Simulizi: Msegemnege

Simulizi: Msegemnege

Shukrani mkuu.

Natamani kila siku niwe naweka, lakini muda wa kuandika ndio tatizo.

Awali nilitaka niandike "off JF" kwanza yote hadi iishe, lakini PM zilizidi za kutaka niweke simulizi...
Shukran brother,nafurahi umetekeleza ushauri wa kutupia katikati ya wiki kisha jumamosi tena maana kwa wiki mara moja tunakua tumeanza kusahau mtiririko wa stori unavyoenda,sasa tunavumilia hadi jmosi tena tukutane na tupio😂 lingine.
Ila watu wa jf kiboko kudadeki😂,
Mmeona mambo ya sehemu inayofuata mara sijui episode inayofuata yamekua mengi sasa ni matupio ya JBourne59 baada ya Analyse kutupatia vi portion 😂
 
Tupio la XXV - Makao


Ilipoishia…



Omari akachukuwa nakala ya ile meseji kisha akaipiga picha na kuituma.

Omari: “I sent you a photo, did you see?”

Nasreen: “Ok, I’ve just seen it, but I need to see the original, and if you don’t mind make a video call so that I make sure I’m talking to the one who real found the bottle.”

Omari: “Okay, will call you in fews minutes, I have to go back home”

Nasreen: “Ok, Omari, I’m so eager to see you and the message”

Omari akazima data kisha akatoka mle ukumbini haraka na kudandia DCM iliyomfikisha Ukwamani.

Akiwa chumbani kwake, akaitoa ile barua ‘original’ na akawasha data kwenye simu kisha akapiga video call…



Sasa endelea…


(Video call)


Omari: “Haloo!”

Nasreen: “ Hi, you are handsome!”

Omari: “Oh, thank you…”

Nasreen: “Is that your room?”

Omari: “Yes, me living with my parents”

Nasreen: “Owh, you’re living with your parents in the same room?!”

Omari: “No, no ,no, me live my room and my parents their room”

Nasreen: “Okaaay, now show me the original paper you found in the bottle”

Omari akaichukua ile karatasi orijino, akaikunjua kisha akaelekezea kwenye jicho la kamera ya simu yake…

Nasreen: “Yes, adjust the distance a bit so that I see well”

Omari akasogeza nyuma kidogo simu yake

Nasreen: “Yes, wow, that is the original one, good, now what about the bill attached?”

Omari akafunua mchago wake kisha akatoa kibunda cha elfu kumi kumi zilizokamilisha kuwa milioni moja

Nasreen: “What are those?! You are own money?”

Omari: “This is what I found on the bottle also…”

Nasreen: “I instructed to keep one bill, where is it?”

Omari akaelewa na kukumbuka alipoiweka ile noti moja ya Bahrain, akaitoa kwenye wallet kisha akamuoneshea kupitia camera

Nasreen: “Yes, that is 20 bill of Bahrain dinar, zoom a bit so that I can see well”

Omari akafanya kama alivyo elekezwa hadi Nasreen aliporidhika na muonekano kisha akasema…

Nasreen: “Oh yes, it’s exactly same number as recored before I put them in the bottle”

Nasreen: “Okay Omari, how much is that you showed me ealier”

Omari: “One Million Tanzanian Shillings”

Nasreen: “Wait a second…”

Nasreen akafanya hesabu zake haraka haraka kisha akasema

Nasreen: “It looks like you have all the money I put in the bottle, so wonderful”

Omari: “No, I spent about one lakhi and twenty buying this smartphone…”

Nasreen: “One lakhi?!!”

Omari: “Yes, one hundred thousand and twenty thousand Tanzania shillings”

Nasreen: “So you are telling me, you can buy a smartphone with just one hundred thousand in your country?”

Omari: “Yes”

Nasreen: “What’s the make of your phone?”

Omari: “Itel”

Nasreen: “I see”

Nasreen: “You are so honest Omari”

Waliendelea kuongea pale weee lakini wote wakivunja kiingereza ingawaje walikuwa wanaelewana.

Omari alikuwa na kichwa kizuri kwenye kuhifadhi mambo, ni kwamba alivyomaliza darasa la saba, kichwa chake hakikushughulishwa na mambo mengi hivyo kilikuwa na nafasi ya kutosha kuhifadhi vitu ndio maana hata kusoma kiingereza na kuongea aliweza kwa muda mfupi.

