SIMULIZI: Pete ya Mfalme wa Eden

SIMULIZI: Pete ya Mfalme wa Eden

shukran mkuu,tuendelee natamani kuona kifo cha huyo baradhuli jamal
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN
MTUNZI:JAFARI MPOLE
SEHEMU YA 21

ILIPOISHIA
* Jamal apandishe hasira kuona kama ni dharau na maneno ya kashfa kwake, alijikuta akiunyanyua upanga wake kwa nguvu huku kila mtu akipata kuona kinachoendelea pale uwanjani.*

TUENDELEE.
Bila kuchelewa Jamal aliushusha upanga ule na kumchana yule askari mgongoni mwake na kumfanya apige kelele sana na watu wote wakashuhudia tukio lile. Tukio ambalo lilimfanya Samir ashangaa na kuona ile ndoto ambayo ameiota ilienda tofauti na vile anavyoona pale.
Kila mtu alistaajabu kuona vile hata Mfalme alijikuta akisimama pale alipo baada ya kuona Jamal akifanya shambulio lile kwa askari wake. Baadhi ya watu walionekana kumshangilia Jamal kwa kuona amefanikiwa kushinda pambano hilo akiwemo Lutfiya ambaye aliona ushindi bila shaka unakaribia kwenda kwa Jamal. Mfalme Faruk alifurahi sana na kumpigia makofi mwanawe kwa kufanikiwa kushinda pambano lile. Hakuwa na jinsi Mfalme Siddik aliamua kurudi kukaa japo moyoni anaumia kuona askari wake ameshindwa tena kaumizwa vibaya.Walikuja watu maalumu wakamchukua yule askari na wengine wakamtoa yule mtu aliyeuliwa na Samir.
Jamal alikitoa kinyago chake na kuanza kutamba sasa pale uwanjani nakujikuta alishangiliwa na watu wakimkubali kwa mapigo yake na kuona anafaa kumlinda Maya muda wote. Samir alibaki kumtazama Jamal kwa yale mambo aliyofanya,alibaki kujiuliza sana kuhusu ndoto ile kama ndio tayari ilipangwa iishe hivi au kuna jambo lengine lazima limhusi Maya pia!. Hakupata jibu kamili juu ya jambo hilo na kubaki kuushika mkono wake uliojeruhiwa na taratibu wakaanza kutoka mule uwanjani kwenda kupata mapumziko.
Kila mtu akawa anaongelea sasa fainali ya watu wawili waliobaki, hakuna aliyetegemea kama Samir mpaka sasa ameweza kufika katika hatua hii ya sasa.
Kwa Maya aliona ni kama ndio mwisho wa Samir pale na nafasi ile inayogombaniwa itaenda kwa Jamal, hii ni kutokana na kuumia mkono wake Samir. Hali hiyo kila mmoja wapo akiwemo Mfalme Siddik ilimfanya naye awe na hofu hiyo juu ya kijana wake. Kwa jinsi ambavyo ameonekana Jamal akipambana na baadhi ya washiriki waliopita na kufanikiwa kuwaangusha hadi yeye kufika hapo.
Muda huo Samir alikuwa akiuguza mkono wake mule ndani walipofika. Alifunga kitambaa ile sehemu iliyojeruhiwa na kisu na baada ya muda akamzarazama Jamal aliyekuwa hana habari.
Alichokifanya ni kuunyanyua ule mkono ulio na pete kisha akashika lile jeraha huku akitamka maneno fulani lengo ni kupata ahueni kwenye mkono ule apate kuendelea na mpambono dhidi ya Jamal ambaye muda huo alikuwa amekaa kama kawaida yake huku akiwa ameweka upanga wake mbele. Muda huohuo Samir alipotoa mkono wake alipata kuona jeraha lile limepotea na kurudi kawa awali. Alitabasamu kuona vile na kupata tumaini la kuendelea, na baada ya muda kadhaa washiriki hao wawili waliitwa uwanjani kuweza kukamilisha kile ambacho kimekuwa kikisubiriwa na kila mtu.Watu wote walishangilia baada ya kuwaona Jamal pamoja na Samir wakisimama katikati ya uwanja huku kila mmoja wao akiwa ameshika upanga wake mkononi. Maya alikuwa mwenye hofu juu ya Samir hasa jinsi anavyoonekana kuwa mwenye jeraha lililofungwa kwa kitambaa. Mfalme Faruk akawa anatabamu tu na kuona ndio muda wa kushuhudia mwanaye akichukua ubingwa huo. Walisogezwa karibu na na kubaki kutazamana huku Jamal akimyazama Samir huku akiwa mwenye kutabasamu, tabasamu la kinafki ndani yake.Yule mtangazaji akaanza kuwapa maelezo ya pambano hilo wanalilotataji kianza, na baada ya dakika kadhaa alirudi nyuma na kuacha jukwa limilikiwe na watu wawili.

Kelele za kushangilia zilisikika pande zote iila mtu akimshangilia yule ambaye amemvutia kwa kupambana kwake.
Kila mmoja wao alikuwa makini sana dhidi ya mwenzake na hata Jamal alipoanza kupeleka mashambulizi kwa Samir mwenzake alikuwa makini pia kuzuia asije kujeruhiwa na upanga mkali wa mtoto wa Mfalme Faruk. Hakika watu walikuwa makini kutazama mpambano wa kumtafuta mtu mmoja aweze kuwa mlinzi wa binti wa Mfalme Maya. Mfalme alikuwa akitazama kuona kijana wake Samir akionesha uwezo ambao hakuna hata mmoja wa watu waliotegemea kama angeweza hata kumpiga mtu mmoja kati ya wale wote waliokutana naye na kuweza kuwashinda. Hakika alikuwa akipambana na Jamal muda ule bila kuhofia kitu hali iliyowafanya baadhi ya watu washangae maana aliomekana kuumia mkono awali. Alileta upinzani mkubwa sana kwa Jamal ambaye muda wote alikuwa akitafuta namna ya kumdhibiti mpinzani wake. Dalfa alikuwa akitazama mpambano wa wawili wale na kuona jinsi ambavyo kila mtu akionesha kuwa makini sana japo lengo lake likiwa kwa Samir.
Jamal alivyoona anazidi kuzuiwa na Samir ikabidi atumie njia mbadala ya kumdhibiti mpinzani wake, alirudi nyuma kujipanga upya kisha akaingiza mkono wake ndani ya nguo aliyovaa kifuani na kuurudisha kama kawaida huku akimtazama Samir akiwa anahema kwa kasi. Alinyanyua upanga wake na kushika kwenye makali kwa mkono ule alioutoa ndani ya nguo yake na kuanza kufuta upanga ule. Jambo lile likamfanya Dalfa kule alipo atambue kuwa Jamal kuna kitu amekipaka kwenye upanga ule japo hakutaka kusema lolote na kubaki kushudia nini kitatokea.
Alikuwa hana habari Samir baada ya kupata kutazamana kwa sekunde kadhaa walijikuta wakisogeleana kila mtu akiwa na moto wa kummaliza mwenzake. Watu walizidi kushangilia tu kiasi cha kumfanya hata Mfalme Siddik apate furaha kuona jinsi mpambano ule ulivyo mkali ambao hafi dakika hiyo haikujulikana nani atakaeibuka kuwa mshindi.
Samir alijitahidi kadri ya uwezo wake na kwa bahati ya Jamal akapata nafasi ya kumchana kwa upanga ule Samir kwenye uleule mkono wake ambao awali alipata kujeruhiwa. Maumivu aliyoyasikia yalimfanya arudi nyuma kwanza huku akitazama mkono ule uliochanwa kwa upanga ukibubujika damu. Mfalme Faruk alifurahi sana na kuona huo ndio ushindi kwa mwanaye. Muda ule alipata kumuona mwanaye akifanya tukio lile la kupaka sumu ambayo ni yeye ndiye aliyempatia mwanaye kipindi akiwa anajiandaa kwaajili ya kuja Eden kwenye mpambano huo. Hivyo sumu ile ikishagusa tu kwenye damu basi ni dhahiri kwamba haitachukua dakika tano mtu huyo kuweza kupoteza maisha.
Jamal baada ya kulifanikisha zoezi hilo akawa mwenye kujiamini na kusubiri muda maalumu apate kutazama hali ya mpinzani wake inavyobadilika muda hadi muda.
Samir alijikuta anaanza kuona mkono ukiwa mzito sana kana kwamba umekufa ganzi hadi upanga wake wake alioshika ukamdondoka mkononi. Alistaajabu sana kuona tukio hilo likimkuta hali ambayo hakuwahi kuona toka awali. Aliinama chini kushika ule upanga lakini alichokitegemea hakikuweza kutokea. Hakika mkono wake ulikuwa hauna kabisa nguvu ya kuweza kushika chochote.
Maya na Malkia walishangaa kuona Samir akienda chini na kupiga magoti huku akiushika mkono ule aliokatwa na upanga wa Jamal. Hakuna aliyefahamu kwamba kuliwekwa nini kwenye upanga ule huku watu wakijua Samir ameenda chini kwasababu ya maumivu ya upanga aliyokatwa. Jamal aligeuka na kumtazama baba yake aliyekuwa akitabamu tupale alipo, alitikisa kichwa chake kumuamuru mwanaye amalize kazi ili nafasi iliyokiwa ikigombewa itue kwake Jamal. Tararibu akaanza kupiga hatua Jamal kusogea pale alipo Samir akiwa amepiga magoti chini, alimzunguka na kuwa nyuma yake akawa anamtazama tu akitafakari ammalize kwa staili gani.
Watu wengi waliokuwa wakimshangilia Samir walinyamaza kimya na wengine kushika tu midomo yao hawaamini kile ambacho anakwenda kufanyiwa mtu wao.
"Mama Samir anauliwa!"aliongea Maya akionesha kuwa na huruma na Samir. Hata Mfalme Siddik alibaki kumeza mate pale alipo hana jinsi maana ndio sheria ya mchezo huo ulivyo ili apatikane mshindi. Taratibu Jamal alionekana kunyanyua upanga wake ule ambao aliupaka sumu kali sana inayomtesa Samir muda ule. Hata mdomo wae ukaanza kuonesha kukauka kutokana na sumu ile kuwa kali sana. Alijikuta akiitazama ile pete yake tu na kujitahidi kuongea lakini hakuweza maana hata sauti ilikuwa ngumu kutoka, akabaki kujisemea tu moyoni huku akiitazama pete yake
" Sitojali kama kuna mtu anaitwa Dalfa ananitazama, nahitaji kushinda hili pambano ili niweze kumuweka salama Maya. Huyu mtu nina wasiwasi naye simuamini tangu nilipomuona ndotoni.. NAHITAJI NIUNYANYUE HUU UPANGA NITUMIE NGUVU ZILIZOPO NDANI YAKE ILI NIMZIDI HUYU MTU.."alisema Samir huku akifanya kwa vitendo, alipeleka mkono wake ule kwenye upanga wake na kujikuta akiukamata barabara na kuunyanyua. Na muda huohuo Jamal ndio alikuwa akilishusha panga lake kumkata mgongoni Samir lakini alishangaa kuona upanga wake unazuiwa pindi ulipofika sehemu aliyokusudia kukata. Samir alizuia kwa kuliweka panga lake na taratibu akanyanyuka na kuchoropoka pale kwenye hatari. Umati wa watu ulionyamaza ukaanza kupiga shangwe kuona Samir ameinuka tena. Dalfa ndio akapata kuamini kile alichokisubiri muda wote kuwa Samir zile nguvu anazo na sasa anazirumia kulikamilisha swala hilo. Alirudi nyuma na kukaa vizuri Dalfa huku akitabasamu baada ya kubaini hilo. Maya pamoja na Mfalme walijikuta wakifurahi kuona Samir ameinuka tena na kuendelea na mpambano. Mfalme Faruk alibaki kutoa macho haelewi kile ambacho anakiona mbele yake, hata mwanaye pia alibaki kushangaa tu kumuona Samir ameinuka tena pale na kuweza kuukamata upanga wake tena.
Lutfiya aligeuka kumtazama Mfalme Faruk maana walichokipanga kimekwenda tofauti na vile walivyotegemea.
Kwa ujasiri wa kupambana Jamal akasogea kwa Samirna kuanza kupambana naye tena lakini safari hii alikipata cha mtemakuni. Samir akionekana kuwa mwepesi maradufu kila ashambuliwapo anakwepa na kuwa nyuma ya adui wake kisha humchana kidogo kumpa maumivu Jamal. Alisirika sana kuona kibao kimeanza kumgeukia gafla, hakutaka kukubali kushindwa alimfuata zaidi kumdhibiti lakini hakuna alichofanikiwa zaidi ya kukatwa na upanga ule wa Samir. Mwisho wa siku hasira zilipozidi kumuandama akajikuta akipambana bila kutumia akili na hapo ndipo Samir akaweza kumvizia kwa kumpiga mtama wa nguvu Jamal akala mweleka hadi chini na alipotaka kunyanyuka alishuhudia upanga ukiwa shingoni mwake kumaanisha amewahiwa hana ujanja. Alitazama na kukutana na sura ya Samir ikiwa inatiririka jasho, bila huruma Samir alinyanyua upanga wake kutaka kutimiza ndoto ile aliyoota isije kutokea hapo mbele na alipotaka kummaliza Jamal alisikia akiamuria aache.
"Inatosha..inatosha.. Hongera kijana kwa kuweza kuwa mshindi wa hili pambano. Ushindi umebaki EEEDEN.."alinyanyuka Mfalme Faruk na kuyasema hayo baada ya kuona angempoteza mwanaye pale. Watu walishangilia sana hata Mfalme na familia yake kwa ujumla ilifurahi kwa kuona aliyetoka kwenye falme hiyo ndio ameibuka kuwa mshindi. Walitoka watu kwenye majukwaa na kuingia uwanjani kwenda kumbeba Samir kwa furaha ambayo waliyopata kuona Samir amewainua.
Mfalme,Malkia,Maya na wageni wengine walioalikwa walinyanyuka na kuanza kupiga makofi kumpongeza kijana huyo. Mfalme Faruk alikuwa akipiga makofi kwa unafiki moyoni akiwa na hasira isiyopimika kuona mwanaye amefeli kupata nafasi ya kuwakaribu na Maya binti wa Mfalme, . Lutfiya alijuwa hana raha kabisa na kuamua kuondoka kabisa ndani ya uwanja.
Dalfa alinyanyuka na watu wake akionesha kuridhikia na kile kilichotokea.
"Hatimaye nimepata kuona nilichokihitaji, huyu leo nammaliza na kuzichukua nguvu zangu zirudi kwangu hatuwezi kuwa wawili."alisema Dalfa huku akitazama uwanjani akimuangalia Samir akiwa juu amebebwa kwa furaha na watu wa Eden.
ITAENDELEA
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN
MTUNZI:JAFARI MPOLE
SEHEMU YA 22

ILIPOISHIA
* huyu leo nammaliza na kuzichukua nguvu zangu zirudi kwangu hatuwezi kuwa wawili."alisema Dalfa huku akitazama uwanjani akimuangalia Samir akiwa juu amebebwa kwa furaha na watu wa Eden.*

TUENDELEE
Mfalme aliwashukuru wageni wake aliyowaalika kwa kuweza kufika katika swala hilo. Mfalme Faruk alijenga tabasamu zito akiweka utofauti wa kile kilichopo moyoni mwake , alibaki kutazama tu uwanjani na kuona jinsi Samir anavyoshangiliwa na kupongezwa. Alipotazama sehemu alizoumizwa zilirudi na kuwa na majeraha kusudi watu wasipate kuuliza lolote.
Baada ya kumalizika hayo alirudi kwenye hali yake ya kawaida huku wengine wakimpungia mikono jwa kama pongezi.

Siku hiyo ikawa ya heshima kwa Samir ambaye alirudi zake kwenye chumba chake na kujilaza akiwa hoi kwa uchovu. Aliutazama ule mkono wake na kuona gafla ukianza kurudisha yale majeraha ambayo ameyapata akiwa anapambana na kubaki kushangaa wakati yalipotea na mkono ukarudi kama awali. Sekunde kadhaa kupita mlango wa chumba chake uligongwa na kumfanya haraka ainuke pale kitandani na kwenda kuufungua. Alipata kuona mzee mmoja akiwa na vijana wake wawili wakia wameshika vyungu vya udongo.
"Pole sana kwa uchovu na majeraha uliyopata ukiwa kwenye uwanja wa mapambano, pia hongera kwa kuweza kushinda na kuwa Mlinzi wa binti wa Mfalme."alisema mzee yule akiwa mwenye tabasamu.
"Asante sana mzee."alijibu Samir akiwa ameshikilia mlango wake.
"Mfalme ametuagiza tuje kukupa matibabu maana uliumia sana, na baada ya kufanikisha hilo atakuhitaji kwenye chakula cha jioni hivvyo ujiandae Samir."alisema yule mzee na kuwageukia vijana wake wakatua vile vyungu. Ilimbidi Samir atoe kiti pale nje na kukaa ili apate kutibiwa na hapo ndio akapata kufahamu kwanini majeraha yale yalirudi tena yenyewe.
Moyoni alijikuta mwenye kufurahi sana maana ni heshima kubwa kula chakula pamoja na Mfalme hivyo akawa anatabasamu tu huku yule mzee akimpaka baadhi ya dawa za asili na kumsafisha kidonda kile.

Siku hiyoEden nzima ilikuwa ikimzungumzia Samir kwa kuweza kupata nafasi ya kuwa mlinzi wa binti wa Mfalme. Hakuna aliyemtegemea kama angeweza kujitokeza na kushiriki mapambano hadi kuibuka mshindi na kuleta furaha kwa watu wa Eden. Si wote waliofurahia ushindi wa Samir wengine kwao ilikuwa ni maumivu na kuzidi kupata hasira. Lutfiya muda huo wa jioni alikuwa na wenzake kwenye nyumba moja wakijadili akiwa pamoja na Mfalme Faruk.
"Tumefeli tena kwa mara nyengine, kijana mdogo yule ametushinda tena na hata sielewi imekuwaje na kwanini amekuwa ni yeye tu anazuia mipango yetu."alisema Mfalme Faruk akionesha kuchukizwa na ushindi ule wa Samir. Wote walinyamaza walimsikiliza Mfalme wao akiporomosha maneno ya hasira sana baada ya kijana wake kushindwa kupata nafasi ile waliyokuwa wakiihitaji.

Muda huo Jamal alikuwa kwenye chumba kimoja ndani ya falme naye akipewa matibabu kadhaa,alikuwa hana raha kuikosa nafasi ile ambayo wamekuwa wakihakikisha wanaipata ili lengo lao litimie.
Baada ya muda aliingia Genarali mkuu wa Eden akiwa na baadhi ya askari na kuwakuta baadhi ya watu wakimtibia Jamal mule ndani.
"Karibu katika falme ya Eden. Mfalme ameniagiza nije kwako kukuangalia maendeleo yako, unajisikiaje kwasasa.?"aliongea yule Generali akimtazama Jamal akiwa amekaa kwenye kiti akipata huduma.
"Niko sawa kwasasa baada ya kupata matibabu."aliongea Jamal akiwa anamtazama yule Generali.
"Naamini utakuwa salama zaidi kwa muda mfupi, Mfalme ametuma nije kukutaarifu kuwa hapo baadae utahitajika kujumuika kwenye chakula cha pamoja ili muweze kukaribishwa katika Eden, umekuwa ni askari wa Eden kuanzia sasa na ni ahadi ambayo aliitoa Mfalme kwa watakaofika hatua ile mliofika hivyo unakaribishwa sana Eden kuanzia sasa."alisema yule Generali kisha akawageukia wale watu waliokuwa wakimtibu Jamal na kuwataka wahakikishe waamaliza kwa wakati. Baada ya dakika kadhaa Generali aligeuka na kuondoka mule ndani akiwa na watu wale waliokuwa wakimfuata nyuma.
Jamal alibaki kutafakari swala hilo la kuingizwa moja kwa moja kwenye jeshi la Eden kulitumikia. Ilikuwa ni heshima kubwa kuonekana kama ni mmoja wa askari wa Eden lakini kwa Jamal ilikuwa ni tofauti kabisa, hakuwaza wala kufikiria kama atakuja kuwa hivyo. Yeye ni mtoto wa kifalme na alishiriki mashindano yale ili apate nafasi moja tu, ya kuwa Mlinzi wa Maya lakini mwisho wa siku imekuwa ni tofauti na vile alivyotegemea.

