SIMULIZI: Pete ya Mfalme wa Eden

SIMULIZI: Pete ya Mfalme wa Eden

SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN 35

Faraj aliipiga fimbo yake chini kwa nguvu na kupata kuonekana moto ukitanda kama mpaka ili kuwazuia askari wale wasipite. Askari wote walishangaa kuona moto ule uliowafanya farasi wao wafurukute kurudi nyuma kuhofia kuungua. Rahim alibaki kushangaa pale alipo haelewi imekuwaje.

"Anatumia nguvu za kichawi!"alistaajabu Rahim baada ya kutambua mtoto yule anatumia nguvu za kichawi. Alihamaki kuona moto ule ukianza kutanda kuwazunguka na kujikuta wamewekwa kati na moto ule na kubaki kuhaha. Faraj aliwatazama tu na kuona jinsi ambavyo hawaamini kile wanachokiona. Hasira zilimpanda Rahim kuona vijana wake wanaanza kuingiwa na woga,ilimbidi awape amri ya kusonga mbele zaidi na askari wale wakapata morali wa pita kwenda mbele.

Waliwaamu farasi wao wasöge mbele kuvuka 6to ule,walitoka spidi ya hali ya juu hali iliyofanya Faraj autazame moto ule kwa macho makali sana ule moto ukazidi kuchochea mara mbili yake, hata farasi wale walipofika pale walijikuta wakisimama gafla kuhofia kuungua na kufanya askari waliokuwa juu yao wadondoke mbele na kuuvaa moto ule askari wote. Wakaanza kupiga mayowe kuhitaji msaada maana nguo zao zimepamba moto. Iliwabidi wajitupe chini na kuanza kugaragara moto upate kuzima. Hali ile ilimfanya Rahim asiamini kile anachokiona mbele yake,alibaki ametulia juu ya farasi wake. Faraj alitazama taratibu akaanza kusogea alipo Rahim, aliuvuka moto ule bila hofu na kusogea hadi pale akizidi kumuaminisha Rahim uwezo alionao. Walibaki wakitazamana kwa muda kadhaa na Faraj akapata kumfahamu Rahim.

"Mtoto wa Mfalme Faruk,nini kimekuleta pamoja na askari wako katika ardhi yangu?"aliuliza Faraj akimtazama Rahim.
"Nimemfuata Maya,namuhitaji hilo ndilo lengo langu mimi."alisema Rahim.
"Nani amekwambia kama Maya yupo hapa angali yeye ni binti wa Mfalme wa Eden."
"Mimi naamini tu yupo katika makazi haya,yupo... tena yupo na mlinzi wake Samir."aliongea Rahim akiwa anajiamini.

"Sawa hata kama wapo,imekuwaje awali ukawatuma askari wenu wamvamie Samir jioni ile na leo unakuja na askari wengine unasema unamtaka Maya wakati leo mmedhamiria kuwavamia watu kwenye makazi yao."alisema Faraj akiwa mwenye kujiamini sana. Rahim alinyamaza kutafuta la kusema na muda huohuo Maya pamoja na Samir ndio walikuwa wakifika eneo hilo na kukutana na hali ile askari wote wakiwa chini wanaugulia majeraha. Walikimbia haraka kusogea pale waliposimama Faraj pamoja na Rahim ambaye kitendo cha kuwaona tu wakina Maya alishtuka akiamini kweli wawili hao ni wazima.
"Faraj, vipi upo salama?"aliuliza Maya akiwa na wasiwasi.

"Mimi ni mzima kabisa, tumetembelewa na mtoto wa Mfalme Faruk na amekuja hapa anasema anakuhitaji wewe, kuna mmepanga mkutane?"aliuliza Faraj na kumfanya Maya ageuke kumtazama Rahim,alimsogelea hadi pale alipokaa juu ya farasi wake.

"Nilishatangaza mbele ya wazazi wangu pamoja na wako kwamba sipo tayari kuolewa nawewe,na mtu niliyemchagua ni huyu hapa ambaye tumepewa adhabu ya kutelekezwa kwenye msitu wenye wanyama wakali. Nini kimekuleta tena hapa na umejuaje kama nipo hapa?"aliuliza Maya akionekana kuwa mkali juu ya swala hilo.

"Maya hebu nifikirie mimi japo mara moja,hakika nakupenda na ndio maana wazazi wetu kwa pamoja wamelipitisha na kulibariki swala hilo,hebu tazama maisha unayoishi huku,wewe sio mwanamke wa kuishi huku vijijini una heshima yako Eden. Tafadhari nikubalie turudi Eden nitamshawishi baba yako afute adhabu yako uwe ni mtu wa Eden."alisema Rahim akijaribu kumshawishi Maya.

"Naomba niongee kauli ya mwisho na sitopenda nirudie tena, Sipo tayari kuolewa na wewe , naomba uniache na maisha hayahaya ninayoishi kwasasa."alisema Maya na kugeuka nyuma kuwataka waondoke. Faraj aligeuka na kuongoza njia huku wenzake wakimfuata.

Walimuacha Rahim aliwa anawatazama tu hadi walipotoweka, alipiga kelele kwa hasira zilizopo moyoni mwake huku moto ule ukianza kutulia taratibu. Aliwatazama askari wake na kuona wakiugulia maumivu huku wengine wakiungua sana mwilini.
"Huyu mpumbavu Samir ndiye anayemfanya Maya anione si lolote."aliongea Rahim akionesha kuchukizwa na jambo hilo,aliona mtu anayemuwekea kizuwizi ni Samir hivyo lazima ammalize ili lengo lake litimie.

Baada ya muda kupita Maya na wenzake walikaa mahala kujadili juu ya swala lile lililotokea.
" Huyu mtu sidhani kama ndio itakuwa mwisho wa kutufuatilia hapa,maana anaonekana kuwa upande wako Maya."aliongea Samir.
"Hata afanyaje sitaweza kukubaliana naye, siwezi."alikuwa kwenye msimamo mzito Maya.
"Mimi nadhani anakuhitaji kwa maslahi yake binafsi na si upendo. Asingekuja na askari wote wale ni wazi kwamba alikuja kwa shari."alisema Faraj akimtazama Maya.
"Na taarifa kwamba sisi tupo hapa wamezipata wapi?"aliuliza Samir.
"Hapa mimi nina mashaka itakuwa kuna ambaye anawapa taarifa hizi."aliongea Maya na kuwafanya wenzake wahisi jambo hilo likawa kweli. Waliweka moyoni mwao kwamba kuna mtu anashirikiana na Rahim kwenye jambo hili. Iliwabidi wajitose kumnasa mtu huyo wanayemuhisi hivyo.

Tangu kuondoka kwa Maya ndani ya falme hakukuwa shwari hasa kwa upande wa Mama yake. Muda wote Malkia Rayat alikuwa kwenye mawazo tele juu ya mwanaye. Muda mwengine alidiriki hata kufikiria mbali kujitoa sadaka naye katika msitu ule maana Maya alikuwa ni muhimu sana katika maisha yake. Hali hiyo ya Malkia ilimfanya hata Mfalme Siddik kukosa raha. Aliichukia sheria ya adhabu ile ambayo imemgusa na kutoa furaha katika familia yake. Muda wote amekuwa akimtazama mkewe akiwa mwenye huzuni. Alinyanyuka na kuondoka sehemu hiyo ili asizidi kuumia kwa kile kilichotokea kwa binti yake anayedhaniwa tayari ameuawa kwa wanyama wakali kule msituni.

Kwa Jamal,ilikuwa ni kama amekosa kitu mwilini mwake baada ya kumkosa Maya,alifahamu ndio mwisho wa mipango yao waliyopanga ili kuipata Eden kupitia binti wa Mfalme. Alichoamua ni kutaka kuachana na uaskari ili arudi katika taifa lao kama mtoto wa Mfalme Faruk. Hakuona sababu ya kulitumikia jeshi la Eden wakati mtu aliyemfanya awe askari hayupo tena na hatambuliki Eden.

Hadi kufika jioni ya siku hiyo kila mtu alionekana kutulia nje ya nyumba yake wakiwa makini kuhofia huenda wakaja majeshi mengi zaidi kuwavamia hivyo kila mmoja hakucheza mbali na kwake. Kwa Samir na Maya haikuwa hivyo na wala hawakuonesha kuwa na hofu hata kidogo. Walitoka ma kwenda mtoni kama ilivyo kawaida yao. Walipofika wakatafuta mahala na kuketi wakiongea mambo yao. Maya alipakumbuka nyumbani kwa akina Jafari nchini Tanzania na kumtaka jioni ile waende kwa mara nyengine na ni wazi kwamba amevutiwa na mazingira yale. Samir alitabasamu tu na hakuwa na jinsi akafanya vile alivyotaka Maya. Walikamatana mikono na sekunde chache tu wakapotea kabisa eneo lile. Walikuja kutokea chumbani kwa Jafari hali iliyomfanya Maya atabasamu kuona wamerejea tena.

Alifarijika sana Maya kuwa pale,hata alipotazama nywele zake zilibadilika na kuwa fupi zenye kusukwa. Alibaki akicheka tu kicheko ambacho kilimfanya Jafari amfumbe mdomo asije kusikika. Alimuacha mule chumbani na kutoka nje kuangalia usalama kwanza. Alimuona shemeji yake akiwa jikoni anapika muda ule,taratibu akapiga hatua kusogea hadi pale na matani ya hapa na pale yakaendelea.
"Kaka yuko wapi?"aliuliza Jafari akiwa amekamata kisu akikatakata nyanya kumsaidia shemeji yake aliyekuwa anakorogea uji wa ugali.

"Kwani amekwambia anarudi leo? Tangu jana si kaondoka kupeleka mzigo wake wa Mahindi Dar na hapa kurudi hadi kesho au keshokutwa si unajua kazi zao wakipata mzigo hukohuko wanaunganisha kwenda mkoa mwengine."maneno yale yakamfanya Jamal awe na amani baada ya kusikia hivyo kwamba kaka yake hayupo.
"Kwahiyo analala kwako leo?"aliuliza shemeji mtu na swali lake lilimshtua Jafari,akajikuta anapatwa na kigugumizi.
"Nani,."
"Si nimemuona amerudi jioni hii akaingia geto kwako."alisema shemeji na kumfanya Jafari atambue kumbe Maya anajulikana kufika kwake,alijichekesha tu pale ili jambo lile liishe.
"Ila shemeji angalia mtoto wa watu huyo usimharibu,wote mnasoma msijisahau nkaja kuleta aibu katika familia."aliongea Shemeji maneno ya busara kumweleza Jafari. Aliyaelewa maneno yale na kuendelea kusaidiana kupika.
Hata baada ya muda walipoivisha aliandaa chakula na kumpa Jafari akale na mwenza wake jambo ambalo lilimfanya Jafari apate kufurahi kwa kupata shemeji mwenye upendo kwake.
Alipoingia chumbani akamkuta Maya kashabadilisha nguo na kujifunga taulo lililopo mule ndani. Taratibu Maya Alimsogelea Jafari na kumpokea chakula kile akionesha kuwa mchangamfu hata Jafari akashangaa. Alitabasamu tu na kusogea hadi pale Maya alipoweka chakula kile na baada ya kunawishana mikono wakaanza kula. Hakuwa mwenye kuchagua chakula Maya,alikula ugali ule bila kujali kama ndio kwa mara ya kwanza kula chakula hicho,alijua fika hata siku za mbele atakuwa akija huku hivyo chakula kitakuwa ni hicho.
"Usiku umeingia huu."aliongea Maya akiwa anapeleka tonge mdomoni.
" Kwahiyo.."
"Hatutaweza kurudi Gu Ram kwa muda huu,tutalala tu hapahapa."aliongea Maya akiwa mwenye kujiamini, Jafari alitabasamu kwa kusikia maneno yale na kwakuwa ni wapenzi hapajuwa na shaka juu ya uamuzi aliouchukua Maya.

Asubuhi na mapema Rahim alikuwa anaongea na baba yake baada ya kupata kifungua kinywa.
"Sasa umeamua vipi baada ya kutambua hilo?"aliuliza Mfalme Faruk akimtazama mwanaye aliyeonekana kutokuwa na furaha usoni mwake.
"Bado naamini nina nafasi ya kuwa naye, hapa ninapoongea nikitoka naenda Eden."
"Eden? Kufanya nini tena Eden?"
"Nakwenda kukutana na Mfalme Siddik,nimueleze ukweli kwamba Maya na yule mlinzi wake wapo kwenye kijiji kile hawajafa. Nadhani kwa kufanya hivyo kutanipa nafasikwa Mfalme akanifikiria tena,bado sijafeli baba niamini."aliongea Rahim kwa kujiamini sana huku akimtazama baba yake.
ITAENDELEA.
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN 36

Asubuhi ya siku iliyofuata Jafari alipata kuamka pale kitandani huku akimtazama Maya aliyelala naye usiku wajana. Ajabu hakuweza kumuona pale kitandani hali iliyomfanya ashtuke. Alikurupuka pale kitandani na kuanza kutazama huku na kule bila mafanikio. Ilimbidi anyanyuke na kuelekea nje kumtazama.
Moyo wake ulipata kutulia baada ya kumuona Maya akiwa jikoni pamoja na shemeji akimfundisha kumenya viazi. Alibaki kutabasamu Jafari kwa kuona mara ya kwanza binti wa Mfalme anafanya kazi, aligeuka na kurudi zake ndani na sekunde kadhaa kupita akatokea Nadhra mule chumbani, taratibu akasogea na kukaa kitandani alipo Jafari.
"Umekuwa adimu Nadhra siku hizi."aliongea Jafari akimtazama Nadhra.
"Kuna jambo lilitokea na nikaamua kulifanya bila ya kukushirikisha,na imepelekea hata kuwa kimya kuja kukutembelea."alisema Nadhra akionekana kun'gaa kwa uzuri alionao.
"Jambo gani limetokea hadi ushindwe kuniambia.?" aliuliza Jafari na kuona akishikwa mkono.
"Jafari ,naomba unisamehe kwanza kwa kufanya maamuzi bila kukushirikisha, mimi sio tena Nadhra yule uliyekuwa unamfahamu, nimemfuata baba yangu kule alipokwenda lakini nikijuwa fika kwamba nimekuacha ukitekeleza kile kilichopangwa. Lengo hasa la kupata uwezo ulionao ni kuhakikisha unaivunja mila na destuli za Eden juu ya watu wenye uwezo wa nguvu kama zetu. Wewe ndiye wa kuibadilisha Eden kuwa mpya. Mataifa mengi wanaitamani Eden kwa kitu kimoja tu."alisema Nadhra.
"Kitu gani hicho? Na kwanini watu wengi wanaifuatilia Eden?"aliuliza Jafari akimtazama Nadhra.
"Ni Pete ya Mfalme wa Eden. Na endapo akaipata mtu yeyote pete hiyo basi hakuna yeyote wa kumpindua kwa namna yeyote ile,na mtu huyo ndio atakuwa Mfalme wa taifa hilo la Eden."alisema Nadhra na maneno yakamshangaza Jafari.
"Inamaana pete hii niliyonayo ni tofauti na hiyo inayosakwa na watu.?"
"Pete hii uliyonayo ni mara kumi ya pete hiyo inayotamaniwa na kila mtu aipate. Inauwezo mkubwa sana na ndio pete iliyojazwa nguvu zote za wafalme wa Eden waliopita."alisema Nadhra na maneno yake yakamuingia Jafari akapata kuelewa.
"Nimejitoa sadaka kwaajili yako Jafari ili ufanye kazi hiyo,mimi naamini utafikia lengo japo kuna changamoto nyingi utakumbana nazo ila yakupasa kuvumilia na kusonga mbele. Pete uliyonayo haina kazi tena kwasasa maana unaingia kwenye mtihani wa kuipata pete ya Mfalme wa Eden, pete hiyo inatafutwa na watu wengi hivyo yakupasa uwe makini katika maisha yako."alisema Nadhra na maneno yake yakamshtua Jafari.
"Inamaana... inamaana sitakuwa na uwezo wa kufanya lolote tena? Sasa itakuwaje kama haitafanya kazi angali sisi tupo huku.?"
"Na ndio maana nimekwambia nimejitoa mimi ili kazi hii uifanye wewe maana tayari umetengeneza mazingira ya kujulikana Eden,nitakupa nguvu na uwezo nilionao mimi utakuwa unatumi a ukiwa unapigania kuitafuta pete hiyo."alisema Nadhra.
"Nadhra,inamaana umejitoa kwaajili yangu?"aliongea Jafari kwa sauti ya huruma lakini haikumfanya Nadhra abadili maamuzi yake. Palepale alinyanyuka huku akimtazama Jafari,alinyanyua mikono yake kushika kichwa cha Jafari huku akiongea maneno ambayo hayakuweza kueleweka kwa haraka. Gafla tu mwili wake ukaanza kutoa moshi mweusi kila sehemu huku Jafari nuru ikianza kummulika kichwani na kujikuta akiyafumba macho akihisi kuna vitu vinaingia mwilini kwa kasi sana na muda huohuo hali ikaanza kubadilika mwilini mwake,kizunguzungu kilianza kumzonga na kushindwa kupata hata nguvu ya kuendelea kukaa pale,taratibu akaanza kulegea mwili na sekunde kadhaa mbele akadondokea kitandani na kupoteza fahamu.

Baada ya muda kupita Rahim ndio alikuwa akiwasili Eden akiwa na askari wawili tu waliomsindikiza ,moja kwa moja wakaaza kuelekea katika falme ili apate kukutana na Mfalme. Taarifa za kuwasili Rahim ndani ya mji wa Eden zilimfikia Mfalme Siddik pamoja na Malkia wakiwa wanatoka kupata kifungua kinywa. Iliwabidi waelekee ukumbini kukaa kusubiri ugeni huo uweze kufika huku wakiwa na maswali imekuwaje mtoto wa Mfalme aweze kurejea mwenyewe. Muda mfupi Rahim aliweza kuwasili na wale askari waliomsindikiza,alikaribishwa kwa heshma kubwa na kupelekwa hadi pale ukumbini ambapo alipata kuwaona viongozi wa taifa hilo wakiwa wametulia.
Alitoa heshima kama ilivyoada na kufanya viongozi hao wampokee na kumkaribisha akapata kukaa.
Waliongea mambo mengi ya kimaendeleo na mwishowe Rahim ikambidi aeleze kilichomleta.
"Nimeona nije asubuhi na mapema kuja kuwaeleza jambo,nafahamu mmekuwa na shauku za kufahamu kwanini nimerejea tena mapema hivi. Upendo wangu kwa binti yenu hauwezi kufutika japo ameelekeza hisia zake kwa mlinzi wake,hata siku ambayo wanatolewa ndani ya Eden kupelekwa kwenye msitu ule sikuwa nyuma kuhakikisha kama ni kweli Maya niliyempenda anakwenda kuachwa msituni."aliongea Rahim huku akiwatazama wawili hao.
"Ah Rahim, hayo yamepita hatupaswi kuyaongelea tena,ilikuwa ni adhabu ilikuwepo toka enzi na enzi hivyo haitapendeza kukumbushia maana hata sisi inatuuma."alisema Mfalme Siddik kwa sauti ya upole akionesha kweli kuumizwa na jambo lile.
"Askari wenu wameifanya kazi ile kwa ufasaha kuhakikisha wanawaacha kwenye ule msitu,ila walipoondoka huku nyuma haikujulikana imekuwaje ila nimepata taarifa kutoka kwa askari wangu kuwa Maya pamoja na Samir wapo kwenye kijiji cha Gu Ram wanaishi huko."maneno yale yalimshtua Malkia Rayat akajikuta akisimama pale alipo.
"Unasema!!.. Inamaana Maya wangu bado anaishi?"aliuliza Malkia akiwa mwenye kutetemeka baada ya kusikia hivyo.

Upande wa pili Jamal alimfuata Generali mkuu akiwa kwenye ofisi yake. Alimpa heshima kama mkubwa wake wa majeshi akakaribishwa kukaa.
"Hapana mimi si mkaaji sana,nimekuja kwako kukupa taarifa moja tu na nimeamua kutoka moyoni mwangu."alisema Jamal akiwa anajiamini lengo ni kumweleza Generali kuhusu kuacha uaskari na kurudi katika taifa lao.
"Eh jambo gani hilo Jamal ambalo unataka kuniambia?"aliuliza Generali huku akimtazama Jamal, alitazama chini na mwishowe akanyanyua uso wake kuongea.
Muda huohuo akaingia askari mmoja bila kubisha hodi na moja kwa moja akatoa saluti kwa Generari.
"Generali kuna taarifa imefika kwa Mfalme muda huu kwamba binti wa Mfalme Maya pamoja na Samir bado ni wazima na wamekutwa wakiishi katika kijiji cha Gu Ram."aliongea askari yule na maneno yale yakamsimamisha Generali kwa mshangao. Aligeuka kumtazama Jamal ambaye naye alibaki kushangaa baada ya kusikia taarifa hiyo.
"Unasemaje? Bado wanaishi?" ni maswali mfulilizo yakimtoka kinywani Jamal akiwa haamini kinachoelezwa pale.
"Ndio,na hapa nimeagizwa na Mfalme nimuite Generali."alisema yule askari akaeleweka. Hakutaka kuchelewa Generali akaanza safari ya kuelekea kwa Mfalme kumsikiliza huku nyuma akifuatwa na askari yule.
Jamal alibaki akishangaa baada ya kusikia kama Maya na Samir ni wazima hali ya kuwa waliachwa kwenye msitu ule wa wanyama wakali. Alijikuta akiuziba mdomo kumaanisha kile alichokuwa anataka kumweleza Generali amekifuta baada ya kujua Maya yumzima hivyo nafasi anayohitaji bado ipo. Haraka naye akatoka mule ndani kwenda kusikiliza kinachozungumzwa kwa Mfalme.

