Simulizi ya Kijasusi: C.O.D.EX.

Simulizi ya Kijasusi: C.O.D.EX.

53.
Baada kushuhudia tukio hilo nilitupilia mbali wazo la kukuokoa bali niliamua nikupe mafunzo kama kawaida na uendelee kuwa chini ya uchunguzi maalum. Na ndio maana ulivyotoroka wakati ukiwa na miaka kumi na mbili nilikuachia uishi nje kwa muda wa mwaka mzima, nilifanya hivo ili kukujenga kiakili kuwa kuna maisha nje ya kambi. Na ulivyotoroka mwezi uliopita unadhani nini kilitokea, ulitoroka baada kuona moto umezuka. Moto niliuwasha mimi mwenyewe ili kukupa nafasi hiyo na yote hio ni kukutaka ulipe kisasi cha familia yako" Alimaliza kuongea na kumuangalia Alex usoni.
"Kwa we nani" Alex aliuliza, "we kweli kilaza kama mpaka saa hivi umeshindwa kunitambua, mimi ni General David kiongozi Marine Base 71" alijibu na kucheka kidogo. Alex alitoa macho kama mjusi aliebanwa na mlango maana katika watu ambao alikuwa anawachukia wakati akiwa kambini. "Ina maana mara zote wakati natoroka wewe ndio ulikuwa chanzo" Alex aliuliza kwa mshangao kisha akaendelea "na kule kambini umetokaje sasa".
"Sasa ikiwa nimeweza kukutorosha wewe, iweje mimi nishindwe kutoroka" aliongea General David, "baada ya kupata taarifa za kuthibitika kuwa umefanikiwa kukimbia nilitega bomu ofisini kwangu na kutoroka kabla ya kulipuka na kwasababu lilikuwa kali sana halikuacha ushahidi wowote ule hivyo wanaamini mimi nimekufa" alijibu.
*************************
"Tumepokea taarifa kutoka kwa watu wetu ambao wapo nchini Brazil kuwa Project 75 ameonekana Rio De Janeiro" aliingia Martin ofisini kwa bosi wake na kutoa taarifa. "Vipi umeshatuma vijana huko" aliuliza Mr Clinton, "ndio nimemtuma Project O" alijibu Martin. "Ataweza kutekeleza kazi huyo" aliuliza, "katika wote huyu ndie ana uwezo unaolingana na project 75 kwa hiyo usijali mkuu, mara hii mambo yatakuwa sawa kabisa" Martin alijibu huku akitabasamu. "Tuone wakati huu utatotokea wapi" Mr Clinton alijisemea moyoni. Baada kuwasilisha ripoti hiyo Martin alitoka ofisini, Mr Clinton alinyanyua simu na kumpigia secretary wake. Maggy alifika ofisini mara moja baada kukata simu, Mr Clinton alianza mambo yake yake yakipuuzi lakini alikutana na kibao kizito kilichomuangusha chini. Aliinuka kwa hasira na kutoa bastola lakini alikuwa kashachelewa maana alihisi kitu cha baridi kikigusa katika paji la uso, "ukileta ujinga nakufumua ubongo, kawafanyia malaya wenzako upuuzi kama huu mimi sie tumeelewana" alifoka kwa hasira Maggy. "Sawa nimekuelewa" Mr Clinton alijibu huku akimeza funda kubwa la mate maana alihisi kama kifo chake kina karibia. Baada hapo Maggy alirudisha bastola yake na kuondoka, Mr Clinton aliishia kula kwa macho tu huku akijilaumu kwanini amemuachia kirahisi namna ile.
Beach ya Copacabana ilikuwa imechangamka siku hiyo kuliko siku nyingine nyingi, kwa mbali alionekana kijana mmoja akiwa anatembea taratiu huku mkononi akiwa amebeba boksi dogo. Alionekana hayuko sehemu hiyo kupata upepo bali alikuwepo eneo hilo kikazi zaidi. Alikuwa akielekea sehemu aliokuwa amelala Alex ambae alikuwa akiota jua, alikuwa bize akisikiliza mziki lakini alianza kuhisi hali ambayo si ya kawaida. Mshale wa hatari uligonga kichwani mwake, alitoa earphone masikioni na kuanza kuangaza pande zote za pwani hiyo na ndipo akamuona yule mtu aliekuwa akija upande wake. Yule jamaa alifungua lile boksi na kutoa bastola ndogo iliofungwa kiwambo cha kuzuia sauti na kuanza kumshambulia Alex.
 
54.
Kwa kasi ya ajabu Alex alifanikiwa kuondoka kwenye kitanda alichokuwa amelala na kuruka pembeni, uwezo wa kujitetea wakatai huo uikuwa mdogo sana kwa sababu hakuwa na silaha yoyote ile. Yule jamaa hakuwa mwengine isipokuwa project 0, huyo ndie anaefuata kwa hatari baada Alex. Yeye hakujali watu aliendelea kumwaga risasi tu na kila aliepita mbele yake alikwenda na maji, "simama na weka silaha chini" iliskika sauti ikitokea nyuma ya Alex. "Inspecta usisogee huyo jamaa atakuua" Alex aliongea lakini alikuwa kashachelewa, yule askari alichezea risasi ya kichwa na kudondoka kama mzigo. Alex hakulaza damu alirukia bastola ya yule asakari, alipoinuka tu alianza kushambulia. Alifanya kama njia ya kujinunulia muda wa kutoroka eneo hilo maana ilikuwa pazito. Na kweli mbinu yake ilifanikiwa na hapo hapo alitoweka katika mazingira ya kutatanisha.
Alifika chumbani kwake na kufungua begi lake, alitoa vipande vipande vya chuma na kuanza kuviunga. Dakika tano baadae akawa amemaliza kuviunga na kupata batola kamili, alitoa magazine za kutosha kisha akavaa nguo zake za kazi na kuziweka magazine hizo. Alichukua simu yake na kukuta ujumbe uliomwambia ujio wa Project 0, "ahaa kumbe wewe ndio project zero, basi wacha nikuonyeshe kama ziro haina thamani ikiwa mwanzo" alijisemea moyoni na kutoka chumbani kwake. Uko chini katika hoteli hiyo palikuwa pamevurugwa na project 0, "project 75 jitokeze upambane na mwanaume mwenzio" alifoka kwa hasira na kumfumua ubongo dada wa mapokezi kisha akaendelea kuongea "kama ukiendelea kujificha nitauwa mtu mmoja mmoja mpaka waishe".
.
"Umesema nitoke nipambane na mwanaume mwenzangu sasa mbona unauwa wanawake au ndio wenzako" Alex aliongea huku akitoka katika lifti na kujibanza pembeni kwenye ukuta. "Waache hao, hii vita ni kati yangu mimi na wewe" Alex aliongea na kutabasamu, na kweli project 0 aliwaachia watu wote aliokuwa amewakamata. Alex alitoa bastola yake na kuanza mashambulizi ya kasi, project 0 nae alijibu mashambulizi hayo. ulikuwa ni mwendo wa kujibizana kwa risasi tu, mashambulizi yalendela kuwa ya na namna hiyo kwa muda mrefu huku wakitupiana maneno ya kejeli. "mi nahisi wewe ni mjinga, yaani umetumwa kuja kukinunua kifo chako au sio" Alex aliongea akiwa amejificha sehemu, "hahaha,.. mimi nimekuja hapa kuchukua roho yako" Project o alijibu.
"hivi wewe unalijua hata jina lako" Alex aliuliza, "project o ndio jina langu" alijibu. "mi nlijua tu utakuwa zezeta, hata jina lako hulikumbuki" Alex aliendelea kujibu majibu ya hovyo. "kama vipi tuoneshana ni nani mwanaume halisi kati yetu" Alex aliongea na kusimama kisha akaweka bastola pembeni, "nilikuwa nataka sana tuchapane kwa mkono na sio msaada wa bastola" project 0 aliongea huku akisimama na kuweka bastola pembeni. " sawa tuoneshane" Alex alijibu na kuchomoka sehemu aliokuwa amesimama kama mshale na kumvaa project 0. Mkono si wa kitoto ulianza kutembea huku kila mmoja akionyesha uwezo wake. Kila mmoja alipokea masumbwi kadha kutoka kwa mwenzake lakini upande project 0 hali ilikuwa mbaya sana mwisho akaona bora akimbiie bastola yake. Na Alex kama alimsoma hivi na yeye akaruka pembeni na kuokota bastola yake na kuanza kutupiana risasi tena.
Risasi zilizidi kumiminwa, huku kila upande ukijitahidi kumshambulia mwenzake. Alex alichomoka sehemu aliokuwa amejificha na kwa kasi na wepesi aliokuwa nao. Alijirusha upande mwengine huku akishambulia, alipokaa sawa alitoa magazine katika bastola yake ndogo na kuangalia imebakiwa na risasi ngapi. "risasi sita, zinatosha kunitoa hapa" alijesemea moyoni na kuirudisha magazine katika bastola yake. Aliokota chuma kidogo pembeni na kukirusha, ghafla uliskika mlio wa bastola.
 