Huku upande wa pili kwa Dalfa aliweza kutafuta mahala pa kuweka kambi na vijana wake, na usiku ulipofika alitoka na kuanza safari ya kuelekea kwenye falme lengo ni kuzipata nguvu za Samir naye aweze kummaliza kabisa pasiwepo na mtu huyo tena katika ulimwengu.
Baada ya muda kupita Samir aliweza kuelekea mahala ambapo ameagizwa kufika jioni ile, alivaa vyema na kuingia ndani ya falme moja kwa moja akaelekea sebuleni ambapo kulikuwa na ukumbi mkubwa ulioandaliwa vyema kwaajili ya kupata chakula. Hata alipofika mtu wa kwanza kuiona sura yake alikiwa ni Maya akionesha kuwa na tabasamu mwanana lililomfanya hata Samir mwenyewe akumbuke mbali. Alimkimbuka msichana anayempenda sana kule shuleni, Aziza.
"Oh Samir karibu sana japo sio mgeni wa eneo hili karibu Samir sogea hiku."alisema Mfalme Siddik na kuwafanya Malkia Rayyat na Maya wageuke kumtazama Samir aliyeonekana kutabasamu huku mkono wake mmoja ukifungwa bandeji. Taratibu akaanza kusogea pale huku akionesha kuwa na hofu maana si kazi rahisi kuweza kusogea kwenye meza moja na familia ya Mfalme. Baadhi ya askari walibaki kumtazama tu wakiwa wanatabasamu maana hawaamini jama ni yule Samir ambaye kwao hakuwa lolote wakimdharau lakini mwishowe amekuja kujulikana ni zaidi ya watu wenye nguvu zao, kikubwa ni kwamba sasa amekuwa zaidi ya vyeo vyao vya uaskari. Alipofika sehemu ile alisogea askari mmoja alivuta kiti nyuma ili Samir apate kukaa, hata yeye alistaajabu kuona vile lakini hakujali na kuona kama ni kawaida kwake alisogeana kukaa na kuanza kushuhudia meza ile ilivyopendeza kwa vyakula mbalimbali vilivyotanda mezani pale.
"Kuwa huru Samir, haya ndio maisha ambayo umeyapigania kwa jasho lako hadi kuyapata. Halafu umenifanya niamini kwamba watu wapole siku zote wana mambo mazito moyoni kumbe ni mpambanaji mahiri na mwenye uwezo mkubwa sana katika kutumia upanga ndani ya vita! Hakika nimependezwa na upiganaji wako naamini Maya atakuwa kwenye mikono salama."alisema Mfalme Siddik akiwa ameshika glasi ya juisi ya mazabibu.
"Usijali Mfalme wangu, nina imani Maya atakuwa salama siku zote katika uangalizi wangu."alisema Samir na kukamata uma na kisu akaanza kusogeza mnofu kwenye saani na kuanza kukatakata kuanza kula.
"Mimi umenifurahisha pia kuona nafasi hii imechukuliwa na kijana wa Eden tena ambaye tumemzoea na tunamfahamu kiundani zaidi. Sasa uanze maisha mapya kama mlinzi wa binti yangu na usahau maisha yako ya awali."alisema Malkia Rayyat na kumfanya hata Maya atabasamu, alimtazama Samir akiwa mwenye furaha kuambiwa vile na muda huohuo Jamal aliwasili akiwa na askari wawili walio muongoza hafi kufika hapo. Alikaribishwa na yeye na kusogea kwenye meza ile akijenga tabasamu mwanana. Aligongana macho yake na Samir ambaye alionesha tabasamu kwamba wafurahie mualiko ule. Jamal alitabasamu tu lakini moyoni hakuwa na furaha kuhusu Samir, hakutegemea kama anaweza akazidiwa ujanja pale uwanjani na mtu kama huyo. Muda wote pale mezani wakiwa wanakula alikuwa akimtazaka sana Samir haamini kama ndiye mtu aliyemuweka chini na kuchukua ushindi ule. Waliongea mambo mengi na familia hiyo ya kifalme na baada ya muda kila mmoja wao akaenda kupelekwa kwenye makazi yake mpya waweze kupumzika usiku huo. Kwa Samir ilikuwa ni furaha kuona anapatiwa heshima kama hiyo,na ndio ulikuwa mwisho wa kuishi kwenye kibanda chake kuanzia usiku huo. Alipewa chumba kimoja karibu na chumba cha Maya lengo ni kuwa karibu na binti huyo kumuwekea ulinzi.
Maya alibaki kutabasamu tu akiwa chumbani kwake,hakumtegemea Samir kama ndio atakuwa mlinzi wake. Alimzoea sana muda wote hasa akikumbuka akiwa anaongea naye muda mwingi na kumpa ushauri. Kwa upande wake alikuwa ni mshauri wa mambo mengi ambayo alikosa maamuzi,hivyo ushindi wa Samir ulimfanya ajione mwenye faraja sana maana atakuwa karibu na rafiki yake huyo.
Huku wa Jamal bado alikuwa na kinyongo juu ya ushindi ule wa Samir,alijitupa kitandani na kuanza kutafakari mambo kadhaa ambayo walipanga na wenzake lakini mwishowe mtu mmoja ndio anakuja kuwaharibia.
"Huyu mtu ni wa kumfuatilia nijue kwanini anakuwa kikwazo katika mambo tunayopanga siku zote"alisema Jamal akiwa anatazama paa la nyumba akiwa amejilaza pale kitandani.
Usiku huo ulikuwa mwanana kwa Samir ambaye aliandaliwa sehemu mpya ndani ya falme,alikumbuka jinsi alivyopigania nafasi ya kuwa mlinzi wa Maya na mwishowe amefanikiwa japo amepitia mitihani kadhaa. Alimkumbuka Jamal ambaye ndiye alionekana kuwa ni kikwazo kwake hadi akapata kuota lile tukio kuhusu kukatwa kichwa Maya. Alipolikumbuka hilo moyo wake ukaanza kumfikiria Jamal kwa mambo mengi sana akimuwekea wasiwasi akihisi ujio wake sio wa heri.
"Napaswa kuwa makini sana dhidi ya huyu mtu,mbona moyo wangu unakosa raha pindi niikumbukapo ile ndoto! "aliongea Samir akiwa amejilaza kitandani akitafakari hayo .
ITAENDELEA.
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN
MTUNZI:JAFARI MPOLE
SEHEMU YA 23

ILIPOISHIA
* "Napaswa kuwa makini sana dhidi ya huyu mtu,mbona moyo wangu unakosa raha pindi niikumbukapo ile ndoto! "aliongea Samir akiwa amejilaza kitandani akitafakari hayo.*

TUENDELEE.
Taratibu akaanza kunyemelewa na usingizi na baada ya muda mfupi ukamchukua. Usiku huo ndio Dalfa alikuwa akiwasili karibu na jengo lile la kifalme. Alilitazama na kutafakari kujua wapi aanzie na mlengwa mkuu ni Samir ambaye muda huo alikuwa akiuchapa usingizi. Ulinzi ulishamiri kila kona ya jengo hilo kuku askari wakionekana kutembea usiku kucha kuhakikisha usalama. Yote hayo kwa Dalfa hakuweza kutetereka wala kuwa na hofu dhidi ya ulinzi ambo umewekwa. Bila kuhofia lolote alianza kusogea kwenye geti kubwa lile na kuona walinzi wakiwa wanamtazama tu bila kumzuia muda huo. Alipita pale kwenye ulinzi mkubwa na kuingia ndani ya falme,kitendo hicho kikafanya ile pete aliyovaa Samir ianze kumbana kidole bila yeye kuhisi kama kuna maumivu hayo akiwa kwenye usingizi.
Alifika mahala Dalfa na kuanza kuangaza huku na kule akitafuta kujua alipo Samir. Kwa hisia alizonazo akapata kujua yupo chumba gani,taratibu akaanza kuingia kwenye falme huku askari wakiwa wametanda kila kona lakini hawakuweza kumuona. Alizidi kwenda ndani zaidi bila kuwa na wasi hadi alipofika kwenye chumba husika akasogea hadi pale mlangoni akawa anautazama huku macho yake yakiwa yamebadilika na kuwa makali huku akiushika ule mlango na kufanya lile komeo lililofunga kwa ndani kuweza kufunguka. Aliufungua mlango na kuanza kuingia ndani usiku ule. Kulikuwa kumetulia sana huku kelele za maaskari kwa nje zikisikika wakipiga doria kuhakikisha usalama. Alisogea mpaka pale alipolala Samir huku akiwa na macho ya kutisha na kufunua shuka alilojifunika Samir na kuweza kumuona amelala akiwa hana habari. Alitabasamu Dalfa na kuanza kunena maneno kadhaa huku akimuangalia mlengwa wake na kushuhudia miale meupe ikitoka
machoni mwake na kupenya mwilini mwa Samir. Aliendelea kuyatamka maneno ya kichawi lengo ni kuzitoa zile nguvu zote zilizopo kwa Samir kuzihamishia kwake. Zoezi hilo lilimchukua muda hadi kuweza kumaliza na baada ya kujirisha kulikamilisha hilo aligeuka zake na kuondoka. Alipofika mlangoni alisita na kugeuka kumtazama Samir,alifikiria ammalize kabisa ili asipate kumsikia mtu huyo akiendelea kuishi lakini alipojiridhisha kuwa tayari kumtoa nguvu zile hakuona haja ya kummaliza. Aliamua kutoka mule ndani na kuelekea kwa Maya ili amjaze tena ule ugonjwa . Na hata alipofika alipofika chumbani kwa Maya alifanya kile alichokusudia usiku huo. Alipomaliza hakutaka kuendelea kukaa tena mule alitoka zake na kurudi mahala walipofikia na watu wake akiwakuta wanamsubiri usiku ule.
"Vipi umefanikiwa?"aliuliza kijana wake mmoja.
"Dalfa ashindwi na kitu hasa kile alichokipanga, hii Eden itakuwa yangu tu muda si mrefu, na safari hii
sidhani kama watachelewa kunifuata maana nimeweka uchawi mzito kwenye mwili wa Maya. Hatupaswi kuendelea kukaa tena hapa tunaanza safari ya kurudi Mashari ya mbali usiku huu tusubiri ugeni wa Mfalme na Malkia wa Eden wakija kunikabidhi Eden."alisema Dalfa na kuwafanya watu wake wafurahi kusikia hivyo.
Haraka wakaanza kukusanya mizigo yao na kuweka kwenye farasi wao usiku uleule wakaanza safari ya kurudi kwao.

Ndoto mbaya zilianza kumtawala Maya usiku ule huku akianza kutokwa na jasho sana mwilini. Alikuwa mwenye kuweweseka pale kitandani na kuona kama anatishwa na viumbe vya ajabu,alitamani kunyanyuka lakini mwili ulikuwa mzito sana. Alitamani kupiga kelele lakini mdomo haukuwa tayari kuongea,ulikuwa mzito kana kwamba amefungwa kinywa chake kutoweza kutamka lolote. Hakika mateso aliyoyapata yalimfanya atoe tu machozi kwa kilio cha moyoni. Alijikuta akimtaja Samir kama mlinzi wake wa sasa japo sauti
haikuweza kusikika ikitoka.

Samir alishtuka kutoka usingizini baada ya kusikia akiitwa kwa sauti ya juu sana iliyomfanya akurupuke pale kitandani. Alitazama huku na kule na kushangaa yupo chumbani kwake,Tanga. Alijua kuna jambo huenda lilitokea na ndio sababu ya kurudishwa huku usiku huo. Aliitazama pete yake na kuiona ipo kidoleni kwako.
"Nini kimetokea mbona nimerudi huku usiku huu?"aliuliza Samir huku akiitazama pete yake.
"Dalfa aliingia kwenye falme usiku huu na akafika mahala ulipolala,lengo ni kuzichukua nguvu zako na ndio maana umerudishwa huku,hali ya Maya sio nzuri tayari amemuweka uchawi wa kumdhuru akijua ameshazichukua nguvu ulizonazo hivyo Maya hataweza kusaidiwa na yeyote, muwahi Maya kabla hakujapambazuka arudi hali yake ya kawaida mtu yeyote asijue kimetokea nini."ilisema ile pete na kumfanya Samir atambue sababu za yeye kurudishwa htku,alihisi ile sauti kali iliyomshtua kutoka usingizini bila shaka ni Maya anahitaji msaada. Haraka alinyanyuka kutoka kitandani na kuchutama chini akiongea maneno fulani gafla akapotea mule ndani.
Alikuja kutokea yupo ndani ya chumba cha Maya na kuweza kushuhudia Maya akiwa anapepesuka pale kitandani huku jasho likimtiririka. Haraka alisogea Samir pale kitandani na kumshika Maya mkono na kujikuta akin'gan'ganiwa na binti huyo wa Mfalme kana kwamba anahitaji msaada. Alipeleka mkono wake kichwani kwa Maya na kuanza kuongea lugha isiyoeleweka. Huku Maya alipata kumuona Samir ndotoni akiwa anapambana na viumbe vya ajabu vilivyotaka kumdhuru Maya ambaye alionekana kujificha sehemu akiangalia vita ile. Viumbe wale walikuwa ni wengi sana lakini mwanaume alijitahidi kupambana nao. Walionekana wakitoa moto mdomoni mwao kumtupia Samir ambaye aliukinga kwa mkono wake hali ilifanya Maya ajione mwenyewe akishangaa baada ya kuona uwezo ule wa ajabu alionao Samir. Mwishowe akapata kuona viumbe wale wakiuawa na Samir ambaye alionekana kuchoka hoi baada ya kazi hiyo,Maya alianza kutoka pale alipojificha na kuanza kumsogelea Samir akionekana ameinama huku akihema sana huku wale viumbe wakiwa chini . Taratibu akamshika Samiri mkono na muda huohuo Samir pale kitandani kwa Maya alikuwa anahema kweli kwa kazi nzito ya kuutoa uchawi ule kwa Maya,alipata kuona akishikwa mikono yake na Maya aliyekuwa pale kitandani akiwa kwenye usingizi mzito.
"Samir.."aliita Maya akiwa bado amelala.
Samir alimtazama baada ya kuona Maya ameongea japo hakuweza kufumbua macho yake. Samir alitabasamu tu na kumshika Maya shavuni ambaye muda huohuo akalala usingizi mzuri usiokuwa na ndoto za kutisha. Alipohakikisha uzima huo kwa Maya naye akarudi chumbani kwake kupumzika.

Alikuwa mwingi wa mawazo na kubaki kutafari namna pete ile inavyomsaidia sana katika mambo mengi. Alinyanyuka na kukaa akimtafakari Dalfa.
"Huyu mtu ameshafahamu
nipo vipi ndio maana ananifuatilia kiasi hiki. Anamuumiza Maya ili aipate Eden kwanini asimdhuru Mfalme mwenyewe anaumiza watu wasiokuwa na hatia!."alisema Samir akimjadili Dalfa kwa kile anachokifanya kwa Maya na kuona ni unyanyasaji kwa binti huyo. Alijilaza tena kitandani kuutafuta usingizi akiwa amechoka sana kwa kazi aliyoifanya.

Asubuhi kulipo pambazuka Jamal alipata kuamshwa kwaajili ya kufanya mazoezi akiwa kama askari wa Eden. Hakuwa na jinsi alitii kile alichoambiwa na kuelekea kwenye uwanja wa mazoezi kujumuika na wenzake. Huku Samir alielekea hadi kwa Maya na kugonga mlango,aliporuhusi aliingia na kukuta wasichana wawili wakiwa wanampamba Maya apate kupendeza. Alisogea hadi pale na kumpa heshima binti huyo wa Mfalme.
" Samir umefika! Na ndio nilikuwa nakuulizia hapa."alisema Maya akiwa anawekwa urembo kwenye nywele zake.
"Nimefika binti wa Mfalme,nipo kwaajili ya kuanza kazi yangu ya kukuweke
a ulinzi."alisema Samir na kumfanya Maya atabasamu. Dakika kadhaa alimaliza kuwekwa vizuri kisha akawaruhusu wafanyakazi hao waendelee na kazi zengine.
Taratibu wakaanza kutoka mule ndani wakimuacha Samir akiwa amesimama pale ndani. Muda huohuo Lutfiya alikuwa akipita zake njia ile na kuweza kuwaona wale wasichana wakitoka mule ndani kwa Maya,hakuwa na lakusema naye alipita kuendelea na safari yake lakini alipofika mlangoni pale alipata kusikia sauti ya Samir mule chumbani kwa Maya,alitazama pande zote pale alipo na alipohakikisha hakuna mtu eneo lile alisogea taratibu pale mlangoni akatega sikio apate kusikia yanayozungumzwa ndani.
" Safari gani hiyo unayoizungumzia?"aliuliza Samir akimtazama Maya akiwa amekaa kwenye kiti akikitazama kioo kikubwa kilichopo mbele yake.
"Nahitaji twende tena kule kwenye kile kijiji,si unakumbuka niliwaahidi nitarudi siku moja! Sasa naona muda umekwenda sikutimiza ahadi yangu kwao,hivyo leo nimepanga twende tena na nafurahi safari hii umekuwa na mamlaka ya kunilinda na sio mfanyakazi wa kutumwa kama awali,hivyo naomba ujiandae."alisema Maya akionesha kutabasamu.
"Sawa nimekuelewa binti wa Mfalme,nakwenda kujiandaa."alisema Samir huku akimtazama Maya vile aliuyopambwa,hakika alikuwa mwenye kupendeza sana hasa uzuri wa asili aliokuwa nao. Hakuwa anafahamu lolote kuhusu kijiji hicho wala mahala kilipo akahisi huenda ni yule Samir mwenyewe ndiye alioweza kuelekea huko na Maya
Taratibu Samir akageuka na kuanza kuondoka baada ya kujiridhisha kuwa Maya ni mzima kabisa na hakuna aliyetambua kulitokea nini usiku.
"Halafu Samir..."aliongea Maya na kumfanya Samir ageuke tena kumtazama.
"Endelea kama mwanzo kuniita Maya na sio mtoto wa Mfalme ."alisema Maya na Samir akakubali. Lutfiya kule mlangoni alipopata kusikia hayo haraka akatoka pale mlangoni na kuendelea na safari yake.
Maya alibaki kumtazama tu Samir baada ya kukumbuka wale viumbe waliokuwa wakitisha wakipambana na Samir.
"Ile ni ndoto gani mbona ilikuwa inanitisha vile?. Na mbona kama nilimshika kweli Samir mikono yake,mmh ndoto gani hii mbona haijawahi kunitokea.!"alisema Maya akiwa pekeake mule chumbani kwake.

Huku kwa Lutfiya akiwa anatembea zake alipata kumuona Jamal akiwa ametulia sehemu na wenzake wakiwa wamepumzika, alijisogeza maeneo ya na Jamal akapata kumuona Lutfiya akiwa amesimama akajua kuna jambo. Taratibu akasimama na kusogea hadi pale.
"Vipi Lutfiya!"
"Kuna safari leo Maya anaenda na Samir,kuna kijiji kinaitwa Gu Ram nje ya mji wa Eden, kiongozi wao ni mtoto mdogo na anapendwa sana na kila mtu kutokana na ukarimu na maneno ya busara."
"Kwahiyo tunafanyaje,na mimi ndio nimeshaingia kwenye jeshi la kifalme."alisema Jamal huku wakiwa makini wasije kusikiwa wanacho kizungumza.
"Jamal hizi ndio nafasi za kufanya jambo kwa Maya na hata huyu Samir,hatuna haja ya kuendelea kukubali kuvurugiwa mipango yetu. Wewe ndio una sauti ya kumfanya lolote Samir maana siamini kama amekushinda nguvu na kupambana ilitokea bahati tu akapata nafasi ile."
"Haya nimekuelewa,na vipi kuhusu Maya? Tunafanyaje kwake.?"aliuliza Jamal na kumfanya Lutfiya aangali pembeni kwanza kisha akamsogelea Jamal na kuanza kumnon'goneza jambo fulani. Jamal alitabasamu baada ya kusikia ushauri huo alioambiwa na Lutfiya.
ITAENDELEA
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN.
MTUNZI:JAFARI MPOLE
SEHEMU YA 24

ILIPOISHIA
Jamal alitabasamu baada ya kusikia ushauri huo alioambiwa na Lutfiya.

TUENDELEE
"Hapo sawa nimekuelewa, wacha nilifanyie kazi hilo."alisema Jamal .
"Sawa fanya hivyo mimi ngoja nimtumid ujumbe Mfalme Faruk apate kujua kinachoendelea."alisema Lutfiya na Jamal akaliafiki swala hilo kisha akarejea kukaa na askari wenzake.

Mfalme Siddik alikuwa amepumzika juu kabisa ya jengo la kifalme akiwa na mkewe wakiitazama Eden yao asubuhi ile. Walipata kuwaona wananchi wao wakiendelea na kazi mbalimbali ya kujenga Taifa hilo hali iliyomfanya Mfalme afurahi kuona vile.
"Nazidi kupata hamasa ya kulipenda Taifa langu kila siku hasa nikiangalia wananchi wangu wanavyoishi kwa amani na upendo, Eden ndio Taifa pekee lenye mfano wa kuigwa katika kila jambo."alisema Mfalme akiwa anaangalia Taifa lake.
"Mimi bado nipo njia panda sielewi ingekuwaje kwasasa tungekuwa raia wa kawaida huku Taifa hili likiwa mikononi mwa Dalfa."
"Siku zote usifanye maamuzi ya haraka kabla ya kujadili na moyo wako, kama ungeridhia kukubaliana na mikataba ile ya Dalfa tusingekuwa hapa muda huu na jina la mfalme pamoja na Malkia ndio lingeshia siku ile." alisema Mfalme Siddik
"Ila kuna watu wanaonekana ni wa kawaida hawana umuhimu sana lakini kiukweli bila ya Samir basi heshima yetu ingeshuka. Yeye ndio kafanya nisiendelee kumsikiliza Dalfa baada ya kunipa habari kwamba Maya ameamka,na nilipanga kumpa adhabu kali nikijua alinidanganya na wewe ndio umemtuma afanye vile kunifikishia taarifa za uongo,tumshukuru sana Samir."alisema Malkia Rayyat.
"Ndio maana nilipopata ushauri kutoka kwa wazee kipindi kile kuwa nimfukuze Samir kutokana na muonekano wake wa kazi sikuwasikiliza. Watu kama hawa wanafaida kubwa sana katika maendeleo,ana haki ya kushkuriwa maana hata sielewi alipitaje njiani hadi kukuwahi wewe kabla ya sisi kufika."alisema Mfalme wakizidi kumsifia Samir. Wakiwa kule juu walipata kumuona binti yao Maya akiwa juu ya farasi huku Samir naye
akipanda kwenye farasi wake ambaye alibebeshwa baadhi ya mizigo kwaajili ya safari. Maya aligeuka na kuwatazama wazazi wake kule juu huku akiwa mwenye tabasamu mwanana. Aliwapungia mkono wa kuwaaga nao hawakuwa na hiyana,walimruhusu kwenda safari hiyo akiongoza na Samir kuelekea kwenye kijiji cha Gu ram.
Jamal alipata kuwaona wakianza safari hiyo na kuamua kusimama pale alipo na kuelekea nje ya jengo la kifalme akiwasindikiza wakina Maya kwa macho. Alitazama huku na kule na kuona hakuna mtu anayemuona,haraka akatoka pale kuelekea sehemu ambayo walikuwa wakikutana watu wa Taifa lao mara kwa mara.

