Simulizi ya kijasusi: Nafsi zilizotelekezwa

Simulizi ya kijasusi: Nafsi zilizotelekezwa

HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 14

Issa alimsisitiza akitafute kitabu na kukisoma kisha akielewe na wakati huo alikuwa amekipata kitabu chenyewe tayari kwenye mkono wake ila hakuwa amekipitia na kuweza kujua ndani yake kilikuwa kimeandikwa nini. Alizidi kuchanganyikiwa kwa sababu alionekana kutafutwa mno, alikuwa akipata taarifa chache chache kumhusu ikiwa hakuwa anaelewa sababu ya hayo yote kutokea, kichwa chake kilikuwa kizito kufunguka juu ya kila ambacho kilikuwa kinaendelea kwenye maisha yake.

Alikumbuka kwamba kuna siku mchungaji aliwahi kumsihi kwamba ikitokea siku amekufa basi ahakikishe anamtafuta kijana huyo Issa kuna maelekezo ya mhimu angempa, alikuwa na kifaa cha mawasiliano kwenye mwili wake Issa ndiyo maana yeye binafsi hakupata taabu ya kuweza kumpata. Alimuona tangu akiwa anatoka kwenye ile hoteli ambayo alikuwa amekifikia ila hakutaka kukurupuka kwa sababu hawakuwahi kukaa pamoja huko nyuma au kufahamiana hivyo wangefahamiana kwa njia ya kuvamiana, alikuwa anamfuatilia kwa mbali Issa akiwa anapita vichochoro vingine ili mtu huyo asije akashtukia hiyo ishu ila kufanya hivyo kulimfanya apoteze lengo lake baada ya kukuta kuna mtu mwingine ambaye alikuwa amemuwahi ili kulitekeleza jambo hilo na mwisho wake akakosa kumhoji Issa maswali ambayo alitakiwa kumhoji.
Kwenye mfuko wake alikuwa anatembea na picha ya mwanamke ambaye yeye binafsi hakumjua kwamba huyo mwanamke alikuwa ni nani ila aliwahi kusisitiziwa kwamba asije akaipoteza hiyo picha kwa sababu ina mengi ambayo ilikuwa inayazungumza kuhusu maisha yake. Aliitoa hiyo picha na kuiangalia kwa umakini, akairudisha kwenye mfuko wake na kunyanyuka taratibu akaanza kuondoka hilo eneo kuelekea lilipokuwa gari yake aina ya BMWX5 nyeusi. Aliiwasha na kuondoka mitaa hiyo ya Kariakoo na kuelekea huko ilipo hospitali ya Amana.
Alipitia njia ya Fire na kuiacha ambapo aliishika njia ya Msimbazi, kulikuwa hakuna foleni wakati huo zaidi ya utulivu ambao ulishamiri. Alikunja barabara ya Karume na ndani ya muda mfupi akawa amepita mpaka lilipo soko la Ilala, alipunguza mwendo na kuanza kutembea taratibu mpaka alipo ikaribia barabara ya kukunja ilipo hospitali ya Amana akasimamisha gari yake na kuizima. Alitoka na kuanza kutembea kwa miguu mpaka alipo ipita hospitali hiyo akiwa anakagua namba za nyumba taratibu. Aliangalia saa yake ilikuwa inasoma saa tisa usiku.
Alikunja mkono wake wa kushoto, kwa mbali taa ilikuw ainamulika vizuri aliona namba ya nyumba ikiwa inang’aa vyema kupitia ule mwanga uliokuwa unamulika. Alisogea mpaka eneo lile, pembezoni mwa ukuta wa geti aliona damu ambayo baada ya kuigusa aligundua kwamba ilikuwa mbichi bado hivyo akawa na uhakika kwamba mtu wake alikuwa ameingia pale kama ambavyo alielekezwa na kijana Issa. Aligusa geti la mlango huo akagundua kwamba lipo wazi hivyo hakupata shida kuingia na kujua kwamba aliye ingia hapo alionekana kuwa na haraka ndiyo maana hakukumbuka hata kuweza kulifunga vizuri.

Ndani ya geti hilo kulikuwa na uwanja mdogo na nyumba moja tu pekee ambayo ndiyo alikuwa akiitazama, alisogea mpaka ulipo mlango wa kuingilia ndani nao haukufungwa, hapo akawa na imani zaidi kwamba mtu wake aliingia muda mfupi uliopita na huenda ilikuwa ni hofu ya kupoteza damu nyingi ndiyo maana alikuwa anafanya vitu kwa pupa mpaka akasahau kwamba alikuwa anaikaribisha zaidi hatari ndani mwake mwenyewe.
Aliichomoa bastola yake ambayo alikuwa akiitumia mara chache kwenye harakati zake kwa sababu bastola haikuwa njia sahihi kukipata kile ambacho alikitaka kwa kuyatoa maisha ya watu kwa uharaka mkubwa. Aliugusa mlango huo kidogo kuongeza nafasi ya yeye kupita na kutokezea ndani ghafla akiwa tayari kukabiliana na kila hali ambayo angekutana nayo ndani ila sebule haikuwa na kitu zaidi ya masofa, tv kubwa iliyozimwa na friji kubwa likiwa linamtazama.

Alitulia baada ya kusikia kelele za maji yakitiririka bafuni akajua moja kwa moja mtu wake alikuwa bafuni. Aliipakia bastola yake kiunoni kwa sababu hata huyo wa bafuni bila shaka hakuwa na silaha zaidi ya kuingia huko kujisafisha na kujitibia jeraha lake. Edison alikichomoa kisu chake ambacho huenda ndicho alikuwa akikiamini zaidi na kutembea bila hofu kuelekea ndani ya bafu hilo, alipo likaribia alijua kabisa kwamba aliyekuwa ndani hakuwa amejiandaa kwa jambo lolote baya hivyo aliukanyaga huo mlango kwa nguvu na kuingia nao ndani.
Ilisikika sauti ya maumivu ndani bila shaka Jacob alikumbana na hiyo dhahama ya ghafla ambayo hata yeye hakutegemea kukutana nayo wakati huo. Mlango ulivunjika na vipande vya mbao vikampata tumboni, alitoa sauti ya kilio, alikuwa hajapata hata muda wa kujipanga vizuri kwa sababu alikuwa anasafisha na kuweza dawa kwenye mkono ambao ulichanwa muda mfupi uliokuwa umepita ndipo akavamiwa, alishtuka wakati kisu kinampatia maumivu kwenye ubavu wake wa kushoto.
Alijivuta nyuma kisu kicho kikachomoka, mwilini mwake alikuwa amevaa taulo tu pekee hivyo alilivua na kulirusha alipokuwa Edson, lilidakwa na kuvutwa akateleza kwenye maji ya chini akajikuta anaenda mzima mzima, alirudishwa na ngumi ya uso na kudondokea kwenye sinki la maji ya kunawia ambalo lilishikana na kioo. Sinki hilo lilipasuka na kioo kikavunjika, hakukata tamaa Jacob, aligeuka na teke za nyuma ambalo alilizungusha kwa nguvu ila hakuwa na bahati. Mguu wake wakati unazunguka ulikita kwenye kisu ambacho kilizama kwenye kisigino, kisu kilizamishwa zaidi na kutolewa, kisigino kikawa hakifai tena akabaki anatoa sauti ya uchungu na kutia huruma huku akiwa anachechemea.
Edson alikuwa amevaa suti ambayo ilimpendeza ila nafsi yake ilikuwa ni tofauti na kupendeza kwake kwa sababu huruma haikuwa sehemu ya maisha yake.
“Frash iko wapi na kwanini umemuua Issa?”
“Hahahah unahisi unaweza ukasaidia kwa lolote? Issa alitakiwa kufa kama wewe ambavyo unatakiwa kufa mpuuzi wewe”
“Unanifahamu mimi?”
“Hakuna mtu ambaye hakufahamu wewe! Umetafutwa kwa miaka mingi sijui ulijificha wapi ila kwa sasa umeshajulikana kwamba bado upo hapa nchini kwahiyo ni suala la muda tu kabla hujapatikana na kuuawa”
“Mimi ni nani?”
“Inasikitisha mwanaume ambaye una kesi ya kuhusika na mauaji unajifanya haujui wewe ni nani, hahah au ndiyo mbinu ambayo umetumia kujificha kwa wakati wote huu? Lazima ufe kama alivyokuwa mke wako” alikuwa makini kusikiliza maelezo yale ila neno mke ndilo lilimshtua, aliitoa ile picha mfukoni na kumuonyesha Jacob haraka haraka
“Unamaanisha huyu ni mke wangu?”
“Acha kuniigizia, unatembea na picha ya mkeo halafu unaniambia humjui? Mtoto wako si angekuwa mkubwa sasa kama angepewa nafasi ya kujifungua” Jacob alizidi kumshangaza Edison ambaye kila neno alilokuwa anaambiwa lilionekana kuleta kitu kipya kwenye moyo wake mpaka akabaki anajishangaa.
“Bosi wako ni nani?”
“Hilo huwezi kuja kulijua hilo labda siku ambayo utaingia kaburini tena kwa mara nyingine kwa sababu watu walijua umekufa wewe hivyo kwenye dunia hautambuliki kama upo hai tena” kauli hiyo ilimfanya amkwide Jacob kwa sababu alikuwa anahitaji maelekezo ili atoke gizani ambako alikuwepo lakini muda haukuwa rafiki kwake kwa sababu Jacob alianza kutoa damu nyeusi mdomoni akiwa anatapa tapa. Alimfungua mdomo wake akagundua naye alikuwa na kidonge cha kuyatoa maisha yake awapo kwenye hatari ya kutoa siri kama ambavyo ilikuwa kwa yule mwanaume ambaye alimuua Lego wakati anatafuta kile kitabu nyumbani kwa mchungaji japo aina za hivyo vidonge ilionekana kuwa tofauti kuwa kuwa wa kwanza alitoa povu ila huyu wa sasa alitoa sumu nyeusi mdomoni.
Edson alichoka, alisogea kwenye kile kioo ambacho kilikuwa kimepasuka pasuka na kuanza kujiangalia huku naye kwenye vioo hivyo akionekana kama mtu ambaye mwili wake umepasuka pasuka na hivyo ndivyo alivyokuwa anajiona ndani yake. Alijihisi kama mtu ambaye alikuwa ndani ya jangwa asubuhi anapo amka asijue aelekee wapi kwa ajili ya kuupambania uhai wake. Aliangalia kila sehemu ya bafu hilo kuona kama angepata kitu chochote kile lakini hakuna cha maana ambacho alikiona zaidi ya pakiti tano za kondomu ambapo tatu zilikuwa zimetumika tayari.

UKURASA WA 14 umefika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 15

Alitoka mpaka sebuleni ambapo aliangaza kila sehemu ila hakuona cha maana chochote. Alipo geukia upande wake wa kushoto alifanikiwa kuona sehemu iliyokuwa na mlango na bila shaka alijua huo ni mlango wa kuelekea vyumbani. Baada ya kuufungua mlango huo aligundua kwamba ndani kulikuwa na vyumba viwili vya kulala. Aliingia kwenye chumba cha kwanza ila hakupata kitu cha maana chochote mpaka alipo ingia ndani ya chumba cha pili ambacho aligundua kwamba ndicho kilikuwa kinatumika na Jacob kwa ajili ya kulala kwa sababu aliyakuta yale mavazi ambayo yalikuwa na damu yakiwa juu ya kiti kimoja.

Aliangalia kwenye mifuko ya ile suruali huku shati akiitupa chini na kufanikiwa kuipata ile frash ambayo Jacob aliichukua kwa Issa. Alikagua kila sehemu, hakupata kitu chochote kile kwa namna watu hao walivyokuwa makini kwenye kazi zao, zaidi zaidi alikutana na pakiti zingine za kondomu kwenye plastiki ya kuhifadhia taka pamoja na vipande vingi vya sigara bila shaka mhusika alikuwa anapenda ngono na uvutaji wa sigara. Edison akawa hana namna ya kufanya zaidi ya kwenda kuangalia kilichopo ndani ya hiyo frash pamoja na kusoma kitabu ambacho alisisitiziwa kuweza kukipitia huku akiwa kwenye mshangao mkubwa hususani baada ya kuongezewa jambo lingine la kuwa na mke ambaye alidaiwa kuwa marehemu mpaka wakati huo. Alitoka na kusogea mpaka ilipokuwepo gari yake, alipanda kinyongea na kuondoka hilo eneo mithili ya mtu ambaye alikuwa amelazimishwa kufanya jambo hilo.

Hayo mambo yote yalikuwa yametokea ndani ya siku moja pekee. Kuvamiwa kwa Edison akiwa kigogo mwisho, mchungaji kuuawa ndani ya kanisa Mabibo, Yohani Mawenge kujikamatisha ndani ya kituo kikubwa cha polisi cha Entebbe, Leyla kutekwa ndani ya uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere, Issa kuuawa na Jacob lakini hata Jacob mwenyewe kuweza kuuawa na Edison akiwa anautafuta ukweli kuhusu maisha yake na kuhitaji kujijua zaidi yeye ni nani kwa sababu alionekana kuwa mgeni wa nafsi yake mwenyewe.











Leyla M. Patrick.
Mrembo wa haja, aliyeumbwa na dunia ikaukubali uumbwaji wake, mwanamke ambaye aliamua kulichanua tabasamu bora mbele ya uso wa dunia huku sura yake nzuri na laini ikizidi kuifanya dunia ijivunie kuweza kumpata kama kiumbe hai. Alikurupuka kutoka usingizini ambapo hakujua alitumia muda gani kuweza kuwa kwenye usingizi huo. Wakati anashtuka alikuwa kitandani, kitanda safi ambacho kilipambwa ndicho alichokuwa amekitumia kupumzika hivyo akahitaji kuamka hapo lakini alirudi tena kujilaza baada ya kushindwa kunyanyuka kutokana na mikono yake kuwa mizito kuliko kawaida. Aligeukia upande mmoja wa mkono wake ndipo alisonya kwa hasira baada ya kugundua kwamba mikono yake yote miwili ilikuwa imefungwa pingu.

