Simulizi: Mimi na Mimi

Simulizi: Mimi na Mimi

Jc ,, kaacha kuendelea kupost hii story baada ya kuona kuna wahuni ,, wameichukua hii story bila ridhaa yake na kwenda kuipost huko Fasihinet.com

Kwa kweli wanaofanya hivi wanastahili kuchukuliwa hatua kali za kisheria kama inawezekna ,,, haiwezekani mtu anajipinda anaandika story wewe unakuja una copy na kupest sehemu nyingine na kujifanya wewe ndiyo mwandishi kwa kweli hiki si kitu kizuri kabisa
 
Umepata kuona mtu kapost kazi yangu huko? Nipe jina analotumia huko tafadhali
 
MIMI NA MIMI 3

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Siri, Tamaa, Hila, Usaliti, Ukatili, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA NANE

★★★★★★★★★★★★★

Stella na Deborah walishangazwa na jinsi nilivyonyanyuka namna hiyo nusu nimfanye mtoto adondoke, na msaidizi wa kazi akaja kwa mbele zaidi akiniangalia kwa umakini kiasi.

"Mamu, unamaanisha nini?" nikauliza kuielekea simu, ikiwa bado sikioni.

Mariam, akiendelea kupumua kwa presha upande wa pili, akasema, "Mimi sijui... tumekuta amelala chini... hapumui..."

"Ma' mkubwa yupi?" nikauliza.

"Ma' mkubwa Zawadi..." Mariam akasema.

Nikaingiwa na wasiwasi zaidi.

Stella akasimama, Deborah pia, naye akanisogelea huku akiuliza kwa sauti ya chini, "Nini?"

"Uko na nani Mamu?" nikaongea na simu.

"Niko na shangazi, mama mkubwa Jamila, mama Shabani, na Ankia amekuja. Ma..."

Kwa kuwa sikumjibu Stella upesi, aliendelea kusimama mbele yangu akinitazama kwa subira, na msaidizi wa kazi akataka kumchukua mtoto kutoka sofani lakini Evelyn akamgomea na kushuka, halafu akasimama karibu na mguu wangu kunishikilia. Nikamshika mtoto pia huku bado umakini wangu ukiwa kwenye simu, nami nikasikia sauti ya Ankia kutokea huko ikiuliza 'Ni JC?' naye Mariam akasema, 'Eeeh.' Kidogo tu ikaonekana kwamba Mariam alimpa Ankia simu, kisha...

"JC..." Ankia akasikika.

"Ankia, nini kinaendelea?" nikauliza kwa utulivu kiasi.

Stella akanionyesha kwa ishara ya kiganja kuwa alitaka kujua pia, nami nikaitoa simu sikioni na kuweka mfumo wa sauti ya juu kwa spika. Deborah akatusogelea pia.

"Bi Zawadi amepoteza fahamu! Sijui... yaani, sijui kama amepoteza fahamu au... hapumui, tunampepea lakini hapumui..." Ankia akaeleza kutoka simuni.

"Yuko chini?" nikauliza.

"Eeh. JC, tunatakiwa tumpeleke hospitali, Miryam tumemwambia anakuja kutoka kazini maana hamna usafiri wa.... eh Mungu wangu... sielewi tunafanyaje yaani..."

"Mapigo yake ya moyo yanadunda?" Stella akauliza.

Ankia akatulia kwanza, kisha akajibu, "Ndiyo... siyo kwa haraka lakini... yanadunda taratibu..."

Nikasema, "Ankia..."

"Abee..." akaitika.

"Unajua kufanya CPR?" nikamuuliza.

"Ndiyo nini?" Ankia akauliza.

Stella akaichukua simu yangu na kusema, "Chukua mto, uweke chini ya miguu yake, hakikisha inakuwa kwa juu kidogo. Yaani awe amelala chali, sawa? Halafu vishikanishe viganja vyako kwa pamoja, viweke kifuani kwake uanze kupampu... si umeshawahi kuona hiyo?"

"Kama madaktari wanavyofanya?" Ankia akauliza.

"Eeh ndiyo," Stella akasema.

"Jaribu Ankia, harakisha..." nikamwambia hivyo.

Ukimya ukafuata, ikionekana Ankia alianza kushughulikia ushauri wa Stella.

"Atakuwa na Asthma," Stella akaniambia.

"Sidhani. Sijawahi kumjua huyo mama kuwa na..." nikaishia hapo.

"Ni nani?" akauliza.

"Ni mama yake na... Miryam," nikamjuza.

Stella akatikisa kichwa kuonyesha uelewa na kuendelea kuniangalia.

"Ankia vipi?" nikauliza kuielekea simu.

Sikupata jibu upesi, zaidi zikawa zikisikika sauti za vitu kukwaruza na nini, kisha za wengine wakiongea hivi na vile kunifanya nitambue kwamba mmojawapo alikuwa Fatuma wa dukani. Labda huyo ndiye ambaye Mariam alisema ni mama Shabani.

Ndipo sauti ya Mariam ikasikika akisema, "JC, JC..."

"Eh Mamu, niambie..." nikaitika.

"Mama ameanza kupumua!" akasema hivyo.

Nikafumba macho kwa kuhisi ahueni, nami nikauliza, "Nini kinaendelea?"

"Ankia na shangazi wamemwamsha. Wamem... wamempa pumzi kifuani akazinduka..." Mariam akasema.

"Eh, afadhali..." Deborah akasema.

Sauti ya Ankia simuni sasa ndiyo ikasema, "JC... Bi Zawadi kaamka, ameanza kupumua tena."

"Ni bora. Anajisikiaje, yaani... ameweza kuongea?" nikauliza.

"Ngoja..."

Baada ya Ankia kusema hivyo kweli nikangoja kidogo, kisha...

"JC..." sasa ikawa ni sauti ya Bi Jamila aliyoita jina langu.

"Naam mama," nikaitika.

"Asante sana baba. Tunashukuru sana. Ankia amesema umemwambia jinsi ya kumsaidia Zawadi, jamani nashukuru," Bi Jamila akaongea kwa hisia.

"Hamna shida mama, usijali kabisa. Na... siyo mimi, ni daktari mwenzangu hapa ndiyo... ametoa ushauri mpaka... aam... nafurahi imefanikiwa," nikaongea kwa hisia pia.

"Mpe shukrani zangu sana," Bi Jamila akasema.

"Usijali mama, tuko pamoja eh? Mpe pole mama yetu, jitahidini kumfikisha hospitali na Mungu yuko pamoja naye atakaa sawa," Stella akaongea hivyo.

"Amen mwanangu. Nakushukuru sana," Bi Jamila akasikika.

"Yuko vipi sa'hivi? Anajisikiaje?" nikauliza.

"Tumemsaidia kupanda kitandani, amekunywa maji, anasema anahisi kizunguzungu tu kidogo kwa hiyo ametaka kulala kwanza. Tunamwangalia mpaka Miryam afike halafu tutaona inakuwaje..." Bi Jamila akaniambia.

"Sawa mama. Mwangalieni kwa ukaribu... ikiwa kuna badiliko lolote litajitokeza kabla... kabla Miryam hajafika, nipigieni tu. Sawa?" nikamwambia.

"Ubarikiwe baba. Asante sana," Bi Jamila akatoa shukrani.

"Amina," nikajibu.

"JC..." Ankia akasikika.

"Eeh, Ankia... unaonaje hapo? Bi Zawadi ana usalama kweli?" nikauliza.

"Naona yuko poa kidogo. Nahisi atakuwa alipandwa na presha labda, sijajua. Yaani tumeogopa!" Ankia akaeleza.

