Boogman
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 2,439
- 5,612
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kijeeee tuuu
Kama uliweza kusubiri kwa wiki kama mbili sidhani kama jumatano itakuwa mbali
VISASI
The President And I(Mimi Na Rais)- Sehemu Ya Kumi Na Moja
Lello Mmassy  February 07, 2019

Stanza Mambo Ni "Tetema"
“Tunaelekea wapi Joe”, Habibu alimuuliza Joe baada ya kuona wanakatiza mitaa ya Shenyang bila kuongea neno.
“Just follow me boy” (We nifuate tu dogo), Joe alijibu kiufupi ila kwa kujiamini.
“Kaka, sikufikiri hata siku moja kama maisha yangu yatakuja kuharibika ndani ya siku chache namna hii. Nilipoambiwa ninafanya kazi na wewe niliona ni heshima kubwa na nilifurahi sana lakini ukweli kwa sasa ninajuta sana.
Natamani hata wakati ule ulipokuwa unatuambia ule mpango ningetia hata neno la kukataa leo ningelitumia kama utetezi mbele ya Rais. Sasa nilibaki kimya naonekana na mimi nimeridhia”, Habibu alijiongelesha huku wakitembea.
Joe ndiye aliyekuwa ametangulia mbele na Habibu akifuata kwa nyuma.
“Kwani hukuridhia?”, Joe alihoji kwa ufupi sana.
Jibu hilo lilizidi kumtia wazimu Habibu, chuki ya ukweli ilianza kujengeka dhidi ya Joe. Aliwaza kuwa inawezekana Joe hajali lile lililotokea ambalo limemuharibia maisha kama yeye alivyoharibu yake miaka michache iliyopita.
Wakati Joe akiwa anapiga hatua kwa kasi yeye Habibu alisimama na kumwacha Joe kama hatua tatu hivi kisha akamwita.
“Joe. Nashukuru kwa yote uliyonifunza na kufanya nawe pamoja. Naelekea kujisalimisha ubalozini. I can no longer handle this”, Habibu alimalizia.
Joe aliposikia hivyo alisimama na kugeuka, alimwangalia Habibu kwa muda kama wa dakika moja kisha alipiga hatua kumsogelea na alimfikia karibu.
“Habibu, wewe ni Rais mtarajiwa wa Stanza. You need to be as strong as the president should be. We are almost there Habibu, this is just a shortfall on the process, but it should not stop us.
You’re a traitor to Costa either way, whether you return, or you follow me, pull up your socks, wipe the dusts and continue with the mission. You are as good as dead in Costa’s hands, that you know.’’
Joe aliendelea kumuasa Habibu kwa namna aliyoona ingepunguza hofu na kukata tamaa kulikoanza kushamiri machoni mwake.
‘’Sisi ndio wa kuikomboa Stanza, sisi ndio wa kujitolea kuifanya Stanza iwe vile watu wanafikiria iwe. Tumebeba matumaini yao na ya vizazi vijavyo” Joe aliendelea.
“I need you to put in your mind that you are not the only one hurting, my family is in Stanza, but the cause we are both fighting for is bigger than I, it is bigger than you and I combined. It is also more important than family and career, it is the future of our country and the next generations. Some sacrifices must be made.”
(Nahitaji uelewe kuwa si wewe pekee unaumia, familia yangu ipo Stanza. Lakini kile tunachokipigania ni kikubwa kuliko mimi, kuliko wewe na mimi pamoja, ni kikubwa kuliko familia na hata kazi yako. Hii ndiyo baadae ya taifa letu na vizazi vijavyo. Ni lazima kujitoa muhanga), Joe aliendelea kumsisitiza Habibu
‘’Na wewe ni lazima usimame kujua nini ulikuwa ukikipigania toka ukiwa chuoni. Umepata nafasi ya kukifanya kuwa kweli kwanini unaogopa?”, Joe alikuwa akiongea na Habibu huku amemkazia macho na kumgusa kwa kidole kifuani. Aliongea kwa kuchanganya lugha kuonyesha msisitizo.
