Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
DahMIMI NA MIMI 3
A Story by Elton Tonny
Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Siri, Tamaa, Hila, Usaliti, Ukatili, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa
R-rated 18+
Enjoy!
★★★★★★★★★★★★★★★★★
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Nikaendelea kumkumbatia Miryam kwa dakika kadhaa, yeye akiwa amejibana kwangu kunihisi zaidi kwa kuwa alipenda sana cuddling, na ilikuwa ni ukimya tu wa utulivu ulioendelea baina yetu baada ya kuwa nimempa ukweli kuhusiana na Festo. Nililileta jambo hilo upesi kwa manufaa ya Miryam, ili hatimaye nimweke huru mwanamke wangu kutoka kwenye fikira za huyo mwanaume kuwa mtu wa kumwamini kwa asilimia zote. Najua Miryam alilichukulia hili kwa uzito, kama jinsi ambavyo ilikuwa kwa yule kaka yake aitwaye Joshua. Sasa ndiyo ningetakiwa kuhakikisha namweka Festo mbali kutoka kwetu, na hiyo njia ingenihitaji nimhusishe askari Ramadhan.
Lakini kwanza, ingebidi suala la penzi letu kurudi mahala pake litiwe mhimili uliofaa kwa pande zote zilizotuzunguka; familia yangu, familia yake, mwanangu Evelyn, na Adelina. Hasa huyu mwanamke. Alikuwa mstaarabu sana Adelina, lakini kumfikishia tu taarifa kwamba ninarudiana na Miryam ghafla namna hii najua ingemchanganya sana, kama siyo kumuumiza. Lakini ningefanya nini? Miryam ndiyo alikuwa mwanamke kwangu ambaye hata kama ningekuwa nimeshamwoa Adelina, akinipigia tu simu niende kwake ku-cheat, ningefanya hivyo. Kinoleo cha chuma changu kigumu sana ilikuwa ni yeye. Bado nilimpenda sana, na sasa akiwa na ujauzito wangu yaani ndiyo kabisa nisingeweza kuangalia kwingine tena. Ingepaswa tu kuwa hivyo.
Miryam, akiwa bado amejilaza kifuani kwangu, akauliza, "Nini kitafuata sasa?"
Nikiwa nazilaza nywele zake taratibu, nikamwambia, "Nitashughulikia kila kitu, usijali. Wewe jitahidi tu kutojipa stress kuanzia sasa."
"Kwa uliyotoka kuniambia, sidhani kama hiyo itakuwa rahisi..." akasema.
"Mhm... usiogope. Festo hajui kama nimekwambia haya, anafikiri sitawahi kukwambia. Kwa hiyo hata wewe kwa sasa jifanye tu kama haujui ili nifanikiwe kwanza kumwondoa kutoka kutoka kwenye maisha yetu," nikamwambia hivyo.
Miryam akajitoa taratibu mikononi mwangu na kuniangalia, naye akasema, "Unamaanisha..."
"Nitajua la kufanya, usiwaze. Superman wako hapa, au umenisahau?" nikamwambia kiutani.
Miryam akatazama pembeni kiufikirio, kisha akasema, "Natamani ningeyajua hayo mapema... ningemwambia anikome kabisa. Unachosema ni kwamba, sitakiwi kumwambia chochote kabisa... niweke distance, lakini isiwe wazi wazi sana?"
"Yeah. Ni kwa sasa tu lakini. Bado simwamini. Mpaka labda nijionee kwa hakika amegeuka kuwa askofu, ndo' nitakuwa na amani. Na tena hata na hapo siyo sana..."
Miryam akatabasamu kiasi.
"Ila wewe usihofu lolote. Acha tu aendelee kujifanya rafiki mwema wakati mimi nafanya jambo kujua nyendo zake za wakati huu. Na lazima tu atakamatika tena," nikamwambia hivyo.
Miryam akatikisa kichwa kwa uelewa, naye akasema, "Sijawa na muda wa... niseme... ku-reflect sana, yale ambayo tuli...."
Simu yangu ikaanza kuita, kitu kilichomfanya Miryam asitishe kuzungumza. Nikaivuta na kuangalia mpigaji, kukuta namba ngeni kabisa, nami nikaitolea sauti na kuiacha iite hivyo hivyo tu.
"Ulikuwa unasema?" nikamuuliza Miryam.
"Pokea simu kwanza," Miryam akasema.
"Ah, achana nayo..."
"Ni nani?"
"Hata sijui... namba ngeni."
"Kwa nini hupokei sasa?"
"Mimi kupokea namba ngeni, a-ah... sipendi," nikamwambia.
"Inaweza ikawa muhimu... je kama ni mtu unayemjua?" akasema hivyo.
"Atume ujumbe. Me huwa... dah! Na we' uko kama Ankia yaani," nikamwambia.
"Kwa nini?"
"Ahah... basi tu. Ila achana nayo. Endelea na ulivyokuwa una...."
Nadhani simu ilikuwa imeshakata, lakini ikaanza tena kuita na kukatisha maneno yangu. Nilipoichukua kutazama mpigaji, namba ilikuwa ile ile, nami nikamwangalia Miryam kwa njia ya kukerwa.
Miryam akaichukua simu na kusema, "Labda ni Adelina..."
"Siyo namba yake hiyo..." nikajitetea upesi.
Miryam akafanya kupokea, halafu akaniwekea sikioni kwa kushurutisha. Nikabaki nikimtazama usoni tu, na yeye akawa akinionyesha kwa ishara kwamba niongee. Upande wa aliyenipigia haukutoa sauti yoyote, nami nikaona nimridhishe tu mwanamke wangu.
"Hello..."
Nikasema hivyo, na sikusikia jibu lolote lile, isipokuwa ikawa ni kama vile pumzi ilishushwa upande wa pili wa simu, nami nikakunja uso kimaswali.
"Hello... Halloo? Nani?"
Hata kwa kusisitiza hivyo, sikupata jibu, nami nikapiga ulimi kwa kuudhika na kuitoa simu sikioni.
"Haongei?" Miryam akauliza.
"Umeona sasa haya mausumbufu? Ndo' maana sipendagi kupokea namba ngeni, wengine wanabeba sauti ya mtu unashangaa nimerogwa, wananigeuza msukule..." nikamwambia hivyo.
"Ahahah... ila Jayden..."
"Ni kweli. Nini sasa hicho?"
"Acha woga bwana. Nani akuroge?" Miryam akasema hivyo.
"Ahaa... sawa. We' wape support sasa..." nikamwambia hivyo.
Nikaiwekea kizuizi namba hiyo ili isije kunisumbua tena, na nilipomtazama Miryam, nikakuta ananiangalia kwa hisia za furaha sana.
"Vipi?" nikamuuliza hivyo huku nikitabasamu kiasi.
Akatikisa kichwa kuonyesha hamna kitu.
"Niiini? Niambie..." nikamsemesha kichokozi na kumbonyesha shavuni.
Akatabasamu na kusema, "Hamna kitu. Niliku-miss sana tu."
Nikatabasamu pia na kusema, "Kiukweli... hata mimi."
Akabaki kunitazama kwa hisia.
"Ningejitahidi kukuondoa kichwani... lakini... hapa yaani... bado ulikuwa unasumbua sana," nikamwambia hivyo huku nikijishika kifuani, kumwonyesha moyo.
Akatabasamu kwa hisia na kusema, "Kama naona jinsi utakavyokuja kuwa baba mzuri sana kwa binti yetu," akaniambia hivyo.
Nikakunja uso kimaswali na kusema, "Binti, eh? Umejuaje atakuwa wa kike?"
"Najua tu. Ninahisi," akaniambia.
"Acha mambo yako wewe. Ama umeshaenda kujikagua bila me kuwepo?"
"Hahah... no, bado. Jamani, si ndo wiki mbili... sijui tatu tu?"
Nikatabasamu kwa hisia.
"Akue-kue kwanza. Tutakuja twende pamoja tuone kama hisia zangu za kweli," akasema hivyo.
"Duh! Tayari nina mwali, aje na mwingine tena, si itakuwa soo?"
"Kwa nini?"
"Nitawadekezaje wote kwa pamoja?"
"Ndiyo utajibeba. Yaani itabidi wote uwape mapenzi asilimia mia, hakuna kupendelea."
"Hilo ni uhakika. Usijali. Mtoto wetu tutamtunza vizuri zaidi ya sana. Na kama wa kike kweli, yaani atalindwa huyo mpaka itabidi atafute starring wa kuja kumtorosha..."
Miryam akacheka kwa furaha.
"Unafikiri nakutania? Yaani sitataka mtu yeyote amguse," nikamwambia.
"Unaongea hivyo utafikiri hujawahi kuhusika kutorosha watoto wa watu pia!" akaniambia hivyo.
"Hap... yaani..."
Miryam akasema, "Hayo mambo na mwanetu atayapitia tu, wazazi wote huwa wana sera zile zile ila hutaweza kumzuia ayafanye..."
"Wee! Hakuna. Hii ni tofauti, me na we' tulivyo wazuri hivi, unafikiri mtoto wetu atakuwaje? Kila mtu atataka kumpandilia, hiyo ni no!" nikaongea kwa shauku.
"Hahahah... ila wewe..."
"Me nakwambia, we' ngoja..."
"Hapo utakuwa baba, ama mbepari?"
"Yote sawa tu. Lakini habari ndo' hiyo."
"Na akiwa wa kiume je?" Miryam akauliza.
"Akiwa wa kiume? Aaa huyo utadili naye wewe, kupandishiana besi na mtu sitataka, la sivyo...."
"Itakuwa ni mangumi kila siku," Miryam akamalizia maneno yangu.
Nikacheka kidogo. Maongezi yakaanza kuchangamsha.
"Tutakuharibia jiko bure kwa mateke, ya nini? Utakuwa unambembeleza tu, me kudekeza dume itakuwa noma," nikamwambia kiutani.
"Ahah... atakuwa kama wewe tu. Ulivyo mjeuri," akaniambia.
"Ndo' itabidi umfunde awe kama wewe. Wa kiume si wa mama? Itakuwa yako peke yako..."
"Utanitelekezea mtoto ndani ya nyumba moja..."
"Yaani humo humo."
"Ahahah... haya bwana, umeshinda. Ila me bado nahisi huyu wa kike. Atakuwa wako zaidi kufunda," akaniambia hivyo kwa hisia.
"Na kudeka atadeka mno. Siyo siri Mimi, ninaingoja kwa hamu siku utakayojifungua. Nitampenda huyo mtoto!" nikamwambia.
"Mpaka me utanisahau..."
"Ah, we' utakuwa wa kazi gani sa'?"
Akasonya kidogo na kunipiga kifuani kimasihara.
Nikacheka kidogo huku nikianza kuisugua shingo yake laini taratibu, nami nikasema, "I can't wait. Yaani... hiyo ni siku ambayo utaniongezea furaha zaidi ya ninayohisi wakati huu mpaka kufikia wakati huo. Umeli-change game yaani."
"Mhmhm... kwa maneno hayo Jayden utadondosha hadi milima," akasema.
"No, siyo ya utupu. Namaanisha kila nilisemalo," nikamwambia kwa hisia.
"Asante," akaongea kwa kasauti kake katamu.
Nikaanza kuzichezea nywele zake laini taratibu.
"Umeshawaza jina?" akaniuliza.
"La kumpatia mama kayoyoo?" nikatania.
"We! Koma," akanikanya.
"Hahahah... sirudii tena, nisamehe..."
"Unamwita mwanangu majina gani hayo, a-ah..."
"Okay, okay, natania. Ila nina rundo kibao la majina nayoweza kufikiria kumpa kijacho, sema... nataka nisikie ya kwako kwanza," nikamwambia.
"Ili tukubaliane vizuri?"
"Eeeh, tuweke option mezani halafu tuchanganue pamoja mpaka tupate linalofaa..."
"Ahahahah..."
"Mbona unacheka?"
"Yaani mtu anaweza kuona hii kama upuuzi, hivi kweli tuamue jina sasa hivi mimba yenyewe ndiyo kwanza ina wiki?"
"Shida ni ipi? Jina la mtoto... yaani wewe... hujui tunamuamulia kitu ambacho ataishi nacho maisha yake yote? Lazima tufanye ma-conteplatation na ma-compilation mpaka tupate linalofaa. Miezi tisa ikiisha ubishi utakuwa umeisha," nikasisitiza.
"Mmh!"
"Usishangae bwana. Niambie, ulikuwa umeshawaza jina?"
"Yes, nimeshawaza. Me napenda moja tu kama wa kike, sina rundo kama wewe," akaniambia.
"Ahahah... haya liseme," nikamwambia.
"Napenda... akiwa wa kike tumwite Dahlia," akasema hivyo.
"Eh!" nikashangaa.
"Nini?"
"Hee! Umenimaliza..."
"Hahahah... kwa nini?"
"Jina zuri, yaani nilifikiri nikisema Bianca ndo' ningekumaliza, ila we' kiboko kwenye majina," nikamsifia.
"Chezea," akajisifia kwa kurusha nywele zake kwa kiganja.
"Hahah... kwa nini unapenda hilo?" nikauliza.
"Ni zuri. Lilivyo tu. Kuna maua yanaitwa hivyo, nikawaza mwanangu aitwe Maua, lakini kwa njia rare..." akaniambia.
"Ahaa, siyo ile ya Maua Sama, ila maua, lakini specific kwa aina?"
"Hahahah... ndiyo. Rose, Lily, na mengine-mengine yanatumika sana. Dahlia ni adimu. Kwa huku Bongo naona. Unaonaje?" akauliza.
"Ah, pigia mstari. Unasikia Dahlia? Jina ndiyo hilo, na tayari maandalizi ya cheti yanaanza," nikaongea na tumbo lake.
Miryam akanichapa kofi dogo begani, nami nikatabasamu na kuendelea kuchezea shingo yake taratibu.
Ukimya ukafuata baada ya hapo, tukikaa kuangaliana kwa hisia za upendo, na kweli macho yetu yakaambiana kuwa tulihitaji kuuhisi zaidi huo upendo. Nikautelezesha mkono wangu kufikia shavu lake laini na kuanza kumsogelea usoni, na yeye vilevile akaitikia hilo kwa kunikaribia zaidi. Tukaikutanisha midomo yetu na kuanza kupeana busu tamu sana, kwa hisia tukionyeshana namna tulivyokuwa na hamu za juu kuelekeana, na kwa kweli nilikuwa nimekosa sana penzi la huyu mwanamke. Hii ilijibumba kuelekea sehemu bora hata zaidi kwa siku ya leo tofauti na matarajio yoyote niliyokuwa nayo, nami nikaona niifanye iwe hivyo.
Nimemnyonya midomo kwa dakika nzima kabisa, kisha nikashuka na shingoni kwake, nikianza kumpandishia hamu hata zaidi. Miryam hakuwa na pingamizi, tena zaidi akanishika kichwani na mgongoni kunitia hamasa niendelee huku akianza kupumua kimahaba, ndipo kwa pamoja tukashtushwa na sauti fulani kutokea nje. Nikasitisha kumpa penzi Miryam na kutazama upande wa mlango, na sauti hiyo iliposikika mara ya pili, nikatambua lilikuwa geti, likifungwa naona. Hapo nikaelewa kuwa bila shaka ingekuwa ni Simba ndiye aliyerejea, na ni wakati mbaya sana jamaa alikuwa ameamua kurudi muda niliokuwa natengeneza wakati mzuri.
Nikamwangalia Miryam, kukuta ananitazama kwa subira, nami nikasema, "Huyo ni Simba."
"Simba?" Miryam akauliza, akiwa hajaelewa.
"Ni rafiki yangu. Amekuja majuzi tokea Mwanza..." nikamwelewesha.
"Ooh... yule mliyekuwa naye jana?"
"Yeah. Ndiyo huyo."
"Sawa. Ndiyo uliniambiaga ana vituko sana?"
Nikatabasamu kiasi na kusema, "Ndiyo. Amepunguza kidogo, ila bado hajaacha."
