Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Yaan hii part ya doctor na mwanachuo ndio inanivutia zaidi kuliko part zote alafu deus amemshamjua vero ila vero bado hajagutuka.
 
Yaan hii part ya doctor na mwanachuo ndio inanivutia zaidi kuliko part zote alafu deus amemshamjua vero ila vero bado hajagutuka.
Amemjua kama ni binti wa Boss Kelvin ila hajamjua kama ndie pacha wanayechati naye kila siku,,
 
👍👍😂Kongole Sana kwa mtunzi wa hii kazi unajua sana.
Tukiachana na hayo, Leo jaribu kuijazia zaidi😂😂 ishu ya Sheria imeshavunjika mpaka sasa.


"unaishi kwa wazazi wako?” aliuliza tena Deus, “ndiyo naishi kwetu, vipi naonekana mzee?” aliuliza Veronica huku anacheka kidogo, lakini haikuchekesha kwa Deus, ambae ndio kwanza akatupa swali jingine, “baba yako ni mfany…..”

weka mzigo wa kutosha mtunga Sheria keshaharibu wewe ni nani mkuuu😅🤣😅🤣😅🤣😅
Shushan mzigo wa kutosha mpaka Deus ajishtukieee🥰🥰🥰🥰
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA KUMI NA NNE
MTUNZI: Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA KUMI NA TATU :- “asante mfalme wangu, uwena Maisha marefu” alisema mzee James akionyesha tabasamu pana la furaha, “bwana James sasa ningependa kusikia kutoka kwako pia” alisema mfalme na kutulia kumsikiliza bwana James, “mtukufu mfalme, ukweli sikuwahi kujihusisha na watu hao hata mara moja, lakini jana usiku nilipigiwa simu na…..” alisema James na kusita kidogo, kisha akamtazama mke wake, “ni nani huyo alikupugia simu bwana James?” aliuliza king Elvis, kwa sauti, yenye shauku…..…. ENDELEA…

Ilimshtua kidogo James, ambae bado alikuwa anamtazama mke wake kama vile anamuomba msaada wa jibu, nae akamonyesha ishara ya mdomo kwamba amuambie ukweli, na kabla hajatoa jibu lolote, akasikia sauti ya mfalme Elvis, “hallow bwana James, bado unasikia?” hapo mzee James akaigeukia simu yake haraka, “ndio nipo na kusikia” alijibu mzee James ambae kichwani mwake alikuwa anatafakari jambo juu ya jibu ambalo analihitaji mfalme, je ni kweli amueleze aliepiga simu, ili hali hakuwa na ushaidi kuwa Chitopela ndie muhusika mkuu wa kikundi cha UMD, au akae kimya mpaka itakapo bainika.

Lakini baada ya kuchakata akaona ni vyema kufanya linalofaa kwa wakati ule,“ndio bwana James, ulisema ulipokea simu kutoka kwa nani?” aliuliza mfalme akionyesha hamu kubwa ya kumfahamu muhusika wa kundi hilo, “ndiyo mtukufu mfalme, nilipokea simu kutoka kwa mtu ambae hakujitambulisha akisema anahitaji kuongea na mimi juu ya biashara, nilipoenda nikawakuta wakina Kadumya, nao wakaniambia wanataka niwafadhili kuingiza silaha nchini, nilipokataa. walitka kuniuwa, bahati nzuri akatokea kijana mmoja hivi ni mtoto wa askari wa zamani wa #mbogo_land, bwana Deus Nyati, sidhani kama ni kweli yupo UMD, ila nae alikimbia nchini kwa kusingiziwa kuwa ni UMD” alielezea bwana James na wakaongea mawili matatu na king Elvis kabla ya kukata simu, huku wakipeana ahadi ya kuwasiliana kila itakapoitajika.********

Yap! sasa uchunguzi mkali chini ya TSA, ulianza kufanyika, juu ya wazazi wa kijana Deus, lengo ni kutaka kujuwa Deus ni nani asa na ametokea wapi, sababu shuku kubwa ni kwamba, Deus alikuwa ni askari wa MLA, alie jiunga na jeshi la Tanzania, pengine ni kwakutaka habari za kiusalama za jeshi la ulinzi la Tanzania, au alikuwa na mpango wa kuhujumu jeshi na serikali ya Tanzania kwa ujumla, tayari taarifa zilisha tawanywa sehemu tatu muhimu, ikiwemO TRA, ambako ndio sehemu ambayo taarifa zinaweza kupatikana kirahisi, TSA songea, na pia taarifa zilienda #mbogo_lan kwamakachero wa Tanzania waishio nchini humo, katika imvuri cha watumishi wa barozi.

Lakini ukiachilia ilo, TSA wengi sasa walikuwa mitaani wakiendelea msako wa siri, kama raia wengine, walikuwepo walio jifanya boda boda, walikuwepo waliojifanya maderva wa taxi, na wapo wengine, waliojifanya raia wa kawaida mitaani, mida hii mkurugenzi wa TSA kanda ya dar es salaam, bwana Elisha Eric, alikuwa ofisini, ana anasubiria taarifa toka sehemu mbali mbali, alizoweka mitego yake, mala akapokea toka kwa mmoja wa mawakara wake, aliekuwa mtaani anaendelea na ukusanyaji wa habari, “mkuruenzi, taarifa mpya zilizo naswa kwenye redio ya polisi, katika frequance 3, ni kwamba, dereva wa BMW jeusi, yani Deus Nyati, yupo na Veronica James, wameonekana mitaa ya Kufulu, barabara ya malamba mawili, kuelekea Kinyerezi, na wamefanikiwa kuwakimbia polisi” taarifa hii ilimshtua sana bwana Elisha, pamoja nawana usalama wenzake, aliokuwanao pale ofisini.

