Abdallahking
JF-Expert Member
- Mar 19, 2018
- 3,985
- 10,840
- Thread starter
- #21
C.O.D.EX. 1 ................... SEHEMU YA 14
Baada ya hapo mashine ilijifunga na kuwaka taa nyekundu ndani ya mashine hiyo. "nakutakia usingizi mwema" iliongea ile computer na ghafla usingizi mzito ukanichukua.
*****.
"We David si unakwenda kwenye interview leo" baba alifungua mlango wa chumba changu na kunishtua, nilikurupuka kutoka kitandani na kuangalia saa yangu ya mezani. Iliniambia saa moja kamili asubuhi, na natakiwa niripoti white house saa moja na nusu kwaajili ya hiyo interview.Hapo nilikuwa na miaka ishirirni na ndio kwanza nilikuwa nimaliza chuo kikuu katika cozi ya IT. Niliingia chooni haraka na kujisafisha kisha nilirudi chumbani kwangu na kuvaa suti aliyoninunulia baba. Hata chai sikunnwa nilitoka nduki mpaka kwenye gari yangu na kuelekea ikulu.
Dakika ishirini na nane nilikuwa mapokezi na kuelekezwa sehemu nnayo takiwa kuwepo, nilipofika nilishangaa kuona msururu wa vijana wakisubiri na wengine walikuwa wakitoka katika chumba cha interview huku machozi yakiwatoka, hiyo ilikuwa ni dhahiri kuwa walikosa kazi hiyo. NIkiwa katika hali hiyo niliskia jina langu likiitwa. Niliitika na kuelekea mlangoni, mlango ulifunguliwa nikaingia. Alinihoji maswali ya kawaida kwanza kisha wakanisogezea computer na kunambia nihack system ya white house, nilitabasamu kidogo kwa sababu kuhack ndio kitu nnachokipenda katika maisha yangu. Wakaniekea saa mbele na kunambia nina dakika tano tu za kufanya hivo.
Saa ilipobonyezwa tu na mimi nikaanza maujuzi yangu, kila nilivojaribu nilifika pahali nikakwama lakini baadae nilishtuka kama kuna mtu mwengine pia anahack computer ninayo tumia. kwanza lazima nimzuie halafu ndio niendelea na kuhack. Nilipoangalia saa niligundua kuwa dakika mbili na nusu zishateketea, niliongeza kasi na kufanikiwa kumzuia anaehack compuetr niliopewa ndani ya sekunde arobaini tu. Hapo niliongeza kasi mara dufu huku nikitumia ufundi wa hali ya juu kufanya kazi hiyo ngumu, dakika nne na sekunde hamsini na sita ndio muda niliomaliza kuhack na kufanikiwa. Kisha nikiwapa computer yao. Hawakushangaa sana, mmoja aliondoka nayo na baada dakika kadhaa alirudi huku akionyesha uso wa simanzi, mapigo ya moyo yalianza kwenda mbio na kijasho chembamba kikaanza kunitoka. "samahani umejitahid sana lakini hujafikia kiwango tulichokitaka" aliongea na kunionyesha mlango uliokua na alama ya kutokea. Kiunyonge niliiuka na kuelekea kwenye mlango huo, lakini nilipoufungua nilishangaa kuona hakuna hata mtu mmoja aliekuwa akisubiria kuingia kwenye chumba hicho. Lakini sikutilia maanani kwani mawazo yote yalikuwa mbali sana nikikumbuka jinsi nilivyokuwa natamani sana kulitumikia taifa langu.
Ghafla nikiwa katika dimbwi hilo la mawazo kengele zinazoashiria hatari zilianza kulia, na kwa mbali niliona kikundi cha watu kikija upande wangu wakiona kama kuna mtu wanamlinda. Na kila walivyosogea niligundua kuwa alikuwa ni raisi, nilianza kuetetemeka huku nikishangaa, waliponikaribia mmoaja wao alinivuta na kunambia "mlinde raisi" nilitaka kumwambia kuwa mimi sio mlinzi lakini nilichelewa kwani risasi zilianza kurindika na kunibakisha nisiwe na chaguo zaidi ya kumlinda raisi lakin Ukweli hata kukamata silaha nilikuwa sijui. .