Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA SITINI NA MBILI
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
TULIPOISHIA SEHEMU YA SITINI MOJA: Kitendo ambacho kilizuwa msuko suko kwa Sheba ambae aliyumba kidogo akibakiza nchi chache sana kijibamiza kwenye kioo cha mbele kutokana na ile brake, huku akipelekwa pembeni na kujigonga kwenye mlango halafu akaa sawa na kugeuza uso wake nyuma kuona anacho kikimbia Dereva wake mpya, lakini hakuona chochote zaidi ya kushuhudia gari likiendelea kutililika kwa speed kuingia kwenye yale makazi, “au huyu nae ni mmoja kati ya watu wanao tufukuzia?” alijiuliza Sheba huku anageuza usi wake kumtazama Deus kwa macho yaliyojaa mashaka, “unadhani unafanya nini Deus?” aliuliza Sheba, huku anapeleka mkono kwenye vungu ya kiti chake na kuikamata bastora.. ..…….endelea….

wakati huo huo akaliona gari likisimama ubavuni mwa nyumba ile iliyokuwa kwenye kile kijipori cha miti ya kupanda, “sikia binti, sipendi bunduki, ni vyema ukitulia na kujiandaa kwa mambo yajayo, kuliko kunitolea macho” alisema Deus huku anatazama kwenye side mirror ya upande wake.

Kuona hivyo Sheba nae akageuka kabisa, kutazama nyuma ambako mwanzo hakuona kitu, “kuna nini? mbona hakuna kit….” kabla hajamaliza kuuliza alichotaka kuuliza, akaiona pikipiki moja ikipita kwa speed kuelekea upande ambao na wao walikuwa wanaelekea, “nadhani jibu umelipata, kuna watu wanatufuatilia kila tunapoenda, hivyo tunapaswa kuwatangulia hatua kadhaa mbele” alisema Deus, huku wakiendelea kuisindikiza ile piki piki kwa macho mpaka ilipopotelea upande wa kwa matius, “mh! we ulijuaje kama wanatufuatilia?” aliuliza Sheba kwa sauti yenye wasi wasi na mshangao, huku anamtazama Deus aliekuwa anaingiza gia ya uwani, (ya kurudi nyuma) na kukanyaga mafuta kwanguvu, na gari lika chomoka mbio kurudi nyuma, ungesema linaenda mbele, tena kwenye barabara ya lami.

Deus ambae hakujibu mara moja swali la Sheba, baada yake alitembeza gari kwa speed kali, akirudi nyuma, kuona hivyo Sheba kwa hiyari yake akafunga mkanda haraka na kusikilizia gari likizidi kurudi nyuma kwa speed ya kilomita sitini kwa saa, huku moyoni mwake akiombea gari lisipatwe na chochote cha kulitoa barabarani, wakati huo Deus ambae alionekana kutokuwa na wasi wasi, alizidi kukanyaga mafuta mpaka alipoikuta ile barabara ya zamani ya morogoro na alipoifikia tu, akashika hand brake huku anakata kona kushoto na kufanya gari lizunguke nusu duara na kutazama upande wa pili wa barabara, kisha akaipachika gia namba D, na kukanyaga mafuta huku anashusha hand brake, gari likachomoka kwa speed kuingia kwenye ile njia inayoelekea barabara ya morogoro ya sasa.

Naam walipoifikia sasa, walikuta kulikuwa na magari mengi, yanayo katiza kwenye barabara hiyo yakiwa katika mwendo kali, lakini huwezi amini alichokifanya Deus, aliingia barabarani na speed hizo hizo nakuingiza gari barabarani akivuka upande wa pili kakunja upande wa kulia wa barabara yaani upande wakurudi mjini, kisha akakanyaga mafuta kwa nguvu na hapo akaonekana akiovertake magari kadhaa, kabla ya kuingia picha ya ndege, ambapo hakuzubaa, aliivuka kwa speed kali, akiwaacha watu wakishangaa na alipofika mwishoni mwa mtaa huu wa picha ya ndege akaingia upande wa kushoto wa barabara, akiifuata barabara ya vumbi, ambayo aliiingia kwa speed ile ile mpaka alipoikuta barabara ya roliondo, akakata kulia na kuelekea roliondo sokoni, ambapo baada ya kutembea kilomita moja, akakutana na njia panda ya kunduchi, akaachana na ile Roliondo Sokoni, ambako sasa ni stendi ya dala dala akaifuata hii iendayo mnada wa mbuzi, akaingia na speed ile ile, ungesema gari lilikuwa katika mashindano ya magari.*******

Naaam Mzee Nyati na mke wake wakiwa wanendelea kuperuzi na kuangalia vita vya waandishi wa habari na watoa maoni, juu ya kitendo cha serikali kumuachisha jeshi kijan Deus Nyati, mara wakasikia simu ya mzee Nyati inaita, na bahati mbaya namba ilikuwa ngeni, “nani tena huyo, isije kuwa ni maswala hayo hayo ya Deus” alisema mzee Nyati huku anaipokea simu ile na kuiweka sikioni, “hallow, habari yako” alisalimia mzee Nyati, “nzuri shikamoo mzee” ilikuwa ni sauti ya kiume yenye nidhamu, “marahaba kijana nakusikiliza maana namba imekuja ngeni” alisema mzee Nyati kwa sauti iliyochangamka, “naitwa luten Kasian toka MMJ, yani makao makuu ya jeshi, bila shaka wewe ni bwana Frank Nyati?” aliongea ile sauti upande wapili wasimu.

