Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA TANO
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WATSAPP: 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA NNE: “ok! nipe hali ya uzito wa mzigo, daraja la mzigo, na usalama wa usafirishaji” aliuliza kijana wetu, ambae alikuwa anaendelea kuendesha gari kwa speed kama vile analazimika kwenda na muda flani, wakati huo walikuwa wanakaribia njia panda ya Moroco, “uzito, haufiki hata kilo, usalama ni mkubwa sana, thamani yake laki mbili” alijibu yule mwanamke kwa sauti ile ile, ambayo kama unauwezo wa kujaji mtu kupitia sauti ungejuwa kwa, uzuri wa mwanamke huyu, siyo wataratibu, na ni mwanamke wa mjini, mwenye maisha ya hali ya juu. endelea

Hapo dereva wetu akashusha pumzi ndevu ya kuchoka, maana yeye amezowea kusafirisha mizigo ya hatari, lakini sasa anaambiwa kuwa, mzigo hakuwa na hatari yoyote, na thamni yake ni laki mbili, hapo akaona kuwa ni utani, lakini kutokana na utaratibu wake namba 7, hakutakiwa kudharau kitu wala mtu, “ok! malipo elfu hamsini, utanipatia nikifisha mzigo, lakini utatakiwa kuzingatia kuwa, hakuna ujanja, huo ni utaratibu namba 5” alisema dereva, akitaja elfu hamasini kwa kutegemea kuwa mwanamke huyu, angeona bei kubwa, na kughairi mpango, “wala usiwe na wasi wasi, natukienda sawa, nita kuongezea mala dufu ya elfu hamsini” alisema yule mwanamke, huku akizidi kuipooza sauti yake, “ok! mpango umekubaliwa” alisema dereva na kukata simu, wakati huo, anapunguza mwendo kuingia njia panda ya Moroco, na kukata kushoto kuelekea barabara ya mwenge, kisha akaongeza mwendo, pasipo kujari sms zilizokuwa zinaingia kwenye ile simu yake nyingine, muda wote mschana mdogo Zamda akiwa anamtazama kijana huyu, kwa macho ya viulizo, na kushindwa kupata jibu.*******

Yap! wakati kama huu, kusini mashariki mwa Tanzania, pembezoni mwa mto Ruvuma, kaskazini mashariki mwa msumbiji, ndani ya nchi ndogo ya kifalme, nchi iliyosaahulika katika ramani ya dunia, kutokana na kuchelewa kutambuliwa na umoja wa mataifa, nchi ya mbogo #land_land, inayoongozwa na mfalme Elvis Mbogo wa kwanza, mwenye makazi yake katika ngome ya dhadhabu, kwamaana ya Golden Castle, iliyopo ndani ya jiji la Treanch Town, kwa maana ya Treanch Town City.

Tuachane na King Elvis, twende kusini mwa mji huu wa TT, mpaka nje kidogo ya jiji Hilo la Trench Town, ni pembezoni mwa barabara ya kuelekea upande wa msumbiji, katika kitongoji kidogo cha Mmajile, (mmemaliza), mji ulikuwa umechangamka kwa burudani, kama ujuwavyo mji huu, jioni na nyakati kama hizi, watu hutumia muda wao na familia zao, au wapenzi wao, kupata burudani katika bustani za viunga vya jiji, huku wakipata vinywaji na vitafunwa mbali mbali.

Hayatuhusu hayo, sisi twendeni moja kwamoja mpaka kwenye jengo moja kubwa, la ghorofa kumi na mbili, ambao lilikuwa alijamaliziwa ujenzi wake, lililokuwa limezungushiwa uzio wa mabati, kama wafanyavyo wakandarasi wengine wanapofanya ujenzi mkubwa kama huu.

Ndani ya uzio huo yana onekana magari nane ya kifahari, ni jambo la kawaida kwa nchi hii kuona magari kama haya, maana wanachi wengi ni mtajiri, lakini licha ya magari hayo nane, pia kulionekana vijana kumi na tano, walio valia nguo nyeusi, kwa maana ya suruali nyeusi za jinsi, na tishert nyeusi, zilizo kamata miili yao, kichwani kofia nyeusi za cap, waswaili uita kapelo, mikononi mwao wakiwa na bunduki aina ya HECKLER &KOCH G95 toka GERMANY ASSAULT RFLE 5.56MM, H K G 95, yaani hecler & koch G 95, iliyotengenezwa nchi germany assault refle yenye mtutu wa mzingo mill miter 5.56, kwa faida ya msomaji, ni aina ya silah iliyotumika kumuuwa Osama bin laden mwaka 2011.

Wakionekana kuwa makini sana, katika ulinzi wa eneo hilo, lenye mwanga hafifu, vijana hawa walionekana wakiwa wamejipanga kwa kuachiana nafasi ya mita kati ya kumi mpaka kumi natano eneo lote la mbele.

Achana na eneo ili kwa nje, huko ndani katika moja kumbi za jengo hilo, lenye giza, zilionekana taswira za vimvuli vya giza, vya watu kama sita hivi, ambao kiukweli usingeweza kuona sura zao, walionekana kuwa katika mpango flani mzito sana, “bwana James Carvin, alitoroka nchini mwaka 1988, na kukimbilia tanzania, ambako anaalianzisha tena biashara zake na kuwa mfanyabiashra mkubwa na tajiri” alisema mmoja wao, aliekuwa amesimama mbele yao, huku wengine watano, wakiwa wamesima kwa kutengeneza nusu mwezi, huku wakionekana kumsikiliza kwa umakini mkubwa sana.


“bwana James Carvin, ambae kwa sasa anamiliki viwanda vikubwa vya vyakula unga na vinywaji, huko Tanzania, alikimbia nchini, akikwepa tuhuma za uhaini, alionekana kuwa alikuwa anafadhiri kikundi cha kijeshi cha waasi wa zamani, kilicho fahamika kwa jina la harakati za uhuru kwa damu” alisema tena yule ambae walikuwa wanamtazama, ambae kwa haraka alionekana kuwa na umri mkubwa zaidi yao, “naamini bwana James atakuwa na hasira kali sana na serikali, hivyo akielezwa anachotakiwa kufanya juu yetu, lazima ataungana na sisi, na kutusaidia kulipia kontena ishirini za silaha mabomu na risasi, kwaaajili ya mapinduzi, pamoja na kutusaidia chakula kwaajili ya askari wetu waliopo msituni” alisema yule jamaa, ambae licha ya kuwa gizani, na rangi yake kuwa nyeusi, pia alikuwa amevalia koti refu jeusi, suruali nyeusi, viatu vyeusi, na kofia ya duara yeusi yenye kuziba uso wake.


“Lakini mheshimiwa, itakuwaje kama atakataa, maana Jemes nikama mtu wa kufata sheria pia” aliuliza mmoja kati yao, ambae alionekana kuvalia nguo zinazofanana na wale vijana wa nje, “sikia bwana Tambwe, fanya kama nilivyo kuagiza, mweleze kwamba, mimi nimesema, kuwa, endapo tutachukuwa nchi hii, yeye atakuwa huru kuchimba dhahabu, kufanya biashara bila ushuru wowote, pia atapewa eneo kubwa sana la kufungua biashara yake na pia atapewa kandarasi ya kuchimba gass na mafuta, lazima atakubari tu, na kumbukeni kuwa mzigo hupo njiani, sikutatu baadae unatia nanga Queen Irine Bay, lazima tuwe na fedha ya kulipia kwa wale jamaa watukabidhi mzigo wetu” alisema yule alie itwa Mheshimiwa, safari hii akionyesha msisitizo mkubwa, “lakini mheshimiwa, nadhani itakuwa vizuri kama tukiwa na mpango mwingine, maana uwezi kujuwa James atasemaje” safari hii alishauri mtu mwingine, na siyo yule alie itwa Tambwe, huyu alikuwa amevaa suit nyeusi na kofia nyeusi.


Hapo mheshimiwa akatulia kidogo kama sekunde tano hivi, kisha akamtazama yule alie shauri, “sasa nimekuelewa, bwana Kadumya, mpango wapili upo, na utatekelezwa muda mchache sana baada ya huu wa kwanza kushindikana” alisema mheshimiwa ambae mpaka sasa hatuja mfahamu kwa jina, huku wale wengine wakimsikiliza kwa umakini mkubwa sana, “Kadumya hakikisha vijana wako wanafwata maelezo, ikiwa pamoja na endapo huu wakwanza utashindikana, wamuuwe James, kisha watahamia kwenye mpango wa pili, ambao nita wapa muda mfupi baada ya mpango wa kwanza, japo sitegemei kama James akiona mitutu ya bunduki usoni mwake, ataweza kusema hapana” alisema Mheshimiwa akionekana kuwa mwenye uhakika zaidi.


