93 - 94
Siku ya kuripoti mafunzoni ilifika na mapema niliwasili katika kambi tulioambiwa, tulipewa maelekezo yote yaliokuwa yanatuhusu na baada hapo tukaanza mazoezi. Kwakweli yalikuwa mazoezi magumu sana kuliko nilivofikiria, ulifika wakati nilifikiria hata kutoroka lakini kila nilipokumbuka hadi niliompa baba nilipata ujasiri na kuendelea na mazoezi. Nilichunika chunika vya kutosha mpaka basi. Ila mwisho nilizoea maumivu na kuendelea na mazoezi bila shida yoyote ile. Muda wa mazoezi ulimaliza na tulikabidhiwa vyeti vyetu pamoja na nguo za kazi, siku hiyi ilikuwa ni ya furaha sana kwa kila mtu ambae alishieiki katika mazoezi yale magumu. Baada ya sherehe fupi tulipew ruhusa ya kurudi nyumbani huku tukisubiri kupangiwa vituo vya kufanyia kazi. Baba alionesha furaha ya hali ya juu sana, alinifanyia kasherehe kadogo hivi. "mwanangu jukumu ulilobeba sio dogo na sio kila mtu atakua na furaha na wewe, kwa hiyo ujiandae vilivo" maneno yalitoka kinywani mwa baba akinihusia. Nilitikisa kichwa kuashiria nimemuelewa, baada ya siku ya mbili nilipokea simu kuwa nimepangiwa kituo kikuu. Hiyo ilikuwa furaha nyingine kwa sababu sikupangiwa mbali na nnapo kaa. Siku ya pili niliwasili kituoni na kutambulishwa kituoni pamoja na kutambulishwa kwa mtu ambae nitakuwa nashirikiana nae. Alikuwa anaitwa Mike, alikuwa mtu mcheshi sana na alikuwa mchangamfu na mchapa kazi. Mike alikuwa mzoefu katika kazi hio, alikuwa na zaidi ya miaka mitatu. Mwanzo kila mtu alinisangaa kituoni kutokana na kovu langu usoni lakini kadiri siku zilivyokwenda walinizoea na kutokana na kujichanganya kwangu nao basi ilikuwa rahisi sana kupata marafiki wengi. Baada ya wiki moja nilipangiwa kazi ya kwanza nje ya kituo, na ilikuwa ni kuongoza msafara wa waziri mkuu katika eneo karibu na kituo chetu. Haikuwa kazi ngumu kabisa hasa ukizingatia ilikuwa ni kufunga njia tu wakati msafara unapita. Nilimaliza na kuripotu kituonim, Maisha kama askari wa kawaida yaliendelea kuwa mazuri huku kila siku sifa zangu zikizidi kutapakaa kutokana na uchangamfu wangu.
Siku moja nikiwa na Mike katika mgahawa mmoja hivi nikipata chai, ghafla tulisikia mlio wa risasi na bila kuchelewa tulitoka huku mikono ikiwa viunoni ambako kulikuwa na bastola zetu ndogo. Tulishuhudia gari moja likitupita kwa kasi huku mtu mmoja akiwa ametoa kichwa nje na kushambulia, tuliingia kwenye gari yetu na kuanza kuwafukuza. Ukweli Mike alikuwa dereva mzuri sana maana aliweza kumudu gari na kukwepa gari nyingi akiwa katika mwendo kasi. Nilitoa kichwa nje na kuipiga gari tuliokuwa tunaifukuza risasi katika tairi ya nyuma na kusababisha ipoteze muelekeo na kugonga nguzo pembeni. Walishuka watu watatu na kuanza kutushambulia, kwa bahati mbaya risasi moja ilimpata Mike begani. Sikuhitaji kufikiria mara mbili, niliteremka kwenye gari na kujificha pembeni kwenye mlango kisha nikatoa radio call na kuomba msaada. Wakati nasubiri msaada mashambulizi yalizidi kuwa makali kawa sababu wale majambazi walikuwa wanatumia silaha nzito sana. Wakati nikiendelea kushambuliana nao nilishutuka mlango ukifunguliwa na Mike akajiangusha chini kisha akanipa ishara niende nyuma kwenye buti. Nilifanya hivo bila kuchelewa, nilifika nyuma na kukuta buti limeshafunguliwa, nilikuta bastola aina ya shotgun na SMG. Nilibeba zote mbili na kurudi mbele ambako Mike alikuwa akiendelea kupambana nao. Nilimkabidhi SMG lakini akanambia nitumie mimi yeye akachukua shotgun. Hapo sasa moto ulizidi kuwa mkali maana sasa uwezo wa silaha ulikuwa unafanana. Baada ya dakika chache msaada ulifika na hapo tukafaikiwa kuwakamata, gari ya wagonjwa ilifika na Mike pamoja na raia kadhaa waliojeruhiwa katika pambano hilo waliwahishwa hospitali punde baada ya kupatiwa huduma ya kwanza. Niliporudi kituoni, mkuu wa kituo aliniita ndani moja kwa moja nikajua kuwa hizo ni lawama. Lakini haikuwa hivo, mkuu wa kituo