Simulizi ya kweli..... SHANGA YA BIBI ILIVYONIPA UMAARUFU!!
Msimuliaji................ KIDAWA
Sehemu ya 27
Tulipoishia......Sabrat ameingiwa na tamaa,anataka kubaki duniani,je Jabir atamruhusu?
Songa nayo.....
"Sabrat siwezi kumuacha uishi duniani!"
"Unamaanisha nini jabir?"
"Nikikuacha huku utafanya fujo,istoshe stakuwa nikikuletea kafara kila alhamis sababu wa kunifanya nifanye ivyo hayupo!"
"Kwa hiyo Jabir umekata tamaa?unamaanisha nini kusema hayupo Kidawa ni mkeo wa ndoa!"
"Hujui tu wameenda kwa mtu wa aina gani kunizuia nisiwe Karibu nae!Nikimsogelea hata kidogo ntaungua kama karatasi!"
"Sawa wewe umekata tamaa,mimi je?"
"Unamaanisha nini sabrat?"
"Namaanisha kuna mtu nampenda!"
"Nani?Suma?!"
"Ndiyo,nampenda siwezi kumuacha!"
"Umechelewa Sabrat,Suma hutomgusa tena kwani mkandarasi wa yote haya ni mke wa Suma!Na ni wewe umesababisha bila kutembea na mume wake hadi ukafanya waachane hasingefanya hivi,pengine mimi ningeweza kumrudisha Kidawa nyumbani na wewe ungeendelea kuishi kama kawaida!"
"Haiwezekaniiiiii!!Suma ni wanguuuu!!!"
Alipaza sauti Sabrat huku machozi ya damu yakimtoka!
"Kuwa mpole Sabrat,na kumbuka kuwa Suma anampenda Kidawa siyo wewe!!!"
"Hata kama!sirudi ujinini mimi!"
"Hakuna namna tena inabid urudi nyumban!
"Sirudi!!"
Alisema Sabrat kisha akakata minyororo akafanya timbwili kikatokea kimbunga kikali sana!!
Jabir na nguvu zake aliziwa ujanja,Sabrat akawaponyoka akapotelea mbali!
Jabir alibaki na maskitiko hakiamini ulimwengu hautakuwa salama kabisa sababu ya Sabrat!
********""""""********
Mke wa Suma alikuwa njiani anarudi akiwa na furaha moyoni kwa kushinda vita kali ya kupambana na majini!
Tayari kamwekea kinga mume wake na yeye mwenyewe!
Ili kujaribu kama mumewe amenasuka akamtumia meseji!
"Nakupenda mume wangu!"
Hazikupita hata dakika mbili Suma naye akatuma meseji!
"Nakupenda pia mkewangu,njoo nyumbani nimekumiss sana,njoo unipikie kile chakula nachokipenda!"
"WOW!",alishtuka mke wa Suma hasiamini kama ni mume wake ndiye katuma ujumbe ule!
"Dahh!afadhali yani ningelegea kidogo ningempoteza mume wangu dahhh!
******""""""*******
Suma alikuwa kazini,lakini ghafla alijikuta anamkumbuka Sana mkewe .
Alimkumbuka kiasi kwamba akaanza kujiona mkosefu mbele yake,kitendo chake cha kuchepuka alikuwa anakiona cha kawaida,lakini sasa aliuona ukubwa wa dhambi yake!
"Ila nimemkosea sana mke wangu!napaswa kumuomba msamaha!"
"Lakini naanzaje anzaje? Na talaka nilishampa?"
Mawazo yalikuwa ni mengi sana,kazi haazikwenda sawa kabisa!
Mawazo yale hata yeye yalimshangaza sana,kumkumbuka mkewe namna ile ilikuwa zamani Sana!
Enzi zile za yale mapenzi ya kuonana kwenye glasi.
Yale mapenzi ya kushindwa mpaka kula usipomuona.
Picha ilimvuta ikamkumbusha zamani enzi zile anakutana na mkewe,kabla ya kuitwa mama fulani.
Kipindi kile anaitwa Aisha,alikuwa Aisha kweli,alitingisha kila kona ya mtaa.
Akakumbuka alivyopata tabu kumpata,ilimchukua miezi sita mpaka kumpata!
Licha ya uzuri wa sura na umbo lake la kuvutia,Suma alimkuta Aisha na bikra yake!
Alijilaumu sana kwa mabaya aliyomfanyia!
"Kwanini nafanya hivi?Ina maana mkewangu siyo mtamu tena?hapana siyo kweli!!Au uzuri wake umeisha?hapana siyo kweli!!
"Ivi watoto wangu wakijua nayomfanyia mama yao siwatanichukia sana?"
Suma alijiuliza maswali na kuyajibu mwenyewe!
Akiwa katika mawazo iliingia meseji kwenye simu yake,hakuamini alichokiona.
Kwake ilikuwa ni kama kitu alichokuwa anakisubiri kutoka kwa mkewe!
"NAKUPENDA MUME WANGU!"
Alijikuta anaruka kwa furaha kama kashinda milioni za biko au tatu mzuka!
Siku hiyo alitoka kazini mapema akapita super market uko akanunua vitu mbali mbali,akiamini hiyo ni siku mpya kwao,kama ni mapenzi basi wamejivua gamba!
Alinunua na zawadi nzuri kama chupi na sindiria(jamani hivi vichupi kama zawadi wadada wanavipendaga sijui kwanini)
Alipomaliza aliviingiza kwenye gari lake akapanda!
Alipokaa tu kwenye kiti kabla hata hajawasha taa,alihisi kama kuna mtu nyuma yake!
Alipogeuka alimuona mwanamke mzuri mwenye sura ya kihindi akiwa amevaa mavazi mekundu,alikuwa mrembo haswa!!!
Alishtuka akataka kushuka kwenye gari lakini milango haikufunguka!
JE HUYO MWANAMKE NI NANI?NA VIPI SABRAT ALIENDA WAPI?USISAHAU KUHUSU KIDAWA NA SHANGA ZAKE!