“Joe, I didn’t plan my career to end up miserably like this brother. I am…I am…”, Habibu alishindwa kumalizia na kuanza kulia. Ilikuwa ni ngumu kuamini kuwa huyo anaelia ni balozi wa Stanza nchini India. Usingeamini.
Joe alipoona vile hakika huzuni ilimwingia, aliona kabisa amemwingiza kijana wake kwenye misheni ambayo haikuwa saizi yake. Alijiona amefanya kosa sana kuamini ustahimilivu wa mambo alio nao yeye na Macha ni sawa na hawa vijana. Alielewa hisia za Habibu na alijua kweli amemwingiza mahali pagumu.
“Habibu, I will help you out of this and you will be free”, Joe alimwambia Habibu aliyekuwa amejifunika na kitambaa cha jasho ili wapita njia wasijue kama analia.
“Mtuhumiwa wa kesi ya uhaini anawezaje kumsaidia mwenzake?”, Habibu alihoji bila kutoa kitambaa usoni.
“Nifuate. Kwa sasa sio salama sana kurudi ubalozini, acha kwanza nipige simu mbili tatu. Sawa?”, Joe alimjibu Habibu.
“Sawa kaka”, Habibu alijibu kama mtoto mdogo. Hakika kama kuingizwa choo cha kike basi hapa aliingizwa cha vikongwe kabisa.
********************************************
Mara baada ya Pius kuachwa pale uwanja wa ndege na Joe na Habibu kuondoka, baada ya muda alishtuka na kujikuta amekaa juu ya choo amelala.
Hakuelewa, alijipapasa na kukuta kila kitu anacho isipokuwa Simu aliyokuwa akitumia pamoja na kile kinasa sauti alichokuwa amerekodia mazungumzo yote ya safari nzima ya Korea Kaskazini ikiwepo na majadiliano yote.
Alisimama na alipotaka kutoka aligundua amefungiwa mlango kwa nje. Aligonga sana na hatimaye mtu mmoja alieingia maliwatoni alimfungulia. Alianza utaratibu wa namna gani atafika ubalozini.
**********************************************
Joe na Habibu waliambatana na mlinzi mmoja wa kichina wa pale uwanjani pamoja na afisa mmoja wa usalama wa ubalozi wa Korea pale China aliekuwa amekuja kuwapokea kina Joe.
Baada ya Pius kutokomea katika hali isiyotarajiwa pale kiwanjani haraka yule afisa wa usalama wa ubalozi wa Korea aliyetumwa kuwapokea kina Joe alishafanya mawasiliano na Ubalozi na kuwapa taarifa kuwa kuna mambo hayapo sawa.
Ni Ubalozi wa Korea uliofanya mawasiliano na uongozi wa ulinzi wa uwanja wa Shenyang ili kumsaidia Joe kumtafuta Pius kwa kutumia kamera za CCTV. Ni yeye baada ya kushuhudia sintofahamu kati ya Joe na Pius, Joe alimwomba ahakikishe anampatia simu na kile kinasa sauti alichokuwa nacho Habibu.
Kwa kutumia ‘style’ ya mapigo wakorea wanaiita jug-eun yaani kifo cha uzima basi yule afisa wa usalama alifanikiwa kumzimisha Pius katika hali ya utaratibu kabisa na kumfanya apoteze fahamu na kisha kuchukua simu na kile kinasa sauti na kumkabidhi Joe.
Jug-eun ni aina ya mapigo ambayo ni ya ufundi wa hali ya juu. Mtu aweza kukusogelea karibu hata katikati ya kusanyiko la watu halafu akakupa hilo pigo moja kimya kimya ukaishia kupoteza fahamu bila hata kutoa mlio. Akishakupiga anakushika hapo hapo na kukuegemeza kwenye bega lake na kuanza kutembea na wewe kama mtu anaemsaidia mgonjwa na hakuna atakaeweza kugundua kama umepoteza fahamu.
Ni pigo hilo Pius alipigwa eneo la shingo kwa nyuma na aligutuka baada ya dakika 15. Wakati pigo hilo likitokea na vitu kuchukuliwa watu waliopo kwenye control room ya kamera za CCTV walifanikiwa kukata kipande cha tukio lile na kisha kuunganisha baada ya tukio kwisha bila kuonyesha mpishano wa sekunde hata moja. Walilifanya hili kitaalamu wakiongozwa na afisa kutoka ubalozi wa Korea aliejulikana kama Sam Si.
