mhanuzi wangu
Senior Member
- Dec 18, 2024
- 125
- 72
Mida yake ndiyo hii.Anaitikia kuwa anaweka alafu haweki, haaminiki hata kidogo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mida yake ndiyo hii.Anaitikia kuwa anaweka alafu haweki, haaminiki hata kidogo.
Wacha tuone..Mida yake ndiyo hii.
Sema jamaa anatugalagaza vibaya mno, familia wanachapika kiboya sana🤣😂😂😂😂UMDWacha tuone..
Wapi mkuuúu😭😅😂🤣Poleni jaman kuna mambo naweka sawa kisha tunamalizia simuliz yetu
Kuna jamaa zangu hapo naona wanawaza usiku wa mapacha unapitaje pitaje yaan kila mtu atalala kwake au inakuwaje 😂
Jamaa zangu wakina Che mittoga Mmea Jr
Hakika nafsi yangu kidogo imeridhika mana toka jana sikupata usingizi nikisubir vigongo vishuke hatimae umeleta mchana huu vipi usiku vitakuja vingine au ndio mpaka kesho mkuu🫣🫣🫣NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA ISHIRINI NA TATU
MTUNZI: Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA ISHIRINI NA MBILI:- “mchoraji” aliita tena Veronica kwa sauti ya kivivu yenye kuonyesha kusisimkwa, “naaam!!! pacha wangu” aliitikia Deus kwa sauti tulivu nzito yenye kuanza kuelemwa na kiu ya bumuunda, (andazi lililotengenezwa kwa ndizi na unga wa maindi) huku anamtazama Veronika ambae alikuwa amefumba macho kama anaesikilizia kitu fulani kinacholeta uroda kwenye mwili wake, “kwani inaruhusiwa kupapasa mzigo?” aliuliza Veronica, kwa sauti ile ile, ambayo sasa iliongezeka kicheko cha kivivu chenye aibu ndani yake. ENDELEA…
Deus anatabasamu kidogo, maana swali hili ni kama la mwanzo, lakini hakutakiwa kutoa jibu linalofanana na lile la mwanzo, “yah! inaruhusiwa, nitapimaje uzito bila kupapasa” alijibu Deus kwa sauti ile ile nzito huku anachukuwa grass ya wine toka mezani na kumpatia Veronica ambae anajiweka sawa kidogo, “asante mchoraji wangu” alisema Veronica kwa sauti iliyo lainika, huku anapokea grass, kisha anainywa kidogo na kumpatia Deus, huku anamtazama usoni kwa macho yaliyolegea, wote wanatabasamuliana kivivu, huku Veronica anarudisha kifua chake kwenye mapaja ya Deus na kulala kama alivyo lala mwanzo, Deus nae anaiweka grass mezani na kuchukua ya kwake, anakunywa kidogo na kuirudisha mezani, kisha anendelea kufanya alichokuwa anakifanya mwanzo, safari hii akienda mbali zaidi, maana alikuwa anacheza eneo kubwa la mwili huu ulioumbika wa mwana dada mrembo Veronica, ambae hata yeye mwenyewe alishangaa kumzoea kwa haraka kijana huyu, pangine sababu ni marafki wa muda mrefu.
Maana Veronica akiwa amelala kifudi fundi kwenye mapaja ya kijana huyu, huku kitu kigumu mfano wa tango au ndizi ya mkono wa tembo, kikiwa kimebanwa na matiti yake juu ya kifua anasikilizia mitekenyo ya kijana huyu, ambae kwa muda mfupi aliomfahamu amegundua kuwa, anatabia zote kuu za duniani, yani upande mmoja akiwa muuwaji wa hatari, lakini pia ni muokoaji mkubwa, upande mwigine akiwa ni mpiganaji mwenye uwezo mkubwa wa kupigana, lakini upande mwingine ni mtetezi na mlinzi wa nguvu mwenye kuaminika, kiasi unaelindwa unafaa kujivunia na kujiona upo sehemu salama, ni mtu ambae licha kuwa na roho ngumu ya kikatili, lakini anahuruma kubwa sana na kupenda kusaidia mtu mwenye kuhitaji msaada bila kujiuliza mara mbili, ukiachilia kuwa mtu mwenye kusimamia sheria zake na kuwa mlinzi wa usalamana sheria za nchi, pia ni mvunjaji wa sheria za nchi kwa shughuli anazo zifanya, huyu huyu mmoja licha ya kuwa na sura na sauti za upole lakini ni mwenye hasira na mkatili ajabu.
