SIMULIZI: Notebook

Cruze

Member
Joined
Jan 10, 2021
Posts
36
Reaction score
60
NOTEBOOK: SEHEMU YA KWANZA

Mshale wa saa ulisimama kwenye 4 na dakika zake ,Carry alikuwa akijigeuza upande wa pil ili alale vizuri Ila mwanga wa jua ulionekana kumkera pindi ulipomchoma usoni, Carry alifumbua macho yake kwa tabu sana na kwa hasira juu ya mwanga ule alianza kujinyoosha taratibu kisha alijisogeza dirishan na kufungua vzr pazia alishtuka sana na kukurupuka kisha alianza kuvaa nguo zake haraka haraka ili atoke mahala pale ,kabla hajamaliza kuvaa alisikia mlango unagongwa. Alisita kufungua Ila alienda kufungua baada ya mgongaj kujitambulisha ni mhudumu.

"Dada samahani kuna business card hii apa nmepewa nkupatie na mwanaume ulyekuja nae usiku "yule muhudum alimwambia Carry huku akimpatia ile Card. Carry hakumjb chochote alichukua ile card kisha akafunga mlango.

"Mungu wang ni nini hichi nmekifanya simfaham ata huyo mwanaume nlyekuwa nae na nmelala nae ,masikn Carry mim ntamueleza nin mama angu ntamwambia nilikuwa wap ila yote haya sababu ya pombe "Carry alionekana ana mawazo ndipo akakumbka jana yake usiku alienda kweny sherehe ya kuzaliwa ya rafk ake Joan, alikunywa pombe sana bahat mbaya akachukuliwa na Edward walyekutana nae kwa mara ya kwanza kwenye hiyo sherehe. Carry aliachan na hayo mawazo aliona ni afadhal awah nyumbani kwanza maana alijiua jins mama yake alivyo mkal.

Carry alivyofika tu nyumbani alikutana na mama yake amekaa nje ya mlango akimsubiri

"Mama samahan jana sikuweza kurud sherehe ilichelewa kuisha"Carry alianza kujitetea kabla hajaulizwa chochote na mama yake
"Mwanangu dunia itakufundisha maana umeshindwa kunielewa mim mama yako"kisha mama ake Carry aliingia ndan ,Carry aliamua kuingia ndan huku akiwa na aibu kwa alichokifanya alikuwa na uchovu sana na kichwa kilmgonga kutokan na pombe alyokunywa usiku,alienda kuoga ili apunguze uchovu, alvyomaliza ndipo alikumbuka kuhus ile card ,aliichukua ili amtafte yule mwanaume ila aliona hakuna haja ya kumtafta maana hawakuwa wapenz isitoshe walilala wote bahati mbaya tu .. alienda kwnye maktaba ndogo iliyopo pale nyumban kwao kisha alichukua notebook ndogo na kuiweka ile business card ndan ya hiyo notebook .

Baada ya week mbil tangu lile tukio litokee Carry akiwa anafua gafla alihis kichef chef na kuanza kutapika sana mama yake alibak akimtazam tu bila kuzungumza chochote aliingia ndan na kushika tamaa alihis kabisa mwanae atakuwa ana mimba

"Leila Leila Leila !!!mama Carry aliita kwa jazba na kwa saut ya juu sana
"Abee mama "aliitika Leila mdogo wake Carry kisha akaenda kumsiklz mama yake
"Mwambie dada yako ajiandae tunaenda hospital sasahiv "
"Kwan mama dada anaumwa?"
"Mpuuzi wewe fanya nilichokwambia sitak maswali"..ilibid Leila afanye alchoambiwa bila kuuliza chochote tena maana mama yake alionekana kuwa mwenye hasira

Carry na mama yake walienda hospital na vipimo vilionesha ana mimba kwel ..mama yake alikasirika sana alimpiga Carry ili amtaje mwnye mimba ikiwezekana achukue jukumu la kulea mtoto pamoja na Carry mwenyewe,,Kiukwel Carry hakuwa na jibu juu ya swal la mama yake maana hakujua wap angempata Edward.

Mama yake aliamua kumuacha, Carry alibak analia tu huku akijilaumu kwann alienda kwenye ile sherehe. Huku akiugulia maumivu alienda kutafuta ile notebook ili achukue ile business card amtafute muhusika wa mimba ampe taarifa ..alitafuta sana notebook bila mafanikio aliamuua kuumuliza mdogo wake kama ameichukua
"Leila kuna notebook ilikuwa kule library umeichukua?
"Aah ndiyo dada niliichukua lakin anayo rafik angu"
"Uwiih rafiki yako yupo WAP???kwann ulichukua bila kunambia Leila jamani "Carry alionesha kuchanganyikiwa kabisa
"Lakin dada tangu umalize chuo ulinambia kila kit u kilichopo library naruhusiwa kutumia na kuchukua muda wowote nikitaka "
"Kuna kitu chochote ulikikuta kwenye ile notebook?"
"Mmh kiukwel sikuikagua na nlimuachia rafik yang siku ya graduation yetu aniandikie no yake bahat mbaya nkaisahau kwake"Leila alitoa maelezo yale kwan ni week 3 sasa zmepita tangu amalize kidato cha sita

Carry aliingia ndan huku amechanganyikiwa hakujua afanye nin ila baada ya muda akapata wazo amtafute rafik ake Joan amuulize kuhus yule mtu ....alichukua simu yake ya mkonon na kumpigia Joan

"Joan samahan unamkumbuka yule kaka niliyecheza nae siku ya sherehe yako"Carry alimuulza Joan baada ya salam
"Ndiyo namkumbka ndo shemej nin"Joan aliweka utan huku akicheka

"Stop joking Joan nipo serious naomba no zake kama unazo au naweza kumpata WAP"

"Kiukwel sifaham chochote maan me mwnyew nlimuona Mara ya kwanza siku ile so sijui nkusaidiaje "...Carry alikata simu hakusubir maelezo mengine zaid ,alimfata Leila ili ampeleke kwa huyo rafik ake(Jescar) mwenye ile notebook ..waliongozana had kwa kina Jescar bahat mbaya waliambiwa walishahama tangu siku 3 zilizopita .
.
..........ITAENDELEA .........
 
SEHEMU YA PILI:

Endelea!!.....

