Simulizi ya Kijasusi: C.O.D.EX.

Simulizi ya Kijasusi: C.O.D.EX.

33.

Siku ya pili mapema nilirudi kule kambini kwaajili ya kuanza mipango ya kuisambaratisha, na kutikana na cheo basi sikusachiwa hata kidogo. niliitumia nafasa hiyo kuingia na nyaya kadha pamoja na vitu muhimu vya kutengenezea mabomu. Kutengeneza mabomu nimejua kwa sababu ni moja kati ya kozi nilizopewa kipindi nataka kuwa sniper. Nilifanya kila kitu changu nikijuwa zimebakia siku mbili tu mpaka mabomu yafike nchini humo. Usiku siku hiyo sikutoka kama ilivyo kawaida, na pia sikulalala nilizunguka zunguka na kujichanganya na wenngine lengo na madhumuni ilikuwa ni kukagua eneo zima ili kwanza nijue wapi kunakaa silaha maana naelewa kuwa ili kumpunguza nguvu adui yako ni lazima umnyang'anye silaha kwanza. Na kweli nilifika kwenye ghala la silaha na kushangazwa na silaha nzito zilizokuwemo katika ghala hilo vikiwemo vifaru ambavyo tayari vimesachorwa bendera ya Al-shabaab, niilkuta na nguo ambazo wanazivaa Al-shabaab katika kutekeleza mashambulizi. Niliangalia kushoto na kulia na nilipoona hakuna mtu mwengine kwenye ghala, nilitoa vitu kama vigololi viwili na kuviingiza kwenye boxi la mabomu aina ya grenade. Vigololi hivo ni mabomu madogo sana lakini ya uwezo wake wa kuripuwa ni mkubwa sana, baada kuviseti niliondoka na kurudi chumbani kwangu. Nilipofika nilianza kutengeza mabomu mengine aina ya C4, natumai wengi mtakua mnaelewa kasheshe ya bomu hili. usiku mzima sikulala, nilihakikisha paki pambazuka niwe tayari nishaakamilisha kazi ile maana siku zilikuwa hamna tena. Ilibakika siku moja tu kabla ya ndege inayokuja na mabomu kufika. Siku nilipanga nikitoka kambini hapo natoka kama sergent Jones lakini nikirudi narudi kama David Robert Mccanon. Asubuhi mapema niliamka na kuungana na wengine katika mazoezi na kwa sababu hata mimi mwenyewe nilitrainiwa na jeshi la marekani hivyo niliafahamu mazoezi yote vzuri sana.
Baada ya mazoezi nilirudi chumbani na kujimwagia maji, baada ya hapo nilikula gwanda safi na wakati nasachisachi nikafungua box fukani hivi na kukuta yale mambo nnayoyapenda. Kulikuwa na pistol semi-auto, revolver, shotgun, mashine gun six rounds, AK47 pamoja na mwana nimpendae kuliko wote sniper.

Nilijkuta nikitabasamu bila kutaka lakini swali likawa ni jinsi ya kutoka nazo humo kambini maana huruhusiwi kutoka na silaha. Niliumiza sana akili maana kwa wakati nilizihitaji kuliko kitu kingine chochote "nitatoka nazo tu" nilijisemea na kutafuta begi la kutilia silaha nikaanz kuziweka humo, ilibidi nizipangue ili kuepuka kushtukiwa. Kazi hiyo niliifanya kwa nusu saa, mara mlango ukagongwa. Nilipofungua nikakutana na kijana

“sergent unahitajika chamber kuu" aliongea na kuondoka, nilijiandaa na kuelekea huko, nilipofika nilikutana na raisi mstaafu akanipa karatasi na kunambia nchukue vijana wengine watatu tuelekee baharini sehemu ambayo ndege ndio ingetua kwaajili ya kufanya maandalizi ya mwisho kabla ya kufika kwa ndege hiyo ambayo itatua baharini.
 
34.

Niliitika na kutoka na kuelekea sehemu ya mazoezi, niliwakuta wanajeshiwengine wakiwa wapiga story. Bila kuchelewa niliwaita wanne na kuwaambia wajiandae, waliitika na kuelekea vyumbani mwao na mimi nilikwenda chumbani kwangu na kubeba lile begi. Mpaka hapo niliona Mungu yuko karibu nami, nilitoka na kuelekea sehemu ya magari na kuwakuta wakinisubiri. Naam na kila mmoja alitoka kamili gado maana ilikuwa ni kuweka ulinzi. Tuliingia kwenye gari na kutoka kambini kwa mwendo mdogo, haikuwa ngumu kufika sehemu ile. Tulipofika nikatoa ile barua na kusoma
.
" hakikisha vijana ulowachukua ndio wanaobeba mabomu na kujitoa muhanga, tumia jina la nchi yetu kuhakikisha wanakubali na wakikataa wauwe wote" nilishtuka sana baada kusoma ile barua mpaka wale vijana wakaniuliza imeandikwa nini.

"mnajua tunalotaka kulifanya ni hatari sana" niliwauliza,

"ndio lakini tunafanya kwa ajili ya nchi yetu" mmoja wao alijibu.

"Ukishafanya kwa ajili ya nchi yako wewe unalipwa nini" nilimuuliza kwa hasira kidogo, alikaa kimya.

"Nikikwambieni kuwa mimi sio sergent Jones mtaamini" niliwauliza tena, walicheka kidogo wakizani nafanya utani.

"najua mtakuwa mshawahi kusikia kuhusu mtu anaeitwa David Robert Mccannon" niliwauliza tena "dah! naskia huyo jamaa ni hatari hata awepo mita miatano hakukosi na sniper yake" mmoja alijibu

"halafu naskia anachapa mbaya yaani ni hatari kuliko ukoma" mwengine alidakia,

"halafu naskia ni mtaalamu sana na anaweza kujibadilisha kuwa mtu yeyote yule" mwengine aliongea na ghafla wote wakanyamaza na kuniangalia. Baada kuona wakiwa na waswas na hapo ndio nikavua kile kinyago kisha nikwapa ishara wasijaribu kuto kunyanyua silaha zao "huyo David ndio mimi, lakini kawaida yang huwa siuwi mtu ambae sijakusdia" niliwaambia na kidogo wakapumua maana waliona hali ilishakuwa mbaya. Kisha nikawarushia ile karatasi, baada ya kuisoma walitumbua macho kama mijusi waliobanwa na milango.

"hiyo ndio faida mnayoipata kwa ajili ya kuitumikia nchi yenu, nyie mnakufa huku wenzenu wakirudi nyumbanii wanapandishwa vyeo na nyie picha zenu zinavalishwa maua na kuwashiwa mishumaa halafu wanasema hawa wameuza maisha yao kwa ajili ya nchi hii halafu mnasahaulika kabisa" niliwaambia na kuonekana maneno hayo yamewaingia kisawasawa vichwani. Baada ya hapo niliwasimulia mkasa wangu wote na kuwashishi kuungana na mimi ili tufanye kazi ya kuikimbo nchi isio na hatia kuingia matatani.
Walikubali kwa moyo mmoja, tulikubaliana kuwa ikifika ndege tunawateka marubani kisha wao wanne wanaondoka na ndege ile kurudi nayo marekani hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya usalama wao. Baada ya maongezi mawili matatu nilichukua lile begi na kumwaga silaha zote lakini zilikuwa zimepanguliwa, walishangaa kuoa vile.


"nani anaweza kuzipanga hizi bila kukosea" niliwauliza lakini hakuna hata mmoja aliejibu hiyo ilimaanisha kuwa hakuna hata mmoja ambae anaweza. Basi niyaka kuwaonyesha kama mimi ni moto wa kuotea mbali, nilitoa kitambaa cheusi na kujifunga machoni kisha nikakaa chini na kuanza kuzipanga. Nilianza na sniper, nilweza kufanya hivo kwa sababu kila kipande nilichokishika nilijua ni cha bastola gani. Kipindi nikiwa training, nilifundiswa kuunga silaha katika kiza kizito na kunawakati niliunga silaha wakati nakimbi kwenye mabonde na milima.
 
35.

Siku nyingine ilikuwa hatari zaidi, niliunga wakati nashambuliwa japo hazikuwa risasi za kwenli lakini usiombe zikakupata uanweza kupoteza fahamu. Nusu saa baadae nilikuwa nimeshamaliza kuunga zote, nilipofungua macho niliwakuta wote wakiwa hawaamini nilichokuwa nakifanya. Nikawaambia kuwa hayo ni mambo ya kawaida hasa unapopewa mafunzo ya kuwa muuaji. tulipiga stori nyingi sana huku tukujaribu kuzoeana, kiza kiliingia nikawaambia wafungue mahema na wapumzikie. Mimi nikatoka kidog na kurudi kule nyumbani kwangu, nilipofika niliingia moja kwa moja katika kile chumba cha serjent Jones. Nilimkuta akiwa kalegea kwa njaa, nikamwambia asihofu mimi sitamuua ila nilihitaji akae pale kwa muda kidogo ili niweze kumaliza kazi zangu. Japo alikuwa lakini hakuacha kunyesha kama anachuki juu yangu. Basi nkamchoma sindano yenye Glucose ndani yake ili kunfanya aweze kuendelea kuishi. Nilichukua baadhi ya vitu muhimu na kuvificha sehemy nje ya nyuma hiyo, nilipohakikisha hakuna ushaahidi kama nilikuwa pale nilimchoma sindano ya usingizi kisha nikamfungua na kumuacha ili akiamka arudi kambini. Baada hapo niliondoka na kurudi kule baharini kwaajili ya kuipokea ndege ambayo ilikuwa inaingia asubuhi. Nilipofika niliwakuta wale wanajeshi wakiwa makini sana maana nilipotokeza tu mmoja wao aliinua mtutu wake na kuelekeza kwangu. Nikamuonesha ishara ambayo tulikubaliana na hapo akanitambua, usiku huo mimi sikulala japo wao wote walila. mapema alfajiri niliwaamsha na kuwaambia wajiandae kwani muda si mrefu ndeg itatu, kisha nikatoa karatasi ndogo pamoja na flash nikamkabidhi mmoja wao na kumwambia wakifika tu amkabidhi karatasi ile pamoja na flash muheshimiwa raisi. Waliponiuliza vipi kuhusu mimi, nikawajibu tutakutana makao makuu nyumbani huko. Wakati tukiendelea kuongea kwa mbali niliiona ndege ikitua katika maji na taratibu tukasogea mpaka karibu na maji hasaa, ilisimama na rubani akashuka nilimpa ishara kuwa sisi ndo tulokuja kumpokea lakini alionesha kuwa na wasiwasi maana alijua sergent ndio mpokeaji, nililishtukia hilo na kabla hajafanya chochote nilimpasua kichwa. Nikawapa ishara haraka waingie kenye ndege na waondoke,na wao bila kuchelewa walfanya hivo. Kwa mbali nilianza kusimia milio ya gari ikija upande wetu, hivyo nikawapa ishara waondoke haraka. Na mimi nikatafuta sehemu nikajificha maana eneo loe hilo nilikuwa nimetega mabomu, kwa mbali ni niliiona ndge ikizama kwenye mawingu. Nilitabasamu kidogo nikajua ule muda wa kuwamaliza umefika.
Nilitulia sehemu niliojificha mpaka walipoingia katika eneo lenye mabomu na hapo hapo gari zao kadhaa ziliripuka na kuwafanya wasimame. Njia pekee ya kupanda nao ilikuwa ni kwa mfumo kombolela, sikutaka kutumia silaha zang kwanza maan nilijuwa nikizimaliza wataniua. Nilichokuwa nakifanya ni kuwavizia na kuwaua pasi na wengine kujua, kwa kweli mchezo huo ulinifurahisha sana hata sijui kwanini. Walipoona hali imekuwa mbaya waligeuza na kukimblia kambini kwao,ila kabla hawajaondoka niliwahi kuingia chini ya mvungu wa gar moja na kukamata ipasavyo nisije nikaanguka.
 