"Kama Maya ni mzima basi nami nitaondoka nikaishi naye,nampenda mwanangu sitakubali niwe mbali naye safari hii."alisema Malkia Rayat akiwa amesimama na mwenye shauku ya kutaka kumuona mtoto wake.
"Unamaana gani kusema hivyo?"aliuliza Mfalme akimtazama mkewe.
"Tambua hilo tu kwamba sitaweza kuendelea kumfikiria mwanangu,nimekuwa sina raha kwa kujua tayari nimempoteza mwanangu lakini kama ni mzima sitaweza kukubali niwe mpweke kiasi hiki tena."aliongea Malkia akionesha kuwa na msimamo wa kile alichoamua.
Muda huohuo akafika Generali na kumsogelea Mfalme kwa kumpa heshima na kusimama kumsikiliza.
"Bila shaka taarifa umeipata kuhusu binti yangu."
"Nimeisikia Mfalme japo imenishangaza sana,niombe samahani kwa niaba ya askari wangu nadhani wao ndio wamefanya makosa kutokuwa makini juu ya swala hilo."alisema Generali kwa upole akiwaombea msamaha askari wake.
"Kwa taarifa zilizofika nimepata kutambua askari hawana kosa lolote juu ya swala hilo. Mtu pekee ninayemuhisi ni Samir,huyu naomba achunguzwe kwa umakini sana huenda akawa ananguvu tofauti na binadamu wengine."alisema Mfalme Siddik na kauli yake ikawashtua watu wote waliopo mahala pale.
"Mh Mfalme,kitu gani kimekufanya uamini hayo unayosema?"aliuliza Generali baada ya kutoamini kile alichokizungumza Mfalme dhidi ya Samir.
"Tangu kuumwa kwa Maya hadi Malkia kuamua kwenda Mashariki na mbali,ni Samir ndiye aliyewahi kufika kule na kuweza kumzuia Malkia,nilikaa nikifikiria alifika muda gani kule angali sisi tumetumia siku mbili bila kulala njiani na ajabu hata hatukufika tumekutana nao njiani wakirejea. Samir siku zote ni mzembe wa kupitiliza amepata wapi ujasiri na nguvu za kupambana uwanjani hadi kuibuka kuwa mshindi. Na tukio hili ndilo linanifanya niamini haya yote kwamba huyu kuna nguvu za kichawi anazitumia."aliongea Mfalme na kila mtu akaanza kuhisi huenda kinacho zungumzwa ni cha kweli.
"Kwahiyo unataka tufanye jambo gani kwa Maya na Samir?"aliuliza Generali huku Rahim akiwa makini kusikiliza.
"Natoa amri kama Mfalme hawa watu waletwe hapa mara moja,ukweli utapatikana hapahapana sheria ifuatwe"alisema Mfalme akitoa amri na kuvunja amri ile ya wawili wake kutokanyaga tena Eden. Haraka Generali akapokea oda ile na kuwaanda askari wake akiongozana na Jamal kuelekea kwenye kijiji cha Gu Ram.
"Nimeamini kweli huna mapenzi na binti yako,pia huna hata shukrani kwa msaada alioutoa Samir dhidi ya Maya. Hata kama anatumia nguvu za kichawi ila katumia kumuokoa binti yako,hivi bila ya Samir wewe si ungekuwa raia wa kawaida tu Eden ingetawaliwa na Dalfa!."alisema Malkia akionesha kukasirika sana kwa maamuzi aliyoyachukua Mfalme. Hakutaka kuendelea kukaa pale alitoka nje na yeye akapanda kwenye farasi wake kwenda kumuona mwanaye katika kijiji hicho cha Gu Ram. Mfalme alibaki kusimama akishuhudia mkewe akiondoka. Rahim alikuwa pembeni akitabasamu tu na kujua lazima sheria ya Eden itamuadhibu Samir kwa kujulikana kwamba anatumia uchawi,ni wazi kwamba lazima anyongwe mpaka kufa.
ITAENDELEA
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN 37

Baada ya muda kupita Jafari aliweza kufumbua macho yake
pale kitandani. Tangu alipopoteza fahamu muda ule alivyokuja Nadhra hakuweza kuelewa ilikuwaje na nini kilitokea muda ule. Moja kwa moja akatoka mule chumbani na kuelekea sebuleni kutazama kalenda iliyoko ukutani. Alishusha pumzi baada ya kutambua ilikuwa ni bado ni siku ileile ya Jumapili. Fikra zilimfanya ahisi huenda jambo lile alilofanyiwa na Nadhra limechukua siku kadhaa. Alisogea na kukaa kwenye kiti akitafakari ilivyokuwa. Alitazama vidole vyake na kuona bado pete ile ipo kidoleni. Alinyanyua mkono wake na kutazama ile pete lengo ni kutaka kujua kama kweli haina kazi kwasasa. Punde tu akatokea shemeji akiwa ameshika chupa ya chai.
"Mkeo yupo shapu kweli katika kazi sema anaonekana kwao in mtu wa kupikiwa maana hana hata anachojua kwenye kupika."alisema Shemeji huku akiweka chupa ile mezani. Jafari aliachia tabasamu baada ya kuambiwa hivyo. Ni wazi kwamba Maya hakuna anachojua maana ametoka kwenye familia ya kifalme. Kuna muda alitamani amueleze shemeji yake lakini nafsi inasita na kulifanya ni kama siri ya wao pekee.

Huku kwa Faraj tangu siku ya jana alikuwa akiwatafuta Maya pamoja na Samir maana walipotea gafla tena bila hata kuaga wanapoelekea. Lakini kadiri muda ulipozidi kwenda akapata kutambua huenda Samir amemueleza ukweli Maya wapi alipotokea na ikamfanya amuoneshe ili apate kuamini. Kidogo hofu na mashaka juu yao yakapungua maana alihisi wamepata tatizo ndani ya Gu Ram.
Baada ya muda kupita kikosi cha askari wa Eden kilikuwa kinakaribia katika kijiji cha Gu Ram. Generali alikuwa mstari wa mbele akiwaongoza vijana wake. Pembeni alikuwa Jamal akionekana kuwa makini katika kazi hiyo wanayokwenda kuifanya. Malkia Rayat alikuwa nyuma sana hadi kuweza kuwafikia lengo ni kutaka kumuona binti yake baada ya kupata taarifa kwamba yupo hai. Huku kwa Jafari baada ya muda kwenda aliona ni wakati wao kurejfa Guram maana lengo la kurudi kwao ni kumuonesha Maya mahala alipotokea. Ilimbidi amweleze Maya ili wapate kurejea Gu Ram maana tangu waondoka hawakuweza kuwasiliana na mwenyeji wao Faraj.

Generali alifanikiwa kuwasili katika kijiji hicho akiwa na askari wake. Watu waliokuwa njiani waliweza kuwaona na kuwatambua kwa mavazi yao kwamba ni askari wa taifa la Eden. Kwa heshma ya taiea hilo wananchi wakawa wanainamisha nyuso zao chini kuwapisha askari hao wapite. Moja kwa moja Generali na watu wake wakaelekea kwenye nyumba ya Kiongozi wa kijiji hicho maana ni miaka mingi hakuweza kufika kijijini hapo. Wananchi nao wakawa wanafuata nyuma kwenda kushuhudia nini sababu za ujio huo wa askari wa Eden.
Muda wote huo Faraj alikuwa nje ya eneo lake amekaa akiangalia mandhari ya hapo, alishapata kutambua kuwa kuna ugeni uliofija katika kijiji chake na muda mfupi waliwasili pale katika nyumba ya kiongozi wa kijiji hicho. Askari walitanda kila kona ya eneo lile kuweka ulinzi kama waliowafuata wamo ndani wasipate kuwatoroka. Faraj alisimama kutoka pale alipokaa akiwatazama askari wale, Generali alishuka kutoka kwenye farasi wake bada ya kusimama kisha akaanza kumsogelea Faraj pale alipo akiwa hamfahamu. Alisimama kwa sekunde kama ishirini wakitazama wenyewe bila yeyote kuongea.
"Inamaana hufahamu jeshi hili linatokea Taifa gani hadi usitoe heshima?"aliongea Generali akimtazama Faraj akionekana mtoto bado.
"Laiti angesimama mbele yangu Mfalme wa Eden au Malkia ningefanya hivyo japo kwa kuamua pia."alisema Faraj.
"Hata hivyo unadhani nalingana na wewe?"
"Huenda ukawa na umri mkubwa lakini usipate kubarikiwa upeo na heshima. Huenda umri wangu ndio ukakufanya uwe na kiburi cha kutosalimia. Wewe ni mgeni katika ardhi yangu unapaswa ujitambulishe baada ya salamu na si mimi nianze kukusalhmu."alisema Faraj akiwafanya hata askari waliokuwa pembeni akiwemo Jamal waone ni maneno yenye dharau kwa Generali wao. Wakataka kusogea pale kumkamata lakini Generali akanyanyua mkono kuwataka waache.
Alibaki kutabasamu tu huku akimtazama Faraj.
"Unataka kunambia wewe ndio kiongozi wa hapa?"aliuliza General na jibu alilopata ikabidi astaajabu maana hakumtegemea kama anaweza kuwa kiongozi kwa umri ule. Baada ya kufahamu hilo ilimbidi arudi kwenye kile kilichowaleta.
"Bila shaka unafahamu ujio wa watu wawili katika kijiji chako, binti wa Mfalme pamoja na mlinzi wake wapo humu. Tusingependa sisi tuutimie nguvu kulikamilisha hili,tunahitaji kwa busara zako uwaamuru watoke Mfalme Siddik anawahitaji mara moja."alisema Generali na kumfanya Faruk atabasamu kusikia hivyo. Aligeuka kumtazama Jamal pamoja na askari wengine kisha akarudi kumtazama Generali.
"Ninavyofahamu mtu akifukuzwa kwenye mji kamwe hawezi tena kurejea mahala alipofukuzwa, taarifa za kuachwa kwenye msitu watu hao wawili nilizipata na kujua tayari watu hao wameshaliwa na wamyama wa msituni. Imekuwaje mnawata futa watu ambao mmewasindikiza hadi msituni mkawaacha huko mkijua watakufa?"alisema Faraj kwa sauti kubwa yenye kujiamini. Generali alibaki kumtazama tu kwa kuguswa na maneno yale. Baadhi ya wanakijiji walistaajabu kusikia swala hilo maana hawakuwa wanafahamu sababu za Samir na Maya kurejea katika kijiji chao.
"Amri ya Mfalme ifuatwe popote pale bila kipingamizi,hivyo unapoombwa kwa upole ujue unaepushwa na vurugu katika eneo hili,shida yetu ni hao watu wawili waamur watoke ili mahala hapa pawe salama."alisema Generali akiwa anamaanisha kile anachokisema.
"Sijawakaza kuingia ili muangalie,ila naongea kwa amani tu hao watu hawapo hapa."
"Wamekwenda wapi?"
"Sifahamu hata mimi."jibu hilo halikumfanya aamini kinachozungumzwa pale Generali, alitoa amri ya askari wake waingie mule ndani kupekua na askari wakafanya hivyo huku wengine wakiwa nje kuweka ulinzi. Watu wakabaki kuongea chinichini tu kila mtu akisema la kwake kwa kile kinachoendelea pale. Askari mule ndani walipekua kila sehemu bila mafanikio takribani dakika kumi nzima. Mwishowe walitoka nje na kumueleza Generali kwamba hakuna mtu yeyote ndani. Aligeuka kumtazama tena Faraj aliyekuwa hana shaka.
"Wameenda wapi wawili hawa?"aliukiza kwa mara nyengine huku safari hii hakuonesha kuwa na furaha hata kidogo.
"Laiti ningelijua walipo basi ningeliwaambia tangu awali, lakini ninachoongea hamkiamini mnachokitaka ni nini kwangu?"alisema Faraj akiwa anamtazama Generali.
"Nadhani hunifahamu ndio maana unanichezea akili... Mkamateni haraka!"alitoa amri hiyo na mara moja askari wawili wakasogea pale na kumkamata mikono Faraj,hakuwa mwenye kupepesuka wala kuhofia jambo. Alibaki kumtazama tu Generali pale aliposimama.
"Mnafanya makosa kuja katika ardhi yangu na kunifanya hivi mbele ya watu wangu. Mnapoelezwa ukweli jaribuni kuwa waelewa ili mpate kusaidiwa."alion gea Faraj kwa busara na upole.
"Kipi cha ukweli unachokiongea hapa,unataka kusema hawa watu hawakufika hapa?... Eti nyie watu hamkuwaona binti wa Mfalme wa Eden pamoja na mlinzi wake?"aliuliza Generali kwa ukali lakini hakuweza kujibiwa na raia yeyote pale. Kwa hasira alizonazo na kujua kwamba anadharauliwa na watu wote pale,alitoa upanga wake na kumuwekea Faraj shingoni mwake lengo ni kufanya kile alichokusudia. Watu walishtuka kuona hivyo na kuwatia hofu huenda kiongozi wao akadhurika. Wakawa wanaanzisha zogo kutaka kiongozi wao aachilie, iliwabidi Jamal na askari wengine wawazuie raia ambao walikuwa wanakuja juu. Faraj alikuwa anatazama tu kinachoendelea hali iliyomfanya ahisi huenda kikamtokea kitu kibaya maana amewekewa upanga shingoni. Aliikamata bakora yake vyema ili apate kujitoa mikononi mwa askari wale waliomkamata.
"Muacheni mara moja!"ilisikika sauti iliyowafanya watu wote wageuke kutazama ilipotokea. Kila moja aliinamisha sura chini baada ya kumuona Malkia Rayat akisogea mahala pale. Ilimlazimu Generali atii kile alichosema Malkia,aliuto upanga wake na askari wake wakamwacha Faraj alikuwa anataka kujitetea muda ule. Malkia alisogea hadi pale na kuwataka askari warudi nyuma kumuacha Faraj pekeyake. Alionekana kuwa mwenye huruma na kujali utu,jambo hilo lilijidhihirisha pale alipoinama kupiga magoti huku akimshika Faraj mkono.
"Bila shaka wewe ndiye unayeongoza watu wa Gu Ram,ni kiongozi wa kijiji hiki."aliongea Malkia huku akionesha tabasamu usoni mwake.
Faraj alitabasamu huku akimtazama Malkia usoni mwake.
"Mimi ndiye, Gu Ram ndio ninayo iongoza kwasasa."alisema Faraj kwa sauti ya upole.
"Samahani kwa hiki ninachotaka kuuliza kwako, ni kweli Maya yuhai?"aliuliza Malkia huku akiwa amemshika mkono Faraj.
"Si Maya tu hata Samir ni mzima pia."maneno yale yakamfanya Malkia afurahi sana,alizidi kumsogelea Faraj.
"Naweza kuwaona hata mara moja?"
"Kiukweli hawapo kwasasa,ila huenda wakarejea hapo baadae maana sifahamu hata walipoelekea."alisema Faraj.
"Ila wanaishi hapa kwenye mji wako?"
"Ndio,na maamini watarejea hapahapa."alisema Faraj na kushuhudia Malkia akinyanyuka haraka na kugeuka kumtazama Generali.
"Hamtaweza kuwapata kwa muda huu,nimeongea na mwenye mji huu amewataka muondoke mrudi Eden, wakirejea ataongozana nao kuwakabidhisha kwa Mfalme. Hampaswi tena kuendelea kukaa hapa."alisema Malkia kumuamuru Generali aondoke na askari wake.
"Lakini Malkia hii ni amri ya Mfalme ameitoa turudi na hawa watu hataweza kutuelewa tukirejea mikono mitupu."alisema Generali.
"Na mimi ndio nimesema mrudi huyu atawaleta naminikiwemo,amini hilo."alisema Malkia na kumfanya Generali awe na mashaka katika kuchukua maamuzi. Lakini mwishowe akaelewa yaliyoongelewa na Malkia,aliwaamuru askari wake waondoke. Jamal alikuwa na wasiwasi kwa kile alichokiamua Malkia na kuhisi huenda anataka kuwageuka. Hata walipofika njiani ilimbidi amueleweshe Generali kuwa wanapaswa kuwa makini katika swala hilo. Waliamua kurejea Eden kwakuwa Malkia ndiye aliyetamka maneno yale na hawakuweza kumpinga.

Huku nyuma Faraj alimkaribisha Malkia huku wananchi wakianza kuondoka eneo lile baada ya kuona amani imerejea.
Walikaa na kuongea mambo mengi pale nje wakivuta muda kuwasubiri wakina Maya kama watarudi.
"Nimepata faraja kusikia mwanangu na Samir bado wanaishi. Nilikata tamaa na kujua sina tena mtoto katika dunia hii. Sitakubali nimpoteze tena Maya nimejua kuumia pindi alipoondoka Eden."alisema Malkia akionesha kuwa na shauku ya kumwona mwanaye. Faraj alibaki kumtazama tu huku akiwa mwenye kutabasamu.
Muda mchache tu walipata kuonekana Maya na Samir wakiwa wameshikana mikono kwa furaha. Wanakijiji walipata kuwaona wakawa wanawafuata ku taka kufahamu walikuwa wapi muda wote. Hali ile iliwatia mashaka wawili hao na kuhisi huenda kuna jambo limetokea maana si kawaida kwa watu kuwa na wasiwasi kiasi hicho. Hawakutaka kuongea lolote hadi walipofika kwa Faraj. Macho ya Maya yaligongana na ya mama yake na kila mmoja wapo akawa mwenye kushangaa. Alinyanyuka pale alipo Malkia na kuanza kumkimbilia mwanaye ambaye naye alikuwa mwenye furaha sana na kujikuta wakikumbatiana muda ule. Samir alitabasamu huku akitoa heshima kwa Malkia wake.
ITAENDELEA.
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN 38

Iliwabidi watulie mahala waongee Maya pamoja na Malkia huku Faraj akiongozana na Samir kuelekea nje kidogo ya mahala pale.
"Niwie radhi kwa kile kilichotokea sikuweza kukwambia maana ilikuwa ni gafla tu safari yenyewe. Na sikupanga kama tutakaa muda mrefu huko maana Maya ndio ameniomba tubaki."alisema Samir wakiwa wanatembea.
"Sikuwa na hofu sana baada ya kufahamu Maya yupo mikononi mwako, kam wote ni wazima basi ni jambo jema."alisema Faraj na kumfanya Samir amtazame.
"Nimeonana na Nadhra leo."alisema Samir na maneno yale yakamfanya Samir asimame. Alimgeukia Samir aliyekuwa naye anamtazama.
"Amekuambia nini dada'ngu? Na yupo wapi kwasasa."ni maswali yaliyomfanya Samir atafute namna ya kujibu.
Upande wa pili Malkia alikuwa anaelezwa na binti yake hali halisi ilivyokuwa pindi walipotupwa kwenye msitu ule hadi sasa wapo hai. Ilimfanya ashtuke kupata ukweli wa mambo baada ya kuambiwa uwezo alionao Samir.
"In amaana Samir anatumia nguvu za kichawi?"aliuliza Malkia akiwa haamini kile alichosikia.
"Nguvu zake ni sawa na alizonazo Faraj,hawa watu si wabaya na wanatumia uwezo walionao kusaidia watu."alisema Maya akijaribu kuwatetea.
"Umeamini vipi kama ni wema kwako? Huenda wakawa wanakuzunguka wakipanga kukufanyia jambo baya."
"Nawaamini sana na sio watu wabaya kwangu. Mama.. Labda nikwambie tu ukweli usioujua, huyu si Samir unayemfahamu wewe,huyu ni mtu kutoka taifa lengine kabisa na nimepata kwenda huko na ndio tumetoka huko muda huu. Yote aliyonifanyia ndio nimeamini kuwa huyu ni mtu sahii kwangu, yeye ndio alinisaidia kipindi mnahangaika kwenda kwa Dalfa ili nipate kupona,yeye ndio alikuzuia wewe usikubaliane na mikataba ile ya Dalfa. Hayo tu ni matukio yanayodhihisha kwamba si wote wenye kutumia nguvu hizi ni wabaya. Ufalme umeshikilia sheria ambazo zinawaumiza hawa wat. Unadhani angekuwa mbaya angekukataza kuiuza Eden mikononi mwa Dalfa! Ndio maana nimekuwa na amani ya kuishi hapa Gu Ram najua kuna amani na usalama kwangu, sijafikiria kujuta kuondoka Eden hata mara moja."alisema Maya akionesha kuwa na furaha. Malkia hakuamini kuambiwa kama ni Samir ndiye aliyefanya yote hayo. Alielezwa mengi kuhusu wema wa mtu huyo huku akilazimishwa aamini kwamba si wote walio na nguvu hizo wanatumia uchawi.

Upande wa pili Generali na askari wake waliweza kuwasili Eden, moja kwa moja akaelekea kwa Mfalme ambaye alikuwa pamoja na Rahim hadi muda huo. Kitendo cha Generaki kuja mikono mitupu kilimsht ua Mfalme hadi akanyanyuka pale aliposimama.
"Vipi! Kuna nini kimetokea.?" alikuwa na shauku kubwa ya kufahamu kilichojiri.
"Tumeweza kufika hadi kwenye kijiji kile na tukambana Kiongozi wa pale aweze kunieleza wapi walipo Maya na Samir lakini Malkia akaingilia kati kutaka tumuache. Na ni yeye pekee ndio aliyeongea na yule ki gozi na kuelezwa. Alitoa amri kwamba turudi ili watakaporejea wawili hao atarudi nao hadi kwako wakukabidhi."alisema Generali kwa upole.
"Akhh.. Malkia mbona ananiingilia katika maamuzi yangu sana! Inamaana yeye pia amebaki huko?"aliuliza Mfalme na Generali akamjibu sawiya. Aliyakumbuka maneno ya mkewe huyo kwamba hawezi kunyamaza angali anafahamu mwanaye bado yupo hai. Kauli hiyo ilimpa mashaka na kuona huenda kuondoka kwake ndio safari ya moja kwa moja. Hakutaka yatokee hayo yote kwa kuikosa familia yake yote, alimuamuru Generali waongozane wote pamoja na askari kurudi tena Gu Ram ili apate kurejea nao watu anao wahitaji.
Muda huo Jamal alikuwa mahali akiwa na Lutfiya akimueleza hali halisi ilivyokuwa. Kidogo wakapata kuona kuna matumaini tena ya kumpata Maya. Walichofanya ni kumtumia ujumbe Mfalme Faruk kumueleza hali halisi. Walichukua njiwa na kutuma ujumbe huo mara moja wapate kufanya jambo.

