.
Simulizi ya kweli....... SHANGA YA BIBI ILIVYONIPA UMAARUFU!!!!
Msimuliaji............ KIDAWA
Umri .......... 18+
Sehemu ya 14
Tulipoishia...... Kidawa anarudi nyumbani akiwa na shauku ya kumuona Bi Sandra ili ampe ufundi asionekane gogo kitandani kama wanavyosema lakini anakuta wamefunga Bi Sandra yuko hospital,anaenda hospital Bi Sandra anapata nafuu hadi anamtuma Kidawa ampikie chakula anachopenda......
Songa nayo.......
Nilipika vizuri,maana kwenye mapishi niko vizuri nilifundishwa vzuri na Bi Sandra mwenyewe!
Nilivyomaliza nilijiandaa kisha tukatoka na mama pia kwenda hospitali,tulipanda gari ya mama mpaka hospitali.
Nilikuwa na tabasamu pana usoni nikiamini sio muda mrefu ntakuwa kungwi wa mapenzi,usoni nilijawa na tabasamu pana lenye matumaini!
Tulifika tukashuka mimi na mama tukaanza kupiga hatua zetu kwenda kwenye wodi binafsi alikolazwa Bi Sandra.
Njiani tulikutana na machela iliyobeba mwili wa mtu ambaye ni wazi kashapoteza uhai wake,hiyo haikutushitua,maana pale ni hospital ivyo kufa na kuzaliwa ni kila siku,tuliingia ndani ya wodi nilichokiona kiliniogopesha nilikuta kitanda kikiwa kitupu tena kimetandikwa vizuri kama hakuna mtu alilala pale!
Mkono wangu ulioshika kapu uliachia likaanguka chini,mikono nikaiweka kichwani huku nimepigwa butwaa!!
Nilitoka nakimbia mbio nikielekea njia niliyokutana na ile machela huku nyuma mama akawa ananifuata huku ananiita!!
"Kidawa!Kidawa mwanangu we kidawaaa!!!"
Sikujali nilikimbia huku machozi yakinitiririka kwa kasi,watu walibaki wananishangaa tu hawakujua kwanini nakimbia,walinzi walianza kunikimbiza Ila hawakunipata mpaka nikawaona wale manesi wanaosukuma ile machela!
Nilifika nikasimama mbele yao ghafla nao wakasimama wakawa wananiangalia kama wananishangaa.
Sikuwajali nilifika nikafunua shuka jeupe sikuamini nilimuona Bi Sandra wangu kafumba macho yake hatikisiki wala hawezi tena kugeuza shingo yake kuniangalia!
Bi Sandra alikuwa amefumba macho huku anatabasamu,machozi yalinitoka safari hii nililia peke yangu,Bi Sandra hakulia tena sikuona chozi lake Ila tabasamu lake!!!
Mama naye alifika pale pamoja na wale walinzi,waliotaka kunishika mama akawazuia..
"Hapana msimguse,muacheni amlilie mama yake!"
Mama alinisogelea akapiga magoti pembeni yangu na yeye machozi yalimtoka pia .
"Mama!Bi Sandra ameondoka mama,aliniambia hawezi kusafiri hadi anione mama,Bi Sandra kanisaliti mama,alisema atahairisha safari kwa ajili yangu mamaa!"
Mama alilia tu hakuongea neno lolote wote tulimpenda Bi Sandra.
"Mamaaaaaa!!,amkaaaaaaa mama yangu amkaaaa mamaaaaaa nani atanipikiaaaaaa mamaaaaaaa umeondokaaaa nani atanifundishaaaaaaaa mamaaa wananicheka chuoniiiiiiii!"
Wale manesi walianza kusukuma machela yao wakionyesha huzuni kubwa ,kilio changu kiliwafanya baadhi wamwage machozi!
Nilitaka kuizuia machela Ila walinzi wakanizuia nikabaki nimekaa chini nikigalagala zaidi ya yule jamaa aliyeachwa na Hamida!
Nikiwa pale alikuja Daktari aliyekuwa anamhudumia Bi Sandra akasimama kisha akatoa karatasi akanipatia!!
"Huu ni ujumbe wa marehemu kwako alisema usimpe mtu asome zaidi yako hata mimi sijasoma,tunza ahadi yake!"
Nilichukua ule ujumbe nikauweka kwenye sindiria,mama akanishikria mkono tukaanza kuondoka hadi kwenye gari sikuwa na nguvu za kutembea peke yangu.
Tulirudi nyumbani tukakuta kumbe baba kaishatangaza msiba nyumbani,baadhi ya watu walishafika!
Taratibu zillifanyika Bi Sandra akapumzishwa kesho yake.
