MIMI NA MIMI
A Story by Elton Tonny
Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Yasiyotazamiwa
R-rated 18+
Enjoy!
★★★★★★★★★★★★★★★★★★★
SEHEMU YA THELATHINI NA SITA
★★★★★★★★★★★★★★★★★★★
"Well?"
Swali hilo la Bertha likanifanya nimtazame usoni tena baada ya yeye kuona nimebaki kimya tu. Bado nilikuwa nalitafakari pendekezo lake la kuja kukaa naye hapa hotelini.
Nikamuuliza, "Kweli unataka nije tukae wote?"
"Ninajua nilichokisema. Amua. Utakuja hapa, au?" akauliza hivyo kwa uhakika.
Nikatulia kidogo, kisha nikatikisa kichwa kuonyesha kwamba nimekubali na kumwambia, "Sawa. Nitakuja tukae pamoja."
Akaonekana kuridhishwa na jibu hilo, naye akashusha pumzi ya utulivu.
"Itabidi nije kwenda kufata vitu vyangu baadaye," nikamwambia hivyo.
"Eeh, baadaye. Sasa hivi tunatoka. Si uko vizuri?"
"Whenever you are ready."
"Good. Tunaingia Kivukoni kwanza, halafu... huo mkono umefanyaje?" akauliza hivyo kiudadisi.
Alionekana kuwa na haraka, kwa hiyo nikamwambia, "Nilijikata tu kidogo, hakuna tabu. Twend'zetu."
Akatoka mbele yangu na kwenda kubadili viatu alivyokuwa amevaa, akivaa vile kama mabuti ya kike ya khaki pamoja na koti fulani zito la manyoya kwa juu lililoonekana kuwa la gharama, naye akasema, "Utazunguka nami na huto tundala twako ama utavaa viatu? Chukua zile pale sneaker..."
"Ah, hamna bana. Leo nataka miguu iwe free. Twende tu, niko poa," nikamwambia hivyo.
Akachukua kimkoba kilichokuwa kitandani na kuanza kuja upande wangu, naye akasema, "Jiweke tayari HB. Nahitaji personality yako ya kibabe na ya u-smart uionyeshe vizuri mbele ya wote tutakaokutana nao. Leo tunaenda kutana na watu wenye mifuko bila Festus kuwepo. Nikikutambulisha kwao kumbuka kwamba uko na Queen, kwa hiyo..."
"Nijionyeshe kuwa King. Usiogope. Nina wewe," nikamwambia hivyo.
"Ungekuwa umekuja na mtoko kama suti ndiyo wangekuona kuwa King. Hapa watakuona kama lowlife tu," akasema hivyo.
Nikatabasamu kidogo na kusema, "Ndiyo point yenyewe. Wataona una uwezo mzuri sana wa kutafuta vitu vyenye thamani hata kutokea majalalani. Me ni dhahabu yako, na leo ndo' unaenda kuwaonyesha kwamba umenitoa udongoni ili nije kuwaongezea ufanisi," nikamwambia.
Akawa ananiangalia kwa utathmini.
Nikaishika hereni yake sikioni na kisha shingo yake, nami nikamwambia, "Usiwe na hofu madam wangu. State unayotaka utaijenga tu. Twende ukawawashie sasa."
Akatabasamu kiasi kwa kiburi na kutikisa kichwa kukubali, naye akasema, "Let's go," kisha akatangulia kutoka.
Nikakaza meno yangu na kushusha pumzi, kisha nikageuka pia ili kwenda na mwanamke huyu.
Nikiwa namfuata kwa nyuma, nilikuwa nawaza tu kuhusu uamuzi nilioamua kuuchukua wa kuja kukaa na mwanamke huyu badala ya kubaki Mbagala ili kuendeleza msaada niliokuwa nampatia Mariam. Si kwamba sikutaka tena kumsaidia, lakini nilikuwa tu nimewaza labda kwa wakati huu ningetakiwa kukaza fikira zangu kwenye ishu ya madam Bertha zaidi kwa kuwa nilikuwa nalisogelea lengo langu la kumwangusha kwa ukaribu hata zaidi.
Mariam alihitaji msaada wenye utaalamu mwingi zaidi ya ule niliokuwa nampatia hata kama alikuwa ameonyesha nafuu mwanzoni, kwa hiyo najua ilipaswa tu kufika wakati ambao ningetakiwa kukaa pembeni. Labda sasa ndiyo ulikuwa huo wakati.
Hata hivyo nilihitaji zaidi kuwa jinsi ambavyo nilikuwa tokea nimefika huko Mbagala, yaani nisijiachie mno kulemewa na hisia za kujali sana ambazo sikutaka ziongoze maamuzi yangu badala ya kukazia fikira lengo muhimu zaidi la likizo yangu. Kupumzika. Isingekuwa salama mno kuendelea kujiingiza kwenye mambo ya watu wengine baada ya kuhakikisha namweka Bertha mahala anapostahili, kwa kuwa hiyo ndiyo aina ya maisha niliyokuwa nataka iwe ya kwangu.
Sababu nilizijua mwenyewe, na kukumbukia jambo hili sasa kukawa kumenirudishia akili ile ile niliyokuwa nayo mwanzoni ya kuacha kuwa "soft" mno. Ningetakiwa kujitahidi sana, na kufikia sasa, sikujua kama ingewezekana, maana ile hali ya kujali sana ilikuwa imeshaanza kuiteka mno nafsi yangu. Huo u-soft ungetoweka kweli? Lingekuwa jambo la muhimu sana kujiondoa tu kwenye yale mazingira ili niweze kufanikiwa, ndiyo sababu nikaona kuja kukaa na adui yangu kwa wakati huu kungesaidia kufanikisha hayo.
★★
Bwana, tukaanza mizunguko na huyu mwanamke. Aisee! Bertha alinipeleka sehemu za ukweli na kunikutanisha na watu mpaka viongozi wa serikali niliokuwaga nawaona mitandaoni tu na runingani, wakiwa ndani ya huu mtandao wao wa madawa ya kulevya pia na kufurahia maisha ghali sana kwa kufanya mambo mengi ya kifisadi.
Oh, nilijua hayo yote kwa kuwa na mimi nilihitaji kujionyesha kuwa komredi wa masuala haya, na Bertha alikuwa ananioshea kwao kwa kuonyesha kwamba utashi wangu ungekuja kuibua faida kubwa kwenye biashara zao pia. Sikutarajia kwamba bado alikuwa na baki la madawa yale niliyokuwa nimetengeneza, lakini ndiyo alikuwa anaitumia kuwaonyeshea mfano na kuniachia uwanja ili niwaelezee namna ambavyo nilibuni kitu cha namna hiyo na jinsi ambavyo kingetawala soko kuanzia nchini
mpaka hata nje.
Hawa watu alionikutanisha nao hawakuwa wale ambao niliwakuta kule African Princess casino, bali hawa walikuwa wale wenye pochi nene ambao ndiyo walinunua na hata kuuza madawa pia; wakiwa ndiyo watu waliofikiwa na mambo haya kwa usalama kupitia daraja la ulinzi, yaani Festo. Sijui inaeleweka?
Lengo la madam Bertha lilikuwa kuongeza kama "jeshi" la watu ambao wangesaidia kwenye maandalizi yote ya vifaa, mahala, mpaka utengenezaji wa hii kitu kwa kiwango kikubwa, lakini kwa njia ambayo ingekuwa ya siri zaidi ili isitambulike kwa vyombo vya usalama kama maaskari.
