Simulizi ya kijasusi: Nafsi zilizotelekezwa

Simulizi ya kijasusi: Nafsi zilizotelekezwa

FEBIANI BABUYA

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2022
Posts
1,916
Reaction score
3,850
NINI SIRI YA NAFSI ZILIZO TELEKEZWA?

Inahusu nini, inamhusu nani, kipi kipo nyuma yake? Ungana nami kwenye mtiririko huu uweze kuelewa NAFSI ZILIZO TELEKEZWA inahusu nini.

Mwaka 1991, ni mwaka ambao umoja wa nchi za Kisovieti ulidondoka baada ya kushindwa kwenye vita baridi dhidi ya watu wa Magharibi hususani Marekani. Baada ya vita hiyo kuisha kulikuwa na sababu nyingi sana zilizo wafanya washindwe ikiwemo utaifa na mchango wa nchi za magharibi.

Kwa madhara makubwa ambayo yalipatikana, nchi ya Urusi ilikaa chini kufanya tathmini ili kujua ni wapi walifanya makosa mpaka jambo hilo likatokea nchini mwao. Moja kati ya sababu kubwa ambazo walizipata ni kufeli kwa shirika lao la kijasusi la KGB kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kiusalama kwa asilimia miamoja, waliamini kwamba huenda kama shirika hilo lingekuwa imara mapema na kutekeleza majukumu yake kwa usahihi basi wangeishinda vita hiyo.

Sasa mjadala ukawekwa mezani, walishindwaje? Ndipo ikanukia harufu ya usaliti ndani yao, iligundulika kwamba ndani ya shirika lao kuna watu ambao walikuwa wasaliti na usaliti wao ndio ambao ulifanya shirika hilo kuyumba na kufeli. Sasa wasaliti walikuwa nani na nani? Jina ambalo lilitokezea kwenye makablasha yao ni jina la mwanamke wa miaka ishirini na mitano (IRINA ESPANOVICH). Sasa IRINA ni nani na alitokea vipi kwenye hiyo orodha ya wasaliti?

IRINA ESPANOVICH alikuwa ni jasusi mbobevu ndani ya shirika hilo, Moja kati ya wapelelezi ambao waliaminika mno kiasi kwamba akapata bahati ya kuolewa na moja kati ya maafisa wakubwa ndani ya shirika hilo la KGB. Kuolewa kwake na kiongozi mkubwa wa shirika hilo ikawa nafasi ya yeye kupata taarifa nyingi na za siri za shirika hilo kwa njia ya kawaida ama kuziiba kwa sababu huyo mwanaume alikuwa akiishi naye nyumba moja. Sasa kwenye ule mchakato wa kuwatafuta wasaliti, waligundua kwamba kuna akaunti ndani ya Urusi ilipokea mabilioni ya fedha kutoka ndani ya nchi ya Marekani na walipo jaribu kuichunguza akaunti hiyo ili wajue sababu ya msingi ya pesa nyingi kiasi hicho kutumwa kwa mtu ambaye taifa lake lilikuwa vitani na nchi hiyo ni ipi! Ndipo wakagundua kwamba akaunti hiyo ilikuwa inamilikiwa kwa siri na mwanamke huyo IRINA ESPANOVICH.

Baada ya kuunganisha doti, wakagundua kwamba hizo pesa zilitoka ndani ya shirika la kijasusi la Marekani CIA ambalo wengi huwa wanaamini kwamba ndilo shirika namba Moja kwa ubora zaidi duniani kutokana na kuwa na bajeti kubwa ya uendeshwaji wake. IRINA alipokea pesa nyingi ambazo hata angefanya kazi miaka mia-moja asingeweza kuzipata, CIA wamtumie pesa kama nani? Ikahitimishwa kwamba huyo ndiye msaliti ambaye alikuwa akiwauza kwa CIA ndiyo maana walifeli hivyo ikatolewa amri kwamba asakwe popote alipo, akamatwe, ateswe kisha auawe mrembo huyo.

Bahati ikawa upande wake, mlinzi mkuu wa mumewe akampatia taarifa kwa simu kwamba Maam you are to be killed (unatakiwa kuuawa) hawa watu wanajua kila kitu hivyo KIMBIA (RUN). Alikuwa hatarini hivyo hakuwa na muda wa kupoteza akapotea haraka, KGB hawakumpata mwanamke huyo hivyo ukaanza msako wa kimya kimya kwa sababu waliogopa kuziweka taarifa hizo wazi kwani zingewavua nguo kwa kuonekana ni wazembe mpaka yote hayo yanatokea na hawana taarifa! Hawakutaka aibu wakaamua kuifanya siri kumtafuta huyo DOUBLE AGENT IRINA ESPANOVICH.

Kupotea kwake Urusi mikononi mwa KGB ambao walimpachika jina la LUNATIC GIRL, ukawa mwanzo wake wa kuingia ndani ya nchi ya Tanzania. Kwanini iwe Tanzania? IRINA alipiga hesabu zake akagundua kwamba kama angeenda nchi kubwa hususani ambazo zina usambaaji wa taarifa haraka wangekuja kumpata tu siku moja hivyo alihitaji kuishi sehemu ambayo hata KGB wenyewe wasingeidhania kwamba anaweza kuwepo na ile amani ambayo imetawala Tanzania ikamvutia kuishi hapa kwani ingekuwa ni ngumu kuja kujulikana kwamba yupo hapa. Yes, mpango ulikuwa sahihi sasa Tanzania angeishije na angeweza vipi kujilinda? Ukawa mwanzo wa kuanzisha jamii ya Siri ambayo aliiita LUNATIC SOCIETY, jina ambalo alipewa na KGB kwa usaliti wake. Kumbuka alikuwa mgeni hivyo asingeweza kuianzisha jamii hiyo mwenyewe ikamlazimu kumtafuta mtu.

Macho yake yakadondokea kwa Novack Nyangasa, mdogo wa raisi wa Tanzania ambaye aliamini angekuwa na nguvu ya kumpeleka anapo pataka yeye. Alimshawishi mwanaume huyo kwa urembo wake na kumpa mpango mzima juu ya utajiri ambao wangeenda kuutengeza, Novack akatokwa na mate ya uchu, akakubali. Jamii hiyo ikaanzishwa kwa nguvu ya mdogo wa raisi ambapo waliwasajili watu wakubwa; wanasiasa wakubwa, maprofesa, wanafalsafa, madaktari bingwa, wafanya biashara wakubwa na kila ambaye walimuona anafaa. Baadae raisi akazipata habari, akachukia sana na kumuita mdogo wake IKULU.

Akamtaka aifute jamii hiyo kwa mwezi mmoja tu pekee, huo mwezi ukatumika kummaliza yeye, raisi akawekwa kati akatakiwa kufa ili jamii hiyo iwepo. Moja kati ya mipango mikakati ambayo waliiweka ili kujilinda ni kuanzisha chuo cha kuwatengeneza vijana hatari kwa ajili ya ulinzi na kufanya kazi yao kwa nguvu pale ambapo ingebidi, zoezi hilo likatua mikononi mwa jasusi wa zamani wa Tanzania ambaye aliachana na kazi hiyo baada ya kuhusika na mauaji ya watu wengi sana, NIKOLAI GIBSON. Mwanaume huyo kwenye moja ya mazao yake alifanikiwa kumtengeneza kijana wa kuitwa YOHANI MAWENGE, bwana mdogo ambaye alimuokota Tandale kwa Tumbo akililia mapenzi na kutaka kujiua kisa uchi wa mwanamke.

Alimfunza namna ya kuwa mwanaume akampa begi la pesa akale maisha kwa mwezi mzima, alale na wanawake warembo ambao aliishia kuwaona kwenye runinga ili ushamba umtoke kisha baada ya hapo alikuwa na kazi naye. Alitengenezwa kikawa kiumbe cha kutisha na Kazi yake ya kwanza ikawa kwenda kumuua mcheza KAMARI mmoja huko BAMBALI Senegal na alitakiwa kurudi na bilioni 30 zilizokuwa mkononi mwa bwana huyo..... Huyu tuna mengi ya kuyasoma kwake ni mhimu sana.

Ukawa mwanzo wa mwanamke huyo wa KGB kuitawala Tanzania kwa miaka takribani thelathini. Lakini baadae Moja kati ya makosa makubwa ambayo waliyafanya ni kumuua mwanasayansi aliyedaiwa kuwa binadamu mwenye akili zaidi nchini.

NAFSI ZILIZO TELEKEZWA ni zipi na za nani?
Kulikuwa na utata wa maisha ya mwanaume Edison, bwana ambaye hakuwa na kumbukumbu na kwenye mfuko wake alikuwa anatembea na picha ambayo walidai ni ya mkewe, bwana huyu alikuwa akishangaa kwa sababu yeye binafsi hakuwa na kumbukumbu yeyote kama aliwahi kuwa na mke au familia. Kitu cha kushangaza kwa EDISON ni kwamba alikuwa anatafutwa ili auawe kuliko hata pesa inavyo tafutwa na maskini mpaka yeye mwenyewe akawa anashangaa.

Hali hiyo ilimlazimu kwenda kuishi maisha ya chini sana huko Kigogo Mwisho ili awe salama kwani hakuna ambaye angempata kirahisi akiwa kwenye maisha ya kifukara huko lakini usiku mmoja mvua ikiwa inanyesha akiwa ndani ya kijumba kibovu kwenye mkeka, anapokea simu ambayo ilimtaka atoweke eneo hilo kwa dakika kumi na tano vinginevyo angekufa. Aliduwaa ila hakuwa na namna aliondoka haraka ila kabla hajafika mbali akavamiwa na wanaume wa kutisha ambapo alimuua mmoja akafanikiwa kutoroka.

Safari yake ikawa ni kwenda kwa mlezi wake ambaye ndiye alimpa taarifa hiyo na ndiye alimtaka akaishi huko Kigogo mapaka mambo yakae sawa ili akampe ukweli wa kwanini anatafutwa sana? Kufika kwa huyo mlezi wake ambaye alikuwa ni mchungaji wa KKKT pale Mabibo Mwisho karibu na hosteli za wanafunzi wa NIT, alimkuta mtu huyo yupo kwenye hatua za mwisho za uhai wake. Hakumwambia kitu zaidi ya kumtaka aende nyumbani kwake kwenye banda la mbwa akachukue kitabu ambacho kingemfunulia ukweli kwamba yeye ni nani, kwanini hana kumbukumbu, maisha yake kabla yalikuwaje na kwanini anatafutwa sana na watu ambao yeye alidai hawajui!

EDISON alishangaa baada ya kuambiwa kwamba anatafutwa kwa kuhusika na mauaji ya makomando TISA wa kikosi maamulu cha KOM (KILL ON MISSION).akabaki ameduwaaaa!!!!!!!

Ilishawahi kukukuta kwenye maisha yako ukatakiwa kumuua mama yako mzazi kwa mkono wako mwenyewe? Hilo ni jambo baya na gumu lakini Yes, kuna mwanaume alitakiwa kumuua mama yake aliye mzaa ili nchi iwe salama. Je huyu naye hatima yake ilikuwaje?

Kuna uhusiano gani kati ya hizo NAFSI ZILIZO TELEKEZWA, IRINA ESPANOVICH na EDISON?

Unataka kumjua zaidi IRINA ESPANOVICH? Unataka kuijua kiundani LUNATIC SOCIETY? Unataka kujua uhalisia wa maisha ya EDISON kabla na baada ya hapo? Hizo nafsi ZILIZO TELEKEZWA ndizo hizo za makomando TISA (9) ambao alidaiwa kuwaua au kuna mengine nyuma ya mlango wa siri? Ungana nami kwenye simulizi yangu bora zaidi kuwahi kuiandika kwa mkono wangu.

1. Storyline yake ni kali sana
2. Dialogue (majibizano) yake ni kali sana.
3.Haitabiriki kabisa (huwezi kutabiri kinacho tokea baadae)
4.Lakini pia ina actions kali mno.

Simulizi hii imetoka tayari na unaweza kuipata kwa shilingi ELFU SITA (5000 tu za kitanzania). Unaweza ukalipia 5000 yako kwa namba hizi ili uipate muda huo huo. Inapatikana kwa Softcopy.

0621567672 (HALOPESA)..... WhatsApp.
0745982347 (M-PESA)
0714581046 (TIGO-PESA)
0689440143 (AIRTEL MONEY)

FEBIANI BABUYA

Lipia muamala wako Kisha nicheki nikutumie yote, ama unaweza ukanicheki WhatsApp, ukatuma sms ama ukapiga cm kama utakuwa na swali lolote.

CIAO.
IMG-20240711-WA0001.jpg
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA KWANZA

SURA YA 1.
MIMI NI NANI?

MZIZIMA
Mvua zilizokuwa zimeambatana na upepo mkali zilikuwa zikiendelea kulisumbua jiji la bandari ya Salama, jiji la kale ambalo watu wa zamani walilijua kama mzizima. Mvua hizo ziliwafanya Tanesco wapate kisingizio kizuri kabisa cha kuweza kuukata umeme ambao ulikuwa unaimulika mitaa mbali mbali na kuonyesha umaridadi wake.

Kwenye chumba kimoja maeneo ya Kigogo Mwisho alionekana ndani mwanaume mmoja, kuonekana kwake kulidhihirisha wasiwasi na hofu ambayo ilikuwa imeugubika uso wake na simanzi ikauzidisha upole wa ile sura yake ambayo haikuwa ikionekana vyema huenda kwa sababu ya kukosekana kwa mwanga. Uso wake ulitoa taarifa ya kwamba maisha yake hayakuwa salama ndiyo maana alikuwa hana amani wala kuwa na utulivu wa kutosha, alikuwa ameketi kwenye mkeka ambao ulikuwa umetandikwa chini kwenye chumba kidogo cha hovyo ambacho kiligubikwa na joto kali kwa kukosa nyenzo mhimu za kupambana na joto. Sanjari na hilo udogo wa chumba nao ulichangia kwa kiasi kikubwa.
Mwanaume yule alijizoa kutoka kwenye ule mkeka na kusimama, alijisogeza kwenye dirisha dogo ambalo lilifunikwa kwa tambala kuu kuu lilolokuwa chafu, alifunua kidogo pazia hilo ili kujua kama nje kulikuwa na chochote lakini hakufanikiwa kuona jambo lolote lile zaidi ya radi ambazo zilikuwa inamulika kila wakati kwenye kiza totoro kilicho lifanya jiji hilo kuwa na utulivu ambao sio kawaida yake. Alirudi tena kwenye mkeka wake akiwa anatweta kwa jasho kutokana na joto kali huku akiwa anajifuta jasho hilo kwa kutumia shati lake ambalo lilikuwa mwilini.

Akiwa anaendelea kuhema kwa hesabu maalumu ambazo alizijua yeye na nafsi yake, alihisi kama kuna kitu kinamtekenya kwenye mfuko wake wa suruali, hapo ndipo akakumbuka kwamba kwenye mfuko huo alikuwa amehifadhi kisimu kidogo ambacho alikuwa amekifunga funga kutokana na uchakavu ambao kilikuwa nao. Aliipokea haraka simu hiyo ambayo namba yake haikuwa na jina na kuiweka kwenye sikio lake.
“Ondoka haraka kwenye hilo eneo, una dakika kumi na tano tu za kuyaokoa maisha yako, vinginevyo unakufa” sauti ya upande wa pili iliongea kwa msisitizo kisha simu ikakatwa. Alibaki kwenye mshangao mithili ya mtoto ambaye alikuwa ametelekezwa na mama yake mzazi huku akiamini kwamba alikuwa na usalama wa kutosha kwa sababu mama yake alikuwa karibu.

Alijizoa kivivu huku moyo wake ukiwa unamuenda mbio, alisogea kwenye ule mkeka na kuukunja upande wa juu ambapo eneo hilo kulikuwa na udongo ambao ulijazwa, aliufukua haraka haraka na kukitoa kimfuko cha plastiki. Alikifungua na ndani yake kulikuwa na pesa za kigeni maarufu kama dola huku pembeni yake kukiwa na bastola moja pamoja na kisu kimoja. Alizoa pesa haraka haraka na kuzitupia kwenye mfuko wake, bastola akaipachika kwenye kiuno chake huku kisu akikishika mkononi.
Alipafukia kama alivyokuwa amepakuta mwanzo na kuurudishia ule mkeka kwa mara nyingine tena kisha akanyanyuka na kuanza kutoka nje. Baada ya kufika mlangoni alikuwa amepoteza dakika tatu tayari, aliufungua mlango taratibu kisha akaangaza kila upande ili kuona kama angefanikiwa kuona kile ambacho alikuwa ameambiwa kinaenda kutokea lakini hali ilikuwa shwari kabisa hivyo akajitosa kwenye maji ya mvua na kuanza kutembea haraka haraka ili kuelekea kilipokuwepo kituo cha magari.
Alikunja kona ya kwanza akiwa anapishana na sauti ya kudondoka kwa maji, akakutana na uwazi ambao ulikuwa na mita kama kumi na tano, sehemu ambayo ilimshtua kidogo kwa sababu moyo wake ulimuenda mbio isivyokuwa kawaida. Alitembea haraka haraka ili aweze kulivuka eneo hilo salama huku kwenye mkono wake kisu akiwa amekishikilia vyema, ila hakupiga hatua hata kumi akahisi kabisa kulikuwa na harufu ya mtu ndani ya eneo hilo hali ambayo ilimfanya kupunguza mwendo na kumfanya aanze kutembea taratibu.

Aligeuka kuangalia nyuma yake, hakuona kitu zaidi ya anga ambalo lilikuwa linamcheka hivyo akahitaji kuendelea na safari yake tena lakini nafsi iligoma kabisa, moyo wake ulikuwa mzito na hakuwa mtu wa kuupuuzia huo mlango wake wa sita ambao ulikuwa wa hisia. Alishuka chini kama anajilaza kifudi fudi lakini hakufika chini kwa sababu ule mkono wenye kisu ndio ambao ulitangulizwa kisu ndicho kikafika chini na hata baada ya kufika pale chini kwa mkono wake hakuzubaa, alijigeuza kwa sarakasi kwa kuuviringisha mwili wake hali ambayo ilimfanya atue pembeni.

