Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA KUMI NA MBILI
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA KUMI NA MOJA :- aliuliza mkurugenzi Elisha, hapo mzee James akawatazama mke wake na binti yake kama vile anawauliza nimwambie au nisimwambie, “mh! kwakweli leo ni mara yangu ya kwanza kumuona” alisema bwana James, na hapo mkurugenzi akamuomba kuwa, endapo atasikia au kukumbuka lolote juu ya kijana huyo basi amueleze mara moja.

“baba nimesikia unataja Deus Nyati amefanyaje?” aliuliza Carloline kwa namna fulani ya kwamba anamuulizia mtu anae mfahamu, “vipi kwani unamfahamu” aliuliza mzee James, huku anamuonyesha Caloline ile picha ya kijana Deus Nyati…….…….…... ENDELEA…

Mama Caroline na Caroline mwenyewe wakatazama picha, “ndiyo namfahamu, ni rafiki yangu” alijibu Carloline huku anachukua simu mikononi kwa baba yake na kuitazama vizuri huku uso wake ukiachia tabasamu lenye mshangao ndani yake, huku mama Caroline akimtazama mume wake alietoa macho ya mshangao kumtazama binti yao Caroline, “hooo! Nimekumbuka, ulisema huyu askari unamfahamu kivipi?” aliuliza mzee James, huku anamtazama binti yake kwa macho ya mashaka, maana ile furaha usoni kwa binti yake hakuijua ni ya nini, wakati muda mfupi walikuwa kwenye simanzi na ukichukulia pia mtu anae mtazama kwenye picha, ni mtu hatari sana mwenye dalili ya kiarifu, “si yule rafiki yangu niliekuwa nae kwenye ajari ya tren mpaka akaniokoa” alisema Caroline, akionyesha furaha ya wazi kabisa usoni kwake.

Hapo mzee James nikama alizidisha mshangao wake, “inamaana yule kijana wa wakati ule ndie huyu?” aliuliza mzee James huku anamtazama mke wake kwa macho ya kuhitaji jibu toka kwake, mke wake akaitikia kwa kichwa kukubali kuwa huyo ndie kijana anae zungumziwa, “kwani baba wewe unamfahamu vipi, au anahusika vipi na mambo haya?” aliuliza Carloline, huku anarudisha simu kwa baba yake, “huyu ndie dereva wa gari la kukodi alieniokoa kule hotelini, amechukua shilingi elfu moja ya #mbogo_land, baada ya mimi kukosa fedha ya kumlipa” alijibu mzee James, ambae kiukweli fedha ile aliitunza kwa muda mrefu sana ikiwa na kumbu kumbu nzito sana kwake, yaani ukiachilia vitambulisho ambavyo vilishaisha muda wake vya nchi yake #mbogo_land, ile noti ya elfu moja, ambayo ni sawa na Tsh 10,000/= ndio alama pekee ya nchini kwake aliyokuwa amebakia nayo.

Kauri huyo ilimfanya Carloline aachie kicheko, “baba yani unaikumbuka elfu moja, wakati amekusaidia, basi mimi nitakutafutia nyingine” alisema Carloline, huku mama na baba yake wakiwa wanamtazama, “Carlo, hiyo noti ni muhimu sana kwa baba yako, maana anakumbukumbu nayo sana” aljibu mama Veronica, kisha akamgeukia mume wake, “lakini baba Carlo, nadhani hiyo noti siyo kitu kwa msaada aliokupa yule kijana, ukichukulia ulishindwa kumlipa kwaajili ya msaada aliokupa” alisema mama Veronica na hapo mzee James mwenyewe akarekebisha, “hapana haikuwa kwaajili ya kuniokoa, ilikuwa ni kwaajili ya usafiri wa kunifikisha nyumbani” hapo Carloline na mama yake wakatazamana kwa mshangao, “kwahiyo kupigana kote ilikuwa ni msaada tu?” aliuliza mama Carloline.******

