Simulizi: Lisa

Simulizi: Lisa

LISA KITABU CHA NANE (8) SIMULIZI........................LISA KURASA..................361 - 365
PRESENT: SIMULIZI ZA DULLY

Sura ya: 361
Jua la mchana la uvivu liliangaza kutoka dirishani na kuangukia kwenye sura nzuri ya Lisa.
Akainama kutazama simu yake na kutabasamu kwa upole. Hata sauti yake ilikuwa laini. “Kwa hiyo mtashukia Dar es Salaam?”
"Ndiyo mpenzi, nimepata ndege ya moja kwa moja." Pamela alijibu upande wa pili wa simu. “Unaweza kutusubiri Nairobi. Sitakaa sana Dar, ni siku moja au mbili tu.”
“Hapana. Nitaenda kuwapokelea Dar, ni siku nyingi hata hivyo sijaenda kwenye jiji la nyumbani.” Lisa alinyamaza na kuinua kichwa chake, akionekana kuwa

katika hali nzuri. “Msafiri salama, utawapa hai hao malaika wangu.”
•••
Ndege kutoka Marekani ilitua kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Airport, majira ya saa tatu usiku. Lisa alisubiri kwa zaidi ya dakika kumi kabla ya kumuona Pamela akitoka akiwa na wapenzi wake wawili.
Lucas alikuwa amevaa shati la rangi ya bluu la mtindo wa Kiingereza. Ingawa mwili wake ulikuwa mdogo, sura yake ndogo iliyopendeza kupita kiasi iliwafanya watu waliokuwa wakipita hapo kumtazama.
Kwa upande wa Suzie alikuwa amekaa juu ya sanduku alilokuwa akiburuta Pamela. Mabutu yake mawili ya nywele kichwani yaliyumbayumba kwa

kupendeza. Watoto hao wawili walipomwona Lisa, walifurahi sana. Suzie aliruka chini mara moja kutoka kwenye sanduku na kumkimbilia kwa furaha.
“Mama, mama...”Suzie akaruka mikononi mwake mara moja, na kumganda mama yake kama luba.
Moyo mdogo wa Lisa ulilainika na machozi yalikaribia kumtoka. Tangu wazaliwe, hakuwahi kutenganishwa na watoto hao wawili kwa muda mrefu.
“Mama.” Lucas alijizuia zaidi, lakini macho yake pia yakawa na machozi.
"Sweetie, njoo hapa." Lisa alinyoosha mikono yake na kuwakumbatia.
"Jamani, ni bora kuwa na watoto wangu

wa kuzaa mwenyewe. Yaani mlipomwona mama yenu tu mimi tena basi,” Pamela alitania, “Mimi nawanunulia peremende kila siku lakini mnanisahau mara tu mnapomwona mama yenu.”
Suzie aliukunja mabega yake. “Godmother, fanya haraka na wewe uzae watoto tupate kaka na dada mdogo.”
“Asante kwa baraka.” Pamela alipiga kelele.
Lisa alisimama na kutabasamu. “Pole kwa safari na karibu tena nyumbani. Nimewaandalia chakula kitamu sana cha jioni. Nisingekuwa na watoto tungeanzia bar”
Pamela akacheka. "Hakika, twende."

Pamela alipokuwa anataka kuondoka ghafla sauti ya mshangao ikasikika nyuma yao.
“Pamela, ni wewe?” Ingawa ilikuwa imepita miaka mitatu, bado aliikumbuka vyema sauti hiyo.
Pamela aligeuka na kuwaona Patrick na Linda wakitoka nje ya geti.
Baada ya kutengana kwa miaka mitatu, Patrick alionekana mtu mzima zaidi na alionekana mpole kuliko hapo awali.
Kwa upande wa Linda, hakuwa amebadilika sana. Alikuwa amevaa tisheti nyeupe na sketi iliyofika magotini. Mikono yake miwili ilikuwa imeuzunguka mkono wa Patrick kiundani. Ilikuwa wazi kwamba walikuwa wapenzi.
Hata hivyo, Patrick alionekana

kumsahau Linda aliyekuwa pembeni yake na kumtazama tu Pamela bila kupepesa macho. Jeans yake ya rangi ya blue mpauko ilifafanua vyema miguu yake minene iliyonyooka, na mwili wake wa juu ulifunikwa na fulana nyepesi ya kijivu. Shati la drafti lilikuwa limefungwa kwenye fundo kwenye kiuno chake, likifunua kiuno chake kidogo.
Ngozi yake ilizidi kung’aa kwa weupe wa asili na nywele zake zilikusanywa nyuma ya kisogo na kufungwa kufichua mashavu yake yenye dimpozi. Macho yake yalikuwa makubwa na yenye kung’aa, yalimfanya aonekane mtu wa makabila mchanganyiko. Miaka mitatu ilikuwa imeacha alama kwenye uso wake, lakini ilimfanya kuwa kijana zaidi na mrembo.
Patrick alionekana kusahau mpaka

kupumua. Kando yake, Linda alisema kwa mshangao, “Pamela, ni wewe kweli. Umerudi? Tulikuwa na wasiwasi sana juu yako wakati huo tulipoona picha na video zako chafu mtandaoni. Uko salama?"
Patrick aliganda. Ndio, sasa alikumbuka. Miaka mitatu iliyopita, kulikuwa na habari kwamba Pamela alijirahisisha kwa Thomas Njau. Kisha Thomas alimfanyia mambo ya kisodoma na kurekodi video ambayo aliisambaza mtandaoni kwa watu kuona. Japo video hiyo haikuwa na uthibitisho wa kutosha kwamba aliyekuwa akifanyiwa kitendo hicho ni Pamela, teknolojia ilifanya kazi yake na kuuaminisha umma kuwa mwanamke huyo alikuwa ni Pamela. Habari chafu mara nyingi husambaa haraka, ndiyo maana tukio hilo la Pamela lilienea kwa kasi.

Muda mfupi baadaye, kulikuwa na habari kwamba alienda ng’ambo ili kukwepa aibu iliyomkuta. Macho ya Patrick ghafla yalijawa na karaha na tamaa.
Pamela kiasili hakuonyesha mabadiliko yoyote machoni mwake, akacheka tu na kusema. “Linda, unanipaka chumvi kwenye vidonda vyangu mara tu unaponiona, kwani hakuna habari nzuri za kuongelea hadi ukumbushie tukio baya kama hilo? Bado wewe ni wa ajabu tu kama zamani."
Sura ya Linda ilibadilika kidogo huku akijifanya ameziba mdomo kujionyesha kuwa amejawa na hatia. "Samahani-"
“Usiombe msamaha,” Patrick alisema kwa upole, “Kwa kuwa ulithubutu

kufanya mambo kama hayo, kwanini unachukia yakiongelewa na wengine?”
Pamela aliinamisha kichwa chake. Huyu ndiye mwanaume ambaye hapo awali alikuwa akimpenda sana. Lakini, kwa sababu tu ya habari za uwongo, angeamini uwongo wa Thomas kuliko yeye.
Lisa hakuweza kujizuia. “Patrick Jackson, Pamela alikuwa nawe kwa muda mrefu lakini bado humfahamu vya kutosha?”
“Namfahamu vizuri sana.” Patrick alisema kwa dharau. “Nilipokuja kumtafuta mara ya kwanza huko Nairobi, alimbusu mwanaume mwingine hadharani tena mbele yangu. Ni wazi kwamba mtindo wake wa maisha umekuwa mchafu baada ya kufika

huko.”
"Patrick, usiseme hivyo." Linda akahema. "Pamela huenda alikuwa akijaribu kukukomoa wakati huo. Thomas Njau ni Mkurugenzi wa Kampuni kubwa tu, hata hivyo. Huenda alikuwa akijaribu kutafuta mtu aliye na hadhi ya juu ili akuonyeshe, lakini iliishia... kumrudisha nyuma. Hata hivyo, Pamela, nataka kukukumbusha. Wakati mwingine unapotafuta mwanamume, bado unapaswa kuzingatia tabia yake.”
Pamela alitumbua macho kwa kuchukia. “Uko sahihi. Sikuangalia tabia ya mtu wakati wa kupata mpenzi wangu wa kwanza. Wakati huo, nilisema kwamba rafiki yake wa utotoni ambaye aliendelea kumsumbua alivutiwa naye, lakini hakuniamini. Tazama sasa. Kwa

kweli waliishia kuwa wapenzi."
Uso wa Linda ulijawa na aibu, akamtazama Patrick ambaye naye alikosa cha kusema.
Pamela aliinama chini na kusema, “Nilimwambia mpenzi wangu huyo wa kwanza kuhusu hilo lakini alinilaumu na kusema hakuna kinachoendelea. Sasa nikifikiria juu yake, kwa kweli najilaumui sana. Nilipaswa kuondoka mapema. Badala yake, niliishia kuchelewesha uhusiano wa kimapenzi wa mtu fulani kwa miaka mingi sana. Mimi ni mjinga sana."
Rangi kwenye nyuso za Patrick na Linda zilibadilika mfululizo.
Linda aliuma mdomo wake na kusema kwa hatia, “Pamela, umeelewa vibaya. Amini usiamini, sikuwa na hisia zozote

na Patrick wakati huo, lakini baada ya wewe kuondoka, nilihisi kwamba alikuwa na huzuni sana. Baadaye, nilipokuwa nikimriwadha, sikuweza kujizuia kumpenda.”
“Huzuni?” Pamela alipigwa na butwaa.
“Ndiyo, nilikuwa na mfadhaiko sana.” Patrick alisema kwa sauti ya chuki. “Nilitapeliwa na mwanamke mnafiki kama wewe kwa miaka mingi sana,”
Pamela alishtuka sana hata ubongo wake ulikuwa umevurugika. "Pia nilikuwa kipofu kabisa kwa kupoteza miaka mingi ya maisha yangu na mtu wa kuchukiza kama wewe. Hapo zamani, nilifikirije kuwa wewe ni mpole na mwenye upendo? Nilikuwa kipofu kabisa.”

Pamela hakuweza kuwa na wasiwasi tena na akamshika mkono Lucas na kuondoka.
"Subiri, huyo ni mtoto wako?" Patrick akatazama kwa udadisi.
Pamela alitaka kukiri kwamba alikuwa mtoto wake, lakini Lucas alizungumza kabla yake, “Yeye ni aunty yangu.”
Linda alisema, “Sijawahi kusikia habari za Forrest kufunga ndoa. Je, ni mwanae wa haramu?”
Sura ya: 362
“Oh jamani, mmesahau? Mtindo wangu wa maisha ni mbaya sana, hivyo ni kawaida kwangu kupata mtoto mmoja au wawili wa haramu,” Pamela alitabasamu na kucheka.

Lakini, uso wa Patrick ulibadilika sana. “Ni kweli ni mwanao wa haramu?”
“Mjinga wewe,” Lucas alimdhihaki, “zaa na wewe wa kwako umwite mtoto haramu, mimi siyo mtoto haramu!”
“Unasemaje wewe mtoto? Nitakufinyaaa!” Patrick alikasirishwa na maneno ya yule mtoto na kukaribia kumshika.
"Jaribu tu kumwekea mkono wako uone." Pamela alishika mkono wake.
Patrick ambaye alikuwa mrefu kuliko yeye alishangazwa na maumivu ya mkono wake. Akamkazia macho Pamela, lakini alimtazama tu kwa dhihaka. Alipatwa na mshtuko kidogo alipokumbuka kwamba alikuwa akimwangalia kila mara kwa

kumwabudu. Moyo wake ulimuuma ghafla.
“Patrick Jackson, natumai kwamba tutakapokutana tena wakati ujao, usithubutu hata kunisalimia. Watu husema kwamba mapenzi ya kwanza ni mazuri, lakini mimi nakuona unachukiza kama nzi.” Pamela aliuachia mkono wake na kuondoka na Lisa.
Walipotoka, Patrick aliendelea kumtazama nyuma. Alimchukia waziwazi, lakini miaka yote hii, hakuwahi kufanikiwa kumfuta moyoni mwake.
“Patrick, uko sawa?” Linda kwa haraka akaja na kumshika mkono huku akimtazama kwa karibu.
"Si chochote." Patrick alikuwa hayupo.

Linda alipomuona hivyo alichukia kwa siri.
Ndani ya gari. Lisa alicheka akisema, "Patrick bado anakupenda sana. Bado aliendelea kukutazama tulipoondoka."
"Kwa hiyo?" Pamela alichungulia dirishani. “Baada ya tukio la Thomas, kila mtu alinisuta na kunisema sana. Huyu mpenzi wangu wa zamani pia alinitumia ujumbe akisema sijiheshimu.”
“Usijali Pamela. Sisi sote tumeteseka kwa kitu kimoja. Sote wawili tulikumbana na wahuni kwenye mapenzi yetu, wewe Linda na mimi ni Sarah” Lisa alilalamika.
“Hakika. Sitarudia tena makosa." Pamela alijipa moyo. Alikataa kuwa na

bahati mbaya hivyo tena.
"Sawa, natumai utakuwa bora kuliko mimi," Lisa alisema kwa dhati.
“Godmother, usijali. Ukishindwa kupata mwanaume mzuri, nikikuwa mkubwa nitakulinda,” Lucas alisema kwa uvivu.
"Lucas wangu ni mtu mtamu sana." Lisa alimkumbatia na kumpiga busu, na kufanya masikio yake kuwa mekundu.
"Mama, mama, na mimi nataka pia." Suzie alimkumbatia na yeye pia akataka busu.
“Kwanza kabla ya yote shosti nimezikumbuka kweli chipsi vumbi za uswazi na nyama za kuku, tuanweza kuzipata wapi sasa hivi?” Pamela aliuliza ghafla.

“Muda wowote unapata, lakini nyumbani nimewandalia chakula cha jioni kitamu sana...” Lisa alimwambia.
“Sawa, tupite uswazi basi nichukue hata vimiguu vya kuku tu kupoza hamu hamu.” Pamela alisisitiza.
Lisa akawapeleka sehemu moja huko Msasani. Hapo palipatikana kila aina ya chakula cha uswahilini, haswa chpisi, mishikaki, nyama za kuku, mihogo na vingine kama hivyo.
Wale watoto wawili walifurahia sana chipsi na nyama za kuku. Walikula na kujilamba hadi matumbo yao yakakosa nafasi kabisa.
Suzie aliinua mdomo wake mdogo mwekundu na uliojaa mafuta, na mkononi akiwa ameshikilia vipapatio

vya kuku vilivyokaangwa, akisema, “Hatimaye ninaelewa kwa nini Godmother huzungumza kila mara kuhusu chakula cha nyumbani, kumbe ni kitamu hivi?”
“Ni kitamu eeh?” Lisa aliuliza akitabasamu kwa bintiye.
“Ni kitamu sana. Sitaki kurudi Marekani tena. Nataka kubaki hapa na kula chipsi na kuku kila siku.” Suzie alisema huku akilazimisha kubugia vipande vya chipsi vilivyojazwa tomato sauce.
“Sawa mwanangu.” Lisa alihisi maumivu ya moyo.
"Sitaki kurudi pia," Lucas alisema kwa uso uliotulia,mdomoni akiwa amerundika minofu ya kuku wa kukaangwa. "Nataka nikae na wewe

nikulinde."
Sauti za watotowale zilimfanya Lisa acheke, lakini akasema kwa uzito, “Hamtaweza kukaa huku mkiwa bado wadogo. Baba yenu akiwajua atawaiba na kuwapeleka mbali na mimi, au nyie mnapenda kwenda kukaa na mama mbaya wa kambo?”
"Ndio," Pamela aliyekuwa busy muda mrefu akifakamia nyama za kuku wa uswazi alisema ghafla, "Mama yenu anawapenda sana, lakini baba yenu ni mhuni, hana huruma kabisa."
Watoto hao wawili waliinamisha vichwa vyao, wote wawili wakiwa kimya kwa muda.
Baada ya kumaliza kula, Lisa aliwapeleka Masaki, mtaa wa Buzwagi

ambako alinunua lile jumba la kifahari la Alvin siku za mwisho kabla hajaondoka kwenda Nairobi. Jumba lilikuwa kubwa na tulivu na muda wote lilikuwa likitunzwa na Jumbe, kijana wa kazi ambaye muda wote aliliweka jumba hilo katika mazingira nadhifu.
Siku inayofuata, Lisa aliamka mapema na kuandaa kifungua kinywa cha kupendeza kwa wapenzi wake wadogo.
"Wapenzi, mama atapumzika pamoja nanyi leo. Baadaye nitawapeleka beach kwenye uwanja wa michezo, sawa?" Lisa alisema kwa upole.
“Sawa.” Suzie akawa na furaha.
"Mama nataka uninunulie mpira." Lucas alisema aliokuwa akichungulia dirishani kwenye bustani kubwa iliyokuwa nje.

"Unavyotaka mwanangu."
Muda huohuo, Pamela alitoka nje ya chumba cha wageni akiwa amevalia nguo za kupendeza. Alijipaka vipodozi vyepesi usoni, na nywele zake ndefu zilishuka mabegani mwake. Alikuwa amevalia viatu vya visigino virefu."
"Watoto wangu, ninaonekana mrembo?" Pamela akasogea kwenye meza ya chakula
Suzie alipiga makofi. “Wewe ni mrembo sana. Wewe ni mzuri kama yule mwanamke anayeimba kwenye tv."
“Ooh! Msichana wangu wewe ni mzuri sana. Nitakuzawadia chokoleti." Pamela alitupa kipande cha chokoleti juu.

Lisa alimtazama Pamela kwa jicho la kumsifia pia na kuchombeza. “Kama usingesema kuwa unaenda kuhudhuria kongamano linalofanywa na SE Group, ningefikiria kuwa unaingia kwenye shindano la urembo.”
"Unajua nini? Nimesubiri wakati huu kwa muda mrefu sana. Tukio la leo ni muhimu sana kwangu kuanza zoezi langu la kulipiza kisasi kwa Rodney Shangwe wa Osher Corporation. Alinifukuza hapo awali, lakini hah! Siwezi kusubiri kuona macho yake ya huzuni na majuto sasa,” Pamela alisema huku kichwa chake kikiwa juu.
“Sawa, fanya haraka kula. Ondoka ukimaliza, usije ukaachwa na ndege.” Lisa alisema huku akizuia kicheko.
“Ni masaa mawili tu kutoka Dar hadi

Nairobi. Mkurugenzi wa SE Group ametuma ndege binafsi kuja kunichukua, sina presha. Kongamano halitakuwa na maana ikiwa mimi sitahudhuria.” Pamela alijigamba.
•••
Katika Jumba la kifahari la Rodney Shangwe.
Baada ya mpishi kutoa kifungua kinywa, msaidizi wa Rodney alimpa ratiba na kusema, “Bwana Shangwe, mwanakemia wa kimataifa wa vipodozi, Nicole, atakuwa akizungumza jukwaani kwa ajili ya kongamano la SE Group saa saba mchana wa leo. Ungependa kwenda? SE Group imetuma mwaliko.”
Rodney alikunja uso na kukoroma. "Huyu jamaa, Bwana Erick Malugu, ameweza kumwalika Nicole?"

“Ndiyo.” Msaidizi akapumua. "Lakini, Nicole ni wa kushangaza sana. Tumemwalika aje Kenya mara nyingi sana lakini amekuwa akikataa kila mara. Nilifikiri kwamba haipendi Kenya, lakini sikutarajia angekubali ghafla kuja wakati SE Group, mpinzani wetu kibiashara, alipomwalika. Osher ipo juu kuliko SE katika kiwango cha hadhi na brand. Watu wenye akili wangechagua kushirikiana nasi badala yake.”
Rodney alikitumbukiza kichwa chake katika mawazo mazito. "Je, Nicole amesaini mkataba wa ushirikiano na SE?"
"Hapana, lakini inasemekana kwamba Nicole anakuja Kenya wakati huu kutia saini mkataba na SE. Nilisikia kwamba ana fomula ya kipodozi cha kuzuia

kasoro za ngozi na kuimarisha ngozi mikononi mwake. Itakuwa shida ikiwa zitanunuliwa na SE. Baada ya yote, bidhaa zilivumbulia na Nicole miaka hii zimekuwa bidhaa maarufu ulimwenguni kote na hadi 80% ya watumiaji wanarudi kununua bidhaa hizo tena.”
Baada ya kuambiwa hayo, Rodney alihisi kuudhika. "Wataalamu wa vipodozi katika kampuni yetu wote hawana maana. Tunawekeza pesa nyingi sana kwao kila mwaka, lakini hawajawahi kufanya chochote cha kuridhisha.”
Msaidizi wake alikunja midomo yake na kusema, “Mkurugenzi wa Idara ya utafiti na maendeleo humsifia kila Pamela Masanja, mwanamke aliyewahi kufanya kazi Osher miaka minne iliyopita. Alikuwa na kipaji kikubwa, lakini inasikitisha kwamba—”

"Nyamaza." Rodney alimtazama msaidizi wake kwa ukali. “Pamela Masanja ni mwanamke asiyefaa. Hakuna kitu cha kusifia juu yake. Wataalamu wa vipodozi kama yeye wanaweza kupatikana kote nchini. Sitaki kumsikia!”
"Hiyo ni sawa. Pamela Masanja hakika hayuko kwenye kiwango sawa na Nicole.” Msaidizi alikubali kwa kichwa alipoona bosi wake akiwaka.
"Hata iweje, hatuwezi kuruhusu Nicole kushirikiana na SE Group." Rodney aliinuka ghafla. “Nipatie hiyo kadi ya mwaliko. Nitaenda kwenye kongamano la SE na kukutana na Nicole mimi mwenyewe. Nikienda kibinafsi, bila shaka atalazimika kunionyesha heshima fulani.”

Sura ya: 363
Katika hoteli ya nyota tano. Sankara Nairobi. Saa sita adhuhuri.
Baada ya Rodney kukabidhi kadi ya mwaliko na kuingia, Bwana Erick Malugu wa SE Group alimkaribisha kwa furaha. “Bwana Shangwe, karibu, karibu sana. Nilijua utakuja leo. Nilisikia kwamba Osher Corporation ilikuwa imemwalika Nicole mara kadhaa lakini siku zote ilikataliwa, kwa hivyo sikuwa na matarajio mengi nilipomwalika. Lakini ni nani aliyejua kwamba angekubali kwa urahisi?”
“Hongera sana, Bwana Malugu." Rodney alitabasamu vibaya. "Lakini

anakuja tu kuhudhuria kongamano, sio kushirikiana na wewe. Usisherehekee haraka sana, Bwana Malugu.”
“Hiyo ni kweli. Lakini Nicole pia amekubali mwaliko wangu usiku wa leo ambapo tutazungumza kuhusu fomula fulani ya kipodozi adimu.” Bwana Malugu alicheka. “Samahani, Bwana Shangwe. Ikiwa tutapata fomula hiyo, mauzo ya bidhaa zetu kwa nusu ijayo ya mwaka hakika yatapita yako."
Midomo ya Rodney ikatetemeka. Bwana Malugu akampigapiga begani. "Lakini Bwana Shangwe, hautajali, sivyo? Familia ya Shangwe ina viwanda vingi sana. Hata kama Osher Corporation itapotea, bado una kampuni nyingi katika tasnia zingine unaweza kuchukua. Tunaweza hata kuwa washirika wakati huo."

Rodney alikunja uso kwa ukali, uso wake mzuri ukasinyaa na kuwa mbaya ghafla. Ndiyo, familia ya Shangwe ilikuwa katika viwanda vingi, lakini wakati huo huo, familia ya Shangwe ilikuwa na watoto wengi na wajukuu. Osher Corporation pekee ndiyo ilikuwa mikononi mwake. Kama ingemfia, hakuwa na jeuri ya kudai kampuni nyingine kutoka kwenye familia yao. Ikiwa kampuni ingemfia mikononi mwake, angechekwa na familia zingine za Shangwe. Ilibidi ampate Nicole.
Kama mgeni muhimu wa kongamano la siku hiyo, Nicole angetokea tu wakati muhimu. Saa saba kamili mchana, mwenyeji alipiga makofi.
“Tumkaribishe mwanakemia mahiri wa vipodozi kutoka Marekani, Nicole. Nicole haitaji utangulizi. Akiwa na umri

wa miaka 25, alifundishwa na Mwalimu Simpson, mtu ambaye alianzisha tasnia ya urembo wa anasa. Leo, Nicole anafanya kazi na brand nyingi za juu za kimataifa. Mwaka jana, lipstick zake za mfululizo wa Sapphire alizobuni zilivunja rekodi kwa mauzo ya kimataifa."
Chini ya macho ya umati, mwanamke aliyevaa nguo ndefu ya kifahari alijongea kwenye jukwaa la ukumbi wa ‘The Kenyatta International Conference Centre’. Mwanamke huyo alikuwa na sifa maridadi, pua iliyonyooka, na macho yaliyoeleweka vizuri. Alionekana mzuri na mrembo kama waridi linalochanua.
Rodney aliminya kwa nguvu glasi ya maji iliyokuwa mkononi mwake, na kusababisha maji kumwagika na kulowesha mkono wake. Hata hivyo, hakutambua hilo. Hakutarajia kamwe

kuwa Nicole, mwanakemia maarufu wa vipodozi angekuwa... Pamela Masanja. Alikuwa ni mwanamke ambaye aliwahi kumdharau. Maneno ya kiburi aliyokuwa ameyasema asubuhi ya siku hiyo yalionekana kumpiga usoni.
Akiwa jukwaani, macho ya Pamela yalimtoka kabla ya kumwangukia kila mtu. Kwa tabasamu, alisema, “Halo watu wote. Mimi ni Nicole, ninayejulikana pia kama Pamela Masanja.”
Watazamaji walisimama, wakalikumbuka jina hilo la kawaida.
“Ndiyo, niliwahi kufanya kazi kama mkemia wa vipodozi katika kampuni ya Osher, lakini haikuchukua muda Osher kunishutumu kwa wizi na utovu wa nidhamu. Walinifungia kuajiriwa na

kampuni zote za vipodozi nchini. Kimsingi sikuweza kupata kazi nchini wakati huo.”
Pamela alitabasamu huku akiongelea maisha yake yaliyopita. Alimtazama Rodney ghafla. "Bwana Shangwe, baada ya miaka mitatu, najiuliza ikiwa bado unaamini kuwa kweli nilikuibia? Ikiwa ningefanya hivyo, ningekuwa na hadhi niliyo nayo leo?"
Kila mtu mara moja akamtazama Rodney. Kila mtu aliyekuwepo alikuwa aidha ni mkurugenzi wa kampuni fulani au mtendaji wa ngazi za juu. Wote walielewa kuwa huo ulikuwa mchezo wa kitoto kwa Bwana Rodney kumkandamiza mkemia mdogo wa vipodozi.
Isitoshe, ikiwa Pamela aliiba kweli,

angewezaje kuwa mwanakemia mkuu wa vipodozi na maarufu? Watu walitegemea nguvu ya kusema.
Akiwa ametazamana na umati wa watu, Rodney alikunja ngumi zake kwa siri zilizokuwa kwenye magoti yake. Uso wake mzuri ulikuwa karibu kugeuka majivu. “Sikuwa na habari nyingi kuhusu matukio ya mwaka huo. Labda... watu walio chini yangu walinipa taarifa potofu.”
Baada ya muda, Rodney aliweza tu kuweka uso wa ujasiri na kuelezea. 'Ndio hivyo?"
Pamela alitabasamu kwa utamu na kusema kwa sauti ya mzaha,
“Bwana Shangwe, uamuzi wako wa kunifukuza na kunifungia miaka minne iliyopita uliniumiza sana. Lakini sina budi kukushukuru. Ulikuwa kikwazo

kwenye njia yangu ya mafanikio. Kama si wewe, nisingekutana na Mwalimu Simpson baada ya kuondoka nchini.”
Kisha, Pamela akaachana na Rodney na kuingia kwenye kiini cha kongamano. Alizungumza kuhusu baadhi ya utaalamu wake juu ya bidhaa za vipodozi.
Hapo awali Rodney hakutaka chochote zaidi ya kumpiga teke, lakini kwa sababu fulani, kadiri alivyokuwa akisikiliza, ndivyo alivyokuwa akivutiwa zaidi. Ilibidi akubali kwamba Pamela Masanja alikuwa na uzoefu na ujuzi. Kwa kweli alikuwa bora zaidi kuliko wanakemia wa vipodozi katika kampuni yake.
Mwishoni mwa kongamano, mwandishi wa habari ghafla alisema, "Bi. Masanja,

nakukumbuka. Miaka mitatu iliyopita, tukio lako na Thomas Njau lilizua gumzo kubwa. Nilisikia kwamba ulijilahisisha kwa Thomas—”
Uso wa Bwana Malugu ulibadilika huku akimkodolea macho mwandishi huyo. "Unatoka wapi? Usizungumze ujinga.”
“Ninasema ukweli. Tukio hilo liliibua hisia wakati huo. Bi Masanja alinajisiwa na Thomas Njau na kupelekwa hospitalini,” mwanahabari alisisitiza kauli yake kwa nguvu.
Umati wa watu uliingiwa na kizaazaa, na macho yao walipomtazama Pamela nayo yakawa ya ajabu.
Tabasamu zuri usoni mwa Pamela likabaki. Alinyanyua miguu yake mirefu na kushuka kutoka jukwaani kwa

utulivu, akimsogelea mwandishi huyo hatua kwa hatua bila hata chembe ya woga machoni mwake.
“Mara zote mimi husema kwamba wanawake lazima wajitahidi kujitegemea. Wakati msimamo wako ni wa chini sana na hata kama hujawahi kufanya chochote kibaya, unapokutana na mtu anayetegemea mamlaka na watu wenye nguvu nyuma yake ... mkosaji ambaye huwadhalilisha na kuwadhulumu wanawake atakuwa mwathirika mwishowe."
“Bi. Masanja, unamaanisha kusema...” Kulikuwa pia na waandishi wengine ambao walisimama polepole na kuuliza.
Pamela alisema kwa upole, “Huu ndio ukweli nyuma ya kile kilichotokea wakati ule. Nilimkataa Bwana Njau mara nyingi

aliponinyemelea, kwa hiyo aliweka kinyongo na kunivamia ndani ya nyumba yangu. Alinipiga kwa nguvu kwa nia ya kunibaka. Kwa bahati nzuri, rafiki yangu alifika kwa wakati.
“Ingawa nilikuwa sawa, mimi na rafiki yangu tulijeruhiwa na kulazwa hospitalini. Kama mnavyojua, dada mdogo wa Thomas Njau anaungwa mkono na Mwenyekiti wa KIM International. Dada wa Thomas anakaribia kuolewa katika familia ya Kimaro hivi karibuni. Wakati huo, ningewezaje kushindana na familia ya Kimaro?”
Mwandishi alifoka, "Kwa maneno mengine, unajaribu kusema kuwa ni Bwana Kimaro aliyemuunga mkono Thomas Njau na kukuundia kashfa?"

Pamela alisema kwa unyonge, “Ikiwa huniamini, unaweza kuchambua mambo mengine yote ambayo Thomas Njau amekuwa akijihusisha nayo kwa miaka mingi. Miaka iliyopita, mwanafunzi wa chuo kikuu alilazimika kujiua baada ya kubakwa na Thomas. Mwishowe, Thomas alimtegemea dada yake mdogo na akaondoka mahakamani bila hatia.
"Miaka hii michache, pia alikuwa amelazimisha wanawake wengi kutoa mimba. Hadi sasa, hakuna mtu kutoka kwa familia yenye heshima ambaye yuko tayari kuolewa naye. Ningewezaje kupenda kipande cha takataka kama yeye?"
Kila mtu alivuta pumzi ya baridi. Wote walijua kuwa mdogo wa Thomas Njau alikuwa karibu kuolewa na Alvin Kimaro. Maneno ya Pamela yalikuwa ni sawa na

kumwita Alvin takataka.
Rodney hakuweza tena kujizuia. "Pamela Masanja, ninakusihi uangalie maneno yako. Usifikiri kwamba wewe ni mtu asiyeweza kuguswa kwa kuwa sasa unajulikana katika tasnia ya vipodozi.”
Sura ya: 364
“Ninasema tu ukweli kuhusu mwaka huo. Kuna uhusiano gani na mimi kutoguswa?" Pamela alijibu huku akicheka.
“Unathubutu kusema mbele ya kila mtu kwamba Thomas Njau ni muungwana, Bwana Shangwe? Sahau, neno 'muungwana' ni kubwa na tata sana. Wacha tutumie neno "heshima". Je, Thomas ana heshima hata hivyo?"

Rodney aliwekwa njia panda. Kila mtu aliifahamu tabia ya Thomas. Rodney angekuwa tayari kushusha hadhi yake na kusema kwamba Thomas Njau alikuwa na tabia nzuri? Kwa kweli asingeweza kusema, huvyo. Kwa kweli, hakuwahi kukutana na mtu mchafu kama huyo hapo awali. Ikiwa sio kwa ukweli kwamba alikuwa kaka yake Sara, angeweza hata kumkana kwamba hamjui.
Pamela alitabasamu na kucheka kwa furaha moyoni mwake. Alikuwa akifanya kazi kwa bidii katika miaka mitatu iliyopita ili kulipa fedheha zote
alizopitia wakati huo.
Lisa hakuwa peke yake aliyeshikilia chuki za nyuma; Pamela pia.
Ni wazi alikuwa mwathirika katika tukio

hilo la Thomas lakini kashfa zikamgeukia yeye kwa kuitwa majina machafu. Hakupenda. Popote alipoenda, alinyooshewa vidole. Hata watu wealiomuheshimu hapo awali aliokuwa akiwasiliana nao walianza kumtumia meseji katikati ya usiku, wakiuliza ingegharimu kiasi gani kulala naye kwa usiku mmoja.
Alipoondoka, alikuwa kama mbwa mnyonge aliyepotea, lakini sasa ulikuwa wakati wa yeye kurejesha tena hadhi yake katika jamii hatua kwa hatua.
Pamela kwa mara nyingine tena aligeukia kipaza sauti cha mwandishi na kusema, “Ni vizuri kwamba umegusia tukio la Thomas Njau. Ngoja nimtangazie Thomas kuwa nimerudi! Uliponitisha wakati huo, niliweza tu kumeza maneno yangu, lakini ukweli utafichuliwa mapema au baadaye.”

Kisha akageuka na kuondoka.
Rodney pia alionekana kupotea katika mawazo kwa muda. Alipochukua hatua kubwa kujaribu kumfuata, Bwana Malugu alimzuia. "Bwana Shangwe, tangu ulipomfukuza talanta kama Bi. Masanja miaka mitatu iliyopita, anakuchukia sana. Usimfuate tena. Nadhani hataki kukuona pia.”
“Ondoka njiani,” Rodney aliamuru huku akiwa na uso wa mkali.
"Fomula iliyo mikononi mwa Bi. Masanja itakuwa ya SE Group." Bwana Malugu alimtazama machoni bila kukata tamaa. Katika kura ya maegesho kwenye ghorofa ya kwanza ya basement ya hoteli.
Gari la michezo lilikuja.

Katika maegesho ya magari kwenye ghorofa ya kwanza ya basement ya hoteli.
Gari la kifahari likajongea. Pamela alifungua mlango wa gari na kukaa kwenye kiti cha abiria. Mara tu baada ya kufunga mkanda alipokea simu ya video kutoka kwa Lisa.
Hapo hapo Suzie alikandamiza midomo yake kwenye na kumbusu. “Godmother, wewe ni mzuri sana. Umeongea vizuri sana."
“Mmeona?” Pamela alishangaa kwa furaha.
"Kulikuwa na matangazo ya moja kwa moja." Lisa akajitokeza kwenye simu yake. "Ingawa si watu wengi walioitazama, habari zitaenea polepole."

"Hakika nitalipiza kisasi kwa kile kilichotokea mwaka huo." Pamela aliuma mdomo. “Simuogopi Thomas Njau. Ni kwamba Alvin Kimaro, ambaye yuko nyuma yake, anasumbua kidogo.”
“Usijali, chukua muda wako. Hebu tufanye kazi pamoja. Tayari nilimwambia Big V achapishe ulichosema. Sasa ngoja tuone.” Lisa alimwambia kwa furaha. “Rudi Dar mara moja, nimekuandalia chakula.”
Katika sofa walilokuwa wamekaa, Suzie aligeuka na kumnong’oneza Lucas, “Kaka, Alvin Kimaro ndiye baba yetu mchafu?”
“Ndiyo.” Lucas alikunja uso na kutikisa kichwa.

Suzie aliuma mdomo wake na kusema kwa hasira, “Kwanini baba yetu ni mchafu? Alimuumiza Mama, na alimuumiza pia Godmom. simpendi hata kidogo.”
“Hata mimi simpendi.” Lucas tayari alimtambulisha Alvin kama adui yake.
•••
Kile ambacho Pamela alisema kwenye kongamano hilo kilisukumwa polepole kwa vyombo vya habari na Big V, na kwa hivyo, habari za zamani za miaka mitatu iliyopita zilichimbwa tena.
[Namkumbuka huyu binti sasa. Miaka mitatu iliyopita, ilisemekana kwamba alimtongoza Thomas Njau, hivyo alikaripiwa na kila mtu.
Watu hata walimrushia mayai viza wakati anatembea.]

[Anashangaza. Yeye ni mwanakemia maarufu wa vipodozi sasa. Sijui ni kwanini, lakini kwa namna fulani naamini kwamba anasema ukweli. Labda ni kwa sababu yeye ni mrembo.]
[Kwa kweli nilitaka kusema hivi miaka mitatu iliyopita. Tabia ya Thomas Njau kweli si nzuri, lakini hakuna aliyeniamini.]
[Nina jamaa wa mbali ambaye alifanya kazi katika New Era Advertisings na mara kwa mara alitongozwa na Thomas. Mwishowe, alijiuzulu kwa sababu asingeweza kuvumilia tena.]
[Thomas Njau ni fisadi maarufu katika jiji hili. Nilikuwa na mwanafunzi mwenzangu wa chuo kikuu ambaye alivutia umakini wake, lakini alimkataa.

Mwishowe, alimlazimisha kwa nguvu akamsababisha hadi ajiue. Familia yake ilimshtaki, lakini haikufaa. Alitetewa na wakili bora kabisa.]
[Kila mtu anajua kwamba dada yake mdogo ni Sarah Njau.
Anafanya ushenzi tu kwa sababu anajua shemeji yake ni Alvin Kimaro.]
Mambo yalipoanza kuwa mbaya, Hans akaenda kuripoti kwa Alvin. Wakati huo Alvin alikuwa akiongozana na Sarah kujaribu mavazi yake ya harusi.
“Pamela Masanja?” Alvin bila ufahamu alimfikiria Lisa aliposikia jina hilo. Kipindi hicho alikuwa akijaribu kila awezalo kutofikiria juu yake. Hata hivyo, sasa jina la Pamela lilipotajwa, tukio la miaka mitatu iliyopita nalo lilijirudia tena akilini mwake.

"Ndio, inaonekana anataka kufichua ukweli kuhusu tukio la Thomas Njau miaka mitatu iliyopita." Hans Aliitikia na kusema, “Kwa kuwa sifa ya Thomas Njau imekuwa duni miaka hii, maoni yote mabaya ni dhidi yake. Sasa, watu kwenye mtandao... wanazungumza kuhusu Bi. Njau na wewe.”
“Wanasema nini?” Alvin aliuliza kwa uso wa hasira.
"Wanasema unatumia nafasi yako kuwadhulumu wengine."
Alipokuwa akijaribu mavazi ya harusi, sura nzuri ya Sarah ilibadilika aliposikia maneno hayo. Hakuwahi kufikiria kuwa Pamela angetokea tena. Si alikuwa tu mfanyakazi mdogo chini ya Rodney wakati huo? Aliwezaje kurudi tena kwa

nguvu kama Lisa?
Sarah aliuma meno lakini haraka akasema kwa hatia, “Samahani, Alvin. Sikutarajia tukio lile lingeweza kukuletea shida tena, lakini tayari nimeshawahi kumpa onyo kaka yangu kuhusiana na hili. Anajiheshimu sana sasa hivi.”
Hans hakuweza kujizuia kusema, “Lakini... niliona baadhi ya watu kwenye mtandao wakisema kwamba Bwana Njau... mara nyingi huwanyanyasa wafanyakazi warembo katika kampuni.”
Uso mzuri wa Alvin mara moja ukapoa. Sarah alimlaani Hans kwa siri, lakini uso wake ulionyesha huzuni tu. “Kwa kweli sikujua kuhusu hilo. Labda kuna mtu aliajiri watu kutoa maoni hayo... "
“Inatosha. Zuia jambo hilo kwanza.”

Alvin akageuka kumuamuru Hans. “Bila shaka.”
Baada ya Hans kuondoka, Sarah alimshika mkono Alvin. “Alvin, kuhusu suala hili, ni kaka yangu ndiye aliyemkosea Pamela. Vipi kuhusu mimi kumfidia dola milioni moja?”
"Ikiwa unafikiri kweli kwamba alikuwa na makosa, basi mwambie afunge mdomo wake." Alvin alikasirika bila kifani. "Yeye ndiye alikuwa na makosa lakini alikimbilia kwa waandishi na kusema kwamba Pamela alimtongoza. Ikiwa sivyo kwamba yeye ni kaka yako, ningemuua tayari.”
Mwaka huo, pia alikuwa Thomas Njau ambaye alimfanya kupoteza watoto wake kwa njia isiyo ya moja kwa moja.

Alvin alijawa na karaha kwa mwanaume huyo sasa.
Sarah alishtushwa na hasira iliyokuwa machoni mwake, na macho yake yakawa mekundu huku akiomba msamaha kwa haraka, “Samahani, ni kosa langu. Sikupaswa kuwa mbinafsi na kukuomba umwokoe kwanza.” “Sahau, si kosa lako. Hata hivyo, siku za usoni, sitajali iwapo ataishi au kufa tena,” Alvin alisema kwa kuudhika.
“Sawa.” Sarah alizuia machozi yake. "Alvin, je! vazi hili la harusi linanipendeza?"
Alvin alimtazama kwa kawaida na kutikisa kichwa. "Tutanunua hili." Kisha, akatoka nje. Kwa sababu fulani, alihisi kwamba ikiwa nguo hiyo ingevaliwa na Lisa badala yake,

ingekuwa nzuri zaidi.
Sarah alimtazama yule mtu wa nusu nusu na kukanyaga mguu wake kwa hasira.
Sura ya: 365
Wakati huo huo, Thomas alimpigia. "Sarah, yule b*tch Pamela Masanja amerudi. Wakati huu, hakika nitammaliza!”
Uso mrembo wa Sarah mara moja ukaangaza kwa mguso wa karaha. "Funga mdomo wako. Huu ni wakati mgumu kwani nitafunga ndoa na Alvin hivi karibuni. Usiniletee balaa.”
Thomas alishtushwa na karipio la ghafla. "Lakini haukuona alichosema

Pamela kwa waandishi wa habari"
“Alvin tayari ameweka mtu wa kuzima jambo hilo. Ikiwa una kinyongo, basi subiri baada ya harusi yangu.” Sara alisema neno baada ya neno, “ ikiwa kitu kitaenda vibaya, sitakusaidia."
“... Sawa.” Thomas alikata simu bila kupenda, lakini moyoni hakufikiri kwamba jambo lolote lingeharibika. Akageuka, akapiga simu. "Nenda utafute anapoishi huyo b*tch Pamela Masanja."
•••
Katika hoteli ya kifahari ya ‘The Concord Hotel & Suites.’
Mhudumu alimuongoza Pamela na kusimama kwenye mlango wa chumba cha faragha. "Hiki ndicho chumba

ambacho Bwana Malugu alipanga kwa ajili yako."
"Asante." Pamela aliusukuma mlango na kuingia ndani.
Rodney alikuwa ameketi mbele ya skrini ya kale. Alivaa shati la kahawia na vifungo viwili vya kwanza vilikuwa vimefunguliwa. Mikono ya shati ilikuwa imekunjwa, na macho yake yalikuwa makali kwenye uso wake mzuri, na kumpa mtazamo mbaya lakini wa mapenzi.
“Keti.” Akaelekeza kwenye kiti kilichokuwa kando yake.
Pamela hakuweza kuwa na wasiwasi naye na akageuka kuondoka, lakini alipojaribu kufungua mlango, aligundua kuwa umefungwa.

“Usiondoke. Kula. Chakula hakitakuwa na ladha kikiwa cha baridi.”
Rodney aliinuka na kumburuta hadi kwenye kiti. “Bi. Masanja lazima ulijisikia vizuri ulipokuwa ukizungumza kwenye kongamano leo. Nakubali, umenishangaa. Nilikosea juu yako hapo awali. Ninakupa toast hii kama msamaha, sawa? Una furaha sasa?"
Rodney alijimiminia glasi ya mvinyo mwekundu na kuinywa. Pamela aliitazama glasi ya mvinyo iliyokuwa mezani kwa muda kabla ya kwenda kumimina mvinyo ndani yake.
Rodney alifurahi, akifikiri kwamba alitaka kutoa toast, lakini bila kutarajia, aliinua mkono wake na kumwaga mvinyo wote kwenye uso wake mzuri.

"Pamela Masanja!" Uso wa Rodney ulibadilika sana. Alipokaribia kukasirika, Pamela alichukua chupa ya divai, akaifungua kola yake na kumimina vilivyomo ndani ya shati lake. Mvinyo ulikuwa baridi, na kusababisha Rodney kupiga kelele.
Aliruka pembeni na kuvua shati haraka, lakini suruali yake ilikuwa tayari imelowa. Suruali yake ilishikamana kwa nguvu kwenye mapaja yake, ikionyesha mistari ya kuvutia.
"Pamela Masanja, unataka kufa?" Rodney alikasirika. Hakuna mtu aliyewahi kuthubutu kumfanyia hivi. Mwanamke huyu alikuwa mwendawazimu! Anathubutu vipi kummwagia mvinyo?!
Alikuwa amepoa sana baada ya kuvua

nguo zake. Alitetemeka, na kwa macho yake, hakutaka chochote zaidi ya kumla akiwa hai.
Kwa upande mwingine, Pamela alikuwa akitabasamu kwa furaha. “Nilifikiri haujaamka kabisa, kwa hiyo nilikumiminia mvinyo. Rodney Shangwe, nadhani umezoea sana kutetemekewa kwa kuwa bwana mdogo tajiri sana. Hujawahi kunitendea haki hata kidogo. Wakati ule, ili kumsaidia Sarah Njau, ulitamka sentensi ya kawaida ambayo karibu kuharibu maisha ya juhudi zangu. Kama hukunipenda, ungenifukuza tu. Kwanini ulilazimika kunifungia kabisa kwenye tasnia?”
Kadiri alivyozidi kusema ndivyo alivyozidi kupata hasira. Aliivunja chupa, na kusababisha vipande vya chupa kusambaa kila mahali.

Rodney aliruka kwenye kiti kwa woga na nusura ateleze kwenye vipande vya chupa. Baada ya yote, hakuwa amevaa shati. "Pamela Masanja, usifikiri kwamba sitathubutu kukupiga!" Rodney alimfokea.
"Endelea. Hata usiponipiga nitakupiga.” Pamela alitumia uma kuokota kipande cha nyama ambavyo vilikuwa bado vya moto kutoka kwenye sahani na kumrushia Rodney.
Rodney aliitazama jinsi chumba kilivyokuwa kimechafuka kwa fujo za kila aina na kumtisha, "Pamela Masanja, nitaita polisi ikiwa utatupa kipande kingine."
"Endelea. Zaidi sana, nitaambiwa kulipa pesa. Naweza kumudu.” Pamela

alimtupia kila kitu mezani.
Rodney hakuweza kukwepa na aliweza tu kukimbilia kushika mikono ya Pamela. Mikono ya Pamela ilikuwa imezuiliwa, hivyo akageuza kichwa chake na kumng'ata kwa nguvu sikioni.
“Sawa!” Rodney alipiga kelele baada ya kuumwa na kuushika sehemu fulani ya mwili wake bila fahamu. Matokeo yake, alihisi kitu laini mikononi mwake. Alipogundua alichokuwa akikamata, tayari alikuwa amepigiwa goti katikati ya mapaja yake na Pamela. Macho yalimtoka kwa maumivu.
Ghafla, aliweza kuelewa maumivu ya Alvin siku nyingine. Haishangazi alikwenda hospitali kwa uchunguzi. Inaumiza sana.
"Tamu eeh?" Pamela alimtazama kwa

dhihaka. “Yako haina maana hata hivyo.”
"Yangu hayana maana?" Rodney alijikunja kwa maumivu na nusura apoteze pumzi.
“Umewahi kuitumia kwa nani?” Pamela alicheka. “Umejitolea kwa Sarah Njau, lakini ataolewa na Alvin Kimaro hata hivyo. Hatakuwa na nafasi katika maisha yako. Unapaswa kuwa towashi tu. Sijawahi kuona mwanaume mjinga kama wewe.”
"Pamela Masanja, thubutu kusema neno moja zaidi..." Macho meusi ya Rodney yalikuwa yamefunikwa na hasira.
“Nimesema kitu kibaya? Nilishakuambiaga muda mrefu. Wewe ni

mwanaume lakini bado una kelele kuliko mwanamke. Kuwa mwanamke katika maisha yako yajayo basi...”
Kabla Pamela hajamaliza, Rodney alimkimbilia na kumg’ata.
Macho yalimtoka Pamela na bila fahamu akajaribu kumpiga tena goti sehemu zake za siri. Wakati huu, Rodney alikuwa amejiandaa na kubana miguu yake haraka. Pamela alipoteza stepu na mwili wake ukaanguka moja kwa moja kwenye mikono ya Rodney. Wakati huo, sauti ya hasira ya Bwana Malugu ilisikika nje ya chumba akimfokea mhudumu. "Mara nyingi mimi huja kwenye hoteli hii. Siamini kuwa ulimleta mgeni wangu kwenye chumba cha mtu mwingine. Mgeni wangu akipata madhara yoyote, sitakusamehe...”

Ndani ya chumba, Pamela aliogopa na kujitahidi sana. "Rodney Shangwe, niachie!"
"Hapana." Rodney aliuma mdomo wake kwa ukaidi na hakumuachilia.
Pamela hakuwa na chaguo ila kuuma, na kwa sababu hiyo, wote wawili waliangukia kwenye sofa.
Kisha, mlango ukafunguliwa. Bwana Malugu na meneja wa hoteli waliingia ndani haraka. Waliona tukio la shauku ndani na walipigwa na butwaa mara moja.
Bwana Malugu alikasirika sana hadi uso wake ukakunjamana. Rodney alilegea, na Pamela akamsukuma kwa nguvu. Ingawa nguo zake zilikuwa safi, kulikuwa na alama za meno kwenye midomo yake na rangi ya lipstick yake

iliacha alama kwenye uso wa Rodney kwa uwazi sana.
“Bwana Malugu, uko kwa wakati. Yeye-”
"Nicole, ninaelewa. Alikutongoza, sivyo?”
Bwana Malugu alikatisha maneno yake. Alimkazia macho Rodney kwa ujeuri ambaye hakuwa amevaa shati na suruali yake ikiwa imelowa. "Bwana Shangwe, unaenda mbali sana. Kwa ajili ya kupata fomula tu, unawezaje kufanya kitu kama kuuza utu wako?"
Ingekuwa ni mtu mwingine, angekuwa na hasira kabisa. Lakini, Radney hakuwa na aibu. Alijipangusa kwa utulivu pembeni ya mdomo wake na

kutabasamu huku akiinua nyusi zake. "Bwana Malugu, unaweza pia kujaribu kuuza utu wako, lakini Bi. Masanja anaweza kufikiria kuwa wewe ni mzee sana."
Uso wa Bwana Malugu ulilegea. Pamela alichukua kitambaa na kujifuta pembeni ya mdomo wake kwa nguvu huku akimkazia macho Rodney. “Pole, Bwana Shangwe, lakini nadhani wewe ni mchafu sana. Mdomo wako huo ni kama choo cha umma. Nimechukizwa.”
TUKUTANE KURASA 366-370
ONYO: Ni marufuku kusambaza, kukopi wala kuuza kazi hii kwani endapo kama tutakubaini basi sheria itachukua mkondo wake (By: Official Dully)
 
LISA KITABU CHA NANE (8) SIMULIZI........................LISA KURASA.................366 - 370
PRESENT: SIMULIZI ZA DULLY

Sura ya: 366
"Ulibusu choo hiki cha umma kwa
furaha." Rodney akakonyeza macho.
“Na ulinivua nguo zangu na kunimwagia
divai. Nimependa michezo yako ya
kusisimua kama hii.”
Kwa maneno yake, meneja wa hoteli na
Bwana Malugu wote walimtazama
Pamela kwa njia isiyo ya kawaida.
Alionekana mrembo sana, lakini bila
kutarajia, alikuwa jasiri na asiyejizuia
kwa ndani.
“Bullsh*t!” Uso wa Pamela ukawa
mwekundu kwa hasira.
Rodney alihisi faraja kadiri alivyozidi
kumuona vile, na macho yake yalimtoka
kwa fujo. “Sahau, sitasema mengi
kuhusu mambo fulani. Baada ya yote,

mwonekano wangu wa sasa unaweza
kuthibitisha kila kitu.”
“Wewe una wazimu!” Pamela akampiga
kofi na kuondoka.
"Halo, vipi kuhusu formula?" Rodney
alifoka nyuma yake bila aibu.
"Endelea kuota!" Pamela aliondoka, na
Bwana Malugu akamfuata mara moja.
Mara tu walipotoweka, Rodney alipiga
chafya mara moja. Alianza kutetemeka
huku akimpigia kelele msaidizi wake
pale nje. "Herbert, vua koti lako na
unipe."
Damn it! alikuwa anaenda kuganda
hadi kufa kwa baridi la Nairobi.
Hakuwa amekula pia.
Herbert alimvulia Rodney koti lake

kimyakimya. "Bwana Shangwe,
mazungumzo ya fomula yaliendaje?"
“Ilikuwa sh*t. Hatukuwa hata tumeanza
kuongea kuhusu fomula na yule
mwanamke tayari ameshaanza
kugombana nami.” Rodney alimtazama
kwa ukali. “Mfuatilie Bwana Malugu.
Haijalishi ni njia gani unayotumia,
usiwaruhusu tu kusaini mkataba. Narudi
nyumbani kuoga.”
Baada ya kuoga kwenye jumba lake la
kifahari, Rodney alikasirika zaidi
alivyofikiria juu ya Pamela. Akampigia
Chester, akisema, “Uko wapi? Niko
katika hali mbaya. Njoo tunywe pamoja
nami.”
"Njoo mahali pa kawaida. Nipo na
Alvin.” Chester alimwambia.

Rodney alipofika aliwakuta Alvin na
Chester pekee yao. “Ni nyinyi wawili tu?
Wako wapi Cindy na Sarah?”
Uso wa Alvin ulikuwa umezama kwenye
giza la mawazo totoro. Hakuongea, na
haikuwezekana kukisia hali yake.
Chester alitazama juu na kutabasamu.
"Kwa hiyo tunatakiwa kuongozana na
wanawake kila mahali tunapokwenda?
Halo, nini kilitokea kwa mdomo wako?
Hiyo ni nadra. Umeumwa na
mwanamke?"
Kwa maneno hayo, Alvin naye
alimtazama kwa uvivu.
Rodney alisema kwa hasira, “Sio
mdomo wangu tu. Angalia sikio langu.
Iiling’atwa hadi likatoka damu. Pamela
Masanja, lazima alikuwa mbwa katika

maisha yake ya zamani. Kitu cha
kwanza alichofanya ni kunimiminia
chupa nzima ya divai mwilini. Nilikaribia
kuganda.” Kufikia hapo aligugumia
kidogo kabla hajasema kwa aibu, "kwa
hiyo, Chester, nisaidie kufanya
uchunguzi. Sehemu yangu ya chini
inauma kama nini baada ya Pamela
kunipigia kwa goti. Alvin, hatimaye
ninaelewa uchungu uliohisi.”
Chester alitoa macho kwa kuchukia.
“Potelea mbali. Mimi si daktari wa
andrology, lakini usijali. Alvin hakuweza
kutembea moja kwa moja alipokuwa
amepigwa nyeti zake na Lisa wakati huo, lakini alikuwa sawa mwishowe.
Sidhani kama kuna shida yoyote
itakutokea.”
“Sawa.” Rodney aliguna, “Pamela na Lisa kimsingi ni mtu na dadake. Hata

mienendo yao ni sawa. Je, walikuwa na
mshauri mmoja walipopotea katika
miaka michache iliyopita?”
"Labda." Chester alimtazama Alvin
kimaana.
Alvin aliwasha sigara. Alipokuwa
akisikiliza maneno ya Rodney, moyo
wake ulijikunja na kutabasamu.
"Alvin, unatabasamu nini?" Rodney
aliuliza.
“Hakuna kitu.” Alvin akainua midomo
yake. Hapo awali alitaka kutoka nje na
kupumzika kwa sababu alikuwa
amekasirika, lakini Rodney alipokuja na
kueleza mambo yake, moyo wake
ulipumua kidogo.
•••

Masaki. Dar es Salaam.
Lisa aliwarudisha nyumbani watoto
wake wawili baada ya kucheza siku
nzima.
"Mama, nataka kucheza kesho pia."
Suzie alimkumbatia Lisa na kukataa
kumuachia.
"Sawa, tutaenda kwenye aquarium
kesho."
Lisa alikuwa akijiandaa kwenda kuoga
wakati alipopokea ujumbe wa whatsapp
kwenye simu yake uliotumwa na
muuguzi wa hospitali kupitia simu ya
baba yake. [ Bi. Jones, tafadhali njoo
hospitalini sasa. Shinikizo la damu la
Bwana Ngosha lilipanda ghafla usiku
huu. Tulimpiga dripu lakini halijashuka.]

[Sawa, haraka mjulishe daktari kuhusu
hali yake. Nitakuwa hapo muda si
mrefu.]
Baada ya Lisa kukata simu, hakuwa na
namna zaidi ya kupanga safari ya
haraka kuelekea Nairobi. Alikata tiketi
kwenye mtandao ya ndege iliyokuwa
inaondoka muda wa karibu zaidi na
baada ya kuoga na kujiandaa haraka
haraka, aliwakusanya watoto wake na
kuelekea uwanja wa ndege. Masaa
manne baadaye alikuwa amefika
kwenye makazi yake huko Karen
Estate, Nairobi.
Ilikuwa ni usiku tayari, mida ya saa nne
hivi. Aliwaambia watoto wake wawili,
“Babu yenu hajisikii vizuri, kwa hiyo ni
lazima niende hospitali sasa hivi
kumuona. Mtabaki hapa nyumbani
mlale sawa? Godmother wenu atarudi

baada ya muda mfupi."
"Mama, tunaweza kwenda kumsalimia
babu pia?" Lucas aliuliza huku
amekunja uso.
“Sasa si wakati mzuri. Zaidi ya hayo,
babu ni dhaifu sana hawezi
kuzungumza na nyie. Tunaweza
kwenda kumtembelea wakati fulani
baadaye.” Lisa alijua wanawe
hawakuwa wasumbufu.
Aliwabembeleza hadi alipoona
wameanza kukole usingizi.
Baada ya kuwafariji watoto wake wawili
wapenzi, alikimbia hospitali akiwa hoi.
Akiwa njiani kwenda huko, alimpigia
simu Pamela, akimtaka arudi nyumbani
mapema.
Kumbe wale watoto wawili walikuwa

wamevunga tu kulala ili kumridhisha
mama yao. Baada ya Lisa kuondoka,
Suzie alikuwa wa kwanza kuamka.
Alikagua nyumba nzima kutafuta
vitafunwa. “Hehe. Nilijua mama
angeficha chokoleti hapa. Alidhani
nisingejua.”
Suzie akamtupia Lucas pakiti ya
chokolate. “Unaitaka?”
“Sili kitu alichotukataza mama, alisema
tutakuwa bubu.” Lucas alimjibu huku
akiifuata laptop ya mama yake iliyokuwa
mezani. Alipenda sana kuchezea
kompyuta tangu akiwa mdogo kabisa.
Suzie hakuelewa ni kwanini mama yao
aliwakataza kula chokoleti mara kwa
mara. Aliona aina hii ya chakula ni tamu
sana. Alihisi kwa kuwa mama yake
hakufurahia yeye kula chokoleti, baba

yake huenda angemruhusu. Hivyo
Suzie akatamani kumtafuta Alvin.
Lucas aliwasha laptop. Na kwa kuwa
eneo lile lilikuwa limeunganishwa na wi-
fi, laptop ilishika mtandao wa internet
mara moja. Lucas alikuwa anapenda
sana kutazama katuni kwenye mtandao
wa Youtube. Pamela alimfundisha jinsi
ya kuingia huko kupitia simu na
kompyuta na kwa sababu Lucas alikuwa
na akili nyepesi ya kitoto, alikariri
haraka.
Baada ya kufungua Youtube, mtandao
ulionyesha video ambazo Lisa alipenda
kutazama mara kwa mara. Kwa hivyo
video nyingi zilizomuonyesha Alvin na
Sarah zilionekana.
“Woooh! Lucas, ni baba yetu mchafu!”
Suzie aliruka kwa mshangao. Wote

waliifahamu vizuri sura ya baba yao
kwani walionyeshwa na mama yao
kwenye picha na video za simu.
“Bonyeza hiyo video tumuone baba...”
Suzie aliingiwa na shauku ya ajabu.
Muda mfupi baadaye, Lucas akabofya
video mojawapo na video ikaanza
kutembea. Suzie aliyekuwa anakula
chokoleti alimsogelea Lucas. "Wow, ni
mtu mzuri sana! Yeye ni mzuri zaidi
kuliko mjomba Kelvin. Lazima nipate
mchumba ambaye ni mzuri kama yeye
nikikuwa mkubwa."
“Baba yetu ni mchafu.” Lucas alimkazia
macho. "Mama labda alidanganywa kwa
sababu alikuwa na mawazo kama
yako."
“Woooh, baba anaongea, anasemaje

baba?” Suzie akatoa macho yake. Alvin
alikuwa akihojiwa na waandishi wa
habari kwenye video hiyo.
Lucas alijibu kwa sauti ya chini, “Mm.
Kulingana na habari, anaenda kuoa
mapema mwezi ujao. Mwanamke
ambaye atamuoa ni Sarah Langa, na
hivi ndivyo anavyoonekana.”
Suzie akaikazia macho sura ya Sarah
aliyeonekana pembeni mwa Alvin, kisha
akakunja midomo yake. “Ni mbaya
sana. Yeye siyo mrembo kama Mama.
Baba yetu mchafu ana mke mbaya
sana."
“Ndiyo.” Lucas alikodoa macho.
“Wamemuumiza mama. Ni lazima
tulipize kisasi kwa ajili ya mama.”
“Hakika, hakika. Kwa hivyo tutalipaje
kisasi?" Suzie alisisimka.

Wakati huo, ghafla sauti ya ajabu
ilisikika kutoka nje. Kulikuwa na watu
wanakuja!
Sura ya: 367
“Shhhh!” Lucas alimfanyia Suzie ishara
ya kunyamaza. Haraka akafunga laptop.
Kisha, akamvuta Suzie na kutafuta
mahala pa kujificha.
Akiwa na wazo, alimwaga nguo chache
kutoka kwenye sanduku kisha akamvuta
Suzie ndani ya lile sanduku na kuweka
nguo chache juu yao, halafu akalifunika
bila kufunga zipu. Wawili hao walikuwa
wamejikunja ndani kwa pamoja kama
sungura.
Suzie alipokuwa amejikunja huku
akishusha pumzi, alijisikia vibaya sana.

Aliuliza, “Unafanya nini Lucas? Lazima
ni Godmother anarudi—”
Kabla hajamalizia sentensi yake, Lucas
alimziba mdomo. "Nyamaza.
Godmother havuti sigara, we hujasikia
harufu ya sigara?” Lucas alijibu kwa
sauti ya kunong’ona. Alipomaliza tu
kuongea, mlango wa nje ukafunguliwa
kwa nguvu. Baadaye, sauti ya mtu wa
kushangaza ilisikika.
“Vega, sioni mtu yeyote hapa, lakini taa
zimewaka.”
"Anaweza kuwa kajificha. Nenda
ukaangalie pande zote."
Watu wachache walisikika wakiingia
chumbani. Walipekua kabati la nguo na
chini ya kitanda na kuonekana kukata
tamaa. "Hakuna mtu, bana, Vega."

“Umeangalia mpaka bafuni, stoo,
jikoni... ?” Mtu yule kwenye simu alizidi
kusisitiza. Wale jamaa mle ndani
wakasambaa kila kona kutafuta, lakini
hawakuona mtu.
Macho ya jamaa mmoja yakaangaza
kwenye chumba hicho. Akakazia macho
kwenye sanduku lililokuwa kwenye
kabati la nguo. Je, anaweza kuwa
kajificha humu? Aliponyoosha mkono
wake kulifungua, mtu aliyekuwa nyuma
yake alimpiga teke. “Una akili kweli
wewe! Unafikiri mtu mzima anaweza
kutoshea kwenye sanduku dogo kama
hilo?”
Alinyamaza kwa muda kabla ya
kuangaza huku na kule na kusema
kwenye simu, “Bwana Vega, hakuna
mtu humu.”

“Sawa. Vunja kila kitu ndani ya
nyumba."
Kwa hayo, nyumba ya Lisa ikageuka
kuwa Ukraine. Vurugu ya vitu vikivunjwa
hovyohovyo ilisikika kwa kishindo.
Walivunja chupa za mvinyo, vioo vya
makabati na dressing table, madirisha,
vyombo vya jikoni, TV, pamoja na
kupora vitu vya thamani. Baada tu ya
kumaliza kuvuruga kila kitu ndipo
waliondoka wakiwa wameridhika.
Dakika kumi hivi baada ya wao
kuondoka, Lucas alifunua sanduku na
kutangulia kutoka kisha akamtoa pia
Suzie nje. Suzie alitoka akiwa na
mawenge ya woga, hivyo alihisi
kizunguzungu na kuanguka. Kwa bahati
mbaya aliangukia kipande kikubwa cha
chupa ya mvinyo ambacho kilimchoma

kichwani. Kichwa chake kilianza kuvuja
damu kwa wingi.
“Kaka, inauma sana...” Suzie
alimtazama kwa sura ya maumivu akiwa
na pakiti ya chokoleti mkononi mwake.
“Usiogope, Suzie. Nitakupeleka hospitali
sasa hivi.” Lucas alikuwa na wasiwasi
sana hivi kwamba machozi yalitiririka
kwenye uso wake ambao kawaida
ulikuwa mtulivu.
Muda mfupi baada ya Suzie kuumia,
Pamela akaingia, alishangaa kukuta
nyumba ikiwa kwenye vurugu kiasi kile
huku Lucas akiwa anahangaika na
Suzie. Hakukuwa hata na jirani
aliyejitokeza kusaidia.
Lucas alilia alipomuona Pamela,
“Godmother, Suzie ameumiaa.”

"Nini kimetokea?!" Pamela aliuliza kwa
mshtuko huku akimtumbulia macho
Suzie aliyekuwa akivuja damu kwa
wingi. Hapohapo akapiga simu kuita
ambulensi kishaakawabeba wale watoto
kushuka chini.
Wakiwa njiani kwenda hospitali, Pamela
alimpigia simu Lisa kumpa taarifa.
"Mungu wangu! Nimerudi tu na kukuta
nyumba yako kwenye fujo. Nimewaita
polisi. Suzie ameumia.”
“Nini kimetokea? Suzie kaumia? Hali
yake ikoje?” Lisa ambaye alikuwa
amewasili hospitalini, mara baada ya
kusikia maneno ya Pamela aliingiwa na
huzuni nyingi. “Alijijeruhi vipi? Je, ni
serious?”
“Lisa, hata mimi sijui kilichotokea.
Nitazungumza nawe baadaye. Suzie

amezimia. Nimepiga simu ambulensi na
sasa nampeleka hospitalini.” Pamela
alisikika akiwa amekabwa.
Wimbi la hofu lilimkumba Lisa, karibu
kumfanya apoteze akili yake.
Haraka akakimbia kwenda kwenye
hospitali nyingine. Alipofika alimuona
Lucas akiwa amesimama kinyonge
kwenye korido peke yake. Mikono na
uso wake ulikuwa umetapakaa damu.
Mara alipomuona Lisa, akajitupa
kwenye mikono yake huku akilia.
“Mama, Suzie ameumiaaa....”
“Usilie. Niambie kilichotokea.” Lisa
alifuta madoa ya damu usoni mwake
kwa uchungu.
“Muda mfupi baada ya wewe kuondoka,
watu wachache waliingia ndani ya
nyumba yetu, kwa hiyo nikaenda

kujificha kwenye sanduku la suti pamoja
na Suzie. Hawakutuona, lakini mwisho
walivunja kila kitu. Tulipotoka kwenye
sanduku, Suzie aliangukia chupa
ikamkata kichwani.”
Katikati ya maelezo yake, Lucas
alidondosha kilio. “Nilikuwa nimemziba
mdomo Suzie muda wote ili asipige
kelele.”
Lisa alitetemeka kwa hasira. Kamwe
katika ndoto zake za ajabu hakutarajia
kwamba kuna mtu angekuwa na ujasiri
wa kuvunja na kuingia ndani ya nyumba
yake. Aliogopa kufikiria nini kingetokea
kwa watoto hawa wawili ikiwa Lucas asingechukua hatua ya kijasiri kama
hiyo. Alikuwa amevunjika moyo na
mwenye hatia. Kama mama, alishindwa
kuwalinda watoto wake waliporudi hapa.

Muda mfupi baadaye Pamela alitoka
kwenye chumba cha daktari. Alikuwa
kampakata Suzie wakielekea kwenye
wodi kwa ajili ya mapumziko.
“Vipi hali ya Suzie?” Lisa aliuliza kwa
wasiwasi.
"Ametoka kwenye hatari."
Pamela alimkazia macho yake ya
huruma kwa Suzie ambaye alibaki
amepoteza fahamu. Kipaji cha uso cha
mtoto huyo mdogo kilikuwa kimefungwa
kwa kutumia bandeji, na mashavu yake
ya rangi ya waridi yalikuwa yamepauka.
"Hawa watu ni wakatili. Wanawezaje
kumdhuru mtoto?" Pamela alinyamaza
kwa muda kabla ya kuuliza bila kujali,
"Hii haimuhusu Thomas kweli?"
“Pengine.” Lisa aliitikia kwa kichwa bila

huruma. Alikuwa na maadui wengi
sana. Ikiwa Melanie na Damien
wangetaka kuchukua hatua dhidi yake,
wangefanya hivyo lakini wasingetumia
nguvu kiasi hicho.
"Yote ni makosa yangu," Pamela
alisema kwa hatia, "nilimchana makavu
Thomas hadharani wakati wa mkutano
wa waandishi wa habari leo. Lazima alichukia. Anajua nitakuwa nimefikia
kwako. Tayari alikuwa na ujasiri wa
kutosha kuingia nyumbani kwangu
miaka mitatu iliyopita, kwa hiyo sidhani
kama kuna jambo lolote anaogopa
kufanya.”
“Ndio. Alipokamatwa miaka mitatu
iliyopita, hata hakwenda jela. Ndiyo
maana sasa hana woga.” Sura ya
kusikitisha iliosha uso wa Lisa.

Pamela akainua midomo yake.
"Naogopa kwamba Alvin ... atamtetea."
Kifua cha Lisa kilihisi kubana. Aligeuza
kichwa chake na kumtazama Suzie.
Hasira kali ikamjia. Sarah Njauna
Thomas Njau! Ilimbidi kuwalipa
waliomuumiza bintiye!
Wakiwa kwenye wodi ya faragha, Lucas
alimwangalia Suzie na kusema kwa
huruma. “Mama, lilikuwa kosa langu.
Nilipaswa kuzima taa. Nilishindwa
kumtunza vizuri Dada!”
“Lucas, acha kujilaumu. Ulifanya kazi
nzuri. Ulikuwa sahihi kwa kuacha taa
ikiwaka.” Lisa alimkandamiza mabegani.
"Lazima watu hao walikuwa wakitazama
nyumba yetu kutokea chini. Walijua
kuwa taa zetu zinawaka, ungezima
ghafla, wangejua kuna mtu amejificha

ndani ya nyumba. Kwa hali hiyo,
wangegundua kuwa wewe na Suzie
mko kwenye sanduku. Mwishowe, nyote
wawili mngetekwa.”
"Mama, ni nani hao watu waovu?"
Lucas aliuliza huku akiwa amejilaza
mikononi mwake. "Nataka kulipiza kisasi
kwa niaba ya Suzie."
“Wewe ni mdogo sana kufikiria mambo
hayo. Suzie atakuwa sawa tu.” Lisa
alimtuliza mwanaye, lakini
asingewaruhusu wale waliomuumiza
Suzie kutoka kwenye ndoano.
Kwa wakati huo, daktari aliwatembelea
wodini. “Uchunguzi unaonyesha mtoto
amepoteza damu nyingi, lakini hatuna
damu ya kutosha aina ya AB hapa. Kwa
kuwa wewe ni mama yake, je, damu
yako ni AB pia?”

"Hapana." Uso wa Lisa uligeuka kuwa
mbaya.
Lucas alikunja mikono yake na kusema,
“Mama, yangu ni—”
"Hapana. Wewe ni mdogo sana kuweza
kutoa damu yako,” daktari akakatisha
sentensi yake. “Mgonjwa anahitaji
mililita 500 za damu.
Hata mtu mzima hawezi kuvumilia ikiwa
atatoa damu nyingi hivi. Mtoto hakika
ataanguka. Baba wa mtoto yuko wapi?"
“Baba?” Lisa alikunja ngumi. Ikiwa Alvin
angejua kuhusu hili, bila shaka
angemnyakua Suzie kutoka kwake.
Sura ya: 368

Kwa wakati huu, Lucas alivuta mkono
wa Lisa. “Mama, tunaweza kwenda
kumtafuta mjomba Jack.?” Jack Kimaro
ndiye pekee kutoka familia ya Kimaro
aliyefahamu uwepo wa watoto hao.
Alimsaidia Lisa kutoroka na mara kwa
mara alikwenda Marekani kumsalimia
hadi alipojifungua. Lucas na Suzie
walimfahamau vizuri.
Baada ya kupigwa na butwaa kwa
muda, Lisa mara moja akampigia Jack
simu.
Jack aliharakisha kifka hospitalini
pale ndani ya dakika kumi. “Vipi hali ya
Suzie? Mara tu nilipojua kuwa kuna
jambo limempata, nimepita taa nane
nyekundu kuwahi hapa.”
"Asante, Jack." Lisa alimshukuru sana.
“Suzie bado anaendelea na matibabu

ya dharura. Anahitaji mililita 500 za
damu.”
"Nina damu sawa na yeye. Fanya
haraka uchukue damu yangu.” Jack
alikunja mikono yake bila wasiwasi
zaidi.
“Subiri kidogo. Tunahitaji kuthibitisha
aina ya damu yako kwanza.”
Nesi alimshusha haraka haraka. Baada
ya kuthibitisha aina yake ya damu,
mililita 500 za damu yake zilitiwa
mishipani Suzie. Pamoja na hayo, hali
ya Suzie iliboreka taratibu.
"Jack, sijui jinsi ya kutoa shukrani zangu
kwako wakati huu." Lisa alihisi kwamba
alikuwa na deni kubwa la Jack.
"Hakuna wasiwasi. Baada ya yote,
Suzie ni mwanangu kiukoo.”

Kwa sura ya kuhuzunisha, Jack
alimaliza chupa ya maziwa. Alikuwa
mzima wa afya, lakini kutoa mililita 500
za damu bado kulimfanya ahisi
kizunguzungu kidogo. “Nenda
ukamwangalie Suzie. Nitapumzika hapa
kwa muda.”
•••
Kulipopambazuka, polisi walifika na
kumwambia Lisa, “Tumewatambua watu
waliovunja vitu vya nyumbani kwako.
Walikuwa wahuni kutoka jirani, na tayari
tumewakamata. Walikiri kwamba
walivunja nyumba yako kufanya wizi.
Tulipata vito na pesa taslimu. Angalia
na uhakikishe kama hivi ndivyo vitu
walivyoiba nyumbani kwako.”
“Ndiyo.” Lisa alivitazama vile vitu na
kuvipokea.
“Sawa. Kesi imefungwa."

Polisi walipokuwa tayari kuondoka,
Pamela alisema kwa kutoridhika, “Ni
wazi, haukuwa wizi. Kuna mtu aliwalipa
ili kulipiza kisasi kwetu.”
“Inatosha, Pamela. Polisi wamefanya
walichoweza.” Lisa alimsimamisha na
kuwaacha polisi waondoke.
"Nina uhakika Thomas amewahonga,"
Pamela alisema kwa hasira.
Lisa alicheka. “Bila shaka. Naam,
mazoea hujenga tabia. Kadri Thomas
anavyofanya matendo maovu zaidi,
ndivyo anavyozidi kuwa stadi. Kabla ya
hili, Alvin alilazimika kusafisha uchafu
wake. Sasa, anaweza kushughulikia
mambo peke yake vizuri hivi kwamba
hatahitaji hata msaada.”
"Kwa hiyo tutamwacha tu?" Pamela

aliuliza bila kuridhika.
"Tutaenda naye polepole. Lakini...
sitaweza kuishi vizuri hadi niwalipe.”
Lisa alimkabidhi Lucas kwa Pamela.
“Natoka nje mara moja, mtazame.”
“Mama, unaenda wapi?” Lucas aliuliza
kwa wasiwasi.
“Naenda kununua kifungua kinywa.
Nitarudi hivi karibuni. Mwangalie dada
yako kwa sasa.” Lisa alitoka hospitali
baada ya kumtuliza Lucas.
•••
8:00 asubuhi, katika jumba lake la
kifahari, baada ya Alvin kumaliza
kifungua kinywa, Sarah alitabasamu
kwa upole na kusema, “Kwa kuwa bado
ni mapema, unaweza kunisindikiza
hospitalini? Nahitaji kuchoma sindano."

Siku hizo, Sarah ilibidi atembelee
hospitali mara nyingi sana kuchoma
sindano ya kuchochea mwili ili aweze
kufanikiwa matibabu ya In vitro
Fertilization (IVF), au upandikizaji wa
mimba kwa njia ya matibabu.
Aliposikia ombi lake, Alvin aligeuka na
kumkazia macho yake magumu. “Kwa
kweli, hakuna haraka ya sisi kupata
mimba. Kwa kuwa bado ni
vijana, hatujachelewa kufanya hivyo
baada ya kufunga ndoa.”
“Alvinic, mimi si kijana tena. Ninataka
kuwa na watoto haraka iwezekanavyo
na kujenga familia na wewe. Siogopi
maumivu. Sijali kuteseka kwa ajili yako,”
Sarah alijibu kwa upole huku
akiizungusha mikono yake shingoni.
"Sawa, nitakupeleka huko." Alvin

aliinamisha macho chini kwa kuomba
msamaha. Ikiwa sio kwa sababu
hakuweza kufanya naye mapenzi,
asingelazimika kwenda kwenye shida
zote za kupitia IVF.
Lisa alikuwa sahihi kwa kusema
kwamba uzazi kwa njia ya IVF
kuliwaweka wanawake katika hali
mbaya.
Gari ilipowashwa tu na kuelekea nje ya
geti, ghafla gari aina ya SUV ilipita
kwenye geti la chuma na kuelekea
kwenye gari la Alvin.
Alvin aligeuza usukani kwa haraka ili
kulikwepa. SUV ilielekea kwenye maua
na kugonga kwenye dirisha la nyumba.
Baadaye, vioo vilivunjika na vipande
kutawanyika ardhini.
Lisa alifungua mlango kwa teke. Akiwa

amevaa jozi ya buti za Dk. Martens na
jeans, aliruka kutoka kwenye SUV kwa
macho ya kutisha.
Alvin alimkazia macho, huku Sarah
akiiweka mikono yake kiunoni huku
akitetemeka. Alionekana kuwa na hofu.
“Anapanga kufanya nini Alvinic? Hii
inatisha. Karibu atugonge.”
Alvin alifungua mlango kwa huzuni na
kutoka nje ya gari. Kuona fujo pale uani,
aliruka kwa hasira. "Lisa Jones,
unatamani kifo mapema asubuhi?
Nimetosha na vitimbi vyako sasa.”
“Mimi pi nimechoshwa na nyinyi wawili
pia.” Lisa akamsogelea taratibu huku
macho yake yakionyesha hasira.
“Kwanini sikufaulu kuwaua ninyi wenzi
wasio na aibu sasa hivi?”

“Wewe ni mgonjwa! Nenda ukachukue
dawa yako.” Alvin alimtazama Lisa kana
kwamba ni kichaa.
Sarah alishuka kwenye gari na
kumshauri Lisa kwa huzuni, “Tulia Lisa.
Najua habari za ndoa yangu na Alvin
labda zimekuchanganya, lakini
unachofanya sasa ni kinyume cha
sheria. Nimepiga simu polisi hivi punde.”
Alvin alishikwa na butwaa. Kisha, Sarah
akaeleza bila kujali, “Ameenda mbali
sana wakati huu. Umeona uharibu
kwenye ua wetu? Kwa bahati nzuri,
hakuna mtu aliyegongwa. Ikiwa
hatutamfundisha somo sasa hivi,
atafanya ujinga wa kiwango kikubwa
wakati ujao.”
Alvin alinyamaza kwa muda. Alijua
kwamba Lisa alikuwa bado anampenda,

lakini tabia yake ya ukichaa ilimtia hofu
sana. Aliona hitaji la kumfundisha somo
pia.
Akiwatazama wawili hao, Lisa
alidhihaki. “Acha kuwaza mambo kupita
kiasi. Nilikuja hapa sio kwa sababu nina
wivu na ndoa yako. Ninataka kukuonya
kwamba hasira yangu ina mipaka yake. Sarah Langa, bora uendelee kumkanya
Thomas. Watu wachache waliingia
ndani ya nyumba yangu na kuvunja vitu
vyangu jana usiku. Ni Thomas tu ndiye
aliyewatuma.”
“Kwanini umsingizie kaka yangu, una
ushahidi?” Sarah alichukia.
"Pamela alimuumbua Thomas mbele ya
vyombo vya habari wakati wa mchana
na tukio la uvamizi lilifanyika nyumbani
kwangu usiku huo huo. Inawezaje kuwa

bahati mbaya?” Lisa alifoka. “Ijapokuwa
wale watu ambao wamekamatwa kwa
kuingia ndani ya nyumba yangu ni
wahuni tu, aliyewaelekeza atakuwa ni
Thomas. Haiwezi kuwa mtu mwingine
yeyote.”
Uso wa Alvin ulibadilika kidogo. Hapo
ndipo alipoona sura ya Lisa iliyopauka
na macho yaliyovimba. Ilionekana kuwa
hakuwa amelala jana yake usiku.
"Ni Thomas ndiye amefanya?" Alvin
akageuza kichwa chake na kumtazama
Sarah kwa ukali.
“Hapana... Hapana.” Bila kujua lolote
kuhusu jambo hilo, Sarah alianza
kuingiwa na hofu. “Nilimpigia simu kaka
yangu jana. Alisema kuwa hatajali
maneno ya Pamela na hatamletea
shida. Lisa, nadhani umewaudhi watu

wengine. Huwezi kumlaumu ndugu
yangu kwa sababu tu unanichukia.”
“Sihitaji kukukumbusha jinsi Thomas
alivyo na jeuri ya kijinga, sivyo? Miaka
minne iliyopita, tayari alikuwa na ujasiri
wa kutosha kuingia ndani ya nyumba ya
Pamela na kutaka kumbaka. Licha ya
kujua kuwa nilikuwa mjamzito wakati
huo, alithubutu kunisukuma! Zaidi ya
hayo, dada yake ataolewa katika familia
ya Kimaro hivi karibuni. Angeogopa
kufanya nini?"
Lisa alimtazama Alvin kwa hasira.
"Endelea kumtetea Thomas milele. Kwa
sababu yake, sifa yako itaharibiwa
mapema au baadaye. Kila mtu
atachukizwa na jinsi unavyomsaidia na
kumsaidia.”
Sura ya: 369

Alvin alishtuka na kujikuta anakunja
ngumi bila kujijua. Aliongeza sauti yake
na kuuliza, “Thomas alikusukuma miaka
mitatu iliyopita?”
“Hata kama angefanya hivyo?
Ungejali? Pia alimpiga rafiki yangu na
kujaribu kumsumbua, lakini uliamua
kunitisha na baba yangu kwa ajili ya
mwanamke huyu. Baada ya miaka
mingi sana, hujisikii kuwa na hatia
kuhusu hilo, Alvin? Naam, sidhani kama
unafanya hivyo kwa sababu wewe si
tofauti na Thomas. Nyinyi wawili ni
mashetani katili tu.”
Ikiwa Alvin asingemsaidia Thomas tena
na tena, Thomas angekuwaje na ujasiri
wa kufanya jambo kama hilo sasa na
hatimaye kumuumiza Suzie? Alipofikiria
jinsi mtoto wake alivyokuwa na
uchungu, macho ya Lisa yalibadilika na

kuwa mekundu. Hakuweza kujizuia
kutetemeka pia.
“Wewe endelea tu kumtetea Thomas.
Jana aliharibu nyumba yangu, na mimi
leo nimeharibu mahali pako. Akimuua
rafiki yangu kesho, nitaondoa uhai
wako!” Macho ya Lisa yalijaa chuki.
Ndani ya moyo wake, Alvin alihisi hasira
sana bila sababu za msingi.
Hakupenda jinsi Lisa alivyomchukia.
Hata hakupenda sura yake ya machozi.
Punde, polisi walifika. "Bwana Kimaro,
ni yeye ndiye aliyeingia nyumbani
kwako na kufanya fujo?" Polisi
walitembea kuelekea kwa Lisa.
"Achana naye. Sitafuatilia suala hili,”
Alvin alijibu ghafla.

