SEHEMU YA 454
βNajua wengi sana mtashangaa imekuwaje kuja kusimama hapa mbele na kutoa ujumbe huu ninaotaka kutoa, kwanza naomba mtambue kwamba sina nia mbaya ila nimekuja kwa upendo tu. Kuna kitu nimejiuliza sana jana usiku na ndio kimenifanya leo nije kuzungumza hapa, nimejiuliza san asana NINI MAANA YA MAPENZI? MAPENZI NI NINI? MAPENZI NI KITU GANI? Nimejiuliza sana ndugu zangu, ila nikasema naomba kupeleka kwa wadau labda watanisaidia kwa kile nilichonacho. Mimi kama Bahati nakiri kwenye umati huu mkubwa kuwa nilimpenda sana Ericana bado nampenda ndiomana nimekuja hapa kwani nimeona kama nampenda basi nimuache afurahi na furaha ya Erica ni kuolewa na Erick, asante Erick kwa kufanikisha hilo. Erica hakunipenda mimi kimapenzi ila alinipenda kama binadamu mwenzie, ila swala la kutonipenda kimapenzi halikumfanya anitenge kwani alinijali na kunithamini na kufikia hata hatua ya kuniokoa kutoka kwenye gonjwa la ukimwi, unaweza sema alifanya yote hayo sababu alinipenda kimapenzi hapana, ila aliniokoa sababu ndani mwake kuna upendo wa dhati na ndani mwake kuna kitu kinaitwa kujali. Naweza sema Erica ni mwanamke wa tofauti sana, na Erick ni mwanaume wa tofauti sana, nilimpenda Erica ila yeye hakunipenda na ikawa ngumu kutimiliza swala la mapenzi, ila Erica na Erick ndio maana halisi ya neno mapenzi kwa nionavyo mimi, nimefikiria na kuchambua nimeona mapenzi ni kupendana, kama mna mengine mtayaongezea ila nimeona mapenzi ni kupendana. Mungu awajaalie Erica na Erick nawaombea mpate watoto mapacha tena wakike na wa kiume nao muwaite Erica na Erick, asanteniβ
Watu walipiga makofi, mama Erica aliinuka kwenye kiti chake na kwenda kumpokea Bahati maana hakuamini kama Bahati angeweza kuongea vitu vya maana kiasi kile, alijua tu angelia lia pale mbele kuwa anampenda sana Erica.
Basi watu wengi wakafatana na mama Erica kwenda kumsindikia Bahati na kumpongeza.
Ulifika muda wa watu kwenda kusalimiana na maharusi na kugonga glasi za vinywaji kwa pamoja, ni muda huu ambao Derick alienda pia, ila alipofika pale Erick alimvuta karibu na kumnongβoneza,
βSasa kile alichofanya Bahati ndio tunaita uanaume yani kule ndio kuwa mwanaume unakubaliana na matokeo sio mwanume unakuwa na wivu na dada yakoβ
Derick aliondoka na kurudi kwenye kiti ambapo pembeni yake kuna mdada alikuwa akivutiwa nae aliamua kutoa swaga zake,
βNakupenda, natamani na mimi ifikie wakati nifunge ndoaβ
βIla umenipenda lakini mimi ni mjamzitoβ
βOoh sawa, ila hata hivyo sidhani kama utanikubali maana mimi ni muathirikaβ
Yule dada akamwambia,
βNatamani kupata mume wa kunioa sana, na wala sijali kuhusu kuathirika kwako kama utanikubali na mimba yanguβ
βKweli umenikubalia? Unaitwa nani?β
βNaitwa Siwema, na wewe je?β
βNaitwa Derick, naomba twende kwa mama yangu pale akufahamu Siwema tafadhaliβ
Basi Derick na Siwema waliinuka na kwenda alipokaa mama yake Derick.
Kuna meza alikaa James, Dora na watu wengine akiwemo George, Dora alimtania George,
βNa wewe utaoa lini eeeh! Au bado unasubiri kuoa bikra?β
βAaah Dora mbona hilo wazo limepotea kwangu sema tu sijampata wa kumuoaβ
Pembeni yake kulikuwa na binti aliyebeba mtotot mdogo mikononi, alimwambia George
βNioe mimi basiβ
James na Dora walicheka kisha Dora akamwambia George,
βEeeh mke huyo kajitokezaβ
George alimuangalia Yule mwanamke na kumwambia,
βDada, mimi natafuta muathirika mwenzangu maana mimi nina ukimwiβ
Nipo tayari kuishi na wewe hivyo hivyoβ
βUnaitwa nani dada?β
βNaitwa Nasmaβ
Dora akajaribu kumshauri Nasma,
βUsiharakie sana kuolewa angalia maisha yako na mtoto, usikimbilie kuolewa mdogo wangu. Unatakiwa kuangalia maisha yako yani ukauzoe ukimwi sababu ya kutamani kuolewa! Hapana kwakweli, jifikirie mara mbiliβ
Ujumbe ule ulimuingia Nasma ingawa alikuwa na hamu sana ya kupata mume na kuolewa tu.