Baada ya kuongea sana na Nasreen hatimaye wakahitimisha kwa siku hiyo…

Nasreen: “I will call you tomorrow in shaa Allah after swalatil ‘isha”

Omar: “Ok, thank you”

Nasreen: “Bye”

Omari akawa na furaha sana kwa kuongea na rafiki wa mbali, rafiki aliye mpata kwa bahati nasibu (ee ndugu msomaji, hii sasa ndiyo bahati nasibu, wengi huchanganya kati ya bahati nasibu na kamari. Kamari ni mchezo unaodhulumu wengine na kumpa mmoja faida kiasi lakini mwendesha Kamari hufaidika zaidi, unaweza kusema bahati nasibu ni ‘zari’.

Siku hiyo Omari alilala akiwa na amani na wala hakumshirikisha yoyote mle ndani mwao.
---


Jana yake, baba yake Omari alisoma ‘oda’ kwenye ubao wa matangazo kazini kwake kwamba keshokutwa (kesho) mapema saa moja asubuhi anatakiwa aripoti makao makuu, hivyo afike ofisi ya siioo (CO ) akachukue barua ya maelekezo. Wakati akimueleza mke wake alionekana akiwa na wasiwasi mwingi kana kwamba kuna jambo baya litaenda kutokea kwake.

“Nimeitwa makao, sijui hata kuna nini, ni mimi tu kwenye kambi yetu ambaye nimeitwa, sijui ndio naenda kupewa barua ya kustaafu ama kuachishwa kazi…”

“…lakini kama ingekuwa kuachishwa kazi kwa makossa yangu lazima ningepelekwa kortimasho kwanza nihukumiwe…”

Afande Juma alikuwa hana furaha akiwa anamueleza jambo hilo mkewe. Akachukuwa buti zake mpya na kuanza kuzisafisha kisha kuzipiga dawa ya viatu (kiwi). Alitumia muda mrefu kuving’arisha hadi aliporidhika, viatu vilikuwa vinang’aa kiasi cha kuweza kujiona ukiviangalia hususani kwnye pua ya buti.

Asubuhi saa kumi afande juma aliamka, akaoga na kujiandaa kwa kuvalia nadhifu. Alivaa sare zake mpya ambazo alikuwa hapendi kuzivaa, akavaa na nishani zake zote alizozipata nchini baada ya kutekeleza fatiki kadhaa kwa umahiri lakini pia alivaa nishani yake aliyopata alipotoka mafunzo ya vilipuzi huko ughaibuni. Akavaa buti zake na akaving’arisha tena kwa pamba laini aliyokuwa nayo kwenye mfuko wa suruali. Hakika alipendeza.

Saa kumi na moja na nusu alitoka nyumbani hadi ukwamani stendi ya daladala ambapo alipanda gari za kwenda Mwenge, hapo Mwenge akapanda gari za kwenda Posta na akashukia kituo kiitwacho ‘Palm beach…” kutokea hapo alivuka barabara na kuelekea makao kwa kutembea kwa miguu. Kwa kuwa ilikuwa bado ni mapema, alitembea taratibu ili asitokwe na jasho pia asichafue viatu vyake.

Alienda moja kwa moja hadi lango kuu…

“Jambo afande!” baba Omari alisalimia kwa ukakamavu pale getini alipokutana na askari jeshi wa zamu aliyemruhusu kuingia sehemu ya mapokezi.

“Jambo!, habari za huko utokako lenzkoplo!” Aliitikiwa salaam baada ya kusalimia tena huku akipiga saluti kwa mkuu wa askari wa zamu waliokuwepo hapo mapokezi…

“Wewe lenzkoplo hebu jitambulishe kwanza!” Sauti nyingine ya kukoroma ilisikika, alikuwa ni mteule daraja la pili ambaye alikuwa amevalia mkumbulu maridadi kabisa(sash) akiwa anamnyooshea fimbo yake (walking stick) baba Omari…

“Emtii saba kenda (ngapi ngapi) alitaja namba, natokea miatano ishirini na moja keijei, lenzkoplo Juma Bakari Omari Sa! (sir)” Kwa ukakamavu kabisa afande Juma alijitambulisha kama inavyotakiwa… ingawaje mteule yule alimfanyia dhihaka jeuri tu ama kutaka kumpa kashkash kidogo kama ilivyo kawaida kwa mkubwa kumpa kashkash kidogo mdogo. Ni kawaida kwa kila aingiaye hapo lazima ajitambulishe kwa askari maalumu wa hapo mapokezi ambapo kuna wataalamu wa kada za ulizi jeshi.