Wakiwa njiani stori za hapa na pale ziliendelea huku Maya akikumbushia matukio ya nyuma ambayo kwa Samir yalikuwa ni mageni kwake lakini hakutaka kuonesha kwamba hafahamu lolote.
"Kwahiyo tunapoenda huko tunarudi muda gani Maya?"aliuliza Samir akiwa anamtazama Maya huku farasi wao wakitembea mwendo wa taratibu.
"Safari hii tutakaa sana kama siku nne hivi maana nahitaji kuwa nao karibu watu wa Gu Ram, kuna mambo mengi najifunza nikiwa karibu na yule mtoto, tangu upate kushinda pale uwanjani na kuwa mlinzi wangu nimejikuta naamini yale maneno yake kuhusu wewe. Tazama sasa Eden sasa haikutazami kama Samir yule waliyemzoea,una heshima yako Eden kwasasa na huenda ukafika mbali zaidi."alisema Maya na maneno yale yakamfanya Samir awe na shauku ya kumuona mtoto huyo.

Huku kwa Jamal alipofika kwa wenzake akawapa kazi ya kufanya,waelekee kijiji kile cha Gu Ram kuwachunguza kujua kitu gani Maya amefuata huko. Pia wahakikishe wanammaliza Samir asiweze kurudi tena Eden. Baada ya kupatiwa taarifa hiyo haraka wakaanza safari ya kuelekea kwenye kijiji kile kuweka kambi wakiwasubiri watu waliowafuata.

Ujumbe uliweza kufika kwa Mfalme Faruk baada ya Lutfiya kutuma ujumbe kupitia njiwa yule wanayemtumia. Alifurahi baada ya kujua kuna mpango kabambe umeandaliwa na unapaswa ufanyike haraka sana. Alimuita mkuu wa majeshi yake aandae vijana kadhaa kwaajili ya kuifanya kazi hiyo. Waliteuliwa vijana kumi na watatu kwaajili ya kufanya kazi hiyo na bila kuchelewa wakaanza safari ya kuelekea kwenye kijiji cha Gu Ram. Walipanga kufanya jambo la tofauti ili wapate kufanikiwa kile wanachokihitaji. Baada ya mambo yote kwenda sawa Mfalme Faruk alirudisha ujumbe kupitia njiwa yule, Lutfiya alipata kuusoma ujumbe huo na kupata tumaini jipya la uhakika kuona idadi watu waliotumwa kwenda kukamilisha kazi hiyo wanatosha . Alimpasha habari hizo Jamal ambaye alikuwa na furaha kuona hata baba yake anamuunga mkono kwenye hilo. Wakabaki kusubiri kupata taarifa ambazo zitawafanya wafurahi.

bvBaada ya masaa kadhaa safari ya Maya na Samir iliweza kufika tamati baada ya kuwasili kwenye kijiji kile. Watu wengi waliwakimbia kuweza kuwakaribisha
ndani ya kijiji chao wakiwemo watoto. Maya alishuka kwenye farasi na kujikuta akizingirwa na watoto wengi waliomsogelea pale,alifurahi sana kwa upokeaji ule na kuamua kuwashika mikono baadhi ya watoto na kuanza kutembea kuelekea kwa kiongozi wa kijiji hicho. Samir alitabasamu tu kuona umati ule wa watu wakimfuata Maya. Naye alipokelewa baada ya kushuka kwenye farasi wakaja vijana wawili wakamchukua farasi yule na kumpeleka mahala apate kupumzika. Naye akafuata njia aliyoelekea Maya na watoto wale. Walifika kwenye nyumba moja iliyojengwa kwa ubora wake kuliko nyumba zengine na muda huohuo akapata kutokea mtoto mwenye kukadiriwa umri wa miaka mitano akiwa ameshika bakora yake fupi akiwa kwenye mavazi ya kifalme akiwatazama wageni hao kwa tabasamu.
Samir alipomtazama yule mtoto alipata kujua huenda ndye aliyekuwa akizungumziwa na Maya wakiwa safarini. Alishangaa kuona umri wake mdogo na inasadikika ndio anayeongoza kijiji
hicho. Maya alisogea hadi pale alipo mtoto yule na kupiga magoti, yule mtoto alimsogelea na kumshika kwenye paji la uso kama ishara ya kumkaribisha na kumbariki awe mwenye amani. Samir kuona vile naye akasogea hadi pale na kupiga magoti na mtoto yule akasogea kwa Samir na kumshika kwenye paji la uso gafla akapata kuona mkono wake ukitetema pindi alipomshika Samir. Yule mtoto alishtuka na kurudi nyuma hatua mbili kumtazama Samir vizuri. Aliwatazama wanakijiji wake waliozunguka eneo lile kuwatazama wakina Maya.
"Tumepata ugeni leo katika Taifa letu dogo la Gu Ram,ugeni huu umekuja na baraka tele na kuleta kitu kipya ndani ya ardhi yetu na naamini hata mimea na viumbe hai wengine watashangilia siku ya leo."alisema yule kiongozi mtoto na sekunde kadhaa mbele matone ya mvua yakaanza kudondoka kuwafanya watu washangae. Kila mmoja alishangaa kuona mvua inaanza kunyesha na kila mtu akawa anakimbia kwake kwa furaha
kadhaa safari ya Maya na Samir iliweza kufika tamati baada ya kuwasili kwenye kijiji kile. Wazee, vijana na watoto waliwakimbia kuweza kuwakaribisha
kwenda kuyakinga maji hayo, Samir alishangaa kuona hali ile ya gafla tu na kushuhudia Maya akinyanyuka.
"Tuingieni ndani jamani mvua itanyesha kubwa sana kwa muda."alisema yule kiongozi mtoto na kugeuka nyuma kuongoza njia kuingia ndani akifuatiwa na Maya. Samir aligeuka na kuona jinsi watu wanavyo shangiria mvua ile.
"Inamaana walikuwa hawapati mvua hawa mbona wanafuraha hivyo!"alisema Samir akishuhudia furaha ya wanakijiji baada ya mvua ile.Aligeuka na kupiga hatua naye akaingia ndani. Alibaki kushangaa pindi alipotaza ndani kulivyo, ilikuwa ni nyumba yenye thamani kwa ndani lakini aliyeitazama nje aliiona ni ya kawaida. Mapambo ya kila aina yaliweza kuipendezesha nyumba ile hali iliyofanya Samir abaki kushangaa. Walikaribishwa na kuweza kusogea kukaa kwenye viti,mwenyeji wao alisogeza kiti chake na kuweza kukaa huku mvua ikizidi kunyesha nje.
"Nimekuwa nikiwakumbuka kila siku tangu nilipoondoka mara ya kwanza,maneno yako yenye ushauri ndani yake nimekuwa nikiyafuata kila siku na siku hizi za karibuni nimekuwa na amani sana moyoni japo nilipatwa na maradhi makubwa ambayo kila mtu Eden aliniombea niweze kupona. Nashkuru kwa ushauri wako Faraj."alisema Maya akimtazama yule mtoto aliyeonekana kusikitika baada ya kupata taarifa hiyo ya maradhi.
"Pole sana Maya, unajua siku zote binadamu tumekuwa watu wa tamaa sana katika maisha yetu,swala la maradhi yako nilipata kusikia na nikatamani kuja Eden kukupa msaada lakini sheria zenu zilinitia hofu nikahofia maisha yangu na huenda baadae ningekusaidia kisha wakanigeuka kwakuwa natumia nguvu za kichawi."alisema mtoto yule aliyefahamika kwa jina la Faraj. Maneno yake yakamfanya Samir ashtuke na kumtazama baada ya kutaja mambo ya nguvu za kichawi.
"Ni kweli sheria ya Eden hairuhusu mtu mchawi na endapo akijulikana huna adhabu yake ni kifo, nilijaribu kumueleza kuwa sio wote wanatumia nguvu hizo kwa ubaya lakini hakuweza kunielewa, mwisho wa siku naumwa mimi wanatafuta watu wenye nguvu za kichawi waweze kunisaidia nirudi katika hali yangu. Na nimesikia walitaka hata kuitoa Eden iwe mikononi kwa yule Mfalme wa mashariki ya mbali,Dalfa. Na sijui nani aliyenisaidia hadi kurudi katika hali yangu hii."alisema Maya huku akisikilizwa na Faraj pamoja na Samir ambaye alikuwa kimya muda wote.
Faraj alinyanyuka pale alipokaa na kumsogelea Maya pale alipo akamshika vidole vyake huku akivibinya taratibu.
"Kuna mtu amejitolea kukusaidia katika maisha yako,yeye ndio amekufanya hadi sasa uitwe Maya tena maana uchawi ule ungekutoa uhai,ulikuwa nusu ya kufa ila yeye ndiye amekusaidia hadi sasa unaishi tena."alisema Faraj na kumfanya Maya ashangae,Samir kusikia vile alishtuka na kujua huenda Faraj aweshamtambua kuwa yeye ndiye aliyetoa msaada ule.
"Una maana gani kusema hivyo Faraj?"aliuliza Maya akiwa hajapata kuelewa.
"Tambua tu hivyo Maya kuwa yupo ambaye anakuangalia muda wote kwa kukulinda na kuhakikisha usalama wako, tutaongea siku nyengine hiyo mada naona mvua imeacha kuyesha,mimi ngoja niwaache naingia kwenye ibada,karibuni sana Gu Ram maana hapa ni kwenu, Samir karibu sana."alisema Faraj na kumpa heshima Samir kwa kuinamisha uso wake chini kisha akauinua na kuelekea zake kwenye chumba chake cha ibada.
Maya akawa njia panda kwa maneno yale ya Faraj.
"Kumuelewa yataka umakini sana,lakini kadiri ya muda unavozidi huenda ukapata kujua nini anamaanisha mimi nishamzoea maneno yake."alisema Samir akitaka asijulikane kama ni mgeni ndani ya kijiji hicho cha Gu Ram.
"Namuamini Faraj huenda anachosema kipo japo sijapata kujua kiundani zaidi."alisema Maya akiwa mwenye kutafakari. Ilimbidi Samir aanze kubadilisha mada tofauti ili amtoe Maya mawazo hayo ya kufikiri. Muda huohuo wale watu wa Mfalme Faruk ndio walikuwa wanaingia katika kijiji hicho cha Gu Ram lengo ni kummaliza Samir ili wampate Maya kuna jambo wanahitaji kulifanya kwake.
NINI KITAJIRI NDANI YA KIJIJI HICHO? USIKOSE SEHEMU IJAYO.
 
PETE YA MFALME WA EDEN 25

Walifika sehemu wakaweka kambi kwenye nyumba moja ambayo walikuwa wameandaa mazingira ya mahala pa kufika. Walipokelewa na mtu mmoja ambaye alikuwa yupo upande wao.
"Hawa watu wamekuja kwa mara nyengine,Maya amekuwa akipendwa sana na wanakijiji wa hapa hivyo mnapomfuatilia Samir muhakikishe hakuna mtu ambaye ataona tukio hilo,wanakuwaga na matembezi ya kwenda mtoni mida ya jioni hivyo muda huo ndio mzuri kuutumia kukamilisha jambo hilo."alisema mtu huyo ambaye ndio mwenyeji wa watu hao wa Mfalme Faruk,muda huohuo wale watu waliotumwa na Jamal ndio walikuwa wanawasili na kufika kwenye nyumba hiyo kuungana na wenzake.
Maelezo waliyopewa wakayaridhia na kuamua kukaa kusubiri jioni ifike. Muda huo walitoka watu wawili na kuongozana na mwenyeji wao huyo kuwapeleka huko mtoni wapajue ili hapo baadae asiweze kuonekana kama alikuwa anashirikiana nao. Huku upande wa pili Jamal aliendelea na kulitumikia jeshi la Eden,kwa uwezo wake wa kutumia upanga kwenye mapambano ulimfanya hata Generali mkuu ahamasike kumpenda sana. Siku hiyohiyo alimuita na kukaa mahala waongee.
"Nimekuwa nikitazama kipawa na akili unazotumia nimekuona una kitu cha ziada kwenye akili yako, na hii ndio inavyotakiwa hasa kwa askari wa kifalme,mimi naamini ukiendelea hivi siku utakuja kuwa mkubwa zaidi ya hapa ulipo."alisema Generali akimwagia sifa Jamal alibaki kutabasamu.
"Sawa Generali mjuu nitahakikisha nazidi kukuwa kiakili siku hadi siku."
"Sawa endelea na kasi hiyo,kesho kwenye mazoezi ya Alfajiri nitakupa nafasi ya kuwaongoza wenzako naamini utalifanya hilo."
"Bila shaka Generali,nitafanya hivyo kesho Alfajiri."alisema Jamal na kuagwa na Generali huyo akaondoka zake. Alijisiki furaha kuona ameanza kuaminiwa na Generali mkuu wa majeshi yote ya Eden.
"Hii ni nafasi mpya imejitokeza sitakubali kuipoteza hata kidogo nihakikishe nafika pale nilipokusudia."alisema Jamal akimtazama Generali akitokomea.

Siku hiyo Maya alikuwa mwenye faraja sana ndani ya kijiji cha Gu Ram,ilifika muda aliweza kutoka anatembezwa na kiongozi wa kijiji hicho Faraj huku wakifuatwa nyuma na Samir akiwa kama mlinzi wa Maya.
"Hata mimi sikuweza kuamini kama ndio atakuja kuwa mlinzi wangu,ila nimefurahi maana kwasasa amepata kuheshiwa na watu,ameamua kuonesha uwezo wake ndani ya uwanja na hakuna aliyetegemea."alisema Maya akiongea na Faraj.
"Niliwahi kukuambiaga kuwa siku zote hata kama ukiongoza watu wako usimdharau mtu wa chini yako na kumuona si lolote maana huenda siku moja akakusaidia sehemu ambayo hukuwahi kutegemea.Ilikuwa ni bahati kwa Samir na sasa amekuwa mtu wa kukuangalia na uzuri wake mmekuwa kama ndugu toka awali hivyo hakuna shaka."alisema Faraj wakiwa wanatembea taratibu kuzunguka mji huku kwa mbali jua likionekana kuchomoza baada ya mvua kunyesha kwa muda.
Samir mwenyewe alikuwa akiwasikiliza tu wakiongea kuhusu yeye. Alikuwa akimtazama Faraj vile alivyo,akikumbuka yale maneno aliyoongea muda ule alibaki kuustaajabu tu.
"Ina maana naye ana nguvu kama nilizonazo mimi?"alijiuliza Samir moyoni mwake akiwa nyuma pembeni ya Maya.
"Hapana,nguvu nilizokuwa nazo chache sana kuliko ulizonazo wewe. Ndio maana ulipowasili tu kwenye taifa langu nikakujua mapema kuwa una kitu tena kikubwa sana,"Samir aliyasikia maneno hayo na kumfanya ashangae,Faraj aligeuka kumtazama huku akitabasamu baada ya kuongea vile kwa hisia bila kutoa sauti. Samir alishangaa kusikia vile na kujua mtoto yule anauwezo wa ajabu na hakutaka kuuonesha kwa watu. Alibaki amenyamaza tu akiwasindikiza huko wanapoenda baada ya kufahamu tayari amejulikana na Faraj. Siku hiyo walitembea sehemu mbalimbali kwenye kijiji kile wakiangalia vitu mbalimbali vinavopendezesha kijiji hicho hasa mazingira kwa ujumla. Kwa mbali yalionekana maji yaliyokuwa yanatiririka kutoka milimani,Samir alivutiwa sana na mazingira yale.
"Aise kunavutia sana yaani hadi raha ukiyaona maji yale yanavyotiririka."alisema Samir na kumfanya Maya atabasamu.
"Wewe unayasifia tu lakini kupiga mbizi muoga kwelikweli."alisema Maya.
"Mimi najua mbona! Nayakata maji kama sina akili nzuri."alisema Salim na kuwafanya Maya na Faraj watazamane,wakaanza kucheka wenyewe baada ya kuona Samir anajisifia hali ya kuwa anajulikana kwa jinsi alivyo muoga wa maji. Hata yeye alijishtukia baada ya kujua kuwa anajulikana kama Samir. Faraj akabadilisha mada nyengne huku wakiendelea kuzunguka kijiji hicho. Muda wote huo wale askari wa Mfalme Faruk walikuwa ndani ya nyumba waliyofika wakiangalia muda tu,walikuwa wanahamu ya kumaliza kazi yao mapema waweze kurejea kwa Mfalme kumpa taarifa. Walifika sehemu Maya akaona watoto wakiwa wanacheza hivyo naye akajisogeza na kuanza kucheza nao. Faraj na Samir wakawa wanamtazama tu Maya akiwa anafurahi na wale watoto.
"Anaupendo kwa kila mtu na ndio sababu anayo heshima kubwa hapa kwetu,nakuomba sana umlinde sana katika maisha maana atakuja kuwa tegemezi hapo mbele."alisema Faraj akiwa amekaa sehemu pamoja na Samir wakiwatazama watoto wakiwa wanacheza na Maya kwenye matope.
"Nafahamu hilo ndio maana nimehakikisha napata nafasi ya kuwa mlinzi kwake."alisema Samir na kumfanya Faraj ageuke kumtazama.
"Hebu niambie umetokea taifa gani, na hizi nguvu umezipata vipi?"aliuliza Faraj na kumfanya Samir ashushe pumzi kwanza.
"Nimetokea bara la Afrika,mimi ni mtanzania na nilipata kukabidhiwa nguvu hizi baada ya pete hii kuingia kidoleni hapa."alisema Samir akimuonesha Faraj kile kidole chenye pete. Faraji aliitazama pete ile na kujikuta akiushika mkono ule wa Samir ambaye alibaki kumtazama tu Faraj. Alitumia dakika tano na sekunde ka dhaa kuutazama mkono ule na kuichunguza ile pete yenye maandishi madogomadogo ambayo aliweza kuya fahamu. Aliurudisha mkono ule huku akiachia tabasamu.
"Nimeangalia matukio hapa kadhaa yaliyopita, hakika una bahati ya kuipata pete hii. Pete iliyobarikiwa na yenye uwezo mkubwa wa kufanya kitu chochote kwa muda sahihi, ni PETE YA MFALME WA EDEN. Mfalme wa kwanza kuitawala Eden na ndio alikuwa mwenye nguvu ya kupambana hata na majini ambao walikuwa wakitaka kuigeuza Eden kuwa mji wao. Lakini sasahivi imekuwa ni tofauti Mfalme wa Eden ndio amekuwa mstari wa mbele kukataza nguvu hizi ndani ya Taifa hilo. Ila fahamu kwamba kuwa na pete hii ni ishara kwamba utakuwa kiongozi wa Eden hapo mbeleni japo utapitia vikwazo vingi ila yakupasa uvumilie."alisema Faraj na kumfanya Samir aelewe hali halisi.
"Unamfahamu Nadhra au marehemu baba yake aliyenyongwa mbele ya Mfalme Siddik"?aliuliza Samir huku akimu angalia Faraj.
"Mimi ndio mtoto wa mwisho wa mzee Jailan,mzee ambaye amenyongwa katika falme ya Siddik,na Nadhra ni dada yangu. Haya yote Maya hayafahamu na sitaki ajue kabisa maana akijuwa kuwa baba yangu ndiye aliyemfanya kuuguanusu ya kufa basi naamini hata upendo wake utabadilika na hata kuleta chuki."alisema Faraj na kumfanya Samir atambue kumbe Nadhra binti aliyemfanya aijue Eden ndiye dada wa kiongozi huyu mdogo wa Gu Ram.

"Yupo wapi Nadhra sasa?"
"Pia naye ana mji wake kama mimi hapa. Upo mbali sana na anawaongoza watu wenye nguvu kama za kwetu,hii ni baada ya kuona Eden kumekuwa na sheria zinazowaadhibu wakaamua kwenda kuanzisha mji wao huko wanaishi."alisema Faraj akizidi kumueleza Samir mambo mengi sana. Hata baada ya muda kupita Maya alirejea akiwa amechafuka sana kutokana na kucheza kwenye matope na watoto wale hali iliyomfanya Samir amshangae maana amekuwa kama mtoto. Walibaki kumcheka tu na baada ya muda wakarejea nyumbani kwa Faraj.
Hata jioni ilipoanza kuingia Maya akamtaka Samir waelekee mtoni kawa ilivyo kawaida yao. Kwa Samir ilikuwa ni mara yake ya kwanza lakini hakutaka kujionesha kama ni mgeni huko waendako.
Njiani aliongea mambo mengi ya kumuaminisha Maya asiweze kuona utofauti wowote. Hata walipofika Samir alisikia furaha sana pindi alipofika sehemu hiyo,hakika ilikuwa yenye kupendeza huku maua mbalimbali yaliyojiotea pembezoni mwa mto huo yakizidi kueanya sehemu hiyo ivutie. Maya alijisogeza kwenye jabali moja na kuanza kupunguza nguo zake hali iliyomfanya Samir abaki kumtazama binti huyo. Hakika Maya alikuwa mwenye umbo lenye mvuto wa aina yake,hii ilijidhihirisha hasa pale alipobaki na nguo nyepesi iliyofunika mwili wake kuanzia kifuani hadi kwenye mapaja yake, na hata aliposogea kwenye maji na kujirusha kuanza kupiga mbizi ilimfanya Samir apatwe na hamu ya kutaka kuyaingia maji yale. Alimuona Maya akiibuka na kufanya nguo ile nyepesi aliyovaa iuchore mwili wake,hali iliyomfanya Samir ashindwe kujizuia. Taratibu akavua viatu vyake na nguo kadhaa akabaki na bukta ya ndani na kusogea karibu na maji.
"Utayanywa haya maji shauri yako!"alisema Maya akifahamu fika Samir hana ujanja kwenye maji. Alibaki kutabasamu mwenyewe na muda huohuo akajitosa majini hali iliyomfanya Maya acheke,gafla akapata kuona Samir akitapata kuyapiga maji kuonesha anahitaji msaada. Maya alitabasamu na kuanza kukata maji kusogea pale alipo Samir,alishangaa mikono ya Samir inazama chini na kutoweza kuonekana. Ilimbidi azame ndani kumtafuta lakini hakuweza kumwona hali iliyomfanya awe na hofu huku akiibuka juu na kuanza kuangaza huku na kule. Alishangaa kumuona Samir yupo mbali akiwa anachezea maji huku akicheka kumtazama Maya ambaye alipata kustaajabu. Ilimbidi Samir atoke kule huku akipiga mbizi hadi pale alipo Maya na kumuacha akiwa anashangaa haamini.
"Kumbe ulikuwa unanidanganya siku zote kuwa hujui kuogelea!"alisema Maya huku akimtazama Samir aliyekuwa anatabasamu tu na kujirusha akazama ndani ya maji,Maya alifurahi kuona vile ikawa ni mchezo sasa baina yao.
Muda huo wale askari ndio walikuwa wakelekea maeneo ya mtoni wakiwa wamejiandaa kikamilifu lengo ni kummaliza kabisa Samir kisha wamchukue Maya. Kule mtoni wakiwa wanaendelea kufurahi Samir aliona pete yake aliyovaa ikiwa inambana kwenye kidole muda ule akiwa ndani ya maji, alimbidi anyanyuke na kuutazama mkono ule uliokuwa na pete akapata kuona kuna askari kadhaa wanafuata njia ile ya kuelekea mtoni hali iliyomfanya awe na mashaka juu yao. Alimtazama Maya aliyekuwa hana habari akiendelea kupiga mbizi. Alitokaharaka kwenye maji na kuqnza kuvaa nguo zake Maya akashangaa.
"Vipi mbona gafla hivyo?"aliuliza Maya akiwa anamtazama Samir.
"Toka kwenye maji tuondoke haraka!."aliongea Samir na kumfamya Maya ashangae.
"Kuna nini mbona sikuelewi Samir?"
"Nahisi sehemu hii si salama, njoo uvae nguo haraka tuondoke Maya niskilize."alisema Samir akionesha kuwa makimi na anachoongea. Hata Maya alishangaa kuona hivyo ila kwakuwa ameshakuwa ni mlinzi kwake ikabidi amsikilize na afuate vile mlinzi wake anavyosema kwa usalama zaidi. Haraka alitoka kwenye maji yale na kuanza kuvaa nguo zake huku Samir akiwa anatazama kila sehemu kwa usalama.
ITAENDELEA
 
PETE YA MFALME WA EDEN 26

ILIPOISHIA
kwakuwa ameshakuwa ni mlinzi kwake ikabidi amsikilize na afuate vile mlinzi wake anavyosema kwa usalama zaidi. Haraka alitoka kwenye maji yale na kuanza kuvaa nguo zake huku Samir akiwa anatazama kila sehemu kwa usalama.