36.
Malengo yangu ilikuwa nijitahidi kuwa hai mpaka siku ya pili msaada kutoka marekani utakapofika lakini raisi mstaafu ilikuwa ni lazima afe tena kwa mikono yangu. Waliingia kambini na moja kwa moja kuelekea ofisini kwa bosi wao, na haukupita muda ilipigwa honi ya hatari na wote walikusanyika na mimi nikiwemo lakini kwa vile mavazi yangu yalifanana na yao hawakunijua. Mbele alisimama sergent Jones "tumepata tatizo kubwa sana, na tunatakiwa kuanzia sasa tuwe makini sana maana kuna mtu anaitwa David Robert Mccannon. Huyu mtu ni hatari sana kuliko mnavofikiria na anawezakuwa yoyote miongoni mwetu, sasa baada kutano huu tuelekee kwenye ghala la silaha. Hii ni vita na vita hii tunapambana na mtu mmoja tu". Alimaliza kuongea na hapo walianza kuelekea katika ghala lakini kabla wahajafikia, nilitoa remote ndogo na kubonyeza kitufe papo hapo ghala liakaripuka wote wakabaki wameshangaa tu. Nilirudi chini ya mvungu wa ile gari na kutoa silaha zangu kisha nikaingia ndani bila kutambulikana kwa sababu kila mtu alikuwa akijaribu kuokoa maisha yake..
"simama" niliskia sauti ikitokea nyuma yangu, nilisimama ila sikugeuka maana sauti ile niliijuwa kama Serjent Jones, alikuja kunishika bega ili nigeuke na mimi sikusita niligeuka ila iliyangulia ngumi nzito iliogota usoni mwa serjent Jones. Alishtuka sana baada kuniona "afadhali tumekutana ili tumalize deni kati yetu" aliongea huku akisimama, "hakuna kutumia silaha wala kuita mtu, hapa ni mimi na wewe na mmoja tu kati yetu ndie atakaetoka mzima" aliendelea kuongea na kunifanya nitabsamu. nilivua silaha zote nkaweka pembeni na yeye akatoa bastola ndogo na kuitupa chini. Alinifwata kwa kasi huku akirusha ngumi kadhaa ambazo nilifanikiwa kuzikwepa bila shida, alipoona vile aligeuka na kuja tena lakini safari hii alikuwa makini zaidi. Alirusha ngumi kadhaa ambazo ziliishia mikononi mwangu kwa kuzipangua na kumtandika ngumi nzito ya tumbo. Alitoa sauti ya maumivu japo hakutaka nijue kama imemuingia, kwa kasi ya ajabu nilimfata na kurusha ngumi kadhaa ambazo chache alifanikiwa kuzipangua lakini nyingine ziliingia sawa sawia katika mwili wake. Kinachonisaidia mimi ni kwamba situmii aina moja ya ngumi katika kupanda,huwa nachangaya. Kama hapo nilitumia aina ya mchezo unaitwa tai boxing, baada kumuona ana mawenge nikabadilisha kukaa katika mkao unaojulikana kama nekoashidat, huo ni mkao wa saba katika karati. Nilimdanganya kwa mguu wa mbele na bila mategemeo alijikuta akiambulia teke zito la shingo na kumtupa huko. Ila alikuwa mbishi kwelikweli alisimama ila kabla hajakaa sawa, niliinama na kurudi juu na mfumo wa ngumu wa boxer, nilimtandika ngumi ya kidevu maarufu kama uppercut na kumrusha juu kabla hajatua nikamsindikiza na teke la tumbo na moja kwa moja alienda mpaka kweny chuma kilichoingia mgongoni na kutoke tumboni.
Baada hapo niliokota silaha zangu na kuondoka, nilianza kumsaka raisi mstaafu bila mafanikio yoyote. NIliingia katika chumba kimoja na kabla hata sijaangaza vizuri nilihisi kitu kizito kikinipiga kichwa na kupoteza fahamu. Nikuja kushtuka baada kumwagiwa maji ya uso, na nilipofungua macho nilimuona raisi mstaafu akiniangalia huku akicheka kwa dharau."unajua mi nilidhani mtu anakufa mara moja tu lakini kwa wewe imekuwa tofauti, mara hii nakuahidi utakufa kweli na hutaonekana tena duniani" aliongea huku akichezea bastola yake ndogo. "labda katika ndoto zako ndio nitakufa lakini kaa ukijua wewe utakufa mwanzo kabla yangu" niliongea kwa hasira. "hahaha... sasa hebu jiangalia wewe ndie uliefungwa kwenye kiti halafu chini ya kiti hicho kuna bomu, unasema nitakufa mimi mwanzo" alijibu huku akicheka. Nikajisemea kasahau huyu kama katika kichwa changu kuna GPS tracker, na ninauwezo kuhack kitu chochote ambacho kina mfumo wa mawasilino. basi bila kuchelewa nikaanza kuihack remote ya bomu ambalo lipo chini kwenye kiti nilichokaa. wakati huo yeye alikuwa akiongea tu bila kujua kuwa wala nilikuwa sijui anaongea nini. Nilipohakikisha nishaivuruga remoti ile nilianza kuzungusha viganja vyangu ili nione kama kuna uwezekano wa kuvitoa katika pingu alionifunga.
 
37.
MWISHO C.O.D.EX. 1
(SEASON 1)



Ila sikufanikiwa, "muda wako wa kuishi duniani umwekwisha, kwa heri maana naskia jeshi la nyumbani lishafika kuja kuniokoa" alisema huku akiondoka. Hiyo ndio ikawa nafasi pekee ya mimi kutoka katika kiti hicho, kwa nguvu zangu zote nilijirusha na kuanguka, kiti kilivunjika na mimi bila kuchelewa nikasimama, nilikiteuwa kiganja changu kimoja ili nitoe pingu na nikafanikia japo maumivu yalikuwa makali lakini sikujali. NIlitoka chumbani humo huku nakimbia kumfata, kisha nikatuma kodi kupitia kichwa changu na lile bomu likaripuka. Nilimkuta akiwa kasima huku anacheka, nilimvizia na kumtia kabali kisha nikamvuta ndani na kuingia nae katika chumba kimoja hivi. "leo nataka nikuonyeshe maumivu ya kuungua na moto" nilimwambia huku nikimwagia mafuta ya taa, "tafadhali usinichome,nina familia inanitegemea" alijaribu kujitetea. "unajua saa hivi kama una familia, lakini kipindi ukinitenganisha na familia yangu hukujali kama ningeteseka kiasi hichi" nilijibu huku machozi yakinitoka. "Mungu akuingize katika moto mkali kuliko yote huko unakokwenda, nakutakia safari ya misukosuko iliojaa mateso, manyanyaso na fedheha" niliongea maneno hayo kuwasha kibiriti na kukiangusha kwenye mafuta. Alipiga kelele lakini wala sikujali nilitoka nje na kukuta kumeshaanza kupambazuka, sikutaka kusubiri niliondoka eneo hilo na kutafuta pahali nikajisafisha, mwili wangu niliuhisi umekuwa mwepesi. Nilivaa mavazi ya kiraia kisha nikatoa simu na kumpigia yule kijana aniletee taxi.
Hakukaa sana alifika na taxi, niliingia na kumwambia amwambie dereva anipeleke auwanja wa ndege. Muda huo mawazo yangu yote yalikuwa kwa mwanangu Christina na mke wangu mtarajiwa Tania. Nilifika uwanja wa ndege na kumlipa yule dereva, kisha nikatoa mfuko mdogo nikamkabidhi yule kijana na kumwambia "hizo ni dola elfu tano, anza maisha yako upya na ujiajiri mwenyewe" alifurahi sana. tuliagan na mimi nikaingia ndani na kukata ticket ya kuelekea marekani, masaa kadhaa baadae ndege ilitua. Nilishangaa sana nilipotoka nje baada kuona gari za serekali zikiwa zinanisubiri, ukweli nilijua tayari naenda kuozea jela lakini kabla sijaamua la kufanya nilimuona kija mmoja kati ya wale wanne akija. KIdogo nilikaa sawa, alipofika aliniambia kuwa nahitajika white house. Tuliingia kwenye gari na kuelekea huko, nilikutana na raisi na kuongea mambo mengi lakini nikamwambia siko tayari kufanya kazi ile tena na sasa nataka kuanzisha maisha yangu ili niwe na familia yangu. Alinielewa na kuaguza nipewe ulinzi mpaka Califonia ambako ndipo alipokuwa mwangu Christina. Japo mwanzo hakunijua lakini kwa msaada wa baba mkwe wangu mambo yalikuwa mazuri. Nilitoa simu yangu na kumpigia Tania na kumuuliza yupo nchi gani, alinijibu kuwa yupo London. NIkamwambia apnde ndege aje Califonia nae hakupinga, siku ya pili mapema nilikwenda kuompokea na kumpeleka nyumbani. kwa vile mi sikuwa na wazazi,niliwafanya wake zangu kama wazazi wangu na kuwaeleza kila kitu. Walikubali na baada miezi miwili Tania aliacha kazi ya ndege na tukafunga ndoa. Na mpaka sasa tunaishi pamoja na tuna watoto wanne,Christina ambae anamiaka 22 na ni personal secretary wa rais, Jeff ambae ana miaka 18 na yuko high school, Edward ambae ana 12 na yuko junior school na wa mwisho ni Tatiana ambae ana mika 3 na yuko baby class.
.
NA MIMI SIE DAVID ROBERT MCCANNON KWA SABABU ALIKUFA SIKU ILE NILOMUUA ADUI YANGU MKUBWA.

JINA LANGU NI JAMES ALLEN
MWISHO.

HUU NI MWISHO WA C.O.D.E.X season one.
Kwa Season two, kaa hapahapa.

Tariq Haji anawapa shukrani wote mliokuwa mnamsapoti katika kazi hii kwa hali na mali na kumkosoa kwa makosa ambayo mliyaona.
Bado anajifunza kupitia waandishi wengine, hivyo anaomba zaidi muwe mnamfunza hasa pale mnapoona makosa ambayo yanajitokeza kwake mara kwa mara, yaani yale ambayo yanaonekana kwake ni ubovu na si yale ya bahati mbaya.

Kaa tayari kwa Season Two.

