Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Mkuu
Kama zote tu πŸ˜…
Jana ukatupiga kamba halafu ukapotelea mitini du!!! πŸ₯±πŸ₯±πŸ€­πŸ€­πŸ₯±πŸ€­πŸ€­
Sema Nini, kuwa makini huko, huwaga siyo watu wa zuri kabisa. Yaani mpaka Wana michezo ya kuridhishana bila ya tendo, chezea vijana wa UMD! πŸ€£πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜­πŸ€£πŸ€£πŸ˜…πŸ€£πŸ˜…
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA ISHIRINI
MTUNZI: Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA KUMI NA TISA:- Kimya kikatawala, kila mmoja akiwaza la kwake kabla Veronica hajaamua kuwakilisha ombi lake, "samahani kaka, naweza kupiga simu moja tu kwa rafiki yangu" aliuliza Veronica, huku anajaribu kumtazama Deus, lakini anashindwa, "nani huyo ni huyo uliekuwa unachati nae?" alizungumza Deus pasipo kumtazama Veronica, "ndiyo nataka kuagana nae" alisema Veronica, huku anachukua simu yake toka mezani, "mh! unawezaje kuagana na mtu ambae upo nae, au nimekosea kwamba unataka kumpgia mchoraji?" aliuliza Deus na kumfanya Veronica atoe macho ya mshangao kwa kuthibitisha kuwa, huyu mbele yake ndie mchoraji aliekuwa anachati nae wakati wote, ni rafiki yake wa muda mrefu ambae ambae hawa kuwahi kuonana toka wamekuwa marafiki, "mchoraji umenijuaje" aliuliza Veronica huku anamtazama Deus kwa macho ya mshangao, wakati huo deusi alikuwa anaendelea kula bila kumtazama Veronica. ENDELEA…


Veronica alimtazama kijana kwa macho ya mshangao na kutokuamini, huku akijiuliza maswali kadhaa kichwani mwake, β€œJe huyu kweli ni mchoraji wake, kama ni yeye kweli kwanini wakutane katika mazingira kama haya, ukweli hawezi kuwa mmoja wa wakina JJ, maana asinge wauwa namna ile, β€œau ni mpelelezi aliekuwa anawapeleleza wakina JJ, lakini hapana, mbona nimefahamiana nae kabla ya kufahamina na JJ, sasa kwanini alinidanganya ni muuza vyombo, au ni jambazi ndio maana alinidanganya hakutaka nimjue, lakini mbona mimi nilimdanganya, au alikuwa ananijua toka zamani, lakini alikuwa anazuga kuwa hanijui” maswali hayo ya Veronica yalimfanya aanze kumuogopa kijana huyu mwenye mvuto na kujikuta anachukua simu yake na kuipiga namba ya mchoraji.


Ukweli Veronica anashangaa kuona simu ya mwenyeji wake kijana dereva inaanza kuita, anaimua uso wake kumtazama kijana huyu ambae anaonekana ameachia tabasamu jepesi huku anaendelea kula taratibu na kushushia kinywaji chake pasipo kuhangaika na ile simu iliyokuwa inaendelea kuita. ******


Huko #mbogo_land, mambo yalikuwa mazito, kwa upande wa bwana Dickson Chitopelah, ambae mpaka sasa ni kama alikuwa amesahau kabisa kuhusu jukumu la kuimarisha ulinzi kwenye mipaka ya nchi hii kama alivyo agizwa na mfalme wa nchi hii, maana alionekana akihangaika na kupiga simu kila wakati kuwasiliana na Captain Kobwe ambae ni OC yaani Offcer of Campany, ikiwa na maana ofisa mkuu wa kombania, ambae alikuwa anaongoza msafara wa kuelekea dar es salaam Tanzania, kuongeza nguvu kwa kina Kadumya.


