MIMI NA MIMI 3
A Story by Elton Tonny
Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Siri, Tamaa, Hila, Usaliti, Ukatili, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa
R-rated 18+
Enjoy!
β
β
β
β
β
β
β
β
β
β
β
β
β
SEHEMU YA TANO
β
β
β
β
β
β
β
β
β
β
β
β
β
Niliishiwa pozi. Huyo ndiye mgeni mwenye Range ambaye Shadya alisema amefika hapo? Kwa nini sikuwaza kabisa kwamba ingeweza kuwa yeye? Festo alifikaje huku wakati kama huu, na alikuja kwa dhumuni lipi? Ilinishtua kwa kweli, kwa sababu ni kwa wakati mwafaka kabisa ambao mimi na Miryam tulikuwa tukipitia hali yenye kutatanisha ndiyo jamaa akawa amefika ghafla namna hiyo. Alijua kuhusu haya yaliyokuwa yanatokea? Yaani... sikuelewa.
Alitoka tu mlangoni hapo na kusimama nyuma yake Bi Jamila na Bi Zawadi, nasi tukabaki kutazamana usoni kwa macho yaliyofahamiana vyema sana. Alikuwa amevalia kwa njia nadhifu, asiwe na utofauti wowote kutoka kwa jinsi nilivyomkumbuka kimwonekano. Nikaacha kumwangalia na kutazama pembeni kwanza, nikiwa najaribu kuusoma mchezo uliokuwepo hapa, kisha nikamwangalia Miryam usoni tena. Alitulia tu na kunitazama kama vile kusubiri niseme lolote lile ili nimwondolee kero, na ni kitu kilichonivunja sana moyo. Kwamba nilihisi ameanza kuniona kuwa kero. Wote hapo nje walitulia kimya tu, wakitutazama mimi na bibie kungoja drama.
Kwa sauti tulivu, nikamuuliza Miryam, "Umepoteza simu?"
Akabaki kuniangalia kama vile hataki kujibu.
"Kwa nini haukuja?" nikamuuliza.
"Wapi?" akaniuliza.
"Najua umeziona sms zangu zote. Kwa nini haukujibu? Na kwa nini haukuja?" nikamuuliza pia.
"Nina mambo mengi," akanijibu hivyo.
"Mmm... kwa hiyo kama usingekuwa na mambo mengi ungekuja?"
"Labda," akajibu kibaridi.
"Okay. Nimekurahisishia kazi basi. Nimeona nikufate me mwenyewe. Twende nje tukaongee," nikamwambia hivyo.
"Hatuna chochote cha kuongelea," akasema hivyo.
"Kabisa?"
"Kabisa."
"Kwa hiyo... kila kitu kiko poa?"
"Yeah, kila kitu kiko poa."
Nikatulia kidogo nikimtazamaaa, kisha nikamuuliza, "Unapofanya haya unayoyafanya Miryam, unakuwa unamaanisha nini?"
"Simaanishi chochote. Na sijafanya lolote. Ni wewe tu ndiyo umebaki kulazimisha vitu visivyowezekana," akaniambia hivyo.
"Visivyowezekana kivipi? Miryam mimi na wewe hatuja-share damu, na haya yote hakuna ambaye angeweza kuyaona...."
"Jayden, inatosha. Hakuna lolote ambalo utasema wala kufanya litabadili hali," akanikatisha.
"Hali ipi? Kweli unataka kusema kwa sababu tu tumejua kuna uhusiano wa kifamilia basi ndiyo ifute kila kitu ambacho mimi na wewe tumepitia? Eh? Kila kitu ambacho tumefanya?" nikamuuliza kwa hisia.
Akabaki kuniangalia kwa hisia makini.
Bi Jamila akasema, "JC mwanangu, tutafute muda, au mtafute muda mwingine mzuri wa kuongelea haya mambo kwa sababu huu siyo wakati mzuri."
"Nini, kwa sababu Festo amekuja?" nikamuuliza.
Wote wakabaki kimya, huku jamaa akiwa ananiangalia kwa utulivu pale nyuma.
"Ahah, Miryam bana! Kwa hiyo, una mambo mengi, huwezi kukutana nami, ila kupanda Range za watu kuzurura mpaka usiku ndo' unaweza..." nikamwambia hivyo.
Akabaki kuniangalia tu kwa mkazo.
"Kwa hiyo kilichokuwa kinakufanya uwe bize eti, ni kutafuta... backup plan ya kumwondoa JC kwenye taswira, si ndiyo? Umemwita na huyu jamaa ili akusaidie kunipotezea, au?" nikamuuliza Miryam.
"JC, acha kuongea hivyo," Bi Zawadi akaniambia.
