NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA AROBAINI NA TATU
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA AROBAINI NA MBILI: “mimi ndio na fahamu toka zamani” alisema Carolina huku anainuka na kukaa pembeni ya mama yake, ni wazi kabisa, alikuwa macho toka wageni hawa wanaingia ndani ya nyumba yao, Issa na Michael wakamtazama Carolina kwa mshangao, “hoooo! kwahiyo shemeji, binti yako alikuwa anafahamiana na Deus Frank, toka zamani, hata haya yaliyotokea hayakuwa bahati mbaya, kwamba mulimuomba Deus awasaidie kumuokoa baba yenu na baadae dada yake” aliuliza Issa, kwa sauti ya ung'amuzi wa kinoko, huku wote wakitoa macho kwa mshangao, huku wametoa macho yenye viashiria vya kiumbea...ENDELEA...
Ni kama walikuwa wanajaribu kuwahusisha wao na kijana Deus Nyati, “hapana sio kwamba walikuwa wanafahamiana kabisa, ila waliwahi kukutana kwa siku moja tu wakiwa safarini” alisema mama Veronica na kuanza kusimulia ile safari ya binti yake aliyoamua kupanda tren, na jinsi ilivyopata ajari, kisha Deus kuwaokoa wakina Carolina na wenzake, “siku hiyo ndiyo ilikuwa ya kwanza na ya mwisho kwa Carolina kumuona Deus, mpaka leo hajamuona tena, japo imekuwa rahisi kwa yeye kuikumbuka sura yake mara alipoiona kwenye simu” alijibu mama Veronica huku Carolina akiwa ametulia pembeni yake anasikiliza mama yake aliekuwa anatoa maelezo kwa watu wale wawili ambao walijitambulisha kama wanausalama.
Hapo wakina Makame, wakatazamana tena, ni kama waliongea jambo fulani na kukubaliana, sekunde chache baadae wakamtazama Veronica, “kwahiyo akikuona anaweza kukutambua?” aliuliza Makame, hapo Caroline alitulia kidogo, kama vile anatafuta jibu, na baada ya utulivu wa sekunde kadhaa, Carolina akatoa jibu, “mh sidhani kama atanitambua, nilikuwa mtoto sana, ila nikimkumbusha mimi nani, lazima atanikumbuka tu, maana hawezi kusahau lile tukio la ajari ya treni” jibu hilo alilitoa Caro mwenyewe, na hapo wanausalama wawili walitabasamu kwa Pamoja, “vizuri sana, wewe ndie utasaidia kupatikana kwa dada yako kirahisi, maana hatujui anampango gani, ila kama wewe utakuwepo na ukamkumbusha urafiki wenu wa zamani lazima atamtoa dada yako kwa haraka na bila shida yoyote” alisema Makame, na kwa sauti iliyochangamka, ugesema amevumbua jambo fulani la ukweli.
Ni kama walijua kuwa Carolina ana hamu kubwa ya kukutana na kijana Deus Nyati, maana kusikia hivyo Carolina aliinuka haraka toka kwenye kochi, “sawa, hakuna shida twendeni, ngoja nikavae” alisema Carolina, huku anatambea kuelekea chumbani kwake, huku mama yake akimtazama binti yake kwa macho ya mshangao, kabla haja wageukia wakina Makame, ambao walionekana kutabasamia mafanikio yao, “lakini tutawaamni vipi” aliuliza mama Veronica, huku anawatazama wakina Makame kwa macho ya mashaka, “hooo! Kumbe hatujakuonyesha vitambulisho vyetu” alisema Michael Njogopa, huku anaingiza mkono mfukoni mwake na kutoa kitambulisho, kisha akamuonyesha mama Veronica, ambae alikitazama kwa sekunde kadhaa, ambapo alitazama picha tu na kumpatia, huku Issa nae akiwa anamkabidhi cha kwake, “inatosha, najua sitoweza kumzuia Carlo kwenda huko kwa Deus, wacha na mimi nijiandae niongozane na nyie” alisema mama Carlo, huku anainuka na kuelekea chumbani kwake.******
Naaam! Msafara wa magari ya jeshi la ulinzi la kikundi cha marine special force, cha magari nane, ambayo sasa yalikuwa yamesha gawana maeneo ya ulinzi na mitego, manne yakiwa yamebakia relini na manne yakiwa yanazidi kusonga mbele, yalipishana na magari mengi sana ya polisi yaliyokuwa yana tembea kuelekea upande wa relini.
