Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA ALOBAINI NA MOJA
MTUNZI: Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA AROBAINI: Kufumba na kufumbua anastuka kuna mtu yupo karibu yake ile anageuka kujihami, tayari kisu kimesha penya kwenye chemba ya moyo wake na kabla hajaanguka chini yule askari anamdaka na kumlaza chini taratibu, kisha askari anatazama upande wa camera yetu, ambayo kumbuka ipo usoni kwa mtu, imevaliwa kama miwani, anaonyesha ishara ya kwamba mmoja apite, hapo mmoja anaonekana akipita kwa mwendo wa tahadhari akifuatiwa na camera na kuibukia upande wa mbele wa hema ambako wanakutana na askari mwingine MLA, yule aliepitia upande wa pili, hapo wakaonyeshana ishara ya kuingia ndani ya hema. .....…….ENDELEA…

Hapo wakachomoka askari wawili, ambao tofauti na wenzao, wao walishika bunduki aina ya Uzi Gun, yenye viwamba sauti, wakasogelea haraka mlango wa hema huku wengine wawili wakifuatilia na kusimama mlango mwingine wakuingilia kwenye upande ambao mwanzo aliingia major Kwanguru, nao wakiwa na bunduki mkononi mwao kama walivyo kuwa wenzao wawili.

Hapo anaonekana mmoja wao akihesabu kimya kimya kwa ishara ya vidole, yani bila kutoa sauti, “moja, mbili, tatu” wote wanne wakaingia mule ndani kwa haraka sana” wakifuatiwa na wengine wawili kila chumba, “ambapo kwenye chumba cha Chitopela walimkuta bwana chitopela amekaa kwenye kitanda amevaa lile joho la kulalia, amefumba macho anasikilizia utamu anao upata toka kwenye mdomo wa mwanamke aliepiga magoti mbele yake, ni kelele za uoga za wale wanawake ndizo zilizo mfanya afumbue macho na kukutana uso kwa macho na askari wa MLA, hata yule mwanamke aliekuwa analamba mwiko wa bwana Chitopelah aliacha haraka na kufanya kama wenzake walivyofanya kuziba vifua vyao na vitumbua, “tulieni kama mlivyo hakuna mmoja kujitikisa” ilisikika sauti ya mmoja kati ya wale askari wa MLA, kama ilivyopenya kwenye masikio ya wakina Sixmund kupitia zile hear phone.

Yap! wakati hayo yanaendelea upande wapili wa chumba cha Chitopela, upande wapili wa chumba cha Kwanguru askari wanavamia kama tunavyoona kupitia tv B, wanamkuta bwana Kwanguru akiwa amelala katikati ya wanawake wawili waliokuwa uchi kabisa, huku yeye kwanguru akiwa na joho la kulalia, “tulia hivyo hivyo” anasema mmoja wao, lakini neno hilo lililotoka kama amri linaonekana kuparaza, maana Kwanguru anageuka haraka na kupelaka mkono kwenye mchago wa kitanda, kisha mkono unaibuka na bastora aina ya Barreta, lakini kabla hajaielekeza kwa askari wale anakutana na risasi ya kichwa katikati ya paji la uso, zinasikika kelele za wale wanawake, ambao askari mmoja anawatupia nguo wanawake wale kwaajili ya kujihifadhi maungo yao nyeti, kisha wanatoka huku wakati huo pale nje wanaweza kuona magari matatu ya MLA yanaingia pale kambini na kwenda kusimama mbele ya eneo la wazi, askari wanashuka kwa haraka wakiwa na bunduki zao mikononi.

Wakati hayo yanatendeka, waziri Chitopela aliekuwa amekaa kitandani alionekana kutabasamu pasi na wasi wasi wowote, mbele ya askari wanne ambao mmoja wao anaokota nguo chini na kuwakabidhi wale wanawake, nao wanazivaa ili kuhifadhi sukari zao, nao wanavaa kwa haraka, kisha wanatolewa nje na askari mmoja, “Dickson Chitopela upo chini ya ulinzi, utapekwa Treanch Town City, kwaajili ya mahojiano” alisema mmoja wa askari alieingia mule ndani, Chitopela akatikisa kichwa kwa dharau huku anatabasam.

Na wale wanawake wanaungana na wenzao nakupelekwa kwenye magari yale, ambayo pia kulikuwa na watu wengine waliokuwa wanaletwa kwaajili ya kupakizwa kwenye magari yale wakiwepo askari wa UMD waliokamtwa kama mateka na wengine ambao walikuwa pale kama wafungwa na UMD, ambao wengi wao walikuwa ni raia na askari wachache wa MLA ambao walikuwa wanalazimishwa kujiunga na jeshi hili la waasi wa UMD, pia walikuwepo wanawake wahamiaji walioletwa huku kwaajili ya kuwaburudisha askari wa UMD, wanawake ambao wengi wao walikuwa ni wahamiaji toka nchi za jirani, ambao walidanganywa kuwa wangekuja kupewa ajira nzuri.

Mule ndani ya chumba cha Chitopela, askari mmoja anaonekana ana msogelea chitopela akiwa na kifungio cha kamba kwaajili ya kuifunga mikono ya waziri huyu, ambae bado hajatangazwa kutolewa wadhifa huo, “kwahiyo mnakubaliana ya kuwa tutaendelea kutawaliwa kiukoo?” aliuliza Chitopelah kwa sauti isiyo na wasi, hakuna aliemjibu zaidi yule askari aliikusanya mikono ya Chitopela na kuifungia kwa nyuma, “ok! labda tufanye hivi, humu ndani mpo wanne, fungueni hilo sanduku hapo pembeni, kisha muchkue kilichopo na mimi niache niondoke kwa kupitia hapo nyuma” alisema Chitopela, safari hii kwa sauti iliyoanza kupoa kidogo, lakini hakuna aliemjibu zaidi ikasikika sauti toka kwa yule aliekuwepo mule ndani, “kazi imekamilika lengo tunalo mkononi” alisema yule askari wa mule ndani, na hapo sauti nyingine ikasikika, “mtoe nje”.

Naaam kusikia hivyo, Sura ya Chitopela, inabadirika na kuonekana kunyongea, “yani munakataa fedha kwaajili ya kujifanya wazalendo?” alisema Chitopela kwa sauti yenye ujeuri uliofifia, “inuka twende” alisema askari aliekuwa anamfunga Chitopela huku anamvuta toka kitandani alipokuwa amekaa, “kuwa na heshima we askari, kumbuka mimi ni brigedia general na waziri pia” alisema Chitopela akionyesha ukali kidogo, hapo akakutana na kitako cha bunduki cha usoni, ambacho kilileta matokeo ya kweli, maana Chitopela alionekana akizimia na kuanza kwenda chini taratibu akidakwa na askari mmoja aliekuwa karibu yake.

Wanamkokota Chitopela mpaka nje, ambako wanakuta bado watu wanaendelea kupanda kwenye magari, “taarifa makao makuu, mpango umekamilika kabisa, lengo limepatikana” hii ilikuwa ni taarifa ya kwenda makao makuu ya operation, “ok! safari ya kurudi ifanyike, hellcopter tatu zipo hewani, wekeni alama sehemu ya kutua, hellcopter moja” alisema major general Sixmund, “nimekupata afande” ilisikika sauti toka kwenye hear Phone.

Dakika chache baadae zikaonekana hellcopter tatu zikiwa zinasogea kwenye anga la kambi lile, ambapo wao walitupa baruti nyepesi ya kuonyesha alama yenye mwanga mweupe, mwanga ambao uliifanya moja kati ya zile Hellcopter tatu zishuke sehemu ile, wakati huo huo magari yalikuwa yanaanza kuondoka eneo lile kuelekea upande wa kusini mwa Tanzania, yani kaskazini mwa #mbogo_land, yakiwa na baadhi ya askari wa MLA, na wale mateka na wafungwa, huku Hellcopter ikiwa inapakia baadhi ya askari wanne waliobakia ambao walishirikiana kumpakiza Chitopela aliekuwa amepoteza fahamu, kisha hellcopter inainuka na kuondoka zake, kushika uelekeo wa kusini yani #mbogo_land.*******

Naaam! kati ya watu ambao mpaka mida hii ya saa tisa za usiku walikuwa macho, ni TSA yani Tanzania Secret Agent, nao walikuwa makini wakifuatilia kila hatua ya msako uliokuwa unaendelea, maana sio tu kumfuatilia kijana Deus Nyati, sasa ilishageuka na kuwa msako na mapambano dhidi ya kikundi cha waasi cha UMD, lakini mkuu, habari zinasema kuwa askari wa MLA na wale wa Jeshi la ulinzi wanaelekea kisarawe, sidhani kama kuna hata mmoja anae jua, wanaenda kukutana sehemu gani huko kisarawe “pia hatujui wanampango gani na yule kijana Deus Nyati, maana Jeshi la ulinzi wanamuhitaji, polisi nao wanamuhitaji, hatujui kuhusu MLA, lakini hata sisi pia tunamuhitaji, tujue yeye ni nani hasa” alisema mmoja wa wajumbe waliokuwepo pale ofisini kwa mkurugenzi Elisha Eric, “mpaka hapo kuna umuhimu wa sisi kwenda huko” alisema Elisha, huku akiongeza kuwa ajulishwe mkurugenzi wa kisarawe TSA, ilia toe mtu wa kufuatilia nyenendo za MLA na jeshi la ulinzi, ili wao wajue wanaelekea wapi, “lakini pia ni muhimu sana, kama tutatafuta sababu ya sisi kuwepo pale” alishauri mmoja wao.

Wajumbe wote wakaunga mkono, na kuona hilo swala lilikuwa na ukweli, lakini sasa ni sababu gani ambayo itawafanya wao waende kule kisarawe, maana endapo wataenda bila sababu wataonekana kama ni wanausalama waliokuja kuangalia tu, endapo watatoa hoja ya kumchukua Deus, lazima watakutana na vizingiti toka jeshi la ulinzi na jeshi la polisi, ambao wote watakuwa na hoja za msingi, maana polisi walikuwa na kibali cha kumkamata Deus aliekuwa akitafutwa kama dereva BMW jeus, gari lililoshiriki uharifu huko Arusha, “jeshi la ulinzi wao ndio wakwanza kumtafuta Deus Nyati, na kikawaida ni mtu wao, maana yule ni askari wao ndio wenye jukumu la kumkamata na kumstaki katika mahakama ya kijeshi” aliwakumbusha mwenzao mmoja.

Naam, baada ya kujadili kwa muda mrefu, mmoja akapata jibu, “nimepata wazo” alisema huyo mmoja wao, “wazo gani hilo?” aliuliza mkurugenzi, huku wote wakiwa wameamishia macho na masikio kwake kusikiliza hilo wazo, “mke wake yupo nyumbani, twendeni tuka mchukue, kwa maana ya kumpeleka eneo la tukio kumuona binti yake, kule tutawaambia, tumemleta kwasababu mama wa watu alikuwa ana wasiwasi mkubwa na binti yake” alisema yule mjumbe, “halafu baada ya hapo” aliuliza Elisha, “baada ya hapo, hakuna atakae kuwa makini na sisi, hivyo tutaanza mipango ya kumtorosha Deus, ambae tutajifanya kama tuna msaidia, na yeye lazima ataunga mkono mpango wetu, na kama akiunga mkono ndio tutamteka na kumleta ofisini kwa mahojiano” alisema yule mjumbe, akiona kuwa ametoa mpango kubwa wa maana.

Hapo akasikia kicheko kikubwa na kikali toka kwa wenzake, kisheko ambacho hata yeye kilimshangaza, “mnacheka nini sasa, au sijaeleweka?” aliuliza yule mjumbe akiwashangaa waliokuwa wanamcheka, “umeeleweka kaka, lakini kabla hujafanya hivyo nenda kaage familia yako na watu wote ulio wanaandika kwenye urithi” alisema Elisha Eric, hapo wakacheka tena, “tatizo hamja nisikiliza mpaka mwisho, yule hatumchukui kama mwizi wa kuku, yule tuna mteka pamoja na wote atakao kuwanao kwenye gari moja, kwa kuwategea dawa ya usingizi” alisema mjumbe, na hapo vicheko vikapungua na wote wakakubaliana nae kwa kutikisa vichwa vyao chini juu.********

Naaam usiku ulizidi kuyoyoma, masaa yalizidi kuhesabu, sasa ni saa kumi za usiku, majeshi ya UMD yanaezidi kuyoyoma pori kwa pori kulekea upande wa pili wa msitu huu wa Kazimzumbwi, unao pakana na msitu wa misegese, askari wanaonekana wakiwa na silaha nzito, silaha zilizoshiba, makombora mazito ya RPG, masanduku ya risasi na silaha zao walizidi kusongea mbele wakifuata njia za ng’ombe na chochoro za wachoma mkaa kuelekea kaskazini mashariki, walipanda milima na kushuka mabonde, ambayo kwa msimu huu wa mvua, yalikuwa yana madimbwi madogo madogo ya maji, ndio wakati ambao Kadumya aliekuwa kati kati ya kundi alipoona simu yake inaita.