"Aisee..." nikasema hivyo na kupiga ulimi kiasi.

"Uko na nani sasa hivi JC? Nimemsikia mwanamke huyo anaongea... ni nani yako? Uko hospitali?" Ankia akauliza.

Stella akakunja uso kimaswali, nami nikasema, "Hapana, siko hospital. Ni daktari mwenzangu lakini. Uliweza kufanya CPR vizuri eh?"

"Tumejitahidi. Shadya kanisaidia na yeye angalau mpaka mama wa watu akaamka," Ankia akasema.

"Angalau. Basi sawa, kuna ishu namalizia kufanya hapa. Tutawasiliana. Kama utakuwa karibu, uniambie lolote likizuka pia..." nikasema.

"Nitarudi ndani, sa' kwa hiyo baadaye si unaweza tu kumwuliza Miryam hali ya Bi Zawadi, JC?" Ankia akasema hivyo.

Nikatulia kidogo, Stella akinikazia macho bila kuacha, nami nikasema, "Sawa. Mwachie pole yangu Mamu pia, mwambie asiwe na hofu tena, eh? Ma' mkubwa wake atakuwa sawa," nikamwambia hivyo.

"Haya, asante. Baadaye," Ankia akaaga.

Hatimaye nikaishusha simu, na hapo ndani macho yote yalikuwa kwangu.

"Aisee, tsk... dharula hizi," nikasema hivyo.

"Hmm imetia huruma kweli, kuwasikia hao wanawake walivyokuwa wanahangaika hapo! Mama wa watu atakuwa alipandwa na presha eti?" Deborah akasema hivyo.

"Inawezekana. Sijui yaani, ni mwanamke mwenye nguvu, sijawahi kumwona hata akiumwa, kwa hiyo... nimeshangaa," nikasema hivyo.

"Na ndiyo huyo Ankia anaanza kukuuliza mpaka uko na mwanamke gani? Anataka kujua ili ampe taarifa Miryam eti?" Stella akaongea kikejeli.

Nikalikalia kimya swali lake na kumnyanyua Evelyn kumbeba.

"Miryam ndiyo mtoto wa huyo mama aliyezidiwa?" Deborah akauliza.

Kwa jinsi alivyouliza hivyo ilionyesha tayari alikuwa na ujuzi fulani kuhusiana na Miryam, labda kutoka kwake Stella, nami nikamjibu, "Ndiyo, ni mama mkubwa wake. Wanaishi pamoja."

"Ahaa... bora, Mungu amesaidia lakini," Deborah akasema.

"Sijui ingekuwaje kama angeacha kupumua kwa muda mrefu, ikiwa wasingekupigia sa'hivi, kesho zingekuwa taarifa zingine. Siyo kwamba naombea mabaya," Stella akasema.

"Ni kweli, uko sahihi. Asante Stella... kwa ulichokifanya kumsaidia," nikamwambia hivyo kwa upole.

Stella na Deborah wakaangaliana na kutabasamu kiasi, naye mama wa mwanangu akasema, "Usijali. Twendeni tukale sasa, usije ukachelewa kwenye C-section zako."

Aliongea kwa njia ya utani kidogo, nami nikatabasamu tu na kuwaruhusu wanawake wanitangulie mbele kuelekea meza ya chakula, huku mimi nikifuata na mtoto. Ingawa hali ya utulivu ilirejea tulipoanza kupata chakula kizuri pamoja, bado ishu ya Bi Zawadi ilizunguka sana kichwani. Nilikosa amani kufikiria ni nini ambacho kilimsababishia yule mama tatizo hilo la ghafla sana, na wazo la matatizo yetu ya kifamilia kuwa chanzo halikuwa mbali sana. Ikiwa ni hivyo, basi sote tulimtia mkazo mbaya sana mama yule, huenda ukimwamshia hata liugonjwa kwa kuwa alisumbuliwa na hali iliyoendelea baina yangu, Miryam, na familia zetu; hususani mimi kuachana na binti yake. Kwa hiyo kwa hapo ningehitaji kufanya jambo fulani kuhakikisha hali haiwi mbaya zaidi ya jinsi ilivyoonekana kuwa.

★★★

Jumanne ikafika. Usiku uliotangulia baada ya kumaliza mlo mtamu kwake Stella, nilikaa kama nusu saa zaidi kucheza kwa muda mfupi na mwanangu na kisha ndiyo nikaelekea hospitali kufanya niliyohitaji kabla ya kujipumzisha kidogo. Na Evelyn hakutaka nimwache kabisa kwa hiyo wakati nikiondoka alinililia kwa hisia mno. Upendo aliokuwa nao mtoto kunielekea ulinipa amani sana, jumuisha na mambo yaliyokuwa yameanza kwenda vizuri kwangu na Adelina pia, lakini bado upande wangu wa hisia uliokuwa na matatizo yake ulinitekenya mara kwa mara, kwa njia mbaya yaani, hasa baada ya tukio la usiku huo kuhusiana na Bi Zawadi.

Asubuhi hii nilipoanza baadhi ya kazi zangu niliweza kupata taarifa za mwanamke huyo, kupitia Tesha. Tumeongea kwa simu akanifahamisha kuwa alifika nyumbani saa sita usiku hivi na kukutana na hali yenye huzuni, na dada yake alikuwepo pia akisisitiza wampeleke mama mkubwa wao hospitali. Bi Zawadi, baada ya kuamshwa ili apelekwe hospitali, hakutaka kuondoka kwa muda huo akisema hali yake si mbaya sana, na kama ni hospitali basi wangekwenda wakati mwingine. Kimtazamo, waliona mama huyo alijitahidi kujikaza ila ni wazi hakuwa na nguvu za kutosha, kwa hiyo Tesha akaniambia walilazimika kumtoa kwa ulazima ingawa aliwapinga. Usiku huo huo wakampeleka hospitalini, na ndiyo wakagundua kiwango cha sukari kwenye mwili wa Bi Zawadi kilikuwa kimeshuka.

Iliwashangaza wengine kwa sababu Bi Zawadi hakuwahi kupatwa na matatizo ya sukari, lakini kwa maelezo ya daktari aliyempima inaonekana mwanamke huyo alikabiliwa na mkazo mbaya usiojionyesha, kwa sababu ya mawazo, na kwa wiki hizi chache hakuwa akila vizuri. Kuna vyakula ambavyo mwili wake ulizoea, na alivipendelea, ndiyo sababu haikuwahi kuonekana ana tatizo lolote kabla ya jana kwa kuwa kwa sasa kiwango cha ulaji wake kilipungua na presha ya huo mkazo ndiyo ikamjia vibaya mpaka kumfanya apoteze fahamu. Na kama jana Mariam na wengine wangechelewa basi madhara yangekuwa makubwa zaidi.

Kwa hiyo wakampatia dawa, hapo hapo hospitali na za kutumia nyumbani kwa majuma kadhaa, na angetakiwa kuanza kutumia sukari na vyakula vyenye sukari kwa ukawaida kila siku mpaka haii yake itulie. Na la muhimu hata zaidi ingetakiwa ajitahidi kuondoa msongo, endapo kama kuna jambo lilimhangaisha sana basi wapendwa wake wamsaidie kulidhibiti lisimnyime afya njema. Kwa kweli ishu ya Bi Zawadi ilinigusa mno, hasa nikikumbukia namna ambavyo huyo mama alinipenda sana tokea siku ya kwanza nimefika huko kwao. Na naelewa chanzo cha afya yake kuyumba ilikuwa mkazo wa matatizo yangu na Miryam, kwa hiyo ilikuwa muhimu mimi pia nihusike kumsaidia zaidi kudhibiti hali yake isiwe mbaya.

