Simulizi: Mimi na Mimi

Simulizi: Mimi na Mimi

MIMI NA MIMI 2

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Siri, Tamaa, Hila, Usaliti, Ukatili, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KUMI NA TATU

★★★★★★★★★★★★★★★★★

Baada ya Festo kuniambia niwe makini, Bertha akaonyesha kukerwa naye kiasi na kumwonyesha kidole chake cha kati kwa njia ya utani, kisha akanivuta zaidi ili tuondoke. Hata Dotto, ingawa hakusema lolote, akawa amenionyeshea dole gumba kirafiki, ili kutuliza hali baina yetu, lakini nilikuwa nimeishiwa raha na amani kabisa yaani, siyo siri. Tena sifichi, yaani bado nilihisi adrenaline mwilini ikiwa juu kiasi kwamba miguu ilikuwa ikitetema kiasi, lakini baada ya sekunde chache ikatulia.

Tukashuka ngazi na madam mpaka huko nje kichwa kikiwa na mawazo tu, naye Bertha akaona anipe ruhusa ya kuwa dereva wa gari wakati huu ili nimwendeshe mpaka alipotaka twende akapate kiamsha kinywa, kisha hotelini kwake. Nikawasha tu ndinga, nisiwe na jambo lingine lolote akilini lililopita kuziba taswira ya jinsi wale watu walivyouawa mbele yangu, nami nikaliondoa gari kutoka kwenye jengo hilo upesi.

"Haaahh... what an epic start of a day!" Bertha akasema hivyo kwa furaha tukiwa mwendoni bado.

Nikaendelea tu kuwa makini na uendeshaji.

"JC yaani najihisi kama vile nimetoka kwenye set ya movie, sikutanii! Ile ya Captain America Civil War ile, sema tu hii ikiwa bloody zaidi hahahah..."

Alionekana kuwa mawinguni yaani, lakini sikujali kabisa maneno yake na kuendelea kuendesha kama vile nimegandishwa.

"Vipi JC? Bado tu una-sulk?" akaniuliza hivyo.

Nikabaki kimya.

"Hey, si naongea na wewe?"

Nikavuta pumzi na kusema, "Niko makini tu na uendeshaji. Kichwa hakipo sawa."

"Kwa nini kisiwe sawa?"

"Mambo mengi tu..."

"Kama?"

"Ah, Bertha..."

"Nini? Ongea. Unataka kusema hao washenzi kufa ndo' imekuuma saaana?"

"Siyo hivyo, sikuwa tu tayari..."

"Tayari na nini? Kwa hiyo haujafurahi kwamba maadui zetu wamekufa?"

"Bertha, sijawahi kufanya kitu kama hicho, sawa? Kuangalia mtu akiuawa mbe...."

"Ulitaka wenyewe ndiyo watuue kwa hiyo?"

"Labda kunge-kungekuwa na njia nyingine ya...."

"Njia gani? Hii ni conscience yako tu inakusuta, si ndiyo? Ulikuwa unataka kujiunga nao at one point kwa kuamini maneno ambayo Chaz alikwambia. Nadanganya?"

Nikahisi hasira na kuliegesha gari pembeni ya barabara kwa kasi sana, naye Bertha akashtuka na kuniangalia kwa mshangao makini.

Nikamwambia, "I wasn't ready! Bertha... can you imagine, nini kingetokea kama ningefika tu hapo na kum-shoot Dotto nikifikiri kweli alikuwa anataka kukuua? Nini kingefuata baada ya hapo?"

"Well, lucky for us... hiyo haikutokea. Don't be tripping JC. Hiyo imeshaisha, sijui ambacho kinakusumbua ni nini," akaniambia hivyo.

Nikafumba macho huku nikishusha pumzi kutuliza hisia, nami nikamwangalia na kusema, "Sikuwa tayari, Bertha. Leo... ni kitu ambacho sikuwahi kufikiria kingekuja kuwa sehemu ya maisha yangu... lakini sasa hivi nitapaswa kuishi nikijua na mimi nilikuwa na mchango kwa yaliyotokea leo. Naomba uelewe. Bado siko kama wewe."

Akafumba macho pia na kushusha pumzi, huku akitikisa kichwa kwa kukereka kiasi, naye akaniangalia na kusema, "Nataka uiondoe hiyo 'bado' kutoka kinywani mwako, JC. Sitaki kusikia unaitapika tena. Ni part ipi ya hili game iliyokufanya ufikiri hatutakuja kufanya vitu kama hivi? Eh? Na tena hata haujaua mtu leo! Mbona una-trip kihivyo mtu wangu?"

"Inaweza ikawa rahisi kwako, lakini sijawahi kuua mtu, na sidhani... kama nitaweza kuja...."

"Kuua? Kwa nini? Kwa kuwa we' ni daktari?" akaniuliza hivyo.

Nikamtazama kwa umakini sana.

"Hujawahi kuniambia moja kwa moja, lakini najua wewe ni daktari. Hukuniambia pia, ila najua ulienda kwa Festo kutafuta bastola ili ujilinde..." akaniambia hivyo.

Nikatazama pembeni.

"Unaweza usiniambie lolote kukuhusu JC, lakini nakuelewa. Umeacha maisha ya udaktari kwa sababu umeona yanakuboa, si ndiyo? Ukanipata mimi, ukaona hii ndiyo sehemu unayofaa kuwa. Kwa nini unaanza kuogopa tena sasa? Ukiwa ndani ya hili game unapaswa uelewe kuwa kuna kufa ama kupona, and you gotta do everything necessary to survive. Usije kukonyeza hata siku moja mbele ya kifo JC, nakufundisha, nisikilize..."

Nikamwangalia usoni kwa macho makini.

"Usifikirie mara mbili kabisa. Mtu akikutishia kukuua, unapaswa uwe tayari umeshamuua kwenye akili yako kabla yeye hajaifikia hiyo hatua. Sudi alipokunyooshea bastola siku ile tupo Red Room, kuanzia hapo tayari nilijua angekuja kujaribu kukumaliza, na mimi pia. Sikufumba macho, maana ikiwa ningeyafumba, leo ni mimi na wewe ndiyo tungekuwa tunalamba mchanga. Huu umekuwa kama mfano, ipo siku haya yanaweza yakajirudia maana watu... watu wanapenda rebellion. Wanapenda kutaka kufanya mapinduzi. Sikuzote kuwa mindful, uwe tayari kuchukua hatua zinazohitajika kuchukuliwa ili ubaki kuwa hai, and on top. Ukiona black mamba anakukaribia utamwangalia tu eti kisa hujawahi kuua?"

Nikatikisa kichwa kukanusha.

"Sasa! Kwa nini mtu atishie kuyaondoa maisha yako halafu umwangalie tu ayaondoe? Huo utakuwa ni ujinga kwako. Narudia tena JC. Umechagua kuwa na mimi ili uje kuwa on top, na kwa sababu unanipenda. Si ndiyo? Basi ukiwa na mimi... uwe tayari kufanya kitu chochote kile kwa ajili yangu. I mean it. Uwe tayari kuua, JC. Hakuna mtu wa kufanya killing test dummy, kwa hiyo ikitokea retaliation, live... uwe tayari kuua. Sijui umenipata?"

Aliongea kwa njia yenye kusihi sana, nami nikaangalia mbele na kutikisa kichwa kukubali kwa shingo upande.

Akanishika shingoni na kusema, "Hey, niangalie."

Nikamtazama.

"Hautakiwi kufanya nini ukiwa mbele ya kifo, JC?" akaniuliza.

"Sitakiwi kukonyeza," nikamjibu.

"Good. So, kione kikiwa kinakuja kwako kutokea mbali, ili kikikufikia uwe tayari kukigeuza kirudi kilipotoka. That's how we survive in this game. Ukiwa mzembe, ukiendelea kuwa soft... utakufa haraka sana, na itakuwa kuchelewa kujutia kuingia kwenye hili game kwa sababu tayari litakuwa limeshakumeza. Sijui unanielewa?" akaniambia hivyo.

Mh!

Mwana nikatikisa kichwa kuonyesha uelewa kweli, naye akaiachia shingo yangu na kutazama mbele huku akiegamiza mwili wake vizuri kwenye siti.

"Nitafutie ka-McDonald basi. Nina hamu kali ya kula hamburger," akaniambia hivyo.

Nikarudisha umakini wangu tena kwenye usukani na kuliingiza gari barabarani, nami nikaendesha kuelekea upande ambao ungekuwa na mgahawa mmoja mzuri kama McDonald's kweli ili madam ajilie alivyotaka, na bado rundo la mawazo likiwa limekilemea kichwa changu.

★★

Tukapata mgahawa mmoja mzuri na kujumuika kula hicho cha asubuhi, kwa utulivu tu pamoja tukala hizo baga nzito kwelikweli mpaka kushiba, naye akalipia kisha tukaingia barabarani tena ili kurudi hotelini kwake mara moja. Alihisi uhitaji wa kujisafisha mwili kisha tuondoke tena kwenda kwenye biashara zake kama ilivyokuwa kawaida, na kama vile hakukuwa na lolote zito lililotokea kwa hii asubuhi.

Tumekuja kufika kwenye chumba cha hoteli alipokaa ikiwa imeshaingia saa sita mchana, na huko nje kulikuwa na wingu zito lililoonyesha nia ya kutaka kushusha mvua ya maana, kwa hiyo kulikuwa na hali ya ugiza ndani ya chumba chake iliyofanya awashe taa na kuipa sehemu hii hali ya usiku-usiku yaani. Bado nilikuwa kama sina raha, Bertha ndiye aliyekuwa akizungumza zaidi kuhusu kuliuza lile gari lake lingine la Harrier ili apate pesa ya kuchezea, lakini ni kama nilikuwa simsikii kabisa.

Nikakaa tu sofani na kutulia wakati yeye alipokuwa ameanza kuvua nguo zake, halafu akapokea simu ilipoita na kuzungumza na mtu fulani kuhusiana na masuala ya usambazaji wa madawa na malipo kwa wafanyakazi wao. Nikatoa simu yangu mfukoni kuangalia ujumbe uliokuwa umeingia, na oh ikaja kwa surprise, ilikuwa ni askari Ramadhan. Nikamwangalia Bertha, ambaye alikuwa ametoa nguo zake na kubaki na sidiria na nguo ya ndani nyeupe tu, nami nikaufungua ujumbe huo na kuusoma upesi.

'Tulikuwa kweny mission nyingin huku Ilala. Nisharud, utanipa update mpya. Kesho kesho-kutwa uhakika'

Ukasomeka hivyo. Alikuwa ametumia namba yake ya kisiri, na baada ya kuusoma huo ujumbe nikaufuta upesi Bertha alipokuwa ameanza kuja upande wangu huku bado akizungumza na mtu wake. Akakaa sofani karibu nami kwa kukunjia mguu mmoja juu, akijibinua mgongo kiasi kuelekea mbele ili akikaribishe vyema kifua chake kwangu, nami nikawa namwangalia kwa utulivu tu. Akawa anachezea-chezea ndevu zangu hafifu upande wa shavu, kisha ndiyo akakata simu na kuweka mkono wake mmoja kifuani kwangu.

"Kuna wajinga wanasema nawaonea eti kisa nimechelewa kuwapitishia malipo leo, re-up zenyewe wanazofanya zinayumba, lakini bado wanalalamika. Maneno meengi. Si nimetoka kukwambia? Umeona jinsi watu wanavyopenda rebellion? Basi tu ili tuanze mizozo, halafu tufikie pabaya..." akasema hivyo na kusonya.

Mimi nikaangalia mbele tu kwa utulivu.

Akaonekana kunitathmini kidogo, kisha akasema, "Una uhakika hautaki twende kuoga wote?"

Nikatikisa kichwa kukubali.

"Mmm... JC! Ndo' kusema bado nyundo ya Thor imekugonga namna hiyo?"

Nikatabasamu kiasi na kusema, "Sijui hata unamaanisha nini."

"Yaani hauna raha kabisa. Unawaza nini bwana?"

"Kuwaza lazima madam. Ah... hivi ikitokea pale pakajulikana? Itakuwaje? Hm?"

"Pajulikaneje?"

"Inaweza ikatokea... dharula... watu wenu mpaka waje wapasafishe, wenye jengo wanaweza wakafika, au... ile miili tu kwanza wanaitoaje pale huu mchana wote, inawezekana kuna CCTV camera za nje, na... kuna mlinzi pia. Exposure huoni iko high?"

"Una-panick mno, hakuna vitu vya namna hiyo... we' umeona CCTV wapi?"

"Sijaona sawa, lakini kuna mlinzi. Hata kama mtamlipa, anaweza akaja akawataja baadaye ikiw...."

"Mlinzi yupi?" akanikatisha kwa kuuliza hivyo.

Nikaendelea kumwangalia usoni kwa umakini. Akapandisha nyusi kama vile kutaka kunielewesha jambo fulani, nami nikawa nimemwelewa. Aisee! Na mlinzi wangemuua. Dah! Nikatazama pembeni tu nikihisi kuchoka zaidi.

"Usiwe na presha. Tunajua jinsi ya ku-handle mambo vizuri, so just... tulia. Acha kuwaza mno. Come on, be a man," akaniambia hivyo na kunipiga kidogo shavuni.

Nikamwangalia na kuuliza, "Kwa hiyo una shaka kwamba me siyo mwanaume?"

"Sina shaka, ila ndo' umeanza kunipa mashaka. Ukiiacha hii kitu ikutikise namna hii, kweli utaweza wewe kubeba mengine yanayokuja?"

"Unamaanisha nini?"

"Charles amekufa. Nataka nikupe hoteli ya Buza na pale Masai, uzi-handle," akaniambia hivyo.

Nikawa makini zaidi na kuuliza, "Nini?"

"Yeah. Tena nakupa zotezote. Lakini utaweza kubeba wewe?" akaniuliza hivyo.

"Ahah... Bertha subiri, usifanye maamuzi haraka-haraka. Me... sidhani kama nitaweza kubeba hizo biashara kweli..."

"Well sina mtu mwingine wa kumpa, awe kichwa huko. Nahitaji mtu ambaye... namwamini," akasema hivyo.

"Kwa hiyo na Chalii ulikuwa unamwamini?" nikamuuliza pia.

Akanikazia macho yake kama kuuliza 'nini?'

"Sorry Bertha, yaani... ni jambo zuri kujua unaniamini, thanks, lakini mimi hayo mambo si...."

"Nakupa hizo sehemu, JC. Utake usitake," akasema hivyo.

Nikabaki nikimtazama machoni kwa umakini.

"And anyway, sina... sina mpango yaani hata wa kuziangalia, maana... nahisi kama vile scent yote ya Charles imetapakaa huko. Nakupa. Handle utakavyoona inafaa. Full stop," akasema hivyo.

"Unamaanisha hazina faida sana kwako?"

"Yeah. Kwa hiyo, nakupa, yaani kama, nakuachia. Ukiamua kuuza ukanunua gari, sawa tu. Ndo' zawadi zangu kwako, kwa hiyo ukiamua kuzitunza au kuzitupa... ni wewe tu. Zishakuwa zako," akaniambia hivyo.

"Ila Bertha! Unapenda kuchezea vitu wewe..."

"Kuchezea? Si ni vyangu? Najenga vingine bora zaidi, hivyo naona kama vimeshapitwa..."

"Halafu ndo' unaniachia mimi? Kwamba na me nimepitwa sana?"

"Ahahahah... utajiju. We' fanya unaloona kuwa sawa huko, yaani hayo maeneo sa'hivi sitaki kugusa kabisa. Kinachotakiwa nikuhalalishe tu huko, halafu uendeshe mambo unavyoona inafaa. Ila ndo' utumie zawadi zako vizuri. Nimesota sana mpaka zikawa kubwa vile..."

"Halafu sasa hivi unazitupa?"

"Agh... whatever. Don't blow a brain gasket," akaniambia hivyo kwa kutojali.

Alikuwa yuko mawinguni kwelikweli yaani, sidhani hata alikuwa akifikiria upande hasi kwa wakati huu maana alihisi kuwa kila kitu kingekwenda vizuri sana kutokea hapa baada ya kuwaondoa Sudi na Chalii Gonga, lakini ambalo hakulijua ni lile ambalo lingekuja kumpiga vibaya mno kama giza la ghafla pale ambapo umeme wake ungekatwa.