Naam baada ya hapo hawa kutumia muda mrefu mahala pale, wakaagana, “Kadumya, hakikisha vijana wako, wanapanda ndege kesho mapema, kuelekea Tanzania, nguo na silaha watazikuta huko huko, kwa bwana Mbwambo, kule temeke kaburi moja” alielekeza Mheshimiwa, kabla hawajaondoka zao, kwa namna ya siri kama vile Hawakuwa pamoja.******


Naam turudi kigamboni, ambako tayari polisi walisha kagua magari yote yaliyokuwa yana subiri kuingia kwenye kivuko yani Pantoni, pasipo kuliona BMW jeusi, na kuamua kurudi walikotoka, huku CP Ulenje akitoa maagizo askari wasambae maeneo yote kulisaka gari ilo, na yeye pamoja na askari watano wakaelekea upande wa mji mwema, kwenda kumwona bwana Songoro.


Ilikuwa ni safari ya dakika kumi na tano, mpaka kufika kwenye nyumba ya bwana Songoro, iliyo jitenga ndani ya eneo moja kubwa lililozingikwa na vichaka vifupi na minazi mirefu, sehemu ambayo walipofika tu, wakapokelewa na bwana Songoro alie simama sambamba na yule mwanamke, ambae sasa alikuwa amevalia chupi aina ya bikini na sidilia kifuani kwake, kati kati ya eneo la mbele la ile yumba kubwa, huku wakionekana watu waliokuwa wanagala gala chini kwa maumivu makali, huku wengine wakiwa wamepoteza fahamu zao, idadi yao ikifika zaidi ya kumi, huku zikionekana silaha mbali mbali zajadi na zile za kisasa, yani visu mapanga na bastora, vikiwa vimetawanyika eneo lile, huku baadhi ya ya watu hao wakionekana kuvujwa na damu , toka kwenye majelaha mbakubwa, katika sehemu mbali mbali za miili yao.


CP Ulenje alitoa macho kwa mshangao, “Songoro unasema alikuwa kijana mmoja tu?” aliuliza CP Ulenje kwa mshangao, “ukweli sikuwai kufikiria kama kuna mtu anaweza kuwa kama yule kijana, hakika namwitaji na tena namwitaji nimkate kiungo kimoja baada ya kingine” alisema Songoro kwa sauti iliyo jaa chukizo na kasiriko, “vijana tayari wapo kazini, naamini muda siyo mrefu watamtia nguvuni” alisema Ulenje, wakati huo wanaingia ndani, na kukagua watu wengine walio kuwa bado wanagala gala kwa maumivu, wapo waliolalamikia mbavu wapo waliolalamikia nyuso zao, na wapo walio lalamikia miguu yao, ilimradi kila mmoja wao alipata anacho stahili, “unampango gani na hawa watu Songoro” aliuliza Uledi , wakati wanaendelea kukagua mle ndani, “wajinga hawa wanawezaje kupigwa na mtoto mrembo kama yule” alisema Songoro ambae hakuonyesha dalili ya kuwa saidia vijana wake, waliokuwa wanataabika pale chini, “huyo kijana atakuwa tatizo hapa mjini, inabidi apatikane haraka sana” alisema CP Ulenje, huku anatoa simu, kubofya namba kisha akaipiga na kuweka sikioni.


Simu haikuita muda mrefu, ikapokelewa, “OCD mambo ni mazito, kuna uvamizi mkubwa umetokea huku mji mwema kigamboni, kwa mfanyabiashara Songoro, agiza gari la wagonjwa lije huku, pia peleka taarifa vituo vyote vya polisi, hapa mjini, msako mkali uendelee, malengo ni BMW jeusi, kamata kila anae hisiwa mpaka apatikane, na taarifa itolewe kuwa ni mtu hatari sana huyo” alisema CP Ulenje, mara tu baada ya simu kupokelewa, “sawa mkuu inatekelezwa” alijibu OCD, na hapo Ulenje akakata simu, kisha akamtazama Songoro, “hakiki hakikisha unaondoa hizo silaha hapo nje” alisema Ulenje, kwa msisitizo.*******


Naam barabara ya bagamoyo, mtaa wa tegeta, njia panda ya kwasharifu, linaonekana gari moja jeusi aina ya ford ranger likiwa limesimama pembeni ya barabara hiyo, huku mtu mmoja, mwenye mwonekano wa miaka 40, akiwa amesimama ubavuni mwa gari ilo, huku uso wake, ukionekana kujawa na mashaka mengi, mara kwa mara alikuwa anatazama saa yake, na kisha kutazama upande wa mjini, ni wazi alikuwa anatarajia kuona mtu au gari likitokea upande huo….. hivi huyo mzee James atakubari mpango wa mheshimiwa, ebu tuone kitakacho tokea. basi… endelea kufwatilia mkasa huu wa #NYUMA_YA_MLANGO_WA_ADUI, inayo kujia hapa hapa jamii forums
Nzuri
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA TISINI NA TISA:- “huyu kwa kuowanisha picha za TRA katika kumbu kumbu ya namba ya ulipaji kodi ya TIN tumeweza kulinganisha picha ya huyu mwanamke” alisema mmoja wa watu toka TSA, aliekuwa anatafuta utambulisho wa watuhumiwa, alipokuwa anatoa taarifa kwa mkuu wa kitengo hicho kanda ya dar es salaam, “endelea nakusikiliza” alisema yule mkurugenzi wa TSA, na hapo huyo wakala akaendelea, “huyu anaitwa Veronica James Kervn, anamiaka ishirini na nne, kazi yake ni doctor, anaishi dar es salaam” alieleza wakala….….ENDELEA…

Na hapo mkurugenzi akauliza swali, “makazi na hospital anayofanyia kazi?” aliuliza mkrugenzi, “tumesha tuma taarifa kwa wakala wetu kule wizara ya afya ajaribu kuangalia jina hilo kwenye orodha ya madoctor walio sajiliwa nchini ili kujua hospital anayofanyia kazi” alisema yule wakala wa TSA, “utanipatia jibu haraka utakapopata taarifa toka wizara ya afya, na sisi turudishe wizara ya mambo ya ndani iliwaweze kumnasa mtuhumiwa wao” alisema mkurugenzi kabla hajakata simu.********

Naam!!!, huku mbezi makabe, tayari bwana Zaid tambwe, alikuwa ameshalifikia gari na kujaribu kuchungulia ndani, lakini ni wazi hakuona kitu, ni kutokana na vioo vya giza vya gari lile, hapo anatoa ishara kwamba wa shuke toka kwenye gari, Veronica anamtazama dereva, ambae anatulia kama sekunde tano hivi, kisha anashusha pumzi ndevu, ni kama vile hakupenda kushuka toka kwenye gari.

Veronica anamuona Dereva anabofya kitu fulani kilichoa andikwa lock, karibu na kirungu cha gia kati kati ya seat yake na ile ya dereva, halafu ana bofya tena kidude kwenye mlango wake, hapo unasikika mlio wa “ti!!! ti!! ti!!” “chukua begi lako sasa unaweza kushuka” alisema Deus huku na yeye anafungua mlango wa gari na kutoka nje ya gari kwa namna ya pekee kabisa, wakati dereva huyu machachari anashuka toka kwenye gari, anapeleka mkono kwenye mguu wake wa kulia na kugusa sehemu ya mguu karibu na shingo ya kiatu, ni kama anahakikisha kitu fulani sehemu ile.

Wote wanashuka toka kwenye gari, tayari Veronica yupo na begi mkononi, “mzigo wenu huu hapa, John yupo wapi?” aliuliza Veronica kwa sauti ambayo ilionyesha wazi kujawa na wasi wasi, “nifuateni” alisema Zaid Tambwe pasipo kutoa jibu lolote kwa Veronica, baad yake alianza kutembea kuelekea kwenye lango la jengo lile kubwa kama ukumbi mkubwa wa mikutano au burudani, na wao wakamfuata.