Tesha alinijuza kwamba ndugu zake wangekaa na mama mkubwa wao kusubiri amalizie dawa za maji alizotiwa, na baadaye angeruhusiwa kurudi nyumbani. Nikatumia muda mfupi kumsalimia mama huyu kwenye mida ya saa sita mchana, kupitia simu yake mwenyewe tukaongea kwa njia nzuri kabisa, na alionyesha kufurahi kweli mie kumjulia hali. Nikamwambia nikipata nafasi ndefu ya kutoka kazini ningekuja huko kumtembelea, naye akaniomba niifanye hiyo kuwa ahadi isiyovunjika kwa kuwa alinikosa sana. Alihitaji sana kuniona, akisema anahisi angekuwa sawa kabisa nikienda. Kwa hilo nikamwambia asiwe na shaka, na ndiyo tukaagana nikiwa nimejisikia vizuri zaidi.

Ambacho kingefuata ingekuwa kuendelea na kazi, na nikapanga ratiba mapema ya muda ambao ungefaa kuondoka na kurejea haraka pia bila kusababisha hitilafu kwa wagonjwa; nikimpanga daktari mwenzangu mwingine ajaze sehemu yangu mpaka nikirudi. Hakungekuwa na utata.

★★

Piga kazi, piga kazi, dirisha dogo la kunipa nafasi ya kuondoka likapatikana saa kumi na mbili jioni. Na hata sikuwa nimepata wagonjwa wengi mno kwa leo, sanasana kuangalia haii za waliolazwa na wachache waliohitaji vipimo, sindano, na dawa, kwa hiyo nikaondoka muda huo kuelekea Mbagala. Niliamua kubeba kifaa fulani maalumu cha kupima kiwango cha sukari, ambacho nilitaka kwenda kumwachia Bi Zawadi endapo kama hakupatiwa huko hospitali, pamoja na dawa za virutubishi muhimu mwilini. Kiukweli, nilijitahidi kuiweka akili yangu sawa, kwamba hapo ningeenda kumsalimia mgonjwa, na siyo kufanya biashara zingine. Ya kutarajia yangekuwa mengi lakini sikutaka kuyakazia fikira hata kidogo. Lengo lingekuwa moja, kumwona Bi Zawadi, basi.

Nikiwa njiani, Simba akanipigia, naye akasema ndiyo alikuwa kwenye daladala kutokea Mbezi kwenda Makumbusho, ili arejee huko nyumbani kwangu. Nikasema sawa, mimi nilikuwa na shughuli nyingi kama kawaida kwa hiyo tungeonana wakati ambao tungeonana tu; sikujua kama ningerudi nyumbani kabla ya Jumapili. Alikuwa na funguo ya ziada ya pale kwangu kwa hiyo asingepata shida, na akasema alikuwa na mambo mengi ya kuzungumza pamoja nami kuhusu unyama waliofanya na rafiki yetu huko Segerea. Nilipoagana naye, nikamtumia Adelina ujumbe wa salamu na viemoji vya upendo, lakini sikupata jibu upesi. Nikajua alikuwa bize, kwa hiyo nikakaza mwendo mpaka kufanikiwa kuifika Mzinga ikiwa imeingia saa moja jioni.

Baada tu ya kuifikia nyumba yake Miryam, nikatulia kidogo ndani ya gari nikiwa nimerudiwa na kumbukumbu za kilichotokea mara ya mwisho nimefika hapo. Alivyoongea. Niliyoongea. Festo. Na tena kuwaza tu hilo jina kukanikumbusha ni namna gani kulikuwa na mambo mengi yasiyofaa asiyojua Miryam kumhusu mtu huyo, lakini haikujalisha tena. Alitaka kusonga mbele, na mimi nilikuwa nimeshaanza kusonga mbele pia. Ikiwa ningemkuta huko ndani sasa hivi, sijui ningetendaje kumwelekea, lakini sikupanga kukaa kwa muda mrefu na sikutarajia kumkuta kwa kuwa nadhani bado alikuwa huko kazini kwake kwa mida hii. Kwa hiyo ningejitahidi kuwahisha lengo lililonileta hapo na kuondoka.

Basi, nikashuka kutoka garini na kulikaribia geti. Duka la Fatuma lilikuwa wazi lakini hakuwemo, na nje hakukuwa na watu, hivyo nikagonga mlango wa geti na kungoja. Hazijapita sekunde nyingi na mlango huo ukafunguka, sura ya kwanza kuiona hapo ikiwa ni ya binti Mariam.

"JC!"

Mariam akaniita kwa shauku na kunisogelea upesi, akinikumbatia kwa furaha. Nikarudisha upendo wake pia, naye aliponiachia akaushika mkono wangu kunivuta tuingie ndani pamoja. Ni baada tu ya kuingia hapo ndani ya geti ndiyo nikaona kwamba gari la Miryam lilikuwepo, na wanafamilia wachache walikuwa wameanza kutoka pale ndani kuja upande wangu. Alitangulia Shadya, akafuatia Bi Jamila, Ankia, Fatuma, na mama Chande yule, kisha bibie Miryam mwenyewe akatoka pia. Mimi na Mariam tukasimama usawa wa gari lake bibie, nikiwa namwangalia Miryam alipotoka mlangoni huku akishikiza mkono wake kwa Bi Zawadi aliyetembea karibu yake huku akitabasamu. Nikafurahi sana kumwona mama huyo, ingawa tabasamu langu lilikuwa hafifu tu, na Mariam akanisogeza karibu zaidi kama kunikutanisha na wengine.

"Woooow!" Ankia akasema hivyo na kunikaribia.

Tukakumbatiana, nami nikamwambia, "Mambo?"

Akaniachia na kusema, "Safi. Karibu. Unazidi tu kuwa handsome."

Wengine wakacheka kidogo.

"Ahah... asante. Mama shikamoo?" nikamsemesha Bi Jamila kwa ustaarabu.

"Marahaba baba. Karibu," Bi Jamila akaniambia hivyo huku akitabasamu kiasi.

Nikamwangalia Bi Zawadi, huku jicho likiona namna ambavyo Miryam alishusha macho yake chini tu, nami nikasema, "Shikamoo mama?"

"Marahaba. Hebu kuja hapa," Bi Zawadi akaniambia hivyo.

Nikamsogelea karibu zaidi na kumkumbatia, Miryam akijisogeza pembeni kidogo, naye Bi Zawadi akasema, "Nimekumiss sana mwanangu."

"Mimi pia," nikamwambia hivyo.

"Za huko?" Bi Zawadi akauliza.

"Salama tu," nikamjibu.

"Mama hajambo?" akauliza tena.

"Mzima wa afya," nikamwambia.

Wengine wakawa wakituangalia kwa subira, Ankia akiwa amesogea karibu na aliposimama Miryam, nami nikamwachia Bi Zawadi na kuanza kumwangalia kwa udadisi.

"Mh... cheupe una uhakika unaumwa? Mbona uko fire sana?" nikatania.

Bi Zawadi na wengine wakacheka kidogo, naye Shadya akasema, "Yaani ile jana ungemwona! Ilikuwa kama fire kabisa."

Nikatabasamu kiasi na kumwamkia Shadya pia, naye akaitikia vizuri. Nikawasemesha na wengine pia kwa salamu, ndipo macho yangu yakawa hayana budi kumtazama na Miryam. Alikuwa akiniangalia, lakini hapo tu nilipomtazama ndiyo akashusha macho yake na kuangalia chini. Nikaona Ankia akimbonyeza bibie kwa nyuma sijui, na macho ya Miryam yakacheza huku na huku kwa njia iliyoonyesha wasiwasi. Najua wote walikuwa wanasubiri kitakachofuata kuelekea sisi wawili, nami nikaamua kuondoa utata.

