Simulizi: Mimi na Mimi

Simulizi: Mimi na Mimi

Sijui kwann kama namchukia hivi Mimi
JC nae kilaza sana si amwache apambane na shida zake
Mpenz njoo basi tuwekee moja
 
MIMI NA MIMI

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Tamaa, Hila, Usaliti, Siri, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!


★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE

★★★★★★★★★★★★★★★★★


Nikamwangalia Miryam usoni na kuona jinsi ambavyo aliniangalia kwa hasira sana, na ni hapa ndiyo nikawa nimeweza kumwona Mariam pia, akiwa amesimama karibu na kaka yake huku wote wakinitazama kwa kuchanganywa na yaliyotokea hapo. Bi Zawadi alikuwa ameweka kiganja chake kwenye mdomo wake huku akiniangalia kwa kutoamini, na Bi Jamila alinitazama kwa mshangao sana pia.

Nikajipa utulivu tu, nami nikamwambia Miryam, "Sawa. Nimekuelewa. Sitajihusisha tena kwa lolote lile ambalo halinihusu. Sipendi yeyote kati ya hawa aumie. Ila... watakapoumia safari hii Miryam... ujue itakuwa ni juu yako."

Nilimalizia maneno hayo ya mwisho nikiwa nimemnyooshea kidole mwanamke huyo, naye akanikazia macho yake hata zaidi. Sikusubiri lingine tena. Nikatoka hapo kibarazani na kuvaa malapa yangu miguuni, nisiweze kuwaangalia wengine baada ya hicho kilichotokea.

"JC baba..." Bi Jamila akaniita kwa upole.

Sikuitika wala kumwangalia, nami nikaanza kuondoka hapo.

Nikamsikia Tesha akisema, "Da' Mimi... ndiyo nini haya? Mmefanyaje, mbona sielewi...."

Najua maongezi kwenye hiyo familia kuhusu hilo suala yangeendelea tu baada ya mimi kuwa nimewaacha, na nilikuwa nimejawa na hasira moyoni kutokana na kuharibikiwa na moja kati ya mambo yaliyokuwa yananipa nguvu sana. Kosa tu Miryam kukutana na Bertha ndiyo likawa limesababisha haya kutokea.

Nikaingia ndani kwa Ankia na kuwakuta mashosti zake wakiwa wanakula, huku Ankia akitazama tu TV. Niliwapita bila kusema lolote, na nadhani Ankia aliona kwamba nilikuwa nimeudhika. Nikaingia chumbani na kukaa kitandani, nami nikawa najaribu kuisawazisha akili yangu ili ipate utulivu, lakini nikashindwa.

Nikaamua kubadili mavazi na kuvaa nguo nyepesi, kisha nikaanza kufanya mazoezi ya kuchangamsha mwili ili akili yangu ipotezee masuala ya kuvunjika moyo, lakini wapi. Nikaambulia kujilowanisha tu kwa jasho.

Sikupenda hisia za namna hii kabisa. Sijui nilianza kuwaje. Sawa, kuwajali hawa watu niliwajali, lakini hili suala la kuwaza sana juu ya fikira za Miryam kunielekea ndiyo lililokuwa linanihangaisha. Sikuwa mtu wa kujali sana nani ananifikiriaje na hata kama ningekuwa nimetoka kutibuana na mtu, lingekuwa suala la kuishia hapo hapo na mimi kuendelea na mambo mengine; labda ikiwa tu niliyetibuana naye angetaka kuliendeleza.

Ila Miryam! Alikuwa anafanya akili yangu iwe kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe, ikipambana kutaka kumtoa akilini lakini ikishindwa kufanikisha hilo. Ningehitaji kutafuta njia ya kunisahaulisha maana hizi hisia huwa zinaboa sana.

Kidogo tu baada ya kuacha hizo push-ups na sit-ups, Ankia akawa ameingia chumbani hapo na kunikuta nikiwa nimekaa chini; nikiegamia kitanda tu.

Akafunga mlango na kuja karibu nami, naye akauliza, "Vipi?"

Sikumwangalia, lakini nikatikisa kichwa kidogo kuonyesha hakuna kitu.

"Mbona kama una huzuni? Nini kinakusumbua?" akaniuliza hivyo kwa upole.

Nikabaki kimya tu nikitazama mbele.

Akashuka na kuchuchumaa karibu na miguu yangu, naye akasema, "Nimemsikia Miryam wakati anafoka hapo nje."

Nikamwangalia usoni.

"Tesha kanitumia sms pia. Anasema haelewi kinachoendelea, ana-kutext lakini haumjibu. Nini kimetokea hapo JC?" akaniuliza hivyo kwa upole.

Nikashusha pumzi kiasi, nikihisi kuvunjika moyo, nami nikamwambia, "Amenielewa vibaya. Nilikuwa najaribu kuwasaidia tu lakini... kanisoma vibaya."

"JC unajua kabisa kwamba Miryam huwa hapendi watu kujiingiza sana kwenye masuala ya familia yake. Nilikwambia kabisa siku ile. Sawa unamsaidia mdogo wake, lakini... mengine unayaacha tu. Ona sasa mpaka mmefika huko kwenye kupigiana kelele..."

"Hiyo ndiyo nini? Kwa hiyo unamaanisha nikiona nyoka anataka kuwang'ata basi niwaache tu... niwaangalie tu. Kisa? Miryam atanuna? Hayo siyo maisha Ankia..." nikamwambia hivyo kwa uhakika.