Tuachane na magari ya jeshi la ulinzi, tuyafuate ya polisi, ambayo yalikuwa katika mwendo mkali sana, sisi twendeni kwenye gari la ACP Ulenje, ambalo alikuwa yeye dereva wake na mlinzi wake mmoja tu, ndani ya gari hilo, ambapo tuna muona Ulenje akiwa na simu sikioni, huu ndio wakati aliokuwa anaongea na koplo Cheleji.
Ni kwamba wakati ule anaongea na Songoro, aliekuwa ameepuka kifo toka kwa akina Cheleji, na muda huo huo anasikia sauti ya mshangao ya Uled Songoro, ikitaja Dereva, na baadae Kufuatia miguno ya maumivu makali, ambayo yalifuatiwa na kishindo cha kuanguka na ukimya wa muda, uliovunjwa na sauti ya tulivu yenye upole wa hali ya juu, japo ilikuwa ni mara yake ya kwanza, lakini haikuwa vigumu kwa yeye Ulenje kugundua kuwa muongeaji ndie dereva mwenyewe, na mbaya zaidi alimtaja kwa jina.
Ilimshtua sana Ulenje, sio tu kutajwa jina na kijana huyu hatari, tatizo ni kwamba kijana huyo, amesha tambua kuwa yeye ni nani na anajiusisha na nini, lakini Ulenje alijiambia kuwa hakutakiwa kujilegeza mbele ya kijana huyu.
Hapo Ulenje akaachia kicheko Kizito cha kuhesabu, “hooooo! dereva, kwanza hongera kwa kuondoa hiyo kero, sasa tuna weza kufanya mpango” alisema Ulenje kwa sauti fulani tulivu, ambayo mara nyingi hutumiwa na watu wenye uwezo mkubwa kifedha, na mipango endelevu ya kupata fedha, “nipo kwenye mpango, siwezi kuingia kwenye mpango mwingine” ilisikika sauti tulivu toka upande wa pili wa simu.
Ulenje ambae alihisi kuwa, kijana dereva amesha jua kuwa yeye ni kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi wa Ilala, hivyo ilikuwa ni lazima kumthibiti Deus Nyati, kabla hajafanya lolote la kijinga ambalo linaweza kujulisha jamii yeye ni nani na anashiriki mipango gani ya kiharifu, “hii ni kwaajiili ya usalama wako, maana sasa tupo njiani tunakuja hapo ulipo, ni kundi kubwa la polisi wenye silaha, , na unatakiwa kuondoka mara moja, hakika hautoweza kuchomoka mbele ya kundi kubwa kama hili, vinginevyo inabidi umwage damu nyingi za askari wasio na hatia, na kitu ninacho kijua kwako ni kwamba wewe sio muharifu na haupendi uharifu, vipi sasa tutaweka mpango ili na mimi nikusaidie kuondoka hapo?” aliuliza Ulenje kwa sauti yake ile ile ya kiboss, “huwa sivunji sheria zangu, labda wewe usikilize toka kwangu, waambie watu wako wasinisogelee, maana mimi sio muharifu, na kila kitu kinaenda kuisha salama” ilisikika sauti toka upande wa pili wa simu, sauti ambayo utulivu wake ulitaka kumshawishi Ulenje adhanie kuwa, ilikuwa ni swala la utani.