Nikiwa namtazama kwa njia ya kawaida tu, nikasema, "Za saa hizi?"

Miryam akaniangalia usoni, kwa sekunde chache nikiona hali fulani hivi mpya kutokana na namna alivyonitazama. Jibu lake kwa salamu yangu likakawia, na ile nimeona anataka tu kuitikia, nikaacha kumwangalia na kumtazama Bi Zawadi tena.

"Nimekuletea zawadi cheupe wangu," nikasema hivyo huku nikimwonyeshea kimfuko nilichoshika.

Niliweza kuona namna Miryam alivyoishia hewani baada ya mie kumkwepa upesi, naye akashusha macho kwa kubabaika kiasi.

"Zawadi gani baba?" Bi Zawadi akaniuliza.

"Dawa," nikamwambia.

"Aaah..." Bi Zawadi akafanya hivyo, kitu kilichofanya wengine wacheke kidogo.

"Sa'hivi utakuwa mtu wa dawa tu mama, mpaka kieleweke," akasema hivyo Fatuma.

"Na unavyojua jinsi sipendi za hospitali... JC umeniletea mateso zaidi," Bi Zawadi akatania.

Nikatabasamu kiasi, naye Mariam akatoka upande wangu na kusogea karibu na dada yake.

"Karibu ndani baba... utakuwa umechoka na kazi, karibu ndani ukae kidogo," Bi Jamila akaniambia hivyo.

Nikatulia kidogo kwanza, nami nikasema, "Haina shida, nime... nilitaka tu kumwona cheupe kidogo nimwachie na hizi, halafu..."

"JC nawe unawahi wapi?" mama Chande akanikatisha.

"Bado kulikuwa na kazi kazi, yaani nimezitelekeza kidogo tu, ila natakiwa niwahishe," nikamwambia.

"Me nilitaka ukae bwana... tumekumiss," Bi Zawadi akasema.

Niliona namna ambavyo Shadya, Bi Jamila, Ankia, na Mariam walimwangalia Miryam kwa hisia na kunitazama pia kuonyesha uelewa wa hali yenye utata iliyoendelea hapo. Sikutaka kuingia ndani kwa sababu ya Miryam, na ni wazi yeye alilitambua hilo.

Nikamsogelea Bi Zawadi tena nikimkumbatia na kusema, "Nimekumiss sana pia."

"Si ndiyo uingie ndani sasa, ukae tule na mastory?" Fatuma akaniambia.

"Labda wakati mwingine dada. Ona... najua umeshapewa dawa, ila kuna hizi unaweza kutumia pia kuongeza virutubisho muhimu kwenye mfumo wa insulini," nikamwambia hivyo Bi Zawadi.

"Ndiyo nini?" akauliza kwa hofu.

Wengine wakacheka kidogo, nami nikamwambia, "Kinachosaidia mambo ya sukari mwilini yaani. Itakuwa nzuri kwa ini lako pia, na... unaweza kutumia pamoja na mama, itakuwa nzuri kwenu nyote."

Nilimaanisha Bi Jamila, naye akasema, "Sawa mwanangu, asante sana."

Nikazitoa chache na kuanza kuwaelekeza jinsi ya kuzitumia, dawa pamoja na kile kifaa, na kwa sekunde chache nilitambua Miryam alikuwa akiniangalia kwa hisia makini, lakini sikujali tena kumtazama.

Nilipomaliza, Bi Zawadi akauliza, "Sasa utarudi lini tena kututembelea? Hivi umekuja kugusa tu na kupaa."

Nikatabasamu kiasi na kusema, "Tutaangalia na ratiba. Ikiwa itawezekana, tunakutana sehemu kuonana... kama mambo yakiwa yamebana sana."

"Kwa nini isiwezekane sasa? Na hapa ni nyumbani JC, unakuja muda wowote yaani, siyo kuonana kwingine..." Bi Zawadi akaniambia.

Nikajitabasamisha tu na kuangalia chini.

"Ndo' hataki hivyo..." Shadya akasema kiutani.

"Hamna, siyo hivyo. Naahidi tutaonana tu tena, ni suala la mipango," nikawaambia.

"Jamani..." Bi Zawadi akasema.

"Inabidi niwahi, kuna wagonjwa kama wote yaani wanahitaji japo kuona kasura kangu ili wapone," nikatania.

Mama Chande na Fatuma wakacheka kimbea kidogo, huku wengine wakitabasamu isipokuwa Miryam, naye Bi Jamila akaniambia, "Haina shida baba, wahi tu kazini. Tumefurahi sana kukuona leo."

"Yeah, sana," Bi Zawadi akasema.

"Sisi wote tumefurahi," Ankia akasema hivyo na kumshika Miryam begani kunipa maana fulani hivi.

Nikamtazama tu Mariam na kumwambia, "Nitakupigia Mamu tuongee kidogo, eh? Naona ushakuwa mjuzi wa simu siku hizi."

"Ujuzi mbona upo tokea muda?" Mariam akasema hivyo.

"Okay. Hatusemi, hatusemi..." nikamwambia hivyo huku nikinyanyua mikono kama kujihami.

Wengine wakacheka kidogo, naye Mariam akasema, "Nipigie kesho."

Nikamwambia, "Sawa dear. Broop."

Nilimwonyeshea kutetemesha vidole kwa mbali, naye Mariam akaiga na kusema, "Broop."

"Ma' mwenye nyumba... nitakucheki," nikamwambia Ankia.

Akaninyooshea kidole kama kukanya kimasihara na kusema, "Ole wako uache."

Nikatabasamu na kuwaambia wengine, "Me ngoja niwaache sasa. Panapo majaliwa tutaonana."

Kwa pamoja wakasema haya, sawa, ufike salama, isipokuwa Miryam pekee. Ukimya na utulivu wake mpaka ungemfanya mtu afikiri hakuwa hapo, nami nikamwangalia kwa ufupi. Aliponitazama, nikabana mdomo kiasi na kutikisa kichwa mara moja kama ishara ya kumuaga yeye, na hapo hapo nikaacha kumwangalia na kugeuka. Ni wakati tu nageuka jicho lilikamata mjongeo wa mwili wake Miryam kama anataka kuja upande wangu, lakini ilikuwa kwa msukumo ulionielewesha kwamba ni Ankia ndiye aliyemfanyia hivyo. Inaonekana alikuwa akishawishiwa kujaribu maongezi nami, labda anifate, lakini nikapuuzia kabisa hilo na kuendelea kuondoka mpaka kuingia garini.

Nikatulia kwa ufupi nikitafakari hali hiyo yote, kidogo mapigo yangu ya moyo yakifanya riadha kutokana na hisia za majuto. Yaani kwa nini nilikuja hapo tena? Kuna hali mbaya tu ya moyoni inakuwepo japo kihalisi sikutaka kabisa kuiendekeza. Na haikuwa na maana tena. Kilichonileta nilikikamilisha, hivyo nikawasha gari na kuondoka huko nisiwe na mpango wa kurudi tena. Maisha yangetakiwa kusonga tu hata kama mapito yalikuwa karibu nami sana.