Ujumbe kupitia njiwa yule uliweza kumfikia Mfalme Faruk na baada ya kuelewa kilichoandikwa ndani yake gakutaka kupoteza muda alitoa amri ya askari wengi sana kuwahi kwenye kijiji kile kabla Mfalme Saleh na jeshi lake hawajafika. Huku Jamal naye alijichanganya na askari wenzake wakiongozana na Mfalme kuelekea Gu Ram.
Baada ya muda kadhaa Malkia Rayat alikaa na Samir wakiongea mambo kadhaa. Hapakuwa na siri tena juu ya Samir kwa uwezo alionao na hata jina lake pia. Malkia alihitaji kupata uhakika kutoka kwa Samir kama ni kweli hana nia mbaya na Maya maana amekuwa n mashaka hayo tu moyoni mwake.
Alimtoa hofu hiyo Malkia na kumhakikishia kwamba Maya yupo katika mikono salama. Kauli ile ikamfanya Malkia apate faraja na kuwa na matumaini juu ya mwanaye. Alijikuta anamuamini Samir baada ya kutambua anatumia nguvu za kichawi kwa kusaidia watu na si kudhuru. Maya alikuwa sehemu akiwatazama wakiwa wanaongea, alifurahi sana kuona hata Malkia amekuwa muelewa wa haraka kuhusu Samir. Hakuonesha kukwazika wala kushangaa sana baada ya kuelezwa kuhusu Samir.
Baada ya muda kadhaa ikambidi Malkia awaweke pamoja Maya pamoja na Samir na kuwaeleza sababu za askari wale kufika hapo Gu Ram.
" Na kwakuwa nimewbmuru waondoke bila kuwapata naamini lazima watatumwa tena maana Mfalme amekuwa ni mtu wa kutopingwa katika jambo lake lolote aliloamua liwe" alisema Malkia huku akimtazama mwanaye.
"Inamaana anataka turudi ili atuue au? Kama adhabu kashatupatia tumetelekezwa ndani ya ule msitu hivyo swala la sisi kuwa hai yeye linamuhusu nini?"aliongea Maya akimshangaa baba yake kwa maamuzi yake.
"Tatizo lililopo ni kwa upande wa Samir, ameanza kumhisi huenda akawa anatumia nguvu za kichawi maana si rahisi kwa mtu wa kawaida kutupwa katika msitu ule kisha akaendelea kuishi. Hivyo anamhisi hivyo na huenda kama wakibaini kuwa ni kweli wakampa adhabu kama ilivyo kawaida kwa mtu mwenye kosa hilo."aliongea Malkia kwa upole na maneno yale yakamtia hofu Maya,aligeuka kumtazama Samir akiwa hana la kuongea baada ya kusikia hivyo,alibaki kumsikiliza tu Malkia.
"Ila naamini hakuna kitakachoharibika wala msiwe na hofu juu ya hilo."aliwapa moyo juu ya hilo akiwa mwenye kujiamini na kuwafanya Samir pamoja na Maya wabaki kutazamana.

Muda ulizidi kwenda mbele na hatimaye Askari wa Mfalme Faruk walifika kijijini hapo. Mkuu wa kikosi hicho alitoa amri moja tu kama walivyoagizwa kufanya.
"Unaingia kila nyumba kuangalia watu tunanwataka kama wapo,yeyote atakayeleta ubishi chinja bila kuhofia jambo."alisema askari huyo na kuwapa mori wenzake wakawa tayari kwa jambo ìlo,muda ulipofika walianza kazi hiyo kuingia kwenye kijiji hicho kupekua kila nyumba.
Huku wakiwa hawana habari pale nje wakiongea mambo yao walishangaa kumuona Faraj akitoka ndani haraka na kusimama mlangoni. Hali ile ikamfanya hta Samir ahisi huenda kuna jambo limetokea. Alisimama na kumsogelea Faraj pale aliposimama.
"Vipi kuna tatizo umepata kutambua?"aliuliza Samir akiwa namtazama Faraj.
"Nahisi kuna waru wameivamia Gu Ram, nasikia harufu ya damu hapa."alisem Faraj akiwa anazidi kuangalia kila sehemu. Alipoona hali inazidi kubadilika aliingia ndani na punde tu akatoka akiwa ameshika ile bakora yake.
"Ingieni ndani msitoke hadi tutakaporejea."alisema Faraj akiwataka Maya na Malkia waingie ndani. Haraka wakanyanyuka pale walipokaa na kuelekea ndani huku Samir pamoja na Faraj wakienda kuangalia kulikoni.

Hawakuwa na huruma askari wale wa Mfalme Faruk kila mtu aliyeleta kipingamizi kuwazuia walimkita upanga wa tumbo na kupoteza maisha ya watu. Watu walikimbia kwenye nyumba zao wakihofia kuuawa maana askari wale hawakuonesha mchezo kwenye jambo hilo. Samir na Faraj walipokaribia eneo husika walipishana na watu waliokuwa wakikimbia kuelekea walipotoka wao. Baadhi ya askari walipata kumuona Samir hali iliyowafanya wawataarifu na wenzao kwamba mmojawa wale wanao wahitaji wamepata kumuona. Ikawabidi wasogee pamoja wakimtazama Samir akiwa anakuja bila wasi. Askari wale walitazamana huku wakiachia tabasamu kuona mtu wao anajileta mwenyewe. Wakashuka kwenye farasi wao huku wakiwa wameshika mapanga kila mmoja.
Faraj alitazama pembeni na kuona baadhi ya raia wake wameuawa na askari hawa,alijisikia vibaya sana maana yeye ndio mtu wa kuwalinda watu wake wasipatw e na matatizo lakini ameruhusu waumizwe na hata kupoteza maisha.
"Faraj hawa mimi nawamudu wewe rudi kule ukawaangalie Malkia na Maya kwa usalama saidi."alisema Samir akiwa anatazama askari waliokuwa mbele yao. Hakuweza kukubaliana na maneno haya ambayo hayakumuingia akilini kabisa. Aliona askari wale wakianza kuja kwa kasi lengo ni kuwavamia pale waliposimama,walipokaribia tu Faraj akanyanyua bakora yake na kuishika kwa mikono miwili gafla tu ikabadilika na kuwa upanga mkali wenye kumeremeta. Samir alitoa upanga wake na waliposogea wale askari mapanga yakaanza kuchukua nafasi yake. Faraj pamoja na udogo alionao lakini alikuwa yupo vizuri kwenye kupambana jambo lililowaacha askari wale washangae maana hawakumdhania kama ataweza kuwapa changamoto kama hiyo. Askari hao walikuwa na umoja hasa baada ya kuona wanapambana na watu wanaojua kutumia upanga vizuri. Na muda huohuo Mfalme Siddik ndio alikuwa akiwasili katika kijiji hicho hju akifuatwa na askari wake akiwepo Generali pamoja na Jamal. Walipatwa na mshangao baada ya kuona baadì ya nyumba za kijiji hicho zikiwaka moto huku kelele za watu zikisikika. Hali hiyo ikameanya Mfalme ashangae. Iliwabidi wazidi kusogea mbele kujua imekuwaje. Huku Faraj alizidi kuonesha umahiri wake kwa kila anayesogea mbele yake anakata. Alipoona wanazidi kuja kwa wingi akaamua kuzitumia nguvu zake za kichawi kuzidi kuwapunguza askari hao. Alimfanya hata Samir naye afanye hivyo tena kwa uwezo wa hali ya juu. Alimudu kuachia pigo moja lililoweza kuwadondosha askari wanne kwa pamoja huku macho yake pamoja na Faraj yakibadilika na kuwa makali sana. Na muda huohuo Mfalme pamoja na askari wake kwa ujumla wakapata kufika kwenye tukio hilo na kushuhudia kwa macho yao jinsi Samir alivyobadilia na anavyopambana na watu wale. Jamal kuona vile akataka kwenda kutoa msaada kwa Samir ili baadae wapate kumkamata lakini Mfalme akamtuliza ili wapate kuangalia zaidi pindi Samir anapotumia nguvu zile akiwa sambamba na kiongozi mdogo Faraj.
ITAENDELEA.
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN 39

Hakuna aliyetegemea kumuona Samir akiwa anapambana na askari wale kwa uwezo ule. Jamal alibaki kushangaa kile ambacho anakiona mbele yake. Alikumbuka siku ile ndani ya uwanja akiwa anapambana na Samir na kuanza kuhisi huenda nguvu hizi ndio zimemsaidia Samir hadi kuja kuwa Mlinzi wa binti wa Mfalm. Kwa kujua hilo akataka kujenga mazingira ya kujiaminisha kuwa yeye ndio alistahili kupata nafasi hiyo.
"Huyu mtu anaonekana ni muda mrefu anatumia nguvu hizi,tazama jinsi alivyo mzoefu katika kupambana huku akitumia uchawi."alisikika Generali akiongea na kumfanya Mfalme azidi kuamini kwa kile anachokiona mbele yake. Hawakuwa wanafahamu lolote kama wanaangaliwa muda huo. Walifanya kile wanachokiona kwao kitaleta amani katika kijiji hicho lengo ni kuwamaliza askari wale maana wamekuja kwa nia ya kuua watu. Muda mfupi tu waliweza kuwamaliza wote huku wakionekana kuchoka kwa kupambana. Wakiwa kwenye hali hiyo makofi yalisikika mfululizo na kuwafanya wageuke kutazama sauti hiyo inapotokea. Walipatwa na mshangao baada ya kumuoni Mfalme akiwa anaendelea kupiga makofi kuashiria amefurahishwa na uwezo walio uonesha wawili hao kwa kuwamaliza askasi zaidi ya ishirini. Waligeuka kutazamana baada ya kufahamu kile walichokifanya kimepatwa kuonekana na watu wengi.
"Safi sana,nimependa mbinu mlizotumia."alisema Mfalme akionesha tabasamu usoni mwake. Dakika chache kupita alibadilika na kuwa na sura ya hasira.
"Siku zote umekuwa mkimya kumbe ulikuwa ni miongoni mwa wanaotumia uchawi! Nilitokea kukuamini sana lakini baada ya kupata wasiwasi juu yako na leo ndio nimeiaminisha nafsi kwa kile nilichokuwa nakifikiria. Binti yangu hawezi kulindwa na mchawi hata siku moja,kufanya hivyo ni sawa na kuruhusu uchawi ndani ya falme yangu.... Lazima uadhibiwe kama sheria ya Eden inavyofuatwa ka yeyote yule aliyejulikana ana nguvu hizo,mkamateni haraka."alitoa amri hiyo Mfalme na haraka askari wakashuka kwenye farasi na mapanga yao wakaharakisha kumsogelea Samir pale aliposimama. Faraj kuona vile alisimama mbele ya Samis kuzuia kile kinachotaka kutokea.
"Mbona unabadilika hivyo Mfalme wa Eden? Huyu mtu pamoja na binti yako si uliwafukuza katika taifa lako wasikanyage tena! Haitoshi ukawapa adhabu ya kutupwa kwenye msitu wenye wanyama wakali mkijua fika hawataishi hata siku isingeisha wangeliwa na wanyama wa porini. Imekuwa ni bahati leo ni wazima na baada ya kutambua kwamba hawatakiwi Eden wamekuja hapa kuanza maisha yao mapya. Na hadi sasa hawa watu wanajulikana ni wa kijiji changu. Nakuheshimu kwakuwa ni Mfalme wa Taifa kubwa, waache watu wangu waishi kwa amani, kama uliwakataa ukaona hawastahili kuishi Eden basi huku hawa watu wanaheshimiwa na watu wote hapa kijijini."alisema Faraj kwa kujiamini sana na maneno yake yenye ukweli ndani yake yalianza kumwingia Mfalme na hata Generali aliyeko pembeni anatazama kinachoendelea.
"Unaongea nini wewe mbele ya Mfalme? Unapanga sheria zako mbele ya utawala wa Eden!"alifoka Jamal na kumfanya hata Mfalme ageuke kumtazama maana alikosa la kusema.
Faraj alimtazama Jamal akionekana kukereka kwa kile kilichozungumzwa.
Kwa kumtaza tu kwa muda akapata kumtambua vilivyo hata lengo lake.
"Mtoto wa Mfalme Faruk, Mfalme mwenye kutamani siku moja kuupindua utawala wa Eden kisha ammilikishe wewe. Hivi kabisa umeamua kuacha heshima ya kuitwa mtoto wa Mfalme ambaye siku moja utakuja kurithi nafasi ya baba'ko. Lakini ukajitoa kwenda kugombania nafasi ya kuwa mlinzi wa binti wa Mfalme wa Eden. Ulijua utakapofanikiwa kupata nafasi ya kumlinda Maya ndio mtakayemtumia katika kufanikisha mambo yenu."alisema Faraj na maneno yale yalimshtua Mfalme.
Jamal kusikia vile alipata mshtuko baada ya kujua tayari siri yao imevuja.

tena mbela ya Mfalme Siddik.
"Unaongea kuhusu nini wewe!"alikuja juu Jamal akitaka kujitetea kwa kile kilichozungumzwa na Faraj.
"Huo ndin ukweli,upo Eden kwa maslahi ya taifa lako wewe na bac yako. Kitendo cha Samir kuwa mlinzi wa Maya kiliwauma sana na mmekuwa mnafanya njama za kummaliza Samir,hata walipoadhibiwa kutupwa msituni mlikyuwa mnafuatilia kila hatua kujua kinachoendelea.
"Acha mara moja kutupakazia mabaya ili upate kuonekana mwema kwa Mfalme Siddik. Samir amekutwa na uchawi na lazima sheria ya Eden ifuatwe maana huyu ni mti wa Eden tu."aliongea Jamal akizidi kujiwekea mazingira ya kutojukana.
"Ahaa,kama unaongea mbele ya Mfalme uongo wako unadhani nani atamuamini hata siku ukaja kuwa kiongozi wa Eden maana hilo ndilo linalowafanya msilale siku zote,mmewatuma askari wenu kuja kummaliza Samir ili mpate nafasi ya kuonekan bora kwa Mfalme."alisema Jamal na kusogea kwa askari mmoja aliyekuwa chini amekufa kisha akavua nguo yake ya juu, vazi lililopo ndani liliwafanya watu wote wa pale washangae. Hapo ndipo Jamal akakosa la kusema baada ya kuonekana askari wa taifa lao wakiwa kwene vazi hilo. Walikuja kwa nguo tofauti ili wasipate kujulikana na hatimaye imekuwa tofauti.
Mfalme Siddik alistaajabu kuona tukio hilo mnele ya macho yake,alimgeukia Generali ambaye hakuwa na la kusema akabaki kuwa kimya muda wote.
"Hapana.. Hapana.. Hii ni njama tu na hakuna ukweli wowote. Mfalme nakuhakikishia baba yangu ni rafiki mkubwa sana kwako na hawezi kufanya hivi. Hawa wametengeneza hili swala amini ninayokwambia. "alisema Jamal akiwa mwenye kujitetea muda wote. Mfalme aliwaamuru askari kadhaa kwenda kuihakiki ile miili ya askari wanaosadikika ni wa Mfalme Faruk. Walisogea hadi pale na kupekuwa baafhi ya alama na hata mavazi yale ukweli ukabaki kuwa palepale kwamba ni watu wa Mfalme Faruk. Alisikiyika sana Mfalme Siddik baada ya kuona hata rafiki yake kumbe anaombea mabaya na kuitamani taifa la Eden. Alikasirika sana kusikia hivyo na muda huohuo akatoa amri Jamal akamatwe mara moja,askari wakafanya hivyo kama alivyotoa amri Mfalme ya kumkamata Jamal. Alizidi kukataa kwamba jamvo lile wamelitengeneza Samir na Faraj ili wazigombanishe Falme hizo mbili lakini kwa Mfalme hakuweza kuamini hilo. Muda huohuo walimfunga kamba na kumuweka kwenye farasi askari kadhaa wakaanza kurejea naye Eden wakamuweke selo wasubiri kitakachoamuriwa.

Mfalme alikosa hata la kusema baada ya kutambua ukweli kwamba Eden yake inamezewa mate na falme za jirani. Alinitokeza Malkia Rayyat akiwa sambamba na binti yake Maya wakifika katika eneo lile. Mfalme alipomuona binti yake moyo wake ulikumbwa na wimbi la faraja kuamini kweli yuhai. Bila kujali lolote Maya alisogea hadi alipo Samir na kumkamata mkono kuonesha yuko pamoja naye.
"Nimejaribu kumueleza binti yako kuhusu amri yako uliyotoa ya wao kurudishwa Eden lakini imekuwa kinyume kwao. Hivyo sikuweza kuwalazimisha baada ya kuona wanaishi kwa amani. Hakuna haja ya kuwasumbua tena kama umeshaamuru kuwa ni haramu kwao kukanya Eden basi huwezi ukawachukua kuwaadhibu watu uliowatoa sadaka. Nimekaa hapa kwa muda mchache tu lakini najiona mwenye amani pia,uchawi unaotumiwa na watu hawa ni kwaajili ya kusaidia katika matatizo na kujihami mbele ya adui zao, sijaona sababu ya kuchukia tena jambo hili kama limekuwa na faida kwa watu, nitafurahi sana nikiishi hapa muda mrefu na si kurudi tena Eden, Faraj... Ningetamani kupata ruhusa kutoka kwako ya kunifanya niwe raia wa kijiji hiki,hakika nitashuru kama utanikubalia."alisema Malkia Rayyat na kuwafanya watu wote washangae kwa kauli yake hiyo. Mfalme Siddik alishtuka kusikia hivyo,hakutaka kabisa swala hilo litokee hata kidogo. Lakini kwa Malkia alikuwa anamaanisha kweli kile alichoongea,hakuona hamu ya kuendelea kukaa katika taifa ambalo hana furaha angali mwanaye anaishi mbali naye.
"Hapana sitapendezwa na jambo hilo,haitaleta picha nzuri kuona Malkia wa taifa langu anaishi mbali na sehemu yake,tafadhari naomba usifanye hivyo."alisema Mfalme akionesha upendo kwa mkewe. Mtu wa pekee anayepaswa kuruhusu hilo alikuwa ni Faraj, yeye ndiye mwenye kuamua kumkubalia Malkia aishi Gu Ram au laa. Hata yeye alikuwa kwenye wakati mgumu juu ya swala hilo huku Malkia akionesha msimamo wake wa kuwa upande wa binti yake. Mwisho wa siku ikambidi atumie busara na hekima ili kulifanikisha swala hilo kila mmoja apate kuridhia.
"Nafasi ya Malkia kuishi hapa ni kubwa mno maana ameshapata kutambua mji huu ni wa amani. Ila ningependa kutaka jambo kwa Mfalme, endapo Malkia akiondoka nawe Eden basi Maya na Samir sitataka wasumbuliwe tena. Na endapo Malkia akiishi hapa basi sitaruhusu mtu yeyote kutoka kwenu kuja kuleta vurugu kwa hawa watu. Hivyo nakupa nafasi hizo mbili uchague moja wapo."alisema Faraj huk akimtazama Mfalme. Alimtazama Generali akiwa naye anamuangalia Mfalme ili apate kuamua moja kati ya hayo mawili. Aliitazama familia yake ikiwa pale karibu na Faraj na kupata picha kwamba taifa lake si lolote japo linapendwa na wengi. Kama hata familia yake inakataa kurejea Eden ni wazi kwamba kuna tatizo ambalo anahitajika kulifanyia kazi.
Aliona afanye maamuzi magumu ambayo aliona ndio sahihi kwake na hakutaka kupigwa na yeyote.
NI MAAMUZI GANI ATAYACHUKUA MFALME?USIKOSE SEHEMU IJAYO
 
* SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN* 40

Alirudi nyuma na kupanda kwenye farasi wake huku watu wakimuangali. Alimtazama Malkia akiwa amesimama karibu na Faraj.
"Utaishi hapa kuanzia sasa, ila fahamu bado utabaki kuwa Malkia wa Eden siku zote. Wewe ni mkewangu na siku zote itabaki kuwa hivyo."alisema Mfalme n kuamuru jeshi lote alilokuja nalo ligeuze kurejea Eden. Walitii amri hiyo askari wote huku baadhi yao wakistaajabu kwa uamuzi aliouchukua Mfalme kwa kumruhusu Malkia kuishi Gu Ram. Generali alishangaa sana kwa jambo. Ni wazi kwamba Mfalme ameiacha familia yake pamoja na Samir kuwa huru waishi huru. Generali walifuata na askari wengine kurejea sasa Eden wakiongozwa naMfalme baada ya kuamuru Malkia na wengine waachwe pale.
Maya alimsogelea mama yake na kumkumbatia baada ya kufahamu wapo hutu kwasasa kuishi kijijini hapo. Samir aligeuka kumtazama Faraj aliyekuwa akiangalia majeshi yale ya Eden wakitokomea kabisa kwenye kijiji chao.

Baada ya muda iliwabidi wawape taarifa watu ambao muda wote walikuwa wamejificha ndani ya nyumba zao. Taratibu wakaanza kutoka kwenye makazi yao na kuanza kuzunguka kuhakikisha usalama. Waliona watu wengi wameuawa pale chini wakiwa wanapambana, iliwabidi wawakusanye na kwenda kuwatupa kwenye mto maana hawakutaka kuwazika katika ardhi yao watu ambao walidhamiria kuwaua.
Kwa umoja wao wakaanza kusaidiana kujenga upya baadhi ya nyumba ambazo zimepatwa kuchomwa moto na watu wale waliovamia. Malkia pamoja na mwanaye walikuwa mstari wa mbele katika kwenda kutafuta miti ya kujengea nyumba za wananchi. Watu waliomfahamu kwa heshima aliyonayo kama Malkia hawakutegemea kama anaweza akafanya kazi hizo na watu wa kawaida jambo ambao yeye binafsi hakutaka litokse. Alikuwa karibu na watu akishirikiana nao katika matatizo hayo yaliyowakumba.
Jioni ya siku Faraj aliwakusanya wananchi wake nje ya nyumba yake na kuanza kuwapa maneno yenye busara na kuwatoa hofu kwa kile kilichotokea siku hiyo. Aliwapa ujasiri wa kutoogopa watu ambao wanaingia katika ardhi yao kwa lengo la kuwadhuru.