Ila, kufikiria kwamba nilikuwa nimetoka kujitahidi kumwokoa muda mfupi nyuma ili tena nije kuona anaporomoka kulinipa mvurugo mwingi sana wa kihisia. Yaani moyo wangu haukuwa na msimamo sahihi kujua ulitaka nini kutokea hapa ilipokuja kwenye suala la huyu mwanamke. Mambo yalikuwa yamekwenda mbali sana, na sikuwa na njia ya kuyabadilisha yale yaliyokuwa yakija.

Nikiwa bado natafakari tu, Bertha akaingiza kiganja chake ndani ya T-shirt langu na kunishika tumboni, naye akasema, "Bado tu kale ka-scene pale tulipokuwa kanazunguka kichwani kwako, eh? Ukikumbukia jinsi hao mafala walivyokula chuma... doesn't it turn you on?"

Aliongea kwa njia ya kuamsha hisia za kimahaba huku akiukaribia uso wangu, nami nikamwangalia usoni kwa utulivu.

"Vile nilivyompiga Chaz risasi... tah, tah! Wasn't that f(......) hot?" akasema hivyo na kunilamba shavuni.

"Kwa hiyo... hivi tuseme kama ningekuwa nimekugeuka na kukusaliti kiukweli, ungeniua na mimi?" nikamuuliza hivyo.

Mishipa ya shingo yake ikatokeza akiwa ananiangalia kwa utafakari, naye akarudisha uso wake nyuma na kutazama pembeni, kisha akasema, "Acha kuwaza hayo bwana, nimekwambia. Hauwezi kunisaliti, najua hilo. Kwa hiyo kukuua ni kitu ambacho siwezi kufanya."

"Lakini vipi ikitokea, ikitokea tu nikakusaliti Bertha? Utanifanya kama Chalii?" nikamuuliza tena.

Akaniangalia na kusema, "Sitaki kuongelea hayo mambo, JC. Usiharibu mood yangu bwana, niko lifted, unakuwaje?"

Nikashusha pumzi na kukishika kiganja chake taratibu, nami nikamwambia, "Bertha, najua hatujakutana katika mazingira mazuri sana. Mambo ya mbeleni... yanaweza yakabadilika...."

"Unataka kusema nini, JC? Niambie ukweli," akanikatisha kwa kusema hivyo.

Nikabaki nikimtazama machoni kwa utulivu.

"Unahisi utanisaliti? Hm? Kwamba utanichoka na utapata mwanamke mwingine unayeona ni mzuri sana zaidi yangu, si ndiyo? Au tayari una mwanamke mwingine?" akauliza.

Hiyo haikuwa maana yangu, yaani hakuwa hata na wazo kabisa kuhusu uwezekano wa usaliti nilioongelea kuwa wa kumpindua yeye na watu wake kabisa.

Nikamwambia, "Sijamaanisha hivyo."

"We' nimeshakuelewa JC. Unafikiri nitakufanyia kama nilivyomfanyia Chaz, kwa hiyo unaogopa. Lakini siwezi kukufanyia hivyo. Nakupenda," akaniambia hivyo kwa hisia.

Dah!

"Na nimekwambia ukiwa na mimi akili yako inapaswa kuwa sehemu moja, usiitangishe sana, utapata ma-stress tu. Sasa hivi wa kutupa hayo mastress nimeshawaondoa, kinachobaki ni mimi na wewe. Angalia hilo. Focus kwenye hilo. Usiwaze sijui unaweza ukanisaliti... we' ni mtu mzima JC, na ni mmoja mwenye msimamo, I know. Kwa nini ufikiri unaweza kunigeuka? Unigeuke kwa kipi labda? Iweke mindset yako inapopaswa kuwa, hautafanya lolote lile baya kwangu. Mimi naamini hilo. Kwa nini we' ushindwe?" akaniambia hayo.

Nikainamisha tu uso wangu.

Akanishika kidevu na kunitazamisha kwake huku akisema, "Usiogope. Wewe ni wangu. Nitafanya kila kitu kukulinda kama wewe ulivyoweza kunilinda. Unajua, nili-imagine ikiwa Dotto angekuwa amenigeuka kiukweli, basi leo... mimi na wewe tungekufa pamoja. Ulikuwa tayari kwa ajili ya hilo, na hiyo ni sababu tosha kwangu kuamini mpaka mwisho kwamba hauwezi kuniumiza. Nimeona upendo wako kwangu JC, kwa hiyo achana na stress kuanzia sasa hivi ili mimi nikuonyeshe wa kwangu. Sawa?"

Nilijikuta hadi napenda ufasaha wake katika kuongea, lakini bado moyo ulikuwa ukiniuma sana. Kujua kwamba alikuwa amenipenda kikweli, lakini mimi nisingeweza kumpenda namna hiyo, na bado ningehitaji kumtupia kwa maaskari ili akutane na mkono wa haki wa sheria. Yote kwa yote, Bertha bado alikuwa mwanamke aliyefanya mambo mengi yasiyofaa, kwa hiyo hata kama roho ingeniuma vipi, ningetakiwa kuacha kile ambacho askari Ramadhan alikuwa amekisema kwenye ujumbe alionitumia kitokee. Hakukuwa na namna.

Baada ya madam kunibembeleza kwa hayo maneno, akanifuata mdomoni na kuanza kunibusu kimahaba sana. Sikuwa katika hali nzuri kihisia kunifanya nisisimke, lakini kadiri alivyoendelea kunionyesha hamu yake kwangu, ndivyo nami nikaanza kupanda taratibu. Akanikalia kabisa na kuendelea kunionyesha upendo wake, nami kiukweli sikuwa nikitaka tena jambo hilo kwa sababu nyingi, lakini kuliacha litokee ikawa ni lazima.

Kwa hiyo nikamruhusu afanye kila alichotaka kwenye mwili wangu ili kunipa mapenzi yake matamu, tukapiga mechi kwa mtindo wa kuendesha farasi akiwa amenikalia hapo hapo sofani, na alikuwa anaruka! Kisha tukaipeleka mpaka bafuni na kuoga pamoja bila kuacha kupeana penzi. Nilihakikisha namridhisha kwa wakati huu kwa sababu nilijua ingekuwa ni mara ya mwisho, kwa hiyo ningekuwa nimemwachiapo kumbukumbu nzuri kiasi kabla ya mbaya ambayo angekuja kubaki nayo wakati ambao angekamatwa.

Hivyo ndivyo karata dume ilivyopaswa kuchezwa mpaka kufikia mwisho wa mahusiano yangu na huyu mwanamke, na hayangechelewa kufikia tamati, lakini najua kwa njia moja ama nyingine yangeniacha nikiwa nimevurugwa mno. Kutojali sana, ndiyo kitu nilichokuwaga najaribu kukimbia na kujifanya hakipo kabisa kwenye mfumo wangu, lakini hii hali ilikuwa ikithibitisha vingine. Nilimjali Bertha, hata kama alikuwa mbaya, nilikuwa nimemjali. Lakini ndiyo ningetakiwa kumwachia tu, kama msemo wake, nitake nisitake.

★★

Kwa hiyo baada ya mechi tamu iliyomridhisha madam, akawa ameamua kuvaa vizuri tena ili atoke kwenda kushughulikia biashara zake. Ilikuwa twende pamoja, lakini nikasingizia kuwa sikujihisi vizuri, yaani sikuwa na umakini uliofaa kumsindikiza huko na hivyo ingekuwa bora tu kama ningeenda kule Ubungo kwenye supermarket kumalizia nini na nini, maana wenzangu wangekuwa wamelemewa na mengi bila mi' kuwepo.

Lakini Bertha akaona anidekeze kidogo. Akaniambia niende tu kwangu nikapumzike, maana aliona hii siku ilikuwa nzito mno kwa hiyo sabato fupi kutoka kwenye biashara zake ingekuwa bora kuchukua. Na kweli, nilihisi uhitaji wa kupumzika kiakili na kimwili. Akanipa na hela, eti nitakula na kuichezea kidogo kwa kunywa hata bia, nami nikamshukuru na kuamua kuvaa, kisha nikamwacha hapo hotelini kwake ikiwa ni mida ya saa tisa alasiri. Mvua kubwa ilikuwa imenyesha na kukata, kwa hiyo hali ya unyevu ilikuwa imetapakaa kwingi na mawingu kuficha jua bado.

Mpaka napanda daladala kwenda Mbagala na safari kuanza, bado nilikuwa nimetekwa kimawazo sana. Yaani, kuangalia yale mauaji leo, nilijiona kama vile nilitoka kwenye ndoto mbaya tu, na hii sehemu ya maisha yangu haikuwa kweli. Ila, hakuna chochote ambacho ningeweza kubadilisha kuhusu kilichowapata Sudi na Chalii Gonga. Wazia kama kweli Dotto angekuwa pamoja nao, ningekuwa wapi sasa hivi? Kwa hiyo kihalisi nilitakiwa kushukuru Mungu kuendelea kupumua, ingawa yaliyotokea bado hayakuwa yenye kuridhisha.

Sikuwa hata na hamu ya kushika simu, sijui niwasiliane na nani, yaani nilitaka tu kufika kwa Ankia na kulala kabisa. Baga niliyokula saa tano ilinitosha, na nimekuja kufika Mzinga kwenye mida iliyoelekea saa kumi na moja. Hakukuwa na msongamano wala nini. Nikatembea tu mpaka kwa Ankia, nikiwa sina bastola yangu tena, nami kweli nikaingia pale ndani mpaka chumbani na kujitupia tu kitandani kama mzigo.

Mwili ulikuwa umechoka kiasi shauri ya mechi ndefu niliyocheza na Bertha, na bado viungo viliuma-uma kiasi shauri ya kuwa nimeanza kunyanyua chuma, kwa hiyo nikaona nijaribu kuvuta usingizi tu ili nipumzike ipasavyo, lakini ukanigomea. Yaani nilijigeuza na kujigeuza, wapi, mpaka inaingia saa moja yaani bado nilikuwa kitandani tu nalazimisha usingizi, lakini ni mawazo na mawazo tu ndiyo yaliyoendelea kunisumbua.

Nikaona niachane na kitanda na kunyanyuka kwenda kukojoa kwanza, kisha nikawasha taa za ndani na nje na kurudi kitandani tena. Nikachukua simu yangu na kuangalia hili na lile, na bado yule Kevin hakuwa ameacha kunitumia jumbe za kuniuliza kama nilikuwa nimeshaongea na dada yangu kuhusu ugomvi wao. Ndiyo nikaamua kumtumia ujumbe nikisema kuwa ni wiki hii ndiyo ningekwenda kumwona Jasmine, hivyo ningezungumza na dada yangu huyo kwa niaba yake kwa hiyo asiwe na hofu.

Kevin akawa amerudisha jibu la shukrani na kuniambia nimjulishe yatakayojiri, nami nikamkubalia. Kidogo tu, Tesha akawa amenipigia, na nilipopokea akaniuliza ikiwa nilikuwepo hapa nyumbani tayari. Nilipokubali, akasema ndiyo anakaribia kufika huku akiwa anatokea sokoni huko Mzinga, kwa hiyo angekuja hapa kunicheki. Hakukuwa na shida na hilo, na kweli baada ya dakika kadhaa jamaa akaingia hapo kwa Ankia na moja kwa moja kuja mpaka chumbani kwangu. Ankia hakuwa amerejea bado.

Tesha akaja mpaka kitandani na kukaa, akiwa na mwonekano wa kawaida tu wa kinyumbani, nami nikajivuta na kukaa kwa kuegamia mto mwanzoni mwa kitanda.

"Oya, vipi unaumwa?" akaniuliza hivyo.

"Hamna. Nimechoka tu," nikamwambia hivyo.

"Mizunguko mingi, au siyo?"

"Yeah."

"Kamepiga leo ile mchana!" akasema hivyo.

"Nini, mvua?"

"Eeh. Ilikukuta huku?"

"Hamna, nilikuwa Makumbusho bado. Na wewe? Ilikukutia wapi?"

"Kwa Happy."

"Ooh, kumbe ulienda Tandika?"

"Mm-hmm."

"Sawa. Mzima huyo mke wako?" nikamuuliza.

"Eeh, alikuwa ameni-miss kidogo. Nikaenda kumcheki, amekuja na dada yake pale. Ndiyo nikatambulishwa, eti mashemeji," akasema hivyo na kutabasamu.

"Mhm... na we' utakuja kumtambulisha Happy lini?" nikamuuliza.

"Ah, bado bwana..."

"Anaonekana anakupenda sana. Kwani unaogopa nini?"

"Hizo siyo mambo zangu, kaka. Nitakuja labda kukupeleka wewe kwanza akujue brother wangu, lakini kumleta huku? Hamna."

"Kwa hiyo hutaki kuacha lifestyle ya kurukaruka? Hutaki kutulia na mmoja?" nikamuuliza.

"Muda wa kutulia utafika tu. Sa'hivi naona bado bro. Na sometimes naweza kufikiri nitatulia na huyu afu' tunakuja kutibuana tu. Nishawahi kuleta demu hapo, akatibuana hadi na mama hao... sitaki hayo yajirudie," akasema hivyo.

Nikatabasamu kiasi na kutikisa kichwa taratibu.

Akasema, "Hata kazi ya maana bado sijapata, nadandia opportunity hapa na pale, hazishiki, natuliaje na mwanamke kama Happy ambaye tayari ana kazi yake. Ye' ndo' anilee?"

"Ee, si anakupenda? Kwani kuna shida gani?"

"Aa wewe, unazingua. Masuala ya me kuanza kukalia kigoda kumpikia siyawezi," akasema hivyo, nasi tukacheka kidogo.

Nikamwambia, "Uko sahihi. Ni muhimu upate kazi. Huwa unatafuta?"

"Eeh, kaka. Sema, me JC... kazi sijui za ndoo zege, siwezagi kabisa. Za maofisini ndo' zinanifaa. Natuma maombi kama yote, wengine matapeli tu, si unajua? Huku pakikubali, ukaingia, unalaghaiwa, agh, unarudi mwanzo tena. Yaani... nataka nipate sehemu ya uhakika, bro. Hela nzuri yaani, nitoke nikae na mwanamke wangu," akaniambia hivyo.

"Yeah, ila sa'hivi Bongo kubagua kazi Tesha, unajua jinsi maisha yalivyo magumu. Ni bora uwe na sehemu umeegamia hata kama bado iko chini, ili uende unapanda, kuliko kungoja for the perfect job. Umri unaenda rafiki yangu," nikamwambia.

"Unasema kweli, bro. Ninaelekea 26 sa'hivi, usingekuwa wizi wa Joshua ningekuwa nimetumia mali yangu vizuri sana kuendesha maisha... ila hiyo ishapita. Natakiwa nitafute changu. Da' Mimi mwenyewe analemewa naona, mambo kibunda ananyooshea mkono, lakini sometimes na yeye simwelewi. Sijui anataka nikae nyumbani kimoja?" akaongea hivyo.

"Kwa nini useme hivyo?" nikamuuliza.

Akasema, "Yule jamaa'ake anayemtongozaga, Festo, anayekujaga hapo 'skani..."

Nikawa makini na kuuliza, "Amefanyaje?"

"Alitaka kunipa ofa kufanya kazi... kwenye kampuni yake, anapofanyia. Nikamwambia sister, akanikatalia. Nisikubali eti," akasema hivyo.

Nikatulia kidogo, kisha nikamuuliza, "Kwa nini Miryam alikukatalia?"

"Si hamtaki jamaa? Sasa... anafikiri nikikubali hizo favor na nini, mwamba atakuwa anajirahisishia kuingia pale. Mimi hapendagi watu waingie kwa shortcut, yule jamaa anaonekana ana hela, ashawahi kujaribu kumnunulia mavitu da' Mimi, akayakataa. Huwezi jua, labda hata... unaweza ukakuta ana limke huko mikoani ama hizo hela za utapeli, si unajua?" akasema hayo.

Nikaangalia tu chini na kutikisa kichwa kukubaliana na hilo.

"Da' Mimi hataki kabisa za kupewa na wanaume, naelewa. Ila ndo' sa' me nikikubali kufanya kazi huko, kwani jamaa atambeba kwa lazima? Si ananisaidia tu?" Tesha akaongea hivyo.

"Hapana, dada yako yuko sahihi. Usikubali lolote kutoka kwa huyo mwanaume," nikamwambia.