Baada ya tukio lile afisa wa usalama wa Ubalozi wa Korea akiwa hajui kwa nini Joe ameomba yafanyike yote yaliyofanyika alidhani wangeambatana nae Ubalozi kwao kisha aelekee ubalozi wa Stanza pale Beijing lakini Joe aliomba aachwe aende anapopajua yeye na kisha atawasiliana nao.
Alimsihi sana asiseme lolote lililotukia ili kutoleta hali ya taharuki. Joe hakutaka ijulikane kwa Korea kuwa alikuwa na mpango wa kumtoa Rais Costa madarakani kabla ya muda. Aliona ni mapema sana Rais Kim kumjua kiundani namna ile.
***************************************
“Franco-Domino-Chi”, Ni maneno Stanley Macha aliyomnong’oneza Meshack wakati Meshack akichukua beji yake na bastola.
“Aye Sir”, Meshack alijibu kwa sauti ya chini sana sikioni mwa Stanley Macha isiyoruhusu mtu yeyote kusikia.
Vijana wengine watatu wa usalama wakiwa wamesimama hatua kama tatu kutoka walipokuwa Macha na Meshack walimwongoza Macha kuelekea ofisi ya Rais Sylvester Costa.
Franco-Domino-Chi ni ‘code’ ya kiusalama ya mawasiliano kati ya Macha na Meshack. Maneno yale yalimtaka Meshack afanye mambo matatu makubwa, kwanza yalimpa taarifa kuwa Macha hatafanya jambo lolote la ajabu kwa hiyo Meshack asiogope, pili abakie akiwa amejikita katika majukumu yake kwa utulivu na tatu, siri yake bado haijagundulika hivyo asihofu kwa sasa.
Watu wa usalama mara nyingi hutumia maneno machache kumaanisha kurasa nzima. Hii huwasaidia kuwasiliana ndani ya muda mfupi lakini mambo mengi. Huweza kuamua kufanya kidole kimoja kikinyooshwa basi kumaanisha mambo matatu mpaka manne.
Meshack alimwelewa Macha na kukubali. Meshack alikuwa sehemu ya mpango mkakati lakini akitumiwa na Macha kwa siri na utaalamu mkubwa. Yeye aliwekwa aje kuwa kiungo mmaliziaji lakini bahati mbaya mambo yamekwenda ndivyo sivyo hadi kufikia wakati ule.
Macha alishaelewa kuwa Meshack atakuwa katika hali mbaya hivyo alihitaji kumtia moyo na kumfanya atulie asije akashawishika kutamka lolote katika kujihami ama kujisafisha mbele ya Rais. Japo mpango mzima na wahusika wote alikuwa nao Macha na Joe tu na hata baadhi ya wahusika wenyewe hawajuani.
************************************
Baada ya Rais Sylvester Costa kupata mpango ule na kusikia zile sauti alizotumiwa na Jenerali Ernest Nduta alichanganyikiwa.
Alimwagiza mkuu wa majeshi haraka aongeze ulinzi pale Ikulu, alimkabidhi Sabinasi Paulo aongoze intelijensia ya Idara ya Usalama wa Taifa na kuhakikisha kama kuna uwezekano wa kuwajua wahusika wengine basi haraka hilo lifanyike. Kwa ufupi aliona ni kama anapinduliwa muda huo.
Rais Costa alikuwa akizungukazunguka meza ya ofisi yake huku aking’ata kucha asijue nini kinatokea. Taarifa zile zilimchanganya sana. Hupenda kusema kazi ya Urais inamchosha sana lakini wakati ule alionyesha fika ni kwa jinsi gani anapenda cheo kile na kamwe hayupo tayari kukiachia.
Alikuwa akipiga simu kila mahali na kila saa kuulizia nini wameweza kukigundua kingine. Mathalani, alitaka sana kuongea na Pius lakini jitihada zote za kumpata zilikuwa zikishindikana.
