Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA TISINI NA TISA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA TISINI NA NANE:- “kwa hiyo kaka yangu, nikishawapa hili begi lenu muna muachia John?” aliuliza Veronica huku anamtazama huyu kijana asiefanana na kazi anayoifanya, “mpaka sasa umesha vunja sheria mbili, kumbuka hakuna kujuana majina, pia mimi sijui lolote, kazi yangu ni kukufikisha eneo la tukio tu” alisema Deus kwa sauti yake tulivu huku macho ameyakaza mbele. .….ENDELEA…

Hapo Veronica akatulia kidogo kutafuta namna nyingine ya kuuliza usalama wake na wa mchumba wake JJD, “lakini kaka, nyie mulijuaje kama JJ ni mchumba wangu, na kwanini mulimchagua yeye na siyo mtu mwingine?” aliuliza Veronica, swali ambalo aliliweka kama kipimo kuona kama Dereva huyu atalijibu vipi, “dada mbona maswali ni mengi sana, au una wasi wasi na kazi unayoifanya? ni vyema ungemshauri huyo mchumba wako mufunge ndoa ukatulie nyumbani na kulea watoto kuliko kuranda usiku unavunja mabenk ya watu” alisema Deus, akionyesha kutokupendezewa na ushirika wa Veronica katika tukio lile la kijambazi.

Maneno hayo yanamshtua sana Veronica, ambae anamshangaa kijana huyu kwa kumdhania yeye ni jambazi, “weeee nani jambazi, mimi ni doctor, tena ni professional, nyie si ndio mume mteja JJ, ili nikawachukulie hela mulizoiba pale benk” alisema kwa sauti ya hamaki doctor Veronica.

Hapo ni kama Deus alipata picha fulani ya tukio na mpango wa wateja wake wale, “ni vyema ukaa kimya dada yangu sababu sina msaada wowote kwako” alisema Deus, huku anatazama GPS, ambayo iliwez kumuonyesha kuwa alikuwa amebakiza mita mia tano kufika kituo cha mwisho wa safari yake ile,na kweli Veronica akatulia na kutazama mbele akisubiri matokeo ya mwisho baada ya kufika kituo cha mwisho na kukabidhi fedha.*****

Yap! sasa turudi mbezi mwisho, ambako tunawakuta polisi wa kituo cha mbezi nao wanaendelea kukagua camera za pale benk, na kuona jinsi tukio lote lilivyokuwa, jinsi mschana mrembo alivyo ingia akionekana mwenye wasi wasi, ambae pia hakuonekana kuwa ni mteja, maana alifika na kuketi kwenye kiti cha wangojeao, hata baada ya majambazi watatu kuvamia na wanaanza kutekeleza tukio la uporaji.

Anaonekana mmoja kati ya wale majambazi, akipiga risasi hewani na kuamuru watu walale chini, nao wanalala kwa haraka pamoja na yule mwanamke mwenye wasi wasi na pia waliweza kuona jinsi jambazi mmoja alivyochukua begi toka kwa mteja, ikionekana wazi kabisa kuwa walisha mlenga mteja yule, maana hawakuchukua kitu kingine chochote toka kwa mteja mwingine yoyote zaidi ya lile begi na kisha anaonekana yule jambazi akitembea kuelekea alikolala yule mwanamke mrembo mwenye wasi wasi.

Naam yule jambazi anapomkaribia yule mwanamke mwenye wasi wasi, ghafla umeme unakatika na giza linatanda, hali ambayo ina dumu kwa sekunde chache, kisha taa zinawaka, na hapo majambazi hawaonekani tena baada yake wanaonekana polisi wanne, “hebu subiri hapo, rudisha kidogo hiyo video” alisema yule inspector na yule mama akisaidiwa na mfanya kazi mmoja wakiume aliirudisha nyuma ile video walifanikisha kuonyesha sehemu ambayo inamuonyesha mwanamke mrembo akiinuka toka chini na kuchukuwa begi ambalo hapo mwanzo hakuwa nalo na kutoka nje sambamba na watu wengine, huku polisi nao wakijichanganya na wale raia waliokuwa wanatoka ndani.