“unauhakika kuwa, ulichokisikia ndio hicho unacho tueleza sisi?” aliuliza Elisha Eric, kwa sauti yenye mashaka, yani kuto kuamini kile alicho kisikia, toka kwa wakara wake, “ndiyo mkuu, hivyo ndivyo polisi walivyo peana taarifa, na hivi tunavyoongea lazima watakuwa Morogoro road, maeneo ya kuanzia mbezi mpaka kiluvya madukani” alisema yule wakara, akionyesha kuwa na uhakika na kile alichokisema, “sawa nimekupata, lakini mudawote, jitaidini muwe karibu na naeneo ambalo Deus anaonekana” alisema mkurugenzi na kukata simu.

Elisha Eric anaachia tabasamu, “jamani, ni mambo juu ya mambo, kazi inazidi kupamba moto” alisema Lisha akiwatazama wenzake kwa awamu, wemzale wanatega masikio kwa hamu ya kusikiliza taarifa mpya, “dakika chache baada ya Veronica kuonekana akishiriki wizi, tunapata taarifa kuwa alitekwa na UMD, lakini sasa inakuja taarifa kuwa yupo mikononi mwa Deus Frank Nyati, je yupo salama au nako ameteka?” aliuliza Elisha, na wenzake wakacheka kidogo, “kwa hiyo alimwokoa baba kisha akaenda kumteka mtoto?” aliuliza wakara mwingine, kwa sauti yenye mashaka, “hiyo aiwezekani, maana ni lazima ange mchukuwa moja kwa moja bwana James” alijibu mwingine, “sasa huyu Deus ni nani, na kwa nini anafanya hayo yote, au mzee James amemkodi kwenda kumchukuwa binti yake, maana kama alionekana kinyelezi, hiyo ilikuwa ni safari ya kurudi nyumbani” alisema bwan Elisha, wote wakatazamana.

Ni wazi kuna jmbo walilishuku, "kwahiyo mkuu, kama bwana James amemtuma huyu dereva akamwokoe binti yake, inamanisha kuwa, bwana james yupo katika mtandao wa watu, wanao tumia Deus Nyati, kama dereva kodi" alisema mmoja wa wanausalama waliokuwa na mle ndani na bwana Elisha, "kwahiyo unataka kusema kuwa, James anamfahamu Deus, muda mrefu uliopita?" aliuliza mkurugenzi Deus, huku anamtazama yule wakara, kabla ajajibu, hapo hapo wakara mwingine akadakia, "sizani kama inaweza kuwa hivyo, ila nahisi ni kwamba, Deus ni wakara wa serikali ya #mbogo_land. ambae baada ya kumwokoa bwana James, akapewa jukumu la kumwokoa Veronica" alisema wakara, wingine akipingana na yule wakwanza, "kwahiyo bado tunarudi kule kule, kwamba private Deus ni MLSA, na aliingia Jeshi la ulinzi kama mpelelezi wa siri" alisema mkurugenzi Elisha, na wengine wakaunga mkono, "basi tusubiri taarifa toka Songea kwa Haule (james bond, soma kiapo cha damu) na huko #mbogo_land, wao ndio wata tuonyesha mbivu na mbichi" alisema mkurugenzi Elisha, ambae akuonyeshaa dalili ya kwamba ata watawanyisha wajumbe wake, kwenda kupumzika.*******

Naam!! wakati kikundi maalumu cha jeshi la wananchi cha spcial marine force, kikiwa kina weka kituo kidogo maeneo ya kiluvya gogoni, wakati huo huo huku bwana Songoro na kikundi chake wakiwa wamesimama Kiluvya kwa komba hawajui waelekee wapi, maana tayari walishaachwa kama solemba, wakati huo huo magari takribani kumi na tano ya jeshi la polisi yanaonekana yakiwa katika speed ya ajabu yanakatiza mtaa ya Luguruni kuelekea mbezi, huku yakilindimisha ving'ora na bocon za rangi nyekundu na blue juu ya vichwa vya magari yao, huku askari wakionekana nyuma ya magari hayo wakining'inia na silaha zao, hizi zote ni mbio kuliwahi BMW jeus, kama wao walivyo liita farasi.