Hapo mzee Nyati akamkamtazama mke wake, huku akiachia tabasamu pana na kumuonyesha ishara ya dole gumba la juu, “yes! mimi ni baba mzazi wa Deus” alijibu mzee Nyati, kwa sauti ile ile iliyochangamka, “ok! nashukuru sana kukupata ni hivi tumejaribu kumpigia kijana wako, kwenye simu yake ya mkononi, lakini hapatikani tukaona tukupigie wewe ambae amekutaja kama mtu wake wakaribu, ujumbe ni kwamba kesho mapema kabla ya saa moja na nusu anatakiwa kufika makao makuu ya jeshi, ofisi ya CDMP, bila kukosa” alisema luten Kasian, “sawa hakuna shida nitampigia, pengine ni network tu ndio maana hapatikani” alisema mzee Nyati kwa sauti iliyoonyesha wazi ufahari aliokuwa anajisikia, japo hakujuwa Deus anaitiwa nini huko makao makuu ya jeshi.

Naam baada ya simu kukatika, mzee Nyati akamatazama mke wake, “nilikuambia mama Deus hawawezi kumfukuza kazi kienyeji hivi, si unaona sasa wanamuita tena” alisema kwa majisifu mzee Nyati na mke wake, alieonekana kufurahishwa na jambo lile akaachia kicheko cha furaha, “lakini yasije kujirudia kama yale yaliyo jitokeza miaka ya nyuma kwako” alisema mama Deus, huku anamtazama mume wake aliekuwa anapiga simu kwa Deus, lakini simu haikupatikana, “huyu mpuuzi anafanya nini sasa, hajuwi kama wenzake wanamtafuta huko” alisema mzee Nyati, huku anarudia tena kupiga simu ile, ambayo licha ya kurudia mara kadhaa, lakini bado simu haikupatikana.*******

Yap! mtaani mambo yalikuwa moto moto, habari ni juu ya askari aliefukuzwa jeshi ziliendelea kusambaa na kugonga vichwani mwa watu, kila mmoja akiendelea kuzungumzia kwa namna yake, huku wengi wakilalamika na kukosoa utaratibu wa kufuata sheria, kama zilivyo ainishwa pasipo kuangalia mazingira ya utendaji wakosa, japo utaratibu huo ndio utaratibu ambao uliliwezesha jeshi hilo kuwa katika nafasi tatu za juu za majeshi yeye nidhamu Afrika, huku wachambuzi wakitaja kuwa MLA, ndio jeshi pekee lenye nidhamu kwa kiwango kikubwa Africa, kwa maana ya namba moja.

Habari hii inamfikia mwana mama tajiri, Monica, akiwa amekaa seat ya abiria mbele ya gari lake la kifahari, akipekuwa simu yake kusoma habari mbali mbali kwenye mitandao ya kijamii, huku kulia kwake kuna dereva wake na seat ya nyuma yake kuna mschana mrembo, mschana mwenye muonekano wa kuwa mtoto wa tajiri mkubwa, mwenye mkadirio wa miaka kati ya kumi na nane na kumi na tisa, ni mmoja kati ya watoto wa Monica, “sioni sababu ya wao kupiga kelele, kama wenyewe wameona hawafai basi ujuwe watakuwa na askari wengi kama hao” alisema Monica wakati huo anasoma habari hii, “nini hiyo mama?” aliuliza mschana seat ya nyuma, “si hawa hapa nao wametuchosha na kelele zao za huyu Deus Nyat..” alijibu yule Monica, kisha akasia kidogo, “mh! Nyati, nakumbuka zamani kule #Mbogo_land kulikuwa na askari wa MLA, aliemuokoa mfalme mara mbili, lakini mwisho wake alitoweka nchini kipindi cha uhaini” alisema Monica kwa mshangao.

Wakati Monica anamsimulia mwanae habari hiyo, wakati huo huo, mschana huyo mrembo nae, alikuwa anapekuwa simu yake, kama vile kuna jambo anahitaji kulithibitisha yeye mwenyewe na bahati nzuri, hakuchelewa kuipata habari hiyo na kuithibitisha, “we! mama unamaanisha ni huyu Deus” aliuliza yule mschana kwa mshangao mkubwa, huku akimuonyesha mama yake picha ya askari Deus Frank Nyati, iliyoambatana na habari ya askari kufukuzwa kazi, “ndiyo huyo huyo, si huyu hapa” alisema Monica huku anaonyesha picha ya askari huyo, kwenye simu yake, “hebu muone alivyo na sura ya upole” alisema Monica kwa sauti ya masikitiko.

Hapo mschana mrembo na mzuri, aliachia tabasamu lililoingiliana na mshangao, “jamaniiii, kumbe kaka Deus alijiunga na jeshi” alisema yule mschana kwa sauti fulani ambayo, hata wewe ungejuwa alikuwa katika msisimko wa furaha, “we umemfahamia wapi huyu, ulisoma nae?” aliuliza Monica huku anageuka kumtazama tena mwanae, safari hii akionyesha kumshangaa, maana kwa jinsi alivyoonekana kwa wakati ule, ungejuwa kabisa kuwa Deus alikuwa ni muhimu kwake, “we mama kwani humjui huyu?” aliuliza yule mschana, ambae sio tu urembo na uzuri wa sura, pia alikuwa na uzuri wa umbo na sauti tamu, “nimjulie wapi, kwani wewe una mfahamu” aliuliza Monica huku akiitazama ile picha kwa umakini zaidi, “we mama umemsahau huyu, huyu ni Deus alieniokoa kwenye ajali ya Tren wakati ule nasoma Njombe” alisema mschana huyo huku anamtazama mama yake.

Hapo Monica akaachama mdomo kwa mshangao wanguvu, “weeee unasema kweli, tungejuwa mapema si tungeenda kumpatia zawadi kama tulivyo ahidi” alisema Monica, ambae sasa alikuwa anatoka mjini kuelekea nyumbani kwake upande wa Kinyelezi, “ipo siku tutakutana nae tu, na hivi ameanza kutajwa kwenye vyombo vya habari, wala sina wasi wasi” alisema yule mschana alieonekana kuwa na jambo kubwa zaidi ya zawadi ya mama yake kwa kijana huyo kitu ambacho hata mama yake alishakiona.

