Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Dah, naona umefanya kutuonjesha moja tu 😂😂
 
Muda bado hiyo imejipost tu 😅
Mkuu mambo vipi mpemba? Ndiyo naingia sasa
1738865804539.jpg
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA NNE
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA NA TATU:- Hapo Veronica akatazama vyema kuona kile ambacho Kafulu anachotaka kumfanyia dereva mpole, “sina hakika kama kweli umeshajiandaa kuona kile ninachofanya kwa mtu anaevunja utaratibu wangu” alisema Deus kwa sauti ile ile tulivu, safari hii akitabasamu kidogo na kumtazama Veronica, ambae pia alikuwa anamtazama kwa macho ya huruma, japo muhurumiwaji alikuwa anatabasamu, likiwa ni tabasamu la kwanza kuliona kwa kijana yule ambalo lilimfanya Veronica auone uzuri wa sura ya kijana wetu huyu ambae aliamini muda mchache ujao anaenda kupoteza maisha, maana wale jamaa rafiki zake JJ, hawakuonyesha kuwa na mchezo hata kidogo. ….ENDELEA…

Lakini kitu cha kushangaza, Veronica aliona yule kijana bado amemkazia macho, ni kama kuna kitu alikuwa anamueleza, ndipo alipomtazama vizuri kijana yule akijaribu kuona kama atamuelewa, kile anachojaribu kumueleza, lakini hakumuelewa chochote, pengine angekuwa na muonekano wa kutaka kupambana, basi angedhania anampa ishara fulani ya kujandaa na jambo, lakini kwa namna ambayo Veronica alimjona kijana huyu na kumchukulia kama mnyonge fulani anae tafuta kifo hakuweza kudhani kama anamuambia kitu cha kujiokoa.******

Naaaam, jiji liliendelea changamka, polisi walizidi kuzagaa mitaani wakifanya msako wa nguvu, lengo likiwa katika makundi manne, moja likiwa ni vijana waliovamia hotel wakiwa na silaha, ambao walionekana wakishambulia jengo la sisterfada hotel kwa nje.

Pili likiwa ni kundi linalo sadikiwa kuwa ni UMD toka #mbogo_land, kundi ambalo linahusishwa na utekaji nyara wa mfanya biashara James Kervin, kundi la tatu ni kijana ambae ameondoka na tajiri James pale hotelini, kijana ambae anatafutwa na jeshi la ulinzi akajibu mashitaka ya utoro jeshini.

Huyu ni private Deus Frank Nyati, ambae sio tu anatafutwa na jeshi la ulinzi, pia alikuwa anatafutwa kama dereva wa BMW jeusi ambalo limesha onekana likishiriki mauaji Arusha mjini na pasipo vyombo vya ulinzi na usalama kung’amua sehemu alipo kijana huyo machachali, na msako wa kundi la tatu ambae ameshiriki kwenye tukio la ujambazi na wizi wa fedha katika benk ya uhifadhi wa mali binafsi za wananchi.

Huyu ndie doctor Veronica James, mschana mrembo na mtoto wa mfanyabiashara tajiri Africa na mmiliki wa viwanda na makampuni makubwa, ambae sasa yupo na dereva wa BMW S7 jeusi, na kwa pamoja wote wawili wapo mikononi mwa wafuasi wa UMD wanatazamana na kifo.

Wakati huo haya yote yakiendelea, twendeni sisterFada Hotel ambako sasa uchunguzi ulikuwa unaendelea kwenye chumba namba nane cha ghorofa ya tatu, chumba ambacho ukiachilia kutapakaa kwa damu na matundu ya risasi kwenye kuta za chumba, pia kulikuwa na maganda kadhaa ya risasi, “hii ni risasi ndogo kwa SMG, lakini sio ya bastora wala Uzi Gun” aliuliza mwana TSA mmoja kati ya wale wanne waliokuwa wanaendelea na uchunguzi, aliekuwa ameshika ganda moja la risasi kwa kutumia kibanio maalumu, huku wote wanne wakiwa wamevaa groves za kitabibu, mikononi mwao, “sijui itakuwa ni bunduki ya aina gani, ni ngeni machoni pangu” alisema mwingine ambae pia alikuwa ameshika ganda jingine la risasi, linalofanana na lile aliloshika mwenzie.