Mahesabu yake yalikuwa sahihi kwa sababu wakati anashuka pale chini, juu yake kilipitishwa kisu kutoka kwenye mikono ambayo ilionekana kuwa na nguvu kubwa na lengo la mtu huyo halikuonekana kuwa kumzimisha tu bali alikuwa anahitaji kuondoka na nafsi yake moja kwa moja. Hata baada ya kutua pale chini hakuzubaa kwa sababu alijua huenda akampa adui nafasi nzuri ya kuweza kufanikisha jambo lake kitu ambacho hakutaka kiweze kutokea kwake yeye ndiyo maana alijiviringisha kwa sarakasi na kutua pembeni. Kujiviringisha kwake kulimfanya kulikwepa buti zito la ngozi ambalo lilikuwa limeshushwa na mwanaume ambaye alionyesha kuwa na uhasama naye mkubwa mithili ya mtu ambaye alimuibia mkewe, buti hilo kama lingefanikiwa kutua kwenye mgongo wake basi asingefanikiwa kutembea tena kwenye maisha yake yote.

Kiza kinene kilimfanya mwanaume huyo ashindwe kumtambua mwanaume ambaye alikuwa amekuja mbele yake ila mwanga wa radi ulimumulika mtu huyo ambaye bila shaka alikuwa ni mweusi usoni akiwa kwenye ghadhabu isiyo pimika. Aliukunjua mkono wake ambao ulikuwa na kisu kwa sababu alijua kwamba anatakiwa kufa wakati huo asipo yatetea maisha yake, hakupata muda wa kutosha wa kupiga tathmini juu ya uwezekano kama alikuwa anamfahamu mwanaume huyo kwa sababu alikuwa anamjia kwa kasi pale alipokuwepo huku mabuti yake yakiwa yanapiga piga kwa nguvu kwenye maji ambayo yalikuwa yametuama chini.
Miguu yenye nguvu miwili ilikuwa inakuja kwenye uso wake, kama bahati tu, tope lililokuwa chini lilimsaidia kuteleza kidogo na kurudi nyuma hali ambayo iliifanya miguu hiyo kumkosa na badala yake akarushiwa maji machafu usoni ambayo yalimuingia kwenye macho. Mtetemo wa ardhi aliusikia vyema baada ya ile miguu ambayo ilimkosa kutua chini na kukita kwa nguvu. Aliyafumbua macho yake haraka ili kujilinda, alichelewa kwenye mahesabu, ngumi ilizama kifuani na kumfanya ahisi kama kuna mtu alimpasua na shoka.

Ngumi hiyo ilimburuza mpaka karibu na ukuta mmoja wa nyumba ambapo hakuruhusu kuufikia bali mguu wake ndio ulitumika kama ngao baada ya kuurusha na kukita kwenye ukuta wa nyumba hiyo ambao ulitingishika kwa nguvu na kutulia. Alitaka kujipanga vyema alihisi kuna kitu kinawaka kinakuja pale alipo, alifanikiwa kukikwepa kisu ambacho kilikuwa na makali ya kutosha, kilimbaraza kidogo kwenye bega lake na kumpatia maumivu lakini hakulizingatia hilo kwanza badala yake alikuwa anaangalia namna ya kumkabili mwanaume huyo ambaye bado alikuwa anakuja mithili ya mtu ambaye anachajiwa huku kisu chake kikizama kwenye ukuta wa nyumba hiyo ya tofali.

Alifanikiwa kuziona ngumi mbili zilizokuwa zimeulenga uso wake, alijisogeza pembeni na kumpa mtu huyo nafasi ya kumpatia goti la ubavu kisha akiwa anasikilizia maumivu mwanaume yule alikichomoa kile kisu na kukizamisha kwenye mbavu za mwanaume huyo hali iliyomfanya kutoa sauti kali ya mguno wa maumivu. Sasa alikuwa anajiona anakufa kizembe bila hata kumjua mtu ambaye alikuwa anamvamia hapo alikuwa nani.
Alisogea hatua mbili nyuma macho yake yakiwa makini kwenye kile kiza huku ubavu wake ukiendelea kuitoa damu taratibu ambayo ilikuwa inatoka kwa fujo mpaka wakati huo, yule mwamba ambaye alikuwa anaelekea kupata ushindi, baada ya kukichomoa kisu chake alikuwa anasogea kwa hatua chache ambazo zilimpa uhakika wa ushindi. Kusogea kwake mvamiaji naye alihisi kama kuna kitu hakipo sawa, mbele yake mtu aliyekuwa anamuwinda ni kama ghafla tu hakumuona na radi ilipo piga aliona mtu huyo akitokea pembeni yake ambapo alifanikiwa kuipangua ngumi yake moja lakini mkono ambao ulikuwa na kisu ulizama kwenye kifua chake.

Ndiyo kwanza tunaufungua ukurasa wa kwanza kabisa wa simulizi hii ya kusisimua. Ungana nami mpaka mwisho tuweze kuugusa wino huu bora mno.

NAFSI ZILIZO TELEKEZWA.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA PILI

Alijaribu kuutoa mkono huo kwa nguvu lakini hakufanikiwa baada ya kushindiliwa na ngumi nyingine ya kwenye chembe iliyo mpa maumivu makali. Aliachiwa akiwa amejishika kifuani sehemu ambayo ilitobolewa huku akiwa amepinda maana ile ngumi ya chembe ilimuingia vizuri. Alijikaza na kukizungusha kisu chake kwa nguvu kumsogelea mtu wake pale alipokuwepo, alirusha mkono ambao ulikuwa na kisu ukapita karibu na shingo ya mwanaume ambaye alikuwa amevamiwa hivyo akapiga hewa. Wakati anajipanga kuurudisha tena alijikuta hata kisu kinamponyoka kwenye mkono wake baada ya kupigwa ngumi nzito za haraka haraka kifuani kwake ambazo zilikifanya kifua kilainike, uzito wa zile ngumi kifua kisingeweza kuuhimili.
Aliachiwa akiwa anayumba yumba, mguu mzito ulitua kwenye shingo yake na kumshusha chini kwa nguvu, alipotua chini alipigwa teke la uso ambalo lilimfanya agale gale akiwa anaburuzwa na nguvu ya ule msukumo wa lile teke. Mwanaume ambaye alikuwa kwenye mavazi makuukuu alimsogelea akiwa na kisu chake mkononi na kufika mpaka pale chini ambapo alikuwepo mwanaume yule aliye mvamia. Alijaribu kunyanyuka kwa nguvu ila alirudi chini baada ya kushindiliwa kisu cha kwenye bega karibu kabisa na ilipokuwa shingo.
“Mimi na wewe tunafahamiana kabla ya hapa?” ilikuwa sauti nzito ambayo ilitoka kwa yule mwanaume ambaye alikuwa amevamiwa akiwa anamuuliza mgeni wake.
“Lazima uf….” Yule mwanaume hata hakukamilisha sentensi yake kuna risasi ilimkosa na kutua kwenye ukuta, alishtuka baada ya kugundua kwamba kumbe mvamiaji hakuwa mmoja ndani ya hilo eneo hivyo alikizamisha kisu chake kwa nguvu kwenye shingo ya mwanaume yule kisha akakitoa na kujigeuza kwa sarakasi ambayo ilimfanya atue kando na baada ya pale aliichomoa bastola yake haraka na kuruhusu pia risasi ziende ule upande ambao alihisi unamshambulia lakini mtu huyo hakuonekana kuwa wa kawaida na yeye alikuwa amejeruhiwa hivyo akawa anatafuta namna ya kuweza kutoweka ndani ya lile eneo.
Alidunda kwenye ukuta ambao ulikuwa karibu na alipo simama, alijivuta na kudondokea upande wa pili na kuishia kwenye vichochoro ambavyo vilimezwa na kiza totoro. Mwanaume mmoja mwenye miraba minne ndiye alikuwa amefika pale akiwa ameghadhabika mno, alitafuta kila kona ya ule ukuta lakini hakuona mtu, licha ya kumsindikiza mwanaume huyo kwa risasi za kutosha lakini bado hakumpata. Alirudi pale alipokuwa mwenzake na kumsikitikia tu kwani alikuwa kwenye dakika za mwisho kuweza kushindana na kifo, alichanwa vibaya kwenye shingo yake kiasi kwamba alikuwa anahangaika huku na huko kwa maumivu hivyo mwenzake akaamua kumfanyia msaada kwa kumpiga risasi ya kichwa ili apumzike.

EDISON
Ndilo lilikuwa jina la mwanaume ambaye alikuwa amefanikiwa kuwakimbia wanaume waliokuwa wamemvamia eneo lile la kigogo mwisho. Licha ya kuwa na maumivu makali kwenye ubavu wake huku damu zikiendelea kumtoka kwa wingi kwenye mwili wake, haikuwa sababu ya kumfanya aweze kusimama ndani ya eneo hilo kwani hakujua wavamiaji walikuwa wangapi na kwa hisia zake ni kwamba hawakuwa tayari kuweza kumuacha hai.
Mwanaume huyo alikuwa anaendelea kulaani hali ile ambayo ilimkuta huku mvua ikiendelea kumzomea kwa kumnyeshea kiasi kwamba alilowa chapa chapa. Baada ya kufanikiwa kutoka ndani ya eneo lile, alikimbia kwa spidi kali akiwa anavikata vichochoro kadhaa mpaka pale alipokujuja kutokezea eneo la Mti Pesa. Mazingira yalikuwa kimya na tulivu huku akiwa anaona boda boda chache ambazo zilikuwa zinatokea ilipo bar ya King’ole.

Haikuwa dhamira yake kusimama ndani ya lile eneo hivyo akaendelea kushuka njia ambayo ilikuwa inaelekea Mabibo mwisho huku akiwa makini na mwendo wake. Macho yake yalikuwa makali kiasi kwamba hakuonekana kuwa mtu wa kawaida, aliingiza mkono kwenye mfuko wake mmoja wa nyuma na kutoa kimfuko kidogo ambacho alikuwa amekikunja, alikifungua na ndani yake kulikuwa na vidonge kadhaa na kichupa kidogo ambacho ndani yake kilikuwa na kimiminika.
Alikifungua kile kichupa na kukimwagia kile kimiminika sehemu iliyo tobolewa huku akitoa sauti ya miguno ya maumivu makali mpaka akaukunja uso wake lakini haikuwa sababu ya yeye kusimama. Alikitupa kichupa hicho kwenye mtaro wa kupitishia maji machafu huku akifungua pakiti ya vidonge na kumeza kimoja kisha vingine akavirudisha kwenye kimfuko chake kile, sekunde chache zilizo fuatia licha ya mvua kuendelea kumwagikia mwilini mwake lakini kile kidonda kilianza kukauka na damu ikaacha kutoka.

Hakuyasikia tena maumivu mwanaume na wakati huo alikuwa amefika ilipo shule ya Loyola, hakunyoosha na barabara ya msikitini badala yake alichepuka mkono wake wa kushoto kuiacha bara bara ya rami na kuifuata barabara ya vumbi iendayo TOT huku akiwa anaongeza mwendo taratibu. Baada ya kufika mbele alikutana na njiapanda hata hivyo hakujiuliza mara mbili akanyoosha na barabara ambayo ilikuwa imekunja kulia. Alianza kukimbia taratibu na kadri muda ulivyokuwa unazidi kwenda ndivyo alivyokuwa anaongeza spidi mpaka alipofika karibu na kanisa la KKKT ambalo lipo karibu kabisa na hosteli za Mabibo ambazo wanazitumia wanafunzi wa chuo cha NIT.
Edison alikuwa anatembea kuelekea ulipokuwa mlango wa kanisa hilo lakini alipunguza mwendo baada ya kuhisi hali ambayo haikuwa sawa ndani ya eneo hilo. Kilicho mshtua ni baada ya kuona mlango upo wazi halafu usiku wa maneno kama huo huku ndani yake ikionekana mishumaa imetaradadi na kufanya eneo hilo kuwa na mwanga japo maeneo mengine yalikuwa na kiza cha kutosha. Alichomoa bastola yake na kunyata kupitia nyumba ambazo zilikuwa jirani kabisa na eneo hilo mpaka alipo ukaribia mlango wa kanisa hilo kubwa.
Alichungulia ndani kwa umakini, hakuona mtu yeyote yule lakini alipo angalia chini kwa umakini aligundua kwamba kuanzia pale mlangoni alipokuwepo kulikuwa na maiti za wanaume ambao walikuwa kwenye suti zao. Watu hao walikuwa wamekufa kwa kupigwa risasi, aligundua kwamba hakukuwa na hatari kwa wakati huo kwa mazingira yalivyokuwa kwani watu ambao walionekana kufika hapo walikuwa wameikamilisha kazi yao hivyo hawakuwa na kingine cha kuweza kukisubiria.

Aliipakia bastola yake ndani ya kiuno chake na kuingia humo ndani kushuhudia walinzi walivyokuwa wamekufa. Alisikitika mno huku uso wake ukiwa na wasiwasi akiwa anaangaza huku na huko, bila shaka kuna mtu alikuwa anamtafuta ndani ya eneo hilo. Aliitoa ile simu yake ndogo kwenye mfuko wake na kuipigia ile namba ambayo kwa mara ya mwisho ndiyo ilimtahadharisha kwamba alikuwa na dakika kumi na tano tu za kuweza kuyaokoa maisha yake vinginevyo alikuwa anaingia kwenye hatari kubwa.

Simu ile ilianza kuita kwa fujo madhabahuni eneo ambalo lilikuwa limezuiwa na meza moja ya mninga ambayo ilikuwa ya gharama kubwa, alikimbilia eneo hilo na ndipo aliona kuna mtu ananyoosha mkono wake kana kwamba alikuwa anampa ishara alipo ila kwa taabu mno. Eneo hilo alikuwa ameketi mchungaji wa kanisa hilo, mwanaume ambaye alikuwa na umri wa kiutu uzima ndiye ambaye mwili wake ulikuwa umechakaa pale chini huku simu ya kisasa ikiwa pembeni yake inaita kwa fujo.
Edson alimkimbilia mwanaume yule mtu mzima na kumnyanyua akamuweka kwenye mapaja yake akiwa mwingi wa simanzi na usoni ameduwaa kama mtu ambaye alibananishwa na benki kwa kushindwa kulipa madeni kwa wakati.
“Nini kimetokea?” aliuliza kwa upole akiwa anahangaika kupekua namba kwenye simu yake, bila shaka alikuwa anatafuta ni msaada wa kuweza kumfikisha mwanaume yule sehemu ambayo ingekuwa salama kwa kujaribu kuokoa maisha yake lakini mwanaume yule alimzuia akiwa anatoa damu kwenye mdomo wake.
“Naomba unisamehe sana kwa sababu nimeshindwa kukulinda, nimeshindwa kutekeleza wajibu wangu” alitamka kwa shida mwanaume yule akiwa anaendelea kutoa damu nyingi kwenye mdomo wake.
“Nani amefanya haya?”
“Nenda nyumbani kwangu, kuna kitabu kidogo kipo chini ya banda la mbwa ukifungua chini kuna maelezo yote ya mhimu, hakikisha unakipata kabla mtu yeyote hajakitia kwenye mkono wake na uondoke haraka hili eneo kwa sababu polisi wanaweza kufika muda wowote ule na hutakiwi kuua polisi kwa sasa” aliongea kwa msisitizo huku mikono yake ikilegea na kushuka chini roho ikawa inaacha mwili. Edison aligubikwa na simanzi huku akiuachia mwili huo na kuibeba simu ya mchungaji huyo, alitoka na kupotea jumla ndani ya eneo hilo ambalo halikueleweka lilikuwa na nini hasa mpaka kanisa kulindwa namna hiyo.

UKURASA WA PILI UNAFIKA MWISHO
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA TATU

Edisoni baada ya kutoka ndani ya lile eneo alipishana na polisi ambao walikuwa wanaingia lakini wasingeweza kumuona kwa sabaabu alikuwa ametoweka tayari. Alitembea haraka haraka kuelekea Mabibo Mwisho ambapo baada ya kufika hapo alichukua boda boda, licha ya boda boda huyo na wenzake ambao walikuwa hapo kumshangaa kwa namna alivyokuwa amechakaa lakini hakujali kwani alitanguliza pesa mbele hivyo boda akawa hana namna zaidi ya kumbeba na kumpeleka kule ambako alikuwa anahitaji kufikishwa haraka.

Safari haikuwa ndefu kwa sababu ilienda kuishia Lego, karibu na lilipo jengo kubwa la Ubungo Plaza. Edison alishuka hapo na kujiweka sawa kisha akarudi nyuma hatua kadhaa na kuingia kwenye njia nyembamba ambayo ilimfanya atokezee nyuma kabisa ya jengo hilo, alitembea kwa muda kidogo na kutokezea kwenye nyumba moja ambayo ilikuwa nzuri ila haikuwa kubwa. Rangi yake nyeupe iliifanya nyumba hiyo kuonyesha umaridadi wake kwa mumeta meta, taa safi ambazo zilifungwa ziliifanya kuendelea kuwa bora kwenye macho ya mtazamaji.
Alitembea taratibu kwa sababu hakuwa na imani na sehemu yoyote ile ambayo alikuwepo wakati huo hali ambayo ilimfanya kuwa makini zaidi. Alisogelea mpaka lilipokuwepo geti kubwa jeusi ambalo lilinakshiwa kwa chuma kizito, geti hilo lilikuwa linaelea kwa maana hiyo ni kwamba lilikuwa limefunguliwa na aliyekuwa amelifungua hakukumbuka kulifunga vizuri ili liweze kushika kwa usahihi, hapo akajua kwamba kulikuwa na ugeni ndani ya eneo hilo ukiacha yeye.
Aliichomoa bastola yake na kuanza kunyata kuelekea ndani baada ya kulifungua geti hilo taratibu, baada ya kuzama ndani kabisa ndipo aliona kuna watu watatu nje wakiwa kama wanabishana. Wote walikuwa wamevaa mavazi ya kiraia ya kawaida tu ila walikuwa na silaha zao mikononi. Alishagazwa na ukimya mkubwa ambao ulikuwepo hilo eneo kwa sababu lilikuwa na mbwa hivyo taa ya hatari ikawa imewaka kwenye ubongo wake kwamba huenda hata mbwa walikuwa wameuliwa.
Hakuwa na muda wa kuanza kujishauri kwa muda mrefu hivyo akakwea taratibu mpaka lilipokuwepo gari ndani ya uzio huo ili ajipange vyema. Upande wa kulia wa eneo hilo kulikuwa na tenki kubwa la lita 10000 kwa ajili ya kuhifadhia maji. Alifunga kiwambo cha kuzuia sauti kwenye bastola yake na kuachia risasi mbili ambazo zilienda kutoboa sehemu moja kwenye lile tenki na kufanya kuwa na tobo kubwa ambalo lilianza kutoa maji kwa fujo na kuwashtua wanaume wale watatu ambao walikuwa wanabishana ndani ya lile eneo kwani wote waligeuka kushangaa sauti ya maji iliyokuwa inamwagika kwa nguvu huku mvua ikiwa ni manyunyu tu.

