Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Aliachia kimoja chali,inabid mwandishi atafutiwe dapox hii premature eja** inatuacha na arosto (jokes) 🙂
ameongeza vingine,ila anajua kutuacha na kiu maana imeishia patamu kwel
 
  • Thanks
Reactions: Sax
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA SITA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA NA TANO:- Hapo Deus Frank Nyati, hakumjibu Veronica, baada yake akatazama kushoto na kulia kuona kama kuna njia nyingine anaweza kuitumia kupishana na magari yale, lakini ukweli ni kwamba, ile barabara ilikuwa inaishia pale kwenye ile nyumba ambayo dakika chache zilizopita, ilikuwa ni uwanja wa vita, Deus akazima taa za gari huku macho ameyaelekeza mbele, “funga mkanda” alisema Deus kwa sauti tulivu kama kawaida yake….…... ENDELEA…

Sauti ambayo hata Veronica aliona kijana huyu akiitumia wakati wote, hata kipindi anapambana na wakina JJ.

Veronica hakusubiri aambiwe mara ya pili, akafunga mkanda haraka na kumtazama kijana yule mwenye sura ya upole na roho ngumu ya kinyama, ambae alikuwa anayatazama magari matatu mbele yao yaliyokuwa yanakuja kwa speed kali sana.********

Wakati huo huo, kule Hotelini Sisterfada, mawakala wanne wa TSA, wanashuka toka kwenye lift katika flow ya nne na kuelekea moja kwa moja kwenye mlango wa namba nne, wakipishana na vijana wanne waliokuwa wanasubiria lift, nao hawa kuwajari, maana hata muonekano wao haukuwa wa ajabu sana kiasi cha kuwatilia mashaka.

Wale wana TSA wanasogelea mlango ule na kisha mmoja wao anagonga mlango mara mbili mfululizo, lakini hapakuwa na jibu lolote, mgongaji akajaribu kushika kitasa na kukinyonga, mlango haukufunguka, ilionyesha kuwa mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani na hapo ndipo, wale mawakala walipo gundua kuwa wame fanya kosa la kuja chumba namba nane ghorofa ya nne, bila hata mtu mmoja wa utawala pale hotelini.

Lakini kabla hawaja fanya lolote, mara mlango wa chumba ukafunuliwa na mbele yao akasimama mwanadada wa nguvu mwenye umbo mwanana la kuitwa mama watoto na siyo baby, maana kuna umbo la kuitwa mama fulani na kuna umbo la kuitwa baby au sweat.

Wanausalama waliganda kwa sekunde kadhaa wakimtazama mwanadada yule alievalia tauro jeupe la hotel ile, niwasaidie tafadhari?” alisema yule mwanamke ambae mpaka dakika hii nywele zake zilikuwa tim tim, pengine ni kwaajili ya kazi ambayo imetoka kufanyika huko ndani, haikuonyesha dalili kama kulikuwa na tukio lolote la kimapigano limetokea muda uliopita humo ndani.

Kwanza kabisa wote wanne walitazama juu ya mlango ili kuhakikisha kama kweli mlango ule ulikuwa ni wachumba namba nane, kweli ulikuwa mlango wa chumba namba nne, wakajikuta wanatazamana kama vile wanaulizana, nani aeleze kile wanacho kihitaji, maana waliona kama wamekosea chumba, “hiki ndio chumba namba nane, je wewe ndie ulimpokea kijana mwenye box jekundu?” aluliza mmoja kati ya mawakala wale, huku wote wakimtazama yule mwanamke ambae sio tu kuvutia, ila pia alikuwa anashawishi kwa kutimiza ndoa katika tendo.

“mnamzungumzia yule dereva, ndiyo aliniletea mzigo wangu” aliitikia yule mwana dada, ambae tunamfahamu kwa jina la Emmy au mama Spesioza, “ok! tuna maswali machache tunahitaji kukuuliza” alisema yule mmoja wa wana TSA, “hakuna shida, karibu ndani” alikubari Emmy na kuwakaribisha wale wana usalama wa taifa la Tanzania kanda ya dar es salaam, nao wakaingia ndani.