“Kimweri vijana wako wameshafanikiwa kufika uwanja wa ndege wa Shenyang?”, Rais Costa aliwasiliana na balozi Kimweri kutoka Beijing China.
“Ndiyo Mkuu, wamefika lakini kamera zimeonyesha alitoka nje ya uwanja ndio bado tunafuatilia” Kimweri alijibu.
“Fanyeni hima mniambie kijana wangu Pius yupo wapi kama mnashindwa niambieni nitapiga simu Ikulu”, Rais Costa aliongea kwa ghadhabu.
“Tunajitahidi mkuu”, Kimweri alijibu
Wakati anamalizia kuongea na simu mlango wa ofisi ya Rais Costa ulifunguliwa na alikuwa ni Meshack akimwingiza Stanley Macha.
“A traitor”(Msaliti), Rais Costa alifoka kwa hasira na kumkaribia kwa kasi Stanley Macha na kumpiga ngumi ya uso.
“Mh. Rais”, Macha alijibu kwa unyenyekevu na kujishika alipopigwa na kutulia.
Rais Costa alikuwa amefura kwa hasira.
“How did you manage to fool me all along? It has been a long time Macha, for the past 8 years I believed you were protecting me and the best interest of our nation, and you were conspiring to overthrow constitutionally, legitimate president who was elected through democratic processes? How could you? Son of a bitch”.
(Uliwezajie kunidanganya kwa kipindi chote? Ni muda mrefu Macha, kwa miaka nane sasa niliamini unanilinda na kulinda maslahi ya nchi yetu, kumbe ulikuwa unakula njama za kumpindua Rais halali aliyechaguliwa kwa misingi ya katiba, aliyechaguliwa kwa michakato ya kidemokrasia? Mwanaharamu mkubwa!), Rais Costa alizidi kung’aka kwa hasira.
Hakika haikuwahi kutokea hata siku moja Rais kuonekana katika hasira ya namna ile. Ilimtisha kila mtu, hakuna aliyeongea wala kumsogelea. Macha alibaki kimya.
“Nimekukosea nini mimi? Nimekunyima kitu gani? Tell me, tell me now Macha”, Costa aliendelea kuongea huku macho yake yakiwa mekundu kama yaliyojaa damu. Hasira ilimzidi kipimo.
“Am I not doing enough for this country? Am I not delivering? then why? Why are you doing this? Then do it, am here. Do it, tell me to get out and I will leave this office and let you be if that is what you wanted. Is it not what you want?”.'
(Je sifanyi vya kutosha kwa ajili ya nchi hii? Sitekelezi? Kwanini lakini? Kwanini unafanya haya? Haya, nipindue, nipo hapa. Nipindue, niambie nitoke nje na nitaondoka nikuachie Urais huu kama ndicho utakacho. Sivyo?), Rais Costa aliongea mfululizo huku akizungukazunguka ndani ya ile ofisi.
Macha alibaki kimya akiwa ameinamisha kichwa chini.
“Mh. Rais…”
“Shut up” (Nyamaza), Costa alimkatiza Macha alietaka kuongea jambo.
“Meshack hakikisha familia ya huyu mbwa na ya Joe zote zimewekwa chini ya ulinzi popote zilipo na mtoeni huyu mbele yangu. I don’t have timen to listen to traitors. Just get him out of my sight”. (Sina muda wa kusikiliza wahaini. Mtoe machoni mwangu sasahivi), Rais Costa aliagiza kwa hasira kuu.
Vijana wawili walimshika Macha mkono ili wamwelekeze mahali wanapokwenda kumuhifadhi kwenye moja ya nyumba za siri za idara ya usalama wa taifa ambapo atakaa huko muda wote wa uchunguzi chini ya uangalizi mkali.
Meshack alipotaka kutoka tu Gideon msaidizi wa Rais aliekuwa akifuatilia kasheshe lile alitia neno.
“Meshack subiri. Mh. Rais, kitendo wanachokifanya hawa kina Joe na Macha ni kitendo cha ajabu sana, kwanza umefanya hekima sana kumsitiri mimi ningeshapiga mtu risasi”. Gideoni kama kawaida yake alianza unaa.
