Simulizi: Mapenzi ya Mungu hayakwepeki mtoto wa mfalme alikufa licha ya baba yake kujenga ghorofa la vioo ili kumlinda

Simulizi: Mapenzi ya Mungu hayakwepeki mtoto wa mfalme alikufa licha ya baba yake kujenga ghorofa la vioo ili kumlinda

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Kuna mfalme alijaliwa kupata mtoto wa kiume. Yule mtoto alikuwa na afya njema, sura ya kuvutia alivutia hata wageni waliofika kwa mfalme. Mfalme alimpenda yule mtoto kama roho yake.

Mtoto yule alipofikisha miaka minne, Mungu Mwenyezi alimtaarifu mfalme kuwa mtoto yule atakufa siku si nyingi. Mfalme akasema moyoni nitamlinda mtoto huyu kwa uwezo wangu wote kifo kisimsogelee.

Mfalme alijenga nyumba ya ghorofa akitumia vioo ili aone kila mtu na kila kitu kinachoingia na kutoka kwenye nyumba ile. Alitafuka wafanya kazi na kuwa pa amri wakae na mtoto ghorofani wasishuke chini mahitaji yao yote watatimiziwa.

Siku moja Mfalme akiwa kwenye baraza alipita mtu anauza mtoto wa kondoo. Ndama yule alikuwa mweupe aliyejaa sufu. Mtoto wa mfalme kumuona alilia na kugalagala akimtaka acheze nae.

Vijakazi vilimwambia yule mtu, tupe huyo ndama tumpe mtoto ili aache kulia, baba yake akimaliza baraza atakupa pesa yako. Mtoto wa mfalme alipewa ndama achezee, Khee kumbe ndama alikuwa na nyoka mdogo kwenye sufu, alimgonga mtoto wa mfalme. Kwakuwa sumu ilikuwa kali sana mtoto aliaga dunia kablahata Baba yake hajamaliza baraza.
 
Back
Top Bottom