Wakati huo huo bwana Chitopelah ambae kila muda ulivyokuwa unaenda alizidi kuona mambo yanazidi kupanuka, toka kupata fedha kwa bwana James mpaka kuanza kumsaka mzee huyu asifichue siri, pia kumpata binti yake na dereva ambao wanafedha na kuzipata fedha walizo nazo, pia alikuwa anapekuwa simu yake kubwa kuangalia Makala ambazo alimueleza Chiropo azipost, ambazo ndani ya muda mfupi zinaonyesha kuwa zimesomwa na watu wengi, na wengi wametoa maoni ya kuishutumu serikali ya nchi ya #mbogo_land, kwamba haitendi haki kwa wachangiaji, ambao wengi wao sio raia wa mbogo land, β€œbora wabadili uongozi na kuweka uchaguzi huru” hayo ni maoni ya mchangiaji mmoja, huku wengine wakionekana kuwa tofauti kidogo, wamechoka ugari katika amani hao wapuuzi, wajaribu kuandamana waone kama kilicho watokea wenzao huko Libya” maoni hayo haya kumpendeza Chitopelah, ambae kwa lugha ya #mbogo_land jina hilo likiwa na maana ya KIMEELEMEA.


Naam akiwa anaendelea kunywa pombe huku anaperuzi mtandaoni, Chitopelah anaziona habari nyingine za kusisimua zaidi, ambazo anazisoma zaidi ya mara mbili, β€œaskari Deus Nyati, amemteka mtoto wa tajiri James Kervin, β€œhivi ina maana hawa ni kweli hawajui kinachoendelea au wanapanga kufanya jambo fulani?” aliuliza Chitopelah huku anaanza kuvuta kumbu kumbu ya jioni ya leo alipoletewa taarifa ya kwamba kuna askari wanaenda Tanzania kwenye zoezi, na baadae anagunduwa kuwa, hakukuwa na zoezi lolote nchini Tanzania, hivyo kulikuwa na mpango wa operation ya kwenda kukutana na mshukiwa wa uasi wa zamani wa UMD, β€œna kama walianza kufuatilia kabla hata james haja watoroka wakina Kadumya, basi kuna uwezekano wa kwamba, tayari walikuwa na taarifa fulani ya UMD” aliwaza Chitopelah ambae alikuwa na uhakika na vijana wake kuwa watafanikisha kupata fedha za kulipia usafiri wa silaha, na pia watafuta ushaidi kwa kuwauwa James Deus na binti wa mzee James.*******


Naam! nje kidogo ya jiji la dar es salaam, kilomita nne toka kibamba chama, upande wa kusini kando kando ya mtaa wa mloganzila, kwenye barabara moja ya vumbi ambayo ilikuwa katika matengenezo ya kuelekea kwenye kiwango cha lami, iliyokatiza pembeni ya eneo moja kubwa lililokuwa linaashiria kuendelea kwa ujenzi mkubwa katika eneo lile, linaonekekana gari moja la polisi aina ya land rover defender, liliko kuwa limesimama pembeni ya barabara, huku wakionekana askari polisi ambao idadi yao inafikia kumi na moja, kila mmoja akiwa amekaa kwa namna ya peke yake, wapo waliokuwa wamesimama nje ya gari, wengine wakiwa wamekaa juu ya gari wanasinzia, pia wapo waliojitenga pia wapo walio wawili waliokuwa wamekaa ndani ya gari mbele, mmoja seat ya abiria na mmoja kwenye kiti cha dereva wakisinzia.


Naam wakiwa katika mapumziko ya dharula, ambayo wasingeweza kuyafanyia kule barabara kuu, maana ingeonekana ni utegevu wa kazi, huku wanazungumzia umakini na wepesi wa dereva wa BMW, mara ghafla, wanamulikwa na mwanga wa taa za gari, wanapotazama vizuri wanagundua kuwa yalikuwa magari mawili yaliyokuwa yanakuja upande wao, β€œoya kuna wengine wameamua kuja kupumzika huku au?” aliuliza mmoja wao, huku wote wakiwa wanajiweka sawa isionekane kama walikuwa wanasinzia, β€œsidhani, mbona kama sio magari ya polisi hayo” alisema mwingine huku wakiyatolea macho magari yake ambayo bado yalikuwa yameachia taa kubwa pasipo kujihangaisha kupunguza mwanga hata kidogo, β€œhapana huyo sio dereva wa polisi, lazima angepunguza mwanga, hebu wasimamisheni hao” alisema askari aliekuwa amekaa kwenye seat ya mbele ya abiria, hapo askari mmoja akaingia barabarani na kunyoosha mkono juu, akionyesha ishara ya kuwasimamisha wale waliokuwa wanakuja, huku kila mmoja wao akiwaza kuwa wamepata dili la haraka haraka, maana hakuna gari la kawaida ambalo lingeelekea upande huu usiku kama huu, labda kama walikuwa wanasafirisha vitu ambavyo sio halali, na inapotokea Fursa kama hii, lazima mtu aache milion kadhaa, na polisi hawa kugawana kwaajili ya kujipooza kwa uchovu wa kazi ngumu wanazofanya, japo ni kinyume na maadili ya kazi yao.