Huyu mschana mwenye mkadilio wa miaka kumi nane au kumi na tisa, ni Caroline, huyu ndie yule yule aliekutana na Deus miaka mitano iliyopita, kule mjini makambako na kupanda Tren ya mizigo….…….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
Pamoja na watu wangu wa nguvu woodpecker24 Doctor G moneytalk na wengineo tupo pamoja like za kutosha tuendelee...
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA SITINI NA TATU
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
TULIPOISHIA SEHEMU YA SITINI MBILI: Huyu mschana mwenye mkadilio wa miaka kumi nane au kumi na tisa, ni Caroline, huyu ndie yule yule alie kutana na Deus miaka mitano iliyopita, kule mjini makambako, na kupanda Tren ya mizigo….…….endelea….

Ambayo baadae ilipata ajali maeneo ya Morogoro, na baada ya hapo hawakuweza kuonana tena wala kila mmoja kujuwa mwenzie yupo wapi, “kaa ni yeye hawakushatahili kumfukuza kazi na tukimpata tutampatia kazi kwenye moja ya viwanda vyetu, tena hata ikibidi kumpeleka shule, tutafanya hivyo ili apate nafasi nzuri” alisema mama Caroline kuiweka sawa furaha ya mwanae Caroline.******

Naam Sheba ambae mwanzo aliona kama uendeshaji wa Deus haukuwa mzuri alitulia kwa dakika kadhaa ndani ya gari lile, akishuhudia gari likienda kwa mwendo wa kasi sana, kasi ambayo hakutegemea kama angeweza kuendesha mwendo ule kwenye njia kama hii, “mh! Deus, ulijifunzia wapi kuendesha gari namna hii” aliuliza Sheba ambae wasi wasi na uoga wake vilionekana wazi kabisa kupitia sauti yake, nianze kukujibu swali gani? lile la nimejuaje kama tunafuatiliwa au hili la chuo cha udereva?” aliuliza Deus, ambae sasa alikuwa makini kutazama barabara na mguu wake ukiwa umeng’ang’ania kikanyagio cha mafuta, “ni vyema ukibijibu maswali yote” alisema Sheba na kumfanya Deus atabasamu kidogo, ikiwa ni mara ya kwanza toka ameingia kwenye gari, “chuo hakija nifundisha kuendesha gari namna hii, chuo nilienda kupata kibari cha kuendesha gari, gari amenifundisha baba yangu” alijibu Deus, ambae hakuacha kukimbiza gari, hiyo ilikuwa ni saa tisa na robo za Alaasiri.

Deus akamueleza Sheba kuwa, kuna jambo aliligundua, mara baada ya yeye Sheba, kumueleza kuwa walikuwa wanatafutwa na vyombo vya dola, ndipo alipodhania kuwa lazima wangesimamishwa na polisi pale mzani, maana polisi wangekuwa wamesha sambazambaza namba za gari hili na aina ya gari kwenye kila kituo cha askari wa usalama barabarani na wakaguzi kwaajili ya kulikamata, lakini walipovuka, bila kikwazo akajuwa lazima wangezuiliwa pale TAMCO, napo wakapita bila kikwazo, hapo Deus akagundua kuwa waliokuwa wanawafukuzia wapo nje ya sheria, hata kama wao ni watu wa serikali, kwahiyo wanawafatilia kimya kimya kwenye barabara ambayo wao wangeitumia, ndio maana akaamua kutegeneza mtego wa kumbaini anae wafuatilia na kumuona yule alie bebwa kwenye pikipiki, “na sasa tunabadili njia, tunapitia hii ya bagamoyo maana wao wote mawazo yao wameyaweka kwenye barabara ya morogoro” alisema Deus,l na kumfanya Sheba amtazame kwa mshangao, “mh! basi wewe ni mtu hatari sana” alisema Sheba, huku anatazama mbele, ambako sasa waliyaona maungio ya barabara ya bagamoyo, Deus akapunguza mwendo na kuingia barabarani akikata upande wa kushoto, kuelekea bagamoyo, “inaonyesha mpaka sasa na wewe humjui adui yako” alisema Deus kwa sauti yake tulivu, huku anakanyaga mafuta kwa nguvu na kutokomea kabisa upande huo wa mji mkongwe wa kihistoria.*******

Yap! tukirudi Kibaha sasa tunaenda mpaka kongowe, ambako tunakuta gari aina ya Land rover mia na kumi, mali ya jeshi la polisi likiwa lina ingia kwenye kituo cha dala dala, huku limebeba askari sita nyuma yake, huku SMG nane zikiwa zimelazwa kwenye skafu ya gari lile na seat ya abiria wa mbele akiwa amekaa koplo Cheleji, ni yule ambae muda mfupi uliopita alikuwepo pale Kiluvya Madukani.

Naam mara baada ya gari kusimama, anasogea yule askari ambae mwanzo tulimuona pale kibaha picha ya ndege, akisogea kwenye mlango wa abiria wa mbele, “sijaelewa jinsi alivyo nitoka toka, ila nina uhakika watakuwa wameenda uelekeo huu” alisema yule jamaa, ambae mwanzo alikodi pikipiki kwaajili ya kulifuatilia BMW jeusi, “una uhakika kwamba hawakuchepuka sehemu?” aliuliza Cheleji, akionekana kuwa na shaka juu ya taarifa ya yule mwenzie, “nilipofika kwa Matius na kuwakosa nikarudi tena na njia ile ile, lakini sikuwaona tena, ndio nikaingia barabara ya lami, na kuanza kuwa fukuzia” alisema yule jamaa, “ok! ingia ndani ya gari, tuelekee chalinze, kama wameenda huko, lazima watakutana na wale wa bagamoyo au wanaotoka Morogoro” alisema Cheleji, na yule mwingine akaingia kwenye gari akiungana na mwenzake walipanda nyuma ya gari, kisha gari likaondoka kwa speed kuelekea Chalinze.