"Lakini ya kwao siyo ya kwako JC. Utalazimisha? Yote hayo kwa faida gani? Unajitoa kusaidia halafu mwisho wa siku uje kutimuliwa vumbi?"

"Siyo hivyo Ankia. Miryam kajaji hii situation vibaya tu... na siyo makosa yake. Ila ndo' yameshamwagika sasa. Hakuna yaani... imekwisha hiyo," nikamwambia hivyo.

"Kwani amekwambiaje?"

"Nisimsogelee tena Mariam," nikamwambia.

"Ih! Kisa nini JC?" akauliza kimshangao kiasi.

"Ni... ni mambo mengi Ankia. Ngoja tu nitulie kwanza, nitakuja kukwambia," nikamwambia hivyo kwa sauti ya chini.

Alikuwa ananitazama kwa hisia za huruma, naye akasema, "Sawa. Kuna ugali kwenye hotpot, ukitaka..."

"Hapana, sihisi njaa. Naenda tu kupiga maji af' naingia kulala," nikasema hivyo bila kumwangalia.

Akaitikia tu kwa kusema "Haya," kisha akasimama na kuondoka.

Sehemu kubwa ndani ya moyo wangu ilikuwa ikihisi hasira sana japo nilijitahidi kujidhibiti. Si ile kujua kwamba uko sahihi kabisa katika jambo fulani lakini kwa wengine unakuwa unaonekana kama vile umepotea? Miryam hakuamini niliyomwambia, Ankia naye akawa anaongeza kunifanya nihisi kama vile hatia yote ilikuwa yangu, yaani dah! Hapa hamna kabisa.

Nikasimama tu na kuamua kwenda kuoga hatimaye, nisitake tena kujali habari zozote zile kunizunguka kwa wakati huu. Shwaa bafuni, shwii chumbani. Mapema ya saa nne tu nikawa kitandani tayari na taa zikiwa zimezimwa, nikikaa kucheza game mpaka kufikia saa nane kabisa, ndiyo hatimaye nikaweka simu pembeni na kuutafuta usingizi.

Mawazo ya hapa na pale kuhusiana na jambo lililokuwa limetokea yalinikawiza kweli kuupata usingizi, lakini mwishowe ukawa umeniiba. Siyo siri, hizo zilikuwa ndiyo stress za kujitakia!


★★★


Nimekuja kuamka asubuhi ikiwa ni saa tatu, usingizi bado ukinivuta, na kilichokuwa kimenishtua ni mwito wa simu yangu. Sikutaka hata kuijibu lakini nilipoichungulia na kukuta mpigaji ni mke wake Chalii Gonga, madam Bertha mwenyewe, nikaona nimsikilize. Lazima angekuwa na jipya kunitafuta asubuhi yote hii.

Jipya lenyewe likawa tu kwamba nilipaswa kwenda huko kwake hotelini, ingawa hakusema kwa dhumuni lipi wakati huu, ishu iliyokuwepo ilinihitaji kwenda huko upesi eti hata kama sikuwa nimekunywa chai. Nikamwambia haina shida, anipe muda mfupi nijiandae kisha ningefika huko ndani ya saa moja tu. Swaga za asubuhi.

Baada ya kuachana naye nikatoka kitandani na kuchukua vifaa vya usafi wa mwili, kisha nikaelekea nje ili kujisafisha. Ankia alikuwa ameshaamka na kufanya mambo yake kama kawaida, na japo tulipeana salamu ya asubuhi lakini hakukuwa na uchangamfu kama ilivyokuwa imezoeleka.

Nikaoga tu na kurudi tena chumbani, na nilipokuwa nataka tu kuanza kuvaa kimtoko, Ankia akawa amekuja kuniambia aliniwekea chai. Nilitaka kusema sikujisikia kunywa, lakini nikamtazama na kuona jinsi alivyoonyesha kunijali sana, nami nikaamua kumkubalia tu. Sikutaka kumvunja moyo.

Kwa hiyo nikajitengeneza vizuri mwilini na kuvaa nguo nyepesi kwanza, kisha nikaelekea sebuleni kupata kiamsha kinywa. Alikuwa ametengeneza chapati za mayai, nami nikapiga mbili na chai kisha kumshukuru kwa fadhili yake. Hatukuongea sana, hasa kuhusiana na ishu ya jana, zaidi tu ya Ankia kusema alijua mambo yangekaa sawa baada ya muda fulani, na mimi ndiyo nikawa nimemwambia kwamba ninaelekea Sinza kwa muda huu.

Basi, nikarudi chumbani tena na kuanza kuvalisha mwili wangu nguo safi, lile T-shirt jipya la blue-nyeusi pamoja na jeans yangu nyeusi, nami nikawa najifikiria nivae zile ndala mpya ama viatu vyangu vyeupe. Mmm... viatu ndiyo vingefaa zaidi, na ile tu ndiyo nataka kuanza kuvivaa, nikasikia sauti ya mgeni aliyekuwa amefika hapo na kukaribishwa na Ankia.

Isipokuwa tu sauti yake haikuwa ngeni, nami nikatambua kwamba ilikuwa ni Tesha. Nilijua tu dogo alikuwa amenifata, nami nikawa najilaumu kwa nini sikuwa nimeondoka mapema zaidi kwa sababu najua angeanza maswali mengi hapa, kitu ambacho nilitaka kuepuka.