Getini hapo baadhi ya watu ambao hawavai mavazi yao vizuri huzuiliwa kuingia na kuambiwa wakavae vizuri. Angalau usivae suruali ya kubana, ama mlegezo, ama jeans zilizo na viraka vya urembo na mfano wake, ama gauni fupi, au sketi fupi, ama za kuangaza ama nguo za kushikwa mwili na mfanowe…

Wengi wakijua siku hiyo anaenda makao, basi hujitahidi kuvalia ipasavyo, ila wale wa mara ya kwanza halafu hawajui dress code, hupata tabu sana! Na hivi ndivyo watu ama jamii inatakiwa iwe, uvae nguo sahihi sehemu sahihi, siyo unavaa shaghala baghala ama ‘shabby’ halafu unaenda sehemu zenye kutunza nidhamu, utajuwa hujui.

Mapokezi hapo aliandikisha kama kawaida na kupewa kadi maalumu ya wageni ambayo alitakiwa aivae muda wote akiwa ndani ya wigo.

“Eee kumbe umekuja kwenye paredi ya leo, basi nenda jengo lile ukasubiri, utakuwa wengine wapo humo…”

Afande mmoja wa pale mapokezi ambaye alikuwa amevaa kiraia alimuelekeza sehemu ya kusubiria baada ya kumsikiliza shida aliyoijia.

“Jambo afande!” Alisalimia alivyoingia jengo lile na kukuta askari wenzake wenye vyeo vikubwa zaidi yake. Aliitikia mmoja tu wengine wakiwa wamenyamaza kimya, siyo kwa dharau, bali ndio utaratibu wao wavaa mabakamabaka.

Alikuta kuna makundi mawili, moja la wenye nyota nyota mabegani na lingine wenye mbavu mbavu na wasio na mbavu na wenye kolokolo mikononi (likitu kama saa hivi)

Ni kwamba siku hiyo hapo makao, kulikuwa na paredi fupi ya kuwatunuku vyeo na nishani mbalimbali kwa baadhi ya askari. Afande Juma naye akawa mmoja wao.
---


Flash Back


Kulikuwa kunahitajika askari kadhaa kwenda Yugoslavia kusomea masomo ya kati ya milipuko na masomo ya juu ya milipuko.

Jenerali wa nyota moja, afande Gema, aliitisha mafaili ya askari wote aliokuwa nao kwenye mafunzo ya kati ya milipuko miaka kadhaa iliyopita huko Jamhuri ya Czech. Baadhi walikuwa wamekufa na wachache wamestaafu. Katika majina hayo afande Juma naye alikuwemo.

Brigedia Gema alikuwa mkufunzi wa kitengo cha mafuzo ya nje ya nchi. Akiwa anapata mafunzo yake ya juu huko Czechoslovakia, afande Juma naye alikuwa anapata mafunzo ya kati huko huko lakini kambi tofauti. Hivyo walikuwa wanafahamiana.

Afande Juma alikuwa mtaalam aliyefuzu vizuri, lakini faili lake lilichafuka kwa utovu wa nidhamu kwenye kikosi chake hususani tangia alivyotoka Dafur.


Flash Forward


Ile sherehe fupi ilifanyika, na katika paredi ile, afande Juma akarejeshewa mbavu zake mbili na ua, hivyo sasa akawa na mbavu tatu na ua moja na kufanya awe sajini mtumishi (staff sergeant). Ilikuwa siku ya furaha sana kwa stafu sajent Juma ambapo alikabidhiwa na fimbo yake rasmi ya kutembelea.


Flash Back Again

Baada ya Brigedia Gema kupitia faili la lenzkoplo Juma, ndipo akakutana na maelezo ya kiongozi wake kwenye kombania (oosii), na mtunza nidhami wa kambi ‘rejimento sajenti meja’ yote yakimuelezea tabia zake za ulevi na kwamba wanasubiri afikishe miaka 45 tu ambapo ilikuwa ni miezi michache baadaye astaafu wa achane naye.