55.
Ulipokata tu aliinuka na kupiga risasi moja tu iliokwenda moja kwa moja mpaka kwenye goti la project 0 ambae alipiga kelele za maumivu. Na bila kuchelewa alikimbilia sehemu aliokuwepo na kumnyang'anya bastola. "najua umeahidiwa zawadi nono ukiniuwa lakini kaa ukijua kuwa wameshindwa wenye uwezo kuliko wewe" Alex aliongea na kumuekea bastola katika paji la uso, "hahaha... hata ukiniuwa mimi ujue kuna wengine watakuja kuendelea nilipopaacha" aliongea kijana huyo ambae alionekana kutokukiogopa hasa kifo. "sawa waache waje tu, na mimi nitakuwa nawauwa mpaka pale watakapoacha kunifatilia maisha yangu" Alex aliongea na kufyetua risasi kisha akachukua kile kifaa cha kuwasiliana "nawatangazia vita rasmi, mtalipa kwa mlioiendea familia yangu na kama mlikuwa mnadhani sijitambui mmekosea naitwa Alex Juniour" aliongea na kukikata kile kifaa.
*******************
"Kosa kubwa tunalolifanya ni kwamba tunajaribu kumuwinda simba kwa kutumia nyati, hatuwezi kumnasa hata siku moja, simba anawindwa na simba mwenzie" aliongea Mr Robert katika kikao cha siri kilichokuwa kikiendelea katika moja kati ya ofisi kubwa za kipelelezi mjini New york nchini Marekani. "Unamaanisha kwamba wanajeshi wetu wote hawana maana si ndio" alifoka mwengine, "tuseme hivyo ni sahihi kabisa, wanajeshi wetu wote hawawezi na hawatoweza kumtia mbaroni huyu kijana" alijibu. "sasa wewe kuna mtu unamfahamu ambae anaweza kuifanya kazi hii" aliongea mkuu wa kikao hicho, "ndio namfahamu na ndio mtu pekee anaeweza kumtia kizuizini huyu kijana" alijibu. "na mtu huyo ni nani" aliuliza tena mkuu wao kwa shauku. "mtu mwenyewe ni Project X" alijibu Mr Robert.
"Robert hebu tuambie huyo mtu ana kipi hasa ambaco wanajeshi wetu hawana" aliongea Mr Clinton, "project X ndio mtu wa kwanza kufanikiwa wakati wa uhunguzi wa mwanzo wa CODE X, analingana kila kitu na Alex. Kwa maana nyingine yuko rank moja na Alex na hivyo ndio maana anakuwa mtu wa pekee ambae atafanikisha kumtia Alex mbaroni" Robert alijibu kwa kujiamini sana huku akitabasamu. "kwa sasa unajua yuko wapi" Aliuliza Mr Clinton, "nipeni siku tatu tu nitawaletea hapahapa ofisini" Robert aliongea na wote wakatikisa vichwa kuanshiria kuwa wamekubaliana nae. "jamani acheni masihara mujue huyu kijana ni hatari" aliongea Helen, "na kawaida yao wakiweka ahadi lazima waitimize kwa hiyo tusijiachie tu kutegemea mia mia kama atatiwa mbaroni, tuwe tayari kwa lolote litakalotokea" aliendelea kuongea.
*****************************.
"Habari yako Mr Allen" Robert aliongea na kuka katika kiti cha pembeni katika mgahawa mmoja mjini Florida nchini Marekani. "safi, unataka nini na kama ni lile swala tuliloongea mwanzo acha tu niondoke" Alijibu lakini alionekana kukerwa. "hamna shida we ondoka tu lakini ntakufungulia kesi ambayo najua utashindwa kuiepuka" alitisha Robert, ilibidi Mr Allen atulie ili kumsikiliza. "hapa sis tunaongelea maisha kwa ujumla, wewe nisaidie kumtia mkononi Alex mimi ntakusaidia kukufuta katika ubao wa blacklist" aliongea Robert. "wewe ndio unaongelea maisha na unataka kunituma kwenye kifo changu, kijana umri umekwenda tayari nini kinachokufanya ujiamini kama nitaweza kumkamata Alex" alijaribu kujitetea Mr Allen.
"unajua Alex hahitaji mtu mwenye nguvu ili kukamatwa bali anahitaji mwenye uwezo wa kufikiri kama yeye ili aweze kugundua mbinu na mipango yake kabla hajafanya chochote, na kwa sasa hakuna mtu mwenye uwezo wa kufikiria kama Alex isipokuwa wewe" Robert aliongea. "mimi nawafahamu sana nyinyi mkitaka lenu mpaka liwe, iwe kwa njia ya kawaida au yoyote ile" Mr Allen aliongea na kukunja uso. "nashkuru umelifahamu hilo, nakupa siku mbili unipe jibu" Robert alimaliza kuongea na kuondoka, alimuachia bahasha ndogo mezani. Allen James aliichukua na kuondoka lakini kichwani alikuwa na mwazo kibao, maana alielewa hatari iliokuwa mbele yake ikiwa atakubali au atakataa.
 
56.
Alirudi nyumabani kwake akiwa na sura ya huzuni, "mume kuna tatizo gani" mkewe aliuliza. "we acha tu, twende chumbani nikakueleze kila kitu" alijibu na kuongoza njia. Walipofika chumbani alimueleza kila bila kumifcha chochote kile. "si ukatae tu" mkewe aliongea, "kukata sio tatizo, litakalotokea baada ya kukataa ndio tatizo" Alijibu Mr Allen. "we unadhani serekali ya nchi hii inakuacha tu huru hasa baada kufanya matukio makubwa, wakikuacha ujue wanakuacha kwa sababu zao maalum" alimfafanulia mkewe. "sasa tunafanyaje" aliuliza mkewe, "sikia usiku ntaongea na watoto, wakati huo we fanya mpango wa kuelekea Qatar, na usinipigie simu mpaka nitakapokupigia mimi" aliongea kwa masikitiko, mkewe mwanzo alikataa lakini alijaribu kumuelewesaha mpaka akaelewa. Usiku aliwaita watoto wake wote na kuwaeleza hali halisi, wote walikubaliana nae na kukubali kuondoka na mama yao siku ya pili. Christina hakuwepo kwenye kikao hicho, alikuwa mbali sana katika mafunzo maalum ya kikomando.
Siku ya pili mapema familia yake yote iliondoka na kumuacha peke yake, alifungua kabati lake na kuangalia vifaa vyake vya kazi. Alitoa suti moja kali sana na kuvaa ikiambatana na viatu vyeusi vilivyong'aa, shingoni alining'iniza tai maridadi kabisa. katika sehemu ya nyuma ya kabati hilo aliiondoa nguo na kubonyeza kitufe, sehemu hio ilifunguka na kisha akaingia. Hicho kilikuwa ni chumba maalum cha siri na ndipo alipokuwa ameweka silaha zake zote pamoja na passport zake. Alichagua vifaa ambavyo vingemsaidia kufanikisha kazi hiyo ngumu, alipordhika na maandalizi hayo alitoka na kurudisha kila kitu kama kilivokuwa. Alitoa simu yake na kumpigia Robert "tukutane wapi" aliongea Mr Allen, "subiri hapo hapo kwako, natuma helicopter sasa hivi" Robert alijibu na kukata simu.
Nusu saa baadae helicopter ilitua mbele ya nyumba ya Mr Allen na bila kuchelewa alipanda na safari ikaanza. Helicopter hiyo ilitua makao makuu ya kitengo cha upelelezi mjini Washington DC, Robert alikuwa akimsubiri kwa hamu "karibu Washington" aliongea baada Mr Allen kushuka. Kisha akamfanyia ishara amfata, walitembea mpaka walipofika katika chumba maalum ambacho wengine wote walikuwa wakimsubiria mbabe wa Alex kwa hamu. Ila alipoingia tu Mr Clinton alicheka "ina maana huyo mzee ndio atakaeweza kumkamata Alex".
Maneno hayo yalimkera sana Mr Allen na bila kuchelewa aliingiza mkono nyuma ya koti lake na kutoa kisu kidogo. Kwa nguvu alikirusha kikaenda kuchoma pembeni ya kichwa cha Mr Clinton katika kiti, Mr Clinton alimeza funda kubwa la mate kisha akasema kwa nguvu "makamateni". Walinzi kama sita hivi waliokuwemo katika chumba hicho walisogea mpaka alipo Allen na kutaka kumshika lakini walichokutana nacho wanakijiua wenyewe. Mmoja alirusha kirungu kwa nguvu lakini Allen alikiona na kukikwepa kisha akamzadiwa ngumi nzito ya shingo na kumfanya aanguke kama mzigo, na hapo akaanza kuwachakaza wengine. Dakika tatu baadae wote walikuwa chini hoi "usihukumu kitabu kwa gamba lake la nje" aliongea maneno hayo huku akiweka tai yake vizuri.
 
57.

.
Wote waliokuwepo katika chumba kile walibakia mdomo wazi kwani hawakutegemea kabisa kama mzee kama yule ambae kwa haraka utafikiri ana miaka kati ya hamsini na hamsini na tano atakuwa na uwezo kiasi kile. "Jamani huyu ndie project X au unaweza kumita Allen James lakini jina lake halisi ni David Robert Mc cannon" Aliongea Robert na hapo sasa ndio wengi wakamtambua, "karibu Project X" aliongea Helen, "samahani niite Allen, Project X halina tofauti na ukiniita mbwa" alijibu huku akiwa amekunja sura kuashiria kama hapendi kuitwa vile. "hakuna shida Mr Allen" Helen alijibu huku akijibabaisha, "Sawa kwanza nina masharti yangu" aliongea Allen.
"Yapi hayo" Mr Clinton aliuliza, "la kwanza sitaki familia yangu ihusishwe na kitu chochote, pili sitapokea amri ya yoyote kati yenu isipokuwa Robert na tatu nataka kazi niifanye peke yangu sihitaji msaada wowote kutoka kwenu" alimaliza. "hakuna shida yoyote" Mr Clinton alijibu, "tuongee sasa" Allen aliongea na kuvuta kiti na kukaa. Kikao kilifanyika kwa muda wa robo saa mpaka wakafikia makubaliano, "Kwa taarifa tulizozipata Alex ameonakana Hongkong jana" Robert aliongea.
************************
Baada mshikemshike wa Brasil Alex aliondoka na kuelekea Hongkong, hii ilikuwa ni mbinu ya kuwapoteza ili wasijue anaelekea wapi. Usiku alitoka katika hoteli aliofikia kwa ajili ya kunyoosha miguu, alifika katika bar moja hivi na kuingia ili apate kinywaji. Alikaa kwenye meza moja na mrembo fulani hivi lakini Alex alipomuangalia tu aligundua kuwa hakuwa mtu wa kawaida na alionekana pale kikazi zaidi. Muhudumu alifika kusikiliza oda ya Alex, aliagiza alichotaka na muhudumu akondoka. "habari yako mrembo" alivunja ukimya, "safi mambo vipi" alijibu. "powa, mimi naitwa Alex" Alex alijitambulisha, "nashkuru kukufaham" alijibu kisha akatulia.
"Wewe unaitwa nani" ilibidi amuulize, "kulijua jina langu ni kujitia matatizoni tu" yule msichana alijibu na kutoa sigara. Wakati wote huo alikuwa akiangalia meza fulani hivi, walikuwa wamekaa watu wanne waloonekana kama wakifanya biashara. Alex aliwaangalia watu wale na kugundua kuwa walikuwa ni wafanya biashara za madawa ya kulevya. Aliingia mtu mwengie na kwenda mpaka kwenye ile meza na kumnong'oneza mmoja, ghafla baada kumnong'oneza yule jamaa aliinuka na kutoa bastola na kuielekeza katika meza aliokaa Alex na yule mschana. Kwa kasi ya ajabu yule mschana aliruka pembeni na kutoa bastola katika pochi yake, Alex nae hakulaza damu aliruka pembeni na kupiga teke ile meza waliokaa kisha akajificha nyuma. Vurugu lilianza ndani ya bar hiyo huku watu wakikimbia ovyo, yule mschana aliendelea kuwashambulia wale watu. Alex nae akaona si vibaya kama angemsaidia, alitoa bastola yake na kuanza kushambulia.
Ghafla alisikia ukwenzi mkali wa maumivu, alipogeuka alimuona yule mschana akigaragara chini huku akitoka damu mkononi, alipoona hivo aliisogeza meza upande wa yule mschana kisha yeye akabetuka kwa nguvu kutoka chini na kuanza kuwafata wale watu huku akijitahdi kukwepa risasi zao. Alipowafikia tu aliwachakaza ile mbaya, walipoona hali imekuwa ngumu waliamua kukimbia. Alex alitaka kuwafukuza lakini alikumbuka kuwa yule mschana ameumia. Alirudi sehemu aliyomuacha lakini hakumkuta, ilibidi atoke nje na kuanza kumatafuta na baada kumtafuta sana alifanikiwa kumuona akiwa anajikokota.
 