Lakini ile kuingia tu, wakaona kuna mtoto amelala kitandani, “hooo!!! kummbe upo na mtoto hapa, kwani wewe sio mwenyeji wa hapa jijini?” aliuliza mmoja wa wanausalama huku wote wakimtazama mtoto alielala kitandani, “yule siyo mtoto ni mume wangu” alijibu Emmy, na wakati huo huo yule alielala kitandani anafunua shuka na kuwatazama wale wanausalama, habari zenu.

Kweli alikuwa ni mtu mzima, tena ni baba hasawaaaa, lakini ni mfupi kama mtoto wa miaka tisa kumi ana kumi na moja kama sio kumi na mbili, nakuwafanya wale wanausalama wakitoa macho kwa mshangao, wale wanausalama wawili wakakaa kwenye kochi, huku wawili wakibakia wamesimama, Emmy akiwa amekalia kitanda ambacho bwana Eze alikuwa amelala.*******

Yap! koplo Cheleji akiwa amekaa seat ya mbele ya gari la mbele upande wa abiria, lilikuwa linatembea kwa speed kali sana na kulisogelea jengo walilolikusudia, jengo ambalo waliambiwa kuwa yule kijana hatari dereva wa BMW jeusi yupo hapo, na wanatakiwa wawahi kabla hajasababisha maafa mengine kama aliyo sababisha kule hotelini sisterfada, aliweza kukaza macho mbele kutazama eneo lile la jengo, ambalo zaidi ya magari kadhaa yaliyokuwepo pale nje yani land rover puma, idadi sita na BMW jeusi moja, hapa kuonyesha dalili ya uwepo wa mtu yoyote.

Naam, hapo magar matatu ya polisi, yanaingia kwa fujo eneo lile na ile wanagia tu wakasikia ngurumo ya gari kama vile mnyama duma, ile wanatahamaki tayari wakaliona BMW jeusi, likiwasha taa kali na kuwamulika kwa namna ya kuchukiza.

Ni wakati wanapambana na mwanga mkali wa taa, huku polisi wale waliokuwa nyuma ya gari wakishindwa kushika bunduki zao vyema kutokana na mwendo mkali wa magari yale, wakaliona BMW likichomoka kwa speed kali kuelekea kule wanakotokea, hivyo wakapishana huku wote wakiwa katika speed kali.

Tunaweza kuona magari haya matatu ya polisi, yakijaribu kukamatishwa brake kwa nguvu na kusababisaha magari hayo kukosa uelekeo na kuyumba kidogo kabla ya kukaa sawa na kuanza kugeuka, tayari BMW lilikuwa limesha fika usawa wa land rover puma la bwana Kadumya, ambalo kwa namna ya ajabu tunao jinsi lilivyo kwepwa na BMW ambalo lilipita pembeni kidogo ya land rover nakutokomea zake huku nyuma yakifuatiwa magari yale ya polisi.

Kadumya hakutaka kugeuka kama wenzake, akaelekea moja kwa moja mpaka kwenye lile jengo, ambako alipofika tu, alishuka pamoja na wale vijana wake wawili, ambao kiukweli ndio waliokuwa ni wazima, maana wale watatu walikuwa wamesha chezea risasi sehemu mbali mbali za miili yao huku mmoja akiwa marehemu kabisa.

Pale nje hapa kuwa na mtu yoyote, wala dalili ya mtu kuwepo eneo lile, “isiwe kama navyo waza jamani” alisema general Kadumya, huku anatembea kwa haraka kuingia ndani akifuatiwa na wale vijana wake ambao sasa walikuwa wamebeba bunduki zao wazi wazi.

Naaam, Kadumya aliekuwa mbele, ile anaingia ndani ya jengo lile ambalo wanalitumia kama sehemu ya kuweka sawa mipango yao na kukamilisha matukio yao, kwanza anahisi amekanyaga kitu ambacho kitaka kumtelezesha, ile anakaa sawa ananusurika kujikwaa kwenye kitu kilicho lala chini mfano wa gunia au gogo.