Kitendo bila kuchelewa, akatoa simu yake haraka na kutazama jina la mpigaji, alikuwa ni Ulenje, akaipokea mara moja akitegemea kuwepo kwa taarifa nzuri, “niambie kamanda wangu” alisema Kadumya, mara baada ya kuiweka sikioni, “sikia kaka safari hii usifanye makosa, huyu mpuuzi nimesha jua sehemu aliyopo,” alisema Ulenje, kwa sauti yenye msisitizo, “niambie Ulenje, yupo wapi huyu mjinga nina jeshi zima, hawezi kuniepuka safari hii, alisema Ulenje kwa sauti yenye hamu na shauku kubwa sana, “wapo huku huku porini, upande wa ile barabara muliyotumia kujia toka mjini, cha msingi nyie njooni sawa wa reli, muwe macho upande wa kusini wa reli, kuanzia ziro mpaka mita mia sita, hakuna anae jua zaidi yangu uwepo wa huyu mshenzi eneo hilo, najua kwa kuwa sisi tunaenda kule, kama bado yupo eneo lile basi atakimbilia huko kwenu, vinginevyo mpaka sasa atakuwa anakuja huko kwenu, kwasababu kuna vijana wangu tayari wapo eneo lile” alisema Ulenje na hapo Kadumya hakusubiri simu ikatwe, “simamaaaa kuleeeee” alipiga kelele Kadumya huku anakata simu na kuiweka mfukoni. .....…….ENDELEA




NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA AROBAINI NA MBILI
MTUNZI: Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA AROBAINI NA MOJA: cha msingi nyie njooni sawa wa reli, muwe macho upande wa kusini wa reli, kuanzia ziro mpaka mita mia sita, hakuna anaejua zaidi yangu uwepo wa huyu mshenzi eneo hilo, najua kwakuwa sisi tunaenda kule, kama bado yupo eneo lile basi atakimbilia huko kwenu, vinginevyo mpaka sasa atakuwa anakuja huko kwenu, kwasababu kuna vijana wangu tayari wapo eneo lile” alisema Ulenje na hapo Kadumya akusubiri simu ikatwe, “simamaaaa kuleeeee” alipiga kelele Kadumya huku anakata simu na kuiweka mfukoni. .....…….ENDELEA

Hapo askari wote waliokuwa wanatembea kwa kufuata mstari mmoja, kwamaana ya mstari mmoja, yani single file walisimama mara moja na kutuli kimya kabisa, “wote sogeeni kwangu” alisema Kadumya na wale askari zaidi ya hamsini wakaanza kujikusanya pale alipokuwepo Kadumya Kobwe na Kafulu ya JJD.******

Yap! mwana dada Veronica akiwa ndani, akiwa hajamuona kabisa Dereva wa gari jeusi aina ya BMW kijana mpole ambae ametoka kuokoa Maisha yake na heshima yake, kijana ambae ni Rafiki yake wa muda mrefu, kijana ambae leo hii amekuwa mpenzi wake na kupeana nae penzi kwa mara ya kwanza, ambae alitoka muda mfupi uliopita, japo hakusema anaenda kufanya nini, lakini tayari ile kauri ya wamebeba silaha ilisha mjulisha mrembo huyu kuwa mpenzi wake huyo anaenda kufanya jambo zito huko nje, ni kama alishaanza kuijua tabia ya mpenzi wake huyo, zaidi aliweza kuwaona vijana wawili wakiingia ndani ya jengo hilo, na baada ya muda mfupi sasa anayaona magari mawili ya jeshi la polisi yakisimama nje ya jengo lile huku yamebeba askari kadhaa wenye bunduki mikononi mwao, “jamani Deus, ondoka huko nje wapo wengi na bunduki” alisema Veronica, akijisemea mwenyewe.

Nadhani sasa hatuwezi kuona vyema kile kinachoendelea zaidi ya hapo itapendeza kama tukitoka nje tukashuhudie kinachotokea, njia tunayopitia ni hii ya ngazi, ambayo inaenda kutokea uvunguni mwakitanda, katika chumba cha kwenye nyumba ya juu, nyumba ambayo haijamalizwa ujenzi wake, ambako tunakuta kile kitanda na nguo chache zilizotundukwa kwenye kuta isiyopigwa lip.

Tunaelekea sebuleni, ambako tumuona kijana Deus, akiwa amesimama pembeni ya dirisha, anaweka simu ya Songoro mfukoni mwake huku macho yake yanachungulia nje, ambako anayaona magari mawili ya polisi, huku polisi wakiwa wameshuka toka kwenye magari yale na bunduki zao mikoni, Deus anatazama chini ambako inaionekana miili ya Songoro na kijana Side, ikiwa imelala chini huku imezungukwa na vidimbwi vya damu, na bunduki zao zikiwa pembeni ya miili yao, bunduki iliyokuwa pembeni ya Songoro ikionekana kufunguliwa na mkebe wake wa risasi ukiwa mkononi kwa Deus, huku kifuniko cha mitambo kikiwa kimezama shingoni kwa Songoro, “sina la kufanya” anajisemea Deus, huku anaokota bunduki ya Side na kutazama kama ina risasi za kutosha, anaona kuwa zilisha pungua kidogo, anatazama mkebe wa Songoro, nao hivyo hivyo, anazibua ile magazine ya Songoro na kutoa pring yake, ikifuatiwa na risasi, ambazo anazikinga mkononi, huku anaelekea upande wa chumba kimoja chenye giza nene, wakati huo anapachika zile risasi kwenye mkebe wa Side, yani alikuwa anajazia, wakati huo hatujui aliongea nini na bwana Ulenje, maana hatukusikia maongezi yao.******

Naaaaam, lisaa limoja baadae, bwana Dickson Chitopela, anahisi giza nene lilikuwa limetanda usoni mwake, kichwa kilikuwa Kizito kama vile amefungwa kitu Kizito, baridi ilikuwa inapenya kwenye mwili wake, hapo taratibu anajitahidi kufumbua macho yake ilikupata nuru, lakini kwa uhakika hakuna hata chembe moja ya mwanga inayofikia macho yake, Chitopela anastuka sana, pengine anahisi kuwa ameshakuwa kipofu, akiwa na hofu kubwa sana ana jaribu kupapasa usoni, akikagua macho yake ili kuhakikisha kama macho yake yalikuwa mazima, ukweli macho yake ni mazima.

Chiitopela anarudisha kumbu kumbu zake lisaa limoja lililopita, anakumbuka kuwa alikuwa chini ya ulinzi wa MLA marine commando, ambao alijaribu kuwashawishi na baada yake akajikuta anapigwa na kitako cha bunduki na kuona giza usoni mwake, giza ambalo limedumu mpaka sasa hivi.

Baridi kali inamfanya Chitopela aliekuwa amekaa chini kabisa sakafuni ajipapase mwilini mwake, anagundua kuwa zaidi ya joho la kulalia mwilini mwake hakuwa na vazi jingine lolote, “inamana huu ndio mwisho wangu, ndoto zangu zote zakuchukua nchi hii zimepotea” aliwaza Chitopela huku anajiinua toka sakafuni na kupapasa kwa mikono yake akitafuta kujua alikuwa katika chumba au sehemu ya aina gani, lakini hatua nne tu, anajikuta amegusa ukuta, anaenda upande wa kushoto nako hatua mbili tu anajikuta amegusa ukuta, anaenda upande wa kulia, huku kidogo ana tembea hatua sita kabla ya kugusa ukuta, anageuka na nyuma na kuanza kutembea, ambapo anapiga hatua kama nne tu, anakutana na ukuta ulioambataba na mlango wa chuma.

Ni kweli alikuwa ndani ya chumba, lakini chumba ambacho hakikuwa na dirisha hata moja ambalo lingeweza kupitisha japo mwanga kidogo, Chitopela anajaribu kuwaza na kubashiri yupo kwenye eneo gani la nchi yao, yani chumba hiki kipo kwenye jengo gani la kambi gani la kijeshi, hapa #mbogo_land, anatamani aite mtu yoyote aje amueleze yupo wapi, lakini kuita kwake mtu ni sawa na kuwajulisha kuwa alikuwa amesha rejewa na fahamu.

Lakini wazo lake hilo alikusaidia kitu, maana muda mfupi baadae akashangaa kuona ule mlango mgumu wa chuma Kizito ukifunguliwa, na ghafla chumba kikanurulishwa na mwanga mkali sana wataa toka nje ya chumba, ambao ulipenya mlangoni na kuangazia mule ndani. ********

Lakini tunapo tazama nje kupitia madirisha yaliyokuwa wazi, tuna yaona yale magari mawili ya jeshi la polisi, tayari askari walikuwa wamesha shuka toka kwenye magari yale na silaha zao mikononi mwao, na kwa ukaribu zaidi tuna muona Koplo Cheleji aliekunja sura kwa hasira anatazama lile jengo bovu bovu na kwa umakini wa hali ya juu, anatazama kwenye aridhi na kuona nyayo za watu wawili zikiingia kwenye jengo lile, bila shaka ni wakina Songoro, hapo anatoa redio call yake, “hallow vituo vyote, hiki ni kituo namba saba, upande wa relini, askari wanne wapo chini, narudia tumeshambuliwa, askari wawili wapo chini na adui yupo mbele yetu tunapambana nae” alisikika Cheleji, ambae wakati huo alikuwa anafungua mlango wa gari na kushuka, kisha anaonyesha ishara wale askari, kwa kuonyesha kama vile anawahesabu, na kila aliemuonyesha alielekea upande alio onyeshwa.

“tumekupata, tumekupata namba saba, na sisi tupo njiani kuja uelekeo wako, hakikisheni munaenda sambamba na maadui, wasiondoke machoni penu, tunakuja kuongeza nguvu” ilisikika sauti bila kujitambulisha, lakini niwazi ilikuwa ya kamanda Nyambibo, “tupo nae sambamba, na hakikisha safari hii hawezi kutukimbia” alijibu Cheleji kwa sauti ya kujiamini, huku anawatazama askari nane aliotanguliza mbele, wanne wakizunguka upande wa kushoto wanne upande wakulia, yeye akiwa amebakia na askari wa tano, yeye akiwa wa sita.

Askari wale nane wa jeshi la polisi walioneka wakikimbia kwa haraka pasipo tahadhari yoyote kulizunguka lile jengo ambalo ni kama lilitelekezwa, au mwenye jengo hakuwa na fedha ya kuliendeleza, ila ni wazi kuwa lilikuwa linakaliwa na mtu, na kama sio kuishi basi alikuwa anakuja na kuondoka, maana mazingira ya nje yalionyesha hivyo, hasa kwa muonekano wa ile bustani ambayo ilikuwa imemelesha vyema mimea yake, na mtu huyu alionyesha kuwa na uwezo fulani wa kimaisha, ni kutokana na nyayo za matairi ya gari, pengine amelisusa kwasababu ni mbali na mjini, au huduma nyingine za kijamii, sio kwamba najiuliza mimi, ila ni koplo Cheleji, ambae alishangaa sana, kwa kuhisi kuwa yale yalikuwa ni maficho ya Songoro, ilishangaza sana, maana hakuwahi kufikiria kuwa Songoro alikuwa na maficho upande huu na yeye asijue.

Ok! Cheleji kwa kuona kuwa askari wake tayari wamesha zjnguka eneo lile, hapo na yeye anawapa ishara askari wengine wawili kwamba waelekee kwenye mlango wa mbele wa kuingilia ndani ya nyumba ile, ambayo ni wazi wakina Songoro walikuwa wameingia, nae akawafuata askari wale wawili wenye vyeo vya constable, ambao sasa walikuwa wameshaufikia mlango wa jengo lile lililojaliwa na giza nene, huku mitutu ya bunduki zao ikiwa mbele tayari kushambulia chochote ambacho watakutana nacho mbele yao.

Cheleji akiwa anawafuata wale askari wenzake kwa mwendo wa tahadhari, akawaona wanaingia mule ndani ya jengo na sekunde chache baadae, unaonekana mwanga hafifu wa tochi ya simu, ndani ya chumba kile cha sebule chenye madirisha wazi, ukifuatiwa na ukulele toka kwa mmoja kati ya askari alieingia mule ndani, “afande chelejiii njoo uone huku” ilikuwa ni sauti ya juu yenye kujawa na mstuko na uoga wa hali ya juu, Cheleji akaongeza mwendo kukimbilia mule ndani, ambapo ile anaingia kwa msaada wa tochi ya askari wake, anawaona wakina Songoro na kijana wake wakiwa wamelala chini, huku wakiwa na majeraha makubwa shingoni, Cheleji alijumlisha muda ambao askari waliingia ndani na muda ambao walitumia kufanya mauwaji yale “huuu! Mumewezaje haraka hivi?” aliuliza Cheleji kwa sauti ya mshangao, huku anawatazama wale askari wawili waliokuwa wametazama pembeni wakishindwa kuwatazama wakina Songoro kwa kile ambacho kimewakuta, hakika ni vifo vya kinyama.