58.
"Wewe huoni kama umeumia sana" aliropoka alipomfikia, "kwanini unanifata huoni kama unahatarisha maisha yako" aliongea yule mschana kwa tabu kidogo. "sasa kati yangu na wewe nani yupo katika hatari" aliongea Alex na kujaribu kumshika bega kisha akaendelea "mi najua kama wewe ulikuwa unapeleleza". Yule mschana aliposikia maneno hayo aliruka pembeni na kutoa bastola "wewe ni nani" aliuliza. "weka bastola pembeni mimi siko hapa kukudhuru" Alex alijibu huku akitabasamu. "nambie wewe ni nani" alifoka sasa yule mschana, "si nimekwambia naitwa Alex au ushasahau" Alex alijibu.
"Najua kama jina lako ni Alex" Alifoka yule mschana akionekana kuzidiwa na maumivu. Bastola ilimdondoka na hapohapo akaanguka chini na kupoteza fahamu. "nilijua tu hutoweza kusatahamili maumivu lakini kwa kweli sijawahi ona mwanamke mkakamavu kama wewe" Alex alijisemea moyoni huku akihisi mwili wake wote umekuwa baridi. Alimbeba na kurudi nae hotelini, alipoingia chumbani kwake alimuweka juu ya meza na kisha akatoa vifaa vyake vya huduma ya kwanza. Kitu cha kwanza alichikifanya ni kuitoa risasi mkononi mwa mschana huyo kisha akamsafisha kidonda hicho na kumfunga bendeg..
Baada hapo alimbeba na kumlaza kitandani, lakini alishidwa kuyatoa macho yake katika sura ya mschana huyo mrembo kupitiliza. "hivi mtoto mzuri kama wewe, kwa nini unachagua kazi ngumu kama zetu wakati kazi nyingine za hadhi yenu zipo" alijisemea moyoni Alex. Alijitahidi kuyaonda macho yake katika sura ya binti huyo lakini alishindwa kabisa, "we Alex unafikiria nini hebu tafuta njia uende huko acha kushangaa kazi ya Mungu" alijisemea mwenyewe na kuelekea sebeleni kwa ajili ya kuupitisha usiku ambao ulikuwa mrefu sana kwake.
Alikuja kushtuka jua lishatoka, alisimama na kuanza kunyoosha viungo kama kawaida yake kisha akaelekea chooni kupiga mswaki. Alipotoka alielekea chumbani na alipofungua tuu mlango yule mschana alikurupika huku akihema. "niko wapi hapa" aliuliza kwa wasiwasi, "usijali uko sehemu salama kabisa" Alex alijibu huku akifungua kabati. Yule mwanamke alihisi kitu tafauti mwilini mwake alifunuwa shuka na kuchungulia akajikuta akitoa macho baada kugundua kuwa amebadilishwa na nguo. "umenifanya nini" aliuliza huku akitoa macho, "we unahisi nemekufanya nini" Alex alijibu bila kumuangalia.
Yule mschana alichomoka kwa kasi na kumvaa Alex na kuanza kumshushia makonde ya haja, Alex alijaribu kuyakwepa lakini baadhi yalimuingia. Alifanikiwa kumtoka mikononi "duh wewe mbona mkorofi kiasi hicho, we unadhani nimekufanya kitu kibaya. Mimi nimekutoa tu risasi iliganda mkononi na kukubadilisha nguo, sijafanya kingine" Alex aliongea huku akihema. Hapo alijiangalia mkononi na kukuta bendeg, "oh samahani si unajua watu wengi wanajichukulia point ikiwa mwanamake hajielewi" Alibadilika ghafla na kuwa mpole. "bila samahani hata ingekuwa ni mimi nisingekuelewa kwanza" Alex alijibu huku akijishangaa na kujiuliza mbona mwepes sana kwa binti huyo. Alex alitoa suruali yake moja na kumrushia, baada kuvaa walitoka wakaelekea sebeleni.
 
59.
"sorry kwa lililotokea jana" alianza kuongea yule mschana "jina langu Scarlet" alijitambulisha. "jina zuri" Alex alijibu, "we umesema unaitwa Alex si ndio" aliendelea kuongea Scarlet, "yeah" Alex alijibu. "imekuaje ukajua kama mimi ni mpelelezi" Aliuliza kwa shauku, "kwa sababu mimi mwenyewe ni kama wewe tu" Alex alijibu. "na wewe pia mpelelezi" aliuliza kwa mshangao, "si mpelelezi kama unavofikiria, mimi ni muuaji wa kimataifa" Alex alijibu na kuzidi kumshangaza binti huyo. Waliendelea kuongea mambo mengi sana kama kwamba walikuwa ni marafiki wa muda mrefu. Wakati wanaendelea na maongezi simu ya Alex iliita "kuna nini" alipokea na kuongea kwa hasira, alisikiliza simu kwa makini na baada kukata mudi yake ilibadilika ghafla. "wewe unaelekea wapi ukitoka hapa" Alex aliuliza, "kuna pahali nakwenda ambapo itakuja helicopter kunichukua" Scarlet alijibu. Alex aliinuka na kuelekea chumbani kwake na kungia bafuni, alioga na alipomaliza alirudi sebeleni kashabadilisha nguo. "hii sehemu haifai tena tuondoke" Aliongea a Scarlet alimuelewa anamaanisha nini. Walitoka hotelini na kuelekea sehemu ambayo scarlet anakuja kuchukuliwa na wenzake.
**********************************
Ndege inakanyaga ardhi ya Hongkong na anaonekana mzee mmoja wa makamo akishuka akiwa na briefcase ndogo. Hakuwa mwengine isipokuwa Allen James ambae ndie rasmi aliekabidhiwa kazi ya kumtia Alex nguvuni. Alitoka mpaka nje ya uwanja na kuangaza huku na kule mpaka alipoona gari nyweusi aina ya mercides benzi. Kwa mwendo wa taratibu alitembea mpaka ilipo na kuingia, aliwsha gari na kwenye kioo ikatokea ramani inayomuonyesha hoteli anayokaa Alex ilipo. Aliondoa gari hiyo kwa mwendo mdogo na kuelekea inapomuelekeza ramani. Alifika nje ya hoteli hiyo na kushuka, aliingia ndani na hakuuliza chochote mapokezi. Moja kwa moja mpaka kwenye lifti na kuelekea gorfa ambayo chumba cha Alex kilikuwepo, kwa umakini wa hali ya juu alifungua mlango na kuingia. Alitembeza macho chumba kizima na kuyaangalia madirisha yote. Alipofika kweny dirisha moja alisimama na kuangalia nje, aliangalia kwa umakini wa hali ya juu na bila kusita alitoa bastola yake kiunoni na kufyatua risasi iliopasua kioo na kuelekea gorofa jirani. "mbinu hizi ni za kitoto sana" alijisemea na kujibanza ukutani.
Kumbe Alex alikuwa ametega gorofa jirani na hilo akiwa na bunduki yake ya kudungulia, lakini Allen alishtuka na kumtungua yeye kwanza bahati nzuri Alex aliwahi kuinama hivyo risasi iliopita kwenye darubini ya bunduki yake ilimkosa na kama angechelewa kidogo tu basi risasi ile ingeingia jichoni. "si nilikwambia alitumwa wakati huu kukukamata, unatakiwa ukajipange upya kabla ya kumvaa" . Alikuwa akiwasiliana na mtu kupitia kifaa maalum alichokiweka sikioni. "huyi ndio Allen James" aliongea kwa taharuki, "kabisa ndio mwenyewe huyo, au wanamuita Project x. Huyo ndugu ni balaa na usipokuwa makini huenda akakuzidi katika mchezo huu ambao umeuanzisha wewe mweyewe".
 
60.