alinisifu kutokana na ujasiri wangu hasa ukizingatia bado nilikuwa mgeni kati anga hizo. "karibu katika matatizo" mkuu wangu aliongea maneno hayo ambayo kwa haraka sikuweza kuifahamu maana yake, Baada ya hapo niliruhusiwa kurudi nyumbani kupumzika. Lakini nilipofika nyumbani nilimkuta mzee akiwa amevimba kwa hasira, nilipojaribu kumuuliza kuna tatizo gani hakunijibu kitu na kuinuka akaingia zake ndani. Hapo kichwa kilijaa mawazo, basi niliingia chumbani kwangu na kujifanyia usafi kisha nikatoka. Nilipofika ukumbini nilimkuta mzee akiwa anaangalia taarifa ya habari, nilimsalimia kisha nikakaa pembeni yake. "jemedari mzuri anazuia uhalifu na wakati huo huo ana hakikisha mtu asiehusika hapati jeraha lolote, na pia jemedari mzuri ni yule anaehakikisha mwenzake hajeruhiwi" alianza kuongea maneno hayo kisha akaniangalia na kunambia "umefanya vizuri lakini unatakia ujitahidi na kuhakikisha usalama wa raia". Baada kuongea maneno hayo alinikabidhi karatasi nyeupe ambayo haikuandikwa kitu, kisha akanipa ishara nisiongee kitu na niihifadhi ile karatasi..
Baada maongezi mafupi na baba chakula kilikuwa tayari, wote tulisogea mezani na kupata chakula cha usiku. Tulipomaliza niliaga na kuingia chumbani kwangu kulala, na kutokana na uchovo wa mchana, usingizi ulinizoa nilipogusa tu kitanda. Nilikuja kushtuka baada kuota ndoto mbaya sana, nilipoangalia saa nikagundua ilikuwa saa kum na moja usiku. Niliamka na kujiandaa, niliingia jikoni na kuandaa chai na vitafunuwa vya asubuhi. Nilipomaliza niliandika ujumbe na kuuacha mezani kisha nikatoka. Kitu cha kwanza nilichokifanya, nilielekea hospitali kwenda kumuangalia Mike ambae alikuwa anendelea na matibabu. Baada ya hapo nilielekea kituoni kwa ajili ya kuanza majukumu yangu ya kila siku. Kila mtu kituoni alikuwa akinisifu, na magazeti hayakuwa nyuma nayo. Kila gazeti liliandika linavojisikia "tunahitaji polisi kama huyu", "Waabudu matatizo kaeni pembei, simba jike kaingia mtaani". "mamilioni ya pesa yaoolewa". Hivyo ni baadhi ya vuchwa vya habari vya magazeti machache, niljifanya kama siyashughulikii lakini moyoni nilikuwa nnafuraha na kichwa kilikuwa kikubwa kama dunia kwa sifa. Niliendelea na majukumu yangu ya kila siku kama polisi, baada ya mwezi mmoja Mike alirudi kazini na kuendelea kama kawaida. Wakati huo jina langu lilikuwa lishasambaa na kila mtu alikuwa anataka kunijaribu na kila aliefanya hivo alikutana na kisiki. Baada ya Mike kurudi alianza kunipa mazoezi mengine ya kupigana, kila siku baada ya kazi tulikutana Gym na kuoata mazoezi kadhaa ya kujiweka powa. Maana alinambia kuwa niko hatarini sana kutokana na sifa zangu, mpaka majambazi sugu na wale wanasiasa watakuwa wananiwinda hivyo ni lazima niwe fiti, nisiwe nategemea silaha tu. Na pia alinishauri nihame nyumbani ili familia yangu iwe salama kutokana na mikono ya wabaya. Nililiwasilisha wazo hilo kwa mzee nae hakupinga alikubali na taratibu za kutafuta nyumba zikaanza, haukipita muda nilikuwa na kwangu. Kumbuka hapo nilikuwa na miaka ishirini tu na tayari nilishakutana na vikwazo vingi sana katika kazi yangu.Niliendelea na majukumu yangu huku nikiendelea kupokea mafunzo ya ngumi kutoka kwa Mike, ambae alionekana kama komando. Maana mazoezi aliyokuwa ananipa hayakuwa na tofauti na yale nliokuwa nayaona katika TV na movie mbalimbali wakifanya makomando. Miaka miwili ilipita huku nikiwa nimepandishwa cheo mara mbili, siku hiyo baada ya kumaliza mazoezi. Mike aliniita na kunambia kuwa anataka kuanambia kitu. Mapigo ya moyo yalianza kudunda na kihasho chembamba kikaanza kunitoka. "nimemaliza kazi niliopewa na General, natumai umeiva vya kutosha sasa" aliogea maneno hayo na kuniacha njia panda na kumuomba anielezee. Na hapo ndio akafunguka kuwa yeye ni Leutenant General Mike Kings, na alipewa kazi ya kuhakikisha kuwa naiva vya kutosha katika mafunzo ya kijeshi hasa kwenye mkono.