Mwanzo hakuweza kuona vyema kutokana na mwanga hafifu uliopo mwanzoni mwa jengo lile, hivyo Kadumya ana toa simu yake na kuwasha tochi anacho kiona sasa ndicho kinamfanya aache mdomo wazi huku anatazama chini, ambapo palikuwa pame tapakaa damu kama vile sehemu ya machinjio ya ng’ombe,

Naam hapo Kadumya akamulika tochi maeneo ya jirani kuifuatilia ile damu, hapo akakutana na mwili wa askari wake akiwa amelala chini huku damu zikimtoka eneo la kifuani, Kadumya akiwa mwingi wa wasi wasi hofu na hasira akaendelea kumulika maeneo ya jirani na pale aliposimama, anakutana na mwili wa pili, mara wa tatu wanne, mpaka miili sita, huku yote ikiwa imelamba risasi, sehemu mbali mbali za miili yao, “huyu mtu au jini, amewezaje huyu mshenzi” aling’aka Kadumya huku anatazama kule kwenye taa, ambako hakukuwa na mtu wala dalili ya mtu aliesimama, katika eneo lile.

Na kabla hajafanya lolote Kadumya simu yake inaanza kuita, anaitazama haraka kuona jina la mpigaji, “mhe shimiwa” ndivyo anavyo muita waziri wa Ulinzi na usalama wa taifa wa #mbogo_land, nitamweleza nini huyu paka… .…... ENDELEA…



NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA SABA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA NA SITA:- Na kabla akafanya lolote Kadumya simu yake inaanza kuita, anaitazama haraka kuona jina la mpigaji, “mhe shimiwa” ndivyo anavyo mwita waziri wa Ulinzi na usalama wa taifa wa #mbogo_land, nitamweleza nini huyu paka… .…... ENDELEA…

Alijiuliza Kadumya mwenye kujiita general, akiwa amesimama katikati ya vidimbwi vya damu, huku anaitazama simu yake mkononi ambayo ilikuwa inaendelea kuita.*******

Turudi sisterfada hotel, ndani ya chumba namba nane cha ghorofa ya nne, ambako Emmy na wageni wake walikuwa wanaendelea na maongezi yao, huku bwana Eze, akiwa anasikilizia maongezi toka ndani ya shuka la hotel, “yule kijana ni yupi na alikuja hapa kuleta nini na aliondokaje na wale walio mvamia walikuwa wakina nani ni kwanini walimvamia?” aliuliza mmoja wa wale mawakara wa TSA.

Na hapo Emmy akaanza kueleza hadithi yake, japo sina uhakika kama alikuwa anaweza kueleza ukweli halisi mbele ya bwana Eze aliekuwa anasikiliza kila kitu, huku akiombea asije akaamshwa kujibu maswali magumu kuhusu mahusiano yake na wakina Songoro, ambao ni wazi kabisa wao ndio waliofanya shambulizi na lazima watakuwa wamesha bainika,m kuwa ni wao na tatizo lililopo ni kwamba, yeye Eze wakati anaingia hapa hotelini aliongozana na wakina Songoro.

“nina kawaida ya kupumzika nje ya nyumba yangu, nafanya hivyo kama burudani na kubadili mazingira” hivyo ndivyo mwana dada Emmy alivyoanza kueleza, “leo pia niliamua kupumzika hapa hotelini, lakini nilikuwa nimesahau nguo zangu, nikaagiza yule dereva aniletee, nae akafanya hivyo” Emmy alieleza pia, wakati dereva ana mletea nguo zake alizo zisahau ofisini kwake, yani saloon, ndipo mume wake yani bwana Eze akashuku kuwa yeye anachepuka na kijana yule, ndipo alipo kuja kufumania, yule kijana alipojua kuwa anafumaniwa nikashangaa anatokea dirishani” alieleza Emmy.

