C.O.D.EX. 1 ................... SEHEMU YA 10
“Sawa Lim.” Akakubali Idris. “Kwa hiyo nikufuate lini uje ukae kwangu siku nzima.” Akatupa kete nyingine muhimu.
“Nitakupa taarifa kwenye simu, siwezi kukujibu hapa.” Limasi akaivunja ile kete iliyotupwa na Idris kwa jibu hilo.
“Sawa. Nasubiri mlio wako wa simu.” Idris akakubali huku anampatia kadi yake ya biashara Limasi ambaye aliipokea na kabla hajatoka garini, Idris alimvuta tena na kumuingizia tena ulimi wake kinywani. Wakabadilishana tena ndimi zao na ndipo Limasi aliposhuka garini na kwenda ndani ya nyuba anayoishi.
ENDELEA.
Akiwa na dada yake, Limasi alikuwa haamini kama aliweza kuingia mkenge kirahisi namna ile na kujikuta anachukua busu laini na nyevu la Idris.
“Yaani Tim mimi hata sijui nilikuwaje. Akili yote ilinihama.” Akawa anamuhadithia dada yake huku yupo kitandani kakamata mto wake na Timasi alikuwa akimtazama huku tabasamu hafifu likiupamba uso wake. “Nilikuwa napata msisimko wa ajabu ambao hadi sasa kama siiuelewi vile. Sijui kanipa nini yule mwanaume.” Maneno hayo yakamfanya Timasi naye akae kwenye kitanda cha Limasi na kuzishika nywele za dada yake kwa kuzilaza kwa nyuma.
“Lim. Hayo ndio mapenzi. Ndivyo yalivyo. Uhamisha akili na hupoteza kabisa kujiamini. Na saa nyingine, hata ngvu za mwili. Damu yote hujaa msisimko, unaopoteza nguvu kilaini. Kwa hiyo, usijali sana, ndivyo yalivyo na nafurahi kwa wewe kuingia huko tena. Naimani Idris ni mtu sahihi kwako.” Limasi alimuangalia dada yake kwa macho ya huruma, au tuseme macho ya kudeka.
“Dada naogopa kuumia mimi. Tayari waliniumiza hawa watu, na huyu akiniumiza mimi nitaishi kweli?” Safari hii aliongea huku akitamani kutoa machozi.
“Idris, ndilo chaguo sahihi. Wale wengine kumbuka niliwahi kukuonya. Ila huyu, nakuhakikishia, upo sehemu sahihi na utafurahia mapenzi.” Akajibiwa Limasi.
“Kaniomba niende kwake. Sijui niende lini.”Akachomekea na suala la kwenda kwa Idris.
“Sema anakuja keshokutwa. Ndio anatoka huko Afrika Kusini. Akija na ukasalimiana naye, unaweza kwenda hata mwezi mzima.” Timasi akamuelezea kuhusu kuja kwa mume wake ambaye yupo Afrika Kusini. Na maneno hayo yakampa faraja Limasi kwani alianza kujihisi hali ya kumpenda Idris kwa siku hiyohiyo moja. Hapo ndipo ule usemi wa mapenzi ni kama magugu maji, unapanda asubuhi, saa sita unakuta yametapakaa kiwanja kizima. Unatimia.
“Mwezi nzima. Sasa si bora nihamie.” Akaongea huku anacheka Limasi ambaye kwa muda mfupi tu! Ule ukanjanja wake ulipotea na alikuwa msichana mwenye hekima.
“Kuwa huru Lim. Wala usiogope, Namuamini sana Idris, yaani namuamini kuliko wale wengine. Jitahidi kumtunza awe wako pekee.” Akaongeza maneno mengine ambayo yalikuwa kama msumali wa mwisho kwenye kugongelea hisia za mapenzi kwenye moyo wa Limasi.
Hadithi ikawa hiyohiyo usiku huo hadi wakapitiwa na usingizi wakiwa hapohapo kwenye kitanda cha Limasi.