“Gideon, nimekasirika sana na hawa watakiona cha mtema kuni. Kama Joe nilimfanyia vile kwa miaka miwili bila kugusa roho yake akaniona mimi ni mjinga wakati huu naua mtu”, Rais Costa alijikuta anaropoka azma yake ya kumuua Macha na Joe popote atakapopatikana.
“Lakini sasa Mh Rais nilikuwa nashauri, mambo haya unajua mara nyingi hayafanywi na watu wawili ama watatu ni mnyororo mrefu na watu wa kukufanya ujue mnyororo huo ni Macha na Joe hivyo nashauri usiwapoteze mapema…….
Tunawahitaji sana. Huyu Macha aingizwe kwenye mahojiano yenye mateso makali mpaka aseme nani wanashirikiana nae. Joe nae atafutwe, najua vijana wetu hawashindwi kumpata ndani ya muda mfupi. Hata hivyo kumbuka kina Joe wametoka kwenye misheni huko Korea unahitaji kupata mrejesho. Siku mbili tatu hizi Rais Kim atataka kusikia kutoka kwako utamjibu nini?”
“Unaongea kweli Gideon lakini taarifa zote alikuwa amebeba Pius, anazo. Nitazipata”, Rais Costa alijibu kwa majigambo.
“Sawa utazipata lakini bado ninashauri familia za hawa mabwana zisiguswe kabisa. Kufanya hivyo utasababisha taharuki na watu watataka kufahamu nini kimetoka. Ninashauri jaribio hili lisijulikane kabisa, tena hata Mkuu wa Majeshi mwambie afanye siri. Wakuu wake wa vikosi wasijue maana kumbuka ni wao walitaka kukupindua kipindi cha nyuma na kina Joe na Macha wakazima lile jaribio sasa huwezi jua kuna masalia yao na wakijua utaamsha tena hisia”, Gideon aliendelea kuchangia.
Wakati wa mazungumzo yote hayo Meshack alikuwa amesimama pale akisubiria maelekezo mengine.
Rais Costa alitafakari ushauri wa Gideon na kuunga mkono japo roho ilimuuma sana kuziacha familia za Joe na Macha bila kuzipa shida.
“Meshack ziache familia zao kwanza nitakupa maelekezo baadae”, Rais Costa alimalizia na Gideon na Meshack walitoka na kumwacha Rais Costa mwenyewe.
Akiwa bado amesimama ghafla aliingia Jenerali Ernest Nduta Mkuu wa Majeshi.
“Nduta, tell me what’s going on” (Nduta niambie nini kinaendelea), Rais Costa alimpokea Nduta kwa swali.
“Mpaka sasa taarifa za kiintelijensia zinaonyesha hali ni shwari. Tumefanya full intel scan kwa miezi zaidi ya sita nyuma na hakuna mawasiliano yoyote yaliyobainisha mpango huu.
Actually, timu yangu inaendelea kukagua kama kuna mawasiliano yoyote kutoka nje na watu wa ndani ili kujua labda kuna mkono wa nje, lakini kwa sasa hali ni shwari. Nadhani ulikuwa ni mpango ambao bado ulikuwa ni mchanga sana”, Nduta alimpa taarifa fupi Rais Costa.
Wakiwa bado wanaongea ghafla simu ya Sabinasi Paulo, kijana aliyekaimishwa ukuu wa Idara ya Usalama wa Taifa baada ya Macha kuwekwa chini ya ulinzi iliingia.
“Mh Rais, tumempata Luteni Jenerali Pius” Sabinasi aliongea kwa kifupi.
“Put him through” (Muunganishe hewani), Rais Costa alitaka kuunganishwa nae.
“Mh. Rais Salamu”, Pius alisikika akiongea kwa sauti ya unyonge.
“Pius, upo salama? Pole sana kijana wangu”, Rais Costa aliongea kwa sauti ya upole na mahaba mazito kwa Pius.
Alimuona ni shujaa kuliko mashujaa wote aliowahi kuwasoma kwenye historia. Kitendo cha kuweza kumpenyezea taarifa kuwa mtu kama Macha anaemwamini anapanga mipango miovu dhidi yake kilikuwa ni msaada mkubwa kupitiliza. Alitamani hata palepale atoe amri vitabu vyote vya mitaala vya historia viwafute watu kama kina Mkwere na Njelilila wanaoonekana ni mashujaa na kumwandika Pius Kihaka.