Naam Veronica alitembea kuongozana na wale wanaume wawili huku wakiwapita vijana walioshika bunduki, ambao baadhi yao aliweza kuwa kumbuka kuwa aliwaona kule mbezi, huku kichwani mwake akipanga kuwahi kumpeleka JJ Hosptal na kumtibu yeye mwenyewe majeraha ya vidonda atakayokuwa nayo maana sio kwa damu ile iliyo chafua nguo zake.

Wote watatu wanaufikia mlango na kuingia ndani, huku Veronica anazidi kupata wasi wasi, anawaza jinsi macho yake yatakavyo kabiliana na kumuona mchumba wake akiwa katika hali mbaya ya mateso, hata wanajikuta ndani ukumbi mkubwa sana wenye mwanga hafifu, Veronica anajitahidi kutazama kwa umakini lakini hawezi kumuona JJ akiwa amelala chini kama video ilivyoonyesha.

Wanazidi kutembea kusogea mbele zaidi ambako angalau kuna mwanga ambao watu wanaweza kuonana na kila wanavyosogea wanaanza kuwaona watu wakiwa kule wanakoelekea, eneo linatisha na kuogofya, Veronica anatamani aruhusiwe haraka kuondoka na mchumba wake, sasa anao gundua kuwa ata wale watu walipo mbele yao, baadhi wanabunduki mikononi mwao, lakini licha ya kuwaona watu wale hawezi kumuona JJ.

Hatimae wanafika pale walipokuwepo watu wale wenye bunduki, Veronica haoni dalili ya JJ wala alama ya damu eneo lile, kitu cha kwanza kukiona Verinica ni mkoba wake na simu yake ya mkononi vikiwa juu ya kiti cha plastic, “Kafulu yupo wapi?” anauliza Tambwe na wakati huo huo mlango mmoja wa pembeni unafunguliwa, wanatokea watu wawili, Veronika anageuza uso wake kuwatazama watu wale, ambao ni Kafulu na bwana Mbwambo, wote wakionyesha nyuso za tabasamu, muda wote Deus alikuwa ametulia kama vile anasoma akili za watu na mazingira.

Veronica anatoa macho kwa mshangao kiasi cha lilebegi kumtoka mkononi, “John, nini unanifanyia, inamaana ulikuwa unanidanganya?” aliuliza Veronica kwa mshangao mkubwa huku anamtazama Kafulu, ambae yeye alimuita John, ambae muda huu alikuwa amesimama karibu kabisa na mtu ambae yeye aliwahi kukutana nae mara moja na kutambulishwa kama ni mjomba wake John, ndie ambae alipangwa kusimamia taratibu zote za kuchumbiana kwao.

Hapo wote wakacheka kwa pamoja kikiwa ni kicheko cha dharau na sanifu, doctor Veronica James, mimi naitwa Enock Kafulu, na sio John Joseph Daud kama ulivyopenda kuniita” alisema kafulu huku anamsogelea Veronica, “ila usiwe na wasi wasi, usiku wa leo tutafanya kile tulichopanga kukifanya leo, au unasemaje mpenzi wangu?” aliuliza huyu mwanaume ambae hakuwa na hata tone moja la damu huku anapitisha mkono wake kwenye kichwa cha Veronica na kupapasa nywele zake ndefu zilizofungwa kwa namna ya kupendeza, “John naomba niache niende, kama unahitaji fedha nitakupatia, tafadhari naomba uniache niende, usinifanyie hivyo” alisema Veronica huku anaachia kilio cha taratibu.

Haikusaidia kitu, ndio kwanza Kafulu, anachuchumaa na kulishika lile begi, halafu anafungua zip na kuifungua kisha anazamisha mkono ndani ya begi na kuibuka na kibunda cha noti za elfu kumi kumi, “kazi nzuri mpenzi, sasa nina kila sababu ya kukuburudisha usiku kucha” alisema Kafulu huku anatoa simu yake mfukoni, na kumpigia Kadumya, “naomba John, usinifanyie hivyo niache niende nyumbani” alisema Veronica, huku anazidi kuangua kilio.

Lakini pasipo kujali maombi ya Veronica Kafulu anatoa kauli ya kukatisha tamaa, “lakini Veronica kwani ni vibaya kulala na mwanaume ambae amekufanya utoke kwenu usiku kumfuata yeye?” alisema kafulu huku Deus akionekana kuchoshwa na maongezi yasiyo muhusu, “jamani John, naomba uniache niende, kama begi lenu nimesha waletea” alisema Veronica kwa sauti ile ile iliyo ambatana na kilio, lakini ndio kwanza JJ anasikilizia simu ipokelewe.

Hakika ilitia huzuni sana kumuona mwanamke mrembo kama yule akiangua kilio, japo Deus alishaona vilio vingi tena vya wanaume wa rika mbali mbali wanao kabiliana na vifo, lakini kilio cha mrembo huyu kilifika moyoni, Deus akamtazama Kafuru, akamuona anasikilizia simu, ambayo ni wazi ilikuwa bado inaita, “nadhani kazi yenu nimeshaimaliza, je sasa naweza kupata fedha zangu?” aliuliza Deus, na hapo Kafuli akamuonyesha mkono wa kumzuia kuongea na sekunde hiyo hiyo simu ikapokelewa, “ndiyo Enock, kuna lolote?” iliuliza sauti toka upande wapili wa simu, “mkuu tayari wote wawili tunao hapa na mzigo upo” alisema Kafulu, huku anarudisha mkono wake kichwani kwa Veronica, ambae muda wote alikuwa anatetemeka, “safi sana, sasa fanya kama nilivyo kueleza, na mimi napiga simu kwa bwana James, kumueleza ujanja wake ulipoishia, yeye si anajifanya mjanja” alisema mwanaume wa upande wa pili wa simu.******

Naam viongozi wa serikali ya watu wa #mbogo_land, walianza kupokea taarifa ya kwamba, wanatakiwa kukutana kwenye ukumbi wa mikutano, kuna jambo la dharula linalohusu uasi wa bwana James, hivyo walipewa nusu saa tu, wote wawe wamefika ukumbini.

Taarifa hii ilimkuta bwana Chitopela akiwa nyumbani kwake sebuleni anakunywa pombe kali, huku anaperuzi kwenye mtandao kutazama matukio yanayoendelea huko Tanzania na maoni juu ya taarifa ya ushiriki wa bwana James UMD, pia aliweza kufurahishwa na taarifa ya tukio la ujambazi ambalo lim tokea mbezi kwenye jengo la benk ya uhifadhi wa mali binafsi za wananchi, “safi vijana kazi inaenda vyema” alisema Chitopelah huku anafungua ujumbe kwenye simu yake, “saa tano kamili mawaziri na wakurugenzi wote pamoja na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wanahitajika kwenye ukumbi wa mkutano wa ikulu, kuna dharula ya mambo ya kiusalama inayohusu ushirika wa James Kervin, kujiweka wazi kuwa ni mfadhili wa UMD” mara baada ya kusoma ujumbe huo, waziri huyu wa ulinzi bwana Dickson Chitopela, aliachia kicheko kikubwa cha kufurahia, “sasa James atajua hajui” alisema Chitopela huku ananyakua glass yenye pombe na kuipeleka mdomoni, kisha akagumia mafunda mawili magumu, kisha akaiweka glass mezani na kuinuka zake akaelekea chumbani, ambako hakukaa hata dakika tano, akatoka akiwa amevaa vazi la juma mosi, vazi la muonekano wa kitaifa, yani lenye ubunifu wa kiasili, kisha akaondoka zake kutoka nje.********

Yap! huko songea, captain Amos Makey anapata amri ya kuondoka kuelekea dar es salaam, “mutatumia dakika arobaini na tano kufika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere, ambapo mutapokelewa na jeshi la ulinzi la Tanzania, ndio ambao watawapeleka Nyumbani kwa bwana James” alisema generali Sixmund, wakati anatoa amri ya kuondoka, “pia inabidi mfahamu kuwa jukumu lenu lime badirika, toka kumkamata bwana Janes na kumleta nchini, na kuwa kumlinda bwana James na familia yake, na kumleta nchini kwaajili ya usalama wake” alisema Sixmund huku akisisitiza kuwa, daraja la mpango bado ni siri, “acha watu wajue kuwa munaenda kumkamata James kwa tuhuma za uasi, kwasababu sasa serikali inaenda kutangaza” alisema lakini juu ya kumkamata mzee James, tunafanya hivi kwaajili ya kuwapumbaza washirika halisi wa UMD, ambao wataamini kuwa tume liwazika na uongo wao” alisema General Sixmund, “nimeinakiri mkuu, naomba kuondoka” alisema Captain Amos akiwa anaagana na fande wake.

