SIMULIZI: Pete ya Mfalme wa Eden

SIMULIZI: Pete ya Mfalme wa Eden

mireille

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2020
Posts
529
Reaction score
589
PETE YA MFALME WA EDEN
MTUNZI:JAFARI MPOLE
SEHEMU YA 01

Asubuhi ya Saa mbili kijana Jafari alikurupuka kutoka kitandani,alipotazama saa yake ya mkononi ambayo aliiweka karibu na mto alipolala kwa lengo la kumuamsha kwa kutegesha alamu,lakini ajabu siku hiyo hakuweza kusikia muito wa saa ile ikimuamsha jambo lililomfanya haraka anyanyuke na kuanza kuvaa nguo zake za shule haraka haraka.

“yaani leo nachezea stiki za Bokeloo, na u timekeeper niliopewa ndio mimi nimekuwa mchelewaji,Mungu wangu leo mh“alisema kijana Jafari akiwa anavaa viatu vyake haraka bila ya soksi,alipohakikisha yupo sawa alinawa uso wake kisha akachukua begi lake na kuanza safari ya kuelekea shuleni ambapo ni mbali kidogo kutoka kijiji cha Kabuku ambacho ndipo anaishi kijana huyo na alipogika njiani akakata kipande cha tawi la muarobaini na kutengeneza mswaki wa kijiti huku safari ikiendelea kuelekea shule. Ilimchukua dakika 35 za kukimbia tu hadi kufika mazingira ya shuleni hapo huku akionekana kuhema sana kwa kuchoka na jasho likimmiminika kiasi cha kulowesha nguo zake. Alisogea mbele kidogo akaanza kunyata na kwa mbali alisikia bakora zikitua mwilini kwa mtu hali iliyomfanya ajibanze kwanza mahali.Alipotazama kwa makini mbele alipata kushuhudia rafiki yake wa darasani Fanuel akiwa amelala chini akichapwa bakora kwenye makalio.

“duh hata jamaa leo kachelewa? Mungu wangu nisaidie"alisema Jafari na kuanza kutafuta njama ya kuingia darasani bila kuonekana maana wanafunzi wote walikuwa washaingia darasani wakichungulia tu kuona watu walio chelewa wakipata adhabu ya viboko kutoka kwa Mwalimu mkuu wa shule hiyo ya KWALUDEGE SECONDARY. Alipotazama pembeni akaona kuna wanafunzi watano wanatembea wakielekea kwenye bustani hivyo akaona njia pekee ya yeye kuepuka bakora ni kujichanganya kwa wale wanafunzi apate kupenya hadi kuingia darasani. Taratibu akanyata kwa ustadi wa hali ya juu hadi kufanikiwa kuzama kwenye lile kundi ambalo walipomuona Jafari walicheka tu na kuendelea na kazi zao za pale kwenye bustani huku naye akishirikiana nao huku akipanga njama ya kuingia darasana ambapo ni karibu na bustani hiyo waliyopo. Alipo piga ramani na kuona Mwalimu mkuu yule amezubaa akakimbia haraka hadi darasani kwao akaingia na kikimbia kukaa kwenye kiti chake huku baadhi ya wenzake wakianza kucheka maana walishamuona tangu anafanya ujanja wake.Dakika moja mbele akaja kijana mmoja pale karibu yake.

“mwanangu sio kama umesevu ulivyoingia humu.. Bokeloo anakuja huku kashatuhesabu tuliowahi ana namba zake na tuliopo humu ni 36 tu.“alisema kijana huyo na kumfanya Jafari ashtuke kusikia vile. Akaona ni msala wa yeye kuendelea kuwa pale darasani bora atoke tu, na alipotaka kufanya hivyo gafla tu aliona mlango unafunguliwa na kuingia Mwalimu mkuu Bokeloo akiwa ameshika bakora zake tatu huku sura yake ikionesha kuwa na hasira. Alipiga macho darasa zima huku akihesabu watu waliopo mule ndani,akajikuta akirudia tena na tena.

“hesabu zangu zinakataa, kuna mtu amezidi humu“alisema Mkuu huyo na baadhi ya wanafunzi wakaanza kumtazama Jafari aliye onekana kutetema mwili huku akijitahidi asionekane hali ile akawa anatoa vitabu vyake kwenye begi na kuanza kuvipanga.

“simameni wote“alitoa amri hiyo mkuu na wote wanafunzi wa darasa hilo la Form 4 wasimame.

“namba moja apite mbele“alisema Mkuu na mwanafunzi mwenye namba hiyo akapita mbele,hali hiyo ikazidi kumfanya Jafari akose amani na kukumbuka ule usemi KIFO CHA NYANI MITI YOTE HUTELEZA, hakukuwa na ujanja wowote ikabidi asubiri tu kukamatwa. Namba ziliendelea hadi kufika 34 na kubaki wanafunzi watatu waliosimama akiwemo Jafari ambaye alijikuta akiomba Mungu tu kwa woga uliomjaa.

“eh Mungu wangu nishushie muujiza huyu mzee hata akinikamata asiniadhibu hata bakola moja, unajua nilivyo mbovu katika kuvulia bakora mimi mja wako,doh saa imeniponza leo“alijisemea moyoni Jafari huku tumbo likiunguruma kwa woga akabaki ameinamisha tu kichwa chini huku wenzake wawili waliobaki wamesimama naye wakasogea mbele baada ya kutajwa namba zao akabaki yeye tu. Hapo ndipo akasikia vicheko vya wenzake wakicheka baada ya kumuona amebaki yeye tu kwenye viti.

“wewe ndio ulikuwa unanisumbua muda wote hapa hebu kuja huku, nyie rudini mkakae wewe kima njoo hapa alaah.“alisema Mkuu na wanafunzi wakarudi kwenye viti vyao huku Jafari akisogea pale mbele na kushikwa mkono na Bokeloo.

“wewe una makosa mawili kwanza, kwanza wewe ni TIME KEEPER ulipaswa uwahi kugonga kengele ndio watu wahesabu namba saa moja kamili,leo kengele nimegonga mimi mwenyewe saa moja na dakika 15 hivyo umeharibu ratiba nzima ya shule leo mpaka sasa vipindi havijaanza,utabeba adhabu hii peke yako lazima uwajibike,twende huku.“alisema Mkuu akitoka nje na kijana Jafari aliyeshikwa mkono. Watu wakawa wanatazama tu madirishani wakitaka kushuhudia adhabu gani atakayopatiwa.

Upande wa pili katika nchi ya kifalme kunaonekana kuna mkusanyiko wa watu katika uwanja mmoja nje ya jengo la kifalme. Kwenye jukwaa ambalo ni maalumu kwaajili ya kutoa hukumu anaonekana babu mmoja akiwa amefungwa kamba kwenye nguzo ya mti mrefu huku mwili wake ukiharibika kwa kupigwa sana na askari wa kifalme. Alichoka mwili mzima akisubiri hukumu yake tu ambayo ilisadikika mzee huyo ni mchawi na baya zaidi ameweza kumroga mpaka binti wa kifalme ambaye hadi sasa bado yu taabani kitandani hanyanyuki. Mzee huyo alipokamatwa na kubinywa ili aweze kueleza dawa ya kumtibu binti huyo alikataa katakata na kusema hawezi kusaidia falme haramu inayoongozwa na Mfalme Siddik hivyo ilibidi Mfalme Siddik atoe amri ya kumnyonga mzee huyo kwa kumkashifu Mfalme kisha waangalie namna nyengine ya kumsaidia binti wake maana hakukuwa na jinsi maana mzee yule aliapa kutomponesha binti huyo. Basi siku hiyo ya hukumu watu walifurika sana akiwemo hata binti wa mzee huyo aliyeitwa Nadhra. Yeye alikuwa mstari wa mbele kabisa akiwa mwenye huzuni sana akimtazama baba yake huyo akiwa amenin‘ginizwa kwenye nguzo kubwa akisubiri hukumu yake ambayo kila mmoja aliifahamu hukumu ya mtu mchawi,ni kunyongwa mpaka kufa.
Mzee huyo akiwa pale juu huku damu zikimtiririka alipata kumuona mwanaye pale mbele akiwa analia tu,alitabasamu baada ya kumuona mwanaye.

“Nadhra...usilie binti yangu,ukifanya hivyo utanifanya huko niendako niwe na huzuni kuwa nimemuacha binti muoga,simama kwenye msimamo nilio kwambia na hiyo pete kaitupe sehemu yeyote ya kengele kabla ya hukumu yangu kama unataka niwe nawe kiroho siku zote“alisema Mzee huyo moyoni mwake lakini kwa uwezo alio nao Nadhra alipata kusikia yote aliyosema baba yake.

“mimi naamini nguvu zako baba sio za kudhuru mtu, wana kuhukumu bure tu hawa watu wa kifalme.“alisema Nadhra moyoni mwake akiwa anawasiliana na baba yake aliyekuwa juu ya nguzo.

“hilo sio la kuliongelea kwasasa,fanya kile nilichokueleza hapo awali haraka.“alisema Mzee yule na binti yake akamuelewa. Waliangalina kwa mara ya mwisho mtu na mwanaye kila mtu akitokwa na machozi kisha Nadhra akageuka na kuondoka zake akipita katikati ya halaiki ya watu waliofurika kushuhudia hukumu hiyo.

“PISHA NJIA MFALME ANAPITA...“ilisikika sauti ya maaskari na kuwafanya watu waache njia kubwa ya msafara wa Kifalme ukiwasili sehemu ile.Nadhra alipata kuutazama tu msafara ule ukimpita akiwa naye amesimama pembeni hadi Mfalme Siddik alipopita akiwa juu ya farasi na wafuasi wake na kufika kwenye jukwaa lile alilopo baba wa Nadhra. Kiliandaliwa kitanzi maalumu kwaajili ya kukamilisha hukumu hiyo na hapo ndipo Nadhra akapata akili kumbe aliagizwa kufanya jambo. Haraka akaanza kukimbia sasa kwenda kutafuta mahala popote pale palipo kengele ili apate kuitupa pete aliyo agizwa na baba yake upate kusikika mlio kutoka kwenye kengele kwa imani yao ndio itakuwa afadhari ya baba yake atakuwa amejitoa kiroho katika mwili ambao utanyongwa hivyo ataendelea kuishi kama kawaida lakini hataweza kuonekana kama awali. Na asipofanikiwa Nadhra ni kwamba baba yake atakufa kabisa pindi atakapo nyongwa.

ITAENDELEA
 
SIMULIZI: PERE YA MFALME WA EDEN
MWANDISHI:JAFARI MPOLE
SEHEMU YA 02

ILIPOISHIA
Na asipofanikiwa Nadhra ni kwamba baba yake atakufa kabisa pindi atakapo nyongwa.

TUENDELEE

Muda huo baada ya kitanzi kuwa tayari yule Mzee alishushwa taratibu na kusogezwa kwenye kitanzi akaingizwa kichwa chake na askari mmoja akisubiri tu amri kutoka kwa Mfalme. Mfalme alipanda kwenya lile jukwaa na kusimama kuwatazama wananchi wake.

“kwa kawaida na sheria za Eden atakapo bainika mtu yetote anatumia uchawi basi kunyongwa mpaka kufa ni adhabu yake pindi atakapobainika, huyu mzee ni adui wa falme yangu ametumia uchawi kumdhuru binti wa kifalme hali yake ni mbaya sana,amethubutu kuutukana ufalme mzima na hata kunitukana mimi.. hivyo hukumu yake nii......“alisema Mfalme Siddik.

“K I F O O O“walisema wananchi kwa sauti kubwa sana wakijibu, jibu ambalo lilimfanya Nadhra kule alipo asikie na kugeuka kuangalia sauti ilipotokea, Akajua sasa baba yake anakwenda kunyongwa kweli, Kila akiangalia pembeni ya kila sehemu hakuna mahala palipo na kengele apate kuitupa ile pete, Alijikuta akilia kwa sauti kama kuchanganyikiwa akiwa anakimbia huku na kule.

Muda huo huo kule shuleni Jafari alikuwa akiongozana na Mwalimu mkuu aliyejawa na hasira sana.
“wewe nakuadhibu mbele ya shule nzima na kuanzia leo nakuvua uTIME KEEPER nampa mtu mwengine,kagonge kengele kwa mara ya mwisho watu waje paredi,haraka“alisema Mkuu na kumfanya Jafari anyon‘gonyee kusikia ndio anafutwa cheo chake cha kugonja kengele. Alitembea taratubu hadi kuifikia kengele ile na kuchukua kile kichuma akikiangalia sana na kuona ndio mara yake ya mwisho kukishika chuma kile kama akifutwa cheo hicho. Alikasirika sana na alichokifanya ni kuigonga kengele kwa hasira zote tena mfululizo bila kusimama. Kitendo cha kugonga kengele ile kwa nguvu zote sauti iliyotoka pale ilisikika hadi Eden na kwa mbali alipata kuisikia Nadhra ambaye alitega sikio kusikiliza sauti ile inatoka wapi ili awahi kutupa ile pete lakini kila akiweka umakini wa masikio yake sauti anaona inatokea juu angani tu na sio kusini wala kaskazini wala Mashariki wala Magharibi hali iliyomfanya azidi kuchanganyikiwa na kujikuta akiitoa ile pete na kuishika mkoni. Alichokifanya ni kucheza mchezo wa bahati nasibu tu liwalo na liwe, alifumba macho na kuomba kwa imani yao kisha akairusha juu angani ile pete akiweka dhamira ifike kwenye kengele aliyoisikia. Kitendo cha kuirusha tu pete ile alisikia watu wakishangilia kuonesha tayari baba yake kashanyongwa, alienda chini kama mzigo kwa kupiga magoti.

“naamini nimeifanya kazi yako baba japo sina hakika kwa nilichokifanya, ni kuomba na kusubiri matokeo ya kilichofanyika.“alisema Nadhra huku chozi likimtiririka haelewi kama jambo alilo lifanya limefanikiwa au ndio laa kashampoteza baba yake?

Upande wa pili Jafari akiwa mwenye hasira zake pale kwenye kengele akizidi kuigonga mfululizo alimfanya hata Mkuu wa Shule acheke baada ya kuona kweli kijana anagonja kengele kwa mara ya mwisho kama alivyomuambia na kweli hakuwa mwenye kutania. Alipanga kumtoa Jafari kwenye uongozi wa kuangalia muda wa vipindi kutokana na uchelewaji wa kijana huyo.

Wanafunzi madarasani walianza kutoka kuelejea paredi lakini ajabu Jafari aliendelea tu na kuipiga kengele ile bila kusimama. Gafla tu zile kelele za kengele zikaanza kubadilika na kuwa miungurumo ya radi na ni yeye pekee ndiye aliyekuwa anasikia hivyo ikabidi atazame wenzake na kuona hawana habari wanaelekea paredi. Alishangaa kuona kile chuma kinakuwa cha moto sana hali iliyomfanya akitupe chini. Alipotazama mkononi aliona umebadilika na kuwa mwekundu kama ameungua na cha ajabu ni kuona Pete kwenye kidole huku akisikia maumivu taratibu kwenye mkono huo.

“haya mazingaombwe gani tena jamani hivi? hii pete imetokea wapi tena? Na kugonga kengele hivi ndio nipate maumivu haya jamani hadi kubabuka mikono?“alisema mwenyewe Jafari akiwa anautazama mkono wake. Akasikia anaitwa Paredi na haraka akaelekea kutii wito huo.

Kule kwa Nadhra akiwa amekaa pale aliona upepo mkali ukivuma na kutengeneza kitu kama kimbunga kilichosogea karibu yake.

“Ni mtu mmoja pekee ndiye aliyenifanya niwe hivi kulikoni kuuliwa na falme ya Siddik,huyu mtu yupo nchi ya mbali sana na ni wajibu wako umtafute muwe wote kuna kazi kubwa ya kufanya,yeye ndio atakuwa badala yangu hivyo mtakuwa pamoja muda wote.“ilisikika ile sauti ikitokea kwenye kile kimbuka kikali Nadhra akawa anakinga macho yake vumbi lisije kuingia, aliifahamu kuwa ni sauti ya baba yake mzazi ambaye muda mchache alikuwa kwenye adhabu ya kunyongwa.

“huyo kiumbe anatokea wapi? Na ana uweo mkubwa kama sisi?“aliuliza Nadhra.

“hadi sasa ana nguvu za ajabu ambazo zitawasaidia wakati wote japo yeye hafahamu kama anazo,nitakuonesha mahala anapo patikana uende kumshawishi ili uje naye huku mfanye ile kazi kwa pamoja,ukirejea nyumbani utapata kujua mahali hapo anapopatikana,sitawaona tena hadi mambo yatakapo kwenda sawa,niwatakie kazi njema.“ilisema ile sauti ya mzee kisha kile kimbunga kikapotea gafla na kumfanya Nadhra atambue sasa maneno aliyoambiwa.

Muda huo huo aliweka mikono yake chini na kutamka maneno fulani akapotea pale alipo gafla na kutokea nyumbani kwao, haraka akaelekea kwenye chumba kimoja na kufungua mlango akenda kwenye kabati akatoa beseni dogo kisha akaliweja mezani na kulijaza maji kiasi chake,akaanza kuyazungusha yale maji huku akitamka maneno fulani ya kichawi na gafla ndani ya maji ikaonekana tukio ambalo linapata kuendelea shuleni KWALUDEGE ambapo Jafari alionekana kupiga magoti chini huku Mwalimu mkuu akiongea mbele ya wanafunzi wote.

Kitendo kile kilimstaajabisha sana Nadhra baada ya kuona ni kitu kigeni katika macho yake.Ni nchi ambayo hakuweza kuitambua kabisa wala mazingira ambayo anayaona pale,kitu pekee alichokibaini ni pete ambayo alimuona kijana Jafari ameivaa na kujua ndio ile pete aliyoirusha juu angani. Hapo ndipo akabaini huenda huyu ndiye kijana aliyeambiwa na baba yake kuwa atakuwa naye muda wote kuikamilisha kazi fulani,aliisogeza ile picha ya Jafari akiwa pale chini amepiga magoti na kuanza kumchambua kujua kila kitu.

“anaitwa Jafari.. ana miaka 22... ni mtanzania... ni mpiga kengele wa shule... anaishi na kaka yake... anaadhibiwa kwa kosa la kuchelewa hadi kuharibu ratiba ya vipindi vya shule...ana nyota kali iliyozimwa na ndugu zake kutofanikiwa katika maisha...anapenda lakini hapendwi....mmh“yote hayo aliyaona Nadhra kupitia kwenye yale maji huku akimtazama kijana huyo akiwa kwenye ile adhabu.

Alitabasamu baada ya kumfahamu kuwa ndiye mtu pekee ambaye atakuwa naye katika harakati nzima ya kufanya kazi ambayo baba yake anahitaji iwe.

“muda si mrefu nitakuwa na wewe Eden,naamini tutashirikiana vyema.“alisema Nadhra huku akimtazama kijana Jafari ambaye alionekana akilala chini ili aadhibiwe bakora, alichokifanya Nadhra ni kuishika tu ile bakora kwa kuingiza mkono wake kwenye yale maji. Bakora ambayo Mkuu wa shule hiyo aliinyanyuka ipasavyo kumchapa Jafari matakoni, na kweli kila mtu alishuhudia bakora ile ikitua matakoni mwa Jafari ambaye alikunja sura kuona inashuka lakini ajabu hakuona maumivu yeyote yale katika mwili wake na kubaki kumtazama mwalimu huyo aliyekuwa akishusha bakora akijua zinamkolea kijana huyo hadi zilipofika sita akaacha na kumtaka anyanyuke kijana huyo huku baadhi ya wanafunzi wakishangaa kuona leo mwenzao hakuweza hata kutetereka kwa fimbo zile.

“Hii nakupa onyo kwa mara ya mwisho, tena nimejikuta nakusamehe bure uendelee na kitengo chako utakaporudia tena basi nampa mtu mwengine uongozi huo, leo umetufanya tunapoteza ratiba ya vipindi kwaajili yako maana watu walikuwa wanasubiri kengele kugonjwa wakafanye usafi lakini wapi watu wanaongea tu na kuweka vigenge vya umbea na muda wa masomo umefika, kwa mara ya mwisho mbele ya wanafunzi wenzako utakapo chelewa tena aisee utachimbua visiki vitano vya nguvu peke yako, haya rudi huko“alisema Mr. Bokeloo na kumfanya Jafari arudi na kuungana na viongozi wenzake waliokuwa nyuma ya wanafunzi. Muda wote huo alikuwa akizuga kuumia makalio lakini moyoni alikuwa na maswali mengi juu ya jambo lile imekuwaje hadi imetokea vile. Alitazama pembeni yake na kugongana na macho ya msichana Aziza ambaye alitokea kumhusudu sana, alijikuta akijenga tu tabasamu usoni mwake baada ya kutazamwa na mrembo huyo ambaye kwa aibu alitazama mbele kumsikiliza Bokeloo akiendelea kuongea.

“Kengele imegongwa kwa jambo moja tu, baada ya Break Fast kutakuwa na kikao baina ya walimu na wanafunzi wa kidato cha nne wote, hivyo basi kengele ya saa nne ya kunywa chai ikigongwa muende mkirudi mkae darasa moja watakuja walimu kuna mambo tunahitaji kuyaweka sawa, baada ya kusema hayo wote rudini madarasani kwenu“alisema Mwalimu huyo na kuwafanya wanafunzi wote warudi madarasani na yeye akaelekea zake ofisini mwake.

Jafari aligeuka na kuelekea zake darasani na muda huo huo akatokea msichana mmoja aliyefahamika kwa jina la Elizabeth ambaye ni rafiki sana wa karibu na kijana huyo.

“baba leo umezichezea sita za Mkuu, pole sana aisee maana tukawa tunaskia tu mlio wa bakora PAAH...PAAH... yule mzee kiboko kama anaua nyoka.“alisema Eliza akiwa amemshika mkono Jafari.

“mh ina maana mlikuwa mnasikia sauti ya bakora zikitua?“aliuliza Jafari maana hakusikia sauti wala maumivu yeyote yale ya fimbo zile.

“eh baba ndio kusema stiki zilikuzidi ukawa husikii au?“alisema Eliza na kumfanya Jafari awe njia panda,haelewi hili swala linakuwaje tena.

“eh naona Aziza amekuvisha Pete aisee, mambo ni mukidee aisee duu.“alisema Eliza baada ya kuiona ile pete mkononi mwa Jafari ambaye baada ya kusikia vile ndipo akakumbuka kumbe alikuwa na zoezi la kuutazama mkono wake pale alipokuwa akigonga kengele na kuhisi maumivu makali sana hadi kuumia. Aliunyanyua ule mkono wake na kuutazama akaona upo kawaida ile michubuko ikiwa imepotea na kuwa sawa tu. Alishika kile kidole chenye pete ambayo ilikuwa na maneno madogo madogo ya lugha isiyo eleweka.

Alichokifanya ni kuivua maana hakufahamu ilimpataje hadi ikawa kwenye kidole chake, lakini kila akiivua inashindikana kana kwamba imegandia pale kidoleni.

“Eliza.. unajua mimi sielewi hii pete imefikaje hapa kidoleni.. na nashangaa haitoki sijui nini tena hii jamani eh“alisema Jafari akiendelea kujaribu kuivua ile pete.

“acha kuleta muvi za kibongo wewe... wewe sema bwana mzigo kanivalisha Wifi yako tu basi sasa unanificha nini,mimi kuna kitu niliwahi kukuficha Jeffy, acha zako bwana..ngoja nielekee maliwato kabisa nikiingia darasani ni kupiga msuli tu.“alisema Eliza na kuelekea zake chooni akijua mwenzake anatania, akamwacha Jafari akiendelea zake kupambana na ile pete itoke kidoleni kwake.

“Mungu wangu haya mabalaa gani tena jamani eh..!“alikasirika sana kuona inashindikana kutoa ile pete hadi alipoona mwalimu wa somo Kiswahili anaingia darasani kwao naye akaamua aende kwanza darasani zoezi la pete atalifanya akitoka darasani.

ITAENDELEA
 
SIMULIZI: PETE YA MFALME WA EDEN
MTUNZI:JAFARI MPOLE
SEHEMU YA 03

ILIPOISHIA
“Mungu wangu haya mabalaa gani tena jamani eh..!“alikasirika sana kuona inashindikana kutoa ile pete hadi alipoona mwalimu wa somo Kiswahili anaingia darasani kwao naye akaamua aende kwanza darasani zoezi la pete atalifanya akitoka darasani.

