Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA ISHILINI NA TISA
MTUNZI: Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA ISHILINI NA NANE:- alisema Songoro, kwa sauti yenye ubabe ndani yake, mpaka hapo ACP Ulenje aliona wazi kuwa anaenda kuharibikiwa kabla jua hailijachomoza, hivyo ni lazima achukue maamuzi magumu “sawa bwana Songoro, pengine umejipanga, ila itabidi nikuongezee nguvu ya askari na silaha” alisema Ulenje kwa sauti tulivu mfano wa mtu alie kubaliana na msimamo wa Songoro, “hapo sasa ndio umeongea point, sasa nakutana nao wapi hao askari?” aliuliza Songoro, akionyesha kufurahia mpango wa Ulenje, hakujua kuwa kilichopangwa na Ulenje ni zaidi ya mipango yake ya kikatiri aliyowahi kuifanya… ENDELEA..

“umesema mpo ndani kidogo upande wa kulia pembeni mwa reli?” aliuliza Ulenje, “ndiyo, kuna kinjia fulani hivi, tena naona kuna alama za matairi ya gari, inaonyesha njia inayotumika sana” alijibu Songoro pasipo kujua kuwa anaelekeza hatari kuja upande wake, “sawa sawa subiri hapo mpaka vijana wangu watakapo kuja” alisema Ulenje, na Songoro akakubari mara moja akidhania kuwa Ulenje kubari kufuata anavyotaka yeye.******

Ndani ya golden house kwa mfalme Elvis Mbogo wa kwanza, mtoto wa king Eric wa pili na Malkia Doctor Irene, ambae sasa alikuwa ametulia huku macho yake kwa mpenzi wake huyu ambae hadithi ya kukutana kwao inapendeza na kusisimua zaidi ya ile ya #UMEKOSEA_LAKINI_TAMU, akmwambia “aya mke wangu, sasa nakusikiliza, hebu fafanua unachowaza” alisema Elvis kwa sauti ya upole.

Na hapo Vaselisa akaanza kuongea kwa ile sauti yake tamu, kama kinubi cha mfalme Suleiman, “mume wangu, kwanza kumbuka kuwa wewe na general Sixmund, ndio watu pekee munao endesha huu mpango wa siri, kwa maana hiyo hakuna mwingine ambae anafahamu juu ya hilo, na mpaka sasa tayari mumeshatilia mashaka makubwa juu ya njama kubwa iliyofanyika wakati wa operation ya kwanza ya mwaka 92, ambayo iliendeshwa na huyo huyo Chitopelah, ambae hajui kama kuna watu wameshaipata orodha ya askari na wanausalama walioshiriki katika operation ile….” Wakati malkia Vaselisa anaendelea kueleza anachokihisi, mara simu binafsi ya king Elvis ikaanza kuita.

King Elvis akaichukua simu haraka na kuitazama, akaona kuwa mpigaji alikuwa ni major General Sixmund, hii hakujiuliza mara mbili, akaipokea mara moja na kuweka sauti ya wazi ili wote wawili wasikie kitakacho ongelewa, “ndiyo Sixmund, kuna jipya lolote?” aliuliza Elvis kwa sauti iliyojaa shahuku, “mtukufu mfalme, licha ya kuwepo kwa habari mbaya, ila pia kuna habari njema” alisema Sixmund, nae akianza kama alivyoanza Chitopelah muda mfupi uliopita, “anza na hizo mbaya” alisema Elvis, ambae safari hii, alionekana kuwa na wasi wasi mara mbili, akihofia kupewa taarifa kama zile za Chitopelah, ambazo zingethibitisha kuwa ni kweli kuna waasi ndani ya serikali yake.

Naam, Major General Sixmund akaanza kueleza huku mfalme Elvis na malkia mwenye umri mdogo kuliko malkia wote kwa kipindi hicho, wakisikiliza kwa umakini, “mtukufu mfalme, taarifa mbaya ni kwamba, kati ya watu ishirini na tano katika orodha ya wanausalama walioshiriki operation ya mwaka 92, watu ishirini na tatu wote wametoweka katika mazingira ya kutatanisha, kama sio kifo basi ni kuacha kazi ghafla na kupotea kabisa, huku tukikosa kumbu kumbu muhimu zote za watu wale” alieleza Sixmund, na hapo mfalme akamtazama mke wake, ambae pia alikuwa anamtazama kwa mshtuko na mshangao, “Habari njema ni kwamba kati ya wawili walio salia, ambao Habari zao zimeatikana ni Waziri Chitopela ambae katika mpango wetu, tumepanga kutomuhoji chochote, maana yeye ndie aliekuwa kiongozi wa zoezi lile, hatuna uhakika kama mahojiano yetu na yeye hayatoleta madhara katika taifa letu” alisema Sixmund.

Na hapo Elvis akadakia, “na huyo mwingine ni nani na yupo wapi?” aliuliza Elvis aliekuwa na shauku kuu, “huyo mwingine ni sajent taji Ashraff Kibwana wa MLA, na baadae MLSA, ambae alitoweka miezi michache baada tu ya kumalizika kwa operation ile ya kuondoa waasi, na ameanza kuonekana miaka michache iliyopita huku magharibi katika nje ya kitongoji cha Komwe, anaishi kama mkulima muhamiaji masikini” alieleza Sixmund, ambae pia alieleza kuwa tayari wamesha tuma askari kwaajili ya kwenda kufanya nae mahojiano, “tunaamini kuwa huyo atakupatia majibu sahihi tunayo yahitaji” aliitimisha Sixmund, na hapo Elvis akamtazama mke wake kama vile anawazo fulani lenye mashaka akilini mwake, ni sawa na mke wake ambae pia alikuwa anamtazama kama yeye, “ok! katika hali yoyote, Ashraff apatikane, mimi nipo njiani, nieleze nikukute wapi nataka kusikia mahojiano kwa masikio yangu” alisema Elvis wakati huo yeye na mke wake walikuwa wameshainuka toka kitandani na kuelekea kwenye kabati la nguo za kawaida ambazo mara nyingi huzitumia katika matembezi yao binafsi na ya siri.

Kitu cha kujua msomaji ni kwamba kuna wakati ambao Elvis na Vaselisa, huwa wanakuwa na tamaa ya kufanya matembezi wakiwa kama raia wa kawaida, hivyo huvaa kikawaida na kuingia kwenye gari kisha kuondoka zao kuelekea mitaani hasa nyakati za usiku, ambako utembea sehemu mbali ikiwemo kwenye viunga ya bustani za TT City, ambako hupenda kutumia sehemu zile kufanyia utani wa kimapenzi na michezo ya wapenda nao, vitu ambavyo walivifanya sana wakiwa Tanzania miaka michache iliyopita. *******

Yaaap! Kilomita zaidi ya nane toka njia panda ya kisarawe na kibaha, magharibi mwa kisarawe ndani ya msitu wa Kazi Msumbwi katika machimbo ya kokoto laini na mchanga, bado wakina Kadumya wanaonekana wakiwa wamesimama na magari yao mawili wanasubiria wenzao ambao tayari walikuwa wamesha karibia.

Muda wote bwana Kafulu, ambae siku za nyuma alikuwa anajiita JJD, alikuwa anawaza kuhusu kitu kilicho mtokea kule makabe na kuona kama alidhalilishwa vibaya sana, hasa akikumbuka jinsi ambavyo alionyesha umwamba mbele ya Veronica na kijana Deus, ambae dakika chache baadae akamchapa kama mtoto na kuondoka na Veronica akiwa amechukua fedha ambazo zingesaidia katika mpango wa mapinduzi, “mshenzi sana huyu, hakutaka kuniachia nifungue kitumbua toka kwenye box mimi mwenyewe, aliwaza Kafulu ambae baada ya kuwaza kwa muda akapata wazo, “mkuu mimi na wazo ambalo litatusaidia kumpata yule Dereva na Veronica pamoja na fedha zetu” alisema Kafulu, akimueleza Kadumya aliekuwa amesimama pembeni yake wote wanavuta bangi, “mpango gani huo Kafulu?” aliuliza Kadumya kwa sauti ya tabu kidogo kutokana na kuubana moshi wa bangi mdomoni na puani.

Hapo Enock Kafulu akaanza kueleza mpango wake ambao ulikuwa ni kujifanya wateja wapya na kumpigia simu Deus, wakimueleza sehemu ya kuchukuwa abiria au mzigo, “ili akiingia hapo, tayari askari wetu watakuwa wanamsubiri kuwaweka chini ya ulinzi” alieleza Kafulu na hapo likaonekana tabasamu usoni kwa Kadumya, “upo sawa kabisa Enock, tena safari hii ni vyema kama tukitumia simu yako” aliunga mkono Kadumya ********

Naaaam, Songea mkoani Ruvuma, giza lilikuwa limetanda kweli kweli, mji ulikuwa kimya kabisa, ni wazi watu walikuwa wamelala mida hii ya usiku mkubwa, lakini basi nyumbani kwa mzee Frank Nyati iliyopo mtaa wa Making’inda, bado tunamuona mzee huyu akiwa ametulia sebuleni na simu yake sikioni, ni wazi alikuwa anampigia mtu fulani ambae hakuwa na mpango wa kupokea simu hiyo, “kwanini huyu mpuuzi hapokei simu, lazima ajue kuwa MLA wapo dar kuwa saidia na kwamba kila anachokifanya ni kwaajili ya nchi yake ya asili nchi ya baba yake nchi ya babu zake” alijisemea mzee Frank, ambae mpaka sasa alikuwa ameshapiga simu zaidi ya mara kumi bila kupokelewa.

