Simulizi: Lisa

Simulizi: Lisa

"Chochote unachofikiria," Eliza alijibu kwa unyogovu. "Ikiwa unafikiri nina nia ya siri au nataka kuangalia bahati ya Sarah inavyoisha, sijali.”

Baada ya kuutoa moshi huo, macho ya Chester maridadi yaliganda kidogo.
Muda mfupi baadaye, alinyanyuka polepole na sauti yake ilikuwa baridi kama barafu. "Nadhani unamchukia Sarah, lakini huna historia na Sarah. Au... unatazama kwa niaba ya mtu fulani.” Eliza alikaa kimya.

Hata hivyo, moyo wake ulishikwa na woga.

“Eliza, niambie. Je, Charity bado yuko hai?" Chester ghafla akashika kidevu chake. "Kwa kuwa alikuwa rafiki yako wa utotoni, haiwezekani aje kwako ikiwa hajafa."

“Ha…” Eliza alionekana kama anasikia mzaha. Macho yake mazuri yalionyesha hasira ya chuki. “Unafikiri mtu anaweza kuruka kwenye bahari iliyochafuka bila kufa? Ikiwa una uwezo, basi nenda ujaribu mwenyewe. Amekufa. Pia nilitamani ... asife.” Ingawa roho yake ilikuwa bado hai, mwili wake ulikuwa umekufa milele.

“Kwa kweli sielewi kwanini unaendelea kuhangaikia. Iwapo Charity amekufa au la, na nini na wewe?"
Eliza alicheka. "Usiniambie kuwa yeye ni mmoja wa wanawake ambao ulikuwa nao siku za nyuma."

Chester aligeuka na kufumba macho. Pia hakujua ni kwanini alikuwa akihangaika sana kujua kama Charity amekufa au la. Labda ilikuwa dhamiri yake ya mwisho.

"Ulidhania sawa. Alinipenda sana zamani. Alinipenda hadi kufa,” Chester aliinua midomo yake myembamba aliposema neno baada ya neno.

Moyo wa Eliza ulikaribia kupasuka kwa hasira. "Nadhani ikiwa nyinyi wawili mlikuwa na uhusiano hapo awali, lingekuwa jambo la kusikitisha zaidi maishani mwake.”

“Unawezaje kuwa na uhakika hivyo? Wewe si yeye,” Chester alitabasamu kwa ubaya.


“Namfahamu. Yeye ni mtu mwenye kiburi. Lazima atachukizwa sana na mwanaume kama wewe ambaye anajua tu jinsi ya kuingia kwenye joto anapoona wanawake, "Eliza alisema kwa baridi.

Macho baridi ya Chester yalitetemeka na huku miguu yake mirefu ikimkaribia. “Kwa vile ulisema kwamba ninaingia kwenye joto nikiona mwanamke, labda unasema kweli. Niko kwenye joto ninapokuona sasa hivi.”

Umbo refu la mwanaume huyo na lililo wima lilimkandamiza. Moyo wa Eliza ukazidi kukaza na bila fahamu akapiga hatua mbili nyuma hadi mwili wake ukagonga ukuta wa nyuma yake. Mikono ya Chester ilikandamiza ukutani, na kuuweka mwili wake katikati yake na ukuta. Harufu hafifu, tamu ya mwili wa mwanamke huyo ikaingia puani mwake.
Mwili wake uliganda.
Ilikuwa ni harufu aliyoisikia kwa mara ya kwanza katika usiku wake wa kukumbukwa.

Hakufikiria juu yake hapo awali na alipuuza.
Hata hivyo, harufu aliyoizoea ilipoibuka tena, bado angeweza kuikumbuka.
Baadaye, aliuliza na kugundua kuwa ilikuwa shampoo ya nywele ya Charity aliyoitumia. Alipenda kutumia aina hiyo tu.
Hakutarajia Eliza angetumia aina hiyo pia. Akatazama chini. Mwanamke mikononi mwake alitazama juu yake, macho yake meusi na yenye kung'aa yakificha mlipuko mkali wa hasira. Alionekana kama yeye. Alifanana naye sana. Koo la Chester lilimtoka huku kichwa chake kikiwa moto, akainamisha kichwa chake na kumbusu midomo yake mizuri kwa nguvu.


Ingawa alikuwa na wanawake wengi hapo awali, msukumo huu ulikuwa umetoweka kwa muda mrefu sana. Midomo yake ilkuwa na rdha sawa na ile ya kumbukumbu yake,
tamu kama jeli.
Alishindwa na ladha ya midomo yake na hakuweza kujizuia.


Eliza aliganda. Hakuwahi kufikiria kwamba Chester angekuwa... hana haya. Alikuwa anaoa hivi karibuni. Hata kama alijua kwamba hakuna uaminifu wa ndoa inapokuja kwa watu kama yeye, angalau angemheshimu kwamba yeye ni rafiki wa utoto wa Charity, lakini, bado alikuwa mbabe sana. Je, alikuwa na kiburi kiasi kwamba hakuwa na mipaka ya maadili? Kufikiria kwamba aliwahi kumpenda mtu kama huyo. Eliza alihisi kichefuchefu, akachukia sana.