*************
Ilikuwa ni ngumu sana kuamini yaliyotokea kwangu kiukweli nilikuwa katika wakati mgumu sana.
Ilinichukua wiki nzima kuanza kuzoea na kula japo si sana muda mwingi nilimkumbuka mama yangu wa hiyari!!
Nikienda jikoni nakuwa kama namuona anapika,sebuleni namuona akifanya usafi na nikiwa ndani mtu akija kuniamsha nahisi ni yeye ndiyo ananiita!
Ndipo nulipokumbuka ile barua aliyonipa yule daktari niliitoa nilipoihifadhi nikaanza kuisoma!
Iliandikwa hivi....
Kwako mwanangu,binti yangu wa pekee,popote ntakapokuwa ntakutambulisha kama mwanangu umeishi ukiniaminisha ivyo binti yangu Kidawa,hujui tu vile nilikuwa nafurahi ulipokuwa unaniita mama!
Wewe ndiyo unanifanya niende safarini nikiwa natabasamu,chozi lako limenionyesha ni jinsi gani una upendo wa kweli kwangu.
Japo roho yangu inaniuma nimekufundisha kupika,nimekufundisha vyote Ila nilisahau kukufundisha kitu kinachokusumbua Sasa mwanangu! Sijakufundisha mapenzi najuta Kidawa mwanangu.
Naskitika uzuri wako umefunikwa na kufichwa na kasoro ndogo iliyopo ndani yako .
Kama nilivyokwambia Safari yangu ilifika na tiketi nilikuwa nayo,Ila sikupanda basi nikagoma kuondoka mpaka nikuone mwanangu kipenzi!
Nashukuru ulikuja,Israel akakubali kunipa pumzi tena niongee na wewe.nimefurahi sana mwanangu.
Sasa sina sababu tena basi limenirudia,namuona mama na baba zangu wananiita namuona pia na mpenzi wa moyo wangu ananiita,mwanaume niliyempenda kuliko mwanaume yoyote duniani ananiita sio muda ntaonana nae!
Najua sikuachi vizuri mwanangu Ila ntakupa maelekezo yupo wa kukutendea makubwa zaidi yangu.
Funga Safari hadi Tanga wilaya ya Lushoto shukia sehemu moja wanapaita vuga road pale utachukua pikipiki wakupeleke kwenye Kijiji cha Kilwai ukifika ulizia kw Bi Mwana mtoto,kama tatzo ni mapenzi atakufanya uwe kungwi wa mahaba na kama kuna uchawi atakutibu pia!!!
Sina mengi mikono inakosa nguvu ya kuandika angalau nina amani nina amini utatabasamu na utakuwa kungwi kati ya makungwi!......
Narudi nyumbani ntakusubiri huko safari yako ikifika ntakutumia tiketi mwanangu,ntakupokea huku ni kuzuri kuliko huko mwanangu!!!!
...............
Nilimaliza kusoma machozi yakanitoka nikaanza kupanga nguo zangu kwenye kibegi changu,sikupanga nguo nyingi sana nilichukua tu kama tatu.Mama aliingia akanikuta napanga nguo zangu
"Mwanangu una Safari?"
"Narudi chuo mama!"
"Hakijafunguliwa bado lakini?"
"Siwezi kukaa hapa mama,namuona Bi Sandra kila Kona!"
"Basi safiri na Baba yako anaenda Dubai kesho kutwa!"
"Sisafiri mama naenda chuo kuna rafiki zangu nimewazoea huko!"
"Sawa nenda mwanangu!!"
"Ahsante mama!"
"Akaunti yako ina pesa!"
"Ina laki nne!"
"Ntakuingizia laki sita nadhani zinatosha utumie!"
"Ntashukuru!"
"Mbona hauna furaha mwanangu?"
"Unahisi huu ni wakati wa furaha kwangu?"
Nilimuuliza swali mama ambaye aliondoka bila kunijibu,ndivyo walivyo wazazi wangu wanaamini pesa ni kila kitu, nikikohoa tu pesa hawana muda wa kujua nasumbuliwa na nini.Waliniingizia pesa ambazo sikuwa hata na matumizi nazo ,nimemwambia lakini nne lakini ukweli Nina kama milioni mbili benki.
Muda mwingine mama ananiingizia pesa baba naye ananitumia sijui hawaambiani?mi sijui!!
Kulikucha nikabeba begi langu nikawaaga wakataka wanibebe mpaka chuoni nikakataa,nikatoka nikachuka bodaboda mpaka ubungo nikakata tiketi ya Basi la Tanga linaloenda Lushoto!
Safari ikaanza!!!!
JE KIDAWA ATAFANIKIWA KUMPATA BI MWANA MTOTO ,NA JE HUYU BIBI NI NANI?? USIKOSEEEEEE