NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA THELATHININA TATU
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA THELATHININA MBILI:- Naaam kabla hatujaenda kwenye maficho ya Deus, twendeni moja kwa moja Mbogo Land jijini TT, mtaa Sizwe kwenye nyumba ya MLA kusikiliza mahojiano kati ya MLA na askari wa zamani wa MLA alieshiriki kwenye operation ya kutokomeza waasi ndani ya serikali ya #mbogo_land, kipindi cha utawala wa mfalme Eugen, wa ishirini na tano, operation ambayo inasadikiwa iliangamiza watu muhimu na wazalendo wa kweli wanchi hiyo....…….ENDELEA…
Sanjent taji Ashraff Mbwana, akiwa amesimama ndani ya chumba chenye mwanga hafifu, na meza ya chuma yenye viti viwili vya chuma, anaonekana kuwa mwenye wasi wasi mwingi na sura ya kukata tamaa, na kujua kuwa sasa anaelekea kupoteza maisha, tena kwa kifo cha kikatili, kitu ambacho aliwahi kukishuhudia kwa askari na wanausalama wenzake miaka mingi iliyopita akiwa kijana mdogo, kitu ambacho kimewatokea baadhi ya askari wenzake waliokuwepo kwenye mpango wa kuondoa waasi ndani ya serikali ya mfalme Eugen, “sasa zamu yangu, sina hakika juu ya familia yangu, sijui na wao watakufa kifo gani” aliwaza Ashraff, ambae anajuafika mpango ule wa kuwauwa yeye na askari wenzake ulihusisha na vizazi vyao, ili visije kulipiza kisasi hapo baadae.
Ukweli bwana Ashraff alikuwa katika wakati mgumu sana wa kungojea kifo chake kama alivyoamini, japo kiuhalisia, mambo yalivyokuwa yanaenda, ilikuwa tofauti na jinsi wenzake walivyo tendewa, mfano walivyokuwa wanaingia katika chumba kama hiki, kwanza kabisa waliingia wakiwa wamezibwa nyuso zao, huku wamefungwa pingu za minyororo mikononi na miguuni, “kumbe wapo wengi sana, yani hata kanal Jastin nae ni mmoja wao” aliwaza Asharaff na wakati huo mlango wa chumba kile, ukafunguliwa na akaonekana askari mmoja mwenye cheo cha luten alievalia vazi la working dreass, lenye rangi ya kaki iliyoiva kwa suruali na kaki mpauko kwa shati, kofia nyeusi, baller hart yenye nembo ya jeshi la #mbogo_land, na viatu vyeusi vyenye kung’aa sana.
Alikuwa mgeni machoni pake, maana ni miaka mingi toka yeye akimbie jeshi, hivyo vijana wengi waliandikishwa hapa katikati, “staff sajent Ashraff Mbwana, kuna viti viwili humu ndani umeshindwa kujichagulia hata kimoja?” aliuliza luten, huku anakaa kwenye kiti kimoja kati ya vile viwili, “sidhani kama nina haja ya kukaa, wakati najua kuwa nauwawa muda wowote” alisema staff sajent wa zamani Ashraff Mbwana kwa sauti ya kukata tamaa, kiasi cha kumfanya yule luten wa MLA, acheke kidogo, “bwana Ashraff, kwanini unahisi kifo ndio kitu pekee kinacho kustahili?” aliuliza luten yule huku anamtazama Ashraf, “sidhani kama kuna haja yakupoteza muda kwa maswali ya kejeri, kukibwa naomba nafasi nitoe ombi langu” alisema Ashraff, kwa sauti yenye kusihi na kuombeleza, “ombi la aina gani hilo bwana Ashraf” aliuliza yule luten huku anatoa kofia kichwani na kuiweka mezani.
Hapo bwana Ashraf akamtazama yule luten kwa sekunde kadhaa, kama vile anajiuliza kwamba ombi lake litakuwa na maana au ndio kazi bure, lakini akapiga moyo konde na kuwakilisha ombi lake, “chochote ambacho kitanikuta, naomba msiwaguse watoto wangu na mke wangu” alisema Ashraff, kwa sauti nyonge yenye kuomba na kusihisi, kiasi kwamba hata wale waliokuwa chumba cha pili wanafuatilia maongezi yale, walitazamana kwa mshangao, “kwanini anahisi familia yake itakuwa hatarini?” aliuliza Malkia Vaselisa huku anamtazama major general Sixmund.