★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★

Whatsapp +255 678 017 280
 
Mwamba Elton, ingefaa ukatupia nyingine leo, tumekaa sana kusubiri hii
 
Broop! 👍
 
SEHEMU YA TISA

★★★★★★★★★★★★★

Siku ikaja mpya, Jumatano. Baada ya kuondoka huko Mzinga hiyo jana nilipotoka kumwona Bi Zawadi, moja kwa moja nilielekea hospitalini tena kuendelea na majukumu. Hakukuwa na longolongo lolote, kazi ziliendelea tu mpaka mida ya saa tano ambapo Adelina alinitafuta hatimaye kujibu ujumbe wa salamu niliomtumia awali. Kiuhakika alikuwa amebanwa na kazi sana jana na alichoka, akitoka huko kazini kwake baada ya kumaliza masaa ya ziada. Kwa hiyo nilimsihi tu apumzike, na huenda leo tungeonana kwa kuwa ningeweza kupata mbadilishano wa zamu na daktari mwingine ambaye angefanya kazi kwa upande wangu kuanzia jioni.

Sasa ikiwa ni alfajiri tu, baada ya kuamka na kujiweka safi kuelekea jukumuni, simu yangu ikaita, na baada ya kutazama mpigaji nikatulia kidogo. Ni kutotarajia kabisa kwamba askari Ramadhan angenipigia, siyo kwa sababu ya muda, bali kwa kukumbukia mambo mengi tuliyopitia wiki chache nyuma. Mwanaume huyo alinisaidia kwa vingi, na hasa kwa sababu vingi hivyo vilihusisha mambo mabaya, mwito wake kwangu sasa ukaniwekea hali makini. Hakuwa amenitafuta wala mimi kumtafuta tokea mara ya mwisho nimeongea naye kuhusiana na mdogo wake yule madam Bertha, aliyeitwa Beatha, hivyo udadisi wa akilini juu ya nini angetaka kuniambia wakati huu ulikuwa mwingi.

Nikapokea, na upande wa pili sauti yake Ramadan ikasikika akisema, "Hallo..."

"Yeah, kaka... habari?" nikajibu.

"Safi. Za siku?"

"Mungu anasaidia. Vipi wewe?"

"Kwema kabisa. Mambo yamekaaje huko kwenu?"

"Ah, kwa kipindi hiki mambo mengi yamebadilika ndugu yangu. Nilishatoka kule, sasa hivi niko Muhimbili," nikamwambia.

"Oooh, umerudi hospitali?"

"Ndiyo, likizo imeisha..."

"Okay..."

"Vipi harakati za usalama zinakwendaje?"

"Bomba tu."

"Eti eh? Mission mission kama zote mnamaliza bila shida kabisa?"

"Ah, hamna. Pamepoa sana sasa hivi toka tulipomalizana na yale ya Bertha, ndiyo maana nikaona nikucheki tujue kama umepata mkate mpya uturushie..."

"Ahahahah... hamna, hata mie kwa upande wangu ni utulivu tu sa'hivi," nikamwambia.

"Mwezi umepita sasa, nimeona nikusalimie kijana wetu wa faida," akaniambia hivyo.

Aliongea kwa njia iliyoonyesha hakukuwa na lolote zito, nami nikasema, "Asante mkubwa. Ila alfajiri yote hii, mwanzo nikadhani kuna case mpya."

"Haapana... ni kujuliana hali tu. Ulitusaidia sana kwa zile ishu, we' ni kama comrade hapa," akasema hivyo.

"Asante sana," nikamwambia.

"Basi, tutawasiliana wakati mwingine, ni vizuri kujua uko poa. Wasalimu familia," akaniambia.

Nikasema, "Sawa sawa. Halafu hivi, kuna na...."

"Ndiyo?" akaitikia.

"Ile ishu nilikwambia kuhusu mdogo wake Bertha..." nikamkumbusha.

"Ooh, sawa. Yule mweupe... uliniambia anaitwa...."

"Beatha."

"Sawa. Ndiyo, tulifanya research kuwahusu, na inaonekana hilo siyo jina lake," akaniambia hivyo.

Nikawa makini zaidi.

"Huyo mdogo wake Bertha anaitwa Tamiah Celestine. Hiyo Celestine ni surname yao wote, na wametoka kwa watu wa ukabila fulani wa huko Kenya," akaniambia hivyo.

Nikashangazwa kiasi na taarifa hii, nami nikamuuliza, "Unataka kusema Bertha alikuwa mkenya?"

"Ni watu wa huko, ukoo yaani, wenyewe wamezaliwa Tanzania na sijui sana kama walikuwa na uhusiano na wanaukoo wao, ila hawa wawili wamezaliwa na mwanamke mtanzania," akasema.

"Kwa hiyo ni kusema baba yao, ukoo wa baba yao... ndiyo wa huko nje?"

"Ndiyo. Detail zao nyingi zipo derailed, kwa mambo aliyofanya Bertha huku na wenzake hayakuhusiana na familia yake iliyo huko nje..."

"Wanaukoo wake wapo Kenya?"

"Kwa inavyoonekana, ila sina uhakika. Hakuwa na tie zozote na watu hao."

"Aliwahi kuniambia alipofungwa jela hakutaka wazazi wake na familia ijue kuhusu hilo, nilichukulia ni huku huku Tanzania. Labda alimaanisha wa huko Kenya," nikamwambia.

"Tutajuaje? Hakuna chochote kinacho-suggest kwamba alikuwa na mawasiliano na watu wa huko, na hata huyu Tamiah tumemcheki ila haonekani kujihusisha na biashara alizokuwa akifanya dada yake," akaniambia hivyo.

"Kabla Bertha hajafa kalinifata kunionya kabisa... kana ule moto kama wa dada yake, sikuona ni busara kumchukulia easy maana you never know... wanaweza kuwa na ishu zao mahala pengine na njia tofauti na zile tulizotibua," nikamwambia.

"Ahah... uko makini sana JC. Yote unayosema ni kweli, lakini kama nilivyokwambia... hatujaona lolote tena. Huyo Tamiah... mara ya mwisho najua alikuwa spotted huko Arusha... anasoma, kwa pesa za dada yake. Siyo muda mrefu atasahau yote hayo na kugeuka jiko la mtu huyo. Kama walikuwa na mipango wamebakiza kufanya, sa'hivi imeshindikana tena maana wameogopa tulipoporomosha himaya zao. Kwa hiyo usiwaze. Vile vitisho na nini... chukulia kama upepo tu, havitakuumiza..." akaniambia hivyo kiuhakika.

"Tamiah..." nikasema hivyo kwa sauti ya chini.

"Usimuwaze sana, yaani sasa hivi yale mambo yote yameshakufa na Bertha, tunaangalia vingine," akaniambia.

"Sawa sawa mkuu, asante sana. Hujaacha kuwa baraka kwangu," nikamwambia.

"Hah... kama wewe tu. Take care, wacha tuingie kazini," akaniambia.

"Likewise," nikamjibu kwa kuaga.

Simu ikakatwa, na kwa sekunde chache nikatafakari mazungumzo hayo mafupi niliyofanya na askari huyo. Uhakika alionipatia kuelekea suala la Beat... oh, hapana. Ni Tamiah. Jina la mdogo wake Bertha ndiyo lilikuwa hilo, ikiwa ni mara ya pili napata kujua kwamba majina yake niliuofahamu mwanzo yalikuwa ya uwongo. Hii ilikuwa sababu tosha kunifanya nihisi kwamba kuna kitu zaidi kilifichika kuelekea mwanamke yule, tofauti kabisa na mambo yote askari Ramadhan aliyonijulisha leo hii. Ingeonekana kama upepo wa Bertha kwenye bahari ya maisha yangu ulikuwa umekatika, lakini bado sikuwa na uhakika wa kutosha kama upepo wa Tamiah ulitoweka kabisa. Ulianza kidogo siku ambayo alinisemesha kwa kitisho, na ungeweza kugeuka kuwa mkubwa na kusababisha dhoruba kali sana kwenye maisha yangu wakati ambao nisingetarajia. Nilikuwa mpaka nimeshaanza kuyaweka pembeni kabisa mambo hayo baada ya kifo cha Bertha, lakini sasa ningejitahidi kutafuta mwanga zaidi juu ya huyu Tamiah ili niondoe hasara yoyote ambayo angeweza kuniletea; endapo kama ingekuwa hivyo. Hii tunaita tahadhari kabla ya hatari.

