Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Shukrani sana Mkuuu
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA THERASINI NA MOJA
MTUNZI: Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA THERASINI:- Hapo Ulenje akamwona CP Nyambibo, akiwa tazama wenzake kwa macho ya mshangao na kiulizo, nao wakaonekana kuwa na hali kama ya mkuu wao Nyambibo, ni wazi walishangaa kusikia maneno yale toka kwa kamanda huyu wa ngazi za juu za jeshi la polisi, hasa kanda maalumu ya dar es salaam, hata yeye mwenyewe alijiona kama amekosea kuongea jambo lile ambalo aliamini kuwa wenzake hawana ufahamu nalo, ulenje akamuona Nyambibo anamgeukia na kumtazama kwa macho ya mshangao…....…….ENDELEA…

Kabla haja sogeza uso wake karibu na usawa wasikio lake yeye Ulenje, β€œni aibu ACP hufuatiliii taarifa ya hiki kinachoendelea, Deus na hawa jamaa ni maadui wakubwa, japo wote wanahitajika wakamatwe haraka iwezekanavyo” alinong’ona yule CP Nyanmbibo kabla haja wageukia askari na kuanza kugawa majukumu kutokana na mikoa.

Ambapo katika mikoa ya kipolisi mitatu, miwili yani temeke na Kinondoni, ilielekea kazi mzumbwi na mmoja wa Ilala ulibakia nyuma, huku makamanda wote wakiwa katikati.

Dakika kumi mara baada ya magari ya polisi yenye askari wa temeke na Kinondoni kuondoka, ndipo Cheleji na Othman walipo gawana majukumu, β€œsasa kaka wakati ndio huu, ni vyema kama tutaondoka haraka tukamalize kazi, kisha tutoe taarifa itakayo warudisha wale na kuacha kuwafuatilia wakina Kadumya” alisema Cheleji, kisha kimya kimya na kwa usiri mkubwa wakaingia kwenye magari yao na kuanza kuondoka kwa kuachiana nafasi ya dakika kadhaa, kiasi cha kutokuwa shtua wenzao kwamba magari yale yanaondoka kwa kazi maalumu.


Yaaap! Akiwa ameshtushwa kwa maneno ya Dereva wa BMW jeusi, msafirishaji Deus Frank Nyati, mzee James ambae pia aliweza kuisikia sauti ya binti yake akiongea kwa mahaba na kijana yule hatari akiwa chumbani kwake mzee huyu, anapiga simu haraka kwa binti yake, ambae dakika chache zilizopita amejaribu kumpigia bila mafanikio.

Lakini safari hii, bahati nzuri kwake, simu inapokelewa mara moja, β€œbaba hujajalala mpaka saa hizi” mzee James anakutana na sauti ya binti yake, ambayo haikuwa na wasi wasi hata kidogo, β€œnitalalaje wakati sina uhakika wa usalama wako Vero, hebu niambie ni kweli upo na huyo kijana Dereva” aliuliza mzee James kwa sauti ya kunong’ona.

Hapo ilitumia sekunde kadhaa kujibiwa, ni wazi Veronica alikuwa anaomba ruksa ya kueleza ukweli, β€œndiyo baba, kwani wasi wasi wako nini, si nilikuambia kuwa nipo salama, tena nyie ndio munapaswa kujiangalia sana, maana hawa majambazi hata hawaeleweki, yaani hadi polisi wengine wanasaidiana nao” aliongea Veronca, na wakati huo huo mzee James alikuwa anasikia sauti ya kiume ikiongea na simu nyingine, japo hakusikia kinachoongelewa na mwanaume huyu ambae kwa vyovyote alikuwa ni Deus Nyati.

Hapo kidogo ni kama mzee huyu alipoa, β€œhuku kuhusu sisi ondoa wasi wasi, tunalindwa na majeshi ya ulinzi, pia hata jeshi la #mbogo_land lipo hapa kutulinda na mwisho watatupeleka nchini kuonana na mfalme” ilimshtua kidogo Veronica, β€œmh! Unasema majeshi ya Mbogo land kuonana na mfalme?” aliuliza Veronica kwa mshangao, β€œndiyo tena hapa tunakusubiri wewe tu” alisema mzee James, huku safari hii akitoka chumbani na kuelekea sebuleni aliko lwaacha wenzake, β€œhizo Habari tumesha zipata, lakini wasi wasi wangu ni huyo kijana, utawezana nae kweli maana anasheria zake hizo ukiivunja moja hata kama amekisaidia vipi anaweza kuchinja mara moja” alisema mzee James, huku watu waliokuwa sebuleni wakisikia sauti yake, maana sasa alikuwa anakaribia sebuleni, mzee James akabofya kitufe cha kuruhusu sauti ya wazi.

Hapo wote wakapata nafasi ya kusikia sauti ya Veronica, β€œwala usiwe na wasi wasi baba, Deus ni Rafiki yangu wa siku nyingi” sauti hii ya Veronica ambayo iliwafikia watu wote waliokuwa sebuleni, usingedhania kuwa ndie aliekuwa amewajaza watu hapa sebuleni kwenye nyumba ya baba yake, maana ilikuwa ni sauti ya kujiachia kama vile mtu aliepo nyumbani kwake au ofisini kwake, na pengine hotelini na mpenzi wake.