Ni swali ambalo kama asingeuliza malkia, basi mfalme Elvis angetangulia kuuliza, “kwa kweli sija fahamu, na sijui kama itahusiana na taarifa za mwanzo ambazo zinaonyesha kuwa askari wote walio toweka au kuuwawa hata familia zao pia zilitoweka” alijibu Sixmund, na wote wakakubali kwa kutikisa vichwa vyao wakionyesha wameelewa maelezo ya Sixmund, huku wanarudisha macho yao kwenye kioo, ambako mahojiano yalikuwa yanaendelea.
Ombi la Ashraf, linamfanya luteni wa jeshi la #mbogo_land acheke kwa mara nyingine, “ashraf, hebu kaa chini tuanze maongezi, sasa hii ni amri ya kijeshi” alisema luten, “afande familia inauma, naomba familia yangu isiingizwe kwenye hili, alisema tena Ashraf, huku akaa kwenye kiti upande wapili wa meza, “Ashraf, kwanini unahisi kuwa serikali inaweza kufanya jambo la kipuuzi kama hilo, kwamba kesi ya kwako tuiingize familia yako?” aliuliza luten, ikiwa ni swali ambalo wakina Elvis walikuwa wanatamani sana kusikia jibu lake, “hakuna asiejua kuwa wote waliuwawa na familia zao pia” alisema Ashraf, na kufanya, iwe kama mahojiano yameanza juu kwa juu.
Hii ilitoa mwanga fulani kwa waliokuwa wanasikiliza, “kwani hilo lilikuwa ni agizo la serikali?” aliuliza malkia Vaselisa, akimtazama general Sixmund, “hapana alikuwa agizo la serikali, ila ilichukuliwa kama habari za uongo, lakini yeye sijui kwanini anaongea hivyo, kwasababu ni mmoja kati ya watu waliokuwa wanatoa adhabu hizo” alijibu sixmund, kisha wote wakaamishia macho yao kwenye kioo, “nadhani staff sajant Ashraff una mengi ya kutueleza, hebu kwa sasa jibu kwanza maswali yangu huku ukitambua kuwa kuanzia wewe na familia yako mupo salama, napia swala hili haliusiani na familia, tumeileta hapa kwasababu ya usalama wao” alisema yule luten, pasipo kumtazama staff sajent Ashraf, ambae alimtazama afisa huyu kwa macho ya kutokumuelewa, “unamaanisha nini afande, kwamba hapa mumenileta kuhoji kilichotokea?” aliuliza Ashraf kwa sauti ya kuto kuamini, “imekuwa vyema umejua nini nakihitaji kwako” alisema yule luten ambae sasa tunaweza kuliona jina lake kwenye kibandiko kilicho ning’inizwa kwenye juu ya mfuko wa kulia wa shati lake, “Elia Enock” ndivyo lilivyosomeka jina lile, “ina maana nipo hapa kuhojiwla na jeshi la serikali ya mfalme nasio washirika wa UMD?” aliuliza Ashraf kwa sauti yenye mshangao, “ndio bwana Ashraff, tena unatakiwa kutoa ushirikiano na kujibu maswali yangu vizuri” alisema luten Elia, huku anamtazama Ashraf usoni, “kama ni hivyo haukuwa na haja ya kunishika kama mwizi, ingefaa unipigie simu tu na mimi ningekuja mara moja” alisema Ashraf, na akionyesha kuwa mwenye kuanza kuwa na Amani, “naitwa luten Elia Enock, ni askari wa kitengo cha Amored Recce, hii inahusiana na operation tokomeza uasi, ya mwaka 1992” alisema yule luten, “sawa, nipo tayari kujibu chochote utakacho taka kujua, kwaajili ya taifa langu, cha msingi nihakikishie usalama wangu na familia yangu” alisema Ashraf, ambae mpaka hapo alionyesha wazi kuwa alishaondokewa na wasi wasi, japo kwa mbali alionyesha mashaka, “ondoa shaka juu ya usalama, hebu nieleze juu ya operation yenu, na jinsi mulivyokuwa munawagundua waasi, na jinsi mulivyo washugulikia, na kama kuna kingine unakifahamu juu ya wezako waliotoweka, na pia sababu za wewe kuacha jeshi na kutoweka nchini” alisema luten Elia, huku anamtazama Ashraf, wakati huo wakina king Elvis, wakiwa wametega masikio yao kusikiliza mahojiano**********
Naaam wakati kule mbogo mahojiano yanaendelea, huku jijini dar es salaam kijana Deus Nyati akiwa nyumbani kwake na mgeni wake, nae ametoka kuongea na baba yake, ikiwa tayari ameshaongea na simu nyingine mbili, moja toka kwa mzee James, ambae ni baba wa Veronica James, mwanamke mrembo ambae sio tu kuwa rafiki wa muda mrefu wakimtandao, pia kwa sasa ni mpenzi wake.