Naam baada ya kukata simu, Amos akawageukia askari wake na kuwaeleza, “zoezi limegeuka, na tuna paswa kulijuwa hilo, imebainika kuwa tajiri James sio muasi, ila kuna ujanja umefanyika ili kuipumbaza serikali na kufanya izidi kumchukia Jame na serikali ina wasi wasi kuwa pengine waasi wakamuua James ili lawama ziende kwa serikali” alisema Amos, ambae alihitimisha kwa kutaja jukumu lao la sasa, “kwasasa kazi yetu ni kumlinda James na familia yake” alimaliza Amos na wote wakaanza kuingia kwenye magari, safari ya kuelekea airport.******

Naam sasa tuangazie nyumbani kwa tajiri mkubwa, bwana James, bado hofu ilikuwa imetanda familia ilikuwa ina wasiwasi juu ya Veronica, ambae mpaka dakika hii, alikuwa hajapatikana katika mawasiliano yake simu ya mkononi, hata zile sehemu ambazo walihisi kuwa wanaweza kumpata, kama vile kazini kwake walisema hawajui lolote juu ya Veronica.

Mzee James tayari alisha piga namba ya kijana John, ambae ni rafiki wa bnti yao, lakini simu ilieleza kuwa haipatikani, kwa maana nayo ilikuwa imezima, “inamaana gani hawa wawili wapo kwenye matatizo au wameshaingia mikononi mwa UMD” alijiuliza mzee James akiwa amekosa amani kabisa moyoni mwake, “baba Vero ni bora kama ukitoa taarifa polisi, pengine Vero amekamtwa na hawa majambazi” alishauri mke wa mzee James yaani mama Veronica.

Naam!!!, wakati wanafamilia hawa wanafikiria kutoa taarifa za kuto kuonekana kwa Veronica, ambae hakuwa na taratibu za kuchelewa kurudi nyumbani bila sababu za msingi, ghafla simu yake inaanza kuita, wote wanaitazama simu ile ambayo wanahisi kuwa ni simu toka kwa Veronica, lakini walipoitazama wakaona kuwa ni namba isiyojulikana, kwa maana ilikuwa imefungwa kwa kificho, mioyo ya wanafamilia inaanza kwenda kasi, kwa hofu kubwa iliyo wajaa, maana walijua fika ile simu haikuwa njema kwao.

Mzee James hakuwa na chaguo lingine zaidi ya kupokea ile simu, anaipokea na kuiweka sikioni kisha anategemea kusikia sauti ya mpigaji, nikweli alifanikiwa, maana alianza kwakusikia kicheko kibaya cha kuchukiza, toka upande wapili wa simu, “bwana James, pengine ulizania umenikimbia, ingekuwa hivyo kama kusinge kuwa na kitu cha kutukutanisha” ilisikika sauti yenye dharau na vitisho, toka upande wapili, “Kadumya, unamaanisha nini?” aliuliza James kwa sauti yenye uoga na wasi wasi, huku familia yake ikiwa inamsikiliza kwa umakini, “kwani hapo nyumbani mpo wote au hujali kuhusu doctor Veronica?” ilikuwa ni sauti ya kukera yenye taarifa ya kugofya masikioni mwa mzee James, “unataka nini kwangu tafadhari usimdhuru binti yangu” alisikika mzee James akiomba kwa sauti yenyekutetemeka kwa uoga na wasi wasi….….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA MOJA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA:- ilisikika sauti yenye dharau na vitisho toka upande wa pili, “Kadumya, unamaanisha nini?” aliuliza James kwa sauti yenye uoga na wasi wasi, huku familia yake ikiwa inamsikiliza kwa umakini, “kwani hapo nyumbani mupo wote au hujali kuhusu doctor Veronica?” ilikuwa ni sauti ya kukera yenye taarifa ya kugofya, masikioni mwa mzee James, “unataka nini kwangu tafadhari usimdhuru binti yangu” alisikika mzee James akiomba kwa sauti yenye kutetemeka kwa uoga na wasi was….….ENDELEA…

Hapo kikasikika kicheko kingine cha dharau toka kwa Kadumya, upande wa pili wa simu, “kwa kuwa umekubali huwezi kutukimbia bwana James, basi tuna mpango wa kufanya ili umpate binti yako, subiri simu yangu nusu saa ijayo” alisema Kadumya na kukata simu, “wamemfanyaje Vero?” aliuliza mama Vero huku sauti yake ikiambatana na kilio, lakini mzee James hakuweza kujibu zaidi kuinamisha uso wake na kujishika kichwani.

“baba inabidi uwajulishe wanajeshi wakamchukue dada” alisema Caroline ambae alionyesha wasi wasi mkubwa juu ya usalama wa dada yake, “nadhani itakuwa vyema tukisubiri simu ya Kadumya tusikie anasemaje” alisema mzee James huku anajaribu kupiga simu ya binti yake lakini bado haikupatikana, na hapo kichwani mwake yakaanza kutiririka mawazo, kama vile ambavyo mke wake na binti yake Caroline waliwaza, na kikubwa walicho waza ni kile ambacho waasi wa UMD watakacho mfanya mpendwa wao, na kitu cha kwanza walichofikilia, ni kubakwa, kitu ambacho kisinge kwepeka, na ukichukulia kuwa Vernica alikuwa ni mschana mzuri kuliko uzuri wenyewe, hivyo lazima kila ambae angekuwa karibu na Veronica lazima angeshawishika kumbaka.

Jambo la pili ni kwamba, wasinge waacha salama hata baada ya kukubaliana na kukamilisha makubaliano, wakihofia kufichuka kwa mipango yao na kubainika kwa kiongozi wao bwana Chitopela ambae sasa ni kiongozi wa wizara muhimu katika serikari ya mfalme Elvis, wa #mbogo_land, “wacha nimpigie waziri Kasanzu” alisema mzee James huku anabofya namba ya waziri Kasanzu na kuipiga, maana yeye ndie mtu alieweza kuwasiliana nae kwa haraka.********

Mitaani polisi walikuwa wamezagaa jiji zima, wakiendeleza msako, usingeweza kupita kilomita moja pasipo kupishana na gari la polisi lenye kubeba askari kadhaa, basi ungekutana na kikundi cha polisi watembeao kwa miguu wakiwa na bunduki zao, bila kusahau wenye pikipiki huku wakisimamisha magari waliyo yashuku, ukiachilia mbali polisi hao watembea kwa miguu pikipiki na magari, basi kulikuwa na vizuwizi vya barabarani, ndani ya jiji na vile vya nje ya jiji ambavyo vilikuwa vinazuia na kukagua magari yote yanayotoka na kuingia jijini, wote wakiwa na lengo la kumkatama dereva mwenye BMW jeusi S7.

Naam lakini ndani ya magari matatu ya polisi aina ya land cruzer puma yaliyopo katika msako huo yalikuwa na lengo tofauti kabisa, lengo ambalo walipewa na mkuu wao wa kazi bwana CP Ulenje.

Ilikuwaje mpaka wakapewa jukumu hilo, ni baada ya koplo wa polisi Cheleji kubaini kuwa, kijana alie muokoa tajiri james pale sisterfada hotel ni kijana Deus Nyati, askari wa jeshi la ulinzi mwenye rekodi ya kufanya vizuri kwenye mapambano ya jeshi la mtu mmoja na ndie dereva wa BMW jeusi ambalo waliwahi kulifukuzia miezi michachache iliyopita kwa lengo la kupora dhahabu na gari lile jipya bila mafanikio, wakiambulia kumkosa na kushuhudia vifo kadhaa, na leo kulikuwa na mpango wa kumwingiza mtegoni ili washirika wao wakina Kadumya wamkamate.

Cheleji anapiga simu kwa CP Ulenje, ambae anamuambia aelekee makabe haraka pamoja na wenzake ishirini ili wakaongeze nguvu ya kupambana nae, maana kijana huyo siyo mtu wa kawaida, hivyo mida hii walikuwa walikuwa wameshafika mbezi mwisho na wanakata kona kulia kuingia barabara ya goba safari ya makabe kumdhibiti kijana huyo.*******

Naam!! taarifa ya matukio ya usiku huo yalizidi kusambaa mitandaoni, huku kila sekunde habari mpya zikiongezeka kama ilivyo onekana taarifa ya kutangazwa kwa bana James Kervine kuwa mtu hatari anae tafutwa na serikali ya #mbogo_land, akichukuliwa kuwa ni adui na muhamasishaji wa mapinduzi kwa njia ya damu katika nchi hiyo.