Hata mama Veronica na Carolina waliokuwa wamekaa kwenye kochi moja walionekana kushangazwa, maana wakati Carolina akiwa anatoa macho kwa mchangao, tayari mama yake alikuwa ameshainuka mbio mbio, akamfuata mume wake, β€œuna uhakika ni Vero? huyo kijana…..” mzee James hakumaliza kuongea tayari mke wake alisha pokonya simu, β€œwe Vero, kama unasema kweli sasa kwanini hurudi nyumbani unatuweka roho juu juu wenzako?” aliuliza mke wa mzee James ambae ndie mama yake Veronica kwa sauti ya ukali kidogo, β€œmama jamani si nilisema wakati tuna kuja huko polisi walitushambulia, tumekaa sehemu mpaka kesho tutarudi maana wakituona tu watatushambulia tena” alisema Veronica kwa sauti ya kudeka, kama mtoto anaeomba ruksa ya kulala kwa Rafiki yake.

Hapo captain Amosi Makey akanyoosha mkono kwa mama Veronica kuomba simu, β€œhaya kuna mtu anataka kuongea na wewe” alisema mama Vero kabla hajatoa simu kwa Amos Makey, troop kamanda wa kikundi maalumu cha uchunguzi wa kivita toka MLA, β€œmtu gani tena mama?” aliuliza Veronica, lakini tayari simu alikuwa nayo Amos Makey, β€œnaitwa Kaptain Amos Makey toka ML..” hakupewa nafasi ya kumaliza kujitambulisha, tayari simu ilishakatwa, β€œamekata” alisema mzee James, huku anaichukua simu na kuipiga tena, lakini ilifanikiwa kuita mara moja tu na ikakatwa tena, na walipo jaribu kupiga tena wakasikia simu haipatikani kwa maana ilikuwa imeshazimwa, wote wakatazama kwa macho yenye wasi wasi mkubwa, huku Carlolina, akiwa anatabasamu kwa fadhaha, β€œmh! najua tu, dada hawezi kukwepa kwa kaka Deus” ilimchomoka Veronica kwa sauti ya chini, lakini iliyosikika vyema kabisa na wao wakamtazama, huku mama yake tu akiwa anajua alicho maanisha Carolina.******

Naaam tukienda machimbo ya kokoto kule Kazimzumbwi, na sasa tunaona magari ya kijeshi, yakiwa yamesimama na askari UMD wakionekana wakiwa wanashusha baadhi ya mizigo toka kwenye gari, ambayo ni maboxi ya silaha, tayari kujiandaa kwa majukumu yaliyo waleta.

Kaptain Kobwe anaonekana akiwa amesimama na wakina Kadumya, huku Kadumya mwenyewe akiwa anaongea na simu kwa sauti ya wazi, huku wenzake wasikie kinachoongelewa, β€œhallow bwana Dereva, ni bahati haujalala mpaka sasa maana tuna kazi ya kufanya usiku huu” alisema Kadumya kwa sauti nzito yenye mikwaruzo, β€œok! nakusikiliza” ilikuwa ni sauti tulivu ya Dereva, toka upande wa pili wa simu, sauti ambayo licha ya utulivu na upole wake, lakini yeye aliiona kuwa ni kama sauti ya mzimu au jini lenye hasira, β€œkuna mzigo toka stendi maili moja unatakiwa upelekwe bagamoyo” aliongea Kadumya, huku Kafulu na kobwe wakimsikiliza pembeni na kutabasamia chini chini, β€œuzito wa mzigo” ilisikika ile sauti ambayo sio tu Kadumya ndie alieichukia, hata Kafulu yani JJD, aliiona kama ni chukuzo kubwa.

Kadumya akamtazama Kafulu, ambae pia alikuwa anamtazama akionyesha pia hakuwa amejiandaa kwa swali kama hilo, β€œkilo kumi” alijibu Kadumya kwa kuona kuwa Kafulu hakuwa na msaada, β€œmuda na sheria zako tafadhari” ilisikika sauti ya Deus Nyati, sauti ambayo ilimfanya Kobwe asiamini kile alichokisikia juu ya mtu huyu anae sadikiwa kuwa ni hatari sana, β€œmuda ni saa tisa na nusu, sheria ni kuzingatia muda” alisema Kadumya kwa sauti ile ile ya mikwaruzo, na wote wakatulia kusikiliza atachoongea dereva, lakini kikapita kimya pasipo Dereva kuongea, β€œhallow dereva, bado tupo pamoja, nitajie malipo yatakuwa kiasi gani?” aliuliza Kadumya, ambae niwazi alijua kuwa Dereva alikuwa hewani na anamsikia vyema, β€œnadhani malipo safari hii yatakuwa makubwa zaidi ya yale ya mwanzo” alisema Deus, kwa sauti ile ile tulivu, lakini maneno aliyoyaongea yaliwashtua wote watatu, hata Kobwe pia alishtuka.