"Alvini." Sarah aliuma mdomo. "Yeye
karibu -"
"Nimesema kwamba sitafuatilia suala
hilo, basi!" Alvin aligeuka na kuingia
ndani ya gari bila kujishughulisha
kumtazama Sarah. Muda si mrefu
aliendesha gari na kuondoka.
"Alvini." Sara kadiri alivyozidi
kumkimbilia, ndivyo alivyozidi kuachwa
nyuma. Alvin alisahau kabisa kuhusu
ahadi yake ya kuongozana naye hadi
hospitali kwa ajili ya sindano.
“Unajisikiaje sasa kwamba
mwanamume wako mpendwa
anakuacha kama hakujui?” Sauti ya
Lisa isiyojali ilisikika masikioni mwa
Sarah.
Sarah aligeuka na kumtazama Lisa.
Jinsi alivyochukia alitamani kumpasua.

Sarah mara akajivuta. "Lisa Jones,
usiwe na majivuno. Alvin
amechanganyikiwa tu na vurugu zako.
Isitoshe, ulikuwa ukimshtaki tu Thomas
bila ushahidi wowote.”
Ikiwa Lisa angekuwa na ushahidi wa
kitendo cha Thomas, asingeenda pale
kuzua fujo. Badala yake, angemshataki
Thomas polisi moja kwa moja. Wakati
huo, Thomas hakuwa amemwomba
Sarah msaada. Ilimaanisha kwamba
alikuwa amejiandaa vya kutosha hata
Lisa asingeweza kumfanya chochote.
“Ndio, sina ushahidi, lakini hiyo
haimaanishi kwamba Alvin
hatalichunguza. Kwa vile ni kaka yako,
unadhani Alvin hatamshuku?
Sarah Langa, unaweza kumlaghai Alvin
ili akubaliane nawe, lakini huwezi

kubadilisha tabia yake kwa mbinu
potofu ya hypnosis. Yeye si mtu mbaya,
lakini kwa sababu yako, analazimika
kumvumilia Thomas tena na tena. Mara
moja au mbili ni sawa, lakini wakati
anaharibu zaidi na zaidi, watu wengi
huko nje wataanza kumkosoa Alvin kwa
kumsaidia na kumsaidia Thomas.
Unafikiri Alvin atafanya nini wakati
huo?” Lisa alipomaliza kuongea, uso wa
Sarah ukaanguka. "
Lisa alikunja midomo yake juu na
kuangaza huku na huko. “Pia, jumba hili
lilikuwa la Alvin na nyumbani kwangu.
Uliiba mahali pangu na hata unatumia
kitanda nilicholalia. Huoni aibu?”
Kwa hayo, Lisa moja kwa moja
alielekea kwenye gari lake bila
kuangalia sura mbaya ya Sarah.
Aligeuka na kuondoka.

Sara alikata tamaa kabisa. Muda
kidogo, akatoa simu yake na kumpigia
Thomas. "Ulituma watu waharibu
nyumba ya Lisa?"
"Hapana, niliwatuma kwa Pamela,"
Thomas alijibu kwa majivuno.
Sarah alipoteza utulivu wake. "Pamela
sasa anakaa kwa Lisa, kwa hivyo
uliharibu nyumba ya Lisa! Asubuhi ya
leo, Lisa alikuja hapa kuanzisha
ugomvi."
“Anathubutuje kuja huko?! Shemeji
atashughulika naye, sawa?" Thomas
aliongeza bila kujali, “Usijali. Mimi siwezi
kuingia matatizoni. Wale watu
nilowatuma kuchafua mahali hapo
wameshakamatwa kwa wizi. Polisi
watawachukulia tu kama wezi na
hawatanishuku. Zaidi ya hayo,

nimewapa pesa kimyakimya, kwa hivyo
watafanya siri.”
Sarah alishusha pumzi ndefu na
kuuliza, “Umewapaje pesa hizo za
kimyakimya?”
"Nilimwambia msaidizi wangu
kuihamisha pesa kwenye akaunti za
benki za familia zao."
Wakati huo, Sarah alikuwa akihema
kwa hasira. "Kumbe wewe ni boya?
Alvin anaweza kugundulika kwa urahisi
ikiwa atachunguza.”
"Shemeji atachunguzaje suala hili?"
Thomas alishangaa. “Unaweza
kuzungumza naye na kumshawishi.
Kama shemeji yake, mimi sio muhimu
kuliko Lisa?"

"Lisa alikuja hapa na kuongea mengi,
na zaidi ya hayo, Alvin bado ana hisia
kwake. Kama ndugu yangu, unaweza
kuacha kuwa mzigo kwangu? Siku zote
nimekuwa nikikuambia kuwa unaweza
kufanya chochote unachopenda baada
ya ndoa yangu kupita. Kwanini huwezi
kungoja?” Sarah alikazia macho baada
ya kukata simu.
Walisema wachezaji wasio na uwezo
wanaweza kuharibu timu.
Ijapokuwa Thomas alikuwa kaka yake
wa tumbo moja, angejikuta katika
matatizo makubwa mapema au
baadaye ikiwa angeendelea
kusababisha matatizo. Labda ulikuwa
wakati wa kuachana naye?
Baada ya kuondoka nyumbani, Alvin
alimpigia Hans. "Nenda ukaangalie ni
nini hasa kilitokea nyumbani kwa Lisa

jana usiku."
Kwa vile Hans alikuwa na mtu
anayefahamiana naye ambaye alifanya
kazi katika kituo cha polisi, alipata
habari hizo katika muda usiozidi dakika
kumi.
“Bwana Kimaro, wanaume wanne
walivamia nyumba ya Miss Jones
mwendo wa saa nne usiku wa jana.
Kwa bahati nzuri, Bi Jones alikuwa
hospitalini wakati huo kwani shinikizo la
damu la Joel lilikuwa limeongezeka.
Vinginevyo, angekutana na watu hao
wa kutisha... Nilisikia wanaume hao ni
wakatili ambao kila mara wanahusika
katika ujambazi na wizi.” Hans
alisimama ghafla katika hotuba yake.
Moyo wa Alvin ulishuka. Hata kama Lisa
angekuwa na ujuzi fulani wa kimsingi

wa kupigana, labda asingeweza
kuwashinda wanaume hao wanne
wakatili. Angekabiliwa na wanaume hao
wanne usiku, mwanamke mrembo
asingeweza kuwashinda. Anaweza hata
kubakwa!
Alvin bila fahamu akakaza mikono yake
kwenye usukani. "Kuna maeneo nyeti
katika kitongoji hicho. Ulinzi wa eneo
hilo ni mkali, kwa hiyo walithubutuje
kuingia ndani ya nyumba na kuiba vitu
saa nne usiku?"
"Ndio, hii ni kesi ya kwanza nzito
ambayo imetokea huko. Polisi
wamewakamata wahalifu hao wanne.
Wahalifu hao walidai kwamba walisikia
Miss Jones ndiye mrithi wa Ngosha
Corporation na walidhani yeye ni tajiri,
kwa hivyo walikwenda huko kutafuta
vitu vya thamani.

“Hata hivyo, ni mara yangu ya kwanza
kusikia wezi wakivunja kila kitu ndani ya
nyumba. Walivunja kila kitu
kilichoonekana hadi nyumba ikakosa
kutambulika. Haifai hata kwa binadamu
kukaa hapo sasa. Inaonekana walikuwa
wakilipiza kisasi.”
Alvin akasugua kichwa chake. Baada ya
muda, alisema kwa ukali, "Nenda
ukachunguze ikiwa tukio hili linahusiana
na Thomas."
Saa moja baadaye, Alvin alipokea
taarifa kutoka kwa Hans alipokuwa
ofisini. “Msaidizi wa 'Thomas'
alihamisha pesa kwa wanafamilia
wanne wa watuhumiwa waliokubali
kumlinda. Kila mmoja wao alipokea
shilingi milioni moja za Kenya.”
Alipomaliza tu sentensi hiyo, Alvin

aliyekuwa ameketi kwenye kiti cha ngozi
aligeuka na kurusha faili alilokuwa nalo.
“Hans, unafikiri... ninamdekeza Thomas sana eeh?” Uso mzuri wa Alvin uligeuka
kuwa mbaya, na mdomo wake ulipinda
na kuwa tabasamu la huzuni.
Hans alishindwa cha kusema. Sio tu
kwamba Alvin alikuwa akimtendea
Thomas kwa ukarimu sana, lakini pia
alikuwa ameenda hadi kuvuka msingi
wa maadili. Hata hivyo, Hans
alimkumbusha Alvin kwa tahadhari, "Ni
kwa sababu huwezi kuvumilia kuona Bi
Njau akiwa amekasirika, sivyo?"
Sura ya: 370
Sura ya huzuni ikaangaza machoni
mwa Alvin. Aliinamisha kichwa chini na

kufikiria. Hakika, alikuwa akifanya kila
kitu kwa ajili ya Sara. Miaka mitatu
iliyopita, hakutaka kumwokoa Thomas,
lakini alifanya hivyo dhidi ya dhamiri
yake kwa sababu ya Sarah. Hii ndiyo
sababu Lisa alikuwa amemwekea
kinyongo. Hatimaye, alipoteza watoto
wake, yote kwa sababu ya mipango
yake. Wakati fulani uliopita, Alvin hata
alipinga kesi dhidi ya dhamiri yake ili
kumuokoa Thomas aliyeharibu maisha
ya binti asiye na hatia. Lakini nini
matokeo yake? Badala ya Thomas
kubadili tabia yake, alizidi kuwa na
ujasiri na matendo yake maovu.
Alvin ghafla aliibuka kutoka kwenye lindi
la mawazo na kusema. "Peleka ushahidi
kwa polisi,"
Hans alipigwa na butwaa kwa muda.
"Lakini ikiwa Bi Njau atagundua-"

“Ikiwa atakuja kuniona kwa sababu ya
jambo hili, usimruhusu aingie. Alvin
aligeuka kwenye kiti chake cha ngozi na
kutazama nje ya dirisha.
“Sawa.” Hans aliitikia kwa kichwa na
hatimaye akahisi ahueni. Hatimaye,
dhamiri ya Bwana Mkubwa wake ilikuwa
inaamshwa polepole.
•••
Thomas alikuwa amemkumbatia
sekretari ofisini kwake tayari kumfanyia
jambo fulani. Mfanyakazi mmoja aliingia
ghafla kwa wasiwasi. “ Bwana Njau.
Msaidizi wako alichukuliwa na polisi
sasa hivi."
Thomas aliinuka mara moja, na
sekretari aliyefadhaika mikononi mwake
akaanguka chini. Kwa wakati huo,

hakuwa hata na wasiwasi juu yake.
Haraka akatoka nje na kupiga namba ya
Sarah. “Dada kuna tatizo.
Msaidizi wangu amechukuliwa na
polisi.”
“Kwanini unaogopa? Hukumkumbusha
Msaidizi wako yale niliyokuambia?"
“Nilifanya..."
“Usiwe na wasiwasi basi. Bila kujali ni
kiasi gani unamlipa, hakikisha tu
midomo yake imefungwa. Pia, afadhali
ujirekebishe kuanzia sasa au sitaweza
kukuokoa.” Sarah alichukia sana mara
baada ya kukata simu.
•••
Hospitalini, Lisa alipokuwa akimlisha
Suzie uji mikononi mwake, Pamela
alipokea simu.

Baada ya hapo, Pamela alisema, "Kuna
habari njema na mbaya. Habari njema
ni kwamba polisi walipiga simu na
kuniambia kuwa kuna
ushahidi unaoonyesha kuwa wezi hao
walikodiwa na mtu mwingine. Ni
msaidizi wa Thomas ambaye
alihamisha pesa kwa wanafamilia wao.”
Lisa aliinua kichwa chake na kusema,
"Kuhusu habari mbaya, msaidizi wa
Thomas amekiri kosa hilo?"
“Ndiyo! Ina maana kwamba Thomas
bado ametoroka kwenye kitanzi tena,”
Pamela alipumua. “Lakini unajua ni
nani aliyewasilisha ushahidi kwa polisi?
Ni Alvin! Ulimfanya nini asubuhi hii?”
“Nilimpaka dawa machoni. Nadhani
anaona vizuri sasa.” Ndani ya moyo

wake, Lisa alishusha pumzi.
Kwa kweli, alikuwa amecheza kamari
kwa kwenda huko asubuhi ya siku hiyo
ili kuanzisha fujo. Aliweka dau kwamba
Alvin bado alikuwa na hisia kwake na
asingeweza tena kuvumilia tabia ya
Thomas. Alikwenda kwake na
kumkumbusha kwamba Thomas
alihusika moja kwa moja kwa kupoteza
watoto wao miaka minne iliyopita. Kwa
bahati nzuri, alishinda Kamari yake!
"Wewe ni noma!" Pamela aliinua kidole
gumba.
“Godmother, mdomo wako uliumwa na
mbu? Umevimba.” Suzie ambaye
alikuwa akinywa uji huku akiwa
amejilaza kwenye mikono ya Lisa,
aliinamisha kichwa chake na
kumtazama Pamela kwa udadisi.

Pamela mara moja aliona aibu. "Mbwa
aliniuma."
"Lazima mbwa atakuwa mrefu kwani
anaweza kuuma mdomo wako," Suzie
alisema kwa tabasamu.
Pamela alimtazama Suzie kwa
mshangao huku mikono yake ikiwa
kiunoni. “Kwa kuwa unaweza
kunidhihaki, maana yake ni mzima.
Lakini ulikuwa unalia na kuomba
kukumbatiwa na peremende kwa mama
yako sasa hivi.”
Suzie alipiga kelele na kujipenyeza
kwenye mikono ya Lisa tena. "Mama,
inauma tena."
“Uliumia vibaya sana wakati huu
mwanangu. Acha nikubusu." Ni baada

tu ya Lisa kumkumbatia na kumbusu
kwenye shavu ndipo mtoto mdogo yule
alitabasamu kwa uchangamfu. Baada
ya yote, kichwa chake kilijeruhiwa
vibaya. Baada ya kunywa uji, Suzie
alihisi kusinzia.
Siku chache zilizofuata, Pamela alikuwa
na shughuli nyingi akimsaidia Lisa
kusafisha nyumba yake huku Lisa
akimhudumia Suzie hospitalini. Akiwa
na kazi nyingi sana, kwa kawaida
alifanya kazi huku akimtunza Suzie.
Lucas alikaa wodini kwa siku hizi tatu
bila kutoka nje. Alihisi ndiye
aliyesababisha majeraha ya Suzie.
Jack aliwatembelea tena usiku moja
usiku. Jack aliyabana mashavu ya
Suzie taratibu na kusema. “Suzie, ngoja
nikusindikize usiku huu, sawa? Mwache

mama naye akapumzike nyumbani.”
“Hakika, hakika. Ninakupenda zaidi,
Mjomba Jack. Suzie alimuonea huruma
mama yake pia. Mara moja akasema,
“Mama, unaweza kumpeleka kaka
nyumbani kwanza. Wacha nilale na
Uncle Jack.”
“Yeye ni mwanangu hata hivyo. Hakika
nitamtazama kwa makini.” Jack alimtoa
wasiwasi Lisa.
"Sawa." Lisa aliitikia kwa kichwa huku
akielewa nia ya bintiye. "Nitakuletea
chakula kizuri kesho."
Lisa alipoondoka na Lucas, alimuona
Jack akicheka na Suzie ambaye
alionekana kufurahihi. Hakuweza
kujizuia kukumbuka wakati Suzie
alipozaliwa tu. Siku zote Suzie alikuwa

akilia na hakupenda mtu mwingine
yeyote kumbeba isipokuwa Lisa. Hata
hivyo, Jack alipoenda kuwatembelea,
Suzie alikubali Jack kumbeba, na wala
hakulia. Pia Suzie alifurahia kuwa karibu
na Jack hasa. Ndiyo maana Lisa
alimuacha naye kwa moyo mweupe.
Pengine huu ulikuwa ni mfano wa
msemo 'damu ni nzito kuliko maji', au
pengine, ni kwa sababu Jack alikuwa na
mfanano wa kupita kiasi na Alvin. Mtoto
angeweza kuhisi.
Suzie alipokuwa mikononi mwa Jack
usiku, alimnong’oneza kwa ghafla,
“Anko Jack, baba yangu mchafu ana
upendo kama wewe anapokuwa na
watoto?”
Jack alipigwa na butwaa. Alipomwona
mtoto huyo mrembo ambaye uso wake
ulikuwa umepauka kwa sababu ya

majeraha yake, hakuweza kujizuia
kusema, “Kama yeye akimuona
mrembo kama wewe, hakika atakuwa
rafiki yako. Je! unatamani kuwa na ...
baba?"
"Sijui." Ghafla, Suzie alipiga kelele huku
macho yake yakiwa mekundu. "Watu
wale walipoingia usiku huo, niliogopa
sana. Nilikuwa nikifikiria... ingekuwa
vizuri kama nini ikiwa Baba alikuwa
karibu, lakini sikumwambia Mama
kuhusu hilo. Niliogopa angekasirika.”
"Wewe ni mtoto mzuri sana, Suzie."
Jack akashusha pumzi ndefu.
Alvin lazima awe amepigwa na laana.
Ikiwa Jack angekuwa na mtoto mzuri
kama huyo, bila shaka angemlea kama
binti wa kifalme. “Kama kuna chochote,
unaweza kunitafuta. Nichukulie tu kama
baba yako, sawa mtoto mzuri?”

“Sawa.” Suzie alilala taratibu huku
akimuegemea Jack.
Asubuhi iliyofuata, muuguzi
alimkumbusha Jack ampeleka Suzie
kwenye ghorofa ya nne kwa uchunguzi
wa ubongo wa CT ifikapo saa mbili
asubuhi.
Jack alimvalisha Suzie barakoa yake
vizuri kama alivyoagizwa na Lisa
walipokuwa wakitembea kwenda huko.
Lakini, Suzie alivua kinyago chake mara
tu alipoingia kwenye chumba cha CT.
Mara tu uchunguzi wa CT scan
ulipofanywa, Suzie alitoka akiwa
hajavaa barakoa yake. Mtu fulani
alimgonga Jack mgongoni kabla
hajamvisha Suzie barakoa.
Alipogeuka, Bibi Kimaro alikuwa

akimwangalia Suzie kwa mshangao.
"Jack, huyu ni mtoto wa nani?”
Akiwa amepigwa na bumbuwazi
moyoni, Jack aligugumia, “Bibi, kwanini
uko hapa?”
“Nakuuliza huyu ni mtoto wa nani.” Bibi
Kimaro alikuwa na wasiwasi sana hivi
kwamba alivuta sikio lake moja kwa
moja.
“Yeye... Ni mtoto wa rafiki yangu.” Mara
tu Jack alipomaliza kuzungumza, Bibi
Kimaro alimpiga kofi. “Unathubutu vipi
kunidanganya?! Unafikiri macho yangu
yamekufa, huh? Angalia jinsi
mnavyofanana. Je, ni binti yako wa
haramu?”
Jack alishtuka sana hivi kwamba sura

ya kutokuamini iliosha uso wake.
“Hapana, mimi...”
TUKUTANE KURASA 371-375
ONYO: Ni marufuku kusambaza, kukopi wala kuuza kazi hii kwani endapo kama tutakubaini basi sheria itachukua mkondo wake (By: Official Dully)
 
LISA KITABU CHA NANE (8) SIMULIZI........................LISA KURASA..................371- 375
PRESENT: SIMULIZI ZA DULLY

Sura ya: 371
“Unathubutu vipi kuendelea kukana?!
Utakataa mpaka nimpeleke akapime
DNA?” Bibi Kimaro aling'aka kwa ukali.
Jack akachanganyikiwa mara moja,
ilionekana kana kwamba kulikuwa na
kitu kwenye koo lake. Ikiwa uchunguzi
wa DNA usingeonyesha kuwa yeye ni
baba yake lakini ulionyesha kuwa Suzie
alikuwa na uhusiano naye, ingeleta
shida kubwa.
"Mtoto mdogo, niambie kama yeye ni
baba yako." Bibi Kimaro alitabasamu
kwa upole huku akiinamisha kichwa
kumtazama Suzie. “Mtoto wa
kupendeza kama nini. Kwa mashavu
yake laini na macho angavu, alifanana
kabisa na Lea alipokuwa mdogo.” Bibi
Kimaro alishangaa jinsi Suzie
alivyoumia paji la uso. “Hapana,
umejeruhiwa vipi kitukuu wangu

mpenzi?” Isingekuwa uzee wake, Bibi
Kimaro angembeba Suzie.
Jack alitetemeka pale Bibi Kimaro
alipomwita Suzie kitukuu wake.
Suzie aliinua kichwa chake na
kumtazama Bibi Kimaro kwa udadisi.
Aliposikia Jack akimwita Bibi yake,
akajua Bibi Kimaro alikuwa nyanya
yake. Alipoona tabasamu la urafiki la
bibi yake, Suzie alikuwa tayari
anampenda bila kujua.
Suzie alikulia katika nchi ya kigeni tangu
umri mdogo na alikuwa amezungukwa
na wanafamilia wawili tu, yaani Lisa na
Lucas, watu wengine walikuwa na babu
na babu, lakini yeye hakuwahi kuwaona.
Alitamani kuwa huru na bibi yake pia.
Wazo likamjia kichwani ghafla. Alitikisa
kichwa kabla hajaizungushia mikono
yake shingoni mwa Jack, akiita, “Baba.”
Jack akashtuka.

“Ona anakuita baba na bado unakataa?
Watoto hawatasema uwongo." Bibi
Kimaro alipiga kichwa chake kwa
nguvu.
Jack alijihisi mnyonge. Ni lini alikuwa na
binti ambaye hivi karibuni alikuwa
nanatimiza miaka minne?
“Hi, Bibi mkubwa,” Suzie alimsalimia
Bibi Kimaro kwa utamu.
"Aww, wewe ni mzuri sana. Wewe ni
mtiifu sana, mwenye adabu, na
mwerevu. Tayari unaweza kunitambua
kama nyanya yako mara moja.
Umegunduaje? “Moyo wa Bibi Kimaro
uliyeyuka.
Bibi Kimaro alikuwa na watoto na
wajukuu wengi, lakini mara nyingi
walimkera baada ya kukua—hasa
wajukuu zake.

Willie alikuwa mchezeaji wa wanawake
tu, ilhali Alvin ndiye aliyesababisha kifo
cha watoto wake. Jack, kwa upande
mwingine, bado alikataa kuoa.
Sasa kwa vile Bibi Kimaro hatimaye
alikutana na kitukuu, alianza kumpenda
sana.
“Baba amekuita Bibi sasa hivi, kwa hiyo
lazima utakuwa nyanya yangu,” Suzie
alijibu kwa sura isiyo na hatia, “Baba
huzungumza kila mara kuhusu wewe.
Alisema wewe ni mzuri sana ....”
"Hakika wewe ni kitukuu wangu
mpenzi." Bibi Kimaro alikuwa anazidi
kumpenda. Alimtazama kwa ukali Jack.
“Unatisha sana. Unawezaje kuthubutu
kunificha mtoto mzuri kama huyo?!"
Jack alishindwa kabisa kusema. Ni lini
uongo aliwahi kumtaja nyanya yake
mbele ya Suzie? Mtoto huyu mjanja
alikuwa na ustadi mkubwa wa kuigiza.

“Nitapiga simu kwa mama yako sasa
hivi.” Bibi Kimaro akatoa simu yake na
kumpigia Lea.
Simu ilipopokelewa kwa Lea, Bibi
Kimaro alisema kwa furaha, "Hongera,
Lea. Una mjukuu.
Lea ambaye alikuwa anafanya kazi
ofisini, aliduwaa kidogo. Hakuweza
kujua mjukuu huyo alitoka wapi. “Sarah
ana mimba?”
“Kwanini nishabikie mimba ya huyo
mwanamke? Nilipokuja hospitalini
kumtembelea Aunty Lola leo, nilikutana
na Jack ambaye alikuwa na msichana
mdogo. Msichana anaonekana
kufanana naye kabisa. Ningeweza
kusema kwa urahisi kuwa ni binti yake.
Ikawa kweli nilipowauliza.” Bibi Kimaro
aliongeza kwa tabasamu, “Fanya
haraka na uje umwone. Mpenzi huyu

hakika anapendeza. Lakini paji la uso
wake limejeruhiwa, na inavunja moyo
wangu kuona hivyo. Naam,
nitazungumza nawe baadaye. Nahitaji
kumpigia simu baba yako sasa.”
Baada ya simu kukatika, Lea alibaki
ameduwaa. Kwa kuzingatia kwamba
Jack hakuwa na mpenzi, alikuwaje na
binti ghafla?
Mara Lea akampigia simu Mason.
Ilichukua muda mrefu kabla ya kujibu
simu, "Ni nini tena?"
Mara tu aliposikia sauti yake, moyo wa
Lea ulisisimka. "Mason, mbona unakosa
subira unapojibu simu zangu sasa?
“Hapana, niko na Baba na Mama
kwenye nyumba ya familia ya Campos.
Sitaki tu uniulize kuhusu mahali nilipo
na unikaripie tena.”
Maneno ya Mason yalimwacha Lea
akiwa na hasira. Licha ya kujua kwamba

alikuwa haipendi familia ya Campos,
aliendelea kuwatembelea mara kwa
mara. Hata alilala huko nyakati fulani.
Inavyoonekana, hakuweza kuwa na
wasiwasi juu ya hisia zake tena. Alihisi
kweli kwamba Mason alikuwa
amebadilika.
Lea hakujisikia kubishana naye muda
huo. "Mama yangu alinipigia simu sasa
hivi na kuniambia kwamba Jack ana
binti ..."
"Kwani kuna tatizo gani yeye kuwa na
binti?"
"Hapana. Naomba uje unichukue
twende huko pamoja tukamwone. "
Bibi Kimaro tayari alikuwa amewajulisha
kila mtu katika familia hiyo.
Jack harakaharaka akamtumia Lisa
ujumbe kwa siri akimwambia asije na
Lucas baadae.

Lisa, ambaye alikuwa njiani kuelekea
hospitalini, alihisi kuwa ni upuuzi.
Binti yake mzuri alimwacha kwa usiku
mmoja tu, alikuwa binti wa Jack sasa.
Jack hakuwa mwaminifu kabisa.
Katika muda usiozidi saa moja, Mzee
Kimaro, Lea, Mason, Valerie, na
Spencer walifika. Wote walikuwa na
mashaka mwanzoni. Hata hivyo,
walipoiona sura ya Suzie,
hawakuthubutu kuwa na shaka zaidi.
Alifanana sana na Lea alipokuwa
mdogo.
Lea alipigwa na butwaa kumwona Suzie
kwa mtazamo wa kwanza. Alikuwa
mwanamke aliyependa kazi, kwa hiyo
hakuwahi kufikiria kuwa na watoto na
wajukuu wengi. Lakini, alipomwona
mjukuu mzuri kama huyo ambaye
alionekana kama yeye alipokuwa
mdogo, moyo wake karibu ukayeyuka.

Alipomkaribia tu, Suzie alimtazama na
kusema, “Najua. Lazima utakuwa bibi
yangu."
“Nilikuambia hivyo. Suzie ni mwerevu
sana, kama inavyotarajiwa kwa mjukuu
wa familia ya Kimaro.” Bibi Kimaro
alikuwa na shauku kama mtoto.
Lea alicheka pia. “Ndiyo, mimi ni bibi
yako. Ulijuaje?"
Suzie aliinamisha kichwa chake na
kufikiria kwa muda. “Unafanana kidogo
na baba yangu, kwa hiyo nilifikiri lazima
utakuwa bibi yangu.
Halafu, unaponitazama na
kutabasamu... inaonekana tofauti
kabisa. Inaonekana kama bibi ambaye
alikuwa jirani yangu, anapokuja
kumchukua Nicky.”
“Nani? Nicky?”

“Ni mtoto mwenzangu wa jirani. Ana
babu na bibi yake, wanampenda sana.
Lakini mimi sikuwa na babu na bibi,”
Suzie alisema kwa huzuni huku
akiinamisha kichwa chake, lakini
akatabasamu tena kwa haraka. "Lakini
sasa nimewapata."
"Ndio, una bibi na babu kuanzia sasa."
Lea alijisikia vibaya na kumbeba Suzie
mikononi mwake. Kisha, alimkodolea
macho Jack. “Kwa kweli ulinituficha
jambo muhimu sana kwa muda mrefu,
nitashughulika nawe baadaye.”
Mzee Kimaro akakoroma. “Mjukuu wa
familia ya Kimaro alihuzunika sana hadi
akawaonea wivu wengine kwa kuwa na
babu na bibi. Watoto wanahitaji upendo
wa familia zao. Ulipaswa
kumtambulisha mapema. Halafu, mama
yake ni nani? Kwanini alimuacha Suzie
peke yake hapa?”

Jack alikuwa tayari amefikiria kisingizio.
Alieleza mara moja, “Kwa kweli, sikujua
kuhusu kuwepo kwake kabla ya hapa
pia. Nimefahamu tu juu yake hivi majuzi.
Mama yake ni mhudumu tu kwenye
baa. Nilifikiri kwamba alikuwa mrembo
wakati huo, kwa hiyo... nilimtunza kwa
muda. Baada ya hapo nilichoka,
nikampa pesa na kumuacha aondoke.
"Nilimwambia moja kwa moja kwamba
hakuwa mzuri kwangu na kwamba
haikuwezekana kwake kukubalika katika
familia ya Kimaro. Lakini sikuwahi
kufikiria kwamba angekuwa mjamzito
wakati huo. Aliaga dunia kutokana na
kansa muda fulani uliopita, na aliniachia
mtoto. "
Baada ya kusikia maneno yake,
machozi yalimtoka mara moja Suzie.
"Mama... "
“Sawa, usilie. Bibi atakuwa na wewe
kuanzia sasa. “Lea alikipapasa kichwa

chake kidogo sana. “Njoo, huyu ni babu
yako. "
"Suzie. "Mason alimtabasamu na
kusema, "Kwanini ninahisi kwamba
anafanana zaidi na Alvin?"
“Hiyo ni sawa. Nina hisia hiyo pia,
"Valerie alisema.
Moyo wa Jack ulirukaruka. Alisema,
“Kwani kuna tatizo lolote kuhusu hilo,
mimi na Alvin si tulizaliwa na mama
mmoja?”
”Ni kawaida. Wasichana wengine
hufanana na baba zao wadogo," Bibi
Kimaro alilalamika," Kama mapacha wa
Alvin wangekuwa hai, wangekuwa
karibu na umri wa mtoto huyu pia."
Sura ya: 372

“Mama acha kutaja yaliyopita. Labda
Mungu hakukusudia wajukuu wa Kimaro
wapitie kwa Lisa. "Valerie alifurahia
sana, lakini hakuweza kujionyesha.
“Sawa, nadhani mazingira ya hospitali
hii si mazuri. Wacha turudi nyumbani.
Ajiri timu bora kabisa ya madaktari
wamtibie Suzie nyumbani asipate shida
ya kukaa hospitalini, “Mzee Kimaro
aliamuru.
Suzie alikuwa kitukuu wa kwanza wa
familia ya Kimaro. Ilibidi alelewe kwa
uangalifu.
Wakati familia ya Kimaro inatoka
hospitali pamoja na Suzie, Lisa alitoka
kwenye kona ya ukuta huku akiwa
amemshika mkono Lucas. Ungekuwa ni
uwongo kusema kwamba hakuwa na
hasira wala huzuni. Alipomwona Suzie
akiwa na furaha mikononi mwa Lea,
alihisi kukosa raha moyoni mwake pia.

Ingawa Suzie hakuwahi kusema hivyo
kwa sauti, Lisa alijua kwamba Suzie
alikuwa akiwaonea wivu watoto wengine
waliokuwa na babu na bibi zao.
Labda hiyo ingekuwa bora japo
haikuwa sawa. Ikiwa Suzie angerudi
kwa familia ya Kimaro kama binti ya
Jack, wanafamilia wa Kimaro
wangemthamini. Alvin asingepigana
naye kwa ajili ya Suzie pia. Ni kwamba
binti ambaye alikuwa amejitahidi sana
kumlea alikuwa ghafla na familia ya
Kimaro sasa. Alijisikia mnyonge na
kufadhaika.
“Lucas, unamtamani Suzie? Je! unataka
kurudi kwa familia ya Kimaro pia?" Lisa
alimtazama mwanae.
Lucas akatikisa kichwa. “Sipendi.
Napenda kuwa na Mama siku zote ila
nimemkumbuka dada.” Alimshika Lisa
mkono kwa nguvu baada ya kusema

hivyo. Ikilinganishwa na Suzie, sura ya
Lucas ilifanana zaidi na ya Lisa.
Lisa alienda kwa moyo mpole na
kumkumbatia kwa nguvu.
“Mama usihudhunike sana. Dada huyo,
Suzie, anaona inapendeza kwa sasa.
Hakika atakukumbuka siku chache tu
baadaye, "Lucas alisema kwa utulivu.
“Sawa. "Lisa alipumua. Ghafla
aligundua kwamba watoto walihitaji
ndugu wengine wa familia pia. Kwa
vyovyote vile, hata umng’ang’anieje
mtoto, ipo siku atawatafuta tu ndugu
zake.
"Lucas, kwa kuwa Suzie amechukuliwa
na familia ya kifahari, sio lazima urudi
Marekani peke yako."
“Kweli?” Lucas aliinua kichwa chake
kwa macho ya kumetameta.

“Ndiyo. Nitakutafutia chekeche.
Nitalijadili na Uncle Jack na
kukuandikisha wewe na Suzie katika
shule moja ya chekechea. Lakini huwezi
kuishi nami kwa sasa. Babu yako
anaruhusiwa kutoka hospitalini siku
chache baadaye. Unaweza kuishi na
babu yako kwa muda na unisaidie
kumtunza pia.”
“Hiyo ni sawa mama. Hatimaye naweza
kukutana na mtu mzuri pia.
•••
Suzie alifurahi alipofika kwenye nyumba
ya familia ya Kimaro kwa mara ya
kwanza. Alishangaa kuona jumba
lilivyokuwa kubwa, na maua yalikuwa
yakichanua kila mahali. Kulikuwa na
wanyama wengi wadogo wa kupendeza
pia. Angeweza hata kuogelea na
kupanda farasi hapo.
Alimwambia Lea kwa furaha, “Bibi,
napapenda hapa. Sijawahi kuona

nyumba nzuri kama hii."
Lea na Bibi Kimaro walikuwa
wakitabasamu kutoka sikio hadi sikio.
Ilikuwa nadra kuona Mzee Kimaro
katika hali nzuri pia. “Hii ni nyumba yako
kuanzia sasa. Kuna uwanja mkubwa wa
michezo nyuma ya jengo hilo pia.”
“Kweli? Ikiwa kuna uwanja wa michezo
hapa, hiyo inamaanisha kutakuwa na
watoto wengine ambao watacheza
nami?” Suzie aliuliza kwa furaha.
Mdomo wa Mzee Kimaro ukawa mzito
ghafla. Uwanja huo mkubwa wa
michezo ulijengwa kwa ajili ya mapacha
wa Lisa, lakini hakuwahi kufikiria kama
angepata kitukuu mwingine ghafla.
Lea alisema kwa upole, “Hakuna watoto
wengine. Ilitayarishwa na babu na bibi
zako kwa ajili ya vitukuu vya familia ya
Kimaro. Lakini itabidi usubiri hadi upone

ndipo uende huko kucheza. Twende
zetu. Njoo, Bibi atakupeleka kwenye
chumba cha watoto sasa hivi.”
Bibi Kimaro alimnong'oneza Jack
aliyekuwa nyuma yake, “Hatukujua
kwamba una mtoto, kwa hivyo
hatukutayarisha chumba kipya cha
watoto. Lakini chumba hiki pia ni kipya.
kilitayarishwa kwa ajili mapacha wa
Alvin hapo awali."
Jack alijisemea moyoni. ‘Mambo
yaliyokuwa yameandaliwa kwa
mapacha hao bado yameishia kuwa ya
kwao. Hayakutolewa kwa watu wasio
sahihi.’
“Ni sawa, Bibi. Chumba hicho kiko
sawa.” Jack asingeweza kupinga.
Lakini, kuwa na mtoto aliyefanana
kabisa na Alvin lilikuwa bomu la wakati
pia. Ipo siku lingeripuka tu. Lucas
angeweza kufichuliwa kwa sekunde

yoyote. Alipaswa tu kuruhusu mambo
kuwa kama yalivyokuwa. Suzie alikuwa
salama zaidi na familia ya Kimaro.
“Sawa. "Bibi Kimaro alihisi kwamba
Jack alikuwa akizidi kuwa mkarimu na
mkomavu. “Suzie, mwambie Bibi jina
lako kamili.”
Suzie, ambaye bado alikuwa na furaha,
alisema tu, "Jina langu ni Susan Jones."
“Jones?” Kila mtu alipigwa na butwaa
huku macho yake yakiwa ya ajabu.
Valerie aliendelea kupepesa macho.
"Inaweza kuwa jina la mwisho la mama
yake ni Jones ..."
Jack alihisi moyo wake kupasuka.
Alijiweka sawa na kusema kwa haraka,
"Ni bahati mbaya, lakini kuna watu
wengi wenye majina ya Jones kama jina
lao la mwisho, sawa?"

"Inatosha. Haijalishi Suzie ana jina gani
la mwisho. Itabidi alibadilishe iwe
Kimaro hata hivyo, " Mzee Kimaro
alisema kwa ukali.
“Sitaki kuwa na Kimaro kama jina langu
la mwisho.” Suzie alipomsikia,
alishangaa sana hivi kwamba alikuwa
karibu kulia na kulia. "Sitaki kubadilisha
jina langu la mwisho."
"Sawa, hatutabadilisha ikiwa hutaki. Sio
jambo la dharura. " Bibi Kimaro
aliangaza macho kwa Mzee Kimaro. “
Amefiwa na mama yake na tayari
unamlazimisha kubadili jina lake la
ukoo? Nenda naye polepole. Mbona
unakuwa na haraka hivyo?” Mzee
Kimaro alihuzunika kutokana na
kuzomewa.
Walipofika kwenye chumba cha watoto,
Suzie alikipenda sana. “Bibi, napapenda
sana hapa. Pamejaa midori

ninayoipenda na rangi ya kupendeza.
Kuna hata slaidi. Ingekuwa bora kama
Lucas angekuwa hapa.”
“Lucas?* Kila mtu alipigwa na butwaa
kwa mara nyingine tena.
Moyo wa Jack ulitetemeka tena. Kisha,
akamsikia Suzie akisema, “Yeye ni rafiki
yangu pia. "
“Oh. Kila mtu alielewa mara moja.
Kwa muda mrefu wa siku, Jack alihisi
kana kwamba moyo wake ulikuwa
kinywani mwake. Akamtazama Suzie
kana kwamba anamtazama bwana
mdogo. Kila wakati alimchunga ili
akiropoka neno lolote lenye utata awahi
kusafisha hali ya hewa.
Lea akamtazama. “Kwa kuwa una mtoto
sasa, itabidi urudi kuishi hapa.
Unapaswa kutumia muda wako zaidi

pamoja naye na sio kufikiria tu
kustarehe huko nje.
"Lazima urudi kabla ya saa moja usiku
kila siku kuanzia sasa," Bibi Kimaro
aliamuru.
Suzie akakumbatia paja lake. "Baba,
nakupenda."
Jack alitaka kulia kwa sauti, lakini
hakuweza. Kwa siku nzima, Suzie
alichukuliwa kama binti wa kifalme.
Baada ya saa moja, Mason alimwambia
Lea, "Nina kitu cha kufanya, kwa hivyo
nitaondoka kwanza."
"Unaenda wapi? Tunamfanyia Suzie
karamu usiku wa leo. Wewe ni babu wa
Suzie, unatakiwa uwepo.” Lea
alikasirika kidogo. "Jack ni mtoto wako
wa kumzaa."

“Si tumeonana tayari? Nilimpa hata
pesa ya mfukoni. Zaidi ya hayo, nina
mambo ya kushughulikia.” Mason
aliondoka baada ya kusema sentensi
chache.
Uso wa Lea ulijawa na hasira. Jack
alisogea na kuuliza, “Kwanini Baba
anaondoka? Si anakaa kwenye sherehe
ya Suzie?”
“Alisema ana jambo la kufanya.” Lea
alifikiria na kuuliza, “Sasa, baba yako
alimpa Suzie pesa ngapi za mfukoni?”
Midomo ya Jack ilisogea na kusema bila
raha, “Dola 1,000 tu.”
Ingawa Suzie hakuwa binti wa Jack, kila
mtu alimtendea Suzie kwa furaha
wakiamini ni binti yake.
Spencer na Valerie walimpa shilingi za
Kenya laki mbili kila mmoja. Mzee

Kimaro hata alimpa Suzie kadi binafsi
ya benki mara moja.
Ikilinganishwa na kiasi walichotoa, pesa
za mfukoni za Mason zilikuwa chache
sana hivi kwamba zilimfanya Jack,
mtoto wa Mason, ahisi kukata tamaa.
"Dola 1,000?" Lea alikata tamaa kabisa.
Asingejali kama angekuwa ni mtoto wa
Alvin, lakini Jack alikuwa mtoto wake wa
kumzaa!
Mbali na hilo, Mason hakuwa maskini
hata kidogo. Hata alikuwa amempa
mpwa wa mbali wa familia ya Campos
dola laki moja hapo awali, lakini alitoa tu
dola 1,000 kwa mjukuu wake wa damu?
“Mama, wewe na Baba... Ni nini
kinaendelea kati yenu?” Jack hakuweza
kujizuia kuuliza, “Ninahisi kama hamko
sawa sikuhizi...”

Sura ya: 373
“Wewe pia umeona? Lea alicheka kwa
uchungu. "Jack, unadhani baba yako ni
mtu wa aina gani?"
Jack alifungua kinywa chake kwa
sekunde, lakini mwishowe alinyamaza.
Miaka mitatu iliyopita, kila mtu alikuwa
amemshuku wakati picha za Alvin katika
hospitali ya magonjwa ya akili zilipovuja.
Ni Jack pekee ndiye aliyejua kwamba
hakuwa na hatia.
Alipojua kwamba habari hizo zilitoka
kwa familia ya Campos, alikuwa na zaidi
au chini ya kukisia kuwa ni Mason ndiye
aliyefanya hivyo. Baba yake anaweza
kuonekana mpole na asiyejali mambo
mengi, lakini kile kilichoonekana nje
kinaweza kuwa si kweli.
Kwa bahati mbaya, haijalishi aliuliza

kiasi gani, Mason hakuwahi kujibu
maswali yake moja kwa moja. Miaka
yote hiyo, Jack alihisi kukosa hewa
akifanya kazi katika Kampuni ya KIM.
Lakini, Mason hakuwahi kutaja
chochote kuhusu kumsaidia hata
kidogo. Muda ambao Mason alikaa
naye haukuwa mwingi kama ule ambao
Mason alitumia na Jerome.
Wakati wowote Jack alipoenda kwa
familia ya Campos, watu wa hapo
wangekuwa na urafiki wa juu juu tu
kwake. Kuna wakati mmoja alitaka kuwa
na hisa katika mradi mpya wa baba
yake mdogo kwa sababu alifikiri
haukuwa mbaya. Hata hivyo, ba’mdogo
wake alitoa kisingizio akisema kwamba
tayari alikuwa ametoa mradi huo kwa
watu wengine kwani haukuleta faida
nyingi.
Jack aligundua baadaye kwamba
ba’mdogo wake hakufanya mradi huo

bali alimwacha mpwa wa upande wa
mke wake awe na hisa katika mradi
huo. Yeye aligeuka kuwa duni kwa
mpwa kutoka upande wa mkewe.
Si hivyo tu, lakini wakati mmoja
alipoenda nyumbani kwa familia ya
Campos kwa Mwaka Mpya alipokuwa
mdogo, aliona kwamba Bibi yake
alikuwa na pipi zake za kupendeza
katika mfuko wake. Bibi alisema
peremende zimeisha alipomuomba,
lakini alimwona akimpa Jerome
peremende kwa siri. Alikuwa mjukuu
wake pia.
Hatimaye alifikiri kwamba labda ni kwa
sababu jina lake la mwisho lilikuwa
Kimaro. Kwa hivyo, ingawa familia ya
Campos ilikuwa hatua kwa hatua kuwa
familia ya pili yenye utajiei mkubwa
nchini Kenya, Jack bado alijiweka mbali
nao.

“Mama mimi ni mtoto wa damu wa baba
kweli?” Jack aliuliza swali hilo ghafla.
Lea alipigwa na butwaa kwa muda kisha
sura yake ikaingia giza. Akasema,
“Wewe ni mtoto wa nani kama si wa
baba yako? Unataka kusema nilikuwa
na uhusiano wa kimapenzi na mtu
mwingine?"
“Hicho sicho nilichomaanisha. Sahau,
nilikuwa namaanisha hanijali kama mimi
ni mwanaye." Jack aliondoka baada ya
kusema.
Akili ya Lea ilizunguka kwingine.
Hakuweza kujizuia kukumbuka mambo
fulani ya zamani. Siku alipopata ujauzito
wa Jack, alikuwa ametoka tu kuachana
na Mike Tikisa. Alikuwa katika hali
mbaya na akalewa. Ni Mason ndiye
aliyemrudisha nyumbani baadaye. Bila
kujua, alifanya mapenzi na wote wawili
kwa nyakati tofauti.

•••
Ndani ya Ofisi za Kampuni ya KIM
International.
Baada ya mkutano wake kuisha, Alvin
alitazama simu yake na kuona missed
call nne kutoka kwa Bibi Kimaro.
Akampigia tena. Bibi Kimaro alimkemea
kwa ukali, “Uko busy tu na huyo
mwanamke, Sarah? Hupokei hata simu
zangu."
"Nilikuwa kwenye mkutano," Alvin
alielezea bila hasira.
“Sawa basi. Njoo nyumbani baada ya
kutoka kazini. Kutakuwa na karamu
kwenye jumba la kifahari usiku wa leo.
Mama yako hajakuambia bado?"
“Unafikiri atanipigia simu?”
"Sawa basi," Bibi Kimaro alisema kwa
furaha, "Tumegundua kwamba Jack,

mdogo wako, ana binti wa nje. Sikujua
juu yake mwanzoni, lakini nilikutana nao
leo. Ah, mtoto huyo mdogo ni mzuri
sana. Usiku wa leo, ningependa kuona
kila mwanafamilia wa Kimaro anakuja
na kushiriki karamu kwa ajili ya mdogo
wangu mpenzi. Wewe kama anko wake,
lazima uwepo. Lazima uandae zawadi
na kumtunza pesa ya mfukoni pia."
"Jack ana binti wa nje ?" Alvin
akashangaa. Alijisikia faraja isiyo ya
kawaida. Ikiwa Jack tayari alikuwa na
binti wa nje, Lisa asingefikiria
kuchumbiana naye.
"Alikuwa binti wa nje ya ndoa, lakini
yeye si wa nje tena. Yeye ndiye bintiye
rasmi wa familia ya Kimaro. Yeye ndiye
binti mdogo kabisa katika familia.
Bibi Kimaro alimkumbusha Alvin, “Kwa
njia, Suzie ana zaidi ya miaka mitatu
lakini bado hajafikisha miaka minne.

Unaponunua zawadi, zinunue kulingana
na umri wake. Pia, acha nikufahamishe
kwamba ninamruhusu Suzie atumie
chumba ambacho kilitayarishwa kwa
ajili ya mapacha hao hapo awali. Hata
hivyo hautakitumia sasa hivi.” Alikata
simu baada ya kumaliza kuongea.
Alvin aliishika simu yake na kuduwaa
kwa muda mrefu. Ikiwa watoto wa Lisa wangekuwa hai, wangekuwa karibu na
umri huo pia.
Wakati huo simu yake iliita tena. Sarah
ndiye aliyepiga simu. “Alvinic, bado
unatakiwa kufanya kazi kwa saa za
ziada leo? Si ulikubali kunipeleka
hospitali kuchoma sindano baadaye?”
“Sina muda leo. Lazima niende kwa
babu baada ya kumaliza kazi yangu, ina
naweza nisirudi nyumbani,” Alvin
alieleza.

Sarah aliuma mdomo. “Bado
unanikasirikia kwa sababu kaka yangu
alituma watu kuharibu nyumba ya Lisa?
Alvinic, kwa kweli sikujua juu yake.
Nilimwonya hapo awali, lakini wakati
mwingine hanisikii. Samahani. Sifa yako
imeharibika kwa sababu nina mbaya
kaka kama huyo...”
"Sarah, acha yaliyopita yawe yamepita.
Lakini nakushauri ujiweke mbali naye.
Tayari ana uwezo wa kujiokoa,” Alvin
alimkatisha. Kusikiliza maneno yake
mara moja au mbili kungemfanya
amhurumie, lakini, aliposisitiza mara
nyingi sana, ilimfanya azidi kumchukia
zaidi Thomas.
“ Sawa,” Sarah alijibu kwa aibu.
"Kwa kweli nina jambo la kushughulikia
nyumbani kwa babu leo."
Baada ya Alvin kukata simu, alimuomba
Hans amuandalie zawadi mtoto huyo.

Wakati Hans aliposikia kwamba Jack
alikuwa na binti nje wa miaka mitatu,
alishikwa na butwaa.
“Mbona umeduwaa? Nenda haraka.”
Alvin alimkazia macho.
Baada ya Hans kutoka nje, mara moja
akapata sehemu na kupiga namba ya
Lisa. "Bi Jones, binti wa nje wa Jack
anaweza kuwa ..."
“Uko sahihi. Ni Suzie,” Lisa alimweleza
Hans kila kitu kinyonge.
Hans alipigwa na butwaa.
Hakuna aliyejua kuwa 'kuharibika kwa
mimba' kwa Lisa miaka mitatu au minne
iliyopita lilikuwa jambo ambalo yeye na
Jack waligushi ili kuwaokoa watoto wa
Alvin waliokuwa hatarini.
Hapo nyuma, Lisa alikuwa ametokwa na
damu nyingi baada ya Alvin

kumsukuma. Watoto walikuwa karibu
kupotea, lakini bado walinusurika
mwishowe. Wakati kila mtu alijua kuwa
mimba hiyo imeharibika. Zaidi ya hayo,
hata kama Lisa angezaa mapacha hao,
bila shaka asingeweza kupata malezi ya
watoto hao. Watoto bila shaka
wangedhulumiwa ikiwa wangeanguka
mikononi mwa Sarah.
Kwa hiyo, alikuwa amewasiliana na
Jack. Jack mara moja alimhonga daktari
na kumwambia daktari amwambie kila
mtu kwamba mimba ya Lisa ilikuwa
imeharibika.
Hans alifikiri Alvin angemtaliki Lisa na
kumwacha aondoke baada ya
kuharibika kwa mimba, lakini hakuwahi
kufikiria kwamba Sarah angemchochea
Alvin kumpeleka Lisa kwenye hospitali
ya wagonjwa wa akili. Yeye na Jack
walikuwa na wasiwasi sana katika
kipindi hicho cha wakati.

Kama suluhisho la tatizo hilo, waliamua
kudanganya kifo cha Lisa baadaye na
na kumsafirisha kwenda nje ya nchi
ambako watoto wake walizaliwa salama
huko Marekani.
Hans hakutarajia kwamba Suzie
angerudi kwenye familia ya Kimaro
kama binti wa Jack mwishowe. Hii
ilikuwa kwa bora pia. Angalau Suzie
angeweza kurudi kwa familia ya Kimaro
kwa mara moja na asilengwe na Sarah
pia.
Kwa kuwa ilikuwa zawadi ya binti
mdogo, Hans alienda kwenye duka la
watoto mara moja na kununua nguo
nyingi na vifaa vya kuchezea ambavyo
wasichana wadogo wangependa. Ni
wazi, alitumia kadi ya Bwana Kimaro
kulipia. Bwana Kimaro alikuwa na deni
kubwa mno kwa bintiye.

Sura ya: 374
Saa kumi na mbili na nusu za jioni, gari
aina ya Sedan iliingia kwenye nyumba
ya familia ya Kimaro. Baada ya Alvin
kushuka kwenye gari, Hans alifungua
buti. Uso wa Alvin ulibadilika baada ya
kuona buti limejaa hadi ukingoni. "Ni
nani aliyekuruhusu kununua vitu vingi?"
Hans akapepesa macho. "Yeye ndiye
mwanachama mdogo zaidi wa familia
ya Kimaro. Nilisikia kwamba Bibi Kimaro
amefurahiya sana. Familia ya Kimaro
haijachangamka hivi kwa muda mrefu,
kwa hivyo nilinunua zawadi zaidi.”
Alvin alishtuka. "Huyo si mtoto wangu
hata hivyo."
Kwa kweli, huyo alikuwa mtoto wake,
ndiyo maana Hans alimunulia zawadi
nyingi vile.

Alvin alipanda ngazi. Alipoingia tu ndani
ya jumba hilo, msichana mdogo ambaye
nywele zake zilikuwa zimefungwa
kwenye mabutu mawili akikimbia.
Aligeuza kichwa chake alipokuwa
akikimbia na kusema, “Paka alikimbia.
Ninamfuata.
"Usikimbie, kidonda chako bado
hakijapona." Lea alikuwa amemaliza
kuongea ndipo Suzie alipowavamia
miguu ya Alvin na kuanguka chini.
“Mtoto, tazama mbele yako
unapotembea.” Alvin akainama na
kumsaidia kuinuka.
Suzie aliinua macho na kuiona sura ya
Alvin karibu. Ulikuwa ni uso ambao
alizoea kuuona kwenye picha na video
tu, na sasa alikuwa akiuona laivu. Siku
chache zilizopita, Lucas alikuwa
amefungua video kwenye mtandao na

akamwonyesha. Lakini, baada ya
kukutana na Alvin katika maisha halisi,
Suzie aligundua kuwa anaonekana
mzuri zaidi kuliko alivyokuwa kwenye
picha. Hapana, alikuwa mzuri zaidi
kuliko ma-uncle wake wote waliokuwa
karibu na mama yake.
Suzie alijua kuwa huyo ni baba yake
mkorofi. Baba yake mchafu pia alikuwa
na mwili mzuri. Shati lake jeusi la
kawaida lililochomekewa kwenye suruali
ya rangi ya kahawa lilionyesha
kikamilifu kiuno chake chembamba na
miguu mirefu.
Macho yake yakaangaza mara moja.
Ingawa alipaswa kumchukia, alikuwa
mzuri sana hivi kwamba hakuweza
kupinga kumpenda. Alvin aliinamisha
kichwa kumtazama pia yule binti
mdogo. Alikuwa na mng’aro wa kitoto
kwenye mashavu yake dodo na alikuwa
mrembo kama mwanasesere mzuri.

Alivin alihisi mvuto wa ajabu na
kumpenda kwa mtazamo wa kwanza.
Alipoona kichwa chake kimefungwa
bandeji, hakuweza kujizuia kumuonea
huruma pia. Ilikuwa ni hisia ya kuvutia.
Ni wazi hakuwapenda watoto hapo
awali. Labda ni kwa sababu mtoto huyo
alifanana naye.
Hakuweza kuelewa. Kwa nini mtoto wa
Jack alifanana naye sana?
“Suzie, uko sawa?” Wakati huo, Lea
alimkimbilia. Baada ya kumuona Alvin,
Lea alishindwa kujizuia kumtazama pia
Suzie. Naye akakubali. “Si ajabu Aunty
Valerie alisema Suzie anafanana na
wewe. Mnafanana kweli.”
“Bibi, niko sawa. Huyu ndiye Uncle
Alvin?" Suzie alipepesa macho yake
makubwa. "Anko Alvin anaonekana
mzuri sana."

"Ndiyo, huyu ni Anko Alvin," Lea
alisema huku akitabasamu.
“Anko Alvin, nakupenda sana.” Suzie
aligeuka na kulikumbatia paja la Alvin.
Alvin alipigwa na butwaa, na bila
fahamu alinyoosha mikono yake
kumbeba. Msichana mdogo alikuwa
mwepesi sana, na alikuwa na harufu
nzuri ya maziwa.
“Bwana Mkubwa, hizi ndizo zawadi
ulizomnunulia Binti Mdogo.” Hans alileta
rundo la nguo na midori.
"Wow, nazipenda! Zite ni nzuri kwangu.
"Suzie alitoka kwenye kumbatio lake.
Alikimbia na kutazama nguo na midori.
Macho yake yalikuwa yamejipinda huku
akitabasamu. Alikuwa akitabasamu
kutoka sikio hadi sikio.
Alvin alitabasamu bila kupenda. Alidhani
Hans alikuwa amenunua vitu vingi sana

hapo mwanzo, lakini ghafla alihisi kuwa
hakununua vya kutosha.
“Umenunua hizi?” Lea alimtazama kwa
mshangao. "Hiyo ni nadra."
Wakati huo, Suzie alikimbia upande wa
Alvin. Akampa ishara kwa kidole. "Anko
Alvin, inama kidogo." Baada ya
kuinama, Suzie alisimama kwa vidole
vyake na kubusu shavu lake. "Asante,
Anko Alvin."
Alvin alihisi kana kwamba moyo wake
unabanwa na mkono kwa wakati huo.
Hakuweza kueleza hisia zake. Alihisi
kama... Alimpenda binti yule mdogo
sana. Alikuwa na hamu ya kung'oa
mwezi na nyota kutoka angani kwa ajili
yake ikiwa alitaka.
Hata hivyo... Suzie alikuwa binti wa
Jack. Jack, ambaye Alvin alimdharau
zaidi tangu alipokuwa mdogo. Ikiwa

watoto wake wangekuwa hai,
wangekuwa wa kupendeza sana, sivyo?
Alvin akatoa kadi kwenye pochi yake na
kuiweka mikononi mwa Suzie. "Hizi ni
pesa za mfukoni kwako."
Macho ya Lea nusura yaanguke chini
kutokana na mshtuko.
Hakutarajia kamwe Alvin angekuwa na
urafiki kwa binti ya Jack. Mbali na hilo,
Alvin alimtendea kila mtu kwa ujeuri
Suzie labda ndiye pekee aliyepata
ukarimu maalum kutoka kwake.
"Hii ya nini? Babu wa baba alinipa kadi
pia. Yule Baba Mkubwa alinipa pia,
inatosha. ” Suzie alimrudishia Alvin kadi.
"Siwezi kuchukua hii."
Alvin alifurahi. Ilionekana kama mama
yake alikuwa amemfundisha vizuri. "Ni
sawa. Kadi hiyo ulipewa na babu yako,
wakati hii umepewa na mimi. Ina maana
tofauti. ”

“Suzie, chukua kadi. Anko wako ana
pesa nyingi hata hivyo. Usipoteze,” Lea
alimkumbusha.
Suzie aliinamisha kichwa chake na
kuwaza. Hiyo ilikuwa sawa pia.
Angeweza kumpa Lucas moja ya kadi.
Ingawa hawakujua kuwepo kwa Lucas,
aliweza kuweka sehemu ya kila kitu
alichopokea kwa ajili ya Lucas. Isitoshe,
je, isingempa faida mama yake wa
kambo katili ikiwa asingechukua pesa
za Baba yake mchafui?
“Sawa.” Baada ya Suzie kujibu kwa
sauti ya kitoto, aliushika mkono wa
Alvin. "Anko Alvin, unaweza kwenda
kuona paka pamoja nami?"
Lea alidhani Alvin angemkataa kabisa
Suzie. Alipotaka kuwakatisha, Alvin
alikubali bila kutarajia. Hata alimruhusu
Suzie apande mabegani mwake na

kumpeleka nje kucheza.
Valerie alitembea huku akila karanga.
Alisema, "Wale ambao hawajui bora
zaidi watafikiri kwamba wao ni baba na
binti."
“Uko sawa.”
Ilikuwa ni usiku sana baada ya tafrija
kumalizika. Alvin alikaa usiku kucha
katika nyumba ya babu yake. Katika
miaka mitatu iliyopita, alienda hapo
mara chache sana kwa sababu
kulikuwa na athari nyingi za Lisa hapo.
Usiku, alipumzika chumbani kwake.
Labda ni kwa sababu aliendelea
kuwaza juu ya watoto wawili
aliowapoteza hapo awali ndipo
hakuweza kulala. Ghafla, sauti ya mtu
akigonga mlango nje ilisikika. Aliinuka
na kufungua mlango. Suzie alikuwa
amevalia seti ya pajama za kupendeza

za dubu. Alisimama mlangoni kwa
huzuni huku akipepesa macho. "Anko
Alvin, tunaweza kulala pamoja?"
"Unaweza kulala na baba yako," Alvin
alisema kwa upole.
'Sipendi kulala naye. Anakoroma na
kuna kelele nyingi,” Suzie alifoka na
kusema kwa namna ya kuchekesha.
“Sawa. “Alvin akainama na kumbeba.
Juu ya kitanda, Suzie alimng'ang'ania
kama luba. Punde, alilala fofofo.
Alvin alipomtazama, bila kufafanua
alimsikia msichana mdogo akinong'ona
'Baba'.
Moyo wake ulijawa na uchungu. Labda
ilikuwa wakati wa kujenga familia yake
mwenyewe. Vinginevyo, kwa nini aone
wivu kwa Jack kwa kuwa na binti mzuri
kama huyo? Baada ya kufikiria upuuzi

kwa muda, alilala pia. Sura ya: 375
Alipozinduka, ni kwa sababu kuna mtu
alikuwa akivuta kope zake. Alimsikia
mtoto akicheka kitoto pia. Akafumbua
macho. Alipigwa na butwaa kwa muda
alipoona Suzie amekaa na makorokoro
mengi kitandani.
“Anko Alvin, hii ni ya nani?” Suzie ghafla
akamuonyesha pete.
Alvin alishikwa na butwaa. Alipotazama
vizuri aliona ni pete ya almasi ya waridi
ya bei ghali, yenye uzito wa gramu
13.14. Alifikiri ilionekana kuwa ya
kawaida, lakini hakuweza kukumbuka.
"Umeipata wapi hii?"
“Kuna kisanduku kidogo kabatini. Kuna
namba nyingi juu yake. Nilicheza nayo

tu na ikafunguka.”
Suzie alikuwa anadanganya. Kwa kweli,
aliweka namba za siku ya kuzaliwa ya
mama yake. Lakini, hakujua kwamba
ingefungua. Walipokuwa wakiishi
Marekani, mama yao aliwaelekeza
kufungua kila kitu kilichohitaji namba ya
siri kwa kutumia namba za tarehe yake
ya kuzaliwa. Lucas na Suzy walikuwa
wamekariri namba hizo, na Suzie
alifanya tu kama kujaribu kwenye
kisanduku hicho. Hiyo ilithibitisha
kwamba Mama yake aliwahi kuishi
katika chumba hicho hapo awali.
Alvin alikosa la kusema. Alijua kuwa
Suzie alikuwa anazungumza juu ya
sanduku la usalama. Lisa alikuwa
amekaa katika chumba hicho miaka
mitatu iliyopita. Yeye ndiye aliyeweka
namba za siri pia. Baada ya Lisa
kuondoka, vitu vyake vingi vilivyokuwa
ndani ya chumba hicho viliondolewa,

isipokuwa sanduku la usalama. Hakuna
mtu aliyelifungua kwa sababu
hawakujua namba za siri.
Kabla ya hili, Alvin hakujali hata kidogo
na hakuwahi hata kufikiria kuifungua.
Hakutarajia kwamba yule mtoto mdogo
angefungua kwa bahati mbaya.
“Ni...pete, tu” Alvin alisema kwa sauti ya
hovyo.
“Ni yako, Anko Alvin?" Suzie aliuliza
kwa udadisi.
“Siyo yangu Lakini nadhani najua ni wa
nani. Nitamrudishia.” Pamoja na
kumbukumbu zake dhaifu, Alvin
alikumbuka aliwahi kumnunulia pete
hiyo Lisa kwenye duka la ‘The Only
Love In Life’ kipindi kile mara baada
mapenzi yake ya siri na Lisa
kubumburuka.

“Sawa.” Suzie aliweka pete kwenye
kasha lake na kwenda kuosha uso
wake.
Wakati wa kifungua kinywa, Jack
alikuwa wa kwanza kufika kwenye meza
ya chakula akiwa na Suzie. Alikunja
sura na kusema kwa sauti ya chini,
“Suzie, mama yako akigundua kuwa
unamganda sana Alvin, atakasirika
sana, unajua hilo?” Jack alikuwa karibu
kulia, lakini machozi hayakutoka.
"Baba, kwani utamwambia?"
"Kwa hiyo bado unakumbuka kuwa kwa
sasa mimi ndiye baba yako? Akili zako
zote zimeishia kwa Alvin baada ya
kurudi jana. Uliniacha baada ya kulala
katikati ya usiku. Mtoto wewe, usiharibu
mipango.”
“Anko Jack, umenielewa vibaya.
Natumia sura yangu tu kama mtego.”

Suzie alinong’ona. “Ninamsaidia Mama
kumfundisha somo mama yangu wa
kambo mkatili.”
Kichwa cha Jack kilikuwa karibu
kulipuka. “We mtoto hebu nenda
ukavae. Mama yako aliniambia
nikupeleke chekechea moja na Lucas.”
“Hiyo ni nzuri. Nina kadi ya pesa
ambayo nataka kumpa Lucas,” Suzie
alisema kwa sauti ya dhati. Jack alihisi
kuwa ilikuwa kazi sana kudili na mtoto.
Muda mfupi baadaye, watu wengine wa
familia ya Kimaro walikuja kupata
kifungua kinywa pia. Alvin alitoka
chumbani kwake akiwa na kisanduku
cha kung’aa. Queenie alipoona
kisanduku hicho kizuri hakuweza
kupinga kukifungua ili kutazama.
Alishangaa, "Hii si pete ya almasi?"
Alvin aliinua kichwa chake na

kumtazama huku akikunja uso.
"Unashangaa nini kuhusu pete?"
"Kaka mkubwa, unapanga kumpa
Sarah?" Queenie aliuliza kwa sauti ya
uchungu. "Ni pete ya gharama sana.
Nimeipenda kweli. Niliiona kwenye duka
la ‘The Only Love In Life’ nikatamani
sana ningevaa siku moja.”
Alvin alishika mdomo. "Ikiwa uliipenda
sana, kwa nini hukununua yako
mwenyewe?"
“Ni mwanamke gani angejinunulia? Ni
mwanamume ndiye anayemnunulia
mwanamke.” Queenie alipiga kelele.
Baada ya kifungua kinywa, Alvin aliingia
kwenye gari yake aina ya Sedan. Baada
ya gari kuondoka Sherman Mountain,
alimwagiza dereva, "Nipeleke Mawenzi
Investments."
•••

9:30 asubuhi, Lisa alikuwa anaingia
ofisini kwake baada ya kumpeleka
Lucas shule ya chekechea. Alipokaribia
kupanda juu kutoka sehemu ya
maegesho, aliona sedan nyeusi ikiwa
imeegeshwa mbele ya lango la kuingilia
kwenye lifti. Umbo refu la Alvin lilikuwa
limeegemea Sedan.
“Mbona uko hapa tena?” Lisa alimfuata
kwa hatua ndefu. "Bwana Kimaro,
huwezi kuegesha gari hapa."
Alvin akafungua kifungo kimoja cha
shati lake sehemu ya kifua chake.
Alichukua kisanduku kidogo cha
kung’aa kutoka kwenye gari lake.
Akakifungua na kutoa pete ya almasi
iliyokuwa ndani yake. “Hii... ni yako.”
Lisa alipigwa na butwaa. Pete hiyo
ilikuwa imenunuliwa naye kwa ajili yake
hapo awali kwa gharama kubwa. Ilikuwa
pia ushahidi wa upendo wao. Alikuwa

akiitunza kwa uangalifu hadi miaka
minne iliyopita alipokata tamaa.
Hakukumbuka hata alipokuwa
ameitelekezea. Ilikuwa ni zawadi ya pili
ya gharama ambayo Alvin alimnunulia
ukiacha ile ya Mkufu wa Malkia. Kwa
bahati mbaya vyote havikuwa na maana
kwake tena.
"Ilikuwa yangu, lakini sasa sio yangu
tena." Lisa alitabasamu, lakini macho
yake yalikuwa chini. Alificha hisia hizo
ngumu machoni pake.
"Unamaanisha nini?" Alvin alikunja uso.
"Ulinipa kama zawadi hapo awali, lakini
labda haukumbuki," Lisa alisema kwa
utulivu.
Macho ya Alvin yalisinyaa. "Lazima ni
wewe ndiye ulinilazimisha nikununulie."
Lisa alicheka. “Fikiria vyovyote

unavyotaka, lakini tambua kwamba
tumeachana sasa. Unaweza kumpa
Sarah.” Alipita mbele yake baada ya
kusema.
Alvin alishika mkono wake na kumzuia.
Akaweka kisanduku cha pete mikononi
mwake. “Sarah hatataka kitu ambacho
umevaa hapo awali. Chukua."
Lisa alitazama chini kwenye sanduku.
Alihisi hali ya kujidharau. Kumbe
alikuwa akimpa tu kwa sababu Sarah
hakutaka? “Sawa.” Alichukua kisanduku
na kuondoka.
Baada ya kuingia ndani ya ukumbi
ambapo lifti zilikuwepo, kulikuwa na
pipa la taka kwenye kona. Lisa
akakitupa kisanduku cha pete ndani
yake.
Macho ya Alvin yakachomoka. Alisema
kwa ukali, “Unatupa kitu cha bei ghali

namna hiyo?”
"Kwa kuwa ulitaka niichukue, nina haki
ya kuamua wapi pa kuipeleka."
Lisa alibonyeza kitufe cha lifti ya
kibinafsi ya VIP. Aliingia kwenye lifti,
akafunga milango na kuondoka.
Alvin alitembea hadi kwenye pipa la
takataka. Alitoa kile kisanduku cha pete.
Kuangalia pete ya almasi mle ndani,
alianza kuwaza kwa umakini kwa mara
ya kwanza. Alikuwa amepoteza
kumbukumbu nyingi sana, lakini
zilikuwa kumbukumbu gani? Alifikiri
alikuwa akimchukia Lisa muda wote.
Hata hivyo, kwa nini ampe pete ya
almasi ikiwa anamchukia? Je,
angekubali kwenda Coco Beach na
Lisa, sawa na alivyosema Chester,
ikiwa alimchukia sana?
TUKUTANE KURASA 376-380

ONYO: Ni marufuku kusambaza, kukopi wala kuuza kazi hii kwani endapo kama tutakubaini basi sheria itachukua mkondo
wake (By: Official Dully)
 
LISA KITABU CHA NANE (8) SIMULIZI........................LISA KURASA.................376 - 380
PRESENT: SIMULIZI ZA DULLY

Sura ya: 376
Ilikuwa karibu saa sita mchana
aliporejea KIM International. Sarah
alimpelekea chakula cha mchana.
“Alvinic sijakuona tangu jana.
Nimeku’miss sana. Nilikuandalia
chakula cha mchana maalum kwa ajili
yako.” Sarah alifungua vyombo vya
chakula.
“Sawa.” Alvin alichukua uma. Alipotaka
kula, mlango ukasukumwa. Kichwa
kidogo cha mtoto kilitokea nyuma ya
mlango. Alvin alipotazama, Suzie
alikimbia mara moja huku akirukaruka.
“Nilikukumbuka sana.” Alijitupa kwenye
kumbatio la Alvin.
Sarah alipoteza utulivu alipomuona

Suzie. "Huyu mtoto... hawezi kuwa binti
yako, sawa ..."
“Hapana, huyu ni binti wa Jack. ” Alvin
alimbeba Suzie kwenye mapaja yake.
Aligundua kuwa kamwe hawezi kuwa
mkali mbele ya Suzie. “Si ulikuwa kwa
bibi yako? Kwa nini umekuja hapa?”
"Nilikuja kwenye kampuni na Daddy,
lakini yeye ana shughuli nyingi za
kufanya. Nimechoka kukaa peke yangu,
kwa hiyo nilikuja kukutafuta wewe, Anko
Alvin.” Suzie aligeuza macho yake kwa
Sarah. “Huyu Aunty pia ni mfanyakazi
wa kampuni?”
Moyo wa Sarah uliopata nafuu ulipata
mshtuko mwingine. Ni kwa jinsi gani
hasa alionekana kama mfanyakazi?
“Hapana, yeye ni mchumba wangu,”
Alvin alieleza.

“Habari, Aunty,” Suzie alimsalimia
Sarah kwa uchangamfu.
“Hujambo.” Sarah alitabasamu kwa
unyonge. "Alvinic, sikuwahi kujua
unapenda watoto. Inaonekana
tunatakiwa kuwa na wa kwetu haraka.
"Ndio," Alvin alijibu kwa utulivu, "Labda
ni kwa sababu mtoto huyu anafanana
sana na mimi."
"Ni sawa. Mtoto wetu wa baadaye
atafanana na wewe zaidi.” Sarah
alitabasamu huku mikono yake ikiwa
imeziba mdomo wake.
Macho ya Suzie yalikuwa chini.
Alionyesha sura ya kukata tamaa na
kuushika mkono wa Alvin kwa nguvu.
"Anko Alvin, si utanipenda tena wakati
utakuwa na mtoto wako mwenyewe?"
Macho yake meusi yalijawa na hofu na
kukata tamaa. Uso wake ulikuwa

umepauka, na paji la uso bado lilikuwa
limefungwa bandeji.
Alvin alihisi kubanwa moyoni.
Alimbembeleza kwa sauti ya chini,
akisema, “Usijali mtoto mzuri. Hata
nikiwa na mtoto siku za usoni, bado
nitakupenda wewe Suzie.”
"Asante, Anko Alvin." Suzie akampa
kiss shavuni.
Uso wa Sarah ukawa mgumu. Ingawa
Suzie alikuwa na umri wa zaidi ya miaka
mitatu tu, alimchukia haswaa msichana
huyo mdogo. Zaidi ya hayo, Alvin
alimfurahia sana Suzie na kumtendea
kwa upole sana.
"Alvinic, leo sisi-"
“Anko, hiki ndicho chakula chako?”
Suzie aliuliza ghafla na kumkatisha
Sara.

“Ndiyo.” Alvin aliona matarajio katika
macho ya binti mdogo. "Una njaa?
Unataka kula?”
“Sawa. ” Suzie alichukua kijiko na
kuanza kuchota chakula. Alikunja uso
baada ya kutafuna kidogo. "Wow, kina
ladha mbaya sana. Sio kitamu kama
cha kupikwa kwa mama yangu."
Uso wa Sarah ulikaribia kubadilika
kutokana na hasira. Suzie alionja tu
chakula alichotengeneza na kusema
kwamba kilikuwa na ladha mbaya.
Alvin hakugundua kwani alijisikia sawa
na Suzie. Alifikiri kwamba chakula hicho
kilikuwa na ladha mbaya pia. "Mama
yako alikuwa akipika chakula kitamu
sana?"
“Ndiyo, mama yangu alitengeneza
chakula kitamu sana, nyama choma ya

nguruwe, kababu, kachori sambusa...”
Kwa namna fulani, Alvin ghafla
alikumbuka vyakula ambavyo Lisa
alikuwa amemtengenezea. Ingawa
ulikuwa umepita mudi, bado aliweza
kukumbuka ladha yake. Alikuwa na
uhakika kwamba Suzie angeipenda pia.
"Ah, ghafla nimekumbuka mapisgi ya
mama yangu. ” Macho ya Suzie yakawa
mekundu ghafla, machozi yakaanza
kumlenga lenga.
Alvin alihisi maumivu moyoni mwake.
Alikumbuka Lea alimwambia jana yake
kuwa mama wa msichana huyu mdogo
alikuwa amefariki kutokana na saratani.
“Usilie. Nitamuomba mtu
akutengenezee nyama choma ya
nguruwe ukitaka kula.”
“Lakini ninamkumbuka mama yangu.
Nimemkumbuka sana.” Suzie alizidi

kulia.
Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Alvin
kukumbana na mtoto aliyekuwa akilia.
Alikuwa katika hofu na katika hasara.
Aliweza tu kumtazama Sarah ili kutafuta
msaada.
Lakini, Sarah hakuwa na uzoefu na
watoto pia. Si hivyo tu, bali pia
alimchukia Suzie kutoka ndani ya moyo
wake. Sarah alisita kwa muda na
kuongea kwa kigugumizi, “Kwanini
msimtafute mama yake? Watoto daima
wanataka kuwa karibu na mama zao.”
Sarah alifikiri kwamba Jack alikuwa na
binti wa nje na kwamba utambulisho wa
mama wa mtoto haukuwa wa heshima
kwa familia ya Kimaro. Kwa hivyo,
familia ya Kimaro ilimrudisha mtoto, na
kumzuia mama yake. Hata hivyo, Suzie
alilia zaidi aliposikia maneno ya Sarah.

Alvin alimtazama Sarah kwa hasira
baada ya kusikia maneno yake.
Akasema, “Mama yake tayari
ameshafariki! ”
Moyo wa Sarah ukapandwa hasira
kutokana na kupigiwa kelele.
“Ningejuaje...”
Hata hivyo, Alvin aliweza kusikia tu kilio
cha Suzie wakati huo. Hakuwa na
wakati wa kumjali Sara. "Unapaswa
kurudi kwanza." Akambeba Suzie na
kuelekea kwenye migahawa ya kampuni
hiyo.
Sarah ambaye alibaki nyuma
alikanyaga miguu kwa hasira. Huyo
mtoto alitoka wapi? Alikuwa na chuki
naye sana.
Wapishi maarufu wa migahawa
iliyozunguka kampuniya KIM
International waliagizwa kupika vyakula
alivyopenda Suzie. Lakini, Suzie alionja

mara chache tu kabla ya kulia tena.
“Sipendi. Sio nzuri kama alichopika
Mama. Chakula cha mama kina ladha
safi na harufu nzuri,. Kwa kweli, tayari
najua... kwamba siwezi tena kupata
chakula kama cha Mama tena.”
Alipokuwa akiongea, vijito viwili vya
machozi vilimtoka, lakini, hakutoa sauti
ya kilio. Hakujua kuwa wakati analia
vile, ilizidisha uchungu wa moyo wa
Alvin. Mtoto huyu mdogo alikuwa mjanja
sana.
Alvin pia alijua aina hiyo ya maumivu.
Alipokuwa mdogo, ingawa alikuwa na
mama, ilikuwa ni kana kwamba hakuwa
naye.
“Suzie, twende tkwa baba yako, sawa?”
Kwa kweli Alvin hakuwa na chaguo.
“Sawa, mwambie baba anipeleke kwa
Aunty Lisa. Kupika kwa Aunty Lisa pia

ni sawa na mama yangu. Chakula
chake ni kitamu” Suzie akafuta machozi.
“Aunty Lisa?” Alvin akanyamaza.
"Unamaanisha Lisa Jones?"
“Sijui, namuita tu Aunty Lisa. Yeye ni
mzuri sana. Ni mrembo zaidi ambaye
sijawahi kumuona, na ananitendea
vizuri sana. Je, atakuwa mama yangu
mpya?” Suzie ghafla akainua macho
yake yasiyo na hatia na kuuliza.
Alvin akapagawa ghafla. Jack Kimaro
amelaaniwa! Hata alikuwa amempeleka
binti yake kukutana na Lisa? Alitaka
kweli kumfanya awe mama yake?
Mdomo wa Alvin ulitetemeka kwa
nguvu. Lisa kuwa mke wa Jack na
mama wa Suzie mpya? Kufikiria tu
kulisababisha hasira kumpanda kutoka
ndani kabisa ya moyo wake.
"Haiwezekani kuwa mama yako." Alvin
alijikuta akimpinga yule mtoto.

“Kwanini? Nataka kila wakati kula
chakula cha Aunty Lisa,” Suzie alisema
huku akiinamisha kichwa.
Alvin alimtazama kwa muda na
kumnyanyua. “Nitakupeleka kwake na
kumwambia akupikie. ”
“Sawa! ” Suzie nusura aruke kwa
furaha.
Sura ya: 377
Saa saba mchana, Alvin kwa mara
nyingine tena aliingia kwenye ofisi za
Mawenzi Investments. Hata hivyo,
mlinzi katika maegesho ya chini ya ardhi
hakuruhusu gari lake kuingia baada ya
kusikia maagizo ya Lisa.
Hapo kulikuwa na lifti ya VIP ya kuingilia
moja kwa moja kwenye ofisi ya Lisa.
Angeweza tu kuingia kupitia lango kuu
la kuingilia ndani ya kampuni hiyo.

Mhudumu wa mapokezi alipomuona
Alvin akiwa amemshika mtoto wa miaka
mitatu na kitu ambaye alikuwa akitema
picha yake, alipigwa na butwaa kabisa.
Walinzi waliokuwa mlangoni nao
walizidiwa nguvu, kila mmoja akaanza
kuongea kwa minong'ono.
“Ee Mungu wangu, huyo ni binti wa
Bwana Kimaro?”
“Bila shaka. Lazima atakuwa binti yake
wa kumzaa.”
“Lini ghafla amepata binti mkubwa kiasi
hicho? Anaonekana ana zaidi ya miaka
mitatu. Mama yake anaweza kuwa Bosi
wetu? Ninahisi kama anafanana kidogo
na Bi Jones.”
“Inawezekana sana.”
Hakuna aliyethubutu kumzuia Alvin,
akatembea bila kipingamizi mpaka

kwenye ofisi ya Lisa. Lisa alikuwa
akikutana na wasimamizi kadhaa wa
idara wakati Alvin alipoingia ghafla na
Suzie mikononi mwake.
Siyo wasimamizi kadhaa wa idara tu
ambao walipata hofu, lakini hata Lisa
alihisi roho yake ikikaribia kuondoka
kwenye mwili wake.
“Mwenyekiti Jones, huyu ni... mtoto
wako na Bwana Kimaro? ” Meneja
mmoja aliuliza kwa tahadhari.
Lisa alikuwa njia panda. Je, angeweza
kukataa? Je, Suzie alikuwa
amefichuliwa ndani ya siku mbili tu?
Hapo hapo, Suzie alimtazama na kuita
kwa upole, “Anti Lisa, nilikukumbuka
sana.”
Nini? Ubongo wa Lisa haukuweza
kupata mawazo ya haraka ya Suzie.

“Yeye ni binti wa mdogo wangu.” Alvin
aliwakazia macho wasimamizi.
“Samahani, lakini naomba mtoke nje
kwa muda. Nahitaji kuzungumza na
mwenyekiti wenu.”
"Ndiyo ndiyo."
Nguvu ya kutisha ya Alvin iliwafanya
wasimamizi kuogopa sana nusura ya
kushindwa kupumua. Waliondoka
haraka mahali hapo na kuwaacha.
Mara moja, ofisi ilikuwa kimya.
Suzie alikumbatia shingo ya Lisa na
kusema, “Mimi ghafla nimekumbuka
chakula cha Mama. Baba alinileta
nijaribu chakula chako siku moja na
kilikuwa kitamu. Kina ladha nzuri kama
alichopika Mama, kwa hiyo
nikamwomba Anko Alvin aniletee
kwako.” Kisha, alimkonyeza Lisa kwa
siri.
Lisa alihisi kichwani kikiwa kimekufa

ganzi. Alitoka kuwa mama hadi kuwa
Aunty. Ikiwa Alvin asingekuwa karibu,
angekuwa amemfinya tayari.
Haya yote yalihusu nini? Lakini alielewa
ujanja wa Suzie.
Lisa hakujibu, uso mzuri wa Alvin
ulizama na kusema, “Umesikia
alichosema Suzie? Msichana anataka
kula kchakula chako."
"Hapana, lakini kwanini mko pamoja?"
Lisa alijipapasa na kujiambia atulie na
awe na akili timamu. “Yeye si binti wa
Jack?”
"Kwa hivyo tayari unajua kuwa Jack ana
binti?" Sauti ya Alvin ilibeba uchungu
ambao hata hakuufahamu. Hakukasirika
kwa kuwa Lisa hakumwambia kuhusu
hilo, bali kwa sababu alikuwa karibu
sana na Jack japokuwa tayari alijua
kuwa ana mtoto wa kike.

"Niligundua hivi karibuni." Lisa
hakuweza kuhangaika naye
akamsogelea Suzie kumchukua.
"Unataka kula nini?"
"Nyama ya nguruwe choma, na samaki
wa kuoka."
Lisa alijihisi jasho. Hamu yake ya kula
na ladha yake ya chakula ilifanana
kabisa na ya mtu fulani. “Sawa, twende
tukanunue sasa, sivyo?”
Kwa kuwa binti yake kipenzi alitaka
kula chakula chake, kwa kawaida Lisa
ilimbidi aweke kazi pembeni na kwenda
kumhudumia. Alivaa koti dogo la suti na
kumuongoza Suzie nje. Hakuwa
amemtazama Alvin tangu mwanzo hadi
mwisho.
Alvin aliyepewa bega baridi alikunja uso
na kuwafuata. “Unapikia wapi?”