Imedhaminiwa na BURE SERIES​

 
2.jpg


Simulizi : C.O.D.EX. 2
Mwandishi : TARIQ HAJI
Imeletwa kwenu na: BURE SERIES


SEHEMU YA 38




"Mkuu Marine base 71 imepata tatizo" aliigia Hansen huku akihema katika ofisi kubwa za CIA Marekani, "unasemaje wewe?" aliinuka huku akifoka Ms Helen. "Ndio taarifa tulizozipata muda huu na inasemekana mmoja kati ya wale vijana ambao wapo katika project inayoendelea ametoroka" Hansen aliongea huku akijiweka sawa. "Shit bila shaka huyo atakuwa Project 75" aliongea Ms Helen aliongea huku akijishika kiuno, "hebu waambia wawakague halafu watuambie ni yupi ambae ametoroka" alimaliza kuongea na Hansen akatoka..
Ms Helen alikaa kwenye kiti chake na kushusha pumzi kwa nguvu, maana aliwaza awaambie nini wakubwa wake. Robo saa Hansen alirudi tena huku akiwa na huzuni, "wala hujakosea, alietoroka ni project 75" aliongea Hansen. "Hapo ndio kwenye tatizo kubwa maana unafahamu mara ya mwisho alivotoroka ilituchukua mwaka mzima mpaka kumkamata" Ms Helen aliongea huku akikuna kichwa, alionesha kuchanganyikiwa. "Na kipindi kile alikuwa na miaka kumi na tatu tu, sasa saa hivi ana miaka kumi na nane unadhani tutafanyaje na ikiwa ataendelea kukaa uraiani itakuwa hatari kwetu sisi" aliendelea kuongea Ms Helen huku akionyesha kukata tamaa. "Sasa tunafanyaje mkuu" Hansen aliuliza, "wewe nenda kaendelee na mambo mengine" Ms Helen alijibu na Hansen akaondoka.
"Habari bosi kuna tatizo huku limetokea, naomba kesho asubuhi nije kuonana na wewe" Ms Helen alitoa simu yake na kupiga. Baada kukata simu alibeba begi yake na kutoka ofisini, siku hiyo ilikuwa imeharibika kabisa hata hamu ya kufanya kazi iliondoka kabisa.
**********************************
Jitihda za kuzima moto ambao ulikuwa ukiendelea kuitekeketeza Marine Base 71 ziliendelea huku wakijitahidi kuuzuia moto huo usisambae sehemu nyingine. "Mkuu tuna tatizo kubwa, project 75 ametoroka" sajenti Louise aliongea, "ah huyo dogo anatabu sana, tuma boti sita ndogo zifanye msako atakua hajafika mbali" General David alijibu na kutoa amri ziachie boti kadhaa kwa ajili ya kumtafuta project 75. Sajent Louise aliondoka na kuelekea kwenye vikosi maalum vya msako, alitoa amri hio boti sita ziliingiz kazini kumsaka kijana machachari na hatari kuliko wote na hakuwa mwengine bali ni project 75.
Muda uliyoyoyoma lakini haikurudi hata moja, muda ulizidi kukatika bila kuwepo kwa mawasiliano kati ya wale walikwenda kumtafuta na kambi yao. "Vipi kuna majibu yoyote" aliuliza General David wakati akiingia ofisini kwa na kumkuta sajent Louise huku akiwa amejiinamia. "Habari ni mbaya tu mkuu, nimefanya vile ulivonambia lakini, umepita muda mrefu bila mawasiliano na wale waliokwenda, ndio nikaamua kutuma kikosi kingine kwenda kuangalia lakini wamerudi na boti tano zikiwa na miili iliotapakaa damu halafu mafuta ya boti hizo zote yalikuwa yamekwisha" alijibu sajent Louise.
"Dah huyu kijana ana balaa kwa kweli," sawa wacha niwasiliane na makao makuu niwape taarifa za kutoweka kwa Project 75" aliongea General David na kwenda moja kwa moja kwenye mkonga wa simu ambao ulikuwa umewekwa pembeni. "Hali ni mbaya kwa kweli, na alietoroka ni Project 75" aliongea kwenye mkonga huo na baada mangezi machache alikata simu na kukaa kwenye kiti chake huku akiwa ameshika kichwa asijue nini la kufanya. Jitihada za kuuzima moto huo zilifanikiwa lakini ulichukua muda mrefu sana hivyo vitu vingi viliteketea. Wanajeshi kwa pamoja walisaidiana kutoa mabaki ya vitu vilivyoungua.
Marine Base 71 ni moja kati ya kambi kubwa za siri ambazo hazijulikani na raia wa kawaida, ni miongoni mwa kambi ambazo kunafanyika uchunguzi juu ya swala zima la kuweza kuzalisha wanajeshi ambao watakuwa na uwezo kuliko kawaida. Kambi hii ipo katika kina kirefu sana cha maji katika kisiwa kimoja miongoni mwa visiwa vinavyopatikana katika bahari ya Pacific. Kwa jumla kambi kama hiyo zipo zaidi ya kumi lakini hii ndio ilikuwa kubwa kuliko zote. Na serekali imeamua kufungua kambi hizo kwa siri baada ile kemikali aina ya Cindrex ootliviaso deca endroline X (CODE X) kugundilika baada ya aliekuwa mtu wa kwanza kuitengeza kupoteza ushahidi kabisa ili isiendelee kutumika.
 
39

Mwanasayansi huyo aliejulikana kwa jina la Melinda alipoteza ushahidi juu ya kemikali hiyo baada kugundua madhara itakayosababisha ikiwa itaingia mikononi mwa watu wabaya. Lakini kama ilivyoada ya wanasayansi kutokubali kushindwa jambo, walianza kufanya uchunguzi tena kupitia nakala maalum waliopewa na mwanasayansi ambae alimsaliti Melinda na kuuza uchunguzi huo. Kazi haikuwa rahisi katika kufanikisha hilo lakini walijitahdi kadiri ya uwezo huku wakiahidiwa donge nono ikiwa wataitengeza tena. Na ndipo mwanasayansi mmoja anejulikana kwa jina la Dr Hudson alipofanikiwa kuitengeza tena kwa mara nyingine.
(siku tatu baadae)
Watu wengi walionekana kukusanyika katika eneo moja kweny fukwe za bahari, walionekana kushangaa kitu fulani na minong'ono ya hapa na pale iliskika. "Hebu mguse labda ni mzima", "hapana usimguse sasa hivi gari ya wagonjwa itafika kumchukua", walisikika watu wakiongea huku kila mmoja akiongea la kwake. Dakika moja mbele gari ya wagonjwa ilifika na bila kuchelewa walishuka na machela kwenda mpaka alipo mlengwa. Kwa uangalifu na tahadhari ya hali ya juu walimnyanyua na kumuweka kwenye machela kisha wakaelekea kwenye gari na safari ya hospitali ikaanza.
Kutokana na sheria zinavosema kuwa gari ya wagonjwa ikiwa inapita gari nyingine zote zinatakiwa kukaa pembeni kuipisha. Robo saa walikua washafika hospitali, kitanda kilishushwa kwenye gari na kukimbizwa wodi ya wagonjwa mahututi. Madaktari walifika na kuanza kutoa huduma, kutokana na chumvi shati ilikuwa imegandana na mwili hivyo ilibidi ichanwe lakini kwa umakini wa hali ya juu. "Bado moyo wake unapidunda lakini katika kasi ndogo sana" daktari mmoja aliongea, walimpatia huduma za haraka ili kuhakikisha wanaokoa maisha yake. "Doh sijawahi ona binaadamu mwenye roho ngumu kama huyu" aliongea daktari mmoja huku akiwapongeza wenzake kwa kazi nzuri waloifanya, "wakushukuriwa ni Mungu kwa kweli" alijibu daktari mmoja wa kike.
****************************.
"Je kuna taarifa zozote za kuonekana pahali Project 75" Mr Clinton aliuliza, "mpaka sasa hatujapokea taarifa zozote, huenda akawa amezama baharini labda" alijibu Rodriguez, "hahaha unadhani atakufa kirahisi kiais hicho, sisi tusubiri tu maana hata bila kumtafuta atakuja mwenyewe kwetu" alijibu Ms Helen. "Acheni kubishana ujinga nyinyi, mnadhani ni jambo la kukaa tukabishana wakati tunaelewa wazi kuwa akirudi huyu kijana basi maisha yetu yatakuwa hatarini" alifoka Mr Clinton, na wote wakanyamaza kimya. "kesho kutakuwa na kikao cha dharura kuhusu huyu Project 75, wote mnatakiwa mufike, haya tawanyikeni" aliendelea Kufoka Mr Clinton.
Wajumbe wote wakatawanyika na kurudi katika sehemu zao za kazi. "hallow muheshimiwa raisi, ndio naelewa na tunajitahidi kadiri ya uwezo wetu kuhakikisha tunamtia mbaroni. Sawa mkuu nimekuelewa hakuna shida, nakutakia jioni njema" Mr Clinton alimaliza kuongea na simu kisha akaipiga na chini kwa hasira "naapa ukikamatwa utajuta kuzaliwa mshenzi mkubwa wee" alijisemea huku akitetemeka kwa hasira. "Rose niletee simu nyingine" Mr Clinton aliitwa kwa nguvu na kutoa agizo, papo hapo mlango ulifunguliwa akaingia binti mmoja mrembo sana mwenye asili ya kivenezuela akiwa na boxi jeupe mkononi. Alilifingua na kutoa simu mpaya kisha akaiokota ile ilovonjwa na kutoa sim card kisha akaitia kwenye ile simu mpya. "Bosi tayari simu yako" aliongea kwa taratibu huku akimkabidhi ile simu, "unahitaji kingine chochote" aliuliza. "Nihitaji nitakwambia hebu nitolee sura yako hapa nisije nikakupiga risasi bure" alijibu kwa hasira na Rose bila kuuliza jambo alitoka nje na kurudi katika sehemu yake ya kazi.
 