Hapo kwa haraka unaweza kushangaa kwamba wanaona huruma, wakati na wao wametoka kuuwa muda mfupi uliopita, na pia walikuwa wanawatafuta watu hawa ili wawauwe pia, “mh!” aliguna kwa mshtuko Cheleji, ni baada ya kugundua kuwa wauwaji wa Songoro sio askari wake, kwa jinsi hiyo mule ndani kutakuwa na mtu mwingine ambae ni hatari zaidi.

Naam kwa kugundua hilo, haraka sana Cheleji ana tazama kushoto na kulia, mbele na nyuma, mule ndani ya sebule ya nyumba hii, ambayo haijamaliza ujenzi, haoni mtu mwingine zaidi ya yeye na askari wake wawili, na wakati huo huo anasikia simu yake inaita toka mfukoni, ana ingiza mkono mfukoni na kutoa simu yake, huku anawatazama wale askari wake na kuwapa ishara ya kutawanyikia vyumbani kwaajili ya msako.

Mara moja askari mwenye simu ya tochi anazima tochi na kuungana na mwenzie kuelekea upande wa vyumbani kwa mwendo wenye tahadhari kubwa sana, wakati huo yeye mwenye anapokea simu na kuiweka sikioni pasipo kutazama mpigaji, na kabla hajaongea lolote akasikia sauti toka upande wa pili, “sikia Cheleji, kuna kitu lazima mujue” ilikuwa ni sauti ya Ulenje, ambayo ilikuwa na wasi wasi kiasi, “kitu gani mkuu” aliuliza Cheleji kwa sauti ya chini huku anawatazama wale vijana wake, ambao sasa walikuwa wanatembea kwa tahadhari kufuata milango tofauti ya mule ndani.

Wakati mmoja akiwa anaufuata mlango uliowekewa kiwambaza dhaifu cha bati, huku mwingine akiwa anaelekea upande wa chumba mfano wa jiko, ungetambua hivyo,l kutokana na kidrisha kidogo kwenye ukuta unao peana mgongo na chumba cha maakuli, yani dianing room, “sikia Cheleji, musiwafuate wakina Songoro tayari wamesha uwawa” alisema Ulenje kwa sauti yenye tahadhari nyingi. ********


Yap, wakiwa sebuleni wamejilaza kwenye makochi yakifahari, Carolina na mama yake, mara wanashtuliwa na mlango uliokuwa unagongwa, toka nje, “nani?” aliuliza afisa mteule daraja la pili Simon Karaghe, wa jeshi la ulinzi, kuna wageni toka makao makuu ya TSA wanahitaji kukuona, hupaswi kuwa na wasi wasi, kwasababu tumewakagua na tumeridhika kuwa ni wao wenyewe” alisema askari mwenye malaka ya juu ya msajent, yani surgent major, ambae kwa sasa alikuwa ameachiwa jukumu la kusimamia ulinzi pale nyumbani kwa mzee James, yani kinyerezi, “sawa” aliitikia mama Veronica, huku anamtoa Caroline miguuni mwake na kumlaza pembeni, akionekana kupitiwa na usingizi, kisha yeye akaende kufungua mlango.

Naam baada ya mlango kufunguliwa, wanaingia wanaume wawili watu wazima, “pole sana kwa usumbufu pole sana kwa kukuamsha usiku huu, pia pole sana kwa haya matukio ya kutwa nzima” alisema mmoja kati ya wale wawili, “kweli hatuwezi kupoa mpaka ni hakikishe yule kijana amemkabidhi binti yangu salama kwa baba yake” alijibu mama Veronica huku anaongoza kwenye kochi, akifuatiwa na wale jamaa wawili walio tambulishwa kama wanausalama, “usiwe na wasi wasi shemeji, hilo linaenda kuisha, ndio maana na sisi tupo hapa kuhakikisha binti yako sio tu anapatikana, ila pia anapatikana akiwa salama kabisa” alisema yule alieongea mara ya kwanza, huku wanakaa kwenye makochi bila kusumbua usingizi wa Carolina, “kwa majina mimi naitwa Issa Makame, na huyu mwenzangu anaitwa Michaer Njogopa, alitambulisha yule alieongea muda wote, “ok! karibuni nawasikiliza” alisema mama Veronica ambae alikuwa wa kwanza kukaa karibu na pale alipokuwa amelala binti yake.

Hapo kwanza wanausalama wakatazamana, kama vile wanaulizana, aanze nani kuongea, lakini ni kama haikuwa kitu, kwasababuni wazi muongeaji alikuwa anajifahamu, “shemeji sisi tunahitaji kujua mambo machache kabla ya kuelekea kisarawe, ambako Deus anaweza kuja kumleta binti yako” alisema yule wa kwanza, alie jitambulisha kwa jina la Issa Makame, “kwahiyo mukitoka hapa munaenda huko walikoenda wakina baba Vero?” aliuliza mama Carolina, kwa sauti yenye kuhamasika, “ndio, tukitoka hapa tunaelekea huko” safari hii alijibu Michael Njogopa, “henhee! Mlitaka kuniuliza nini labda?” aliuliza mama Veronica.

Issa Makame na Michael Njogopa wakatabasamu kidogo, maana maswali hayakuwa katika malengo yao, kikubwa walihitaji kuongozana na mama Veronica kuelekea kisarawe kwenye makutano na dereva wa BMW jeusi, “tuna fahamu kabla ya wakina mzee James kuondoka, tayari walikuwa wamewasiliana na mtu ambae anamshikilia binti yenu, sisi tulitaka kujua kama mulikuwa munamfahamu mtekaji toka siku za nyuma?” aliuliza Issa Makame, “ndiyo mtekaji alipiga simu kwa baba Vero, akasema kuwa wanae Vero, hivyo asubiri aelekezwe cha kufanya ili kumpata Vero akiwa mzima” alisema mama Veronica, na hapo Issa akaongeza swali la mtego, “hooo! sasa ilikuwaje mpaka akakubali kumrejesha binti yako, mumesha fanya alicho taka mukifanye?” hapo mama Veronica aliachia kicheko chepesi cha mguno, “hapana hawakuwahi kupiga tena simu, nadhani huyo kijana Deus aliwahi kumuokoa Veronica” alisema mama Veronica, na hapo wakatazamana tena.

Niwazi walishangaa kusikia mke wa James anafahamu kuwa Veronica aliokolewa na Deus Nyati, hooo kwahiyo ni watu ambao wanafahamiana toka muda mrefu” aliuliza bwana Njogopa, na hapo ghafla Carolina akakurupuka toka pale alipokuwa amelala, “mimi ndio namfahamu toka zamani” alisema Carolina huku anainuka na kukaa pembeni ya mama yake, ni wazi kabisa alikuwa macho toka wageni hawa wanaingia ndani ya nyumba yao, Issa na Michael wakamtazama Carolina kwa mshangao, “hoooo! kwahiyo shemeji, binti yako alikuwa anafahamiana na Deus Frank toka zamani, hata haya yaliyotokea haya kuwa bahati mbaya, kwamba mulimuomba Deus awasaidie kumuokoa baba yenu na baadae dada yake” aliuliza Issa, kwa sauti ya ung'amuzi wa kinoko, huku wote wakitoa macho kwa mshangao, huku wametoa macho yenye viashiria vya kiumbea..…….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao Kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA AROBAINI NA TATU
MTUNZI: Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA AROBAINI NA MBILI: “mimi ndio na fahamu toka zamani” alisema Carolina huku anainuka na kukaa pembeni ya mama yake, ni wazi kabisa, alikuwa macho toka wageni hawa wanaingia ndani ya nyumba yao, Issa na Michael wakamtazama Carolina kwa mshangao, “hoooo! kwahiyo shemeji, binti yako alikuwa anafahamiana na Deus Frank, toka zamani, hata haya yaliyotokea hayakuwa bahati mbaya, kwamba mulimuomba Deus awasaidie kumuokoa baba yenu na baadae dada yake” aliuliza Issa, kwa sauti ya ung'amuzi wa kinoko, huku wote wakitoa macho kwa mshangao, huku wametoa macho yenye viashiria vya kiumbea...ENDELEA...

Ni kama walikuwa wanajaribu kuwahusisha wao na kijana Deus Nyati, “hapana sio kwamba walikuwa wanafahamiana kabisa, ila waliwahi kukutana kwa siku moja tu wakiwa safarini” alisema mama Veronica na kuanza kusimulia ile safari ya binti yake aliyoamua kupanda tren, na jinsi ilivyopata ajari, kisha Deus kuwaokoa wakina Carolina na wenzake, “siku hiyo ndiyo ilikuwa ya kwanza na ya mwisho kwa Carolina kumuona Deus, mpaka leo hajamuona tena, japo imekuwa rahisi kwa yeye kuikumbuka sura yake mara alipoiona kwenye simu” alijibu mama Veronica huku Carolina akiwa ametulia pembeni yake anasikiliza mama yake aliekuwa anatoa maelezo kwa watu wale wawili ambao walijitambulisha kama wanausalama.

Hapo wakina Makame, wakatazamana tena, ni kama waliongea jambo fulani na kukubaliana, sekunde chache baadae wakamtazama Veronica, “kwahiyo akikuona anaweza kukutambua?” aliuliza Makame, hapo Caroline alitulia kidogo, kama vile anatafuta jibu, na baada ya utulivu wa sekunde kadhaa, Carolina akatoa jibu, “mh sidhani kama atanitambua, nilikuwa mtoto sana, ila nikimkumbusha mimi nani, lazima atanikumbuka tu, maana hawezi kusahau lile tukio la ajari ya treni” jibu hilo alilitoa Caro mwenyewe, na hapo wanausalama wawili walitabasamu kwa Pamoja, “vizuri sana, wewe ndie utasaidia kupatikana kwa dada yako kirahisi, maana hatujui anampango gani, ila kama wewe utakuwepo na ukamkumbusha urafiki wenu wa zamani lazima atamtoa dada yako kwa haraka na bila shida yoyote” alisema Makame, na kwa sauti iliyochangamka, ugesema amevumbua jambo fulani la ukweli.

Ni kama walijua kuwa Carolina ana hamu kubwa ya kukutana na kijana Deus Nyati, maana kusikia hivyo Carolina aliinuka haraka toka kwenye kochi, “sawa, hakuna shida twendeni, ngoja nikavae” alisema Carolina, huku anatambea kuelekea chumbani kwake, huku mama yake akimtazama binti yake kwa macho ya mshangao, kabla haja wageukia wakina Makame, ambao walionekana kutabasamia mafanikio yao, “lakini tutawaamni vipi” aliuliza mama Veronica, huku anawatazama wakina Makame kwa macho ya mashaka, “hooo! Kumbe hatujakuonyesha vitambulisho vyetu” alisema Michael Njogopa, huku anaingiza mkono mfukoni mwake na kutoa kitambulisho, kisha akamuonyesha mama Veronica, ambae alikitazama kwa sekunde kadhaa, ambapo alitazama picha tu na kumpatia, huku Issa nae akiwa anamkabidhi cha kwake, “inatosha, najua sitoweza kumzuia Carlo kwenda huko kwa Deus, wacha na mimi nijiandae niongozane na nyie” alisema mama Carlo, huku anainuka na kuelekea chumbani kwake.******

Naaam! Msafara wa magari ya jeshi la ulinzi la kikundi cha marine special force, cha magari nane, ambayo sasa yalikuwa yamesha gawana maeneo ya ulinzi na mitego, manne yakiwa yamebakia relini na manne yakiwa yanazidi kusonga mbele, yalipishana na magari mengi sana ya polisi yaliyokuwa yana tembea kuelekea upande wa relini.

Tuachane na magari ya jeshi la ulinzi, tuyafuate ya polisi, ambayo yalikuwa katika mwendo mkali sana, sisi twendeni kwenye gari la ACP Ulenje, ambalo alikuwa yeye dereva wake na mlinzi wake mmoja tu, ndani ya gari hilo, ambapo tuna muona Ulenje akiwa na simu sikioni, huu ndio wakati aliokuwa anaongea na koplo Cheleji.

Ni kwamba wakati ule anaongea na Songoro, aliekuwa ameepuka kifo toka kwa akina Cheleji, na muda huo huo anasikia sauti ya mshangao ya Uled Songoro, ikitaja Dereva, na baadae Kufuatia miguno ya maumivu makali, ambayo yalifuatiwa na kishindo cha kuanguka na ukimya wa muda, uliovunjwa na sauti ya tulivu yenye upole wa hali ya juu, japo ilikuwa ni mara yake ya kwanza, lakini haikuwa vigumu kwa yeye Ulenje kugundua kuwa muongeaji ndie dereva mwenyewe, na mbaya zaidi alimtaja kwa jina.

Ilimshtua sana Ulenje, sio tu kutajwa jina na kijana huyu hatari, tatizo ni kwamba kijana huyo, amesha tambua kuwa yeye ni nani na anajiusisha na nini, lakini Ulenje alijiambia kuwa hakutakiwa kujilegeza mbele ya kijana huyu.