"Nyumbani, bila shaka. Siwezi kupika
hapa. Lazima niende dukani kwanza."
Lisa alimtazama tena kwa unyonge.
"Rudi tu ofisini kwako.
Nitamjulisha Jack aje kumchukua
baadaye.”
"Hakuna haja. Nimemleta Suzie hapa,
kwa hiyo nitamrudisha mwenyewe.”
Alvin aliweka mikono mfukoni na
kutembea kando yake, akionekana
kupoa na kupendeza.
Wakati wote watatu wakipita kwenye
korido, wafanyakazi wote
wakawatazama.
“Si Bwana Kimaro anaoa? Kwanini bado
anakuja kumuona Mwenyekiti Jones?”
“Huoni? Wana mtoto pamoja. Maadamu
wana mtoto, wawili hao hawawezi
kuvunja uhusiano. ”
“Msichana huyo kwa kweli anafanana

na Alvin Kimaro. Hakika ni binti yake wa
kumzaa.”
Kadiri Lisa alivyokuwa akisikiliza
maneno yao, ndivyo mazungumzo yao
yalivyozidi kuongezeka.
Alvin aliposikia sauti za wafanyakazi
hao, bila kujijua alimtazama Lisa.
Alimshika Suzie huku Suzie
akiikumbatia shingo yake. Walionekana
tu kama jozi ya upendo ya baba, mama
na binti.
Alvin alipoteza mawazo kwa muda.
Ikiwa watoto wao wangekuwa hai, labda
kile ambacho wafanyikazi walisema
kingekuwa kweli. Angeweza kusema
kwamba bila shaka angekuwa mama
mzuri.
Katika maegesho, Lisa alifungua gari
lake, lakini Alvin aliwahikwenye mlango
wa dereva. “Nitaendesha gari. Uketi

naye kwenye kiti cha nyuma."
“Wacha Anko aendeshe,” Suzie alisema
haraka. Lisa hakuwa na jinsi zaidi ya
kumpa funguo Alvin.
Alvin akawasha gari kwa kasi. Kupitia
kioo cha nyuma, alimwona Suzie akiwa
amekumbatiana na Lisa.
Kwa muda, alihisi kama watatu hao
walikuwa familia na alikuwa akimpeleka
mke wake na mtoto wake kwenda
kufanya manunuzi. Hisia hiyo
haikumchukiza. Kinyume chake, alihisi
kwamba kifua chake kilijaa hadi
ukingoni.
Katika kiti cha nyuma, Lisa
alimnong’oneza Suzie sikioni, “Wewe
mpuuzi mdogo. Huogopi kugunduliwa?”
"Siwezi, mama. Wote wanaamini
kwamba mimi ni binti wa Anko Jack,”
Suzie alisema kwa upole, “Mwanamke

yule katili alienda kwenye kampuni
kumtafuta baba yangu mchafu asubuhi.
Simpendi hivyo nikamdanganya atoke
nje. Mama, nakusaidia kulipa kisasi."
Lisa hakujua acheke au alie, lakini
moyoni mwake kulikuwa na utamu.
Binti yake mwenye akili za haraka
alikuwa na akili kweli. “Sawa. Kaa mbali
na huyo mwanamke. Bado wewe ni
mdogo, kwa hivyo hujui jinsi watu
wanaweza kuwa wa kutisha. Mama
hataki kukupoteza.”
“Sawa. Baba mchafu ananipenda sana.
Hakika nitamfanya anipende zaidi ya
yule mwanamke mbaya,” Suzie alisema
kwa kujiamini.
Lisa alimtazama kwa umakini. "Suzie,
unampenda Alvin?"
“Yuko sawa. Yeye ni mzuri, kwa hivyo
yeye sio mtu mbaya." Macho ya Suzie

yalikuwa yanametameta
alipozungumza. Ilikuwa wazi kwamba
alimpenda.
Naam, ilikuwa wazi binti yake alikuwa
amemfuata linapokuja suala la ladha
yake kwa wanaume. Alijali uso wa
mwanaume tu na si kingine. Angepaswa
kumsomesha Suzie baadaye.
Katika maduka makubwa, Lisa
alichukua toroli na kumbeba Suzie ili
akae humo. Hata hivyo, Suzie alikuwa
mzito sana na hakuweza kumwinua juu
vya kutosha. Kisha, Alvin akaja na
kunyoosha mkono kumshika Suzie kwa
nguvu, na kumweka kwa urahisi kwenye
toroli.
Aliutazama mkono wake, na Alvin
akatabasamu kidogo alipomtazama.
"Wanaume wana nguvu zaidi."
Lisa alitabasamu. “Ndiyo, una nguvu
kuliko mimi. Vinginevyo,

nisingesukumwa chini na wewe na
kupoteza watoto wangu.”
Tabasamu kwenye pembe za mdomo
wake likatoweka taratibu. Alijua kwamba
alikuwa akizungumza miaka mitatu
iliyopita. Alipomsukuma chini, aliishia
kupoteza watoto. Uso wa Alvin mara
moja ukageuka kwa huzuni.
Suzie aliuliza bila hatia, “Anko, kwa nini
ulimsukuma Aunty Lisa? Ulikuwa
unamjua kabla ya hii?"
“Lo, hatukujuana tu. Tulikuwa...
tumezoeana sana,” Lisa alisema kwa
kumaanisha.
“Oh, ninaelewa. Mlikuwa kwenye
mapenzi,” ghafla Suzie alisema kwa
kutambua. Lisa akaduwaa.
Alvin hakuthubutu kuendelea na
mazungumzo hayo akatazama huku na

huko ili kubadilisha mada. “Nyama za
nguruwe ziko wapi?”
"Kuna chokoleti! Nataka kuinunua.”
Suzie ghafla alielekeza mbele.
"Hapana. Meno yako yataoza.” Lisa
alikataa mara moja.
"Anko, nataka kula chokoleti. ” Suzie
alifoka na kuanza kudeka kwa Alvin.
“Sawa. Ni sawa ikiwa unakula mara
moja kwa wakati. ” Alvin alimruhusu bila
masharti.
Lisa alihisi kichwa kinamuuma. Suzie
angeharibiwa uozo huo. Baada ya
kununua viungo, wote watatu walirudi
Karen Estate. Alvin alipoingia ndani
aliona samani zote za ndani
zimebadilika. TV, kiyoyozi, sofa, jokofu,
na hata vitu vya jikoni vilibadilishwa.
Alijua kwamba Thomas Njau alikuwa

ameivunja nyumba yake, lakini
hakutarajia uharibifu kuwa mkubwa
sana. "Je, ... samani zote
zilibadilishwa?"
“Si unaona mwenyewe? Hata Ukuta
ulihitaji kubadilishwa rangi. Kila kitu
kiliharibiwa kabisa. ” Lisa alimtazama
kwa hasira.
Alvin alinyamaza kwa muda kabla ya
kutoa kadi ya benki mfukoni na
kumkabidhi. “Iligharimu kiasi gani?
Nitakufidia.”
Alifikiri kwamba Lisa angeweza kukataa,
lakini bila kutarajia, alichukua bila neno.
“Unapaswa kutufidia,” Lisa alisema kwa
upole, “alikwepa jela, lakini
hakulazimika kulipa hata senti moja.
Kwa kweli unapaswa kuzungumza na
familia ya Njau. Huku sio kuomba
msamaha wa dhati.”

Sura ya: 378
Lisa alipeleka vyakula jikoni kupika.
Suzie alikaa kwenye sofa na kutazama
Tv. Baada ta muda, harufu nzuri ilitoka
jikoni. Alvin alikuwa hajala chakula cha
mchana, hivyo tumbo lake lililalamika
kwa kusikia harufu ile ya kuvutia.
Dakika 40 baadaye, Lisa alitoa chakula
jikoni na kuweka mezani. Alvin
alitazama nyama ya nguruwe
iliyochomwa, ndizi, samaki wa
kuchomwa, kachumbari na madikodiko
mengine pale mezani, na akajikuta
anapata hamu ya kula kwa njia
isiyoelezeka.
Lisa alimpa Suzie sehemu yake. Alvin
hakutarajia kuhudumiwa, hivyo akaenda
kujitafutia sahani. Hata hivyo, alipokuja,
hakukuwa na kitu chochote kwenye
mabakuli. Vyote vilikuwa vimeishia

kwenye sahani za Suzie na Lisa
"Lisa, chakula changu kiko wapi?"
Macho yake yalimtoka.
“Kwani ulisema unataka kula? Isitoshe,
nilikubali kumpikia Suzie tu, sio
wewe. Tayari ni saa tisa mchana na
bado hujala, Bwana Kimaro?”
Alvin akauma mdomo. “Tumeambata
wote mjini mjini mchana huu kukua
chakula. Ningepata wakati gani wa
kula?”
“Lo! Ikiwa una njaa, unaweza kwenda
kumtafuta Sarah. Siwajibiki kwako.” Lisa
alimsaidia Suzie kupata vipande bora
zaidi vya nyama ya nguruwe choma na
kuchambua mifupa kutoka kwenye
samaki kabla ya kumpa. Mashavu ya
Suzie yalikuwa yamejaa wakati akila,
akionekana kama nguruwe mdogo.
“Anko Alvin ameacha chakula tele ofisini

alicholetewa na mchumba wake.” Suzie
akapasua jipu. “Hana hata njaa. Kama
ana njaa ataenda kula chakula chake
kibaya.”
“Umesikia?” Lisa alicheka. “Umeacha
chakula cha mkeo huko halafu unakuja
kudowea chakula cha mtoto.”
Baada ya kumeza chakula, Suzie
alisema huku akimtazama Alvin kwa
jicho la pembeni kana kwamba
anamrusha roho. “Upishi wako ni mzuri
sana, Mama.”
Alvin aliyebaki ameduwaa na sahani
yake kubwa mkononi, alimeza mate ya
uchu. Alijua chakula hicho kilikuwa
kitamu, hivyo alitaka kukila pia.
Ni kana kwamba Suzie alikuwa akisikia
mawazo ya ndani ya Alvin. Kwa huruma
alimpa kipande cha nyama ya nguruwe.

“Hebu onja kidogo Anko Alvin mapishi
ya Aunty yangu.”
Alvin alikipokea kipande kile na
kukitupia mdomoni fasta. Kilikuwa
kitamu sana! Angeweza kula chote peke
yake kama angeachiwa. Hata hivyo,
Suzie alimpuuza baada ya kumpa
kipande kimoja tu. Lakini hakumzuia
kula. Angeweza tu kutumia uma
kuchukua chakula mwenyewe.
Lisa hakuwa amepika chakula kingi, na
baba na binti yake walikuwa waroho
kweli kwenye nyama. Kwa muda mfupi,
nyama ya nguruwe iliyochomwa ilikuwa
karibu kumaliza.
Suzie alishika bakuli na kusema kwa
huzuni, “Anko, umetosha. Zimebaki nyama zangu mimi bado sijashiba.”
Alvin alipokitazama kile chakula kitamu
kikiingia mdomoni mwa Suzie, tumbo

lake lilizidi kumkosesha raha. Alitamani
ampokonye.
Lisa alisafisha meza na kumpa Suzie mtindi uliotiwa strawberry ili ashushie
chakula chake. Suzie alikunywa
kikombe kikubwa kwa kuridhika na
kushukuru, "Maziwa ni matamu, Mama."
Mikono ya Lisa ilitetemeka. Ilikuwa ni
mara ya pili sasa Suzie anajisahau na
kumuita Lisa ‘Mama’.
Alvin alimtazama Suzie kwa mshangao.
"Umemwitaje?"
Suzie nusura akose cha kujitetea. Lakini
kwa haraka akarekebisha mambo na
kusema, “chakula cha Aunty Lisa ni
kitamu kama cha mama yangu, ndiyo
maana najisikia kama nipo na mama.
Aunty Lisa, si baba atakuoa ukuwe
mama yangu, seti eeh?”

Lisa alichoka kwa uwezo wa kuigiza wa
bintiye na kwa upole akampigapiga
kichwa chake. "Ukipenda nitakuwa."
Alvin kidogo atapike nyama zote
alivyosikia hivyo. Lisa awe mke wa
Jack?
“Nataka ukuwe mama yangu.” Upesi
Suzie aliitikia kwa kichwa na kupepesa
macho kwa nguvu na kusababisha
machozi kumdondoka. “Kila ninapokula
chakula chako, Aunty, namfikiria Mama.
Sasa hivi, nilikufikiria kama mama
yangu.” Kisha, ghafla akaruka mikononi
mwa Lisa. "Aunty, unaweza kuwa mama
yangu?"
Umahiri wa malkia yule mdogo wa
maigizo ulikuwa ukiongezeka haraka
sana. Hata Lisa, aliyejiita gwiji wa
kuigiza, hakuweza kuendana na
mdundo wa bintiye. Ilikuwa ni huruma
kwamba msichana huyu hakuwa tasnia
ya uigizaji. Kwa kweli angeweza

kucheza kama nyota wa watoto.
Kabla hajajibu, sura ya Alvin ikabadilika
na kusema kwa sauti ya hasira.
"Hapana."
Suzie alimtazama na kuogopa sana
hadi akajizika mikononi mwa Lisa.
Alianza kulia. "Anko anatisha sana."
"Mbona unakuwa mkali sana kwa
mtoto?" Lisa alimtazama kwa hasira.
Alvin hakuwa na nia ya kumtisha Suzie,
lakini wazo tu la Lisa kuolewa na Jack
liliufanya moyo wake ukose raha bila
hiari yake. "Suzie, samahani." Haraka
haraka akaomba msamaha kwa sauti ya
chini. “Lakini wewe bado ni mdogo, kwa
hiyo kuna baadhi ya mambo huelewi.
Aunty Lisa hawezi kuolewa na baba
yako.”
"Kwanini isiwe hivyo? sielewi.” Suzie

alijifanya kutojua. “Baba hajaoa, na
Aunty Lisa pia hajaolewa. Kwanini
wasioane?”
“We mtoto, nimesema haiwezekani,
husikii? ” Alvin alizidiwa na hasira na
kukataa kabisa. “Aunty Lisa ni mke
wangu wa zamani kwa hivyo hawezi
kuolewa na baba yako. Babu na babi
zako hawatakubali.”
“Oh.” Suzie alifikiria jambo hilo kwa
uzito. “Sasa kwa nini usimuoe Aunty
Lisa, Anko? Kwa njia hiyo, Aunty Lisa
pia atakuwa mtu wa familia yangu.”
Baada ya maneno yake kuanguka,
sebule ikawa na kimya cha ajabu.
Alvin alimtazama Lisa kwa mshangao.
Lisa aliinamisha kichwa chake na
kuweka banio la nywele nyuma ya
masikio yake, akionyesha wasifu wake
mzuri na wa upole. “Hatuwezi,” alisema

kwa upole. "Tulifunga ndoa hapo awali,
lakini tuliachana kwa sababu
tulishindwana. Anko wako ataoa hivi
karibuni pia. Atakuwa na mke
mpendwa, kwa hiyo lazima ukubali hilo.”
“Oh, nakumbuka sasa. Atakuwa ni yule
Aunty nilimwona asubuhi. ” Suzie ghafla
akampa Alvin sura ya kufurahi. “Anko,
wewe una hasara sana. Chakula cha
mkeo si kizuri, sitakuja kwako, lakini
ninaweza kuja kwa Aunty Lisa wakati
wowote nikitaka kula chakula kitamu.”
Alvin alihisi kama amepooza tena, na
maneno yale yalimkosesha raha sana.
Hakuwa amefikiria hivyo hapo awali,
lakini kwa wakati huo aligundua
kwamba alipendelea kutumia muda
wake mwingi na Lisa badala yake.
Wawili hao walikuwa wameendana
vizuri walipoambatana na Suzie kwenye
supermarket. Ikiwa wangekuwa familia
ya watu watatu, wangeweza kula

vyakula vitamu vilivyopikwa na Lisa na
mara kwa mara kwenda kwenye uwanja
wa michezo pamoja. Hiyo ilikuwa
imekaa vizuri sana.
Hata hivyo, alielewa kwamba tayari
alikuwa ameamua kumuoa Sarah.
Hakukuwa na kurudi nyuma kwa
mambo mengi.
“Sawa, unapaswa kuondoka sasa.
Tayari nimempigia simu Jack. Atakuja
kumchukua Suzie baadaye.” Lisa
alimfukuza Alvin. “Haikuwa rahisi
kumaliza kukarabati nyumba hii. Sitaki
Thomas Njau anikodishie tena watu wa
kuharibu mahali hapa ikiwa familia ya
Njau itagundua kuwa uko hapa.”
Alvin alikasirika. “Hakuna haja,
nitaondoka na Suzie. Hujui kutunza
watoto hata kidogo, kwa hiyo sikuamini
kuwa utaitunza vyema hazina ndogo ya
familia yetu ya Kimaro."

"Sijui kutunza watoto?" Lisa alidhani
amesikia mzaha. Alikuwa peke yake
akilea watoto wawili. Mpaka hapo
anamwona Suzie, ni yeye ndiye
aliyemlea.
“Nimesema kitu kibaya?” Alvin aliuliza
kwa jeuri.
"Sawa, kila kitu unachosema ni sawa.
Nendeni sasa.” Lisa akawafukuza. “Nina
jambo la kufanya baadaye.”
“Anti Lisa nitamwambia baba kesho
aniletee kwako tena. ” Suzie alipunga
mkono. Ingawa hakutaka kuondoka
upande wa mama yake, ikiwa
angesisitiza kukaa kwa muda mrefu,
baba yake mchafu angetilia shaka.
Alvin alimbeba Suzie pale chini na
kuchuchumaa huku akimwambia kwa
umakini, “Suzie, huwezi kuendelea
kumwambia baba yako akulete kwa

Aunty Lisa.”
"Kwa nini isiwe hivyo?" Suzie alikasirika
mara moja. “Anko, kama ningejua
mapema nisingekuomba uniletee kwa
shangazi. Ninampenda sana, lakini
huniruhusu kukutana naye.”
Sura ya: 379
"Sikuzuii kumuona." Alvin alikunja
midomo yake myembamba na kusema
kwa kufadhaika, "Kama unataka
kumuona, mimi ndo nitakuleta kwake,
lakini sio baba yako."
"Kwanini isiwe baba?" Suzie aliinamisha
kichwa chake huku akitazama kwa
udadisi machoni mwake. “Anko
unampenda Aunty, ni wivu huu?”
Macho meusi ya Alvin yalipungua
ghafla. Alimpenda Lisa? Je, ilikuwa wazi

sana hata mtoto mdogo kama Suzie
angeweza kusema?
“Usiongee upuuzi. ” Uso wake mzuri
uligeuka na kukunjamana. "Mtoto
unajifanya kujua nini maana ya
kumpenda mtu?"
"Najua jinsi ilivyo. Kulikuwa na mvulana
mzuri jirani yetu, na wakati wowote
wasichana wengine walipocheza naye,
sikufurahi sana.” Suzie alipiga kelele na
kusema, “Huo ni wivu.”
Kichwa cha Alvin kilianza kumuuma.
Alihitaji kuzungumza na Jack, ili Suzie
asianze kuchumbiana akiwa shule ya
chekechea.
“Sawa, huelewi. nitakupeleka kwa baba
yako.” Alvin aligundua kuwa kichwa
chake kingemuuma zaidi ikiwa angeendelea kujadiliana naye.

"Anko, kama unampenda Aunty, basi
unapaswa kunileta kwake kila siku."
Suzie alikunja ngumi na kumtia moyo.
“Suzie, tayari nina mchumba. Siwezi
kuwa na tamaa kama za fisi. Na pia
acha kuingilia mambo ya watu wazima,
sawa?” Alvin alimueleza kwa umakini na
kumuonya muda huo huo.
Baada ya kuwafukuza baba na binti,
Lisa aliendesha gari hadi shule ya
chekechea kumchukua Lucas. Mvulana
mdogo alikuwa amevalia sare ya shule
ya rangi ya machungwa ambayo
ilimfanya aonekane mzuri sana na
mzuri.
"Lucas, siku yako ya kwanza shuleni
ilikuwaje? Ilikuwa ya kufurahisha?"
Aliuliza kwa wasiwasi.
“Hakuna hata raha. Wote ni watoto
sana,” Lucas alisema kwa dharau.

"Nadhani natakiwa kwenda shule ya
wakubwa."
“...Um, huwezi. Bado wewe ni mtoto,
kwa hiyo inabidi ubaki kwenye tabaka la
chini.” Lisa akahema.
Watoto wake wawili walionekana
wakubwa kutokana na haiba zao.
Utasema wana miaka mitano au sita.
Kile lichokikuta Lucas wanafundishwa
watoto wenzake yeye alikuwa anajua
kila kitu. Alikuwa ameshaanza hata
kujua kusoma maneno mengi ya
kingereza.
Tabia ya Lucas ilikuwa kama Alvin,
lakini upendeleo wake wa chakula
ulichukua nafasi ya Lisa. Wakati huo
huo, tabia ya Suzie ilikuwa nadhifu na
ya ajabu kama Lisa, lakini upendeleo
wake wa chakula ulichukua nafasi ya
Alvin.
Joel aliruhusiwa kutoka hospitalini siku

hiyo. Kwa hivyo, Lisa alimpeleka Lucas
kwenye jumba la Ngosha.
Ingawa Lisa alikuwa tayari
amemwambia Joel mapema, bado
alifurahi sana alipomuona Lucas.
“Lucas, kwanini usiishi hapa na babu
kuanzia leo?”
“Sawa babu. Naweza kukutunza.” Lucas
alisema kwa upendo.
Joel alifurahishwa sana, na Lisa
akamkumbusha, “Baba, tafadhali weka
utambulisho wa Lucas kuwa siri kwa
wakati huu. Ni bora kutoruhusu watu wa
nje kumuona. ”
“Lakini huwezi kuendelea na jambo hili
milele...” Joel alitafakari. “Unaogopa
Alvin atakunyang’anya watoto? Au
utatangaza baada ya Sarah kupata
mtoto?”

“Baba huelewi Alvin ni mtu wa aina gani
sasa? Hata kama ana mtoto mwingine,
hataruhusu watoto wa familia ya Kimaro
kulelewa nje. Kwa hali yoyote, usijali.
Nina mpango wangu mwenyewe." Lisa
kisha akabadilisha mada. "Vipi kuhusu
kampuni, imekuwaje tena?"
Joel alipumua kwa kusikia hivyo. “Babu
na bibi yako wamechanganyikiwa.
Wamemruhusu Melanie kurudi kazini
tena. Damien na bintiye wako kwenye
nyumba ya kifahari wakijaribu
wawezavyo kuwafurahisha babu na bibi
yako. Kwa bahati mbaya, afya yangu si
nzuri.”
"Jambo muhimu ni kwamba Melanie na
Damien ni sehemu ya ukoo wa familia
ya Ngosha, kwa hiyo ni jambo la
kawaida kwa Bibi na Babu kuwa
wapole kwao." Lisa alimfariji.” Baba,
hakuna haja ya kuwa na wasiwasi.

Nitakusaidia kukabiliana nao baada ya
siku chache.”
Kwa muda huo, mtu ambaye Lisa
alitaka kushughulika naye zaidi, alikuwa
Sarah Njau.
Baada ya kumkabidhi Lucas kwenye
jumba hilo la kifahari, hatimaye Lisa
aliondokana na wasiwasi wake wa
hkugunduliwa na Alvini. Akiwa na
watoto hao wawili, ilikuwa kama bomu
linaloweza kulipuka wakati wowote.
Usiku, baada ya Lucas kulala, Lisa
aliondoka kwenye jumba la Joel.
Alipofika kwenye gari, akapiga namba
ya Logan. “Vipi hali ya Hisan Gadaffi?”
“Jamaa huyo anapenda kucheza
kamari, kunywa pombe, na kulala na
malaya kila siku. Hata alilala na
wanamke kumi kwa siku mbili
mfululizo.” Logan akahema. "Sarah huja
mara tatu kwa wiki na kukaa kwa masaa

saba hadi nane kila wakati. Nitashangaa
sana ikiwa Alvin Kimaro hana ugonjwa
wowote wa zinaa. Ikiwa sivyo, ataupata
mapema au baadaye."
"Nyamaza." Lisa alipapasa paji la uso.
Kila mara alizungumza juu ya kitu kama
hicho wakati alipompigia simu, na
ilimfanya ahisi wasiwasi sana. "Mipango
ikoje na watu tuliowasiliana nao?"
“Imekwisha, lakini nadhani ametumia
pesa nyingi alizonazo. Atamwomba
Sarah pesa tena hivi karibuni. Nadhani
Sarah hataweza kumpa pesa zaidi.”
"Kama ningekuwa Sarah, bila shaka
ningetegua bomu hili kabla sijaolewa,"
Lisa alisema huku nyusi zake zikiwa
zimeinuliwa.
"Unamaanisha..."
“Lazima tumuweke Hisan hadi siku ya

harusi. Vinginevyo, nitawapelekeaje
zawadi yangu kubwa?”
"Nimeelewa." Logan alibofya ulimi
wake. Hii ndiyo sababu wanaume
hawapaswi kamwe kuwaudhi wanawake
kwa sababu baadhi ya wanawake
hawakuweza kusamehe kirahisi.
•••
Siku inayofuata. Kwenye makazi ya
kifahari ya Kimaro.
Jack alikuwa amemaliza kifungua
kinywa na alikuwa karibu tu kwenda
kazini wakati Suzie alipomkumbatia
upesi. “Baba, nataka kwenda na wewe
kwenye kampuni. Nimemkumbuka Bibi.”
Jack alimnyanyua kwa hasira. “Usifikiri
sijui. Unataka kumtafuta Alvin badala
yake.”
“Anko, nilifikiria jambo hilo usiku kucha
jana na nikaona jinsi ya kulipiza kisasi
kwa Mama yangu na kukabiliana na

mama huyo wa kambo mkatili.” Suzie
alimtazama kwa kumsihi. “Lazima
niende. Kwa njia, huwezi kunichukua
mchana. Ninahitaji kulala usiku mzima
na yule mama wa kambo mwovu, kwa
hivyo lazima ushirikiane nami. Tayari
nimetayarisha mpango. Nitakupa
baadaye.”
Kuangalia jinsi alivyokuwa na ujasiri wa
kulipiza kisasi, Jack alikosa la kusema.
Kwa kuwa hakuweza kumkatalia,
alienda naye ofisini. Labda hakukaa
kwa muda mrefu kwenye kampuni jana
yake, lakini kila mtu katika kampuni
alijua kwamba familia ya Kimaro sasa
ilikuwa na binti wa kifalme.
Ingawa alijulikana kama binti wa Jack,
Alvin alimpenda sana, na pia alikuwa
mjukuu wa Makamu Mkurugenzi Lea
Kimaro. Mara baada ya Suzie kufika
ofisini, alienda ofisini kwa Alvin bila
kipingamizi.

“Anko naomba usinichukie,” Suzie
alisema kwa huzuni baada ya kuingia
ndani. “Baba alisema ninaudhi. Alisema
kuwa ni kosa langu kwamba hawezi
kwenda nje kutembea usiku tena na
lazima arudi nyumbani mapema. Anko,
mimi ni msumbufu?"
"Bila shaka hapana." Alvin alihisi kama
alikuwa na wasiwasi mwanzoni.
Hata hivyo moyo wake ulimuuma sana
aliposikia maneno ya Suzie na papo
hapo akamkasirikia Jack. Angewezaje
kusema kitu kama hicho kwa mtoto?
"Nitamwita baba yako na kumfundisha
somo." Alvin kisha akachukua simu
yake.
Suzie haraka akamshika mkono.
“Hapana, sitaki nyie wawili mgombane
kwa sababu yangu. Ninajua kwamba
Baba ananipenda, lakini... hataki
kuandamana nami kama Mama

alivyofanya. Anko, sitakusumbua.
Unaweza kuendelea kufanya kazi.
Nitakaa hapa na kuchora." Hapo akatoa
ubao wake wa kuchora na kukaa
kwenye sofa huku akichora kwa utiifu.
Alvin alifurahi sana na kumwambia
sekretari wake alete vitafunwa. Baada
ya kukaa siku nzima, Alvin alipokea
simu kutoka kwa Jack jioni. “Kaka,
nitatoka kunywa pombe na marafiki
zangu usiku huu. Unaweza kunitunzia
Suzie usiku wa leo?”
Sura ya: 380
"Tangu lini tulielewana vizuri?" Alvin
aliamini zaidi juu ya kile Suzie alisema.
"Jack Kimaro, tayari una binti. Una
miaka mingapi? Unahitaji kutambua
kuwa wewe sasa ni mzazi na kuchukua
jukumu kwa binti yako. Suzie

anakuhitaji.”
“Lakini nahitaji uhuru. Haya, kusema
ukweli, nilifurahi sana kuwa na binti
mwanzoni, lakini baada ya siku chache,
ikawa shida. Sina uhuru, na Suzie
hataki kulala na bibi yake, kwa hiyo
naweza kukukabidhi wewe tu kwa kuwa
anakupenda.”
Kisha, Jack akakata simu. Alvin
alitazama chini na kumwona Suzie
mwenye machozi, ambaye alisema,
"Baba hanipendi tena."
“Hapana, baba yuko busy. Utalala kwa
Anko usiku wa leo, sawa?" Ilimuuma
Alvin kumuona akilia.
"Anko, samahani kwa kukusumbua."
Ujanja wa Suzie ulimfanya Alvin
amlaani Jack mara elfu kumi.
•••
Katika Jumba l a Kifahari la Alvin.

Sarah aliposikia sauti ya injini, mara
akajipodoa na kutoka nje kwa furaha.
Hata hivyo, hali yake ilizidi kuwa mbaya
alipomwona msichana mdogo begani
mwa Alvin. “Alvin, huyu mtoto...”
"Atalala hapa usiku wa leo," Alvin
alieleza kwa ufupi. "Mwambie Aunty
Zara ampikie chakula kingi zaidi."
“Sawa. ” Damu ya Sarah ilichemka. Hivi
majuzi, Alvin alikuwa vuguvugu kwake,
kwa hivyo alitaka kumfurahisha na
kupata ukaribu naye usiku huo. Hata
hivyo ujio wa Suzie ungeharibu furaha
yake.
Suzie alisema kwa utamu, “Habari,
Aunty. Wewe ni mrembo sana.”
"Asante. Wewe pia ni mzuri sana...”
Sarah alipongeza kwa ukaidi.

Wakati wa chakula cha jioni, simu ya
Alvin iliita. Alimtazama Suzie mwenye
tabia njema na kumwambia Sarah,
“Mwangalie kwa muda.” Kisha,
akachukua simu yake na kuelekea
pembeni ili kuipokea.
“Aunty, unaweza kunisaidia samaki?
Siwezi kuifikia.” Suzie alinyooshea
kidole samaki aliyependezwa naye.
Sarah alimpa kipande kisha
akampuuza. Kwa sababu fulani, kadiri
alivyomtazama mtoto, ndivyo
alivyomchukia zaidi.
Baada ya muda, alisikia sauti ya
msichana akikohoa kwa uchungu. Alvin
ambaye alikuwa amemaliza kuongea na
simu, alirudi na kumuona msichana
huyo akiwa amejikunja usoni
akionekana kuwa na maumivu makali.
Alimtazama samaki kwenye bakuli lake

na mara moja akagundua kuwa alikuwa
amekabwa na mfupa. Kwa hiyo,
alimmiminia glasi ya maji kwa haraka.
Hata hivyo, Suzie alikuwa bado
anaumwa. Kwa bahati nzuri, AuntyZara jikoni alikuwa amechukua hatua haraka
kwa kumletea juisi ya Apple.
“Anko...” Suzie alipopata nafuu,
alimshika Alvin na kuanza kulia.
“Sasa uko sawa.” Alvin akampigapiga
mgongoni. Kwa muda mfupi nyuma,
aliogopa sana hivi kwamba alitokwa na
jasho baridi.
“Nafikiri... hatupaswi kupika samaki
wakati ujao, ” Sarah alisema kwa
wasiwasi. "Ni rahisi kwa watoto
kusongwa na mifupa."
Bila kutarajia, maneno hayo
hayakumpendeza Alvin. "Kula samaki
kunawafanya watoto kuwa smart na

wenye akili. Samaki huyu hana mifupa
mingi, lakini hukuzingatia na ukampa
sehemu yenye mifupa mingi zaidi. Si
nilikuambia umtunze?”
Alimfikiria Lisa ghafla jana yake.
Alikuwa amepika samaki pia, lakini
alichagua mifupa peke yake na
kuichunguza kwa makini kabla ya
kumlisha Suzie.
Zamani, kila mara Alvin alihisi kwamba
Sarah alikuwa mwangalifu. Lakini, sasa
aligundua kuwa ingawa wote hawakuwa
wazazi, Lisa alikuwa mvumilivu zaidi
kwa watoto.
Sarah, ambaye alikuwa ameshtakiwa
ghafla, alipigwa na butwaa. Macho yake
hayakuweza kujizuia kuwa mekundu,
akataka kuongea.
Ilikuwa ni wakati huo ambapo Suzie
alivuta mkono wa Alvin na kusema,

“Usimlaumu Aunty. nilikuwa mzembe.”
Alvin akatikisa kichwa. "Anko
atakuchambulia mifupa."
Chini ya mwanga wa rangi ya manjano,
Sarah aliuma mdomo na hakutaka
chochote zaidi ya kumpiga kofi Suzie.
Baada ya chakula cha jioni, Suzie
alitaka kuoga. Alvin hakuwa na uzoefu
wa kuwaogesha watoto, hivyo aliweza
kumuomba tu Aunty Zara amuogeshe.
Hata hivyo, Suzie akatikisa kichwa.
“Mama alisema siwezi kuruhusu watu
nisiowajua wauangalie mwili wangu.
Aunty Sarah, unaweza kuniogesha?”
Alimtazama Sarah kwa matumaini.
Kichwa cha Sarah kilisisimka. “Mimi...
sijui pia...” 'Mbali na hilo,
hatujafahamiana kihivyo, sawa?'

"Basi sitaoga.” Suzie aliinamisha kichwa
chini. “Anko pia hawezi kuniogesha.
Haifai kwa yeye kunigusa mimi mtoto
wa kike.”
Alvin alicheka na kumgeukia Sarah.
“Muogeshe tu. Hujafikiria kupata mtoto?
Unaweza kupata uzoefu kwanza.”
Sara alikanyaga miguu yake na
kujifanya kama mtoto
anayedeka. “Sitaweza peke yangu
kuwajibika kwa mtoto. Wakati ukifika,
hakika tutaajiri house girl. Kazi kama
kumuogesha mtoto, kumfulia na
kumlisha ni za housegirl bana. Mimi kazi
yangu ni kukufurahisha wewe.”
Suzie aliinamisha kichwa chake kwa
sura ya mshangao. “Lakini wakati wote
nilioogeshwa na Mama, na hata alifua
nguo zangu. Alisema mimi ni mtoto
wake wa thamani zaidi. Ingawa baba
alituwekea watumishi, mama pekee

ndiye aliniogesha hata kama
amechoka.”
Uso wa Sarah ukawa ngumu. Moyoni
alijua kuwa mama Suzie alikuwa ni
mfanyakazi wa baa tu, kwa hivyo ni
lazima awe masikini wa kuajiri
housegirl. Aliposikia maneno ya Suzie,
alisema tu kwa sauti ya upole, "Hiyo ni
tofauti."
"Ni tofauti gani?" Suzie akazidi
kuchanganyikiwa.
Sarah hakujua jinsi ya kumjibu, lakini
alipoona macho ya Alvin yanazidi kuwa
meusi, hatimaye akasema, “Sawa,
nitakuogesha.”
Alitaka tu kumuogesha Suzie haraka
iwezekanavyo na kumaliza kesi.
Kwa hiyo, akaenda kujaza maji kwenye
sinki. Suzie alipoingia ndani, mara
alilalamika maji yalikuwa ya baridi sana,

kisha akalalamika kuwa ni ya baridi
sana. Baada ya kurudi na kurudi, Sarah
alipoteza subira pole pole. Uso wake
mzuri ulionekana kuchukuzwa zaidi na
zaidi.
Aliweza tu kumuonya kwa sauti ya chini,
“Nyamaza. Ukithubutu kufanya fujo
tena, sitamruhusu Anko wako akulete
hapa tena.”
Suzie alimtazama kwa hofu. Sara
alipoona hivyo, alisema, “Afadhali
uniamini. Ninakaribia kuolewa na anko
wako, na tutapata watoto siku zijazo.
Anko wako hatawahi kuwa baba yako.
Haijalishi anakupenda sana, atabaki
kuwa anko tu. Baba yako hana baba
sawa na anko wako pia. Je! unajua
kuwa baba yako na anko wako
wamekuwa na uhusiano mbaya tangu
wakiwa wadogo? Kwa kawaida
hawazungumzi vizuri kamwe.” Sarah
aliongea maneno hayo kama

anayemwambia mtu mzima.
Suzie alitazama chini na kudhihirisha
hali ya woga. Aliacha kuongea yote
mara moja.
Sarah akatabasamu na kushusha sauti
yake tena. “Lakini usijali. Maadamu
wewe ni mtiifu na usimkasirishe anko
wako namimi, sitakuchukia.”
“Asante Aunty. Sitaki kuoga tena.” Suzie
alitoka kwenye maji na kutetemeka. "Ni
baridi sana."
“Vumilia tu...” Sarah alikuwa amemaliza
kusema wakati Suzie alipojitupa
mikononi mwake.
Suzie alikuwa amelowa kabisa, hivyo
nguo za kulalia za hariri za bei ghali za
Sarah pia zililowa maji na mapovu ya
sabuni. Sarah alimsukumia mbali bila
fahamu. Hapo ndipo Suzie alipoanguka

chini na kuanza kulia.
“Suzie, kuna nini?” Alvin alisikia kilio cha
kuhuzunisha cha mtoto pale ndani na
mara akaingia bafuni. Hata hivyo
alichokiona ni Sarah akiwa amekaa
kwenye stuli huku Suzie akiwa amekaa
uchi kwenye sakafu ya baridi huku
akilia.
TUKUTANE KURASA 381-385
ONYO: Ni marufuku kusambaza, kukopi wala kuuza kazi hii kwani endapo kama tutakubaini basi sheria itachukua mkondo
wake (By: Official Dully)
 
Dah hii ni kiboko.Mkuu tupia zaidi ukipata muda.Asante sana@Chubbylady
 
Salute kwako mwandishi na wote mliochangia kuandaa hii simulizi yaani inanifunza baadhi ya vitu kwenye maisha ya kila siku....Tupia zaidi upatapo mda.
 
LISA KITABU CHA NANE (8) SIMULIZI........................LISA KURASA.................381 - 385
PRESENT: SIMULIZI ZA DULLY

Sura ya: 381
Tukio hilo liliifanya damu ya Alvin
kuchemka, na moyo wake ulishindwa
kujizuia kujikunja kwa maumivu. Haraka
akavuta taulo la kuogea na kukimbilia
kuufunga vizuri mwili huo mdogo. Kisha,
akamchukua Suzie mikononi mwake na
kutoka kwa haraka kutoka bafuni.
Suzie akiwa amebebwa hadi chumbani
kitandani alilia sana. “Inauma... ni baridi
sana...” Alvin aliigusa ngozi yake, na
alipoona kuna baridi kali, aliuangalia
mwili wake kuona jeraha kwenye kiwiko
chake.
“Suzie, ni sawa. Anko atakuvisha mara
moja.” Alvin alichukua blanketi na
kumzungushia. Alipogeuka tu,
akagongana na Sarah aliyekuwa akija
na seti ya nguo za watoto.

Sara alionekana kuchanganyikiwa na
huzuni. “Alvin, samahani. Sikujua jinsi
alivyoanguka ghafla...”
“Nilikuambia umuogeshe, lakini ulifanya
hivi? Ulikuwa umeketi tu pale
alipoanguka.” Ilikuwa ni mara ya
kwanza kwa Alvin kushindwa kuzuia
hasira yake dhidi yake.
Wimbi la hasira isiyoelezeka lilimjia
Sarah. “Mimi sikumaanisha kumuacha.
Nilishtuka sana hivi kwamba sikuweza
kujua la kufanya.”
Macho ya Sarah yalimtoka kwa sauti
yake. Aliuma mdomo na kumsogelea
Suzie. "Suzie, Aunty atakuvisha."
“Hapana, sitaki univalishe. ” Suzie
alirudi nyuma kwa woga, macho yake
yakiwa yamejawa na upinzani.
“Ondoka. nitamvalisha.” Alvin
akazichukua zile nguo na kumsaidia

haraka Suzie kuvaa.
Pembeni, Sarah alikunja ngumi kwa
hasira na uso uliopauka. Hakuamini
kuwa Alvin alikuwa akimikasirika mara
kwa mara kwa sababu ya mtoto. Je!
hiyo ilikuwa ni lazima kweli? Suzie hata
hakuwa mtoto wake.
Baada ya kuvaa, Alvin alimbeba Suzie
hadi chumba cha pili.
Alipochukua marashi, Suzie alishtuka
na kujificha upande mmoja huku
machozi yakining'inia kwenye kope
zake. “Sitaki.”
“Tulia, Suzie. Utajisikia ikiwa utapaka
marashi.” Ingawa Alvin alikuwa na
huzuni sana, ilimbidi azungumze kwa
sauti nzito.
“Sitaki. Sitaki kukaa hapa tena.
Namtaka Mama. Namtaka kwenda kwa
Aunty Lisa.” Suzie alizika uso wake

mdogo na kulalamika. Kulikuwa na
kidokezo cha hofu juu ya uso wake.
“Aunty Lisa atakuwa amelala kwa sasa.
Suzie, kuwa msichana mzuri, sawa?"
Alvin alimfariji.
Hata hivyo, Suzie alilia tu. "Simtaki
Aunty Sarah, Nimemkumbuka Aunty
Lisa. Sitaki kuwa hapa tena.”
Alvin alishindwa cha kusema. Muda
wote huo, Suzie alikuwa na tabia nzuri
na muelewa mbele yake. Hata kama
alilia, ni kwa sababu alimkumbuka
mama yake au kwamba Jack alimwacha
peke yake.
Lakini, hiyo ilikuwa mara ya kwanza
kumwona kama hivyo.
“Kwanini hupendi kuwa hapa? Si
ulisema unataka kuja kuishi na Anko?”
Hofu ilitanda usoni mwa Suzie, lakini

aliuma meno na hakusema neno lolote.
“Suzie, unaweza kusema unachotaka
kusema. ” Alvin alikipapasa kichwa
chake taratibu.
Suzie alimtazama kwa muda na ghafla
akajitupa kifuani mwake. “Anko
hatamchukia Suzie?”
"Bila shaka hapana. Suzie, wewe ni
mrembo sana.” Alvin alisikitika aliposikia
sauti ya makini ya mtoto.
“Lakini... Lakini Aunty alisema
hutanipenda.” Suzie alikabwa na
kunong'ona, "Alisema utapata watoto
siku zijazo, na hutampenda Suzie tena."
Uso mzuri wa Alvin ulizama ghafla.
“Unamaanisha Aunty Sarah?”
“Ndiyo.” Bila kujua nini kingine cha
kufanya, Suzie alitikisa kichwa chake
kidogo kwa sauti ya woga. “Alisema

wewe na baba mna baba tofauti, na
wewe humpendi baba, na nyote hamna
uhusiano mzuri. Ikiwa ... nitazuia
uhusiano wako, aunty hatanipenda
tena, lakini ... sikuingilia uhusiano
wako.” Macho yake yalizidi kububujikwa
na machozi tena, akarudia kusema,
“Anko, Suzie hakuingilia uhusiano wako
na Aunty. Hivyo...
kwa hivyo usinichukie, sawa? Nataka
Aunty na wewe muwe wazuri kwangu.
Ninaogopa kwamba Baba hatanitaka
tena, na Anko hatanipenda pia.”
"Hapana, anko anakupenda." Alvin
alisema kwa sauti ya chini, “Suzie, lini
Aunty alikuambia mambo hayo?”
"Nilipokuwa nikioga," Suzie alisema kwa
upole.
Alvin alitetemeka. Ikiwa ni mtu mwingine
angemwambia maneno hayo,
asingeamini. Hata hivyo, Suzie alikuwa

tu mtoto asiye na hatia wa miaka mitatu
au minne. Alikuwa katika umri ambapo
asingeweza kusema uwongo, kwa hivyo
lazima iwe kweli. Hakufikiria kamwe
kwamba Sara angesema jambo kama
hilo pia.
Je, alimlaumu Suzie kwa sababu tu
alimkemea kidogo wakati wa chakula
cha jioni? Hakuwa akifahamu upande
huu wa Sarah. Wakati wote huo, Sara
aliyemjua alikuwa mwanamke mpole,
mwenye kujali, mkarimu, na
mchangamfu.
Alifikiri kwamba wangepata watoto
wakati ujao, kwa hiyo bila shaka Sara
angekuwa mwenye subira sana
kuelekea watoto. Hata hivyo, baada ya
kumpeleka Suzie hapo siku hiyo,
aligundua kwamba Sarah hakuwa na
subira na watoto kabisa.
Hiyo ilikuwa sawa, lakini angewezaje
kusema maneno ya kikatili hivyo kwa

mtoto ambaye alikuwa amefiwa na
mama yake? Je, Sara alibadilika, au
hakuwa akimfahamu kiundani?
“Suzie, mwambie Anko. Umeangukaje
bafuni sasa hivi?" Alvin aliuliza kwa
sauti ya chini.
Suzie aliuma mdomo wake mdogo, na
hofu ikatanda machoni mwake.
“Lazima useme ukweli. Anko anapenda
watoto waaminifu.” Macho ya Alvin
yalikuwa mazito.
“Sawa... Nilikuwa nasikia baridi sana
nilipotoka kwenye sinki, kwa hivyo
nilitaka Aunty anikumbatie. Lakini labda
Shangazi alichukia kwamba
nililowanisha nguo zake, hivyo
akanisukuma hadi sakafuni.” Karibu na
mwisho, machozi ya Suzie yalitiririka
tena usoni mwake. “Anko, naomba
usimlaumu Aunty, atazidi kunichukia.
Mimi... Namkumbuka Aunty Lisa.

Ananipenda sana. Sipendi tena hapa.”
“Sawa, nitakupeleka kwa Aunty Lisa.
Usilie.” Alvin akamnyanyua na kuelekea
nje.
“Suzie bado anaumia? Tumwite
daktari?” Sarah alikuja mara moja
aliposikia harakati. Wasiwasi ulifichwa
kwenye sauti yake.
Alvin akamtazama tena. Alipomuona
usoni, alijiuliza kwa mara ya kwanza.
Je, kweli alikuwa na wasiwasi kuhusu
Suzie? Ikiwa alikuwa, kwanini alisema
maneno hayo ili kumtisha mtoto? Ikiwa
alikuwa, kwanini amsukume mtoto
kwenye sakafu yenye baridi kali kwa
sababu tu aliogopa nguo zake zikilowa?
Alvin ghafla aligundua kuwa hakuweza
kumsoma. Pengine, chini ya safu hiyo
ya ngozi ilificha Sarah Njau wa ajabu
ambaye hakumuelewa.

"Hakuna haja. Nitamrudisha kwa bibi
yake.” Alvin aligeuka na Suzie mikononi
mwake na kuondoka bila kuangalia
nyuma.
Alipoona mwonekano wake wa hasira,
Sarah alikanyaga miguu yake kwa
hasira. Macho ya Alvin yalimfanya
akose raha kidogo.
Je, Suzie alimwambia kitu? Ilikuwa
haiwezekani. Alikuwa bado mtoto
mdogo na alikuwa amefiwa tu na mama
yake. Hiki kilikuwa kipindi ambacho
angejaribu kila awezalo kuwafurahisha
wengine ili apate upendo wao.
Sura ya: 382
Alvin aliendesha gari hadi Karen Estate.
Hata baada ya kugonga mlango kwa
muda mrefu, hakuna aliyejibu. Aliweza
tu kutoa simu yake na kupiga namba ya
Lisa. “Uko wapi?”

Kilichomjibu ni sauti ya sinema ikicheza.
"Uko na nani kwenye sinema?" Sauti ya
Alvin ilisisimka ghafla.
"Erick Malugu." Lisa alisema kwa
unyonge.
Uso mzuri wa Alvin ukiwa
umekunjamana. Alitamani sana
kumkemea, lakini tayari walikuwa
wameachana, hivyo hakuwa na sababu
ya kumshtaki. “Rudi sasa hivi. Suzie
amejeruhiwa. Niko mlangoni kwako.”
"Nini?" Sauti ya Lisa ya woga ilisikika.
“Amejeruhiwa vipi? Jack yuko wapi?"
"Sijui. Jack ni mtu asiyewajibika.
Alimtelekeza kwangu na kwenda
kunywa pombe na marafiki zake. Njoo
haraka. Suzie analia na anasema
anakutaka.” Kwa kweli Alvin hakutarajia
mengi aliposema hivyo. Baada ya yote,
Suzie hakuwa binti wa Lisa.

Kwa mshangao, Lisa alisema, “Sawa,
nitarudi sasa hivi.”
Baada ya kukata simu, Alvin aliinamisha
kichwa chini na kumtazama Suzie
pembeni yake. Hakutarajia kwamba
Lisa angemjali sana Suzie. Ilikuwa ni
kama Suzie alikuwa binti yake.
Upande wa pili, Lisa alikata simu na
mara moja akamwambia Erick Malugu,
“Samahani, kuna kitu kimetokea
nyumbani. Nahitaji kwenda."
“Nitakurudisha." Wote wakainuka.
"Hakuna haja, nitarudi peke yangu."
Lisa aliondoka haraka eneo lile.
Mara baada ya kuingia kwenye gari,
haraka akampigia Jack. “Kwanini Suzie
yuko na Alvin? Unajua kwamba
alameumia? Jack Kimaro, ingawa Suzie
si binti yako, bado ni mwanao.

Unawezaje kutokuwa na wasiwasi zaidi
juu yake?"
“Ameumia? Jack alishtuka. “Subiri, sina
makosa. Alikuwa ni mtoto
wako ambaye alitaka kwenda kwenye
jumba la Alvin. Hata aliniambia nijifanye
kama baba asiyewajibika. Unafikiri ni
rahisi kwangu?"
Lisa alihisi maumivu ya kichwa ghafla.
“Ana mpango wa kufanya nini?”
“Alisema alitaka kukusaidia
kumfundisha yule mama wa kambo
mwovu somo.”
Lisa alisugua alisugua kichwa chake.
“Okey, samahani. Sikujua kuhusu hilo.
Alvin amempeleka Suzie nyumbani
kwangu sasa, kwa hiyo inabidi niwahi
haraka. "
"Inaonekana kama Suzie ana uwezo

mkubwa. Kwa vile alimdanganya Alvin
aje kwako wakati huu wa usiku, nadhani
anataka kukuunganisha na Alvin tena.”
Jack alicheka kwa furaha.
“Hah. Sipendezwi na kipande cha mbwa
sh*t kama Alvin Kimaro."
Baada ya Lisa kukata simu, hakuwa na
wasiwasi tena. Aliamini kwamba jeraha
la Suzie haliwezi kuwa kubwa.
Msichana huyo wa ajabu lazima awe
amefanya makusudi.
Lisa alitoka kwenye lifti na kumwona
Alvin akiwa ameegemea mlango wake
huku Suzie akiwa ameketi mabegani
mwake. Mikono yake yote miwili ilikuwa
kichwani mwake huku akitazama katuni
kwenye simu ya Alvin. Tukio hilo
liliufanya moyo wa Lisa kupata
kigugumizi.
Alipokuwa mjamzito wa mapacha,

alikuwa amejaa matarajio kama hayo.
Alikuwa ameiwazia picha hiyo hapo
awali. Kwa kuwa Alvin alikuwa mrefu
sana, alifikiri binti yao mtarajiwa bila
shaka angeweza kukaa kwenye
mabega yake na kucheza. Sasa ingawa
alikuwa amekata tamaa, tukio hilo
lilitimia.
Hata hivyo, ilikuwa ni kwa muda tu.
Alirudi kwenye fahamu zake na bila
fahamu akawa mkali. "Alvin Kimaro,
umemruhusu vipi mtoto kucheza na
simu yako?"
Suzie alishtuka sana hadi simu
ikadondoka kutoka kichwani kwa Alvin
skrini ikiwa imetazama chini. Korido
lilikuwa kimya sana kwa muda. Alvin
kisha akainama kumshusha Suzie chini
na kuchukua simu. Skrini nzima ilikuwa
imevunjika.
Macho ya Suzie yalimtoka kwa hofu.

“Anko, samahani. Sikumaanisha.”
“Ni sawa, ni simu tu. Nitapata mpya.”
Alvin alimtuliza kwa upole.
Moyo wa Suzie wenye hatia ulitulia
taratibu.
Lisa alishtuka baada ya kuona hivyo.
Katika kumbukumbu yake, Alvin alikuwa
mwenye hasira, mkali, na jeuri.
Hakutarajia kamwe kwamba kungekuwa
na upande wenye joto kwake. Au ni kwa
sababu walikuwa na uhusiano wa
damu? Lakini, alikunja uso haraka tena.
"Malezi yako siyo mazuri."
9
Baada ya kulaumiwa, Alvin alimtazama
kwa kutoridhishwa. "Una ujasiri gani
kusema hivyo? Kama usingemkaripia
ghafla, angeshtuka na kudondosha
simu yangu? Wewe ndiye mwenye
makosa.”
“Alvin Kimaro, huelewi kabisa? Bado ni

mtoto, na simu yako ina mambo mengi,
kwa hivyo anaweza akaona mambo ya
ajabu humo. ” Lisa alimsogelea Suzie
kwa umakini sana. "Mtoto nipo sahihi au
sio sawa?"
Alvin alidhani Suzie ataogopa na
kuanza kulia. Alipotaka kumkaripia Lisa,
Suzie alitii kwa kichwa. "Nilikosea
Aunty. Sitacheza na simu ya wakubwa
tena.”
“Ikiwa unataka kutazama katuni,
unaweza kuwasha TV na kutazama kwa
muda. Lakini huwezi kuzitazama
kwenye simu za watu wazima.” Sauti ya
Lisa ilibadilika na kuwa ya upole tena
sana.
Suzie aliitikia kwa utiifu na hata
kunyoosha mikono yake kwa Lisa kwa
ajili ya kumkumbatia. Lisa
akamnyanyua, na Suzie akauzika uso
wake mara moja mikononi mwa Lisa.

Wale ambao hawakujua wangefikiri
kwamba walikuwa mama na binti. Alvin
alishangaa sana.
Kabla hajatafakari, Lisa aligeuka na
kumwambia, “Usitumie simu yako kama
kitu cha kumbembelezea mtoto tena.
Simu ya mtu mzima ina
mambomengiambayo yanaweza
yakamdhuru maisha yake yote. Kwa
kuwa simu yako ilmepasuka, unapaswa
kuchukua kama somo."
Alvin alikosa la kusema. Sio tu kwamba
alipoteza simu, lakini ilionekana pia
ilistahili kuvunjwa. Alisema kwa
kuudhika, “Kama usingechelewa kurudi,
nisingemruhusu Suzie acheze na simu
kwa sababu niliogopa angechoshwa.
Ulirudi dakika arobaini nzima baada ya
kukupigia simu. Ulisitasita sana
kuachana na Erick Malugu?”
“Ndio. Kwa kweli nilitaka kuondoka na

Erick usiku wa leo. Usingemleta Suzie
hapa ghafla, nisingemuacha arudi peke
yake. ” Lisa akatoa funguo na
kumtazama kwa kuchukia.
“Umemjua Erick kwa muda mfupi tu,
lakini unataka kutoka naye usiku kucha?
Lisa, wewe ni kigeugeu sana.”
Alvin alikereka. Alipopiga akilini mwake
picha ya Erick na Lisa wakiwa kitandani,
alihisi kutamani kuua mtu.
Kwa kuhisi macho yake, Suzie alijikunja
mikononi mwa Lisa kwa woga. "Anko,
unatisha."
Alvin aliganda. Je, alikuwa anatisha
kiasi hicho?
Lisa alifungua mlango huku akisema.
“Wewe ni kichaa. Je, mimi ni kigeugeu
vipi? Tayari tumeachana, kwa hivyo ni
kawaida ikiwa nitawasiliana na

wanaume wengine. Hakuna jambo la
ajabu kwa mimi siku moja moja
kumwagilia roho.”
Uso wa Alvin uliingia giza alipokuwa
akisikiliza maneno hayo, na ngumi
zilijikunja mpaka zikakaribia kupasuka.
Lakini, Lisa alionekana kutogundua.
Alimbeba Suzie hadi kwenye sofa na
kumuuliza kwa upole,
“Umeumia wapi?”
"Kwenye mkono wangu." Suzie aliinua
mkono wake.
Lisa alikunja mkono wa Suzie, na
alipoona kiwiko chake kilikuwa na
michubuko, alikunja uso. “Umeumia
vipi?”
Suzie alinyamaza akimtazama Alvin, na
Alvin akatazama pembeni kwa
mashaka. "Alianguka."

“Ni sawa. Utakuwa sawa baada ya
kupaka mafuta.” Lisa akaitoa viksi na
kumpaka Suzie.
Tangu alipokuwa na watoto, alikuwa na
mazoea ya kuweka mafuta kwa ajili ya
majeraha ya kuanguka nyumbani kwa
sababu ilikuwa kawaida kwa watoto
kujikwaa.
“Anti Lisa, nina njaa,” Suzie alisema
ghafla.
“Hukula chakula cha jioni?” Alvin
alichanganyikiwa. "Hukushiba?"
"Anko, naweza kusema ukweli?" Suzie
alipiga kelele.
"Endelea."
“Chakula cha Aunty Sara si kitamu
kama cha Aunty Lisa,” Suzie alisema na
kushusha kichwa haraka. “ Mpishi wa
nyumbani kwa bibi pia hapiki kama vile

Aunty Lisa. Upikaji wa Aunty Lisa ni wa
ajabu sana.”
Sura ya: 383
Alvin hakujua la kusema.
"Kweli, ni kawaida kwa watoto kupata
njaa wakati huu. nitakufanyia... chips
maya.” Lisa alikipapasa kichwa cha
Suzie na kugeukia jikoni. Suzie
alimfuata mara moja nyuma nyuma
kama paka anayetamani kulishwa.
“Si vizuri kwa mtoto kula chipsi usiku
sana." Alvin alimkosoa huku akikunja
uso. Alikuwa analipisha kwa kumlaumu
kwa kumpa Suzie simu mapema.
Lisa hakumjali na kutoa viazi kadhaa
kutoka kwenye kikapu. Kisha, akaanza
kuvimenya kwa ustadi mkubwa. Viazi
vitano tu vilitoshea sahani ya kumtosha

Suzie. Wakati huo mafuta tayari
yalikuwa yamechemka.
Alipotumbukiza viazi kwenye mafuta
alitoa mayai matatu kwenye friji. Kisha,
alitenganisha maganda na ute wa
ndani.
Viini vya yai nyangavu vilifanya vidole
vyake vionekane vyembamba, na
viganja vyake vilivyo safi na vyeupe
vilimpa Alvin shauku ya kumshika.
Alvin alipoteza mawazo kwa muda hadi
Suzie akamjibu, “Chipsi anayofanya
Aunty Lisa ni tamu sana.”
“Suzie, unaonekana unajua kila kitu. Ni
kana kwamba unamfahamu sana.” Alvin
alikuwa na shaka.
Lisa alijibu bila kuinua kichwa chake, "Ni
kwa sababu Jack mara nyingi humleta
hapa, haswa ... baada ya mama yake
kuondoka."

Hapo ndipo Alvin alipoelewa, lakini
alizidi kuchukizwa.
Aliifanya chipsi kuwa ya haraka sana
kwani ilimaliza kutengenezwa kwa chini
ya dakika kumi.
Alvin aligundua kuwa mayai yake
yalikuwa yamekaangwa pembeni kwa
mafuta ya blue band na kuongezewa
humo vipande vya karoti, hoho na
kitunguu kwa mbali. Alimtengea mtoto
pamoja juisi ya zabibu na tomato sauce ya kutengenezwa nyumbani. Ilionekana
kunoga sana, yenye afya zaidi kuliko
chipsi kutoka huko nje. Ilikuwa nzuri
kwa watoto kula.
Wakati harufu hiyo ilipojaa jikoni, hata
mtu mzima kama yeye alitamani kula.
Suzie aliketi kwenye meza ya kahawa
na akala chipsi yenye harufu nzuri. Kwa
kweli, Alvin alikuwa na wivu kidogo.
Alikuwa na wivu kuwa Suzie ni mtoto.
Alichokifanya ni kusema tu, na Lisa
angemfanyia chochote.

Alipokwenda jikoni tena, ilikuwani kwa
ajili ya kusafisha tu jiko. Mwanga wa
njano ulimwagika juu ya kichwa chake.
Ijapokuwa kwa kawaida alionekana
kama vixen mwenye kupendeza wakati
wa mchana, sasa alionekana kama
mwanamke aliyetoa haiba ya uzazi.
"Inaonekana ... unajua mengi kuhusu
watoto. ” Alvin ghafla akasema, “Kwa
kawaida, wanawake ambao si wazazi
huwa hawana msaada sana linapokuja
suala la watoto, lakini Suzie
anakupenda sana na kukuchukulia
kama mama yake.”
Moyo wa Lisa ulirukaruka. Alvin hakujua
kwamba Suzie hakumchukulia Lisa
kama mama yake, bali Lisa alikuwa
mama yake. Lakini, hakuthubutu
kuweka wazi hilo.
Alijifanya mtulivu huku akipiga mswaki.
“Bila shaka najua mengi. Nimesoma

vitabu vingi sana vya malezi nilipokuwa
mjamzito, lakini kwa bahati mbaya,
sikupewa fursa ya kutumia ujuzi huo.
Labda hutaelewa hisia hiyo.
“Nilipokuwa ng’ambo, nilifikiria watoto
niliowapoteza nilipowaona watoto
wengine, na moyo wangu ulitulia.
Nilifikiria kwamba ikiwa watoto wangu
wangekuwa bado hapa, bila shaka
wangekuwa wazuri kama wao. Kwa
hiyo, baada ya muda, nilianza kupenda
kucheza na watoto na kuwazoea
polepole.
"Hah, sahau. Kuzungumza na wewe ni
kama kutupa lulu mbele ya nguruwe,
lakini nina furaha sana kwamba Suzie
ananipenda. Ni mtoto maskini sana.”
Kulikuwa na maumivu yasiyoelezeka
moyoni mwa Alvin. Asingeelewaje?
Kama yeye, kumuona Suzie mara nyingi
kulimkumbusha kuhusu watoto wake

mwenyewe. Alikasirika, kisha
akabadilisha mada. “Kwa nini umsaidie
Jack kumtunza binti yake? Je! huoni
yeye ni...mtu aliye na maisha machafu
ya kibinafsi?”
"Samahani, sidhani kama yuko." Lisa
alimtazama kwa kuchukia. “Angalau
hakuwa na mchumba aliyemchumbia na
kumuacha na hakumlazimisha mke
wake kutia sahihi hati za talaka kwa ajili
ya mwanamke mwingine. Hata awe
mchafu, uchafu wake haupo wazi, lakini
wewe ni mpuuzi kabisa. ”
Alvin, ambaye alipuuzwa tena,
hakuweza kupata maneno ya kujibu.
Alijihisi mnyonge, mnyonge kweli kweli.
Hata hivyo, Lisa alikuwa tayari
amempuuza. Alipotoka nje, Suzie
alikuwa amemaliza kula na kububujikwa
furaha.
“Ni kitamu. Ninahisi usingizi sasa."

“Wewe nguruwe mdogo. Unatakiwa
kupiga mswaki kwanza." Lisa akatoa
mswaki mpya kabisa wa watoto na
dawa ya meno kwenye begi lake.
Alvin alishtuka. "Kwanini unayo hiyo
kwenye begi lako?"
“Nilinunua pale chini mapema. Kwa
kuwa umechelewa kumleta Suzie,
nilidhani atakulazimika kulala hapa.”
Lisa kisha akamuongoza Suzie mpaka
bafuni.
"Subiri, mswaki wangu uko wapi?" Alvin
aliuliza, “Sijisikii vizuri kumuacha Suzie
hapa peke yake. Mimi pia nalala.”
“Samahani, lakini siruhusu wanaume
kulala nyumbani kwangu, na sitaki
ndugu wa Sarah waharibu nyumba
yangu tena,” Lisa alisema kwa ukali.
“Sarah... hajui kama niko hapa,” Alvin

alisema bila kufafanua. “Nitalala kwenye
chumba cha wageni. Kwa vyovyote vile,
siwezi kumuacha Suzie peke yake.”
“Aunty, mwache tu Anko alale hapa,”
Suzie alimuomba kwa upole. "Nataka
abaki pia."
Lisa alimtazama kwa siri, na Suzie
aliinamisha kichwa chini na kutoa ulimi
nje.
“Sawa. Ikiwa unataka kulala hapa,
unaweza kulala kwenye sofa. Mlango
unaofuata ni chumba cha Pamela.
Amerudi Dar es Salaam, lakini vitu
vyake vyote viko kitandani, kwa hivyo
sidhani kama ni vizuri kulala huko.”
Baada ya hapo, Lisa alimpeleka Suzie
chumbani kwake na kufunga mlango.
Alvin aliusukuma mlango wa chumba
cha pili na kukata tamaa kwa kutazama.
Kulikuwa na vitu vingi vya kike ambavyo

Alvin alihisi kinyaa kuvigusa. Mwishowe,
aliamua kulala kwenye sofa.
Ingawa ilikuwa karibu majira ya joto,
usiku ulikuwa bado baridi. Baada ya
kulala kwa muda, alihisi baridi.
Alichoweza kufanya ni kugonga mlango
wa chumba cha kulala Lisa.
Suzie alifungua mlango na kusugua
macho yake yenye usingizi. “Anko, kuna
nini?”
“Suzie, Aunty Lisa yuko wapi? Je,
unaweza kuniruhusu nichukue
blanketi?” Alvin alichungulia ndani na
hakumuona Lisa, lakini kulikuwa na
sauti ya maji ya bomba bafuni.
“Aunty anaoga. Tuna blanketi moja tu,
lakini nadhani kuna shuka."
"Shuka itafaa." Mara Alvin akaenda
kuchukua shuka. Ikiwa angengoja hadi

Lisa atoke, labda asingempa blanketi.
Akiwa anarudi sebuleni, alitazama
bafuni bila kujijua. Taswira ya Lisa
ilimfanya damuyake kuongeza mbio
kwenye mishipa yake. Hiyo ni kwa
sababu Lisa alikuwa anaoga huku
mlango ukiwa umefungwa nusu tu.
Ubongo wake ulimtoka machoni. Lisa
alipogeuka kutoka kuoga, haraka Alvin
akachukua shuka na kutoka nje. Mlango
ulipofungwa, Lisa alifikiri alikuwa
amesikia harakati kutoka ndani ya bafu.
Mara akatazama nje lakini hakuona mtu
yeyote.
Hata hivyo, kulikuwa na hisia ya aibu
isiyoelezeka ndani ya moyo wake.
Hapo zamani, Lucas alipokuwa na
Suzie, alihisi utulivu na kufunga mlango
wa bafu wakati wa kuoga. Sasa,
kulikuwa na mtu mmoja tu chumbani.
Ingawa Suzie alikuwa amejilaza, kama

mama, bado alikuwa na wasiwasi. Kwa
hivyo, hakufunga mlango.
Hakusahau kuwa kulikuwa na
mwanaume ndani ya nyumba pia.
Ingawa alifunga mlango wa chumba cha
kulala, vipi ikiwa Suzie angeufungua?
Kwa hayo, haraka akavaa nguo zake na
kutoka nje. Suzie alikuwa amelala
kitandani, lakini shuka kwenye kitanda
ilikuwa imetoweka.
Sura ya: 384
"Alvin aliingia sasa hivi?" Lisa alimuuliza
Suzie.
"Ndio, baba mchafu alisema alikuwa
anasikia baridi, kwa hivyo nilifungua
mlango na kumruhusu aingie kuchukua
shuka," Suzie alisema kwa sauti ya
usingizi.

Lisa alitazama kwa mbali kutoka
mlangoni hadi kwenye bafu. Hakika
ilitosha kwa Alvin kuona kilichokuwa
kikitokea bafuni, na mlango ulikuwa
umefungwa nusu wakati akioga. Kwa
kufikiria tukio hilo, mara moja alitaka
kujiua kutokana na aibu na hasira.
Alivuta sikio la Suzie na kulifinya, “Kwa
kuwa unamwita baba yako mchafu,
kwanini unamjali? Kama anasikia baridi,
kwanini usimuache. Kwanini ulimruhusu
aingie? Hukujua nilikuwa naoga?”
“Mama kwani kuna kosa gani?” Suzie
alipepesa macho kwa kuchanganyikiwa.
“Hujui kosa lako?” Lisa alieleza kwa
hasira, “Mama alikufundisha kwamba
huwezi kuruhusu watu usiowajua
wauone mwili wako. Ndiyo sababu
sipendi Alvin anione nikioga.
Unaelewa?"

"Lo, baba mchafu lakini alishawahi
kukuona zamani, si hivyo?” Suzie
alisema, nusu-ukweli. Uso mzima wa
Lisa ukawa mtupu.
"Mama, basi samahani, sitarudia tena,"
Suzie alisema kwa wasiwasi.
"Nyamaza!" Lisa alijikuta ghafla
akishindwa kuongea na bintiye.
"Mama, haujaniambia nini kitatokea
ikiwa baba mbaya atakuona ukioga."
Suzie alikunja uso na kuuliza kwa
udadisi, “Je, alifanya jambo baya? Je,
anapaswa kukamatwa? Je, tunapaswa
kuwaita polisi?”
“Kwa kifupi... Kwa kifupi, si vizuri. Ni
mbaya sana.” Kwa hasira, Lisa
alibadilisha mada akiwa amefadhaka.
“Sawa, umeumiaje leo? Niambie ukweli
haraka.”

“Ni kwa sababu mimi... nilimruhusu yule
mama wa kambo mbaya aniogeshe.
Wakati huo, nilimtesa kwa makusudi, na
akanisukuma chini, "Suzie alisema kwa
furaha. “Mama, hukuona jinsi baba
alivyokuwa na hasira. Uso wa yule
mama wa kambo mwovu ulikuwa
mbaya sana wakati baba mchafu
alipomkaripia...”
Nusu ya kuongea, ghafla Suzie
aligundua uso usiopendeza wa Lisa.
“Mama, kuna nini?”
"Wewe mtoto hivi unafikiria nini?" Lisa
aliinua kichwa chake ghafla na kumpiga
vibao kadhaa. “Nilikuambia nahitaji
unifundishie somo Sarah? Una miaka
mingapi?"
“Mama...” Suzie alilia kwa uchungu.
Lisa alimtazama kwa macho mekundu.
"Susan Jones, wewe ni mtoto mjinga

sana. Unaweza kumfanyia Sarah hivyo
leo kwa sababu yeye bado hujui wewe
ni nani. Shukuru Mungu kwamba
alikusukuma tu leo. Itakuwaje kama
hutamwona mama tena?”
Suzie aliingiwa na hofu. Lisa akamshika
mikononi mwake. “Mama hataki
umlipizie kisasi, sawa? Mama ana
mipango yake mwenyewe. Ninachotaka
ni wewe kukua na afya njema. Usiende
kwenye nyumba ya Alvin tena. Kuanzia
sasa, unapaswa kukaa kwa bibi yako
kwa utii.
Kwa nini usiende chekechea na Lucas?
Hujammiss Lucas?”
"Ndio, nimemkumbuka." Suzie alikabwa
na kusema kwa sauti ya chini, “Pole
mama. Nilikupa wasiwasi.”
“Mama hataki uumie kwa sababu mama
anakupenda sana, kwa hiyo lazima
ujipende pia. Umeelewa? ” Lisa alisema
kwa upole.

“Ndiyo.” Upesi Suzie alilala mikononi
mwa mama yake.
Kwenye sofa sebuleni, akiwa na shuka
tu, Alvin hakuwa na baridi tena. Kwa
kweli, mwili wake ulihisi joto kama
volkano. Alipofumba macho tu, akili
yake ikajawa na picha za Lisa akioga.
Ilikuwa ni hisia ya ajabu lakini
iliyozoeleka.
Zamani, hata Sara angekuwa amevaa
kwa kuvutia kiasi gani, hakuwahi kuhisi
hisia kama hizo mbele yake. Hata hivyo
kumtazama Lisa mara moja tu kulitosha
kuufanya mwili wake kuwaka moto.
Hii haikuwa mara yake ya kwanza
kumuona hivi, lakini haijalishi ilikuwa
kabla au baada ya kuachana, alikuwa
na mvuto mkubwa kwa mwanamke
huyo. Mwishowe, hakuwa na la kufanya
zaidi ya kuoga maji baridi. Baada ya

kuoga maji baridi, alijilaza kwenye sofa
akihisi baridi kuliko hapo awali. Shuka
ilikuwa nyembamba sana hivi kwamba
alilala kwa shida usiku kucha.
Siku iliyofuata, Alvin, ambaye mara
chache aliugua, aliamka na mafua na
homa kali. Suzie bado alikuwa amelala
fofofo. Hata hivyo, Lisa alikuwa na
mazoea ya kuamka mapema na
kuandaa kifungua kinywa.
Kwa kuwa mtoto huyo alilala hapa usiku
kucha, ilimbidi aandae chakula kizuri.
Wakati akipita sebuleni, alijitahidi
kutoitazama sura iliyolala kwenye sofa.
“Ahem.” Kikohozi cha Alvin kilisikika.
Alijifanya hasikii na akatoa pakiti ya
tambi kwenye jokofu.
"Nina mafua." Sauti ya mzuka ya Alvin
ilisikika mlangoni.
Alimpuuza. Aliogopa kwamba ikiwa

angegeuka, angeweza kukumbushwa
tukio la aibu jana na asingeweza
kujizuia kumpiga teke.
"Nimesema nina mafua," Alvin alisema
tena kwa upole huku akimsogelea.
"Sijali kama una mafua." Lisa aligeuka
na kumtazama kwa macho yake meusi
na matupu.
Macho makali ya Alvin yalimtazama kwa
haya usoni mwake. Kisha, akatazama
juu na kusema bila kupenda, “Yote ni
kwa sababu nilikuona jana unaoga.
Mwishowe, sikuweza kujizuia kuoga
maji baridi, kisha nikashikwa na homa.”
Wote walikuwa watu wazima, hivyo Lisa
alijua vizuri kwa nini alienda kuoga maji
baridi. Hata hivyo, ilimfanya aaibishwe
na kukasirika zaidi. “Vipi bado una
ujasiri wa kusema hivyo? Ni nani
aliyekuruhusu kuingia chumbani

kwangu jana?"
"Nilikuwa najisikia baridi, na hukunipa
shuka. Ni kosa lako kutofunga mlango.”
"Ninawezaje kuwa na uhakika na
kufunga mlango wakati mtoto yuko peke
yake chumbani?"
Alvin aliacha kuongea na kumtazama
kwa umakini. Kadiri alivyokuwa akimjali
Suzie, ndivyo alivyozidi kuuona utu
wake. Alikuwa makini kwa Suzie bila
kujali ni mtoto wa nani, tofauti na Sarah,
ambaye alikuwa mzembe kiasi cha
kumfanya Suzie asongwe na mfupa wa
samaki. Ikiwa Lisa angekuwa mama,
bila shaka angekuwa mama mzuri.
“Mbona unanitazama?” Lisa alijisikia
vibaya kutokana na kumtazama.
Midomo yake ikaachana kidogo, na
alikuwa anakaribia kuongea wakati

alihisi kooni kuna mwasho. Akatazama
pembeni na kukohoa kwa nguvu.
Mkono wa Lisa uligusa paji la uso wake
ghafla, na Lisa akashusha macho yake.
"Una homa kidogo."
“Mm. ” Akamtazama kwa shauku.
Wakati huo, alionekana kama mtoto
dhaifu. Alifanana kidogo na Suzie
alipokuwa mgonjwa.
Lisa akasema, “Nenda hospitali.
Usimwambukize Suzie.”
“Huh?” Uso mzima wa Alvin ukawa
mweupe kwa hasira. Alifikiri kwamba,
angalau, angejali kuhusu homa yake, na
amwandalie kifungua kinywa kitamu,
lakini kumbe alikuwa na wasiwasi kwamba angemwambukiza Suzie
badala yake.
"Lisa Jones." Akauma mdomo. Hisia

zilizochanganyika za mfadhaiko,
kuudhika, na manung’uniko zilimjaa, na
mwili wake ukayumba bila raha.
Lisa bila fahamu alinyoosha mkono
kumshika mkono wake na kukuta
mikono yake pia inawaka moto.
Alipumua kwa upole. Hakukuwa na
namna zaidi ya kumsaidia. "Kwanini
usilale kwanza kitucha moto?
Unapaswa kula kitu cha moto kabla ya
kuchukua dawa. Kunywa dawa kwenye
tumbo tupu kutaumiza tumbo lako."
Uso wa Alvin uligeuka juu chini huku
uso wake ukiwa umewaka kwa furaha.
“Una wasiwasi na mimi?” Alifurahi
kuona alikuwa na wasiwasi kuhusu yeye
kuumiza tumbo lake.
“Jamani, huo ni ushauri wa kawaida tu,
sawa? Kama hujali kuumiza tumbo lako,
nitakupa dawa sasa hivi.” Lisa alikosa la
kusema kwa kuhisi aibu.

“Je, ni vigumu kukubali kwamba
unanijali?" Alvin alijiamini kabisa.
"Kwa hivyo ikiwa nitakubali? Jamani,
dunia nzima imeshajua kuwa unaoa.
Utamwacha mchumba wako wa utotoni
kwa msichana mbaya kama mimi?” Lisa
alimdhihaki kabla hajaingia jikoni kupika
tambi.
Sura ya: 385
Alvin alitazama kivuli chake kimyakimya
kikitoweka. Ijapokuwa alijua kwa muda
mrefu kwamba alikuwa na mawazo
fulani juu yake, alijipa moyo kwamba
mawazo hayo hayakutosha kuathiri
hisia zake kwa Sarah. Lakini, kile kitu
kilichotokea usiku wa jana kilikuwa
kimebadilisha mtazamo wake juu ya
Sarah.

Labda Sarah hakuwa mwema kama
alivyowazia, na Lisa hakuwa mbaya
kama alivyofikiri. Lakini bado
alijiaminisha kuwa hisia zake kwa Lisa
haziwezi kumpindua Saraha moyoni
mwake.
Tambi ilikuwa rahisi sana kuandaa.
Ndani ya dakika kumi, ilikuwa tayari
kuliwa. Alvin aliifuta sahani ya tambi
ndani ya dakika chache. Ilikuwa tu ni
tambi ya kawaida, lakini Lisa alikuwa
ameiroga na kuwa ya tamu sana.
Ilionekana kana kwamba anapoona
chakula cha Lisa, anakuwa na hamu
nzuri kila wakati.
Baada ya kula tambi, kikombe cha maji
ya moto na vipande vya tangawizi
viliwekwa mbele yake pamoja na
kkwangulio.
"Hutanisaidia kukwangua tangawizi na
kuchanganya?" Alvin aliinua nyuso

zake. Alionekana kama mtoto ambaye
hakutaka kugusa chochote kwa sababu
alikuwa hajisikii vizuri.
“Namba ya Sarah nipatie. Nitampigia
simu na kumwambia aje akusaidie
badala yake.” Lisa akatoa simu yake.
Hakuwahi kukutana na mwanamume
asiye na shukrani kama Alvin. “Kwa
mtindo huu hata kama ungesema
nikuelekeze chooni, ungeniita
nikutawaze baada ya kumaliza.”
Alvin alinyanyuka kimya kimya na
kukwangua tangawizi peke yake. Uso
wake dhaifu na wa kupendeza
ulimfanya aonekane mwenye huzuni.
Dakika ishirini baadaye, sauti ya kilio
ilisikika chumbani. Lisa alikimbia mara
moja. Muda si muda, Suzie aliacha
kulia, na sauti ya vicheko ikasikika. Alvin
alienda mlangoni na kumuona Lisa
akisuka nywele za Suzie pale kitandani.
Punde, Suzie alivalia kama binti wa

kifalme, mzuri na mrembo.
Joto likajaa ghafla moyoni mwake.
Asubuhi hii mapema ilimfanya ahisi
kama walikuwa familia ya watu watatu.
Hata hivyo, katika muda mfupi tu,
kengele ya mlango ililia. Hans
alisimama mlangoni kwa heshima.
“Bwana Mkubwa, Bi Jones kanipigia
akisema kwamba hujisikii vizuri.
Nitakupeleka hospitali sasa hivi.”
Uso wa Alvin ukazama. Alimtazama
tena Lisa, ambaye alikuwa akitoka na
Suzie. “Ulimpigia simu Hans?”
“Duh? Nina shughuli nyingi. Sina muda
wa kukutunza. Isitoshe, hatuna
uhusiano wowote mimi na wewe. Siwezi
kukaa na mume wa mtu nyumbani
kwangu, nitashikwa ugoni. Hans,
mpeleke.” Lisa aliongea huku
akimtengea Suzie kifungua kinywa.

Suzie alikuwa na pancakes, mayai ya
kuchemsha, na juisi. Alikumbuka bakuli
la tambi alilokuwa nalo. Kwa mara
nyingine tena, Alvin alihisi kama
hakutendewa haki kwa kupewa sahani
ya tambi peke yake.
“Anko nimesikia una mafua. Unapaswa
kwenda hospitali haraka." Suzie
alimtazama kwa huruma. "Baba atakuja
kunichukua na kunipeleka shule ya
chekechea baadaye."
“Shule ya chekechea?” Alvin aliganda.
“Ndio, Aunty Lisa aliniambia jana usiku
kwamba niende shule ya awali.
Nitakuwa na marafiki wengi huko ili
nisijisikie mpweke tena. Na sitalazimika
kukunisumbua kazini wakati wa
kupumzika tena.”
Suzie alikuwa na sura ya kujali. Hata

hivyo, Alvin alihisi huzuni Hakuwa na
wasiwasi hata kidogo na alipenda sana
usumbufu wa Suzie. Ikiwa angeenda
shule ya chekechea, bila shaka
asingemwona kwa muda mrefu. “Suzie,
hunisumbui,” Alvin alisema kwa bidii.
“Najua, lakini Anko anakaribia kuoa.
Aunty Lisa alisema kuwa Aunty Sarah
hatakuwa na furaha ikiwa utanisindikiza
kila siku. Sitaki anichukie,” Suzie
alisema bila hatia.
Alvin alimtazama Lisa kwa hasira.
“Nimesema sangapi maneno hayo?”
Macho mazuri ya Lisa yalimpa
changamoto. “Au unafikiri Sarah hawezi
kulea mtoto?”
Ikiwa ingekuwa zamani, Alvin angeweka
dau kwamba Sarah hakuwa mtu wa
aina hiyo, lakini sasa, hakuwa na
uhakika. Alikenua meno yake kwa Lisa.

“Fanya haraka uondoke, usije
ukamwambukiza Suzie mafua.” Lisa
alimfukuza tena.
Alvin aliamua kujiuzulu tu kuondoka.
Mara moja akiwa ndani ya gari, alitoa
amri. "Nipeleke ofisini. Tayari
nimekunywa tangawizi najisikia vizuri.
Sihitaji kwenda hospitali.”
Hans alimtazama na hakusema kitu
kingine chochote. Baada ya yote,
ukiweka kando ugonjwa fulani wa akili,
Bwana wake alikuwa na afya kabisa.
Hakuwahi kupata homa mwaka mzima,
siku hiyo ilikuwa ya kwanza.
“Oh sawa. Piga simu na mwambie Jack
aje kwa kampuni mara moja. Kisha,
upange jambo la dharura asipate nafasi
ya kuondoka ofisini.,” Alvin alisema
tena. Hakutaka kuiona sura ya upendo
ya Jack, Lisa, na Suzie wakiwa pamoja.

