Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Kabla sijasoma huwa na angalia post za mwishoni za aliyeanzisha uzi

Nimeona umeandika sehemu ya.... Nne

Harafu ukaenda..... Sita?

Umeruka au?
Hakuna sehemu ambayo imerukwa, kuna baadh ya sehem huwa naunga kwenye post mmoja, ningeruka watu wa humu eeeeh wangenirudisha asubuh asubuh.
 
  • Thanks
Reactions: Sax
Hakuna sehemu ambayo imerukwa, kuna baadh ya sehem huwa naunga kwenye post mmoja, ningeruka watu wa humu eeeeh wangenirudisha asubuh asubuh.
Nafikiri Jana na Leo iwe kaulimbiu Yako sasa. Tunakusubili Leo ufanye kweli mkuu maana kumepowa mno na ukizingatia hata vibe la Chasambi limekata ghafla.
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA NANE
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA NA SABA:- Mpaka hapo Chitopelah hakuwa na haja ya kuelezwa kilicho wakuta watu wake, maana neno wote wameuwawa kasoro Kafulu, ilimaanisha watu zaidi ya kumi wameuwawa, maana alikuwa anafahamu mpango mzima na jinsi watu walivyo jigawa.

Hapo akasikia vishindo vya Kadunya akikimbia, niwazi alikuwa anakimbilia kule alikokuwepo Kafulu, ambapo sekunde kama tano hivi baadae… .…... ENDELEA…

Chitopela akiwa bado ameshika simu sikioni, akamsikia Kadumya akiongea, “Kafulu, ilikuwaje mpaka imekuwa hvi?” aliuliza Kadumya kwa sauti yenye kumsimanga Kafulu, “sheria mkuu, tulivunja sheria” alijibu Kafulu kama mtu aliechanganyikiwa, ilimshangaza kidogo Chitopelah, ambae hakutaka kuongra kwanza mpaka Kadumya amalize kuhoji kilicho tokea, “sheria gani unazungumzia Kafulu, hebu rudisha akili zako unijibu maswali yangu” sasa Kadumya alifoka, “mkuu tumevunja sheria mkuu, kwani huja nielewa?” Kafulu nae alipaza sauti kwa kufoka, akisahau kama yule ni mkubwa wake wa kazi, labda kwa kuwa ni waasi, lakini majeshi yote duniani tangu ezi za waisrael wakati wanaunda jeshi lao la kwanza kuivamia palestina nidhamu kwa kiongozi ni lazima,

Chtopelah akatoa macho kwa mshangao, akijua sasa vijana wake wanaenda kufarakana, “nataka nijue sheria za nini Kafulu na fedha zipo wapi pamoja na yule mwanamke?” aliuliza Kadumya kwa sauti ya kufoka pia, “ni sheria za dereva mkuu, tumevunja sheria za Dereva, na hivi ndivyo anavyowafanya watu wanao vunja sheria zake, atakuwa ameondoka na fedha na yule mwanamke pia” hapo ilibakia kidogo Chitopela aanguke kwa kupoteza fahamu, lakini aliishia kupatwa na kizungu zungu na kujiegemeza kwenye seat ya gari, “huyu mbwa anae jiita Deus Nyati, sasa amechokoza moto, lazima asakwe, fedha zipatikane na auwawe kinyama” alisema Kadumya kwa sauti iliyojaa hasira na chuki.

Jina hilo alilolitaja Kadumya, lilimshtua kidogo Chtopelah, sio kwa sababu alishawahi kuzipata Habari za huyo mtu hapo kabla, wakati wa zile Habari za madoctor kuokolewa toka mateka ya waasi huko DRC, ila pia sasa aliweza kukumbuka jina la mtoto wa askari wa zamani MLA, bwana Frank Nyati, “kabla ya kusaka inabidi tujipange hasawaa” ilisikika sauti ya Kafulu ambayo ilikuwa na kila dalili ya kukata tamaa.

Hapo nikama alimpandisha hasira Kadumya, maana kilisikika kishindo cha kofi, hatujui lilituwa wapi katika mwili wa Kafulu, maana alisikika akipiga kelele za maumivu, “mkuu usithubutu, tena kunigusa, kwani ni kosa langu?” aliuliza Kafulu akiwa katika maumivu makali, “nikosa lako, nimepiga sana simu kukueleza kuhusu huyu mtu kuwa ni hatari lakini huku pokea, ulikuwa unawaza kuhusu yule Malaya tu” alifoka Kadumya, na hapo Chitopela akaamua kukata simu, maana alihitaji kuwaza jambo gani lifanyike ili fedha zipatikane na kulipia usafirishaji wa silaha toka china, “wote mpo sahihi, inabidi tujipange tumsake tuzipate fedha na kumuulia mbali huyo mshenzi” alijisemea Chitopela huku ana bofya simu yake kupiga kwa mtu alimsave kwa jina la Kwanguru.********

Yaap! Songoro na kundi lake linaingia mbezi mwisho njia panda ya goba, hapo wanakutana kizuwizi cha askari wa jeshi la polisi kilichoambatana na askari kumi wenye silaha mikononi mwao, vizuizi vilikuwa vinene, kimoja kilikinga upande wa kutokea mjini, kimoja kilikinga upande wa kutokea kibaha, kingine kilikinga upande wa kutokea stendi ya Malamba mawili na kimoja upande wa goba, kila upande walisimama askari wawili, huku wawili wakibakia pembeni kutoa msaada upande wowote ambao, ungehitaji msaada, macho yao yalikuwa kwenye BMW jeus, japo walikagua kila
gari binafsi lililopita pale kiasi kwamba sasa foleni ilianza kuongezeka kila sekunde iliyopita.

Naam huo ndio wakati ambao, yalisimama magari mawili, moja likiwa ni Toyota Prado na Toyota Noah, yote yakiwa ni meusi, kila moja likiwa na watu watano wenye bunduki, hata walipoona kizuwizi wakaweka silaha zao kwenye sakafu ya gari na kupandisha vioo vya nyuma, huku wakipunguza mwendo na kusimama nyuma ya magari sita yaliyokuwa mbele yao yanakaguliwa, japo ukaguzi ulionekana kuwa ni waharaka haraka, sababu magari yaliyokuwepo pale haya kuwa lengo la kizuwizi, lakini wao pia waliona kuwa magari yale yana wachelewesha.*******

Naaam!!!! Njia panda ya mbezi, kule msakuzi ghafla polisi waliokuwa kwenye magari wanashangaa kuona gari walilokuwa wanalifukuzia kwa kuangalia taa limetoweka ghafla, mwanzo walidhania kuwa kuna mwinuko, eneo lile na kwamba gari litakuwa limepotelea upande wa pili, lakini hata walipofukuzia hawakuona dalili ya gari lolote.

Baada ya kuona kuwa, wametembea kwa mwendo wa mita mia tano bila dalili ya kuliona gari lile, wakaamua kusimama mbele kidogo ya kituo cha kanisani, ambapo kulikuwa na sehemu ya matengenezo ya magari, uoshaji magari na uzibaji wa pancha sambamba na duka la vipuli, iliyokuwa upande wa kulia kama unaelekea mjini na muda huo ilikuwa imesha fungwa.