Emmy aliendelea kusimulia kuwa, wakati yupo ndani anajiandaa kufungua mlango kuona nani alikuwa anagonga, mara akasikia milio ya risasi, “ilionyesha kuwa kuna watu walikuwa wanamshangulia yule Dereva” alieleza Emmy, “hapo na mimi nikafungua mlango na kumuona huyu mume wangu akiwa na watu wawili waliokuwa wamekuja kumsadia kufumania” hapo ukawa mwisho wa maelezo yake.

Wanausalama wakatazama kuona kama kuna ambae alikuwa na swali kwa mwanadada huyu, “dada umesema walikuwa watu wawili, mbona camera zinaonyesha walikuwa watu wengi sana tena wenye bunduki, je unajaribu kuficha kitu?” aliuliza mmoja wa wanausalama, “mimi niliwaona wawili, tena hawakuwa na bunduki yoyote” alijibu Emmy, kwa kujiamini, “ok! unamfahamu vipi kijana huyu Dereva, je unaweza kututajia jiba lake” aliuliza mwanausalama huyo, hapo Emmy akatulia kidogo kabla hajajibu, “hakuna kujuana majina, hiyo nisheria yake namba moja, na yeye nilimpata njiani wakati nakuja hapa hotelini, nikamkodi akanichukulie nguo zangu” alijibu Emmy.

Hapo wanausalama wakatazama tena kama kuna mwenye swali kwa mwana dada huyu, mwenye umbo tepetishi, lililohifadhiwa kwenye tauro la hotel, “dada uliwezaje kumfahamu kuwa ni dereva wa kukodi, je mnafahamiana toka zamani?” aliuliza mwana usalama mmoja, “sikuwa na mfahamu toka zamani, ila siku chache zilizopita nilimkuta karibu na saloon yangu, akipewa mzigo aupeleke sehemu, ndipo na mimi nilipomuona leo nikaona nimkodi yeye” mpaka hapo ni kama waliishiwa maswali kwa Emmy.

Lakini hawakuishia hapo, wote wakamgeukia bwana Eze, wakionyesha kutoridhika na namna ambavyo wamefanya mahojiano, huku bwana Eze amelala muda wote, “samahani mzee, unaweza kutujibu maswali yetu machache?” alisema mmoja wa wanausalama wale.

Hapo bwana Ezee akatoka kitandani huku shuka likiwa mwilini, “inamaana mke wangu hamja muamini anacho waleza?” aliuliza Eze kwa sauti ya yenye ukali kidogo, “ni maswali mengine kabisa ambayo tunataka kukuuliza na sio yale ambayo mkeo ametujibu” alisema mwanausalama wale.

Naam baada ya bwana Eze kujiweka sawa, ndipo wanausalama hawa walipoiona sura yake vizuri na kubaini kuwa ndie mtu alieingia na wale vijana wenye bunduki ndani ya hotel, japo ilionyesha akishuka kwenye gari tofauti na lile walilokuja nalo wale jamaa ambao walikuwa na kiongozi mwingine ambae kwa mujibu wa camera, ndie aliongoza vijana kushambulia jengo kwa upande wa nje, “Samahani bwana mzee, unaweza kutueleza uhusiano wako kati yako na wale vijana waliokuwa wamebeba bunduki, ambao video inakuonyesha unaingia nao ndani ya hotel?” aliuliza mwana usalam mmoja mara baada ya bwana Eze kujiweka sawa.

“ukweli wale watu siwafahamu, ila nimekutana nao hapo nje tu, nikaona kuwa wananifuata huku juu, wakaja mpaka hapa kwa kuwa na mimi nilikuwa nawaza kufumania nikashindwa kuwauliza walikuwa wanataka nini mibunduki yao, lakini wakati mke wangu anafungua mlango, huko nje nikasikia risasi na wale jamaa, wakaondoka kukimbilia huko ghorofa ya nne, wakaniacha mimi na mke wangu” alieleza Eze, akijitahidi kuto kuonyesha wasi wasi wowote,

Hapo maswali yakaanza, “mzee unasema walikuacha na mke wako na mke wako anasema ulikuwa na watu wawili waliokuja kukusaidia kufumania, sasa hao watu wawili wako wapi kwa sasa” aliuliza mwanausalama mmoja, “wao niliwaambia waondoke zao maana hawakuwa na sababu ya kubakia hapa” alisema Eze.