"Sasa nifanye nini kwa maana tayari kashaiharibu bunduki yangu" Alex aliuliza na kwa maara ya kwanza anajikuta akiingiwa na hofu na mwili wake kuwa wa baridi. "cha kufanya toroka na uje Russia, muda wa kuonana mimi na wewe umefika" , "hakuna shida, wacha nitafute mbinu mbadala ya kuchomoka hapa bila kushtukiwa"Alex aliongea na kuipangua bunduki yake aina ya M21 na kuirudisha katika begi lake. Alishuka gorofa hilo kwa umakini na alippfika chini aliingia kweye gari aliokuja nayo na kutoweka eneo hilo.
***********************.
Baada ya kufika sehemu ambayo Scarlet anakuja kuchukuliwa, Scarlet alitoa kifaa maalum kidogo na kukibonyeza. Dakika kumi baadae ilifika helicopter "kwa heri Alex na nashkuru kwa msaada wako, na kuhusu tabia yangu usijali kwa sababu THIS IS THE REAL ME, ipo siku nitakulipa wema wako" Alipanda kwenye helicopter na kuondoka. "dah kwa hiyo ndio wananiletea kizee wakati huu, ama kweli wamechoka. Alitoa kifaa maalum cha mawasilino na kukiweka masikioni kisha akakiwasha "naomba unielekeze sehemu ambayo nitapata vifaa vya kazi" aliongea Alex, "Alex huyo jamaa ni balaa, kila uanchokifanya wewe yeye tayari alishakifnya. wewe leo unatafutwa watu wachache tu, yeye alikuwa akitautwa na serekali America na bado amewauwa mpaka viongozi wakubwa wenye ulinzi mkali sana".
"Lakini kipindi hicho sio saa hivi eti" Alex aliongea kwa dharau, " mi nakushauri tulia kwanza ujipange ndio umkabili laa sivyo atakushinda tu". "nimekwambia unielekeze duka la silaha na siyo kuanza kunipa mawaidha" Alex alifoka kwa hasira. "sawa nenda mpaka kwenye hoteli uliofikia katila maegesho ya magari kuna toyota nyeupe chukua na kila kitu utakuta humo". Baada maongezi hayo Alex alirudi katika ile hoteli na kuchukua gari alioelekezwa. Alikuta ramani ya maduka yote yanayouzwa silaha a bila kuchelelewa aliwasha gari na kuondoka.Alinunua kila alichotaka na kuondoka, alirudi kule kule hotelini lakini hakuingia katika hoteli aliyofikia badala yake alipada katika gorofa la pembeni yake na kwenda kujitega sehemu aliokuwa na uhakika hatoonekana. Alipanga sniper yake na kuweka kila kitu tayari kwa ajili ya kazi "we mzee umechoka na maisha subiri nikusaidie kukupeleka kwa muumba" aliongea na kutabasamu.
*****************************
Baada kutoka gorofa lile aliingia kwenye gari na kuondoka kwa kasi bila kujua kama Allen alikuwa tayari chini akimsubiri, baada Alex kuondoa gari tu Allen nae aliwasha na kuanza kumafatilia. "doh hiki kizee balaa" Alex alijisemea moyoni lakini alipoangalia kwenye kioo cha pembeni akagundua kama kuna gari inamfatilia. "ntumie ramanai ya jiji zima hili"Alibonyeza kile kifaa cha mawasiliano na kuongea na muda si mrefu katika omputer ya gari yake ilitokea ramani ya Hongkong yote. Aliongeza mwendo wa gari na Allen nae hakuwa nyuma ila yeye hakuhitaji ramano mji mzima alikuwa anaujua kama kiganja chake cha mkono. Sasa ilikuwa ni fast and furious maana wote wawili walikuwa mafunfi katika kumudu gari. Alex alijitahidi kumtoroka mzee huyo lakini wapi ngoma ilikuwa nzito, wakati Allen akiendelea kumfukuza Alex aliangalia kwenye kioo cha pemebeni na kugundua kuwa kuna gari zinamfatilia. Alichikifanya aliacha kumfukuza Alex na kubadilisha njia ili awatoroke na hiyo ndio ikawa nafuu kwa Alex.
Allen alizidi kukanyaga mafuta na alifka katika kona na kuserereka, gari yake iligeuka ilipotoka hivo akawa yuko uso kwa uso na gari ya waliokuwa wanamfatilia. Alitoa bastola yake na kutoa mkono nje kisha akaanza kuishambulia ile na kuisababishia kugongana na gari nyingine.
 
61.
Alivuta handbreak na gari yake ikaserereka tena na kugeuka ilipokuwa ianaelekea kisha akakanyga mafuta na kutoweka. "ndio umefanya nini vile sasa" Robert alilalamika wakati anangea na Allen kupitia kifaa maalum, "umesahau kama tulikubaliana kazi hii nitaifanya peke yangu bila kufuatwa fuatwa" Alijibu Allen akionekana kukerwa na kitendo kile. "sasa kama leo nimeshambulia gari mara nyingine nitawauwa kabisa muje kubeba mizoga, na mukiendelea kunifatilia nitawafanya kitu ambacho hata Alex hatokufikia kwa ubaya" Aliongea Allen na kukata simu, "Allen, Allen" Robert aliita lakini wapi. "mi niliwaambia musifanye mukajifanya hamuelewi sasa mnaona, huyu ni hatari zaidi kuliko Alex. Hivi hamjui kama yupo namba mbili kwenye Blacklist" Alifoka Robert kuwaambia kina Mr Clinton na wengine waliojifanya kukiuka masharti ya Allen James.
Alex alifika uwanja wa ndege na kukata ticket ya kuelekea Urusi, "hivi huyu Allen ndio mbabe sana ama vipi, haiwezekani kizee kinishinde. Kwani ana nini hasa kinachomfanya awe special kuliko mimi" hayo yalikuwa ni baadhi ya maneno aliokuwa akijisemea moyoni baada kupata pigo kubwa kutoka kwa Allen James. Muda wa kupanda ndege ulfika na abiria wote waliingia kwenye ndege na safari ikaanza, safari yote Alex hakupata usingizi hata kidogo alikuwa akiwaza na kuwazua mbinu za kumchapa Allen.
Allen baada kukata mawasiliano na makao makuu ya upelelezi alitafuta mgahawa na kikata akaaanza kuwaza ni sehemu gani aliokwenda Alex. "kama natafautwa na Marekani, nitakwenda nhi gani ambayo nitakuwa salama" alikuwa akijiuliza swali hilo kichwani mwake. "kwa vyovyote vile nitakwenda nchi ambayo ina mkwaruzano mzito na Marekani na hiyo itakuwa ni Urusi tu" alipata jibu na kunuka sehemu aliokaa moja kwa moja mpaka kwenye gari yake na safari ya kwenda uwanja wa ndege ilianza. Njiani aliwasiliana na Robert aone kama atapata majina ya abiria walioondoka siku hiyo, majina yalipatikana lakini la Alex halikuwemo. Hata hivyo alikuwa na uhakika kama Alex atakuwa ameelekea urusi. Alifika uwanja wa ndege na kukata tiket, muda ulifika na safari ikaanza.
*********************************
Ndege ilituwa mjini Moscow majira ya saa saba usiku, kijana Alex alishuka na kuelekea njea ya uwanja. Ujumbe uliingia kwenye simu yake na kumpa maelekezo, alifata maelekezo hayo. "karibu Moscow" Nicolay aliongea na kumpa mkono Alex, "asante" Alex alijibu. Nicolay alimwabia, amfuate na kuongoza njia. Walifika mpaka kwenye gari na safari ya kuelekea asipopajua Alex ikaanza, ilkuwa ni safari ndefu na hatimae walifika. Alex alishuka na Nicolay akaoandoka, mlango ulifunguliwa "karibu nani Mr Alex" Christine aliongea. Alex aliingia bila kuuliza hata swali moja, alipelekwa mpaka katika chumba ambacho angelala kwa usiku huo. "Saa hivi pumzika, tutaongea kesho" Christine aliongea na kuaga. Alex aliingia bafuni na kujimwagia maji kisha alirudi chumbani na kujilaza kitandani na kutokana na uchovu wa safari usingizi ulimchukua ghafla.
 
62.

Siku ya pili mapema asubuhi Alex aliamka na kama kawaida yake kufanya mazoezi kwa ajili ya kuweka mwili sawa. Aliingia chooni na kujifanyia usafi, baada kumaliza kila kitu ndani ndipo akaamua kutoka nje. Alikuta chakula mezani, "habari zaasubuhi" Christine alimuuliza. "nzuri tu" Alex alijibu na kukaa kwenye kochi. "kariu mezani tupate kifunguwa kinywa halafu tuingie kazini kuna mambo mengi sana unatakiwa uyajue" alisemea Christine huku akisimama na kuelekea mezani Alex nae hakuwa nyuma hasa ukizingatia jana yote baada kula asubuhi hakula tena mpaka wakati huo. Wakati wanakula "hivi umenijuaje" Alex alivunja ukimya, "nilijua tu utaniuliza swali hilo" Christine alijibu kisha akaendelea.
"Mimi nakujua kuliko unavojifahamu wewe mwenyewe, ila kiufupi nilikuwa nikifanya kazi kama secretary katika kitengo cha upelelezi nchini Marekani lakini kutokana na mambo ambayo bosi wangu alikuwa akinifanyia ilibidi niache kazi kwa kufeki kifo, mpaka muda huu tunaoongea wanaamini nimekufa. Na nilijipa ahadi moyoni kama lazima nitalipa kisasi" Aliongea Christine huku macho yake yakionesha ishara ya kujaa maji. "dah pole sana lakini kwanini ukanisaidia" Alex aliuliza, "ni kutokana na kuwa na ugumu kulipa kisasi mimi kama mimi ndio maana nikaamua kukusaidia kwa sababu mimi na wewe tunashare adui mmoja" Alijibu. Maongezi yalienedelea mpaka walipomaliza kula. .
Christine aliinuka na kumwambia Alex amfuate, moja kwa moja walielekea katika chumba maalum ambacho kilikuwa kimepambwa na computer nyingi sana. "karibu humu ndio ofisini kwangu" aliongea Christine na kukaa kwenye kiti, "unafanya kazi peke yako humu" aliuliza kwa mshangao Alex. "ndio, ila nina wasaidizi wangu ambao ndio wale waliokuletea bahasha na yule alikuja kukupokea uwanja wa ndege. "si mchezo" Alex alijikuta akisema tu maneno hayo, "ok hatuna muda wakupoteza muda si mrefu Allen James atajua uko wapi, inabidi tufanya haraka na tuondoke eneo hili" Christine aliongea.
"hivi imekuaje huyu Allen akawa hatari kiasi hichi" Aliuliza Alex, "huyo mzee ni miongoni mwa watu wa mwanzo kujaribiwa na kemikali ya CODE X, mwanzo kemikali hiyo ilikuwa kali sana na wenzake wote walikufa wakati wa mchakato. hata hivyo mkewe ndie mtu ambae aliivumbua kemikali hiyo, na baada kugundua madhara yake ikiwa itaangukia mikononi mwa wa baya. Aliiharibu na kupoteza ushahidi wote, na pia aliitengeza keikali nyingine kwa ajili ya kuizimuwa lakini matokeo yake ndio akatengeza kiumbe kama huyo" Christine alimueleza, Alex alikuwa hoi baada kusikia hivo "sasa huyu jamaa nitapamabana nae vipi unadhani". "hatuna haja ya kupamabana nae, tunachotakiwa kufanya ni kumkwepa tu mpaka tuhakikishe tunamaliza kazi yetu.