Ulenje ambae sasa alikuwa anaona magari ya mbele kabisa yana karibia kwenye njia ambayo walitakiwa kukata kushoto kuingia ndani ya msitu kwa kufwata maelekezo ya koplo Cheleji, alichekecha akili kwa haraka na kupata jibu, “sikia kijana, najua unanifikiria tofauti sana, ila ni wazi utahitaji msaada wangu, sisi tunakaribia kuingia kwenye hii njia ambayo inakuja huko uliko, cha kufanya wewe nenda ndani zaidi” alisema Ulenje, kisha akakata simu, kisha akaanza kuchekecha, namna ya kumthibiti Deus, na watu pekee wenye silaha nzito ni wakina Kadumya, yani UMD.
Baada ya kuwaza kwa muda mfupi, ndipo Ulenje alipompigia simu Kadumya na kumueleza juu ya kumshambulia Deus, huku akiwaelekeza njia atakayoitumia, na baada ya kumaliza kuongea na Kadumya ndipo Ulenje anaposikia muito wa redio call toka kwa Cheleji, akitangaza vifo vya askari wanne wa jeshi la polisi, na kwamba yeye Cheleji anahakikisha adui hawakimbii, hapo Ulenje akagundua kuwa, bado kijana wake hakuwa anamtambua adui yake ni nani, na kwamba sio Songoro ambae tayari alikuwa amesha poteza maisha na tayari dereva alishatoa tahadhari kwa askari yoyote atakae mfuata.
Hapo ndipo alipokuwa amempigia simu koplo Cheleji, ili kumjulisha kuwa wasimsogelee kijana yule hatari, baada yake wawaachie kazi hiyo wakina Kadumya, ambao tayari alishawapa taarifa za uwepo wa deus upande ule, ndio ule wakati Cheleji alikuwa anaongea na simu ndani ya lile jengo lisilomaliza ujenzi wake, “sikia Cheleji ondoa askari eneo hilo haraka sana, huyu ni Deus Nyati, yule dereva wa gari jeusi” alisema Ulenje kwa sauti yenye msisitizo, lakini hakusikia jibu au kitendo chochote ambacho kingeashiria kuwa, Cheleji alishamuelewa na saa anatekeleza.********
Naaam sijui tumuite Waziri, au aliekuwa Waziri wa ulinzi na usalama wa #mbogo_land, kwa king Elvis wa pili, mheshimiwa Dickson Chitopelah, au rais mtarajiwa wa #mbogo_land, kama alivyo kuwa anajiaminisha hapo, sasa alionekana akiwa anatoa macho kwanguvu ili kujaribu kumtambua mtu aliekuwa anaingia, mtu ambae ni wazi alikuwa askari wa jeshi la #mbogo_land, yani MLA jeshi ambalo hata yeye alishawahi kulitumikia, akikomea kwenye ngazi ya brigedia General, “bwana mkubwa, nadhani sasa umesha amini kuwa, tayari sasa upo sehemu ya kuvuna ulichopanda”Chitopela alimsikia yule jamaa akiongea na kwa haraka sana Chitopelah akaitambua ile sauti, kuwa ni ya General Sixmund.
Ilimchukiza na kumtia hasira Chitopela, mtu ambae asubuhi ya leo ametoka kumpigia saluti, halafu sasa hivi anamuongelesha kwa dharau kiasi hiki, lakini licha ya kuwa na hasira Chitopela, alijuwa fika kuwa, hawezi kumfanya lolote, zaidi ni kutafuta njia ya kujitoa katika hatari ya kufungiwa kwenye tumbo la ng’ombe wa chuma,l na kuwashiwa moto wa makaa ya mawe chini ya tumbo la ng’ombe yule.
Kwanza Chitopela akaachia kicheko fulani, ambacho licha yakujitahidi kiwe kikali, lakini kilimezwa na maumivu ya mwili, hivyo kiliishia tumboni, ujue vicheko kama hivi vina maana kubwa sana kwa mtu ambae yupo katika wakati mgumu kama huu wa Chitopela, maana ya kicheko hiki ni kwamba, Chitopelah alikuwa anachukua usikivu wa general Sixmund, ambae ni kweli atulia na kumsikiza alikuwa anataka kuongea nini, “general nadhani mpaka hapa unahisi kuwa tayari mume maliza kazi” alisema Chitopela, kwa sauti fulani ya kujikamua.