Hapo Ulenje akaachia kicheko Kizito cha kuhesabu, “hooooo! dereva, kwanza hongera kwa kuondoa hiyo kero, sasa tuna weza kufanya mpango” alisema Ulenje kwa sauti fulani tulivu, ambayo mara nyingi hutumiwa na watu wenye uwezo mkubwa kifedha, na mipango endelevu ya kupata fedha, “nipo kwenye mpango, siwezi kuingia kwenye mpango mwingine” ilisikika sauti tulivu toka upande wa pili wa simu.

Ulenje ambae alihisi kuwa, kijana dereva amesha jua kuwa yeye ni kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi wa Ilala, hivyo ilikuwa ni lazima kumthibiti Deus Nyati, kabla hajafanya lolote la kijinga ambalo linaweza kujulisha jamii yeye ni nani na anashiriki mipango gani ya kiharifu, “hii ni kwaajiili ya usalama wako, maana sasa tupo njiani tunakuja hapo ulipo, ni kundi kubwa la polisi wenye silaha, , na unatakiwa kuondoka mara moja, hakika hautoweza kuchomoka mbele ya kundi kubwa kama hili, vinginevyo inabidi umwage damu nyingi za askari wasio na hatia, na kitu ninacho kijua kwako ni kwamba wewe sio muharifu na haupendi uharifu, vipi sasa tutaweka mpango ili na mimi nikusaidie kuondoka hapo?” aliuliza Ulenje kwa sauti yake ile ile ya kiboss, “huwa sivunji sheria zangu, labda wewe usikilize toka kwangu, waambie watu wako wasinisogelee, maana mimi sio muharifu, na kila kitu kinaenda kuisha salama” ilisikika sauti toka upande wa pili wa simu, sauti ambayo utulivu wake ulitaka kumshawishi Ulenje adhanie kuwa, ilikuwa ni swala la utani.

Ulenje ambae sasa alikuwa anaona magari ya mbele kabisa yana karibia kwenye njia ambayo walitakiwa kukata kushoto kuingia ndani ya msitu kwa kufwata maelekezo ya koplo Cheleji, alichekecha akili kwa haraka na kupata jibu, “sikia kijana, najua unanifikiria tofauti sana, ila ni wazi utahitaji msaada wangu, sisi tunakaribia kuingia kwenye hii njia ambayo inakuja huko uliko, cha kufanya wewe nenda ndani zaidi” alisema Ulenje, kisha akakata simu, kisha akaanza kuchekecha, namna ya kumthibiti Deus, na watu pekee wenye silaha nzito ni wakina Kadumya, yani UMD.

Baada ya kuwaza kwa muda mfupi, ndipo Ulenje alipompigia simu Kadumya na kumueleza juu ya kumshambulia Deus, huku akiwaelekeza njia atakayoitumia, na baada ya kumaliza kuongea na Kadumya ndipo Ulenje anaposikia muito wa redio call toka kwa Cheleji, akitangaza vifo vya askari wanne wa jeshi la polisi, na kwamba yeye Cheleji anahakikisha adui hawakimbii, hapo Ulenje akagundua kuwa, bado kijana wake hakuwa anamtambua adui yake ni nani, na kwamba sio Songoro ambae tayari alikuwa amesha poteza maisha na tayari dereva alishatoa tahadhari kwa askari yoyote atakae mfuata.

Hapo ndipo alipokuwa amempigia simu koplo Cheleji, ili kumjulisha kuwa wasimsogelee kijana yule hatari, baada yake wawaachie kazi hiyo wakina Kadumya, ambao tayari alishawapa taarifa za uwepo wa deus upande ule, ndio ule wakati Cheleji alikuwa anaongea na simu ndani ya lile jengo lisilomaliza ujenzi wake, “sikia Cheleji ondoa askari eneo hilo haraka sana, huyu ni Deus Nyati, yule dereva wa gari jeusi” alisema Ulenje kwa sauti yenye msisitizo, lakini hakusikia jibu au kitendo chochote ambacho kingeashiria kuwa, Cheleji alishamuelewa na saa anatekeleza.********

Naaam sijui tumuite Waziri, au aliekuwa Waziri wa ulinzi na usalama wa #mbogo_land, kwa king Elvis wa pili, mheshimiwa Dickson Chitopelah, au rais mtarajiwa wa #mbogo_land, kama alivyo kuwa anajiaminisha hapo, sasa alionekana akiwa anatoa macho kwanguvu ili kujaribu kumtambua mtu aliekuwa anaingia, mtu ambae ni wazi alikuwa askari wa jeshi la #mbogo_land, yani MLA jeshi ambalo hata yeye alishawahi kulitumikia, akikomea kwenye ngazi ya brigedia General, “bwana mkubwa, nadhani sasa umesha amini kuwa, tayari sasa upo sehemu ya kuvuna ulichopanda”Chitopela alimsikia yule jamaa akiongea na kwa haraka sana Chitopelah akaitambua ile sauti, kuwa ni ya General Sixmund.


Ilimchukiza na kumtia hasira Chitopela, mtu ambae asubuhi ya leo ametoka kumpigia saluti, halafu sasa hivi anamuongelesha kwa dharau kiasi hiki, lakini licha ya kuwa na hasira Chitopela, alijuwa fika kuwa, hawezi kumfanya lolote, zaidi ni kutafuta njia ya kujitoa katika hatari ya kufungiwa kwenye tumbo la ng’ombe wa chuma,l na kuwashiwa moto wa makaa ya mawe chini ya tumbo la ng’ombe yule.

Kwanza Chitopela akaachia kicheko fulani, ambacho licha yakujitahidi kiwe kikali, lakini kilimezwa na maumivu ya mwili, hivyo kiliishia tumboni, ujue vicheko kama hivi vina maana kubwa sana kwa mtu ambae yupo katika wakati mgumu kama huu wa Chitopela, maana ya kicheko hiki ni kwamba, Chitopelah alikuwa anachukua usikivu wa general Sixmund, ambae ni kweli atulia na kumsikiza alikuwa anataka kuongea nini, “general nadhani mpaka hapa unahisi kuwa tayari mume maliza kazi” alisema Chitopela, kwa sauti fulani ya kujikamua.

Hapo General Sixmund, akaona kuwa kuna umuhimu wa kupata habari zaidi ambazo zinaweza kuwasaidia kumaliza jukumu zito la kuangamiza kikundi cha UMD, “unazani kuna lolote unaweza kufanya bwana Chitopela?” aliuliza Sixmund, ambae sasa alikuwa amesha mfikia Chitopela, “Sixmund, kuna kitu lazima ukijue, ni kwamba kunikamata kwenu kutachochea mauwaji makubwa ambayo yataanza kutokea muda mfupi ujao, maana mimi nilipanga mapinduzi yasio na umwagaji damu, lakini msimamizi anaefuatia baada yangu hawezi kufanya mapinduzi kama nilivyopanga mimi” alisema Chitopela kwa kujiamini, maana bado alikuwa na dalili za kucheka kile kicheko chake, “ni nani huyo msaidizi wako, na sasa yupo wapi na askari wake?” aliuliza Sixmund.

Hapo kicheko cha Chitopelah kikakijirudia, “unadhani mimi ni mjinga kiasi hicho, yani nikueleze maficho ya watu ambao wanahitaji kuja kufanya mapinduzi, labda kwa msaada wako na wenzako ni kwamba, ukiachilia kuwa na watu wengi sana ndani ya serikali hii ya kipuuzi, ambayo unaendelea kuipigia magoti na kuisujudia kila siku, pia kuna silaha nzito ambazo kwa shambulio la kushtukiza litakalo fanyika hamuwezi kuzuia vifo vya raia wa nchi hii, kama mupo tayari tukae chini msikilize sisi tunahitaji nini” alisema chitopela kwa kujidai, “unadhani ni muhimu sana serikali kukaa chini na kikundi kidogo cha wahuni kama vile UMD?” aliuliza Sixmund kwa sauti ya taratibu, “pengine umesahau kuwa kukosekana kwangu ndani ya UMD, ndio chanzo cha mauwaji makubwa, ambayo yataishangaza dunia, na pia fahamu kuwa ni mimi pekee ndie mwenye uwezo wa kutoa amri kwa UMD na wakaelewa” alisema Chitopelah.

Sixmund alitulia kidogo, akitafakari maneno ya Chitopela, ukweli kichwani mwake Sixmund aliona kuwa ni maneno ambayo yalipaswa kutiliwa maanani na kufanyiwa kazi, hivyo baada ya kuwaza kwa sekunde kadhaa, Sixmund akamtazama Chitopela, “vizuri bwana Chitopelah, umefanya vizuri kutupa hiyo habari” alisema Sixmund, kisha akageuka na kutoka nje ya kile chumba, Chitopelah akimsindikiza kwa macho, huku akilini mwake akifurahia kufanikiwa kwa mpango wake, maana alimini kuwa, mpango huu, sio tu kuchelewesha wasimuue, pia ungempa nafasi ya kutoka kabisa kizuwizini, maana endapo wangekubari kukaa chini na kujadili amani kwa pamoja, yeye angetoa masharti mengi sana, ambayo yangemsaidia, ikiwa na kuomba uangalizi wa mataifa makubwa ambayo yange simamia usalama wake.********


Naaam koplo mwenye utiifu mkubwa kwa ASP Ulenje, akiwa bado na simu sikioni, alionyesha kushtuka baada ya kusikia kuwa kijana Deus Nyati, yani dereva wa BMW jeus S7, yupo maeneo yale, na kwa hali aliyoikuta pale sebuleni, Cheleji alijua kwamba, kijana huyo hatari yupo mule mule ndani ya jumba lile chakavu, anashtuka na kumtazama yule aliekuwa amesimama mbele ya mlango dhaifu wa mabati, ambae alikuwa anajaribu kuufungua, lakini kabla hajamueleza chochote, akasikia kishindo kikubwa cha “tihiii!” hapo Cheleji akageuza uso wake kutazama upande alioingia yule askari mwingine, hata kabla macho yake hayajapata uwezo wakutambua vizuri kilichopo mbele yake aliweza kuona kitu kama furushi likiwa hewani kuja upande wake, yani pale sebuleni na kujibwaga chini mita kadhaa toka alipokuwa yeye.

Sasa anaweza kuona kuwa ni askari wake, ambae alituwa akiwa mtulivu, hakujuwa kama ni amepoteza fahamu au amekufa, ile anamtazama yule mwingine amueleze kuwa watoke nje haraka, anamuona yule askari aliesimama kwenye mlango, akiwa anaanguka chini kama furushi la mbegu za viazi vitamu, huku pembeni akionekana mtu aliekuwa anakuja upande wake kwa mwendo wa haraka. ..…….ENDELEA


NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA AROBAINI NA NNE
MTUNZI: Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWA MATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA AROBAINI NA TATU: Sasa anaweza kuona kuwa ni askari wake, ambae alituwa akiwa mtulivu, akujuwa kama ni amepoteza fahamu au amekufa, ile anamtazama yule mwingine amweleze kuwa watoke nje haraka, anamwona yule askari alie simama kwenye mlango, akiwa anaanguka chini kama kufushi la mbegu za viazi vitamu, huku pembeni akionekana mtu alie kuwa anakuja upande wake kwa mwendo wa haraka. ..…….ENDELEA…

Kiukweli Cheleji alikuwa anajua sifa tabia na uwezo wa kijana yule, hasa anapoona adui yake anabunduki, hivyo basi kitendo bila kuchelewa, Cheleji ambae hakujisumbua kutumia bunduki yake, alijirusha usawa wa dirisha na kutokea nje, hakujali jinsi alivyojibwaga, wala simu yake iliyo anguka chini, akajiinua haraka, “njooni huku adui huyu hapaaaaaa” alipiga kelele Cheleji, huku anakimbia kwenda kutafuta maficho, akiacha askari wake ambao hawakuwa wanajuwla adui yao ni nani, na kwamba walidhania kuwa bado wanapambana na wakina Songoro, wakiwa wanakimbilia upande ule aliotokea Cheleji na kuanza kumimina risasi kupitia dirishani.

Hakika zilisikika kelele nyingi za mikohowo ya risasi za SMG, tukio lililodumu kwa dakika nzima, maana wengine walipoishiwa risasi walibadili mikebe na kuendelea kumimina risasi mfululizo, mpaka walipokoma kwa kuishiwa risasi, wakiamini kuwa, kwa risasi walizo mimina mule ndani, sio tu hao adui zao ila pia, hakuna kiumbe chochote mule ndani kitakachokuwa hai, kuanzia nzi mbu hata mijusi.

Lakini ile wanasitisha mapigo tu, ghafla wakasikia “pah! pah! pah!” ni milipuko ya risasi toka nyuma yao, huku wale wa mwisho mwisho, wakiwashuhudia wenzao wakianguka kama maroboti yaliyoishiwa chaji, huku na wao wakipokea vitu kama misumari yenye moto,l vichwani mwao na kuanguka kama mabua makavu ya mtama yaliyokutana na chikwakwa, kile kisu cha Jensen kwenye KIAPO CHA DAMU KWA DAMU niwazi adui yao alikuwa ameshahama eneo lile muda mrefu uliopita, na kutokea ubavuni mwao, kisha kuwafanyia shambulio la upande, yani Frank attack.