"Samahani unaweza kujua walipohamia ?"Carry alimuulza yule jiran aliyewapa taarifa za kuhama kwa kina Jescar
"Wamehamia mtaa wa tatu tu hapo sio mbali sana "
"Naomba unisaidie kaka angu unipeleke kama hutojal"
"Sawa nisubirin dakika mbili nakuja"
"Dada hiyo notebook ina nini mbona unaitafuta sana "Leila alimuuliza Carry baada ya yule Jiran kuingia ndani
"Ina kitu cha muhimu nakihitaj sio lazima ukijue "
"Looh dada bhas me siendi nmechoka narud nyumbani we pelekwa mwenyewe "
"Nitakupiga sasahivi we Leila tena wewe ndo sababu wa haya halafu unaniletea ujinga hapa mfyuuu .."Carry alimsonya na alionesha kuchukizwa sana ,kabla Leila hajajibu chochote yule jiran alirud kisha wakaanza safar ya kuelekea huko kwa kina Jescar ...
"Dada nyumba yenyewe ile paleeee mnaweza mkaenda tu"yule Jiran aliwaonesha kwa mbal hakutaka kufika huko kwasabab kulionekan kuna watu weng nje
"Wap hapo?au ndo pale kwenye watu wengi?"Carry aliuliza
"Eewaaah ndo hapo hapo hujakosea mnaweza kwenda maana nmeacha shughul zangu zinanisubir "
"Asante kaka kwa msaada wako"Carry na Leila walianza kuelekea kwenye nyumba waliyooneshwa huku Leila akiwa amenuna
"We vuta domo hilo ujinunishe lakini sitokwambia urud nyumbani "Carry alianza kumsema mdg wake
"Dada tangu saa 10 tumetoka nyumbani sahivi saa 12 me nmechoka kutembea njaa inauma"
"Mitoto mingine sijui ipoje usindekee mie hapa maan naona unazid kunitibua tu "
"Laah dada jamani"
"Dada dada!heee kwanza sikia nikwambie nenda pale kamuulizie huyo Jescar mim ntakusubir hapa "
"Dada watu wengi me naogopa kwenda "
"Hivi hicho kichwa chako kina nin lakini huon me nkienda ntaleta maswal zaid nna shida gan na yule mtoto,ukirud ntaend kununulia chps sawa ee..Carry aliongezea ili kumbembeleza mdg wake akubal kwenda .Leila aliondoka huku amenuna vilevile japo alipojua atanunuliwa chips akapata na nguv za kutembea
"Shikamoo Bibi"Leila alimsalmia mmoja wa watu waliokuwepo wamekaa nje hakujua kuna kitu gan kinaendlea japo alihis kuna msiba baada ya kusikia watu wakilia kule ndani
"Marahaba mjukuu wangu"alijibu yule bibi kizee
"Poleni kwa msiba Bibi"Leila alitoa pole kiuoga uoga
"Alikuwa mtani wangu sana ,Juzi alikuja nyumbani alionekana mzima na mwenye furaha !leo hayupo jamni !!mtaa unazidi kuishiwa na watu wenye busara ameniacha mpweke sana .bibi kiza ..."yule bibi alianza kutiririka bila kuulizwa alikuwa na uhusiano gani na marehemu na alionekana ana uchungu sana kumpoteza huyo bibi kiza aliyekuwa rafik ake sana
"Pole bibi kazi ya mungu haina makosa "Leila alivuta kumbukumbka Jescar alishawah kumwambia kuhus huyo bibi yake waliyezoea kumuita kiza kwasababu hakuweza kutamka kisa na alipenda sna kulitumia hilo neno kiza hivyo leila alijua kwamba Jescar amefiwa na bibi yake alikaa pale kwa dakika kadhaa kisha akaanza safar ya kurud kwa Carry japo Carry hakuw mbal na hapo
"Notebook iko WAP??" alimuulza Leila maana alivyomuangalia mikonon hakuwa ameshika chchte
"Dada nimekuta kuna msiba "
"Mmmh ndomana watu wamejaa pale ee"
"Ndiyo Jescar amefiwa na bibi yake "
"Umeonana na huyo Jescar umemuuliza kuhus kilichokupeleka?"
""Looh!!Dada huon kilichotokea halafu nianze kumuomba kitu.kisicho na maana""
Carry alimkata jicho LA hasira hilo kisha akaanza kuongoza njia ya kwenda nyumbani .Hadi wanafika kwao ilikuwa mida ya 1:30 usiku walimkuta mama yao akiwa bado kafura na hasira juu ya mimba ya Carry
"Wewe Carry usiniharibie mwanangu kwa kumzururisha usiku na kumpeleka akalete mimba isiyokuwa na baba wala mtu wa kumlea "mama yake Carry alimdaka Carry kwa hayo maneno
"Lakin mama"...
"Mshenz mkubwa wewe ntokee hapa zaa na wa kwako akuite mama ,afadhal baba yako angekuwa hai huenda ungemsikiliza yeye ...nitokee hapa ...""Carry akifukuzw na mama yake,kiukwel alizid kujisikia vibaya juu ya yale maneno ya mama yake isitoshe hakujua anamptaje muhusik wa mimba alienda kujikunyata pembezon mwa kitanda huku akilia sana ..mdogo wake aliingia na kumkuta Cary akilia ,Leila alipata kaz ya kumbembeleza Carry ad aliponyamaza ,walipata wasaa wakuzungumza Carry akamwambia ukwel wote Leila kuhusu hiyo mimba yake..
"Usijal dada nitakusaidia kuipata hiyo notebook na nina Iman card unayoitaka utaipata "Leila alimfarij dada yake na kumuahid kesh yake angeweza kwenda kwenye msiba akajaribu kuona kam atapata chochote .
* ************************************
Asubuh sana Carry aliamka na kuanza kufanya usafi ,Leila aliingia jikon na kuandaa chai kisha kuitenga mezan ,Carry alikuwa wa kwanza kuanza kunywa chai maan usiku hakuweza kula alikuwa na njaa mnoo
"Wewe Carry nimetafuta hela kwa jasho langu ili nile na watoto wangu sijatafuta hela ya kulisha kitoto kisichokuwa na baba ,baba wa huyo mtoto aje hapa ndo unywe hiyo chai" Carry alipewa hayo maneno na mama yake hata kabla hajamaliza nusu chapat ..
"Nimekuelewa mama Nitamleta "
"Sio ntamleta nataka ukamlete sasahivi ,,,hivi we mtoto huko chuo ndo ulifundishwa kubeba mimba isiyokuwa na baba???.....Carry alivyoona maneno ya mama yake yanazd ilibid anyanyuke akakae nje tu huku akiona maisha magum Kutokana na maneno ya mama yake ..aliwaza kwa muda mrefu sana hakupata majibu juu ya maisha yake ,alilia kwa uchungu sana ,kumbe muda wote Leila alikuwa amekaa pemben akimtazama dada yake alimuonea huruma sana ,aliamua kwenda kujiandaa ili aende kwa kina Jescar
*******************""""**********************
Leila alikuta watu weng hakujua kam wameshazika au bado ,alipitiliza ad ndani kwa kina Jescar hakuelewa ni wap alipo Jescar ,alijaribu kuangalia angalia kama ataelewa chochote ila aliona ni vyema kam angeuliza mtu yoyote ,
"Kaka!kaka !"Leila alimuita mkaka mmoja aliyeonekan ana haraka sana ,yule kaka alisimama kumsikiliza
"Hivi hapa wameshazika?Leila alimuuliza
"Hapana bado "yule kaka alijibu
"Je wahusika wa msiba watakuwa chumba kipi et ..?"
"Mimi ni mmoja wao"
"Aah nilikuja kumpa pole Jescar samahn"
"Jescar hayupo wametangulia kijijin tunaenda kuzika huko ,mim ni kaka yake naitwa Edward "
"Ah sawa kaka je mnaondoka saa ngap ?na mim naweza kwenda?"
Kabla hajamjibu Edward aliitwa na mbaba mtu mzima hivyo aliacha kuzungumza na Leila ,lakin Leila akawa amepata mwanga hivyo aliona bora arud nyumban akampe zile taarifa Dada yake .Alimkuta Carry bad amekaa nje alionekan dhaif sana kutokan na kushinda njaa Leila alimuonea hurum alienda kumletea chakula ale kisir sir kbla mam yao hajatoka nje ,Carry alikula harak haraka sana alvyomlz walikaa na kuanza kuongea ,Leila alimuelezea alichokikut huko msiban lakin hakumtajia jina la kaka yake Jescar,Carry alisikitika sana ,alijionea huruma juu ya maisha yake ,hakuwa nakaz wala chochote cha kumuingizia pesa ,na manyanyaso ya mama yake yalimchosha ,
"Dada usiwaze sana utafanikiwa "Leila alimwambia dada yake baad ya kumuona amezama kwenye mawazo sana
"Mdogo wangu mimba Ina week mbil tu lakin mama ananinyanyasa sana huyu mtoto tumbon si kwamba atakula chakula akakimlza ila mama anachonifanyia ..kabla hajamaliza kuongea mam yake alitokea
"Eeh we mjinga nmekusikia kila kitu nkwambia na bado bila kumleta huyo mwnye mimba uondoke kwangu,sijakulea uje uniabishe kias hichi,"
"Mama ...?"Leila alimuita mama yake
"Nilishasema sitak ujinga nyumban kwangu "kisha akaondoka zake ...
Carry aliamua kuondoka akatembee tembee apunguze mawazo ,akati yupo njian alipata wazo aende kule msiban ,....
Baad ya nusu saa tu alifika pale msiban bahat mbaya au nzur alikuta watu wakijiandaa kusafirisha msiba,na watu wengi walionekan Kutaka kwenda huko kijijin kuzika ,hakujifikiria mara mbili aliona ni bora aende na yeye maana hakuwa tayr kurud kwao kupokea yale maneno ya mama yake ,alipanda ndan ya gar,baada ya kuona watu wanaanza kuingia kwenye gar kuelkea kijijin .Kiukwel Carry alionekana mwenye mawazo sana na alinyong'onyea Kupita kias ,Japo wengi wao walidhan ana mawazo kwasabab ya msiba .Ila wakat amekaa ndan ya gar akisubir safar ianze alishangaa kumuona mtu kama Edward ,alishuka kwenye gari haraka haraka ili amuwah yule mtu bahat mbaya hakuweza kumuona alikuw ameshajichanganya na watu wengine hivyo haikuwa rahis kumuona tena .
,wakat anaangaza angaza huku na kule kumtafta mtu alyehisi ni Edward ,alishtuka kuguswa bega na mtu ,aligeuka nyuma harak kumuona ni nan alyemgusa
"Samahan dada kuna kitu unatafuta ?"alimuuliza huyo kijana aliyemgusa Carry began
"Hapana, hakuna kitu"Carry Alijibu huku akiwa na waswas
"Nimekuona muda mrefu unahangaika nkahis unahitaj chochote nkusaidie "
"Kuna mtu tu nlimfananisha usijal "
"Oukey me naitwa Alex ,nngependa tufahamiane zaid" alijitambulisha yule kaka
"Sio muda sahihi wa kufahamiana huon tupo msiban?"kisha Carry alipanda ndan ya gar ,baad ya muda kidogo walianza kuimba nyimba za msiba na safar ya kwenda kuzika kijijin ilianza .Carry alijiinamia tu alikuwa anawaza juu ya mtu alyemuona hakuwa na uhakika ni Edward mwenyw au alimfananisha,pia hakuelewa huko kijijin haswa anafata nini maana haikuwa rahis kupata kile anachokitafuta .