Kama tu namna ambavyo yeye na wale wengine wa kwenye kundi lake walivyokuwa na sehemu ya siri ya kukutana kule casino, alihitaji msukumo wa haraka (boost) ili awe na sehemu salama ya kufanyia uumbaji wake wa hili suala, kama vile tuseme duka kubwa la nguo au kiwanda kidogo ambacho kingeonekana kutengeneza mikate, lakini kiwe na sehemu ya siri ya kuendeshea huo mfumo kimya kimya, ndani kwa ndani.
Hawa "wanunuzi" na "wawekezaji" walionekana kufurahishwa sana na sampo waliyoonjeshwa na njia yangu ya kuwashawishi, na nilifanya ionekane kama vile nililielewa hili game kwa ufasaha wa hali ya juu, hivyo matokeo yakawa mazuri na asilimia kubwa ya hao wote wakaahidi kuweka ufadhili wao kwa madam Bertha.
Alifurahia sana huyu mwanamke, kila mara ambayo tungeingia kwenye gari lake ili kufanya mzunguko mwingine angeniambia jinsi ambavyo aliiona hii ishu ikija kuiva mapema tu shauri ya kubarikiwa kwangu kuwa na kichwa kizuri, bila kujua mwenzake hapa nilikuwa natunza notisi zingine tofauti ili kuja kuyasomesha haya mambo yote somo kubwa.
Tulizunguka kwa watu hao mpaka kufikia saa kumi na mbili jioni, na ndani ya wakati huo tulikuwa tumepita sehemu nzuri tukala pamoja, Bertha akanipitisha kwenye maduka makubwa ya nguo na mitindo ambako alikuwa na mashosti wa kishua pia na kunionyeshea kwao, akanunua nguo na viatu pia; yaani mood yake ikawa nzuri tofauti na ilivyokuwa nilipomkuta pale hotelini.
Alikuwa akipata mialiko kutoka kwa hao marafiki zake ya kwenda kwenye party zao pamoja nami, maana wengi walimsifia kuwa alipata mwanaume mwenye mvuto sana, naye akasema haikuwa na shida ila kama wangeniiba, angewaonyesha nini maana ya maumivu ya mwiba. Yale masihara ya wanawake kwa nje nje tu ila kumbe kwa ndani wanamaanisha.
Kwa hiyo hiyo saa kumi na mbili tulipokuwa tumeanza kurejea hotelini kwake, alikuwa akiongea mambo mengi sana juu ya mipango yake kutokea hapo baada ya mikutano yetu na wale watu wa majuu, lakini mimi nilivutwa umakini na mawazo kuelekea simu yangu. Kuna wakati Bi Zawadi alikuwa amenipigia lakini sikuweza kupokea nikiwa na Bertha, na hata Tesha hivyo hivyo pia.
Sasa ndiyo mama huyo akawa amenitumia ujumbe kunijulia hali, na kusema kwamba kwa wakati huu Mariam alikuwa ametolewa kwenye ile hospitali na kupelekwa na dada yake kwenye nyingine, na kama nikipata nafasi niweze kwenda pale kwao ili tuongee mawili matatu. Sikuona kuwa vizuri kumkaushia tu mama wa watu, kwa hiyo nikamtumia ujumbe mfupi kumwambia sawa, tungeonana, na pia kuomba radhi kuzikosa simu zake shauri ya kuwa bize.
Baada ya Bertha kuona niko makini sana, akauliza ikiwa nilikuwa nimeanza kuwaza tena mambo ya familia, nami nikamwambia hapana, kichwa tu kiliuma shauri ya kutolala kwa masaa mengi. Ndiyo tukapita kwenye duka moja la dawa na mwanamke huyu akanifatia yeye mwenyewe, halafu akarudi na kuendelea kuendesha. Alikuwa anafanya vitu kama hajali sana, ile 'haya shika hizo hapo, kunywa,' huku akizirusha dawa kwangu, nami nikawa namtazama tu kwa kumsoma vizuri.
Nilielewa kwamba Bertha hakuwa mtu wa kuonyesha ana udhaifu, lakini sasa nikaanza kutambua kuwa alikuwa na udhaifu mpya; mimi. Hakutaka nilione hilo ili nisiwe shida kwake, lakini tayari nikawa nimeliona. Labda ndiyo nilikuwa kwenye hatua za mwanzo za kuwa kama udhaifu wake bila yeye mwenyewe kutambua, ama tayari alikuwa ameshatambua lakini hakutaka iwe wazi, yaani iwe wazi kwake yeye mwenyewe.
Aliogopa yale yale ambayo alipitia kwa Chalii Gonga, na alikuwa sahihi kuogopa, kwa sababu mimi ndiyo ningekuja kumvunja vibaya mno mpaka angeshangaa. Alikuwa ameanza kunitendea kwa njia fulani ya kudekeza mno toka niliposhiriki naye tendo na yeye kunielezea kisa chake na mume wake, na naona hata ukali aliokuwa ananionyesha alipoona nakosea ulitokana na kuumia rohoni kabisa na siyo tu kwa kuwaza kwamba angepata hasara.
Kwa hiyo mimi ningetakiwa kuendelea kujiweka karibu naye zaidi na kumwonyesha kwamba namjali ili ifike mahala fulani aniamini kwa asilimia zote kabisa, na ndiyo ingekuwa njia nzuri ya kumlegeza na kumwangusha yeye na watu wake bila kunihisi nikija kinamna hiyo. Hatua ya kwanza ingekuwa ni kumridhisha kwa kuja kukaa pamoja naye. Hii ingekuwa noma!
★★
Basi, tukawa tumeingia maegesho ya hotelini ikiwa ni saa moja ya saa mbili usiku, na kweli kwa sasa maumivu ya kichwa yalikuwa yamefifia baada ya kutumia hedex muda mfupi kabla ya kufika. Alikuwa akiendesha gari lake la Harrier, na baada ya kushuka akanibebesha mifuko yake ya shopping na kutangulia mbele yangu kama vile boss anayefatwa na kijakazi. Alipenda huo wadhifa!
Mimi kimya kimya nikamfata tu, nikiwa nahisi uchovu machoni maana bado usingizi ulikuwa unaniita, nasi tukaingia chumbani kwake baada ya kukifikia. Joto nilihisi likiwa kali sana mwilini, na yeye alikuwa akisema anahisi joto sana lakini sijui ni kwa nini alikuwa ameamua kuvaa nguo nzito na kuzunguka nalo nusu siku nzima. Eti wa kishua!
Kwa hiyo nilipoweka mizigo pembeni, moja kwa moja nikaanza kuvua nguo zangu ili niweze kwenda kujimwagia maji kwanza, na ile tu ndiyo nataka kuvua suruali, Bertha naye akawa anazitoa nguo zake mwilini na viatu bila kuwa amenigeukia, hivyo nikakisia kuwa huenda alitaka kwenda kuoga pia.
"Unaingia kujimwagia?" nikamuuliza hivyo.
Akanigeukia baada ya kuwa amebaki na sidiria nyekundu na nguo ya ndani nyekundu pia, naye akatikisa kichwa kukubali huku akivua hereni zake.
Nikaahirisha kwanza kuitoa suruali, nami nikasema, "Kwa hiyo nisubirie umalize kwanza halafu ndiyo nifate."
Akaweka hereni zake pembeni na kuanza kuja mpaka niliposimama, naye akaniuliza, "Hilo lilikuwa swall, au maelezo?"
"Nilikuwa nakwambia," nikamsemesha kwa sauti ya chini.
"Kwa hiyo unataka niingie bafuni peke yangu, halafu we' ufanye nini?"