TUENDELEE

Basi alielekea mahali pake na kukaa kisha akatoa daftari na kuendelea kumsikiliza mwalimu huyo wa Kiswahili aitwae Madam Negele. Alichukua chaki na kuandika somo analofundisha kisha akaandika mada ya siku hiyo na kuwageukia wanafunzi wake.
“haya naomba tuendelee leo, nakumbuka jana tuliishia katika kuchambua mifano ya Hadithi, Riwaya na shairi. Na tulishamaliza kuelezea namna ya Hadithi na Riwaya zinavyokuwa na mifano yake nikawapa, ila kwenye Simulizi ya kubuni nilielezea na nikatoa mfano kidogo wa ile simulizi ya NDOTO YA AJABU jinsi ilivyokuwa si ndio.?“aliuliza Madam Negele.
“ndiooo...“walijibu wanafunzi na mmoja wapo akasimama.
“ila Madam ile simulizi hukuimalizia aisee tamu sana ile tungeomba leo umalizie mfano wako“alisema Kijana mmoja aliyeitwa Ayubu, Madam alitabasamu huku akiwaangalia wanafunzi wake waliokuwa wakimuunga mkono kijana Ayubu.
“jamani ile ni ya kubuni tu na haina ukweli wowote..ila sawa wacha nisimulie kidogo maana tupo kwenye kipindi chake, niliishia wapi?“aliuliza Madam na kijana Jafari akasimama.
“pale ambapo Mfalme Saleh na Malkia Samira walipokuwa wakitoka kule Pangoni halafu nje Sabiha na Malik walikuwa wamejificha wakiwasubiri wawamalize, “alisema Jafari na kukaa chini.
“duh mpo makini kweli maana nilishasahau, haya basi bwana Mfalme na Malkia Samira walitoka mule pangoni wakiwa na furaha sana maana washafungishwa ndoa na Mfalme wa mwanzo wa taifa la Eden na pia wakapewa zawadi ya tufe lile na kila mmoja akakabidhiwa pete ambayo ni zaidi ya ulinzi kwao.“alisema Madam na kumfanya Jafari akumbuke ile pete alionayo kidoleni, aliitazama na kuanza kujenga hisia kama ni yeye ndiye Mfalme amevaa ile pete ambayo ni zaidi ya ulinzi kwake.
Alijikuta akijilaza kwenye dawati akiitazama ile pete kwa umakini sana huku akiyapitia maneno yaliyoandikwa kwenye pete hiyo ambayo hakuweza kuyatambua. Alisikia akiguswa bega lake na kumfanya ainuke pale alipoegemea kwenye dawati.
Alishangaa kumuona msichana ambaye hakuweza kumfahamu kwa sura, uzuri wake uliochangiwa na macho makubwa yalion‘gaa yalimfanya Jafari amtazame kwa muda bila kuchoka, yule msichana aliachia tabasamu la aibu huku akimtazama Jafari.
“Karibu Eden...“alisema msichana yule na kumfanya Jafari amshangae, lilipotajwa jina la Eden akakumbuka ni nchi ambayo ni ya kifalme na aliisikia kutoka kwa Madam Negele aliyewasimulia Simulizi ya NDOTO YA AJABU. Ndipo akili zikamjia kuwa alikuwa darasani muda huo, akajikuta akitazama mbele ili kumuona Madam aliyekuwa akiwasimulia Simulizi darasani, ajabu ni kwamba hakukuwa na Madam wala ubao kwa mbele, alipotazama pembeni kuangalia wanafunzi wenzake hakuona hata mmoja na kujikuta akiona vitabu vingi vikiwa ndani chumba hicho. Alijitazama pale alipokaa na kukuta amekaa kwenye kiti ambacho ni tofauti na dawati la shule KWALUDEGE. Ilimbidi asimame ghafla kwa kuogopa akawa anatazama huku na kule na kuona hali ambayo ni tofauti kabisa na mazingira ya darasani alipokuwepo.
“huna haja ya kuogopa Jafari, upo Eden kwasasa, na mimi ndio mwenyeji wako kuanzia sasa, naitwa Nadhra.“alisema mrembo yule akijitambulisha kwa Jafari ambaye bado hakuweza kuelewa.
“wewe...wewe... kama ushirikina wenu pelekeni huko, mimi nilikuwa darasani nasoma naomba nirudishe uliponikuta samahani sana sikujui hunijui na sitaki kukujua kwanza, nirudishe darasani niendelee kusoma.“alisema Jafari akiwa haelewi mazingira ambayo amejikuta yupo ghafla.
“sawa nitafanya hivyo ukitaka, ila nimekuleta Eden ufahamu mazingira ya huku mara moja kabla hatujaanza kufanya kazi pamoja.“
“wewe ndio uliniweka hii pete kidoleni!? "aliuliza Jafari akiwa anamtazama Nadhra.
“sijakuweka mimi ila ilikufuata yenyewe, hiyo ni kama zawadi kwako na huenda ikakusaidia kwenye maisha yako.“alisema Nadhra na kumfanya Jafari aitazame ile pete, alikumbuka lile tukio la kuchapwa bakora na Mwalimu mkuu lakini ajabu hakuweza kusikia maumivu yeyote na kuhisi huenda ni kwaajili ya pete hiyo. Akiwa kwenye tukio la kuitazama pete ile ghafla akasikia sauti tu ikimuita.
“we Jafari...“alistuka na kutazama mbele yake.
“jana hukulala kwenu? Hebu amka kanawe uso nje kwanza ndio urudi darasani nahisi hata tulicho kijadili hapa hukusikia nenda nje kwanza kanawe“ ilikuwa ni sauti ya Madam Negele aliyekuwa mbele ya darasa, Jafari alibaki kutazama darasa zima akiona anaangaliwa na wenzake. Alishangaa baada ya kuzidi kuona maajabu maana sekunde chache tu alikuwa akiongea na Nadhra ajabu saivi anajiona yupo tena darasani. Hakutaka kuonesha utofauti wowote akanyanyuka na kutoka nje moja kwa moja akaelekea kwenye bomba la maji na kufungulia akaweka kichwa chake maji yakaanza kutiririka. Aliona ni kama ndoto huenda akawa anaota baada ya kuambiwa na Madam kuwa alikuwa amelala darasani.
“itakuwa ndoto tu hii..“alijisemea mwenyewe akikataa kuamini ukweli wa mambo, lakini kitu pekee kilichomfanya achanganyikiwe ni ile pete ambayo bado ipo kidoleni kwake, aliitazama kwa umakini bila kuelewa. Alikumbuka maneno yale ya Nadhra kuwa huenda ikawa ni zawadi kwake ya maisha, alipokumbuka tena tukio la kuchapwa alianza kuhisi huenda ikawa sio ndoto tena bali ni ukweli. Taratibu akajikuta akianza kuamini mambo yale japo moyo unakuwa mzito kukubali.
Aliitazama tena ile pete kwa umakini.
“ina maana haya mambo yapo kweli? Nilikuwa nahisi ni Simulizi tu za kubuni kumbe yaweza kuwa kweli, sasa kwanini mimi? Hakuonekana mtu mwengine zaidi yangu mimi tu.? "alijiuliza sana Jafari bila kupata jibu kamili, aliamua kunyanyuka zake na kurejea tu darasani huku moyo wake taratibu ukianza kuamini matendo yaliyomtokea siku hiyo. Alipokaa kwenye dawati lake na Madam yule akawa anaandika ubaoni kazi ya kufanya wanafunzi.
“hii kazi nitaikusanya Ijumaa, leo Jumatano hadi siku hiyo mtakuwa mmemaliza, nahitaji kila mmoja wenu atunge kisa cha kuvutia ambacho hata mtu akisoma asisimke au kama ni kisa cha kutisha aogope kabisa, na nitoe tu ahadi kwa atakayefanya nikavutiwa na simulizi yake nampa ofa ya kula chakula na sisi walimu kwa wiki nzima atapumzika kula mapure (makande) ya shule na wenzake.“alisema Madam kwa tabasamu na kuwafanya wanafunzi wote wafurahi kusikia hivyo maana chakula wanachokula walimu ni tofauti na chakula cha wanafunzi. Kila mtu alitamani nafasi hiyo aipate yeye endapo akiandika simulizi itakayomvutia Madam Negele.

Baada ya kuondoka mwalimu huyo darasa likabaki na maongezi kuhusu kazi hiyo waliyopewa, kwa Jafari yeye hakuwa mwenye kufuatilia kazi hiyo waliyopewa yeye alikuwa akijadili tu na nafsi yake namna itakavyokuwa baada ya kufahamu kuwa ile pete iliyopo kidoleni kamwe haiwezi kutoka , aliona ni vyema akaonana na yule msichana Nadhra ili amuelezee kwa kina zaidi juu ya swala hilo.

Masaa yalizidi kwenda na muda wa mapumziko ulipofika Jafari kama kawaida yake alielekea kwenye kengele apate kugonga, alipoikaribia akawa na woga baada ya kuona ndio sehemu alipoipata ile pete, akajipa moyo na kukamata kile kichuma akagonga kengele kama kawaidia na wanafunzi baada ya kusikia wakaanza kutoka madarasani kwenda kupata kifungua kinywa kwenye mikahawa iliyopo pembeni na shule yao.


Muda huo akapita msichana Aziza na Jafari alipo muona ilibidi amfuate.
“Aziza...“aliita Jafari na kumfanya Msichana huyu asimame na kugeuka, alipomuona Jafari alibinua mdomo na kuangalia mbele.
“mambo vipi“alisalimia Jafari baada ya kumkaribia Aziza.
“poa tu..“
“si unaelekea kunywa tea.. tuongozane basi.“alisema Jafari na kupiga hatua kuongoza njia.
“we mwanaume mbona unanifuatilia sana? Si nilishakwambia lakini sitaki mazoea na wewe au husikii mwenzetu!“alisema Aziza kwa sauti na baadhi ya wanafunzi waliokuwa wakipita pembeni waliwatazama na kuendelea na safari yao.
“jamani taratibu basi tusiwafaidishe watu, mimi nimeongea kwa wema tu jamani sina nia mbaya lakini“
“awe Wema awe Diamond mimi hainihusu, sitaki kuongozana na wewe na narudia tena kukwambia sihitaji mazoea na mlugaluga sawa, hebu nipishe uko..“alisema Aziza na kumpushi Jafari akaendelea na safari yake. Jafari alibaki kumtazama tu mrembo huyo aliyejaaliwa uzuri na nyuma ameumbwa sawiya kabisa na ndio sababu iliyomfanya Kijana huyo ajaribu bahati yake mara kwa mara kwa mrembo huyo bila mafanikio.
“dah mimi sijui nina kizizi gani yarabbi...haya bana..“alisema Jafari na kuchanganya mwendo naye akaenda zake kupata chai akashangaa kuona ameshikwa mkono akiwa anatembea na alipotazama akamuona ni Eliza best wake na ni mtani wake pia.
“unajua nilikuwa nakukimbilia ila nilipokuona umesimama na wifi ikabidi nisimame tu niwaache mmalizane kwanza wapendanao.“alisema Eliza akiwa mwenye tabadamu usoni. Jafari alitazama msichana huyo akiwa na hasira zake mwenyewe za kukataliwa.
‘Eliza unapoelekea sasa nakutia kofi unikasirikie.“
“ah mimi mbona kupigwa nishazoea mwenzio, ipite siku bila kupigwa sisikii raha yani we nipige tu Jeffy, ila aka mwenzangu kama mmegombana wenyewe mkamalizane wenyewe mimi hainihusu.“alisema Eliza.
“hivi lini niliwahi kukwambia Aziza amenikubalia tukawa wapenzi mbona unakuza mambo we boya.?“alisema Jafari akionesha kukasirika.
‘acha ujinga Jeffy... ina maana tangu siku ile bado tu unaimbisha haelewi?“aliuliza Eliza na kumfanya Jafari akose jibu la kumpa.
“dah Jeffy unazingua, mimi najua mambo fresh yule ndo wifi ndio maana nakutaniaga sana kumbe dah...aisee nsamehe bure sikujua, ila nini tatizo, wapi umekwama naweza kukusaidia.“alisema Eliza na kumfanya Jafari amtazame tena.
“hanitaki ndio alivyoniambia, na kila siku ninavyomsumbua kumuelewesha ndio anaona namsumbua, nahisi leo ndio amenitapika kabisa na kuniambia nikome kumfuatilia.“alisema Jafari akiwa amesimama na Eliza karibu na mkahawa.
“ah achana nae basi utaumia bure ukipenda kwa mtu asiyekupenda, wanawake wapo wengi mbona unachagua tu wewe, hata hivyo nilisikia ticha Saidi anamfukuzia pia sasa sielewi kama ndio kashampata hadi Aziza anakukatalia wewe ama vipi, ila hiyo nimeisikia sina uhakika kama ni kweli.“alisema Eliza na kuzidi kumchanganya Jafari.
Wakaamua waache kwanza mada hizo watafute chai maana baadae wana kikao na walimu wao.
ITAENDELEA
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN
MTUNZI:JAFARI MPOLE
SEHEMU YA 04

ILIPOISHIA

TUENDELEE

Upande wa Eden katika jumba la kifalme wahudumu walikuwa wakitumwa tu huku na kule na waganga wa jadi pamoja na wataalamu wa mambo ya kichawi kuhakikisha wanamsaidia binti wa kifalme ambaye inasadikika yupo kitandani takribani wiki nzima. Kila mganga anayeletwa pale anafanya mambo yake na kutoa dawa za kutumia lakini inashindikana. Uchawi ambao ulioachwa na baba wa binti Nadhra ni mkubwa sana kiasi kwamba hakukuwa na mtaalamu wa kuweza kuutoa uchawi huo. Mwisho wa siku mganga wa mwisho aliposhindwa kumtibu binti huyo alimfuata Mfalme Siddik na kumpa heshima yake kisha akakaa kumueleza.
“hapa utaita kila mganga aje kumsaidia binti yako lakini ninachokwambia ndio ninachokiona kwenye utaalamu wangu, uchawi ulio tupwa kwenye mwili wa mwanao ni uchawi wa miaka mingi iliyopita. Uchawi huu ulitumiwa na binti wa kifalme wa zamani aliyeitwa Sabiha, yeye alikuwa na pacha wake ambaye ndiye alikuwaga Malkia wa enzi hizo akiwa na mumewe aliyeitwa Saleh, hivyo huyo Sabiha baada ya kufariki ndugu yake yeye ndio akawa Malkia wa Eden akawa anaiongoza vyema miaka yote. Sasa naye baada ya kufariki kwenye vita moja huko Mashariki ya mbali kuna mtu alifahamika kwa jina la Dalfa aliweza kuchukua nguvu zake na kujimilikisha yeye na ni Mfalme wa nchi ya huko Mashariki. Sasa uchawi aliotupiwa Binti yako ni ule wa Malkia Sabiha uliochukuliwa na Dalfa hivyo kama kupona huyu basi ni lazima apatikane mtu ndani falme yenu mwenye nguvu kama hizi ili aweze kuutoa uchawi huu,au laa apatikane huyu Dalfa muweze kumshawishi aje kumtibia binti yenu jambo ambalo sidhani kama litakuwa jepesi maana ana sheria kali sana."alisema Mzee yule mganga akimueleza Mfalme Siddik akiwa pembeni na Mkewe Malkia Rayat.
“Kama unapajua hata kesho twende huko Mashariki ya mbali tukaongee naye huyo Dalfa amponeshe mwanangu, anateseka sana“alisema Malkia Rayat akionesha kuumizwa na tatizo lililomkuta binti yake.
“Malkia wangu... tatizo sio kuonana na Dalfa tatizo ni matakwa anayohitaji yatimizwe, historia yake huyu mtu amechukua falme za watu nne na sasa anazimiliki yeye na ni kutokana na makubaliano tu kama haya baadhi ya wafalme ambao wanataka msaada kutoka kwake, yeye anawapa sharti la kuzichukua falme zako au eneo la utawala wa Mfalme huyo na wanakubali kusudi matatizo yao yaishe na ndio maana akapewa jina la MFALME WA MASHARIKI YA MBALI. Sasa nahofia tukaipoteza pia Eden ikawa mikononi mwa Dalfa."alisema yule na jambo hilo kwa Mfalme hakutaka kulisikia kabisa, anaipenda Eden kupita maelezo hawezi kuiacha ikachukuliwa kirahisi.
Wakati yeye akiifikiria Eden yake mkewe Malkia Rayat alikuwa akimfikiria binti yake kuhusu ile hali aliyonayo. Ni kama amekufa japo mapigo ya moyo yakisikika tu yakifanya kazi mara moja moja sana jambo lililomfanya Malkia huyo ahofie kumpoteza kabisa binti yake.
Basi mzee yule alipo waeleza yote hayo akanyanyuka na kuondoka zake akiwaacha wenyewe waamue moja kati ya hayo aliyowaeleza.
“Siddik nisikilize kwa makini,Maya ndiye mtoto wetu pekee tuliojaaliwa kuzaa na hatuna mtoto mwengine zaidi yake, yeye anatuangalia sisi tumsaidie katika maisha yake ili aje kuwa na matendo kama yetu,mimi naamini tunaweza kumtafuta huyo Dalfa na tukakaa naye tukaongea akachagua kitu hata chengine ili tu amsaidie mwenetu, nakuomba sana uwe jasiri kwa hili katika kuokoa maisha ya Maya."alisema Malkia Rayat.
“Huyu mtu yeye anataka kumilikishwa Falme,anakusaidia kisha wewe Mfalme au Malkia unakuwa raia tu wa kawaida yeye ndio anakuwa Mfalme,hadi kuitwa Mfalme wa Mashariki ya mbali juwa kuwa anajulikana, hawezi kukusikiliza kama hutatoa nchi yako jambo ambalo katu sitalifanya hata kama nimelala usingizi,Eden itabaki kuwa Eden."alisema Mfalme Siddik kwa kusisitiza.
“Una maana gani sasa moyoni mwako kama baba wa Maya? Una maana bora afe mwanao ili wewe uendelee kuongoza watu?si ndio una maana hiyo?nijibu.."alisema Malkia Rayat kwa ukali na kumfanya hata mumewe akose jibu la kusema, alinyanyuka Malkia na kuondoka zake kwenda chumbani kwa binti yake huyo aliyeko kitandani tu wahudumu wakimfuta futa na kumuangalia muda wote. Alitokwa na machozi mama mtu baada ya kuzidi kuumia kuona hali ya mwanaye pale kitandani,alisogea mpaka pale na kukaa kisha wale wahudumu wakaamka na kumpa heshima kisha wakatoka zao nje kumuacha mama akimuangalia mwanaye kwa huzuni.
“Maya mwanangu,mimi mama yako nakuombea tu lazima utapona ni lazima, huwezi kuniacha mimi au baba yako tukiwa hai wakati wewe bado kijana unapaswa kuongoza hii Eden kama Malkia kama mimi mama yako, amka mwanangu...amkaaa!"alisema Mama mtu huku akiushika mkono wa mwanaye na kuuweka shavuni kwake. Muda huo Mfalme alikuwa akichungulia tu na kuona jinsi mkewe anavyomlilia mwanaye, hata yeye kama baba aliumia sana kuona binti yake yupo kama maiti tu pale kitandani,aliyazuia machozi yasimbubujike na kugeuka akaondoka zake pale.
Alijifungia chumbani kwake akitafakari sana swala linaloendelea,kichwa chake kilijigawa mara mbili kiakili kuwa aende kwa Dalfa amueleze matatizo ya mwanaye na atakapotaka kuichukia Falme ya Eden akubali kisha mwanaye apone naye Mfalme awe raia wa kawaida kama wananchi wake? Au aendelee na Ufalme wake kama kawaida lakini akijua mwanaye si wakupona tena lazima atakufa!. Ni maswali ambayo alikaa akiyatafakari mwenyewe zaidi ya lisaa lizima bila kupata majibu.

Dakika chache aliingia Malkia Rayat akionesha kupooza huku sura ya majonzi ikimtawala,alisogea hadi kwa mumewe ambaye naye alisimama na kumkumbatia mkewe wakabaki wamekumbatiana wawili hao.
“Mfalme... naomba umsaidie mwanangu...nakuomba sana..“alisema Malkia Rayat akiwa kama mama sasa, kauli yake ilimliza hata Mfalme na kuona kama anaombwa na raia wake wa kawaida na sio Malkia wala mkewe, hii ina maanisha kwamba ufalme wala umalkia si kitu mbele ya damu yao bora wakubali tu kuupoteza uongozi wao ili mtoto wao apone.
Mfalme alijitahidi sana kukubaliana na mkewe lakini moyo unakataa kabisa na kujikuta akishikiria msimamo wake kama Mfalme,alimuacha tu mule ndani mkewe akatoka zake nje kutafuta namna ya kufanya.

Kesho yake asubuhi Malkia Rayat baada kutafakari kwa kina zaidi na kuona huenda akampoteza mwanaye bora ajiongeze kama mama maana yeye ndio mwenye uchungu zaidi,aliamua kutoka ndani ya falme akiwa na mpambe wake mmoja bila Mfalme kujua akamfuata yule mzee aliyewapasha habari kuhusu Dalfa,mzee huyo alipomuona ni Malkia ilibidi ampe heshima yake naye Malkia akapokea na wakakaa kuongea.
“Sikai sana hapa nimekuja nina jambo moja tu nahitaji kutoka kwako,nataka unielekeze wapi nitampata Dalfa."alisema Malkia na kumfanya yule Mzee ashtuke baada ya kujua huenda ndio anataka kwenda kuweka makubaliano na Dalfa.
“Mh lakini Malkia hilo swa...“
“Nimekwambia unielekeze wapi anapopatikana Dalfa.!"alisimama kwenye msimamo wake Malkia na kumtia mkwara yule Mzee ikabidi akubali tu,akamuelekeza japo kwa shingo upande akijua sasa Eden inaenda kuuzwa.
“Haya nitaenda huku kuonana naye na naomba uwe kimya nisisikie lolote ukilifikisha kwa Mfalme juu ya tulichoongea,nikutakie siku njema.“alisema Malkia na kuondoka zake baada ya kupata maelekezo ya kina zaidi anapopatikana Dalfa, akaondoka na yule mpambe wake kurudi kwenye falme.
Aliandaa farasi maalumu kwaajili ya safari ya kuelekea Mashariki ya mbali lengo ni kukutana na huyo Dalfa wapate muafaka,alimuaga mumewe kuwa anaelekea zake kuzunguka huko mipakani na kurejea hapo baadae Mfalme akamruhusu bila ya kujua kuwa mkewe anaenda safari ya mbali. Malkia aliondoka zake na mpambe wake safari ikaanza kuelekea huko.

Siku hiyo jioni Jafari alikuwa zake nyumbani kwao ambapo anakaa na kaka yake na shemeji yake ambaye yumjamzito, muda mwingi anatumia kusaidia kazi za pale ndani kutokana na hali ya shemeji yake.Siku hiyo aliamua kusonga kabisa ugali huku shemeji yake akimtazama tu na kubaki kutabasamu.
“Nakwambia huyo mwanamke utakayempata atafaidi kwakweli."alisema Shemeji mtu na kumfanya Jafari atabasamu.
“Sio kufaidi tu na kunenepa kabisa maana atakula mapochopocho hata yeye hakuwahi kupika."alisema Jafari akiendelea kuusonga ugali. Shemeji katika hali ya kumuangalia Jafari akisonga ugali alipata kuiona ile pete ikiwa inan‘gaa.
“Kumbe ushavalishwa na pete kabisa mumewangu huko,mlete basi mke mwenzangu anisalimie.“alisema shemeji mtu na kumfanya Jafari azuge tu.
“Hii ni ya urembo tu bwana shemeji wala sio yenyewe, ila akipatikana namleta wala usijali utakuwa unakaa kama hivyo anakusaidia kupika wewe si mke mkubwa bwana."alisema Jafari na kumfanya shemeji yake atabasamu tu na kuendelea na maongezi mengine. Hata chakula kilipokuwa tayari waliandaa na kula wawili hao na baadae kila mmoja akajipumzisha.
Jafari aliingia chumbani kwake na kutulia kitandani akiitazama ile pete.
“sasa kila mtu anaiona hii pete siku broo akija kuiona si ndio itakuwa balaa atakaponiambia niivue na kitu kimegoma kutoka hiki."alisema Jafari huku akiitazama ile pete, kwa mbali aliona kitu fulani kwenye ile pete ilibidi asogeze kidole kile karibu na macho yake.
Alipata kuona tukio ambalo linaendelea, wanawake wawili wakiwa kwenye farasi wakiwa spidi wanaelekea sehemu fulani,alishindwa kuelewa ni wakina nani wale na kubaki kuangalia tu wakizidi kwenda.
“hawa ni akina nani tena?“alijiuliza mwenyewe pale huku akitazama pete ile kile anachokiona.
“ni Malkia wa Eden, Rayat yupo na Mfanyakazi wake wakielekea Mashariki ya mbali kukutana na Dalfa ambaye ni mtu mwenye uwezo wa kumponyesha mtoto wa Mfalme aitwaye Maya“ilisikika sauti kutoka kwenye pete ile ikiongea, Jafari alishangaa kusikia vile akawa anaigeuza geuza ile pete kuona wapi inapotokea sauti ile. Alivyorudisha kidole kama awali aliona yule Malkia na mfanyakazi wake wametolewa na kuona mtu mwengine tena akiwa amelala kitandani.Alipojua kuwa kumbe pete ile ni zaidi ya zawadi kwake ilibidi aizoee tu na kujikuta akiitumia tena kuuliza.
“na huyu je ni nani?“
“anaitwa Maya Siddik, ndio Binti wa Mfalme Siddik, yupo hapo kitandani siku ya nane sasa hakuweza kuamka kwa maradhi, ndio mama yake pamoja na yule mfanyakazi wameenda Mashariki ya mbali kutafuta msaada kwa huyo Dalfa.“ilisema ile pete na kumfanya Jafari aisogeze ile pete vizuri amtazame huyo binti wa kifalme hammadi..... alipomuangalia vizuri sura yake ni vile vile kama alivyo msichana aliyempenda sana shuleni kwao lakini yeye hapendwi, Aziza.

IMEKUWAJE AZIZA AKAWANAFANA VILEVILE NA MAYA..TUKUTANE KESHO SEHEMU IJAYO.
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN
MTUNZI:JAFARI MPOLE
SEHEMU YA 05

ILIPOISHIA
Jafari aisogeze ile pete vizuri amtazame huyo binti wa kifalme hammadi..... alipomuangalia vizuri sura yake ni vile vile kama alivyo msichana aliyempenda sana shuleni kwao lakini yeye hapendwi, Aziza.