Lakini mbele kidogo kama mita ishirini hivi, upande wa kushoto wa barabara palikuwa na vibanda vya biashara sambamba na maduka ya kawaida, majiko ya chips na wachoma mahindi, watu walionekana hawakuwa wengi sana, ila uchangamfu wa eneo ulikuwepo wa kutosha, huku boda boda wakiwa wametega piki piki zao, kususubiri abiria.

Koplo Cheleji, anashuka toka kwenye gari na kusogelea upande waliosimama boda boda, huku anasikia maongezi ya watu waliokuwepo eneo lile, “unadhani ni kweli mzee James anafadhiri hilo kundi la waasi?” aliuliza mmoja kati vijana watano waliokuwa wamekaa pembeni ya kibanda cha muuza CD, “kwani inashindikana nini, yule mzee anamkwanja mrefu wewe” alijibu mwingine ambae sidhani kama alikuwa ametoa jibu lengwa la swali, “acha ujinga wewe, sisi tuna zungumzia, kama kweli mzee James anaweza kufanya hivyo, kwa heshima aliyonayo” alielekeza mmoja wao, “huu ni mchongo, nasikia tangu zama za mfalme Eugen wa 2, walishataka kumuuwa huyu jamaa, akakimbia nchi ya #mbogo_land, sasa wamekuja kwa mbinu mpya ya kutengeneza picha yupo na waasi ili wamkamate wakamuuwe” alisema mwingine, “mh! Nchi kubwa kama ile hawawezi kufanya kitu bila kuchunguza wewe, ni kweli yule mzee anafadhili hawa mabandidu” alisema mwingine akitaja jina bandidu.

Bandidu sina hakika kama ndivyo waswahili tunvyo takiwa kuita, ila neno halisi ni bandit, au unaweza kutamka bandits, ikiwa na maana ya wakabaji wezi wa kuvizia barabarani, watekaji wa magari ya wasafari, japo wengine utumia kwa mtu mkorofi na mkatili.

“lakini jamani, hebu tuongee huku tuna fikiria kidogo, unadhani mzee kama yule jinsi anavyo saidia watu na fedha aliyonayo anaweza akafanya hivyo kwaajili gani?” aliuliza yule wa kwanza kuuliza, huku mwingine akidakia, “halafu kwa nini usijiulize kwanini ameokolewa na huyo jamaa aliekuwa anamiminiwa risasi” alisema mwingine, Lakini koplo Cheleji hakuwajali, japo maongezi yale hayakumpendeza, kwasababu yalikuwa yanaelekea ukwelini.

Cheleji alienda moja kwa moja kwa madereva wa bodaboda, ambao pia walikuwa na maongezi kama yale, “yani nimetoka mbezi sasa hivi hakunogi, polisi wametanda kama wote” hayo ni moja ya maongezi ya boda boda, lakini Cheleji hakuyajali, “oya dogo mambo vipi?” alisamia Cheleji huku akimlenga dereva mmoja wa boda boda aliekuwa amejilaza juu ya piki piki yake, boda boda wote wanashtuka na kumtazama cheleji, huku maongezi yakikoma ghafla, “poa bro, hoo!!! shikamoo” alisalimia yule kijana huku anakurupuka na kushuka toka kwenye boda boda yake, “poa, vipi umelionagari fulani dogo jeusi aina ya BMW, limepita hapa?” aliuliza Cheleji, na kabla mlengwa hajajibu, akajibu mwingine, “unazungumzia BMW moja kali hivi?” aliuliza yule mwingine na mwingine akadakia, “limepita kitambo sana limeenda huko msakuzi” alijibu yule mwingine jibu ambalo silo Cheleji alilolihitaji.

“naulizia kama limepta sasa hivi kuelekea mbezi” aliuliza cheleji ambae alidhania kuwa aliejibu hakuwepo wakati gari linapita, “mimi sijatoka kabisa hapa wala alijarudi, labda kama limepitia ile barabara ya kati kwenda kutokea stendi ya zamani” hilo jibu ndilo lililomfumbua akili bwana Cheleji nakujikuta akiachia tusi la nguoni, “kum.. make, huyu dogo anajifanya mjanja sana” alisema Cheleji akiwa anageuka na kurudi waliko kuwa wenzake, huku anatoa simu mfukoni na kupiga kwa boss wake, yani CP Ulenje, kumpatia taarifa ya kile ambacho kimetokea.

Akiwa anasikilizia simu ipokelewe, Cheleji anaingia kwenye gari na kumwamuru dereva aendeshe kuelekea mbezi kwa kupitia upande wa barabara ya goba.********

Naaam Ndani ya BMW, safari ilikuwa ngumu sana kwa mwanadada Veronica, ambae muda wote alijiona kama vile ameshikilia roho yake mkononi, unafuu anakuja kuupata mara baada ya kuingia kwenye safu za maduka ya mbezi mwisho, ambapo dereva huyu alipunguza mwendo na kwenda taratibu kusogelea upande wa barabara kuu, “mwisho wa safari yako tafadhari” aliongea Dereva kwa sauti tulivu ya upole, huku macho yake yana tazama barabara kuu ambako kulikuwa na foleni ya magari, japo haya kuwa mengi sana, “naomba nipeleke nyumbani kinyerezi, alijibu Veronica huku anafungua mkoba wake na kuingiza mkono, ambao unaibuka na simu yake ya mkononi.

Ni kama Deus alikuwa na ushauri mwingine kwa mrembo huyu, “nakushauri kwanza upeleke fedha kituo cha polisi, sehemu ambayo itakufutia makosa na tuhuma, maana mpaka sasa lazima utakuwa umeingia kwenye orodha ya waharifu, na polisi watakuwa na picha yako kwasababu lile jengo lina camera kila kona” alisema Deus Nyati, huku anaingia kwenye njia inayo unganisha maungio ya barabara kuu ya Morogoro na kujikuta amekwama nyuma ya magari mengine, “kaka Dereva, kwa sasa siwezi kujipeleka polisi lazima kwanza nifike nyumbani nikutane na baba, nae amuite mwanasheria, ndipo niende nao kituo cha polisi na wewe utakuwa shahidi” alisema Veronica huku anabonyeza kiwashio cha simu yake, ambayo ilikuwa imezimwa kwa zaidi ya masaa mawili sasa.

