Jackpiano
JF-Expert Member
- Apr 19, 2025
- 560
- 756
Simulizi za kusisimua na fundisho kwa vijana:kijana alivyoingia kwenye mtandao wa wizi wa magari – Safari ya Subaru Legacy ya Gongolamboto hadi Arusha
Baada ya kumaliza kidato cha nne mwaka 2019, maisha yalikuwa magumu. Nilikodishiwa bajaj na binamu yangu ili nijikimu. Nilifanya kazi kwa juhudi, lakini pesa haikutosha. Ndipo nikakutana na mteja mmoja wa kawaida tu, aliyenifanya nigeuke kuwa dereva wa "mambo ya haraka".
Baada ya kunitumia mara kadhaa, aliniingiza rasmi kwenye mtandao wa wizi wa magari. Tulikuwa tunaiba magari ya aina maalum—Subaru, Altezza, na Harrier—kisha tunayauza kwa maduka ya vipuri mikoani.
Tukio la Subaru Legacy – “DILI LA GONGOLAMBOTO”
Usiku mmoja tuliambiwa kuna Subaru Legacy mpya imesimama Gongolamboto karibu na duka moja la vifaa vya ujenzi. Ilikuwa na tracker lakini waliijua mbinu ya kuiblock mara moja ikiwashwa.
Mpango ulikuwa mkali:
Mmoja wetu alikuwa analinda upande wa barabara kama mwangalizi.
Mtaalamu wa ECU alifanya kazi ya kufungua gari kwa kutumia device maalum yenye uwezo wa ku-scan na ku-silent alarm.
Gari lilipoamshwa, tulilitoka nalo kimya kama vile ni la kwetu.
Tulikata njia kupitia Banana, tukavuka Kinyerezi, tukapitia njia ya porini kuelekea Mbezi tukashika Morogoro Road usiku wa manane. Tukiwa na gari, tulikuwa kimya sana, huku mmoja akiwa kwenye gari nyingine nyuma akitupatia ulinzi na tahadhari.
Ilipofika Mlandizi, tulikutana na kijana mwingine aliyekuja na number plate bandia. Tuliibadilisha, tukajaza mafuta, na safari ya kuelekea Arusha ikaanza.
Tulifika Moshi saa kumi na moja alfajiri, tukalipumzisha kwa dakika 30 kwenye nyumba moja ya kuhifadhi magari. Saa mbili asubuhi, likapelekwa kwa fundi anaye-specialize kuvunja magari kwa ajili ya kuuza spare. Pesa iliingia haraka—laki tano kila mmoja na ahadi ya kazi nyingine wiki inayofuata. Nitaeka part 2 sio poa