"Nasubiri umalize."
"Halafu?"
"Na me nikajimwagie."
Akaniangalia kwa macho yenye umakini, ili nione kwamba alikuwa anatoa maana fulani.
Nikiwa nimeshamwelewa, nikasema, "Madam... siyo kwamba labda... nimechoka tu yaani..."
"Mbona unakuwa unapenda sana kujitoa akili?"
"Siyo hivyo. Ila... kwa ishu za jana, kutolala, mizunguko ya leo, yaani... joto liko high mno. Najua unataka kidogo angalau, ila..."
"Siyo kidogo. Nataka joto high. Sample nzima ya coke imeenda, na wewe haujatengeneza nyingine. Sina cha kunipaisha, kwa hiyo acha kudeka, uje huku bafuni uni(.....)," akasema hivyo.
"Madam..."
"Au haujui cha bafuni huwa kitamu?" akasema hivyo na kuanza kuifungua suruali yangu.
Aisee! Hawa wanawake wangeniua. Sababu kuu ya uchovu niliyokuwa nikihisi ilitokana na kukosa usingizi wa kutosha lakini pia uliongezwa zaidi na mechi ya asubuhi niliyocheza na Rukia. Bertha hakujua kuhusu hilo, kwa hiyo kwa kiasi fulani ilikuwa ni makosa yangu, ukitegemea sasa mwanamke huyu alijiona kuwa kama mmiliki wangu baada ya mimi kumwambia leo kwamba ningefanya atakayo kwa asilimia zote. Alichokisema kingetekelezwa tu, nitake nisitake.
Kwa hiyo akanitolea suruali yangu, na ingawa nilikuwa naona uzito katika kufanya jambo hili, mimi pia nikaanza kumtolea nguo zake za ndani. Mahaba yakaanza, taratibu, kwa kuwa Bertha alionekana kutaka zaidi raha kwa njia ya starehe wakati huu tofauti na jinsi ambavyo alipenda fujo zaidi. (........).
(.........).
(.........).
Humo bafuni sasa ndiyo tukaanza kucheza. Alikuwa ameshika ukuta na kunibinulia kalio lake jeupe, nami nikawa namtandika pigo kali lakini kwa ustaarabu, huku maji yakitumwagikia. Bafu lilikuwa safi sana. Mwanamke akaonyesha kutaka raha ya ulimi hekaluni mwake, nami nikampa.
Nikambeba kwa kuinyanyua miguu yake na kuukandamiza mgongo wake ukutani na kuanza kumnyonya haswa kwa kuweka kichwa changu katikati ya mapaja yake, naye akawa anakatika tu na kuzungusha kiuno na miguno ikitoa mwangwi bafuni hapo. Alionekana kunogewa, lakini nikamshusha na kumwambia tuishie hapo maana nilikuwa....
Bertha asikilize sasa? Akanirukia, nami nikamdaka mapaja nusu tuanguke, kisha akauingiza msuli wangu ndani yake tena huku nikiwa nimempakata hivyo hivyo. Akaanza kujirusha-rusha na kujisugua huku mikono yake ikiishikilia shingo yangu, akiguna na akiniangalia kwa macho yenye kuonyesha yupo ile sehemu ya "koleza," na aisee nilikuwa nimechoka.
Ikabidi nitoke pamoja naye, nikiwa nimempakata hivyo hivyo, na tukiiacha mashine ya kutoa maji inayamwaga tu bafuni humo. Tukiwa bado tumelowana nikampeleka mpaka usawa wa kitanda na kumshusha, naye akaanza kunilamba shingoni na kuichua mashine yangu kwa kiganja chake.
"Bertha... Be... madam.... tuishie hapa..."
Nikawa najaribu kumzuia, lakini akaendelea tu na fujo zake.
Nikamshika mabega na kumfanya anitazame usoni, na kwa upole nikamwambia, "Bertha please..."
Akanitazama kwa macho yenye umakini, naye akasema, "Unasema umechoka? Mbona mshedede wako upo hewani?"
"Ahh... we' wa moto mno ndo' maana, ila utaishiwa upepo sasa hivi tu nikitulia. Uchovu nilionao ni fatigue... mahitaji ya kulala. Chochote kingine nitakachofanya kitaniboa tu kwa sasa hivi..." nikamwambia hivyo.
"Kwa hiyo kumbe nakuboa?" akauliza hivyo.
Nikashusha tu pumzi na kutazama chini kiuchovu, maana najua alikuwa ananielewa ila basi tu alikuwa anaweka ujeuri wake.
Akatulia kidogo akiniangalia kwa ufikirio, kisha akasema, "Kwa hiyo unataka kulala?"
"Yeah," nikamjibu hivyo kwa sauti ya chini.
"Hauli kwanza?"
"Sa'hivi saa moja. Acha tu nilale kidogo, nitakula baadaye," nikamwambia.
"Mmm... haya. Panda kitandani ulale," akaniambia.
"Naomba... taulo ni...."
"Aa, we' lala tu hivyo hivyo. Panda," akasema hivyo na kuelekea kwenye kabati.
Pamoja na kuonekana kwamba aliudhika kwa sababu ya kukatishwa utamu wake, sikuwa na hali yoyote ndani yangu kunifanya nijali. Nilitaka kulala. Kituo kikuu. Nikajitupia tu kitandani hapo baada ya kuvaa boksa hata ingawa sikuwa nimekauka vya kutosha, na madam Bertha akawa amesaidia kufanya ndani hapo pawe na hali nzuri zaidi baada ya kuwasha AC.
Si muda mrefu sana baada ya kuwa nimejilaza na usingizi ukawa umenivuta, nami nikauruhusu unibebe hatimaye.
★★★
Usingizi niliokuwa nao ulinivuta sana, yaani nilikuwa naamka na kusinzia tena na tena mpaka nilipokuja kufumbua macho na kutulia kabisa baadaye. Kulikuwa na hali ya ugiza ndani hapo, na nikiwa kitandani bado, nikahisi kama vile mwili wangu ulikuwa umeshikwa usawa wa ubavu kutokea nyuma, hivyo nikajigeuza taratibu na kukuta ni Bertha mwenyewe; akiwa amesinzia pia karibu na mwili wangu.
Sikuwa nimetarajia kabisa jambo hili, maana alionyesha kuwa na imani kubwa sana kunielekea mpaka kufikia hatua ya kulala pamoja nami namna hii, nami nikajisawazisha vyema kwa kupitisha mkono wangu nyuma ya mwili wake na kumfanya alaze kichwa kifuani kwangu.
Alikuwa ndani ya sidiria na nguo ya ndani nyeupe pekee, sehemu kubwa ya mwili wake wote ukiwa tamasha la wazi kwa mimi kuona. Kumwangalia akiwa amesinzia leo tena kulimfanya aonekane kuwa mtu asiye na dosari kabisa, yaani alikuwa na sura nzuri na isiyo ya hatia tofauti kabisa na jinsi ambavyo utu wake ulikuwa.
Nikaona nitulie tu na kutazama juu. Bila shaka muda ulikuwa umeenda sana mpaka Bertha kuja kulala tu pamoja nami, na pia ilionyesha kwamba hakuwa na mizunguko mingine kwa siku hiyo tofauti na ile tuliyoifanya kuanzia saa sita siku hiyo. Pamoja na ukaidi wote lakini na yeye alihitaji kupumzika. Sasa hivi ndiyo kukawa na yale mawazo huru zaidi kichwani kwangu baada ya kutoka usingizini.