Taarifa hii iliyotolewa na msemaji wa ikulu ya Golden House ili washtua watu wengi sana, huku kila mmoja akiipokea kwa namna ya pekee, maana wapo waliochukulia kama kukosa utulivu na busara kwa King Elvis, na kwamba amekurupuka, pia wapo walio sema kuwa serikali ya #mbogo_land ilikuwa sahihi kabisa kuchukuwa maamuzi yake kwa mtu ambae kiukweli anatumia fedha zake kuiporomosha amani ya nchi ambayo ilidumu kwa muda mrefu ikiwa ni tamaa binafsi za kutaka kumiliki mali za nchi hiyo ambayo inaongozwa kwaa namna ya kufurahisha na usawa kwa wananchi ambao huduma zote muhimu wanazipata bure.

Swala hili liliwashangaza sana viongozi wa serikali ya Tanzania, maana wao walichojua ni kwamba bwana James ametumia busara kubwa sana kukataa kuwasaidia UMD, kwaajili ya kuiokoa nchi yake kutoka kwenye machafuko makubwa ambayo pengine yange ingia kwenye kumbu kumbu za mauaji makubwa kuwahi kutokea afrika kama ilivyo kwa Rwanda na nchi nyingine kama Libya, Liberia na Sieralion, sasa mfalme Elvis anamaana gani kufanya hivyo, maana yake akimpata James kinacho fiatia ni adhabu kali sana.

Wakati huo ndio wakati ambao, Mkuu Jeshi la polisi anatoka kupokea taarifa ya kushangaza inayoeleza kuwa mwana dada mrembo, doctor Veronica anahusishwa na tukio lililotokea mbezi, yani tukio la uporaji wa fedha pale PTSH, yani, Private Tresure Saving House mbezi mwisho mkabala na stendi ya malamb mawili,

“inawezekanaje hii, yani wakati baba yake tajiri mkubwa africa akiwa ananusurika kutekwa na hao waasi wa UMD, halafu binti yake ambae sio tu mtoto wa tajiri, pia ni nidoctor mkubwa mwenye kuaminika anashiriki ujambazi?” aliuliza mkuu wa jeshi la polisi ambae tayari alikuwa na wakuu mbali mbali wa vitengo ndani ya jeshi hilo la polisi, “mkuu mimi nadhani haijalishi kama ni amelazimishwa au amefanya kwa hiyari yake, atakapo kamtwa yeye na wenzake ndipo tutapata jibu” alishauri mkuu wa kitengo cha upelelezi, itakuwa vyema kama msako ukiwa wa haraka sana kabla hajauwawa kwaajili ya kuzuia kutoa ushaidi” alisisitiza mkuu wa jeshi la polisi na wakati huo huo simu yake ikaita.

Nae akaichukua toka mezani na kutazama jina la mpigaji, ilikuwa ni simu toka kwa waziri wa mambo ya ndani, wizara ambayo pia inasimia jeshi hilo la polisi nchini, “hallow mheshimiwa habari za saa hizi” alisalimia CGP yani Chief General Polisi. “daaah! leo kazi ipo, CGP, kuna tukio jingine hapa, mtoto wa bwana James mschana Veronica James mwenye miaka ishirini na nne, anashikiliwa na UMD, bado hawajatoa tamko, ni vyema ukawajulisha vijana wako waliopo mitaani wanao endelea na msako waingie katika jukumu lao” alisema waziri wa mambo ya ndani toka upande wapili wa simu,

Taarifa hii ni kama ilitoa jibu kwa CGP, “mheshimiwa, pia kuna taarifa ya kwamba huyo mwanamke ni mmoja wa washukiwa katika tukio la uporaji wa fedha kule mbezi kwenye jengo la uhifazi wa mali binafsi za wanachi” alisema CGP, “inachanganya kwa kweli, lakini sio mbaya nyie ni polisi na munajua cha kufanya, kwanza apatikane huyo mwanamke yeye andie atakae eleza vizuri” maongezi ya waziri na mkuu wa jeshi la polisi yaliisha hivyo na mara moja CGP akatoa amri kwa mkuu wa jeshi hilo kanda maalumu ya dar es salaam kwamba awaeleze makamanda wake wa mikoa ya kanda maalumu ya dar es salaam, wawajulishe askari wao taarifa hiyo.*****

Wakati huo bwana Kadunya aliekuwa amesha karibia njia panda ya msakuzi kupitia njia ya stendi ya zamani ya mbezi mwisho ndani ya gari akiwa na marehemu mmoja, vijana wa tatu majeruhi na wawili wazima mmoja akiendesha gari na ndio wakati ambao aliona simu yake inaita na alipoitazama akaona kuwa mpigaji ni CP Ulenje, hakuipuuza maana alikuwa ni mtu muhimu sana katika usalama wao hapa Dar es salaam hasa kwa sku kama ya leo ambayo ilikuwa na matukio mazito.

Hivyo akaipokea mara moja na kuiweka sikioni, niambie bwana kaka, kuna inshu?” aliuliza Kadumya kwa shahuku, “vipi mumesha mkamata huyo dereva?” aliuliza Ulenje kwa sauti yenye wasisi, “tayari yupo mikononi mwetu, vipi kuna tatizo mbona kama una wasi wasi” aliuliza Kadumya kwa sauti ya mshangao, “basi vijana wako vizuri, waambie vijana wako wawe nae makini sana” alisema Ulenje, huku akionekana kupatwa na uafadhali, “kwanini Ulenje, kwani ana tatizo lolote?” aliuliza Kadumya kwa sauti ya kutokujali, “labda kama unawaamini sana hao vijana wanao mshikiria huyo dereva, lakini pia vijana wangu ishirini wapo njiani wanaelekea huko kuongeza nguvu” alisema CP Ulenje kwa namna ya fulani ya mashaka, “ana nini cha zaidi huyo fala?” aliuliza Kadumya kwa sauti ya kutokujali, yani alidharau.

Hapo Ulenje akacheka kidogo, “naamini hujui kwamba mtu uliemshikilia ni sawa na kuingiza nyoka ndani ya nyumba aje kukamata panya” alisema Ulenje, ambae wazi kabisa hakuhitaji dharau wakati ule, Kadumya akacheka kidogo, acha utani Ulenje, unadhani kuna mtu wa kunizidi ujanja? tena mbele ya wanaume wa shoka wenye silaha” alisema Kadumya kwa sauti yenye kujiamini akimaliza na kicheko.

Ni kama Ulenje aligundua jambo, “hoooooo! sasa nimegundua kuwa hujui chochote kuhusu Deus Frank” alisema Ulenje safari hii kwa sauti yenye msisitizo, hapo kidogo Kadumya akashtuka kidogo na kabla hajauliza lolote, Ulenje akadakia, “huyo ni askari mtoro wa jeshi la ulinzi mwenye mafunzo ya juu ya special force na kwa kifupi ndie mtu alietoka kumchukua James Kervin chumba namba nane cha ghorofa ya tatu pale sisterfada hotel, sasa je una uhakika wa kuwa vijana wako safari hii watamdhibiti?” lilikuwa swali toka kwa CP Ulenje.

Ukweli swali hilo alikujibiwa zaidi Kadumya alionekana kuwa na mshtuko mkubwa, wakati anakata simu na kuanza kubofya simu yake, kumpigia Kafulu huku kichwani mwake zikiwa zinapita picha za matukio yaliyotokea lisaa limoja lililopita kule sisterfada ndani ya chumba namba nane cha ghorofa ya pili.. ….….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA MBILI
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA MBILI:- Ukweli swali hilo halikujibiwa zaidi Kadumya alionekana kuwa na mshtuko mkubwa, wakati anakata simu na kuanza kubofya simu yake kumpigia Kafulu, huku kichwani mwake zikiwa zinapita picha za matukio yaliyotokea lisaa limoja lililopita kule sisterfada ndani ya chumba namba nane cha ghorofa ya pili.. ….….ENDELEA…

Kadumya akiwa anaonekana mwenye wasi wasi, akapiga simu na kuiweka sikioni nayo ikaanza kuita.********

Naaam usiku ulikuwa mrefu, usiku ulikuwa na mambo mengi sana, usiku ulikuwa na pilika nyingi za kila namna, wakati polisi wakiwa mtaani na msako wa nguvu, tayari askari thelathini wa jeshi la ulinzi kikosi cha 85, specia marine force kilikuwa kina jiandaa kuingia katika sako wa nguvu, huku wakitegemea taarifa toka TSA na jeshi la polisi kujua Deus Nyati ataonekana maeneo gani ili wakamchukue na kumpeleka makao makuu ya jeshi ambako angefungwa kwa mwezi mmoja ikiwa ni adhabu ya utoro kazini kisha angerudishwa kazini.