Hali hiyo ilimfanya mmoja wao aelekee lile eneo huku wawili wakiingia ndani na silaha zao, yule mwanaume alifika lile eneo na kushangaa tobo la risasi ambalo aliamini kwamba kati yao hakuna hata mmoja ambaye alikuwa ameirusha hivyo akashtuka kwamba huenda lile eneo lilikuwa lina mtu mwingine. Aligeuka haraka nyuma yake lakini muda haukuwa sahihi kwake, modomo wake ulikutana na kisu cha mtu ambaye alionekana kuwa na hasira iliyo kithiri kwenye macho yake huku kwenye mkono mwingine akiwa ameishika bastola ambayo bila shaka hakutaka kujisumbua kabisa kupunguza risasi kwa kuitumia wakati alikuwa na uwezo wa kutumia njia nyingine.

Mwanaume huyo alikufa akiwa anahangaika kuweza kuongea neno lolote ila mwisho wa siku hakuna neno hata moja ambalo alifanikiwa kulitoa kwenye kinywa chake. Edisoni alitembea taratibu kuelekea ulipokuwa mlango wa kuelekea ndani, alichungulia sebuleni hakuona mtu hivyo akaachana na wazo la kuingia kwanza na kuelekea mwishoni mwa ukuta wa nyumba hiyo ambapo alifanikiwa kuchungulia lilipokuwa banda kubwa la mbwa, mbwa wote wawili ambao walikuwa ndani walikuwa wamekufa kwa kupigwa risasi maana miili yao ilikuwa inavuja damu kwa msaada mkubwa wa mwanga wa taa ambao ulikuwa eneo lile aliliona hilo.
Licha ya maelekezo kumtaka aweze kuingia ndani ya lile banda kuchukua kitabu lakini hakufanya hivyo kwa sababu alikuwa na kazi ya kufanya bado. Alirudi kwenye ule mlango wa kuingilia ndani akiwa na haraka kidogo tofauti na mwanzo, alichungulia ndani na kumuona mwanaume mmoja akifakamia matunda ambayo bila shaka aliyakuta kwenye friji, aligeuka na kupiga risasi zote ambazo zilikuwa kwenye bastola kwenye lile tenki la maji hali ambayo ilifanya kasi ya maji kuongezeka kumwagika na kufanya kelele kuwa nyingi.

Alimuona mwanaume yule akishtuka na kutoka nje, Ed alijibanza kwenye mlango mkono wae ukiwa na kisu, mwanaume yule alitokezea nje lakini akarudisha kichwa haraka ndani baada ya kuona mwenzake alikuwa amelala pale chini karibu na lile tenki la maji. Kurudisha kwake kichwa ndani ilikuwa pona pona yake kwa sababu alipishana na kisu ambacho kilikuwa kimelenga kutoboa shingo yake na huenda kingetokezea upande wa pili lakini hata hivyo hakwenda mbali kwa sababu ilikuwa ni ghafla na mhusika alikuwa amejitokeza mbele yake ambapo alimdaka kwa nguvu na kumvutia nje kisha akaupiga mlango teke ili wamalizane wenyewe wawili.

Mwanaume yule hakuwa mlaini, alijivuta nyuma huku akirusha teke ambalo lilikita kwenye ukuta baada ya kumkosa Ed ambaye aliinama chini, mwanaume yule wakati anarusha teke lingine Ed naye alikuwa ameurusha mkono ambao ulikuwa na kisu kwa nguvu hivyo teke hilo likakutana na kisu kikali ambacho kilitoboa kwa nguvu eneo la goti na kumfanya mwanaume huyo ahitaji kupiga kelele ila kelele zake alihitaji kuzipiga huku akiwa anainama. Kuinama kwake kwa maumivu ambayo aliyapata kulipelekea kuzamishiwa kisu kwenye koromeo kisha akakutanishwa na kisigizo cha uso ambacho kilimchomoa kwenye kisu hicho na wakati anatua chini, alikuwa maiti tayari.

Wakati Ed anammalizia mtu yule, alisikia hatua za mtu kutoka ndani ambazo zilikuwa zinaita jina ambalo bila shaka alijua ni la yule ambaye alikuwa amemuua wakati ule. Ukimya ndio ambao ulimfanya mwanaume wa ndani kutoka kwa tahadhari kubwa akiamini nje hakukuwa salama. Alitoka mzima mzima akiwa na bastola kwenye mkono wake ila aliganda baada ya kushuhudia mwili wa mwenzake ukiwa unavuja damu pale chini, damu ilikuwa bado mbichi na ya moto baada ya kuigusa. Alinyanyuka akiwa na ghadhabu moyoni, aligeuka kila upande lakini hakuona mtu ila akagundua kwamba chini kwenye mwanga wa taa kulikuwa na kivuli cha mtu hali ambayo ilimpa ishara kwamba juu ya paa la nyumba kulikuwa na mtu mwingine ambaye hakuwa mwenzake.

Aligeuka haraka na kurusha risasi ambazo zilipishana na mwanaume huyo ambaye alikuwa juu ya hilo paa la nyumba akiwa anashuka hivyo zikamkosa. Ed wakati anatua chini hakusimama kwa sababu mwenzake alikuwa na bastola kwenye mkono wake. Mwanaume yule wakati anakaa sawa alishuhudia kisu kikiwa kinakuja kwa kasi upande wake, alirudi nyuma kidogo kukikwepa huku akijiandaa kufyatua risasi lakini hakubahatika kuipata hiyo nafasi kwa sababu Ed alikuwa mbele yake na teke lake moja ambalo alilizungusha kwa nguvu lilitua kwenye ule mkono wenye bastola na hatimaye bastola akawa imemtoka mkononi yule mwanaume ambaye alitabasamu.
“Umewezaje kupona bwana mdogo?” swali lake ambalo lilimshangaza yeye mwenyewe baada ya kugundua mtu ambaye alikuwa hapo ndiye ambaye usiku huo walitumwa watu kumuua na huenda alitakiwa kuwa amekufa mpaka wakati huo lakini hakuweza kujibiwa badala yake alipewa mtihani wa ngumi nzito ambazo zilikuwa zinakuja kwake. Aliinama chini akiwa anazunguka na kunyanyuka kwa miguu yake ambayo ilitua kwenye kifua cha Ed kwa nguvu hata hivyo Eddy hakuwa mnyonge kabisa kwani naye aliachia ngumi moja ambayo ilitua kwenye mguu hivyo kila mtu akarudi nyuma akiwa anasikilizia maumivu ambayo mwenzake alimpatia.

Wote walinyanyuka kwa kasi kubwa kudhihirisha ubora wao huku yule mwanaume hesabu zake zikiwa ni kuiwahi ile bastola ila MUNGU alikuwa upande wake kwa sababu zile hesabu zake za kuweza kuiwahi ile bastola pale zingemponza vibaya baada ya kisu kutua pale na kumkosa vidole vyake. Aliyainua macho yake na kugundua kwamba alikuwa amefikiwa, alipigwa na mguu wa usoni ambao ulimpeleka ukutani, akiwa ukutani alishindiliwa na goti la tumbo ambalo lilimfanya apige kelele huku akiwa anarusha ngumi kivivu iliyokutana na ngumi ya Ed kiasi kwamba mifupa ilivunjika ikiitikia kwa nguvu.

UKURASA WA TATU unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA NNE

“Nani amewatuma kufanya haya ambayo mnayafanya leo?” Ed aliuliza swali lakini mwanaume yule aliishia kumcheka tu huku akiwa anatoa damu mdomoni mwake.

“Lazima ufe, lazima ufe hahahahah hahaha” hiyo ndiyo ilikuwa kauli ya mwanaume yule ambaye alimpandisha Ed hasira na kumfanya ampige na vidole viwili kwenye jicho lake ambalo lilitoboka hapo hapo na kuzalisha kelele kwa bwana yule. Ed alienda kukiokota kile kisu chake na bastola ya mwanaume yule ambaye alikuwa ana uhakika kwamba ilikuwa ni lazima amwambie ukweli wa kilichokuwa kinaendelea ila kwa bahati mbaya wakati anageuka na silaha hizo yule mwanaume alikuwa anatokwa na povu mdomoni, alikuwa ameng’ata ulimi wake ambao ulikuwa unatumika kuhifadhia vidonge vyenye sumu ili kuweza kujipunguza mwenyewe kuliko kusema kile ambacho alikuwa ameulizwa.

Ed alisikitika huku akijongea taratibu kuelekea ndani ambapo baada ya muda aligundua kwamba eneo hilo halikuwa na mtu mwingine bali walikuwa ni hao watatu tu. Alitoka nje mpaka lile eneo ambalo lilikuwa na banda la mbwa, alilifungua eneo lile na kuwatoa wale mbwa nje kisha akaanza kutafuta sehemu ambayo ingekuwa na uwazi, baada ya kuzungusha zungusha kisu chake kuna sehemu aligundua kwamba kisu kilizama hivyo akakilazimisha kwa nguvu na eneo hilo likaonyesha uwazi wa ndani. Alizungusha kwenye lile tobo mpaka alipo utenganisha mlango wa chuma ambao juu ulikuwa na zege lake akaufunua kwa nguvu. Ndani yake kulikuwa na kashimo kadogo ambako kalimfanya ainame na kuchukua box la chuma ambalo lilikuwa ndani yake funguo ikiwa juu yake.

Alilifungua na kukutana na kakitabu kadogo ambako kalikuwa kameandikwa kwa mkono wa mtu na sio mashine. Alikabeba na kutoka kwenye banda hilo kisha akarudi ndani ambako alikwenda kuoga na kuingia kwenye chumba kimoja ambacho alikitumia kubadilishia nguo na kuvaa nguo safi. Baada ya hapo alisogea kwenye shelf moja iliyokuwa ukutani, aliifungua kwa namba maalumu na kutoa mabunda mengi ya pesa kuyapakia kwenye begi kisha akachukua funguo na kutoka nje ambako alichukua lile gari la kifahari ambalo alilikuta pale nje na kuweza kutokomea kusiko julikana usiku huo wa manane.




JNIA
“Una muda gani tangu uanze kufanya hii kazi?”
“Ni miaka mitano sasa”
“Unajiskiaje kufanya kazi kama hii?”
“Mhhh kwangu hii kazi ni zaidi ya nafasi ya dhahabu, haya maisha ni marahisi kama mmekaa vijiweni na washkaji zako mnayachambua kwa kuangalia watu walio fanikiwa lakini haya maisha ni magumu kwenye uhalisia wake kuliko unavyo yafikiria, ndiyo maana wanao teseka ni wengi kuliko walio fanikiwa”
“Upo sahihi kwa hilo lakini unahisi ni sahihi kwa hii kazi ambayo tunaifanya? Kazi ambayo inayapunguza maisha ya watu, kazi ambayo inaacha vilio kwa familia zingine? Naona kama hatuko sawa”
“Nisikilize ndugu, haya maisha hayakupi nafasi mbili, una nafasi moja tu kwenye maisha yako na hiyo nafasi kama ukicheza nayo vibaya basi habari yako inaishia hapo hivyo ni wewe unavyoweza kuzichanga karata zako. Mimi nimeishi kila aina ya maisha, nimeishi maisha magumu, nimeishi maisha ya kukosa kila kitu kiasi kwamba kinacho tokea mbele yako haijalishi kimetoka kwa nani au kwa masharti gani huna namna zaidi ya kukipokea tu. Mimi nimeishi nikiwa mtu mwenye huruma kwenye maisha yangu kwa sababu nimekuzwa na kanisa lakini baadae nikaja kugundua kwamba hii dunia sio rafiki kabisa kwa watu wema. Walimwengu hawakumbuki juu ya mema yako ambayo uliwahi kuyafanya bali wanakumbuka kwamba ni nani mwenye pesa nyingi na jina kubwa na hapo ndipo nilipokuja kuchukia kuwa mtu mwema na huruma nyingi kwa sababu zilikuwa zimeyaponza maisha yangu;”

“Huruma yangu ilinifanya nikae jela miaka miwili kwa kosa la mtu mwingine na ajabu baadae akaja kunikataa, hakuna jambo ambalo nimelifanya kwa huruma na likaja kunilipa baadae mpaka nafikisha umri huu. Mimi sikuwahi kutaka kabisa kuendelea kwenye maisha yale ya umaskini, umaskini ni rahisi kuutaja lakini ni kitu kibaya kwenye haya maisha kwa sababu utakuwa mtu wa kujifariji na kauli za wahamasishaji wa mitandaoni tu ila kiuhalisia dunia inakuwa haitambui uwepo wako. Nilitaka niwe na kila kitu kwenye maisha yangu bila kujalisha natumia njia gani kuvipata hivyo vitu na leo ninapo ongea na wewe naweza kwenda popote pale na naweza kumnunua mwanamke yeyote ninaye mtaka mimi lakini naishi sehemu ambayo wanadaiwa kuishi watu wenye ukwasi zaidi ndani ya taifa hili, mpaka hapo unaniuliza kama naipenda hii kazi?” mwanaume mmoja ambaye alikuwa amezama kwenye maelezo na mwenzake ambaye alionekana kujutia kazi ambayo ilikuwa imewaweka hapo alimpa mwenzake maelezo kwa kina huku akiwa anavuta sigara ndani ya gari ambayo walikuwepo na kuutolea moshi dirishani kwa mbwembwe uso ukiwa siriasi.

“Na huyo mtu ambaye ulifungwa kwa ajili yake baada ya hapo kiliendelea nini juu yenu?”
“Nisikilize Paschal, huu ulimwengu hauna kumbukumbu, hakuna taarifa ambazo huwa zinahifadhiwa juu ya kile kizuri unacho kifanya labda uwe mtu mashuhuri. Nilikuwa tayari nimemsaidia, sasa unahisi angenikumbuka tena kwa lipi kapuku mimi? Alichukulia kwamba ni kama duniani hakuwahi kuzaliwa mtu kama mimi basi akaendelea kula maisha huku mimi nikikumbana na dhoruba la wanaume wa shoka huko jela ambako ukiwa legelege unaweza kuishia kuwa mke wa mtu ila mimi sikutaka kufikia hatua hiyo. Jela ilinibadilisha na kunifanya kuwa mwanaume, jela ilinikuza na kuyafanya maisha yangu yawe mapya kabisa kwa kujiunga na vikundi vya watu ambao walikuwa wakiogopeka kule. Wakati natoka jela nilikuwa mtu mwingine kabisa, sikuwa yule ambaye nilienda miaka ya nyuma na maisha ya jela yalinifanya niwe na maamuzi magumu mno. Yule bwana nilimuua yeye na familia yake yote kwa ule uhuni ambao alinifanyia kwa kushindwa kuheshimu kujitoa kwangu” maelezo yake hayakuwa na mwisho mzuri kwa sababu yalikuwa yanatisha.

“Dunia ina mambo ya kutisha sana”
“Jitahidi Paschal usiwe sehemu ya hizo stori za kutisha ukiwa kama mhanga kwa sababu utateseka ni bora uwe ndiye mwendeshaji wa hizo sehemu na sio mhanga” maelezo yao yalikuwa yamenoga lakini walikatishwa na simu ambayo ilianza kuita kwa fujo. Mwanaume huyo aliitazama simu hiyo na kuipokea
“Wameanza kushuka tayari”
“Kuna haja ya mimi kuja huko?”
“Hapana, tunakuja naye muda sio mrefu”
“Hazitakiwi kuzidi dakika kumi inatakiwa muwe mmetoweka humo ndani” mwanaume huyo aliongea akiwa anaikata simu na kumgeukia huyo ambaye alijulikana kama Paschal.
“Zima kamera zote ndani ya dakika ishirini ili zinavyorudi kwenye hali yake tuwe tumetoweka ndani ya hili eneo” aliongea kwa msisitizo mwanaume huyo akiwa anaitazama saa yake ya mkononi. Hayo wazungumzo yao walikuwa wanayafanyia nje ya uwanja wa ndege wa JNIA ulipo DAR ES SALAAM na watu ambao alikuwa anaongea nao walikuwa ndani ya uwanja huo wa ndege sehemu ya mapokezi wakiwa kama wenyeji ambao walikuwa hapo kuwapokea wageni wao.

Ukurasa wa nne unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA TANO

Kwenye eneo la kupokelea wageni, wenyeji walikuwa na vibango vyao vya majina mikononi kama ishara ya kutambuana kirahisi na ndugu zao lakini kwenye hilo eneo walikuwepo wanaume wanne ambao walikuwa wanaranda randa huku wakiwa na vifaa vya mawasiliano kwenye masikio yao na kuonekana kama walikuwa ni watu ambao walikuwa wanateta jambo fulani la siri. Ndani ya muda mfupi uliofuata lilitokea jambo la kushtukiza ambalo lilizua taharuki eneo hilo baada umeme kukatika ghafla kisha ukasikika mlio wa risasi. Eneo lilichafuka na kuwa uwanja wa vita hali ambayo ilifanya kuwe na mtafaruko mkubwa kwa dakika kadhaa huku watu wakiwa wanahaha huku na huko kuziponya nafsi zao.