Taarifa za kuuawa kwa askari wake aliowatuma katika kijiji kile zilimfikia Mfalme Faruk pindi Lutfiya alipomtumia ujumbe kama ilivyo kawaida yao. Kubwa na lenye kumpandisha hasira ni pale alipoambia kuwa mwanaye Jamal amekamatwa kwa kujulikana lengo lao hasa ni kuupindua ufalme wasasa wa Siddik. Alipandwa na hasira zisizo na kipimo akitambua kwa vyovyote mwanaye atapewa adhabu ya kuuawa, alishindwa kukaa mahala pamoja kila akifikiria jambo lililompata mwanaye. Usiku huo aliamua kupanga majeshi yake yote lengo ni kuivamia Eden kuweza kumtoa mwanaye katika kifungo hicho. Askari wote walijiandaa ipasavyo wakiweka silaha zao vema tayari kwa safari ya kuelekea Eden. Baada ya muda Mfalme alitoka na kusimama mbele ya jeshi lake kuwapb maelekezo.
"Kila mtu afahamu anaenda kupambana lengo ni kumkomboa Jamal,wamemkama baada ya kujua ukweli kwamba tunampango wa kuipata Eden. Hivyo basi kwa hili tunalokwenda kulifa nya tukifanikiwa kuwadhibiti jeshi la Eden basi tumefanya kazi moja kwa faida mbili. Nadhani ndio utakuwa usiku wa kuipindua Eden na kuitawala. Itakuwa ni sherehe kubwa kwetu kwa kufanikiwa jambo letu, kila mtu awe na moyo wa ujasiri kathka hili, T U N A I N G I A V I T A N I I I."alisema Mfalme Faruk na askari wote wakapata morari wa kufanya kile walichoambiwa, walipiga kelele za kushangilia kwa kile kilichoelezwa na Mfalme. Bila kucgelewa Mfalme aliongoza safari hiyo na askari wote wakafuata nyuma wakiwa kwenye farasi huku mbaramwezi ikiangaza usiku huo.

Upande wa pili Mfalme Siddik aliongozana na Generali hadi kwenye selo ambayo Jamal amehifadhiwa. Alikuwa mwenye hasira sna pindi alipotambua kwamba lengo la Jamal kuja Eden ni kuweka mazingira ya kuudidimiza ufalme wa sasa wa Eden. Walimkuta akiwa amefungwa kamba mikononi na kunin'ginizwa juu akionesha kuchoka sana. Mfalme alimsogelea hadi pale akiw a amekunja sura.
Alimpiga ngumi ya shavuni na kumfanya Jamal ayasikie maumivu hayo huku damu zikianza kumtoka. Generali alibaki kushuhudia tu kinachoendelea..
"Inamaana lengo lenu ni kuja kunipora uongozi wangu mjimioikishe! Kwanini hamridhiki na Taifa lenu mkalijenga na kuliendeleza! Kipi kimewafanya hadi muitamani Eden yangu?"aliuliza Mfalme akiongea kwa hasira sana lakini Jamal hakuweza kuongea lolote. Hali hiyo ilimfanya Mfalme azidishe hasira, alishusha ngumi nzito iliyotua tumboni kwa Jamal aliyeugumia kwa maumivu anayosikia.
"Nieleze ukweli kitu gani kinawafanya muitamani Eden!?"alifoka Mfalme kwa hasira hadi Generali akafahamu hapa Jamal anaweza kuuliwa kwa hasisa alizo nazo Mfalme. Alitamani kuingilia lakini huwezi kumzuia Mfalme pindi afanyapo jambo lake. Hasira za Mfalme hazikuwa ndogo,alizidi kumpiga Jamal akiwa pale amefungwa kamba lengo ni kumtaka aseme sababu hasa za kutaka kuivamia Eden.

Huku mashariki na mbali, Dalfa baada ya kufanya mambo yake kwa uwezo alionao akapata wazo la kurejea tena Eden, aliona njia rahisi ya kumpata Samir ni kumfanyia jambo Mfalme Siddik. Alijua kwa kufanya hivyo lazima binti yake Maya ambaye ndio yupo sambamba na mtu wake lazima atataka kwenda kumuona baba yake na itafanya waongozane pamoja na Samir na hapo atapata kufanikisha swala lake.
Safari hii alichukua nguvu na silaha zake zote akiamua kulivalia kibwaya jambo hilo na hakutaka kufeli tena. Aliingia kwenye mahala pake pa kufanyia ibada na kufanya maombi yake apate kupotea pale alipo atokee karibu na Eden aikamilishe kazi hiyo.
Huku majeshi ya Mfalme Faruk yalizidi kuja kwa kasi huku mwenyewe akionesha kuwa na hasira sana,kila akimfikiria kijana wake na kuhisi huenda anapata mateso makubwa usiku huu. Alijikuta akizidisha kasi kwa farasi wake kusudi awahi kumkomboa mwanaye.
Huku Eden ulinzi uliendelea kama kawaida wakihakikisha usalama wa raia. Hata ndani ya falme kila kona askari walitanda kuweka ulinzi. Muda huo Mfalme Siddik alikuwa zake chumbani kwake akitafakari mambo yanavyoenda. Mpaka muda huo Jamal hakuweza kusema lolote lile na kumfanya Mfalme awakabidhi askari wake kumuadhibu hadi apate kusema wanamipango gani wa kutaka kumpindua yeye na falme yake. Aliumiza kichwa sana na huku akiwa mwenye hasira kuona rafiki yake Faruk amethubutu kuitaka Eden aifanye kuwa ni kiongozi.
"Kamwe sitakubali mtu baki kuja kuichukua Eden hata awe nani, kama Siddik nipo hai hakuna wa kuitawa Eden yangu, hakuna.."aliongea Mfalme akiwa anaweka msisitizo.
Baada ya muda kupita usiku ukizidi kuwa mkubwa, Lutfiya alichukua chakula na kuanza kuelekea mahala alipohifadhiwa Jamal. Tangu alipokamatwa hakuweza kupata chakula chochote hadi kufika usiku ule. Alinyata huku akiwa makini asije akaonwa na askari mahala anapotaka kwenda. Alifika hadi karibu na selo ile na kupata kuona walinzi wawili wakiwa wamesimama mlangoni macho makavu wakiwa makini kuhakikisha Jamal ndani ya selo hatoki. Aliumiza kichwa afanyaje kuwatoa askari wale lakini hakupata njia sahii ya kufanya. Gafla alishangaa anazibwa mdomo na mtu nyuma yake na kugeuzwa, alishtuka kumuona ni Generali aliyekuwa pale. Alishikwa mkono kusogezwa pembeni kwanza huku akiwa ameshika chakula kile.
"Umefuata nini huku usiku huu?"aliuliza Generali akimtashangaa Lutfiya. Alibaki kujin'gatan'gata maneno akijua tayari amekamatwa.
"Huku hakuruhusiwi mtu yeyote kufika, ni hatari kwako ukikutwa huku muda huu."alisema Generali.
"Nisamehe Generali, ila sikuja kwa niya mbaya nilibeba hiki chakula kwaajili ya yule askari aliyekamatwa, bila shaka atakuwa mwenye njaa maana ni muda yupo humu bila kula."alisema Lutfiya akiongea kwa huruma. Generali alikitazama chakula kile na kuona ni kweli. Alichukua chakula kile na kumtazama Lutfiya alikuwa akitazama chini kama heshima.
"Kitafika usijali,usingeweza kumpatia chakula hiki maana askari walikatazwa asipewe chakula na mtu yoyote. Haya rudi haraka usije ukakuwa huku."alisema Generali na kumfanya Lutfiya ashukuru kwa kusaidiwa kazi hiyo. Alipopiga hatua kadhaa mbele akasimama, kwa huruma aliyooneshwa n Generali aliona naye ampashe habari yenye kuyalinda maisha yake. Aligeuka nyuma kumtazama Generali aliyebaki kushangaa kuona amesimama.
"Huenda usiku wa leo kukamwagika damu hapa Eden, kuwa makini na maisha yako Generali."alisema Lutfiya kwa mafumbo kisha akageuka na kuondoka haraka eneo lile.
Alibaki kushangaa kwa maneno aloambiawa na msichana huyo.
"Usiku wa leo kukamwagika damu? Eden hii au? Anamaana gani kusema maneno haya ya kutisha?"ni maswali ambayo Generali hakuweza kuyapatia jibu na kubaki kutazama njia aliyoondokea nayo Lutfiya. Alitazama chakula kile kwa muda huku fikra zake zikihama kwa kile alichoambiwa. Aliamua kuondoka na kusogea hadi kwenye ile selo na wale askari wakampa heshima kama mkubwa wao. Alifunguliwa mlango na kuingia ndani ambapo alimkuta Jamal akiwa dhoful hali,kwa kipigo alichopata kilimfanya awe hoi huku damu nyingi zikimtoka mwilini mwake. Huruma ilimjia Generali huku akimsogelea kijana wake,alimtazama jinsi alivyochakazwa kwa kupigwa hadi kukosa nguvu ya kusimama vizuri. Alijitahidi kunyanyua sura yake na kupata kumuona Generali akiwa mbele yake.
"Ge ne ra liih... Nitoe hapa..wananiua hawa. Mfalme ataniua!"alitoa sauti ya upole na yenye huruma ndani yake Jamal akihitaji msaada wa kutoka pale alipo. Generali hakuwa na namna ya kumsaidia muda ule. Alifungua kile chakula na kuanza kumlisha Jamal akiwa vilevile amesimama.
"Amekileta Lutfiya hiki chakula,na kuna maneno ameniambia ambayo sikuweza kuyaelewa hadi sasa..* Huenda usiku wa leo kukamwagika damu hapa Eden, kuwa makini na maisha yako Generali.*. Maneno haya yameniacha njia panda sijafahamu anamaanisha nini."alisema Generali huku akimlisha Jamal kile chakula. Aliposikia vile alianza kufurahi Jamal na hata kucheka baada ya kusikia hivyo. Akazidi kumshangaza Generali aliyekuwa anamtazama tu.
"Wanakuja... Wanakuja kuipindua Eden. Ni kweli damu zitamwagika, na endapo nikitoka katika mateso haya Mfalme atakuwa ni sadaka kwa usiku wa leo."alisema Jamal akionesha dhahiri kuwa na hasina na Mfalme Siddik. Hapo ndipo Generali akapata kutambua kumbe kauli ile ya Lutfiya ilikuwa na maana kubwa namna hiyo. Hapo ndipo akafahamu huenda swala hili limepangwa na watu wengi akiwemo msichana huyo Lutfiya aliyekuwa akiishi humo muda mrefu sana.
NINI KITAJIRI HAPO EDEN.. DALFA NAYE HUYOO..
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN 41

"Inamaana hata huyu msichana mnafahamiana naye?"aliuliza Generali na kumuona Jamal akitikisa kichwa kumaanisha ndilo jibu sahihi.
"Nadhani mzee alikuwa na maana kubwa kuongea nawewe na kukueleza mengi kuhusu mimi, nadhani muda ndio huu, naomba uwe upande wangu kuhakikisha swala hili tunalikamilisha."alisema Jamal huku akimtazama Generali akiwa ameshika chakula kile. Alimuweka katika wakati mgumu wa kutafakari swala hilo kwa umakini zaidi.
Dalfa aliweza kuwasili Eden mapema sana baada ya kutumia nguvu za kichawi kumtoa kule mashariki na mbali.
Usiku huo bila kuchelewa alianza kusogea kwenye falme ili kutimiza azma yake. Muda huo kila raia alikuwa amepumzika ndani kwake mji mzima ulikuwa kimya huku vishindo vya askari vilisikika wakiwa wanatembea huku na kule kuhakikisha usalama. Alitembea bila kuhofia lolnte Dalfa, alipishana na askari njiani bila kumsimamisha kuhoji. Ni wazi kwamba amedhamiria kufanya jambo hilo kwa uwezo wake unaomfanya aogopwe na kila mtu uwezo alionao ulimfanya asionekane na askari yeyote hadi alipoingia ndani ya falme husika. Moja kwa moja alielekea chumbani kwa Mfalme akijua kwa muda huu lazima atakuwa amejipummzisha.
Na muda huo Mfalme alikuwa kitandani usingizi hauji abadani kila akifikisi matukio yanayomkabili. Hadi sasa anaishi mbali na familia yake jambo ambalo hakuwahi kufikiria kama lingeweza kutokea. Ilikuwa ni familia ya furaha pindi waishipo pamoja,lakini furaha imepotea baada ya binti yake kugundulika kuwa na mahusiano na mlinzi wake. Alijikuta akisikitika tu kwa kile kilichotokea maana ni aibu na pia adhabu ile ilimgusa moyoni kama mzazi. Hukuwa na la kufanya kwa binti yake kama msaada wa kuikwepa adhabu hiyo jambo ambalo alihisi ndio sababu ya Malkia kuchukia na hata kutotamani aendelee kuishi tena Eden hasa baada ya kutambua binti yao yumzima
Akiwa kwenye kutafakari hayo alipata kuona taa inaanza kufifia mwanga na mwishowe kuzima yenyewe. Alishangaa kuona hali hiyo ambayo haikuwahi kutokea hapo awali. Gafla ile taa ikawaka tena mwanga mkali na kufifia tena gafla, ikawa ni kama mchezo hali ambayo ilimtia hofu Mfalme na kuinua pale kitandani kusogea karibu na taa. Alipotaka kuishikaa gafla ikazima na kufanya giza lichukue nafasi yake mule chumbani. Upepo ukaanza kuvuma nje na hali ya hewa gafla ikabdilika na matone ya mvua yakaanza kudondoka taratibu na hatimaye ikanyesha kubwa kabisa. Muda huo Mfalme Faruk ndin alikuwa anaingia ndani ya Eden huku akifuatwa na majeshi yake yaliyokuwa moto kupambanda siku hiyo ili wamkomboe mtoto wa Mfalme wao.
Huku Mfalme hali ile ilimfanya apatwe na hofu kuona hali ya hewa kubadilika gafla,radi za kumulika mwanga zilirindima na kufanya Mfalme apate akili ya kwenda kufunga madirisha. Alipofunga dirisha na kugeuka nyuma alipata kushtuka baada ya kuona kuna mtu amepita mbele yake na kupotea. Alitoa macho kutazama vizuri huku akiangalia huku na kule bila kuona kitu. Ilimbidi apapase hadi kufika kwenye droo ya kabati na kuchukua tochi, akawasha na mwanga ukaweza kumulika chumba kile huku akimulika huku na kule kuangalia kama kuna anayemfanyia vitisho hivyo. Punde tu mwanga wa taa ukarejea na kurudi kama awali hali iliyompa imani ya usalama Mfalme na kumtoa hofu. Aligeuka kurudisha tochi ile ambayo ilimsaidia kwa muda mchache sana. Alipotaka kurudi zake kitandani kupumzika alishangaa kumuona mtu mbele yake akiwa amesimama, ilimbidi amtazame kwa makini kumuangalia, alishtuka baada ya kumfahamu mtu yule aliyeko mbele yake.
"Unashangaa kunikuta muda huu nipo hapa ndani kwako?"
"Dalfa! Nimi kimekuleta Eden, na umefuata nini hapa ndani kwangu?"aliuliza Mfalme baada ya kumtambua Dalfa ndiye aliyeko mbele yake.
"Shida yangu ni kumpata Samir kwas asa, ila nitataka nitataka kitu chengine hapo baadae. "alisema Dalfa huku mvua kubwa ikinyesha.
"Samir hayupo Eden, na sidhani kama ataweza kurejea tema katika ardhi hii. Sasa sijui utampataje."alisema Mfalme akimtazama Dalfa.
"Ni rahisi kumpata,na ipo siku atakuja tu akiwa na binti yako."alisema Dalfa na kuanza kubadilika macho kuwa ya kutisha. Mfalme kuona vile akajua ni uchawi anaotumia Dalfa. Akataka amuwahi akihofu kudhurika, alikimbilia upanga wake na kuushika vyema akageuka kupambana na Dalfa, ajabu hakuweza kumuona tena mule ndani hali iliyomfanya ageuke kila pande kutazama bila kumuona. Dalfa alitokea nyuma ya Mfalme na kuanza kupandisha uchawi wake mikononi akidhamiri kumuwekea Mfalme Siddik ambaye alipogeuka tu alishuhudia akikabwa shingo yake kwa mkono. Alitaka kunyanyua upanga wake lakini haukuweza kunyanyuka, ni wazi kwamba Dalfa amezuia hilo. Taratibu uchawi ule ukaanza kushuka na kuingia mwilini mwa Mfalme.
Baada ya muda aliachiwa na hapo Dalfa akajua tayari lengo lake limetimia. Mfalme akawa anafurukuta pale alipoachwa,alienda chini kwa kupiga magoti huku akihisi vitu vizito vinazama kwenye koo lake na kumfanya ashike shingo yake kujaribu kuzuia vile vitu anavohisi kuzama ndani lakini haikuwa rahisi. Hali ile ilimfanya hata ashindwe kupumua vizuri na gafla akadondoka chini kwa kukosa pumzi ya kutosha. Dalfa alitabasamu baada ya kufanikisha azma yake. Alijua kwakufanya hivyo lazima familia ya Mfalme itafika kujua hali yake na Samir hatamuabha Maya pekeake lazima ataongozana naye. Aliweka mipango yake swa mule ndani ya chumba kile akikijaza uchawi ili hata akiondoka apate kujua kinachoendelea siku zote. Alipokamilisha zoezi lake gafla tu akapotea kurudi Mashariki na mbali.

Mfalme Faruk alitoa amri kwa askari wake waanze mashambulizi ya kupambana na askari yeyote anayewazuia wao kuingia ndani ya falme kuweza kujua kuna vita nje inaendelea. Majeshi ya Eden yakaanza kutoka ndani ya falme sasa kwenda nje kuwapa msaada wenzao,hakika hilikuwa ni vita ya aina yake usiku ule huku mvua ikizidi kushika kasi. Wafanyakazi ndani ya falme wakawa wanarandaranda huku na kule kila mmoja akijaribu kuyaokoa maisha yake.
Lutfiya baada ya kufahamu hali imeshabadilika alianza kufanya mipango ya kurejea tena kule selo alikofungwa Jamal.
Moja kwa moja Generali alitoka na askari watano na kwenda kumuwekea ulinzi. Hata alipofika alibisha hodi lakini hakuweza kujibiwa. Ilimbidi aufungue mlango na kuingia hadi ndani ambapo alimkuta Mfalme akiwa kitandani amelala. Alisogea hadi pale na kuanza kumuamsha huku akimweleza hali iliyopo huko nje. Ajabu kila anavyozidi kuongea haoni dalili za Mfalme kuweza kuamka,akahisi huenda amepatwa na tatizo haraka akamgeuza Mfalme na kushangaa kuona ni wa baridi mwili mzima. Alipeleka sikio lake kifuan i kusikiliza mapigo ya moyo lakini jibu alilolipb lilimfanya ashtuke bila kuamini. Aligeuka kuwatazama askari wake ambao nao walikuwa wakimtazama na kupata kujua huenda Mfalme amepatwa na tatizo. Generali alibaki kujiuliza na imekuwaje hadi Mfalme kuuawa angali watu waliowavamia hawajaingia ndani ya Falme. Aliyakumbuka maneno ya Lutfiya muda ule na kuhisi huenda ndiye mtu pekee aliyefanya mauaji hayo,ni wazi kwamba Mfalme amefariki kwa kile anachokiona mbele yake. Alipandwa na hasira sana maana hakutegemea kama atampoteza kiongozi wake kwa namna hiyo. Ilimbidi atoke kwa hasira na kutokuwa na huruma tena juu ya kile alichoombiwa na Jamal alitoka akiwa mwenye jazba huku askari wale wakimfuata. Hata alipofika nje aliutoa upanga wake na kuanza kukimbia kwenda kuunganana askari wake kupambana na askari wa Mfalme Faruk.
Huku ndani Lutfiya alifika karibu na selo ile na kumuona amesimama askari mmoja tu pale mlan goni akilinda. Alijitwisha ujasiri wa kummudu askari yule na bila kuhofia lolote alijitokeza na kusogea hadi pale aliposimama askari yule. Alimshangaa kumuona msichana huyo akimfuata.
"Unataka nini huku muda huu?"alisema yule askari aliyejazia kwa mwilini wake wa mazoezi. Alishuhudia msichana huyo akimsogelea huku akiwa mwenye kujilegeza kimwili. Alimshika askari yule na kuanza kumpapasa, kwa ujio ule ukamfanya yule askari akizi zihame kutoka kwenye kazi yake na kumtamani Lutfiya. Alishindwa kuvumilia alijikuta akimvuta msichana huyo aliyetoa mguno wa mahaba akizidi kumpagawisha yule askari akajisahau. Jamal alipata kusikia kelele hizo na kujua kuna kinachoendelea hapo nje.
Yule askari alianza kushusha mabusu kedekede kwa Lutfiya aliyekuwa anamvizia askari huyo akae sawa. Alimuacha auchezee mwili wake na mwishowe akamkumbatia kwa mahaba na hapo akatoa kisu kidogo alichokiweka kiunoni na bila huruma akamkita nacho shingoni askari yule aliyepiga ukelele wa maumivu huku akiishika shingo yake na kwenda chini damu zikitiririka. Lutfiya alimtazama tu bila huruma anainama na kuchukua funguo iliyo kiunoni kwa askari yule na kufungua mlango ule wa selo.
Haraka alisogea kwa Jamal ambaye alitabasamu kumuona ni Lutfiya ndiye aliyemsaidia. Alifunguliwa kamba za mikononi na kuwa huru. Alimkumbatia Lutfiya kwa kuweza kumuokoa katika selo ile.
"Wamekuja,Eden yote askari wetu wametanda kupambana na askari wa Eden."alisema Lutfiya akiwa anampatia upanga Jamal.
"Sawa,ngoja nimtafute kwanza Mfalme kwasasa, ila kuwa makini Lutfiya."alisema Jamal akimwambia msichana huyo jasiri, alimuitikia na Jamal akatoka mule ndani haraja kuelekea kwa Mfalme ana hasira naye.
ITAENDELEA.
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN 42