Lakini Veronica anaacha kuwasha simu na kumtazama Deus, ambae alikuwa anacheka kidogo, “unacheka nini, una maanisha huwezi kuwa shahidi, wakati hata wewe mwenyewe walitaka kukuuwa” aliuliza Veronica kwa sauti ya mshangao, “umekosea dada yangu, sio tu kwenda kutoa ushahidi kituo cha polisi, ukweli ni kwamba hakuna amtu yoyote anaetakiwa kujua mimi ni nani” alijibu Deus, huku anatazama mbele kabisa, kutazama kinacho sababisha foleni, “kwahiyo wewe ndie dereva wa BMW aliesababisha mauwaji huko Arusha, kwanini sasa wanakutafuta wakati wale watu walikuwa ni majambazi” aliuliza Veronica, huku anabonyeza tena simu yake na sasa ikawaka, “yah! ni mimi” alijibu Deus, kwa sauti tulivu, huku macho yake yenye utambuzi yaliweza kuona polisi wakikagua gari la tatu toka gari lao, yani gari la mbele kabisa, “upuuzi, tunahitaji kuondoka hapa” alisema Deus huku anatazama nyuma kwa kutumia side mirror, akaona kuna gari lina kuja nyuma yake na kusimama nyuma ya gari lao, Veronica anashtuka na kutazama mbele kuna nini kwani, “kuna kizuwizi cha polisi, bila shaka sisi ndio walengwa, japo ni vigumu kujua kama tupo Pamoja” alisema Deus, huku anatazama mbele ambako gari la mbele lilikuwa linaruhusiwa na kubakiza gari moja tu mbele yao. .…... ENDELEA MDAU




NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA TISA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA NA NANE:- “yah! ni mimi” alijibu Deus, kwa sauti tulivu huku macho yake yenye utambuzi yaliweza kuona polisi wakikagua gari la tatu toka gari lao, yani gari la mbele kabisa, “upuuzi, tunahitaji kuondoka hapa” alisema Deus huku anatazama nyuma kwa kutumia side mirror, akaona kuna gari lina kuja nyuma yake na kusimama nyuma ya gari lao, Veronica anashtuka na kutazama mbele, kuna nini kwani, “kuna kizuizi cha polisi, bila shaka sisi ndio walengwa, japo ni vigumu kujua kama tupo Pamoja” alisema Deus, huku anatazama mbele, ambako gari la mbele lilikuwa linaruhusiwa na kubakiza gari moja tu mbele yao. .…... ENDELEA…

“mh! hii road block inatuhusu, hivyo kaa tayari?” alisema Deus kwa sauti tulivu, huku analitazama lile gari la mbele ambalo sasa lilikuwa linakaguliwa, “mimi naona hakuna ubaya, tuna weza kujisalimisha mbele ya polisi kama ulivyo sema, tena ngoja ni mpigie baba ili aje kwenye kituo tutakacho pelekwa” alisema Veronica huku anabofya simu yake ambayo ilikuwa inaingiza jumbe mbali mbali, nae akaipiga namba ya baba yake na kuiweka simu sikioni nayo ikaanza kuita.

Deus yeye alikuwa makini anatazama eneo lile, huku kichwani mwake anawaza na kuwazua macho anayatembeza pande zote.********

Naam! Kaskazini mashariki mwa #Mbogo_land, yani kusini mashariki mwa Tanzania, ndani ya msitu mkubwa na mnene wa Karanga njete, msitu unao ungana na msitu mkubwa wa selous, maeneo ya kilimasela na msela nyoko.

Neno nyoko limezoeleka kama tusi kwa watu wengi wanao tumia lugha ya Kiswahili, ila neno hilo lenye asili ya mkoa wa Mara wilaya ya musoma vijijini, yani butiama kwa watu wenye asili ya wajita, neno hili limegawika mara mbili, likitamkwa Nyokomwana, lina beba maana ya mama, ila ukiitaji mapanga tamka Nyoko.

Giza lilikuwa limetanda ndani ya msitu huu wenye kilomita zaidi ya mia tatu, eneo ambalo lenye Wanyama wa kila aina, wakiwepo wakubwa na wadogo wakali na waharibifu, ndege wengi wa aina mbali mbali, wazuri na wakupendeza, pia walikuwepo wale wa usiku na wenye kuogopesha.

Naam kilo mita kama sabini toka mpaka wa Mbogo land na Tanzania, upande wa Tanzania, yani mkoani Ruvuma wilaya ya Tunduru, usiku huu kwa mbali unaweza kuona miale ya moto inayo angaza na kueneza nuru eneo lile la ndani ya msitu, ambapo ukitazama vyema unaweza kuona, vibanda vidogo vdogo vilivyo jengwa kwa maturubai na yenye Ngozi ngumu na vingine vikijengwa kwa miti na nyasi kavu.

Ukisogelea eneo lile sasa una weza kuona kuwa eneo lile, lilikuwa na vibanda vingi sana, sambamba na watu wengi wa jinsia tofauti, yani kike na kiume, walio valia mavazi chakavu ya kijeshi wenye sura zilizochakaa kama mavazi yao, wachache walikuwa na bunduki mikononi mwao, wao walikuwa wamekaa pembezoni mwa eneo lile lililozungushiwa miba na miti iliyo chongolewa, (kuchongwa) sambamba na waya wa uzio, huku watu hao wenye muonekano wa kiuanajeshi, walioshika bunduki aina ya SMG, wakiwa wamekaa kwa vikundi vidogo vidogo vya kati ya watu wawili mpaka wanne, katika mashimo ya kuhami na kupigania, yani mahandaki, huku wenzao wakionekana wakiendelea na burudani mbali mbali, pasipo kujari kama ni harali au haramu.

Wapo waliokuwa wanacheza karata, huku wakivuta bangi na sigara wakishushia pombe haramu ya gogo wanayo itengeneza wao wenyewe pale pale, kambini kwao,

Wapo waliokuwa wana choma nyama za swala ngiri (kasongo) na Wanyama wengine wa porini, waliowindwa bila ruksa ya serikali, pia kama ujuavyo, katika kundi kama ili lenye watu jinsia mchanganyiko, hawakukosa watu waliojifungia kwenye vibanda vyao au vichakani wakipeana vitumbua.

Katikakati ya kambi hilo lenye muonekano wa kijeshi, kuna hema kubwa lililojengwa kwa ustadi mkubwa, lililozungukwa na wanaume kumi mwenye bunduki na makombora mikononi mwao.

kushoto mwa hema hilo, yanaonekana magari ishirini mchanganyiko, yani aina ya land rover puma na Nissan hard top na magari aina ya ashok layland toleo la stallion, yote yakionekana kuwa mazima na mapya kabisa.

Pale nje ya Hema hilo ambalo kimtazamo ni la kiVIP, anaonekana mwanaume wa makamo, akiwa amelala kwenye kitanda kilicho tengenezwa kwa kamba amezungukwa na wanawake wawili waliokuwa wanamkanda mwili wake, huku yeye akiwa anavuta sigara bwege yake akishushia pombe kali iliyokuwepo juu ya meza ndogo pembeni ya kitanda cha kamba.

Mara simu yake inaanza kuita, mmoja kati ya wale wanawake anaichukua toka kwenye meza ile ndogo na kutazama jina la mpigaji, “mkuu, kuna simu yako toka kwa mtu anaeitwa muheshimiwa” alisema yule mwanamke akionyesha kuwa hakuwa anamfahamu mpigaji wa simu hiyo.