Nikaanza tu kuvaa viatu upesi, na ndipo mlango wa kuingilia chumbani hapa ukafunguka. Nikanyanyua uso na kumwangalia rafiki yangu, ambaye alisimama hapo mlangoni huku akinitazama kwa umakini, nami nikaendelea kufunga kamba za viatu.

"Oy," akasema hivyo.

"Niaje?" nikamwambia hivyo bila kumwangalia.

"Siyo poa. Yaani siyo poa hata kidogo mwanangu," akasema hivyo.

Akaja kabisa mpaka kufikia hapo kitandani nilipokaa, nami nikatulia kwa kuegamiza kiwiko changu kwenye mguu, lakini sikumwangalia usoni.

"Oya, yale ya jana ndo' yalikuwa mambo gani? Mm? Mbona we' na Mimi mkachafua kibaraza namna ile... afu', from nowhere tu yaani?" akaniuliza hivyo kwa upole.

Nikainamisha uso kwa kukosa namna ya kuelezea.

"Tatizo nini mwanangu? Unajua hiyo show ya jana haijakaa sawa kabisa? Nimeshindwa kuelewa. Nini kimetokea mpaka da' Mimi akazingua kivile... eh?" akauliza tena kwa kusisitiza.

"Kuna mambo mengi, Tesha. Tulipishana tu kauli na sister, na..."

"Kupishana kauli ndo' mpaka akupige banzi?" akanikatisha.

Nikabaki kimya tu.

"Sielewi JC. Kaka... niambie tu, kwa nini mlizinguana vile? Miryam kufanya hivyo ni mpaka awe amekasirika mno, na wewe sidhani ka' unaweza kumkaririsha kihivyo bro. Ningeelewa tu hata kama mngesema ilikuwa misunderstanding ya kiutu uzima. Ila hazisuluhishwagi hivyo, yaani wote jana mlikuwa tofauti, yaani mwana, si...."

"Ungemuuliza, angekwambia tu," nikamkatisha huku nikiwa nimeinamisha uso bado.

"Mimi hawezi ropoka kaka, unamjua vizuri. Hata mama hajawaambia lolote zaidi tu ya kusema kwamba sasa hivi hautaendelea kuwa daktari wa Mariam... hasemi nini umefanya mpaka kufikia hiyo hatua. Kaka me na we' si tunaelewana? Unashindwa tu kuniambia hili suala? Umemfanyaje? Umemtongoza akakataa au?"

"Tesha!" nikamwita kiukali kiasi.

"Sasa unataka nifikirie nini? Umeanza kuwa kama siyo mwana," akasema hivyo kwa mkazo.

Nikanyanyua uso na kumwangalia, nikiona wazi jinsi alivyokuwa ametatizika kwelikweli, nami nikamwambia, "Kama dada yako hajakwambia chochote, basi ujue na mimi sina cha kusema. Sitaki kutengeneza mvurugo wowote kwenye familia yenu, sawa? Chukulia kwamba... anachokifanya Miryam ni sahihi. Labda tu ndiyo umefika wakati wangu kuacha kumsaidia Mariam, kwa hiyo ni kuendelea kufanya mambo mengine tu. Hivyo."

Akaanza kutikisa kichwa kuonyesha hakubaliani na hilo, naye akasema, "Eti umefika wakati, ndo' uache kumsaidia Mamu, usije nyumbani tena, tukaushiane tu utadhani tumefanyiana ubaya, ndiyo nini sa'? Mi' siwaelewi aisee. Yaani... afu' we na Miryam sometimes huwa mnakuwa mna vichwa vigumu, yaani sijui mkoje! Ah..."

Akapiga ulimi mdomoni mwake kwa njia ya kuudhika, naye akanyanyuka kutoka hapo kitandani na kuelekea nje ya chumba.

Nikafumba macho na kuinamisha uso kwa huzuni, nikiwa najihisi vibaya sana kuhusu namna ambavyo rafiki yangu alikuwa anataabika, lakini hakukuwa na pointi yoyote ya kuanza kumwelezea mengi yaliyofanya mpaka nikagombana na dada yake. Sikutaka tu mengine yazuke maana nilimjua vizuri sana Tesha, kwa hiyo kumwacha gizani kwa wakati huu ilikuwa bora kwa ajili yake.

Japo kiukweli, roho iliniuma sana kila nilipofikiria hatari ambayo ilikuwa inamnyemelea Mariam kuwa karibu naye zaidi halafu mimi kuwa nimepewa kizuizi cha kutomsaidia tena. Zamu hii kama ni kifo ndiyo kilipangwa juu ya huyo binti, basi kingempata tu, kwa sababu sikuona namna nyingine tena ya kuweza ku... aisee! Hii kitu ilininyima raha sana.

Nikaona nibebe vyangu tu ili niondoke eneo hili, na angalau huenda ningekuta mambo mengine huko Sinza kwa adui-rafiki yangu ambayo yangesaidia kuniondolea msongo wa suala hili la Miryam.

★★

Masaa kama mawili hivi kupita nami nikawa nimefika hotelini kwake madam. Yaani niliondoka Mbagala na moja kwa moja kuja huku, nisijali nani wala nini kingine kiasi kwamba hata yule askari mpelelezi Ramadhan aliponipigia wakati nipo pande za Vunja Bei, sikupokea simu kabisa.