Naaaam wakati huo huo, askari waliokuwepo kwenye magari wakaanza kushambulia kule ilikosikika milio ya risasi, bila kuona wanae mshambulia, kuona hivyo, Cheleji akachomoka mbio, toka kwenye kichaka na kukimbilia yalikosimama magari akimini kuwa shambulizi la wenzake linge saidia kumkinga yeye na kuweza kufika kwenye gari, maana hakukuwa na namna zaidi ya kuondoka eneo lile.

Lakini haikuwa bahati yake, maana alisikia milipuko kadhaa ya risasi, sambamba na miali ya moto yenye kasi na nguvu ya ajabu ikigonga kwenye magari yao, huku wenzake kuanzia dereva na wale askari wengine wawili waliobakia, wakipoponyoka, toka kwenye magari na kuanguka chini, hapo Cheleji akajua kuwa kama asipo pambana, basi anaweza akapoteza maisha, hivyo akageuka haraka huku anaishika bunduki yake vyema.

Kitendo bila kuchelewa, Cheleji aliminya trigger kwa nguvu na kwa kuing’ang’ania, akifanya risasi zitoke mfululizo mpaka aliposikia kacha! ikimaananisha kuwa mkebe wa risasi ulikuwa tupu, hapo kwa pupa akachomoa magazine na ilikuwa imebebeshwa tatu kwa Pamoja, wakitumia mpira wa manati kuzifunga pamoja.

Alipomaliza kubadili mkebe wa risasi, akatazama upande ule hakuona dalili ya uwepo wa mtu yoyote alie hai, wakati huo anauona mwanga wa simu yake, ulioangaaza mita chache toka kwenye nyumba ile isiyo isha ujenzi wake usawa wa dirisha ambalo alitokea yeye, ni wazi ilikuwa inaita, wakati huo huo mianga ya taa za magari ilianza kuonekana upande wa barabarani, ikiwa imebakiza mita chache sana kuifikia ile njia panda ya kuingilia pale kichakani. ********

Yap! Milindimo ya risasi ilisikika umbali mkubwa sana, ukiachilia msafara wa mgari ya polisi na kundi la Marine special force waliokuwa relini, pia hata lile kundi la marine special force ambalo sasa lilikuwa linakaribia njia panda ya kisarawe na manero mango, nao walisikia milipuko ile kama walivyosikia UMD waliokuwa kilomita kama nne ndani ya msitu, na msafara wa MLA na askari wa jeshi la ulinzi la Tanzania, ambao sasa walikuwa wamesha maliza kisarawe mjini wanaelekea misitu ya visamvu kuelekea njia panda ya manero mango.

Lakini pia kuna watu wawili walioshuhudia tukio hilo kwa njia tofauti na ile ya wengine, wao maana wakati Ulenje akiwa ndani ya gari na simu sikioni mwake, anasikiliza mwanzo mpaka mwisho na jinsi milindimo ya risasi ilivyosikika ikirindima kupitia simu yake, huku mwana dada mrembo Veronica, akitazama kupitia screen kubwa mbele yake, inayoongoza camera za ulinzi, ambae aliweza kuona jinsi mtu anaemuita mpenzi wake, anaetarajia kumuita mume siku za mbele, akinyofoa roho za watu kama yupo kwenye mchezo wa kuigiza, maana kitu ambacho unatakiwa ufahamu ni kwamba, camera za ulinzi zilizofungwa kwenye nyumba hii, zilikuwa na kifaa ambacho kinaitwa night vision, ambacho husaidia kuona kwenye giza vizuri, kuliko hata aliekuwa eneo husika.

Naaam kwa kusikia milipuko ile UMD ambao bado walikuwa wamesimama wanapeana majukumu, wakaamini maneno ya Ulenje kwamba, dereva wa BMW alikuwepo maeneo yale, “haya jamani nadhani mmesikia wenyewe, kuwa windo letu lipo mbele yetu, cha msingi kumbukeni kuwa yeye ndie mwenye fedha ambayo itamfanya kila mmoja wetu kuwa mtu mkubwa ndani yaserikali yetu, kila mmoja wetu kujichagulia majengo mazuri na kumiliki gari analolihitaji, mke mzuri watoto wenye maisha mazuri” alisikika Kadumya, huku Kafulu akisubiri kusikia Kadumya akitoa tahadhari juu ya Veronica, “sasa basi mutakuwa katika makundi matatu, moja litakuwa na mimi moja kafulu na moja Kobwe, na wale watakao kuwa na mimi watakuwa katikati nyuma, kobwe atakuwa kushoto na kafulu kulia, kwahiyo tutakuwa katika mpango wa mbili juu, kwa maana ya two up fomartion” alisema Kadumya.

Naaam hapo yakiwa makundi matatu, yote yakiwa na silaha nzito, kisha wakajipanga kama walivyo amuriwa, lakini kabla amri ya kuondoka haijatolewa, Kafulu akadakia, “sikiliza tangazo toka kwangu” hapo wote wakatulia kimya, hata Kadumya akatulia kimya lakini akimshangaa Kafulu, maana hakutarajia kama atakuwa na lolote la kutangazia kikosi kizima kilichokuwepo hapa, “vyovyote itakavyo kuwa, kumbukeni kuwa, yule mshenzi yupo na fedha zetu,pamoja na mschana Veronica, ambae namuhitaji akiwa mzima kabisaaaaa, ana denia la kulipa kwangu” alisema kafulu, na kwa wale ambao hawakujuwla anamaana gani, hawakuwa na shaka lolote, ila Kadumya alitikisa kichwa kwa masikitiko, hakutaka kupingana na Kafulu kwa kuchelea kwamba, atazidi kumvunja nguvu ya kufanya jukumu la kuongoza askari, katika mpango wa kumkamata Deus na kuchukua fedha zao.

“haya sikiliza kutoka kwangu” alisema Kadumya, na utulivu ukaendelea kutawala, “wote kaa tayari kwa kuondoka” alisema Kadumya kwa sauti yake ya kikamanda, huku anawatazama wale askari wake waliokuwa katika vikundi vitatu, “ondokaaaaa” alisema Kadumya na hapo vikundi vikaanza kuondoka kwa kushika uelekeo, kama walivyo elekezwa, wakati huo kwa mbali waliweza kuona nuru za taa za magari mengi, yakija upande wao, lakini yalikuwa mbali kidogo, ni kama kilomita nne toka pale walipokuwepo wao. *******

Naaam! akiwa ametoka amesikia majibizano ya risasi kwa kupitia simu ya Cheleji, ambayo ilikuwa wazi muda wote wakati risasi zikisikika, bwana Ulenje ambae alijuwla fika kuwa, wakina Cheleji wanapambana na Deus Nyati, hata mapigano yalipo tulia akajaribu kuita, “hallow Cheleji, cheleji unanisikia, hebu jibu chochote “wanapambana na Deus Nyati” alijisemea Ulenje, akiwa bado ameweka simu sikioni, lakini hakupata jibu lolote.

Akiwa ameingiwa na hofu, juu ya askari wake, anakata simu na kuipiga tena, nayo inaanza kuita mara moja, na kwa bahati nzuri licha ya kuita kwa muda mrefu, lakini baadae ikapokelewa, wakati huo tayari walikuwa wamesha kata kona kuelekeea upande wa kushoto ambako wakina Cheleji walikuwepo. *******

Kitu ambacho Ulenje hakujua ni kwamba, mara baada ya Cheleji kuifikia simu aliinama haraka na kuikota, lakini ile anainuka tu, akashtuka kuona kuna mtu amesimama mbele yake, ile anaishika vizuri bunduki yake ili kumshambulia mtu huyu ambae licha ya uwepo wa giza, lakini aliweza kumtambua kuwa ni kijana Deus Nyati.

Hakika haikuwa bahati yake bwana Cheleji, maana aliweza kuhisi kitu chenye ncha kali kama kiwembe kiki pita shingoni mwake na kumkata mawasiliano ya juu na chini, na kumfanya agande, kama vile ameamrishwa na mkuu wa gwaride fulani, huku damu zikimtoka kwa wingi shingoni mwake, sekunde kadhaa zilitosha kwa Cheleji kuganda wima, maana kilichofuatia ni kuanguka kama mtu aliokatwa kwa msumeno wa nyororo, wakati huo tayari mianga ya gari ilikuwa imesogea, na kubakiza kama mita mia mbili au mia tatu, kufika pale,

Deus anaokota simu, ambayo bado ilikuwa inaendelea kuita, anatazama jina la mpigaji na kuona kuwa alikuwa ni afande Ulenje, kama ilivyokuwa kwa yule wa kwanza, Deus akaipokea na kuiweka sikioni, “Cheleji vipi mmesha muuwa Deus Nyati?” aliuliza Ulenje kwa sauti yenye hofu na wasi wasi mkubwa.

Kwanza kilianza kicheko, kabla ya mguno mdogo mwepesi, “ina maana afande Ulenje huku nielewa nilipokuambia kuwa waambie askari wako wasinisogelee?” aliuliza Deus kwa sauti tulivu huku anaingia ndani ya ile nyumba chakavu, hapo Ulenje mwenye alijikuta anaachia kicheko cha machungu, “inamana umewauwa askari wote, Pamoja na Cheleji” aliuliza Ulenje kwa sauti iliyojaa machungu, ni swali ambalo bila shaka kama kuna aliesikia zaidi yake basi mwili ulimsisimka, “nadhani kuna kitu hujawahi kusikia kuhusu mimi Ulenje, mimi ni mtu wakutimiza kile ninacho ahidi” alisema Deus kwa sauti yake ile ile ya upole, huku anatembea haraka kuingia kwenye kile chumba cha mlango wabati, akiwa na MSG kisu chake mkononi.

Ni wazi maneno yake yalitikisa moyo wa Ulenje, ambae sio tu kuumia, ila pia alikasirishwa sana, “jiandae we mpumbavu, leo ndio mwisho wako, unakamtwa na nina kuuwa mwenyewe kwa mkono wangu” alisema Ulenje kwa sauti iliyojaa machungu, hapo Deus akaachia kicheko hafifu sana, “dah! sidhani kama utaweza kufanya hivyo, maana mpaka sasa umebakiza muda mfupi sana, wakulitumikia jeshi kama ACP, zaidi ya hapo muda mfupi ujao unaenda kuwa raia katika gereza lolote ambalo kuna watu kibao uliowafunga kwa uonevu, na hiyo ni afadhari yako, vingenevyo unaweza ukawa tayari umekatwa shingo yako, maana unastahili kifo, kutokana na uovu wako” alisema Deus kwa sauti yake ile ile, ungesema anaongea kuhusu jambo la kawaida, kisha akakata simu na kuingia kwenye mlango mdogo, uliopo kwenye uvungu wa kitanda.*******

Naaam Major General Sixmund anaonekana akiibukia kwenye kolido refu ndani ya ile nyumba ya MLA, waliyo fanyia mahojiano na bwana Ashraff, anaungana na kanali Jastin, “Jastin kuna kazi ya kufanya, wasiliana na vikosi vidogo ya Amour AR, wakae tayari kusubiri majukumu” alisema Sixmund, huku anafungua mlango wa moja kati ya vyumba vingi, vilivyo jipanga kwenye ile kolido, kisha wote wawili wakaingia kwenye chumba kile kikubwa chenye muonekano wa ofisi, “ndio afande” aliitikia kanal Jastin, huku anatoa simu yake na kuanza kupiga simu, wakati huo Sixmund nae akiwa anafanya hivyo hivyo.