Miryam akaanza kujirekebisha na kukaa vizuri, si kwa ukaribu sana na mimi yaani, nami nikamwangalia kiumakini.
"Unataka kwenda wapi sasa?" nikamuuliza.
"Hamna. Nipo. Siyo poa tu lakini rafiki yako aingie atukute hivi," akaniambia.
"Mm? Asa' huyo mjinga-mjinga unafikiri atafanya nini hata akikuta nakufanya hivi..."
Niliposema hivyo, nikaanza kumtekenya Miryam mwilini na kusababisha aanze kucheka na kujitahidi kunikwepa, lakini nikamkazia kwangu na kuendelea kumtekenya kwa makusudi zaidi.
"Lakin... Jay... acha.... wewe... a-ah...."
Akawa akijitahidi kujitoa kutoka hapo huku mimi nikimkaza zaidi, na ndiyo wote tukatambua kwamba mlango wa kuingilia ndani ulifunguliwa. Nikatazama hapo na kumwona Simba, akiwa amevaa kimtoko yaani, na simu ikiwa sikioni kwake akionekana kuzungumza na mtu. Alisimama hapo na kuelekeza macho yake kwetu kwa njia ya kutotarajia kutukuta tumekaa sofani huku tukitekenyana, halafu akaachama mdomo kuonyesha hali ya sintofahamu; kama kuhisi ameingia na kutushtukiza tukitaka kufanya jambo fulani la kivyetu. Miryam akajisawazisha vyema tena na kujisogeza pembeni, huku mimi nikitabasamu, naye Simba akamalizia maneno machache kumwelekea mtu wa kwenye simu na kutuangalia tena.
Jamaa akasema, "Samahanini jamani... nimerudi wakati mbaya...."
"Wakati mbaya wapi? Hujui kupiga hodi?" nikamuuliza kimasihara.
"Jayden!" Miryam akanong'ona kunielekea.
Nikatabasamu na kumwangalia.
"Ah, haina shida kaka. Usijali. Za saa hizi?" Miryam akamwambia.
"Salama. Karibu sana," Simba akaongea kwa namna yenye heshima.
"Asante," Miryam akamjibu.
Nilibaki kumwangalia Simba kwa jicho makini tu, naye akabana midomo yake na kisha kupepesa macho yake huku na huko kama kubana hisia za uajabu wa kile alichokikuta kinaendelea hapo. Nilielewa upesi alikuwa anawaza nini, nami nikaona niendelee kumtesa kwa kutosema chochote kabisa.
Miryam, akiwa kama ameona jambo fulani, akasema, "Jayden... ngoja me nikimbie."
"Ih, wewe!" nikamshangaa.
Simba akavua viatu na kisha kusema, "Nimechoka kweli, mizunguko mingi. Ngoja niingie kujipumzisha kidogo. Poleni kuwa... kuwashtua."
"Basi unajifanya kastaaarabu..." nikamwambia hivyo.
Miryam akatabasamu kiasi na kunipiga mkononi kwa kiganja chake.
Simba akacheka kidogo kwa pumzi na kusema, "Huyu jamaa akamwone daktari, hata kututambilisha hamna, anaanza mambo gani sijui..."
"Kwa kweli..." Miryam akapigia mstari.
Nikamtazama kwa kuudhika, kimasihara.
Simba akaja upande wetu na kumpa mkono Miryam, ambaye akaupokea, naye akamwambia, "Naitwa Fred. Au ukipenda niite Simba."
"Sawa kabisa. Me naitwa Miryam. Na, Simba ndo' linafaa," Miryam akaongea kwa urafiki.
Simba akakiachia kiganja chake na kusema, "Haya. Ngoja niwaache basi, yaani usingizi!"
Miryam akatabasamu tu na kutikisa kichwa kukubali, mimi nikiwa namwangalia Simba kama vile nina uadui naye, na yeye akanishusha na kunipandisha wakati mimi ndiyo nilikuwa nimekaa, halafu akaelekea upande wa chumbani baada ya hapo.
Miryam akacheka kidogo na kusema, "Naona mnapendana sana."
"Ah, mjinga huyo..." nikasema hivyo.
"Kwa nini sasa jamani?"
"Kilichomtuma arudi sasa hivi nini?"
"Ahahahah... nilijua tu!" Miryam akasema hivyo kwa furaha.
Nikajifanya nimenuna.
Akanishika kiganjani na kuniambia, "Mwache mwenzio bwana. Hayo yapo tu, hata kwa wakati mwingine."
Nikamwangalia na kutabasamu kiasi.
Miryam akatabasamu pia, kisha akaangalia simu yake na kusema, "Nahitaji kwenda Jayden."
"Wapi?"
"Kuna sehemu nilipanga nimpeleke Mamu leo, kabla hujanipigia kukutana nawe. Muda umeenda, ila ngoja tu nimwahi. Tuta..."
"Usijali. Nenda kamjali Mamu. Hata hivyo nilikushtukiza, so... naelewa. Usijali," nikamwambia hivyo.
Akatikisa kichwa kuonyesha uelewa, kisha kwa pamoja tukasimama na kuanza kuelekea nje. Mahusiano yetu yakiwa yamerejea hewani tena, haikuonekana hata kama vile tuliwahi kuachana kwa njia mbaya hapo nyuma, na sasa ingekuwa ni kusonga kwa kasi ya 6G mpaka mwisho. Kwa uimara wote, hili tunda nisingeacha liliwe na mtu yeyote yule zaidi ya mimi pekee. Nikamtoa mwanamke wangu mpaka kulifikia gari lake, nikakumbatiana naye na kumwahidi kumtafuta baadaye, kisha tukapiga busu tamu ya kuagana na yeye kuingia ndani ya gari lake. Nikamfungilia geti, naye huyo akaondoka zake huku akiniacha najihisi kuridhika sana moyoni.
Baada ya kufunga geti, nikarejea ndani, na ile nimeingia tu nikaweza kumwona Simba akiwa usawa wa friji, akionekana kuvaa nguo nuepesi sasa na kutoa tofaa moja humo, kisha akaling'ata na kuelekeza macho yake kwangu. Hakusema lolote, na mimi sikusema lolote, lakini njia yetu ya kuangaliana iliongea mengi zaidi ya jinsi ambavyo tungesema kwa midomo, na nilielewa akili yake ilipokuwa.
Hatimaye, nikavunja ukimya na kumuuliza, "Nini?"
Akaendelea kunitazama kwa njia hiyo hiyo tu.
"Sema unachotaka kusema Simba. Hiyo lugha ya macho siielewi," nikamwambia hivyo kikejeli.
Simba akafumbua mdomo na kuonekana kutaka kusema jambo fulani, nikingojea kusikia maoni yake, kisha akafanya ishara ya kuufunga mdomo wake kwa zipu na kubaki ameufunga hivyo hivyo. Nikamnyanyulia kidole cha kati kuonyeshwa sijapendezwa, naye akaanza kuondoka huku akijaribu kula tofaa eti kwa namna hiyo hiyo ya kufunga mdomo kwa zipu. Nikatabasamu kiasi na kutikisa kichwa kwa kusikitika. Ni wazi Simba alikuwa akihukumu uamuzi wangu aliokuta nimeuchukua hapo baada ya maongezi yetu jana, na nikiwa nimemwonyesha kuwa huo ndiyo ulikuwa uamuzi sahihi kwangu, sasa umakini wangu ungetakiwa kuelekezwa mahali pengine muhimu ili niurasmishe zaidi uamuzi huo. Adelina.
★★
Jioni haikuchelewa kufika baada ya Miryam kuwa ameondoka kwangu. Kama Simba tu, mimi pia niliamua kujipumzisha kidogo, na baada ya kuamka na kula ndiyo nikapata nafasi ya kuongea na rafiki yangu huyo kuhusu suala langu na Miryam. Simba alikuwa msikivu tu, akiweka matani pembeni na kuelewa sababu zangu vizuri hasa baada ya mimi kumwonyesha ripoti ya DNA, na ishu ya ujauzito wa Miryam. Kilichokuwepo sasa ingekuwa kuzungumza na Adelina, na hapo niliona pangekuwa na ugumu wa aina yake. Kiukweli nilikuwa nimeshaanza kumpenda yule mwanamke, lakini, si kama nilivyokuwa nampenda Miryam. Ni moyo tu. Sasa kilichonitatiza ingekuwa ni kujua njia gani ya kumwambia uamuzi wangu bila kumfanya anifikirie vibaya. Na najua angeumia sana dada wa watu.
Simba akanishauri nimtafute mapema tu na kumwomba tuongee, kwa sababu tayari nilikuwa nimesharudiana na Miryam, kwa hiyo nitake nisitake, ya Adelina ningepaswa kuifuta. Hawa hawakuwa kama wanawake wa kutumia ama kuchepukia tu, ni watu waliokuwa serious na maisha. Kwa hiyo kuchagua mmoja na kuachana na mwingine ilikuwa lazima. Alikuwa sahihi, na kwa msingi huo kweli nikawa nimemtafuta Adelina na kuzungumza naye. Akiwa zake kazini, nikamwambia ningependa tukutane siku fulani ya karibuni, labda jumapili hasa kwa sababu asingekuwa na kazi, lakini Adelina akaniambia angependa tuonane leo leo endapo kama nisingekuwa nimebanwa na kazi. Alinikosa sana. Dah!
Nikamjulisha kwamba nisingekwenda kazini kwa siku chache kutokea leo, kwa hiyo nilikuwepo tu, na kwa hilo akasema basi niende kwake kwenye mida ya saa mbili hivi, angekuwa ameshafika. Alitaka sana tuonane. Shauku yake ya kuniona ilikuwa ile ya mapenzi, nikijua alitaka twende tuchangamshane na nini baada ya yale yaliyotokea usiku wa jana kuvuruga mipango yetu, lakini matarajio yake yangekwenda ndivyo-sivyo. Ingenipasa nikamvunjie ukweli huko huko kwake, hata kama ingemvunja moyo. Sikuwa na namna. Kwa hiyo nikamkubalia, na baada ya kuagana, nikakaa kwa muda mfupi kupitia hiki na kile kwenye mitandao na kisha nikaanza kujiandaa kimwili kabla sijaelekea huko kukamilisha hili zoezi.
★★
Imefika mida ya saa moja na arobaini hivi ndiyo nikatoka kwangu na kuanza kuelekea huko Kinyerezi. Njiani, niliweza kuwasiliana na mwanangu Evelyn kupitia simu ya Deborah, dada yake Stella. Mwanangu alichangamka sana, akinionyesha mti mkubwa wa Krismasi ambao uliletwa hapo nyumbani, na mapambo mengine ambayo yalianza kuwekwa kabla ya siku hiyo kufika kwa ajili ya kusherehekea. Tukaongea vizuri sana pia na Deborah, ambaye akauliza ningeenda kuwaona lini tena maana mimi na Stella tulikuwa bize kweli. Nikamwambia ningejitahidi kufika huko siku chache zijazo, na labda tungefanya kukutana sehemu fulani nzuri ili tushiriki mlo mzuri pamoja.
Tukaagana vyema baada ya hapo, nami nikawa nimeingia pande za huko Mbezi kwenye mida ya saa mbili na nusu hivi. Kulikuwa na msongamano hapo kati lakini baada ya dakika chache nikawa naisaka Kinyerezi mpaka nilipofanikiwa kuyafikia maeneo ya nyumbani kwake Adelina. Nilifika tu hapo na kutulia kwa sekunde chache, nikihisi wasiwasi eti. Sijui kwa nini nililiona hili jambo kuwa gumu zaidi ya kuingia chumba cha upasuaji na kukata-kata maogani ya mwili wa mtu, ila hapa ujasiri ulihitajika. Hisia za mtu zilikuwa muhimu sana, kwa hiyo ningeenda huko ndani na kujaribu kuonyesha ninazijali za Adelina, japo najua zingeumizwa kwa kiasi chake.
Kwa hiyo nikaliacha gari hapo nje na kulisogelea geti la nyumba hiyo. Nikausukuma mlango wake mdogo, ambao ulikuwa wazi kiasi, nami nikaelekea hadi mlangoni kwake Adelina na kutulia hapo kwanza. Hisia za kunirudisha nyuma zikawa zimeniingia tena, nikiwaza na kuwaza ni itikio gani lingetoka kwa huyo mwanamke baada ya kumwambia kilichonileta, na kabla sijamaliza kujishauri wala kugonga hodi, mlango ukafunguliwa kutokea ndani. Nikatazama hapo na kumwona Adelina, akiwa anatoka huku akitabasamu kwa furaha, na moja kwa moja akanikaribia na kunikumbatia kwa upendo mwingi.
Mwili wake wenye joto zuri sana ulinisisimua, hata zaidi kwa sababu nilikuwa nimeshamzoea mno, na sasa kumletea habari ambayo najua ingemvunja moyo, kulifanya hisia zangu ziwe juu kupindukia. Lakini nikajitahidi kujipa utulivu na kurudisha kumbatio lake, yeye akiendelea kunibana kwa sekunde chache kama kusikilizia mwili wangu, kisha akaniachia na kunitazama usoni kwa hisia.
"Mambo?" Adelina akanisemesha hivyo kwa sauti yake ya kistaarabu.
"Safi," nikajibu kistaarabu pia, japo jibu lenyewe likanifanya nijihisi mnafiki.
"Vipi? Mbona kama umepoa?" akauliza, akiwa bado kanishika kwa ukaribu.
"Ah... niko sawa. Wewe ndiyo utakuwa umechoka sana najua," nikamwambia.
"Eeh, ila... umekuja sasa, najisikia energized. Karibu," akanisemesha kwa uchangamfu kiasi.
Alitaka tuanze kuelekea ndani, lakini nikaendelea kusimama hapo hapo na kusema, "Adelina... kuna ishu nataka tuzungumzie."
"Ee, njoo sa' ndani tuongee. Unataka tuongelee hapa hapa nje?" akasema hivyo.
Nikakosa hata cha kujibu, naye akanishika mkono na kunishawishi kuingia ndani pamoja naye. Nikaingia, na alipokuwa akiurudishia mlango mimi nikaendelea tu kusimama hapo kati, ndipo ile nimegeuka tu kumtazama papo hapo akawa amenifikia na kujitupia kwangu, akiufuata mdomo wangu kuanzisha denda nzuri baina yetu. Alinipamia kiasi, na kwa kuwa sikujiandaa ilikuwa karibu niweweseke naye vibaya, lakini nikajitia nguvu na kumkaza kwangu pia, nikikishika kiuno chake wakati yeye akiwa ameshaanza kuula mdomo wangu kana kwamba alihisi njaa ya miaka. Alinibusu kwa mtindo wake ule mzito sana, akionyesha hamu kubwa kunielekea, na hilo lilifanya nisisimke zaidi, ninyanyuke bila kulazimika.
Sikutaka niifanye hali hii ionekane kuwa ajabu sana kwake, kwamba labda nimwambie aache, hapana. Angejisikia vibaya sana endapo kama ningelipa suala nililoleta hapa kasi kubwa ya ughafla, hivyo nilitaka kupeleka mambo taratibu tu. Alivaa kinguo laini sana kwa juu kama satini, na khanga iliyomfunika kutokea kiunoni ilikuwa nyepesi pia. Mwili wake ulihisika vyema kwangu, ukinipa hamu pia ya kutaka alichokitaka kiendelee, lakini nilijua sikupaswa kuendeleza jambo hili. Alianza kama kunisukuma ili tulielekee sofa na kuendeleza penzi, na kweli tukalifikia na kukaa pamoja, Adelina akionyesha nia ya kutaka kunilalia kwa juu, hivyo akawa akiendelea kunisukuma huku akinibusu kwa hamu.
Lakini ndiyo hapo nikajitoa midomoni mwake na kusema, "Adelina..."
Akaitikia kwa mguno, huku akiwa amenishikilia kichwani na kunitazama kimahaba.