Naam, kamishna wa polisi, Keneth Paul Ulenje, akiwa nyumbani kwake anasubiria taarifa toka kwa wakina Cheleji, bado kichwani mwake alikuwa anawaza namna ya kuwasadia washirika wake, ambao alikuwa anaamini endapo watafanikiwa anapata fedha nyingi sana, na sio mara moja, ila itakuwa siku zote kwasababu mpango wa washirika wake ulikuwa ni kupindua ile nchi Tajiri ya #mbogo_land, “sasa hii inshu ya wizi wa kule benk ikijulikana itawaharibia sana, na pengine inaweza kugundulika kuwa kuna polisi wanahusika na jambo hili, maana tayari wale wajinga wamesha yaona magari ya polisi yana ingia pale Makabe” aliwaza Ulenje, huku macho kwenye television iliyokuwa inaonyesha wachumbuzi wa habari za matukio ya kigaidi, ambapo watangazaji watatu walikuwa wanajadiri tukio lililotokea usiku wa siku ile, “Kadumya amekosea sana kumuingiza huyu yule dereva kwenye jambo hili” aliwaza Ulenje, ambae moyoni mwake alijua fika kuwa, kuhusishwa kwa dereva wa BMW jeusi katika mpango huu ni kosa kubwa sana, na pengine kila kitu kikaharibika, “lazima nifanyake jambo la haraka ili kuweka sawa jambo hili” alisema Ulenje huku anachukua simu yake na kuipiga namba ya Cheleji.

Simu iliita kwa muda mfupi kabla haijapokelewa, “vipi Cheleji, mumesha fika kinyerezi, aliuliza CP Ulenje kwa sauti ya chini kama vile hakutaka mke wake aliekuwa chumbani asikie anacho ongea, “mkuu tupo tumeshafika kinyerezi na sasa tumesha gawana maeneo, wengine wameenda kuzuia barabara ya kutokea segerea, wengine wameenda kuzuia barabara ya kutokea Kimara, na mimi nipo kwenye barabara hii ya kutokea mbezi, mbele kidogo ya shule ya Kifulu” alijibu koplo Cheleji kwa sauti ya kawaida tu, ambayo isinge msumbua msikilizaji kugundua kuwa walikuwa wametulia sehemu, maana hakukuwa na dalili ya kwamba wapo kwenye gari linalotembea.

“Ok! sasa nisikilize kwa umakini” alisema Ulenje kwa sauti ile ile ya chini, “ndiyo afande” alijibu Cheleji akionyesha kuwa, alikuwa tayari kupokea maelekezo, “ujue muda mfupi ujao itabainika kuwa yule dereva yupo na mtoto wa James, na hapo ndipo askari wote watakapo badili mawazo yao na kusahau kuwa Dereva nae mtuhumiwa na kumpatia ulinzi mkubwa ili wafike sehemu salama, na ukizingatia kwa sasa wakina Kadumya hawana uwezo wa kupambana na jeshi la polisi, wala huyo kijana, kwasababu wapo wachache” alieleza Ulenje na kuweka kituo kidogo huku Cheleji akiwa anasikiliza kwa umakini mkubwa, “wewe fanya hivi, tumia redio call, wasiliana na vituo vyote, jifanye unawapa tahadhari kuwa, huyo dereva yupo na mtoto wa James, itafsirike kuwa yeye ndie mtekaji wa yule mwanamke” alisema Ulenje akionyesha kupangilia mpango wake, nimekupata mkuu, tena itakuwa vizuri sana ili tuzidi kumuongezea maadui huyu fala” alijibu Cheleji kabla hawajakata simu.********

Yap! Mita mia sita toka njia panda ya goba, mita hamsini toka kituo cha polisi, (cha zamani) pale mbezi kwa Yusufu, upande wa kulia wa barabara kuu ya Morogoro, linaonekana BMW s7 jeusi, likiwa limeegeshwa huku limezimwa taa, japo engine yake bado ilikuwa ina unguruma, lime tazama upande wa barabara kuu ya Morogoro, ambako yanaonekana magari mengi ya polisi, yanakatiza kwa speed kali, kuelekea upande wa kibaha.