"Amekunywa huyu," Shadya akasema.
"JC, twende huku ndani basi...." Ankia akajaribu kunisemesha na kunishika, lakini nikauondoa mkono wake kwangu taratibu.
Nikamsogelea Miryam karibu zaidi na kumwambia, "Mimi, come on... let's talk about this, eti? Just me and you."
Nilimsemesha kwa kubembeleza na kuishika mikono yake, lakini akaitoa taratibu mwilini mwake na kuniambia, "Hakuna lolote limebaki la kuzungumzia, Jayden. Jinsi mambo yalivyo ndiyo yanapaswa kuwa hivyo hivyo. Naomba uende nyumbani."
Nilibaki nikimwangalia kwa kutoamini yaani, kwa kuwa maneno yake yalituma maana fulani kwangu ambayo bado sikutaka kukubaliana nayo. Akafumba macho kiufupi, kisha akageuka na kutaka kurejea ndani, lakini nikauwahi mkono wake na kumgeuzia kwangu kwa kasi.
"Miryam..." nikamwita kwa hisia.
"Jayden, niachie..." akaniambia hivyo.
"Unamaanisha nini? Hm? Nini, kwamba mimi na wewe ndiyo basi, au?" nikamuuliza.
Shadya akasema, "Tumeshagundua kwamba nyie ni ndugu JC... kuendeleza mahusiano haita...."
"Shangazi..." Tesha akamwita kama kumzuia asiendelee kuongea.
Festo akasema, "JC, tuliza hisia. Haya mambo mnaweza...."
"Kaa kimya, Festo! Hayakuhusu!" nikamwambia hivyo kwa hisia kali na kumnyooshea kidole.
"Eh, Mungu wangu!" Bi Zawadi akasema hivyo.
Festo alibaki kuniangalia kwa utulivu tu, mimi hapo nikiwa nimeshapandwa na mzuka yaani kama angeleta ujinga wake nisingesubiri kuvuruga hali ya hewa.
Miryam akautoa mkono wake kwangu na kusema, "Jayden, sitaki malumbano sasa hivi. Nimekwambia uondoke."
"Siondoki mpaka ieleweke una tatizo gani Miryam. Kwa nini hutaki tukae tuzungumze kuhusu hili jambo? Kunikwepa ndiyo itasuluhisha lolote linalofanya unione kuwa kama kero sasa hivi, ama?" nikamuuliza kwa hisia.
"Jayden, familia zetu zinaingiliana. Hatuwezi kuendelea kuwa karibu tena! Ni kipi ambacho huelewi na unahitaji kuzungumzia zaidi, eh?" Miryam akanisemesha kwa uthabiti.
"Miryam suala la familia zetu kujuana haliondoi uhusiano tuliojenga kufikia sasa. Hata kama damu zetu zingekuwa zinaingiliana, hiyo haimaanishi tungeacha kupendana, kwa sababu tulikuwa tumeshapendana kabla hatujajua hilo..."
"Hivi Jayden, unaelewa unachokiongea kweli?" akaniuliza.
"Sijui, labda we' ndiyo unieleweshe..." nikamwambia.
"Tesha na Mariam ni wadogo zetu. Mimi na wewe hatuwezi kuwa kitu kimoja kwa kuwa tuna damu zao ndani ya mishipa yetu. Unataka tuendekeze ubinafsi na kufumbia jicho jambo zito kama hilo?" Miryam akaongea kwa hisia.
"Tatizo ni hilo kweli Miryam, au basi tu unataka tuanze kuzungushana mpaka tufike pasikofikiwa? Ikiwa tusingejua kuhusu haya mpaka tunafunga ndoa, ingetuzuia kuendelea kupendana eti tu kwa sababu tumechangia uzazi kwa wadogo zetu?" nikamuuliza.
"Lakini Jayden, kwa nini unakuwa huelewi?" Miryam akaongea kwa hisia.
"Shida siyo suala la undugu Miryam, kuna kitu kingine tu kinakusumbua mpaka ufanye haya. Una tatizo gani? Kwa nini hutaki kuniambia? Kwa nini unakuwa hivi?" nikamuuliza kwa hisia mpaka machozi yakaanza kunivizia.
Akawa ananitazama kwa hisia huku akipumua kwa nguvu.
"Niambie. Nini kinakusumbua?" nikamuuliza.
Akakaza hisia zake zaidi, naye akasema, "Siwezi tena Jayden. Yote... yote tuliyofanya... nikifikiria tu ukweli kwamba tumefanya mengi endapo kama... kama mimi na wewe tungekuwa ndugu wa damu kweli... ingekuwaje?"