Ambae sasa alitumia mikono yake miwili, kumkanda kanda Veronica, ambae aliona mikono ya kijana huyu ikishuka mpaka kwenye makalio yake na kuanza kuyaminya minya taratibu, “choraji vipi nguo yako imenipendeza eehn?” aliuliza Veronica, ambae alijua wazi kuwa kwa jinsi umbo lake lilivyo, na uvaaji aliouvaa, ambao hata nyumbani kwao huwa hathubutu kuvaa namna hiyo, lazima kijana angekuwa katika hali tata, “sanaaaa, mpaka naionea wivu hii truck kwa jinsi ilivyokukamata” alijbu Deus ambae hakuacha kukanda kanda makalio ya mwanadada huyu, ambae nae alizidi kujilegeza na kutoa ruksa ya miminyo ifanyike vyema, wote wanacheka kivivu.
Deus Hakuishia hapo, anashusha mikono yake mpaka mwisho wa makalio, ndipo yanapoanzia mapaja, anatumia vidole gumba kukanda paja la ndani, anafanya kama anazungusha, hapo ni kama kuna kitu kinamkuta Veronica ambae anatanua kidogo mapaja yake, huku vidole vya miguu yake vikikosa utulivu, hata pumzi ya mihemo ya mwanamke huyu, ilianza kusikika wazi wazi sambamba na vijisauti ya kulalamika fulani ya “mh! mh!” hata wakati mwingine Veronica alionekana akikaza makalio yake kusindana na kile alichokuwa anakipata wakati ule.
Sijui kama Deus alikuwa hajuwi anacho kifanya, au alifanya makusudi kile alichokifanya, maana licha ya hayo yote, lakini bado aliendelea kupekecha sehemu hiyo ya mapaja manene ya Veronica, akizidi kushusha vidole vyake mpaka kwenye vungu za mapaja haya, kama kuna kitu alikusudia kukigusa kule uvunguni, “mchoraji” aliita Veronica kwa sauti ya mgonjwa mwenye hali mbaya, “naaaam pacha wangu” aliitikia Deus kwa sauti nzito, tulivu kama ya msimuliaji wa hadithi za mbogo edgar, “kwani…. Kwani… inaruhusiwa ku…kufanya hivi?” aliuliza Veronica kwa sauti ile ile ya tabu, huku anasikilizia vidole vya mchoraji wake, ambavyo kila vilivyo zungushwa kwenye mapaja katika vungu za mwanamke huyu mrembo, vidole vile vilikuwa vinakandamiza mashamvu ya kitumbua kile ambacho ungesema mpikaji aliweka vijiko viwili baada ya kimoja, yalisuguana na kuvinyanga kunde iliyomea kwenye shamba hili la bibi na kuifanya ilowe maji yenye utelezi yaliyo lowesha shamba lote, mpaka lile bonde la kati kati likawa na unyevu unyevu mwingi sana kiasi cha kufaa kuchomeka muhogo kama pando la msimu.