Upande wa pili polisi walikuwa wanaendelea na msako wa nguvu, njia zote za jiji zilishikiliwa na polisi, wananchi hawakuweza kutembea bila sababu za msingi, maana wapo walioangukia kwenye mikono tandikaji ya polisi wasio na subira baada ya raia hao kushidwa kujibu maswali mepesi kama vile, “unaenda wapi” unatoka wapi” “kwanini unazurula usiku” na mengine kama hayo,

Pia ulinzi wa Jeshi la ulinzi ulikuwa unaendelea nyumbani kwa bwana James, hakuna mtu alie ruhusiwa kukatiza eneo hilo, haijirishi ni nani, japo ilikuwa ni usmbufu kwa raia na wakazi wa pale lakini kwa namna ya pekee walielezwa faida ya kutii amri ile pasipo kulazimishwa.

Askari wa MLA, kitengo cha AR nao walikuwa wanaingia ndani ya ndege tayari kuanza safari ya kuelekea Dar es salaam kukamilisha jukumu la kumlinda James Kervine pamoja na kumpelaka sehemu salama ambayo ni nchini #mbogo_land, pekee.

Huko mbogo land kwenyewe sasa, tayari viongozi wakubwa wa serikali ya nchi ya #mbogo_land, walikuwa kwenye ukumbi mdogo wa mikutano pamoja na waandishi wa serikali, ambao walikuwa na camera zao vinasa sauti na karamu na karatasi zao kwaajili ya kuchukua matukio ya kikao hiki.

Mawaziri pamoja na wazee wa baraza na viongozi mbali mbali wa vyombo vya ulinzi na usalama wa #mbogo_land, waliokuwa wanamsubiri mfalme Elvis kwaajili ya kuanza kikao sasa walisikika wakiongea kwa sauti za kunong’ona, huku wakionyeshana baadhi ya habari kwenye simu zao kubwa, kama vile I pand, tablet na simu ndogo za kisasa, hata wengine walichukua laptop zao ndogo za kisasa ambazo pia walizitumia kutazama habari hizo za kushtua sana zilizokuwa zinamuonyesha tajiri James mwenye asili ya #mbogo_land, akiwa na kiongozi wa jeshi la waasi wa UMD, ambao wamekuwa wakitishia nchi ya mbogo land kwa muda wa miaka ishirini na nne sasa.

Muda wote bwana Chitopelah alikuwa kimya kwenye kiti chake, mara kwa mara anatazama simu yake kuona kama kuna taarifa yoyote toka kwa Kadumya, mtu ambae alipanga kumpa jukumu la kuwa mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wa #mbogo_land, wakati watakapo chukua nchi na yeye kuwa raisi.

Chitopelah, aliendelea kusikiliza minong’ono ya wenzake mule ndani ya ukumbi, “kwahiyo bwana James miaka yote hii bado ana nia ya kupindua nchi” Chitopelah, alimsikia anauliza mmoja kati ya wale waliokuwepo ndani ya ukumbi akiongea na mwingine aliekuwa jirani yake upande wa kushoto, “hizi ni tamaa za ajabu sana, yani nchi kama hii yenye kila kitu na maisha mazuri kwa kila mwanachi unatafuta mapinduzi gani tena kama sio kutaka kuuza nchi kwa wezi” alisema mwingine ambae kiukweli mnong’ono wake ni kama ulimgusa kidogo Chitopela, hasa ule msemo wa “hizi ni tamaa za ajabu” ni kweli zilikuwa tamaa za kumiliki nchi hii yenye kila kitu.

Minong’ono iliendelea mule ndani ya ukumbi ambao ukichilia mawaziri na wazee baraza pia kati ya wanausalama waliokuwepo mule ndani, walikuwepo mkuu wa majeshi na wakuu wake wa vitengo, yani mkuu wa mafunzo na mipango vita, ndani na nje ya nchi, pia alikuwepo mnadhimu mkuu, afisa mkuu wa uchunguzi na utambuzi wa jeshi, mkuu wa polisi jeshi, mkuu wa mawasiliano, mkuu wa miradi na fedha, wakuu wa kamand mbali mbali, ikiwa anga maji na ardhini, na pia alikuwepo mkuu wa kitengo cha uchunguzi wa kivita, yani AR Comander, ambae ni major general Sixmund.

“lakini ni kweli kile tunacho kisikia au kuna ujanja umefanywa na UMD au wapinzani wake wakibiashara?” aliuliza mmoja kati ya wale wawili waliokaa karibu na mheshimiwa chitopela, waziri wa ulinzi, “naamini mfalme atachukua maamuzi sahihi ilikukomesha kabisa swala hili” alisema mjumbe mwingine.

Wakati minong’ono ikiendelea, mara yakasikika makofi mawili, “pa pa! wote wakatulia na ukumbi ukawa kimya, waziri mkuu akasimama, “mtukufu mfalme anaingia” alisema waziri mkuu watu wote wakasimama juu, na kama kuna alievaa kofia akaitoa kichwani na kuishika mkono wa kushoto, huku wanainamisha vichwa vyao chini, “huu ndio ujinga nisioutaka” Chitopela alinung’unika kimoyo moyo huku anakata jicho la wizi upande wa kushoto ambako kulikuwa na lango kubwa la kuingilia ukumbini.

Naam wanaonekana waschana wanne warembo, waliovalia kanga au vitenge vilivyofungwa kwa namna ya ufupi na kuacha baadhi ya sehemu za mwili zikiwa wazi, kama vile kuanzia magotini kushuka chini eneo dogo la tumbo na mabega na mikono waliobeba mabakuri makubwa ya dhahabu wakitembea kwa madaha na kutia mikono yao kwenye mabakuri yale na kuibuka na maua mazuri mchanganyiko, kisha kuyamwaga juu ya zuria jekundu huku nyuma yao akionekana Mfalme Elvis akitembea juu ya zuria lile jekundu na kuyakanyaga maua yale mazuri, huku akifuatiwa na vijana wawili waliovalia kaptura na vishati vidogo, ambavyo havikufungwa kifuani “maisha marefu kwa mfalme Elvis kwanza” zilisikika sauti za wajumbe waliokuwa mle ndani, huku wanaweka mkono wa kulia kifuani na vichwa wameviinamisha chini

Ukiyastaajabu ya mussa basi utayaona ya firaun, maana wakati wengine wanamtakia maisha marefu king Elvis mbogo wa kwanza, Chitopela alimtakia la kwake, “maisha mafupi kwa mbwa huyu kwanza” ndivyo alijisemea Chitopela kimoyo moyo huku akiibia kumtazama Mfalme huyu kijana aliekuwa ameinua mkono wake juu kutoa baraka kwa watumishi wake hawa, “mwisho wako unakaribia we mshenzi, kabla ya kukukata kichwa, nitahakikisha umeona na kujua kila kitu kuanzia kuona maisha mapya ya raia wa mbogo land na umjue muhusika wa mipango hii ya kibabe ambayo itakutoa madarakani.

Wati King Elvis anaelekea kukaa kwenye kiti chake cha dhahabu sasa turudi Tanzania. ambako mambo bado mabichi. ********

Naam sasa turudi kule mbezi makabe, ambako Veronica alikuwa analia huku anajilaumu kwa kuingia kwenye penzi la mtego pasipo kujua mtu aliemdhania kuwa anaenda kuwa mume wake ni jambazi mkubwa, “mh! sina hakika kama unacho kifikiria ni kitu cha kweli, nakushauri ujiandae kwa mabadiliko ya ratiba” Veronica anakumbuka maneno ya Mchoraji, yani ni yule rafiki yake wa kwenye simu, ambae mfanyabiashara ndogo ndogo wakutembeza, ambae licha ya kuwa katika urafiki kwa muda mrefu, lakini hakuwahi kukutana nae wala kutoa utambulisho halisi zaidi alimdanya anasoma chuo cha biashara huko mkoani Mbeya.