40
"Dokta yule kijana ameamka" aliingia nesi mmoja ofisini na kusema, bila kupoteza muda dokta aliinuka na kuelekea katika wodi aliokuwa amelazwa Project 75. "Habari yako kijana, mimi naitwa dr Jacob sijui wewe mwenzangu unaitwa nani" alijitambulisha dr Jacob. "Jina langu ni Alex Jr" alijibu Project 75, "hapa niko wapi" kisha akauliza, "uko hospitali" alijibu Dr Jacob. "Najua kama niko hospitali ninachotaka kujua niko nchi gani" alianza kuongea kwa hasira. "Punguza jazba kijana, uko South Africa" Dr Jacob alijibu, Alex Jr alishtuka aliposikia kama yuko South Africa na swali lilomjia ni kuwa amefikaje nchini humo.
"Hebu tueleze imekuwaje ukakutwa ufukweni" aliuliza Dr Jacob, swali lilikuwa gumu sana hasa ukizingatia hataki kusema ukweli kabisa kuhusu alipotoka "Amm meli nliokuwa nafanya kazi imekutana na dhoruba na kuzama, mimi peke yangu ndio nimefanikiwa kuokoka kwa sababu nilikuwa katika chumba maalum cha kuhifadhia data, chumba hicho huwa kinachelewa kuingia maji na kina mlango wa dharura ambao moja kwa moja unakwenda mpaka zilipo boti za uokozi" kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa akili Alex alifanikiwa kutnga uongo huo na kufanikiwa kuwafanya wote waamini kuwa meli yao imezama. "Basi kwa sasa kuwa na amani kabisa mpaka afya yako itakapokaa sawa ndio tutaanza mchakato wa kuwatafuta ndugu zako" aliongea Dr Jacob. "Nashkuru kwa ukarimu wako" alijibu Alex na kujilaza kitandani huku akipanga nakupangua jinsi ya kutoroka hospitali hapo maana alielewa akiendelea kukaa hapo kutawatia matatizoni wote waliohusika na kumuhudumia.
"Kuna taarifa yoyote kuhusu project 75" aliuliza Mr Clinton, "hakuna mkuu" Ms Helen alijibu. "Hebu nambieni nyie wote kuwepo hapa halafu mkashindwa kugundua ni wapi alipo huyu mwehu, hivi muna faida gani". "Usijali mkuu tumeshatuma taarifa kwa maagent wetu waliokuwepo pande zote za dunia, tunaamini kuwa atapatikana" aliongea Rodriguez. "Bosi mheshimiwa raisi kashafika" aliingia Rose na kutoa taarifa. "Sawa, jamani tuelekee ukumbi wa kikao".


"Mr Clinton nategemea kupata majibu ya kuridhisha kutoka kwako" Raisi aliongea na kudhihirisha kuwa amechukizwa na utendaji mbovu wa kazi wa watu hao aliokuwa akiwaamini sana. "Ah kwa kweli mkuu mpaka sasa hakuna taarifa nzuri hata moja" alijibu kiunyonge Mr Clinton. "Shit, siku hizi umekuwa mvivu sana Mr Clinton" alifoka Raisi. "Lakini usijali mkuu tumeshasambaza taarifa kwa maagent wetu wote na tunaamini muda si mrefu tutapata majibu" alijaribu kujitetea Mr Clinton. "Nakupa wiki moja tu, huyo mpuuzi apatikane akiwa hai au amekufa" alifoka Raisi na kisha akainuka na kuondoka. "Dah, yaani huyu bwana mdogo ananitesa kiasi hichi" alijisemea moyoni akiumia kupita maelezo.
Kikao kiliendelea baada raisi kuondoka, walijadiliana nini cha kufanya wakimpata Project 75. Ndipo wakafikia muafaka kuwa wakigundua sehemu alipo basi watume wauwaji nguli kwenda kummaliza na kurudisha mzoga huo Marekani. Kikao kilimalizika na watu wote wakatawanyika na kurudi majumbani kwao.
*******************
 
41.
"Eti nesi hii ni hospitali gani" aliuliza Alex wakati Nesi akimpa dawa za kupunguza maumivu, "hii ni Cecilia Makiwane Hospital" alijibu yule Nesi, "ah sawa" aliitika na kuchukua vidonge kisha akameza. "Usiku wa leo lazima niondoke hapa" alijisemea moyoni na kuanza kupanga mchakato wa kutoroka, wakati akiendele kupanga alichkuliwa na usingizi mzito kutokana na dawa alizokula.
"Nimesema muue", "siwezi kufanya hivo, siwezi kumuaa mdogo wangu", "sawa kama huwezi", "wewe shika bastol, haya muue yeye sasa". "hapana siwezi kumuaa kakaangu", "sikiliza mwanangu hii bastola haina risasi, kwa hiyo hapa tunajifunza kutumia tu sawa, sasa ielekeze mbele halafu bonyeza hicho kidude" alianza kubembelezwa, na kwa sababu ya akili ya utoto alifanya hivyo lakini, Ghafla Alex alishtuka kutoka usingizini huku jasho likimtoka. Alipoangalia nje mvua ilikuwa inanyesha ikiambatana na upepo mkali.
Alianza kuchomoa mashine zote zilizokuwa mwilini mwake na kushuka kitandani. Alipokanyaga tu chini alianguka kutokana na kukosa nguvu kabisa, kwa msaada wa kitanda alisimama na kuangaza pande zote za chumba hicho ndipo akaona kabati. Alisogea mpaka kwenye kabati hilo na kulifungua, alikuta vichupa vingi vya dawa lakini alichukua kimoja tu chenye vidonge vyenye glucose ya kutosha kuzalisha nguvu kwa muda mfupi. Alimeza viwili na kisha akachukua na vidonge vya kukata maumivu, dakika kumi baadae alianza kuchangamka na hapo kazi ikawa imeanza.
Alisogea mpaka dirishani na kwa bahati nzuri lilikuwa dirisha la kuburizika hivyo kulikuwa nanafasi kubwa ya yeye kupenya. Alipenya nakutoka nje kabisa kwenye varanda, akaanza kutemebea taratibu huku akijitahidi asiteleze. Alifanikiwa kutoka nje kabisa ya Hospitali bila kugundulika, tatizo lilikuwa hajui aende wapi maana alikuwa mgeni katika eneo hilo. "Oya wewe simama" alisikia sauti kwa nyuma, alipogeuka akakutana na sura nyeusi inayotisha "toa kila kitu ulichokuwa nacho" alifoka yule mtu huku akitoa kisu..
"Sina kitu labda nikupe hii gauni la hospitali na vidonge" alijibu Alex, "unasemaje bwana mdogo" alinguruma yule mtu. "Hujasikia au vipi" Alex alijibu kwa dharau. "Unaleta jeuri sio" alifoka yule na kusogea kwa kasi sehemu alipo Alex, Alex alimkwepa na kumsindikiza na teke zito la mgongo. "bwana mdogo hapa sipo bora uondoke tu" aliongea Alex huku akiwa anaondoka, yule mtu alirudi tena lakini wakati Alex hakumkwepa, alimtandika ngumi nzito ya kuromeo na kulivunja. Yule jamaa alianguka chini kama mzigo na kukata moto. Alex hakuchelewa alimvua nguo na kuzivaa kisha akatafuata njia na kuondoka eneo hilo.
"Dr yule kijana ametoroka" Nesi aliwasilisha taarifa hizo punde tu baada Dr Jacob kufika ofisini, "eti nini" Dr Jacob aliuliza kwa mshangao. "Duh ngoja niwasiliana na polisi kwanza" aliongea kisha akatoa simu na kupiga polisi, muda si mrefu walifika hospitalini hapo na kupewa taarifa zote pamoja na picha alipigwa wakati hajitambui. Baada hapo polisi walipiga simu katika vituo mbali mbali kuwapa taarifa pamoja na kutuma picha za Alex.
 
42.
"Mkuu kijana yuko South Africa" ujumbe uliingia katika simu ya Mr Clinton, na bila kuchelewa akampigia simu Helen na kumueleza. Baada ya mazungumzo hayo, Helen alitoa simu nyingine na kupiga, "halo, Gerald kuna kazi, kuna kiti moto huko South Africa tunataka ukichinje" alimaliza kuongea na kukata simu. Baada kupokea agizo hilo Gerald ambae yuko Durban South Africa alichukua vifaa vya kazi na safari ya kuelekea alipoelekezwa ikaanza. "Halo Dr Jacob, mimi ni Alex na naomba unisikilize kwa makini. Jambo ulilolifanya linahatarisha maisha yako hivyo fanya kama nitakavo kwambia. Akija mtu yoyote kukuuliza kuhusu mimi mwambie kila kitu usimfiche hata kimoja maana hiyo ndio njia pekee ya wewe kuokoa maisha yako" simu ilikatika bila Dr Jacob kuongea chochote.
"Asante kwa msaada wako" Alex aliongea wakati akimrudishia simu dada mmoja ambae alimuomba kisha akaondoka. Kwa sababu alikuwa na vidonge vya glucose hakupata tabu ya kutafuta chakula.
"Habari za kazi dada" Gerald alimsabahi, "nzuri nikusaidie nini" alijibu. "naomba kuonana na Dr Jacob" aliongea, "leo hana appointment na mtu" alijibu dada huyo lakini alihisi kitu kama cha baridi kikimgusa mkononi. "Na wewe leo huna appointment na Mungu lakini nitakupeleka hivyo hivyo ukamuone" Gerald aliongea huku akimgusa mkono kwa bastola yake. "nenda chumba upande wa kushoto" yule mschana alijibu huku akitetemeka, "mtoto mzuri hawi mbishi na ole wako useme kitu" Gerald aliongea na kuirudisha bastola yake kweye koti kisha akaondoka na moja kwa moja mpaka ofisini kwa Dr Jacob.
"Habari za saa hizi Dr" aliongea wakati akifunga mlango. "sina ahadi ya kukutana na yoyote yule" alijibu bila kuangalia. "mimi pia huwa sina ahadi ya kukutana na mtu siku zote lakini nikitaka tu huwa nakutana nae" Gerald aliongea kisha akatoa bastola na kuiweka kwenye meza. Dr Jacob alishtuka baada kuiona na kukumbuka maneno ya Alex. "naomba unieleze kila kitu unachojua kuhusu kijana uliemtibu hapa" aliongea Gerald. "Mimi natibu watu wengi hapa siwezi kuwakumbuka wote" Dr Jacob alijaribu kucheza na nyoka. "Narudia kwa mara ya mwisho la sivyo ntakufanya kitu ambacho utajuta maisha yako yote" Gerald alifoka kwa hasira.
Dr alipoona hali sio akakubali kutoa ushirikiano, alimueleza kila kitu bila kumficha hadi mwisho. "Dr asante kwa ushirikiano wako na nakutakia kazi njema" Baada kuridhika na maelezo hayo Gerald alishukuru na kuondoka. "Duh binaadamu wengine hawana hata chembe ya huruma" Dr Jacob alijisemea moyoni na kutoa kitambaa kwa ajili ya kujifuta jasho lilirowanisha koti lake japo ndani ya ofisi yake kulikuwa na AC.
"Halow mkuu, ndio nimeshamaliza hatua ya kwanza, sasa naingia mitaani kumtafuta. Usijali mkuu kazi itakwisha tena kwa haraka tu" Gerald alipiga simu na kutoa taarifa hizo, alimaliza kuongea na kurudi kwenye gari yake na kuondoka eneo la hospitali. Alex akiwa mitaani anazurura kama mtu ambae anatafuta kitu, ghafla anashangaa watu wanaanza kutimua ovyo, wenye maduka wanafunga, wenye migahawa wanafunga na kila mtu anatafuta pa kujificha.
 
43.