Kwa sekunde kadhaa macho yangu yalipokuwa yametazama juu, akili yangu ilikuwa inawaza kuhusu hili suala la kutoka na wanawake walionitaka kwa kipindi hiki, yaani kila mmoja baada ya mwingine. Kuna wanaume huwa wanalilia kupata vitu kama hivi lakini hawavipati pasipo kutoa gharama, mimi ambaye nilikuwa napewa bure kila kukicha na wanawake wa kila aina eti ndiyo nikawa naona kero. Utamu unakuwepo ndiyo ila kuna mambo mengine ambayo yalikuwa muhimu kufikiria. Kama nini? Magonjwa.
Nilikuwa najiachia kupita kiasi mpaka nikawa sitazami alama za usalama. Ingekuwa jambo la kumshangaza yeyote mimi kuwa daktari halafu nikawa naishi kwa mtindo wa kiholela. Ningepaswa kurudisha akili yangu mahali sahihi zaidi, na ndiyo ningetakiwa kupata kitu ambacho kingenisaidia kufanya hivyo. Ingekuwa ngumu kwa sababu hata kukitafuta nilikuwa sikitafuti, badala yake ni matatizo tu ndiyo yalionekana kunitafuta mimi.
Haya mahaba ya hapa na pale na kule na huko hayakuwa mazuri, na kwa kuwa sasa nilikuwa nimeazimia kukazia akili yangu kwenye suala la huyu mwanamke, Bertha, ingetakiwa kuwa mimi na yeye tu kuanzia sasa. Lakini ningetakiwa kuwa makini sana ili nifanikiwe kutimiza lengo langu la kuwa naye kwa wakati huu bila kujikuta nimeshikizwa sehemu ambayo sikupaswa kushikika.
Namaanisha kuwa, Bertha alionyesha wazi kwamba alihitaji ukaribu wangu kwake uwe zaidi ya biashara tu, hata kama hakuwa amesema, niliona kabisa kwamba alikuwa ameanza kunipenda. Kwa hiyo hapa ningepaswa kumaliza huu mchezo bila kuhusisha hisia, niwe mkatili kweli kweli ili siku ya kuja kumbwaga chini kusiwe na kitu fulani kama kumwonea huruma, maana hiyo ingekuwa ni udhaifu kwangu. Alikuwa ameshanionyesha namna gani alivyokuwa mkatili, na ndiyo maana sikutaka kulisahau hilo ili hatimaye nije kuukomesha.
Dakika kadhaa kupita nikiwa nimekaa kutafakari, nikahisi kubanwa na haja ndogo, hivyo nikajitoa mwrilini kwa mwanamke huyo na kushuka kutoka kitandani. Nafikiri nikawa nimemfanya aamke, nami nikamtazama na kuona ananiangalia kwa macho mazito ya usingizi.
"Unaenda wapi?" akauliza hivyo.
"Kukojoa," nikamjibu hivyo kwa ufupi.
Nikaelekea mpaka bafuni, nikatoa haja na kurudi chumbani tena, nami nikaichukua simu yangu na kutazama muda kukuta ni saa kumi na moja alfajiri. Kiukweli nilikuwa nimelala sana. Kwenye simu yangu kulikuwa na taarifa kutoka kwa watu walionitafuta kama askari Ramadhan, Tesha, Ankia, na yule Rukia. Rukia sanasana ndiye aliyekuwa msisitizaji wa kunipata maana alipiga na kutuma jumbe kadhaa za kunitaka tukutane, lakini ndiyo ikawa imepita hiyo. Sikuona haja ya kuisumbua akili yangu na suala lake, nami nikasogea mpaka usawa wa sofa na kusimama hapo.
"Wee... si uje ulale?" sauti ya Bertha kutokea kitandani ikasema hivyo.
Nikamwangalia na kuona kwamba alikuwa ameunyanyua mwili wake juu kiasi ili anitazame, nami nikamwambia, "Hamna... usingizi ushakata. We' lala tu, nitakaa hapa. Panakucha muda siyo mrefu."
"Njoo ukae macho huku bwana. Toka huko," akasema hivyo.
Nikatabasamu tu, kisha nikamfata mpaka hapo kitandani na kujilaza vile vile kwa kumruhusu akilalie kifua changu.
"Sa' unataka kukaa kwenye baridi wakati joto liko hapa, we' vipi?" akasema hivyo huku akijibana zaidi kwangu.
"Sikutaka kukusumbua," nikamwambia hivyo huku nikimtekenya taratibu mkononi na mgongoni.
"Najua tu ni njaa inakuwasha, sijui nani alimwambia ulale bila kula," akaongea kwa sauti ya chini.
"Nitakula baadaye," nikamwambia.
"Ni Jumapili. Tuko free sana. Ufate vitu vyako baadaye halafu urudi huku tufanye mambo mengine..."
"Yes madam."
"Mhm... napenda ukisema hivyo," akaongea kwa sauti yenye hisia.
"Nini? Yes madam?"
"Yeah..."
"Kwa nini?"
"Sijui hata. Wengi wakiniita hivyo... nahisi... pride. Ila wewe ukiitumia madam... sijui ni kwa nini tu lakini, najisikia... vizuri..." akasema hivyo kwa sauti iliyofifia.
Akawa ameanza kufunguka yeye mwenyewe, nami nikatabasamu tu na kuendelea kumpa bembelezo kwa kiganja changu taratibu.
Akasinzia tena baada ya dakika chache, na sasa ikawa imeshaingia saa moja asubuhi. Alikuwa sahihi kiasi kuhusiana na mimi kutokula jana maana kwa sasa hivi nilihisi njaa iliyoelekea kuwa kali kwa asubuhi hii, na mpaka kufikia mida ya saa mbili hivi bado alikuwa amenilalia tu, hivyo nayo njaa ilikuwa ikiongezewa uzito kutokana na uzito wa mwili wake juu yangu.
★★
Ndani ya dakika chache kwenye muda huu simu ikaanza kuita, mpigaji akiwa Rukia, nami nikaitolea sauti maana nisingeweza kumjibu na Bertha akiwa hapo. Lakini nilitaka kuongea na mwanamke huyo pia, nimweleze kwamba jana nilitingwa shauri ya dharura na nitunge hadithi yoyote kuhusu mimi kusafiri ili niweze kumkwepa mazima.
Ni baada tu ya simu kukata ndiyo mlango wa chumba hiki ukaanza kugongwa. Inaonekana Bertha hakuwa mbali sana kiusingizi kwa hiyo kugongwa huko kwa mlango kukafanya aamke. Akaniangalia usoni kiuchovu, nami nikamuuliza ikiwa alikuwa na mgeni kwa asubuhi hii. Akasema hapana, inawezekana tu ilikuwa ni room service ama labda Dotto ndiye aliyekuwa amefika hapo, kwa hiyo akaniambia niende kufungua.
Nikamwacha hapo kitandani akijinyoosha, nami nikavaa suruali yangu upesi na kuichukua kadi ya mlango, kisha ndiyo nikaenda kuufungua. Aliyekuwa anagonga alirudia kufanya hivyo kama mara nne kabisa shauri ya mie kuchelewa kiasi, na baada ya kufungua mlango, dah! Yaani sikuwa nimetarajia kabisa kwamba ingekuwa ni Chalii Gonga! Mume halali wa madam, ndiye aliyekuwa hapo.