Lakini mpaka wanafika njia panda ya malamba mawili na wanakutana ambapo walikutana na magari mengine manne ya polisi, tatu yakitokea upande wa mjini na jingine ni lile la wakina Cheleji, lakini hawakuwa wameliona BMW jeus, wala dalili ya gari hilo, hakika ilishangaza sana, “atakuwa amepitia wapi huyu mshenzi, tena amemteka mtoto wa mzee James” alisema koplo Cheleji, huku wengine wakimsikiliza, tena kati yao walikuwepo waliomzidi cheo, wakiwepo ma sajent na major, ma inspector ma super lutenat, hakuna alieamini kilichotokea, maana licha ya speed kali na uharaka walio utumia kuwahi pale mbezi, lakini bado wanalikosa gari lile, cha kushangaza zaidi ni kwamba, ukiachilia magari yaliyotokea kibaha na huku kinyerezi, pia kulikuwa na magari yaliyotokea mjini, kwa maana kama BMW lilielekea upande huo wangekutana nalo, “hakuna haja ya kuzubaa hapa, tunaingia mitaani kulisaka hilo gari, lazima litakuwa halijafika huku” alisema polisi mmoja mwenye cheo cha lutendant, na hapo polisi wakaingia kwenye magari na kuanza kuondoka kuelekea maeneo mbali mbali ya pale mbezi wakipishana na magari mawili aina ya land rover puma yaliyokuwa yanaelekea upande wa kibaha.******

Naam, sasa basi wakati vyombo vya ulinzi na usalama vikiwa mitaani vina msaka kijana Deus Nyati vikisahau kuhusu UMD, kitu ambacho wao hawakukijua ni kwamba tayari BMW S7, lilikuwa limesha kamata barabara ya vumbi ya kisarawe kupitia kisopwa mkoani pwani na kwenda kutokea kwenye reli ya kati, kisha taratibu likaanza kuambaa ambaa na njia hiyo hafifu yenye mawe mengi, na sasa mwendo wa BMW ulikuwa mdogo mdogo, giza lilikuwa nene na la kutisha, misitu minene na vichaka vikubwa, hapakuwa na dalili za makazi ya watu wala dalili ya mwanga wa taa au karabai maeneo ya karibu na pale, zaidi ya taa zilizo onekana mbali sana za mji wa kibaha na dar es salaam, pengine ni mwanga wa taa za gari hili aina ya BMW s7 ambalo sasa, lilikuwa linaangazia mwanga hafifu, uliowekwa makusudi kuepuka kuonekana mbali, yani ngao mbele ya adui zake.

Safari ilikuwa kimya kimya watu wawili yani Deus Nyati na mschana Veronica, kila mmoja akiwaza la kwake kichwani, wakati mwadada Veronica alikuwa anawaza juu ya usalama wake, hasa ukichukulia kwamba alishaona kuwa mambo yamekuwa mazito upande wake, maana hata baadhi ya askari wa jeshi la polisi ni maadui zake, na vipi kuhusu huyu kijana dereva mwenye uso wa upole, ambae kuuwa ni kazi ndogo sana kwake, huku anampeleka wapi na itakuwaje kama akienda kumfanyia vitendo visivyo faa, ukichukulia yeye ni mzuri na anatamanisha.

Lakini hata hivyo kijana huyu ambae hakuonyesha kuwa na nia ovu juu yake ndio msaada wa pekee kwake, maana hata kama akiomba ashushwe na yule dereva angekubari, unadhani yeye angefika wapi na ule msitu, hata kama kusingekuwa na hatari ya watu au wanyama lakini kwa uoga angejikuta anazimia, hivyo kilicho bakia ni kutengeneza urafiki na kijana huyu ili usalama wake uendelee kuwepo.
Deus yeye alikuwa anawaza juu ya muunganiko wa matukio yanayoendelea, matukio yanayohusiana na UMD, kundi ambalo ukiachilia kumteka mzee James na binti yake ni kundi ambalo pia, lilihusika kumsababishia baba yake matatizo makubwa huko #mbogo_land mwaka 1992, “naitwa doctor Veronica, nipo hospita ya mkoa wa pwani” alijitambulisha Veronica huku anaachia tabasamu, ambalo hata yeye alitamani dereva aone hilo tabasamu ambalo mara zote huamsha matamanio ya wanaume, “umevunja sheria namba moja” alisema Dereva kwa sauti tulivu ya upole, ambae hakuonyesha dalili ya kumtazama Veronica...Naam Usiache Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unaokujia hapahapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA KUMI NA TANO
MTUNZI: Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA KUMI NA NNE :- Deus yeye alikuwa anawaza juu ya muunganiko wa matukio yanayoendelea, matukio yanayohusiana na UMD, kundi ambalo ukiachilia kumteka mzee James na binti yake ni kundi ambalo pia lilihusika kumsababishia baba yake matatizo makubwa huko #mbogo_land mwaka 1992, “naitwa doctor Veronica, nipo hospita ya mkoa wa pwani” alijitambulisha Veronica huku anaachia tabasamu ambalo hata yeye alitamani dereva aone hilo tabasamu ambalo mara zote huamsha matamanio ya wanaume, “umevunja sheria namba moja” alisema Dereva, kwa sauti tulivu ya upole, ambae hakuonyesha dalili ya kumtazama Veronica. ..…. ENDELEA…

Hapo Veronica akashtuka kidogo, maana hakutarajia jibu la dereva kuhusu sheria ya hakuna kujuana majina, ambayo alimsikia akimueleza JJ kule makabe, “samahani nilisha sahau” alisema Veronica kwa sauti fulani kama vile hakujali kitu, japo moyoni mwake alikuwa ana uoga fulani huku anaweka sawa simu yake na kuibofya, huku ametega sikio kwa Dereva kusikiliza kama atasema lolote juu ya msamaha aliouomba, lakini ikawa kimya, nae akahisi kuwa pengine Dereva hakuridhika kwa uombaji ule, “lakini mimi nilidhania tumesha kuwa marafiki na tunapaswa kufahamiana” alisema Veronica huku akijaribu kujitabasamulisha, “unawezaje kumuamini mtu kwa haraka hivyo,? wakati mwanaume ambae umekaa nae mwaka mzima amekugeuka ndani ya siku moja tu” alisema dereva huku amekaza macho yake mbele.