Alijikuta amebakia peke yake ambae amesimama barabarani, "wewe ndio unajifanya nunda eenh" alisikia sauti nzito ikitokea nyuma. "Halafu anaonekana kama nguruwe hivi" aliongea mwengine lakini kwa lugha ya kimila, "nguruwe ni wewe mweneyewe" Alex alijibu kwa kimila hivohivo na kuwashangaza wale waliovamia. "Huyu dogo anataka kufundshwa adabu kidogo" aliongea jamaa mmoja ambae alionekana kama ni mkuu wa kikosi hicho.
"Amose hebu mtengeze huyu dogo" yule kiongozi aliongea, lilitoka jitu moja kubwa sana na jeusi lenye kutisha ile mbaya. Alex alirudi nyuma kidogo kwa ajili kupata nafasi ya kumsoma mpinzani wake. Alimuangalia kwa makini wakati anakuja mbio upande wake, alipomkaribia tu, Alex alimkwepa na kusogea pembeni. Lile jiti likageuza na kumfata kichwa kichwa, Alex alikunja ngumi na kukaza miguu, lilipomfikia tu alivurumisha masumbwi manne ya nguvu iliompata kwenye sehemu ya maungio ya bega na kufanikiwa kumtegua mikono yote miwili.
Alex alirudi nyuma ili amalize kazi lakini kabla hajafanya hivo alisikia mlio wa risasi na alipoangalia vizuri alimuona yule kiongozi wa kundi hilo akianguka chini huku akiwa na tobo katika paji la uso. Kwa kasi ya ajabu alimsogelea yule aliekuwa kipigana nae na kumgonga shingoni katika mshipa wa fahamu na kumfanya azimie.
Moto ulianza kuwaka kati ya wale majambazi na mtu aliempiga risasi kiongozi wao, lakini mtu huyo alikuwemo ndani ya gari na alifanya mashambulizi yote akiwa ndani ya gari. Alex aliangalia mpambano huo kwa umakini na akagundua kuwa wanaepambana nae ni mtu aliyebobea. "hamuwezi kushindana nae huyo, atawamaliza wote bora mukimbie" Aliongea kwa nguvu kisha akachomoka mpaka walipo wale majambazi, "nipeni silaha, huyo hamumuwezi na ananitaka mimi" aliongea Alex na kuwashangaza wote pale, "okoeni maisha yenu, huyo niachieni mimi" aliendelea kusisitiza Alex.
Walikubali na kumpatia bunduki moja kubwa aina ya AK 47 na bastola mbili ndogo, "sasa pambana na mbabe mwenzio" Alex aliongea na kulenga tayri ya mbele ya gari ya anaewashambulia, alifyetua risasi na kuipasua tairi hiyo. Gari ilisimama na yule mtu aliekuwa ndani akashuka, naam hakuwa mwengine isipokuwa Gerald. "Project 75 bora ukubali yaishe, maana nimeambiwa nipeleka mzoga wako" aliongea huku akicheka, "mi nahisi wamekutoa kafara tu maana wao wenyewe wananitambua mimi nani" Alex alijibu, "tutaona" Gerald alijibu na kuanza kumimina risasi.

.
Alex alitulia na kumuacha japo azifaidi risasi zake ili atakapomuua asije akalalamika hajazitendea haki risasi zake. "acha kujificha kama mtoto wa kike" Gerald aliropoka, "unajua ningekuwa mimi ndio wewe ningekimbia tu tena kama mbwa koko na mkia wangu katikati ya miguu" Alex alimjibu kwa kumkejeli. Maneno hayo yalimkera sana Gerald, na kujikuta akitoka kichwa kichwa sehemu amabayo alikuwa amejificha ila kitu ambacho hakukitambua ni kuwa tayari alikuwa kashalalengwa na Alex. Kitendo cha kutoa sura tu Alex alimchapa risasi ya uso, "nilikwambia mimi ukadhani nakutania, nenda kwa amani na Mungu akulaze mahali panapostahiki amen" Alex aliongea huku akisimama na kuelekea ulipo mwili wa Gerald, alimsachi na kuchukua simu kisha akapiga. "ehe kazi imekwendaje" Mr Clinton alipokea kwa shauku ya kutaka kujua, "kazi imekwenda vizuri sana,nimeshamuua Gerald na sasa nasubiri mwengine chambo mwengine mtakaemtuma, lakini kaeni mkao wa kula nikishawamaliza nyungunyungu wenu nawafuata nyinyi" Alex aliongea na alipoaliza akavunja simu.
 
44.
Alikwenda mpaka walipojificha wale majambazi na kuwakabidhi silaha zao, "unakwenda wapi" aliuliza mmoja wao. "naenda zangu" alijibu kimkato, "umetusaidia leo tunaomba uje na sisi" aliongea yule mmoja wao. Alex alikubali na kwa pamoja walisaidiana kumbeba Amose na kumuingiza kwenye gari na safari ikaanza.
*****************
"ah, https://jamii.app/JFUserGuide" Mr Clintona aliropoka kwa nguvu na kutoa bastola kisha akavunja vioo na tv katika ofisi yake, "bosi punguza hasira" Rose aliingia ndani na kumuomba. "huy Alex huyu mwanaharamu mkubwa, hebu ita kikao cha dharura" aliongea na kutoa amri.Dakika kumi walikuwa kwenye kikao. "jamani taarifa ni mbaya, Gerald ameuwawa" aliongea Mr Clinton, "mi niliwaambia Project 75 ni namba nyingine" Alijibu Helen. "mimi nahisi nina wazo" Rodriguez alisimama na kuongea, "haya tuambie wazo lako" Mr Clintom alijibu. "kwa nini tusiwatumie wengine ambao ni kama yeye" Aliongea lakini kwa kusitasita, "unamaanisha tuwatumie Project waengine" Aliongea Mr Clinton. "ndio, labda tutaweza kufanikiwa kumkamata" alijibu Rodriguez. "wazo zuri lakini sidhani maana Project 75 ndie pekee ambae amemaliza mchakato wote wa CODE X" Helen aliongea. "nafahamu hilo lakini huyu kwa kuwatuma wauwaji wa kawaida kamwe hatutaweza kumkamata" Aliongea Rodriguez. "sawa nimelisikia wazo lako na nitalifanyia kazi" Aliitika Mr Clinton, kila mtu alitoa wazo lake na mwisho walikubaliana wakutane baada siku tatu kwa ajili ya majibu na kikao kikavunjwa. Mr Clinton alirudi ofisini kwake akiwa hana hata hamu ya kufanya kazi, "Rose njoo mara moja" alinyanyua mkonga wa simu na kumuita secretary wake. Baada ya kukata tu simu Rose aliingia "nikusaidie nini mkuu" aliongea, "njoo karibu" Aliongea kiupole Mr Clinton. Rose baada kusikia hivo alijua ni kitu gani amekusudia bosi wake, kila Mr Clinton alipokuwa anahasira alimuita Rose na kufanya ne mapenzi kama sehemu ya kupunguza hasira na kujiliwaza. Japo Rose alikichikia sanakitendo hicho lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali maana Mr Clinton ndie aliemfanyia mchono mpaka akafikia pale alipo.
Basi mwanadada huyo alifunga mlango na kusogea mpaka katika meza ya bosi wake, na bila kuchelewa Mr Clinton alimvamia na kutekeleza haja yake mpaka aliporidhika. Rose alivaa nguo zake na kutoka ofisini, "Afadhali sasa" Mr Clinton alijisemea moyoni. Rose alielekea mpaka chooni na kuanza kulia maana tabia hiyo ya bosi wake ilimkera sana, yeye kufanywa kama chombo cha kujiliwazia "ipo siku utalipa kwa unacho nifanyia" Rose alijesemea moyoni na kujiweka sawa kisha akarudi katika sehemu yake ya kazi. Siku hiyo ilimuendea vibaya sana maana mpaka muda wa kutoka ofisini unafika tayari alikuwa kashafanya mapenzi na bosi wake mara nne. Na wakati anatoka Mr Clinton alimuita tena na kupata cha kuondokea. Kwa kweli hakuna siku aliodhalilika binti huyo kama siku hiyo. "kila kitu kina mwanzo na mwisho wake" alijisemea moyoni akiwa kwenye gari yake kuelekea nyumbani kwake, "na leo ndio mwisho wa manyanyaso haya" aliongea na kuzidisha mwendo wa gari lake..
 
45.

Siku ya pili mapema katika taarifa za habari kulikuwa na habari moja iliosema" ajali mbaya imetokea na gari hiyo inasadikika kuwa ni ya dada mmoja anaejulikana kwa jina la Rose, chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi aliokuwa akiendesha mschana huyo".
"Kweli ni yeye au wamekosea" aliongea Mr Clinton baada kusikia taarifa hiyo, "ndio mkuu na ushahidi tushaupata" alijibu Martin. "Ah sawa kazi ya Mungu haina makosa" alijibu huku akioenakana mwenye hzuni sana. Na kwa vile hakuwa na ndugu karibu serekali ilisimamia maziko yake, na yalipokamilika waliomboleza kwa siku kadhaa na kila mtu kurudi kazini kuendelea na kazi yake.
"Karibu Alex hapa ndio nyumbani" aliongea mmoja kati ya wale vijana walioondoka na Alex, "mimi naitwa Leonard" alijitambulisha, "yuko wapi yule mwenzenu niliepambana nae" Alex aliuliza. "tumemlaza ndani" Leonard alijibu na Alex akaomba aonyeshwe chumba alicholazwa. Aliingia na kuanza kumnyoosha zile sehemu alizomtegua, wengine walikaa kimya wakimuangalia anachokifanya. Amose alipiga kelele za maumivu makali sana aliyoyapata wakati Alex anayarudisha mabega sehemu yake.
"Tayari, pumzika kwa sasa baada masaa mawili utakuwa sawa" Alex aliongea na kusimama. "Hivi wewe ni mtu wa aina gani" aliuliza kijana mmoja, "ah mimi ni mtu wa kawaida tu" Alex alijibu huku akimshika kichwa kijana huyo ambae alionekana kufurahia kitu hicho. "Hivi kwanini mumeamua kufanya hivi, kwanini mnakuwa waharibifu" Alex aliuliza wakati akikaa kwenye kigogo cha mti. "inabidi tufanye hivi ili tule, maisha yetu ni magumu sana" Leonard alijibu, kwa sasa alionekana kama kiongozi baada kiongozi wao kupigwa risasi na Gerald.
"Sio lazima muibe ili mule, nyie kama mimi bado ni vijana mna nguvu za kutosha kufanya kazi na kujikomboa kimaisha kuwa vibaka sio suala jema kabisa" Alex aliongea kama mshauri sasa, "na wewe kama nani unatuambia hivo" jamaa mmoja aliongea kwa hasira. "mimi, mimi ni mtu mmoja mbaya na hatari sana, na hapa nilipo natafutwa na jeshi la America" Aliwavunjia dafu kisha akaendelea "mimi najaribu kutafuta maisha ya kawaida nimechoka maisha ya kuwa mtumwa wa ujinga, sasa nawashangaa nyie mna ardhi nzuri hapa, mnaweza hata mkalima na kupanda miti ambayo inazaa mapema, mkauza mkapata pesa japo za kula".
"Laiti mimi ningekuwa katika nafasi yenu wala nisinge hangaika kutafuta silaha na kukaba watu, rafiki zangu bado mnayo nafasi ya kurekebisha makosa yenu" Alex alisisitiza. "Kwani we huna fursa hiyo" Leonard alimuuliza, "sina kabisa, muda wowote ntakamatwa na adhabu yangu itakuwa ni kifo tu" Alex alijibu. "Kwa sasa kaa na sisi hapa" Leonard aliongea na Alex akakubali.
************************************
"Karibu Russia madam, mimi naitwa Nikolay" aliongea mwanaume wakati akimpokea mwanadada mmoja mrembo sana. "Asante mimi naitwa Christine" alijibu mwanamke huyo na kuingia kwenye gari, Nikolay aliweka mizigo kwenye buti na yeye akaingia kisha akampa dereva ishara waondoke. "kila kitu nilichoagiza kipo tayari" Christine aliuliza, "ndio madam kila ulichosema kipo" Nikolay alijibu. Safari iliendelea kwa muda mrefu sana mpaka walipofika katika nyumba fulani nje kidogo ya mji wa Moscow.
 