.
Allen James anatoka nje ya uwanja wa ndege mjini Moscow, "Alex utakuwa umejificha wapi" Aliongea na kutafuta mgahawa wa karibu na kuingia. Alitoa laptop yake na kuanza kuhack computer za uwanja ndege kwa ajili ya kuangalia kama atapata chochote cha kuanzia. Lakini bahati mbaya sana hakukuta hata video moja iliomuonyesha Alex, tayari Christine alishafuta picha na video zote zilizomuonyehsa Alex. "vizuri sana lakini hapa umegonga mwamba ulioizamisha titanic" Allen alijisemea moyoni na kuatabasamu, kisha akaanza kuhack katika mafaili yaliofutwa. "bingo" Alijisemea baada kuzipata video zilizofutwa na zilimuonyesha Alex akitoka uwanjani. Video zilionyesha kila kitu mpaka alivopokewa na Nicolay, alifanikiwa kupata namba za gari ya Nicolay. "wacha mchezo uendelee" aliongea na kufunga laptop yake kisha akaondoka kwenye mgahawa huo. Alikodi taxi na kuelekea mpaka anapokaa Nicolay, aligonga mlango "nani wewe na unataka nini" alitoka mwanamke mmoja wa makamo hivi. "naomba kuonana na Nicolay" aliongea kwa upole, "Nicolay ndio nani" aliongea na kutaka kufunga mlango. Allen aliweka mguu na kutoa bastola yake na kumuwekea katika paji la uso, yule mwanamke alianza kutetemeka huku kijashi chembamba kikimtoka. "hakuna haja ya kuekeana bastola" ilisikika sauti ikitokea nyuma, "karibu" Nicolay aliongea kwa tabasamu. Allen aliingia na kumshukuru. Nicolay aliumuonyesha ishara yule mwanamke na kuondoka, "mimi nataka kujua tu kuhusu sehemu alipo Alex" Aliongea Allen. "na nisipokwambia je utanifanya nini" Nicolay aliongea kwa kujiamini, "utaniambia tu hata kama itabidi nijue kwa kutoa tone moja moja la damu katika mwili wako basi nitafanya hivo" Alijibu Allen akionekana kuwa hana masihara hata kidogo na jambo aliloongea.
 
63.

NIcolay alikaa kimya akiwaza kitu, "akikuuliza chochoe wewe mwambie tu maana hatoondoka mpaka apate jibu analoliyaka" aliakumbuka maneno ya Alex. Ndio wakati Allen alivyokuwa anabasihana na yule mwanamke, Nicolay alimpigia simu Christine na kumwambia kuwa Allen yupo nyumbani kwake, Christine alishindw ajibu nini na ndipo akampa Alex simu. Alex baada kupewa simu alimwambia kuwa amwambie anachotaka kujua jwa sababu pangechimbika kama asingemwambia ukweli. "sawa unataka kujua alipo Alex" aliuliza Nicolay, "ndio we nambie tu yuko wapi na wala sitokugusa" Allen alijibu. Basi Nicolay hakuwa mbishi tena alimwabia sehemu alipo Alex, na Allen aliondoka bila hata kumgusa unywele. "doh kiasi Alex amuogope huyu mtu" Nicolay alisijisemea moyoni huku akijifuta kihasho kilichokuwa kikimtoka japo kulikuwa na naridi kali wakati huo..
"Sasa tunafanyaje" Christine alimuuliza Alex baada kumsikia akimwambia Nicolay amwambie Allen anachotaka. "ikiwa Nicolay atamwambia ukweli nina uhakika Allen hatomdhuru so sisi tutafute makazi mengine maana hapa hapafai tena" Alex alijibu. Bila kuchelewa walianza kufungasha mizigo yao na walipohakikisha wamechukua vitu muhimu Alex akasema "we tangulia katafute pakukaa, niache hapa ili tusije tukamponza Nicolay, akifika Allen hapa nitajaribu kumpotezea muda halafu nitamtoroka". "acha na hilo wazo lako, unadhani utaweza kumtoroka kirahisi rahisi hivyo" Christine aliongea huku akionyesha wasiwasi. "we nenda haraka mi najua nitamtokaje huyu kiumbe" Alex aliongea kwa ukakamavu na Christine alikubali na kuondoka. Alex alijipanga ikiwemo na kukagua silaha zake ambazo angezitumia kukabialiana na Allen.
Dakika kumi tu baada kuondoka Christine, Allen alitia timu eneo hilo na kuanza kulikagua kabla hajaingia ndani. Alifika mlangoni na kutoa bastola yake ndogo kisha akaifunga kiwambo cha kuzuia sauti. Aliribu kuufungua mlango ukafungunguka bila shida yoyote, ile kuingia tu Alex alianza kumimina risasi lakini kutokana na wepesi wa Allen alifanikiwa kuruka pembeni na kujibanza kwenye kipembe. "mi nilijua tu huwezi kukimbia kwa sababu unataka kujua kitu gani hasa nnacho ambacho wewe huna" Allen aliongea, "humu ndani ni mimi au wewe lakini wote wawili hatutoki" Alex alijibu kwa hasira. "punguza hasira kijana"Allen aliongea na kutoka sehemu alipokuwa amejificha huku akishamblia kwa risasi. "hivi huoni kama unatumika tu, baada kukaa kwako na familia yako" Alex aliongea kujaribu kumvuruga. "sasa wewe ungetulia kwenye kambi yako, uandhani mimi ningekuwa hapa kukuwinda" Allen alijibu akionekana ana wasiwasi hata kidogo. Alex alichungulia ili aone Allen uko wapi, alipotoa tu kichwa alikoswakoswa na risasi.
"Sijakukosa hiyo ujue, nimefanya makusudi ili ujisalimishe na kila mtu akaendelea na maisha yake" Allen aliongea huku akicheka. "kama unahisi wewe unajiweza kwanini tusichapane mkono" Alex aliongea huku akitoka sehemu aliokuwa amejificha. "halafu mimi pia nlikuwa nataka iwe hivo maana nina miaka mingi sana, sijapigana na mikono yangu inawasha sana" Allen alijibu na yeye akatoka sehemu aliyojibanza. Ni kwa mara ya kwanza Alex anamuona kwa ukaribu zaidi, alishangaa kuona mtu anaemuita mzee kumbe ni kijana kabisa. "ulidhani nitakuwa kikongwe, asante kwa dawa alionipa mke wangu umri unakwenda lakini kasi ya kuzeeka ni ndogo" Allen aliongea baada kugundua mshangao wa Alex. "natumai hutoniangusha, isije ikawa ni mpambano wa sekunde kadhaa tu" Alex aliongea na kunja ngumi kisha akamfata Allen kwa kasi, Allen alimkwepa na kumzawadia ngumu tatu nzito za mbavu na moja ya kifua. "acha kuja kama nguruwe kijana utaumia" Allen aliongea baada kuhisi ngumi zake zimegonga ndipo.
Alex alikohoa kidogo na alihisi kitu kama maji kikimtoka mdomoni, na alipojigusa akagundua kuwa alikuwa akitoka damu. Lakini hakulijali hilo, alijiweka sawa na kumfata tena. Wakati huu alikuwa makini sana, alisukuma masumbwi kadhaa lakini Allen aliyakwepa yote na kumtadika teke zito la kifua lakini Alex aliliona na kurudi nyuma na kabla Allen hajakaa sawa, Alex alirudi mbele kwa kasi na kurusha ngumi nzito ilipenya sawasawa kwenye kifua cha Allen. Allen alipoona kashachelwa kuizuia ngumi hiyo alipiga hatua moja nyuma na kukaza misuli ya kifua, ngumi hiyo ilimpata lakini haikuwa kali kama alivyotegemea Alex. "so mbaya kumbe ukitulia unaweza kupambana vizuri tu" Allen aliongea na kutabasamu.
 
64.
Mpambano uliendelea huku Alex akionekana kuzidiwa na Allen, Allen alirudi hatua kadha nyuma ili kumpa Alex uwanja wa kupumua maana alielewa shughuli imemuelemea, Alex alipoona hali mbaya alikimbilia bastola yake lakini alipogeuka Allen alikuwa kashatoweka tayari. Alimtafuta nyumba nzima bila mafanikio yoyote, wakati akiendelea kufanya hivo simu yake iliita na alipoipokea "leo si siku ya kukumata nilikuwa nakupima uwezo tu lakini nasikitika umeniangusha sikutegemea kama anaesifiwa kuwa yuko rank moja na mimi ni mwepesi kiasi hicho, kajipange upya lakini kaa ukijua nitaendelea kukufatilia" simu ilikatika, Allen James ndie aliepiga simu hiyo. Alex alijikuta akiumuka kwa hasira maana yale maneno yalikuwa yamejaa dharau, siku hiyo ndio siku ambayo alihisi amedhalilika vibaya. Alikaa kwenye kochi na kumpigia Christine simu, baada kupewa malezo alipo mwanamke huyo. Alex alitoka na kuelekea huko lakini alikuwa amekasirika vibaya.
******************************
Mafunzo makali yaliendelea katika kambi moja hivi iliokuwepo jangwani, "ukiendelea hivo hutomaliza mafunzo" aliongea mtu ambae alikuwa akisimamia mafunzi hayo. "nani kasema mimi sitamaliza haya mafunzo" Agent Darling ama Christina au mtoto wa Allen James alijibu. "wengi walisema hivo lakini wakaachia mafunzo njiani" alijibu mwanaume huyo huku akitabasamu. "hata mimi nina imani utamaliza ikiwa utajitahidi sana maana mafunzo haya kila siku yanazidi kuwa magumu" alienedelea kuongea mwanaume huyo. Baada mazoezi Christina alimtafuta mwalimu wake huyo, "hivi mbona unaoenekana mdogo kuliko cheo ulichokuwa nacho" alimuuliza.
"Mimi nilinngia jeshini nikiwa mdogo sana" alijibu kisha akaendelea "si uliwahi kusikia kuna mtu anatumia jina la Ghost kama jina lake la kazi". "ndio" Christina alijibu, "sasa huyo mtu ndio mimi" Alijibu na kumuangalia Christina usoni, "wewe ndie Supreme commando Jeff the Ghost" aliuliza kwa mshangao. "ndio ni mimi" Jeff alijibu, Christina alibaki ametoa macho tu kwa sababu katika watu ambao alikuwa akiwakubali mmoja ni Jeff. "mafunzo haya ni magumu sana lakini matunda yake acha kabisa, ukisikia mtu anacheo cha THE ONE AND THE ONLY, ujue ni mtu wa kuogopwa sana ni zaidi ya commando" Jeff aliongea maneno hayo na kuona uso wa Christina ukichanua kwa tabasamu..
"haya nambie imekuaje" Christine alimuuliza Alex alipofika hoteli aliyopanga, "acha tu kweli yule jamaa ni kiboko, kwa kweli amenitimba kisawasawa" Alex alijibu huku akishika upande wa mbavu za kulia. "mi nilikwambia Allen ni hatari sana" Chrstine aliongea, "lakini cha ajabu ameniachia wakati alikuwa na uwezo wa kuniua" Alex aliongea kwa sintofahamu. "achana na mambo hayo kwanza hebu badilisha nguo tuende hospitali kwanza maana naona hali yako si nzuri. Alex alikubali lakini aliposimama miguu ilikataa kumuonyesha ushrikiano kabisa alijikuta anaanguka na macho yake yakaanza kutandwa na ukungu na kwa mbali akaanza kuona kiza. Alijitahidi kupambana na hali hiyo lakini wapi kila sekunde kiza kiliongezeka na hatimae akapoteza fahamu kabisa, Christine alijaribu kumuamsha lakini wapi. Alitoa simu na kupiga namba za dharura, haukupita muda gari ya kubebea wagonjwa ilifika na Alex akawahishwa hospitali.