Wakati safari ya Chalinze ikiwa inashika kasi ndipo Cheleji alipo piga simu, kwa CP Ulenje, simu ambayo haikuchukwa muda mrefu kupokelewa, “Niambie Cheleji, vipi mumesha wakamata?” aliuliza CP Ulenje mara baada ya kuipokea ile simu, “afande kuna shida kidogo, tumelipoteza gari, ila sasa tunaelekea Chalinze, maana tunahisi wameelekea huko” alijibu Ulenje na hapo ni kama alimshangaza Ulenje, “Ulenje mbona unafanya mambo ya ajabu, unawezaje kuelekea Chalinze, wakati hauna uhakika kama wametoka nje ya mji, hebu rudini pale Picha ya ndege mkachunguze walikoelekea, ikiwezekana ulizieni hata kwa traffic pale kwa Matius, wao lazima watakuwa wameliona hilo gari” alisema Ulenje.

Bila kuoji mara mbili, Cheleji akatoa ishara kwa dereva ageuze gari walikotoka, nae akafanya hivyo, huku simu ya Cheleji ikiwa bado sikioni, anaendelea kupokea ufafanuzi toka kwa CP Ulenje kwa Cheleji kuwa, kama waliweza kutoweka kwa haraka namna hiyo, basi lazima watakuwa katika speed kali, speed ambayo lazima askari wa usalama barabarani, wange wasimamisha, “kwa hiyo na uhakika hawajatoka nje ya mji, huko chalinze waachie hao wengine” alisisitiza Ulenje, kabla ya kukata simu, wakati huo tayari gari lilikuwa limeshika kasi kuelekea upande wa mjini.*******

Naaam wakati hayo yanaendelea huku Kibaha, Dakika thelathini baadae, maeneo ya Msata, mita mia mbili karibu na njia panda ya bagamoyo, ndani ya mkoa wa pwani, linaonekana BMW S 7, likitokea upande wa bagamoyo, kwaspeed kali ya kilomita mia moja themanini kwa saa, likisogelea njia panda ile ambayo inaunganisha barabara itokayo Chalinze kuelekea mikoa ya kaskazini, yani Tanga, Kilimanjaro na Arusha, na gari hilo lenye speed ya Puma, linapokaribia round about ile, linapnguza mwendo zaidi na kuingia mzungukoni, kisha kushika uelekeo wa kaskazini.

Gari linaonekana likwa mwendo wa speed ya kilomita arobaini kwa saa na kuongeza speed taratibu kila lilipozidi kusogea, hata lilipokuwa limemekaribia mzani lilikuwa katika speed ya kilomita hamsini kwa saa, hiyo ilisaidia hata askari wa usalama barabarani alitazame kwa macho pasipo kulisimamisha, maana halikuonejana kuwa na makosa yoyote na kwa bahati nzuri kwa wakati ule lilionekana kuwa namba za usajili wa muda, namba ambayo hupewa gari pale tu linaposhushwa bandarini, kabla ya kusajiliwa upya, namba ambayo hutumika ndani ya siku tisini tu, yani miezi mitatu.

Naam mara tu baada ya kuvuka pale mzani, gari likaongeza mwendo mara dufu, ndani ya sekunde kumi na tano, kama ungekuwa na king’amua mwendo kama ambavyo waswahili tunapenda kuita torch, basi ungewezakushika kichwa kwa speed ambayo ungeishuhudia, ilikuwa ni speed ya kilomita mia tisini kwa saa, na haikuishia hapo, speed iliendelea kuongezeka kila sekunde ilipo sogea, huku kioo kidogo cha video pale kwenye dash board ya gari ikionyesha picha ya ramani ya GPS, ya muundo wa satellite (setelaiti) ramani ambayo iliweza kuonekana vyema, mfano wapicha halisi ya umbo la dunia, kama linavyoweza kuonekana toka angani, lilionyesha jinsi wanavyo karibia mto wami.

“sina shaka na uendeshaji wako Deus” alisema Sheba na kwa mara ya kwanza akiachia tabasamu pana, huku anajilaza kwenye kiegemeo cha kiti aliyokalia, Deus akujibu kitu zaidi kukanyaga mafuta kulifuata daraja la mto wami, ambapo wanaelekea kuuacha mkoa wa pwani, wakati huo tayari zilisha pita dakika ishirini toka itimie saa kumi za jioni kwa saa za afrika ya mashariki.*******

Naam King Elvis na mke wake Vaselisa, wakiwa kwenye eneo la bustani nzuri yenye kupendeza, wamezungukwa na marembo wa maua pamoja na walinzi, wanapunga upepo hapa kwenye jumba la Dhahabu, yaani ikulu ya #mbogo_land, alionekana kuwa mwenye mawazo mengi, yaliyo mkosesha amani, kitu ambacho hata mke wake alikigundua, japo hakujuwa ni kitu gani kime mnyima amani mume wake, “mume wangu mpendwa ni muda mefu sana sijawahi kukuona ukiwa katika hali kama hii, vipi kuna jambo lina kutatiza?” aliuliza Malkia Vaselisa mwanamke mzuri alietajwa kuwa katika oroha ya wanawake wazuri kabisa duniani.

Swali la malkia ni kama lilimgutusha Elvis toka kwenye mawazo, “hooo! ni mambo ya utawala, ukweli yanaumiza kichwa” alisema Elvis, huku anajiweka sawa kwenye kiti chake, kilicho nakshiwa kwa dhahabu na madini mengine, yenye thamani, kiti ambacho angekiokota moneytalk au woodpecker24 wange nunua mtaa mzima na majumba na mali zote za mtaa na wakazi wa mtaa huo wangewaajili kulima mashamba, na kufanya kazi kwenye viwanda vyao, ambavyo wange vianzisha kwa fedha hiyo hiyo, pia fedha inayo bakia wangeinunua simba na ndio ingekuwa mwaka wao wa kwanza kuchukua club bingwa maana wangetumia fedha hiyo hiyo kuhonga marefa waibebe timu na Doctor G angeacha hiyo kazi akajenga hospital za kwake (hayo ni mawazo ya rafiki yangu Mduku aliyoyatoa siku alipokiona kile kiti cha King Elvis wa kwanza siku tulivyotembelea #mbogoland kwenye ndoa ya Radhia) .…….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
Shukrani sana mtunzi ila kila inapoishia ndiyo hamu ya kutaka kujua kitachojiri inazidi hongera kwako kwa utunzi mzuri.
 