Ndani ya gari Veronica anamtazama kijana huyu mwenye sura ya upole, aliekuwa anatazama mbele upande wa barabarani kwa macho yake tulivu pasipo kuonekana dalili yoyote ya wasi wasi usoni pa kijana huyo, ambae umahili wake katika mapigano na kwenye kuendesha gari umemshangaza doctor Veronica.

Veronica anawaza mambo mawili matatu juu ya kijana huyu, kwanza muonekano wake wa kiume, “kwanini mkaka mzuri kama huyu anafanya kazi za hatari kama hizi?” anajiuliza Veronica ambae kwa mara ya kwanza leo anakutana na mwanaume ambae haonyeshi dalili ya kumtazama kwa matamanio, kama ilivyo kwa kila mwanaume anaekutana nae, kiasi cha yeye kushangaa, “inamaana na yeye hajanitamani, mbona hanitazami au majambazi hawapendi, lakini mbona JJ ni jambazi lakini alinitamani?” alijiuliza Veronica huku anajitazama kidogo eneo la mapajani na kisha kumtazama tena Deus kwa macho ya wasi wasi, “umesema unakaa kinyerezi sehemu gani dada?” anauliza kijana kwa sauti tulivu huku macho yake ameyaelekeza mbele.

Hapo nikama Veronica anazinduka toka kwenye, mawazo yake “ndiyo… ndiyo nakaa kinyerezi, ni pale pale kinyerezi mwisho unaingia kushoto” alisema Veronica kwa sauti ya kubabaika kiasi cha kumfanya Deus ashangae kidogo, “sidhani kama una haja ya kuwa na wasi wasi, jione kuwa upo sehemu salama” alisema Deus, kwa sauti yeka tulivu, ambae akuondoa macho yake mbele hata kidgo, bado alikuwa anatazama magari yanayopita barabarani.

Kikapita kimya kifupi huku wakiendelea kutazama magari, sasa hapakuonekana magari yoyote ya polisi zaidi ya magari ya watu binafsi yaliyokuwa yanakatiza barabarani, kama siyo kwenda kibaha basi kwenda mjini, “sasa tunaweza kwenda” alisema Deus, huku anaingiza gia na kutembea taratibu kusogelea barabara kuu, huku macho yake yakitazama kwa umakini mkubwa kulia na kushoto, akifanya makadirio ya magari maana hakutakiwa kusimama hata kidogo pembeni ya barabara.

Mkadilio ulikaa sawa kushoto na kulia, magari yalikuwa umbali wa mita kama mia nne, japo magari ya upande wa kushoto yalionekana kuwa katika mwendo mkali, hata hivyo Deus akakanyaga mafuta kwa nguvu kuingia barabarani huku mwanga hafifu wa taa za BMW, ukisaidia kuvuka barabara salama, na kuingia uapnde wa pili wa barabara, wakiingia barabara ya zamani ambayo inaenda kutokea stendi ya Malamba mawili.

Naaam, ile gari lina vuka tu, nyuma yao wakasikia magari yakipita kwa kasi ya ajabu, wakati Veronica anageuza shingo kutazama nyuma, Deus alikuwa anatazama kupitia side mirror, kwa pamoja wakaweza kuyaona magari manne ya kijeshi yakikatiza kuelekea upande wa kibaha, “sasa hawa wanajeshi nao wanaenda wapi?” aliuliza Veronica akionyesha kustaajabishwa na kile alichokiona, “sina jibu la kweli, lakini kama inahusiana na wizi ulioufanya tutajua tu” alisema Deus huku anaendesha gari kuelekea upande wa mbezi kupitia barabara ya zamani, “mimi sio mwizi” alisema Veronica, akionyesha kutokupendezwa na kauli ya Dereva.