Kale kahisia ka kukatishwa tamaa kalikuwa kamenilemea mno yaani mpaka nikawa sijui nini kilichopaswa kuwa cha muhimu kutanguliza kwanza, lakini nilikuwa nimeamua kumweka madam Bertha mbele zaidi ili niwe chini ya hali tofauti ambayo ingenifanya nipotezee hisia hizi mbaya. Ikiwa hilo lingewezekana.

Baada ya kuwa nimefika kwenye mlango wa chumba chake, nikaugonga na kusubiri. Ilimchukua mwanamke huyo karibia dakika tano kuja kunifungulia, sijui hata alikuwa anafanya nini, lakini baada ya kumtazama hapo alipokuwa amesimama, fikira zangu zote zikavutwa na mwonekano aliokuwa nao. Nilikuwa nimetoka kumwona jana tu lakini kwa jinsi alivyokuwa anafanana sasa, ilikuwa kama vile hatujaonana kwa muda mrefu.

Alikuwa amevaa nguo nyepesi sana mwilini; ki-T-shirt cha njano chenye sura ya Pikachu, lakini kikiwa kimekatwa tumboni mpaka kufikia usawa wa kifua chake. Yaani macho ya Pikachu yalikuwa kwenye pande za matiti yake, ambayo yalikinyanyua kinguo hicho kuelekea mbele. Kitovu chake chenye pini ndogo kikiwa nje, alivaa kikaptura kifupi chenye uwazi, yaani hakikumbana, kutokea kiunoni mpaka katikati ya mapaja yake.

Kilichokuwa kimefanya aonekane mpya zaidi ilikuwa ni nywele zake kichwani. Alikuwa ameutoa ule msuko wake na kunyoa kabisa, akiwa kabakiza nywele nyingi kiasi kwa juu na kupunguza zaidi kwa pande za kichwa, na zilikuwa zimepakwa dawa iliyozifanya zing'ae na kuviringika kuzungukia kichwa chake.

Akiwa amesimama huku mguu wake mmoja akiusogeza mbele na kuusimamisha kwa vidole, alionekana kama mwanamke malaya anayesubiria mteja kwenye mlango wa kuingilia vyumba vya madangulo, tena vile vile vya kule Ubungo, na alishika sigara kwenye vidole viwili huku akiniangalia kwa macho ya kutojali.

Sikuonyesha hisia yoyote ile nilipokuwa nikimwangalia, na kwa mara nyingine tena nikamshusha taratibu mpaka miguuni na kuanza kumpandisha tena.

Akaniuliza, "Nini?"

Nikamwangalia usoni, kisha nikatikisa kichwa kuonyesha hakuna lolote.

Akanishusha kwa macho ya dharau kiasi, naye akageuka na kuanza kuelekea ndani zaidi ya chumba hicho. Nikafata pia, nami nikaufunga mlango na kumgeukia. Alikuwa anapunguza majivu ya sigara kwenye chombo kidogo usawa wa droo la kitanda, kisha akaivuta simu yake iliyokuwa kitandani na kunigeukia, naye akaanza kuja tena upande wangu.

Nilikuwa nimeshatambua kwamba hakuwa amevaa sidiria wala nguo ya ndani kwenye hiyo Pikachu na kikaptura chake, lakini sikukaza sana fikira zangu huko. Alipenda uzungu sawa, na inawezekana alikuwa bonge moja la malaya, lakini kilichonipeleka hapo kilikuwa kitu kingine, hivyo nikatulia tu kumsikia angeanza na kipi.

Akawa amenifikia karibu zaidi, kisha akasema, "Naomba simu yako."

Sikuelewa sababu ya yeye kuanza na hilo moja kwa moja, lakini nilijua haingekuwa busara kuanza maswali. Nikiwa makini tu, nikaitoa simu yangu mfukoni na kumwonyeshea kwa chini. Akaichukua, kisha akaanza kubofya kwenye kioo cha simu yake. Simu yangu ikaanza kuita, nami nikamwangalia usoni kwa umakini kwa sababu sikuelewa kwa nini alifanya hivyo.

Akacheka kidogo kwa pumzi, naye akasema, "Kumbe umeni-save "Madam?" Nilidhani ningekuta umeni-save 'Bitch.'"

Sikuona jambo lolote lenye umuhimu kutokana na kitendo chake, kwa hiyo nikatazama pembeni tu bila kuonyesha hisia yoyote.

Akaniangalia kwa umakini, kisha akasema, "Nini? Mbona grim sana leo?"

Nikatikisa kichwa kuonyesha hamna kitu.

"Sasa mbona umevimba? Umekuwa Zuchu? Navimba, navimba, navi... ahahahah..." akaongea kimasihara.

Inaonekana alikuwa kwenye mood nzuri kweli leo, lakini sikuonyesha kujali kabisa maneno yake.

"Okay, cut the shit. Una shida gani?" akaniuliza hivyo baada ya kuona sicheki.

"Hamna shida. Niambie ikiwa kuna ishu unataka tufanye. Jambo lolote, nipe kazi yoyote..." nikamwambia hivyo.

Akanitazama usoni kwa umakini, naye akasema, "Ili iweje? Kuna kitu unataka kupotezea?"

"Hapana, nataka kushughulika na ulichoniitia..."

"Ili iweje? Nijibu kwanza," akasisitiza.

Nikatazama pembeni tu.