TUENDELEE
Alipohakikisha Maya amemaliza kuvaa nguo zake akamkamata mkono na kuanza kuondoka pale mtoni haraka.
Maya alikuwa akipelekwa tu mkukumkuku huku akimtaza Samir kwajinsi anavyoonekana kuwa makini na kazi yake. Walifika mahala kasi ile ilimchosha binti huyo wa mfalme na kuamua kuutoa mkono wake mikononi mwa Samir akasimama hali iliyomfanya Samir abaki kumshangaa.
"Hebu niambie umeona nini pale mtoni mbona unanipeleka haraka kiasi hiki?"aliuliza Maya akiwa anahema huku akimtazama Samir.
"Maya.. nimejikuta napatwa na hofu ya gafla sehemu ile nikahisi huenda kuna kitu kibaya kitatokea pale ndio maana nikaona niepuke na hofu ile iliyojaa gafla."alisema Samir akiwa hataki kumweleza Maya ukweli kama ameona nini.
Wakiwa kwenye maon ygezi hayo gafla wakashangaa wanazingirwa na watu wakiwa juu ya farasi huku nyuso zao zikiwa zimefunikwa na kitambaa wasipate kutambulika. Maya kuona vile alishangaa na haraka akakimbilia nyuma ya Samir na kumshika mkono akionesha kuwa na woga. Samir alikuwa anawatazama jinsi wale watu walivyokuwa wanazunguka pale waliposimama huku wakiwa wameshika mapanga marefu kuashiria wamekuja kwa shari. Mmoja wao alitoka nyuma na kumpiga kikumbo Maya akadondoka chini ili wapata uhuru wa kumshambulia Samir. Alishtuka kuona Maya ameangushwa na kufikia uso ulipata jeraha. Alipatwa na hasira Samir kuona vile na muda huohuo akasikia upanga ukimkata mgongoni na kubaki kupiga ukelele wa maumivu huku akienda chini. Alinyanyua macho yake kumtazama Maya na kuona akivuja damu kwenye paji la uso wake, alipatwa na hasira sana na kuamua liwalo na liwe hata kama Maya akimtambua kuwa yeye ni nani,alitazama chini kutaka kutumia nguvu zake za kichawi ili apate kupambana na watu wale waliodhamiria kummaliza. Alipotaka kubadilika gafla kikatokea kimbunga kikubwa sana kilichowafanya farasi waliopandwa na watu wale waanza kudodoka kwa upepo ule mkali na wav wale wakadondoka huku vumbi likitawala sehemu ile,na dakika chache kukatulia. Wale walitoa macho kushangaa kilichotokea. Hawakuamini kumuona mtoto mdogo akiwa pale katikati na kuwafanya waamini ndiye alisababisha kutokea kwa kimbunga hicho. Kwa pamoja wakasimama wakiwa wameshika mapanga yako na muda huohuo Samir naye akanyanyuka pale chini akiwa na maumivu mgongoni. Watu wale wakaanza kuwavamia wakina Samir ambaye aliweza kupambana nao bila ya kuonesha uwezo wa nguvu alizonazo. Maya alinyanyuka na kukaa pembeni akitazama na kumuona Faraj anavotumia nguvu zake kuwadhibiti wale watu. Alikuwa akiwaadhibu kama mtu mzima akimwacha Maya astaajabu kuona vile, huku Samir alifanikiwa kuwamaliza watu kadhaa kwa upanga wake ambao alipata kukabidhiwa na Nadhra kipindi alichokuwa akielekea uwanjani kupambana. Hakuwa na huruma na mtu alikata watu kwa hasira isiyopimika huku damu zikitapakaa mgongoni mwake, hali ile iliyomfanya Maya amuamini Samir na kuona kweli alichokifikiria muda ule kilikuwa sahii. Watu wale walijikuta wanabaki wanne tu na wenzao wnte wameuliwa wakatazamana na kuafikiana bora wakimbie kuyaokoa maisha yao,hata walipopata upenyo walikimbia na kuacha farasi zao pale Faraj akabaki kuwatazama tu. Samir alichoka hoi huku akionekana kuwa na majeraha mwilini mwake. Haraka Maya akakimbia hadi alipo Samir huku akionesha kuwa na hofu juu yake na Faraj akasogea pale.
"Nipo sawa tu Maya wala usijali.."aliongea Samir akimuondoa hofu Maya aliyeonekana kuonesha sura ya huruma.
"Hapana umeumia sana Samir."alisema Maya na kuchana nguo yake kisha akaanza kumfunga Samir mgongoni. Faraj alitazama tukio lile na kuona upendo na huruma alionayo moyoni mwake. Samir mwenyewe alibaki kumtazama tu Maya na kuona jinsi gani alivyo na upendo juu yake.Alitamani aunyanyue mkono wake walau amshike Maya lakini nafsi yake ilisita na kubaki kumeza mate tu.
"Utaweza kutembea au nikubebe?"aliuliza Maya baada ya kumfunga vyema Samir kwenye jeraha lile,aliposikia swala la kubebwa alishtuka na kupata nguvu ya kusimama.
"Nguvu ninazo natembea vizuri tu ona..!"alisema Samir akiwa mwenye kuchangamka japo maumivu anayasikia sana. Hakutaka kuona anabwebwa na mwanamke na isingeleta picha nzuri kwa watu wanaowataza njiani. Faraj alilijua hilo na kubaki kutabasamu,alisogea na kumkamata mkono Samir huku akimtazama Maya.
"Nguvu anazo za kutembea hivyo,tumuache atembee mwenyewe."alisema Faraj na kugeuka kuanza kuongoza njia ya kurudi nyumbani jioni ile. Alifuata Samir kutembea naye huku akiugulia maumivu yake hali iliyomfanya Maya apate kumuona akiwa vile, alipiga hatua na kwenda kuukamata mkono wa Samir kuanza kutembea wote pamoja kurudi nyumbani kwa kiongozi wa kijiji hicho, Faraj.

Asubuhi ya siku iliyofuata mapema sana Walifika watu wawili nyumbani kwa Faraj wakimkuta nje amekaa akifanya mazoezi ya viungo. Hata walipofika walimpa heshima yake kama Mfalme wao,alinyanyuka na kupewa taarifa moja iliyomfanya ashtuke kusikia hayo.
"Muda mchache anaweza akafika hapa hivyo uwe tayari kumsikiliza."alisema mmoja wa wale watu na Faraj akapa kuelewa. Hata walipoondoka dakika kadhaa alifika askari mmoja akiwa juu ya farasi, Faraj alipata kumuona akishuka askari ya yule akamtambua kwa mavazi yake aliyovaa kuwa anatokea Eden. Alipofika pale alitoa heshima baada ya kujua mtoto huyo ndiye anakiongeza kijiji hicho, Faraj alimkaribisha kwa tabasamu mwanana.
"Bila shaka wewe ndio kiongozi wa Gu Ram,na siku ya jana umepata ugeni ulio na baraka na heshma kubwa, binti wa Mfalme wa Eden amefikia kwenye kijiji chako."alisema yule askari kwa kauli ya upole.
"Unayosema ni sahihi, na hapa ni sehemu ya heshima na salama kwake. Nahisi atakuwa amepumzika muda huu."alisema Faraj na kumfanya yule askari ashtuke kusikia hivyo.
"Inamaana wapo ndani?"swali hilo lilimfanya Faraj amtazame yule askari. Kwa kuona ataulizwa kwakile alichosema ilimbidi aipindue mada.
"Inamaana amelala mpaka sasa?"aliuliza tena yule askari.
"Nahisi amelala maana jana walitembea sehemu nyingi sana."alisema Faraj na muda huohuo Samir akatoka ndani akiwa tumbo wazi huku akionekana kufungwa nguo mahala alipopata jeraha. Alipomtazama yule askari alishtuka baada ya kumjua kuwa ni Jamal, wakabaki wametazama kwa muda kadhaa huku Faraj akiangalia tukio hilo.

Basi baada ya muda aliweza kuamshwa Maya na kuonana na Jamal wakakaa sehemu huku Samir akiwa pemben kwa Maya.
"Mfalme amenituma kuja kukupa habari kwamba unahitajika kurudi haraka leo hii,kuna ugeni unatoka taifa la kusini kuja Eden, hivyo kama binti pekee wa Mfalme unapaswa uwepo pindi watakapofika."alisema Jamal akiwa anamtazama Maya kwa jicho la aina yake. Samir alikuwa akisikia kinachoongelewa pale .
"Kwanini sikupewa taarifa hiyo mpaema na jana tu ndio nimetoka huko,tunaharibiana mambo na utaratibu niliopanga,nitaanzaje kuwaeleza watu kama naondoka leo wakati nimeshawapa tumaini la kukaa takribani siku nne."aliongea Maya akionekana kutopenda taarifa ile.
"Elewa kwamba sio mimi niliyesema haya,Mfalme Siddik ndio kanituma nikuletee taarifa hiyo."alisema Jamal akiwa mwenye kujiamini kwa kile anachokisema. Ikambidi Maya ageuke kumtazama mlinzi wake Samir ambaye alishusha pumzi na kutikisa kichwa chake akimaanisha amsikilize baba yake anachosema, aligeuka nakumtaza Jamal.
"Sawa nitafuata anachosema baba."alisema Maya na kunyanyuka pale alipokaa na kuingia ndani huku akimwacha Samir akiwa pale nje amesimama karibu na Jamal. Alistaajabu kuona Maya muda ule alimtazama Samir ili apate ushauri kama akubaliane na kile alichosema Jamal kutoka kwa Mfalme. Kikubwa zaidi kilichomstaajabisha muda ule akiwa anaongea na Faraj hadi akashtuka ni pale alipoambiwa Maya amepumzika ndani angali anajua fiki walitumwa askari zaidi ya kumi na watatu kuja kummaliza Samir na kumteka Maya hivyo alishtuka kusikia watu hao bado wapo. Alimtazama Samir akionekana kuwa na majeraha mwilini mwake na kuhisi huenda alidhurika wakati anapambana na askari wale waliotumwa na baba yake pamoja na vijana wake wawili.

Kwa Samir alikuwa na mashaka juu ya ujio huu wa Jamal,tangu mwanzo amekuwa na mashaka naye tangu alipoota ndoto ile, hakutaka kuendelea tena kusimama pale alitoka kuelekea kwa Faraj muda huo, Jamal akabaki pale akionesha kukasirika hadi kupiga teje mti uliokuwa pembeni yake.
"Na hili nalo tumeshindwa! Ah mpaka nachoka sasa huyu mtu tumfanyaje!"alisema Jamal baada ya kushuhudi Samir yupo salama japo amemkuta na majeraha akijua fika ni kwasababu ya kupambana askari wale wa baba yake waliotumwa kummaliza Samir na kumchukua Maya.
ITAENDELEA
 
PETE YA MFALME WA EDEN 27

Alielekea moja kwa moja kwa Faraj ambaye muda huo alikuwa amepumzika baada ya kufanya mazoezi ya asubuhi ile. Hata alipomuona Samir alijua kuwa ndio amekuja kuagwa baada ya kupata habari kuwa wanahitajika kurejea Eden.
"Imekuwa gafla sana safari yenu ila hakuna jinsi inahitajika mrudi kama alivyosema Mfalme Siddik."alisema Faraj akiwa anafuta jasho.
"Ni kweli lazima turudi Eden kama alivyoagiza Mfalme."aliongea Samir.
"Ila siku zote uwe karibu na Maya,kuna watu watamuwinda na kutaka kumtumia kusudi wapate urahisi wa kuupindua ufalme wa Siddik ili wamiliki Eden. Japo nipo kwenye kijiji hiki lakini pia ninauchungu na Eden,nimezaliwa huko na daima nitakuwa raia wa Eden japo tumekimbia kuhofia kuuliwa kwakuwa hatutakiwi. Ni mapema sana endapo Maya akakufahamu kuwa wewe ni nani. Hakikisha siku zote Maya hajui lolote kuhusu wewe maana huenda ikaleta matatizo."alisema Faraj na kumfanya Samir amuelewe.
"Sawa nimekuelewa. Nitahakikisha inakuwa siri."alisema Samir na muda huo Maya ndio alikuwa anatoka ndani baada ya kuwa tayari kwa kuianza safari. Jamal alimtazama na kuachia tabasamu baada ya kuona anatazamwa na Maya. Alikuja Samir na kusimama karibu na Maya huku Jamal akiwatazama.
"Upo tayari?"aliuliza Samir huku akimtazama Maya aliyeitikia na kumfanya Samir atabasamu, alimkamata mkono Maya na kuelekea Mahala walipohifadhiwa Farasi wao. Jamal alishangaa kuona vile na kujiuliza imekuwaje hadi Samir kama mlinzi kuweza kumshika mkono binti wa Mfalme. Ikamtia mashaka kuona kama wamefikia hatua ya kushikana hivyo basi ni wazi kwamba kutakuwa na ugumu kwa watu hawa kuweza kuwatenganisha. Alipanda kwenye farasi wake na kuwafuata,na baada ya muda Maya alimuaga Faraj pamoja na baadhi ya wanakijiji hicho na safari ikaanza kurudi Eden.

Huku upande wa pili Mfalme Faruk alionekana kumzaba kibao askari mmoja aliyekuwa amepiga magoti akiwa na mwenzake. Ni wale askari ambao waliweza kukimbia kifo pindi walipomvamia Samir kule maeneo ya mtoni. Taarifa zile zilikuwa kero na mbaya kwa Mfalme huyo na kuona anazidi kufeli kila mipango ambayo wanaiandaa.
"Huyu mtu auliwe mara moja na binti wa Mfalme apatikane haraka sitaki kusikia lolote zaidi ya hayo."alisema Mfalme Faruk akionesha kukasirika. Ilibidi wale askari waitikie na kutii amri ile kuweza kukamilisha kile anachotaka Kiongozi wao.
Huku Eden kulianza kupambwa kila mahala ndani ya falme baada ya kufahamika kuna ugeni kutoka taifa moja lenye kuheshimika sana. Mfalme pamoja na Malkia Rayat walikuwa wakiwatazama wafanyakazi wao wakiwa wanachakarika siku hiyo ya ugeni huo.
"Hawa sijui watafika salama huku maana nimekuwa na mashaka juu ya maisha ya mwanangu."alisema Malkia akiwa na wasiwasi kwa Maya.
"Mimi sioni sababu za wewe kuwa na hofu kubwa hiyo maana yupo na Samir pamoja na Jamal watahakikisha wanamrudisha salama hapa wala usijali."alisema Mfalme akimtoa hofu mkewe,wakaendelea kuangalia maandalizi yale.

Hadi siku hiyo Dalfa tanu afike kwenye taifa lake hakuweza kupata wala kusikia habari zozote kuhusu Maya ambaye anajua fika kwa uchawi aliyomuwekea siku ile angepata kuona ugeni wa Mfalme au Malkia wa Eden ukiwasili hapo lakini imekuwa kinyume na matarajio yake. Ilimbidi atoke kuelekea kwenye chumba cha kufanyia maombi yake. Hata alipotaka kukaribia aliona askari wawili wakisogea kwake ikabidi asimame.
"Vipi kuna habari gani mpya?"aliuliza Dalfa huku akiwatazama watu wake hao.
"Tumepata habari kwamba ufalme wa Joha unakwenda Eden kukutana na Mfalme wa Eden,na lengo hasa ni kuzungumza kuhusu ukaribu wao wakitaka watoto wao waowane na kuunganisha mataifa hayo mawili kwa udugu."alisema askari mmoja akimweleza Dalfa ambaye alishangaa kusikia taarifa hiyo mpya.
"Na hivi tunavyoongea huenda ugeni huo upo njiani na huenda jambo lao likafanikiwa maana falme hizi zimekuwa na urafiki sana."alisema askari mwengine wakimpatia habari hizo Mfalme wao Dalfa.
"Sawa.."alisema Dalfa na kugeuka kuendelea na safari yake akaingia kwenye chumba chake cha maombi. Taarifa zile alizopewa zilimfanya ashindwe kuelewa mambo anayoyasikia. Anafahamu fika kwamba Maya amemuwekea uchawi ambao asingeweza kuamka kabisa hadi yeye atakapokwenda kutoa uchawi huo kwa Maya. Alifanya hivyo baada ya kujua tayari ameshamtoa nguvu zote Samir usiku ule na ndio maana hadi siku ya leo ameona kimya imemtia mashaka sana. Alisogea kwenye chombo chake cha kutazama matukio yanayoendelea na moja kwa moja akapata kuona jinsi falme ya Eden inavyopambwa siku hiyo huku Mfalme Siddik akiwa mwenye tabasamu. Hali ile ikamfanya Dalfa ashangae. Alihisi kuanza kuchanganyikiwa hasa pale alipotaka kufahamu hali ya Maya kwa muda huo, macho yalimtoka baada ya kuona Maya akiwa juu ya farasi huku Jamal na Samir waki wa pembeni kwake. "Nini tena mbona sielewi hapa!"aliongea Dalfa akiwa anatazama kwenye beseni kubwa lililokuwa na maji ndani yake akitazama wakina Maya wakiwa kwenye farasi wakionekana kurudi Eden. Alipatwa na hasira sana Dalfa na kujikuta akipiga teke yale maji na kumwagika pale ndani. Hasira alizonazo alitamani kurudi tena Eden muda ule baada ya kujua huenda bado Samir anazo nguvu zile. Alitoka mule ndani na moja kwa moja akaelekea zake chumbani kwake kutuliza akili kwanza.