46.
"Hii ndio nyumba ulioagiza" Nikolay aliongea kisha Christine alishuka kwenye gari na kuingia kwenye nyumba hio. "Ni nzuri sana na inanifaa" Aliongea baada kuridhika na ukaguzi mfupi aliofanya, baada ya hapo Nikolay alirudi kwenye gari na kushusha mizigo yote na kuingiza ndani. Alipomaliza Christine alimlipa kiasi alichokihitaji cha feha na kumuongeza kidogo ili kumfunga mdomo. Nikolay aliaga na kuondoka, "sasa subiri niwaoneshe mimi ni nani" aliongea Christine huku macho yake yakirowa machozi. Christine hakuwa mwanamke mwengine bali alikuwa ni Rose ambae inasadikika amekufa mwezi mmoja nyuma.
Katika ajali ambayo inasadikika kuwa amekufa hakuwa yeye bali ilikuwa ni mtu ambae ametengenezwa na kufanana na yeye kabisa kila kitu, hiyo ni kazi malum aliokuwa akiisimamia yeye mwenyewe kama njia moja wapo ya kufanikisha lengo lake la kutoroka kwa kufeki kifo. kabla ya ajali ile alipita katika sehemu ambayo kazi ile ilikuwa ianendelea, aliwauwa wote waliohsika na kutengeneza sanamu hilo ili kujihakakikishia usalama. Baada hapo aliliingia kwenye gari na kuondoka..
Alipofika karibu na daraja moja hivi, alishuka kwenye gari na kulihamishia lile sanamu ubande wa dereva kisha akachukua kibao kizito na kukiweka kwenye sehemu ya kukanyagia mafuta na kuliacha gari likaenda kugonga kwa nguvu kwenye vyuma vya dara hilo. Baada hapo alikwenda mpaka ilipo gari kisha akatoa mfuko wa kihifadhia damu ambapo ndani ya mfuko huo kulikuwa na damu yake mwenyewe na kulimwagia sanamu hilo na nyingine akamwaga katika kioo cha mbele na nyengine akaeneza kwenye dashboard. Kisha akaliwasha moto na kuhakikisha linateketea lote.
"Kazi nzuri" Alex aliongea baada kutoka shambani na wenzake ambao aliwachukulia kama ndugu zake, ni mwezi mzima umepita sasa tokea Alex awe nao. "Leonard nahisi muda wangu wa kuondoka umefika" alimwita rafiki yake kipenzi pembeni na kumueleza. "Mbona mapema sana, tumeshakuzoea" Leonard alijibu kwa masikitiko, "nikiendelea kukaa hapa nyinyi nyote mtakuwa hatarini sana, hivyo kuwaokowa nyinyi inabidi niondoke" alijaribu kumueleza uhalisia wa mambo.

"Siwezi kukaa sehemu moja zaidi mwezi, ni lazima nibadilishe makazi mara kwa mara" alizdi kumuelewesha mpaka mwisho akaelewa. "Lakini ongeza japo wiki moja tu" Leonard alimuomba na Alex akakubali japo shingo upande maana machale ya hatari yalishamcheza. Walirudi na kuungana na wengine kwa ajili ya kupata chakula cha jioni.
"Taarifa zozote juu ya Project 75" aliuliza Mr Clintona wakati wakiwa kwenye kikao, "ndio tumefanikiwa kugundua sehemu alipo ila bado tunataka tupate uhakika" alijibu Martin. "Vizuri sana kijana" Mr Clinton aliongea huku akitabasamu. Kikao kiliendelea mpaka kilipofikia tamati na kila akatawanyika. Mr Clinton alirudi ofisini kwake huku moyo wake ukiwa umejawa na furah baada kusikia kuwa sehemu aliokuwepo Project 75. "ngoja uone nitakachokufanya mpuuzi mkubwa wewe" alisema kwa nguvu mpaka akajishtukia.
"Leonard usigeuke na nisikilize kwa makini, kuna mtu anatuftilia na bila shaka atakuwa mpelelezi. Sasa fanya hivi wewe pita njia yako na mimi nipite yangu tukutane nyumbani" Alex aliongea baada kushtuka kama wanafatiliwa. Leonard alikubali na kila mtu akaelekea njia yake, yule aliekuwa akiwafatilia alielekea upande aliokwenda Alex. Alex alitembea mpaka sehemu yenye viti vya kupumzikia na yule mtu alifika pale akakaa pembeni yake na kuweka bahasha kisha akainuka na kuondoka.
Alex aliichukua bahasha hio na kuondoka eneo hilo, alitembea mpaka alipofika sehemu ambayo alihisi ni salama na kuifungua. Alikuta vipande vya simu, alivitoa na kuiunga simu kisha akaiwasha, muda mfupi baada kuwaka simu ilianza kuita. "we nani" aliuliza baada kupokea, "punguza jazba kijana" upande wa pili wa simu ulimjibu, "najua hunijui lakini mimi nakujua na niko tayari kukusaidia kama utataka".
 
47.

"Sitaki msaada wako" Alex alijibu kwa hasira mpaka wapita njia wakamuangalia, "ni sahihi kabisa kutomuamini mtu, lakini niamini nataka kukusadia tu". "utanisaidiaje, jisaidie mwenyewe kwanza", "kwa sasa wewe huko hatarini ila rafiki zako wako hatarini kwani tayari wanaokusaka washajua uko wapi, na wala usihangaike kurudi kwani utakutana na miili tu ya marafiki zako"
********************
"Sisi tunataka mtueleze tu Project 75 yuko wapi" Project 52 aliuliza kwa mara nyingine tena, "sisi hatumjui huyo project 75" Amose alijibu. "Naona hawa madogo wanajifanya manunda" Project 66 aliongea huku akikoki bastola yake. "Basi kama hawajui, wacha tuache salamu tu akija atatutafuta" Project 78 aliongea na kuwamiminia risasi wote. Yote hayo yanafanyika Leonard akiwa anashuhudia kwa mbali, alipotaka kwenda alizuia na mtu, alipogeuka alikutana na Alex. "Usiende watakuuwa na wewe, tuondoke eneo hili" Alex alimnong'oneza, "wamewauwa ndugu zangu na wao lazima wafe" Leonard aliongea kwa hasira huku machozi yakimtoka.
"Leonard kuwa mwanaume shupavu, kubali leo ipite ili ujipange na kesho" Alex alizidi kumsihi rafiki yake huyo. Leonard alikubali na kuondoka eneo hilo, wakiwa njiani simu iliita tena. "unataka nini" Alex aliongea kwa gadhabu, "nenda mpaka pale ulipopewa bahasha kuna gari aina ya jeep, chukua hio gari na angalia tv yake utakuta ramani itakayokuelekeza katika hoteli" kisha simu ikakatika. "Leonard tukazane wasije wakatukuta njiani, hao jamaa hawajui utani hata kidogo" Alex aliongea huku akizidi kukazana nae Leonard alifanya hivo. Walifkika mpaka sehemu aliyopewa bahasha Alex na kukuta Jeep kama alivyoelekezwa.
Alifungua mlango na kuingia kisha akamfungulia Leonard nae akaingia, alipowasha tu ikatokea ramani kwenye kitv cha gari hio. Aliweka gia na kuondoka, njia nzima Leonard alikuwa akilia mpaka walipofika katika hoteli ilioonyeshwa kwenye ramani. "Leonard futa machozi mtu wangu, ukiendelea kulia haitakusaidia chochote kile" Alex aliongea akijaribu kumnyamazisha. Leonard alifuta machozi na wote wakashuka kweny gari na kuelekea mapokezi, "jina tafadhali" mtu wa mapokezi aliuliza baada salamu, Alex alishindwa aseme jina gani na ghafla ukaingia ujumbe kweny simu yake na alipoangalia akakuta ni jina lake. .
"Jina ni Alex Jr" alijibu, "karibu sana Mr Alex jisikie uko nyumbani" alijibu yule mtu wa mapokezi na kumkabidhi funguo Alex. "Asante" Alex alijibu na kuondoka, moja kwa moja alielekea mpaka chumba chenye namba iliokuwepo kwenye ufunguo. Alifungua na wote wakaingia ndani, Leonard alikaa chini na kuendelea kuomboleza. "lia mpaka uridhike" Alex aliongea na kuingia chooni kwa ajili ya kuoga, alimaliza na kurudi ndani. Alifungua kabati na kutoa suti moja kali na kuvaa. "Leonard kaoge tuje kupanga mpango wa kulipa kisasi" Alex alimwambia, hiyo ilikuwa kama shoti kwa Leonard maana alisimama na bila kupoteza muda aliingia chooni na kuoga. Alipotoka alikuta suti kwenye kitanda ikiwa na kikaratasi "pendeza kwanza". Alivaa suti hiyo na kuonekana kama inamusha hivi kwa sababu ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuvaa suti tokea azaliwe.
Dakika kumi Alex alirudi na chakula na wote wakala na kunywa hadi wakashiba, "sasa kichaa wangu nambie wapi nitapata silaha nzito nzito" Alex alimuuliza Leonard. "Yako machimbo mengi tu kama uko tayari tuende" Leonard alijibu akionekana mwenye furaha. "Sasa mbona unaendelea kukaa" Alex aliongea akiwa kashasimama, Leonard aliinuka na kwa pamoja wakatoka mpaka nje ya hoteli hiyo. Walielekea mpaka kwenye maegesho ya gari na kuingia kisha Alex akalitoa gari hilo kwa fujo mpaka walinzi wakashanga. Kwa uenyeji wa Leonard katika mji huo mashariki mwa South Africa walifanikiwa kufika eneo husika bila shida yoyote ile.
 
48.