“Lakini nikiangalia ngamba ya risasi, ni sio ya Tanzania” alisema yule wa kwanza, huku anatazama nyuma ya kitako cha cha ile risasi, mwenzie nae akafanya hivyo, wakat huo wale wengine walikuwa wanaendelea kukagua chumba huku wanapiga picha kila wanacho kishuku au kuamini kitasaidia katika uchunguzi, “hii inabidi tuipeleke makao makuu wakachunguze na kujua ni risasi toka nchi gani” alisema yule wapili, huku mwingine kati ya wale wawili waliokuwa wanaendelea kukagua akidakia, “hiyo inaonyesha kuwa kundi la kwanza, halina uhusiano na hili la pili, maana wale walikuwa na SMG” alisema yule mwingine na hapo ikazua maswali mengine.

“sasa kama wale wengine walikuwa na smg, nani alikuwa na silaha hii, maana wote wametoka bila silaha” swali hili toka kwa yule wa kwanza lilipata jibu haraka, “kwani hujaona wale jamaa walikuwa na mabegi makubwa, zile ni silaha, tena kila mmoja alikuwa na silaha yake, kasoro yule mmoja, sijui ndio kiongozi wao” alisema yule wa pili, huku mwingine akipata jibu lenye swali la kushangaza, “sasa kama silaha ni za wale waliokuwa ndani na James, huyu kijana alietoka na bwana James alikuwa na silaha gani, maana ameingia na kibox na ametoka mikono mitupu, na kwa vyovyote damu hizi ni za wale wenye silaha” hapo wote wakajikuta wanatazama kwa mshangao, ikionyesha kuwa wameshapata jibu, “yule kijana hatari sana, ina maana ameweza kuingia humu na kuwachakaza hawa jamaa wakiwa na silaha zao?” mshangao huo ukakumbusha jambo.

Hapo ni kama wote wanne walipata jibu na wazo la juu ya nini walikisahau, “chumba na nane, ghorofa ya nne” alisema mmoja wao, kisha wote wakatoka haraka mle ndani, na kuelekea kwenye lift.******

Naam mida hii msafar wa magari mawili wa bwana Songoro ulikuwa unakatiza kimara mwisho, hii ni baada ya kuelezwa na bwana Ulenje kuwa mtu wanae mtafuta atakuwa maeneo ya mbezi, kuna kazi anaifanya huko, “huyu mpuuzi sijali kama anatafutwa na nani, au amevuruga mipango ya nani, nikimkamata nitamyonga kwa mikono yangu mwenyewe” alisema Songoro, ambae sasa licha kuwa kwenye gari, alikuwa na chupa kubwa ya pombe pembeni yake, aliyokuwa anaendelea kuinywa kwa pupa, huku njiani wakipishana na polisi waliokuwaa katika msako.

Bwaba songoro hakujua kuwa lengo la Ulenje, kwamba yeye akaongeze nguvu ya kumshambulia dereva wa BMW, ambae sasa ameshatambua kuwa ni kijana hatari sana, tofauti na washirika wao wanavyo mdhania, ndio maana akawaelekeza wakina Songoro waelekee huko, ili kuwasaidia wakina Kadumya pasipo wao wenyewe kujua kama wanatoa msaada.*********

Naaaam huko makabe, ndani ya ukumbi ambako Deus, baada ya kumpa ishara ya kukaa chini Veronica, wazi Deus aliona kuwa mwanamke huyu hakumuelewa chochote, “dada lala chini na ufumbe macho” alisema yule kijana dereva, kwa sauti ambayo hata wewe ungejuwa ni utani, maana hata doctor Veronica alibakia ametoa macho ya mshangao akimtazama kijana huyu,m anaeleta utani mbele ya kifo.

Lakini kwa upande wa Kafulu ambae wakati huo aliiskia simu yake inaita, alishtuka kidogo, maana sio kwa utani ule anaouleta dereva, wakati mtu yoyote lazima angekuwa anatetemeka kwa uoga baada ya kuleta masihara kama yale.

Lakini licha ya kushtuka huko kabla hajafanya lolote, ghafla akashtuka kichwa cha Dereva kikishuka usoni mwake na kutua kati kati ya macho yani juu ya mgongo wa pua na kuyumba kurudi nyuma huku akijishika sehemu hiyo ambayo haikuchelewa kuanza kutoa damu, kuona hivyo yule kijana wa pembeni aliekuja kumchukua ampeleke huko gorogotha, akainua buduki yake na kuielekeza kwa Deus kwa lengo la kumpiga risasi, lakini alishachelewa kwuharaka wa ajabu sana, Deus alivilingika kama tairi la gari huku mkono wake wakulia ukipitia kisu kwenye mguu wake wa kulia na ile fumba na kufumbua, tayari Deus alisha shika eneo la kati la bunduki ile SMG, ya yule msindikizaji, huku kisu kikigotesha mpini wake kwenye chembe ya moyo ya kijana huyu, ambae aliacha mdomo wazi, uliokuwa ukianza kumwaga damu kama ilivyokuwa kwenye ile sehemu ya chembe ya moyo, ambapo palimwaga damu, nyingi zilizo lowesha mkono wa Deus.*******