ITAENDELEA ......
 
SEHEMU YA TATU;


Mida ya saa 9 hiv walifika huko kijijin ,Carry alianza kujiskia vibaya hivyo alikaa pemben kabisa ,alijitenga na watu wala hakuhudhuria makaburin,masikn Carry hakujua kaka yake Jescar ,ndye Edward amtafutaye na vile tu amejitenga na huku Edward alisimama kutoa muongoz mfup baada ya mazish yale nini kitafuata kwaniaba ya mama yake na baba yake ,hivy ikawa bahat mbaya kwa Carry kutokumuona Edward kwa wakt ule ,Carry alipokuw amekaa kule alianza kujckia kichefuchef alitapika sana,isitoshe hakula kwa muda mref hvyo alikosa nguvu ata za kunyanyuka pale alipokuwa amekaa alianz kujihis kiznguzungu .

**************************************************
Carry alishtuka yupo kitandan huku kichwa kikimuuma sana ,hakuelewa yupo wap alijarb kujiinua pale kitandan lakin hakuwa na nguv ,baada ya muda kidogo aliingia Alex akiwa ameshika mfuko wa chips mkononi ,Carry alishtuka kumuona Alex mbele yake

"Usiogope mrembo upo salama "Alex alimwambia Carry
"Nimefikaje hapa kwann nipo na wewe?"
"Tulia kwanza hal yako si nzur hutakiw kupanic ,ntakuelezea kila kitu usijal ,kula kwanza "
"Siwezi nahitaj kuujua ukwel kwanza "
"Ok ,kama nlivyojitambulisha tangu mwanzo ,mim ni Alex ,nlvyokuona pale msiban nliendelea kukufatilia tartb ,had tunafika kule kjijin nlikuwa nakufatilia ,ndipo nlpokukuta umeanguka na umepoteza faham nlkuchukua nkakupandisha kwenye gar yang ,nkakuleta mjin ,nkaona ni vyema nkufkishe nyumbn kwangu kwanza .
"Ooh Asante sana Alex kwa msaada wako "
"Usijal Lkn ingekuwa vzr kam nngekutambua hata jina lako maan ulikataa kabisa kuntajia"
"Naitwa Carry"Carry alijib kwa aib maan alimtelea nyodo ila ndo mtu pekee aliyeweza kumsaidia ,alipewa chakula akala ,alivyoangalia saa ilikuwa saa 4:30 hivyo haikuw rahis yeye kuondoka usiku huo kwenda nyumban kwao ilimbd alale palepale .
Asubh aliamka ila alikutana na ujumbe kutoka kwa mama yake,kwamba amelala nje hivyo hakutakiwa kabisa kurud nyumban ,Carry alinyong'onyea hakujua ataenda wap ,Alex Alibisha hod kisha akaingia chumban kwa Carry baada ya kukaribishwa ,alimjulia hal Carry na kumuulza atatumia vitafunwa gan,Carry alijibu atakula chochote ,hivyo Alex alitoka kwenda kuandaa chai ,muda huo Carry aliutumia kufikiria atamuombaje Alex aweze kubak pale hata kwa siku kadhaa ,baada ya muda Alex alirud alimtaka Carry akaoge kisha aje kunywa chai Carry alifanya hivyo na baada ya muda wote walikuwa mezan ,Carry alishangaa ukubwa wa ile nyumba isitoshe Alex Alionekana ni kijana mdogo tu ,isingekuwa rahis kuwa na utajiri
"Hivi unaish na nan hapa?"Carry alivunja ukimya na kuamua kumuuliza Alex
"Naish peke ang,kwanini umeuliza hivyo,?"
"Amna nimeshangaa tu kuona nyumba kubwa halafu sion watu"
"Labda niishi na mrembo Carry "Alex aliongea huku akitabsam
"Mmmh ,wifi yangu yupo wap?"
"Hauna WiFi Carry ,n hivi unaish wap,una umr gan?,n una mishe gan?"
"Nna miaka 24 ,naish...kabla hajamaliza kuongea Carry alijihis kichechef alikimbia nje kutapika ,Alex alimfata na kumhudumia baad ya muda alimrudisha ndan kupumzka ,Carry alimuomba Alex aondke lkn Alex alisisitiza asubir apone kisha atamruhus kuondoka ,Carry hakumuweka waz Alex kam ni mjamzto hivyo alikaa kimya tu ili akae pale kwa siku kadhaa kabla Anapanga mikakat ya maisha yake.
*************************************************
Baada ya week mbili ,Carry alishazoea kukaa na Alex na walizoeana sana ,waliish kam kaka na dada ,Alex hakuwah kumtamkia Carry kam anampenda au la.
Siku hiyo mida ya saa 11 jion,Carry aliamua kwenda chumban kwa Alex kupekua pekua ajue Alex anafanya kaz gan maana alijaribu sana kumuuliza lakin hakuambiwa chochote .Alifungua droo za kabat ya nguo hakuona chochote cha tofaut ,alikagua sana lakn hakuambulia chochot ,ila alishtuka baada ya kuinua godoro ,alikuta bastola pamoja na pakt mbili za madawa ya kulevya alitamani kupiga kelele ila hakuwez kupiga kelele maana Alex alikuwa ameshafika na alikuwa kasimana mlangon akimtazama Carry.
"Unatafuta nini Carey ?"Alex alimuuliza kwa jazba sana huku akiwa amemshika Carry mkono wake
"Naomba unisamehe Alex ,amna nachokitfuta "Carry alijibu huku akilia kuomba msamaha
"Sijaweka mpelelez nyumban kwangu ,nlikusaidia tu Ila sikutegmea ungefanya ujinga wa namna hii,"kisha akamnasa kibao Carry akaangukia kitandan
"Nisamehe Alex "
"Nan amekutuma ufatilie maisha yang ?,sema haraka kabla cjakupasua hicho kichwa chako
Carry alijitetea sana lakin Alex hakuweza kumsikiliza ,Alex alianza kutoa mkanda wa surual ,kisha alimfata Carry pale kitandan na kutaka kumbaka ,
"Nisamehe Alex sitorudia tena ,usinfanyie unyama kama huu ,Alex nina mimba mim usinfnyie ukatil "Carry alizid kujitetea na kuhangaika kujinasua kwa Alex
"Ooh ,mwenye mimba ndo mzur ,hiv wewe malaya eee ,yan kumbe nimekusaidia wewe na hicho kijus tumbon halafu unanletea ujinga hapa,sasa leo utanjua sura yang halisi"Alex alimchania gaun Carry ,alibak uch ,hiyo ilizidisha matamanio kwa Alex na kuzid Kutaka kumbaka Carry ,Carry alipiga kelele sana Ila kutokana na ukubwa wa nyumba isingekuw rahis mtu yoyote kusikia zile kelele ,ila kabla Alex hajatimiza anachokitaka alisikia mtu akimuita seblen hvy alimuachia Carry na kujiweka vizur kisha alitoka seblen ,kwenda kuangalia ni nan anayemuita