Ukweli hapo Veronika akaona ukweli ndani ya maneno ya Dereva, lakini haikuwa kama anavyoongea dereva, maana licha ya wao kukutana muda mfupi uliopta lakini tayari dereva alishaonyesha msaada mkubwa kwake, “lakini nitofauti na wewe” alijibu Veronica huku anaanza kupekuwa simu yake kwenye namba zilizo pigwa, “dada ni vyema ukakaa kimya na kujizuia kuvunja sheria zangu” alisema Deus kwa sauti ya taratibu, huku macho yake ameyaelekeza mbele na sasa alikuwa anaiacha reli na kuingia barabara ya kuelekea kisarawe.

Hapo Veronica akaona hapakuwa na urafiki mahali hapa, hivyo akabofya namba ya baba yake na kupiga ile namba, lakini ile anaiweka sikioni tu akamsikia Dereva akiongea kwa sauti tulivu, “dada kuwa makini na simu, usimueleze baba yako tuko wapi au tunaenda wapi na usimueleze upo na nani, hii ni hatari kwetu, maana kitu unachotakiwa kujua hata baba yako hajuwi maadui zake ni wakina nani” alisema Deus, na kumshangaza Veronica, ambae alimtazama Deus kwa mshangao huku anajiuliza, “amejuaje kama naongea na baba” alijiulizaVeronica huku simu ikiwa sikioni inaendelea kuita. ******

Naaam akiwa anaanza kuona kuwa mambo yanaanza kumuendea kombo bwana Chitopela alikuwa nyumbani kwake mbele ya compute mpakato, yaani Lap top, akikagua maandishi fulani yalivyo andikwa kwa mtindo wa Makala, yakiwa na kichwa cha habari, WANANCHI MBOGOLAND KUANDAMANA, KUKUMBUKA MAUWAJI YA WATU WASIO NA HATIA YA MWAKA 1992.

Maandishi hayo yaliyoandikwa kwa mtindo wa Makala yalisema kuwa, wananchi wa nchi ya #mbogo_land, wamepanga kwa siri kufanya maandamano siku yoyote watakayo itangaza siku za karibuni, kwa kile kinacho daiwa kukumbuka mauwaji ya askari wanausalama wa serikali, yaliyofanyika mwaka 1992, ikidaiwa ni mauwaji ya uonevu yaliyofanywa na mfalme wa kipindi hicho King Eugen wa 25, yaliyo kuwa ni mauwaji ya kionevu na yaliyokiuka haki za kibinadamu.

Naam! Chitopelah, aliekuwa anasoma makala hiyo huku anakunywa pombe yake iliyopo katika chupa kubwa, akajikuta anatabsamu kidogo huku anafungua kurasa nyingine, nayo ilikuwa na habari nyingine yenye kichwa cha habari, WANACHI WAHOFIA KUANZA KWA MAUWAJI MENGINE NCHINI MBOGO LAND, nayo ilikuwa na maelezo yafuatayo,

Kufuatia kwa taarifa ya kusakwa kwa Tajiri mkubwa afrika mwenye asili ya mbogo land, ambae anaishi uhamishoni nchini Tanzania baada ya kukimbia mauwaji ya uonevu mwaka 1992, wananchi wameshikwa na hofu kubwa ya kuanza kwa mauwaji kama yale yaliyotokea nchi humo mwaka 1992 kwa mujibu wa baadhi ya wanachi, sasa wanaangalia uwezekano wa kukimbia nchi na kutafuta nchi salama kwaajili yao na familia zao, hata hivyo baadhi wamemuomba mfalme Elvis, kutafuta njia nyingine ya kutafuta amani na waasi wa UMD kuliko kutumia nguvu ambazo zitasababisha mauwaji kwa wananchi wasio na hatia kama ilivyotokea mwaka 1992.

Chitopelah, akishia hapo, akafungua kurasa ya tatu ambayo pia kama zingine, ilikuwa na Makala, yenye kichwa cha habari WANANCHI WAUKATAA UONGOZI WA KIFALME #MBOGO_LAND, Makala hii bwana chitopela aliisoma huku anatabasamu kwa jinsi ilivyo andikwa kiufundi, “kile kinachoonekana kama ni uungaji mkono wa kundi la kiharakati la UMD, wananchi huko #mbogo_land, wameanza kuonyesha dalili za kuipinga serikali ya kifalme na kuanza kudai serikali ya kisiasa, hasa kutokana na vikao vya siri vya wanaharakati wanchi hiyo na upangwaji wa maandamano ya kupinga uongozi wa kifalme, huku wengine wapanga kuuomba umoja wa mataifa kuingilia kati swala hilo, “hapo lazima wasahau kama kuna UMD nakuanza kuwatafuta raia wanaotaka kuandamana” alijisemea Chitopelah huku anacheka kwa dharau na mafanikio, wakati huo huo anachukua simu yake na kumpigia bwana Chiropo, shushushu wake aliepo ubalozi mdogo huko songea Tanzania, “lazima nifanye jambo ili kuwaongezea kazi hawa wajinga na kuwanyima uwezo wa kufikiri” alijisemea Chitopelah huku akisikilizia simu iliyokuwa inaendelea kuita.