“Nipo salama Mkuu, japo nina maumivu makali sana shingoni nadhani walinipiga na kitu kizito. Sasa nipo hapa ofisi zetu za ubalozi wananipatia huduma ya kwanza”, Pius aliongea kwa unyonge sana.
Pigo la jug-eun halikumwacha salama. Alihisi amepondwa na chuma kizito kumbe ni mkono tu.
“Pole sana. You have the package of your visit to North Korea, right?” (Una nyaraka zote zinazohusu safari yenu ya Korea Kaskazini, si kweli?) Rais Costa aliuliza kwa shauku.
“Hapana Mh Rais walichukua taarifa zote”, Pius alijibu.
“Son of a bitch! ****” (Mwanaharumu huyu), Rais Costa alitukana kwa kummaanisha Joe.
“Sabi, andaa mpango wa kuhakikisha Joe anapatikana ndani ya wiki moja akiwa hai ama amekufa. Kama kuna chochote utahitaji kwangu nikusaidie ama kuidhinisha niambie. Huyo kijana wa mawasiliano aliyekuwa akishirikiana na Macha hapo Idarani nae apelekwe ‘sehemu salama’ hata kama alikuwa akifuata maagizo ya mkuu wake, akamatwe na awekwe kizuizini haraka. Nahitaji safu nzima ya vijana wako hapa ikulu ibadilishwe na ianze kuchunguzwa haraka.
Nduta, naomba baada ya siku tatu unipe uhakika kuwa hakuna kikosi ama mkuu wako yeyote wa kikosi aliyekuwa akihusika na mpango huu. Nawategemea ninyi.” Rais Costa alitoa maagizo.
“Sawa mkuu”, wote kwa pamoja Sabinasi na Nduta waliitikia huku Nduta akiwa ameitika kwa kupiga saluti.
“Kimweri, andaa mpango Pius afanyiwe matibabu kama yatahitajika na afike Stanza haraka”, Rais Costa alimwagiza balozi Kimweri aliyekuwa kwenye simu akifuatilia mazungumzo yale.
“Sawa mkuu”, Kimweri aliitikia.
Simu ilikatwa na Nduta alitoka na Rais Costa kubaki ofisini mwenyewe. Alichukua simu na kumpigia tena Sabinasi.
“Sabi, andaa mpango Sara arudi Stanza haraka. Na safari zangu zote za kimataifa zifute mpaka hapo nitakaposema vinginevyo. Sitoki kwenda popote. Sawa?”, Rasi Costa aliagiza.
“Sawa mkuu” Sabinasi alijibu.
Sara ni mke wa Rais Costa na alitajwa na Joe kuhusika katika mpango huo. Wakati hayo yakitokea alikuwa amekwenda Ontario Canada kuhudhuria mkutano wa wiki moja wa wake wa Marais Duniani.
Rais Costa alishindwa kumvumilia arudi, alitaka arudi haraka na ahojiwe na kutaja wanaohusika kama anawafahamu. Japo alishindwa kuamini ni kwa vipi mke wake anaweza kuhusika kutaka atolewe madarakani. Alichukizwa sana.
Aliwaza sana jinsi anavyompa mke wake kila anachohitaji lakini bado anahusika katika mipango miovu dhidi yake. Alitaka afike hata siku hiyo hiyo.
Isitoshe, Rais Costa aliagiza safari zote zifutwe, hakutaka kutoka nje ya mlango wa Ikulu. Alijiona hayupo salama hata kidogo. Hakumwamini yeyote na alihisi saa na wakati wowote anapinduliwa na hivyo alitaka abaki kuhakikisha hali inakuwa shwari.
Rais Costa kichwa kilimuuma sana siku ile.
“Shit”, Costa alijikuta akitamka kwa hasira huku akipiga ukuta pale ofisini kwake alipokuwa mwenyewe.
***************************************
“Meshack, niambie hali ikoje huko”. Joe alikuwa akiongea na Meshack kwa njia ya WhatsApp call kupitia namba ambayo Meshack huitumia kwa kazi maalum tu.