Nikabaki nikimtazama kwa huzuni na kutikisa kichwa.
"Hili jambo siyo dogo. Tungeweza kuwashawishi wengine namna tunavyoelewana haijalishi ni namna gani nimekuacha kiumri, lakini sasa hivi tutawashawishi vipi waelewe...."
"Miryam, kwa nini ujali kuhusu watu...."
"... waelewe mahusiano yetu, no Jayden, usipuuzie ukweli kwamba mahusiano yangu me na wewe yanawaathiri watu wengine pia ndani ya familia zetu. Tutajenga suto kubwa ambayo sidhani kama niko tayari kuibeba," akaongea kwa hisia.
"Nilikwambia nini kuhusu wewe kubeba kila kitu mwenyewe? Hili siyo pambano lako pekee, Miryam, niko nawe, niko kando yako, kwa lolote lile tutakalo-face, itakuwa ni sisi wawili, kwa pamoja...."
Akawa anatikisa kichwa kukataa.
"... mpaka tutashinda. Miryam... Miryam..."
Nikamsogelea karibu zaidi na kumshika shingoni, lakini akajirudisha nyuma.
"Mi.... ah, Miryam nashindwa kuelewa... unataka nini? Tutaondoka ukitaka, sawa? Tutaenda mbali ikiwa hutaki ku...."
"Jayden, hapana. Hii imeshakuwa too much. Tumeshajaribu mengi, lakini nimeona... na wewe umeshaona kabisa kwamba... labda me na wewe hatujapangiwa kuwa pamoja. Labda fate zetu haziendani, na hizi ndiyo ishara..." akaniambia.
"Oh, God..." nikanena hivyo kwa huzuni.
"Inabidi tu tulikubali hilo. Unanielewa?" akaniambia.
Nikamtazama machoni kwa mkazo.
Akajifuta machozi upesi kwa uimara na kusema, "Naomba uende nyumbani. Familia yangu imeshakuwa na rep ya kutosha kutengeneza drama hapa nje, imetosha. Nenda Jayden."
Nikaendelea kumwangalia tu, yaani kama vile sijasikia yote aliyotoka kusema.
Ankia akanisogelea na kusema, "JC... hebu twende."
"Halafu nini?" nikamuuliza Miryam hivyo.
Miryam na wengine wakaendelea kunitazama tu.
"Niende nyumbani, halafu nini? Nisahau kila kitu? Ni... nikusahau Miryam?" nikamuuliza hivyo.
Miryam akabaki kimya tu.
"Unajua Miryam vitu vingine siyo vya kuongelea juu juu tu bila kufikiria. Unaposema imekuwa too much kwako kupokea maumivu wakati hujajipa muda wa kuya-face pamoja nami, wewe ndiyo unakuwa mbinafsi. Unafikiri kila kitu utabeba wewe tu, hujafikiria kwamba hili pia linaniathiri mimi? Lakini uko shuta kweli kunitolea.... eti unaniambia niondoke... niondoke? Unataka nikuache Miryam? Kweli umeshalifikiria hilo vizuri kabisa, au ni pressure tu ndiyo inakufanya uongee hivyo?" nikamuuliza.
"Unataka niseme nini, Jayden?" Miryam akaniuliza kwa mkazo.
"Nataka useme kwamba unanipenda," nikamwambia hivyo kwa uhakika.
Akabaki kuniangalia kwa hisia.
"Nataka useme kwamba unanihitaji, kwamba hutaki niende... kwamba unajua nikiondoka hautakuwa na furaha tena, kwa sababu unajua moyo wako utafunga... na itakuwa ni milele," nikamwambia hivyo kwa hisia.
Miryam akadondosha chozi na kulifuta haraka, huku wengine wakiwa bado wanatazama igizo hili lililozidi kuwa zito sana, naye akajikaza na kuniangalia kwa uimara, kisha akasema, "Hayo mambo hayawezekani tena."
Nikatikisa kichwa kwa huzuni na kupiga ulimi mdomoni.
"Na wala usijali kuhusu moyo wangu. Utapata tu mwingine wa kupenda," akaniambia hivyo.
"Ohh please... wewe Miryam? Umpende nani mwingine, huh? Huyu?" nikaongea kwa hisia kali huku nikimnyooshea kidole Festo.
"JC..." Ankia akaniita kwa upole.
"Huyu ndiyo mtu unayefikiri unaweza kumpenda?" nikamuuliza Miryam kwa mkazo.
Miryam akasema, "Ndiyo."
Nikamwangalia machoni. Hata na wengine wakamtazama Miryam baada ya yeye kusema hivyo.
"Nitampenda yeye," Miryam akaniambia hivyo.