Akaitisha faili la afande Juma kutoka kitengo maalumu ya mienendo ya wanajeshi, ndipo akakuta mapendekezo yaliyofanya afande Juma aitwe kwenye kurudishiwa mbavu zake. Ni kwamba kwa miezi miezi minne mfululizo afande Juma ameonesha nidhamu ya hali ya juu, kwamba ameacha kulewa na ana ushirikiano kazini na wenzake na mwenendo wake kwa ujumla umerudi kama zamani na hata afya yake imeimarika kuliko ilivyokuwa miezi sita nyuma.


Flash Foward


Baada ya sherehe ile, stafu sajenti Juma alitakiwa aripoti ofisi ya Mkuu wa mafunzo (CI-OT) kitengo cha mafunzo ya nje ya nchi.

“Jambo sir!” Ssgt Juma alihoti na kupiga salute kali akimsalimia Brigedia Jenerali Gema ambapo jenerali huyo wa nyota moja aliitikia kwa kukakamaa na kubana mikono kwakuwa kofia yake ilikuwa mezani, kisha akasimama akampatia mkono afande Juma kwa ishara ya kusalimiana.

Waliongea mengi, nasaha nyingi, kukumbushiana drill za nchini Czech kwingi na hatimaye afande Gema akasema...

“Nataka uende sinia kozi ya amnushen, wewe pamoja na wenzako kadhaa, na ukitoka huko itabidi uende semina fupi kwenye chuo chetu cha uongozi (endisii) ili nikupendekeze upatiwe kolokolo…”

“Mwezi mmoja baada ya leo utapata maelekezo kikosini kwako juu ya utaratibu mzima wa safari, roja sofa?”

“Roja ova sa!”

Baada ya maongezi mengine ya kawaida, waliagana na kuondoka.

Wakati anatoka getini pale alipo saini, safari hii sahihi yake ilianza na ‘ssgt’ badala ya ‘lc’ hadi yule askari jeshi akamtania…

“Sasa nani senior kati yangu na yako…” wote wakacheka.

Ni kwamba yule aliye mapokezi naye ni stafu sajenti, lakini kwa mujibu wa namba zao za jeshi, afande Juma ndiye alikuwa senior…

“Mimi Sinia, soma namba hiyo…” Afande Juma alijibu kisha wote wakacheka.

Alivyokuwa anatoka getini, yule askari jeshi aliyemfungulia mlango safari hii alikuwa amesimama kando na geti likihudumiwa na askari mwingine ambaye pia ni MP, ilibidi akauke kumsalimia…

“Jambo afande!” alisalimia yule MP wa kwanza huku yule mwenye kushughulika na geti akimfungulia geti dogo apite.

“Jambo, endelea!” alijibu salamu huku akiitoa fimbo yake kwapani na kuanza kutembea nayo kwa mikogo!

“Hapa kwanza nielekee maeneo ya Diamond Jubilee nikapate chakula…” alijisemea huku akitembea kuelekea upande huo wa diamond jubilee.



Inaendelea…
 
Tupio la XXVI – Possesed


Ilipoishia



Onesmo aliweka hadharani baadhi ya mambo ya watu kila wakimhoji hadi wakamfukuza aende bwenini.

“Hahahaaa, leo tumejua siri zenu…” Yule mwalimu wa kunong’ona alirudia tena kunong’ona akiwaambia walimu wenzake akiwemo mwalimu wa nidhamu ambaye siri yake ilikuwa ya aibu zaidi.


Sasa endelea…


Onesmo hakuadhibiwa, akaruhusiwa kwenda bwenini, lakini walimu hao wakaazimia kumfuatilia ili kujua zaidi maana hata Jose, msimamizi wa bwalo alishuhudia kwa kusema naye alitabiriwa kuokota hela na kweli jioni ile aliokota noti ya elfu kumi alipokuwa akirudi nyumbani kwake.

Maisha ya shule ya Junior yakabadilika kutoka kuonewa na kuandamwa na wanafunzi kutaka kujuwa mambo kadha wa kadha yasiyoweza kujulikana kwa sababu ya umbali nk.

“Baba yangu mie yuko wapi sasa hivi…” hili ni moja ya maswali aliyoanza kuulizwa Onesmo na wenzake

Naye wala hakuwa na hiyana, sijui utoto ama nini, akawa anajibu tu, “Yupo kazini, yupo sehemu fulani…” hivyo yani.
---


“Huyu mtoto ana mapepo!” alisema mwalimu mmoja…

“Eee, si ndiyo yale wayaitayo mapepo ya utambuzi?...” alichangia mwalimu mwingine

“Mmmh, sasa tufanyeje, si atakuwa anatuumbua huyu kila siku…”

“Hapana, mbona hasemi hadi aulizwe…” alijibu mwingine.