"Ona... kuna kitu naomba tuongee... tuongee kwanza," nikamwambia.
"Tutaongea baadaye bwana. Nimeku-miss..." akasema hivyo taratibu.
Akaanza kunibusu shingoni huku akiweka jitihada ya kuanza kuvuta T-shirt langu, nami nikaishika mikono yake na kusema, "No. Inabidi tuongee sasa hivi."
Nilimsemesha kistaarabu, lakini alipositisha alichokuwa akifanya na kunitazama, ilikuwa kwa njia yenye umakini zaidi.
"Kuna nini?" Adelina akauliza hivyo.
Nikajivuta na kukaa vizuri, nami nikasema, "Ni kuhusu mimi na wewe."
Adelina akajisawazisha vyema pia na kusema, "Mimi na wewe tumefanyaje?"
Nikaangalia pembeni kwanza nikijiandaa kumweleza.
"Kuna kitu nimekosea JC?" Adelina akauliza hivyo.
Nikamwangalia upesi na kusema, "Hapana, siyo hivyo. Hujakosea popote."
"Nini sasa, mbona unanitia wasiwasi? Kuna tatizo gani?" akauliza akiwa makini zaidi.
Nikawa nikimwangalia kwa hisia sana, nami nikamwambia, "Nimekutana na Miryam leo."
Adelina akapandisha nyusi kiutambuzi, halafu akatikisa kichwa kuonyesha uelewa, kisha akasema, "Sawa. Na?"
"Tukaongea. Nilitaka tu kujua alicho... alichotaka kuniambia jana, maana... kwa sababu ya pressure na nini, nilikuwa sija...."
"Kwa hiyo we' ndo' umemtafuta leo?" akanikatiza.
Nikabaki kimya, nikimtazama na kuona hali yenye uzito kwa jinsi alivyoniangalia.
"Niambie," akasema.
"Ndiyo. Nilimtafuta," nikajibu.
"Okay. Kwa hiyo akasema nini kingine tofauti na... kujaribu kukuomba msamaha?" akauliza.
Nikatazama pembeni kwanza, kisha nikamwambia, "Ana ujauzito."
Adelina akatikisa kichwa kuonyesha uelewa, kisha akabana midomo yake na kuangalia pembeni pia.
Nikamwambia, "Ana wiki chache tu... alikuwa anataka nijue."
Adelina akashusha pumzi, kisha akasema, "Sasa itakuwaje? Kama nyie ni ndugu, na ana ujauzito... mtafanyaje?"
Nikamwangalia na kusema, "Miryam siyo dada yangu."
Adelina akaweka uso makini.
"Ilibidi twende hospitali kupima kwanza DNA, majibu yakaja negative. Ni... suala tulilotakiwa kufanya mapema sana, lakini... haya mambo... yalituchanganya sana, kwa hiyo..." nikaishia hapo na kubaki nimemwangalia tu.
Adelina akasema, "Unataka kurudiana naye?"
Nikashindwa kutoa jibu. Alienda moja kwa moja kwenye pointi hiyo akiwa na nia ya kutaka kujua nilichotaka, na niliona bado alikuwa na imani kwamba ningechagua kumtaka yeye.
Adelina akacheka kwa pumzi na kusema, "Haita-make sense kufikiria unataka kurudiana naye. Kama nyie siyo ndugu, basi... hiyo itawapa nafasi ya kuwa... wazazi... kwa mtoto wenu... na..."
Aliongea kwa njia ya kujipa matumaini, lakini kwa jinsi ambavyo nilimtazama, nadhani tayari alielewa nilitaka kuelekea wapi.
Akasema, "Ngoja kwanza JC. Usiniambie unafikiria... kwanza... Miryam si ana huyo mtu wake? Mmeongea leo... jana alipokufata akakwambia anataka mrudiane, kwani tayari ameshaachana na yule mwanaume?"
Nikaangalia pembeni kwa huzuni.
"Ongea basi JC! Don't leave me hanging!" akaongea kwa hisia kali zaidi sasa.
Nikakishika kiganja chake na kusema, "Nisamehe Adelina."
"Ahh..." akafanya hivyo na kuinamishia uso wake kiganjani.
"Ona... najua tulikuwa tumeanzisha kitu kizuri, na... nimefurahia sana kuwa nawe kwa huu muda, ila..."
"Ila nini?" akanikatiza.
Nikabaki kimya.
"JC mbona unakuwa hueleweki? Si ulisema mwenyewe kwamba humtaki Miryam tena? Eh? Si uliniambia kwake ndiyo umemaliza?" akaongea kwa hisia.
"Najua Adelina. Yale yote yaliyotokea ndiyo...."
"Kwa hiyo ulikuwa unanitumia tu kupoza maumivu, ulikuwa unasubiria yakipoa na Miryam akirudi, mimi unitupe..." akasema kwa hisia sana.
"Hapana, siyo hivyo..." nikajaribu kumsogelea zaidi ili nimbembeleze.
Adelina akawa ameinamishia tu uso wake kiganjani, akionekana kukosa amani kabisa.
"Adelina nisikie. Sina nia ya kukuumiza. Na... kusema kweli, nimekupenda pia japo tumekuwa pamoja kwa muda mfupi. Nilikuwa bado najitahidi... nilijitahidi kumwondoa Miryam moyoni kwa ajili yako... lakini... bado..." nikajikuta naishia hapo tu.
Adelina akatikisa kichwa kwa njia ya kusikitika sana, akiegamia kiganja chake bado, kisha akaunyanyua na kujifuta machozi upesi ambayo sikuwa nimeweza kuyaona kabla. Hilo likanifanya niingiwe na hisia mbaya sana, kuona kwamba mwanamke huyu alikuwa akilia, nami nikamshika mkononi na kumsogelea karibu zaidi.
"Adelina..." nikamwita kwa upole.
Adelina akafumba macho yake na machozi kuendelea kumtoka, kilio kisichokuwa na sauti yoyote lakini kikionyesha uchungu mwingi sana. Aisee!
Nikamshika usoni na kujaribu kumtazamisha kwangu, nami nikamwambia, "Adelina... usilie... please..."
Akaendelea kuonyesha sononeko tu.
Nikamwambia, "Tafadhali naomba unisamehe Adelina. Sikutaka iwe hivi... I swear. Nina... ninakujali sana Adelina. Na nimekupenda pia. Lakini kwa jinsi mambo yalivyo... yaani... sitaki kukuumiza... hata zaidi kwa sababu... najua sitakuwa fair nikisema nigawanyishe moyo wangu kwa watu wawili. Unastahili kupendwa kwa moyo wote, na mimi najua ni mpumbavu mkubwa sana kukuingiza kwenye matatizo yangu namna hiyo, na sasa imekuja kuwa hivi tena... hukupaswa kuja kuiona hii siku. Naomba unisamehe sana kwa kukutendea hivi. Sikuw... Adelina... please... nakuomba usilie..."
Nilijitahidi sana kumbembeleza, yeye akiwa anajipangusa machozi kwa huzuni nyingi, kisha akajitoa kwangu na kunyanyuka, moja kwa moja akiuelekea mlango wa kuingilia ndani hapo. Nilibaki nikimtazama kwa hisia sana, na yeye alichofanya ikawa ni kuufungua mlango huo, halafu akaendelea kusimama hapo hapo bila kuniangalia tena. Ilikuwa ni ishara tosha kwangu kwamba alinitaka niondoke, na kwa kweli nilihisi mvurugo wa hali ya juu. Sikujua nifanye nini upesi ili kumtuliza maana aliendelea tu kuonyesha huzuni nyingi mno kwa machozi yaliyomdondoka.
Nikasimama, nikiwa na lengo la kumfata yeye ili niweze kumsemesha tena na kumfariji, lakini nilipomfikia karibu akanyanyua kiganja chake kunizuia nisimkaribie, na akasisitiza niondoke kwa kuutikisa mlango kidogo. Dah! Nilipondeka sana moyoni. Alitazama pembeni, akijitahidi kujikaza sasa, mtu mzima aliyehisi maumivu ya kutendwa na kijana mdogo, yaani! Nilikosa hata namna ya kuanza kupiga hatua kuondoka maana sikutaka kumwacha namna hiyo. Ikanibidi nilazimishe kumpa kumbatio, ili aone kwamba nilimjali sana licha ya haya yote, lakini Adelina hakutaka nimguse. Hakuongea, lakini akaniondoa mwilini mwake na kutikisa kichwa kukataa kabisa faraja yangu, na najua kwake ilionekana kuwa ya kinafiki tu. Kwa usawa wote. Ningefanyaje?
Ikanibidi tu nitoke hatimaye, nikiwa nimejawa na simanzi nzito, na baada tu ya kutoka akaufunga mlango upesi sana. Nilihisi kuchoka mwenyewe yaani. Haya maisha yangu haya! Mambo niliyosema hapo ndani kwake yalikuwa kweli. Sikutaka kumuumiza zaidi ingawa yeye angeona ni kama nimemuuza tu, kwa namna yoyote ile nilijua angejisikia vibaya sana. Na ndiyo, hata mimi ilinifanya nijihisi hatia kwa kweli. Ni kama nilikuwa nimemtumia tu dada watu, na sasa nikawa ninamtema baada ya kumchoka. Ila haikuwa hivyo kihalisi. Nisingejisikia vizuri hata kidogo kuacha mambo baina yangu na Adelina katika sehemu mbaya, hivyo ningetakiwa kutafuta wakati mwingine ili niongee naye tena na kuweka hali ya amani zaidi kati yetu.
★★★★★★★★★★
ITAENDELEA
★★★★★★★★★★
Whatsapp +255 678 017 280
Daaaah ety hata adelina lishangazi linalizwa na mapenzi daah mwandishi unajua kinomaa anMIMI NA MIMI 3

Bless up master Tony 🙏MIMI NA MIMI 3
A Story by Elton Tonny
Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Siri, Tamaa, Hila, Usaliti, Ukatili, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa
R-rated 18+
Enjoy!
★★★★★★★★★★★★★★★★★
SEHEMU YA KUMI NA NNE
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Tukakaa pamoja kupata chakula, na Miryam alijitahidi kuonyesha yuko sawa na kushiriki maongezi pamoja na wengine tulipoendelea kufurahia pindi hiyo. Maongezi yalimhusu Evelyn zaidi na vituko vyake, ikifanya Stella awe mtawala wa mazungumzo zaidi, hivyo kwa kadiri kubwa Miryam alikuwa mtulivu. Nilijaribu kurudisha umakini kwake pia kwa kuzungumzia ishu ya Bi Zawadi kuumwa hapo juzi, na angalau mwanamke wangu akapata nafasi ya kuzungumzia moja mbili tatu za huko kwao; akikazia kwamba mambo yalikuwa sawa zaidi kwa kipindi hiki.
Tumekuja kurudi masofani baada ya kushiba ikiwa ni kwenye mida ya saa tano, na mzee Manyanza bado hakuwa amerejea. Usiku ukiendelea kusonga, Miryam akaniambia ingembidi tuondoke kwa sababu ya kesho kuhitajika kazini mapema, na hilo likaniacha nikijihisi kama mpotezaji. Lengo lililotuleta hapo halikutimia, lakini nilielewa sababu. Nikamjulisha mama ya kwamba tungeondoka sasa, na hilo halikusikika kuwa jambo jema kwake. Hata yeye aliona ni kama hakupata muda wa kutosha kuongea na Miryam pia, maana najua angekuwa na nia ya kutaka kuzungumzia mambo muhimu pamoja na sisi wawili, ila uwepo wa wengine ulikwamisha hilo.
Akamtaka Miryam alale hapa nyumbani leo, ili huo muda wa kuongea upatikane baadaye, lakini ndiyo bibie akamweka wazi kuhusu kazi. Ingawa hivyo, akaahidi kuja tena wakati mwingine, labda kesho, ili hilo lifanyike. Stella alikuwa mtulivu wakati huu, naona alihisi kwamba kuna mambo mazito yaliyokuwa yakiendelea lakini hakuuliza lolote. Evelyn aliletwa ili amtembelee bibi yake, lakini sasa mwanangu akawa amesinzia, hivyo mama akamwambia Stella amwache Evelyn alale tu hapo, halafu kesho angemwijia endapo kama dogo angesumbua 'mama, mama.' Stella naye alihitajika kuondoka leo leo akapumzike kwa ajili ya kazi kesho pia, hivyo akakubaliana na ombi la mama akisema kuwa Deborah ndiyo angekuja kumchukua mtoto hiyo kesho. Alipajua hapa pia.
Kwa hiyo tukaanza kumuaga mama na Stella, na Miryam akapewa kumbatio la upendo kutoka kwa mama na kuambiwa asiache kurudi ili watumie muda mwingi zaidi pamoja. Tena akatania kwamba Miryam aje siku fulani yeye mwenyewe ili wakae na kunisema mpaka nipaliwe na maji popote nitakapokuwa nayanywa, nami nikawaambia sitapaliwa ng'o hata wakiongea mpaka midomo ivimbe. Mzee alikuwa amepiga simu tena kumwambia mama angeweza kufika nyumbani kwenye mida ya saa sita, lakini kwa muda huo sisi tungekuwa tumekwishaondoka.
Wakati tunaelekea kwenye magari, Stella akiwa bado huko ndani, mama akaniuliza kabla sijaingia garini ikiwa kulikuwa na jambo lolote lenye utatizo baina yangu na Miryam, maana alihisi ni kama vile tulileta jambo zito hapo. Nikamwondolea wasiwasi kwa kumwambia kila jambo lilikuwa sawa, na angeelewa dhumuni letu kuja ni lenye kumletea amani nyingi wakati ambao tungeweza kuliongelea. Hivyo angetakiwa tu asubiri, kesho panapo majaliwa tungerejea ili kuzungumza. Hakuwa na neno mama yangu, na kwa hapo ndiyo tukahitimisha matembezi yetu hapa kwa siku ya leo. Nikampatia Simba funguo za gari, na rafiki yangu akaanza kutuendesha huku mie nikikaa siti za nyuma pamoja na bibie.
Safari hiyo fupi ya kwenda kwa mama ilikuwa ya malengo ambayo hayakuweza kufikiwa kwa ukamili, ingawa najua iliacha alama nzuri pale. Ujio wa Stella na mwanangu haukutegemewa, na haukuwa mbaya, ila kumfanya mpaka Miryam aanze kuumwa tumbo ilionyesha kuna aina fulani ya wasiwasi aliokuwa nao bado. Labda hisia zake nyingi ziliathiri sana mfumo wake wa uzazi pia, na kwa hilo ningehitajika kuangalia kama kuna njia hususa ya kumsaidia atulize hali yake ili isije kuleta shida kubwa baadaye. Tukiwa mwendoni alipiga simu kwao na kuzungumza na Mariam, akimwambia alikuwa njiani kurudi lakini angechelewa, hivyo wafunge tu geti mpaka muda ambao angefika.
Dakika tulizokata mpaka kuifikia nyumba niliyoishi pale Bamaga hazikuwa na maongezi mengi, na Simba alikuwa mtulivu zaidi kwa pindi hii baada ya kuwa amezungumza na mtu fulani kwenye simu. Tulipofika kwangu ndiyo ikawa wazi ni nani, baada ya Simba kuniambia kwamba angekwenda mahali fulani hapo mbele mara moja, akitumia gari langu, na angewahi kurejea. Hapo bila shaka angekwenda kwa mshangazi wake, na mimi nikilijua hilo vyema nikasema tu sawa, na upesi jamaa akamuaga Miryam na kuondoka; akituacha tunaingia ndani ya geti.