"Kwa nini?"

"Tumia tu akili ya kuzaliwa Tesha. Kuna wanawake wangapi? Kwa nini anafosi sana kumpata dada yako? Inaweza ikawa siyo kwa nia nzuri, na Miryam anaelewa hilo, ndiyo maana akija hapo anamchekea tu lakini siyo kwamba anamwelewa wala nini... Bongo hii kama unavyojua, ni kuwa makini. So uwe smart pia Tesha. Kama ulivyosema, huwezi jua. Usikubali vyote tu vya kupewa. Pambania unavyotaka kuwa navyo," nikamwambia hivyo.

Akatikisa kichwa kuonyesha uelewa, naye akasema, "Sawa. Ndo' pambano liendelee."

"Vipi hapo home, wako poa?" nikamuuliza hivyo.

"Eeh. Dah, kaka yaani tulikuwa excited kinyama na birthday ya ma' mkubwa Jumamosi, asikwambie mtu..." akasema hivyo.

"Eee, afu' kweli. Ni Jumamosi! Ah, cheupe wangu atakua. Imewahi kufika eti? Kesho kutwa tu," nikamwambia hivyo kwa shauku kiasi.

"Eeh, ila na matatizo yameitangulia sasa, sijui hata kama tutaisherekea mwanangu," akasema hivyo.

"Kwa nini?" nikauliza.

Akasema, "Kaka... nilipokwambia da' Mimi amelemewa, yaani elewa amelemewa kichizi..."

Nikiwa nimeshajua ambako angeelekea, nikatazama pembeni tu kwa utulivu.

"Kuna deni nasikia la milioni ngapi sijui anatakiwa alipe, kwa sababu ya yale mautumbo ya Joshua, kaka. Huo mwezi uliopita, ametupa hela nyingi kinoma kwa ajili ya Mamu, huko dukani, ma' mkubwa Jamila, kusapoti ndoa ya Doris, mambo kibunda tu, na sasa hivi hili limekuja tena. Hapo alipo anahaha kuitafuta hiyo hela, sijui wamempa muda gani, ila ni mfupi sana... anakuwa na mawazo huyo... mpaka namwonea huruma," akasema hivyo.

Nikashusha pumzi kiasi na kuuliza, "Amekwambia hayo yeye mwenyewe?"

"Hamna, ma' mkubwa, cheupe wako ameniambia. Waliongea, dada akamwambia, na hataki sisi wengine tujue maana anataka amalizane na hilo kabla ya birthday, ila... nimeshaona kama linampiga vibaya mno. Sijui itakuwaje akishindwa kuwalipa, ndiyo maana nilikuwa natamani hata ningekuwa na kazi tayari mwanangu, kukaa hivi navaa suruali tu halafu sina pepa... ufala tu," akaongea hivyo kwa mkazo.

Jambo hilo likawa limerudi kichwani na kuanza kufanya mizunguko yake kama kawaida, nikiwa nakumbukia maneno ya mzee wangu ile asubuhi wakati nikiwa kwenye boda. Tesha hakujua undani wa kile ambacho Miryam alikabili, lakini mimi nilielewa kwamba kilikuwa kizito sana.

Kwa hiyo tukaendelea kuongea mambo ya hapa na pale kuhusiana na jambo hilo na sherehe ya Bi Zawadi Jumamosi, nikijitahidi kuonekana kuwa sawa kihisia tu hadi Ankia aliporejea hapa tena na kujiunga nasi. Mwanamke alikuwa ameleta chakula kwa ajili ya kupika, yaani unga wa ugali na samaki zilizokaangwa na viungo vyake, na baada ya muda mfupi tu akaenda huko jikoni kwenda kupika.

Mimi na Tesha tukaendelea kuwa pamoja hapo hadi mida ya saa tatu jamaa alipoaga kurudi kwao, ndiyo nikamtoa mpaka nje na kumwambia awasalimie wa kwao, nisingeweza kwenda leo kuwaona mpaka kesho, kisha baada ya hapo nikaamua kukaa subuleni na mwenye nyumba wangu.

Sikuwa na uchangamfu yaani, nikiwaza mambo niliyojionea leo, tatizo la Miryam, ishu za familia yangu mwenyewe ambazo mama alitaka sana nije kwenda huko nyumbani ili tuzizungumzie, na kile ambacho kingetokea kwa Bertha baada ya askari Ramadhan kutibua biashara zake. Kichwa kilikuwa kimechemka haswa, hali yangu ya kihisia ikiwa imeshuka bado mpaka na Ankia akauliza ikiwa nilikuwa naumwa.

Lakini nikamwondolea wasiwasi, na baada ya kuwa amemaliza kupika tukala pamoja, huku tukitazama TV, na tukaendelea kupeana ushirika mpaka kufikia mida ya saa tano kabisa. Ankia alikuwa ameanza kuchat mno kwenye simu yake kwa huo muda, na niligundua kuwa aliyekuwa akichat naye ni Bobo. Inawezekana tayari jamaa alikuwa ameanza kumtokea, lakini mwanamke hakutaka kuweka wazi jambo hilo kwangu kwa hiyo nikaona nijikaushe tu kama vile sikujua.

Akawa ameamua kuelekea chumbani akidai kwamba angelala mapema, wakati naelewa alitaka kupigiana simu na jamaa huko huko! Nikasema sawa tu, yeye aende na mimi ningefanya ufungaji wa hii milango kuanzia huko nje, naye alipoondoka, nikaona nizime tu TV na kubeba funguo ili niende nje kufunga geti, kisha ndiyo ningerudi na kujimwagia kwanza kabla ya kwenda chumbani kupumzika ipasavyo.

Nilipokuwa nimetoka ndani na kuufikia ukuta wa uzio, upande wa nyumba yao Tesha ambao ulikuwa na ile taa iliyoungua haukuwa ukitoa mwanga, kumaanisha hakuwa amebadilisha taa bado, hivyo kulikuwa na giza kuuelekea huu wa kwetu. Nikiwa ndiyo naelekea kuuvuka ili niende huko getini, matobo ya ukutani yakaniruhusu nione upande wao wa varandani hapo nje, na kwa uhakika, bibie Miryam alikuwa amekaa pale kwenye kiti chake kama alivyozoea.

Nikaahirisha kusonga mbele zaidi na kusimama kumwangalia, na kwa sehemu niliyosimama asingeweza kuniona kwa sababu giza lilinificha kiasi, kwa hiyo nikaamua kuegamia ukuta kabisa na kuendelea kumwangalia. Bibie alikuwa amekaa kwa utulivu tu, na urembo wake wote aliojaliwa kuwa nao ukinifanya nimwangalie kwa hisia, akitazama mbele kama mtu aliyezama kwenye mawazo sana, na ninaelewa alikuwa akitafakari vitu vingi mno.

Labda kama angepewa muda wa kutosha, basi hilo suala la shamba angelitatua vizuri sana, ila yaani ni kesho tu alitakiwa kuamua la kufanya kati ya mambo mawili aliyokuwa amepewa kuchagua, na najua alikuwa akijiuliza ni kipi alichopaswa kuamua ambacho kingekuwa sahihi si kwake tu, bali na kwa mdogo wake Mariam, na familia yote kwa ujumla.

Nikamwona Mariam akitoka huko ndani kwao na kumfata Miryam hapo nje akiwa na shauku ya kumwonyesha dada yake jambo fulani, nami nikatabasamu kiasi baada ya kumwona binti. Miryam pia akatabasamu kwa hisia na kumsikiliza mdogo wake, ambaye alitaka waende ndani pamoja ili amwonyeshe, na bibie akawa amekubali. Mariam akatangulia huku akionekana kufurahi, naye Miryam akaacha kutabasamu na kutazama pembeni kama vile raha imemtoka tena. Alitia huruma!

Lakini akashusha pumzi tu na kunyanyuka taratibu, naye akajibebea kiti chake na kuelekea ndani bila kutambua kwamba nilikuwa hapo nikimwangalia. Nilitaka sana kumsaidia huyu mwanamke. Sikupenda kumwona hivyo. Na hasa baada ya kuongea na Tesha muda mfupi nyuma kuhusu jinsi dada yake alivyokuwa mkali kwenye masuala ya shortcut, ndiyo nikawa nimeona hakukuwa na njia nyingine ya kumsaidia Miryam isipokuwa kuchukua hatua ambayo najua huenda isingemfurahisha kabisa. Na mimi ndiyo nikaamua kuichukua hiyo hatua sasa, hata kama ingemkwaza.

★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★

Full Story WhatsApp or inbox

Whatsapp +255 678 017 280
 
Msaidie mchumba JC hawezi kukwazika maana hata yeye anakupenda pia
 
MIMI NA MIMI 2

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Siri, Tamaa, Hila, Usaliti, Ukatili, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KUMI NA NNE

★★★★★★★★★★★★★★★★★

Siku ya Alhamisi ikafika. Nililala usingizi mtamu tu kana kwamba sikuwa na matatizo kabisa, na pia nilikuwa nimemwota Miryam. Labda shauri ya yeye kuwa sehemu kubwa pia ya fikira zangu, ama tu ile jana usiku nilipojiweka pale ukutani na kumtazama sana ndiyo kulifanya nikamwota bibie, lakini ndoto hiyo ilinifanya niamke nikijihisi amani kwa sababu ilikuwa nzuri. Lakini sitaisimulia!

Ikiwa ni saa mbili sasa, nikajitoa tu kitandani na kwenda kuanza harakati za usafi ili niweze kuondoka haraka. Sehemu niliyokuwa nikielekea ndiyo sehemu ambayo nilipaswa kwenda ili kuchukua hatua ya kumsaidia bibie Miryam na tatizo lake kama nilivyokuwa nimejiahidi jana, na najua ikiwa angekuja kutambua jambo hili, basi angekwazika kiasi na mimi. Si unajua jinsi Miryam alivyokuwa? Lakini nilikuwa tayari kwa lolote lile, maadamu nihakikishe kwamba tatizo lake lingemwondoka.

Kwa hiyo nikavaa vizuri, na Ankia alikuwa ameshaamka na yeye pia kujiandaa kuelekea dukani kwake, lakini mimi nikamtangulia kuondoka na kuagana naye vizuri kuja kuonana baadaye. Nilitaka kuharakisha kufika huko na kurudi huku ili nije nimwone binti Mariam, maana nilitaka kuangalia afya yake ya ubongo iliendelea vipi zaidi.

Katikati ya safari ya kuelekea huko nilikuwa nikichat zaidi na Dina, mwanadada huyo akiniambia kuwa angekuja huku Jumamosi kwenye sherehe ya kuzaliwa kwake Bi Zawadi, kwa hiyo alikuwa na hamu kubwa ya kuniona tena.

Nilijua kutokea hapo ningepaswa kufanya jambo fulani ili kuzimisha kale kamchezo nilikokuwa nimeanza kufanya na Dina, maana alionekana kutaka kukaendeleza lakini mimi sikutaka hivyo tena. Ningetakiwa tu nimwelezee kistaarabu na aelewe kwamba nisingeweza kuwa pamoja naye tena kimwili, kwa sababu sasa hivi nilikuwa nimempenda mtu mwingine. Nilitaka kuwa wa huyo mtu mwingine pekee, hata kama bado hakuwa anajua kwamba nampenda.

Basi, nikafanikiwa kufika huko nilikotaka kwenda na kilichonipelekea kikatiki, kisha upesi nikageuza tena kurudi Mbagala. Nikawa nimewasiliana na Adelina pia, nikimpa mwaliko usio rasmi wa kuja kwenye sherehe ya Bi Zawadi, naye akasema angejitahidi kuwepo. Nilipofika maeneo ya Rangi Tatu, nikaamua kuingia kwenye mgahawa mmoja na kunywa supu na chapati mbili kwanza, kisha ndiyo nikarudi barabarani kuelekea Mzinga.

Kila kitu kilifanyika upesi tu yaani, nimekuja kufika Mzinga saa sita mchana, nami nikapita dukani kwa Ankia na kumsalimia, nikimkuta na marafiki zake hapo na mishebeduo yao, nami ndiyo nikaelekea moja kwa moja mpaka nyumbani kwake Miryam. Gari lake halikuwepo, bila shaka akiwa amekwenda kazini, na najua isingechukua muda mrefu sana kwake kutambua mchongo niliokuwa nimeenda kufanya leo, lakini ambayo yangefata yote kwa yote yangekuwa sawa tu kwangu. Nilikuwa tayari.

Nikafika mlangoni na kugonga hodi, nami nikakaribishwa kwa sauti nzuri ya Bi Zawadi. Nikaingia sebuleni hapo na kuwakuta mama wakubwa pekee wakiwa wameketi sofani kwao, wakitazama kipindi cha dini kwenye TV, nami nikawasalimu vizuri na kuketi pia.

"Naona mnamcheki Mwamposa," nikawaambia hivyo.

"Eeh, kuna ibada special ya kukanyaga mafuta wanafanya leo. Sisi kwenda huko mbaali, kwa hiyo tunafatilia hapa..." akaniambia hivyo Bi Zawadi.

"Ahaa... sawa. Naisikiaga," nikasema hivyo.

"Hujawahi kufika kwa Mwamposa?" akaniuliza hivyo Bi Jamila.

"Nimeshawahi. Kuna... shangazi yangu, wa Arusha, alikuwa amekuja mwezi wa kwanza hapo kwa ajili ya maombi na nini... ndo' nikawapeleka huko yeye na mama..." nikawaambia hivyo.

"Ahaa... na mama yako huwa anaenda?" Bi Jamila akauliza.

"Eem... akiweza. Siyo kwamba... ni mwabudu kabisa wa huko, yeye anaendaga kwenye kanisa fulani lipo kule Goba... la Evangelistical nini sijui... jina refu," nikamwambia hivyo.

Wakacheka kidogo kwa pamoja, naye Bi Zawadi akauliza, "Ni kubwa?"

"Eeh, kubwa. Zuri. Lipo karibu kabisa na nyumbani, huwa hata anatembea," nikamwambia.

"Ahaa, sawa," cheupe akaonyesha uelewa.

"Mamu yupo ndani?" nikawauliza.

"A-ah, ameenda sokoni na Tesha. Wameenda kufata nyama," Bi Zawadi akanijibu.

"Ahaa, nilijua tu. Ikiwa ni nyama, Mamu kusindikiza ni lazima," nikawaambia hivyo.

"Hahahah... kweli. Yaani anataka aione ikiwa mbichi buchani, mpaka ikija kuiva. Anapenda nyama!" Bi Zawadi akasema.

"Ahah... sisi wote. Na angalau, aendelee kuwa anatoka-toka kama hivyo... ni kitu kinachomsaidia sana," nikawaambia.

"Ni kweli. Ila tu ndiyo hatakiwi kufika mbali mno, maana... hali yake bado bado, si ndiyo?" Bi Zawadi akauliza.

"Eeh, kufika mbali mno, hasa akiwa peke yake... mpaka baadaye kidogo. Sa'hivi bado," nikamwambia hivyo.

Bi Zawadi akatikisa kichwa kuonyesha uelewa.

"Umependeza JC. Uliamkia wapi leo?" Bi Jamila akaniuliza hivyo.

Nikacheka kidogo na kusema, "Nilienda tu hapo mbele kidogo. Na mbona niko kawaida tu jamani..."

"Mmm, kawaida wapi? Wakati ukipita huko wanawake wote wanakuangalia," Bi Zawadi akasema hivyo.

"Ahah... cheupe na masihara yako bwana..." nikamwambia hivyo.

"Na wewe hujioni ulivyo cheupe JC? Hivi kwanza utaoa lini, tunataka tumwone mchumba wako," Bi Jamila akasema hivyo.

Mimi na Bi Zawadi tukacheka kwa pamoja, nami nikamwambia, "Siku siyo nyingi, nitaoa tu."

Bi Jamila akasema, "Ee baba, uoe. Una kazi yako safi, ukipata mwanamke mzuri unatulia naye, unazaa na watoto..."

"Yaani JC, Jamila anapenda masuala ya ndoa! Hapa mpaka utakubali kuoa msichana atakayemtaka yeye," Bi Zawadi akasema hivyo kwa utani.

Nikatabasamu tu kwa furaha.

