Simulizi: Shanga za Bibi zilivyonipa umaarufu

Simulizi: Shanga za Bibi zilivyonipa umaarufu

Simulizi ya kweli..... SHANGA YA BIBI ILIVYONIPA UMAARUFU!! (season 2)
Msimuliaji................ KIDAWA
Umri................18+

Sehemu ya 30 (MWISHO)

SABRAT & JABIR
Sabrat alikasirika sana,kitendo cha kumgusa Suma akapigwa na shoti kilimuuma sana!
Moyoni aliapa kutomuacha salama mke wa Suma!
Alianza kumtafuta kwa udi na uvumba,tatizo hakuwa akimuona kabisa!
Jabir alimtafuta sana Sabrat aliyekuwa anawakimbia kila alipowaona!
Hatimaye walimuona,wakagundua Sabrat anaishi juu ya mti!
Wakamuwinda hatimaye wakamkamata wakamrudisha ujinini,kule walimfungia kwenye gereza la majini watukutu!
Jabir aliamua kukata tamaa na Kidawa,akiamini hatoweza kuwa naye tena!
Ila moyoni alimchukia sana Kaka yake akiamini yeye ndiyo chanzo cha Kidawa kuondoka sababu ya kuingiliwa kila siku!
"Wewe ndiyo umesababisha mke wangu aondoke!"
"Na wewe ulisababisha nikamuacha mkewangu!"
Walikuwa wanatambiana kila kukicha hatimaye wakaamua kuoa majini wenzao!
Waliamua kuheshimiana hakuna aliyekula tamu ya mwenzie!Wakaamua kuishi kama ndugu wanaopendana Sana!!!

SUMA NA MKEWE

Mapenzi yao ni kama yalikuwa yamezaliwa upya!
Walipendana kama watoto mapacha na kufuatana kama kumbi kumbi!
Maisha yao yaligeuka na kuwa yenye furaha!
Suma aliamua kuwa mtu wa dini sana tena swala tano kabisa!
Mambo ya dunia na warembo wake aliamua kuyatupilia mbali,macho yake yakazibwa na pazia hata hasimuone mwanamke mrembo zaidi ya mke wake!
Mke wa Suma naye alimuonyesha mapenzi mazito mume wake!
Maisha yao yakafunikwa na tabasamu pana!

*********"""""**********

Kwangu mimi maisha yangu hayakubadilika sana!Sasa yatabadilikaje na nyege zipo kila siku!
Nilijitahidi tu kujizuia na kutokuchanganya wanaume kama zamani!
Isipokuwa mwanaume naye usipomchanganya anakuchanganya yeye japo ndiyo nachoka mimi!

Japo nimepitia maisha mengi magumu na yaliyojaa maumivu na changamoto nyingi!
Bado sijakata tamaa, bado namsubiri mwanaume wa maisha yangu!
Kama mwanamke natamani kuwa na familia nami niwe nampikia mume wangu!
Lakini Kidawa sijui nachota ya mchele,wakija ndege wanadonoa na kuondoka!
Hii inaniumiza lakini navumilia,naamini ipo siku ntampata wangu wa kweli!!
Kwa sasa niacheni niruke ruke kama ndege aliyekosa makazi!
Ntafanyaje kama fungu langu ni la kukosa?
Ngoja nikwambie kitu,unajua sisi wanawake au wanaume waliofanikiwa kimaisha huwa tuna dhana moja tu!
Sio kwamba hatutongozwi,tunatongozwa sana Ila tatizo tunaamini kuwa kila anayekutongoza anataka mali zako!
Na hii ni kwa sababu ni ngumu kumjua mwenye mapenzi ya kweli ukiwa na hela!
Kwani asilimia tisini kama sio mia watakuja wakitaka pesa zako tu!
Ndiyo maana majimama yanalea vitoto tu mtaani yakiwa yanajua ni ngumu kupata mwenye mapenzi ya kweli!
Kwa hiyo anapokuwa na kibenteni anajua sawa kile kibenteni kinamtumia Ila na yeye anakitumia kwa hiyo wanatumiana!😂😂😂
Kubadilisha wanaume nimeacha ila ukinizingua kwanini nisikubadilishe😂😂.
Inabadilishwa figo sembuse wewe nyau tu!😂😂😂.
Hela zangu nimetafuta kwa tabu staki stress!

Jamani! jamani!msiogope mapenzi ya kweli yapo!Tena yapo simnamuona Suma alivyonipendaga japo ni mchepuko?
*************
Maisha yangu yalisonga Ila kilichoniumiza sana ni shanga zangu,ziliniuma sana!
Siyo kwamba nilikua gogo Ila nilikuwa nazipenda,na pia zinanikumbusha safari ndefu na mambo niliyopitia hadi kufika kuwa kungwi!
Sikujua nitaipata wapi maana hata Jabir hakunitokea tena!
Sikuwa na wa kumuuliza zaidi nilibaki na msongo wa mawazo tu,kila shanga nilizonunua nilihisi hazinipendezi kama SHANGA YA BI MWANA!!

Kama muujiza siku moja nikiwa nafagia uvunguni,ghafla nikaiona shanga niliitoa haraka,sikuamini ilikuwa ni SHANGA YA BIBI ILIYONIPA UMAARUFU!!!
Nilipiga kelele kama chizi,kama vile mwanafunzi anayehisi ana mimba halafu ghafla akaziona siku zake!
Nilivaa shanga nikasogea kwenye kioo,kiukweli ilinipendeza sana nikajikuta nimesema kwa sauti!!
"PIGA KELELE KWA SHANGA AKEEE!!!"

**************MwishO******************
Ahsanteni sana mwisho wa hii hadithi nyingine nzuri zaidi!
Credit to jack mambo mtunzi
Like his page story za mambo fb

Safi sana... Story nzuri sana...

Chapter Closed...



Cc: mahondaw
 
Nimeisoma kwa wiki moja.
Ni nzuri japo inavuryga mwili wakati mwingine.
Asante Mtunzi
 
Back
Top Bottom