190km/hr..,
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA SITINI NA NNE
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
TULIPOISHIA SEHEMU YA SITINI TATU: kiti ambacho angekiokota moneytalk au woodpecker24 wange nunua mtaa mzima na majumba na mali zote za mtaa na wakazi wa mtaa huo wangewaajili kulima mashamba, na kufanya kazi kwenye viwanda vyao, ambavyo wange vianzisha kwa fedha hiyo hiyo, pia fedha inayo bakia wangeinunua simba na ndio ingekuwa mwaka wao wa kwanza kuchukua club bingwa maana wangetumia fedha hiyo hiyo kuhonga marefa waibebe timu na Doctor G angeacha hiyo kazi akajenga hospital za kwake (hayo ni mawazo ya rafiki yangu Mduku aliyoyatoa siku alipokiona kile kiti cha King Elvis wa kwanza siku tulivyotembelea #mbogoland kwenye ndoa ya Radhia) endelea nayo ….

“Kuna jambo gani tena, au ni lile la askari kuacha kazi?” aliuliza malkia Vaselisa kwa sauti ya unyenyekevu, sauti ambayo mala nyingi huitumia anapohitaji kumuondoa mume wake toka kwenye mawazo ya kiunyonge, “hilo ni moja wapo maana leo nimengundua kuwa kuna baadhi ya askari waliacha jeshi kipindi cha vugu vugu la kundi la UMD, mmoja wao akiwa askari mtiifu na shujaa luten kanal Frank Nyati, alie muokoa mara kadhaa King Eugen wa 25, lakini pia nimegundua kuwa kuna dalili za kurudi kwa kundi la UMD, inawezekana wakina Frank Nyati wanaunda tena kundi hilo?” aliuliza Elvis, sasa akimtazama mke wake ambae pia alionekana kuvuta kumbu kumbu flani.

Uvutaji wa kumbu kumbu ambao ulimfanya achelewe kumjibu mfalme, ambae alimtazama mke wake kwa umakini mkubwa huku akisubiri jibu la mwanamke huyo, ambae kikawaida Elimu yake haikuwa kubwa sana, ila alikuwa na busara zilizo mzidi kimo, “hapa najaribu kuwaza hilo jina nimelisikia wapi halafu siyo muda mrefu” alisema malkia Vaselina huku akijaribu kuvuta kumbu kumbu zaidi, “Nyati…. nyati … Nyati, hoooo! sawa, huyo ni mtazania” alisema Vaselisa, alijaribu kupotezea habari ya huyo ya mtanzania alieitwa Nyati, “amefanyaje huyo mtazania?” aliuliza King Elvis, huku akitazama mke wake.

Mke wake ambae ukiachikia shuguri zake za kusimamia maswala ya jinsia na watoto pamoja na afya, katika nchi ile ya #mbogo_land, akisaidiana na mwanamama Thesilia Martin, mama yake Careen wa kwenye simulizi ya KIAPO CHA FUKARA hiyo ni baada ya kushindwa kuongoza peke yake, kutokana na Elimu ndogo aliyokuwa nayo Malkia huyo, ambae sasa anaendelea kupata Elimu ya chuo baada ya kushauriwa na mama mkwe wake yaani Malkia doctor Irene Simon wa kwenye simulizi ya UMEKOSEA LAKINI TAMU kwamba ajiendeleze Elimu ili awezekuongoza wizara hiyo, ambayo ni lazima kwa mke wa Mfalme.

Pia mwana huyo ambae pia ni mmoja kati ya waschana wadogo kupata kuwa wake wa viongozi wakubwa wanchi alikuwa anapenda sana kuperuzi mitandao ya kijamii ili kuijuwa dunia na kujifunza zaidi, “hukuwahi kusikia habari za Deus Nyati?” aliuliza Vaselisa kwa mshangao, “nisingekuuliza mke wangu, hebu nipe habari zake” aisema King Elivs na kujiweka sawa ili awezekupata habari za mtu huyo ambae mwanzo alihisi anaweza kuwa ndie Nyati ambae alitoweka nchini kwake.

Naam Malikia Vaselisa akaanza kueleza kisa cha askari mtanzania, alie waokoa mdoctor watatu, wa umoja wa mataifa huko nchini Congo na baadae kukutwa na hatia ya jaribio la ubakaji, akishinda kesi kwa kuonekana amesingiziwa na kwamba ulikuwa ni mpango wa IDFNALLU, lakini anaondolewa UN kwa kosa la kufanya jukumu nje ya mkataba na mwisho nchi yake inamfukuza kazi kwa kuliaibisha taifa, “bado sijafanya ujinga huo, hapo lazima ningevunja sheria za nchi yangu, kwa kumuacha askari aendelee na kazi” alisema King Elvis, mwishoni mwa hadithi toka mke wake, “pengine kuna askari wengi wa namna hii, hivyo hawahofii kumpoeza mmoja kwa heshima ya nchi” alisema Vaselisa ambae licha ya kuchanganya damu ya Mmakonde na mwarabu, lakini maisha yake kwa kiasi kikubwa aliishi Dar es salaam.