Hans alikosa la kusema. Aliweza mara
moja kukisia nia ya Bwana Mkubwa
wake.
“Pia...” Alvin akaongeza tena, “Nenda
ukamchunguze Erick Malugu.”
Hans hakuweza kujizuia kusema,
“Bwana Mkubwa, nijuavyo mimi, familia
ya Malugu ni familia ya kuheshimika
sana. Erick Malugu ni mstaarabu,
mwenye kipaji, mwenye tabia njema...”
“Inatosha.” Hans alikatishwa na uso
mkali. “Nataka mapungufu yake. Kila
mtu ana udhaifu wake, kama vile
kutokuwa mwaminifu, kashfa, au kuwa
na mazoea mabaya.”
Hans alikasirika. “Nilisikia hana kashfa
yoyote. Erick ni mtu mungwana na
mpole, huwezi kumkuta maeneo
mabaya...”
“Sitaki ulichosikia. Ulichosikia kinaweza

kuwa si kweli.” Alvin alimkumbusha.
“Kuna vitu vingine vinavyoweza
kumfanya aonekane hafai. Kwa mfano,
miguu yake inanuka? Au mdomo wake
unanuka? Labda hana nguvu za kiume,
au ana sifa za kishoga. Yoyote kati ya
hayo yatafaa.”
“... Vizuri sana.” Hans alishtuka kwa
aibu. Alielewa kuwa Alvin alikuwa
akijaribu tu kuweka kabari kati ya Erick
na Lisa. Hans hakujua ni nini Alvin
anataka. Alikuwa karibu kuoa hivi
karibuni, lakini bado alikuwa akimdhibiti
mke wake wa zamani.
Wakati Alvin anaingia ofisini, Sarah
alikuwa amekaa kwenye sofa kwa muda
mrefu. Alipomwona, mara moja aliuliza
kwa wasiwasi, “Suzie yuko wapi? Yuko
sawa?”
Alvin aliinua macho yake kumtazama.
Sasa kwa vile alikuwa hajisikii vizuri,

alichokuwa akitaka ni amani na utulivu.
Hata hivyo, sura ya Sara ilikuwa
imevuruga tena akili yake.
“Sarah, niambie. Suzie alianguka vipi
jana usiku?” Alvin aliuliza ghafla.
Moyo wa Sarah ulitetemeka, akakosa
raha baada ya kuona uso wa Alvin
ukiwa umekufa. Hakujua kama Suzie
alikuwa amemweleza juu ya kile
kilichotokea jana yake usiku.
Alipomuona akiwa kimya, uso mzuri wa
Alvin ulizidi kuwa mweusi zaidi. "Je! ni
ngumu kujibu swali langu?"
“Ulielewa vibaya. Nilihisi tu kwamba
ninawajibika kujua hali yake kwa kuwa
alianguka nikiwa naye.” Sarah aliuma
midomo yake na kusema bila kufafanua,
“Ni kosa langu. Ikiwa ningekuwa
mwangalifu na mvumilivu zaidi, labda
asingeanguka. Samahani."
Alvin alimkazia macho. Ikiwa ingekuwa

zamani, angeweza kuchagua kumfariji
bila masharti. Hata hivyo, kilio cha Suzie
usiku wa kuamkia jana kilimfanya awe
na akili timamu na kutambua kwamba
ingawa Sarah alijilaumu, lakini sababu
zilizomfanya Suzie aanguke hazikuwa
wazi.
Ilikuwa ni kama... Suzie hakuanguka
kwa sababu Sarah alikuwa mzembe.
Ilikuwa ni kwa sababu Sarah alikuwa na
wasiwasi kuhusu kulowanisha na
kuchafua nguo zake, hivyo
akamsukuma Suzie chini.
"Sarah, hupendi watoto?" Aliuliza
ghafla.
Sarah alishtuka, lakini alijaribu
kudumisha tabasamu usoni mwake.
“Bila shaka nawapenda. Watoto hawana
hatia na wanapendeza, kama malaika
wadogo. Nawapenda sana.”
TUKUTANE KURASA 386-390

ONYO: Ni marufuku kusambaza, kukopi wala kuuza kazi hii kwani endapo kama tutakubaini basi sheria itachukua mkondo wake (By: Official Dully)
 
LISA KITABU CHA NANE (8) SIMULIZI........................LISA KURASA.................386 - 390 PRESENT: SIMULIZI ZA DULLY

Sura ya: 386
Alvin akainua midomo yake. Sarah
alimshika mkono na kushusha macho
yake. “Alvin, najua kosa langu la jana
usiku lilikukera sana, lakini ilikuwa ni
mara yangu ya kwanza kumshika mtoto,
kwa hiyo nilishindwa. Ninaahidi
sitafanya tena katika siku zijazo.
Unaweza kumletea Suzie mara nyingi
zaidi kucheza wakati ujao, na ninaweza
kufanya mazoezi zaidi kuhusu jinsi ya
kutunza watoto.”
“Mazoezi? Unataka ufanye mazoezi
kwa Suzie” Alvin alikunja uso. “Yeye ni
mtoto mdogo tu. Ulifanya uzembe
kidogo tu ukamjeruhi. Hata mfupa wa
samaki tu ulishindwa kutoa ukampalia.
Unataka umfanyie mazoezi ili umuue
kabisa?”
Akiwa na uso uliopauka, Sarah alieleza

upesi, “Hilo silo nililomaanisha.
Nitakuwa makini sana. Sitaruhusu
jambo kama hilo litokee...”
“Sarah, sidhani kama unafaa kuwa na
mtoto kwa sasa.” Alvin akamkatisha
ghafla.
“Kwanini? Kwa sababu tu sikumtunza
Suzie vizuri jana?” Sarah alikuwa na
wasiwasi sana hivi kwamba alikaribia
kulia. “Alvin, huoni kuwa hivi karibuni
umekuwa na upendeleo? Yeye ni mtoto
wa Jack, sio wako. Ndiyo, nakiri
kwamba sikufanya kazi nzuri, lakini
huwezi kuninyang’anya haki yangu ya
kuwa mama. Nina hakika nitakuwa
makini sana na mtoto wangu
mwenyewe.”
"Sarah, kwanini ulimtishia mtoto kuhusu
kuharibu uhusiano wangu na wewe?"
Alvin alikuwa tayari hajisikii vizuri, hivyo
Sarah alipoanza kulia, alipasuka kwa

hasira moja kwa moja. “Kwa sababu
yeye si mtoto wangu, ulimwambia kuwa
mimi na baba yake hatuelewani na
kwamba yeye ni mimi nitabaki kuwa
Anko wake tu. Ulisema kwamba
akiharibu uhusiano wetu, utanifanya
nisimpende nikiwa na mtoto siku za
usoni.”
Sarah alipigwa na butwaa. Alifikiri
kwamba ukimya wa hofu wa Suzie jana
yake baada ya kumtishia ulimaanisha
kwamba tishio lake lilifanikiwa. Baada
ya yote, Suzie alikuwa bado mdogo
sana. Ustadi wa kuzungumza wa watoto
wengi katika umri huo usingekuwa
mkubwa kiasi hicho, Suzie alikuwa na
ubongo gani? Hata hivyo, yule mtoto
mnyonge aligeuka na kumwambia Alvin.
Alvin alimshutumu, “Ulimsukuma chini
kwa sababu tu amelowanisha nguo
zako. Muda wote, alikuwa anaoga peke
yake huku wewe ukicheza na simu

yako. Sarah, huna huruma. Hupendi
watoto hata kidogo. Huna upendo."
Tofauti na Lisa, ambaye angepika
kifungua kinywa chenye lishe na
vitafunwa kwa mtoto, na pia kuchana
nywele zake na kumpigisha mswaki, na
hakuthubutu hata kufunga mlango wa
bafu alipokuwa anaoga kwa sababu
alikuwa na wasiwasi na mtoto, Sarah
alikuwa hafai kuwa mama. Kadiri
alivyokuwa akiwalinganisha ndivyo
alivyohisi Lisa alikuwa bora zaidi.
Wakati fulani, alitaka hata kumuacha
Sarah awatunze mapacha wa Lisa,
akifikiri Sarah angewatunza vizuri.
Lakini, ukweli ni kwamba alimtishia
mtoto ambaye alikuwa na umri wa
miaka mitatu tu. Vipi kuhusu watoto
wadogo basi? Hakuthubutu kufikiria juu
yake.
Midomo ya Sarah ilitetemeka. Kwa

muda wa miaka mitatu kuelekea minne
aliyokaa naye, ndiyo kwanza Alvin
alimtazama kwa kukata tamaa na hasira
machoni mwake.
Wimbi la wasiwasi likatawala juu yake.
Sarah alibubujikwa na machozi ya hatia.
" Samahani. Sikuweza kujizuia, na
sikumaanisha. Jana, wakati
nikimuogesha Suzie, wakati mmoja
alisema maji ya baridi, na nilipoongeza
joto akasema ya moto sana. Nilihisi
ananifanyia usumbufu wa
makusudi,kwa hivyo nikakosa subira
kwake.
“Ndio maana nilisema maneno yale
kumtishia. Lakini hiyo ni kwa sababu
niliona kwamba baadhi ya kina mama
huwatia adabu watoto wao namna hiyo.
Sikumaanisha ubaya wowote. Nilihisi tu
kama Suzie hanipendi.”
"Lakini unapaswa kukumbuka kuwa

Suzie amempoteza mama yake."
Alvin hakuweza kuwa na wasiwasi wa
kubishana naye tena. “Kwa vyovyote
vile, watoto si mbwa au paka. Ikiwa
unaamua kuwazaa, unapaswa
kuwatunza vizuri. Mambo mengi lazima
yafanywe na wewe mwenyewe. Huwezi
kutegemea yaya kwa kila kitu. Baada ya
yote, yaya hakumzaa mtoto. Utajuaje
kama yaya atakuwa mwema kwake?"
Kama yeye tu. Alikuwa akinyanyaswa
na yaya wake. Kwa hiyo, Alvin alitaka
kuhakikisha kwamba watoto wake
wanakua wakizungukwa na upendo wa
wazazi.
“Nitafanya. Nitawatunza watoto wetu
vizuri,” Sarah alisema huku machozi
yakimtoka.
“Sarah, siwezi kukuamini. Nadhani sisi
bado ni vijana. Hebu tusahau kwanza
kuhusu kupata watoto sasa hivi.

Tutapanga tena kuhusu hilo wakati
fulani baadaye. ” Alvin kisha akatazama
pembeni. “Unaweza kuondoka sasa.
Bado nina mambo mengi ya
kushughulikia. Vilevile, huna haja ya
kuandaa chakula changu cha mchana
na kuleta tena. Nataka uwe na kazi ya
kufanya badala ya kutumia maisha yako
kunizingatia mimi tu.” Alipomaliza
kuongea, alikaa kwenye kiti cha ofisi na
kuanza kufanya kazi.
Sarah alikasirika sana hivi kwamba
alikaribia kupatwa na wazimu.
Hata hivyo, alichoweza kufanya ni
kuigiza sura ya uchungu wakati akitoka
nje ya ofisi ya Alvin. Hakuwahi kutarajia
kuwa ndoa yake aliyoifanyia kazi kwa
bidii sana ingeishia kuchafuliwa na
mtoto badala ya Lisa.
Alipofika tu kwenye maegesho ya
magari, Hisan Gadaffi alimpigia
Sara."Nihamishie shilingi milioni 100

sasa hivi. Nina ukata wa pesa taslimu.”
Sarah akaruka kwa hasira. “Nimekupa
pesa nyingi sana muda si mrefu uliopita.
Unanichukulia kama mashine ya
kuchapisha pesa? Unajua jinsi ilivyo
ngumu kupata shilingi milioni 100?"
"Ni vigumu kupata kiasi hicho, lakini si
kazi kwa Alvin." Hisan alisema bila
kujali, “utaolewa na mwanamume tajiri
zaidi nchini Kenya hivi karibuni. Nusu ya
mali yake itakuwa yako.”
Maneno yake yaliifanya damu ya Sarah
kuchemka. "Hiyo ni sawa. Lakini
atashtuka ikiwa nitaendelea kutumia
mamia ya mamilioni ya shilingi kwenye
kadi yake.”
"Sema tu kwamba unanunua vitu,"
Hisan Gadaffi alijibu kwa kukosa subira.
"Harakisha! Kwa kweli nimekaribia
kukata tamaa.”

“Tafadhali, Hisan. Huwezi kutumia pesa
vizuri? Usifikiri kuwa sijui unaitumia kwa
kucheza kamari, kunywa pombe na
kuwagonga wanawake. Niligundua
kuwa umeleta wanawake kwenye
ghorofa langu mara kadhaa. Bora
usiambukizwe.”
“Nyamaza na uchunge mdomo wako.
Ninaweza kukutegemea wewe
kunitimizia mahitaji yangu ikiwa sitaleta
wanawake ndani? Unafurahia maisha
yako na Alvin, mimi je, huh?
Ukinivuruga nitaliamsha dude,mapema
au baadaye!”
Sarah alihisi kana kwamba anapigwa
kofi usoni. Muda mfupi baadaye,
alishusha macho yake. "Sawa, nitakupa
pesa."
Baada ya kukata simu, macho yake
yalimtoka kwa hasira na kuapa kumuua.

Ilimbidi ajiondoe kwa Hisan. Baada ya
hayo, taratibu akatoa simu yake na
kupiga namba fulani...
•••
Muda mfupi baada ya Suzie kumaliza
kifungua kinywa chake, Lisa alipokea
simu kutoka kwa Jack. “Lisa, siwezi
kufika. Nilikuwa nimekaribia kufika
kwako Alvin akaniambia nirudi ofisini
maana kuna kitu cha dharura
kimetokea. Nilifanya haraka kurudi,
nikakabidhiwa rundo la nyaraka za
kufanyia kazi. Ishu ni kwamba
hataniruhusu nitoke hadi nilimalize
kuhakiki nyaraka zote. Ni wazi alikuwa
anajaribu kunizuia nisikuone. Ni mtu wa
vitimbi sana."
Lisa alishikwa na neno ghafla. “Ni sawa.
Nitampeleka Suzie mwenyewe shule ya
chekechea.”
"Endelea. Nimezungumza na mkuu wa
shule mapema,” Jack alisema kwa

hasira. “Nitamchukua Suzie jioni.” “Sawa.”
Lisa basi alimpeleka Suzie kwenye
shule ya mapema. Suzie alikuwa katika
darasa moja na Lucas. Hata mwalimu
wa shule ya awali alikuwa hajui kuwa
Suzie na Lucas ni mapacha, kwani Lisa
alitaja tu kuwa walikuwa marafiki
wakubwa.
Sura ya: 387
Muda mfupi baada ya Lisa kuondoka,
Suzie alijaza kadi mkononi mwa Lucas.
"Hii ni kutoka kwa baba yetu mchafu.
Ichukue na uitumie wakati wowote
unapotaka. Mimi pia ninayo. Babu wa
baba alinipa."
“Sitaki.” Lucas alimrudishia Suzie na

kumkumbusha, "Susan Jones, unatumai
kuwa baba yetu fisadi atarudiana na
Mama?"
Suzie aliona hatia. "Kwa kweli ... Baba
yetu mchafu anavutia zaidi katika
maisha halisi kuliko kwenye picha.
Tutakuwa na heshima ikiwa tutatungana
naye ... "
Lucas alishindwa cha kusema. Alijua
kuwa dada yake si mtu wa
kutegemewa, ukizingatia kuwa alivutiwa
na watu wenye sura nzuri.
“Usisahau kuwa ataoa mwanamke
mwingine. Yeye ni mpuuzi. Kama si
Mama, ambaye alitulinda wakati huo,
tusingeokoka.” Suzie alinyamaza papo
hapo. “Pia, usisahau jinsi Anko Kelvin
anavyotutendea vizuri," Lucas
alimkumbusha bila kuficha. "Wakati
wote huu,
Anko Kelvin amekuwa akimsubiri
Mama.”

“Sawa. Sitawaunganisha.” Suzie
aliinamisha kichwa.
Siku hiyo, mwalimu wa darasa lao
alizungumza juu ya mada muhimu
inayoitwa "Huwezi Kunigusa", ili
kuwatahadharisha watoto dhidi ya
unyanyasaji.
Mwalimu alisema kwa dhati, “Watoto,
ikiwa mgeni anataka kukugusa uso,
mgongo, au kifua, lazima usimruhusu,
sawa? Pia, usivue suruali au shati yako
mbele ya mgeni. Mwili wetu ni wa
faragha na haupaswi kuonyeshwa kwa
wengine.”
Aliposikia hivyo, Suzie alitumbua macho
yake kama panzi. Mwishowe, aliinua
mkono wake na kuuliza, "Mwalimu,
itakuwaje ikiwa mtu ataona mwili wangu
uchi?"
“Ikiwa anakuchungulia makusudi,

unaweza kumsemea kwa mkubwa aliye
karibu." mwalimu alijibu kwa umakini.
"Suzie alitafakari kwa huzuni. “Anko
aliuona mwili wa Aunty, alimchungulia
makusudi, je, Aunty angemsemea kwa
nani?” Mwalimu alikosa la kusema.
“Ahem. Ahem.” Ilimchukua mwalimu
muda kabla ya kupata fahamu zake na
akajibu kwa kusitasita, “ kwa hali hiyo,
kama ni watu wazima, mwanamume
anapaswa kubeba jukumu. Mwanaume
akiuona mwili wa Mwanamke ni lazima
awajibike kwa mwanamke kwa kumuoa.
Vinginevyo, anachukuliwa kuwa mhuni.”
Suzie hakuonekana kuufahamu ujumbe
wa mwalimu. Si ajabu Mama yake
alikasirika jana usiku. Aligundua
kuwa Alvin alikuwa mhuni.
Baada ya mapumziko, Suzie aliazima
simu ya mwalimu ili ampigie Alvin.

"Anko Alvin, niko shuleni."
“Mm. Umetulia?” Alvin aliuliza kwa
upole.
"Ndio, nimetulia. Anko Alvin, mwalimu
wangu alinifundisha kitu leo. Anasema
mwanaume akiuona mwili wa
mwanamke, lazima awajibike kwa
mwanamke kwa kumuoa,” Suzie
alisema kwa upole. “Uliuona mwili wa
Aunty Lisa jana usiku.”
Alvin hakuweza kupata maneno ya
kumjibu.
“Usifikiri sijui kilichotokea. Aunty Lisa
aliniambia jana usiku. Mwalimu wangu
alisema lazima uwajibike kwa kumuoa.
La sivyo, wewe ni mhuni.”
Baada ya hapo, Suzie alikata simu.
Alvin aliposikia maneno hayo akiwa
ofisini, uso wake mzuri ulibadilika na

kuwa mbaya. Hakuweza kuamini
kwamba mtoto mdogo kama Suzie
alikuwa akimfundisha somo.
Akiwa anaishangaa simu yake, tukio la
jana yake usiku lilimjia kichwani. Ghafla,
moyo wake ulishtuka, na alitaka kusikia
sauti ya mwanamke huyo. Baada ya
kusita kwa muda, Alvin akaitafuta
namba ya Lisa na kuipiga.
"Ndiyo, Bwana Kimaro?" Sauti nzito ya
mwanamke ilisikika.
Kwa namna fulani, alikasirika. “Ulinipa
dawa gani asubuhi hii? Najisikia vizuri
zaidi. ”
"Keflex."
“Oh.”
“Nakata simu sasa hivi.”
"Subiri." Mara Alvin akamsimamisha
Lisa. "Ni brand gani?"

“Sikumbuki. Hata hivyo, inapatikana
kwenye duka la dawa.” Lisa akakata
simu mara moja.
Alvin alikunja uso na kumpigia tena.
Alikuwa akizidi kupandwa na jazba.
Alichotaka ni kusikia sauti yake tu.
"Unataka nini, Alvin?" Sauti ya Lisa
ilijawa na papara, lakini Alvin hakuhisi.
Tayari alikuwa mgonjwa, lakini wakati
huo, alihisi homa kidogo tena.
“Nataka nikukumbushe tu kutokana na
wema wa moyo wangu kuwa Erick si
mtu mzuri. Ananuka miguu, na zaidi ya
hayo, anavutiwa na mashoga.
Anajiweka karibu nawe kwa sababu
wewe ni mrithi wa Ngosha Corporation.
Usifikiri kwamba anakupenda.”
“Sio kazi yako.”

Jibu la Lisa lilimfanya ashikwe na
hasira. “Nimekukumbusha tu kwa
sababu wewe ni mke wangu wa zamani.
Sitaki kukuona ukidanganywa na
kuaibishwa.”
“Asante, lakini sidhani kama Erick ana
miguu inayonuka. Nitamleta nyumbani
usiku wa leo ili kujua kama anavutiwa
na mashoga.” Lisa alipomaliza kuongea,
akakata tena simu.
Alvin alikasirika sana hadi akaivunja ile
simu ya mezani mara moja.
Hans, ambaye alikuwa amesimama
mlangoni na kukaribia kuingia
chumbani, aliona aibu. Kwa kweli, Erick
hakuwa na miguu yenye harufu mbaya
wala hakupendezwa na mashoga.
Bwana Kimaro ameweza kufikia hatua
ya kumrushia matope mpinzani wake
wa mapenzi kwa ajili ya kuchafua jina?
Baada ya hasira za Alvin kupungua,

alianza kukohoa kwa nguvu.
“Bwana Mkubwa, nadhani unapaswa
kushauriana na daktari wa kitaalamu
kwa maagizo. Bi Jones si daktari.” Hans
alihisi hali ya Alvin haijatengemaa kwani
uso wake ulikuwa umelowa jasho.
Alvin alimkazia macho na kusema kwa
msisimko, "Mpigie Chester."
Hii ilimweka Hans katika hali mbaya.
Ilimfanya Dokta Choka aonekane kama
daktari wa kibinafsi wa Alvin.
Hans alimpigia Chester simu. Chester
pia alikuwa hana la kusema, lakini
hatimaye alikuja na dawa ya kawaida ya
homa. "Alvin, huwezi kushauriana na
daktari wa familia yako?"
Alvin alifungua pakiti ya dawa na
kuchukua vidonge kadhaa kulingana na
mwongozo. Kwa sauti ya kishindo,
alisema, “Chester, sijisikii kuoa.”

"Nini?" Sura ya mshangao iliosha juu ya
uso wa Chester. “Una tatizo gani tena?”
"Sijui." Alvin aliegemea kiti kwa unyonge
huku akihisi homa. Labda alijua
alichotaka kwa sababu alikuwa
mgonjwa. “Nimebadili mawazo yangu.
Simpendi Sarah kama nilivyokuwa
nikimpenda tena. Sasa ... ninachofikiria
ni Lisa tu.”
Chester alikunja uso na kumtupia jicho.
“Nimekuambia kwa muda mrefu ufikirie
kwa makini. Ulipoenda na kuachana na
Lisa, nilifikiri ulikuwa wazi juu ya kile
unachotaka. Alvin, lazima uelewe
kwamba hakuna kitu kinachoweza
kutibu majuto. Kila mtu anajua kwamba
unafunga ndoa na Sarah. Hoteli na
tarehe zimepangwa, na kadi za mwaliko
wa harusi pia zimetolewa. Ukighairi
harusi ghafla, nini kitatokea kwa Sarah?
Unajaribu kumchimbia kaburi akiwa

hai?"
Mwonekano wa kutojiweza na hatia
uliangaza machoni mwa Alvin.
Chester aliendelea. “Zaidi ya hayo,
aliumia alipokuwa ng’ambo wakati huo.
Kwa kuwa umekuwa naye kwenye
uhusiano kwa miaka kadhaa, unafikiri
atawezaje kukabiliana na maisha yake
kwa vile humtaki tena?”
Chester akamtazama. "Wewe ndiye
uliyechagua njia hii na kusisitiza kurudi
pamoja na Sarah. Hakuna
aliyekulazimisha.”
Alvin alinyamaza kwa muda. Hakujua
kwanini alimchukia sana Lisa miaka
mitatu iliyopita lakini alivutiwa naye tena
miaka mitatu baadaye.
“Chester, sidhani kama nilimchukia Lisa
miaka mitatu iliyopita. Yote ni kwa
sababu nilipoteza kumbukumbu zangu

wakati huo, au nisingempa pete ya
uchumba.”
“Kwa kweli humchukii. Kama si kifo cha
Maurine, ninyi nyote wawili
msingetengana.” Chester alisema kwa
kawaida. Kisha, akasimama na
kumkumbusha, “Alvin, hakuna kurudi
nyuma. ”
Alvin alikaa kimya kwa muda wa lisaa
limoja kwenye siti. Labda aligundua hilo
kwa kuchelewa sana.
Sura ya: 388
Katika chumba cha faragha
kilichofichwa, Sarah alikuwa amengoja
kwa zaidi ya dakika kumi kabla ya
mlango kusukumwa polepole. Mtu
mmoja, ambaye alijidhihirisha katika hali
ya heshima, aliingia polepole. Kutoka

kwenye uso wake, alionekana kuwa
mvivu na mzembe. "Kwanini
unanitafuta, Bi Njau?"
“Ningependa kushirikiana nawe.”
Akimtazama usoni, Sarah alitoa
tabasamu hafifu na tulivu.
“Hakuna tunachoweza kushirikiana.
Nadhani umenielewa vibaya, Bi Njau.
Nina shughuli nyingi. Kama hakuna
kingine...”
"Maurine aliyemhudumia Alvin miaka
mitatu iliyopita hakuwa Maurine halisi,"
Sarah alimkatisha na kuanza
kumpanga. "Alipogundulika baadaye,
ulimbadilisha na Maurine halisi. Isitoshe,
Maurine huyo wa bandia alipokuwa na
Alvin, aliendelea kumlisha Alvin dawa
ambayo ilizidisha hali yake ya ukichaa,
ikiwa ni pamoja na kuharibu
kumbukumbu zake.”

Uso wa mtu huyo ulizidi kuwa na
wasiwasi zaidi na zaidi. Taratibu akaketi
mkabala na Sarah huku akitabasamu
kwa huzuni. "Unajua mambo mengi, Bi
Njau. Nini kingine unachojua?”
“Kama nisingetokea wakati huo, Alvin
angeweza kuwa tayari
amechanganyikiwa," Sarah alisema.
“Ni vizuri unajua. Umeharibu mpango
wangu." Mwanaume huyo akaushika
mdomo wake. "Una ujasiri gani wa kuja
kutafuta ushirikiano na mimi?"
Sarah alicheka. “Sidhani kama
ungependa asili yako ya kweli ifichuliwe,
na nina ushahidi nayo. Nilipoanza
kumtibu Alvin miaka mitatu iliyopita,
niligundua kuwa dawa yake ilikuwa
imechafuliwa. Ilikuwa mbinu ya
kitaalamu sana kwa sababu hakuna
mtu, isipokuwa mwanasaikolojia mahiri
kama mimi, ambaye angegundua.”

Yule mtu akanyamaza. Sarah
akammiminia kikombe cha kahawa.
"Nina ufahamu mzuri wa kile
kilichotokea miaka mitatu iliyopita.
Maurine bandia alikuwa Lina. Kuhusu
mahali alipo Lina kwa sasa, naamini
hakuna mtu mwingine anayejua
isipokuwa wewe tu.”
“Mimi?” Mwanaume akacheka.
“Kwa kuwa umeweza kuficha siri hii
kutoka kwa Alvin, Rodney na Chester,
nina uhakika si wewe pekee uliyehusika
nayo. Lazima kuna mtu mwingine
nyuma ya jambo hili,” Sarah alisema
huku akitabasamu, * Kwa kweli,
ninakushukuru sana kwa kuharibu
uhusiano wa Alvin na Lisa niliporudi.
Ulisababisha hata Charity, mtu
niliyemchukia zaidi, aende jela, jambo
ambalo limeniwezesha kuiharibu familia
ya Njau bila juhudi. Kwa muda mrefu
nilitaka kuwa marafiki na wewe.”

"Huogopi kwamba Alvin atagundua?"
Mwanamume huyo alidhihaki, “Wewe ni
mwanamke mbaya sana. Cha
kushangaza ni kwamba Alvin
hajakugundua japokuwa analala na
wewe kila siku.”
Sarah aliugulia kisirisiri kusikia hivyo.
Angewezaje kulala na Alvin wakati kila
siku alikuwa akilala chumba tofauti?
“Unataka nikusaidie vipi?” mtu huyo
aliuliza baada ya muda.
“Mtu huyu." Sarah akamkabidhi picha.
"Muueni, na tutakuwa washirika wazuri
katika siku zijazo."
“Anakuletea shida gani?”
"Sitaki kumpoteza Alvin." Sarah akauma
meno. Hakuna aliyempenda zaidi Alvin
kuliko mimi. Anachotaka kufanya ni

kuniharibia.”
Mwanaume huyo alichukua picha.
•••
Siku mbili baadaye. Pamela alirudi
kutoka Dar hadi Nairobi usiku.
Lisa mwenyewe alimchukua airport.
“Jamani, niliondoka kwa siku chache tu,
na Suzie tayari amekuwa binti wa Jack.
” Pamela alisema kwa huzuni, “ Basi,
hawawezi kurudi Marekani pamoja
nami. Nitakuwa mpweke peke yangu
huko. Au nihamishe ofisi yangu hapa
Nairobi? Wazazi wangu wanatumaini
kwamba nitarudi pia.”
“Ndio, hakika.” Lisa kisha akauliza,
“Kwani SE Group si walikuomba
ushirikiane nao? Unaweza kufanya kazi
nao na kushindana Osher Corporation
pamoja.”
“Nikizungumza hivi, wale watu kutoka

Osher Corporation wamekuwa
wakinipigia simu kila siku. Wameomba
msamaha na kuniomba nirudi.” Kwa
kutajwa kwa jambo hili, Pamela alikuwa
mtupu sana.
Wakati huo, simu yake iliita na arifa ya
simu inayoonyesha 'Rodney Shangwe'.
Pamela alimtazama Lisa na kuinua
kichwa chake kabla ya kugonga kwa
kiburi kitufe cha kukatia simu. “Ha, huu
ni ujinga. Alinipuuza nilipomsihi mara ya
mwisho, lakini sasa ametoka kwenye ligi
yangu.”
Lisa alicheka. "Hakika italeta shida kwa
Rodney ikiwa utafanya kazi na SE
Group. Familia ya Shangwe ina watoto
wengi. Rodney ana dada mkubwa na
kaka mdogo ambao wote wana uwezo
mkubwa. Lakini kama mtoto wa kati,
hana uwezo mkubwa sana. Ana binamu
kadhaa pia katika familia yake kubwa.
Ikiwa atashindwa kufanya vizuri katika

kampuni yake mwenyewe, familia ya
Shangwe hakika itapoteza imani
kwake.”
"Ni bora ikiwa yeye sio mrithi wa familia
ya Shangwe, au ataharibu maisha yao
ya baadaye," Pamela alidhihaki. "Ni
bora kwake kuwa msaidizi wa Sarah."
Lisa alipokuwa anataka kuzungumza,
ghafla Logan akampigia simu. Sauti
yake upande wa pili ilisikika kukasirika.
"Damn, Hisan Gadaffi amekufa."
Uso wake ulibadilika. “Si nilikuomba
umlinde? Nini kimetokea?"
"Ulikisia kwa usahihi. Hisan
alishambuliwa njiani nilipokuwa
nikimfuatilia usiku wa leo. Akiwa njiani
kuelekea nyumbani, watu wanne
walimvamia, wakampiga risasi akiwa
mbali,” Logan alisema kwa kuudhika.
“Baada ya kumuua, watu hao walimvuta

ndani ya gari na kwenda kumzika
kwenye mlima usio na watu, lakini
hawakujua kwamba nilikuwa
nikiwafuata.”
"Uko wapi sasa?"
"Bado niko mlimani, lakini watu hao
wameondoka." Logan alinyamaza kwa
muda kabla ya kuendelea, "Watu hao
walikuwa wamevaa vinyago, kwa hiyo
sikuweza hata kuwatambua."
Lisa alishangaa. "Kwanini Sarah
ajihusishe na watu wa aina hiyo?"
“Nafikiri... hatumwelewi vya kutosha.
Baada ya yote, mwanamke huyu
alinusurika huko Somalia chini ya
udhibiti wa mtu mkatili kama Hisan.
Labda kuna mtu anayemsaidia kwa siri.”
Logan aliaibika sana aliposema,
“Samahani, ulikuwa uzembe wangu.”

Hakuna aliyeelewa ustadi wa Logan
zaidi ya Lisa. Tayari alikuwa na uzoefu
halisi wa vita licha ya umri wake mdogo,
kwa hivyo watu hao lazima wawe na
nguvu sana kuweza kumuua Hisan chini
ya ulinzi wa Logan.
“Umefanya vizuri. Ingawa nilikuomba
umlinde Hisan, ninaelewa kuwa
hukuweza kufanya lolote chini ya hali
hizo. Nisingetaka utoe maisha yako ili
kumuokoa pia.” Lisa aliongeza kwa
upole, “Nina hakika hawakutarajia
ungewafuata. Jaribu na utafute njia ya
kuwaarifu polisi kuhusu maiti ya Hisan.
Hisan alikuwa akienda hotelini kila mara
na kuwapeleka wanawake kwenye
ghorofa la Sarah, kwa hivyo polisi
wakifuatilia habari hiyo kwa Sarah.
Nadhani ndoa ya Sarah haiwezi kwenda
kwa njia yake.” Lisa aliweka simu yake
chini huku uso wake ukiwa na huzuni.
"Nimekuwa nikimchunguza Sarah nchini

Marekani kwa siri katika kipindi cha
miaka mitatu iliyopita.” Alimwambia
Pamela. “Nilidhani nilimuelewa vizuri,
lakini ikawa kwamba nilimdharau. Kwa
kuwa aliweza kupata kundi hilo la watu
wakatili kumfanyia kazi, lazima asiwe
mwanamke wa kawaida.”
“Unapaswa kuwa makini. Kwani una
Suzie na Lucas sasa,” Pamela
alimkumbusha.
“Sawa.” Bila kujali ni nani aliyekuwa
akimsaidia Sarah kwa siri, Lisa aliona
haja ya kufichua asili yake halisi.
Sura ya: 389
Katika Jumba la Kifahari la Alvin. Punde, Sarah akapokea simu. "Mtu huyo ... ameshughulikiwa."

Macho ya Sarah yaliangaza. "Kazi nzuri.
Nyie mna ufanisi kweli. Je, umeiweka
sawa maiti yake?"
“Imezikwa mlimani. Hakuna mtu
anayeweza kufika huko.”
“Asante.”
Mtu wa upande mwingine alicheka.
“Bado huna haja ya kunishukuru. Kwa
kuwa sasa nimekusaidia, utahitaji
kurudisha fadhila wakati ujao.”
“Sawa.” Sarah akauma mdomo.
Hakuwa na wasiwasi tena kwamba
kutakuwa na kurudi nyuma kwenye
safari yake. Ilikuwa ni kitulizo kikubwa
kujua kwamba Hisan, ambaye alikuwa
mwiba kwake, alikuwa ameuawa.
Muda mfupi baadaye, sauti ya injini ya
gari ilisikika kutoka nje.

Mara aliposikia gari likiingia, Sarah
akashuka chini. “Alvinic, umerudi kwa
wakati ufaao. Mpangaji wa harusi
amenitumia mpango wa ukumbi leo, na
hivi ndivyo ukumbi wetu wa harusi
utapambwa. Iko sawa?"
Alvin aliitupia jicho la kawaida tu pale
alipompa simu yake. “Kadiri
unavyopenda, ni sawa. Naenda kuoga
sasa hivi.”
Sarah alitazama mgongo wake na
ghafla akapiga miguu yake kwa
kuchanganyikiwa. “Alvin, sema kweli
iwapo haupo tayari kunioa. Tangu
tulipoamua kuoana, hujawahi
kusumbuliwa na jambo lolote kuhusiana
na harusi yetu. Bado hatujapata cheti
cha ndoa, na harusi yetu ni wiki ijayo.
Bado unakumbuka hilo?"
Alvin akageuza kichwa chake. Mara
alipokutana na macho yake ya huzuni,

moyo wake ukashtuka. Wakati wote
huo, alifikiri kwamba kumuoa Sara
ilikuwa furaha. Lakini, hivi karibuni
jambo hili llilikuwa kama uzito mkubwa
akilini mwake.
Sarah hakuweza kujizuia kulia machozi.
“Najua kilichompata Suzie juzi ni kosa
langu, lakini nimejitafakari. Hutaki nipate
ujauzito, kwa hivyo sijapiga sindano
yoyote tena. Nini kingine unataka
kutoka kwangu? Je, ni kwa sababu
hunipendi tena? Kila siku, unatoka
nyumbani mapema na kurudi kwa
kuchelewa. Hukuwa hivi hapo awali.
Tangu Lisa arudi...”
“Inatosha.” Alvin akamkatisha.
“Bado sijamaliza,” Sarah alishindwa
kujizuia kumpigia kelele. Alilia kama
alikuwa kwenye hatihati ya kuvunjika.
“Najua siwezi kukuridhisha, na unaona
ni karaha kunigusa. Lakini wewe ndiye

ulisisitiza kuwa na mimi, Alvinic.
Sikutaka pia kuharibu ndoa yako na
Lisa. Nimekaa kando yako kwa miaka
mitatu, na ulimwengu wote unajua
kwamba tunafunga ndoa. Ukiamua
kuniacha sasa, nitafanya nini na maisha
yangu? Unajaribu kunizika ningali hai?
Tulipokutana katika hospitali ya
magonjwa ya akili tukiwa na umri
mdogo, ulisema kwamba utanilinda
milele tutakapokuwa nje. Je, umesahau
kuhusu hilo? Ninakupenda, na upendo
wangu kwako haujawahi kubadilika.
Lakini vipi kuhusu wewe?”
Matukio katika hospitali ya magonjwa ya
akili yalimwangazia akilini mwake. Alvin
aliposikia kilio chake, moyo wake
ulitawaliwa tena na hatia na kujilaumu,
bila kujali alikuwa amegeuka kuwa mtu
wa aina gani. Chester alikuwa sahihi
kwa kusema kwamba hakuna kurudi
nyuma. Ikizingatiwa kuwa mwanamke
huyu alikuwa ametumia muda mwingi

wa ujana wake juu yake, lazima
asimkatishe tamaa.
"Samahani, nina mengi kwenye kichwa
changu hivi karibuni. Nitaenda nawe
kwenye ukumbi wa harusi kesho.” Alvin
alisema kwa sauti ya chini.
Hakumfikiria Lisa tena. Wakati huu,
angeweza kumshinda.
Siku ya harusi yao ilikuwa inakaribia
zaidi na zaidi. Kesho yake akiwa ofisini,
baada ya mkutano kumalizika mchana,
Alvin alisimama na kuwa karibu
kuondoka. Hapo ndipo mkurugenzi
mmoja wa kike alipomwendea Lea na
kusema kwa tabasamu, “Unaenda wapi
jioni hii? Twende tukapige maji
baadaye, sawa?.”
“Siwezi. Jack yuko kwa safari ya kikazi,
kwa hivyo nahitaji kumchukua mjukuu
wangu baadaye," Lea alijibu kwa
tabasamu.

“Wow, kidogo nisahau kwamba wewe ni
bibi tayari. Bado unaonekana kama
msichana mdogo."
Mkurugenzi wa kike na Lea walianza
kuzungumza kwa furaha. Alvin
akawaendea na kusema, “Mnaweza
kwenda, nami nitamchukua Suzie.
Ninakwenda kumtafutia mavazi. Nahitaji
awe msichana wangu wa maua kesho
kutwa.”
Lea alipigwa na butwaa, lakini baada ya
kusitasita akaitikia kwa kichwa. “Sawa
basi.” Kwa kuzingatia kwamba wanawe
hawakuwa na uhusiano wa kirafiki,
alitumaini kwamba Suzie angefanya
kazi kama daraja kati yao.
•••
Katika mlango wa shule ya chekechea.
Wakati Alvin alipofika, watoto walikuwa
bado hawajaruhusiwa kuondoka.

Alipoona umbo lake refu na la kifahari,
mlinzi wa getini alionyesha heshima
yake bila kujua.
Ingawa watoto wengi katika shule hiyo
ya awali walikuwa na wazazi matajiri,
ilikuwa nadra kuona mzazi kama yeye
ambaye alikuwa na hisia kali ya
mamlaka.
"Bwana Mkubwa, naomba kujua
umekuja kwa ajili ya mtoto gani?" Mlinzi
alimuuliza kwa adabu.
“Niko hapa kwa ajili ya Susan Jones,”
Alvin alijibu bila kujali.
“Yuko katika darasa la awali. Darasa la
awali lina shughuli za nje sasa.
Mlinzi huyo alimuongoza kwa adabu
mpaka ndani ya boma. Haikupita hata
dakika moja wakafika mahali ambapo
shughuli za nje zilikuwa zikifanywa.

Kikundi cha watoto kilikuwa kikicheza
kwa furaha katika eneo hilo kubwa.
Alvin alimuona Suzie ndani ya sekunde
chache kutokana na mavazi yake ya
waridi yenye kuvutia, na alikuwa
mrembo zaidi kati ya wasichana hao.
Wakati anakaribia kumsogelea Suzie,
ghafla alimuona akiruka kwenye slaidi
na kumshika mkono mtoto mdogo
aliyevalia sare ya rangi ya machungwa.
Suzie aliuvuta mkono wa mvulana
mdogo kwa nguvu na kukanyaga miguu
yake kwa ustaarabu. "Lucas, unataka
kwenda nami kwenye msumeno?"
"Hapana, siipendi." Mvulana huyo
alionekana mzuri na asiye na hatia.
"Hapana. Nataka tu ucheze na mimi.”
Suzie aliuvuta mkono wa mtoto huyo
bila kukusudia kuuachia.

Uso mzuri wa Alvin ukaingia giza.
Tayari angeweza kusema kuwa Suzie
alikuwa ni mtoto ambaye angevutika
kirahisi kwa watu wenye sura nzuri.
Hapo awali alikuwa na wasiwasi
kwamba angeingia kwenye uhusiano
katika umri mdogo. Lakini, hakutarajia
kwamba angeshika mkono wa mvulana
kwa ustadi katika siku chache za
kwanza za shule ya awali.
Aligeuka, akipanga kumfundisha
kwamba haikuwa sawa kwa wavulana
na wasichana kugusana kimwili.
“Suzie.” Akapiga hatua kuelekea kwake.
Suzie na Lucas wote walishangazwa.
"Anko Alvin." Suzie mara moja
akamkimbilia Alvin na kumzuia njia.
Lucas alichukua nafasi hiyo kukimbia.
Kwa kupepesa macho, alikuwa
amejipenyeza kwenye mtaro wa
kuteleza.

Alvin alikunja uso. “Ni rafiki yako mpya
hapa? Kwanini alinikimbia mara tu
aliponiona?”
"Hakujui, kwanini abaki hapa na
kukusalimia?" Suzie aliinamisha kichwa
chake. "Zaidi ya hayo, labda ulimtisha
kwa sauti yako ya nguvu sasa hivi. Anko
Alvin, kwanini umekuja kunichukua
leo?”
“Baba yako hayupo kwa safari ya kikazi,
kwa hiyo nimekuja kukuchukua. Twende
zetu.” Alvin alinyoosha mkono wake
kuelekea kwake.
“Sawa. Nitamjulisha mwalimu wangu na
kuchukua begi langu.”
Suzie alikurupuka na kumshika mkono
Alvin huku wakielekea darasani
kuchukua begi lake.
Mwalimu alipomkabidhi Suzie kwa Alvin,

mapigo ya moyo yalimuenda mbio
baada ya kuona sura nzuri ya Alvin.
“Madam, utendaji wa Suzie
unaendeleaje?” Alvin aliuliza ghafla.
Alifikiri kwamba Jack hakuwajibika,
hivyo aliona haja ya yeye kujua zaidi
kuhusu Suzie kwa hiari yake.
“Anafanya vizuri sana. Suzie ni
msichana mchangamfu. Tayari amepata
marafiki wazuri siku yake ya kwanza
hapa, na ana uhusiano wa karibu sana
na Lucas,” mwalimu alijibu huku
akitabasamu.
“Lucas?” Alvin alikunja uso huku
akiwaza.
"Tuondoke sasa, Anko Alvin." Suzie
akiwa hana raha, mara moja akamvuta
kwa kuhofia kwamba angemwona
Lucas.
“Mm. Baada tu ya Alvin kumbeba Suzie

na kuondoka alishusha pumzi. "Suzie,
Lucas ndiye uliyekuwa umeshikana
naye mikono sasa hivi?" Alvin aliuliza
ghafla.
Sura ya: 390
“Ndiyo,” Suzie alijibu kwa woga.
“Suzie.” Alvin aliinama ghafla na
kusema kwa dhati, “Nyinyi wawili bado
ni wachanga, kwa hiyo ni sawa. Lakini
unapoendelea kukua, unahitaji kuelewa
kwamba huwezi kumshika mvulana tu
mkono.”
“Oh.” Suzie aliitikia kwa kichwa. Yeye
kamwe hakuwahi kushika mkono wa
mvulana mwingine asiyemjua. Kwa
kuwa Lucas alikuwa kaka yake,
haikujalisha. Lakini hakuweza kuweka
wazi kwa Alvin,
"Unaweza kujaribu kuchanganyika na

wasichana," Alvin alishauri.
“Anko Alvin, usinipangie marafiki,” Suzie
alisema huku akihema.
Alvin hakusema neno baada ya
kudharauliwa. Sawa, alikuwa bado
mdogo sana kuelewa. Angeweza
kwenda naye tu polepole.
Hakujua kuwa Lucas alikuwa amejificha
nyuma ya mlango, akimwangalia wakati
anamchukua Suzie.
Mwalimu alikuwa na hisia kwamba
Lucas alivutiwa na Suzie kwa kuwa na
mzazi wa kwenda kumchukua, hivyo
alimfariji kwa upole, “Lucas, usijali.
Familia yako itakuwa hapa kukuchukua
hivi karibuni."
“Mm.” Lucas aliachia macho yake. Huyo
alikuwa ni baba yake mchafu. Ilikuwa ni
mara ya kwanza kwa Lucas kusikia

sauti ya baba yake mchafu, na alikuwa
mrefu sana pia.
Lakini, hivi karibuni angeoa mwanamke
mwingine. Tofauti na Suzie yule
mpumbavu, Lucas asingeweza
kudanganywa kirahisi hivyo. Hakuwahi
kumkubali baba yake mchafu.
•••
Siku iliyofuata, kwenye Makaburi ya City
Park Cemetery.
Lisa na Pamela walibeba mashada
mawili ya maua na kutembelea
makaburi ya Boris na Jennifer. Baada
ya kutafuta kwa muda mrefu, hatimaye
waliyapata. Mbele ya kaburi kulikuwa na
shada la maua na majivu ya pesa za
karatasi.
"Kuna mtu alikuja na kutoa heshima
zake?" Pamela aliyatazama maua
mapya. “Haikuwa Sarah na Thomas,
wale viumbe waovu, sivyo?
Sidhani kama wao wana utu wa kufanya

hivyo.”
"Bila shaka, sidhani kama wanaweza
kuwa wao." Lisa aliona ni ajabu pia.
Baada ya yote, hakuna mtu kutoka kwa
familia ya Njau aliyekwenda hospitali
kumtembelea Boris alipokuwa mgonjwa.
Pia, kwa kuzingatia kwamba haikuwa
tukio maalum siku hiyo, kwanini mtu aje
na kutoa heshima kwao?
"Naam ... inaweza kuwa kwamba
Charity bado yuko hai?" Pamela aliuliza
ghafla.
Lisa alipigwa na butwaa kidogo.
“Nilisikia hawezi kuogelea. Tangu
alipojitosa baharini, kuna uwezekano
mkubwa kwamba alikufa.”
"Sio tu kwamba amekufa, lakini hata
kaburi lake hamuwezi kuliona kwa
sababu atakuwa aliliwa na samaki."
Ghafla, sauti ya Thomas ya dhihaka

ilisikika nyuma yao.
Lisa aligeuka na kuwaona Sarah na
Thomas wakiwakaribia, wote wakiwa na
mashada ya maua mapya. Sarah
alikuwa amevalia vizuri katika vazi
jekundu la maxi. Hakuonekana kama
alikuwa hapo kutoa heshima zake kwa
Boris na Jennifer. Badala yake,
alionekana kama anahudhuria hafla ya
kufurahisha.
Thomas alitoa kicheko kibaya huku
akimkazia macho Pamela. "Sio mbaya.
Sijakuona kwa miaka mitatu, na bado
unaonekana kuwa mdogo. Hahh, bado
nakumbuka jinsi ulivyoonekana
nilipokuvua nguo wakati huo.”
Uso mzuri wa Pamela ulibadilika ghafla.
"Thomas Njau, bado unanitafuta siyo?"
“Mbona unanikoromea? Unafikiri
unanitisha kwa sababu sasa wewe ni

mwanakemia maarufu wa vipodozi?”
Sura ya dharau iliwaka usoni mwa
Thomas. “Hata hivyo, ninakupa tu
ushauri wa bure, kumbuka kufunga
milango yako unapolala usiku.
Ninaweza kuja kukutafuta katikati ya
usiku.” Kwa hayo, bila aibu aliangua
kicheko.
Ijapokuwa Sarah alichukizwa na
maneno ya Thomas ya kuudhi,
hakujishughulisha na kumzuia
alipokumbuka maneno ya dharau ya
Lisa na Pamela.
“Una uhakika... utathubutu tena kuja
kunitafuta?” Pamela ghafla akainuka na
kumsogelea Thomas polepole.
“Unataka kufanya nini? Unataka
kunipiga, sivyo? Wewe tu? Haha...”
Kabla Thomas hajamaliza sentensi
yake, Pamela alikuwa amempiga ngumi
nzito usoni.

Thomas aliporudi kwenye fahamu zake,
alilenga ngumi kwa Pamela kwa hasira.
Lakini Pamela alihepa, akamtupa
begani, na baadaye akaanguka chini.
Ardhi ilijaa changarawe, na baada ya
sekunde chache, mwili wa Thomas
ulianza kumuuma sana. “B* tch...”
“Unaweza kuongea tena kwa jeuri,
huh?” Pamela akamkanyaga usoni.
“Kaka.” Sarah aliingiwa na hofu sana
hivi kwamba sura yake ilibadilika kabisa.
Alikimbia kuelekea kwa Pamela ili
kujaribu kumshika, lakini Lisa alikuwa
mwepesi wa kutosha kusimama mbele
ya Pamela.
"Hey, wanasuluhisha mambo yao ya
zamani. Kwanini unataka kuingilia?
Waache tuone nani mbabe.”
Ushauri wa Lisa nusura ufanye Sarah

alipuke kwa hasira. Sarah hakumjali
sana Thomas, lakini kwa kuwa sasa
walikuwa pamoja, kumtazama akipigwa
mbele yake kulimdhalilisha pia.
“Fanya haraka uwaite polisi, Sarah.
Mjulishe Shemeji Kimaro na Rodney,”
Thomas alifoka kwa uchungu. Hakujua
ni nini Pamela alipitia kwa miaka mingi
ambacho kilimpa uwezo wa ngumi za
chuma. Makonde yake yalikuwa
yamemwacha katika maumivu makali.
“Pamela Masanja, wewe b*tch, hakika
nitashughulika nawe baadaye.
Usikimbie ikiwa una ujasiri. Nitatafuta
watu wachache na kukufanya
mtungo...”
“Una mdomo mchafu sana. Acha
nikutengeneze.” Pamela alinyanyua jiwe
la ukubwa wa wastani na kuligonga
mdomoni mwake. Yowe la huzuni la
Thomas lilijaza makaburi. Zilikuwa

kelele zilizomshtua msimamizi wa
makaburi.
Uso wa Sarah ulibadilika kidogo kabla
hajatoa simu yake ili kumpigia Alvin.
Lakini, alipokumbuka jinsi Alvin
alivyomchukia sana Thomas siku za
karibuni, alighairi na kumpigia simu
Rodney badala yake. Badala ya
kumzuia Sarah, Lisa alimtazama tu jinsi
alivyokuwa akipiga simu.
Msimamizi wa makaburi alifika.
“Mnafanya nini jamani? Ikiwa mnataka
kupigana, nendeni mahali pengine. Huu
sio ulingo wa masumbwi. Msivuruge
amani ya wafu.”
Sarah alipokuwa anakaribia kuongea,
Pamela alikuwa tayari anaitikia kwa
kichwa huku akiwa amejifunika uso
wake. “Sawa, sawa. Samahani.
Nilishindwa kujizuia nilipomwona mtu
huyu. Yeye ni mtoto wa mjomba wangu,

na mjomba wangu alikufa kwa sababu
yake. Mjomba wangu alikuwa na umri
wa miaka 50 tu. Hawajawahi hata kuja
kumpa heshima mjomba wangu tangu
tumzike miaka michache iliyopita.”
Thomas alitoa macho huku akitaka
kujieleza. Hata hivyo, mdomo wake
ulikuwa umeumia vibaya kwa kupigwa
ngumi na jiwe kiasi kwamba meno yake
machache yalikuwa yamedondoka.
Ilikuwa chungu sana kufungua kinywa
chake, hivyo hakuweza kuzungumza
vizuri.
Meneja akahema. "Baada ya kusimamia
makaburi haya kwa muda mrefu,
nimeona kila aina ya watu. Kuna baadhi
ya makaburi ambayo hakuna mtu
aliyewahi kuja kutoa heshima zake kwa
zaidi ya miaka kumi. Kama kizazi kipya,
mnahitaji kuwa na dhamiri ya maadili.”
“Mm. Sitampiga tena. Kwa kuwa ndivyo

anavyofanya, hakuna maana kumpiga,”
Pamela alisema kwa huzuni huku
akimziba Thomas mdomo.
“Sawa. Toeni heshima zenu tu na
muondoke." Msimamizi aliondoka mara
baada ya kumaliza sentensi yake.
Sarah alikuwa na kichaa sana hadi uso
wake ukapauka. “Nyinyi wawili...
mnachukiza sana. Baba yangu alikuwa
mjomba wako lini? Huna aibu?”
“Angalau sisi tunayemchukulia kama
mjomba, Nyie je? Mnamjua hata kama
ni baba yenu kwenu?." Pamela kisha
akamuachia Thomas, ambaye uso wake
ulikuwa umevimba.
Thomas alitamani angempasua Pamela,
lakini kwa kuwaza jinsi
alivyomshughulikia, aliogopa sana
kumsogelea tena. Ingawa yeye peke
yake alikiri asingemuweza, alichopanga

kufanya ni kutafuta watu wachache zaidi wa kukabiliana naye. Kufikia wakati huo,
angeweza kumuua.
“Nyie... Subirini... Subirini kidogo.”
Thomas aliugulia maumivu. “Dada
yangu... anaolewa kesho. Atakuwa...
kuwa...Bi. Kimaro... Kisha... nitalipiza
kisasi kwenu. ” Thomas alitoa maneno
kwa tabu sana.
Lisa aliyatupia macho maua yaliyokuwa
mkononi mwa Sarah. "Tsk. Je, ulikuja
hapa ili kujionyesha kwa baba yako?”
Baada ya kutajwa kwa ndoa yake siku
iliyofuata, Sara alifurahi. “Kama binti
yake, inabidi nimjulishe kuwa nitaolewa
kesho. Nyinyi hamna uhusiano wowote
na familia ya Njau, kwa hivyo ni wakati
wa kupotea."
“Kweli. Potelea mbali,” Thomas alisema.

TUKUTANE KURASA 391-395
ONYO: Ni marufuku kusambaza, kukopi wala kuuza kazi hii kwani endapo kama tutakubaini basi sheria itachukua mkondo wake (By: Official Dully)
 
LISA KITABU CHA NANE (8) SIMULIZI........................LISA KURASA.................396 – 400
PRESENT: SIMULIZI ZA DULLY

Sura ya: 396
Wanafamilia wa Kimaro walinyamaza
papo hapo. Ingawa familia ya Malugu
haikuweza kulinganishwa na familia ya
Kimaro, bado walikuwa familia ya
wasomi. Kwa kuongezea, utambulisho
wa Lisa ulikuwa tofauti sasa. Ilikuwa
kawaida tu kwamba familia ya Malugu
ingemtaka aolewe katika familia yao.
Hata Valerie alibaki kimya, lakini alihisi
kuchanganyikiwa. Hakutarajia kuwa
Lisa bado angekuwa maarufu hata
baada ya kuachwa.
Kwa upande mwingine, ingawa Alvin
alikuwa akipiga toast na wageni,
aliendelea kutazama kile kinachotokea
upande wa Lisa. Erick alipopita, mikono
yake kwenye glasi yake ya divai ilikaza
bila hiari.

"Alvin, Chester." Ghafla, Rodney
akatokea kwa haraka. Bado alikuwa amevaa nguo zake za jana. Alikuwa
amelewa pombe, na shati lake lilikuwa
limekunjwa.
Chester alimtazama kwa dharau.
“Angalia mwonekano wako. Angalau
ulipaswa kubadilisha nguo zako kabla
ya kuja."
“Sikuwa hata na hamu ya kubadilika.
Ninakaribia kufa kutokana na hasira,”
Rodney alifoka. “Mimi-”
“Ni wakati wa kujiandaa kwa sherehe.
Bibi arusi anaweza kutokea muda
wowote kuanzia sasa hivi.” Msimamizi
wa sherehe alikuja na kukatiza maneno
ya Rodney.
Rodney alionekana kuhuzunika, lakini
hakuna aliyemjali. “Sawa.”

Alvin aliitikia kwa kichwa, na macho
yake yalikuwa chini. Aliwaambia
Chester na Rodney waende kumchukua
Sarah.
Sherehe ya harusi ilianza kwa wakati
mwendo wa saa sita na nusu mchana.
Sarah alivalia vazi maridadi la harusi
lililomfanya aonekane kama binti wa
kifalme. Alitembea polepole akiburuta
shera refu jeupe. Alivaa kishada
kichwani, na kilipambwa kwa almasi
nyingi. Iliwafanya wanawake
waliohudhuria harusi kuwa na wivu.
Aliingia kwenye gazebo nyeupe na
kusimama uso kwa uso na Alvin,
aliyekuwa amevalia suti nyeupe.
Alikuwa na mwonekanoa kipekee
uliyomfanya awe na sura nzuri.
Moyo wa Sarah ulianza kwenda kasi.
Alikuwa akingoja kwa muda mrefu sana
siku hii, na hatimaye ikafika.

Akamtazama kwa haraka Lisa
aliyekuwa kwenye bustani. 'Ha,
mwishowe, Alvin ananioa!' Alijiwazia
kwa furaha.
Katika siku zijazo, angekuwa na watoto
na Alvin. Kila alichokuwa nacho
kingekuwa chake.
“Alvini...” Sarah alimtazama Alvin kwa
upendo.
Alvin alikuwa na hisia tofauti. Tayari
alikuwa ameamua kumuoa Sarah muda
mrefu uliopita. Aliamua tu kufanya
harusi kwa sababu alikuwa na deni la
Sara. Hata hivyo, kwa kuwa sasa wakati
huo ulikuwa umefika, alihisi kana
kwamba kuna jiwe kubwa
linaloukandamiza moyo wake.
Msimamizi wa sherehe alishika kipaza
sauti na kuanza kuuliza, “Mr. Alvin
Kimaro, unamchukua Bi. Sarah Langa

Njau kama mke wako wa ndoa? Je,
unaahidi kuwa mwaminifu kwake pekee,
kumlinda, na kumthamini, kwa utajiri au
umaskini zaidi, katika ugonjwa na afya?”
“Nina...” Alvin alikunja ngumi.
Alipokuwa karibu kusema neno la
mwisho, kundi la polisi liliingia ndani.
"Samahani, tuko hapa kwa shughuli za
kipolisi." Mkaguzi mmoja alimsogelea
Sarah na kusema, “Bi.
Njau, polisi waligundua mwili wa mtu
mgeni kando ya mto siku mbili zilizopita.
Tunashuku kuwa unahusiana na kifo
chake. Tafadhali twende kituo cha polisi
pamoja nasi kwa uchunguzi."
Wageni wote walishtuka. Sara alihisi
kana kwamba alikuwa akianguka kutoka
mbinguni hadi kuzimu. Alisema kwa
sura ya kusikitisha, “Sijui unazungumzia
nini. Sijui mtu yoyote wa kigeni mimi.”

“Una uhakika humtambui?” Inspekta
alimwonyesha picha ya Hisan Gadaffi.
“Baada ya uchunguzi wetu, tunaweza
kuthibitisha kwamba mwanamume huyu
amekuwa akiishi katika nyumba iliyo
chini ya jina lako. Si hivyo tu, ulikuwa
ukiingia na kutoka katika nyumba hiyo mara kwa mara siku chache zilizopita.
Tunashuku kwamba ulishiriki naye
uhusiano usiofaa.”
Uso wa Alvin uligeuka kuwa mbaya
sana. Ni nini kinachoweza kuwa aibu
zaidi kuliko kundi la polisi
linalomshutumu bibi arusi wake kwa
kuwa na uhusiano wa kimapenzi usiofaa
wakati wa sherehe ya harusi yake?
Wageni pia walizusha kelele. Hakuna
mtu aliyetarajia kwamba
wangeshuhudia tukio hilo la
kushangaza wakati wa kuhudhuria
sherehe ya harusi ya Bwana Kimaro.

“Ni ukweli?”
“Je, polisi wanasema Sarah alikuwa na
uhusiano wa kimapenzi na mwanaume
huyo wa kigeni?”
"Hicho ndicho hasa alichomaanisha."
“Hilo haliwezekani, sivyo? Nilisikia
wamependana kwa zaidi ya miaka kumi.
Mbali na hilo, kwa mwonekano wa
nguvu wa Alvin, je Sarah anahitaji hata
kutafuta mwanaume mwingine?”
"Haha, labda hawezi kumridhisha."
Majadiliano ya wageni yalifika masikioni
mwa Alvin. Alionya kwa uso wa
wasiwasi, “Sarah ni mke wangu.
Tafadhali zingatieni maneno yenu
mnapozungumza." Alitoa sura ya
kutisha ambayo ilisababisha hata
mkaguzi mzoefu wa polisi kutetemeka.
Hata hivyo, muda mfupi baadaye,

Inspekta alijipa ujasiri na kusema tena,
“Ni kweli kwamba marehemu alishiriki
uhusiano wa kimapenzi na Bi Njau.
Tunafanya hivi kwa ajili yako pia, Bwana
Kimaro. Unataka kuoa katika mazingira
ya kutiliwa shaka, Bwana Kimaro? Au
una uhakika kwamba unamuelewa
kabisa yule mwanamke aliye karibu
nawe?”
"Inatosha. Ingawa wewe ni polisi, kuna
wageni wengi hapa leo. Inabidi
uwajibike kwa maneno yako. Nilikutana
na mtu huyo wa kigeni
unayemzungumzia hapo awali kwa
sababu alikodisha nyumba yangu.
Nilikuwa tu nikiwasiliana naye kuhusu
nyumba, lakini wewe unageuza
ionekane kuwa tulikuwa na uhusiano
usiofaa. Hii ni kashfa kubwa mno. ”
Sarah alishikwa na kiwewe cha hofu.
"Hiyo ni sawa. Sarah si mtu wa aina
hiyo.” Rodney hakuweza kujizuia tena

akajitokeza kuwavaa polisi. “Unafikiri
unaweza kumharibia mwanamke sifa
kwa sababu tu wewe ni polisi?
Hamzingatii hata kuwa hii ni siku ya
harusi yake?”
Inspekta alikunja uso na kusema kwa
unyenyekevu, “Jeshi la polisi
halikurupuki tu, linafanya kazi kwa
weledi. Mpaka tunakuja hapa, ina
maana kwamba tuna ushahidi mwingi
mikononi mwetu. Una uhakika unataka
niwaorodheshe mmoja baada ya
mwingine hadharani kabla hujaniruhusu
nimtoe mtu huyu?”
Sarah alianza kuingiwa na hofu baada
ya kusikia hivyo. Aliambiwa kazi ilikuwa
imefanywa kikamilifu, na mtu huyo hata
alisema mwili wa Hisan ulizikwa
kwenye milima isiyo na watu. Kwanini
ilionekana kando ya mto ambapo
iligunduliwa na polisi?

Polisi walikuja ghafla na kumkamata.
Hakujua ni kiasi gani polisi walijua
kutokana na uchunguzi wao katika siku
hizi mbili.
Alvin alimtazama Sarah kimya kimya.
Bado hakuamini kuwa Sarah angekuwa
na uhusiano wa kimapenzi na
mwanaume mwingine. Hata hivyo,
macho ya polisi yaliyojaa uhakika
yalimfanya anyamaze wakati huo.
"Alvin, waache polisi wampeleke
kwenye kituo cha polisi kwa uchunguzi,"
Mzee Kimaro alisema kwa sauti kubwa,
"Harusi ya leo imeahirishwa kwa muda."
Mzee Kimaro aliposema hivyo, kila mtu
pale ukumbini alishtuka. Hakuna
aliyetarajia kwamba harusi hiyo ya
karne ingefutwa ghafla. Uso mzuri wa
Sarah chini ya vipodozi maridadi
ulipauka papo hapo. Alikuwa amesubiri
kwa muda mrefu sana hadi siku hiyo
ifike. Alikuwa karibu kuwa Bi Mdogo wa

familia ya Kimaro. Alikuwa akiingoja
siku hii kwa muda mrefu sana.
"Alvinic." Aliushika mkono wa Alvin kwa
nguvu.
Ikiwa arusi ingeghairiwa, angeukosa
ubibi-arusi na kila mtu aliyemwonea
wivu hapo awali angemwona kuwa
kicheko cha taifa zima. Zaidi ya hayo,
sifa yake ingeharibiwa.
Alimtazama inspekta kwa kusihi.
“Unaweza kuturuhusu tumalizie harusi
kabla sijaenda na wewe kituo cha
polisi? Itachukua muda kidogo tu.
Tafadhali, hii ndiyo siku muhimu zaidi
maishani mwangu.”
Macho ya mkaguzi hayakuyumba.
Kama asingegundua baadhi ya mambo,
angevumilia na asingesitisha harusi
yake.
Sura ya: 397

Hata hivyo, afisa huyo wa polisi alihisi tu
kumdharau Sarah kutoka ndani ya
moyo wake. Hakufichua kila kitu kwa
heshima ya Kimaro family.
"Alvin, tunapaswa kushirikiana na
uchunguzi wa polisi," Mzee Kimaro
alisema kwa sauti ya amri, "Ikiwa hana
hatia, harusi itafanywa tena siku chache
baadaye. Familia ya Kimaro haina
uhaba wa pesa za kufanya harusi
nyingine, lakini, bibi mdogo wa baadaye
wa familia ya Kimaro lazima awe
mwanamke aliye na rekodi safi.”
"Alvin, hebu fanya kama babu yako
anasema." Bibi Kimaro alikubali kwa
kichwa. Hawakuwa wamewahi
kumpenda Sarah hata hivyo. Alvin ndiye
aliyeng’ang’ania kumuoa, hivyo
hawakuwa na jinsi.

Kwa vile polisi walikuwa hapo na kudai
kuwa Sarah alikuwa ana uhusiano wa
kimapenzi na mwanaume mwingine,
ingethibitika kuwa ni kweli,
wasingemuacha Alvin aendelee na
ndoa.
Hata kama Alvin angemuoa Sarah,
ilibidi wachunguze kila kitu kwa kina.
Baada ya yote, ilikuwa ndoa ya pili ya
Alvin. Ikiwa angeoa na kuachwa tena,
familia ya Kimaro ingegeuka kuwa
mzaha machoni pa umma.
Sarah alifadhaika. Alisema kwa macho
mekundu, "Babu, najua kuwa
umenichukia muda wote, lakini leo ni
harusi ya Alvinic na mimi."
“Tayari nimeshaweka wazi maoni
yangu. Sisi, familia ya Kimaro, haturudi
nyuma juu ya neno letu kuhusu harusi.
Tunashirikiana tu na uchunguzi wa

polisi. Ikiwa huna hatia, bado kutakuwa
na harusi." Mzee Kimaro alikasirishwa
na Sarah. Alifanya ionekane kama
alikuwa anajaribu kuwatenganisha yeye
na Alvin.
"Alvin, fanya kama babu yako
anavyosema," Lea alisema.
“Twende zetu.” Inspekta alikosa subira
pia. Alikuwa na polisi wawili pembeni
akawaambia wamtoe nje Sarah. Kisha,
akamgeukia Alvin na kusema, “Bwana
Kimaro, labda bado hujaelewa kuhusu
hili. Mtu huyo wa kigeni aliuawa. Hii ni
kesi ya jinai, na ni shtaka kubwa sana.”
Alvin, ambaye alitaka kusema kitu,
alinyamaza. Alikuwa mwanasheria
mahiri, hivyo alijua mengi kuhusu
masuala ya uhalifu. Sarah alikuwa ni
mshukiwa tu, hakutuhumiwa kuhusika
moja kwa moja katika kesi hiyo. Ilikuwa
ni kesi ya jinai, ya mauajia, kwa hivyo,

haikuwezekana kabisa ikiwa angetaka
kumruhusu Sara abaki.
“Sarah, unahitaji tu kushirikiana na
uchunguzi wa polisi,” alimwambia Sarah
kwa upole, “naamini kwamba huna
hatia. Nitakuwekea dhamana hivi
karibuni. Tutafanya harusi yetu siku
nyingine.”
“...Alvinic, sina hatia. Alvinic,
nitakusubiri.” Baada ya kusikia maneno
yake, Sara hakuhisi faraja. Badala yake,
moyo wake ulianguka katika kina cha
kukata tamaa. Alihisi baridi. Hakuwahi
kuhisi kupotea au kuwa na wasiwasi
kama alivyokuwa wakati huo. Aliogopa
kwamba Alvin angejua kuhusu yeye na
Hisan.Hata hivyo, hakuweza kupiga
kelele wala kulia kwa hofu. Vinginevyo,
angefichuliwa zaidi. Aliomba tu kwamba
polisi wasigundue chochote. Kwa njia
hiyo, bado angeweza kuolewa na Alvin
baada ya siku chache.

Harusi ilisimama ghafla. Alvin akatulia
haraka. Aliwaambia wageni, “Wageni
wapendwa, ninaomba radhi kwa dhati.
Nyinyi nyote mlikuja kuhudhuria harusi
yetu huku kukiwa na shughuli nyingi,
lakini tulikutana na tukio hili. Najisikia
kufadhaika sana na kujuta pia. Ingawa
harusi ya leo lazima ikatishwe, bado
mnaweza kukaa na kufurahia mlo na
vinywaji kabla ya kuondoka.”
Joel, ambaye alikuwa ameketi kwenye
meza ya tatu kutoka nyuma,
akamgeukia Lisa na kumwambia, "Lisa,
tunabaki kula?"
“Kwa ajili ya nini? Sio kama hatuna
pesa za kula chakula mahali pengine.”
Lisa akaweka glasi yake chini na
kusimama. Baada ya yote, alikuwa
amekuja tu kutazama tukio hilo
alilolitarajia. Aliridhika sana baada ya
kushuhudia tukio hilo la kuvutia. Ilikuwa

wakati wake wa kuondoka.
Joel alimfuata Lisa mara moja alipoona
kwamba alikuwa karibu kuondoka.
Wageni wengi waliondoka pole pole
baada ya kuona mtu akiongoza.
Wangeweza kula mahali popote, lakini
kila mtu alitaka tu kwenda nje na
kusengenya iwapo Sarah alikuwa
amemdanganya Alvin au la.
Wakati Mzee Kimaro alipoona wageni
wakiondoka mmoja baada ya mwingine,
alivunja glasi kwa hasira. “Ni fedheha
iliyoje! Huyu ndiye mwanamke
unayesisitiza kumuoa?”
“Babu, Sarah anafanyiwa figisu na mtu
mwingine katika tukio hili. Ninaamini
kwamba hana hatia.” Alvin alijaribu
kumtetea Sarah kwa sura mbaya.
"Nilimfahamu tangu nilipokuwa katika
hospitali ya magonjwa ya akili.
Ninamuelewa Sarah vizuri.”

"Hakuna mtu anayeweza kuelewa mtu
mwingine kabisa," Lea alisema ghafla
baada ya kumtazama Mason kama
kidokezo. Hapo awali alifikiria kuwa
anamjua Mason vizuri, lakini aligundua
katika siku za hivi karibuni kwamba
hakuwahi kumjua kabisa mtu ambaye
alikuwa amelala karibu naye kwa zaidi
ya miaka 20. Alvin alikuwa mtoto wake.
Huenda alifuata nyayo zake.
"Mama yako yuko sawa." Bibi Kimaro
aliitikia kwa kichwa. “ Usitulaumu kwa
kughairi harusi sasa hivi. Kama wazee
wako, tunatumai tu kwamba unaweza kuoa mwanamke mwenye rekodi safi.
Polisi walisisitiza kumchukua Sarah
ingawa kulikuwa na wageni wengi sasa
hivi. Nadhani ni lazima wawe
wameweka mikono yao juu ya kitu...”
Willie hakuweza kujizuia lakini kupata
ujasiri wa kusema, “Kaka mkubwa,

nadhani ni bora kuchunguza hili pia kwa
kina. Nimeona wanawake wengi, na
wengi wao wana—”
Alvin alimpiga jicho kali kabla
hajamaliza sentensi yake. "Nitaenda
kituo cha polisi ili kumdhamini Sarah
kutoka jela." Aligeuka na kuondoka
baada ya kusema.
"Alvin, tunaenda nawe." Rodney na
Chester walimfuata.
Wakiwa njiani kuelekea kituo cha polisi,
Rodney alisema kwa hasira, “Hao
maafisa wa polisi wamevuka mipaka.
Hawakuweza kuchagua wakati mzuri
zaidi wa kuchunguza jambo hili?
Kwanini walilazimika kumchukua Sara
wakati wa harusi yake? Si
wanamuaibisha Sarah hadharani?
Hawana hata maadili ya kuzingatia sifa
ya mwanamke. Je, familia za watu
mashuhuri zitazungumzaje kuhusu Sara
kuanzia sasa?”

Akaiwasha simu yake. "Angalia, sasa
kila mtu kwenye mtandao anajua kuwa
ninyi mmeghairi harusi. Kila mtu
anamsema vibaya Sarah.”
“Chester...” Alvin alimtazama Chester.
“Usijali. Tayari nimepiga simu. Kunamtu
atazima kashfa hii kwa kuweka kashfa
zingine za watu mashuhuri." Chester
alikuwa kishafahamu Alvin alitaka nini
toka kwake.
Baada ya kufika kituo cha polisi,
Superintendent Kaboye, aliyekuwa
msimamizi wa kesi hiyo, alikutana na
Alvin binafsi baada ya Alvin
kumwonyesha leseni ya uwakili wake.
“Samahani, Bw. Kimaro. Mshukiwa
bado yuko katikati ya mahojiano.
Hatuwezi kukuruhusu dhamana bado,”
Superintendent Kaboye alisema kwa
sauti nzito.

Alvin alikunja uso na kusema kwa sauti
nzito, “Tayari nimeshawasilisha nyaraka
zinazohusiana. Kwanini siwezi
kumweka dhamana?”
"Kuna pande nyingi sana zinazohusika
katika kesi hii. Inahusiana kwa karibu na
Polisi wa Shirikisho la Kenya pia.
“Si ni mgeni tu huyu aliyeuawa? Kwanini
Polisi wa Shirikisho la Kenya
wanahusika?” Rodney aliuliza bila
furaha.
“Ngoja nikuelezee. Jina la marehemu ni
Hisan Gadaffi. Tayari tumethibitisha na
Interpol kwamba marehemu alikuwa
ametenda mara makosa mengi huko
Somalia, Marekani, Uingereza, Dubai
na hata kwenda jela mara kadhaa.
Baada ya kufika Kenya, tuligundua
kuwa kulikuwa na uhamishaji wa pesa
wa dola milioni 1 kutoka kwa akaunti ya
benki ya Bi. Njau hadi kwa Hisan. Hisan
alikuwa akiishi katika nyumba ya Bi.

Njau pia. Alitembelea kasino za kamari
na baa mara kwa mara.
“Idara ya uchunguzi ya foresinc
ilipofanya uchunguzi wa mwili wa Hisan,
waligundua kwamba alipata uraibu wa
dawa za kulevya hivi majuzi. Kwa
kuchunguza harakati zake ndani na nje
ya baa, tuliongozwa hadi kwa wateja
wachache wa kike wa baa hiyo.
Tuligundua kwamba Hisan mara nyingi
aliwapeleka wanawake tofauti kwenye
nyumba ya Bi Njau, na watatu kati ya
wanawake hao ni waraibu wa dawa za
kulevya pia.”
Macho ya Alvin yalikuwa kama
yanataka kuanguka. "Unasema kwamba
Sarah alimpa Hisan dola milioni 1?"
“Ni kweli kabisa. Dola laki 5 za kwanza
zilitolewa zaidi ya mwezi mmoja uliopita,
na nyingine laki 5 zilitolewa hivi karibuni.
Tumethibitisha kuwa pesa zote

alizotumia Hisan zilitolewa na Bi. Njau.
Kulingana na habari iliyotolewa na jirani
wa karibu, Sarah angeenda kwenye
nyumba yake angalau mara tatu kwa
wiki. Mara nyingi angetumia saa sita
hadi saba huko.
"Hapo awali tulifikiri kwamba Bi Njau
alikuwa akitumia dawa za kulevya
alipokuwa na Hisan, lakini daktari
alimpima tu damu na ripoti ilitoka hasi
kwa dawa. Kuna uwezekano gani
mwingine wakati mwanamke anakaa
katika nyumba moja na mwanamume
kwa muda mrefu kama huo? Tulikagua
kamera za uchunguzi pia... Kulikuwa na
nyakati chache ambapo nguo za Bi.
Njau zilikuwa tofauti alipotoka kwenye
ghorofa na zile alizovaa mwanzo...”
Superintendent Kaboye alimpa Alvin sura ya huruma. “Ndiyo maana watu
wetu hawakuwaruhusu nyinyi wawili
kuendelea na harusi. Ilikuwa kwa ajili

yako.”
Alvin mwili mzima ulimuuma.
Sura ya: 398
Damu iliyokuwa ikitiririka katika mwili wa
Alvin mara moja ikabadilika na kuwa
baridi. Matukio ya Sarah akimsubiri
nyumbani kila siku arudi kutoka kazini
yalizidi kumulika akilini mwake.
Alikumbuka sura yake ya kupendeza, ya
fadhili na safi.
Polisi walimwambia kwamba Sarah
alitumia masaa sita hadi saba katika
ghorofa lake na mwanamume mwingine
mara kadhaa kwa wiki. Mbali na hilo,
nguo zake zilikuwa tofauti alipoingia na
kutoka nje ya nyumba ...
Sarah alisema mtu huyo alikuwa
mpangaji wake. Hata hivyo, ilikuwa ni

lazima kutumia muda mwingi na
mpangaji? Kwanini amdanganye? Kwa
kweli, sababu ilikuwa rahisi. Ni kwamba,
hakumwelewa Sarah vya kutosha.
Alikumbuka akisema kwa ujasiri
kwamba anamwamini. Ghafla, aliona ni
jambo la kuchekesha. Mawazo tu ya
kuwa Sarah amemgusa mtu mchafu
kiasi hicho hapo awali yalimfanya Alvin
ajisikie karaha kabisa kwa wakati huo.
Kwa bahati nzuri, hakuwahi kufanya
ngono na Sarah hapo awali.
Si yeye tu, bali Rodney na Chester wote
walishtuka pia. Hasa Rodney, ambaye
macho yake yalikuwa ya damu, alibisha
waziwazi. “Hilo haliwezekani. Sarah si
mtu wa aina hiyo.”
Superintendent Kaboye alisema, “Siku
zote tunazungumza kulingana na ukweli
tunaposhughulikia kesi. Hivi sasa, Polisi
wa Shirikisho la Kenya wanafuatilia

dawa hizo. Zaidi ya hayo, Hisan alikufa
kutokana na kupigwa risasi. Wakati wa
kifo chake ulikuwa chini ya wiki moja
iliyopita. Tunashuku kuwa Bi. Njau
alikodisha mtu kumuua Hisani ili kuzuia
uhusiano wake usiofaa usifichuliwe
kwani alikuwa karibu kuolewa.”
Mwili wa Rodney ulitetemeka. Alipiga
kelele, “Sarah angewezaje kumuua
mtu? Hawezi hata kuua samaki.”
“Hii ni tuhuma yetu tu. Bado tuko katikati
ya uchunguzi. Ikiwa hakuhusika katika
mauaji hayo, tutamwachilia baada ya
uchunguzi wa Polisi wa Shirikisho la
Kenya kukamilika,” Superintendent
Kaboye alisema.
“Sawa.” Alvin hakujua jinsi gani alitoka
nje ya kituo cha polisi.
Akili yake ilijawa na maneno ya Sarah
aliposema kuwa mtu huyo mgeni
alikuwa mpangaji tu. Ha, mpangaji?

“Alvin, inabidi umuamini Sarah.” Rodney
alimshika bega Alvin. Alisema kwa
hasira, “Siamini kwamba Sarah ni mtu
wa aina hiyo.”
"Rodney, labda sisi sote tumesahau
kuwa Sarah pia ni mwanamke wa
kawaida." Chester aliwasha sigara.
"Wanawake wana mahitaji yao pia, na
Alvin hajawahi kumtosheleza."
Alvin alishangaa. Je, hiyo ilikuwa
sababu? Hata hivyo, alikuwa
amemwambia Sara waziwazi hapo
awali kwamba angeweza kuondoka
ikiwa asingeweza kumvumilia. Yeye
ndiye alisema ni sawa na kwamba
hakujali kuhusu mambo hayo. Je, ni
maneno gani kati ya hayo yalikuwa ya
kweli na yapi yalikuwa ya uwongo?
Alvin ghafla akagundua kuwa huenda
hakuwahi kumuelewa Sarah ipasavyo.
” Bullsh*t! ” Rodney alimkazia macho

Chester na kutema maneno machafu.
“Nilichosema ni ukweli. Vinginevyo,
kwanini kuwe na wanawake
wanaowadanganya waume zao, si
kiakili tu bali kiroho pia? Si kwa sababu
hawawezi kuvumilia upweke?” Chester
alivuta sigara yake kwa muda mrefu.
"Kuhusu dola milioni 1 ambazo Sarah
alimpa Hisan, nadhani alitishiwa."
Hakukuwa na shaka kwamba Chester
ndiye aliyekuwa mtulivu zaidi kati ya
wanaume watatu wakati huo. Alvin naye
akalitambua hilo haraka.
Ikiwa Sarah alitaka tu kufanya mapenzi
na mwanaume huyo, asingempa dola
milioni 1.
"Wacha tuzungumze juu ya suala hili
tena baada ya kutoka nje."
Muda kidogo Alvin alifungua mlango wa
gari na kuingia ndani. Mambo mengi
sana yalitokea siku hiyo. Alitaka tu

kutulia kwa muda na kufikiria
mustakabali wake na wa Sarah.
Dakika chache baadaye, alimpigia simu
Hans. "Ninahitaji habari zote kuhusu
kesi ya Sarah."
Sarah alitumia siku moja na nusu tu
katika kituo cha polisi. Lakini, siku hiyo
moja na nusu alihisi kama mwaka.
Alihojiwa na polisi kila dakika.
“Unajua kuwa Hisan alitumia dawa za
kulevya?
“Je, Hisan alitumia pesa zako kununua
dawa za kulevya? Kwanini ulimpa dola
milioni 1?
"Ulienda kwenye ghorofa mara chache
kila wiki na ukatumia saa nyingi huko.
Nguo zako zilikuwa tofauti ulipotoka na
ulipoingia, na jinsi ulivyotembea
ulionekana kana kwamba unaficha kitu.

Je, unashiriki uhusiano gani na Hisan?
“Kwanini hukutoa taarifa polisi wakati
Hisan alipopotea?
"Unajua kuwa aliingiza wanawake
kwenye ghorofa?
"Je! ulijua tayari kuwa amekufa?"
Sara alijaribu kuwa mtulivu mwanzoni
mwa jambo hilo, lakini maswali yao
makali yalimlazimisha kukataa kila kitu
mwishoni. “Sikufanya hivyo. Hakuna
kilichotokea kati yangu na yeye hata
kidogo.”
“Sarah Langa Njau, tayari tumepata
picha za uchunguzi kutoka maeneo ya
karibu na nyumba yako. Ukiendelea
kukataa kushirikiana nasi na kukataa
kusema lolote, tutakuwa na sababu ya
kushuku kuwa ni wewe uliyemkodisha
mtu kumuua Hisan.”

