Mkuu tupe the meaning of Msegemnege
Asili yake ni neno SEGEMNEGE
Segemnege ni KIELEZI
Kielezi huelezea kitendo (KITENZI) jinsi kilivyo fanyika.
Mf.
Nourhan anatembea "taratibu"
Neno ANATEMBEA ni 'kitenzi' (kitendo)
Neno TARATIBU ni 'kielezi', kwa kwa mukhtadha husika anaelezewa jinsi Nourhan anavyotembea.
Msegemnege ni vivyohivyo kielezi, na maana yake kwa maneno mengine ni 'Shaghalabaghala', 'a~bila mpangilio', 'hovyo hovyo', nk.
---
Tangia alivyomuacha mke wake wa kwanza, mambo yake yanaenda segemnege.
---
Simulizi hii ni msegemnege
(m) hapo nimeongezea kuvunisha tu!
Kama vile baadhi ya watu wa Tanga, Mombasa na Zanzibar wavumishavyo maneno...
mf.
Meli => Jimeli...
Honda => Jihonda...
kama vile baadhi ya watu wa kanda ya ziwa wavumishavyo maneno...
mf.
Baiskeli => Libaiskeli
Moyo wangu umekudondokea => Limoyo langu limekudondokea
Kama vile watu wa kanda ya magharibi wavumishavyo maneno kwa kudunisha...
Hela => Kahela
Simu yake nzuri => kasimu kake kazuri.
Bila kuwasahau baadhi ya watu wa nyanda za juu kusini...
Sanduku => Gusanduku
Nyumba kubwa => Gunyumba gukubwa
Nk
___
Bila shaka umepata mwanga.