Naaaam kitu cha kushangaza ni kwamba, magari yale ambayo sasa yalikuwa yamesha wakaribia kwa mita kama arobaini au therasini na tano, ndio kwanza yakaongeza mwendo, kiasi kwamba yule askari akalazimika kuruka pembeni, maana bila hivyo angekutana na kifo kama sio vilema vya kudumu, β€œwashenzi hawa ingieni kwenye gari tuwafukuzie” alisema yule askari wa mbele mwenye cho cha sajenti, na hapo askari wakaanza kuingia kwenye gari kwa haraka, huku magari yale yakiwapita na kutimua vumbi jingi.


Na hapo hata kabla hawajamaliza kupanda kwenye gari ambalo tayari lilisha washwa na dereva wao, mara ghafla wakasikia, β€œpah!! pah! pah! pah! pah!” ilikuwa ni milipuko ya risasi, zilizokuja usawa wao, zikifuatiwa na kelele za maumivu na maugulio, huku askari wakitawanyika kila mmoja alieweza kukimbia kutafuta maficho yake, hakuna aliekumbuka kurudisha mapigo kwa washambuliaji, ambao ndani ya dakika moja, tayari walikuwa wamesha toweka usawa wa macho yao, na ndipo wao walipoanza kukaguana ilikujua hali zao.


Hapo wanagundua kuwa katika kumi na moja waliokuwepo pale, tayari watatu walikuwa wameuwawa, wawili wamejeruhiwa mmoja tumboni na mmoja mguuni, huku gari lao likiwa limetobolewa tairi moja la nyuma upande wa kushoto, hapo hapo kiongozi wao yule sajent anachukua simu ya upepo na kuita msaada kwa kundi lililopo maeneo ya karibu, β€œhallo vituo vyote, hapa ni kituo 16, tunaomba msaada, tumeshambuliwa na farasi wawili wageni, location mloganzila inapojengwa hospital, watatu wapo chini, wawili xray, narudia tumeshambuliwa na farasi wawili wageni, sio yule mweusi, uelekeo ni mloganzila, watatu wapo chini wawili xray, tunaomba msaada wa haraka, farasi wetu wa blue amepigwa mguu mmoja hawezi kutembea” aliongea yule sajent wa polisi kwa kusisitiza.


Hapo wakaanza kusikia majibu β€œnamba saba tupo njiani, kilomita mbili toka kibamba, tupe nguvu ya adui” alisikika mmoja akiongea kwenye redio call, β€œwanasilaha kubwa inakelele sana, inaonyesha wapo wengi wanashambulia kwa pamoja” alijibu sanjent huku wale majeruhi wanapiga kelele za maumivu, β€œnamba 25 tupo nyuma ya namba 7, tunakuja na farasi wawili, washuhulikie na huduma ya kwanza, tunakuja sasa hivi” majibu mengi yalikuwa ni kwamba, wanaelekea eneo lile la tukio. ******


Yap!!! simu Deus inadelea kuita, Vero anamtazama kijana huyu dereva kwa macho ya mshangao na uoga, anajiuliza kama atakuwa ameingia kwenye mikono salama au yupo kwenye hatari kama ile ya mwanzo, au hatari zaidi ya ile ya mwanzo.
Kitu ambacho Veronica hakujua hapo mwanzo ni kwamba, wakati yeye anaingiwa mashaka ya kwamba anae chati nae yupo karibu yake, kumbe tayari Deus alikuwa amesha mtangulia hatua chache mbele, ni baada tu ya kusema kuwa na yeye anaanza kula, na haikuwahi kutokea hata siku moja katika kuchati kwao akasikia pacha wake akisema anakula saa sita za usiku, hapo ndipo alipokumbuka kuwa, wakati ule alipomueleza anaenda kuoga, nae akajibu anaenda kuoga, na pia hata pacha aliposema amememaliza na Veronica ndio alikuwa amemaliza kuoga na kutokea sebuleni, hata wakati ule anaongea na baba yake na kumuona mschana huyu alivyo onekana na ile truck aliyo mpatia, na kujilaumu akamuona anaenda kukaa na kutuma ujumbe na wakati huo huo, ujumbe ukaingia kwake na hapo ndipo Deus alipoa anza kufananisha matukio ya mwanzo toka wapo kule makabe, anakumbuka Veronica aliita John, akimtaja yule mpenzi wake wa bandia, yani Kafulu, Deus anakumbuka kuwa mpenzi wa pacha wake anaitwa JJ, hapo ndipo Deus alipoamua kumfuatilia kwa umakini mwanamke huyu nakuona kuwa Veronica anapokea sms zake.