Wakati huo tayari luten Enock Kafulu, alisha maliza kuongeana na mkuu wake yani kanali wa zamani wa MLA, ambae sasa anajiita Genneral, yani bwana Kadumya muda mfupi uliopita, kijana huyu anaweka simu mfukoni na kumgeukia Deus, ambae alikuwa amesimama anamtazama kijana mwenzie huyo ambae pengine alimzidi kama miaka minne au mitano. “dereva siku nyingine jifunze kuwa na heshima pale mkubwa wako anapo ongea na simu” alisema Kafuru huku anamtazama Deus aliesimama mita kama tatu toka aliposimama Veronica, “ni kama ambavyo wewe unavyopaswa kuheshimu watu wengine na kutimiza ahadi ulizo ziweka” aliongea Deus kwa sauti tulivu, huku anamtazama Kafulu, yani kijana huyu ambae Veronica anamtambua kama JJD.

Kafulu alicheka kidogo, tena kicheko cha dharau huku anatikisa kichwa kwa masikitiko, “hivi unaitwa nani dereva” aliuliza Kafuru huku anaanza kutembea taratibu kutoka pale alipokuwepo Veronica na kumsogelea Deus, “jikumbushe sheria namba moja, hakuna kujuana majina” alisema Deus kwa sauti tulivu ya taratibu, kama vile hakuwa anapenda kuongea.

Hapo ndipo Veronica alipobaini kuwa dereva hakuwa mmoja wa akina John, na kwamba alikodiwa tu kumleta pale, akainua uso wake na kumtazama kijana huyu, ambae sasa ndio anapata nafasi ya kumtazama vyema usoni na kuiona vizuri sura yake ya upole, kiasi cha kushindwa kuelewa kama anaogopa au ndivyo alivyo.

“dereva unadhani sheria namba moja ni muhimu kwako kwa sasa, muda ambao inabidi ulipie dhambi ya kukimbia na dhahabu zetu?” aliuliza Kafulu kwa sauti ya kujiamini, kama vile mwalimu wa darasa la pili anaongea na mwanafunzi alieiba kichongeo cha mwenzie.

Kauli hii inamshtua kidogo Deus, hapo anakumbuka kazi yake ya kwanza kabisa akiwa na mwanadada Sheba toka nchini Ethiopia, lakini alichokumbuka ni kwamba, dhahabu ilikuwa ni mali ya tajiri wa Sheba, japo alikuwa ameinunua kwa njia isio halali, na kwamba kuna kundi la watu lililoshirikiana na polisi walitaka kuziiba zile dhahabu.

“sijawahi kufungua mzigo wa mteja wala kukimbia na mzigo wa mteja wangu, hii ni sheria namba kumi” alisema dereva kwa sauti tulivu, sauti ambayo inamfanya Kafulu na wenzake wacheke kidogo, maana waliitafsiri kuwa ni sauti iliyokubaliana na matokeo, “dereva unadhani ni wewe tu ndie unaesimamia sheria zako, haya sisi tuna simamia sheria zetu” alisema Kafulu, ambae sasa alikuwa amesimama karibu kabisa na kijana huyu mwenye sura ya upole kama vile mnyonge, “lakini haikufanyi uvunje sheria za mtu mwingine, ni vyema kama ukinipatia malipo yangu kisha nikaondoka zangu kabla hujaendelea kuvunja sheria zangu nyingine” alisema Deus kwa sauti ile ile ya taratibu….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
Imeishia pazuri ngoja tuone kama deus atatoka na happ
 
Imeishia pazuri ngoja tuone kama deus atatoka na happ
Deusi atageuza hilo pagale lao kuwa machinjio kisha ataondoka na mchumba Ili wakajuane kuwa wao ndio pacha na Mchoraji pembeni wakiwa na manoti yaliyochukuliwa bank.

Nahisi itakuwa hivyo.
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA TATU
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MBILI:- “dereva unadhani ni wewe tu ndie anae simamia sheria zako, haya na sisi tuna simamia sheria zetu” alisema Kafulu, ambae sasa alikuwa amesimama karibu kabisa na kijana huyu mwenye sura ya upole kama vile mnyonge, “lakini haikufanyi uvunje sheria za mtu mwingine, ni vyema kama ukinipatia malipo yangu kisha nikaondoka zangu, kabla hujaendelea kuvunja sheria zangu nyingine” alisema Deus kwa sauti ile ile ya taratibu….ENDELEA…

Sijui ni kwanini hawa jamaa waliangua kicheko, ila nadhani hata Veronica, kama isingekuwa tatizo lililopo mbele yake basi angecheka pia, maana sauti iliyokuwa inatamka maneno hayo, yani haikufanana kabisa na kuongea vile sehemu kama ile, “eti sheria, sheria kwenye himaya yangu” alisema Kafulu kwa sauti yenye dharau iliyoambatana na kicheko cha dharau pia.

Hapo dereva, yani Deus anatikisa kichwa kwa masikitiko, “hivi dereva, unasimamiaje sheria zako hasa unapokutana na wababe kama sisi?” aliuliza Enock kwa dharau kisha yeye na wenzake kuangua kicheko cha sanifu, “mjinga sana wewe, yani unaweka sheria na unashindwa kuzilinda” alisema kwa dharau Kafulu huku anageuka kumtazama kijana mmoja alieekuwa amesimama kama mita moja toka alipokuwepo akiwa na bunduki mkononi, “dogo, njoo mchukuwe bwana Dereva mpeleke gorigotha” alisema Kafulu huku yeye anageuka na kuelekea aliposimama Veronica, “bwana Mbwambo, mimi nitakuwa chumbani na shemeji yenu nikampe alichotaka kukipata, naenda kula matunda ya uvumilivu” alisema Kafulu wakati huo kijana mmoja mwenye bunduki alipiga hatua kumsogelea Deus na bunduki yake mkononi.

Hapo ni kama Deus hakupenda kitendo kile, maana alitazama pande zote za mule ndani kama vile alikuwa anakagua mazingira ya mule ndani ikiwa ni watu na vitu kwa ujumla, lengo likiwa ni kuona kama kuna madhara makubwa yanaweza kutokea mule ndani endapo ataamua kukomesha dharau iliyoonekana kushamili mahali pale, “samahani mheshimiwa” aliita Deus kwa sauti tulivu huku anamtazama kafulu ambae tayari alikuwa amesha mkaribia Veronica, ambae alikuwa anatetemeka na kutoa kilio cha chini chini cha kukata tamaa, huku akihisi ule msemo wa mchoraji wake unaenda kutimia, kwamba awe tayari kwa mabadiliko yoyote yatakayotokea.*******

Naam! King Elvis moja kwa moja anaenda kukaa kwenye kiti chake cha enzi za tangu na tangu, kiti ambacho alikikalia babu mpaka sasa wajukuu wanaendelea kukikalia na wale wamwaga maua wakatoka na kuwaacha wale walinzi wakiwa wamesimama pembeni ya mfalme kushoto na kulia, ndipo mfalme akaonyesha ishara ya kwamba watu wakae, nao wakakaaa kwenye viti vyao, “wazee wa baraza, mawaziri, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalam na wasaidizi wenu, leo ni mewaita hapa usiku huu kwaajili ya kutoa tamko rasmi la kiusalama linaloikabili nchi yetu kwa sasa” hivyo ndivyo alivyonza kuongea mfalme Elvis, ambae kiukweli ukiachilia maswala madogo madogo aliyo wahi kukutanayo ya kiuchumi na kiusalama nchini mwake, lakini hili la sasa lilikuwa kubwa na zito sana kwake,

Hapo watu wote ukumbini wakajibu kwa pamoja, “tupo hapa kukusikiliza mtukufu mfalme” hapo Mfalme akavuta pumzi kidogo, huku anazungusha macho ukumbini kutazama sehemu aliyokaa major General Sixmund, mpaka alipomuona, nae akaonyesha ishara ya kushusha uso wake chini taratibu, kwamba yupo, ni mara chache sana kutokea, pengine ni kwasababu ya kuwa wao wawili ndio waliokuwa wanaujua ukweli, “kwanza kabisa natangaza lasmi, uwepo wa kundi la zamani la waasi, wanaojiita UMD, kundi ambalo tuliamini kuwa lime tokomezwa miaka ya 1994” alisema tena King Elvis, huku watu wote mle ndani wakimsikiliza kwa umakini, hasa waziri wa ulinzi na usalama wa taifa muheshimiwa Dickson Chitopelah, hii nikutokana na mambo mawili makuu.