Swali la Vero lililotoka katika hali ya msisimko na miugulio ya utamu, lilikuwa jepesi kwa Deus, ambae aliamua toa jibu ambalo lilijaa mtego, “hailuhusiwi, vipi niache?” aliuliza Deus, huku anasitisha kuzungusha vidole vyake kule uvunguni, “hapana endelea hiyo sheria tunaifuta” alisema Veronica akionekana kutokuwa na utani hata kidogo juu ya kile alichokisema, hapo Deus akaendelea taratibu huku Vero akizidi kujilegeza na kutanua mapaja yake kuachia nafasi kwa mikono ya Deus iweze kupenya vizuri uvunguni, “kumbe inawezekana kufanya bila kuingiza” ilimchomoka Veronica bila kutegemea, huku Deus akitabasamu na moyoni anajisemea “nani alisema chakula kitamu kina liwa kwa macho” *********
Naam! Wakiwa wameshafika kwenye reli ya kati, na kuanza kuambaa ambaa pembezoni mwa reli, Kadumya na wenzake ambao tayari walikuwa wameikuta barabara yenye uafadhali, waliongeza mwendo ili polisi ambao sasa walionekana kwa mbali sana wasiweze kuwakuta, “sasa tume chokoza nyuki, lazima jeshi zima litahamia huku kutusaka” anasema Kadumya huku anatoa simu yake na kubofya sehemu ya namba zilizo pigwa, “lakini hatukuwa na namna, maana tungesimama wale washenzi wangeona huu uchafu (akimaanisha ile miili ya wale askari wake) na hapo ingeukwa tatizo kubwa sana” alisema Kadumya, huku anakagua namba za simu na kuipiga namba ya captain Kobwe, ambayo haikuwa mbali sana.
Simu inaita kidogo, kisha inapokelewa, “ndiyo mkuu, habari ya huko” alisikika captain Kobwe, toka upande wa pili wa simu, sauti ambayo ilionyesha wazi alikuwa kwenye gari lililopo kwenye mwendo wa kasi sana, “mmefika wapi kwa sasa?” aliuliza Kadumya, “kwa sasa mkuu, tunaikaribia Nangurukulu, lengo letu baada ya masaa manne tuwe tumeshaingia dar es salaam na kukutana na nyie” alisema Kobwe.
Japo ndiyo hali halisi, lakini bado Kadumya aliona kama vile ni muda mwingi sana, “Kobwe jitahidini bwana, si unajua kuwa lazima tufanikishe kupata fedha usiku huu ili tuondoke hapa Tanzania, na isitoshe sasa hivi tumeanza kuandamwa na polisi, tunahitaji sana msaada wenu” alisema Kadumya, na wakati huo huo akasikia simu yake inatoa mlio fulani wa kiashirio cha kuwa kuna simu inataka kuingia, “usijali mkuu, tumekuja na silaha nyingi sana, hakuna mtu atachomoka hapo” alisema Kobwe kwa kujinasib, “sawa, kata simu nipokee simu nyingine” alisema Kadumya, na kweli Kobwe akakata simu, na hapo ikaonekana simu ya Ulenje ikiwa inaingia.