Alipofika alipelekwa moja kwa moja mpaka kwenye chumba cha matibabu ya dharura kwanza ili kupewa hatua ya kwanza ya matibabu. Baada hapo alipelekwa chumba cha wagonjwa mahututi na kianza kupewa matibabu. Christine alibakia nje akingojea majibu kutoka kwa daktari ambae alikuwa anamshughulikia Alex. "wewe ndie ndugu wa mgonjwa" alitoka datkri mmoja na kuuliza "ndio" Christine alijibu. "Sawa sasa ni hivi, tumefanikiwa kumstablize mgonjwa lakini hatujui lini ataamka kutoka a kuumia sana hasa sehemu za ndani" Daktari aliongea. "kwani kitu gani alichoumia sana" aliuliza kwa shauku Christine. "amevunjika mbavu mbili za kulia, na nyingine mbili zina ufa, pamoja na kuchanika baadhi ya mishipa mikubwa ya damu" alijibu daktari.
"Sasa anaweza kuchukua siku ngapi mpaka kupata fahamu zake" aliuliza tena. "hatujui kwa kweli, inategemea na nguvu ya mgonjwa wako" alijibu daktari. "asante kwa taarifa zako" aliongea Christine na kukaa kwenye kiti akiwa anamawazo kibao kichwani. Siku mbili zilipita na bado Alex alikuwa chini ya uangalizi maalum wa madaktari, japo hali yake ilikuwa ikiendelea vizuri lakini bado hakuamka. Alionekana mtu mmoja ndani ya mavazi ya kidaktari, alielekea kwenye ngazi na kupanda taratibu bila wasiwasi. na alipofika gorofa ya tano alikata kulia na kuelekea chumba ambacho alikuwa amelazwa Alex.
 
65.

Aliingia ndani na kufunga mlango kisha akakaa pembeni ya kutanda. "kijana ndio unataka kulipa kisasi ukiwa katika hali hiyo, dhaifu namna hiyo" aliongea daktari ambae hakuwa mwengine ila ni Allen James, "huwezi kuondoka mapema kiasi hicho, ni lazima uamke ili na mimi nikamilishe kazi yangu" aliendelea kuongea Allen James akionekana kusikitishwa na udhaifu wa Alex katika kuhimili kishindo kidogo tu. Mapigo ya yaliokuwa yakisomwa katika computer maalum yalianza kuongezeka huku upumuaji wa Alex ukianza kubadilika. "hivo ndivo ninavotaka lazima uamke" aliongea Allen huku akitabasamu, hali ilizidi kubadilika. "amka ili tuendelee kucheza kamchezo ketu, lazima uamke commando hawezi kukaa kitandani siku zaidi ya tatu" Aliendelea kuongea huku akicheka.

Kwa mbali Alex alianza kusiki mawimbi ya sauti na alihisi kama anaifahamu vile, alijaribu kupambana na usingizi wake wa kifo ili kurudi hewani. "ndio, hivo ndio commando anatakiwa awe" Allen aliendelea kuongea manen ambayo yalitikisa ngoma za masikio za Alex na kuufanya ubongo wake ambao ulikuwa umelala kurudiwa na maisha huku akiitambua sauti hio kuwa ni ya mtu aliepeleka kwenye ulimwengu wa kiza. Ghafla Alex alifungua macho na ana kwa ana akakutana na sura ya Allen James aliekuwa akitabasamu. Alex alitaka kuinuka lakini Allen alimzuia na kumwambia"bado acha haraka subiri kwanza wala usiwe na wasiwasi mimi nimekuja kama rafiki kuja kukuona tu na wala sina nia ya kukudhuru" aliongea Allen na kumrudisha Alex kitandani.
"Natumai karibuni tutaonana tena vitani Alex Jr" aliongea Allen na kuinuka kisha akaminyia jicho na kuweka kidole mdomoni kama ishara ya kumwambia asije akaongea kitu kisha alifungua mlango na kuondoka. Dakika mbili baadae daktari alifika huku akihema, "viipi kijana unajisikiaje" Aliuliza. "niko powa" Alex alijibu , doctor alizikagua computer zote na kufanya tathimini ya haraka mpaka aliporidhika. Aliwaita wasaidizi wake na kuzifungua mashine zote ailizokuwa zikimsaidia Alex na baada ya hapo walimuhamisha chumba na kumpeleka katika wodi za wagonjwa wa kawaida.
Baada hapo doctor alimpigia simu Christine na kumueleza hali halisi kama ilivyo, haukupita muda mrefu Christine alifika hospitali na moja kwa moja alikwenda katika chumba alicholazwa Alex baada kuamishwa ICU. "unajisikiaje" swali la kwanza alilomuuliza, "ah najiskia fresh tu" Alex alijibu huku akitabasamu. Taratibu za kutoka hospitali zikafanyika na akaruhusiwa kuondoka aende kumalizia kujiuguza nyumbani. Alipewa baadhi ya dawa za kumsaidia, walitoka Hospitali na kuanza safari ya kurudi bila kujua kama kulikuwa kuna mtu ana wafatilia katika gari nyingine. Lakini ghafala kioo cha mbele cha gari iliokuwa ikiwafatilia kipasuka na damu nyingi ikaruka. "nimesema sitaki kuingiliwa katika kazi yangu" Allen aliongea huku akiliangalia bomba la sniper yake likitoa moshi baada kufyatua risasi..
**********************************
"Bosi mtu wetu aliekuwa akimfatilia Alex ameuwawa" Aliingia Martin ofisini kwa Mr Clinton na kutoa taarifa hizo, "unasemaje wewe" aliongea huku akisimama. "ndio amepigwa risasi lakini mpaka sasa hatujajua aliempiga ni nani" alijibu na kuongezea. "we unadhani atakuwa nani kama si Allen James" aliongea kwa hasira Mr Clinton, "niitie Robert" alitoa agizo na bila kuchelewa Martin alitoka na kuelekea ofisini kwa Robert na kumpa taarifa ya wito huo. "naam bosi" alifikia na kuongea, "umemuona mbwa wako alichokifanya" alifoka Mr Clinton,"mi mbona sina mbwa" alijibu Robert. "unajifanya humjui mbwa wako Allen James" aliongea kwa sauti kubwa, hapo hapo Robert alivua kitambulisho chake na kuchomoa bastola yake kiunoni pamoja na funguo za ofisi na kuziweka mezani.
 
66.



"Una maana gani kufanya hivi" alifoka Mr Clinton, "kwani hujui maana yake au vipi" sasa na Robert alipandisha kifua. "nimeacha kazi rasmi leo, siwezi kuvumilia ushenzi wako. we utamuitaje binaadamu mwenzio mbwa wakati unajua ameacha familia yake nyumbani kuja kukuasaidia wewe wakati anajua kabisa huenda matokeo ya kazi hiyo yakamgharimu maisha yake. Kwani Allen alisemaje kuhusu kazi hii, ataifanya peke yake bila msaada wenu sasa kilichokutuma upeleke watu wako ni kitu gani.
"Na kama hujui mimi ndie niliemwambia kama bado unamfatilia na ndie nliempa ruhusa ya kumuua mtu wako" Robert alimaliza kuongea na kuondoka. Mr Clinton alinyanyua mkonga wa simu na kutoa amri akamatwe na bila kuchelewa wanajeshi wakaingia ndani yamjengo na kuanza kumuwinda Robert. Ambalo hawakuliju kuhusu Robert ni kwamba alikuwa mmoja kati ya watu watano wa mwanzo pamoja na Allen waliofanyiwa jaribio la CODE X. Ila yeye alipewa jina la HUMAN KILLING MACHINE (H.K.M), mashine ya kibinaadamu ya kuuwa. Alipogundua kama imetolewa amri akamatwe alijibanza pahali, na mwanajeshi wa kwanza kupita alimkamata na kumvunja shingo. Kisha akahukua bastola na kuanza kukimbia, kila mwanajeshi aliepeita mbele yake alichezea risasi.
Risasi kwenye bastola aliokuwa anatumia zilikwisha, hivyo aliitupa na kuendelea kukimbia. Kwenye kona ghafla alitokea mwanajeshi, Robert alidunda na kupiga sarakasi ya mbele na alipotuwa tu alibiringitia chini na kufika alipo mwanajehi huyo. Hakuchelewa alibetuka kutoka chini na kumtandika teke zito la kidevu lililomrusha mwanajeshi huyo na kumbamiza ukutani. baada hapo alichungulia kwenye ngazi na kuona kundi la wanajeshi likipanda juu, alirudi kwenye koridoo na kuangalia disrisha moja la upande wa kulia ambalo lilikuwepo mita kadhaa kutoka alipo. Na kwa sababu alilielewa jengo hilo vizuri hakusita alifyetuka kama risasi na kwa kasi ya ajabu alikwenda moja kwa moja kuruka.
Alipasua dirisha katika gorofa ya thalathini na kutoka, kutokana na kasi aliokuwa nayo alifanikiwa kupenya katika kioo cha gorofa jirani na kuangukia kitandani. Aliinuka na kuweka suti yake sawa kisha akatoa check ya bank na kumkabidhi mwanaume aliemkuta katika chumba hicho. "wakitaka uwalipe utawapa hio sawa" aliongea na yule mwanaume alingisha kichwa kuashiria amekubali. Baada hapa Robert alifungua mlango na kutoka, alifika chini na kukuta mtu anashuka kwenye pikipiki, "niazime usafiri wako" aliongea huku akimnyang'anya funguo kijana huyo na alipoleta ubishi alichezea ngumi ya kifua na kuanguka chini kama mzigo.
Aliwasha na kutoweka eneo hilo kama vumbi, "ametutoroka" aliripoti mwanajeshi mmoja. "nyie ama kweli hamuna faida" alifoka Mr Clinton, "mkuu kuna tatizo" aliingia Martin huku akihema. "nini tena" Mr Clinton aliuliza, "njoo mwenyewe ujionee" aliongea Martin na kutoka ofisini, Mr Clinton alifata nyuma. Alifika katika chumba ambacho alipelekwa na Martin. Macho yalimtoka baada kukuta miili ya wanajeshi zaidi ya thalathini ikiwa imelazwa. "nani aliefanya hivo" aliuliza, "Robert mkuu" Alijibu Martin. "haiwezekani na alivyo boya vile" aliongea kwa dharau. Maggy aliingia na laptop ndogo mkononi ikionyesha video kwa jinsi Robert alivyokuwa akitekeleza mauaji, Mr Clinton alipoiona tu hiyo video alipata mshtuko wa ghafla na kuanguka chini na kupoteza fahamu.
**********************************
 
67.