Nilikuwa nimeanza kumwambia Miryam aone busara ya leo kulala hapa hapa kwangu kwa sababu mida ilielekea saa sita, mpaka afike huko Mbagala muda ungekuwa umeenda sana, lakini akaniambia haikuwa na shida. Alitamani sana kubaki nami pia, ila ndiyo kazi nayo ilimhitaji awajibiike hasa kwa sababu ndiyo siku za mwanzo tu toka ameanza kuifanya. Tukaahidiana kukutana kwa siku ya kesho bila shaka, kisha akaingia kwenye gari lake la Mark X lililo jipya kabisa bado na kulitoa mpaka nje ya geti, nami nikaenda hapo na kuingia garini ili niagane naye ipasavyo. Nilivutiwa sana na jinsi ambavyo harufu yake Miryam ilienea ndani ya gari zima, nami nikafumba macho kwa sekunde chache nikiivuta kuisikilizia kama mraibu vile.
"Vipi?" Miryam akauliza hivyo.
Nikamwangalia na kusema, "Napenda harufu yako. Umeijaza humu kote."
Akatabasamu na kutikisa kichwa kiasi.
"Huko Benki kesho si unatakiwa ufike saa mbili juu ya alama?" nikamuuliza.
Akaniangalia na kusema, "Ndiyo. Yaani... kazi ndiyo zinaanza muda huo."
"Kwa hiyo ni kuamka saa kumi na mbili, kujiandaa, kwenda. Tsk... utachelewa kufika, utalala masaa machache, na hiyo hali yako sasa hivi inahitaji ulale masaa mengi. Si ungelala tu hapa hapa?" nikamwambia.
Miryam akatabasamu kiasi na kusema, "Nikisema nilale hapa hapa, najua hayo masaa yatapungua kuliko unayofikiria nitapungukiwa kwa kurudi nyumbani."
Nikatulia kwanza, na baada ya kuelewa alichomaanisha, nikatabasamu kiasi na kutikisa kichwa kama kutoamini. Miryam akaendelea kutabasamu.
"Me siyo mhuni kihivyo," nikamwambia.
Akacheka kidogo na kulalia usukani.
Nikamwangalia kwa hisia za furaha, nami nikamuuliza, "Unajisikiaje lakini sa'hivi? Tumbo..."
Akaniangalia na kusema, "Limeachia. Najua itatokea tena, litaanza kuvuta mara hapa, mara pale, ila... halisumbui sana."
"Kuna vyakula utatakiwa uanze kula zaidi kwa kipindi hiki, halafu na... mazoezi-mazoezi pia," nikamwambia.
"Mh? Mapema hivi?"
"Ndiyo."
"Ahah, hamna... bado bado bwana. Hii hali wala isikutie presha, niko sawa," akasema hivyo kwa uhakika.
Nikaendelea kumwangalia kwa hisia makini.
Alipoona hivyo, akasema, "Unaniangalia kama vile kuna jambo zito unataka kusema."
Nikatikisa kichwa kukanusha na kusema, "Hamna. Nimewaza tu kitu."
"Kitu gani?" akauliza.
"Nakumbuka ma' mkubwa wako aliwahi kusema hujawahi kubeba ujauzito kabisa. Hilo ni kweli?" nikamuuliza.
Miryam akatikisa kichwa kukubali.
"Hata mara moja?"
"Hapana. Nilikwambia sikuwa active sana kushiriki tendo... tokea muda. Na hata mara ambazo nilikutana na mwanaume... sikuwahi kubeba mimba," akaniambia.
Nikatikisa kichwa kuonyesha uelewa.
"Unawaza nini?" akauliza.
"Nafikiria uje tena Muhimbili. Upime," nikamwambia.
Akazima gari kwanza, kisha akaniuliza, "Unahofia nini?"
"Hiyo ishu yako ya tumbo inaweza ikawa shida kubwa ambayo bado haijakomaa. Hatutataka ikomae, siyo?"
"Ahah... hamna, labda... ni kwa sababu labda ndiyo mwanzo tu wa kuzoea hii hali, inaweza isiwe shida kubwa sana," akasema.
"Yeah, unaweza ukawa sahihi, ila nitataka tuhakikishe. Uje... upigwe CT scan, tuangalie," nikamwambia.
"CT sc... Jayden..."
"A-ah, Miryam... usikatae. Najua baadhi ya watu walioona kitu kama yako kuwa ishu ya kawaida tu, halafu baadaye ikapelekea placenta zao ziwe dhaifu sana. Hiyo inaweza ikatokea kwako pia, tusipuuzie uwezekano. Mtoto anaweza asikue vizuri, na wewe ukaumia zaidi baadaye," nikamwambia kwa upole.
Akatikisa kichwa kuonyesha uelewa, naye akaniambia, "Sawa. Tutafanya hivyo basi. Asante."
Nikaendelea kumtazama kwa utulivu.
"Sikutaka tu iwe gharama na nini... ningeweza tu kufanya kipimo cha kawaida, lakini... una njia yako ya kusisitiza huwa sina budi kukubali," akasema hivyo.
"Si ndiyo maana nikakupata? Au umesahau nilivyosisitiza kipindi kile?" nikamwambia kiutani.
Akatabasamu kiasi na kunishika kiganjani.
Nikamwambia, "Najua leo haijaenda kama tulivyotarajia. Nataka kujua kama uko sawa Mimi."
Akaniangalia na kusema, "Niko sawa Jayden, acha kuwaza."
Nikamwangalia kwa utathmini.
"Ahah... unanitendea kama yai sa'hivi wakati juzi tu hapo ulikuwa umevimba, umenikasirikia, hutaki kabisa kunisemesha," akaongea kiutani.
Nikaangalia mbele na kusema, "Ah, huwezi kunilaumu. Na me najua kununa."
Miryam akacheka kidogo kwa pumzi.
Nikamwangalia tena, kisha nikapitisha kiganja changu shingoni kwake na kuanza kuitomasa taratibu. Akawa akiniangalia kwa macho yenye uvutio, nami nikamwambia, "Nakupenda."
Akatabasamu kwa hisia, kisha akanisogelea usoni na moja kwa moja kuufuata mdomo wangu kunipa denda moja tamu kuliko hata msosi wote tuliokula huko kwa mama, kisha akajitoa taratibu na kunong'oneza maneno, "Nakupenda pia."
Tukaendelea kulaziana vichwa vyetu huku akiwa amefumba macho yake, mimi nikishika tumbo lake kwa chini na kufanya kama kulibembeleza kwa kiganja changu, naye akaushika mkono wangu huo na kuupitisha mgongoni kwake, akijiruhusu kuulalia mwili wangu ili nimpe kumbatio zuri la kumfanya ajisikie fahari. Nikaendelea kumshikilia na kumpapasa kwa njia ya kubembeleza sana, kana kwamba alitaka kusinzia mikononi mwangu, kisha dakika chache zikapita ndiyo akajitoa kwangu taratibu na kuniangalia kwa hisia.
"Nafurahi sana kurudi mikononi mwako tena. I'll never forsake you again," akaongea hivyo kwa hisia.
Nikatabasamu kiasi na kumwambia, "I know. Hata mimi pia, ninathamini sana uwepo wako kwenye maisha yangu. We ni sehemu kubwa ya mambo yanayonifanya niwe na furaha Miryam. I will never forsake you again."
Akatabasamu pia na kusema, "Kwa maneno sitakufikia."
Nikatikisa nyusi kwa kujitutumua na kusema, "Kombe ni langu."
Akacheka kwa pumzi na kujirudisha kuketi sitini vizuri, naye akaushika usukani na kusema, "Basi..."
"Usiku mwema," nikaongea kwa ajili yake.
Akatabasamu na kusema, "Na we' pia."
Nikamwambia, "Uendeshe vizuri, ufike salama. Sitalala mpaka nione ujumbe wako unaosema 'nimefika mume wangu, lala salama, I love you daddy... mwah mwah mwah!'"
"Mm... ahahah... tsk, we' ni matatizo..." akaongea kwa furaha.
"Ole wako sasa," nikamwambia hivyo na kufungua mlango kushuka.
Nikatoka na kusimama hapo nikimwangalia tu bado, nami nikamrushia busu kwa ishara ya mdomo. Yeye vilevile akarusha busu kwa kutumia kiganja, lakini nikatania kwa kumwonyesha kwamba busu hiyo ilinipita na kupotelea hewani, hivyo anirushie nyingine. Akarudia tena huku akitabasamu, nami nikarudia huo huo utundu kwa mara nyingine. Sasa akanikazia macho kama kuudhika eti, nami nilipomsisitizia ailete ya tatu, zamu hii akaituma moja kwa moja kwa mdomo wake, nami ndiyo nikaipokea na kuituliza moyoni. Tabasamu lake sasa lilionyesha amani nyingi sana, naye ndiyo akawasha gari hatimaye na kuanza kuliondoa eneo hilo, akiniacha namsindikiza kwa macho na kumpungia mkono kumuaga. Huu ndiyo ungekuwa mwanzo wa amani ya penzi letu kurudi mahali pake.
★★★
Jumamosi ilipoingia, mambo hayakuwa mengi kwa upande wangu zaidi ya kupumzika hata zaidi, kula, kuburudika na sinema kidogo, na kuongea na mpenzi wangu wa moyo. Miryam angekuwa kazini leo pia mpaka jioni, na kwa namna tulivyoyaacha mambo sehemu ya moto sana usiku wa jana baada ya kuondoka Goba kwa mama, sote tulitaka kuonana tena baadaye na kutumia muda mwingi zaidi tukiwa pamoja. Nilikuwa nimependekeza niende kwao kule kumtembelea Bi Zawadi jioni ili Miryam akitoka kazini anikute pia, lakini akaonelea hilo kuwa jambo la kungoja kwanza. Tena, kwa leo alitaka iwe mimi na yeye tu, yaani akitoka kazini, arudi nyumbani kujiandaa, halafu tungekutana mahali ambapo ningependelea ili tule pindi yenye kusisimua.
Nilihisi hilo lingeelekea pazuri sana kwa leo, kwa hiyo kamshawasha ka kutaka muda usonge ili jioni ifike haraka kalikuwa juu sana. Simba alirudi asubuhi ya siku hii baada ya kulala huko alikojua, akiwa amevunja ahadi yake ya kuwahi kurejea, lakini haikuwa na noma kwangu maana nilielewa mabiti yake. Tena mjeshi akatumia muda mrefu kunisimulia kuhusu mwanamke aliyekuwa ameenda kukutana naye, akijisifu kumpa kipondo cha uhakika mpaka kitanda chote kutepeta kwa kulowana. Nikamshauri tu awe makini na hii mishangazi ya Dar, na kwamba kama mke wake angejua huko Mwanza ndiyo pangetikisika wakati ambao angerudi.
Basi, ikawa ni kutulia tu nyumbani hadi mida ya mchana, na nikiwa nimeshafikiria muda niliohitaji kutumia nje ya kazi, nikawa nimeongea na daktari wangu mkuu huko hospitali kumwambia kwamba kikazi ningeweza kurudi angalau kwenye Jumatano. Sijui kama ilikuwa wazi kwake kwamba nilitia uzushi mwingi, maana Krismasi ilikuwa Jumatatu, kwa hiyo akaniambia kiutani kwamba alijua nimeondoka ili kuja tu kula bata na siyo matatizo wala nini. Nikaapa kabisa kwa kusema haikuwa hivyo, na kwamba ndiyo, ningesherehekea Krismasi kama wengi lakini hilo halikuwa jambo lililofanya nikatishe muda wa kufanya kazi kwa siku chache. Maelewano yakawa ni mazuri tu kwa upande huo.
Nikawaza nitoke kidogo, kwenda mahali fulani kutembea kwanza, na wazo zuri la sehemu ya kwenda likanijia. Sikuwa nimeenda kumwona Jasmine kwa wiki chache sasa, hivyo nikaamua kujiandaa vizuri ili nikatumie muda wote uliobaki kuwa huko mpaka wakati ambao ningeweza kukutana na Miryam. Nikamwambia na Simba twende pamoja, lakini akawa na mpango wa kwenda kwingine kwanza, hivyo akasema angefika baadaye kwa dada yangu kumsalimu pia. Alipajua kwake. Kwa hiyo nikawa nimempigia Jasmine kumwambia nilipanga kupita huko kumsalimia, naye kwa furaha akasema niende maana alinikosa pia. Hivyo, nikaondoka kwangu ikiwa ni kwenye mida ya saa nane, nami nikamtumia Miryam ujumbe kwa simu kwamba akishatoka kazini anishtue.
Safari ya kwenda huko Segerea kwa Kevin, mume wa Jasmine, ilichukua kama robo tatu ya saa hivi, nami nikafika huko na kupokelewa vyema na dada yangu kipenzi. Nyumba yao ilikuwa kubwa pia, geti na mambo mazuri-mazuri ya kishua yaani, na Jasmine alikuwa anazidi kung'aa tu. Baada ya kujifungua mwili wake halisi ulirudi, akiwa na ulingano fulani na mwili wa Miryam kwa unawiri, na wakati huu alikuwa akipumzika tu na kuwajali mapacha wake wazuri kama yeye. Nikafikia kuwasalimia mapacha, wakiwa bado wadogo kweli na kufurukuta-furukuta kwenye vitanda vyao vya watoto, na walipewa matunzo bora kwelikweli kwa jinsi ambavyo Kevin na Jasmine waligharamika kuweka kila aina ya huduma kwa ajili yao hapo ndani. Wafanyakazi wa ndani walikuwa wawili kabisa.
Kwa hiyo tukapata chakula kidogo, na baada ya Jasmine kushughulika na mahitaji ya watoto na kuwapumzisha, tukakaa kwa utulivu kuzungumza. Hatua za mwanzo zilikuwa ni kujuliana hali, ndoa na familia yake, wakati huu Jasmine akiwa ameridhishwa na njia ya Kevin ya kumtendea tofauti na ilivyokuwa mwanzoni. Alipata amani zaidi, akisema Kevin aliyempenda mwanzo kabisa ndiye aliyekuwa amerejea kwa kipindi hiki, akiwa mume na baba bora. Ila ndiyo hakuwa na uhakika wa asilimia zote maana alitujua wanaume vizuri na mambo yetu. Ilipofikia upande wangu wa mambo, jasmine alitaka kujua niliendeleaje, na ndiyo nikaona nimfungukie kwa mengi yaliyokuwa yametokea tangu ule usiku tulipojua mahusiano ya mama na Bi Jamila.
Nikamweleza hatua iliyokuwa imefika sasa, ujauzito wa Miryam, na kurudiana kwetu ambako kulifanya twende jana kwa mama kutaka kuongelea mambo mengi muhimu. Jasmine alishangazwa zaidi baada ya kugundua kwamba mimi na Miryam hatukuwa na undugu, akitaka nimwelezee uhakika wangu ulikotoka, na ndiyo nikamwambia kuhusu kipimo cha DNA tulichofanya ile juzi kilichothibitisha zaidi kwamba hatukushiriki damu kwa njia yoyote. Ikawa imebaki kujua upande wa Mariam na Tesha.
"Eeh! Haki ya Mungu," Jasmine akasema hivyo, tukiwa tumekaa sofani pamoja na glasi zenye juice mikononi, mida ikiwa imeshafika saa kumi na mbili.
"Ndo' hivyo," nikaongea pia.
"Sasa hiyo mizungusho yote ya Miryam, mpaka kuanza kusumbuana jamani, si mngekuwa tu mmeenda kupima mapema mkajua?" akaniambia.
"Ile ishu ilitushtua wote, kama unavyojua. Alikuwa na njia yake ya tofauti ku-process..."
"A-ah, hata kama. Me nakwambia ukweli, Miryam wako alikuwa anajitanguliza yeye tu. Si ndo' mpaka kukataa kuonana nasi, kuongea, kisa tumeambiwa tuna undugu basi ndiyo akataka kukata nyuzi zote na siye..."
"Uliongea naye lini Jas, ukamwomba mkutane, akakataa?"
"Si nilisikia ulimfata hadi kwao kumwomba mwongee ila akakufukuza?"
"Nani alikwambia hivyo?"
"Nina mitandao yangu."
"Ah, haijalishi tena. Kikubwa sasa hivi mambo yanarudi mahali pake, ndiyo maana nikakwambia wewe kwanza ili kama kuna hard feelings zozote kutoka kwako..."