TUENDELEE

Siku hiyo jioni Jafari alikuwa zake nyumbani kwao ambapo anakaa na kaka yake na shemeji yake ambaye yumjamzito, muda mwingi anatumia kusaidia kazi za pale ndani kutokana na hali ya shemeji yake. Siku hiyo aliamua kusonga kabisa ugali huku shemeji yake akimtazama tu na kubaki kutabasamu.
“nakwambia huyo mwanamke utakayempata atafaidi kwakweli “alisema Shemeji mtu na kumfanya Jafari atabasamu.
“sio kufaidi tu na kunenepa kabisa maana atakula mapochopocho hata yeye hakuwahi kupika “alisema Jafari akiendelea kuusonga ugali. Shemeji katika hali ya kumuangalia Jafari akisonga ugali alipata kuiona ile pete ikiwa inan‘gaa.
“kumbe ushavalishwa na pete kabisa mumewangu huko, mlete basi mke mwenzangu anisalimie. “alisema shemeji mtu na kumfanya Jafari azuge tu.
“ya urembo tu hii bwana shem wala sio yenyewe, ila akipatikana namleta wala usijali utakuwa unakaa kama hivyo anakusaidia kupika wewe si mke mkubwa bwana “alisema Jafari na kumfanya shemeji yake atabasamu tu na kuendelea na maongezi mengine. Hata chakula kilipokuwa tayari waliandaa na kula wawili hao na baadae kila mmoja akajipumzisha.
Jafari aliingia chumbani kwake na kutulia kitandani akiitazama ile pete.
“sasa kila mtu anaiona hii pete siku broo akija kuiona si ndio itakuwa balaa atakapo niambia niivue na kitu kimegoma kutoka hiki."alisema Jafari huku akiitazama ile pete, kwa mbali aliona kitu fulani kwenye ile pete ilibidi asogeze kidole kile karibu na macho yake. Alipata kuona tukio ambalo linaendelea, wanawake wawili wakiwa kwenye farasi wakiwa spidi wanaelekea sehemu fulani, alishindwa kuelewa ni wakina nani wale na kubaki kuangalia tu wakizidi kwenda.
“hawa ni akina nani tena? “alijiuliza mwenyewe pale huku akitazama pete ile kile anachokiona.
“ni Malkia wa Eden, Rayat yupo na Mfanyakazi wake wakielekea Mashariki ya mbali kukutana na Dalfa ambaye ni mtu mwenye uwezo wa kumponyesha mtoto wa Mfalme aitwaye Maya“ ilisikika sauti kutoka kwenye pete ile ikiongea, Jafari alishangaa kusikia vile akawa anaigeuza geuza ile pete kuona wapi inapotokea sauti ile. Alivyorudisha kidole kama awali aliona yule Malkia na mfanyakazi wake wametolewa na kuona mtu mwengine tena akiwa amelala kitandani. Alipojua kuwa kumbe pete ile ni zaidi ya zawadi kwake ilibidi aizoee tu na kujikuta akiitumia tena kuuliza.
“na huyu je ni nani?“
“anaitwa Maya Siddik, ndio Binti wa Mfalme Siddik, yupo hapo kitandani siku ya nane sasa hakuweza kuamka kwa maradhi, ndio mama yake pamoja na yule mfanyakazi wameenda Mashariki ya mbali kutafuta msaada kwa huyo Dalfa.“ilisema ile pete na kumfanya Jafari aisogeze ile pete vizuri amtazame huyo binti wa kifalme hammadi..... alipomuangalia vizuri sura yake ni vilevile kama alivyo msichana aliyempenda sana shuleni kwao lakini yeye hapendwi, Aziza.
“hee, anaitwa nani umesema?“
“anaitwa Maya Siddik, ni binti wa Mfalme Siddik“. ilisema ile pete na kumfanya Jafari acheke.
“hapana bwana huyu ni demu tunasoma naye shule moja anaitwa Aziza bwana na sio Maya.“alisema Jafari akiwa anatabasamu baada ya kumuona Maya akiwa yupo vilevile kama alivyo Aziza msichana aliyemkataa Jafari.
“ni ufanano wa sura tu, ila matendo, tabia na nchi ni tofauti.“ilisema ile pete.
“nitaamini vipi sasa kama sio Aziza ninayemjua mimi wakati sura yake naifahamu kabisa kuwa ndiye."alisema Jafari.
“fumba macho yako“ilisema ile pete na kumfanya Jafari ameze mate kwa woga, ikabidi afumbe maana amesema mwenyewe.
“haya fumbua“ ilisema ile pete na kumfanya Jafari aanze kufumbua jicho taratibu kama anachungulia kitu huku akitazama huku na kule, aliona yupo mahala tofauti kabisa ikabidi afumbue macho yake kabisa. Alishangaa kuona hayupo tena pale chumbani kwake na kujikuta yupo kwenye chumba tofauti kabisa. Chumba kilichopambwa na maua na picha mbalimbali ukutani, alipo zitazama picha zile sasa akaona wazi sura na umbo la binti wa Mfalme, Maya akiwa kwenye tabasamu na mavazi tofauti tofauti ya heshima. Utofauti aliouona ni kuwa Maya anaonekana mwenye nywele ndefu zenye kun‘gaa zikifika mgongoni, hapo ndipo Jafari akaamini kweli wamefanana sura tu na Aziza. Basi alitazama vitu vingine na kuzidi kuangaza huku na kule na mwishowe akapata kumuona mhusika mwenyewe akiwa amelala kitandani. Jafari alibaki kumtazama tu mrembo huyo na kuanza kupiga hatua taratibu kusogea pale kitandani na kumuona Maya kwa macho yake kabisa.
“Ma..ya“ aliita Jafari kwa sauti ya chini baada ya kumuona mrembo Maya, hakika ni vilevile alivyo Aziza ambaye anampenda sana lakini upendo wake si chochote kwa binti yule.
Alinyanyua mkono wake na kushika nywele zake laini na kujikuta Jafari akitabasamu tu.
Ghafla akarudishwa chumbani kwake kule kama awali.
“ah sasa mbona umenirudisha tena huku?“alilalama Jafari maana alitamani kumshika zaidi binti yule.
“nilikupeleka Eden mara moja tu ukaone utofauti ya Maya na Aziza, nadhani umeshaona utofauti wao“ilisema ile pete.
“sawa nishaona, naomba nirudi basi tena nimuone vizuri Maya.“alisema Jafari baada ya kunogewa na mahali pale.
“unapaswa ukaribishwe rasmi Eden, awali Nadhra alikupeleka na kukukaribisha ukakataa na kutaka urudishwe darasani uendelee na masomo yako, vipi leo upo tayari akukaribishe Eden? “ilisema pete ile, na bila kipingamizi Jafari akaridhia mwenyewe.
“ nipo tayari sasa“alisema Jafari na kujiongeza mwenyewe akafumba macho sekunde tatu tu kufumbua akajikuta yupo kwenye kiti akiwa na Mrembo Nadhra akiwa amejaa tabasamu usoni mwake.
“Jafari, karibu sana Eden..“alisema Nadhra na kumfanya Jafari atabasamu baada kuanza kuzoea sasa hali ile.
“asante sana“alisema Jafari.
“leo ni siku kubwa sana kwako na naamini utaifurahia, sijui kama utalikumbuka jina langu?“. Alisema Nadhra na kumtazama Jafari ambaye alilisahau jina la mrembo huyo, lakini alipotambua uwepo wa pete ile akajikuta akiuliza moyoni na kutajiwa.
“unaitwa Nadhra “alisema Jafari na kumfanya Nadhra atabasamu baada ya kujua sasa mhusika anaanza kuzoea zawadi aliyopewa.
“nimefurahi kwa wewe kulijua jina langu, karibu tena Eden“alisema Nadhra na kumfanya Jafari atazame kile chumba walichopo, kulikuwa na vitabu vingi sana vimepangwa kama Maktaba.
“na hapa ni wapi tulipo? “aliuliza Jafari na kumfanya Nadhra anyanyuke na kuanza kutembea.
“ni chumba ambacho baba yangu alikuwa akitumia kusoma mambo ya kale na kupitia vitabu hivi na hata kuvifanyia kazi.“alisema Nadhra akishika shika vitabu, ilimbidi Jafari naye asimame pale alipo na kuanza kutembea tembea kuangalia baadhi ya vitabu hivyo.
“baba yako alikuwa msomi na mpenzi wa kusoma vitabu eh?“
“bila shaka, alipenda sana kuiga mambo ya zamani maana anaamini hapo zamani watu wa Eden waliishi kwa amani na upendo tofauti na sasa“
“mh kwani sasa wanaishi vipi?“
“hakuna uhuru kama mwanzo, awali kulikuwa na watu waliokuwa na zawadi za asili uwezo na nguvu za ziada kuliko viumbe wengine, na walizitumia kusaidia watu na mambo mema na ni wachache sana waliotumia nguvu hizo kuwadhuru watu, lakini Eden ya sasa haiangalii huyu mbaya wala mzuri wao wakikujua kuwa una uwezo huo wakikukamata hukumu yako ni kama aliyopata baba yangu... walimnyonga mpaka kufa.“alisema Nadhra na kumfanya Jafari ashtuke na kujiwa na huruma baada ya kufahamu kumbe baba yake na msichana huyo amefariki.
“pole sana Nadhra.. na unataka kuniambia hata wewe pia una nguvu hizo kama za baba yako? “aliuliza Jafari na kumfanya Nadhra aitike kwa kutikisa kichwa kuwa anazo pia.
“na imekuwaje mimi niwe hapa Eden, nahusiana nini na mambo yenu haya?“aliuliza Jafari na kumfanya Nadhra amsogelee na kuushika mkono ule uliokuwa na pete, akashika kile kidole na kuivua ile pete kiulaini kabisa hali iliyomfanya hata Jafari ashangae maana ilikuwa kazi kweli kuitoa pete ile.
“hii ndio sababu, siku ambayo baba yangu anapewa hukumu ya kunyongwa ndipo siku ambayo pete hii ilipata kuwa kwenye kidole chako, niliagizwa na baba kuwa kama nahitaji kuwa naye kiroho basi niitupe pete hii kwenye kengele yeyote ile iwe ni kama njia moja wapo ya kumpata tena lakini katika kutafuta kwangu kengele nilikosa nilisikia sauti ya kengele ikipigwa kwa mbali hivyo nikaamua kuitupa pete hii juu angani nikiwa na imani ifike kwenye mlio niliousikia, na kwa bahati ni wewe ndiye uliyekuwa ukipiga kengele shuleni kwenu na ndio maana pete ile ikajivisha kwenye kidole chako. Hiyo ni bahati kwako na hata baba yangu amefurahi kwa kuweza kumfanya aishi tena japo si kama zamani.“alisema Nadhra na kumfanya Jafari afahamu sasa ukweli wa pete ile.
“ina maana.. nilivyokuwa napiga kengele shuleni mlio ulifika hadi huku? Duuh"
*huo ndio ukweli, na kwa kuwa umeweza kumfanya baba yangu awe anaishi kwa namna nyengine basi ameridhia yeye uwe badala yake.“
“badala yake? kivipi yaani, niwe mimi ndio baba yako?“alisema Jafari na kumfanya Nadhra aachie tabasamu.
“sina maana hiyo, maana yangu ni kwamba zile nguvu zake zote wewe ndiye utakaye kuwa nazo kwa sasa na yeye amesharidhia hivyo.“alisema Nadhra na kumfanya Jafari avute funda moja la mate kwanza maana ameshaambiwa fika kuwa wenye nguvu hizo wakikamatwa adhabu yao ni kunyongwa mpaka kufa.
“naomba niulize swala moja tu...lengo hasa ni nini la mimi kutaka nirithi nguvu za baba yako, kuna kitu gani kinaendelea hapa kati ambacho mimi sikijui?“
“iko hivi, kama nilivyo kueleza awali baba yangu ni mtu anayependa kusoma vitabu vya kale, alipokuwa akiisoma Eden ya zamani iliyokuwa ikiongozwa na Wafalme kama Yassir, Saleh na malkia Samira uongozi wao ulikuwa wa upendo muda wote baina ya raia na ufalme, vilevile nguvu hizi zilikuwa kwa watu wengi ambao walikuwa huru kwa kujilinda wao wenyewe na kusaidia wengine hasa katika matatizo ya kifalme, tofauti na sasa wanataka kuua kabisa mambo hayo na Mfalme awe ni mtu wa kuogopwa na watu wake siku zote jambo ambalo halikuwepo hapo awali ndani ya Eden. Eden imegeuzwa sio Eden ile ya uhuru wa watu na ndio maana baba yangu akatumia njia ya kumuadhibu Mfalme kwa kumsababishia binti yake asipate kuamka kitandani kwa muda wa masiku mengi ili akubali na kuwaachia watu wenye nguvu za asili waendelee kuishi kama wengine na si kuwanyonga kama anavyofanya, hivyo basi wewe ndio utakuwa mtu pekee wa kuhakikisha swala hili linakaa sawa utumie akili na nguvu utakazopewa kumshawishi Mfalme Siddik akakuelewa"alisema Nadhra kwa kina zaidi kumuelewesha Jafari ambaye aliyasikia yote na kujua sababu ya yote haya. Alimkumbuka yule binti wa kifalme aliyemuona kweli akiwa kitandani tu kumbe aliyefanya haya ni baba yake Nadhra na lengo ni kumfanya Mfalme Siddik akubaliane na matakwa yao, akaona kweli kuna haja ya kufanya jambo ili haya mambo yawe sawa watu wapate kuwa na amani na Eden yao. Alitafakari kwa kina na kuona wacha ajitoe kimasomaso kama nguvu atakuwa nazo basi hakuna haja ya kuogopa.
“sawa... nitakuwa na wewe katika swala hili Nadhra.“alisema Jafari kwa ujasiri na kumfanya Nadhra afurahi akamsogelea na kumkumbatia kwa kuona ameeleweka.
Basi taratibu za kupatiwa nguvu za mzee yule zikafanyika ndani ya chumba kile ambapo Jafari ilimbidi alazwe kwenye meza ndefu kisha Nadhra akaanza kufanya maombi yake kwa kutumia nguvu za ajabu, roho ya mzee wake ilifika nayo ikaanza kutoa sasa nguvu zake zote na kumkabidhi rasmi kijana huyo ambaye alikuwa akitokwa na jasho jingi sana mwilini na hata baada ya muda alipoteza fahamu baada ya zoezi lile kukamilika.

ITAENDELEA
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN
MTUNZI:JAFARI MPOLE
SEHEMU YA 06

ILIPOISHIA
roho ya mzee wake ilifika nayo ikaanza kutoa sasa nguvu zake zote na kumkabidhi rasmi kijana huyo ambaye alikuwa akitokwa na jasho jingi sana mwilini na hata baada ya muda alipoteza fahamu baada ya zoezi lile kukamilika.

TUENDELEE
Upande wa pili ilikuwa ni msako kila mahala ndani ya Eden baada ya kufahamika Malkia pamoja na mfanyakazi wake mmoja kutojulikana walipotokomea, askari wa kifalme walienda mpaka mipakani kwa Eden kuwatafuta wakizunguka na farasi zao huku na kule bila mafanikio jambo lililomfanya Mfalme azidi kuchanganyikiwa maana mwanaye mgonjwa na mkewe pia ndio hivyo akihisi amepotea. Hakuwa nyuma na yeye alihakikisha anashiriki zoezi hilo kikamilifu kuhakikisha Malkia anapatikana.Yule mzee aliyempa ramani Malkia ya kufika kwa Dalfa alikuwa tu kimya muda wote akificha ile siri japo moyo wake unamuuma sana kuona Eden inakwenda kuuzwa na Malkia, hadi askari na Mfalme walipoanza kukata tamaa jioni kabisa ikiingia ndipo mzee yule uzalendo wa kuficha siri ile ukamshinda ilimbidi amueleze ukweli wote Mfalme Siddik ambaye baada ya kuambiwa hivyo alistaajabu.
“ATI NINII?..“
“Ndio hivyo Mfalme wangu, Malkia aliniziba mdomo nisiongee kuhusu swala hilo lakini kwa akili yangu naona Eden inakwenda kuwa mikononi mwa Dalfa jambo ambalo sidhani kama utaliafiki na ndio maana nimeona bora nikueleze tu ukweli.“alisema Mzee yule na kumfanya Mfalme akasirike sana kusikia hivyo. Hakutaka hata kuchelewa aliandaa jeshi la watu elfu moja naye akiwemo na kuanza safari ya ghafla kuelekea huko Mashariki ya Mbali kuwahi kama wataweza kulizuia jambo hilo ambalo Malkia aliwahi kwenda huko mapema.
Alifika mbali sana na mfanyakazi wake na walikwenda mbele walipata kuona kijiji kimoja ikabidi wasogee hapo na kutafuta mahala pa kupumzika kwanza maana usiku ulishaingia.
Walifika kwenye nyumba moja ambayo ilikuwa karibu na njia ya kuelekea na safari yao ikabidi wafike hapo kuomba hifadhi, walimkuta Mzee mmoja ambaye baada ya kuwaona akafahamu ni watu wanaotoka Eden.
Mpambe wa Malkia aliyeitwa Faisar ndiye alikuwa akiongea na mzee yule na kumueleza kuwa aliye naye ni Malkia wa Eden, mzee yule kusikia vile ilibidi atoe heshima kwa Malkia Rayat na kuweza kuwakaribisha ndani, Aliwaandalia chai ya moto usiku ule na Malkia pamoja na Faisar wakapokea na kuanza kunywa huku maongezi ya hapa na pale kwa mzee yule yakiendelea.
“Eden inakumbukwa hapa kijijini kutokana na matukio ya nyuma yaliyowahi kutokea, kuna mwanamama mmoja alikimbia kutoka Eden na kuja kujihifadhi hapa akiwa na watoto wawili na ilisafikika mtoto mmoja alipewa na Mfalme wa kipindi hicho akimbie naye maana walizaliwa mapacha na mmoja ilibidi auawe kama ilivyo mila za Eden kipindi hicho, sasa waasi kusikia hivyo ilibidi wamtafute mama huyo na kufanikiwa kutambua kuwa alikuwa kijiji hichi, walichokifanya ni kuchoma moto nyumba zetu ikawa ni vita sasa na kwa bahati Mfalme aliwasili na kuanza kuwadhibiti akishirikiana na wanakijiji hadi wale waasi wakatoweka lakin waliacha majonzi kwenye kijiji waliua watu wengi na kiharibu mali zetu kipindi hicho ningali kijana.“alisema Mzee yule akisikilizwa kwa makini.
“nilipata kusimuliwa hayo matukio aisee kumbe ni kijiji chenu ndio kimekumbwa na balaa hilo, poleni sana.“alisema Malkia akiwa ameshika kikombe.
“tushapoa na ndio hivi tunaendelea na maisha mapya hayo yalipita muda sana.“alisema Mzee yule na maongezi yakaendelea.
“haya mlikuwa mnaelekea safari ya wapi?“aliuliza Mzee yule na kumfanya Malkia amtazame Faisar.
“tunaenda mbali kidogo na mji kuna mtu tunaenda kuonana naye ndio maana tukaona wacha tutafute hifadhi kwanza ili hapo kesho mapema tuweze kuendelea na safari.“alisema Faisar.
“ahaa basi sawa mtapumzika hapa usiku huu na hapo kesho mtaweza kuendelea na safari yenu“alisema mzee yule na kuwafanya Malkia na mfanyakazi wake wamshukuru kwa ukarimu wake, waliandaliwa sehemu ya kulala na mzee yule ambaye alionekana kuishi mwenyewe tu.

Asubuhi kulipo pambazuka baada ya kutoa shukran kwa Mzee yule Malkia alitoa kidani cha dhahabu na kumkabidhi mzee yule kama shukrani kwake na safari ikaanza tena kuelekea huko.
Huku nyuma Mfalme alikuwa na askari wake aliotoka nao kwenye falme kuelekea nao hukohuko Mashariki ya Mbali kuwahi kumzuia Malkia asije kufanya lolote na Dalfa.

Upande wa pili kwa Jafari asubuhi ya siku hiyo akiwa zake darasani akiendelea na masomo yake alipata kuona kuna mwanga wa kun‘gaa ukitokea kwenye pete yake hali iliyomfanya ashtuke na kuamua kuiziba pete ile kwa mkono wa pili. Ilimbidi aushushe mkono huko chini ya dawati na kutazama pete ile ikimuonesha binti wa kifalme Maya akiwa bado amelala pale kitandani huku pembeni akionekana mfanyakazi mmoja aliyekuwa akimhudumia lakini akionekana kuwa na wasiwasi huku akichungulia huku na huku ili asionekane. Alitoa kichupa kidogo ambacho kilikuwa na unga fulani kisha akaukoroga kwenye maji yaliyopo kwenye bakuli huku akiwa mwenye wasiwasi. Jafari akahisi huenda mtu yule kawa si mwema kwa Maya.
“wewe unataka kufanya nini hapo?“alisema Jafari kwa sauti na kufanya darasa zima wageuke kumtazama Jafari. Aliponyanyua kichwa akashangaa kuona anatazamwa na ghafla wanafunzi wakaanza kuangua kicheko huku Mwalimu wa Hesabu aliyekuwa ubaoni ilibidi amshangae Jafari.
“wewe una kichaa? Unaongea na nani?“aliuliza Mwalimu yule na kumfanya Jafari akose jibu la kusema, hakutaka tena kukaa alinyanyuka na kusogea mbele kwa mwalimu.
“nahisi sipo sawa naomba niende nje mwalimu“alisema Jafari na bila kujibiwa akafungua mlango na kutoka nje akikimbia hadi uwani. Aliitazama ile pete na kuona bado yule mfanyakazi anakoroga ule unga kwenye maji.
Alitamani kupotea tu ghafla atokee kule lakini alishindwa afanyeje, akajikuta akikasirika na kukunja ngumi kwa mkono ule aliovaa ile pete kuona huenda kuna kitu anafanyiwa Maya, na kitendo cha kukunja ngumi tu akapotea ghafla na kutokea pale pale chumbani ambapo Maya alikuwa amelala. Na kweli alimuona mwanamke yule akiwa anaingiza kitambaa kwenye yale maji aliyochanganya na unga ule na kutaka kumkanda kanda Maya.
“wewe unataka kufanya nini? “alisema Jafari na kumshtua yule mwanamke akatupa kile kitambaa na kurudi nyuma, alipomtazama Jafari akajikuta akijenga tabasamu.
“ah hehe.. Samir umefikaje hapa...ah nilikuwa namfutafuta Maya jasho. “alisema yule mwanamke akionekana kutokuwa na amani.
“nini..? umeniitaje....Samir?“ali aliuliza Jafari baada ya kusikia akiitwa jina tofauti na lake.
“hee sasa unataka nikuite nani? “alisema mwanamke yule na kumfanya Jafari ajishangae kwanza. Ajabu alipojiangalia akajiona yupo kwenye mavazi tofauti na nguo zake za shule, alikuwa kwenye mavazi ya kizamani nguo zilizoishaisha hadhi yake zikiwa zimechakaa, hakika alistaajabu sana kujiona vile na alipoangalia kidoleni kwake pete ile kama kawaida ipo. Alihisi huenda ndio ilivyopangwa iwe hivyo na kuendelea kumtazama yule mwanamke.
“sasa mbona umeshtuka sana hadi ukatupa kitambaa, kuna kitu kinachoendelea hapa?“
“mh wala hakuna kitu, umenishtua tu“alisema mwanamke yule.
“sawa, ila naomba nimfute mimi jasho leo Maya wewe kafanye kazi nyengine.“
“hapana wewe kazi zako ni nje na si huku ndani hivyo huwezi kufanya hivi hata Mfalme au Malkia akikuona huku utapata tabu, nenda zako tu.“alisema Mwanamama yule aliyefahamika kwa jina la Lutfiya na kuokota kile kitambaa. Jafari akaona ni ujinga kumruhusu huyu mtu aendelee na jambo lile, alimsogelea na kumpokonya kile kitambaa kisha akachukua yale maji yaliyo changanywa kwa unga ule na kuyamwaga. Lutfiya alishangaa huku akiyatazama maji yale.
“haa yaani unamwaga maji yaliyoandaliwa kwaajili ya Maya?“
alisema yule Lutfiya na kumfanya Jafari amtazame kisha akamsogelea zaidi mpaka.
“ndio nimemwaga, ulitakaje sasa, ninaweza nikayapiga deki haya nikupake mwilini mwako ili nione ulitaka kumfanya nini Maya“ alisema Jafari akimtia mkwala yule mwanamke ambaye kusikia vile akahisi huenda jambo lake alilotaka kulifanya limejulikana.
“basi Samir tuyaache hayo, naomba na leo nitunzie siri hii kama umeona chochote, nakuomba sana na nitakulipa kama vile tulivyolipana.“alisema Lutfiya na kumfanya Jafari ashangae. Maneno yake yalimfanya ahisi hapa kati kuna kitu kinaendelea na huyu mama si mwema kwa Maya.
“nakuomba utoke nje tu kwanza.“alisema Jafari na kumfanya hata yule mama ashangae.
“mimi nitoke nje tena Samir?..siwezi kutoka tena wewe mfanyakazi wa nje ndio utoke umesahau sheria za Falme?.. siwezi kufanya tena jambo hili."
“leo nataka utoke tu niache mimi humu, ukibisha basi naenda kumwambia Malkia juu ya mambo yako.“alisema Jafari akiwa hana anachojua chochote zaidi ya tukio la siku hiyo tu. Mwanamke yule kusikia hivyo ilibidi atoke tu na kumuacha Jafari mule ndani.

ITAENDELEA.
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN
MTUNZI:JAFARI MPOLE
SEHEMU YA 07

ILIPOISHIA
“leo nataka utoke tu niache mimi humu, ukibisha basi naenda kumwambia Malkia juu ya mambo yako.“alisema Jafari akiwa hana anachojua chochote zaidi ya tukio la siku hiyo tu.Mwanamke yule kusikia hivyo ilibidi atoke tu na kumuacha Jafari mule ndani.

TUENDELEE
Aligeuka na kumtazama Maya akiwa amelazwa pale kitandani na taratibu akamsogelea hadi pale na kukumbuka siku ile aliwahi kufika hapa na akafanikiwa kumshika Maya nywele zake na gafla akajikuta amerejea darasani, lakini leo yupo dhahiri pale na kuamua kulikamilisha zoezi la siku ile, alisogeza mkono wake na kuanza kushika nywele za Maya zilizokuwa ndefu hali iliyomfanya Jafari atabasamu na kusikia raha hasa pale aliitazama sura ya Maya ila vile vile alivyo Mrembo Aziza.
“Maya..wewe ni mrembo kweli, ila pole sana kwa hili lililo kupata“alisema Jafari huku akiendelea na zoezi la kumshika Maya, Lutfiya alikuwa anachungulia kwa nje na kushudia Maya akishikwa vile.
“hee... Samir haogopi kumshika Maya, huyu anatafuta matatizo na Mfalme ngoja aonekane.“alisema huku akimtazama Jafari akiendelea kumshika tu Maya.

Kwenye falme Jafari anajulikana kama Samir na inaonekana ni mtu ambaye yupo kila siku na ni mfanyakazi wa nje akihakikisha kazi zote za nje kama kuwapa majani Farasi na kufanya usafi kwenye jengo la kifalme lote.

Hadi kufika mchana wa siku hiyo Malkia na mwenzake walianza kuwasili ndani ya ardhi ya mashariki ya Mbali ambapo ndipo anapopatikana mtu anayeitwa Dalfa,walizidi kuingia ndani zaidi ya mji hup na kukutana na idadi ya watu wengi maeneo ya Sokoni
Taarifa za kuwasili kwa Malkia wa Eden zilimfikia Dalfa mwenyewe akiwa zake kwenye ibada maalumu ya kuabudu sehemu maalumu ndani ya jengo lile la falme yake.Alipopata taarifa ya kuwa Malkia wa Eden amekuja kumtembelea alishangaa sana maana Eden ni taifa kubwa mno na linasifika kwa kila kitu hasa utawala wake mkali. Alielekea sehemu ya kukutana na wageni na kweli akapata kumuona Malkia Rayat akiwa sambamba na mlinzi wake wamekaribishwa sehemu tulivu,alifika pale na kuyoa heshima kwa Malkia huho kisha akakaa na kuanza kujadili mambo.
“Taifa lango dhalili limepata kutembelewa na kiongozi mtukufu wa Eden, ni bahati iliyoje hii “aliyasema hayo Dalfa akiwa mwingi wa tabasamu.
“ni heri kutembeleana kama hivi tukapata kujuana na kusaidiana kwa matatizo katika falne yetu.“alisema Malkia na kumfanta Dalfa atabasamu.
“huenda ikawa kweli juu ya maneno yako, nami ni miongoni mwa watu wanaosaidia sana viongozi wakubwa, kama kuna tatizo Eden basi tujuzane ili tufikie muafaka wa swala hilo.“aliyasema hayo Dalfa na kumpa nafasi ya kuongea Malkia.
“matatizo ni moja ya changamoto katika mataifa yetu, leo mimi ila kesho huenda ukawa wewe mwenye tatizo hivyo msaada kutoka moyoni unahitajika kama umeguswa na tatizo la mwenzako.Ni kweli Eden ina tatizo, na ni ndani ya falme ikinigusa mimi hasa. Ni binti wa Mfalme amepatwa na balaa, huenda nikasema ni kama amekufa hivi maana ni siku ya sita sasa inaenda kutimia wiki moja Maya amelala tu haamki,inasadikika kuna mzee mmoja aliweza kumtupia uchawi ambao ndio chanzo cha yote haya na alipobanwa ili aweze kutoa kitu alichoweka kwa Maya alikataa katakata na kuona bora afe, na kweli falme ikamnyonga... tumejaribu kila mtaalamu aweze kutoa msaada wake lakini wapi hadi tumetoa ofa kwa wananchi kwa mganga yeyote atakayeweza kufanya kazi hiyo atapata zawadi, wamejitokeza wengi mwisho hakuna kilichofanikiwa. Ni mtu mmoja tu aliyenipa ushauri kuwa huenda Dalfa akafanikisha hili na Maya akapata kuwa salama kama awali hivyo nikaona hakuna haja ya kuendelea kukaa nikafunga safari ya kuja huku lengo ni kuonana.na wewe uweze ninisaidia kwa hilo“alisema Malkia kwa unyonge sana, Dalfa alimtazama kisha akatabasamu kisha akasimama na kuanza kutembea tembea kwa kujiamini.
“kwa Dalfa swala hilo ni dogo sana na jinsi ulivyoongea nimeelewa kitu,uchawi wa kumfanya mtu awe kama amekufa ni mbaya sana na huenda muda wowote mtu huyo akafa kweli, uchawi huo alikuwa nao Malkia wa zamani Sabiha, na ni mimi ndiye mtu pekee niliyeweza kuoambana.naye kipindi hicho na kufanikiwa kumdhibiti na kuchukua nguvu zake, alikuwa na nguvu za ajabu sana ambazo hadi sasa nazitumia mimi, kuna mzee alikuja kuiba ujuzi wa nguvu hizo na akakimbia na baadhi ya vitu ambavyo nilivihitaji japo sikuweza kumuona, na huenda ndiye huyo mtu alimfanya binti yenu hadi leo awe mfu aliye hai, mmenisaidia kumuua mtu huyo sasa naimani hakuna mwenye nguvu hizo tena ni mimi pekee ndiye niliye nazo..“alisema Dalfa na kuanza kucheka sana baada ya kusikia hivyo kisha akamgeukia Malkia, alikuja mpambe wake Dalfa na kuleta karatasi zikizoonyesha ramani na mataifa mbalimbali kisha akampa Malkia aangalie
“tazama mwenyewe, taifa la Googolee,Nakya,Sabhaa,Niang na mengine madogo madogo viongozi wake walikuja kwangu kutaka msaada na mikataba yao hiyo tuliandikishana kama kupeana ahadi, nawasaidia na wao wananiachia ardhi yao, ndio maana Dalfa anaitwa MFALME WA MASHARIKI mataifa hayo yote yapo chini yangu. Nakuhakikishia Maya atapona kabisa maana damu yako haiwezi kupotea angali wewe unaona,wewe ndio mama una uchungu na mtoto wako unajua umepata tabu gani hadi Maya kufikia umri huu hivyo unatakiwa kusimama kama mama kuhakikisha mwanao anatoka kwenye umauti huo wa mateso, kama upo tayari Eden iwe chini yangu tuandikishiane hapa, sihitaji mali, sihitaji dhahabu,almasi wala siraha bali ardhi yako, ardhi ya Eden ndio kitu kinachotakiwa hapa, kama upo tayari tunaanza safari sasa hivi kurejea Eden,na kama hutolikubali hili basi subiri tu matokeo siku Saba kuanzia leo kama zikipita Maya ataitwa marehemu.“alisema Dalfa na kumfanya Malkia azidi kuchanganyikiwa baada ya kuambiwa hivyo, alitegemea ampe mali zote za thamani ili mwanaye apone lakini Dalfa alisimama kwenye msimamo wake akiitaka Eden tu.
Alimtazama mfanyakazi wake ambaye naye alikuwa njia panda akisubiri tu uamuzi wowote atakao uchukua Malkia juu ya swala hilo,alipoangalia mikataba ile ya viongozi mbalimbali ambao wameacha mataifa yao kwaajili ya kusaidiwa na Dalfa akaona kweli taifa si lolote mbele ya utu wa binadamu. Hasa yeye binti yake wa kipekee ndiye mwenye tatizo hilo.Nafsi na moyo wake ukaridhia afanye makubaliano hayo ili leo hiyo hiyo aondoke na Dalfa kwenda kumtibu binti yake.