Veronica anakata simu na simu ya Deus inaacha kuita β€œDoctor Veronica, hupaswi kushtuka wala kuogopa, mimi ndie rafiki yako mchoraji, hatimae leo tumekutana” alisema Deus kwa sauti tulivu huku anainuka na kuelekea kwenye kabati la vinywaji, β€œsamahani kaka, naomba unieleze we ni nani, na unataka nini kwangu?” aliuliza Veronica kwa sauti ambayo kama ungeisikia ungesema anakaribia kujikojolea kwa uoga aliokuwa nao, lakini deus Nyati hakumjari, ndio kwanza alifungua kabati na kuchukua grass moja kisha anarudi nayo mezani, huku uso wake ukiwa na tabasamu β€œmarafiki wenye bahati mbaya, tamaa ya kukutana inaishia kwa mmoja kuogopa sana na mwingine kujawa na furaha” alisema Deus, kwa sauti tulivu lakini yenye utani na kumfanya Veronica abadilike ghafla na kutamani kuangua kicheko, lakini kinaishia njiani na kubakia anamshangaa mtu huyu, ambae wakati wote ni mpole na mtulivu, hata wakati mgumu kama huu β€œacha utani mchoraji naomba uniambie we ni nani na unataka nini kwangu?” aliuliza Veronica, huku anakizuia kicheko kwa kuhofia kucheka mbele ya adui yake.


Deus hakuonyesha dalili ya kujibu swali la Veronica, ndio kwanza akamimina wine kwenye grass ya pili na kumsogezea Veronica, β€œni vyema tukanywa wine kwa pamoja kusherehekea siku yetu ya kukutana, japo najilaumu kwa kuchelewa kukufahamu, ila ningejilaumu zaidi kama ningetimiza mpango wangu wa kutokutana na wewe” alisema Deus, ambae hakuonyesha dalili yoyote kwamba kuna kitu anaficha, au yupo kama vile ambavyo Veronica anawaza, β€œkaka unaweza kunieleza wewe ni nani jamani, huoni kama unanitisha mwenzio?” alisema Veronica huku anapokea grass toka kwa Deus, na kuishikilia mkononi kama vile amepewa sumu, β€œdoctor, ulizaliwa hospital gani huko mbogo land” swali la Deus linamshtua zaidi Veronica β€œqueen Taus hospital, lakini umejuaje kama nilizaliwa #mbogo_land” aliuliza Veronica, ambae uraia wake ulikuwa ni kati yake na wazazi wake ambao waliondoka mbogo land miaka mingi iliyopita,


Deus anatabasamu kidogo, kisha anakunywa kidogo wine yake na kumtazama Veronica usoni, ambae anamuona bado ameshikwa na mshangao, yeye anatabasamu kidogo, β€œDoctor, kitu ambacho hukijui ni kwamba mimi na wewe ni zaidi ya tulivyodhania” alisema Deus kwa sauti tulivu ya upole, huku tabasamu la furaha likionekana usoni, furaha ambayo inamshangaza Veronica, ambae bado ana maswali mengi kichwani, β€œkivipi, wakati siku zote tumekuwa tukidanganyana majina, ina maana wewe unanifahamu toka zamani?” anauliza Veronica, huku anaweka glass mezani.... ENDELEA Mdau



NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA ISHIRINI NA MOJA
MTUNZI: Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA ISHILINI:- Deus anatabasamu kidogo, kisha anakunywa kidogo wine yake na kumtazaama Veronica usoni, ambae anamuona bado ameshikwa na mshangao, yeye anatabasamu kidogo, β€œDoctor, kitu ambacho hukijui ni kwamba, mimi na wewe ni zaidi ya tulivyo dhania” alisema Deus kwa sauti tulivu ya upole, huku tabasamu la furaha likionekana usoni, furaha ambayo inamshangaza Veronica, ambae bado anamaswali mengi kichwani, β€œkivipi, wakati siku zote tumekuwa tukidanganyana majina, ina maana wewe unanifahamu toka zamani?” anauliza Veronica huku anaweka glass mezani. ENDELEA…