Naaaam!!!!! gari aina ya land rover Puma, lilikuwa linakaribia njia panda ya msakuzi, Kadumya, akiwa mwenye hofu na wasi wasi ya kuvurugika kwa mipango yao kama ilivyokuwa kule hotelini, tena ikivurugwa na kijana yule yule ambae ana jina linalofanana na askari wa zamani wa MLA, alishikilia simu yake sikioni, akisilizia ipokelewe, japo iliita muda mrefu bila kupokelewa, “mpuuzi, kwanini hupokei simu Kafulu” alipiga kelele Kadumya huku anapiga tena simu na kuiweka sikioni, huyu mshenzi usikute ametupa simu pembeni anamtomb…., yule binti, na hivyo kalivyo kazuri na alikakosa mwaka mwaka mzima” alisema Kadumya huku anasikilizia simu.

Wakati huo huo gari lao likasimama ghafla kiasi cha kumshangaza Kadumya, kama sio kuyaona magari matatu ya polisi yakikatiza kwa speed mbele yao yakielekea kule walikokuwa wanaelekea wao na kila gari lilikuwa na polisi kadhaa nyuma yake, wote wakiwa wameshika silaha mikononi mwao, “jamani, huyu mjinga nimetoka kuongea nae muda mfupi uliopita sasa kwanini hapokei simu?” alijiuliza Kadumya, huku dereva wake akiondoa gari kuelekea upande ule, yalikoelekea magari ya polisi…... ENDELEA



NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA TANO
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA NA NNE:- Wakati huo huo gari lao likasimama ghafla kiasi cha kumshangaza Kadumya, kama sio kuyaona magari matatu ya polisi yakikatiza kwa speed mbale yao yakielekea kule walikokuwa wanaelekea wao na kila gari lilikuwa na polisi kadhaa nyuma yake, wote wakiwa wameshika silaha mikononi mwao, “jamani, huyu mjinga nimetoka kuongea nae muda mfupi uliopita, sasa kwanini hapokei simu?” alijiuliza Kadumya, huku dereva wake akiondoa gari kuelekea upande ule, yalikoelekea magari ya polisi…... ENDELEA…

“Ongeza mwendo, lazima tukamdhibiti yule mpuuzi” alisema Kadumyabna dereva wake akaongeza mwendo,l pasipo kujari ubovu wa barabara hii.******

Naaam!!!! huko mbezi makabe, sasa mambo yalikuwa yamepamba moyo, wakiwa hawajategemea kuona tukio lile la ghafla na la kushtukiza wale wengine nao, wakaanza kukoki bundiki zao na kuelekeza mitutu ya bunduki zao kwa Deus, ambae ni kama alijua kinachofuata, maana alinyakuwa ile bunduki toka kwa mpigaji huyu aliekuwa anapambania maisha yake katika dakika za mwisho, kisha akamgeukia Veronica.

Mpaka hapo mwanadada mrembo Veronica ambae bado alikuwa amesimama anashangaa kinachotokea, alijihisi ni kama yupo ndotoni, maana hakuwai kuwaza kama anaweza kushuhudia jambo kama lile toka kwa mtu kama huyu, ambae kimuonekaano ni mpole na mtulivu, “shambuliaaaa” alipiga kelele Kafulu huku anajirusha upande wa kushoto, ambako kulikuwa na mzigo wa mbao, nadhani zilikuwepo kwaajili ya ujenzi, hapo kitendo bila kuchelewa sasa Deus, akiwa ameishika ile bunduki akapiga hatua tatu, haraka kumfuata Veronica aliekuwa bado amesimama anashangaa kwa macho yaliyojaa hofu ya kushuhudia mauaji ya kikatili, ambae sasa aliona wale jamaa wanne wakielekeza bunduki zao kule walikokuwepo wao na kujua kuwa asingeweza kuepuka risasi tano au kumi, katika mwili wake.

Lakini ghafla akamuona Dereva akimzoa pale alipo simama na kuruka nae wakiangukia upande wapili wa mzigo wa sementi, huku milipuko ya sirisasi mfurulizo ikisikika, Veronica ambae mwanzo alidhania kuwa wanaenda kujipiga chini vibaya, akashangaa kujikuta amefika chini akiwa juu ya dereva ameshikwa vyema kabisa kwa namna yenye usalama wa hali ya juu, hakuhisi kujigonga sehemu yoyote zaidi ya ubichi wa damu toka kwenye mkono ya dereva.