Siku hiyo kule Eden Jafari alikuwa hado ndani mule kwa Maya, baada ya kujiridhisha na kuhalikisha usalama wa Maya alitoka zake nje na kuzunguka jengo la kifalme kwa umakini. Hakika lilivutia sana huku wafanyakazi wengi wakitembea huku na kule kila mtu akiwa bize.Alivutiwa na mandhari ya jengo hilo na punde tu akajikuta amerejea maeneo ya shuleni kwao.Alitabasamu tu baada ya hali hiyo kuanza kuizoea. Alirudi zake darasani kuendelea na vipindi.
Baada ya muda wa kipindi kuisha Jafari alielekea kugonga kengele kuashiria vipindi vyengine kuendelea.Lakini alipomakiza zoezi hilo akitaka kupiga hatua kurejea darasani alipata kuona kidole chake alichovaa pete kinambana, na alipotazama alipata kuona picha ya Malkia akiwa anatazama kwenye meza moja kukiwa na makaratasi huku akiwa anaonekana mwanaume amesimama.kumtazama.
“hii nini tena...eti..“alisema Jafari akiiukiza pete ile.
“ni Mashariki ya mbali, ndani ya jumba la Mfalme wa mashariki anaitwa Dalfa, Malkia ameenda huko kutaka msaada wa kumponesha binti yake maya, na hiyo ni mikataba ambayo Malkia ameamua kuweka saini yake ili Maya apone, na endapo akipona basi Eden inakuwa mikononi mwa Dalfa ambaye ana mpango wake muhimu anataka kuufanya.“ilisema ile pete na kumfanya Jafari akiwa amesimama pale ashangae,alistaajabu kusikia vile.
“ina maana Mfalme hata amekubaliana na swala hii?“
“hapana hajakubaliana nalo abadani, yupo njiani anawahi kama ataweza kumzuia Malkia kusaini, naamini hataweza kumuwahi yupo mbali sana.“
“mh sasa itakuwaje ina maana Eden inakwenda kupotea kirahisi hivi?kwani mimi siwezi kumfanya Maya apone?“
“ni rahisi wewe kumponesha Maya, ila kama utafanya hivyo juwa kwamba maisha yako yote yatakuwa Eden.“
“mmh na kama nikiwa huko vipi kuhusu shule huku? Na vipi nyumbani si watanitafuta!“
“Jafari wa huku atabaki na kuendelea kuishi na ataonekana kama Jafari ila wewe ukienda kule hautakuwa tena Jafari, utaitwa Samir.“ilisema ile pete na kumfanya Jafari pale alipo akumbuke jina la Samir alivyokuwa akiitwa na yule mfanyakazi Lutfia.
ITAENDELEA
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN
MTUNZI:JAFARI MPOLE
SEHEMU YA 08

ILIPOISHIA
....wewe ukienda kule hautakuwa tena Jafari, utaitwa Samir.“ilisema ile pete na kumfanya Jafari pale alipo akumbuke jina la Samir alivyokuwa akiitwa na yule mfanyakazi Lutfia.

TUENDELEE
Alibaki kutafakari achukue umuzi gani kati ya hiyo aloambiwa maana kinachokwenda kutokea ni kukubaliwa tu Malkia aweze kusaini ile mikataba.
"Kama mimi nina uwezo wakumponesha Maya kuna haja gani ya Malkia kuendelea kumsujudia Dalfa? Hapana .."alisema Jafari moyoni huku akiitazama ile pete, alichokifanya ni kuomba pete ile iweze kumtoa pale alipo haraka awahi kule Mashariki ya mbali.
Punde tu akapotea eneo lile la shule na hakuna hata mmoja ambaye aliyeweza kuona tukio hilo.
Huku upande wa pili Mfalme alikuwa anazidi kuja na viikosi vyake huku akiwa juu ya farasi. Kuna fikra zinamtuma huenda mkewe akawa tayari kashaigawa Eden kwa Dalfa. Akifikiria hivyo moyo unamwenda mbio anachapa farasi ili aweze kuongeza kasi zaidi huku jeshi likimfuata.

Malkia alitazama mikataba ile na taratibu akaanza kuonesha ishara ya kukubaliana naye. Alikamata unyoya wa ndege ambao unatumiwa kama kuchovya kwenye wino ili ipate kuandika kwenye karatasi. Alitazama ule mkataba na taratibu akaanza kuchovya kwenye wino apate kuweka saini yake. Dalfa alikuwa akitazama tu akijawa na shauku ya kuipata Eden kupitia jambo hilo huku kikosi cha majeshi ya Mfalme Siddik pamoja naye wakiwa wanawasili ndani ya jiji la Mashariki ya mbali na bila kupoteza muda wakaelekea kwenye makao makuu anayokaa Dalfa.

Malkia hakuwa aliona bora liwe hivyo wawe maskini lakini binti yake apate kuwa mzima. Alishusha pumzi kwa nguvu na kuanza kupeleka mkono kwenye karatasi na ghafla mlango ukapata kufunguliwa kana kwaba ameingia mtu. Wote walisitisha zoezi hilo na kuangalia mlangoni. Malkia alistaajabu kumuona mmoja wa watanyakazi wake wa ikulu ameweza kufika hapo.
"Wewe ni nani unaingia humu bila kutoa heshima, umetokea wapi? "aliuliza Dalfa akionesha kukasirika huku akimtazama yule mtu. Malkia alipomuona mtu huyo.
"Samir...! Umefuata nini huku wewe?"alistaajabu Malkia baada ya kumuona mtumishi wake akiwa hapo muda huo. Taratibu Samir alisogea akaanza kusogea pale walipo huku akimtazama Dalfa kwa jicho la aina yake. Alishapata historia ya mtu huyo jinsi anavyojimilikisha ardhi za watu pindi awasaidiapo. Alisogea karibu na Dalfa kabisa waabaki wanatazamana wawili hao huku Malkia akishangaa kumuona mtumishi wake huyo dhaifu leo amekuwa mwenye kujiamini kiasi hicho. Hata mlinzi wa Malkia Faisar alibaki kushangaa jambo hilo kumuona Samir amekuwa jasiri sana.
"Dalfa.. kiongozi mwenye wadhifa mkubwa, kiongozi mwenye nguvu kubwa na tajiri wa ardhi zitokazo kwenye mikono ya koo na falme mbalimbali. Unajisikiaje kukumbatia falme za watu hivyo na kumiliki vilivyomo ndani yake kuwa vyako?. Hivi Dalfa, hauna ubinadamu wewe wa kumsaidia mtu matatizo yake hadi na wewe ufaidike kwa kumshusha mtu wadhifa wake na kumpokonya ardhi yake anayowaongoza watu! huna ubinadamu kwanini?"aliongea Samir(Jafari) akiwa mwenye kujiamini bila kujali mtu huyo ana uwezo mkubwa kiasi gani.
Maneno yake yalimtia hasira Dalfa akawa anamtazama kwa ukali Samir aliyekuwa hana hata woga wa kuongea. Hata Malkia alibali kushangaa huku akiwa ameshikilia unyoya ule.
"Samir... unaongea upumbavu gani wewe mbona sikuelewi, Na umejuwaje kama tupo huku? Nani kakuleta hapa.?"aliongea kwa ukali Malkia na kumfanya Samir ageuke kumtazama Malkia Rayyat.
"Ninachokiongea Malkia wangu ni cha maana kubwa sana, huyu mtu anachokifanya sio ubinadamu hawezi kumsaidia mtu bure bila kujinufaisha na yeye."aliongea Samir akiwa mwenye kujiamini. Alionekana wa tofauti sana maana maneno anayoongea kwao ni kama mageni. Anaona vile anavyoishi yeye akiwa Tanzania basi ndio kama wanavyoishi huko Eden na ndio sababu kuongea yote hayo akiona hakuna ubinadamu wa kusaidiana hadi walipane kwa namna hiyo.
"Naomba uniache nimalize swala hili hali ya Maya nadhani unaifahamu."akiongea Malkia huku akisogea kwenye ule mkataba aweze kuandika kukubaliana na Dalfa. Samir alisogea hadi pale na kulichukukua ile karatasi akaikunja ya kugeuka kumpatia Dalfa mwenyewe aliyebaki kushangaa kijana huyo.
Alimtazama Malkia huku akiwa mwenye kujiamini Samir.
"Maya yupo salama ameamka."aliongea Samir na maneno yale yaliwashtua wote mule ndani.
"We Samir.. unachokiongea una uhakika nacho au?"aliongea Faisar akiwa pembeni mwa Malkia.
"Umesemaje..Maya ameamka?"alistaajabu Malkia akiwa anamtazama Samir hadi kudondosha ule unyoya. Dalfa habari zile zilimshtua na kutoamini kile asemacho yule mtumishi wa Malkia huku akimtazama kwa makini.
"Ninachokisema ni cha kweli kabisa Malkia na ndio maana nimefika hapa kukupatia taarifa hii, Maya amepona hivyo tunaweza kurudi tu Eden."alisema Samir na kumfanya Dalfa aangue kicheko pale wakageuka kumtazama akionekana kufurahi.
"Hivi ugonjwa uliopo kwa Maya mnaujua au mnausikia!. Waganga wenu wangapi wameweza kumtibia wakashindwa na mwishowe wanawaambia muende kwa nani!. Hahahahaha....Dalfa ndiye mtu pekee anayeweza kumfanya Maya akaweza kuamka. Ila kama hamtoamini hakuna shida rudini Eden mkaendelee kumuuguza mgonjwa wenu ila mtarudi tena hapa hahahahaha."alicheka sana Dalfa na kusogea kwenye kiti chake kukaa.
"Nendeniii mnachelewa."alisema Dalfa akiwa mwenye kutabasamu hali iliyomfanya Malkia awe njia panda. Samir hakutaka kusubiri tena alimsogelea Malkia na kumkamata mkono hali iliyowashangaza watu wote mule ndani. Akaanza kuongoza njia akiwa na Malkia wakitoka nje, Faisar mwenyewe alibaki kushika mdomo kuona mtumishi wakiume amemshika Malkia mkono wake jambo ambalo haliruhusiwi kwa mtu yeyote kumshika Malkia zaidi ya Mfalme Siddik. Alibaki kumtazama tu usoni huku akiwa anapelekwa tu na Samir wakitoka hadi sehemu walipo wahifadhi farasi zao.
"Hebu niache wewe, nani kakupa ruhusa ya kunishika kiasi hiki! Hivi leo umeingiwa na ujasiri gani wa kufanya vitu hivi kwa kujiamini."aliongea Malkia akiwa amekasirika kwa kushikwa vile. Hakuwa anajua Samir kama lile ni kosa kubwa sana alilofanya ikabidi azoee sasa sheria za huko taratibu. Alijirudi na kuwa mpole huku akiomba samahani kwa kile alichokifanya. Malkia alipanda kwenye farasi akiwa amenuna sana.
"Narudi Eden, ole wako nimkute mwanangu hali yake ipo vilevile hakika kichwa chako kitakuwa halali kwangu."alisema Malkia Rayyat akionesha kukasirika sana, aliruhusu farasi wake na kuanza kukimbia spidi kurejea Eden.
Faisar ilibidi amsogelee Samir akimtazama kwa makini, alisogea mpaka kwenye kinywa chake akimnusa huenda labda alikuwa amekunywa pombe na ndio maana amekuwa na ujasiri sana siku hiyo.
"Mbona una ninusa hivyo wewe?"
"Hebu niambie ukweli Samir, leo imekuwaje mpaka umechangamka kiasi hicho? Na nani kakwabia kuwa sisi tupo huku."aliuliza Faisar akiwa anamtazama Samir usoni.
"Ni yule mganga ndiye aliyetoa taarifa hizo na hadi sasa tunaongea Mfalme na jeshi lake wanakuja huku wakijua fika kuwa Malkia amekuja kwa Dalfa akubaliane naye kuitoa Eden ili Maya apone."alisema Samir na kumfanya Faisar ashtuke baada ya kujua kumbe Mfalme ameshajua.
"Sasa Maya ameponaje na wakati tulimuacha akiwa kwenye hali mbaya?"
"Ndio hivyo sasa wewe tambua kuwa Maya amepona."alisema Samir kwa ufupi hahitaji kuulizwa maswali mengi.
Faisar alipanda kwenye farasi wake na kuanza kuondoka.
"Sasa mbona unaniacha nipandishe na mimi."alisema Samir.
"Wewe ulikuja vipi huku?"aliongea Faisar akiwa amesimamisha farasi na kumtazama Samir.
"Ah samahani basi endelea na safari yako muwahi Malkia haraka."alisema Samir na kumfanya Faisar asikitike huku akitabasamu. Hivyo ndivyo wanavyomtambua Samir kuwa kidogo ana ugonjwa wa kusahau na mtu dhaifu sana ndio maana akapewa kazi kwenye falme ya kufanya usafi ndani ya falme ikiwa pamoja na kulisha farasi majani.
Alisogea pembeni na kuitazaa pete ile na kuomba apate usafiri wa farasii na punde tu akatokea farasi mweusi mbele yake hali iliyomfanya atabasamu. Alipanda farasi huyo safari ikaanza kurejea Eden baada ya kumzuia Malkia asiandike chochote kwenye mkataba ule.
Huku kwa Dalfa hakuwa na wasiwasi juu ya Maya na kuona ungonjwa alionao binti huyo hakuna wakuweza kumponesha zaidi yake maana nguvu zile anazozitumia yeye tu na hakuna mwengine, hivyo alijiamini kuona lazima watarudi tena kutaka msaada.

Njiani Malkia akiwa sabamba na Faisar walipata kuona majeshi mbele yanakuja. Wakiwatazama vizuri walipata kutambua kuwa ni majeshi ya Eden yakiongozwa na Mfalme Siddik aliyekuwa mbele. Alishtuka lakini hakukuwa na jinsi ilimbidi ajikaze na kukubaliana na lawama zote zitakazomshukia kutoka kwa mumewe. Mfalme alisogea hadi pale alipo Malkia na kubaki kumtazama kwa hasira huku majeshi yake yakiwa nyuma.
"Umeshaigawa Eden yangu kwa Dalfa?" ni swali lililomfanya Malkia Rayyat atazame tu chini. Faisar alimtazama Malkia wake aliyekuwa hana la kusema ikabidi amtetee.
"Mfalme wangu, Hat..."
"Naomba unyamaze wewe nikiwa naongea na mkewangu. Tena wewe ndio sababu unawezaje kumruhusu Malkia akatoka nje ya Eden bila kuniambia lolote. Mmeshaigawa Eden yangu ndio mnarudi sasa mnaenda kukaa wapi sasa,!"alifoka kwa ukali sana Mfalme.
"Hatukufanya lolote baada ya kuambiwa Maya ame.."
"Nyamaz...! Nini? Hebu malizia ulichokuwa unakisema."alisema Mfalme baada ya kumsikia Faisar akiwa anataka kuongea kitu.
"Baada ya kuambiwa kuwa Maya amepona ndio Malkia akaacha kufanya lolote na ndio maana tunarudi kuona kama ni kweli Maya amepona."alisema Faisar na muda huohuo Samir ndio alikuwa anafika sehemu ile na kuwakuta wakiwa wamesimama pale wakiongea. Alitazama yale majeshi jinsi walivyo wengi akabaki kuengaenga tu maana mambo hayo amekuwa akiyaona kwenye runinga tu.
"Maya amepona? Taarifa hizo amewapa nani?"aliuliza Mfalme akistaajabu kuambiwa vile. Faisar alimgeukia Samir kumtazama na kumfanya Mfalme ageuke naye kumtazama Samir.

ITAENDELEA.
 
SIMULIZI😛ETE YYA MFALME WA EDEN
MTUNZI:JAFARI MPOLE
SEHEMU YA 09

ILIPOISHIA
"Maya amepona? Taarifa hizo amewapa nani?"aliuliza Mfalme akistaajabu kuambiwa vile. Faisqr alimgeukia Samir kumtazama na kumfanya Mfalme ageuke naye kumtazama Samir.

TUENDELEE
"Samir ndio katuambia"alisema Faisar na maneno yale yalimfanya Mfalme acheke sana huku akimtazama Faisar. Alishuka kwenye farasi na kuanza kusogea taratibu pale aliposimama farasi wa Samir. Alimshika farasi yule huku akiwa mwenye kutabasamu. Samir alikuwa anatamzama tu Mfalme jinsi alivyokuwa akifurahi, furaha ya kuona hawakuweza kufanya kitu chochote kwa Dalfa. Na yote ni kwasababu ya Samir ambaye ndiye aliyewahi kumzuia Malkia Rayyat.
Alirudi kwenye farasi wake na kumpanda kisha akageuka alipotoka akiwatazama majeshi yake aliyoongozana nayo.
"Tunarudi Eden muda huu hakuna kibaya kilichotokea. Eden bado ni ya Siddik."aliongea Mfalme huyo na kuwafanya wau wote washangilie kuona hakuna kilichoharibika.
Malkia Rayyat alibaki kutazama tu na kuona majeshi hayo yanaanza kugeuza. Alimtazama Samir ambaye naye baada ya kuona anatazamwa akawa anaangalia kwa kuibia. Safari ikaanza wote wakirejea Eden huku Malkia akiwa anamuwazia tu mwanaye kwa kile alichosikia kutoka kwa Samir. Alikuwa na hamu ya kujua kama ni kweli au laa, na kama sivyo basi kile alichoahidi kukifanya kwa Samir zima akitekeleze.

Huku kwa Dalfa hakuwa na wasiwasi kabisa juu ya kuimiliki Eden. Baada ya kuwasili Malkia kwake na kumueleza hali halisi moyoni alianza kujiwekea tumaini la kuimiliki Eden. Muda mchache mbele alifika mkewe ambaye ni Malkia wa Taifa hilo la Mashariki. Alisogea hadi pale alipo mumewe naye akakaa kweuye kiti chake huku akimtazama Dalfa akiwa mwenye furaha.
"Nategemea kuimiliki Eden majuma kadhaa yajayo."alisema Dalfa na kumfanya mkewe Malkia Saadie ashangae.
"Unataka kuniambia alifika hapa Mfalme wa Eden leo ?"
"Alifikia mkewe na ndio aliyetaka msaada juu ya yule binti yao."
"Sasa imekuwaje, ameshakubaliana nawe?"aliuliza Malkia Saadie.
"Alionekana wazi kukubali hadi kushika wino ili apate kundika makubaliano yetu, gafla tu akatokea Mtumishi wake kuja kumpasha habari Malkia kuwa binti yule amepata nafuu na kuamka."
"Ati nini? inamaana ndio basi tena?"aliongea Malkia Saadie akionesha kushtushwa na habari ile.
"Haiwezi hata siku kutokea hivyo. Naamini uchawi ambao anao binti yule ni Dalfa pekee ndiye anaweza kuutoa kwenye mwili ule na Eden inakuja kuwa yangu, hilo ondoa shaka Malkia wangu."alisema Dalfa akimtuliza mkewe ambaye maneno yale yalimpa tumaini la kuweza kuwa ndani ya Eden kama Malkia.

Njiani Samir alikuwa akitafakari kama kweli alichokisema kinaweza kutokea kweli au laa. Alijipa imani ya kuwa lazima Maya atakuwa salama kutokana na vile aliyoambiwa na ile pete. Alichokifanya ni kutaka kutangulia yeye kabla ya msafara huo haujafika kwenye falme ili akapate kujua kuhusu Maya.Alisogea mpaka mbele alipo Mfalme.
"Mfalme, nahitaji niwahi Eden ili nisafishe falme iwe safi maana hakuna mtu wa kufanya kazi hiyo kule."alisema Samir akiwa juu ya farasi, Mfalme alimtazama huku akiwa mwenye kutabasamu.
"Mfalme, nahitaji niwahi Eden ili nisafishe falme iwe safi maana hakuna mtu wa kufanya kazi hiyo kule."alisema Samir akiwa juu ya farasi, Mfalme alimtazama huku akiwa mwenye kutabasamu. wsijali nitajaribu kukutetea maana umefanya Eden iwe mikononi mwangu tena.,wahi haraka kabla hatujafika"alisema Mfalme Siddik na kumfanya Samir atii alivyoambiwa. Alimruhusu farasi aongeze spidi huku akimshikilia kwa nguvu asije kudondoka. Mpambe wa karibu na Mfalme alijisogeza kwa Mfalme akiwa anamtazama Samir akiwa anatokomea.
"Huyu Mfalme nina wasiwasi naye sana tangu kipindi kile cha kuwapoteza askari wetu akiwa ameongozana nao lakini mwishowe akarejea pekeyake angali hawezi kupambana. Sasa leo hii huku amefikaje na amefuata nini huku?"alihoji yule mpambe aliyefahamika kwa jina la Fakiy.
"Awali nilishtuka kumuona huku Samir lakini nilipopata kutambua kuwa yeye ndiye aliyemzuia Malkia asiweze kuandika lolote kwenye ile mikataba basi sina shaka naye kabisa. Samir hana lolote analojua akili zake mwenyewe unazijua hivyo ukimtilia shaka naona ni sawa na bure Fakiy.
Wacha akasafishe mabanda ya farasi usimfikirie hivyo."alisema Mfalme akiwa hana shaka na Samir. Fakiy akabaki kuvuta pumzi na kuishusha baada ya kuona Mfalme anamuamini Samir,safari iliendelea ya kurejea Eden. Kuna mambo awali Samir akiweza kuyafanya na kuwapa mashaka kuwa huenda akawa anashirikiana na baadhi ya mataifa mengine na ndio maana hata Fakiy amekuwa na mashaka naye hadi leo.

Samir alipofika mbele akaona atulie sehemu na kumuweka farasi pembeni kisha akaitazama ile pete akihitaji kuona hali ya Maya kule ndani. Muda mfupi tu alipata kuletewa kuona Maya akiwa bado yupo kitandani akiwa na wafanyakazi ambao walikuwa wakihudumia kumkanda kwa maji ya moto.
Alipatwa na hofu ya kutokujiamini kama ataeza kweli kumsaidia Maya kuweza kuamka pale kitandani.Alijipa moyo na kuona lazima atalifanikisha swala hilo,aligeuka kuweza kupanda farasi wake ajabu hakuweza kumuona yule farasi pale alipomuacha. Alitazama huku na kule bila kutambua alipokimbilia. Aliitazama pete ile na kuona ndio msaada kwake wacha aituie. Ilimbidi aitazama ile pete na kuomba aweze kufika Eden muda huo, alifumba macho yake na sekunde kadhaa aalipofumbua alijikuta yupo kwenye zizi la farasi. Alistaajabu huku akitazama huku na kule bila kuona mtu yeyote aliyeweza kuwa karibu na mahala hapo. Haraka alitoka mule ndani yaa zizi na kuanza safari ya kuelekea ndani Falme.Alipowasili tu baadhi ya wafanyakazi walmshangaa.
"Wewe ulikuwa wapi muda wote unatafutwa,tazama maeneo yalivyo machafu hivyo, unajisahau sana Samir ndio maana unadharaulika na kila mtu humu ndani utakuwa lini wewe?"alisema mfanyakazi mmoja akiwa amebeba tenga la matunda na kuamua kuelekea zake ndani akimuacha pale Samir akiwa amesimama.
"Ina maana huyu Samir alikuwa vipi anadharaulika sana humu ndani? Maana kila mtu Samir Samir, nami natakiwa niende na tabia hiyohiyo ya Samir nisije kujulikana hapa ikawa balaa."alisema Jafari baada ya kujua mwenye jina la Samir alikuwa akidharauliwa sana ndani ya falme. Ilimbidi naye aishi maisha hayohayo ya kudharauliwa asije kuonekana tofauti, alipokumbuka swala la Maya haraka akaelekea ndani kujua atamsaidiaje.
Alifika ndabi na kuona wafanyakazi wakiendelea kuzunguka huku na kule kumhangaikia Maya. Hakuwa anaruhusiwa kuingia ndani mara kwa mara lakini alijitahidi asipate kuonekana na macho ya watu wengi hadi alipofika kwenye mlango wa chumba ambacho binti huyo wa kifalme amehifadhiwa. Alipochungulia aliona baadhi ya wafanyakazi wakiwa wanamhudumia Maya mule chumbani. Aliittazama pete ile nakuongea maneno kadhaa punde tu wale wafanyakazi wakaanza kutoka mmoja mmoja mule ndani. Alijibanza mahala hadi walipotoka wote naye taratibu akaingia mule ndani na kuusogea hadi pale kitandani. Alimtazama Maya akiwa bado amelala pale huku sura yake ikimfanya Samir amkumbuke Aziza msichana anayesoma naye shule moja mkoani Tanga. Alimeza funda moja la mate na kuupeleka mkono wake kichwani kwa Maya. Alishangaa kuna maneno yanatokea mbele yake.
"Yatamke maneno hayo huku ukiuweka mkono kifuani kwake."ilisikika sauti kutoka kqenye ile pete na kumfanya Samir afuate kile anachoambiwa. Aliupeleka mkono wale kifuani kwa Maya nana kuyatazama yale maneno yaliyokuwa mageni kwake akajitahidi kuyasema.
" vamos partir dentro de uma hora....vamos partir dentro de uma horaa.....vamos partir dentro de uma horaaa" aliona moshi mweusi ukitoa puani na kwenye masikio ya Maya, akabaki kushangaa tukio hilo ambalo hakutaraji kuona hivyo. Gafla Maya akatema donge la damu na papo hapo akapata kufumbua macho huku damu zikimtoka mdomoni huku akiwa anahema kama mtu aliyekimbizwa. Samir kuona vile alishtuka sana, haraka akachukua kitambaa na maji ya moto kidogo yaliyo pembeni akaanza kumfuta damu ile.
"Maya.. umeamka!"alisema Samir akimtazama Maya akiyekuwa anahitaji kuinuka kuweza kukaa. Samir alimsaidia kumnyanyua huku akiweka mto ukutani Maya akapata kuegamia.
Akawa anazama mule ndani kulivyo na kuona kuna madawa kibao yaliyokuwa pembeni,alimtazama Samir akiwa anamfuta futa damu na hapo ndipo akapata kujiona jinsi alivyo akiwa amefunikwa mashuka mazito.
"Samir.. nini kimetokea kwani mbona nipo kitandani?.Na imekuwaje natokwa na damu hivi."alisema Maya akiwa anajitazama jinsi alivyo.
Hakujua amjibu nini muda huo lakini punde tu alishangaakuona wafanyakazi wa mule ndani wakiingia na kushikwa na butwaa hawaamini kile ambacho wanakiona.
Walianza kupiga mayowe ya furaha na kuwafanya watu.huko wasikie huku wakisogea hadi pale na kuanza kumkumbatia Maya ambaye muda wote alikuwa hata haelewi nini nimetokea. Nafasi hiyo ndio aliitumia Samir kutoka mule ndani baada ya kujua jambo alilopaswa kulifanya limefanikiwa. Alipata furaha kuona vile huku akitoka nje na kupishana na watu wakikimbia kuelekea kumuona Maya baada ya kupata taarifa kuwa ameamka.
ITAENDELEA
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN
MTUNZI:JAFARI MPOLE
SEHEMU YA 10

ILIPOISHIA.
Alipata furaha kuona vile huku akitoka nje na kupishana na watu wakikimbia kuelekea kumuona Maya baada ya kupata taarifa kuwa ameamka.