Moja yeye akiwa kama waziri wa ulinzi hili swala linamuhusu moja kwa moja, japo ilishangaza kwa nini hakupewa taarifa kabla ya kuitishwa kikao, pili alisikiliza kwa umakini mkubwa ili kumsoma mfalme na kujua anaelewa nini juu ya UMD na mwenendo wao ili aweze kuzitumia kufanikisha mapainduzi yake, huku akiwa anaamini kuwa tayari mzigo wa fadha upo mikononi mwao, fedha ambazo zitawapa uwezo wa kuzipata silaha zao, silaha ambazo zita wawezesha kuipindua nchi na kuingia madarakani,

“kundi hilo lililoanzishwa na watu wachache wenye tamaa ya kujibinafsishia nchi yetu, bado linaongozwa na yule yule kanari wa zamani wa MLA, muasi Erasto Kadumya, ambae amekuwa akiongoza kundi hilo haramu toka mwaka 1992” hapo Chtopela akaonekana kushtuka kidogo na mapigo ya moyo yakaanza kwenda mbio, sio kwamba alihofia kuwa Kadumya amebainika, hapana, sio kwasababu hiyo, maana Kadumya anafahamika muda mrefu kuwa ni kiongozi wa kundi hilo la wanaharakati wa mchongo, kilicho mpeleka mbio mapigo ya moyo, je kuna mwingine amebainika.

“pia kundi hilo linaloendelea kupata ufadhili toka kwa mfanya biashara mkimbizi toka nchini kwetu, yani bwana James Kervin, inasadikika kuwa kuna uwepo wa viongozi wengine wa kundi hilo ndani ya serikari yetu, viongozi ambao huwashawishi askari na wanausalama wetu kuacha kazi na kujiunga na kundi hilo” alisema Mfalme na hapo Chitopela, akatazama chini kwa kukwepesha uso wake usionekane na mtu mwingine na kubaini mshtuko wake, maana hakuamini kwamba, mfalme alikuwa anayajua hayo yote pasipo yeye kujua kama mfalme anajua.

“hatua zilizo chukuwaliwa kwa haraka kimeagizwa kikosi cha AR, ambacho kilienda Tanzania jioni ya leo kwaajili ya kushiriki zoezi la pamoja la ujirani kiende kumkamata bwana James, ambae ataletwa nchini kuja kujibu mashtaka yake ya kujaribu kushiriki uasi, ikiwa pamoja na kumtaja kiongozi wao mkuu” alisema mfamle Elvis, ambae mara zote walizoea kumuona akiwa katika sura ya tabasamu na kutoa hotuba zenye hadithi za utani.

“Mwisho natoa maagizo kwa waziri wa ulinzi na mkuu wa majeshi, kuandaa vikosi ambavyo vita weka kambi za muda kwenye njia ya maji ya mto ruvuma, upande wa mashariki ambako tunadhani waasi wanaweza kutumia kuleta silaha nchini” mfalme alipomaliza kusehem hivyo akasimama juu na watu wte wakasimama mule ukumbini wakiinamisha vichwa vyao kama wakati mfalme anaingia, wanadada wa maua nao wakakimbia ndani haraka na kuanza kumwaga maua huku wakitembea kuelekea nje, mfalme na walinzi wake wakifuata.

Hapo Chitopela akashusha pumzi ndefu, kwa maana hakuamini kama kwa uchunguzi ule na mambo ambayo mfalme amebaini kwamba bado hajajulikana kiongozi wa kundi lile la UMD, “mumefanya kosa kubwa sana” alijisema kimoyo moyo bwana Chitopela huku akimkata jicho baya mfalme aliekuwa anapotelea nje ya ukumbi.

Baada ya kuhakikisha mfalme ameshatoka, wajumbe nao wakaanza kutoka huku wakiongea hili na lile, ikiwa ni juu ya taarifa ya mfalme, “akisha letwa ni vyema kama atahojiwa kwa kina na kistaarabu ili aweze kujieleza vizuri, pengne ni mipango ya maadui zake kumchafua tu” hiyo ni baadhi ya sehemu ya maongezi ya wajumbe wale, “sijui ni nani huyu kiongozi wao, nadhani james akikamtwa ataeleza kila kitu” alisema mjumbe mwingine huku bwana Chitopelah ambae pia alikuwa anatoka nje ya ukumbi, akiachia tabasamu la dharau na kujisemea kimoyo moyo, “mutamkamata sasa, labda kama ni bahati yenu”

Ukweli chitopela aliamini kuwa Kadumya ata fanikiwa kumpata James kwa kumtumia binti wa mfanyabiasha huyo, “mheshimiwa, nadhani ni vyema ukatupa rukasa ya kuanza kupanga vikundi vya ulinzi sehemu ambazo zinaweza kupitika kirahisi” alishtuliwa Chitopelah na sauti toka pembeni yake.

Alipotazama, huyu alikuwa ni mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, akiwa ameambatana na wasaidizi wake, ni sawa general, unaweza kuanza kufanya hivyo, lakini hakikisha napata muundo mzima wa ulinzi wa mipakani mata tu utakapo maliza kuupanga” alisisitiza Chitopela kabla hajawaagana na kila mmoja kuelekea kwenye gari lake.

Naam ile chitopela anaingia kwenye gari, akapiga simu kwa Kadumya kumueleza kinachojili huku #mbogo_land, na kumsisitiza kumpata bwana James haraka iwezekanavyo na kumuua ili serikali ionekane imefanya hivyo na kuanza kutupiwa lawama na mataifa mbali mbali pamoja na jumuia za kimataifa.

Lakini ile anapiga tu, akasikia sauti ya kike inamueleza, “namba ya simu unayopiga kwa sasa haipatikani, tafadhari jaribu tena baadae********

Naaam!!! huko makabe sasa, Veronica ambae hakutamani kabisa kile ambacho Kafulu alipanga akamfanyie, anamuona mchumba wake huyo tapeli wa mapenzi akisimama na kugeuka kule alikokuwepo Dereva ambae alikuwa anamtazama kwa sura yake ya upole, “vipi Dereva, kuna kitu ungependa kusema kabla hujakata roho?” aliuliza Kafulu, huku anamtazama Deus, “umesha vunja sheria nyingi sana katika makubariano yetu, ni vyema kama ukinipatia fedha yangu ili niondoke” alisema Deus kwa sauti yake tulivu pasipo kuonyesha dalili yoyote ya utani, huku anamtazama Kafulu ambae alitikisa kichwa kwa masikitiko, nikama alikuwa anamsikitikia kijana huyu kwa dharau alizozionyesha, japo kiuhalisia Deus alikuwa anaongea ukweli mtupu.

Kafulu akatulia kwa sekunde kadhaa akiwatazama wenzie kwa awamu, kisha akamtazama Deus kwa sekunde mbili, anawaza amfanye nini huyu dereva mdhaifu anamletea dharau, kisha akaachia kicheko cha dharau, “kwahiyo Dereva, unadhani utafanya nini kama ukiendelea kuwepo hapa na sheria zako zikavunjwa zote na mwisho ukauwawa pia?” aliuliza Kafulu kwa sauti ya dharau, kama vile anaongea na mtoto mdogo huku anatembea kwa mwendo mdogo wa taratibu kumsogelea Deus, ambae hakujibu mpaka Kafulu aliposogea, Vero akajua kuwa kwa mara ya kwanza anashuhudia mtu akiuwawa kwa risasi au kwa kipigo cha mbwa mwizi.

Hapo Veronica akatazama vyema kuona kile ambacho Kafulu anachotaka kumfanyia dereva mpole, “sina hakika kama kweli umeshajiandaa kuona kile ninachofanya kwa mtu anaevunja uratatibu wangu” alisema Deus kwa sauti ile ile tulivu, safari hii akitabasamu kidogo na kumtazama Veronica, ambae pia alikuwa anamtazama kwa macho ya huruma, japo muhurumiwaji alikuwa anatabasamu, likiwa ni tabasamu la kwanza kuliona kwa kijana yule ambalo lilimfanya Veronica auone uzuri wa sura ya kijana wetu huyu, ambae aliamini muda mchache ujao anaenda kupoteza maisha, maana wale jamaa rafiki zake JJ, hawakuonyesha kuwa na mchezo ata kidogo. ….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
Back
Top Bottom