“Hali ni tete mkuu, we are almost cornered. Sabinasi kapewa kitengo na wewe unamjua alivyokuwa haivi na wewe na Macha”, Meshack alijibu
“Damn it! Ila wakati nikifikiria namna ingine ya kufanya nakutegemea wewe uendelee kunipa taarifa”, Joe alimwambia Meshack
“Tumebadilishwa wote, hivi ninapoongea na wewe nimepangwa nikawe afisa usalama jimbo la Kinyunyu. Yani Joe huu mpango achana nao kaka. Umeshindwa vibaya”, Meshack aliongea kwa kukata tamaa.
“****”, Joe nae alijikuta akitukana. Hakika aliwekwa pabaya. Kwa mara ya kwanza aliona kushindwa kukiwa mbele yake.
Jimbo la Kinyunyu ni moja ya majimbo yaliyopo pembezoni kabisa mwa Stanza, mpakani na nchi ya Rangaba inayosifika kwa warembo barani Afrika. Ndipo huko Sabinasi alipomtupa Meshack baada ya kupangua maafisa usalama wa pale Ikulu. Kiufupi alipangua haswa.
“Ok Meshack nitakutafuta tena”, Joe aliagana na Meshack kiunyonge.
“Una maanisha Meshack alikuwa Sehemu ya mpango”, Habibu aliekuwa akisikiliza ile simu alihoji.
“Ndiyo, ila huyu kazi yake ingekuwa mwishoni sana. Sasa ndio hivyo tena”, Joe kwa mara ya kwanza alimjibu Habibu katika hali ya kukata tamaa.
Habibu nae kwa mara ya kwanza alianza kumsikitikia Joe badala ya kujisikitikia yeye. Alimwangalia Joe katika hali ya kumwonea huruma. Aliona nia njema iliyopo ndani ya Joe lakini inayoendea kushindwa.
“Joe, you still have power brother. Una taarifa muhimu ambazo Rais Costa atazihitaji. Unaweza kuzitumia hizo kukaa nae mezani”, Habibu alimpa moyo Joe.
Yale makabrasha yote ya safari ya Korea Kaskazini alikuwa ameyashika Joe. Rais Kim alikuwa akisubiri simu ya Rais Costa kukiri kupata majibu na hivyo mambo mengine yaendelee.
Kauli ya Habibu ilimpa moyo Joe kwa kiasi fulani.
“Ni kweli Habibu”, Joe alijibu kwa tabasamu la kulazimishia. Hakutaka kumvunja moyo Habibu aliyeona ameshaanza kupata moyo.
“There is one person left untouched. If he gets caught, then I will declare this a mission impossible and surrender” (Kuna mtu mmoja tu amebaki bila kuguswa. Kama na huyu akishtukiwa na kukamatwa nitakiri rasmi mpango huu kushindwa na nitajisalimisha) Joe alimwambia Habibu huku akichukua simu yake na kufungua ‘game’ yaClash Royale.
Clash Royale ni ile ile ‘game’aliyokuwa akiitumia kuwasiliana na Macha kwa siri, na huyu anaetaka kuwasiliana nae ni mtu wa tatu mwenye ile game katika mpango ule. Wakiwa watatu tu yaani Joe, Macha na huyu anaewasiliana nae sasa ndio haswa ‘masterminds’ wa mpango huu.
“Who is that? (Nani huyo?), Habibu aliuliza kwa shauku.
“Just pray that he is still in position to carry on with the mission Habibu or else consider yourself screwed”, (We omba sana huyu jamaa bado awe kwenye nafasi nzuri ya kutusaidia kuendelea na misheni Habibu, tofauti na hapo jihesabu umekwisha) Joe alijibu kwa jibu lililotoka moyoni kabisa. Wazungu wangesema ‘a sincere reply’
******************************
Usikose Kuendelea Kufuatilia Mfululizo Huu Wa Pili Wa Riwaya Hii Ya Kusisimua.Sehemu Ya 12 Itakujia Jumatano.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sio mbali kama sehemu ya 11 yenyewe imechukua zaidi ya wiki 2Jamani j5 km mwaka vile