Pia kijana wetu alikuwa ametoka kuongea na kanali wa zamani wa UMD, ambae sasa anajiita general Kadumya, “kwanini ulimkatia simu baba yako” aliuliza Deus, huku anaweka simu mezani, “alimpa simu sijui nani wa MLA” alisema Veronica huku anajiweka vizuri kwenye mapaja ya Deus, hakuonyesha kujali chochote, “huyo ni askari wa jeshi la #mbogo_land, ndio watu pekee ambao tunapswa kuwaamini kwa sasa” alisema Deus, wakati huo anapeleka macho yake upande wa kushoto wa sebule kwenye kona kabisa,ambapo macho yake yanatua kwenye tv kubwa yenye kuonyesha picha fulani katika mgawanyo wa vipande vinne, na kama ilivyo kuwa mwanzo, video ya kipande cha cam 2 iliwaonyesha waume kama kumi hivi wenye bunduki wakiwa wamesimama pembeni ya magari yao, nikama walikuwa wanasubiria kitu fulani,
Macho yao karibu wote walikuwa wameyaelekeza upande wa barabara ya kwenda kisalawe na sio kule iliko nyumba yao, “hawa watu, mbona siwaelewi, wanahitaji nini huku?” alijiuliza Deus, huku anamuweka pembeni Veronica na kuisogelea ile TV kubwa, “kwani hao ni wakina nani” anauliza Veronica huku na yeye anainuka na kumfuata Deus, kule alikokuwa anaelekea, “sidhani kama nina wafahamu…” alisema Deus, huku anabofya kitufe fulani kwenye king’amuzi kulicho kuwa na jukumu la kuongoza kamera zote nne zilizo wekwa kwenye nyumba hii.
Kipande kilichoandikwa cam 2 kikajaa kwenye tv yote, na sasa ungeweza kuwaona vyema watu wenye bunduki, watu ambao hawakuwa na muonekano wa kijeshi au kipolisi, “kwa hiyo ni wahalifu, kwasababu hakuna mtu anawinda ndani ya msitu huu” aljiuliza Deus, huku anatazama vizuri ile video kwenye TV, “inawezekana wakawa ni wenzake JJ” aliuliza Veronica, huku anamkumbatia Deus kwa nyuma, “sidhani” alijibu Deus, huku anaitazama kwa umakini mkubwa ile video, ni kama kunakitu alikihisi au kungundua, “japo kwa umbali waliopo siwezi kuona vyema sura zao, ila naweza kumuona huyo aliesimama pembeni ya gari la nyuma, ni mmoja kati ya watu walionishambulia mwanzo kabisa pale hotelini” alisema Deus, ambae alizidi kueleza kuwa, “huyu sio mwingine ni Songoro, yeye ndie aliekuwa ananishambulia kabla sijaingia kwenye ugomvi na hawa UMD” alisema Deus, akionyesha kutoamini anachokiona, kwenye ile screen kubwa, “sasa wamejuaje kama tupo hapa?” aliuliza Veronica kwa sauti yenye wasi wasi na mshangao.