Hapo General Sixmund, akaona kuwa kuna umuhimu wa kupata habari zaidi ambazo zinaweza kuwasaidia kumaliza jukumu zito la kuangamiza kikundi cha UMD, “unazani kuna lolote unaweza kufanya bwana Chitopela?” aliuliza Sixmund, ambae sasa alikuwa amesha mfikia Chitopela, “Sixmund, kuna kitu lazima ukijue, ni kwamba kunikamata kwenu kutachochea mauwaji makubwa ambayo yataanza kutokea muda mfupi ujao, maana mimi nilipanga mapinduzi yasio na umwagaji damu, lakini msimamizi anaefuatia baada yangu hawezi kufanya mapinduzi kama nilivyopanga mimi” alisema Chitopela kwa kujiamini, maana bado alikuwa na dalili za kucheka kile kicheko chake, “ni nani huyo msaidizi wako, na sasa yupo wapi na askari wake?” aliuliza Sixmund.
Hapo kicheko cha Chitopelah kikakijirudia, “unadhani mimi ni mjinga kiasi hicho, yani nikueleze maficho ya watu ambao wanahitaji kuja kufanya mapinduzi, labda kwa msaada wako na wenzako ni kwamba, ukiachilia kuwa na watu wengi sana ndani ya serikali hii ya kipuuzi, ambayo unaendelea kuipigia magoti na kuisujudia kila siku, pia kuna silaha nzito ambazo kwa shambulio la kushtukiza litakalo fanyika hamuwezi kuzuia vifo vya raia wa nchi hii, kama mupo tayari tukae chini msikilize sisi tunahitaji nini” alisema chitopela kwa kujidai, “unadhani ni muhimu sana serikali kukaa chini na kikundi kidogo cha wahuni kama vile UMD?” aliuliza Sixmund kwa sauti ya taratibu, “pengine umesahau kuwa kukosekana kwangu ndani ya UMD, ndio chanzo cha mauwaji makubwa, ambayo yataishangaza dunia, na pia fahamu kuwa ni mimi pekee ndie mwenye uwezo wa kutoa amri kwa UMD na wakaelewa” alisema Chitopelah.
Sixmund alitulia kidogo, akitafakari maneno ya Chitopela, ukweli kichwani mwake Sixmund aliona kuwa ni maneno ambayo yalipaswa kutiliwa maanani na kufanyiwa kazi, hivyo baada ya kuwaza kwa sekunde kadhaa, Sixmund akamtazama Chitopela, “vizuri bwana Chitopelah, umefanya vizuri kutupa hiyo habari” alisema Sixmund, kisha akageuka na kutoka nje ya kile chumba, Chitopelah akimsindikiza kwa macho, huku akilini mwake akifurahia kufanikiwa kwa mpango wake, maana alimini kuwa, mpango huu, sio tu kuchelewesha wasimuue, pia ungempa nafasi ya kutoka kabisa kizuwizini, maana endapo wangekubari kukaa chini na kujadili amani kwa pamoja, yeye angetoa masharti mengi sana, ambayo yangemsaidia, ikiwa na kuomba uangalizi wa mataifa makubwa ambayo yange simamia usalama wake.********
Naaam koplo mwenye utiifu mkubwa kwa ASP Ulenje, akiwa bado na simu sikioni, alionyesha kushtuka baada ya kusikia kuwa kijana Deus Nyati, yani dereva wa BMW jeus S7, yupo maeneo yale, na kwa hali aliyoikuta pale sebuleni, Cheleji alijua kwamba, kijana huyo hatari yupo mule mule ndani ya jumba lile chakavu, anashtuka na kumtazama yule aliekuwa amesimama mbele ya mlango dhaifu wa mabati, ambae alikuwa anajaribu kuufungua, lakini kabla hajamueleza chochote, akasikia kishindo kikubwa cha “tihiii!” hapo Cheleji akageuza uso wake kutazama upande alioingia yule askari mwingine, hata kabla macho yake hayajapata uwezo wakutambua vizuri kilichopo mbele yake aliweza kuona kitu kama furushi likiwa hewani kuja upande wake, yani pale sebuleni na kujibwaga chini mita kadhaa toka alipokuwa yeye.