Licha ya kujaribu kuwa tambua wale polisi hawa kufanikiwa hata kidogo kujua hata sura ya mmoja wao, “hawa sio polisi wa kweli, nao ni majambazi, kama majambazi wengine” alisema yule sajenti, na yule afisa akadakia, “kwahiyo waligawana mara tatu, majambazi, polisi na huyu mwanamke” alisema yule insp, wakati huo yule meneja akiwa ametoa macho kwa mshangao, ni mara baada ya kusikia kuwa, wale aliodhania kuwa ni polisi nao walikuwa ni majambazi, “jamani na huyu mwanamke pia ni jambazi, mbona hafanani na ujambazi” alisema yule mwanamke kwa sauti ambayo ilionyesha wazi kutokuamini anacho kiona, “hebu tutoleeni nakala ya picha za hao wahusika wote tuitume kwa RCO RPC na staff officer” alisema inspector huku anatoa simu yake na kupiga kwa OCD kumpatia taarifa ya kilichotokea mbezi luis.*******

Naaam ndani ya jiji kubwa la TT, kwenye makazi ya mfalme wa nchi hii ya #mbogo_land, yani Golden House, king Elvis akiwa ametulia anasubiri simu toka Tanzania inayompa jibu la ombi lake la kuweza kumshikilia bwana James na kumleta katika nchi ya asili yake kuja kueleza ukweli kama anashiriki katika kundi la wahlasi wa UMD au laa, na kama anashiriki, kwanini anafanya hivyo na wakina nani ni viongozi wa kundi hilo.

Mara mfalme anapokea simu, toka jijin dar es salaam Tanzania, kwenye ubalozi wake mkubwa, “salaam mtukufu mfalme wa #mbogo _land, uishi maisha marefu mfalme Elvis wa kwanza” ilisikika salamu toka upande wa pili wa simu, “salaam mtumishi mwema, baraka zangu zikawe juu yako, haya nipe majibu ya maombi yetu” alisema king Elvis, ambae licha usiku kuzidi kwenda, lakini yeye na mke wake hawakuonyesha dalili ya kwamba wanatakiwa kulala.

“mtukufu mfalme, ombi lako lile kwa ukuu wako, na urafiki ulionao na Tanzania mpaka sasa ombi lako limeshakubaliwa, askari waje na watapokelewa uwanja wa ndege na kupelekwa moja kwa moja nyumbani kwa James”alisikika balozi, ambae pia aliendelea kueleza, “mtukufu mfalme, pia kuna taarifa ni muhimu ukazisikia” alisema balozi na kutulia kidogo akisubiri ruksa ya kuongea, “nakusiliza barozi” alijibu mfalme Elvis ambae aliona kama anacheleweshwa, maana ilibidi atoe amri ya kuondoka kwa askari wa AR yani Amoured Recce, “mtukufu, taarifa za mwanzo ambazo zinasubiri uthibitisho ni kwamba, bwana James leo mapema alishikiliwa mateka kwa muda na kiongozi wa UMD, anaejiita General Kadumya, lakini bahati nzuri, kuna mtu alimuokoa na mpaka sasa hajajulikana ni nani, japo serikali ya tanzania inashuku kuwa, anaweza kuwa ni MLA au MLSA, aliekuwa anawafuatilia, baadae James aliomba msaada serikalin, nao wamempatia ulinzi wa jeshi la ulinzi” alieleza balozi.

Hapo Mfalme akakumbuka maneno ya general sixmund wakati anampatia taarifa ya bwana Frank Nyati, “vipi kuhusu hao wakina Kadumya, wamekamatwa?” aliuliza Elvis, kwa sauti iliyojaa uchungu hasira na shahuku, “bado hawajakamatwa, lakini serikali inatafuta uthibitisho ili waanze kuwasaka wahusika” alisema balozi, “sawa barlozi, vijana wapo njiani” kabla hawajaagana na kukata simu.