“Inawezekana hata kufaulu kwake ni kwa ajili ya mdude hayo hayo…” alisikika mwalimu mwingine

“Sasa tufanyeje…” alisema mwalimu wa taaluma.

“Tumshirikishe mkuu wa shule kwanza…” Mwalimu mwingine alisema.

“Pia tuwashirikishe watu wa maombi ya kiroho labda watatusaidia…”

“Wana maombi hawaruhusiwi kwenye kanuni za taasisi yetu…” Ilikuwa kauli ya Mkuu wa shule baada ya kushirikishwa suala lile.

“Tuache tu kwakuwa hakuna madhara anayoleta kwa wenzake, tukazanie kwenye kumuongoza kitaaluma lakini mwalimu wa malezi jitahidi kuwa naye karibu na kumjenga kwenye maadili mema…” Alimaliza hivyo mkuu wa shule.
---



Miaka miwili baadaye, ile familia ya mama ustaadhi ilihamishiwa mkoa mwingine, walikuwa ni wafanyakazi wa serikali, lakini Zawadi yeye alirudi kwao Iringa.

“Nataka nikasalimie nyumbani…” hayo yalikuwa maneno ya Zawadi akiyarudia mara kwa mara aliposikia habari za kuhamia mkoani Dodoma.

Bahati nzuri walimruhusu, wakamfanyia shopping kwa ajili yake na zawadi za kwenda nazo kwao. Sehemu kubwa ya hela za shopping zilikuwa ni sadaka za waumini kule nyumbani kwa mama Junior, maana kila akipata hela yeye alikuwa akizipeleka nyumbani kwa dada yake.

Nyumba ya mama Vai ikapata pigo la kuondokewa na binti muhimu aliyebadilisha maisha yao na kuwa mazuri.

“Ninawaageni, wiki ijayo nitarudi kwetu Iringa kusalimia, dada na mumewe wao wanahamia Dodoma. Mungu akipenda tutaonana wakati mwingine…” Zawadi alisikika akiwa anawaaga waumini pale nyumbani kwa mama Onesmo.

Waumini walihuzunika sana lakini waliamua nao kumtafutia zawadi za kwenda nazo nyumbani, hivyo alimuomba jumapili ijayo awepo ili wampatie zawadi zake.

Siku tano baadaye, familia ya mama ustaadhi ilihamia Dodoma, lakini Zawadi yeye aliomba asipakiwe kwenye basi la kwenda Iringa siku hiyo badala yake apelekwe kwa mama Onesmo ili asubiri Jumapili akutane na waumini kisha Jumatatu ndio apande basi la kwenda Iringa.

Zawadi aliomba kwenda shuleni kumuaga Onesmo ambaye sasa alikuwa darasa la sita. Ilikuwa siku ya jumamosi baada ya jumuiya na kupata kifungua kinywa, walifanya ziara kwenda St. Anne. Walinunua zawadi za chocolate za kupeleka shuleni kwa wanafunzi wote wa darasa lake.

Zawadi alimuaga rasmi Onesmo kuwa yeye ataenda kusalimia nyumbani, na wataonana siku yoyote panapo majaaliwa. Onesmo alihuzunika, maana alikuwa ameshamzoea Zawadi kama dada yake. Hatimaye wakarudi nyumbani.
---


Wakati Zawadi anasindikizwa kwenda Msamvu stendi, aliwaomba wapitie kwanza kwenye kituo cha kulelea watoto waliokuwa wakiishi kwenye mazingira magumu na yatima kilichopo katika kati ya mji wa Morogoro. Huko Zawadi alikabidhi mizigo yake yote pamoja na hela zote alizopewa nyumbani kwa mama ustadhi na nyumbani kwa mama onesmo, akabakiwa hana chochote cha kubeba wala kushika mkononi.

Mama Junior na Mama Rose walishangaa sana na kumuuliza kwanini anagawa kila kitu...

"Zawadi, mbona unatoa vitu vyote!, sasa nyumbani utaenda mikono mitupu?..." Vai aliuliza

"Mungu ni mwema, nitafika tu na zawadi za kupeleka zitapatikana" Alijibu Zawadi kisha akaendelea...