Wakati Kanal Jastin akiwa anawasiliana na wakuu wa vikosi vidogo vidogo, vyenye ukubwa wa Troop, Sixmund alikuwa anapiga simu kwa captain Amos Makey, ambae alipokea mara moja, “nipe maendeleo Makey” alisema Sixmund, mara baada ya simu kupokelewa, “afande mpaka sasa, inaonyesha UMD wapo wengi sana huku Tanzania, wanaendelea kupambana na jeshi la polisi na kusababisha maafa makubwa kwa askari hao, ila sisi tunaenda kukutana na Deus Nyati, ambae anataka kutukabidhi doctor Veronica mtoto bwana James ili tuanze safari mara moja” alijibu captain Amos Makey, ambae ni wazi alikuwa ndani ya gari lililokuwa linatembea, “ok! hakikisheni munapata habari kamili, na ikiwezekana kuondoka mara moja baada ya kumpata Veronica” alisema Sixmund, kabla hajakata simu. ..…….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI Unao Kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA AROBAINI NA TANO
MTUNZI: Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA AROBAINI NA NNE: “afande mpaka sasa inaonyesha UMD wapo wengi sana huku Tanzania, wanaendelea kupambana na jeshi la polisi na kusababisha maafa makubwa kwa askari hao, ila sisi tunaenda kukutana na Deus Nyati, ambae anataka kutukabidhi doctor Veronica, mtoto bwana James ili tuanze safari mara moja” alijibu captain Amos Makey, ambae ni wazi alikuwa ndani ya gari lililokuwa linatembea, “ok! hakikisheni munapata habari kamili na ikiwezekana kuondoka mara moja baada ya kumpata Veronica” alisema Sixmund, kabla hajakata simu. ..…….ENDELEA…

Mara baada ya kukata simu, Sixmund akapiga simu kwa king Elvis, ambae pia kwa usiku ule hakuwa amegusa hata lepe moja la usingizi, maana hata simu hii ilipoita mara moja tu ya pili akaipokea, “ndio general, maana leo nimesha kubali kuwa hakuna kulala” alisikika Elvis, kwa sauti yenye uchovu mwingi wa usingizi, “naamini utalala vyema kesho baada ya hili kuisha” alisema Sixmund kwa sauti yenye utani kidogo, “unaamini swala hili ni la leo tu?” aliuliza Elvis kwa sauti yenye mashaka, “mtukufu mfalme, naamini kwa umahili wa kijana Deus, UMD waliopo Tanzania wataangamia, na kitu cha kufurahisha tayari tupo na kiongozi wao, pili muda mfupi ujao Deus anaenda kumkabidhi Veronica kwa MLA, na wao wataanza safari ya kuja #mbogo_land, na bwana James atatoa ushaidi wake” alisema Sixmund, “hooo sawa, vipi kuna lolote lililokufanya unipigie simu usiku huu?” aliuliza mfalme Elvis.

Na hapo ndipo Sixmund, akaanza kueleza kuhusu maongezi yake na Chitopela, “na amesisitiza sana kuwa yeye ndie pekee anaeweza kutuliza UMD wasitishe mipango yao ili kunusuru mauwaji makubwa ya raia” alimaliza Sixmund kuelekezea, “ok! ni wazo zuri, au wewe una mpango gani Six?” aliuliza mfalme, “mtukufu mfalme, mimi na wazo moja tu, nalo ni kumfanya atuambie kikundi kukubwa kipo wapi na kinasimamiwa na nani, maana wote tumeshuhudia jinsi alivyoweza kufarakanisha serikali na raia, pia kuwafanya baadhi ya wanausalama na askari wetu, waichukuie serikali” alisema Sixmund, “kwahiyo unataka nifanyaje Six, aliuliza Mfalme, “mtukufu mfalme, tunaomba kibali chako tuanze mahojiano na Chitopela” alisema Sixmund, “ok! kibali kimetolewa, ila kumbukeni kuwa nahitaji kukutana na Deus Nyati na bwana Frank” alisema Mfalme na bila kuongeza neno akakata simu.

Hapo General Sixmund akamtazama kanal Jastin, “huyo mjinga aingie chini ya handaki, wachukue watesaji wa special force, wamchangamshe kidogo, wasimuue ila wamfanye aseme kundi la askari lipo wapi na kiongozi wao ni nani” alisema Sximund na hapo Jastin akapiga salut na kugeuka nyuma tayari kuondoka, “Jastin, tumieni kila kitu kinachopaswa kutumika, ikibidi tumieni mtomolelo” alisema Sixmund, akitaja kifaa ambacho hata mimi nikikitaja au kusikia kinatajwa hakika mwili unasisimka, maana matumizi yake sio mazuri sana.********

Yap! Vikundi vya kijeshi na vile vya kiusalama, vilizidi kusogea maeneo husika, tayari magari ya ya ubalozi wa #mbogo_land, pamoja na yale ya jeshi la ulinzi, yalisimama njia panda ya kibaha, wakiyakuta magari ya jeshi la ulinzi Marine Special Force, yakiwa yameegeshwa kwa kificho katika eneo lile la njia panda, kama ukiwa makini ungeweza kuwaona askari wa kundi hilo maalumu lenye askari wenye mafunzo ya kiwango cha juu cha kivita, walikuwa wanajipanga kwenye vichaka na maficho yaliyozunguka eneo lile, hata mzee James na baadhi ya askari waligundua uwepo wao, baada ya kusimama na kumuona kamanda mmoja mwenye cheo cha major akibuka toka kwenye kingo za daraja dogo lililopo pale njia panda.

Captain Amos akashuka toka kwenye gari na kumsogelea yule Major, ambae ni wazi alikuwa anatafuta kiongozi wa ule msafara, “jambo afande” alisalimia captain Amos, na yule Major akaitikia, “jambo captain, tupo hapa kuungana na nyie kwaajili ya kumsubiria Deus Frank Nyati, pia kutoa ulinzi endapo eneo hili litavamiwa” alisema yule major, akieleza dhumuni la uwepo wao eneo lile, “ndiyo afande hatuna cha kupinga, japo uwepo wenu ni uvunjifu wa mkataba wangu na Deus Nyati” alisema Amos Makey, “achana na huo upuuzi wa sheria, nani alisema muharifu kama huyu anaweza kuwa na sheria zake, yeye atafuata sheria zetu” alisema yule major, kwa sauti ya kujiamini, “sawa, lakini tunaomba mtuachie tumalizane nae kwanza, kisha muanze operation yenu juu yake” alisema Makey, na Major akakubaliana nae, kisha kila mmoja akashika nafasi yake, wa pale pale akabikia kuwa wa pale pale na wamafichoni akawa wa mafichoni.*******

Yaaap! Mwana dada Veronica, mwenye degree ya uganguzi, ambae alikuwa ameshuhudia mauwaji makubwa yaliyofanywa na mchoraji wake, mara anaweza kuona magari mengi ya polisi yakija toka upande ule ule yalipotokea magari mengine, “haooo wengine wanakuja, jamani atakamatwa” alisema Veronica kwa sauti yenye wasi wasi na uoga wa wazi.

Lakini wakati anajisemea hivyo pia kwenye kipande cha video iliyo andikwa cam 4, anaona kwa mbali dalili ya watu wanao tembea kuja kule waliko wao, “wengine hawa huku, atafanyaje jamani, rudi ujifiche ndani” anasema Veronica, ambae kiukweli hakuonyesha kushtushwa na mauwaji ya kutisha aliyoyafanya Deus, ila anaonekana kuhofia usalama wa kijana huyu, ambae sasa ni mpenzi wake, hivyo ni wazi alisha zowea kile anachokifanya mpenzi.

Sekunde chache baadae, akiwa bado anawaza juu ya usalama wa mpenzi wake, mara anaona mlango unafunguliwa na Deus akaingia ndani, “tunatakiwa kuondoka mara moja, kabla hawaja gundua maficho yetu” alisema Deus akionekana mwenye uharaka wa ajabu, “tutatokaje na wao wamesha karibia na wengine wale kule” alisema Veronica akionyesha camera namba nne, Deus nae akatazama, “pumbavu ni UMD, wamesha pewa habari na huyu Ulenje mshenzi” alisema Deus, huku anaweka simu ya Cheleji kwenye mfuko alioweka simu ya Songoro, “lakini kuna kitu nita wafanyia, wataisoma habari kwenye vichwa vyao” alisema Deus, huku anaiweka sawa bunduki yake na kuikagua risasi, aliporidhika akaipachika kifuani, “tuondoke sasa” alisema Deus, huku anamshika mkono Veronica na kuanza kutembea nae kuelekea kwenye mlango wa kutokea.

Hiyo ndiyo ilikuwa safari ya kutoka nje, Deus akihakikisha anafunga milango, kila walipo toka, Veronica alishangaa kuona wanayaacha magari na kutooka nje kwa kutumia mlango wa kutokea mgari, uliotengenezwa kwa mfumo wa lift, hata walipo maliza kupanda juu akafunua kipande fulani cha bati na hapo wakakutana na kitu kama main switch, Deus akabonyeza off, ikimaanisha kuwa umeme umekatwa nyumba nzima ya kule chini, akapekuwa pembeni na kutoa tochi, ambayo hakuiwasha, baada yake, wao wakapenya kwenye lile gate dogo la mabati, na kuzunguka nyuma ya nyumba, kisha wakaingia kichakani na kutokomea magharibi, kule ambako Veronica aliona kuna watu wanakuja.

Naam wakati wao wanaingia kichakani wakasikia ngurum za magari ya polisi yakiwa karibu kabisa na ile nyumba yao. *******

Haya sasa, huko TT City #mbogo_land, mambo yalikuwa tofauti na vile Chitopela alivyodhania kuwa ataweza kuwashawishi MLA na serikali ya mfalme Elvis kumuacha huru ili aweze kuongea na UMD, huku yeye lengo lake likiwa ni kupata uhuru ili aweze kukamilisha lengo lake la mapinduzi.

Lakini akiwa na mawazo hayo, ndani ya kile chumba kifinyu chenye giza nene na sakafu yenye ubaridi wa ajabu, huku akiwa amevalia joho la kulalia, mara akaona tena lango lina funguliwa na wakaingia askari wanne wa MLA walioziba sura zao kwa vitambaa vyeusi wakiachia macho pekee, Chitopela anahisi kuwa mpango wake umeanza kufanya kazi.

Moja kati ya wale wanne anamfunga kitambaa cheusi usawa wa macho yake, hilo bado alimfanyi Chitopela kuamini kuwa mpango wake umeshindwa, anashikwa mikono huku na huku, anakokotwa kutoka nje ya chumba, hajui wanampeleka wapi, anatamani kuuliza lakini anakaa kimya, maana anaamini anapelekwa sehemu ambayo anaenda kuachiwa huru kutokana na mpango aliousuka.

Safari inaendelea kimya kimya, hata wanaanza kushuka ngazi nyingi na defu kiasi, chitopela, anaamini kuwa jengo aliloletwa japo hakulifahamu lipo sehemu gani, kwamba ni ghorofa na sasa wanashuka gazi, anawaza hivyo mpaka wanapo ifikia sakafu nyoofu, ikionyesha wamesha fika chini, Chitopela anagundua kuwa bado wapo ndani na sio nje kama alivyodhania, anajipa moyo kuwa walikuwa kwenye kolido la kutokea nje, hata walipoufikia mlango fulani ambao unafunguliwa na kuingia ndani yake, kisha akatolewa kitambaa usoni na kujikuta akiwa ndani ya chumba chenye mwanga hafifu, chumba ambacho muonekano wake ulishtua moyo wa Chitopela, ambae alizungusha macho yake kutazama ndani na kujionea vitu ambavyo ukivitazama kwa haraka ungedhania ni kiwanda cha kutengenezea masufuria au majiko ya bati, maana kulikuwa na vifaa vingi vya kukatia na kugongea kama vile nyudo, misumeno, tindo na makoleo, vingine vya kuchomea, kama vile spok zenye ncha kali, bisibisi za kila aina, vitu ambayo vinge kushangaza ni vifaa kama vile vile nondo zenye ncha kali zilizo ning'inizwa juu kwa kutumia minyororo kama vile nondo za buchani, pia kitu chenye tobo uvunguni, na jiko kubwa la mkaa, ambalo muda huu lilikuwa limekolea moto vibaya sana, ungesema kuna mtu anafanya biashara ya nyama choma mule ndani, pia ukichilia hayo yote kulikuwa na vitu viwili ambavyo vingekushangaza hata wewe.

Moja, ni kitu mfano wa mgongo wa ng'ombe au farasi lenye ukubwa wakimo cha cha mbuzi, ambavyo lilikuwa na vitu kama vifunguo vya mikanda ya chuma iliyokuwa inaning'inia juu na pembeni, na kitu cha pili ni banda lenye paka wawili, ambao ukiwatazama vizuri hawakuwa na meno kabisa, ukiachilia hilo ni wale watu wawili, wenye miili mikubwa waliovalia vinyago vya kutisha.

Pengine Chitopela alishajua dhumuni la chumba kile na kazi ya vifaa vile, maana alionekana kutoa macho ya mshangao yaliyochanganyika na uoga wa hali ya juu, japo alionekana kujikaza kidogo, "sidhani kama hii itafanya kazi, nadhini mshauri wa mfalme ni hatari kuliko UMD, maana haitakii mema nchi hii na anapenda kuona machafuko yakitokea" alisema Chitopela huku anajitahidi kuachia kicheko ambacho kilimezwa na pumzi na uoga, "labda ni kuambie kitu rais mtarajiwa wa #mbogo_land, wewe ndie unaetakiwa kuiokoa nchi hii, kama ulivyoanza kuibomoa, ndio maana tumekuja hapa kukushawishi uongee yale tunayo hitaji kuyajua" alisema mmoja kati ya wale watu wawili wenye miili mikubwa walio valia vinyago.

Nadhani Chitopela alihisi kuwa vile ni vitisho, vyenye lengo la ushawishi wa kumfanya aseme kile ambacho alimueleza Sixmund kuwa anakifahamu, ambayo ni sehemu askari wapo na wanaongozwa na nani, hivyo Chitopela akaona kuwa anatakiwa kuwa imara, akilegea kidogo hatokaa atoke mule ndani, na mwisho atashtakiwa na kuhukumiwa kifo kama ilivyo sema sheria ya uhaini kuwa adhabu ya msaliti wa nchi ni kifo ndani ya tumbo la ngombe wa chuma, maana bwana chitopela alicheka kidogo, "mnadhani ni rahisi hivyo, vipi kama nitakufa kabla sijawaeleza munachotaka?" alisema Chitopela kwa sauti yenye dharau kiasi fulani.