Na sasa ndio aligundua kuwa kijana huyu, licha ya kuwa na muonekano mzuri, pia alikuwa na nguvu kama simba wa tunduru na mwenye kifua kipana ambacho kinafaa kuwa mto wa kulalia mwanamke mrembo kama yeye.

Milipuko ya risasi iliendelea kusikika, vishindo vyepesi mfano wa vipisi vya nondo viligoga kwenye mifuko ya cement iliyowakinga wakina Deus, na kutibua vumbi vumbi kwa fujo, Veronica aliziba masikio kwa uoga huku anafumba macho.

Kwa haraka Deus akamgeuza vero na kumuweka chini kwa namna ya pekee, kisha akaweka kisu chake kwenye sehemu ya mguu pale alipohifadhiaga, halafu akaikamata ile SMG, kisha akatoa mkebe wa risasi na kuikagua kama ina risasi, akaona risasi zipo za kutosha, akaupachika tena na kukikoki, kisha akatulia, “usiinue kichwa” alisema Deus, akiwa ametulia pale chini, huku ameishika vyema bunduki yake, doctor Veronica akaitikia kwa kichwa akionyesha wazi kujawa na uoga mkubwa kwa kile ambacho kilikuwa kinaendelea, mambo yalifanyika kwa haraka sana, muda ambao haukuzidi dakika moja.

Naaam baada ya risasi kulindima kwa muda kama wa sekunde kumi na tano hivi, mara ghafla milipuko ya risasi ikakoma, na kufwatia na milio ya kacha kacha, ikionyasha kuwa washambuliaji waliishiwa na risasi, hapo Deusbakainuka kwa haraka, huku bunduki yake ameilaza usawa wa bega, kitako kikibanwa vyema kwenye mnofu wa kwenye bega lake la kulia, shavu la kulia lime lala kwenye kitako cha bunduki hiyo huku amefumba jicho lake la kushoto na jicho la kulia kiliunganisha kilengo cha nyuma na cha mbele.

Naam ndani ya sekunde mbili, tayari vijana wanne walikuwa wamesha anguka chini, vichwa vyao vikiwa vimepasuriwa na risasi toka kwenye bunduki ya kijana Deus Frank Nyati, hapo Deus akaruka juu na kutua upande wa pili wa ile mifuko ya cement na kuanza kutembea kwa hatua zenye tahadhari huku akizungusha macho yake kushoto na kulia kuona kama anaweza akampata mtu mwingine zaidi ya Kafulu aliejificha nyuma ya mbao, ambae kiukweli hakuwa na silaha yoyote.

Na wakati anakaribia zile mbao, mara ghafla akamuona mtu mmoja anachomoka toka kwenye maficho na kukimbia mlango mmoja kati ya milango mitano iliyopo kwenye ukuta wa kushoto wa ule ukumbi, ambae kiukweli hakuwa na bahati, maana alipewa risasi moja ya mguu na kujibwaga chini, huyu alikuwa ni bwana Zaid Tambwe, yule aliemfuata Veronica kule bar, kusikia hivyo Mbwambo nae ambae lishajua kuwa waliingia choo cha kike, akainuka na huku ameshika bastora mkononi, lakini kabla hajafyetua risasi yake, tayari risasi mbili zilikuwa zimesha ingia kifuani kwake.

Nadhani hata Kafulu ambae simu yake ilisikika ikiita toka pale mafichoni nae ni kama alishajua kuwa ameingia choo cha kike, maana ainuka taratibu huku mikono ameweka juu, “aya bwana Dereva umeshinda” alisema Kafulu huku anajitoa mafichoni na mikono ameinua juu, damu zikiendelea kuchuruzika usoni mwake Deus hakujibu chochote, zaidi aliendelea kumsogelea Kafulu, ambae bado alikuwa anamtazama Deus, Kafulu akaona kama vile hajaeleweka, “sikia Dereva fungua lile begi chukua fedha unazohitaji, uondoke zako na uniachie huyo mwanamke” alisema tena Kafulu na wakati huo vikasikika vishindo vya watu wakiingia ndani ya ule ukumbi,

“mheshimiwa siwezi kuingia makubaliano mapya na wewe, ila nataka uwe balozi kwa wenzako ambao hawapendi kufuata sheria na taratibu tulizo wekeana kwamba hivi ndivyo navyo wafanyia wapindishaji wa sheria” alisema Deus, kisha kwa haraka sana akampiga kitako cha bunduki usoni kwa Kafulu ambae alipoteza fahamu kabisa na kuanguka chini kama mzigo.