Deus hakuongea chochote zaidi ya kuongoza gari, nadhani Veronica alitafsiri kama ni dharau, “kaka ni vyema ukafuta kauli yako, mimi ni mtu mwenye heshima zangu, siwezi kuwa mwizi, nadhani unafahamu kilichotokea” aliongea Veronica akionyesha wazi amechukizwa na kitendo cha kuambiwa wizi alioufanya, “kwani kauli yangu itabadili ukweli?” aliuliza Deus kwa sauti tulivu, huku anakanyaga mafuta kuisogelea njia panda ya malamba mawili, “ukweli gani, kwamba nimefanya wizi?” aliuliza Veronica, ambae hakutaka kukumbuka gari lake aliloliacha kwenye bar iliyopo maeneo yale yale waliyokuwa wanakatiza, “ukweli wa kwamba tumeshiriki wizi, nadhani mpaka sasa ndivyo jamii inavyotambua” alisema Deus, ambae alikuwa anapunguza mwendo kuingia njia panda ya malamba mawili.

Ni kama Veronica alikuwa ameelewa maana ya maneno ya dereva wake, “ilikuwa ni mtego wa muda mrefu sana” alisema Veronica kwa sauti tulivu ya upole iliyojawa na huzuni huku anatazama jinsi wanavyoiacha barabara ya mbezi na kuingia malamba mawili, “aliniraghai kwa muda wa mwaka mzima, matokeo yake anakuja kuniteka nyara, sijui hatakuwa ametumwa na washindani wa baba kwenye biashara?” aliuliza Veronica, huku safari ikiendelea na sasa walisha ikamata barabara ya malamba mawili, ambayo wakati huo ilikuwa katika ujenzi, kikapita kimya kifupi kama vile Veronica alikuwa anaongea peke yake, hata hivyo ni kama Veronica alishaanza kuelewa Deus ni mtu wa aina gani, “lakini sijawai kusikia baba akizungumza kuwa na maadui katika Maisha yake” alisema Veronica, huku anaunda tabasamu usoni mwake, tabasamu ambalo alitamani sana kama dereva huyu mpole angeliona, Dereva ambae alionekana kuwa katika hali ya utulivu fulani kama kuna kitu anatafakari, “lakini siwezi kujua, maana binadamu wanapotaka lao wapo tayari kufanya lolote” alijisemesha Veronica, ambae ungesema alikuwa anaongea pake yake.

Ukweli ni kwamba, wakati huu kijana Deus ambae licha ya kuwa makini na barabara huku anaendesha gari kwa speed ya wastani, lakini pia kichwani mwake alikuwa anajaribu kufananisha safari yake kinyerezi usiku huu, huku kinyerezi, alikokuwa amemleta mzee James aliemchomoa mikononi mwa UMD, kama ina mahusiano na safari hii ya huyu mwanamke mrembo, “japo naamini tutaonana tena, lakini niseme tu asante kaka yangu kwa kuniokoa toka kwa wale washenzi” alisema Veronica akiwa katika hali ya tabasamu, huku anagaeuza uso wake kumtazama tena kijana Deus, ambae mpaka sasa hakuwa anamfahamu jina.

Lakini Veronica ambae alitegemea kusikia sauti ya kijana huyu, akashangaa kuona kama kijana yule hakuijali ile asante na baada yake kinapita kimya kifupi, Veronica akaingiwa na wasi wasi, maana ukimya wa kijana huyu ungesema anapanga kitu juu yake na ukweli ni kwamba hapakuwa na mtu ambae angeweza kumuokoa toka kwa kijana huyu.

Lakini wakati Veronica anawaza hayo, mara ikasikika sauti tulivu ya Dereva, “umesema unakaa kinyerezi mwisho?” aliuliza Deus, na hapo Veronica akatabasamu kidogo, “ndiyo, tena sio mbali na barabara” alijibu Veronica, “upande wa kushoto kama unatoka huku?” aliuliza tena Deus, kwa sauti ile ile tulivu ungesema kile alichokua anakiulizia kilikuwa ni kitu cha kawaida tu, “unaishi kwa wazazi wako?” aliuliza tena Deus, “ndiyo naishi kwetu, vipi naonekana mzee?” aliuliza Veronica huku anacheka kidogo, lakini haikuchekesha kwa Deus, ambae ndio kwanza akatupa swali jingine, “baba yako ni mfany…..” kabla hajamaliza kuuliza swali hilo, Veronica akadakia, “kumbe umenifahamu eeh, mimi ni mtoto wa James Kelvin” alisema Veronica akiachia tabasamu pana sana huku anamtazama Deus, na sasa Veronica akapata bahati ya kumuona Deus akiwa anaachia tabasamu fulani la kivivu, “mh! ndio kwanza kuna kucha, andaa akili na mwili, kwamba lolote linaweza kutokea kuanzia sasa” alisema Deus kwa sauti tulivu kama vile alikuwa anafanya jambo fulani la utani wakati huo walikuwa wanapandisha kilima cha shule ya msingi Kifulu.