Hapo mwanaume huyu, ananyoosha mkono, kupokea simu huku akionyesha kushangazwa na simu ile nyakati za usiku mkubwa kama ule na yule mwanamke anampatia simu akiwa tayari ameshaipokea, “hallow mheshimiwa, mbona usiku sana mkuu, kuna usalama ukweli?” aliuliza mwanaume wa makamo, “hakuna muda wakuulizana maswali bwana Kwanguru, chukua askari hamsini wenye uwezo mzuri wa kulenga na kushambulia, waliokamilika kivita silaha zote mpaka makombora ya RPG, risasi na mabomu ya kutupa kwa mkono safari tanzania tumia barabara ya mashariki kuelekea dar es salaam” ilisikika sauti yenye haraka toka upande wapili wa simu.

Ilimshtua kidogo mwanaume mtu mzima, kiasi cha kujiinua toka kitandani huku simu ikiwa sikioni, “samahani mkuu lakini…” alitaka kuongea bwana Kwanguru, lakini kabla hajasema lolote, mheshimiwa akamuwahi, “kwanguru hakuna lakini, safari ianze sasa na mtatumia masaa matano tu kufika dar es salaam, nataka mpaka jua linachomoza tayari mume mmesha maliza jukumu na mnarudi kambini kujiandaa na upokeaji wa silaha, maelezo zaidi mutayakuta kwa Kadumya huko dar es salaam, kuhusu fedha za utawala mtakutana na Choropo Tunduru” alisema muheshimiwa na simu ikakatwa, “khaaaa kazi imeanza” alisema Kwanguru huku anainuka kabisa toka kitandani, “mwambie captain Kobwe, afolenishe askari hamsini wa kombonia A” alisema Kwanguru akimtazama mwanamke mmoja, “ambae alipiga salut na kuondoka zake, “na wewe mwambie Kazola aandae mabomu na risasi haraka” alisema Kwanguru huku anachukua chupa ya pombe na kuigugumia, huku yule mwanamke anapiga salut na kuondoka zake, wakimwacha yeye anavaa shati.******

Naam, Ulenje akiwa nyumbani kwake anaonekana anamaliza kuongea na simu, “nilimuambia Kadumya achukue tahadhari mapema, lakini akajifanya mjuaji sasa hilo gari limeelekea wapi?” aliuliza Ulenje kwa sauti ya kulalamika, “itakuwa limeelekea mbezi sisi ndio tunaelekea huko” ilisikika sauti ya cheleji toka upande wa pili wa simu, “ok! Nawapigia simu wakina Songoro wawe makini pale mbezi, nyiefanyeni haraka kufika hapo na haitakiwi wakamatwe na polisi wengine kabla yenu” alisisitiza Cheleji na kukata simu, hapo Ulenje hakupoa akapiga simu nyingine haraka na kusikilizia ipokelewe.**********

Yap! ofisi mbali mbali za ulinzi na usalama ndani ya jiji la dar es salaam, ndio kwanza zilikuwa kama kuna kucha, maana wakati mkurugenzi wa TSA jiji la dar es salaam akiwa ofisini na wasaidizi wake, wakati huo huo mkuu wajeshi la polisi Tanzania nae alikuwa na wasaidizi wake ofisini kwake, huku mkuu wa mafunzo na utendaji kivita ndio alikuwa anaingia makao makuu ya jeshi kukutana na kikundi maalumu cha marine special Force, kilicho andaliwa kwaajili ya kumkamata private Deus Frank Nyati.

Lakini katika ofisi za TSA kanda ya dar es salaam, wanaonekana watu sita waliozunguka meza kubwa ya duara, yenya Majarada kadhaa juu yake, “tumetumiwa picha nyingine za washukiwa toka sehemu ya tukio, ambazo sasa zinaonekana vyema” alisema mkuu wa TSA dar es salaam, huku anafunua jarada moja, ambalo lilikuwa na picha kadhaa za watu mbali mbali, waliokuwepo kwenye tukio la pale sisterfada hotel.

Lakini kati ya picha hizo, picha ya kijana Deus Nyati ilikuwa katika nakara nyingi zaidi, ambazo alitawanya kwa wenzake, “huyu ni Deus Nyati, askari wa jeshi la ulinzi, mwenye mafunzo ya special Force, ambae anasadikika kuwa alimuokoa bwana James” alisema mkurugenzi wa TSA, ambae pia hakuishia hapo, “tayari nimetoa maagizo zitumwe picha kwa njia ya simu kwenda kwa James ili athibitishe mtu aliemtoa pale Hotelini, kama ni huyo au sio huyo” alisema mkurugenzi, ambae pia alitoa tamko, “agizeni wanausalama Wote wa wilaya za mkoa huu wa dar es salaam, waingie kazini haraka, maana tunamuhitaji huyu kijana, ili tujue zaidi ya kuwa askari wa jeshi la ulinzi na pia dereva wa BMW jeusi, yeye ni nani, inawezekana ni mwanausalama wa MLSA, alieishi tanzania kama shushushu kiasi cha kujinga na jeshi la ulinzi, kama sio kwanini ameweza kuja kumuokoa bwana James” alisema mkurugenzi.********

Naam sasa turudi mbezi njia panda ya goba, Songoro ambae alikuwa kwenye gari la mbele kati ya magari yake mawili, huku mbele yake kukiwa kumebakiza gari moja, ili wao wakaguliwe, mara anaona simu yake inaita akaitoa mfukoni na kuitazama, “tena afadhari huyu mpuuzi anapiga, ngoja nimwambie awaambie hawa ng’ombe wake watuache tupite” alisema Songoro, huku anapokea simu na kuiweka sikioni, “vipi Ulenje, unahabari mpya” aliuliza Songoro kwa shahuku, “nisikilize vizuri, unatakiwa kuwa makini sana, lile gari linakuja mbezi kutokea msakuzi” alisema Ulenje na kumfanya songoro ainue uso wake na kutazama upande wake wa kulia, yani kwenye barabara inayotoka Goba, ambako anaona magari kadhaa yaliyokuwa kwenye foleni, “hakikisheni hamumpotezi” alisema Ulenje, akionyesha kusisitiza.

Lakini sidhani kama Songoro alikuwa bado anamsikiliza Ulenje, maana Songoro alionekana kutoa macho yenye udadisi na kutokuamini, “jamani, hivi ni macho yangu, au….?” Aliuliza Songoro huku anashusha simu toka sikioni, akiwa amesha msahau Ulenje, na hapo wenzake pia wanatazama kule anakotazama mwenzao ambae anaweka simu mfukoni, bila kuikata na kuchomoa bastora toka kwenye mkebe wa dash board.