"Ooh ,Edward karbu mshikaj "Alex alimkarbisha Eddy baada ya kumkuta seblen akimsubir
"Dah!mwanangu nmegonga sana nkaamua kuingia moja kwa moja ndan,halafu nmeingia ndan nakuita unankaushia"Edward alilalamika kwa Alex
"Nipo ndan na shemej yako nilikuw nmelala bhn"
"Mlete mke wetu ,nimuone bhasi "Edward aliweka utan ,lakin Alex aligoma kabisa,maan hakutakaEdward ajue kinachoendelea
"Sawa bhan nibanie kumuona shemej,but anyway me nimekuja kukuona maana tangu uondoke siku ile kwenye msiba gafla gafla hatujaonana tena ,"
"Aah siunajua majukum ,yan nilikuwa bize kwel ,nisamehe kwnza kwa kutokukaa had mwisho wa msiba"
"Usijal ,kila kitu kimeenda sawa na week ijayo nampeleka dogo South Africa Mzee kamtaftia chuo huko "
"Uende ukapate watoto wazur huko,maan wabongo wanazingua sikuhizi "
"Acha mambo yako Alex ,me kuna mwanamke nampenda ,nmempa no yang anitafute lakin mpka leo hajanitafuta ,mwez sasa umepita naona kimya tu,Alex alianza kumcheka Edward ,Ila kabla maongez yao hayajaendlea simu ya Edward iliita ,na alikuw mama yake Alimtaka aende nyumban .
Kumbe muda wanazungumza Carry alikuwa kajibanza anawasilikiza hakujua tena kama Alex yupo na Edward anayemtaka yeye,alikuwa ameshavaa nguo zingine ,alishika viatu mkonon,.Alex alvyotoka kumsindikiza Edward, Carry alitumia huo upenyo kutoka nje kupitia mlango wa nyuma .
Bahat ilkuwa kwake alifanikiwa kutoroka kutoka kwenye mikon ya Alex ,ila tatz hakujua aelekee wap aliwaza sana ila aliona afadhal ajitoe ufaham aende nyumban kwao ,maan hakuw na sehem nyngn ya kwenda .
Alifika nyumban kwao mida ya saa 3 kasoro aligonga mlango ,baada ya muda Leila alimfungulia mlango ,alifurah sana kumuona Dada yake maan hawakuonana muda mref ,kisha alimkarbisha ndan ,muda huo mama yao alikuwa amesindikiza wagen ila baada ya dk 5 aliingia mama mwenye nyumba na kumkuta Carry akiwa amekaa pale seblen na Leila
"Mbona upo peke yako?mjinga mwenzako yupo wap?"Carry alidakwa n hayo maswal kutoka kwa mama yake
"Shikamoo mama "badala ya kumjibu swal Carry aliona ni vyema akamsalmia kwanza
"Shika na ya kwako ,hiyo salam ingekuwa ya muhimu sana ingemleta mwenye hiyo mimba,nachokitaka ni majibu ya maswal yang tu "
"Lakin mama ungesubir nijieleze yaliyonitokea kwanza"
"Unieleze nin mjinga wewe ,kam hujaja na huyo mwanaume uondoke kwang sasahv nkifumba macho nkifumbua urud uko uko ulipotoka "Carry hakuwa na jinsi ilibd anyanyuke tu aanze kuondka ,Leila alimuonea huruma sana dada yake Ila hakuw na namna ya kumsaidia ,ila alimfata kabla hajafika mbal ,akampatia noti ya shilling elfu 10 ,ili imsaidie mbele ya safar ,Carry alilia sana alijiona kam ni yatima ,hakutegemea kam mama yake angemfukuza usiku ule .


ITAENDELEA .........
 
SEHEMU YA NNE :,

Bhs bhana Carry aliamua kwenda kwa Joan ,aligonga mlango kam mara 3 ndipo Joan alifungua mlango ,
"Ooh karibu mpenz ,mbona usiku usiku hiv hata bila taarifa ,"Joan alianza maswal hata kbla hajamkarbisha ndan
"Shoga angu hata bila salam?"
"Ujio wako umenishangaza ,saa 5 hii kwema kwel?"
"Jaman Joan ,tutaongea vizur nkaribishe kwanza npumzke ntakueleza tu "
" ndan huwez kuingia nipo na shemej yako "
"Joan mwenzio sina hata pa kulala nljua kwako ntapata msaada"
"Msaada??msaada gan unautaka halafu vip si una kwenu wewe umeshindwa nin kulala huko".
"Joan nina matatizo nsaidie mwenzio "...
"Joan mlete alale kwangu tu me nipo mwenyewe leo ,"mpangaj mwenzake na Joan aliingilia yale maongez
"Husna una uhakika na unachokisema lakin?"Joan alimjibu Husna kwa swal
"we mlete bhn we ,kaendendelee na mamb yako tutaonana asubuh ,kuhus huyu niache mim.muda wote huo Carry alikuwa amekaa kmya tu hakuelew chochote ila alichokuwa anakitaka apate sehemu ya kujiegesha tu kwa usiku ule,alichukuliwa na Husna wakaingia chumban kwake ,Husna alimchangmkia Carry utadhan alkuwa anamjua siku nying ,alipewa chakula alivyomaliza kula aliamua kujipumzisha .
Alishtuka saa 3 asubh alijikuta yupo peke ake chumban ,aliamka akatandika Kitanda vizur ,kisha akatoka nje,alimkuta Husna anafua
"Za asubh dada "Carry alimsalmia Husna
"Salama tu mdg wang ,umeamkaje "
"Salama tu dada sijui ww"
"Salama tu ,naona jana ulikuwa umechoka sana had ukalal na nguo zako ulizovaa "
"Ee dada nilikuw nmechoka sana ila kidogo sahiv uchovu umepungua "
"Mwenzetu naona ndo unaamka "Joan alfika
"Umetoka wap huko Joan"Carry alimuulz
"Nmetoka kumsindikiza mgen wang ,vp kwan"
"Rafiki angu hujaach tu tabia yako ya ukorof "
"Shoga ang maisha yenyew ndo haya niwe mpole ili iweje ?",eb kwanza nieleze yaliyokukuta maan umekuja kuleta mzg kwa watu.Carry alishusha pumz kwnza ila aliamua kuwaeleza ukwel tu ,yaliyomtokea Husna aliskitika na kumpa pole ,
"Sikia Carry nkwambie ,kwangu ntakukaribisha tutakaa wote hapa ila sitak uwe mzgo kwang ,sio mim Joan natok kuhangaika uko mwenzang uje kula tu na hicho kijus chako ,kwanza mimba yako ina mda gan vile "
"Inaelekea miez miwil sasa"
"Oh vizur kumbe unawez kufanya kaz kabisa,me nachotaka ujishughulishe sawa"
"Nimekuelewa Joan ",waliendlea endlea kupiga story badae Joan aliaga anatoka ,Carry alibak na Husna ,ndipo Carry alitumia huo muda kumwomba Husna amsaidie kutafuta kitu cha kufanya
"Mdogo wang labda nkuunganishie napofanyia kaz mim kam utahitaj"
"Kaz gan dada,mim yoyote ntafanya tu"
"Kuna lodge hapo mtaa wa pil si mbal na hapa huwa nafanya usaf pale na kufua mashuka ,kama utaweza nawez nkakuunganishia "
"Carry alijifkria sana kuhus hiyo kaz ila aliona ni bora akubal tu kufanya kaz ilmrad Joan asije akamfukuza kbla hajajipanga kwa chochote .
Asubuh aliamka mapema ,alijiandaa walitoka na Husna had Golden Lodge ,walimkuta boss ,Husna alimtambulisha Carry kam mdogo wake,Yule boss alimkubal Carry aanze kufanya kaz pale .