Waliongea mawili matatu juu ya Deus Nyati, kabla hawaja badili maongezi, pasipo mfalme kufahamu au kulijuwa jina la tatu la askari huyo, shujaa mwenye bahati mbaya.*********

Yap! saa kumi na moja kasoro gari la polisi, lilikuwa kwenye soko dogo maarufu kama mnadani pale kwa matius, njia ya kwenda Efatha, askari saba, wakiwa nyuma ya gari huku koplo Cheleji, akionekana akiwa amesimama kwenye kibaraza cha nyumba moja, pale pembeni ya barabara inayotenganisha nyumba kadhaa upande wa kushoto na soko likiwa upande wakulia mbele yake wakiwa mafundi wa kushona, tume zowea kuwaita mafundi cherehani, mnasema hamjaliona gari dogo jeusi jipya hivi, BMW likipita hapa?” aliuliza Cheleji, akionekana kuishiwa nguvu, baada ya kukosa kile alicho tegemea, “yaani kaka lingepita tunge liona, maana hapa yanapita magari machache sana na yote tumeyaona kama hilo lingepita nalo tungeliona tu” alisema mmoja kati ya wale fundi cherehani wa kiume alieonekana kuwa na umri mkubwa zaidi ya wote, aliekadiriwa kuwa na miaka hamasini na tano, “ok! sie tunaondoka ila kama mtakumbuka chochote au kuliona gari hilo mutatueleza maana tutapia baadae” alisema Koplo Cheleji, wakati anaaga na kundoka kuelekea kwenye gari.

Naam Koplo Cheleji akaingia kwenye gari ambalo wenzake walikuwa wanamsubiri, kisha gari likaondoka kuelekea barabara ya zamani ya Morogoro na walipoikuta wakafuata upande wa kuelekea picha ya ndege yaani kule ambako yule mwenzao aliliona BMW 7 likielekea.

Gari aina ya land rover mia na kumi, lilitembea taratibu huku wote wakiwa makini kutazama kushoto na kulia kama wangeweza kuliona BMW S7, lakini mpaka wanafika pale kwenye msitu, hawa kuwa wameliona gari lile wala dalili ya uwepo wa gari ilo.

Lakini wakati wanataka kukatiza kwenye njia ya kuingia kwenye ile nyumba iliyopo kwenye kichaka cha miti ya kupanda ghafla dereva akasimamisha gari, “afande naweza kuona kuna gari liliingia barabara hiyo njia hapo” alisema dereva wa lile gari la polisi, ambae alikuwa kule mbele ya gari na Cheleji hapo Cheleji nae akatazama kwenye sakafu ya barabara, inayoingia kwenye ile nyumba na kuona alama za tairi za gari akazifuatilia na kuziona zinatokea kwenye ile nyumba, “mh! mbona kama ni gari la ile nyumba” alisema Cheleji, huku anarudisha macho yake upande wa barabara lakini usawa wa sakafu ya barabara ambapo tairi za gari zilizo futika zilionekana kuvuka barabara, “lakini afande unadhani mwenyeji wa eneo hili anaweza kupitisha gari kwenye barabara hii?” aliuliza dereva, huku wakitazama tairi za gari zilizovuka upande wa pili wa barabara.

Naam! hapo nikama Koplo Cheleji alibaini jambo jipya, mh! hebu subiri kidogo, inawezekana hawa washenzi walishtukia kuwa wanafuatiliwa, wakaja kujibanza hapa na Mao alipopita tu wao wakarudi walikotoka na kubadili njia, kama huamini hebu kwanza uone” alisema Cheleji huku anafungua mlango wa gari na kushuka chini, kisha akaelekea kwenye ile nyumba ya kichakani, huku akimuacha dereva anaegesha gari pembeni ya barabara.

Cheleji alitembea kwa haraka kuifuata ile nyumba, huku anatazama kwa umakini alama zile za tairi za gari mpaka alipofika nazo kwenye ile nyumba, na kuziona zikiwa zimeishia ubavuni mwa nyumba, ile ambayo kiukweli ilikuwa kimya kiasi, japo walionekana kuku na bata wakizurula eneo lile la nyumba ile tulivu.

Cheleji akasogelea lango na kugonga hodi mara kadhaa, lakini hakupata mrejesho wowote toka ndani, akarudia tena na tena lakini mambo yakawa vile vile, Cheleji akiwa amekata tamaa ya uwepo wa wenyeji akageuka ili kuondoka, lakini kabla hajapiga hatua hata moja, akasikia michatoka ya vishindo vya mtu upande wa ndani, akiufuata mlango, Cheleji akasimama na kusikilizia kifuatacho.

Nikweli sekunde chache baadae, mlango ukafunguliwa akaibuka kijana mmoja wakati ya umri wa miaka kumi na tisa au ishirini, mwenye uso wa tabasamu na ukarimu, “karibu bro, pole sana maana nilikuwa na jiuliza hii hodi ni huku au?” alisema yule kijana, ambae alionekana wazi kuwa alikuwa ametoka kwenye kazi fulani ngumu, iliyomfanya achafuke nguo zake chakavu, alizokuwa amezivaa, “kwa hiyo ukashindwa kuacha upuuzi wako nakuja kusikiliza mara moja, ukaamua unichomeshe mahindi hapa mlangoni?” aliuliza Cheleji kwa sauti kavu isiyo na utani hata chembe, kiasi cha yule kijana mkarimu kujikuta akibadiri sura yake toka katika hali ya tabasamu, na kuwa katika hali ya uoga na wasi wasi.

Kijana anatazama barabarani, macho yake yana kutana na gari la polisi, hapo ndio anakosa kabisa uwezo wa kujiamini na kuzidi kujawa na wasi wasi,”samahani kaka nilikuwa ndani ya banda la kuku, nafanya usafi ndio maana sikuweza kusikia vizuri” alisema yule kijana kwa sauti ya kuombeleza….endelea…. kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unaoo kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA SITINI NA TATU
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
TULIPOISHIA SEHEMU YA SITINI MBILI: Huyu mschana mwenye mkadilio wa miaka kumi nane au kumi na tisa, ni Caroline, huyu ndie yule yule alie kutana na Deus miaka mitano iliyopita, kule mjini makambako, na kupanda Tren ya mizigo….…….endelea….