"Haiko hivyo bwanaa, nampatia tu kijana wetu baraka zangu, apate mke mzuri. Au siyo JC?" Bi Jamila akasema hivyo.

"Kabisa. Na haitachukua muda mrefu sana nitampata mwanamke anayenifaa, baraka zako zimeshasomeka," nikamwambia hivyo.

"Sasa je!" Bi Jamila akamwambia hivyo mwenzake.

"Haya bwana. Kwa hiyo JC, wewe mpaka sasa hivi uko single bado?" Bi Zawadi akaniuliza.

Nikatikisa kichwa kukubali.

"Mmm, kweli?" Bi Zawadi akafanya hivyo.

"Kabisa," nikamhakikishia.

"Asa' unasubiri nini baba? Si utafute mtu?" Bi Zawadi akasema hivyo.

"Nataka kuwa mwangalifu, cheupe wangu. Vijana wengi siku hizi hatujatulia, kwa hiyo nikitaka kutulia na mwanamke mmoja, natakiwa niwe na uhakika kwamba yeye pia atatulia na mimi," nikamwambia hivyo.

"Sikiliza JC. Wanawake waliotulia, wapo, sidhani ni tabu kuwapata. Wapo. Tena wengi tu. Au nadanganya?" Bi Jamila akasema.

"Ni kweli. Ila nafikiri anamaanisha kwamba, kazi ipo kwenye kumpata anayemfaa YEYE sasa. Huku Dar wengi wameshayageuza maisha ya mapenzi kuwa biashara na starehe za muda tu, unakuta anaoa, kidogo wameachana, hayo siyo. Baba... kawatafutie huko kwenu, Mwanza, au Shinyanga huko kwa wasukuma, huku hapana," Bi Zawadi akasema hivyo.

Akanifanya nicheke kwa furaha sana.

"Yaani unataka JC aoe wasukuma?" Bi Jamila akamuuliza hivyo.

"Kwani wasukuma wana shida gani? Siyo wote ni washamba bwana. Si eti JC?" Bi Zawadi akaniuliza.

"Yeah, siyo wote. Inategemea," nikamwambia.

"Eeeh. Na sijamaanisha kwamba uoe msukuma, au mshamba. Uoe mwanamke mwenye maadili, ndiyo nachomaanisha. Ah, nyakati hizi wengi wameshatekwa na utandawazi, mara fesibuku, sijui twita, na kujali nywele, vinguo vyenye kuonyesha uchi, na kioo tu muda wote. Unaweza ukapata mwenye maadili na hayo mambo anayajua, lakini anayaona kuwa ya kawaida sana... yaani la msingi, awe mke anayejua nini maana ya kuwa mke, akishajua amekuwa mwanamke. Si unaelewa?" Bi Zawadi akanipa mawaidha.

Nikatikisa kichwa kukubali na kuegamia mkono wa sofa kwa kiwiko changu huku nikishikisha kiganja kwenye taya kuwapa umakini zaidi.

"Jamila amesema wapo wengi, ila kweli ni kazi kumpata anayekufaa. Unakuta wakati mwingine unapata mtu anajionyesha mtakatifu, kumbe...."

"We! Ndani ni mchafu! Hivi vitabia-vitabia wanavyokuwa navyo watoto wadogo hawa wanavitoa kwa mama zao wasiowafunza maadili kwa sababu na wenyewe wanaendekeza tabia za kijinga, na... hayo mautandawazi. Na, na hivi siku hizi yanasambaa haraka... mpaka inakuwa ngumu sana kujua nani ana hizo tabia, au nani hana, kwa hiyo unaweza ukachukulia kama vile wanawake wooote wako hivyo hivyo," Bi Jamila akaniambia hayo.

Bi Zawadi akasema, "Ni kweli kabisa. Hee! Nimeona... ile juzi, ulivyotupeleka kule Sinza..."

Nikamtikisia nyusi kukubali.

"Kulikuwa kuna wadada kule, yaani jinsi wanavyovaa! Mpaka nikafikiria nilikuwa nimetoka kwenye dunia nyingine na kwenda tofauti na niliyoijua miaka mingi ya nyuma. Wanawaiga wazungu, kwa kila kitu. Na sasa hivi imeshakuwa kawaida tu kwao kuyafanya hayo mambo yaani, utawaambia nini?" akasema hivyo.

"Mambo yamebadilika sana," nikamwambia hivyo.

"Eeeh. Ndiyo maana unatakiwa uchague mwanamke kwa hekima sana. Ni busara kwako kuendelea kusubiri JC," Bi Zawadi akaniambia hivyo.

"Lakini siyo usubiri mpaka uzeeke sasa, ama utumie ujana wako kuchezea-chezea watoto wa watu weee..." Bi Jamila akaniambia hivyo.

Nikacheka kidogo huku nikiwa nimefumba mdomo, na bado nikiwa nimeegamia taya.

"Ahahah... kweli, ndiyo mambo yenu na Tesha hayo," Bi Zawadi akasema hivyo.

"Hamna, me siko hivyo..." nikajitetea.

"Eeee, JC..." Bi Zawadi akasema hivyo kwa njia ya kusuta, nasi sote tukacheka pamoja.

"Mnayoongea ni ya kweli kabisa. Me mwenyewe... nafikiria kutulia na mwanamke mmoja tu. Nimeshajionea mengi, na huu ndiyo wakati mwafaka kwangu. Nimeshamwona mwanamke anayefaa kuwa mke mzuri kwangu, na nitafanya kila kitu kuhakikisha nampata," nikawaambia hivyo.

"Kweli JC?" Bi Jamila akaniuliza hivyo.

Nikatikisa kichwa kukubali.

"Safi sana. Litakuwa jambo jema yaani ukioa, tukamwona mke wako. Tena... tuombe Mungu Mimi na yeye apate mume mzuri, aolewe atulie na ndoa yake. Ndiyo jambo nalohitaji sana kuona kabla Mola hajanichukua," Bi Jamila akaongea kwa hisia.

Nikaguswa sana na maneno hayo ya huyu mama, nami nikakaa vyema zaidi na kutazama chini kwa utafakari.

Bi Zawadi akamshika mwenzake kiganjani na kumwambia, "Usianze kuongelea masuala ya kufa bwana. Kila kitu kitaenda vizuri; Doris huyo anaolewa, Tesha ataoa, Mariam atapona na ataolewa pia. Mimi ataolewa wa kwanza kabisa, na sisi tutakuwepo kumpa support yote anayohitaji. Mpaka na wajukuu tutacheza nao. Au siyo JC?"

Nikatabasamu kiasi na kutikisa kichwa kukubaliana naye.

Bi Jamila akaonekana kulengwa kabisa na machozi, ikionyesha kweli hicho ni kitu alichokuwa na hamu nacho zaidi, naye akasema, "Natamani tu mambo yangekuwa rahisi kwa binti yetu. Anahangaikia vitu vingi sana mpaka anakosa muda wa kujijali yeye mwenyewe. Anateseka."

Nikawaangalia wanawake hawa kwa hisia sana, naye Bi Zawadi akanitazama usoni.

"Miryam bado anahangaishwa na suala la wizi wa Joshua, JC. Unakumbuka nilipokwambia ile juzi kuhusu simu yake... niliposikia anaongea na mtu fulani kuhusu madeni na nini..." Bi Zawadi akaniuliza hivyo.

Ikanibidi nitikise tu kichwa kuonyesha uelewa wa alichoongelea kama vile ni hapo hapo alipokuwa akiongelea ndiyo nilielewa, bila yeye kujua nilikuwa nafahamu kila kitu kwa undani zaidi.

Akasema, "Kumbe wale watu ambao Joshua alitaka kuwauzia shamba la Mamu walikuwa wanamdai pesa nyingi, milioni 20 huko kabisa! Wameuza nyumba yake Joshua wakapunguza deni, lakini lililobaki Miryam ndiyo anatakiwa awalipe. Na ni kubwa. Ametuambia asipoweza kulipia, eti watamnyang'anya shamba la Mariam."

"Aisee! Poleni sana. Amesemaje Miryam? Ameweza kupata ya kuwalipa, ama atawaachia shamba?" nikauliza hivyo kama vile sijui.

Bi Jamila akasema, "Hamna, hataki kuuza kiwanja cha mdogo wake. Alikuwa amekusanya ili awapelekee kidogo leo, ametoka ndo' kwenda huko kwanza, sijui wapi..."

Nikamwangalia usoni kwa umakini, nami nikamuuliza, "Amepeleka pesa kuwa... kuwalipa?"

"Eeh. Na tena hakuwa amepata ya kutosha, kwa hiyo sijui sa' kama watakubali kumpa muda zaidi ili amalizie, au ndo' zamu hii shamba la Mamu litabebwa kabisa," Bi Zawadi akasema hivyo.

Nikaangalia pembeni tu kwa utulivu.

"Alikuwa hataki tujue, hakutaka kutupa presha... lakini tumejua ndo' na ye' akatuelezea. Sasa hivi tunasubiri kuona itakuwaje, maana...."

Bi Zawadi alipokuwa akisema hivyo, tukasikia sauti ya geti nje likifunguliwa na kufungwa.

"Tesha na Mamu hao," Bi Zawadi akasema hivyo baada ya kukatisha maneno yake.

"Ni vyema Mariam asisikie lolote kuhusu haya, si ndiyo baba?" Bi Jamila akaniambia hivyo.

"Ndiyo. Nina imani kila kitu kitakuwa sawa, wala msijipe msongo warembo wangu. Kila kitu kitaenda vizuri tu. Miryam atafanikiwa," nikawatia moyo kidogo.

Wakaonekana kufarijiwa na maneno yangu, na ndiyo mlango wa kuingilia ndani hapo ukawa umefunguka na Mariam kuwa wa kwanza kuingia akiwa amebeba mfuko. Binti akafurahi sana kuniona, naye akaja mpaka sofani nilipokaa na kuketi pia, kwa njia ya kawaida tu siyo ile ya kurukaruka sana, naye akanisalimu vizuri na kuniambia alikuwa ameenda sokoni. Tesha pia akaingia, na baada ya kusalimiana naye kirafiki, akakaa na kuanzisha mazungumzo yenye kuchangamsha pamoja nasi wote.

Mariam akafata vyombo huko jikoni na kuvileta hapo sebuleni ili aanze kukata nyama. Alitaka nione namna ambavyo aliweza jambo hilo yeye kama yeye, naye akakaa karibu nami kabisa huku akijitahidi kukata vipande vidogo na kuniangalia kwa matumaini ya kupata sifa kutoka kwangu. Na sikumnyima hilo. Nikamsifia sana kwamba aliweza, na baada ya kuwa amemaliza hiyo kazi akapeleka hivyo vitu jikoni tena na kujisaifisha, kisha akarejea kwetu na kukaa.

Ni Bi Zawadi ndiye akanyanyuka baada ya muda mfupi ili kwenda kuanza kutengeneza mboga, kwa hiyo tukabaki hapo sebuleni tukipiga story na binti Mariam na kufanya michezo rahisi yenye kuchemsha ubongo ambayo iliendelea kuonyesha matokeo mazuri zaidi kwenye ufahamu wa Mariam, kwa kuwa akili yake ilikuwa imefunguka zaidi.

★★

Nikaendelea kuwa hapo mpaka kufikia mida ya saa tisa alasiri, na tayari Bi Zawadi alikuwa ameshaunga mboga akisaidiwa na 'assistant' wake Mariam, huku Tesha akiwa amewapa mkono kwenye usongaji wa ugali. Kwa hiyo tukaponda ugali na nyama hapo, pamoja na chinese, na baada ya kushiba tukaendelea kuketi pamoja sebuleni kupeana mitazamo yetu tofauti-tofauti kuhusiana na sherehe ya kuzaliwa kwake Bi Zawadi.

Muda kama huu ulikuwa mzuri sana, kuweka mambo mengine mengi pembeni na kufurahia ushirika na hawa ndugu, lakini bado haikuwa rahisi mno kuacha kukengeuka juu ya fikira zenye kuutatanisha ubongo wangu. Kuna kitu ambacho nilikuwa nawaza sana, na ni kwa kuendelea kukaa pamoja na marafiki zangu ndiyo ilifanya nizidi kukiwaza shauri ya kusubiria mno matokeo ya maamuzi niliyokuwa nimechukua ile asubuhi. Na hatimaye, kusubiri huko kukafikia ukomo wake.

Simu yangu ikaanza kuita. Mpigaji? Bibie Miryam. Kwa sekunde chache nikabaki nikiitazama tu simu mpaka ilipokata, kisha akapiga tena. Nikaamua kutoka hapo ndani na kwenda varandani, nami nikapokea na kumsikiliza. Hakuongea mengi. Akauliza nilikuwa wapi, na nilipomwambia nipo huku kwao, akasema niende kule dukani kwake ili anione, mara moja! Woi! Bibie alisikika kuwa makini kwelikweli, kwa hiyo sikuwa na njia ya kumkatalia.

Nikamwambia sawa, isingenichukua muda mrefu sana kufika huko, naye akakata simu. Nilikuwa nimeingiwa na msisimko kwa kujua ambacho kingeenda kutokea huko, lakini si kwamba niliogopa ama nilikuwa na wasiwasi sanaaa. Nilikuwa tu nimetarajia hili, ila sikudhania angeniita huko ofisini kwake kabisa, na kwa njia fulani nikaona mwito wake kwenda huko kuwa wa busara; najua aliyotaka tuzungumzie hayakuwa na nafasi iliyotosha kuzungumziwa huku kwake ama kwenye simu.

Hivyo, nikarudi pale sebuleni na kuwaaga sasa wapendwa wangu, nikisema kuna mahali nilihitajika mara moja ila haingechukua muda mrefu sana kurudi huku, nao wakaonekana kuridhia na kunitakia matembezi mema huko nilikokuwa naenda. Ikiwa ndiyo inaelekea kuingia mida ya saa kumi, nikatoka hapo na kwenda kwa Ankia ili kujiweka sawa zaidi. Tena nikaamua kujimwagia kabisa na kuvaa kwa njia nzuri ambayo ingenipa mwonekano 'fresh,' ndiyo nikatimka upesi utadhani nilikuwa nimeitwa kwenye date.

Usafiri wa daladala nikapandia hapo Mzinga mpaka Rangi Tatu, kisha kutokea Zakhem hadi huko Kijichi kama kawaida nikapelekwa na bajaji. Kamoyo kalikuwa kanadunda, lakini ulikuwa ni msisimko tu yaani wa kutegemea mengi, na utayari wa lolote ambalo ungetokea ndiyo ulinifanya nijitahidi kutulia zaidi kihisia. Nikashushwa kwenye kituo cha Upendo, na sasa ilikuwa imeshaingia saa kumi na moja, ndiyo nikaelekea taratibu kwenye duka kubwa la bibie huku watu wengi wa hizo pande wakinitazama sana.

Mimi nikaendelea kulielekea tu hilo duka, ikiwa umepita muda wa wiki chache tokea mara ya mwisho nilipofika hapo, na kupitia milango yenye vioo katikati nikaweza kumwona Soraya akiwa amesimama kwa hapo ndani, karibu kabisa na meza yake ya usaidizi. Nikatabasamu kiasi na kufikia hapo mlangoni, maana ulikuwa umepita muda, na yeye kutokea humo ndani akawa ameangalia upande wangu na kuachama kiasi akionekana kushangaa.

Kisha mtoto akaanza kucheka kwa haya, akijifunika uso kwa kiganja chake, nami nikafungua mlango na kuingia ndani hapo mpaka kufikia aliposimama yeye. Alionekana kufurahi kweli yaani, na kama nilivyokuwa nimemzoea, alivaa hizi baibui nyeusi pamoja na ushungi mweupe ulioficha sehemu kubwa ya kichwa chake na kuacha uso wazi, sehemu za mwili wake mnono ambazo zikionekana zaidi ikiwa ni viganja tu na miguu yake myeupe iliyokuwa ndani ya makhirikhiri nzuri nyeusi.

Akawa anatabasamu kwa shau, huku akiniangalia kwa aibu, nami nilikuwa nimepanga kumkazia lakini nikashindwa kujizuia kucheka kidogo kwa pumzi na kutikisa kichwa kidogo. Akajikaza zaidi na kuniangalia usoni kwa ile njia kama kuniambia 'ila wewe,' katika maana ya kwamba nimemtesa sana mpaka sasa halafu ghafla tu natokea namna hiyo bila onyo wala nini.