Simu iliita bila kupokelewa mpaka ilipokatika yenyewe, lakini hakuchoka alipiga tena kuisikilizia, safari hii haikuita sana ikapokelewa, “naam muheshimiwa, vipi kuna jambo jipya? maana mimi toka nimewaacha hotelini sijawafuatilia tena” alisikika Chiropo ambae sauti yake ilionyesha wazi kuwa alikuwa ametokea kwenye usingizi, “achana na hao wapuuzi, sasa hivi wapo njiani wanaelekea dar es salaam kuna kazi nataka uifanye usiku huu nitakutumia kwenye emaill yako ipost kwenye ile page yetu ya uvumi” alisema Chitopelah huku anabofya computer yake kwaajili ya kutuma zile kurasa zenye Makala kwa bwana Chiropo, “hakuna shida mkuu, wacha niwashe computer” alisema Chiropo.******

Naam!!! tukirudi jijini Dar es salaam, jiji bado lilikuwa linapilika za kutosha, wakina Kadumya na Kafulu walikuwa kwenye msafara wao mdogo, wanaelekea upande wa kibaha kwa lengo la kutafuta msitu wa kwenda kuwa subiri wenzao, wanaotokea mbogo land kupitia kusini, huku kwenye gari wakiwa na miili ya wale wenzao, waliouliwa na kijana Deus Nyati, miili ambayo wanategemea waje kusaidiwa kuifukia, maana wao peke yao wangeshindwa.
Msafara huo wa magari mawili unaenda mpaka kibamba CCM na kuingia upande wa kushoto, ambako wanaingia kwenye barabara iliyokuwa inachongwa, kwa maana ilikuwa kwenye matengenezo, nao wanaifwata barabara hiyo kuelekea misitu ya kisopwa, huku kila mmoja kichwani mwake akimfikiria kijana Deus Nyati kwa kile alichowafanyia kijana huyo, kila mmoja kwa wakati wake, wakati msafara huo unaendelea kutimia vumbi pia angani tuna weza kuiona ndege ndogo ya kukodi, iliyokuwa inatokea nyanda za juu kusini, sasa ilikuwa inatafuta uelekeo wa kisarawe gogo la mboto ili iweke miguu yake kwenye njia za kurukia za uwanja wa ndege wa walimu Nyerere.

Ukiachilia UMD, sasa twendeni nyumbani kwa bwana James kule kinyerezi, sasa maongezi yalikuwa yamebadilika baina ya wanafamilia hawa, walikuwa wanasimuliana umahili wa kijana Deus Nyati, mzee James akisimulia jinsi kijana alivyo pigana kwa namna ya kipekee kule SisterFada, lakini pia binti yake Carloline, alikuwa anasimulia hadithi ambayo hajawahi kuisahau, licha ya miaka saba kupita ni kipindi anakutana nae makambako na kupanda nae tren, huku akimlea kama mdogo wake na kisha kumuokoa yeye na wafanyakazi wengine wa tren, lakini pia hawakuacha kuzungumzia kuhusu simu ambayo ilikuwa imepigwa na king Elvis, “kwahiyo mume wangu, akipatikana Veronica tunaondoka hapa Tanzania?” aliuliza mama Carlo, “yes, ni muhimu kutii amri ya mfalme, maana kila kitu kinaenda kuisha” alisema mzee James na kuongeza kuwa, “lakini hatuwezi kukiacha kile ambacho tumekianzisha hapa Tanzania miaka mingi iliyo pita, hivyo tunaishi Tanzania na #mbogo_land” alisema mzee James.

Wakati wanaendelea kuongea hili na lile, mara simu ya mzee James inaita, wote wakatazama jina la mpigaji kwa macho ya shauku, hawakuweza kuona jina la mpigaji zaidi ya kuona namba ngeni, “mkurugenzi TSA” alisema mzee James, huku anachukua simu yake na kuipokea, “naaam mkurugenzi” alisema Mzee James huku anaweka simu katika sauti ya wazi, “kuna maswali machache tunahitaji kukuuliza bwana James, ni kuhusu Deus Nyati” alisikika mkurugenzi TSA, bwana Elisha Eric, “naam nakusikiliza mkurugenzi” alisema bwana James, na hapo maswali yakaanza, “ulisema bwana Deus, hukuwahi kumfahamau kabla ya leo ni kweli bwana James?” aliuliza mkurugenzi kwa sauti tulivu yenye umakini mkubwa, “ndiyo hakika ni leo ndio kwanza nakutana na kijana huyo, lakini kuna taarifa mpya pia toka kwa binti yangu” alisema mzee James, “ipi hiyo bwana James?” aliuliza mkurugenzi kwa sauti iliyojaa shauku.