TUENDELEE.
Ilikiwa ni jambo la kushangaza kwa Maya kuona kila mtu aliyefika pale akiwa anafuraha ya kumuona kana kwamba hakuweza kuwepo muda mrefu sana. Lutfiya alikuwa tu pembeni akiwatazama wenzake wakionesha kufurahi baada ya Maya kuweza kuamka. Hakupenda kabisa jambo hilo muda wote alionesha kukunja mdomo huku akijiuliza imekuwaje jambo hilo likawa gafla hivyo aweze kuamka.
Huku kwa Maya alikuwa akisikiliza tu maongezi ya wafanyakazi baada ya kuuliza imekuwaje hadi aweze kuwa pale kitandani.
"Maya.. ni wiki ya pili sasa ulikuwa hapo kitandani, haikujulikana umezimia au umekufa maana kila mganga wa jadi unayefahamu kuwa ni hodari katika masuala hayo amefika kukutibia lakini hakuna tumaini lolote. Ikafika wakati watu tulikata tamaa na kusubiri tu matokeo yatakavyokuwa sisi tutayapokea. Maana wazazi wao wamehangaika sana kutafuta dawa walau uweze kurudisha uhai kama awali."alisema mfanyakazi mmoja akimweleza Maya. Alibali kushangaa baada ya kipata kuambiwa kuwa ni zaidi ya siku kumi alikuwa amelala tu pale kitandani. Akili ilivurugika kabisa huku akitazama kitanda kile ambacho kiliweza kumbeba kwa siku zote hizo. Alijaribu kuvuta kumbukumbu kuweza kujua kilitokea kitu gani hadi kupelekea kuwa hivyo lakini hakuweza kupata kumbukumbu zozote.
" Mama na baba yangu wapo?"aliuliza Maya huku akiwa ameshikilia shuka.
"Hivi tunavyoongea Mama yako alielekea Mashariki ya mbali kwenda kutafuta masaada wa kuweza kukusaidia, na tulivyosikia ni kwamba endapo watakapoipata dawa hiyo ya kukuponya wewe basi Eden inakuwa si mali ya Mfalme Siddik,kuna mtu anaitwa Dalfa na huyo ndiye mtu ambaye alikuwa anaumwezo wa kukuponesha ungonjwa wako. Ulitupiwa uchawi wa kifo kabisa na ndio maana mama yako akaona bora aitoe Eden aimiliki Dalfa lakini wewe upone."alisema yule mfanyakazi.
"Uchawi? Inamaaa walitaka waniue?Ni nani huyo alifanya jambo hilo.?"aliuliza Maya akiwa anashauku ya kutaka kufahamu mhusika wa tukio hilo.
"Kuna mzee mmoja na tayari Mfalme amweza kumpa adhabu yake,amenyongwa hadi kufa baada ya kujulikana anatumia uchawi uliokupumbaza siku zote hizo ukawa kama mfu. Hivi tunavyoongea naamini hata wanganga wakija kukuona upo mzima watashangaa maana kila mmoja alikuja kutumia nguvu zake imeshindikana."alisema yule mfanyakazi na kauli hiyo ikamstaajabisha sana Maya baada ya kutambua kweli alikuwa nusu kufa.
Akawa anatafakari mwenyewe kama juhudi za kuokoa maisha yake kila mmoja alishindwa imekuwaje ameweza kuamka gafla hivyo?.
Mtu pekee aliyeweza kumuona pindi aliyafumbua macho yake ni Samir na alipata kumuona akiwa anamfuta damu. Alikosa uhakika wa kuamini kama mtu aliyemuona anaweza kufahamu chochote kuhusu hali hiyo. Alishukuru tu kuona yupo salama kwa muda huo na taratibu wakamuandalia maji kisha wakamchukua kwenda kumsafisha mwili.

Taarifa za kuweza kuinuka binti waMfalme zikaanza kutapakaa jiji zima hali iliyowafanya watu washangilie sana maana walikuwa wakifanya maombi kwaajili yake.
Hadi kufika usiku vigingi vya moto viliwashwa jiji zima kufurahia kurejea kwa binti wa Mfalme, mji wa Eden ukawa unatoa mwanga hata kwa baadhi ya mataifa mbalimbali walipata kuona mwanga ule na kuhisi huenda kuna kitu cha furaha kimetokea. Mfalme Siddik akiwa na Malkia Rayyat waliweza kuona pia mwaga ule na kuwafanya washangae huku majeshi ya askari wa Eden wakiwa nyuma yao.
Walitazamana baada ya kutambua miale ile ya moto ilikuwa ikitoka katika taifa lao la Eden na kufahamu kuwa huenda kuna jambo zuri limetokea. Hakuna kati yao wawili aliyeweza kuamini kile ambacho wanakihisi muda huo, wakabaki kutazama tu na kuanza kuongeza spidi farasi zao ili wafike haraka maana bado ni mbali sana.

Usiku ulipozidi watu wakaanza kuelekea zao kupumzika kila mtu mahala pake. Shuhuli ikawa kwa Samir ambaye hafahamu mahala pa yeye kwenda kupumzika. Alibaki kushangaa tu akiwa amesimama huku baadhi ya askari wakiwa wanatembea huku na kule ndani ya jengo hilo la kifalme kuweka ulinzi.
Ilibidi ajitoe akili na kumfuata askari mmoja aliyekuwa amesimama.
"Wewe Samir vipi mbona hadi sasa upo macho?"aliuliza yule adkari akiwa ameshikilia upanga wake huku akiwa kwenye vazi la kiaskari.
"Naomba msaada wako ndugu yangu,mahala ninapolala nahisi kuna nyoka sijui maana naona vitu vinagongana tu sielewina mimi ni muoga sana wa nyoka, nisaidie kuweza kumtoa nyoka huyo."alisema Samir akiweka sura ya huruma huku askari yule akitabasamu tu. Alimtia konzi la kichwa kisha akaanza kuongoza mjia yule askari. Samir alibaki kushikia kichwa chake kwa maumivu makali baada ya kupigwa konzi, taratibu naye akafuata kule ambapo anaelekea askari yule.
Walifika kwenye kibanda kimoja kilichopo karibu na zizi la farasi na askari yule akaspgea hadi mlangoni na kuona umefungwa na kufuli, akamgeukia Samir.
"Naona matani yamezidi sasa, huyo nyoka umemsikiaje wakati hata mlango hujaufungua!."alisema yule askari na kumfanya Samir ashangae. Hakutegemea kama ni yeye ndio ataishi kweye kibanda hicho ambacho hakikuonesha kama kuna mtu anaishi humo.Kwa hasira yule askari akamsogelea Samir na kumpiga makonzi kadhaa kichwa huku mqenye akojaribu kuyazuia kisha akaondoka zake yule askari.
Alibaki kumsindikiza tu kwa macho hadi alipotokomea.
"Haaah! ina maaa humu ndio kwangi?!... Hahahaha, hili balaa sasa."alisema Samir na kuanza kusogea hadi pale kwenye mlango. Aliingiza mikono yake mfukoni na kuona funguo moja akawa anaitazama. Alishikwa na butwaa baada ya kuona funguo hiyo ambayo anaitumia kule kwao Handeni kwenye chumba chake. Alishindwa kuelewa imekuwaje hadi kufika pale,aliingiza kweye kile kitasa na kufungua na kushuhudia mlango ukifunguka. Taratibu akaanza kuingia mule ndani na kuwasha chemli iliyokuwa pembeni, akapata kuona kitanda cha kamba kikiwa kimetandikwa vizuri na mito ya sufi, huku pembeni kukiwa na meza yenye vitabu vingi juu yake. Taratibu akaanza kusogea pale mezani na kuvuta kitu akakaa na kushika kitabu kimoja. Gafla akatokea yule msichana Nadhra akiwa mwenye tabasamu huku amesimama pembei ya Samir.
"Umenishtua! sikutegemea kama utatokea muda huu."alisema Samir akiwa anamtazama Nadhra, alisogeza kiti naye akakaa huku akishika kitabu kimoja.
"Nimekuja tu mara moja kukusalimia, naona umeanza kuzaewa mazingira ya hapa Eden. Hivyo ndicyo alikuwa akiishi Samir wa awali, kila mtu alikuwa akimdharau kwakuwa ni dhaifu, ila tambua kwamba hapo ulipo unauwezo wakufanya chochote kile ambacho nguvu za kawaida haziwezi kufanya. Na kuhusu kuamka kwa Maya yoyote atakaye kuhisi au kukuuliza usiseme lolote fanya kama haufahamu kitu, Nadhani kuna watu wameshamuhisi Samir wa mwanzo."alisema Nadhra na kumfanya Samir ashangae.
"Wamemuhisu kwa lipi? amefanya jambo gani kwani.?"
"Alilaghaiwa na baadhi ya watu wa taifa fulani awe anatoa siri za ndani ya Falme. Akawa mara kwa mara anatoka na kukutana nao kwa siri kuwapa baadhi ya taarifa za siri kutoka ndani ya falme. Nadhani kuna watumishi wa Mfalme wamelijua swala hilo na wakaanza kumfuatilia tangu siku hiyo. Na nikwambie tu jambo geni kwako, Samir mwenyewe ameuliwa na wale watu aliokuwa anawapelekea taarifa kutoka ndai ya falme na wamemzika kabisa. Hivyo hakuna yeyote huku Eden anayefahamu kama Samir ameuawa hivyo sura,nguo na muonekano wako hivyo ulivyo ndio Samir alikuwa hivyohivyo... Wacha niondoke nitaonana na wewe siku nyengine."alisema Nadhra na kumfanya Jafari atambue kwamba kumbe analitumia jina la mtu ambaye ameshafariki. Muda huohuo Nadhra akatoweka huku akimuacha Samir akiwa ameelewa baadhi ya mambo. Alikiweka kile kitabu alichoshika na kusogea kwenye kile kitanda kujilaza na kuanza kuutafuta usingizi huku mji mzima ukiwa wenye furaha kwa tukio kubwa lililotokea.

Asubuhi kulipambazuka na kila mmoja akawa anafanya kazi zake ambazo amepangiwa kufanya. Hata kwa Samir baada ya kusafisha maeneo kadhaa ya falme akawa anasafisha mabanda ya farasi.
Kule ndani Maya alikuwa amepambwa vizuri na kuandaliwa chakula. Akasogea mezani pale kisha Lutfia akafika kumnawisha binti huyo wa kifalme. Alikuwa akimtazama kwa jicho la chuki sana bila Maya kufahamu kama anatazamwa vile. Baada ya kumaliza kufanya zoezi hilo alitoka zale nje na moja kwa moja akaelekea nyuma ya jengo la kifalme. Alitazama huku na kule kisha akaingiza mkono wake kwenye titi lakw la kushoto na kutoa karatasi iliyofungwa kama barua. Alinyoosha mkono mbelw kama anapokea kitu kutoka mbinguni na dakika kadhaa akatokea njiwa na kutua kwenye mkono wake. Haraka aliifunga ile karatasi kwa kamba kwenye mguu wa njiwa yule na baada ya kulikamilisha hilo akruhusu aondoke ndege huyo akapeperusha mabawa yake kuelekea sehemu, naye Lutfiya akageuza na kurudi zake ndani ya Falme.
NINI DHAMIRA YA LUTFIA? USIKOSE SEHEMU IJAYO.
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN.
MTUNZI:JAFARI MPOLE
SEHEMU YA 11

ILIPOISHIA
Haraka aliifunga ile karatasi kwa kamba kwenye mguu wa njiwa yule na baada ya kulikamilisha hilo akruhusu aondoke ndege huyo akapeperusha mabawa yake kuelekea sehemu, naye Lutfiya akageuza na kurudi zake ndani ya Falme.

TUENDELEE
Siku hiyo majeshi ya mfalme ndio yalikuwa yanawasili Eden huku Malkia pamoja na Mfalme Siddik wakiwa mbele wanaongoza njia.Walipokelewa kwa heshimanjia nzima baada ya kuingia Eden,kila mtu alishuka chini kutoa heshima kwa viongozi hao waliokuwa juu ya farasi zao wakielekea kwenye falme. Hata walipokaribia kwenye jengo la kifalme baadhi ya askari waliokuwa eneo hilo waliinama na kupiga goto moja chini kutoa heshma hiyo kwa viongozi hao. Samir alipata kuona hilo naye akaiga kama walivyofanya wenzake kwa kutoa heshima huku mfalme akishuka kwenye farasi na taratibu akasogea kwa mkewe na kumsaidia kumshusha. Wakaanza kuongoza njia kuelekea ndani wakiwa wameshikana mikono huku malkia akiwa na hamu kubwa sana kujua kuhusu mwanaye. Samir alibaki kuwatazama huku akitabasamu na muda huohuo akashangaa anasukumwa na askari mmoja pembeni yake.
"We boya umesimama tu hapa hebu peleka farasi zizini unashangaa tu hapa.!"alisema yule askari na kumfanya Samir akumbuke kazi yake hiyo,haraka akasogea kwa farasi wale na kushika kamba kuwapeleka kwenye zizi.
Huku ndani walipoingia moja kwa moja walielekea chumbani kwa binti yao huku wakiona wafanyakazi wa ndani humo wakiwapa heshima yao,hata walipofika baada ya kuufungua mlango ule walistaajabu kumuona Maya akiwa amepambwa vyema akiwa ni mwingi tabasamu usoni. Hali ile ikamfanya mama yake ashindwe kujizuia akasogea hadi pale na kumkumbatia mwanaye huyo.
"Oh mwanangu siamini kama upo mzima leo,nimekuwa na mashaka juu ya maisha yako Maya hadi kuamua kwenda mbali sana."alisema Malkia Rayat akiwa amemkumbatia mwanaye,alijikuta hata anatoa chozi kwa furaha baada ya kufahamu kuwa Maya ni mzima.
"Nimeambiwa yote mama,na nimeona jinsi gani umekuwa mwema kwangu muda wote umekuwa ukinihangaikia mimi niweze kurudisha fahamu,nipo salama mama yangu na nafuraha kukuona tena."alisema Maya akiwa mwenye kutabasamu huku akiwa amekumbatiana mama yake.
Mfalme alikuwa anawatazama mtu na mwanaye huku akiwa mwenye furaha,alisogea pale naye akamshika mwanaye kumpa pole kwa kile kilichotokea. Ikawa ni furaha kwao kuona binti yao yupo salama tofauti na walivyomuacha.
Baada ya muda mfalme alitoka na kumuacha Malkia mule ndani na kuelekea chumbani kwake kujipumzisha. Alianza kuwaza mambo tofauti na kujihisi alikosea kitendo cha yeye kukataa Eden isiweze kuchukuliwa na Dalfa ili binti yao aweze kupona. Alihisi ataonekana wa tofauti hasa kwa Maya endapo atakapoambiwa kuwa baba yake hakutaka kuiachia Eden yake, hivyo alikuwa radhi Maya afe kuliko kuiruhusu Eden iwe mikononi mwa Dalfa.

Muda huohuo mlango ukagongwa na askari wawili wsionekana kuingia na kusogea karibu na Mfalme.
"Ehee mmefanikiwa.?"aliuliza Mfalme akiwa anawatazama askari wake.
"Hadi sasa tukuweza kumpata wala kujua alipo. Ila wengi wanasema amekuwa akionekana mitaani mara kwa mara."akisema askari mmoja akimueleza Mfalme.
"Mmefika walipokuwa wanaishi?"
"Ndio Mfalme tumefika na hatukuweza kumuona. Na tumepata kuona vitabu vingi sana mule ndani huku vengine vikiwa havijulikani ni lugha gani iliyotumika kuandikwa mule."alisema askari wapili wakiwa wamesimama imara kumueleza Mfalme Siddik.
"Huyu binti atafutwe pale alipo, nahisi hatakuwa kimya kwa kile tulichofanya kwa baba yake hivyo yatupasa kumuwagi mapema kumkamata. Na nyumba hiyo mtoe kila kitu ndani muvichome moto nje maana huwezi juwa kama kuna uchawi ambao bado upo umewekwa humo ndani, mkawape taarifa wale waganga muongozane nao kulifanikisha hilo swala huenda likaenda kimila."alisema Mfalme Siddik na kuwafanya askati wake wamuelewe kila anachosema. Walitii amri hiyo na kugeuka kuondoka zao kuifanya hiyo kazi. Muda huohuo Malkia Rayat akaingia na kumkuta kumewe akiwa amekaa.
"Kuna jambo linaendelea.?"aliuliza Malkia akiwa anamtazama Mfalme.
"Yule mzee mchawi tuliomuua ana binti yake aliyekuwa akiishi naye. Napata mashaka juu yake pia huenda akawa anashirikiana na baba yake. Huenda pia akawa anajipanga kufanya kitu ndani ya falme hii kama kulipa kwa kile alichofanyiwa baba yake. Hivyo nisingependa yote yatokee hayo ndio maana nimewapa kazi askari ya kumtafuta huyo binti na kuchoma moto vitu vyote vilivyomo kwenye nyumba yao, wachaei huwagana mambo ya kuacha urithi hivyo sitaki tena yajirudie kwa mwanangu yale yaliyotokea."alisema Mfalme akionesha msimamo wake, Malkia aliafikiana naye jambo hilo.

Ilibidi waongozane na wale waganga moja kuelekea kwenye nyumba inayosadika baba yule mchawi alikuwa akiishi humo na binti yake. Msafari huo wa gafla ulimfanya hata Samir ashangae na kushikwa na sintofahamu. Alishangaa pete yake aliyovaa inambana na kumfanya anyanyue mkono wake kuitazama.
"Samir nakuomba sana uende na hao watu wanataka kuingia nyumbani kwetu wafanye uhatibifu. Kuna kitabu chekundu kimefungwa kwenye kitambaa nakuomba sana ukichukue wasikiharibu. Ni muhimu sana kwangu naomba msaada wako."ilisikika sauti ya Nadhra na kumfanya Samir atambue kwamba msafari ule kumbe unaelekea nyumbani kwa akina Nadhra.
Harakanaye akachukua farasi na kuanza kuwafuata wale askati waiwa na baadhi ya waganga wao.

Upande kwa pili kwenye Taifa moja jirani na Eden lilikuwa na maadhimisho ya kuwakumbuka baadhi ya viongozi wao siku hiyo. Mfalme wa taifa hilo Faruk alikuwa akiwaongoza wananchi wake katika sikukuu hiyo ya kuwakumbuka viongozi waliotawala nchini humo.
Pembeni aliongozana na kijana wake wakiume Bilal akiwa amechorwa masizi mekundu kwenye paji la uso kama mila zao katika maombi hayo. Mila na destuli zao zilifuatwa huku baadhi yao wakianda vyakula mbalimbali. Kwao ilikuwa ma sherehe ndani ya Taifa hilo na siku hiyo ilikuwa kubwa kwao hasa kwa Bilal ambaye alikuwa akisubiri jambo fulani kwa hamu sana. Baada ya mila kadhaa na kufanya matambiko na wazee wa zamani Mfalme huyo alinyanyuka na kijana wake na kuanza safari ya kuelekea kwenye falme yao kupumzika. Walipanda farasi wao huku nyuma askari kadhaa wakiwasindikiza kuwalinda. Waliwapita wananchi waliokuwa wakitoa heshima mtu na mwanaye huyo hadi walipotoka kwenye sehemu hiyo ya sherehe wakiwaacha waendelee kula kwa pamoja.
"Ulishawasiliana na Lutfiya kule Eden,"aliuliza Bilal akiwa juu ya farasi huku akimtazama baba yake.
"Ni muda niliwatuma watu wakapate habari kuhusu lile swala lakini hadi sasa sikupata jibu kamili."alisema Mfalme Faruk akiwa anapelekwa na farasi wake taratibu kuelekea kwenye falme.
"Hili swala lisichukue muda hivyo baba tunaweza kufeli mpango wetu."
"Usijali naamini kila kitu kitakwenda sawa,namuamini Lutfiya kwa muda mrefu sana hawezi kutuangusha."alisema Mfalme akiwa mwenye tabasamu.
Muda mfupi tu waliona njiwa mweupe akiwa angani na tatatibu akaanza kushuka usawa ule. Mfalme alinyoosha mkono na kumfya njiwa yule atue pale mkononi mwake. Alimpekuwa na kuona amefungwa kikaratasi mguuni ikambidi amfungue na kuchukua kuifungua palepale. Aliisoma kwa umakini mkubwa huku Bilal akiwa anamtazama tu baba yake usoni akionesha kuwa makini kusoma maelezo yaliyo kwenye karatasi lile.
Baada yamuda aliweza kumaliza kusoma, alivuta pumzi na kuishusha kwa nguvu huku akimtazama kijana wake.
"Vipi kuna kitu gani kipya?"aliuliza Bilal akiwa anamtazama baba yake.
"Maya ameamka, na lile zoezi nililompa Lutfiya limefeli pia, kuna mtu mule aliweza kumuona akifanya lile jambo la kumuwekea ile dawa Maya hivyo ikambidi aache."alisema Mfalme na kumfanya mwanaye akasirike sana kusikia vile. Wote wakawa hawana raha kabisa baadaya kupokea taarifa hizo maana hawakutegemea kama wanaweza kufeli mpango wao huo. Walibaki kimya kila mtu huku taratibu wakielekea zao kwenye falme.

Huku nyuma baada ya kuwasili kwenye nyumba ile askari wote wakaanza kuingia mule ndani na kuanza kutoka kila kitu kilichokuwa mule. Raia wa kawaida walishangaa jambo hilo na ratibu waaanza kujaa sehemu ile wakishuhudia askari wae wakifanya kazi hiyo yakurusha vitu nje kuhakikisha kila kitu mule ndani kimetolewa. Samir alijichanganya na wananchi waawa wanatazama kinachoendelea huku macho na akili yake yote kikiwa kwenye kitabu alichoambiwa. Alisimama Mganga mmoja na kuwageukia wananchi huku akia ameshika pembe ya ndefu ya Tembo.
"Nyumba hii alikuwa akiishi mtu ambaye aliyeweza kumuweka uchawi binti wakifalme na kila mtu analijua hilo,hivyo leo tunachoma moto kila kitu kilichopo huku na ni baada ya binti wa kifalme kuweza kurudi katika hali yake ya awali na sasa yumzima. Kila mtu atashuhudia kinachokwenda kutokea hapa tunachoma uchawi wote ambao uliweza kubaki humu ndani huenda ungeweza kuwadhuru hata raia wa kawaida na hata kwa falme pia. Na Mfalme ametoa zawadi nono kwa mtu yeyote ambaye ataweza kumuona binti wa mzee yule mchawi popote pale basi atoe taarifa haraka kwa askari wa kifalme haraka sana."alisema yule mzee na kuwafanya watu wote watambue lengo hasa la askari wale kutoa vitu ndani. Walimalizia kwa kuvitoa vitabu vyote na kuvitupa sehemu moja, Samir alipata kuona kitabu kile ambacho aliambiwa ahakikishe kisichomwe moto wala kuharibika.
Alishuhudia kuona mafuta yanaletwa na askari kadhaa kwaajili ya kunyunyiza kila kitu vipate kuchomwa moto, wale waganga wakaanza kazi yao ya kufanya maombi pale ili waweze kuvunja nguvu zote za kichawi eneo lile.
Samir alijisogeza karibu na vitabu vile akawa anakitazama kile kitabu huku akiona askari wakiwa wametapakaa sehemu ile kuhakikisha.kila kitu pale kinateketea kwa moto.
ATAKICHUKUAJE KITABU HICHO? USIKOSE SEHEMU YA 12.
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN.
MTUNZI:JAFARI MPOLE
SEHEMU YA 12

ILIPOISHIA
* Samir alijisogeza karibu na vitabu vile akawa anakitazama kile kitabu huku akiona askari wakiwa wametapakaa sehemu ile kuhakikisha.kila kitu pale kinateketea kwa moto.*

TUENDELEE
Alitazama kwa makini sehemu ile kuona mafuta yakianza kumwagwa na askari kwenye vitu vingine huku wakizunguka. Pembeni aliona farasi amesimama pale huku akiwa amevishwa mangozi ya kuwekea baadhi ya mizigo kama maji nakadhalika. Aliona afanye kitu ili aweze kukitoa kitabu kile pale.
Alitazama huku na kule kuangalia hakuna anayemtazama kisha akaiangalia ile pete yake na kuanza kuongea maneno kadhaa huku ajiwa amefumba macho yake. Sekunde kadhaa baada ya kufumbua macho alipotupa macho yale pele mbele hakuweza kuona kile kitabu kilichokuwa pale. Vilimwagiwa mafuta vyote vilivyosalia pale na vitu vyengine kisha kikaletwa kiberiti na kuweza kuwasha vitu vyote pale. Watu waianza kusogea nyuma na wengine kuanza kuondoka zao baada ya kuona zoezo hilo linakwenda tamati. Wale waganga walikuwa wakimalizia kusoma mambo yao pale huku moto mkubwa ukiwaka eneo lile.
Zoezi hilo walibaki wale askari wakilimalizia na taratibu baadhi yao wakaanza kurejea kwenye falme wakiwa na wae wanganga. Samir alipeleka macho kwa yule farasi aliyekuwa karibu na kitabu kile na kuona mganga mmoja ndiye amepanda juu yake wakianza safari ya kurejea kwenye falme. Naye alipanda kwenye farasi wake kuondoka na wenzake.
Huku kwenye falme Maya alikuwa juu ya falme akiitazama Eden jinsi inavyoonekana kwa chini, alipata kuuona moto ule uliokuwa ukiwaka mbele kidogo na kutambua kuwa ni oda aliyotoa baba yake. Aliwaona watu wakirejea kutoka kule na mmoja wapo akiwa Samir.
Alibaki kumtazama tu na kumuona jinsi alivyo bize na kumtazama farasi mmoja aliyepandwa na mzee mmoja.
Hakumtilia maanani sana aligeuka na kushuka kule juu naa kuelekea zake chumbani kwake, alifungua nlabgo na kuingia moja kwamojq akajitupa kitandani huku akiuqcha wazi mlango. Lutfiya alikuwa anamchunguza sana Maya kila nyenendo anazofanya, kuna jambo ahitaji kulifanya kwa Maya ikiwa kama moja ya kazi aliyopewa aifanye na Mfalme Faruk. Alijisogeza hadi pale mlangoni mwa chumba cha Maya akiwa anazuga kufutafuta vumbi ukutani lakini macho yakokaye yakiwa makini kuchungulia ndani.
Alipata kumuona Maya akiwa amejilaza kitandani hali ikiyompelekea Lutfiya ageuke kutazama kama kuna mtu aliyekaribu anamuona. Alihakikisha usalama huo taratibu akaingoza mkono kwenye matiti yake na kutoa kikaratasi kilichofinyagwa,akaanza kukifungua huku akionesha kuwa na wasiwasi kuogopwa kukutwa pale. Alichota unga fulani uliokuwa ndani ya karatasi ile na kuanza kumtazama Maya aliyekuwa hana analojua akiwa amejipumzisha kitandani. Akaunyanyua mkono wake ulioshika unga ule na kuanza kunyunyizia pale mlangoni kusudi Maya atakapotoka aweze kuukanyaga. Ni wazi kwanba hakuwa mwema kwa binti wa Mfalme na yote haya anayafanya kwaajili ya Mfalme Faruk. Alipolikamilisha zoezi hilo akaanza kunuia maneno fulani pale huku akitazama pale chinii alipomwaga unga ule na mwengine kuuelekezea kwa Maya, alishangaa anasukumwa na kitu nyuma yake hali iliyomfanya haraka afiche kile kikaratasi chenye unga ule kiaje kuonekana, alipogeuka kutazama alishangaa kumuona Samir akiwa amebeba tenga kubwa la nguo.
"Eh samahani kwa kukusukuma Lutfiya sikujuakaa upo mbele."aliema Samir akionesha hakuwa anafahamu kinachoendelea.
"Ah wewe umefuata nini huku?."aliongea Lutfiya kwa sayti ya chini huku akionesha kuwa na hasira.
"Nimetumwa nilete nguo za Maya zimetoka kufuliwa. Ndio nampelekea, samahani kidogo nipishe"alisema Samir na kumfanya Lutfiya ashtuke kusikia hivyo, ilibidi amzuie Samir akijua kupita kwake mlangoni kutaharibu nipango yake.
"Hebu subiri kwanza, unataka kuingia nani kakuruhusu? Maya anaoga na hata mimi kaniambia nisubiri hapa nje akimaliza ndio niingie."
"Ah sasa inakuwaje.?"
"Wewe uache tu huo mzigo hapa nikiingia nitampelekea."aliema Lutfiya huku akimtazama Samir aliyeonekana kutojua lolote.
"Ah usijali Lutfiya wacha nimsubiri tu hapahapa akimaliza nitaingia tu, nataka nikamjulie hali pia maana tangu jana sikuweza kuona."alisema Samir na kutua kile tenga chini naye akaka. Hali ile ikamfanya Lutfiya amtazame Samir kwa jicho la hasira kwa kuona anamharibia mipango yake.Aligeuka Samir na kuutazama mlango ukiwa wazi haukufungwa.
"Una maana Maya anaoga huku mlango ukiwa wazi kweli?"aliuliza Samir huku akimtazama Lutfiya.
"Ndio maana amenimbia nisubiri hapa mlango pasitokee mtukutaka kuingia ndani."alisema Lutfiya na Samir akanyanyuka zake na kuusogeoea ule mlango hali iliyofya Lutfiya ashangae. Aliposogeapale akaanza kutazama chini na kuweza kuuona ule unga ukionea kumwagwa pale, hakutaka kuonesha kama ameona lolote aligeuka na kwenda kwenye tenga lake na kulinyanyua na kurudi pale mlangoni .
"Wewe Samir unataka kufanya nini?"alishangaa Lutfiya akiwa amemkodolea macho Samir, hakutaka kumjibu lolotea aliusukuma ule mlango na kumfanya Lutfia amzuie kwa kumshika mkono.
"Hebu rudi wewe..!" alionekanakupagawa Lutfiya lakini maneno yake hayakuweza kunzuia Sanir kuingia mule ndani huku akiiruka ile dawa ambayo Lutfiya aliiweka pe mlangoni kwaajili ya Maya.
Samir aliingia na kumfayq Maya yanyuke pe kitandani na kuweza kumuona Samir akiwa amebebalile tenga.
"Eh pole sana jamani, sasakwaini wamekupa wewe huu mzigo uulete wakati sio kazi yako?"aliongea Maya huku akimzama Samir aliyekuwa anatua lile tenga.
"Naona wote wanafanya kazi ndio maana nikaona nikuletee nguo zako Maya."alisema Samir.
"Haya asante sana Samir."akisema Maya huku akiwa mwenye tabasamu.
"Umeshamaliza kuoga mara hii?"aliuliza Samir na swali hilo likfanya Lutfia pale mlangoni ashike mdomo kusikia vile.
"Mh mbona nilioga mapema sana, nupo tu nimepumzika hapa."alisema Maya.
Samir kusijia vile akageuka kutazama mlangoni alipotokea.
"Lutfia ingia kumbe tayari alishamaliza kuoga."alisema Samir kwa sauti hadi Maya akashangaa.
Maneno yale yalimfanya Lutfiq pake mlangoni ashike kichwa kuona Samir anazidi kumharibia.
"Kafanyaje Lutfia mbona unamuita?"aluliza Maya akiwa haelewi kinachoendelea.
"Nilimkuta hapo mlangoni nikiwa nataka kuingia akanizuiq na.kusema ulikuwa unaoga ndio maaa nikashangaa kukuta umepumzika."aliongea Samir na kumfanya Maya ashangae, Lutfiya hakuwa na jinsi aliamua kuingia mule ndani na kuituka ile dawa aloweka mwenyewe na kufanya iharibike kile kitu alicho dhamiria kukifanya kwa Maya. Taratibu alisogea hadi pale waliposimama.
"Kwani uliingia humu Lutfia nikakwambia naoga?"aliuliza Maya akiwaanamtazama Lutfia aliyekuwa anatazama tu chini kwa aibu.
"Nisamehe binti wa Mfalme, sikutaka mtu akusumbue ukiwa umepumzika maana umetoka kwenye misukosuko hivyo isingependeza ukasumbuliwa."alijitetea Lutfiya.
"Hapana wala usijali kuhusu hilo, mimi nipo sawa kwasasa na huyu alikuwa analeta hizi nguo tu hakuwa na shida."aliongea Maya.
"Sawa nimekuelewa binti wa Mfalme."
" Haya mnaweza kwenda wote mniache sasa."alisema Maya na kuwafanya Samir na Lutfiya wageuge kuondoka zao.Hata waipotoka nje Samir aliongoza njia yake moja kwa moja kueleea kwake huku Lutfiya akimtazama kwa hasira sana kuona amemharibia mipango yake kwa mara pili,aligeuka na kuongoza njoa yake.