Zilipita dakika ishirini ndipo umeme ukarudi, baada ya umeme kurudi kuna wanaume wanne walikuwa chini ndani ya mavazi ya suti zao wakiwa wamepigwa risasi za kwenye mapaji ya uso watu wakiwa wametawanyika hovyo kila sehemu. Lilikuwa jambo la kushtusha kwa sababu ilitokea ghafla bila kutarajiwa kabisa lakini haikuwa sababu ya kuamini kwamba halikutokea, tayari lilikuwa limetokea. Askari wa usalama ambao walikuwa eneo hilo iliwalazimu kuwakusanya wananchi ambao walikuwa wamesambaa hovyo kwa hofu huku wengine wakiendelea kukimbia kila sehemu na kusababisha idadi kubwa ya majeruhi.
Jambo la kushangaza ni kwamba wanaume walio uawa walikuwa ni wavaa suti tu wanne, hakuna mtu mwingine yeyote yule ambaye alikuwa ameguswa katika eneo hilo hivyo likahesabika kama tukio la kigaidi lakini wakati hayo yote yanaendelea ndani ya uwanja huo msafara wa gari tatu ulikuwa umenyoosha njia ya vingunguti kuelekea Kariakoo huku barabarani ukipishana na gari za polisi ambazo zilikuwa zinakwenda kwa kasi kubwa huko uwanja wa ndege kutokana na tukio ambalo lilikuwa limetokea. Kikosi hicho ambacho kilitokea uwanja wa ndege, kilikuwa maalumu kwa ajili ya kumteka binti mrembo ambaye alikuwa amefika ndani ya uwanja ule na walifanikisha hilo zoezi bila shida yoyote na sasa mwanamke huyo ambaye haikujulikana walikuwa na kazi ipi naye, alikuwa kwenye mkono wao tayari.
JNIA ilifungwa, vurugu na mauaji ambayo yalitokea yalifanya watu kutokuwa na uhakika na usalama wao hivyo kila mtu akawa ametawanyika upande wake huku wengine wakifanikiwa kutoka nje kabisa na kukimbilia walikokuwa wanakujua wenyewe kama sio kwa sababu ya presha lakini wengine walitulizwa na kuwekwa sehemu moja ili mtu yeyote asije akapata tatizo.

Baada ya muda mfupi kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam, Raymond Kono alikuwa anawasili eneo hilo baada ya kupokea taarifa za kushtua kuhusu usalama ndani ya uwanja huo wa ndege mkubwa ambao unategemewa nchini. Baada ya kuwasili eneo hilo, aliikagua ile miili ya wale wanaume ambao walikuwa wameuawa kisha akamhitaji afisa mkuu wa usalama wa uwanja wa ndege kuweza kumpa taarifa zote juu ya kile ambacho kilitokea.
“Hawa watu wanaonekana kuuawa na mtu mmoja kutokana na jinsi walivyo uawa, unaweza ukanipa taarifa juu ya hili ndugu Jonas Moba!?”
“Ni jambo ambalo limetokea kwa haraka ila nahisi sio mtu mmoja ambaye amehusika kuua wote kwa sababu muda ambao umetumika ni mchache na kwa kiza kile mmoja asingefanikiwa hivyo walikuwa ni watu wengi ambao wanahusika na ni maelekezo ambayo walikuwa wamepewa ili kuweka ugumu kwenye kupatikana kwao baada ya hili tukio”
“Unasema unahisi?”
“Ndiyo”
“Hii sehemu ina ulinzi wa kamera kila kona, sasa unaniambia vipi kwamba unahisi?”
“Kwa sababu kamera zote zilizima na umeme ukakatwa na vyote vilipokuja kurudi tukio lilikuwa limetokea tayari kwahiyo sina uhakika na wahusika ambao wamehusika moja kwa moja”
“Kwamba kuna moja kati ya vijana wako wameisaliti nchi yao kwa kuzima kamera?”
“Bado siwezi kuthibitisha jambo hilo kwa sababu inaonekana ni mtu kutoka nje ndiye alifanya zoezi la kuzima kamera”
“Naomba unipeleke kwenye chumba cha kamera na uhakikishe hawa watu wote wanarejeshwa makwao saivi tena wakiwa salama kabisa”
“Sawa kiongozi”

Watu hao waliongozana mpaka ndani ya chumba ambacho kilikuwa kinatumika kuongozea kamera, ndani ya chumba hicho kulikuwa na vijana wa kike na wa kiume ambao walikuwa wakitwetwa kubonyeza tarakishi kwa haraka mno ili kuona kama wanaweza kuyaweka mambo sawa kwani kile ambacho kilitokea hakikuwa kitu kizuri kwa usalama wa taifa lakini walionekana kushindwa kuzipata zile taarifa ambazo walikuwa wakizitaka kwa wakati ule.
“Nionyesheni video ya dakika kumi nyuma kabla ya hili tukio kutokea” kamanda aliamuru ili kuweza kujipa uhakika kama anaweza kumuona mhusika hata mmoja ambaye angeweza kuanza naye kwenye hilo zoezi lake. Haikuchukua muda mrefu, dakika moja ilitosha kuwarejesha nyuma kidogo kuangaza kile ambacho kilikuwa kinaendelea humo ndani. Kwenye ile video ambayo ilirudiwa mara mbili ndipo kamanda wa polisi akashtuka, aliwaona wanaume tofauti wanne ambao walionekana kuwa watu wa kawaida wakiwa wamekuja kwa lengo la kuwapokea wageni wao ila aliwashtukia kwa sababu walikuwa wanaonekana kuwa makini kwenye maongezi na watu ambao hawakuwa wanaonekana.
Watu hao walikuwa wamejigawa kwenye maeneo manne tofauti wakiwa wanalitekeleza zoezi lao hilo. Kwenye mikono yao wanaume hao kila mmoja alikuwa na kibao chenye jina, hakutaka kukurupuka akataka kuhakiki uhalali wa majina ambayo watu hao walikuwa wameyabeba. Majina yote manne hayakuwepo kwenye listi ya wasafiri ambao walikuwa wamefika ndani ya eneo hilo, hilo likamuongezea mashaka na mwelekeo wa kazi yake ambayo ilikuwa imeanza.
Alizitaka picha za watu hao zikuzwe haraka, ndipo aligundua kwamba kwenye masikio yao wote walikuwa na mawasiliano wakionekana kufanya mazungumzo ambayo yalikuwa ya muda mfupi. Baada ya muda kidogo watu hao waliangalia saa zao kwa wakati mmoja na muda haukupita umeme ukawa unakatika lakini hilo jambo lilitokea muda mfupi baada ya binti mrembo kutokezea mapokezi akiwa na walinzi wake wanne. Hapo ndipo muda mfupi uliofuata, umeme ulikatika na kamera zote zilizima na kila kitu kilipokuja kurudi mauaji yalikuwa yametokea tayari huku watu wahitaharuki na kuanza kutoka nduki baada ya kushuhudia mauaji na yule binti mrembo hakuwepo.
“Kuhusu huu uzembe ambao umetokea hapa kwenye mikono yako Jonas tutaushughulikia baadae lakini hapa kuna mambo mawili ambayo tunatakiwa kuyashughulikia. Jambo la kwanza nataka kujua kwamba hawa watu ni akina nani, jambo la pili nataka kujua kwamba ni kwanini wamemteka huyu mwanamke? Kwa sababu ni dhahiri walikuja kwa lengo hilo tu na hili sio shambulio la kigaidi kama mlivyokuwa mnadai, kama ingekuwa hivyo basi kungekuwa na madhara makubwa na mauaji ya watu wengi na wasingetumia ustaarabu namna hii wangehakikisha watu wanapata madhara pamoja na vitu vyetu. Kwahiyo mpaka wanakuja hapa mlengwa wao alikuwa anafahamika, baada ya kujua haya nitahitaji kujua kwamba imewezekaje watu kuingia na silaha mpaka huku mapokezi kirahisi tu namna hii?” Kamanda alikuwa amefura kwa hasira wakati anampa maelekezo yake afisa mkuu wa kitengo cha usalama wa hapo uwanja wa ndege.
Watu wale wote wanne zilihitajika taarifa zao kwa sababu picha zilikuwepo, kati yao ni mmoja tu pekee ambaye taarifa zake zilikuja na wengine hawakuonekana kuwahi kutokea duniani kitu ambacho kiliacha maswali mengine mengi. Damasi Kazimoto, ndilo jina pekee ambalo lilitokea kwenye picha ya mwanaume mmoja kati ya wale wanne ambao walionekana uwanja wa ndege. Taarifa zake zote mwanaume huyo zilikuwa zinaonekana vyema kabisa, alikuwa mzaliwa wa kijiji cha Tambani, Mkuranga na kabila lake alikuwa ni Mndengereko.
Alikuwa ni mwanajeshi wa zamani wa jeshi la wananchi la kujenga taifa ambalo alijiunga nalo baada ya kumaliza tu shule ya upili. Damasi umri wake ulikuwa unasoma miaka thelathini na minne kwenye komputa hizo kubwa ambazo mbele yake ndipo alikuwepo kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam. Jambo la kushangaza kwenye taarifa hiyo ni kwamba mwanaume huyo alikuwa amekufa miaka miwili ambayo ilikuwa imepita na wakati anakufa ndipo alikuwa na miaka thelathini na minne hivyo kama angekuwa hai maana yake angekuwa na umri wa miaka thelathini na misita.

UKURASA WA TANO umefika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA SITA.

Wote waligeukiana na kuangaliana bila kupata jibu lolote la kueleweka juu ya jambo hilo, taarifa zilizo fuatia zilielezea namna alivyokuwa amekufa kwenye oparesheni ya kijeshi. Alikuwa miongoni mwa wanajeshi ambao walichaguliwa kwenda kutoa msaada ndani ya nchi ya Somalia kupambana na kundi la waasi la Al-Shabaab na ndipo ikarudi maiti yake yeye. Swali ambalo walibaki nalo ni kwamba iweje mtu ambaye alikuwa amekufa miaka miwili huko nyuma aweze kuonekana tena ndani ya uwanja wa ndege akiwa hai? Kamanda akaandika taarifa za mwanaume huyo kwenda note-book yake ndogo halafu akaweka alama ya kiulizo.
“Nataka kujua sababu hasa ambayo imewafanya wawepo hili eneo kumteka huyo mwanamke na hilo hatuwezi kulijua bila kumfahamu kwanza huyo mwanamke ni nani?” maelezo yake ndiyo yalifanya wahamie kwenye picha ya mwanamke ambaye alionekana kuwa ndiye mlengwa wa watu hao kuwepo eneo hilo kwa sababu walinzi wake ndiyo walio uawa. Picha ilikuwepo hivyo zoezi halikuwa gumu kuzitafuta taarifa zake.

Leyla M. Patrick, ndilo jina ambalo lilijitokeza pembeni mwa picha hiyo. Hakukuwa na taarifa yake yoyote ya maana wa kuwapa mwongozi zaidi ya kuonyesha kwamba alikuwa yatima binti huyo mrembo. Wote wakabaki wameduwaa, kwamba ni bahati mbaya wavamiaji wengi kutokuwepo taarifa zao lakini naye mvamiwaji taarifa zake zisiwepo? Kivipi? Hilo likaleta mashaka makubwa miongoni mwao. Kamanda wa polisi akabaki ameduwaa kwa muda kwanza akiwa analitafakari hilo jina kwa umakini hususani ile herufi ya katikati ambayo ilikuwa ni M.
“Patrick Magebe!” akatamka kwa sauti ya chini ambayo ikawafanya wote kumgeukia, yeye ndiye alionekana kulijua jina hilo kuliko watu wengine.
“Unamfahamu huyu mtu?”
“Ndiyo huyu alikufa kwenye ajali ya ndege miaka mingi ambayo imepita, litafuteni hilo jina kwenya mtandao haraka” alikuwa kama amezinduka kutoka usingizini kamanda na kuhitaji jina la mtu huyo litafutwe kwa sababu alionekana kuwa alikufa kwa kipindi kirefu kidogo ambacho kilikuwa kimepita na kama angekuwa ni yeye alihitaji kujua ana mahusiano yapi hasa na mrembo huyo ambaye alitekwa uwanja wa ndege.
Mtu huyo alikuwa mashuhuri enzi za uhai wake, hilo likasaidia taarifa zake kupatikana kirahisi, alikuwa ni mfanya biashara mkubwa wa madini. Tajiri huyo alikufa kwenye ajali ya ndege yeye na familia yake yote wakiwa ndani ya jiji la Antananarivo ambako walienda kwa ajili ya likizo. Taarifa hizo zilikuwa za kushtusha, kama alikufa yeye na familia yake yote inakuwaje atokee mtu mwingine mwenye jina lake ambaye kimsingi alikuwa na umri wa binti ambaye angeweza kuwa wake? Huyo Leila ni nani hasa? Ndilo swali ambalo lilianza kuusumbua ubongo wa kamanda huyo mkubwa wa jeshi la polisi akibaki ameduwaa tu asijue angeanzia wapi kulishughulikia jambo hilo.

“Huyu binti anatakiwa kupatikana kwa namna yoyote ile kwa sababu ndiye ambaye pekee anaweza kutupatia jibu la sababu ya kilicho tokea leo pamoja na kuwapata ambao wamehusika. Lakini nahitaji kujua yeye ni mtoto yupi wa yule tajiri wakati taarifa inaeleza kwamba tajiri huyo alikufa na familia yake yote, hili jambo linaweza kutufikisha sehemu nzuri huenda kuna mambo mengine ambayo hatuyajui yakawa sehemu ya hili. Mimi naenda saivi Tambani Mkuranga kuweza kuonana na familia ya Damasi ili nijue kama kweli alikufa na kama alikufa basi tujue huyu ni nani” kamanda alitoa maelezo akiwa anatoka kwenye hicho chumba kuelekea Mkuranga wakati huo huo wa usiku kwa sababu alijua usiku huo au asubuhi yake IGP alitakiwa kuwa na taarifa yote ya kilichotokea lakini hata mamlaka za juu zingehitaji taarifa ya kila kilicho tokea, aliona hiyo ni sehemu ya kujipatia ujiko kwa wakubwa hivyo alikuwa anajituma vilivyo.

Raymond Kono ambaye alikuwa kamanda wa jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam, aliwachukua vijana wake kadhaa na kuondoka nao kuelekea Mkuranga. Gari yao iliendeshwa kwa spidi ili kuweza kuwahi kufika eneo hilo, walipita Vikindu na hatimaye ndani ya saa moja wakawa wamefika Mkuranga. Waliulizia nyumbani kwa mzee Kazimoto ambaye ndiye alikuwa baba mzazi wa Damasi, kwa sababu sakata la mwanae kufariki vitani lilikuwa maarufu! Ilikuwa ni rahisi tu kuelekezwa kwake.
Walifika eneo hilo ambalo ndipo palikuwa nyumbani kwa mzee huyo, alikuwa anakaa pembezoni kidogo sehemu ambayo ilikuwa na minazi mingi. Nyumba yake ilikuwa tofauti na za wengine wote ambao walikuwa wamemzunguka kwa sababu ilikuwa bora. Hayo yalikuwa matunda ya mwanae Damasi ambaye alikuwa mwanajeshi na baada ya kufa walipata mafao ya kutosha ya kumfanya yeye kuishi maisha safi na familia yake tofauti na wanakijiji wengine wa hapo Tambani. Mzee Kazimoto umri ulikuwa umeenda kidogo lakini kwa sababu ya kula vizuri bado alikuwa na afya njema, alishtushwa kupokea ugeni mzito kama huo nyumbani kwake tena majira ya usiku.
“Karibuni, jisikieni mpo nyumbani”
“Asante mzee wangu, pole kwa kukusumbua na usiku wote huu ila ni maswala ya ulinzi na usalama wa nchi hivyo tukawa hatuna namna”
“Nalielewa hilo, nawasikiliza vijana wangu” bwana Raymond ambaye kiumri alikuwa mdogo kwa mzee huyo kwa kuwatazama tu, alizamisha mkono wake mfukoni na kuitoa simu yake ya kisasa, aliifungua na kuikuza ile picha ya Damasi kwenye simu na kumsogezea mzee Kazimoto aweze kuitambua picha hiyo.
“Huyu unamfahamu mzee wangu?”
“Ndiyo, ni mwanangu marehemu”
“Alikufa lini na kipi kilimuua?”
“Ni miaka miwili sasa imepita, alifia akiwa kazini huko Somalia na ndiye ambaye ametufanya sisi kama familia kuishi maisha mazuri, bila yeye sijui ningekuwa wapi leo. Namkumbuka sana mwanangu”
“Pole mzee wangu, naelewa maumivu ya kumpoteza mtu ambaye ni mhimu na mhimili mkubwa wa maisha yako lakini hilo sio ambalo limenileta hapa”
“Kipi kimekuleta?”
“Muda huu kuna watu wamevamia uwanja wa ndege na kusababisha mauaji ya watu wanne na kumteka mwanamke mmoja, kwenye orodha ya hao watu ambao walikuwepo uwanja wa ndege leo, hata mwanao aliku………” mzee huyo hakuruhusu kamanda huyo aweze kuimalizia sentensi yake;
“Umesema nani?”
“Damasi Kazimoto”
“Nadhani mtakuwa mmekosea”
“Hapana mzee wangu, hiyo picha niliyo kuonyesha hapo ni picha ya leo”
“Mwanangu amekufa miaka miwili iliyopita sasa unaniambiaje kwamba yupo hai?” Kamanda hakutaka kubishana, akaitafuta video ambayo alikuwa ametumiwa na watu wa uwanja wa ndege ambayo ilikuwa inawaonyesha wanaume hao wanne na Damasi akiwepo. Mzee Kazimoto alibaki ameganda kwa muda midomo ikiwa inamtetemeka, hakutarajia kuona jambo kama hilo kwenye maisha yake huku bado akiwa mgumu wa kukiamini kile ambacho alikuwa anakiona mbele yake.
“Hili linawezekanaje?”
“Mzee nina imani huenda kukawa na watu mawili, labda mwanao hakufa au kama alikufa basi kuna mtu anatumia sura yake ya bandia ili kujificha kwenye hicho kivuli asije kukamatwa. Naomba unipeleke mahali ambapo alizikwa kama hautajali mzee wangu”
“Sawa haina shida” mzee huyo alijibu ila alionekana kutokuwa sawa, bado ni kama hakuwa akiiamini hali ile.