Hali hiyo pia ilikuwa huko kinyerezi dar es salaam, katika nyumba ya bwana James, mtaa ulikuwa kimya kabisa, japo baadhi ya nyumba za jirani na nyumba ya bwana James, walionekana watu wakiwa wanachungulia katika madirisha yao, lakini ni katika hali ya umbea tu kuona kitu kinachoendelea kwa wale askari wa jeshi la ulinzi walio zunguka uzio wa jengo la bwana James.

Lakini upande wa ndani ya nyumba hiyo ambayo ilikuwa imepewa ulinzi mkali sana, sasa tuna waona watu ishirini, yani askari kumi na sita wa MLA, askari wa jeshi la Tanzania na bwana James wakiwa na familia yake, bwana James akiwa anapiga simu ya binti yake ambayo iliita muda mrefu bila kupokelewa, kitu ambacho kilikuwa kinampatia wasi wasi mkubwa juu ya usalama wa binti yake, “isijekuwa yule kijana ameshapatana na wale washenzi awapatie Veronica kwa malipo, aliwaza mzee James huku anawatazama watu wengine mle ndani.

Askari walikuwa busy na mipango yao, mke wake alikuwa na binti yao Caroline wamekaa kwenye kochi moja wanasinzia kutokana na kulemewa na usingizi, “lazima nifanye jambo kabla mambo hayajawa mabaya zaid na binti yangu kufikishwa kwenye mikono ya UMD” aliwaza mzee James huku anainuka toka kwenye kochi na kuelekea chumbani akiwa na simu yake mkononi. *******

Naaaam! Sasa turudi Visegese, sasa tuyaona magari yale Matano ya polisi, manne yakiwa ni magari ya viongozi wakuu wa jeshi hilo ngazi ya mkoa, yaliyokuwa yanakatiza eneo lenye kibarabara hafifu kilicho tokomea upande wa kulia wa barabara na gari la nne katika msafara ndani yake yupo bwana Ulenje, ambae anaonekana akibofya bofya simu yake kwa namna ya kuingia kwenye sehemu ya miito iliyopita, anaonekana kukwama kwenye namba zilizo ambatana na jina la Cheleji, na bwana Ulenje anaipiga namba ile ambayo inaita kwa muda mfupi kisha inapokelewa, “ndiyo afande” ilisikika sauti toka upande wa pili wa simu, “sikia Cheleji, kuna kazi ya kufanya” alisema Ulenje, na kuanza kutoa maagizo kwa askari wake huyu anaemuamini kuliko wote.

Wakati huo sisi tunaachana na magari yale, tunaelekea upande kulia wa barabara, tuna fuata ile barabara ndogo ambayo mbele tuna wapita wakina Songoro waliokuwa wamesimama sehemu wakipata mapumziko ya kuvuta sigara bwege, huku Songoro mwenyewe akinywa pombe yake, kila mmoja wao akiwa na silaha yake mkononi, maongezi yao yalikuwa ni namna watakavyo muadhibu Dereva wa BMW na kummalizia kwa kifo chenye maumivu makali, “dogo anabahati sana, yani tunge mnasa pale hotelini angejisahau hata yeye mwenyewe kwa kitu ambacho tungemfanyia” aliongea Side kwa namna ambayo ungesema anazungumzia kukamata kuku wa kisasa, hakika wangejua nadhani wangeachana na mpango wao na kufuata maelezo ya Ulenje.

Tunaachana na wakina Songoro, tunasogea mbele zaidi umbali kama wa mita mia mbili, ambapo pana nyumba ya chakavu yenye kuzungukwa na mashamba madogo ya mboga mboga yaliyostawisha mboga mboga vizuri kabisa, tunaingia ndani ya nyumba hii moja kwa moja chini kabisa eneo la sebuleni hakuna mtu yoyote, tunaelekea chumbani kwa Deus ambako safari hii kabla hatujaingia ndani, mara mlango unafunguliwa na wanatokea wapenda nao wawili, waliokutana kwa mara ya kwanza na kuzindua penzi lao katika siku hii ya kwanza, safari hii tunamuona Deus alievalia bukta pekee bila tishert akiwa amembeba kifuani mwanadada mrembo Veronica alievalia truck suti na tishert nyingine, sura zao zikiwa zimetawaliwa na matabasamu ya furaha, macho yao yanatazama kwenye simu ambazo zilikuwa zimetulia, nao wanaishia kwenye makochi, Deus anamlaza Veronica kwenye kochi kubwa na yeye anakaa pembeni, lakini Veronica anajiinua kidogo na kujilaza kwenye mapaja ya Deus.

Naaam ile wanaanza kumiminiana wine kwenye grass mara simu ya Deus inaanza kuita, safari hii sio ile simu yake binafsi, ni simu ya kazi, Deus anaitazama akijaribu kuangalia kama ni mteja anaemfahamu au mpya, anaona kuwa ni mteja mpya, Deus anaichukuwa simu kwa tahadhari kubwa huku anajiuliza isije kuwa ni wakina Kadumya wameamua kutumia namba ngeni ili wajaribu kupanga mipango yao fake kwaajili ya kumnasa awapatie Veronica na Fedha, na pengine kumuangamiza kwasababu amesha jua wao ni wakina nani.

Deus akapiga moyo konde na kupokea simu na kukaa kimya ili kusikiliza sauti ya mpigaji wa simu yake, “hallow kijana Dereva, mimi ni mteja wako, naitwa bwana……” ilisikika sauti yenye kunong’ona toka upande wa pili wa simu na kabla hajamaliza kuongea mtu huyo Deus akamuwahi, “kabla ya yote unataka kuvunja sheria namba moja “HAKUNA KUJUANA MAJINA” alisema Deus kwa sauti tulivu kama ilivyo kawaida yake, huku Veronica alietulia juu ya mapaja ya Deus Nyati, akimtazama kijana huyu mpole wa sura na uongeaji, lakini mbaya kwenye ulaji wa kitumbua na mapigano...…….ENDELEA MDAU, COMMENT LIKE VINAMPA HAMASA MTUNZI YA KULETA HUU MKASA KWAN NDIO ATAJUA KUWA KUNA WATU WANAFUATILIA...

NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA THELATHINI

TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA ISHIRINI NA TISA:- Deus akapiga moyo konde na kupokea simu na kukaa kimya ili kusikiliza sauti ya mpigaji wa simu yake, “hallow kijana Dereva, mimi ni mteja wako, naitwa bwana……” ilisikika sauti yenye kunong’ona toka upande wapili wa simu, na kabla hajamaliza kuongea mtu huyo, Deus akamuwahi, “kabla ya yote unataka kuvunja sheria namba moja “HAKUNA KUJUANA MAJINA” alisema Deus kwa sauti tulivu kama ilivyo kawaida yake, huku Veronica alietulia juu ya mapaja ya Deus Nyati, akimtazama kijana huyu mpole wa sura na uongeaji lakini mbaya kwenye ulaji wa kitumbua na mapigano...…….ENDELEA…

Kijana ambae sio tu kwa kuwa amemsaidia kutoka mikononi mwa watu ambao walipanga kumfanyia kitu kibaya, ila pia ni mtu ambae amekuwa Rafiki yake kwa muda mrefu japo hawakuwahi kukutana mwanzo, na leo ikiwa siku yao ya kwanza kukutana amejikuta amezama kwenye penzi lake pasipo kujari tabia yake ya kuuwa bila kujiuliza mara mbili, “hoooo! Samahani kijana nilisahau, lakini nakuahidi sitovunja sheria hata moja” ilisikika sauti ya mwanaume mtu mzima, “ok! nafasi ya mwisho, ongea mpango bila kuvunja sheria” Veronica alimsikia Deus akiongea kwa sauti ile ile tulivu, japo hakujua anaongea na nani, ila kiukweli alijua anaongea na mteja wake maana tayari alisha sikia mambo ya sheria.

“kijana sijui nisemeje maana siwezi kujitambulisha kama ilivyo sheria yako namba moja, ila ninahitaji uniletee binti yangu kwa kiasi chochote unachohitaji” ilisikika ile sauti ya mtu mzima yenye kunong’ona toka upande wa pili wa simu ni wazi hakutaka watu wengine wamsikie, “sehemu ya kumchukuwa na sehemu ya kumpeleka?” aliuliza Deus Frank Nyati, mwenye jina la utani, msafirishaji au mchoraji, “sehemu ya kumchukua ni pale ulipompeleka na sehemu ya kumleta ni kinyerezi mwisho nyumbani kwangu, hapo Deus akajua kuwa anaongea na bwana James Kelvin, akamtazama Veronica ambae alikuwa amelala pajani mwake huku macho ameyaelekeza kwake, macho yao yalipokutana, Veronica akajitabasamulisha na Deus nae akatabasamu, “mpango umekataliwa, nitakua navunja sheria namba 4” alisema Deus, kwa sauti ile ile kama hataki vile, kisha akataka kukata simu, lakini kabla hajakata simu mzee James akawahi, “subiri kijana, kuna mpango gani mwingine juu ya binti yangu?” aliuliza mzee James kwa sauti ambayo ilionyesha wazi kuwa alikuwa amesha changanyikiwa kusikia vile, maana Sheria namba nne inasema hakuna mpango juu ya mpango.