Polisi walimnyooshea kidole huku
wakisema neno kwa neno, “Lazima
uelewe kwamba wewe ni mtu wa karibu
zaidi wa Hisan. Ni bure hata
ukificha mambo maana Alvin tayari
anajua kila kitu. Alikuja kituo cha polisi
jana jioni. Vinginevyo, unadhani kwa
nini bado hujaachiliwa kwa dhamana
hadi sasa?”
Wakati huo, Sara alihisi tu kama anga
lilikuwa karibu kuanguka. Jambo
ambalo aliogopa zaidi bado lilitokea
mwishoni. Hapana, haukuwa wakati
wake wa kufadhaika. Kwanza,
asingeweza kwenda jela. Isitoshe,
Hisan aliuawa na watu wengine.
Hakuhusika katika jambo lolote baada
ya hapo. Haikuwezekana kwa polisi
kutambua kwamba yeye ndiye
aliyemuua Hisan.
Baada ya kukaa kimya kwa zaidi ya

dakika kumi, macho ya Sarah yakawa
mekundu. Alianza kulia ghafla. "Sikuwa
na nia ya kuficha chochote ..."
Saa moja asubuhi ya siku iliyofuata,
Sarah aliachiliwa kwa dhamana. Bado
alikuwa amevaa mavazi ya harusi
kutoka jana yake. Hata hivyo, baada ya
kukaa muda mwingi katika kituo cha
polisi, vazi jeupe lilikuwa limebadilika
kuwa na rangi isiyoeleweka. Urembo
wake pia ulichafuliwa. Alionekana kama
mzimu wa kike.
Alvin alikuwa akisubiri nje. Baada ya
kumuona, alama ya kushangaa
iliangaza machoni pake. Sarah katika
kumbukumbu zake alikuwa mrembo,
lakini hakujua ni lini alianza kumuona
wakuchukiza.
"Alvinic, Alvinic." Sarah alipomwona,
machozi yalimtoka. Alinyanyua gauni
lake na kumkimbilia huku

akijikwaa.Alitaka kujirusha kwenye
kumbatio lake, lakini, Alvin alimkwepa
haraka. Sarah alimuangalia kwa sura
tupu. Maumivu, majuto, na maumivu
yalimwangazia macho yake.
“Alvinic, sikukudanganya makusudi.
Nililazimika kufanya hivyo. Mtu huyo
alikuwa mmoja wa wahalifu walioniteka
nyara huko Somalia. Unapaswa kujua
jinsi tukio hilo lilivyokuwa la uchungu
kwangu. Mimi si msafi tena, lakini mtu
huyo alionekana tena kama pepo.
Alisema alikuwa na picha na video
zisizofaa za maisha yangu ya zamani.
Sikuwa na chaguo. Niliogopa kwamba
utanichukia ikiwa utagundua, basi
nikampa pesa. Nilimpa dola milioni 1
lakini yeye hakuridhika. Alitaka nifanye
naye ngono.” Sarah aliinama chini huku
akilia kwa uchungu. “Nilihisi
kuchukizwa. Kila alipokuwa akinigusa,
nilihisi kuchukizwa sana hivi kwamba
nilitaka hata kujiua. Alvinic, nilifanya

makosa. Nimekukosea, lakini haikuwa
makusudi. Nakupenda. Ulikuwa tayari
umechukizwa na mimi hivi kwamba
ungenikataa kila nilipokugusa. Niliogopa
kwamba ungenichukia hata zaidi ikiwa
ungeona picha hizo.”
"Simama." Alvin alinyoosha mikono
yake kumsaidia kuinuka. Sarah
akajitupa kwenye kumbatio lake. Alilia
huku akimkumbatia. “Alvinic, usiniache.
Nitakufa bila wewe.”
Mwili wa Alvin ukakakamaa. Kwa kweli,
polisi walikuwa tayari wamemwambia
kuhusu mambo haya kabla ya kumtoa
gerezani. Bado alikuwa amemlaumu
Sarah kwa ujinga wake hapo awali.
Alipaswa kumwambia kwamba kuna
mtu anayemtishia.
Hata hivyo kilio cha Sarah kilimfanya
aelewe kuwa huenda suala hilo
lilitokana na kukataa kumgusa mara

kwa mara na kumfanya azidi
kutojiamini. Hakumlaumu sana tena,
lakini bado alijisikia vibaya.
“Sarah tulia. Hebu turudi nyumbani
kwanza.” Alvin alimsaidia kuingia
kwenye gari. Hans alikuwa mbele
akiendesha gari.
Sura ya: 399
Katika safari nzima Sarah aliuegemeza
mwili wake kwenye kifua cha Alvin.
Aliendelea kueleza, “Alvinic, Hisan
amekufa sasa. Sitakukosea kuanzia
sasa. Hebu tufanye kama ngoma droo,
sawa? Hukufanya mapenzi na Lisa
kitambo pia? Ninajua yote juu yake.
Ulikaa kwa siku mbili nyumbani kwake.
Alvin alicheka kwa uchungu moyoni
mwake. Alisema anampenda Sarah,
lakini alifanya ngono na Lisa. Kwa
upande mwingine, Sarah alisema

alimpenda kwa zaidi ya miaka kumi,
lakini bado alikuwa akifanya mapenzi na
mwanamume mwingine kabla ya ndoa
yao.
Hiyo ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza
kupoteza uhusiano wao.
Je, kweli angeweza kuendelea kuwa
pamoja na Sara? Je, uhusiano kama
huo haukuwa mchafu?
"Alvinic, sema kitu. Ninakuomba, sema
tu kitu. Unanitia hofu.” Sarah alianza
kulia tena huku akiwa hajielewi.
“Sarah, nijibu kwa umakini. Je, una
uhusiano wowote na kifo cha Hisan?”
Macho makali ya Alvin yalimtazama.
Mtazamo wake ulionekana kama
anataka kumchoma mtu.
Sarah alitetemeka. Alisema, “Hisan
alikufa kwa kupigwa risasi. Ningempata
wapi muuaji ambaye angeweza kufanya
kitu kama hicho? Ningekuwa na uwezo

huo, ningekuwa nimeshughulika naye
zamani sana. Nisingeruhusu kuendelea
kutishwa na Hisan.”
Alvin alibana midomo yake kwa ukimya.
Hakusema neno. Sarah aliendelea
kusema, “Hisan alifanya mambo mengi
mabaya nje ya nchi. Baada ya kuja
Nairobi, aliendelea kucheza kamari na
kutumia dawa za kulevya. Alikuwa na
maadui wengi sana.”
“Inatosha, nimekuelewa.” Hatimaye
Alvin alisema kitu. Baada ya kuongea,
aligeuza kichwa chake na kutazama nje
ya dirisha.
Sarah alitazama wasifu wake mzuri wa
pembeni. Akashusha pumzi ya raha
ndani kwa ndani. Hata hivyo, bado
alikuwa na mashaka mengi moyoni
mwake. Nani aliuchimba mwili wa
Hisan? Ni nani aliyekuwa akimpa wakati
mgumu nyuma ya pazia?

Hakujiamini, lakini kwa bahati nzuri,
Alvin alikuwa amechagua kumwamini.
Baada ya kufika nyumbani, Alvin
alimpeleka ndani. Alipoona masanduku
yake sebuleni, Sarah hakujisikia vizuri.
"Alvinic, tunahamia mahali pengine?"
“Sio wote wawili, ni mimi tu. ” Alvin
alipapasa kichwa chake. Hali ya
kulazimisha maamuzi magumu
iliangaza kwenye macho yake finyu.
“Samahani, Sarah. Nadhani sote
tunahitaji muda wa kutulia.”
Sarah alipigwa na butwaa. Hakuweza
kuamini. Je, Alvin hakuwa ameamua
kuacha kufuatilia jambo hilo? Mbona
aliamua kuondoka ghafla?! Hapana,
asingeweza kumruhusu aondoke.
Sarah akamshika mkono Alvin. “Alvinic,

usiende. Nakuomba. Itachukua nini ili
unisamehe? Kadiri utakavyosema, niko
tayari kufanya lolote.”
“Sarah, usifanye hivi...” Alvin alijaribu
kuusukuma mkono wake mbali.
Hata hivyo, ni kana kwamba Sarah
alikuwa amepagawa. Uso wake ulikuwa
na michirizi ya machozi. "Ikiwa unataka
muda wa kutuliza akili yako, unaweza
kufanya hapahapa. Sitakusumbua.
Alvinic, kila mtu huko nje ananiona
kama mzaha sasa. Ukihama ghafla
hivyo watu hao watanionaje? Watafikiri
kwamba mimi ni mchafu. Sitaweza
kuinua kichwa changu kwa maisha
yangu yote. Kama hunitaki, afadhali
nife! ”
“Sarah, unanitishia?” Sauti ya Alvin
ilitanda kwa hasira ambayo inaweza
kuufanya moyo wa mtu kutetemeka bila
hiari yake.

Sarah aliogopa. Alitikisa kichwa.
"Hapana, Alvinic, kwani hatuwezi tu
kukaa chini na kuzungumza kwa
amani? Tumefahamiana kwa miaka 20.
Tumekuwa na hisia kwa kila mmoja kwa
zaidi ya miaka kumi na tulipitia magumu
mengi pamoja. Kwa kweli haikuwa rahisi
kwetu kufika hapa tulipo leo.”
Alvin alimtazama kwa kuchanganyikiwa.
“Sarah, nimefikiria sana katika siku hizi
mbili. Kwa kweli, sikuwahi kufikiria hata
mara moja kuwa ulikuwa mchafu. Hata
hivyo, ukweli kwamba siwezi kukugusa
umekuwa kizuizi katika mioyo yetu
ambayo hatuwezi kuishinda. Kila
mwanamke ana mahitaji yake ya
msingi, na siwezi kukidhi kwa ajili yako.
Tayari nimekusamehe, lakini siwezi
kujifanya kana kwamba hakuna
kilichowahi kutokea hapo awali.
Unaelewa?"
Kufikiria tu wanawake wengi ambao

Hisan alilala nao na nyakati alizofanya
mapenzi na Sarah zilimfanya Alvin
achukizwe na wazo la kumkumbatia.
Wangewezaje hata kuzungumza juu ya
kuwa pamoja kwa maisha yao yote?
"Unamaanisha nini?" Sarah alifadhaika
na kufedheheka. "Mwishowe, unafikiria
tu kuwa mimi ni mchafu?"
“Sarah si umechoka? Wakati wowote tunapopingana, utaleta jambo hili kila
wakati." Alvin alikuwa na sura ya
uchungu. "Kama ningekuchukia kwa
kuwa mchafu, nisingekuwa na wewe
tangu mwanzo."
“Basi kwanini unaondoka?” Sarah
aliomba kwa huruma, “Alvinic, usiende.
Nitakuambia kila kitu kuanzia sasa.
Sitakuficha chochote, sawa? Sehemu
yangu yoyote ambayo unadhani
haitoshi, nitaibadilisha.”

“Sarah, samahani. Nimechoka sana.”
Alvin alivuta mikono yake. Alichukua tu
masanduku yake, akageuka na kutoka
nje.
Sara alikuwa kwenye hatihati ya
kusambaratika. Alizuia masanduku yake
na kumkataza kuondoka. “Ulisema
unahitaji mapumziko, kwa hivyo nenda
utarudi. Sitakuruhusu kuondosha vitu
vyako. Alvinic, nakubali kwamba
nilikosea, lakini ulilala na Lisa pia.
Ulisaliti hisia zetu hapo awali pia.
Naweza kukusamehe kwa hilo, kwa nini
wewe usinisamehe?! ”
Alvin alipomwona akiwa ameshikilia
masanduku yake, akikataa kumwachia,
alikerwa na kilio chake pia. Kwa hivyo,
aliacha vitu vyake na kuondoka mara
moja. Hakujua ni kwanini yeye na Sara
wamekuwa hivyo.
Katika kumbukumbu zake, kila alipojihisi

mchovu au mpweke, siku zote aliweza
kujihisi kuwa na amani ilimradi tu
amwone Sarah. Hata hivyo, wakati huo
Sara alikuwa kama mlima mkubwa
unaousukuma moyo wake. Kila
alipomkabili, alihisi uchovu usioelezeka.
Wakati Alvin alipotoka kwenye jumba
lake la kifahari, alihisi hatia fulani
moyoni mwake. Wakati huo huo, alihisi
utulivu pia.
Hans aliwasha gari. Alvin aliingia
kwenye gari na kuwasha sigara. Aliuliza
bila shaka, "Hans, mimi ni muhuni
mkubwa?"
“Bwana Kimaro, wewe si muhuni. Wewe
tu... humpendi Bi Njau tena.” Hans
alisema kisha akajiwazia. ‘Uliacha
kumpenda muda mrefu uliopita, lakini ulidanganywa tu na hali ya akili ya Bi.
Njau,'
“Simpendi?” Alvin alitabasamu kwa

uchungu. "Nilikuwa nikifikiria kwamba
nitampenda milele."
"Kuna kizuizi kati yako na Bi. Njau,"
Hans alisema, "Furaha ni kitu muhimu
zaidi wakati watu wawili wana uhusiano.
Lakini sikuwahi kufikiria kuwa ulikuwa
na furaha kila nilipokuona ukitoka
kwenye jumba hilo.”
Alvin alishikwa na butwaa. Je, hakuwa
na furaha? Alipofikiria juu yake,
ilionekana kuwa sahihi. Hakujua ilianza
lini, lakini angependelea kufanya kazi
kwa saa za ziada kwenye kampuni
kuliko kuwahi kurudi nyumbani.
Hans alipoona kwamba Alvin alikuwa
katika butwaa, aliendelea kusema,
“Mbali na hilo... hata ukivumilia jambo
hili, polisi walikuwa wamejitokeza
hadharani kumtoa Bi. Njau siku hiyo.
Watu wengi tayari wamepata habari
hizi. Ikiwa bado utasisitiza kuwa pamoja

na Bi. Njau, haitamkasirisha tu Mzee
Kimaro na Bibi Kimaro tu, lakini watu wa
nje watakudhihaki pia.”
“Usiseme zaidi.” Alvin alikunja ngumi
zake zilizokuwa zimetua kwenye miguu
yake.
Ilikuwa harusi ya karne hiyo, lakini
mwishowe akawa kicheko cha karne.
Sura ya: 400
Baada ya Alvin kuondoka bila kusita,
Sarah alivunja kila kitu alichokikuta pale
nyumbani mithili ya mwendawazimu.
Sehemu nzima ilikuwa imepambwa kwa
maua ya Rose kutokana na harusi. Hata
hivyo, ilikuwa ni kana kwamba maua ya
waridi mekundu yalikuwa yakimdhihaki.
Alipaswa kuwa bibi mdogo wa familia ya
Kimaro sasa, mtu ambaye Kenya nzima
ilimhusudu. Kwanini alianguka kutoka

mbinguni hadi kuzimu mara moja?
Aunty Zara aliyekuwa jikoni aliogopa
sana hata hakuthubutu kutoka nje.
Wakati huo, Maya alikimbilia ndani kwa
hasira. “Tulia Bi Njau. Bwana Mkubwa
ana hasira tu. Atarudi baada ya muda
mfupi.”
"Maya, unafikiri mimi pia ni chukizo?"
Sarah aliuliza huku akilia.
“Hapana, najua hukuwa na chaguo. Bi
Njau, umepitia magumu mengi sana.
Bwana Kimaro hana fununu hata
kidogo.” Maya alikasirika kwamba Alvin
alikuwa hana huruma. Bi Njau ni wazi
alimpenda sana.
"Asante, Maya," Sarah alinong'ona,
"Wewe pekee ndiye kutoka kwa watu
wa Alvin ambaye bado uko upande
wangu sasa. Lazima unisaidie
niendelee kumuangalia. Nina wasiwasi

kwamba Lisa anaweza kuchukua fursa
hii. Bila shaka, kunaweza kuwa na
wanawake wengine pia.”
“Usijali. Nitakusaidia kuendelea
kumuangalia. Nitakuambia ikiwa
chochote kitatokea,” Maya alisema,
akiuma mdomo.
“Sawa, Maya. Sitasahau udada wetu.”
Sarah akamkumbatia.
Baada ya Maya kuondoka, Sarah
alipiga namba ya mtu fulani kwa hasira.
“Si ulisema kwamba ulizika mwili wa
Hisan milimani kusikokuwa na watu?
Kwanini mwili wake uligunduliwa na
polisi kando ya mto?”
“Watu wangu walikuwa wazembe.
Naona walikuwa na mikia ikiwafuatilia
walipozika mwili,” mtu huyo alisema kwa
sauti ya chini.
Sarah alikasirika. “Nilidhani una uwezo

mkubwa sana. Nyie mmeniweka
matatani muda huu. Harusi ilikatishwa,
na mimi na Alvin hatuelewani. Ikiwa
ningejua nyinyi mngekuwa bure,
ningefanya kila kitu mimi mwenyewe
wakati huo."
Mtu wa upande mwingine wa simu
alidhihaki kwa ujeuri, “Sarah Langa
Njau, hukuniambia kwamba mtu huyo
alitumia dawa za kulevya. Hukuniambia
pia kama ulifanya naye ngono hata.
Huwezi kunilaumu kwa matendo yako
machafu. Kama nisingekuwa na
mawazo ya haraka, karibu ningejiingiza
katika matatizo yako. Bado sijamaliza
deni langu na wewe. Kando na hilo,
unapaswa kufikiria kile ambacho bado
unacho ambacho ni muhimu kwangu.
Ukitoka kwa Alvin, wewe si kitu
kwangu.”
Simu ikakatika bila huruma.
Sarah alishangaa. Alishika simu yake

kwa nguvu. Alijua wakati wote kwamba
machoni pa kundi hilo la watu, hakuwa
na jeuri. Kwa hivyo, angeweza tu
kuwashikilia kwa nguvu Alvin, Rodney,
na Chester. Wimbi la hofu lilimkumba.
Akapiga namba ya Rodney.
Nusu saa baadaye, Rodney alikimbia
haraka.Sarah alikuwa tayari ameosha
uso wake na kubadili nguo nyeupe.
Alikaa kwenye sofa sebuleni huku
akinywa mvinyo. Muonekano wake
ulikuwa wa mtu aliyekata tamaa, lakini
ulikuwa na mguso wa usafi pia.
"Sarah, acha pombe." Rodney
alinyakua glasi yake ya divai. Kumuona
mwanamke aliyekuwa akimpenda kwa
siri tangu akiwa mdogo katika hali hiyo
kulimtia uchungu.
"Rodney, hunichukii?" Sarah alitazama
juu kwa macho mekundu. “Huoni kama
ninachukiza?”

Rodney hapo awali alihisi uchungu
kwamba malaika wa moyo wake
alikuwa amelala na mwanamume wa
ajabu. Hata hivyo, akimwangalia akiwa
hivyo, alimuonea huruma ajabu. “Sarah,
ulikuwa mjinga sana. Kwanini
hukutuambia? Tunajua kuhusu mateso
yote uliyopitia wakati huo. Tunaelewa
kuwa ulikuwa mwathirika na hujali hata
kidogo. Ulimdanganya Alvin wakati huu.
Hakuna mwanadamu anayeweza
kustahimili hilo.”
"Niliogopa kwamba nyinyi hamtaweza
kunielewa ikiwa mngeona picha. Nilitaka
tu kuweka sehemu ya mwisho ya
heshima yangu. Sikutarajia kamwe
kwamba ningepoteza heshima yangu
iliyobaki pia.”
Sarah alitabasamu kwa huzuni. "Alvinic
aliondoka, na harusi haiwezi kufanywa
tena. Kila mtu lazima awe
anazungumza kunihusu na kunidharau.
Siwezi kuikubali tena. Nilitamani kufa

wakati ule pia, lakini nilibaki kimya
nilipomfikiria Alvinic. Sikuwahi kujua...
nilipaswa kufa tu wakati huo.” Alichukua
chupa ya mvinyo na kuinywa moja kwa
moja baada ya kusema. “Usinizuie.
Acha nife kwa kunywa tu.”
“Usiwe hivyo. Labda Alvin atakuwa na
hasira kwa muda tu. Mpe muda.”
Rodney alichukua chupa ya mvinyo kwa
nguvu.
Sarah akauma meno yake na kusema,
“Hakika nitamshauri Alvin arudi, lakini
itakuwaje kama hatarudi?” Sarah
alikuwa na sura ya kuchanganyikiwa.
“Nitafikiria kitu. Hata kama hatarudi...
Huna haja ya kuogopa. Nitakuwa
msaada wako zaidi kila wakati, "
Rodney alisema kwa dhamira.
•••
Katika ofisi ya Alvin Kimaro.

Taa zilikuwa zimewaka kwa usiku
mzima, lakini Alvin alikuwa bado
anafanya kazi. Kila mtu katika kampuni
hiyo aligundua kuwa bosi wao amekuwa
mchapa kazi kabisa. Zamani, bado
angerudi nyumbani kupumzika baada
ya kufanya kazi kwa saa za ziada, lakini
sasa, hakurudi nyumbani kabisa.
Alifanya kazi mchana na usiku.
Alvin hakuwa na hisia juu yake. Hata
hivyo, wafanyakazi wa idara ya
sekretarieti ambao walifanya kazi kwa
saa za ziada na kukaa naye usiku
kucha hawakuweza kuvumilia tena.
Walimlilia msaidizi wake, Hans,
amshauri Alvin.
“Bwana Hans, tafadhali mshauri Bwana
Kimaro arudi kupumzika. Hata mtu wa
kawaida hataweza kuvumilia ikiwa hali
hii itaendelea. Tunajua Bwana Kimaro
anapitia magumu ya kutengana na
mkewe, lakini hawezi kutufanya

tuteseke pamoja naye.”
“Hiyo ni kweli. Nina mke wangu na
watoto nyumbani. Watoto wangu
hunipigia simu kila siku kuniambia
wanani’miss.”
Usemi wa Hans ulikuwa wa kusikitisha
sana. "Bwana Kimaro aliachana lini na
mkewe? Ni upuuzi gani wote
mnaozungumza?”
"Bwana Hans, tumesikia yote tayari,"
sekretari alisema kwa sauti ya chini,
"Wakati wa harusi, Bi Njau alichukuliwa
na polisi. Nilisikia kwamba tayari
amepewa dhamana, lakini Bwana Kimaro hakuwahi kutaja chochote
kuhusu kufanya harusi nyingine. Hata
harudi nyumbani sasa. Hii ina maana
kwamba Bi. Njau alikuwa
amemdanganya Bwana Kimaro.”
“Bi Njau alikuwa akiwaza nini? bosi

wetu ni mzuri sana. Alikuwa haridhiki na
nini?”
“Ni kweli, bosi wetu ni mrefu na mwenye
nguvu. Ni wazi kwa mtazamo kwamba
anaweza kudumu kwa muda mrefu
sana. Bado Sarah alishindwa
kuridhika?"
"Labda bosi anaonekana kuwa na
nguvu kwa nje tu?"
Hans, ambaye aliwatazama
wakiendelea kusengenya, alihisi
kukasirika.
Ikiwa wangeendelea hivi, Alvin
ingevuliwa. “Fungeni midomo yenu.
Mnamsengenya bosi wenu kwenye
kampuni? Hamtaki kufanya kazi tena?"
Hans alionya.
Wakati huo, Lea aligonga mlango na
kuingia ndani. "Alvin yuko wapi?"

"Ofisini. ” Hans alimwendea haraka na
kusema, “Makamu Mkurugenzi, lazima
umshawishi Bwana Mkubwa, apumzike
japo kidogo. Amekuwa akifanya kazi
bila kuchoka kwa siku mbili na
hajapumzika.”
Lea alifungua mlango na kuingia ndani,
akifunga mlango nyuma yake.
Alvin aliyekatishwa aliinua macho yake
yenye damu. “Kwanini upo hapa?”
“Hata kama hutaki kurudi nyumbani,
sekretari wako na wasaidizi wako
wengine hawawezi kuendelea kufanya
kazi nawe saa za ziada mchana na
usiku. Ni watu wenye familia.” Lea
akavuta kiti na kuketi. Alishusha pumzi
baada ya kuona sura ya Alvin
iliyochoka. Siku zote alikuwa akifikiri
kwamba Alvin hakuwa kama yeye hata
kidogo, lakini sasa, aligundua kwamba
Alvin alimfuata zaidi. Njia aliyoipitia
ilikuwa sawa kabisa na yake. “Sasa

unapanga kufanya nini na Sarah?”
Alvin akaminya midomo yake
myembamba kimya kimya. Siku hizo,
Sarah alikuwa akimpigia simu mara kwa
mara na kumtumia meseji, lakini
alizipuuza zote.
Lea alikunja uso. “Pamoja na kwamba
sifahamu undani wake, hukuwahi kutaja
kufanya harusi nyingine na Sarah tena,
maana yake walichokisema polisi siku
hiyo kilikuwa sahihi. Sarah alifanya
jambo ambalo lilikuvunja moyo.”
Nitasuluhisha mambo yangu
mwenyewe. Sihitaji uingilie kati.” Uso
mzuri wa Alvin ukawa umejikunja.
“Ikiwa amekukwaza kweli, familia ya
Kimaro haitamkubali kamwe," Lea alisema kwa uthabiti, "Alvin, labda
hukuwahi kumuelewa vyema Sarah
Njau hapo kwanza.”

Ingekuwa zamani, labda Alvin angejibu,
lakini kwa namna fulani, aligundua kuwa
kweli alikubaliana na Lea kwa wakati
huo.
Sarah angewezaje kurudi bila
kuonyesha hata chembe ya hatia baada
ya kulala na Hisan mara nyingi? Hata
alionyesha mapenzi makubwa sana kwa
Alvin.
Je, ni kwa sababu Sara alikuwa hodari
sana katika kuficha mambo yake?
Kama Hisan asingekufa, angeendelea
kumtishia Sarah. Labda baada ya
kuoana, Sara angeendelea kulala naye.
Ikiwa ingekuwa kabla ya ndoa, Alvin
angeweza kuvumilia kwa sababu ya
Lisa, lakini vipi baada ya ndoa yao? Ni
mwanaume gani angeweza kukubali
hilo? Isitoshe, vipi ikiwa Sara angepata
mimba ya mtoto wa mwanamume
huyo? Kadiri alivyozidi kulifikiria, ndivyo
matokeo yalivyokuwa ya kutisha zaidi.

Lea alishusha pumzi ndefu na kusema
kwa uchungu, “Nichukulie tu kwa mfano.
Nilikuwa nikisema kwamba nilimuelewa
Mason na hata nilipigana na wewe kwa
sababu yake, lakini miaka hii, amekuwa
akipunguza zaidi na zaidi kunijali. Je,
amebadilika?
Labda sivyo. Labda siku zote alikuwa
ameuficha huo upande wake. Familia
ya Campos ilihitaji usaidizi na ulinzi wa
familia ya Kimaro, kwa hivyo alinivumilia
na sikutambua kamwe. Nimekuwa naye
kwa zaidi ya miaka 20. Tulikutana chuo
kikuu, lakini nimeanza kumwelewa
polepole mtu huyu nikiwa na umri wa
miaka 50.” Baada ya pause, Lea
aliendelea na sauti yake laini. “Usifikiri
kwamba unamuelewa Sarah kabisa kwa
sababu tu umemjua kwa muda mrefu.
Lazima uelewe kwamba alinaswa na
mwanaume mwingine nje. Kwa
kuongezea, alitoweka nje ya nchi kwa

miaka michache. Watu hubadilika.
Kadiri wanavyopata uzoefu, ndivyo
wanavyobadilika zaidi.”
Alvin akatikisa kichwa. Ndiyo, Sarah
alikuwa ametoweka kwa miaka
michache nje ya nchi.Angewezaje kujua
kama alikuwa amebadilika au la? Lea
hakuweza kuelewa Mason baada ya
miaka 30. Vipi kuhusu yeye? Alimjua
Sarah kwa miaka 20 tu.
“Alvin, wewe si mtu wa kawaida. Wewe
ni kiongozi wa familia ya Kimaro na
unasimama juu ya piramidi. Wengine
watakuwa makini na ndoa yako.
Umeachana mara moja, na hii ilitokea
wakati ulikuwa karibu kuoa kwa mara ya
pili. Itakuwa doa kwenye maisha yako.”
Lea alisimama na kusema kwa uzito,
"Fikiria ipasavyo juu yake." Alimaliza
sentensi yake na kugeuka kuondoka.

LISA INAENDELEA KWENYE KITABU CHA 9
Tunaimani unaendelea kuburufika na mfululiozo wa simulizi yetu pendwa inayokwenda kwa jina la LISA lakini mpaka kufikia hapa tunahitimisha kitabu cha 8 na tukukaribishe katika kitabu cha tisa ambacho kitakujia hivi punde kikubwa ni kusubiri na kuwa mvumilivu.
Ahsante sana
ONYO: Ni marufuku kusambaza, kukopi wala kuuza kazi hii kwani endapo kama tutakubaini basi sheria itachukua mkondo wake (By: Official Dully)
 
LISA KITABU CHA NANE (9) SIMULIZI........................LISA KURASA.................401 – 405
PRESENT: SIMULIZI ZA DULLY

Sura ya: 401
Alvin alikaa peke yake kwenye kiti cha
ofisi kwa muda mrefu hadi mlango
ukagongwa. Kisha, kichwa kidogo cha
Suzie kikaingia kutoka nje. "Anko,
naweza kuingia?"
Ingawa Alvin alikuwa katika hali mbaya,
moyo wake ulibadilika mara moja baada
ya kumuona yule mtoto akiwa makini na
mwenye shauku ya kutaka kuongea
naye.
“Suzie, si ulienda shule ya awali leo?”
Alvin aONA bado amevaa sare
nyekundu ya shule ya awali.
Suzie aliinamisha kichwa chake na
kusema. "Bibi alisema una hali mbaya,
kwa hivyo nimekuja kukufariji."
Moyo wa Alvin ukapata joto ghafla.

Hakutarajia Lea angemjali hata kwa
wakati kama huo.
"Uncle, hii ni kwa ajili yako." Suzie
alikimbia na kupanda kwenye mapaja
yake. Alifungua kiganja chake, akifunua
kipande cha chokoleti ndani yake. "Kila
wakati nikiwa katika huzuni, nitaacha
kulia baada ya kula chokoleti."
Alvin alimtazama na kutabasamu.
Kisha, msichana mdogo alifunua
chokoleti na kuitia kinywani mwake.
Alvin mara chache alikula pipi, lakini
wakati alipouma kipande cha chokoleti,
kilikuwa kitamu.
"Uncle, unajisikia vizuri sasa?" Suzie
alimtazama kwa macho ya kumetameta.
"Vizuri zaidi. Asante, Suzie.”
Akamsugua kichwa kidogo.
“Mmh. Anko, mwili wako... unanuka!”

Suzie alisema ghafla kwa sura ya
kuchukiza.
Alvin aliganda. Hakuwa amelala sana
katika siku mbili zilizopita, hata kuoga.
“Nimekuwa... nimekuwa bize na kazi
siku hizi na kusahau kuoga. Nisubiri
hapa. Nitaenda kuoga mara moja sasa.
” Alvin kwa shida akamuwashia Suzie
TV.
“Sawa.” Suzie aliketi kwenye sofa kwa
utii na kuangalia katuni.
Alvin aliingia kwenye bafu lillilo katika
ofisi yake. Alijiosha kuanzia kichwani
hadi miguuni. Alibadilika na kuvaa
suruali nyeusi na shati jeupe. Alitoka na
mwonekano wa kupendeza na wa
kifahari.
Macho ya Suzie yakaangaza. “Anko
wewe umekuwa mzuri sana. Twende
kwenye miadi.”

Alvin alishindwa kujizuia kucheka.
"Wewe mpuuzi mdogo, unajua hata
miadi ni nini?"
"Niliiona kwenye TV. Watu kwenye TV
huwa wanaenda kwenye miadi." Suzie
alicheka. "Twende kwenye amusement
park. Nataka kwenda kucheza."
“Sawa.” Alvin alikubali bila kufikiria.
Kwa kweli, pia alikuwa ameona kuwa
inachosha sana kufanya kazi mfululizo
kila siku. Hata hivyo, hakutaka kwenda
nje kukabiliana na Rodney na Chester.
Ikiwa asingekuwa Suzie, angependa
kutumia wakati wakati wake peke yake.
Alipoendesha gari kuelekea kwenye
uwanja wa burudani wa Two Rivers
Theme Park, simu ya saa ya Suzie iliita.
Mama yake alikuwa amemnunulia simu
ndogo ya saa ambayo ilikuwa ikipokea

na kupiga simu kutoka kwa Lisa tu.
Sauti ya kupendeza ya kike ilisikika.
“Suzie, nipo getini. Uko wapi?” Ilikuwa
sauti ya Lisa.
Moyo wa Alvin ulirukaruka. Aligeuka
nyuma kumwangalia Suzie na kumuona
akiinamisha kichwa chini kumwambia
kujibu sauti ile kwenye saa yake, “Tupo
kwenye gari. Tutafika hapo sasa hivi.”
Baada ya simu kuisha, Alvin aliuliza
haraka. “Umemwalika Aunty Lisa?”
“Ndiyo.” Suzie alitikisa miguu yake.
“Kwanini hukuniambia mapema?” Alvin
alikasirika.
"Hata Aunty Lisa hajui kama nipo na
wewe, anajua kuwa nipo na baba."
Suzie alitoa ulimi wake nje. “Bibi
alisema mmeachana na Aunty Sara,
kwa hiyo nikamuuliza baba wanaume

wanapaswa kufanya nini
wanapoachana. Baba alisema kuwa
jambo bora kwa mwanaume baada ya
kuachana ni kutafuta mke mwingine.
Mtu mwingine ninayemfahamu ni Aunty
Lisa.”
Alvin alikosa la kusema. Kweli?
Alionekana kwamba machoni pa
wengine alikuwa ameachana? “Um...
kwa hiyo wewe ukamkaribisha Aunty
Lisa na alikubali kirahisi hivyo?”
“Ndiyo.” Suzie aliitikia kwa kichwa. “Kwa
sababu nilimdanganya na kumwambia
nilikuwa na Baba.”
Alvin akaishiwa pozi. Ilibainika kuwa
mwanamke huyo alikubali kwenda
kwenye uwanja wa burudani kwa
sababu tu... ya Jack? Je angemwambia
kwamba alikuwa na yeye angekubali?
Alvin alikasirika kwa siri. Lisa bado
alikuwa naye moyoni.

“Kwa hiyo ungemwambia kuwa upo na
mimi asingekubali?” Alvin aliuliza ghafla.
“Ndiyo.” Suzie alipiga kelele.
“Nilimwambia Aunty Lisa kuwa nataka
unipeleke kwake kwa chakula cha jioni
kwake, lakini akasema nikiwa na wewe
hataniruhusu niende kwake. Alisema
kwamba anakasirika akikutazama tu.”
Mara Alvin alihisi moyo wake ukimuuma
kwa hasira. Je! msichana huyu alikuwa
akijaribu kumfariji au kumkasirisha?
“Kwanini basi unataka nimuoe mtu
anayenichukia?”
“Nilifanya jambo baya?” Suzie aliinua
midomo yake alipoona hasira usoni
mwake. “Basi nitampigia baba simu na
kumwambia aje. Anko, unaweza
kurudi.”
"Uliniita hapa na sasa unaniambia

nirudi?" Alvin alihisi kana kwamba kisu
kilikuwa kikimpasua moyoni. Msichana
huyo alianza kumkera.
“Siwezi kumwambia Aunty Lisa arudi.
Yeye ni mwanamke.” Suzie
alimuangalia bila hatia.
Alvin alikosa la kusema. Msichana huyo
alipokaribia kupiga namba ya Lisa
kwenye saa yake tena, Alvin alitamka,
“Acha, usipige. Tayari nimeshawasha
gari kwa hiyo sitaweza kurudi.”
“Kwa hiyo upo tayari kuchumbiana na
Aunty Lisa?” Uso wa kitoto wa Suzie
ulionyesha dokezo la ucheshi.
“Uchumba gani? Usiseme ujinga.
Ninakusindikiza tu kwenye uwanja wa
burudani."
Safari nzima ikawa ya kimyakimya hadi
wakafika kwenye viwanja vya burudani

vya Two Rivers Theme Park, Limuru
Road jijini Nairobi. Baada ya Alvin
kuufungua mlango na kushuka chini,
alijitazama kwenye kioo cha dirisha.
Kwa bahati nzuri, alikuwa ameoga kabla
ya kutoka nje. Kasoro pekee ni
kwamba, shati lake halikupigwa pasi
ipasavyo.
Alichomekea shati lake kwenye suruali kwa haraka huku akijitazama dirishani.
Kisha akazitazama ndevu zake ambazo
hazikunyolewa. Hakuwa amepumzika
vizuri siku hizi mbili, hivyo miacho yake
yalikuwa yamevimba kidogo pia.
Mlango ukafunguliwa ghafla na Suzie
akatoka akiwa amekunja mikono yake
kiunoni. "Anko, mbona unajitazama
kwenye dirisha?"
“Shati langu lilikuwa limekaa vibaya kwa
hiyo nilikuwa naliweka sawa. ” Alvin
akapunguza sauti yake na kubadilisha

mada. “Angalia, kuna peremende pale.
Nitakununulia moja.”
“Sawa! ” Suzie alikengeushwa kwa
mafanikio.
Dakika tano baadaye, wawili hao
hatimaye walitembea hadi kwenye
mlango wa bustani ya burudani. Kabla
hawajafika, tayari Alvin aliiona sura ya
Lisa pale getini. Alikuwa amevaa jeans
na fulana nyeupe, pamoja na jozi ya
viatu vyeupe. Nywele zake ndefu nyeusi
zilivutwa na kufungwa nyuma kama
mkia wa farasi. Kwa sura yake nzuri,
alionekana mrembo kiasi kwamba Alvin
hakuweza kung'oa macho yake kutoka
kwake.
Hapo hapo, Alvin aONA wanaume
kadhaa wakimtazama. Kijana
aliyefanana na mwanafunzi wa chuo
kikuu alisimama mbele yake ili
kuanzisha mazungumzo. "Dada,

naweza kukuongeza kwenye
WhatsApp?"
Chini ya mwanga wa jua, uso safi wa
kijana huyo ulionekana wenye haya.
Lisa alishtuka. Alikuwa karibu
kutabasamu na kukataa, lakini sauti ya
chini na ya sumaku ilisikika ghafla.
“Mke, samahani kwa kuchelewa.”
Kijana huyo aligeuka nyuma na kuiona sura ya Alvin, nzuri na yenye heshima.
Hakutarajia Lisa angekuwa ameolewa
kwani alionekana mdogo sana. Mtoto
wao pia alikuwa mkubwa. “Mimi...
samahani. Sikujua kama umeolewa.
Samahani kwa kukusumbua." Yule
kijana aligeuka haraka na kukimbia
baada ya kuongea.
Lisa alimkazia macho yule mtu
aliyelaaniwa ambaye alitokea ghafla.
“Mke wako ni nani? Afadhali uangalie
mdomo wako."

"Ndio Anko, tangu lini Aunty Lisa akawa
mke wako?" Suzie aliuliza kwa udadisi
huku akila pipi yake.
“Niliogopa kwamba angedanganywa na
wavulana hao wadogo wa chuo.” Alvin
alionyesha dharau ya ndani kabisa.
“Lisa Jones, una miaka mingapi? Je,
huoni aibu kutabasamu kwa wavulana
wadogo kiasi hicho? Je, unajua maana
ya neno ‘kujiheshimu’? Unataka
kuwabemenda vijana wadogo?”
“Nina umri wa miaka 26. Mvulana huyo
anaweza kuwa na umri wa miaka 20.
Nitambemendaje?” Lisa alimrukia kwa
maneno ya hasira. "Kuna wanawake
wakubwa wanaoolewa na vijana
wadogo kila mahali sasa hivi, pole!"
“Kwa hiyo unatamani kuolewa na kijana
mdogo, sivyo?” Hewa karibu na Alvin
ilikua na joto ghafla.

Lisa alikunja mikono yake na kudharau,
“Kwa hiyo ni sawa kwa mwanamume
mkubwa kuoa binti mdogo na siyo
kinyume chake? Wewe si ni mkubwa kuliko mimi? Ulipokuwa shuleni, hata
sikuwa nimetungwa mimba. Mbegu za
baba yangu zilikuwa bado hata
hazijatarajiwa kukutana na yai la mama
yangu.”
Alvin aliduwaa. "Lisa Jones, afadhali
ufikirie kabla ya kuongea. Kumbuka
kwamba kuna mtoto hapa."
Lisa akabadili mada haraka haraka. “By
the way, mbona upo na Suzie?
Jack yuko wapi?" Lisa alimtazama
ghafla Alvin kwa unyonge.
Sura ya: 402
“Kwa hiyo mimi sijakaribishwa mahali hapa? Au ndo umem’miss Jack kiasi

hicho?" Tabia yake ilimfanya Alvin kuwa na hasira.
“Jack ni mwokozi wangu. Kwa upande wako wewe ni mwanaume ambaye tayari una mwanamke mwingine.” Lisa alidhihaki, “ Ninaogopa kushtakiwa kwa ugoni ikiwa nitapigwa picha kwa bahati mbaya na mapaparazi nikiwa na wewe. Kwani, mradi kuna jambo lolote linalomuumiza mpenzi wako Sarah Njau, hutasita kusukuma lawama kwangu.”
Alvin alihisi huzuni kwa kukosolewa kwake. Alijua kwamba alikuwa amefanya mambo mengi ya kumuumiza kwa sababu ya Sara zamani. "Mimi na Sarah hatutafunga ndoa."
"Unatania?" Lisa aliinua kichwa chake makusudi kwa mshangao. “Si utafanya harusi nyingine? Je! yale ambayo polisi walisema ni kweli? Alifanya hivyo na

mwanamume mwingine - "
"Lisa Jones," Alvin alimkatisha kwa ukali na jeuri. Sauti yake ililipuka kama ngurumo.
Suzie aliogopa sana hata mkono wake ukatetemeka na ile pipi ya bigboom ikaanguka chini. Kisha, akaanza kulia. “Anko unamtisha Aunty!” Alijificha nyuma ya Lisa kwa hofu.
Lisa haraka akamchukua msichana yule mdogo. Alipoona machozi ya Suzie, alimtazama Alvin kwa hasira.” Sarah ndiye aliyekusaliti, mbona unanikaripia mimi tena? Nenda kamkoromee Sarah kama una uthubutu. Unapenda tu kunifokea kila wakati. Potelea mbali. Nitaache na Suzie wangu. Kampani yako haihitajiki.” Kisha, akambeba Suzie hadi kwenye uwanja wa burudani.
Alvin aliyebaki nyuma alikunja ngumi

kwa kuudhika. Alipowatazama wawili hao wakimwacha mbali zaidi na zaidi, miguu yake mirefu ikawafuata kwa haraka. “Suzie ni mwanangu. Hata kama anataka kucheza, atacheza na mimi.”
“Anko sikutaki. Wewe ni mkali sana.” Suzie alimkataa bila huruma.
Alvin alisimama na kusema kwa sauti nyororo, “Suzie, sikumaanisha hivi sasa hivi...”
“Anko, hutakiwi kuniomba mimi msamaha, bali Aunty Lisa,” Suzie alisema kwa uzito.
Alvin alimtazama Lisa lakini alimuona tu akiendelea kusonga mbele. Hakumtilia maanani hata kidogo. Alihisi huzuni.
Suzie alimtazama kwa kumtia moyo. “Mwalimu wangu alisema kwamba

mwanamume wa kweli huomba msamaha anapojua kwamba amekosea.”
Alvin akaishiwa pozi. Alipotazama macho ya mtoto yule asiye na hatia, alihisi kana kwamba asingekuwa mwanamume ikiwa asingeomba msamaha. Alinyamaza kimya na kuushika mkono wa Lisa. Akipunguza sauti yake, alisema, “Samahani. Nimekuwa katika hali mbaya tangu majuzi na nilmekukaripia kwa sauti kubwa sasa hivi. Usiichukulie vibaya.”
Lisa aligeuka kwa hasira kumtazama machoni, lakini Suzie
akawahi akasema, “Aunty Lisa, msamehe tu. Anko pia anatia huruma. Tayari ni mkubwa sana lakini aliachana na mke wake bila hata mtoto. Baba yangu ni mdogo kuliko yeye lakini tayari ana binti mkubwa kama mimi.”

Alvin alionekana kuchomwa vibaya na kisu kisichoonekana. Uso wake mzuri uligeuka na kuwa mbaya kwa huzuni. Ikiwa asingemsukuma Lisa kwa bahati mbaya wakati huo, mapacha wake wangekuwa wakubwa vile vile, sawa? Lakini sasa, hakuweza kuhimili uchungu wake.
Lisa alitazama sura yake iliyojawa majuto na wasiwasi. Alijisikia furaha. "Sawa, sitabishana na wewe kwa vile Suzie amezungumza kwa ajili yako, lakini ikiwa bado unataka kufuatana na sisi, basi kuwa mstaaribu. Hasira zako usizimalizie kwetu." Kisha, akamwongoza Suzie kwenye michezo ya kushangaza.
Alvin aliwafuata wawili hao kwa nyuma. Kwenye michezo yote ya awali Lisa hakumpa nafasi Alvin ya kucheza ya Suzie. Hatimaye, walipoenda kwenye gurudumu la Ferris, Lisa alimruhusu

ampeleke Suzie kwa vile yeye aliogopa urefu.
“Kwanini unaogopa gurudumu la Ferris? Mbona mimi siogopi?" Suzie hakukubali na kumsisitiza Lisa ajiunge. Wote watatu walikaa kwenye kibanda kimoja. Alvin alikaa upande mmoja huku Suzie na Lisa wakikaa upande wa pili.
Ilikuwa sawa mwanzoni, lakini kibanda chao kilipoinuka, miguu ya Lisa ilidhoofika. Alishika nguzo pembeni kwa woga na hakuthubutu kutazama chini. Alvin aliitazama sura yake ya uoga na kuhisi kufurahishwa bila kuelezeka. Alikuwa amemjua kwa muda mrefu, lakini hakujua kamwe kwamba alikuwa akiogopa urefu. Hakuthubutu hata kukaa kwenye gurudumu la Ferris.
Kwa sababu fulani, ghafla alitaka kumtisha. Wakati gurudumu la Ferris lilipofikia kilele chake, alitikisa kibanda

kwa makusudi. Jumba liliyumba polepole, lakini Lisa aliogopa sana hivi kwamba moyo ulimdunda kwa kasi ya ajabu. Mwili mzima ulikuwa ukimtetemeka, lakini hakutaka kumtisha Suzie, akachuchumaa pembeni ya siti na kujikunyata kama mpira. Meno yake yalikuwa yakigongana kwa sababu ya hofu.
Moyo wa Alvin ulijawa na raha kumuona Lisa akiogopa vile. Alinyoosha mkono, akamvuta Lisa mikononi mwake na kumkumbatia kwa nguvu. Joto kali la mwili wake lilimfunika, na kumfanya amtegemee bila kujua. Hakuweza kujizuia kulishika shati lililokuwa kifuani mwake.
Hata hivyo, alipokumbuka kuwa alimtisha, aliinua mkono wake na kukibana kifua chake kwa nguvu. “Alvin Kimaro, wewe ni mkorofi! Kwa nini ulinitisha?”

Alvin alitaka kukasirika, lakini aliposikia sauti nyororo ya mwanamke huyo, hakuweza kukasirika hata kidogo. Alisikia harufu nzuri ya nywele zake na kuukumbatia mwili wake laini, akihisi moyo wake ukijaa hadi ukingoni.
Kisha, sauti ya Suzie iliyokasirika ikasikika. "Hmph, nyinyi wawili mnakumbatiana na kuniacha pembeni?" Lisa aONA haya na kutaka kujitoa kwa Alvin, lakini gurudumu la Ferris bado lilikuwa juu na alizidi kuogopa, kwa hivyo miguu yake ilikuwa dhaifu.
"Endeleeni na mambo yenu, nitajiangalia mwenyewe.” Suzie alichungulia dirishani bila woga.
Lisa aliinamisha macho chini kwa huzuni na aibu. Alvin alitazama chini na kuona kope zake zikicheza mithili ya feni. Takriban dakika tatu baadaye,

kibanda chao kilikuwa hatua chache kutoka chini na mara moja Lisa alijitenga na mikono yake na kuketi kando ya Suzie.
Macho ya Alvin yaliganda kwenye kumbatio lake tupu na akamkumbusha, “Hiyo ilikuwa ni raundi ya kwanza tu. Bado kuna raundi moja zaidi."
“Nashuka. Nyie mnaweza kuendelea. ” Lisa aliogopa sana. Suzie alikuwa mdogo na hakuwa na hofu ya kupanda gurudumu la Ferris, lakini yeye, aliogopa sana.
"Sitaki kukaa hapa tena. Haifurahishi hata kidogo. Nataka kupanda mashua.” Suzie alikuwa tayari ameona kitu cha kuvutia zaidi sehemu nyingine.
Alvin alihuzunika kwa kutoswa, lakini aliweza tu kuwafuata wawili hao nje. Walizunguka kwa muda mrefu kwenye

uwanja huo wa burudani. Hatimaye, waliingia kwenye mgahawa kula.
Baada ya Lisa kuagiza chakula, wote watatu walikaa kwenye meza ya dirishani na kula. Alvin hakupendezwa na vyakula hivyo na alipata chupa ya soda tu kunywa wakati sauti za wanandoa wachanga zilisikika ghafla kutoka upande mwingine.
'Kipapatio hiki cha kuku ni kitamu. nitakupa.” Msichana huyo kwa furaha alichukua kipapatio cha kuku na kukiweka kwenye sahani ya mvulana.
Mvulana huyo alimtazama msichana huyo kwa unyonge. “Sijakuelewa. Unanipa tu vitu ambavyo hutaki kula mwenyewe.”
“Hehe, ni kwa sababu wewe ni mpenzi wangu. Ni jukumu la mpenzi kula kile ambacho mpenzi wake hataki.”

"Woi, ni kazi sana kuwa mpenzi wako." “Hebu jaribu kusema hivyo tena?”
“Nilikuwa natania tu. ” Mvulana huyo alichukua vipande vya kuku na kula kwa huzuni.
Alvin aliganda. Tukio hilo lilimpa hisia alizozizoea, kana kwamba aliwahi kuzipata hapo awali. Ghafla, sauti ya mwanamke ilisikika akilini mwake. ‘Kwa nini huwezi kula nilichokula? Je, ni kwa sababu unanichukia? Au hunipendi tena?’
Hata hivyo, kabla hajafikiria zaidi, kulikuwa na maumivu ya kutoboa kichwani mwake. Soda iliyokuwa mkononi mwake ilianguka chini na kumwagika. Uso wake mzuri ulibadilika kwa maumivu.

Suzie na Lisa walishtuka. Wakamtazama kwa wakati mmoja. “Anko , uko sawa?” Suzie alionekana kuwa na wasiwasi.
“Niko sawa tu. Nitaenda uani kunawa uso wangu. ” Alvin alienda chooni kwa haraka.
Sura ya: 403
Lisa alichanganyikiwa hadi akawageukia wanandoa wale pembeni. Alishtuka na kukumbuka kitu tangu zamani. Yeye na Alvin pia walikumbana na maneno kama hayo hapo awali walipokula kwenye ufukwe wa Coco Beach huko Dar es Salaam.
Akiwa anawaza hayo, ghafla akasikia sauti ya mhudumu. “Bibiye, uko sawa? Mwanamume uliyekuja naye amezimia nje ya mlango wa choo."

Lisa alitazama upande wa bafuni ambapo kundi la watu walikuwa wamekusanyika. Alikimbia na kusukuma umati wa watu, na kumuona Alvin akiwa amepoteza fahamu.
“Alvin... Alvin...” Alimvuta na kuita jina lake kwa muda mrefu, lakini alipokataa kuitika, alipiga simu kuita ambulensi haraka. Muda si mrefu gari la wagonjwa lilifika na kumpeleka Alvin hospitali.
Suzie alionekana kuwa na wasiwasi. "Mama, nini kimetokea kwa baba mchafu? Kwanini alizimia ghafla?”
Lisa alikunja uso. Alishuku kuwa huenda Alvin alikumbuka kitu baada ya kusikia mazungumzo ya wanandoa hao mapema,kwa hiyo kumbukumbu zake zikamrudia kwa nguvu na kukizidia kichwa chake. Lakini, mwanasaikolojia hapo awali alisema kuwa ni 0.1% tu ya watu waliolazwa akili wanaweza

kupona. Wengine wanaweza kupata nafuu lakini wakawa mazuzu.
Wakati huo, mlango wa Emergence Room ulifunguliwa na daktari akatoka. “Bwana Kimaro amenaguka kutokana na uchovu. Inavyoonekana hajalala kwa siku chache. Ninaamini amekaa kwa muda mrefu bila kupumzika, na kusababisha ugonjwa wa neva wa ubongo ambao ulisababisha kuzirai.”
Lisa alikosa la kusema. Mwanzo alifikiri kwamba Alvin alizimia kwa sababu alichochewa na kumbukumbu za zamani. Naam, ilionekana alikuwa amefikiria mbali sana.
Wakati huo, Chester na Rodney pia walifika. Alvin alipopelekwa hospitali, watu waliokuwa kwenye chumba cha dharura walikuwa wamemjulisha Chester. Rodney alikuwa pamoja naye, hivyo wawili hao walifika pamoja.

Hata hivyo, Rodney alipomwona Lisa nje, alipandwa na hasira. "Lisa Jones, kwanini uko hapa? Wewe ni kama mzimu unaomsumbua Alvin. Je, unajaribu kumrejesha Alvin kwako kwa sababu harusi yake na Sarah imeghairiwa kwa muda? Ninakuonya, bora ukae mbali na Alvin.”
“Mbona wewe ni mkali sana?” Suzie alimkazia macho Rodney kwa hasira.
"Watoto wadogo kama wewe wanapaswa kujiepusha na masuala yanayohusu watu wazima.” Rodney alimkazia macho Lisa. "Kuna wanaume wengi chini ya anga, kwanini unamng'ang'ania Alvin tu? Je, huoni aibu kuwa mchepuko?”
"Mchepuko?" Lisa alicheka. “Sawa, nina makosa hata nifanye nini. Sikupaswa kupiga 000 na kumleta Alvin hapa.

Ningemwacha afe badala yake.” “Wewe ndiye ulimleta hapa?”
“Kumbe? Alvin akiamka kumbuka kumwambia anilipie gharama za matibabu. Sina mpango wa kutumia pesa zangu kumtibu mume wa mtu.” Lisa alisema kwa ujeuri na kumbeba Suzie moja kwa moja. Alihisi kwamba IQ yake ingepungua ikiwa angeendelea kuzungumza na Rodney.
“Usidhani sijui unataka Alvin akulipe ili umpigie baadaye. Alvin atafunga ndoa na Sarah, acha kuota!” Rodney alimfokea nyuma yake. Kisha, akatoa simu yake na kutaka kumpigia Sarah.
Chester alichukua simu yake na kumfokea, “Huwezi kumwacha Alvin awe na amani na utulivu? Hukusikia alichosema daktari? Alvin hajalala kwa siku kadhaa na yote ni kwa sababu ya

Sarah. Hajalala vizuri tangu tukio lile na Sarah.”
“Ninamwita Sarah ili amtunze,” Rodney alieleza, “hawawezi kuendelea hivi, inabidi waelewane.”
"Lakini inabidi ungoje hadi Alvin apate nafuu kidogo. Ataumwa na kichwa akimuona tena Sarah sasa hivi.” Chester alikasirika. “Si unajua kwanini hapokei simu zetu tena? Ni kwa sababu hataki kusikia tukizungumza kuhusu Sarah. Mpe muda.” Rodney alikasirika na hakuweza kusema chochote kingine.
Alvin alipoteza fahamu kwa siku nzima kabla ya kuamka. Alipofumbua macho, ni Chester pekee aliyekuwa amekaa wodini. “Rafiki nakuomba upumzike vya kutosha baada ya hapa. Sitaki kuhudhuria mazishi yako ikiwa utakufa ghafla,” Chester alitania.

Alvin alisugua kichwa chake. “Kwanini nipo hapa?” Alikumbuka mara ya mwisho alikuwa na Suzie na Lisa, wakila mgahawani katika bustani ya burudani.
“Haujapumzika kwa siku nyingi, jambo lililopelekea kuzirai kutokana na kushindwa kufanya kazi kwa mishipa ya ubongo. Lisa ndiye aliyekuleta hapa. ” Chester akamtazama pembeni. “Badala ya kusema ulikuwa umezimia, ni bora kusema ulilala kwa sababu ulikuwa umechoka sana. Unafikiri umetengenezwa kwa chuma?”
Alvin alifumba macho yake kimya kimya.
“Sawa, una njaa? Nitampigia Hans— ”
Alvin akamkatisha Chester ghafla. "Nakumbuka ulisema kwamba nilikula Coco Beach na Lisa hapo awali."

"Ndio, mbona unaniuliza ghafla?"
"Je, niliwahi kwenda na mwanamke mwingine yeyote hapo awali?" Alvin aliuliza.
“Ningejuaje?” Chester alihisi kutokuamini. "Lakini sidhani. Kwanini?”
"Si chochote." Alvin, mara moja akaketi. Akatupa shuka la hospitalini na kubadili nguo na viatu. “Nisaidie utaratibu wa kuagwa. Naondoka.”
"Alvin Kimaro." Chester alikasirika sana. "Unaweza kuichukulia afya yako mwenyewe kwa uzito?"
“Sasa sijambo. Niko sawa." Alvin alifungua mlango.
Maya, ambaye alikuwa akingoja mlangoni, mara moja alisema, “Bwana

Mkubwa, unaenda wapi? nitakupeleka.”
“Kwanini uko hapa?” Macho makali ya Alvin yalimpita Maya na kuruka kwa woga.
Maya alikuwa mwanachama wa ONA na jukumu lake lilikuwa kumlinda Sarah. Ni mara chache sana angekuja kumtafuta kama Alvin asingemwita. Alikuwa hapo kwa ajili ya kumtazama tu kwa ajili ya Sara.
“Kazi yako sasa ni kumlinda Sarah. ” Macho meusi ya Alvin yalijaa ukali ghafla. “Maya Chande, wewe ndiye mtu wa karibu zaidi na Sarah. Ina maana, hukumuona kabisa alipoenda kwenye ghorofa kila wiki kumtafuta Hisan?”
Maya alishtuka. “Bwana Mkubwa, kwa kweli sikujua. Ingawa ni jukumu langu kumlinda, yeye ana mambo yake binafsi wakati mwingine na siwezi kumuangalia

kila wakati. Sikujua kama alikuwa akifanya mambo kama hayo. Lakini usijali, katika siku zijazo, nita—”
"Unahitaji tu kumlinda kwa sasa asije akachukua maamuzi magumu sana. Anaweza kuwa na yeyote anayetaka. Huna haja ya kuniambia kuhusu hilo tena.” Kisha, Alvin akageuka na kuondoka.
Maya alipigwa na butwaa. Alimaanisha nini kwa kusema hivyo? Je, alikuwa anaachana na Sarah kistaarabu? Haraka alimfuata, lakini kabla hajamkaribia, Alvin alimtazama kwa ukali. “Hujasikia nilichosema? Watu wa ONA wote wana majukumu yao. Nitakupigia nikikuhitaji. Hakuna haja ya kunilinda.” Alisema na kuondoka bila kuangalia nyuma.
Wakati huo, Maya hakuthubutu kumfuata tena kwani aliogopa kuibua

mashaka yake.
Nusu saa baadaye, gari la Alvin lilikuwa limeegeshwa chini ya ofisi za Mawenzi Investments. Alvin alipokuwa akijiandaa kushuka kwenye gari, ghafla aONA BMW nyeusi ikiwa imeegeshwa kando ya barabara. Muda si muda, Erick alitoka ndani huku akiwa ameshika maua. Alikuwa akipiga simu kwa Lisa.
Uso wa Alvin ulibadilika na kujawa huzuni huku akiufunga mlango kwa nguvu baada ya kutoka kwenye gari. Alichukua hatua kubwa kuelekea kwa yule mtu.
“Sawa, nitakusubiri,” Erick alisema kwa upole huku kivuli kirefu kikimfunika. Akageuka na kuuona uso wa Alvin wa kupendeza. "Bwana Kimaro, habari." Erick alitabasamu kwa umaridadi. Ingawa mara nyingi hakukutana na Alvin, aONAna naye mara chache sana

kwenye karamu mbalimbali za watu mashuhuri alizoalikwa.
Macho makali ya Alvin yalitazama maua ya waridi mkononi mwake. "Hayo ni kwa ajili ya Lisa?"
“Ndiyo, Lisa aliniambia mara ya mwisho kwamba anapenda maua ya waridi— ” Kabla Erick hajamaliza, maua mikononi mwake yalipokonywa kutoka kwake. Alvin alichukua maua na kuyasukuma moja kwa moja kwenye pipa la takataka lililokuwa karibu naye.
"Alvin Kimaro, unafanya nini?" Hasira ilionekana kwenye uso mzuri wa Erick.
"Kaa mbali na Lisa ikiwa unataka familia ya Malugu kuendelea kuwa kwenye ramani." Alvin alimuonya.
“Huna nafasi ya kuingilia mambo yangu na ya Lisa. Najua ni mke wako wa

zamani, lakini nyinyi wawili tayari mmeachana. Huna haki ya kuingilia mambo yake,” Erick alidhihaki.
“Hukunielewa? Usidhani sijui unamfuata Lisa kwa sababu ya utambulisho na hadhi ya familia ya Ngosha. Mwishowe, ni kwa ajili ya familia ya Malugu. Lakini inabidi uelewe, ukiniudhi, nitasema neno moja tu na riziki ya familia yako itakuwa ya shida.” Macho ya Alvin yalikuwa yamejawa na hasira, na sauti yake ya chini ilionyesha kuwa uvumilivu umekwisha.
“Alvin Kimaro, huwezi kumwacha Lisa aende zake? Nani katika mji huu hajui kuwa tayari uko na Sarah Njau? Kama hadhi yako huoni kwamba unajidhalilisha kwa kuendekeza michepuko?” Erick alikuwa kijana asiye na makuu na alikasirishwa na matendo ya Alvin ya dharau.

"Ndio, sina aibu, lakini watu wasio na aibu wanaweza kufanya chochote. Unataka kunijaribu?" Alvin alimtazama kwa macho ya kuchoma.
Erick aliogopa kiasi fulani. Kwa wakuu nchini, Alvin ulikuwa mlima usioweza kupandwa. Akauma meno na kuondoka kwa hasira.
Sura ya: 404
Hata hivyo, baada ya gari hilo kutembea umbali usiozidi mita 200, Erick alimpigia simu Lisa tena. “Lisa, samaki amechukua chambo. Utanishukuruje kwa hili?”
Akiwa amesimama mbele ya dirisha na kutazama chini, Lisa alitabasamu kwa upole. “Nitakuandalia chakula cha jioni siku nyingine.”
“Sihitaji chakula. Unahitaji tu kuja na

muundo wa kipekee wa nyumba yangu mpya.” Erick aliguna.
"Bado una ujasiri wa kuniuliza kuhusu muundo wa nyumba? Kama nisingalikuwa ngao yako, familia yako ingalikulazimisha kwenda kwenye miadi ya uchumba.”
“Usiseme hivyo. Si tulikubaliana?”
“Sawa, nitakupa muundo wako baada ya mwezi mmoja.”
Baada ya Lisa kukata simu, midomo yake ilijikunja kwa kejeli. Siku hizo, Nairobi nzima ilifikiri kwamba Erick alikuwa akitoka na Lisa kimapenzi. Hata hivyo, hakuna aliyejua kwamba Erick na yeye tayari walikuwa wanajuana tangu akiwa huko Marekani. Alikuwa amemuona kwa macho yake Erick akiingia na kutoka katika mahusiano na wanaume kadhaa. Ndiyo, wanaume!

Mwanaume huyo alipenda mahusiano na wanaume wenzake.
Lisa alimtazama Alvin pale chini. Akitazama chini kutoka ghorofa ya 30, umbo la mwanamume huyo lilikuwa ndogo kama mchwa. Hata hivyo, mchwa huyo hatimaye alikuwa amemeza chambo. Lengo la Lisa lilikuwa ni kumuaminisha Alvin kuwa yeye alikuwa anatoka na Erick, na Alvin tayari alikuwa ameshaamini hilo.
‘Alvin Kimaro, nitakupa ladha ya kuhisi jinsi inavyouma kuona mpenzi wako wa zamani akiwa na mwanamume mwingine.' Lisa alijiapia.‘Sarah Njau, nitakupa ladha ya kuhisi jinsi inavyouma kunyang'anywa mpenzi wako.’ Hata kama Alvin alilazwa kiakili, asingemsamehe.
Alvin alisimama chini kwa dakika kumi kabla ya kumuona Lisa akitoka nje ya

jengo hilo akiwa amevalia suti ndogo ya rangi ya chungwa. Nywele zake ndefu zilikusanywa na kubanwa kisogoni, zikifunua hereni ndefu za tassel zilizoning’inia masikioni mwake. Lisa alitazama eneo lile na kwa haraka akamuona Alvin akinyata kuelekea kwake.
“Kwanini uko hapa?” Alimuuliza kwa makusudi.
“Ulikuja kumpokea nani? Erick Malugu?” Alvin alidhihaki, “Lisa Jones, hebu niambie, Erick anapenda wanaume, wewe umempendea nini?”
Macho ya Lisa yalimtoka. Alvin aliwezaje kuyafahamu hayo? Hakuna mtu katika Nairobi ambaye alijua kwamba Erick alipenda wanaume.
Alvin aONA sura ya Lisa iliyoshtuka.Tabasamu likaangaza usoni

mwake. Alikuwa ametupa tu jiwe gizani lakini hakuwa na uhakika kama lingempata, lakini bila kutarajia alimwamini. “Hata hivyo, nasema ukweli. Nakushauri ukae mbali naye,” Alvin aliongeza.
Lisa alimkazia macho na kutoa simu yake ili kumpigia Erick.
Alvin akasema, “Erick tayari ameondoka.”
"Alvin Kimaro, ulimfanya nin?" Lisa alimkazia macho.
"Nilimwambia kuwa aache kukufuata, akaondoka bila neno," Alvin alisema kwa dharau. "Yeye ni mwoga kama panya."
Lisa akaguna. Kama asingemfahamu Erick vizuri, angeamini upuuzi wa Alvin. Mtu huyu alisema uwongo bila kuja na ushahidi kwanza.

Alvin alipoona ameacha kuongea na kumtazama kwa sura yake nzuri, akakohoa kwenye ngumi. “Nilikuja hapa kukushukuru kwa kunipeleka hospitali jana. Kwanini nisikufanyie chakula cha jioni usiku wa leo kama shukrani?”
“Asante, lakini sihitaji. Jana nilikupeleka hospitali kwa wema tu na kuishia kuzomewa na marafiki zako wazuri. Walisema kwamba mimi ni kama mzimu unaokusumbua na kwamba ninachukua fursa hiyo kurudiana pamoja nawe. Niliwaambia wakukumbushe unilipe gharama zangu za matibabu, lakini wakasema nilitaka tu kisingizio cha kukupigia." Lisa aliinua mikono yake kwa ujeuri na kumdhihaki, “Ikiwa nitakubali kwenda kula chakula cha jioni nawe, nitayaumiza masikio yangu kwa kwa maneno yao makali tena.”
“Unamzungumzia Rodney?” Alvin

alikasirika ghafla. Ikiwa sivyo kwa sababu walikuwa marafiki bora kwa miaka mingi, alitaka sana kumpiga ngumi. "Usisikilize upuuzi wake."
“Alvin Kimaro, sijui unataka nini kutoka kwangu.” Lisa alionekana kukasirika. “Kwa sababu yako, huwa nazomewa na wengine. Je, humpendi Sarah Njau? Mbona huwa unakuja kunitafuta? Je, umesahau kwamba kwenye harusi siku chache zilizopita, wewe binafsi ulisema kwamba utafanya harusi nyingine na Sarah baada ya siku chache? Au ni kwa sababu Sarah alifanya jambo ambalo limekuangusha, ulikuja hapa kwangu kwa kupoza machungu yako? Mimi sio kipozeo chako."
Uso mzuri wa Alvin ulijawa na aibu. Kila neno alilosema Lisa lilianguka usoni mwake kama kofi. Kama mwanamume, aONA aibu.

"Alvin Kimaro, acha kuwapa watu matumaini na kuwafanya wakate tamaa." Lisa aligeuka na kuondoka.
Alvin aliganda. Alipomwona Lisa akiondoka, bila fahamu alimshika mkono. “Jana, tulipokuwa tunakula Mgahawani, baadhi ya
kumbukumbu ziliangaza akilini mwangu. Hapo awali... sidhani kama nilikuchukia kiasi hicho.”
Mwili wa Lisa ukawa mgumu. Alikuwa na mashaka hayo jana yake, lakini hakutarajia angekumbuka kitu.
"Haiwezekani mimi na Sarah kuoana tena." Alvin alipoona Lisa amesimama kumsikiliza, aliendelea, "Nimehama kutoka Oasis na kumwacha Sarah peke yake. Sidhani kama nipo tayari kumuoa tena."
"Kwa hiyo unataka kunifanya kama tairi

lako la spea? Unakimbilia kwangu kwa sababu tu mambo yako yameenda vibaya kwa Sarah.” Lisa alitupa mkono wake kwa hasira. "Nadhani ni kwa sababu umegundua kuwa mpenzi wako wa utotoni na penzi lako la kwanza sio safi kama ulivyofikiria, kwa hivyo unajuta. Kwa kuwa hakuna wanawake wengine karibu nawe, ulihisi kuchoka na badala yake ukaja kunisumbua.” Kadiri alivyozidi kuongea ndivyo alivyokuwa na hasira. Macho yake yaliwaka moto wa hasira na machozi.
Moyo wa Alvin uliuma sana. Alifungua kinywa chake kwa shida.“Siyo hivyo.”
"Alvin Kimaro, sitaki kuumizwa na wewe tena." Lisa aligeuka na kuondoka.
Alvin alimfuata Lisa. Alipomwona Lisa akirudi kwa uthabiti, alihisi kwamba ikiwa hakuweka wazi mambo fulani, angeweza kumpoteza milele. “Usiende.

Kwa kweli, nilikupenda tangu zamani. Hii ilikuwa mara ya kwanza kueleza kikamilifu mawazo yake ya kweli.
Lisa akanyamaza, Alvin akashusha sauti yake kwa huzuni. “Lakini sikuweza kusema kwa sababu nimemfahamu Sarah kwa muda mrefu na nina deni kubwa kwake. Nisingeweza kumwangusha, hivyo ningeweza kuchagua tu kuachana nawe. Sielewi kwanini nilibadilisha mawazo yangu pia. Ninapenda tu kutumia wakati wangu na wewe zaidi. Ninapokuona na Jack au Erick, huwan naumia sana.
“Ndio hivyo?" Lisa aligeuza macho yake mekundu kwake na kumtazama kwa tabasamu la kejeli. "Alvin Kimaro, umechanganyikiwa sana na Sarah. Ulisema kwamba unanipenda, lakini inaweza kulinganishwa na hatia uliyo nayo kwa Sara? Wakati mwingine

atakaposema neno dhidi yangu, utaniacha bila huruma tena. Je! kusikia juu ya mvulana ambaye alilia mbwa mwitu na kuwaita wanakijiji kumbe anawadanganya? Na siku alipotokea mbwa mwitu wa kweli hakuna aliyejitokeza kumsaidia kwa sababu wote walijua alikuwa akiwadanganya. Mimi ndiye mwanakijiji katika hadithi hiyo. Sina imani nawe tena.”
"Hapana, ni kweli ... haiwezekani kati yangu na Sarah." Alvin akatikisa kichwa. Baada ya kuzungumza, alihisi utulivu. Alionekana kweli hakumpenda Sara tena. Alikuwa amechoka kila wakati alipokuwa naye. Hata harusi yao ilikuwa imemjaza mfadhaiko.
“Kwa vyovyote vile, sitakuamini. Sitaki kuwa dampo la mafadhaiko yako. Siku mambo yakiwa mazuri kwa Sarah, unaniacha kwa kashfa kama zote. Siku mambo yakikuchachia, unarudi kwangu

ukiwa mpole kama njiwa. Hapana, sitaweza tena. Usinifuate tena.” Lisa alimkazia macho na kuondoka kwa kasi akiwa amevalia viatu vyake virefu. Alionekana kana kwamba anaogopa kwamba angemfuata.
Alvin alikasirika. Tayari alikuwa ameeleza hisia zake za kweli, lakini bila kutarajia, hakuitikiwa vizuri hata kidogo. Labda alikuwa amemuumiza sana hapo awali.
Sura ya: 405
Usiku, Lisa alimwambia Pamela kuhusu hilo wakati wanakula.
"Nini? Alvin Kimaro alikuambia kweli kwamba anakupenda?" Pamela alifurahi sana. “Safi sana! Sasa unaweza kumnyanyasa huyo mhuni hadi kumuua.”

“Siyo rahisi hivyo." Lisa akahema. “Unadharau hisia kati ya Alvin na Sarah. Lazima nichukue hatua moja baada ya nyingine.”
"Hapana, Sarah tayari ametupwa mkono." Pamela alitaka kutapika akiwaza tu. "Hakuna mwanaume ambaye anaweza kukubali hilo."
“Unamdharau Sarah. Hukusikia kuwa alitoka kituo cha polisi siku iliyofuata? Lazima alimwambia Alvin kwamba alilazimishwa na Hisan. Lazima aliondoa hasira ya Alvin. ”
Lisa alisikitika kidogo. Alikuwa ametumia juhudi nyingi kumgundua Hisan, lakini mwishowe, aliishia kufa kwa namna fulani. Hapo awali alitaka Hisan aishi na kumfanya Sarah aingie kwenye vita vikali na Alvin.
"Labda nibadilishe mpango." Wakati

Pamela anakaribia kuuliza swali, ghafla kengele ya mlango ililia. Alitazama tundu la kuchungulia na kuona kwamba ni mwanamume mwenye sura nzuri wa makamo. Alienda kufungua mlango.
“Wewe ni... Bi. Masanja, sivyo?” Mzee yule wa makamo akatabasamu kwa upole. "Mimi ndiye mjakazi mkuu wa familia ya Shangwe. ”
Pamela alijaribu kufunga mlango bila fahamu, lakini jamaa yule alikuwa na haraka na bila kutarajia, papo hapo akawa kishaingia ndani. Kisha, walinzi wawili shupavu wakatokea nyuma yake.
"Mnataka nini?" Pamela alikuwa na hisia mbaya. Je, familia ya Shangwe ilikuwa hapa ili kumsababishia matatizo kwa sababu aliharibu sifa ya Rodney hapo awali?
“Bi. Masanja, usiogope. Hatuna nia

yoyote mbaya. Ni kwamba mzee wa familia yetu anataka kuzungumza nawe.”
“Kunanini cha mimi kuzungumza na mzee wa familia yako? Kuhusu nini? Siko huru. ” Pamela hakuamini kwamba alichosema jamaa yule ni kweli. Alijuta sasa. Hakupaswa kuwaita waandishi wa habari ili kufanya tukio la kumdhalilisha Rodney. Hakuwa na uwezo wa kupigana na familia nzima ya Shangwe.
“Bi. Masanja, usiogope. Kama nilivyoeleza hapo awali, hatuna nia mbaya,” mjakazi alisema kwa uvumilivu.
“Niliharibu sifa ya Rodney Shangwe, najua. Kwa hivyo mtasemaje kuwa hamna nia mbaya na mimi?"
Pamela hakuamini familia hizi hata kidogo. Siku za nyuma, Lisa aliitwa na mzee wa familia ya Kimaro na uso wake

uliishia kuharibika. Alikuwa hajapata hata mpenzi bado. Hakutaka kuharibika sura au kufungiwa kwenye jela ya familia ya Shangwe.
"Ikiwa hautashirikiana nasi kwa hiari, tutalazimika kukupeleka huko kwa nguvu." Mjakazi alipumua kwa kukosa uvumilivu.
Lisa alipoona walinzi wanakaribia kuingia ndani, akasogea. "Pamela, nitaenda nawe."
“Bi. Jones, huyo...” Mjakazi wa Shangwe alikunja uso. Pia alikuwa amesikia habari za Lisa. Alikuwa mrithi wa familia ya Ngosha.
"Ninaamini kuwa familia ya Shangwe ni ya busara. Ikiwa kuna jambo lolote la kusema, tunaweza kulizungumza. Kusema kweli, sitakuwa na raha kumruhusu rafiki yangu aende huko

peke yake.”
"Vizuri sana." Mjakazi akaitikia kwa kichwa. "Twendeni pamoja."
"Lisa, kweli unataka kwenda na mimi?" Pamela alikuwa na wasiwasi. Wawili hao hawaikujua vizuri familia ya Shangwe hata kidogo. Nani alijua kama wangeishia kuingia kwenye tundu la simba?
“Ni sawa. Ninaamini familia ya Shangwe haitafanya mambo kuwa magumu sana kwetu kwa sababu ya baba yangu.” Lisa alikuwa na uhakika na maneno yake.
Hata hivyo baada ya kuingia kwenye gari bila aibu alimtumia Alvin meseji ya kuomba msaada. Hakuwa na chaguo. Ingawa alimchukia, aliamini angekuwa msaada kwao kwa nyakati ngumu, kama yeye anavyokuwaga msaada kwake kwenye nyakati ngumu. Baada

ya yote, kila mtu katika jiji la Nairobi alipaswa kumuonyesha Alvin heshima fulani.
Saa moja baadaye, gari liliingia kwenye jumba la kifahari la familia ya Shangwe. Hali ya majengo ya kifahari ya familia ya Shangwe ilikuwa tofauti na ya Kimaro. Yote yalikuwa ni makazi ya kifahari lakini yenye ladha tofauti. Gharama ya kutunza mti wowote kwenye uwanja wao ingeweza kununua nyumba kubwa huko uswahilini.
Baada ya kupita mlangoni, Pamela alimwona mwanamke mrefu na mwembamba mbele yao akitembea. Mwanamke huyo alitembea kwa kasi sana hivi kwamba Pamela hakuwa na wakati wa kuona wasifu mzuri wa mwanamke huyo, lakini ilitosha kumshangaza.
"Nini tatizo?" Lisa aligeuka nyuma

kumtazama.
Pamela aliushika mkono wake kwa hisia na kunong'ona, "Ulimwona mwanamke huyo sasa hivi? Anaonekana kama... mpenzi wa zamani wa kaka yangu. NiONA picha yake kwenye simu yake hapo awali."
Lisa aliganda. Alimjua Forrest Masanja lakini hakuwa akimfahamu kwa undani. Baada ya yote, Pamela alikuwa amesema kila mara kwamba angemuunganisha Forrest naye. Lakini, Forrest kila wakati alionekana kikauzu zaidi, asiye na tabasamu na asiye na mapenzi, ambayo ilimfanya ahisi kutovutiwa naye. Hakuweza kabisa kuelewana na Forrest.
“Hilo haliwezi kuwa. Sijawahi kusikia kaka yako ana rafiki wa kike.” Lisa alikataa.

“Aliwahi kuwa na mpenzi mara moja tu alipokuwa akisoma nje ya nchi. Sikuwahi kukutana naye hapo awali, lakini nilimwona kwenye picha.” Baada ya Pamela kumaliza kuongea kwa kunong'ona kwa hisia, aligeuka na kumuuliza yule mjakazi, "Bwana, yule mrembo aliyepita sasa hivi ni nani? Yeye ni mrembo sana.”
"Huyo ndiye binti mkubwa zaidi wa familia yetu ya Shangwe."
Mjakazi aliposikia Pamela akimwoongelea mwanamke huyo kwa upendo sana, alivutiwa zaidi.
Akifikiria kwamba Pamela angeweza kuwa bibi wa pili wa familia ya Shangwe katika siku zijazo, mjakazi hakuweza kujizuia lakini kuongeza, "Kwa sasa ni mwenyekiti wa Shangwe Corporation ambayo ni kampuni ya familia, na kwa kawaida ana shughuli nyingi sana."

“Binti mkubwa wa Familia ya Shangwe?” Pamela alipigwa na butwaa kidogo.
Lisa alimtazama kwa tabasamu lisilo wazi. "Ndio, ex wa kaka yako ndiye miss mkubwa zaidi wa familia ya Shangwe."
“Sikuwa nauhkika sana. Labda nilikosea.” Pamela alikosa raha ghafla. Aliamini kwamba kaka yake hakuwa na uwezo huo.
Muda si mrefu, walifika kwenye jumba kuu na kuwaona watu watatu wakiwa wamekaa ndani. Aliyeketi katikati alikuwa ni mzee mwenye nywele nyeupe lakini uso wa fadhili. Pembeni yake alikaa mwanamume wa makamo mwenye uso mzuri na mwanamke wa makamo aliyejipodoa vilivyo. Mwanamke huyo alionekana kufanana kidogo na Rodney, na ilionekana wazi kwa mtazamo kwamba walikuwa wazazi

wa Rodney.
“Babu, Anko, Aunty, habari,” Pamela na Lisa waliwasalimia kwa heshima kwa wakati mmoja.
Mjakazi alieleza kutoka upande, “Huyu ni Bi. Lisa Jones, binti wa Bw. Joel Ngosha. Yeye ni rafiki mzuri wa Bi. Masanja na alikuja kwa sababu alikuwa na wasiwasi.”
Mzee Shangwe aliitikia kwa kichwa. Watu wengi kwenye jamii ya watu mashuhuri walikuwa wakizungumza juu ya Lisa hivi karibuni, na kila mtu alivutiwa na kipaji chake cha kipekee.
Baada ya yote, hakuna mtu wa kawaida ambaye angeweza kuwa mbunifu bora zaidi katika umri mdogo kama huo. Ikiwa Pamela aliweza kuwa na urafiki na mtu kama huyo, ilimaanisha kuwa alikuwa na heshima.

TUKUTANE KURASA 406-410
ONYO: Ni marufuku kusambaza, kukopi wala kuuza kazi hii kwani endapo kama tutakubaini basi sheria itachukua mkondo
wake (By: Official Dully)
 
LISA KITABU CHA NANE (9) SIMULIZI........................LISA KURASA.................406 - 410
PRESENT: SIMULIZI ZA DULLY

Sura ya: 406
Watu wa familia ya Shangwe waliweka macho yao kwa Pamela. Baada ya kwenda nyumbani usiku huo, Pamela alikuwa ameondoa vipodozi na alikuwa amevaa jeans ya kawaida ya denim na fulana.
Hata hivyo, uso wake ulikuwa safi na macho yake yalikuwa safi. Uso wake mzuri ulionekana mwororo. Familia ya Shangwe iliitikia kwa kuridhika.
“Je, kuna kitu unanihitaji kutoka kwangu?" Pamela alihisi wasiwasi akiwatazama. “Naweza kujieleza. Ni Rodney Shangwe ambaye alinisingizia kwa wizi miaka mitatu iliyopita na

kunifanya nishindwe kubaki katika tasnia ya vipodozi nchini. Wakati huu, nimemrudishia tu kwa mabaya aliyonitendea.”
Mzee Shangwe alikoroma kwa ukali. “Je, familia ya Shangwe ni familia ambayo unaweza kushindana nayo? Umeharibu sifa ya Rodney. Mama yake alitaka kumpangia mke hapo awali, lakini sasa, wanawake wote kutoka familia mashuhuri wanamkwepa.”
"Sidhani kama angekubali hata kama mngempangia wanawake wengine." Pamela hakuweza kujizuia kunung'unika. Mtu pekee aliyekuwa akilini mwa Rodney ni Sarah”
“Sijali kuhusu hilo.” Mzee Shangwe

aligonga meza. “Kwa kifupi, watu wanaochafua familia ya Shangwe watalipa gharamai. Kwa sababu yako, familia ya Shangwe inadhihakiwa.”
Mzee Shangwe alifunua sura yake ya heshima. Bila kusema, Pamela aliruka kwa mshtuko, na hata Lisa alikuwa na wasiwasi kidogo.
"Mzee Mshangwe,” Lisa alijikaza na kuingilia ghafla. “Ingawa sijawahi kukutana nawe hapo awali, nilisikia juu ya mihadhara yako mikali juu ya nidhamu unayowapa wazao wako. Siku zote nilifikiri kwamba wewe ni mzee mwenye busara na mwenye usawa, lakini sikutarajia kwamba wewe si tofauti na wale wazee wa familia kubwa ambao huwaonea walio dhaifu.”

Uso wa Jason Shangwe ulibadilika kidogo. “Bi. Jones, tafadhali zingatia maneno yako. Hata babu yako akija, hatathubutu kusema hivyo na baba yangu.”
“Nilichosema ni ukweli. ” Lisa aliinamisha kichwa chini. "Zaidi ya hayo, sababu ya tukio hilo ni kwa sababu Rodney alikuwa amemnyanyasa Pamela kwa kutumia hadhi yake. ”
Mzee Shangwe aONA aibu kwa kukosolewa, lakini kutokana na lengo lake, aliweka sura ya ujasiri kwenye uso wake. Alisema kwa ukali, “Inatosha, usije ukaniita sina akili. Pamela Masanja, ngoja nikuulize.