Hapo moja kwa moja Kadumya akajuwa kuwa tayari anakuja kupewa taarifa za tukio la shambulizi walilo lifanya muda mfupi uliopita, akaipokea na kuiweka sikioni, “niambie Ulenje, kuna jipya huko?” aliuliza Kadumya kwa shauku, “tayari mmesha likoroga, jeshi lote la polisi lina elekea misitu ya kisarawe, kwani mpo wapi sasa hivi” aliuliza Ulenje, “tunakaribia kwenye makutano ya reli na barabara ya kisarawe tunatafuta maficho ili tuwasubiri wenzetu ambao wapo njiani wanakuja kutusaidia kumsaka huyu bwana mdogo na huyu binti wa James, maana bado wanafedha yetu” alisema Kadumya, wakati huo walikuwa wanaiona barabara inayotoka kibaha kwenda kisarawe, “sawa fanyeni haraka sana, mkiikuta barabara ya kisarawe nendeni kushoto mpaka muikute ile Maneromango, halafu muende kulia mukatafute maficho, mkihitaji msaada nipigieni haraka, mimi na makamanda wengine tupo njiani tuna elekea huko, kwahiyo kuweni makini sana” alisisitiza Ulenje kabla ya kukata simu.******
Naaam sasa twendeni mbogo land, ambako kikundi cha ARR, kama wenye we wanavyo ita A dubble R, kwa maana ya Amoured Recce Regiment, chenye namba 91, na vishikizo vyake, kwamaana ya vikikosi vidogo vidogo kama kile cha fuvu la simba, mambo yalikuwa moto moto, watu walikuwa na pilika kama vile mchana, ofisi ya uchunguzi na utambuzi wa usalama wa ndani, tayari walikuwa wamesha hangaika sana kusaka orodha ya watu waliohusika katika msako wa waasi ndani ya serikali, lakini hawakufanikiwa, licha ya kutumia watu wao waliopo vitengo mbali mbali ndani ya jeshi na serikali kwa ujumla, lakini kitu cha kushangaza hapakuwa na hata nyaraka moja iliyosalia inayo wahusu askari MLA na mawakala wa MLSA walioshiriki katika msako huo wa mwaka 1992, operation ambayo ilichangia kuondoa watu wengi muhimu katika nchi, ikiwa majeshini na kwenye vyombo vingine vya ulinzi na usalama, pia ilimhusisha Tajiri James Kervin.
“Jamani tumehangaika vya kutosha kupata hii orodha bila mafanikio, lakini tume bakiza sehemu moja tu, nayo ni ikulu” alisema luten Mahadhi Salum, aliepewa kazi ya kusimamia jukumu hilo nyeti la kutafuta wahusika wa operation tokomeza wahaini, “afande ni hatari sana kuchunguza ikulu, maana mfalme akijua tutaingia kwenye kosa la kutokuwa na Imani na king Euge, lakini tuna mfahamu Chitopelah, aliekuwa nsimamizi wa zoezi hilo, kwanini asitupatie majina ya watu wachache waliohusika na msako ule” alishauri koplo Michael, ambae alikuwa katika kikundi cha uchunguzi, “hilo wazo zuri, inabii tuongee na afande Six ili afanye utaratibu wa kumpata Waziri na kufanyanae mahojiano, si unajua kwa sasa yeye ni mheshimiwa” alisema luten Mahadhi, pasipo kujuwa wanae mkusudia, ndie mtu hatari zaidi ya hatari yenyewe kwa usalama nchi na jukumu lao siri.*******
Naaam! nadhani sasa ni wakati mzuri wa kurudi kule mdidimua, ambako tuliwaacha vijana hawa wawili walio kuwa wanavunjiana sheria walizo ziweka wao wenyewe, ambao sasa hivi bado tuna wakuta wakiwa vile vile, yani Veronica amelala mapajani kwa Deus, amejilegeza kweli kweli akisikilizia utamu wa kupekechwa kunde ya shamba la bibi, huku akitamani kufanyiwa kitu zaidi ya vile anavyo fanyiwa, akihisi kwamba kuna utamu mkubwa sana upo mbele yake, lakini kabla hajafikiria kumshawishi Deus, wote wanashtuliwa na mlio wa simu ya Veronica……. ENDELEA MSOMOJI WANGU.