Ukweli ni kwamba, ilikuwa ni vigumu kwa Deus, kuingia mpango wa biashara juu ya Veronica ambae ukiachilia kuwa katika hatari ya kuvamiwa na kushambuliwa muda wowote huku baba yake akikosa msaada wa kumlinda, na pia alishapanga kuwa asingefanya kazi ile tena, na ili apate nafasi ya kuishi kama mtu wa kawaida, maana kamafedha tayari alikuwa nayo, lakini kubwa zaidi ni kwamba, mschana huyu kwa sasa ni mpenzi wake na wameshaingia katika makubaliano ya kuchumbiana.

Deus akamtazama tena Veronica, ambae bado alikuwa anamtazama kama vile aamini kama mtu alie kuwa ana wasiliana nae kila siku ndie huyu mbele yake, na kwamba anaenda kuwa mpenzi wake wa siku zote, hakufikiria kuhusu kile anachoongea kwenye simu ya kwamba kina muhusu yeye, “tayari huyo yupo kwenye mpango uliotangulia, siwezi kubadiri mpango wa mwanzo” alisema Deus, kwa sauti ile ile, ambayo kama unafahamu matendo yake ungesema ile sauti ni ya kuigiza, na siyo sauti yake halisi, lakini ukimtazama usoni, ungejua kuwa Deus anaupole ni waasili.

Maneno yale ni kama yalimshtua zaidi mzee James, ambae ni wazi alihisi kuwa tayari binti yake alikuwa katika mpango wa kupelekwa kwa wakina Kadumya kama alivyo hisi mwanzo, “nakuomba kijana, nipo tayari kukulipa mara tano zaidi ya malipo uliyoaidiana na hao washenzi” ni Deus pekee ndie aliekuwa anasikia sauti ya mzee James aliekuwa analalamika, “mzee nimesema siwezi kuingiza mpango juu ya mpango mwingine, huwa nasimamia sheria zangu” Veronica alimsikia mpenzi wake huyu akiongea kwa sauti ya upole kama vile hakumaanisha alichokisema, “jamani mchoraji wangu si umkubalie tu, mbona kama mteja wako anakuomba sana” alisema Veronica kwa sauti nyororo iliyojaa mahaba makubwa, Deus anamtazama huku anatabasamu nakukata simu.

Lakini ile anakata simu na wakati huo, simu hiyo hiyo ikaanza kuita tena, “bado hujamalizana na mteja wako, huyooo anapiga tena” alisema Veronica huku anaachia tabasamu la kivivu, kama unge waona wawili hawa basi ungejua kuwa bado muda ilikuwa ni mapema sana.

Deus akaitazama namba ya mpigaji wake, ambae mwanzo alijua kuwa ni mzee James, yani baba wa binti huyu, lakini alipotazama ile namba haikuwa na mfanano wowote na ile namba ya mwanzo, akaipokea na kuiweka sikioni. Na wakati huo huo ikasikika simu ya Veronica nayo inaanza kuita, Veronica anaitazama anaona kuwa ni baba yake ndie aliekuwaa anapiga, Veronica akamtazama Deus, kama vile anamuomba apokee simu, nae akamuonyesha ishara ya kwamba apokee, wakati huo nayeye simu ilikuwa sikioni na macho kwenye kioo cha TV kubwa kwenye kona ya kulia ya sebule, ambapo kijana wetu aliweza kuona kipande cha camera na mbili, kukiwa na watu kumi waliosimama nje ya magari yao, mawili huku bunduki zao zikiwa mikononi. ********** Naam huko #Mbogo_land, ndani ya mtaa tulivu unaonakaliwa na viongozi wenye hadhi ya kipekee, kama vile wajumbe wa kamati za serikali, mawaziri na wazee wa mabaraza mbali mbali, ulikuwa kimya kabisa, kama ulivyokuwa mji mzima wa Treach Town, moja kati ya majiji ya kifahari duniani, ikiwa namba mbili kwa starehe kutoka kwa jiji la paris, na jiji la kwanza kwa usafi na utajiri duniani.

Nalo lilikuwa kimya kabisa, maana tayari watu walikuwa wameshalala, hata kama ulilala masaa kumi na mbili ya mchana, lakini ifikapo saa nane za usiku, lazima utapatwa na japo kalepe ka usingizi, labda kama ukiwa na kazi ya kufanya au mafunzo maalumu ya kuvumilia uchovu wa usingizi, japo mida hiyo lazima utahisi kitu fulani mwilini mwako, japo inakuwa tofauti kwa mtu aliepo bar.

Nyumbani kwa Waziri Chitopela, mambo yalikuwa tofauti kidogo, yeye licha ya kuhisi usingizi mkali, lakini bado alijitahidi kunywa pombe yake na kuendelea na mipango yake ya kimapinduzi, huku anasuka properganda moja kubwa, ambayo ingeshtua nchi nzima ya #mbogo_land, lengo ni kutoa nafasi kwa majeshi yake yafanikishe lengo.

Naam sasa bwana Chitopela, anaonekana akimaliza kuandika kitu fulani kwenye computer mpakato yake na kutuma kwa mtu fulani, kisha akachukua simu yake na kuipiga, simu haikuita sana ikapokelewa, “afadhari Chilopo umetambua kuwa leo sio siku ya kulala” alisema Kadumya mara baada ya simu kupokelewa, “siwezi kulala mkuu wakati najua siku za mapinduzi zinakaribia” alisikika Chilopo kwa sauti yenye kuelemewa na uzito wa usingizi, “ok! changamka tufyetue mabomu mawili mazito, tayari nimesha kuwekea kwenye email yako” alisema Chitopelah na Chilopo akakubaliana nae, “bila shaka mkuu, inatekelezwa sasa hivi” alisema Cholipo, sambamba na sauti ya kuliza kwa kitanda, ikionyesha wazi kuwa Chilopo alikuwa ananyanyuka toka kitandani, “ok! nakutakia mafanikio bwana Chilopo, Waziri wa Habari ajae” alisema Chitopela kabla ya kukata simu.

Ile anakata simu, bwana Chitopela, kabla hajaweka simu mezani akaisikia ikitekenye mkono wake, kwa mtetemo wa muito, akaitazama kuona mpigaji, nae alikuwa ni Kobwe, mkuu wa kombania A, ya batallion ya UMD, akaipokea maea moja, “niambie Kobwe, natarajia kusikia habari njema” alisema Chitopelah, kwa shauku, ndio mkuu habari njema ni kwamba sasa ndio tunaingia sehemu ya makutano na wakina Kadumya” ilisikika sauti toka upande wa pili, hapo Kadumya akatazama saa yake, ilikuwa inasoma saa nane, “mwendo mzuri bwana Kobwe, nasubiri taarifa zaidi za kazi” alisema Chitopela, kabla ya kukata simu.*********

Naaam, wakati huo huo, magaharibi mwa TT City, barabara ya kutokea Komwe, katika mashamba yaliyopo pembezoni mwa mto Bhumbu za Kwala, magari manne ya kijeshi yalionekana yakitembea kwa kasi ya nguvu, Askari mtoro wa MLA staff sajent Ashlaff Kibwana akiwa mwenye hofu kubwa na pasipo kuamini kile kinacho mtokea, alikuwa amekaa ndani ya gari zuri la kijeshi, lenye muonekano wa gari la ki VIP, pembeni askari wawili wenye bunduki zao, aina ya Uzi, pia nyuma kabisa walikuwa askari wawili wenye bunduki kama hizo, na seat ya mbele ya abiria pia kulikuwa na askari mwenye bunduki, hakika licha ya MLA kumueleza mzee Ashlaff, kuwa hawakuwa na lengo baya kwake na kwa familia yake, ambao walikuwa kwenye gari la nyuma yake, lakini ulinzi na ujio wa askari hawa wajeshi ambalo hapo mwanzo aliwahi kulitumikia.

Dakika ishirin baadae, tayari magari yale yalikuwa yamesha ingia mjini, nae bwana Ashlaff akitazama mitaa ya jiji lile ambalo kwa miaka mingi hakuwa na uwezo wa kutembea akiwa huru, safari inaenda moja kwa moja mpaka Mtaa wa Sizwe, ni mmoja kati ya mitaa tulivu katika jiji la Trench Town na wenye sifa ya kukaliwa na viongozi wakubwa wa ulinzi na usalama.

Moja kwa moja magari yanaenda kusimama mbele ya lango kubwa la chuma lililoshikizwa kwenye kuta kubwa na imara, ukuta licha ya kuwa mrefu na wenye ulinzi wa umeme, lakini pia kulikuwa na askari kadhaa MLA, waliokuwa wamesimama nje ya lango lile na bunduki zao mikononi.

Lango linafunguliwa na magari yote yanaingia ndani, ambako pia wanakutana na magari mengine ya kifahari zaidi kasoro gari moja dogo ania ya Toyota caldina, huku wakionekana askari kadhaa wenye bunduki wakiwa wamesimama imara wakitazama pande zote za ukuta ule pasipo kuhangaika na magari yale yaliyokuwa yanaingia.