Deus yeye anabugia mvinyo na kuongeza mwingine kwenye glass, huku bado tabasamu limetawala usoni mwake, β€œkwanza kabisa tumezaliwa siku moja, ndani ya nchi moja, na katika hospital moja” alisema Deus, japo sauti yake ilikuwa tulivu, lakini ilionyesha furaha ya wazi, β€œkwahiyo wewe ni askari toka mbogo land, bado munamfuatilia baba yangu?” aliuliza Veronica kwa sauti mshangao wenye kuchukia, hapo Deus anakataa kwa kichwa, huku anachukua glass ya wine na kuiweka mdomoni, anapiga funda na kuweka mezani, β€œsasa wewe ni nani?” aliuliza Veronica ambae bado hakuwa na amani kabisa, β€œmimi naitwa Deus Nyati ni mtoto wa askari wazamani wa MLA, ambae ni kama baba yako, nae alikimbia nchi baada ya kusingiziwa kuwa ni muasi wa UMD” alisema Deus na kuweka kituo kidogo, japo ilikuwa ni kwaajili ya kunywa wine na kuongezea nyingine, lakini pia alitoa nafasi kwa Vero kushangaa.


Baada ya kumeza funda moja Deus akaendelea, β€œpia mimi ni askari wa zamani wa jeshi la Tanzania, kama uliwahi kusikia nilifukuzwa jeshi miezi mitatu iliyopita” alisema Deus, na hapo Veronica akadakia β€œhapana sio wewe, Deus Nyati niliemsikia aliachishwa jeshi akitokea congo vitani, wakati wewe ulikuwa hapa dar es salaam wakati wote” alisema Veronica akipingana na Deus, β€œhukumbuki na wewe ulikuwa Mbeya chuoni?” alisema Deus na hapo Veronica kikamponyoka kicheko, β€œsawa bwana haya endelea kunisimulia” alisema Veronica huku anachukua glass na kuiweka mdomoni na kupiga funda moja, kisha akabakia ameishikilia wine,k huku anakunja nne na kufanya hips zake zizidi kuonekana vyema na kumtamanisha Deus, β€œsikuweza kutoa utambulisho wangu kwako, kwasababu ya kazi nyeti niliyokuwa naifanya, pili niliamini kuwa utakuwa ni Rafiki wa muda mfupi na urafiki wetu utaishia mtandaoni, ukichukulia nilidhania kuwa ni kweli tupo mbali mbali” alisema Deus na hapo Veronica akacheka huku Deus akiishia kutabasamu, β€œsasa je ningekuambiaje kwamba mimi ni mtoto wa James Kervin, mwenzako napata usumbufu wa wanaume kama nini?” alijitetea Veronica, kwa kueleza sababu ya kudanganya utambulisho wake, β€œsio mbaya, leo kila mmoja amemfahamu mwenzie” alisema Deus kwa sauti ya upole lakini sasa ilianza kuchangamka.


Veronica ambae haamini macho yake kwa kumuona mwanaume huyu, mwenye muonekano mzuri wa kuvutia kwamba ndie yule mtembeza biashara aliekuwa anachati nae siku zote na kumfanya mtu wake wa karibu, nandie walie kubaliana kuwa, endapo JJ asipokuwa sahihi, kwake, basi mchoraji wake ndie angemuoa, β€œLakini Deus, baba amejuaje kama nipo na wewe, kwani mnafahamiana nae” aliuliza Veronica huku wakiendelea kunywa wine, β€œbaba yako nimekutana nae leo kwa mara ya kwanza, na kitu ambacho unapaswa kukijua ni kwamba, wewe na baba yako mupo kwenye mkasa mmoja” alisema Deus na kumfanya Veronica ashtuke kidogo, β€œunamaana gani Deus?” ulikuwa ni mstuko wenye hofu, β€œwaliokuteka wewe ndio waliomteka baba yako hapo mwanzo” alisema Deus na kumsimulia Veronica jinsi ilivyokuwa, kuanzia alivyomuokoa mzee James na kumfikisha nyumbani, kisha kumlipa elfu moja ya #mbogo_land, β€œkwahiyo baba alivunja sheria za Dereva?” aliuliza Veronica huku anacheka kwa furaha, β€œdah! sijui nikikutana nae itakuwaje, maana nilimtolea macho kisha nikaondoka zangu” alisema Deus akionyesha kujutia kile alichokifanya, shauri yako umemkorofisha mkwe wako….” alisema Veronica na kujikuta akisita ghafla na kumtazama Deus usoni, huku akionyesha wazi kujishtukia.********