Ilikuwa ni vita ya aina yake huku majeshi ya Mfalme Faruk yakiwa na hasira dhidi ya adui zao. Hawakuwa tayari kupoteza nafasi hiyo kubwa siku hiyo. Walipambana kwa juhudi zote kuhakikisha wanawadondosha askari wote wa Eden. Nao hawakuwa nyuma kuwazuia watu hao na kutokubali Eden ipate matatizo. Ilikuwa ni siku ya kumwaga damu kulinda jina la Eden. Generali alitoka ndani ya falme kuungana na vijana wake kuwamaliza wale wavamizi. Alionesha kuxa na hasira sana hakutaka kuwa na huruma pindi anapoushusha upanga wake kwenye mwili wa mtu. Hali ile ikamfanya Mfalme Faruk ashangae maana walishakaa kuongea naye hivyokitendo anachokifanya Generali ni sawa na kuwageuka. Haraka naye akashuka kwenye farasi na kukamata upanga kuingi vitani. Alikuwa ni mpambanaji mzuri wa kutumia upanga hali iliyofanya kwa muda wa dakika kadhaa kuangusha askari wa Eden tisa huku akizidi kusogea mbele kumfuata Generali.
Jamal alipofika nje ya chumba cha Mfalme akaupiga teke kwa nguvu mlango ukapata kufunguka. Lutfiya alipofika pale alipata kuona Jamal akiingia mule ndani,haraka naye akafuata kupata kushuhudia kinachoendelea. Alisogea mpaka pale alipolala Mfalme na kuanza kumuamsha kwa nguvu apate kumhoji maneno kadhaa kabla hajafanya kile alichokusudia. Kitendo cha kumgeuza Mfalme kilimfanya hata yeye awe na mashaka baada ya kuona mwili ukiwa legevu. Lutfiya alipofika pale alimuona Jamal akiwa anamuamsha Mfalme bila tumaini.
"Amka usinizuge hapa!"alifoka Jamal akihisi Mfalme anaigiza kuwa vile. Haraka Lutfiya akasogea pale na kupeleka sikio lake kifuani mwa Mfalme. Kulikuwa kumetulia hakukusikika mapigo ya moyo akifanya kazi, ni wazi kwamba Mfalme amefariki. Aligeuka kumtazama Jamal alikuwa anashangaa.
"Nini! Nini kimetokea?"aliuliza Jamal akiwa kama kachanganyikiwa.
"Inaonekana amekata roho muda tu."
"Ati nini! Amekufa.? Ah hapana hebu muamshe nami nimuadhibu kwa vile alivyonifanya. Muamshe..!"alifoka Jamal lakini hakukuwa na ujanja. Lutfiya alinyanyuka na kusimama pembeni akimuacha Jamal ahakikishe mwenyewe. Taratibu alisogea hadi pale na kumtazama Mfalme vile alivyo,alishka upande wa moyo wake akapaka kutambua kuwa kweli umesimama. Hasira zote alizokuwa nazo zilipotea zote na kujiwa na moyo wa ubinadamu.
"Imekuwaje mbona sielewi?"aliuliza Jamal akimtazama Lutfiya. Hakukuwa jibu lengine tofauti na kile wanachokiona mbele yao. Ilimbidi arudi nyuma Jamal huku akijiuliza maswali maana hakuna jeraha lolote mwilini mwa Mfalme.
"Tuachane na hili swala twende tukatoe msaada kwa wenzetu huko nje."alisema Lutfiya na kuanza kutoka mule ndani. Jamal hakuwa na jinsi aligeuka naye kutoka nje.
Generali alizidi kuwapunguza askari wa Mfalme Faruk ambaye naye hakuwa nyuma kuwadondosha watu wa Eden huku akiwa anazidi kumsogelea Generali amba e hakuwa anafahamu kama anafuatwa. Hata alipomkaribia walipata kutazamana huku kila mmoja akiwa anahema sana. Walirushiana mashambulizi kadhaa kisha wakasogeleana kila mmoja akionesha kukwazika.
"Mbona unaenda kinyume na tulivyopanga Generali? Inamaana umenisaliti?"aliongea Mfalme huku panga lake likiwa limezuiwa lisipenye mwa Generali.
"Hatukupanga kufanya mauaji kwa Mfalme, tulitaka tumtoe madarakani lakini si kumuua. Mnamtumia Lutfiya ameweza kumdhuru Mfalme na kumuua, sitaweza kukubaliana swala hilo hata kidogo."alisema Generali akiwa mwenye hasira sana.
"Nini...? Inamaana Mfalme ameuawa?"alipatwa na mshangao baada ya kusikia taarifa hizo.
"Unauhakika Lutfiya kama ndiye aliyefanya jambo hilo?"
"Nani mwengine wa kumhisi aliyekuwa na tafauti na Mfalme, alifahamu kama mnakuja ndio maana amerahisisha kazi hiyo. Alijuwa fika kwamba kuna vita itatokea."alisema Generali huku askari wao wakizidi kuchinjana bila huruma.
"Hawezi kufanya jambo zito hilo mwenyewe hana ujasiri huo. Na isitoshe kama Mfalme amekufa hakuna haja ya kumlaumu mt u lengo letu ndio litatimia kwa wepesi,kikubwa wewe ni kuungana nasi tuwe kitu kimoja,utakuwa hata waziri pindi Eden ikiwa mikononi mwetu."alisema Mfalme Faruk akimtamanisha Generali ambaye maneno hayo akayatafakari mara mbilimbili.
Jamal alipotoka mule ndani na bila kuangalia sura ya mtu. Alitumia uwezo wa kutumia upanga kuwapunguza askari wengi wa Eden. Hakika kulionesha kila dalili za Eden kushindwa angali wapo katika ardhi yao,hali iliyofanya Generali atazame majeshi yanavyozidi kupungua kila dakika. Mfalme Faruk akazidi kumshawishi awe upande wao akijua Generali ndiye mwenye kauli ya kuamrisha askari wake nini wafanye.

Wakati yanaendelea yote hayo Faraj pamoja na Samir walikuwa wameshapata ishara kwamba Eden ipo kwenye matatizo.
"Lakini ni haramu kwangu kuikanyaga Eden, tayari tumeshafukuzwa hatuna mamlaka ya kurudi tena."aliongea Samir akiwa anamtazama Faraj wakiwa kwenye jabari wamekaa.
"Siku zote mitihani lazima iwepo katika maisha,tambua kwamba ilikuwa ni changamoto tu ambazo hata huko mbeleni utakumbana nazo. Siku ile nilikueleza kuhusuiana na yale niliyoota kwamba kuna pete unavalishwa,amini kwamba wewe ndiyo Mfalme mpya wa Eden na hakuna mwengine wa kuweza kuisaidia isipokuwa wewe mwenyewe. Wanagombea Eden wakijua kuna Pete ambayo ni muhimu sana pindi ikipatikana, na kamwe hawataweza kuipata maana hawafahamu ilipo."alisema Faraj na maneno yake yakaanza kumfumbua akili Samir.
"Inamaana hakuna anayejua ilipo pete hiyo?"
" Kwasasa hakuna anayefahamu ilipo, niliwahi kufuatilia swala hilo na kusoma vitabu vingi vya kale nikapata kutambua mengi,na nilipokaribia kujua ilipo pete hiyo nilisita, maana ningefahamu ndio ningekuwa kiongozi ila nilishaapa kwamba sitakuja kuio ngoza Eden. Taifa lililoua wazazi wangu nisingeweza kuwa kiongozi wao maana ningehisi nawakosea wazazi wangu."alisema Faraj huku Samir akipata kujua kumbe Faraj alikataa mwenyewe. Alitoa kiboksi kidogo Faraj kisha akampatia Samir.
"Ndani yake kuna funguo, funguo ya kuufungua mti wa ufalme. Mti uliopo ndani ya msitu ule mliotakiwa kuingia mule. Mimi naamini utafanikiwa kuipata pete hiyo endapo utakapoufungua huo mti."alisema Faraj huku akimkabidhi Samir kiboksi kile.
"Ni ule msitu tuliopaswa kutupwa! Mh, na nitaujuaje huo mti kama ndio maana ule ni msitu!"
"Muda wote unaotembea hakikisha hicho kipo nkononi mwako, ndicho kitakuelekeza hadi sehemu husika. Cha msingi ni kuwa makini tu."alisema Faraj akimueleza Samir. Maneno yale yalimlaa akilini na kuona ana kazi kubwa ya kufanikisha zoezi hilo.
"Ila usimweleze mtu yeyote swala hili hata Maya pia, kamilisha kila kitu wewe mwenyewe na hapo ndipo watakapojua."alisema Faraj.
Samir alipata kuelewa na kushika yote aliyoelezwa. Ilimbidi anyanyuke huku akitazama mazingira ya pale walipo ndani ya Gu Ram.
"Wacha nielekee Eden,nikafanye kile ninachokiona ni sahihi na chenye kuleta amani kwa watu."alisema Samir na Faraj akasimama pia huku akimtazama.
"Naamini utafanikiwa, ipo siku utakuja kuwa mkubwa sana katika kutawala."alisema Faraj akimpa mori ya kufanikiwa Samir. Alimpa mkono kama kumuaga na baada ya zoezi hilo akakamata upanga wake Samir na muda huohuo Maya alipata kutokea na kuwaona wawili hao wakiwa wamesamama pale lakini alichelewa. Samir alipotea gafla akimwacha Faraj pale akiwa mwenye kutabasamu.
"Faraj?"aliita Maya na Faraj akageuka kumtazama. Alisogea Maya hadi pale alipo Faraj na kusimama pale alipotoka Samir.
"Ameelekea wapi Samir mbona gafla hivyo?"aliuliza Maya akimtazama Faraj.
"Kuna mahala ameenda ila hatachelewa kurudi."alisema Faraj akificha ukweli. Maya alikuba li maelezo yale na kurudi nyuma akitazama pale aliposimama Samir,akapeleka mkono wake wa kulia kama kumpa baraka huko aendako. Lakini kitendo cha kushika tu pale chini naye akapotea, hali ile ilimshtua Faraj asijue imekuwaje.
Haraka akaanza kukimbia kurudi kwake kuangalia kwenye vitabu vya kale maana jambo lile ni ishara ya kitu fulani.

Huku Eden mambo yalizidi kwa upande wa askari wa Eden. Kwa maneno yale aliyoahidiwa Generali moyo wake ulitekwa na matamanio ya madaraka kama alivyoahidiwa na Mfalme Faruk. Na taratibu akaanza kuwajaza sumu ya maneno baadhi ya askari wake kwamba warudi nyuma na kukubali kushindwa. Kauli hiyo ilishangaza wengi ambao wanauchungu na taifa lao. Lakini Generali alisimama kwenye neno lake akiwaamuru askari wake wakubali kushindwa angali bado wana nguvu za kupambana.
Taarifa hiyo ikaanza kusambaa kwa askari wote kuwa wakubali kuwa wameshindwa. Hii inamaana kwamba majeshi yao hayana uwezo wa kupambana na majeshi ya Mfalme Faruk. Kwakuwa Generali ndiye aliyesema iliwalazimu kufuata amri huku wakijua kushindwa kwao ndio kunawapa nguvu wapinzani wao kuitawala Eden rasmi. Kauli ile iliwafanya wakina Jamal na askari wao wafurahi sana na kuona kile walichokidhamiria kinakwenda kuwa. Lutfiya alishangilia sana kuona taifa lake linakwenda kushika madaraka.
Wakati hayo yakiendelea nje huku ndani ya chumba cha Mfalme alipata kutokea Samir moja kwa moja. Alipotazama pale kitandani alishtuka kumuona Mfalme akiwa vile,taratibu akamsogelea na kuanza kumuita. Gafla Maya naye akapata kutokea palepale akiwa ameweka mkono chini. Alipotazama chumba kile kwa makini alishtuka kufahamu ni chumba cha babake. Alimuona Samir akiwa pale anamtikisa Mfalme akionesha kulala. Naye akasogea hadi pale na kumfanya hata Samir ashangae maana hayana uwezo wa kupambana na majeshi ya Mfalme Faruk. Kwakuwa Generali ndiye aliyesema iliwalazimu kufuata amri huku wakijua kushindwa kwao ndio kunawapa nguvu wapinzani wao kuitawala Eden rasmi. Kauli ile iliwafanya wakina Jamal na askari wao wafurahi sana na kuona kile walichokidhamiria kinakwenda kuwa. Lutfiya alishangilia sana kuona taifa lake linakwenda kushika madaraka.
Wakati hayo yakiendelea nje huku ndani ya chumba cha Mfalme alipata kutokea Samir moja kwa moja. Alipotazama pale kitandani alishtuka kumuona Mfalme akiwa vile,taratibu akamsogelea na kuanza kumuita. Gafla Maya naye akapata kutokea palepale akiwa ameweka mkono chini. Alipotazama chumba kile kwa makini alishtuka kufahamu ni chumba cha babake. Alimuona Samir akiwa pale anamtikisa Mfalme akionesha kulala. Naye akasogea hadi pale na kumfanya hata Samir ashangae maana aliondoka kule kwa siri na hayana uwezo wa kupambana na majeshi ya Mfalme Faruk. Kwakuwa Generali ndiye aliyesema iliwalazimu kufuata amri huku wakijua kushindwa kwao ndio kunawapa nguvu wapinzani wao kuitawala Eden rasmi. Kauli ile iliwafanya wakina Jamal na askari wao wafurahi sana na kuona kile walichokidhamiria kinakwenda kuwa. Lutfiya alishangilia sana kuona taifa lake linakwenda kushika madaraka.
Wakati hayo yakiendelea nje huku ndani ya chumba cha Mfalme alipata kutokea Samir moja kwa moja. Alipotazama pale kitandani alishtuka kumuona Mfalme akiwa vile,taratibu akamsogelea na kuanza kumuita. Gafla Maya naye akapata kutokea palepale akiwa ameweka mkono chini. Alipotazama chumba kile kwa makini alishtuka kufahamu ni chumba cha babake. Alimuona Samir akiwa pale anamtikisa Mfalme akionesha kulala. Naye akasogea hadi pale na kumfanya hata Samir ashangae maana aliondoka kule kwa siri na aliyemuona ni Faraj.
"Samir baba yangu kafa ni Faraj.
"Samir baba yangu kafa kule kwa siri na aliyemuona ni Faraj.
"Samir baba yangu kafa nywa nini?"aliuliza Maya na kuanza kumuita baba yake. Aliita na kuita bila kuona Mfalme kuinuka,hapo ndipo kilio kikaanza kwa binti huyo wa Mfalme huku Samir akiwa anamtazama Mfalme aliyeonekana kweli amefariki.

Huku mashariki ya mbali Dalfa alibaki kutabasamu baada ya ule uchawi aliouacha mule ndani ya chumba cha mfalme umemjulisha kwamba Samir amefika.
"Sikuachi safari hii, nachukua kila kilicho kwenye mwili wako na ndio muda muafaka wa kuimiliki Eden."alisema Dalfa akiwa kwenye chumba chake cha kufanyia ibada. Alichukua mkuki wake mrefu wenye maandisha ya kichawi na bila kuchelewa akapetea kuelekea Eden.
NINI KITAJIRI EDEN? USIKOS
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN 43

Hadi muda huo Eden ilikuwa tayari imeshikwa na Mfalme Faruk baada ya askari wote wa Eden kukubali kile walichoagizwa kufanya na Generali mkuu. Askari wa Faruk walipiga kelele za furaha baada ya kufanikiwa kuwanyamazisha majeshi ya Eden. Mfalme alimtazama Generali kwa tabadamu na kumsifu kwa kile alichokifanya.
Furaha aliyokuwa nayo Lutfiya haikuwa ya kawaida maana alifanya mengi sana kuihamikishia taifa lake linaikamata na kuitawala Eden kama walivyopanga. Ikawa ni sherehe ya kushangilia ushindi huo wakizunguka kila mtaa usiku ule huku wananchi wakiwa zao ndani wakichunfulia yanayoendelea nje. Kwa kuona shangwe zile zikizidi kila dakika wakaamini Ufalme wa Siddik umepinduliwa na sasa tawala mpya inaingia madarakani.
Baada ya muda ilibidi Generali awaeleze askari wake wote hali halisi ya Mfalme wao. Wote walipiga magoti chini kwa huzuni baada ya kusikia Mfalme Siddik ameuawa.
Baadhi yao walipatwa na hasira sana na kujua huenda hawa waliowavamia ndio waliofanya mauaji hayo lakini hawakuwa na jinsi wanafuata amri kutoka kwa Generali wao.
Huku ndani ya falme ilikuwa ni huzuni kwa Maya akimtazama baba yake pale kitandani akiwa tayari amekata kauli. Hali ile ilimfanya Samir akumbuke tukio la nyuma kabisa pindi Maya alipokuwa kitandani akiugua. Alihisi na hili pia laweza kuwa kama lile la awali. Alimshika magega Maya na kumtaka akae kwanza pembeni kisha akasimama karibu na mwili wa Mfalme. Alimtazama kwa dakika kadhaa huku Maya akiwa anajiguta machozi akionesha kuwa na uchungu.
Samir alishika masikio ya Mfalme na kuyaziba kwa vidole huku akinena maneno fulani na kuanza kubadilika taratibu macho yake yakin'gaa sana. Ilimchukuwa dakika kadhaa na hata alipotoa vidole vile moshi mweusi ulianza kutoka masikioni mwa Mfalme na hata puani. Hali hiyo ilimstaajabisha sanaMaya na kujikuta akisimama taratibu huku akimtazama baba yake akitokwa na moshi ule mweusi sana ambao ulionekana kuna nafsi za viumbe wakiwa wanafurukuta kuonesha hawakutaka kutolewa ndani ya mwili ya mwili wa Mfalme Siddik. Hata baada ya kuzidi kuomba sana Samir akiuyoa ule uchawi ndani ya mwili huo alipata kuona Mfalme akitapika damu iliyomshtua Maya.
Samir alichukua kitambaa na kuanza kumfuta Mfalme na hapo ndipo Maya akakumbuka siku ile ambayo alikuwa kitandani akiugua, na siku alipoamka alipata kumuona Samir akimfuta damu kama hivyo anavyofanya sasa. Akapata tumaini jipya huenda baba yake naye akawa mzima. Haraka akasogea pale na kumtazama baba yake, ilikuwa ni bahati kuonekana Mfalme akianza kupumua kwa mara nyengine.
"Amewekwa uchawi ndio maana, ni kama ilivyokuwa kwako awali."alisema Samir akiwa anamtazama Mfalme pale kitandani.
"Ni nani sasa aliyefanya haya?"aliuliza Maya huku akionekana kuwa na hofu.
"Huyu lazima atakuwa Dalfa,ndiye mwenye uwezo wa kufanya haya na nadhani hili amelifanya kusudi baada ya kufeli kwako."alisema Samir na Maya aliposikia jona la Dalfa alizidi kuogopa. Hakuna asiyemfahamu Dalfa kwa jinsi alivyo na uwezo wa kutumia nguvu za kichawi.

Muda huohuo Dalfa ndio alikuwa anawasili ndani ya Eden. Alishangaa kuona umati wa askari wakiwa nje wanashangilia na kupongezana kwa furaha kubwa. Ajabu ni kwamba hakuona raia yeyote nje usiku huo. Alisikia kwa mbali kuna mtu anamwita akiwa ndani ya nyumba. Kwakuwa hakujua kinachoendelea na kubaki njia panda ilimbidi asogee kule alipoitwa.
"Wewe huna uoga hata na vita hii kubwa lakini bado upo nje,rudi kwako haraka watakuua hawa."alisema mzee mmoja aliyemeita Dalfa. Maneno yale yakamshamgaza Dalfa.
"Vita?... Vita gani tena?"aliuliza Dalfa.
"Wewe ulikuwa wapi kwani? Eden imechafuka hakuna raia anayeweza kutoka nje muda huu. Lisaa lizima yanasikika mapanga tu huku nje. Damu kila mahala watu wanachungulia tu waone kinachoendelea. Na bila shaka tukatawaliwa na Mfalme Faruk maana ndio askari wake wanashangilia kw furaha baada ya kuwazidi majeshi ya Eden."alisema yule mtu na maneno yake hayo yalimshtua Dalfa baada ya kujua kumbe kuna ambao wanaitaka Eden, wanapambana siku hiyo kwaajili ya kuupindua utawala wa Mfalme Siddik. Hakutaka kuendelea kuwa pale haraka akatoka nje kuelekea mahala alipokusidia. Yule mtu alimshangaa Dalfa kuona kama anajiingiza kwenye matatizo.

Kule ndani Maya bado alikuwa akimtazama baba yake akiwa pale kitandani. Taratibu Mfalme akaanza kufumbua macho yake na kukutana na sura ya binti yake Maya. Alijikuta akilitaja jona hilo na kiupeleka mkono shavini kwa binti yake baye alipata kuaxhia tabasamu lenyekumfariji baba yake.
"Maya..nisamehe sana binti yangu sikuweza kukutetea na kusimama upande wako,ikasababisha uwe mbali na Taifa lako,uwe mbali na wazazi wako.. Nisamehe sana binti yangu."alisema Mfalme akiongea kwa sauti ndogo. Maya alijisoheza kwa baba yake na kumkumbatia kuona hakuna haja ya kuendelea kumchukia mzazi wake. Mfae aligeuka na kumtazama Samir aliyekuwa amesimama kando yake.
Samir, Dalfa anakutafuta na nahisi amefahamu kama unatumia nguvu za kichawi. Ni mtu mbinafsi anayetaka kuwa yeye pekeake hivyo kuwa makini katika maisha yako juu ya huyu mtu. Amekuwa akiitamani pia taifa hili na nadhani safari hii atafanya jambo aweze kulipata taifa hili. Kama unatumia nguvu hizo basi tumia kwa kuwasaidia watu, tumia kwa kuisaidia Eden isichukuliwe na mtu yeyote. Na daima usikae mbali na Maya ipo siku atakusaidia na mtafika mbali katika maisha yenu."alisema Mfalme na kuushika mkono wa Samir huku Maya akitazama tu. "Samir.. Naomba unisaidie jambo.."aliongea Mfalme na kumfanya Samir atege sikio akimtazama Mfalme kwa makini maana anaonekana hali yake si nzuri.
Ilibidi Mfalme Faruk akusanye askari wote akishirikiana na Generali wakasimama kwenye uwanja mkubwa. Mfalme Faruk akasimama kwenye sehemu maalumu na kuanza kujigamba kwa kuupindua utawala wa Siddik. Aliwaunganisha askari wa mataifa hay o mawili kuwa kitu kimoja kuanzia siku hiyo. Aliongea mengi na mwishowe akampandisha Generali ambaye naye alitoa sifa kwa Mfalme Faruk huku akiitangaza rasmi taarifa ya kufariki kwa Mfalme Siddik. Taarifa ambayo hata watu waliokuwa wamejifungia pindi wakiposikia waliumia sana na hata kushindwa kujizuia kulia kwa kumpoteza Mfalme wa Eden.