Hapo ile mijitu ambayo zamani ilikuwa inaitwa power, ikatazamana kwa sekunde kadhaa kisha wote kwa pamoja wakaangua kicheko kikubwa sana, tena kibaya kama vile kilio cha mtu alieumwa na nge sehemu za siri, "ok! hebu tuone uvumulivu wako mheshimiwa rais" alisema mmoja wao, kisha akatoa ishara fulani kwa wale askari wanne waliokuja nae, ok tutarudi kumuona mheshimiwa Chitopela, hebu turudi tanzania tukajue kinacho endelea.*********

Tanzania dar es salaam mambo yalikuwa yanazidi kupamba moto, marine special force kundi la kwanza likiwa karibu kabisa na reli, ambayo ipo mita chache toka ilipo nyumba ya bwana Deus Nyati, lilikuwa limetulia kimya kabisa, wakisubiri amri ya kusonga mbele kuelekea njia panda, ambako wenzao walikuwa wameelekea huku wakitazama magari ya polisi yaliyokuwa yanatokomea porini upande wa magharibi.

Magari ambayo inatupasa twende nayo sambamba ili kuona kilichotokea, na tunaona yakiwa yamesimama mita mia mbili toka pale ilipo nyumba ya Deus Nyati, yani walisimama pale kwa koplo Othman, ambae alikuwa na miili mingi ya watu waliovalia mavazi ya kiraia, "hawa ni wakina nani, nao ni UMD au wengine" aliuliza Nyambibo, lakini kabla Othman hajatoa jibu, akawahi kamanda mwingine wa mkoa wa Konondoni, "nadhani ni wale walio onekana wamevamia hotel wakiwa na silaha, wakimshambulia yule kijana Dereva" alijibu hivyo na wote wakakubaliana nae, "inaonyesha walikuwa na ugomvi na dereva, kama sio walikuwa wanasaidia UMD" alisema Kamanda wa mkoa wa kipolisi temeke, wakati huo Ulenje akiwa anaonekana kujawa na hofu kubwa, kama sio lile giza lililokuwepo basi wenzake wangekuwa wamesha tambua wasi wasi wa Ulenje, ambae maneno ya Deus nyati yalikuwa yanajirudia kichwani mwake, "kama sio kukata kichwa chako" ilimuogopesha sana Ulenje.

"sasa huku walikuwa wanafuata nini, wakati hawakuwa wanakimbizwa na polisi yoyote, maana polisi walikuwa busy na dereva wa gari jeusi?" aliuliza Nyambibo, "inawezekana walikuwa windo lao lipo maeneo ya karibu, nadhani unakumbuka ujumbe tuliopewa kuwa popote atakapoonekana Deus Nyati asishambuliwe, maana jeshi la ulinzi linamuhitaji akiwa hai" alikumbusha RPC kinondoni….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao Kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA AROBAINI NA SITA
MTUNZI: Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA AROBAINI NA TANO: "sasa huku walikuwa wanafwata nini, wakati hawakuwa wanakimbizwa na polisi yoyote, maana polisi walikuwa busy na dereva wa gari jeusi?" aliuliza Nyambibo, "inawezekana walikuwa windo lao lipo maeneo ya karibu, nadhani unakumbuka ujumbe tuliopewa kuwa popote atakapoonekana Deus Nyati asishambuliwe, maana jeshi la ulinzi linamuhitaji akiwa hai" alikumbusha RPC kinondoni….ENDELEA…..

Ambae baada ya hapo akamgeukia Othman, "ok! koplo askari wengine wapo wapi?" aliuliza nyambibo, huku anamtazama Othmani ambae kama wange mtazama vyema alikuwa amejawa na wasi wasi, maana alijua kuwa wanachokifanya hakikuwa sahihi, "wameelekea huko mbele, walikuwa wanawafatilia wenzetu waliokuwa wanawakimbiza maadui" alijibu Othman.

Baada ya jibu hilo, ikatolewa amri ya kusonga mbele na magari yakaendelea kusonga mbele, ambapo hatua chache mbele wakakutana na miili mingine ya askari ikiwa imelala barabarani, hii iliwashtua sana, hasa kamanda Nyambibo, ambae alitoa amri ya kusonga mbele, huku wakiacha gari moja lenye askari watano waipakie miili kwenye gari.

Magari yalisonga kwa kasi ya ajabu, pasipo kujua kuwa walikuwa wamesha karibia eneo la tukio, huku askari wakiwa na tahadhari kubwa sana, maana hawakujua adui yao yupo upande gani na ana uwezo kiasi gani, ukichukulia ndani ya usiku mmoja tayari wenzao kadhaa walisha poteza maisha.

Naam magari yanaibukia kwenye eneo la wazi, lenye nyumba ambayo ilikuwa haijamaliza ujenzi wake, ambapo gari la mbele lilisimama kwa brake za ghafla baada ya kuona magari mawili mbele, huku magari mengine ya nyuma yakisimama kwa mtindo huo huo, hali iliyozuwa taharuki na askari wakianza kuruka hovyo hovyo toka kwenye magari na kukimbilia vichakani kutafuta maficho sambamba na wakuu wao wakidhania kuwa adui ameonekana huko mbele, lakini wakashangaa kuona waliokuwa kwenye gari la mbele, wakishuka toka kwenye gari na kuanza kutembea kuyafuata magari ya mbele, ambayo yalikuwa yameeshambuliwa na risasi chache.

Hiyo haikuwa shangazo kwao, ila walishangaa na roho zao sekunde chache baadae, baada ya kuona miili ya watu wanne waliokuwa wamelala chini pembeni ya magari yao, huku wakiwa wanachuruzika damu toka kwenye matundu ya risasi, kabla hawaja maliza kushangaa na kunung'unika wanaona miili mingine mbele yao, ina washangaza zaidi, hasa pale wanapo tazama mbele ya ile nyumba chakavu, ambapo waliona askari wengi walikuwa wamelala chini pembeni ya silaha zao, "mama yangu, nini hiki?" ilimtoka Nyambibo aliekuwa anatazama jinsi askari wake walivyo uwawa kama kuku waliotiliwa sumu, hakika alisahau hata kutoa amri ya kufanya msako eneo, kitu ambacho kilifanywa na RPC temeke, "zunguka eneo haraka, chochote utakacho kuta halali yetu" alisema RPC Temeke, na hapo askari wakaanza kuzunguka ile nyumba kwa tahadhari kubwa, huku wengine wakiwa wanatazama ile miili kwa maana ya kuikagua wakisaidiana na wakuu wao.********

Yaaap sasa turudi, #mbogo_land, pale Treanch Town City, kwenye nyumba ya siri ya MLA, katika chumba kilichopo chini ya jengo hilo kubwa la kisasa, ambako kila tunapo zidi kukisogelea chumba hicho tuna sikia sauti za mvumo wa upepo wa vuuuup!, ukifuatiwa na kishindo cha waaap!, ikimaliziwa na kelele za maumivu makali.

Tunapata hamu ya kuona kinachotokea, tunaingia ndani na sasa tunamuona bwana Chitopela akiwa uchi kabisa, amelala juu ya lile sanamu mfano wa mgongo wa ng'ombe, lenye kima cha mbuzi, huku akiwa amefungwa kwa vibanio vya chumba, shingoni, kiunoni, mikononi na miguuni, huku wale jamaa wawili wenye miili mikubwa na vinyago vya kutisha wakiwa wamesimama kushoto na kulia mwa Chitopela, huku wameshika mijeredi mirefu iliyotengenezwa kwa waya wa kopa.

Walichokuwa wanakifanya ndio kilitisha sana, maana mmoja alitulia mjeredi ukiwa chini, wakati mwenzie akiwa ameinua mjeredi kwa kiwango cha nyuma ya mgongo wake kisha anaushusha kwa kasi ya mia mbili kilomita kwa saa, vuuuuup nakukita mgongoni kwa Chitpela, waaap "mtaniuwa jamaniiii heeeee!" ilikuwa ni kelele ya kilio cha Chitopela, kilicho ambatana na maumivu makali kupita kiasi, lakini kama vile hawakuwa wanasikia kilio cha Chitopela, mtu ambae masaa machache yaliyopita alikuwa anasimama kama waziri wao, mwingine tayari alikuwa ameshainua mjeredi wake na kuhushusha kwa Chitopela, kama alivyofanya mwenzie ambae pia sasa alishainua mjeredi na kuushusha, na kila mjeredi uliposhuka mgongoni uliacha alama ya mchirizi ambao ulianza kutoa damu.

Mizunguko sita ya mijeredi ilitosha kukomesha kilio cha Chitopela, sio kwamba hakusikia tena maumivu, ila ni kwamba alishapoteza fahamu hapo kipigo kikasitishwa, "mfungueni mfungeni kwenye kiti cha mapenzi" alisema mmoja kati ya wale wachapaji, na hapo wale askari wawili kati ya wale wanne waliomleta chitopela wakamfungua chitopela toka kwenye mgongo wa ng'ombe, wakimnyakuwa juu juu, mpaka kwenye kiti chenye uwazi chini na kumfunga mikono na miguu usawa wa mapaja na kumuacha akiwa amezimia korodani zikiwa zina ning'inia kwa chini pale kwenye uwazi wa kiti sehemu ya kukalia.*******

Sasa turudi misegese, kule porini nje ya jiji la dar es salaam tanzania, ambako sasa Deus aliekuwa na mwanadada Veronica mita kadhaa, toka kwenye ile nyumba yake wamejificha wana watazama polisi waliokuwa wanachachalika kukuzunguka na kuikagua ile nyumba, huku wakipeana report, waliweza kusikia kila kitu na kuona baadhi ya matendo yao, "mkuu kuna watu wengine huku ndani" ilisikika sauti ya askari wa jeshi la polisi, "afande mmoja ni muhalifu mkubwa anaefahamika, ni bwana Uled Songoro alisema mwingine.

Wakati huo huo ikasikika report nyingine, "afande kuna chumba kinaonyesha kuwa kuna mtu anaishi humu" kwakuona hivyo Deus akaona kuwa atachelewa mpango wa wake wa kumpeleka Veronica kwa wazazi wake, hivyo akaachana nao na kuanza kujipanga na Veronica wake, "sikia Vero nitaenda kukuacha pale mbele, utanisubiri hapo mpaka nitakaporudi, usiondoke atakikitokea nini, lazima nitarudi kukuchukua" alisema Deus na Veronica akaitikia kwa kichwa, kukubaliana na mpenzi wake huyu.********

Naaaam, nusu saa baadae Chitopela anashtuliwa na maji ya baridi yaliyomwagwa mwilini mwake, anashtuka na kujikuta akiwa amekaa kwenye kiti ambacho ile sehemu ya kukalia ilikuwa wazi, kama vile yupo chooni huku korodani zake zina ning'inia, anatamani aziweke vizuri lakini anashindwa maana alikuwa amefungwa mikono na miguu, anainua macho yake anawaona wale jamaa wawili wakiwa mbele yake, "haya muheshimiwa raisi, nadhani sasa unaweza kujibu maswali yetu, kundi la askari lipo wapi?" aliuliza mmoja wao na hapo Chitopela, akatulia kidogo akitafakari kwamba akitoa jibu lazima atakuwa ameshapoteza uwezekano wa yeye kutoka mahali hapa, na pengine kuuwawa kabisa, hata hivyo ukweli halisi ni kwamba hapa kuwa na kundi lililosalia, baada ya wote kuuwawa kule kambini kwao na wengine wapo tanzania wakimsaka Deus wachukue fedha za kununulia silaha.

Ukweli hakuwa na ujanja zaidi ya kuleta kiburi ili waamini kuwa anacho anachojivunia, "mnadhani nikifa mimi peke yangu ni hasara kwa mapinduzi tunayo yatarajia, tena mapindu ambayo yataleta mauwaji makubwa hapa nchini" alijibu Chitopela kwa sauti iliyojawa na uchovu mkubwa wa maumivu, "tunakuuliza tena bwana Chitopela, kabla hatujakuletea mrembo akunyonye korodani, kama walivofanya wale warembo kule porini, kundi lako liko wapi na lipo na nani?" aliuliza tena yule jamaa, "ni vyema mkitambua kuwa sito wajibu chochote mpaka niongee na Sixmund, nimuambie kuwa hakuna kitu zaidi ya UMD kukaa meza moja na serikali na kuongea juu ya amani ya nchi hii" alijibu Chitopela, na hapo ni kama alifungulia kile kicheko cha kukera toka kwa miamba hii miwili.