Nikiwa namtazama kwa utulivu tu, nikamwambia, "Mambo vipi Soraah?"

Midomo yake ikawa inakunjamana-kunjamana tu kuzuia tabasamu eti, naye akasema, "Safi."

Nikaona alikuwa amebeba mkoba wake begani, hivyo nikamuuliza, "Ndiyo ulikuwa unaondoka?"

Akavuta kichwa chake mara moja kwa njia ya kukubali huku akinitazama kwa matumaini yaani.

"Pole na kazi mwaya," nikamwambia hivyo.

"Asante. Jamani! Yaani kama vile mwaka umepita," akasema hivyo.

"Toka tulipoonana?"

"Eeeh. Yaani mpaka nikafikiri sitakuja kukuona tena JC," akaongea kwa hisia.

"Nipo. Mambo mengi tu," nikamwambia hivyo.

"Jamani! Mhm... we' haya..."

"Sikudanganyi. Maisha yangu yamejaa misukosuko, we' acha tu. Ku-balance muda kwenye kila kitu... inakuwa ngumu sometimes. Kuna sehemu tu zimenimeza sana sasa hivi," nikamwambia hivyo.

"Sawa. Me sina shida, wala usijali," akasema hivyo kiupole.

"Vipi familia?"

"Wazima. Sijui wewe?"

"Wako good pia. Nimefurahi kukuona Soraya, nilikukumbuka," nikamwambia hivyo.

"Kweli?"

"Yeah."

"Kwa hiyo ulikuwa umekuja kuniona?"

"Aa... ndiyo. Nilikuwa nataka kuzungumza na Miryam, nikaona nije kukuona na wewe," nikampa moyo kinamna hiyo.

Akaibana midomo yake kiasi na kuniangalia kwa njia fulani ya mashaka.

"Nini?" nikamuuliza hivyo.

"Niambie ukweli JC. Sasa hivi umeshapata mwanamke mwingine eti?" akaniuliza hivyo.

Nikabaki nikimtazama machoni tu kwa utulivu.

"Haina shida, me naelewa. Nilishakwambia. Ila ndiyo bado nakuhitaji. Kama, kama nilivyokwambia JC, hata kwa mara moja ya mwisho nahitaji kuwa nawe tu..." akaongea hivyo bila woga.

"Umeni-miss sana?"

"Mno."

"Sasa una uhakika gani hiyo mara ya mwisho unayoitaka haitakufanya unihitaji zaidi baada ya muda kupita, Soraah?" nikamuuliza hivyo kwa upole.

"Eh... siyo... yaani, nitajitahidi kujizuia tu..."

"Kwa nini usiweze kuanzia sasa?"

"Mh! JC? Ndo' kumaanisha kwamba hunitaki tena kabisa?" akauliza hivyo.

"Sina maana hiyo, we' ni mwanamke mzuri sana. Ila..."

"Ndiyo umeshanitumia, ukamaliza," akanikatisha.

"Siyo hivyo..."

"Niambie tu JC kama hutaki kabisa kuni...."

Maneno ya Soraya yakakatishwa baada ya mlango wa ofisi ya boss wake kusikika ukifunguka, nasi kwa pamoja tukatazama huko. Miryam mwenyewe akatoka. Pigo zito kiasi moyoni mwangu likadunda, nduhh!

Mwanamke huyo akasimama usawa wa huo mlango baada ya kuniona, na alionekana makini kweli. Alikuwa amevaa shati la kike, likiwa ni jeans yenye rangi ya usamawati uliolowana, akilikunja mikono kufikia viwiko vyake, pamoja na suruali nyeusi iliyombana kiasi japo ilikuwa pana kufikia chini. Alinitazama kwa umakini sana, kisha akaanza kuja mpaka hapo nilipokuwa na Soraya na kusimama pia.

"Dada, me ndiyo naenda. JC amefika, anataka mzungumze," Soraya akaongea kama vile mtu aliyejishtukia.

Bila kumwangalia, Miryam akamjibu, "Sawa, ufike salama," huku akiwa amekaza macho yake kwangu tu.

Nikashusha pumzi tu kujipa utulivu, naye Soraya akamshukuru na kuniaga mimi pia kistaarabu, akinionyeshea ishara kwa vidole vyake viwili kwa chini kuwa 'tutawasiliana,' kisha huyoo akaondoka zake. Nikamwangalia Miryam usoni, na kweli, macho yake yalionyesha dhahiri kwamba alikuwa amekwazika sana na mimi, na nilielewa kwa nini. Alikuwa ameshikilia karatasi iliyochapishiwa maandishi maalumu mkononi, naye akainyanyua juu kiasi kama kunionyesha, nami nikaitazama.

"Hii ni nini, Jayden?" swali lake la kwanza kabisa kwangu likawa hilo.

Nikiwa naelewa vizuri karatasi hiyo ilihusiana na nini, nikamwambia, "Usichukulie vibaya Miryam. Nilitaka tu kusaidia."

"Kwa nini ufanye hivyo? Nilikuomba?" akaniuliza tena.

"Hapana, ila...."

"Nani amekupa haki ya kuamua kufanya kitu cha namna hii bila kuniambia? Eh? Jayden umekuwaje?"

"Najua usingekubali wachukue shamba la mdogo wako, ni haki yake, na haustahili hii adhabu ambayo Joshua amekuachia Miryam kwa sababu najua haukuwa tayari kui...."

"Jayden, unakosea. Wewe siyo mwamuzi wa maisha yangu. Unanijua vizuri, si ndiyo? Ulikuwa unajua kabisa kwamba nisingekubaliana na hili, lakini bado ukafanya hivyo. Kwa nini?"

"Kwa sababu najua hukuwa na pesa ya kutosha," nikamwambia hivyo.

"Ooh, kwa hiyo wewe ndiyo mwenye pesa ya kutosha sana mpaka ukaenda tu na kuwapa milioni 10, 'hee... shikeni hizi hapa?'"

"Sijamaanisha hivyo."

"Nilikuwa na njia ya kwenda kusuluhisha hili tatizo Jayden. Lakini umeingia na kunikatia katikati, unajua sipendi hivyo, ningefanikiwa kuwapa...."

"Miryam nisikilize. Wasingekubali uwape kiasi kidogo, sijui uje uwaongezee tena... hawangekubali. Hiyo ilikuwa ni mechanism kuku-force utoe pesa yote kwa mkupuo, ama walichukue shamba la Mariam... deadline ilikuwa ni leo leo, na kama usingefanikiwa Miryam, wangebeba kila kitu. Wangetaifisha kila ulichonacho, na mahakama ilikuwa upande wao. Usingeweza kufanya lolote," nikamwambia hivyo kwa msisitizo.

Akabaki akinitazama usoni huku akipumua kwa uzito kiasi.

"Sijakukatia katikati kwa sababu labda... nimekuona hauna, ama me ninazo sana, no. Nimefanya tu hiyo gesture ndogo kukusaidia we' na familia yako kuepuka hiyo shida Miryam..." nikamwambia hivyo kwa upole.

"Gesture ndogo? Umetoa milioni 10... milioni 10 Jayden kulipia matatizo yangu, halafu unaiita gesture ndogo?" akaniuliza hivyo.

Nikabaki nikimtazama kwa hisia.

"Na hayo yote ya me kutaifishwa mali zote umeyajua vipi? Eh? Ulikuwa unafatilia kila kitu?" Miryam akauliza tena.

Nikaangalia chini na kushusha pumzi kiasi.

"Ahah... okay, so, umeenda kutoa milioni zako kumi ili kunisaidia, yeah? Natakiwa nikurudishie," akaniambia hivyo.

"Hapana, sihitaji unirudishie," nikamwambia hivyo.

"Hau... hauhitaji? Milioni 10 umezitoa, mfukoni kwako mwenyewe, ili tu kunisaidia, halafu hautegemei lolote?"

"Sitegemei chochote Miryam. Nimeshakwambia toka mwanzo, nafanya tu kukusaidia," nikamwambia hivyo kwa upole.

"Hapana. Siwezi kuamini. Hizo pesa umezitoa wapi? Kwamba uzichezee tu kwenye matatizo yangu mimi ambaye hata hunijui vizuri, halafu ziishie tu hewani? Ni nini unachotaka Jayden?" akaniuliza kwa mkazo kiasi.

"Sitaki chochote. Kama ni ngumu kwako kuamini kwamba nachotaka tu ni kuwasaidia, hilo ni tatizo lako Miryam. Siyo kila mtu anataka tu gain. Na... hiyo pesa ilikuwepo tu, nilitunza... na... imetokea dharula kama hivyo... ndiyo nimetumia..." nikajaribu kumshawishi.

Akabaki akinitazama kwa umakini sana.

"Miryam, sikudanganyi. Nimefanya hivi pia ili kumsaidia na Mamu. Hilo shamba... hicho kiwanja kinaweza kuja kumsaidia sana baadaye, nyie wote... unalijua hilo, ndiyo maana unampambania. Nimekupa mkono kidogo tu kuendelea kuhakikisha hukipotezi, kwa nini unafanya ionekane kama nimekukosea sana? Eh? Hata shukrani ndogo tu ya moyoni Miryam, hauhisi kabisa?" nikamuuliza hivyo kwa hisia.

"Ahh... Jayden tatizo hunielewi. Siyo kwamba sina shukrani kwa sababu ya msaada unaonipa, Jayden... sitaki tu niwe na deni zaidi kwako... umeshafanya mengi mno..." akaongea hivyo kwa hisia.

"Nilikwambia lini utunze madeni kwangu? Eh? Kwa nini bado unahisi kwamba unatakiwa kunilipa? Sijafanya hivi ili unilipe Miryam. Tena nafanya hivi kwa sababu...." nikaishia hapo tu na kubaki nimemtazama.

"Najua unapenda tu kutusaidia, sijakataa. Lakini Jayden, mimi ndiyo nilivyo. Msaada kama huu kuupokea kijuujuu tu, halafu niseme asante, ndiyo imeisha? Siwezi. Hiyo pesa uliyotoa ingeweza kuwa na umuhimu fulani mkubwa kwenye maisha yako, lakini umeimalizia yote kwangu wakati kwa muda huu sina uhakika wa kuweza kuirudish...."

"Na ndiyo maana nimekwambia hauhitaji kulipia lolote..."

"Hapana Jayden, lazima nipambane mpaka nikurudishi..."

"Miryam, nisikilize. Huo umuhimu wa pesa unaoongelea ndiyo umefanya nimeitoa sasa hivi. Unanielewa? Nisingekaa kusubiri... kuona Mariam anataifishwa haki yake kwa sababu ya upuuzi wa Joshua, na wewe naelewa hali yako ndiyo maana nikaona nisaidie. Sihitaji unilipe, na wala usijisikie hatia kwa lolote, nimetoa kwa kupenda, siyo ili kupata faida. Please Miryam..." nikamsihi.

Akauliza, "Lakini kwa nini? Eh? Unataka kuniambia umetafuta pesa hiyo yote... umeitunza... halafu uje tu kuitoa kwetu kinamna hiyo? Umeangalia mbele kweli? Vipi ikiwa utajisababishia hasara kwa kufanya maamuzi bila kufikiri...."

"Miryam...."

"... bila kufikiria matokeo ya baadaye? Sawa unajali, lakini kwa nini mpaka ufikie hatua hiyo? Siyo rahisi kwangu kutohisi hatia hata kama unaniambia nisihisi hivyo, maana ninaweza nikawa sababu ya kukunyima kitu fulani mbeleni kwa sababu umekaa kuhangaikia matatizo yangu. Kwa nini unajibebesha mizigo yangu Jayden? Unapata faida ipi kwa kulipia hasara ya mtu mwingine bila kujali mato...."

"Kwa sababu nakupenda Miryam!" nikajikuta nimeropoka.

Miryam akabaki akinitazama kama vile hakunisikia vizuri.

Mapigo yangu ya moyo yalikuwa yameongeza kasi, nami nikainamisha uso na kusema, "Samahani, ni... nilikuwa sitaki ku... kukwambia kihivyo, ila..."

Nikamtazama na kukuta bado ananiangalia kwa njia ya kutoelewa yaani. Najua nilimchanganya.

Nikajipa ujasiri zaidi na kumwambia, "Miryam... hakuna kingine kinachonisukuma kufanya haya isipokuwa ya hisia nilizonazo kwako. Sipendi kuona... unaumia. Ninafanya yote... chochote nachoweza kwa ajili yako kwa sababu nakupenda. Nakupenda sana."

Nilimwambia hivyo huku nikimtazama machoni kwa hisia sana, naye akawa ananiangalia kwa njia ya kawaida, lakini nilielewa kuwa hakutarajia niongee maneno hayo hata kidogo. Ama labda tayari alikuwa ameshakisia ila alitaka tu niyaseme, eti? Sikujua, ila itikio lake lilionyesha kweli hakutegemea. Kiukweli mimi mwenyewe sikuwa nimefikiria kabisa kwamba ningemwambia hii kitu kwa huu muda, lakini tayari mtama ukawa umemwagika.

Nikamsogelea karibu zaidi kwa ujasiri wa hisia zangu kumwelekea na kuishika mikono yake kwa chini, nami nikamwambia, "Sihitaji unilipe. Moyo wangu ndiyo unaniongoza kufanya yote kwa ajili yako, na ninapenda kuyafanya. Ni kwa sababu nakupenda sana Miryam."

Nilikuwa karibu zaidi na uso wake mzuri sana, akiwa ananiangalia kwa macho yenye utafakari mwingi, naye akaidondosha karatasi aliyokuwa ameshika huku akiwa amekaza macho yake kwangu tu. Kisha, taratibu akaitoa mikono yangu kutoka kwenye yake na kujisogeza nyuma kidogo. Nikabaki namwangalia tu kwa hisia. Yeye akawa ananiangalia kama haamini vile, ile yaani, 'hivi huyu kijana ametoka kabisa kuniambia mimi hivyo?' Ha, hapa kazi nilikuwa nayo!

Nikasema, "Miryam...."

Akanyanyua kiganja chake kunizuia nisiendelee, nami nikatulia. Alionekana kuwa makini sana sasa hivi, naye akasema, "Ndiyo lilikuwa lengo lako."

Ah!

Nikawa nimeshaelewa anataka kuelekea wapi, nami nikatulia tu na kuendelea kumwangalia usoni.

Akasema, "Yote hayo, ulikuwa unayafanya ili... faida ambayo ungepata iwe... mimi."

Nikafumba macho na kukaza meno. Mchezo akauelewa... tofauti kabisa yaani!

Akauliza, "So that was your play? Kwamba ufanye haya yote ili uje kunipata mimi kama tuzo?"

"Miryam jamani..." nikamwita kwa sauti ya kubembeleza huku nikitikisa kichwa taratibu.

"Nimeelewa, nimeshakuelewa. Kila kitu ungefanya kwa ajili ya Mamu, Tesha, familia yangu, ili... uje kumzoa Miryam. Na mimi ningefanya nini? Ningekubali tu out of a show of gratitude..."

"Miryam, usiongee hivyo. Ninakupenda kweli..." nikasema hivyo kwa hisia.

"Koma!" akaniambia hivyo kwa mkazo huku akinyanyua kidole chake kimoja.

Dah! Nikatulia.

"Hivi kweli... me nafikiri... yaani, me nadhani sina njia ya haraka kukulipa kwa msaada wote ulionipatia lakini kumbe tayari ulikuwa umesha-capitalize kila kitu! Miryam ndiyo angekuwa malipo!" akaongea kwa hisia za kuvunjika moyo.

"Oh God, Miryam! Kwa nini uwaze hivyo?" nikamuuliza kwa hisia.

"Unataka niwaze nini kingine kinacho-make sense? Tafadhali Jayden, niambie unanitania rafiki yangu... ndiyo nitakuelewa," akasema hivyo.

Nikabaki nikimwangalia kwa hisia tu.

"Ahh... Sikutegemea unifanyie mchezo kama huu. Yaani, mimi? Unaniambia... wewe... unipende mimi??" akauliza hivyo kwa hisia.

"Kwa nini nisikupende?" nikamuuliza pia.

"Ahah..." akafanya hivyo na kutikisa kichwa chake kama kusema haamini.

"Miryam nisikilize..."

"Simama hapo hapo, usinisogelee!" akanizuia kumfata.