“lenyewe, ni yeye dereva wa BMW” alisema dereva wa gari lile la songoro, na wengine wakitazama na kuthibitisha kuwa, waliloliona upande ule ni gari walilokuwa wanalitafuta, “ok! andaeni bunduki zenu tayari kumshambulia yule mshenzi” alisema Songoro, huku anakoki bastora yake…….…... ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA KUMI
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA NA TISA:- “lenyewe, ni yeye dereva wa BMW” alisema dereva wa gari lile la songoro na wengine wakitazama na kuthibitisha kuwa waliloliona upande ule ni gari walilokuwa wanalitafuta, “ok! andaeni bunduki zenu tayari kumshambulia yule mshenzi” alisema Songoro huku anakoki bastora yake…….…... ENDELEA…

“mkuu kuna kizuwizu na kuna polisi hapa” alisema mmoja kati ya wafanyakazi wa Songoro, ni yule alietoka kwa Eze, yani kijana Side, “lakini ni muhimu tumpate kabla polisi hawajampata” alisema Songoro, huku akishusha bastora yake usawa wa dash board, huku wote macho wameyaelekeza kule ambako kuna gari la wakina Deus, nadhani itakuwa sawa kama tukimshambulia mara atakapoondoka eneo hili” alishauri Side na kama vile Songoro hakauelewa ule ushauri, “sawa, sasa shuka ukawaambie hao wanyuma wajiandae kumfukuzia na kumshambulia huyo mpuuzi” alisema Sonoro na haraka sana Side akashuka toka kwenye gari na kulifuata gari la nyuma yao ambalo lilikuwa na wenzao pia.*******

Naaam nyumbani kwa tajiri James Kelvin, bado hali ya unyonge ilikuwa imetawala, wote walisahau amani yao na kuwazia usalama wa Veronica ambae inasemekana yupo mikononi mwa UMD, huku taarifa nyingine zina muhusisha na tukio la uporaji katika benk ya uhifadhi huko mitaa ya mbezi luis.

Wakati familia hii inasubiria simu toka kwa kiongozi wa kundi hilo lenye lengo la kupindua uongozi wa nchi ya kifalme ya #mbogo_land, mara simu ya mzee James inaanza kuita, wote wanashtuka na kumtazama mzee James, ambae anaitazama simu yake haraka, mapigo ya moyo yakienda mbio kwa wasiwasi kuu aliyokuwa nayo, lakini anapo liona jina la mpigaji mzee huyu anaonekana kushtuka, “Vero” anasema mzee James huku anaipokea simu yake haraka na kuiweka sikioni, “hallow” anaita mzee James kwa sauti ya chini iliyo nyongea, akidhania kuwa moja kwa moja mpigaji atakuwa ni mtekaji wa binti yake, hivyo alitegemea kusikia akijibiwa na sauti nzito yakiume.

“baba, kumbe John ni jambazi yeye na wenzake waliniteka halafu wakanipeleka benk..” kabla hajamaliza tayari mama yake alisha dakia, “Vero mwanangu upo salama kweli, vipi hawaja kuumiza?” aliuliza mama Veronica ambae ni wazi kabisa hakuamini kama binti yake anaongea katika hali ya kuwa huru, “nipo salama mama, kuna mkaka amenisaidia kutoroka” alisema Veronica kwa sauti ya kuwa mwenye furaha, “upo wapi sasa niwaambie polisi waje kukuchukua?” aliuliza mzee James na hapo hakujibiwa na Veronica, baada yake akasikia sauti ya kiume, “dada kaa tayari kwa kuondoka” ilikuwa ni sauti tulivu, sauti ambayo ni kama haikuwa ngeni kwa mzee James, “hallow Vero, niambie upo wapi, ni nani huyo anakupeleka wapi?” aliuliza mzee James, kwa sauti yenye wasi wasi mwingi, lakini akagundua kuwa simu tayari ilikuwa imekatika, maana wakati huo huo simu yake ikaanza kuita tena, ilikuwa namba ngeni.

Kiunyonge mzee James akaipokea ile simu iliyokuwa inaingia, “hallow, James Kelvin naongea hapa, aliongea mzee James kwa sauti ili yokosa matumainu, huku mke wake na binti yake Caroline wakimtazama mzee huyu kwa macho yaliyokosa matumaini, “naitwa Elisha Eric, mkurugenzi TSA, kanda ya dar es salaam, pole kwa matatizo bwana James” ilisikika sauti toka upande wa pili wa simu.

Jina hilo sio geni masikioni mwa mzee James, kwa maana anamfahamu huyu mkurugenzi wa TSA, “asante mkurungenzi ni bahati umepiga simu wakati sahihi, maana nimetoka kuongea na binti yangu sasa hivi alikuwa ametekwa na kutumiwa kwenye uvamizi wa benk, lakini sasa amesha toka kwenye mikono ya UMD, hivyo naomba msaada wa kumpata na kumpeleka sehemu salama” alisema James, kwa sauti yenye uhitaji wa msaada, “ni taarifa nzuri bwana James, unaweza kutuleza kwasasa yupo wapi?” aliuliza bwana Elisha Eric.

Hapo ni kama bwana James akaingiwa na unyonge kidogo, “huo ndio mtihani, kabla hajasema simu ilikatika” alisema mzee James, huku familia yake wakifuatilia maongezi yake, “una hakika kweli amefanikiwa kutoka mikononi mwa watekaji?” aliuliza bwana Elisha Eric, akionyesha kutia mashaka, “ndiyo, ametoka kunipigia yeye mwenyewe, lakini sijui kwa nini, hakumaliza maongezi” alisema mzee James, “ok! Tuna omba ushirikiano wako pindi atakapo piga tena, muulize sehemu aliyopo na utujulishe mara moja” alisema Elisha Eric, kisha akaendelea.

“Pili bwana James, nina maswali mawili kwako” alisema Elisha Eric na kuweka kituo kidogo, kuona kama bado bwana James alikuwa Pamoja nae, “naam nakusikiliza bwana Elisha” alijibu bwana James, akionyesha wazi yupo tayari kujibu maswali, “ok! kuhusu kijana aliekuchukua toka Sisterfada hotel, anaitwa nani na ni mara ya ngapi unakodi usafiri wake” aliuliza Elisha Eric, “hapana sijawahi kumfahamu hapo mwanzo, na kuhusu jina, hakuna juana, hii ni moja ya sheria zake” alisema mzee James, “hooo, kumbe anasheria kabisa, hakuwahi kujitambulisha kuhusu kazi yake au kama ni mwanausalama toka #mbogo_land?” aliuliza tena Elisha.

Lilikuwa ni swali lenye kibu kama lile la kwanza, japo sasa mzee James aliweka nyongeza, “mkurugenzi, labda ni kufafanulie kidogo, ni kwamba huyu bwana yeye ni msafirishaji, na anasheria zake, sheria namba moja hakuna kutambuana na mteja, ni mpole sana, anaongea mara chache, sikuweza kuongea nae sana, ila aliniuliza kuhusu tukio la mwaka 1992 huko #mbogo_land” alimaliza kueleza mzee James.

Na hapo kikapita kimya cha sekekunde chache, ni kama bwana Elisha alikuwa anatafuta swali jingine, lakini hapo hapo mzee James akaonekana kukumbuka kitu, ila anawezekana anamafunzo makubwa ya kijeshi, maana anapigana isivyo kawaida, aliweza kuwapiga UMD kama vile watoto wadogo, ndio maana hata mimi nilijihisi salama kumtumia kunileta nyumbani” alieleza bwana James.