Mpaka hapo wanausalama hawakuwa na maswali zaidi japo wangekuwa makini wangebain kipishan kwa majibu, baada yake wakachukua majina na utambulisho wa wanandoa hawa wa uongo pamoja na namba zao za simu, “tukiwahitaji tuta wasiliana na nyie” alisema mmoja wa wanausalama wale, ambao waliona kuwa Eze na Emmy hawakuwa na msaada wowote juu ya uchunguzi ule, japo kama wange komaa na Eze wange pata japo mwanga wa uchunguzi wao, zaidi walipiga simu kwa mkurugenzi, na kutoa taarifa ya kamili ya uchunguzi wao.*****

Naam akiwa anatetemeka, huku anatoa macho kwa uoga, mwana dada mrembo doctor Veronica James, aliekuwa ameshikilia seat ya BMW S7, kama vile hakuamini mkanda wa usalama aliojifunga kutokana na mwendo ambao gari lile lilikuwa linaenda, katika ile barabra ya ovyo, yenye mawe na mabonde, japo kwa muundo wa gari hili, walikuwa kama vile wapo kwenye barabara ya lami kwa jinsi gari lilivyokuwa limetulia pasipo mitikisiko.

Deus Frank Nyati, aliendelea kukanyaga mafuta huku akipangua gia kila apoona inafaa, kama sio kushuka basi kupanda, macho yake yakiwa makini kutazama mbele, kule anakoelekea, mara kadhaa akizikosa kosa pikipiki za abiria, zilizokuwa zina kuja mbele yake bila utaratibu, mara chache akipeleka macho kwenye side mirror na kutazama yale magari matatu yaliyokuwa yana wafukuzia kwa speed kali, ambayo kwa sasa yalionekana kwa mbali sana.

Naam Veronica akiwa amepoteza matumaini ya kufika salama nyumbani kwao, kabla hajapoteza Maisha au kupata ulemavu kwa ajari, aliendelea kuliona gari likitembea kwa mwendo ule mkali wa kugofya, na hata walipofika eneo la njia panda ya mbezi kutokea stend ya zamani ghafla akaona gari linazimwa taa kisha akamuona dereva kwa haraka akiachia mkono wake wa kushoto toka kwenye stearing na kushika kirungu cha parking brake, wengi huita heand brake na kuipandisha nusu huku anakata kona upande wa kulia.

Hapo Veronica akaliona gari linasotesha tiri zake, na kugeukia upande ule wa kulia kisha akashusha ile heand brake na kukanya mafuta huku ana liweka gari sawa na kutokomea upande huo, kitendo ambacho kilimuacha Veronica akiatetemeka mpaka tumbo la chakula na mapigo ya moyo akiyahisi yamesimama, akamtazama dereva akamuona ametulia anaendesha gari, macho ameyaelekeza mbele, uso wake ukionyesha utulivu ule ule, ambao aliuona kuanzia pale mbezi na kule ndani kwa akina JJ, yani Kafuru, ndivyo alivyomuona sasa na kumshuhudia akiwasha taa kwa mwanga hafifu, huku wa kimulika kuta ndefu kushoto na kulia, zilipo jengwa kama uzio wa wenye maeneo hayo.*******

Naam huko #mbogo_land, bwana Chitopela, akiwa njiani ndani ya gari peke yake, anaelekea nyumbani kwake, wakati mkono mmoja umeshika kiongoza gari, mkono mmoja ulikuwa sikioni umeshikilia simu, ambayo ilikuwa inaita, hii ilikuwa karibu mara ya tatu anapiga, mara mbili ilimuambia simu inatumika, safari hii ndio ilibahatika kuita na bahati nzuri zaidi ilipokelewa, “Kadumya, mbona unatumika sana, ujue huu sio wakati wa kuzubaa, mambo yanazidi kupamba moto” alisema Chitopelah kwa sauti yenye ukali wa kufoka.