"kaka nadhani mheshimiwa anahitaji mrembo wa kumburudisha" alisema mmoja wao, huku anafuata bakuri lililokuwepo juu ya meza ya chuma, kisha akasogea nalo pale alipokwepo chitopela na kufamnya bwana Chitopela aisikie harufu ya samaki wabichi, ni kweli ilikuwa ni shombo la samaki wabichi, aligundua ilo, mara baada ya yule jamaa, kuanza kupakaza ile shombo kwenye korodani za Chitopela zilizokuwa zinaning'inia uvunguni mwa kiti kile, "unafanya nini wewe" aliuliza Chitopela, huku akiwa mwenye wasi wasi na uoga mkubwa, maana hakujua maana ya kitendo kile, "subiri uone bwana Chitopela" alisema yule aliekuwa amesimama, huku anatembea kuelekea kwenye banda dogo la kisasa lenye paka wawili wakubwa wasio na meno, akafungua kidogo na kumtoa paka mmoja kisha akamuachia.

Hapo yule paka akunusa mara mbili, moja kwa moja akakimbilia kwenye vungu ya kiti alicho kalia Chitopela, hapo chitopela alishtuka nyanya zake zikizama mdomoni kwa paka, ambae sijui alikuwa anawaza nini, maana alipozidumbukiza mdomoni tu, akaanza kuzivuta kwa nguvu kwa kutumia fizi zake, lakini zikateleza na kutoka mdomoni, paka hakukubali kushindwa akadumbukiza tena zile kengere na kuzibana kisawa sawa, hapo maumivu makali aliyasikia bwana Chitopela, ambae alipiga kelele kama mtoto kwa maumivu aliyo yasikia, lakini hakuna aliemsikia wala kumuonea huruma, na yeye hakukata tamaa, hakuwa tayari kueleza chochote maana hakuwa na ukweli wowote wa kueleza.

Kiminyo cha paka kibogoyo, kilikoma baada ya chitopela kuzimia kwa mara ya nyingine, ikiwa ni mzimio wa tatu kwa usiku huu mmoja, wale jamaa wakatoa paka na kumrudisha bandani huku wakiwarushia chakula maalumu chenye radha na harufu ya samaki, "huyo muacheni hapo hapo, wewe andaa mtomolelo alisema yule mmoja.**********

Naaaam! makundi matatu ya UMD katika mwendo wa msambao, yani walitawanyika mwanzo mwisho mwa eneo ambalo walikusudia kulichunguza, katika mpango wa mbili juu, waliendelea kusonga mbele huku wakiwa makini kuangalia pande zote kuona kama kuna sehemu Deus Nyati atakuwa amejificha baada ya kuwaona maana walijuwa lazima angekimbilia upande waliopo wao.

Lakini wakiwa wanazidi kutembea mbele, mara ghafla wakashtuka kusikia "pah! pah! pah" ilikuwa ni milio ya risasi iliyoshambulia kundi la kulia mbele, "tumepigwa shambuliaaaa" alipiga kelele Kobwe na hapo ikasikika milimo mingi ya risasi toka kwa UMD makundi yote matatu, askari walishambulia huku wanakimbilia mbele kule ziliko tokea risasi, ambako ni kule walikokuwa wanaelekea wakiamini kuwa alieashambulia alikuwa mita chache mbele, hawakujua kuwa kuna kitu wanakiita hawakujua kama Deus anawachonganisha na askari polisi

Milio ya risasi ilisikika eneo lote la msitu, na kuwafikia jeshi la polisi ambalo lilikuwa kilomita kama mbili mbele yao, pamoja na special force Marine waliokuwa kule relini, "sikiliza toka kwangu, hao washenzi wanashambulia huku wanakuja huku kwetu, lazima na sisi tupambane nao, umakini wa hali ya juu unahitajika, sitaki kuona askari mwingine anapoteza maisha" alisema kamanda nyambibo, ambae mwisho akatoa amri ya askari kusonga mbele.

Wakati huo huo Special force wa pale relini, ambao lengo lao lilikuwa ni kumpata Deus Nyati akiwa hai, wakaona itakuwa vyema kama wataingilia kati mapambano yale, isije kuwa mtu wao ndie yupo kwenye matatizo, hivyo wakaingia porini na kusonga mbele, kwa njia ya pembeni lengo lao ni kuwa piga shambulio la upande.********

Naaam turudi TTCity, kwenye nyumba ya siri, ambako sasa Chitopela alikuwa amesha zinduka na kumuona mmoja kati ya ile mijamaa miwili, akiwa anaunguza kitu mfano wa spook ya baiskeri kwenye jiko lile la moto, kama vile anaechoma nyama, mwanzo alielewa kile kifimbo cha chuma kinakazi gani katika mwili wake, lakini dakika moja baadae akamuona yule jamaa akitoa kile kichuma kilichokuwa kimebadirika rangi na kuwa nyekundu, akikichukua na kumsogelea, kisha akashika dudu ya mzee huyu, ambae sasa alianza kulia kama mtoto, maana tayari alisha tabiri kinacho fuata, ni kwamba kile chuma kilikuwa kinaenda kupitishwa kwenye tundu la mkojo, ikiwa na moto wake, hakika moyo unasisimka, hii ndio mtomolelo, ambao sasa ulikuwa unasongezwa taratibu kuelekea kwenye kichwa cha dudu usawa wa tobo la mkojo, "niachieni nitasemaaaa" alipigalele Chitopela, na hapo yule jamaa akaacha kufanya alichotaka kufanya, "ok! ongea sasa, kundi lipo wapo na lipo na nani" alisema yule mmoja wao, huku mwingine akiwa anarudisha mtomolelo kwenye jiko.

Hapo bwana Chitopela, aliesema kuwa atasema, iliaachiwe, akawaza kidogo namna ya kuepuka kuwatia ghazab wawili hawa, aliwaza kidogo kisha akapata jibu, nitaongea na Sixmund, nita mueleza kila kitu, naomba msiningize mtomolelo" alisema Chitopela kwa sauti yenye kuombeleza, baada ya hapo wawili hawa wakakutana pembeni kujadili ombi la bwana Chitopela.**********

Naaam misegese wanaonekana UMD wakizidi kusonga mbele, mbio mbio, lakini wakiwa kati kati ya sambali yao, eneo lenye wanda wa juu, ghafla wanashtuka wakianza kushambuliwa kwa risasi, ambazo zinaonyesha wazi kuwa ni kutoka kwa kundi kubwa la watu na sio kijana Deus kama walivyo tegemea, hapo na wao wanaanza kujibu mashambulizi kwa kutumia silaha zote walizo nazo, mabomu na makombora, eneo linageuka mchana kwa mianga ya mabomu na makombora, watu wanajeruhiwa na wengine wanapoteza maisha, vita ni kubwa kupita kiasi, wakati UMD wanakaribia kulishinda jeshi la polisi, mara wanaanza kushambuliwa toka upande wa kushoto nao ni marine Special force, ambao kazi yao sio ndogo na hainakujaribu

UMD wanaona mambo magumu, Kobwe anapoteza maisha katika mapambano, lakini Kadumya na Kafulu wakiwa wameishiwa risasi wanatokomea porini, na kuutafuta uelekeo wa mjini ili wakafanye mpango wa kusafiri kurudi kambini kwao kule mpakani mwa tanzania na mbogo land, ndio wakati ambao Deus na Veronica walikuwa wanajaribu kusogelea nyumba yao ya maficho ili wakachukue gari na kuondoka zao wakiamini kuwa polisi wata kuwa kwenye mapigano na ndipo walipo waona watu wawili wanakuja upande wao, nao wakajificha na kuwatazama vyema.

Wakiwa wamejificha wanawatazama watu wale waliokuwa wanakuja kwa mwendo wa haraka bila tahadhari wakawasikiwa wanaongea, "nivyema ukamweleza mkuu kilichotokea" hii ilikuwa ni sauti ya JJ, yani Kafulu sauti ambayo Vero aliitambua kwa haraka sana, hapo Deus alichomoa kisu chake na kukaa tayari ni kweli walikuwa Kadumya na Kafulu, ambao walikubariana wapige simu kwa Chitopela, ili amueleze kilichotokea, nayo inapokelewa na general sixmund, ambae alikuwa ofisini anajaribu kuikagua ile simu, "hallow bwana Kadumya, unaongea na General sixmund, vipi unalolote la kumueleza ndugu yako, Chitopela?" ilimshtua sana Kadumya, ambae anashindwa kuogea na kubakia ameshika simu akitazama Kafulu, huku wakipunguza mwendo na kuwa kama wameshiwa nguvu za miguu.

Akiwa hajui lakufanya wala kuongea, mara ghafla wote wawili wakashtuka kuona kitu kama mnyama simba au chui kikiwavamia na kupita na na shingo ya Kadumya, ile kutahamaki kuwa ni binadamu tayari kafulu alikuwa amesha dungwa kisu cha tumbo na kuganda akisikilizia maumivu, huku anatazama yule mtu wa ajabu, "dereva" alisema kwa shida Kafulu, huku anatazama Deus Nyati, "yupo na mimi JJ, nadhani hicho ndicho unachostahili wewe mshenzi kwa yale yote uliyo yafanya na uliyotaka kunifanyia" Kafulu anageuka kumtazama mtu wa pili kuongea ambae sauti yake haikuwa ngeni masikioni mwake, alimuona Veronica aliekuwa amejawa na hasira kari sana, ambae hakusubiri kuambiwa alichukuwa na kumpokonya kisu toka kwa mpenzi wake Deus na kukishidilia tena tumboni kwa Kafulu, "hufaikuishi we mshenzi jambazi mbakaji" alisema Veronica huku anazidi kushindilia kisu mara kadhaa tumboni kwa Kafulu, hata alipo anguka chini alimfuata na kuendelea mpaka Deus alipomzuia, "Vero tayari amesha kufa, tunahitaji kuondoka hapa" alisema Deus, huku anatoa Veronica kwa Kafulu.******

Naaaam, Sixmund anapeleka ujumbe kwa mfalme kuwa kadumya amesha uwawa na Deus Nyati, maana aliskia maongezi ya tukio kuipitia simu ya Chitopela na Chitopela aliposikia kuwa kundi lake limeangamizwa alilia kama mtoto, akijua kuwa mwisho wake utakuwa mbaya kuliko ule wa sajent samuel doe.

Kijana Deus Nyati anafanikiwa kumfikisha Veronica kwa baba yake na yeye akakamatwa na Special Force kwa njia ya amani, nae akakubari kuongozana nao mpaka makao makuu ya jeshi la ulinzi, huku TSA wakishindwa kumpata, japo faida ilikuwa kwa Caroline, ambae anakutana kwa mara ya pili na kijana Deus, lakini safari hii kama shemeji yake, Deus anakabidhi ushaidi kwa TSA, ikiwa ni simu mbili yaani ya Songoro na Cheleji, ambazo zote zikaenda kutumika kama ushaidi kwa Ulenje, huku yeye mwenyewe akifikishwa katika mahakama kuu ya kijeshi, ambako anashinda kesi kwa kutolewa ushahidi na bwana Simba mdogo na binti Zamda mtoto wa kaka yake Simba, pia Veronica nae alitoa ushahidi, kwamba Deus hakuwa muhalifu ila alisaidia kuokoa watu katika njia ngumu, mwisho akaachiwa huru kwa maelekezo kwamba arudi jeshini, kitu ambacho Deus alikifanya, lakini baada ya mwezi mmoja aliandika barua ya ombi la kuacha kazi, huku akiwa amepokea ujumbe toka kwa king Elvis ambae alitaka aende nchini mbogo land.

Ulenje na wafuasi wake waliobakia kama wakina Othmani, walifikishwa mahakamani na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela, huku bwana James akienda kukamilisha ushaidi wa kwamba Chitopela ndie mpangaji wa mipango yote ya mapinduzi, ambapo Chitopela alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifo cha tumbo la ng'ombe wa chuma, alilia sana Chitopela akiomba msahama lakini haikuisaidia kitu, zaidi ni kwamba bwana Frank Nyati alipewa heshima zake kama kanali wa MLA, na serikali kumtaka yeye na familia yake kurudi Mbogo Land, kitu ambacho hakukipinga, alirudi nchini akiwa kama shujaa yani yeye na kijana wake Deus, na hii ilikuwa kwa bwana James, ambae sasa anavibari vya kuishi katika nchi mbili, huku binti yake Veronica akiwa ameolewa na kijana Deus, na sasa Veronica ni doctor wa Malikia Vaselisa, huku Deus akiwa ndani ya MLA mwenye cheo cha luten Kanali, na mkufunzi wa mbinu za mapigano na utumiaji wa silaha ndogo ndogo.

MWISHO HAKUWA MZURI SANA, HII NI KUTOKANA NA WAKATI MGUMU NILIONAO KWA UPANDE WA VIFAA VYA KUZALISHIA HADITHI, NAOMBA ISIJIRUDIE KWENYE KIAPO CHA DAMU KWA DAMU YA CAPTAIN CHUI... ASANTENI KWA KUWA NAMI MWANZO MPAKA MWISHO, MWISHO WA SIMULIZI HII NDIO MWANZO WA SIMULIZI NYINGINE, TUKUTANE KWENYE SIMULIZI IJAYO.
RAMADAN MUBAARAK ........
 
Back
Top Bottom