Mkono niliokuwa nimeunyoosha kumwelekea Festo ukashuka taratibu, baada ya kuhisi kitu kikali kikiwa kimeuchoma moyo wangu kutokana na kusikia maneno ya Miryam. Sikuamini yaani. Yaani alikuwa kabisa ametoka kuniambia kwamba atampenda Festo badala yangu? Alinimaliza! Nikaangalia chini nikiwa nimeishiwa pozi hata zaidi, na chozi nililojitahidi kuzuia lisitiririke likanitoka.
"Dah! JC, kaka nisikilize..." Tesha akanisemesha hivyo.
"JC... Mimi..." Bi Zawadi akasikika pia akituita.
Nikamtazama Miryam usoni na kuona alivyokuwa akiniangalia kwa huzuni, machozi akijitahidi kuyazuia, nami nikamwambia, "Unajua Miryam... yaani ingekuwa bora kama ungenikata-kata kwa mapanga kuliko kuniambia hivyo. Ulichokisema... kwangu ni kibaya kuliko hata kifo!"
"We' JC wewe!" Shadya akasema hivyo.
"JC... acha kuongea hivyo. Hey... nakuomba uje nasi," Adelina akanisemesha hivyo hatimaye na kunishika mkononi.
"JC... hebu twende," Ankia naye akaniambia hivyo.
Miryam aliendelea kunitazama tu kwa njia imara, nami nikamwangalia Festo pale nyuma yake. Mwanaume huyo alinitazama kwa umakini, akijifanya mtulivu tu wakati bado sikuwa nimesahau rangi zake zote alizokuwa nazo, lakini kwa wakati huu sikuona uhitaji tena wa kuendelea kulazimisha mambo hapo. Miryam alikuwa ameusema uamuzi wake mpya, tena hadharani, na mimi sikuwa sehemu ya huo uamuzi hata chembe. Nilikuwa nafanya nini hapa?
Nikageuka hapo hapo na kuanza kuelekea upande wa geti, Ankia na Adelina wakija nyuma yangu, na kuna baadhi ya watu waliokuwa wamesimama sehemu hiyo, wakinipisha nilipojitoa getini hapo. Yaani sikutaka kujali tena yaliyoendelea pale, moyo wangu ulikuwa umevunjika sana baada ya mwanamke huyo kuniambia yale maneno. Nilipofika nje sikwenda garini, bali nikaelekea kwenye nyumba ya Ankia mpaka kule ndani kwake. Nadhani wanawake hawa walifikiri nilitaka kwenda kukaa nao na kuzungumza kidogo, lakini mie nikakielekea chumba nilichokuwa natumia hapo na kuanza kuzitoa nguo zangu kabatini, upesi nikizishindilia ndani ya begi. Najua walikuwa nyuma yangu wakinitazama, na ni Ankia ndiye akaanza kunisemesha.
"JC, mbona unapaki nguo?" akaniuliza hivyo.
Sikujibu. Nikaendelea tu mpaka nikamaliza na kulifunga begi.
Akaendelea kusema, "Tukae basi kwanza tuongee, eh? Najua unaumia lakini nakuomba kwanza... ukae... JC..."
Nikawa nimeshalibeba begi na kuanza kuelekea mlangoni, nami nikasimama na kuwatazama kwa njia iliyowapa ujumbe kuwa nilihitaji wanipishe ili niondoke.
"JC, sikiliza. Tuongee kwanza, eti? Weka begi chini tuongee," Ankia akaniambia hivyo.
Nikatikisa kichwa kukataa, nami nikataka kupita katikati yao kwa lazima. Lakini Adelina akaweka kiganja chake kifuani kwangu kunizuia, nami nikamtazama machoni kwa hisia za mkazo.
"Siyo salama kwako kuendesha ukiwa umekunywa JC. Nitakuja na wewe," Adelina akaniambia hivyo.
"Adela..." Ankia akamwita kama kumzuia.
"Nipe funguo, nitaendesha," Adelina akaniambia hivyo.
Nikamtazama kwa hisia makini kwanza, nami nikasema, "Nimefika hapa bila shida. Nitarudi hivyo hivyo."
"Hapana JC. Siwezi kukubali uendeshe ukiwa namna hii. Nipe funguo," Adelina akaniongelesha kwa ustaarabu thabiti.
Nikiwa sitaki kuvurugwa zaidi, na kwa heshima niliyokuwa nayo kumwelekea, nikatoa tu funguo mfukoni na kumpatia, kisha nikawapita bila kusema lolote na kuelekea huko nje.
Nikamsikia Ankia akisema, "Lakini Adela, tulikuwa hata hatuja...."