★★

Basi, kazi zikaanza, taratibu muda ukisogea mpaka kwenye saa sita mchana nikapigiwa simu na mama. Akanijulisha kuhusu Stella, akisema aliongea naye jana na kuhisi furaha yake baada ya mimi kuanza kumhudumia mtoto na hata kwenda kwake, na ni jambo ambalo lilimpa furaha mama pia. Ushauri wote aliokuwa amenipatia kuhusiana na hilo sasa akaona umezaa matunda mazuri, na akaomba nafasi ikipatikana tuje tukutane wote kwa pamoja nyumbani kufurahia ushirika na mwanangu Evelyn. Nikamwambia ningeutafuta muda huo, na siku siyo nyingi tungeonana kutimiza hilo.

Maongezi yalipoingia kwenye kujua hali zetu binafsi zilikuwaje, mama akataka kujua endapo kama nilishaongea na Miryam kwa lolote tena lililohusiana na zile ishu zilizozuia mipango ya ndoa, na ndiyo nikawa nimemtaarifu kwamba kwa sasa hatukuwa pamoja, wala kufikiria kuwa pamoja tena maana tuliachana kwa urasmi. Nikamwambia hatukuhitaji kuongelea chochote zaidi maana Miryam alitaka kusonga mbele, na mimi tayari nilikuwa nimeshaanza kusonga mbele pia, kwa hiyo yale yote yangebaki kuwa historia.

Mama alifikiri kwamba kuna sehemu ndani yangu bado iliumizwa sana na haya yote na akataka nije niende tuongee kwa mapana zaidi, lakini nikamwambia hilo halikuwa na haja kabisa. Kuwa sawa nilikuwa sawa, na ningeendelea kuwa sawa zaidi kwa kutojilazimu kurudi-rudi nyuma kuyaangalia hayo tena. Kwa hilo akasema haikuwa na shida, na kwamba kwa wakati huu alijihisi yuko sawa hata zaidi kuja kuzungumza na mama mkubwa wa Miryam, Bi Jamila, kuhusu yaliyopita, na akiwa anataka kusawazisha hali baina ya familia zetu iwe nzuri. Jambo hilo likaonekana kuwa jema sana kwangu, nami nikamwambia tungepanga kuja kuonana na mwanamke yule ili kwanza afanye maongezi naye, halafu baadaye familia kiujumla. Amani na mpangilio mzuri ungefuata bila shaka.

Baada ya kumaliza maongezi na mama, nikawa nataka kwenda kupata chakula kwanza maana asubuhi yote sikuwa nimetia chochote tumboni, lakini ni hapo hapo tu Ankia naye akawa amenipigia. Nikapokea, na baada ya kujuliana hali mwanamke huyo akafanya maongezi kuhusu jinsi nilivyofika pale kwao jana kumsalimia Bi Zawadi ndiyo yawe dhumuni kuu la kunipigia. Ankia alitaka kujua ni kwa nini nilitenda kwa jinsi nilivyotenda kumwelekea Miryam. Mh? Nikamuuliza alimaanisha nini, naye akasema nilimtendea vibaya kwa kutomsemesha na kumwacha akijisikia vibaya sana.

Alikuwa akinilalamikia yaani, kwamba Miryam aliishiwa raha kabisa kwa sababu yangu, nami nikamwambia Ankia ishia hapo hapo. Alitaka niongee nini na yule mwanamke? Nilikuja kwa ajili yake ama Bi Zawadi? Na kumsemesha, sikumsemesha? Alikuwa anataka nimbebe au hayo mawazo Ankia alikuwa anayatoa wapi? Nikamwambia Ankia kama amenipigia kunitibua ni bora akate simu na asinipigie tena ikiwa hana jambo lingine la kusema. Ndiyo akaanza kuja chini et ooh... siyo hivyo, nilimwonea tu huruma, hakusema chochote lakini yeye ni rafiki yangu namwelewa.

Nikamwambia sikufanya chochote kibaya pale, labda kama kibaya kwa Miryam ilikuwa mimi kufika hapo kwake, ndiyo sababu sikutaka hata kuingia ndani. Nikamweleza kwa ufupi kwamba mawazo ya namna hiyo hayakufaa, kwa yeye Ankia, kwa sababu tayari Miryam aliweka uamuzi wake mbele ya watu wote kuhusu mahusiano yetu wiki chache nyuma, na ni kwamba tumeachana, sasa sijui angekuwa na matarajio yapi kwa sasa hivi tena wakati alinibwaga yeye mwenyewe. Mimi hata kujenga hali ya urafiki na Miryam sikufikiri ni jambo ambalo lingewezekana, kwa hiyo nikamwomba Ankia aweke hizo mada pembeni kabisa; akitaka tuongee mambo, yawe mambo yaliyonyooka. Akawa anaguna-guna tu na kusema sawa, ila ikitokea nafasi ya mimi kuongea na Miryam, eti nisikwepe maongezi na nijaribu kumsikiliza mwanamke huyo.

Ankia alinishangaza kwa kweli, ni kama vile alikuwa akitaka kusema jambo fulani hivi, lakini akajizuia, mpaka nikahisi labda hapo aliweka simu kwa mfumo wa sauti ya juu na Miryam mwenyewe alikuwa pembeni yake, kwa hiyo nikaamua tu kumuaga na kukatisha mazungumzo hayo. Yaani nilikuwa nimetoka tu kwenye hali ya amani baada ya kuzungumza na mama halafu Ankia naye akaja kunivutugia mambo. Sasa mimi na Miryam kwa wakati huu tuongelea nini? Tuanze kuongea na kujichekesha kinafiki utadhani hakukuwa na damu mbaya kati yetu, ndiyo walitaka hivyo? Sikuhitaji hayo mambo tena. Na sikutaka kuendelea kuyafikiria. Nikaweka namba ya mpenzi wangu Adelina na kumpigia hapo, nami nikatoka ofisini kwenda kutafuta chakula kwanza huku nikiwa nimeanza kuzungumza naye. Araah!

★★

Siku ikaendelea kutembea vyema, na hata Ankia kunipanda kichwani muda ule kukasahaulika. Nimekuja kumaliza kazi zangu saa moja jioni na kuachia wengine ili nikapumzike, lakini tayari nikawa na mipango mingine kwa usiku huu. Muda ule nimeongea na Adelina, tulipanga kutoka baadaye kwenda kujifurahisha kidogo, yeye akiwa na nafasi kutoka kazini saa mbili, hivyo nikamwambia ningempitia kule kwake akishafika. Alikuwa amenikosa mwenyewe, akitaka kweli tufurahie usiku huu hata kwa masaa machache, kwa hiyo nisingemvunja moyo. Moja kwa moja nikarudi kule kwangu, na tayari rafiki yangu Simba alikuwepo akifurahia kutazama mechi kwa utulivu. Tukasalimiana vyema na kujuliana hali, nami nikatulia pia kwa muda mfupi kisha nikamwambia ningetoka tena kwenda sehemu fulani na mtu.