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA ISHILINI NA NNE
MTUNZI: Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA ISHILINI NA TATU:- Naaam! nadhani sasa ni wakati mzuri wa kurudi kule mdidimua, ambako tuliwaacha vijana hawa wawili walio kuwa wanavunjiana sheria walizo ziweka wao wenyewe, ambao sasa hivi bado tuna wakuta wakiwa vile vile, yani Veronica amelala mapajani kwa Deus, amejilegeza kweli kweli akisikilizia utamu wa kupekechwa kunde ya shamba la bibi huku akitamani kufanyiwa kitu zaidi ya vile anavyo fanyiwa, akihisi kwamba kuna utamu mkubwa sana upo mbele yake, lakini kabla hajafikiria kumshawishi Deus, wote wanashtuliwa na mlio wa simu ya Veronica……. ENDELEA…
Deus anataka kuichukuwa ile simu lakini Veronica ana mzuia mkono, kwamba anendelee kufanya kile alichokuwa anamfanyia, na kiukweli alikuwa amenogewa kweli kweli, “mchoraji kweli haiwezekani, naona kama nashindwa, haiwezekani bila kufanya, yani najisikia raha unavyo nifanya hivi” alisema Veronica kwa sauti iliyo zidiwa kweli na kiu ya kitu fulani. ******
Naaam, huko #mbogo_land mambo yalikuwa yanazidi kusonga mbele, major Gen Six anapigiwa simu toka kikosi kidogo cha Lion Skull, fuvu la simba, mpigaji akiwa ni canal Jastin Johnson CO wa kikosi cha uchunguzi cha Lion Skull Base, akaipoea na kuiweka sikioni, wakati huo alikuwa ofisini kwake na watu watatu, nao wakifuatilia habari na matukio yanayoendelea huko Tanzania, “ndiyo Jastin, kuna jipya lolote?” aliuliza major General Sixmund, “mkuu ukweli jipya ni mambo ya kushangaza sana, hatujafanikiwa kupata nakara hata moja ya orodha ya askari waliohusika katika operation ya kutokomeza wa haini nchini” alisema kanali Jastin na kumshangaza kidogo Major Sixmund, “inawezekana vipi, wakati kila kitu kipo kwenye mpangilio wa computer” aliuliza Major general Sixmund kwa sauti ya mshangao “mkuu inaonekana huo ulikuwa ni mpango wa muda mrefu, na kuna mtu aliifuta ilikufanya uchunguzi kuwa mgumu” alijibu kanali Jastin Jonhson, CO wa kambi ya jeshi ya fuvu la simba, “unachosema kinaweza kuwa kweli, maana sio tu hatuwezi kufanya mahojiano na Chitopela, ila ni kwamba hatakiwi kujua kabisa kama tunaitafuta ile orodha” alisema Major general Sixmund, sasa ulikuwa unashaurije kanali, maana ni lazima tupate hiyo orodha?” aliuliza Sixmund, “mkuu najua licha ya kukosekana kwa orodha hii sehemu zote, lakini lazima itakuwepo kwenye ofisi ya nyumbani kwa mfalme” alisema kanali Jastin hakuwa na maana ya kwamba yeye Sixmund afanye mpango wa kuipata tokea huko.
Japo niliona kuwa itakuwa ngumu kidogo kuomba nyaraka kwenye ofisi ya nyumbani kwa mfalme, lakini major general Sixmund aliona kuwa, hakuwa na budi kufuatilia orodha hiyo, ambayo ni kweli kabisa, sehemu ya mwisho ambayo kwa vyovyote inaweza kupatikana ni golden house, “sawa nitawasiliana na mfalme mwenyewe, japo inahitaji busara na akili nyingi sana kumueleza swala hili, vinginevyo anaweza kuchukulia kuwa tunakosoa teuzi ya mfalme Eugen” alisema Sixmund kabla ya kukata simu na kubofya namba nyingine ya mfalme wa nchi hii ndogo na tajiri inayotamaniwa na matajiri wakubwa duniani.*******
Nyumbani kwa mzee James Kelvin, ambae sasa alikuwa na familia yake na askari kumi na nne wa MLA yani #Mbogo_Land Army, wenye mafunzo makubwa ya mbinu za kivita na uchunguzi katika uwanja wa vita pamoja na luten Jimmy Stuart wa jeshi la Tanzania, ambae alikuwa anaongoza platoon moja iliyokuwa inaendeleza ulinzi nje ya uzio wa nyumba ya tajiri James Kelvin kuimarisha ulinzi, “kwanini dada Vero hataki kusema sehemu alipo au amekatazwa na huyu aliemteka?” aliuliza Carolina kwa sauti ya hofu.