Moja kwa moja alirudi kwenye kibanda chake na kujilaza kweye kitanda huku akishusha pumzi kwa uchovu. Aligeuza kichwa na kutazama kike kitabu akiwa amekiweka pembeni ya kitanda, taratibu alinyoosha mkono na kukichukua akawa amekishika huku akikitazama. Alikumbuka muda ule alipopeleka farasi zizini wakiwa wametokakule mtaani kuchoma vitu vya ile nyumba ya akinq Nadhra na ndio muda hata wale waganga nao wakiweza kuwaingiza farasi wao kwenye zizi hilo. Na walipoondoka ndipo nafasi hiyo aliitumia kusogea kwayule farasi ambaye muda ule alikuwa karibu na vile vitabu kabla ya vile vitabu kuchomwa moto. Aliweza kumshika farasi yule kwenye ile ngozi aliyovalishwa ikiwa kama ni kifaa cha kuwekea maji na vitu vyengine. Aliongea maneno kadhaa na kufanya pete ile iliyopo kidoleni kuwaka na kuweza kuona kitabu kile kwenye lile ngozi. Alikichukua na haraka akatoka mule zizini na kwenda kukihifadhi kwake, akiwa ndani alishangaa kuona pete ile ikiwa inambana sana na alipotazama aliona tukio ambalo lilikuwa likiendelea muda ule. Alimuona Lutfiya akiwa mlangoni kwenye chumba cha Maya. Hali ile ikamfanya Samir atambue kuwa kuna jambo baya Lutfiya anataka kulifanya kwa Maya, haraka alichoropika mule ndani kama upepo n kuelekea huko kujaribu kumuwahi Lutfiya.
Yote hayo alikuwa akiyakumbuka akiwa amekishika kitabu hicho pale kitandani. Alianza kuwa na wasiwasi kuhusu Lutfiya maana ni tukio la pili sasa anapata kumuona akitaka kumfanyia Maya. Nafsi yake ilimsuta kuendelea kunnyamazia Lutfia kwa matendo yake yale muda huohuo akanyanyuka na kuelekea moja kwakoja kumfuata Lutfia.
ITAENDELEA
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN
MTUNZI:JAFARI MPOLE
SEHEMU YA 13

ILIPOISHIA
Nafsi yake ilimsuta kuendelea kunnyamazia Lutfia kwa matendo yake yale muda huohuo akanyanyuka na kuelekea moja kwa moja kumfuata Lutfiya.
TUENDELEE

Huku upande wa pili Mfalme Faruk baada ya kukaana kutafakari kwa kina kuhusu kazi aliyompatia Lutfiya kule Eden kuweza kufeli, alitafuta njia nyengine ya kulikamilisha swala hilo. Muda huohuo Jamal aliingia na kumkuta baba yake akiwa ametulia kwenye kiti chake cha kifalme akitafakari.
"Ni muda sasa umepita tangu umpe kazi yule mwanamke na sioni chochote kinachoendelea, kama imeshindikana hivyo tutafute njia nyengine ya kufanya."aliongea Jamal huku akimtazama baba yake.
"Jamal.. hili swala sio la mara moja kama unavyofikiri, elewa kwamba ile ni falme kama ilivyo hii. Tazama askari waliopo nje na ndani wakiweka ulinzi na ndio vivyo hivyo ilivyo mule ndani ya falme ya Eden. Huyu msichana anafanya kila jitihada kuweza kufanya kazi tunazompa na sio kama hafanyi, anafanya lakini kunakuwa na vizuwizi vya hapa na pale. Hivyo hupaswi kukata tamaa mapema hivyo na tambua hili swala ni kwaajili yako hivyo ukijifanya kuwana haraka unaweza kukosa tunacho kihitaji."alisema Mfalme Faruk akimtazama mwanaye.
"Sawa nimekuelewa, lakini tunavyokwenda taratibu tunafanya swala hili liwe gumu zaidi, hii ndio nafasi ya siai kuhakikisha Maya tunamteka kiakili kusudi aonekane alitoka kuugua. Sasa tukichukua muda watu wote wakamuona amerudi hali yake ya kawaida tukija kufanya jambo letu lazima litachunguzwa ijulikane chanzo."alisema Jamal na kumfanya baba yake atazame pembeni kulitafakari swala hilo. Aliona anachoongea mwanaye ni swala la msingi sana.
"Sawa umeongea jambo la msingi sana kuujali muda,nitatuma ujumbe kwa Lutfiya aweze kujitahidi kwenye hilo."alisema Mfalme akimtia moyo mwanaye.

Huku kwa Samir aliweza kumuona Lutfiya akiwa zake kwenye korido moja wapitayo watu akifanya usafo. Alimsogelea hadi pale jambo lililomfanya hata mwanamke huyo ashangae kuona anafuatwa.
"Samir una shida gani muda huu wa kazi?"aliuliza Lutfiya akiwa ameshika kitambaa akisafisha kuta za mahala pale na baada ya kumuona Samir ikabidi asitishe zoezi holo.
"Shida yangu ni wewe."aliongea kwa kujiamini huku akimtazama Lutfiya.
"Unataka nini kutoka kwangu?huu muda sio wa kuanza kuongea lakini.!"
"Sikuja kuongea ila itakuwa ni kitendo cha marmoja tu endapo ukiniambia unataka kumfanyia Maya kitu gani?."aliuliza Samir huku akiwa anamtazama Lutfiya kwa umakini zaidi.
"Samir.. mbona sikuelewi unamaanisha nini?"aliongea Lutfiya akijifanya hajaelewa chochote.
"Kipi hujaelewa hapo? inamaana unavyofanya kwa Maya hujui,mara ya ngapi sasa nakuuta ukiwa katika matukio ya ajabu, mwanzo ulitaka kumpatka nini sijui Maya nilipotokea ukaanza kujikosha, leo tena umeweka sijui madawa gani mlangoni kwake, ulikuwa na lengo gani naye?ulitaka awe chizi au umuue?"alisema Samir akiwa amemkazia jicho Lutfiya.
"Haa jamani Samir sikuwa na maana hiyo,naomba tu tuyamalize hayo nisamehe kwa kilichotokea."
"Kwanini hukutaka niingie ndani ukanidanganya Maya anaoga?. Nataka nijue tu unampango gani na Maya , au nikamwanbie mwenyewe?"
"Ah hapana nakuomba sana usiende kuongea lolote kwa Maya kuhusu mimi nakuomba sana Samir."alibembeleza Lutfiya baada ya kuona swala hilo linaweza kuwa kubwa.
"Nahitaji kujua tu ukweli yote hayo unayomfanyia Maya ni kwasababu zipi?"alisema Samir na hali ile ikamfanya Lutfiya awe mpole. Baada ya kubanwa sana aliona aeleze tu ukweli huenda asipofanya hivyo anaweza kukamatwa siku .
"Wewe Samir unafanya nini hapo muda huu.!"ilisikika sauti ya Malkia na kumfanya Samir ashtuke baada ya kujua ni Malkia,alimpa heshima yake pale huku Lutfiya akiona ndio nafasi ya yeye kuepukana na Samir. Haraka aligeuka na kuendelea na kazi yake.
"Muache mwenzako afanye kazi Samir usimsumbue, hebu nenda nje kaendelee na kazi zako huko."alisema Malkia na kumfanya Samir ageuke na kuondoka zake eneo lile akiwa ameshindwa kujua sababu za Lutfiya kuweza kufanya mambo yote hayo.
Malkia alimtazama hadi alipotokomea Samir kisha akamsogelea Lutfiya.
"Kuna jambo nahitaji kulifahamu Lutfia."alisema Malkia na kumfanya Lutfia ageuke kumtazama Malkia Tayat kumsikiliza.
"Jambo gani Malkia wangu?"
"Ni kuhusu Maya mwanangu."
"Maya? kafanya kitu gani Maya?"
"Hapana, ni kuhusu tukio ambao lilitufanya tukeshe na kuhangaika kila sehemu kwaajili ya tatizo lake. Waganga wamefanya kila njia kumponesha lakini ilishindikana. Nataka nijue aliamka mwenyewe au kuna sababu ambazo zimepelekea yeye kuweza kurudisha uhai tena?"aliuliza Malkia na swali lake hilo likamuweka njia panda Lutfiya.
"Malkia, nini una maanisha lakini. Mimi nadhani hayo maswala tungeyasahau kabisa maana yatakutia mawazo yasiyo na msingi, na jambo la kushukuru Maya yupo salama sasa tupo naye tena na hili ndilo tulikuwa tukilisubiri muda wote hata ukaamua kwenda Mashariki ya mbali ili Maya aweze kuamka."alisema Lutfiya akimueleza Malkia Rayat.
"Sio kwamba nimechukia kurudi kwa mwanangu laa, nina furaha sana kumuona tena akiwa mwenye tabasamu muda wote. Ila akili inafikiria mbali sana, nahisi uchawi bado unaendelea kwa mwanangu. Na huenda mtu aliyemfanya hivi mwanangu si yule mzee pekeyake huenda kuna watu wengine wanazidi kumuandama mwanangu. Sina uhakika wa asilimia zote kama Maya amepona kabisa, nina wasiwasi juu ya mwanangu huenda wakawa wamempa uhuru kwa muda."aliongea Malkia Rayat akionesha kuwa na mashaka juu ya binti yake.
"Mh swala hilo sikuwa nalifikiria kabisa Malkia wangu, ila uliponiambia tu hata mimi nimejawa na hofu moyoni. Maya inabidi aangaliwe sana asiwe mwenye kuachwa tu huru muda mrefu."aliongea Lutfiya.
"Nina mpango wa kumfutia mtu wa kuweza kumlinda, safari zake za kwenda kuzunguka baadhi ya miji akiwa na wenzake wa kawaida sitaki tena niisikie nahofia lisije kutokea kama la kipindi kile huko njiani waavamiwa yakaanza matatizo yaleyale."
"Cha msingi ni hicho apewe ulinzi wa kutosha."alisema Lutfiya akichangia mada hoyo na kumpa ushauri Malkia. Moyoni alipata tunaini jipya la kuona kuna nafasi kumbe ya kuendelea kujaribu tena jambo kwa Maya. Kama Malkia hadi sasa ana wasiwasi kuwa mwanaye huenda hajaona basi hata akimfanyia kitu alichoagizwa kufanya na Mfalme Faruk kwa Maya hatajulikana kama ni yeye bali itadhaniwa ni ugonjwa uleule unamsumbua. Malkia aligeuka na kuondoka zake baada ya kupata ushauri kwa mfanyakazi wake huyo bila kujua si mwema upande mengine.

Wazo la kumuwekea ulinzi Maya hakubaki nalo mwenyewe akimjulisha na Mfalme Siddik swala hilo. Wakawa wanajadili namna ya kuwapata watu mahodari wa kumlinda binti yao. Njia pekee ya kulifanikisha hilo ni kutoa matangazo kwa raia ambaye mwenye nguvu na shababi wa kweli wakiandaliwa mapambano baina yao ili apatikane mshindi aweze kuwa mtu wa kumlinda Maya muda na wakati wowote. Vipeperushi vilisambaa Eden na nje ya Eden kote kuhusu mashindano hayo ya kumtafuta shababi.
Upande wa mhusika mwenyewe Maya hakupendezwa na hatua ambayo wazazi wake wameichukua. Hakupenda swala la kulindwa kila wakati maana aliqnza kuyazoea maisha ya kuwa na uhuru muda wote.
"Hii ni kwaajili ya kukulinda mwanangu na si vingine."alisema Mfalme akiwa chumbani kwa binti yake baada ya kunpelekeea taarifa hizo.
"Sijapenda mlivyofanya baba, muda wote nitakuwa nasimamiwa tu na mtu sitapata uhuru wa kufanya mambo yangu."aliongea Maya akiwa amenuna.
"Uhuru unaotaka wewe ndio umepelekea wewe kupata matatizo hayo, umeenda na wenzako mnevamiwa na watu huko mmerudi wachache wengine wameuliwa huko, hata siku moja haijapita na wewe ukaanza kuugua na kukupelekea ukapoteza fahamu wiki mbili nzima umetutia wasiwasi, mimi kama baba ndio nimeamua hivyo kwaajili ya usalama wako."alisema Mfalme Siddik na kugeuka kuondoka zake akiwa tayari amefikisha ujumbe huo kwa mwanaye. Maya alikasirika sana lakini na kujituoa kitandani akichukia uamuzi ule wa wazazi wake, hakupenda maisha ya kulindwa.

Taarifa za mapambano hayo zilimfikia Dalfa kule Mashariki ya mbali na kumfanya akasirike baada ya kutambua kumbe ni kweli Maya ameweza kuamka. Hadi wanamtafutia ulinzi basi ni wazi kwamba binti huyo yupo salama kiafya.
" Hili swala limewezekana vipi?ni nani ameweza kumtoa uchawi ule bila kutumia nguvu zangu,?aaaaaah."alikasirika sana Dalfa baada ya kujua ameikosa Falme ya Eden, alijua kwa vyovyote lazima Malkia Rayat angerudi tena kwaajili ya mwanaye hivyo kazima wangekubaliana tu kuiacha Eden iwe mikononi mwa Dalfa ambaye ndio alikuwa akitarajia hilo siku zote kuimikiki Eden taifa maarufu. Haraka akatoka zakena kwenda kwenye chumba chqke cha kufanyia maombi yake huko.Hata alipofika aliufunga mlango na kuanza kubadilika sura kuwa ya kutisha sana. Alisogea kwenye kalai moja likiwa kwenye moto huku likiwa na mafuta ndani yake. Alinyoosha mkono huku akiongea msneno fulani kwa lugha ya kichawi na kufanya mafuta yale yatulie kama maji angali moto unawaka sana. Alizidi kuomba huku akiwa amefumba macho yake mkono wake ukiwa umeelekea kwenye mafuta yale na dakika kadhaa alipofumbua macho yalikuwa yanawa kama paka na kwenye yale mafuta kukawa kunaonesha tukio lililopita pindi Maya alipokuwa kitandani amelala akiwa hajitambui, lengo ni kujua kitu gani kilitokea hadi kuweza kumfanya Maya akaamka.

JE SAMIR ATAJULIKANA KUWA NI YEYE NDIYE ALIYEMSAIDIA MAYA? USIKOSE SEHEMU IJAYO.
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN.
MTUNZI:JAFARI MPOLE
SEHEMU YA 14

ILIPOISHIA
Jafari alifunika daftari lake na kusimama naye kutoa heshima na alipotazama mbele kwa Mwalimu huyo alshtuka baada ya kumuona yule Mwalimu.
* TUENDELEE*
Alibaki kumtazama Mwalimu yule ambaye ana siku kadhaa pale shuleni ni mgeni, ilaa kwa Jafari ilikuwa tofauti kidogo baada kuitambua sura.
"Mfalme?"alishangaa Jafari baada ya kumuona mwalimu yule anafanana vilevile na Mfalme Siddik. Alishudia kuona mwalimu huyo akisogea hadi kwenye meza moja na kuweka vitabu vyake huku mkono mwengine akiwa ameshika bakora zaidi ya tatu. Aligeuka kuwatazama wanafunzi baada ya kuitikia salamu aliyopewa.
"Kaeni chini...Viongozi wa darasa naomba mkusanye madaftari yote, naamini siku tano zimetosha kuifanya kazi ambayo nimewapa,tangu Ijumaa hadi Jumatatu kama wewe hukumaliza kazi yangu basi ni makusudi hayo,kama wewe umefanya hesabu zangu 25 ili tu umalize na nisahihishe nikute umepata hesabu kuanzia 15 kushuka chini ni makusudi hayo. Kama wewe unajua umekopi kwa mwenzako na kuhamishia kwako nikute majibu na njia zinafanana kwa watu kama pia ni makusudi maana umeshindwa kushirikisha ubongo wako. Na mimi watu wote wanaofanya makosa kwa makusudi katika somo langu lazima niwanyooshe wakae mstari mmoja na wenzao. Hatuwezi kuwa kwenye msafara mmoja lakini wengine fikra zipo nyumbani kwao."alisema yule mwalimu akiwatazama wanafunzi wa darasa hilo.
Jafari alibaki kumtazama yule mwalimu vile anavyoogea ni vilevile ambavyo Mfalme Siddik anavyozungumza. Alijikuta akitabasamu tu baada ya kuona ni maajabu hayo anayoyaona mbele yake.
Viongozi wa darasa wakaanza kupita kwa wenzao wakikusanya kazi hiyo. Kuona hivyo Jafari aliichukua karatasi ile ya maswali na kuiweka kwenye daftari lake kisha akalifunika na kuliweka pale mezani huku akishika kwa mkono wake ambao amevaa ile pete. Aliomba maneno yake kadhaa huku akiwa amefumba macho na muda huohuo Monitor akapia pale akihitaji kulikusanya daftari lile. Alifumbua macho na moja kwa moja akalifunua lile daftari na kushuhudia maswali yale yakiwa yamechambuliwa kwa uweledi mkubwa kana kwamba aiyefanya kazi hiyo ni yeye. Hata yeye hakuamini kuona vile na hapo ndipo akaona kweli pete ile ni muhimu sna katika maisha yake. Alikusanya daftari lile na kuendelea kumtazama mwalimu yule.

Alionesha kutokuwa na utani kabisa na wanafunzi, muda wote alikuwa anaonekana kuwa makini na kazi yake hiyo hasa pale alipotaka kufahamu kama kuna ambaye hakufanya kazi hiyo.Alipohakikisha hakuna aliagiza viongozi wa darasa hilo kuchukua madaftari yale wapeleke ofisini.
"Leo sitafundisha chochote ila nitakapomaliza kusahihisha kazi hii hata baadae nitakuja na kama niivyosema wale watu wangu wa makusudi mjiandae."alisema Mwalimu yule na kutoka zake mule darasani baada ya madaftari yale kupelekwa ofisini kwake.Hapo wanafunzi wote wakaanza kushukuru Mungu kwa kuona wamepewa uhuru maana walikuwa wameingiwa na woga.
"Huyu ticha naona amekuja kwa kasi sana hapa shuleni,atapoa tu we subiri hajakutana na wababe, sasa
we mwalimu hata wiki haijaisha tayari wanafunzi wameanza kukuogopa duh!"alisema mwanafunzi mmoja na kuwafanya hata baadhi ya wenzake wamuunge mkono kwa kile alichokisema. Wakawa wanamuongelea mwalimu yule huku Jafari akisikiliza tu kinachoendelea huenda akasikia hata jina la mwalimu huyo ili apate kufananisha na mtu anayemjua.
Baada ya muda vipindi vengine viliendelea hadi ulipofika muda wa mapumziko kengele iligongwa na wanafunzi wakaelekea kupata kifungua kinywa. Muda huo ndio Jafari aliutumia kupata uhakika juu ya yule mwalimu, alimuona Eliza akiwa anaelekea kwenye chai akamkimbilia kumuwahi wakawa wanatembea wote.
"Baba Azizaaa vipi uko powa."alitania Eliza akionesha kutabasamu.
"Hebu acha ujinga wako bwana, ..hivi Eliza yule mwalimu anaitwa nani maana jina lake nimelisahau kidogo.."
"Mwalimu yupi tena ?"
"Yule mgeni aliyekusanya madaftari."
"Dah halafu umenikumbusha, kumbe ile kazi uliifanya ukawa unanidanganya mshkaji wangu si fresh Jafari.."aliongea Eliza akiwa anampa lawama Jafari.
"Dah usinifikirie vibaya rafiki yangu nilijua unanitania muda ule ndio maana nikakujibu vile, nisamehe sana."aliongea Jafari kwa upole.
"Mimi nilikuwa sijamaliza kweli sio utani, sema fresh nilikopi kwa Rosemary ila sasa sijui itakuwaje yule ticha akijua kama tumeibiana majibu,"
"Mimi sidhani kama ataweza kupitia kila daftari kuona kama watu wameigaliziana mpaka njia, vile ni vitishi tu, haya hebu nikumbushe jina lake basi."
"Yule si Mwalimu Sadiki na wewe jana tu kalirudia jina lake mara kwa mara."
"Sadiki? Mhh... Sadiki au Siddik?"aliuliza Jafari na swali lake hilo likaonekana kumkera Eliza.
"Kwani una matatizo ya masikio sikuhizi? Utanikera sasahivi Jeff. Anaitwa Sadiki."alisema Eliza na kumfanya Jafari abaki kushangaa. Kwa namna fulani aliona jinsi majina hayo mawili yanavyoshabihiana hali iliyopelekea kuwa na wasiwasi juu ya mwalimu yule.
"Haya shemeji huyo anapita."alisema Eliza na kumfanya Jafari ageuke kutazama, alimuona Aziza anapita kuelekea kwenye chai. Akabaki kutabasamu tu huku akiwa anaongozana na Eliza nao wakielekea huko. Muda wote alikuwa akimtazama Aziza kwa umbo na vile alivyo akapata kuona jinsi alivyofanana na Maya kule Eden. Hapo ndipo akapata kujua kweli duniani ni wawili wawili lakini kwa upande wa Mwalimu Sadiki hakuweza kuamini maana aliona hata majina jinsi yalivyo shabihiana na kujipa moyo atalifuatilia swala hilo hapo badae.

Huku Eden mambo yalizidi kupamba moto kila sehemu. Ilikuwa ikisubiriwa siku ya kesho ambayo ndio mashindano hayo yatarindima kwenye uwaja maalumu kwaajili ya mpambano. Watu walikuwa wakijifua kikamilifu kuhakikisha wanapata ushindi siku hiyo. Kwa Lutfiya yeye bado alikuwa na kazi ya kuhakikisha swala lake linafanikiwa kabla ya siku hiyo. Alihakikisha siku hiyo anatumia njama yeyote ile kuhakikisha nafanya swala lake. Alitoka kwake na kuelekea upande wa jikoni kwanza kuhakikisha kama kuna idadi zaidi ya watu. Kwa bahati alipata kumuona msichana mmoja peke yake akiwa anaandaa chakula muda huo.
"Hii nafasi sipaswi kuichezea tena ni kuongeza umakini tu."alijisemea mwenyewe akiwa anatazama kule jikoni. Muda huohuo alianza kusogea hadi pale jikoni na kumfanya yule msichana amuone Lutfiya.
"Naona unaandaa chakula kwaajili ya Mfalme pamoja na Malkia."
"Ndio, leo nimeona niandae mapema maana kuna kazi zinanisubiri hapo baadae."
"Upo peke yako leo?"
"Ndio, wenzangu wametoka kwenda sokoni kutafuta mboga za kesho."alisema yule msichana huku akiwa shapu kuendelea na kuandaa.
"Dah pole sana, wacha nikusaidie baadhi ya kazi mwenzangu haya vyombo vya kumuwekea Maya chakula viko wapi.?"alisema Lutfiya akisogea kwenye sufuria na yeye, yule msichana aliona ni wema anaofanyiwa kusaidiwa kazi. Alichukua vyombo hivyo na kumpatia Lutfiya aliyepokea na kuanza kuweka chakula huku akimtazama mara kwa mara yule msichana. Dakika kadhaa kupita akiweza kuweka mambo sawa msichana yule na akanyanyua vyakula na kuelekea sebuleni kuandaa mezani. Lutfiya alibaki kumtazama tu aliondoka na kuona ndio muda pekee wa yeye kufanya kile kilichomleta. Aliingiza kifuani na kutoa kikaratasi kidogo kilichokuwa na unga fulani wa rangi. Akaanza kuchota kwa mkono na kuanza kunyunyizia kwenye chakula kile kilichopaswa kwenda kwa Maya.
Alipolikamilisha zoezi hilo alikirudisha kikaratasi kile na kuendelea na kazi nyengine. Muda huohuo yule msichana alirejea na kumkuta Lutfiya akimsaidia hata kuosha vyombo.
"Jamani nashkuru sana leo kwa kunisaidia hivi maana leo ningezunguka kila kazi ningeifanya mimi."
"Usijali kuhusu hivi, sote tunafanya kazi kwenye falme hivyo kusaidiana ni jambo la kawaida sana. Itafika siku na wewe ukiwa hauna kazi unaweza ukaniona nimebanwa na kazi ukanisaidia pia."
"Ni kweli kabisa usemacho"alisema msichana yule bila kuelewa kilichoendelea. Baada ya muda alichukua kile chakula na kupeleka kwa Maya. Hapo ndipo Lutfiya akabaki kutabasamu na kuona kazi yake inakwenda kukamilika, alibaki kumtazama tu msichana yule akitembea kuelekea chumbani kwa Maya,naye akaamua kutoka mule jikoni baada ya kumaliza kazi yake iliyomleta akaondoka kuendelea na mambo yake.
Aliweza kuingia mule chumbani na kumkuta Maya amejipumzisha kitandani, taratibu kwa heshima akasogea hadi kwenye meza iliyopo pembeni na kuweka kile chakula. Akaanza kuandaa pale kila kitu na alipokamilisha aliweza kumkaribisha Maya aweze kusogea mezani kupata chakula.
"Sawa nakuja wewe kaendelee na kazi."alisema Maya akiwa amejilaza kitandani. Yule msichana aligeuka na kuondoka zake baada ya kukamilisha kazi yake. Dakika chache kupita alishuka pale kitandani na kuelekea kwenye ile meza iliyoandaliwa vyakula. Alisogeza kiti na kukaa pale huku akiweka sahani ili apate kupakuwa chakula.