Huku njiani kwa Maya muda wote alikuwa kimya juu ya farasi, Samir alikuwa akimtazama na kuhisi huenda kuna jambo Maya analitafakari.
"Maya.. Unawaza nini muda wote?"aliuliza Samir na kauli yake hiyo ikamfanya Jamal azidi kuamini kwamba Samir amekuwa na ukaribu sana na Maya hadi kumuita kwa jina lake badala ya kumtukuza kama mtoto wa Mfalme.
"Ah kuna jambo linanipa wakati mgumu sana pindi nikilitafakari, na najikuta nakosa jibu lililo sahihi."alisema Maya wakiwa kwenye farasi wamepunguza mwendo.
"Unaweza kunishirikisha pia huenda nikapata ushauri wa kukupa!"alisema Samir na kumfanya Jamal atege sikio kwa makini naye apate kusikia, Maya alimgeukia Jamal kumtazama naye akabaki anamuangalia. Akajua huenda hapaswi kusikia maongezi hayo hivyo alimsimamisha farasi wake na kuwaacha Maya na Samir watangulie mbele naye akafuata nyuma.
"Huu ujinga yaani nimekuwa mlinzi wao huku nyuma,sijui wanataka kuongea nini hawa?"alilalama Jamal mwenyewa akiona wakina Maya mbele yake wakiongea.
"Hao wageni ambao wanakuja wanatoka kwenye taifa moja la falme ya Joha, na dhumuni na ujio wao ni kuja kujadili na baba yangu kuhusu kuunganisha falme hizi mbili ziwe kitu kimoja."alisema Maya na kumfanya Samir amtazame.
"Wasiwasi wako upo wapi hapo? Huwaamini hao watu wa Joha?"aliuliza Samir na kumfanya Maya ageuke umtazama.
"Sina maana hiyo, wanataka mtoto wa Mfalme aje kunioa mimi niwe mkewe,na swala hilo litafanya falme hizi mbili kuwa kitu kimoja. Hakika moyo wangu umekuwa mzito kukubali swala hili,sihitaji kuolewa kwenye koo ya ufalme wowote na ndio nimepanga kutoka moyoni mwangu."alisema Maya akionesha kuwa na huzuni juu ya swala hilo. Samir alimtazama na kumuonea huruma baada ya kujua msimamo wa Maya japo ni ngumu kulizuia maana Mfalme ndiye mwenye kuamua hayo yote.
"Nipe ushauri Samir nifanye nini na hapa ndio wanakuja leo hawa watu,na naamini hawataondoka hadi maswala ya ndoa yakamilike hivyo kama nitaoleoa basi nitaondoka nao kurudi kwenye falme yao ya Joha."alisema Maya na kumfanya Samir ashangae kusikia hivyo.
"Inanipa wakati mgumu sana kukushauri maana Mfalme Siddik anakupenda sana kama binti yake,na kama ugeni huu una urafiki na falme ya baba yako maana yake hatakubali kupata aibu kwa ugeni huo,lazima atafanya kile ambacho ataona ni heshima kwake na kwa falme nzima."alisema Samir na kuzidi kumchanganya Maya.
"Sasa unanishauri vipi mbona unazidi kuniweka kwenye wakati mgumu?"aliongea Maya akionesha kuchanganyikiwa na swala hilo. Samir alibaki kutazama chini huku akisusha pumzi kutafakari itakuwaje. Muda wote Jamal alikuwa nyuma yao kama hatua kumi bila kusikia lolote linalozungumzwa na wawili hao. Alijaribu kutega sikio kwa umakini bila mafanikio hali iliyomfanya achukie sana.
"Maya,nitakuambia tukifika Eden usijali."alisema Samir.
"Huu ndio muda wa kunieleza Samir ili nijipange nitasemaje mbele yao na hakuna muda mwengine tutakaopata kuonana, tambua kwamba kama nitaolewa basi hata wewe ndio itakuwa mwisho wa kuwa mlinzi kwangu maana kila kitu atakipanga mwanaume huyo."aliongea Maya na kumfanya Samir ashtuke kusikia hayo,alipiga moyo konde.
"Niamini Maya nitakwambia tukifika Eden na lazima nitapata tu nafasi ya kukuona. Nitakapokwambia sasa utakuwa mwenye hofu na kukuzidishia mawazo kama utaweza kulifanya jambo hilo,hivyo muda wa kwenda kuonana na wageni ndio nitautumia kukueleza wazo langu,kwasasa niache nitafakari wazo ninalolifikiria."alisema Samir na kumpiga farasi wake aongeze spidi,Maya akabaki kumtaza tu Samir akienda mbele zaidi. Jamal akapata muda wa kumsogelea Maya pale mbele alipo.
"Vipi upo salama?"aliuliza Jamal na kumfanya Maya ageuke kumtazama.
"Nipo salama ndio."alijibu Maya naye akapiga farasi wake akaongeza kasi ya kwenda mbele zaidi, Jamal aliwatazama tu bila kuelewa kimetokea nini,ilimbidi naye aongeze kasi kwenda nao sawa.
ITAENDELEA
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN 28

Baada ya kila kitu kwenda kama kilivyopangwa wakawa wanasubiri ugeni huo uweze kuwasili kwenye falme. Japo Malkia Rayat muda wote alikuwa akimfikiria mwanaye maana ndiye mtu muhimu katika ugeni huo. Akiwa kwenye hali hiyo walifika askari wawili na kuweza kutoa taarifa kwamba wageni waliowasubiri wanaanza kuingia Eden hali iliyowafanya watabasamu japo binti yao hakuweza kufika hadi muda ule. Wananchi walianza kuwashangilia kwa mapokezi makubwa yenye furaha. Mfalme Joha akiwa sambamba na familia yake pamoja na askari wake zaidi ya 30 waliosindikiza ufalme huo. Watu walijipanga njiani kuwakaribisha wageni hao waliokuwa kwenye farasi wao walifika askari wa Eden takribani kumi kuupokea msafara huo na kuanza kuwaongoza kuelekea kwenye falme.
"Hakika watu wa Eden ni wanyenyekevu sana na wanaonekana wakarimu. Mfalme Siddik lazima ajivunie kwa hili."aliongea mtoto wa kiume wa Mfalme Joha aliyejulikana kwa jina la Rahim.
"Pia wana umoja wa hali ya juu kakima maisha yao ya kawaida,hii inafanya jina la Eden likue siku hadi siku kwakuwa na wananchi wenye umoja wa kufanya kazi."alisema askari mmoja wa Eden akimueleza mtoto huyo wa Mfalme.
Stori za hapa na pale ziliendelea hadi walipofika kwenye ufalme ambapo walipokelewa kwa furaha kubwa sana na wenyeji wao. Askari wa mataifa hayo mawili walikaribishana na kuwa pamoja kwa siku hiyo baada ya wafalme wao kuweza kukutana siku hiyo.Walikaribishwa sehemu husika na kuweza kuka kuongea pande hizo mbili. Muda huohuo wakina Jamal ndio walikuwa wanawasili Eden,njiani walipata kuona jinsi mitaa ilivyopambwa vizuri kwaajili ya ugeni ule. Moyo wa Maya ulimwenda mbio baada ya kuona hali na kujua ugeni wa ufalme wa Eden umeweza kuwasili katika ufalme wao. Aligeuka kumtazama Samir ambaye naye alikuwa akishangaa ile hali.
Hata walipokaribia na jengo la kifalme walipata kuwaona wasichana watano wanaofanya kazi chumbani kwa Maya wakisogea kuwafuata. Hata walipofika walimsimamisha Maya na kumtaka ashuke kwenye farasi wake.
"Kuna nini mbona mnataka ashuke hapa?"aliuliza Jamal akiwa haelewi.
"Tumeagizwa na Malkia kuwa tumchukue Maya tupite naye mlango wa pili ili asionekane na ugeni uliokuja kuwa ni mtu wa kutembea,huyu ni mwari hivyo si vizuri kuwa nje kwa muda huu."alisema mmoja wa wale wasichana na kauli yake ile ilimshtua Jamal kusikia taarifa hiyo. Alimgeukia Maya ambaye baada yakusikia hivyo alimtazama Samir.
"Bado tu unatafakari jambo la kunishauri Samir?"aliuliza Maya na kumfanya Samir amtazame.
"Fuata ulichoambiwa na wahudumu wako kwanza muda sio mrefu nitakueleza."alisema Samir na kuona Maya anashuka kwenye farasi wake akionesha kukata tamaa,alishikwa mkono na wasichana wale wakaanza kutembea naye kupitia mlango wa pili asipate kuonekana.
Jamal alibaki kutazama tu asijue kitu gani kinaendelea hapa kati. Alimuona Samir anasuka kwenye farasi wake na ilibidi naye ashuke kwenye farasi kumfuata Samir aliyekuwa anakokota farasi wake huku akionekana kuwa kwenye mawazo. Alitangulia mbele na kumzuia Samir asiende mbele.
"Kuna kitu gani kinaendelea kwa Maya mbona sielewi hapa?"aliuliza jamal huku akimtazama Samir kwa umakini.
"Hebu naomba uniache nahisi kuchanganyikiwa nikitafakari,niache nikapumzike Jamal."alisema Samir na kusogea pembeni aweze kuendelea na safari yake lakini Jamal hakutaka kumruhusu aondoke.
"Tafadhari Samir niambie kuna nini kinaendelea hapa!" Samir alimtazama Jamal baada ya kuongea vile.
"Unataka ujue kitu gani tena na umesikia pale kwamba Maya ni mwari kwasasa inamaana anataka kuolewa. Sasa kuna kitu gani wataka ujue?"alisema Samir huku akimtazama Jamal.
Maneno yale yalizidi kumchanganya Jamal baada ya kusikia Maya anataka kuolewa. Muda huohuo Lutfiya alitokea pale na kukuta Jamal akiwa amesimama na Samir,ilimbidi asite kusogea pale na dakika chache akamuona Samir akiondoka zake kuelekea chumbani kwake. Haraka akakimbia kumfuata Jamal aliyekuwa mnyonge baada ya kuambiwa vile na Samir.
"Jamal.."aliita Lutfiya na kumfanya Jamal ageuke na kukutana na sura ya mwanamke huyo. Ni wazi kwamba amekuja kumueleza kuhusu taarifa hizohizo za kuolewa kwa Maya. Hii inamaana kwamba endapo atakapoolewa Maya basi swala lao ndio limefeli kabisa na hawataweza kupata nafasi ya kumtumia Maya,walibaki wametazamana tu wasijue nini wafanye kwa muda ule.
Samir alijitupa kitandani baada ya uchovu wa safari. Kikubwa hasa kilichomtia kwenye wakati mgumu ni swala la Maya kuhusu kuolewa kwake na mtoto wa Mfalme Joha. Aliafakari ampe ushauri gani Maya kabla ya muda kuweza kufika. Aliitazama pete yake kwa umakini na kuusogeza mkono ule karibu yake.
"Nimpe ushauri gani Maya aweze kuufuata ukawa ni afadhari kwake?"aliuliza Samir huku akiitazama pete yake.
" Kuna mawili ya kufuata kama itawezekekana, Maya akiolewa na ukoo wa Joha siku tano mbele Mfalme na Malkia wa Eden watauliwa na watu fulani,atakayeimiliki Eden ni Maya ambaye ndiye mke wa mtoto wa Joha hivyo Eden itakuwa mikononi mwa ukoo wa Joha na siku za mbeleni watamgeuka Maya na kujimilikisha Eden kuwa yao. Kama utataka hili lisitokee basi mueleze Maya kuwa unampenda na unataka uwe mume kwake. Hili litakuwa zito kwakuwa mtapaswa kuondoka Eden kama atakukubalia,maana ukoo wowote wa ufalme haupaswi kuwa na mahusiano na mfanyakazi yeyote wa kifalme,lakini ndio njia pekee ya kuzuia Malkia Rayat pamoja na Mfalme Siddik kutouliwa. Hivyo unakazi ya kumshawishi Maya kwa muda mfupi uliobaki."ilisema ile pete na kumfanya hata Samir anyanyuke pale kitandani maana anayoelezwa ni mazito.
"Inamaana huu ugeni sio mwema katika taifa hili?"aliuliza Samir.
"Watakaa hapa kwa muda wa siku nne,na kila siku wanayokaa ndio wanabadilika na kuitamani falme hiyo. Kuna mambo mengo yatatokea na ukizembea unaweza hata kujulikana wewe nani na inaweza kukuweka kwenye matatizo,hivyo yakupasa kuwa makini katika mambo yako yote."ilisema pete na kumfanya Samir ashushe pumzi kwa hofu. Alijikuta anasimama kutoka pale kitandani na kutaka kwenda kuonana na Maya amueleze hali halisi ili wainusuru Eden pamoja na viongozi wake maana inakwenda kufa. Alisimama kwa dakika kadhaa akitafakari ataanzaje kumueleza Maya akamuelewa yale aliyoambiwa na pete yake. Alipiga moyo konde akafungua mlango na kuelekea sehemu husika.

Huku sebuleni maongezi yalipamba moto baina ya pande hizo mbili,ilikuwa ni furaha kubwa sana kwa Mfalme Siddik kukutana na rafiki yake huyo wa muda mrefu Mfalme Joha.
"Naamini urafiki wetu unakaribia kuwa ndugu muda si mrefu,falme zetu zikiwa kitu kimoja hakuna wa kuziingilia wala kuleta matatizo. Hakuna asiyefahamu ukoo wa Joha ulivyojizatiti katika majeshi yenye kutumia silaha za uhakika,dhahabu zilizosheheni kwenye ardhi yangu,wacha tulifanikishe swala hili la watoto wetu watuunganishe falme hizi mbili,na hii ni zawadi kidogo niliyokuandalia Mfalme Siddik."alisema Mfalme Joha na kumfanya askari wake mmoja asogeze sanduku kubwa lililojaa dhahabu ndani yake na kuliweka mezani,Mfalme Joha akamsogezea sanduka lile karibu yake hali iliyomfanya Mfalme Siddik aachie tabasamu zito huku akilikamata sanduku lile.
"Hakika mmependelewa ardhi yenye mali za thamani kama hizi. Nimepokea na nimefurahi kwa zawadi yako hii uliyoandaa."alisema Mfalme Siddik na kumfanya hata mkewe afurahi.
"Hiyo ni zawadi yangu kama baba, ila mhusika mwenyewe naye ameandaa zawadi yako kwako."alisema Mfalme Joha na mwanaye Rahim akasimama kwa heshima,alimsogelea mlinzi wake na kupokea kiboksi kidogo na kumsogelea Malkia Rayat akamkabidhi. Hata alipofungua alipata furaha kuona vidani ni mikufu ya dhahabu ikiwa kwenye kiboksi kile,hakika aliifurahia zawadi ile na kumshukuru sana Rahim.
Hakuishia hapo kijana huyo lilikuja sanduku la nguo mbalimbali zenye mapambo ya dhahabu na yenye heshma kubwa akampatia Mfalme Siddik, hakika walijua kuziteka furaha za viongozi hao wa Eden ikawa ni furaha zaidi ya maelezo.

Huku kwa Samir alikuwa amesimama kwenye mlango wa chumba cha Maya huku akionekana kuzuiwa na msichana mmoja pale mlangoni.
"Nahitaji kuongea naye dakika mbili tu nawaomba."alisikika Samir akimbembeleza msichana yule.
"Hebu kuwa muelewa basi Samir,Maya yupo anaandaliwa akakutane na wageni hakuna ruhusa ya mtu yeyote kukutana naye kwa wakati huu."alizidi kuweka msimamo msichana yule.
"Nakuomba mfuate Maya mwambie Samir anataka kuongea na wewe,akikataa nitaondoka hapa mlangoni."alisema Samir na kumfanya yule msichan a amtazame. Ilibidi afanye hivyo kumfuata Maya alikuwa ndani anapambwa ili akaonane na wakwe zake.
"Binti wa Mfalme,kuna mtu yupo nje anahitaji kuonana na wewe muda huu,nimejar.."
"Ni nani? Samir? Samir ndio anahitaji kuonana na mimi?"aliuliza kwa haraka Maya na kuwafanya hata wale wasichana wote waliokuwa mule ndani washangae. Yule msichana alimuitikia kuwa ndiye mwenyewe akashuhudi Maya akitoka mbio kuelekea mlangoni huku nyuma akiwaacha midomo wazi wale wafanyakazi wake.
Alijihisi mwenye furaha na kujawa na shauku ya kutaka kujua jambo pindi alipomuona Samir pale mlangoni.
"Niambie sasa Samir, nafanyaje?"aliuliza Maya huku akimkamata mikono Samir kutaka ampe ushauri. Samir alijikuta akimeza funda moja la mate ili amueleze ukweli Maya.

ITAENDELEA
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN 29

"Maya, hakika niliuficha ukweli ulio moyoni mwangu kwa muda mrefu sana,nimekuwa nikihofia kukwambia toka awali nikihofia kufukuzwa na Mfalme lakini tangu nilipopata kufahamu ukweli kutoka moyoni mwako nimejikuta napata nguvu ya kuongea haya mbele yako... MAYA HAKIKA NAKUPENDA.. na ninaongea kutoka moyoni kwamba nakupenda sana,umekuwa mtu wangu wa karibu siku zote na ni wewe pekee uliyeniamini na kunifanya kama ndugu kwako. Tafadhari naomba unifanye niwe wako."aliongea Samir huku akimtazama usoni Maya ambaye maneno yalimfanya apoe.
"Samir mbona unazidi kuniweka kwenye wakati mgumu,sielewi ujue hadi sasa."alisema Maya akionesha kuchanganyikiwa.
"Maya elewa kwamba huu ndio muda sahihi wa kuanza mahusiano baina yetu,kama hutaki kuolewa na ugeni huu ambao upo hapa kwaajili ya kusubiri ndoa basi ndio muda pekee wa mimi na wewe kufanya jambo ambalo litaweza kuvunja mpango huo wa kuolewa na falme ya Joha."
"Unataka tufanye jambo gani Samir,unafahamu fika desturi za Eden hasa katika familia za kifalme kuwa na mahusiano na mfanyakazi yeyote wa Mfalme. Huoni itakufanya upate adhabu ya kuondolewa uishi mbali na hapa?"
"Hilo ndio kusudio langu,nahitaji mimi na wewe tukaishi mbali na hapa,kama utakataa kuolewa na kijana wa Mfalme Joha na ukanitaja mimi kuwa ndiye uliyenichagua,haitakuwa na kipingamizi tena na nipo tayari kuondoka Eden lakini na wewe uwe na msimamo wa kuondoka na mimi,najua itakuwa ni aibu kwa Mfalme na hasira zake lazima atakufukuza nawewe pia."alisema Samir akizidi kumvuta Maya.
"Mh Samir unataka tufukuzwe halafu tukaishi wapi maana nafahamu lazima baba yangu ataweka amri kwa mataifa mbalimbali ili wasitupokee."aliongea Maya akiwa hana raha kabisa.
"Maya ninachokiongea hapa sio kwamba nimetengeneza ili nikusaidie usiolewe laa, ninaongea kutoka moyoni nakupenda na ningependa hapo mbeleni tuje kuwa na famili ia yetu. Hivyo maswala ya wapi tutaishi ni baada ya moyo wako kuridhia maneno yangu na uwe na utayari wa kuwa na mimi. Nikwambie tu ukweli nimejitolea kufa uwanjani siku ile kuhakikisha napata nafasi ya kuwa mlinzi wako ili nizidi kuwa karibu nawe,na Mungu amesaidia nimeipata nafasi hiyo na alijua nilifanya kwakuwa nakupenda. Nimejitolea kukulinda katika maisha yako yote,hata tukienda kuishi msituni juwa kwamba mimi nipo kwaajili yako,nakuomba sana unikubalie Maya."aliongea Samir na maneno yake matam yalimfanya Maya amtazame Samir aliyeonekana kuongea kutoka moyoni.
"Samir, nitafanya kile unachotaka ila naomba uniahidi kwamba utakuwa upande wangu."aliongea Maya akiwa ameishika mikono ya Samir.
"Muda wote katika maisha yako nitakuwa nawe hadi mmoja kati yetu atakapotangulia,niamini Maya nafanya haya yote kwakuwa nakupenda."alisema Samir na kushuhudia mdomo wa Maya ukitua kwenye kinywa chake,hata yeye alishangaa maana hakuamini kama anaweza kumshawishi binti huyo wa Mfalme. Hakuwa na jinsi naye alishiriki kwenye tendo hilo kikamilifu wakabaki kukumbatiana wawili hao.
Yote hayo yalikuwa yakiendelea pale mlangoni kwa ndani wale wafanyakazi walikuwa wametega masikio yao kusikiliza maongezi yale. Walibaki kushika midomo yao hawaamini kile ambacho wamesikia.

Baada ya muda Maya alirejea mule ndani kumaliziwa kupambwa baada ya kukubaliana na kupanga mambo na Samir. Wale wasichana wakawa wanampamba huku muda mwingi wakitazamana,hali ile ilimfanya Maya atambue huenda wamesikia kilichoongelewa muda ule. Hakutaka kujali alikuwa mwenye kujiamini na kuona hata wakijua haina tatizo maana muda mfupi atakwenda kuongea mbele ya wazazi wake na watu wa Joha.
Huku kwa Samir alikuwa mwenye kutafakari sana baada ya kuweza kumweleza Maya ukweli. Alibaki kusubiria kitakachotokea pindi Maya atakapoonea ukweli.
"Sina jinsi,nitakubaliana na uamuzi wowote atakao utoa Mfalme kwa kile kitakachokwenda kutokea, sifanyi haya kwaajili ya Maya,nailinda Eden yote hasa Mfalme na Malkia waliokuwa katika wakati mgumu."alisema Samir akimeshika tama akitafakari haya. Hakutaka kuendelea kupoteza muda alitoka kuelekea nje kuandaa usafiri wao endapo wakitaka kuondoka na Maya.
Huku upande wa pili Jamal alielekea kwenye nyumba ambayo wamekuwa wakikutana mara kwa mara kupanga mikakati yao. Hata alipofika aliweza kuwakuta wale wenzake wakiwa na majeraha,ni muda ule walipokwenda kumvamia Samir kutaka kumuua na ndio walionusurika kukimbia pindi wenzao walipouawa. Dakika kadhaa alifika Lutfiya na kuungana na wenzake,lengo hasa ni juu ya taarifa za Maya kutaka kuolewa. Taarifa ambayo kwao ni tofauti hawakupenda swala hilo litokee,walitaka hapo baadae wamfanye Maya awe na mahusiano na Jamal ili aweze kuolewa. Hivyo ugeni huo wa Falme ya Joha haukuwa mzuri kwao kuona wanawaingilia katika jambo lao.
"Tunafanyaje sasa hapa maana hili swala limezidi kunichanganya akili."alisema Jamal akiwatazama tu wenzake.
"Njia rahisi ya kulizuia hili ni kummaliza huyo mtu anayetaka kumuoa mtoto wa Mfalme wa Eden,nadhani kwa kufanya hili itapelekea kuwa na nafasi tena ya wewe kumpata."alisema mmoja wa wale watu akimtazama Jamal.
" Nahisi ndio njia peke ya kulizuia hili,akiuliwa yule mtoto wa Mfalme Joha kila kitu walichopanga wao kitavurugika. Watarudi katika taifa na kumuacha Maya kama kawaida."alisema Lutfiya akimuunga mkono mwenzake.
"Nani sasa ataifanya kazi hii maana kwasasa nimekuwa nategemewa kwenye jeshi muda mwingi nakuwa nipo kazini."aliongea Jamal.
"Hili swala mmoja kati yenu alifanye,ataingia kwenye falme aikamilishe kazi hii. Nimefanya matukio mengi na nimekua nikihisiwa vibaya na Samir hivyo safari hii tuwatumie nyie muifanye hiyo kazi."alisema Lutfiya akiwatazama wale wenzao. Walikaa kimya kwa muda kadhaa na mwishowe mmoja wapo akajitolea kufanya jambo hilo. Jamal alimpa moyo na hamasa ya kulitekeleza swala hilo. Ilibidi wamuandae na kuhakikisha wanashirikiana naye hadi kumuelekeza chumba ambacho Rahim atapataka kupumzika. Baada ya kupanga hayo Jamal na Lutfiya walirejea kwenye falme kila mtu kwa muda wake maana kila wanapokutana hakuna anayewafahamu kwamba wanalengo gani dhidi ya ufalme wa Eden.