Watu ishirini waliokuwepo ndani ya sebule kubwa ya nyumba hii, yani askari kumi na saba pamoja na mzee James mke wake na binti yao Carloline, walikuwa kimya wanasikiliza simu ambayo ilikuwa inaendelea kuita kwa sauti ya wazi kabisa bila kupokelewa, huku jina la mpigiwaji likiwa linaonekana doctor Veronica, “atakuwa amepumzika sehemu” alisema Luten Jimmy wa jeshi la ulinzi la Tanzania, akijaribu kuondoa wasi wasi kwa familia ya bwana James, ambayo ilionekana kuwa na wasi wasi na binti yao, “sidhani kama anaweza kuwa amepumzika, wakati ameshikiliwa na huyo mtu ambae hatumfahamu” alisema mama Carl, akionyesha kukata tamaa, “ila kuna kitu mimi nahisi” alisema captain Amos Makey troop kamanda wa ART, wote wakamtazama Makey, kama ishara ya kusikia kile anacho kiwaza, wakati huo simu ilikuwa inaacha kuita na sauti ya kike inasikika ikisema “namba unayopiga haipokelewi, jaribu tena baadae” mzee James anaichukua simu kwa lengo la kupiga tena, “binti yenu ni kweli yupo salama, sababu yupo na Deus Nyati” alisema captain Amos Makey, huku anamzuwia mzee James kupiga tena simu, “hapana, amesema hayupo na Deus Nyati” alisema Carloline, ambae kichwani mwake aliamini kuwa siku chache zijazo atakutana tena na kijana yule, ambae aliwahi kukutana nae akiwa mschana mdogo.
Hapo Amos ambae alikuwa anatoa simu yake mfukoni na kupiga namba za mzee Frank Nyati, aliishia kutabasamu tu, wakati huo watu wote waliokuwa ndani walikuwa wanamtazama kuona alikuwa anafanya nini, na sekunde kadhaa baadae wakamwona anaanza kuongea, “samahani kwa usumbufu Afande, hata hivyo nilijuwa ungekuwa umeshalala” alisema captain Amos Makey, kisha akatulia kutoa nafasi kwa yule anaeongea nae, ambae hakusikika kwa wengune, “ni kweli usingizi hauwezi kuja mpaka ujue kijana yupo katika hali gani” alisema Amos Makey, ambae pia akaendelea kuongea, “nilitaka kukujulisha kuwa tuliingia salama dar es salaam, na pia mfalme ameshukuru sana kwa ushirikiano wako” alisikika Amos Makey akiongea, “ni jambo la kushukuru bwana Amos, ila nashukuru pia kijana wangu amefika kwenye maficho yake salama” alisema Nyati, ambae wengine hawakumsikia zaidi ya Amos ambae alikuwa anaongea nae kupitia simu, “hoooo ni vizuri sana afande, kama ameshafika kwenye maficho yake, lakini bado kuna utata kidogo, nadhani umesikia kuwa Deus amemteka biiii…….” Alisema Amos, huku anamtazama mzee James, kwaishara ya kuomba msaada wa jina, “Veronica” alisema James kwa sauti ya kunong’ona, huku anamuonyesha ishara Amos abofye kuiruhusu sauti ya wazi, nae Amos akafanya hivyo huku ana ungia juu kwa juu, “Bi Veronica James, ni mtoto wa bwana James, vipi unafamahamu lolote?” aliuliza Amos na kukaa kimya kusubiria jibu, huku kila mmoja mle ndani akimtazama yeye.