"Ahah... HB boy umekumbwa na nini? Tuambiane," akasema hivyo.

"Sijakumbwa na chochote madam..."

"Naonekana kama mjinga kwako?"

"Nimesema hivyo?"

"Ndiyo unachotaka kumaanisha..."

"Kwani ni lazima ujue? Vitu vingine ni personal madam, hata nikikwambia hautanisaidia kwa lolote, ya nini sasa? Ah..." nikaongea hivyo kwa kuudhika.

"Yaani unanisemesha mimi hivyo?" akaniuliza.

"Ah, we' ndo' umenifosi..." nikasema hivyo na kusogea pembeni.

Nilikuwa nahisi hasira-hasira tu yaani, na ni hali ambayo nilitaka ikome lakini ndiyo ikawa inazidi kukua tu. Nikafumba macho na kushusha pumzi, huku nikipitisha kiganja changu kwenye paji la uso.

Bertha akawa amekuja hapo niliposogea, naye akasema, "Niambie."

Nikamtazama machoni.

"Niambie nini kinakusumbua, huwezi kuwa hapa huku akili yako iko maili mia tisa mbele. Sema," akaongea hivyo.

"Haina haja ya..."

"Wewe sema. Tatizo nini? Una shida na pesa?" akaniuliza hivyo.

Nikatazama pembeni na kutikisa kichwa kukataa.

"Nini sasa? Demu wako kakuacha au?"

"Sina demu bana."

"Wewe huyo ukose?"

Nikatulia tu.

"Au ni matatizo ya familia? Ni... mzazi anaumwa au?" akaongea kwa sauti yenye kujali kiasi.

Nikamwangalia, nikiwa nimeshangazwa kiasi na hilo, nami nikatikisa kichwa kukataa tena.

"Sasa shida ni nini? Kinachokuwangisha hivyo ni nini, kuna jambo lingine tofauti na hayo lililo kubwa mpaka kukukosesha raha kihivyo?" akauliza kwa kusisitiza.

"Me mwenyewe hata sielewi. Sijui kwa nini nakuwa hivi..." nikajikuta namfungukia mwanamke huyu.

Akawa ananitazama kwa hisia makini, naye akasema, "Kwani umekuwaje? Niambie..."

"Aa... yaani... hhh... sijui hata nise..." nikapatwa na kigugumizi cha maneno.

Bertha wa wakati huu alionekana kuwa tofauti sana na nilivyokuwa nimemzoea, adui kama adui, akawa ananionyesha hisia-mwenzi (compassion) kwa kuonyesha anataka kunisikiliza.

Nikamwangalia usoni, kisha nikamuuliza, "Hivi madam... imeshatokea ukawahi kukaa... ukafikiria labda... ifikie wakati ubadili maisha unayoishi?"

"Unamaanisha nini?" akaniuliza hivyo kwa sauti ya chini.

"Kila mtu huwa anapewa mkondo wa kufuata kwenye maisha yake, sawa? Vile anavyoamua kuufuata au kuachana nao na kuangalia mwingine... ni juu yake, si ndiyo? Sasa... huwa inafika wakati ambao utaanza kuona kwamba kuchagua mkondo wa maisha yasiyofaa kunaweza kukuletea matatizo, si ndiyo? Na kuna vitu vitakupa maonyo. Ukivipuuzia halafu ukapatwa na hayo matatizo... hiyo itakuwa ni juu yako, si ndiyo? Hakutakuwa na mtu mwingine wa kulaumu ila wewe, si ndiyo?" nikamwambia hivyo kwa sauti tulivu.

Bertha akaendelea kunitazama kwa umakini ulioonyesha kwamba alikuwa akitafakari hayo niliyomwambia, nami nikawa namwangalia kwa subira ili nione itikio lake kutokana maneno yangu. Lakini ghafla, mwanamke huyu akaanza kucheka kwa sifa sana, akiinama na kupiga makofi kuonyesha kwamba nilikuwa nimemchekesha sana, nami nikaelewa kwamba hakuwa amenichukulia serious.

"Ahahah... ahah... yaani HB bwana! Eti si ndiyo... si ndiyo... si ndiyo... unatoa neno kama mzee wa upako! Hahahah... na sadaka nakupa aisee ahahah..."

Akaendelea tu kucheka na kwenda upande wa kitanda, nami nikamwangalia kwa utulivu tu.

"Kinachokuhangaisha ni hicho? We' unawaza hayo ya nini? This life, no stress. Ishi baba. Siku hizi jema ndiyo baya, baya ndiyo jema. Matatizo, matatizo kitu gani? Matatizo ni ya washamba walioachwa tu na wakati, watu kama sisi tunakula raha kwa sababu tunaishi kwa akili. Sijui unanielewa? Peleka hayo mahubiri yako sehemu nyingine HB, siyo hapa. Hapa hizo zote ulizoongea ni pumba," akaongea namna hiyo.

Kweli. Huyo ndiyo Bertha niliyekuwa namfahamu. Hiyo yote aliyoiita pumba ilikuwa ni kitu kilichofanya nisumbuke sana rohoni, kwa sababu nilikuwa najimaanishia mimi mwenyewe kwa sehemu kubwa ya yale niliyomwambia.