Yap!!! magari manne ya polisi yanaingia kwenye eneo la tukio pale karibu na eneo panapojengwa hospital ya mloganzila tawi la muhimbili, β€œwameelekea wapi hao?” anauliza askari mwenye cheo cha nyota tatu aliekaa seat ya mbele ya gari la kwanza, β€œwameelekea huku mbele, dakika tatu zilizopita” anasema yule sajent, wakati huo askari wa gari la nyuma kabisa wanashuka toka kwenye gari lao kuanza kupakiza miili ya askari watatu pamoja na kuwasaidia wale majeruhi kupanda kwenye gari, β€œbadilisheni tairi, hao wengine wapelekwe hospital, sisi tunaenda kuwa fuata” alisema yule ASP, na hapo gari linaondoka huku likifuatiwa na mengine mawili, wakiwaacha wenzao wanasaidia kuondoa majeruhi na marehemu na kubadili tairi la gari.


β€œHallow taarifa kwa vituo vyote, kituo namba saba na ishirini na tano tunafukuzia farasi wapya, ulekeo kisopwa na rudia, uelekeo kisopwa, nguvu zaidi inahitajika” alisema yule askari mwenye nyota tatu na hapo vituo vingine vikaanza kuitikia, vikionyesha kuwa na wao walikuwa njiani kuelekea upande huo uliotajwa, huku mawasiliano hayo yakidakwa na redio nyingi sana za vyombo vya ulinzi na usalama vya hapa jijini dar es salaam.


Naam!!! dakika mbili na nusu baadae, wakiwa wamesha tembea kilomita tatu kasoro, tayari magari haya yaliyopanda na kushuka milima na mabonde kwenye barabara mbovu, sasa kwa mbali sana, kiasia cha kilomita kama nne mbele yao, waliweza kuona taa nyekundu za nyuma ya magari mawili zikipotelea kwenye misitu ya kisopwa upande wa relini, β€œongeza mwendo bado tupo nao mbali sana” alisisitiza ASP, na dereva akaongeza mwendo huku wenzao wakazidi kufuata kwa speed ile ile ya gari la mbele. *****


Huku porini wawili hawa, walio sahau vita na kuzama kwenye maongezi, walikuwa bado wamepigwa na mshangao mtamu, Kufuatia ile kauli ya Veronica, β€œmkwe?” aliuliza Deus, kwa sauti fulani ya utani, japo kiukweli moyoni mwake Veronica alivutiwa na kijana huyu mwenye muonekano wa kuvutia, lakini hakutakiwa kusema hivi, hata hivyo akapata jibu, β€œnatania tu, kwani hukumbuki tulicho kubaliana endepo JJ nae angekuwa mwanaume wa ovyo” alisema Veronica na wote wakacheka kwa pamoja, lakini huku wanaonena aibu, β€œpangine ilikuwa ni bahati yangu, ndio maana wote uliokutana nao wakawa hawakufai” alisema Deus, ni kama wote walisha sahau vita iliyopo mbele yao, maana walionekana kuongea na kucheka kwa furaha, β€œtena nimekumbuka, hivi ulijuaje kama JJ anasema uongo” aliuliza Veronica, ambae sasa macho yake hayakubanduka usoni kwa Deus.


Swali hilo linamfanya Deus atabasamu huku anainua uso wake kumtazama Veronica ambae anatabasamu pia na kuzidisha uzuri wake, ambao unazidi kumtamanisha Deus Nyati, β€œunadhani kuna mwanaume ambae anaweza kuvumilia kukuona ukiwa mtupu mbele yakebna kuishia kushikan shikana?” aliuliza Deus, na kumfanya Veronica achie tabasamu lenye mchanganyiko wa aibu, β€œkwanini bwana, mbona kawaida tu” alisema Veronica huku anaweka glass mezani, kisha anainuka toka alipokaa, huku kishati alichovaa, kikiinuka kidogo na kuacha wazi, sehemu ya tumbo, macho ya Deus yanatua eneo lile lenye tumbo dogo, huku akipata kuona kitovu cha mwana dada kilicho tumbukia ndani pamoja na pindo ya chupi ya mwanamke huyu ambayo ni kama inazidi kumfanya awe mtamu kimapenzi, kiasi cha bwana kaka kujikuta akiamsha dudu, β€œbado hatujamalizana, ngoja kwanza niende chooni” anasema Veronica, huku anaelekea upande wa chumba chake na Deus anamsindikiza kwa macho, ambayo yana tazama eneo la kiuno kushuka chini, kwakweli ni hatari na nusu, yani Deus anashuhudia makalio ya mwana dada huyu jinsi yanavyo tikisikika kwa namna ya kipekee na kupendeza na kutamanisha pia.