Hapo kikasikika kicheko toka upande wa pili wa simu, yani kwa bwana Frank Nyati, “hapana bwana, hajamteka, ila yeye ndie aliemtoa mikononi mwa UMD, utekajinyara huo ulifanywa na UMD, wakimtumia askari wa UMD mmoja anaitwa Enock Kafulu, ambae alibadili jina na kujiita John Joseph akijifanya mchumba wa huyo binti kabla ya kumteka, hivyo ni mpango wa muda mrefu” alifafanua mzee Frank Nyati, huku watu wote wakisikia maongezi hayo kwa uwazi kabisa.
Hapo watu wote wakatazamana huku wanapeana ishara ya kukubarian na bwana Amos, huku tabasamu zikichanua kwenye nyuso zao kasoro Carolina, ambae ni kama hakupendezwa na jambo lile, sijui alikuwa anawaza nini, “sasa tuna weza kupata uelekeo wa eneo hilo ili tukatoe msaada kwa Deus?” aliuliza Amos huku yeye na wenzake wakitegemea jibu la kukubaliwa toka kwa kanali wa zamani wa MLA, yani bwana Frank Nyati, “ni wazo zuri, lakini siyo jema sana, kwaajili ya kuzuia vifo zaidi” alisema Frank na hapo watu wote wakatazamana kwa mshangao, bila shaka walikuwa na maswali yanayofanana, “vifo zaidi kivipi afande, maana ni muhimu tumpate Veronica ili familia hii iweze kusafiri kuelekea #mbogo_land kukutana na mfalme” alisema Amos kwa sauti yenye busara na msisitizo, “Amos nadhani kuna kitu bado serikali haija gundua, mpaka sasa Deus ameshauwa UMD wengi sana, ambao sio tu wapo hapa tanzania, ila wapo na silaha za kisasa, na sio wao peke yao pia wapo polisi wa Tanzania ambao wanashirikiana na UMD, hivyo basi endapo mtaenda kuwafuata, lazima watu wabaya waliopo katika operation hii watawafuata na kujaribu kuwashambulia wakina Deus, nakitu ambacho unahitaji kujua ni kwamba, Deus siyo mtu wakijiuliza mara mbili linapokuja swala la kulinda usalama wake na watu wake wa karibu, ndio maana nakushauri kuwa muwe watulivu, mpaka wakati utakapofika wa kujua nani ni nani” alisema mzee Frank na wote wakakubaliana kwa vichwa.
Wakati maongezi hayo yanaendelea, huku nako Carolina, alikuwa anamnon’oneza jambo mama yake, “mamaaaa kwani Dada anajua kuwa Deus ni rafiki yangu?” aliuliza Carlo kwa sauti ya kunong’ona, lakini mama yake akapotezea na kuweka umakini kwa mume wake, ambae aliingilia maongezi ya Amos na bwana Nyati, “bwana Nyati ni mimi James, habari za siku nyingi” alisalimia mzee James, japo hakuwahi kuwa karibu na bwana Frank zaidi ya kuwahi kumsikia kutokana na matukio ya kishujaa aliyo wahi kuyafanya kwa kumuokoa mfalme Eugen mara kadhaa, “habari bwana James, pole kwa yote yaliyokukuta” alisikika Frank kwa sauti ya wazi kabisa, “asante bwana Frank, pole na wewe pia, kutoka shujaa wa nchi mpaka mkimbizi” alijibu mzee James, kikafwatia kicheko toka upande wa pili wasimu, “lakini mwisho wa siku yote yanaenda kuisha” alisema kanali wa zamani wa MLA bwana Frank Nyati na James akadakia, “bahati nzuri yanaenda kuisha, kabla hawajafanikiwa kwa lolote” alisema James, huku na yeye anacheka kidogo, kuonyesha kwamba, walikuwa wanaongelea kitu ambacho wanaombea kitokee.