Baada ya dakika kama kumi Lutfiya aliongoza njia kuelekea kwa Maya ili apate kuona kama jambo ambalo amelifanya limeanza kufanya kazi. Moyoni alikuwa mwenye furaha sana akijua kila kitu kinakwenda sawa. Alipita sehemu kwenye korido na kuweza kumuona Samir akiwa anatokea njia ya kuelekea sebuleni walipo Mfalme na Malkia wakiwa wanakula, walipishana kama hawajuani huku akimtazama akiwa ameshika kitenga akielekea nje. Alipofika mbele Lutfiya aligeuka kumtazama Samir aliyeonekana hana habari kinachoendelea. Alimsindikiza kwa kumsonya kuonesha hampendi maana amekuwa akimvurugia mipango yake yote. Aligeuka kuongoza njia hadi alipofika nje ya chumba cha Maya, alitazama huku na kule kuangalia kama kuna mtu maeneo yale. Alipohakikisha usalama upo alisogea kwenye dirisha na kuchungulia ndani akapata kumuona Maya akiendelea kula. Hapo akapata tumaini la kuona kazi yake imefana. Alishangilia pale dirishani na baada ya kuonesha furaha yake hiyo alisogea mpaka pale mlangoni kisha akagonga hodi na kuingia.
Alimuona jinsi Maya anavyoendelea kula pale mezani bila kujua kinachoendelea. Taratibu akasogea hadi pale.
"Lutfiya vipi.!"aliongea Maya akionekana kunyanyua kipande cha nyama ya kuku na kukipeleka mdomoni kutafuna.
"Ah samahani binti wa Mafalme, nilikuja kwaajili ya kuangalia kama umemaliza kula ili nipate kutoa vyombo."
"Bado nakula uje baadae."alisema Maya akiendelea kula.
Lutfiya aligeuka huku akiwa ni mwingi wa furaha akaanza kuondoka mule ndani.
"Halafu, pitia kwa mama yangu umwambie Nashkuru sana kwa chakula chake."alisema Maya na maelezo yale yalimfanya Lutfiya asielewe yanamaana gani.
"Sijakuelewa una maana gani binti wa Mfalme."aliongea Lutfiya akitega masikio yake kumsikiliza Maya.
"Hujasikia au hujaelewa,nenda kwa mama umwambie Maya anasema asante kwa kile chakula alichompa Samir kuniletea, umeelewa..?"aliongea Maya na kumfanya Lutfiya ashtuke kusikia maneno hayo. Alitengeneza tabasamu usoni mwake na kumuitikia Maya kisha akatoka zake nje.
Alihisi kuvurugwa akili baada ya kutoka nje, alisimama sehemu na kuanza kutafakari maneno ya Maya.
"Inamaana na hili swala Samir ameliingilia? Amejuaje kama nilifanya?"alijiuliza Lutfiya na kubaki njia panda. Alipokumbuka muda ule wakiwa wanapishana na Samir aliweza kuona ameshika kitenga akitoka nacho nje. Hakuweza kufahamu ndani yake kulikuwa na nini. Hapo ndipo akaanza kuhisi huenda kuna jambo Samir amelifanya, haraka akatoka na kuelekea alipoenda Samir kujua alibeba nini mule kwenye kitenga.
ITAENDELEA.
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN
MTUNZI:JAFARI MPOLE
SEHEMU YA 15

ILIPOISHIA
* Hapo ndipo akaanza kuhisi huenda kuna jambo Samir amelifanya, haraka akatoka na kuelekea alipoenda Samir kujua alibeba nini mule kwenye kitenga.*

TUENDELEE
Upande wa pili Dalfa alikuwa njiani na vijana wake wawili wanakuja ndani ya mji wa Eden na lengo hasa ni kumtambua mtu ambaye amekuwa akimtilia mashaka. Alifumba macho yake na kuanza kuvuta hisia huku akichanganya na nguvu zake kujua kinachoendelea Eden.Upeo wake wa kufikira ulimfanya aone zile nguvu ambazo anazitilia shaka kwa yule mtu bado zipo Eden hali iliyomfanya afumbue macho haraka baada ya kutambua kile alichokiona huenda kikawa kweli. Akazidi kupata hamasa ya kufika Eden haraka kumpata mtu huyo.

Lutfia alifika nje na kuzunguka nyuma ya jengo kwenye zizi la farasi na kuweza kumuona Samir akiwa anawatupia kuku panoja na jiwa wengi sana chakula. Alipotazama kwa makini alipata kuona ni punje za wali Samir akiwa anawapq wale ndege huku wengine wakionekana kulewa na kuishiwa na nguvu kabisa baada ya kula chakula kile. Hapo ndipo Lutfiya akapata kutambua kile chakula alichotia unga ule kwa lengo la kumdhuru Maya endapo angelikula chakula kile. Alijikuta akikasirika sana baada ya kuona mpango huo tena amefeli. Alimuona Samir akinyanyuka pale alipokaa na kugeuka kumtazama wakabaki wakiangaliana. Samir akapiga hatua na kusogea pale alipo Lutfia ambaye alibaki kuangalia tu pembeni akionesha kukasirika.
"Naomba uniambie leo, kwanini unataka kumdhuru Maya?. Mara ya ngapi hii nimekuwa nakuona ukijaribu kumuwekea vitu vya hatari.?"aliongea Samir huku akimtazama Lutfiya kwa jicho la hasira sana.
"Samir nisikilize.. haya mambo wewe hayakuhusu usitafute matatizo mengine. Kaa mbali na Maya usijaribu kunizuia kwa lolote lile kuanzia sasa, fuata kilichokuleta humu kwenye falme fanyakazi zako."aliongea Lutfiya kwa kujiamini sana baada ya kuona sasa akizidi kumhofia Samir anaweza asifanikiwe kabisa kile alichowaahidi wenzake.
"Wewe.. hunijui sikujui nimekukuta tu humu na kukupa heshima kama mfanyakazi kwenzangu. Siwezi kukaa kimya nikukuona ukijaribu kumdhuru binti wa Mfalme. Yule ni Malkia wetu wa baadae iweje umfanyie visakama hivi, amekukosea nini au kuna watu wanakutuma uje kuharibu hii furaha iliyopo sasa?. Ina maana haufurahia kupona kwake, ulitaka afe si ndio."aliongea Samir akiwa makini na kile asemacho. Lutfiya mwenywe alishangaa kuona Samir aliyemzoea hivi leo anaongea kwa kujiamini sana. Mwanaume aligeuka na kuwatazama wale kuku na njiwa wote wakiwa hoi pale chini na wengine wakionekana kufa kabisa.
"Nimekuvumilia kwa mambo uliyokuwa ukifanya nyuma sasa imetosha, ni muda wa kuyaeleza mambo yako kwa mhusika. Ulitaka kumuua Maya kwa sumu hebu ona.. wewe sio binadamu wakuishi kwenye falme hii."alisema Samir akimueleza ukweli Lutfiya aliyebaki kutulia tu hana neno la kusema. Samir alimpushi Lutfiya pale alipisimama na kupita kuelekea zake.
"Sawa endapo ukienda kusema kwa Maya nami naelekea kwa Mfalme kumueleza ulivyotaka kumbaka Maya. Hapo ndipo tutakapojua nani ataondoka kwenye falme hii."alisema Lutfiya na kumfanya Samir asimame gafla na kushindwa kuendelea mbele na safari. Aligeuka nyuma kumtazama Lutfiya aliyekuwa anamuangalia Samir.
"Unasemaje,?Mimi nilitaka kumbaka Maya,? Wapi na lini."aliuliza maswali kwa mkupuo Samir baada ya swala hilo kutolielewa vyema.
"Lini? Unajifanya kusahau kile ulichotaka kukifanya usiku ule Mayabakiwa kitandani?"alisema Lutfiya na kumfanya na kumfanya Samir ashangae habari hizo ambazo kwake ni ngeni. Alijua huenda mwenye jina la Samir ndio alitaka kufanya tukio hili. Taratibu akaanza kukosa ujasiri wa kuendelea na msimamamo wake wa kupeleka taarifa zile kuhusu Lutfia. Alilitafakari swala hilo na mwisho akageuka na kwenda hivyohivyo ndani. Alimuacha Lutfiya pale nje akiwa ameshika kichwa kuona mambo yamezidi kuwa magumu kwake.
"Kama nitafukuzwa humu basi lazima nayeye atafukuzwa sitakaa kimya."alisem Lutfiya akiwatazama wale kuku wakiwa pale chini wengi wao waionekana kukata roho. Hakujali kuhusu hilo aligeuka naye kuelekea ndani ya falme kujua kinachoendelea kama Samir ataongea kweli.
Samir alifika ndani na kukutana na mfanyakazi mmoja wa ndani.
"Malkia alikuwa anakuhitaji, yupo ukimbini."akisema msichana yule na kugeuka kuondoka zake. Samir aliposikia hivyo haraka akaongoza njia kuelekea ukumbini, alipata kumuona Malkia akiwa amekaa na Mfalme wakiwa wanapata kinywaji.
"Vipi ulifikisha chakula kile?"aliuliza Malkia akimtazama Samir aliyesogea pale na kutoa heshima kwao.
"Ndio nilifikisha Malkia wangu, na amekushukuru kwa kumpatia chakula kile."alisema Samir.
"Sawa chukua na hii umpelekee."alisema Malkia akinyanyua bilauli lenye kinywaji ndani yake, Samir alipokea na kugeuka kuelekea kwa Maya kumpati.
"Maya ameanza kumuamini Samir hadi kumtua leo chakula angali wafanyakazi wapo."alisema Mfalme akimtazama Samir akitokomea.
"Ni maamuzi yake naona leo kaamua kumtuma Samir."alisema Malkia wakawa wanaendelea kupata kinywaji.

Samir akiwa anaelekea kwa Maya njia alijikuta akihema baada ya kuona amefanya kazi kubwa sana siku hiyo. Muda ule ambao Lutfia alikuwa akiandaa kuweka unga wenye madhara kwa Maya kwenye chakula kule jikoni huku upande wapili Jafari aliweza kutambua baada ya kuona ile pete yake ikimbana, na alipoitazama aliona tukio lile Lutfiya akiwa ananyunyizia ule ule unga kwenye chakula cha Maya hali iliyopelekea Jafari atoke mbio akiwa zake kwenyw mgahawa anakunywa chai na moja kwa moja akaelekea kwenye vyoo vya shule lengo. Hata alipoingia mule aliitazama pete ile na kuanzakuongea maneno fulani na gafla akajikuta yupo kwenye choo ndani ya falme. Alitoka haraka na kuumiza kichwa atazuiaje swala lile ili hata yeye asijulikane wala kuulizwa amelijuaje swala hilo. Alielekea kwa Malkia akimkuta yupo mezani anakula pamoja na Mfalme.
"Malkia wangu,Maya ameniagiza kwako anasema angependezwa leo kula chakula ambacho kimeandaliwa kwaajili yenu wazazi wake apate kuonja ladha hiyo."alisema Samir akiwa anamtazama Malkia Rayyat. Alishangaa kusikia hivyo akageuka kumtazama mumewe wakabaki kutazamana.
"Una uhakika na hicho unachokisema Samir.?"aliuliza Mfalme akiwa anamtazama Samir.
"Bila shaka, ni maneno ya binti yako Mfalme wangu na ndio kaniagiza nifikishe hili kwa mama yake."alisema Samir akionesha kweli anamaanisha. Malkia alianza kuamini kile asemacho Samir. Kwa kuona ni kwaajili ya afya ya mwanaye wacha atoe kile chakula. Aligawa nusu ya vyakula vilivyokuwepo pale mezani na kumruhusu Samir achukue umpelekea Maya. Haraka Samir alifanya zoezi hilo huku akiwaacha Mfalme na Malkia wamtazame tu. Muda ule chumbani Maya alivuta kitu na kukaa, akasogeza sahani na kupakuwa chakula anachotaka kula. Alipotaka kupeleka kijiko mdomoni aliona mlango ukifunguliwa na kumuona Samir akiwa ameshika vyakula. Ilimbidi abaki kushangaa tu na kuona Samir anasogea pale.
"Umeshakula hata kijiko kimoja?"aliuliza Samir akiwa anahema sana.
"Umenishtua maana ndio nilikuwa naanza kula Samir, haya mbona umekuja na vyakula hivi.?"aliuliza Maya akiwa haelewi. Bila kuchelewa alianza kutoa kile chakula cha mezani kilichoandaliwa ambacho ndio kiliwekewa ungaunga ule na Lutfiya. Alipomaliza akamuwekea mezani sasa chakula kile alichopewa na Malkia kisha akamtazama Maya.
"Nimeagizwa Malkia nikupatie chakula hichi ambacho amekichagua kwaajili ya mwanaye, hakika anakujali na kukupenda na amenisistiza ukipokee upate baraka zake."alisema Samir na kumfanya Maya atazame kile chakula, hakika kilikuwa kinavutia sana.
"Una uhakika kweli kama amekuagiza hivyo.?,"
"Bila shaka, nimeagizwa hivyo na Malkia Rayyat."alisema Samir na kumfanya Maya asipoteze muda alisogea vizuri na kuanza kula chakula kile.
"Haya ondoka na hicho chakula chengine sitaweza kula."alisema Maya akiwa anaendelea kula chakula kile akicholeta Samir.
Alikichukua na kuweka kwenye kitenga kisha akatoka nacho nje, hapo moyo wae ukawa umetuliana baada ya kuona ameokoa maisha ya Maya kwa mara nyengine, na muda ule alipotoka ndipo akapishana na Lutfiya njiani na wala hakutaka kumtazama maana alifahamu kuwa anakwenda kupata uhakika wa kazi aliyokuwa ameifanya.

Yote hayo alikuwa akikumbuka Samir muda ule aliokuwa amepewa bilauli lile kupeleka tena kwa Maya. Hata alipofika aliingia na kumpatia Maya kile kinywaji kisha naye akageuka kurudi zake kupumzika akiwa amenyamaza kusema lile swala la Lutfiya.
ITAENDELEA
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN.
MTUNZI:JAFARI MPOLE
SEHEMU YA 16

ILIPOISHIA
* Hata alipofika aliingia na kumpatia Maya kile kinywaji kisha naye akageuka kurudi zake kupumzika akiwa amenyamaza kusema lile swala la Lutfiya.*

TUENDELEE
Mwenyewe alikuwa alimtazama Samir muda wote na kufahamu swala lake halikuweza kufikishwa kwa Maya. Alishusha pumzi na kurudi zale kuendelea na kazi yake.
Baadae askari wa Eden walianza kutembea mji mzima wa Eden mitaani kuwatangazia wananchi kuweza kufika siku ya kesho kwaajili ya kutazama mapambano ambayo yanahusisha kumpata shababi wa kuweza kumlinda binti wa kifalme,Maya.
Watu walizidi kujitokeza kujiandikisha ili kujaribu bahati zao kama wataweza kuibuka kuwa washindi. Hadi kifika jioni hiyo uwanja maalumu ulioandaliwa kwa siku ya kesho. Mfalme Siddik alianza kuwaagiza baadhi ya askari wake kupeleka mualiko kwa baadhi ya Mataifa jirani ili kuweza kushuhudia mashindano hayo.

Huku kwa Jamal baada ya kuwa kujua kinachoendelea alikuwa amejiandaa kwaajili ya mpambano huo wq kesho Alipata chachu ya kuzidi kutamani ushindi kwasiku ya kesho mara baada ya kutambua ana watu wanaomuunga mkono yeye ili kuweza kumteka Maya kiakili. Wanajua fika wakilifanikisha hilo basi wanauwezo wa kufanya chochote ndani ya Eden kwa maana Maya ndiye mtoto pekee kwa Mflame Siddik na mkewe Malkia Rayat.
"Ushindi kesho lazima ili tufikie malengo yetu, nimetembea Eden kwenye mitaa na kuona jinsi baadhi ya watu wakijiandaa kwaajili ya kesho lini sijaona mtu wa kuweza kupambana nami. Nakuhakikishia baba hii nafasi tuliyokuwa tukiisubiri kwa muda mrefu naamini imewadia."alisema Jamal akiwa mwenye kujiamini. Baba yake alimtaza tu huku akitabasamu kwa furaha akiamini kile asema mwanaye. Alimtia moyo sana siku hiyo na baadae Jamal akiingia zake sehemu ya kufanyia mazoezi yake Alisogea mbele na kuvua nguo yake ya juu. Alionekana kutuna kifua huku mkono wake uliojazia ulimfanya ajiamini sana licha ya kuwa ni mtoto wa Mfalme. Alipiga hatua kadhaa na kutoa upanga mrefu uliokuwa pembeni umehifadhiwa kisha akaukamata kwa mikono miwili na kurudi nyuma hatua tatu. Alitoa heshima kwa kuinama chini kidogo kisha akaanza kuonesha ujuzi wake wa kutumia upanga kwa weledi mkubwa sana huku akionekana.kuwa mwepesi mwili wake. Hakika alikuwa fiti kwenye kupambana hali iliyomfanya baba yake aliyekuwa akichungulia nje atabasamu tu na kuona kweli amepata kidume.
Muda huohuo askari mmoja aliingia na kumfanya Mfalme atoke kule aliposimama akimtazama mwaaye akasogea alipo yule askari.
"Vipi kuna tatizo?"aliuliza Mfalme Faruk akiwa anamtazama askari yule.
"Hapana Mfalme,kuna askari wa Eden wamefika wapo nje wanashida na wewe, hivyo nimekuja kukupa taarifa hiyo kuwa wanahitaji kukuona."alisema yule askari.
"Umesema Askari wa Eden?"
"Ndio Mfalme wangu,"alisema yule askari na kumfya Mfalme huyo asitambue nini kilichowaeta askari hao. Alimpa amri yule askari akawakaribishe askari hao kisha naye akaelekea ukumbini kukaa akiwasubiri kujua wamekuja kwa dhumuni gani.
Dakika kadhaa waliingia askari wawili wa Eden na walipofika kwa Mfalme hiyo waliinamisha vichwa chini kumpa heahima yake kisha wakanyanyuka. Mfalme alijenga tabasamu usoni na kuwakaribisha wakae.
"Hapana sisi sio wakaaji Mfalme Faruk,tumekuja hapa kuleta ujumbe kutoka kwa Mfalme wetu Siddik."alisema askari mmoja na kutoa karatasi moja iliyokunjwa na kumpatia Mfalme huyo. Aliipokea huku akiwana shauku ya kujua kilichoandikwa.
"Inahusu nini lakini?"aliuliza Mfalme huyo akimtazama yule askari.
"Siku ya kesho kutakuwa na mapambano ya kumtafuta shababi wakuweza kua mlinzi wa binti wa Mfalme katika kiwanja kikubwa cha Eden hivyo kwa heshima yako Mfalme Siddik anakuomba uhudhurie siku hiyo ili kuonesha ujirani wa mataifa haya mawili. Hivyo anakuomba sana ufike siku ya kesho."alisema yule askari na kumfanya Mflame yule aelewe kilichodhamiriwa mule kwenye ile karatasi. Hakuona haja ya kuendelea kuifungua.
"Sawa hakuna tatizo, mwambieni tutakuwa pamoja."alisema Mfalme Faruk na kuwafanya wale askai waombe ruhusa ya kurejea Eden muda huo. Mfalme aliwaruhusu naye akarudi kuelekea kwa Jamal aliyekuwa anaendelea na mazoezi yake jioni ile. Alipomuona baba yake ameingia mule ilibidi asimamishe zoezi lake.
"Kuna taarifa nimepokea hapa kutoka Eden."
"Eden? Taarifa inahusu nini?"aliuliza Jamal akiwa ameshikilia upanga wake huku mwili wake ukitiririka jasho.
"Mfalme Siddik amenialika kwenye mashindano hayo hivyo nami nitakuwa miongoni mwa watu watakaotazama kinachoendelea kwenye kiwanja vile."alisema Mfalme na taarifa zile zilimfurahisha mwanaye na kujikuta wote wakifurahi baada ya kuona wanapata nafasi zaidi.

Usiku huo kwa Mfalme Siddik aliuuyumia kuelekea kwa binti yake kumuangalia. Alimkuta Maya akiwa anasoma vitabu mule ndani, akigonga mlango na taratibu akaanza kusogea hadi pale alipo binti yake aliyeonekana kuwa makini na kusoma. Alitazama kitabu kile kichokuandikwa EDEN YA MFALME SALEH. Alijikuta akitabasamu tu Mfalme baada ya kutambua mwanaye anamsoma aliyekuwa Mfalme wa Eden miaka ya nyuma.
"Unajua Eden ni Taifa ambalo tangu hapo awali lilikuwa na historia ya kipekee. Viongozi wake walikuwa mashuhuri sana na wenye nguvu huku wakiheshimika kila kona na kila Taifa ambalo lilikuwa na askari wake. Majeshi ya Eden yalikuwa yalikuwa imara sana na kuogopwa na kila Taifa ndio maana vita zao zilikuwa dhidi ya mataifa yenye kuongozwa na viongozi wenye kutumia nguvu za kichawi kwa maana tangu enzi hizo Mfalme wa kwanza wa Eden ambaye ni Saleh alikuwa na nguvu kubwa sana za ajabu hivyo aliweza kuwadhibiti wabaya wake."alisema Mfalme Siddik na kumfanya Maya amtazame.
" Inamaana hata Mfalme Saleh alikuwani mchawi.?"aliuliza Maya.
"Bila shaka, alikuwa ni zaidi ya wengine na uchawi wake haukuwa kama wa wengine. Aliutumia kuwasaidia wananchi wake katika shida na hata vita."
"Sasa kwanini unakataza uchawi Eden baba wakati hata Mfalme mwenzako alikuwa hivyo!."
"Binti yangu Maya, muda na zama zinabadilika. Uchawi wa Mfalme Saleh haukuwa wa kudhuru tofauti sasa, kila mtu anatumia uchawi kumdhuru au kumkonesha mwenzake. Na ndio maana nilipoliona nikaweka amri ya kuuawa wachawi wote bora tuishi kawaida tu. Tazama hata wewe walivyokufanya, ulifanya kosa gani sasa binti yangu!, ni chuki tu za watu na ndio maana sitaki kusikia uchawi tena hapa Eden."alisema Mfalme na maelezo yake yakamuingia mwanaye. Alikitazama kile kitabu na kupata swala la kumuuliza baba yake.
"Huyu Mfalme Saleh alitokea Bara gani.?"
"Mfalme huyu alikuwa mzawa hapa Eden na Mkewe Zainab alikuwa pia mtu wa Eden na katika mwisho wa maisha yao waliacha vitu vingi ili wafalme wajao waweze kifuata. Kitu pekee ambacho kilikuwa cha tofauti ni pale ambapo ilipatwa kuachwa alama ya kiganja cha mkono iwe kama nembo na ishara ya Mfalme atakayekuja kuitawala Eden na ilisadikika alitokea Bara la Afrika.
Hivyo wafalme wote walioweza kuitawala Eden walijua ipo siku Eden itakuja kutawaliwa na mfalme wa aina hiyo."alisema Mfalme Siddik akiwa anamueleza mambi binti yake.
"Ahaaa ndio maana nimesoma kurasa nyingi humu nimeona likitajwa hili Bara la Afrika ambalo ametokea Mfalme huyu anayeitwa Saleh. Kumbehiki kitabu ni cha Mfalme Saleh aliyetokea Bara la Afrika."
"Ndio, hiki kitabu kinamuhusu yeye. Aliweza kuibadilisha Eden kutoka kwenye ubaguaji wa rangi za watu hadi leo hii tunaishi na watu weusi kama ndugu na wengi wamezaliana ndani ya Eden, tupo nao siku zote."alisema Mfalme Siddik na kumfanya Maya atambue historia fupi ya Mfalme Saleh.
"Kwahiyo hata hawa wakina Samir wametokana na huyu Mfalme Saleh?"
"Sio Samir tu wengi unaoona na ngozi nyeusi wametokana na uzao huo wa Mfalme Saleh."alisema Mfalme na kuzidi kunuelewesha binti yake ambaye hakuona umuhimu wakuendelea kusoma kitabu tena,akawa anasimuliwa mambo mengi sana baba yake.
Taratibu akaanza kuona jinsi watu weusi walivyo na upendo kwa watu na umuhimu pia katika maisha ya wengine.
Mwishowe Mfalme aligusia swala la kesho na kumtaka Maya aweze kua na furaha ya swa hilo maana myu anayetafutwa ni kwaajili yake ili aweze kumlinda katika maisha yake. Alimuelewa baba yake na kukubaliana naye kwa jambo hilo ambalo awali hakupendezwa nalo lakini mwisho wa siku aliona muhimu kwake kuweza kuangaliwa kama binti wa kifalme. Baada ya muda waliagana mtu na mwanaye kisha Mfalme akatoka zake na kuelekea kulala na mkewe. Maya alikitazama kile kitabu na kubaki kutabasamu. Alifurahishwa na jinsi Mfalme huyo alivyoleta mabadiliko katika taifa hilo la Eden na kuona ni mfano wa kuigwa. Alisogea nacho kile kitabu hadi kitandani akapanda na kujilaza, alifungua kurasa kadhaa akaendelea kukisoma huku usingizi ukimnyemelea na muda mfupi akapitiwa na usingizi huku kitabu kile kikiwa kifuani mwake.

Alionekana msichana mmoja akiwa hoi amepiga magoti chini ya ardhi huku sura yake iliyozibwa na nywele zake ikiangalia chini kufanya asiweze kuonekana vizuri,mikono yake ikiwa imefungwa minyororo huku pembeni akionekana mtu mmoja aliyekuwa amejifunika sura yake akiwa nyuma ya msichana huyo akiwa ameshika upanga wenye kun'gaa. Kwa mbali alionekana kijana mmoja akiwa anakuja eneo lile akiwa anachechemea huku mkono wake wa kulia uliokuwa umeshika upanga ukiwa unavuja damu. Alikuwa akihema sana kuonesha ametoka kupambana na watu wengi sana.
Alipofika pale alipata kuona yule mtu akipeleka upanga ule shingoni kwa yule msichana pale chini huku akitabasamu.
"Ukitaka kumsaidia huyu pambana na mimi, ukinishinda atakuwa huru umemsaidia. Na endapo nikakushinda au ukakataa kupambana nami basi kichwa cha mtu wako huyu nitakifyeka kwa upanga huu kama hivi..."alisema yule mtu kunyanyua upanga wake juu, yule msichana taratibu akaanza kunyanyua sura yake kumtazama yule kijana alikekuwa mbele yake akionekana kuvuja damu mkononi akiwa hoi. Kijana yule alipomtazama vizuri yule msichana alishtuka baada ya kuifahamu sura ile na muda huohuo alishuhudia upanga wa yule mtu ukipita shingoni mwa yule msichana kama fyekeo na kukata kichwa. Yule kijana alishangaa kuona tukio lile huku akishikwa na bumbuwazi, hasira zilimpanda na kujikuta akipiga kelele kwa nguvu...
"HAPANAAAAAA....."