Kauli hii ili mshtua sana Veronica, “kwanini unasema hivyo, kwani inamhusisha baba yangu hii?” aliuliza Veronica huku anamtazama Deus, ambae alikuwa amaliza kipando kile na kukaa sawa akiitazama shule ya Kifulu, na hapo Veronica ambae alikuwa anasubiria jibu, akashangaa gari linashikishwa brake za ghafla kuashiria kuwa mbele kulikuwa na kitu sio cha kawaida, nae akatazama mbele kule wanakoelekea, akaliona gari la polisi sambamba na polisi wengi wenye bunduki wakiwa barabarani.…. ENDELEA MDAU USISAHAU KUACHIA LIKE NA COMMENT KIDOGO YA KUMPA HAMASA MTUNZI.




NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA KUMI NA TATU
MTUNZI: Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA KUMI NA MBILI :- Kauli hii ilimshtua sana Veronica, “kwanini unasema hivyo, kwani inamhusisha baba yangu hii?” aliuliza Veronica, huku anamtazama Deus ambae alikuwa amaliza kipando kile na kukaa sawa akiitazama shule ya Kifulu, na hapo Veronica ambae alikuwa anasubiria jibu, akashangaa gari linashikishwa brake za ghafla, kuashiria kuwa mbele kulikuwa na kitu sio cha kawaida, nae akatazama mbele kule wanakoelekea, akaliona gari la polisi sambamba na polisi wengi wenye bunduki wakiwa barabarani.…... ENDELEA…

“vipi utawakimbia na hawa?” aliuliza Veronica, huku anawatazama polisi wale ambao kabla hata dereva hajatoa jibu la kinachofuata, doctor Veronica James kwa macho yake aliweza kuona polisi wale wakiinua bunduki zao kulielekezea gari lao.

Hapo hofu kubwa ya wazi inaoneka usoni kwa Veronica, “mamaaa!! Wanataka kutuuwa!!” alipiga kelele Veronica ambae sasa ndio alimini kuwa walikuwa na maadui wengi kuliko alivyofikiria, lakini wakati huo huo aliweza kumuona kijana huyu pembeni yake, ambae hakuonyesha dalili yoyote ya hofu akikanyaga clutch na kuweka gia ya uwani.

Naaaam kilicho tokea hapo weka kwanza kiporo, sasa twendeni kwanza nyumbani kwa bwana James, ambako ni kilomita kadhaa toka pale walipoliwepo wakina Veronica. ******

Pale nyumbani wanafamilia walikuwa bado wapo katika hali ya sitofahamu, bado hawakujua Veronica yupo katika hali gani huko aliko, huku wanashuhudia habari ya kutangazwa kwa msako mkubwa wa bwana James, anaetafutwa na serikali ya #mbogo_and, akitangazwa kama Adui wa taifa hilo la asili yao, hali ambayo inazidi kuwatia huzuni wanafamilia, “inamaana hawa watu hawajaamini bado kuwa mimi ni muathirika wa hili?’ aliuliza mzee James kwa sauti yenye kukata tamaa, “lakini baba Vero, kwanini usiwaambie ukweli watu wa #mbogo_land kuhusu mtu anae jiusisha na mpango wa mapinduzi kama ni huyo Chitopelah, we mtaje tu” alisema mama Veronica ambae alikuwa anafahamu fika kuwa aliempigia simu mume wake na kumueleza juu ya kikao kilicholeta utata ni mheshimiwa chitopelah, ambae ni Waziri wa ulinzi na usalama wa nchi ya #mbogo_land, akidai ni kao cha kibiashara, matokeo yake ni utekaji na uasi.