Sasa anaweza kuona kuwa ni askari wake, ambae alituwa akiwa mtulivu, hakujuwa kama ni amepoteza fahamu au amekufa, ile anamtazama yule mwingine amueleze kuwa watoke nje haraka, anamuona yule askari aliesimama kwenye mlango, akiwa anaanguka chini kama furushi la mbegu za viazi vitamu, huku pembeni akionekana mtu aliekuwa anakuja upande wake kwa mwendo wa haraka. ..…….ENDELEA
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA MIA MOJA NA AROBAINI NA NNE
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
WHATSAPP: 0743632247 (KWA MATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA MIA MOJA NA AROBAINI NA TATU: Sasa anaweza kuona kuwa ni askari wake, ambae alituwa akiwa mtulivu, akujuwa kama ni amepoteza fahamu au amekufa, ile anamtazama yule mwingine amweleze kuwa watoke nje haraka, anamwona yule askari alie simama kwenye mlango, akiwa anaanguka chini kama kufushi la mbegu za viazi vitamu, huku pembeni akionekana mtu alie kuwa anakuja upande wake kwa mwendo wa haraka. ..…….ENDELEA…
Kiukweli Cheleji alikuwa anajua sifa tabia na uwezo wa kijana yule, hasa anapoona adui yake anabunduki, hivyo basi kitendo bila kuchelewa, Cheleji ambae hakujisumbua kutumia bunduki yake, alijirusha usawa wa dirisha na kutokea nje, hakujali jinsi alivyojibwaga, wala simu yake iliyo anguka chini, akajiinua haraka, “njooni huku adui huyu hapaaaaaa” alipiga kelele Cheleji, huku anakimbia kwenda kutafuta maficho, akiacha askari wake ambao hawakuwa wanajuwla adui yao ni nani, na kwamba walidhania kuwa bado wanapambana na wakina Songoro, wakiwa wanakimbilia upande ule aliotokea Cheleji na kuanza kumimina risasi kupitia dirishani.
Hakika zilisikika kelele nyingi za mikohowo ya risasi za SMG, tukio lililodumu kwa dakika nzima, maana wengine walipoishiwa risasi walibadili mikebe na kuendelea kumimina risasi mfululizo, mpaka walipokoma kwa kuishiwa risasi, wakiamini kuwa, kwa risasi walizo mimina mule ndani, sio tu hao adui zao ila pia, hakuna kiumbe chochote mule ndani kitakachokuwa hai, kuanzia nzi mbu hata mijusi.
Lakini ile wanasitisha mapigo tu, ghafla wakasikia “pah! pah! pah!” ni milipuko ya risasi toka nyuma yao, huku wale wa mwisho mwisho, wakiwashuhudia wenzao wakianguka kama maroboti yaliyoishiwa chaji, huku na wao wakipokea vitu kama misumari yenye moto,l vichwani mwao na kuanguka kama mabua makavu ya mtama yaliyokutana na chikwakwa, kile kisu cha Jensen kwenye KIAPO CHA DAMU KWA DAMU niwazi adui yao alikuwa ameshahama eneo lile muda mrefu uliopita, na kutokea ubavuni mwao, kisha kuwafanyia shambulio la upande, yani Frank attack.
Naaaam wakati huo huo, askari waliokuwepo kwenye magari wakaanza kushambulia kule ilikosikika milio ya risasi, bila kuona wanae mshambulia, kuona hivyo, Cheleji akachomoka mbio, toka kwenye kichaka na kukimbilia yalikosimama magari akimini kuwa shambulizi la wenzake linge saidia kumkinga yeye na kuweza kufika kwenye gari, maana hakukuwa na namna zaidi ya kuondoka eneo lile.