*************************************************
Leila alikuwa anaenda sokon,bahat nzur wakati yupo njian alikutana na Jescar,Jescar alikuw wa kwanza kumuona Leila
"Leila jaman mbona upo busy hivo hugeuk hata pemben "
"Nina mawazo acha tu hata sijakuona kabisa,vip lakin mzima wewe,za masiku ?"
"Salama tu nlipata msiba ndomana nlishindwa kabisa kukutafuta"
"Nilisikia kuhusu msiba ,na afadhal hata nimekuona vip notebook nlyokupa unayo?
"Ninayo dear ipo nyumban "
"Naomba twende ukanipe yan ni ya muhimu sana"
"Nilikuwa nafata tiket ya ndege kesho kutwa naondoka naelekea south Afrika,ila twende tu nyumban nkakupe kwanza halafu ntaenda huko ,
"Nashukur sana jamn utakuw umenisaidia sana
"Mbona unaonekan una haraka hv Leila "
"Aah twende tu kwnz ukanipe nachokitak mengine tutaongea tu ",..Walianza safar ya kwenda kwa kina Jescar ,walifika lakini Leila aligoma kuingia ndan alimsubir nje .
Jescar alikutana na kaka ake Edward akiwa race anawah kutoka nje ,
"We Jesar umeshika nn mkonon "
"Notebook ya rafik angu nampelekea yupo hapo nje"
"Ebu niione ...kabla hajaangalia simu yake iliita hivyo aliondoka ,Jescar alitoka nje na kumpa ile notebook Leila ,Kitu cha kwanza Leila aliangalia bussiness card aliiona na alifurah kwel alimuaga Jescar harakharak ili akampe taarifa dada ake .
*************************************************
Carry akiwa kazin anafanya usaf ,alisikia simu yake ikiita mpigaj alikuwa ni mdogo wake ,aliipokea ile simu haraka ,
"Da Carrie nna good news "leila aliend direct hakuanz hat na salam
"Mmmh heb nipe na mim nzsikie "
"Guess zinahusu nin kwanza"
"Nahis mama atakuwa amekubal nrud nyumban "
"Umekosa ...bt soon utakuw na furah dada ni hv nimeipata ile card unayoitafuta"
"Woow kwel Leila ?unayo hapo?"
"Ndiyo ninayo dada "
"Sikia me nakutumia msg nkuelekez nilipo halaf unletee"
"Sawa dada ",Leila alikata cm alisbr maelekez ,haikuchukua muda msg iliingiia ,alielekezwa pale kazin kwa Carrie ,Leila hakupoteza muda alichukua kibag chake kdg cha mgongon aliiweka ile notebook ikiwa na Card ndan yake ,alifika barabran alipanda bajaj lakin anapoelekea kulkuw kuna kaumbal kidgo hv aliweka pemben kibag chake halaf yeye akalala .
"Sister umeshafka "Leila alishtuliwa na saut ya dereva bajaj
"Aah nilipitiw na usingz ,kumbe ndo mbal hiv ,ila asante kaka ,kisha Leila alianza kuondoka kwasabab naul alishamlipa hv haikuw na haja ya kuendlez mazungumzo .Alifika Golden lodge alimkuta dada yake akimsubr ,walipokean kwa furah tu na baad ya salam ,Leila anagundua kasahau kibeg chake kwenye bajaj
"Dada nmesahau bag lang kweny bajj ndo lina kila kitu"
"We Leila wewe acha masihara kwenye vitu kam HIV"
"Me sitanii kwel da Carry nmesahau bag lang hata naul ya krudia nyumbn sina na sim yang nmeisahau "
"Hiv Leila unawezaje kusau kitu kam hcho au ulikuw unandangnya Ley?"
"Dada sijakudangnya nakwambia ukwel niamn"
"Chukua naul hii hapa nenda nyumban "
"Dada lakin usikasirike "
"Nenda tu Ley "Carry alikuw kachukia alihis mdg wake alikuw anamtania alimrudishia ile ile elf kum aliyompag maan hakuw na hela yyt zaid ya hiyo ,Leila aliichukua kinyonge na kuanz kuondoka .

*******************
Mimba ya Carry haikuw inaonekana ,na ilimpenda haswa ,alizid kuonekan mremb tu na umbo lake zur lilionekana japo alikuw na maisha magum kwa wakt ule alijitahid kufanya kaz kwa bidiii ili apate hela japo kwa siku alkuwa analipwa 7000,kila siku kwa Joan alikuwa anatoa 3000 kwaajil ya chakula.Siku Hiy Carry alirud amechoka balaa ,alimkuta Joan anamsbr mlangon ,
"Vp mbn umekaa mlangon usiku huu kuna nin"
"Nimekaa nakusubir wewe Carry"
"Mmmh unantisha ,enhe nambie"
"Carry leo nna mgen ,hauwez kulala hapa leo"
"Joan jamn ungenambia mapema sahv uck huu naenda wap"
"Shoga ang me sijui we angalia ustaarb mwngn me namchelewesha mgen wang,tutaonan asbh bhc,halafu hilo swal la kwenda wap sio LA kwang.. .Joan aliingia ndan na kufunga mlango na funguo Carry alienda kugonga mlango wa Husna .
"Da Husna samahn kwa usumbuf"
"Bila samahan mdogo wang "
" Naomba unisaidie hifadh nilale kwa leo tu Joan ana mgen ,na hakunipa taarif Mapema".
"Mmmh ,Jamn kwnn Joan kakufnyia hv"
"Ata sielew dada ,naona ameshanichoka"
"Nataman nkusaidie lakin na mim leo npo na shemej yako"siku zote Carry alijua Husna hakuw na mume kwasabab umr wake ulishaenda japo alikuwa anajiweka aonekane kama msichan ,Carry hakusubr hata cha ziada alianza kuondoka tu huku amenyong'onyea hatare .Aliona ni kher arud kule anapofanyia kaz lbda atapata hata hifadh ,bahat nzur anafka anakutan na boss wake anatoka na gar ,boss alivyomuona Carry alisimamisha gar akamuita Carry .
Carry alianz kupiga hatua taratib kuelekea alipo boss wake ,muda wote huo boss mtu alimuangalia Carry kwa macho ya matamanio ,mwendo wake wa madaha na umbo lake no 8 lilionekan vizur licha ya kuvaa dela ,hiyo ilizdsha matamanio kwa boss wake japo alimuangalia kwa nje tu
"Shikamoo boss "Carry alimsalimia boss wake ,kwasabab umr wake ulkuw umeenda na alionekana atakuw na watoto wakubwa tu
"Carry unataka kuninyima nin had unipe hiyo salam"
"Amna boss samahan"
"Halafu me naitwa Derick hiyo Boss iweke pemben"
"Mmhmmh"
"Hiyo miguno sasa,mwenzako hoi huku ,"
"Boss bhna ,Carry alitabsam na dimpoz zake zilionekan vzr ,
"Woow nimependa hayo mashimo kweny mashav yak,bt naomba upande kwenye gar tukakae sehem tuongee kidogo "
"Usiku sahv boss me siwez kwenda na wewe popote"
"Unaogopa nin Carry "
"Namuogopa mkeo"
"Nan kakwambia mim nimeoa "
"Na uzee huo hujao?????"
"Achan na hayo bhan we ingia kwenye gar twende"
Carry wala hakukataa tena maan aliona ni afadhal aende huko akapoteze mawazo isitoshe hakuwa na sehemu hata ya kulala.