Mimi ndiye niliyekuwa nimemwonya Miryam kuhusu hatari iliyokuwa karibu sana na mdogo wake, lakini hakutaka kukubali. Ikiwa baya lingetokea, bado ningejihisi vibaya mno haijalishi nini kilikuwa kimetokea baina yangu na yule mwanamke; nisingeweza kujisamehe endapo kama Mariam angeumia huku na mimi nikiwa pale pale. Ila ndiyo kutokea hapa ningeweza vipi tena kumsaidia yule binti? Dada yake alikuwa amenipiga marufuku kwenye wakati mbaya sana!

Nikawa nawaza mengi haswa kwenye kichwa changu, na umakini wa macho yangu ukawa kwenye kifua chake Bertha. Mimi bila kutambua hilo upesi, nafikiri nikawa nimemfanya mwanamke huyo adhani kwamba nilimtazama yeye kwa kuzubaishwa na ufikirio fulani kumwelekea, naye akanyanyua kiganja chake kunielekea na kupiga vidole vyake kwa sauti.

Nikashtuka machoni na kumtazama usoni, naye akasema, "Mbona unataka kutoa udende? Umeona nini?"

"Udende haujanitoka, kwa hiyo jua sijaona lolote," nikamwambia hivyo.

Sura yake ikageuka kuwa makini, naye akasema, "Njoo hapa."

Nikamfata mpaka hapo aliposimama, nami nikatulia tu nikimwangalia kwa utulivu.

Akasema, "Unajifanya una majibu eh?"

"Kuna kibaya nimeongea kwani?"

"Uwe na breki kwenye maneno unayoniambia. Kumbuka kwa nini uko hapa, na mimi ni nani kwako. Usinijibu ovyo kisa tu una stress za kipuuzi," akaniambia hivyo.

"Hivi... ahah... madam una tatizo lolote na mimi, au? Maana nimeshajisafisha fresh mpaka umeniweka upande wako, lakini unanitendea kama vile me sijui... mtumwa labda..."

"Kumbe? Ulifikiri we' ni nini? Yaani wewe ni sawa na kinyago cha pambo tu kwangu. Utanipendezeshea himaya yangu kwa muda, halafu... ukisha-expire nakutupa," akasema hivyo.

Nikaangalia pembeni na kusema, "Hilo nalijua."

"Sasa je? Unajikuta uko high kisa nini... uko top floor na mimi, ama ile kulala kitandani kwangu? Kuwa care dogo... hili tako la gharama sana. Narudia kukwambia nione kama malikia na uwe unakaa kimya, usinijibu ovyo ovyo tu kwa sababu nakuruhusu uingie chumbani kwangu. Hauna utofauti wowote na Eliya wewe..." akasema hivyo.

Nikamwangalia usoni kwa umakini, nami nikamwambia, "Mambo gani tena hayo madam?"

Akiwa anavuta sigara yake, akasema, "Nini? Kwani uwongo? We' ulivyo soft, hauna utofauti wowote na shoga."

Kisha akapuliza moshi usoni kwangu kwa makusudi. Kudadeki! Hizi dharau zilikuwa zimeanza kuzidi kiasi sasa, na ukitegemea na hasira iliyokuwepo ndani yangu, nikajikuta naukamata mkono wake ulioshika sigara na kuukung'uta kwa nguvu ili sigara yake imtoke kiganjani, nayo kweli ikarukia upande mwingine wa chumba.

Bertha alishtuka kiasi, naye akanitazama usoni kwa mkazo na kuashiria kutaka kufanya kitendo cha ujeuri, lakini nikauzungushia mkono wake kufikia mgongoni kwake na kuukaza, na mwili wake ukawa umesogea karibu zaidi na wangu.

"Hivi we' ni mse.... niachie!" akasema hivyo kwa ukali.

Akawa anajaribu kufurukuta kwa nguvu, na kani yake ikafanya wote tuangukie kitandani, mimi nikiwa juu yake na yeye akilala chali chini yangu, na mkono wake nikiwa bado nimeukaza. Nafikiri nilikuwa namuumiza maana alionyesha sura ya maumivu kiasi.

Nikamwambia kwa sauti ya chini, "Nakuwa mkimya kwa sababu ninataka faida kutoka kwako, lakini sipendi dharau kama mwanaume yeyote. Nimeshakwambia mimi siyo boya, na mimi siko kama huyo mpuuzi wako. Kama huwezi kuniheshimu basi kaa tu na hilo moyoni, siyo lazima uniambie hayo maneno ya kashfa. Siko hapa kuwa rag doll wako, na mimi siyo Chalii, niko nawe kikazi. Basi. Nitumie kama mwanaume kwenye kazi, na siyo begi la kupanchia. Sawa?"

Akawa ananitazama kwa hisia kali sana, naye akasema, "Na wewe unajiita mwanaume? Kisa nilikuruhusu unibusu, ama?"

"Ahah... usimzomee simba ukiwa mbali, msogelee ndiyo utajua kwa nini ana meno makali," nikamwambia hivyo.

"Ya kwako yako wapi?" akaniuliza hivyo kibabe.

"Nisogelee uyaone," nikamwambia hivyo.

"Kwani hapa niko mbali?" akauliza kwa ubabe tena.

Ahaa? Kumbe alikuwa anakitaka? Angekipata!

Nikaanza kuuachia mkono wake niliokuwa nimeukazia nyuma ya mgongo wake, na ni hapa sasa ndiyo ikawa wazi kwangu kwamba kifua cha mwanamke huyu kilikuwa kimefunuka kabisa kwa chini, nami nikayatazama matiti yake. Yalikuwa meupe yenye chukuchuku nyeusi tii, zikiweka mzunguko mkubwa kwenye matiti utadhani yalikuwa yameunguzwa na moto.