Kwa sekunde chache, tukabaki tunaangaliana machoni kwa njia makini sana, kila mmoja wetu akiwa hajatarajia kuiona sura ya mwenzake hapo bila shaka, na kwa kutoamini alichokuwa amekiona, Chalii Gonga akacheka kwa mguno na kutikisa kichwa kiasi. Kunikuta kwenye chumba cha hoteli cha mke wake asubuhi, nikiwa kifua wazi, na mimi mwenyewe kumfungulia mlango, ilitosha kabisa kumwelewesha kwa nini wiki kadhaa nyuma alikorofishana na mke wake juu yangu. Yaani mimi ndiyo nilikuwa nakula mali yake.
Akalamba midomo yake na kushikanisha viganja vyake kwa mbele, akinitazama kama vile anasubiria niseme kitu au nijieleze labda, lakini sikumwonyesha hisia yoyote usoni na kuendelea kumtazama pia kwa ujasiri.
"Hey, vipi... ni nani?"
Sauti yake Bertha ikasikika kutokea nyuma yangu akiuliza hivyo, nami nikaachia uwazi zaidi mlangoni ili kumruhusu Chalii aingie. Alikuwa ameweka uso makini sana, akiwa amevalia kofia nyeusi kichwani, T-shirt pana jeupe, suruali ya jeans ya samawati, na viatu vyeupe miguuni. Akanipita kwa kunipamia kiasi begani, nami nikamtazama tu na kurudishia mlango.
Bertha alikuwa amejilaza kitandani bado, na baada ya kumwona Chalii, akaweka uso makini na kujikalisha, huku akiuziba kiasi mwili wake kwa shuka. Nikaelekea sehemu yenye sofa na kuvaa T-shirt langu, kisha nikaendelea kusimama kwa hapo nikiwaangalia.
"Chaz? Ume... umepajuaje hapa?" Bertha akamuuliza hivyo jamaa.
"We' ni mke wangu B... unajua kukutafuta ni lazima. Na nimehangaika kweli mpaka kukupata yaani," Chalii Gonga akasema hivyo.
"Unataka nini? Ulishindwa kupiga simu?" Bertha akamuuliza.
"Nimekuja kuongea na wewe, mke wangu," Chalii Gonga akamwambia hivyo.
Mm?
Nikamwangalia mwanaume huyo kwa macho makini. Aliposema hivyo, nilihisi kama vile alikuwa na nia mbili.
Bertha akaendelea kumtazama usoni kwa subira, kisha akasema, "Nini sasa? Ongea!"
Chalii akanitazama kwa ufupi, kisha akamwambia, "Wewe kama wewe. Hatakiwi kusikia mtu mwingine."
"Kulikuwa na ulazima gani wa kuja? Ulishindwa kupiga simu?" Bertha akamuuliza hivyo kwa mkazo.
"Ni muhimu sana, ndiyo maana. Dogo... tupishe tuongee," Chalii akasema hivyo kwa kuelekeza maneno hayo kwangu.
Lakini nikaendelea kusimama hapo hapo kama vile sijamsikia. Akanitazama usoni kwa mkazo.
Bertha akanitazama pia, kisha akamwambia, "Hauwezi ukaja tu kwangu na kuanza kutoa amri kama vile kwako. Ongea shida yako, huwezi... nenda. Sioni utofauti wowote ukiongea kwenye simu na ana kwa ana, na... iwe mwanzo na mwisho, kuja hapa... bila kunipa taarifa. Ukinikuta uchi je?"
Maneno hayo yakanifanya nitabasamu kiasi na kuangalia pembeni, kisha nikamtazama jamaa.
Chalii Gonga akawa anamwangalia mwanamke huyo kwa njia fulani... sijui tu yaani, lakini ilikuwa kama vile anamchora hivi.
Bertha akamwambia, "Umenielewa? Mwanzo... na mwisho. Nenda. Utaniambia madudu washa yako kwenye simu. Go!"
Chalii Gonga hakuonekana kuudhika baada ya Bertha kumsemesha namna hiyo, badala yake akatabasamu tu kidogo na kuangalia chini, kisha akageuka na kuondoka.
Njia yake hiyo ya kuitikia kufukuzwa sehemu hii ilionyesha hila fulani hivi, nami nikapata hisia kwamba kuna jambo lililokuwa likiendelea kutoka kwa mwanaume huyo kumwelekea madam. Yaani, ni kama kuna kitu fulani ambacho Chalii Gonga alikuwa anataka kufanya, na kuja kwake leo hapa haikuwa tu ili aongee na madam, ila aone kama angeweza kufanya hicho kitu.
"We' naye, si ungefunga tu huo mlango ulipoliona lisura lake hapo nje? Sijui nani akakutuma umruhusu aingie humu..." Bertha akasema hivyo na kusonya kidogo.
Nikamfata mpaka hapo kitandani na kukaa karibu yake, naye akaniangalia kwa umakini. "Hii ndiyo mara ya kwanza Chalii amekuja hapa?" nikamuuliza.
"Eeh. Atakuwa amenisaka mpaka akafanikiwa, maana sasa hivi sina habari naye. Kwani vipi?"
"Naona kama vile alikuwa anakuchora."
"Ahah... Chaz? Asa' unadhani hilo ni jipya kwangu? Mwache achore mpaka aumwe, ila ndo' nilishagakwambia... hawezi kufanya chochote. We' unaogopa kwa sababu amekukuta humu?"
"Hapana, siyo hivyo. Bertha... nina mashaka na ujio wa Chalii hapa. Amekuja kivingine yaani..."
"Nimekwambia usiwaze. Charles anajua hawezi kunifa...."
"Ndiyo hicho madam. Anajua hawezi kufanya chochote kwako moja kwa moja, lakini usipuuzie ukweli kwamba anaweza akatafuta njia isiyo ya moja kwa moja. Anachokifanya ni... anakikuza tu kiburi chako madam, uendelee kumchukulia simple, lakini yeye siyo mpumbavu. Hakutarajia kunikuta hapa, ndiyo maana kaondoka bila kutimiza motive yake. Kuwa care... anaweza akakuzidi akili," nikamwambia hivyo kwa sauti hakika.
Akawa ananiangalia kwa yale macho makini sana, naye akasema, "For once... umeongea point. Tuseme kwa mfano tayari ameshafanya hizo measure. Ungenishauri nifanyeje?"
"Utafute... ujue kapajuaje hapa. Uwe mwangalifu na vitu ambavyo vitahusiana moja kwa moja na hii sehemu... labda hata usile chakula kutoka kwenye hii hii hoteli, precaution tu. Amefanya umakusudi wa kuja hapa, na nafikiri alitaka tu uone kwamba hata ukienda wapi... atakupata. Anafikiri unanitumia mimi kama vile kumkomoa tu, kwa hiyo na yeye atataka kukuonyesha kwamba yumo kwenye game. Labda itakuwa vizuri ukiacha kumchukulia easy madam... huwezi kujua akili yake inawaza nini," nikamwambia hivyo kwa utulivu.
Akatazama pembeni kwa mkazo. Eee, yaani yale macho ya hila!
Nilikuwa nimempampu vizuri kweli, nami nikamwambia, "Ngoja nikaoge. Naenda Mbagala kufata vitu vyangu, afu' tutakutana baadaye. Poa?"
Akatikisa kichwa mara moja tu kukubali, nami nikambusu shavuni na kisha kuelekea bafuni. Sikujua Bertha angeshughulikia suala hilo kwa njia gani, lakini kumpa huo ushauri haikumaanisha kwamba nilimjali sana, badala yake nilikuwa naangalia usalama wangu pia nikiwa upande wake.