*****
HUKO Marekani, hali ilizidi kuwawia ugumu baada ya kutompata Idris Iris ambaye alikuwa Tanzania. Walipeleleza kila mahali lakini hawakupata jibu la alipokuwepo Idris. Waliweza kuchukua kamera za barabarani pamoja na za uwanja wa ndege ambao Iris alikwenda, lakini hamna walichoshuhudia. Waliangalia hadi pass za wasafiri wa wiki nzima ndani ya Marekani, lakini hawakumuona Idris wala jina ambalo walihisi ndilo analotumia.
“Mmefikia wapi Ally?” Alifoka kwenye simu Uzo baada ya mkuu wa CIA kupokea simu yake.
“Hamna kitu Uzo. Naomba unipe muda wa kuendelea kumtazama. Na pia kama unavideo za Dokta Ice, naomba uzilete hapa ili tuchunguze mambo kadhaa.” Akaongea Ally.
“Video zipo hadi za siku yake ya kufa. Hilo halina tatizo. Baada ya nusu saa, zitakuja hapo kwa ndege maalumu.” Maneno hayo yalienda sambamba na Uzo kukata simu na kumfanya Ally atoke ofisini kwake na kwenda kusimama kwenye kioo kikubwa ambacho kiliungwa kwenye kompyuta na kuonesha nchi nzima ya Marekani. Wafanyakazi wengi walikuwa wanaendelea kucharaza kompyuta zao, yote ni katika utendaji wao wa kazi.
Wakati hayo yanaendelea kujiri ndani ya Jiji la New York huko Marekani, ndani ya Jiji la Arusha, Tanzania, Idris alikuwa anapapasa kiuno hadhimu cha mwanadada Limasi ambaye alikuwa bado kalala na kajifunika shuka jeupe lililotandikwa kwenye kitanda cha Idris. Usiku mmoja uliopita, ni kelele na lugha za mapenzi ndizo zilizuka kwenye nyumba kubwa ya Idris. Idris aliendelea kuchezea kiuno cha Limasi ambacho kilikuwa kimefunikwa kwa shuka.
“Bwana niache nilalee.” Sauti ya puani ilimtoka Limasi baada ya kuona kashikashi za Idris zinazidi kwenye kiuno chake.
“Kwani nimekukataza jamani.” Naye Idris akajibu.
“Sasa ndio nini hivyo?” Akaendelea kuuliza kwa sauti yake ya puani.
“Basi tu, napenda hivi.” Akajibu tena Idris.
“Je nikifanya hivi.” Limasi akakatika kwa minato na kuzidi kumfanya Idris ahisi yupo dunia nyingine ya kisasa kuliko ile ya sasa hivi ambayo maisha magumu kuliko chuma.
“Ndio maana napapasa hapo kwa sababu jana mambo yaliyokuwa yanatokea, sikuyaelewa kabisa ni kwa sababu gani. Ni hichi ndio kilikuwa kinahusika?” Akafunguka yake Idris.
“Unaonaje kwani?” Safari hii Limasi alinyanyuka kabisa na kufunua shuka walilokuwa wamejifunika. Miili yao ambayo ilikuwa inangozi pekee, ikaonekana na macho yao kwa pamoja walikuwa wanaona jinsi ngozi zao zilivyobarikiwa.
“We’ ni mzuri Lim.” Maneno hayo yakamfanya Limasi asogee kwa Idris na kumlaza kifudifudi, kisha akampandia kwa juu kama farasi na kusogeza kinywa chake hadi kwenye kinywa cha Idris. Tendo la kuchukuliana mate, likapamba moto.
“Id, nimekuheshimu hadi hapa nipo katika kifua chako. Sipo hivi, ila unastahili zawadi hii. Lakini sijui mimi nastahili zawadi gani toka kwako.” Akaongea baada ya kunyonyana ndimi kwa dakika kadhaa huku bado akiwa kamdandia kama farasi.
“Huna unachostahili zaidi ya hicho kidoleni.” Maneno yalimtoka Idris na kumfanya Limasi atazame kwenye kidole chake. Hapo alikutana na pete ndogo lakini imenakwishiwa na jiwe la almasi inayopendeza sana.