Deus akageuza uso wake na kumtazama Veronica, “wala hawajafahamu kama tupo hapa, pengine wamehisi tume kuja huku lakini kamwe hawawezi kuifikia sehemu hii” alisema Deus, huku anarudisha camera kama ilivyokuwa mwanzo, na kufanya zote nne zionekane kwenye kioo cha TV, “sasa itakuwaje wakijua kama tupo hapa?” aliuliza Veronica kwa sauti iliyojaa uoga na wasi wasi, “watakuwa wamesha karibia kifo, maana safari hii sitowaacha hai” alisema Deus kwa sauti ya upole na tulivu, kama vile anazungumzia jambo la kawaida kabisa, huku wote wanarudi kwenye kochi na kukaa kama walivyo kuwa wamekaa mwanzo, japo safari hii, dakika chache baadae Veronica akaanza kusinzia na mwisho kupitiwa na usingizi mzito juu ya mapaja ya Deus Nyati.*******
Naaam, wakati huo huo kundi la pili la polisi, yani wilaya ya kinondoni, lilipokea amri ya kusimama sehemu waliyopo na kupewa amri ya kuingia porini kuanza kusaka kiashiria chochote cha uwepo wa watu wanao wasaka, yaani kundi la waasi wa UMD, askari wana gawana makundi ya watu watano watano mpaka siita na kuingia porini na bunduki zao, ikiwa tayari msako wa mguu kwa mguu ukiwa umeshaanza, askari wanatembea wakiwa makini sana, wapo waliofuata vijinjia vyembamba vilivyoingia ndani ya msitu ule, kasoro magari mawili ambayo yaliagizwa kufuata barabara ya kuelekea machimbo ya kokoto, nayo yanaondoka huku yakiwa na askari saba kila gari, watano nYuma na wawili mbele wawili yani viongozi wao pamoja na dereva, wote wakiwa na bunduki zenye kusheheni risasi, hawakujua kuwa mita mia nne mbele yao kuna kitu kilikuwa kimeandaliwa kwaajili yao.
Wakati hayo yanaendelea porini, tayari magari mawili ya polisi yalikuwa yanaingia kwenye hospital teule ya tumbi kwaajili ya kupeleka miili ya watu zaidi ya kumi waliyoikuta porini, na sekunde chache baadae yakaingia magari matatu toka vitengo mbali mbali vya kiusalama, wapo TSA, wapo polisi na pia walikuwepo MLAS toka ubalozi wa #mbogo_land, waliokuwa wameitwa kujaribu kutambua miili ya wale watu kama wanaweza kuwa ni raia wa nchi yao, ikiwa ni taarifa waliyopewa mara tu baada ya taarifa hii kufika makao makuu ya jeshi la polisi , na TSA, ambao wakaona itakuwa vyema ubalozi wa #mbogo_land, wakija kutambua watu hawa walio hisiwa kuwa ni UMD,jopo la watu kumi na mbili liliongoza moja kwa moja kwenye jengo la kuhifadhia miili ya watu waliofariki tayari kwenda kukagua na kuwatambua.*******
Yap! Songoro akiwa na wenzake pale kichakani, wanasubiri kuongezewa nguvu kama walivyo ahidiwa na Ulenje, mara kwa mbali wakaanza kuona mwanga wataa za magari yakitembe kwenye barabara kuu, hawakuchelewa kutambua kuwa yalikuwa magari matatu, sekunde chache baadae mwanga ukatoweka, niwazi magari yalipotelea kwenye bonde. ....…….ENDELEA
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA THELATHINI NA NNE
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWA MATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA THERASINI NA TATU: Yap! Songoro akiwa na wenzake pale kichakani wanasubiri kuongezewa nguvu kama walivyo ahidiwa na Ulenje, mara kwambali wakaanza kuona mwanga wa taa za magari yakitembe kwenye barabara kuu, hawakuchelewa kutambua kuwa yalikuwa magari matatu, sekunde chache baadae mwanga ukatoweka, niwazi magari yalipotelea kwenye bonde…….ENDELEA…
Hapo wote wakiwa wamekaza macho kwa umakini kutazama barabara kuu, wakayaona magari yale yakiibuka moja baada ya jingine sambamba na ngurumo za magari yale na hapo wanaweza kushuhudia magari yale yakitembea kwa umbali kama wa mita mia moja mbele, kisha yanakata kona upande wa kushoto, upande waliopo wao nao wakatabasamu na kuamini kuwa sasa wanaenda kuunganisha nguvu zao na jeshi la polisi, hawakujua walicho andaliwa na kamanda Ulenje kupitia kijana wake Cheleji.