Alimsukuma kwa nguvu, lakini kifua cha mwanamume huyo kilikuwa imara sana.
Hakuwa na jinsi zaidi ya kumng'ata kwa ukali mpaka damu zikamtoka.
Chester alihama ghafla. Eliza alimsukuma na kumpiga kofi usoni. Ofisi nzima ilikaa kimya baada ya kupigwa kofi.


“Unathubutu kunipiga?” Macho ya Chester yalikuwa mazito, kama nyoka mwenye hasira kali.
 
“Kwanini nisingethubutu kukupiga? Nisipompiga tapeli aliyejaribu kunishambulia, je, ninapaswa kukunyamazia au kukupeleka nyumbani kukutana na wazazi wangu?” Eliza alicheka.

"Vizuri sana, Eliza Robbins. Umenikera kabisa safari hii. Kwa vile uliniita tapeli, nitakuonyesha jinsi nilivyo tapeli.” Chester alimnyanyua kiunoni na kumtupa kwenye sofa huku akimkandamiza mwili wake mrefu.
"Chester Choka, wacha niende!" Eliza kwa kweli hakutarajia mtu huyu kuwa kichaa kiasi hicho. Zaidi ya hayo, Chester alifanya kazi mara kwa mara na alikuwa na nguvu sana. Alipobanwa naye hivi, nguvu zake zilikuwa kama chungu ukilinganisha na tembo.

Hata alipoinua mguu wake kwenda juu, Chester alibana miguu yake na kucheka kwa sauti ya chini. "Una kazi sana."

Macho ya Eliza yalimtoka kwa hasira. "Chester choka, ikiwa unataka kucheza na wanawake, kuna wengi kwako wa kuchagua. Mbona unanikera sana? Kwa sababu mimi ni rafiki wa Charity? Unapenda sana kucheza na akina dada? Huogopi kwamba...mpenzi wako atakufa bila amani?"


Kufa bila amani?
Maneno matatu yalimgonga kama nyundo. Mwili wa Chester uliganda. Eliza alichukua nafasi hiyo kumsukuma. Haraka akaweka vizuri nguo zake na kutoka nje ya ofisi haraka.

Bila kutarajia, baada ya kupiga hatua kadhaa, alimuona Cindy akiwa amebeba begi huku akitembea juu juu. Alipoona nguo za Eliza zikiwa rafu pamoja na alama shingoni, alitupia macho kwenye mlango wa ofisi ya Mkurugenzi nyuma ya Eliza na macho yake yakamtoka kwa dharau.

“Eliza, sikutegemea ungekuwa rahisi kiasi hicho, au umekuwa hivyo siku zote? Watu katika kampuni walikuita mtukufu na mwema, lakini ikawa wewe ni kama hivi.”

Eliza alimtazama kwa dharau na kugeuka kuondoka bila kuangalia nyuma.

“Simama. Huoni kwamba Cindy anazungumza na wewe?” Kando ya Cindy, msaidizi wake Ada alipaza sauti, “Haya, hukumsikia Cindy akizungumza nawe? Je, wewe ni kiziwi? Hutaki kufanya kazi katika kampuni tena?"

Hata hivyo Eliza alimpuuzia kabisa kana kwamba hakuwasikia na kuondoka zake. Ada alikasirika. "Cindy, huyo b*tch anakukosea heshima sana."

“Ni sawa. Yeye atakuwa ni mchepuko wa Mkurugenzi Mutui. Tayari ana mke. Ulifikiri atamuoa?” Cindy alicheka kwa madaha na kwenda mbele kuusukuma mlango wa ofisi.


Alipoona sura ya Chester imekaa kwenye sofa, mara moja alipigwa na butwaa. Mwili wake mzima ulionekana kuganda. Alichungulia ofisini lakini hakumuona kabisa Shedrick Mutui. Yaani yule aliyekuwa na Eliza sasa hivi... alikuwa Chester? Hiyo inawezaje kuwa?
 
"Hakuna haja ya yeye kuuliza." Ghafla sauti ya kike ya kivivu na ya kupendeza ilisikika badala ya Alvin. Rodney aliitazama simu yake. Ilikuwa saa mbili asubuhi. Ni nini hiki? Ilikuwa ni mapema sana lakini tayari walikuwa pamoja?
Au Lisa na Alvin walilala pamoja jana yake usiku? Alihisi kama alipata shambulio lingine la mapenzi tena.
Rodney alikesha kibarazani kwa Pamela akipigwa baridi.

Alvin na Lisa alikesha kitandani wakipeana mahaba.

Rodney itabidi ajiongeze kutimiza sharti la pamela ili naye awe anakesha kitandani na Pamela 😀
 
Alipoona sura ya Chester imekaa kwenye sofa, mara moja alipigwa na butwaa. Mwili wake mzima ulionekana kuganda. Alichungulia ofisini lakini hakumuona kabisa Shedrick Mutui. Yaani yule aliyekuwa na Eliza sasa hivi... alikuwa Chester? Hiyo inawezaje kuwa?
Pole yake kilaza Cindy 😂😂
 
Rodney alikesha kibarazani kwa Pamela akipigwa baridi.

Alvin na Lisa alikesha kitandani wakipeana mahaba.

Rodney itabidi ajiongeze kutimiza sharti la pamela ili naye awe anakesha kitandani na Pamela [emoji3]
[emoji1787][emoji1787]na ule mdomo wa Pamela ataweza ata kulala nae siku ikaisha maana ashindwi kumuamsha usiku wagombane
 
Back
Top Bottom