“Id?” Akauliza huku katanua midomo yake. “Hii umeweka saa ngapi.” Bado alikuwa haamini. “Na kwa nini……” Akashindwa kumaliza kauli yake baada ya Idris kumvuta kwake na kuanza kunywa kinywaji cha mapenzi. Na mwisho wa yote, walijikuta wakilia kilio cha utamu, utamu ambao uliwafanya waahidiane mambo kibao ambayo sidhani kama wangekuwa hawapo katika dunia hiyo, wangepeana kizembe hivyo.
****
Baada ya mwezi mmoja. Si CIA, FBI wala C.O.D.EX waliokuwa wanataarifa za mwanajeshi aliyepotea (A missing Soldier). Wote walishindwa kutambua ni wapi alipokuwepo Idris Iris. Walichoka na kushindwa kabisa kuendelea kumtafuta mwanaume yule ambaye kwa wakati huo, alikuwa amefanya harusi kubwa sana na kumuoa rasmi Limasi.
Harusi ilikuwa kubwa sana Jijini Arusha. Kila ambaye aliweza kuhudhuria, alikubali harusi ile licha ya upande wa Idris kuwakilishwa na watu wachache sana akiwepo dereva wake pamoja na marafiki wa dereva huyo ambao walisimama kama ndugu wa Idris.
Kwa upande wa Limasi, alikuwa ni mwenye furaha kila mara. Familia za wazazi wake, zilifika katika harusi ile. Na ndugu wa mume wa Timasi nao walifika kunogesha harusi ile iliyokuwa babu kubwa jijini.
“Kwanza napenda kumshukuru MUNGU kwa kunipa pumzi leo, hadi nimesimama hapa kwenu. Bila yeye, mimi si kitu,” Sauti ya Limasi ilipaa baada ya kupewa wasaha wa kuongea. “Pili nimshukuru dada yangu Timasi, yeye ndiye kila kitu kwangu hasa baada ya wazazi wetu kuondoka duniani. Yeye na mumewe, wamekuwa bega kwa bega hadi nikafika hapa leo. Mume wangu Idris, umekuja kuwa wa muhimu sana kwangu. Nakuahidi nitakuheshimu na kukutunza daima. Hilo ndilo kubwa. Wazazi wangu popote walipo, juweni kuwa nawapenda sana na nimewakumbuka sana.” Kimya kikatawala wakati wa maneno hayo machache. “Pia ndugu wa baba na mama na wageni wote mliofika, sina cha kuwapa zaidi ya upendo wangu kwenu. Nawapenda sana jamani.” Watu wote ndani ya ukumbi wakanyanyuka na kupiga makofi kwa maneno hayo machache aliyoyaongea Limasi.
Upande wa mwanaume, pia Idris aliongea na kuhadithia historia ya uongo kuhusu wazazi wake. Wapo walioguswa na wapo waliosikitika sana na kuamua kumpa pole. Hivyo ndivyo harusi ya Idris na Limasi ilivyochukua nafasi katika Jiji la Arusha na wakati huo, mashirika ya kipelelezi na kijasusi, yakiwa yanamtafuta kwa udi na uvumba.
****
“Uzo, umeona hii video?” Ally Ahmed Ally, Mkuu wa CIA, alikuwa anacheza video ambayo ilikuwa inaonesha jinsi Uzo alivyokuwa anamlazimisha Dokta Ice ataje mambo aliyoyafanya. Video hiyo ndio ilionesha kifo cha Dokta Ice pia.
Walikuwa wamekutana kwa mara nyingine ili kupata muelekeo sahihi wa kumsaka Idris na siku hiyo, Ally alikuwa ana ahueni juu ya majibu ya kile wanachokitafuta.
“Hiyo video, mimi nilikuwepo, halafu unaniuliza kama nimeiona tena? We’ vipi bwana?” Alibwata Uzo.
“Yawezekana ukaigiza filamu lakini ukuwahi kuiangalia, ndio maana nimekuuliza.” Akaongea Ally.
“Nenda kwenye mada husika Ally.” Waziri wa Ulinzi ambaye alikuwepo wakati anatoa majukumu ya kumsaka Idris, aliongea na kumfanya Ally asimame na kwenda pale kwenye video.