Naam kwa macho yao wakina Songoro na vijana wake wanayaona magari yale yakija kwa mwendo wa taratibu na kila sekunde yakizidi kuonekana hata ngurumo zake kusikika vyema na kwa uwazi kuwa ni magari aina ya land lover, ambayo mara nyingi humilikiwa na jeshi la polisi, hivyo wakina Songoro hawakuwa na wasi wasi zaidi ya kujiandaa kupanga mikakati ya namna ya kusaka na kumkamata kijana Deus Nyati Dereva wa BMW S7 jeusi’
Lakini magari yale yakiwa yame bakiza mita kama mia ishirini kuwafikia, yanaonekana yakisimama Songoro na wenzake hawajui kinachoendelea, maana mwanga mkali wa taa za gari la mbele, ulikuwa unawamulika usoni, hata hivyo wanatulia kuwasubiri, hawakujua kuwa wenzao sasa walikuwa wanashuka toka kwenye magari yao na kuingia vichakani kwa kugawana maeneo, wakijipanga kwa namna ambayo ingewapa raha muda mfupi ujao.
Yap! Tukiwa bado maeneo ya kisarawe, msako bado ulikuwa unaendelea, sasa makundi yote yalikuwa yametwanyika kwa makundi ya kimkoa kama walivyopangwa ndani ya msitu wa kazimzumbwi, sasa kila RPC alikuwa na kundi lake, japo idadi kubwa ya askari walikuwa ndani ya msitu wakifanya kazi katika wakati mgumu, katika operation hii ya ghafla, maana hata tochi, walitumia za kwenye simu zao, wakuu wao ambao ni RPC na ma OCD walikuwa kwenye barabara, pamoja na walinzi wachache ndani ya magari yao.
Ndio wakati ambao Ulenje aliutumia kuongea na watu wake yani wakina Cheleji na wakina Kadumya, “sikiliza Kadumya, mnachotakiwa kufanya ni kuwa watulivu, kuna tukio litatoea muda mfupi ujao na askari wote wataondoka kuelekea upande wapili wa msitu huu, na nyie mutapata nafasi ya kuhama eneo hili kwa haraka, nitawapa njia ya kupita” alisema Ulenje, ambae licha ya kuwa katika jukumu hili zito, lakini pia alikuwa anashirikiana na waasi kutekeleza jukumu lao ambalo mpaka sasa, lilikuwa limesha poteza uelekeo kwa asilimia kubwa, “vipi kama tutaenda moja kwa moja nyumbani kwa James kumchukuwa na kumlazimisha atimize matakwa yetu, hasa wakati huu serikali na yetu na dunia nzima inaamini kuwa yeye ni UMD?” aliuliza Kadumya kwa sauti ya kunong’ona, ni wazi sasa alikuwa katika maficho.
Ukweli Ulenje alikumbuka kuwa, Kadumya na wenzake hawakuwa na njia yoyote ya kupata habari na kujua kinachoendelea huku mjini, hivyo habari walizonazo zilisha pitwa na wakati, “ondoa hilo wazo Kadumya, ni vyema kama mukitumia njia yoyote kumpata binti yake, maana tayari James yupo kwenye ulinzi mkubwa jeshi la ulinzi na MLA” alisema Ulenje kwa msisitizo, “lakini wao si wanaamini yeye ni muasi?” aliuliza Kadumya akionyesha kuwa na uhakika na hisia zake, “sikia Kadumya, we niamini mimi, mpaka sasa serikali imeweka macho kwenu kuwa ndio waharifu pekee, na James analindwa kama shujaa ili kumuepusha na hatari zozote toka kwenu, ndio maana hata yule kijana Dereva anaeleka kuonekana shujaa kwa kumuokoa mtoto wa james, na kingine cha kuzingatia ni kwamba, ile miili mulioiacha kule porini imesha chukuliwa na inapelekwa hospital, napengine tayari watu toka ubalozi wa #mbogo_land, wameshaenda kuwatambua” alisisitiza Ulenje.