Simba kama Simba akataka kujua ni nani, na nilipomfahamisha kuwa ni Adelina, akataka kuja pamoja nami pia ili amwone kwa mara ya kwanza. Ilitakiwa kuwa kitu ya mimi na mpenzi wangu pekee, lakini Simba akasisitiza kuja, akisema angekunywa mbili tatu tu pamoja na "shemeji mpya" kisha angetuacha baadaye tuwe pekee. Sikuona shida kwa hilo. Kwa hiyo tukajiandaa kikawaida tu, ikiwa inaelekea saa tatu, tukaondoka hapo nyumbani nikiwa naelewa Adelina tayari angekuwa ameshaondoka kazini. Simba akawa ananipigisha story kama zote wakati tuko njiani kuelekea huko Kinyerezi, na katikati ya safari Adelina akanipigia kuniambia kuwa aliningojea huko kwake tayari hivyo niwahi kabla muda haujayoyoma mno.

Kweli, nikajitahidi kuwahisha, mpaka tumefika kwake mrembo ilikuwa inaelekea kuingia saa nne, shauri ya umbali. Nikamwita, kwa sababu tayari alikuwa amejiandaa ingepaswa kuwa atoke, apande kwenye gari, twende. Simba alikuwa ameketi siti ya mbele pembeni yangu, lakini hapo akashuka na kwenda kukaa ya nyuma ili Adelina akija akae ndiyo pembeni yangu. Baada ya dakika chache, kweli mwanamke huyo akatoka, tukimwona namna alivyopendeza kwa kuvalia kiblauzi chekundu chepesi na suruali nyeusi ya skinny iliyoling'ata umbo lake nono vyema, na Simba akawa amekubali. Kwamba kweli nilijua kuchagua wanawake. Sikumwambia kihalisi ni mimi ndiye niliyekuwa nimechaguliwa na mwanamke huyo, ila hiyo ikaishia hapo. Adelina kusifiwa ilikuwa jambo zuri kwangu. Alikuwa ameumbika kweli.

Kwa hiyo akaja mpaka ndani ya gari, akiwa amependeza kweli usoni, nasi tukapiga busu ya kinywa akiwa hajamwona Simba huko nyuma. Ndiyo ile nimemwonyesha, akacheka kwa haya na kufunika mdomo wake, nao wakatambulishana sasa mmoja na mwenzake; nikimwambia Adelina kwamba huyo Simba ndiyo rafiki aliye "best" katika marafiki wote nilionao. Nikageuza gari, mwendoni tukaingia tena, na Adelina akiwa ameniuliza tunakokwenda, nikamwambia leo tungeenda kujiburudisha club. Hakuwa ametarajia hilo, hasa kwa kuwa alipitisha muda mrefu kwenda sehemu kama hizo, kwa hiyo nikamwambia ajiandae kupagawa na burudanj leo mpaka asahau uchovu wowote wa kazi. Akaonyesha utayari wa hilo. Simba alikuwa mtulivu tu.

Basi, tukafika na kuegesha gari mbele ya jengo la club moja kubwa kwenye maeneo ya Mbezi Luis, sijui ndo' panaitwa hivyo, nasi tukaingia huko na kukuta tayari watu wameshajaa na kufurahia muziki na vinywaji. Aisee watu walijua kujitumbuiza. Yaani ulikuwa unaingia club unahisi ni kama umefika nyumbani. Palichangamka sana. Nikamwambia Adelina tucheze, lakini kwa jinsi alivyokuwa, mwanzoni aliona uzito na hata kudai hajui kucheza. Ahaa? Nikamvuta mpaka sehemu tuliyoweza kusimama na kuagiza vinywaji, hapo tukaanza kupiga pombe sasa. Mwanamke alitaka kuwa mstaarabu kwenye kunywa lakini nikamshinikiza anywe mpaka ahisi kichwa kimebondwa japo kidogo, na hilo lilipofanikiwa, ndiyo nikamwingiza sasa kati. Simba hakuwa nyuma.

Hali ya hewa ikiwa imechangamka, watu wakijirusha, kunywa, kula, kulana, tukaanza kucheza muziki. Adelina alijirusha pia, kila mara muziki mpya uliopendwa na wengi ukipigwa alikuwa akirukaruka na kunichezea kwa ukaribu kwa mitindo iliyonisisimua sana, na kadiri muda ulivyokwenda nikazidi kufurahia sana pindi hii. Watu hata ambao sikuwafahamu walikuja kujichanganya na sisi, wakicheza na mimi, wakicheza na Adelina na Simba, na pombe ikiendelea kunyweka kila nafasi ndogo ilipopatikana ya kupumua. Kuna wakati nikawa nikiangalia simu na kukuta namba ngeni kabisa ikiwa imenipigia mara kadhaa, lakini mvutano wa burudani hapo club ukanizuia kuijali na kuweka simu mfukoni tu. Nikawa nahisi muda umeanza kwenda sana, na nilitaka kujirusha hapa club lisiwe jambo la mwisho kufanya mimi na mpenzi wangu mpya. Leo nilitaka tuvaane angalau kidogo.

Nikataka nimfate, nimshike ili kumvuta pembeni na kumwambia tuondoke kwenda kujilia bata yetu faraghani, na nilipomkaribia alikuwa akicheza pamoja na Simba kwa shangwe nyingi. Nikamsemesha, lakini hakunielewa, macho yake yakiwa yamelegezwa na pombe kiasi, hivyo nikawaomba wote wawili tusogee usawa wa kaunta moja ili tupumue kidogo. Wakatii, na tulipokwenda upande ambao haukuwa mbali sana na kaunta, nikamwambia Simba kimasihara kuwa muda uliisha, hivyo abebe virago vyake asepe ili mimi na Adelina twende kwingine. Wote wakacheka sana, utani na masihara zaidi yakianza hapo huku Adelina akinishikilia kiunoni na kusikiliza maneno ya Simba, nami nikazungusha macho huku na kule kwanza kabla sijawaambia tuondoke kwa pamoja; ilhali Simba hakutaka kuondoka. Pisi nyingi amwachie nani eti? Si ndiyo ile nimepiga jicho hivi tena nikawa nimemwona Miryam pale usawa wa kaunta! Heel

Nilishtuka. Niliganda. Nilihisi pigo zito kiasi moyoni mwangu kutokana na kutotarajia kabisa kumwona sehemu hiyo, na nikajikuta nimeendelea kutulia na kubaki nimemtazama kwa umakini. Yaani alikuwa amesimama umbali mfupi kutokea sehemu ambayo sisi tulikuwa, pale kwenye kaunta la tender wa vinywaji, akitazama kwangu moja kwa moja kabisa. Alikuwa amevaa vizuri, T-shirt nyeupe na suruali jeans yenye kubana, na macho yake yaliniangalia kwa njia iliyoonyesha wazi kwamba alitegemea kabisa kuniona, yaani hakushtuka, ni kwamba alikuwa ameshaniona kwa muda mrefu tangu tumefika sehemu hiyo. Sikuwatazama wenzangu tena baada ya macho yangu na Miryam kukutana namna hiyo, lakini nilielewa wao pia walikuwa wameshaona nilikoangalia, na najua Adelina akabaki kusubiri jambo fulani litokee.