"Haina shida Ankia, nitamsindikiza tu halafu nitaenda kwangu pia. Anahitaji kupumzika, lakini nataka kuhakikisha anafika salama," Adelina akasema hivyo.
Nikatoka hapo ndani na kwenda mpaka garini kwangu, bado watu wakiwepo sehemu hiyo ya nje, nami nikaingia tu na kutupia begi langu siti za nyuma. Nikiwa nimeketi siti ya pembeni na usukani, nilikuwa nikiitazama nyumba yake Miryam kwa mkazo sana, nikimwona Tesha anakuja sehemu ya hapo nje na kusimama pamoja na vijana kama wawili-watatu hivi, ambao walionekana kuongea na kuelekeza macho yao upande wa gari langu. Adelina akaja mpaka ndani ya gari langu na kuingia kwenye usukani, naye akaniangalia kwa ufupi usoni. Nikiwa nataka tu kuondoka eneo hili, nikatulia na kufumba macho nisisubiri kingine zaidi. Gari likawaka, na mwanamke huyu akaniondoa taratibu eneo hilo lililokuwa limeniacha na majonzi mengi moyoni mwangu.
β
β
Adelina akaniendesha kwa mwendo usio wa haraka kabisa, na mwanamke huyu mtulivu alikuwa akijaribu kunisemesha mara kadhaa kuhusu hali yangu, lakini sikumjibu hata kidogo. Nilikuwa ndani ya hisia mbaya sana kiasi kwamba sikujua tunaenda wapi na sikujibu hata aliponiuliza uelekeo aliopaswa kupita ili anifikishe kwangu. Na kiukweli sikumtendea haki dada wa watu, maana alichokuwa akifanya ni kujitahidi tu kunisaidia. Lakini mawazo na hisia zangu hazikuwa mahala sahihi kwa pindi hii, nilivurugwa ile mbaya. Yaani nilihisi hasira kali mno kwa maneno ambayo Miryam aliyasema mbele ya kila mtu. Eti ingekuwa afadhali ampende Festo na si mimi? Ningeweza kuua mtu aisee, na sikudhani ningewahi kuwaza kufanya hivyo.
Kuna mahali tukafika, barabarani, na askari wa usalama kwa eneo hilo akatusimamisha. Ilikuwa ni kuchekiwa tu kwa gari na mwendeshaji, na Adelina alionyesha leseni yake na kufanya maongezi mafupi na askari huyo, kisha akatuachia tusonge mbele. Kiukweli alikuwa amenisaidia sana maana endapo kama ningeshikwa naendesha huku nimelewa ingekuwa kujitia hatiani. Ila bado nilikuwa kwenye hisia za kutojali, na Adelina aliendelea kujaribu kunisemesha bila kupata itikio lolote. Ikafikia hatua akasimamisha gari eneo moja, na kuliangalia nikatambua palikuwa kwenye barabara iliyoelekea Kimara.
Adelina akanishika begani na kuniambia ninavyokaa kimya inamkosesha amani sana, na ile nimemwangalia tu, niliona sura yenye kujali sana ya mwanamke huyu ilivyokuwa ikinitazama, lakini umakini wangu ukawa huko nje zaidi. Niliona jengo lenye kumbi ya starehe na baa ya vinywaji, nami bila kusema lolote, nikafungua mlango na kutoka ndani ya gari. Nikavuka barabara na kwenda huko bila kujali kuangalia kushoto wala kulia, nikimwacha Adelina anajiuliza ninakwenda wapi bila shaka.
Akili mbele tu, nikaingia kwenye kumbi hiyo na moja kwa moja kuelekea kaunta kupombeka. Aloo! Najua niliwavutia wengi waliokuwepo, nikafuatwa kabisa na baadhi ya wanawake ili wapate baraka kutoka kwangu, lakini sikuwa na muda nao. Nikakaa kitini na kuagiza kileo kikali, spirit yaani, na sikuwa na mpango wa kuichanganyia na soda wala nini, yaani chupa nzima nilipanga kuinywa hadi iishe. Ndiyo nilikuwa nimetoka tu kuimimina kwenye glasi kidogo pale niliposhikwa mkono kwa chini, na aliyenishika nilipomgeukia nikakuta ni Adelina.
"Wewe, JC... mambo gani haya?" akaniuliza kiumakini.
Nikabaki nikimtazama kwa umakini pia, na hatimaye nikamwambia, "Nakunywa kidogo. Kaa nikuagizie."
Akabaki kuniangalia kwa kukereka, nami nikavuta glasi yenye kileo na kuishusha yote kooni kwa kishindo. Ilikuwa kali! Nikatulia kwa sekunde chache nikisikilizia hilo pigo, kisha nikatulia na kumwita bartender, mwanamke mtu mzima ila matata.