“hilo aliwezekani mke wangu, ujue ni rahisi sana kuongea na kusikilizwa, lakini kuaminiwa ndiyo kazi ilipo, hata hapa tulipo inasaidia ni sababu, wakina Kadumya wameonekana kwenye cctv, pale hotelini, na vipi kama aliepiga simu hakuwa chitopelah mwenyewe?” aliuliza mzee James, na hapo hata Caroline ambae alikuwa anaonekana kufurahi kwa kuiona picha ya kijana Deus kwenye simu ya baba yake alikubaliana na baba yake, “ni kweli mama, mambo mengine yanahitaji ushaidi wenye nguvu”.alisema mzee James, huku anajaribu kupitia maoni ya wasomaji, ambao kwa asilimia kubwa ni wateja na watumiaji wa bidhaa zake, wapo waliopingana na habari ile wakidai ni mbinu ya serikali ya #mbogo_land kumuangusha tajiri huyo ambae alihama nchi yao miaka mingi iliyopita, huku wengine wakidai ni mbinu chafu toka kwa matajiri wenzake ambao wanahitaji kumuangusha ili asiwape ushindani katika biashara.

Lakini pia walikuwepo ambao walionyesha wazi kuwa wanaamini kuwa James, anahusika moja kwa moja na ufadhiri wa genge hilo lenye mpango wa mapinduzi, huku wengine wakitoa maoni yao kwa kulaani jambo hilo, wakimlenga moja kwa moja tajiri James, wakidai kuwa tajiri James ameonyesha tamaa ya ajabu, amesahau kuwa kwa tamaa yake damu nyingi itamwagika, tena ya watu wasio na hatia, na kilichomuuma zaidi bwana James na familia yake ni kwamba, wahusika hawakutajwa hata kidogo, lawama zote zilienda kwake.

Naam wakati wanafamalia wanaendelea kusoma maoni na kutazama habari mitandaoni na kwenye television, mara simu ya bwana James ikaanza kuita na kwa kuwa ilikuwa mkononi akaitazama kwa haraka nakuona kuwa namba ya simu ilikuwa ngeni, hapo akaipokea haraka sana, akijua itakuwa inatokea kwa mkurugenzi wa TSA, ambae ametoka kumpigia muda mfupi uliopita, “ndiyo mkurugenzi kuna lolote?” aliuliza mzee James, huku familia yake ikimsikiliza kwa umakini huku wakimtazama usoni, “bwana James Kervin, pokea salaam toka kwa mfalme wako king Elvis Mbogo wa kwanza” ilikuwa ni sauti tulivu sana iliyosikika toka upande wa pili wa simu, hapo mzee James akatoa macho kwa mshangao kuwatazama mke wake na binti yake kama vile mzee huyu ameshikwa na butwaha, kiasi cha wanafamilia hawa kutamani kusikia alichokisikia mzee James, ambae walidhania anaongea na mkurugenzi wa wakala wasiri wa Tanzania jiji la dar es salaam.*******

Naaaam! Sasa turudi shule ya msingi kifulu, akiwa ametoka kuongea na mkuu wake wakazi, muda mfupi uliopita, koplo wa jeshi la polisi, kijana Cheleji, aliekuwa amesimama mita chache toka kwenye gari aina ya Toyota land cruzer, mali ya jeshi la polisi lililosimama katikati ya barabara, lililo zungukwa na polisi kadhaa, huku polisi wengine wakiwa wamekaa kwenye body la gari hilo, macho wameyaelekeza upande wa mbezi, wakitazama kwa umakini, wakitazama kila gari lililokuwa linatokea upande huo huku wakiwaza mwisho wa kazi hii utakuwa ni saa ngapi, na je ni kweli watafanikiwa au ndiyo itakuwa kama ilivyo kuwa safari ya Arusha wakati ule wa kufukuzia dhahabu.