Furaha ilizidi kushamiri ndani ya ufalme,pongezi za hapa na pale ziliendelea baada ya kupeana zawadi zile. Ilifika muda walihitaji kumuona binti wa Mfalme maana tangu walipowasili hawakuweza kuona hata sura yake. Malkia Rayat alinyanyuka na kuanza kupiga hatua kuelekea chumbani kwa Maya. Rahim alimtazama baba yake na kuoneshdana ishara kwamba mambo yanakwenda sawa kama walivyopanga.
Maya alikuwa karibu na kioo amekaa huku akijitazama vile alivyopambwa na wasichana wale ambao eiimaliza kazi yao vyema na yote ni kwaajili ya kuolewa na mtoto wa Joha. Akiyakumbuka maneno ya Samir na jinsi walivyopanga kufanya. Alishusha pumzi kidogo maana swala hilo linahitaji kuwa na ujasiri wa aina yake kuongea mbele ya wageni na wazazi wake.
"Litakalokuwa sawa ila nafanya yote kwaajili ya furaha yangu,siwezi kuwafurahisha watu angali moyo wangu unakwenda kupata mateso."alisema moyoni Maya na muda huohuo mama yake akaingia akionesha kuwa na furaha moyoni,alimsogelea binti yake pale alipo na kumbusu shavuni.
"Hakika leo ni siku nzuri na yenye kuleta furaha kwenye ufalme huu,kile tulichokuwa tunakisubisi siku zote hatimaye kimewadia. Familia ya Mfalme Joha imefika muda mrefu na sasa wanahitaji kukuona na hata mumeo mtarajiwa anahamu ya kukuona."aliongea Malkia Rayat akiwa na tabasamu mwanana huku akimtazama binti yake kwenye kioo kikubwa kilichopo mbele yake akionekana kurembwa haswa.
"Sawa nimesikia."alijibu kwa mkato Maya huku akijitazama kwenye kioo kile.
"Hupaswi kuwa hivyo sasa Maya,tengeneza tabasamu uonekane mwenye furaha,au hujafurahia ugeni huu?"alisema Malkia na kumfanya Maya asimame na kutazamana na mama yake.
"Mama, unakumbuka kauli yangu ya mwisho nilisemaje kuhusu kuolewa?"
"Mayaaa, hebu usifanye wazazi wako tuingiwe na aibu,baba yako alikukataza kushikilia msimamo wako huo,bado tu hujaubadilisha moyo wako? Hebu sahau yote ili lifanyike jambo kubwa hapa Eden kwa hizi familia mbili."alisema Malkia na kushuhudia Maya akitikisa kichwa kutokukubaliana naye.
"Siwezi kubadili maamuzi yangu eti nisiwatie aibu!, hivi nawezaje kuwafurahisha ninyi kwa siku kadhaa halafu nije kuwa na majuto katika maisha yangu yote ya ndoa. Nilishasema siko tayari kuolewa na falme yeyote ile,na kama huamini ngoja uone kinachokwenda kutokea hivi sasa."alisema Maya na kutoka pale chumbani moja kuelekea ukumbini walipokaa wageni wote pamoja na Mfalme Siddik. Malkia kusikia hivyo haraka naye akatoka kumkimbilia mwanaye huku akimtaja jina lake.

Huku chini wakiwa hawana habari walizidi kuongea mambo mbalimbali. Muda huohuo akapata kuonekana Maya akisogea pole walipo huku kila mmoja wapo akimtazama. Rahim alibaki kuachia tabasamu baada ya kumuona mwanamke ambaye anategemea kuwa mkewe siku za karibuni. Watu wote walimtazama Maya kwa vile alivyopendeza,hakika hata Mfalme Joha alifurahi kuona mwanaye anapata chaguo lililo sahihi. Aliwasili Jamal na kusimama mahala ambapo baadhi ya askari waliochaguliwa kuwepo eneo hilo. Alimtazama Rahim pale alipokaa na kuona ndiyo mtu anayepaswa kuuawa. Alitazama pembeni na kumuona Lutfiya naye akiwa amesimama na baadhi ya wafanyakazi.
"Binti yangu mpendwa,hakika umependeza sana siku ya leo, naamini hata mumeo mtarajiwa anasikia faraja kukuona."alisema Mfalme Siddik huku akiwa mwenye tabasamu. Maya alimtazama baba yake huku sura yake haikuwa yenye furaha, na muda huohuo mama yake ndio alikuwa anakuja akionekana kuharakisha,hata alipofika pale aliwashtua watu kwa mwendo wake.
wakawa wanamtaza. Maya aligeuka kumtazama mama yake akionesha kuwa na wasiwasi, na kweli alikuwa anahofu mwanaye kuongea maneno mabaya mbele ya umati ule wa watu pale ukumbini walipokaa
"Samahani jamani, Maya nakuomba tuongee mara moja"alisema Malkia Rayat akitaka kugeuka kwenda sehemu aongee na binti yake.
"Nitakuja subiri kwanza niyaseme machache mbele ya wageni wangu na baba yangu Mfalme wa Eden."alisema Maya kwa kujiamini na maneno hayo yakamshtua mama yake akageuka kumtazama. Haraka akamsogelea pale alipo kutaka kumkamata mkono watoke mahala pale.
"Hebu mpe uhuru wa kuongea mtoto, muache aseme alichopanga kutueleza."alisema Mfalme Joha na kumfanya Malkia amuache Maya na kujenga tabasamu la kutengeneza.
Watu wote wakanyamaza kimya huku wakimuangalia Maya wamsikie kitu gani ambacho amepanga kukisema.
ITAENDELEA
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WWA EDEN 30

"Mioyo yenu imekuwa na furaha siku ya leo mkiwa mnasubiri jambo ambalo litawaunganisha kuwa familia moja."alisema Maya na kuwatazama wageni wale huku Mfalme Siddik akiwa mwenye tabasamu.
"Huenda mkawa na furaha kwa upande wenu lakini katika moyo sina hata chembe ya furaha kwa hilo mnalolitaraji. Moyo wangu haupo tayari kuolewa na falme yeyote ile na kauli hii naisema mbele ya watu wote ili mfahamu hilo."alisema Maya na maneno yake yakawa sumu katika mioyo ya watu hususani Mfalme Siddik ambaye alikasirika gafla kwa kuyasikia maneno ya binti yake.
"Unaongea upumbavu gani wewe Maya?"alifoka Mfalme na kutaka kunyanyuka lakini Mfalme Joha akamzuia pale alipo.
"Si mara ya kwanza baba kukueleza juu ya hili lakini umekuwa unataka iwe ni lazima jambo ambalo sitalikubali abadani."aliongea Maya na kuzidi kumtia hasira baba yake,aligeuka kumtazama Rahim.
"Siku zote ndoa ni maridhiano baina ya watu wawili waliopenda na, mimi na wewe tulikaa lini tulikubaliana kwa maongezi tulifanikishe hili? Mimi nikwambie ukweli ulio moyoni sina upendo wowote na wewe na wala usitegemee ukaja kuwa mume kwangu."alimpa ukweli kutoka moyoni bila kujali wapo watu wengi eneo lile.
"Kila mtu ana uhuru wa kumchagua yele ambaye moyo wake umeridhia kuwa naye,sitakuwa tayari kuwa na mtu ambaye hayupo katika fikra za.."
"Usizidi kunikera Maya,askari mkamateni haraka sana.!"alitoa amri hiyo na mara moja Jamal aliharakisha pamoja na askari wawili wakamkamata Maya mikono.
"Sijamaliza,naomba kila mtu afahamu sina mapenzi na Rahim hata chembe,yupo ninayempenda naye anajua hilo."alisema Maya na kuwafanya watu wote wamtazame,hata Jamal na wale askari walimtazama baada ya kusema hivyo.

Huku kwa Samir alikuwa tayari kashaanda farasi wa Maya pamoja na farasi wake ikiwa ni maandalizi endapo wakifukuzwa na Mfalme. Alipohakikisha hilo amelikamilisha alirud i zake chumbani kwake huku akiwa ni mwingi wa mawazo. Akiwa anaukaribia mlango mkuu alishangaa kuon askari wapatao ishirini wakikimbia na kumzuka pale,hali iliyomfanya asimame na kubaki kwenye mshangao akiwatazama askari wale walioweka mikono yao kwenye mapanga yalionin'ginia kiunoni tayari kwa kuyatoa kumkabili Samir endapo ataleta tafarani. Akiwa kwenye mshangao huo alitokea Generali mkuu akiwa ameweka mikono nyuma,walifungua duara lile akapita kisha na kumsogelea Samir aliyebaki kushangaa tu. Ngumi nzito ilituwa shavuni kwa Samir akaenda chini huku akishika shavu lake,alishuhudia damu zinamwagika kutoka mdomoni mwake,aligeuka kumtazama Generali aliyeonekana kuwa na hasira.
"Kupewa nafasi ya kuwa mlinzi wake ndio umeona njia nzuri ya kuanzisha mahusiano naye,sasa utaenda kuishi msituni upambane na wanyama wakali,huwezi kumtia aibu Mfalme kiasi hiki."alifoka Generali na kugeuka.
"Mleteni huku aongee."ali amuru akamatwe Samir aingizwe ndani akajibu mbele ya Mfalme. Alikamatwa na kuanza kupelekwa ndani,alijua tayari Maya ameongea kila kitu,alikuwa na hofu juu ya swala.
"Huwezi kuongea maneno hayo mbele yangu mimi,umenitia aibu kubwa sana Maya."alisikika Mfalme Siddik akifoka kwa ukali huku akimtazama binti yake,Malkia Rayat ilibidi awe mpole tu baada ya kuona mumewe amepandisha hasira. Muda huohuo aliingia Generali huku nyuma akifuatwa na askari wake waliomuweka Samir chini ya ulinzi.
"Huyu mjinga ndio amekuteka akili hadi unakosa heshima hata kwa mzazi wako."alisema na kugeuka kumtazama Samir.
"Sikutegemea kama utakuja kufanya jambo hili katika falme yangu, Samir niliyemlea mimi muda wote leo amekuja kunigeuka na kutaka kuchuma mmea wangu nilioupanda mwenyewe. Sitahitaji kusikiliza la mtu nakupa uhuru uondoke hapa Eden ukatafute mji wowote wa kuishi nje ya Taifa langu,ole wako nikuone unakanyaga tena hapa ,haraka naomba uondoke.!"alisema Mfalme Siddik akiwa amekasirika sana huku Mfalme Joha akimtaza Samir aliyekuwa ameinamisha tu kichwa chini. Rahim alimkata jicho Samir baada ya kujua ndiye mtu aliyemfanya asikubalike kwa Maya.
Hata alipogeuka kutaka kuondoka Maya alimkamata mkono angali naye ameshikwa na wakina Jamal.
"Baba, Samir hawezi kuondoka Eden pekeyake kama kupendana ni sisi ndio tumependana hivyo hata kama ntanilazimisha sitakuja kumpenda mtu mnayemtaka nyiye, chaguo langu ni moja tu,Samir."aliongea Maya na maneno yake hata mama yake yalimchoma na kujua kweli mwanaye amependa. Watu wote walielewa kweli Maya amedhamiria kuwa na Samir. Mfalme Joha alisimama na kupiga makofi kadhaa huku akijenga tabasamu,watu wote wakageuka kumtazama hata Mfalme pia.
Aligeuka kumtazama Mfalme Siddik.
"Siku zote usilazimishe jambo ambalo haliwezekani maana unaweza ukaumia ama likakuchosha. Muache mwanao afanye uamuzi anaotaka" aliongea kwa upole mfalme joha akijaribu kumtuliza mfalme siddik aliyeonekana kuwa mkali sana. ilimbidi mfalme aite baraza la wazee wakaingia mahala kukijadili swala hilo huku kila mv akiwa akiongea lakwake juu ya jambo hilo, jamal alimtazama samir akiwa ameshikiliwa na askasi pali karibu yao,moyoni alipatwa na hasira baada ya kufahamu kumbe samir pamoja na maya walikuwa wapenzi, swala hilo lilimfanya hata lutfiya apate kuhisi ndio sababu ya samir kuwa karibu kila anapotaka kufanya jambo baya kwa maya, malkia alibaki kumtazama tu binti yake huku akisikitika na kuona huenda likaamuliwa lolote na wazee pi i watakapopata muafaka wa swala hilo. Mfalme Joha alimsogelea mwanaye na kujadili naye mambo fulani pale walipokaa wakisubiri muafaka utolewe na Mfalme Siddik. Huku Maya alikuwa ameinama tu chni pale alipokamatwa na wakina Jamal ,ilisikika tu minon'gono pale ukumbini kila aliyeko eneo hilo alilipokea swala hilo kwa namna yake. Baada ya muda Mfalme Siddik alitoka sambamba na wazee wale na kurudi kukaa sehemu zao. Kila mtu alitulia kimya huku wakimtazama Mfalme aliyeonekana akiwa amenuna. Maya na Samir walikuwa wenye hofu wakisubiri kitakachoamuliwa na Mfalme.
Alinyanyuka mzee mmoja na kusogea pale mbele akasimama huku watu wakimtazama.
"Baraza la wazee wa Eden likiwa chini ya Mfalme Siddik limekaa na kuchukua uamuzi wa pamoja na kumfikishia Mfalme. Hata yeye ameridhia sheria ifuatwe kam inavyotaka."alisema Mzee yule na kumfanya Malkia Rayat aanze kulia baada ya kufahamu kinachojiri.
"Kuanzia sasa Samir pamoja na Maya hawatatakiwa kuonekana katika Taifa la Eden milele."watu walihamaki baada ya kusikia hivyo,wengine hawakuamini kama itatokea adhabu hiyo.
"Ufalme unasheria zake na ni kosa kubwa Mfanyakazi wa falme kuwa na mahusiano mtoto wa kiume au binti wa Mfalme na endapo litatokea hilo basi mmoja kati ya hao auliwe na mwengine atupwe msituni,lakini Mfalme amekataa kushuhudia kifo cha mmoja kati ya hawa hivyo wote watapelekwa kutupwa msituni na hawataruhusiwa kurudi Eden maisha yao yote."alisema Mzee yule na kumaliza maelezo yake akarudi kukaa. Mfalme Joha alitabasamu kusikia vile,kuna namna amefikiria na kuona huo ndio muda pekee wa yeye kufanya kitu.
Malkia alijikuta akijikuta akimsogelea mwanaye na kumkumbatia pale huku akionekana kulia maana hatakuja kumuona tena. Mfalme Siddik alijikaza kutosikia maumivu kama baba lakini moyoni aliumia sana,hakukuwa na namna ya kulizuia hilo Maya na Samir lazima waondoke Eden. Aliumi sana kwa kuona ameingia aibu kwenye falme ya Joha kwa maneno yale ya binti yake kuonesha kutokuwa tayari kuolewa na ukoo huo. Kubwa na ndio linalobeba adhabu ya kuwafukuza wawili hao ni kuwa na mahusiano baina ya mtoto wa Mfalme na mfanyakazi wa mfalme.
Taratibu Maya alimsogelea baba yake hadi pale alipo na kuinama chini kuishika miguu ya baba yake kama kuchukua baraka. Hata alipomaliza alirejea nyuma na kufanya hivyo kwa mama yake pia ambaye alijikuta akimnyanyua mwanaye na kumkumbatia huku akionekana mwenye majonzi
Generali aliwaamuru askari wafanye kazi na mara moja walianza kuwatoa wawili hao huku Malkia Rayat akitolewa mwilini mwa binti yake wakiwa wamekumbatiana, Maya alijihisi huzuni kumuona mama yake akiwa katika hali ile,alishuhudi kuona mama yake akikimbia kuelekea chumbani kwake,ni wazi kwamba ameshindwa kuvumilia kumuona binti yake huo akitolewa katika taifa alilozaliwa.

Taarifa nje zikapata kusikika na kuwafanya wananchi watoke wote majumbani kwa kwao na kusimama nje.
Hata walipotoka Samir na Maya walipanda kwenye farasi wao kila mmoja na kuanza kusindikizwa na askari kumi waliochaguliwa na Generali akiwemo Jamal. Wafanyakazi wa Maya waliokuwa wakimhudumia waliumia sana kuona bosi wao anaondoka ndani ya falme hivyo hawatakuwa na kazi tena katika falme. Lutfiya alibaki kutazama tu msafara ule unavyoondoka pale na kuona mipango yao imekufa bila shaka. Wananchi walimpa heshima Maya kwa kuinamisha vichwa chini kuonesha bado wanamheshimu. Lakini walipewa mgongo wakaanza kumshambulia Samir kwa maneno na hata kumrushia vitu kama mayai na nyanya mbovu. Iliwabidi askari waingilie kati kmkinga Samir asizidi kuchafuliwa,alibaki kuinamisha kichwa chini tu huku akiona kama ni fedheha kwake kufanyiwa vile.
Malkia Rayat alikuwa juu ya chumba chake akitazama dirishani na kuona Maya na Samir wakiiaga Eden.
"mungu awatangulie huko muendako naamini mtaishi muda mrefu."alisema malkia Rayat akiwaombea uzima maya pamoja na samir.
ITAENDELEA
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME 31

Huku nyuma Mfalme Siddik aliwaomba radhi familia yote ya Mfalme Joha kwa kile kilichotokea. Hata yeye hakutegemea kusikia yale ambayo yamemchoma moyoni. Hapakuwa na jinsi waliona hakuna haja ya kulaumiana kwa jambo lile na kuamua kuachana nalo. Hata zawadi zile walizotoa waliamua kumpatia Mfalme Siddik kwa moyo mmoja. Waliongea mambo mengi siku hiyo na baadae iliwalazimu waage ili kuweza kurejea kwenye taiea lao. Mfalme Siddik aliwapatia magunia ya vyakula ikiwa kama shukrani yake ili kuweza kusahau yale yaliyotokea. Walipokea mizigo hiyo askari na kuanza safari ya kurudi kwenye ufalme wa Joha. Rahim alibaki kuitazama Eden vile ilivyo,roho ilimuuma san maana alitegemea kumuoa Maya kungemfanya akaheshika Eden.
"Nimeagiza vijana kadhaa wawafuatilie wajue wanaachwa kwenye msitu gani,bado nina tumaini la kuja kupata heshima Eden,nitampata tu Maya na yule mpumbavu lazima auliwe."alisema Rahim akionesha kukwazika sana kwa kumkosa Maya. Mfalme Joha alibaki kumtazama tu na kusikia lengo la mwanaye huyo .
Mfalme Siddik alirejea chumbani kwake na kumkuta mkewe akiwa amesimama tu pale dirishani akitazama nje. Alijuwa bila shaka alikuwa akiwatazama wakina Maya wakiondoka. Alishusha pumzi kidogo kabla ya kuongea lolote huku akiinamisha kichwa chake. Alifahamu kuwa adhabu ile imemuuza hata mkewe maana Maya ndiye mtoto wao wa pekee hivyo kuondoka kwake ni sawa na kumfanya Malkia ajione hana mtoto tena. Taratibu alipiga hatua pale alipo kumsogelea mkewe,akamshisha bega.
"Haikuwa na jinsi,sheria za Eden ndio zinatuongoza."aliongea Mfalme kwa sauti ya upole.
"Nafahamu hilo,nami sina jinsi nitabaki kuwa Malkia tu nisiye na mtoto kwasasa. Sijui huko aendako atakuwa hai kwa muda gani au atakufa lini."aliongea Malkia na maneno yale yalimchoma Mfalme Siddik. Hakuwa na jinsi maana binti yake amehukumiwa kwa sheria zilizowekwa Eden.

Taarifa za binti wa Mfalme kufukuzwa ndani ya taifa la Eden zilimfikia Mfalme Faruk hali iliyomfanya ataharuki.
"Wameelekea wapi kwasasa?"
"Wanakwenda kutelekezwa kwenye msitu na askari wa Eden."alisema kijana mmoja aliyeileta taarifa hiyo akitokea Eden.
Alichoka Mfalme Faruk maana taarifa hiyo ilimfanya aamini swala la kumtumia Maya katika njama yao ili waipate Eden kwa njama hiyo imegonga mwamba. Alitafakari namna ya kufanya na mwishowe akapata jibu alilohisi litaleta maana.
"Yuko wapi Jamal kwasasa.?"aliuliza swali akitaka afahamu mwanaye alipo.

Safari ilikaribia kuishia ukingoni baada ya kuukaribia msitu ambao unasadikika kuwa na wanyama wakali. Hapo ndipo walipaswa kuachwa Samir pamoja na Maya kama adhabu ilivyotolewa. Walikuwa wakiutazama msitu ule jinsi ulivyo mkubwa na kuwafanya watazamane kuona ni wao ndio wanapaswa kuingia huwo. Baada ya dakika kadhaa walifika mwanzo wa msitu huo na kuonekana njia kubwa ambayo ni ya kupita watu na usafiri wao.
"Huu ndio msitu wa mpaka wa Eden unapoingia kwenye msitu huu kuanza kuifuata njia hiyo hautambuliki kuwa upo Eden,hilo ni taifa lengine tena. Hivyo basi hiyo ndio njia yenu ya kupita kuwa nje ya Eden,mkatafute mji wa kuishi huko muendako kama mtafanikiwa kupita salama ndani ya msitu huu. Sisi safari yetu imeishia hapa tutasimama hapa kuhakikisha mmepita hapo ndipo turudi."alisema kamanda wa kikosi hicho akimtazama Samir aliyekuwa makini kusikiliza. Aligeuka kutazama msitu ule uliokuwa unasikika sauti mbalimbali za wanyama na ndege. Jamal alibaki kuwatazama tu Maya na Samir,taratibu huruma ikaanza kumjia pale akiwa juu ya farasi.
"Nendeni haraka!"alisema askari yule na kumfanya Maya aanze kutangulia,Samir na akafuata wakinyoosha njia ile kuingia mule ndani huku askari wakishuhudia wakitokomea watu hao. Walisimama kwa dakika kadhaa pale hadi walipojiridh isha kuwa wamefika mbali na wao wakageuka na kuanza safari ya kurejea Eden. Jamal alibaki kuutazama tu ukubwa wa msitu ule na kuwa na mashaka juu ya maisha ya wawili hao.