Ambayo baadae ilipata ajali maeneo ya Morogoro, na baada ya hapo hawakuweza kuonana tena wala kila mmoja kujuwa mwenzie yupo wapi, “kaa ni yeye hawakushatahili kumfukuza kazi na tukimpata tutampatia kazi kwenye moja ya viwanda vyetu, tena hata ikibidi kumpeleka shule, tutafanya hivyo ili apate nafasi nzuri” alisema mama Caroline kuiweka sawa furaha ya mwanae Caroline.******

Naam Sheba ambae mwanzo aliona kama uendeshaji wa Deus haukuwa mzuri alitulia kwa dakika kadhaa ndani ya gari lile, akishuhudia gari likienda kwa mwendo wa kasi sana, kasi ambayo hakutegemea kama angeweza kuendesha mwendo ule kwenye njia kama hii, “mh! Deus, ulijifunzia wapi kuendesha gari namna hii” aliuliza Sheba ambae wasi wasi na uoga wake vilionekana wazi kabisa kupitia sauti yake, nianze kukujibu swali gani? lile la nimejuaje kama tunafuatiliwa au hili la chuo cha udereva?” aliuliza Deus, ambae sasa alikuwa makini kutazama barabara na mguu wake ukiwa umeng’ang’ania kikanyagio cha mafuta, “ni vyema ukibijibu maswali yote” alisema Sheba na kumfanya Deus atabasamu kidogo, ikiwa ni mara ya kwanza toka ameingia kwenye gari, “chuo hakija nifundisha kuendesha gari namna hii, chuo nilienda kupata kibari cha kuendesha gari, gari amenifundisha baba yangu” alijibu Deus, ambae hakuacha kukimbiza gari, hiyo ilikuwa ni saa tisa na robo za Alaasiri.

Deus akamueleza Sheba kuwa, kuna jambo aliligundua, mara baada ya yeye Sheba, kumueleza kuwa walikuwa wanatafutwa na vyombo vya dola, ndipo alipodhania kuwa lazima wangesimamishwa na polisi pale mzani, maana polisi wangekuwa wamesha sambazambaza namba za gari hili na aina ya gari kwenye kila kituo cha askari wa usalama barabarani na wakaguzi kwaajili ya kulikamata, lakini walipovuka, bila kikwazo akajuwa lazima wangezuiliwa pale TAMCO, napo wakapita bila kikwazo, hapo Deus akagundua kuwa waliokuwa wanawafukuzia wapo nje ya sheria, hata kama wao ni watu wa serikali, kwahiyo wanawafatilia kimya kimya kwenye barabara ambayo wao wangeitumia, ndio maana akaamua kutegeneza mtego wa kumbaini anae wafuatilia na kumuona yule alie bebwa kwenye pikipiki, “na sasa tunabadili njia, tunapitia hii ya bagamoyo maana wao wote mawazo yao wameyaweka kwenye barabara ya morogoro” alisema Deus,l na kumfanya Sheba amtazame kwa mshangao, “mh! basi wewe ni mtu hatari sana” alisema Sheba, huku anatazama mbele, ambako sasa waliyaona maungio ya barabara ya bagamoyo, Deus akapunguza mwendo na kuingia barabarani akikata upande wa kushoto, kuelekea bagamoyo, “inaonyesha mpaka sasa na wewe humjui adui yako” alisema Deus kwa sauti yake tulivu, huku anakanyaga mafuta kwa nguvu na kutokomea kabisa upande huo wa mji mkongwe wa kihistoria.*******

Yap! tukirudi Kibaha sasa tunaenda mpaka kongowe, ambako tunakuta gari aina ya Land rover mia na kumi, mali ya jeshi la polisi likiwa lina ingia kwenye kituo cha dala dala, huku limebeba askari sita nyuma yake, huku SMG nane zikiwa zimelazwa kwenye skafu ya gari lile na seat ya abiria wa mbele akiwa amekaa koplo Cheleji, ni yule ambae muda mfupi uliopita alikuwepo pale Kiluvya Madukani.

Naam mara baada ya gari kusimama, anasogea yule askari ambae mwanzo tulimuona pale kibaha picha ya ndege, akisogea kwenye mlango wa abiria wa mbele, “sijaelewa jinsi alivyo nitoka toka, ila nina uhakika watakuwa wameenda uelekeo huu” alisema yule jamaa, ambae mwanzo alikodi pikipiki kwaajili ya kulifuatilia BMW jeusi, “una uhakika kwamba hawakuchepuka sehemu?” aliuliza Cheleji, akionekana kuwa na shaka juu ya taarifa ya yule mwenzie, “nilipofika kwa Matius na kuwakosa nikarudi tena na njia ile ile, lakini sikuwaona tena, ndio nikaingia barabara ya lami, na kuanza kuwa fukuzia” alisema yule jamaa, “ok! ingia ndani ya gari, tuelekee chalinze, kama wameenda huko, lazima watakutana na wale wa bagamoyo au wanaotoka Morogoro” alisema Cheleji, na yule mwingine akaingia kwenye gari akiungana na mwenzake walipanda nyuma ya gari, kisha gari likaondoka kwa speed kuelekea Chalinze.

Wakati safari ya Chalinze ikiwa inashika kasi ndipo Cheleji alipo piga simu, kwa CP Ulenje, simu ambayo haikuchukwa muda mrefu kupokelewa, “Niambie Cheleji, vipi mumesha wakamata?” aliuliza CP Ulenje mara baada ya kuipokea ile simu, “afande kuna shida kidogo, tumelipoteza gari, ila sasa tunaelekea Chalinze, maana tunahisi wameelekea huko” alijibu Ulenje na hapo ni kama alimshangaza Ulenje, “Ulenje mbona unafanya mambo ya ajabu, unawezaje kuelekea Chalinze, wakati hauna uhakika kama wametoka nje ya mji, hebu rudini pale Picha ya ndege mkachunguze walikoelekea, ikiwezekana ulizieni hata kwa traffic pale kwa Matius, wao lazima watakuwa wameliona hilo gari” alisema Ulenje.