Waliongea mawili matatu kabla James hajaenda kwenye lengo kuu, “sasa bwana Frank, nadhani unafahamu kijana wako yupo na binti yangu, unaweza kunihakikishia usalama wake” aliuliza James kwa sauti fulani yenye kuhitaji uthibitisho, huku Caroline akiwa anasikilizia kwa umakini, ni kama alijikuta anakitu fulani kinamfanya asitamani dada yake kuwa karibu na Deus, “James, wewe ni shuhuda wa kile anachokifanya Deus, kama aliweza kukusaidia kwa mtu ambae wameshakaa zaidi ya masaa matatu” alisema mzee Nyati, kwa sauti yenye uhakika wa kile anacho kisema, ni kweli namuamini kijana wako, na ameshawahi kumsaidia binti yangu Carlo, lakini wasi wasi wangu ni kwamba, mpaka sasa hajajitambulisha kwake, na sina uhakika kama Veronica ataweza kutimiza na kufuata sheria za kijana wako” alisema mzee James, akionyesha kuwa na mashaka na usalama wa binti yake,
Wakati maongezi ya mzee James na bwana Nyati yanaendelea, Carlo nae hakuacha kumsumbua mama yake, “mama dada yupo na Deus” lakini mama akampotezea tena, akiweka umakini kwenye maongezi ya mume wake na bwana Nyati, “ondoa mashaka bwana James, hakika binti yako ana bahati kubwa sana, maana ameaminiwa na Deus mpaka kufika kwenye maficho yake ambayo hata mimi sijawahi kufika” alisikika mzee Nyati.
Hapo Carlo akamtazama mama yake ambae bado hakuwa anamjali, “mama unasikia huko, ongea na baba, amwambie awaambie wakina dada wapokee simu niongee na yule kaka” alisema Carlo kwa sauti ya kum’bembeleza mama yake, ambae alimpotezea tena, akimsikiliza mume wake aliekuwa anaongea na bwana Frank, “sawa bwana Frank, naamini kuwa kijana wako atamtunza binti yangu” aliongea bwana James, kabla hawajaagana na kumuachia Captain Amos, “sawa afande sisi tunasubiri wakati muafaka ili tuende tukatoe msaada, na hii taarifa tunaimani itatoka kwako, baada ya kuwasiliana na Deus” alisema Amos, kabla ya kuagana na Frank Nyati ambae ni baba mzazi wa kijana Deus Nyati.
Mara baada ya simu kukatwa, mama Carlo akamshika mkono binti yake na kuondoka nae kuelekea upande wa chumbani, kimya kimya, moja kwa moja wakaingia kwenye chumba cha Carolina, “haya niambie ulichokuwa unaniambia” alisema mama Carolina, “kwani we mama hujui?” aliuliza Carlo, kwa sauti iliyojaa aibu, huku anatazama pembeni, “najua kuhusu nini?” aliuliza mama Carlo, huku anamtazama binti yake kwa jicho lenye hasira kidogo, “kwani mama hujui kuwa Deus rafiki yangu toka nikiwa mdogo” aliuliza Carlo kwa sauti ambayo ilionekana wazi kuficha neno mpenzi. ……. ENDELEA KUFUATILIA MKASA UNAOFUATA WA TEMBELE LA UANI UTAKAO KUJIA HAPA HAPA jamii forums MWISHO WA MKASA HUU NDIO MWANZO WA MKASA MWINGINE USIKAE MBALI
Usiku vinakuja mkuuHakika nafsi yangu kidogo imeridhika mana toka jana sikupata usingizi nikisubir vigongo vishuke hatimae umeleta mchana huu vipi usiku vitakuja vingine au ndio mpaka kesho mkuu🫣🫣🫣
😅NExt episode iwe ni ya deus tu.
Fanya kweli kiongozi👍Usiku vinakuja mkuu
Mr (+_+)
Mida ya wanga.Usiku vinakuja mkuu
Kuhusu yajayo, kule kwa mapacha hamna jipyaaaa, tuliosoma ile KAZI ya "Asali haitiwi kidole" tayari Kuna mwanga tunapataa.Naona kama muda haufiki,,