"Me niwe na hard feelings za nini sasa? Hamna mtu aliyenikosea, niko zangu huku nimejituliza," Jasmine akasema.
"Sawa. Kama vipi, mtafute Miryam mwongee tena, yuko poa zaidi sasa hivi," nikamwambia hivyo.
"Mimi kujipendekeza J siwezi. Siyo keamba nina kinyongo, wala... tena namkubali sana Miryam. Ila ndiyo sikujisikia tu fresh. Tulianza kuwa kama ma-best kabisa, afu' ghafla tu akakatisha mawasiliano," akaniambia.
"Nimwombee samahani tu. Alikuwa ameumizwa na vingi," nikamwambia kiupole.
"Haina shida. Kama mnarudiana, sawa. Mambo yakiwa fresh mtaoana, na hiyo ni ikiwa Tesha pia na Mariam siyo wadogo zetu," akasema.
"Hata kama tutakuwa tume-share baba na hao wawili, mimi na Miryam tutakuwa pamoja tu. Nimeshachoshwa na visa vyote vinavyojaribu kuzuia niwe naye," nikaongea kwa uhakika.
Jasmine akacheka kidogo na kupiga viganja vyake, naye akasema, "Umechizishwa na huyo mwanamke, sijawahi kuona."
Nikatikisa nyusi kukubali.
"Kwa hiyo jana mmeenda nyumbani, lakini haukumwambia mama kuhusu Miryam kuwa na mimba?" Jasmine akauliza na kunywa juice yake.
"Eeh. Kama nilivyokwambia, Stella alikuja, kwa hiyo..."
"Akawaharibia?" akanikatiza.
"Siyo hivyo. Mazingira tu yali-change kwa Miryam, akaona ni busara tukingojea na kuongea na wazazi baadaye. Na mzee hakuwepo hata hivyo," nikamwambia.
"Mhm... bado sielewi," akasema.
"Kuhusu?"
"Kuhusu nyie. Simba kaniambia tayari ulikuwa na demu mwingine, ila Miryam alipokuja kusema ana mimba, ukamwacha instantly," akaniambia.
"Dah, Simba naye mbea! Umeongea naye lini?"
"Ahahaha... juzi. Alinipigia. Na si ni kweli?"
"Sawa, eeh ni kweli. Unataka kusemaje?" nikamuuliza kistaarabu.
"Well, nawaza kama Miryam asingekuwa amepata mimba, angeendelea kukuchunia tu, au vipi? Naona ni kama alikuwa anatafuta sababu ya kutaka mrudiane hata baada ya yeye mwenyewe kukufukuza, na mimba ikawa njia rahisi. Ni wazi mwenzio huyo anajua kurusha tantrum nyingi, lakini hana msimamo. Kama wewe tu," jasmine akaniambia hivyo.
Nikaweka uso makini na kusema, "Mbona unaongea kwa chuki sana? Hujapenda me kurudiana naye?"
"Sijasema hivyo..."
"Sa' mbona unampondea sana?"
"Nimekwambia nachowaza tu, sijampondea mtu yeyote mimi. For what its worth, mnafaana. Mko tayari kufanya mambo yaende kwa njia ya kuwafaidisha nyie hata kama yatawaumiza wengine, such ni jinsi mnavyopendana," akaniambia hivyo.
Nikatabasamu na kutikisa kichwa kidogo, nami nikasema, "Unajikuta mama ushauri. Lakini hilo siyo kweli. Sisi wote tulikuwa tunatafuta namna ya kusonga mbele, hm? Sidhani kama yeye alifikiria kuhusu ujauzito, hata kama alitaka turudiane, siyo kwamba angetumia mimba kama kigezo. Unajua kama tungekuta sisi ni ndugu ukweli, hilo lingekuwa tatizo. Hali zilikuwa tu ngumu kwa hisia zetu sote dada, ndo' maana mambo yameenda vibaya-vibaya."
"Ni kweli lakini," Jasmine akasema hivyo kwa utulivu.
"Yeah, kwa hiyo... kuumiza wengine... itatokea tu, siyo kwamba mimi au yeye tumefanya makusudi. Huyo dada niliyekuwa natoka naye tuliongea, akaelewa, anamjua Miryam, kwa hiyo... siyo kwamba nimeacha mtu vibaya," nikamweleza kwa ufupi.
"Haya. Ni vizuri. Kilichobaki ndiyo kuhalalisha ndoa sasa kama sikosei. Uharakishe tule keki," Jasmine akasema hivyo.
Nikacheka kidogo, na ni wakati huu ndiyo simu yangu ikaanza kuita. Kuangalia mpigaji nikakuta ni Miryam, nami nikapokea kumsikiliza. Tayari alikuwa ameshatoka kazini, tena leo saa kumi tu, akafika nyumbani, na sasa alikuwa anaanza kujiandaa ili aje tukutane. Alitaka kujua tunaenda wapi, nami nikamwambia aje yale maeneo ya kule Stesheni ambako tulipandia treni za mwendokasi kipindi kile, kuna sehemu nzuri yenye hoteli maridadi maeneo ya huko tungeingia. Aliona kama ni mbali sana, lakini nikambembeleza aje tu kwa kusema maandalizi nilikuwa nimeshafanya. Akalegeza na kukubaliana nami.
Baada ya kumalizana naye, ikanibidi nimuage Jasmine sasa, yeye akiwa ananihukumu kwa kutaka kumkimbia kabla ya msosi wa jioni na Kevin kurudi, lakini nikamwambia tungepangia hilo wakati mwingine. Nikakumbatiana naye kwa upendo na kwenda kuwaona wapwa wangu pia, waliokuwa wamesinzia kwa pamoja, kisha ndiyo nikamwacha dada yangu ili kwenda kuonana na mpenzi wangu. Hatimaye jioni niliyoingojea kwa hamu ikawa imefika.
★★
Nilihitaji kwenda kwangu kwanza ili nichukue zile zawadi ambazo nilinunua kwa ajili ya bibie, kisha ndiyo nikaelekea huko nilipomwambia tukutane, nikiipita Kisutu na kuingia mitaa yenye barabara ambayo ingetupeleka mpaka kwenye hoteli niliyodhamiria kutumia muda mzuri na bebe mama wangu mtarajiwa. Kama kungekuwa na muda wa kutosha tungeenda huko Hyatt Regency tena, lakini nilitaka tu kumpa mwanamke wangu kamguso ka mazingira mapya kwa leo. Najua angekuwa amechoka kiasi kwa kazi za siku, hivyo nilipanga kumchangamsha haswa hadi aridhike na uamuzi wake kulirudia tena penzi letu.
Nilifika maeneo ya stendi ya Stesheni na kwenda kuegesha gari usawa wa barabara iliyokinzana na majengo yenye maghorofa marefu sana, nikiona iwe jambo jema kumngoja Miryam afike hapo ili tusindikizane hadi kwenye hoteli ile. Iliitwa Golden Tulip, City Center, katikati ya jiji yaani. Ilikuwa moja ya hoteli maridadi sana, na Miryam angehitaji kuufahamu uelekeo vyema zaidi ndiyo sababu nikaona nimngojee sehemu aliyoijua kabla hatujaenda moja kwa moja huko. Sikudhani angekuwa akipajua kabisa. Kwa hiyo nikamngoja hadi imeshaingia mida ya saa mbili, ndiyo akawa amefika eneo hilo na kukutana na mimi pale nilipoegesha gari.
Tukakutana ndani ya gari lake, nikiwa nimeingia humo baada ya kutoka sehemu ya benchi la kusubiri nilikokuwa nimekaa na wadau wachache, nasi tukakumbatiana kwa upendo na mimi kujiruhusu kuutathmini uzuri wake kwanza. Kama kawaida yake, alijiweka katika hali ya urembo wa kadiri tu, lakini kwa uzuri aliokuwa nao ni kama ilipitiliza. Akiwa amevaa blauzi nyepesi ya njano na suruali yenye kubana ya kijivu, alivutia sana usoni kwa namna alivyozitengeneza nywele zake kwa kuziachia zimwagikie mgongoni, huku mbele akileta chache zifunike paji lake la uso kwa namna wazungu waitayo "bangs." Ulikuwa mwonekano fulani mpya kwangu kumwona nao kabisa, hivyo nilivutiwa mno kujua alifahamu mitindo mingi yenye kupendezesha hata kwa kiasi alichojiwekea.
Baada ya Miryam kuuliza tunaelekea wapi, nikabaki nikimtazama tu kwa hisia, naye akasema, "Hatutamaliza kilichotuleta huku kote ikiwa utaendelea kunikodolea tu hivyo."
Nikaacha kumwangalia na kutazama mbele, nami nikacheka kidogo kwa pumzi.
Miryam akacheka kidogo pia, naye akasema, "Umekuwa mkimya. Kwema lakini?"
Nikamwangalia na kusema, "Kwema. Nilikuwa nakuangalia tu."
"Kwani hujawahi kuniona?"
"Siyo kuhusu hilo. Ni unavyojiweka yaani... simple tu, lakini... inakuwa ni kama kila siku nakuona kwa mara ya kwanza," nikasema hivyo.
"Wacha!" akaongea kikejeli.
"Ahahah... Nini sasa? Unabisha?"
"Sijabisha. Hilo unalijua mwenyewe..."
"Ninafurahi tu kukuangalia," nikamwambia kwa hisia.
"Asante. Hata we' una... unavutia," akasema hivyo.
Nilibaki kumwangalia kwa umakini baada ya yeye kusema hivyo na kunitazama kwa njia fulani kama vile anajikaza, nami nikamuuliza, "Uko sawa?"
Akatikisa kichwa kukubali.
"Vipi? Mbona naona kama unataka ku..."
"Tunaenda wapi?" akanikatiza kwa kuuliza hivyo, akitazama mbele.
"Huko mbele tu. Karibu na kituo cha Ferry," nikamwambia.
"Sawa. Twende basi," akasema hivyo kwa sauti ya chini na kukishika kiganja changu.
Nilianza kuhisi ni kama anakaza hisia fulani, nami nikasema, "Naona kama uko juu-juu, sijui chini-chini... umechoka sana?"
Akatikisa kichwa kuonyesha hana uchovu.
"Tumbo je?" nikauliza.
Akaniangalia na kusema, "Hamna. Twende tu Jayden, kama unachukua gari lako, me nitakufata, tuna... tuwahi."
Nikakunja uso kiasi na kutabasamu, nami nikamuuliza, "Miryam vipi?"
Akabaki kunitazama kwa hisia fulani hivi, makini, ila kama legevu.
Nikamsogelea usoni na kusema, "Niambie. Sijawahi kukuona namna hii yaani. Unatoa expression fulani usoni si... sielewi. Nini shida?"
Akabana midomo yake kiasi na kisha kusema, "Ninahisi... desire."
Alisema hivyo taratibu sana, kwa sauti tamu ya chini, nami nikaachia tabasamu kwa kupendezwa na maneno hayo. Inaonekana hamu yake kwangu ilikuwa kali mno yaani mpaka akawa hatulii, nami nikasema, "Pole. Usijali. Naenda kuku-fix."
Miryam akanikazia macho na kubana tabasamu lake, halafu akanipiga mguuni na kuangalia pembeni kwa njia fulani ya manung'uniko ya deko.
Nikatabasamu kiasi na kusema, "Sawa. Naenda kwenye gari, nifuate."
Akatikisa kichwa kukubali hilo.
Raa!
Mambo mazuri yangefuata hapa, si unajua wanasemaga hawa watu huwa wanapanda mizuka sana wakiwa na hizi hali zao, na macho ya Miryam yalionyesha hilo kwelikweli kutafsiri vyema maana ya neno alilolisema, "desire," kuwa hamu nzito sana ya kutaka huo mzuka upozwe. Kwa hiyo nikafungua mlango, na kabla sijashuka, simu yangu ikaanza kuita. Ilikuwa kiganjani, na hapo hapo nikaona mpigaji alikuwa ni Stella. Ohoo!
Sijui angekuwa anahitaji nini, lakini nilihisi angeweza kuvuruga hii ya leo kama ningepokea na kuzungumza naye. Ila... nikaona nipokee tu na kushuka kutoka kwenye gari, huenda hii ingemhusu mwanangu, na hilo lilikuwa muhimu. Lakini kama ingekuwa mambo mengine, ah, ningempiga chini na kurudisha umakini wote kwa mwanamke wangu mwenye "desire." Leo ingekuwa denja!
Baada ya kuweka simu sikioni, nikasema tu, "Hallo..."
"Ba' Evelyn..."
Nilikuwa karibu kuufunga mlango wa gari lake Miryam, lakini nikaishia kusimama hapo kwanza baada ya kusikia sauti hiyo iliyoniita kutokuwa ya Stella. Ilikuwa ni Deborah, dada yake. Aliiniita kwa njia fulani ya haraka sana, kama vile mtu aliyeshtuka, na hilo likanitia umakini.
"Deborah?" nikaita.
"Baba Evelyn, tuko hospitali sasa hivi. Njoo haraka tafadhali!"
Mh!
Deborah alisema hivyo kwa sauti makini, ikionyesha kulikuwa na dharula mbaya sana na siyo tu labda alikuwa hospitali kumtembelea Stella.
Nikauliza, "Kuna nini dada?"
"Evelyn anaumwa. Sana. Kazirai, haamki!" Deborah akasema hivyo.
Eh!
Nikabaki nikitazama mbele nikiwa nimekaza macho, mtu ambaye angeniangalia angedhani niko sawa tu na ninasikiliza anayezungumza kwenye simu kwa umakini, lakini wasiwasi mwingi ulikuwa umeanza kuniingia.
"Sielewi, unamaanisha nini?" nikamuuliza kwa sauti tulivu.
"Hata sisi hatujui, yaani ndiyo tumemfiikisha sasa hivi," akaniambia.
"Stella?"
"Ndiyo, tupo naye. Ana.. anahangaika hapa kujua shida nini, mtoto hajaamka tokea jioni..."
Nikafumba macho na kutuliza hisia, nami nikatikisa kichwa kwa kusikitika.
"Stella amechanganyikiwa, kashindwa hata kuongea, amenipa simu akaniambia nikutafute. Nakuomba uje baba Evelyn," Deborah akasema hivyo.
Nikatazama ndani ya gari lake Miryam na kumwona, akiwa ananitazama tu baada ya kuona nimeishia kusimama tu hapo hapo, nami nikainamisha uso kiasi na kumwambia Deborah kwenye simu, "Sawa. Nakuja."
Baada ya kumwambia hivyo, nikashusha simu na kuangalia mbele kwa kuhisi vibaya moyoni, nikiwaza hali ya mwanangu, na pia ya mpenzi wangu hapo.
"Jayden..."
Miryam akaniita kutokea ndani ya gari, nami nikamwangalia na kisha kuingia tena, nikikaa na kumtazama kwa hisia za huzuni.
"Vipi? Kuna tatizo?" akauliza kwa kujali.
"Evelyn anaumwa. Wamempeleka hospitali, wanasema amezidiwa. Hajaamka," nikamwambia hivyo.
Miryam akaangalia mbele na kusema, "Masikini! Yuko hospitali gani?"
"Itakuwa Rabininsia," nikasema hivyo.
"Basi, twende pamoja tukamwone. Inaweza kuwa kitu serious, ni muhimu uwepo," Miryam akasema hivyo.
Nikabaki nikimtazama kwa hisia za kujali zaidi.
"Twende, muda usije kukutupa. Huku tutakuja wakati mwingine," akaongea kwa njia iliyoonyesha uimara.
"Miryam..."
"Usiwaze kuhusu sisi, tuta-make time tu. Mtoto kwanza, anakuhitaji," akaniambia hivyo kwa uhakika.
Nilijisikia vibaya kwamba tamaa yake ya kuwa nami leo ilikatishwa namna hiyo, lakini nilihisi shukrani na uthamini kwa jinsi ambavyo alinitanguliza kwanza kabla yake yeye mwenyewe. Nikamkumbatia kwa upendo na kusema, "Asante."