Mzee Ashlaf ambae hakuwa na pingu wala kibanio cha Kamba, licha ya kuwa alihakikishiwa usalama wake, lakini bado alionekana kuwa na wasi wasi juu ya usalama wake na familia yake, mzee huyu anaona magari yana simama, askari wanashuka mara moja, “mzee kumbuka upo na familia yako, hatutaki kuipa wasi wasi na mashaka yoyote familia yako, hivyo utafuata kile tunacho kueleza bila kujaribu kufanya ujanja wowote” alisema askari aliekuwa amekaa seat ya mbele ya gari lile alilopanda Ashlaf, ambae kwenye kosi za shati lake jeusi la sare za uvamizi wa usiku, ungeona nyota mbili kila upande, ikimtambulisha kuwa ni mwenye cheo cha luten.

Hapo bwana Ashlaf anatazama kwenye gari la nyuma na kuwaona mke wake na Watoto wake wakiwa wanashuka toka kwenye gari na kusimama pembeni ya gari lile, huku wakionekana kushangaa, kwa maana ya kutokujua kinachoendelea, ila nyuso zao zilionyesha kuwa na uoga kwa kiasi kikubwa, “bila shaka, afande, lakini naomba msiushishe familia yangu kama mlivyofanya kwa wengine” alisema Ashraff ambae alionekana kutokuwa na imani na wana MLA hawa, “ondoa shaka na ushuke kwenye gari” alisema yule luteni wa MLA kwa sauti ya chini, ni wazi hakutaka mke na watoto wawili wa bwana Ashraf wasikie maongezi yao.

Naaam bwana Asraff ana shuka toka kwenye gari, na wakati huo huo anamuona askari mmoja wa kike akija mbele ya mke wake na Watoto wake na kuwaongoza kuelekea ndani ya jengo lile, na wakati huo huo wakati wao wanaingia ndani, wanapishana na kanali Jastin, “safari itaishia hapa, hatuendi LS Base, mpelekeni kwenye chumba cha mahojiano” alisema kanali Jastin Johnson, kisha akarudi ndani ya jengo lile la kifahari, usingefikilia kuwa ni jengo linalomilikiwa na jeshi la ulinzi la nchi hii ya kifalme.******

Naaaam! Sasa turudi njia panda ya kisarawe, ambapo tuna wakuta askari wa jeshi polisi, PT yani Polisi Tanzania, wakiwa bado wamekaa kwa vikundi, huku wengine wakiwa wametafuta sehemu za kujiegesha na wengine wakianza kusinzia kabisa kutokana na muegesho ule.

Tofauti na kundi dogo la askari kumi na tano, ndani ya jeshi hili linalo aminiwa na serikali, walio kuwa wamesimama pembeni kabisa katika vikundi vidogo vidogo wakiendelea kuwasha mienge ya sigara na bangi, na ndio wakati ambao koplo wa polisi Cheleji, aliekuwa na koplo Othman alikuwa anamaliza kuongea na simu, “kaka kimeumana” alisema Cheleji, huku anaweka simu mfukoni na kutoa mkebe wa risasi kwenye bunduki yake, akaitazama kama ina risasi, akagundua kuwa ilikuwa nazo lakini chache, nadhani alizitumia kuwashambulia wakina Deus kule barabara ya malamba mawili, “vipi mkuu anasemaje?” aliuliza Othman, kwa sauti yenye shauku, huku anamtazama Cheleji aliekuwa anaweka ule mkebe wa risasi kwenye kifuko kilichopo kiunoni mwake na kutoa mkebe mwingine uliosheheni risasi, “kuna kazi relini inabidi ikafanyike” alisema Cheleji, huku anaupachika mkebe wa risasi kwenye bunduki yake.

Wakati wanaongea hayo, wakati huo huo, wakayaona magari yanaingia pale njia panda, yakitokea upande wa kibaha, hakuna alieuliza ni magari ya nani, tayari walishajua ujio wa wakuu wao, hivyo haraka sana wakajikusanya mbele ya magari yale kwaajili ya kusikiliza amri za matarajio.

Dakika mbili baadae tayari viongozi walio tangulia na askari pale njia panda, walikuwa wameshaanza kutoa taarifa za mwanzo kwa mkuu wa polisi kanda ya dar es salaam, “afande mpaka sasa uelekeo wa waharifu ni kazimzumbwi, hatuna uhakika kama huku walikoelekea ndiko kwenye makazi yao au wamekimbilia kwasababu ya kujificha kwa muda” alisema yule Assistant inspector, “vipi kuhusu yule mualifu Deus Nyati, yule Dereva mwenye gari jeusi, kuna taarifa zozote za kufahamu sehemu alipo kwa sasa?” aliuliza CP Nyambibo, huku Ulenje na wenzake wakiwa wanasikiliza taarifa zile, “afande zaidi ya taarifa za kuonekana barabara ya maramba mawili hakuna taarifa nyingine ya kuonekana kwake” alisema yule inspector.

Hapo Kamanda Nyambibo akawatazama wenzake, yani makamanda wa polisi mikoa, “mnashaurije sasa?” aliuliza Nyambogo, akiwazama kwa zamu, “afande nashauri tusi jiziuke na hawa wenye magari peke yao, muhimu zaidi ni yule dereva wa gari jeusi” alisema kamanda Ulenje, lakini Nyambibo akaonekana kutokukubaliana na wazo hilo, “ujue Ulenje mpaka sasa Deus Nyati hajawa hatari kama walivyo hao jamaa, kwasababu mpaka sasa wamesha uwa polisi, lakin Deus amekuwa akitukikimbia tu” alisema CP Nyambibo na Ulenje akaona ndio nafasi ya kutoa ushauri, ambao utawapotosha wenzake na kuwaokoa wakina Kadumya, hivyo haraka sana akadakia, “naitakuwaje kama Deus Nyati ni mshiraka wa hao wengine, huoni kama tukimpata yeye itatusaidia kuwapata hao wengine?” alisema Ulenje.

Hapo Ulenje akamuona CP Nyambibo akiwa tazama wenzake kwa macho ya mshangao na kiulizo na mshangao, nao wakaoi

Hapo Ulenje akamuona CP Nyambibo akiwa tazama wenzake kwa macho ya mshangao na kiulizo na mshangao, nao wakaonekana kuwa na hali kama ya mkuu wao Nyambibo, ni wazi walishangaa kusikia maneno yale toka kwa kamanda huyu wa ngazi za juu za jeshi la polisi, hasa kanda maalumu ya dar es salaam, hata yeye mwenyewe alijiona kama amekosea kuongea jambo lile, ambalo aliamini kuwa wenzake hawana ufahamu nalo, ulenje akamuona Nyambibo anamgeukia na kumtazama kwa macho ya mshangao…....…….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao Kujia hapa hapa jamii forums
Shukrami sana Mkuuuunekana kuwa na hali kama ya mkuu wao Nyambibo, ni wazi walishangaa kusikia maneno yale toka kwa kamanda huyu wa ngazi za juu za jeshi la polisi, hasa kanda maalumu ya dar es salaam, hata yeye mwenyewe alijiona kama amekosea kuongea jambo lile, ambalo aliamini kuwa wenzake hawana ufahamu nalo, ulenje akamuona Nyambibo anamgeukia na kumtazama kwa macho ya mshangao…....…….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao Kujia hapa hapa jamii forums
Shukrani sana Mkuuu
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA THERASINI NA MOJA
MTUNZI: Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA THERASINI:- Hapo Ulenje akamwona CP Nyambibo, akiwa tazama wenzake kwa macho ya mshangao na kiulizo, nao wakaonekana kuwa na hali kama ya mkuu wao Nyambibo, ni wazi walishangaa kusikia maneno yale toka kwa kamanda huyu wa ngazi za juu za jeshi la polisi, hasa kanda maalumu ya dar es salaam, hata yeye mwenyewe alijiona kama amekosea kuongea jambo lile ambalo aliamini kuwa wenzake hawana ufahamu nalo, ulenje akamuona Nyambibo anamgeukia na kumtazama kwa macho ya mshangao…....…….ENDELEA…

Kabla haja sogeza uso wake karibu na usawa wasikio lake yeye Ulenje, “ni aibu ACP hufuatiliii taarifa ya hiki kinachoendelea, Deus na hawa jamaa ni maadui wakubwa, japo wote wanahitajika wakamatwe haraka iwezekanavyo” alinong’ona yule CP Nyanmbibo kabla haja wageukia askari na kuanza kugawa majukumu kutokana na mikoa.

Ambapo katika mikoa ya kipolisi mitatu, miwili yani temeke na Kinondoni, ilielekea kazi mzumbwi na mmoja wa Ilala ulibakia nyuma, huku makamanda wote wakiwa katikati.

Dakika kumi mara baada ya magari ya polisi yenye askari wa temeke na Kinondoni kuondoka, ndipo Cheleji na Othman walipo gawana majukumu, “sasa kaka wakati ndio huu, ni vyema kama tutaondoka haraka tukamalize kazi, kisha tutoe taarifa itakayo warudisha wale na kuacha kuwafuatilia wakina Kadumya” alisema Cheleji, kisha kimya kimya na kwa usiri mkubwa wakaingia kwenye magari yao na kuanza kuondoka kwa kuachiana nafasi ya dakika kadhaa, kiasi cha kutokuwa shtua wenzao kwamba magari yale yanaondoka kwa kazi maalumu.