Walishuka kwenye gari na kuingia ndani wakifuata vichochoro kadhaa mpaka walipofika katika nyumba moja hivi ambayo kwa nje tu unakaribishwa na moshi wa bangi. "nisubiri hapa nikaongee nao" Leonard aliongea na kuingia ndani ya nyumba hiyo. Baada dakika tano alirudi na kumfanyia ishara Alex amfate, "karibu ndugu tumesikia unataka vitu vizuri basi hapa ndio kwao. Tuna kuanzia bastola ndogo ndogo mpaka makombora, wewe tu mkwanja wako" aliongea mtu mmoja mwenye rasta chafu hivi huku mkononi akiwa na kipande cha bangi.
"Asante hebu kwanza nipatie hicho kipisi cha bangi kilichobakia nishtue ili nipate mzuka wa kuchagua" Alex aliongea huku akinyoosha mkono, kama ilivo ada ya rasta ni watu ambao wako na amani sana, alimpa kipande na Alex akapiga mafunda ya fasta huku akitoa moshi kama jiko la kuni zilizorowa maji.
Baada kupata pafu kadhaa, alisogea mpaka ilipo mitutu na kuanza kuchagua, aliendelea na zoezi hilo mpaka aliporidhika "hizi kwa sasa zitafanya kazi yangu" Aliongea Alex huku akiweka mitutu kadhaa kwenye meza. Yule jamaa aliziangalia kwa makini kisha akamuangalia Alex, "unavoonekana umebobea kwenye kuchagua silaha nzuri na makini" aliongea kisha akamtajia bei. "Leonard nenda kwenye gari kuna begi jeusi njoo nalo" Alex aliongea na Leonard bila kuchelewa aliondoka na haukupita muda alirudi akiwa na begi jeusi mkononi.
"Kuna pesa kwenye begi hili, angalia kama zitakutosha au nikuongeze" Alex alilisogeza lile begi karibu na muuzaji. Alilifungua na kuziangalia kisha akatabasamu, "usiwe na wasi wasi zinatosha hizi" alijibu na kusimama. "Nimefarijika kufanya biashara na wewe Mr Alex" Aliongea na kumpa mkono, "hata mimi nimefarijika, ni mategemeo yangu tutaendelea kufanya biashara vizuri zaidi huko mbeleni" alijibu Alex huku akitabasam.
Baada ya hapo walibeba dhana zao za kazi na kuondoka, "tunarudi hotelini au vipi" Leonard aliuliza. "Hapana kurudi kule ni kujipeleka katika mdomo wa mamba, wale jamaa watakuwa washaajua kama tuko pale hivyo watakwenda kututafuta. Ila kwa sababu saa hivi ni usiku sana watafika pale mapema asubuhi na wataelekea chumbani kama wahudumu wa hoteli" Alex alimjibu huku akizidi kukanyaga mafuta. "Sasa tunakwenda wapi" Leonard aliuliza tena, "tunaelekea kule kule hotelini lakini tutakaa kwenye gari" Alex alijibu huku akizidisha umakini kweny usukani.
Walifika mpaka karibu na hoteli waliofikia mwanzo lakini walikaa mbali kidogo na kupaki gari katika maegesho ya barabarani na kupumzika. Kutokana na uchovu usingizi mzito ulimchukua Leonard, Alex hakulala kabisa usiku huo alikuwa akiandaa silaha ambazo atazitumia asubuhi kutuma salamu kwa wanaomfatilia maisha yake. Kulipambazuka "oya umelala sana kumekucha kaka" Alex alikuwa akimuamsha Leonard ambae alionekana kuwa na usingizi mzito.
"Ah mapema kaka wacha nipatilize kidogo" Alijibu kivivu, "oya acha zako wewe, amka upashe mwili kuna kibarua kizito" Alex alizidi kumkera mpaka Leo akaamka na kushuka kwenye gari kwa ajili ya kupasha. Wakati Alex akiendelea na maandalizi yake, alichungulia nje na kwa mbali aliwaona maadui zake wakiingia katika ile hoteli. "Leonard ingia kwenye gari haraka" Alex aliongea kwa sauti kubwa na Leonard akaingia. "unaweza kazi ya utunguaji (sniper)" alimuuliza, "ndio ila si sana" Leonard alijibu..
"Sawa chukua hili begi na panda juu kabisa ya gorofa hili, ukifika kaa usawa na dirisha la pili kutoka kushoto halafu jipange" Alex aliongea na kumkabidhi begi Leonard. "chukua na hiki kifaa, kitatusaidia katika mawasilino" Alex aliendelea kuongea na kumkabidhi kidude fulani hivi. Leonard alikipokea na kukiweka sikio la kushoto kisha akashuka kwenye gari na kuelekea alipoambiwa.
 
49.
Alex alichukua kila alichohisi kitamsaidia na yeye pia akashuka kwenye gari na kuelekea hotelini, moja kwa moja alielekea mpaka gorofa ambayo chumba chake kilikuwepo. Alitembea kwa umakini mpaka katika mlango wa chumba chake, na kwa umakini wa hali ya juu aliuchunguza mlango huo ili ahakikishe kama walishafika chumbani kwake au laa. Aliporidhika kuwa hawajaingia alifungua na kuingia kisha akaufunga na kusimama mbele, "unaniona nilipo" aliongea, "nakuona kaka" Leonard alijibu. "Basi wa kwanza akiingia atasimama hapa, atakuwa anaangalia dirisha. Usimruhusu akainua kichwa, akisimama tu mpasue kichwa au mchimbe moyo" Alex alimueleza Leonard kwa umakini.


"Nimekusoma mkubwa" Leonard alijibu huku akiikoki bunduki yake. Baada kama dakika tano hivi mlango uligongwa lakini Alex hakujibu "jiandae" aliongea kwa sauti ya chini, "on position" Leonard alijibu. Baada kuona kimya mlango ulifunguliwa taratibu na project 52 akawa wa kwanza kuingia. kama alivyotegemea Alex, baada kuingia tu alisimama mbele ya mlango na Leonard hakufanya makosa alimchapa risasi ya kichwa. "vizuri sana kijana" Alex aliongea, "sasa we tulia hapo na usome mchezo kupitia darubini yako, kuwa makini ntakuuliza baadae" Alex aliongea na kucheka kwa sauti ya chini. "umesomeka mkuu" Leonard alijibu huku akicheka kwa nguvu kidogo.
Alex alikuwa amejifcha ndani ya kabati la nguo, akiwa na mitutu mkononi. Baada Project 52 kutandikwa risasi, waliokuwa nyuma yake walisita kuingia kwa sekunde kadhaa. Mlango ulisukumwa taratibu na kwa umakini wa hali ya juu, alitangulia project 66 ambae ni mwanamke na kufuatiwa na project 78. "atakuwa kajificha wapi huyu mwehu" aliongea Project 66, "kwa akili zake huyu atakuwa amejificha nje katika varanda" Alijibu project 78 na wote wakaelekea varanda.
Muda wote Alex alikuwa akiwasikia na alitamani kucheka "wapumbavu sana hawa, ina maana hawakucheza hata kombolela walivokuwa wadogo. Ah lakini sishangai sana kwa sababu haya ndio madhara ya kulelelewa kama makuku ya nyama hata yakitolewa nje ya banda yanashindwa hata kutafuta chakula" aliongea hayo moyoni huku akitabasamu. Walipofika mmoja aifungua dirisha na kuchungulia lakini hakuona mtu, hapo Alex alitoka kwenye kabati na kumimina risasi huku akitafua sehemu ya kujifcha.
"Aghh" ulisikika ukwenzi wa maumivu na ghafla project 66 alianguka chini na kusogea pemebeni kwa ajili ya kujificha. Kisha aliangalia sehemu aliopigwa risasi na kusema "unadhani utatoka leo", "swali hilo ujiulize mwenyewe" Alex aljibu huku akibadilsha magazine na kuweka ambayo imejaa risasi. "Project 75 kubali kama umeshindwa na hatutakuuwa" project 78 aliongea huku akijaribu kuchungulia, lakini mara alikoswa na risasi. "Duh huyu jamaa ni balaa" alijisemea moyoni, "project 66 vipi unaweza kuendelea na mpambano" aliuliza project 78.
"Mimi mbona niko sawa" alijibu huku akijiweka sawa, baada kuongea hivo aliinuka na kuanza kushambulia hovyo n Alex aliitumia nafasi hiyo kumueka matobo kadhaa upande wa moyo. "Project 66 amepigwa risasi" Project 78 aliongea, "fanya lolote utoke humo ndani" upande wa pili ulijibu. "Sawa mkuu" Project 78 alijibu, alichomoka alipokuwa amejificha huku akipiga risasi bila mpango lakini Alex alitulia akisikiliza sauti ya bastola inaeleka upande gani.
Project 78 alifanikiwa kufika mlangoni, aliurukia na kuanguka nao nje kisha akainuka na kuanza kukimbia. Alex hakuchelewa aliinuka na kuanza kumkimbiza, Project 78 alikimbilia mpaka kwenye ngazi na kuanza kushuka. Alex alikuwa nyuma nae akimfukuza bila kupiga risasi akiepuka asije akapiga mtu asie na hatia. Watu wote waliokuwa wakitumia ngazi walikaa pembeni baada kuona wawili hao wakikimbizana na bastola mikononi. Project 78 alifanikiwa kufika chini kabisa lakini bahati ikawa mbaya kwake alijikwaa na kuanguka, bastola yake ikaangukia mbali kidogo na alipodondoka..
Alipojaribu kuinuka aifate alijikuta akichezea teke zito la tumbo.
 
50.
"Mimi nilidhani una ubavu wa kupambana na mimi kumbe ni mbwa koko tu" Alex aliongea kwa kejeli, aliirudisha bastola yake kiunoni na kumuinua. Alianza kumtembeza kichapo,kila Project 78 alivojitahidi kuzuia mashambulizi hayo alijikuta akichezea ngumi zisizi na idadi. Bahati nzuri alifanikiwa kuponyoka mikononi mwa Alex na kumkimbilia mschana na kumuweka kama ngao "ukinisogelea namuua huyu" aliongea kwa tabu kidogo.
Wakati Alex anafikiria nini cha kufanya ghafla project 78 alianguka chini huku akiwa na tobo katika paji la uso. "usiwaze sana kaka, kazi imekwisha" Leonard aliongea huku akiiangalia bomba ya bunduki iliyokuwa inatoka moshi. "Kazi nzuri, sasa tukutane kwenye gari haraka" Alex aliongea na kuanza kukimbia, alifika kwenye gari na sekunde kadhaa mbele Leonard alifika na kuingia. Alex aliiondoa gari kwa kasi ya ajabu sana, "ni lazima tutoke nje ya mji kwanza" aliongea huku akiwa makini na barabara. "Hakuna shida we nyoosha tu hiyo njia" Leonard alijibu, Alex aliongeza mwendo na kufungulia mziki kabisa.