Unakubali kwamba umeharibu sifa ya Rodney?”
"Ndio, ninakubali ..." Pamela alitikisa kichwa bila kufafanua. “Lakini-”
“Lakini isingekuwa yeye, usingekwenda nje ya nchi mwaka huo na usingekuja kuwa mwanakemia wa vipodozi mwenye kipaji kikubwa kama ulivyo leo,” Mzee Shangwe alimkatiza. "Ni kwa sababu ya unyonge aliokupa ndio ulikufanya kuwa hivi ulivyo leo."
Pamela alipigwa na butwaa. Mzee Shangwe tayari alikuwa mzee sana. Angewezaje kuwa hivyo... bila aibu? "Kwa hivyo, kulingana na wewe, ninapaswa kumshukuru Rodney Shangwe badala yake?" Aliuma

mdomo wake na kuuliza kwa kejeli.
Mzee Shangwe alitikisa mkono wake bila huruma. "Hiyo sio lazima. Lazima tu umlipe fidia Rodney. Kwa kuwa umeharibu sifa yake na kuwafanya wanawake wengine kuogopa kuolewa naye, jitoe kama fidia kwake.”
Pamela alipigwa na butwaa. Mzee Shangwe alikuwa akisema nini? Kwanini hakumuelewa hata kidogo?
Mdomo wa Lisa ulitetemeka. "Ina maana unataka Pamela ... aolewe na Rodney?"
“Hasa.” Mzee Shangwe aliitikia kwa kichwa. “Hatuna chaguo lingine. Mama yake alikuwa amempangia ndoa, lakini yote yaliharibiwa na

yeye.”
Kisha, akamwonyesha binti-mkwe wake kwa siri.
Wendy Karia, mama yake Rodney, alisema bila aibu, “Ndiyo, mwanamke huyo alikuwa mwanamke mzuri sana. Wangeweza kuoana. Lazima umlipe fidia kwa ndoa.”
"Hapana." Pamela alitetemeka huku kichwa chake kikimtingisha kama njuga. “Familia yangu ni maskini sana. Watu kama mimi hawastahili familia ya Shangwe."
Mzee Shangwe alikoroma. “Tayari tumechunguza historia yako. Familia ya Masanja ni moja ya familia tajiri zaidi huko Dar es Salaam. Ingawa hukustahili hapo awali, sifa ya Rodney

si nzuri kwa sasa, kwa hiyo tunaweza kukukubali.”
Pamela alitaka kulia. “Rodney hanipendi, na mimi pia simpendi. Hakuna haja ya kujaribu kitu ambacho kwa macho meupe hakiwezekani.
"Hisia zinaweza kuzaliwa na kukua kwa wakati." Wendy alishawishi.
“Mimi ni mchafu na sistahili kuwa na Rodney. Niliharibiwa na Thomas Njau hapo awali. Kila kitu kilipakiwa mtandaoni wakati huo, kwa hivyo nendeni mkaitazame. Watu wengi wanajua kuhusu hilo.” Pamela alijipaka matope jina lake moja kwa moja.
“Tayari tumechunguza. Hukunajisiwa,” Jason Shangwe

aliongeza.
Pamela, hakuelewa ajitete vipi. Aliuma mdomo na kusema. “Kwa vyovyote vile, sitaolewa na Rodney hata nikifa. Iwapo mnafikiri nimeharibu sifa ya Rodney, jisikieni huru kulipiza kisasi kwangu kwa njia yoyote ile. Ikiwa mnataka niolewe na mtu kama yeye, bora mniambie nife, nitakuwa tayari nife kuliko kuolewa naye. Ni fisadi ambaye ubongo wake huvutwa kirahisi na wanawake wenye sura mbili za kijanja kama Sarah. Nitakuwa mwendawazimu kuolewa naye.”
“Wewe...” Shinikizo la damu la Mzee Shangwe lilipanda.
Kuona hali ya mambo inazidi kuwa

ngumu na tata, Lisa hakuweza kujizuia kuingilia, “Um...Hakuna haja ya kubishana kuhusu hili. Nadhani mnaweza pia kumshawishi Rodney kwanza badala ya kumwomba Pamela amlipe fidia. Bila shaka hata Rodney angechagua kifo badala ya kukubaliana na hili.”
"Tutamfanya akubali," Mzee Shangwe alisema kwa ujasiri.
Lisa naye alikosa la kusema kabisa.
“Lisa twende. Maneno matupu hawataMayaewa. ” Pamela alimshika Lisa na kukaribia kuondoka.
Walinzi kadhaa wakawazuia mara moja. Uso wa Lisa ulibadilika.
Wakati huo, aONA umbo la Alvin refu

na imara likitokezea kwenye jumba. Alikuwa amevaa nguo zilezile za mchana, shati jeusi na suruali nyeusi. Walakini, wakati huo, alionekana kama tofauti.
"Unafanya nini hapa?" Punde, Alvin alienda mlangoni. Akayafagia macho yake meusi na mazito kwa walinzi waliomsimamisha mlangoni.
Walinzi walitambua utambulisho wake na mara moja wakatoa njia kimyakimya.
Alvin akaingia kwa hatua kubwa, macho yake yakatua kwa Lisa aliyekuwa mlangoni. Alipomuona akimtizama kwa macho yake makubwa na yenye kung'aa, hakuweza kujizuia kuwaza ujumbe wa WhatsApp ambao alimtumia akiwa

amepumzika nyumbani kwake.
Lisa alikuwa ametoka tu kumwambia asimfuate mchana, lakini alimtumia ujumbe wa WhatsApp jioni.
Alvin alijifanya kutomuona na akageuka kuwasalimia watu wa familia ya Shangwe. “Babu Derek, kwa nini umewaita hapa?”
Mzee Shangwe alimpa ishara Pamela kwa kidevu chake. “Msichana huyo mwongo aliharibu sifa ya Rodney, kwa hiyo sikuwa na la kufanya. Nina wasiwasi kwamba Rodney hatapata mke, kwa hiyo nataka amuoe.”
Alvin naye alishtushwa na wazo la yule mzee. “Rodney anajua kuhusu hili?”

"Nilimwambia hapo awali." Mzee Shangwe alihema sana. “Alvin, Rodney si kijana tena. Siwezi kumtazama akipoteza maisha yake namna hii.”
Alvin alikabwa kwa muda. Alijua kuwa Rodney alikuwa na hisia na Sarah. "Babu, ni lazima niwalete watu hawa wawili leo, kwa hivyo kuwa na subira, usifanye mambo kuwa magumu."
"Kumbe mlitayarisha mtetezi kabla?" Mzee Shangwe alimkodolea macho Pamela. “Nitakapokuona tena, natumaini utakuwa mke wa mjukuu wangu. Ukikubali Rodney akuoe, nitakupa 10% ya hisa za Shangwe Corporation.”

Pamela alipigwa na butwaa na kutikisa kichwa. "Naweza kupata pesa peke yangu. Kwanini nikubali kushiriki na familia yako Shangwe kwa sababu ya pesa? Sizihitaji.”
Familia ya Shangwe ilishangaa, bila kutarajia Pamela alikataa bila kusita.
"Babu, inaonekana huwezi kumshawishi." Alvin alicheka. Akamshika mkono Lisa na kuondoka zake. Pamela akawafuata
Sura ya: 407
Baada ya kimya cha dakika nzima, Mzee Shangwe alipiga meza kwa furaha. "Anachukulia pesa kama uchafu? Hakika ninamfanya Pamela

Masanja kuwa mke wa mjukuu wangu. Apende asipende.”
Jason alikasirika, lakini Wendy alikuwa makini zaidi. “Alvin alikuwa amemshika Lisa mkono mapema. Hiyo ina maana gani? Je, wanarudiana tena? Si ataomuoa Sara?”
“Hawakuridhia jambo hilo. Nilisikia Sarah alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu mwingine kabla ya harusi yao. Familia ya Kimaro kamwe haina mpango wa kufanya harusi nyingine," Jason alisema.
“Hapana! Iwapo Sarah hataolewa na Alvin, kuna uwezekano mkubwa ataangukia kwa Rodney. Kijana huyo mjinga humlinda Sarah kila wakati. Inabidi tutafute njia ya kumfanya

Sarah aolewe hivi karibuni,” Wendy alisema kwa wasiwasi, “Sitakubali Sarah aolewe na Rodney kamwe.”
Mzee Shangwe na Jason pia walitikisa viichwa. Mwanamke kama Sarah Njau lazima asiingie kwenye familia ya Shangwe.
Muda si mrefu baada ya kutoka nje ya jumba kuu la familia ya Shangwe, Lisa aliutoa mkono wake kwa nguvu kutoka kwa Alvin. Alvin alitazama chini kiganja chake tupu na kumtazama kwa hasira. “Sijala kwa sababu nilikimbilia hapa ili kukuokoa.”
“Kwa hiyo? Kama ulituokoa ni lazima nikuache unishike mkono?” Lisa alimtazama kwa ukali. “Basi

usinisaidie wakati ujao. Zaidi, Pamela atakuwa mke wa rafiki yako mzuri.”
Pamela, ambaye alikuwa akitembea nyuma, alitaka kutapika damu.
Lisa akamgeukia Pamela na kumuuliza. "By the way, unajua 10% ya hisa za Shangwe Corporation zina thamani kiasi gani ?"
“Ningejuaje? Sipendezwi na—”
“Angalau dola milioni 40.” Alvin alidakia
Pamela alihesabu kwa vidole vyake. Ilikuwa pesa ambayo asingeweza kuipata hata kama angefanya kazi kwa maisha yake yote, lakini bado aliipuuza. "Sahau. Hata kama utanipa dola milioni100, siko tayari kuwa na

mpumbavu kama Rodney Shangwe ambaye anajua tu jinsi ya kumlinda b*tch mwenye nyuso mbili kama Sarah Njau.”
Pamela alimtazama Alvin kimakusudi. “Lisa, sitaki kufuata nyayo zako. Ikiwa Rodney ataniambia nipotee na nisipotee, ninaweza kulazwa katika hospitali ya magonjwa ya akili. Sitakuwa na mtu wa kunisaidia kama wewe.”
Alvin aliguna kwa hasira. Kwa kweli alikuwa na hamu ya kumtupa Pamela kwa familia ya Shangwe sasa. Alikuwa tu amefanya upendeleo kidogo, lakini aliharibu kila kitu.
"Haki? Ndiyo maana lazima uwe mwangalifu unapopata mwanaume,”

Lisa alisema kwa kumaanisha. "Hasa wale wanaume ambao hupoteza akili zao wanapokutana na b*tches za nyuso mbili. Inabidi ukae mbali nao.”
Baada ya kutoka nje ya makazi ya Shangwe, Alvin alikemewa sana na wanawake wale wawili. Alijiona kama mtu mwenye akili na mwenye nguvu. Vinginevyo, hangeweza kuongoza KIM International na familia nzima ya KImaro huku akiwa amezungukwa na mbweha, lakini, machoni pa wanawake hao wawili, alikuwa mjinga tu. Ilifanya uso wake mzuri kubadilika.
“BwanaKimaro...” Wakati huo, Hans alisimama mbele ya wale watatu akiwa kwenye sedan. “Umeniita kwa—” "Mrudishe Pamela." Alvin alimkokota Lisa bila neno hadi kwenye gari lake

mwenyewe. Tayari alikuwa amevumilia Pamela kama mtu wa tatu asiyehitajika kwa muda mrefu sana.
"Alvin Kimaro, acha. Ninaishi na Pamela, tunaweza kurudi pamoja." Lisa alirudisha mkono wake kwa nguvu lakini hakuweza kujinasua kutoka kwenye mkono wake. Mwili wake ulibanwa kwenye kiti cha gari na Alvin.
“Hata ukisemaje, nimekuokoa leo, kwa hiyo inabidi uniandalie chakula cha jioni. Nina njaa,” Alvin aliinua uso wake mkali na kusema kwa haki.
Lisa alitazama sura yake iliyodhamiria na alijua kuwa asingeweza kujinasua kutoka kwake, kwa hivyo akafunga mkanda wake bila kupenda. "Unataka

kula nini?"
"Naweza kula chochote ninachotaka?" Macho ya Alvin yakaangaza. Kabla Lisa hajajibu, tayari alikanyaga kanyagio.
Njiani, alipiga simu. "Peleka kilo 10 za nyama ya nguruwe kwenye Makazi ya Sayuni."
Kama ilivyotarajiwa...Lisa alihema sana. Hakika Alvin alikuwa Alvin. Ubabe wake haukubadilika kamwe.
Muda si muda, gari lilisimama nje Zion Residence. Hapo ndipo mahali alipohamia Alvin baada ya kujitenga na Sarah na kumuacha mtaa wa Oasis. Nyumba aliyoishi Alvin ilikuwa ni jengo lenye ghorofa sita. Alvin alikaa

kwenye ghorofa ya juu.
Walipotoka kwenye lifti, Lisa aONA mifuko minne ya nyama imewekwa mlangoni, mara moja kichwa kilimuuma.
Alvin akaingiza neno la siri kwenye mlango huku Lisa akiona na kugeuka na kumwambia, “Umeipata hiyo? Unaweza kuja wakati wowote hata kama sipo."
Lisa alidhihaki, “Kwanini nije hapa? Ili kukupikia? Mimi si yaya wako, na wewe pia hunilipi.”
“Hilo silo nililomaanisha...” Alvin alikosa la kusema na kujihisi hoi.
“Kumbe ulimaanisha nini? Unataka

nije hapa kuoga na kulala nawe?” Lisa alisema bila huruma, "Kwako, hizo ndizo kazi pekee nilizo nazo."
“Sikujua hapo awali. Sitafanya hivyo katika siku zijazo.” Alvin alimtazama kwa macho ya kina.
Lisa angeweza kuteka macho meusi ya mtu huyo na uso mzuri hata akiwa amefumba macho. Aliposikiza sauti yake ya chini na yenye sumaku, moyo wake ulikuwa ukirukaruka kama maharage yanayotokota jikoni.
Alvin akafungua mlango, Lisa akaingia. Iliweza kuonekana kwamba Alvin alikuwa amehamia hapo muda si mrefu. Nyumba nzima ilionekana ukiwa, na ilikuwa wazi kuwa mahali hapo hakuishi mtu kabla. Hakukuwa

na dalili zilizonyesha kuwa jiko lilitumiwa hapo awali.
"Ulihamia mahali hapa kwa siri ili uweze kuingiza wanawake kwa kumzunguka Sarah?" Lisa hakuweza kujizuia kumdhihaki.
“Nilihamia hapa siku chache zilizopita. Sitarudi kwenye jumba la Oasis tena. Nilifikiria kwenda kuishi kwenye jumba la baharini huko Mombasa nikaona ni mbali,” Alvin alieleza kwa subira, “Nataka kula nyama ya nguruwe choma kama ulizomtengenezea Suzie mara ya mwisho.” Alipokuwa akiongea, alileta mifuko minne ya nyama ya nguruwe.
Uso wa Lisa ulitetemeka. "Usinaimbie unataka nitengeneze nyama zote hizi

usiku wa leo?" Ikiwa ndivyo, bila shaka angegeuka na kuondoka mara moja.
Alvin alitazama chini kwa sekunde kadhaa na kutoa mfuko wenye kama kilo nne hivi za nyama. “Pika tu hizi.” Lisa alipigwa butwaa. Jamani! Kuanzia mwanzo hadi mwisho, Alvin alimchukulia tu kama mpishi. Je, alipendana vipi na mwanamume kama yeye hapo awali? Sahau. Angeweza kuvumilia kwa ajili ya mpango wake. Alifumba macho na kuvaa aproni kabla ya kwenda jikoni kupika.
Alvin alikaa sebuleni akitazama TV. Alitazama nyuma mara kwa mara na kuona mtu mwenye shughuli nyingi jikoni. Moyo wake ulihisi joto.

Hapo awali alipokuwa peke yake hapo, alihisi kwamba mahali hapo palikuwa patupu na kwamba kuna kitu kilikosekana. Sasa, akagundua kwamba palikuwa pamekosa mwanamke. Hakuwa na uzoefu wa aina hii ya hisia hata wakati anaishi katika mtaa wa Oasisi. Ingawa Sarah na Aunty Zara walikuwa pale, hakuwahi kuhisi hivi hapo awali.
Lisa alitumia saa moja na nusu kabla ya kumaliza kuandaa nyama. Alikuwa amechoka kiasi kwamba mikono yake ilishika ganzi na tumbo lilikuwa likiunguruma.
Alvin alitazama vyombo vilivyowekwa pale mezani. Kulikuwa na nyama ya nguruwe iliyochomwa, na nyama ya nguruwe rosti, pamoja na

nyama ya nguruwe ya kukaanga. Ndizi zilizochomwa na nyingine za ku-rosti, pamoja na kachumbali.
Alvin alikula kwa kuridhika kwelikweli. Baada ya kula, aliweka iliyobaki kwenye jokofu. Alipogeuka, akamuona Lisa akiwa amekaa akichezea simu yake. Vyombo vilivyokuwa mezani vilikuwa havijaondolewa hata kidogo.
“Vyombo vioshwe...” Aligonga meza na kumkumbusha kwa sauti ya chini.
Lisa aliinua macho kutoka kwenye mchezo wake na kumtazama kwa macho ya makali.
Alvin alieleza, "Hakuna yaya hapa nyumbani, kwa hivyo hakuna mtu wa

kufanya mambo haya."
Lisa alicheka. Historia ilikuwa inajirudia. Alizidi kuhisi kwamba tangu zamani alikuwa mjinga kwa kumpenda. “Alvin Kimaro, kuna faida gani mtu kama wewe kutaka mwanamke? Unapaswa kukaa peke yako maisha yote." Lisa aliinuka moja kwa moja na kuondoka zake. Kumtazama tu kulimtia hasira.
Sura ya: 408
Alvin alipomuona Lisa akifungua mlango na kutaka kuondoka, akasogea na kumshika mkono. “Ikiwa hutaki kuosha vyombo, basi usioshe. Sema tu -"
"Alvin Kimaro, inatosha. Ulituokoa

kutoka kwa familia ya Shangwe usiku wa leo, kwa hiyo nilipika kwa saa mbili na kukulipa kwa fadhila. Isitoshe, nilikuokoa pia jana. Ni kosa langu kuwa mpole.” Lisa alidhihaki, “Usinitafute siku za usoni. Sitaki kukupikia kwa uchungu na kuishia kuwajibika kuosha vyombo na kusafisha baada ya kukupikia pia. Ninapendekeza upige simu namba hii ikiwa unahitaji kitu katika siku zijazo. ” Lisa akatoa simu yake na kuvuta mawasiliano ili amuoneshe.
Alvin aONA kuwa namba hiyo imehifadhiwa kama 'Wakala wa Utunzaji wa Nyumba'. Uso wake mzuri ukasinyaa ghafla.
Lisa alikumbusha kwa dhati, “Usifikiri kwamba watunza nyumba ni

wanawake wakubwa. Kuna wengine ambao ni vijana na hawajaolewa. Unaweza kuchagua yoyote kati yao ukiona anafaa kwako.” Kisha akaufunga mlango na kuondoka zake. Ilikuwa ni kana kwamba ilikuwa inamkera sana kumtazama.
Kifua cha Alvin kilimpanda kwa hasira. Wakati anamfuata, sura yake ilikuwa imetoweka. Aliporudi ndani na kuona meza imejaa vyombo vilivyotumika. Alihisi huzuni. Alikuwa ametoka tu kumtaka aoshe vyombo. Je, kulikuwa na haja ya kuongea mambo mengi hivyo? Ikiwa hakutaka kuosha, basi angesema hivyo tu. Haikuwa kama alikuwa akimlazimisha aoshe vyombo.
Alichukua simu yake na bila fahamu

alitaka kumpigia Chester kwa ushauri, lakini mara akaacha. Chester na Sarah pia walikuwa marafiki. Ikiwa Chester angegundua kuwa Alvin alikuwa na Lisa, bila shaka angeanza kumsumbua tena.
Alifikiria jambo hilo na kuingia mtandaoni kwa jina tofauti ili kuficha utambulisho wake, na kuuliza: [Nilimwalika msichana ninayempenda kupika nyumbani, lakini nilipomwomba aoshe vyombo, alikasirika na kuondoka. Je, ni kosa langu au mwanamke huyo ana akili finyu sana?]
Chini ya nusu saa baada ya kuichapisha, sehemu ya maoni ililipuka.

[Oh Mungu wangu, siwezi kuamini kwamba kuna mtu aliuliza swali kama hili. Mwanamke huyo atakuwa na bahati mbaya kiasi gani kupendwa na mwanamume kama huyu?]
[Una ujasiri mwingi wa kuuliza ikiwa mwanamke huyo ana mawazo finyu! Wewe umeyapima mawazo yako na kyaona ni finyu kiasi gani?]
[Rafiki, kama mwanamume, ninakuambia hili kwa fadhili kwa ujasiri: Hutaweza kupata rafiki wa kike kama huyu.]
[Nadhani hupaswi kupata rafiki wa kike. Pata tu mfanyakazi wa nyumbani.]
[Kama ningekuwa mwanamke huyo, si

tu ningekimbia, ningekublock pia.]
Alvin alikasirika sana alihisi kana kwamba anakaribia kulipuka. Wanamtandao hawa walikuwa wamerukwa na akili. Walimaanisha nini kusema alikuwa na mawazo finyu? Walimaanisha nini
kusema asingeweza kupata rafiki wa kike? Siku zote alikuwa akifuatiliwa na kila aina ya wanawake.
Alikasirika na kufuta chapisho hilo. Alijilaumu kwa kuuliza swali lisilo na maana kama hilo mtandaoni.
Baada ya kufuta chapisho hilo aliitafuta namba ya Lisa na kumpigia. Hata hivyo, kilichomjibu ni sauti ya kike ya kiotomatiki ikisema, "Namba ambayo umepiga haipatikani kwa sasa." Kisha akajaribu tena dakika

moja baadaye lakini akapata jibu lile lile. Dakika tano baadaye, bado ilikuwa vile vile.
Nusu saa baadaye, alikuwa na uhakika kwamba kweli alikuwa amechezea block. F*ck.
•••
Baada ya Lisa kurudi nyumbani kwake, Karen Estate, Pamela, ambaye alikuwa ametoka kuoga, mara moja alikimbia na kumkonyeza macho. "Hebu niangalie kama nguo zako ziko sawa. Halo, nguo zako zimekunjamana na nywele zako zimetibuka sana. Unaonekana umechoka pia. Je, nyinyi wawili...” Pamela alitabasamu kiutata.
Lisa alifuta macho yake yenye usingizi. “Ondoa mawazo hayo machafu. Nilikwenda kwake na

kumpikia kwa saa mbili. Nina mikwaruzo kwenye mikono yangu kutokana na kukata nyama nyingi sana.”
Pamela kimya aliitazama mikono yake yenye rangi nyekundu na akakosa la kusema.
Lisa alionekana kama anataka kulia na akalalamika, "Kilo 10 za nyama. Nilizikatakata kwa muda mwingi kabla ya kumwekea kwenye friji. Kisha, nilimpikia nyama ya nguruwe iliyochomwa, rosti, nyama ya nguruwe kukaanga, ndizi, kachumbari... Nilikuwa nimemaliza kula akaniuliza kwanini siendi kuosha vyombo. Mimi...?!” Alikunywa glasi kubwa ya maji kwa hasira. "Hivi, unaweza kuamini kwamba sikunywa hata glasi

ya maji nyumbani kwke?"
Pamela akampiga bega kwa huruma. "Ulikuwa kipofu kiasi gani kumpenda hapo awali?"
“Unajua kwamba mimi pia ni kipofu?” Lisa alitazama juu na
kuhema. “Niliblock namba yake mara tu nilipotoka. Inatia hasira kiasi gani.”
"Umefanya vizuri. Lazima uwe umechoka. Nenda kaoge kisha ulale.” Pamela alimfariji. "Ninaamini kwamba baada ya tukio hili, moyo wako utakuwa mtulivu na hatakusumbua tena."
•••
Kesho yake asubuhi mida ya saa mbili, Alvin alipotoka kwenye lifti kuingia ofisini kwake, alimsikia Hans

akiongea na wanawake kadhaa katika idara ya katibu kwenye korido.
"Hans, niONA mwanamume mcheshi sana kwenye group la facebook jana akiuliza swali mtandaoni jana. Mwanamume huyo aliuliza, 'Nilimwalika msichana ninayependa kupika nyumbani, lakini nilipomwomba aoshe vyombo, alikasirika na kuondoka. Je, ni kosa langu au mwanamke huyo ana mawazo finyu sana?' Mungu wangu, kweli dunia ni kubwa. Kuna kila aina ya wanaume wa ajabu huko nje."
Hans alicheka. “Huyo mtu ana kichaa. Alimwalika mwanamke nyumbani pake, akamwomba ampikie, akampikia, kisha akamtaka aoshe vyombo pia? Msumbufu wa namna hii

atakimbiwa na wanawake wote.”
"Haki? Hata alikuwa na ujasiri wa kuuliza swali mtandaoni! Inatosha kuwa hajitambui, lakini alikuwa na jeuri ya kumtuhumu mwanamke huyo kuwa na mawazo finyu sana.”
"Kuna wanaume wa ajabu zaidi siku hizi. Ni bora kukaa mbali na watu kama hao ikiwa utakutana nao."
Wakati fulani, kila mtu ghafla alihisi baridi ikitoka nyuma yao. Ilikuwa karibu kiangazi, lakini waONA kana kwamba kulikuwa na baridi zaidi kuliko majira ya baridi.
Mtu mmoja aliita, "Bwana Kimaro." Walipotazama nyuma, waONA sura nzuri ya Alvin lakini yenye huzuni.

“Bwana Mkubwa...” Hans alieleza kwa woga, “Saa za kazi hazijaanza, kwa hivyo sisi...”
"Hans. ” Alvin alimwangalia kwa macho ya kifo. “Ingia ndani.” Kisha, Alvin akaingia ofisini.
Hans alimfuata kwa hofu na kufunga mlango. “Bwana Kimaro, samahani. Sitawahi kuzungumza tena na wengine kwenye korido...”
“Hans, mtu mwendawazimu mliyekuwa mkimjadili hapo awali ni mimi.” Alvin akavua koti lake na kulitupia kwenye kiti chake cha ngozi. Macho yake yalikuwa ya huzuni. “Mimi ndiye niliyeuliza swali hilo mtandaoni. Mwanamume yule yule

uliyesema hatapata rafiki wa kike maishani mwake.”
Hans alishtuka. Alikuwa na hamu ya kujiua papo hapo. Ni maneno gani ya kuudhi aliyoyasema hapo awali? Hakuweza kukumbuka hata kidogo. “Bwana Mkubwa, samahani. Sikujua, ” Hans aligugumia, “Ni... nilifikiri ni mhuni tu na mtu asiyejitambua wa kawaida. Bila shaka... kwa mwanamume mtanashati, tajiri, na mashuhuri kama wewe, kuna wanawake wengi walio tayari kukupikia na kukuoshea vyombo. Haiwezekani kwako kukosa rafiki wa kike.”
Alvin alikoroma kwa hasira. "Hivyo sivyo nilivyokusikia ukisema."

Moyo wa Hans uliruka hadi kifuani mwake. Hakutaka kitu zaidi ya kutoweka. Hakuweza kuelewa. Si yeye peke yake aliyekuwa akipiga porojo. Mbona bosi alikuwa anamsumbua yeye tu?
"Basi nijibu swali hili." Alvin aligonga meza na kusema kwa sauti kubwa, “Lisa... Kwanini alikasirika na kuondoka? Je, kweli nilifanya kitu kibaya? Nifanye nini sasa?”
"Bwana Mkubwa, kwa heshima zote, kwa sasa ... kwanini usimchumbie tu kama bado unampenda?" Hans aliuliza kwa makini.
Alvin alimdhihaki na kumtazama. “Ni lazima nimchumbie? Unapaswa kumjua Lisa vizuri kuliko mtu yeyote.

Amenipenda kwa muda mrefu, lakini nilimuumiza siku za nyuma na kumfanya akose raha. Hata hivyo, ninajishusha kwa ajili yake.”
Sura ya: 409
Hans alicheka sana. Alvin alikuwa bosi wake wa muda mrefu, alimjua hakuwa na uzoefu kwa wanawake hivyo akamshauri kwa heshima. "Bwana Mkubwa, kama nyinyi wawili mnapendana au la, siwezi kujua. Ninachojua ni kwamba, wanawake wanapenda kudekezwa. Unawezaje kumwita mwanamke nyumbani na kumwomba akupikie, kisha, ukamwomba aoshe vyombo? Unatafuta mwanamke, si mfanyakazi wa nyumbani. Lisa ana majukumu makubwa ya kuongoza kampuni kama

wewe, ni heshima kubwa hata hivyo kutenga muda wake kukupikia. Hukupaswa kumwambia pia akuoshee vyombo. Kwa jinsi unavyomchulia, inamfanya tu Bi Jones ajisikie kuwa yuko nawe kama yaya wako tu. Mwanamke yeyote atakosa raha.”
Sarah hayuko hivyo. ” Alvin alishindwa kujizuia kusema.
Hans alikosa la kusema. Ikiwa Sara hakuwa hivyo, basi kwanini hakwenda kwa Sara badala yake? Hata hivyo, Hans bado alijifanya kushangaa na kusema, “Je, Bi. Njau amewahi kuosha vyombo hapo awali? Inaonekana ni kawaida Aunty Zara ndiye anayefanya kazi hiyo.”
Alvin alipigwa na butwaa. Ilikuwa

kweli. Ingawa Sarah alipika mara kwa mara, usafi wa vyombo na jiko ulifanywa na Aunty Zara au Maya. Kulikuwa na vijakazi nyumbani kwake wa kufua nguo na kusafisha nyumba.
Hans alipumua. "Bwana Mkubwa, unapaswa kuelewa hili vizuri. Wanawake wanapaswa kudekezwa. Si una vijakazi wengi tu?”
"Lakini napenda vyakula vya kupikwa na Lisa, na hata vyombo vyangu vikisafishwa naye najisikia furaha sana," Alvin alisema kwa kuudhika.
"Basi unaweza kujifunza kuosha vyombo mwenyewe. Atapika, na utaosha vyombo. Kwa hali hiyo unaweza kumfanya avutiwe nawewe bila kulazimika kumkera... Unaweza kujifunza kutokana na jinsi Erick

Malugu anavyomdekeza.”
"Kwanini nijifunze kutoka kwa huyo hayawani?" Alvin alidhihaki kwa dharau, “Erick Malugu, unawezaje kumlinganisha na mimi?”
Kuanzia kichwani hadi miguuni, hakuna kitu ambacho Isaka alikuwa nacho ambacho kililingana naye.
“Nilikosea. Nimeongea sana.” Hans mara moja akajipiga kofi kinywa chake mwenyewe. "Ikilinganishwa na wewe, Erick ni kama uchafu kwenye viatu vyako."
Alvin alishika kalamu yake ya chemchemi kwa hasira. Muda kidogo baadaye, aliiacha na kusema kwa sauti ya ukali, "Nenda ununue maua ya

waridi yaliyojaa gari na uyatume Mawenzi Investiments."
Hans alitokwa na jasho. Mtu huyo alisema tu kwamba hatajifunza kutoka kwa Erick, lakini alisahau maneno yake mwenyewe kwa kufumba na kufumbua. “Ndiyo.” Hans alijibu kwa heshima na akatoka kwenda kununua maua.
Alifurahi sana kuona jinsi Bwana Mkubwa wake na Bi Jones walikuwa wanaendelea. Ingawa hypnosis ya Alvin haikuweza kuondolewa, haikumzuia kumpenda Lisa tena.
•••
Lisa alikuwa amerudi tu ofisini kwake baada ya mkutano na ghafla, akagundua kuwa ofisi ilikuwa imejaa maua ya waridi. Alihisi kama

ameanguka kwenye bahari ya waridi. Mdomo wake ulitetemeka alipogeuka na kumuuliza Amba, msaidizi wake, “Ni nani aliyeleta haya?” Alipozungumza tu, simu yake ikaita. Ilitoka kwa namba isiyojulikana, kwa hivyo aliijibu. Sauti ya chini na ya upole ya Alvin ilisikika. “Umeyapenda maua niliyotuma?”
Lisa alipapasa paji la uso na kumdhihaki, “Mbona umenitumia maua mengi? Unataka nikupikie na kukuoshea vyombo tena?”
“Ni kwa ajili ya kukuomba msamaha,” Alvin alisema kwa sauti ya chini, "Sikupaswa kukuomba kuosha vyombo jana usiku, na sikupaswa kukuomba upike. ”

“Usinidhihaki. Wewe ni Bwana Alvin Kimaro. Kukupikia ni heshima yangu,” Lisa aliuma meno na kusema kwa sauti ya huzuni.
“Nitakupikia usiku wa leo, sawa?" Alvin alibembeleza kwa upole. “Nitaosha vyombo pia."
“Asante, lakini sitaki kula chakula chako. Naogopa utanitilia sumu.” Lisa alikuwa amejaribu kula chakula chake zamani na kilikuwa kibaya sana.
"Basi nitakupeleka ukaangalie filamu."
"Hapana." Lisa alikata simu moja kwa moja. Licha ya kujua kwamba alipaswa kushikamana na mpango wake badala ya kutenda hivi, hakuweza kujizuia kukasirishwa na

tukio hilo la jana yake usiku.
Alipokatiwa simu, Alvin alikasirika sana. Akawasha laptop yake lakini akashindwa kuona neno lolote lililoonyeshwa pale. Ilipofika saa tisa alasiri, aliwasha gari na kuelekea shule ya awali.
Mlinzi wa getini alimfahamu, hivyo akaruhusiwa kwenda kwenye mlango wa darasa hilo. Watoto walikuwa wameamka tu kutoka kwenye usingizi wao wa machana na walikuwa wakinywa juisi ya matunda. Suzie alikuwa ameketi kando ya mvulana aliyevalia shati jeupe. Alikuwa akisoma kitabu huku akiwa ameinamisha kichwa chake chini. Alichukua juisi yake kwa siri na kuinywa.

Kijana aliinua kichwa chake. Baada ya hapo, alikunja uso wake na kumkazia macho Suzie kama onyo. Suzie alitoa ulimi wake nje kwa njia ya ukorofi sana. Alipomwona Alvin kupitia dirishani, alishtuka sana hivi kwamba akakaribia kuuma ulimi wake.
Lucas alitazama upande uleule na kutetemeka sana. Jamani! Alvin alikuwa ameona uso wake. Alikumbuka kuwa mama yake alimwambia kwamba anafanana naye sana.
Wimbi la hisia lilimkumba Alvin aliyekuwa amesimama nje. Alipomwona mvulana huyo kando ya Suzie muda huo, aONA sura yake si ngeni kabisa. Baada ya kumwangalia mara mbili mbili, Alvin aligundua

kuwa sura ya mtoto huyo ilifanana sana na ya Lisa. Kwa kweli, mvulana huyo alikuwa toleo dogo la uso wa Lisa. Tofauti pekee ni kwamba uso wa mtoto huyo ulimfanya aonekane mzuri zaidi.
Suzie na Lucas wakiwa wamekaa pamoja, kila aina ya mawazo ya mshtuko yalimtawala Alvin. Ikiwa mapacha wake wangalkuwai hai, mvulana angefanana na mvulana huyo. Je! kila kitu kinaweza kuwa cha bahati mbaya tu?
"Anko Alvin, kwanini uko hapa?" Kwa wakati huu, Suzie alitoka mbio akiwa na sura isiyopendeza.
“Suzie, ni mvulana gani uliyekuwa unacheza naye sasa hivi?” Alvin

alichuchumaa na kuuliza kwa upole.
"Anaitwa Lucas." Suzie aliinamisha kichwa chake na kuuliza kwa mshangao, “Kwanini unauliza jina lake?”
“Hufikirii kuwa anafanana na Aunty Lisa?” Mikono ya Alvin ilitetemeka bila kujizuia.
"Ndio, ndio maana ninahisi uhusiano naye. Tunacheza pamoja kila wakati, na yeye ni rafiki yangu mkubwa, " Suzie alijibu kwa tabasamu.
Alvin alikodoa macho na kubana midomo yake. "Ingia ndani na uendelee kucheza kwa muda. Nitakuja tena baadaye kukuchukua.”
“Oh, sawa.” Maneno yake yalimtia

wasiwasi Suzie.
Aliporudi, Lucas alimkimbilia na kumuuliza kwa wasiwasi, "Alisema nini?"
"Inaonekana baba yetu mchafu ameanza kukushuku." Suzie alikuwa mwisho wa akili yake. Lucas alikunja uso. "Usiwe na wasiwasi. Mama alipoamua kunileta hapa, nilikuwa tayari nimejitayarisha kwa ajili ya nyakati kama hizi.”
Alvin aliwasiliana kwa haraka na mkuu wa shule na kuuliza maelezo ya Lucas. Jina kamili la Lucas lilikuwa ni Lucas Ngosha. Baba yake alikuwa Sheldon Ngosha, ambapo mama yake alikuwa Sabrina Wanjala. Kwa shida ya Alvin, Lucas alikuwa mdogo kwa

Suzie kwa miezi sita na nusu. Alvin alikunja uso kwa nguvu akishangaa kwanini Lucas anaonekana mkubwa kuliko Suzie na wakati huohuo akiwa mdogo kiumri.
“Ndiyo. Mtoto huyo ni mrefu sana, labda kwa sababu wazazi wake ni warefu. Hali kama hii ni ya kawaida tu kwa watoto." Mkuu wa shule alitabasamu na kusema, “Hapo awali, hatukutaka kumkubali kwa vile ni mdogo sana. Lakini hatimaye, tulimkubali kwa vile wazazi wake wanatoka katika familia ya Ngosha na walivutana nasi.”
"Familia ya Ngosha?" Alvin akajiuliza sana.
Baada ya kutoka nje ya ofisi ya mkuu

wa shule, mara akamuagiza mtu mmoja kutoka ONA kuichunguza familia ya Ngosha.
Sura ya: 410
Punde, alipokea habari fulani. "Bwana Kimaro, kuna mtu anayeitwa Sheldon Ngosha katika familia ya Ngosha. Yeye ni binamu wa Joel. Ingawa ameoa kwa miaka mingi, Sheldon hana mtoto wa kiume. Muda mfupi uliopita, mpenzi wake wa zamani alimletea mvulana wa miaka mitatu.
"Sheldon alisikia kwamba mvulana huyo ni mtoto wake, kwa hivyo akafanya kipimo cha DNA mara moja. Ilithibitisha kuwa Lucas ni mtoto wake wa kumzaa. Sasa, Sheldon na mpenzi wake wanamchukulia Lucas kama

mtoto wao mpendwa. Kwa sababu hiyo, mke wake anakasirika sana hivi kwamba anagombana naye kila mara.”
“Nitumie picha ya Sheldon. Nataka kumtazama.” Alvin aliamuru.
Chini ya dakika moja baada ya kutoa agizo lake, Alvin alipokea picha ya Sheldon. Aligundua kuwa Sheldon na Joel wanafanana kabisa. Kwa kuzingatia kwamba Lisa alifanana na Joel, haikushangaza kwamba Lucas alifanana na Lisa.
Alvin aliwasha sigara na kuhisi kana kwamba mwili wake umeanguka ghafla kutoka angani hadi chini. Kweli, muda si mrefu alikuwa amerukwa na akili. Kwa kweli alishuku kuwa Lucas na Suzie

walikuwa mapacha ambao Lisa alikuwa amebeba ujauzito wao. Hata hivyo aliendelea kuwa na mashaka mengi moyoni mwake. Jack alipata mtoto ghafla nje ya ndoa na mtoto huyo alifanana kabisa na Alvin. Muda huo huo, Sheldon naye alipata mtoto wa kiume nje ya ndoa mwenye umri sawa na wa mtoto wa Jack, na mtoto huyo alifanana kabisa na Lisa. Huu unaweza kuwa mfanano wa habati mbaya kweli? Tena isitoshe watoto hao walionekana kujuana walipokuwa shuleni, na walicheza pamoja muda wote.
Labda Lisa alimhadaa kuhusu mimba wakati huo? Inawezekana Jack aliwahonga wahudumu wa hospitali hiyo ili wamwambie kuwa mimba yake imeharibika na baadaye Lisa

amekufa. Hata hivyo, alipokumbuka kiasi cha damu alichopoteza Lisa alipompeleka hospitali wakati huo, hakuwa na imani kama mapacha hao wangeweza kuwa hai. Alijiona kana kwamba ni mwendawazimu.
“Anko Alvin, Bibi alisema unapaswa kuvuta sigara kidogo.
Uvutaji sigara haufai kwa mwili.” Suzie aliyekuwa amebeba begi lake la shule akatokea mbele yake. Huku mwanga wa jua ukiangaza kwenye mashavu yake ya kitoto, alionekana kama mwanasesere mzuri.
Licha ya kuhisi maumivu makali ndani yake, alilazimisha tabasamu. “Mbona umetoka?”
“Madarasa yanakaribia kuisha.

Mwalimu wangu aliniruhusu nitoke kwani tayari unanisubiri nje.” Suzie aliinamisha kichwa chake na kuuliza, “Anko Alvin, unaonekana... una huzuni kidogo.”
“Mm. Nilikuwa nikifikiria jambo fulani, jambo ambalo... siwezi kamwe kujisamehe.” Alvin aliinama na kumgusa kichwa. "Hebu tumwombe Aunty Lisa ajiunge nasi kwa sinema, sawa?"
“Huh?” Suzie aliduwaa kwa muda. “Lakini... Lakini mimi bado ni mdogo. Ninaweza kutazama sinema za katuni pekee
" Wacha tuangalie sinema za katuni basi," Alvin alijibu kwa kusita.

“Ndiyo. Hebu tuangalie Kung Fu Panda.”
Muda mfupi baadaye, Alvin aliwasili Mawenzi Investments. Suzie kisha akampigia simu Lisa. “Anti Lisa nakusubiri hapa chini na baba. Shuka sasa, sawa?”
Dakika Lisa aliposikia Suzie akimwita 'Aunty Lisa', alikuwa na uhakika kwamba si Jack aliyekuwa naye. Suzie alipokuwa na Jack, kila mara alikuwa akimwita Lisa 'Mama'. Sasa, msichana huyu mdogo alikuwa bingwa katika kudanganya watu. Siku zote aliwapendelea wageni kuliko mama yake mwenyewe.
Lisa alipumua na kujibu, "Sawa. nashuka.”

Alvin aliyekuwa amekaa kwenye kiti cha dereva alionekana kusononeka. Alvin alijua kuwa Lisa alishuka moja kwa moja bila kuuliza swali kwa sababu alidhani anaenda kukutana na Jack. Alitaka Lisa aachane na tabia hizi mbaya siku moja. Alitaka kumjulisha kuwa alihitaji kujiweka mbali na shemeji yake.
Muda mfupi baadaye, Lisa akatokea mbele ya Alvin na Suzie. Suzie aliteremsha dirisha na kumpungia mkono kwa furaha. Mara Lisa akatembea kuelekea kwenye gari. Hazikupita sekunde, Alvin akatoka na kufungua mlango wa nyuma. "Tutafuatana na Suzie kutazama sinema."

“Mimi...” Midomo ya Lisa ilitetemeka.
Alvin aliwasha simu yake na kumuonyesha tiketi. "Nimenunua tikiti yako, na haiwezi kurejeshwa."
Lisa alikosa la kusema baada ya kuitazama. “Unanipeleka kutazama katuni?”
“Aunty Lisa, mimi ndiye niliyependekeza filamu hii.” Suzie aliinua kichwa chake kwa huruma na kumtazama Lisa. “Sijawahi kuingi kwenye jumba la sinema maishani mwangu.”
“Wewe mtoto mwongo.” Lisa akamvuta sikioni Suzie. “Kwanini ulinidanganya kuwa upo na baba

yako?”
Suzie alisema kwa uchungu, “Pole. Nisingekuambia kuwa niko na Baba, usingeshuka.”
"Nilijua mapema kuwa unadanganya," Lisa alisema kwa hasira.
Macho ya Alvin yalimtoka na kumtazama Lisa kwa hisia tofauti. "Hii ina maana kwamba ... ulishuka tu kwa sababu ya Jack?"
Lisa alimtazama kwa macho yake makubwa, na alionekana kuwa na hasira. Lakini, tukio hilo liliwafanya waonekane kama wanandoa wanaogombana. Midomo ya Alvin ilijikunja huku akimtazama anavyopandwa na hasira.

Kwa sababu ya Suzie, Lisa hatimaye alikubali. Alvin aliwapeleka kwanza kwenye mgahawa unaofaa watoto. Wote watatu waliagiza pizza ya nyama. Alvin alihisi kuwa ladha ya pizza ilikuwa ya wastani na sio ya kupendeza kama nyama zilizopikwa na Lisa. Aliacha kula baada ya kumega mara chache.
Suzie alipepesa macho na kusema, “Anko Alvin, hukumaliza chakula chako. Ni uharibufu ulioje! Utapata njaa muda si mrefu, we jishaue tu."
“We! Iwe mwanzo na mwisho kuongea hivyo na wakubwa. Kujishaua ndo nini?” Lisa alimfokea.
Alvin alitabasamu kwa kuridhika tu.

Walipokuwa wote watatu, walionekana kama familia ya kupendeza na watu waliwatupia jicho la husuda sana. “Ni sawa. Bado nina kiporo nyumbani, naweza kwenda kula baadaye,” Alvin alisema huku akimwangalia Lisa kwa upole.
Lisa alikaribia kusongwa na chakula chake. Alipotazama juu na kukutana na macho yake, uso wake mzuri ulikunjamana kidogo.
Alvin alijawa na furaha moyoni alipoiona sura yake. Moyo wake ulidunda kwa furaha hata mwenyewe hakujua ni kwa sababu gani. Hakuwahi kujihisi hivi hata alipokuwa kwenye uhusiano na Sarah enzi hizo mapenzi yao yakiwa motomoto. Hakuwahi kutarajia kuwa angepata

hisia kama hizo wakati huu.
"Nini? Una kiporo cha jana usiku?” Suzie alishangaa. “Hiyo si nzuri. Chakula kimekaa kwa muda mrefu sana. Nilisikia kula viporo ni mbaya kwa afya yako.”
“Huelewi. Kiporo ni kitamu.” Alvin aliendelea kumkazia macho mwanamke aliye mkabala na yeye.
Suzie aliitikia kwa kichwa. "Labda ni kiporo cha nyama choma ya nguruwe, sivyo?"
“Siyo tu nyama ya nguruwe. Kuna kitu tamu ndani yake ambacho hukijui.” Alvin alitoa tabasamu hafifu. "Ladha tamu inapoingia mwilini mwangu, ninahisi utamu moyoni mwangu pia."

“Aunty Lisa, unajua ni kitu gani hiki kitamu?” Suzie alimtazama Lisa kwa bumbuwazi. “Ili na mimi niweze kuhisi utamu moyoni mwangu wakati ujao pia.”
"Hata mimi sikijui hicho kitu, labda muulize Anko Alvin,” Lisa alimtania kabla hajainamisha kichwa chake na kuendelea kula pizza.
Baada ya kumaliza chakula, wote watatu walielekea kwenye ukumbi wa sinema. Alvin alikuwa amembeba Suzie begani, huku Lisa akiwa ameshikilia koti la Suzie. Kwa watoto wengine, watatu kati yao walionekana kama familia.
Walipokuwa wakingoja nje ya ukumbi

wa sinema, watoto wengi walikuwa wamesimama pale. Wengine walikuja na baba au mama zao. Wote wakamtazama Suzie kwa kumshangaa.
“Mama, msichana huyo mdogo ana bahati kweli. Baba na mama yake wote wawili wamemleta kwenye sinema.”
"Mpenzi, baba yako hana chaguo ila kufanya kazi ya ziada ili kupata pesa zaidi."
"Natamani baba na mama yangu wangenisindikiza. Ona, baba yake ni mzuri na mama yake ni mzuri.”
Baada ya kusikia maneno hayo, Suzie aliinua kichwa chake huku akionyesha mbwembwe. Alipoiona sura ya Suzie, Lisa alitabasamu kwa upole lakini

wakati huo huo alijihisi kukasirika.
Suzie pia alikuwa anawaonea wivu watoto walioandamana na wazazi wao wote wawili alipokuwa nje ya nchi. Hii pia ndiyo ilikuwa sababu hasa Lisa hakuweza kuvumilia kukataa ombi la Suzie la kwenda kutizama katuni pamoja naye.
Lucas alipita akilini mwake ghafla. Zilikuwa zimepita siku kadhaa tangu amtembelee Lucas mara ya mwisho. Lisa alimuonea huruma ghafla. Alitamani na yeye angekuwa pamoja nao.
TUKUTANE KURASA 411-415

ONYO: Ni marufuku kusambaza, kukopi wala kuuza kazi hii kwani endapo kama tutakubaini basi sheria itachukua mkondo wake (By: Official Dully)
 
LISA KITABU CHA NANE (9) SIMULIZI........................LISA KURASA.................411 - 415
PRESENT: SIMULIZI ZA DULLY

Sura ya: 411
“Mbona umeduwaa? Unawaza nini” Alvin aliushika mkono wa Lisa ghafla na kumtazama kwa makini. "Mnataka kula nini tena? Twendeni tukanunue."
“Nataka... nataka popcorn,” Suzie alisema kwanza.
"Unadhani mimi ni mlaji kama nyinyi?" Lisa aligugumia, lakini Alvin alijisikia hovyo.
Alvin akajibu kwa umakini, “Mimi sio mla hovyo. Ninapenda tu upishi wako."
"Na mimi pia. Upikaji wa Aunty Lisa ni bora zaidi ya wa mama wote." Suzie akaenda pamoja nao.
Kwa kuona jinsi Alvin na Suzie walivyofanana kimuonekano, macho ya Lisa yakawa ya upole. "Nataka juisi ya

zabibu."
Baada ya kumkabidhi Suzie kwa Lisa, Alvin aligeuka na kwenda kununua juisi ya zabibu. Akiwa amekaa mikononi mwa Lisa, Suzie alinong'ona kwa ghafla, "Mama, baba yangu mchafu... anajaribu kukurudisha kwake?"
"Hujui chochote we mtoto, nyamaza." Lisa alibana ncha ya pua ya Suzie.
"Mama, nahisi ... Baba mchafu ni mzuri sana." Suzie alimkazia macho ya huruma. “Kwanini usifanye hivyo? Nyie tu... mnapendeza mkiwa pamoja.”
Lisa alipigwa na butwaa kwa muda. Kwa kweli, aligundua mapema kwamba Suzie alikuwa na nia ya kumuunganisha na Alvin. Japokuwa Suzie alitarajia hilo lingetokea, Je, Lisa angeweza kusahau madhara aliyosababishiwa na Alvin kwa ajili ya Suzie? "Siyo rahisi kama

unavyofikiri. Aunty Sarah hataweza kumuachia baba yako kiurahisi, na baba yako mchafu anaweza kututupa wakati wowote kwa ajili yake.”
“Kweli? Ikiwa ndivyo alivyo, sitamsamehe tena,” Suzie alijibu kwa kufoka.
Suzie hakujua kwamba kama isingekuwa msaada wa Jack na Hans, yeye na Lucas wangepoteza maisha. Lisa asingeweza kusahau mateso na unyonge huo.
Muda si mrefu Alvin alirudi na popcorn na juisi. Kisha, wote watatu wakaingia kwenye ukumbi wa sinema pamoja. Suzie alikuwa ameketi kati ya Alvin na Lisa. Hata hivyo, Alvin alihisi yuko mbali sana na Lisa, hivyo akamuweka Suzie kwenye mapaja yake na badala yake akaketi na kugusana kabisa na Lisa. “Suzie, nitakuruhusu ukae kwenye

mapaja yangu, sawa? Mtu mrefu aliye mbele yako anaweza kukuzuia, kwa hivyo hutaweza kuona skrini. ”
Suzie aliitikia kwa kichwa akidhani kuwa alichokisema Alvin ni kweli.
Lisa alikosa la kusema. Mara akagundua mkono wa Alvin umewekwa nyuma ya mgongo wake.
Lisa alimkazia macho, lakini Alvin alisema kwa uso ulionyooka, "Bega langu linauma, kwa hivyo ninanyoosha mkono wangu."
Lisa aligeuza macho yake kwenye skrini kwani hakuweza kuwa na wasiwasi juu yake. Lakini, sinema za katuni za watoto zilikuwa za kuchosha sana. Suzie pekee ndiye alikuwa amezama kwenye sinema.
Lisa aliinamisha kichwa chini. Aliwasha simu yake ili kucheza baadhi ya michezo.

Mkono wa Alvin ukatua begani mwake. Alikuwa amevaa vazi jepesi la hariri, hivyo aliweza kuhisi mkono wake laini ukipenya kabisa kwenye ngozi yake.
“Alvin...” Lisa alitazama juu na kumkazia macho.
Alvin aliondoa mkono wake kwa aibu. Kisha, akachukua chupa ya juisi ya zabibu iliyowekwa kati yao na kuinywa.
“Hiyo ni yangu.” Lisa kwa hasira akashusha pumzi ndefu.
“Haijalishi,” Alvin alimsogelea na kumnong’oneza sikioni. Kupumua kwake kwa jinsi ya kiume kulimfanya Lisa awe na mwasho moyoni na kitetemeshi kwenye uti wake wa mgongo. "Tumeshea mate mara nyingi sana hivyo hakuna ajabu tukishea juisi."

Lisa alibana paja lake bila huruma. Huyu mhuni anathubutu vipi kutoa maneno yasiyo na aibu? Ikiwa ukumbi wa sinema haukuwa na giza vile, bila shaka angeweza kumuona uso wake ukiwa umekunjamana kwa wakati huo.
Hakujisikia tena kuinywa ile juisi kwa vile Alvin alikuwa amekunywa. Hata hivyo, alihitaji kukata kiu yake vibaya sana. Hakuwa na jinsi zaidi ya kuinywa tu hiyo juisi.
Katikati ya sinema hiyo, Alvin aliinuka na kuelekea chooni. Lisa alipomuuliza Suzie kama angependa kwenda chooni, Suzie akatikisa kichwa na kusema hapana. Hata hivyo, Lisa alipombeba, alihisi mkojo wa joto ukitoka kwa Suzie ambao ulilowesha suruali yake. Uso wa Lisa ukaganda. Kama wangekuwa nje muda huo, angemchapa.
“Samahani mama. ” Suzie alifahamu

jambo baya alilokuwa ametoka kufanya. Huku machozi yakimtoka, nusura aanze kulia.
"Kwanini ulisema hapana nilipokuuliza unataka kukojoa?"
“Sikutaka kukosa sinema hiyo, na nilifikiri ningeweza kuvumilia!” Suzie alijibu kwa unyonge.
Lisa alishindwa kusema chochote, akashusha pumzi. “Sawa. Acha kutazama filamu. Lazima ubadilishwe. Vinginevyo, utapata homa."
Alimbeba Suzie na kutoka nje. Alvin, ambaye alikuwa akitoka nje ya choo, alitokea kuona unyevunyevu kwenye nguo ya Lisa sehemu ya mapajani.
“Suzie alinikojolea. Ni lazima nimtafutie seti mpya ya nguo ili asipate homa.” Lisa alieleza.
Kwa bahati nzuri, kulikuwa na maduka

chini ya ukumbi wa sinema. Muda si muda Lisa alinunua seti mpya ya nguo ili Suzie abadilishwe. Alijinunulia nguo mpya kwenye duka la nguo za wanawake na kubadilisha pia. Kwa kuwa alikuwa na sura nzuri, suruali yoyote ingempendeza.
Msaidizi wa duka kando yake alimsifu, “Bwana, mke wako ana sura nzuri sana, na pia anaonekana mrembo. Ni kama mwanamitindo bila kujali anavaa nguo gani.”
Alvin akatabasamu. Neno 'mke' halikuwahi kusikika la ajabu sana kwake. "Mpatie nguo zote za saizi yake." Alvin alitoa kadi ya malipo kwa msaidizi wa duka moja kwa moja. Msaidizi wa duka alipigwa na butwaa. Alikuwa tajiri kiasi gani?
Wakati Lisa anatoka akiwa amevalia suruali mpya ya jeans, muuza duka

alikuwa tayari ameshapakia furushi la nguo. “Bibi, mumeo amenunua nguo zote za duka hili zenye saizi yako. Umebarikiwa sana!”
Lisa akahamishia macho yake kwa Alvin huku midomo ikicheza. "Mbona unanunua nguo nyingi hivi?"
"Muuzaji amesema unaonekana mzuri ukizivaa." Alvin akatabasamu.
Lisa alipapasa paji la uso wake. "Hakuna nafasi ya kutosha nyumbani kwangu kuweka nguo hizi zote ..."
“Utaziweka katika nyumba yangu ya Zion Residence, basi. Unapokuja kukaa, hutalazimika kubeba nguo zako,” Alvin alijibu kwa namna ya kujihesabia haki kana kwamba... wawili hao walikuwa kwenye uhusiano rasmi.
Lisa alikosa la kusema kabisa baada ya kuona sura yake isiyo na aibu. "Naweza

kujua kwanini nije kukaa huko?"
“Usipokuja na kukaa kwangu, unapanga kukaa sehemu ya nani? Sitakuruhusu kukaa katika nyumba za wanaume wengine,” Alvin alisema kwa njia ya ubabe na ya uchochezi.
Lakini, Lisa hakuwa na nguvu ya kubishana naye tena. Kwa kuwa alitaka kutumia pesa, angemruhusu. Kwa vyovyote vile, yeye ndiye angeamua kukaa au kutokaa mahali pake.
Alvin aliishia kumnunulia zaidi ya seti 100 za nguo Lisa, ambaye mwanzoni alitaka tu kununua suruali moja ya jeans.
 Alvin aliandika anwani ya Zion Residence katika fomu ili kutuma baadhi ya nguo huko. Kisha, alimsaidia Lisa kubeba zingine kurudi nyumbani.
Wakati wote watatu waliposhuka kwenye lifti, Joan Halua, rafiki wa

Sarah, ambaye alikuwa akinunua vitu, aliwaona. Hapo hapo akawapiga picha na kumtumia Sarah kwa njia ya WhatsApp. [Sarah, nini kinaendelea kati yako na Alvin? Nilimwona tena akinunua nguo na Lisa. Wamenunua nguo nyingi mno.]
Kusema kweli, Joan hapo awali alikuwa amempenda Sarah kwa kuwa mchumba wa Alvin. Alikuwa ametumia muda mwingi na juhudi kujikombakomba kwa Sarah kwa sababu hiyo. Hakutarajia hilo mwishowe...
Kila mtu alijua kuwa Sarah asingekuwa mtu wa matawi ya juu bila kumtegemea Alvin, ikizingatiwa kuwa alikuwa mwanasaikolojia tu. Angehitajika tu wakati kulikuwa na mgonjwa wa akili.
Sarah alipoona picha, aliruka kwa

hasira. Kipindi hicho, Alvin alikuwa akipotezeasimu na meseji zake. Hata mlinzi wa ofisi yake angemzuia kuingia. Ilionekana kana kwamba alikuwa ametupwa kabisa.
Sarah alihisi kuwa Alvin bado ana kinyongo naye, lakini hakutegemea kwamba angeenda kumtafuta Lisa. Hata alikuwa akimsindikiza kwenda kufanya manunuzi ya nguo. Pamoja na wote wawili kuambatana na mtoto, walionekana kama familia. Mbaya zaidi aliweza kuhesabu nguo ambazo Alvin alimnunulia kwa kutumia vidole vya mkono mmoja. Sarah karibu akaenda wazimu.
Hapana! Ilibidi amzuie Alvin kuwa na tabia hii! Dokezo la chuki lilimwangazia machoni pake. Alifungua mlango na kumwita Maya.
Sura ya: 412

Wakiwa njiani kurejea Karen Estate, simu ya Alvin iliita ghafla. Alipoitoa na kuitazama, akagundua kuwa ilikuwa ni simu inayoingia kutoka kwa
Sarah.
 Akakunja uso, akabonyeza kitufe cha kuzima sauti kabla hajaitupa simu pembeni.
Lisa aliyekuwa amembeba Suzie kwenye kiti cha nyuma, alibaki akihema huku akitazama tu. Muda mfupi baadaye, simu yake iliita tena. Ni Maya ndiye aliyempigia simu wakati huo. Maya kawaida hakumpigia simu. Kwa hiyo, Alvin aliitikia simu haraka. " Kuna nini?"
“Oh hapana, Bwana Kimaro! Umeme katika jumba ghafla ulizima ghafla. Bi Njau aliposhuka chini, alikosea kukanyaga na kuteleza kwenye ngazi kwa bahati mbaya. Amejeruhiwa, na anavuja damu nyingi,” Maya alisema

kwa wasiwasi.
Uso wa Alvin ulibadilika. “Nenda ukaite gari la wagonjwa limpeleke Sarah hospitali. Narudi sasa hivi.”
Alipokata simu hiyo, alikanyaga moto mpaka gari likakaribia kupaa na mara akafika kwenye lango la kuingilia kwenye jengo la nyumba ya
Lisa.
 “Nitamwacha Suzie na wewe hapa usiku wa leo. Kesho nitakuja kumchukua asubuhi.”
Wakati huo, Suzie alikuwa tayari amelala mikononi mwa Lisa.
 Lisa alikodoa macho. Alipotazama sura safi na tamu ya Suzie, moyo wake ulimuuma ghafla. Muda si mrefu, mtoto huyu mdogo alikuwa amesema kwamba babake mchafu alikuwa mzuri sana, kwa hiyo alitaka Lisa warudiane naye.

Hata hivyo, muda mfupi baadaye alikuwa akiwatelekeza bila kusita na kwenda kukutana na mwanamke mwingine.
“Sasa kwa kuwa yeye ni mzito sana, unafikiri ninaweza kumbeba juu mpaka kwenye lifti peke yangu?” Lisa alitoa kicheko cha kejeli.
Alvin alipigwa na butwaa na akajibu bila kufikiria tena, “Basi nitambeba.”
“Alvin, mbona unakimbilia kuondoka? Huna hata wasiwasi kuhusu mtoto wa mdogo wako. Hii ni kwa sababu tu kuna jambo limempata Sarah?” Ghafla, Lisa alimkazia macho. Kwa kweli, alikuwa amesikia sehemu fulani za mazungumzo alipokuwa kwenye simu.
Alvin aliguna, akitaka kumdanganya. Hata hivyo, baada ya kuona macho yake meusi lakini angavu, alishindwa

kusema lolote. Muda mfupi baadaye, hakuweza kujizuia kueleza, “Kulikuwa na giza ndani ya jumba. Sarah hakuweza kuona gizani, hivyo akaanguka alipokuwa akishuka ngazi...” "Si kuna mtu aliyepiga simu kwa gari la wagonjwa kumpeleka hospitali?" Lisa aliuliza kwa ukali.
 "Maya ameita gari la wagonjwa. Sasa mbona unakimbilia huko? Wewe ni daktari? Au bado ni mpenzi wake? Mume wake?”
Baada ya kusikia maneno ya Lisa, Alvin alianza kuonekana mnyonge.
“Yeye... Amejeruhiwa vibaya sana...” Baada ya muda fulani ndipo alipolazimisha sentensi hiyo kutoka kinywani mwake.

Lisa alicheka tu kwa kebehi. "Alvin, mwishowe, bado una wasiwasi juu yake. Unahisi una jukumu kwake. Bado una hisia kwake, bila kujali kama

unamtendea kama mwanafamilia, mpenzi, au mtu unayemuhurumia. Kwa kawaida na bila kujua umemfanya kuwa kipaumbele chako cha juu."
“Usinielewe vibaya, Lisa. ” Mikono ya Alvin iliyokuwa imeshikilia usukani iliganda.
"Kuna mtu karibu naye sasa, na zaidi ya hayo, uliniambia kuwa haiwezekani tena nyinyi kuoana. Kwa hivyo kwanini unataka kuharakisha huko?" Lisa alilazimisha tabasamu. “Alvin, ukisisitiza kuwa na tabia hii, ningekushauri uache kunifuatafuata.
 Ni bora ubaki kuwa na Sarah. Kwa kweli sitaki unifanye niteseke na kunitendea isivyo haki.”
“Ninaenda kumtazama tu mara moja. Wewe unazidisha mambo. ” Uso wa Alvin ulijikunja. "Nina hakika kuwa wewe ndiye ninayekupenda."

“Unanipenda, lakini utaenda kwa Sarah mara tu jambo litakapomtokea. Lakini mimi? Nilivamiwa na ndugu yake na hakuna lolote ulilolifanya. Unanipendaje kwa mfano?” Lisa alijua kwamba Sarah alifanya mambo kama hayo makusudi. Alijua kuwa Sarah angejiumiza ili tu apate huruma ya Alvin.
Ni wazi, Sarah alikuwa ameanguka kutoka kwenye ngazi wakati wa giza kwa nia moja tu ya kumfanya Alvin aende huko.
 Lakini, Lisa hakumruhusu Alvin kuingia kwenye mtego wa Sarah. Hakumruhusu Alvin aelekee huko usiku huo.
"Alvin, ikiwa bado unajiona kuwa na hatia kwa yaliyompata, basi endelea kubeba jukumu lake, lakini uachane kabisa na mimi. Huwezi kuwa na uhusiano na mimi na kuendelea kumjali Sarah kwa wakati mmoja. Ingawa amefanya jambo baya, bado unamvumilia. Ukiendelea kufanya hivi,

nitaanza kukudharau.” Lisa aliinua kichwa chake kama twiga mwenye majivuno, macho yake yalikuwa mazito kwa kumaanisha. “Nataka ujue kwamba usipomwacha Sarah aendelee na maisha yake, atafikiri ana nafasi ya kurudiana na wewe. Ikiwa hali ndiyo hii, mwanamume yeyote ambaye anavutiwa naye hataweza kumkaribia na kumfuatilia. Huwezi kumzuia kuolewa na mwanaume mwingine wakati hutaki kumuoa, sivyo?”
Midomo myembamba ya Alvin ilitetemeka. "Bila shaka hapana. Natumai kuwa atafurahi pia. ”
“Basi sio lazima ujisikie hatia kwake, kwa kweli. Baada ya yote, ulikuwa tu kwenye uhusiano na Sarah. Hujazaa naye mtoto wala hujawahi kumpa mimba. Umemsaidia hata Thomas kwa kumzuia kupelekwa jela mara kadhaa, na pia umeitetea sana New Era

Advertisings kila wakati. Juu ya kwanini nyie hamkuishia kuoana, nadhani mnajua jibu kuliko mtu mwingine yeyote.”
Maneno ya Lisa yalimfanya Alvin ahisi raha ghafla. Licha ya kujua kwamba alikuwa na badiliko la moyo wake, bado alihisi kuwa amejawa na hatia kwa sababu ya ahadi yake ya wakati huo kwa Sarah.
 Baada ya Sarah kurejea, aliweza kutibu ugonjwa wake, lakini hakuweza kufanya naye mapenzi.
Lisa alikuwa sahihi. Alvin na Sarah walikuwa kwenye uhusiano tu na hawakuwahi kulala pamoja. Hapo awali, Alvin alitamani kwa dhati kumuoa Sarah. Isingekuwa kuonekana kwa Hisan, angeishia kumuoa Sarah. Alikiri kwamba Sarah alihuzunika, lakini si yeye aliyechangia maisha yake ya zamani yenye kuhuzunisha.

Lisa kisha akaendelea, “Mimi si mtu asiye na huruma hata hivyo. Ikiwa kusingekuwa na mtu kando ya Sarah, ingekuwa sawa kwangu ikiwa ungetaka kwenda kumsaidia kwa kuwa wewe ni mpenzi wake wa zamani. Lakini kuna mtu yuko naye sasa na kakake Sarah yuko hapahapa Nairobi. Ukitaka kwenda huko, sitakupa nafasi ya pili.” Kwa hayo, akafungua mlango wa gari na moja kwa moja akatoka huku akiwa amembeba Suzie.
“Sawa, siendi huko.” Alipoona anatoka, Alvin haraka akafungua mkanda wake na kumfuata. Akamchukua Suzie kutoka mikononi mwake huku macho yake yakimetameta. “Kwa hiyo unaweza kunipa nafasi nyingine usiku wa leo?” Alvin alianza kusukuma bahati yake. "Baada ya yote, ulikuwa unajaribu kunidhibiti sasa hivi."

“Nilikudhibiti lini? Nilikuwa nasema ukweli tu.” Lisa alianza kushindwa kujizuia. Kama asingetumia muda mrefu kumfundisha Alvin, angeenda kumtafuta Sarah. Anathubutu vipi kuuliza swali kama hilo.
"Unawazimu? Una wivu?” Mdomo wa Alvin ulijipinda na kuwa tabasamu mbaya.
 Ingawa alizuga kuwa na uso mkali, alijua kwamba alikuwa na wasiwasi juu yake.
“Unawaza kupita kiasi. Sitaki mambo yawe kama hapo awali uliponipiga teke na kunitaliki mara baada ya kulala pamoja. Alvin, ninachotaka ni hali ya usalama. Sitaki kuwa siku zote nitakayetupwa wakati wowote.”
Lisa alipomaliza kuongea, alitangulia mbele bila kuangalia nyuma.
Baada ya kuona nywele zake nyeusi zikipeperushwa na upepo wa usiku na

mikunjo yake mizuri, moyo wa Alvin uliumia kwa namna fulani. Alvin alimfuata na kuingia ndani ya nyumba. Kisha, akamweka Suzie juu ya kitanda katika chumba chake cha kulala.
“Kesho, nitampeleka Suzie shule ya chekechea. Sio lazima uje kumchukua. ” Lisa alimlaza Suzie kitandani.
“Oh!” Macho ya Alvin yalipita ndani ya nyumba ile. Aliinua uso wake kwa hisia ya kukata tamaa “Nilifikiri ningelala hapa usiku huu. Naweza hata kulala kwenye kochi.”
“Unaota ndoto?” Baada ya kutumbua macho, Lisa alimtoa chumbani kwa ukali. "Pamela atarudi muda si mrefu. Itakuwa shida ukilala hapa."
"Katika hali hiyo, ... naweza kulala kwenye kochi katika chumba chako cha kulala." Alvin alimtishia kwa sauti ya

chini, “Huogopi kwamba nitaenda hospitali kumtafuta Sarah ikiwa utaniruhusu niende?” Hakutarajia maneno hayo yangemkera Lisa.
Lisa alimjibu kwa kuchukia sana. “Kama unataka kumtafuta, hiyo ni biashara yako. Sio kama nimekufunga miguu yako hata hivyo."
Safari hii, moja kwa moja alimsukuma nje ya mlango mkuu na kuufunga kwa nguvu.
Sura ya: 413
Alvin alitikisa kichwa chake kwa kuudhika. Alijilaumu kwa kumuudhi kwa maneno yake ya kijinga. Alipogeuka tu, akamuona Pamela akitoka kwenye lifti huku akipiga kelele.
 Macho yao yalipokutana, Pamela alishikwa na butwaa. "Alvin, kwanini uko hapa tena?"

Alivin alishangaa. Alimaanisha nini aliposema 'tena'? Hata
hivyo, hakupenda kumuona Pamela kwani alikuwa ameharibu nafasi yake ya kukaa na Lisa.
 “Ofisi yako si ipo Marekani? Unaondoka lini?” Alvin aliuliza bila huruma.
“Kuondoka?” Pamela alipigwa na butwaa. “Sina mpango wa kuondoka. Nitabaki Nairobi kufanya kazi."
Kichwa cha Alvin kilimuuma kwa kuwaza gurudumu hilo la tatu ambalo lingeendelea kubaki hapo. Alivuta uso mrefu na kuuliza, "Kwa hiyo, utaendelea kukaa na Lisa?"
“Bila shaka. Sisi ni marafiki, na tunategemeana. Lisa yupo single na mimi nipo single, kwa hiyo hatuna wasiwasi.”
Alvin akafikiria kwa muda na ghafla

akatoa simu yake kutoka mfukoni mwake. Alibofyabofya kidogo na kumwambia Pamela. "Hii hapa ni virtual card ya nyumba ya ghorofa mbili yenye ukubwa wa mita za mraba 40, iliyopo kwenye mtaa wa Brighton Gardens. Ghorofa hii ina kila kitu ndani. Kadi hii ya kieletroniki ina maelezo yote ya umiliki wa nyumba. Nitawaambia watu wangu wabadilishe jina na kuweka lako. Namba za siri za kufungua kila mlango zimo kwenye hii virtual card.
Hamia huko na ni yako kuanzia leo na kuendelea.”
Pamela alipigwa na butwaa. Ingawa hakuwa amekaa Nairobi kwa miaka mingi, alijua kwamba Brighton Gardens ulikuwa ni mtaa mmoja wapo wenye nyumba za gharama kubwa zaidi huko Nairobi. Kwa kuzingatia kwamba ilikuwa katikati mwa jiji, kila senti mita moja ya mraba ya ardhi ilikuwa na thamani kubwa mno.
 Kweli Alvin alimpa

nyumba kama hiyo bure? “Unaitaka?” Alvin alimuuliza.
“Ndiyo!” Pamela alikubali haraka haraka, akifikiri kwamba ingekuwa ni kupoteza fursa adimu kukataa ofa kama hiyo. "Nitaondoka kesho."
“Mm. Alvin aliitikia kwa kuridhika. Alimtumia hiyo virtual card iliyokuwa na maelezo yote ya nyumba kwenye simu yake. Baada ya hapo, aliingia kwenye lifti na kuondoka. Hatimaye, aliweza kulitoa gurudumu hili la tatu nje.
Baada ya Pamela kufungua mlango na kuingia ndani ya nyumba, haraka akamkimbilia Lisa. Alionyesha kadi kwenye simu yake, akisema, "Jamani.
 Sasa hivi, Alvin amenipa nyumba yenye ghorofa mbili kwenye mtaa wa Brighton Gardens. Alisema ni mita za mraba 40.”

Lisa alikuwa anakunywa maji na akayatema mara moja. Akiwa ameduwaa, Lisa alikazia macho kwenye kadi ya kieletroniki iliyoonyesha anuani ya nyumba. Alihisi kukosa la kusema. "Kwa hiyo umemwambia kuwa utahama?"
"Ndiyo, najua uhusiano wenu unaendelea vizuri hivi karibuni, kwa hivyo sitakaa hapa na kuwasumbua nyinyi... Hehehe." Pamela alicheka kwa furaha. "Zaidi ya hayo, ninaweza kukupa nyumba hiyo baadaye."
“Ni sawa. Mimi ni tajiri na sitamani nyumba. ” Lisa aONA ni ujinga. Labda Alvin alivaa kofia ya dola kumi kwenye kichwa cha senti tano. Walipoachana kabla ya hii, hakupokea nyumba kutoka kwake, lakini alikuwa tayari kutumia dola milioni 10 ili tu kumfukuza Pamela, ambaye alikuwa gurudumu la tatu

machoni pake. Ilikuwa ni kama anajaribu kuua mbu kwa bunduki.
Lisa hakuweza kuwa na wasiwasi kuhusu Pamela. Aligeuka na kwenda kuoga.
Baada ya kuoga, alirudi kitandani kwake na kufungua WhatsApp. Aligundua kuwa mtu aliyekwenda kwa jina 'Ni Wako Pekee' alikuwa amemfikia.
Lisa alihisi kukosa raha na akajitenga kimawazo kwa muda. Wakati Alvin na Lisa walikuwa wakipendana kwa sana hapo awali, Alvin alikuwa amebadilisha jina lake la WhatsApp kuwa hilo.
Muda mfupi baadaye, Alvin alimtumia ujumbe wa WhatsApp. [Uliblock namba yangu ya mwisho, kwa hivyo nilipata namba mpya.]
Lisa hakujibu. Kisha, Alvin akamtumia

selfie. Alikuwa amevaa vazi la kuogea ambalo lilikuwa limefungwa ovyo. Mbali na uso wake mzuri, tumbo lake la misuli lililofunikwa na matone ya maji ya kumeta pia lilikuwa likionekana. Japokuwa Lisa aliwahi kumuona mwanaume huyo kuanzia utosini hadi unyayoni, hakuweza kujizuia kuona haya usoni kwa kuuona mwili wake uchi. Alvin alikuwa akijaribu kufanya nini?
Kwa wakati huo, alicheza ujumbe wa sauti ambao alikuwa amepokea. Sauti nzito ya kiume ya mwanaume huyo ilimfanya ajisikie kana kwamba umeme unapita mwilini mwake na kumfanya aishiwe nguvu.
“Mpenzi, nipo nyumbani. sikwenda popote.”
Mpenzi? Upuuzi ulioje! Uso wa Lisa ulimtoka. Mtu huyu alikuwa hana aibu

kweli.
Hata hivyo, Sarah lazima angekuwa na wazimu kwamba Alvin hakwenda kumuona usiku huo.
 Baada ya kufikiria kidogo, Lisa alimtumia emoji ya busu. Baada ya kutuma emoji, uso wake ukabadilika na kujawa aibu tena. Alitaka tu kumpagawisha mwanaume huyo na kumchokoza Sarah kwa makusudi.
Mara Alvin alipoona emoji ya busu, alihisi msisimko mkubwa ndani yake. Mjeledi wake uliamka, na kumsababishia usumbufu kwa sababu isiyoelezeka. Akajilaza huku akimwazia Lisa akimbusu.
Wakati huo, ghafla aliketi kitandani na kumtumia Lisa ujumbe maneno mawili tu: [Nataka kesho.] Kisha, akakimbilia bafuni kuoga maji baridi.

Hakuwahi kusisimka na Sarah licha ya kuwa naye kwa muda mrefu. Kamwe katika ndoto zake kali hakufikiri kwamba emoji rahisi kutoka kwa Lisa ingemfanya awake kwa msisimko. Akatoa kicheko cha uchungu.
Alipotoka bafuni, simu yake ikaita tena. Maya alimpigia. “Bwana Mkubwa, si ulisema unakuja? Bi Njau analia hospitalini. Anakataa kufungwa bandeji.”
Alvin alikasirika kwa namna fulani. "Ni mwili wake, sio wangu! ”
Maya aliogopa alipomfokea. “Lakini Bi Njau anakuhitaji sana sasa, Bwana Mkubwa. Siku zote hizi ukiwa haupo, hajaweza kula wala kulala vizuri. Kwa sababu hiyo, hakuwa na nguvu ndiyo maana akaanguka kutoka kwenye ngazi wakati wa kukatika kwa umeme usiku wa leo. Daktari alisema kuwa miguu yake imejeruhiwa. Ikiwa

hatatibiwa mara moja, anaweza kuwa mlemavu katika siku zijazo.”
Maneno ya Maya yalionekana kama uzito mkubwa kwenye akili ya
Alvin.
 Kwa mara ya kwanza, hakuhisi hatia. Badala yake, alihisi kuishiwa nguvu.
 Kama Lisa alivyosema, alikuwa tu katika uhusiano na Sarah. Kwanini ilionekana kana kwamba alipaswa kuwajibika kwa maisha yake yote?
“Sawa, nitakuja,” alinong’ona baada ya muda fulani.

Katika hospitali, Maya mara moja alimwambia Sarah kuhusu hilo. Sarah alisisimka. Alijua kwamba Alvin angeenda hatimaye. Sarah alikuwa amekasirika baada ya Alvin kutokwenda alipopigiwa simu na Maya mara ya kwanza. Lakini, alifurahi

kwamba Maya alifanikiwa kumshawishi mwishowe.
Alikuwa amepanga wakati wa Alvin kuonekana tu, kungekuwa na waandishi wa habari wakiwapiga picha. Kisha, kila mtu katika Kenya angejua kwamba jambo fulani lilikuwa limempata Sarah na Alvin ndiye aliyekuwa wa kwanza kukimbilia hospitalini kumwona kwa wasiwasi. Ha! Tayari angeweza kufikiria kulalamika kwa Lisa kwa hasira kesho yake. Lisa alikuwa akijaribu kumpokonya mtu wake. Lakini, mara Sarah alipotoa agizo, Alvin angemmwaga Lisa bila huruma.

Dakika 20 baadaye.
 Sarah alipomwona Alvin hospitalini, haraka akajilaza kitandani na kujifanya kutoa machozi ya kukata tamaa. Ili kupata huruma ya Alvin, Sarah alikuwa amejiangusha bila huruma kutoka

kwenye ngazi siku hiyo. Paji la uso, miguu na mikono yake vilijeruhiwa.
 Alionekana mwenye huzuni sana.
“Alvinic, hatimaye umefika. Nilifikiri sitaweza kukuona tena.” Sara alipomwona, alianza kulia kwa uchungu. Alinyoosha mikono yake na kuanguka katika mikono yake. Alvin alishindwa kujizuia kumshika, au angeanguka kutoka kitandani.
Sura ya: 414
"Alvinic, nimekukumbuka sana." Sarah akajiegemeza kwenye mikono ya Alvin, machozi yake yakilowanisha shati lake. “Siku hizi nimekuwa nikijitafakari. Nilikuwa mjinga sana na mpumbavu. Ninaapa kwamba sitakukosea tena. Rudi kwangu. Nimekukumbuka sana.”
Alvin alikaza macho na kumweka

kitandani. Baada ya hapo, aligeuka na kumwambia daktari nje, "Ingia ndani umtibu."
"Hapana. Usiponiahidi, sitatibiwa. ” Sarah alijitahidi kwa fadhaa.
Alipoiona sura yake, macho ya Alvin yalimtoka kwa hasira. Uso wake mzuri ulidhihirisha polepole hali ya
ukali.
 “Inatosha. Acha kutumia mwili wako kunitisha.”
Hakujua ni kwanini Sarah amekuwa msumbufu na asiye na akili. Hata sasa alikuwa akimtishia, hiyo ndiyo mbinu ambayo alikuwa akiichukia zaidi. Ilikuwa mara yake ya kwanza kutumia sauti ya kutisha hivyo kuzungumza na Sarah.
Baada ya kupigwa na butwaa kwa muda, Sarah alianza kulia zaidi. "Sipendi kuwa na tabia kama hii pia lakini ninaweza kufanya nini? Siwezi

kujizuia kufanya hivyo.”
"Sarah, kwanini tusitengane bila kuwa na kinyongo?" Alvin hakuguswa na kilio chake hata kidogo. Badala yake, alihisi wimbi la uchovu likimuandama. “Miguu yako ni yako. Hata ukiwa kilema siku za usoni, sitawajibikia kwa sababu si mimi niliyekuangusha kwenye ngazi.”
Sarah aliutazama uso wake mzuri bila kuamini. Siku zote alikuwa mpole na mvumilivu kwake. Lakini siku hiyo, alikuwa na mawazo tofauti kabisa juu yake.
“Bwana Mkubwa, tafadhari usimkasirishe Bi. Njau tena. ” Maya akawa na wasiwasi. “Umesahau kuwa Bi Njau ndiye aliyekutibu ugonjwa wako? Kama isingekuwa kwa Bi Njau kukutana na wewe katika hospitali moja ya wagonjwa wa akili kama wewe, usingekuwa na ujasiri wa kutosha

kusimama hapa leo ukiwa mzima hivi."
“Hiyo ndiyo sababu niliamua kumuoa, lakini yeye ndiye aliyefanya mambo ya hovyo,” Alvin alisema kwa uchungu, “Sasa, nimekuwa kicheko miongoni mwa kila mtu kwenye jiji hili. Wakati polisi walipofunua uozo wako wakati wa harusi yetu, nilivumilia na kukusamehe. Lakini kwa nini usiniruhusu niende? Kama si kifo cha Hisan, ungeendelea kufanya naye matendo hayo mabaya. Sarah, usinichukulie kama mjinga.”
Uso wa Sarah ukageuka kuwa na huzuni. "Nisingefanya, Alvinic. Usinifikirie vibaya sana.” Ghafla alitupa blanketi sakafuni kama mwanamke mwendawazimu na kulia kwa uchungu. “Kwanini wewe
kunifanyia hivi? Hisan alinilazimisha kufanya hivy. Si kwamba nilifanya kwa sababu nampenda. Hata mimi ilikuwa ikiniumiza pia.”

“Bi Njau, usihangaike. Miguu yako imejeruhiwa.” Maya alimwambia Sarah na kumsihi Alvin bila utulivu, “Bwana Mkubwa, punguza sauti yako na umsikilize. Ikiwa ataendelea kuwa na tabia kama hii, miguu yake inaweza kuwa na ulemavu."
Kumtazama Sarah alivyokuwa mjeuri, Alvin alijihisi kuishiwa nguvu hadi kichwa kikaanza kumuuma. Aligeuka na kuwaambia wahudumu wa hospitali, "Mkandamizeni tu chini na mumfunge majeraha yake kwanza."
Wahudumu wa hospitali hiyo walitazamana kwa muda. Kisha, walifuata maagizo yake na kumkandamiza Sarah kitandani. Sarah, ambaye alikuwa amejifanya kushindwa kujizuia, hakuwahi kutarajia Alvin kuwa mkatili kiasi kile. Alifikiri kwamba angembembeleza. Sasa alipokuwa

akiomba wafanyakazi wamfunge, alikasirika sana hivi kwamba aliendelea kupiga mateke. Hata alimjeruhi mfanyakazi wa hospitali kwa teke lake.
Alvin alimwendea na kumshika mguu wake mmoja ili daktari ampake dawa kwenye majeraha yake.
 Hata hivyo, daktari alipomaliza kumpaka dawa, Sarah aliivua bandeji. Alisema katikati ya kilio chake, "Hapana. Bila wewe, bora niwe kilema. ”
Baada ya kuchokozwa tena na tena, Alvin alipandwa na hasira. “Basi, endelea na uwe kiwete. Sihitaji kuwajibika kwa maisha yako.”
"Alvin, hivi ndivyo unavyomjibu Sarah leo?" Rodney ambaye alikuwa ameingia ghafla, alitokea kusikia maneno ya Alvin na akashindwa kujizuia mara moja. “Ni mwanamke wako! Yeye ni mchumba wako! Unapaswa kuchukua jukumu kwa

ajili yake." Rodney alimvuta Alvin pembeni. Huku akiwa amekata tamaa, alimuelekeza Sarah pale kitandani ambaye alikuwa ameumia sana. “Umesahau kuwa uliahidi kumtunza? Na hivi ndivyo ulivyomuumiza?”
“Nimemuumiza vipi?” Papara za Alvin zilikuwa zimefikia kikomo. "Rodney Shangwe, wewe si mimi. Hujui lolote.”
“Ninachojua ni kwamba ikiwa hutamuoa Sarah, sifa yake itaharibika milele,” Rodney alijibu kwa hasira, “Anakupenda. Unadhani alifanya mambo hayo yote makusudi? Yeye ni mwathirika. Zaidi ya hayo, bado unajihusisha na Lisa, lakini Sarah hakusema lolote. Ni nini kinakupa haki ya kumkosoa?”
“Umemaliza?” Alvin alishindwa kujizuia. “Nimesema mimi na yeye hatuwezikuendelea tena. Sina mjadala

kwa hilo.”
“Umekuwa naye kwa zaidi ya miaka kumi. Ikiwa sio wewe, basi ni nani anayepaswa kuwajibika kwa hilo?" Rodney aliuliza kwa hasira.