Walitoka hapo na kutembea kwa dakika kumi wakawa wamefika sehemu ambayo ilikuwa na makaburi mengi, bila shaka yalikuwa ni ya familia. Mzee huyo alinyoosha moja kwa moja mpaka kwenye kaburi moja ambalo lilikuwa limejengewa na kuwaeleza kwamba hapo ndipo ambapo mtoto wake alipumzishwa miaka miwili iliyopita. Lengo la Raymond Kono kufika hapo alitaka kuhakiki urefu wa lile kaburi kama lilikuwa linaendana na urefu wa Damasi, aliliangalia kwa umakini kwa kulizunguka huku akiwa anaangalia vipimo vya urefu wa Damasi kwenye simu pamoja na picha yake mpaka alipo ridhika.
“Mzee wangu utusamehe na pole kwa kukusumbua, nimejiridhisha kwamba Damasi alikufa na huyu kwenye picha ni mtu mwingine ambaye anatumia picha ya mwanao ili kufanya uhalifu. Nakuahidi kwamba tutampata mapema tu na atapata adhabu kali ya kutumia picha za watu ambao wanatakiwa kupumzika kwa amani kwa ajili ya kufanya udhalimu wake” maelezo hayo yalifuatiwa na polisi na kamanda wao kumpa mkono wa asante ya ushirikiano mzee Kazimoto na kutoweka huku yeye akiomba kuachwa pekeyake kwenye kaburi la mtoto wake.

UKURASA WA SITA unafika mwisho.
 
4500 tu kumalizia mpaka mwisho 106.

0621567672 (HALOPESA).....WhatsApp

0745982347 (M-PESA)

0714581046 (TIGO-PESA)

FEBIANI BABUYA
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA SABA

ENTEBBE POLICE STATION
MASAA NANE (8) KABLA YA LEYLA KUTEKWA JNIA.
Ndani ya ardhi ya Yowel Kaguta Mseven, raisi ambaye alinukuliwa mwaka 1986 akidai kwamba tatizo kubwa la Afrika ni viongozi kung’ang’ania madarakani lakini kitu cha kushangaza hata yeye mwenyewe baada ya kuingia madarakani alinogewa kiasi kwamba mpaka leo imeshindikana kuweza kutoka kwenye kiti hicho cha Ikulu.

Entebbe ina historia kubwa husuani wakati wa utawala wa Iddi Amin Dada kiongozi ambaye aliandikwa na makala nyingi kwa ubaya, alichorwa kama kiongozi asiye faa na vyombo vingi vya habari na magazeti mengi huku wengine wakidai kwamba ulikuwa ni mpango wa kumchafua na wengine wakiamini kwamba kila kilicho ongelewa kilikuwa cha kweli. Jiji la Entebbe linaweza kukumbukwa kwa mambo mengi ila mambo makubwa zaidi ni mawili, kwanza ni ile vita maarufu ya Kagera ambayo mwalimu Nyerere aliamua kumuonyesha bwana Iddi Amin kwamba Tanzania sio nchi ya kuichezea chezea japo vita yoyote madhara yake huwa ni mabaya kuliko faida lakini mwalimu alishinda.

Jambo la pili ni makomando wa Israeli kwenda kuwakomboa mateka ndani ya jiji hilo ambao walikuwa wapo chini ya ulinzi wakiteswa kwa amri ya Iddi Amini, jambo ambalo lilipelekea kutengenezwa kwa movie iitwayo OPERATION ENTEBBE. Tuachane na umashuhuri wake wa historia jiji hilo ambalo huenda ukilitaja kwa wana Uganda au wana Afrka ya Mashariki basi huwa wanalikumbuka kwa mengi ya zamani leo linatupatia kisa kingine kikubwa huenda kikawa cha tatu kwa kukumbukwa kwenye historia ya taifa hilo.

Saa saba kamili mchana, umbali wa mita kadhaa kutoka kilipo kituo hicho cha polisi kikubwa kiitwacho ENTEBBE POLICE STATION, mwanaume mmoja alishuka kwenye tax akiwa na suti yake na begi la safari mkononi. Baada ya kushuka ndani ya hiyo tax alilipa ujira wake na kumtaka dereva aondoke bila kumpatia chenji, alisimama kwa umbali akiwa analitazama jengo kubwa la kituo hicho cha polisi akiwa na tabasamu hafifu kwenye uso wake, tabasamu ambalo lilikuwa linaenda kufungua ukurasa mwingine ndani ya kituo hicho cha polisi.
Ukiachana na suti yake ghali ya blue ambayo ilikuwa mwilini mwake, kichwani alikuwa na kofia kubwa aina ya pama ambayo ilikuwa rangi sawa na suti yake, chini kabisa mguuni alikuwa na kiatu cheusi ambacho kiling’aa na kwa jua lilivyokuwa limewaka kilizidi kuwa maridhawa ndani ya mwili wake. Begi lake jeusi alikuwa ameliweka mkono wa kulia huku mkono wa kushoto akiwa ameishikilia simu yake ndogo ya kufunua, alilitazama kwa umakini jengo lile akiwa anatafakari mengi kwenye mfumo wake wa akili. Hatimaye aliifunua ile simu yake na kuiweka sikioni.

“Initiated” ndilo neno moja pekee ambalo alilitoa kwenye kinywa chake kisha aliirushia simu yake chini na kuikanyaga mpaka ilipo bakia vipande vidogo vidogo, laini ndogo ilionekana chini, hakuinama kuiokota bali aliisukumizia kwenye tundu dogo ambalo lilikuwa limetokea mtaroni hivyo kusingekuwa na namna ya laini hiyo kuja kupatikana tena. Baada ya kuhakikisha jambo hilo lipo sawia kama alivyotaka, sasa alianza kujongea taratibu kuelekea kilipo kituo hicho kikubwa cha polisi.

Alifika mapokeni na kueleza kwamba alikuwa anahitaji kuelekea ndani ambapo kwa aina ya mavazi yaliyokuwa mwilini mwake, hakupata upinzani mkubwa ila alitakiwa kwenda kukaa sehemu ya kuweza kusubiria ili ikifika zamu yake aitwe na kwenda kusikilizwa, alikutana na idadi ya watu wengi ndani ya sehemu kubwa ya ndani ya kituo hicho kila mtu akiwa na yake ya kuyamalizia hapo. Watu wengi ambao walikuwa wanampita, walikuwa ni weusi tii na haikumshangaza kwa sababu ndiyo asili yenyewe ya watu wa Uganda walivyo.

Baada ya kuona kila mtu yupo na lake, alisimama na kusogea katikati ya eneo hilo akiwa na begi lake mkononi, aliinama na kuifunua soksi yake ambapo aliitoa bastola kwenye soksi yake nyeusi na kupiga risasi nyingi juu ambazo zilipelekea watu kuanza kusambaratika kwa mbio kuokoa uhai wao lakini wengine wakilala chini kwa uoga wa kupatwa na risasi. Lilikuwa ni jambo la sekunde chache mwanaume huyo kujikuta akiwa amezungukwa na maaskari ambao walikuwa na mitutu ya hatari wakisubiri kumshambulia yeye.

Baada ya kuona amezungukwa na kupokea amri ya kujisalimisha haraka kutoka kwa mkuu wa kituo hicho ambaye aliingia hapo kutoka kwenye ofisi yake baada ya muda mfupi tangu isikike milio ya risasi, mwanaume huyo aliiachia bastola yake chini pamoja na begi lake akiwa anapiga magoti chini na kunyoosha mikono yake juu akiwa mwingi wa tabasamu kwenye uso wake. Polisi walimzunguka haraka na mmoja alimpiga na kitako cha bunduki kwa jazba ambayo alikuwa nayo, ilikuwa ni aibu kubwa mtu kuvamia kituo kikubwa kama hicho cha polisi na kuanzisha vurugu ambazo zilikuwa zimeleta kashikashi kwa watu ambao walifika hapo kutatua shida zao.
Kitako cha bunduki kilimpata kwenye pua yake ambayo ilipasuka kidogo na kuanza kuvuja damu, alifungwa pingu na kusogezwa alipokuwepo mkuu wa kituo ambaye alimzaba kofi kali usoni mwake na kumtamkia;

“Umeingia sehemu mbaya ambayo utatamani usingeijua kwenye maisha yako” licha ya kufanyiwa hayo yote mwanaume huyo aliishia kutabasamu tu na kuwaangalia watu hao kwa dharau kisha akabebwa kuelekea kwenye chumba cha mateso na mahojiano ili akawaambie yeye ni nani hasa na alifuata nini hapo kiasi kwamba hakuogopa kuruhusu risasi zitoke kwenye batola yake japo hakumuumiza mtu yeyote.

Taa nyekundu zilikuwa zinawaka na kuzima ndani ya chumba ambacho kwa mwonekano tu hakikuwa salama kwa binadamu kukaa kwa muda mrefu kama sio kufika kabisa. Chumba kilikuwa kikubwa ambacho kilikuwa chini ya ardhi ndani ya kituo hicho kikubwa cha polisi, ndani yake hakikuwa na mapambo mengi bali mashine kadhaa ambazo zilikuwa zinaendana na mashine za mikono za kusagia kahawa lakini zile sehemu za kuvesha mikanda zilikuwa kubwa na ngumu zaidi pembeni yake kukiwa na minyororo migumu ambayo ilikuwa inatumika kama mikanda yake.

Zilikuwa mashine nne ambazo ziliwekwa kwenye pembe tofauti tofauti, kulikuwa na viti kadhaa vya umeme na kiti kimoja cha chuma ambacho kilikuwa katikati ya chumba. Upande wa mbele wa chumba hicho kulikuwa na meza moja kubwa ambayo juu yake kulikuwa na vifaa vya chuma na mabox kadhaa yakiwemo ya huduma ya kwanza, pembeni ya meza hiyo kulikuwa na mipira kadhaa ya maji yenye nguvu na kasi kubwa. Hicho ndicho chumba ambacho alikuwa ameletwa mwanaume ambaye utambulisho wake bado haukufahamika ila alikuwa na jeuri ya kuvamia kituo kikubwa cha polisi nchini Uganda.

Alipo fikishwa ndani ya chumba hicho, hakuonekana kuwa na presha japo vitu alivyo viona humo ndani ni wazi kwamba hakuwa anavitarajia kuvikuta. Alihema kwa nguvu wakati huo alipigwa na mtama wa kushtukiza nyuma ambao ulimfanya adondoke chini, hakubembelezwa bali alivuliwa nguo kwa nguvu na kubakia na boxer tu pekee. Maaskari ambao walionekana kuwa na hamu naye wakisubiri amri walimfunga minyororo minne kwenye mwili wake, miwili kwenye mikono yake na miwili kwenye miguu yake kisha minyororo hiyo ikavalishwa kwenye zile mashine.

Mashine ziliwashwa na kuanza kumvuta taratibu mpaka alipokuwa anaelekea hewani bila kukanyaga chini ndipo zikazimwa, alitakiwa kuongea vizuri kwamba yeye ni nani na kipi kilimuingiza ndani ya hilo eneo na kuleta taharuki. Aliingia mkuu wa kituo akiwa kwenye vazi lake, alimsogelea mtuhumiwa wake pale alipokuwa anaelea na kumwangalia kwa umakini kwenye uso wake bila kupepesa macho macho.
“Wewe ni nani?” alirudia kuuliza mara mbili lakini mwanaume huyo hakujibu kitu chochote zaidi ya kubaki anamtazama tu, alihitaji aletewe fimbo. Alipewa na kuanza kumshughulikia mwanaume huyo ambaye aliishia kucheka kwa sauti licha ya fimbo kali ambazo zilikuwa zinapita kwenye mwili wake, mwili wake ulikuwa umekomaa kiasi kwamba mpiga fimbo alikuwa anapoteza muda wake tu kufanya zoezi hilo.

Aliacha mara moja na kuhitaji vitu vya mwanaume huyo viletwe ndani humo ambapo walikagua kwenye suti yake na kukuta sigara moja aina ya CIGAR pamoja na pochi ndogo, zaidi ya hapo hakukuwa na kitu kingine ndani yake. Walipo ifunua waleti hiyo walikutana na pesa za mataifa sita yenye thamani kubwa duniani zikiwa zimerundikwa ndani pamoja na paspoti mbili. Paspoti moja ilikuwa ya taifa la Tanzania lakini ya pili ilikuwa ni ya nchi ya Uganda, wakabaki wameshangaa kwamba mtu huyo paspoti hizo zote mbili alikuwa anafanyia nini? Kwenye paspoti zote kulikuwa na picha zake ambazo zilifanana, alikuwa anaonekana kuwa na kipara ila kwa wakati huo alikuwa na nywele kichwani kwake, hilo lilionyesha kwamba alipiga picha hizo kitambo kidogo. YOHANI MAWENGE ndilo jina ambalo lilikuwa linasoma kwenye paspoti zake zote mbili.

UKURASA WA SABA unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA NANE

Ikabidi walichukue na begi lake ambapo kwenye begi waliikuta laptop moja tu pekee, waliiwasha ikawaka bila kukutana na upinzani wowote ule. Kwenye ile laptop kulikuwa na faili moja tu pekee ambalo walijaribu kulifungua lakini likagoma kwa sababu lilikuwa linahitaji nywila ili kuweza kufunguka na hapo ndipo mkuu wa kituo hicho akamgeukia tena mwanaume huyo akiwa anatoa ishara kwa vijana wake kuchukua ile mipira ya maji ili kumchangamsha akili kidogo. Maji yalifunguliwa na kumfanya achakae ndani ya dakika kadhaa tu, maji yalikuwa yana ubaridi mno na yalikuwa yanatoka kwa kasi kubwa ila mwanaume huyo alibaki ametulia tu akiinamisha kichwa chini japo yale maji yalionekana kabisa kumkolea kwenye mwili wake.

Alipigwa shoti kadhaa ambazo zilimfanya apige kelele huku zile mashine zikiwa zinavutwa na kuanza kumtanua kwa lazima, kama zingeenda kwa kasi zaidi basi zingeweza kumgawanyisha vipande vidogo vidogo.

“Mimi na wewe tuna mengi ya kuzungumza ila kabla ya kunijibu kipi kimekuleta hapa nahitaji unitajie namba za siri za kufungulia lile faili.

“Nadhani ulitakiwa kunisikiliza kwanza kabla ya kufanya maamuzi ya kijinga kama haya, maamuzi ya kuanza kunitesa bila kujua nataka nini na kwanini nimekuja hapa yanaweza kukuingiza matatizoni wewe na vijana wako wote kwa sababu haya mateso mtayalipa” ndilo jibu la jeuri ambalo alilijibu mwanaume huyo ambaye jina lake lilikuwa linasoma Mawenge Yohani. Mkuu wa kituo alicheka sana akiwa amemkazia macho, alishangaa mtu ambaye alikuwa anaweza kumuua muda wowote bado alikuwa na jeuri ya kumjibu kwa dharau namna hiyo.

Alisogea kwenye meza na kuchukua nyundo moja ambayo alirudi nayo na kumkita nayo mwanaume huto tumboni kwa hasira bila kumuuliza kitu.

“Andika mwaka wa kuzaliwa mtoto wako wa kiume, ndilo neno la siri la kufungulia kwenye hilo faili” mkuu wa kituo ni kama bado hakusikia ama alisikia ila hakuelewa ambacho mwanaume huyo alikuwa amekiongea. Mtoto wake wa kiume alikuwa anaingia vipi kwenye hilo sakata kiasi kwamba mwaka wake wa kuzaliwa ndilo liwe neno la siri? Na huyo mtoto huyo mtu alimfahamia wapi? Akiwa amebaki ameduwaa alisogea kwenye laptop hiyo na kuingiza mwaka wa mwanae kuzaliwa na kweli lile faili lilifunguka likiwa na video kadhaa na nyaraka kadhaa ndani yake ambazo zilikuwa zimewekwa kwa mfumo wa mafaili.

Aliifungua video ya kwanza lakini jambo la kushangaza ni kwamba video hiyo ilikuwa na yeye na mkewe wakiwa wanafanya mapenzi kwenye mvua nje ya nyumba yake, aliitoa haraka na kuifuta ili vijana wake wasiweze kuiona na alipiga marufuku mtu yeyote kuweza kuigusa laptop hiyo kisha akamgeukia mwanaume yule ambaye alikuwa amenasa hewani akiwa hana ujanja wa kujinasua kwenye ile minyororo migumu na mizito. Mkuu wa kituo alitoa bastola kwenye kiuno chake na kumsogelea bwana Yohani akiwa na jaziba kali hali iliyo mfanya kuanza kuchuruza jasho jingi kwenye uso wake na mwilini kwa ujumla huku mdomo wake ukiwa unatetemeka kama mtu ambaye alikuwa anataka kuongea jambo ila kuna kitu kilikuwa kimemkaba shingoni na kumfanya asiwe na huo uwezo.

“We, wewe ni nani?” aliuliza kwa sauti ya mamlaka hata vijana wake walisogea nyuma kwa uoga, hawakuwahi kumuona kiongozi wao akiwa kwenye hali ya hatari kama hiyo na yote ni baada ya kufungua video ile ambayo hawakujua hata ndani yake aliona nini mpaka kufikia hatua ya kubadilika ghafla.
“Nadhani sasa tunaweza kuongea” Yohani aliongea kwa tabasamu huku akiwapa ishara askari waliokuwa pembeni kumshusha hapo maana alikuwa amechoka. Mkuu wa kituo aliwapa ishara wamshushe na kumfunga kwenye kiti kisha akawataka vijana hao watoke nje, yeye ndiye binafsi angefanya mazungumzo na mwanaume huyo. Alisogea kwenye kona moja na kubonyeza kitufe cheusi ambacho kilifanya kamera zote humo ndani kuzima kisha akarudi na kiti kingine ambacho kilikuwa konani na bastola yake mkononi, waliketi wakiwa wanatazamana ili wafahamiane kiundani zaidi.
“Wewe ni nani?”