Hatua za ujio wa mtu ziliyatekenya masikio yake, akagundua kwamba humo ndani lazima kulikuwa na kamera kwa sababu isingewezekana aamke tu halafu wahusika walitambue hilo. Aliyanyanyua macho yake kivivu kuelekea kwenye pembe moja ya chumba hicho, tabasamu la uchovu lilichanua kwa mbali baada ya kuiona taa moja kubwa ya umeme. Kwa macho ya wengi ilikuwa ni taa ya kawaida lakini taa hiyo ilikuwa ni kamera, akawa mtulivu; jambo hilo wala halikumshtua, alilitarajia mapema.

Mlango wa kioo cha shaba ulifunguliwa, ukaonekana mguu ukiwa ndani ya buti ambayo ilifanania na zile za mafundi wa Tanesco wanazo zitumia hususani wanapokuwa kwenye matengenezo ya nguzo au sehemu yoyote ile yenye hatari ya umeme. Mguu huo juu yake ulifuatia na suruari moja ya samawati ambayo ilikuwa na mifuko mingi na mikanda ambayo ilikuwa inabembea mpaka pembezoni mwa viatu, akatambua aliyekuwa anaingia hapo alikuwa ni mtu kweli. Alilithibitisha hilo baada ya mtu huyo kumalizia mwili mzima ukadondokea ndani ya chumba.

Mwili mrefu ulikuwa umesimama mbele yake, mwili uliotunzwa kwa mazoezi makali na ustadi mkubwa ulitosha kumtahadharisha kutokuwa na masiara. Mwanaume huyo suruali yake iliyo ishia kiunoni ilikuwa imeunganishwa na vest nyeusi ambayo aliichomokea ndani ya suruali hiyo huku shingoni akiwa na cheni ndogo ya dhahabu. Kichwani alikuwa na rasta ambazo alizifungia kwa nyuma, hapo ndipo akakumbuka kumwangalia usoni kwake, alikuwa mweupe wa wastani na midomo yake kwa mbali ilikuwa inatakuwa na rangi nyeusi ambayo ilipishana kwa mbali na rangi yake asilia.
Haikumchukua dakika kujua kwamba rangi ya mdomo iliathiriwa na sigara ambayo aliithibitisha kwenye mkono wa mwanaume huyo ambaye baada ya kugundua kwamba mwanamke huyo anamkadiria aliiweka mdomoni mwake na kuimeza akiwa hajaizima. Ule moshi ambao aliupuliza ulipotezwa na harufu safi ya manukato ambayo ilikuwa imeenea ndani humo, wote wakiwa wanategeana kuanza kuongea.

Bwana yule ambaye sura yake haikuwa ya kirafiki, alimkadiria Leyla kuanzia chini ya miguu mpaka kwenye paji lake la uso. Alikuwa mrembo wa haja huenda ndiyo sababu iliyomfanya yeye kukaa na kumkadiria kwa muda mrefu namna ile, na ile nguo ambayo ilikuwa ndani ya mwili wake basi ilileta shida kwenye nafsi ya bwana yule ila kwake ilikuwa ni tofauti. Hakuwa pale kwa sababu ya mapenzi, wanawake hawakuwa kitu kwenye kichwa chake kwani kama angewahitaji walikuwepo warembo zaidi ya huyo kwenye makasino mbali mbali ndani ya jiji na uwezo alikuwa nao wa kuwapata muda wowote. Alijongea kukisogelea kitanda na kumwangalia kwa utulivu Leyla, bastola ambayo ilikuwa pembezoni mwa kiuno ikaonekana vizuri, Leyla akajua anatakiwa kuwa na ustaarabu kwenye maongezi yake hata hivyo mrembo huyo hakuwa na papara, bastola halikuwa jambo geni kwake.

“Leyla Patrick, nilipo iona picha yako kwa mara ya kwanza sikutarajia kukutana na binti kama wewe, nilijua huenda ni mtu mkubwa, mtu mwenye cheo ambaye kuna jambo la maana lipo nyuma yake kiasi cha kumpa kiburi lakini ni mwanamke mrembo wa aina yako. Kwanini umeamua kujiingiza kwenye jambo zito kama hili?” sauti ya utulivu ilipenya kwenye ngoma za masikio yake na kumuongezea utulivu wa kumsiliza mwanaume aliyekuwa anashangazwa na umri wake pamoja na urembo uliompa umaridadi kwenye uso wake.
“Mmewaua vijana wangu wanne, unajua gharama ambayo mnatakiwa kuilipa?” swali lilimshangaza mwanaume huyo ambaye alikuwa mbele yake, kujiamini kwa binti huyo kukampa mashaka, moyo ukapigwa na ganzi akihisi labda alikuwa anaota bado, lakini wapi alikuwa mbele yake tena wakiwa wawili tu ndani ya hicho chumba. Leyla sura yake ilikuwa na utulivu na sio wasiwasi wa kuhitaji msamaha wa kuachiwa hapo.
“Naweza kukubaka, naweza kukufanyia jambo baya na dunia haitajua upo wapi wala kipi kilikukuta, kwanini unajitwika ugwiji na kujifanya mjuaji?”
“Saimoni, mimi na wewe wote tunajua kwamba ungehitaji kuniua basi nisingekuwa hai mpaka wakati huu. Mnanihitaji nikiwa mzima zaidi ya nikiwa nimekufa kwa sababu bosi wako atakuua kama mimi nikifa. Nahitaji vijana wako wanne wauawe mbele yangu ndipo mimi na wewe tunaweza kuzungumza” Leyla aliongea kwa kujiamini akiwa hana hata tone la wasiwasi.
“Umelijuaje jina langu?”
“Unahisi nipo hapa kwa bahati mbaya?”
“Wewe ni nani?”
“Huna haja ya kunijua kwa sasa, nifungulie hapa, ua hao watu wanne kama malipo kwa mauaji ya walinzi wangu kisha baada ya hapo nahitaji kuongea na bosi wako sio wewe” Leyla, alikuwa anajiamini kupitiliza hali ambayo ilimfanya Saimon kugwaya. Haikuwa bure mwanamke kuwa na ujasiri wa kufanya hayo ambayo alikuwa anayafanya. Saimon aliitoa bastola yake na kuilengesha kwa Leyla jambo lililo mfanya Leyla kuangua kicheko kizito.
“Weka bastola yako chini Saimon, hili kosa hauwezi kulifanya. Nina mabilioni ya pesa ya bosi wako kwenye mkono wangu. Ukifanya hili kosa itakula kwako hivyo fanya nilicho kuagiza, nahitaji kuongea na huyo bosi wako” Saimon alitulia akiwa hana usemi, alitafakari maneno ya mwanamke huyo na kuirudisha bastola mahali pale ambapo ilikuwepo mwanzo.

UKURASA WA 15 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 16

“Ulijua kama tutakuteka?”
“Kutekwa ulikuwa mpango wangu, ningeamua wewe hapo usingekuwa na uwezo wa kunipata abadani! Fanya haraka niongee na bosi wako kwa sababu nina ratiba zangu inatakiwa nizianze leo baada ya kutoka hapa” Leyla aliibadilisha sura yake na jambo hilo aliongeza kulifanyia msisitizo zaidi, sura yake haikuwa ya kirafiki tena bali shari! Siamon akawa mtulivu na kutoka nje ambapo baada ya dakika alirudi akiwa na wanaume wawili walioshiba.
Walimfungulia Leyla na kumtoa nje ambapo walielekea kwenye chumba kikubwa ambacho kilikuwa na skrini za kutosha. Akiwa hapo, waliletwa wanaume wanne ambao walikuwa wamefungwa, hao walikuwa wametolewa kafara ya kuuawa kama ambavyo alihitaji mwanamke huyo. Hapo ilionekana skrini moja ikibadili mawimbi yake, mbele yake akiwa anaonekana mwanamke ambaye sura yake ilikuwa imefunikwa kote asiache hata sehemu ndogo ya kumpa mwanya mtazamaji kumfahamu.
Wanawake hao wawili waliangaliana kwa muda kila mtu akiwa anamkadiria mwenzake na kuongea pekeyake kwenye nafasi yake. Leyla alisogea kwenye sofa akakaa na kukunja mguu wake kwa mbwembwe mdomo akiwa ameubinua.
“Bila shaka wewe ndiye Madam Kate!” aliongea kwa kujiamini, kauli ambayo ilimshtua mwanamke ambaye alikuwa upande wa pili.
“Umefanikiwa vipi kulijua hilo jina?”
“Mpaka nakutafuta ujue nina taarifa zako nyingi, unafanya biashara chafu ndani ya soko jeusi (black market) ambako hata mimi nimewahi kuwepo huko hivyo huwa nawatafiti watu wengi hususani watu ambao ninaweza kuwa na matumizi nao”
“Hiyo ndiyo sababu ilikufanya ukaiba madini yangu?”
“Ndiyo, kwa sababu mimi na wewe nahitaji tufanye kazi pamoja kwa sasa”
“Umeambiwa kwamba ninatafuta mtu wa kufanya naye kazi?”
“Unatafuta ndiyo maana nipo hapa, kama haupo tayari basi sahau kabisa kuhusu kuyapata madini yako”
“Umefanikiwaje kufanya haya yote?” Leyla alisimama na kuichomoa ile bastola ambayo ilikuwa kwenye kiuno cha Saimoni kwa kasi na kuwatandika risasi za vichwa wale wanaume wanne ambao walikuwa wameletwa pale mbele yake.
“Ni miaka kadhaa iliyopita, nilipata kusikia kuhusu jamii yenu ya siri, jamii ambayo ilikuwa ina nguvu kubwa lakini watu wengi waliamini kwamba huenda ni nadharia tu zinatengenezwa kama ambavyo ulimwengu umezoea kuwahadaa watu ila ilikuwa ni tofauti kwangu. Jambo hilo lilikuwa tofauti kwangu, tangu siku nipate hizo taarifa, sijawahi kuzipuuzia hivyo ukawa mwanzo wangu wa kuweza kuanza kufuatilia kwa undani kuhitaji kujua kama ni kweli hiyo jamii ipo na kama kweli ipo, inajihusisha na nini na kuanzishwa kwake kuna sababu zipi?”;
“Baadae sana nikaja kugundua kwamba ni kweli kuna baadhi ya hadithi za hiyo jamii hali ambayo ilinifanya nianze kuchimba ndani zaidi hususani kujiunga na hayo masoko meusi ambako najua watu wa kariba kama hizo ndiko ambako huwa wanatokea. Huko baada ya kutumia pesa nyingi nilikuja kulipata jina lako la Madam Kate ambaye ni maarufu kwa ufanyaji wa biashara haramu ambazo zinakupa pesa nyingi. Nikataka kujua kwanini huyu ni mwanamke halafu ana jina kubwa namna hii? Ndipo nikaja kugundua kwamba wewe ndiye ulikuwa nyuma ya usimamizi wa hii jamii kwa mlango wa nyuma na kwa usiri mkubwa mno. Nikatamani kukupata wewe lakini ikashindikana hivyo nikawa na nafasi moja tu pekee ya kuweza kuonana ama kuwasiliana na wewe, kupotea na mzigo wako wa thamani kubwa na ndicho nilikifanya”
“Nilitumia nguvu kubwa kufanikisha kulipata hilo mpaka nilipofanikiwa kupata jina la kampuni ambayo ulikuwa unaitumia kwenye usafirishaji. Nikamteka mmoja ya wafanyakazi wa nafasi za juu wa kampuni hiyo ambaye baada ya kumtesa alinipa ukweli wa mambo na mizigo ambayo ilikuwa inasafirishwa karibuni. Hiyo ndiyo ikawa njia rahisi mimi kuupata mzigo wako na kwa sababu nilijua ukija kulitambua hilo ungemlazimisha akwambie ukweli, nikaamua kumuua. Je unataka kujua sababu ambayo ilinifanya mimi nifikie hatua na maamuzi magumu ya kukuibia mtu hatari kama wewe?” Leyla alitulia baada ya kuweka maelezo machache ambayo yalimfanya mwanamke ambaye alikuwa upande wa pili kusikitishwa na jambo hilo, lilikuwa kosa kubwa kukosea kuchukua tahadhari ambazo zingeweza kumleta madhara makubwa kwenye hizo biashara zake.
“Unataka nini binti? Kwa sababu unaonekana unanifahamu sana na kama nikikuacha hai itakuwa hatari kwangu”
“Ni kweli nayajua mengi kutoka kwako ila nilishindwa kitu kimoja tu, sijafanikiwa kuujua uhalisia wako kwenye maisha ya kila siku kwamba wewe ni nani na una kazi gani. Nategemea kulijua hilo mepama kwa sababu inanishangaza mwanamke kuwa na nafasi kubwa na kuendesha jamii ya siri ambayo inadaiwa kumiliki watu wa kutisha sio jambo la kawaida”
“Haujanijibu swali langu Leyla”
“Baada ya kupotea na mzigo wako, nilijua mtaanza kumtafuta mhusika kwa udi na uvumba ili aseme mzigo uko wapi kisha mmuue. Mimi nilicho kifanya ni kutengeneza utambulisho feki ambapo niliwapa taarifa kuhusu mimi binafsi, niliwatumia hadi picha yangu huku mkinilipa pesa nyingi baada ya kuwasaidia kumjua aliye husika na wizi wa madini yako na kuamini kwamba kupitia mimi mngeweza kumpata kirahisi hivyo tangu nakuja Tanzania taarifa zangu nilizianika wazi ndiyo maana mkapata taarifa. Wakati mnakuja pale uwanja wa ndege binafsi nilikuwa najua ambacho kinaenda kutokea kwa sababu mlikuwa na taarifa zangu zote na zoezi limeenda kama nilivyotaka mimi, nipo naongea na wewe sasa hivi”
“Sikutegemea binti mdogo kama wewe kuwa na akili kubwa kiasi hiki. Kwanini?”
“Nadhani unajua kwamba Patrick Magebe alikufa miaka kadhaa iliyopita?”
“Ndiyo”
“Haikukushangaza kuona mimi naitwa Leyla Patrick Magebe?”
“Ndiyo maana upo hapa kunijibu maswali hayo”
“Patrick mimi ndiye nilimua na familia yake yote”
“Binti umechanganyikiwa?”
“Ningekuwa nimechanganyikiwa basi usingekuwa na hiyo nafasi ya kuongea na mimi wakati huu. Baba yangu alikuwa mwanasheria miaka mingi iliyopita, alipata taarifa juu ya kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inamhusu Patrick Magebe lakini kwa sababu ya nguvu ya pesa aliyokuwa nayo bwana yule, kesi ikawa inapotezewa na kila mtu kujifanya haioni. Baba yangu kama mwanasheria ambaye alikuwa analipenda taifa lake akaamua kulivalia njuga swala hilo ili mtu huyo apate ile adhabu ambayo anastahili. Unajua kilicho tokea? Baba yangu aliuawa mbele ya familia ya Patrick Magebe”;
“Tulilifuatilia jambo hilo kwa umakini na ukaribu lakini hakuna majibu ambayo tuliyapata ya kueleweka. Kila tulikoenda tuliambiwa baba yetu alikuwa tapeli hivyo huenda wenzake walimuua kwenye hizo harakati zao haramu. Ilikuwa inatuuma kwa sababu baba yetu alikuwa mtu safi, alikuwa baba bora zaidi tangu siku mama alipokufa na kutukabidhi kwenye mikono yake, lakini mbali na hilo baba alikuwa mtu mzalendo mno! Ila dunia haiwataki mashujaa kifo chake ikawa sherehe kwa wengi wakawa wanatukebehi sisi”
“Tulifanya maamuzi ya kufanya uchunguzi wenyewe na baada ya muda nilipata fununu za kifo chake kuhusiana moja kwa moja na bwana Patrick Magebe. Nilizichunguza mwenyewe kwa mkono wangu na kuthibitisha kwamba yule bwana ndiye ambaye alikuwa amehusika. Mimi sikuwahi kufikiria kumuua! Lengo langu ilikuwa ni kwamba ahukumiwe kwa sheria ya jamhuri lakini tunarudi pale pale, huwezi kwenda na tajiri mahakamani ukategemea kushinda, hiyo ni vita ambayo unatakiwa kuimaliza mtaani mwenywe”
“Familia yake ilitukana na kutukebehi, wakadai huenda tumechanganyikiwa kwa sababu baba yetu alikufa kwa ujinga wake. Wote walitukana na kututishia kutufunga kwa kuanza kuwachafua kwa kitu ambacho hawakijui, wakatishia na kutuharibia kazi zetu tukaamua kutulia na kupotezea hilo jambo. Binafsi sikuwahi kulipotezea lile kwa sababu lilikuwa moyoni bado hivyo nikaanza jitihada za kutafuta kulipa kisasi kwa mpango wangu”