Wakati wakiwa wanaendelea kuwaza na kuwazuwa, mara ghafla wanaliona BMW jeusi likiibuka kilimani mita kama sabini tu mbele yao na kupunguza mwendo kwa ghafla, “oyaaaa! Gari hilo hapo, shambuliaaaaa” alisema Cheleji kwa sauti ya juu huku anaweka sawa bunduki yake na kuikoki, wakati huo wanaliona lile gari likisimama ghafla na kuanza kurudi nyuma kwa speed kali sana kama vile lilikuwa linaenda mbele.

Polisi nao hawakuzubaha, wakaanza kumimina risasi kulilenga lile gari, huku wakitegemea kuwa muda wowote kama sio kwaajili ya risasi, basi kwaajili ya mwendo mkali wa kurudi nyuma uliokuwa unaendwa na lile gari, lazima gari lingeacha njia na kuingia mtaroni.

Lakini huwezi amini kilicho tokea, ni kama dereva wa BMW alikuwa anafahamu tabia ya bunduki hizi za SMG walizo kuwa wanatumia polisi, maana alikuwa anarudisha gari nyuma, huku amebana upande wa kushoto wa barabara, milindimo ya risasi ilipoanza tu, ghafla dereva akahamia upande wa kulia wa barabara na kuwafanya polisi wale wasitishe mapigo na kulenga upande ule wa barabara, na ile wanaanza kushambulia tu wakajikuta wanashambulia patupu,

Kwa faida watu wangu, tabia moja wapo ya SMG ni mtutu wake kusukumwa juu kwa nguvu ya mtoko wa risasi, tofauti na silaha kama semi automatic rifle, yani SAR ambayo ukimbilia upande wa kulia, hivyo kwa mpigaji wa SMG ni vigumu sana kulenga malengo yanayokimbia kuelekea pembeni, labda kama anapiga risasi moja moja au mpigaji awe na mafunzo mazuri ya utumiaji wa silaha hiyo.

Kwa maana hiyo sasa, polisi wale walijikuta wakipiga hewa mpaka walipoliona gari likizunguka kwa ghafla sana na uharaka wa ajabu na kutazama lilikotoka na kuchomoka mbio za ajabu kupotelea mteremkoni, “ingieni kwenye gari haraka” alipiga kelele Cheleji, huku na yeye anaongoza kukimbilia garini na bunduki yake mkononi, wenzake wanamfuata na kuingia garini, dereva anaondoa gari haraka kuelekea ule lilikoelekea BMW, wakati huo Cheleji anachukua redio call na kuminya kuruhusu msemo, “hallo vituo vyote, taarifa muhimu kwa wote, mnanipata over” aliongea Cheleji,l huku safari inaendelea na mbele yao waliweza kuona taa za gari zikipotea kwa mbali, “na ruadia tena, vituo vyote, taarifa muhimu, munanisikia jamani” alisema Cheleji, na hapo vituo vikaanza kujibu kama ilivyo kawaida, huku vituo vingi vikijibu kuwa vipo Kiluvya kwa komba, “taarifa kwenu, dereva wa farasi mweusi, ndie mtekaji watoto wa mzee James, narudia tena, dereva wa farasi mweusi ndie mtekaji wa binti wa mzee James, na sasa farasi mweusi anaelekea mbezi, elewa uelekeo ni mbezi” alisema Cheleji, ikiwa ni kutimiza maagizo ya mkuu wake bwana Ulenje, “tupo njiani tuna kuja over” hayo ni majibu toka kwenye vikundi vingine, gari lilikuwa speed, japo hawakuona tena dalili ya uwepo wa BMW s7 mbele yao.********

Mzee James kama ambae hajaamini alicho kisikia toka kwa mpigaji wa simu, akatoa simu sikioni na kutazama namba ya mpigajibambayo anashuhudia kuwa ni kweli kuwa ni namba ya kutoka #mbogo_land, na wakati huo huo kwa haraka sana Carloline akawahi simu ya baba yake na kubofya sehemu inayo ruhusu sauti ya wazi, “sa..sa.. salaam mtukufu mfalme, maisha marefu kwako mfalme Elvis wa kwanza” aliitikia mzee James na kuwafanya mke wake na bnti yake wazidi kushangaa, maana tayari walishajua kuwa, mzee huyu alikuwa anaongea na mfalme wa #mbogo_land “baraka zangu ziwe juu yako sana mzee James” alisikika king Elvis akiongea kwa sauti ya taratibu.