Yaaap! Akiwa ameshtushwa kwa maneno ya Dereva wa BMW jeusi, msafirishaji Deus Frank Nyati, mzee James ambae pia aliweza kuisikia sauti ya binti yake akiongea kwa mahaba na kijana yule hatari akiwa chumbani kwake mzee huyu, anapiga simu haraka kwa binti yake, ambae dakika chache zilizopita amejaribu kumpigia bila mafanikio.

Lakini safari hii, bahati nzuri kwake, simu inapokelewa mara moja, “baba hujajalala mpaka saa hizi” mzee James anakutana na sauti ya binti yake, ambayo haikuwa na wasi wasi hata kidogo, “nitalalaje wakati sina uhakika wa usalama wako Vero, hebu niambie ni kweli upo na huyo kijana Dereva” aliuliza mzee James kwa sauti ya kunong’ona.

Hapo ilitumia sekunde kadhaa kujibiwa, ni wazi Veronica alikuwa anaomba ruksa ya kueleza ukweli, “ndiyo baba, kwani wasi wasi wako nini, si nilikuambia kuwa nipo salama, tena nyie ndio munapaswa kujiangalia sana, maana hawa majambazi hata hawaeleweki, yaani hadi polisi wengine wanasaidiana nao” aliongea Veronca, na wakati huo huo mzee James alikuwa anasikia sauti ya kiume ikiongea na simu nyingine, japo hakusikia kinachoongelewa na mwanaume huyu ambae kwa vyovyote alikuwa ni Deus Nyati.

Hapo kidogo ni kama mzee huyu alipoa, “huku kuhusu sisi ondoa wasi wasi, tunalindwa na majeshi ya ulinzi, pia hata jeshi la #mbogo_land lipo hapa kutulinda na mwisho watatupeleka nchini kuonana na mfalme” ilimshtua kidogo Veronica, “mh! Unasema majeshi ya Mbogo land kuonana na mfalme?” aliuliza Veronica kwa mshangao, “ndiyo tena hapa tunakusubiri wewe tu” alisema mzee James, huku safari hii akitoka chumbani na kuelekea sebuleni aliko lwaacha wenzake, “hizo Habari tumesha zipata, lakini wasi wasi wangu ni huyo kijana, utawezana nae kweli maana anasheria zake hizo ukiivunja moja hata kama amekisaidia vipi anaweza kuchinja mara moja” alisema mzee James, huku watu waliokuwa sebuleni wakisikia sauti yake, maana sasa alikuwa anakaribia sebuleni, mzee James akabofya kitufe cha kuruhusu sauti ya wazi.

Hapo wote wakapata nafasi ya kusikia sauti ya Veronica, “wala usiwe na wasi wasi baba, Deus ni Rafiki yangu wa siku nyingi” sauti hii ya Veronica ambayo iliwafikia watu wote waliokuwa sebuleni, usingedhania kuwa ndie aliekuwa amewajaza watu hapa sebuleni kwenye nyumba ya baba yake, maana ilikuwa ni sauti ya kujiachia kama vile mtu aliepo nyumbani kwake au ofisini kwake, na pengine hotelini na mpenzi wake.

Hata mama Veronica na Carolina waliokuwa wamekaa kwenye kochi moja walionekana kushangazwa, maana wakati Carolina akiwa anatoa macho kwa mchangao, tayari mama yake alikuwa ameshainuka mbio mbio, akamfuata mume wake, “una uhakika ni Vero? huyo kijana…..” mzee James hakumaliza kuongea tayari mke wake alisha pokonya simu, “we Vero, kama unasema kweli sasa kwanini hurudi nyumbani unatuweka roho juu juu wenzako?” aliuliza mke wa mzee James ambae ndie mama yake Veronica kwa sauti ya ukali kidogo, “mama jamani si nilisema wakati tuna kuja huko polisi walitushambulia, tumekaa sehemu mpaka kesho tutarudi maana wakituona tu watatushambulia tena” alisema Veronica kwa sauti ya kudeka, kama mtoto anaeomba ruksa ya kulala kwa Rafiki yake.

Hapo captain Amosi Makey akanyoosha mkono kwa mama Veronica kuomba simu, “haya kuna mtu anataka kuongea na wewe” alisema mama Vero kabla hajatoa simu kwa Amos Makey, troop kamanda wa kikundi maalumu cha uchunguzi wa kivita toka MLA, “mtu gani tena mama?” aliuliza Veronica, lakini tayari simu alikuwa nayo Amos Makey, “naitwa Kaptain Amos Makey toka ML..” hakupewa nafasi ya kumaliza kujitambulisha, tayari simu ilishakatwa, “amekata” alisema mzee James, huku anaichukua simu na kuipiga tena, lakini ilifanikiwa kuita mara moja tu na ikakatwa tena, na walipo jaribu kupiga tena wakasikia simu haipatikani kwa maana ilikuwa imeshazimwa, wote wakatazama kwa macho yenye wasi wasi mkubwa, huku Carlolina, akiwa anatabasamu kwa fadhaha, “mh! najua tu, dada hawezi kukwepa kwa kaka Deus” ilimchomoka Veronica kwa sauti ya chini, lakini iliyosikika vyema kabisa na wao wakamtazama, huku mama yake tu akiwa anajua alicho maanisha Carolina.******

Naaam tukienda machimbo ya kokoto kule Kazimzumbwi, na sasa tunaona magari ya kijeshi, yakiwa yamesimama na askari UMD wakionekana wakiwa wanashusha baadhi ya mizigo toka kwenye gari, ambayo ni maboxi ya silaha, tayari kujiandaa kwa majukumu yaliyo waleta.

Kaptain Kobwe anaonekana akiwa amesimama na wakina Kadumya, huku Kadumya mwenyewe akiwa anaongea na simu kwa sauti ya wazi, huku wenzake wasikie kinachoongelewa, “hallow bwana Dereva, ni bahati haujalala mpaka sasa maana tuna kazi ya kufanya usiku huu” alisema Kadumya kwa sauti nzito yenye mikwaruzo, “ok! nakusikiliza” ilikuwa ni sauti tulivu ya Dereva, toka upande wa pili wa simu, sauti ambayo licha ya utulivu na upole wake, lakini yeye aliiona kuwa ni kama sauti ya mzimu au jini lenye hasira, “kuna mzigo toka stendi maili moja unatakiwa upelekwe bagamoyo” aliongea Kadumya, huku Kafulu na kobwe wakimsikiliza pembeni na kutabasamia chini chini, “uzito wa mzigo” ilisikika ile sauti ambayo sio tu Kadumya ndie alieichukia, hata Kafulu yani JJD, aliiona kama ni chukuzo kubwa.

Kadumya akamtazama Kafulu, ambae pia alikuwa anamtazama akionyesha pia hakuwa amejiandaa kwa swali kama hilo, “kilo kumi” alijibu Kadumya kwa kuona kuwa Kafulu hakuwa na msaada, “muda na sheria zako tafadhari” ilisikika sauti ya Deus Nyati, sauti ambayo ilimfanya Kobwe asiamini kile alichokisikia juu ya mtu huyu anae sadikiwa kuwa ni hatari sana, “muda ni saa tisa na nusu, sheria ni kuzingatia muda” alisema Kadumya kwa sauti ile ile ya mikwaruzo, na wote wakatulia kusikiliza atachoongea dereva, lakini kikapita kimya pasipo Dereva kuongea, “hallow dereva, bado tupo pamoja, nitajie malipo yatakuwa kiasi gani?” aliuliza Kadumya, ambae niwazi alijua kuwa Dereva alikuwa hewani na anamsikia vyema, “nadhani malipo safari hii yatakuwa makubwa zaidi ya yale ya mwanzo” alisema Deus, kwa sauti ile ile tulivu, lakini maneno aliyoyaongea yaliwashtua wote watatu, hata Kobwe pia alishtuka.

Maaan hakuna alie amini kijana huyu angetoa kauli kama hii, ambayo ilionyesha wazi kuwa amegundua kuwa huu ni mkataba wa pili, “unamaana gani safari hii dereva” aliuliza Kadumya kwa sauti yenye utulivu wakulazimisha, japo kwa macho tuliweza kuona wasi wasi na mshangao aliokuwa nao, “najua hukutakiwa kufahamu, ila wewe ni mteja wangu wa mwisho na ulikiuka sheria tisa ndani ya lisaa limoja tu” kuanzia kutojuana majina, kutumia bunduki nidhamu, kufungua mzigo, na hata ile muhimu ya malipo” ilisikika sauti ya dereva, yaani Deus Nyati akiongea kwa utulivu ule ule kama vile hakuwa anatilia msisitizo yale aliyoyaongea, “lakini umeuwa vijana wangu wengi sana, haya tuaache hayo, nieleze safari hii utahitaji kiasi gani kukamilisha jukumu?” aliuliza Kadumya, ambae nikama alikuwa anajaribu bahati yake baada ya kuona amesha shtukiwa.

Wote wakatega sikio kusikia atakachoongea Deus Nyati, “gharama ya safari hii itakuwa ni roho yako, na huyo mpuuzi niliempa nafasi nyingine ya kutubu dhambi zake, na sio roho za hao wapuuzi wenu ambao hamja wafundisha vyema kupambana na mtu kama mimi ” alisema Deus Nyati kwa sauti ile ile, ambayo hata akiongelea mambo ya hatari utasema anaungama dhambi zake kwa unyenyekevu, hapo wote watatu wakatazamana kwa mshangao juu ya kujiamini kwa kijana huyu mwenye sauti ya kanisani au msikitini, kisha wakatazama kule waliko vijana wao, ambao walikuwa wanaweka sawa silaha zao, ambazo zilikuwa ni zile kipimo cha kati yani SMG, AK 47, MMG, RPG na mabomu ya kutupa kwa mkono, stick heand grenade, defensive na offensive heand grenade, huku wakiwa na vifuko vya makombora ya RPG, na kwamba Deus angeweza kuchomoa roho ya mtu hata mmoja endapo angeingia ndani ya mtego wao.