Bila kuoji mara mbili, Cheleji akatoa ishara kwa dereva ageuze gari walikotoka, nae akafanya hivyo, huku simu ya Cheleji ikiwa bado sikioni, anaendelea kupokea ufafanuzi toka kwa CP Ulenje kwa Cheleji kuwa, kama waliweza kutoweka kwa haraka namna hiyo, basi lazima watakuwa katika speed kali, speed ambayo lazima askari wa usalama barabarani, wange wasimamisha, “kwa hiyo na uhakika hawajatoka nje ya mji, huko chalinze waachie hao wengine” alisisitiza Ulenje, kabla ya kukata simu, wakati huo tayari gari lilikuwa limeshika kasi kuelekea upande wa mjini.*******

Naaam wakati hayo yanaendelea huku Kibaha, Dakika thelathini baadae, maeneo ya Msata, mita mia mbili karibu na njia panda ya bagamoyo, ndani ya mkoa wa pwani, linaonekana BMW S 7, likitokea upande wa bagamoyo, kwaspeed kali ya kilomita mia moja themanini kwa saa, likisogelea njia panda ile ambayo inaunganisha barabara itokayo Chalinze kuelekea mikoa ya kaskazini, yani Tanga, Kilimanjaro na Arusha, na gari hilo lenye speed ya Puma, linapokaribia round about ile, linapnguza mwendo zaidi na kuingia mzungukoni, kisha kushika uelekeo wa kaskazini.

Gari linaonekana likwa mwendo wa speed ya kilomita arobaini kwa saa na kuongeza speed taratibu kila lilipozidi kusogea, hata lilipokuwa limemekaribia mzani lilikuwa katika speed ya kilomita hamsini kwa saa, hiyo ilisaidia hata askari wa usalama barabarani alitazame kwa macho pasipo kulisimamisha, maana halikuonejana kuwa na makosa yoyote na kwa bahati nzuri kwa wakati ule lilionekana kuwa namba za usajili wa muda, namba ambayo hupewa gari pale tu linaposhushwa bandarini, kabla ya kusajiliwa upya, namba ambayo hutumika ndani ya siku tisini tu, yani miezi mitatu.

Naam mara tu baada ya kuvuka pale mzani, gari likaongeza mwendo mara dufu, ndani ya sekunde kumi na tano, kama ungekuwa na king’amua mwendo kama ambavyo waswahili tunapenda kuita torch, basi ungewezakushika kichwa kwa speed ambayo ungeishuhudia, ilikuwa ni speed ya kilomita mia tisini kwa saa, na haikuishia hapo, speed iliendelea kuongezeka kila sekunde ilipo sogea, huku kioo kidogo cha video pale kwenye dash board ya gari ikionyesha picha ya ramani ya GPS, ya muundo wa satellite (setelaiti) ramani ambayo iliweza kuonekana vyema, mfano wapicha halisi ya umbo la dunia, kama linavyoweza kuonekana toka angani, lilionyesha jinsi wanavyo karibia mto wami.

“sina shaka na uendeshaji wako Deus” alisema Sheba na kwa mara ya kwanza akiachia tabasamu pana, huku anajilaza kwenye kiegemeo cha kiti aliyokalia, Deus akujibu kitu zaidi kukanyaga mafuta kulifuata daraja la mto wami, ambapo wanaelekea kuuacha mkoa wa pwani, wakati huo tayari zilisha pita dakika ishirini toka itimie saa kumi za jioni kwa saa za afrika ya mashariki.*******

Naam King Elvis na mke wake Vaselisa, wakiwa kwenye eneo la bustani nzuri yenye kupendeza, wamezungukwa na marembo wa maua pamoja na walinzi, wanapunga upepo hapa kwenye jumba la Dhahabu, yaani ikulu ya #mbogo_land, alionekana kuwa mwenye mawazo mengi, yaliyo mkosesha amani, kitu ambacho hata mke wake alikigundua, japo hakujuwa ni kitu gani kime mnyima amani mume wake, “mume wangu mpendwa ni muda mefu sana sijawahi kukuona ukiwa katika hali kama hii, vipi kuna jambo lina kutatiza?” aliuliza Malkia Vaselisa mwanamke mzuri alietajwa kuwa katika oroha ya wanawake wazuri kabisa duniani.

Swali la malkia ni kama lilimgutusha Elvis toka kwenye mawazo, “hooo! ni mambo ya utawala, ukweli yanaumiza kichwa” alisema Elvis, huku anajiweka sawa kwenye kiti chake, kilicho nakshiwa kwa dhahabu na madini mengine, yenye thamani, kiti ambacho angekiokota moneytalk au woodpecker24 wange nunua mtaa mzima na majumba na mali zote za mtaa na wakazi wa mtaa huo wangewaajili kulima mashamba, na kufanya kazi kwenye viwanda vyao, ambavyo wange vianzisha kwa fedha hiyo hiyo, pia fedha inayo bakia wangeinunua simba na ndio ingekuwa mwaka wao wa kwanza kuchukua club bingwa maana wangetumia fedha hiyo hiyo kuhonga marefa waibebe timu na Doctor G angeacha hiyo kazi akajenga hospital za kwake (hayo ni mawazo ya rafiki yangu Mduku aliyoyatoa siku alipokiona kile kiti cha King Elvis wa kwanza siku tulivyotembelea #mbogoland kwenye ndoa ya Radhia) .…….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
hahahaa mimi siwezi kununua simba,yanga yangu nimuachie nani
 
190km/hr..,
012_i_combi.jpg
 
mkuu shukrani sana,muendelezo tafadhali.
 
Back
Top Bottom