Hapo Ulenje akasikia Kadumya akishusha pumzi nzito, ikifwatia sauti ya kunong’ona, “ngoma nzito” ilikuwa sauti yenye dalili za kukata tamaa, sauti iliyomtia simanzi Ulenje, ambae aliamini kufanikiwa kwa wakina Kadumya ndio kufanikiwa kwake na kuwa na maisha mazuri, “hapana Kadumya, haiwezi kuwa hivyo, usiku mkubwa huu, bado tuna muda wa kukamilisha hili na nyie kuondoka na fedha, cha msingi mkipata nasifa wagawe vijana wako, wengine watafute maficho ya yule dereva na wengine wapambane na polisi” alisema Ulenje pasipo kufikiria hatari itakayo wakuta polisi wenzake.**********
Yap! Taarifa za ukaguzi na utambuzi wa miili ya watu iliyokutwa porini, ziliwafikia haraka sana TSA na kurudishwa makao makuu ya jeshi la polisi, ili nao wathibitishe vijana saba ambao ni watanzania waliowahi kushiriki makosa kadhaa ya ujambazi, na kisha kutoweka kusiko julikana, huku pia baadhi yao wakibainika kuwa ndio vijana walioshiriki tukio la wizi wa fedha pale mbezi kwenye jumba la uhifadhi wa mali binafsi za wananchi, kati yao walikuwepo na wale polisi, waliofika kwenye tukio mapema.
Wakati huo huo MLSA wa ubalozi wa mbogo land, wakituma taarifa nchini kwao kwaajili ya wakutambua baadhi ya watu waliohisiwa kuwa, wanaweza kuwa ni raia wa nchi yao, na pengine waliwahi kuwa watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama wa serikali ya mbogo land, picha za marehemu wale, zikiambatana na maelezo ya tukio na taarifa fikirika juu ya vifo vyao, kwamba inahisiwa waliuwawa katika mapambano wakati wa kumuokoa mschana Veronica James, binti wa mfanya biashara mkubwa Africa bwana James Kelvine.********
Naaaam kijana Deus Frank Nyati, akiwa sebuleni kwake ametulia kwa muda fulani, akitafakari juu kile ambacho ameelezwa na baba yake ya kwamba inabidi ashirikiane na MLA kuhakikisha anamfikisha Veronica salama kwa baba yake, ambae sasa amepewa ulinzi wakutosha kwa ushirikiano wa majeshi mawili, yani MLA na jeshi la ulinzi la Tanzania, “lakini hata kama nikikaa nae muda wote mwisho nitampeleka wapi, zaidi nitamuweka katika wakati mgumu na hatari zaidi, maana natafutwa na vikundi vinne, polisi wa Tanzania wananitafuta, jeshi la ulinzi linanitafuta, yule bwana alienishambulia hotelin (songoro) ananitafuta na UMD nao wananitafuta” aliwaza Deus Nyati, ambae mwisho akachukua maamuzi sahihi, “hakuna namna, lazima nimpeleke Veronica kwa baba yake, na mwisho wa yote nitamrudia” alijisemea Deus, huku anachukua simu yake na kutazama saa, tayari ilishatimia saa tisa za usiku.