Nilimwangalia Miryam kwa mkazo, lakini kihisia, nikiwa nahisi mapigo yangu ya moyo yanadunda kwa kasi zaidi kumwelekea yeye. Sijui kwa nini tu, ni kama bado alikuwa na athari kubwa moyoni mwangu. Kuna kitu nilianza kuhisi kinanitia msukumo, yaani msukumo wa kama kutaka kumwelekea pale alipokuwa amesimama, na hata nyendo za mwili wake zilionyesha hivyo pia, sema ikawa kama vile sote tunasubirishiana. Ndipo kikatokea kitu ambacho kikafanya msukumo huo uvurugike kabisa. Kutokea upande wake wa kulia akamfikia mwanaume ambaye nilimfahamu vyema sana, Festo mwenyewe! Tarajio lolote ambalo kona ndogo ya sehemu ya moyo wangu lilikuwa limeanza kujengwa likatokomea papo hapo. Nilijisikia vibaya sana kuona picha hiyo.

Festo alikuwa ameshikilia bia mbili za kopo, akimfikia Miryam na kuonekana kutaka kumpatia moja, jambo lililonihakikishia kwamba walikuja sehemu hiyo pamoja. Ah, kudadeki! Sijui kwa nini, lakini nikahisi nikichomwa kweli na jambo hilo. Si nilijiambia nisingejali tena? Lakini bado nikahisi kuumia. Sikutoa macho yangu kwao, na najua wenzangu pia walikuwa wakitazama upande wake Miryam. Simba akawa akinitikisa kuniita 'oya, vipi?' lakini sikumwitikia hata kidogo. Miryam hakupokea kinywaji ambacho Festo alitaka kumpa kwa kuwa aliendelea kunitazama tu, na hilo likafanya jamaa atazame upande wangu. Aliponiona, hakuonyesha hisia zozote za kushangaa na kutulia tu, nami nikaacha kuwaangalia wao kwa pamoja na kumtazama Adelina na Simba pembeni. Adelina alinitazama kwa hisia makini kiasi.

"Tuondoke," nikamwambia Adelina hivyo.

Na sikusubiri anipe jibu, hapo hapo nikageuka nikiwa nimeushika mkono wake na kuanza kuondoka. Simba akaniomba nisubiri kwanza, akiuliza tunaenda wapi, lakini sikukatisha hatua zangu, na hata nilipouachia mkono wa Adelina najua wote kwa pamoja walinifuata kwa nyuma. Ingekuwa kwamba nimemwona Miryam pekee hapo basi labda ningevunga tu na kuendelea na mambo mengine, ila kumwona akiwa na Festo, kulinikata stimu kabisa. Tena yaani hata sijui ilikuwa vipi eti na wenyewe wakawa ndani ya club moja na sisi kwa muda huo huo. Hapa pasingekalika tena kwangu, ila najua bado wenzangu walihitaji kuendelea kupata wakati mzuri, na mimi nisingeacha matatizo yangu yawavurugie furaha yao. Hivyo nikawaza tu tukiondoka sehemu hiyo tuelekee nyingine eneo tofauti, na huko tungesaidiana zaidi kusahau mikazo yetu; yangu sanasana.

Nikiwa nimetangulia, tukazifikia ngazi kupitia mlango wa nyuma wa jengo hilo na kuanza kuelekea chini, pale niliposikia jina langu likiitwa na sauti niliyoifahamu vyema kabisa.

"Jayden..."

Ilikuwa ni Miryam. Sikugeuka, na hatua zangu zikafifia kiasi lakini sikuacha kutembea. Kwa jinsi ilivyosikika, sauti yake ilionyesha kwamba alikuwa akitufuata kutokea kule ndani, bado akiwa hajazifikia ngazi, nami nikaona niongeze kasi ya kushuka ili nimwepuke upesi.

"Jayden..." sauti yake ikasikika tena.

"JC... kuna mtu anakuita..." Simba akanisemesha kutokea nyuma yangu.

Sikujibu wala kugeuka na kuendelea kuukata mzunguko wa ngazi ili niwahi kutoka sehemu hiyo, na sasa ikawa wazi kwamba Miryam alikuwa ametukaribia, akishuka ngazi upesi pia kama vile anakimbia.

"Jayden... subiri..."

Ih! Alikuwa anataka nini? Yaani, wakati huu niliokuwa najitahidi kusonga mbele bila yeye, yeye tena akaanza kunikimbiza ili kunirudisha nyuma, siyo? Tena alinionyesha wazi kwamba na yeye alikuwa ameshaanza kusonga mbele na huyo Festo wake, sasa sielewi alihitaji nini zaidi kutoka kwangu. Mizinguo, ama? Sikutaka kabisa kusimama, na ikiwa ndiyo imebaki mistari miwili kuzimaliza ngazi kufikia chini, Miryam akawa amefanikiwa kuwapita Simba na Adelina na kunishika mkononi upesi, jambo lililofanya nigeuke kwa kasi kumwangalia. Alishikilia mkono wangu kwa nguvu, akiuvuta fulani hivi yaani kunizuia, ili nisimame, huku akipumua kwa kasi kiasi, na macho yake yakinitazama kwa hisia nyingi za huzuni.

"Jayden..." akaita.

Nikaendelea kukaza macho yangu usoni kwake kwa umakini.

"Samahani..." akaniambia hivyo huku machozi yakimlenga.

Nikaendelea tu kumwangalia.

"Tafadhali... naomba unisamehe mpenzi wangu..." akasema hivyo.

Sauti yake tamu aliyotumia kuniambia hivyo ilifanya nihisi kuyeyuka moyoni, yaani aliongea kwa hisia huku akikikaza zaidi kiganja changu, nami nikajikuta nalengwa na machozi kwa sababu ya hisia nilizokuwa nikificha kulazimisha kutoka.

Machozi yake yakamwagika, akikinyanyua kiganja changu kukikaribisha na uso wake, na kwa sauti tetemeshi akaniambia, "Nakuomba... naomba tuongee... tafadhali..."

Alionekana kutaka kusema kitu fulani muhimu sana zaidi tu ya kuomba samahani kwa maneno aliyoniambia ule usiku. Nikakosa hata cha kumjibu, hapo tukiwa tumesimama sehemu ambayo watu na wapenzi wao wangepita na kututazama kwa kudhani tunatengeneza sinema, na ndipo kutokea ngazini kuelekea juu nikamwona Festo akiwa amefika hapo na kusimama. Alisimama kwa huo umbali akitungalia, nami pia nikimwangalia, na Miryam pamoja na wengine wakamwangalia. Miryam akiporudisha macho yake kwangu, nikamwangalia pia, kisha nikakivuta kiganja changu kutoka kwake kistaarabu tu, yeye akiwa kama hataki kukiachia, na nilipofanikiwa kukiondoa, hapo hapo nikamwacha na kuendelea kushuka ngazi.

Bila kugeuka nyuma wala nini, nilisikia sauti yake ya chini ya kilio, akionekana kuhuzunika sana, nami nikakaza hisia zangu kiume na kuelekea moja kwa moja mpaka garini kwangu; Adelina na Simba wakiingia pamoja nami. Sikutaka hata kuzungumza, nikawasha tu gari, na hapo ndiyo hisia zikanilemea zaidi na kujikuta tu naishia kuukaza usukani kwa mikono yangu. Miryam bado alikuwa anaudundisha mno moyo wangu, mpaka sasa nikawa sielewi kile nilichotaka au kuhitaji mimi binafsi kuelekea suala langu na huyo mwanamke. Nadhani Adelina aliona namna ambavyo nilikuwa nimevurugika kihisia, naye akiwa kwenye siti pembeni yangu, akakishika kiganja changu na kukikaza kama kunitia moyo bila maneno. Sikumwangalia, bali nikashusha tu pumzi kujipa utulivu, kisha ndiyo nikaliondoa gari sehemu hiyo.

★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★

WhatsApp +255 678 017 280
 
Huko kwenye WhatsApp tunachangia kiasi gani mkuu? Nachoka kusubiri
 
Back
Top Bottom