“Hilo sio swali la msingi kwa sasa, jambo la msingi ulitakiwa kuniuliza kwanini nipo hapa” Yohani hakuwa na wasiwasi kwa sababu alionekana kuwa na uhakika wa kile ambacho alikuwa anakifanya na alijua kabisa kwamba wangefikia sehemu hiyo ambayo walikuwa wameifikia kwa wakati huo.
“Unanijibu kwa jeuri hivi unajua kwamba naweza hata kukuua na hakuna kitu kitatokea na hakuna mtu ambaye atajua kama uliwahi kuwepo!” maneno ya mkuu wa kituo yalimfanya Yohani kucheka akiwa anamtazama.

“Nina uhakika hilo ni kosa ambalo huwezi kulifanya bwana Odong kwa sababu baada ya kuiona ile video nina uhakika kwamba umetambua sijaja kwa bahati mbaya hii sehemu hivyo tusipoteze muda tuende kwenye jambo ambalo limenileta hapa moja kwa moja”

“Unajua nini kuhusu mimi wewe?”

“Nakujua wewe huenda kuliko hata ambavyo unajijua wewe mwenyewe. Miaka miwili iliyopita ulikuwa askari kanzu mwenye cheo cha chini, ulikuwa na maisha magumu kama ambayo wanayo askari wengine wa kawaida huku ukiwa unafanya kazi kwenye kituo kidogo cha polisi huko Kampala lakini kichwani mwako ulikuwa na mahesabu yako mengi juu ya kuusaka utajiri. Ulikuwa unajihusisha na uchezaji wa kamari haramu mtaani ambazo sheria ya nchi yenu hairuhusu huku ukishinda kwenye madanguro na kununua malaya ambao wanaiuza miili yao ukimuacha mkeo nyumbani”;

“Baada ya kuteseka kwa muda kimaajabu ulipata nafasi ya kuja kuwa mkuu wa kituo hiki kikubwa bila hata kujua hiyo nafasi uliipataje na ulivyo mjinga uliamua kutofuatilia kabisa ukihisi wewe ndiye mtu mwenye bahati kabisa ndani ya taifa hili ukaanza kuzitumbua pesa na kuishi maisha safi. Unaishi ndani ya ARKRIGHT CITY kwenye jumba la kifahari ambalo haliendani kabisa na mshahara wako. Labda nikuulize swali rahisi tu, ile video ambao umeiona humo ndani ukasita na kuangalia zingine au kuimaliza ni yako au sio wewe?” swali lilikuwa gumu kwake akaishia kuguna tu asiongee lolote na kumfanya Yohani kuendelea na maelezo yake.

“Umefanya uchafu mwingi ambao ukifika kwa umma basi wewe na mabosi zako hamtakuwa na kazi tena na huenda taifa likaingia kwenye machafuko makubwa au vita vya wenyewe kwa wenyewe na ukisoma mafaili yote na kutazama video zote utaelewa vizuri zaidi. Nina siri zako nyingi na ushenzi wako wote ambao umeufanya, video zako za ngono zipo zaidi ya kumi mle na sio wewe na mkeo tu zingine mpaka na wake wa viongozi wa dini na wake wa mabosi zako lakini baya zaidi zipo mpaka za mkeo akiwa anafanya mapenzi na wanaume wengine japo hayo sio mhimu sana kwa sasa”;

“Jina lako wewe unaitwa Akello Odong, una mke mmoja wa ndoa ambaye anaitwa Adong Akello Odong na watoto watatu, Othieno ambaye ndiye wa kiume pekee, Akite ambaye ndiye binti yako mkubwa na ndiye mtoto wa kwanza kwenye familia yako lakini pia una mtoto wa kike wa mwisho aitwaye Amara. Othieno ambaye kwa sasa ana miaka ishirini na miwili mwaka jana alimbaka mtoto wa kike mwenye miaka kumi na mitano na kumuua na wewe ulijua kabisa lakini ukalificha hilo na kuifuta hiyo kesi kwa ujanja ujanja wako. Taarifa zake na video zake ninazo na najua hili ndilo mhimu zaidi kwako kwa sababu mwanao akijulikana ananyongwa na wewe unafungwa kwa kulificha hili”

“Humo ndani ya hiyo laptop kuna taarifa za viongozi wako wakubwa na listi yao kwa ujumla na ushenzi wote ambao wanaufanya na kama ushahidi huo ukiwekwa wazi basi utaelewa kwamba ni kwanini nchi yenu inaweza kuingia kwenye vita mbaya vya wenyewe kwa wenyewe kwani wananchi hawatakubali. Lakini wakubwa zako wao wanaweza kujitetea kwa namna wajuayo wao vipi wewe hapo ambaye ni mkuu tu wa kituo unahisi hautakuwa miongoni mwa wale ambao watatolewa kafara?”

“Unataka nini kwangu?” bwana Akello aliuliza akiwa anatetemeka na jasho jingi linamtoka kwenye mwili wake, kuhusu yeye na familia yake mtu huyo taarifa zote ambazo alizitoa zilikuwa za kweli kabisa na ndilo jambo ambalo lilimtisha mpaka wakati huo.

“Masaa kumi kuanzia sasa kitengo maalumu cha counter terrorism kutoka kwenyes shirika lenu la kijasusi la ISO kitakuja kunichukua hapa na kwenda kunihoji mimi kwa sababu kwa kilicho tokea hapa huenda watahisi kwamba mimi ni miongoni mwa magaidi ambao wanaiweka Uganda kwenye hali ya hatari lakini kabla ya mimi kwenda huko kuna kazi ambayo nataka nikupe wewe hapo”

UKURASA WA NANE unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA TISA

“Una maana gani kusema unachukuliwa baada ya masaa kumi yajayo na haya umeyafahamia wapi”
“Hizi ni hesabu ndogo ambazo zinatokana na utaratibu wa sheria za nchi fulani, kwa mtu kama mimi ni rahisi kuishi na hizi hesabu kwa sababu nimeishi haya maisha kwa muda sasa”
“Unataka nifanye nini?”
“Kuanzia sasa yakipita masaa nane Tanzania kuna tukio la mauaji na utekwaji wa mtu litatokea kwenye eneo la mhimu kwa taifa lakini linaweza kuzuiwa kama nitafanya mawasiliano ndani ya nchi ya Tanzania”
“Bado sikuelewi, hili jambo ulitakiwa ulifanye ukiwa nje ya kituo hiki, sasa kwanini umesubiri uje hapa ndipo uanze kuhitaji kufanya mawasiliano na watu hao?”
“Kufanya mawasiliano nje ya mikono yenu ingekuwa ni hatari kwangu ila nikifanya mawasiliano nikiwa kwenye mikono ya mamlaka za Uganda kwangu ni salama zaidi ndiyo maana nimefanya hili. Nahitaji kuongea na kamishna wa jeshi la polisi wa nchi ya Tanzania na kama ikishindikana mimi kuongea naye basi inatakiwa niongee na raisi wa Tanzania”
“Kwani wewe ni nani hasa mpaka uhitaji kuongea na hawa viongozi wawili wa nchi?”
“Hilo halikuhusu, najua wewe hauna mamlaka ya kunifanya mimi niweze kuongea na hawa watu moja kwa moja ila naweza kufanya hivyo kupitia viongozi wako wa juu, kazi yako unatakiwa uwapatie taarifa waje hapa haraka niwape maagizo ya nini cha kufanya”
“Hakuna kiongozi ambaye anaweza kukubali kuja kuongea na mtu wa kawaida kama wewe kirahisi namna hii kwa sababu haiwezekani”
“Nenda kwenye lile begi ambalo umeikuta laptop na uangalie chini yake kuna zipu ngumu imejibana konani, ifungue halafu utakacho kikuta niletee hapa” Bwana Akello bado alikuwa njiapanda asielewe huyo mtu alikuwa na maana gani lakini aliamua kutii maagizo na kuinuka kwenye kiti chake kama mtoto mdogo. Ndani ya hilo begi aliikuta saa moja ndogo ambayo juu yake ilikuwa inasoma masaa kumi na hapo ndipo akashtuka na kumkimbilia Yohani.
“Hiki ni nini?”
“Hilo ni bomu ambalo lipo ndani ya Uganda, bomu hilo linauwezo wa kuua watu walio karibu mpaka elfu hamsini na kujeruhi watu karibia elfu tano walio mbali kama likilipuka na linalipuka ndani ya masaa kumi kama ambavyo linajionyesha kwenye hiyo saa hapo. Nina uwezo wa kulifanya bomu hilo likasimamishwa ila nahitaji viongozi wako wakubwa waje hapa kunisikiliza mara moja”
“Unapanga kuangamiza wananchi wa taifa hili? Unadhani naweza kukuacha hai au tunaweza kukuacha hai kwa huu ujinga ambao unaufanya?”
“Wewe hapo hauna lolote la kufanya mpaka sasa, halafu unavyo chelewa kufanya maamuzi huenda hata familia yako ikaingia matatizoni kwa sababu wote watakufa” neno familia ndilo lilimchanganya, alisimama na kupiga simu haraka kwa mkewe kuulizia usalama wa familia hiyo. Alicho jibiwa na mkewe kilimtisha, kuna wanaume wawili wenye suti zao walikuwa wamefika kwake kumtafuta lakini mkewe akawapa taarifa kwamba alikuwa kazini na baadae kama angerudi angempa taarifa ya ujio wao nao wakaahidi wangerudi tena baadae.
Alipaniki na kumsogelea Yohani akiwa anakimbia, akamkwida kwenye shingo yake akiwa anamtikisa kwenye kile kiti huku akimtishia na bastola kana kwamba alikuwa anaweza kumuua wakati huo huo.
“Weka bastola yako chini na unisikilize” alimuachia kwa jaziba huku akiwa anahema na kuinama pembeni akiwa anamwangalia bwana huyo kwa jicho kali lililo fuga kisasi.
“Kwa sasa unafanya kazi chini yangu, kuanzia leo utafanya ninacho kitaka mimi na kama ukienda kinyume sio kukudhalilisha tu bali wewe na familia yako wote mtakufa na wewe utakuwa wa mwisho. Kuna namba nakupatia ambayo utaitumia baadae kwenda kwenye hoteli moja ipo ndani ya Kampala, utaelekezwa chumba cha kwenda, kuna mtu utamkuta huko kuna maelezo atakupatia ya nini ambacho unatakiwa kukifanya kipindi ambacho mimi sitakuwepo wewe ndiye utakuwa unatimiza majukumu yangu” Odong alibaki anajishangaa na kujicheka, ilikuwa ni ajabu ndani ya dakika kadhaa tu alijikuta anakuwa kibaraka wa mwanaume ambaye alitakiwa kuwa mfungwa wake.
“Ipo siku nitakuua”
“Kama huna uwezo wa kuniua kwa sasa Odong basi kwenye maisha yako hautakuja kupata nafasi nyingine kama hii ya kuweza kuniua tena. Baada ya dakika tano, wapigie simu viongozi wako wakubwa waje hapa niongee nao na kama wakinielewa basi mambo yatakuwa sawa ila kama watajifanya kuwa na vichwa vigumu basi taifa lenu litaingia sehemu mbaya. Mimi naenda kuhojiwa na ni matumaini yangu kama ikishindikana leo basi kesho nitaongea na hao viongozi wa Tanzania kisha masaa ishirini na manne baada ya mimi kukamatwa na ISO nitatoroka na kupotea kabisa hivyo wewe ndiye ambaye unapaswa kuhusika kunitorosha”
“Umechanganyikiwa wewe, mimi nikutoroshe mtuhumiwa ambaye unataka kuliingiza taifa langu kwenye matatizo?”
“Kumbuka unafanya kazi chini yangu kwa sasa hivyo mimi ndiye ambaye nakupa amri ya nini cha kukifanya na nini cha kutokifanya. Chukua hiyo laptop futa video ya kwanza mpaka ya kumi ndizo zako na vingine vyote viache ni vya viongozi wako na baada ya hapo ifunike kama hujaigusa kwa sababu wakijua umeziangalia utakuwa hatarini, hao nataka wajionee wenyewe ujinga wao. Sina lingine la kuongea na wewe kwa sasa wapigie simu hao watu nina shida nao wewe nitakutafuta kwa mara nyingine nikiwa nataka tuonane tena” Odong kwanza alikaa chini, hakuelewa huyo binadamu alikuwa wa aina gani mpaka kuwa na imani na hatua zake zote ambazo alikuwa anazifanya namna hiyo. Odong aliambiwa alete kalamu na karatasi ambavyo alikuwa navyo mfukoni, kuna namba alitajiwa, akaziandika na kuzitia kwenye mfuko wake akiwa anatetemeka na kuanza kumuogopa Yohani.
Yohan hakuonekana kuwa binadamu kama yeye, alionekana kuwa kiumbe wa tofauti na wanadamu wengine kwa sababu wakati huo alitakiwa kuutumia kujitetea ili aachiwe lakini alizidi kumuweka mkuu wa kituo njiapanda. Alisogea kwenye ile laptop, akafuta video ambazo alielekezwa na kuifunika kisha akatoka ndani ya hicho chumba na kukifunga kabisa ili mtu mwingine yeyote asije akaingia humo ndani huku yeye binafsi akiwa amechanganyikiwa.

Yalipotea masaa mawili bila taarifa yoyote wala ujio wa mtu yeyote ndani ya chumba chake Yohani, ikawa inasoma saa tisa alasiri na madakika kadhaa ndipo aliona mlango huo ukiwa unafunguliwa. Aliye ingia hapo alikuwa ni IGP wa taifa la Uganda, Okumu Odinga, vazi lake lilikuwa limependezeshwa na uwingi wa nyota ambazo alizipata kwa kazi nzuri ambayo alikuwa ameifanya kwa muda mrefu ndani ya serikali yake.
Huyo ndiye alikuwa mkuu wa idara zote za kipolisi ndani ya taifa hilo, alifika hapo baada ya kupata taarifa za kushtua kutoka kwa mkuu wa kituo cha ENTEBBE ambaye alikuwa ni kijana wake wa kazi. Alisogea mpaka alipokuwa Yohani kwa msaada mkubwa wa taa zenye mwanga wa kutosha zilizo nururisha chumba hicho huku kwenye mkono wake akiwa na zile paspoti mbili za mwanaume aliyekuwa mbele yake kwa wakati huo.
“Una miaka mingapi kijana?” Aliuliza swali wakati huo akiwa anakivuta kiti na kukaa umbali kidogo kutoka alipokuwepo Yohani ila mwanaume huyo aliishia kumwangalia tu huyo mheshimiwa na kusikitika bila kumjibu jambo lolote lile.
“Unajua umejiingiza sehemu mbaya, nimepewa taarifa zako masaa mawili yaliyo pita lakini sikutaka kuyapa uzito kwani nilihisi watakuwa vibaka tu ambao huwa wanatafuta majina yao kwa nguvu ili watokeze kwenye kurasa za magazeti ila nimeamua kuja baada ya Ogong kunisisitiza kwa ukubwa juu ya mimi kuwepo hapa. Mimi ni kiongozi mkubwa wa usalama wa taifa hili, nimeacha majukumu mengi mpaka kufika hapa hivyo niambie haraka ni mambo gani ambayo yanahatarisha usalama wa taifa hili mpaka kuna ulazima wa mimi kukusikiliza?”

UKURASA WA TISA unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA KUMI

“Hili taifa lako lipo hatarini na bado masaa nane tu yatokee maafa ya kihistoria lakini hilo unaweza kulizuia wewe hapo na kwa bahati mbaya siwezi kuongea mpaka nipewe ninacho kitaka”
“Unavyo ona hii serikali unahisi kwamba ni genge la wahuni kiasi kwamba unaweza kuja hapa na kudai unacho kitaka wewe? Hilo bomu ambalo unadai lipo kwenye taifa hili ni stori za kutunga bwana mdogo, hili taifa ni salama kuliko unavyo fikiria wewe. Niambie jambo la maana ambalo unahisi litanishawishi mimi kukuacha hai kwa kunisumbua kuja hapa”
“Mwezi uliopita nchi yako ilivamiwa kwa kiongozi mmoja kutekwa lakini mkaudanganya uma kwamba lilikuwa ni genge la wahuni tu lakini kiongozi hakutekwa hususani baada ya kukutwa ametelekezwa kwenye uwanja wa gofu mkabala na Akright city. Wiki mbili baadae waziri wa ulinzi alipata ajali lakini alifanikiwa kupona, kitu ambacho hamukukiweka wazi na mkayafanya kwa usiri mkubwa japo mlimkuta waziri amepigwa risasi moja kwenye bega lake. Hizi ni taarifa za ndani ambazo hakuna mwananchi yeyote yule anajua na baada ya hapo mmepanga kwa sasa kumbambikizia kesi ya ugaidi kiongozi wa upinzani ili mmtoe kwenye ramani. Haya yote yanafanyika kwa usiri mkubwa na viongozi wakubwa kiasi kwamba ni taarifa ambayo ipo kwa watu wachache, bado unataka nikuaminishe kwamba nipo siriasi na ninacho kiongea?”
“Wewe ni nani?”
“Ungeniuliza kwanza nataka nini”
“Hata nikikuuliza haina maana kwa sababu siwezi kukupa zaidi ya kukuua, unajua kupitiliza na hii sio salama kwetu”
“Too late kuhitaji kuniua kwa sasa. Nahitaji immunity”
“Umechanganyikiwa?”
“Ongea na mshauri mkuu wa raisi nipatiwe immunity from proseution kwa ajili ya ulinzi wangu, nitakupa taarifa za hili bomu lilipo ila baada ya hapo hakuna mtu anatakiwa kunigusa. Najua nitachukuliwa na kwenda kuwekwa kizuizini na ISO ila nahitaji baada ya mahojiano niweze kuwa huru”
“Hilo ni jambo ambalo haliwezekani. Tuna uwezo wa kukutesa mpaka useme ni wapi hilo bomu lilipo kama ni kweli unayo yaongea”
“Unapoteza muda wako kamanda, nahitaji kuongea na kamshina wa jeshi la polisi wa Tanzania au raisi wa Tanzania waje hapa kunifuata ikishindikana kabisa niongee nao kwa njia ya simu, nina maagizo ya kuwapa. Yafanyie kazi hayo mambo mawili ambayo ninayataka na nchi yenu itakuwa salama ila bila hivyo baada ya masaa nane yajayo kutakuwa na historia mbaya ndani ya hili taifa”
“Najiuliza maswali mengi, nina imani wewe ni mtanzania, kwanini kama ulitaka jambo hili lifanyike usiende moja kwa moja kwenye serikali yako uzungumze nao? Kwanini Uganda? Na baada ya kuzungumza na hao viongozi wako mwafaka wako ni upi hasa? Unahitaji kuwaua kwenye taifa letu tuingie vitani na Tanzania? What is it you want?”
“Nenda kaniandalie immunity from proseution kabla haujachelewa. Kama unaona hili jambo natania basi subiri ndani ya masaa sita uone kitakacho tokea ndani ya nchi ya Tanzania. Baada ya tukio hilo kutokea, kumbuka mtakuwa na masaa mawili tu ya kuweza kuwaokoa wanananchi zaidi ya elfu hamsini ambao wanaweza kufa na kupata madhara makubwa ndani ya taifa hili” IGP alicheka kwa nguvu akiwa anamwangalia mwanaume yule mtata bila kummaliza. Hakuwa na uhakika na maneno yake lakini kwa namna fulani yalianza kumtisha na kuhisi kwamba huenda jambo hilo lilikuwa na siri ndani yake hata hivyo alisimama na kutembea hatua chache kisha akageuka na kurudi karibu na alipokuwa amefungwa Yohani.
“You better be right boy, kwa sababu kama unacheza michezo ya kitoto na hii serikali, utaishia sehemu ambayo haujawahi kuifikiria”
“ You have six hours to make your decision commander” ndilo jibu ambalo Yohani alimpa kiongozi huyo ambaye hakugusia kabisa suala la laptop huenda alipuuza bila kujua kilichokuwepo ndani. Sasa kazi ilikuwa kwake kufanya maamuzi ya busara ndani ya masaa sita ambayo yalikuwa yanafuata.