Nikatulia tu.

Akaanza kusema, "Nakuthamini sana Jayden. Wewe ni... rafiki mzuri. Nakuona kama mdogo wangu, tunaweza hata tukataniana kama unavyotaniana na wadogo zangu, lakini... sipendi ipite mipaka. Kabisa yaani, hebu fikiria kwa umakini, sawa? Wakati mwingine inaweza ikawa tu ni..."

"Sijakwambia nilichofikiria, Miryam. Nimekwambia ninachohisi. Nakupenda," nikamwambia hivyo kwa uhakika.

"Acha ujinga Jayden! We' siyo mtoto. Nina... nina mambo mengi ya kufikiria, mambo mengi ya kufanya, halafu unaniletea vitu gani hivi? Kama ndiyo shukrani unayoitegemea kutoka kwangu kwa kunisaidia mpaka sasa, tambua kwamba umeenda mbali sana. Mbali mno ambako hakuna ukomo. Huwezi kufika popote ukiendekeza hizo... hhh..." akaishia hapo na kushusha pumzi tu.

Dah! Hivi kweli kungekuwa na njia nzuri ya kumwelewesha huyu mwanamke ili aelewe? Nikabaki namwangalia tu kwa hisia zilizoanza kuwa huzuni kutokana na kuvunjika moyo sana.

Akasema, "Nitatafuta namna ya kuulipa wema wako. Nashukuru kwa kila kitu... ila naomba hapo ndiyo iwe mwisho."

Aisee!

Akashusha pumzi kiasi kwa njia ya kufadhaika na kutikisa kichwa chake, kisha akageuka na kuondoka sehemu hiyo kurudi ofisini kwake, akiniacha nimesimama kama zoba vile. Mpaka nikaukumbuka wimbo wa Banana Zorro!

Ni kweli kabisa. Nilichokuwa nimefanya ile asubuhi ilikuwa kwenda kule kwenye kampuni ya mzee na kukutana na mwakilishi wake aliyekuwa akishughulikia suala hilo la shamba, ama kiwanja kama wenyewe walivyoliona, na nilitoa pesa zangu mwenyewe kwa ukamili kulipia hiyo fidia waliyokuwa wakihitaji. Kwa kiasi fulani niliwaumiza kwa sababu bado walikuwa wakilihitaji shamba la Mariam, lakini hawakuwa na jinsi ila kuzipokea pesa hizo nilizolipa kwa niaba ya Miryam.

Inaonekana baada ya Miryam kuwa amekwenda huko pia muda fulani leo ndiyo akakutana na hilo badiliko, na ndiyo akapewa na hizo karatasi za kuthibitisha miamala iliyokuwa imefanywa kwa sababu mimi wasingeweza kunipa kutokana na kutokuwa mmiliki moja kwa moja. Angekuja kuletewa yeye kibinafsi baadaye na ingemshtua kama nilivyotarajia, ila kwenda kwake huko leo ndiyo kukawa kumempa huo mshtuko uliofanya aniite hapa ili kunisema; kama kawaida yake. Na sasa suala hilo moja likawa limezua hili lingine. Mapenzi.

Nilijua tu asingenichukulia serious kirahisi namna hii, na pia ukitegemea na nyakati hizi kuwa zenye kumchanganya akili bado, yaani naelewa angeona suala hili kuwa upuuzi mtupu. Nilikuwa nimeshalemewa mno na hizi hisia, hata kama sikutaka kumwambia kwa namna hii lakini kwa njia moja ama nyingine nilijua ningetakiwa tu kumwambia, na maswali yake ya kwa nini na kwa nini ndiyo yakawa yamenilazimu kuropoka.

'Timing' haikuwa sahihi, yaani huu haukuwa wakati sahihi kabisa wa kumfikishia mwanamke huyo hisia zangu. Nilikuwa nimejichanganya kweli, lakini kutokea hapa hakukuwa na jinsi tena ila kukubali kwamba tayari alijua ukweli. Ukweli wangu. Ambacho kingetakiwa kufuata ingekuwa kumfanya atambue ukweli wake yeye pia uliokuwa ndani ya moyo wake, kwa kuwa mimi nilikuwa nimeshauona, ila yeye hakuutambua. Nilikuwa na imani kabisa kwamba bado sikufeli kwa huyu mwanamke, hivyo ningefanya kila kitu kuhakikisha namkamata na kumfanya awe wangu.

Najipiga mara mbili kifuani. JC!

Dah!!!JC🥺🥺🥺fans wake lazma tuwe na majonzi kwa kukataliwa kwake😔
 
Bora kasema ukweli plan A (a) imezingua haijaleta matokeo ninahamu ya planA(b) itakayo leta matokeo am too excited 😊 kumuona JC na miryam wako katika love 💕
 
Usijali mwamba JC huuo demu akilala usiku ataanza kutafakari uliyoyasema atakumbuka namna macho yako yalivyokuwa yanaonyesha dhamira ya kweli.
Kwanza demu mwenyewe anakuelewa sana ila inaonekana alikuwa anajioni hatoshi kwako sasa umelipua amebaki na duwaa.
Soon tutashuhudia MIMI akiliwa na JC
 
Shida ni festo😂😂😂alafu kashaambiwa take care
 
MIMI NA MIMI 2

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Siri, Tamaa, Hila, Usaliti, Ukatili, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KUMI NA TANO

★★★★★★★★★★★★★★★★★

Baada ya Miryam kwenda tu ofisini kwake na kujifungia, nikageuka zangu na kuanza kuondoka hapo ili nirudi tu Mzinga. Ingawa nilikuwa nimetoka kumfunulia mwanamke niliyempenda hisia zangu, bado nilikuwa na mtihani kwake wa kuhakikisha nafaulu kumshawishi azikubali, kwa sababu sikutaka 'hapana' yake moja tu imaanishe ndiyo nimempoteza. Yaani sikuwa tayari kwa ajili ya hilo. Ningefanya kila kitu kuhakikisha Miryam anakubali kwamba ana hisia kwangu pia.

Ingeweza kuonekana kwamba najipa moyo bure tu, lakini hapana, hisia zake kwangu ni kitu ambacho nilihisi pia. Kuna nyakati tulikuwa tunakaa, tunaongea kidogo, tunataniana kidogo, na mara nyingi angeniangalia kwa njia iliyoonyesha hisia nyingi kwangu. Hata maisha yake yalipotishiwa ile juzi, alionekana kujali hali yangu zaidi ya yakwake, kitu ambacho hakingewezekana endapo kama tu angekuwa ananiona kuwa "mdogo" wake wa kawaida. Hayo yalikuwa maneno ya kujihami tu.

Kuna sababu iliyomfanya asitake kukubali kuwa mimi ningeweza kumpenda yeye, huenda akidhani nilitaka tu kumchezea, ama labda aliniona kuwa mdogo mno kwake, bado hakujiona kuwa tayari kuwa na mtu kimahusiano. Kwa vyovyote vile, nilitakiwa kumfungua macho, aachane na mitazamo ya namna hiyo, na aone kwamba upendo wangu kwake ulikuwa wa kweli. Kwa hiyo nisingemwacha, hata kama angesema ama kufanya nini.

Bwana, nikawa nimeamua kupanda bajaji na kuelekea mpaka Zakhem, na baada ya kushuka, nikaendelea kutembea taratibu kuelekea kule kwenye daladala ili nipande tena, na ndiyo nikawa nimepigiwa simu na mama yangu. Nilipenda kuzungumza na mama katika hali tulivu, kwa hiyo sikupokea kwanza shauri ya kuwa barabarani nikipishana na makelele kama yote. Nikaamua kugeuza tena, nikarudi mpaka kwenye mgahawa maridadi wa Zakhem, nami nikatafuta sehemu ya mbele huko na kukaa.

Mhudumu aliponifata, nikamwambia tu aniletee 'milkshake' moja nipoze koo, naye akasepa. Ndiyo nikampigia mama sasa, yaani yeye alikuwa wa kunipigia mara moja, akinikosa, anaacha; labda kama kungekuwa na tatizo kubwa. Kwa hiyo nikampigia zamu hii, na alipopokea tukasalimiana vizuri na yeye kunijulia hali.

"Niko poa tu ma. Jasmine anaendelea vizuri?" nikamuuliza.

"Eeeh. Yupo tu. Ukuje bwana, tumeku-miss," akasema hivyo.

"Nitakuja. Hii hii wiki au ijayo," nikamwambia hivyo.

"Sawa. Nilikupigia kukuuliza kitu. Nasikia eti umetoa... yaani umelipa milioni kumi leo kwenye kampuni, kufidishia hela za mtu fulani aliyekuwa anadaiwa. Ni kweli?" akauliza.

"Mhm... ni mzee amekwambia?"

"Hapana, nina watu wa kunipa taarifa. Na hilo siyo la muhimu..."

"Well... yeah. Ndiyo mama, ni kweli. Nimetoa hiyo fidia," nikamwambia.

"Umetoa milioni hizo zote kwa ajili ya nani J?"

"Ni msichana fulani wa huku. Ni mgonjwa wangu. Nilipokwambiaga kuna mtu namsaidia huku, ndiyo huyo msichana sasa," nikamwambia.

"Mpaka milioni kumi? Ni... anaumwa sana, au? Yaani... Frank alikuwa anamdai hizo hela ndiyo ukaona umtolee?"

"Ni mambo mengi mama. Sijui hata nianzie wapi kuelezea," nikasema hivyo.

"Nieleweshe tu hata kwa ufupi. Napenda tu kujua kwa nini umefanya hivyo, siyo kawaida sana," akaniambia hivyo kwa upole.

Milkshake yangu ikawa imeletwa hatimaye, na mhudumu akasepa.

Nikashusha pumzi kiasi na kusema, "Mama... yaani nimefanya hivyo kiukweli kwa sababu... huyu msichana amenikumbusha mengi ambayo wewe ulipitia. Toka nimeanza kumsaidia, nimemwona kama wewe kabisa... jinsi ulivyoteseka kipindi kile... yaani... ni kama vile yeye tu alivyoteseka sasa...."

"Okay..."

"Sijui ni-delve zaidi ndani kwenye detail..."

"Hapana, Jayden, inatosha. Usijali. Nimekuelewa," akaniambia hivyo kwa upole.

"Yeah, ndiyo hivyo. Ila siyo kwamba namlinganisha na wewe, lakini... yeye na familia yake kwa ujumla... ni watu ambao nimetokea kuwapenda, na kuwajali sana," nikamwambia hivyo.

"Anaitwa nani?" akauliza.

"Mariam," nikamjibu.

"Na, ni mkubwa? Ukisema msichana, ni kwamba ni mwanamke tayari au...."

"Ni mdada, mdogo. Alikuwa na tatizo, matatizo... kwenye ubongo. Matatizo hayo ubongo ndiyo yalimfanya awe kama mtoto, so... nimejitahidi kumsaidia mpaka sasa angalau anaendelea vizuri," nikamwelezea.

"Amepitia hali ngumu?"

"Mno. Kiumri Nuru hajamwacha sana, ila alikuwa na behavior za mtoto mdogo shauri ya hili tatizo tunaita ASD. Ana kaka yake, alikuwa anataka kumwibia yeye na ndugu zake mali zao... hapo juzi akamteka na kupanga kumuua ili afanikiwe kufanya hayo yote. Tulimkuta akiwa karibu sana kubakwa na kuchinjwa mama, na hana kosa lolote kabisa, she's so innocent..." nikamwambia hayo.

Akasema, "Masikini! Ah... pole kwake. Imenigusa sana kujua umetoa msaada kwa mtu namna hiyo yaani, sijui kama Jasmine anaweza kufanya hivyo..."

"Ahah, piga, ua, galagaza..."

"Ahahahah... una moyo mzuri Jayden. Umenifurahisha sana. Basi, mwanzoni nikafikiri labda umetoa na mahali huko bila sisi kujua..." akasema hivyo.

"Ahahah... hapana. Ya mahali lazima mjue, na muda bado," nikamwambia hivyo.

"Sawa. Nimeelewa. Haya, me acha nikuage sasa. Halafu... umepanga kuja lini kabisa?" akauliza.

"Mmm... nimefikiria nije labda Jumapili, au Jumatatu kama Jumapili haitawezekana," nikamwambia hivyo.

"Sawa, ila ndiyo utaniambia kwa uhakika. Vipi ukija naye?" mama akasema hivyo.

"Nini? Nani?" nikamuuliza.

"Huyo Mariam. Ukija, kama utaweza njoo naye nimwone," akaniambia hivyo.

Nikatabasamu kwa hisia na kusema, "Sawa. Nitajitahidi kuja naye."

"Haya. Uwe care huko eh? Tutawasiliana," akaniaga.

"Poa, usisahau kunifinyia shavu la huyo kibonge," nikamwambia hivyo kiutani.

"Hahah... haya sawa."

Hapo ndiyo nikakata simu na kuanza kushusha kinywaji changu taratibu.

Nilifurahia sana hayo maongezi na mama yangu, si unajua jinsi uvutano uliopo kati ya mama na mwana unavyokuwaga wa hali ya juu? Ndivyo ilivyokuwa na huyu mzazi wangu. Sehemu kubwa ya utu wangu mzuri nilikuwa naitoa kwake, na nilipenda sana aliposema kuwa alitaka kumwona Mariam, hivyo ningehitaji kufanikisha hilo kwa kumpeleka binti nyumbani ili ajuane na watu wa familia yangu. Kidogo kidogo tu, ingeanza na Mariam, na hatimaye ingekuja kumfikia bibie Miryam mwenyewe.

★★

Nilipomaliza kinywaji changu, tayari usiku ulikuwa umeshaingia, na baada ya kulipa ndiyo nikaondoka kuelekea Mzinga. Katika hali yangu ya kuwa na mawazo mengi, nikawa nimeamua kufanya zoezi la kutembea mpaka Mzinga badala ya kupanda usafiri, maana sikuhisi uhitaji wa kuingia gym leo. Nigepumzika kidogo. Kwa hiyo taratibu tu nikajongea kutoka hayo maeneo ya Rangi Tatu mpaka nikafika Mzinga ikiwa imeshaingia saa mbili usiku, nami nikaelekea makwetu moja kwa moja.

Nilipofika upande wa nje wa nyumba yake Ankia, nikaweza kuona familia ya Miryam ikiwa imekaa pale varandani, yaani wote walikuwa nje, nami nikaamua kwenda kuwasalimia tena kabla sijarudi huku kuoga. Nilipoingia hapo getini kwao, gari la bibie lilikuwemo, na Miryam mwenyewe alikuwa pamoja na familia yake hapo nje. Alikuwa amesharudi. Ni yeye pekee na Tesha ndiyo waliokuwa wamekaa kwenye viti, huku wakina Bi Zawadi, Bi Jamila, Mariam, pamoja na Shadya, wakiwa wamekaa mkekani kwenye uvaranda.

Mariam kama kawaida yake akanyanyuka na kuja kukutana nami ili kunikumbatia, nami sikumnyima hilo. Nilipomwangalia Miryam, alikuwa ameketi kitini huku akiwa makini kweli na simu yake, kama mtu asiyejali ujio wa mgeni yaani, na nilielewa kwangu mimi ingekuwa namna hiyo kutokea hapa na kuelekea mbele. Alikuwa amevaa dera zuri sana la njano mwenyewe, Mariam akiwa amevaa dera pia, nami nikasogea mpaka hapo varandani pamoja na binti na kusalimiana na wengine pia.

Tesha akataka anipishe ili niketi kitini, lakini nikamwambia hakukuwa na uhitaji kwa sababu nilitaka kwenda kujisafisha mwili kwanza, kwa hiyo yeye akae tu. Nilisemeshana na wengine kwa njia ya uchangamfu sana, lakini Miryam alionekana kutotaka kujihusisha na hayo maongezi kabisa. Hakutaka kabisa mazoea na mimi tena. Nilikuwa namwangalia mara kwa mara, yeye asiniangalie hata mara moja, kisha akanyanyuka na kuelekea ndani.

Nikawekwa wazi kwamba Miryam alikuwa anawarekebishia wengine msosi huko ndani, wakisema aliwahi kurudi hiyo jioni, na mimi nikaona niwaage sasa ili niende tu pale kwa Ankia kuuweka mwili sawa. Lakini kabla sijaondoka, bibie Miryam akawa ametokezea hapo mlangoni na kusimama, naye akanitazama usoni moja kwa moja.