UKURASA WA 16 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 17

“Na huo ndio ukawa mwanzo wa mauti yao, niliua familia nzima bila kuacha hata ushahidi ndiyo maana mpaka leo dunia inajua ile familia ilikufa kwa ajali ya ndege ila uhalisia ni kwamba niliwaua wakiwa ndani ya ile ndege kisha nikasababisha ajali huku mimi nikipotea na parachuti” Leyla alitoa maelezo ya kumhusu Patrick Magebe, habari ambayo hata kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam ilimchanganya kwa sababu tajiri huyo alikuwa amekufa miaka mingi iliyopita.
“Ulifanikiwa vipi kufanya hayo?”
“Kwa sababu nilikuwa miongoni mwa wahudumu wa ile ndege”
“Sasa ilikuwaje ikakutwa miili kamili ya watu waliopanda wakati mwili wako haukuwepo?”
“Mimi nilimuua mhudumu mmoja na kutengeneza sura ya mfanano wake nikaivaa, hivyo hakuna aliyeshtuka lakini mapema kabla ya jambo lile kutokea kuna mtu ambaye nilikuwa nimemuingiza ndani ya ile ndege kwa kumuahidi kiwango kikubwa cha pesa. Yule ndiye nilimtoa sadaka kwa sababu hakuwa akijua kinacho endelea akatulia mahali ambapo nilimficha mimi kwenye chumba kikubwa cha silver na kwa ukubwa wa ile ndege binafsi hakuna mtu ambaye angekuwa na muda wa kuzungukia sehemu zote kwani hilo linafanywa na wafanyakazi wakati wanafanya usafi. Yule ndiye alikuja kukaa kwenye nafasi yangu baada ya ile ndege kulipuka”
“Who are you girl?” alikuwa mtaalamu wa kusuka mipango ambayo ilimvutia madam Kate, alitaka kumfahamu yeye ni nani haswa kama sio Leyla M. Patrick.
“Nicola Aidan Semzaba”
“Whaaaat! Yule mwanasheria mbobevu Aidan Semzaba ndiye alikuwa baba yako mzazi?” Madam kate alishangazwa pakubwa na jambo hilo hata sura yake ilionekana kubadilika kiasi kwa sababu ni wazi alikuwa akimjua sana mtu huyo aliyekuwa amezungumziwa.
“Yes, mimi ndiye mtoto wake wa pili na wa mwisho”
“What do you want?”
“Namhitaji Edjr. Edison” alilitaja jina hiyo kwa msisitizo na hasira ambayo ilidhihirika kwenye macho yake yaliyokuwa yanawaka moto. Hapakuwa pema.
“Kwanini?”
“Alimuua kaka yangu”
“Kivipi?”
“Miaka michache iliyopita, Edjr alikuwa kiongozi wa kikosi cha makomando tisa na yeye akiwa wa kumi. Kilikuwa ni kikosi maalumu ambacho serikali ilikitengeneza nje ya wale makomando wengine kwa ajili ya kutoa misaada hususani kwa wananchi ama mataifa mengine ambayo ni rafiki yanapo ingia kwenye dhahama kubwa. Kwenye kile kikosi ambacho Edjr alikuw akiongozi kulikuwa na kaka yangu Daniel Aidan Semzaba”;
“Huyo ndiye mtu pekee ambaye nilibakiwa naye kwenye maisha yangu hivyo alikuwa kila kitu kwangu baada ya baba kufa. Kikosi chao kiligawanywa mara mbili kwenda kwenye mataifa mawili tofauti, kikosi cha kwanza kilienda nchini Kongo kuweza kusaidia serikali kupambana na makundi ya uhalifu huko Goma na Kitchanga lakini kikosi cha pili cha watu watano ambacho kaka yangu alikuwepo na Edjr mwenyewe kilielekea Somalia ambako wakati ule kikundi cha AL-SHABAAB kilikuwa kimejipatia umaarufu mkubwa na kwa bahati mbaya miongoni mwa wananchi ambao waliwateka na kuwaua, walikuwepo watanzania kumi. Walikuwa wamekufa sita na wanne walitakiwa kurudishwa nyumbani ndipo kikatumwa hicho kikosi huko”;
“Baada ya siku tatu tu kupita ilirudi miili tisa ya makomando hao wakiwa kwenye majeneza kwa kusalitiwa na mwenzao Edjr ambaye aliwauza na kuwaua huku kaka yangu akifa kwa risasi ambayo iligundulika kwamba ilikuwa inatoka kwenye bunduki iliyokuwa inamilikiwa na Edjr mwenyewe hivyo bila shaka alimuua mwenyewe. Baada ya hilo kutokea mwanaume huyo yeye alipotea kabisa kwenye uso wa dunia, akawa mtu wa kujificha ficha lakini baadae akaja kuonekana ndani ya jiji hili na kisha hakuonekana tena”;
“Kipindi anaonekana ndipo niligundua kwamba wewe na jamii yako mnamtafuta na nyie kwa sababu ambazo mwanzo sikutaka kuzijua na hata sasa sijali kuhusu hizo sababu ila namhitaji huyu mtu kwa udi na uvumba tena akiwa hai kwa sababu kuna maswali ambayo nahitaji anijibu na nitamuua kwa mkono wangu mwenyewe. Sasa nakujibu swali la kwamba ni kwanini niliiba madini yako na kuhitaji kukutana na wewe; ni kwamba nataka tusaidiane mimi na wewe na watu wako kumtafuta. Najua wewe una nguvu kubwa kimamlaka hivyo chini ya kivuli chako nitakuwa salama kufanya kile ambacho ninakitaka kwa sababu hakuna atakaye nigusa. Kama ukinisaidia kwa hili tukafanya kazi pamoja, baada ya kumpata mimi nitakurudishia mzigo wako wote ambao una zaidi ya bilioni miambili na nina uhakika hauwezi kuuruhusu upotee kirahisi hivi kwa ajili ya kumlinda mtu ambaye hana uhusiano wowote na maisha yako wewe” Nicola aliongea kwa uchungu na hasira ya kitu ambacho bila shaka kilikuwa kimemkaba kwa muda mrefu kwenye nafsi yake, alimpa chaguo madam Kate kama angehitaji kuupata mzigo wake mkubwa wa dhahabu ambao ulikuwa umepotea kwenye mazingira ya ajabu. Alimwangalia binti huyo kwa jicho lenye maswali mengi, jicho lenye udadisi wa kutaka kuijua sababu ya binti huyo kujiamini namna hiyo.
“Wewe ni binti tena ambaye hata miaka thelathini na mitano haujavuka, kwa umri wako wa miaka thelathini na miwili unahisi unaweza kumkamata mtu ambaye alikuwa kiongozi wa kikosi hatari cha makomando?”
“Nahitaji nyezo za kazi kama watu wa serikali, kulindwa na mamlaka, kupewa taarifa za namna ya kuweza kumpata ila kuhusu mimi nina imani hautaki kunijua kiundani, nimeishi pale Mlimani Morogoro kwenye kambi ya makomando nikipata mafunzo, nikaenda kuishi nje kwa muda kupata mafunzo, nina imani sina ulazima wa kuwaua watu wako kikatili ndipo utambue kwamba mimi ni mtu hatari ambaye ninaweza kuiteketeza hii kambi yako ndani ya dakika kumi tu” aliongea kwa kujiamini huku akiuma meno yake.
“Na hiyo jamii ambayo umeisema unaijua vipi?”
“LS (The LUNATIC SOCIETY) sina taarifa nyingi zaidi kuhusu nyie ila najua mpo na mnafanya shughuli za hatari za kutisha na ni mfumo ambao una mpaka viongozi wakubwa wa kiserikali ndani ya Afrika mashariki yote japo nasikia pia kuna viongozi wa mataifa mengine ya mbali wameanza kuingizwa huko kama raisi wa Bulgaria HIRISTO RADOSLAV, kwahiyo naweza kuwa na manufaa makubwa pia kwako”
“Deal, you are in” ndiyo kauli ambayo ilitoka kwa madam Kate kumjibu Nicola kwamba alikuwa ameruhusiwa kujiunga nao kama alivyo hitaji lakini wakati anajibiwa hivyo, skrini ilizima na madam Kate akapotea hewani, mazungumzo yalikuwa yameisha. Mazungumzo yalimpa furaha Nicola na kumfanya atabasamu kwa sababu alikuwa amepiga hatua kubwa ya kumpata adui yake ambaye alikuwa amemsaka kwa muda mrefu bila mafanikio. Adui ambaye alimuulia kaka yake wa damu na wa pekee, adui ambaye ni Edison. Edison mwenyewe mpaka wakati huo alikuwa anadai kwamba hajijui yeye ni nani na mambo ambayo anaambiwa hata hakuwa anayakumbuka. Ni kweli? Twende sawa.

UKURASA WA 17 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 18

SURA YA 3

The LUNATIC SOCIETY (LS)
Jamii ya siri nyuma ya mlango wa jina la jamii ya wendawazimu. Ni umoja wa siri ambo ulianzishwa mnao mwaka wa 1992, jamii hii ilianzishwa mara tu baada vita biridi kukoma na umoja wa nchi za kisovieti kudondoka mwaka 1991. Kudondoka kwa umoja wa nchi za kisovieti sababu kubwa zinatajwa kuwa sababu za ndani hasa mambo ya utaifa huku wengine wakimrushia lawama raisi Gorbachev kwa maamuzi yake ya kuruhusu uchaguzi wa mfumo wa vyama vingi ambao waliamini kwamba ulianza kuyumbisha utawala wa kikomyunisti.
Ukiacha sababu hizo lakini pia matokeo mabaya ya vita baridi ambayo ilianza mwaka 1947 na kuja kukoma mnamo mwaka 1991, vita ambayo ilihusisha pande mbili, wetern block iliyokuwa ikiongozwa na mataifa makubwa kama Marekani, Uingereza na Ufaransa dhidi ya Estern block ambayo ilikuwa ikiongozwa na umoja wa kisovieti. Vita hiyo iliisha vibaya kwa upande wa block ya mashariki baada ya kusababisha kudondoka kwa umoja huo na kusababisha kutokea kwa dola kumi na tano ambapo kila dola ilitaka kujitawala yenyewe kama Estoni, Ukraine na zingine.
Mchango wa vita baridi kupelekea kudondoka kwa umoja huo kunafananishwa na kwamba ni block ya magharibi chini ya Marekeni ndiyo ambao ulisababisha yote hayo kupitia vitu kama; kuunga mkono juhudi za wakwamisha umoja wa kisovieti, kuhamasisha tamaduni ya magharibi ndani ya umoja ya kisovieti, kuweka vikwazo kwa nchi za block ya mashariki kutopata nafasi kwenye masoko makubwa ya magharibi na kwenye teknolojia. Lakini pia kwenye upande wa kusambaza na kumiliki taarifa, magharibi ndio ambao walikuwa wanamiliki usambazaji wa taarifa hivyo kuwanyima nafasi hiyo estern block ambao walikuwa wanapambania kuweza kupata nafasi hiyo lakini hawakufanikiwa kwa sababu magharibi walijaribu kutumia vyombo vyao hivyo kusambaza propaganda ambazo ziliwaweka umoja wa kisovieti kwenye nafasi mbaya na hatimaye baadae kuja kugawaanyika na kudondoka kabisa.

Baada ya vita hivyo vya baridi kufika ukomo na umoja huo kudondoka, nchi ya Urusi ilikaa chini na kuanza kufanya mahesabu yake ili kujua ni wapi walikosea na ni watu wapi ambao waliwakwamisha kwenye vita hiyo. Moja kwa moja macho yakaelekezwa kwenye shirika lao la kijasusi la KGB, wengi waliamini kwamba kufeli kwa shirika hilo ndiyo ilikuwa sababu kuu ya taifa hilo kushindwa kwenye vita baridi hivyo wakaamua kufanya uchunguzi wa kina kuyaweka bayana yaliyokuwa yanaendelea ndani ya shirika hilo.
Kwenye uchunguzi wao, licha ya madhaifu mengi ya viongozi wa shirika hilo wa nafasi za juu lakini waligundua kwamba kuna watu ambao walikuwa kama wasaliti ndani yake, baadhi ya maagent (maajenti) hawakuwa upande wao licha ya kuwa raia wa nchi hiyo! Wakajumlisha kwamba wengine walikuwa ni mamluki ambao walitumiwa na magharibi kwa ajili ya kuwadhoofisha kwa utoa siri za ndani za shirika hilo jambo ambalo lilipelekea wao kuyumba kwa namna kubwa. Ikatolewa amri watu hao waweze kusakwa kwa udi na uvumba na kuweza kuuawa.
Kwenye majina ya watu ambao walitakiwa kukamatwa ndani ya KGB likatokeza jina la mwanamke mmoja, IRINA ESPANOVICH. Huyu alikuwa ni jasusi ndani ya shirika hilo ambaye alifanya kazi kubwa lakini baadae jina lake likatokeza kwenye orodha ya wasaliti ambao walikuwa wanahitajika kupatikana haraka na kuweza kuuawa.