**************
"Tumepoteza mawasiliano na project 78" Ms Helen aliongea huku akivua kifaa maalum cha mawasiliano, "shit" Mr Clinton alifoka. "Huu ni mwanzo tu, hali ikiendelea hivi sisi wote vibarua vyetu viko mashakani kuota nyasi" aliendelea kuongea. "Tupunguze jazba kwanza halafu tukae kitako tupange mipango mengine maana huu ndio umefeli" Rodriguez aliongea huku akiweka tai yake vizuri. "Yeah hilo ndio la kufanya sasa" Martin alichangia. "Mkuu kuna simu kutoka ikulu" aliingia Maggy ambae alikuwa secretary mpya baada aliekuwa secretary wa zamani kufa.
Mr Clinton alikwenda ofisini kwa ajili ya kuongea "hali ni tete mpaka sasa, tumeshapoteza watatu kati ya project wetu bora kabisa" Aliongea kwa unyonge. Baada ya maongezi ya muda mrefu alikata simu na kurudi alipokuwa mwanzo. "Kuna mpya gani huko" Ms Helen alimuuliza punde tu baada ya kufika, "hakuna mpya" Alijibu kwa mkato akionekana kuwa na mawazo mengi sana.
"Inabidi ufike Durban kwanza kisha nitakupa maelekezo zaidi" ilikuwa ni sauti kwenye simu, baada maongezi hayo alirudi mpaka kwenye gari. "Inabidi tuelelekee Durban kwanza " aliongea na kuingia kwenye gari, Leonard aliingia na safari ikaanza. Njia nzima walikuwa kimya huku kila mmoja akiwaza la kwake. Safari ilikuwa ndefu lakini walifanikiwa kufika salama bila matatizo yoyote, na kwa sababu waliingia usiku hivyo walitafuta hoteli na kupumzika.
Asubuhi mapema uliingia ujumbe kweny simu ya Alex ukimwambia mahali na saa, aliamka bila kumshtua Leonard na kutoka alikwenda mpaka sehemu ambayo aliambiwa kwenye ujumbe na kusubiri. Ulipofia ule muda alioambiwa alikuja mtu na kumkabidi bahasha kisha akaondoka. Alex baada kupokea bahasha ile alirudi hotelini kisha akaifungua, alikuta passport pamoja na vitambulisho kadhaa tiket ya ndege pamoja na kikaratasi kidogo kilichoandikwa Rio De Janeiro Brazil.
Baada ya hapo aliingia chooni na kujimwagia maji na kuvaa kwa ajili ya safari. "Leonard , mimi inabidi niondoke mtu wangu" aliongea, "wapi tena" aliuliza Leonard. "Naelekea Brazil" Alijibu, "dah haina noma kaka, mi nashukuru kwa msaada wako katika kulipiza kisasi cha wadogo zangu" Alijibu huku akitabasamu. "Sasa ni hivi katika gari kuna pesa nyingi tu na zinaweza kukusaidia, zichukue na uanze maisha upya" Alex aliongea. "Hakuna shida nimekuelewa" alijibu Leonard na kisha akajiandaa na kumsindikiza rafiki yake uwanja wa ndege. "ipo siku nitakulipa wema wako" Leonard aliongea maneno hayo wakati akimuaga Alex, "sawa" Alex alijibu na kuingia ndani ya uwanja huo.
******************
 
51.
Maisha ya Allen James yalikuwa ya amani kabisa, jioni hiyo alikuwa na familia yake katika fukwe moja hivi mjini Florida. Kwa kweli alikuwa amesahau kabisa machungu alioyapata kipindi cha nyuma, " Mume wangu unawaza nini" Aliuliza mkewe Tania. Mwanamke ambae uzuri wake haujapingua hata kidogo machoni mwa Allen James. "Siwazi kitu" alijibu huku akitabasamu na kumuangaliwa mkewe ambae nae pia alikuwa akitabsamu. "Baba inuka" aliongea Christina ambae muonekano wake haukuwa tofauti n alivyokuwa mama yake Melinda. "Unataka nini" aliuliza baba ake, "halafu unajua siku hizi umekuwa mvivu sana" Christina alijibu huku akimsukuma mgongoni, "we mtoto wee kuwa na adabu, babaako huyu" Tania aliingilia kati. "Mama mimi si mtoto tena nina miaka ishirini na tano sasa" Christina alijibu.
Wakati akiendelea kubishana na wazazi wake simu yake iliita "Agent Darling unahitajika ikulu, kaa tayari helicopter inakuja kukuchukua hapo hapo ulipo". "Hii mijitu hainipi hata nafasi ya kukaa na familia yangu" aliongea kwa hasira kidogo. "Kazi au" Babaake alimuuliza, "hata sijui wamesema nahitajika tu ikulu" alijibu na kwa mbali alisikia mlio wa helicopter na sekunde kadhaa mbele ilifika eneo hilo na kutua. Alishuka kijana mmoja na kuelekea alipo Christina au Agent Darling kama anavojulikana akiwa kazini.
Alitoa heshima na kisha akamuambia amfuate "nahisi piknik yangu itakuwa imeishia hapa" aliongea Christina huku akiondoka taratibu. "Kama ni kazi ya kwenda kumchapa mtu hakikisha unamfundisha heshima kisawasawa" Allen James aliongea kwa nguvu mpaka watu waliokuwa pembeni walishangaa. "Duh mi wazazi wengine hasa makatili" alisikika mtu mmoja akiongea pembeni yao. "Na wewe unataka kuchapwa" Allen James aliongea na kumuangalia.
Ndege ilikanyaga ardhi ya Brazil mjini Rio de Janeiro, "hewa safi kabisa" aliongea Alex wakati anashuka ndege akiongozana na abiria wengine. Alitoka mpaka nje ya uwanja na kukuta watu na mabango ya fukwe tofauti tofauti. Ujumbe uliingia kwenye simu yake ukiwa umeandikwa Copacabana, aliinua macho na kutafuta bango lililoandikwa hivyo. Alipoliona alinyoosha mkono na dereva alipouona mkono, haraka bila kuchelewa alimfata na kumsaidia mabegi mpaka kwenye gari. Safari ilianza "karibu Rio" aliongea yule dereva, "asante" alijibu Alex. Safari haikuwa fupi na dereva alionekana kuwa mcheshi sana jambo ambalo lilimfurahisha Alex.

.
Walifika mpaka katika pwani hiyo iliyozungukwa na mahoteli makubwa makubwa na yenye mvuto wa aina yake. Alex alimlipa dereva kiasi cha fedha alichohitaji na kuingia katika hoteli moja hivi na kuchukua chumba. Kutokana na uchovu wa safari alioga na kujitupa kitandani, usingizi nao haukucheza mbali ulimchukua ghafla na kuanza kumuhamisha katika maeneo tofauti kabisa. "Baba Alex si nilikwambia usiwaite watoto wote wawili Alex, ona sasa hata wakifanya kosa kila mmoja anasema yeye ndie amehusika", "mke wangu hiyo sio shida, sasa hao si watoto tu wakikuwa wataaacha". "Mpige risasi mdogo wako", "hapana siwezi kumuua mdogo wangu". Ghafla Alex alishtuka kutoka usingizini huku jasho jingi likimtoka, ni ndoto hiyo ambayo inajirudia kila siku lakini kutokana na kuwa alifutwa kumbukumbu huwa anahisi ni kitu ambacho hakijawahi kutokea.
 
52.
Alipoangalia saa yake ilikuwa ni saa kumi na moja jioni, aliamka na kuvaa mavazi ya kutembelea baharini na kutoka hotelini.Kwa kweli fukwe hiyo ilipendeza sana, na watu wengi walionekana kufurahia upepo wake. Alex alitembea tembea katika ufukwe huo huku akiwa ameshika dafu na kufurahia maji yake. Alifika sehemu na kuamua kupumzika, wakati akiwa amekaa alikuja mtu pembeni yake na kukaa.
"Habari yako Alex Junior" aliongea yule mtu, Alex alishangaa kulisikia jina hilo. "Najua utakuwa unajiuliza nimelijuaje jina hilo" alizidi kuongea yule mtu, "wewe utakuwa hunijui ila mimi nakufahamu kinaga ubaga". Alex aligeuka na kumuangalia anaeongea na kugundua alikuwa mtu mmoja mzee sana lakini alivomuona tu alihisi kama kumfahamu. "Hivi tumewahi kuonana mimi na wewe" aliuliza Alex akiwa na wasiwasi, "ndio lakini miaka mingi sana" alijibu huku akitabasamu. "Alex, Alex, Alex" yule mzee aliita jina hilo mara tatu ghafla Alex akaanza kuhisi kichwa kinamuuma, vitu kama kumbkumbu vilianza kugongana kwa kasi ndani ya kichwa chake na kujikuta akiishiwa nguvu na mwisho akaanguka na kupoteza fahamu kabisa.
Alikuja kushtuka akiwa chumbani kwake na yule mzee akiwa pembeni yake, "unafanya nini chumbani kwangu" aliuliza akijaribu kukaa lakini bado kichwa kilikuwa kinamuuma. "Unajua tatizo lako unajaribu kuzipinga kumbukumbu zako" aliongea yule mzee, "unamaanisha nini kusema hivyo" Alex aliuliza kwa mshangao. "Si unakuwa unaota ndoto za ajabu ajabu" aliongea yule mzee, "ndio" Al alijibu Alex. "Sasa ni hivi, hizo unazoota si ndoto ni kumbukumbu zako mwenyewe zinarudi lakini wewe unapingana nazo na ndio maana mara nyingien zinakuangusha" aliongea yule mzee.
"Acha kunizungusha we mzee, nambie ukweli kuhusu mimi" alifoka Alex. "sasa umeona bado una hasira zako za ajabu" aliongea yule mzee kisha akaendelea "umeletwa huku ili kuja kuujua ukweli kuhusu maisha kabla ya kufika hapo ulipo leo, Alex Alex Alex. Babaako ndie alikuwa akiwaita hivo baada kufanya makosa, ukweli ni kwamba wewe ni wa pili katika familia yenu. Wa kwanza alikuwa anaitwa Alex Seniour na wewe ni Alex Juniour, mlikuwa watundu kupindukia na siku zote mukifanya makosa munasingiziana. Wewe na kaka yako mumepishana mwaka mmoja tu na mlikuwa mukipendana sana na ndio maana mukifanya kosa aidha mupigwe wote au muachiwe wote. Mimi nilikuwa mlinzi wa babaako wakati huo na nlikuwa naelewa mambo mengi sana pamoja na siri nzito ambazo hata mamaako hakuzijua.
Siku moja wakati tupo safarini babaako alipokea simu ya vitosho kutoka makao makuu ya kipelelezi nchini, baada kupokea taarifa hizo haraka tuligeuza na kurudi nyumbani. Lakini bahati haikuwa upande wetu,tulifika nyumbani lakini tulikuta nyumba inamalizika tena kwa moto. Baba ako alipata mshtuko mkubwa na kupelekea kupoteza maisha lakini akiwa katika hali aliniachia kazi moja kama ikiwa kuna hata mmoja kati ya wanafamilia atakuwa amepona basi niondoke nae mimi. Lakini baada moto kuzimwa mifupa iliokutwa ni ya mtu mmoja tu ambae ni mama ako, kuanzia hapo nikaanza kufanya uchunguzi wa siri na nikafanikiwa kugundua kuwa nyote wawili mumechukuliwa na serekali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi maalum wa kemikali inayojulikana kama CODE X. Hapo sasa ikabidi nirudi tena kwenye gwanda ili niweze kuingia katika kambi ambazo zinasadikika kuwa watoto wengi mayatima wanapelekwa huko. Na kutokana na kazi nilioifanya kuitumikia nchi kipindi niko jeshini haikuwa tabu kuaminiwa lakini siku niliofika ndio siku niliokuta wewe na kaka yako mnapewa jaribio la kuuwana lakini kaka ako alishindwa na wewe ulipokabidhiwa bastola ilikuwa haina risasi hata moja. Kuna mtu alikuwa nyuma yako na ndie aliepiga risasi na kumuua kakaako huku ukidhani wewe ndie uliemuuwa. .
 
Back
Top Bottom