"Nipe ripoti"aliongea mtu mmoja, "kila kitu kinakwenda kama kilivyopangwa" alijibu Robert. "kazi nzuri sana" alipongeza yule mtu. "ikiwa mambo yatakwenda hivi mpaka mwisho basi itakuwa vizuri sana" aliongea yule mtu. "unaweza kwenda kupumzika" Robert alipewa ruhusa na kutoka, "mkuu, kazi inakwenda kama ulivyopanga" yule mtu alinyanyua simu na kupiga. "usijali hakuna hata mmoja atakaeshtukia mchezo mzima, lets them play the dirty game" aliongea kwa majigambo huku akicheka..
Alex na Christine wala hawakushtuka kama wanafatiliwa, waliekea mpaka katika hoteli waliopanga. Lakini Alex alikuwa na mawazo sana kuhusu Allen kuja kumtembelea hospitali na alitaka kumwambia Christine lakini akakumbuka ishara aliopewa na Allen wakati anaondoka. Kwa jinsi alivyokiweka kidole mdomoni ni dhahiri hakutakuwa kumwambia mtu yoyote ujio wake. "karibu tena" Christine aliongea, "asante" Alex alijibu na kuelekea chumbani kwake. Na kwavile walikodi apartment kila mtu alilala katika chumba chake. Alipofika chumbani kwake aliingia bafuni na kujimwagia maji japo bado alihisi maumuvi makali lakini alijikaza kiume.


Alirudi ndani na kukaa kitandani huku akiendelea kuwaza, ghafla uliingia ujumbe kwenye simu yake "kuanzia sasa usimuamini mtu yoyote hata huyo mschana unaekaa nae..... Allen James". "kwanini" Alex alijibu ujumbe huo, "ukifika muda nitakwambia lakini nahisi kuna kamchezo kachafu unachezewa" Allen alijibu. "unasemaje wewe unataka kunitenganisha na mtu anaenisaidia si ndio" Alex alindika ujumbe na kutuma. "Kesho tukutane 18''20 saa A6:3M" Allen alituma ujumbe huo kwa njia ya kodi maalum ambazo watu wa aina yao tu ndio walizielewa. "sawa" Alex alijibu na kuweka simu pembeni kisha akajilaza kitandani.
Siku iliofuata Alex alitoka mapema asubuhi, "unaenda wapi" Christine alimuuliza. "ah naenda kutafuta dhana za kazi" Alex alijibu, "nikusindikize" Christine aliongea. "hapana na nashkuru ila ntakuwa sawa tu" Alex alijibu na kutoka. "mhh mbona kabadilika ghafla"Christine alijisemea moyoni, baada Alex kutoka tu Christine alifungua begi lake na kutoa simu nyingine. "habari yako mkuu" aliongea baada simu kpokewa, "ndio ila nahisi Alex kashaanza kushtuka" "ok hamna shida". Alimaliza kuongea na kukata simu "yatukuke mapinduzi" Christine alijisemea na kukunja ngumi kisha akaiweka kifuani kama ishara ya kutoa heshima.
Alex alitembea kwa umakini wa hali ya juu huku akihakikisha hakuna anaemfuatilia, alifika mpaka katika jengo aliloambiwa afike na kupanda lifti kuelekea juu kabisa. "unakwenda na muda kijana" Allen aliongea punde tu baada Alex kufika, "usiwe na wasiwasi kuanzia sasa mimi sio adui yako kabisa lakini nataka kukusaidia" Allen aliongea na kumshangaza Alex. "unataka kunisaidia kivipi" aliuliza ka mshangao, "kijana mimi pia niliwahi kuwa katika hali kama yako wakati fulani kwa hiyo naelewa ni kiasi gani unateseka kutaka kujikomboa na utumwa wa akili" aliongea Allen na kutoa kitu mfukoni kisha akakirusha kwa nguvu lakini Alex alikiona na kukidaka na alipoangalia vizuri aligundua kama kilikuwa kisu kidogo.
"Umeniita uje kuniuwa" aliongea kwa hasira Alex, "hapana siwezi kumuua mgonjwa kisha nikajisifu nimefanya kazi" Aliongea Allen na kutabasamu. "akili yako ni kama yangu tu, lakini wewe bado hujajizoesha kuitumia inavotakiwa" Aliongea Allen kisha akaendelea "we unadhani kwanini mara zote mbili nilizokutana na wewe nimekushinda, ni kwasababu nilikuwa nafikiria hatua moja au mbili mbele yako". "sijakufahamu" Alex aliongea "sisi ni watu amabao tuna uwezo mkubwa sana wa kufikiria, kama saa hivi najua kama unataka kutoa bastola ili uniue" Aliongea huku akicheka na kweli Alex alikuwa na bastola ndogo mfukoni ambayo ilikuwa tayari imeshakokiwa vizuri tu.
 
68.

"Umejuaje" Alex aliuliza huku akitoa macho, "mi si nimekwambia nafikiria hatua moja au mbili mbele yako" Allen alijibu."usijali utajua jinsi ya kusoma mchezo wa aina yoyote ile" aliendelea kuongea Allen kisha akampa ishara amfuate na Alex nae alifanya hivo bili kusita mpaka alipofika mwisho wa jengo hilo kabisa. "we unadhani kwa nini Rose anakusaidia" aliongea Allen, "Rose ndio nani" Alex aliuliza, "ah nimesahau kumbe anatumia jina la Christine" alijibu huku akitabasamu. "ananisaidia kwa sababu anataka na mimi nimsaidie kulipa fedheha alioipata kutoka kwa bosi wake" Alex alijibu kwa kujiamini kwasababu ndivyo alvyoamini.
"Umechezwa akili kiajana" aliongea Allen na kumshika bega Alex, "una maanisha nini" Aliuliza. "we unadhani ni rahisi sana mtu kufanya hivo, hapana kijana. Kuna mchezo unachezewa hapa, kwanza wewe ni miongoni mwa watu wanotafutwa kwa udi na uvumba Marekani yote. Sasa basi Christine au Rose jina lake halisi anakutumia kuondoa vikwazo vyote katika njia ya mkuu wake kuelekea utawalani. Wewe ndie unaekwenda kufanya mashambulizi ikiwa utakamatwa basi yeye atakuacha ufe mikononi mwa serekali. Au pili ikiwa utafanikisha kazi ya kuwauwa watu wote ambao wapo katika list yake basi kuna vijana wake ambao huwa wanakufatilia kwa siri watakuuwa ili kupoteza ushahidi..
Wakati huo huo nimetumwa mimi kuja kukumata nikurudishe mikononi mwa serekali, lakini nilichogundua ni kwamba wamenituma makusidi wakielewa kuwa sitakuuwa wala kukukamata bali utajifunza mbinu zaidi kupitia mimi. Hapa sasa ndipo unapokuja mchezo mchafu na kaa tayari na kuumia kwa ntakachokwambia, kuna kikundi maalum cha watu wamejipanga kuiingiza dunia katika machafuko. Hicho kikundi kinaitwa "THE REVOLUTIONARIES" (WANA MAPINDUZI), kiongozi wao bado sijamjua ila Christine, Mr Clinton, Robert na wengine wengi wanamtumikia bila kujua kama wanawindana wenyewe kwa wenyewe"Alimaliza kuongea na kumtazama Alex amabe alikuwa haamini anachokisikia.
"Huo upuuzi umetoa wapi" Alex aliongea, "kijana huu si upuuzi bali nakutahadharisha tu ujiandae kiakili kwa chochote kila kitakachokukuta" Allen alijibu na kumwagalia kwa makini. "ukitaka kuugundua ukweli fanya hivi, kwa sababu wao wanatuchezea mchezo mchafu na sisi tuwaingizie mchezo ndani ya mchezo wao ili tujue nani kiongozi wao na hapo ndio tutaweza kuokoa maisha yetu na ya wale tunaowapenda pamoja na dunia kwa ujumla. Kitendo cha kuondoka hapa mimi na wewe si marafiki bali ni maadui kama mwanzo tu na kaa ukijua nikikutana na wewe kwenye anga zangu nakuchapa kama kawaida lakini ukiwa makini utajifunza mengi"Allen aliongea na kumpa mkono Alex kama ishara ya urafiki. Alex aliupokea na kutabasamu, "acha tuwaoneshe kama sisi si panya wa maabara kututumia wanavotaka" Alex alionea na kumfanya Allen atabasamu "that is the spirit boy" Allen aliongea huku akiondoka.
****************************
Kikao cha siri kilikuwa kikiendelea katika makao makuu ya THE REVOLUTIONARIES, ajenda ya kikao hicho ilikuwa ni kukusanya ripoti kuhusu mienendo yao. Ripoti zote zilikuwa zinaridhisha "vizuri sana wanangu, mnanipa furaha sana" Aliongea mtu alievalia gwanda jeshi, alikuwa anafanana na Hitler katika ubora wake. "hatua ya kwanza imekwisha, sasa tunaelekea hatua ya pili ya kuwaondoa viongozi wote ambao wamekataa kuungana nasi" aliendelea kuongea, "hatua hii ni muhimu sana na hakutakiwi kutendeke makosa yoyote yale na ikiwa itafeli mujue hatutafika pale tunapopataka"."tumekuelewa mkuu na tunakuahidi kuwa hakutatendeka makosa yoyote yale na kazi itakwenda kama ulivyopanga" walijibu wote kwa pamoja na kusimama. Na tena kwa pamoja wakakunja ngumi na kusema YATUKUKE MAPINDUZI.
 