ITAENDELEA !..........
 
shukran,endelea basi kushusha vitu
 
SEHEMU YA TANO :;

Moja kwa moja Carry na boss wake Derick walienda hoteln ,watu weng walionekana kuwashangaa Derrick na Carry na wengine walicheka Carry hakuelewa wanacheka nin aliwapuuzia tu ,aliangalia kilichowapeleka pale ,kwanza walipochagua meza ya kukaa ,Derick alimvutia Carry kit na kumkaribisha kwa manjonjo akae
"Karibu ukae malkia wang"
"Mmmh boss kwann unafanya hiv ,inakuwa kam nmekudharau na kukuvunjia heshima "
"No Carey ucjal halafu nilkwambia uniite Derrick sio boss plz "
"OK Derrick "
"So ungependa kula chakula gan mpnz ,na kinywaj gan?"
"Mmh mpnz tena tang lin jamn nkawa mpnz wako"
"Una maswal wewe agiza kwanza chakula mengn tutazungumza "
"Nakula chochot tu utakachoagiza wewe"muhudum aliitwa na Derrick alimuagiza chips ,kuku mzima na glass mbil za mvinyo ,chakul kililetwa kwa wakat ,hivy walianz kula huku wakipiga story za hapa na pale
"Carry kwhy umesem una degree ya biashara?
"Ndiyo ,baht mbaya sijabahtik kupata kaz"
"Usijal muhim umeshakutan na mim kila kitu kitakuw sawa"
"Kwel boss????"carry hakuamin alichokisikia
"Carry ukiniita boss me nitakasirika sasa ,"
"Samahan najisahau tu"
Bhc waliendlea na mazungmz huk Derrick akimuahd kumtftia kaz ,walivyomaliza kula ndipo Derrick akata kumrudisha carry nyumbn Ila sasa tatizo kwa Carry hakuwa na sehem ya kwenda kulala ilabid atumie uongo
"Unajua sahv muda umeshaenda hata nkienda nyumban hawatonfungulia mlango "
"Jaman bhas twende ukalale kwangu asubuh ntakurudisha nyumban kam hutojal ,be free kwang nakaa peke ang sijaoa ,Carry alijidai kukakataa kataa lakin mwisho alikubal .Hao walipanda kwenye gar had nyumban kwa derrick ,walivyofika kwel hakukuwa na mtu yoyote kulikuw kimyaaa haswaaaa ,Derrick alijarib kumtoa waswas asiogope ,kisha alimuonesha chumba chake atakacholala wakaagan wataonan asubuh ,...Lakin baada ya nusu saa ,Carry alisikia mlango wake ukigongwa ,alijua atakuwa ni Mr derick hivyo alifungua mlango kidog tu alichungulia aonekane sura bhc ..
"Samahan unawez ukanruhus kuingia ndan"
"Lakin Derrick nlishajiandaa kulala na siwez kukuruhus kuingia ndan".
"Kwanin nisiingie Carry!"
"Kwasabab sijavaa but sorry"muda huo Carry alikuw kafunga taulo tu
"Aah usijal kuna issue natka unisaidie mara moja ukishansaidia me natoka nkuache upumzike "
Carry alijifkria ila aliona amkarbishe tu ndan kwasabab mwenye nyumba kashasema ,japo muda huo alikuw kavaa kitaulo kifup tu mapaja yote nje na mzgo huku nyuma ulionekan vizur ,Mzee wa watu macho yalizid kumtoka ,mate yalmtoka utadhan mbwa kaona fupa la nyama ,moja kwa moja alienda kukaa kitandan na kumuita Carry aliyekuwa bado amesimama ,Carry alijisogez Kitandan akakaa mbal kabisa na Mzee ,lakin huyu Mzee asiyekuw na stara alimsogelea karb na kuanza kung'atang'ata maneno
"Unajua nin Carry "
"Sijui kitu".
"We ni mzur Sana"
"Nalitambua hilo"Carey alimjib short ilmrad asiendlee kuongea vitu vya kijinga
"Rang yako ya chocolate imenivutia sana "..alianza kupeleka mkono wake kwenye mapaja ya Carry ,Carry alishtuka na alichukia sana alimtoa ule mkono na alienda kusimam mbal na Derrick ,Mzee alivyoona hivyo alisimama na kumfata Carry na kusema direct anachokitaka
"Carry sitak kuzunguk sana naamin ushanielewa nachokitaka,wewe sio mtoto "
"Lakin wewe ni kama baba yang "
"Kama baba yako lakin mim sio baba yako wala siwez kuwa na bint kam wewe sijazeek kias hicho"
"Looh!!mzee wewe na mvi zote hzo bado unakataa tu?"
"Mvi kitu gan ,we nipe uone kam ntashndw kufunga magol"
"Me sitak na siwez ".
"Hahaha !kwang lazima utake tu kwa lazima "alimshika Carry ili afanye nae kwa lazima ,Carry aliona akipiga kelele hapo hakun atakayemsaidia ilibd acheze na akil ya huyu mzee
"Aah jaman vitu vizur havitak kulazimishana ".
"Inabid tulazimishe wakat mwingine maan hutak kunipa"
"Sikia nkwambie Derrick ,unajua hata mim nilikuw nataka ila nilitaka tu kujua je unatak kwel au unantania"muda huo Carry alizungumza nae huku anamchezea chezea kifua japo alikuwa amevaa vest tu ,alikuw mara aivute huku mara ashike ndevu ,yote hayo yalimpagawisha mzee wa watu akil ikamruka akabak amezuba tu asijue aseme nin aliishia kushika kiuno cha Carry tu Ila Carry alijitahd kumtoa mikon yake kwa akil sana ,

"Mpenz naomba tufnye kesho leo nimechoka sana plz "Carry Alijitahd kubana saut na kudeka kidogo ,huku amemlalia kifuan maan Mzee alikuw amemzd uref kidog
"No Carey I can't wait ,me nataka leo"
"Me natak nkuburudishe ufurah na uenjoy kuwa na mim so ukitak leo hutonfaid,vizur kam ikiwa kesh itakuwa vizur zaid"Carry alizd kushusha maneno pale ad mzee akaelewa somo maana Alishachanganyikiwa na hiyo mipapaso ya Carry ,hivyo alikubal kuondoka kwenda chumban kwake ,alivyotoka tu Carry alifunga mlango na ufunguo ,alikaa kitandan akaanz kulia ,alifikiria ana mikos gan kwenye maisha yake maan kila akipata msaada lazima aulipie hawez kusaidiwa bure ,alilia sana mwsh alipitiwa usingiz akalala.