Lakini haikuwa bahati yake, maana alisikia milipuko kadhaa ya risasi, sambamba na miali ya moto yenye kasi na nguvu ya ajabu ikigonga kwenye magari yao, huku wenzake kuanzia dereva na wale askari wengine wawili waliobakia, wakipoponyoka, toka kwenye magari na kuanguka chini, hapo Cheleji akajua kuwa kama asipo pambana, basi anaweza akapoteza maisha, hivyo akageuka haraka huku anaishika bunduki yake vyema.
Kitendo bila kuchelewa, Cheleji aliminya trigger kwa nguvu na kwa kuing’ang’ania, akifanya risasi zitoke mfululizo mpaka aliposikia kacha! ikimaananisha kuwa mkebe wa risasi ulikuwa tupu, hapo kwa pupa akachomoa magazine na ilikuwa imebebeshwa tatu kwa Pamoja, wakitumia mpira wa manati kuzifunga pamoja.
Alipomaliza kubadili mkebe wa risasi, akatazama upande ule hakuona dalili ya uwepo wa mtu yoyote alie hai, wakati huo anauona mwanga wa simu yake, ulioangaaza mita chache toka kwenye nyumba ile isiyo isha ujenzi wake usawa wa dirisha ambalo alitokea yeye, ni wazi ilikuwa inaita, wakati huo huo mianga ya taa za magari ilianza kuonekana upande wa barabarani, ikiwa imebakiza mita chache sana kuifikia ile njia panda ya kuingilia pale kichakani. ********
Yap! Milindimo ya risasi ilisikika umbali mkubwa sana, ukiachilia msafara wa mgari ya polisi na kundi la Marine special force waliokuwa relini, pia hata lile kundi la marine special force ambalo sasa lilikuwa linakaribia njia panda ya kisarawe na manero mango, nao walisikia milipuko ile kama walivyosikia UMD waliokuwa kilomita kama nne ndani ya msitu, na msafara wa MLA na askari wa jeshi la ulinzi la Tanzania, ambao sasa walikuwa wamesha maliza kisarawe mjini wanaelekea misitu ya visamvu kuelekea njia panda ya manero mango.
Lakini pia kuna watu wawili walioshuhudia tukio hilo kwa njia tofauti na ile ya wengine, wao maana wakati Ulenje akiwa ndani ya gari na simu sikioni mwake, anasikiliza mwanzo mpaka mwisho na jinsi milindimo ya risasi ilivyosikika ikirindima kupitia simu yake, huku mwana dada mrembo Veronica, akitazama kupitia screen kubwa mbele yake, inayoongoza camera za ulinzi, ambae aliweza kuona jinsi mtu anaemuita mpenzi wake, anaetarajia kumuita mume siku za mbele, akinyofoa roho za watu kama yupo kwenye mchezo wa kuigiza, maana kitu ambacho unatakiwa ufahamu ni kwamba, camera za ulinzi zilizofungwa kwenye nyumba hii, zilikuwa na kifaa ambacho kinaitwa night vision, ambacho husaidia kuona kwenye giza vizuri, kuliko hata aliekuwa eneo husika.
Naaam kwa kusikia milipuko ile UMD ambao bado walikuwa wamesimama wanapeana majukumu, wakaamini maneno ya Ulenje kwamba, dereva wa BMW alikuwepo maeneo yale, “haya jamani nadhani mmesikia wenyewe, kuwa windo letu lipo mbele yetu, cha msingi kumbukeni kuwa yeye ndie mwenye fedha ambayo itamfanya kila mmoja wetu kuwa mtu mkubwa ndani yaserikali yetu, kila mmoja wetu kujichagulia majengo mazuri na kumiliki gari analolihitaji, mke mzuri watoto wenye maisha mazuri” alisikika Kadumya, huku Kafulu akisubiri kusikia Kadumya akitoa tahadhari juu ya Veronica, “sasa basi mutakuwa katika makundi matatu, moja litakuwa na mimi moja kafulu na moja Kobwe, na wale watakao kuwa na mimi watakuwa katikati nyuma, kobwe atakuwa kushoto na kafulu kulia, kwahiyo tutakuwa katika mpango wa mbili juu, kwa maana ya two up fomartion” alisema Kadumya.