"Mpe huyu yoyote anayotaka," nikamwambia huku nikimshika Adelina begani.
Adelina akautoa mkono wangu begani kwake na kumwambia mwanamke huyo, "Sitaki chochote."
Mwanamke huyo akabaki kututazama.
Nikiwa nimeshamimina kinywaji tena, nikasema, "Kama hutaki kunywa agiza msosi ule."
Adelina akabaki kuniangalia kwa mkazo.
"Au ulikula kwa Ankia?" nikamuuliza.
Tayari divai ilikuwa imeanza kunikoroga vyema, naye Adelina akasema, "Kwa hiyo muda wote nimekusemesha kwenye gari ulikuwa husikii? Ulitaka kuja kuongelea bar?"
Nikapuuzia swali lake na kupachika goli la pili la pombe hiyo kali balaa.
"JC mbona unakuwa hivi? Nikuache tu si ndiyo?" Adelina akasema.
"Hamna... kaa unywe," nikaongea kilevi.
"Hebu twende JC..."
Adelina akajaribu kunivuta lakini nikamwekea mgomo.
"Tabia si nzuri hii, kulewa haitasaidia lolote. Unajidanganya ukifikiri ndiyo itasuluhisha matatizo yako..." akaniambia hivyo.
"Hamna... ila inayapunguza," nikamwambia hivyo na kutabasamu.
"Hakuna! Unayaongeza tu na unajiumiza. Hebu acha," akaongea kwa hisia kali.
"Adelina nenda ukalale... matatizo... matatizo yangu... hayakuhusu..." nikamwambia hivyo.
Nikaongeza pombe na kutaka kunywa tena, hapo wenge zito kichwani likiwa limeshaniteka, lakini Adelina akaikwapua glasi hiyo na kuiweka pembeni kwa hasira.
Akamwita bartender na kutoa hela yake mwenyewe kumpatia. "Shi'ngapi hiyo?" akamuuliza.
Nikacheka kilegevu, na baada ya kuambiwa bei Adelina akalipia na kisha kunishika mkono kwa nguvu.
"JC nyanyuka," Adelina akaniambia.
"Sijamaliza kilichoni...."
"Nimesema twende!" akanikatisha kwa kunikaripia.
Nikautoa mkono wangu kutoka kwake kwa nguvu sana na kusema kwa hasira, "Niache bana! We' vipi?!"
Niliuvuta mkono wangu kwa njia iliyosababisha Adelina aweweseke kunielekea, na ikawa kama vile nimemsukumia upande wa kaunta nusu ajipige hapo. Kuna watu najua walianza kututazama sana, hata bartender, naye Adelina akaniangalia usoni kwa kutatizika. Nikapatwa na hisia mbaya baada ya kutambua nilichofanya, na mwanamke huyu akaangalia tu chini kwa ufupi, kisha akaniwekea funguo za gari langu ndani ya mfuko wa suruali na kuanza kuondoka sehemu hiyo. Aliondoka huku nikimtazama bila kuacha, nami nikarudiwa na utambuzi ulionifanya nitoke hapo pia ili niwahi kumfata.
Pombe niliyokunywa kabla sijaenda kwa Miryam kujumuisha na hii ya sasa ilifanya nihisi kulewa hata zaidi, kwa hiyo nguvu mwilini ilivutwa. Lakini nikajitahidi kutoka na kuanza kuelekea kule nilikoliona gari langu, na kwa hakika sikuweza kumwona Adelina upande huo. Nilipoangaza huko na kule, nikamwona mwanamke huyo akielekea sehemu ambayo angesimama ili kungoja daladala, na kiukweli hisia mbaya zikazidi kunipata. Sikumtendea kwa heshima. Akafika hiyo sehemu na kusimama pamoja na watu wengine, nami nikaelekeza hatua zangu huko kumfuata. Nilipomkaribia, aliniangalia kwa njia ya kawaida tu, hivyo nikajitahidi kuuweka utimamu kisawasawa ili nisiongee pumba na kumwomba samahani kwa kilichotokea.
"Adelina..."
Akanyanyua kiganja chake kwa chini kama kunizuia nisiendelee, halafu akatazama upande mwingine kuonyesha namna gani alikwazika.
"Adelina samahani... sija...." nikakosa hata cha kusema.
Inaonekana gari alilokuwa akilingojea likawa limefika, naye akaashiria kutaka kulifata lakini nikamshika mkono ili nimzuie.
"Adelina please... nisikilize..." nikamwomba.
"Niachie bwana JC..." akaniambia hivyo kwa kuudhika.