Hapo bwana James akaanza kueleza hadithi ya binti yake ya kuokolewa na kijana huyo huyo, miaka mingi iliyopita, “hooo! Nakumbuka hilo tukio, kumbe alikuwa ni kijana Deus” alisikika mkurugenzi, ambae pia aliongeza swali, “sasa bwana James, sisi tuna taka kujua kama kuna mkataba wowote umeingia na Deus Nyati au kama mnadaiana kitu au kama munaugomvi wowote na kijana huyo” alisema Elisha..…. ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao Kujia hapa hapa jamii forums
 
🚶🏃🏃🏃🤸🤸🤸🏂🏂🪂🪂🪂🏄🧟🚣🚣🚣🚣🦸🦸. Mala paaaàp, nmefika.

Mda ndio unakaribia Dj weka vituúu😂🥰😂😂😂😂😂😂🤣🤣😂😂🤣😭
 
😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭🤣🤣😂😂😂😂😂😅😅😅😅patupu!!!!
 
huyu mtunzi nae sijui vp jana usiku hajapost kama ilivyo ada yake na mpaka sahizi hajaonekana humu..bila shaka anafurahia valentine day kuna mahali kafungiwa huyu tusubiri aachiliwe huko..mkuu fanya vipande sita leo kama zawadi kwa fans wako humu.. tufurahi pamoja nawe maana si kwa kufungiwa huko.
 
Kwani Leo Kuna tukio Gani? 🤣😂🤣😂😂😂😂🤣😂🤣😂🤣😂😂 Naona mtaani kwetu vijana wameadimika🤣😂😂😂🤣😂🤣🤣
 
nitarudi siku story itapoisha utaratibu wakutuma story ubadilike mara nyingi wasomaji tunapenda kujipa furaha kusoma kwa urefu mpaka tunapoweka nukta ya kula na kunywa c mwandishi kutuma story robo robo .....
 
huyu mtunzi nae sijui vp jana usiku hajapost kama ilivyo ada yake na mpaka sahizi hajaonekana humu..bila shaka anafurahia valentine day kuna mahali kafungiwa huyu tusubiri aachiliwe huko..mkuu fanya vipande sita leo kama zawadi kwa fans wako humu.. tufurahi pamoja nawe maana si kwa kufungiwa huko.
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA KUMI NA SITA
MTUNZI: Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA KUMI NA TANO:- Hapo bwana James akaanza kueleza hadithi ya binti yake ya kuokolewa na kijana huyo huyo miaka mingi iliyopita, “hooo! Nakumbuka hilo ilo tukio kumbe alikuwa ni kijana Deus” alisikika mkurugenzi ambae pia aliongeza swali, “sasa bwana James sisi tunataka kujua kama kuna mkataba wowote umeingia na Deus Nyati, au kama mnadaiana kitu au kama munaugomvi wowote na kijana huyo” alisema Elisha..…. ENDELEA…

Lakini bwana James akakataa kata kata, kuwa toka alivyoachana na kijana huyo hakuwasiliana nae tena, “lakini alipoondoka hapa alikuwa kama amechukia kwasababu tulishindwa kufikia mwisho mzuri juu ya malipo, yeye alikuwa anahitaji cash mkononi na mimi sitembei na fedha nyingi” alifafanua James, “unadhani hiyo inaweza kuwa sababu ya Deus kumteka binti yako?” aliuliza mkurugenzi swali ambalo hata halikumshtua James wala familia yake, yani mke wake na binti yake, “hapana mkurugenzi, Veronica hajatekwa na Deus, Veronica ametekwa na UMD ambao walinipigia simu, na ninacho kijua mimi Deus ndie alieniokoa toka kwa UMD” alisema mzee James akionyesha kuwa na uhakika wa kile anacho kisema.

Hapo kikapita kimya kifupi, ni kama James alikuwa anatafakari majibu ya James, “hallow mkurugenzi, kwani kuna lolote limetokea kati ya binti yangu na huyo Deus?” aliuliza mzee James, “ndiyo bwana James, taarifa za mwisho, zinasema kuwa binti yenu ameshikiliwa na Deus, mwanzo walionekana mbezi na sasa wameonekana kifulu barabara ya kinyerezi malamba mawili” alisikika mkurugenzi na kuwafanya wanafamilia hawa watazamane kwa mshangao, “sidhani kama ni kweli, maana kwa kile Deus alichowafanyia wakina Kadumya sifikirii kama wanaweza kuwa pamoja, lazima mutakuwa mumekosea, isitoshe Veronica alinipigia simu na akaongea vizuri tu akionyesha kuwa yupo salama” alisema James, akionekana kuanza kuchanganyikiwa kwa hofu na wasi wasi tofauti na familia yake, yani mke wake na binti yake, “ok! wacha tuendelee kuchunguza, kisha tutakujulisha, ila kama ukipata habari yoyote na sisi tujulishe, alisema mkurugenzi na kukata simu.