IRINA ESPANOVICH

Alikuwa mwanamke wa miaka ishirini na tano tu kwa wakati huo, moja kati ya mazao bora ya uwekezaji wa KGB. Huyu alipokea pesa nyingi kwa ajili ya kuuza siri za shirika lake kwa nchi ya Marekani na kilichokuja kumfunga ni baada ya kutumia moja ya akaunti zake binafsi kupokea mabilioni ya pesa kutoka kwenye akaunti ambayo haikuwa ikijulikana ni ya nani. Baada ya vita kuisha wakati unafanyika uchunguzi mkali na kwa usiri mkubwa ndani ya shirika hilo ndipo hilo jambo likaja kugundulika, pesa ambayo alikuwa ameipokea mwanamke huyo ilikuwa ni nyingi kiasi kwamba kwa kazi yake hata kama angehudumu miaka sitini bado asingeweza kupata pesa nyingi namna hiyo, hivyo akawa tageti ya kwanza ya shirika hilo.
IRINA alikuwa mama wa familia ya mtoto mmoja na mke pia, mumewe alikuwa miongoni mwa viongozi wa juu wa KGB ndiyo maana alitumika mwanamke huyo kwa sababu alifanikisha kumuibia mumewe siri za ndani na kuziuza. Mumewe hakuwa na huruma na mkewe, alihitaji auawe kwa namna yoyote ile lakini kabla hilo halijafanyika, dereva na mlinzi wa mumewe alimpigia simu na kumtaka atoweke haraka kwa sababu alimsikia bosi wake akiongea kwenye simu kwamba mkewe anatakiwa kukamatwa muda huo huo kwa usaliti wa taifa lake.
Baada ya kuipokea taarifa hiyo, alitoroka ndani ya taifa lake na kiasi kikubwa cha pesa pamoja na vito vya thamani vya mumewe. Kwa mara ya kwanza alikimbilia ndani ya Ukraine lakini aliona hapo muda wowote angekamatwa hivyo alitafuta sehemu ambayo ni salama kwake, akaamua kukimbilia ndani ya taifa la Marekani ambao ndio aliwasaidia. Licha ya kuwa huko, alijua wazi atakuja kupatikana siku moja kulingana na ukubwa wa usambaaji wa taarifa ndani ya taifa hilo hapo akacheza karata nyingine ya kutafuta taifa ambalo ni dogo kinguvu kwenda kujificha, alijua kuwepo kwenye taifa dogo kungemfanya awe salama kwani hakuna mtu angehangaika kumtafuta huko.
Baada ya kufanya tafiti zake ndipo karata yake ikadondokea ndani ya nchi ya Tanzania, hapo akafunga safari kwa siri kutoka Marekani na kuja Tanzania ambapo baada ya muda alianza kutafuta namna sahihi ya kufanya mambo yake. Akili ikamuonyesha mdogo wa raisi wa Tanzania wa nyakati hizo, Novack Nyangasa. Hiyo ndiyo ikawa hesabu yake ya kwanza kabisa ndani ya ardhi ya Tanzania. Kwanini iwe mdogo wa raisi wa nchi, alitaka kufanya naye nini IRINA? Twende pamoja.
Lengo kubwa la Irina kumtumia mdogo wa raisi kama karata yake ya umuhimu ni kwa sababu ya nafasi ambayo alikuwa nayo mtu huyo, kuanzia nguvu ya kifedha pamoja na nguvu ya mamlaka ambayo ilikuwa nyuma ya raisi Justin Nyagasa. Kwenye kurasa za siri za mashirika ya kipelelezi duniani mwanadada huyo alikuwa anatafutwa kila sehemu na picha yake ilisasishwa huko ila kwa bahati nzuri dunia hiyo ilikuwa ni dunia ya siri ambayo siyo kila mtu anaifahamu.
Walimchafua huko kwao na kumuita LUNATIC GIRL ikiwa na maana ya binti mwendawazimu lakini zilikuwa ni taarifa za siri kwa sababu kama ingejulikana basi KGB wangeonekana ni wadhaifu mbele ya ulimwengu na hawakuwa tayari kuliweka wazi jambo hilo ndiyo maana ikawa ni siri yao wenyewe kuhakikisha wanalimaliza jambo hilo chini chini. Irina kutokana na uzuri wa asili uliokuwa umekithiri kwenye mwonekano wake alifanikiwa kumshawishi Novack Nyangasa ambaye alikuwa na mke na watoto wawili tayari kuzama kwenye penzi lake.
Alivutia zaidi ya wale warembo wa dunia, macho yake ambayo yalikuwa na ublue hayakumuacha salama mdogo wa raisi akaona amepata bahati ya mtende ya pekee kabisa kuwa na mwanamke huyo, akazama kwenye mapenzi mazito asijue huyo alikuwa ni agent wa KGB. Kuzama kwenye penzi na mlimbwende huyo ambaye alijitambulisha kama anatokea ndani ya nchi ya Panama ila wazazi wake wana asili ya Urusi ambako aliishi babu yake, alidai kwamba hakuwahi kupata mwanaume akampenda lakini alimuona bwana huyo anamfaa. Novack akajaa kichwa na kuamua kumpenda mwanamke asiyemjua kiundani zaidi, akaisahau hata familia yake lakini mwenzake alikuwa na mipango mingine tofauti ambayo aliamini mwanaume huyo angekuja kuijua baadae akiwa kwenye himaya yake tayari.
Irina alikuwa na pesa nyingi, pesa ambayo alihitaji imfanye awe mwanamke mwenye nguvu duniani, awe mwanamke wa kuogopwa akiwa anaendesha mambo yake kwa kutumia mlango wa nyuma na alijua hayo yote atayafanikisha akiwa na mtu mwenye nguvu pembeni yake ndiyo maana Novack lilikuwa chaguo lake sahihi. Mpango wa kwanza ukawa ni kuanzisha jamii yenye nguvu, jamii ambayo itajumuisha watu wa taaluma mbalimbali; wanasiasa mbalimbali, wanafalsafa, maprofesa, watu wenye vipaji vikubwa bila kuwasahau wafanya biashara wakubwa kwa kuwawezesha njia za kufikia ndoto zao lakini wakiwa chini ya jamii hiyo na kwa ambaye angeenda kinyume basi alitakiwa kufa.

UKURASA WA 18 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 19

Mlengo wake ulikuwa ni kuwa jamii ya siri yenye nguvu ambayo ingefanya jambo lolote kwa wakati wowote na kwa muda wowote ule, ila lengo kuu la siri lilikuwa ni Irina kujiwekea ulinzi kwa sababu alijua kumiliki jamii hiyo ingekuwa ni ngumu kwa yeye kuja kupatikana kwenye uso wa dunia na kama kuna mtu angekuwa anamtafuta basi kwa kuwa na watu wengi wenye nguvu taarifa hizo angezipata mapema na kujua namna ya kujilinda. Alimshawishi Novack ambaye alikuwa amezama kwake, alimpa fununu kuhusu taasisi ambayo ana mpango wa kuianzisha, akamweleza faida za mabilioni ambazo wangezipata kutoka kwenye mradi huo! Pesa hununua mpaka nafsi, licha ya kuwa na pesa za kutosha kutokana na biashara zake nyingi alizokuwa anazifanya, Novack alitokwa na mate ya hamu, akaingia kwenye kumi na nane za Irina. Akakubali.
Ndipo ukawa mwanzo rasmi wa kuanzisha kitu kinaitwa LS (The LUNATIC SOCIETY) akitumia lile jina ambalo aliitwa na shirika lake baada ya kuwasaliti. Jamii hiyo ilianza kutafuta watu ambao walikuwa wamewalenga kwa nguvu iwe ni kwa hiari au kwa lazima, waliogoma familia zao zilitekwa, ndugu zao waliteswa, mali zao zilipotea na kuporwa kwa siri kubwa hivyo wengi wakawa hawana namna kwa sababu nyuma yake alikuwepo mdogo wa raisi ambaye alikuwa na nguvu kubwa ya kiutawala japo hayo yote alikuwa anayafanya bila kaka yake kujua.
Walisajiliwa watu wengi wenye nguvu nchini, ikawa ni jamii ambayo inamiliki kila aina ya watu ndani yake kwa sababu pesa ilikuwepo, wakawa wanafanya biashara haramu kwa ajili ya kujipatia pesa nyingi na kila ambaye aliingia huko hakutamani tena kutoka kwa aina ya pesa ambazo walikuwa wanazitengeneza. Ukawa mwanzo wa jamii hiyo kufanya kazi na kuotesha mizizi ikiwa nyuma ya huyo mwanamke kutoka Urusi.

Kwa bahati iliyokuwa mbaya raisi alifanikiwa kupata taarifa za chini chini juu ya uwepo wa watu hao nchini, alishangaa alipo sikia kwamba jamii hiyo ilikuwa inaendeshwa na mdogo wake wa damu, akalazimika kumuita Ikulu ili kujua ukweli wa taarifa hizo. Mdogo wake hakusita kumpa ukweli kaka yake, alimweleza kinaga ubaga na kumkaribisha yeye kama mkubwa wa nchi na kumuahidi kwamba huko kulikuwa na siti yake ya VIP iliandaliwa muda mrefu ila ulikuwa unasubiriwa muda sahihi wa kufika na kumweleza jambo hilo, mheshimiwa akagoma.
Alikataa kabisa kuruhusu jambo kama hilo kufanyika ndani ya taifa lake, aliipenda mno Tanzania hivyo hakuwa tayari kuruhusu nchi iharibike tena yeye akiwa madarakani. Akamuonya mdogo wake na kumpa tahadhari kwamba sio kwa sababu yeye ni mdogo wake basi anaweza kufanya lolote ambalo analitaka yeye, akasisitiza kwamba anampa mdogo wake mwezi mmoja asije akalisikia tena jambo hilo kwenye maisha yake vinginevyo atasahau kama wao ni ndugu. Mpango wa kumshawishi raisi ukagonga mwamba kwa sababu alichukizwa na jambo hilo hususani kufichwa na ndugu yake kutoka hatua ya kwanza mpaka mpango unakamilika, kugoma kwake kama mkubwa wa nchi likawa ni tatizo lingine ambalo lingeitingisha jamii hiyo ya siri. Irina akaja na mpango mwingine mezani baada ya kuipata ripoti hiyo. Mpango wa kumtoa raisi madarakani au kumuua.
Huo mpango ukawa mgumu kwa Novack, kivipi amuue kaka yake? Kwa sababu ya pesa tu!? Hapana kama pesa anazo na kaka yake ndiye kamfikisha pale alipo kwa wakati huo, sasa kivipi amsaliti ndugu yake ambaye wametoka mbali? Roho ikagoma, damu ni nzito kuliko maji! Novack akagoma kabisa kutekeleza jambo hilo kwani alidai anampenda kaka yake sana. Irina akatolewa nje na jaribio lake la kwanza, mwanamke huyo akasikitika mno na kumkumbusha Novack waliko tokea na umoja huo na ukizingatia kwa wakati huo alimdanganya kwamba alikuwa na mimba yake ili amkamate vizuri. Sasa kama yeye asipo msikiliza hasa kama kiongozi mwenzake nani angempa sikio lake na ngoma za masikio zikakubali kumsikia? Abadani! Hakuwepo zaidi ya Novack.
Mwanamke huyo alimuweka wazi kwamba washirika wenzao watawaona wao ni wadhaifu na watu wa kuyumbishwa hivyo hawana hata sifa za kuwa viongozi wa jamii hiyo, kama shida ilikuwa ni ndugu mbona hata wao wakati wanaingizwa ndani ya jamii hiyo ndugu zao waliteswa na wengine wakauawa! Kwamba wao hawakuwa na uchungu na ndugu zao ila viongozi ndio wenye uchungu? Irina akamuweka wazi Novack kwamba katiba yao ilikuwa inaeleza vizuri kwamba haijalishi ni nani ila ikitokea akawa kipingamizi kwenye umoja huo ni lazima aondolewe mara moja duniani na kama sio hivyo basi wao kama viongozi ilitakiwa mmoja wao afe hususani ambaye anapingana na katiba ili aje kiongozi mwingine mwenye uwezo wa kufanya maamuzi sahihi.
Kwa maana hiyo na kwa maelezo hayo ikawa ni kwamba kuna uwezekano Novack akampoteza Irina ambaye alikuwa amempenda na tayari alikuwa na mimba yake, lakini pia huenda yeye mwenyewe alitakiwa kufa kwa sababu ndiye alihitaji kwenda kinyume na katiba yao. Kufa? Hapana bado aliyapenda mno maisha yake, Novack akabaki njiapanda asijue aende na njia ipi. Alimpenda mno kaka yake lakini maisha yake yeye binafsi yalikuwa ni mhimu zaidi hata ya huyo kaka yake, afanye nini? Bora apungue kaka lakini sio yeye.
Kumuua kaka yake akaona hapana bora wamtoe Ikulu ila awe hai, alijua baadae angekuja kumuomba msamaha na wakayamaliza kwa sababu wao ni ndugu tena walio nyonya ziwa moja kwa kuachiana. Shida ikaja, kama akitolewa na kuwa hai bado alikuwa ana mizizi mirefu serikalini na kuna viongozi ambao bado walikuwa watiifu kwake hivyo lazima angewatumia watu hao kufanya kisasi kama sio kupambana na watu hao na mwisho wa siku wakaja kujulikana kwa yale ambayo wanayafanya. Njia pekee ya kuwa salama ikawa ni kuyachukua maisha yake, Novack alikuwa mzito kuyakubali maamuzi hayo lakini akawa hana namna, raisi wa nchi akawekwa kikaangoni, ni lazima roho yake ichukuliwe ili aingizwe madarakani raisi ambaye wangemtaka wao. Raisi anauawa, kivipi?
POLONIUM-204, ndilo likawa suluhisho la kumuua raisi wa nchi, kwanini? Kwa sababu ni njia salama zaidi ambayo hakuna mtu angeweza kuishtukia hivyo hata uchunguzi usingefanyika kwa ukubwa kiasi cha kuwashtua wananchi. Polonium 204 ni sumu mbaya sana ambayo iingiapo mwilini inaanza kuathiri mfumo wa ufanyaji kazi wa mwili kama mapafu, figo na viungo vingine kushindwa kufanya kazi kwa usahihi hali ambayo inaweza kupelekea mhanga kuanza kupoteza nywele na koo kuvimba hali inayomfanya mhanga kupumua kwa shida.
Ilichaguliwa hiyo kwa sababu ni sumu hatari ambayo inaua taratibu hivyo hata mtu kushtuka ni ngumu mno, zitaanza dalili za mbali ambazo walijua zingewafikia wananchi na kujua kama raisi wao anaumwa hivyo hata siku akifa wasingeshtuka kwani habari za kuumwa kwake wangekuwa nazo. Uliwekwa muda wa mwezi mmoja tu ndio ambao raisi alikuwa anatakiwa kuishi ili watu wasishtuke.
Mpango ukawa umekamilika, kilichokuwa kimebaki ni nani wa kumpatia raisi hiyo sumu? Novack ndilo likawa jibu rahisi kwa sababu yeye alikuwa na uwezo wa kuonana na kaka yake muda wowote ambao aliutaka na hata Ikulu alikuwa anaingia bila kukaguliwa. Alitakiwa kumuua kaka yake kwa mkono wake mwenyewe jambo ambalo kwake lilikuwa gumu na zito isivyo kawaida lakini hakuwa na namna. Iliandaliwa nyaraka ambayo ilikuwa na maelezo ambayo binasfi aliamini kaka yake angeyasoma kwa namna moja ama nyingine kwa sababu barua ikitoka kwake ilikuwa inamfikia kaka yake mwenyewe na anaisoma yeye mwenyewe.
Ndani ya nyaraka hiyo ndiko ambako ilipakwa hiyo sumu hivyo mtu ambaye angeivuta ikaingia ndani, basi siku za kuishi kwake zingeanza kuhesabika na huyo alikuwa ni raisi mwenyewe ambaye alitakiwa kufanyiwa hivyo. Mpango ulikamilika, nyaraka hiyo ilifikishwa kwa raisi na Novack mwenyewe ambaye alidai kwamba aliyafikria maneno ya kaka yake na alikuwa tayari kuachana na ule mpango na maelezo yote yalikuwa kwenye nyaraka hiyo. Kaka mtu akafurahishwa na maamuzi ya mdogo wake kwani hakupenda waingie kwenye mgogoro hivyo akaifungua nyaraka hiyo akiwa mwenyewe ofisini kwake ili asome maelezo ya mdogo wake, hilo ndilo likawa kosa ambalo liliiachia umauti nafsi yake.
Aliivuta ile sumu bila kujua, akafurahia maamuzi ya mdogo wake asijue kwamba alikuwa anaenda kufa taratibu bila haraka. Baada ya siku kadhaa kupita mwili ulianza kuchoka na kuishiwa nguvu hivyo mheshimiwa akawahishwa hospitali na wananchi wakaarifiwa kwamba raisi wao anaumwa lakini baada ya siku kadhaa wakaambiwa amepata nafuu. Hospitali daktari wa raisi alikuwa ni mwanachama wa LS ndiyo maana walijua mpango wao ungetimia kwa asilimia zote, hakuwa anamtibu mheshimiwa kwa kuipunguza ile sumu mwilini bali alikuwa akimpa dawa zingine za kumpa nguvu mheshimiwa tu kwa siku kadhaa lakini sumu iliendelea kumteketeza ndani kwa ndani.
Ilipofika wiki ya tatu, daktari alipewa maagizo kwamba ni wiki ya mwisho ya raisi huyo kuishi hivyo amchome sindano nyingine ya kummaliza haraka, zoezi likaenda kama lilivyopangwa, raisi akazidiwa na wananchi wakataharuki. Wiki moja baadae makamu wa raisi akautangaza msiba mbele ya vyombo vya habari huku ikidaiwa kwamba raisi amekufa kwa sababu ya kansa ya damu ambayo ilimtafuna kwa muda mrefu. Wananchi hawakushtuka kwa sababu ni mwezi mzima walikuwa wana taarifa za kuumwa kwake na kulazwa mara kwa mara ila walitamani kwamba lingefanyika jambo raisi wao akasaidiwa zaidi ya pale kwani walimpenda, lakini nani angebadili uhalisia na ukweli huo? Alikuwa amekufa mheshimiwa na karata ya ushindi ikadondokea mikononi mwa IRINA ESPANOVICH. Hivyo ndivyo LUNATIC SOCIETY ilivyo anzishwa na kuotesha mizizi yake ndani ya ukanda wa Afrika ya mashariki.