Maaan hakuna alie amini kijana huyu angetoa kauli kama hii, ambayo ilionyesha wazi kuwa amegundua kuwa huu ni mkataba wa pili, β€œunamaana gani safari hii dereva” aliuliza Kadumya kwa sauti yenye utulivu wakulazimisha, japo kwa macho tuliweza kuona wasi wasi na mshangao aliokuwa nao, β€œnajua hukutakiwa kufahamu, ila wewe ni mteja wangu wa mwisho na ulikiuka sheria tisa ndani ya lisaa limoja tu” kuanzia kutojuana majina, kutumia bunduki nidhamu, kufungua mzigo, na hata ile muhimu ya malipo” ilisikika sauti ya dereva, yaani Deus Nyati akiongea kwa utulivu ule ule kama vile hakuwa anatilia msisitizo yale aliyoyaongea, β€œlakini umeuwa vijana wangu wengi sana, haya tuaache hayo, nieleze safari hii utahitaji kiasi gani kukamilisha jukumu?” aliuliza Kadumya, ambae nikama alikuwa anajaribu bahati yake baada ya kuona amesha shtukiwa.

Wote wakatega sikio kusikia atakachoongea Deus Nyati, β€œgharama ya safari hii itakuwa ni roho yako, na huyo mpuuzi niliempa nafasi nyingine ya kutubu dhambi zake, na sio roho za hao wapuuzi wenu ambao hamja wafundisha vyema kupambana na mtu kama mimi ” alisema Deus Nyati kwa sauti ile ile, ambayo hata akiongelea mambo ya hatari utasema anaungama dhambi zake kwa unyenyekevu, hapo wote watatu wakatazamana kwa mshangao juu ya kujiamini kwa kijana huyu mwenye sauti ya kanisani au msikitini, kisha wakatazama kule waliko vijana wao, ambao walikuwa wanaweka sawa silaha zao, ambazo zilikuwa ni zile kipimo cha kati yani SMG, AK 47, MMG, RPG na mabomu ya kutupa kwa mkono, stick heand grenade, defensive na offensive heand grenade, huku wakiwa na vifuko vya makombora ya RPG, na kwamba Deus angeweza kuchomoa roho ya mtu hata mmoja endapo angeingia ndani ya mtego wao.

Hapo wote watatu, wakaachia kicheko cha nguvu, kilichojaa dharau, ni kweli walidharau maneno ya Deus, ambae kiukweli, waliamini kuwa anasema vile kwakuwa hakujua kama sasa jeshi lao limekamilika, na kwamba akiingia kwenye mtego wao hawezi tena kuchomoka, kwasababu ukiachilia watu waliokuwa nao, pia walikuwa na silaha kubwa za kivita kwa ngazi ya section, β€œkijana ni vyema ukaanza kujiandaa kwa kile ambacho kinakuja kukupata safari hii?” alisema Kadumya, mara baada ya kumaliza kicheko, β€œlabda nieleze unataka nifanye nini?” aliuliza Deus kwa sauti ile ile, ambayo kwa haraka haraka ungesema alishakubari yaishe, β€œhayo ndiyo maneno ambayo unapaswa kuongea sasa hivi, sio kujipiga kifua mbele ya kundi la wanaume” alisema Kadumya kwa sauti ile ile yamikwaruzo yenye dhaurau kubwa, β€œnakusikiliza mzee jari muda wangu” alisikika Deus kwa sauti ile ile tulivu ya upole.

Hapo wote wakatazamana, huku wanaonyeshana ishara ya dole gumba kuwa mambo yapo sawa, β€œsikia kijana, najua hunifahamu mimi ni nani, lakini nakupa nafasi ya kurekebisha makosa yako, nipatie fedha zangu na huyo mwanamke, tutaachana na wewe” alisema Kadumya kwa sauti yenye msisitizo nakitisho, huku wenzake wakitabasamu kwa kuzuia vicheko vyao visitoke nje ya vinywa vyao, huku masikio yao yakiwa yametegwa kwenye simu ile aliyoishika bwana Kadumya.

Wakati wanategemea kusikia sauti ya uoga ikiomba kujua sehemu ya kupeleka fedha na yule mwanamke, ghafa masikio yao yakanasa sauti ya kicheko cha mguno, yani kicheko cha mtu mzima anaemcheka mtoto mwenye kushindwa jaribio, kicheko ambacho unaweza kusema ni cha masikitiko, β€œnakufahamu mzee, wewe ni Kanali Erasto Kadumya afisa mtoro wa MLA, na sasa unajiita general wa UMD, labda wewe ndiyo hunifahamu mimi, kama ungekuwa unanifahamu, lazima ungetambua kuwa, unapuliza moto wa mafuta ukiwa na ndevu nyingi kidevuni, cha msingi achana na upuuzi huo kabla ndevu hazijadaka moto” alisikika Deus, kwa sauti ile ile ya upole, ikifuatiwa na kicheko cha sauti ya kike toka upande wa pili wa simu, β€œjamani weweee una maneno” ilisikika sauti ya kike, huku wakati huo huo kicheko kikimponyoka Kobwe alieshindwa kujizuia, β€œpumbavu unacheka nini Kobwe” aliuliza Kadumya kwa sauti ya hasira, huku mkono wake ukipitia kwenye kiuno na kuibuka na bostora iliyo elekezwa moja kwa moja kichwani kwa Kobwe, usawa wa paji la uso.