Hapo kama aliechanganyikiwa, mzee James akaingiza mkono mfukoni na kuibuka na kadi yenye namba za simu na sheria upande wa nyuma, “lazima nimpigie, nitamlipa fedha anayotaka amlete Veronica, najua anaweza” alisema James huku anaanza kuandika namba ya simu toka kwenye ile card yenye jina la kampuni msafirishaji, huku Carloline nae akikodoa kutazama zile namba ambazo mpaka dakika hii, hakujua ni namba za nini, “baba hizo namba ni za nini?” aliuliza Carlo, huku anazikodolea macho namba zile kwenye kadi ya biashara, “namba za Deus Nyati” alisema mzee James, huku anaandika namba moja baada nyingine, lakini baba Vero unadhani yule kijana amemteka Vero kweli?” aliuza mama Vero, lakini mume wake hakujibu zaidi ya kuendelea kuandika namba ile.

Naam, kusikia kuwa namba ni za Deus Nyati, nae akatoa simu yake haraka sana, lakini kabla hajaandika namba hata moja simu ya baba yake ikaanza kuita na jina la pigaji likaonekana kuwa ni Veronica, hapo mioyo ya wote watatu ukalipuka kwa mmshtuko na shauku ya kumsikia Veronica, mzee James, huku anarudisha ile card mfukoni, akapokea simu na kuweka sauti ya wazi, lakini wa kwanza kuongea alikuwa ni mama yake. ********

Yap! kusini mashariki mwa TT City, pembeni kabisa ya jiji ili dogo kwa mita za mraba, ndani ya msitu wa mkubwa Karanga njete kituo cha 17, linaonekana gari moja aina ya land rover puma, gari ambazo toka kuanza kutengenezwa kwake kwa toleo la kwanza la Land rover 109 yamekuwa magari tegemeo katika shughuri za kijeshi, hasa kwenye matumizi magumu ya porini na vitani, likichanja mbuga kuelekea kusini zaidi, ambako sasa walibakiza mita chache sana kufika LSB yani Lion Skull Base, (kambi ya fuvu la simba) ambayo ni kambi ya kijeshi inayo kaliwa na kikosi cha wachunguzi wa kivita, ni kambi lenye muundo wa kipekee sana, kambi ambalo kimuonekano ni ndogo lakini lilikuwa na nguvu kubwa ya askari wenye mafunzo mazuri na mbinu kubwa za kivita, pia lilikuwa na silaha nzuri na za kisasa.
Lina onekana gari aina ya land puma likisimama kwenye lango kuu la kuingilia kwenye kambi hilo lenye ulinzi mkubwa kupita kiasi, kuanzia askari watembea ardhini, waliokuwa wanazunguka kambi kwa kupishana, pia walikuwepo askari waliosimama kwenye vituo muhimu, ambayo ni maeneo shawishi kwa adui, kama vile ghara la kuifadhia silaha, store ya vifaa vya utawala na majengo ya utawala, kama vile ofisi hospital na majengo ya mawasiliano.

Pia kulikuwa na askari waliosimama kwenye minara mirefu wakiwa na silaha nzito kuanzia kimo cha kati, MMG kwamaana ya Midium Machine Gun, kama vile xuacial LMG, na nyingine za hivyo, pia kulikuwa na camera kuzunguka kambi ili lenye uzio mkubwa wa kuta, na mifuko ya michanga sand bags, huku kila baada ya hatua kumi kulikuwa na sehemu ya kupigania, yani fighting post.

Askari mkakamavu, alieshikiria bunduki aina ya Uzi Gun ya mwaka 2009, ana litazama gari lile, lililokuwa lina mulikwa na mwanga mkali wa taa, “zima taa za nje kisha washa taa za ndani” anasema yule askari, wakati huo askari wenzake wawili wakiwa wamesimama mita chache toka alipo simama yeye, bunduki zao mkononi, ni kama walikuwa wanasubiria amri ya kushambulia.

Bahati nzuri dereva anazima taa za nje, na kuwasha taa za ndani kama alivyo elekezwa, na kwa msaada wa taa za ndani za gari lile, yule askari mlinzi anaweza kuona watu watatu waliovalia sale kama za kwao, yani vazi la kijeshi la kivita, kwa maana ya combart dress, “abiria washuke abakie dereva” aliamrisha yule mlinzi na hapo milango miwili ya gari ikafunguka, yani wa abiria wa mbele na mmoja wa nyuma, yote ya kushoto ikifuatiwa na watu wawili kushuka toka kwenye gari, “sogea mbele pita kwenye geti dogo” alisema yule askari huku askari mwingine akifungua mlango mdogo ulioambatanishwa na lango kuu, nao wakatembea kuingia ndani kama walivyo elekezwa, “ingiza gari ndani kwa ukaguzi” alisema askari na huku askari mwingine anafungua lango kubwa na kufanya dereva aweze kungiza gari ndani.

Naam baada ya kusogea na kuwatambua wale askari walioshuka toka kwenye gari, askari mmoja akapiga saluti na kusalimia kijeshi, kisha wale wageni wakaingia kwenye gari na kuelekea ndani zaidi ya kambi usawa wa ofisi kuu za kambi wakiawaacha wale walinzi wanaendelea kuimarisha ulinzi pasipo dalili ya kulala wala kusinzia.