Samir na mrembo Maya walifika sehemu wakakuta mifupa na mafuvu ya watu hali iliyomfanya Maya ahofie na kuingiwa na woga.
"Samir.. kwani tunaenda wapi?"aliuliza Maya na kumfanya Samir amsimamishe farasi wake.
"Umeniwahi kuongea hayo maana tunapokwenda hakujulikani."alisema Samir wakawa wamenyamaza kwa muda wakitafakari.
"Unaonaje tukaelekea Gu Ram?"aliuliza Maya.
"Gu Ram?"
"Ndio twende huko,mimi naamini Faraj tukimueleza yote atatuelewa na kutupokea."aliyasema hayo huku akimtazama Samir aliyekuwa anamsikiliza. Maneno yalijitosheleza kwa Samir na kumuunga mkono Maya,ilibidi wageuke na kurudi walipotokea ili wakamate njia ya kulekea Gu Ram. Hata walipotoka nje ya msitu ule walitazama huku na kule hawakuweza kuona mtu yeyote eneo lile na haraka wakaanza safari yao. Kwa mbali walionekana watu wakiwa kwenye farasi wao wakiwawafuata na bila shaka ni wale askari waliotumwa na Rahim,hakutaka kukubali kirahisi kumkosa Maya.

Siku hiyo Dalfa naye ndio alikuwa akiikaribia Eden akitokea katika taifa lake,hakutaka kuamini kama kile alichokifanya kwa Maya hakikuweza kufanikiwa. Alijua bila shaka ni yule mtu aliyekuwa na nguvu kama zake. Njiani alipata kuona askari wa Eden wakionekana kutoka mahala wakirudi Eden,alipowatazama kwa umakini aliweza kumtambua Jamal na kumkumbuka ndiye mtu aliyepambana na Samir siku ile pale uwanjani.
"Wametoka wapi hawa mbona wengi hivi?"alijiuliza Dalfa bila kupata jibu kamili huku akiona msafara ule ukitokomea. Taratibu naye akafuata huku akiwa juu ya farasi wake mweupe.

Baada ya kwenda umbali mrefu kwa kasi iliwabidi wawapunguze kasi farasi wao na kuanza kutembea taratibu wakawa wanaongea mambo yao.
"Unajua mpaka sasa siamini kama tumelifanikisha hili,moyo wangu naona umekuwa na amani kwasasa na wala sina mashka tena."alisema Maya akionesha kutabasamu.
"Nitafurahi kama utaendelea kuwa hivyo muda wote,nipo kwaajili yako Maya."aliongea Samir na kumfanya Maya ajihisi mwenye faraja sana. Wakiwa kwenye furaha hiyo gafla walipata kusikia vishindo vya farasi wakiwa wanakimbia kwa spidi,walipogeuka nyuma walipata kuona wanakaribiwa na kundi la watu nane wakionekana kushika mapanga yao.
"Tukimbie haraka sio wema hawa."aliongea Samir na kumsukuma farasi wake aongeze mbio, Maya naye akafanya hivyo kakini kwa bahati mbaya kilirushwa kisu kikapenya kwenye nyama za mguu wa farasi wake aliyedondoka chini na kumfanya Maya naye aanguke. Hali ile ikamfanya Samir aliyekuwa ametangulia asimame na kurudi nyuma. Haikuwa rahisi muda huohuo wale watu walifika na kuwazunguka kuwaweka kati huku mapanga yakiwa mikononi. Hakujali silaha zile
alishuka na kumsogelea Maya pale alipodonda akamnyanyua.
"Upo salama?"aliuliza Samir bila kujali watu walio wazunguka.
"Samir tupo kwenye hatasi, hawa watu watatuua."alisema Maya akionesha kuwa na hofu. Alisuhudia kuona Samir akitoa kitambaa na kukishika.
"Fumba macho yako Maya."alisema Samir akiwa anatazamana na Maya. Hakuwa na jinsi alifanya vile alivyoambiwa. Haraka Samir akanyanyua kitambaa kile na kuyaziba macho ya Maya kusudi asione kinachoendela muda ule. Alipohakikisha amelifanya hilo alimuacha pale akiwa amesimama kisha akakamata upanga wake na kugeuka kuwatazama watu wale ambao walionekana kuwa na uchu wa kummaliza Samir,wakashuka kwenye farasi wao na kuanza kumsogelea mtu wao. Bila kuchelewa wakaanza kumvamia Samir kutaka kummaliza, hakuwa tayari kudhurika na silaha zile za mapanga alipigana kwa umakini wa hali ya juu. Alipoona wanazidi kumuandama hakusita nguvu zake za ziada pindi aangaliapo pete yake iliyopo kidoleni mwake. Alijikuta anabadilika gafla na kuwa na kasi ya ajabu kuwadhibiti watu wale,hakuwa na huruma nao hata kidogo alichinja kwa dakika chache tu na kubaki watu wawili ambao walistaajabu kuona vifo vya wenzao pale chini na kushuhudia damu nyingi ikisambaa eneo lile. Hawakuwa tayari kuendelea na zoezi hilo,waliona njia ya haraka kuyanusuru maisha yao ni kukimbia maana mtu walitemtegea ni zaidi ya shetani anatumia nguvu za ajabu. Haraka walianza kutoka mbio eneo lile. Samir alipata kuwaona na hakutaka kumuacha hata mmoja akiwa mzima maana walikuja kwa shari,aliokota mapanga mawili pale chini na kuyarusha kwa kasi kwa watu wale ikapata kuzama mgongoni mwao na kuwadondosha chini na kupoteza maisha. Alibaki akihema kwa kazi nzito aliyoifanya kwa dakika chache. Aliwatazama wale watu pale chini na kushindwa kuwafahamu ni watu wa taifa gani lakini alipoweka umakini wa hilo swala akapata kuhisi jambo. Alimsogelea mmoja pale chini na kuivua nguo yake ya juu na kukuta kuna nguo ya pili amevaa. Alipoitazama aliifahamu kuwa ni sare ya askari wa Mfalme Joha jambo ambalo lilimshangaza.
"Inamaana wametuma watu ili watuue?"alijiuliza Samir bila kupata jibu kamili. Haraka akanyanyuka kugeuka kwa Maya na kujikuta wanatazamana. Alikitoa kile kitambaa na kuonekana kama mtu aliyeshikwa na butwaa. Hali ile ikamfanya Samir ashtuke na kuhisi huenda Maya ameona kila kitu na kumjua Samir yupoje. Walibaki wametazamana kila mtu akiwa kwenye hali ya mshangao.
ITAENDELEA
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN 32

"Ni wewe Samir..?!"lilikuwa ni swali ambalo lilimfanya Samir ashindwe kujibu kwa haraka. Mwili wote ulipoa baada ya kuona tayari Maya amemtambua kuwa anatumia nguvu za ajabu.
"Umeanza lini kuwa hivi?"aliuliza Maya akiwa anamshangaa Samir pale alipo, alijikaza na kuanza kupiga hatua hadi pale alipo Maya.
"Maya,haya yote nitakueleza pindi tutakapofika Gu Ram,tafadhari tuondoke."alisema Samir na kuanza kuongoza njia lakini alijikuta akishikwa mkono wake na Maya,aligeuka taratibu kumtazama.
"Nijibu swali langu Samir, umeanza lini kuwa hivi?"aliuliza tena Maya swali ambalo lilimfanya Samir atafakari namna ya kumwambia. Alimsogelea Maya na kumshika shavu huku wakitazamana, hakuona ja ya kumficha tena.
"Siku zote nimekuwa hivi tangu ulipolala kitandani kwa majuma kadhaa na kuwafanya watu wote wa Eden waamini kama hutaweza kuwa hai. Na siku ambayo unaamka mtu wa kwanza uliyepata kumuona ni mimi,na ndio nilifanya uweze kupona pindi nilipojua kwamba uchawi uliotupiwa hakuna ambaye angeweza kuutoa. Na ni mimi ndiye niliyetoka siku ileile kwenda Mashariki na mbali kumzuia Malkia asiandike chochote kwenye mikataba ile ya kuiacha Eden mikononi mwa Dalfa, naomba ufahamu hayo machache kwasasa pindi tukifika nitakueleza tu ila usiniogope mimi sina ubaya kwako Maya,nakupenda naomba ufahamu hilo."aliongea Samir kwa ufupi na kumuacha Maya mdomo wazi haamini kama ni Samir ndiye aliyefanya yale yote. Alimtazama tu Samir na kumuona akigeuka na kumfuata yule farasi wa Maya aliyechomwa kisu mguuni alikuwa amejilaza pale chini akiugulia maumivu. Hata alipomfikia akapiga magoti na kushika ile sehemu iliyozama kisu kile na kuanza kuongea maneno fulani huku taratibu akikichomoa kisu kile. Maya alijikuta akipiga hatua taratibu akishuhudia anachokifanya Samir. Kisu kile kilitoka bila wasi na wala hakukuwa na maumivu kwa farasi yule. Alipolikamilisha hilo akashika kile kidonda na kuachia,hapakuonekana jeraha lolote kwenye mguu wa farasi yule ambaye muda huohuo akapata kunyanyuka na kutembea kama ilivyo awali. Maya alibaki kustaajabu baada ya kushuhudia tukio hilo na kuamini kweli Samir ananguvu za ajabu.
Hakutaka tena kuficha uwezo wake Samir kwa Maya maana tayari alishamuona akipambana na wale askari wa Joha. Alimuamuru Maya apande kwenye farasi wake waendelee na safari huku akimtoa wasiwasi.
Njia nzima Maya alikuwa kimya huku akimtazama Samir, hakumdhania kama yeye ndio amekuwa msaada kwake na hata kwa Eden nzima kwa kumzuia Malkia Rayat kutoweka saini yake kwenye mikataba ile.

Huku upande wa pili Jamal pamoja na askari wenzake waliwasili Eden na kuripoti kwa mfalme kumueleza kuikamilisha kazi ile kama alivyotaka Mfalme. Aliwaruhusu waendelee na ulinzi baada ya kupokea taarifa hizo. Moyo ulimuuma kama mzazi maana anafahamu jinsi msitu ule ulivyo hatari kwa watu wapitao njia ile. Kuna wanyama wakali wa kila aina hivyo si rahisi Maya na Samir kuweza kuwa hai. Hakuwa na jinsi maana sheria ndio imemhukumu mwanaye kwa kosa la kuwa na mahusiano na mfanyakazi. Malkia rayat alikuwa anawataza tu askari wale wakiondoka kwa mfalme baada ya kuleta ripoti ya kuikamilisha kazi ile. Alihuzunika san na kuona ndio mwisho wa kumuona binti yake Maya.
Muda huo Dalfa ndio alikuwa akiwasili Eden,moja kwa moja alisogea katika falme na kupata kuona ulinzi wa askari ukifanya kazi yake. Alitazama pembeni na kuweza kumuona msichana wa kazi akitoka kwenye Falme akiwa ameshika kitenga akielekea sokoni. Akaona njia sahihi na ya kuweza kumfanya akaingia mchana ule bila kujulikana ni kumtumia msichana huyo. Taratibu akaanza kumfuata kule alipokuwa anaelekea.
Huku upande wa pili kwa Rahim hadi muda ule hawakuweza kupata taarifa zozote kwa wale watu aliowatuma kwenda kummaliza Samir na kumchuku a Maya. Alianza kuwa na wasiwasi juu ya hilo hivyo akaamua swala hilo kulifuatilia mwenyewe. Aliandaa askari ishirini na kuanza safari za kuelekea kule msituni kunaposadikika ndipo Maya na Samir walipoachwa huko. Yote hayo alikuwa anayafanya Rahim huku baba yake alikuwa akimuangalia tu na kuona kweli mwanaye amedhamiria kumpata Maya mtoto wa Mfalme Siddik.
Kule kwa Dalfa aliweza kumpata msichana yule baada ya kurejea sokoni na kumchukua kumficha sehemu kisha akajibadili na kuwa kama alivyo msichana yule,alikamata kile kitenga kilichosheheni matunda na mbogamboga akaanza safari ya kuingia kwenye falme. Hakuna aliyemuhisi kuwa yutofauti,alipita kwenye geti kuu kama kawaida akiwa anatazama kwa umakini baadhi ya sehemu kama ataweza kumuona Samir. Alienda hadi ndani na kuanza kupita kila sehemu kumtafuta mtu wake huku akiwa makini kutojulikana anachokitafuta. Alienda moja kwa moja hadi kwenye chumba kile cha Samir. Alipokaribia na chumba hicho alipata kumuona Jamal akiwa anatoka kwenye chumba hicho na kukifunga kwa kufuli kisha akaondoka zake. Hali ile ikamfanya ashangae kuona mtu tofauti ndio anafunga mlango ule kuonesha hakuna mtu ndani.
Hakutaka kuamini hilo taratibu alisogea pale huku akitayama huku na kule kisha akaishika kufuli ile huku akiitazama kwa macho makali ikapata kufunguka.
Huku kwa Jamal alipofika mahala alisimama baada ya kufahamu ameacha upanga wake mule ndani haraka akageuza kurudi kule chumbani.
Dalfa akiwa kwenye umbo na sura ya yule msichana alipoingia hakuweza kumuona yeyote mule ndani,alisogea hadi pale kitandani ambazo siku ile alipokuja usiku ndipo aliposimama akimtoa nguvu zile Samir. Aliushika mto uliopo pale kitandani na kuushika huku akivua hisia kutumia nguvu alizonazo kutambua kuwa mto huo ulilaliwa na mtu tofauti na Samir.
Alichanganyikiwa hapo asijue inakuwaje jambo hilo.
Haraka akatoka mule ndani baada ya kumkosa Samir kwenye chumba chake. Akawa anatembea akiwa anatazama huku na kule kama ataweza kumpata mtu wake. Alishangaa akishikwa mkono kwa nyuma jambo lililomfanya ageuke haraka na kukutana na sura ya askari mmoja akiwa kwenye tabasamu. Yule askari alimvua yule msichana kwenye korido huku akitazama huku na kule kuangalia kama kuna watu.
"ah nimekuwa na hamu na wewe tangu jana uliponiahidi tukutane leo,nadhani ndio muda muafaka huu kama tulivoku baliana."alisema yule askari na kuanza kumtomasa msichana yule,huenda ni wapenzi wenye kujuana muda mrefu. Hali ile ikamfanya Dalfa apate ghadhabu ya kushikwashikwa vile akawa anajiondoa mikononi mwa askari yule aliyetegemea kupata ushirikiano kwa mpenzi wake. Alishangaa kuona mwenza wake hayupo tayari kwenye jambo hilo akawa anamtazama.
"Unanini kwani mbona sikuelewi?"aliuliza askar yule na kushuhudia akishikwa bega.
"usijali mpenzi wangu kwasasa nina kazi nitakutafuta baadae."alisema msichana yule na taratibu yule askari akaanza kwenda chini kama mtu aliye na usingizi na kulala kabisa pale. Aligeuka haraka na kuendelea na safari yake hadi alitoka nje na kwenda kujibadilisha mbele ya safari na kurudi kuwa Dalfa.
Alikasirika sana kwa kumkosa Samir ndani ya falme hali iliyomfanya atafute mahala kwanza atulie huku akiona baadhi ya wananchi wakipita kutoka mashambani.
"Nimeamini sheria zinafuatwa hapa Eden,yaani mfalme ameridhia kabisa binti yake akatelekezwe msituni bila kujali kama ni mwanaye!"alisikika mtu mmoja akiongea huku akiwa amebeba mzigo wa majani kwaajili ya mifugo yao.
"Hiyo ndio maana ya uongozi sio kubagua adhabu ya kuwapa watu fulani wengine unawaacha."
"Ila kwakuwa yupo na Samir huenda akawa na msaada kwa binti wa Mfalme."
"Ah wapi ule msitu una wanyama wakali sana huwezi kuwazuia wasikudhuru,ni wengi na wakali."
"Hebu acheni mada hizo tayari wawili hao kama kufa wameshakufa tangu muda walioondoka Eden,itakumbukwa tu kwamba binti wa mfalme alikuwa na mahusiano na mlinzi wake na wamepata adhabu ya kutelekezwa msituni. "aliongea mtu mmoja akiwa na wenzake watatu wakijadili mada hiyo. Maongezi yao yalims hangaza Dalfa akiw amekaa mahali akiwatazama wale watu wakitembea huku wakipashana habari hizo.
"ina maana hawa watu walikuwa na mahusiano? Ndio maana yule kijana amekuwa akimlinda muda wote ."aliongea Dalfa baada ya kuupata ukweli kuhusu Samir na Maya. Alipopata kufahamu kwamba wawili hao wametelekezwa msituni alijuwa fika swala hilo si hatari kwa Samir kama ananguvu kama yeye. Alijua kwa namna yeyote ile watu hao ni wazima na huenda wapo mahala kujihifadhi. Haraka alisogea kwenye farasi wake na kupanda kuelekea kule msituni kupata uhakika wa kile anachokiwaza.

Huku upande wa pili Samir na Maya waliweza kuwasili katika kijiji cha Gu Ram. Walipokelewa kama ilivyokawaida,wanakijiji wengi waliungana nao kuwasindikiza hadi kwa kiongozi wao Faraj. Alipata faraja kuwaona wageni hao kwa mara nyengine na kuweza kuwakaribisha kwa kuwapa baraka kama ilivyoada na zoezi hilo lilipokamilika watu wakarejea kwenye kazi zao na wageni hao wakapata kuingia ndani baada ya kukaribishwa na mwenyeji wao.
Maongezi ya hapa na pale yaliendelea na hata walipomueleza ukweli juu ya kile kilichojiri Eden kwamba wamefukuzwa hawatakiwi tena katika taifa la Mfalme Siddik.
"Huu ni mtihani mmeupata katika maisha, ila sidhani kama kuna kikubwa cha kuogopesha juu ya uamuzi na sheria iliyotolewa dhidi yenu. Hapa ni nyumbani kwenu karibuni na mtaishi hapa siku zote kama Eden wameweka marufuku kwenu kurejea. "aliongea Faraj akiwafariji.
"hivi ni kweli sitaweza kuonana na mama yangu tena?"aliuliza Maya akiwa anamtazama Faraj.
"Ni rahisi kumuona, ila ni vigumu sana kuonana naye. Kwasasa huesabiwi kama mtoto wa Mfalme kama ilivyo zamani,na wewe ndio mwenye kazi ya kurudisha jina lako pindi utakapohitaji kurejea Eden,ila sio kwasasa yakupasa ukae muda mrefu usionekane ili siku utakayorejea waamini hukuuawa kwenye msitu ule hatari."alisema Faraj na kumfanya Maya apate kuelewa,aligeuka kumtazama Samir aliyekuwa akisikiliza yanayozungumzwa pale. Faraj aligeuka kumtazama Samir pale alipokaa.
"Samir,usiku wa jana nimepata kuota ndoto kuhusu wewe na imekuwa kama bahati mmeweza kuja leo."alionge Faraj na kauli yake ile ikamshtua Samir.
"Ndoto? Ni ndoto gani hiyo?"
"nimeota unavalishwalishwa pete,ni pete yenye thamani kubwa sana katika mataifa,ni Pete ya Mfalme wa Eden. Mfalme wa kwanza kuitawala Eden hii ambayo kwasasa inatawaliwa na Siddik."alisema Faraj na kumfanya Samir ashangae,aligeuka kumtazama Maya aliyekuwa anamuangalia pia.
"Hiyo ndoto inamaana gani Faraj?"
"Huenda ukawa Mfalme hapo mbeleni."aliongea Faraj na kuwafanya Samir na Maya washangae kuambiwa vile.
ITAENDELEA
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN 33

"Inamaana Samir atakuja kuwa Mfalme? Kwenye Taifa gani sasa?"aliuliza maswali kwa mkupuo Maya huku akimtazama Faraj.
"Siwezi tambua ni Taifa gani labda laki kwa ntoto niliyoota ni kwamba anavalishwa pete ya Eden. Na pete hiyo hadi kuivaa ni kwamba umekubalika uitawale Eden."alisema Faraj na kuwaacha Samir na Maya wakiwa wenye kutafakari swala hilo. Alinyanyuka na kuwaacha pale yeye akaenda kwenye chumba chake cha kufanyia ibada.
Iliwachukua dakika tatu bila kusemeshana pale ndani na hatimaye Maya akafungua kinywa chake.
"Mimi namuamini Faraj,ndoto zake zimekuwa na ukweli katika maisha yangu na siwezi kupinga kwa hili pia"
"Lakini nitawezaje mimi kuwa Mfalme?"aliongea Samir akijua fika kuwa yeye ni mtanzania hivyo asingeweza kulitawala taifa hilo.
"Huwezi juwa ni sababu zipi zitakufanya ukawa Mfalme hapo mbeneni."aliongea Maya akimuelewesha Samir wakiwa wenyewe pale walipoachwa.
Huku Eden zilianza kusamb aa kila kona kuhusu kupatikana kwa mwili mfanyakazi wa kike wa mfalme ukiwa kwenye moja ya njia ya uchochoroni akiwa tayari amekufa. Watu walipatwa na hofu juu ya kifo hicho kisichojulikana mhusika wa tukio hilo ni nani. Taarifa hiyo ilimshtua yule askari ambaye ni mpenzi wake na muda mchache uliopita alikuwa pamoja naye lakini alijikuta haelewi kilichotokea mara baada ya mpenzi wake kumshika begani akapoteza fahamu.
Mfalme Siddik pamoja na Malkia walipatwa na mshangao baada ya kufikishiwa taarifa hiyo,ilibidi waongozane hadi kwenda mahala mwili wa marehemu ulipohifadhiwa.
Walifika na baadhi ya waganga wa jadi na Generali kushuhudi. Waliuchunguza mwili huo lakini hawakuweza kuona jeraha lolote mwilini,ilibidi wazee watumie ujuzi wao kutazama zaidi huku Mfalme akitazama tu na mwisho wa siku wakapata kujua ukweli.
"Kuna mtu amenyonga kwa kutumia mkono na hakuna silaha yeyote iliyotumika. Mtu huyo ana nguv u sana maana hakuukaza mkono wake shingoni alijua kwakufanya hivyo kungebaki alama ya vidole vyake."alisema mzee mmoja baada ya kuchunguza maiti ile kwa makini.
Ilibidi Mfalme atoe amri kwa Generali kuwapa kazi askari ya kufanya upelelezi ili abainike mtu huyo aliyefanya mauaji hayo.
Moja kwa moja Generali alitoka hapo na kuelekea kwa Jamal. Inasadikika tangu alipodondoka na kupoteza fahamu hakuweza kuinuka, alifika na kumkuta akiwa amelazwa kitandani huku askari wawili wakiwa pembeni kumuangalia.
"Mmehakikisha hakuna anayefahamu swala hili?aliuliza Generali.
"Ndio hakuna anayefahamu kinachoendelea."alijibu askari mmoja akiwa anamtazama Generali wake..
"Sawa hakikisheni hata Mfalme hafahamu kama huyu amepoteza fahamu. Ah sijui nini kimemkuta Jamal hadi kuwa hivi!"aliongea Generali huku akimtazama Jamal pale kitanda akiwa amelala.