UKURASA WA 19 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 20.

UGANDA.
Yohani Mawenge, alikuwa anajua kitu ambacho kingefanyika ndiyo maana alikuwa amehitaji kitu kinacho itwa IMMUNITY FROM PROSECUSION. Huu ni mkataba au makubaliano ambayo huwa wanaingia serikali ya taifa husika na mtuhumiwa ambayo inamlinda mtuhumiwa ili asikumbane na mkono wa sheria kwa makubaliano ya kutoa taarifa au kuwa msaada kwa serikali juu ya upatikanaji wa wahalifu wengine au kutoa taarifa ambazo zitakuwa na msaada mkubwa wa taifa husika, kama; kutoa taarifa juu ya uwepo wa hatari ya uvamizi ndani ya nchi au kuamua kuwauza wahalifu wenzake kwa kutoa taarifa za namna ya upatikanaji wao kwa serikali ili yeye apone.
Makubaliano hayo aliyafanya wakati amewaahidi kuwapa taarifa juu ya uwepo wa bomu ambalo lilitegwa ndani ya uwanja wa timu ya taifa na siku hiyo kulikuwa na mechi kubwa ya kirafiki kati ya Uganda na Algeria hivyo kama asingetoa taarifa wangekufa maelfu ya watu ambao wangeleta uhasama kati ya taifa la Uganda dhidi ya Algeria. Sanjari na hilo, alikuwa mtaalamu kwenye hiyo tasnia hivyo alijua watu hao hapaswi kuwaamini kwa sababu sio kila serikali huwa inaishi kwenye makubaliano japo kuvunja makubaliano halafu ikajulikana ni mbaya kwa baadae kwani wahalifu wengine au watu wengine wakijua basi hawawezi kuisaidia nchi yako tena.
Sababu hiyo ndiyo ambayo ilimfanya awe na mpango wa pili, mpango namba mbili alikuwa ni mkuu wa kituo cha Entebbe. Huyo ndiye ambaye alikuwa anatakiwa kwenda kumkomboa mtu huyo kwa namna yoyote ile bila yeye kujua alihusishwaje kwenye mpango japo aliambiwa kwamba yeye ndiye ambaye alitakiwa kwenda kumtoa sehemu ambayo angehifadhiwa.
Baada ya mambo yote kufanyika, Yohani alichukuliwa na shirika la kijasusi la nchi ya Uganda lijulikanalo kama ISO na kwenda kuhifadhiwa kwenye dark site ambayo ilikuwa maalumu kwa ajili ya kuwahifadhia na kuwafanyia mahojiano wahalifu wakubwa. Tangu anachukuliwa mpaka anapelekwa huko hakuwa akijua kwamba yuko wapi kwa sababu alifungwa kitambaa usoni, alitolewa kitambaa hicho akiwa tayari yupo ndani ya kambi hiyo ndogo ambayo ni tawi ya shirika hilo. Alikuwa anapitishwa kwenye kodiro moja ndogo ambayo ilikuwa inatosha watu wawili tu kupita, pembeni kulikuwa na vyumba kadhaa ambavyo havikustahili mtu yeyote kuweza kuishi huku ndani yake kukiwa na watu ambao walikuwa wamekondeana na kufubaa hata hivyo hakuna ambaye aliwajali.
Taa zilikuwa zinatoa mwanga hafifu mno kiasi kwamba ungehisi eneo hilo lilitumika kufugia kuku wa kisasa ilihali walikuwa ni wanawadamu wa kawaida. Mazingira hayo yalimpa tahadhari juu ya uhatari wa eneo ambalo alikuwa amefikishwa. Waliliacha lile eneo na kushuka na ngazi kadhaa mpaka walipo ikuta korido nyingine ambayo ilikuwa na umeme vizuri na pana kidogo, ndani ya korido hiyo walifungwa watu ambao angalau walikuwa wapo sehemu nzuri tofauti na mwanzo, akagundua kwamba huenda hao walikuwa ni watu wenye ukwasi ama matajiri ambao walikuwa wanakamatwa kwa sababu mbali mbali ndiyo maana mateso yao hayakuwa makali kama wengine.
Walitembea mpaka sehemu iliyokuwa na lifti, wakapanda na kushuka chini kwa muda mfupi na walipo tokezea hapo, ilikuwa ni sehemu ambayo ilikuwa ni nzuri, sehemu ambayo ilikuwa na shehena ya mitambo na kumpyuta kubwa huku watu wakiwa wanapambana kucheza na tarakishi kwenye kompyuta hizo mbele yao. Wakati anaingia pale kila mtu aliacha alichokuwa anakifanya na kumuangalia kwa umakini mwanaume huyo ambaye hakuwa na hofu licha ya kuwepo kwa eneo ambalo hakuwa an uhakika na eneo ambako lilikuwa linapatikana. Alikumbuka kugeuka nyuma ndipo akamuona yule mkuu wa kituo yupo, jambo hilo lilimpa faraja kubwa, akacheka kwa sauti wasijue ni kipi kinamchekesha ila yeye alikifahamu.
Alipelekwa ndani ya chumba cha mahojiano ambacho kilikuwa na kamera nne kila pembe, kilizungukwa na nondo kila sehemu huku kikiwa kimefunikwa na kioo safi kwa nje. Kulikuwa na viti viwili tu ndani yake ambavyo katikati vilitenganishwa na meza moja ya mninga, aliketishwa upande wa pili akiwa ndani ya pingu na hata miguu yake ilifungwa pingu kwenye meza kisha watu wote wakatoka na kumuacha pekeyake. Hakuwa na wasiwasi Yohani, utulivu ulikuwa sehemu yake huku akiwa anaangaza kila sehemu asielewe alikuwa wapi ila akaamua kuupa muda nafasi.
Baada ya dakika kadhaa alisikia mtu akiwa anakuja eneo hilo kwa sauti za viatu ambavyo vilikuwa vinapiga kelele, aliingia mwanaume mmoja ambaye alikuwa amevaa suti safi na sura pana isiyo na utani. Bwana huyo alikuwa ameishika bahasha ndogo na kalamu ya kuandikia pamoja na kifaa cha kurekodia sauti mkononi mwake, alipofika hapo hakukaa wala kutoa salamu bali aliirushia ile bahasha juu ya meza na kumwangalia Yohani kwa jicho la kufuga kisasi, hata hivyo hakujali.
Aliketi upande wa pili akimpa ishara Yohani aifungue bahasha ile, alisita kidogo ila hakuwa na namna kwani hakujua kipo nini ndani yake. Aliifungua na kukutana na picha kadhaa ambazo zilikuwa zinamuonyesha yeye mwenyewe kwenye matukio tofauti. Picha ya kwanza ilimuonyesha akiwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kampala, picha ya pili ilimuonyesha akiwa karibu na ulipo uwanja wa taifa wa Uganda lakini picha ya tatu alikuwa karibu na hoteli moja kubwa ya kifahari ndani ya Entebbe akiwa amevaa mavazi ambayo ndiyo alikuwa nayo wakati wapo ndani ya hicho chumba cha mahojiano na bila shaka ni picha ambayo alipigwa akiwa anaelekea kwenye kituo hicho.
“Unaweza ukanipa maelekezo kuhusu hizo picha?”
“Inaonekana mmejitahidi sana kunifuatilia”
“Unahisi hii nchi unaweza ukaingia na kufanya unacho kitaka wewe kwa wakati unao utaka wewe wenyewe sio?”
“Una mtu anaye kutegemea ofisa?” swali la Yohani lilimshangaza mtu huyo ambaye alisimama na kugonga meza kwa hasira.
“Ni mara mia unipe majibu ambayo ninayataka kwa sababu vinginevyo nakuua kwa mkono wangu mwenyewe”
“Nimekuuliza kama kuna mtu ambaye anakutegemea kwa sababu dakika chache zijazo unaenda kufa na wenzako” ofisa alibaki ameduwaa asielewe kitu ambacho alikuwa anakiongea Yohani kwa sababu alionekana mfa maji hivyo asingeacha kutapa tapa. Alimcheka kwa dharau na kumpuuza kisha akaketi tena, naye Yohani akacheka kujibu ile dhihaka.
“Niambie aliyekutuma kufanya hili jambo ni nani?”
“Kumbuka nina ulinzi wa taifa la Uganda, nimeingia nao makubaliano hivyo sipo hapa kukujibu wewe maswali bali nipo hapa kwa ajili ya kuwasubiria watu ambao ninataka kuongea nao kutoka Tanzania”
“Hebu nisikilize vyema bwana mdogo, sijali kuhusu serikali imekupatia mkataba wa kukulinda au mdudu gani, uhalisia ni kwamba siwezi kukuacha ukatoka humu ndani bila kunipa kile ambacho ninakitaka. Na unatakiwa kufanya hivyo haraka “ alitamka ofisa huyo akiwa anaiweka bastola yake mezani kwa hasira, Yohani alimuinamia mwanaume huyo na kumsisitizia tena.
“Una dakika tano za kuyaokoa maisha yako, kimbia na utoke kwenye hili eneo unaenda kufa”
“Umepanga kufanya nini?”
“Nilijua serikali yako lazima itanisaliti, mimi sio mjinga kiasi hiki kiasi kwamba niamini kile ambacho mlikuwa mnakifanya. Sina muda wa kukueleza ila nakusisitiza kwamba kimbia ndani ya hili eneo kwa sababu kwa sasa zimbaki dakika tatu na sekunde kadhaa za wewe kuwa hai” hakuonekana kuwa na masiara na anacho kiongea mwanaume. Ofisa huyo akiwa anashangaa kutaka kujua kwamba ni kipi kilikuwa kinaendelea ndipo akasikia sauti ya king’ora. Ilikuwa ni alamu ya hatari kwamba eneo hilo halikuwa salama hivyo kila mtu alitakiwa kuwa tayari kwa lolote.
“Umefanya nini?” alijikuta ananyanyuka na kumkwida Yohani huku akiwa ameiweka bastola kwenye paji lake la uso lakini ni yeye ndiye alikuwa akiweweseka na kuteseka.
“Unapoteza muda mwingi kuuliza vitu vya kijinga, nenda kawasaidie wenzako huko nje wanazidi kufa” alimwangalia Yohani kwa hasira baada ya kutamka kauli hiyo ili ni kweli muda haukuwa rafiki kwake, yeye ndiye alikuwa kiongozi wa eneo hilo hivyo lilikuwa jukumu lake kuhakikisha kwamba kila mtu alikuwa salama.