**************************************************
Asubuh alishtuka mida ya saa 4 hiv ,alipitiliza kuoga maan bafu lilikuw humo humo ,baada ya kuoga alirudishia dela lake ,kisha akatoka had seblen alimkuta Derrick akiangalia runinga ,
"Ooh vip malkia wang umeamkaje "
"Salama tu hunie hof kwako"
"Me nmeamka na arosto zang mamii jana ulinibania leo nlkuwa nakusbr kwa ham kwel"
"Jaman me ni wako tu ,sahiv bado mapema sana ,kwanza ungeenda kazin mengne baadae "
"Mtoto wewe jamn Unankosha kwel haya bhc me naenda kazin Ila nkirud usitoe sabab yoyote "
"Ukirud ni mwendo wa kula raha tu"
"Jamn Nitawah kurud kwaajil yako,halafu chukua hela hiyo apo ukafanye shopping ununue nguo maana jana kule hotelin wat walicheka ulivyovaa,so nataka uendane na hadh yang ,lazima nkupendezeshe mrembo ,"
"Jamn asante sana mpnz sitokuabishan tena",Mr Derrick alimuaga anatoka sasa kisha wakaagan kwa mabusu ila si kwamba Carry alikuw anafurahia ila alifanya kumridhisha tu huyu mzee .
Alivyotoka Carry alihesabu zile hela.alikuta shiling million mbil ,alifurah sana hivy hakupoteza muda alizificha kwenye maziwa kisha akaondoka zake akaanglie ustaarbu mwingne.Hakutaka kurud kwa Joan maana alijua fika akirud kule Mzee derrick atamfata tu .
 
SEHEMU YA SITA ;

Carry aliamua kwend mtaa mwingne kabisa ambapo watu hawamjui wala si rahis kwa Boss wake kumpata ,Alitafuta lodge ya bei rahis apumzike kwanza baada ya hapo akatafute chumba apange .
Mida ya mchana aliamua kutoka nje akatfute chumba ,baht nzur hakufika hata mbal aliona bango limeandikwa no za dalali alizichukua zile no Kisha aliwasilian na dalali aliyefahamika kwa jina la Naseeb ,alimuahd chumba atapata na baada ya siku moja tu kila kitu kitakuwa sawa .
Kwel kesh yake asubuh Musa alimpigia simu Carry na kumjulisha chumba kipo akakiangalie kam ataridhika nacho akilipie .Carry hakupoteza muda alianz safar kuelekea huko alipoambiwa amepata chumba .Alivyofika maeneo hayo Naseeb almwambia amsubr barabrn ye atamfata
"Mambo Carry "
"Pw tu"Carry aligeuka nyum na kupokea salam ilyotoka nyuma ya mgongo wake
"Naitwa naseeb,ndo dalal ulyekuw unawasiliana nae"
"Mmmh umenjujae wakt hujawah kuniona"
"Nimekuona dp whatsup,ndomaan sijapata shida kukufaham "
"Mmmh ,haya hongera "
"Ok twende ukaone chumba chenyew lakin naamin utakipenda "
"Lakin nlkwambia usintftie chumba cha bei ghal "
"Usijal nimelizingatia hilo Carry ".Walifika had kweny hicho chumba ,Carry alikipenda na alkuw tayr kukilipia kwasab mazingr pia yalkuw rafik ,nyumba ilikuw na wapangaj wawil na yeye akiongezeka wanakuw watatu,.Kod ilikuw elf 30 kwa mwez hivyo alimwambia Naseeb atalipia miez mi3 .
"Kwhy madam upo tayar kuhamia lin"
"Mimi leo leo nahamia hapa "
"Ooh kam utahitaj kirikuu cha kukubebea vitu vyak ,kun jamaa namfahm anawez kukubebea kwa bei rahis tu "
"Yan sina kitu hata kimoja cha kubeba "
"Mmh kwahiyo unakuj kukaa hivhv?
"Hapana hapa ndo natak niende mjin nkanunue vitu,"
"Ooh bhas nawez nkakusindikiza kam hutojal au unaend na shemej "
"Mmh amna Ila ntashukur sana ukinsaidia ,..Hao walichukuan had mjin Naseeb ndo alikuw akimuongoz Carry ,hivy carry alisem anachotaka then naseeb anampeleka sehem husika ,.Walinunua Kitanda na godor lake ,mashuka,pazia ,jiko la gas ,vyomb vichache tu ,zulia pamoja na nguo mbil tatu maan nguo zake aliacha nyumban kwao .Had wanamaliz shopping ilikuw jion kabisa na giza lilianz kuingia
"Unaonaje hiv vitu tukavipeleka kesh maan sahv kuhamia usiku utashindw kuvipanga ,isitoshe haujafanya usaf kwenye chumba "
"No naseeb lazim nihamie leo leo kam unawah kwako ,we nenda tu me ntamlizia kila kitu mwenyew"
"Sijamaanisha hivyo madam ,nimejarib kutoa wazo tu ,but ok tufanye hv we sahiv nenda ukafanye usaf then mim nawasilian na yule jamaa wa kirikuu tuanze kupakia vitu had umalize kufanya usaf si tutkuw tumeshafika hapo "
"Asante sana Naseeb ,sikutegemea kam ungekuwa tayr kunsaidia kias hichi"
"Usijal mamii we nenda tumalize hil utanshukuru badae ".Carry aliondoka had kule chumba chake kilipo ,alimkuta jiran yake mmoja yupo nje ,alimsalmia vizur kisha akamuomba ndoo ya kudekia na dekio ,maj yalikuw yanatoka bomban,yule dada aliingia ndan na kumpatia vitu alvyoomba .wakt Carry anadek yule dada alimfata huko chumban kwake
""Shoga mbona hujanambia unaitwa nan "
"Naitwa Carry "
"Me naitwa Mamuu ,shoga angu nmekuja kukwambia ukae mbal na huy mam chumba cha jiran ,hapo yan ni mmbea mtaa mzima kashindikana ,ukijiloga tu kuweka nae ushoga utaumia ,tena hatochelewa kusem unatembea na mume wake ,kuwa makin shoga ohoooo yang hayo tu kwaher,Carry alichoka maan mtu anaongea utadhan kameza kanda ya redio hapo hajajibiw ila katiririka kila kitu .Carry hakutilia maanan aliendlea kufanya usaf ,alvyomaliza alimjulisha Naseeb il walete vitu .
Baada ya nusu saa Naseeb alifika na vile vitu ,walisaidian kushusha na yule dereva baada ya kumaliza dereva aliondoka na kumuacha Naseeb anamsaidia Carry kupanga vitu ndan
"Halafu nilisahau kununua ndoo itabid kesh niende mjin "
"Usijal madam me asubh ntakuletea najua kwa hil varangat lazim utaamka umechoka "
"Nichoke na nin jaman sijafnya kaz yoyote ya maan ,wakuchoka ni wewe bhna"
"Tangu lin mwanaume akachoka mbele ya malkia kama wewe"
"Acha utan wako bhana "walicheka kisha wakaendlea kupanga vitu had wanamaliza ilikuwa saa 6 usiku ndo kila kitu kilikuwa kimekaa sawa
"Sasa mama mim nkuache upumzike na mim nkapumzke"
"Usiku wote huu utaweza kwend kwel?
"Nitawez usijal madame"
"Sijui nkushukuru vip Naseeb maan peke ang sidhan kam nngeweza kumaliza yote haya kwa wakat "
"Ah binadam lazima tusaidiane ,kuw na aman ,Carry alimsogolea na kumhug ,Naseeb alibak kazubaa tu maan ni kitendo cha gafla hakutarajia Ila bumbuwaz ilipomuisha alijikaza akapitisha mikono yake kwenye kiuno cha Carry ,wote walijikuta wanahisia flan hiv ,
"Naseeb Asante sana"Carry alimnong'oneza sikion kisha akajitoa kutoka mikonon mwa Naseeb .
"Nashukuru Carry,halafu kesho nitakuletea karatas za mkataba usign maan mwenye nyumba nakaa nae mtaa mmoja so makabidhian rasm yatakuw kesho ,".
"Sawa Naseeb".Naseeb aliaga anaondka ,hakuwez kusindikizw maan ilikuw usiku sana ,Carry alichukua kile kindoo alichodekia alikiosha vizur halaf akaenda kukoga .,alvyotoka kuoga alijifungia mlango wake Ila kidogo mlango uligongwa na mgongaj alikuw ni Mamuu ,
"Yule ndo shemej eee?"
"Kwanini unauliza hivo "
"Nataka nkwambie tu kuw makin maan huyu mwanamke apo atakuchukulia bwana ako ,usije sema sijakwambia ooh me sitak kuja kuamua ugomv "
"Lakin yule ni dalal tu "
"Dalal ndo hafai kuitw mume?et dalal hahaha umemlipa shingap had akupangie vitu ndan ,nsije sahau kilichonileta naomba ndoo yang nkaoge mie .Alchukua ndoo yake na kuondoka zake ,Carry alishngazwa na huyu dada maan hajal hata kam ni usiku ila anapiga umbea tu ,Carry alijitupia zake kitandan na kuanz kuwaza mawil matatu .Alimkumbka Naseeb gafla ,alimfikria jins alvyo ,mref mweuc wastan ,nywel zke za kishombeshombe ,mwenye mwil uliojazia wastan ,mtaratib na alionekan mwenye huruma na mpenda kusaidia wengine Carry alijikuta akitabasam tu na kutamn angekuwepo na Naseeb kwa wakat ule ,aliwaza sana mwisho alipitiwa na usingiz.