Kuyaona sasa mbashara bila chenga kukasababisha nisimamishe msuli wangu pasipo kuvuta hisia yoyote, na nadhani madam alipotambua ninayaangalia ndiyo akaamua kunitemea mate usoni. Ke!

Sikutarajia hilo, kwa hiyo nikamtazama kwa mshangao sana huku yeye akitaka kujitoa kitandani, lakini ndiyo nikaikamata shingo yake kwa nguvu na kuikaba, nikimkandamizia kitandani tena, kisha nikaliwasha kofi titi lake moja kwa nguvu pia.

Akatoa mguno wa maumivu kiasi huku akiniangalia kwa hisia kali, nami nikaanza kulivuta-vuta kama kulipoza. Nikarudia tena kulitandika namna hiyo hiyo, kisha kulipoza tena, naye akaanza kunyonya mdomo wake wa chini huku sura yake ikiwa imevimba kiasi kutokana na jinsi ambavyo nilimkandamiza shingoni.

Nikaachana na kifua chake na kushusha kiganja changu mpaka katikati ya mapaja yake, nami nikakiingiza ndani ya kikaptura chake na kukiweka kidole changu mahali pake patakatifu. Nikaanza kufanya uchokonoaji kwa nguvu, na macho yake yakaanza kulegea huku uso wake ukijawa na wekundu kwa mbali kutokana na mnigo niliompa, kwa hiyo nikalegeza kiganja changu kiasi.

Pumzi zake zikaanza kusikika zaidi, naye akatanua miguu yake vizuri zaidi ili niendelee kumchokonoa. Nikaendelea kumkuna tu, na ndiyo nikahisi anaishika sehemu yangu ya siri na kuanza kuivuta ili niitoe nje. Ha! Kiko wapi? Nikautoa mkono wake kwangu na kuacha kabisa kumchokonoa kwa vidole vyangu, nami nikajifuta mate yake usoni na kuashiria kutaka kuondoka kitandani hapo. Wee!

Akakurupuka na kunishika kiunoni kwa nguvu, mpaka nikashtuka kiasi, naye akauliza, "Unaenda wapi?"

Sikumjibu na kuendelea tu kumtazama.

Akafanya kuifungua kabisa suruali upesi, kisha akautoa msuli na kuushikilia kiganjani. Akawa anauchua kidogo na kusema, "Maliza ulichokianza... la sivyo nitakuzingua!"

"Lakini me si kinyago kwako?" nikamwambia hivyo.

"Acha ujinga, maliza ulichokianza," akasema hivyo kwa msisitizo.

"Papara ya nini? Umefikiri nakimbia au?" nikamuuliza.

Hakutoa jibu, na badala yake akaanza kuvua kikaptura chake upesi ili aweze kujiwekea mtambo.

Nilikuwa namshangaa kiasi, yaani jinsi ambavyo alifanya hii kitu alionekana kama hakuwa ameifanya kwa muda mrefu, ama labda basi tu aliipenda kama vile alivyokuwa anapenda sana madawa. Na tena mpaka kuniita mimi kinyago halafu baada ya kumwonyesha ubabe wangu ndiyo akaanza kunielewa sasa, ilimaanisha hakuwa mzuri sana kwenye misimamo yake mwenyewe, na alipenda sana vitendo vya ujeuri hata kwenye mapenzi. Wapo wanawake wengi wa aina yake, na mimi ndiyo nikawa nimeelewa hilo zaidi sasa kumhusu yeye.

Hakutaka kuiachia mashine yangu mpaka alipokivua kikaptura chake, naye akajisawazisha vizuri zaidi kwa kutanua miguu yake huku akilenga kuiingiza hekaluni bila kuilainisha wala nini. Nikaushika mkono wake kumzuia, naye akaniangalia machoni.

"Umeniamini vipi ghafla tu kuniruhusu nikuingie?" nikamuuliza.

"We' si mjanja sana? Najua lazima unajitunza," akasema hivyo.

"Utakuwaje na uhakika? Je nikikwambia nina ngoma?"

"Basi niambukize," akanijibu kiujeuri.

"Ama we' ndo' unao?" nikamuuliza hivyo.

"Agh!" akafanya hivyo na kuanza kukisugua kito chake kwa msuli wangu.

"Una njaa sana, eh?" nikamuuliza hivyo.

"Acha ujinga wako, em ni(.....)! akasema hivyo na kuanza kujiingizia.

Macho yake yalikuwa yanalegea lakini aliniangalia kiujeuri sana, nami nikaamua kufanya umakusudi wa kuisukumia kwa nguvu mpaka mwisho! Akapiga kelele ndogo huku akirudisha kiuno chake nyuma, naye akakaza meno yake huku akiniangalia kwa mkazo. Nilikuwa nataka nimpe kipigo cha chuki yaani, na sikutaka kutania, hivyo nikaikamata shingo yake tena na kuanza kumsugua kwa kasi kama vile sina akili.

(.........).

(.........).

(.........).

(.........).

(.........).