Alionekana kuwa makini tu, naye akasema, "Njoo mara moja."

Alikuwa ananiambia mimi hivyo. Kabla hata sijaongea lolote, akarudi ndani, na kiukweli alifanya mapigo yangu ya moyo yakimbie kwa kasi kiasi kwa sababu ya kutojua la kutarajia litokee huko. Alikuwa ananiitia nini huyo? Siyo 'kumchum kumchum' kweli? Nikajitahidi tu kuonyesha niko kawaida, nami nikawaacha wengine hapo na kuingia sebuleni.

Hakuwepo hapo sebuleni, lakini nikaweza kumwona upande wa kule jikoni akiwa kama amesimama usawa wa jiko lao la umeme/gesi anakoroga mambo. Kisha, akafanya kama kuja huku, lakini akaishia hapo kwenye ukuta uliotenganisha sebule na upande huo, na alisimama huku akiniangalia kwa macho makini. Ikawa wazi kuwa alitaka nimfate, labda tuongee bila wengine kuweza kusikia, nami nikajituliza tu kihisia na kumsogelea.

Akarudi nyuma kidogo ili ukuta huo utufiche kiasi, yaani kama vile alikuwa anataka tunong'onezane sijui? Na kiukweli nilikuwa na misisimko ya hali ya juu. Nikasimama mbele yake huku nikimwangalia kwa utulivu, naye akanyanyua mkono wake mmoja juu kiasi. Nikaona ulikuwa umeshika bahasha ndogo iliyokunjwa, nami nikamtazama machoni tena.

Akiwa bado ameinyanyua bahasha hiyo, akasema kwa sauti ya chini, "Hii hapa... milioni tano na laki nane. Natanguliza, nyingine inayobaki nitamalizia. Shika."

Nikabaki nikimtazama machoni kama vile sikuwa nimemwelewa.

Akakichukua kiganja changu na kujaribu kulazimisha kunishikisha hiyo bahasha, lakini nikagoma na kuutoa mkono wangu kwake kwa nguvu. Akanitazama usoni kimaswali, na kwa njia ya kuudhika.

"Unaanza tena kurudi kule kule ulikotoka Miryam," nikamwambia hivyo kwa sauti ya chini.

"Nini?" akauliza.

"Kale kakiburi kako kale... umeanza kukarudisha tena, kisa tu hutaki kukubaliana na nilichosema leo..." nikamwambia hivyo kwa utulivu.

"Sitaki kukubaliana na lolote wala kusikiliza mahubiri yako kwa...."

"Si kwa sababu unajua ni kweli?" nikamkatisha.

Akatulia na kuendelea kunitazama, eti kwa hasira.

"Ni part ipi ya maneno 'sihitaji unilipe' ambayo huelewi, hm?" nikamuuliza hivyo.

"Sijali maneno yako. Nairudisha pesa yote uliyotoa, kwa sababu...."

"Kwa sababu hutaki kuwa na deni kwangu? Ahah... Miryam, hata ufanye nini, huwezi kulipia deni ulilonalo kwangu kwa pesa," nikamwambia hivyo.

Akakunja uso wake kimaswali kiasi.

"Unajifanya hujui?" nikamuuliza.

Akaendelea kunikazia macho.

"Hizo pesa zimeshaenda, Miryam. Deni ulilonalo wewe kwangu, halihusiani kwa vyovyote na hizo hela. Ninachokudai wewe... ni kukiri kwamba unanipenda pia," nikamwambia hivyo kwa ujasiri.

Akaniangalia kama vile mimi ni mtu niliyechanganyikiwa, na kwa sauti ya chini akasema, "Una wazimu wewe!"

"Yeah. Nina wazimu juu yako," nikasema hivyo.

Akasonya kidogo na kutazama pembeni.

Nikatabasamu kiasi na kumwambia, "Najua kuna sehemu ya moyo wako inayoelewa kwamba huo ni ukweli. Najua unanipenda Miryam."

Akaniangalia kiukali na kusema, "Mimi? Mimi nakupenda wewe?!"

"Ndiyo. Ila bado tu hujatambua hilo," nikasema hivyo.

Akaonekana kutaka kusema kitu fulani kwa hasira, lakini akajizuia. Sijui alikuwa anataka kunitukana?

Kwa sauti tulivu, nikamwambia, "Nimegundua kwamba kukufanya utambue hilo ndiyo itakuwa challenge. Ila kwangu mimi. Nilikuwa nimeshaona upendo wako kwangu Miryam, lakini kwa sababu ya haya matatizo na nini... najua ulikuwa umefunikwa mbali sana kutoka kwenye macho yako, ndiyo sababu mpaka sasa hivi wewe hujauona bado. Lakini upo. Mie nimeshauona kwa upande wangu, na we' nitakusaidia uuone pia."

Alikuwa akiniangalia kwa hisia kali yaani, huku mimi nikimtazama kwa yale macho yangu mazuri, naye akasema, "Unajua... nilikuwa nimeanza kufikiri uko sensible, lakini... yaani... bado sana. Unanifanya natamani hata nikuwashe kofi!"

"Oh, please do!" nikamwambia hivyo na kumsogelea zaidi.

Akarudi nyuma kidogo huku akinitazama kimshangao kiasi.

"Sikukwambiaga kipindi kile uliponizibua, ila kofi lako liliacha mark nzuri sana kwangu. Siyo kwenye shavu... moyoni. Ama hujui? Kofi la mpenzi haliumi, ni tamu," nikamwambia hivyo kiuchokozi.

Midomo yake ikatetemeka kiasi huku akiibana kwa njia iliyoonyesha hasira, kisha kwa kunong'oneza akasema kwa ukali, "Mjinga wewe!"

Akanipita upesi na kuanza kuelekea upande wa chumba chake haraka-haraka, akionekana kukasirika mno, nami nikajikuta natabasamu tu na kushusha pumzi kujipa utulivu.

Huu mchezo haungekwenda kiulaini sana mwanzoni, najua, lakini nilijua pia kwamba ungefika tu muda ambao mwanamke huyo angelainika. Alama zote zilizoonyesha kwamba alikuwa ana hisia kwangu nilikuwa nimeshaziona huko nyuma, hata sasa zilikuwepo, kwa hiyo kazi ambayo ingebaki ingetakiwa kuwa kumfanya akiri kwamba alinipenda pia. Na ungekuwa mtihani.

Nikaamua tu kujiondokea hapo mapema kabla hajatoka na panga huko chumbani, nami nikawaaga wengine na kusema kama ningeweza basi hata baadaye ningekuja tena. Ndiyo nikaelekea kwa Ankia na kuoga, mwenye nyumba wangu huyo akiwa ndani tayari, kisha nikakaa pamoja naye sebuleni ili tupatane kwa mambo ya hapa na pale kabla ya mengine kufuata.

Inaonekana Ankia tayari alikuwa ameshatongozwa na Bobo, maana simu haikumshuka kiganjani kwa muda mrefu sana, akitabasamu-tabasamu na kuniangalia kwa sura yenye madaha. Nikamtania kwamba inawezekana siku si nyingi angenitambulisha kwa 'sugar daddy' wake mpya, naye akakataa kwa kusema eti alikuwa akichat na rafiki na kuangalia utani fulani huko Facebook.

Haya bwana, mimi nikatulia tu, lakini hakujua kwamba nilikuwa nafurahi sana kwa ajili yake, kuona jinsi ambavyo aliburudishwa na Bobo. Kidogo kidogo tu hivyo hivyo ningekuja kushtukia jamaa analetwa hapa kama faza hausi! Nikiwa nimeketi sofani bado pamoja naye, nikawa nimetumiwa ujumbe ulionifanya niwe makini zaidi. Ulitoka kwa askari Ramadhan, akiwa amenitumia maneno rahisi yaliyokuwa yamebeba maana nzito sana.

'Shukran kwa jitihada JC, Sodoma na Gomora zinaanguka. Kufikia asubuhi, kazi kwisha.'

Hiyo ilimaanisha kwamba sasa wakati ambao nilikuwa nimetazamia ufike ulikuwa umewadia, lakini ujumbe wake haukunipa hisia yoyote ya uchangamfu, bali nikahisi wasiwasi tena. Wasiwasi tu. Ikanibidi niende chumbani, nami nikampigia Ramadhan kwa namba yake ile ya siri, na uzuri akapokea.

Nikamwomba anipe ruhusa ya kufanya jambo fulani mapema sana ya kesho, na mwanzoni aliona ombi langu kuwa la kipuuzi na lisilofaa, lakini nikamshawishi aniruhusu tu, na mambo yangekwenda sawa. Akawa amenikubalia hatimaye kwa kusema ningefanya nilichotaka lakini kwa kufuata mwongozo wake, nami nikakubali hilo, kisha ndiyo akakata simu. Nikaamua kuahirisha kwenda kwake Miryam tena ili niweze kupumzika mapema, nami nikawahi kupanda kitandani huku nikiwaza mengi mazito mno ambayo yangetokea kwa siku ya kesho.

★★★

Asubuhi na mapema sana nikawa nimeamka, moja kwa moja nikaanza kujiandaa upesi ili niweze kuondoka. Yaani niliamka saa kumi na mbili leo, nikaoga, nikavaa, huyoo nikaondoka upesi. Safari ilikuwa ni moja tu; kwa madam Bertha. Kutokana na jambo aliloniambia askari Ramadhan jana, nilitaka tu kumwona huyo mwanamke, yaani... nimwone tu. Kisha mengine ambayo yangefuata, yangefuata.

Labda tuseme ni moyo ndiyo uliokuwa ukiniongoza kufanya hivi, maana akili yangu ilielewa vizuri kabisa kwamba sikutakiwa kufanya hivi. Kwa yale ambayo askari Ramadhan na watu wao wote wangehusika kufanya leo, najua nilipaswa kukaa mbali, lakini bado ni moyo tu ndiyo ukawa unanisukuma kutaka kuwa huko kwa huyo mwanamke kabla ya yaliyokuwa yakimjia kumfikia. Mtu hata angeweza kuniambia nina akili sita, na kwa wakati huu ningekubaliana na hilo na kumwambia sijali. Huu ndiyo ulikuwa uamuzi wangu.

Nikachukua usafiri kwenda Makumbusho moja kwa moja, nami nikafika huko Mkwajuni Vunja Bei ikiwa imeshaingia mida ya saa tatu asubuhi. Nilikuwa nimevaa kwa njia makini tu, na nilipoekekea huko hotelini nilitambua kwamba kulikuwa na mazingira fulani ya "utayari" yaliyokuwa yameshawekwa kuizunguka hoteli hiyo, kwa hiyo ni mimi tu ndiye niliyetakiwa kwenda huko juu, kumwona madam, kisha baada ya kumaliza biashara yangu nitoke ili kuyaacha hayo mazingira yafanye kazi yake. Ndiyo mwongozo wa kufata niliokuwa nimepewa na Ramadhan. Najua inaeleweka.

Nikapanda mpaka ghorofani huko, moja mbili tatu mpaka mlangoni kwa madam, nami nikagonga hodi na kungoja. Dakika kama mbili hivi zikapita, ndiyo mlango ukawa umefunguliwa, na hapo mbele yangu akawa amesimama madam Bertha mwenyewe. Alionekana makini kweli usoni kwa jinsi alivyokuwa akinitazama.

"JC?"

Akauliza hivyo kwa kuonekana kutotarajia iwe mimi niliyefika hapo kwa asubuhi hii. Alikuwa ndani ya ki-T-shirt chepesi cheupe, ambacho kilikuwa kifupi mno kuonyesha kitovu chake, na alivalia suruali ya michezo, pana kama zile za wahindi. Yaani alionekana kama dancer. Sijui kwa nini, lakini mkono wake mmoja ulikuwa nyuma ya kiuno chake kama vile ameficha kitu. Nikaendelea kumwangalia usoni.

Akauliza, "Unafanya nini hapa asubuhi yote hii?"

Nikiwa namtazama kwa utulivu tu, nikasema, "Nilitaka kukuona."

"Haujawahi kuniona?" akauliza hivyo.

"Kuwa pamoja nawe kabisa," nikamwambia hivyo kistaarabu.

Akaangalia pembeni na kutabasamu kiasi, kisha akasema, "We' umeamka nazo leo, eti? Na kazi je?"

Nikaendelea tu kumwangalia usoni kwa utulivu.

Akasonya kidogo kimasihara na kusema, "Hebu ingia huko."

Yaani hakuwa na habari!

Akarudi ndani, nami nikaingia pia na kufunga mlango. Sasa ndiyo nikaweza kuona kwamba kwenye mkono aliokuwa ameukunjia mgongoni alishikilia bastola, na nikaitambua kuwa ile bastola ambayo Festo alikuwa amenipa, ikionekana Dotto alimletea huku baada ya mauaji ya wakina Sudi, nami nikasimama kwanza na kumtazama tu mpaka alipogeuka na kuniangalia tena.

Akainyanyua hewani bastola hiyo na kusema, "Sipendi wageni wasio rasmi. Muhimu kuwa careful."

Nikatikisa kichwa kuonyesha uelewa.

Akaishusha bastola na kusema, "Haka ka Taurus kazuri. Festus alikuuzia, au alikupa kishkaji tu?"

"Ali... alinigei tu," nikasema hivyo kwa sauti ya chini.

Akanitazama kwa udadisi kiasi, naye akauliza, "Mbona uko hivyo? Kuna tatizo?"

Nikatikisa kichwa kukanusha na kusema, "Niko poa. Kwa hiyo kama isingekuwa mimi na ni mtu usiyemjua, ungem-shoot tu?"

"Eeh, anakula chuma! Unafikiri naogopa visheria-sheria vya kipuuzi vya hoteli? Naweza tu kusema nilivamiwa, na nina haki ya kujilinda," akaniambia hivyo.

"Na haki ya kumiliki gun?"

"Ninayo. We' unanionaje?"

Nikanyoosha viganja juu kiasi kama kumwambia nimeshindwa.

Akasema, "Kaa hapo basi, tena ni vizuri Kantala wangu umejileta ili tuongee."

Nikajipeleka tu mpaka sofani na kukaa, naye akaiweka bastola yake juu ya droo la kitanda na kuja upande wangu.

"Nilikuwa na mpango wa kwenda Mbezi. Kuna spa fulani kule nzuri kichizi, nilikuwa nataka kung'arisha hii ngozi. Ishaanza kufanana na ya Zuchu," akasema hivyo.

Nikatabasamu kiasi na kumwangalia hadi alipofikia sofani na kukaa karibu yangu pia.

"Kama vipi twende wote," akaniambia hivyo.

"Unataka kwenda saa ngapi?"

"Sa'hivi."

"Asubuhi yote hii?"

"Yeah, asubuhi ndo' raha. Na tena... nimechelewa. Yaani hapa nitafika huko saa sita kabisa."

"Si bora tu uahirishe sasa?"

"A-ah, nimekwambia sina undugu na Zuchu..."

"Ahah... lakini si unapenda asubuhi? Ahirisha leo... utaenda siku nyingine..."

"Lini?" akauliza hivyo.

Nikatazama pembeni tu kwa utulivu. Swali lake likanifanya nijihisi vibaya moyoni.

Akaonekana kunitathmini kidogo, kisha akasema, "Hivi wewe... ni nini kwanza kimekuleta hapa... hm? Maana hadi umeanza kunizuia nisiende kupata some quality time kabisa. Nini kinakusumbua? Unataka mnyanduo, au.. unahofia kwa sababu naenda kufinywa-finywa kidogo na wanaume wenye mamisuli na nini eh... wanipakate-pakate kidogo, na madude yao makubwa-makubwa wayatelezeshe hapa weee... siyo kama hicho kiandunje chako?"

Nikajikuta natabasamu kwa furaha, utani wake ukiwa unamfanya apendeze kwa kiwango fulani machoni mwangu, nami nikamwangalia usoni kwa hisia.

"Ahahah... au uwongo?" akaniuliza hivyo.

"Ni kweli. Nahofia hicho," nikamwambia hivyo.

"Sa' si ndiyo maana nimekwambia twende wote? Au unafikiri me niko easy sana nitawaruhusu wanichezee tu?" akauliza.

"Hapana. Najua uko na msimamo," nikamwambia.

"Sasa je! Acha kufeli," akasema hivyo.