Huku ndani ya falme Dalfa alipata kutokea katika chumba kilekile alichopo Mfalme. Ajabu na cha kumshtua ni kuona kupo tupu hakuna mtu mule ndani. Alipatwa na sintofahamu na haraka akatoka na kuanza kuangaza macho kila chumba kuhakisha kama atawapata.
Generali aliendelea kutoa darasa kwa askari wote usiku huo akizidi kuweka ukaribu. Akiwa anayaongea hayo gafla tu wakatokea katikati yao Samir na Maya wakiwa wamemshika Mfalme Siddik. Hakuna aliyeamini kile wanachokiona mbele yao. Generali alishikwa butwaa kumuona Mfalme akiwa hai tena yupo na watu ambao amekwishawafukuza.
Hata Jamal alishangaa huku akimgeukia Lutfiya ambaye alibaki kushika mdomo wake kwakile anachokiona.
"Generali... Kabisa umeamua kulisaliti taifa lako na kuligata kwa mtu asiyestahili!"alisema Maya akiwa anamtazama Generali aliyekuwa amesimama pale mbele. Alikosa hata cha kujitetea akabaki kutazama chini. Mfalme Siddik alimkazia macho Generali baada ya kutambua amekwenda kinyume naye.
"Ni nafasi gani hiiyo mnapeana baina yenu? Ni taifa la nani hilo mnamilikishana kwa kujitangazia mbele ya askari wangu."alisema Mfalme Siddik akionekana kuchoka sana. Akigeuka taratibu na kuwatazama askari wake wakiwa wameinamisha vichwa vyao kwa aibu. Hawakuwa na jinsi maana walifuata amri ya Generali wao baada ya kupatikana taarifa kwamba Mfalme amefariki. Kwapamoja wakaenda chini kupiga goti kuomba msamamaha. Watu waliokuwa ndani wamejificha walipopata kumuona Mfalme kidogo wakapata faraja kwenye mioyo yao.
"Kama unamfuata Generali na uongozi wake mpya nyanyuka usogee upande wao."alisema Mfalme akionesha kuwa makini na kile anachokisema. Jamal pamoja na baba yake walibaki kutazama tu na kushuhudia hakuna hata askari mmoja aliyenyanyuka kuwa upande wao. Mfalme Siddik alirudia kwa mara nyengine kauli hiyo na kuhitimisha kwa mara ya tatu lakini hakuna aliyesimama kusogea.
"Ukimya wenu na kuwa hapa wote ni wazi kwamba mpo nami."alisema Mfalme na sauti kubwa ilitoka kwa askari wale kukubaliana naye.
"Kama mpo pamoja nami basi tambueni ni mimi pekee ndiye ninayetoa amri ya jambo lolote ndani ya Eden,na hapa nimesimama mbele yenu kila mtu afahamu leo ndio itakuwa siku yangu ya mwisho kuitawala Eden na pia ndio itakuwa siku ya kwanza kwa Samir kuitwa Mfalme wa Eden. Nimelitangaza mbele yenu leo kila mtu aelewe nbfahamu hilo na watu wote mliopo ndani kwenu Mfalme wenu wa sasa ni Samir na ndiye nimemchagua mwenyewe nikiwa kama Mfalme, apewe heshima Mfalme mpya...! "alisema Mfalme Siddik na askari wote wa Eden wakaitika na kumpa heshima Samir kama Mfalme mpya wa Een. Watu wote waliojificha majumbani pia walisujudu kama kuonesha ishara ya kutoa heshima kwa Mfalme huyo.
Yeye mwenyewe hakuamini maana ni jambo la kushtukiza alilofanya Mfalme. Jamal na Lutfiya walikasirika kusikia taarifa hiyo kiasi cha kufanya hata Mfalme Faruk afure kwa hasira.

Askari wa Eden wakazidi kumpa sifa Mfalme wao mpya na kuwatia hasira zaidi upande wa majeshi pinzani. Mfalme Siddik alitabasamu kwa furaha kuona bado anapendwa na watu wake, gafla upanga mrecu ukatua mgongoni mwake na kutokeza tumboni mwa Mfalme Siddik tukio ambalo liliwaacha watu wakiwa kwenye mshangao. Maya alibaki ameshikwa na butwaa haamini kile ambacho anakiona mbele yake. Taratibu Mfalme akaenda chini kama mzigo hali iliyowafanya wakina Samir na askari wengine wamkimbilie pale alipodondoka.
NANI ALIYEFANYA TUKIO HILO? TUTAFAHAMU SEHEMU IJAYO.
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN 44

Tukio hilo liliwaacha watu midomo wazi hasa walipo walipomtazama mhusika aliyefanya jambo hilo. Mfalme Faruk aligeuka kumtazama mwanaye Jamal alikuwa euelekeza mkono wake mbele. Ni yeye ndiye aliyerusha upanga ule uliozama moja kwa moja mgongoni mwa Mfalme Siddik na kutokeza upande wa pili.
"Jamal.... Umefanya nini sasa?!"aliuliza Mfalme Faruk akimshangaa kijana wake kea mile alichokifanya. Hata yeye alibaki ameshikwa na butwaa kwa kile alichokifanya maana amechukua maamuzi yake ya haraka ambayo aliona kwake ni sahihi.
Maya alilia sana baada ya kuona hali ile na kubaki kumshika baba yake pale chini huku Samir akimnyanyua Mfalme na kumlanza miguuni mwake.
"Mfalme... "Aliita Samir akiwa anamtazama Mfalme Diddik.
"Samir...nakuomba sana umlinde Maya na mama yake, Mimi sina uwezo tena wa kuendelea kuishi."aliongea Mfalme kwa sauti ya chini sana.
"Hapana baba usiseme hivyo,Mimi bado nakuhitaji tuishi kama awali, Samir hebu msaidie baba yangu, msaidie Samir.."slisema Maya akionekana kuchanganyikiwa. Ilibidi Samir atumie nguvu zake mbele ya watu pale bila kuhofia lolote. Alijaribu kuutoa upanga ule lakini Mfalme alikuwa akilia kwa maumivu makali sana kiasi cha kufanya asitishe zoezi hilo.
"Nasikia maumivu, naumia sana.."alisema Mfalme akihema kwa kasi. Damu zilimmimika eneo like lilipoizama panga lile refu. Hakika ulikuwa ni mtihani jinsi ya kulitoa panga lile hali iliyofanya mwenyewe Mfalme asitake kufanywa lolote maana in wazi kwamba uwezo wa kuendelea kuishi tena haupo. Upanga ulizama sehemu mbaya kiasi cha kufanya asikie maumivu makali sana pindi utolewapo. Eatu ealibaki kumgutumia tu na hata baafa ya muda Mfalme alinyamaza kimya na mwili wake kukosa uwezo wa kuendelea kuwa na nguvu. Mwili ulishatengana na roho na hapo ndipo majonzi yakaanza kwa Maya na askari wengine ambapo walipata kuona tukio hilo. Wote walipiga magoti chini na kuweka vichwa vyao kwenye ardhi kama kutoa heshima ya mwisho kwa Mfalme Siddik. Samir alinyanyuka akiwa na hasira zisizopimika na kugeuka nyuma kutazama upanga ule ulipotokea. Alipata kumuona Jamal akiwa amesimama pale na kufahamu ni yeye ndiye aliyefanya tukio hili.
" Sikuwa na nia ya kufanya kibaya kwenu ila kwa hili sitawacha salama mtalipa kwa hili mlilofanya na sitaruhusu hata mmoja wenu aondoke kwenye ardhi hii akiwa hai."alisema Samir na kuwafanya askari wote wa Eden waliokuwa wanatoa heshima ya mwisho kwa Marehemu wakanyanyuka na kukamata mapanga yao sawiya wakiwa wametoneshwa mioyo yao kwa kuuawa kwa Mfalme Siddik.
Jamal alibaki kutazama tu na kuanza kucheka.
"Baba.. Hakuna kurudi nyuma huu ushindi ni wetu na tunahakikisha Eden inakuwa mikononi mwetu. Tayari tumeshafanikiwa hatua zote kwanini tuhofie sasa!" Alisema Jamal akimjaza ujasiri baba yake na wenzake wengine. Nao hawakuona haja ya kurudi nyuma iliwabidi walimalize swala hilo wakamilishe kile walichokusudia. Mfalme alimtazama Generali ambaye ameigeuka Eden na kuwa upande wao, alitoa amri moja yu ya askari wao wasihofie lolote na vita ianze upya. Huku naye Samir alitoa amri kwa askari Eden kuwafuata adui zao wahakikishe hakuna anayesalia. Vita ikaanza tena upya huku kila mmoja akiwa na hasira zaidi ya mwenzake
Lutfiya kuona vile akaanza kurudi nyuma na kuelekea zake upande wa pili kujificha lakini Maya aliweza kumuona akiwa pale chini amemshika baba yake. Alinyanyuka akiwa na hasira kwa kuuawa kwa Mfalme na taratibu akaanza kumfuatilia Lutfiya kwa nyuma akijua ndiye mtu ambaye alikuwa akitumiwa na Ufalme wa Faruk katika kila jambo baya ambali sasa limeiweka Eden pabaya.
Muda huo Dalfa baada ya kutafuta kila mahala bila mafanikio alitoka nje ambapo alikuta vita ile ikiendelea. Alitazama jinsi hali ile inavyoendelea na kuona jinsi watu wanavyochinjana bila huruma, damu zilimwagika katika ardhi hiyo ya Eden kila askari alikuwa amechafukwa na roho. Hakukuwa na huruma baina ya pamde hizo mbili hali iliyomfanya Dalfa asimame kuangalia kwanza.
Alipata kumuona Samir akipambana akizitumia nguvu zile ambazo muda mrefu Dalfa amekuwa akizifuatilia kuweza kuzichukuwa awe nazo yeye pekeyake. Alifurahi kuona sasa swala lake la kupokonya uwezo ule alionao Samir linakwenda kutimia. Alipotazama pembeni alipata kuona askari mmoja akiuchomoa upanga ule uliozama mwilini mwa Mfalme Siddik na kuutupa pembeni, askari wawili walisogea pale na kuubeba mwili wa Mfalme Siddik kuupeleka ndani kuuhifadhi kwanza ikiwa ni kama heshima. Dalfa akapata kufahamu kumne Mfalme ameuawa. Kwake ilikuwa sawa tu maana kifo cha Mfalme kilimpunguzia kazi maana alipaswa kummaliza hapo mbele pindi atakapoitaka Eden aimiliki baada ya kuhakikisha Samir hana uwezo tena ya kupambana naye.
Huku upande wa pili Lutfiya alielekea moja kwa moja hadi chumbani kwake na kuanza kukusanya kila kilicho chake kwa kujua hakuna tena usalama Eden. Alikuwa akihema sana na kuwa na hofu iliyochanganyika na woga ndni yake kila akifikiria hatua walizopitia na kukaribia kuimiliki Eden lakini hali imebafilika tena. Muda huohuo akatokea Maya na kusimama mlangoni pale, Lutfiya alishtuka kuona vile.
"Unataka kwenda wapi mbona unasomba nguo zako?" Aliukiza Maya akiwa amekamata upanga mkononi.
"Ah..ehee...amna napangapanga tu nguo zangu.. Nikasafishe.. Ah nikazihifadhi." alin'gatan'gata maneno asieleweke anachozungumza.
"Shetani mkubwa wewe.. muda wote unakaa humu ndani pamoja nasi kumbe ni shetani wa kupindukia, umekuwa ukishirikiana na hawa watu kuipindua Eden ya baba yangu. Na mmefanikiwa kumuua pia nadhani ndilo lilikuwa lengo lenu." alisema Maya humu machozi ya hasira yakimbubujika.
"Yani leo ndio mwisho wako mjinga sana wewe." alisema Maya na kumsogelea Lutfiya aliyebaki kutazama tu. Alisogea pale na kumchomeka upanga wa tumbo bila huruma na msichana huyo akabaki kutoa macho baada ya kuzamishwa panga lile likatomeza upande wa pili. Akataka kujitetea muda huo akitaka kulitoa panga lile lakini Maya alilikamata kisawasawa huku akichezesha huku na kule akizidi kumchimba kwa ndani. Alikosa nguvu ya kuendelea kusimama Lutfiya akaenda chini kama mzigo huku damu nyingi zikimtoka. Maya alibaki kumtazama tu na kidogo moyo wake ukapata tulia baada ya kulifanikisha zoezi hilo kwa mikono yake huku akishuhudia Lutfiya akikata kauli palepale.

Huku chini mapambano yalizidi kushika kasi. Safari hii hakuna askati wa Eden aliyemheshimu Generali baada ya kujua kuwa alikuwa akishirikiana na upande wa pili ambao ni adui kwao. Kwa upande wake yeye hakuona haja ya kuhofia lolote ilibidi ashirikiane na Mfalme Faruk kulikamilisha zoezi wanalotaka lifanikiwe.
Huku Samir alikuwa ni zaidi ya katili , aliweza kupunguza askari wa Mfalme Faruk kwa kasi zaidi na kwa muda mfupi sana huku akizidi kusogea mbele zaidi. Na mwishowe akapata kukutana na mtu na baba yake wakiwa mbele wanamtazama Samir aliyeonekana kubadilika kabisa hata macho yake kuwa makali. Mfalme Faruk aligeula kumtazama mwanaye Jamal ambaye hakutaka hata kusubiri alisogea na upanga wale bila kuhofia jambo.
"Sitojali unauwezo kiasi gani nitahakikisha nakumaliza, huwezi kutuvutugia mipango yetu angali tushayakamilisha na kuwa na furaha" alisema Jamal akiwa amekamata panga lake sawiya.
"Kwani kitu gani kimewafanya hadi muitamani Eden angali mnataifa lenu kubwa tu.! Kwanini mnakuwa na mioyo ya tamaa, tazama umemuua Mfalme ndani ya Eden, unamuua kiongozi wa taifa nini unategemea kwa wananchi wake." Alisema Samir akiwa anahasira moyoni.
"Ni pete... Ndicho kitu kikubwa tunachokihitaji sisi na ndio maana tunaitaka Eden kwa hali na maili. Pete ya Mfalme wa Eden wa enzi na enzi ndio tunaitaka sisi, tukiwa ndani ya taifa hili tunauwezo wa kuitafuta kujua wapi ilipo. Usifikirie kutajwa kuwa wewe ndio Mfalme ukadhani utakuwa hivyo kweli,. Huwezi kuiongoza Eden angali unatumia uchawi. Uchawi katika taifa hili ni kosa kubwa sana nadhani wafahamu hivyo. Halafu wewe.. Si ulifukuzwa na mkapewa adhabu ya kutorejea tena Eden. Imekuwaje umerudi tena.!"aliongea Jamak kwa kupaniki, hakika hakufurahishwa na uamuzi wa Mfalme Siddik kumchagua Samir kuwa ndiye Mfalme wa Eden bila kujali kama alikuwa mwenye adhabu. Hali hiyo ndiyo ikamfanya Jamal kummaliza Mfalme kwa upanga wake kwa hasira baada ya kutangazwa vile.
"Huwezi kubishana na Mfalme Siddik kwa maamuzi yake, huenda ameona ninamsaada kwa watu ndio maana amenikubali na kunichagua. Na hapa unaponiona naiongoza Eden ama Mfalme hivyo usifikirie uaongea na Samir yule wa zamani." maneno hayo yalizidi kunuumiza Jamal, hakutaka kusikia mtu mwengine yeyote anaikamata nafadi hiyo. Alinyanyua upanga wake kwa hadira na kumfuata Samir aliyebaki kumtazama Jamal akia kwa hasira zote. Hata alipofika wakaanza kuoneshana kila mtu uwezo wake wa kupambana.
Maneno yale yote yaliyoongelewa pale yalimfanya Dalfa ashtuke baada ya kusikia kumbe Samir tayari ameshatangazwa kuwa ndiye Mfalme mpya wa Eden. Akaona njia pekee ya kumdhibiti kijna huyo ni ile ambayo Jamal anapambana naye. Harka na kwa uwezo wa ajabu akapotea pale na kujibadili kuwa kivuli kikimfuata Jamal akiwa anazidi kujitetea pale kwa Samir. Hakutaka kuendelea kupoteza nguvu zake Samir aliamua kuachia pigo ambalo lingeweza kumuangamiza kabisa Jamal aliyekuwa akitumia upanga wake bila mafanikio. Aliachia shambulizi la aina yake na muda huohuo kivuli hile cha Dalfa kikaingia mwilini mwa Jamal na haraka akakinga mkono wake na nguvu zile za kichawi alizotumia Sir zikadunda pale.
Alishangaa Samir kuona vile maana hakutegemea kama binadamu wa kawaida angeweza kuzuia shambulizi hilo.
Alirudi nyuma Jamal huku akijitazama mwili wake akijihisi ni wa tofauti. Alijiona ni mwenye hali ya hasira dhidi ya Samir, haraka isiyo ya kawaida akamsogelea Samir na kupambana naye, safari hii hata Samir alishangaa kuona Jamal amekuwa na uwezo wa kupambana naye. Alipata kutambua kuwa Jamal yule wa awali sio wa sasa pindi alipojaribu kumkita panga la kifua na papohapo Jamal akapotea na kutokea upande wa pili wa Samir. Hali ile hata Mfalme Faruk alishangaa maana ni uchawi ndio unatumika kufanya jambo hilo. Huku askari wa Eden walizidi kupambana na askari pinzani kwa kila jitihada zao. Wakimfikiria Mfalme wao jinsi alivyouawa kinyama hawakuwa na huruma nao tena. Askari kadhaa wakamzingira Generali akiwa ameshikiria upanga wake, aliwatazama askari wake na kuona ni vijana wake aliokuwa anawafundisha mapambano lakini leo imekuwa tofauti baada ya yeye kuwa upande wa pili. Askari wale bila kuuliza wakaanza kum shambulia Gaenerali bila kumtazama usoni. Walipambana kwa pamoja hawakutaka kukubali kushindwa mbele ya mwalimu wao huyo. Generali alikuwa akiwadhibiti askari hao kwakuwa ameshajua uwezo wao hivyo hakuwa anatumia akili nyingi. Askari wale walipoona wanazidi kupunguzwa ilibidi waongezeke tena wengine zaidi ya hao. Hali ile ilimfanya hata Generali ashushe pumzi akihema kwa kwa kuchoka. Hawakuta kumpa nafasi ya kupumzika walizidi kumuandama.
Huku kwa Mfalme Faruk alikuwa akiendelea kupambana na askari wengine. Hakika siku hiyo ilikuwa ni ya aina yake huku wananchi wakichungulia madirishani usiku ule wa mbaramwezi.
ITAENDELEA
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN 45

Jamal alikuwa akiwashangaza watu wengi kwa kuonekana akipambana na Samir ambaye alifahamika kutumia nguvu za kichawi. Hata Maya baada ya kutoka mule ndani aliweza kuona Samir akiendelea kumdibiti Jamal aliyeonekana kuwa na uwezo mkubwa. Hali ile ikamfanya Samir atambue hapambani na Jamal yule aliyemzoea, ilimbidi atumie nguvu na akili za ziada kuhakikisha anamdhibiti mpinzani wake.
Huku kwa Generali mambo yalianza kuwa magumu, askari wa Eden walimuandama mjubwa wao huo akiyeisaliti Taifa lake na kuwa upande wa adui zao. Walimshambulia General huyo ambaye alijitahidi kuwazuia lajini mwishowe nguvu zilimuisha na kuanza kuruhusu kujeruhiwa katika baadhi ya sehemu za mwili wake kwa mapanga. Alirudi nyuma na kushuhudia damu zikichuruzika mgongoni na sehemu za mikono yake. Alikamata panga lake vyema na kumeza mate huku akiwatazama askari wale waliokuwa hawana masihara juu taifa lao. Umakini wao na umoja ulijidhihirisha pale ambapo Generali akipotaka kuendelea kupambana nao na wakafanikiwa kumkata misuli ya mguu na papo hapo akaenda chini akioiga magoti. Hakuweza tena kusimama muda ule na taratibu akasogea askari mmoja aliyekuwa akiwaongoza wenzake, akawa anatazamana na Generali aliyekuwa ametapakaa damu mwilini.
Hakutaka kuongea naye tena maana ingemfanya amuonee huruma, alinyanyua upanga wake juu na kuupitisha kwa nguvu shingoni kwa Generali aliyekwenda chini kama mzigo huku damu nyingi zikitaoakaa pale chini na ndio ukawa usiku wa mwisho wa maisha yake.
Askari wale walitazamana kila mtu akiwa anahena kwa kazi nzito hadi kuweza kummaliza aliyekuwa Kiongozi wao.

Huku kwa Samir alizidi kupambana na Jamal ambaye alionekana kuwa shapu kukiko vile alivyozoeleka. Jamal baada ya kutambua kuwa anayepambana naye si mtu wa kawaida akaamua kuzidisha ujuzi na kuzitoa nguvu zake za ziada alizonazo. Hali ile ikamfanya hata Dalfa aliyekuwa ndani ya Jamal ashtuke. Uwezo ule wa Samir ulimfanya Dalfa atambue kuwa kuna nguvu za ziada anazo kijana huyo hivyo lazima ahakikishe usiku huo anamtia kila kitu alichonacho Samir ili apate kuwa yeye pekee mwenye uwezo wa kila kitu.