Ilishangaza sana, maana licha ya kusoma habari mitandaoni na kuona jinsi mzee James alivyo ongelewa kama mtu hatari mwana mapinduzi haramu, lakini bado inasikika sauti ya mfalme katika hali ya utulivu na amani kubwa, “asante sana mfalme Elvis wa kwanza, baada ya miaka mingi leo nifuraha kubwa sana kwangu kupokea simu yako mfalme wangu, sasa mtumishi wako nipo tayari kukusikiliza ewe mfalme wangu” alijibu James kwa sauti tulivu, yenye unyenyekevu mkubwa, “hakika ni fahari kwangu kusikia bado unaniita mfalme wako ewe mzalendo wan chi ya asili yako” alisikika mfalme Elis, akiongea kwa sauti tulivu lakini yenye furaha.

Naam baada ya kumaliza kusalimia, ndipo maongezi lengwa yalipoanza, “bwana James nmekupigia usikuu, kwa mambo tatu, moja ni kukupa pole na nakukuomba msamaha kwa kile ambacho baadhi ya watu waliiaminisha serikali kuhusu wewe, ukweli baada ya kugundua kilicho tokea nimehuzunika sana” alisema king Elvis, akionyesha kuwa ni kweli alikuwa anamaanisha anacho kisema, huku Carloline na mama yake wakisikiliza maongezi yale huku wakishangaa kama tayari mfalme alisha fahamu kuwa mzee James hakuwa UMD, sasa kwanini wamemtangaza kama adui wa taifa?,

Lakini walishindwa kuhoji, “naaam! mfalme wangu ni furaha kwangu kama mumegundua ukweli” aliitikia mzee James, “pili bwana James, nichukue nafasi hii kukutaka usiangalie kinachoendelea katika tovuti za serikali, wala watu binafsi juu ya kile kilichotangazwa juu yako, ukweli sisi hatuna ugomvi na wewe, ila kilicho baki ni wewe kukaribishwa tena nchini kwako ili kizazi chako kijekufaidi mema ya nchi ya #mbogo_land, kile unacho kisoma mitandaoni ni mtego kwa wanao amini mpango wao umefanikiwa, lakini iwe siri yako mpaka tutakapo fanikiwa kuwapata wahusika” alisema King Elvis, “naaam mfalme wangu, wewe umesema sina cha kupinga” alijibu mzee James.

Na hapo mfalme akaendelea, “na tatu na mwisho ni kwamba, kuanzia sasa utakuwa na ulinzi wa askari wa MLA, wapo njiani watasaidia na jeshi la Tanzania, wao ndio watakao kulinda mpaka unafika nyumbani pamoja na familia yako” alisema King Elvis, na hapo wanafamilia wanashindwa kujizuia, wanajikuta wakiachia tabasamu la furaha, “asante mfalme wangu, uwe na Maisha marefu” alisema mzee James akionyesha tabasamu pana la furaha, “bwana James sasa, ningependa kusikia kutoka kwako pia” alisema mfalme na kutulia, kumsikiliza bwana James, “mtukufu mfalme, ukweli sikuwahi kujihusisha na watu hawa hata mara moja, lakini jana usiku nilipigiwa simu na…..” alisema James na kusita kidogo, kisha akamtazama mke wake, “ni nani huyo alikupugia simu bwana James?” aliuliza king Elvis, kwa sauti, yenye shauku…..….Anamtaja au hamtaji basi ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
👍Umetisha sana mkuu, nmekuwa na robo saa Bora sana kusoma kipande hiki. 😂🤣😂🤣🤣😂🤣🤣🤣🤣😂😂😂😅
 
Ndio naisoma muda huu wa saa tisa kasoro robo usiku.
Baada ya kuamka usingizini nikaona notification kitu kisha tupiwa.
 
Deusi angempeleka Veronica chimbo kwanza kule kwenye Gheto lake la undergroud,, watulie hata siku mbili hivi kuwapoteza maadui,,
 
Back
Top Bottom