Naam Kingi Elvis akiwa na mke wake, alipoikata simu tu, akabofya simu yake akitaka kupiga simu kwa general Sixmund ili atoe rukasa ya kuanza safari kwenda dar es salaam, lakini kabla hajapiga simu, akaona simu yake inaita, na alipo tazama mpigaji akaipokea haraka, “yani ungechelewa sekunde moja tu wewe ndie ungepokea simu yangu, vipi kuna jipya?” aliuliza king Elvis, kwa sauti yenye shauku, “mtukufu mfalme, kuna habari mpya” huyo alikuwa ni Sixmund, “hen! usiku umekuwa na taarifa nyingi sana, hebu nipe zako na wewe” alisema king Elvis na hapo Six akaanza kumueleza vile alivyo simuliwa na Amos, ambae pia alisimuliwa na luten kanal wa zamani, bwana Frank Nyati.

“hivyo mtukufu, ukweli ni ule ule kwamba, UMD walitaka kumtumia kufadhili malipo ya usafirishaji wa silaha, ambazo zinatarajiwa kuingia nchini, hivyo mfalme nashauri askari waruhusiwe haraka, ili waweze kumfikia James, ambae anaweza kuwa na mambo mengi ya kutueleza, japo kwasasa usalama wake ni mdogo” alieleza Six, “taarifa hizo na mimi nimezipata, ila waeleze vijana kuwa, wahakikishe wanamlinda James na anafika akiwa salama yeye na familia yake, pili bado zoezi liendelee kuwa siri, hasa huu mpango wa kumlinda James, waache wahusika wajue kuwa sisi tunamsaka James kwaajili ya kumshtaki” alisema mfalme ambae akuishia hapo,

“sasa hivi nawasiliana mwandishi wangunkuwa atoe tangazo la kusakwa kwa James na tangazo la kuwa ni mtu hatari katika taifa, ila bwana Six inabidi tulimalize hili, natarajia vijana wako watakapokuwa wanarudi watakuja na vitu viwili, moja waje na jina la kiongozi wa UMD aliepo serikalini, na pili ni kichwa au kiwiliwili cha Kadumya” alisema mfalme kwa msisitizo, “ndiyo mtukufu falme, itafanywa kama utakavyo” alijibu Sixmund, kabla mfalme hajakata simu.*******

Naaam taarifa zilizo ambatana na picha za kijana Deus, zinasafari kwa kasi sana ndani ya jeshi la ulinzi, kuazia kitengo cha MI, yani Military Intelegence, pia ikaenda kitengo cha CDMP, kitengo cha polisi wa jeshi kama haitoshi habari zikaenda mpaka kwenye kitengo cha mafunzo na utendaji wa kivita, kinacho husishwa na operation za ndani na nje ya nchi COT, kitengo cha major general Mbike kifimbo, ambae askari aliekuwa zamu ofisini kwake usiku ule, alituma picha na taarifa zote zinazoeleza mashaka toka kwa TSA kwa mkuu wake huyo wa kitengo.

Bwana Mbike kifimbo alisisimuliwa sana na ile taarifa “ndio yeye huyu, hebu rudisha report haraka TSA, waambie kuwa huyo ni mtu wetu na tulikuwa tunamuhitaji, halafu wewe mwenyewe, nenda chumba mahususi, mwambie afisa wa zamu aandae askari waingie kazini sasa hivi, wamsake mpaka wampate askari Deus Nyati na kila hatua wanayopiga nipate taarifa mapema” alisema major gen Mbike Kifimbobkabla hajakata simu na kupiga kwa mkuu wa majeshi kumpatia taarifa hiyo, nae akamueleza kuwa tayari alisha pata taarifa ya tukio hilo, na tayari jeshi kupitia kikosi namba 1108 cha mbawa za anga, kimesha peleka askari kwaajili ya bwana James ambae inasemekana kuwa alitekwa na waarifu wa kivita wa UMD, na baadae kuchukuwa na kijana huyo, ambae sasa amebakinika kuwa ni Deus Frank Nyati, “fanyeni juu chini apatikane, ila kumbukeni anatumia BMW jeusi” alisisitiza mkuu wa majeshi.********

Naam sasa turudi mbezi makabe, gari aina ya BMW S7 linaenda kusimama mbele ya jengo moja kubwa lililojengwa mfano wa bar, tofauti ni kwamba haikuwa imeanza kutumika, nje wanaonekana vijana sita wenye slilaha zao, mikononi na magari manne aina ya Land Rover Puma.