Wakati Kafulu anaanguka tayari Deus alisha geuka na bunduki yake ikiwa katika mkao wa kushambulia, huku macho ameyaelekeza kule vilikosikika vishindo, yani upande wa mlagoni, ambako aliweza kuona taswira za watu wakiingia ndani mbio mbio.

Hakuwa na sababu ya kusubiri, Deus akafanya anachopaswa kufanya, yani aliamimina risasi mfululizo kwa kuelekea eneo lile lenye giza na taswira za watu, ambapo aliweza kuwaangusha watu kama sita hivi, baada ya hapo hakusubiri waje wengine, akalifuata lile begi lenye fedha walilotoka nalo mbezi na kuelekea pale ambapo alikuwepo Veronica, “inuka tuondoke” alisema Deus huku anamshika mkono na kumsaidia kuinuka, “wameisha wote?” aliuliza Veronica huku anavua viatu vyake vyenye visigono virefu na kuvishika mkononi, kisha wakaanza kutembea kuelekea kwenye lango la kutokea nje, huku wakiendelea kusikia simu ya Kafulu ikiita, “samahani begi langu na simu yangu” alisema Veronica huku amageuka nakuelekea pale alipouona mkoba wake.

Naam Veronica alitembea kwa haraka huku macho yake yakishuhudia miili kadhaa ya watu walio kuwa wamelala chini huku wakivuja damu sehemu mbali mbali za miili yao, hasa maeneo ya kichwa,

Ukweli hali ilikuwa ina gofya, mahali pale, Veronica haraka sana aliunyakuwa mkoba wake pasipo kutazama ndani kuhakikisha simu kama vitu vyake bado vipo, kisha akaanza kukimbia kumfuata Deus huku akimpita yule kijana anae mtambua kwa jina la John, ambae sasa alikuwa amelala chini bila fahamu yoyote.

Veronica alitamani kumfanyia kitu ambacho kinge ituliza roho yake, lakini akakumbuka kuwa itakuwa ni sawa na kupoteza muda, hivyo akaendele kumkimbilia Deus, aliekuwa amesimama na bunduki yake akiielekezea mlangoni kwa umakini mkubwa sana na hata alipomfikia wakaanza kutembea kuelekea nje, njiani wakiruka miili ya wale wapiganaji wengine toka nje ambako walipofika hawakuweza kuona mtu hata mmoja, gari lao lilikuwa bado lina unguruma huku limewashwa taa hafifu.

Deus akatupa ile bunduki ndani ya jengo lile, “mbona umeacha bunduki wakitokea wengine je?” aliuliza Veronica huku anatembea kumfuata Deus, aliekuwa anatembea kwa haraka kulifwata gari aina BMW, “hatuhitaji bunduki” alisema Deus, huku wanaingia ndani ya gari, wakati huo kumbuka hawakuwa wanafahamiana majina.

Wakati huo doctor Veronica nyayo za miguu yake zilikuwa zinawaka moto kwa kutembea peku peku umbali wa mita hamsini tu, “tuondoke watakuja wangine” alisema Veronica kwa sauti iliyojaa uoga.

Naaam lakini kabla hata dereva wetu, Deus Frank Nyati hajaingiza gia kwaajili ya kuondoka, mara wakaona mwanga wa taa ukimulika mita kama mia moja hivi mbele yao, ni wazi ulikuwa ni mwanga wa gari lililokuwa linakuja upande wao,

Na baada ya kutazama vizuri wakagundua kuwa halikuwa gari moja, ila yalikuwa zaidi ya magari mawili, labda tuseme ni magari matatu, japo moja la nne lilionekana kwa mbali lakini hakukuwa na uhakika kama nalo lilikuwa linakuja upande huo ila yote yalikuwa speed, “wanakuja tutafanyaje sasa?” aliuliza Veronica kwa sauti iliyojaa uoga.

Hapo Deus Frank Nyati, hakumjibu Veronica, baada yake akatazama kushoto na kulia, kuona kama kuna njia nyingine anaweza kuitumia kupishana na magari yale, lakini ukweli ni kwamba, ile barabara ilikuwa inaishia pale, kwenye ile nyumba, ambayo dakika chache zilizo pita, ilikuwa ni uwanja wa vita, Deus akazima taa za gari huku macho ameyaelekeza mbele, “funga mkanda” alisema Deus, kwa sauti tulivu kama kawaida yake….…... ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
Back
Top Bottom