Askari wote wanashtuka wanaacha kufanya wanacho kifanya na kutazama upande ule, ambako wanamuona general wao akiwa amemnyooshea bastora mkuu wa kombania yao, ambae anaonekana akiwa anatetemeka kwa wasi wasi na uoga, kwasababu anaijua tabia ya mkuu huyu wa jeshi hili la UMD, mata nyingi akitoa bastora yake huwa hairudi bure,

Kobwe anashikwa na wasi wasi mkubwa, anamtazama Kadumya, ambe macho yake yamemtoka kwa hasira, Kobwe anamtazama Kafulu ambae ndie angehusika na kusuluhisha, lakini anaonekana amesimama pembeni amejishika kiuno, ni kama hakujua kinachoendelea pale, β€œSamahani mkuu, haito jirudia tena” alisema Kobwe kwa sauti ya kutetemeka.

Ilitumia sekunde kadhaa kwa Kadumya kushusha hasira zake na kundoa bastora kichwani kwa Kobwe, β€œunabahati tuna majukumu makubwa, ungekuwa umesha lamba udongo” alisema Kadumya kabla ya kukumbuka kuwa simu ilikuwa hewani, β€œhallow dereva, na jua bado upo hewani na unanisikia, hebu tambua kuwa maneno yako hayachekeshi kama wapumbavu wanavyo dhania, nakupa nafasi ya mwisho ya kunipatia fedha na huyo mwanamke…..” alisema Kadumya kwa sauti ya ukali na vitisho, kabla hajagundua kuwa simu imekatwa, β€œmshenzi amenikatia simu, atajuta kujiingiza kwenye hili, alisema Kadumya kwa hasira, huku ananyoosha mkono kumpatia simu Kafulu.

Lakini licha ya kunyoosha kwa sekunde kadhaa, hakuona mtu akipokea simu, akamtazama Kafulu ambae alionekana akiwamesimama anamtazama kama mzimu, β€œwe fala hebu chukua simu yako, unawaza nini, au sauti ya huyo kahaba ndiyo imekuchanganya, acha ushamba yupo na mwanaume mwingine, kwani wewe tulikutuma ukapendane au ukafanye kazi?” alisema Kadumya, huku Kafulu akikurupuka na kupokea simu yake ambayo ilikuwa inatumiwa na Kadumya, na wakati huo huo simu ya Kadumya ikaanza kuita, akaitoa mfukoni na kutazama mpigaji akaona kuwa ni bwana Ulenje, akaipokea mara moja, ana haikuchukua hata sekunde mbili tayari simu ilikuwa imekatwa, sijui aliambiwa nini.

Maana haraka sana, aliwageukia wakina Kobwe, haya kazi imeenza, polisi wanakuja upande huu, wapangeni askari, kama wataingia hapa wasipate hata nafasi ya kutoa taarifa kwa wenzao, yani nikuwateketeza kabisa” alitoa maagizo Kadumya, na hapo Kobwe akaanza kuwapanga askari huku akiwapa habari za ujio wa adui zao. *****


Naaam huko TT City, mtaa wa Sizwe, ndani ya jumba kubwa la kifahari linalomilikiwa na jeshi la ulinzi la #MBOGO_LAND ARMY, nje wanaonekana askari wakiwa wamezunguka jengo lile ndani ya uzio mkubwa wa kuta, unao lindwa na umeme ikisaidiwa na camera kila kona ya ukuta, magari mengi ya serikali sambamba na gari moja binafsi aina ya Toyota Caldina, tunaingia ndani ya jengo lile la kifahari, ambalo ukitazama kwa haraka, unaweza kusema kuwa ni nyumba ya mtu binafsi, kutokana muundo wake, ukiachilia sebule kubwa yenye kila kitu, ila pia kulikuwa na jiko vyoo na vyumba vya kulala, katika vyumba viwili kati ya vyumba nane vilivyomo ndani ya jengo lile, ambavyo tunafanikiwa kuingia, tunakuta ni vyumba vizuri vyenye kila kitu ungesema ni vyumba vya hoteli moja kubwa ya kifahari.

Chumba cha kwanza tuna wakuta Watoto wawili wa staff sajent Ashraff Kibwana, ambao umri wao ni kati ya miaka saba, kwa mdogo na mkubwa ni miaka kumi na mbili, wote wakiwa ni wa kike, ambao tayari walikuwa wamepitiwa na usingizi, pia chumba kingine tunacho kiangazia, alikuwepo mke wa bwana Ashraff, ambae licha ya kupewa huduma zote lakini bado hakuthubutu kufumba hata kope ya jicho lake, kwa maana alikuwa anawaza usalama wa mume wake, hasa kutokana na matukio kadhaa ya siku za nyuma yaliyomkumba mume wake, kiasi cha kuamua kuacha kazi ya jeshi na kukimbia nchi. …....…….ENDELEA MZEE WA UMD mhanuzi wangu MUNA MPANGO GANI NA POLISI WETU WA TZ MBONA HAWANA BAYA NA NYINYI?




NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA THERASINI NA MBILI
MTUNZI: Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA THERASINI NA MOJA:- Chumba cha kwanza tuna wakuta Watoto wawili wa staff sajent Ashraff Kibwana, ambao umri wao ni kati ya miaka saba, kwa mdogo na mkubwa ni miaka kumi na mbili, wote wakiwa ni wa kike, ambao tayari walikuwa wamepitiwa na usingizi, pia chumba kingine tunacho kiangazia, alikuwepo mke wa bwana Ashraff, ambae licha ya kupewa huduma zote lakini bado hakuthubutu kufumba hata kope ya jicho lake, kwa maana alikuwa anawaza usalama wa mume wake, hasa kutokana na matukio kadhaa ya siku za nyuma yaliyomkumba mume wake, kiasi cha kuamua kuacha kazi ya jeshi na kukimbia nchi. …....…….ENDELEA…

Tunaachana na mke wa bwana Ashraf, tunaenda moja kwa moja mpaka kwenye chumba ambacho ukitazama kwa haraka ungesema ni vyumba viwili tofauti kabisa, ni kweli kulikuwa na milango miwili, lakini unapoingia mlango wa kushoto, ambao tunaweza kuuita mlango wa pili tunakutana na chumba kimoja kipana cha kawaida chenye makochi mawili na viti vinne, vyote vikiwa vimetazama upande wa kulia wa chumba hicho, ambacho kuta yake kati ya kuta zake nne upande huo wa kulia nusu yake ulikuwa ni kioo kitupu, ambacho chini yake palionekana speeker mbili kubwa.

Ukitazama kioo kile na pasipo umakini wowote, ungeweza kuona chumba kingine kipana, chenye meza kubwa ya chuma yenye vishiko fulani kama vile sehemu ya kufungia mtu mkorofi, huku meza hiyo ikiwa imezungukwa na viti viwili, navyo vya chuma kama meza yake.

Sisi tupo ndani ya chumba hiki cha kwanza, ambacho kuna viti na makochi, hatupo peke yetu, tupo na watu wanne, nao ni King Elvis Queen Vaselisa, General Sixmund na kanali Justin Johnson, ni Malikia Vaselisa peke yake ndie alikuwa amekaa kwenye kiti, lakini mfalme na makamanda wa kijeshi wote walikuwa wamesimama, huku wote wanne macho yao yakiwa kwenye kioo kikubwa mbele yao, ambapo kwa uwazi kabisa waliweza kuona mlango wa chumba kile ukifunguliwa, na wakaonekana askari wa MLA waliovalia sare nyeusi, wakiingia mule ndani huku wamemtanguliza mwanaume mmoja mtu mzima, ambae alionekana kuwa na wasi wasi sana, kisha askari wale wanatoka mule ndani wakimuacha yule mwanaume ametoa macho kwa mshangao na wasi wasi, asijue la kufanya, β€œjamani kwanini munanifungia humu” alisikika Ashrafu, akipiga kelele kwa nguvu, β€œfamilia yangu mume ipeleka wapi, mulisema Hamto nifanya chochote” alipiga kelele Ashraf.

Wakati huo huo mfalme anasikia simu yake inaanza kuita, β€œshiiiiiii atajua kama tuna fuatilia mahojiano” alisema Malkia Vaselisa kwa sauti ya kunong’ona, huku anamsihi mume wake kukata simu ile, hapo General Sixmund akajua kuwa Malkia hakujua kuwa kile chumba kimewambwa sauti, β€œmalkia mtukufu wa #Mbogo_Land, upo huru kuongea chochote kwa sauti yoyote, kwa maana sisi tuna wasikia wao ila wao hawawezi kutusikia, mpaka turuhusu sauti zetu kwa kutumia vipanza sauti maalumu” alisema General Sixmund, kwa sauti ya unyenyekevu, wakati huo kanali Jastin anazima speeker za sauti.

Na hapo ndipo shida ilipo, yani katika nchi za kifalme unapo zingumza na familia au koo za kifalme hata kama wewe ni komando, itabidi uongee kwa unyenyekevu kama hivi, tofauti na unapozungumza na viongozi wengine wenye uteuzi wa mfalme, wao utawasalimia kijeshi.

Malkia akacheka kidogo, huku anamtazama mume wake aliekuwa anacheka huku anaitazama simu yake kuona jina la mpigaji, β€œnilijua tunahitajika kukaa kimya” alisema Vaselisa, huku yeye na mume wake wanacheka kwa Pamoja, utajulia wapi haya mambo ya kintelejensia, hebu kwanza nipokee simu naona mwana habari wetu anapiga sijui kuna jambo gani tena” alisema King Elvis, na wote wakakaa kimya wakimtazama mfame akipokea simu pasipo kuweka sauti ya wazi, nae akaipokea na kukaa kimya kwa sekunde kadhaa ni wazi alikuwa anatoa nafasi ya mpigaji kutoa salam, β€œsalaam mtumishi mwema, kipi kimekufanya upige simu usiku huu” ilikuwa ni sauti tulivu ya kifalme, ambae alitulia kwa sekunde kadhaa kusikiliza huku wenzake wakiwa kimya kabisa, wakimtazama mfalme ambae kila sekunde iliyoenda alionekana kubadirika sura mfano wa mtu anaepokea taarifa mbaya.