Na hapo bwana Elisha akamaliza maongezi kwa kusema, “sasa bwana James, kuna picha utatumiwa kwa njia ya Whatsapp, tunaomba umtambue huyo aliepo kwenye picha, kisha utupe jibu kama ni yeye aliekutoa mikononi mwa UMD au sie” hivy ndivyo maongezi yao yalivyo hitimishwa.******

Sasa turudi pale mbezi, kwenye maungio ya barabara ya goba na Morogoro, ambako ilikuwa hivi.

Wakati Veronica anaongea na wazazi wake akitumia simu, huku Deus nae alikuwa anajaribu kuoanisha matukio ya kwamba, wale jamaa walio mkodi na kumtaka kumuuwa, walidai kuwa ndio wamiliki wa dhahabu ambayo aliisafirisha kuelekea kule tarakea, lakini kwa maelezo ya Sheba ni kwamba, walio wauzia dhahabu waliwazunguka na kutumia wanausalama wa Tanzania kutaka kuzipora,

Swali likaja kwamba, kama wale jamaa ambao bado hakuwa anawafahamu ni wakina nani ndio wenye dhahabu, kwanini walitumia polisi kuzitafuta zile dhahabu ili hali wao ni majambazi, na leo ameshuhudia wakipora fedha benk, sawa tuseme zilikuwa ni za kwao na walitumia polisi kihalali, sasa kwanini haikutangazwa kwenye vyombo vya Habari kuwa kuna wizi wa dhahabu umetokea na polisi wale waliowahi kule makabe walijuaje kama yeye na huyu mwanamke wapo kule, je walikuja kuokoa au kusaidia kama walivyo saidia kusaka dhahabu?.

Hapo Deus akapata majibu madogo mawili ya kwamba, wale wanaodai ni wamiliki wa dhahabu ni majambazi, ambao walikuwa wanamuwinda wamuuwe kwa kuwapotezea dhahabu, jibu la pili, ni kwamba wale polisi ni washiriki wa kubwa wa genge hili la kihalifu, ambalo bado hajalijua ni lipi, hivyo hata huyu mwanamke pia yupo katka hatari.

Hivyo basi, moja kwa moja kwa sasa alikuwa na uwanja mkubwa wa maadui, na hatakiwi kumuamini mtu yoyote, wala chombo chochote cha ulinzi na usalama.

Hapo Deus akatazama mbele, akamuona polisi mkaguzi anamaliza kukagua gari aina ya Toyota Caldina lililokuwa mbele yao, huku kisha akampa ishara polisi aliekuwa katika geti kuwa afungue kizuwizi, “dada kaa tayari kwa kuondoka” alisema Deus huku anashika simu ya Vero na kuikata, kisha akaiachia idondoke kwenye mapaja manene ya mwanadada yule mrembo, ambae alibakia ameduwaa huku wote wakimtazama polisi aliekuwa anawaonyesha ishara ya kwamba wasogeze gari mbele.

Deus akaondoa gari taratibu nyuma ya Toyota Caldina lililokuwa linaanza kuondka taratibu kuvuka kwa kwenye kizuwizi ambacho sasa kilikuwa juu, huku polisi akionenakana kulitolea macho ya mshangao lile gari dogo jeusi aina ya BMW, ni wazi alisha liona gari hilo ambalo lilikuwa ni gari lengwa katika kizuwizi kile cha muda, “unataka kufanya nini we kaka?” aliuliza Veronica kwa sauti yenye kuanza kujawa na wasi wasi, lakini dereva wetu hakuonyesha dalili ya kujibu swali la mrembo.

Lakini kikatokea kitu ambacho sio tu polisi yule hakukitegemea, ila pia Veronica na wakina Songoro, raia waliokuwepo pale madereva wa magari mengine hata polisi wengine wakishindwa kutumia bunduki zao, maana kilikuwa ni kitendo cha haraka sana, wakati Toyota Caldina likiwa katikati ya kivuko kile cha bomba la chuma, Deus akajanyaga mafuta kwa nguvu na kuchomoa gari kwa speed kuliovertake lile Caldina, side mirror zikipishana nchi moja tu, kutahamaki BMW lilikuwa limejaa kati kati ya barabara, huku kila mmoja akitegemea kuwa BMW linanyoosha na barabara kuelekea stendi ya malamba mawili, ni kutokana na speed kali iliyokuwa nayo gari lile, hivyo hivyo polisi wa upande wa barabara ya zamani anatupa waya wa miba kwenye barabara ya upande wa kushoto, upande ambao ulikuwa wazi kwaajili ya magari yanayoenda, yaani yaliyo kaguliwa.

Lakini haikuwa hivyo, maana ile ghafla watu wanaliona gari likisota na kusugua tairi kwenye lami, huku likigeukia upande wa kulia wa barabara, yani upande wa kibaha na lilipokaa usawa wa barabara ya upande wa kushoto wa barabara hii ya Morogoro kama vile kinu cha nuclea kime ruhusu kombora kuchomoka, mizinga ya mizzael inavyo chomoka toka kwenye ndege.

Hakika ilipendeza machoni pa watu, japo ilihisiwa dereva ni muhalifu, gari lilichomoka speed ya kufyetuliwa, na ukizingatia magari yalikuwa machache upande wa kwenda, maana mengi yalikuwa yamezuiliwa, yana kaguliwa hapo kama alivyo fanya njia panda.

Naam kuona hivyo, Songoro nae akaamulisha gari liondoke kupitia upande wa pili wa barabara, yani wrong sight ambako kulikuwa wazi, hakukuwa na kizuwizi, wanyuma yake akaunga, “ingieni kwenye gari haraka” alipiga kelele polisi mmoja huku anaanza kukimbilia kwenye defender lilikokuwa limesimama pembeni ya barabara lina unguruma, huku polisi huyo akiongea na ile redio ya miito, wenyewe wanaita radio call, “hallo vituo vyote, mimi ni kituo cha kizuwizi cha mbezi luis, nina ujumbe” alisema yule polisi akiendelea kukimbilia gari, hapo redio yake ikaanza kusikika sauti mbali mbali, zikimjibu, kwa kupeana nafasi, huku kila mmoja akitoa utambulisho wake, na sehemu aliyopo, “tuma, nakupata kutoka kimara” “tuma na kupata toka gongo la mboto” “tuma na kupata toka barabara ya goba” “taarifa kwa vituo vyote, yule farasi mweusi tunae mtafuta, ameonekana mbezi mwisho anakimbilia upande wa kibaha, narudia farasi mweusi, anaelekea kibaha” alisema yule polisi wakati huo gari lilikuwa linanza kuondoka huku askari wengine wakidandia juu kwa juu, wakiwaacha askari wawili tu pale makutano ambao walikuwa wanaondoa kizuwizi ili magari mengine yawezekupita, wakati huo tayari magari ya wakina Songoro yalikuwa yamesha ondoka, kupotelea upande wa mbezi kwa yusufu. …….…... ENDELEA




NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA KUMI NA MOJA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA KUMI :- “taarifa kwa vituo vyote, yule farasi mweusi tunae mtafuta ameonekana mbezi mwisho, anakimbilia upande wa kibaha, narudia farasi mweusi anaelekea kibaha” alisema yule polisi, wakati huo gari lilikuwa linanza kuondoka huku askari wengine wakidandia juu kwa juu, wakiwaacha askari wawili tu pale makutano, ambao walikuwa wanaondoa kizuwizi ili magari mengine yawezekupita, wakati huo tayari magari ya wakina Songoro yalikuwa yamesha ondoka kupotelea upande wa mbezi kwa yusufu. …….…... ENDELEA…

Ambako BMW halikuweza kuonekana kabisa, zaidi walionekana watu wakitazama upande ule huku wakipiga kelele za kishabiki, wakishabiakia magari yaliyoonekana yakipita mbio eneo lile la stendi mpya ya dala dala.

Naaaaam, wakati magari polisi nayo yana ondoka kuelekea upande ule wa mbezi kwa Yusufu, magari mengine matatu ya polisi nayo yaliingia pale kwenye maungio na kukuta magari ya raia, yakigombania kupita pale njia panda, “raia wameshaanza yani kila mmoja anajiona ana haraka ya kuwahi, mpaka wata tengeneza msongamano mwingine” alisema koplo cheleji, ambae alikuwa kwenye gari la mbele kabisa, bahati nzuri kwao wale polisi wawili waliwepo pale, nao wakaanza kusaidia kuongoza magari, hasa wakiuongoza upande wa kutokea goba, ambao wao walikuwa wanatokea, ilikuwa ni kwaajili yao maana wao walipo pita tu, wakaanza kuongoza upande wa kimara ambako pia kulikuwa na magari kadhaa ya polisi yaliyokuwa yameitikia wito wa kwamba farasi mweusi ameonekana upende huo.

Wakati huo huo Cheleji akapokea simu toka kwa Ulenje, “sikia bwana mdogo, haina kupoteza muda, kabla serikali haija fahamu kuwa dereva na mtoto wa James wapo gari moja, haraka sana inabidi muwapate hao wawili, hivyo wahini mukaweke kizuwizi, barabara zote zinazoingia kinyerezi, pia kuweni tayari kwa taarifa yoyote, maana akionekana sehemu itabidi muwahi kabla ya mtu yoyote, alisema Ulenje, safari hii hakuwa na maneno mengi akakata simu,tayari mgari yalikuwa yanakatiza stendi ya dala dala.

Kilicho fuata ni amri toka kwa Cheleji, “kata kona kushoto, tunaelekea kinyelezi, yule demu hatakiwi kufika kwao” alisema Cheleji na dereva wa gari la mbele akapunguza mwendo na kukata kushoto, kwenye barabara ya kutokea stendi ya dala dala, na magari ya nyuma yakafuata. *******

Yap Kadumya akiwa amechanganyikiwa hajui pakuanzia, hasira zime mshika vibaya sana juu ya kilichotokea, anatazama miili ya vijana wake iliyo tapakaa chini, huku mmoja ukiwa ndani ya gari Pamoja na majeruhi, mara anasikia simu yake inaita, anapoitazama anaona kuwa mpigaji ni Chitopelah ambae amemsave kwa jina la mheshimiwa, akaipokea haraka na kuiweka sikioni, “habari za saa hizi muheshimia” Kadumya alisalimia, salamu yake haikupatiwa jibu, baada yake akamsikia boss wake akiongea, Kadumya, huu sio wakati wa kufanya makosa, serikali ya #mbogo_land inamtaka James kwa udi na uvumba, hivyo tayari serikali ya Tanzania nayo itakuwa inamzuia James, ili imkabidhi kwa ART, ambao wapo njiani wanakuja dar, fanyeni juu chini, mumkamate huyo mwanamke kwa kushirikiana na marafiki zetu, hasa yule polisi, ila wakati huo askari wetu hamsini wapo njiani wanakuja huko, utakuwa unawasiliana na mkuu wamsafara captain Kobwe ili mujue mtakutana wapi?” alisema Chitopelah, ambae sauti yake ilionekana wazi kuwa alikuwa katika wakati mgumu.

Hapo Kadumya, aliachia tabasamu la wazi, kuonyesha matumaini mapya, “sawa mheshimiwa, wacha tutafute sehemu ambayo tunaweza kufukia miili ya watu wetu, kisha tujue watatukuta wapi” alisema Kadumya, ambae alionyesha furaha ya wazi kabisa kwa kupata matumaini mapya ya kufanikisha zoezi, upatikanaji wa fedha na kuzuia siri yao kuvuja mapema kabla hawaja tekeleza mpango wao. ******

Naam wakati hayo yanaendelea jiji dar es salaam Tanzania, huko Trench Town City #mbogo_land, mfalme Elvis alikuwa chumbani kwake, ndani ya Golden House, pamoja na mke wake wana jadili juu ya kinachoendelea, huku wanasubiri taarifa za huko dar es salaam, “hivi unakumbuka niliwahi kukueleza juu ya huyu mpiganaji wa Jeshi la ulinzi wa huko Tanzania?” aliuliza Malikia Vaselisa, ambae alikuwa amejilaza kifuani kwa mume wake, “nakumbuka, kumbe ni mtoto wa askari wetu wa zamani aliekimbia nchi kwa kusingiziwa kuwa ni mhaini” alisema king Elvis, ambae alionekana kukosa amani kabisa, sababu mambo yalikuwa yanaenda kasi sana.

Yani leo asubuhi anapata taarifa za uagizwaji wa silaha toka china, uagizaji uliofanywa na kundi la waasi linalo jiita UMD yani Uhuru kwa Mapinduzi ya Damu, pia leo hii hii, anaanza kupata ukweli juu ya Frank Nyati na kutuma watu wafuatilie, na leo hii hii ndio anasikia tukio la utekwaji nyara wa Tajiri mkubwa mwenye asili ya #mbogo_land anaeishi huko Tanzania, utekaji unaofwanywa na UMD, kwa kile kinacho daiwa kumshinikiza afadhili mpango wa kuingiza silaha.

“lakini mume wangu, sijasikia kama umewasiliana na bwana James, unadhani ataridhia kupata ulinzi toka kwa askari uliowapeleka?” aliuliza malkia Vaselisa, ambae kama ukibahatika kumuona wakati huu anaingia kitandani, ungesema kuwa alikuwa anajiandaa kwenda kwenye tafrija au ziara kubwa kwa jinsi alivyo lembeka na kuongeza mvuto mkubwa wa sura yake, “mh! ni vizuri umenikumbusha jambo hilo la busara, japo itakuwa vuzuri nikiwasiliana nae binafsi pasipo kutumia afisa habari wangu, sihitaji watu wengine wajue mpango wangu” alisema Elvis huku ana chukuwa simu yake na kupiga kwa barozi wake aliepo dar es salaam akiwa na lengo la kuomba namba ya simu ya bwana James Kelvin.******

Naaaam, taarifa za tukio la kuonekana kwa gari dogo jeusi aina ya BMW maeneo ya mbezi mwisho zilishasambaa ofisi zote za ulinzi na usalama za hapa jijini dar es salaam, navyo vikazidi kumwaga watu wao mitaani hasa upande wa mbezi mwisho kuelekea kibaha.