Kwa mara ya kwanza maishani mwake, Alvin alihisi kuwa uhusiano wake na Sarah ulimfanya ajisikie kuchoka kabisa. Hakutaka tu kumuoa tena Sara. Ni nini kilmpa Sarah haki ya kumlaumu? Je, yeye ndiye aliyekuwa ametuma mtu wa kumteka nyara Sarah huko Garisa? Je, yeye ndiye aliyewafanya Sarah na Hisan walale pamoja? Hapana.! "Rodney, ikiwa unampenda sana, muoe wewe. Usije kwangu kila wakati ili kunilazimisha niwajibike kwake.” Alvin alipiga hatua kuelekea mlangoni huku akihisi kuvuta sigara.
Baada ya kuutazama uso wa Sarah uliopauka, Rodney alishindwa kujizuia

kumfuata Alvin nje. Akamshika mkono Alvin na kumnong'oneza, “Unadhani sitaki kumuoa? Jambo ni kwamba anakupenda wewe tu.
 Wewe ndiye anayetaka kuwa naye. Alvin, huwezi kumsukumia Sarah kwa mtu mwingine kwa sababu tu hutaki kuwa
naye.
 Yeye ni binadamu, na anakupenda kwa moyo wake wote.”
“Simpendi tena.” Alvin aliinua kichwa chake ghafla. Huku mikondo ya hasira ikitiririka katika macho yake yaliyozama ndani, alionekana kama simba aliyekasirishwa.
"Umesema nini?" Rodney alipigwa na butwaa.

“Unaweza kunichukulia kama mpuuzi. Hata hivyo, haiwezekani nimuoe tena,” Alvin alisema kwa uthabiti.

“Wewe ni mtu wa ajabu kiasi gani!” Rodney alikasirika sana hadi akampiga Alvin usoni. “Lazima Lisa ndiye aliyekujaza upepo tena, sivyo? Nitamuua.”
Rodney aligeuka na kuwa karibu kuondoka. Hata hivyo, Alvin alimzuia na kumwonya bila huruma, “Huruhusiwi kumtafuta Lisa. Haina uhusiano wowote naye. Hata bila yeye, bado sitamuoa Sarah.”
“Usifikirie kunidanganya. Kila kitu kilikuwa sawa kabla ya Lisa kurudi. Nitahakikisha atalipia mateso ya Sarah.” Rodney hakuweza kuwa na wasiwasi kuhusu Alvin.
Wale watu wawili walisukumana na kusukumana kwenye korido. Hatimaye, Rodney alimpiga ngumi kwani hakuweza tena
kumvumilia.
 Hasira za Alvin zilikuwa

zimefika kileleni pia. Wawili hao walianza kupigana kwenye korido.
“Acheni kupigana! ” Chester, ambaye alikimbilia hapo baada ya kusikia habari hizo, aliwaamua haraka. “Nyinyi nyote ni watu mashuhuri. Hamuoni aibu kutazamwa kana kwamba ninyi ni wanyama?”
Wawili hao walishtuka. Hapo ndipo walipogundua kuwa kulikuwa na watazamaji wengi karibu nao.
 Kwa bahati nzuri, Ghorofa hiyo ilikuwa ya wagonjwa wa VIP, kwa hiyo hapakuwa na watu wengi. Wengi wao walikuwa madaktari.

“Endeleeni na kazi zenu. Ikiwa yeyote kati yenu atathubutu kueneza tukio la usiku wa leo, atafukuzwa kazi moja kwa moja,” Chester aliwaonya kabla hajautawanya umati.

Rodney, ambaye uso wake ulijeruhiwa, alitoa maneno ya kikatili kwa Alvin. "Ukithubutu kumwacha Sarah, hatutakuwa marafiki tena."
“Utajua mwenyewe.” Alvin alidumisha uso usio na huruma, jambo ambalo lilimfanya Rodney apate wazimu tena.
“Inatosha, Rodney. Haya ni mambo ya Alvin na Sarah. Kwanini unaendelea kujiingiza?” Chester alimwonya bila aibu, “Zaidi ya hayo, Sarah yuko wodini. Akijua kuwa nyinyi wawili mnampigania, lazima atavunjika moyo.”
Kwa mawazo ya Sarah, Rodney alishindwa hata kusema lolote. Vile vile, Alvin alikaa kimya huku akiwa amesimama upande mmoja.
Wakiwa wodini Sarah alisaga meno aliposikia wawili hao wakipigana.

Hakuwahi kufikiria kuwa Alvin angesema bila huruma kwamba hatamuoa.

Sura ya: 415
Kesho yake asubuhi, nyumbani kwa Lisa.
Lisa alipokuwa akiwaandalia Suzie na Pamela kiamsha kinywa jikoni, Pamela alipiga kelele kutoka nje
ghafla.
 Kisha, akaingia jikoni na simu yake. “Lisa, nitakuonyesha kitu. Usiwe na wazimu.”
Lisa alishika simu na kuitazama. Kichwa cha habari cha stori hiyo kilikuwa 'Sarah Ajeruhiwa, Bwana Kimaro Mara Moja Amkimbiza Hospitali. Kuvunjika Kwa Ndoa Yao-Tetesi Zilikoma.'
Alipobofya kufungua video hiyo,

mwandishi alitoa maelezo ya kina ya habari hiyo. “Harusi ya Alvin Kimaro na Sarah Njau ilighairishwa ghafla hapo awali, na hakukuwa na habari kuhusu ndoa hiyo kufanyika tena baadaye. Uvumi juu ya kutengana kwao umekuwa ukienea kama moto wa nyika. Hata hivyo, mwanahabari wetu aliyekuwa akifuatilia habari hizi kwa karibu usiku na mchana, alipata taarifa kuwa Sarah alikuwa amelazwa hospitalini jana usiku. Muda mfupi baadaye, Bwana Kimaro alikimbilia hospitalini huku akiwa na sura ya huzuni, pengine kwa sababu alikuwa na wasiwasi kuhusu hali ya Sarah. Hadi saa saba usiku mwanahabari wetu alimuona Bwana Kimaro akitoka hospitalini hapo kwa uchovu.”
Lisa alizima habari hiyo moja kwa moja. Kisha, akarudisha simu kwa Pamela. Uso wake ulikuwa shwari na usio na wasiwasi kana kwamba hakuwa

ameguswa na chochote kwenye habari hiyo.
"Uko sawa?" Pamela alimtazama Lisa kwa wasiwasi. Jana yake usiku, Alvin alikuwa amempa hata nyumba ya kuishi kumfanya atoke nje kumpisha Lisa, hivyo alifikiri alikuwa akisisitiza kurudiana na Lisa. Hata hivyo, bado aliishia kwenda kumtafuta Sarah. Hata mgeni kama yeye angekasirika juu yake.
"Bila shaka, sina cha kunifanya nichukie. Lakini nimemdharau mtu huyu asiye na aibu.” Lisa alicheka sana. Jana yake usiku, Alvin hata alimtumia selfie ambayo alipiga nyumbani, na kweli alimuamini.
 'Wa Kwako Pekee'? Nenda kuzimu!
Naam, ilikuwa ni kofi usoni kwake. Ilimfanya atulie na kuwa macho zaidi. “Wacha tupate kifungua kinywa. Baada

ya hapo, nitampeleka Suzie shule.”
Lisa alitenga kifungua kinywa mezani. Baada ya kifungua kinywa, alimkimbiza Suzie hadi shule. Alipomshusha Suzie alikutana na Sheldon aliyekuwa akimshusha Lucas getini.
"Asante tena, Anko Sheldon." Lisa alimshukuru. Ili kumzuia Lucas asishukiwe, Joel alimwomba Sheldon ajifanye kuwa babake Lucas. Kwa bahati nzuri, Sheldon alionekana kama Joel, kwa hivyo hakuna mtu aliyemshuku.
“Unakaribishwa sana. Ni kwa sababu ya baba yako kwamba nilifanikiwa kurudi Ngosha Corporation na kuwa meneja,” Sheldon alijibu huku akitabasamu.
Lisa alitabasamu. Akainama na kumbusu Lucas kwenye paji la uso. "Lucas, hujani’miss?"

“Mimi sio Suzie.” Sura ya kiburi ilivuka uso wa Lucas. Hata hivyo, alinyoosha mikono yake kumkumbatia Lisa ili kupata upendo wa mama
yake.
 “Nitaongozana na wewe kula chakula cha jioni kwa babu yako usiku wa leo,” Lisa alisema kwa upole.
“Mama, nataka kwenda na mimi kwa babu” Suzie alifoka.
"Hapana. Sasa kwa kuwa wewe ni wa familia ya Kimaro, watu watakushuku ikiwa utaendelea kukaa nami kila wakati,” Lisa alimuonya.
Baada ya kuwaacha Suzie na Lucas shuleni, alipokea ujumbe wa WhatsApp kutoka kwa 'Ni Wako Pekee. [ Darling, umempeleka Suzie shule?]
Lisa aliinamisha kichwa na kuutazama. Baada ya hapo, alimblock tena.

Alvin aliendesha gari hadi ofisini baada ya kutuma ujumbe. Akiwa njiani kwenda huko, aliiangalia WhatsApp yake mara kwa mara. Hakupata jibu kutoka kwa Lisa hata baada ya kufika ofisini.
Kwa hasira, akamtumia ujumbe mwingine. [Uko bize na nini? Kwanini hujibu ujumbe wangu?]
Lakini, ujumbe wake ulionyesha tiki moja tu kwa muda mrefu, kwa maana kwamba haujaenda. Wakati huo, aligundua kuwa hakuweza kuona picha yake ya profile tena.
 Alvin alikosa la kusema.
Hii ilimaanisha nini? Jana yake usiku, aliweza kuona picha yake ya profile na meseji zake zilionyesha kupe mbili. Je, alikuwa kamblock tena? Kwa namna fulani, alipata hisia inayowaka katika kifua chake, ambayo pia ilibeba dokezo

la utusitusi, manung'uniko, na kuudhika.
Wakati huo huo, Hans aliingia. "Bwana Kimaro, tafadhali saini hati hii haraka iwezekanavyo."
Alvin alimkodolea macho Hans kwa huzuni. Hans alikosa la kusema. Alikuwa amefanya kosa gani? Alichokuwa anaomba ni saini tu. Hakika, kuwa Msaidizi Mkubwa wa Alvin Kimaro ilikuwa inazidi kuwa ngumu.
"Nipe hati." Alvin alifungua mdomo wake taratibu huku akimwangalia kwa jicho la kifo.
Hans akamkabidhi. Ilikuwa tu baada ya Alvin kusaini ndipo Hans alisema, "Halafu, kuna jambo moja zaidi, Bwana Mkubwa. Umetoa habari kuwa ulimtembelea Sarah hospitalini jana usiku?” Hans akabofya habari ile na kumuonyesha Alvin. "Sasa kwa kuwa

unamfuatilia Bi. Jones, nadhani akiona kipande hiki cha habari, anaweza kuhisi... kukatishwa tamaa."
“Mbona hukuniambia mapema?” Baada ya Alvin kuitazama video hiyo, uso wake uligeuka kuwa na huzuni moja kwa moja. "Ni mwandishi gani?"
“Ni ripota kutoka Udaku Live. Mtandao huu wa habari kila mara huripoti mambo madogo madogo yanayotokea katika jamii. Kila mara kuna wanahabari wanaokesha kwenye majumba ya umma, kama hospitalini, klabu, madukani, polisi na kwingineko wakiwinda habari za udaku.”
Alvin akauma meno. “Ninakupa nusu ya siku ili kufanya mtandao huu wa habari kutoweka. Wakati huo huo, hakikisha habari zote za jana usiku zinafutwa. Pia, waonye makampuni mengine ya habari kwamba yatakabiliwa na matokeo

mabaya ikiwa yatathubutu kuripoti habari zinazonihusu bila ridhaa yangu.”
“Sawa.” Hans pia alihisi kuwa Udaku Live ilikuwa imejitakia kifo.
Baada ya Hans kuondoka, mara moja Alvin aliendesha gari hadi Mawenzi Investments, na kukuta Lisa alikuwa bado hajafika.
Amba alikerwa na jinsi Alvin alivyokuwa akitamba kwenye ofisi ya Lisa. Hata hivyo, kutokana na utambulisho wa Alvin, hakuwa na jinsi zaidi ya kummiminia kikombe cha kahawa ya moto. " Mwenyekiti Jones huwa haji ofisini kila siku. Yeye hufuata ratiba yake binafsi wakati mwingine." Amba alimwambia.
"Mpigie simu na umwombe aje hapa," Alvin alisema kwa sauti ya ukali.

Amba alimpigia Lisa mbele yake. "Mwenyekiti Jones, Bwana Kimaro yuko hapa na anasema kwamba anataka kukutana nawe."
“Nina shughuli nyingi sana siwezi kumsikiliza. Mwambie aende kuzimu.” Lisa alikata simu mara baada ya kumaliza sentensi yake.

Uso wa Alvin ukageuka kwa huzuni mara moja. Amba hakuthubutu kucheka kwa sauti kubwa. Kwa bahati, Alvin aliondoka muda mfupi baadaye ndipo alipoachia kicheko chake hadi mwisho.
Mchana, Alvin alikwenda hospitali tena wakati Rodney akiwa
hayupo.
 "Alvinic, uko hapa." Mara Sara alipomwona, macho yake yaling'aa.
Wakati habari hiyo ilipotolewa asubuhi,

wale wasichana matajiri huko Nairobi ambao walimkwepa Sarah baada ya kusikia ameachana na Alvin, walianza kumpigia simu mara moja kutuma salamu zao. Wengi wao walikuja kumtembelea Sarah asubuhi, na kulikuwa na aina tofauti za vyakula na vinywaji kwenye meza.
Wakati huo, Sarah alikuwa ameridhika sana. Kwa hivyo, hakuweza kuruhusu kumwacha Alvin aende.

 "Unajisikiaje?" Alvin aliuliza kwa sauti ya chini.
"Miguu yangu bado inauma. Daktari alisema mishipa yangu imejeruhiwa.” Sarah alilitazama jeraha lililo pembeni ya mdomo wake. “Samahani, Alvinic. Kwa sababu yangu, uligombana na Rodney. Hukuumia? Ngoja nikuwekee dawa.”

"Hakuna haja." Alvin akatoa hati. “Sarah, nimekuja hapa leo kukuwekea jambo bayana. Mimi...”
“Alvinic, sijisikii vizuri. Hebu tuzungumze kuhusu hilo wakati fulani baadaye.” Mara Sarah alipoona hati miliki kwenye folda, alihisi kuzama ndani kabisa. Haraka akajifanya kujisikia vibaya na kujilaza.
TUKUTANE KURASA 416-420
ONYO: Ni marufuku kusambaza, kukopi wala kuuza kazi hii kwani endapo kama tutakubaini basi sheria itachukua mkondo wake (By: Official Dully)
 
LISA KITABU CHA NANE (9) SIMULIZI........................LISA KURASA.................416 - 420
PRESENT: SIMULIZI ZA DULLY

Sura ya: 416
"Sarah, acha kukwepa jambo hili." Alvin hakujisikia tena kuliburuza jambo lile, kwa hiyo alitenda bila huruma. "Hii ni hati miliki ya jumba la Oasis, ni lako kuanzia leo. Hapa kuna kadi yenye dola milioni 50 ndani, ambazo zinatosha kwako kuishi maisha ya anasa mpaka utakapotoweka duniani. Kwa hayo, naomba uniache huru!”
"Hapana. Sitaachana na wewe. ” Sarah alimwaga thermos ya maji ya moto kando yake kwa fadhaa na hivyo kuunguza mkono wake.
“Bi Njau...” Maya alishtuka sana hivi kwamba mara moja akabonyeza kengele kumwita daktari.
 “Mkono wangu unauma. Unauma sana.” Sarah alianza kulia kwa uchungu.


Maya alimshauri Alvin, “Bwana Mkubwa, Bi Njau bado hajapata nafuu. Kwanini usisubiri hadi apone ndiyo umwingizie mambo mengine?”
Kama hili lingetokea wakati ule, Alvin angevumilia. Hata hivyo, Sarah alikataa kuukubali ukweli huo na aliendelea kuzua fujo tangu jana yake usiku. Zaidi ya hayo, Alvin alikuwa amekaa usiku kucha akifanya kazi jana yake na hakupata usingizi. Huku hisia za kila aina zikimtawala, hakuwa na subira.
“Sarah, usiende mbali sana. Hatuwezi kurudiana pamoja kamwe." Alvin aliiweka ile hati kabla hajageuka na kuondoka. Kila alipomuona Sarah akifanya vituko sasa, kwa namna fulani alikuwa na hamu kubwa ya kukimbia. Pia ilichochea nia yake ya kumaliza uhusiano wake na Sarah.
Wakati analia, Sarah alivunja vitu

vingi.
 Rodney alipofika, aliumia sana kuona mikono yake ikiwa imevimba.
“Rodney, Alvinic ameamua kuniacha. Alinipa vitu hivi na kuniacha.” Sarah alianguka mikononi mwake na kutokwa na machozi. “Mimi ni nani kwake? Mimi ndiye mtu ninayemjali zaidi. Sijali hata utambulisho wake wala utajiri wake.”
"Ameenda mbali sana." Kuangalia nyaraka hizo, Rodney alihisi kwamba Alvin alistahili kufa. Angewezaje kumchukulia Sarah kama jinsi Chester alivyocheza na wale wanawake huko nje? “Sarah acha kulia. Nitashughulika naye kwa niaba yako.” Rodney alikunja ngumi. “Kama Alvin atakuacha, nitakuoa. Sitakuacha uwe kicheko. Ninatoka kwa familia ya Shangwe. Ingawa sina ushawishi mkubwa kama Alvin, familia yangu ina hadhi ya juu pia.”

“Rodney...” Sarah aliduwaa kwa muda. Kisha akatikisa kichwa bila kuamini. "Hapana. Ninawezaje kukuumiza hivi? Zaidi ya hayo, familia yako haitakubali.”
"Mradi nimeamua mimi, familia yangu haiwezi kufanya chochote." Rodney alimfuta machozi yake. "Sarah, nitakuwa karibu nawe kila wakati. Ikiwa unamtaka Alvin, nitafanya chochote ninachoweza kumfanya awe wako tena. Ukiamua kuachana naye, nitakuoa.”
“Asante Rodney.” Sarah akajishikashika mikononi mwake na kulia kwa uchungu.
Sarah alitabasamu kidogo bila Rodney kutambua. Alijiona mwenye bahati kuwa na Rodney kama hifadhi yake. Rodney angeweza asiwe mkuu kama Alvin, lakini mara tu Baba mdogo wake angechaguliwa kuwa Rais anayefuata, Shangwe ingekuwa kwenye kilele cha mamlaka yao.

Wakati huohuo, msaidizi wa Rodney akaingia. “Oh hapana, Bwana Shangwe!”
“Kuna nini?” Rodney alimtazama kwa hasira.
"Angalia, Bwana Shangwe." Akiwa na uso ulioduwaa, msaidizi wake alichukua simu na kumuonyesha. "Mzee Shangwe alihojiwa kwenye ofisi za Shangwe Corporation hivi sasa."
Rodney alibofya kufungua video na kumtazama babu yake akisema, “Takriban miaka 20 iliyopita, niliamua kugawanya mali ya familia ya Shangwe miongoni mwa watoto wangu. Kwa bahati nzuri, watoto hawa hawajanikatisha tamaa kwa miaka mingi. Sasa kwa kuwa Jason anasimamia Shangwe Corporation, sina wasiwasi. Bado ninamiliki 30% ya hisa

za kampuni, ambazo zitapitishwa kwa wajukuu zangu Jessica na Carson katika siku zijazo.”
Mwandishi aliuliza kwa mshangao, "Lakini huna mjukuu anayeitwa Rodney?"
Mzee Shangwe alijibu kwa mkoromo, “Rodney ameniangusha. Hisa za Shangwe Corporation hazitakuwa na uhusiano wowote naye. Ikiwa anapanga kurithi mali ya familia ya Shangwe anaweza kuendelea na ndoto yake.”
Simu ya Rodney ilidondoka chini. Uso wake mzuri ulibadilika. Kisha, akasimama ghafla. "Sarah, nahitaji kwenda nyumbani sasa kwani kuna jambo limetokea."
Akili ya Sarah pia ilikuwa imechanganyikiwa. Hakuwa na hali ya kumshawishi Rodney abaki kabisa.

Muda mfupi uliopita, alifikiri angeolewa na Rodney ikiwa asingeweza kumrudisha Alvin.
 Baada ya yote, aliamini alikuwa mrithi wa Shangwe Corporation na mtoto wa Rais wa nchi wa baadaye. Haikuwa heshima kidogo kuliko kuolewa na Alvin. Lakini, kwa muda mfupi tu, Rodney aliondolewa na familia ya Shangwe kutoka kurithi hisa za kampuni ya familia yao. Bila msaada wa familia yake, Rodney, ambaye alikuwa na Osher Corporation tu, hakuwa chochote. Angekuwa na ndoa mbaya kuliko Cindy. Sarah alikuwa karibu kupata kichaa. Kwanini alikuwa na bahati mbaya?
Rodney alikimbia kurudi nyumbani mara moja.
 Kufika nyumbani, Mzee Shangwe na Jessica walikuwa wakizungumza juu ya mambo ya kampuni.

“Jessica, laiti ungekuwa mwanamume?! Una uwezo zaidi ya Rodney.” Wakati wowote Mzee Shangwe alipomsikiliza mjukuu wake akizungumza kuhusu kazi, alipata hisia.
“Babu, unasikika kana kwamba unatubagua sisi wanawake,” Jessica alisema kwa mzaha.
Wakati tu Mzee Shangwe alipokuwa karibu kuongea, Rodney aliinua mapazia na kuingia ndani. “Babu, je, sina haki ya urithi wa Shangwe Corporation pia? Kwanini ulininyima sifa?”
"Kwa sababu wewe ni mjinga sana." Ilikuwa kana kwamba Mzee Shangwe alitarajia kuonekana kwake, na akaongeza kahawa kwenye kikombe.
Alikuwa mjinga sana? Damu ya Rodney ilichemka kwa hasira. “Mimi ni mjinga

vipi? Tangu nilipozaliwa, nimekuwa mwanafunzi wa haraka zaidi kati ya kila mtu katika familia ya Shangwe kwa chochote ninachojifunza. Mwaka niliofanya mtihani wangu wa mwisho, matokeo yangu yalishika nafasi ya tatu kati ya nchi nzima. Nilisoma hata katika chuo kikuu cha juu zaidi ulimwenguni, Havard. Ulisema hata mimi nina akili kuliko Uncle wangu."
Mzee Shangwe alicheka kijeuri. “Ndio maana nikasema wewe ni mjinga. Bado hujatambua sababu ya
kukukemea.
 Hakika ulikuwa mwerevu ulipokuwa mdogo, lakini unakuwa mjinga kadri unavyokua mkubwa. Sijisikii raha kukupa hisa za Shangwe Corporation. Isipokuwa ... kama utaoa kulingana na mpango wangu.”
Hapo ndipo Rodney alipogundua. "Kwa kusema wazi, hii ni mbinu yako tu ya kunilazimisha kuoa."

“Hapana, hii si mbinu. Ni nafasi yako pekee.” Mzee Shangwe alikunywa kahawa huku akisema kwa utulivu.
"Sitafuata mipango yako na kuoa mwanamke ambaye simpendi." Rodney alifikiria kwa muda na ghafla akasema, "Lakini ninaweza kuoa mke na kukufanya kupata vitukuu hivi karibuni."
“Humaanishi kwamba unamuoa Sarah, sivyo?” Jessica aliuliza.
“Sarah ni mwanamke mzuri. ”...
Mzee Shangwe alitupa kikombe chake sakafuni kabla Rodney hajamaliza kusema. "Ukithubutu kumuoa Sarah, usiwahi kukanyaga kwenye familia ya Shangwe.”
“Babu.” Rodney alishtuka na kukasirika. “Ulisikiliza maneno ya watu, sivyo? Je,

si wewe uliyesema kwamba tuamini tunachokiona na sio tunasikia nini? Sarah hajawahi kunichukulia kama mbadala.”
Jessica alidhihaki. “Ikiwa hajakuchukua kama mbadala, kwanini atataka umuoe baada ya Alvin kumkataa?” Hakuweza kuelewa ni kwanini alikuwa na kaka mjinga namna hiyo.
"Mimi ndiye niliyempendekeza ..."
"Nyamaza na upotee." Mzee Shangwe aliogopa kwamba hasira yake ingeweka afya yake hatarini ikiwa angemtazama Rodney zaidi.
 “Usiongee nami, nimeamua.” Baada ya hapo, Mzee Shangwe aliondoka.
Sura ya: 417
Jessica alimtazama Rodney akiwa hoi. “Babu yuko serious. Unapaswa kufikiria

hili kwa undani. Unaweza kwenda umbali gani bila usaidizi wa familia ya Shangwe?"
“Nimetafakari. Piga, ua, galagaza, sitaoa mtu ambaye simpendi,” Rodney alisema kwa hasira.

Sura ya Jessica ilibadilika, na alama ndogo ya huzuni ikaangaza machoni pake. Kisha, alitoka nje ya sebule na kuondoka pia.
 Rodney alisimama hapo kwa muda kabla ya kutoka nje ya nyumba ya familia ya Shangwe kwa hasira.
Alipofika kwenye gari, alipokea simu kutoka kwa Meneja Mkuu Stevens. "Bwana Shangwe, ununuzi wa kampuni yetu ya Umoja Group ya Tanzania umeshindikana."
"Nini kimetokea? Hukuchukua miaka

miwili kujiandaa kwa ununuzi wa Umoja Group?” Rodney alihisi hasira isiyoelezeka ikimwagika tena.
Hapo awali, alitaka kuchukua fursa ya kununua Umoja Group ili kuiwezesha Osher Corporation iingie katika uzalishaji wa shampoo na hata kuipanua zaidi kimataifa. Kwa njia hiyo, asingehitaji kuwa na wasiwasi na ushindani wa SE Group hata
kidogo.
 Ikiwa kampuni ilitaka kukua zaidi, ilibidi kupanua aina ya bidhaa. Alidhani kwamba kwa kuinyakua Umoja Group bila shaka ingekuwa mwanzo wa mafanikio.
Meneja Mkuu Stevens alicheka kwa uchungu.” Bwana Shangwe, Umoja Group awali ilikubali kampuni yetu kuinunua. Lakini baada ya habari kuwa familia ya Shangwe imeghairi haki yako ya urithi, Umoja Group ilizingatia. Waliogopa kwamba maendeleo ya siku

za usoni ya Osher Corporation huenda yasiwe mazuri bila usaidizi wa Shangwe Corporation, kwa hiyo wakakubali kuiuzia kampuni nyingine kubwa nchini Tanzania.”
“Bullsh*t, kwani nilifika hapa kwa kutegemea Shangwe Corporation? Nilijitegemea.” Bahati haikuwa upande wa Rodney siku hiyo.
“Bwana Shangwe, jambo muhimu zaidi sasa ni kukuza umaarufu wa bidhaa ya Osher Corporation ya kutunza ngozi nchini Kenya.
 Kuna uvumi kwamba Pamela na meneja mkuu wa SE Group wanapanga kushirikiana. Mara tu watakapounda bidhaa mpya, nafasi ya Osher Corporation itaporomoka. Tunaweza hata kuondolewa sokoni.” Meneja Mkuu Stevens aliendelea, "Bidhaa zinaboreshwa na kubadilishwa haraka sana siku hizi. Tunahitaji mkemia bora na wa hali ya juu wa

vipodozi. Kwa kuwa umepoteza usaidizi wa familia ya Shangwe, utakuwa kicheko miongoni mwa familia tajiri nchini Kenya mara tu Osher itakapoanza kuyumba.”
Rodney alishika simu yake kwa nguvu. Mishipa ya nyuma ya mkono wake ilikuwa ikipiga. Hakuwahi kufikiria kwamba yeye, aliyependelewa katika familia ya Shangwe, angekuwa katika hali kama hiyo siku moja.
Osher Corporation ilikuwa damu yake, jasho, na machozi. Ikiwa angepoteza Osher Corporation, angeachwa bila chochote.
"Bwana Shangwe, haijalishi ni nini, lazima umsihi Pamela arudi kwenye kampuni," Meneja Mkuu Stevens alisema kwa uchungu.
 "Tumefikiria kila njia iwezekanavyo. Lakini mwaka huo ulikuwa ni wewe...”

"Nyamaza. Inatosha, nimekupata.” Rodney nusura aivunje simu
yake.
 Hakuwahi kufikiria kuwa ipo siku ambapo ingembidi kumsihi Pamela. Zaidi ya yote, mwanamke huyo hata aliharibu sifa yake siku chache zilizopita, lakini bado alionekana kuwa tegemeo lake. F*ck.

•••
Usiku, Lisa alikula chakula na Joel na Lucas kwenye nyumba ya familia ya Ngosha. Joel na Lucas walipojua kwamba Lisa angekaa usiku kucha, walisisimka. Jumba hilo kubwa lilikuwa tupu sana kwa wao wawili tu na watumishi wachache.
Saa 8:00 usiku, Lisa alipokuwa karibu kujaza sinki la bafuni kwa ajili ya kumuogesha Lucas, wasimamizi wa jengo iliyomo nyumba yake huko Karen Estate walimpigia simu ghafla.

“Bi. Jones, kwa mujibu wa jirani yako, kuna mwanaume amekuwa akikungoja mlangoni kwako tangu jioni hii na bado hajaondoka. Inaonekana ni... mpenzi wako wa zamani. Tuna wasiwasi kwa kuzingatia kuwa juzijuzi hapa ulivamiwa nyumbani kwako.”
“Mpenzi wa zamani?” Pembe za mdomo wa Lisa zilitetemeka. Jirani yake alikuwa amemwona Alvin akiingia na kutoka nje ya mlango wake mara chache kabla. Hata hivyo, hakuwa amejitokeza kwa muda sasa. Jirani yake lazima alihisi Alvin kama mpenzi wake wa zamani, ambaye waliachana naye.
"Ndiyo," wasimamizi walisema, "bila shaka, tunakutaarifu tu. Hatuwezi kuelewa kinachoendelea. Ikiwa kuna mzozo au usumbufu wowote, kati yenu, unaweza kuchagua kuripoti hili kwa polisi. ” Baada ya kukata simu, Lisa alipiga simu mara moja polisi.


•••
9:30 pm
 Alvin aliuegemea mlango wa nyumba ya Lisa na kuitazama simu yake mara kwa mara. Kwanini mwanamke huyo alikuwa bado hajarudi wakati tayari ilikuwa usiku sana? Je, anaweza kuwa kwenye miadi na mwanamume mwingine tena? Laiti Alvin asingefuatilia mahali alipo Erick kabla na kugundua kuwa anafanya kazi kwa saa za ziada kwenye kampuni yake usiku huo, asingesubiri hapo kipumbavu kwa saa saba. Hakuwahi kumngoja mwanamke kwa muda mrefu hivyo awali.
Ding. Sauti ilitoka kwenye lifti. Polisi wachache walimwendea wakiwa wamekunja uso. "Unafanya nini hapa?” Alvin alipigwa na butwaa.
“Ondoka sasa hivi au tutakupeleka kituo

cha polisi.” Polisi walisema kwa uthabitii, “Mmiliki wa hii nyumba tayari imetoa taarifa polisi. Alisema wewe ni mume wake wa zamani ambaye umekuwa ukimsumbua sana hata baada ya talaka hata hathubutu kurudi nyumbani.”
“Alipiga simu polisi?” Uso mzuri wa Alvin ulitetemeka, na akatoa sura ya kutisha. Bila kujua, iliwafanya polisi wahisi kwamba alikuwa mtu mkatili na mwenye tabia mbaya.
“Acha kuongea upuuzi. Kwa hiyo asipige simu polisi na akuache umsumbue?” Polisi mmoja alianza kumsomesha Alvin. “Nimeona wanaume wengi kama wewe ambao bado wanawanyanyasa wake zao hata baada ya kuachwa. Ngoja nikushauri jambo moja. Kwa kuwa tayari mmeachana, ishi maisha yako mwenyewe. Bado wewe utajiita ni mwanamume utaendelea

kumng'ang'ania mwanamke?"
"Vizuri sana." Alvin alikunja ngumi na kuelekea kwenye lifti kwa hatua ndefu.
 Wakati anaingia kwenye lifti, alisikia polisi wakizungumza.
“Hasira za huyu jamaa zinaonekana ni mbaya sana. Ndiyo maana alitalikiwa na mwanamke.”
Baada ya kutoka kwenye lifti, Alvin alitembea hadi sehemu ya maegesho. Akaufunga mlango wa gari kwa nguvu na kupiga simu kwa jamaa mmoja wa ONA.
 “Nitafutie eneo alilopo Lisa. Nataka kujua yuko wapi.”
Muda mfupi baadaye, alitumiwa anwani: [Lisa yuko kwenye jumba la kifahari la familia ya Ngosha.]
Uso wa Alvin ulilegea kidogo. Bahati

nzuri Lisa hakuwa kwenye uchumba na mwanaume mwingine. Kama sivyo ... angeweza kumuua mtu huyo.
•••
Lisa alilala vizuri na Lucas. Asubuhi iliyofuata walipoamka ili kupata kifungua kinywa, mtumishi aliingia na kusema, “Bwana Ngosha, gari moja lilifika mlangoni mwendo wa saa nne usiku jana na limeegeshwa hapo tangu wakati huo. Mlinzi alisema taa kwenye gari ziliwashwa mara kadhaa usiku, hivyo kuna mtu ndani. Gari hilo ni toleo la kipekee.
 Kwa sasa... ni Alvin pekee aliye nayo katika Kenya yote.”
Uso wa Joel ukabadilika ghafla. “Mbona anasubiri mlangoni kwetu? Sijawahi kuona mtu asiye na haya kama huyu maishani mwangu.”
Lucas alimtazama Lisa kwa woga. “Mama...”

“Usijali. Hebu tupate kifungua kinywa chetu kwanza. Nitakutana naye mara baada ya kula.” Kwa hayo, Lisa alijaza sahani za Joel na Lucas.
“Lisa, nisikilize. Kaa mbali na huyo jamaa. Erick ni mzuri pia. Unaweza kumfahamu zaidi,” Joel alimshauri kwa dhati. “Alvin ni fisadi asiyebadilika. Sarah asingepata matatizo, hata asingegeuka na kukutafuta.”
“Najua. Baba, acha Uncle Sheldon ampeleke Lucas shule, na usiruhusu mtu yeyote kujua,” Lisa alikumbusha.
Sura ya: 418
Baada ya kiamsha kinywa, Lisa alitoka kwenye lango kuu la jumba la kifahari la familia ya Ngosha.
Mara Alvin akafungua mlango wa gari na kuelekea kwake. Kwa kuwa hakuwa

nyumbani kwa usiku mbili mfululizo, shati alilovaa lilikuwa limekunjamana, na kulikuwa na tongotongo usoni. Hata hivyo, hilo halikuathiri sura yake nzuri hata kidogo.
“Ulipiga simu polisi jana usiku?” Alvin alimkazia macho Lisa kwa mtazamo wa kutisha.
"Ndiyo.” Lisa alijibu kwa jeuri bila hisia yoyote ya hatia. “Uliendelea kusimama mlangoni kwangu, hukutaka kuondoka. Ulikuwa ni usumbufu mkubwa kwangu. Majirani wananiona mimi ni mtu wa ajabu sana.”
“Wewe...” kifua cha Alvin kilimtoka. Akiwa mwanamume aliyeheshimiwa sana, hakuwahi kudhalilishwa na mwanamke namna hiyo hapo awali.
“Mimi nini? Mimi si mtu ambaye umeniweka kwenye kiganja chako kama

simu yako. Kwamba muda wowote ukitaka kuitumia, unaitumia tu” Lisa alimkemea kwa ukali. "Nakumbuka nilikuambia waziwazi usiku uliopita, kwamba ikiwa utaenda kwa Sarah, hupaswi kujisumbua tena kunirudia."
Lisa alipokumbuka kuwa alimtumia selfie nyumbani kwake lakini akaenda kumtafuta Sarah dakika iliyofuata, alichukizwa naye sana.
“Mimi sikuwa na chaguo. Sarah alianguka chini kutoka kwenye ngazi siku hiyo, na akaumiza mguu wake. Ikiwa nisingeenda, angekataa kutibiwa.
 Mwishowe, nilienda na kumweleza mambo wazi. Unaona? Rodney hata alipigana nami kuhusu jambo hili.” Alvin alimnyooshea kidonda mdomoni. Alichoweza kufanya ni kujionea huruma huku akihema kwa maumivu. "Bado inauma sana."

"Nimekuvumilia sana Alvin, lakini hubadiliki. Wewe ni yule yule tu." Lisa alisema maneno hayo na kudharau.
Alvin alijikaza kwa muda kabla ya kusema kwa ujasiri, “Ndiyo, najua nimekuudhi babe. Uliniambia nisiende na mimi nikaenda. Lakini sikwenda kwa nia mbaya...”
“Nani babe wako? Angalia mdomo wako." Kichwa cha Lisa kilimsisimka kumuita babe wake,
Macho yake makubwa, ngozi laini, na midomo ya waridi yenye majimaji iliufanya moyo wa Alvin kuyeyuka. Iliyeyuka zaidi alipokumbuka emoji ya busu ambayo alimtumia. Alidhamiria kumfanya amsamehe siku hiyo, hata ikiwa ni lazima awe na uso wa jazba. Kisha, polepole angeonja ladha ya kumbusu. “Lisa, tayari nimeshamalizana na Sarah. Simpendi tena, na

haiwezekani nirudiane naye na kumuoa.”
Alvin alishika mikono ya Lisa na kuikamata kwa nguvu. Mtazamo wake wa kina ulikuwa mzito.
 Akili ya Lisa ilizunguka kwa muda.
 Alikumbuka siku za nyuma aliwahi kumtazama kwa dharau na kusema kwamba aliyempenda ni Sara. Kwa hiyo, alipomsikia akisema hivyo kutoka kwa midomo yake myembamba tena, hakuhisi kuguswa. Badala yake, alifikiri ni kejeli.
“Babe, unaweza kunipa nafasi nyingine?” Alvin alifikiri kukaa kwake kimya kunamaanisha kuwa ameguswa. Kwa hiyo, alinyoosha mikono yake na kutaka kumvuta kwenye kumbato lake.
Lakini, Lisa aliweka mikono yake kifuani mwake. “Alvin, sijui nikuamini tena au

nisikuamini. Nimeumizwa na wewe mara nyingi sana sasa. Ninaogopa kwamba nikianza kuwa na matarajio na wewe kwa mara nyingine, Sarah atakupigia simu tena au kukutishia maisha yake. Sijakaa nawe kwa muda mrefu, lakini wewe na Sarah mmefahamiana kwa zaidi ya miaka 10...”
“Hapana Lisa. Sitakuangusha tena.” Alvin akamkumbatia kwa nguvu. “Si unajua mimi ni mtu wa aina gani kwa sasa? Sitasema maneno kama hayo ikiwa sina uhakika wa hisia zangu.”
Uso wa Lisa ulizikwa kwenye kumbatio lake. Mahali ambapo hakuweza kuona, kulikuwa na dhihaka machoni pake. Alimfahamu vizuri sana. Aliweza kutamka maneno yoyote matamu akiwa katika mapenzi. Ndiyo maana alimwangukia tena licha ya kuumizwa naye mara kwa mara. Hata hivyo,

wakati hakuwa katika upendo, alikuwa jeuri, asiye na moyo, na mkatili.

“Babe...” Alvin alipomwona Lisa bado yuko mikononi mwake, wimbi la shauku lilimpanda. "Unadaiwa kunibusu." Baada ya hapo, aliinamisha kichwa chake na kumbusu.
Mkono ulifunika midomo ya Alvin kabla hajambusu Lisa. "Nilikubusu lini?" Lisa alishangaa. Alikuwa karibu kushindwa na ukosefu wake wa aibu.
“Usiku wa kuamkia jana. ” Alvin akatoa simu yake na kumuonyesha emoji ya busu ambayo alimtumia.
Uso mzuri wa Lisa ulishtuka alipoona emoji ya busu kwenye simu. Alifanya hivyo kwa kukurupuka tu kwa nia ya kumfanya mtu huyu amtamani. Hata hivyo, hakutarajia angekumbuka vizuri hivyo.

“Oh, nakumbuka. Lakini... ulienda kumtafuta Sarah mara baada ya kupokea emoji yangu?” Aliuliza huku akitoa tabasamu bandia.

"Hapana." Sura ya Alvin ilikakamaa, na akasema isivyo kawaida, “Nilienda kuoga maji baridi baada ya kuipokea.”
Kwa kuwa walikuwa watu wazima, Lisa alijikuta akielewa maneno yake mara moja. Macho yalimtoka kwa kutoamini kabla ya moyo wake kujawa na msisimko. Hakuwa na la kusema.
 Je! haikuwa emoji tu ambayo kila mtu alikuwa akitumia? Kwanini alikuwa na hisia nayo sana?
Lisa akageuza macho yake. "Ina maana kwamba utakuwa na deni langu nikikutumia emoji ya kukuchapa wakati ujao?"

“Hakika.” Alvin alitazama midomo yake kwa tamaa. Muda mrefu alikuwa akitamani kumbusu.
“Nadhani bado unaota. Siwezi kuendelea kupoteza wakati wangu na wewe. Naenda kwenye kampuni.” Lisa hakujali tena juu yake na akageuka moja kwa moja.
"Subiri, nitakupeleka ofisini kwako." Alvin akamshika mkono na kufungua mlango wa siti ya abiria.

Lisa alitupia macho kwenye kiti cha abiria. "Hapana. Sitaki kuketi mahali ambapo wanawake wengine wameketi hapo awali.” Baada ya hapo, alitembea kuelekea lango kuu la nyumba. Mlinzi tayari alikuwa amelisogeza gari lake getini.
 Lisa alifungua mlango wa gari na kuingia kwenye kiti cha dereva. Hata hivyo, mara moja Alvin aliketi kwenye

kiti cha abiria na kufunga mikanda yake ya usalama.
“Kaka mbona unanifuata? Lazima niende kazini.” Lisa alifoka.
“Nitakusindikiza kazini. Nataka kutumia wakati mwingi zaidi na wewe njiani." Midomo myembamba ya Alvin ilifunuliwa kwa tabasamu. "Nimegundua hata hewa ni tamu ninapokuwa na wewe."
Lisa alitetemeka. "Nyamaza."
Alvin alikunja uso huku akionekana kuwa na huzuni. Hakulala ndani ya gari usiku kucha ili tu aweze kusema maneno haya yenye mguso, ya kimahaba aliyokuwa akijifunza kwenye simu yake.
“Sawa, nitanyamaza. Lakini akili yangu imejaa sauti yako, kwa hiyo haijalishi

tunazungumza au la.” Alitabasamu kwa upendo.
Kona za mdomo wa Lisa zilimtetemeka huku akiweka mkono wake kwenye paji la uso. “Vipi kuhusu gari lako la thamani? Utaliacha tu hapa?"
“Umesema hutaki kulipanda, kwa hiyo silitaki tena. Nitanunua gari jipya.” Alvin akatoa simu yake na kumpigia Hans. Alitazama nembo kwenye usukani wa Lisa na kusema, “Nipatie Aston Martin.”
"Lakini umenunua gari lako muda si mrefu uliopita." Hans alishangaa.
“Siendesha gari hilo tena. Lisa halipendi, kwa hiyo hakuna haja ya kuwa nalo.”
Hans aONA ajabu. "Lakini Aston Martin itakuwa nafuu sana? Hailingani kabisa na hadhi yako.”

"Usijali. Lisa anaendesha Aston Martin pia. Kwa kuwa anaendesha gari nyeupe, unaweza kuninunulia nyeusi. Tutakuwa na magari yanayofanana.” Alvin alikata simu baada ya kusema hivyo. Kubadilishia gari kwake ilikuwa rahisi kama vile kubadilisha mboga tu.
Sura ya: 419
Lisa alizingatia sana kuendesha gari na kumwacha Alvin afanye chochote. Alipokuwa akiendesha gari, Alvin alisema, "Hii sio njia ya Mawenzi Investiments."
“Mm, naenda Ngosha Corporation. Sumu katika mwili wa baba yangu bado haijatoka, kwa hiyo naenda kwa kampuni yake kuangalia mambo yanavyoenda kidogo.”
Kikubwa ni kwa sababu Joel

alimwambia jana usiku kuwa Mzee Ngosha amekubali kumruhusu Melanie kurudi kwenye kampuni. Kwa hivyo, ilibidi aende kujionea yeye
mwenyewe binafsi mipango iliyokuwa inafanywa na Melanie. Vinginevyo, kampuni ya Ngosha ingekuwa kwenye vurugu kabisa kwa sababu ya Melanie na baba yake tena.
'Ikiwa utaenda kwenye kampuni hiyo, inamaanisha kuwa utaingilia masuala ya Ngosha Corporation. Utaweza kusimamia kila kitu?" Alvin alikunja uso aliposikia maneno yake. "Bado utakuwa na muda wa kuwa na uhusiano na mimi kweli?"
"Ni lini nilikubali kuwa na uhusiano na wewe?" Lisa alilalamika.
"Haijalishi unakubali au la kwa sababu hata hivyo nimekubali." Alvin alitabasamu.

Baada ya kumtazama kwa ukimya, Lisa hakuweza kupinga kusema, “Unaweza kurudi na kulala kidogo? Usije ukaniangukia tena na kuzimia.”
“Una wasiwasi na mimi?” Macho ya Alvin yakaangaza.
"Hapana, macho yako yamevimba sana. Inakufanya uonekane kama una uso wa panzi, na inaathiri sura yako. Lisa alimpa maneno yasiyo na huruma.
Alvin ghafla alishindwa cha kusema. Alikuwa na hamu ya kuitoa simu yake ili kujingalia usoni, lakini kiburi na heshima yake haikuruhusu hilo. Badala yake, aliweka tu uso wa kauzu.
Gari iliingia kwenye maegesho ya Ngosha Corporation.
 Lisa alipoegesha gari na kukaribia kushuka, Alvin alimshika na kusema kwa sauti ya

ukali, “Lisa, unaweza. unaniongeza kwenye mawasiliano yako ya WhatsApp? Niondoe kwenye blacklist pia. Usipofanya hivyo, nitakufuata kila uendako.”
Lisa akahema. Kisha, akamuongeza kwenye contacts zake za WhatsApp mbele yake na akaondoa namba yake blacklist. "Naweza kwenda sasa?"
“Sawa.” Alvin alishuka naye kwenye gari huku akiuliza. "Lisa, nilisikia Ngosha Corporation na Campos Corporation wanapanga kuanzisha ubia."
"Kulikuwa na habari hiyo hapo awali, lakini kwa kuwa niko hapa, sitakubali."
Alvin akaitikia kwa kichwa. "Campos Corporation sio watu wazuri. Katika miaka kumi ya ushirikiano waliokuwa nao na KIM International, kimsingi waliinyonya bila huruma. Kuwa

mwangalifu."
Lisa alishtuka, lakini aliitikia kwa kichwa. Baada ya kuingia kwenye lifti, aligundua kuwa Alvin bado alikuwa akisubiri nje. Aliinamisha kichwa chini na kutabasamu. Hakutarajia kuwa siku kama hiyo ingemjia.

Lifti ilipanda na kumuongoza moja kwa moja hadi kwenye ghorofa aliyofanyia kazi Joel. Msaidizi mpya wa Joel, Bwana Goleman, alikuwa akimngojea huko kwa muda. Lisa alipotokea, aliwaongoza wafanyakazi wa wa ofisi ya Joel mara moja na kusema, “Bi Mkubwa, Mzee Ngosha amemleta Melanie kwenye kampuni leo, na kwa sasa wanafanya mkutano.”
"Kwanini baba yangu hajui hili?" Lisa aliinua macho yake kwa mashaka. Ulikuwa uamuzi wa dakika za mwisho kutoka kwa Mzee Ngosha. Wasimamizi

wakuu wa kila idara na wanahisa wachache muhimu walikuwako kwenye mkutano huo. Watu wa Campos Corporation walikuwako hapo pia.
“Ongoza njia. Mimi pia nitaingia kwenye mkutano.” Lisa alikuwa na hisia mbaya. Aligeuka na mara akaingia kwenye lifti tena.

•••
Kwenye chumba cha mikutano
kwenye ghorofa ya 3, Jerome Campos alipomaliza hotuba yake ndefu, alisema, "Kila mtu, sote tunataka kupata pesa. Ikiwa tunataka kupata pesa zaidi, basi lazima tuingie katika sekta ya fedha. Sasa ni fursa nzuri zaidi ya kufanya hivyo. Ngosha Corporation imekuwa ikiendelea vyema katika miaka ya hivi karibuni, lakini bado iko nyuma ikilinganishwa na familia ya Kimaro na familia ya Shangwe. Babu, unaonaje?"
Akiwa hajasimamia masuala ya

kampuni kwa miaka mingi, Mzee Ngosha aliburutwa kwenye mkutano huo kwa lazima tu na Melanie.
Hata hivyo, hotuba ya Jerome ilikuwa imemgusa.
 Alikasirishwa zaidi na ukweli kwamba familia ya Ngosha haikuwa mojawapo ya familia tatu tajiri zaidi nchini Kenya.
“Mzee Ngosha, sema kitu. Tunaamini katika maoni yako. ” Bwana Parker, mmoja wa wanahisa, alimbembeleza. "Sasa kwa kuwa Mkurugenzi Ngosha amelishwa sumu na si mzima kiafya kama zamani, Kampuni ya Ngosha linaweza kukutegemea wewe tu."
“Ndiyo hivyo Mzee Ngosha. Rudi kwenye kampuni.” Wanahisa wachache walimshauri. "Campos Corporation imekuwa ikiendelea kwa kasi kwa miaka mingi, na wamepanda hadi kuwa kampuni ya pili kwa ukubwa nchini Kenya. Nadhani hatupaswi kukosa

nafasi hii ya kushirikiana nao.”
“Ndiyo. Bila kujali chuki za kibinafsi, kama si biashara ya mtandaoni ambayo tumeanzisha hapo awali na Campos Corporation, Ngosha Corporation isingekua haraka sana kwa miaka michache iliyopita. Mzee Ngosha, unapaswa kuongoza kampuni ya Ngosha kwenye utukufu wake tena."
Mzee Ngosha alichomwa moto mara moja na maoni hayo. Ingawa alikuwa amestaafu kwa miaka mingi, bado alikuwa na tamaa kama hapo awali. Sababu ya yeye kustaafu ni kutokana na matatizo yake ya kiafya. Hata hivyo, afya yake ilikuwa imeimarika kutokana na kupata nafuu kwa miaka hii yote, hivyo akaanza kuwa na tamaa tena ya kurudi kazini.
“Mzee Ngosha, ngoja nikuambie ukweli.” Bwana Parker alikwenda

upande wa Mzee Ngosha na kunong'ona, "Ingawa Mkurugenzi Ngosha alimteua Lisa kuwa mrithi wake, jina lake la mwisho bado ni Jones. Ngosha Corporation haiwezi kubadilisha jina lake kuwa Jones Corporation katika siku zijazo, sawa?”
Uso wa Mzee Ngosha ulibadilika. Ikiwa hakuna mtu ambaye
angechomekea jambo hilo, asingetambua kamwe.
Melanie alitabasamu. Aligeuza kichwa chake na kusema, “Babu, nimemsikia Jerome akitaja kuhusu kuanzisha ubia mara nyingi, na kwa hakika inawezekana. Hivi sasa, kuna watu wengi ambao wanataka kuwa wanahisa pia. Kama si ndoa yetu kati ya familia hizi mbili, Jerome asingeipa kipaumbele Ngosha Corporation kwa mradi mzuri kama huo. Lakini ili kuwekeza makumi ya mabilioni ya pesa katika mradi huu,

tutahitaji mtu shupavu kama wewe kufanya uamuzi.”
Mzee Ngosha alishusha pumzi ndefu kabla hajaipiga meza. “Sawa. Nimeamua, basi. ”
"Babu, umeamua nini?" Mlango wa ofisi ulisukumwa ghafla. Lisa aliingia kwa hatua ndefu huku akitabasamu. Alikuwa ndani ya blauzi nyeupe iliyomfanya aonekane hodari na mrembo kupita kawaida.
"Kuhusu kuanzisha ubia na Kampuni ya Campos. Nadhani ni jambo linalowezekana,” Mzee Ngosha alisema huku akitabasamu. "Lisa, kwanini uko hapa leo?"
“Baba alisema Melanie anarudi kwenye kampuni leo, kwa hiyo akaniambia nije niangalie. ” Lisa aliwatazama Melanie na Jerome kwa ufasaha. "Sikujua kuwa

dada yangu alikuwa amepanga kitu kizuri cha kufanya siku yake ya kwanza kurudi."
"Ninafanya tu kwa ajili ya maendeleo ya kampuni," Melanie alisema kwa unyenyekevu. "Mbali na hilo, Kampuni ya Campos tayari imekuwa ikitayarisha hili kwa nusu mwaka. Haiwezi kucheleweshwa tena.”
Macho ya Lisa yalikodoa. Melanie alikuwa mtulivu siku za nyuma, lakini siku hiyo, hakuweza kudumisha utulivu wake. Hakika alibadilika sana tangu Nina aende jela.
"Kwa hiyo umekubali, babu?" Lisa alimtazama Mzee Ngosha.
“Nimemsikia Jerome akieleza kwa undani sasa hivi, na nimeridhika kabisa. Tutapata faida halisi ya zaidi ya shilingi bilioni 10 katika mwaka wa kwanza.

Kwanini tusifanye hivyo?” Mzee Ngosha alijiamini sana.
Lisa alikunja uso. "Babu, wakati mwingine wakati mpango unasikika kuwa mzuri kupita kiasi, itakuwa rahisi ..."
Jerome aliingilia ghafla na kumkatisha. “Bi. Jones, sijawahi kukosa uhalisia. Huu sio ushirikiano wa kwanza kati ya Campos Corporation na Ngosha Corporation pia. Kila mtu yuko wazi juu ya mimi ni mtu wa aina gani, na mimi hutimiza ahadi zangu kila wakati. Baada ya yote, mafanikio ya familia ya Campos leo hayakuja bure. Naelewa una kinyongo na mke wangu, lakini, sio wakati wa kubishana juu ya chuki hizo ndogo linapokuja suala la mambo makubwa zaidi.”
Alichomaanisha ni kwamba ikiwa Lisa asingekubaliana na mpango huo,

ingekuwa ni kwa sababu hakuweza kumvumilia Melanie.
Ndani kabisa, Lisa alihema. Ujanja wa Melanie ulikuwa wa kiwango cha juu. Alikuwa amemshawishi kwa siri Mzee Ngosha kuja kwenye kampuni na kumfanya chambo cha kupitisha uamuzi haramu ya familia ya Campos. Ikiwa Lisa asingeunga mkono uamuzi wake, angeonekana kuendekeza chuki binafsi.
Sura ya: 420
Hata hivyo, Lisa bado hakukubaliana na ushirikiano na Campos Corporation. “Babu, bado naona ni vyema kulichunguza jambo hili kwa kina. Kwa mfano, baada ya ubia kuanzishwa, nani atatoa timu ya wataalamu? Nani atakuwa mkurugenzi mkuu? Ngosha Corporation haifahamu vyema sekta ya fedha, kwa hivyo hatuna rasilimali zinazohitajika pia. Iwapo tutaingia katika

sekta hiyo kwa haraka...”
"Unamaanisha nini? Unahoji uamuzi wangu?” Maneno ya Mzee Ngosha yalikuwa makali. “Lisa, nimekuwa katika ulimwengu wa biashara kwa makumi ya miaka. Nina uzoefu zaidi kuliko wewe. Hakuna haja ya wewe kuingilia tena maswala ya Ngosha Corporation."
“Babu, sio kwamba sikuamini. Nadhani ni bora tujadili hili baba yangu atakaporudi...”
Jerome alisema kwa kejeli, “Bi. Jones, unamaanisha kwamba Mzee Ngosha hana maono kama baba yako?”
Mzee Ngosha alikasirika aliposikia hivyo. "Nimesimamia Ngosha Corporation kwa makumi ya miaka. Hakuna anayejua ulimwengu wa biashara vizuri kuliko mimi. Jambo hili limeamuliwa. Lisa, kwa kuwa huijui

Kampuni ya Ngosha vizuri, unapaswa kuja hapa kujifunza kidogo siku zijazo.” Alisimama baada ya kusema. "Sawa, hiyo inahitimisha mkutano wa leo."
"Babu, nitakupeleka nyumbani." Melanie alimfuata mara moja. Alipotoka, alimtazama Lisa kwa siri.
 Wafanyikazi na wasimamizi wakuu waliondoka polepole. Hakuna hata mmoja wao aliyemjali Lisa.
Jerome alienda kando yake huku akitabasamu na kusema, “Kwa hivyo itakuwaje kama wewe ni mrithi wa Ngosha Corporation? Hakuna anayekuchukulia kwa uzito. Ningekushauri urudi ulikotoka.”
“Jerome, siamini kama wewe ni mwaminifu katika kushirikiana na Ngosha Corporation. Baada ya yote, familia ya Campos ndiyo iliyochukua faida ya KIM International. Je, ninyi

nyote hamkupata utajiri wenu kwa kuidhulumu familia ya Kimaro? Sasa kwa kuwa familia ya Campos ni familia ya pili tajiri zaidi nchini Kenya, nadhani lazima utake kuwa katika nafasi ya kwanza.” Lisa alimtazama Jerome kwa ujeuri. Kusema kweli, hakuwahi kumwelewa Jerome.
Katika ndoa ya Melanie na harusi yake miaka mitatu iliyopita, kila mara alimfikiria kama mtu mcheshi, asiye na adabu, na mtu mwenye majivuno. Lakini, katika miaka mitatu tu, familia ya Campos bila kutarajia ilikuwa familia ya pili tajiri zaidi nchini Kenya. Familia ya Campos haikuwa rahisi. Alikuwa na hisia kwamba kulikuwa na nguvu ya ajabu inayosaidia familia ya Campos nyuma ya pazia.
“Hujakosea. Nataka kuwa katika nafasi ya kwanza." Jerome akagusa kidevu chake. "Angalia, labda tunaweza

kushirikiana pamoja?"
"Babu yangu si ameshakubali ushirikiano wenu wa kipuuzi tayari?" Lisa alikunja uso.
Jerome alicheka. "Nilimaanisha sisi wawili. Nilisikia habari fulani hivi majuzi. Si Alvin anajaribu kukurudisha? Umeridhika na ukweli kwamba alikuacha miaka mitatu iliyopita? Hutaki kumkanyaga fisadi aliyekusaliti hapo awali?”
Lisa alishangaa. Alvin na Sarah walikuwa wametoka tu kujitokeza kwenye habari siku chache zilizopita, hivyo familia zote tajiri nchini Kenya zilifikiri kwamba Alvin na Sarah walikuwa wamerudiana tena. Hata hivyo, Jerome tayari aligundua kwamba Alvin alikuwa akimtongoza.
“Unashangaa? Kwa kweli, familia ya

Campos ina nguvu zaidi kuliko unavyofikiria. Jerome alipeleka mkono wake mbele ili amguse usoni huku akitabasamu.
Lisa alimsimamisha nusu. Alimtazama Jerome usoni kwa dharau. “Shemeji viwango vyangu viko juu sana.
 Huna sifa huna hadhi ya kugusa hata unywele wangu tu. Kwa kawaida, hata sielekezi macho yangu kwa mtu mwenye sura ya wastani kama wewe.”
Baada ya hapo, aligeuka, akipuuza usemi wa kutisha wa Jerome, na akaondoka bila kuangalia nyuma.
Jerome alitazama mwonekano wake mzuri na kuipangusa midomo yake kwa nguvu.
 Ha! Kwa hivyo ikiwa angemdharau? Hakika angemfundisha somo siku moja.

Baada ya kurudi ofisini, kichwa cha Lisa kilizunguka baada ya kupitia nyaraka za Ngosha Corporation kwa muda. Kwa hivyo, alianza kucheza michezo kwenye simu yake.
•••
Lisaalichukua mkoba wake na kuingia kwenye lifti private ya mkurugenzi mkuu wa kampuni. Lifti ilisimama kwenye orofa ya 25, ambapo Melanie alimtazama kwa unyonge na alikuwa karibu kuingia kwenye lifti.
 Hata hivyo, Lisa alibonyeza kitufe cha milango ya kufunga moja kwa moja, akimbana Melanie katikati ya milango.
"Lisa, unajaribu kuniua?" Melanie alipiga kelele. Alikuwa katika maumivu kutokana na kubanwa kati ya milango.


“Una jeuri sana. ” Lisa akabonyeza tena kitufe cha milango iliyofunguliwa na kumsukuma Melanie nje. “Hukuona kilichoandikwa nje? Inasema '
Lifti binafsi ya Mkurugenzi'. Una hadhi gani ya kutumia hii?"
Melanie alicheka. “Si unategemea tu utambulisho wa mrithi ambao Joel alikupa? Lakini sasa, mimi ni mtu muhimu ambaye ninasimamia maendeleo ya siku zijazo ya Ngosha Corporation. Huenda hujui hili, lakini Babu tayari ameidhinisha idara ya fedha kunigawia bilioni 12 ili kuendeleza ubia na Kampuni ya Campos. Hukutarajia hili, sivyo? Ulinifukuza mimi na baba yangu kwa makusudi hapo awali, kwa hiyo usingetarajia kwamba tutarudi kwa nguvu hivi karibuni.”
“Naona umekuwa ukijaribu sana kujipendekeza kwa babu na Bibi nyumbani hivi majuzi. Lakini Melanie,

unapaswa kukumbuka kwamba jina lako la mwisho ni Ngosha. Usiwe mpumbavu kwa kuwa kibaraka kwa wengine. Inabidi uelewe hili. Mara tu utakapokosa thamani yoyote kwa familia ya Campos, unadhani huyo mhuni Jerome, bado atakutaka? Kama hapo awali. Hukulalamika hospitalini kwamba Jerome alikupiga ulipofukuzwa kazi?”
Lisa aliweka nywele zake nyuma ya sikio huku akidhihaki. “Zaidi ya hayo, Jerome hata alijaribu kunichezea kimapenzi, shemeji yake, kwenye chumba cha mikutano asubuhi ya leo. Ikiwa huniamini, unaweza kuangalia picha za usalama mwenyewe.”
Baada ya kusema hivyo, alitoa kidole chake kwenye kitufe cha milango iliyofunguliwa, na milango ya lifti ikafungwa.
 Uso mzuri wa Melanie ulikuwa umekunjamana kwa hasira. Hapo awali alitaka kuondoka kazini,

lakini sasa, alikwenda moja kwa moja kwenye chumba cha usalama.
Baada ya kupata picha za asubuhi hiyo za chumba cha mkutano. Hapo ndipo alipomuona Jerome akinyoosha mkono wake kumgusa Lisa usoni. Harakati zake zilikuwa za kufurahisha. Alama kidogo ya hasira ilipita machoni pake. 'Jerome, wewe ni mwana haramu asiye na moyo,' Melanie aliwaza kwa uchungu.
Wakati huo huo, Lisa alifika kwenye maegesho. Kabla hajafika kwenye gari lake, aliweza kumuona Alvin akiwa ameegemea mbele ya gari lake. Alivaa suruali ndefu nyeupe na shati yenye mistari ya bluu na nyeupe. Kulikuwa na miwani ya jua iliyotundikwa mbele ya shati lake. Alionyesha uwepo wa kupendeza na mzuri. Miguu yake mirefu, haswa, ililinganishwa na miguu ya mwanamitindo.

Lisa alisimama pale na kumsoma kwa muda. Alihisi kama Alvin anazidi kuwa mdogo kadri alivyokuwa anazeeka. Watu wangeweza hata kuamini kwamba alikuwa na umri wa miaka 25.
“Lisa...” Alvin alipomuona anakuja, alifungua mlango wa abiria mara moja.
 Lisa akamkabidhi funguo ya gari na kuingia ndani ya gari.
TUKUTANE KURASA 421-425
ONYO: Ni marufuku kusambaza, kukopi wala kuuza kazi hii kwani endapo kama tutakubaini basi sheria itachukua mkondo wake (By: Official Dully)
 
LISA KITABU CHA NANE (9) SIMULIZI........................LISA KURASA.................421 - 425
PRESENT: SIMULIZI ZA DULLY

Sura ya: 421
Mara Alvin alipoingia kwenye kiti cha dereva, akawasha gari na kuondoka. "Babe, mambo yameendaje huko Ngosha Corporation leo?"
"Hakuna jipya sana. Mambo ni yaleyale tu ya ajabu.” Lisa alisema kwa uchovu. “Ngosha Corporation na Campos Corporation tayari wameamua kuanzisha ubia, na pesa nyingi zimewekezwa. Wana tamaa sana.”
Familia ya Campos ilikusudia kuanzisha kampuni kubwa zaidi ya kifedha nchini Kenya. Kama mambo yangeenda sawa, kampuni tanzu za kifedha za KIM International zingeweza kupikuliwa hivi karibuni. Familia ya Kimaro imekuwa haifanyi maendeleo yoyote katika biashara ya fedha miaka ya karibuni.
Alvin akavaa miwani yake ya jua.

“Lakini... Familia ya Ngosha haina ufahamu wa kutosha wa biashara ya fedha hata kidogo. Je, huogopi kwamba familia ya Campos itakuwa tegemeo lenu ikiwa mtaingia katika sekta ya fedha kwa haraka hivyo?”
"Nilikuwa na mawazo kama hayo pia. Lakini wanahisa tayari wameonja mafanikio matamu wakati wa ushirikiano wao wa awali na Kampuni ya Campos kwenye biashara ya mtandaoni. Wameonjeshwa asali kiduchu sasa wanataka kuchonga mzinga kabisa. Wamedanganywa na kujazwa na tamaa. Melanie hata alimshawishi babu yangu arejee kazini.”
Lisa akahema. Alikuwa amepoteza nguvu nyingi sana dhidi ya Sarah kwa wiki chache zilizopita ma kuwasahau Melanie na baba yake hivyo kuwapa nafasi ya kuibuka tena.

"Ingawa Mzee Ngosha amestaafu kwa miaka mingi, bado ana heshima katika familia ya Ngosha," Alvin alisema. “Melanie ni mjanja sana.
Ikiwa Mzee Ngosha atarudi, atakuwa tegemeo lake kubwa. Kulingana na maoni ya babu yangu, Mzee Ngosha ni... mkaidi kidogo, mjinga, na mwenye majivuno. Kwa kweli, yeye ni mtu anayejiona kuwa ana uwezo mkubwa lakini hana uwezo huo katika uhalisia. Lakini, hakuna mtu anayeweza kumkosoa.”
Lisa aONA aibu. Kama ilivyotarajiwa, maoni ya Mzee Kimaro yalikuwa ya moja kwa moja na sahihi. "Unafikiri Jerome ni mtu wa aina gani?"
Alvin alipapasa usukani na kusema. "Yeye ni mwenye tamaa, na anaweza kufanya lolote ili kufikia lengo lake. Kulingana na ufahamu wangu wa mbinu za kawaida za familia ya Campos, wao

si waaminifu hata kidogo. Hawapo katika kusaidia Ngosha Corporation. Wanataka ushirikiano huu kwa sababu wanafikiri wanaweza kuvuna faida kubwa kutoka kwao. Ubia huu, utainyonya Ngosha Corporation na kuineemesha familia ya Campos.
"Ni wakati tu atakapoinyonya Ngosha Corporation ndipo ataweza kushindana na familia ya Kimaro bila kujizuia."
Lisalishtuka sana na kukaa kimya kwa muda. Alipoona ukimya wake, Alvin alifikiri alikuwa na wasiwasi. Kwa hiyo, alicheka na kusema, “Usifikirie sana kuhusu hilo.
 Ingawa wewe ni mrithi wa Ngosha Corporation, urithi wako utakuwa na nguvu tu wakati Ngosha Corporation iko mikononi mwako. Jina lako la mwisho ni Jones. Kwa macho ya wazee wawili wakaidi wa familia ya Ngosha, bado wewe ni tofauti ukilinganisha na Melanie na Damien,

ambao wamewalea. ”
“Najua. Ndio maana sijisumbui sana juu yake. Kwa kuwa babu yangu anasisitiza kushirikiana na familia ya Campos, basi sitaingilia mambo yao, nisije nikapoteza pande zote mbili.” Lisa aliinua mabega yake bila wasiwasi. "Kusema ukweli, sina uhusiano wowote na familia ya Ngosha na kampuni ya Ngosha."
“Mm, huna haja ya kujali sana Ngosha Corporation. Kwa kuwa utakuwa mke wangu siku zijazo, na KIM International yote itakuwa yako. ” Alvin alimshika mkono ghafla. "Una mtu tajiri zaidi wa Kenya mikononi mwako."
"Sahau. Baada ya yote, wanawake wanapaswa kujitegemea wenyewe. Labda... utaniacha tena. ” Lisa alitoa mkono wake. Macho yake yalikuwa chini kuficha aibu machoni mwake.

“Ni sawa kama huniamini. Nina muda mwingi wa kukuthibitishia hilo.” Alvin alitabasamu kwa utulivu.
Lisa alimtazama kwa pembeni na kumuuliza. "Huna wasiwasi kwamba familia ya Campos itakuwa familia tajiri zaidi Kenya baada ya kuichukua Ngosha Corporation?"
"Hapana. KIM International tayari imewekeza fedha nyingi katika utafiti na maendeleo kwa miaka michache iliyopita. Tayari tumepata mafanikio muhimu pia. Tutapanda juu zaidi katika siku zijazo." Alvin alitabasamu kwa kujiamini. "Familia ya Campos inapata pesa kutoka kwa soko la ndani, wakati KIM International inalenga soko la kimataifa. Hawawezi kamwe kutuzidi.”
Lisa alipigwa na butwaa. Bado alikuwa na sura ile ile ya kupendeza, lakini mng'aro wa kujiamini machoni mwake

wakati huo kwa kushangaza ulimfanya kupoteza sauti yake. Ingawa kijana huyo alikuwa mpuuzi, ilimbidi akubali kwamba alikuwa mfanyabiashara mahiri. Hakuna mwanamke ambaye angeweza kupinga kuvutiwa naye.
Dakika arobaini baadaye, gari lilienda kwenye mgahawa mashuhuri katikati ya jiji. Mambo ya ndani ya mgahawa yalikuwa ya kigeni sana.
Alvin alikuwa tayari ameweka oda mapema na kukuta meza yao imeshaandaliwa. Kulikuwa na hata mtu anayecheza gita karibu na meza yao.
Lisa alifurahia sana chakula hicho. “Nimeona nyie ni wastadi sana wa kuchagua mahali pa kula. Mgahawa ambao Sam na Joseph walinipeleka mara ya mwisho ulikuwa mzuri pia. Moyo wa Alvin uliingia uchungu mara moja. “Wakati ujao, huruhusiwi kwenda kula chakula peke yako na watu wa

jinsia tofauti, hasa Joseph. ”
“Kuna nini kuhusu Joseph? Ni rafiki yangu mkubwa.” Lisa alicheka. "Kama si yeye, Mawenzi Investiments ingekufa kwa sababu yako."
Alvin aONA aibu. Sawa, angeweza kujilaumu tu kwa kufanya mambo mengi ya kihuni na kujipa shida mwenyewe bila kujua. “Ahem. Nilichomaanisha ni wakati mwingine Joseph atakapokuja... tunaweza kwenda kula naye pamoja. Nitamfanyia chakula ili kumshukuru kwa kuokoa kampuni ya babe wangu mzuri.”
“Mradi unalijua hilo." Lisa alimsukumia sahani nzima ya samaki amchambulie miiba. “Unajua kwanini wanawake wana wapenzi? Ni kuwafanya wafanye mambo ya aina hii.”
Alvin aliumwa na kichwa akiitazama ile sahani. Kwa kawaida, yeye mwenyewe

alimmega samaki mara moja tu kila upande kwa uvivu wa kuchambua miiba.
 Hata hivyo, alikuwa tayari kufanya hivyo ili kumfurahisha
Lisa.
 Wakati wa mchakato huo, hata alijichoma kidole chake na kikavuja damu.
“Wewe ni kweli... mzembe.” Lisa alikishika kidole chake na kukitazama kwa muda kabla hajakiweka mdomoni.
Alvin alishtuka. Wakati huo, ilikuwa ni kama volkano ilikuwa karibu kulipuka mwili wake. Pumzi zake zikawa nzito huku akiutazama uso wake mzuri, mdogo kwa macho ya joto.
 Alishuku kwamba alikuwa akimtania kimakusudi.
Midomo ya Lisa iliacha kidole chake tarataibu. Hakusahau kumtazama kwa jicho la uchochezi. Hata hivyo, wanaume walipaswa kuchezewa mara

kwa mara na kupewa mahaba fulani. Ikiwa sivyo, angeachaje hisia nzito kwake?
Alvin alitazama bila kujali kidole chake kilichoacha kuvuja damu. Baada ya muda kidogo, akainua mwiba wa samaki na kujichoma kidole chake kingine. Kisha, akampa kidole chake. "Kinatoka damu tena."
Je, alifikiri alikuwa kipofu? Alikuwa amenogewa, eeh? “Mhudumu.” Lisa aliinua mkono wake na kumpungia mkono mhudumu. “Tafadhali niletee chumvi.”
Alvin alikunja uso. Kwanini ilikuwa tofauti na vile alivyofikiria? “Mbona hunyonyi? Damu inazidi kutoka.”
“Ni sawa. Itakata tukinyunyiza chumvi juu yake baadaye. ” Lisa alitabasamu kama mbweha mjanja.

Alvin aliuliza kwa kukata tamaa. "Kwanini mwanzo ulininyonya na sasa unakataa?"
“Mimi ni kichaa? Watu watafikiri mimi ni kichaa nikiendelea kukunyonya vidole unavyojitoboa makusudi. Isitoshe, huna vijidudu mikononi mwako?” Lisa alishindwa kujizuia kucheka.
Mara Alvin akanyamaza kimya kutokana na kuzodolewa.
Kwa kuwa hakuweza kunyonywa tena, aliweza tu kuizuia damu kwa kitambaa.
"Sahau. Acha nifanye mwenyewe. Mpenzi wangu hana maana tena. Hawezi hata kutoa miiba kwenye samaki.” Lisa alipumua na kuanza kujichambulia samaki mwenyewe.
“Acha, nitakuchambulia.” Baada ya kupata kipigo kingine cha maneno, Alvin aliendelea kuwachambua samaki kwa

utiifu. Alijiona anazidi kuwa mnyenyekevu mbele ya Lisa.
Hata hivyo, alipokumbuka tukio la mwanamke huyo kunyonya damu kutoka kwenye kidole chake, moyo wake ulipiga kwa kasi.
Sura ya: 422
Muda si mrefu Chester akaingia na Cindy. “Alvin, ni wewe kweli. Nilidhani nimekosea. ” Chester alikuwa ameweka mikono mfukoni. Uso wake wa kiungwana ulijawa na mshangao.
Mara nyingi walipokuwa wakila pamoja siku za nyuma, Sarah mara zote alikuwa pamoja na Alvin, na Chester hakuwahi kumwona Alvin hata akimsogezea tu Sarah sahani ya chakula. Alishangaa kumuona Alvin kaatamia sahani ya samaki akichambua mifupa na kumlisha Lisa minofu kama

vile angefanya kwa Suzie.
Cindy alizidi kushangaa. Alijua jinsi Alvin alivyokuwa kauzu wakati wa mikusanyiko ya kawaida, hivyo hakuwahi kutarajia kwamba angeweza kumtendea Lisa vizuri. Cindy aliuma meno kwa siri kwa wivu. Aliamini Alvin hakika angemwacha Lisa. Hata hivyo, mwishowe, ni Sara ambaye hakuwa na maana tena, na alikuwa amepoteza miaka mitatu ya wakati wake kujipendekeza kwa Sarah bure kabisa.
“Bwana Kimaro...” Cindy alijifanya kana kwamba yuko kwenye hali ngumu. “Sikuamini nilipokuwa nikitazama kwa mbali, lakini wewe. ..
 Unaongozana na Lisa. Je! Sarah anajua kuhusu hili? Bado amelazwa hospitalini. Hii ni sawa kweli?”
Alvin alimpiga jicho kali kama mwiba. Cindy alishtuka kana kwamba kisu

chepesi kimepita usoni mwake. "Samahani. Mimi...ninaweza kuwa naingilia sana mambo yako. Labda ni kwa sababu nina uhusiano mzuri na Sarah. Anatia huruma sana sasa. ”
Lisa akachukua maji taratibu. “Ninaona uhusiano wako na Sarah umekuwa mzuri sana siku zote. Vinginevyo, ulijuaje kwamba Alvin alirudi nyumbani kwa Sara baada ya kutoka kula bata kila siku miaka mitatu iliyopita? UONA hata kikwaruzo kwenye shingo ya Sarah siku iliyofuata.
Uso wa kila mtu ulibadilika. Macho ya kina Chester yalikuwa yakimtazama Cindy, na sura nzuri ya Alvin nayo ilikuwa imebadilika kuwa ngumu. “Ni lini... niliacha mikwaruzo kwenye shingo ya Sarah?”
Alvin hakuwahi hata kumgusa Sarah kabisa. Angewezaje kuacha alama za mabusu shingoni mwake?

Cindy alijilazimisha kutulia na kusema, “Lisa, sijui unazungumza nini.”
“Kwa kweli, ninakushukuru sana,” Lisa alisema. "Kipindi hicho, nilikuwa mjamzito na niliwekwa kizuizini na Alvin hadi nilipolazimika kwenda kufanyiwa uchunguzi wa ujauzito. Isingekuwa wewe, nisingejua kuwa vyombo vya habari vilisambaza habari za Pamela kuzagaa mtandaoni. Na hata nisingejua kuwa Thomas alitangaza hadharani kuwa Pamela ndiye aliyemtongoza. Hilo lilinikasirisha sana hivi kwamba nilirudi na kuvunja kila kitu nyumbani. Niligombana na Alvin, jambo ambalo lilisababisha anisukume chini, nikatokwa damu nyingi na kisha mimba ikaharibika.”
Huo ndio wakati alipoteza
mapacha. Alvin alikumbuka na sura yake ilibadilika sana. Lisa alionekana

kana kwamba alikuwa na kichaa siku hiyo. Alichukua hata kisu na kujaribu kumchoma. Hilo lilimfanya ashangae jinsi gani Lisa alikuwa amegundua mambo hayo yote ikiwa alimyanganya hadi simu. Ikawa kumbe ni Cindy ndiye aliyemwambia. Kama si mdomo wake mkubwa, huenda asingepoteza watoto wake wote wawili.
"Kwa hiyo ilikuwa ni wewe?" Alvin alisimama ghafla. Akauvuta mkono wa Cindy na kumkandamiza kwenye meza kwa nguvu. “Nani alikuruhusu kuongea hivyo? Ulimi wako unakusumbua? Ikiwa ndivyo, nitaukatilia mbali.”
Baada ya kuongea, alichukua kisu kutoka mezani.
 Macho ya Cindy yalimtoka kwa woga, mwili mzima ukamtetemeka. “Sikufanya hivyo. Mimi sina hatia. Chester, niokoe.”
“Alvin.” Chester akamshika mkono

Alvin. “Tafadhali nifanyie upendeleo.”
“Unajua ni mdomo wake ulinifanya nipoteze watoto wangu?” Macho ya Alvin yalikuwa makali.

"Achana naye. Usisukumie lawama kwa wengine." Lisa alijifuta mdomo kwa kitambaa kabla hajamuombea kwa ghafla Cindy. “Cindy alikuwa ananiambia ukweli tu. Wakati huo, nilishukuru sana. La sivyo, ningewekwa gizani kama mjinga. Kwa kuwa sasa watoto wamekwenda, si kosa la mtu mwingine bali letu.”
Mwili wa Alvin ukakakamaa kwa aibu. Alijua alitaka kusema kwamba kupoteza watoto wao lilikuwa kosa lake hasa. Thomas ndiye aliyekuwa kichochezi, na ndiye aliyeongeza chumvi kwa jeraha.
Chester alichukua kisu kutoka kwa Alvin na kumtoa Cindy mikononi

mwake.
 “Alvin, tutapanda juu kula chakula chetu. Hatutakusumbua.” Chester alimshika mkono Cindy na kuondoka. Cindy bado alikuwa amedhoofika magotini. Hakuwahi kufikiria kuwa Alvin angekuwa wa kutisha namna ile.
Hata hivyo, hakuwa na shukrani hata kidogo kwa Lisa kwa kumuokoa muda huo. Kama Lisa asingesema maneno hayo, Alvin asingechukia na kumshikia kisu. Kwa siri aliutazama uso wa Chester mzuri, lakini usio tabirika, na hisia za chuki zikaongezeka ndani yake.
Walipoingia kwenye chumba cha faragha, Chester alifunga mlango kwa nguvu na kuwasha sigara. Kulikuwa na athari ya uhasama kwenye uso wake wa kiungwana. “Cindy, huo mdomo wako utaniletea shida siku moja.”
“Chester, samahani. Lisa, Pamela, na

mimi ni marafiki wazuri. Nilifikiri kwamba wakati huo alikuwa anasikitisha sana, kwa hiyo sikuweza kujizuia kusema ukweli,” Cindy alieleza huku machozi yakimtoka.
"Acha uongo wako. Usinichukulie kama mjinga.” Chester aligonga uso wake kwa upole. Alitoa dokezo la ukali na uadui. “Ikiwa unawajali sana, kwanini umekuwa karibu sana na Sara katika miaka mitatu iliyopita? Kwa upande mmoja, unamhurumia Sarah, na upande mwingine, unasema Lisa na Pamela ni marafiki zako. Naam, moyo wako unawahurumia watu wengi sana?” Sauti yake ilikuwa tulivu, lakini kwa Cindy, ilisikika kama mawimbi ya dhoruba. Ilimfanya ahisi wasiwasi.
“Ukiendelea kunizingua, nitaachana
na wewe mara moja, nadhani unanijua vizuri.” Chester alimwonya kwa ukali, “Afadhali ukae kimya kuanzia sasa na

ufunge mdomo wako. Ikiwa sivyo, usifikirie hata juu ya kuigiza kwenye filamu niliyokuunganisha.”
Akiwa na uso uliopauka, Cindy alitikisa kichwa kwa utii. Lisa alikuwa ameharibu kabisa sifa yake kwenye muziki mara ya mwisho. Kando na kushindwa kuonekana katika maonyesho kadhaa katika miezi michache iliyopita, bado alikuwa amepokea ofa ya kuigiza kwenye filamu mpya. Kwa hivyo, alikuwa akimtegemea Chester.
“Chester, nina jambo la kusema... Lakini sijui niseme au nisiseme...” Alisitasita.

"Ikiwa unafikiri halifai, basi funga mdomo wako," Chester alifoka.
"Hapana. Naona inanishangaza tu.” Cindy akauma meno. Ilibidi amalize sentensi yake. “Alvin alimuumiza Lisa

kikatili sana siku za nyuma. Alimweka kwenye kizuizi cha nyumbani na kumfanya apoteze mimba. Hata alimpeleka hospitali ya magonjwa ya akili. Ningekuwa mwanamke nisingemsamehe hata kidogo. Lakini kwa nini yeye ghafla karudiana pamoja naye tena? Anajiskia vizuri kweli?”
“Unajaribu kusema nini?” Macho ya Chester yaliganda.
Cindy alishtuka. "Ninaogopa kwamba Lisa sasa anajaribu kulipiza kisasi kwa Alvin. Hii ni silika yangu kama mwanamke. Sijaribu kumsema
vibaya kwa makusudi. Ninahofia kwamba Alvin Kimaro ataumia mara tu atakapozama sana kwenye uhusiano."
“Nenda kaagize chakula.” Chester alimpiga jicho kali. “Achana na mambo ya watu wengine.”

“Sawa.” Cindy aliitikia kwa kichwa na kutoka nje kwa haraka kwenda kumuita mhudumu.
Chester akavuta sigara yake. AONA ni ajabu pia kwa kile Cindy
aliongea. Kimsingi alikubaliana na mashaka ya Cindy ila hakutaka kuyajadili mambo hayo pamoja naye.
Sura ya: 423
Gari liliegeshwa kwenye eneo la maegesho lambele ya nyumba ya Lisa huko Karen Estate. Lisa alifungua mkanda wake wa kiti. Wakati anakaribia kuteremka kwenye gari, ghafla Alvin alimshika.
Koo lake likamtoka, lakini hakujua la kusema. Walikuwa na wakati mzuri wakati wa chakula. Hata hivyo walinyamaza baada ya Cindy kuja na kuvuruga mambo.