†*†*****†********†*******†*******††*****
Aliamshw na mtu alyebisha hod ,Carry alijiinua kivivu kwel na kwa uchov haswaa ,alijifunga kanga na kufungua mlango
"Ooh Naseeb karib ndan "
"Asante ,me hata sikai nmekuletea vitu vyak hiv hapa "
"Jamn wagen hawaishiag nje ingia hata kidogo tu "Carry alibeba ndoo alizoletew na kuzingiiza ndan ,Naseeb naye ilibid akubal tu kuingia ndan ,walipiga pig story ,walipika walikula had mida yajion hiv ndipo Naseeb aliaga anaondoka .

************************************************
Carry aliamua kuanza biashara ya kuuza vitenge pamoja na nguo ndogo ndogo za kike,hakuw na mtaj mkubwa hivyo biashara yake ilikuw ya kawaida tu na mzgo haukuw mkubwa lakin ilmrad alipata chochote kitu ,ukaribu wake na Naseeb ulizd na walikuw marafik wakubwa tu ,na mimba ya Carry ilikuw inaonekan japo alijitahid kuificha ficha na madela ,kila siku baada ya muda wake wa kufanya kaz kuisha Naseeb alikuw anamfata na kumpeleka had nyumban .Kama kawaida siku hiyo Naseeb alimfata Carry na kumfkisha had nyumban ,aliingia ndan kwa Carry maan alimwambia anahitaj kuzungumza nae .

"Khoo! khoo !khoo!"Naseeb alianz kujikoholesha hali ya kuwa hakuw nakumbkumbk kam anaumwa kifua ,"Sijui hata nianzie WAP"
"Anzia popote tu Naseeb me nakusikilza"
"Carry samahn naomba kujua baba wa mtoto wako "
"Ukishamjua atakusaidia nin ?
"Nahitaj tu kujua Samahan"
"Naona unatak unchefue sahiv naomba uondoke kam huna kingine cha kuongea"
"Carry mbona unakuw mkal hiv,am sorry but nakupenda ndomn nahitaj kujua kitu kuhus wewe,nahitaj kuwa na ww Carie ,nmekujua muda sasa na tumekuw marafik kwa mwez mzima na tena ni zaid ya mwez ,sijawah kuona upo na mtu ndiomaan nkataka kujua il npate ruksa ya kuwa na ww Carry"muda wote Carry alikuw katulia tu anasikilza ngonjera za Naseeb
"Niruhus nkupende ,uruhusu na moyo wako unipende "Carry alikaa kmya muda mrefu then aliamua kuongea alimuelezea kila kitu kuhus hiyo mimba
"Mimba ina muda gan kwa sasa?
"Miez minne"
"Upo tayar niwe baba wa mtoto atakayezaliwa?
"Mmmh Naseeb ,hapana sitak"
"Kwann mama niruhus plz nakuahid ntakuw baba bora kwako ,sitoruhus uteseke wala mtoto wetu hatoteseka "
"Mtoto gan unayemzungumzia Naseeb?
"Huyo alyepo tumbon"
"Mim nitakuw mama na nitakuw baba wa huyu mtoto naomba uondoke"
"Siwez kuondoka had unikubalie omb langu na uzielewe hisia zang tafadhal "Naseeb alipiga had magot huku akilia kam nusu saa nzima aliendelea kulia tu huku akimbembeleza Carry ,Carry aliangalia choz LA mwanaume linavyoshuka Iman ikaanz kumuingia uvumiliv ulimshinda na alishindw kuyashinda majarib ya shetan alikubal kuwa pamoja na Naseeb .Naseeb hakuamin alichokisikia kutoka kwa Carry alifurah mnoo ,walikumbatiana na walikuw tayar kuanza safar yao mpya ya mapenz .

*************************************************
Edward alimpeleka mdogo wake nje ya nchi ,alikaa kule kwa muda kisha alirud nchin na alivyorud tu alikuw na kikao na mama ake .
"Hivi mwanangu sasahiv una umr gan?"
"27 mama ,kijana wako nimekuw ee"
"Hata mim naona umekuwa mwanang,lakin bado hujakuw "
"Kwanin mama ,huon na ndev hiz hapa,au had uzishike mama"Edward alizoea kumtania mama yake
"Ebu acha ujinga hapa uniskilize "
"Jaman mama unatak nkue niwe VIP"
"Nataka uoe Edward ,me nataka nipate wajukuu kabla sijafa "
"Mama muda bado nitaoa tu "
"Edward huon hal yang ,kila siku naumwa umwa tu nikifa je utafurah?
"Hapana mama sitofurah"
"Kwahiyo me natak uoe harak tu"
"Mama me bado sijapata mwanamke wa kuoa na mwanamke wang nliyewah kumpenda hayupo kwa sasa"
"Edward mwanamke wa kumuoa nimeshamuandaa tayar ni wewe tu kujiandaa kuoa "
"Mama maswala ya kuchagulian mke yamepitwa na wakat me sitak unichagulie mwanamke ,halafu sijajipanga kuoa kwa sasa"
"Kama nyumba unayo,gar unalo ,biashara unazo unatak ujipange na nini tena?nakwambia huoi mwanamke mwingine zaid ya Neema "
"Mama lakin "
"Hakuna cha lakin ,mwanang naomba ukubal hili tu mama yako hata nkifika ntapumzika kwa aman "
"Mama mama mama !maneno gan hayo unasema but Ok sawa nimekubal "
"Chereko!!!! chereko!!! jamn asante mwanangu asante sna na kesho nitawakutanisha na Neema najua utampend tu bint wa watu mzur kwel na hana shida .Edward aliitikia tu kinyonge maan hakuwez kumbishia mam yake na alimpenda sana hivyo alikuwa tayar kufanya chochote kwaajil ya mama yake isitoshe kiafya mam yake hakuwa vizur hivyo alihofia kumpoteza na hakuw na uhakika kam atakuja kuweza kuonana na msichan alyekuwa nae kwenye party miez mi4 iliyopita .


......Carry anaanzisha mahusiano na Naseeb,Edward naye amekubali kuoa mwanamke alichaguliwa na mama yake .......Je Carry na Edward watawez kuonana tena au baada ya kuw na mahusiano mengine ndo itakuw mwisho wao..........USIKOSE KIFUATACHO ......

ITAENDELEA .........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…