"HAPANAAAAAA......."akishutuka kutoka kitandani baada ya kusema maneno hayo. Alitazama huku na kule na kuona kiza tu kikitawala mule ndani. Alinyanyuka na kuwasha chemli kwanza kisha akarejea pale kitandani huku akishusha pumzi kwa nguvu. Alikuwa ni Samir muda wote huo alikuwa akiota ndoto hiyo ambayo alijiona dhahiri ni yeye ndiye aliyekuwa akivuja damu mkononi huku akishuhudia msichana yule akikatwa kichwa na mtu ambaye hakuweza kumtambua kutokana na kuificha sura yake. Aliikumbuka ile sura ya yule mwanamke na kubaki kushika mdomo huku akiwa na hofu haamini kile alichokiona ndotoni.
"Hii ni ndoto gani jamani naota?. ndoto ya kutisha...Mmmh hapana.. Huwezi kufa vile Maya angali mimi nipi.. hii ni ndoto tu wala haina ukweli wowote."alisema Samir akijituliza moyo wake baada ya ile ndoto kutokea. Alipuuza na kuona haina ukweli wowote,alizima chemli ile na kujilaza kitandani japo hakuweza kuupata usingizi mapema akiifikiria ile ndoto..

NI NDOTO KWELI AMA?AISEE USIKOSE SEHEMU IJAYO.
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME.WA EDEN
MTUNZI:JAFARI MPOLE
SEHEMU YA 18

ILIPOISHIA
* Bila kupoteza muda washiriki wote walirudishwa ndani na kuchaguliwa watu nane wakaingia uwanjani na kila mmoja akapewa mtu wa kupambana naye, mapambano yakaanza.*

TUENDELEE
Ilikuwa ni kama uwanja wa vita muda ule kila mtu alionekana kuchafukwa na roho kuhakikisha anakuwa mshindi kwa mpinzani wake. Pindi ukizembea unauliwa mara moja maana kila mtu alikuwa na silaha yake kali lengo ni kumdhuru mpinzani wake ili yeye apate kuwa mshindi. Watu walishangilia sana kufanya mapambano hayo yaonekane yenye shamrashamra kubwa sana.
Mfalme pamoja na meza yote ya waalikwa walikuwa makini kuangalia kile kinachoendelea. Maya alibaki kushangaa kuona jinsi watu wanavyotoana roho kwaajili yake. Tangu awali hakupendezwa na kitu hicho lakini ilibidi akubaliane na baba yake ili apate ulinzi katika maisha yale.
Wapambanaji wengine walikuwa ndani ya jengo moja wakichungulia tu jinsi wenzao wanavyopigania nafasi ile. Ndani ya uwanja kila mtu alionesha umahiri wake na mwisho wa pambano waliweza kushinda watu wanne na wengine wakiwa chini wamejeruhiwa vibaya sana huku mmoja akipoteza maisha wakatolewa. Walitangazwa wale washindi na kumfanya Mfalme na watu wengine wanyanyuke kuwapigia makofi kwa kuwapongeza kwa kile walichokifanya.
Walitoka kwenda kupumzika wasubiri kitakachoendelea.
Baada ya dakika kadhaa walitajwa tena watu nane wakaingia uwanjani na pambano likaendelea kama kawaida.

Huku Dalfa na watu wake walifika pale uwanjani na kuingia mule wakioata kuona umati wa watu wakiwa wanatazama mapambano yale.Nao bila kujiuliza wajipanda kwenye majukwaa na kutafuta sehemu wakakaa kutazama kinachoendelea. Dalfa alitazama kule kwenye jukwaa la wakubwa na kuweza kumuona Mfalme Siddik akiwa mwenye furaha kuangalia mapambo yale. Alimuona Malkia Rayat akiwa pembeni na binti yake wakiwa wapo makini kutazama kinachoendelea. Hapo ndipo akapata kuamini kweli binti wa Mfalme ameweza kupona na jambo la msingi ni kumpata yule mtu aliyemponesha binti huyo. Aliangalia tu mapambano yale yanayoendelea pale kiwanjani.

Hakukuwa na huruma baina ya mtu na mtu ndani ya uwanja. Kila mtu alikuwa akijitetea upande wake. Damu zilimwagika,panga zilisikika zikipigana vikumbo hali iliyomfanya Samir kule ndani alipo na wenzake aone kwamba kuna kazi ya kutetea uhai wake pindi aingiapo kwenye uwanja ule. Alitazama juu ya jukwaa walipo Mfalme na watu wakubwa na kuona sura ya Maya akiwa anaangalia huku akionesha kuwana woga. Hapo ndipo akakumbuka ile ndoto ya jana usiku na muda huohuo akageuka kumtafuta yule mtu ambaye alimuona akiwa amejifunika uso. Aliangalia huku na kule na kuweza kumuona mtu yule akiwa amekaa chini akiwa amekunja miguu yake kama yupo kwenye maombi huku panga lake likiwa mbele yake. Samir alilitazama lile panga na kulikumbuka panga lile ambalo yule muuaji wa ndotoni alilitumia kumkata kichwa Maya. Alishtuka sana baada ya kutambua hilo na kuona huyu mtu huenda ndiye yule ambaye alimuona ndotoni na huenda jambo hilo likatokea hapo mbeleni. Ilibidi awe naye makini sana muda wote ili maisha ya Maya yasije kukatishwa kama alivyoona kwenye ndoto.
Watu uwanjani walizidi kupungua tu kila kundi la watu nane wakiingia baso wanne wanaibuka washindi kuendelea na hatua nyengine. Kundi la mwisho liliingia uwanjani na watu wengi wakawa wanamtazama Samir aliyeonekana kuingilia mambo ambayo hana hobi nayo. Jamal alikuwa miongoni mwao na kuweza kupangiwa mtu wa kupambana naye. Samir alikabidhiwa mtu mrefu mwenye mwili mkubwa sana uliojazia aliyeonekana kuwa na rungu kubwa lenye uzito huku mkono mwengine akiwa ameshika mnyororo. Maya akabaki tu kushika mdomo.
"Jamani mbona wamempa jitu lenye nguvu kiasi kile apambane naye?"aliongea Maya akionesha kuwa na hofu sana.
"Haijalishi awe vipi kama amekubali kushiriki kwenye mashindano haya basi amejiamini, ngoja tusubiri atamuepuka vipi."alisema Malkia Rayat na kugeuka kutazama uwanjani. Mfalme alibaki kusikitika tu baada ya kuona dhahiri kijana wake anaelekea kupambana na mtu mwenye nguvu zake.
Pambano likanza na kila mtu akawa anapambana na mtu wake aliyepangiwa. Samir aliutoa upanga wake na kukaa makini sana kumtazama adui yake ambaye alionekana kutokuwa na wasiwasi. Alimtazama Samir na kubaki kucheka tu maana ni mdogo sana lakini hakuwa na huruma maana lazima apatikane mshindi. Alianza kuuzungusha mnyororo wake kumchapa nao Samir ambaye alionekana kuuwa na wepesi wa kukwepa na kuwafanya kidogo watu wawe na tumaini naye kidogo.
Huku Dalfa baada ya kumuona Samir pale uwanjani akipambana aliweza kumtambua kwa sura na kujua ndiye yule mtu ambaye aliweza kumsaidia Maya siku ile hivyo lazima atakuwa na uwezo kama wake. Alibaki kuangalia pambano lile akiwa makini kumuangalia Samir kama atatumia zile nguvu.
Jamal alionekana kuwa makini na mwepesi kwa adui yake na sekunde kadhaa tu akaweza kumbana adui yake na kumchana kwa upanga mgongoni akaenda chini. Watu walimshangilia sana kwa kumaliza pambano lake mapema sana kuliko wenzake. Mfalme Faruk alibaki kutabasamu tu baada ya kuona mwanaye akionesha umahiri wake hadi kuweza kuibuka mshindi kwenye pambano lake la kwanza.
Baada ya muda na wengine wakaweza kufanikisha zoezi hilo na kufanya uwanja mzima abaki yule mtu baunsa pamoja na Samir ambaye alionekana kuzuia sana mashambulizi ya mpinzani wake akizidi kumtia maudhi kuona kijana mdogo anamsumbua mpaka dakika ile.
Hata jukwaa walipo Wafalme walishangaa kuona Samir analeta upinzani mkubwa kwa mtu yule jamba ambalo hawakutegemea ikabidi watu wa Eden waanze kumsapoti mtu wao Samir wakilitaja jina lake kama kumpa mori hadi mwenyewe akashangaa kuona anapewa hamasa ya kushinda.
Yule mtu aliposikia vile aliona kumbe anayepambana naye anajulikana Eden, alizidi kupata hasira kutaka kummaliza kabisa Samir ili awanyamazishe midomo watu wote. Alinyanyua rungu lake kwa nguvu zote na kurusha kwa Samir ambaye kwa wepesi wa hali ya juu akalikwepa. Alishangaa kuona yule mtu anakuja mzimamzima ili ampige kikumbo Samir, kwa weledi wa hali ya juu alipiga msamba kwa chini na kuachia ngumi nzito sehemu za siri za yule mtu ambaye alionekana akienda chini mzimamzima kwa kipigo kile na ukawa ni ushindi kwa Samir. Watu wote walishangaa hawakuamini huku wengine wakimshangilia kwakile alichokifanya.
Maya hakuamini kuona vile akabaki kutabasamu tu na kupiga makofi na mama yake aliyekuwa pembeni yake.
Mfalme alifurahi sana na kubaki kupiga makofi tu kuona kijana wake wa Eden amepata ushindi
"Nilisema mimi huyu kijana anajiamini sana."alisema Mfalme Faruk akimtazama Mfalme Siddik akionesha kutamasamu tu bila kusema lolote. Samir alitoka pale uwanjani na wengine walioshinda akiwemo Jamal na kurudi kupumzika na awamu hiyo ya kwanza ikamalizika na kuwapata washiriki 24 waliobaki huku 24 wengine wakiwa wameshindwa na baadhi yao kupoteza maisha kabisa.
Watu walipumzika robo saa tu na wale washiriki wa awali wakaingia nane na kila mmoja akapangwa na mtu wa kupambana naye na zoezi likaanza.
Ilikuwa ni zaidi ya mpambano kila mmoja alikuwa akijitahidi apate nafasi ya kwenda mbele zaidi. Hata wale baadhi ya askari wa kifalme walioshiriki kwenye mapambano hayo walikuwa makini sana lengo ni kuipata ile nafasi moja ya mshindi. Na katika pambano hilo waliibuka washindi wanne huku majonzi yakiwa kwa Eden kwa kuweza kuwapoteza askari wawili kwenye mpambano huo na kubaki askari wanne wa Eden pamoja na mfanyakazi mmoja wa Samir. Washindi walitoka na kwenda kupumzika huku wale walioshindwa na kupoteza maisha wakitolewa kwenyw uwanja kurusu kundi lengine liingie na mpambano ukaendelea kama kawaida.
Shangwe zilisikika kwa raia waliokuwa wakiangalia mapambano hayo wakiwapa moyo askari watatu waliokuwa katika kundi lile. Walikuwa na uchungu sana baada ya wenzao wawili kuwapoteza hivyo walipambana kishujaa kama askari kuhakikisha wanatetea nafasi zao. Na kweli katika kundi hilo askari wote watatu waliweza kushinda pamoja na mtu mwengine na kuwafanya watu wa Eden wafurahi sana.
Kundi la mwisho likawa ni la akina Jamal, Samir na watu wengine ambao miili yao ilionekana imeimarika kimazoezi huku wakiwa na mapanga marefu na makali sana. Kila mtu alipangiwa wakwake na kwa mara nyengine Samir anapangwa na mtu alionekana kuwa na nguvu na mwili uliojengeka kikamilifu. Hakuwa na jinsi ilibidi akubali kukabiana nalo na mpambano ukaendelea. Jamal alikuwa akipambana kwa staili ya aina yake, hakika alionesha kuwa yeye ni hodari wa kutumia upanga wake. Kama ilivyo kawaida yake dakika kadhaa tu aliweza kumzidi ujanja mpinzani wake na kukata viungio vya miguu na kumfanya mpinzani wake asiweze kusimama kabisa. Watu walimshangilia sana kwa kujua uwezo wake wa kupambana, Lutfiya kule alipo jukwaani alibaki kutabasamu tu na kuona mtoto wa Mfalme wa taifa lao anazidi kupata ushindi. Kwa Samir naye alijitahidi safari hii baada ya kuzoea kupambana, akifikiria likuwa yote anafanya kwaajili ya Maya asiweze kufa basi anapata ujasiri zaidi wa kuendelea.
Lakini kwa Dalfa alibaki kushangaa kuona mtu yule tangu anapambana mwanzo hadi pambano hili la pili hakutumia hata zile nguvu ambazo anafikiri anazo. Hakumuelewa mpaka dakika ile na kuzidi kumchunguza zaidi akiamini ataujua tu ukweli.
Huku kwa wengine wakiwepo askari wa kifalme wawili walipambana kwa juhudi zao lakini mmoja wao akazidiwa maarifa na kujikita akidhibitiwa baada ya kukatwa na upanga tumboni huku mwenzake aliyebaki akipata ushindi.
Samir alizidi kukaza msuri na kwa bahati akapata nafasi ya kupenyeza upanga wake tumboni kwa mpinzani wake aliyekwenda chini na kupoteza maisha papohapo. Watu wa Eden walishangilia sana kuona watu wao wawili katika kundi hili pia wameondoka na ushindi. Taratibu Malkia pamoja na Maya wakaanza kumuwekea imani Samir aweze kufika mbali. Mfalme alipiga sana makofi kuwapongeza washindi wote waliofika hatua hiyo wakiwa wamebaki 12 huku Eden ikiwakilishwa na askari wanne pamoja na Samir wakiwa washiriki wote wamesimama msitari mmoja wakipongezwa kwakufika hatua ile. Samir aligeuka.kuwatazama wenzake waliofika hatua ile, lakini alishangaa kuona yule mtu anayejifunika sura yake tangu mwanzo kabla ya mpambano hakuweza kumuona mpaka muda huo. Alivuta kumbukumbu kuangalia wale watu walioshindwa kuendelea na mashindano hayo kama alikuwepo lakini akili yake inakataa, akabaki kutafakari mtu yule ameenda wapi.
NINI KITAENDELEA, MTU YULE AMEENDA WAPI, NANI ATAIBUKA MSHINDI WA MASHINDANO HAYO.
USIKOSE SEHEMU IJAYO.
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN
MTUNZI:JAFARI MPOLE
SEHEMU YA 19

ILIPOISHIA
* Alivuta kumbukumbu kuangalia wale watu walioshindwa kuendelea na mashindano hayo kama alikuwepo lakini akili yake inakataa, akabaki kutafakari mtu yule ameenda wapi.*

TUENDELEE
Walipewa muda wa kupumzika na kuwaacha watu wakiwa wanahamu kubwa ya kujua ni nani na nani wataweza kufika hatua za mbele zaidi. Washiriki wale 12 walirudi sehemu ya kupumzika na kusubiri baada ya muda waweze kuitwa tena. Wale askari wa Eden walisimama pamoja wakawa wanaongea kama watu wa karibu bila yeyote kujua atapangiwa na nani wa kupambana naye. Samir alikaa sehemu yake akijipumzisha huku akiwa ameshika upanga wake ule. Alitoa kitambaa na kuanza kyfuta damu zilizogandia kwenye upanga ule huku akiwaangalia wale askari wakiwa wameweka kikundi chao wakiendelea kuongea.
Alitazama pembeni na kumuona Jamal akiwa amekunja miguu kama anafanya maombi huku panga lake likiwa mbele yake. Tukio lile lilimfanya Samir amkumbuke yule mtu aliejifunga sura yake isionekane na ghafla hakuweza kumuona tena. Alikaa na kuweka upanga wake kama anavyomuona huyu wa sasa. Alipolitazama lile panga kwa umanikini hapo ndipo akajiridhisha baada ya kutambua ndio huyuhuyu ambaye mwanzo aliweza kumuona pindi akiwa ameificha sura yake. Alijiuliza moyoni kuona imekuwaje sura yake ameificha mara moja tu na pindi alipoingia kwenye mapambano hakuweza kuificha sura yake. Hakuweza kupata jibu kamili juu ya swala hilo lakini alitambua tu kuwa mtu ambaye alimuota kwenye ndoto ndio yule anayemuona pale mbele. Alibaki kumtazama vizuri Jamal aliyeonekana kuwa makini muda wote akiwa si mwenye sura ya kucheka.

Huku uwanjani watu walikuwa wakisubiri kwa hamu muda ufike mapambano yaendelee. Kila mtu alikuwa na shauku ya kujua nani ataibuka kuwa mshindi siku hiyo. Kila mtu alimtabiria mtu ambaye anaona ndio ataibuka kuwa mshindi na kuweza kupewa nafasi ya kumlinda binti wa kifalme. Muda ulizidi kwenda na baadae waliitwa majina washiriki waingie uwanjani.
Waliingia askari wa Eden watatu pamoja na wanaume wengine kukamilisha idadi hiyo ya washiriki sita.
Kila mmoja alipangwa mtu wa kupambana naye, na safari hii askari wawili wa mfalme Siddik waliweza kukutana na kupangiwa kupambana. Waliweka uaskari wao pembeni kila mmoja akipigania nafasi ya kuendelea mbele. Mpambano ulianza huku Mfalme mwenyewe akiwa mwenye hofu kubwa hasa vijana wake hao ambao mmoja wao lazima ashindwe. Watu walishangilia kuwapa hamasa washiriki huku Dalfa akiwa anatazama tu kinachoendelea, lengo lake likiwa kwa Samir na alisubiri muda tu Samir atumie zile nguvu aweze kufanya kitu.
Samir na baadhi ya wenzake mule ndani wakawa wanachungulia tu kuona wenzao wanavyopimana ubavu. Aligeuka kumtazama yule mtu na kumuona bado amekaa hana hata habari kama kuna kinachoendelea.
"Huyu mtu mbona anajiamini sana hivi?"alijisemea moyoni Samir akiwa anamtazama Jamal aliyeonekana kukaa pale chini huku wenzake wakichungulia mapambano yanavyoendelea.

Hakika hakuna aliyetaka kuzidiwa ndani ya uwanja. Kila mtu alionesha umahiri wake na kufanya meza kuu ya wageni waalikwa pamoja na wafalme wapate hamasa ya kuzidi kuangalia kinachoendelea. Miongoni mwa wale askari waliokuwa wakipambana aliweza kumzidi ujanja adui yake baada ya kupitisha shingoni panga na adui yake akaweza kwenda chini na kupoteza maisha papohapo. Samir kuona vile akabaki kufumba macho na kuamua kutoka pale waliposimama asiendelee tena kuangalia, alitafuta sehemu kutulia akisikiliza kelele za mashabiki wakiwashangilia watu ndani ya uwanja. Wale washiriki wengine kila mmoja alikuwa imara katika kutumia silaha ya upanga, jambo ambalo lilikuwa gumu kutabiri nani ataibuka kuwa mshindi. Katika harakati za kupambana walijikuta wakiwahiana na kila mmoja akapeleka upanga tumboni kwa mwenzake hali iliyowafanya watu wote washangae tukio lile walishuhudia wote wakienda chini na kupoteza maisha. Tukio hilo liliendana na tukio la wapiganaji wengine ambao na kwa staili tofauti walirushiana visu vifuani na kusababisha asipatikane mshindi baina yao. Uwanja mzima akawa amebaki yule askari wa kifalme aliyeweza kushinda peke yake na wenzake kupoteza nafasi ya kuendelea. Haikuwa na jinsi watu walimshangilia sana kuona anaitetea Eden vyema na baada ya kupokea sifa hizo hata kwa Mfalme akatoka mule uwanjani kwenda kupumzika.
Liliingia kundi la mwisho na kila mmoja akakabidhiwa mtu wa kupambana naye. Maya alipata kustaajabu pale alipomuona Samir amekabidhiwa askari mmoja wa Eden apambane naye. Hawakuwa na ujanja ilibidi wafanye kama ilivyopangwa huku naye Jamal akipewa askari mmoja apambane naye.
Watu wengi sana walianza kumuwekea tumaini Jamal kwa vile anavyopambana kuonesha umahiri wake. Hali ile ilimpelekea kupata mashabiki wengi wanao muunga mkono hali iliyomfanya Mfalme Faruk atabasamu kuona mwanaye ameweza kukonga nyoyo za watu. Mfalme akawa na hofu juu ya kumpoteza askari wake mwengine maana anapambana na mtu mwenye uwezo mkubwa sana huku upande mwengine akiona Samir akipewa nafasi ya kupambana na askari huyo mmoja wa Eden. Hata mapambano yalipoanza kila mtu alikuwa amemuwekea tumaini mtu wake ambaye anahisi atakuja kuibuka kuwa mshindi. Kila mtu alikuwa makini kupambana na mwenzake huku Samir akiwa anamkwepa tu yule askari.
"Sisi sote ni watu wa Eden na ukiona umeshindwa pambano unadondoka chini ili mwenzio asipate kukuumiza."alisema Samir akiwa anamtazama yule askari aliyekuwa akipambana naye.
"Huu ni mchezo wa kufa au kupona, ulikubali kuingia humu uwanjani na ukakubaliana na kila hali italayotokea humu.Fanya kilichokuleta."alisema yule askari na kuupeleka upanga wake akitaka kumkata lakini alilizuia Samir kwa uhodari.
"Fikiria kuhusu wewe pia nitakapo kudhuru na una nafasi katika falme kama askari wa Eden, hebu fikiria hilo."alisema Samir akimsihi yule askari wapambane kawaida na mmoja wapo akizidiwa asidhurike.
"Unaongea ujinga gani Samir... unadhani nikipata nafasi ya kuwa mlinzi wa Mfalme nitaendelea kuwa askari pia. Nitakuwa zaidi ya askari na ndio lengo langu hilo."alisema yule askari na kuendelea kumuandama Samir aliyeonekana kuzuia tu. Alimtazama Jamal pembeni na kuweza kumuona akiwa amemzidi mpinzani wake aliyeonekana kuwa hoi mapema.

Hali ile Mfalme Siddik aliiona na kujua kuna uwezekano mkubwa wa kumpoteza askari wake. Aligeuka kumtazama Mfalme Faruk ambaye alionekana kutabasamu kuona jinsi mwanaye anavyowadhibiti wenzake. Haikupita dakika mbili Jamal alimpindua yule askari akadondoka chini, alipotaka kifurukuta kujitetea yule askari alishuhudia kuona upanga ukipiga begani ukachana. Alipiga ukelele wa maumivu na kumfanya Jamal aachane naye baada ya kuona amemzidi na kupata ushindi kwa mara nyengine tena.
Watu waliokuwa upande wake wakaanza kumshagilia kwa kelele huku baadhi ya wengine hawakupenda kuona watu wao wa Eden wanapigwa vile. Waligeuza macho yao kwa wengine na kuona hata yule askari aliyebaki akizidi kutetea nafasi yake. Alipambana kadri ya uwezo wake japo alikutana na mtu mwenye uwezo mkubwa sana na mwenye mwili. Aliutumia upanga wake vyema na mwisho akafanikiwa kummaliza yule askari wa kifalme pale na kumfanya Mfalme azidi kupata machungu. Malkia alibaki kusikitika tu pale kuona vijana wa taifa lao wanaisha na wamebaki uwanjani Samir na yule askari mbishi.
Hakuutaka kusikia lolote kwa kile anachoelezwa na Samir ambaye mara kadhaa amekuwa akimtazama Mfalme akiwa anawaagalia. Alishuhudia akipigwa ngumi mzito na kwenda chini na hapo ndipo akapata kusikia watu wakimshangilia yule askari ambaye alizidi kufurahi na kujitapa uwanjani pale akitaka kumaliza kazi. Aligeuka kumtazama Samir pale chini akiwa anatokwa na damu mdomoni baada ya konde lile la shavuni. Alifikiria kile alichoambiwa kuhusu kuipoteza nafasi ile atampoteza Maya hapo akapata hata nguvu ya kusimama na kuwafanya watu wapunguze kelele zile kuona Samir ameamka.
"Nimekwambia toka awali hunisikii basi wacha tugombanie hii nafasi vizuri."alisema Samir na bila woga akamsogelea yule mtu palepale aliposimama. Alicheka sana kwadharau na kutaka kunyang'anyia panga lake Samir akalia kwa kulipiga teke likadondokea pembeni. Wakabaki wakiangaliana tu kwa macho yenye chuki ndani yake huku Samir akiwa amekata ule upanga wake.Hapo Dalfa akawa makini kutazama kuona kama mtu huyo anaweza akafanya lolote kwa yule askari.
"Samir kuwa makini kuna mtu anaitwa Dalfa anakufuatilia. Usioneshe kitu chochote hapo atakujua kuwa wewe ni nani."ilisikika sauti kwenye ngoma za masikio ya Samir na akapata kujua ni Nadhra ndiye aliyeongea vile.

Ilimbidi yule askari atumie ngumi sasa kumdhibiti Samir lakini haikusaida, bila huruma Samir akamchanachana tumboni na upanga ule kwa haraka sana hadi watu wakashangaa kumuona Samir akiwa mwepesi wa hali ya juu. Alishuhudia yule askari akidondoka chini palepale kupoteza maisha na ushindi ukaenda kwa Samir. Watu wengi hawakuamini kuona askari wa Mfalme ameuliwa na mfanyakazi Samir. Maya alistaajabu kuona vile na kubaki kuduwaa tu haamini.
"Kumbe Samir anajua kupambana kiasi hiki. Hadi sasa ameshinda tena anazidi kwenda mbele."alisema Maya nakumfanya hata Malkia abaki kumshangaa tu Samir na kufanya waonekane washindi watatu waliobaki kwenye uwanja.
Mfalme alinyanyuka kuwapigia makofi akafuatiwa na Mfalme Faruk akionesha kufurahi sana, furaha yake ilikuwa kwa mwanaye kuona hadi muda huo amekuwa akishinda mapambano yote aliyopangiwa.
Watu waliwapongeza kwa hatua hiyo waliyofikia. Aliitwa yule askari wa Eden pekee aliyeshinda na kuungana na wenzake watatu waliobaki na kuikamilisha idadi hiyo ya watu wanne Jamal, Samir, askari huyo pamoja na mwanaume mmoja aliyejazia mwili wake.
Mfalme alisimama tena na kuwatazama wale washiriki waliobakii huku akiwa mwenye tabasamu.
"Japo siamini ila utabaki kuwa hivyo tu kuwa mmejitahidi sana wanne nyie mliobaki hadi sasa. Watu 44 wameshindwa kufika hapa mlipo kwasasa ni wazi kwamba nyinyi ni zaidi.
Na sitaki kuwaacha hivihivi japo mmoja wenu atatakiwa kuwa Mlinzi wa binti yangu lakini natoa ofa moja ya kujiunga na jeshi la kifalme. Nadhani kati yenu kuna askari wangu mmoja hapo hivyo basi kama ataibuka mshindi ni yeye basi atakuwa akimlinda mwanangu na siku zote atabaki kuwa na heshima, ila kama hatafanikiwa basii ataendelea na kazi yake. Na kwa hawa wengine natangaza mbele ya watu mshindi wa pili ataingia kwenye jeshi la kifalme kama muongozaji wa majeshi popote pale inapotolewa oda. Hivyo kati yenu watu wanne wawili ndio watapata bahati hiyo. Mmoja anakuwa askari wa majeshi yangu na mwengine anakuwa mlinzi wa binti yangu. Nadhani nimeeleweka na niwatakie ushindi kwa kila mmoja wenu."alisema Mfalme na kuwafanya watu wampigie makofi kwa kile alichosema na kuona ametoa nafasi nzuri kwa watu hao. Kila mmoja wapo baada ya kusikia vile akatamani kuwa mmoja kati ya ambao watafanikiwa kupata nafasi hiyo. Samir alibaki kumeza mate tu na kuona ndio wanaelekea tamati kujua nani ataibuka kuwa mshindi. Aligeuka kumtazama Jamal na safari hii alipata kugongana macho na Jamal aliyeachia tabasamu baada ya kumuona Samir.
NANI MLINZI WA MAYA? NANI ASKARI WA MAJESHI? USIKOSE SEHEMU IJAYO.
 
Back
Top Bottom