Na hapo akanitonya kitu kuwa kuwa polisi ni maandalizi ya kuelekea katika jeshi la nchi hiyo. Baada ya mazungumzo hayo aliniaga na kunambia kuwa tutakuja kuonana tena labda jeshini katika mafunzo maalum. Kisha akaondoka, nilikaa kitako kwanza huku nikijiambia mwenyewe kuwa naota na nikiamka kila kitu kitakuwa sawa. Lakini ukweli ulibaki kuwa ukweli tu, maana siku ya pili nilipofika kazini nikakabidhiwa msaidizi mwengine na nilipouliza kuhusu Mike nikaambiwa kuwa amehamishwa kituo. Hapo sasa nikaamini kuwa ndio ulikuwa mwisho wa kuonana na Mike.
Baada ya miezi sita tokea Mike nilipokea barua kuwa nimeitwa katika makao makuu ya jeshi, na bila kuchelewa nilielekea huko. Nilishanga kumkuta baba akiwa katika Gwanda zake za Kijenerali huku pembei akiwa amesimama Mike katika combat takatifu ya Lt. General. Baada ya robo saa waliingia watu wengine sita wakiwa wameongozana na vijana ambao walikuwa mapolisi kama mimi kisha tukaelekezwa katika chumba maalumu cha vikao. Hapo alisimama baba na kutoa salamu kisha akaanza kuonge "najua wengi mtajiuliza kwanini mumeitwa hapa, ila ukweli ni kuwa toke mwanzo nyinyi mlichaguliwa kujiunga na kikosi maalum cha kupambana wahalifu sugu. Natumai wote mumewahi kusikia kikosi kinachoitwa "THE PIRATES". Na wengi mlikuwa mnadhani ni stori lakini kikosi hichi kipo na ndio kinachopambana na wahalifu sugu hapa nchini na je ya nchi. Na sheria, ili ujiunge na kikosi hichi ni lazima uanze katika ngazi za askari wa kawaida. Hivyo basi hongereni na karibuni katika anga za majanga".
Kuna kitu sikukielewa na nlipotaka kuongea kitu, mzee alinipa ishara kuwa ninyamaze. Baada ya kikao kile kifupi cha utambulisho tulipelekwa katika chumba maalum na kupigwa picha kisha tukaruhusiwa turudi katika maeneo yetu ya kazi na kuambiwa kuwa hiyo ni siri na hakutakiwa mtu mwengine zaidi yetu kujua. Nilirudi kituoni kwangu nikiwa na maswali kadhaa lakini wa kuyajibu alikuwa ni mzee tu. Hivyo nilisubiria mpaka zamu yangu ilipokwisha na kuondoka kituoni lakini sikwenda nyumbani kwangu. Moja kwa moja nilielekea nyumbani kwa wazazi wangu na nilipofika tu baba alitabasamu na kunipa ishara nikae. Na kwa sababu mama alikuwa hayupo nikaona huo ndio mwanya pekee wa kumuuliza maswali yangu. Swali la kwanza lilikuwa ni ilikuwaje hasa akarudia gwanda wakati yeye alishastaafu. Nae akanijibu kuwa kustaafishwa kwake ilikuwa ni moja kati ya mipango ya raisi ili amkabidhi majukumu mengine ambayo yalikuwa ni siri. Akasema kuwa ile siku alipokwenda kukabidhi barua ya kukubali kustaafu, mheshimiwa raisi alimwambia kuwa hajastaafishwa bali alipewa majukumu mengine makubwa zaidi ya kuendesha kikosi maalum cha THE PIRATES.