Nikatabasamu kiasi.

"Halafu kweli. Nilikuwa nataka nikwambie, ile hoteli ya kule Buza imepata mteja, kuna mtu ameinunua," akaniambia hivyo.

"Mh? Juzi tu mpaka leo tayari umeshaiuza?"

"Eeh. Hata hivyo, nilikuwa nimeshaiweka sokoni muda... na nimeiuza cheap tu. Nilikuwa nataka nikwambie mapema ili usijisikie vibaya, nimeiuza zawadi yako... lakini Masai ipo..."

"Ahah... hamna shida, me... hata hiyo siihitaji. Lakini... hizo pesa unafanyia nini sasa?"

Akatabasamu na kusema, "Unazitaka eti? Niambie kama unataka nikupe."

"Hamna, hiyo siyo maana yangu. Naona unakusanya pesa nyingi, umeshanunua na gari, nime... nimehisi kuna mabadiliko unataka... unataka kufanya," nikamwambia hivyo.

"Yeah. Haujakosea. Nafikiri sasa hivi natakiwa kuanza... au niseme, niendelee kusonga, lakini upya. Nataka niache kukaa hapa, nirudi kwenye nyumba yangu... hasa sasa hivi kwa sababu Chaz amekufa, na nataka niifanyie renovation kubwa sana. Iwe kama nimeijenga upya. Nataka... nifungue hoteli na club nyingine ya maana... hoteli kubwa three, au four, au five stars ikiwezekana. Ahah... five stars nimefikiria mbali sana, ila... nataka iwe kama fresh start..." akaongea hivyo kwa uhakika.

Nikabaki nikimtazama machoni kwa utulivu tu.

Akanishika mkono na kuniambia, "Tena... nataka iwe ni fresh start nikiwa pamoja na wewe, JC."

Dah!

Nikaangalia pembeni tu, yaani nikiwa nazidi kujihisi vibaya mno moyoni.

"Hey, usifikiri nina-bug hapa. I mean it. Sawa sitakuwa malaika na nini, lakini JC... nataka sasa hivi... moving forward, iwe ni mimi na...."

"Basi, Bertha... usiseme hivyo," nikamkatisha.

Akaniangalia kimaswali kiasi, nami nikamtazama usoni kwa umakini.

"Bertha... hhh... najua, najua unajitahidi lakini, na naona kuna sehemu kubwa ndani ya moyo wako imeridhia kuwa na mimi, ila... siyo mimi ninaye...." nikajikuta nashindwa kuendelea.

"Nini? Unataka kusema nini?" akauliza.

Nikashusha pumzi tu kwa kufadhaika.

"Kwamba hautaki kuwa sehemu ya mpango wangu moving forward?" akauliza hivyo.

Nikamwangalia usoni kwa utulivu.

"Oh, shida ni nini JC? Kwa sababu nimeiuza hiyo hoteli? Ahah... please, ilikuwa imeshazeeka hata hivyo...."

"Sijamaanisha hivyo Bertha..."

"Sasa tatizo ni nini? Bado tu unasumbuliwa na kilichowapata wakina Sudi? Ndiyo hivyo?" akauliza.

Nikainamisha tu uso wangu.

"Oh JC... ulinifata wewe mwenyewe, ukaniambia unanipenda huku ukijua nature yangu, na bado ukataka tuwe sote through all of this, mpaka sasa... shida ni nini sasa hivi? Kinachokupa was...."

Maneno yake Bertha yakakatishwa baada ya simu yake iliyokuwa mezani kuanza kuita, naye akatikisa kichwa kidogo na kuichukua upesi.

Akaangalia mpigaji na kuniambia, "Kinachokupa wasiwasi ni nini wewe... eh? Nilikwambia be a man, be a man bwana. Ah..."

Alikuwa akimalizia maneno yake kwangu, kisha ndiyo akapokea simu yake. Nikawa namtazama tu kwa utulivu mpaka alipoiweka sikioni kumsikiliza mpigaji, na uso wake ukaonyesha jambo nililokuwa nimetarajia upesi sana. Alishtuka.

"Nini?!"

Neno hilo pekee likamtoka midomoni mwake baada ya kuonekana kuwa amesikia jambo fulani baya na lenye kushangaza mno, naye akanitazama usoni kwa macho yaliyoonyesha hofu kubwa. Nikashindwa hata kuigiza yaani na kuendelea kumwangalia tu kwa hisia za huzuni, naye ghafla akasimama na kuirusha simu yake kwa nguvu hadi ilipopiga ukuta na kuvunjika-vunjika!

"Aaaaah!" akapiga kelele kwa hasira na kujishika kichwani kwa viganja vyake vyote.

Nikasimama pia na kumuuliza, "Nini madam? Nini... nini kimetokea?"

Akawa anatembea mbele na nyuma huku akipumua kwa uzito, naye akasema, "Wameharibu, JC! Wameharibu kila kitu!"

Nikaangalia pembeni kwanza, hapo tayari nikiwa naelewa vizuri kilichokuwa kimetokea, nami nikamuuliza, "Huyo alikuwa nani?"

"Msambazaji wangu mmoja! Hapo amenipigia... anakimbia... anasema maaskari wame-seize majengo yetu YOTE ya biashara! How the hell did this happen?!" akaongea hivyo kwa presha.

Nikaendelea kutulia huku nikikunja ngumi kuzuia hisia zangu.

"No... no, no, no... huyu mpumbavu atakuwa amekosea. F(...)! Naomba simu yako JC. Give me your f(......) phone!" akanifokea kama amechizi vile.

Hili itikio nilikuwa nimelitarajia. Nikaitoa simu mfukoni na kumpatia baada ya kutoa lock, naye akaonekana kutafuta namba ya mtu na kupiga.

"Dotto pokea... pokea Dotto... uko wapi?"

Akaongea hivyo na kisha kutulia, halafu akakaza macho yake kwa nguvu na kushusha mkono wake. Nikamnyang'anya simu yangu kabla na yenyewe hajaitupa!

"Vipi madam? Dotto hapatikani?" nikamuuliza hivyo.

"Hapokei. JC, kama kweli maaskari wamefanya round up kote kukamata biashara zangu, inamaanisha wana... damn! Wame.... kila jengo!" akasema hivyo kwa hisia kali.

Nikaangalia tu chini kwa utulivu.

"Ahh... hhahh... how the hell did this.... Dotto atakuwa wapi? Ama na yeye utaniambia.... na yeye... wanamkimbiza, kila... wanaweza ku.... mpigie Festus JC, now! Mpigie haraka..." akaongea kwa kubabaika na uharakishi.

Akatoka hapo alipokuwa amesimama na kuelekea kwenye kabati la nguo, naye akafunua mlango mdogo humo humo ndani na hapo nikaona sanduku la kielektroni la kutunza, ama kufichia vitu. Nikaendelea kumtazama kwa umakini hadi alipobonyeza namba za kulifungulia (nywila), kisha akafungua kimlango chake na kuanza kutoa mabunda ya pesa nyingi sana, akiyarushia kitandani kwa kasi mpaka alipomaliza yote.

Akachukua mkoba mkubwa na mtupu kutoka kwenye stendi pembeni na kukielekea kitanda, naye akaanza kuziweka pesa hizo mkobani huku akisema, "Kama wameweza kufikia sehemu zangu, sehemu zetu zote kwa mkupuo, na kuwakimbiza wajeshi wangu wote, basi watakuwa wamezinusa na kuzifata biashara za wengine pia. Ni lazima kuwe na leak. Ni lazima! Kuna mtu ametu-snitch... this is impossible, haiwezekani... everything was done so carefully, I can't...."

Alikuwa anaongea haraka-haraka kama vile amepagawishwa na madawa ya kulevya, naye akanigeukia kukuta bado nimesimama tu huku nikimtazama.

"Acha kuzubaa JC! Pick something up, mpigie Festus haraka! We have to get out of here! Hao washenzi wanaweza wakawa wanakuja na hapa, tunapaswa tuondoke ASAP...."

Alikuwa ameshamaliza kuzirundika pesa zote kwenye mkoba, naye akavua ki-T-shirt chake na kukirusha huko, kisha akachukua T-shirt jeusi la mikono mirefu na kulivaa upesi, halafu akaivua na hiyo suruali yake na kuanza kuvaa nyingine tena; ile ile ngumu ya leather yenye kung'aa aliyokuwa amevaa juzi alipomuua mume wake.

"Haiwezekani! Haiwezekani kabisa! Haiwezi kuwa mistake, haiwezi kuwa wameotea tu, eti sehemu zote kwa mpigo mmoja, wamewezaje... wamewezaje kufanya hivyo? Ah, ku(.......)! Just when everything was going so perfectly... JC, tuondoke haraka. Chukua funguo zangu za gari hapo. Harakisha!" akaongea kwa msisitizo.

Nikabaki nikimtazama kwa hisia sana.

"What are you doing?! Unafikiri nakutania? Kila kitu kimeharibika! Hatupaswi kuendelea kuwa hapa, kuna mtu ameni-snitch, JC! Harakisha, mpigie na Festus, tuku...."

Akaishia hapo ghafla.

Alikuwa ameinama tena kuelekea shelfu lililokuwa limebebea viatu, bila shaka akitaka kuchukua viatu avae, naye akatulia kidogo kama vile kuonyesha utambuzi wa jambo fulani ulikuwa umemwingia kichwani. Akasimama wima na kuniangalia usoni kwa umakini sana, mimi bado nikiwa namtazama kwa hisia, naye akashusha pumzi kwa njia fulani kama mtu aliyechoka sana.

"Kwa nini haumpigii Festus?" akaniuliza hivyo kwa sauti ya chini.

Nikaangalia pembeni na kubaki kimya tu.

"JC? Hey... mbona hunijibu?" akauliza tena.

Machozi yakaanza kunilenga kabisa, nami nikainamisha uso wangu tu.

"Ahh... JC! JC umefanya nini?" akauliza hivyo kwa sauti yenye kunong'oneza.

Nikajikaza tu kihisia na kumtazama usoni kwa umakini.

Akaninyooshea kidole chake na kusema, "Wewe... wewe ndiyo umefanya hivi? Kwa nini? Huh? Ume... umeni-umenisnichia kwa mapolisi, JC?"

"Bertha..."

"Yaani... una... oh f(...)!" akasema hivyo na kujishika kichwani.

Nikashusha pumzi tu na kuiweka simu mfukoni, nikiwa nataka nimsemeshe tena.

"Yaani kumbe umekuja hapa, to keep me occupied... unizubaishe... ili... na penyewe waje kunisomba? Eh?" akauliza hivyo.

"Sikia Bertha. Kila kitu kimeenda, siyo kwa jinsi nilivyofikiria kingeenda, ni... mambo mengi, lakini... yaani, sijui hata nikwambieje ila...."

Nikiwa naisaka namna ya kumwelezea, nikaona anatazama pale kwenye droo ya kitanda upesi, nami nikaangalia hapo na kuona kwamba aliiangalia bastola yake. Tukaangaliana tena kwa umakini, naye Bertha akakaza macho yake kwa njia iliyoonyesha hasira zaidi, na ule mjongeo wa mbali wa mwili wake wa kutaka kuelekea upande huo ukanifanya nitambue kwamba alidhamiria kuifata bastola yake ili anifundishe adabu.

Na kweli akageukia huko tena na kuonyesha nia ya kuifata bastola hiyo kwa kuanza kukimbia, nami hapo hapo nikaliruka sofa kwa kasi na kukutana naye wakati ambao tayari alikuwa ameshaikamata bastola yake na kujaribu kuigeuzia kwangu ili anitandike risasi. Nikaiwahi mikono yake na kuupamia mwili wake kwa nguvu kiasi, nasi tukadondokea kitandani huku nikiwa juu yake, na nikiikaza mikono yake ili bastola isigeukie kwangu.

"Bertha, subiri... acha..." nikawa najaribu kumzuia.

"Una(......) wewe! Niachie, mpumbavu, msenge wewe! Unanisaliti mimi?!" akaongea kwa uchungu sana.

"Bertha, nisikilize... please..."

"Niachie, nikuonyeshe, mpumbavu... aahh..."

Alikuwa anajaribu kufurukuta kwa nguvu zake zote, na mimi nikaendelea kumkandamiza ili nipate nafasi moja tu ya kuuachia mkono wake mmoja na kuikamata bastola upesi, na nilipofanya hivyo, ikampa mwanya kiasi wa kukaza zaidi viganja vya mikono yake, hivyo akawa amesababisha risasi moja ifyatuke. We! Hiyo kelele!

Risasi ilikuwa imetandika ukuta na kuacha tobo, na najua sauti iliyokuwa imetoa ingeshtua wengi hotelini hapo. Niliumia kiasi masikioni kutokana na hiyo sauti na kushindwa kuendelea kumkaza zaidi, na hiyo ikampa nafasi ya kujigeuza kidogo na kurusha mguu wake chini yangu. Hapo akawa amenipiga sehemu ya siri na kunifanya niishiwe nguvu zaidi, nami nikalegea na kudondokea chini huku nikihisi maumivu kwenye viungo vya uzazi.

Bertha akajitoa kitandani upesi na kushuka chini, naye akasogea mpaka usawa wa lile sofa huku akiielekeza bastola yake upande wangu. Nilikuwa chini bado huku nikimtazama usoni kwa huzuni, yeye akiwa ananiangalia kwa hasira sana na kupumua kwake kukiwa kwa presha yaani utafikiri alikuwa anataka kupasuka. Dah!

Najua alikuwa na hasira, siyo kwamba kwa sababu angekuwa amepoteza huu mchezo, ila kwa kuwa aliyesababisha aupoteze ilikuwa ni mimi. Najua Bertha alikuwa ananipenda, na ni jambo hilo ndiyo lililofanya akasirike zaidi kwa sababu nilimuumiza moyoni kabisa. Yaani kabisa, toka mwanzo, hakufikiria kwamba mimi ndiyo ningekuwa msaliti wake, hata alikuwa tayari kuondoka na kukimbia pamoja nami, lakini sasa akaona wazi kuwa alishindwa kotekote kabisa. Na ni hilo ndiyo lilinifanya nijione kuwa mbaya yaani.

Nikajitahidi kusimama taratibu, huku bado nikijishika usawa wa kiuno kutokana na kuhisi maumivu, nami nikaendelea kumwangalia usoni kwa huzuni sana kutokana jinsi ambavyo aliniangalia kwa zile hasira zilizomfanya alengwe na machozi na pumzi zake kutetemeka sana. Katika wakati kama huu, ikiwa ingekuwa chini ya hali nyingine, labda kama ingekuwa ni mtu mwingine ndiyo kanishikia bastola namna hiyo, huenda ningetetemeka, lakini hapa, sikuwa na wazo la kuhofia kabisa juu ya maisha yangu.

Yaani, kwa lolote ambalo lingetokea, nilikuwa tayari kuacha litokee, na sikujua tu kwa nini ilikuwa namna hiyo. Nilimwangalia Bertha machoni na kuona namna alivyokuwa akihisi uchungu, na kwa njia fulani ikawa kama vile anaushiriki pamoja nami. Mpaka nikawa nahisi kama vile mimi ndiyo mtenda dhambi kwenye hiki kisa. Nilihisi kama vile nimemwonea yaani.

Nikaangalia chini kwa huzuni sana, kisha nikamwangalia usoni tena na kumwambia, "I'm sorry..."

Sikuwa na lingine la kumwambia.

Uso wake ukakunjamana zaidi, akionekana kupandisha hasira zaidi na zaidi huku akikaza bastola viganjani kunielekea kwa nia kuu ya kutaka kufyatua risasi, nami nikaendelea tu kumwangalia usoni kwa hisia sana mpaka machozi yakajaa machoni kwa huzuni kuu niliyohisi kutokana na kuuona uchungu wake.

Akakaza na meno yake akiwa anataka, na anataka kunipasua kichwa kwa usaliti niliokuwa nimemfanyia, nami nikafumba macho yangu taratibu nikiwa naelewa kuwa huu ndiyo ungekuwa mwisho! Nini kingeniokoa kutoka kwenye hasira ya huyu mwanamke?

★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★
 
Kaka heshima kwako, unajitahid sana kutupia kila siku na leo tafadhari kiongoz
 
hongera JC
 
Dah MAPENZI KONYO
 
Back
Top Bottom