Usingizi wa mang’amu ng’amu ulikuwa umeichukua nuru usoni pake akiwa anasikilizia fukuto la joto ambalo lilikuwa limekibamba chumba alicho kuwepo. Uchovu na njaa ambayo alikuwa nayo ndivyo ambavyo vilimfanya atulie kitini huku akiwa anabahatisha usingizi ambao hata hivyo ulimpata kiasi kwamba akapata nafasi ya kupumzika kidogo. Yohani ndiye ambaye alikuwa amelala kwenye kiti chake alichokuwa amefungwa, yalikuwa yamepita masaa sita akiwa ndani ya chumba hicho tangu mara ya mwisho alipo fanikiw akuongea na IGP.
Alikurupushwa na vishindo vikali vya miguu ya viatu hususani viatu vya kike ambavyo vilikuwa vinatoa kelele zilizo yatekenya masikio yake na kumfanya kushtuka. Mlango wa chumba ambacho alihifadhiwa ulifunguliwa kwa fujo huku ndani humo wakiingia watu wenye silaha nzito, usoni bado alikuwa na wenge lakini aligundua kwamba alikuwa amezungukwa na wanajeshi na sio polisi tena ambao walikuwa ndani ya magwanda yao huku mbele yao akiwa amesimama mwanamama aliyekuwa ndani ya koti la suti nyeusi iliyo ambatana na sketi iliyokuwa imevuka magotini na viatu vya mchuchumio chini ambavyo bila shaka ndivyo vilikuwa vinatoa mlio wa sauti. Pembani yake alikuwepo IGP na upande wake wa kushoto mkuu wa kituo hicho Akello Odong alikuwa ametulia kama mtu ambaye amenyeshewa na mvua kwenye baridi kali.
“Ni saa ngapi saivi?” Yohan aliuliza akiwa anamtazama mwanamama huyo kwa tabasamu.
“Unajua una muda mchache wa kuishi?”
“Hapana mama yangu, ila wananchi wa Uganda ndio wana muda mchache wa kuishi. Nina uhakika mmeniletea nilichokuwa nakihitaji”
“Ni saa tatu na nusu saivi usiku unalijua hilo?” mwanamama huyo aliongea kwa sauti kali ya mamlaka lakini iliyo onyesha uoga ndani yake.
“Hiyo inamaanisha kwamba Tayari ndani ya uwanja wa ndege wa Tanzania Leila Patrick ametekwa, bado mna saa moja na nusu la kuwaokoa wananchi wenu”
“Why are you doing this?”
“Swali zuri lakini sio muda wake wa kulijibu ila kuna siku utakuja kunielewa kwamba ni kwanini nafanya haya na huenda utatamani ningefanya mabaya zaidi ya haya”
“Unajua unazungumzia ni maisha ya watu haya ambayo unayataja kirahisi namna hiyo?”
“Naelewa mama ndiyo maana tupo hapa mimi na wewe ili uweze kuziokoa nafsi za wananchi wako”
“Nipo hapa kwa niaba ya raisi, niambie bomu liko wapi ili nikupe immunity ya kuweza kukulinda”
“Mimi sio mjinga kiasi hicho, nipe hapa niisome nijiridhishe kisha niisaini na wewe usaini na ipigwe picha kabisa muiuplod mtandaoni kisha ndipo niwaambie bomu lipo sehemu gani” mama huyo alimwangalia Yohani kwa hasira ila hakuwa na namna, alitoa amri afunguliwe ili waweze kulimaliza zoezi hilo. Yohani alisimama na kujinyoosha kwa uchovu kisha akahitaji watu hao wamletee suti yake aivae, zoezi ambalo lilifanyika haraka ndipo wakakaa chini na kuweza kusaini mkataba wa kumpa immunity kwa ajili ya ulinzi atakapo maliza hilo zoezi asiguswe na mtu yeyote yule.
Zoezi lilipo kamilika, alihitajika kutoa maelezo juu ya bomu hilo lilipo lakini aligoma na kuhitaji raisi wa Tanzania apigiwe simu kwanza. Hakukuwa na naman zaidi ya mama huyo kutoa amri Ikulu ya Uganda kupiga simu Tanzania ambapo raisi wa Tanzania aliwekwa hewani moja kwa moja kisha akaelezwa kila kinacho endelea kuanzia lile tukio lililokuwa limetokea uwanja wa ndege mpaka mtu huyo kuhitaji kuonana naye au kamishna wa jeshi la polisi la Tanzania. Taarifa ilikuwa ni ya ghafla na ya kushangaza kwa sababu Tanzania mamlaka za ulinzi na usalama zilikuwa zimeingia kwenye kazi ya kuwasaka wahusika ila wakati huo wakapata taarifa kwamba Uganda kuna mtu ambaye alikuwa na taarifa zote juu ya hayo ambayo yalikuwa yanaendelea

UKURASA WA KUMI unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA KUMI NA MOJA

Raisi alikubali kumtuma kamishna wa jeshi la polisi wa Tanzania kwenda Uganda usiku huo huo kuonana na mtu huyo kama alivyotaka. Baada ya mazungumzo kukamilika ndipo Yohani alipo mgeukia mama huyo kumpa maelekezo na wakati huo lilikuwa limebakia saa moja tu linasoma kwenye ile saa ya bomu.
“Leo kwenye uwanja wa taifa kuna mechi kubwa kati ya timu ya taifa ya Uganda dhidi ya timu ya taifa ya Algeria ambao wanakutana kwenye mechi ya kirafiki. Unaona kabisa kwamba ungefanya maamuzi ya kipuuzi basi ulikuwa unaenda kuua raia wa Algeria na nina uhakika wasinge wasamehe kabisa. Ndani ya ule uwanja kuna sehemu ambayo ina jenereta ambalo huwa linafanya kazi umeme unapozima, Ndani ya kile chumba cha jenereta kuna masanduku ya vifaa vya mafundi, kwenye sanduku ambalo lina rangu nyekundu ndani yake kuna begi jeusi na ndani yake ndimo kuna hilo bomu” Aliwapa ukweli wa kile ambacho walikuwa wanahitaji kukifahamu, bomu lilitegwa sehemu mbaya ambapo ilimlazimu mama huyo kupiga simu haraka kwenye vitengo maamulu vya uteguaji mabomu vilivyokuwa karibu na uwanja wa taifa kwenda kushuguhulikia tatizo hilo bila wananchi kujua chochote ambacho kilikuwa kinaendelea kisha akamsogelea Yohani na kumtamkiwa kwa msisitizo.
“Mimi na wewe hatujamalizana, utalipa kwa hili kijana”
“Usijali mama, nina imani tutakuwa na mazungumzo marefu baada ya hapa” Yohani wakati anamaliza kuongea, kuna wanaume ambao walikuwa kwenye suti zao na vifaa vya mawasiliano masikioni, waliingia humo ndani na kumfunga pingu kisha wakatoka naye. Hakuwa na wasiwasi kwa sababu alijua kwamba hao walikuwa ni watu wa usalama wa taifa hilo na ni lazima wangemhitaji kwa uchunguzi japo masaa kumi hayakuwa yamefika bado ila maagizo yake ilikuwa ni kwamba mkuu wa kituo ndiyo ilikuwa karata yake mhimu ya kumfanya atoroke huko anako pelekwa.


SURA YA 2
SOFIA, BULGARIA

SOFIA, ni mji mkuu wa nchi ya Bulgaria, ni miongoni mwa majiji bora duniani ambayo ni kivutio kikubwa cha watalii na wafanya biashara wakubwa kutokana na namna llivyo pambwa na kutengenezwa kiustadi kiasi kwamba limekuwa ni sehemu ya dunia ambayo inayavuta macho ya watu wengi. Ni jiji mashuhuri kwa biashara ya madini hivyo matajiri wamekuwa wakilitolea macho kwa kusaka fursa za biashara ndani ya taifa hilo.

HYATT REGENCY SOFIA
Hii ni hoteli ya kifahari ya nyota tano ambayo ipo chini ya wamiliki wa hoteli maarufu na miongozi mwa hoteli za kisasa zaidi duniani. Hii inapatikana ndani ya nchi ya Bulgaria ndani ya jiji la Sofia.
Ndani ya hoteli hii kulikuwa na ugeni mkubwa kutoka ndani ya nchi ya Tanzania, ugeni ambao ulikuwa mzito kwa sababu ulikuwa ni msafara wa serikali. Raisi wa Tanzania alikuwa amealikwa ndani ya taifa hilo kwenye mkutano wa ziara za viongozi ambao ulikuwa na mlengo wa kudumisha mahusiano ya kidiplomasia baina ya nchi ya kiafrika pamoja na taifa hilo ambalo lilikuwa tayari kutoa msaada kwa baadhi ya mataifa ya Afrika ikiwemo Tanzania ambayo ilikuwa inapewa kipaumbele zaidi ya mataifa mengine.
Lakini pia mwaliko huo ulikuwa unajumuisha kuweza kupata fursa mpya za uwekezaji na biashara kwa maslahi mapana ya taifa pamona na vijana ambao ndio haswa walikuwa walengwa wakubwa wa uwekezaji kwa ajili ya taifa la kesho. Kutokana na kubanwa na majukumu ya raisi wa Tanzania ambaye kwa wakati huo alikuwa ndani ya taifa la Uswisi kuhudhuria mwaliko wa mkutano ambao uliandaliwa na benki ya dunia kwa ajili ya kuangalia namna ya kuisaidia Afrika kwenye mikopo wezeshi ambayo ingetumika kwenye uwekezaji wa elimu, miundombinu na biashara kwa ajili ya maendeleo ya taifa, basi alikuwa amemuagiza waziri mkuu kuweza kuhudhuria mkutano huo ambao ulikuwa unafanyika Ikulu ya Bulgaria.

Kwa sababu ya umuhimu wa jambo hilo, waziri mkuu alisafiri na wawekezaji wakubwa zaidi watanzania kwa sababu wao walikuwa wana uzoefu mkubwa kwenye biashara ya uwekezaji na kuweza kuwa na jicho la tatu kwenye fursa mpya ambazo zingekuwa na msaada mkubwa kwa ajili ya taifa na hao ndio ambao walikuwa wanategemewa hasa kwenye majadiliano ya mezani juu ya mikataba ambayo ilikuwa inatarajiwa kuingiwa kati ya Bulgaria na Tanzania.
Msafara wa waziri mkuu na wafanya biashara wakubwa kutoka Tanzania ambao wao walisafirishwa kwa usiri bila hata wananchi kuweza kung’amua jambo hilo, ulikuwa umefikia ndani ya hoteli ya HYATT REGENCY SOFIA ambapo palikuwa na ulinzi mkali kwa sababu msafara huo ulitakiwa kuwa salama muda wote mpaka utakapo rejea tena Tanzania. Ilikuwa ni ziara ya siku tatu hivyo hawakuwa na muda mrefu wa kuweza kukaa ndani ya nchi hiyo ambayo miaka ya hivi karibuni ilijiunga na jumuiya ya umoja wa nchi za Ulaya.
Saa nne usiku ndio wakati ambao walikuwa wamepanga kukutana na raisi wa taifa hilo aliye itwa HIRISTO RADOSLAV ndani ya Ikulu ambayo inapatikana ndani ya Boyona ambayo ndiyo sehemu ghali zaidi kwa kuishi ndani ya Bulgaria. Siku hiyo ilikuwa ni hafla ya kuupokea ugeni huo na kuweza kufahamiana kwa machache ili kesho yake ndipo mazungumzo rasmi yalipaswa kuweza kufanyika.
Waziri mkuu wa Tanzania Antipati Kisubi alitoa taarifa mapema kwamba wakati wa kujiandaa ulikuwa umefika hivyo ndani ya saa moja ambalo lilikuwa linafuatia wote walitakiwa kuwa tayari kwa ajili ya safari ya kutoka hapo hotelini kuelekea Ikulu ambapo ingewachukua dakika ishirini na tatu tu pekee kuweza kuufikia umbali wa kilomita tisa nukta nne za mraba mpaka ilipo Ikulu hiyo ya Bulgaria.
Taarifa hiyo ilifika ndani ya chumba kimoja ambacho alikuwa ameketi kwenye meza ya kujipodolea mfanya biashara mkubwa kutoka ndani ya Tanzania ambaye alikuwa ameongozana na msafara wa waziri mkuu. Alikuwa ni mwanamama CERSIE MHINA ambaye alikuwa mfanya biashara mkubwa wa biashara ya gesi na mitandao ya simu ndani ya Tanzania na bara zima la Afrika akijihusisha zaidi na uchimbaji wa gesi asilia. Alikuwa ni mwanamke mrembo isivyokuwa kawaida na mwanamke mwenye mafanikio makubwa ndani ya Tanzania, akiwa amepokea taarifa yake ya kujiandaa, simu yake kubwa ya kisasa ambayo ilikuwa kwenye kitanda chake ilikuwa inaita. Alisimama kwa madoido na kuisogelea pale kitandani huku akiachia taulo ambalo lilikuwa kwenye mwili wake na kubaki akiwa uchi bila nguo hata moja.
Aliipokea simu yake akiwa anarudi kwenye kile kioo kikubwa ambacho kilikuwa mbele yake akiwa anajitazama mwili wake kwa jinsi alivyokuwa mrembo japo umri ulimtupa mkono.
“Mpango wa kwanza umekamilika bosi, Leyla yupo kwenye mkono wetu na huko Uganda mipango inaenda kama tulivyo hitaji” sauti ya upande wa pili ilisikika ikiongea kwa sauti nzito na kumfanya atabasamu.
“Naenda kukutana na raisi wa Bulgaria kwa sasa, kazi nzuri hakikisha hakuna mtu yeyote anaingia kati kati ya hili”
“Copy that boss” simu ilikatwa na kurushwa kitandani. alAligeuka na kuupima mwili wake ulivyokuwa mzuri, akacheka kwa sauti kubwa na kujifurahia kwa jinsi alivyokuwa mrembo, baada ya hapo akajiandaa na kutoka ili safari iweze kufanyika maana ni yeye pekee ndiye ambaye alikuwa hajatoka.
Mkutano wa kwanza ulienda vizuri na walipokelewa kwa ukarimu mkubwa lakini baada ya jambo hilo kukamilika, mwanamama huyo alitafuta nafasi ya kuweza kuongea na raisi wakiwa wawili tu pekee. Haikuwa rahisi kuweza kulifanikisha hilo lakini kwa sababu alikuwa ni mfanya biashara mkubwa na lengo lake aliliweka wazi kwamba ni la kibiashara ambalo litakuwa na faida pande zote mbili, alipewa nafasi ya kuweza kuongea na raisi Hristo wakiwa wawili tu kwenye chumba kidogo cha mkutano.
“Sio busara kukutana wenyewe kwenye chumba kama hiki lakini nimeheshimu ukubwa wako ndiyo maana nimekupa nafasi ya kukusiliza japo waziri mkuu akijua hili huenda akajisikia vibaya”

UKURASA WA KUMI NA MOJA unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 12