Mwisho wakamsikia mfalme akisema, β€œsawa agiza watu wetu, wafuatilie chanzo cha mtandao uliotumika kuposti hizo habari” alisema mfalme kabla ya kukata simu, β€œvipi tena kuna habari mpya mtandaoni?” aliuliza Malkia kwa sauti yenye shauku, β€œwapuuzi wamesha post uvumi mwingine, wa kwanza unasema wakuu kadhaa wa jeshi na usalama wa taifa wamejiunga na UMD, ni kutokana na kutokuukubali utawarla wa kifalme, na habari ya pili ni kwamba, wamevumisha kuwa tumetuma askari wa MLA, kwenda Tanzania kumuua bwana James” alieleza king Elvis.

Taarifa hii ilimshangaza kila mmoja mule ndani, β€œtayari mambo yameanza, hebu tusubiri tuone” alisema malkia Vaselisa, akimaanisha kuwa taarifa hizi zimeenda sambamba na zile za Waziri Chitopela, na hapo ni kama king Elvis alikumbuka jambo, β€œvipi kuhusu askari wetu waliopo Tanzania, umewasiliana nao hivi karibuni?” aliuliza mfalme Elvis, huku akimtazama general Sixmund, β€œnajitahidi kuwasiliana nao kila mara, na sasa bado wapo nyumbani kwa bwana James, na wanafanya juhudi za kumpata Veronica ili waweze kuanza safari ya kuja Mbogoland” alisema Sixmund na mke wa mfalme akauliza, β€œwanauhakika na sehemu alipo Veronica?” aliuliza Vaselisa, β€œndiyo wanafahamu, maana mpaka dakika ya mwisho, ilithibitika kuwa Veronica na Deus Nyati walikuwa pamoja” alijibu Sixmund.

Hapo mfalme alitulia kidogo, kama anatafakari jambo, sekunde chache baadae akaongea, β€œhuyu Deus Nyati ni alama katika mapambano haya, maana ni sababu kubwa ya kukwamisha juhudi za utafutaji wa fedha za kulipia silaha za UMD na kufanya sisi tugundue uovu wao” alisema Elvis, akionyesha kuliongea kwa hisia za hali ya juu jambo lile, β€œhata baba yake pia, ni wazi ameonyesha kuwa mzalendo katika nchi yake, ambayo licha ya watu wabaya kumgombanisha na serikali lakini ametoa ushirikiano mkubwa wa kufichua uasi” alisema Malkia Vaselisa, β€œni kweli kabisa, ata record zake zinaonyesha kuwa ni mtu ambae ameitumikia nchi kwa moyo wake wote, kiasi cha kujitolea uhai mara kadhaa kuokoa Maisha ya mfalme Eugen.” Alisema King Elvis, huku wote wanatazama kwenye kioo na kuona mlango wa chumba cha pili ukifunguliwa akaingia askari mwenye cheo cha luten, alievalia suruali ya kaki iliyoiva, na shati la kaki rangi ya kupauka, huku kichwani akiwa amevaa kofia ya duara ya rangi kama ya suruali yenye nembo ya jeshi la #mbogo_land, chini viatu vyeusi vyenye kung’aa kama kioo, β€œJastin washa speeker” alisema general Sixmund. ******

Naaam huko songaea nako, mzee Frank Nyati nae alikuwa katika wakati mgumu sana, licha ya kushikwa na usingizi mkali, lakini muda wote alipambana asitopee kwenye starehe hii ya kisheria, mara baada ya kujaribu kupiga simu mara kadhaa bila mafanikio na kujipumzisha kidogo, na baadae kuona dalili za kusinzia, bwana Frank anaamua kujaribu tena kupiga simu kwa kijana wake kwa mara nyingine tena, lakini bahati nzuri safari hii simu yake inapokelewa mara moja, β€œbaba kwanini hujalala mpaka saa hizi?” ” aliuliza Deus kwa sauti tulivu lakini yenye mshangao, β€œunadani sijalala Kwasababu nina wasi wasi na wewe?” aliuliza mzee Frank, akimalizia kwa kupiga mhayo mrefu wa usingizi, β€œsasa ni kitu gani kinakuweka macho mpaka mida hii?” aliuliza Deus, kama vile anamashaka na jibu la baba yake ambae toka akiwa mdogo hajawahi kuwa na wasi wasi nae, β€œkuna kitu unatakiwa kujua, ni kwamba MLA wapo dar es ni watu ambao unapaswa kushirikiana nao, maana wao pia wapo huko kwaajili ya kumlinda James na kumpeleka #mbogo_land” alisema mzee Frank.