Konda alikuwa akisubiria tupande kwa kuona nyendo za Adelina, lakini nikamwambia, "Hatuendi bro. Tembea."
"Hauendi wewe, me naenda," Adelina akasema hivyo na kujaribu kuutoa mkono wangu kwake.
"No, hauwezi... bro tembeeni tu," nikasema hivyo nikiendelea kuukaza mkono wa Adelina.
Konda alikuwa akinitazama kwa hasira, eti namkosesha buku, na dereva wake akampigia kelele waondoke upesi, hivyo wakatuacha hapo nikimshikilia rafiki yangu bado.
"JC ni nini lakini? Si umeniambia nikuache, unataka nini?" Adelina akaongea kwa hisia.
"Nis.. nisamehe, samahani, unajua... unajua..." nikaishia tu hapo kwa kubabaika.
Akabaki kuniangalia kwa mkazo.
"Tafadhali... naomba uniendeshe. Ni.. siwezi ku... kuendesha ma... sisemi hauna budi, ni makosa yangu... najua... ila...."
Adelina akapiga ulimi kwa kuudhika na kisha kunishika mkononi, naye akaanza kuelekea upande tuliotoka kwa njia ya kunivuta. Na pombe juu lakini mpaka nilihisi aibu. Alinishika hivyo ili kuhakikisha tunavuka barabara kwa usalama, na baada ya kuvuka moja kwa moja tukaelekea kwenye gari langu. Nikampatia funguo, kisha tukaingia na safari kuanza.
Sikujaribu tena kumsemesha kwa kuwa niliona bado aliudhika. Na tena pombe yangu kichwani haikuwa nzito kunisahaulisha mambo kivile, lakini wenge nililohisi likanifanya hadi nisahau simu yangu ilikuwa wapi. Ndiyo nikamuuliza Adelina, nikimwambia mara mbili kwamba nimeimisi simu yangu, lakini wakati huu ikawa ni zamu yake kuninyamazia. Dah! Haya bwana. Nikaona nisitoe kero zaidi, kwa sababu wakati huu mimi ndiye niliyekuwa mkosaji. Nikatulia tu kwenye siti nisijue tulikoelekea.
β
β
Mwendo ulikuwa mrefu kiasi, na kuna mara ambazo ningetazama nje na kutambua kwamba tupo Kimara, Temboni, kuelekea kituo cha mabasi cha Magufuli Mbezi. Pindi nyingi tulisimama sana kutokana na msongamano, na baada ya muda ulioonekana kuwa mrefu tukaingia eneo lililoiacha lami na kusonga kwa dakika chache, kisha gari likatulia. Kichwani pombe ilikuwa imeanza kufifia ingawa bado wenge lilikuwepo, na nikaona Adelina akitoka ndani ya gari. Kuangalia mbele lilikuwa geti lisilopakwa rangi, likiwa la uchuma yaani, naye akaingia hapo na kisha kuanza kulifungua lote kutokea ndani. Sikujua ikiwa hapa palikuwa kwake ama vipi, lakini akarejea tena kwenye gari na kuliingiza ndani, kisha akashuka tena. Hakutaka kunisemesha kabisa.
Bwana, nikajiongeza tu na mipombe yangu kushuka pia, na yeye akiwa ndiyo anamalizia kulifunga geti. Nikapatazama hapo kuyaelewa mazingira, na mbele yangu ilikuwa ni nyumba yenye ukubwa mkubwa kiasi, iliyoonekana kuwa ya kupangisha watu. Millango kwa nje ilikuwa kwa pande mbili, hivyo nikafikiria lazima kuwe na mpangaji mwingine tofauti na Adelina hapo. Moja kwa moja nikaelewa huku palikuwa Kinyerezi, ambako mara nyingi mwanamke huyu alinisisitiza nije kumtembelea, na ni jambo ambalo nilikuwa nikimwahidi kufanya bila kulitimiza. Ona sasa mazingira yaliyokuwa yamefanya nikafika kwake kwa mara ya kwanza! Yalikuwa mabaya, na hilo likanitia huzuni.
Kumwangalia, Adelina akaja niliposimama na kunishika mkononi, naye akaanza kunielekeza kuelekea mlango ambao bila shaka ulikuwa wa ndani alikoishi yeye. Sikuwa na namna ila kuwa mtiifu tu, na aliponiachia ili anitangulie nikawa namfuata taratibu hadi alipofikia sehemu yenye ngazi kama mbili hivi, kisha akaufungua mlango huo. Sikujua ilikuwa saa ngapi, ila palikuwa kimya kweli kuzungukia eneo lote kutokea huko nje. Alipoufungua mlango akanishika tena mkono kunikaribisha ndani bila maneno, nami nikainama na mapombe yangu ili nifanye ustaarabu wa kuvua viatu kwanza.