“Lisa, samahani...” Alvin alijawa na majuto. Ikiwa angejua kwamba alimpenda, asingeweza kamwe kuwa mkatili wakati huo. “Bado unanichukia?”
“Itakuwa uwongo ikiwa nitasema sikuchukii.” Macho ya Lisa yalitetemeka. Kulikuwa na dalili ya uchungu machoni pake. “Kila nikifikiria wale watoto wawili nilipokuwa ng’ambo, nilitamani kukutafuna ukiwa hai. Niliporudi, nilidhamiria kuwafanya wewe na Sarah mteseke. Lakini uliponilazimisha kupata talaka, niligundua bado sikuwa na uwezo wa kwenda kinyume na nyinyi. Na sasa uko hapa, unanibembeleza. Ninahisi mgongano na wasiwasi. Wakati mwingine nataka kurudiana pamoja nawe tena, lakini wakati mwingine ninaogopa sana...”
Alvin alimvuta kwenye kumbato lake

kabla hajamaliza sentensi yake. Akamkumbatia kwa nguvu. “Haitatokea tena. Niamini. Sitakuumiza tena. Nilikasirika mara ya mwisho, Lisa. Hebu tuwe na mapacha tena katika siku zijazo, sawa?"
Lisa alicheka huku macho yake yakiwa chini. Alisikika akiwa hoi. “Unafikiri bahati inaweza kujirudia? Unadhani ni rahisi hivyo kuwa na mapacha?”
'Basi, tutakuwa na watoto wawili. Binti yetu hakika atakuwa mrembo kama Suzie. ” Kwa namna fulani, Alvin aliposema hivyo, ghafla alitamani kupata mtoto wa wao wawili.
“Suzie...” Lisa alitamani kuchekai. Suzie alikuwa binti yake tangu
mwanzo.
 Hata hivyo, hangeweza kamwe kumruhusu Alvin ajue. Mtu kama yeye hakustahili kuwa baba wa mtoto. "Tutazungumza juu ya hili tena

siku nyingine." Alitazama juu. “Usiku wa leo hukula sana. Una njaa? Ninaweza kwenda ghorofani na kukutengenezea rchakula cha fasta.”
Macho ya Alvin yakaangaza. Alifikiri kukumbuka yaliyopita kungeweza kumkasirisha. Yeye, pia, alikuwa na wasiwasi sana, lakini hakutarajia bado angejali tumbo lake. Hasa alipomwalika kwa chakula usiku kama huo, hakutaka kuipiga teke bahati hiyo.
Mara walipofika ghorofani, Lisa alitumia mchele uliobaki jana yake na kumtengenezea Alvin mseto wa wali na njegere. Pia kulikuwa na karoti, hoho, na nyama ndani yake. Chumba kizima kilijaa harufu ya chakula. Alvin alifuta sahani nzima ya mseto.
“Babe, mbona upishi wako ni mtamu sana?” Alvin alilalamika tena. "Nataka kula chakula chako tu kwa maisha

yangu yote."
“Ndio. Wakati fulani ulipata nafasi hiyo, lakini ukanifukuza.” Lisa aliinuka na kukusanya sahani. "Rudi nyumbani, usiku umeenda.”
Alipogeuka, Alvin alikuja kwa nyuma na kukaza mikono yake kiunoni.
 “Sitaki kurudi nyumbani. Nataka kubaki hapa. Naweza kulala kwenye sofa.”
"Alvin, mimi sio mwanamke mwingine yeyote," Lisa alisema kwa upole. “Nilipolala na wewe hapo awali, nilichoambulia ni kufedheheshwa na vidonge vya kupanga uzazi. Wakati huu, nataka kujipenda zaidi. Sitaki kujitoa kirahisi hivyo.”
Alvin alikosa la kusema. Ilikuwa ni kosa lake kwa kufanya mambo mengi ya kihuni. Ikiwa angejua kuwa siku kama hiyo ipo, angerudi nyuma na kujipiga

mara kadhaa.
“Sawa, nitaenda. Lakini nataka busu." Alvin bila aibu akamgeuza na kumbusu midomo yake.
Lisa alikuwa na upinzani kidogo mwanzoni, lakini polepole, alishika kiuno chake. Busu la Alvin lilikuwa refu na la moto. Busu lilipoisha, alisukumwa nje ya mlango huku macho yake yakiwa yamejawa na matamanio. “Babe, nitakuletea kifungua kinywa kesho, sawa?”
“Sawa.” Lisa kisha akafunga mlango, akakimbilia bafuni na kupiga mswaki na kujisafisha vizuri.
 Wazo tu la mdomo wake kumbusu Sarah kabla lilimjaza karaha.
Alvin alikuwa kinyume chake. Mdomo wake ulikuwa mtamu kana kwamba

anakula asali tu.
 Hata baada ya Hans kuendesha gari ili kumchukua, aliendelea kufurahia ladha kinywani mwake.
 Kwa bahati mbaya, busu ilikuwa fupi sana. Ilikuwa ni dakika tano au sita tu. Ingekuwa bora kama ingedumu kwa muda mrefu zaidi.
"Bwana Kimaro, unaonekana kama uko katika hali nzuri." Hans alijua, kwa hiyo alitania kwa ujasiri, “Kama kijana ambaye ametoka tu kukutana na mpenzi wake wa kwanza.”
“Kama?” Alvin alikunja uso kwa kutoridhika. "Kwani mimi si kijana?"
Kama mwanamume katika mapenzi, alijali sana umri wake, haswa kwani Lisa alikuwa mdogo kwake kwa miaka mitano au sita.

“Aha, nilikosea.” Hans aliomba

msamaha kwa haraka. “Ninachomaanisha... umebadilika kidogo, Bwana Mkubwa. Hakukuwa na hisia za aina hii ulipokuwa ukichumbiana na Bi. Njau.”
“Uko sawa.” Alvin naye alitambua hilo, lakini hakuweza kuelewa. Siku zote alikuwa akikumbuka kwamba alimpenda Sarah. Ingawa alipokuwa naye, hakuwa na furaha kila wakati.
Midomo ya Hans ikasogea. Hapo awali alitaka kumwambia kwamba Alvin alifanyiwa Hypnosis na Sarah, lakini alighairi alipofikiria juu yake. Mwanasaikolojia alisema iwapo angejaribu kupata nafuu huenda ingeharibu ubongo wake na kumfanya awe mpumbavu. Aliamua kuacha tu. Angalau kila kitu kilikuwa kikienda vizuri.

Wakati huo Chester alimpigia simu

Alvin. “Miadi imekwisha? Njoo tuzungumze.”
Alvin alitazama muda akakubali kabla hajampeleka Hans kwenye baa aliyokuwepo Chester. Alipofika, Chester pekee ndiye aliyekuwepo.
"Yule mwanamke aliondoka?" Alvin aliketi kando ya Chester. “Chester, utaendelea kumvumilia huyo mwanamke? Sijawahi kuwa na hisia nyingi za Cindy, lakini baada ya usiku wa leo, niligundua kuwa yeye sio mzuri. Hastahili kuwa na wewe.”
"Kuna mambo ambayo hayawezi kusaidiwa." Chester akanywa mvinyo. Macho yake yalikuwa ya kina. " Na wewe je? Unarudiana na Lisa kweli?"
“Ndiyo.” Alvin alikuwa katika hali nzuri usiku huo. Kwa kweli, ingeweza kuwa bora zaidi ikiwa hakukutana na Cindy

katikati.
Chester alimtazama kwa wasiwasi. “Umewahi kufikiria ikiwa Lisaanataka kwa dhati kuwa na wewe au ... kulipiza kisasi kwako?”
Uso wenye furaha na mzuri wa Alvin uliganda mara moja. Alvin akaweka glasi yake ya divai, na ukali wa kutisha ukaangaza machoni pake.
Ikiwa ni mtu mwingine yeyote, angeweza kuwa na hofu. Hata hivyo, Chester alimfahamu tangu wakiwa watoto, hivyo alimuelewa.
Chester aliendelea na uso ulionyooka, “Fikiria ulichomfanyia siku za nyuma kwa sababu ya Sara. Ulimweka kwenye kizuizi cha nyumbani, ulimlazimisha talaka, ulimsukuma chini, ulisababisha kupoteza watoto wake, ulimpeleka hospitali ya magonjwa ya akili kwa matibabu, na orodha inaendelea.

Unafikiri anaweza kuweka kando kabisa kinyongo moyoni mwake hadi kusiwe na chuki iliyobaki?”
Kope za Alvin zililegea kwa kila jambo Chester alisema. Kifua chake kilihisi kama kinapigwa. Ikiwa Chester asingemdokezea, asingethubutu kukumbuka kwamba alifanya mambo mengi ya kumuumiza.

"Unafikiri anajaribu kunirudia kwa ajili ya kulipiza kisasi?" Alvin aliuliza kwa sauti kubwa baada ya muda mrefu.
“Siyo jambo lisilowezekana.” Chester akampiga bega. “Nakukumbusha tu kuwa makini. Usizame ndani sana hadi ukajisahau. Ninahisi ana nia ya kulipiza kisasi kwako.”
Sura ya: 424
Glasi iliyokuwa mkononi mwake

ilipasuka ghafla, na damu nyekundu nyangavu ikatoka na kuchanganyikana pamoja na ile pombe. Uso mzuri wa Alvin ulikuwa na huzuni. “Haiwezekani. Ananipenda. Naweza kuhisi. Sikumpenda mara ya mwisho na ndiyo maana nilienda mbali zaidi, lakini nitampenda kuanzia sasa. Nitampa kila la kheri kwa moyo wangu wote.” "Vema, ikiwa ndivyo unavyofikiria, basi hakuna ninachoweza kufanya. Nimesema kinachopaswa kusemwa. ” Chester alipomuona hivyo alikoroma na kumpa kitambaa. "Sema, kwanini wewe na Rodney mligombana kwa sababu ya mwanamke? Kuna maana gani? Kwa bahati nzuri, mimi sipo kama nyinyi wawili."
“Ha! Kweli, ni nani aliyetuita tuende kunywa pombe usiku kucha alipogundua kuwa Charity alikuwa akitoka na mwanaume mwingine?"

“Usinitajie jinala huyo mwanamke.” Macho ya kina Chester yaliangaza kwa karaha.
“Sawa. Hata hivyo, tayari amekufa. Hakuna maana hata kumjadili." Alvin alichukua kitambaa na kufuta damu mikononi mwake.
 “Umesikia kuhusu lolote kuhusu Rodney? Anaendeleaje sasa?”
“Kushindwa kuinunua Umoja Group imekuwa pigo kwake, lakini hatujui mengi kuhusu mambo ya vipodozi, kwa hivyo hatuwezi kumsaidia lolote." Chester akahema. “Kama angesikiliza ushauri wangu, ningemwambia akubali tu ndoa ambayo Babu Derek amepanga, lakini anakataa. Pengine ni kwa sababu anataka kumuoa Sarah kwa vile wewe umemtema.”
Alvin hakuchangia lolote kwenye hilo, badala yake aliinuka na kuaga,

“Naondoka. ”
Ndani ya gari, akainama kwenye siti akiwaza. Je, kweli Lisa atalipiza kisasi kwake? Je, iliwezekana?
•••
Siku iliyofuata, Alvin alipeleka kifungua kinywa asubuhi na mapema. Lisa alipokuja kufungua mlango, alikuwa bado amevaa pajama ya hariri na uso wake ulikuwa wa kusinzia.
“Alvin, ni saa kumi na mbili asubuhi. Mbona umefika hapa mapema hivi?” Lisa alishangaa.
“Sio mapema. Niliamka saa kumi na moja asubuhi” Alvin alimtazama kifuani, na mashetani yake yakaruka, na mara moja akamsukumia Lisa ndani, akaingia na kufunga mlango.
“Mbona unanisukumia ndani kwa nguvu?” Lisa alishangaa kwa msukumo

ule.
“Sitaki mwanamume mwingine atokee akuone ukiwa hivi. Mwili wako unavutia sana.” Hakutaka wanaume wengine wamuone akiwa amevaa kinguo cha kulalia.
“Leo hii unaona wivu mwili wangu kutazamwa na wanaume wengine, lakini ulipokuja kudai talaka kwa nguvu ulimwacha Maya anivue nguo mbele ya wanaume wa ONA.” Lisa alisimama na kumtazama kwa mshangao.
“Haiwezekani kitu kama hicho.” Alvin alibisha.
“Kweli kabisa Alvin, wewe ni wa kunifanya mimi nidhalilishwe na mlinzi kabisa? Halafu leo hii unasimama mbele yangu na kusema hutaki wanaume wengine wauone mwili wangu?”

“Babe, nimeleta kifungua kinywa. Kwanini usikae ule kwanza kwa amani?” Alvin alimsihi. “Maya ni mtu mdogo sana, kama kweli alifanya hivyo, nitamshughulikia baadaye.”
“Lazima nione unamshughulikia vinginevyo sitaamini kama kweli mapenzi yako kwangu ni ya kweli.”
Asubuhi na mapema, kulikuwa na kijibaridi sana ambacho kilitamanisha mambo fulani. “Nenda ukabadili nguo. Usijaribu uvumilivu wangu.”
Alvin alimwambia kisha, akageuza uso wake na kutazama pembeni.
Lisa alitazama chini, na pembe za mdomo wake zikainua. Ingawa anapaswa kuona haya, alikuwa ametumia hila hii hapo awali walipokuwa wakiishi pamoja huko Dar

es Salaam ili kumshawishi Alvin. Heh. Alvin alipagawa kana kwamba hajawahi kuona mwanamke hapo awali.
Aliingia chumbani kwake na kupitiliza bafuni kunawa uso, kisha akatoka nje baada ya kubadilisha nguo
zake.
 Alvin aliketi kwenye meza ya chakula pamoja na kifungua kinywa alichonunua kutoka kwa mgahawa maarufu wa kifungua kinywa.
"Nimefurahishwa na mpishi bora zaidi katika mgahawa wa ‘Wasp &
Sprout’ aliyeniandalia kiamsha kinywa hiki. Kuna ‘ricotta pancakes’, toast ya parachichi, baby spinach bacon salad, double cappuccino, hot
chocolate...” Alvin aliziorodhesha moja baada ya nyingine.
“Mh! Kifungua kinywa cha kizembe kama nini!” Lisa aliweza kuhisi kwamba kilikuwa kitamu kwa kunusa tu harufu

yake tu. Kwa hiyo, akachukua uma na kuanza kula. Baada ya kula kwa muda, aligundua kuwa Alvin hakuwa amegusa chochote.
“Mbona huli?”
“Sina hamu ya kula. ” Alvin alikuwa anasema ukweli. Hakupendezwa na kitu chochote zaidi ya chakula chake cha nyumbani.

“Hiyo si sawa. Unapaswa kula kifungua kinywa. Nitakulisha.” Lisa aliinua uso wake, kisha, akaweka kipande cha pancake mdomoni mwake na kumwelekea.
Alvin alishusha pumzi. Alikuwa karibu naye kiasi kwamba aliweza kuona kope zake ndefu. Alikuwa akitumia mdomo wake kumlisha.
Alvin awali hakuwa na hamu ya

kifungua kinywa kile, lakini koromeo lake likacheza ghafla. Aliinamisha kichwa chake na kuuma kwenye nusu nyingine ya keki ile.
“Sasa ni kitamu?” Lisa alimtazama kwa tabasamu. Ni kana kwamba mwanga wa jua wa asubuhi ulikuwa unamulika machoni pake.
"Ni kitamu sana." Hakuweza kupinga, Alvin kisha akamvuta kwenye mapaja yake na kuuzika uso wake ndani kabisa ya bega lake. Alihisi kama Lisa alimfanyia limbwata. Walikuwa wakigombana kila siku, lakini bado alivutiwa naye kihisia kuliko mwanamke mwingine yoyote. Hata hivyo, sasa alitambua kwamba mwanamke huyo alikuwa hodari sana katika kuteka hisia zake. Ni wazi alianza kumpenda tena siku chache zilizopita. Lakini sasa, alimpenda hata zaidi.


"Lisa hata kama unataka kulipiza kisasi kwangu, bado nataka kuwa na wewe." Alvin alijizika kwenye shingo yake na kunung'unika.
Mwili wa Lisa ukakakamaa, akamtazama tena. "Unasema nini?"
"Ninahisi kama nimefanya mambo mengi mabaya na ya kihuni hapo awali." Alvin aliukunja uso wake mdogo. "Lisa, hata ukinichukia na kutaka kulipiza kisasi kwangu, sitakuacha uende."
"Alvin Kimaro, sikiliza. Ninakuchukia kweli kwa mambo uliyonifanyia, lakini moyo wangu ni mwepesi kusamehe. Sina nia ya kulipiza kisasi kwako. Ninataka tu kukurudisha kwangu. Ninataka kukuchukua na kukushikilia kwa nguvu mkononi mwangu. Sitajali hata kama Sarah atakuwa mnyonge na asiye na furaha. Wewe ndiye furaha yangu ya pekee duniani.” Lisa

alimchombeza. Asingekuwa mwendawazimu kumweka wazi nia yake ya kumlipiza kisasi. Alitaka tu kumlevya kwa mahaba motomoto, akishakolea ndipo baadaye amteme ili na yeye aonje uchungu wa kuachwa na mtu anayempenda sana.
Lisa kisha akakumbatia shingo yake na kuuliza kwa macho tulivu, “Una wasiwasi kwamba ninakupenda kwa nia ya kulipiza kisasi?"
Alvin hakujua la kusema. Kwa kweli alikubali kuachana na Sarah kwa ajili ya Lisa, lakini maneno ya Chester jana yake yalimtia wasiwasi. Asingeweza kumwambia hivyo Lisa. Vinginevyo, angejisikia vibaya nakumchukia zaidi Chester.
"Najua kwamba Sara amekuwa nawe kwa miaka ishirini. Siwezi kujilinganisha naye." Lisa ghafla akainamia mikononi

mwake. Nywele zake zikamsugua Alvin kwenye shingo yake, akifanya kama nyoka. “Ni kweli, kama si Sarah, ugonjwa wako usingepona. Ni kawaida kwako kuhisi hatia juu yake.”
“Mmhm. ” Koo la Alvin lilikuwa likiwashwa vibaya na nywele zake. Sasa angeweza kuelewa vizuri ni kwanini watu wengi katika nyakati za kale walichanganyikiwa na kumwaga siri zao wakati mwanamke alipokuwa mikononi mwao.
“Lakini...” Lisa alibadilisha mada. “Kuna mtu nataka kumfundisha somo. Usiponiruhusu nitoe hasira yangu, nitakuwa na shaka kuhusu hisia zako.”
“Nani tena?”
"Maya Chande." Lisa aliyatema maneno hayo mawili taratibu. Sauti yake ilisikika kana kwamba alikuwa akiuma meno.


Alvin alishtuka, lakini mara akakunja uso. “Leo umeamka na Maya? Ni kwa sababu ya maneno uliyosema mwanzoni?”
"Ndiyo." Lisa alimtazama kwa chuki. “Siku hiyo alinidhalilisha sana. Kama Hans asingemkaripia, basi angenivua suruali. Sitasahau aibu hii.”
Macho meusi ya Alvin yalikuwa baridi kidogo. Siku hiyo mambo yalikuwa yamechafuka sana. Alichokumbuka ni kwamba alikuwa ametoka baada ya kuwaamuru watafute cheti cha ndoa na aliingia tu baada ya kusikia sauti za Hans na Maya wakirumbana. Hata hivyo, aliona kwamba Lisa alikuwa mzima na amevaa kikamilifu wakati huo.
“Mbona nilikukuta umevaa kawaida tu?” "Unamaanisha nini? Huniamini?” Lisa

alitoka mikononi mwake kwa hasira. "Sina chochote dhidi ya Maya, kwanini nimsingizie mlinzi yule masikini kwa uwongo? Ikiwa huniamini, unaweza kumuuliza Hans na wale wanaume wengine wa ONA waliokuwepo siku hiyo.
 Ikiwa mimi, Lisa Jones, ninakudanganya, sitakufa kifo kirahisi.”
"Sitakuruhusu kuapa juu ya jambo baya kama hilo." Sura ya Alvin ilibadilika huku akionya.
"Nina dhamiri safi kwa sababu sisemi uwongo, kwa hivyo siogopi." Baada ya Lisa kuongea, alipoteza hamu ya kupata kifungua kinywa kilichokuwa mezani. “Alvin wewe ndio unasema unanipenda na hutaki kuniacha. Lakini unapenda nini kwangu? Kulala na mimi? Huna imani nami hata kidogo. Angelikuwa ni Sarah ndiyo kafanyiwa hivi ungejisikia hatia juu yake, lakini mimi? Sistahili hilo.” Lisa alianza kukata tamaa.

“Siyo kwamba sikuamini...” Ingawa ndivyo kinywa chake kilitamka, moyo wake haukuwa na uhakika. Maya alikuwa akimhofia Lisa kwa sababu ya Sarah, kwa hivyo alihisi kwamba Lisa alikuwa akifanya hivi kwa sababu ya chuki yake binafsi.
Lakini, kwa Lisa, kusita kwake kuliongeza mafuta kwenye
moto.
 “Alvin, kwa nini usiende kuchunguza. Sitaki kuamini maneno yangu moja kwa moja.” Lisa aligeuka ghafla na akakunja ngumi kwa nguvu. Alikuwa na sura ya kujizuia usoni mwake. “Sitaki pia unibembeleze. Mlete tu Maya baada ya kufanya uchunguzi na kuujua ukweli." Kisha, akamvuta kutoka kwenye kiti na kumsukuma nje.
Alvin kichwa kilimuuma. Alikuwa mtamu muda mfupi uliopita, na hata alimlisha

keki kwa mdomo wake.
 Aliwezaje kumfukuza kwa kupepesa macho?
Alvin aliingia kwenye gari huku akifikiria sababu ya ugomvi huo. Macho yake yakawa na huzuni, na mara moja akawaita wanachama wawili wa ONA waliokuwa pale siku hiyo ofisini kwake.
Sura ya: 425
Muda si muda, wanachama wawili wa ONA, Ivan na Roy, walikuja ofisini kwake. Walipofika, walimkuta Hans pia.
 "Bwana Mkubwa, kuna jambo la dharura?" Ivan aliuliza kwa heshima. Alvin hakuwa na kawaida ya kuwaita isipokuwa alikuwa na jambo la kufanya nao.
“Nimewaita nyinyi nyote hapa leo ili tu kuwauliza jambo moja. ” Alvin aligonga meza yake kwa mkono. Sauti yake

tulivu iliwafanya watu watatu pale ofisini kukosa raha. “Mtanijibu kweli, sivyo?”
“Ndiyo.” Ivan na Roy mara moja walisema, “Bwana Mkubwa, mradi tu sisi ni wanachama wa ONA, sisi ni wa ONA hata tukifa. Tutakusikiliza wewe tu.”
“Basi, nitakuulizeni kitu. Ni nini kilitokea siku hiyo nilipomlazimisha Lisa Jones atie saini hati za talaka?” Alvin alisimama ghafla. Macho yake yalikuwa yanatisha. "Maya alifanya nini?"
Ivan na Roy vile vile walishtuka. Walikuwa na woga sana wasijue la kufanya. Alvin alikuwa mungu wa ONA, lakini Maya alikuwa mwanamke wa Master Ganja, kiongozi wao, na Lisa alikuwa mwanamke tu ambaye Alvin hakumtaka, kwa hiyo walilifumbia macho. Lakini kwanini aliuliza kuhusu hilo ghafla? Au uvumi waliokuwa

wakiusikia ulikuwa wa kweli? Bwana Kimaro alikuwa akipanga kurudiana naye?
"Hans, ongea kwanza." Alvin akamgeukia Hans. Je, Maya alimvua nguo Lisa?”
Hans alitazama juu kwa mshangao. Ilionekana kama Bi Jones alikuwa akilipiza visasi vyake vya zamani. Kama angekuwa yeye, angefanya
hivyohivyo pia. “Siwezi kusema uongo. Wakati huo, nilimwona Maya akivua koti la Bi Jones, akitoa nguo zake, na maeneo mengi yalikuwa... wazi. Nilimzuia wakati tu anakaribia kumvua Bi Jones suruali. Lakini Maya alidhani nilikuwa nikimfundisha kazi, kwa hivyo alitaka nifanye mimi badala yake. Hapo ndipo ulipoingia.”
Alvin alikunja ngumi na kuwatazama Ivan na Roy. "Sema ukweli."

Ivan aliogopa sana hivi kwamba akasema, "Ni kama Hans alivyosema."
“Kwa hiyo Maya alikuwa anajaribu kumvua Lisa suruali?” Alvin alikodoa macho.
Roy kwa woga alikabwa na mate. "Maya alisema kuwa alihisi Lisa Jones alikuwa ameficha cheti ndani ya suruali yake ..."
Kabla hajamaliza, Alvin alimrushia ngumi kali. Ivan na Roy walipigwa nyeusi na bluu, lakini hakuna mtu aliyethubutu kupigana naye au kufanya fyokofyoko yoyote.
"Kwa hivyo mliona kila kitu." Mishipa katika mikono ya Alvin iliziba. Watu hawa walikuwa wamemwona mwanamke wake, na hakutaka chochote zaidi ya kung'oa macho yao nje.

"Sisi hatukuona chochote." Ivan na Roy walikuwa wakitetemeka. Hawakuthubutu kukiri jambo hilo hata kama lilimaanisha kifo.
“Msingemuonaje? Ninyi wawili ndio mlikuwa mmemkandamiza chini. Lazima mliona kwa uwazi sana.” Alvin alikanyaga mikono yao bila huruma. “Kwanini hamkusema lolote wakati huo? Hata kama nilitaka kuachana na Lisa, bado alikuwa mke wangu wa zamani. Mnathubutuje kumdhalilisha?”
"Samahani, Bwana Mkubwa." Wale watu wawili walipiga magoti chini na kuinama. “Wakati huo ulikuwa unamchukia sana Bi.
 Jones. Tulifikiri unamchukia na kumdharau, na kwa kuwa Maya ni mwenzetu, tulifikiri tunaweza kumfumbia macho.”
Damu ya Alvin ilichemka. Alijua

walikuwa wanasema ukweli. Ni kwa sababu alimdharau Lisa ndipo wakathubutu kumdhalilisha. Mwisho wa siku, ni kwa sababu ya mambo ya kijinga aliyoyafanya yeye mwenyewe. Lisa alipomwambia mapema, alikuwa na mashaka. Alifikiri kwamba alitaka kulipiza kisasi kwa Maya kwa sababu ya Sarah. Sasa kwa kuwa alifahamu ukweli juu yake, hakustahili kusema kwamba anampenda.
Je, alikuwa amefanya mambo mangapi ya kijinga kumuumiza?
Kwa upande mmoja, alisema kwamba hisia zake kwake zilikuwa za kina kama bahari, kwamba angebadilika katika siku zijazo na kumpenda maisha yake yote. Hata hivyo, hakumwamini hata kidogo. Hata akamsababisha kudhalilishwa na mwanachama wa ONA. Haishangazi alikuwa na hasira sana. Alistahili.
Mara Ivan na Roy walikimbia haraka

kana kwamba wameachiliwa.
"Subiri," Alvin aliwazuia. “Nyinyi wawili mlifanya kosa safari hii, kwa hiyo nendeni kwenye chumba cha adhabu cha ONA ili muadhibiwe kwa hiari yenu. Katika siku zijazo, mtamheshimu Lisa kama vile mnavyoniheshimu mimi. Yeye ni mwanamke wangu.”
“Ndiyo. Tutaenda mara moja." Watu hao wawili walipigwa na butwaa.
Hata hivyo, wakati huohuo, walilalamika kisiri. Hapo awali walidhani Sarah ndiye kinara kwa Alvin, lakini ilionekana walikuwa washikilia kuti kavu, na sasa lilikuwa likianguka pamoja nao. Yote yalikuwa makosa ya Maya. Yeye ndiye aliyesababisha hayo.
•••
Lisa akiwa ofisini kwake, Alvin alimpigia simu. "Lisa, shuka. niko chini.

Nilichunguza na kujua ukweli, nitakupeleka Maya.”
“Umechunguza kweli?” Lisa alicheka. “Inaonekana kama hukuniamini.”
Alvin hakuweza kupata maneno ya kumjibu. Alikasirika. Alielewa kabisa maana ya kujipiga risasi mguuni.
"Ni kosa langu kutokuamini. Kuanzia sasa ikiwa utanipenda, unaweza kusema chochote, na nitachagua kukuamini bila masharti. Najua hujawahi kusema uwongo. ”
Lisa alihema kimya kimya. “Inaeleweka. Ulikuwa unaamini kila alichokuambia Sara, lakini hukuamini chochote nilichosema. Kama angekuwa Sarah, kila kitu kingekuwa tofauti.”
“Samahani...” Moyo wa Alvin ulisogea. Ndiyo. Kila mara Lisa alipogombana na

Sarah, Alvin alikuwa akichagua kumwamini Sarah bila masharti. Lakini, baada ya wakati huo, aligundua kuwa labda kuna nyakati ambazo hakuelewana naye hapo awali. Labda Sarah alidanganya pia. Baada ya yote, hakutarajia Maya angefanya kitu kama kile kwani siku hiyo alikuwa nje ya mlango.

"Ninashuka. Nitalipiza kisasi changu kwa siku hiyo,” Lisa alisema kwa ukali ghafla.
“Sawa.” Alvin alikaa chini kwa dakika kumi kabla ya Lisa kuingia kwenye gari.
“Lisa, hii ni zawadi! nilikununulia njiani wakati nakuja hapa.” Alvin akamkabidhi Lisa sanduku. Lisa akalifungua na kuona ni pete, mikufu na hereni za almasi. "Niliona ulikuwa mrembo sana ukiwa umevaa pete mara ya mwisho," Alvin alieleza kwa upole.

"Hii ni zawadi ya kuomba msamaha?" Lisa aliuliza moja kwa moja.
“Ndiyo.” Alvin alijikaza na kujibu kwa uaminifu.
“Sipendi hereni za almasi.” Lisa akalitupa boksi lile kwenye gari. "Ninapenda dhahabu. Almasi ni mawe tu, na ni ya kawaida sana. Inatafutwa sana kwa sababu wanawake wengine wanasema kwamba almasi inawakilisha upendo na uaminifu. Ha! Upendo hauwezi kuthibitishwa na kitu kama hicho. Lakini dhahabu bado ina thamani zaidi. Inaweza kubadilishwa na inapanda kwa thamani. Kama vile wanawake husema mara nyingi, kati ya mwanaume na pesa, pesa ni bora zaidi.”
Alvin alikosa la kusema.
 Alihisi kuwa amemuudhi sana mwanamke huyo siku

hiyo. Ingawa alipofikiria kuhusu hilo, aligundua lilikuwa kosa la Maya. Sasa, alichotaka ni kumfundisha Maya somo.
“Sawa. Nitakupa dhahabu siku nyingine, "Alvin alisema kinyonge baada ya muda. Angemwonyesha kwa matendo yake kwamba kati ya yeye na pesa, angetamani amchague yeye.

Muda si muda, gari liliingia kwenye geti kubwa kwenye Mlima wa Sherman. Ingawa palionekana kuwa pa zamani kidogo, sanamu kwenye korido zilionekana kuwa za zamani zaidi.
Lisa alitazama huku na huku, na Alvin akamweleza, “Hapa ni makao makuu ya ONA.”
Alipigwa na butwaa kidogo. Hakutarajia Alvin angempeleka moja kwa moja kwenye makao makuu ya ONA. Kwa watu wengi, hii ilikuwa mahali pa siri

zaidi. Ilikuwa ni kama vile Alvin anamiliki jeshi dogo, au kikundi cha kigaidi. Ilisemekana kuwa wapiganaji wengi mahiri walikusanyika hapo.
Baada ya gari kuegeshwa, Ivan alijikongoja na kufungua mlango. Lisa alimtazama. Japo uso wa mwanaume huyo ulikuwa na michubuko na kuvimba baada ya kupokea kichapo kutoka kwenye chumba cha adhabu, bado alimtambua kuwa ni mmoja wa watu waliomkandamiza chini wakati wa kumlazimisha kusaini talaka.
Hata hivyo, mtu huyo mara moja akasema kwa hofu, “Bi. Jones, nilikuwa kipofu hapo awali. Tafadhali naomba unisamehe."
“Ni sawa. Najua ulikuwa unasikiliza amri tu.” Lisa alimtazama Alvin. “Mbona umempiga hivyo? Je! hawakutii amri zako tu?”

TUKUTANE KURASA 426-430
ONYO: Ni marufuku kusambaza, kukopi wala kuuza kazi hii kwani endapo kama tutakubaini basi sheria itachukua mkondo wake (By: Official Dully)
 
LISA KITABU CHA NANE (9) SIMULIZI........................LISA KURASA.................426 - 430
PRESENT: SIMULIZI ZA DULLY

Sura ya: 426
Ivan alimtazama Alvin, na taya lake lilikuwa karibu kuanguka chini kwa mshangao. Hii ilikuwa mara yake ya kwanza kumuona Bwana Kimaro akiwa mtiifu kwa mwanamke. Hata Sarah hakuwa amepokea aina hii ya heshima kutoka kwake hapo awali. Ilionekana kana kwamba alipaswa kumheshimu Bi Jones kuanzia siku hiyo.
Roy naye akakimbia huku akitetemeka. “Bwana Mkubwa, Maya yuko kwenye chumba cha adhabu. ” Pua yake ilipigwa hadi ikatoka damu, na ilikuwa inamuuma sana.
“Sawa.” Alvin alimchukua Lisa na kuingia ndani.
Katika chumba cha adhabu, Maya alifungiwa mara tu baada ya kuingizwa humo. Simu yake ikachukuliwa mara

moja, na hali ya wasiwasi moyoni mwake ikazidi kuongezeka.
"Niacheni niende. Nahitaji kwenda hospitali,” Maya aliwakoromea watu waliokuwa mlangoni kwa ukali. “Bwana Mkubwa amenipangia kumlinda Bi Njau hivyo msipoteze muda wangu hapa.”
"Hapana. Inabidi usubiri hapa. Bwana Mkubwa atakuja muda si mrefu,” mlinzi wa getini alisema kwa sauti ya chini.
“Kwanini ameniita hapa? Sikufanya chochote kibaya,” Maya alifoka kwa hasira.
"Una uhakika kuwa haukufanya chochote kibaya?"
Alvin alifungua mlango kwa teke na kuingia ndani akiwa na Lisa. Uso wake mzuri ulikuwa wa baridi.

“Bwana Mkubwa...” Maya alijihisi vibaya alipomwona Lisa kando yake. lakini, hakuthubutu kupiga kelele. Alihisi maumivu ya moyo kwa Sarah, ambaye alikuwa peke yake hospitalini. Baada ya yote, wote walikuwa wanawake. Alihisi kwamba Bwana Mkubwa kweli alikuwa hana huruma sana.
Kisha, Ivan na Roy wakaingia ndani, wakiwa wamejeruhiwa na kupigwa, na kusema kwa uchungu, “Maya, Bwana Mkubwa tayari anajua ulichofanya tulipoenda kwa Bi Jones ili kumlazimisha atie sahihi hati za talaka.”
Macho ya Maya yalitetemeka. Alikuwa karibu kusahau tukio hilo na hakutarajia Lisa angelikumbuka bado. Mara moja, chuki yake kwa Lisa iliongezeka ghafla. "Nilifanya nini? hata sikumbuki. Ni Bwana Mkubwa aliyeniambia nimpekue.”

“Ndio?” Lisa alitabasamu. "Bado unakumbuka uliposema sikioni mwangu kuwa utanivua nguo na kuwaacha hawa wanaume wauangalie vizuri mwili wangu?"
Uso wa Alvin ulibadilika ghafla. Ikiwa sura inaweza kuua, Maya angekufa mara moja. “Ulisema hivyo?”
“Sikufanya hivyo. Ananisingizia,” Maya alikanusha kwa sauti kubwa. “Bi. Jones, huwezi kunisingizia hivi kwa sababu tu ninamlinda Bi.
 Njau. Pia ninafanya kazi kulingana na maagizo ya Bwana Kimaro.
Lisa alicheka na kumtazama Alvin. “Anamaanisha kwamba nikitaka kumlaumu mtu, nikulaumu wewe. Haina uhusiano wowote naye. ”
“Mimi sikufanya hivyo.” Maya alishtuka na kutikisa kichwa kwa nguvu.

Hata hivyo, Alvin pia alikuwa amesikia hivyo. Akasogea mbele na kumpiga teke zito Maya. Maya alianguka chini na hakuweza kusimama kutokana na maumivu ya mwili wake mzima.
"Bwana Mkubwa, huwezi kufanya hivi." Maya alilala chini na uso uliopauka na kusema, “Ni wewe uliniambia nitafute cheti cha ndoa, na ni wewe pia uliniambia nimlinde Bi Njau. Sikufanya chochote kibaya. Bi Jones ni wazi hajanipenda tangu mwanzo. Ameshindwa kushughulika na Bi. Njau, kwa hivyo badala yake ananiletea hasira zake mimi. Unaenda nje ya mstari.”
Macho ya Alvin yalimganda, misuli ya mwili ikasisimka kwa hasira.
Mwili maridadi wa Lisa ukamsogelea ghafla Alvin. Aliinua kichwa chake juu na kutabasamu. “Si ulisema kwamba

wanachama wa ONA wanamtii mtu anayesimamia familia ya Kimaro? Inaonekana mtumishi wako wa chini si mtiifu sana.”
Akiwa ameshtuka, Maya alijitetea kwa haraka, “Acha uchonganishi. Familia ya Chande tumekuwa waaminifu kwa familia ya Kimaro tangu kizazi cha babu yangu. ”
“Vema, mimi ni mpenzi wa Alvin. Wewe unawezaje kunivunjia heshima? Au ni kwa sababu mimi sio Sarah, hivyo unanichukia na kunifanyia uadui? Hata ulimdharau Shani kwa kunilinda. Labda umemlinda Sarah kwa muda mrefu hivi kwamba sasa unamwona kuwa mungu wako wa kike?” Lisa aliinua uso wake. Alikuwa amegonga msumari kichwani.
"Hapana." Uso wa Maya ulipauka. Huko ONA, kitendo cha mwiko zaidi

kilikuwa kutokuwa mwaminifu kwa familia ya Kimaro, na matokeo yake yalikuwa mabaya sana. Kwa hiyo, Maya alikuwa na wasiwasi mno! “Bi. Jones, mbona unanisingizia hivi? Sina kinyongo na wewe. Mimi ni mlinzi wa hali ya chini tu.”
"Wewe ni mwanachama wa ONA, kwa hivyo sio saawa na mlinzi wa kawaida. Wewe kama ONA, una siri nyingi sana za familia ya Kimaro.” Lisa alitabasamu na kumuuliza Alvin, “Naweza kuwa na ujasiri wa kukuuliza swali? Maya amemlinda Sarah kwa muda gani?"
Alvin alikunja uso. "Ikiwa ni pamoja na wakati kabla ya Sarah kutoweka, karibu miaka saba au minane."
"Inaonekana amekuwa akimlinda Sarah tangu alipokuwa mdogo sana." Lisa alisema.

Maya alielewa haraka hoja yake. “Ingawa nimemlinda Bi Njau kwa muda mrefu, ninatii amri za ONA.”
Alvin akasugua kichwa chake. Ghafla akagundua kuwa alikuwa amezembea. Kwa kuwa Sarah alikuwa mtu wa maana sana kwake, alimwambia mkuu wa ONA ampangie mtu aliyekuwa makini zaidi kumtunza. Huyo alikuwa Maya.
Baadaye Sarah aliporejea Alvin alisema anataka kumpangia mlinzi. Sarah alipendekeza mlinzi kuwa Maya kwa sababu alikuwa anamfahamu, na kwa hivyo, alikubali.
Hata hivyo, alikuwa amesahau kwamba kadiri watu wawili walivyokuwa pamoja, ndivyo ilivyokuwa rahisi kwao kuendeleza uhusiano wao wa bwana- mtumishi. Ilikuwa kama Shani na Aunty Yasmine wakiwa na Lisa.

Maya alikuwa akijua siri nyingi za Sarah, na Sarah alimjali sana Maya kwa maslahi kwa sababu hiyo, kwa hivyo Sarah alikuwa na maana zaidi kwake kuliko kawaida.
“Maya, inatosha. Ni ukweli kwamba ulimuumiza Lisa bila mimi kujua. Itabidi ukubali adhabu ya ONA,” Alvin aliamuru kwa ukali.
“Naweza kumpa adhabu mimi mwenyewe? Mimi sijazoea kuona damu na majeraha. Sipendi vurugu, hivyo sipendekezi adhabu ya viboko.” Sauti ya Lisa ilikuwa nyororo na ya upole. Ilifanya watu watake kumsikiliza.
"Unataka kufanya nini?" Alvin aliuliza kwa kujiachia.
"Nataka kumfanyia kama alichonifanyia." Lisa alimtazama Maya, ambaye mashavu yake yalibadilika rangi ghafla. “Kwa kuwa siku hiyo

aliwafanya wanaume hawa wauangalie mwili wangu, nitawaonyesha pia mwili wake leo. Hataweza kuelewa machungu niliyoyapata hadi ajionee wenyewe.”
Alvin alipigwa na butwaa lakini aliitikia kwa kichwa muda mfupi baadaye. "Fanya upendavyo."
"Hapana." Maya alikuwa na hisia mbaya juu yake. “Bwana Mkubwa, naomba utumie tu adhabu ya ONA. Hata utoe viboko vingapi, naweza kuvumilia.”
"Maya, ungependelea kupata maumivu ya mwili kuliko kuvumilia kuvuliwa uchi mbele ya watu? Hii inaonyesha kuwa unaelewa aibu niliyoipata siku hiyo. Kwanini ulinidhalilisha hivyo siku hiyo?” Lisa alicheka. “Usiwafanyie wengine yale usiyotaka wakufanyie. Je, huelewi msemo huu?”
“Sikufanya hivyo. Unanishtaki kwa

uwongo.” Maya alimkazia macho. Chuki iliyokuwa machoni mwake haikuweza kufichwa tena.
"Kila mtu tayari amekiri. Wewe pekee ndiye hutaki kukubali. Una kiburi kama nini.” Lisa alifuatilia kiganja cha Alvin kwa vidole vyake. "Nini unadhani; unafikiria nini?"
"Tutafanya kama unavyosema. Mfungie Maya.” Kisha, Alvin akageuka na kutoka nje. “Sipendi kutazama.”
“Mimi pia...” Ivan na Roy pia walikuwa karibu kutoroka.
“Subirini.” Lisa akawazuia huku akitabasamu. “Mlifurahi sana kunitazama siku hiyo, jambo ambalo linaonyesha mnapenda kuangalia miili ya wanawake. Katika hali hiyo, mtakaa na muangalie."

Ivan na Roy mara moja waligeuka rangi. Alvin aliwatazama tu kwa ukali na kutoka nje.
Maya alifungwa kwenye nguzo na watu wa ONA. Haijalishi alijitahidi vipi, hakuna mtu aliyemsikiliza.
 Lisa aliomba mkasi na kukata polepole nguo za Maya, kipande kwa kipande.
"Lisa Jones, sitakusamehe kamwe," Maya alisema kwa sauti ya chini. Macho yake yalikuwa ya kutisha na yaliyopinda. “Usijione umefika.
 Bwana Mkubwa tu anataka kucheza na wewe kwa sababu ana kikwazo katika kipengele hicho. Hawezi kumgusa mwanamke mwingine yeyote isipokuwa wewe. Anavutiwa nawe kwa sababu hiyo tu. Unaelewa? Wewe ni chombo tu cha kukidhi mahitaji yake ya kimwili.”
Sura ya: 427

Lisa aliganda, na mshangao ukaangaza machoni pake.
 Hata hivyo, Maya alifikiri kwamba alikuwa amekasirishwa, hivyo akasema kwa ukali, “Ikiwa ingewezekana kufanya na Bi. Njau, Alvin hata asingekutafuta. Ikiwa huniamini, subiri utajionea mwenyewe. Alvin atakapomuonja tu Sarah, hutakuwa na thamani kwake. Afadhali unisitiri, la sivyo sitakuacha.”
"Kumbe ndio hivyo?" Lisa alishusha pumzi ndefu na kutikisa kichwa kwa kusitasita. "Nitaenda kumuuliza Alvin baadaye, kama kweli hajawahi kumgusa Sarah."
“Usithubutu.” Maya aliogopa. Alitaka tu kumchokoza Lisa. Ikiwa Alvin angegundua kuwa alimwambia Lisa kitu kama hicho, bila shaka angemuua. Baada ya yote, wanaume walijali sana kiburi chao.

Lisa alicheka. Maya aliogopa, ambayo ilimaanisha kwamba kile alichosema kilikuwa cha kweli. Hakutarajia kuwa hakuna kilichotokea kati ya Alvin na Sarah licha ya kuwa walikuwa pamoja kwa muda mrefu.
 Hii ilikuwa ya kuvutia sana. Kwa hiyo sarah alifanikiwa kuudanganya bongo wake, lakini mwili wake ulipinga kisilika.
Kwa namna fulani, chuki yake kwa mtu huyu ghafla ilipungua kidogo, na hakumwona kama hapo awali.
 “Maya, huelewi kwanini ana rudi kwangu mara kwa mara? Ni kwa sababu ana mimi tu moyoni mwake.”
Mkasi wa Lisa ukaipunguza suruali yake taratibu. Maya hakuwa tena katika hali ya kuzungumza naye kwa sababu alikuwa akipiga kelele kwa aibu.
“Njooni muangalie vizuri. Msiangalie mbali. Nitamwambia Alvin iwapo mtu

yeyote atathubutu kuondoka.” Lisa akawatazama kwa macho wanaume waliokuwa pembeni.
 Kundi la wanaume warefu walitoka jasho baridi na kuwa na wapole sana.
 Sh*t. Walikuwa wamekaa na Maya kwa muda mwingi, lakini hii ilikuwa mara yao ya kwanza kukutana na mkanganyiko huo.
Ilibidi wakubali kwamba Maya alikuwa na umbo zuri, na alikuwa amevaa kitu cha kuvutia sana ndani yake. Hawakuweza kusema hata kidogo. Zaidi ya dakika kumi baadaye, Lisa alitoka chumbani huku akiwa na tabasamu usoni.
Kumuona akiwa katika hali nzuri, Alvin alilegea sana. Akasogea na Lisa akamshika mkono ghafla. "Asante. Najisikia vizuri zaidi.”
"Samahani. Lilikuwa kosa langu.” Alvin

aliomba msamaha kwa dhati. Mwishowe, ni yeye aliyewapa wengine fursa ya kumuumiza.

Lisa alimtazama kwa jicho lisilo la kawaida. Kwa kusema ukweli, kama alivyosema Maya, ikiwa Alvin angeweza kufanya na wanawake wengine pia, labda asingerudi kwake kwa urahisi leo.
“Mbona unanitazama hivyo?” Alvin alishangazwa na sura yake.
"Bwana Mkubwa..." Wakati huo, mwanamume mrefu na mnene wa makamo alipita. "Nimesikia kwamba Maya amekukera?"
“Ndiyo. Master Ganja, unapaswa kumfundisha Maya vizuri ili akumbuke bwana wake wa kweli ni nani.” Kisha, Alvin akamvuta Lisa na kuondoka.
“Huyu ni...” Lisa alishindwa kujizuia

kugeuka nyuma na kumwangalia mwanaume huyo.
Kabla hajaonekana vizuri, alivutwa nyuma na nguvu nyingi. Alvin alimtazama kwa nguvu. "Hauruhusiwi kutazama wanaume wengine kwa udadisi."
Lisa alikosa la kusema. “Sina hobi ya kupenda wanaume wa makamo. Nilitaka tu kujua ni nani."
“Ni mwalimu wa ONA na mmoja wa mabosi wa ONA. Anafuata tu maagizo yangu.” Alvin alimweleza, “Ili kuwa mwanachama katika ONA, ujuzi wa mtu lazima uwe wa juu zaidi. Watu wanaojiunga na ONA pia wanapaswa kukumbana na vikwazo vingi, hivyo ni jambo la kawaida kwamba uwepo wa Mwalimu Ganja ni muhimu sana.”
“Oh.” Lisa aliitikia kwa kichwa.

"Niilikatakata nguo zote za Maya ndani. Nadhani atanichukia sana.”
"Hatathubutu." Ukali wa kutisha ulikuwa ukiwaka machoni mwa Alvin. “Wewe ni mwanamke wangu. Kukuchukia ni sawa na kunichukia. Wale wanaothubutu kwenda kinyume na mimi huwa sinaga huruma nao.”
Lisa alimtazama Alvin kwa siri. Wale wote waliokuwa kwenye kilele cha mafanikio walionekana kuwa na kosa moja - walifikiri hakuna mtu ambaye angethubutu kuwasaliti. Walifikiri kila mtu anapaswa kuwa mwaminifu na kuwaogopa, lakini hawakujua kwamba akili ya mwanadamu ilikuwa ngumu zaidi kuifahamu.
“Nakukumbusha tu. Kwa kuwa Maya alithubutu kunidhalilisha mbele ya macho yako, ina maana kwamba kati yako na Sarah, anaweza kumjali Sarah

zaidi. Usinielewe vibaya. Simlengi kwa makusudi kwani tayari nimeshalipiza kisasi mapema. Natumai utaendelea kufuatilia." Lisa alisema kwa uwazi.
Alvin alishindwa kujizuia kumtazama na kutabasamu. “Una wasiwasi na mimi?”
Lisa aliinamisha kichwa chini na kusema.
 “Hapana.”
Alvin alimshika kwa nguvu. "Babe, katika siku zijazo, nitakulinda kwa nguvu zangu." Badala ya kuwa mtu anayemuumiza kila wakati. Alvin alitoa ahadi moyoni mwake.
•••
Katika chumba cha adhabu, Master Ganja alifungua mlango na kumuona Ivan akimfungua Maya. Jacket ya Ivan ilikuwa imefunikwa juu ya Maya. Mwili wake wa juu ulikuwa umefunikwa, lakini nusu ya chini ilikuwa wazi.
 Vipande

vya suruali vilitawanyika kwenye sakafu. Ilionekana wazi kwa mtazamo kwamba zilikuwa nguo za kike.

“Master...” Machozi ya Maya yalimwagika mara tu alipomwona. “Lisa alinikata nguo zote. Wote waliniona.”
"Nini kimetokea?" Uso wa Master Ganja ulikuwa umekakamaa kwa hasira. "ONA ilikuja lini na adhabu ya aina hii?" Alifikiri ingekuwa mijeledi miwili au viboko vichache.
Ivan alieleza upesi, “Yalikuwa ni maagizo ya Bwana Mkubwa. Alisema kuwa Maya alimvua Bi. Lisa nguo zake hapo zamani, kwa hivyo Bi Jones alikuwa akimpa tu ladha ya dawa yake mwenyewe.”
Master Ganja alivua koti lake na kumrushia Maya. “Twende.”

Maya alilia na kumfuata Master Ganja. Kila hatua aliyopiga, alihisi watu waliokuwa nyuma yake wakimtazama ajabu.
 Haikuwa mpaka Maya na Master Ganja walipoondoka ndipo walianza kujadiliana katika chumba cha adhabu.
“Si ajabu Maya anaweza kuwa demu wa Master Ganja. Sikuwahi kutambua hapo awali, lakini baada ya kuvuliwa nguo leo, niligundua kwamba yeye ni chombo kwelikweli.”
“Weka sauti yako chini. Unafikiri tunapaswa kumwambia Bwana Mkubwa kuhusu uhusiano wa Master Ganja na Maya?”
"Sidhani kama hiyo ni muhimu. Uhusiano wa Master Ganja na Bwana Mkubwa si wa kawaida. Je, ikiwa Bwana Mkubwa atadhani tunajaribu kuwachonganisha? Isitoshe, hukuona jinsi Master Ganja alivyokasirishwa na

kitendo kilichotokea sasa hivi.”
“Hiyo ni kweli. Maya ni mwanamke tu."
Ndani ya chumba, Master Ganja aliingia na Maya akamfuata nyuma. Maya alifunga mlango nyuma yao na kuvua koti lake kabla ya kumkumbatia kiunoni kutoka nyuma. "Mpenzi, nataka kufa! Siwezi kuendelea kuishi katika maisha haya tena.”
Master Ganja akageuka. Alipoona sehemu ya chini ya Maya ambayo haijavalishwa nguo, dokezo la huzuni liliangaza katika macho yake meusi.
"Usiwe mjinga." Ganja alisema kwa upole, “Nimekuonya zamani sana kwamba Sarah Njau ni mtu unayemlinda tu. Kwanini uliingilia kati mambo yake binafsi na Lisa Jones? Unachohitajika kufanya ni kutekeleza kazi ambayo Bwana Mkubwa

alikupangia, basi.”
"Lakini alinisingizia uwongo." Maya alilia sana.“ Nilikuwa nikifuata tu maagizo ya Bwana Mkubwa wa kupekua mwili wake, lakini Lisa akabeba chuki dhidi yangu. Kwanini anitoe sadaka kwa sababu ana chuki na Bi Njau? Bwana Mkubwa pia alipokuwa na uhusiano mzuri na Bi. Njau, angeweza kung'oa mwezi kutoka angani, lakini akiwa na Lisa, maagizo yake yote yakawa kosa letu. Ni vigumu sana kuwa chini ya mtu mwingine.”
“Maya, nyamaza.” Ganja alionya kwa sauti ya chini.
“Nina huzuni na siwezi kujizuia. Inawezekana, huelewi hisia za kuvuliwa nguo mbele ya wanaume wengi.” Maya alitokwa na machozi. “Siwezi kusahau sura yao. Wao... Waliendelea kunitazama kwa kuchukiza sana. Najisikia fedheha sana. Bora nife tu."

Baada ya hapo, aligeuka na kujitupa mlangoni.
“Maya, acha ujinga. Hakuna tatizo.” Master Ganja mara moja akamshika na kumrudisha mikononi mwake kwa nguvu.
“Master, usinizuie. Nifanye nini? Sikustahili wewe.” Maya alilia huku akianguka kifuani mwake.
“Usiwe mjinga. Wewe ndiye msichana ninayekutegemea." Ganja akampapasa nywele zake taratibu.
Sura ya: 428
“Ganja, nishike. Vinginevyo, nitajisikia vibaya sana. ” Maya alishusha kichwa ghafla na kuvuta nguo zile kifuani mwake bila mpangilio.
 Kisha, akambusu.

Master Ganja alikuwa mtu wa makamo. Akikabiliwa na mwili mchanga na wenye shauku wa Maya, hakuweza kujizuia. Mara chumba cha ofisi kikatulia tuli, ni kelele nyepesi tu za kujizuia kufurahia hisia tamu za tendo ndizo zilisikika kwa muda.
Ilipoisha, Maya aliegemea kifuani mwake na kunung'unika huku macho yake yakiwa yamefumba, "Master, ninahisi kuchoka sana wakati mwingine. Siku zote lazima nimsikilize Bwana Mkubwa. Ninaishi kama ... kama mbwa. ”
“Usiongee upuuzi. Tuna deni kwa Alvin Kimaro. Ikiwa si familia ya Kimaro kutulea, tusingekuwa hapa leo.” Ganja akamshika mabega. "Hupaswi kwenda upande wa Sarah Njau kwa sasa."
Maya aliingiwa na hofu. "Lakini Bi Njau ananihitaji sana ..."

"Maya, lazima ukumbuke kuwa Sarah ni mtu tu unayemlinda." Ganja alimkumbusha. “Ukiendelea hivyo, utafukuzwa kwa urahisi kutoka ONA. Unajua jinsi bei ya kuondoka ONA itakavyokuwa chungu? Asilimia za kuishi zitakuwa chache sana.”
Baridi ilitanda juu ya Maya. Ikiwa angetoka ONA, misuli na mishipa yake ingekatwa, angepoteza sanaa yake ya kijeshi, na pesa zake pia zingechukuliwa. Kwa watu kama wao ambao walifanya mazoezi ya karate maisha yao yote, kupoteza sanaa yao ya kijeshi itakuwa sawa na kuwa kilema.
 Alikenua meno kwa siri huku chuki ikizidi kumtoka machoni. Bila shaka angelipiza kisasi kwa hili.
Jioni, muda si mrefu baada ya Maya kuondoka, Master Ganja alipokea simu kutoka kwa Alvin tena. Alvin alisema moja kwa moja, “Nitakupa chaguzi mbili.

Moja, kumhamisha Maya nje ya nchi. Mbili, kumfukuza Maya kutoka kwa ONA.”
Uso wa Ganja ulibadilika kwa hofu. “Bwana Mkubwa, Maya alifanya kosa dogo tu. Tayari ameshatumikia adhabu yake. Ya nini tena kufanya hivyo?”
Sauti ya Alvin ilikuwa kali kidogo. "Master Ganja, usifikirie sijui uhusiano wako na Maya."
Ganja alishtuka. Siku zote alifikiri kuwa Alvin alikuwa hajui. "Bwana Mkubwa kijana, mimi ..."
"Nyamaza. Maya ni mdogo na mrembo, lakini kwa umri wako, ni mwanamke wa aina gani ambaye hujamwona?" Alvin alipunguza sauti yake.
 “Maya si mwaminifu kabisa kwangu tena. Sina imani naye kubaki ONA.”
Ganja alitabasamu kwa uchungu. Maya

alikuwa tofauti kwani alikuwa amemtazama akikua kwenye macho yake. Alipokua kutoka kuwa msichana huyo mdogo hadi kuwa mwanamke mzuri aliyempenda, kitu ndani yake ambacho kilikuwa kimetulia kwa miaka mingi ghafla kilionekana kuwa hai.
"Master Ganja, mbona unahuzunika?" Alvin aliuliza ghafla.
“Hapana, Bwana Mkubwa. Yeye ni mwanamke tu. Lakini, ninaogopa kwamba kumfukuza kutoka ONA tutasababisha taharuki kwa wengine. Wacha tumhamishe nje ya nchi,” Ganja alisema kwa tahadhari. Akiwa kiongozi wa ONA, hakuruhusiwa kuwa na huruma.
“Sawa, basi nitaenda na utaratibu wako. Master Ganja, ninafanya hivi kwa kukuheshimu.”Kisha, Alvin akakata simu.

Ganja akakaza mkono kwenye simu yake. Baada ya muda, alimpigia Maya. “Pakia mizigo na uende Tanzania kwa misheni. Nitakuja kukuona nikipata muda.”
Maya alishtuka. "Unamaanisha nini? Sitaki kwenda Tanzania. Unamaanisha nini utakuja kuniona ukiwa na wakati? Je, sitaweza kurudi tena?”
“Ni maagizo ya Bwana Mkubwa. Umegusa ujasiri ndani yake. Bwana Mkubwa anashuku kuwa wewe si mwaminifu vya kutosha tena.” Master Ganja alitabasamu kwa uchungu. “Alitaka kukufukuza ONA mwanzoni, lakini alinipa chaguo, nikachagua kukuacha uondoke nchini. Maya, nisikilize mimi. Mazingira ya Tanzania pia ni mazuri. Haitakuwa ngumu kwangu kuja huko kukuona mara kwa mara.”

"Sitaki kwenda mbali," Maya alisema kwa mshangao. “Bwana Mkubwa tayari amenipa adhabu kali zaidi. Kwanini bado ananitendea hivi? Je, familia ya Chande inapaswa kuishi kama mbwa kwa vizazi ili kuwa waaminifu kwa familia ya Kimaro?"
"Nyamaza." Ganja alionya. Nitakurudisha baada ya miaka michache hasira yake itakapopungua.
“Haitawezekana. Maadamu Lisa Jones yuko karibu, hakika hataniruhusu nirudi. Bahati mbaya siwezi kuvumilia kukuacha.” Maya alilia.
"Nitakuja kukutembelea mara kwa mara nimesema." Ganja akakata simu, akiwa amekasirika.
•••
Huko hospitali, Sarah alihangaika. Tangu Maya alipoitwa asubuhi, hakuwa

amepiga simu hata mara moja. Hilo lilimpa Sarah hisia mbaya.
Rodney naye hakufika siku hiyo, na aliondoka mara tu alipoenda kumuona jana yake. Alikuwa na haraka kila wakati.
Hapo mwanzo alikuwa nikipenzi cha kila mtu. Kila dakika, iwe ni Alvin, Rodney, au Chester, wote walimzunguka. Lakini sasa, ni mlezi pekee ndiye aliyebaki.
“Bi. Njau, nimekumenya sahani ya matunda.” Mlezi alitoa sahani kwa mbwembwe.
“Hebu tupilia mbali huko.” Sarah alisukuma sahani kwa hasira.
Mlezi naye alikasirika. “Sawa, nitafanya. Mimi ni binadamu pia. Ninakutunza tu kwa sababu unanilipa, lakini pesa inaweza kupatikana popote. Sihitaji kuchuma kutoka kwako. Kwa kweli

nimevumilia sana hasira yako ya kutisha. Si ajabu Bwana Mkubwa hawezi kukustahimili.”
Pamoja na hayo, aligeuka na kuweka vitu vyake na kuondoka.
“Nyinyi nyote ni wapuuzi.” Sara alilaani nyuma yake, lakini mlinzi hakumjali hata kidogo. Ghafla, yeye peke yake ndiye aliyekuwa amebaki wodini.
Aliingiwa na hofu na haraka akapiga namba ya simu ya Alvin. Ilipounganishwa, mara moja alilia. "Alvin, fanya haraka na uje. Niko peke yangu hospitalini. Maya aliitwa ghafla asubuhi, na mlezi naye ameondoka. Nimebaki peke yangu tu, nimekukumbuka sana...”
“Bi. Njau, Bwana Kimaro yuko kwenye mkutano.” Hans alimkatiza.

“Hans...” Sarah alipigwa na butwaa.

“Basi, mara tu mkutano utakapomalizika, unaweza...”
“Bi. Njau, ikiwa mlezi ameondoka, nitapanga mwingine aje huko. Lakini natumai hutaendelea kuwakoromea kwa hasira walezi wengine. Wao pia ni wanadamu, na wote wanafanya kazi kwa bidii ili kupata pesa. Hakuna aliye bora kuliko mtu mwingine.”
Macho ya Sarah yakawa mekundu kwa kila neno alilosema Hans.
“Hans, unamaanisha nini kusema hivyo? Wewe pia unanitazama kama mtu aliyeshindwa? Nakuhakikishia, msimamo wangu katika moyo wa Alvin hauwezi kubadilishwa.”
“Bi. Njau, hilo ndilo ninalopaswa kusema.” Hans alikata simu baada ya kumaliza kuongea.

Sarah alikasirika sana hadi akakaribia kuvunja simu yake. Kwa bahati nzuri, haikuchukua muda mrefu kwa Maya kuja. Lakini, Maya aliangua kilio mara tu alipomwona. “Bi. Njau, Lisa Jones ni mkatili sana...” Kisha akamwambia Sarah kile kilichotokea huko ONA mchana huo.
Sarah mwili mzima ukamtetemeka. Sio kwamba alijisikia vibaya kwa Maya, lakini hakutarajia kwamba Alvin angempenda Lisa ndani ya siku chache tu. Hata akampeleka ONA.
“Maya, samahani. Ni kwa sababu nilikushirikisha kwenye mambo yangu.” Alitoa machozi ya hatia. “Sina maana. Siwezi hata kukulinda. Sasa kwa kuwa nimepoteza uwezo na ushawishi wangu, ninadharauliwa na kuonewa.”
“Bi. Njau, usiseme hivyo. Sijawahi kukulaumu.” Maya alisema kwa haraka,

“Lakini siwezi kukulinda tena. ONA itatuma mtu mpya, lakini ninatabiri kwamba ataondoka baada ya wewe kuruhusiwa kutoka hospitalini. Alvin amerogwa kweli na Lisa Jones muda huu. Yeye ni mpuuzi.”
“Usiseme hivyo,” Sarah alinung’unika. “Lisa kushughulika na wewe ni hatua ya kwanza tu. Ninaogopa kwamba atakuja kwangu hatua ijayo. Daima amekuwa akinichukia kwa kupendekeza nimpeleke hospitali ya magonjwa ya akili kwa matibabu. Mtu mwenye kulipiza kisasi kama yeye hataniacha kamwe.”
“Ndiyo. Rodney Shangwe pia mikono yake imejaa." Maya aliuma meno. “Bi. Njau, usijali. Sitaenda Tanzania. Nitabaki nyuma kisiri ili kukulinda.”
"Lakini wewe..."

“Kweli, kuna kitu sijakuambia. Master Ganja, kiongozi wa ONA, ni mpenzi wangu.” Maya ghafla alisema kwa aibu, "Ananipenda sana, kwa hivyo atanisaidia kutunza siri hii."
"Nini? Sikujua hilo.” Sura isiyo ya kawaida iliangaza machoni pa Sarah, lakini alimshika Maya kwa utulivu na kusema, “Hongera, Maya.
 Una furaha kuliko mimi.”
"Sio lazima." Maya alipumua. "Mwishowe, sisi ni mbwa tu wa Alvin. Siku zote tunapaswa kuwa waangalifu tunapokuwa pamoja.”
“Haijalishi. Wewe ni mrembo na mkarimu, nina hakika kwamba Master Ganja atakupenda daima."
Sarah alimbembeleza Maya hadi alipoondoka.
Sura ya: 429

Kisha, Sarah aliinamisha kichwa chake na kuachia kicheko kidogo.
Hakutarajia Maya kuwa mwanamke wa Master Ganja. Hilo lilimvutia sana.
Ikiwa kweli Alvin asingerudi kwake, asingejali kumwangamiza mtu ambaye angeweza kumchukua.
 Lakini, sasa haukuwa wakati wake.
Alipompigia tena Rodney, sauti yake ilikuwa laini. "Rodney, unafanya nini?"
"Sarah, namsubiri Pamela." Sauti ya Rodney ilisikika. "Sasa, ni Pamela pekee anayeweza kunisaidia kuiokoa Osher, kwa hivyo ninahitaji kumrudisha mwanamke huyo kwenye kampuni."
Damu ya Sarah ilichemka baada ya kumsikia. Moyo wa Alvin ulikuwa umetekwa na Lisa. Halafu sasa, hata mpango wake wa kando, Rodney

alikuwa akimzungukia Pamela siku nzima.
 Kwa kweli alihisikama dunia nzima imepanga kumfanyia njama!
"Rodney, nina hasira sana." Sarah alisikika akiwa na huzuni. "Nilikuwa na Maya, lakini sasa, pia amehamishwa."
"Si amekuwa akikulinda muda wote huu?" Sauti ya Rodney ililipuka ghafla.
"Anafuata tu maagizo ya ONA." Sarah akahema kwa uchungu. “Mlezi aliondoka pia, akisema nina hasira. Kwa kweli sikutarajia kwamba ningeishia katika hali hii.”
"F*ck. Alvin ni mjinga. ” Rodney hakutarajia Alvin angekuwa hana moyo kiasi hicho. Hata kama alitaka kuachana naye, je, ilimbidi awe na kinyongo hivyo na kuwahamisha wafanyakazi wake? “Usifikirie juu yake. Nitakuja mara moja.”
Hata hivyo, alipokata simu na kugeuka

ili kuondoka, alimuona Pamela akiwa amesimama nyuma yake. Hakujua ni muda gani yeye alikuwa amesimama hapo.
Alikuwa amevalia vazi jeupe lililofumwa na kofia nyeupe ya baseball kichwani. Kwa tabasamu hafifu kwenye kona ya mdomo wake, alionekana mrembo na asiyeeleweka mwanzoni.
"Hi, Mwenyekiti Shangwe. Ulijuaje kuwa nimehamia Brighton Gardens?" Pamela alitabasamu. "Bwana Kimaro alikuambia?"
Rodney alikasirika sana baada ya kutajwa kwa Alvin.
 Chester ndiye aliyemwambia. Alikumbuka kuwa hii ni nyumba ya Alvin, lakini aliihamishia kwa Pamela.
Pamela alihema kwa nguvu. “Alvin ni mkarimu kupita kiasi. Nilitaka kubaki na

Lisa, lakini alihisi kwamba nilikuwa ninawaendesha kwa gurudumu la tatu, kwa hiyo akanipa ghorofa hii. Kuishi hapa peke yangu ni nraha sana. ”...
“Umemaliza?” Akiwa njia kumfuata Pamela, Rodney alijiambia kudhibiti hasira yake. Hata hivyo, aligundua kwamba kila alipowasiliana na mwanamke huyu, shinikizo la damu lilipanda. Hakutaka kitu zaidi ya kumkata vipande vipande.
“Hakika. Nimemaliza. Unaondoka?” Pamela alimtazama kimya kimya.
“...Ndio. naondoka.” Rodney alichanganyikiwa aliposema. Alikuwa amemngoja kwa muda mrefu sana, lakini alipotokea, alikuwa kishamuahidi Sara kwamba angeenda.
“Bwana Shangwe, umepofushwa sana na upendo.” Pamela alivutiwa. “Ili tu kumuwahi Sarah, hata hujali kuhusu

kampuni yako. Ikiwa hutafanya kazi kwa bidii, naweza kushirikiana na SE Group katika siku chache zijazo. Bila kutaja, nina fomula mpya niliyotengeneza mkononi mwangu. Matokeo ni mazuri sana, na malighafi sio ghali. Bwana Malugu anaitaka vibaya sana.”
Rodney alifikiria juu ya jambo fulani, na alikuwa karibu kuzungumza wakati Pamela alipogeuka na kuanza kuondoka.
 “Subiri...” Aliongea kwa haraka.
"Nini? Si unaondoka? Si unamuwahi Sarah?” Pamela aliuliza kwa mshangao.
Rodney aliona aibu. Je, angewezaje bado kuwa katika hali ya kumuona Sarah? “Pamela Masanja, tuongee. ”
“Kuongea? Hakuna cha kuzungumza. Kila unapozungumza na mimi, unakasirika na kuanza kupiga kelele.

Kwa hivyo, sina muda wa kubishana na wewe.” Pamela alipunga mkono kwa uso wa kikauzu.
Uso mzuri wa Rodney ulikunjamana kwa hasira. Jamani. Alifanya ionekane kana kwamba ni kosa lake. Yeye ndiye aliyemkasirisha. Kwa kawaida alikuwa muungwana sana kwa wanawake wengine.
“Pamela, najua kwamba nilienda mbali sana hapo awali, lakini unajua kuwa wale wanawake wabaya ulionipambanisha nao mara ya mwisho... Umeniharibia jina?!”
"Unasema nini? Unapaswa kunishukuru. Kama si mimi, wazazi wako wangekulazimisha kumuoa yule binti usiyemtaka. Lakini sasa, kwa sababu yangu, hakuna mtu ambaye yuko tayari kuchumbiwa nawe, kwa hivyo unaweza kuendelea kumngoja

Sarah Njau wako. Siyo nzuri hii?” Pamela alijibu mara moja, na sentensi 'Nilifanya hivi kwa faida yako mwenyewe' iliandikwa kwenye uso wake wa fahari.

Rodney kwa mara nyingine akashusha pumzi ndefu. “Sawa, asante. Wewe ni mfadhili wangu. Je, ninaweza kukununulia chakula cha jioni, mfadhili?”
Pamela akatikisa kichwa. “Sitaki kwenda nje. Nimekuwa nikila chakula cha nje kila siku, na tumbo langu halijisikii vizuri, kwa hiyo nataka kula chakula cha kupika mwenyewe. Unaweza kunipikia?”
"Nini?" Rodney alifikiri alikuwa kiziwi.
“Hutaki? Ikiwa hutaki, basi usahau. Nilifikiri tunaweza kutumia nafasi hii ili tuongee juu yake...”

“Sawa, nitafanya.” Rodney alijikaza kiume na kumfuata. Hakuwahi kufikiria kuwa ingetokea siku ambayo ingebidi asikilize mihemko ya Pamela.
Baada ya kupanda ghorofani, Pamela alijitupa kwenye sofa. Kisha, akararua vitafunio kwenye meza na kuanza kula. “Fanya haraka kupika. Ikiwa chakula kitakuwa kibaya, basi hakuna nafasi ya kuzungumza. Pia, usifikirie hata kumwomba mtu msaada. Mimi ni aina ya mtu ambaye anapenda uaminifu."
Rodney alifungua jokofu kwa uso uliojaa huzuni. Kulikuwa na vitu vingi ndani, lakini ilikuwa tu mtindi, maziwa fresh, na matunda. Hakukuwa na vyakula vya kupikia. Baada ya kutafuta kwa muda mrefu, aliona nyama na samaki waliogandishwa kwenye friji. Aliangalia tarehe. Zinge expire ndani ya muda wa siku mbili.

Alinyamaza kimya akimtazama yule mwanamke aliyekuwa nje na hakujua ni mwanamke wa aina gani. Hakika hakuwa mwanamke mwema, na hakuna mtu aliyetaka mwanamke kama huyo.
Pamela aliingia baada ya kula pakiti ya chips za viazi na kumuona akipunguza baridi ya nyama hiyo. Alikuwa ameipika hapo awali alipoinunua tu. Hata hivyo, kwa kuwa nyama hiyo haikuungwa, ilikuwa na ladha mbaya sana.
 Ndani ilikuwa mbichi pia.
“Unatengeneza nyama? Hiyo ni ngumu kupika." Kutokana na wema wa moyo wake, Pamela alimkumbusha, “Kwanini usishuke chini ukanunue mboga ili kupika chakula chepesi tu?”
"Hakuna haja." Rodney alimtazama kwa huzuni.
Uso wake ulimfanya Pamela amfikirie

mbwa wake huko Dar es Salaam. Kisha, akageuka na kumpigia mama yake simu ya video. “Mama, Milo yuko wapi? Nilimwona mvulana anayefanana na Milo na nikamkumbuka ghafla.
“Mwanaume gani?” Mama yake alicheka huku akileta mbwa mdogo wa hudhurungi haraka. "Lazima aonekane wa ajabu sana ikiwa anafanana na Milo mdogo. Haahaahaaa."
“Si ajabu. Yeye ni kama msichana."
"Oh, unazungumza juu ya wanaume wa kike? Binti mjinga, ukitafuta mchumba, utafute wa kiume. Usiendelee kukaa peke yako. Unapaswa kuanza kuniletea wajukuu.”
Huko jikoni, Rodney alijichukia kwa kusikia maneno hayo. Alimwona mtu aliyefanana na mbwa? Mwanaume huyo alikuwa kama msichana? Alikuwa

effeminate? Dume-Jike? Rodney alikuwa na uhakika wa 100% kwamba Pamela alikuwa akimzungumzia yeye. Hili lilikuwa tusi kwake.
Akajikaza sana jikoni na kushusha pumzi ndefu. Alilazimika kuvumilia.
Baada ya kuzungumza na mama yake kwa zaidi ya dakika 40, harufu nzuri ilikuja kutoka jikoni, na akakata simu ya video.
 Muda si muda, Rodney alitoka na sahani za nyama, Ugali na samaki wa kukaanga.
Pamela alipigwa na butwaa. “Sh*t. Unaweza kupika kweli?" Macho yalimtoka kana kwamba ameona mzimu.
Sura ya: 430
Rodney aliuma meno. “Inabidi ushangae hivyo? Je, ni ajabu kwamba naweza kupika?”

“Ndio. Machoni mwangu, wewe ni bwana mdogo asiye na faida, mwenye kudekezwa ambaye hujui kufanya lolote zaidi ya kufuata maagizo ya Sarah na kufanya matakwa yake kila siku.” Pamela alitikisa kichwa bila kusita.
Rodney alichukia sana. Alipaswa kuweka sumu kwenye sahani mapema ili kumaliza yote.
Pamela alikata kipande kidogo cha nyama na kuonja. ladha ilikuwa ya kushangaza ... nzuri sana. Ilikuwa na ladha ya kweli kama nyama iliyopikwa na mama yake. Ugali ulikuwa laini na hata samaki walikaangwa vizuri.
"Hivi umetengeneza wewe mwenyewe?" Alikuwa na hamu ya kutaka kujua. "Hukuomba wasaidizi wako kuituma kupitia kwa dirisha la jikoni kwa drone?"

"Hapana, nilifanikiwa mwenyewe. Nilipenda kupika tangu nilipokuwa mdogo, sawa?" Rodney alishindwa kuvumilia.
“Hii ni kweli ni ajabu. Kupika kwa Alvin ni majanga, kwa hivyo sikuwahi kufikiria kuwa angekuwa na rafiki kama wewe. ” Pamela akahema tena. Ilikuwa ni mara ya kwanza kumtazama kwa makini Rodney.
Sifa za mtu huyo zilikuwa nzuri, na macho yake yalionekana kama yanaweza kumshawishi mtu wakati wowote. Umbo lake jembamba lilipendeza katika mavazi yoyote. Ikiwa angejiunga na tasnia ya burudani, bila shaka angekuwa aina vijana ambayo wanawake huwa waanapagawa nao.
“Mbona unanishangaa hivyo? Mimi nakuambia, sitaanguka kwa ajili yako.”

Rodney alijisikia vibaya chini ya macho yake na akasema haraka, "Tunaweza kuzungumza juu ya formula sasa?"
“Hakika. Endelea." Pamela akaitikia kwa kichwa.
"Rodney alisema, "Ninajua unataka kushirikiana na SE Group, lakini ni lazima nikukumbushe kwamba SE daima imekuwa chini ya Osher kwa huduma ya ngozi nchini. Kawaida huwalenga wanafunzi. Wanawake wa tabaka la juu wanaidharau bidhaa zao. Ukifanya nao kazi, utakuwa unashusha hadhi yako.
"Pili, SE Group ina maduka machache kuliko sisi, iwe ya ndani au nje ya nchi. Ukichagua Osher Corporation, bidhaa zako zitakuwa na nafasi ya kuwa maarufu nchini kote na nchi jirani. Lakini ukichagua SE, inaweza kuuzwa tu nchini Kenya kwa wingi. Kando na hilo,

Mwenyekiti wa SE Group, Lincoln Malugu, ni bahili na mkatili hata kwa mtoto wake mwenyewe Bwana Erick Malugu.”
"Kama wewe, ni mkatili na huna huruma pia." Pamela alidhihaki.

Rodney alijizatiti na kusema, “Lincoln Malugu ana tabia ya kuhonga wanawake. Anatupa pesa kwa wanawake wa nje lakini hatoi hata senti moja kwa mkewe nyumbani. Niamini. Yeye ni tajiri sana, lakini kijana wake Erick Malugu amesoma kwa shida sana. Mkewe na binti yake mdogo bado wanaishi katika nyumba ya vyumba viwili.. Mara tu kashfa hii ikizuka, itakuwa pigo kubwa kwa SE.
 Baada ya yote, SE inapata pesa kutoka kwa wanawake.
"Je, huogopi kwamba nitamwambia

Bwana Malugu?" Pamela aliinua macho yake.
“Tayari nimetuma ushahidi wote kuhusiana na ulaghai wake kwa mkewe. Labda atafanya tukio hivi karibuni." Rodney alikata nyama yake polepole na kwa utaratibu huku akisema, "Hata kama mke wake hatatoa ushirikiano, nina uwezo wa kulikuza mimi mwenyewe."
"Nakuamini. Nani asiyejua kuwa Alvinarah Media Network ya Kimaro inamiliki nusu ya vyombo vya habari vya mtandaoni nchini humu?” Pamela alicheka. "Bwana Shangwe, inaonekana kama nilikudharau."
“Hapana, hukunidharau. Umeikadiria SE Group kupita kiasi." Rodney alitikisa kichwa.“ Bidhaa zilizosalia za SE hazitoshi kushindana na Osher. Ingawa tumekuwa na migongano mingi

isiyopendeza hapo awali, wewe ni mtu mwerevu, Bi.
 Masanja. Kwanini ufanye mambo yawe magumu kwa pesa na kazi yako?"
Pamela alidhihaki. “Kama nisingepigana sana, maisha yangu ya baadaye yangeharibiwa na nyinyi. Rodney Shangwe, uliza dhamiri yako. Umewahi kujisikia hatia kuhusu mimi?
“Kwako, mimi nilikuwa ni mwanakemia wa kawaida wa vipodozi. Lakini je, umewahi kufikiria jinsi tnilivyojitahidi kupambana kwa ajili ya kampuni yako? Wakati ninyi mlipokuwa mkinywa pombe na kucheza na marafiki zako, nilikuwa bado nachoma mafuta ya usiku wa manane kwenye maabara. Ulipotoka kucheza mpira na kwenda kuvua samaki, nilibaki nyumbani tukipiga vitabu.” Macho ya Pamela hayakuweza kujizuia kuwa mekundu alipokuwa akiongea.

"Unaelewa jinsi ulivyonikatisha tamaa wakati ulinifukuza na kuniblacklist? Tukio la Thomas Njau lilitokea kwa bahati mbaya wakati huo huo, na niliharibiwa kabisa sifa yangu. Sikuweza kupata kazi na sikuweza kukubalika popote, kwa hiyo nililazimika kwenda ng’ambo.
"Kama mgeni, nilidharauliwa hadi nje ya nchi. Sikurudi hata kwenye nyumba yangu kila siku. Kati ya siku 365 kwa mwaka, nilitumia siku 350 kukesha katika maabara na kuzirai mara kadhaa.
"Kuna mara mbili nililala kwenye sakafu baridi usiku kucha na niliamka peke yangu kwenda hospitalini. Nilifikiria kukata tamaa, lakini nilijipa moyo na kupigana ili nirudishe hali yangu ya kujistahi iliyopotea.”
Kadiri alivyozidi kuwaza jambo hilo ndivyo moyo wake ulivyozidi kuwa

mchungu, machozi yakimtoka.
"Halo, usilie." Rodney alijisikia hatia kidogo alipokuwa akimsikiliza, akashindwa kumuona akilia. Alimfanya ajione kama kweli alikuwa na hatia.
"Nina huzuni na kuumia, lakini hauniruhusu nilie." Machozi ya Pamela yalianguka chini kwa matone makubwa.
Hata hivyo, kulikuwa na msemo usemao kwamba mtu akiwa mrembo anaonekana mrembo zaidi akiwa analia. Ilikuwa ni kama matone ya mvua yakianguka kwenye petals za maua.
"Sawa, endelea kulia." Rodney alinyamaza kimya kutokana na kukemea
Kwake.
"Rodney Shangwe, wewe ni mwanaume? Ninalia, lakini bado hujui

jinsi ya kunifariji. Si ajabu huwezi kupata rafiki wa kike.” Pamela akamrushia kitambaa alichokuwa ametumia kujifuta machozi.
"Pamela Masanja, unakosa akili kidogo." Rodney alikasirika.
"Wanawake siku zote hawana akili." Pamela akamfonza. Uso wake uliojaa machozi maridadi, mdogo na mzuri sasa ulikuwa mzuri sana kuutazama.
Kumtazama, Rodney kwa namna fulani alifikiri kwamba ngozi yake ilikuwa nzuri sana, na kwa kweli alionekana mzuri kidogo baada ya kulia.
“Nimefikiria. Tunaweza kushirikiana.” Pamela ghafla alisema, "Fomula ni dola laki 5 kila moja. Wakati huo huo, ninataka pia asilimia 10 ya hisa za Osher Corporation. Kila mwaka, Osher italazimika kuwekeza dola milioni 40

katika kutengeneza bidhaa mpya. Zaidi ya hayo, ninataka kuhudumu kama mkurugenzi wa idara ya R&D (maendeleo na utafiti) ya Osher.” Rodney alishtuka. "Masharti mengine ni sawa, lakini unataka asilimia 10 ya hisa? Huo ni wizi wa mchana.”
“Fikiria jambo hilo. Usiposhirikiana nami, bado nitachagua SE. Hata kama SE inakumbwa na kashfa hasi, mimi natafuta pesa tu. Zaidi ya hayo, unapaswa kuelewa nguvu zangu. Mkemia wa vipodozi mwenye kipawa kama mimi anaweza kugunduliwa lakini hatafutwi. Ikiwa utaichukua nafasi hii au la itategemea wewe.”
Pamela akapangusa pua yake na kuanza kula nyama hiyo kwa raha zake.
 Muonekano huo ulimfanya Rodney ashuku kuwa kilio chake hapo awali kilikuwa ni uzushi tu.

Rodney aliondoka baada ya chakula cha jioni, lakini masharti ya Pamela bado yalikuwa akilini mwake. Kwa hivyo, jambo la kwanza alilofanya ni kuelekea kwenye kampuni kwa mkutano.
Ilipofika saa 11 jioni Sarah alipiga simu, ndipo alipokumbuka kuwa alikuwa amesahau kumtembelea Sarah hospitalini.
“Samahani, Sarah. Nimekuwa busy na mikutano. sikukusudia.”
TUKUTANE KURASA 431-435
ONYO: Ni marufuku kusambaza, kukopi wala kuuza kazi hii kwani endapo kama tutakubaini basi sheria itachukua mkondo wake (By: Official Dully)
 
Back
Top Bottom