UKURASA WA 20 unafika mwisho.
 
3500 tu kumalizia mpaka mwisho 106.

0621567672 (HALOPESA)..
WhatsApp

0745982347 (M-PESA)

0714581046 (TIGO-PESA)

FEBIANI BABUYA
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 21

Kiongozi wa Dark site alitoka nje ya chumba hicho na kushangaa akiwaona vijana wake wakiwa wanahaha na komputa zao lakini wale ambao walikuwa na silaha wakiwa wanajikusanya kusubiri amri yake.
“Nini kimetokea?”
“Geti la nje limevunjwa” mmoja wa wataalamu wa komputa alijibu akiwa anajaribu kuonyesha picha za geti hilo kwa upande wa nje.
“Hili jambo limewezekana vipi?”
“Mpaka sasa hatujajua bosi kwa sababu watu wenyewe wamevaa vitambaa usoni”
“Wapo wangapi?”
“Watatu”
“Watu watatu ndio wavamie sehemu kama hii?”
“Ndiyo kiongozi”
“Watafuteni haraka mniletee hapa” alifoka
“Lakini tayari wameshapenya mlango wa kuingilia ndani”
“Wameweza vipi kufungua mlango huo”
“Kwenye kamera wamaonekana wanne, inaonekana kuna mlinzi wamemteka na ndiye anawapa maelekezo ya nini cha kufanya”
“Andaeni silaha zenu, naombeni maelekezo kila hatua ambayo wanafikia, wavamieni na waletwe hapa haraka” maelezo yake yalimfanya ahitaji kurudi kwenye kile chumba cha mahojiano lakini alisikia sauti ya mtu wa komputa akimwambia kwamba kamera zote humo ndani zilikuwa zimezimwa hivyo wasingejua ni wapi walielekea, alisogea kutazama hakuamini. Walinzi wake walikuwa wanauawa kikatili mno kwa video ambazo zilionekana kabla ya kamera hizo kuzima. Aliitoa simu yake mfukoni na kupiga ili kuhitaji msaada wa dharura nje ya sehemu hiyo kwa bahati mbaya hakukuwa na mtandao, alijaribu kuongea na wataalamu wake wa IT ila kabla hawajafanya jambo lolote mitambo yote ilizima kwa sababu ilikuwa inatumia umeme na mifumo ya umeme ilikuwa imekata, msaada wa pekee ikawa ni kupigania kilichopo mbele yao.
Alikimbia kama amechanganyikiwa kurudi kwenye chumba cha mahojiano ili mtu huyo ampe maelezo watu hao walifanikiwaje kufika na kuingia hapo na huenda kuwa naye kwenye mkono wake wakati huo kungeweza kusaidia jambo hilo kusimama. Lakini kipindi yeye anatoka humo ndani, yule mkuu wa kituo cha Entebbe aliingia akiwa mwingi wa hofu usoni pake, mtu huyo alikuwa na siri zake nyingi na za viongozi wake wa juu, alikuwa anaogopa kama siri hizo zingevuja lingekuwa tatizo lingine kwake hivyo alikuwa na maswali kadhaa kwa mtu huyo ili kujihakikishia usalama wake kwanza na kujua sababu hasa ambayo ilimfanya mtu huyo ampe taarifa kwamba yeye ndiye angetumika kuweza kumtorosha eneo hilo.
“Umeniingiza kwenye matatizo makubwa, hili eneo kuingia huwa ni rahisi ila kutoka kwake ni ngumu mno. Sikuwahi kufika kabla leo ndiyo mara ya kwanza na hata mimi wakati nakuja huku nilizibwa macho ili nisipajue, lengo la wao kunileta mimi huku ni kutoa taarifa za mwanzo ambazo ulinipa lakini pia kuthibitisha maelekezo yako ambayo uliyatoa mwanzo na utakayo yatoa hapa kama yanafanana”
“Nifungulie tuweze kuongea kabla haujachelewa”
“Siwezi kukufungulia kwa sababu sina mamlaka hayo na hata kama ningekuwa nayo bado sitakufungulia”
“Unajua kwanini nimekwambia wewe ndiye utakaye nitorosha ndani ya eneo hili?”
“Hapana”
“Nilijua serikali yako itanifanyia uhuni na ndicho ambacho wamekifanya ndiyo sababu mpango wangu mkubwa ulikuwa ni wewe hapo. Najua baada ya kutoka ofisini ulirudi nyumbani kwako kujua kama familia ipo salama, ulivyofika kule mkeo alionekana kuwa na wasiwasi kiasi kwamba mkakumbatiana kama kufarijiana ila wakati anakukumbatia kuna kifaa cha mawasiliano alikibandika ndani ya kola yako upande wa nyuma ya shingo huko. Unaweza ukamchukia mkeo ila hakuwa na namna kama ambavyo wewe huna namna zaidi ya kufanya ninacho kitaka” maelezo hayo yalionyesha kwamba mkewe alimsaliti, alihamaki na kupaniki ila hakuwa na kauli ilitakiwa awe mpole asikilize maelezo yote.
“Mkeo alionyeshwa video zake chafu ambazo amekuwa akikusaliti na kuugawa mwili wake kwa wanaume wengine, ukiacha hilo amepewa maelekezo kwamba kama angegoma kufanya kama wanavyotaka watu hao basi wangeua watoto wako wote na wewe mwenyewe ungeuawa. Unahisi mkeo angefanya nini zaidi ya kukubali? Akawa hana namna zaidi ya kuifanya kazi hiyo ambayo ameitekeleza kwa ubora wa hali ya juu” Yohani alimeza mate na kutulia akiwa amemkazia macho bwana Odong.
“Mimi nilikuwa najua kabisa kwamba wewe lazima wangekuchukua kuja na mimi huku hivyo kukuwekea kifaa cha mawasiliano nilihitaji watu wangu wajue ni wapi ninapo letwa ili waje kunichukua na kwa wewe na familia yako mmefanikiwa kuifanya kazi yangu kwa usahihi hivyo hakuna kati yenu ambaye atapata madhara, nitawapa nafasi nyingine ya kuishi” Odong alizidi kustaajabishwa na mwanaume wa maajabu huyo ambaye kila alichokuwa anakifanya basi alikuwa anawazidi hatua moja mbele jambo ambalo lilimshangaza.
“Kama lengo lako lilikuwa ni kutoroka, kwanini ukaruhusu mpaka uletwe huku?”
“Unataka kuijua sababu iliyo nileta nchini Uganda? Kwa sababu mara ya kwanza nilikudanganya”
“Ndiyo”
“Mimi sijaja huku kuongea na raisi wa Tanzania wala kamshina wa jeshi la polisi wa Tanzania, nilifanya vile ili niaminike tu ila lengo langu ya kuingia ndani ya nchi hii lilikuwa ni kufika ndani ya hii kambi ya siri ya shirika lenu la kijasusi”
“Kwanini?”
“Kuna mtu anaitwa Kenneth Lawi, ana miezi sita tangu akamatwe na kufungwa ndani ya hili eneo. Alikuwa ni kijana wangu na alikamatwa na madawa ya kulevya na baada ya kukamatwa aligundulika kwamba ana siri nyingi ndani yake, siri ambazo zinaweza kuniweka mimi na washirika wenzangu kwenye matatizo makubwa na kupitia baadhi ya watu wetu ambao wapo ndani ya taifa hili wanadai kwamba amefikia makubaliano na serikali ya taifa hili kuweza kunianika mimi na washirika wenzangu ili yeye aweze kuachwa huru na kuwa chini ya ulinzi wa serikali jambo ambalo halitakiwi kufanyika”
“Kwahiyo umekuja kumsaidia ili asiongee?”
“Ni msaliti tayari siwezi kupoteza muda wa kusema namsaidia, nimekuja hapa kumuua. Hili jambo nahitaji kulikamilisha haraka kisha nitoke humu ndani na wewe nitakuzimisha tu ili wakikupata ukiwa bado upo hai uweze kujitetea maana wewe mwenyewe utakuwa ulipona kwa bahati tu ndani ya uwanja wa vita. Nifungue” Yohani alisisitiza sana, Odong alijifikiria na kwenda ukutani eneo ambalo lilikuwa na funguo, alimfungua mwanaume huyo ambaye alijinyoisha na kuhitaji bastola ya Odong apatiwe yeye. Baada ya kuichukua bastola hiyo alimwangalia Odong;
“Kwahiyo unataka kuniambia kwamba yale mawasiliano hayakufanyika dhidi ya serikali ya Tanzania?”
“Ndiyo walio ongea nao kwenye simu ni watu wangu” Odong alibaki ameduwaa
“Tutaonana wakati mwingine” alitamka na kumtandika ngumi nzito kwenye shingo ambayo ilimdondosha chini bwana Odong akazimia hapo hapo.

Wakati anajiandaa kutoka, malango ulifunguliwa huku mtu ambaye aliufungua akionekana kuwa na jaziba lakini mtu huyo alipiga kelele baada ya kupokelewa na ngumi nzito ya paji la uso kiasi kwamba hata silaha yake mkononi ikamponyoka. Sauti yake ilikuwa kali isiyo na msaada, akiwa anayumba yumba Yohani aliukunjua mguu wake ambao ulitua kwenye mbavu na kukita hapo, ofisa huyo alijibamiza kwenye nondo na kundondoka chini.

UKURASA WA 21 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 22

Yohani alimuonyeshea ishara ya kunyanyuka akiwa amemnyooshea bastola, ofisa huyo akacheka kwa nguvu huku mdomo wake ukiwa unatoa damu kidogo;
“Huwezi kutoka humu ndani, achia bastola yako na ujisalimishe kabla haujasababisha hatari kubwa zaidi mpu……” sentensi yake ya kujiamini ilikatishwa na mlio wa risasi, risasi ilipenya kwenye kiatu chake na kukipasua kiganja ya mguu wake wa kulia, alikuwa bado ameganda akiwa haelewi hiyo risasi iliingia sehemu ipi, alishtuka baada ya mguu ganzi kupotea na kuanza kumletea maumivu.
“Sijaja hii sehemu kupokea ushauri wako, nipeleke alipo Keneth Lawi”
“Siwezi kufanya hiv…..” aliongezewa risasi ya pili juu kidogo ya sehemu ilipokuwepo risasi ya kwanza na kumsababishia maumivu ambayo yalimfanya ahisi kuna mtu alikuwa anatembea na shoti ya umeme ndani ya mwili wake.
“Sipo hapa ili kukubembeleza wewe unipeleke huko ila ni lazima iwe hivyo” ofisa huyo hakuwa na namna zaidi ya kufanya kile ambacho aliamrishwa kukifanya. Baada ya kutoka ile sehemu iliyokuwa na mitambo alishangaa kuona watu wake wote walikuwa wameingizwa kwenye chumba kimoja na wanaume watatu waliokuwa na mavazi meusi wakiwa wameshikilia bunduki zao. Alijaribu kuangalia kila pande, alikuwa anashuhudia maiti za walinzi wake wakiwa wamekufa, hofu ikazidi kutanda kwenye nafsi yake, akawa hana namna zaidi ya kuweza kuongoza njia.
Waliutumia mlango wa siri tofauti na milango mingine, Keneth alikuwa amehifadhiwa sehemu ya siri mno, baada ya kuingiza code kwenye geti moja ambalo lilikuwa nyuma ya ofisi yake mlango ulifunguka ambapo walitembea kidogo na mbele yake kulikuwa na vyumba viwili, ndani ya chumba kimoja ndimo alikuwepo Keneth. Walitembea kwa muda mfupi Yohani akafanikiwa kumuona mtu wake akiwa ndani ya vazi maalumu huku akiwa na ndevu nyingi usoni kwake. Alimtaka afisa huyo afungue sehemu hiyo ambayo ilikuwa inafunguliwa kwa namba za siri ambazo baada ya kuhakikisha ameziingiza alimgeukia yule afisa na kumpiga risasi ya kichwa kisha akaingia ndani.
Keneth alishtushwa na kushangazwa na ujio wa mtu huyo humo ndani kwani hakutegemea wala kufikiria, alibakia na kigugumizi huku midomo ikiwa inatetemeka, Yohani alikuwa anamwangalia huku ameishika bastola vizuri kwenye mkono wake.
“Kiongozi”
“Kwanini umeamua kutusaliti Keneth?”
“Mimi nisingeweza kuwasaliti ndiyo maana mpaka sasa sijaongea”
“Najua hilo kwamba hujaongea ndiyo maana nipo hapa ili kuhakikisha hauongei jambo lolote”
“Usifanye hivyo kiongozi bado nahitaji kuishi nirekebishe makosa ambayo niliyafanya ya kukamatwa”
“Kukamatwa sio tatizo kubwa ila tatizo ni usaliti na unaelewa kabisa kwamba msaliti huwa anafanywa nini. Kwa kuweka mfano hautakiwi kuishi tena Keneth kwa sababu wengine wataona kama kusaliti ni sawa tu, najua kwamba una makubaliano na serikali ya taifa hili ili kutuuza. Hili lingetoka kwa mtu mwingine nisingeshangaa ila kutoka kwako ndilo jambo ambalo limeniumiza na kunishangaza pakubwa”
“Hapana kiongozi nahitaji nafasi nyingine tafadha…..” hakumalizia sentensi yake alipigwa risasi zote ambazo zilikuwa zimebakia kwenye bastola. Baada ya kuhakikisha kwamba amemmaliza mtu huyo, aliwachukua vijana wake na kuondoka ndani ya DARK SITE akiwa amekamilisha kilichokuwa kimempeleka huko bila tatizo lolote.