Mapigo ya moyo ya mwana dada Veronica, yanaanza kuongea kasi, uoga unamshika, wasi wasi unamtawala, Veronica anamuona yule jamaa aliekutana nae kule mbezi kwenye bar, akija kwa mwendo wa haraka akilisogelea gari walilokuwepo, ambalo bado lilikuwa lina unguruma na wao wakiwa ndani, vioo vime pandishwa, anamtazama dereva kijana alie lkaa pembeni yake, anamuona anawatazama wale vijana walioshika bunduki na kusimama nje ya jengo lile, kisha dereva anamtazama huyu jamaa aliekuwa analisogelea gari lao, “kaka naomba muchukuwe begi lenu muniache niondoke na John” alisema Veronica kwa sauti yenye kutetemeka kwa uoga, “zingatia sheria mlizo peana na watu wako, wakukabidhi mtu wako na wewe wakabidhi mzigo wao” alisema Deus kwa sauti tulivu huku moyoni mwake akihisi kumpenda mwanamke huyu, “kama kasingekuwa kajambazi ningejaribu bahati yangu” aliwaza Deus huku anatazama mazingira ya eneo lile.********

Yap, taarifa za wizi wa fedha, katika jengo la uhifadhi wa mali za wananchi zilikuwa zimesambaa katika maeneo mengi ya kiusalama wa nchi, kuanzia kituo cha polisi cha mbezi, kituo cha kimara, makao makuu ya polisi cha magomeni, na pia taarifa zilishafika makao makuu ya jeshi la polisi, na hapo zikaanza juhudi za kutafuta utambilisho wa wausika wa tukio lile la uporaji kwa kutumia picha za zilizopigwa toka kwenye camera za usalama za cctv, ndani ya jengo lile, huku polisi wa jiji zima la dar es salaam wakizagaa jiji zima kuwasaka wezi hao.

“huyu kwa kuowanisha picha za TRA katika kumbukumbu ya namba ya ulipaji kodi ya TIN, tumeweza kulinganisha picha ya huyu mwanamke” alisema mmoja wa watu toka TSA, aliekuwa anatafuta utambulisho wa watuhumiwa, alipokuwa anatoa taarifa kwa mkuu wa kitengo hicho kanda ya dar es salaam, “endelea nakusikiliza” alisema yule mkurugenzi wa TSA, na hapo huyo wakala akaendelea, “huyu anaitwa Veronica James Kervn, anamiaka ishini na nne, kazi yake ni doctor, anaishi dar es salaam” alieleza wakala….. .….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
yaani kusubiri kutwa nzima alafu unakuja kupost kipande kimoja.! ujinga huu ndiomaana nilikushauri uwe unatupia vipande 4 kwa mkupuo mmoja tu ila kwq mwendo huu unatukatisha tamaa kweli..kuwa mnaanza kwa spidi kubwa ila mkishapata wasomaji mnarudi nyuma spidi ya kobe badala ya kuongeza kasi zaidi..au ww huoni watunzi wenzako wanaloleta story humu wanatupia vipande 4 au 5 chap wanaendelea na shughuli zao wala husikii wakipigiwa kelele na lawama.. ila ww mtunzi wetu hapa unabania kinoma hadi tunapata hasira maana unatusotesha siku nzima alafu unaleta kimoko si bora usingepost tu.!
 
Dah,, leo nilale mapema sasa nimekesha sana sababu ya hiki kigongo,, ni balaa, sidhani kama Deusi atamkabidhi mrembo Veronica kwa wale jamaa, ukizingatia chuma BMW S7 bado iko silence hapo inavutwa fasta shwaa,, wana watabaki kuitupia risasi tu na ikumbukwe chuma yenyewe ni bullet proof,, hatari wewe
 
yaani kusubiri kutwa nzima alafu unakuja kupost kipande kimoja.! ujinga huu ndiomaana nilikushauri uwe unatupia vipande 4 kwa mkupuo mmoja tu ila kwq mwendo huu unatukatisha tamaa kweli..kuwa mnaanza kwa spidi kubwa ila mkishapata wasomaji mnarudi nyuma spidi ya kobe badala ya kuongeza kasi zaidi..au ww huoni watunzi wenzako wanaloleta story humu wanatupia vipande 4 au 5 chap wanaendelea na shughuli zao wala husikii wakipigiwa kelele na lawama.. ila ww mtunzi wetu hapa unabania kinoma hadi tunapata hasira maana unatusotesha siku nzima alafu unaleta kimoko si bora usingepost tu.!
Ungeukagua uzi vizur kabla ya kumwaga lawama
 