Hapo wote watatu, wakaachia kicheko cha nguvu, kilichojaa dharau, ni kweli walidharau maneno ya Deus, ambae kiukweli, waliamini kuwa anasema vile kwakuwa hakujua kama sasa jeshi lao limekamilika, na kwamba akiingia kwenye mtego wao hawezi tena kuchomoka, kwasababu ukiachilia watu waliokuwa nao, pia walikuwa na silaha kubwa za kivita kwa ngazi ya section, “kijana ni vyema ukaanza kujiandaa kwa kile ambacho kinakuja kukupata safari hii?” alisema Kadumya, mara baada ya kumaliza kicheko, “labda nieleze unataka nifanye nini?” aliuliza Deus kwa sauti ile ile, ambayo kwa haraka haraka ungesema alishakubari yaishe, “hayo ndiyo maneno ambayo unapaswa kuongea sasa hivi, sio kujipiga kifua mbele ya kundi la wanaume” alisema Kadumya kwa sauti ile ile yamikwaruzo yenye dhaurau kubwa, “nakusikiliza mzee jari muda wangu” alisikika Deus kwa sauti ile ile tulivu ya upole.

Hapo wote wakatazamana, huku wanaonyeshana ishara ya dole gumba kuwa mambo yapo sawa, “sikia kijana, najua hunifahamu mimi ni nani, lakini nakupa nafasi ya kurekebisha makosa yako, nipatie fedha zangu na huyo mwanamke, tutaachana na wewe” alisema Kadumya kwa sauti yenye msisitizo nakitisho, huku wenzake wakitabasamu kwa kuzuia vicheko vyao visitoke nje ya vinywa vyao, huku masikio yao yakiwa yametegwa kwenye simu ile aliyoishika bwana Kadumya.

Wakati wanategemea kusikia sauti ya uoga ikiomba kujua sehemu ya kupeleka fedha na yule mwanamke, ghafa masikio yao yakanasa sauti ya kicheko cha mguno, yani kicheko cha mtu mzima anaemcheka mtoto mwenye kushindwa jaribio, kicheko ambacho unaweza kusema ni cha masikitiko, “nakufahamu mzee, wewe ni Kanali Erasto Kadumya afisa mtoro wa MLA, na sasa unajiita general wa UMD, labda wewe ndiyo hunifahamu mimi, kama ungekuwa unanifahamu, lazima ungetambua kuwa, unapuliza moto wa mafuta ukiwa na ndevu nyingi kidevuni, cha msingi achana na upuuzi huo kabla ndevu hazijadaka moto” alisikika Deus, kwa sauti ile ile ya upole, ikifuatiwa na kicheko cha sauti ya kike toka upande wa pili wa simu, “jamani weweee una maneno” ilisikika sauti ya kike, huku wakati huo huo kicheko kikimponyoka Kobwe alieshindwa kujizuia, “pumbavu unacheka nini Kobwe” aliuliza Kadumya kwa sauti ya hasira, huku mkono wake ukipitia kwenye kiuno na kuibuka na bostora iliyo elekezwa moja kwa moja kichwani kwa Kobwe, usawa wa paji la uso.

Askari wote wanashtuka wanaacha kufanya wanacho kifanya na kutazama upande ule, ambako wanamuona general wao akiwa amemnyooshea bastora mkuu wa kombania yao, ambae anaonekana akiwa anatetemeka kwa wasi wasi na uoga, kwasababu anaijua tabia ya mkuu huyu wa jeshi hili la UMD, mata nyingi akitoa bastora yake huwa hairudi bure,

Kobwe anashikwa na wasi wasi mkubwa, anamtazama Kadumya, ambe macho yake yamemtoka kwa hasira, Kobwe anamtazama Kafulu ambae ndie angehusika na kusuluhisha, lakini anaonekana amesimama pembeni amejishika kiuno, ni kama hakujua kinachoendelea pale, “Samahani mkuu, haito jirudia tena” alisema Kobwe kwa sauti ya kutetemeka.

Ilitumia sekunde kadhaa kwa Kadumya kushusha hasira zake na kundoa bastora kichwani kwa Kobwe, “unabahati tuna majukumu makubwa, ungekuwa umesha lamba udongo” alisema Kadumya kabla ya kukumbuka kuwa simu ilikuwa hewani, “hallow dereva, na jua bado upo hewani na unanisikia, hebu tambua kuwa maneno yako hayachekeshi kama wapumbavu wanavyo dhania, nakupa nafasi ya mwisho ya kunipatia fedha na huyo mwanamke…..” alisema Kadumya kwa sauti ya ukali na vitisho, kabla hajagundua kuwa simu imekatwa, “mshenzi amenikatia simu, atajuta kujiingiza kwenye hili, alisema Kadumya kwa hasira, huku ananyoosha mkono kumpatia simu Kafulu.

Lakini licha ya kunyoosha kwa sekunde kadhaa, hakuona mtu akipokea simu, akamtazama Kafulu ambae alionekana akiwamesimama anamtazama kama mzimu, “we fala hebu chukua simu yako, unawaza nini, au sauti ya huyo kahaba ndiyo imekuchanganya, acha ushamba yupo na mwanaume mwingine, kwani wewe tulikutuma ukapendane au ukafanye kazi?” alisema Kadumya, huku Kafulu akikurupuka na kupokea simu yake ambayo ilikuwa inatumiwa na Kadumya, na wakati huo huo simu ya Kadumya ikaanza kuita, akaitoa mfukoni na kutazama mpigaji akaona kuwa ni bwana Ulenje, akaipokea mara moja, ana haikuchukua hata sekunde mbili tayari simu ilikuwa imekatwa, sijui aliambiwa nini.

Maana haraka sana, aliwageukia wakina Kobwe, haya kazi imeenza, polisi wanakuja upande huu, wapangeni askari, kama wataingia hapa wasipate hata nafasi ya kutoa taarifa kwa wenzao, yani nikuwateketeza kabisa” alitoa maagizo Kadumya, na hapo Kobwe akaanza kuwapanga askari huku akiwapa habari za ujio wa adui zao. *****

Naaam huko TT City, mtaa wa Sizwe, ndani ya jumba kubwa la kifahari linalomilikiwa na jeshi la ulinzi la #MBOGO_LAND ARMY, nje wanaonekana askari wakiwa wamezunguka jengo lile ndani ya uzio mkubwa wa kuta, unao lindwa na umeme ikisaidiwa na camera kila kona ya ukuta, magari mengi ya serikali sambamba na gari moja binafsi aina ya Toyota Caldina, tunaingia ndani ya jengo lile la kifahari, ambalo ukitazama kwa haraka, unaweza kusema kuwa ni nyumba ya mtu binafsi, kutokana muundo wake, ukiachilia sebule kubwa yenye kila kitu, ila pia kulikuwa na jiko vyoo na vyumba vya kulala, katika vyumba viwili kati ya vyumba nane vilivyomo ndani ya jengo lile, ambavyo tunafanikiwa kuingia, tunakuta ni vyumba vizuri vyenye kila kitu ungesema ni vyumba vya hoteli moja kubwa ya kifahari.

Chumba cha kwanza tuna wakuta Watoto wawili wa staff sajent Ashraff Kibwana, ambao umri wao ni kati ya miaka saba, kwa mdogo na mkubwa ni miaka kumi na mbili, wote wakiwa ni wa kike, ambao tayari walikuwa wamepitiwa na usingizi, pia chumba kingine tunacho kiangazia, alikuwepo mke wa bwana Ashraff, ambae licha ya kupewa huduma zote lakini bado hakuthubutu kufumba hata kope ya jicho lake, kwa maana alikuwa anawaza usalama wa mume wake, hasa kutokana na matukio kadhaa ya siku za nyuma yaliyomkumba mume wake, kiasi cha kuamua kuacha kazi ya jeshi na kukimbia nchi. …....…….ENDELEA MZEE WA UMD mhanuzi wangu MUNA MPANGO GANI NA POLISI WETU WA TZ MBONA HAWANA BAYA NA NYINYI?

NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA THERASINI NA MBILI

TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA THERASINI NA MOJA:- Chumba cha kwanza tuna wakuta Watoto wawili wa staff sajent Ashraff Kibwana, ambao umri wao ni kati ya miaka saba, kwa mdogo na mkubwa ni miaka kumi na mbili, wote wakiwa ni wa kike, ambao tayari walikuwa wamepitiwa na usingizi, pia chumba kingine tunacho kiangazia, alikuwepo mke wa bwana Ashraff, ambae licha ya kupewa huduma zote lakini bado hakuthubutu kufumba hata kope ya jicho lake, kwa maana alikuwa anawaza usalama wa mume wake, hasa kutokana na matukio kadhaa ya siku za nyuma yaliyomkumba mume wake, kiasi cha kuamua kuacha kazi ya jeshi na kukimbia nchi. …....…….ENDELEA…

Tunaachana na mke wa bwana Ashraf, tunaenda moja kwa moja mpaka kwenye chumba ambacho ukitazama kwa haraka ungesema ni vyumba viwili tofauti kabisa, ni kweli kulikuwa na milango miwili, lakini unapoingia mlango wa kushoto, ambao tunaweza kuuita mlango wa pili tunakutana na chumba kimoja kipana cha kawaida chenye makochi mawili na viti vinne, vyote vikiwa vimetazama upande wa kulia wa chumba hicho, ambacho kuta yake kati ya kuta zake nne upande huo wa kulia nusu yake ulikuwa ni kioo kitupu, ambacho chini yake palionekana speeker mbili kubwa.