Mimi ni mwanaume, niliona wazi kwamba mwanaume mwenzangu alikuwa amechoshwa kutendewa kama kilaza tu na mke wake; yaani afike kwenye chumba chake, amkute na mwanaume mwingine, aambiwe ondoka, halafu aondoke tu kwa amani? Hapana. Chalii Gonga alikuwa anapanga kitu fulani.
Ushauri niliompa madam ulitakiwa kumfanya aamke na kushughulika na mume wake vizuri, ili niweze kufanikiwa kutimiza malengo yangu bila bughudhi za pembeni kutoka kwa huyo jamaa. Lilikuwa ni suala la kumwangusha Bertha, lakini sikusahau kwamba na huyo Chalii alitakiwa kwenda chini pamoja naye.
Kwa hiyo baada ya mimi kuoga, Bertha akaingia kuoga pia na kisha kuanza kujiandaa kutoka. Mapema ile alfajiri alisema kwa kuwa leo ilikuwa Jumapili basi ingetakiwa kuwa siku ya kutulia tu, lakini sasa hilo likawa limebadilika upesi. Alionekana kuwa makini sana kwa wakati huu, hata nilipokuwa nimeomba kutangulia akawa amenizuia na kusema nitulie mpaka amalize kuvaa, ndiyo tungeondoka pamoja. Akawa anaongea na watu wake kwenye simu kwa ajili ya mikutano fulani ya kuzungusha biashara, yaani madawa, kisha ndiyo tukaondoka hatimaye.
Mpaka kufikia kwenye gari lake, madam Bertha alikuwa akiongea tu na simu yake, na mimi kwa wakati huo nilikuwa nimeiweka simu yangu katika mfumo wa kurekodi sauti bila yeye kutambua, kwa hiyo kuna vitu alivisema ambavyo ningetunza tu kwa ajili ya matumizi ya baadaye. Alikuwa ameshaniamini mno, kwa hiyo hakuonekana kuwa na noma kuongelea mambo mengi mbele yangu kwa kujiachia.
Kwenye gari lake, tulimkuta Dotto, tayari akiwa kwenye usukani, na kwa sababu fulani niliona hilo kuwa na uajabu kiasi. Jamaa alikuwa wa kutokea na kupotea, sikujua sana jinsi gani Bertha alimpangilia lakini nilihisi na yeye hakuwa wa kuaminika kwa asilimia zote. Si unajua me mwenyewe nilikuwa mchongezi? Snitch anamjua snitch. Zilikuwa hisia tu lakini, zilizofanya niwaze hiki na kile hasa kutokana na ishu ya Chalii Gonga kwa asubuhi hii. Ila na huyu Dotto nilipaswa kumweka katika akiba ya mambo ya kujihadhari nayo.
★★
Kwa hiyo Dotto akatuendesha kutokea hapo baada ya kuwa tumeongea vizuri tu kwa ufupi, akiwa amegusia kuyakosa sana madawa yale ya cocaine niliyokuwa nimetengeneza, nami nikamwambia asiwaze kwa sababu muda si mrefu sana ningetengeneza mengine tena. Nilikuwa nimekaa siti ya mbele pembeni yake, nami nikaitumia nafasi hiyo kuwatumia baadhi ya watu muhimu jumbe fupi, hususani askari Ramadhan na Rukia, ambao niliwaahidi kuwatafuta baadaye kwa kusema nipo kwenye ibada. Usinihukumu!
Tukawa tunachanganya story za hapa na pale pamoja na huyu Dotto mpaka madam Bertha alipositisha kuzungumza na simu, kisha ndiyo akaniambia kwamba wangeniacha sehemu fulani ili nielekee huko Mbagala, halafu ndiyo tungekutana baadaye. Sikuwa na neno.
Uzuri ni kwamba, ijapokuwa sikujua madam alikuwa anaelekea wapi, sehemu waliyonishushia ikawa ni maeneo yasiyo mbali sana na uwanja wa Benjamin Mkapa, hivyo Mbagala haikuwa mbali sana kufikia. Bertha akaniambia nikianza tu kurudi kule hotelini nimjulishe ili aweze kuona utaratibu mzuri wa kunipa, endapo kama labda angekuwa hajarudi, nami nikaridhia. Wawili hao wakatembea, nami nikatafuta usafiri kisha kuendelea na safari ya kwenda kwa Ankia.
Yaani mambo yalienda kwa mtiririko, kwa sababu wakati nikiwa mwendoni bado, Ankia akawa amenipigia kuniambia ndiyo alikuwa amefika pale kwake kutokea kule alikokuwa ameenda kumsindikiza Adelina. Alikuwa anauliza sehemu gani nilipo maana alitaka tuongee, nami nikamwambia niko njiani kufika hapo kwake.
Nilielewa kwamba alitaka tuongee kuhusu visa vilivyokuwa vimetokea pale kwao na bibie Miryam, bila shaka akiwa ameyasikia yote baada ya kufika, na mimi pia nikashukuru tu kwamba angalau alikuwepo huko ili kuifanya ishu ya kuondoka hapo kwake iwe rahisi. Ndiyo, ingekuwa vizuri zaidi kuondoka hapo nikiwa nimeongea naye ana kwa ana, badala kama angerudi baadaye na kukuta tu mpangaji wake ameshasepa.
★★
Nikawa nimefika Mzinga hatimaye. Moja kwa moja mpaka kwa Ankia nikitembea taratibu tu, na sasa ilikuwa inaingia saa sita mchana bila kuwa nimeweka chochote kile tumboni. Niligundua kwamba wengi wa watu wa eneo hilo walinitazama kwa njia makini zaidi wakati huu, na nilielewa vizuri kwamba hapo tayari kulikuwa na umaarufu fulani hivi uliojijenga kutokana na kilichotokea baina yangu na Joshua usiku uliotangulia.
Lakini nikiwa si mtu wa kushoboka na watu nikapita zangu tu dukani kwa Fatuma pale nje ya nyumba ya Ankia na kumkuta mwanamke huyo akiwa amekaa na wanawake wengine watatu, nami nikawapa salamu fupi tu bila kuwaangalia. Walijibu kwa njia nzuri huku nikiona jinsi ambavyo waliendelea kunifata tu kwa macho yao mpaka nilipoingia getini. Bila shaka hapo ningekuwa mada kuu muda si mrefu, lakini sikujali.
Nikaenda mpaka ndani, na baada ya kuingia tu sebuleni, nikamkuta Ankia akiwa amesimama usawa wa sofa moja huku akitazama upande wangu, na akiniangalia kwa macho yenye utulivu tu kuonyesha kwamba alikuwa ametegemea ujio wangu. Nikafunga mlango na kusogea mpaka karibu yake, naye akawa ananiangalia kwa njia ya subira tu. Alivalia kwa ukawaida wa nyumbani tu.
"Nini?" nikamuuliza hivyo kwa sauti ya chini.
Akatikisa kichwa kidogo kuonyesha hakuna kitu.
"Unasubiri nikupe maelezo, au?"
"Haina haja ya kuelezea lolote. Yote nimeshayasikia," akaniambia hivyo.
"Nakisia ni mama Chande na umbea wake," nikamwambia.
"Kaniambia kila kitu ndiyo. Ila nimeongea na akina Bi Jamila pia na wenyewe wakaniambia. Kimeumana na huyo Joshua..."
Nikaangalia pembeni kwa njia ya kuudhika baada ya kusikia jina hilo.
"Mama Chande kanisimulia ulivyompiga jana huyo...."
"Adelina umerudi naye?" nikamkatisha kwanza.
Akasema, "Hapana. Yeye yuko huko kwao bado. Ameniambia nikusalimie."
"Kaburi?"