Akaniambia, "Usijali."
Nikamwachia na kusema, "Alright. Nakutangulia."
Akatikisa kichwa kukubali na kusema, "Sawa."
Upesi nikatoka ndani humo na kuliwahi gari langu, bado nikihisi kama nisingekuwa namtendea haki Miryam, lakini nilihitaji sana kwenda kumwona mwanangu. Na nilithamini sana jinsi Miryam alivyoonyesha moyo wa kujidhabihu, hivyo lazima ningekuja kumpa mazuri aliyostahili baada ya haya mengine kutulia. Nikawasha gari langu na kukanyaga mafuta, na mwendo wa kugeuka ukaanza ili twende kujua nini kilikuwa kimempata mwanangu mpendwa.
★★★★★★★★★★
ITAENDELEA
★★★★★★★★★★
Whatsapp +255 678 017 280
Ila hii care ya Mimi 😊MIMI NA MIMI 3

Kumekucha 🔥🔥🔥MIMI NA MIMI 3
A Story by Elton Tonny
Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Siri, Tamaa, Hila, Usaliti, Ukatili, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa
R-rated 18+
Enjoy!
★★★★★★★★★★★★★★★★★
SEHEMU YA KUMI NA TANO
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Ilituchukua muda mrefu kiasi kufika huko Tegeta kutokana na msongamano mkali wa magari, na pia mambo ya hapa na pale ya barabarani. Nilikuwa nimeongea na Deborah tena, zamu hii kwa namba yake, nikimjulisha kwamba niko njiani, nikimwambia awe karibu na simu ili nikifika aniambie wako upande gani kutokana na Stella kutokuwa na muda na simu kwa wakati huu. Ilikata masaa mawili kabisa kufika huko, siyo mchezo, nasi tukawa tumeingia hospitalini hapo ikiwa imefika saa tano. Eneo la hospitali halikuonekana kuwa na purukushani nyingi na watu kama iwavyo pakiwa na mwangaza.
Nikafanikisha kuegesha gari, Miryam pia, nasi kwa pamoja tukashuka na kuanza kuelekea huko ndani ya jengo huku nikimpigia Deborah. Alipopokea nikamuuliza yuko upande upi, naye akaniambia yupo chumba cha wodi ya kupumzikia ya wanawake na watoto kwenye ghorofa ya nne. Upesi tukaifuata lifti, na kweli sehemu kubwa ya ndani kutokea mapokezi na zingine zilikuwa tupu kabisa, isipokuwa ya watu mmoja mmoja walioonekana kuwepo kwa ajili ya waliolazwa, pamoja na wauguzi kadhaa. Lifti ikatuchukua hadi ghorofa ya nne, mimi na bibie tukaelekea wodi alitotuelekeza Deborah, na uzuri kwa kuwa muuguzi hapo alinifahamu, moja kwa moja akanionyesha chumba binafsi ambacho 'doctor' Stella alikuwepo na kuamua kuja pamoja nasi pia.
Tukaingia humo, na kwa uhakika Stella alikuwepo hapo pamoja na Deborah ns msaidizi wake wa kazi, aliyeitwa Melina. Kuangalia kitandani nikamwona mwanangu, akilala tuli kwa kilichoonekana kuwa usingizi ikiwa siyo kwamba alizidiwa, na akiwekewa dripu ya dawa ya maji. Stella aliketi kitini huku Deborah akisimama pembeni yake, na aliinamishia uso wake viganjani huku nikiona wazi kwamba alilia. Mimi na Miryam tukasogea karibu na kitanda zaidi, muuguzi akiwa pembeni, nami nikamsogelea Evelyn na kuanza kuangalia joto la mwili na kukagua macho yake. Alichemka sana. Miryam akasalimiana na Deborah vizuri tu. Melina akamwamkia Miryam pamoja na mimi pia, na Miryam akamwitikia vyema, lakini mimi nikashindwa hata kuijibu salamu yake.
"Stella vipi? Huyu amekuwaje?" nikamuuliza.
Stella akawa analia tu kwa sauti ya chini na kujifuta machozi.
Deborah akasema, "Alilala mapema ile jioni, baadaye Melina akaenda kumwamsha ili ale maana alilala muda mrefu. Ndiyo akamkuta amechemka hivyo. Akaniambia, na me nikamkuta hivyo pia. Kumwamsha, akawa anapumua kwa shida... kama mafua yamemkaba. Nikampigia Stella, ndiyo akaja, tukamleta."
"Alilala saa ngapi?" nikamuuliza.
"Kwenye saa kumi na moja," Melina akajibu.
"Ukamwamsha muda gani?"
"Saa mbili," Melina akajibu tena.
"Jana si alikuwa sawa... ta-tatizo nini Stella? Malaria, au? Mmempa dawa?" nikauliza kwa utulivu.
Stella, akiwa anajikaza kulia, akasema, "Ana polyps."
"Polyps ya?" nikauliza.
"Nasal," akajibu.
Akaniacha nikishangaa.
"Na inaenda kuwa sugu, anashindwa kupumua vizuri," akaniambia hivyo huku akijifuta machozi.
"Nini... wha.... a.. ahh... tokea lini?" nikauliza kwa kutatizika.
"Ina muda, lakini sijawahi kuona sign zozote... hhh... sikujua," Stella akaongea kwa huzuni.
"Ni nini?" Miryam akauliza.
Kwa huzuni nikamwambia, "Ana nyama puani."
"Oh, masikini... pole sana Stella," Miryam akamwambia kwa kufariji.
"Jamani!" Deborah akaongea kwa hisia.
Stella akawa anatikisa tu kichwa kwa kusikitika bila kuacha kulia.
Nikasema, "Kwa hiyo hizo nyama zinaenda kuziba koo la... ona, Stella, kwani Eve hajawahi kuumwa labda, ukatambua ana allergy ama...."
"Hapana, allergy hana, yaani sikuwahi kufikiria kabisa angekuwa na hii kitu," Stella akanikatisha kwa kusema hivyo.
"Dah, Stella mambo gani haya, yaani... mtoto kweli mpaka anazidiwa huna habari? Tukikuta ana cystic fibrosis? Asthma?" nikamwambia kwa hisia.
Stella akaniangalia na kusema, "Unafikiri nimependa? Au nimefanya kusudi? Nakuwa kazini, muda naopata kutumia naye mtoto kachangamka, jana wewe mwenyewe tu ulimwona, unadhani ingekuwa rahisi kugundua? Nhh... nilikuwa... nilikuwa kazini leo, unajua hilo... unasema ni makosa yangu kwamba anaumwa hivi?"
"Sija...."
Miryam akanikatisha kwa kunishika mkono na kusema, "Hapana, siyo makosa yako Stella. Watoto huwa wanaumwa, ni kawaida."
"Sasa mbona mtu wako ananilalamikia mimi? Unatakaje labda, Jayden? Kama unaona simwangalii vizuri si unisaidie kumtunza? We' si upo huko unafanya mambo yako, nimekuzuia?" Stella akaongea kwa hisia za huzuni.
Nikajihisi vibaya moyoni, nami nikamsogelea na kupiga goti moja chini huku nikimwambia, "Okay, okay, samahani. Sipaswi kukulaumu. Siyo makosa yako."
Stella akaendelea kukikaza kilio chake, naye Deborah akasogea pembeni.
"Tusikae kulia Stella, Eve anahitaji msaada chap. Mbona mmekaa hapa tu, si tufanye kitu a...."
"Haiwezekani kumtolea sasa hivi, daktari wa upasuaji hii ishu hayupo, na huwa wanaenda kwa list," akaniambia.
"Ulimpimaje ukajua ana...?" nikauliza.
Stella akabaki kujifuta machozi, hivyo muuguzi yule akasema, "Kwenye CT scan."
"Nilimwomba Juma ampime hapo chini, ndiyo nikajua. Doctor Jeanine hayupo... nimempigia, yuko mbali, ni yeye ndiyo angefanya endoscopy tuwe na hakika la kufanya... hhh... na hata kwa hii dharura, uhakika ni mpaka asubuhi... na hizo process zote, yaa... hhh... Evelyn kukaa mpaka asubuhi hivyo...." Stella akaongea kwa uchungu.
"Pole Stella, tafadhali jikaze. Unahitaji kuwa imara, usilie," Deborah akaongea hivyo na kuja kukaa kitini pia, akianza kumbembeleza Stella taratibu.
Stella akajifunika usoni na kusema, "Labda kweli ni makosa yangu ahhh..."
Aliuficha ule uchungu mkali, yaani sauti yake ilifinya haswa aliposema hivyo, nami nikamkumbatia kwa kukilaza kichwa chake begani kwangu. Akaendelea kulia kwa njia iliyoonyesha alijilaumu pia, hivyo nikaelewa maneno yangu yalimwongezea hisia mbaya sana.
Nikaanza kumfuta machozi, yeye akiangalia chini kwa huzuni, nami nikasema, "Tunahitaji kufanya jambo fulani."
Akaniangalia.
"We have to do something. Sasa hivi," nikasisitiza.
"Kama?" Stella akauliza.
"Umeshampima, umeona hali yake ni mbaya sana, siyo?" nikamuuliza.
Akatikisa kichwa kukubali.
"Inabidi tujaribu kum-operate sisi wenyewe," nikasema.
Stella akashangaa.
"Ba' Evelyn... hiyo ni salama kweli?" Deborah akauliza.
"No. Hapana," Stella akakataa.
"Nisikilize..."
"Nisikilize nini? Unataka kuniulia mtoto?" Stella akaongea kwa jazba.
"Ni puani tu Stella, inaweza hata isiwe lazima kumwingiza OR. Kwa ulivyoniambia, najua ni lazima upasuaji uhusike. Lakini endoscopy si procedure tu ya kuangalia hizo nyama? Vifaa vipo, na kuna madaktari wachache hapa pia wanaweza wakasaidia...."
"Hawajabobea Jayden..." Stella akakakatiza.
"... na tukaweza... ndiyo, najua, lakini sisi wote madaktari Stella, upasuaji tunafanya... tuangalie tu hiyo view puani mwake Evelyn kwa umakini, tutajua namna ya kuzitoa hizo nyama. Hapa hatuwezi tu kumwacha namna hiyo mpaka asubuhi, unafikiri itakuwaje?" nikamuuliza.
Stella akawa anatikisa kichwa kukataa.
"Hatuwezi kupata hospitali nyingine yenye madaktari wanaowezea zaidi kuzitoa? Wamfanyie upasuaji wa dharura? Vipi Muhimbili?" Miryam akauliza.
"Hamna hospitali nyingine wanafanya upasuaji wa nyama za pua. Ni hapa tu," yule muuguzi akamwambia.
"Kweli?" Deborah akauliza.
"Ndiyo," muuguzi akasema.
"Na hapa ndiyo imeshakuwa kuchelewa, hatuwezi kungoja mpaka asubuhi, halafu waje kutuchelewesha zaidi..." nikasema hivyo.
"Jayden hilo siyo... siyo jambo la mchezo. Siyo mguu wala kidole hicho, unataka kuhatarisha uhai wa mtoto wangu," Stella akaniambia hivyo.
"Lakini Stella...."
"Nah, hapana..." Stella akagoma.
Nikamwangalia Miryam, yeye pia akiniangalia kwa hisia makini, nami nikamwambia Stella, "Kwa hiyo tumwache tu... tatizo lizidi kupanda na.... yaani... Stella, tumwache tu?"
Stella akaangalia pembeni huku akikaza machozi yasimtoke, naye akaema, "Nitamshawishi doctor Jeanine atusaidie, mapema kabisa, yaani... iwe isiwe, mpaka Evelyn apone. Nitawalipa madaktari wote ikiwezekana wamtangulize mwanangu kwanza..."
Deborah akasema, "Stella..."
"Lakini kufanya unachotaka, siwezi. Yaani ni bora kama tatizo likimmaliza lenyewe, siyo mimi kushiriki kumuua mwanangu," Stella akaniambia.
Nikabaki kumwangalia kwa hisia za huzuni.
Miryam akamwambia, "Usiseme hivyo Stella, tafadhali. Jayden ana...."
Kabla hajamaliza maneno yake, Stella akanyanyuka upesi na kutupita, akikisogelea kitanda karibu na Evelyn na kuanza kumpapasa hapa na pale. Roho iliniuma. Nikamwangalia Miryam machoni, naye akanitikisia kichwa kama kukanusha, akionyesha kuwa jitihada zangu za kumfariji mama wa binti yangu hazikufaa sana kwa pindi hii. Stella aliumia, nilitakiwa nielewe hilo na nijaribu kumtia nguvu avumilie, siyo kujaribu kusuluhisha kitu ambacho hakikuwezekana kwa muda huo. Nilijihisi kama Shetani wakati huu, yaani sikuwa na suluhisho sahihi kwa ajili ya kutatua hali mbaya ya mtoto, na mpaka mawazo yangu yakaenda mbali kiasi kwamba nikapotea kabisa katika kufikiri vizuri.
Kwa kutambua namna ambavyo nilitoa athari mbaya, nikaona nisimame tu, Deborah pia akasimama, nami nikamwangalia Stella. Alikuwa amenipa mgongo tu huku akiongea na muuguzi pembeni kuhusu jambo lingine ili, naelewa, kwamba ajaribu kupotezea ya dakika chache nyuma. Lakini nikamsogelea karibu na kuushika mgongo wake kwa mikono yangu, naye akanigeukia. Aliniangalia kwa kungojea nimwambie jambo fulani, lakini mimi nikabaki kimya tu nikimtazama kwa kujali. Macho yake yakaanza kujaza machozi, akibana midomo yake kwa kujikaza, nami nikamvuta taratibu na kumkumbatia. Akanibana mgongoni pia kuonyesha alihitaji sana kitulizo kwa namna hiyo, nami nikazidi kumpa alivyostahili.
Pindi hii Stella alinitia sana simanzi, kweli alistahili kumbatio. Hapo hakukuwa na zengwe lolote tena baina yetu kwa kuwa tulijali zaidi hali ya mtoto, na kwa kuona tunahitaji muda wa kuwa pamoja kama wazazi, Miryam akawaomba Melina, Deborah na muuguzi watupishe, yeye pia akiondoka pamoja nao kutuacha mama, baba, na binti chumbani humo. Nikaendelea kumkumbatia Stella kwa kujali, naye akalaza kichwa chake kifuani kwangu na kugeuzia uso kuelekea kitanda ili sote tumtazame binti yetu.
★★
Basi, ikawa ni kukaa hapo pamoja na Stella na mtoto wetu, tukamwongezea na dawa ya maji kupunguza joto hilo. Kulikuwa na baadhi ya madaktari wengine wa usiku waliofika na kutusemesha, wakiangalia hali ya Evelyn na kumpa pole Stella, na alifarijika sana. Kumwangalia Stella akiwa mama mwenye upendo wa hali ya juu namna hiyo kulibadili kabisa mtazamo wowote hasi uliokuwa umebaki ndani yangu kumwelekea. Kweli alikuwa amekua sasa, yaani kiutu, kama vile ambavyo mimi pia nilijitahidi kufanya kipindi hiki.
Wakati huo wote Miryam alikuwepo, akituunga mkono pia kwa kukaa kando yangu, na mpaka inafika saa nane usiku hakujaribu kutafuta usingizi licha ya kwamba nilimwomba mara kadhaa akajipumzishe kwenye moja ya vyumba ndani hapo. Kama mimi ningekaa kumwangalia mtoto mpaka asubuhi, basi na yeye alitaka kufanya hivyo. Lakini nikamsihi sana, alale, nikigusia umuhimu wa kufanya hivyo kwa ajili ya mtoto aliye tumboni mwake. Kwa msisitizo huo ndiyo akakubali, nami nikamwongoza kwenye chumba kimoja ili apumzike huko.