Deus anatulia kidogo, anamtazama Veronica usoni kwa sekunde kadhaa, anausadifu uzuri wa mwanamke huyu, ambae muda mfupi uliopita ametoka kukubali ombi lake la kuowana, kisha anajisemea, “kwaajili yako nitapambana” alijisemea Deus Nyati, huku anapiga namba ya mzee James kwa kutumia simu yake ya kibiashara. ********
Naaaam, mambo yalikuwa yanaenda kasi sana usiku huu wa tarehe ishirini na saba, kwenda ishirini na nane ya mwezi wa pili(usisahau matukio yote haya ni usiku mmoja msomaji), kundi kubwa la watu halikuwa na uhakika wa kulala, maana ilikuwa kama ukilala wamepenyea kwako, mfalme Elvis na Malkia Vaselisa kule mbogo land, bodo walikuwa pamoja na wakina major general Sixmund na kanali Jastin, wanasikiliza maelezo ya mwanajeshi wa zamani wa MLA sajent taji Ashraf Mbwana, “mwaka ule 1992 mimi na wenzangu tulichaguliwa kwenye kikundi maalimu cha kuwasaka na kuwatokomeza waasi ndani ya serikali, ambao ilisemekana kuwa walikuwa wengi, ukiwa ni mpango na maagizo ya mfalme Eugeni, ambae mwanzo hatukujua alipata wapi wazo hilo na taarifa ya uwepo wa waasi ndani serikali, lakini baadae tukagundua kuwa ni Chitopela ndie aliepelaka taarifa za uwepo waasi na mfalme akampatia jukumu la kuwasaka na kuwahoji ili kuwatokomeza kabisa” alisema Ashraf huku wakina Elvis wakimsikiliza kwa umakini mkubwa.
“Operation ilianza kwa kuwakamata wote walio bainika, ambao kiukweli ilishangaza upatikanaji wa taarifa zao, japo baadae tuligundua kuwa taarifa hizo za kiuchunguzi zilitoka kwa kamanda wa operation ile, ambae alikuwa ni luten kanali Dickson Chitopela, ambae baadae alipandishwa cheo na kuwa kanali, kiukweli mwanzo mimi binafsi nilidhania kuwa tulikuwa sahihi kukamata kila tulieambiwa ni muasi, ambao wengine wao ni watu ambao hatukuwategemea kutokana na utendaji wao mzuri kazini na ufanisi kijeshi na kiusalama, tuliwauwa wao na familia zao, tukiambiwa kuwa ni maagizo ya mfalme Eugen” alieleza Ashraf, taarifa ambazo ziliwasisimuwa wakina Elvis.
Ashraf, akiwa mbele ya Luten Elia, akaendelea, “lakini nilikuja kushtuka siku moja mchana, siku ambayo nilimkuta kanali Chitopela akiwa anamliza kuongea na mfalme Eugen, akimueleza juu ya taarifa za mfanyabiashara James Kelvine, kuwa ni mfadhiri mkubwa wa kundi cha waasi wa UMD, kwamba yeye ndie anaewanunulia silaha na kuwapatia mavazi na chakula, pia kuwalipa mshahara na hapo mfalme akatoa maagizo kuwa mfanya biashara yule akamtwe mara moja” alisimua Ashraf, ambae mpaka sasa nadhani alikuwa ameshapata Imani ya kuwa alikuwa sehemu salama.
Ashraf akaendelea kueleza, “Baada ya kumaliza kuongea na mfalme, bwana Dickson Chitopelaha, akanipa simu na kunitaka niongee na James Kelvin, nimueleze kuwa anatakiwa kukimbia nchi mara moja na kwamba serikali imemshuku kuwa yeye ni mfadhili wa UMD, hivyo muda wowote, anakuja kukamatwa, na ukweli ni kwamba akikamatwa hatopata nafasi ya kujitetea, namimi nikafanya kama nilivyo elezwa, nakumbuka James ambae hakujuwa anaongea na nani, maana niliambiwa nisijitambulishe, akanieleza kuwa anahitaji kuonana na mfalme akanushe madai hayo, Chitopelah ambae alikuwa anasikiliza maongezi yetu akananiambia nimueleze kuwa, “hilo ni agizo la mfalme mwenyewe na maagizo aliyoyatoa ni kwamba, akipatikana auwawe mara moja, nilipo mueleza hivyo tajiri James hakusubiri tena kuambiwa mara ya pili, hapo mara moja kaanza mipango ya kukimbia nchi, ambapo masaa matatu baadae, aliondoka nchini akisaidiwa na kikundi cha askari wa MLA, waliokuwa wanashiriki operation wakati ule bwana James akiwa na mke wake na mtoto mmoja wakike”
Nakumbuka zile taarifa zilisambaa nchini nyingi za jirani kupitia maredio na magazeti, na jambo lile lilifanywa makusudi, nakumbuka nilimsikia chitopela akitoa maagizo kwa mtu aliekuwa Tanzania apeleke habari za uasi wa James kwenye vyombo vya habari, ilinishangaza kidogo, na kujiuliza inakuwaje kuwa yeye ndie alietoa taarifa na yeye ndie aliemuokoa bwana James, na sasa yeye ndie anaepeleka uvumi kwenye vyombo vya habari.