"Bado wanajenga. Me nimerudi baada ya kusikia kilichompata Mamu. Sikuwa na amani yaani... nampenda sana sa'hivi kama mdogo wangu," akasema hivyo.
Nikashusha pumzi kiasi na kukaa kwenye sofa, naye Ankia akakaa karibu nami pia.
"JC... yaani kiukweli mambo yanayoendelea kwenye hiyo familia yanasikitisha sana. Na mimi huwa natamani kufanya lolote kuwasaidia maana Miryam aliwahi kunisaidia kipindi fulani kigumu sana, ila ndiyo bado sijawezaga kujua ni namna gani ya kuwa naye karibu zaidi... maana ya kwake hataki mtu mwingine ajihusishe nayo. Leo Bi Jamila kaniambia kila kitu. Siku ile Miryam kakukasirikia ilikuwa shauri ya wewe kumwonya kuhusu Joshua lakini hakukusikiliza. Mama wa watu anasema imemuuma sana, lakini ameniomba nikiongea na wewe nijaribu kuku...."
"Basi, Ankia... inatosha. Naelewa," nikamkatisha kwa kusema hivyo.
"Kweli? Hauna hasira na... Miryam kwa sababu ali..."
"Sijawahi kuwa na hasira kumwelekea huyo mwanamke. Namwelewa vizuri zaidi ya unavyojua," nikamwambia hivyo.
"Kumbe? Unamaanisha unamjua vizuri Miryam?"
Nikatikisa kichwa kukubali.
"Umemjulia wapi?" akauliza.
Nikashusha pumzi na kusema, "Haina umuhimu sana. Ona... yaliyotokea yameshatokea. Natumaini tu mambo yao yatakwenda vizuri sasa hivi. Nafikiri nimemaliza sehemu yangu."
Akaniangalia kwa umakini na kuuliza, "Unamaanisha nini?"
"Naondoka," nikamwambia.
"Nini? Unaondokaje?"
"Yaani naondoka kuondoka. Sitakaa tena hapa."
"Ih! JC? Yamekuwa hayo tena?" akaonekana kushangaa.
"Wala usichukulie vibaya. Kuna ishu tu naenda kufanya kule Makumbusho, kwa hiyo...."
"Ishu gani, JC? Miezi yako ya likizo si bado?"
"Najua, ila..."
"Na ulikuwa umeshalipia mwezi mwingine wa kukaa hapa advance. Mimi hiyo hela nimeshatumia sasa, unataka kusema nikurudishie, au?"
"Hapana, Ankia... usijali. Siyo hivyo wala," nikamtuliza.
"Kwa hiyo... unaondoka... unaondoka lini?"
"Leo."
"Leo?"
"Yeah. Sasa hivi," nikamwambia hivyo.
"Ahah... hiyo ishu ya jana ndo' imekudis kihivyo mpaka umeamua kuondoka tu, eh?" akauliza hivyo kwa njia ya kuudhika.
Niliona wazi kwamba alikuwa amevunjika moyo, nami nikamwambia, "Hata kama isingekuwa imetokea jana, kuondoka ningeondoka tu. Ni kama..."
"Kwa hiyo na Mariam unamwacha tu?" akanikatisha kwa kuuliza hivyo.
Nikabaki nikimwangalia kwa umakini.
"Kama tu ulivyowaacha jana hospitali? Hautaki kumsaidia tena? Akina Bi Jamila mpaka wamehisi umekwazika mno kwa sababu ya Miryam na Mariam. Hivi hata unajua hali yake ikoje sasa hivi?"
Nikapandwa na hisia kusema, "Mimi ni nani Ankia? Me ni stranger tu kwenye hiyo familia. Kama kuwasaidia nimejitahidi, ila.... hhh... ila siwezi kutoa msaada zaidi ya niliotoa. Kama ni mwisho basi ndiyo hiyo jana... watapata tu namna nyingine ya kumsaidia huyo msichana."
Ankia akawa ananitazama kwa ufikirio, kisha akasema, "Naona ushafanya maamuzi yako ila... unayafanya kwa sababu tu ya hasira."
"Siyo hasira Ankia, nimekwambia kuna kazi ya muhimu naenda kufanya," nikasema hivyo kwa mkazo.
"Najua huwa unajivika huu utu wako wa kutojali unapoona inakufaa... ila huu utu siyo wewe JC. Najua unamjali sana Mamu. Sema tu... umeumia. Ndiyo maana unataka kukimbia ili usiwe na hizo hisia, si ndiyo? Hautaki ku...."
"Ankia... inatosha. Acha. Sipendi ku... usiongee hivyo, unanifanya najisikia kama vile nina hatia sana, wakati siyo mimi ambaye..."
"Ehee... hicho hicho ndo' nachomaanisha. JC mimi ni mtu mzima, nimeshakuelewa. Yaani... uko tofauti kabisa na vile ambavyo unataka watu wakuone, halafu wakianza kuuona huo utofauti wako... unaogopa. Ni kwa nini uko hivyo?" Ankia akauliza kwa busara.
Nikabaki kimya tu nikitazama pembeni.
"Watu kama wewe ndiyo huwa wako radhi hadi kuua mtu wakizinguliwa vibaya, eti? Ndiyo maana uliniambia una mkono mbaya sana, hasa kwa watu kama Joshua. Lakini JC, wewe siyo mtu mbaya. Tena... yaani una moyo mzuri sana. Hatufanani kwa mambo tuliyopitia maishani, lakini... naelewa ya kwako hayajawa rahisi sana ndiyo sababu mpaka uko radhi kupambana kwa ajili ya msichana usiyemfahamu... yaani... ni kitu kinachogusa sana. Usifikiri kwamba haina maana, au ni vibaya kuonyesha kwamba unajali. Ila kwa wewe najua ukiacha... itakusumbua sana rohoni... na huyo msichana ataumia pia. Tafadhali JC... usimwache Mamu," akanisemesha kwa upole.
Nikatabasamu kidogo na kusema, "Na we' leo umeamua kucheza karata za ushauri na saha kwangu, eh?"
Akatabasamu kiasi na kusema, "Ndiyo. Sipendi tu kuona unaumia."
"Ankia... una jicho pevu. Ila no... siondoki kisa majungu rohoni. Nina ishu muhimu ya kufanya. Ikiwa nitawahi kumaliza... basi labda nitarudi huku kumalizia likizo yangu. Wala usijali kuhusu me kuumia," nikamwambia hivyo.
"Kweli?"
"Kweli. Hakuna kitu kama mimi kuogopa, we' sijui hata hayo mawazo unayatoa wapi. Achana na tamthilia za wahindi, utapotea," nikajaribu kumtania kidogo.
Akatabasamu huku ameibana midomo yake kiasi, naye akauliza, "Kwa hiyo hii ndiyo bye bye?"
"Siyo forever, nitarudi tu njiwa wangu," nikamwambia hivyo na kumfinya shavu kidogo.
"Nimeshakuzoea sana JC. We' ndiyo umenifanya mpaka nikayaachilia mapito yangu na kuanza kufurahia life tena. Usiondoke please..." akaongea kwa hisia.
"Hata me nimeshazoea kuwa hapa, ndo' maana nikakwambia hii siyo bye bye kimoja. Wala usiogope," nikamwambia hivyo kwa upole.
Akataka kunifata mdomoni ili aweze kunibusu, lakini nikamwekea kizuizi kiasi. Akabaki kunitazama kwa hisia.
"Ankia... tuliyofanya mimi na wewe... nimefurahia sana. Ila kutokea hapa tutapaswa tu kubaki kuwa marafiki... kawaida," nikamwambia hivyo.
