Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Shanga zimekuwa shanga mjini
Enheee muendelezoSimulizi ya kweli.......SHANGA YA BIBI ILIVYONIPA UMAARUFU!!!!
Msimuliaji............. KIDAWA
Umri........18+
Sehemu ya 22
Tulipoishia....Jini Jabir,aliyekuwa kikwazo kwenye mahusiano ya Kidawa amerudi na kumkanya Kidawa juu ya tabia yake ya kubadilisha wanaume leo huyu kesho yule!!!
Songa nayo......
Zilipita siku baada ya Jabir kunitokea niliogopa sana,nikihofia atarudi kunipa ile nuksi iliyonifanya nidharaulike!
Ila kama ujuavyo binadamu tunasahau ndivyo ilivyotokea,nilisahau kila kitu nikaanza upya tabia yangu ikazidi,sikujua ni pepo au nini Ila nilijiskia tu kubadilisha wanaume.
Umaarufu wa Kidawa ukazidi kushamiri si chuoni tu huko hata mitaani!Mitandaoni picha zangu zilikuwa gumzo wafuasi waliongezeka kila kukicha!
Meseji zilikuwa nyingi sana,wanaume wakinitongoza ,na kilicho wachanganya ni shanga zangu nilipopiga picha niliacha kiuno wazi zionekane!
Umbo langu nalo lilikuwa habari nyingine!
Nakumbuka nilipiga picha ambayo ilinipa umaarufu hadi kufuatwa na waandishi wa habari wa mitandaoni kunifanyia mahojiano!Alikuja mwandishi wa habari kunioji
"Kwanini unavaa shanga!"
"Napenda ni kama pambo kwangu na ukiacha matumizi mengine yale ni pambo zuri ningependa kumshauri kila mwanamke wa kiafrika avae!"
"Unavaa kwa sababu baby anapenda au unapenda?"
"Hapana napenda sana kuvaa sijafuata ushauri wa mtu!"
"Unahisi kwanini jina lako linashamiri mitandaoni kwa sasa!!"
"Nahisi ni shanga sababu wanawake wengi wanavaa shanga lakini wanazificha zisionekane lakini tofauti na wao niko huru na shanga zangu nazipenda wananishangaa!"
"Unawashauri nini wanawake wa kitanzania!"
"Waache kuendekeza tamaduni za watu,sawa tunavaa nguo zao na viatu vyao Ila shanga tuvae zetu tuvipende vya nyumbani!"
"Ni msanii gani wa kiume ambaye unampenda sana kiasi kwamba unatamani hata uone siku moja ameku DM?".
"Hahahahahaaaaa!swali gumu sana!"
"Watanzania wangependa kufahamu!".
"Mmhh!namkubali Jack Mambo namkubali sana akija kwetu kuniowa hata mahali ntawaomba wazazi wanisamehe!!"
Hiyo ni siku niliyotembelewa na mwandishi wa habari mmoja wa mtandao mmoja maarufu!!
Sikuamini kama kuzionyesha tu shanga zangu ingekuwa inshu kubwa namna ile!
Nilivyogundua shanga ni inshu nikaanza kupiga picha nyingi nikijiachia na shanga zangu ....
Nikabadili na jina la akaunti nikajiita SHANGA ZA KIDAWA!
Nilianza kupata meseji nyingi kutoka kwa watu wakubwa sana ambao walikuwa wananipa pongezi kwa kudumisha na kupenda asili yangu!
Nyuma ya pazia ilikuwepo siri yangu niliyonayo kuhusu shanga hizi nilizopewa na Bi Mwana.Nazipenda kwa sababu zimenifutia kashfa nilizopata kuko nyuma!
Ila sasa kitu ambacho sikutegemea kumbe hizi shanga hata kuonekana kwake ni dili kwangu!
Nilianza mwaka wa pili chuoni tayari nikiwa maarufu sana Tanzania,iyo ilikuwa ni hatua kubwa kwangu hata zile tabia zangu za kubadili wanaume zilipungua kwa kiasi kikubwa!
Mapaparazi walinifuata kila kona ivyo nisingeweza kujiachia kama zamani.
Mwaka wa mafanikio ni wa mafanikio tu,nilihama hostel nikaenda zangu kupanga nikawa naishi na rafiki yangu Jenny!!
Siku moja nikiwa nimelala alikuja rafiki yangu Jenny anaruka kwa furaha!
"We vipi nimelala bhana!"
"Amka best amkaaaa uone Waziri kakupost!"
"Unasema?acha masikhara ujue!"
"Waziri kakupost ivyo njoo uone!"