“Naelewa hilo mheshimiwa na nashukuru kwa kunipa hii nafasi”
“What is it?”
“Mimi ni miongoni mwa watu ambao wamekuja ndani ya taifa hili kama washauri wakuu wa masuala la biashara, mimi ndiye naweza kutoa kauli ya mwisho kwamba hii biashara inatufaa au haitufai na waziri mkuu pamoja na raisi wakaikubali au wasiikubali hivyo kiufupi ni kwamba naaminika ndani ya nchi yangu. Kupitia hili nataka mimi na wewe tufanye biashara ambayo haitalihusisha taifa japo itafanyika kwa mgongo wa kitaifa”
“Una maana ipi?”
“Nchi yako ni miongoni mwa mataifa maskini zaidi ndani ya bara la Ulaya, jambo ambalo nina uhakika hata wewe haulipendi ila linatokea kwa sababu hauna namna ya kuweza kufanya hivyo nataka nilitoe taifa lako kwenye umaskini lakini mimi pia nahitaji kunufaika kwenye hili. Upo tayari?”
“Endelea nakusikiliza”
“Kwenye tafiti zangu ambazo nimezifanya ni kwamba taifa hili gharama za uendeshaji wa kibiashara sio ghali hivyo nimevutiwa kuja kuwekeza hapa kwa siri lakini pia kwenye baadhi ya faida ambazo utazipata kutoka kwenye mikataba ambayo unaingia na nchi ya Tanzania basi namimi nitakuwa na gawio lako vivyo hivyo nahitaji nitakapo anza kufanya biashara hapa nisilipie kodi”
“Mimi nataka kuisaidia Tanzania kwenye baadhi ya mambo ikiwemo silaha sasa kivipi tena unayaingizia haya mambo wakati huu?”
“Najua kwamba hautaki kuisaidia Tanzania kwa sababu una uwezo, sio kweli. Hata wewe taifa lako linahitaji msaada mkubwa ila unataka kuhakikisha unakuwa na uhusiano mzuri zaidi na Tanzania kwa kuzitolea macho rasilimali zilizopo nani ya taifa letu kitu ambacho una mahesabu ya mbali kwa baadae kwamba utazipata kwa mgongo wa nchi hizi mbili kuwa na mahusiano mazuri yakiwemo ya kibiashara. Sasa mimi nimekuja kukurahisishia hilo ili tusizunguke, mikataba na nchi yako nitatoa ushauri kwamba ni salama na inafaa kwa nchi yetu na utafanya kama nilivyo kwambia” mwanamama huyo alimeza funda la mate kisha akaendelea;
“Najua kwamba hapa dola haitumiki japo kwenye soko la dunia dola ndiyo kila kitu. Naelewa kwamba pesa yako ya Leu (BGN) ni miongoni mwa pesa imara zaidi duniani hivyo badala ya dola ambazo nimezoea kufanyia biashara kwa sasa nataka niwekeze kwenye pesa yako ya hapa kwa sababu haishuki thamani kirahisi. Huenda unajiuliza kwamba biashara ninayo ifanya ya gesi na mitandao hapa mbona haipo? Mimi nafanya biashara ya madini na baadhi ya zingine ambazo nazifanyia kwenye soko jeusi lisilo onekana kwa macho ya wengi na huo ndio mlango ambao nataka niutumie kuingilia hapa kwako” Alikuwa akijiamini na kujiachia CERSIE, hakuwa na wasiwasi, raisi Hristo aliwekewa dili zito mezani ambalo kulikataa ilikuwa ni ngumu. Alinyanyua bilauri lake la wine na kuligida kisha akalitua akiwa mwingi wa tabasamu kwenye sura yake.
“Nilivyo kuona tu nilijua huyu mwanamke kuna jambo lipo nyuma yake kwa sababu kichwa chako kinaonekana kuwa na mengi kimeyabeba. Unaonekana unayajua mengi kuhusu taifa langu, na vipi kama nikisema kwamba sitaki kukubali maongezi yako?”
“Utakosa kila kitu kuhusu Tanzania”
“Na nikisema ndiyo?”
“Tanzania ni nyumbani kwako kuanzia wakati utakao sema hivyo”
“Ni hilo tu?” aliuliza raisi akiwa anasimama na kusogea nyuma ya mwanamama huyo akiwa anachora vidole kwenye shingo yake.
“Nitakupa na zawadi ya mwili wangu muda wowote utakao nihitaji hata kama nipo wapi nitakuwa nafika ulipo”
“Then we have a deal japo sitakiwi kabisa kujulikana kwa namna yoyote ile”
“Hakuna mtu atakaye kuja kujua kuhusu hili, itakuwa ni mimi na wewe ila na mimi nahitaji ulinzi wako siku nikikuhitaji”
“Deal”
“Baada ya kutoka hapa, kuna watu watakuja kukuchukua na kukuleta nilipo tuweze kujuana kiundani zaidi usiku huu” raisi aliongea na kuhitaji kutoka lakini mwanamke huyo alimdaka mkono wake.
“Kuna jambo moja unatakiwa kulifanya”
“Lipi?”
“Wapigie simu kundi lolote la magaidi kesho wavamie msafara wa waziri mkuu lakini hakikisha hawampati”
“Whaaat?”
“Ni mpango wa serikali yangu kukuamini moja kwa moja, kwenye msafara huo hakikisha hakuna mtu yetu hata mmoja wa Tanzania anaumia ila hakikisha kuna walinzi wako wanakufa na vichwa vya habari vitaandika kwamba wanajeshi wako wamekufa kwa sababu ya kuwalinda watanzania. Baada ya hapo utafanya hotuba fupi na kujinadi kwamba upo tayari kufanya lolote lakini sio kuruhusu wageni wako wapate dhoruba yoyote ile na ndiyo maana wanajeshi wako wamejitoa sadaka kwa ajili ya kumlinda waziri mkuu kisha mkutano uendelee kama ulivyopangwa baada ya hapo niamini mimi watanzania wote watakuwa wanakusifia na utapata vingi zaidi ya vile ambavyo nimekutajia” raisi huyo alimwangalia huyo mwanamke ambaye alionekana kuwa mbele ya muda isivyo kawaida, alitabasamu na kutoka bila kuongea jambo.
Alikuwa na uhakika kwamba vyumba vya siri kama hivyo ambavyo watu wanakutaka kufanya mazungumzo ya faragha haviwezi kuwa na vifaa vyovyote vya mawasiliano wala kamera ili kulinda baadhi ya faragha za watu, baada ya raisi kutoka aliitoa simu yake na kuipiga mahali.
“Bulgarian president is working for me now” kisha akaikata simu yake urembo wake ukipambwa na cheko ambalo alilitoa, aliinyanyua bilauri ya waini na kuigida yote kisha naye akatoka ndani ya chumba hicho kujumuika na wenzake.





JANGWANI

Mwanaume mmoja alikuwa anatembea kwa hofu akiwa amejifunika ndani ya hood ili uso wake usiweze kuonekana kwa mtu yeyote ambaye angekutana naye. Ulikuwa ni usiku wa manane kiasi kwamba alikuwa anakutana na mtu mmoja mmoja kwa kubahatisha na hicho ndicho ambacho alikuwa anakitaka yeye asiweze kuonekana kwa watu wengi.
Mwanaume huyo alikuwa ametokea kwenye hoteli moja ambayo ipo maeneo hayo karibu na yalipo makao makuu ya timu ya Yanga mtaa wa Jangwani, Kariakoo. Alishuka na barabara mpaka alipo yakaribia makao makuu ya timu hiyo, alismama na kuangaza kila upande kama kuna mtu alikuwa anamfuatilia ama kumuona lakini alijiridhisha kwamba hali ilikuwa safi hivyo akaendelea na safari yake akiwa anatembea haraka haraka. Alipo fika yalipo makao makuu ya Yanga alikutana na barabara mbili, moja ambayo inanyoosha moja kwa moja na nyinyine ambayo imekunja kushoto kwake, yeye akachagua kukunja kushoto kuelekea mahali ambako kuna stationary nyingi na ofisi nyingi za wachapa vitabu.
Mwendo wake ulikuwa unaongea yale ambayo alikuwa ameyabeba kwenye moyo wake, mita hamsini alizo tembea tangu wakati alipokuwa anakunja ile kona zilimfanya mwili wake kuweza kusisimka na kumfanya asimame, aligeuka haraka lakini hakuona kitu, akahisi huenda ulikuwa ni wasiwasi wake ndio ulimfanya ahisi kuna mtu maeneo hayo hivyo akapuuza hali hiyo na kujishauri kwamba alipaswa kutozidisha kiwango cha wasiwasi kwa sababu kitamfanya apoteze kabisa umakini na kujikuta akijiweka kwenye hatari kubwa zaidi.

UKURASA WA 12 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 13

Kupuuzia hisia zake likawa kosa la kwanza kwa sababu wakati anasimama kuna mtu alikatiza barabara kwa kasi na kupotelea nyuma ya duka moja ambalo lilikuwa kando. Alitembea tena kwa hatua kama kumi na tano moyo ukawa unaenda mbio, hapo akawa na uhakika kwamba mara ya kwanza tu pale aliposhtuka alipaswa kukimbia, kusubiri mpaka kuwa kwenye hali ya moyo kushtuka alikuwa amechelewa kufanya maamuzi yake. Aliona kivuli kwa msaada wa taa ambayo ilikuwa pembezoni mwa kibanda kimoja, alijivuta mpaka nyuma ya nguzo ya umeme na kujibanza.
Buti zito lilitua kwenye ile nguzo ya umeme na kuifanya nguzo hiyo kutikisika kwa nguvu ungehisi itanyofoka pale ila shukrani ziende kwa mafundi wa Tanesco kwa kuiweka vyema zaidi. Aliruka sarakasi kuelekea mbele wakati huo alipokuwa amejibanza kilizungushwa kisu ambacho kilikuwa kimepinda kiasi na kubandua nguzo hiyo kavu. Alitua mbele yake na kugeuka ili kumuona mtu ambaye alikuwa amekuja kukutana naye muda huo, mwanaume huyo alikuwa amejifunika kwa kitambaa cheusi usoni mwilini mwake akiwa amevaa vesti nyeusi na suruali ya jeans pamoja na buti gumu leusi mguuni mwake.
Mwili ulikuwa umevimbiana mithini ya mtu ambaye anashinda gym lakini utofauti wake ni kwamba mwili wake ulikuwa umejigawa mipande mipande ikiwa ni ishara ya kwamba huyo hakuwa mtu wa gym tu bali alikuwa ni mtu hatari kwenye upande wa mazoezi na aina ya mapigo ambayo alikuwa anayatumia ni wazi hakuwa na mpango wa kumkamata mwanaume huyo mbele yake bali alihitaji kumuua. Hakuwa na namna zaidi ya kujitetea mbele ya mtu ambaye yeye hakuwa akimjua kabisa, akaupanga mkono wake vizuri kwa sababu hata yeye mwenyewe hakuwa haba kwenye huo ulimwengu.
“Nipe frash kisha uende zako” sauti yenye nguvu ilisikika kwa mwanaume huyo lakini mwenzake alimpuuza na kuamua kumfuata ili kuyanusuru maisha yake. Alisogea akirusha ngumi moja ambayo ilimkosa mvamiaji, kabla hajajipata vizuri alizunguka teke la chini kisha akajigeuza kwa double kick ambayo iliishia kukita kwenye ile nguzo ya umeme na mvamiaji alikuwa ameruka pembeni kwa kasi ya ajabu kisu kikiwa kinazunguka kwenye mkono wake.
Mavamiwaji hakuchoka kwa sababu alihitaji kwenda na muda akihofia kwamba huenda walikuwa wengi hivyo alipaswa kuimaliza kazi yake haraka. Alivua begi lake ambalo alibebea nguo kadha za kubadilisha na kumrushia mvamiaji ili amchanganye wakati huo alikuwa anakuja kwa nguvu mikono yake ikiwa imavutika kwa namna ilivyokuwa imekazwa, ile begi ilidakwa na kurudishwa kwa kasi kiasi kwamba ilimchanganya yeye mwenyewe hivyo akapoteza mwelekeo, alizolewa na mtama wa ngumi na kumfanya abaki anaelea hewani ambapo alipigwa ngumi ya taya iliyo mpeleka chini na kuhisi taya yake imevunjika.
Alisimama akiwa anajaribu kuachama kwenye mdomo wake, alipigwa na ngumi kali utadhani ni chuma kilipita hapo. Alijipapasa kwenye kiuno chake ila aliishia kujisonya mwenyewe baada ya kukumbuka kwamba bastola yake hakuwa nayo kwa sababu aliipoteza alipo vamiwa mara ya kwanza hivyo msaada wake wa pekee ilikuwa ni mikono. Alivizia kwa kumzunguka mwanaume huyo ambaye alimuacha aende kisha akarudi nyuma hatua chake, yeye wakati anafika mwenzake alikuwa amehesabu hatua kadhaa nyuma hivyo alimkosa na badala yake mvamiaji aliruka sarakasi ya mbele miguu yake ikatua kichwani kwa mvamiwaji akabaki anayumba yumba kichwa kikiwa kizito.
Akiwa hana mwelekeo, alipokea kisu cha shingo ambacho kilizama zaidi upande wa bega lake na kumfanya kuguna kwa maumivu makali. Kisu kilichomolewa huku akisindikizwa na ngumi kali ya kifua iliyo mpeleka mpaka kwenye ile nguzo na kujibamiza hapo. Mwanaume yule hakuwa na huruma naye, alimsogelea pale na kushusha mguu wake ambao mvamiwaji aliinama kidogo ukamkosa na kukita kwenye nguzo ambayo ilibonyea kidogo lakini haikusaidia kitu kwa sababu alikitwa na visu vingi vya tumboni.
Alibakia hana cha kufanya zaidi ya kuhema kwa nguvu huku ile nguzo ndio ukiwa msaada wake wa pekee akiendelea kuvuja damu. Mwanaume yule aliinama pale alipokuwa ameketi yeye na kuanza kumpekua kwenye mifuko yake ambapo aliikuta frash ambayo alikuwa anaitafuta. Aliichomoa haraka na kuikagua mpaka alipo jiridhisha ndipo akaifunua ile hood yake usoni kitu ambacho kilimshangaza mvamiwaji kwa sababu alikuwa akimjua mtu huyo.
“Jacob?”Mvamiwaji alionyesha kushangazwa na mtu ambaye alikuwa hapo wakati huo, alilitambua hilo akiwa hana cha kufanya kwa sababu alikuwa kwenye hali mbaya.
“Unajua mengi Issa ndiyo maana imebidi iwe hivi”
“Na wewe ni mmoja wao rafiki yangu?”
“Maisha yanawashangaza wengi Issa, mimi huwa naangalia namna ya kuweza kuishi tu hayo mengine siyajali”
“Umefikia hatua mbaya, nilikuwa nakuchukulia kama ndugu yangu lakini leo nakufa kwenye mkono wako. Jacob acha hicho unacho kifanya mara moja kwa sababu kuwalinda hao watu sio salama kwako hata wewe ipo siku wakichoka kukutumia watakuua kama mimi”
“Too late kusema hivyo rafiki yangu, pumzika mimi nitaendelea kuangalia namna nzuri ya kunifanya niishi” Issa alitikisa kichwa kwa masikitiko kwa sababu alikuwa anauawa na rafiki yake ambaye yeye ndiye alimpigia simu kumueleza ni wapi alipo ili aje amsaidie. Aliyafumba macho yake, hata hivyo bado alikuwa kwenye hatua za mwisho za kufa ila alijua mtu huyo hawezi kuacha ushahidi zaidi ya kuhakikisha anamuua yeye mwenyewe kwa mkono wake.
Jacob alikirusha kisu chake juu, ilikuwa kikitua kwenye mkono wake basi anatembea na shingo ya huyo ambaye alijulikana kama rafiki yake Issa. Kisu hicho ambacho kilikuwa kinakaribia kwenye mkono wake kabla hakijatua mkono wake ulidakwa, kisha kisu hicho kikafikia kwenye mkono wa mtu mwingine ambaye alikuwa ameongezeka hilo eneo wakati wao wamezama kwenye majibizano mafupi, kilizamishwa kwenye mkono wake na kuichana sehemu kubwa ya mkono wake. Alihitaji kuugeuza uso wake kujua ni nani ambaye aliingia na kumpatia maumivu makali wakati huo ila wakati anageuza uso wake, uso ulifunikwa na kiatu ambacho kiliipasua pua yake kulingana na uzito wa mtu ambaye alikirusha, hali hiyo ikamfanya ayumbe yumbe kuelekea nyuma kwa sababu alikuwa amechuchumaa.
Mkono wake mmoja ambao ulikuwa salama, ulitua chini kujipa balansi, alijigeuza kwa sarakasi ya hewani na kutua kwa kusimama akiwa ameushikilia ule mkono mmoja ulio tobolewa ukiwa unamuwasha kwa namna kile kisu kilivyokuwa kikali. Aliangalia kuanzia chini miguuni ambapo alimuona mwanaume ambaye alikuwa na suti safi na kiatu kinacho ng’aa ila kwa bahati mbaya zaidi hakufanikiwa kumuona mpaka usoni kwa sababu mtu huyo alikuja kwa kasi mno akiwa anatembea kwa zigzaga ambapo alimfikia Jacob aliye rudi nyuma na kurusha ngumi kadhaa lakini hakuwa na uwezo wa kuzuia kasi ya mtu huyo ambaye aliinama kidogo na kumkita na kisigino cha kiatu usoni kisha alipigwa ngumi nyingi kifuani na kuanza kuvuja damu.

Aliona kabisa huyo mtu hakuwa wa aina yake hivyo angekufa, alitishia kama anashambulia akiwa anaona kiza kiza usoni, alipo fanikiwa kuiona nguzo alitisha tena lakini mwanaume ambaye alikuwa mbele yake hakutishika, alirusha mateke mfululizo na alipo pata upenyo alikimbia na kukanya mara mbili kama anapanda juu ya nguzo, alifanikiwa kudunda hapo na kutua juu ya bati la duka moja akaishia upande wake wa pili. Mvamiaji mpya alihitaji kumfuata ila aligundua mtu ambaye alikuwa chini alikuwa akihitaji msaada wa hali na mali hivyo akarudi pale alipokuwepo kwa kasi. Mwanaume huyo sura yake ilionekana wakati anainama pale alipokuwepo Issa, hakuwa mwingine bali Edson ndiye ambaye alikuwa amefika ndani ya eneo hilo.
“Hey, hey tafadhali unaweza ukaniambia kwamba ni kwanini watu hawa wananitafuta sana mimi?” Edson aliongea akiwa anamshika shika mwanaume huyo ambaye macho yake yalikuwa yameanza kufumba kwa mbali huku akiwa anahema na kutoa damu mdomoni mwake.
“Kama umekipata kitabu kitakuongoza, kisome ukielewe. Na yule aliyetoka hapa anaitwa Jacob, alikuwa ni komando mwenzangu ila amenisaliti, mtafute uichukue frash ambayo amekimbia nayo kuna siri ambazo unapaswa kuzijua mle ndani. Kwa sasa ameumia hivyo atakimbilia Ilala karibu na ilipo hospitali ya Amana, pale kuna nyumba ya siri ambayo tulikuwa tunaitumia kukamilishia kazi zetu za siri hivyo atakimbilia pale. Nyumba namba 17” Issa alitamka kwa shida wakati huo akawa anakata kauli, Edson alijaribu kumuita lakini hakuna kitu ambacho angekibadilisha kutoka kwa mwanaume huyo kwa sababu tayari alikuwa amekufa.

UKURASA WA 13 unafika mwisho.
 
Back
Top Bottom