Naaam hapo yakiwa makundi matatu, yote yakiwa na silaha nzito, kisha wakajipanga kama walivyo amuriwa, lakini kabla amri ya kuondoka haijatolewa, Kafulu akadakia, “sikiliza tangazo toka kwangu” hapo wote wakatulia kimya, hata Kadumya akatulia kimya lakini akimshangaa Kafulu, maana hakutarajia kama atakuwa na lolote la kutangazia kikosi kizima kilichokuwepo hapa, “vyovyote itakavyo kuwa, kumbukeni kuwa, yule mshenzi yupo na fedha zetu,pamoja na mschana Veronica, ambae namuhitaji akiwa mzima kabisaaaaa, ana denia la kulipa kwangu” alisema kafulu, na kwa wale ambao hawakujuwla anamaana gani, hawakuwa na shaka lolote, ila Kadumya alitikisa kichwa kwa masikitiko, hakutaka kupingana na Kafulu kwa kuchelea kwamba, atazidi kumvunja nguvu ya kufanya jukumu la kuongoza askari, katika mpango wa kumkamata Deus na kuchukua fedha zao.
“haya sikiliza kutoka kwangu” alisema Kadumya, na utulivu ukaendelea kutawala, “wote kaa tayari kwa kuondoka” alisema Kadumya kwa sauti yake ya kikamanda, huku anawatazama wale askari wake waliokuwa katika vikundi vitatu, “ondokaaaaa” alisema Kadumya na hapo vikundi vikaanza kuondoka kwa kushika uelekeo, kama walivyo elekezwa, wakati huo kwa mbali waliweza kuona nuru za taa za magari mengi, yakija upande wao, lakini yalikuwa mbali kidogo, ni kama kilomita nne toka pale walipokuwepo wao. *******
Naaam! akiwa ametoka amesikia majibizano ya risasi kwa kupitia simu ya Cheleji, ambayo ilikuwa wazi muda wote wakati risasi zikisikika, bwana Ulenje ambae alijuwla fika kuwa, wakina Cheleji wanapambana na Deus Nyati, hata mapigano yalipo tulia akajaribu kuita, “hallow Cheleji, cheleji unanisikia, hebu jibu chochote “wanapambana na Deus Nyati” alijisemea Ulenje, akiwa bado ameweka simu sikioni, lakini hakupata jibu lolote.
Akiwa ameingiwa na hofu, juu ya askari wake, anakata simu na kuipiga tena, nayo inaanza kuita mara moja, na kwa bahati nzuri licha ya kuita kwa muda mrefu, lakini baadae ikapokelewa, wakati huo tayari walikuwa wamesha kata kona kuelekeea upande wa kushoto ambako wakina Cheleji walikuwepo. *******
Kitu ambacho Ulenje hakujua ni kwamba, mara baada ya Cheleji kuifikia simu aliinama haraka na kuikota, lakini ile anainuka tu, akashtuka kuona kuna mtu amesimama mbele yake, ile anaishika vizuri bunduki yake ili kumshambulia mtu huyu ambae licha ya uwepo wa giza, lakini aliweza kumtambua kuwa ni kijana Deus Nyati.
Hakika haikuwa bahati yake bwana Cheleji, maana aliweza kuhisi kitu chenye ncha kali kama kiwembe kiki pita shingoni mwake na kumkata mawasiliano ya juu na chini, na kumfanya agande, kama vile ameamrishwa na mkuu wa gwaride fulani, huku damu zikimtoka kwa wingi shingoni mwake, sekunde kadhaa zilitosha kwa Cheleji kuganda wima, maana kilichofuatia ni kuanguka kama mtu aliokatwa kwa msumeno wa nyororo, wakati huo tayari mianga ya gari ilikuwa imesogea, na kubakiza kama mita mia mbili au mia tatu, kufika pale,
Deus anaokota simu, ambayo bado ilikuwa inaendelea kuita, anatazama jina la mpigaji na kuona kuwa alikuwa ni afande Ulenje, kama ilivyokuwa kwa yule wa kwanza, Deus akaipokea na kuiweka sikioni, “Cheleji vipi mmesha muuwa Deus Nyati?” aliuliza Ulenje kwa sauti yenye hofu na wasi wasi mkubwa.