Ukitazama kioo kile na pasipo umakini wowote, ungeweza kuona chumba kingine kipana, chenye meza kubwa ya chuma yenye vishiko fulani kama vile sehemu ya kufungia mtu mkorofi, huku meza hiyo ikiwa imezungukwa na viti viwili, navyo vya chuma kama meza yake.

Sisi tupo ndani ya chumba hiki cha kwanza, ambacho kuna viti na makochi, hatupo peke yetu, tupo na watu wanne, nao ni King Elvis Queen Vaselisa, General Sixmund na kanali Justin Johnson, ni Malikia Vaselisa peke yake ndie alikuwa amekaa kwenye kiti, lakini mfalme na makamanda wa kijeshi wote walikuwa wamesimama, huku wote wanne macho yao yakiwa kwenye kioo kikubwa mbele yao, ambapo kwa uwazi kabisa waliweza kuona mlango wa chumba kile ukifunguliwa, na wakaonekana askari wa MLA waliovalia sare nyeusi, wakiingia mule ndani huku wamemtanguliza mwanaume mmoja mtu mzima, ambae alionekana kuwa na wasi wasi sana, kisha askari wale wanatoka mule ndani wakimuacha yule mwanaume ametoa macho kwa mshangao na wasi wasi, asijue la kufanya, “jamani kwanini munanifungia humu” alisikika Ashrafu, akipiga kelele kwa nguvu, “familia yangu mume ipeleka wapi, mulisema Hamto nifanya chochote” alipiga kelele Ashraf.

Wakati huo huo mfalme anasikia simu yake inaanza kuita, “shiiiiiii atajua kama tuna fuatilia mahojiano” alisema Malkia Vaselisa kwa sauti ya kunong’ona, huku anamsihi mume wake kukata simu ile, hapo General Sixmund akajua kuwa Malkia hakujua kuwa kile chumba kimewambwa sauti, “malkia mtukufu wa #Mbogo_Land, upo huru kuongea chochote kwa sauti yoyote, kwa maana sisi tuna wasikia wao ila wao hawawezi kutusikia, mpaka turuhusu sauti zetu kwa kutumia vipanza sauti maalumu” alisema General Sixmund, kwa sauti ya unyenyekevu, wakati huo kanali Jastin anazima speeker za sauti.

Na hapo ndipo shida ilipo, yani katika nchi za kifalme unapo zingumza na familia au koo za kifalme hata kama wewe ni komando, itabidi uongee kwa unyenyekevu kama hivi, tofauti na unapozungumza na viongozi wengine wenye uteuzi wa mfalme, wao utawasalimia kijeshi.

Malkia akacheka kidogo, huku anamtazama mume wake aliekuwa anacheka huku anaitazama simu yake kuona jina la mpigaji, “nilijua tunahitajika kukaa kimya” alisema Vaselisa, huku yeye na mume wake wanacheka kwa Pamoja, utajulia wapi haya mambo ya kintelejensia, hebu kwanza nipokee simu naona mwana habari wetu anapiga sijui kuna jambo gani tena” alisema King Elvis, na wote wakakaa kimya wakimtazama mfame akipokea simu pasipo kuweka sauti ya wazi, nae akaipokea na kukaa kimya kwa sekunde kadhaa ni wazi alikuwa anatoa nafasi ya mpigaji kutoa salam, “salaam mtumishi mwema, kipi kimekufanya upige simu usiku huu” ilikuwa ni sauti tulivu ya kifalme, ambae alitulia kwa sekunde kadhaa kusikiliza huku wenzake wakiwa kimya kabisa, wakimtazama mfalme ambae kila sekunde iliyoenda alionekana kubadirika sura mfano wa mtu anaepokea taarifa mbaya.

Mwisho wakamsikia mfalme akisema, “sawa agiza watu wetu, wafuatilie chanzo cha mtandao uliotumika kuposti hizo habari” alisema mfalme kabla ya kukata simu, “vipi tena kuna habari mpya mtandaoni?” aliuliza Malkia kwa sauti yenye shauku, “wapuuzi wamesha post uvumi mwingine, wa kwanza unasema wakuu kadhaa wa jeshi na usalama wa taifa wamejiunga na UMD, ni kutokana na kutokuukubali utawarla wa kifalme, na habari ya pili ni kwamba, wamevumisha kuwa tumetuma askari wa MLA, kwenda Tanzania kumuua bwana James” alieleza king Elvis.

Taarifa hii ilimshangaza kila mmoja mule ndani, “tayari mambo yameanza, hebu tusubiri tuone” alisema malkia Vaselisa, akimaanisha kuwa taarifa hizi zimeenda sambamba na zile za Waziri Chitopela, na hapo ni kama king Elvis alikumbuka jambo, “vipi kuhusu askari wetu waliopo Tanzania, umewasiliana nao hivi karibuni?” aliuliza mfalme Elvis, huku akimtazama general Sixmund, “najitahidi kuwasiliana nao kila mara, na sasa bado wapo nyumbani kwa bwana James, na wanafanya juhudi za kumpata Veronica ili waweze kuanza safari ya kuja Mbogoland” alisema Sixmund na mke wa mfalme akauliza, “wanauhakika na sehemu alipo Veronica?” aliuliza Vaselisa, “ndiyo wanafahamu, maana mpaka dakika ya mwisho, ilithibitika kuwa Veronica na Deus Nyati walikuwa pamoja” alijibu Sixmund.

Hapo mfalme alitulia kidogo, kama anatafakari jambo, sekunde chache baadae akaongea, “huyu Deus Nyati ni alama katika mapambano haya, maana ni sababu kubwa ya kukwamisha juhudi za utafutaji wa fedha za kulipia silaha za UMD na kufanya sisi tugundue uovu wao” alisema Elvis, akionyesha kuliongea kwa hisia za hali ya juu jambo lile, “hata baba yake pia, ni wazi ameonyesha kuwa mzalendo katika nchi yake, ambayo licha ya watu wabaya kumgombanisha na serikali lakini ametoa ushirikiano mkubwa wa kufichua uasi” alisema Malkia Vaselisa, “ni kweli kabisa, ata record zake zinaonyesha kuwa ni mtu ambae ameitumikia nchi kwa moyo wake wote, kiasi cha kujitolea uhai mara kadhaa kuokoa Maisha ya mfalme Eugen.” Alisema King Elvis, huku wote wanatazama kwenye kioo na kuona mlango wa chumba cha pili ukifunguliwa akaingia askari mwenye cheo cha luten, alievalia suruali ya kaki iliyoiva, na shati la kaki rangi ya kupauka, huku kichwani akiwa amevaa kofia ya duara ya rangi kama ya suruali yenye nembo ya jeshi la #mbogo_land, chini viatu vyeusi vyenye kung’aa kama kioo, “Jastin washa speeker” alisema general Sixmund. ******

Naaam huko songaea nako, mzee Frank Nyati nae alikuwa katika wakati mgumu sana, licha ya kushikwa na usingizi mkali, lakini muda wote alipambana asitopee kwenye starehe hii ya kisheria, mara baada ya kujaribu kupiga simu mara kadhaa bila mafanikio na kujipumzisha kidogo, na baadae kuona dalili za kusinzia, bwana Frank anaamua kujaribu tena kupiga simu kwa kijana wake kwa mara nyingine tena, lakini bahati nzuri safari hii simu yake inapokelewa mara moja, “baba kwanini hujalala mpaka saa hizi?” ” aliuliza Deus kwa sauti tulivu lakini yenye mshangao, “unadani sijalala Kwasababu nina wasi wasi na wewe?” aliuliza mzee Frank, akimalizia kwa kupiga mhayo mrefu wa usingizi, “sasa ni kitu gani kinakuweka macho mpaka mida hii?” aliuliza Deus, kama vile anamashaka na jibu la baba yake ambae toka akiwa mdogo hajawahi kuwa na wasi wasi nae, “kuna kitu unatakiwa kujua, ni kwamba MLA wapo dar es ni watu ambao unapaswa kushirikiana nao, maana wao pia wapo huko kwaajili ya kumlinda James na kumpeleka #mbogo_land” alisema mzee Frank.

Hiyo kidogo ni kama Deus hakuielewa au kuikubari, “sasa mimi wananihusu nini?” aliuliza Deus, “wana kuhusu Deus, maana ukiachilia kuwa ulichokifanya kilikuwa ni kujiokoa mwenyewe, lakini pia umefanya kitendo kikubwa na kizuri sana cha kuokoa mtu muhimu katika nchi yako halisi” alisema mzee Frank, “lakini sina mkataba nao wowote na kivipi nitashirikiana nao wakati wao ni wanajeshi na sasa mimi ni raia tena muharifu, unadhani nitaishia wapi baada ya mipango yao kukamilika?” aliuliza Deus kwa sauti ile ile ya upole, sauti ambayo baba yake anaifahamu toka akiwa mdogo.