Ni kama Veronica anajua kuwa anatazamwa, maana anapokaribia mlango wa chumba alichopewa na mwenyeji wake anasimama na kugeuka, anamtazama mwenyeji wake ambae leo anagundua kuwa ni Rafiki yake wa muda mrefu, macho yao yanakutana, wote wanatabasamuliana, β€œmchoraji hebu acha utundu” alisema Veronica kwa sauti yenye utani, wote wacheka kidogo, huku Veronica ambae macho yake yalishanza kulegea kwa kilevi, anafungua mlango na kuingia chumbani. *******


Yap! taarifa ya shambulizi la kunuwia lililofanywa na magari mawili aina ya land rover puma lina enea kwa kasi kila kona ya jiji la dar es salaam, hasa kwenye ofisi za vyombo vya ulinzi na usalama, watu wanataka kushawishika kuwa dereva wa BMW anahusika na shambulizi hilo, lakini upande mwingine inakuwa ni vigumu kuamini, β€œgari kama hilo lilionekana pale sisterfada hotel wakati wa shambulizi” alisema mmoja kati ya wajumbe waliokuwa katika kikao cha dharula cha usiku huu ndani ya ofisi ya mkuu wa jeshi la polisi, β€œndiyo ni kama haya, tena moja wapo ndilo ambalo waliondoka nalo wale UMD waliofanya jaribio la kumteka bwana James” anasema mkuu wa kitengo cha fird force, β€œkwahiyo hawa UMD wameamua kututukana kabisa, sasa lazima watu hawa wakamatwe haraka sana na ikiwezekana wauwawe kabisa” alisema CGP, kwa sauti iliyoonyesha kuchukizwa na kukasirishwa.


CGP hakuishia hapo, anamtazama mkuu wa polisi kanda ya dar es salaam, β€œhakikisha unaenda kusaidiana na makamanda mikoa kusimamia huo msako, sitaki ionekane tumeshindwa kazi mpaka jeshi la ulinzi lije kusaidia, hakikisheni hao wajinga wanapatika hai au wamekufa hiyo haina umuhimu, cha msingi jambo hili liishe kabisa, maana sisi hatuna mahakama ya kuwapeleka hao washenzi” alisema CGP, na hapo kamanda wa polisi kanda maalumu ya dar es salaam akainuka na kupiga salut, ndiyo afande, alisema na kugeuka kisha akaelekea nje ya ukumbi huku anatoa simu yake nakupiga kwa makamanda wa mikoa ya kipolisi ya dar es salaam, ambao wengi walikuwa maofisini wanaongoza msako kwa kutumia redio call, mwisho akampigia bwana Ulenje.*******


Naam!! dakika tano zilitumika, kwa Veronica kumaliza haja ndogo yake na kutoka nje ya chumba akirudi sebuleni, huku uso wake ukiwa umejawa na tabasamu, macho yakionekana kulembuka kwa wine aliyokunywa, β€œmchoraji, mimi nina ombi moja usiku wa leo” alisema Veronica huku anamsogelea Deus pale kwenye kochi, β€œsawa nakusikiliza doctor” alijibu Deus, huku anamtazama Veronica ambae alikuwa anajichekesha, β€œusinitazame bwana nitashindwa kukueleza” alisema Veronica huku anacheka kicheko kitamu kilicho gubikwa na aibu, β€œhaya sema” alisema Deus huku anatazama pembeni, β€œhaya! ombi langu ikiwa ni siku yetu ya kwanza kukutana na siku moja baada ya siku yetu ya kuzaliwa naomba nikae kochi moja na wewe” alisema Veronica huku anajichekesha, wakati huo huo bila kusibiri kukubaliwa tayari alishakaa kwenye kochi la watu wawili alilokuwa amekaa Deus.