Nikaendelea kupampu, hisia zikiwa zinanipanda, lakini akilini mwangu niliyekuwa namwona alikuwa ni Miryam. Sikujua kwa nini, lakini bado alikuwepo tu anazunguka kichwani. Bertha akarusha maji tena, yaliyonilowanisha kiasi nguoni, nami nikaamua kuitoa T-shirt yote na kuianika kwenye kifaa kilichobeba taa karibu na kitanda. Nikaingia tena.

Piga, piga, piga, huku nababua matiti yake makofi na kuyavuta kwa nguvu, naye akamwaga mengine tena yaliyoendelea kumtetemesha tu mapajani. Akili yangu ilikuwa imekazia fikira jambo moja tu, jinsi ambavyo Miryam alinipiga kofi usoni usiku wa jana, nami nikaendelea kumpiga madam kama vile sikutaka kuacha.

Akashika vidole vyake vya miguuni ili kuitanua zaidi na isirudi chini, machoni kukiwa kweupe kama vile hakuna lenzi, na ni hapa ndiyo nikawa nimeiona tatoo ndogo ya ua la waridi chini ya kidevu chake, yaani kuelekea kooni, na sijui kwa nini aliona hiyo kuwa sehemu nzuri ya kuchorea tattoo. Uso wake ulikuwa umelegea wewe, yaani aliachama mdomo na mate yakimtoka kama zezeta, na hatimaye akapasua la nne.

Isipokuwa tu wakati huu, mimi pia nikaanza kushusha haja yangu, lakini nilipotaka kuichomoa mashine, mwanamke huyu akaning'ang'ania ili ibaki ndani yake, kwa hiyo tukawa tunaoshana. Dah, siyo siri nilikuwa nikifanya ujinga wa hali ya juu!

Nikawa nimemlalia kabisa sasa. Kiuno changu kikawa kinashtua, na kila niliposhtuka Bertha alikuwa anaguna kuendana na mishtuko yangu, eti linasikia raha! Nikaanza kutulia, nikiwa nimelaza uso wangu pembeni ya kichwa chake huku nikiihisi harufu ya sigara iliyomtoka mdomoni, nami nikajitoa kwake na kujilaza pembeni.

Kufanya yote haya, yaani ilikuwa ni kama vile najikomoa tu maana sikumpenda mwanamke huyu hata kidogo, ila ndiyo ikawa njia ya kupunguzia hasira kiasi. Mawazo hayakuondoka kabisa, kwa sababu hata hazijapita dakika chache tayari Miryam na Mariam wakawa wamerejea kichwani tena. Waliniteka kiakili hao wanawake.

"Aih... nimechemka! Kumbe unajua eh?"

Sauti ya chini ya Bertha ikiuliza hivyo ikanifanya nimtazame, nami nikakuta anajisugua taratibu kwenye kito chake huku akiniangalia kwa macho legevu.

"Unakutana na wengi wasiojua kwani?" nikamuuliza hivyo.

"Kujua sijamaanisha ku-thrust tu. Nimemaanisha ku-last," akasema.

"Ahahah... muda huwa siyo shida kwangu," nikamwambia.

Nikamwangalia na kuona anajichomekea kidole chake kimoja, kisha akakipeleka mdomoni mwake na kulamba urojo wa hapo huku akiniangalia kwa macho yenye jeuri.

"Dah! We' ni mchafu!" nikamwambia hivyo.

"Cha ajabu? Ama hujui kwamba sisi ni wanyama?" akasema hivyo.

Nikaangalia pembeni tu.

Mlio wa simu yangu ukaanza kusikika, na ilikuwa imewekwa usawa wa upande aliolalia huyu mwanamke.

Akasema, "Nani tena huyo anataka kutuharibia starehe?"

Nikiwa nimejilaza tu, nikamwambia, "Nipasie basi."

Akacheka kidogo kwa pumzi, naye akajiketisha ili aivute simu yangu.

Chafya ikanibana puani ghafla, kwa hiyo nikageukia upande mwingine wa kitanda na kuitoa kistaarabu, mara mbili.

Bertha akasema, "Nani huyu umem-save kwa kichina? Ngoja..."

Kauli hiyo ikanifanya nishtuke kiasi, nami nikamgeukia na kukuta akiwa ameshapokea na kuweka simu yangu sikioni kwake. Ai! Bertha!

Hakukuwa na mtu mwingine yeyote niliyetunza namba yake kwa jina la kichina isipokuwa askari Ramadhan, na ninakumbuka kwamba alijaribu kunitafuta mapema lakini sikumjibu. Sasa bila shaka alikuwa amenipigia tena ili tujulishane juu ya mambo yaliyoendelea upande wa adui yetu, halafu adui yetu ndiyo akawa ameishika simu. Ningekuwa nimejikamatisha vizuri mno kwa madam Bertha endapo kama Ramadhan angesema lolote lile ambalo lingempa tahadhari huyu mwanamke.

Nikajaribu kuikwapua simu yangu kutoka kwake, lakini akanikwepa na kuninyooshea kidole kama kunionya nitulie. Sura yake ilikuwa makini, akionekana kusikiliza jambo fulani kutokea upande wa pili, kisha akaniangalia kwa macho yenye umakini sana. Sijui nini kilikuwa kimesemwa na huyo askari lakini hakikuonekana kuwa kitu cha kumpa furaha madam, na mimi moja kwa moja nikaelewa kwamba nilikuwa nimekwisha.



★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★

Full Story WhatsApp or inbox

Whatsapp +255 678 017 280
 
Back
Top Bottom