Alicho kiongea Deus kilikuwa ni kitu cha kweli masikioni mwake, maana tayari Deus alisha julikana kuwa ndie dereva wa gari jeusi, licha ya hivyo jeshi la ulinzi la Tanzania lilikuwa linamsaka, baada ya kuonekana kuwa na mapungufu katika utoaji wa hukumu ya mwanzo, “kwahiyo umepanga kufanya nini, au utaishi kama mkimbizi Maisha yako yote” aliuliza mzee Frank kwa sauti tulivu, maana ni kweli kijana wake alikuwa katika wakati mgumu sana, “kwanza kabisa naachana na kazi ya usafarishaji, nitajificha kwa miaka kumi, baada ya hapo nitajiweka wazi nikiwa mtu wa kawaida na kuishi na familia yangu.

Mzee Frank akajikuta anacheka kidogo, mwanzo sikujua ni kwanini, ila nikajua baada ya mzee kuuliza swali, “familia ipi unaizungumzia, mke na Watoto wako au mimi na mama yako?” aliuliza huku anacheka kidogo na kumfanya Deus pia aachie kicheko, kama chake yani kicheko cha taratibu, “utafahamu hivi karibu” alijibu Deus, na hapo baba yake akauliza swali kama la mwanzo, “na umepanga nini juu ya huyo binti wa James, maana sasa anasubiriwa na familia yake kwa safari ya #mbogo_land?” aliuliza mzee Frank, safari hii akiweka umakini kwenye swali lake, “nitahakikisha namfikisha sehemu salama kwa mikono yangu” alisema Deus na baba yake akaongezea, “sehemu salama pekee ni kwa baba yake, ambae sasa ana ulinzi mkubwa sana toka kwa mfalme” alisema mzee Frank, “kwa nguvu na akili zangu zote, Veronica atafika akiwa salama” alisikika Deus akisema, sawa ukiwa unahitaji chochote niambie” hivyo ndivyo walivyo maliza maongezi yao na kukata simu, kisha mzee Nyati akampigia simu captain Amos Makey.*******

Yap! Wakati huo huo, upande wa magharibi mwa kisarawe, eneo la msitu wa visegese uliopaka na Kazi mzumbwi, mashariki na kusini, tuna yaona magari matatu ya polisi yakiwa yanatimua vumbi kuelekea upande wa kibaha, na sasa yanakaribia eneo la relini, sisi tunaachana nayo tunaelekea kusini kwenye barabara ya maneromango, kilomita kama nane tu toka njia panda ya kisarawe na kibaha, ambapo tunaona magari ya jeshi la polisi yakiwa yamesimama, sasa kundi la kwanza ambalo ni askari wa mkoa wa temeke, wataanza kufanya msako kuanzia hapa, wakati kundi la pili litasonga mbele” alisikika ACP Kabona, ambae ni OCD wa ubungo, “aliekuwa anasimamia kundi la pili la mkoa wa kipolisi wa Kinondoni.

Kitendo cha haraka, magari yakajitenga kama mafuta na maji, yale ya askari wa Kinondoni, idadi yake tisa, yakaendelea na safari, huku yale ya mkoa wakipolisi temeke, yakibakia pale, huku askari wakishuka toka kwenye magari yale yenye idadi nane, la tisa likiwa la OCD, na kuingia vichakani, nusu wakielekea upande wa kushoto wa barabara, na nusu iliyobakia wakiingia upande wa kulia wa barabara, wakifuata vinjia vya wachoma mkaa kama walivyofanya wenzao wa upande wa kushoto.

Yap! Njia panda nako, askari walikuwa wametulia katika mikao mbali mbali yakimapumziko, kama vile hakukuwa na jukumu zito la kuwasaka wanaume wenye silaha za moto, wapo waliokuwa wamesinzia kwenye magari, wapo waliokuwa wamezama kwenye maongezi, na wapo walikuwa wamezama kwenye mazungumzo na simu zao za mikononi wakisahau jukumu lao la utayari, endapo wenzao watahitaji msaada. Wakati huo kilomita mbili toka pale njia panda kama unaenda kazi mzumbwi, yalionekana magari saba manne yakiwa ya viongozi, na matatu ya askari walinzi wenye bunduki zao, hakika hawa jamaa wamejua kutusumbua” alisema kamanda Nyambibo, akionekana kuchoshwa na swala hili, “hivi wamewezaje kuja kujijenga ndani ya nchi yetu na kujaribu kufanya ujinga kama huu?” aliuliza RPC wa temeke, wakati huo huo ikasikika sauti kwenye redio zao, “hallow namba 1 ya 1, mimi namba mbili A, kuna ujumbe tafadhari” kwa muito huo, wote wakajua kuwa ni alama ya uitaji wa OCD wa temeke, ambae alikuwa anamuita mkuu wa kanda maalumu.

Kwa muito huo kila mmoja akahisi kuwa kuna jambo tayari limetokea, “namba moja A, tuma tafadhar” alijibu kamanda Nyambibo, “mkuu, katika uelekeo wangu, mita kama mia mbili toka barabarani, tumekuta kuna watu wapo chini, ni wazi kabisa watu hawa wameuwawa leo hii na sio muda mrefu sana, kwasababu hata damu zao ni mbichi, hii ni taarifa ya awali” ilisikika sauti ya OCD Temeke, makanamada wakatazamana kwa mshangao, “fafanua ni watu wa aina gani, wenzetu au raia au wale tunaowatafuta?” aliuliza Nyambibo, na kutulia kidogo akitoanafasi kwa OCD kuongea, “kwa muonekano wao ni kundi lile lile, na baadhi wanaonekana kama wale waliovamia benk ya uhifadhi ya mali binafsi” alisema OCD.

Ilishangaza kidogo, “namba mbili A, eleza idadi ya miili hiyo” alisema Kamanada Nyambibo, “afande idadi ni kumi sita, pia inaonyesha ni wazi kuwa kuna gari limeondoka muda mfupi uliopita, maana alama za matairi zinaonekana” alisema OCD, na baada ya hapo, kamanda Nyambibo akatoa tamko, “hallow vituo vyote, sikiliza toka kwangu, kundi namba tatu, sogeeni mbele kwaajili ya kutoa msaada wa kukagua eneo la tukio, kundi namba mbili hapo hapo mlipo simama kisha anza msako wa nguvu pande zote hakikisha unawaangalia walengwa, na sio mtu mwingine, umakini unahitajika” alisema kamanda Nyambibo, wakati huo kamanda Ulenje, akiwa anasikiliza kwa umakini, huku moyoni mwake akiwaza juu ya sehemu waliyopo wakina Kadumya.******

Naaam kabla hatujaenda kwenye maficho ya Deus, twendeni moja kwa moja Mbogo Land, jijini TT, mtaa Sizwe, kwenye nyumba ya MLA, kusikiliza mahojiano kati ya MLA na askari wa zamani wa MLA, alieshiriki kwenye operation ya kutokomeza waasi ndani ya serikali ya #mbogo_land, kipindi cha utawala wa mfalme Eugen wa ishirini na tano, operation ambayo inasadikiwa iliangamiza watu muhimu na wazalendo wa kweli wanchi hiyo....…….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao Kujia Hapa Hapa JamiiForums
 
Du! Hii imekaa pw mkuu, nmecomment kabla ya kusoma.
 
Aiseeeeee🤔🤔🤔🤔🤔🤔.
Naiona familia mda sio mrefu wanaenda kuchapika kama Ngoma.

Tatizo ni Hawa wapuuzi kina Kadumya, wajinga kabisa wanachekacheka TU mda wote.

Chitopela nae ana mipango ya kitoto, yaani mtu unasuka mipango ukiwa umelewa! halafu unataka ushinde! Fala kabisa hili.
Hapa familia sijui itakuwaje du! 🥱🥱🥱🥱🥱🥱🥱🥱🤭🤭🤭🤭🤭UMD
 
Kwani Kadumya si ana H&K G95 ASSAULT RFLE 5.56 MM au hamuiamini? 😅😅
 
Hii hadithi haina maisha marefu.Bora aweke vipande vilivyobaki tuanze nyingine
 
Kwani Kadumya si ana H&K G95 ASSAULT RFLE 5.56 MM au hamuiamini? 😅😅
we jamaa fanya kuongeza vipande angalau 4 au 5..hivi viwili unavyopost havishibishi kabisa ukizingatia tunasota mda mrefu tukisubiri..nawe ulishasema bado una stori nyingi za kuleta humu sasa yanini kurembesha namna hii au unataka uwe kama singano jr. story moja et tunaisoma miaka miwili.! acha kubania mwaga moto bhana.
 
Akiweka vipande 4 au 5 mara 3 tamthilia inakuwa imeisha.Zimebaki episodes chache!
 
we jamaa fanya kuongeza vipande angalau 4 au 5..hivi viwili unavyopost havishibishi kabisa ukizingatia tunasota mda mrefu tukisubiri..nawe ulishasema bado una stori nyingi za kuleta humu sasa yanini kurembesha namna hii au unataka uwe kama singano jr. story moja et tunaisoma miaka miwili.! acha kubania mwaga moto bhana.
Inayokuja naipost yote kwa pamoja 😎
 
Back
Top Bottom