"A-ah, usivue. Ingia tu."
Akanisemesha hatimaye. Nikasimama vizuri na kumtazama, naye akageuka na kuingia ndani kwa kusimama usawa wa mlango, halafu akawasha taa na kuendelea kusimama hapo hapo kama kusubiri nipite. Haikuwa na neno, nikapita. Ndani hapo palikuwa simple tu, masofa matatu ya samawati marefu na mazuri aliyoyapanga kwa kuzungukia kuta, zulia safi na laini chini, nikaona na friji, kiyoyozi cha juu na cha kuongoza kwa mkono pembeni, pamoja na TV pana ya flat screen, bufa, king'amuzi, na vitu-vitu vingine. Kulikuwa na mlango upande wa kushoto ambao ulikuwa wa jikoni, na upande wa kulia chumbani kwake bila shaka. Nikasimama hapo kati nikimwangalia Adelina alipokuwa akimalizia kufunga mlango vizuri, kisha akasogea mbele yangu na kuniangalia machoni.
"Unasikia njaa?" akaniuliza hivyo.
Nikatikisa kichwa kukanusha.
Yeye pia akatikisa kichwa mara moja na kuangalia pembeni, kisha akasema, "Sawa. Itabidi ulale hapo hivi, kwenye sofa, maana... kitanda ni kimo...."
"Haina shida Adelina," nikamkatisha.
Akiwa hataki kunitazama bado, akasema, "Sawa, basi... me naenda kulala. Upumzike pia, hapa hamna mbu... ukitaka nikuwashie na fe..."
"Adelina..." nikamwita kwa upole.
Akaacha kuongea na kunitazama kichini, si machoni.
Nikamwambia, "Adelina naomba unisamehe."
Akasema, "Ah, usijali JC, yashapita hayo achana nayo. Wote tumechoka kwa hiyo... usiku mwema..."
Alitaka na kuondoka lakini nikaushika mkono wake na kumgeuzia kwangu kwa nguvu kiasi, naye akatulia.
Nikiwa namwangalia kwa kujali, nikasema, "Adelina niangalie."
Macho yake hayakuwa mbali sana kuyafikia yangu sababu ya urefu wa mwili wake, lakini bado akaendelea tu kuniangalia kichini. Nikatumia kiganja changu kulishika shavu lake taratibu, naye ndiyo akanitazama machoni hatimaye.
"Nisamehe," nikaongea kwa upole na macho yangu lege.
Adelina hakutoa jibu kwa maneno na kuendelea kuniangalia tu, na kisha matendo yake ndiyo yakaongea. Akapitisha mikono yake kufikia mgongoni kwangu na kunikumbatia taratibu, akiusugua taratibu kama kuniambia nisijali, nami nikapata ahueni moyoni. Nikalirudisha kumbatio hilo na kisha kumwachia, nikimtazama usoni kwa uthamini. Tukiwa tumekaribiana zaidi namna hiyo, tukabaki kuangaliana kwa njia fulani ya subira; mimi nikingoja aseme jambo fulani, na nisijue yeye akingoja nini. Lakini kungoja kwangu aseme jambo fulani kukabadilika ghafla kutokana na kuanza kupatwa na hisia kumwelekea mwanamke huyu. Sikuwahi kumtazama Adelina kwa njia hii, ya hisia, ila sasa ikawepo. Sijui ni pombe tu, au ilikuwa moyo kabisa?
Nadhani hali ikawa namna hiyo hiyo hata kwake pia, kwa sababu baada ya kuangaliana kihivyo, nikahisi mkono wake ukipita ubavuni kwangu na kufanya kama kuishika T-shirt niliyovaa kwa kuivuta fulani hivi, nami nikauangalia mkono wake. Niliporudisha macho yangu usoni kwake, wakati huu ukawa tofauti na jinsi ulivyokuwa awali; si wa kuudhika tena, bali wa hisia. Ah! Hee. Ujumbe ukawa delivadi. Mimi nikiwa mzee wa kupandisha mizuka, sikuchelewa. Huko chini nikaanza kunyanyuka, kwa nguvu hatari, na hali hii ikaniongezea hamu ya kutaka jambo hili liendelee. Tukiwa bado tunatazamana kwa ukaribu, na Adelina akinishikilia ubavuni bado, nikajikuta naifuata midomo yake papo hapo na kuanza kuipiga busu. Mluzi!
β
β
β
β
β
β
β
β
β
β
ITAENDELEA
β
β
β
β
β
β
β
β
β
β
Whatsapp +255 678 017 280