Huyu alikuwa ni Major General Sixmund, mkuu wa kitengo cha uchunguzi wa kivita MLA, ambae alifika kwenye ofisi kuu za Lion Skull Base, ambapo alipokelewa na afisa mwenye cheo cha kanal, ambae kwa hakika ndie mkuu wakambi aliekuwa amesimama nje ya ofisi hizo na maafisa kadhaa wenye vyeo mbali mbali, kuanzia luteni mpaka luten kanal,pia kulikuwa na ma captain na ma major, “karibu afande hawa mbele yako ni maafisa wa kikosi cha LSB” alisema yule kanal, huku anapiga salut na wenzake wakiwa wametulia kwa kubana mikono kwenye mapaja, usawa wa pindo za suruali zao, “asante CO, hatuna muda wa kupoteza, tuanze kikao” alisema bwana Sixmund pasipo kusubiri kuingia ndani, “afande naomba nikupe taarifa mpya za kichunguzi” alisema yule kanal huku wakiwa wamesimama pale pale nje.

Na hapo akaanza kutoa taarifa mpya, “afande taarifa kutoka kwa askari wetu wa uchunguzi wa kutoka angani, wamebaini uwepo wakambi ya waasi wa UMD kaskazini mwa nchi yetu, ni kilomita arobaini toka upande watanzania, mwanzo tulihisi ni kundi la waharifu wa kitanzania, lakini baadae tukabaini mienendo ya kuingia na kutoka Tanzania ya watu toka katika kambi hilo ambalo ukiachilia kujihusisha na uharifu katika vijiji vya Tanzania, na #mbogo_land walivyo karibiana navyo kama vile ubakaji na uporaji, pia wamekuwa wakiendesha mafunzo ya jeshi kunyume na utaratibu” alisema yule kanal, huku akimalizia kwa kutoa simu yake kubwa ya kisasa na kumuonyesha baadhi ya picha na video.

Baada ya kutazama kwa dakika chache, Sixmund akaachia tabasamu la ushindi, “namuona major Kwanguru kwenye hii picha ya mafunzo, kumbe nae alienda huko” alisema Sixmund huku anaonyesha moja ya picha iliyo onyesha vijana kadhaa waliovalia mavazi chakavu ya kijeshi, “wapo wengi, pia kuna huyu koplo nae alitoroka jeshi miaka mitatu iliyopita” alisema CO, huku anaonyesha picha nyingine inayomuonyesha akasri alie valia vazi safi la kijeshi na cheo cha captain, “ni kobwe huyu, nae wamempatia cheo cha captain” alisema Sixmund na wote wakacheka kidogo.

Naam baada ya kumaliza kukagua zile picha, Sixmund akatoa maagizo, “kuhusu hilo kambi subiri amri yangu, taarifa iendelee kuwa siri, ila kwa sasa tuna jambo ambalo inabidi tulichunguze, nalo ni viongozi wa msako wa siri wa kutafuta wahaini ndani ya serikali uliofanyika mwaka 1992” alisema Major General Sixmund, akiongezea kuwa, “dokezo ni kwamba, msako ule ndio uliimarisha kundi baada ya kulitokomeza” alisema Sixmund, lakini hapo hapo CO akakumbusha jambo, “lakini afande, tunaelekea kukosoa uteuzi wa mfalme Eugen wa 25 maana katika historia inasemekana kuwa yeye ndie alie fanya uteuzi huo wa siri, na nina imani kuwa hata majina ya wahusika yatakuwa Golden House, kwenye ofisi ya mfalme” alisema Kanal, lakini Sixmund akuonyesha kujali, “hili ni jukumu la mfalme mwenyewe, hivyo ondoa shaka juu ya hilo, sisi hatuvunji sheria yoyote, maana sasa ndio tunaanza kugundua kuwa hata zile shutuma za mataifa mengine zilikuwa za kweli, na kwamba wale washukiwa walio uwawa hawakuwa UMD, na pengine hata UMD yenyewe haikuwepo, ila ulikuwa ni uvumi wa kuiingiza serikali kwenye kashfa” alisema Sixmund, kabla hajaingia kwenye gari na kuondoka zake, akiwa tayari amesha acha jukumu la uchunguzi.********


Naam vijana wawili wenye asili ya #mbogo_ land, wakike na kiume, yani Deus Nyati na mwana dada Veronica James, wakiwa ndani ya BMW s7 na sasa walishaiacha barabara ya kisarawe na kuingia upande wa kulia wa barabara na kuifuata barabara ndogo “nimejuaje kama unaongea na baba yako, hilo sio muhimu kama kuzingatia niliyokuambia” alisema Deus kwa sauti tulivu, huku anatazama ile njia hafifu waliyo kuwa wanaifuata kuingia porini zaidi, “hallow!! Vero, upo wapi mwanangu?” ilisikika sauti ya mama Vero, toka upande wapili wa simu, ikifuatiwa na simu ya mzee James, “upo salama Vero, hebu tuambie upo wapi tuwalete polisi waje kukuchukua” hapo Veronica alieshindwa kujibu anamtazama Dereva, aliekuwa anaendesha gari, kimya kimya, “dada mbona huongei jamani, ni kweli upo na Deus Nyati?” hilo lilikuwa swali toka kwa Carloline na ndilo swali lililo mfungua mdomo mwana dada Veronica, “Deus Nyati, ndio nani huyo?” aliuliza Veronica kwa sauti iliyojawa na mshangao…..…. ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
Back
Top Bottom