Kwanza kilianza kicheko, kabla ya mguno mdogo mwepesi, “ina maana afande Ulenje huku nielewa nilipokuambia kuwa waambie askari wako wasinisogelee?” aliuliza Deus kwa sauti tulivu huku anaingia ndani ya ile nyumba chakavu, hapo Ulenje mwenye alijikuta anaachia kicheko cha machungu, “inamana umewauwa askari wote, Pamoja na Cheleji” aliuliza Ulenje kwa sauti iliyojaa machungu, ni swali ambalo bila shaka kama kuna aliesikia zaidi yake basi mwili ulimsisimka, “nadhani kuna kitu hujawahi kusikia kuhusu mimi Ulenje, mimi ni mtu wakutimiza kile ninacho ahidi” alisema Deus kwa sauti yake ile ile ya upole, huku anatembea haraka kuingia kwenye kile chumba cha mlango wabati, akiwa na MSG kisu chake mkononi.
Ni wazi maneno yake yalitikisa moyo wa Ulenje, ambae sio tu kuumia, ila pia alikasirishwa sana, “jiandae we mpumbavu, leo ndio mwisho wako, unakamtwa na nina kuuwa mwenyewe kwa mkono wangu” alisema Ulenje kwa sauti iliyojaa machungu, hapo Deus akaachia kicheko hafifu sana, “dah! sidhani kama utaweza kufanya hivyo, maana mpaka sasa umebakiza muda mfupi sana, wakulitumikia jeshi kama ACP, zaidi ya hapo muda mfupi ujao unaenda kuwa raia katika gereza lolote ambalo kuna watu kibao uliowafunga kwa uonevu, na hiyo ni afadhari yako, vingenevyo unaweza ukawa tayari umekatwa shingo yako, maana unastahili kifo, kutokana na uovu wako” alisema Deus kwa sauti yake ile ile, ungesema anaongea kuhusu jambo la kawaida, kisha akakata simu na kuingia kwenye mlango mdogo, uliopo kwenye uvungu wa kitanda.*******
Naaam Major General Sixmund anaonekana akiibukia kwenye kolido refu ndani ya ile nyumba ya MLA, waliyo fanyia mahojiano na bwana Ashraff, anaungana na kanali Jastin, “Jastin kuna kazi ya kufanya, wasiliana na vikosi vidogo ya Amour AR, wakae tayari kusubiri majukumu” alisema Sixmund, huku anafungua mlango wa moja kati ya vyumba vingi, vilivyo jipanga kwenye ile kolido, kisha wote wawili wakaingia kwenye chumba kile kikubwa chenye muonekano wa ofisi, “ndio afande” aliitikia kanal Jastin, huku anatoa simu yake na kuanza kupiga simu, wakati huo Sixmund nae akiwa anafanya hivyo hivyo.
Wakati Kanal Jastin akiwa anawasiliana na wakuu wa vikosi vidogo vidogo, vyenye ukubwa wa Troop, Sixmund alikuwa anapiga simu kwa captain Amos Makey, ambae alipokea mara moja, “nipe maendeleo Makey” alisema Sixmund, mara baada ya simu kupokelewa, “afande mpaka sasa, inaonyesha UMD wapo wengi sana huku Tanzania, wanaendelea kupambana na jeshi la polisi na kusababisha maafa makubwa kwa askari hao, ila sisi tunaenda kukutana na Deus Nyati, ambae anataka kutukabidhi doctor Veronica mtoto bwana James ili tuanze safari mara moja” alijibu captain Amos Makey, ambae ni wazi alikuwa ndani ya gari lililokuwa linatembea, “ok! hakikisheni munapata habari kamili, na ikiwezekana kuondoka mara moja baada ya kumpata Veronica” alisema Sixmund, kabla hajakata simu. ..…….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa
NYUMA YA MLANGO WA ADUI Unao Kujia hapa hapa
jamii forums