Muda huohuo Faraj akapata kuwatokea eneo hilo. Alipata kujua kinachoendelea ndani ya Eden na kujua Samir atakuwa yu matatizoni. Hata alipotazama mbele yake alimuona Samir akizidi kupambana na Jamal ambaye alionekana kuwa makini sana. Hakutaka kuchelewa haraka akasogea mahala pale na kumfanya hata Samir ashangae. Jamal alirudi nyuma akiwa amekamata upanga wake.
"Elewa kwamba unapambana na watu wawili hapa."alisema Faraj huku akimuangalia Jamal akiwa anahema akiwatazama.
"Nililijua hilo mapema ndio maana nimekuwa makini."alisema Samir.
"Huyu nitapambana naye wewe nenda kule msituni kaitafute ile pete, nadhani ndio yenye umuhimu sana."alisema Faraj akimweleza Samir ambaye akapata kuyaelewa maneno yale. Alihofia kuondoka pale huenda akamwachia mtihani mkubwa Faraj. Faraj akampa imani ya kuwa asihofie lolote hali iliyomfanya Samir kuridhia. Dalfa akiwa ndani ya mwili wa Jamal alibaki kutazama tu asijue kinachoongelewa pale. Aliona Mtoto yule akipiga hatua kadhaa kusogea mbele huku Samir akiwa nyuma, taratibu aligeuka na kuondoka zake kuanza safari ya kuelekea kwenye ule msitu usiku ule. Dalfa kuona vile akataka amfuate kujua wapi amapoelekea Samir lakini alishangaa kuona mahala pale waliposimama kukiwaka moto pembeni uliozunguka duara. hata yeye alishangaa ikambidi ageuke kumtazama Faraj aliyekuwa amesimama tu akimuangalia.
"Nishakufahamu kuwa wewe ni Dalfa, na lengo lako hasa ni kuichukua ardhi hii iwe mikononi mwako."alisema Faraj akiwa anamtazama Dalfa aliyekuwa kwenye mwili wa Jamal.
"Wewe ni nani?"aliuliza Dalfa akiwa mwenye kushangaa. Faraj alisogea tena hatua kadhaa mbele akiwa mwenye hasira sana.
"Mimi ndiye niliyestahiki kuwa na nguvu hizo ulizonazo,ila kwa ujanja na tamaa zako ukaiba kutoka kwa baba yangu na kuamua kwenda mbali kuanisha taifa lako. Unatumia vibaya uwezo ulonao na kuamua kuwanyonya
watu na mali zao, kwani huwezi kumsaidia mtu hadi unyan'ganye mali yake. Baba hakuwa hivyo hata kidogo, na nilipata kuambiwa ni wewe ndiye ulimuwekea uchawi Maya ili uje kuichukua Eden pindi watakapokuja kuomba msaada kutoka kwako. Baba yangu alipokea adhabu ya kunyongwa bila kosa lakini alijua nini anafanya, ila kwahilo tu utalipa na sitaweza kukusamehe."alisema Faraj akionekana kuwa hasira.
Dalfa alimtazama na kubaki kucheka mwenyewe. Kauli za mtoto huyo zilimfanya hata yeye ashangae na kuona ni vitisho vinavyoongelewa pale..
"Hadi sasa najikuta mwenye tabasamu,nakaribia kuitawala Eden na nimepata kufahamu kumbe kulikuwa na wengine waliokuwa wanaitaka ardhi hii. Tafadhari mtoto wangu usitafute matatizo yasiyo na lazima."alisema Dalfa na kutaka kupotea eneo lile lakini Faraj kwa uwezo wake akamzuia jambo ambalo hata Dalfa hakutegemea kabisa. Hapo ndipo akafahamu kumbe anayeongea naye anauwezo mkubwa sana kama alionao Samir. Ilimbidi ageuke kumtazama vizuri Faraj pale aliposimama akionesha kujiamini. Dalfa akaona kuna haja ya kupambana na kijana huyo azichukue nguvu hizo kabda ya kumaliza kwa Samir. Aliandaa shambulizi lake imara lakini aliona akirushwa kwa nguvu na upepo mkali hadi kudondokea kwenye moto.

Kitendo kile kilimkasisha Dalfa na kuyanyuka haraka huku akitumia uwezo wake kuuzima moto ule uliokuwa ukitanda kwenye nguo zake. Naye akaanza kujibu mashambulizi na ikawa ni vita ya kutumia uchawi. Huku askari wa Eden walikuwa wakiwamalizia baadhi ya watu wa Mfalme Faruk ambaye muda huo alikuwa amewekwa kati na askari kadhaa wakiwa wamemzingira. Alibaki akihema sana kutokana na kupambana kwa muda mrefu. Aliitazama idadi ile ya askari na kuangalia pembeni kuwaona jinsi askari wake wanavyozidi kumalizwa. Alimuanalia mwanaye Jamal na kuona jinsi anavyopambana na mtoto Faraj wakioneshana uwezo walionao. Alitazama upanga wake ulio mkononi mwake na kuukamata sawasawa. Alinyanyua upanga wake na kuendelea kupambana na askari wale. Wingi wao ulimfanya hata Mfalme ashindwe kuwamudu, walimbana na kufanikiwa kumdhibiti akaenda chini baada ya kupata majeraha kadhaa. Damu zilimchuruzika kutoka mwilini na kubaki kuzitazama tu . Alivuta nguvu zake na kujaribu kuinuka lakini haikuwa rahisi, walipita askari wawili haraka na kumkata tumboni pamoja na shingoni na papo hapo akaangusha upanga wake kwa kukosa nguvu,akaenda chini kama mzigo na ndio ukawa mwisho wa Mfalme Faruk.
Maya pamoja na wafanyakazi wa mfalme wakaanza kusaidia baadhi askari walipata majeraha kwenye vita hiyo na kuwaweka mahala pamoja. Huku upande wa pili Dalfa alizidi kushindana na Faraj muda wote, hata yeye aliona ni dharau kubwa kwa mtu kama yeye kushindwa na mtu wa rika lile. Aliona atumie njia mbadala ya kumkabili Faraj maana amekuwa ni hatari. Alichokifanya ni kujigawa mara mbili huku akitumia nafsi ya Jamal pia wakaanza kupambana na Faraj pale. Awali ilikuwa ni ngumu kwa Faraj kuweza kuwamudu watu hao wawili . Alijikuta akishambuliwa kwa haraka sana hali iliyomfanya arudi kwanza nyuma kujipanga. Haikuwa kazi rahisi usiku huo hasa kwa Faraj ambaye alifahamu kuwa anapambana na nafsi zaidi ya moja pale. Hivyo ikamlazimu kuwa makini sana dhidi ya mhusika mkuu wa yote hayo Dalfa ambaye akili yake ilikuwa kwa Samir na kutofahamu alipoelekea. Ilimlazimu kuzidisha kasi ya mashambukizi kwa Faraj kusudi amfuate alipoelekea Samir.
Hilo alilifahamu Faraj na kuzidi kumbana Dalfa asiweze kutoka mule katikati ya moto.

Huku kwa Samir alikuwa aliweza kuukaribia msitu ule, aliutazama jinsi ulivyokuwa mkubwa na wenye kutisha usiku ule. Sauti za wanyama wakali zilisikika na kuleta hofu hasa kwa binadamu apitaye karibu na msitu huo. Ila kwa Samir ilikuwa ni lazima kuingia ndani ya msitu kuitafuta pete ile inayosadikika ni ya Mfalme wa zama hizo. Hata alipofika kwenye njia ya kuingilia ndani alibaki kutazama tu huku akishusha pumzi kutoa hofu iliyoanza kutanda moyoni. Taratibu akaanza kupiga hatua kuingia ndani ya msitu ule huku milio ya wanyama wakali ikisikika usiku ule.

Kwa uwezo alionao Samir alipoingia ndani ya msitu ule alinyoosha mkono wake mbele ukapata kuangaza mwanga kutoka kiganjani kwake na kuruhusu kutanda mbele yake. Kitendo kile kikiwafanya hata baadhu ya wanyama wakali walikkuwa kando yake watambue kuwa kiumbe huyo si wa kawaida. Alitoa kile kiboksi alichokabidhiwa na kukifungua akikielekezea mbele yake huku akitazama. Alianza kuelekezwa mahala pa kuelekea ambaki ndipo anapaswa afike. Simba na wanyama wakali wengi walikuwa wakimtazama tu huju suti zao kali zikisikika lakini hawakuwa na nguvu hata ya kumsogelea Samir oindi anapotembea. Haikuwa safari fupi kama alivyodhani alizidi kutembea zaidi kuingia ndani huku akiwa anatazama huku na kule akioishana na wanyama wengi ambao walikuwa wakimtazama tu. Hadi alipofika sehemu moja ambapo alipata kuona mwongozo alioushika ukionesha eneo hilo. Alitazama sehemu ile na kuona kuna miti mitatu mirefu sana na ikambidi asogee karibu. Kitendo cha kusogea tu eneo lile yalitokea majoka matatu marefu na yenye meno marefu huku yakirusha moto kutoka kwenyw vinywa vyao. Hali ile ilimuogopesha Samir hadi kuruka kurudi nyuma. Walionekana kuwa na hasira sana na kila mmoja wapo alikuwa amesimama wima katika mti wake...
NINI KITAJIRI HAPO....TUKUTANE KESHO MCHANA KUMALIZIA SIMUKIZI HII.
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN 46 (MWISHO)

Alibaki kuwashangaa nyoka wale na kuona kuna mtihani kwake wa kusogea pale.
"Mbona sikupata habari juu ya nyoka hawa imekuwaje tena?"alijiuliza Samir akiwashangaa nyoka wale wakiwa wenye kutoa cheche za moto huku wakisimama wima. Alitazama kile kiboksi na kuona mahala anapotaka kufika ni kwenye mti ule wa katikati na hakukuwa na njia nyengine ya kufanya zaidi ya kwenda palepale ili aweze kukamilisha zoezi lake la kuipata pete hiyo. Alisimama imara Samir na kushusha pumzi kwanza kuutoa uoga wote ulioanza kumtawala, alinyanyua kile kiboksi na kukifungua, kukaanza kuonekana miale ya mwanga ikichomoza kutoka kwenye kiboksi kile. Miale iliyofanya hata nyoka wale washtuke baada ya kuiona.Tararibu wakaanza kunyongea chini na kupoa kabisa. Hali ile ilimfanya hata Samir atambue ni utii wao na kuheshimu kile alichobeba. Tayari alisogea hadi pale kwenye ule mti na kuona wale nyoka wakimpisha wakakaa pamoja sehemu wakimuangalia Samir anachokifanya.
Bila kuchelewa akaanza kuutazama mti ule kwa makini kutafuta mahala ambapo ataweza kupitisha funguo ile ipate kuingia. Ilimchukua muda mrefu kutafuta hadi alipokuja kufanikiwa kupata alishukuru. Alichomeka ufunguo ule na muda huohuo yule nyoka wa katikati akaanza kutokewa gafla akiwaacha wenzake wakiendelea kumshuhudia Samir.
Muda mfupi tu ule mti ukagawa katikati na kuonekana mwanga mweupe ndani yake uliofnya kionekane kilichopo mule ndani. Samir hakuamini baada ya kuona kuna pete ambayo ilikuwa imewekwa katikati ya mti ule ikiwa inavutia. Alinyoosha mkono kuichukua pete ile huku akiwa mwenye kutabasamu. Wale nyoka walipata kushuhudia pete ile ikishikwa na Samir, hawakuwa na kazi tena ya kufanya taratibu wakaanza kutoweka huku Samir akiwa anaitazama pete ile kwa tabasamu kubwa.

Huku Eden ngoma bado ilikuwa nzito kwa Dalfa dhidi ya Faraj. Japo ni mdogo kiumri lakini uwezo wake alionao ulimfanya aheshimike na hata kutoa jasho Dalfa muda wote. Akaona hapa atakosa kotekote ni bora apotee kumfuata Samir ambaye ndiye mwenye umuhimu naye. Aliwatazama askari wa Mfalme Faruk waliokuwa tayar wameuawa pale chini,alichokifanya ni kuwaweka uwezo kama wake askari watano na muda huohuo wakanyanyuka na kusogea pale alipo Dalfa na kuwapa amri ya kumvamia Faraj nao wakafanya hivyo. Huku yeye alijitoa mwilini mwa Jamal na kumuacha akidondoka chini kwa uchovu maana ametumika pasi na kujua lolote. Haraka Dalfa akapotea eneo lile akifuata harufu tu kujua wapi alipoelekea Samir.
Huku Faraj aliachiwa kazi ya kupambana na askari wale wengi lakini muda huohuo askati wa Eden nao wakafika pale kuungana naye.
"Kuweni makini hawa wamepewa nguvu za kichawi!"alisema Faraj kuwaambia askari wale ambao walimuelewa na bila kusubiri wakanyanyua oanga zao kuingia tena vitani kupambana na askari wale wa Faruk.

Upande wa pili katika falme ya Joha muda huo alikuwa ametulia na kijana wake Rahim wakiwa na baadhi ya makamanda wa majeshi yao.
"Nahisi hadi kufikia kesho yule mpumbavu aliyemchukua Maya wakaondoka atakuwa amedhibitiwa na Mfalme Siddik. Maana hawezi kumdhuru Mfalme akijua ni baba wa Maya, hivyo nafasi hii ndio sisi tunaitumia kukamilisha zoezi letu.. Baba .. mimi naamini kesho tunakwenda kufanya mapinduzi makubwa sana Eden na tutaichukua tu kuwa mikononi mwetu. Tukifanikiwa tu basi swala la kuitafuta pete ile lazima tutaipata tu na hakutakuwa na mtu yeyote wa kututisha."alisema Rahim akionesha kuwa na uchu wa kuimiliki Eden.
Baba yake Mfalme Joha alibaki kumtazama tu na kushusha pumzi.
"Rahim mwanangu, mimi nadhani tusilazimishe kitu ambacho hakiwezekani. Yule kijana tumeshafahamu kuwa anatumia uwezo wa nguvu za kichawi kamwe hatuwezi kupambana naye. Mfano mzuri ni pale tulipopeleka askari wa kwanza wakauliwa wote , tupate funzo kupitia hili kwamba hata kungekuwa elfu hatuwezi kushindana kwa nguvu hizo. Isitoshe anasaidiana na mwenzake hivyo inakuwa ni hatari katika maisha yetu angali hapa tunaishi kwa amani. Kama shida yako ni binti wa Mfalme kumuoa na amekiri kwamba hakuhitaji basi tusilazimishe kitu ambacho hakina faida katika familia yetu. Nakuhitaji sana mwanangu uje kuiongoza falme hii, achana na mambo hayo tena angalia ufalme wako ambao siku chache unakuja kuuongoza. Askari hawa ni muhimu sana katika kutulinda katika siku za baadae hatupaswi kuwapoteza kwa jambo ambalo haliwezaniki. Nakutegemea wewe na wewe ndiye uliyebaki baada ya mama yako kufariki hivyo sitapenda nikupoteze na wewe."alisema Mfalme Joha akimsihi mwanaye aachane na habari za kurudi tena Eden kuanzisha vita. Alinyanyuka pale alipokaa na kuelekea zake chumbani kwake akimuacha Rahim na baadhi ya askari pale wakiwa wamekaa. Alinyanyuka kwa hasira baada ya kuona baba yake amebadili maamuzi waliyokubaliana.
"Hapana siwezi kuliacha swala liende tu kirahisi angali tumepoteza wenzetu kwa swala hili. Hakuna kumsikiliza baba yangu ni mimi ndiye ninayetoa amri ya kwenda Eden kesho alfajiri... sawa..!"alifoka Rahim na kutoa amri hiyo. Askari walitazamana tu na kutii kile alichosema.
Huku kwa Samir alinza kutoka nje ya msitu ule huku akiwa ameshika pete ile ya Mfalme wa kwanza wa Eden. Safari hii pindi alikuwa anapita kwenye njia ndani ya msitu ule hakukuwa na mnyama wala ndege aliyeweza kupaza sauti yake ikapata kusikika. Wote walikuwa kimya wakijua anayepita eneo hilo ni mtu mkubwa sana hivyo inawalazimu kumpa heshima yake. Hakika hata yeye binafsi alipata kuona raha yake na kuona kweli pete ile ina heshima kubwa mpaka kwa wanyama wa msitu ule ambao unaogopwa.
Alipotoka nje ya msitu ule alipata kukumbana na sura ya Dalfa akiwa amesimama mbele huku akiwa ameshika fimbo yake ndefu yenye maandishi ya kichawi.
"Hongera sana kwa kuingia ndani ya msitu huu na kutoka ukiwa hai. Ni wazi kwamba kile ulichokifuata umekipata ndio maana umetoka muda huu. Matumainia kukuona ukiendelea kuishi ukiwa na afya tele hivyo sitapenda nikudhuru mwili wako kijana wangu. Nipatie hicho ilichokipata huko ulipotoka."alisema Dalfa akiwa anamtazama Samir aliyebaki kusimama tu. Dalfa alimtazama Samir mkononi na kuona kile kiboksi akiwa amekishika. Kwa haraka isiyo ya kawaida alifika pale na kumpora kiboksi kile hali iliyomfanya hata Samir ashangae. Alibaki kucheka tu Dalfa alikifungua kiboksi kile na kufanikiwa kuiona pete ikiwa mule na funguo.
"Siku zote nimekuwa nikitaka jambo hili litimie, naamini nakwenda kuwa yule niliyetaka niwe. Kwa kuipata pete hii sidhani kama hata hizo nguvu ulizonazo zitaendelea kuwa katika mwili wako. Nashkuru kwa kunitolea pete hii maana nisngeweza nafahamika mimi ni nani.!"alisema Dalfa na kutoa ile pete na kuanza kuiweka kwenye kidole chake huku akiwa mwenye kutabasamu. Akimtazama Samir ambaye hakuonesha dalili zozote za kumzuia kuichukua pete ile hali iliyomfanya hata Dalfa mwenyewe ashangae.
Taratibu Samir alisogea karibu na Dalfa akiwa hana wasi hata chembe.
"Siku zote ubaya hulipwa kwa ubaya, matendo ambayo umewafanyia watu kuwadhulumu vitu vyao leo ndio unafika kikomo. Ukijifanya unanua kila kitu basi kuna wanaojua kidogo lakini chenye faida sana. Sina sifa za kuupata ufalme kwa faida yangu mimi laa, nipo kwaajili ya kuwasaidia watu wengine pia ili tuwe kitu kimoja.... Pete ya Mfalme wa Eden hii hapa ninayo kwenye kidole changu mimi."alisema Samir akionesha kiganja chake kuonesha pete aliyovaa ikiwa kidoleni.
Hali ile ikamfanya Dalfa ashangae na kugeuka kuitazama pete aliyovaa yeye muda huo. Alishangaa kuona pete ile ikianza kujibana na kufanya kukiminya kidole chake. Taratibu akaanza kuona moshi ukianza kutoka chini ya unyayo wake na kuanza kupanda juu taratibu. Alishangaa sana tukio hilo na kujikuta miguuni akijiona mwepesi sana huku moshi ule ukizidi kupanda kwenye magoti.
"Umenifanya nini wewe mpumbavu!!!"alijikuta akipandwa na jazba baada ya hali ile kushuhudia ikimtokea.
"Hizo nguvu zilizopo kwenye mwili wako sio zako. Hivyo hapo ndio zinakuaga kwa mara ya mwisho zirudi kwa mwenyewe. Usishangae Dalfa haya ndio malipo yako kwa yale uliyofanya."alisema Samir akiwa anamaanisha kweli. Kauli hiyo ikamfanya Dalfa ashangae na kuona ni dhahir nguvu alizonazo zinazidi kunyonywa tu kwa pete ile. Alijaribu kuzia lakini haikuwa rahisi hadi kuangusha fimbo ile alioishika. Alijaribu kupotea arudi katika ardhi yake lakini ajabu alishangaa kujiona amerudi Eden tena pale ambapo alipotoka akishuhudia wale askari aliowaweka nguvu wakianza kuwa wachovu gafla. Hali hiyo ikawafanya askari wa Eden watumie nafasi hiyo kuwakata kwa mapanga hadi kuwamaliza wote, Jamal alikuwa tayari katumiwa sana na Dalfa hivyo hakuwa na nguvu za kuendelea kupambana hali iliyomfanya ashambuliwe na kuuliwa kiurahisi sana na askari wa Eden.