Hiyo kidogo ni kama Deus hakuielewa au kuikubari, β€œsasa mimi wananihusu nini?” aliuliza Deus, β€œwana kuhusu Deus, maana ukiachilia kuwa ulichokifanya kilikuwa ni kujiokoa mwenyewe, lakini pia umefanya kitendo kikubwa na kizuri sana cha kuokoa mtu muhimu katika nchi yako halisi” alisema mzee Frank, β€œlakini sina mkataba nao wowote na kivipi nitashirikiana nao wakati wao ni wanajeshi na sasa mimi ni raia tena muharifu, unadhani nitaishia wapi baada ya mipango yao kukamilika?” aliuliza Deus kwa sauti ile ile ya upole, sauti ambayo baba yake anaifahamu toka akiwa mdogo.

Alicho kiongea Deus kilikuwa ni kitu cha kweli masikioni mwake, maana tayari Deus alisha julikana kuwa ndie dereva wa gari jeusi, licha ya hivyo jeshi la ulinzi la Tanzania lilikuwa linamsaka, baada ya kuonekana kuwa na mapungufu katika utoaji wa hukumu ya mwanzo, β€œkwahiyo umepanga kufanya nini, au utaishi kama mkimbizi Maisha yako yote” aliuliza mzee Frank kwa sauti tulivu, maana ni kweli kijana wake alikuwa katika wakati mgumu sana, β€œkwanza kabisa naachana na kazi ya usafarishaji, nitajificha kwa miaka kumi, baada ya hapo nitajiweka wazi nikiwa mtu wa kawaida na kuishi na familia yangu.

Mzee Frank akajikuta anacheka kidogo, mwanzo sikujua ni kwanini, ila nikajua baada ya mzee kuuliza swali, β€œfamilia ipi unaizungumzia, mke na Watoto wako au mimi na mama yako?” aliuliza huku anacheka kidogo na kumfanya Deus pia aachie kicheko, kama chake yani kicheko cha taratibu, β€œutafahamu hivi karibu” alijibu Deus, na hapo baba yake akauliza swali kama la mwanzo, β€œna umepanga nini juu ya huyo binti wa James, maana sasa anasubiriwa na familia yake kwa safari ya #mbogo_land?” aliuliza mzee Frank, safari hii akiweka umakini kwenye swali lake, β€œnitahakikisha namfikisha sehemu salama kwa mikono yangu” alisema Deus na baba yake akaongezea, β€œsehemu salama pekee ni kwa baba yake, ambae sasa ana ulinzi mkubwa sana toka kwa mfalme” alisema mzee Frank, β€œkwa nguvu na akili zangu zote, Veronica atafika akiwa salama” alisikika Deus akisema, sawa ukiwa unahitaji chochote niambie” hivyo ndivyo walivyo maliza maongezi yao na kukata simu, kisha mzee Nyati akampigia simu captain Amos Makey.*******

Yap! Wakati huo huo, upande wa magharibi mwa kisarawe, eneo la msitu wa visegese uliopaka na Kazi mzumbwi, mashariki na kusini, tuna yaona magari matatu ya polisi yakiwa yanatimua vumbi kuelekea upande wa kibaha, na sasa yanakaribia eneo la relini, sisi tunaachana nayo tunaelekea kusini kwenye barabara ya maneromango, kilomita kama nane tu toka njia panda ya kisarawe na kibaha, ambapo tunaona magari ya jeshi la polisi yakiwa yamesimama, sasa kundi la kwanza ambalo ni askari wa mkoa wa temeke, wataanza kufanya msako kuanzia hapa, wakati kundi la pili litasonga mbele” alisikika ACP Kabona, ambae ni OCD wa ubungo, β€œaliekuwa anasimamia kundi la pili la mkoa wa kipolisi wa Kinondoni.

Kitendo cha haraka, magari yakajitenga kama mafuta na maji, yale ya askari wa Kinondoni, idadi yake tisa, yakaendelea na safari, huku yale ya mkoa wakipolisi temeke, yakibakia pale, huku askari wakishuka toka kwenye magari yale yenye idadi nane, la tisa likiwa la OCD, na kuingia vichakani, nusu wakielekea upande wa kushoto wa barabara, na nusu iliyobakia wakiingia upande wa kulia wa barabara, wakifuata vinjia vya wachoma mkaa kama walivyofanya wenzao wa upande wa kushoto.

Yap! Njia panda nako, askari walikuwa wametulia katika mikao mbali mbali yakimapumziko, kama vile hakukuwa na jukumu zito la kuwasaka wanaume wenye silaha za moto, wapo waliokuwa wamesinzia kwenye magari, wapo waliokuwa wamezama kwenye maongezi, na wapo walikuwa wamezama kwenye mazungumzo na simu zao za mikononi wakisahau jukumu lao la utayari, endapo wenzao watahitaji msaada. Wakati huo kilomita mbili toka pale njia panda kama unaenda kazi mzumbwi, yalionekana magari saba manne yakiwa ya viongozi, na matatu ya askari walinzi wenye bunduki zao, hakika hawa jamaa wamejua kutusumbua” alisema kamanda Nyambibo, akionekana kuchoshwa na swala hili, β€œhivi wamewezaje kuja kujijenga ndani ya nchi yetu na kujaribu kufanya ujinga kama huu?” aliuliza RPC wa temeke, wakati huo huo ikasikika sauti kwenye redio zao, β€œhallow namba 1 ya 1, mimi namba mbili A, kuna ujumbe tafadhari” kwa muito huo, wote wakajua kuwa ni alama ya uitaji wa OCD wa temeke, ambae alikuwa anamuita mkuu wa kanda maalumu.