69.
Alex alirudi katika hoteli waliopanga lakini cha ajabu hakumkuta Christine, wakati anazungukuzunguka alikuta karatasi mezani iliokuwa na ujmbe "kuna kitu nafatilia nitarudi jioni". Baada kuisoma alitabasamu kidogo kisha akaelekea chumbani akiwa na begi alilorudi nalo, alipofika kitandani alilifungua na kumwaga silaha kuanzia ndogondogo mpaka kubwa. Alipanga vizuri na kuhakikisha kuwa zote zina risasi na ziko sawa. Baada hapo aliingia bafuni na kuoga, aliva suti nzuri na iliotulia kisha akarudi sebleni na kukaa.
Christine aliporudi na kumkuta Alex sebleni, ilibidi ashangae kwanza kwa jinsi alivyokuwa amependeza. "wapi tena mbona umevaa suti" aliuliza kwa mashangao, "ah nimeamua tu kutoka kiofisi zaidi" Alex alijibu huku akitabasamu. "sasa mipango tunaanza lini" aliuliza Alex, " we si bado hujapona" Christine aliuliza na yeye. "mi mbona mzima kabisa, nashkuru kwa kemikali walioingiza mwilini mwangu" Alex alijibu huku akitabasamu. "kama ni hivo itakuwa vizuri sana, maana nilijua ungekaa sana" Christine alijibu na kuelekea chumbani kwake. Baada kama dakika mbili hivi alirudi akiwa na bahasaha ya wastani mkononi na kuiweka mezani, kwa muonekano tu Alex aligundua ile bahasha ilikuwa imeletwa kama amri kutoka sehemu fulani "acha tu nicheze kwa sheria " Alijisemea moyoni.
Christine aliifungua ile bahsasha na kutoa picha kadhaa. "huyo kwenye picha anaitwa Marko, yupo hapa Urusi na mmoja kati watu waliohusika na vifo vya familia yako" Christine aliongea huku akimuangalia Alex kwa makini usoni. Sura ya Alex ghafla ilibadilika na kuoneha wazi kuwa alikuwa na hasira. Aliichukua ile picha na kuiangalia kwa umakini sana kisha akairudisha mezani na kuicora alama ya X kwa kalamu nyekundu. "lini anatakiwa aondoke duniani" Aliuliza akionesha kabisa hasira zake..
"Ndani ya masaa arobaini na nane awe tayari ameshatangulia mbele za haki" Aliongea Christine na kuichukua ile picha na kuirudisha katika bahasha, baada hapo alimpa Alex maelezo ya anaweza kumpata mtu huyo. Baada ya maongezi hayo Alex alikwenda chumbani kwake na kubadilisha nguo na kuvaa zile nguo zake maalum za kazi. Alitoa begi la silaha na kuchagua silaha lakini wakati anafanya hivo uliingia ujumbe katika simu yake ukisema "chukua M23...Allen James". Alitabasamu kidogo na kuujibu "asante mkuu". Alitoa begi jingine dogo na kuiweka sniper yake kisha aktoka na kumuaga Christine, alitoka nje na kuchukua gari na kuondoka.
Akiwa kwenye gari uliingia ujumbe mwengine "kuwa makini unafatiliwa", alizdi kukanyaga mafuta na kufanikiwa kuwatoroka walikuwa wanamfatilia. Alifika mpaka kwenye sehemu alioambiwa atamkuta huyo mtu, alipanda gorfa jirani na kwenda juu kabisa. "umechelewa dakika moja" Allen aliongea baada Alex kufika, "duh unafanya nini hapa" Alex aliuliza kwa mshangao. "niko hapa kukupa mafunzo ambayo hujawahi kupewa ukiwa kambini" Allen alijibu bila kumuangalia Alex. "mtu uanetakiwa kumuua bado hajafika, na ni mtu ambae anaheshimika sana katika nchi hii hivyo basi kaa ukijua kuwa ukifanya kosa tu umekwisha naa natumai unalielewa jeshi la nchi hii katika usakaji wake" Allen alimueleza kisha akendelea "risasi inayo takiwa kutumika ni moja tu na hakuna kurudia, ukikosea unatakiwa kukimbia haraka iwezekanavyo. Jingine hutakiwi kutumia darubini kwa sababu wanavifaa maalum vya kisasa ambavyo vinasensa moja matata sana, unatakiwa kutumia macho tu.
 
70.


Na umbali kutoka hapa mpaka atakapokaa ni makadirio ya mita 60. Dakika yoyote kutoka sasa ataingia nakutakia jaribio jema"Allen alimaliza kuongea na kuondoka bila kusubir Alex aongee chochote. Alex alibaki ameshangaa tu huku akijiuliza atawezaje kulenga mita 60 bila kutumia darubini, aliona huo ni mtihani mkubwa sana lakini alijipa moyo kupitia jina la familia yake ilioteketea bila hatia kuwa ataweza kumtungua. Alifungua begi lake kuanza kuipanga sniper yake na kama alivyoambiwa na Allen aliweka risasi moja tu kakaa sehemu ambayo angeweza kumpata vizuri.
Gari sita zilifika nje ya hiteli na Marko akashuka na vijana wake na kuingia ndani, moja kwa moja alielekea mpaka katika meza maalum ambayo huwa anakaa akifika katika hoteli hiyo na kukaa. Ukaguzi ulifanyika na baada hapo walinzi wake walisogea mita kama tano hivi kutoka alipo kwasababu alikuwa akikutana na mtu kuongea kitu ambacho ni siri. Alex alikuwa makini juu huku akipata tabu sana kumlenga kutokana na umbali, wakati akiwa katika hali hiyo uliingia ujumbe kwenye simu yake "tuliza akili yako na fanya kama hakuna kitu kingine mbele yako zaidi ya Marko na pumua taratibu sana hakikisha husikii chochote zaidi ya pumzi yako.... Allen James".
Alifanya hivo na taratibu akili yake ikatulia, baada hapo alifuta kila kitu mbele yake isipokuwa Marko peke yake. Kisha akaanza kupumua taratibu huku akiisikilizia pumzi yake. Mapigo yake ya moyo yalirudi kati hali ya kawaida na alishanga kuona kama hata macho yake yana uwezo kuvuta. Hakupoteza tena muda aliweka kidole kwenye trigger na kufyatua risasi iliosafiri moja kwa kwa moja mpaka kwenye kichwa cha Marko na kuweka saini kama imefika. Marko alianguaka chini kama mzigo na kukata upepo. Bila kuchelewa alirudisha sniper yake kwenye begi na kuanza kuondoka lakini uliingia ujumbe ukimwambia "kwenye mlango wa kutokea juu hapo kuna begi la parachute, chukua na uruke upande wapili wa gorofa na ukatue 18:71 nitakuwa nakusuburi". Alikwenda mpaka kwenye mlango na kuchukua begi na kulivaa, alianza kukimbia na kuruka.
Alifika sehemu alioelekezwa na kumkuta Allen akimsubiri "kazi nzuri, umefaulu jaribio la kwanza" Allen aliongea na kumpa mkono Alex ambae alionekana kuwa na furaha sana. "lakini kitu kimoja, kumbuka ukishafanya kazi ni mwiko kurudia njia uliopita mwanzo, kwa hiyo kabla ya kutekeleza kazi yoyote ile unatakiwa kutengeza mbinu za kuitekeleza kazi hiyo bila kusahau kutengeza mbinu ya kujiokoa (back up plan) ikiwa itatokea utafeli. "nimekuelwa na nashkuru kwa msaada wako" Alex aliongea "tukutane tena katika kazi yako ya pili, na nina uhakika itakuwa ni moja kati ya nchi hizi mbili Uingereza ama Marekani" Allen aliongea na kungia kwenye gari yake kuondoka "dah huyu mzee kumbe ni balaa yaani angekuwa ni adui yangu nina uhakika saa hivi ningekuwa jela au marehemu" alijisemea moyoni huku akicheka na kuondoka eneo hilo. Alirudi mpaka katika ile hoteli alipoacha gari yake na kupanda kisha akaondoka eneo hilo.
"Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa Don Marko ameuwawa kwa kupigwa risasi ya kichwa" hiyo ilikuwa ni taarifaa ya habari ikitangazwa na kituo kimoja cha taifa nchini urusi, habari hiyo iliwaumiza wengi ambao walikuwa wakimtegemea Don Marko. Lakini haikuwa hivyo kwa wale wanaoishi mitaani walionekana kufurahi sana. "afadhali amekufa maana tulikuwa hatuna amani, mtu anajiona kama mungu bwana" alisikika mtu mmoja akiongea. Mfarakano ulitokea katika kikao cha dharura kilichowahusisha watu wakubwa, "hebu tulieni kwanza sasa mukibishana atarudi duniani au vipi" aliongea mmija mabe alionekana kuwa kiongozi wao. "baada kubishana ujinga tutafute nani aliehusika na kifo chake na lazima alipe kwa maisha yake" aliongea kwa hasira sana mpaka akwa natetemeka. .
Wakati kikao kikiendelea aliingia mschana mmoja kumkabidhi mkuu wake bahasha, alipoifungua alikuta picha ya Marko ikiwa na alama ya X na alipoigeuza nyuma akakuta ujumbe "anaefuata atakuwa nani". Aliishiwa nguvu na kukaa kwenye kiti huku akiiweka ile bahasha mezani, wengine waliichukua na kuangalia kilichokuwemo ndani. walishangaa kukuta picha zao zote ambazo zimepigwa wakati huo wakiwa kwenye kikao. Vurugu lilizuka tena huku kila mmoja akianza kumuhisi mwenzake kuwa ndie ambae anahusika na mauaji ya Marko. Kutokana na vurugu kuwa kubwa kikao kilivunjika na kila mmoja akaondoka akiwa kachukia sana
**************************
 
Back
Top Bottom