"Kwani sisi siyo marafiki? Si tulieleweshana kuhusu mahusiano yetu? Shida ni nini sasa hivi nikitaka kukupa kiss ya kuaga?" akauliza hivyo.
Nikashusha tu pumzi na kubaki kimya.
"Mmm... naona umeshapata mwingine huko Sinza, sijui wapi... kakukamata mpaka umechizi, unataka kukimbia tu," akaongea kwa kejeli.
"Wala hata siyo hivyo..."
"Unakataa nini? Hata harufu yako tu nimeona imechange, ni ya huyo huyo mwanamke. Unafikiri sikuwa nimeisikia?" Ankia akaendelea kunikejeli kimasihara.
"Haitajalisha hata kama nikipata mwingine, wewe thamani yako kwangu ina kiwango chake tayari. We' ni wa muhimu kwangu Ankia. Usisahau hilo," nikamwambia hivyo kwa upole na kuvishika viganja vyake.
Akatabasamu kwa hisia, naye akasema, "Asante."
"Haya. Me naenda kuweka virago vyangu nisepe," nikamwambia.
"Si ungekula?"
"Nimekunywa chai ya nguvu hii asubuhi, hapa mpaka baadaye. Na inabidi niwahi..." nikadanganya ili tu niwahishe jambo hili.
"Na kwa kina Miryam je? Unaenda kuwaaga?" akaniuliza hivyo upesi.
Nikatulia kidogo, kisha nikatikisa kichwa kukubali.
"Sawa. Yupo na yeye, itakuwa vizuri ukiongea naye pia," akaniambia.
"Hakuna presha wala. Ngoja nije," nikamwambia hivyo na kunyanyuka.
Nikaelekea mpaka chumbani, na kwa sekunde chache nikabaki kuegamia mlango nikitafakari mambo fulani. Ankia alikuwa sahihi. Nilichokuwa nakifanya sasa hakikunipa raha hata kidogo, lakini niliona ndiyo chenye utimamu zaidi kwa wakati huu. Bado nilikuwa nang'ang'ania kuuvaa utu ule wa kutojali ingawa ilikuwa ngumu sana kufanya hivyo maana tayari moyo wangu ulikuwa umeshikwa na hisia kali sana za kumjali Mariam, kwa hiyo kiukweli, hapa nilikuwa kama vile nakimbia.
Ndiyo. Yale yale ambayo nilimshauri Tesha asifanye kuhusu kukimbia hisia zake, ndiyo niliyokuwa nayafanya sasa. Wakati mwingine inabidi tu, maana ni kweli kabisa kwamba huwezi kushikilia kila kitu.
Kwa hiyo nikavua nguo zangu na kuvaa zingine safi zaidi, kisha nikaweka kila kilichokuwa changu kwenye begi na kutoka. Wakati huu nikavaa viatu vyeupe miguuni, kisha ndiyo nikaenda pamoja na Ankia mpaka pale kwao na Mariam. Wakina Fatuma pale nje walikuwa wanatutazama sana wasielewe kwa sababu gani nimeweka begi mgongoni, nasi tukajali yetu tu na kwenda mpaka ndani kule.
Tuliwakuta mama wakubwa pamoja na Shadya pale sebuleni, na baada ya kuniona, walifurahi sana. Tena walipoona nimebeba begi, walidhani ndiyo nilikuwa nimerejea kutoka sehemu fulani, na kuanza kuniambia kwamba muda siyo mrefu wanaenda pamoja na Miryam hospitali kumwona Mariam kwa hiyo ikiwezekana nijiunge nao, lakini ndiyo nikawapa taarifa ya kuondoka kwangu iliyowaacha wakihuzunika sana. Yaani sana. Sikutarajia wasikitike mpaka kuanza kuniomba radhi kwa sababu walifikiri naondoka kutokana na kukwazwa nao, lakini nikajitahidi kuwatuliza kama tu nilivyomtuliza Ankia. Walikuwa wamenizoea sana.
Kwa hiyo baada ya kuwaelewesha tu kwamba nilikuwa naondoka kutokana na suala la kikazi, nikawaomba wamwambie Miryam ili naye niweze kumuaga, lakini ndiyo wakawa wamenijulisha kwamba mwanamke huyo alikuwa ametoka. Alikuwa ameenda kuonana na mwenyekiti huko, bila shaka kuzungumza naye kuhusiana na mengi ya matatizo yao, hivyo nikawaomba mama wakubwa waje kumpa heri yangu ya kuaga, na nikawaahidi kuja huku tena hasa kwa ajili ya kumjulia hali binti Mariam. Tesha alikuwa hospitali pamoja na mdogo wake kwa wakati huu, hivyo naye ningemtafuta kwa simu kumuaga.
Ilikuwa ni pindi iliyoutia moyo wangu simanzi kiasi, kuona namna wanawake hawa walivyonitazama kwa huzuni, hivyo nikafanya tu kuondoka hapo upesi sana na kuingia barabarani kuelekea Mzinga kabla hisia hazijanilemea mimi pia na kufanya nibadili maamuzi. Yaani!
Tokea mwanzo sikutaka kabisa likizo yangu iwe yenye mambo ya vuta-nikuvute mazito kama hivi, lakini sijui kwa nini tu ndiyo yalipenda kunitafuta. Labda ilikuwa ni Karma, ile kwamba kuna mambo maishani huwezi kuyaepuka hata ukiyakimbia vipi; yatakufikia tu. Ila kwa hapa, nilikuwa nimeamua kuyakimbia haya kwa wakati huu mpaka muda ambao hiyo "Karma" ingekuja kunifata ili niyarudie kwa mara nyingine, ikiwa ni kweli kuna kitu kama Karma.
Sikuwa na presha katika utembeaji wala. Taratibu tu, ijapokuwa niliwaacha wanawake wale kama vile nimewakimbia, huku begi likiwa upande wangu mmoja nyuma ya bega. Nilijihisi kama vile mjeshi anayetoka kwenye 'mission' moja na kisha kuelekea kwenye nyingine ndani ya wakati huo huo, ingawa yangu ya kumsaidia Mariam haikuwa imefikia kiwango cha kuwa 'mission accomplished.' Na hiyo iliuma, basi tu.
Nikafika zangu barabarani, upande ambao watu wangesimama kwanza kusubiri magari yapite kisha ndiyo kuvuka mpaka upande wa pili ili kuchukua daladala za kuelekea Rangi Tatu huko. Ile tu ndiyo nataka kuvuka pamoja na wengine, mkono wangu ukashikwa kutokea nyuma kwa nguvu na ghafla mpaka kunifanya nishtuke kiasi, nami nikamgeukia aliyenikamata namna hiyo na kumtazama kwa umakini. Umakini nilioweka kumtazama mtu huyu ukafifia taratibu na kuniacha nikiwa namwangalia tu kwa kutoamini, kwa sababu sikuwa nimetarajia kabisa kwamba ingekuwa ni bibie Miryam!
Alikuwa amenikamata mkononi na viganja vyake kwa pamoja, akionekana kuwa ametoka kukimbia kutokana na namna ambavyo alipumua kwa uzito, huku jasho likionekana kumtoka kiasi kwenye paji la uso wake. Sikuwa nimetarajia kitu hiki kabisa, nami nikabaki nikimwangalia usoni tu, huku mapigo yangu ya moyo yakianza kudunda kwa nguvu sana pasipo kujua sababu iliyosababisha hilo.
★★★★★★★★★
ITAENDELEA
★★★★★★★★★