Kimya sekunde nne hapakuwa na jibu lolote, Chitopela anashangaa, “Kadumya, vipi mbona kimya unasikia kweli” anauliza Chitopelah kwa sauti yenye mashaka mengi sana, hapo anasikia mvumo wa pumzi ndefu ukishushwa kwa nguvu, toka upande wa pili wa simu, “hali ni ngumu mheshimiwa” alisikika Kadumya kama mtu alie shikwa na bumbu wazi, “ongea Kadumya, au unataka unipime kama nina pressure, kuna nini wewe” aliuliza kwa sauti ile ile ya kukalipia, bwana Chitopelah, “mheshimiwa, ukweli yule kijana ni hatari sana, yani hapa nilipo nimesimama katikati ya vijana wetu waliolala utadhani mbuzi waliovamiwa na simba zizini” alisema kwa sauti ileile ya bumbuwazi bwana Kadumya, “eti kijana gani unamzungumzia huyo?” aliuliza Chitopelah, kwa sauti yenye kushangaa, “ni yule dereva wa BMW jeusi, ambae miezi miwili iliyopita alikimbia na zile dhahabu zetu” alielekeza Kadumya kwa sauti ya kupooza.

Ukweli hii ilikuwa ni Habari mpya sana kwa Chitopelah, Habari ambayo hakuitegemea hata kidogo, lakini haikumshtua sana, “achana nae, cha msingi fedha tumeshaipata, angalia kama kuna wazima kisha muondoke haraka, anzeni safari ya kurudi #Mbogo-Land” alisema Chitopelah, na hapo akasikia mguno mdogo wa chini chini toka upande wapili wa simu, “vipi sijaeleweka, mbona unaguna Kadumya?” aliuliza Chitopela, ambae sasa alikuwa amesimamisha gari kabisa pembeni ya barabara, ambayo mida hii magari yalikuwa machache, japo watu wengi walionekana wamepumzika kwenye viunga vya jiji la Treanch Town.

Kimya kikatanda, Kadumya hakujibu kitu, zaidi Chtopelah anasikia sauti kama za vishindo vya watu upande wapili wa simu, “mkuu!! Mkuu!!” ilisikika sauti ya kiume iliyojawa na hofu na uoga, toka upande wapili wa simu, lakini sio ya Kadumya, Chitopela akajua kuna taarifa mpya inakuja, hivyo nae akatega sikio kusikiliza kwa umakini, “vipi kuna lolote” alisikika Kadumya akiuliza kwa mtu aliekuwa anamuita kwa sauti yenye wasi wasi mwingi, “mkuu wote wameuwawa kasoro Kafulu peke yake ndio anapata fahamu, alikuwa amezimia” alisema yule mtu kwa sauti yenye kutetemeka kwa uoga.

Mpaka hapo Chitopelah, hakuwa na haja ya kuelezwa kilicho wakuta watu wake, maana neno wote wameuwawa kasoro Kafulu ilimaanisha watu zaidi ya kumi wameuwawa, maana alikuwa anafahamu mpango mzima na jinsi watu walivyo jigawa.

Hapo akasikia vishindo vya Kadunya akikimbia, niwazi alikuwa anakimbilia kule alikokuwepo Kafulu, ambapo sekunde kama tano hivi baadae… .…... ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI hapa hapa jamii forums
 
Hii simulizi uiandikie kitabu
Utapiga pesa ndefu.
Simulizi tamu sana.
Simulizi yenye uhalisia wa mambo na haina miujiza ya kufikirika ya nguvu za mizimu, malaika au majini.
Ni kama ile simulizi ya
"Bao tatu za mgeni"
Ni hatari na nusu.
Asante sana
 
Hii simulizi uiandikie kitabu
Utapiga pesa ndefu.
Simulizi tamu sana.
Simulizi yenye uhalisia wa mambo na haina miujiza ya kufikirika ya nguvu za mizimu, malaika au majini.
Ni kama ile simulizi ya
"Bao tatu za mgeni"
Ni hatari na nusu.
Asante sana
Wazo zuri kiongozi
 
Back
Top Bottom