"Nisindikizeni stendi kisha nikatieni tiketi ya kwenda Iringa, nitafika..." Alimaliza.
---


Flash Forward

Saa saba baadaye – “7 hours later”

Iringa, eneo la Gangilonga.

Watu walijazana mtaa mmoja kushuhudia mtoto aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha miaka kadhaa iliyopita...

Gift, alipotea alipotumwa na mama yake kwenda soko kuu lakini hakurudi nyumbani hadi siku hiyo alipopatikana mtaa wa jirani na nyumbani kwao akiwa hajitambui, mchafu wa nguo lakini akiwa na afya njema kwa muonekano wa nje.

Mtaani hapo alipopatikana akiwa amelala upenuni mwa nyumba ya mzee mmoja maarufu, watoto walianza kupiga kelele kwa kusemaa kuna mtoto kichaa amelala nyumbani kwa mzee Mwengwa

Watu walivyo kusanyika ndipo binti mmoja akamtambua na kuanza kisema kwa sauti...

"Huyu ni Jifti, jamani huyu ni Jifti, ni yeye..."

Watu wazima wakakusanyika pia na Mzee Mwengwa mwenyewe pia na ndiye alikuwa balozi wa mtaa huo na mtoto Gift alikuwa ameonekana upenuni mwa nyumba ya balozi huyo.
---


Flash back.

Miaka kadhaa iliyopita, mama mzazi wa Gifti alimtuma binti yake wa pekee kwenda soko kuu la Miomboni kufuata mahitaji.

Mama Gift alimsubiri mwanae bila majibu, wasiwasi ukamuingia, akaenda kwa balozi kutoa taarifa ya kupotelewa mtoto, Balozi akamshauri wasubiri hadi kesho yake ili kama bado atakuwa hajapatikana basi ndio waende kutoa taarifa Polisi.

Saa zilienda, siku ikapinduka, Gift hakurudi nyumbani. Wasiwasi mwingi ukamuingia mama Gifti ambaye mume wake wakati huo alikuwa Mtera kufuata samaki. Yeye (baba Gift) alikuwa akiuza samaki kutoka mtera hapo sokoni miomboni ingawaje yeye alikuwa akiuza kwa jumla.

Mama Gift jua lilipozama "tumbo la uzazi likamuuma na akaaza kulia, majirani wakakusanyika kujua kulikoni, mtaa mzima wakajua like tukio.

Ilikuwa huzuni kubwa. Taarifa zikasambazwa Kanisani anapoabudia, msikitini kwenye spika kulitangazwa kupotea kwa mtoto Gift...

Polisi wazazi wa Gift walifuatilia mara kwa mara labda wangepata taarifa mpya lakini haikuwa hivyo...

Wiki ikaisha, mwezi ukaisha, mwaka ukaisha bila taarifa yoyote ya kuonekana Gift akiwa hai ama akiwa amefariki.

Gift ambaye siku chache alimaliza darasa la saba, hakuonekana tena wala kusikia habari zake popote.

Baada ya mwaka na mwezi mmoja kupita, ilibidi wazazi wa Gifti waweke msiba nyumbani, kukawa na matanga bubu.

Kulifanyika misa ya kumuomba Mungu amtunze mtoto Gift kama yupo hai, na kama amefariki basi amrehemu na kumuweka mahali pema peponi.

Baada ya matanga ya siku tatu msiba ukaisha rasmi na watu wakasahau habari za Gift maisha yakaendelea.

Wiki moja baada ya kuanua matanga ndoto za kwamba Gift yupo hai zikaanza kumuandama mama Gift.

Awali alidhani ni shauri ya mawazo tu ya mwanae wa pekee.

Lakini ndoto ilimirudia kila baada ya siku chache kwa namna tofauti ndipo akamshirikisha mume wake.