β€œok! nipe sheria zako, wakati wakutekeleza ombi lako ambalo limesha tekelezwa kabla ya kukubaliwa” alisema Deus, kwa sauti tulivu huku anamtazama Veronica, ambae alitazama juu kama vile anawaza jambo, kisha akamtazama Deus kama vile anataka amueleze lakini anaonekana kushindwa, β€œusinitazame sasa, si nimekuambia kuwa ukinitazama nashindwa kukueleza” anasema Veronica kwa sauti ya kudeka huku anaziba uso wake kwenye kifua cha Deus, haya sikutazami, niambie sasa” alisema Deus huku anasikilizia matiti ya binti huyu mrembo yakigusa eneo lake la mapajani, β€œsheria ya kwanza, kuna ile sheria yako sijui namba ngapi, ila inasema hivi hakuna kufungua mzigo” alisema Veronica huku anajichekesha, wakati huo alikuwa anahisi dudu ya kijana huyu ikijitutumua na kumgusa kwenye matiti yake magumu, β€œok! ni sheria namba kumi hiyo, nipe nyingine kama unayo” alisema Deus, huku akijitaidi kuzuia dudu yake isiendelee kujitutumua, β€œile sheria yako uliyo mwambia JJ ameivunja, hakuna kutumia bunduki, na wewe usitumie bunduki yako” alisema Veronica, huku anapenyeza mkono kwenye uvungu wa kifua chake na kugusa kitu kigumu kilichokuwa kinagusa matiti yake, Veronica anashtuka na kutoa mkono, kisha anajiondoa kifua kwa Deus, β€œvipi mbona umeshtuka?” Deus anauliza kama vile hajui kilicho msibu pacha wake ambae anatazama chini kwa aibu, β€œmbona tayari imesimama?” aliuliza Veronica kwa sauti iliyojawa na aibu na mshangao, β€œkinini hicho kilicho simama?” anauliza Deus kwa sauti yenye utani ndani yake, β€œsi hiyo bunduki yako” anasema Veronica kwa sauti iliyo jaa aibu, huku anaonyesha kwa kidole, usawa wadudu ya Deus, β€œwala usijari si umesma hakuna matumizi ya silaha... hahahahaaaa hawa wapuuzi watafika asubuh salama hawa? Unataka kujua nini kitatokea? Basi ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
Chochote na ziada πŸ˜…
Saf sana mkuu,πŸ‘πŸ‘πŸ‘

Ila kipande Cha UMD umetuminya zaidi,
Maana umetupitisha site kwa Kasi sana ajabu kuna mafala tayali tumewala vichwaaπŸ€£πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ€£πŸ˜…πŸ€£πŸ˜…πŸ€£πŸ˜…πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ‘πŸ‘πŸ€£πŸ˜…πŸ˜…
 
Saf sana mkuu,πŸ‘πŸ‘πŸ‘

Ila kipande Cha UMD umetuminya zaidi,
Maana umetupitisha site kwa Kasi sana ajabu kuna mafala tayali tumewala vichwaaπŸ€£πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ€£πŸ˜…πŸ€£πŸ˜…πŸ€£πŸ˜…πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ‘πŸ‘πŸ€£πŸ˜…πŸ˜…
Ha ha ha mumeshika serikali makalio subirin cha moto
 
Samahani mkuu nilionja mvinyo kidogo wakat naandikaπŸ‘‰πŸ€£
🀝🀝🀝🀝🀝 Mpaka tupindue utawala kaka au vpπŸ€£πŸ˜…πŸ€£πŸ˜…πŸ€£πŸ˜…πŸ˜œπŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ˜…

Naona UMD mwenzangu umechanganikiwa mapemaπŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ˜‚πŸ˜­πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜…πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£
 
🀝🀝🀝🀝🀝 Mpaka tupindue utawala kaka au vpπŸ€£πŸ˜…πŸ€£πŸ˜…πŸ€£πŸ˜…πŸ˜œπŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ˜…

Naona UMD mwenzangu umechanganikiwa mapemaπŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ˜‚πŸ˜­πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜…πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£
Yaani sifa zote za Deus ninazo mimi hapa 😎
 
Yaani sifa zote za Deus ninazo mimi hapa 😎
Kuwa makini tutakukula kichwa soon,
[πŸ˜…πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€£πŸ€£UMD]
 
Back
Top Bottom