“Sikilezeni hapa kwa makini alichokiongea Dokta Ice.” Akacheza video ile baada ya kuongea maneno hayo.
“Unajidanganya. Mimi ndiye alpha na omega kwenye kutengeneza hiyo kemikali na kuifanya iwe bora zaidi. Nilioshirikiana nao, wote mliwaua. Bado mimi ni jiwe la pembeni.” Maneno hayo ya kwanza yakasikika toka kwenye video, Wote waliokuwepo kwenye mkutano wakawa kimya zaidi.
“Una uhakika Ice?” Swali la Uzo pia likasika
“Unauliza maembe Tanzania mwezi wa kumi mbili?” Jibu hilo likamfanya Bastian, Mkuu wa FBI kurudisha mgongo wake kwenye kiti.
“Inaonekana unapajua sana Tanzania. Hamna kitu wale, tukiamua kuiangamiza ni dakika tano tu.” Ally hakutaka kuendelea kucheza video ile hadi mwisho bali kuirudisha tena nyuma hadi kwenye maneno aliyoona ni picha ya kuanzia kwenye upelelezi wake.
“Unauliza maembe Tanzania mwezi wa kumi mbili?” Akacheza sehemu hiyo kama mara saba kwa kuirudisha rudisha nyuma. Waliokuwepo kwenye kikao wote wakawa wameelewa anachomaanisha Ally.
“Unataka kusema Soldier yupo Tanzania?” Akauliza Uzo na wakati huohuo, Ally alirudi kwenye kiti chake na kukaa kabla hajajibu.
“Hapana. Nachotaka kukwambia, hivi sasa kaoa pia, huko Tanzania. Na hamna mpango wa yeye kurudi huku.” Akajibu Ally.
“Kwa hiyo unaushauri nini Ally?” Akauliza Waziri wa Ulinzi.
“Tanzania ni marafiki zetu sana. Na hawana uwezo wowote wa kutupiga wala kutengeneza silaha kama ile. Kwa nini tusimuache tu?”
“Yule ni zao letu bwana.” Akawaka Uzo. “Tukimuacha halafu akitoka kwenda nchi nyingine je?” Akazidi kupayuka.
“Kwa hiyo tufanyaje Uzo?” Akauliza Bastian, mkuu wa FBI.
“Tukachukue kilicho chetu.” Akajibu kifupi.
“Kwa sasa anauraia wa Tanzania. Anajulikana ni Mtanzania aliyeishi Marekani. Ni ngumu kumrudisha.” Akatiririka Ally.
“Wapelelezi wa kule wanasemaje kuhusu huyu mwanajeshi wetu?” Akauliza Waziri wa Ulinzi.
“Niliongea na Shirika la Siri la Kipelelezi la kule, wakaniambia wao hawawezi kumkamata mtu wa aina ile kabla ya kupata ruhusa toka kwa Rais wao. Tuliwatumia na video za jinsi mwanajeshi yule anavyofanya kazi. Wakasema watamuangalia asifanye ujinga wowote na yaonekana anatabia njema tu.” Akajibu Ally.
“Hamna tabia njema, yule arudishwe tu huku.” Akabwabwaja tena Uzo.
“Walipoongea na Rais, wakaambiwa kuwa jamaa anatakiwa arudishwe Marekani, kweli. Lakini hawataki waajeshi wetu waende kule kumkamata, wakasema watamkamata wenyewe.” Akaongeza Ally.
“Wataweza. Kuna mtu anaweza kumkamata yule Tanzania?” Akauliza Bastian kwa mshangao.
“Ndio. Rais wao alisema anamtu wake anamuamini sana katika hilo.” Akajibu Ally.
“Mh! Ni nani huyo?” Waziri wa Ulinzi akakaa kitako kusikia mtu ambaye hadi Rais wa nchi anamuamini.
“Wanamuita ‘The Undercover Agent’ au Agent Zero.” Akajibu Ally na kuendelea. “Wanasema huyo ndiye tegemeo la nchi ya Tanzania…” Hakumaliza, Waziri wa Ulinzi akamsitisha maelezo yake.
“Basi, namjua huyo. Hamna kitakachoshindikana.” Waziri akaongea.