Ungeukagua uzi vizur kabla ya kumwaga lawama
Hadithi nzuri ila unatuhamisha matukio mpk tunasahau.
Ukigonga ya deus weka mpk anapokula mbususu ya pacha Veronica.
Ukiweka ya tajiri James, weka mpk anapoookolewa.
Kadumya pia na wajeshi wake weka yote.umalizie walivyomalizwa.
Na yule msaliti Chitopela weka walimnasa waPi.
Hatua kwa hatua twende sawa.
 
Nafkiri kila mfuatiliaji angali like episode ya kwanza kumpa support mtunzi na appreciation ya kazi nzuri na mpangili/mtiririko ingependeza mana ni mtu mwenye wa pekee na asiye na tamaa. Pia anaskiliza wadau wake na kutumia busara na hekima sana kudili nao, mana kupitia ivyo itamtangaza zaidi na kuzidi mpa moral ya Karama yake ya utunzi, Ni mawazo tu msini popoe😅
 
Nafkiri kila mfuatiliaji angali like episode ya kwanza kumpa support mtunzi na appreciation ya kazi nzuri na mpangili/mtiririko ingependeza mana ni mtu mwenye wa pekee na asiye na tamaa. Pia anaskiliza wadau wake na kutumia busara na hekima sana kudili nao, mana kupitia ivyo itamtangaza zaidi na kuzidi mpa moral ya Karama yake ya utunzi, Ni mawazo tu msini popoe😅
Nimeisha Like.
 
yaani kusubiri kutwa nzima alafu unakuja kupost kipande kimoja.! ujinga huu ndiomaana nilikushauri uwe unatupia vipande 4 kwa mkupuo mmoja tu ila kwq mwendo huu unatukatisha tamaa kweli..kuwa mnaanza kwa spidi kubwa ila mkishapata wasomaji mnarudi nyuma spidi ya kobe badala ya kuongeza kasi zaidi..au ww huoni watunzi wenzako wanaloleta story humu wanatupia vipande 4 au 5 chap wanaendelea na shughuli zao wala husikii wakipigiwa kelele na lawama.. ila ww mtunzi wetu hapa unabania kinoma hadi tunapata hasira maana unatusotesha siku nzima alafu unaleta kimoko si bora usingepost tu.!
Unatoa povu hivyo umemchangia bando au muda wake huyu mtu ana shuuhuli zake za kufanya jaribu kufikisha hoja yako kistarabu utaeleweka tu
 
Nafkiri kila mfuatiliaji angali like episode ya kwanza kumpa support mtunzi na appreciation ya kazi nzuri na mpangili/mtiririko ingependeza mana ni mtu mwenye wa pekee na asiye na tamaa. Pia anaskiliza wadau wake na kutumia busara na hekima sana kudili nao, mana kupitia ivyo itamtangaza zaidi na kuzidi mpa moral ya Karama yake ya utunzi, Ni mawazo tu msini popoe😅
Wajinga wachache wanashindwa kuwa na lughabza staha
 
Stori iko sawa kabisa,ila ni matumaini yangu utapost hadi mwisho.nakufuatilia kutoka Kenya.
 
Hadithi nzuri ila unatuhamisha matukio mpk tunasahau.
Ukigonga ya deus weka mpk anapokula mbususu ya pacha Veronica.
Ukiweka ya tajiri James, weka mpk anapoookolewa.
Kadumya pia na wajeshi wake weka yote.umalizie walivyomalizwa.
Na yule msaliti Chitopela weka walimnasa waPi.
Hatua kwa hatua twende sawa.
Ukiweka kwa mfumo huo stori haitokuwa na mvuto kwasababu matukio yote yanategemeana kama ulivyoona mzigo wa emmy umekuwa sababu ya kuokolewa mzee james na mengineyo.
 
Back
Top Bottom