Sote tulikuwa tunafahamu kuwa, James hakuwahi kujihusisha na jambo kama lile, lakini hatukuwa na la kufanya, hivyo tulikaa kimya na mashaka yetu, hasa mimi ambae sikujua kinachoendelea, ilinishtua zaidi siku mbili baadae, siku ambayo alikuja kanali mmoja pale ofisini, yeye anaitwa Frank Nyati, alikuwa na historia nzuri sana ndani ya nchi, mimi wakati huo nilikuwa mtunza nyaraka wa kanali Chitopela” alieleza Ashraf, nakuzidi kuwafanya wakina Elvis watege masikio kwa umakini mkubwa.
“nakumbuka ulikuwa mchana, wakati kanali Frank alipofika ofisini na kunieleza kuwa alikuwa anahitaji kuingia ofisini kwa Chitopelah, nika mtolea taarifa nae akaingia, baada ya hapa nilifanikiwa kunasa baadhi ya maongezi yao, ambayo nilimsikia Nyati akimlaumu Chitopelah kwa kuendesha operation ile kinyume na lengo la serikali, huku akimsisitiza kufanyia uchunguzi taarifa anazopewa kabla ya kuchukua jukumu la kuwakamata watuhumiwa na kuwauwa, pia alimsihi asihusishe familia zao, lakini Chitopelah, hakuonyesha kukubaliana nae, na baada yake mara tu kanali Frank alipoondoka tu, nikamsikia Chitopela anaongea na mtu mwingine kwa njia ya simu ya ofisini kwake, “hallow kadu kuna mtu tulimsahau na inabidi auwawe usiku wa leo, nae ni Nyati” alisema Chitopelah, akimueleza mtu huyo, ambae baadae nikagundua kuwa ni Kadumya” alieleza Ashraf huku maelezo yake yakiendelea kumsisimua kila mmoja pale ndani.
Ashraf hakuishia hapo, akaendelea kueleza, “mara baada ya kumaliza kuongea na Kadumya, nikamsikia Chitopela akipiga simu kwa mfalme Eugeni, niligundua hilo wakati akimsalimu, “salaam mtukufu mfalme wa #mbogo_land” sikuwa nasikia sauti ya upande wa pili, ila nilimsikia Chitopela akitoa taarifa ya uchunguzi, “mtukufu mfalme, kuna taarifa mpya ya muasi mwingine, ambae ni mtu aliewahi kuaminiwa ndani ya serikali yako, nae ni kanali Frank Nyati, tumepanga leo tukamkamate nakufanya nae mahojiano” ndivyo alivyosema Chitopela, hakika ilinishangaza sana, sikusikia maamuzi ya mfalme, ila nakumbuka kuwa jioni ya siku ile, ndiyo siku ambayo Frank Nyati alitoweka nchini na hakuonekana tena, mpaka nilipopata taarifa za kijana wake mwishoni mwa mwaka jana akiwa kama askari wa jeshi la ulinzi la Tanzania” alieleza Ashraf, ambae hakuishia hapo akaendelea kueleza.
Mpaka hapo ni kama jopo zima lilikuwa limeshaelewa Chitopela amesimama upande gani katika matukio yale, japo hawakutaka kukatiza maelezo ya bwana Ashraf, “opration iliendelea huku nikiamini kuwa mimi tu ndio nilikuwa sijui kinachoendelea, lakini wakati operation ile ikiwa imesha malizika, ndipo nikagundua kuwa ile operation kwa kiasi kikubwa ilifanywa na UMD, ikisimamiwa na Kadumya, ambae wakati huo tayari alikuwa amesha hesabika kama mtoro kazini” alieleza Ashraf....…….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa
NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa
JamiiForums