Kurudi kwa mwanangu, bado Stella alikuwa macho pia, akiwa kitandani karibu na Evelyn ili kumchunga. Aliegamia ubavu, na kiwiko chake kiliongoza mkono kuegamiza kichwa, mtoto akiwa katikati chini yake. Ila alionekana kuchoka, kwa kuwa alijitahidi kubaki macho lakini usingizi ukawa ukimvuta. Inawezekana aliacha majukumu ya kikazi ili kuwahi kumfata mtoto nyumbani na kumrudisha huku. Msaidizi wake, Melina, alikuwa ameenda kulala pia kwenye chumba kimoja hapo hospitai, na Devotional alilala kwenye sofa pembeni ndani hapo. Nikasogea mpaka pale Stella alipokuwa na kumgusa. Akashtuka kiasi na kuniangalia usoni kivivu.
"Njoo ulale kidogo. Nitakaa kumwangalia," nikamwambia.
Stella akatikisa kichwa kukataa na kumtazama tena mtoto.
"Stella... unahitaji kupumzika..."
Akaonyesha kutotaka hilo kwa kuendelea kukaa hivyo hivyo tu.
Nikamshika mkononi ili nimsisitizie, lakini akautoa wake kwangu na kusema, "Niache Jayden, siondoki humu. Nitamwangalia tu."
Nikamtazama kwa kujali, nami nikamshika shingoni taratibu. Akaniangalia, na hapo nikamwambia, "Njoo. Nakuomba."
Aliniangalia kwa utathmini kwanza, kisha akajinyanyua taratibu huku nikisisitiza kwa kumvuta mkono. Akasimama na kuanza kunifata nilipoelekea kwenye sofa alilokaa dada yake, nami nikamwacha akae hapo, halafu mimi nikakaa kwenye mkono wa hilo sofa pembeni yake.
"Nisamehe Stella, nimeongea vibaya sana muda ule. I'm so sorry kwa hili," nikaongea hivyo kwa upole.
Akabaki mtulivu tu katika hali yake ya majonzi.
Nikapitisha mkono wangu begani kwake na kumvutia kwangu, nikimruhusu aniegamie ubavuni ili aweze kulala sasa, huku nikimbembeleza taratibu kwa kusugua bega lake, naye hakuchukua muda mrefu sana na usingizi ule aliouhitaji ukamjia.
★★★
Sikusinzia hata mara moja, na mara kwa mara ningemsogelea Evelyn kuangalia hali na nini, kisha ningerudi sofani tena. Hizo mara kwa mara Stella alikuwa akiamka pia, na nikishamwambia hali ya mtoto ina usawaziko, angerudi kulala aidha kwa kunilalia kifuani ama pajani. Mpaka inafika saa kumi na mbili ya saa moja asubuhi, ndiyo Stella akaamka kimoja. Hapo ndiyo simu zikaanza kupigwa sasa, akizungumza na watu aliojuana nao hapo hospitali kutuwezesha kushughulika na tatizo la mwanetu upesi iwezekanavyo. Deborah na Melina walikuwa wameshaamka pia, na baada ya Stella kupata uhakika kwa yule tabibu aliyemwita Jeanine, ikawa ni kumtoa Evelyn hapo haraka na kumpeleka kwenye chumba cha upasuaji baada ya kumwandaa kwa ajili ya hilo.
Kweli binti yetu akaanzishiwa upasuaji huo, na hapo tukakaa kungoja atolewe ili mengine yafuate. Stella alihisi ahueni kwa kiasi kikubwa hadi akawa akilia, ile kwamba tumeifikia asubuhi na bado mtoto alikuwa na usalama. Ambacho kingejalisha sasa ni kumtoa humo akiwa salama zaidi na kuomba Mungu asaidie ili tatizo lake likomeshwe kabisa. Tulikuwa ghorofa ya tatu sasa wakati tukisubiria, na ndiyo nikarudiwa na kumbukumbu kuwa Miryam alikuwepo hapo hospitali pia. Hatukuwa tumeonana tena tangu nimemsindikiza kuingia kupumzika ule usiku, na sikujua kama bado alikuwa amelala ama vipi.
Nikaona nimpigie, naye akapokea. Akaniambia ndiyo ametoka tu chumbani, na alikuwa hajisikii vizuri sana mwilini ndiyo sababu akaamua kuketi sehemu fulani huko juu ili hiyo hali itulie. Duh! Nikamwambia atulie hapo hapo, namfuata, nami nikamsemesha Stella juu ya hilo, nikisema watakapomtoa tu Evelyn ikiwa sijarudi anipigie. Hakunijibu lolote na kuendelea kutulia tu na msaidizi wake wa kazi, nami nikaelekea tu ngazini ili nimwahi mama kijacho wangu. Mambo yakaanza kuingiliana sasa. Nimemfikia tu Miryam nikakuta ameketi kitini huku ameinamisha uso, na akionekana kufumba macho. Nikamfata mpaka alipo, nami nikakaa karibu yake na kumfanya anitazame usoni.
"Vipi? Nini kinauma?" nikamuuliza kwa kujali.
"Hamna kinachouma. Najisikia vibaya tu," Miryam akasema.
"Unatakiwa ule, tsk... hebu twende pale chini uchukue na vipimo halafu...."
"No, Jayden... niende tu nyumbani," akanikatisha.
"Ukafanyaje? Uzidiwe zaidi?"
"Siyo mbaya kihivyo, usijali. Na ni kweli, nahitaji tu kula, najua nitakaa sawa," akasema hivyo.
"Ndiyo, unatakiwa ule sana. Inabidi tupitie vitu njiani uende unakula," nikamwambia.
Akatabasamu kiasi na kusema, "Sawa. Vipi Evelyn?"
"Ndiyo wamemwingiza theatre. Atakuwa sawa, najua," nikaongea kwa kujifariji.
"Ndiyo, atapona tu. Poleni kwa kweli..."
"Asante. Hiyo pole inarudi kwako pia."
"Kwa nini?"
"Na wewe ni mama'ake, kwa hiyo hili ni tatizo lako pia," nikamwambia.
Akatabasamu tena na kusema, "Ndiyo, uko sahihi."
Nikamtathmini na kusema, "Ila... huku hatupaswi kukaa. Tushuke haraka nikutafutie chakula, halafu tuone hali yako itakaaje."
"Na Evelyn je?"
"Mama'ake si yupo hapo? Nimemwambia wakimtoa atanipigia. Twende," nikasema hivyo na kunyanyuka.
Miryam akasimama taratibu pia, nasi tukaielekea lifti. Alikuwa akitembea taratibu zaidi ya jinsi nilivyomzoea. Tukashuka hadi chini, na kwa uhakika zaidi nikaamua tu nimpigie Stella ili nimjulishe kuwa nimemtoa Miryam mara moja na sipo mbali, lakini yeye Stella ndiyo akapiga kwangu muda huo huo. Nikapokea kumsikiliza, taarifa ikiwa kwamba tayari wamemtoa Evelyn chumba cha upasuaji na sasa wako huko chumba cha mapumziko wodi ya kupumzikia wanawake na watoto. Dah! Nikamwambia sawa, nakuja. Nimeshusha tu simu, Miryam akaniambia turudi maana alikuwa ameshaelewa, na bila kungoja kweli tukaigeukia lifti tena. Nilihitaji kuona mwanangu anaendelea vipi.
Tulipofika upande wa wodi hiyo, Miryam akaishia kusimama nyuma, nami nikamrudia kwa kuona kwamba alijihisi vibaya zaidi.
"Umechoka?" nikamuuliza.
Akakunja sura kiasi na kusema, "Nahisi kizunguzungu."
"Okay, twende basi ukapumzike humo humo pia. Itakuwa wana...."
"Hapana, Jayden... nenda tu. Mie nitaenda nyumbani," akaniambia hivyo.
"Unaenda vipi nyumbani na kizunguzungu? Tuko hospitali, tulia kwanza tukuangalizie..."
"Jayden..."
Sauti ya Stella akiniita ikanifanya nigeuke, na ni yeye ndiyo akawa akija upande wetu.
"Njoo, Eve anakulilia," Stella akasema hivyo na kuishia hapo mbele.
"Ameshaamka?" nikauliza.
"Yuko macho, twende..." Stella akasisitiza.
Nikamgeukia Miryam, ambaye alinitazama kichovu na kusema, "Nenda."
"Lakini..." nikajikuta naishia hapo tu.
"Jayden... come on, I need you," Stella akasema hivyo.
Aliniambia hivyo huku akinyoosha kiganja chake kunielekea, nami nikamwangalia Miryam tena.
"Nenda, nenda. Nitakuwa sawa. I promise," Miryam akasema hivyo na kufanya kama kunisukuma.
Hatimaye nikagawika, ingawa kwa upande mmoja tu ambao ni wa mwanangu. Nikamfata Stella ambaye bado aliweka kiganja chake kunielekea, nami nikakishika na yeye kuanza kuniharakisha tuelekee chumbani kwa mtoto. Nikageuka nyuma tena kumwona mpenzi wangu, ambaye alibaki hapo kuniangalia mpaka nilipotokomea na kufika kwa mwanangu. Ingawa najua Evelyn alikuwa muhimu sana, kwa kiwango fulani naelewa Miryam alihisi kuwekwa pembeni. Si kwa hili tu, kwa mengi. Tangu turudiane, ilikuwa kama vile yeye anafanya kila kitu kuniunga mkono mimi na si mimi kwake yeye. Ingenibidi nitafute njia ya kusawazisha mambo zaidi baada ya hili la mwanangu kupita, na sasa ndiyo nikatumia muda kuwa baba mzuri kwa Evelyn alipokuwa akiugulia maumivu ya upasuaji aliotoka kufanyiwa.
★★
Kwa hiyo sasa Evelyn akawa ameondolewa hizo nyama puani, na kwa kiasi chake alipatwa na maumivu yaliyomfanya alie sana. Tulijitahidi kumtuliza, na daktari aliyemsaidia akatuambia kuwa upasuaji aliofanyiwa ungesababisha hali za maumivu ya kichwa na koo, hivyo dawa za maji zingehitajika kumtuliza zaidi na kufikia kesho tu angekuwa sawa kurudi nyumbani. Stella akawafahamisha wazazi na ndugu zetu kuhusu jambo hili, na wote wakatuma pole na kuahidi kuja kumwona mtoto. Nilikuwa nikimtumia Miryam jumbe za simu mara kwa mara kuhakikisha kama amefika nyumbani salama, naye kweli akajibu kuwa alijitahidi mpaka kufika huko kwake kwenye mida ya saa tano. Nilimshauri achukue dawa fulani ambazo zingemwongezea nguvu na ale chakula bora na kingi, naye akasema angefanya hayo. Nikamwahidi kufika kwake pia baadaye kuangalia hali yake.
Tumekaa hapo hospitalini mpaka saa saba, na Stella alihitaji kuendelea na majukumu yake ya kitabibu huku mara kwa mara akija kumwangalia mtoto. Deborah, shangazi yake Stella na mwanaye wa kike, na rafiki zake wawili walikuja kumwona mtoto. Mama yangu na Nuru pia walifika hapo mapema zaidi, kwa hiyo Evelyn alikuwa na ushirika mkubwa wa wapendwa pamoja na wasaidizi wao. Ni ndani ya muda huu ndiyo nikawa nimepokea ujumbe kutoka kwa Miryam tena. Aliulizia hali ya mtoto na kuniambia kwamba bado kwa kadiri kubwa alinihitaji sana. Yaani, pamoja na yote, lakini kilichomfanya ajihisi vibaya haikuwa tu kwa sababu ya tumbo wala nini, bali uhitaji wake wenye nguvu sana wa kuwa pamoja na mimi. Nilimwelewa, na nikamhakikishia kwamba ningefanya jambo fulani ili tuwe pamoja labda baadaye, kwa kuwa sasa Evelyn angeielekea nafuu.
Lakini Miryam akaniambia kwamba, alishindwa kujizuia. Alitaka tukutane, sasa hivi. Ilijenga hali ya utata kiasi kwa sababu bado nilihisi uhitaji wa kuendelea kukaa hospitali na mwanangu, lakini nilitaka pia kumpa furaha mwanamke wangu. Kwa hiyo, kupitia ujumbe hivyo hivyo, nikamuuliza alitaka nifanye nini, naye akasema nisisumbuke kwa lolote, bali nimfate tu sehemu ambayo angenielekeza ili niende kumpa alichokihamu sana. Angegharamika yeye mwenyewe. Huu ulikuwa upande wa Miryam ambao ulionyesha msisitizo mwingi kwa namna ngeni kiasi, sikumzoea namna hiyo, lakini naelewa ujauzito ungekuwa unachangia hilo. Kwa hiyo nikataka kumridhisha tu, kutoka hospitalini hapo kwa muda mfupi isingekuwa mbaya, hivyo nikamwomba aniambie wapi alitaka niende kutuliza hamu zake.
Baada ya kuniambia mahali pa kukutana, nikamwambia Miryam sawa, ningekuja baada ya muda mfupi, nami nikamuaga mama na wengine kwa kusema natoka kidogo kwenda kushughulika na ishu fulani upesi, kisha ningerejea. Nikampatia na Stella taarifa hiyo, na upesi nikaondoka Rabininsia. Nadhani hali mbaya ya Miryam ingemwondoka baada ya mini kumtimizia mahitaji yake, kwa hiyo pamoja na kwamba mwili wangu ulikuwa na uchovu, ningejitahidi kwenda kumpa dozi aliyostahili. Mambo yalikuwa mengi!
★★
Basi, nikaendesha gari mpaka kufikia maeneo ambayo Miryam aliniambia niende, na ilikuwa maeneo ya kule kule ambako jana nilipanga kumpeleka, isipokuwa hoteli aliyonielekeza kwenda ikawa tofauti. Alisema alichukua huduma kutoka kwenye hoteli ya Holiday Inn, na niliiekewa kuwa moja ya hoteli ghali hapo jijini. Mwanamke wangu alipendelea mazingira mazuri pia, na kufikiria kwamba angetaka nije sehemu ya gharama ambayo angelipia ilionyesha namna gani hamu yake ilikuwa kubwa kuliko.
Kwa hiyo nikafika eneo hilo na kupeleka gari mpaka sehemu ya kuegesha, kisha kushuka na kuliangalia ghorofa hilo. Lilikuwa kubwa, na sikujua kihususa Miryam alikuwa wapi huko ndani, hivyo nikaanza kulielekea tu huku nikimpigia. Watu kadha wa kadha waliendelea na mambo yao sehemu hiyo, kukiwa na huduma mbalimbali za kifahari walizojipatia hapa na pale, na baada ya kumpigia Miryam mara mbili bila yeye kupokea, nikaamua kusimama kando ya ukuta kwanza. Sijui angekuwa wapi, lakini ingenibidi niendelee kumtafuta.
Nilipotaka kumpigia tena, ujumbe kutoka kwa bibie mwenyewe ukaingia. Akaniambia kwamba yupo ghorofa la nne kwenye chumba maalumu cha kukandwa wanawake, yaani massage, na ndiko alipotaka nimfate. Nikajikuta natabasamu tu, na kiutani nikamuuliza kwa nini aje kufanyiwa massage bila kuniambia mapema, yaani ikiwa ningekuta anashikwa-shikwa na mwanaume mwingine ndiyo angenitambua! Wakati huo nikawa nimeshaanza kuelekea ngazini, kwa kuwa lifti ilikuwa juu bado, naye Miryam akanijibu akisema ndiyo niende sasa ili anitambue vizuri. Najua tu kuna kitu chenye kusisimua sana ambacho mwanamke wangu alikuwa ameandaa kwa ajili yangu, labda ili kunipa ahueni pia kutokana na mkazo niliopitia jana kwa suala la Evelyn, na nilisisimuliwa na wazo hilo kwelikweli.