Nilikurupuka nikamkwapua simu Jenny nikaangalia sikuamini nilihisi mwili unatetemeka nilishindwa kuvumilia machozi yalinitoka!!
Waziri alikuwa amepost picha yangu huku akiwa ameambatanisha maneno yafuatayo!!!
"Angeweza kutumia cheni mikufu au mapambo ya kigeni kama angetaka lakini kaamua kuchagua asili yake,utamaduni wake na kukubali vitu asili vya asili tena kutoka Tanzania kuwa pambo lake la asili.
Amehamasisha wengi sasa naona picha zao wakiwa wamejipamba na pambo za asili.SISI KAMA WIZARA TUMEONA TUFANYE KITU KWA AJILI YAKE,NA MIMI KAMA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII NACHUKUA FURSA HII KUMTANGAZA kidawa KUWA BALOZI WETU WA KUTANGAZA UTALII WA NDANI!
Ningependa aje ofisini tayari tumemtumia namba Dm afike kwa ajili ya Mambo mengine yanayofuata!
Japo kulikuwa na AC ila kijasho kilinitoka nikasimama nikamkumbatia Jenny huku nalia.
"Pole rafiki yangu umepambana sana Hadi kufikia hapo ulipo sasa,kila mtu alikudharau sasa kila mtu atakuheshimu!"
Aliongea Jenny naye machozi yalimtoka siku hii nilipokea simu kutoka kwa mama!
"Hongera mwanangu!"
"Ahsante mama",nilijibu huku nalia.
"Usilie mwanangu,niko na baba yako tunafikiria namna tunavyoweza kusapoti hiki ulichoanzisha!"
"Nashukuru mama!"
Niliongea na mama kisha nikaiweka simu pembeni,sikutaka kuingia Instagram ili niangalie alichonitumia waziri.
Nilipumzika kwanza nikavuta pumzi ndefu nikafakari maisha yangu yaliyopita kuanzia kwa John misukosuko aliyopitia na James alivyonitesa chuoni nilitabasamu tu nikiamini huzuni yako ni tabasamu la kesho!
Niliinuka nikaenda kuoga bafu la ndani kwa ndani,niliziangalia shanga zangu zilizotulia kiunoni kwangu nikatabasam, nikatoka nikamkuta Jenny anabishana na watu mlangoni,
"Jenny vipi?"
"Waandishi Kidawa!"
"Wanataka nini?"
"Wanataka interview!"
"Waambie siyo leo!"
Niliwakatalia waandishi sikutaka kuongea nao chochote mpaka nitoke kwa Waziri niskie kwanza ntaambiwa nini?
Niliingia Instagram nikakuta Waziri kanitumia namba nikazichukua nikapiga ikaita mara moja tu ikapokelewa!
"Haloo Mheshimiwa"
"Samahani nani mwenzangu!"
"Mimi naitwa Kidawa yule wa.....!"
"Subiri!"
Alinikatisha akakata simu kisha baada ya dakika tano ile namba ilinipigia nikapokea haraka huku mikono inatetemeka!
"Haloo unaongea na Waziri!"
"Haloo shikamoo mheshimiwa Mimi ni Kidawa!"
"Okay!marahaba mwanangu nimependa Sana kazi yako!"
"Ahsante sana Mheshimiwa!"
"Heeh!Sasa nadhani ungefika kwenye ofisi zetu ziko Dar ntamtuma dereva aje akuchukue ntampa namba zake muwasiliane!"
"Sawa nashukuru sana!"
"Sawa kazi njema!"
"Nashukuru sana!"
Moyoni nilijawa na furaha,uso wangu ulijawa na tabasamu pana!
Nilipokea simu nyingi sana kutoka kwa watu mbali mbali hadi meseji za wabunifu mbalimbali wakitaka wafanye kazi na mimi!
Niliwasiliana na dereva aliyetumwa kunichukua akafika muda huo nilishajiandaa nimevaa gauni langu nililoshona kwa shuka la kimasai lililonikaa vizuri mwilini kiasi cha kunifanya nionekana msichana halisi wa kitanzania.
Hatimaye Safari ikaanza kuelekea kwenye ofisi ya waziri!!!
KIDAWA HUYO ANAZIDI KUWA JUU KILA LEO!UNAMTABIRIA NINI KIDAWA??UNAHISI KWELI ATATUSUA KWA SHANGA TU!!!
Ya kibongobongo11 kamili kidawa anashuka leo wakuu msijaliView attachment 1438489
Sent using Jamii Forums mobile app
11 kamili kidawa anashuka leo wakuu msijaliView attachment 1438489
Sent using Jamii Forums mobile app