Mama Gift kabila lake ni Mkaguru wa Mpwapwa ambaye aliolewa na kijana mmoja wa kihehe aitwaye Kihwele. Walikutana kwenye shughuli za mnada sehemu iitwayo Kibakwe - Mpwapwa, wakaanzisha uhusiano na hatimaye wakafunga ndoa ya kimila iliyofanyika Mpwapwa kisha kumaliziwa Iringa na wakawa wanaishi Iringa huku kijana Kihwele akiendelea na shughuli zake za minadani hadi miaka ya hivi karibuni alipoamua kufanya biashara kati ya Mtera na Iringa tu na wakati huo tayari walikuwa na binti yao wa pekee aitwaye Gift.
---



Mama baada ya kumshirikisha mumewe, aliamua kusafiri kwenda kwao Mpwapwa ambapo huko alienda kulia kwa wazee kuhusu mwana wake wa pekee kupotea katika mazingira ya kutatanisha lakini sasa kuna ndoto inayojirudiarudia.

Baada ya wiki tatu alirudi Iringa kuendelea na maisha, ingawaje huko alikoenda hakupata majibu yenye kutanzua shida yake lakini wazee waliishia tu kusema, awe mvumilivu, ipo siku mtoto ataonekana.


Flash forward.

Watu wengi walikusanyika kushangaa tukio lile na Balozi wa mtaa akasema…

“Hebu kamwiteni mama Kihwele...” Balozi alipenda kumuita hivyo mama Gift.

Babada ya dakika kadhaa, mama Gifti alifika kwenye tukio lile. Wakati huo mumewe pia alikuwa safarini.

“Kuna mtoto amekutwa amelala hapa upenuni mwa nyumba yangu, na kuna watoto wansema ni jifti, hebu muangalie umtambue…”

Wakati huo yule binti aliyedhaniwa kuwa ni chizi, alikuwa bado amejikunyata, haongei lakini macho yake yanaangaza huku na huku na alikuwa kama anasikia baridi hivyo alipewa kitenge ajifunike, lakini bado alikuwa amekaa chini.

Akiwa na shauku, mama Gift alimtoa kile kitenge alichojifunika, wakawa wanaangaliana! Mama Gift akaachama mdomo, akamshika kwa mikono yake miwili, akamwinua, bado akiwa katika hali ya kuhamanika akamgeuza mgongoni, akashusha kidogo gauni alilovaa…

“Jamani mwanangu Gift….” Akamkumbatia na akaanza kulia

“Ni yeye Gift, nimeona alama yake mgongoni, ahsante Mungu…” aliendelea kulia

Kulipita kilio cha dakika kadhaa huku mama Gift akiwa bado amemkumbatia mwanae. Mwanae ambaye alikuwa bado amezubaa tu waongei bali alikuwa akiangaza macho tu kama vile haelewi kinachoendelea.

“Sasa, kabla ya yote, tukapige ripoti Polisi…” Sauti ya Balozi ilisikika…

“Polisi nenda wewe baba, ngoja nikamuogeshe mwanangu, ngoja nikampe chakula mwanangu…” Mamam Gift alikuwa akilia kwa kuomboleza huku akielekea nyumbani kwake ambapo sio mbali…

“Gift mwanangu, ulikuwa wapi?!” Mama Gift aliendelea kulia

“Hadi tumeweka msiba mwanagu, tulidhani umeshakufa….”
--


Nyumbani mama Gift alichukuwa maji ya moto aliyoyaandaa kwa ajili yake na kumuogesha mwanae huyo huku akimkagua kila sehemu na kumkuta salama hana jereha lolote wala makovu yoyote. Akaingia naye chumbani kwake na kumkagua maeneo ya siri lakini pia alikuta yupo salama, hakuingiliwa halafu ndio akamfunga vitenge na kisha akamfunika na koti la kuzuia baridi.

“Njoo jikoni mwanagu…” mama Gifti alimuongelesha mwanawe…

Akaandaa uji haraka haraka, akaweka ndimu sukari kidogo na siagi kisha akampa mwanawe.

Gift akiwa bado hajatoa neno lolote akapoke ule uji akaanza kunywa.

“Hodi hodi hodi humu ndani…” Ilikuwa sauti ya Balozi

“Habariza muda?” Balozi alisalimia

Alijibiwa kisha akauliza kama ameona mtoto ana hitilafu yoyote.

“Nimemuogeshwa mwenyewe, nimemkagua, hana hitilafu yoyote, lakini bado hajaongea chochote, yupo jikoni anakunywa uji.” Mama Gift alisema.

“Basi vizuri, nimetokea Polisi, wamesema kesho asubuhi tuende na mtoto ili wafanye kazi yao…”
---


Itaendelea Jumamosi panapo majaaliwa
 
Back
Top Bottom