. Yeye mwenyewe alishangaa baada kusikia jina hilo kwani alikuwa akidhani uwepo wa kikosi kile maalum ni maneno tu ya watu. Lakini mhshimiwa raisi alitaka baba akiongoze kikosi hicho ambacho alikuwa akikiongoza mwenyewe kwa muda mrefu, kutokana na majukumukuwa mengi aliamua kukibadhi kikosi hicho kwa mtu ambae ni mzalendo sana na hakuwa mwengine isipokuwa baba. Baada ya hapo ndio akapewa maelekezo yote yanayostahiki, baada kunieleza hivo kidogo roho yangu ilitulia. Basi tuliendelea na mazungumzo mengine mpaka mama aliporudi nikamsalimia na baada dakika kidogo niliaga na kuondoka. Nilirudi nyumbani nikiwa mwepesi kabisa baada ya maswali yangu yote kujibiwa, nilipumzika kwa amani kabisa usiku huo.
Siku iliofuata mapema niliamka na kufanya mazoezi kisha niakaoga na kupata kifungua kinywa, nilipomaliza kila kitu nilitoka na kuelekea kazini. Nilipofika niliambiwa nahitajika na bosi ofisini, na nilipoingia tu alinikabidhi karatasi ya uhamisho wangu. Nilijua tu mambo yashaiva, niliichukua karatasi ile na kurudi nayo ofisini kwangu. Niliifungua na kuanza kuiosoma mwisho iliandikwa "ukiupata ujumbe huu, mara moja fika makao makuu ya jeshi ukiwa na hii karatasi". Nilitoka ofisini kwangu mbio za ajabu na moja kwa moja hadi kwenye gari yangu na safari ikaanza. Nilikanyaga mafuta kisawa kwa mara ya kwanza sikuheshimu hata sheria za barabara. Baada ya dakika kumi nilifika makao makuu na kuwaonyesha ile karatasi wanajeshi waliokuwa getini. Walinipa maelekezo ni wapi natakiwa nifike, bila asante niliondoa gari na kuelekea sehemu ya megesho. Nilishuka na kuanza kukimbia, nilifika katika koridoo ambayo ndio nilipoelekzwa nikakuta karatasi imeandikwa "una sekunde sitini tu kufika juu kabisa ya jengo hili, ukichelewa helicopter ina kuacha" nilihisi kuchanganyikiwa hasa ukizingatia katika koridoo ile kulikua na watu wengi kweli. Nilianza kukimbia huku nikipigana vikumbo na watu wengine lakini wala sikujali, na nilipoona nazidi kuchelewa ilibidi nitumie mafunzo ya ziada ili kuwapita watu hao. Nilivua viatu huku nakimbia, hapo sasa nilianza kuwaruka kwa kukanyaga kuta za koridoo hio. Wengine niliwasukuma kwa nguvu na kuwatupa pembeni, niliongeza mwendo huku akili yangu ikiwa inafanya kazi kama computer. Nilifika juu ya jengo hilo lakini sikuikuta helicopter, nilianza kujilaumu lakini ghafla alitokea mtu kwa pembeni na kunipa ishara nimfate kisha yeye akaongoza njia. Tulifika katika chumba kimoja hivi na kuwakuta wengine wakiwa wananiangalia, mara walianza kupiga makofi. "umetumia sekunde hamsini na tatu" aliongea Mike huku akitbasamu. Baada ya nusu saa tulipewa mabegi na kuambiwa tuongozane na Mike mpaka juu kule, tulipofika tulikuta helicopter ikitusubiri. Tulipanda na safari ikaanza, tukiwa ndani ya chombo hicho tulipewa maziwa kuambiwa tujwe kwa sababu safari ni ndefu sana. Cha ajabu baada ya kunywa tu maziwa hayo macho yalianza kuwa mazito na mwisho wote tukapitia na usingizi mzito. Mimi nikuja kushtuka baada kuhisi hewa nzito, na nilipofungua macho nilishtuka baada kuona chombo tulichopanda kinawaka moto, niliwaangalia marubani wote walikuwa wakivuja damu. Nilianza kuwaamsha wenzangu wengine ambao kwa ujumla wetu tulikuwa saba, wote tulitoa nje ya chombo hicho. Baada kuridhika kuwa hakuna hata mmoja wetu alieumia sana, tulikaa kwanza huku kila mtu akitafakari kuwa ni jambo gani lililotokea. Kutokana na kiza tulishindwa kugundua tuko wapi, na ilibidi tulale hapo hapo. Siku ya pili mapema tuliamka na kila mtu alichukua begi lake alilopewa na kufungua, ndani ya mabegi hayo kulikuwa na combat pamoja na silaha nyepesi na vifaa vya mawasiliano.