Dalfa alibaki kutazama tu asielewe afanye nini huku moshi ule ukizidi kupanda na kufika tumboni. Muda huohuo Samir alitokea naye akiwa amekamata fimbo ile ya Dalfa aliyoiangusha kule. Askari wote wakawa wanatazama kinachoendelea pale huku Maya akisogea taratibu hadi akiposimama Faraj wakiwa wanamtazama Dalfa.
"Huyu mnayemuona hapa ndiye Dalfa.. mtu ambage ameleta tafarani nyingi sana ndani ya Eden. Huyu ndiye aliyemuwekea uchawi Maya akawa kitandani kwa majuma kadhaa kama amekufa,lengo akijua Mfalme na Malkia watamtafuta ili aweze kumsaidia Maya naye aichukue Eden. Huyu ndiye aliyemuua Mfalme Siddik hadi sasa mwili wake upo ndani. Hii yote ni tamaa ya kuitaka Eden. Sidhani kama mtu huyu anastahiki kuendelea kuishi kwa hiki alichokifanya."alisema Samir na taratibu wananchi wakaanza kufungua milango ya nyumba zao kutoka nje kwenda kushuhudia kinachoendelea baada ya kujua mambo yamekuwa shwari. Walifika eneo lile na kumshuhudia Dalfa mwenyewe. Kwa wale waliokuwa wakimfahamu walishangaa kuona leo amekamatika kirahisi. Hasira alizonazo Dalfa alitamani kufanga jambo lakini haikuwa rahisi. Pete aliyoivaa mwenyewe haikuwa ya kawaida, ilizidi kunyonya nguvu zake zote na muda huohuo ule moshi na pete ile vikapotea na kumuacha Dalfa akiwa amesimama pale. Faraj na Samir walitazamana na kufahamu kwasasa Dalfa hana kitu chochote mwilini mwake. Hata yeye mwenyewe alishangaa kuona amekuwa tofauti na alivyo mwanzo. Hapo ndipo Samir akatoa amri auawe kwa kunyongwa lakini Maya akazuia. Watu wote walimtazama Maya kuona amezuia Dalfa asiuliwe. Hata yeye Dalfa aligeuka kumtazama Maya kuona huruma ile aliyonayo akapiga magoti akizidi kuweka kuruma ili apate kusamehewa. Maya alichukua upanga wa Faraj na kumsogelea Dalfa akiwa pale amepiga magoti.
Hali ile ikamfanya Dalfa aangue kilio kuona anakwenda kuadhibiwa kifo. Hata alioposimama karibu yake Maya alibaki kumtazama Dalfa aliyekuwa na sura ya huruma.
"Nakuomba sana Maya.. sitaweza kufanya lolote kuanzia sasa.. nisamehe Maya nakuomba."alisema Dalfa kwa huruma ya hali ya juu. Huruma ambayo haikuweza kumbadilisha Maya kile alichokusudia. Mtu aliyemfanya awe kitandani muda mrefu leo hii anamuomba msamaha, mtu aliyemuua Mfalme ambaye ni baba yake leo hii anhitaji kusamehewa. Hakuweza kusikiliza kauli yeyote kutoka kwa Dalfa na bila huruma aliupitisha upanga wake kwenye shingo ya Dalfa na kuacha damu zikiruka na kuchafua nguo za watu wa pembeni, papo hapo Dalfa akaenda chini na ndio ukawa mwisho wake.
Watu waliangua shangwe baada ya kuona Eden imerudi katika mikono salama tena. Askari na pamoja na wananchi wote wanaenda chini na kuweka vichwa vyao chini kumpa heshima Samir kama Mfalme wao mpya. Hata Faruk pamoja na Maya wakafanya hivyo na kumfanya Samir aangushe chozi la furaha kuona amekamilisha kazi aliyoipanga kuifanya. Hakika usiku huyo ulikuwa ni wa furaha kwa kila mtu japo askari wengi wamepoteza maisha kwa vita hiyo ya usiku.
Iliwabidi wananchi wakisaidiana na askari kuanza kukusanya maiti za askari wao na kuwahifadhi mahala huku maiti za adui zao wakiwachukua na kwenda kuwatupa mbali maporini.
Iliwabidi Samir na Maya waingie ndani sasa kuutazama mwili wa Mfalme Siddik, ni wazi kuwa amefariki na kuwaachia majonzi watu wake. Maya alilia sana kumpoteza baba yake lakini haikuwa na jinsi jambo hilo limefanyika. Ilimlazimu Faraj arudi kule kwenye kijiji chake cha Gu Ram kwenda kumpa taarifa Malkia Rayyat ambaye alishtuka kusikia hivyo. Huzuni na majonzi yalimuandama baada ya kutambua mumewe ameuawa. Bila kusubiri wakaanza safari ya kurejea Eden kwaajili ya mazishi ya mumewe.
Eden nzima taarifa hizo zilisambaa na kila mtu alilia kwa jinsi alivyokuwa akiongoza taifa hilo Mfalme wao. Basi taratibu za mazishi zikaanza kufanyika usiku ule ili panapokucha Mfalme aweze kupelekwa kuzikwa.
Na alfajiri ya siku hiyo Rahim aliongozana na vikosi vya askari wengi kuelekea Eden lengo ni kutaka kuipindua falme hiyo bila kujua kilichotokea.

Hadi kulipopambazuka kila mtu alikuwa tayari kwaajili ya kuuaga mwili wa Mfalme Siddik. Kwenye barabara kuu walisimana watu pande mbili kuusubiri mwili wa Mfalme upite ili waweze kuuaga. Baada ya muda askari wa Eden waliutoa mwili wa Mfalme ukiwa kwenye jeneza na kuanza kulibeba kuelekea kunako makaburi ya wafalme wote waliopita. Mji mzima ulikuwa ni kilio kwa wananchi huku jeneza likipita kuelekea makaburini. Majeshi yote ya askari walikuwa nyuma wakiusindikiza mwili huo. Hakuna aliyebaki ndani kila mtu alielekea makaburini kushuhudia safari ya mwisho ya Mfalme Siddik.

Baada ya nusu saa Rahim aliweza kuwasili na majeshi yake ndani ya Eden. Ajabu wakipofika hawakuona mtu yeyote ambaye anakatiza mitaa zaidi ya kuku na mbwa wa mitaani. Hali ile ikawafanya wapate mashaka. Ilibidi wazidi kusogea mbele hadi walipofika kwenye falme nje na kukuta lango limefungwa.
"Wameenda wapi hawa watu?"aliuliza Rahim huku akiangalia huku na kule na askari wake. Wakiwa katika sintofahamu hiyo waliona ndege wengi wakiruka juu angani wakitokea sehemu moja kuelekea pengine. Ishara ile iliwajulisha huenda kuna watu wanakuja. Wakasimama sawiya na kukamata mapanga yao kujiandaa kwa lolote. Hammadi.... walichokiona mbele yao askari hao wa Rahim wote wakaweka silaha zao chini taratibu kuashiria wamesalimu amri. Idadi kubwa ya wananchi pamoja na askari wa Eden iliwaogopesha sana na kujua kamwe hawataweza kuwamaliza watu wote pale. Rahim aliwashangaa askari wake kuona wamechukua uamuzi ule wa haraka kabla hata hawajapambana.

Hata baada ya kuwasili Samir pale mbele yao ilimfanya Rahim ashangae kuona mtu huyo amevaa mavazi ya kifalme. Walibaki wakitazamana kwa muda, bila kutegemea Rahim alitupa upanga wake chini na kuinama kumpa heshima Samir akikubali kuwa ni Mfalme. Hata askari wake aliunguna naye wakamfuata kumpa heshima ile Samir. Jambo lao walilokuja kulitimiza liliishia hewani baada ya kuona pamoja na kuwa na nguvu za kichawi Samir lakini watu wameridhia kuongozwa naye hivyo hawakuweza kuwabadilisha mawazo yao.
Hawakuwa na uwezo wa kufanya lolote hata Samir alijua fika kuwa walikuja kwa shari, hakutaka kuwadhuru aliwaamuru waondoke haraka sana na Rahim akafanya hivyo pamoja na askari wake kurudi katika falme yao.

Baada ya miezi kadhaa Malkia Rayyat alimkabidhi rasmi Samir falme ile aiongoze naye akawa kama mama wa Maya. Jambo hilo Samir alilikuza na kuamua kuandaa harusi kabisa na kuweza kumuona Maya na kumkabidhi rasmi kuwa Malkia. Maya aliichukua pete ile ya Samir ambayo aliichukua kule msituni na kuweza kumvalisha mumewe huyo na kufanya tukio lile la Faraj alilolitabiri litimie.
Baada ya siku kadhaa kupita Maya alihitaji kuelekea kule nyumbani kwa Jafari. Ilimbidi mwanaume amfuate Faraj kumueleza jambo hilo. Alibaki kutabasamu tu huku akimtazama Samir.
"Sio rahisi tena kurudi kule ulipotoka Samir. Madam umeshaivaa pete hiyo basi maisha yako yatakuwa ni hukuhuku Eden na sio kurudi kule tena. Kule kuna mtu kama wewe na ataendelea kuwepo siku zote ni sawa na wewe jinsi ulivyochukua uhalisia wa Samir. Sahau jina lako la Jafari tena kuanzia sasa wewe ni Mfalme Samir."alisema Faraj akiwa kwenye kijiji chake cha Gu Ram na kumfanya Samir apate kutambua kuwa hawezi tena kurejea Tanga na maisha yake yote ni Eden. Alikubaliana na hali hiyo wakaendelea kuongea mambo mengi sana huku akimpa nafasi Faraj ya kuhama na watu wake kuja kuishi Eden akiwaahidi kuwapa sehemu za kuishi.
Faraj alishukuru kupewa nafasi hiyo lakini hakuwa tayari kuishi Eden, alitamani kuendelea kuishi GU Ram miaka mingi zaidi ili aweke historia.
Samir alimuelewa na baada ya muda aliagana na rafiki yake huyo kurudi zake Eden akiwa kama Mfalme.

MWISHO
 
Aisee asante sana mkuu,kwakwel unafaa umetupa burudani bila arosto,tunasubiri mambo mengine mazuri zaidi
 
Dah! Bonge la stori kaka pia umenikumbusha mbali sana nko Mwanza ila napajua poa Kabuku na Kaludege dah Handeni hiyo Tanga hapo Kwaludege kwa kina Jafari ni bush kinoma ila pako barabarani mi nimekaa sehemu inaitwa Chogo kama miezi miwili mwaka jana so kwaludege ndio njia yetu pale...
 
Kwa kweli ni Hadith nzuri Sana japo Ina vipande vingi vilichanganywa hapa mwishoni mfalme Joha kuitwa Faruk na mengine ila yote ya yote kitu kilitulia sante sana mkuu
 
Hadithi tamu sana, hongera mkuu kwa kuimaliza
 
SIMULIZI: PETE YA MFALME WA EDEN
MTUNZI:JAFARI MPOLE
SEHEMU YA 03

ILIPOISHIA
“Mungu wangu haya mabalaa gani tena jamani eh..!“alikasirika sana kuona inashindikana kutoa ile pete hadi alipoona mwalimu wa somo Kiswahili anaingia darasani kwao naye akaamua aende kwanza darasani zoezi la pete atalifanya akitoka darasani.

TUENDELEE

Basi alielekea mahali pake na kukaa kisha akatoa daftari na kuendelea kumsikiliza mwalimu huyo wa Kiswahili aitwae Madam Negele. Alichukua chaki na kuandika somo analofundisha kisha akaandika mada ya siku hiyo na kuwageukia wanafunzi wake.
“haya naomba tuendelee leo, nakumbuka jana tuliishia katika kuchambua mifano ya Hadithi, Riwaya na shairi. Na tulishamaliza kuelezea namna ya Hadithi na Riwaya zinavyokuwa na mifano yake nikawapa, ila kwenye Simulizi ya kubuni nilielezea na nikatoa mfano kidogo wa ile simulizi ya NDOTO YA AJABU jinsi ilivyokuwa si ndio.?“aliuliza Madam Negele.
“ndiooo...“walijibu wanafunzi na mmoja wapo akasimama.
“ila Madam ile simulizi hukuimalizia aisee tamu sana ile tungeomba leo umalizie mfano wako“alisema Kijana mmoja aliyeitwa Ayubu, Madam alitabasamu huku akiwaangalia wanafunzi wake waliokuwa wakimuunga mkono kijana Ayubu.
“jamani ile ni ya kubuni tu na haina ukweli wowote..ila sawa wacha nisimulie kidogo maana tupo kwenye kipindi chake, niliishia wapi?“aliuliza Madam na kijana Jafari akasimama.
“pale ambapo Mfalme Saleh na Malkia Samira walipokuwa wakitoka kule Pangoni halafu nje Sabiha na Malik walikuwa wamejificha wakiwasubiri wawamalize, “alisema Jafari na kukaa chini.
“duh mpo makini kweli maana nilishasahau, haya basi bwana Mfalme na Malkia Samira walitoka mule pangoni wakiwa na furaha sana maana washafungishwa ndoa na Mfalme wa mwanzo wa taifa la Eden na pia wakapewa zawadi ya tufe lile na kila mmoja akakabidhiwa pete ambayo ni zaidi ya ulinzi kwao.“alisema Madam na kumfanya Jafari akumbuke ile pete alionayo kidoleni, aliitazama na kuanza kujenga hisia kama ni yeye ndiye Mfalme amevaa ile pete ambayo ni zaidi ya ulinzi kwake.
Alijikuta akijilaza kwenye dawati akiitazama ile pete kwa umakini sana huku akiyapitia maneno yaliyoandikwa kwenye pete hiyo ambayo hakuweza kuyatambua. Alisikia akiguswa bega lake na kumfanya ainuke pale alipoegemea kwenye dawati.
Alishangaa kumuona msichana ambaye hakuweza kumfahamu kwa sura, uzuri wake uliochangiwa na macho makubwa yalion‘gaa yalimfanya Jafari amtazame kwa muda bila kuchoka, yule msichana aliachia tabasamu la aibu huku akimtazama Jafari.
“Karibu Eden...“alisema msichana yule na kumfanya Jafari amshangae, lilipotajwa jina la Eden akakumbuka ni nchi ambayo ni ya kifalme na aliisikia kutoka kwa Madam Negele aliyewasimulia Simulizi ya NDOTO YA AJABU. Ndipo akili zikamjia kuwa alikuwa darasani muda huo, akajikuta akitazama mbele ili kumuona Madam aliyekuwa akiwasimulia Simulizi darasani, ajabu ni kwamba hakukuwa na Madam wala ubao kwa mbele, alipotazama pembeni kuangalia wanafunzi wenzake hakuona hata mmoja na kujikuta akiona vitabu vingi vikiwa ndani chumba hicho. Alijitazama pale alipokaa na kukuta amekaa kwenye kiti ambacho ni tofauti na dawati la shule KWALUDEGE. Ilimbidi asimame ghafla kwa kuogopa akawa anatazama huku na kule na kuona hali ambayo ni tofauti kabisa na mazingira ya darasani alipokuwepo.
“huna haja ya kuogopa Jafari, upo Eden kwasasa, na mimi ndio mwenyeji wako kuanzia sasa, naitwa Nadhra.“alisema mrembo yule akijitambulisha kwa Jafari ambaye bado hakuweza kuelewa.
“wewe...wewe... kama ushirikina wenu pelekeni huko, mimi nilikuwa darasani nasoma naomba nirudishe uliponikuta samahani sana sikujui hunijui na sitaki kukujua kwanza, nirudishe darasani niendelee kusoma.“alisema Jafari akiwa haelewi mazingira ambayo amejikuta yupo ghafla.
“sawa nitafanya hivyo ukitaka, ila nimekuleta Eden ufahamu mazingira ya huku mara moja kabla hatujaanza kufanya kazi pamoja.“
“wewe ndio uliniweka hii pete kidoleni!? "aliuliza Jafari akiwa anamtazama Nadhra.
“sijakuweka mimi ila ilikufuata yenyewe, hiyo ni kama zawadi kwako na huenda ikakusaidia kwenye maisha yako.“alisema Nadhra na kumfanya Jafari aitazame ile pete, alikumbuka lile tukio la kuchapwa bakora na Mwalimu mkuu lakini ajabu hakuweza kusikia maumivu yeyote na kuhisi huenda ni kwaajili ya pete hiyo. Akiwa kwenye tukio la kuitazama pete ile ghafla akasikia sauti tu ikimuita.
“we Jafari...“alistuka na kutazama mbele yake.
“jana hukulala kwenu? Hebu amka kanawe uso nje kwanza ndio urudi darasani nahisi hata tulicho kijadili hapa hukusikia nenda nje kwanza kanawe“ ilikuwa ni sauti ya Madam Negele aliyekuwa mbele ya darasa, Jafari alibaki kutazama darasa zima akiona anaangaliwa na wenzake. Alishangaa baada ya kuzidi kuona maajabu maana sekunde chache tu alikuwa akiongea na Nadhra ajabu saivi anajiona yupo tena darasani. Hakutaka kuonesha utofauti wowote akanyanyuka na kutoka nje moja kwa moja akaelekea kwenye bomba la maji na kufungulia akaweka kichwa chake maji yakaanza kutiririka. Aliona ni kama ndoto huenda akawa anaota baada ya kuambiwa na Madam kuwa alikuwa amelala darasani.
“itakuwa ndoto tu hii..“alijisemea mwenyewe akikataa kuamini ukweli wa mambo, lakini kitu pekee kilichomfanya achanganyikiwe ni ile pete ambayo bado ipo kidoleni kwake, aliitazama kwa umakini bila kuelewa. Alikumbuka maneno yale ya Nadhra kuwa huenda ikawa ni zawadi kwake ya maisha, alipokumbuka tena tukio la kuchapwa alianza kuhisi huenda ikawa sio ndoto tena bali ni ukweli. Taratibu akajikuta akianza kuamini mambo yale japo moyo unakuwa mzito kukubali.
Aliitazama tena ile pete kwa umakini.
“ina maana haya mambo yapo kweli? Nilikuwa nahisi ni Simulizi tu za kubuni kumbe yaweza kuwa kweli, sasa kwanini mimi? Hakuonekana mtu mwengine zaidi yangu mimi tu.? "alijiuliza sana Jafari bila kupata jibu kamili, aliamua kunyanyuka zake na kurejea tu darasani huku moyo wake taratibu ukianza kuamini matendo yaliyomtokea siku hiyo. Alipokaa kwenye dawati lake na Madam yule akawa anaandika ubaoni kazi ya kufanya wanafunzi.
“hii kazi nitaikusanya Ijumaa, leo Jumatano hadi siku hiyo mtakuwa mmemaliza, nahitaji kila mmoja wenu atunge kisa cha kuvutia ambacho hata mtu akisoma asisimke au kama ni kisa cha kutisha aogope kabisa, na nitoe tu ahadi kwa atakayefanya nikavutiwa na simulizi yake nampa ofa ya kula chakula na sisi walimu kwa wiki nzima atapumzika kula mapure (makande) ya shule na wenzake.“alisema Madam kwa tabasamu na kuwafanya wanafunzi wote wafurahi kusikia hivyo maana chakula wanachokula walimu ni tofauti na chakula cha wanafunzi. Kila mtu alitamani nafasi hiyo aipate yeye endapo akiandika simulizi itakayomvutia Madam Negele.

Baada ya kuondoka mwalimu huyo darasa likabaki na maongezi kuhusu kazi hiyo waliyopewa, kwa Jafari yeye hakuwa mwenye kufuatilia kazi hiyo waliyopewa yeye alikuwa akijadili tu na nafsi yake namna itakavyokuwa baada ya kufahamu kuwa ile pete iliyopo kidoleni kamwe haiwezi kutoka , aliona ni vyema akaonana na yule msichana Nadhra ili amuelezee kwa kina zaidi juu ya swala hilo.

Masaa yalizidi kwenda na muda wa mapumziko ulipofika Jafari kama kawaida yake alielekea kwenye kengele apate kugonga, alipoikaribia akawa na woga baada ya kuona ndio sehemu alipoipata ile pete, akajipa moyo na kukamata kile kichuma akagonga kengele kama kawaidia na wanafunzi baada ya kusikia wakaanza kutoka madarasani kwenda kupata kifungua kinywa kwenye mikahawa iliyopo pembeni na shule yao.

Muda huo akapita msichana Aziza na Jafari alipo muona ilibidi amfuate.
“Aziza...“aliita Jafari na kumfanya Msichana huyu asimame na kugeuka, alipomuona Jafari alibinua mdomo na kuangalia mbele.
“mambo vipi“alisalimia Jafari baada ya kumkaribia Aziza.
“poa tu..“
“si unaelekea kunywa tea.. tuongozane basi.“alisema Jafari na kupiga hatua kuongoza njia.
“we mwanaume mbona unanifuatilia sana? Si nilishakwambia lakini sitaki mazoea na wewe au husikii mwenzetu!“alisema Aziza kwa sauti na baadhi ya wanafunzi waliokuwa wakipita pembeni waliwatazama na kuendelea na safari yao.
“jamani taratibu basi tusiwafaidishe watu, mimi nimeongea kwa wema tu jamani sina nia mbaya lakini“
“awe Wema awe Diamond mimi hainihusu, sitaki kuongozana na wewe na narudia tena kukwambia sihitaji mazoea na mlugaluga sawa, hebu nipishe uko..“alisema Aziza na kumpushi Jafari akaendelea na safari yake. Jafari alibaki kumtazama tu mrembo huyo aliyejaaliwa uzuri na nyuma ameumbwa sawiya kabisa na ndio sababu iliyomfanya Kijana huyo ajaribu bahati yake mara kwa mara kwa mrembo huyo bila mafanikio.
“dah mimi sijui nina kizizi gani yarabbi...haya bana..“alisema Jafari na kuchanganya mwendo naye akaenda zake kupata chai akashangaa kuona ameshikwa mkono akiwa anatembea na alipotazama akamuona ni Eliza best wake na ni mtani wake pia.
“unajua nilikuwa nakukimbilia ila nilipokuona umesimama na wifi ikabidi nisimame tu niwaache mmalizane kwanza wapendanao.“alisema Eliza akiwa mwenye tabadamu usoni. Jafari alitazama msichana huyo akiwa na hasira zake mwenyewe za kukataliwa.
‘Eliza unapoelekea sasa nakutia kofi unikasirikie.“
“ah mimi mbona kupigwa nishazoea mwenzio, ipite siku bila kupigwa sisikii raha yani we nipige tu Jeffy, ila aka mwenzangu kama mmegombana wenyewe mkamalizane wenyewe mimi hainihusu.“alisema Eliza.
“hivi lini niliwahi kukwambia Aziza amenikubalia tukawa wapenzi mbona unakuza mambo we boya.?“alisema Jafari akionesha kukasirika.
‘acha ujinga Jeffy... ina maana tangu siku ile bado tu unaimbisha haelewi?“aliuliza Eliza na kumfanya Jafari akose jibu la kumpa.
“dah Jeffy unazingua, mimi najua mambo fresh yule ndo wifi ndio maana nakutaniaga sana kumbe dah...aisee nsamehe bure sikujua, ila nini tatizo, wapi umekwama naweza kukusaidia.“alisema Eliza na kumfanya Jafari amtazame tena.
“hanitaki ndio alivyoniambia, na kila siku ninavyomsumbua kumuelewesha ndio anaona namsumbua, nahisi leo ndio amenitapika kabisa na kuniambia nikome kumfuatilia.“alisema Jafari akiwa amesimama na Eliza karibu na mkahawa.
“ah achana nae basi utaumia bure ukipenda kwa mtu asiyekupenda, wanawake wapo wengi mbona unachagua tu wewe, hata hivyo nilisikia ticha Saidi anamfukuzia pia sasa sielewi kama ndio kashampata hadi Aziza anakukatalia wewe ama vipi, ila hiyo nimeisikia sina uhakika kama ni kweli.“alisema Eliza na kuzidi kumchanganya Jafari.
Wakaamua waache kwanza mada hizo watafute chai maana baadae wana kikao na walimu wao.
ITAENDELEA
Kaliiiiiiiii
 
Back
Top Bottom