EDISON
Mwanaume huyu kuna watu walikuwa wanaisaka roho yake kwa udi na uvumba, wengine wakidai kwamba aliwaulia kaka zao huku wengine wakidai aliua makomando wenzake tisa lakini wengine haikujulikana sababu ya msingi ya kuweza kumtafuta kwa hasira huku yeye binafsi akidai kwamba hakuwa anaelewa jambo lolote ambalo lilikuwa likiendelea. Kile kitabu ambacho alikipata nyumbani kwa nchungaji ndicho aliamini kwamba kingempatia majibu sahihi ya kile ambacho alikuwa anakihitaji hivyo alikuwa anatakiwa kukisoma.
Edisoni alikuwa ndani ya jengo moja la zamani, ndipo alipopaki gari yake kwa nje na kuingia ndani huko ili aweze kupata utulivu wa kusoma maandishi hayo ambayo yaliandikwa kwa mkono wa kawaida. Aliketi kwenye kiti cha zamani mbele ya meza moja kuu kuu kisha akaifunua kurasa ya kwanza kujua kilicho andikwa huku nje yakiwa yameandikwa maandishi makubwa yaliyo someka “MIMI NI NANI?” kiulizo hakikuwa na jibu hivyo ndani yake ndiko angeyapata majibu yake. Aliufunua ukurasa wa kwanza ambao juu yake uliandikwa “MAISHA YANGU MPAKA NITAKAPO KUFA”
“Nayaandika haya huenda siku ambayo utafanikiwa kuyasoma nitakuwa sipo duniani, kama niliyo yafanya yalimpendeza MUNGU basi mimi nitakuwa huko mbinguni kama ilivyo ahidiwa. Acha nikukumbushe machache kumhusu MUNGU kijana wangu, ujivuni wa afya njema na kuwa hai huwa unawafanya wanadamu wawaze yale ambayo wao wanaona ni sahihi kwao, huwa wanaweza kukejeli kwa namna yoyote ile kiasi kwamba wanaaminishana kwamba MUNGU hayupo na hata kama yupo basi hana cha kuwafanya. Hayo ni majivuni ambayo huwa yanawatoka watu ambao hawajapitia nyakati ngumu ama wanaishi kwa raha wakati huo ili siku yakiwafika na kuielewa dunia ilivyo mbaya, siku ambayo hawatakuwa na namna ya kuyabeba magumu yaliyo kwenye nyoyo zao zaidi ya kutegemea maombi basi kwa vinywani mwao watakiri kwamba Mungu yupo.”
“Uzima wa maisha usikupe ujivuni wa hivyo, hii dunia haikutokea bahati mbaya, kuna kitu nyuma yake na huyo ndiye MUNGU mwenyewe kijana wangu, unaweza ukashangaa kwamba haya yanatoka wapi, nasema hivi kwa sababu najua kabisa kwamba nitakuwa na muda mfupi wa kuishi kuanzia sasa hivyo ni wajibu wangu kukukumbusha kutenda yaliyo mema na kuifuata njia sahihi ili usije ukaishia kujutia kwenye siku zako za mwisho za uhai wako badala ya kufurahia kuziacha taabu za dunia kwani kifo sio adhabu, kifo kinatakiwa kuwa furaha ya kusherehekewa kwa sababu unaziacha taabu na shida zote za walimwengu na kwenda kupumzika sehemu ambayo hautasumbuliwa tena zaidi ya kuyalipa na kufaidi matunda ya kile ulicho kifanya siku za uhai wako”;
“Historia ya maisha yako inaanzia huko pembezoni mwa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, rujewa. Ndiko chimbuko lako lilipo na hata kaburi la babu yako mzee Edison mwenyewe lipo huko. Babu yako alikuwa ni mkulima mkubwa wa mpunga, alikuwa ni miongoni mwa matajiri wakubwa ambao walikimudu kilimo na kikawalipa, akawa maarufu kila kona ya mji na miji mbali mbali. Alikuwa akilisha mamia ya watu kwa kujitolea huenda ndiyo sababu iliyo mfanya kuwa maarufu zaidi na kuishi miaka mingi kwa kuwa mamia walimuombea hivyo Mungu akampa neema kubwa”
“Licha ya kuwa na ukwasi mkubwa kiasi hicho na familia kubwa, babu yako kuna kitu kilimnyima raha kwenye maisha yake, alitamani kuwa na watoto wasomi kama zilivyo familia zingine lakini hakufanikiwa kwenye hilo. Watoto wake wengi waliishia kuikimbia shule kwa sababu walijua kwao mali zilikuwepo, sasa yanini kujitesa wakati kwao wanapata kila kitu? Wakamwacha elimu aende zake, jambo hilo likampa sonona na kumkosesha raha babu yako. Kuna watu huwa wanasema kwamba kwenye wakati mgumu MUNGU huwa anajitokeza na kuinua watu ndicho ambacho kilimtokea babu yako, katikati ya kukata tamaa alizaliwa mtoto wa kiume ambaye alimpatia jina la Christian. Christian akawa kipenzi cha babu yako, alimpenda mno huyo mtoto na ile hali ya kukata tamaa ndani yake ikaisha, akajikuta ana nguvu mpya, aliuona mwanga mbele yake, mtoto akawa baraka mpya kwenye familia”

UKURASA WA 22 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 23


“Christian aliipenda mno shule, akiwa mdogo tu kitu cha kwanza akiamka alitaka kusoma vitabu, baba yako akamuweka mbali na nduguze ili wasimharibu mwanae wa ndoto. Ukuaji wake Christian alichukiwa na nduguze lakini angurumapo simba mcheza nani? Baba yake ndiye alikuwa mfalme wa familia nani angepinga tena? Hakuna abadani! Kumuweka mbali na ndugu zake ilikuwa ni kwa sababu ya kumkinga kutoka kwenye kuharibika. Akampeleka shule za gharama kubwa ili akajifunze elimu ya makaratasi na elimu dunia, Christian hakuwahi kumuangusha baba yake. Akili za Christian zikaanza kuvuma kila kona ya mji, ikawa miji na sasa ikawa nchi hata kuvuka mipaka ya nchi, mtoto wa mkulima kutoka Mbarali akawa fahari ya wilaya, mkoa na nchi. Mbarali ilikuwa inaimbwa kwa sababu ya jina la Christian Edison, nani angetamba mbele yake? Hakuwepo, baba yake akawa muda wote meno yapo nje kwa cheko la furaha, dume lake linamuwakilisha vyema. Mzazi gani huwa haitaki fahari hiyo? Sio kwa hapa duniani, hapa kila mzazi anaupenda huo ufahari wa kusifiwa na kunadiwa kwa sababu ya mwanae wa damu”
“Christian alipata ufaulu wa madaraja ya juu mpaka akaimudu moja namba ndani ya nchi nzima, ukuaji wake ulizidi kumpa nafasi ya kuwa mtu mwenye akili kubwa zaidi kitu ambacho kilimfanya aichague sayansi, kuchagua kwake sayansi ukawa uchaguzi mbaya zaidi kwenye ufanyaji wa maamuzi ya maisha yake. Lisikushangaze hilo, kuchagua kwake kusoma zaidi sayansi ndiyo sababu ambayo ilileta maafa kwenye familia yake, jambo ambalo hata yeye alilijutia kwa maisha yake yote mpaka siku anapotea kwenye uso wa dunia”
“Christian alichukua nishani za heshima kila pembe ya nchi, hata ukanda wa Afrika ya Mashariki akatamba vilivyo, hakuna sehemu hawakumjua mtoto wa Edison. Wakati anayaanza masomo ya elimu za juu tayari makampuni makubwa duniani na ndani ya nchi yalikuwa yanapigana vikumbo kuihitaji akili yake ambayo waliamini kwamba ingefanya makubwa ndani ya nchi hii na duniani kwa ujumla. Akili yake ikawa inaleta ugomvi kwa watu huku zikianza kutengenezwa stori mbali mbali kwamba kuna watu walihitaji kumtumia mwanasayansi huyo mpya kutengeneza silaha za hatari ambazo huenda zingekuja kuwa tatizo kwa usalama wa watu, akili yake ikaanza kuogopwa tena badala ya kushangiliwa. Wengine waliona hatari mbele lakini wengine waliona fursa mbele kupitia akili yake, kila mtu na jinsi ambavyo anafanya upembuzi wake yakinifu mbele ya wengi”
“Wakati huo alimpata mchumba, mchumba ambaye alikiri kwamba alimpenda vilivyo akawa tayari kumuoa. Alimpatia chuo mwanamke huyo ambaye waliendana kwa vingi, hata alipo lifikisha kwa baba yake mzee huyo alilikubali jambo hilo bila kinyongo na wakati huo umri ulikuwa umemtupa mkono mzee Edison. Rasmi Christian akaingia kwenye maisha ya ndoa ambayo baada ya muda mfupi yalimlipa kwa kumpatia mtoto wake wa kiume ambaye aliamua kumuita jina la baba yake mzazi, Edison na huyo Edison ni wewe hapo ambaye nina imani siku unalitambua hili ni siku ambayo utakuwa tayari umeisoma habari hii”
“Baba yako akili yake ikawa hatari, akili ambayo ilianza kuogopwa kiasi kwamba akawa anapokea barua za vitisho kutoka kwa watu wasio julikana. Serikali ikamuita na kumkalisha chini, akawa chini ya uangalizi wa serikali sasa, serikali ikamlipa pesa nyingi na kumtaka atengeneze sumu ambayo ingekuwa na uwezo wa kumuua mtu kwa muda mfupi, dakika kumi mpaka kumi na tano tu tangu atakapo itumia sumu hiyo na ndio wakati huo huo ambao kulikuwa na siri zilianza kuvuja kwenye mamlaka za siri za usalama kwamba kuna jamii ya siri ambayo ilikuwa imeshaingia nchini, The LUNATIC SOCIETY. Usiumize kichwa juu ya namna ambavyo nilifanikiwa kujua kuhusu hiyo jamii ya siri, ni kwa sababu mimi nilikuwa mpelelezi”
“Baba yako alitengeneza sumu hiyo kama ilivyo hitajika na serikali na mwezi mmoja tu baada ya ule mpango kukamilika ndipo kilitangazwa kifo cha raisi wa Tanzania ambaye alifia madarakani kwa mara ya kwanza Justin Nyangasa na ndio wakati huo pia mamlaka za usalama zilikuwa zimepata taarifa za ujio wa agent wa zamani wa KGB, IRINA ESPANOVICH ambaye aliisaliti nchi yake kwenye vita baridi ambayo iliisha mwaka 1991”
Baba yako alishangazwa na jambo hilo, akahisi kwamba huenda ni yeye ndiye alikuwa chanzo lakini baadae tuligundua kwamba sumu ambayo ilimuua raisi ni POLONIUM 204 ambayo baba yako hakuhusika kuitengeneza, sasa aliyo itengeneza yeye ilitumika wapi na kwanini? Baadae ikagundulika kwamba wakati mheshimiwa akiwa kwenye hali ambayo siyo nzuri kiafya, siku ambayo ilipangwa afe ndiyo siku ambayo alichomwa ile sumu ambayo baba yako aliitengeneza iliyo yachukua maisha yake kwa haraka hivyo baba yako pia akawa amehusika kwenye kifo cha raisi bila kupenda. Jibu la kwanini likawa gumu kulipata ila lilikuja kupatikana baada ya kufanya tafiti na kugundua juu ya uwepo wa jamii hiyo ya siri ambayo ndiyo ilikuwa nyuma ya huo mpango wa kumuua raisi na chanzo ni huyo mwanamke wa KGB
Baba yako alianza kuogopa baada ya kulitambua hilo, alijihisi kuwa na hatia kuhusika na mauaji ya raisi ambaye alipendwa na watu, vipi kama siku wangejua angewajibu nini? Alichanganyikiwa lakini akiwa hajatulia vizuri akapokea habari ya kutisha, habari ambayo alitamani iwe ndoto tu kwenye masikio yake, aliogopa na kuzimia. Hata alipo zinduka hakuna kitu kilichokuwa kimebadilika, familia yake yote ilikuwa imeuawa ndani ya Rujewa, Mbarali Mbeya. Wote walikufa ndani ya usiku mmoja tena bila kuguswa na mtu yeyote yule, lilikuwa jambo la kushangaza, akachanganyikiwa Christian.
Alichukua damu ya ndugu zake wote na kuipima, akaduwaa baada ya kuikuta sumu kwenye miili yao, huenda sumu halikuwa jambo la kushangaza ila kuikuta sumu ambayo yeye ndiye aliitengeneza lilikuwa jambo jingine la ajabu na kusikitisha isivyo kawaida. Alitamani kujitoa roho yake ila akagundua atakuwa anakufuru mbele ya mwenyezi Mungu, sasa anakufuru vipi wakati alimpoteza kila mtu kwenye maisha yake? Alikumbuka neno mtoto hapo akagundua kwamba alikuwa na mtoto wa kiume, mtoto ambaye alikuwa anamhitaji mno kwenye maisha yake ila akashtuka kwamba mpaka wakati huo alizongwa na mawazo ya kuipoteza familia yake kiasi kwamba hakumkumbuka mwanae tena. Wakati anashtukia jambo hilo akagundua kwamba mwanae hayupo wala mkewe hayupo, akachanganyikiwa Christian.
Kwa mara ya kwanza nilimuona baba yako akiwa analia kama mtoto mdogo, uso wake ulikuwa umesawajika kwa kukosa tumaini. Uso uliokata tamaa ya maisha, licha ya ambayo yalimkuta lakini bado hakujua kwamba mkewe na mwanae walikuwa wapi, hilo lilikuwa ni pigo lingine. Christian alikuja kunipigia goti nimsaidie kumtafuta mwanae na mkewe kwani hata mipango ya mwanzo ambayo alijua anaifanya ili kuisaidia serikali haikuwa hivyo, ilikuwa ni kuwasaidia jamii ya LUNATIC SOCIETY kukamilisha mipango yao ambayo hata yeye hakuwahi kuijua kamwe.
Nilimshangaa kwanini ananiachia kazi hiyo na yeye anaonekana kabisa kuhitaji kujitoa, ndipo akaniambia kwamba alikuwa ameambiwa anahitajika kusafiri kwenda mashariki ya kati huko. Serikali ilikuwa imempa kazi maalumu ya kuweza kusaidiana na shirika la kijasusi la MOSSAD, MOSSAD walikuwa wanahitaji wanasayansi wenye uwezo mkubwa wa kuwasaidia kutengeneza nyukilia za hatari ili kuweza kuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kushindana na mahasimu wao Iran. Israel ilifanya michezo ya hatari ya kuwakamata wanasayansi na kuwatumikisha kinguvu kukamilisha mipango yao na wanasayansi hao walipo jaribu kutumika na upande mwingine walitishiwa na kuuawa.
Israel hawakuwahi kuhitaji wanasayansi hao watumike na watu wengine zaidi yao wenyewe na hilo ndilo likawa limemkuta Christian, nikapigwa na butwaa serikali yetu imtoe mwanasayansi wa kutegemewa na taifa kwenda huko kwa sababu zipi na kwa sababu serikali inafaidika na kitu kipi? Sikupata jibu la haraka kwa wakati ule ila baba yako akanifungua kidogo kwamba alikuwa ametengeneza vipande kadhaa vya nyukilia ambavyo aliingia makubaliano na serikali ya Tanzania lakini vipande hivyo baadae vilipotea kwenye mazingira ya kutatanaisha kabla ya kukamilika na yeye akapewa taarifa kwamba anatakiwa kusafiri kwenda Israel serikali ikimpa ahadi ya kufanya uchunguzi wa walio husika na vifo vya familia yake lakini pia serikali ilimpa ahadi kwamba mkewe na mwanae walikuwa wamehifadhiwa ndani ya eneo ambalo lilikuwa salama, yeye alitakiwa kufanya kazi kwa amani huko alikokuwa anaenda.
Hakuwa mjinga kuwaamini watu hao kuhusu familia yake kuwa salama japo hakuwa na namna kwani kama angegoma alijua wazi kwamba alikuwa anaenda kufa. Zoezi hilo akaliacha kwenye mikono yangu mimi niweze kukutafuta wewe na mkewe na kukuweka kwenye mikono yangu mpaka siku ambayo angerudi na kama ikitokea hataweza kurudi basi mimi niwe mzazi wako kwa niaba yake. Aliniachia mali zake zote ndiyo maana tangu uweze kujitambua uliniona mimi kama mtu mwenye mali nyingi ila zile zote ni mali zako ambazo nyingi alirithi kutoka kwa baba yake kwa sababu ndiye mtoto pekee ambaye alibaki hai wakati ule.
Siku ile Christian alitoweka kwenye macho yangu akiwa na haraka na huzuni, sikujua japo nilihisi kwamba huenda ndiyo ilikuwa siku ya mwisho ya mimi kumuona rafiki yangu kipenzi, binadamu ambaye akili yake ilikuwa chanzo cha kuupoteza mwelekeo wa maisha yake. Christian aliniaga akiwa anamwaga machozi ila alikubali kwenda na maamuzi yale ili kumlinda mtoto wake wa pekee, mtoto ambaye ni wewe hapo Edison.