Nikafanikiwa kufika juu upesi na moja kwa moja kukiendea chumba hicho. Kilikuwa na milango mipana ya vioo vizito visivyoonyesha ndani, na nilihisi kungetakiwa kuwa na ruhusa maalumu ya kuingia ama nini, lakini labda ningeikuta humo humo. Nikaingia, na mwonekano mzuri wa ndani humo ulipendeza sana. Palikuwa safi, kama vyumba vya mahoteli makubwa ya wazungu yaani, na kwenye meza ya mapokezi alikaa mwanamume kijana mwenye mwonekano mzuri kisura na kimwili. Bila shaka hii ilikuwa sehemu yenyewe, kwa ajili ya wanawake yaani, na akiwa ananiangalia kwa utulivu nikamfata hapo na kumsalimu. Hakukuwa na watu wengine.
Akaninyooshea kidole kiutambuzi huku akisema, "Mr. Jayden?"
Nikatikisa kichwa kukubali.
"Oh, karibu sana. Mkeo anakusubiri," akaniambia hivyo.
Nikamwambia, "Asante."
Nikaangaza sehemu hiyo, kukiwa na korido fupi lililoonekana kuelekea upande wenye vyumba kama vinne, viwili upande mmoja wa ukuta na viwili mwingine.
Nikamuuliza, "Ni chumba kipi?"
"Yupo deluxe room, kile pale mwishoni..." akanionyesha.
Eti deluxe! Haya bwana.
Nikamtikisia kichwa tu na kuanza kukielekea, huku nikitabasamu kiasi kwa furaha. Miryam alikuwa amechukua na chumba cha kukandwa cha gharama nakwambia, nafasi iwe ya kutoshea mimi pia nipatiwe huduma ikiwezekana, na nilikuwa tayari kwa lolote ambalo lingetokea zaidi tu ya kukandwa. Wakati nimeufikia mlango huo, nikamwona yule jamaa aliyenielekeza akitoka sehemu yake kuelekea nje, nami nikaingia nikiwa naelewa kuwa bila shaka nilipewa uhuru zaidi kuanzia hapo.
Baada ya kukanyaga ndani, mazingira niliyoyakuta yakanishangaza kidogo. Chumba kilikuwa tupu, yaani kikiwa kipana sana, cheupe, ni madirisha ya vioo tu ndiyo yaliyoingiza mwanga hafifu wa ugiza kutokana na rangi yake. Nilitarajia kukuta aidha vitanda vya huduma ama watu, lakini hakukuwa na chochote kile kwenye hicho chumba isipokuwa mimi tu. Nikafikiria kuwa huenda nilikosea pa kuingia, hivyo kurudi kwa nje ingekuwa busa....
Ile nageuka tu nyuma, mlango ukaachia uwazi kuruhusu mtu mwingine kuingia, ikiwa ni yule yule mwanaume wa mapokezi, na aliingia huku akiwa ameninyooshea bastola! Nilishtuka, lakini nikaweza kutulia hapo hapo. Aliinyoosha bastola kwangu huku sura yake ikiwa si ya kirafiki tena kunielekea, na nyuma yake akaingia mwanaume mwingine mweusi mwenye mwili wa kikomando yaani, yeye pia akinyoosha bastola fupi kunielekea. Sikuelewa nini kilikuwa kinaendelea, lakini jambo moja likawa wazi; huu ulikuwa mtego.
Watu hawa kwa pamoja wakaingia kwa njia fulani ya kunizingira, nikiwa kati, na kwa ishara ya bastola yule mweupe akanielekeza nisogee nyuma. Bastola zao zote ziliwekewa viziba sauti, na walionekana kuwa watu mahiri sana kwa lolote kati ya mambo yote waliyofanya. Niliwatazama kwa umakini sana, na nikatii agizo lake kwa kupiga hatua chache nyuma. Ilikuwa kama vile walitaka niache uwazi zaidi kwa ajili ya kitu kingine kufuata, na kiukweli nilianza kuogopa. Nilihofia sana juu ya Miryam. Hawa watu walikuwa nani, na walitaka nini?
Nikajitia ujasiri na kuuliza, "Nyie ni nani?"
"Nirushie simu yako," yule jamaa mweupe akaniambia hivyo.
Nikabaki kumtazama tu kama vile sijamsikia.
"Harakisha," mweusi akaamrisha hivyo.
Nikaitoa simu mfukoni na kumrushia mweupe, naye akaidaka na kisha kuitupa chini kwa nguvu sana mpaka ikapasuka-suka! Nilikuwa nimeshaanza kutaharuki ndani kwa ndani, lakini nikaendelea kutulia na kumtazama mwanaume huyo kwa mkazo.
"Mikono nyuma ya kichwa," akaniamuru hivyo.
Nikairudisha mikono nyuma ya kichwa na kukishika, na kwa umakini nikawauliza, "Mke wangu yuko wapi?"
"Kaa kimya. Tulia hivyo hivyo," mweupe akasema.
Hofu niliyokuwa nayo juu ya Miryam ilizidi kupanda, lakini ilinipa pia ujasiri wa kutowaogopa watu hawa hata kidogo. Nilifikiria zaidi juu ya hali ya mwanamke wangu, angekuwa wapi, ni kutokea muda gani watu hawa walimshika na kuitumia simu yake kunirubuni nije sehemu hii kwa ajili ya madhumuni yao, na ni nani alikuwa akifanya haya. Oh, wazo lenyewe halikuwa mbali. Nilijua kabisa ni nani aliyekuwa akifanya hivi!Kutokea nje ya mlango wa hapo nikaweza kusikia sauti ya mlango mwingine ukifunguka, hatua zikikaribia, na huu wetu ndiyo ukasukumwa na watu wengine zaidi kuingia. Walikuwa watatu; mwanaume mwingine mweusi, mwanamke mweusi pia mwenye mwili mkomavu, akiwa amemshikilia Miryam mikono kutokea mgongoni!
Nilighafilishwa sana na jambo hili, mapigo yangu ya moyo yakianza kukimbia kwa kasi zaidi. Miryam alishikiliwa mikono yake yote iliyorudishwa mgongoni, akiwa na ule ule mwonekano wake wa asubuhi wakati akiondoka hospitali, na mdomoni alifungwa kwa kitambaa kilichozuia sauti yake kutoka. Nywele zake zilivurugika kiasi, akionekana kuwa amelia sana, na baada ya kuniona akaonyesha kutaka kujitoa katika mikono ya mwanamke huyo aliyemkaza, lakini akakandamizwa zaidi ili asijitoe.
Nilihisi hasira sana, nikitaka hata niruke na yeyote kati ya watu hawa, lakini usalama wa mpenzi wangu ulikuwa wa kutanguliza zaidi, hasa ukitegemea na hali yake aliyokuwa nayo. Sikutaka kabisa aumie. Alipumua kwa presha, akiniangalia kwa kububujikwa na machozi, nami nilihisi vibaya mno moyoni kumwona hivyo. Baada ya mwanamke aliyemshikilia Miryam kumtuliza zaidi, mwanaume aliyekuwa amewatangulia akanisogelea karibu na kuniangalia kiudadisi fulani hivi, mimi nikimtazama kwa hasira, naye akacheka kidogo kwa pumzi huku akitikisa kichwa chake kana kwamba ananionea sana huruma. Nilitamani hata nimtemee mate yaani, lakini nikaendelea kujikaza. Alikuwa mtu mzima kabisa kufikia hata miaka 50, lakini mkomavu kama Kishoka.
Akaniangalia kiumakini na kuuliza, "Kwa hiyo ukaja mbio mbio unakenua ukifikiri mtu wako yuko deluxe room uje kula raha tu, eh?"
Nikamuuliza, "Anataka nini?"
"Nani?" akaniuliza.
"Aliyewatuma," nikamwambia.
"Una uhakika gani kwamba tumetumwa? Unaona jini hapa?" akauliza kikejeli.
"Siwajui nyie, hamnijui, kama ni uadui na mtu aliyewatuma basi nipelekeni kwake anifanye lolote analotaka, lakini nawaomba mmwachie huyu mwanamke," nikaongea kwa hisia makini.
Miryam akaanza kuguna huku anatikisa kichwa kama kukataa.
"Kwa hiyo kumbe unalijua hilo? Kwamba una adui?" mwanaume huyu akaniuliza hivyo.
Nikamwambia yule mweupe, "Tafadhali bro, nakuomba sana, mwachieni. Ana... ni mjamzito, hali yake si bora kumweka kwenye pressure kubwa namna hii... tafadhali nawaomba mmwachie, eh? Nitaenda nanyi kokote mnapota...."
"Kaa kimya wewe, mbona unaongea sana?" yule komando akanikatisha.
"Na hakuna bro wako hapa," mweupe akasema.
"Eti bro! Hadi mkojo unataka kumshuka," mwanamke aliyemshika Miryam akasema hivyo.
"Unafikiri tumetumwa na nani?" mzee mbele yangu akaniuliza.
"Festo," nikamjibu.
Nikamtazama Miryam na kuona alivyoniangalia kwa hisia za utambuzi, nami nikamtazama tena jamaa.
Akaniuliza, "Festo ndiyo nani?"
Nikafumba macho na kuinamisha uso kwa hasira.
"Jibu. Festo ndiyo nani?" akauliza.
Nikamwambia, "Ninajua Festo ndiyo anacheza huu mchezo, hakuna haja ya hizi drama, najua anataka ku...."
"Kumbe una maadui wengi eh?" akanikatisha kwa kuuliza hivyo.
Nikaona Miryam anaonyesha sura ya maumivu kutokana na jinsi alivyokazwa, nami nikamwambia aliyemshikilia, "Dada, nakuomba usimkaze hivyo, tafadhali... ana..."
Mwanaume aliye mbele yangu akanitandika kofi zito sana usoni, mpaka nikahisi kizunguzungu baada ya kuinamia pembeni kiasi. Ah! Nikahisi ladha ya damu mdomoni, nami nikaendelea kuinamisha uso huku hasira zikizidi. Niliweza kuisikia miguno kutoka kwa Miryam iliyoonyesha ameanza kulia kwa sauti, nami nikatema damu na kuinua uso kumwangalia tena huyu jamaa mbele yangu bila kuweka mikono kichwani tena.
"Nikiuliza swali, lijibu. La sivyo, kofi litakalofuata halitakuwa lako," akaniambia hivyo na kumgeukia Miryam.
Nikabaki kumtazama tu kwa mkazo, fizi na ulimi zikiuma kweli, naye akaniangalia tena.
Akasema, "Nimekuuliza una maadui wengi?"
Nikamwambia, "Ninaowajua ni wachache. Naweza kudhani wapo wachache lakini ukakuta ninao wengi, kwa hiyo siwezi kujua."
"Ni nani wengine wanaokuja akilini ukimtoa... Festo?" akaniuliza hivyo.
Nikamwangalia Miryam kiufupi, yeye akinitazama kwa huzuni sana, nami nikamjibu jamaa, "Kuna... maaskari wa ulinzi niliwahi kuzinguana nao..."
"Mwingine?" akauliza.
Nikawaza na kusema, "Labda... Joshua... ila yeye yuko jela sasa na wenzake naowaona kuwa maadui."
"Mwingine?" akauliza.
Niliona kwamba huyu jamaa alikuwa anataka niorodheshe watu niliowaona kuwa maadui kwa kusudio fulani, na ingawa sikujua ni lipi, ningetakiwa tu niendelee kumpa aliyohitaji hata kama sikuwa na uhakika kama angewajua niliowasema ama la.
Nikawaza mtu mwingine, nami nikamwambia, "Tamiah."
"Mwingine?"
Nikainamisha uso kiasi, nikianza kuona huu kuwa upuuzi wa hali ya juu, na kwa kukosa mtu mwingine nikamwambia, "Ni hao wachache naowajua. Wengine siwajui."
Akatabasamu kiasi na kuuliza, "Kwa hiyo kati yao wote, ni Festo tu ndiyo unayemfikiria wa kukuleta hapa?"
"Naamini kwa asilimia kubwa ni yeye. Nisikilize tafadhali. Haya yote hayana haja. Ni... nipelekeni kwa bosi wenu, ama kama yupo mwambie aje, niko tayari kuonana naye, akitaka kufanya nini, afanye, kama wewe unataka kunipiga, nipige mpaka uridhike. Lakini nachowaomba tu ni kumwachia Miryam... hana makosa yoyote. Tafadhali..." nikaongea kwa hisia.
"Eti vipi? Tukuachie halafu yeye abaki?" jamaa akamuuliza hivyo Miryam.
Miryam akaanza kutikisa kichwa kama kukataa, nami nikamtazama kwa hisia za huzuni sana.
"Hataki. Anataka kubaki," mwanaume huyu akaniambia hivyo.
Wenzake wakacheka kidogo.
Nikahisi hasira na kusema kwa sauti ya juu kiasi, "Festo! Kama uko hapo, uje...."
"Wewe!" baunsa mweupe aliyeshika bastola akanifokea kiukali.
Mwanaume aliye mbele yangu akanipiga ngumi tumboni iliyofanya nihisi maumivu makali, nami nikajishika tumboni na kukaza maumivu.
"Nitamfumua malaya wako ngumi za tumbo atapike huo uchafu, mshenzi wewe! Unampigia nani kelele? Ama wafikiri tunakudekeza hapa? Unataka nifanye hivyo?" akaniuliza hivyo kwa ukali.
Nikatikisa kichwa kukataa hilo na kumwangalia Miryam. Alikuwa amevutwa nywele kwa nyuma sasa, asiache kulia kwa hisia sana ingawa sauti ilizibwa. Nikahisi maumivu mengi sana kihisia.
Nikamuuliza, "Niambie anataka nini! Eh? Niambie... anataka nini?"
Jamaa akasema, "Wewe."
Nikakaza maumivu zaidi na kumwambia, "Ndiyo maana nimesema nipelekeni kwake, afanye lolote analotaka juu.. akitaka kuniua, aniue... ila mwachieni Miryam jamani... please..."
Niliongea kwa hisia sana, Miryam akilia kwa ajili yangu, na huyu mwanaume akatabasamu kiasi na kuangalia pembeni.
"Tafadhali..." nikamwomba.
Akaniangalia na kusema, "Wala hata hana mpango wa kukuua."
Nikiwa napumua kwa nguvu, nikamwambia, "Vyovyote vile. Kama anataka kunitesa, sawa. Ninachoomba...."
"Aacha kufikiria mateso kijana, hujui mateso ni nini, unaongea tu. Unadhani ukiteswa utatamka hayo maneno 'ooh mwachieni' kujifanya hero kwa ajili ya huyu mwanamke? Tena wewe... utakana kabisa kumjua. Wewe unachojua tu ni kutia mateso watu wengine, hujawahi kupitia mateso, ila... yako yanakuja... kwa wakati wake," mwanaume huyu akaniambia hivi.
Nilibaki nikimtazama kwa umakini kiasi, nikiona maneno yake yamebeba maana fulani pana, nami nikamuuliza, "Wewe ni nani?"
Akacheka kidogo huku akitazama chini kuelekea pembeni, naye akasema, "Anataka kujua me ni nani."
Hakuonekana kama alizungumza na wengine waliokuwemo humo, na ndipo sauti kutokea nje ya mlango ikasikika ikisema, "Labda nimsaidie kwa hilo."
Nilihisi pigo zito sana moyoni mwangu, lililopiga kuendana na mshtuko niliohisi baada ya kuisikia sauti hiyo. Hapo hapo akaingia mtu ambaye sikuwa nimemtarajia hata kidogo, yaani hata chembe. Aliingia taratibu, akija hadi usawa wake huyu mwanaume mtu mzima, na jamaa akasogea nyuma kiasi kama kumpisha ili mja awe mbele zaidi na mimi. Akasimama na kubaki kuniangalia usoni kwa utulivu, mimi hapo nikiwa nimeshindwa hata kuufunga mdomo wangu uliokuwa wazi kwa butwaa lililonipata kwa ughafla wa jambo hilo.
"Bertha?!"
Nilichoka!
★★★★★★★★★★★
ITAENDELEA
★★★★★★★★★★★
Whatsapp +255 678 017 280MIMI NA MIMI 3

Bertha Tena?MIMI NA MIMI 3