Kwa muito huo kila mmoja akahisi kuwa kuna jambo tayari limetokea, β€œnamba moja A, tuma tafadhar” alijibu kamanda Nyambibo, β€œmkuu, katika uelekeo wangu, mita kama mia mbili toka barabarani, tumekuta kuna watu wapo chini, ni wazi kabisa watu hawa wameuwawa leo hii na sio muda mrefu sana, kwasababu hata damu zao ni mbichi, hii ni taarifa ya awali” ilisikika sauti ya OCD Temeke, makanamada wakatazamana kwa mshangao, β€œfafanua ni watu wa aina gani, wenzetu au raia au wale tunaowatafuta?” aliuliza Nyambibo, na kutulia kidogo akitoanafasi kwa OCD kuongea, β€œkwa muonekano wao ni kundi lile lile, na baadhi wanaonekana kama wale waliovamia benk ya uhifadhi ya mali binafsi” alisema OCD.

Ilishangaza kidogo, β€œnamba mbili A, eleza idadi ya miili hiyo” alisema Kamanada Nyambibo, β€œafande idadi ni kumi sita, pia inaonyesha ni wazi kuwa kuna gari limeondoka muda mfupi uliopita, maana alama za matairi zinaonekana” alisema OCD, na baada ya hapo, kamanda Nyambibo akatoa tamko, β€œhallow vituo vyote, sikiliza toka kwangu, kundi namba tatu, sogeeni mbele kwaajili ya kutoa msaada wa kukagua eneo la tukio, kundi namba mbili hapo hapo mlipo simama kisha anza msako wa nguvu pande zote hakikisha unawaangalia walengwa, na sio mtu mwingine, umakini unahitajika” alisema kamanda Nyambibo, wakati huo kamanda Ulenje, akiwa anasikiliza kwa umakini, huku moyoni mwake akiwaza juu ya sehemu waliyopo wakina Kadumya.******

Naaam kabla hatujaenda kwenye maficho ya Deus, twendeni moja kwa moja Mbogo Land, jijini TT, mtaa Sizwe, kwenye nyumba ya MLA, kusikiliza mahojiano kati ya MLA na askari wa zamani wa MLA, alieshiriki kwenye operation ya kutokomeza waasi ndani ya serikali ya #mbogo_land, kipindi cha utawala wa mfalme Eugen wa ishirini na tano, operation ambayo inasadikiwa iliangamiza watu muhimu na wazalendo wa kweli wanchi hiyo....…….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao Kujia Hapa Hapa JamiiForums
 
Du! Hii imekaa pw mkuu, nmecomment kabla ya kusoma.
 
AiseeeeeeπŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”.
Naiona familia mda sio mrefu wanaenda kuchapika kama Ngoma.

Tatizo ni Hawa wapuuzi kina Kadumya, wajinga kabisa wanachekacheka TU mda wote.

Chitopela nae ana mipango ya kitoto, yaani mtu unasuka mipango ukiwa umelewa! halafu unataka ushinde! Fala kabisa hili.
Hapa familia sijui itakuwaje du! πŸ₯±πŸ₯±πŸ₯±πŸ₯±πŸ₯±πŸ₯±πŸ₯±πŸ₯±πŸ€­πŸ€­πŸ€­πŸ€­πŸ€­UMD
 
Kwani Kadumya si ana H&K G95 ASSAULT RFLE 5.56 MM au hamuiamini? πŸ˜…πŸ˜…
 
Kwa vile nimekutag πŸ˜…
Yeah!
Jana nimeisoma kwa simanzi sana, baada ya kuona familia wanafanya ujinga wakati ambao wengine ndiyo kwanza wanashtukia mipango yetu. πŸ₯±πŸ₯±πŸ€­πŸ₯±πŸ₯±πŸ€”
 
Hii hadithi haina maisha marefu.Bora aweke vipande vilivyobaki tuanze nyingine
 
Kwani Kadumya si ana H&K G95 ASSAULT RFLE 5.56 MM au hamuiamini? πŸ˜…πŸ˜…
we jamaa fanya kuongeza vipande angalau 4 au 5..hivi viwili unavyopost havishibishi kabisa ukizingatia tunasota mda mrefu tukisubiri..nawe ulishasema bado una stori nyingi za kuleta humu sasa yanini kurembesha namna hii au unataka uwe kama singano jr. story moja et tunaisoma miaka miwili.! acha kubania mwaga moto bhana.
 
Akiweka vipande 4 au 5 mara 3 tamthilia inakuwa imeisha.Zimebaki episodes chache!
 
Inayokuja naipost yote kwa pamoja 😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…