UKURASA WA 23 unafika mwisho.
 
3500 tu kumalizia mpaka mwisho 106.

0621567672 (HALOPESA)..
WhatsApp

0745982347 (M-PESA)

0714581046 (TIGO-PESA)

FEBIANI BABUYA
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 24

EDWARD PANDE
Hili ni jina langu mimi, sina historia ndefu ya maisha yangu kwa sababu maisha yangu yalianzia pale ambapo mimi nilijikuta naishi wakati akili yangu inaanza kutambua mema na mabaya ya ulimwengu. Siwezi kusema nilizaliwa ila naweza kusema nilijikuta naishi Ujiji Kigoma kwa mwanamke mmoja ambaye alikuwa anafanya kazi ndani ya shirika la wakimbizi ya UNHCR huko Kigoma.
Siku ambayo akili yangu ilianza kukomaa mama huyo alinikalisha kitako, akaniambia kwamba yeye aliniokota mimi nje ya kanisa, kuna mtu alimuona hapo akianiacha kwenye kikapu ambaye ni mwanamke na bila shaka huenda alikuwa ni mama yangu mzazi. Mwanamama huyo alidai kwamba hakujua mtu yule aliacha nini pale na kwa sababu eneo lile lilikuwa likitumiwa na watu wengi basi akahisi huenda wanaweza kuwa magaidi wanaotaka kuua watu waliweka bomu ukizingatia Kigoma ni karibu na Kongo ambako vita zinapiganwa kila siku ya Mungu hivyo akakimbilia eneo lile kujua kwenye kikapu kuna kitu gani.
Ndani ya kikapu, alidai kumuona mtoto mwenye afya ambaye alijaa tabasamu, tabasamu la kutojua alikuwa ameachwa wapi au kutelekezwa malaika yule, alipo mwangalia mtoto yule na kumgusa kidogo, mtoto alicheka na kufurahi huku akiung’ang’ania mkono wake kwa vidole vyake ambavyo havikuwa vimekomaa bado. Kung’ang’aniwa na mtoto yule kukashusha chozi lililokuwa linaongea mengi moyoni mwake.
Hakulia kwa sababu tu ya kusikitika kwa mzazi ambaye alimtelekeza mtoto mzuri kama yule ambaye alimuona kwenye macho yake bali alilia kwa sababu hakuwahi kuipata hisia ya namna hiyo. Kwenye maisha yake alitamani siku moja aamke na kukuta tabasamu la mtoto pembeni yake akiwa amemng’ang’ania na kumsumbua kwa kilio ama kicheko lakini haikuwa bahati kwake. Ni miaka kadhaa ilikuwa imepita tangu alipo olewa na mwanaume ambaye alimpenda lakini aliachwa baada ya kupimwa hospitali na kuonekana kwamba hana uwezo wa kuzaa kwenye maisha yake hali ambayo ilifanya aondolewe kabisa kizazi, likawa pigo kubwa kwenye maisha na mume akamkimbia kwa dhihaka ya kutokuwa na uwezo wa kuzaa huku akidai kwamba mwanamke huyo hakuwa na maana tena ya kuwa hai.
Jambo hilo ndilo ambalo lilimfanya atoe chozi kwa hisia kali, alijiona mwanadamu asiye kamilika mbele za Mungu, alikumbuka miaka hiyo alitumia muda mrefu kumlaumu Mungu kwa kumleta duniani na kumpa adhabu kali namna hiyo, alitamani asingezaliwa kwa sababu wanadamu wasingekuwa na namna ya kumdhihaki au kumtusi mambo ambayo yaliuvunja vunja moyo wake. Huyo mtoto ambaye alimuona mbele yake ilikuwa ni kama nafasi nyingine ambayo Mungu alimpa kwenye maisha yake, lilikuwa tumaini jipya la upendo na hata chozi lake lilipo mdondokea mtoto yule, mtoto alitulia na kumwangalia mwanamama yule kwenye mboni yake ya jicho wote wakatabasamu. Hakujiuliza mara mbili tena alimbeba yule mtoto na kuondoka naye ili akamlee mwenyewe kwa mikono yake.
Hakutaka kujua historia ya mtoto kwa sababu hakuna ambaye angekuwa na uwezo wa kumpatia, hakutaka kujua kuhusu maisha ya nyuma tena ila kwa wakati huo kwenye moyo wake alijiambia kabisa kwamba tayari alikuwa na mtoto wake, huyo kwake alikuwa ni mwanae wa damu ambaye asingeruhusu mtu mwingine aje kumtoa kwenye maisha yake. Yale maisha yakukosa furaha yalikoma, akapata sababu ya kuwa hai, akampata mtu wa kumfanya awe anawahi kurudi nyumbani, Mungu akampa jukumu jipya la kulitimiza kabla ya kumaliza muda wake wa kuwa hai hapa duniani. Hakusita, akampenda yule mtoto ambaye alimpa jina la Edward.
Alimlea kwa upendo, alimpa kila kitu, alimsomesha kwenye shule bora ili baadae yake ije kuwa njema huku muda mwingi akishinda naye kwenye zile kambi za wakimbizi ambako alikuwa anafanya kazi hali ambayo ilimfanya Edward kujenga urafiki na watu wengi wa kule na kuelewa namna watu walivyo teseka na maisha na hawana nyumbani, hiyo ikawa ni ishara nzuri kwake kuweza kumfanya kupaheshimu kwao na mama yake mpaka siku alipokuja kusimuliwa na kuelewa kwamba yule hakuwa mama yake mzazi.
Edward aliye zungumziwa hapo, ni mimi hapa mwenyewe. Mimi ndiye huyo mtoto ambaye aliokotwa siku ile pale kanisani na ndiye mimi huyu niliyepata nafasi ya kuyaeleza haya kwako leo Edison ili uilewe na ikiwezekana kuikumbuka historia ya maisha yako kwa sababu nina uhakika mpaka sasa hakuna jambo unalikumbuka na sababu ambayo inafanya baadhi ya watu kukuwinda sana wewe.
Kufanya kazi kwenye shirika la wakimbizi kulimfanya mama yangu mlezi kuwa na maisha safi hivyo nami nikawa napata kilicho bora. Ubora wa kila kitu ulinifanya kusoma shule zenye hadhi ya juu hapa nchini ambapo nilipofika elimu ya upili ndipo nilikutana na rafiki wa maisha yangu, hapa namzungumzia Christian ambaye ni baba yako mzazi. Mimi na Chris tulishibana vilivyo, tulimshika elimu, tulikuwa na maarifa makubwa ndiyo maana tukaendana lakini siku zote “Siku ya kufa nyani miti yote huteleza” Miti iliteleza kwangu, mama yangu mlezi alipatwa na tatizo kazini, maendeleo yake yaliwashtua wenzake, wivu ukatawala sehemu kubwa ya maisha yao wakatafuta namna ya kummaliza.
Mama alitengenezewa kesi ya kulihujumu taifa, ile kesi ya uhujumu uchumi haikumuacha salama, ilifanya wabebe kila alichokuwa nacho. Hakuweza kuhimili yale maumivu, alipatwa na presha ya moyo ambayo iliyachukua maisha yake, akapotea kama kiza kinavyopotezwa na ujio wa mwanga wa jua kila ifikapo asubuhi ya siku mpya. Kupokea taarifa ile yalikuwa ni maumivu ambayo binafsi nilitamani ningekufa kabla yake ama ningekufa kabla ya mambo yale kutokea. Ukiachilia mbali nilivyokuwa nampenda mwanamke yule lakini maisha yangu yaliutegemea mkono wake kwa asilimia miamoja, sikuwa na jambo, sikuwa na lolote wala chochote, yeye ndiye alikuwa kila kitu kwangu hivyo kuondoka kwake ni kwamba aliondoka na kila kitu changu nami nilitakiwa kuanza na moja kwenye maisha. Nilibaki nimehamaki nikihesabu mawingu hewani, hakuna cha maana ambacho akili yangu ilikiwaza kwa wakati ule zaidi ya kuuchukua uhai wangu.
Niuchukue uhai? Hapana, nitamjibu nini Mungu siku ya mwisho kwa kuuchukua uhai ambao alinipa yeye bure? Niliogopa hilo nikabaki nimejiinamia nalia kwa uchungu. Nilijua baba yako angekuwa na uwezo wa kunisaidia kwa sababu kwa muda ambao mimi nilikaa naye nilijua kila kitu kuhusu maisha yake lakini kwanini nimpe mtu mwingine mzigo ambao natakiwa kuubeba mwenyewe? Sikuruhusu hilo litokee, nikaamua kuondoka kwenye maisha yake na kwenda mbali. Sikwenda mbali na nchi mbali nilikwenda mbali na macho yake huku nikimuahidi kwamba ipo siku ningekuja kumtafuta baada ya mambo yale ya familia kukaa sawa kama ilivyokuwa mwanzo.
Maisha yangu hayakuwa na mwelekeo kwa wakati ule mpaka nilipopita sehemu nikasikia redio ikitangaza nafasi za jeshi, sikuwahi kulipenda jeshi ila lile tangazo liliiamsha akili yangu kwa kupata njia pekee ambayo huenda ingekuwa mkombozi kwenye maisha yangu mapya. Nilitumia nafasi ile kwenda jeshini, sehemu ambako niliyaanza maisha mapya kabisa ambayo sikutaka ukaribu na watu, sikupenda kujihusisha na wanadamu wengine, sio kwamba sikupenda ila sikutaka kwa sababu wanadamu ndio chanzo cha kila jambo ambalo linatokea. Nikajiweka kando pekeyangu huku nikifanya kwa hasira na jitihada kile ambacho kilikuwa kimenipeleka kule.
Maisha yangu ya kule bila kujua yalikuwa kivutio cha wengi, viongozi wa ngazi za juu walipendezwa na aina ya maisha yangu na bila kujua nilikuja kuitwa siku moja na kuhojiwa. Sikuelewa dhumuni la kuhojiwa, nilihisi huenda ni utamaduni wa kila mwanajeshi kuwa vile hivyo nikaendelea na maisha yangu ya jeshi ambayo baadae niliyazoea. Ilipita miezi kumi na mbili ndipo walikuja watu niso wafahamu, watu wale walikuwa ndani ya kaunda suti nyeusi na gari kubwa la kifahari. Sikuwa na hofu kwa sababu walikuja ni kambini lakini muda ambao walikuja haukuwa rafiki kwa mazungumzo kwani wenzangu walikuwa wamelala ila mimi nilikuwa nafanya mazoezi.
Ilikuwa ni kawaida yangu kufanya hivyo na viongozi wengi pale kambini walinizoea hivyo halikuwa jambo la kushangaza, watu wale walinihoji kwa muda wa nusu saa kisha akaitwa mkuu wa kambi na kuniambia kwamba nilitakiwa kuondoka na wale watu, nikaduwaa! Ni akina nani wale watu ambao nilipaswa kuondoka nao? Mkuu hakuniambia ila alinipa pongezi nyingi na kunitakia kila lakheri kwenye majukumu yangu mapya, sikujua anamaanisha nini mpaka tulipotoka pale ndipo niligundua kwamba nilikuwa nimechaguliwa kujiunga na idara ya usalama wa taifa ya nchi iliyokuwa inamiliki shirika la kijasusi liitwalo IBA (INVESTIGATION BUREAUCRACY AGENCY).

UKURASA WA 24 unafika mwisho.
 
Back
Top Bottom