Moja wapo ni jeshi la ulinzi ambalo mpaka sasa, magari yao nane aina ya Amoured Recconisence Super Turbo Vehicle, kama unavyoweza kuita, ARSTV, yenye rangi za combart yalisha katiza makutano ya barabara ya Morogoro na mandera, pale ubungo wakati huo pakiitwa mataa, kila gari likiwa na askari wanne,

Gari zilikuwa katika speed za hali ya juu kuelekea upande wa mbezi mwisho, askar ndani ya magari hayo ya chuma yaliyotengenezwa Urusi wakati huo bado wapo kwenye, USSR, yenye silaha kubwa ya mzingo wa 14 mm inayo fahamika kwa jina la KAPEVETE, walikuwa wanawasiliana kwa tumia redio, P 422, toka gari moja kwenda gari jingine na pia makao makuu ya jeshi, utofauti wa gari hili ambalo wao huliita Boko na Tank, ni kwamba hili lilikuwa na matairi na Tank ambayo nikifaru, chewe kina tumia truck yani minyororo, mfano wa katapila.

Hakuna gari lililokaa barabarani muda huo, magari yote yalijiweka pembeni kupisha msafara huo mkubwa wenye kusisimua, huku wananchi wakiamini kuwa ni kweli jambo lile lilikuwa zito, na kwamba waharifu lazima wakamatwe, japo hakuna aliejua mlegwa hasa ni yupi kati ya washambuliaji wa hotel, washiriki wa UMD, au bwana James na kijana alieondoka nae pale hotelini, hakika kila mmoja alifuatilia habari hii kwa hamu kubwa.

Naam wakati ambao gari aina ya BMW jeus lilikuwa limeelekea upande wa kibaha, magari matatu aina ya Toyota, mali ya jeshi la polisi, yaliyosheheni askari wenye silaha wakiongozwa na koplo cheleji, yakielekea upande wa kinyerezi kama walivyo amuriwa na CP Ulenje, ya kipitia barabara ya malamba mawili, hakika yalikuwa katika speed kali sana.

Upande mwingine, upande wa kuelekea kibaha, yalionekana magari mawili, moja likiwa Toyota Prado lililotangulia mbele likifuatiwa na gari jingine aina ya Subaru forester, nayo yalikuwa speed kali sana yakielekea upande huo huo wa kibaha, nayo yakiwa katika mwendo mkali kama ilivyo kuwa kwa magari mengine manne ya polisi nyuma yao, ambayo yalikuwa yemesheheni askari wajeshi la polisi wenye vyeo mbali mbali waliobeba silaha mikononi mwao, sasa walikuwa wanakatiza maeneo ya makondeko, wakijaribu kulifukuzia BMW s7 ambalo waliamini lazima polisi wa kibaha wange lizuia mbele.

Lakini ukweli ni kwamba, magari ya mbele kabisa yanafika maeneo kiluvya kwa komba, ambako polisi walikuwa wamesha weka kizuwizi ndipo walipo amini kuwa gari lile wamesha liacha walikotoka. *******

Naaam!!!!! nyumbani kwa bwana James, bado hali ilikuwa tete, askari walikuwa wamezinguka nyumba nzima ya Tajiri huyo, wakati ndani ya nyumba hiyo mioyo ya wanafamilia ilikosa amani kabisa, ukiachilia hali ya kuwindwa kwa mzee James, pia mzee James mwenyewe mke wake na binti yao Carloline walikuwa wana hofia juu ya usalama wa Veronica, ambae licha ya kupiga simu na kuongea kidogo na baba yake, lakini simu ilikatika ghafla na sasa wanajaribu kupiga simu lakini hakupokea kabisa.

Wakati bwana James anarudia rudia kupiga simu, mala anaona ujumbe wa njia ya whatsapp unaingia kwenye simu yake, nae anaufungua mara moja, humo anakutana na picha mbili za mtindo wa passport size, zote zikiwa ni picha za yule kijana aliemchukua pale SisterFada, moja ikimuonyesha kijana yule dereva, akiwa amevaa mavazi ambayo alimuona nayo muda mfupi uliopita, na picha nyingine ilimuonyesha akiwa amevalia mavazi ya kijeshi.

Wakati bwana James anatazama picha zile, mara simu yake ikaita, nae akaitazamabkuangalia jina la mpigaji, nae alikuwa ni mkurugenzi wa TSA yani bwana Elisha Eric, akaipokea haraka sana na kuiweka sikioni, “ni yeye bwana mkubwa, kumbe ni askari?” alisikika akiongea bwana James na kuwafanya mke wake na binti yake watamani kutazama picha hizo, lakini simu ile ile, ilikuwa tayari sikioni kwa bwana James, “ndiyo, anaitwa Deus Frank Nyati, ni askari mtoro wa Jeshi la ulinzi la Tanzania, alijibu bwana Elisha.

Hapo bwana James anaonekana kushtuka kidogo, hasa anapoliskia lile jina, sasa anafahamu ni kwanini dereva yule hatari alikuwa anafahamu hadithi yake ya mwaka 92, “hooo! Kumbe, nilishawahi kupata habari zake, lakini sikuwahi kumfuatilia, kumbe ndie bwana Deus Nyati” akiamua kuficha ukweli wa kwamba kijana yule ana uhusiano na askari mmoja wa zamani wa MLA, ambae pia kuna uwezekano wa kuwa nae ni muathirika wa mipango ya UMD, “kuna jambo jingine ambalo unalifahamu juu ya mtu huyu?” aliuliza mkurugenzi Elisha, hapo mzee James akawatazama mke wake na binti yake, kama vile anawauliza nimwambie au nisimwambie, “mh! kwa kweli leo ni mara yangu ya kwanza kumuona” alisema bwana James, na hapo mkurugenzi akamuomba kuwa endapo ata sikia au kukumbuka lolote juu ya kijana huyo basi amueleze mara moja.

“baba nimesikia unataja Deus Nyati amefanyaje?” aliuliza Carloline kwa namna fulani ya kwamba anamuulizia mtu anae mfahamu, “vipi kwani unamfahamu” aliuliza mzee James, huku anamwonyesha Caloline ile picha ya kijana Deus Nyati…….…….…... ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao Kujia hapa hapa jamii forums
 
👍Umetisha sana mkuu, nmekuwa na robo saa Bora sana kusoma kipande hiki. 😂🤣😂🤣🤣😂🤣🤣🤣🤣😂😂😂😅
 
Back
Top Bottom