Kule msituni Rahim aliweza kufika na askari wake hadi kwenye ile njia ya ku ingia ndani ya msitu. Wali2aaki kuutazama msitu ule huku milio ya ndege na wanyama mbalimbali ikisikika. Aliwaamuru askari watano waongoze njia ya kuingia msituni. Nao wakatii amri hiyo ya mtoto wa Mfalme wakaingia huku wakina Rahim wakisikilizia kinachoendele. Haikupita hata dakika mbili walishtuka kusikia kelele za askari walioingia mule wakijaribu kuomba msaada na punde tu kukawa kimya huku sauti ya kuunguruma ya wanyama wakali zikisikika kana kwamba wanagombana. Ilibidi wakina Rahim wasogee pale mahala pa kuingilia na kuona mule ndani ya msitu chui weusi zaidi ya kumi wakiwagombania askari waliokuwa tayari washapoteza maisha pale chini. Walitafunwa kama wanyama wa porini hali iliyowafanya askari wote waliobaki nje waogope, Rahim mwenyewe alishangaa kuona vile na kupata ushahidi huenda hivyo ndivyo ilikuwa pia kwa Samir pamoja na Maya. Alirudi nyuma akiwa hoi amechoka kwa lile alichokiona ni ushahid i tosha juu ya watu aliohitaji kuwapata. Alijikuta akipiga kelele za hasira maana amemkosa Maya akiwa na malengo naye binafsi. Askari waliinamisha vichwa chini wakimsikia Rahim akiwa analalama kwa kutofanikiwa,alisogea kwenye farari wake na kupanda kuondoka zake huku askari wale nao wakifuata baada ya kujua walichokifuata wamekosa. Muda wote huo Dalfa alikuwa mahala anawatazama hadi walipokomea,alijua nawao wamewafuata wakina Samir kwa namna yao. Alisogea hadi pale kwenye njia ile na kusikia chui wale wakiunguruma. Alishuka kwenye farasi wake na kuanza kuingia mule ndani bila kuhofia lolote.
Wale chui wakiwa wanamalizia kutafuna miili ya askari wale wakapata kumuona Dalfa akiwa anajuja bila kuonesha woga,walikaa tayari kwaajili ya kumrukia binadamu huyo lakini kadri anavyozidi kusogea ndipo anapobadilika na kuwa kama wao na zaidi ya hapo alikuwa akiwaka macho yake na kuonekana yenye kun'gaa. Hali hiyo ili wafanya chui wale watambue yule ni zaidi yao,walirudi nyuma taratibu na kuanza kukimbia kila mtu njia yake. Dalfa kwa mnyama huyo mkali alitembea taratibu huku akitazama huku na kule kuona wanyama wakali ndani ya msitu huo. Aliangalia chini ya ardhi akinusa harufu ya kwato za farasi akijua huenda wakina Samir walipita hapa. Na kweli alipata kusikia harufu hiyo akazidi kwenda mbele zaidi. Alifika mahali akapata kuona ndio mwisho wa kwato zile za farasi. Alinusa harufu ile bila kutambu muelekeo walipoenda watu wake anaowataka. Akapata kufahamu huenda walifika hapo na kugeuza kurudi walipotoka. Naye aligeuza na kurejea kule nje baada ya kujiridhisha hayo.

Huku upande wa pili Jamal alianza kurejesha fahamu baada ya kufumbua macho yake. Alitazama mahala alipo na kujikuta amelala pale kitandani,alinyanyuka taratibu na kuhisi maumivu mgongoni. Aliangalia kila kona kwenye chumba kile akiwa pekeake na ndipo kumbu kumbu zikamjia mara ya mwisho alipata kumuona msichana wa kazi akiwa mule ndani,na ni yeye ndiye aliyemtupa Rahim kwa nguvu za ajabu kumrusha akadondoka chini na hakujua kilichoendelea.
"Yule msichana anatumia nguvu za kichawi?"alishangaa Rahim pale alipo na kuhisi huenda ikawa kweli. Hakutaka kuchelewa akashuka pale kitandani na kuvaa nguo zake za uaskari na kukamata upanga wake akatoka nje,lengo ni kwenda kumpasha habari Mfalme kuhusu msichana yule akijua huenda kuna jambo baya amedhamiria kulifanya likaleta matatizo kwenye falme. Hakufika mbali akakutana na Generali akiwa anaelekea kumuona Jamal kule chumbani.
"Jamal umeamka!"aliongea Generali huku wakisogeleana.
"Generali, naelekea kwa Mfalme nikamweleze jambo lililotokea,kuna watu wanatumia uchawi humu kwenye falme na huenda si wema."aliongea Jamal na kumfanya Generali amkamate mkono wakasogea mahala waongee.
"Unamaana gani kusema hivyo Jamal mbona sikuelewi?"
"Kuna mfanyakazi wa kike anatumia nguvu za kichawi,nimemuona akiwa ndani ya chumba kile akiwa anatafuta kitu,na mlango niliufunga kwa kufuli funguo hii hapa ninayo,ameingiaje mule ndani? Na ndio maana nilipomshtua kumuuliza hakuwa na lakujibu nikajikuta narushwa sijui na upepo sijui kimbunga hata sijafahamu na sikujua kiliendelea kitu gani."aliyasema hayo Jamal na kumfanya Generali aelewe sababu za Jamal kukutwa akiwa amezimia.
"Huyo msichana unamfahamu ukimuona?"aliuliza Generali na kuweza kuitikiwa.
"Sasa sikia hili swala tutalifanya bila Mfalme kujua lolote kwanza tupate uhakika na jambo hili, tusikurupuke kumpa taarifa zisiso na uhakika akaja kukubadilikia ukapata adhabu na unaelewa ameshampoteza binti yake hivyo hana huruma kwasasa."alisema Generali na maneno yale Jamal akayaelewa.
"Nahitaji nikuweke kwenye nafasi nzuri hapa Eden,huenda ukaja kuwa nafasi yangu na hata ukafika mbali na ha pa ulipo,niliongea na baba yako akanieleza kuhusu wewe kutaka kuwa askari mashuhuri hapa Eden na naamini utafika unapotaka."alisema Generali na Jamal akafahamu kumbe baba yake tarari alisharahisisha kazi mapema. Alimshkuru kwa kuwa naye karibu na kumpa kipaumbele sana katika mambo mengi. Baada ya kuongea hayo walitoka na kuelekea kumtafuta msichana huyo anayedhania kuwa na nguvu za kichawi.

Upande wa pili Rahim akiwa njiani na askari wake akitafakasi mambo mengi jinsi alivyopanga endapo angempata Maya na kuwa mkewe basi angekuwa na heshma kubwa ndani ya Eden na ndio njia ya urahisi kwake kuja kuimiliki Een kama mfalme. Akiwa kwe fikra hizo alikumbuka wale askari wao waliotumwa kwenye kile kijiji cha Gu Ram na muda huohuo akasimama kuwauliza askari wake kama wanafahamu kijiji ambacho wenzao walitumwa kwenda. Baadhi yao walipafahamu na ikawa ni heri kwa Rahim aliyeamuru waelekee huko. Alikuwa mwenye hasir a za kumkosa Maya hivyo alijiandaa kwa lolote huko wanapoelekea.
Kwa Dalfa alipotoka kwenye msitu ule alirudi kwenye umbo lake la awali huku akionekana kuangaza macho yake kila kona bila mafanikio. Hakupata kutambua wapi walipoelekea wakina Samir maana kitendo cha kutoka nje ya msitu ule hakuna alama yeyote inayoonesha muelekeo wa farasi wakiopandwa na wakina Maya. Alikasirika sana kuona mtu anayemsumbua kiasi hicho ni Samir na aliapa safari hii akimpata lazima ammalize kabisa.
Alichoamua ni kurudi tu Mashariki na kati kutuliza akili kwanza ili ajipange namna ya kumpata Samir maana ndiye mtu pekee anayemnyima usingizi kwakufahamu kwamba anatumia nguvu kama alizonazo yeye.

Baada ya muda kupita Maya pamoja na Samir walitoka na kwenda kutembea sehemu mbalimbali ndani ya kijiji hicho huku maongezi ya hapa na pale yakiendea. Na huo muda muafaka wa Samir kumueleza ukweli Maya kuwa yeye ni nani na ametokea wapi.
ITAENDELEA
 
SIMULIZI😛ETE YA MFALME WA EDEN 34

Safari yao ilikomeshea kwenye jabali moja kubwa wakapanda na kukaa wakawa wanaongea mambo mengi zaidi.
Alitumia muda mwingi kumuelewesha Maya ambaye alibaki kustaajabu tu baada ya kuelezwa kuwa Samir anayemjua yeye si huyu ambaye anamuona kwasasa. Jambo ambalo awali hakuwa mwenye kuamini kwa haraka maana hakukuwa na utofauti baina ya watu hao wawili.
"Jina langu kamili ni Jafari na sio Samir,nilipatwa kuambiwa mwenye jina hili ameshauawa na watu ambao walimpa kazi ya kummaliza Maya. Na baada ya tukio la kupata matatizo bimti huyo wa Mfalme Samir akatumia njia hiyo kuwadanganya kwamba tayari amelifanikisha zoezi hilo,swala likabaki kwenye kulipana na hapo ndipo walipomgeuka na kummaliza wakijua wamesaidiwa kuuawa kwa Maya.
Maelezo hayo yalimshtua Maya na kuona jinsi alivyokuwa akiandamwa na wabaya bila sababu yeyote.
"Hiyo ndio tofauti kubwa kati ya mimi na yeye, nipo kwaajili ya kukulinda na si kukuuza kwa watu wabaya."aliongea Samir akiwa anatazamana na Maya. Alimtoa hofu kwa yale yote mabaya anayofikiria binti huyo wa Mfalme,na kubwa hasa alilofanya Samir ili kumpa furaha Maya ni pale alitaka washikane mikono,Maya hakusita alifanya kama alivyoagizwa na kushuhudia Samir akiitazama pete yake iliyo kidoleni mwake na gafla wakapotea pale walipokaa.
Walikuja kuibuka wapo chumbani tena kwenye viti karibu na meza ndogo iliyosheheni vitabu na madaftari. Samir aliachia tabasamu tu huku akimtazama Maya aliyekuwa akiangaza macho yake huku na kule asijue yupo wapi.
"Ni wapi hapa mbona sipafahamu?"aliuliza Maya akizidi kushangaa,zilisikika kelele za watoto nje wakicheza hali iliyozidi kumshangaza.
"Hapa ndio chumbani kwangu,tupo Tanga sasa nchini Tanzania."aliongea Jafari na kumfanya Maya astaajabu kusikia hivyo. Alinyanyuka haraka na kwenda kufunua pazia la dirishani, mazingira na nyumba za watu jinsi zilivyo zilimshangaza sana na kuona kweli ni tofauti na Eden. Akataka kupiga hatua ili atoke nje kuangalia zaidi mazingira lakini Samir akamzuia.
"Wewe nje hapana, kaka yangu atakuona wakati hafahamu kama wewe upo humu usije kuniletea matatizo hapa."alisema Jafari na kushika kitasa cha mlango.
"Kwani atakugombeza kwa lipi? Naomba niruhusu nitoke nione mazingira yalivyo,nakuomba Samir!"alisema Maya akitaka kutoka nje. Ilimbidi Samir aufungue mlango na kuchungulia kwanza nje ahakikishe kama kuna watu pale nje. Bahati nzuri hapakuwa na yeyote eneo lile akarudisha kichwa chake ndani na kumruhusu Maya atoke nje na haraka Maya akafanya hivyo. Aliona mandhari tofauti na aliyozoea huku akiona kwa mbele watoto wakicheza mchezo wa goroli na wengine wakiruka kamba, alijikuta akitabasamu kwa kuona watoto wale wakiwa wenye furaha na taratibu akaanza kujisogeza.
"Jamani mnaondoka kimyakimya?"ilisikika sauti iliyomfanya Maya asimame na kugeuka nyuma sauti ilipotokea. Jafari alishtuka kumuona shemeji yake anatoka ndani huku akiwa amebeba sahani iliyokuwa na machungwa. Kwa kauli yake ile ilimfanya Samir atambue huenda alifahamu kama Jafari alikuwa na msichana yule mule chumbani. Maya alibaki kushangaa tu na kumgeukia Jafari aliyempa ishara kwamba achangamke.
"Ah samahani nilijua umelala ndio maana nikaona nisikusumbue."aliongea Maya akijenga tabasamu.
"Wala sikuwa nimelala,mimi nilikuwa nawamenyea machungwa wageni,hebu rudi walau utie baraka kidogo."alisema Shemeji mtu na kumtaka Maya arudi kuchukua chungwa,naye akafanya hivyo na kupokea chungwa hilo huku akitoa shukrani. Ilibidi Jafari naye akisogea pale kuchukua kipande,baada ya dakika kadhaa kujiridhisha kwamba swala hilo shemeji yake anafahamu akawa anajiamini. Alimkamata mkono Maya na kumuaga shemeji yake kuwa anamsindikiza. Maya aliaga na kugeuka kuongozana na Samir.
Alianza kumzungusha kwenye mitaa huku Maya akionekana kushangaa tu.
"Halafu mbona najiona mwepesi sana Samir?" aliuliza Maya wakiwa wanatembea pamoja. Samir alitabasamu huku akitazama mbele.
"Labda nyele zako zilikuwa zinakupa uzito."alisema Samir na kumfanya Maya ashike kichwa chake. Alishtuka kuona nywele zake zipo tofauti, ni fupi na zimesukwa kabisa.
"Mungu wangu! Samir nini tena hiki mbona sielewi?"alistaajabu Maya baada ya kuona yupo tofauti.
"Kuna msichana anaitwa Aziza yupo kama wewe ulivyo kasoro yenu ni hizo nywele tu, hivyo ungeonekana wa ajabu kila mtu angeshangaa kuona nywele ndefu zenye kufika mgongoni."
"Inamaana hata mimi kuna mtu nafanana naye?"
"Ndio, anaitwa Aziza. Nasoma naye shule moja."aliongea Jafari na kumfanya Maya ajue kumbe hata yeye pia kuna aliyefanana naye huku Tanzania.
Wakiwa kwenye maongezi hayo akatokea Eliza akiwa anapita njia ile,alitabasamu tu baada ya kumuona Jafari akiwa na mrembo yule. Aliwasalimia kisha akaendelea na safari yake. Jafari alitabasamu na kujua Eliza aepata neno la kuongea endapo wakikutana.

Huku upande wa pili Rahim aliweza kuwasili na askari wake katika kijiji cha Gu Ram. Walikuwa wamesimama sehemu wakikitazama kijiji kile huku Sahim akionekana kuwa na hasira sana. Alitoa amri kwa askari wake wavamie kiji kile na kupiga watu ili iwe fundisho na kisasi kwa kile walichofanyiwa askari wake. Muda huohuo akawasili yule mtu wanayemtumia katika mambo yao na kuwaeleza ukweli halisi.
"Wamerudi tena Maya na yule Samir."aliongea yule mtu na kumfanya Rahim ashangae.
"Unachoongea una uhakika?"aliuliza Rahim akiwa haamini.
"Siwezi kumdanganya mtoto wa Mfalme Faruk,hawa watu wamekuja leo na nimepata kusikia kwamba wamefukuzwa Eden na sasa watakuwa wakiishi hapa."
"Hawa watu kumbe bado wazima....Safi sana!"alifurahi Sahim na kuwageukia askari wake.
"Namuhitaji Maya akiwa mzima huyo mwengine auawe."alitoa amri hiyo Rahim na askari wake wakaipokea,bila kuchelewa wakaanza kusoga mbele kuikamilisha kazi hiyo.
Huku kwa Jafari akiwa anazidi kumzungusha Maya kwenye mita aliona pete yake ikimbana kidoleni na kufahamu huenda kuna jambo. Maya alitazama kumuona Jafari akinyanyua mkono wake kuitazama pete ile,alimuona amebadilika gafla akionesha kukasirika.
"Vipi mbona umebadilika hafla hivyo?"
"Gu Ram kuna matatizo, Rahim na askari wake wameingia kwa shari."alisema Jafari na kumfanya Maya ashangae
"Jamani sasa kwanini wanafanya hivyo! Kwahiyo tunafanyaje.?"aliuliza Maya akionekana mwenye huruma.
Jafari alisogea na kumshika mkono Maya alifahamu wanarudi walipotoka. Na kweli sekunde kadhaa walitoweka pale walipo wakaja kuibuka kule walipokuwa juu ya jabali moja. Haraka bila kuchelewa wakaanza kutoka mbio kurudi kijijini ambapo ndipo sehemu inayotarajiwa kuvamiwa.
Faraj akiwa zake kwenye chumba chake cha maombi alipata kuhisi ishara ya jambo la hatari kuweza kutokea. Haraka akatoka mule chumbani hadi nje na kusimama mlangoni,aliona kuna kila dalili mbaya kutokea. Haraka aliingia ndani na punde tu akatoka akiwa ameshika pembe ndefu iliyojikunja na kuanza kuipuliza kama tarumbeta. Mlio uliotoka pale ulikuwa mkubwa sana uliowafanya wananchi wote wapate kusikia na kujua maana ya mlio huo. Haraka wakaanza kukimbia kila mmoja wao akaingia ndani kwake kufunga milango na kutulia kimya. Muda mfupi kupita waliwasili jeshi hilo la Rahim wakiwa juu ya farasi wao huku wakitazama kila kona bila kuona yeyote.
Walizunguka kila njia kutafuta kama wataweza kumpata hata mtu mmoja lakini haikuwa rahisi.
"Inamaana walijua kama tunakuja! mbona hakuna hata mtu nje?"aliuliza Rahim akiwa mwenye kushangaa.
"Huenda ikawa hivyo,hapa kilichobaki ni kuvunja milango yao na kuwatoa wapate adabu."aliongea askari mmoja aliyekuwa karibu na Rahim ambaye naye alikuwa na wazo hilohilo, bila kuchelewa akawaamuru askari wote wavamie kwenye nyumba za watu, lakini gafla tu wakapata kumuona mtoto mmoja akisogea pale walipo. Mavazi yake ya heshima huku akiwa ameshika bakora kama mzee yaliwashangaza wakina Rahim aliyewasimamisha kwanza watu wake. Alikua ni Faraj aliyesogea pale walipo wakina Rahim.
"Karibuni Gu Ram taifa dogo lenye amani ndani yake."alisema Faraj huku akiachia tabasamu.
"Mtoto,kaa pembeni hatukuja kuongea na rika lenu hivyo kaa mbali kabda sijakubadilikia."alisema Rahim huku akimtazama Faraj,hakumtambua kuwa ni nani kwenye kijiji kile hali iliyomfanya Faraj atabasamu tu huku akitazama askari wote waliokusanyika pale.
Ilibidi Rahim awape ruhusa askari wake waendelee na zoezi lile lakini Faraji aliwazuia kwa kunyoosha mikono yake.
"Nawaomba sana muwaache watu na furaha yao,nimewakaribisha kwa hekima na heshima, siwafahamu nami hamnifahamu ila nimesimama hapa kushikilia amani. Mimi ndiye kiongozi wa taifa hili hivyo lengo la kufika kwenu hapa ni lazima mimi nifahamu maana ninyi ni wageni wangu."alisema Faraj na maneno yalimshangaza hata Rahim kuona mtoto mdogo kama huyo anaongea maneno ya kikubwa na yenye tija ndani yake.
"Yaani mtoto wewe ndio wakupe uongozi!,unaongelea kuhusu kuwaongoza watu au kuwaongoza watoto wenzako?"aliongea Rahim akimdharau Faraj.
"Watoto pia ni watu ujue,ila kwamimi nawaongoza watoto pamoja na hao watu."alisema Faraj na majibu yake yalimchosha Rahim akawaruhusu askari wake wafanye kilichowaleta.
"Nimesema hakuna mtu kupiata hapa,kama hamuwezi kueleza shida yenu geuzeni mrudi mlipotoka,siwezi kuruhusu watu waingie katika ardhi yangu bila kuwafahamu."Faraj alishikilia msimamo wake na safari hii alikuwa mkali sana. Rahim kuona vile akaona ni dharau kwa mtoto mdogo kuwazuia wakati wapo kazini, alitoa amri ya lazima askari wafanye kile alichowaagiza. Safari hawakutaka kumsikiliza yule mtoto wakatoa mapanga yao na kuruhusu farasi waliwapanda kwenda mbele wammalize kwanza mtoto huyo ili wakavunje nyumba za watu.
ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom