Simulizi ya kijasusi: Nafsi zilizotelekezwa

Simulizi ya kijasusi: Nafsi zilizotelekezwa

HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 97

Safari yake ilikuwa ni kuelekea Kinondoni na alikuwa nyuma ya muda hivyo aliitoa gari yake kwa spidi kali mno, kama angekutana na kitu chochote hata kidogo tu barabarani basi angepata ajali moja mbaya ambayo isingeacha hata mfupa wake ukiwa salama. Alifikia kindondoni kwa muda mfupi kutokana na spidi yake, ilikuwa ng’ambo ya eneo kubwa ambalo huwa linatumika kama mnada na muda mwingine watu kufanyia kampeni za biashara zao au siasa ambalo lipo karibu na makao makuu ya OPEN UNIVERSITY ila yeye alikuwa kwa ng’ambo yake.
Kulikuwa kweupe, alikuwa anaonekana mtu mmoja mmoja wengi wakiwa ni wale ambao walitoka kwenye starehe. Watu walionekana kutopita pita kutokana na kwamba eneo hilo Tanesco walikuwa wamepita na umeme wao hivyo maeneo mengi yalikuwa na kiza. Alikunja kushoto kuifuata barabara nyingine ya lami ambayo alinyoosha nayo kwa dakika moja akaiacha gari yake na kubeba silaha zake ambazo zilikuwa kwenye buti yake ya gari. Alitembea kwa dakika moja nyingine akawa amelifikia jengo moja kubwa la kifahari, sehemu hiyo yalikuwa ni makazi ya siri ya mkurugenzi wa shirika la kijasusi la nchi na usalama wa taifa kwa ujumla.
Mwanamama huyo masaa kadhaa nyuma ndiye ambaye alisababisha Aaliyah kuuawa mbele yake lakini kabla mrembo huyo hajafa, alimuomba ahakikishe anamuua mama huyo kwa ajili yake huku akisisitiza kwamba mama huyo kama angeendelea kuishi basi huko mbeleni kungekuwa na matatizo zaidi ya hapo ambayo yalitokea. Mwanamama huyo alikuwa ni mtu wa siri kwa sababu kipindi hicho serikali haikuwa ikiwatangaza hadharani wakurugenzi wa eneo hilo nyeti la usalama kwa sababu za kiusalama hivyo ikapelekea kutokujulikana kabisa kwa watu.
Kutofahamika kwake kulimfanya kuwa na maisha ambayo sio ya ulinzi mkali kila sehemu ili kutoleta maswali mengi kwa watu, alikuwa na nyumba zake nyingi lakini hiyo ilikuwa ni sehemu yake ya siri ambayo mara nyingi alikuwa akiitumia kwa ajili ya kupumzika baada ya kukamilisha mambo yake na eneo hilo lilikuwa na ulinzi lakini walinzi hawakuwa wengi ili kutozua maswali kwa watu wa Kinondoni kwani kushinda na ulinzi mkali awapo maeneo hayo ingezua minong’ono ambayo huenda ingepelekea watu kuanza kumhisi ama kujua anacho kifanya na jambo hilo lingekuwa ni hatari kwa usalama wake na siri za nchi kwani yeye alikuwa ni miongoni mwa watu ambao walikuwa na siri nyingi za taifa.
Kwenye mkono wake alikishika kisu ambacho alikuwa anakiangalia kisha anaukadiria ule ukuta kwa sababu ulikuwa mrefu kiasi, alihema mara moja akauparamia ukuta ule ambapo alichomeka kisu kile akakiacha kimeshika ukutani, alikitumia kama ngazi akakikanyaga na kurukia juu ya ukuta baada ya kugundua kwamba ukuta ule haukuwa na nyaya za umeme zaidi ya Vyuma vikali. Alichungulia ndani kwa sababu nyumba hiyo ilikuwa na umema kwa mbali aliona kuna watu wanaranda randa wakiwa na silaha, aligundua kabisa ni wanajeshi, aliishikiza miguu yake kwenye vile vyuma akainamia ule upande wa chini alipokuwa amekichomeka kisu chake kikali, alifanikiwa kukishika na kukichomoa.
Baada ya hapo alijigeuza na kujivutia tena juu, aliruka sarakasi akatua ndani akiwa anakizungusha kisu hicho kwa hasira kali. Alizunguka nyuma akamuona mwanaume mmoja akiwa anaangalia kila upande, alihisi kama aliona kivuli ila hakuwa na uhakika, alirudi nyuma kwa wasiwasi akiwa makini lakini kwenye kona ambayo alifikia ndipo alikuwepo Edison, alimdaka na kuzamisha kisu kwenye shingo yake kwa nyuma, aliichana vibaya na kumtupa mtu huyo hakuwa anafaa tena.
Alizungukia kwa mbele akawaona wanaume wawili wakiwa wanapiga stori, hawakuwa na bahati kuwa kwenye kazi kama hizo halafu wanaziachia. Alikirusha kile kisu ambacho kilitua kwenye paji la uso la mwanaume ambaye alikuwa upande wake wakati huo alikuwa anaenda kwa zigzaga kuelekea hilo eneo, mwanaume ambaye alimshuhudia mwenzake akipingwa kisu cha paji la uso alipigwa na butwaa lakini aligundua kwamba mvamiaji alikuwa nyuma yake, alihitaji kugeuka ila alitulia, kitu cha baridi kilikuwa shingoni kwake. Ni ule upanga ambao aliupenda ulikuwa kwenye mkono wake
“Bosi wako yuko wapi?” mwanaume huyo hakujibu bali alijaribu kutaka kufanya hila kuweza kukabiliana na mtu huyo, alionjwa kidogo shingo ikachanika ikamlazimu kuwa mpole.
“Yupo ndani ghorofa ya pili, kuna mlango mkubwa mwekundu hicho ndicho chumba chake”
“Funguo za huo mlango ziko wapi?”
“Anazo Batoni”
“Batoni ndo nani?”
“Mlinzi wetu mkuu wa hii nyumba”
“Yuko wapi?”
“Yupo ghorofa ya kwanza”
“Huwa anakaa hapo kwa masaa yote?”
“Ndiyo mpaka bosi aamke”
“Mpo wangapi humu ndani?”
“Walinzi tupo sita”
“Hao wawili wengine wako wapi?”
“Wapo sebule…..” hakumaliza sentensi yake alimaliziwa kwa risasi kutoka kwenye bastola ambayo ilikuwa imewekewa kiwambo cha kuzuia sauti.
Aligonga mlango wa kuingilia ndani kistaarabu, kwa ndani zilisikia hatua taratibu zikielekea mlangoni. Mlinzi wa ndani bila shaka alijua kwamba alikuwa ni mwenzake hivyo hakuona taabu kumfungulia, wakati amefungua alibaki ameduwaa akiwa anamkagua mtu huyo kuanzia juu mpaka chini, alikuwa tofauti kabisa ndipo alishtuka akihitaji kunyoosha bastola ambayo ilikuwa kwenye mkono wake. Ulikuwa muda wa mahesabu kwenye biashara, kichwa chake kilifumuliwa kwa risasi akadondoka chini kama gogo.
Kudondoka kwake ndilo kulimshtua mwenzake ambaye alikuwa ameketi kwenye sofa akiwa anasinzia, wote hao walikuwa ni maafisa usalama. Mwanaume yule kushtuka kwake lilikuwa somo jipya endapo angelipata nafasi ya kuweza kuishi kwa mara ya pili, angehitaji kulala hakutakiwa kuwepo kwenye hiyo kazi. Edison alikanyaga kwenye sofa likampa lifti kwa sarakasi ambapo alitua karibu na alipo mwanaume yule, kutua kwake pale kisu kikali kilizama kwenye koo lake akaongezwa risasi ya mdomoni habari yake ikaisha hapo, Edison akaitupa na bastola yenyewe kwa sababu risasi zilikuwa zimeisha hivyo haikuwa na kazi tena wakati huo.
Alitembea taratibu kwenye ngazi kupandish ghorofa ya kwanza mkononi akiivaa ile chuma ya mviringo huku mkono mmoja akiwa na upanga ambao alikuwa anaubana kwenye koti jepesi ambalo lilikuwa kwenye mwili wake. Aliona kama kivuli kinakuja kwa chini akainama, risasi ilipita juu yake ikaenda kukita kwenye ukuta na kuchimba chimba eneo hilo, aliurusha ule upanga ukakita kwenye ukuta kwa sababu mhusika aliukwepa. Bastola ilifungwa kwenye kiwambo chake ili ikitokea dharura walinzi hao waweze kuzuia makelele kumpata bosi wao.
Alijua hali hiyo haikuwa njema hivyo wakati bwana yule anarusha risasi alitembea kwenye vyumba ambavyo vilijengwa pembezoni mwa ngazi zile ili kutengeneza balansi nzuri wakati mtu anashuka na kupanda. Alitua karibu na alipo mwanaume yule aliyekuwa na sura ngumu na nyeusi isivyo kawaida, bwana yule alijivuta akiachia risai nyingine ambayo ilitoboa koti la Edison ila haikumpata kwenye mwili wake.
Alirusha mkono wake ambao ulikuwa na ile chuma, bwana yule aliipangua ila alirudi nyuma kwa maumivu kwani mkono wake ulikutanishwa na chuma na sio mkono. Alitaka kuinyanyua tena ile bastola yake ila wakati huo hakupewa nafasi nyingine, baada ya kukutanishwa na chuma cha kichwa kisha akaguswa mbele ya mguu wake ambapo aliyumba akakutana na buti la uso, hakukumbuka hata bastola aliko irushia. Alirudi akiwa na jaziba akiwa anairusha mikono yake yote miwili kwa pamoja, aliizungusha ngumi kwa umaridadi mkubwa ikamkosa Edison na kukita ukutani ambapo mkono huo ulidakwa na kuvutiwa pembeni ukashushwa kwa nguvu.
Mkono ulishushiwa lile eneo ambalo upanga ulikuwepo, hivyo kiganja cha mkono kiliachana na mkono wenyewe, bwana yule aliangalia wakati anaona kiganja chake kinaachiwa chini akaanza kulia. Haikutakiwa kelele, aliinama akihema baada ya kugundua kwamba kisu kilizama katikati ya kifua chake, kilishusha chini kukipasua kifua hicho mithili ya kuku wa sikukuu ambavyo huwa anapasuliwa na mtu mwenye uchu mkali kwa kuipania sikukuu hiyo.

UKURASA WA 97 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 98

Kifua kilipasuliwa kiasi kwamba viungo vya ndani vikawa vinaonekana huku damu ikiwa inaendelea kumwagika. Alishuka chini taratibu, Edison aliona mtu huyo anampotezea muda, alimshona buti la kichwa ambalo lilimbamiza ukutani kichwa kikapasuka vibaya. Aliinama na kuingiza kwenye mfuko wa bwana huyo akaipata funguo ambayo aliitumia kufungulia mlango wa mkurugenzi mwenyewe baada ya kupandisha ile ghorofa ya tatu. Aliingia ndani na kumkuta mama huyo akiwa amelala fofofo asijue dunia ilivyokuwa inaenda, aliwashangaa taa kubwa ukiachana na ile ya kitandani ambayo mhusika alisahau kuizima, akaketi kwenye kiti kuangalia mazingira ya ndani ya chumba hicho kilivyokuwa kimejaa vitu vya bei ghali zikiwa ni kodi za wananchi.
Aliangaza kila sehemu mpaka alipofanikiwa kuyaona maji kwenye bilauri karibu na alipokuwa amekaa kwani kiti hakikuwa mbali na kitanda. Aliyachukua na kummwagia mama huyo, alishtuka akiwa anasonya na kutukana matusi mazito ya nguoni, wenge lilimuisha baada ya kuiona vizuri sura ambayo ilikuwa mbele yake ikiwa inamtazama kwa macho makali.
“Walinz……”
“Acha kunipigia kelele, kama walinzi wako wangekuwa hai basi mpaka wakati huu mimi nisingefanikiwa kuwa humu ndani”
“Hili jambo tunaweza kulizungumza mimi na wewe, naweza kufuta kesi zako zote nikakupeleka mbali ukaendelea na maisha mengine ya kawaida” mheshimiwa alianza kujihami mapema kwa sababu hakuwa na msaada. Hata ule usingizi fofofo haukuwepo tena, ungemuona basi usingesita kumfananisha na yule mtu ambaye alitoka kufanya mazoezi yaani alikuwa vyema kumzidi hata yule bondia Michael Tyson.
“Hayo ni maneno ambayo huwa unayatumia kuwahadaa watu ambao unataka kuwafanyia ubaya huku ukitia huruma, watu hao wakihadaika tu wakajisahau huwa unaitumia nafasi hiyo kuweza kuufanya ushetani wako. Najua kila kitu kuhusu wewe hivyo sitahitaji mambo mengi kutoka kwako, sababu kubwa ambayo imenileta mimi hapa ni kukuua wewe ila kabla sijafanya hivyo nahitaji uweze kuniambia kwanini umemuua binti asiye na hatia kama yule?”
“Hakuna mtu ambaye nimemuua huenda kuna mtu amekupa taarifa zisizo sahihi”
“Wale vijana wako wamekuja, nikamoji wa mwisho kabla sijamuua ila kinacho niuma ni kwamba nimeshindwa kumsaidia Aaliyah hivyo naye amekufa, kabla ya kufa ameniomba kwa gharama ya damu yake wewe ufe. Sasa nataka kujua sababu ya msingi ya wewe kumtoa sadaka binti ambaye alikuwa anafanya kila kitu kwa ajili yako na taifa lake”
“Alianza kunifuatilia ndilo kosa lake kubwa”
“Unahisi unastahali kuishi kwa hilo?”
“Mimi naweza kukupa kila ambacho unakitaka, tafadhali usiniue”
“Nikikwambia nirejeshee baba yangu utaweza, nikikwambia namtaka mke wangu na mwanangu utawarudisha? Nikikwambia zile NAFSI TISA ZILIZO TELEKEZWA za makomando wenzangu unaweza kuzijeresha? Jibu ni hapana maana yake hakuna kitu unaweza ukafanya cha kukuweka wewe huru”
“Usifanye hiki unacho taka kukifanya, kumuua kiongozi mkubwa kama mimi hii itakufanya utafutwe hata kwenye mashimo na hautafanikiwa kupona kwa sababu hata raisi hatakuacha hai”
“Nimeua wengi sio wewe tu, kama nimemuua makamu wa raisi itakuwa mtu kama wewe? Huyo raisi wako unaye msema hapo ameniomba tuoane na naenda kuonana naye baada ya kukuua wewe. Anahitaji kuiteketeza jamii hii kwani amechoka hivyo hayupo upande wako” yale maelezo yalimchanganya Lionela Philson, alibaki kama amewehuka akiwa anacheka cheka mwenyewe, alinyanyuka kwenye kile kitanda na kuanza kukimbia lakini alidakwa, akiwa amejifunika taulo tu ambalo baada ya kuanza kukimbia alibakia wazi kabisa bila nguo. Edison alimpiga alama ya X kwenye tumbo mwanamama huyo kwa kumcharanga na upanga wake kisha akausokomezea tumboni ambapo alijinyonga nyonga na kwenda kudondokea kitandani. Alichukua muda mfupi mpaka akapoteza maisha, mwanaume alimwangalia mwanamke yule akiwa anasikitika, alikuwa amechelewa ikambidi kutoka haraka kuelekea gerezani ambako walikubaliana kukutana na mheshimiwa raisi.

Saa nane na nusu, CDF alikuwa nyumbani kwake. Ni muda mfupi tangu alipokuwa ametoka kukutana na Edison, mauaji aliyo yashuhudia yalikuwa yanajirudia kwenye kichwa chake jambo ambalo lilizidi kumpa hofu moyoni. Hakuwa na uhakika kwamba jambo hilo lingeishia wapi kwa sababu kama angekosea kuchagua basi ingekula kwake. Alikuwa amekaa kwenye balcony akiwa anakunywa pombe kali ili kuweza kupooza machungu na kujisahaulisha majanga yote yaliyokuwa yametokea siku hiyo.
Simu yake ambayo ilikuwa pembeni iliita, aliangalia muda ulikuwa umekwenda isivyo kawaida, simu ile ilikuwa ni namba ngeni, akaipokea haraka.
“Pole sana nasikitika kwamba hautakuwa na muda hata wa kuweza kuungama dhambi zako” simu ilimpa hiyo taarifa ikakata, alibaki anajiuliza ni nani ambaye alimwambia maneno yale na alikuwa na maana gani hasa usiku huo. Aliwaza na kuwazua kuna kitu akaona hakikuwa sawa, sehemu ambapo alikuwepo umbali wa mita kama miatatu alikuwa anatazamana na jengo moja refu, kwenye jengo lile kuna sehemu aliona kuna tundu ambalo lilikuwa na mwanga.
Akili ilimjia kwamba mtu yule ambaye alimpigia simu alikuwa anamuaga kumpa taarifa ya kwamba alikuwa anakufa wakati huo. Alipo unganisha matukio hayo mawili aligundua kwamba eneo lile lilikuwa na mdunguaji, alijiuliza mdunguaji huyo alijuaje kama yupo pale muda ule, jibu ni kwamba walinzi wake ndio walimsaliti. Akili ya kukimbia ilimjia kwa kasi, alinyanyuka ili akimbie kwa kuwa aliziamini hisia zake kwamba kwenye lile jengo kulikuwa na mdunguaji. Alikuwa amechelewa, muda ambao aliutumia kuzichambua taarifa hizo ulikuwa ni mwingi mno hivyo mpaka anafanya maamuzi ya kukimbia risasi mbili zilitua kwenye kichwa chake. Alidondoka na kupoteza maisha kimasiara tu akiwa anajipooza machungu, alitakiwa kwenda kujitetea na dhambi zake mbele ya safari.

Barabara ilikuwa nyeupe wakati huo ilikuwa inaelekea saa kumi ya usiku. Gari ya Edison (EdJr) ilikuwa kwenye mwendo mkali kuweza kuwahi kuonana na raisi wa nchi, alikuwa yupo nyuma ya muda ambao walikubaliana. Spidi yake haikuwa ikielezeka huku watu wachache hususani ambao walikuwa wamewahi kuanza kujihangaisha walishangaa kuona mtu akitembea namna hiyo hata wale ambao hawakuwa na makazi waliamshwa na tukio hilo lakini hawakujali kwa sababu haikuwa biashara yao, kila mtu anajali tumbo lake kwenye hili jiji na si vinginevyo.
Ilikuwa inagota saa kumi ndipo alikuwa anaingia kwenye kituo cha mwendokasi ya Gerezani, palikuwa kimya huku getini pakiwa na walinzi kadhaa ambao walikuwa na suti zao, aligundua kabisa kwamba walikuwa ni walinzi wa Ikulu. Alishuka kwenye gari akakaguliwa, baada ya kuona yupo sawa aliruhusiwa kupita ambapo kwenye gari moja ya mwendokasi aliona kuna watu wawili, mmoja alikuwa ameketi na mwingine alisimama, aliona baada ya taa ya gari hiyo kuwashwa akajua ndilo eneo sahihi.
Hatua zake zilielekezwa huko na baada ya kufika, mwanaume aliyekuwa amesimama alikuwa ni mlinzi mkuu wa raisi na aliyekuwa amekaa alikuwa ni raisi mwenyewe. Mlinzi alitoa ishara ya heshima kwa Edison (alikuwa na taarifa za mwanaume huyo na kazi ambayo aliwahi kuifanya miaka ya huko nyuma akiwa ndani ya jeshi) kisha akatoka nje kuwaacha watu hao wawili wakiongea.
“Ni zaidi ya dakika ishirini zimepita nikiwa nakusubiri hapa” ilisikika sauti ya raisi wakati Edisona anasogea ile sehemu ambayo alikuwepo.
“Nilipitia kwa mkurugenzi”
“Wa IBA?”
“Ndiyo”
“Ulikuwa na mazungumzo yapi mpaka uwe na hiyo nafasi ya kukutana naye?”
“Nimetoka kumuua” raisi alimwangalia mwanaume huyo kwa umakini mkubwa kwa sababu lilikuwa ni jambo lingine kubwa mno, huyo alikuwa ni moja ya viongozi wakubwa nchini, kifo chake kingeenda kuleta athari kadhaa hususani kama kuna watu wangeenda kuujua ukweli.

UKURASA WA 98 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 99

“Unahisi ni wazo zuri kwa huo uamuzi ambao umeufanya?”
“Amemua Aaliyah ambaye wakati anakufa aliacha hilo kama ombi lake la mwisho kwamba nihakikishe namuua mwanamama yule kwa sababu kuishi kwake lingekuwa ni tatizo lingine kwani ana watu wengi ambao anandelea kuwasambazia propaganda hivyo kuishi kwake ingekuwa ni hatari ama kupanda kirusi kingine”
“Aaliyah amekufaje?” raisi aliuliza ikiwa ni ishara ya kutozipenda taarifa hizo kabisa kwani alikuwa na mipango mikubwa na binti huyo kwa baadae.
“Walitumwa wale wenzake kuyaondoa maisha yake, kwa bahati mbaya nimeua wote lakini nimeshindwa kuyasaidia maisha yake ilikuwa ni ghafla na kabla ya kufa yeye ndiye ambaye amenielekeza kuhusu wewe hivyo tunaweza kwenda moja kwa moja kwenye jambo ambalo limetukutanisha hapa” Mheshimiwa Faraj Asan alionekana kusikitishwa na jambo hilo, aliangalia nje ya eneo hilo kuangalia namna jiji lilivyokuwa likimeta meta kwa mataa safi ambayo yalikuwa yanamulika kila pembe.
“Kuna kipindi nimewahi kutamani siku moja nikae maisha ya kawaida ya amani kabisa eneo lenye uoto wa asili na utulivu. Niwe na uwezo wa kuangalia asili ya dunia na viumbe vyake, niwe nalishuhudia jua likichomoza na kuzama kwa utulivu bila kelele na watu wala kumkera mtu ama kumwaga damu yake. Ni maisha ambayo yameishia kuwa ndoto tu kwa upande wangu kwani kila ninapo jaribu kushindana nayo naishia kujiumiza mwenyewe ila huu ni wakati ambao natarajia kuipata hali hiyo japo mara moja na hata kama nitakufa basi nife kwa amani. Sikutaka kuishi hivi, hata hiki kiti sikuwahi kukipenda kutoka moyoni ila niliwekwa na watu ambao hawakunipa chaguo lingine zaidi ya kufanya hivi” Mheshimiwa alizama kwenye hisia nzito akikielezea kiti chake cha uraisi ambacho ni wazi hakuwa akikifurahia bali hakuwa na namna ya kuweza kufanya.
“Bado haujaniweka wazi sababu ya kuniitia hapa” Edison alimkumbusha baada ya kuona amezama zaidi kwenye hisia zake binafsi.
“Nimefanya tafiti juu ya jambo la baba yako, ni kwamba kweli alipelekwa huko Israeli kufanya kazi na MOSSAD, jambo ambalo sikuwa nikilifahamu ni kwamba kiongozi wa hii jamii ni mwanamke, nimesikitika pakubwa mno. Mwanamke huyu baada ya kuikimbia nchi yake alikuwa na mpango wa kuweza kulipiza kwa nchi yake hivyo kumtuma baba yako huko Mossad ulikuwa ni mojawapo ya mpango wake wa kufanya malipizi, alifanyaje?”
“Anajua kwamba MOSSAD wanafanya kazi kwa ukaribu na CIA hivyo hizo taarifa ambazo zingekuwa na madhara kwa KGB na Urusi kwa ujumla lazima MOSSAD wangezifikisha kwa CIA. Hivyo baba yako alienda huko kusaidia kuwatengenezea formula za utengenezaji wa mabomu hatari ya nyukilia na baada ya hapo ndipo wakafanikiwa kumuua. Inasemekana kwamba hajaishia hapo tu bali huwa anaendelea kuvujisha siri zake kwa CIA mpaka leo kuhusu Urusi na kwa sababu alikuwa ana taarifa nyingi huwa zinawanufaisha CIA pakubwa.” Alitulia kidogo na kuangalia saa yake kisha akaendelea
“Sasa lengo langu la kukuitia hapa ni kwamba nahitaji tufanye kazi pamoja, nategemea tutafanikiwa lakini kuna kufeli. Kufeli kwa kazi hii ni kufa kwa mmoja wetu kati yangu mimi na wewe lakini kwa mazingira yalivyo ni mara mia nife mimi. Muda mfupi uliopita mkuu wa majeshi ameuawa (Ni taarifa iliyo mshtua sana Edison kwa sababu muda sio mrefu alikuwa na mtu huyo) hivyo kwa sababu hata mkurugenzi umemuua maana yake viongozi wa ngazi za juu wote hawapo na ni hatari japo ni faida kwa upande wetu pia kwani mashambulizi hayatakuwa makubwa. Nitamtoa waziri mkuu kwenye nafasi yake ili tupate mtu mwingine, mtu mmoja ambaye amebaki sina wasiwasi naye jaji mkuu ambaye anaweza kukaimu nafasi yangu kama ikitokea nikifa kwahiyo huyu nitaongea naye ili likitokea lolote nchi isije kurudi kwa hao watu kwa mara nyingine” alitulia akizama fikirani kisha akameza mate na kuendelea kwani haikuwa raisi kuzungumzia kuhusu kuishi kwake ama kufa;
“Mimi nitafanya kila linalo wezekana kuhusu viongozi waliobaki na mambo ya usalama kisha wewe nitakupa unacho kihitaji ili tukamilishe zoezi hili nchi yetu irudi kwetu kwa mara nyingine tena. Jambo ambalo ni la msingi zaidi ni kwamba huyu mwanamke anahitajika akiwa hai hatakiwi kufa” kauli nyingine ambayo ilimshtua Edison.
“Amehatarisha usalama wa taifa hili kwa muda mrefu ni miaka kama thelathini sasa, kwanini aendelee kuwa hai?”
“Unajua saivi duniani vita baridi imekuwa ya moto na haishikiki, muda mrefu tumeonekana kama tumeegemea upande wa Marekani pekee jambo ambalo linaweza kuwa na athari kwa upande wetu kama mkeka utabadilika, kwa maana hiyo tunatakiwa kucheza kote na upande wa Urusi pia na huu unaweza ukawa mwanzo mzuri kwetu. Urusi wametumia mabilioni ya fedha kumtafuta mwanamke huyu bila mafanikio kwa sababu ana taarifa nyeti ambazo huwa wanahisi sio salaam kama zote zikienda kwenye mikono ya maadui zao hivyo sisi tukifanikisha kukamatwa kwake tutakuwa tumejipa pointi kubwa kwa Urusi, tutaimarisha mahusiano yetu kidiplomasia na nchi hiyo jambo ambalo litakuwa na faida nyingi kwetu sisi kwa hapo baadae.”
“Huyu mwanamke anatakiwa kupelekewa kwenye mikono ya KGB kwa mara nyingine kupitia ubalozi wao ambao kwa sasa umefungwa ila watu wao bado wapo kwahiyo mimi nitawasiliana nao mapema hata kama sitokuwepo watu hawa watakusubiri pale, utajitambulisha kwamba wewe ni mtu wangu ambaye ndiye unatakiwa kufika pale kisha utamkabidhi kwao. Hii haitajalisha kama nipo hai au nimekufa huu mpango lazima uwe hivyo kuleta amani ya taifa hili, kama ikitokea sipo na ukapokea taarifa zozote basi mtu wa kwanza ambaye utatakiwa kukutana naye ni jaji mkuu kwa sababu najua wewe utamlinda na kumfikisha Ikulu salama, kama Mungu atanipatia maisha zaidi ya haya basi hili likiisha nitajiuzulu kwenye nafasi yangu. Nakuomba sana kwa ajili ya wananchi pamoja na wale watu ambao wametangulia usipuuzie ombi langu. Ukihitaji jambo lolote muda wowote utaniambia (alimpasia kadi ambayo ilikuwa na namba zake binafsi)” Edison alimwangalia mheshimiwa huyo kwa umakini usoni, uso wake ulikuwa unamwaga machozi akionyesha kumaanisha kile ambacho alikuwa anakiongea. Alisimama na kumpa mkono bila kujibu chochote, raisi huyo alitoka hilo eneo kwa sababu kulianza kupambazuka sasa na ingekuwa hatari kama umma ungejua raisi yupo eneo hilo. Aliondoka akimucha mwanaume kwenye tafakuri nzito juu ya mambo ambayo alitakiwa kuyafanya zaidi kilicho mshtua ni kifo cha mkuu wa majeshi, bila shaka alijua ni wale ambao walikuwa na Nicola, alitulia kwa sababu alijua lazima watamtafuta aende ambako walikuwepo.
Asubuhi kulikucha ila nchi ilikuwa na habari nyingi za kutisha, kiongozi mmoja wa upinzani alitangaza kwenye vyombo vya habari kwamba serikali haikuwa wazi kwa wananchi wake kwa sababu walikuwa wanauficha ukweli. Aliwahakikishia wananchi kwamba taifa lilikuwa kwenye hatari kubwa ila wahusika waliamua kuwafanya wananchi wao ni wajinga na wapuuzi kwa kuwanyima taarifa ambazo zilikuwa ni mhimu kwao. Mpaka wakati huo walidanganya kuhusu kumuua yule komando, alikuwa hai lakini ukiachana na hilo kiongozi huyo alithibitisha kwamba mpaka muda huo makamu wa raisi alikuwa ameuawa lakini serikali iliamua kulikaushia jambo hilo.
Mkurugenzi wa usalama wa taifa na shirika la IBA kwa ujumla naye aliuawa, mkuu wa majeshi alikuwa amekufa ukiacha vifo ambavyo vilipuuzwa vya watu wengine kama kamamda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam, afisa wa polisi Julius Mbandu, wapelelezi wa shirika la IBA na wengine ambao walifanywa kuwa siri kubwa. Kiongozi huyo alidai kwamba hizo habari alikuwa na uhakika nazo kwa asilimia zote miamoja na kama serikali ingesingizia kwamba alikuwa muongo basi aliwaruhusu watu hao wajitokeze hadharani na kama angekutwa anadanganya basi alikuwa tayari kupewa adhabu yoyote kali ya kimahakama kwa kuudanganya umma na kuleta taharuki ndani ya nchi. Mwisho wa yote alidai kwamba inasemekana hata raisi hana mamlaka yoyote ni kibaraka wa watu kadhaa ambao wanaitumia nchi kwa maslahi yao binafsi.
Ni habari ambazo zilizua gumzo jipya nchini, watu walibaki wameduwaa wakiwa hawaamini kama kile ambacho waliambiwa na kukisikia kilikuwa na ukweli wowote ule. Watu walianza kuandamana wakiitaka serikali kujitokeza kujibu tuhuma hizo ukijumlisha hasira walizokuwa nazo kwa vifo kadhaa ambavyo vilikuwa vimetokea nchini walizijumlishia humo humo. Watu walianzisha vurugu mtaani ambapo vituo kadhaa vya polisi vilichomwa ikalazimu jeshi la polisi kuingia mtaani kukamata wachochezi wengine wakipata kipigo kikali huku wananchi wakiendelea kubomoa baadhi ya majengo ya serikali kwa hasira.

Hayo yote raisi alikuwa anayaona na kuyasikia kwa sababu ndiyo ilikuwa habari kubwa nchini asubuhi hiyo na zoezi hilo alijua kabisa lisingeweza kuisha mpaka pale ambapo angejitokeza hadharani kuongea. Kama angeongea kwa wakati huo ingekuwa hatari kwa upande wake hivyo alitakiwa kusubiri lakini wakati huo pia alimuita mlinzi wake mkuu kwani ilikuwa hamsini hamsini kuishi ama kufa, karata yake ilikuwa ni kwa Edison, kama angewapata watu hao haraka basi lazima angeishi ila kama Edison angewakosa watu hao lazima wangemfuata yeye kummaliza.

UKURASA WA 99 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 100

Kuweza kushindana na jambo hilo kwa sababu alikuwa na utayari wa jambo lolote lile alikuwa ameandaa waraka ambao hata angekufa bado ungewasilishwa na kama angeishi basi angeuwasilisha kwa mdomo wake mwenyewe. Alikuwa kwenye ofisi yake ambapo alimuita mlinzi wake wa karibu zaidi ambaye ndiye alikuwa anajua kila kitu chake.
“Tadeo kwa lolote lile ambalo litatokea wewe unatakiwa kuishi kwa gharama yoyote ile”
“Bosi kwanini unaongea hivi?”
“Naweza kuishi au kufa lakini kwa chochote kikitokea basi taarifa hii inatakiwa iwasilishwe kwa wananchi hivyo shika hii bahasha, kama nikifa basi utampatia Edison lakini kama nikiishi taarifa hiyo nitaiwasilisha mwenyewe”
“Unajua kabisa siwezi kuishi kama kuna tatizo litakukuta bosi”
“Hii ni amri sio ombi Tadeo hakikisha inakuwa hivi kwa ajili ya maslahi ya taifa”
“Una uhakika na hili bosi?”
“Ndiyo Tadeo, nahitaji kutulia mwenyewe kwa sasa”
“Sawa bosi” mlinzi wake hakuridhika ila hakuwa na namna kwa sababu hilo halikuwa ombi bali amri ya mkubwa wake. Alitoka kinyonge humo ndani kwa sababu hakuwa na namna ya kufanya.






SURA YA KUMI
MSATA, DAR ES SALAAM
Location ilikuwa inasoma Msata, ilitumwa mida ya saa kumi na mbili jioni kwenye simu ya Edison ikiambatama na maelezo mafupi. Kama alihitaji kumpata mpenzi wake Nicola basi alitakiwa kufika sehemu ambayo location hiyo ilikuwa inamwelekeza. Hilo halikuwa jambo la kupoteza muda tena kwa sababu ndicho alikuwa anakingoja kwa hamu kubwa ili kukata mzizi wa fitna, nafsi yake ilikuwa inamuenda mbio isivyo kawaida kwa sababu huenda ilikuwa ni siku ya kwanza kukutana na mama yake mzazi baada ya miaka mingi sana kupita.
Kutoka Dar es salaam mpaka mpaka kupitia Bagamoyo road yalikuwa yanatumika masaa mawili na dakika arobaini na mbili kufanikiwa kufika huko lakini yeye kwa mwendo ambao aliondoka nao alitumia saa moja na nusu pekee mpaka kutia timu Msata. Alinyoosha na barabara ambayo ilikuwa inaelekea Wami akiwa anaipita miti mingi barabarani kwa kuwa kulikuwa na maeneo mengi ya wazi, alitembea kwa dakika tatu tu ikamtaka akunje mkono wake wa kushoto eneo ambalo lilikuwa na barabara ya vumbi. Alama ile haikuonekana kuwa mbali na pale ambapo alikuwa anakwenda hivyo hata mwendo wake ulikuwa mdogo mpaka pale ambapo alama hiyo ilikita kama alamu inapiga kilele kidoti kile kikiwa kimesimama.
Alijua amefika, aliyainua macho yake kuangalia mbele yake, kulikuwa na jengo moja ambalo lilikuwa kama kiwanda kidogo ambacho kilitelekezwa kwa muda fulani hivi. Hakuamini kwa sababu alihisi lingekuwa ni jumba la kifahari ila hakuwa na namna alishuka ndani ya gari yake, ni ghafla tu walifika wanaume wawili wakiwa na silaha nzito, walimtaka atembe taratibu kuelekea lilipokuwepo lile jengo ambapo alitii amri.

Lango kubwa na gumu lilifunguliwa, hapo aligundua kwamba ndani kulikuwa na walinzi wa kutosha, walimkagua kwenye mwili wake ambapo waifanikiwa kuzitoa bastola mbili na kisu kimoja kikali pamoja na chuma cha kuvaa mkononi. Walimvua hood yake akabakia na vest tu ya ndani ambayo iliwafanya wanaume kadhaa kutoa macho baada ya kuuona mwili wa kidume hicho, mwili ulikubali ukapasuka, sio kwa sababu ya kula sana bali kwa sababu ya kujengwa kwa ukakamavu wa hali ya juu kiasi kwamba ni kama vest ilikuwa inaonewa kuvaliwa kwenye huo mwili.
Alishangaa mbele tena eneo ambalo lilikuwa kama ukuta linajiachia, hapo ndipo alikishuhudia kile ambacho hakukitarajia, yalikuwa mambo makubwa mawili. Jambo la kwanza alimuona Nicola wake akiwa amechakaa kwa mateso ambayo alionekana kuyapitia akiwa amefungwa minyororo miguuni na mikononi wanaume wanne wakiwa wamemzunguka kila mmoja akiwa ameushika mnyororo mmoja. Alishukuru Mungu mwanamke huyo kuwa salama lakini pia alijisikia vibaya kuona kwamba alikuwa anateseka namna hiyo kwa sababu ya uzembe wake. Aliivishwa mno Nicola lakini baada ya kumuona Edison, kiasi fulani alipata tumaini kwa mbali japo kwa mazingira yalivyokuwa alijua kabisa kutoka ndani ya hilo eneo ilikuwa ngumu, uwezekano ulikuwa mkubwa wote kuweza kufia hapo.
Jambo la pili lilikuwa ni kumuona mtesi wake, yule mwanaume ambaye alifanya mpaka akamuachia Damasi ili amsaidie kumpata alikuwa mbele yake. Yohani Mawenge akiwa kwenye ile sura yake bandia alikuwa anamwangalia kwa furaha, hakuonyesha hasira kwenye macho yake bali aliufurahia wakati huo kukutana na mtu amabye alimsaka mno bila mafanikio, waliingia gharama kubwa kumtafuta ila hawakuwahi kumpata wala kujua anako patikana lakini Mungu sio athumani, wakati huo mteja wake alikuwa mbele lilikuwa ni jambo la yeye kujikatia minyama tu wakati huo.
“Hahahaha hahaha you are welcome Edison” aliongea kwa mbembewe akiwa ameinyoosha mikono yake kwa bashasha mithili ya mtu ambaye alikuwa anasubiri kumkumbatia ampendae kisha akapiga makofi kushangilia akiwa anamsogelea Nicola taratibu akimpapasa kwenye shingo yake na kumpiga busu kwenye shavu lake kwa lazima.
“Kwenye maisha yangu tangu niyaanze haya maisha ni kwa mara ya kwanza nimekutana na changamoto kubwa na ngumu kukabiliana na wewe kwa sababu kila hatua ambayo nilikuwa naipita ulikuwa unaniacha hatua mbili nyuma. Jambo hili lilinipa hasira kali na uchungu kwakuwa kwenye maisha yangu hakuna binadamu ambaye amewahi kunipa changamoto ya namna hii lakini mwisho wa yote leo upo hapa. Hahahaha hahaha” alicheka kwa kuifurahia siku hiyo na ugeni wake.
“Wewe ndiye umemuua mkuu wa majeshi?” Edison alitoa sauti kwa mara ya kwanza
“Ndiyo mimi hapa mwenyewe, na sio huyo tu nimeua watu wengi ambao hata idadi yake siikumbuki. Wamekufa watu wengi kama ambavyo wewe na huyu mrembo ambaye nitambaka mbele yako kabla ya kumuua mnaenda kufa kwa mara nyingine kwenye mikono yangu” alibadilisha sura yake akiwa anaitoa ile sura ya Yohani Mawenge akabakia na ile sura yake halisi ya Joel John.
“Mama yuko wapi?” lilikuwa swali kwenda kwa Joel.
“Inashangaza kweli, baada ya miaka yote hii bado unalikumbuka neno mama? Ama kweli siku zote damu ni nzito kuliko maji. Mama yako yupo na anakuona muda huu na jambo zuri ni kwamba yupo hapa hapa hivyo ukihitaji kumuona unatakiwa kufanikiwa kuwamaliza unao waona wote hapa kisha mlango upo wazi” Joel aliongea kwa mbwembwe akiwa anabonyeza limoti iliyokuwa kwenye mkono wake ambapo langu kubwa lilifunguka nyuma yake akapisha pembeni, huko chini kulikuwa na ngazi. Edison hakuona kwa chini zaidi ila lilionekana kuwa eneo ambalo ilitumika gharama kubwa mno kulitengeneza na ni wazi huko chini kulikuwa na nyumba ambayo bila shaka ndiko yalikuwa makazi ya mama yake mzazi.
Alipigwa na butwaa baada ya kuidharau hiyo sehemu mara ya kwanza lakini hakujua ambacho kilikuwa kinaendelea nyuma yake. MwanaumE mmoja aliinyanyua silaha yake baada ya Edison kusogeza hatua moja kuelekea mbela, alipigwa risasi nyingi kwenye kichwa chake mwanaume huyo na Joel mwenyewe ambaye alionekana kukereka na kijana huyo kuingilia sherehe ambayo haikuwa ikimhusu wakati huo aliwageukia vijana wake wengine.
“Hatakiwi kufa wala kuumia kwa haraka namna hii, huyu ni mtu ambaye nimemsubiri kwa miaka mingi niweze kumtia kwenye mkono wangu anijue kiundani zaidi mimi nilivyo. Ukiacha hilo mmemsikia kabisa akidai kumuona mama yake ili akanyonye hivyo asithubutu mtu yeyote yule kumshambulia kwa risasi wala silaha ya namna yoyote ile, itumieni mikono yenu kumleta kwangu namtaka akiwa hai na mzima kabisa” aliwaongelea vijaan wake kwa sauti kali, walikuwa wakimuogopa mno kwa sababu walimjua vyema. Baada ya kuhakikisha somo lake limeeleweka alimgeukia Edison ambaye wengine walikuwa wakimuita EdJr ikiwa na maana ya Edison mdogo kwa sababu baada ya kuzaliwa alipewa jina la babu yake.

UKURASA WA 100 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 101

“Unamtaka mpenzi wako? Unamtaka mama yako? Huo mlango siufungi utakuwa wazi kwahiyo kazi ni kwako, cheza na hao vijana kisha utanikuta huko chini nakusubiri mimi na mama yako. Ni rahisi tu ila kama ukishindwa kufika huko wewe mwenyewe ukaletwa na hawa vijana basi utashuhudia nikimbaka mpenzi wako kwa macho yako na kumuua kisha mimi na wewe tutamalizana baada ya kumuona mama yako. Comon Edison” aliongea kwa mbwembwe akiwa anawakonyeza wale vijana ambao walikuwa wamemshika Nicola, walimkokota kama mbwa kuelekea kule chini ya ngazi kisha naye Joel akashuka huko kuwaachia kazi vijana wake ambao hawakutakiwa kumuua Edison kwani alikuwa anamsubiri wazungumze kiume mtu Bee.
Mwanaume mmoja alitembea kwa kujiburuza kuwahi alipokuwepo Edison, alipigwa ngumi la shingo, alitua chini akakutana na buti ambalo lilimburuza mpaka ukutani, mgongo wake ulivunjika akabaki ametulia vile vile. Walikuwa kumi kwa ujumla wao hivyo mpaka wakati huo walikuwa tisa ambao walibakia pembeni. Alihisi kivuli kinamjia, aligundua mwingine alikuwa amekuja kutoa nyuma, alichana msamba chini mwanaume huyo akampita kwa juu, alinyanyuka ghafla akamdaka kwenye suruali yake ambapo alimgeuza na kukita ngumi kumi kwenye kifua chake.
Kifua kilibaki kilaini kama mpira wa kufuma na karatasi, alisukumwa pembeni kuwapisha wenzake. Walijigawa wanne wanne, wengine mbele wengine nyuma. Edison aliwasogelea wale wa mbele yake kwa kasi kisha akaruka sarakasi ya nyuma ya ghafla kwa sababu alijua kabisa kwamba wale wa nyuma walikuwa wakija kwa kasi upande wake. Hali ile iliwafanya wanaume wale kukutana wenyewe katikati ambapo baada ya yeye kutua nyuma aliwavuta wawili akawagongesha vichwa vyao mara nne vikapasuka vibaya akawarushia kwa wenzake.
Yalikuwa yanatokea mauaji ya kutisha zaidi hata ya yale ambayo yanadaiwa kufanyika huko Rwanda ndani ya gereza la Gitarama. Wanne hawakuwa na uhai, ni wakati ambao alikuwa anawafuata yeye, alitembea kwa kuburuza mabuti yake chini ya sakafu akajigeuza kama analala hewani akiwa anajiviringisha kwa nguvu, walikwepa akadunda kwenye nguzo na kurudi kwa mara ya pili ambayo alitua kwenye shingo ya mmoja na magoti yake, alishuka naye mpaka chini. Mpaka wanatua chini mwanaume huyo alibonyea kwenye mabega yake akitapika damu nyingi kwenye mdomo wake, puani na masikioni. Alikuwa miongoni mwa binadamu ambao walikufa vibaya.
Jambo lile liliwatisha wenzake wakaanza kusukumana kila mtu akiwa anamsakizia mwenzake kuweza kusogea hapo. Mmoja wao alikimbilia kwenye ukuta ambako kulikuwa na nondo nzito na shoka dogo moja yakihifadhiwa hapo kama mapambo. Alimrushia mwenzake mmoja shoka naye akabeba nondo ambayo ilimpa uhakika wa alichokuwa anataka kukifanya, alipata ujasiri wa ghafla ambao ulimfanya kwenda kwa mbwembwe na nondo yake mkononi akiwa anaizungusha, aliirusha kwa nguvu akiwa amemkaribia kumfikia Ed, ilimparaza kidogo kwenye msuli wake baada ya kufanikiwa kuikwepa.
Ilizungushwa kuelekea kwenye paja lake akajivuta nyuma ikamkosa kidogo, alisogea mbele haraka halafu akarudi nyuma kwa hatua kadhaa, kusogea kwake kulimfanya yule mtu airushe ile nondo kwa kutumia nguvu nyingi kwa sababu alikuwa na uhakika kwamba ingekutana na Edison lakini kujivuta kwake kulimfanya mwanaume yule kwenda kinyume na mahesabu yake na kwa sababu alitumia nguvu kubwa alijikuta anakosa babansi akayumbia mbele ambapo alikutana na ngumi ya tumbo akaiachia hata nondo yenyewe. Ilikuwa ni bahati mbaya ilitua kwenye mkono wa EdJr, hakumkopesha aliizamisha kwenye shingo yake na kuichomoa kwa kasi kisha akairusha kwa nguvu.
Wote waliishuhudia ikizama kwenye paji la uso la mwenzao wakiwa wamebaki watatu tu pekee. Mwenye shoka alimeza mate akairusha shoka yake huku akiwa anafuata kwa nyuma, Ed aliinama chini na kuunyoosha mkono wake ambao ulildaka shoka lile wakati linampita akageuka nalo ambapo ilitua kwenye kichwa cha yule bwana. Alikuwa anakufa huku anatetemeka macho yake yakiwa yametoka kwenda kwa muuaji wake, alipasuliwa vibaya kichwa chake asingeweza kuishi tena.
Wale wawili walikuwa wanaangaliana kama kushauriana, mmoja alijikakamua kuweza kumzonga adui yao ila mmoja aliona cha kufia nini akahitaji kukimbia kuelekea kule ndani chini ya zile ngazi ila wakati anakaribia kufika pale shoka lilirushwa kwa nguvu likatua kwenye mgongo wake. Alidondokea kule ndani kama alivyohitaji ila ni wakati ambao alikuwa apumua pumzi ya mwisho mwisho, yule ambaye alibaki mmoja alichomoa kisu kidogo kwenye mfuko wake na kujiua mwenyewe. Hakuweza kuhimili yale ambayo aliyashuhudia kwa wenzake wakati ule. Walikuwa wanauawa kikatili isivyokuwa kawaida ni jambo ambalo lilimuogopesha akaona ni bora ajiondoe mwenyewe aende kwa amani.
EdJr alikuwa anatembea taratibu na kuanza kuzishuka zile ngazi kuelekea huko chini ambako aliambiwa mama yake alikuwa akimsuburi. Ilikuwa ni sehemu ya gharama ambayo ilitengenezwa na msanifu bora wa majengo, kulikuwa na vyumba kadhaa ambapo baadhi ya vyumba kulikuwa na wanawake wanahesabu pesa, kuna vyumba madini yalikuwa yanapimwa na kuwekwa sawa lakini kuna vyumba watu walikuwa wanapima na kuyahifadhi madawa ya kulevya na hiyo ilikuwa ni miliki ya mama yake mzazi.
Hakujali mambo hayo bali alinyoosha kwa njia kubwa kwa sababu alikuwa akiona mbele, mbele kabisa kulikuwa na sebule kubwa mno ambayo ilikuwa ni vito vya thamani. Katikati ya eneo lile kulikuwa na ngazi zilizo pandisha juu eneo ambalo lilikuwa na sofa kubwa la bei ghali isivyo kawaida, hiyo ndiyo sehemu ambayo alikuwa ameketi Boss Lady mwenyewe huku kwa chini yake kidogo akiwa ameketi Yohani Mawenge waweza kumuita Joel John akiwa anavuta Cigar yake bila wasiwasi.
Aliyageuza macho yake na kumuona Nicola akiwa amefungwa na minyororo yake ukutani akiwa amechoka na kuchakaa mno, mwilini mwake alikuwa na kibukta tu na kicloptop damu ikiwa imemtapakaa na miguuni akiwa peku kabisa. Edison aliyarudisha macho yake kule juu ambako hakuwa amepaangalia vyema, hakuamini aisee kumuona mama yake mzazi akiwa amekaa pale juu. Alikuwa ni yule mwanamama ambaye dunia ilimjua kama Cersie Mhina huku soko jeusi likimtambua kama Madam Kate lakini kwa upande wake yeye alikuwa anamtambua kama Zulpha Mazipa.
Alikumbuka mbali sana mpaka chozi likiwa linashuka kwenye mashavu yake, hakuwahi kuombea siku moja kuja kuwa kwenye hali kama hiyo ambapo mama yake ndiye angekuwa adui wa maisha yake lakini wanasema hatima (Fate) huwa haidanganyi, kilicho andikwa kwa namna yoyote ile ni lazima kiweze kutimia. Siku hii yeye ndiye ambaye alitakiwa kuutoa uhai wa mama yake mzazi kwa mkono wake mwenyewe, kibinadamu hiyo ni hatua mbaya na ngumu zaidi kwenye maisha. Haijalishi binadamu huyo alikukosea mangapi na mabaya aliyokufanyia lakini daima hata mbingu zitaandika kwamba ni mama yako mzazi.
Alipitia mengi magumu kwenye maisha yake kwa sababu ya mama yake, maelfu ya watu walikuwa wanapoteza maisha kwa sababu ya mama yake. Baba yake na familia nzima ilipotea kwa sababu ya mama yake, mkewe na mtoto tumboni walikufa kwa sababu ya mama yake, Edward Pande alikufa kwa sababu ya mama yake. Siku hiyo kwa mara ya kwanza alikuwa mbele yake wakitazamana, Edison alishindwa kuyahimili hayo maumivu, alipiga goti chini akiwa anaendelea kutoa chozi lake la kiutu uzima. Hata Nicola ambaye alikuwa kwenye maumivu makali alishindwa kuhimili hali hiyo, alianza kulia kwa sababu alikuwa akimuonea huruma sana Edison, kuvivaa viatu vyake ilihitajika moyo mgumu zaidi ya ule wa paka.
Ilisikika milio minne ya risasi kutoka kwa Joel, aliwaua wale walinzi ambao walionekana kumsogelea Edison pale chini. Ni wale walinzi ambao waliingia humo ndani na Nicola, hakutaka aingilie mtu pambano hilo ndiyo maana alimuua ili wabaki wao wawili tu pekee wamalizane, baada ya kukamilisha hilo aliiweka bastola kwenye kiuno chake akasimama.
“Mamaaaaaaaa” Edison aliita kwa nguvu na kwa hasira akiwa anauinua uso wake, ni wakati ambao Joel alikuwa amedunda kwenye ngazi kadhaa kushuka pale chini. Muda ambao alikuwa anainua uso wake, alikutana na buti likiwa linaelekea usoni kwake, alijaribu kulipangua na mikono ila uzito wake ulikuwa mkubwa, lilimbeba mpaka mbali ambako alitua chini kwa mkono wake mmoja, alijigeuza kwa nguvu akatua kwa kishindo na buti lake na kuanza hali ya mtetemo.
Hilo lilikuwa ni jambo la hatari ila Nicola alikuwa makini kuhitaji kulishuhudia pambano ambalo huenda alilisubiri kwa siku nyingi. Walikuwa ni wanaume wawili ambao waliijua sanaa ya mapigano huenda kuliko watu wote ambao aliwahi kuwaona kwenye maisha yake, hakujali kama angekufa lakini huenda kushuhudia pambano hilo ingekuwa nafasi bora zaidi kwake kuwahi kuona kitu bora kupitia macho yake.
Walikimbiliana kwa nguvu kuelekea katikati ambapo walikutana, Joel alirusha ngumi kali ambayo ilimpuliza Edison kwenye uso wake naye aliukunjua mkono wa kushoto ukatua kwenye kichwa cha Joel aliye rudi nyuma japo hakurudi kizembe alihakikisha buti lake linatua kwenye mbavu ya Edison na kukita ile sehemu ambayo aliwahi kupigwa na kisu ambayo bila shaka haikuwa imepona vizuri, palianza kulowa damu taratibu. Aliume meno yake na kujiweka vyema.

UKURASA WA 101 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 102

Sarakasi mbili za haraka zilimfanya Edison kupangua mguu mzito uliotua kwenye bega lake la kulia mguu mmoja wa Joel ukiwa chini. Aliukita mguu huo na buti lake ukateleza kwa nguvu na kumfanya kukita ngumi yake ya kulia kwenye kifua cha Joel kwa nguvu kubwa ila hata yeye mwenyewe alikutanishwa na mabuti mawili ya kifua ambapo Joel alidondokea kwenye ngazi kwa kutumia mkono wake mithili ya mtu ambaye alikuwa anapiga pushup hakuruhusu kujiumiza kwenye hizo ngazi. Edison aliburuzwa na mateke yale mpaka ukutani ambako mguu ndio ulikita yeye akabaki ameinama mithili ya ule mkao wa nge unavyokuwa.
Alijigeuza kwa sarakasi ambayo ilimfanya atue chini kwa kishindo kuelekea alipokuwepo Joel kwa kasi na nguvu kubwa, alijigonga kidogo mguu wake wa kushoto akajibetua kwa sarakasi ambayo ilimfanya kutua kwenye zile ngazi. Joel alizunguka kwa kupandisha juu kidogo ya ngazi zile, eneo ambalo Edison alikita na mguu ile ngazi ilimeguka kwa kushinda kuuhimili ule uzito ambapo aliona mguu unakuja kwake aliinama chini ukampita akamzoea Joel wakashuka wote chini huku wakiachiana kwa kupeana ngumi za uso wote wawili.
Edison alichana ile vest yake baada ya kuona inamtinga kwani shughuli ambayo ilikuwa mbele yake ilikuwa nzito, hata Joel alifanya hivyo, walikuwa ni wanaume waliokuwa wameshiba vilivyo kwenye miili yao. Joel alikuja kwa kuhesabu miguu yake, aliichezesha mara kadhaa baada ya kufika pale, aliirusha kwa pamoja akiwa anajipinda kama kiwavi ambacho kimeguswa. Miguu ile ilimkita Edison kwenye mabega yake, alituna hayakumpa madhara makubwa. ‘
Hakumpa nafasi joel ya kutua chini alimshambulia kwa ngumi kali tano ambazo zote ziliingia baada ya hapo alimkita na buti la uso kwa kisigizo kiasi kwamba Joel alirudi nyuma hatua kadhaa akiwa kama amelewa. Yale mapigo yalimuingia sawa sawa. Alibaki anarusha ngumi kama ushahidi ili akae sawa, alihisi mtu yule anamjia tena akarudi nyuma mpaka kwenye ngazi ambako alifuatwa, ulichanwa msamba na Edison akamkosa bwana yule akatua kwenye zile ngazi, alizunguka akiwa chini akafanikiwa kumpata Joel kwenye paja lake ambalo lilimpa kadhia kidogo kama kuteguka hivi mpaka akaguna. Alindokea kwenye ngazi akiwa anavuja damu kwenye mdomo wake na mguu kama anavuta hivi hivyo Edison akaenda kwa kasi ambapo alikosea hesabu akateleza kidogo kwenye ngazi alikutana na ngumi ya uso ikamrudisha chini ambako aliyumba mpaka akadondoka chini ila sarakasi ilimnyanyua kwa mara ya pili yeye mwenyewe akiwa amepasuka juu ya jicho na mdomo wake ulikuwa unavuja damu pembezoni maana ulichanika kwa mbali.
Alitaka kukimbilia kule juu ila alitulia baada ya kusikia milio ya risasi, swali lake lilikuwa ni kwamba ni nani alipigwa risasi ndipo akamgeukia mpenzi wake Nicola. Maskini Nicola alikuwa amekula risasi ya tumbo na kwa namna alivyokuwa amefungwa akawa anatoa damu kwa wingi maana damu tumbo lilikuwa limekaza tena alipigwa sehemu ambayo ilikuwa na jeraha. Edison alipatwa na hasira kali ndipo akashangaa anasikia mtu akigugumia kule juu, kuangalia vyema akagundua kwamba hata mama yake alikuwa amepatwa na risasi moja eneo la karibu na shingo yake.
Alipigwa na butwaa kwamba ni kwanini mlinzi ndiye ahitaji kumuua bosi wake? Hakupata jibu zaidi ya kumgeukia Joel akiwa anamwangalia kwa maswali mengi ambayo aliamini mtu huyo ndiye pekee angekuwa na uwezo wa kumpa majibu yake. Joel aliiachia bastola hiyo kwa sababu haikuwa na risasi, ilikuwa na uwezo wakubeba risasi sita, nne alizitumia kuwaua wale vijana wake, moja ilikwenda kwa Nicola na moja ilikwenda kwa mama yake mzazi.
“Nimekwambia utaishuhudia dunia ilivyo mbaya kuwatazama uwapendao wakipotea mbele ya macho yako ukiwa huna la kufanya. Mama yako alionekana kuwa dhaifu kwa sasa kwa sababu ni kama alikuwa anasita sita kukuua hivyo wakubwa walihitaji nimuue lakini niliamua kumpa muda mpaka wewe ukifika ndipo nilifanye hili ukishuhudia kwa macho yako mwenyewe. Sasa kazi ni kwako, sidhani kama utamuokoa mama yako maana nimempiga sehemu mbaya anaweza akadumu kwa dakika tano tu atapoteza maisha ile yule mchumba una nafasi ya kumuokoa kama utatoka humu salama. Kazi ni kwako Edison” maelezo ambayo alipewa yalitosha kabisa kujibu kile ambacho alikuwa anakihitaji.
Aliuma meno yake kwa hasira kali, alikimbia kuelekea kule juu ambako alikuwepo Joel, alirusha ngumi kumi nzito ambazo Joel alikuwa akifanya zoezi la kuzikwepa mpaka alipo kumbana na moja ya kwenye moyo, alihema kwa nguvu akashtuka amepigwa buti la ubapa kwenye sikio ambalo lilimzoa mpaka kule chini. Alifuatwa kama anakufuatwa na mzimu, alikunjuka teke moja kali ambalo lilikutana na ngumi ya Edison na kumpa maumivu makali mno.
Joel ni kama alianza kuzidiwa ukizingatia mguu wake mmoja haukuwa sawa kwa sababu uliteguliwa. Alijigeuza akiwa anchechemea ambapo alitua kwenye kifua cha Edison, alikita hapo Edison alirudi nyuma kidogo anakafanikiwa kuudaka mguu mmoja kabla haujatua chini alipiga ngumi nne mfululizo ambazo zilimpa Joel kilio, hata baada ya kufyatuka kwa nguvu na kumkita Edison buti la uso ambalo lilimtoa damu kwenye pua yake bado haikubadilisha maana halisi kwamba Joel mguu wake mmoja ulikuwa umevunjwa kabisa.
Alisimama kwa mguu mmoja ukiwa hauna nguvu sawa sawa, hakuamini kama ni yeye ambaye wakati huo alikuwa kwenye hali kaam hiyo. Alipiga kelele kwa uchungu mkali akimrukia Edison ambaye alimkwepa kwa kurudi nyuma kisha akauacha mguu wake mbele ambao aliusogeza ukakutana na uso wa Joel, damu iliruka juu kama ng’ombe kachinjwa bila kushikwa vizuri. Alitua chini akiwa anaona dunia inazunguka. Edison alimsogelea pale alipo, alimwangalia mwanaume yule kwa uchungu usio pimika, aliudaka mkono mmoja na kuuvunja vibaya kuanzia kwenye kwapa lakini hakuona kama inatosha.
Alipandisha kwenye ngazi kuichukua ile bastola ambayo ilikuwa imeisha risasi, alirudi nayo wakati Joel akiwa anagalagala chini akijitahidi kunyanyuka lakini uhalisia uliizidi hali ambayo alikuwa nayo. Alimshindilia buti la uso kwa mara nyingine kisha akamdaka na kuizamisha bastola hiyo mdomoni ambapo aliishindilia kwa mguu wake. Bastola ililazimishwa kuzama mdomono, iliuchana chana mdomo vibaya kiasi kwamba hata kulia hakuwa na huo uwezo Joel, alibaki anahema kama mtu ambaye alikuwa na kifafa.
Alimvuta mpaka karibu na alipokuwa amefungwa mpenzi wake, alikidaka kichwa cha Yohani na kukifunga na ile minyororo ambayo ilikuwa inaelewa, alimfungua mpenzi wake kisha akamtaka akamshikisha mnyororo mmoja ambao waliuvuta kwa nguvu Joel ndiye akapandishwa juu mnyororo ukiwa shingoni. Alikuwa anarusha miguu yake nafsi ikiwa inaelekea kuzimu lakini hawakuwa na huruma, walimuua kwa pamoja mwanaume huyo ikiwa ni kama ishara ya kulipa pia kwa Nicola kwa kuuliwa kaka yake Daniel.
Nicola alimuonyesha ishara Edison kuelekea kwa mama yake yeye akiwa anaegamia ukuta basi taratibu ikamlazimu Edison kumsogelea mama yake ambaye alikuwa anamuangalia yeye kwa macho ya kutia huruma na majuto. Hata iweje bado alikuwa ni mama yake aisee, alimsogelea pale na kumuweka kwenye mapaja yake, mama yake alinyoosha mkono na kuyapapasa mashavu ya mwanae.
“Sistahili kuwa mama kwenye hii dunia ila haitabadilisha maana halisi ya kwamba mimi ni mama yako. Nimeyaishi maisha mabaya kwenye historia yangu, nimekuwa muasi wa kutisha kiasi kwamba nimekufanya uishi maisha magumu. Nina uhakika sistahili kusamehewa kwa ambayo niliyafanya lakini ukweli ni kwamba sikuwahi kumpenda baba yako bali nilikutana naye kwa ajili ya kazi, mimi nilitegwa kwake kama chambo tu ili niweze kufanya kazi ambayo niliahidiwa maisha bora”
“Maisha ya uhuru nikiikamilisha kazi, kweli nimeyaishi haya maisha lakini mwisho wa siku nilikuja kugundua kwamba hakuna kitu chenye thamani duniani kama familia ila nililigundua hili nikiwa nimechelewa. Mimi ndiye sababu ya kila amabacho kimekukuta kwenye maisha yako wewe na wenzako kwa sababu nilikuwa na uwezo wa kukizuia hiki. Sina mengi ya kujieleza kwako kwa sababu unajua yote ambayo nimeyafanya na unanijua mimi ni nani tayari lakini ukweli ni kwamba mimi kama mama sijawahi kuacha kukupenda kwenye maisha yangu yote”

UKURASA WA 102 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 103

“Jambo la pekee ambalo leo naweza kukusaidia ni kukuonyesha alipo IRINA ESPANOVICH ambaye bila shaka umemtafuta kwa muda mrefu na baadhi ya watu waliwahi kumtafuta kwa muda mrefu bila mafanikio kwa sababu hawakuwahi kujua kwamba anaishi wapi. Kabla ya kukuelekeza hilo shika hii frash (Aliitoa frash kwenye mfuko wa koti lake na kumkabidhi mwanae), hii ina taarifa zote juu ya biashara ambazo tunazifanya, juu ya watu wote ambao tupo nao na mpangilio wa uongozi kuanzia juu mpaka chini hivyo hii itawasaidia kuweza kuteketeza jamii yote hii kuanzia juu mpaka chini kabisa na taifa kwa mara nyingine linaweza kuwa huru” mama yake aliamua kufa kwa kumpa msaada mwanae, yeye ndiye aliyasababisha hayo hivyo aliona ni yeye pekee tena ambaye alikuwa anaweza kuyamaliza hayo.
“Wakati unamfuata IRINA, wasiliana na watu wa Ikulu haraka kwa sababu imetolewa amri raisi aweze kuuawa na agent Milito ambaye yupo ndani ya Ikulu hivyo raisi yupo kwenye hatari kubwa kwa sababu imegundulika kwamba ameamua kutusaliti. Kumuokoa raisi anaweza kukusaidia kuiweka nchi sawa kwa sababu yeye ni mengi ambayo ameyafahamu kwa sasa ndiyo maana anatakiwa kufa”
“Mwisho kabisa IRINA anaishi ndani ya Pango la Amboni huko Tanga yeye pamoja na mumewe Novack Nyangasa. Maisha yao wameyatengeneza huko ambako waliamua kujenga nyumba chini ya pango hilo na wanaishi kama wako uraiani tu kwa sababu wana utajiri mkubwa isivyo kawaida na hata madini ambayo umeyaona hapo yanawekwa vyema ndiyo mzigo ambao Nicola aliyaiba na baada ya kuteswa sana alitaja ulipo hivyo nao ulitakiwa kusafirishwa kwenye huko Amboni lakini kwa sasa nina imani utaufikisha kwenye mikono salama ya serikali”
“Kama ukifanikiwa kuwamaliza watu hawa basi utakuwa umemaliza kila kitu na mambo yote yataishia hapo na hawa wa huku chini mtawakamata tu kwani huwa wanasubiri amri ndipo wafanye ambayo watu hao wanayataka. Nipe simu yako” Edison hakuwa mbishi, aliitoa simu na kumkabidhi mama huyo, aliiseti Location halisi ya eneo hilo ambalo ndilo alitakiwa kulifikia.
“Kuna mtu mmoja hapo ambaye ni hatari huenda zaidi ya huyu ambaye umemuua hapa kwa sababu ndiye mwalimu wao. Anaitwa Nikolai Gibson, kama ukifanikiwa kumuua huyo basi hao unawafikia kiwepesi tu ila fanya haraka kumsaidia raisi wako, wewe hauwezi kuwahi ila kama inawezekana wasiliana nao kwa njia ya simu” mama huyo alikuwa akiongea kwa uchungu akiwa anatoa machozi.
“Niliyo yafanya hata Mungu najua kwamba hawezi kuja kunisamehe kabisa ila naomba kwenye moyo wako uwe na nafasi hata ndogo ya kuja kunisamehe siku moja mwanangu. Mimi ni mbaya na ni binadamu mpuuzi lakini siku zote bado nitabaki kuwa mama yako na hivi naenda kumuomba msamaha baba yako nina imani naye atanisamehe siku moja” alitamka maneno makali na ya uchungu kisha kukawa kimya. Alikuwa amekwenda zake kupambana kwenye ulimwengu mwingine wa maisha ambayo yaaminiwa kuahidiwa.
Edison alijisikia vibaya lakini jambo ambalo kwake alishukuru MUNGU ni kutomuua mama yake kwa mkono wake maana alijua kabisa kwamba jambo hilo lingemtafuna maisha yake yote. Alipiga simu Ikulu kutoa taarifa kwa raisi kwamba alihitajika kujificha kwenye chumba cha siri ambacho ni salama kisha agent Milito akamatwe haraka kwani ndiye alikuwa muuaji na kukamatwa kwake kungemfanya awataje wenzake na baada ya hapo alipiga simu polisi kuwataka waje eneo hilo ambalo alikuwepo yeye. Alimbeba Nicola wake na kuondoka naye, hakujali aliingia naye kwenye gari na kutoka hapo kwa spidi kali ambapo alipishana na gari za polisi za hapo Msata zikiwa zinaingia hapo kwa mbwembwe ambapo wote waliokutwa mle ndani walikamatwa.
Edison aliendesha gari yake mpaka hospitali kubwa ya Msata ambapo alimshusha mpenzi wake Nicola ili apatiwe matibabu hali yake ilizidi kuwa mbaya kutokana na ile risasi ambayo alipigwa, yeye hakuwa na muda zaidi ya kutafuta sehemu ambayo ilikuwa na Internet Café. Aliingia hapo akiwa anatisha kwa kutapakaa damu kwenye mwili wake ila hakujali zaidi ya kufanya kilichokuwa kimempelea huko. Alizituma zile taarifa zote ambazo zilikuwa kwenye frash Ikulu, alijua yeye hata kama angekufa huko mbele lakini kama raisi atafanikiwa kuishi basi atalimalizia zoezi hilo.
Alitoka hapo watu wakiwa wanamkimbia kwa kupiga makelele kwani ulikuwa kama mzimu, hakuwajali watu hao akaingia kwenye gari ikiwa ni saa nne usiku, safari yake ilikuwa ni kutoka hapo Msata kwenda ndani ya Pango la Amboni huko Tanga, pango ambalo linasadikika kuwa linatisha kwa kiasi kikubwa kwa kumiliki viumbe vya kutisha kama majoka makubwa na wengine wakiwa na imani zingine kama majini ma mizimu kuwepo eneo hilo ila yeye alikuwa anamfuata mwanamke hatari kuwahi kutokea ndani ya ardhi ya Tanzania, Irina Eapanovich ambaye uwepo wake ulihatarisha maisha ya watanzania kwa takribani miaka thelathini.



IKULU.
Mheshimiwa alikuwa ameketi kwenye ofisi yake akiwa na mawazo mengi, alikuwa anaombea Mungu mambo yaende kama alivyokuwa amekusudia. Alifurahia kwa upande fulani kwa sababu alikuwa amempa maagizo jaji mkuu kwani alikuwa akimuamini hivyo aliamini kwamba hata kama yeye angekufa basi kiongozi huyo angesaidia kuliweka taifa sawa lakini aliacha waraka wa kumtoa waziri mkuu kwenye madaraka kama asingefikia muda wa yeye kupata majibu kutoka kwa Edison.
Akiwa ofisini kwake hapo simu yake binafsi ndiyo ilimshtua, ilikuwa ni mara chache kupigiwa simi hiyo kwa sababu ni watu wachache na wenye umuhimu mkubwa ndio walikuwa na namba hiyo. Baada ya kuipokea alipata tumaini jipya kwenye nafsi kwani alikuwa anaisubiri taarifa kutokwa mtu huyo, alikuwa ni Edison ambaye alimtaka aingie kwenye chumba cha siri ambacho hakuna mtu anaweza kuingia huko na mhusika ambaye alikuwa anaenda kumuua usiku huo alikuwa ni agent Milito moja kati ya maagent ambao walikuwa wana nafasi kubwa mno hapo Ikulu na alifanya kazi kwa muda mrefu kwahiyo hakuna mtu hata mmoja ambaye aliwahi kumhisi.
Licha ya hilo aliambiwa anatumiwa taarifa zote ambazo zilikuwa zinahitajika ambazo zilijumuisha vitu vyote vya LUNATIC SOCIETY huku yeye akimuahidi raisi huyo kumrejesha IRINA Dar es salaam kisha simu ikakatwa. Raisi aliona tumaini la kuishi lipo upande wake, alipiga alamu haraka akaingia mlinzi wake mkuu akiwa anakimbia.
“Tadeo, Milito ndiye mtu ambaye yupo hapa kwa ajili ya kuniua na muda wowote kuanzia sasa atatafuta nafasi ya kunifikia ili kuniua hivyo natakiwa kuingia ndani ya SAFE ROOM ila sihitaji kuingia kuingia mwenyewe, tutaenda wote kisha vijana wengine wataifanya hii kazi”
“Mheshimiwa kama ni mtu wa kuifanya hiyo kazi ni mimi hapa, kwa sababu amejulikana atatusaidia kutaja na wenzake hivyo wewe kwa sasa ingia SAFE HOUSE mimi nawaandaa vijana wangu ambao ninawaamini, akija tu hapa namkamata kisha yeye atatujajia na wenzake”
“Hakikisha unakuwa salama Tadeo, hii ni amri”
“Sawa bosi” aliinama kutoa heshima wakati mkubwa wake akiwa anatokea mlango wa dharura ambao ulikuwa wa siri ili kuingia kwenye hiyo SAFE ROOM ambayo ilitengenezwa kwa ofisi maalumu kwa ajili ya ulinzi pale ambapo Ikulu ingekuwa hatarini. Hata kama Ikulu ingelipuliwa raisi angeishi kwa sababu hakukuwa na kifaa ambacho kilikuwa kinaweza kuingia ndani ya chumba hicho zaidi ya jicho lake ambalo ndilo lilikuwa nywila ya kuingilia huko.
Zilipita dakika tano tu kweli mwanaume huyo alisogea hiyo mitaa ambayo ilikuwepo ofisi ya raisi bila kujua kwamba alikuwa mtegoni. Tadeo hakumpakia mafuta, alimkamata na kumpa mateso makali mpaka akawataja wenzake na baada ya kuhakikisha Ikulu imesafishwa raisi aliitisha mkutano wa dharura kwamba vyombo vya habari vyote viwe hadharani muda huo alihitaji kuongea na wananchi wake kuelezea kila jambo ambalo limetokea na kulikuwa na mabadiliko makubwa yalikuwa yanaenda kutokea serikalini.
Mkuu wa kituo cha polisi cha OSTERBAY Kapombe Tyson alikutwa amejinyonga ndani ya ofisi yake akiwa ameacha barua ambao iliandikwa kwa mkono wake mwenyewe. Kwenye barua hiyo alikiri wazi kwamba yeye ndiye alimuua bondia pendwa nchini Wilson Ndamaru kutokana na vitisho vya watu ambao hakuwa anawafahamu kwa kuwa walitishia kuua familia yake yote.

UKURASA WA 103 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 104

Jambo ambalo baadae lilimshtua ni baada ya kugundua kwamba watu ambao walimfanya afanye tukio hilo ilikuwa ni jamii ya siri ambayo ilikuwa inaitwa LUNATIC SOCIETY. Lengo la watu hao kumfanya afanye tukio hilo likuwa ni kuhitaji kumuingiza ndani ya jamii hiyo bila kipingamizi, sasa kwanini walihitaji amuue bondia huyo? Alidai kwamba kulikuwa na sababu kubwa mbili; Sababu ya kwanza ni kwamba bondia huyo aliwahi kugoma kujiunga na watu hao hivyo kwao akawa hana faida ambapo alitakiwa kuuawa, sasa wangemuuaje? Hapo ndipo ikaingia sababu ya pili ambapo walihitaji kumtumia bwana Kapombe kama chambo kukamilisha mambo yao mawili kwa wakati mmoja.
Kumuua kwake bondia huyo kumbe ni tukio ambalo walilipanga kwa muda hivyo walilirekodi na baadae akatumiwa taarifa juu ya vitu ambavyo alitakiwa kuvifanya kwani kama angegoma kila ambacho alikifanya kingewekwa wazi. Kwa presha ambayo alikuwa nayo aliamini kwamba jambo hilo lazima lingefika kwa wananchi na hakujua angewaeleza nini juu ya hilo hivyo akaamua kujiua yeye mwenyewe ila alisisitiza sana kuomba kama kulikuwa na mtu wa kuweza kuitoa jamii hiyo angekuwa amelisaidia taifa kwani baada ya kuwasoma kiundani aligundua kwamba walikuwa ni watu hatari huenda kuliko hata ambavyo walikuwa wanaongelewa na watu.
Watu walisikitishwa na taarifa hizo, nchi ilikuwa inazidi kuingia kwenye mkenge wa hatari kiasi kwamba hakuna raia ambaye alikuwa na imani na jambo lolote ambalo lilikuwa linaendelea tena nchini. Hakuna sehemu hata moja ambayo ilionekana kuwa na amani ndani ya taifa lao ambalo lilisifika kuwa moja kati ya mataifa yenye amani zaidi ulimwenguni.
Mheshimiwa raisi alikwenda mubashara kuweza kuzungumza na wananchi wake juu ya kile ambacho kilikuwa kinaendelea nchi mwake hivyo ikamlazimu kusimulia historia ya nchi yake kuanzia ule ujio wa IRINA EPANOVICH kwa sababu alikuwa na taarifa zote ambazo alitumiwa na Edison. Alisimulia kila kitu ambacho kilitokea kwenye nchi yake akiwemo yeye mwenyewe kama mmoja wa hiyo jamii lakini pia hakuacha kuweka wazi msimamo wake kwa muda huo ambapo alikuwa amekubali kushirikiana na yule komando bora zaidi nchini Edison Christian ambaye alikuwa hai mpaka wakati huo na ndiye huyo alianza kuitokomeza jamii hiyo mpaka wakati huo alikuwa amekwenda kumfuata mwanamama huyo ambaye alikuwa ni jasusi wa zamani wa KGB.
Mheshimiwa aliweka wazi ushetani wote ambao ulitokea nchini kwa kipindi chote hicho mpaka mauaji ya watu ambayo yalikuwa yakifanyika kila siku ambayo ilikuwa inakwenda kwa Mungu. Kama raisi badi alitangaza mabadiliko makubwa ambapo yeye mwenyewe aliahidi kwenda kujiuzulu na mtu ambaye angekuwa sahihi kuliendesha taifa alikuwa ni jaji mkuu wa Tanzania. Pia alitoa amri ya baadhi ya viongozi wakubwa wa serikali ya serikali kukamatwa wakianza na waziri mkuu, mwanasheria mkuu wa serikali, IGP, Katibu muu wa chama tawala pamoja na katibu mkuu kiongoni (hawa miongoni mwao ukimtoa waziri mkuu walikuwa ni wale watu ambao walikuwa wakijifunika sura kwenye kikao wakiwa na madam Kate).
Aliweka uwazi wa kila kitu juu ya mambo ambayo yaliwasumbua watanzania kwa muda mrefu hivyo kwa wakati huo alikuwa anasubiriwa mwanamama huyo ambaye alikuwa ameolewa na mdogo wa raisi wa zamani Novack Nyangasa ambaye ndiye alimsaidia mwanamama huyo kukamilisha mipango yake hasa wa kumuua kaka yake ambaye aliwapinga watu hao kwa nguvu zote. Watu hao wawili walikuwa wakiishi kwenye kivuli cha kudanganya kwamba walikuwa na watoto wawili ila haikuwa kweli, ulikuwa ni uongo wa kutaka kuwaaminisha watu kwamba udhaifu wao mkubwa ulikuwa ni watoto wao hivyo kama mtu angehitaji kuwadondosha alitakiwa kwanza kutumia udhaifu wao.
Hapo angejikuta kwamba anatumia muda mwingi kuusaka udhaifu wa watu hao ambalo lilikuwa jambo la kufikirika tu. Lakini pia mwanaume huyo aliua familia yake kwa mikono yake kwa ajili ya mwanamke huyo Irina hivyo mwisho wa hayo ulikuwa umefika na ni muda mwafaka ambao wananchi walistahili kujua mwenendo wa nchi yao. Ni maneno ambayo raisi Faraji Asani aliyaweka wazi huku yeye mweyewe akiuweka wazi uhalisia wa maisha yake na familia yake kwa ujumla. Hakuwa na nyongeza nyingine, yeye alikuwa amekamilisha wajibu wake hivyo kuhukumu hilo aliwaachia wananchi wenyewe.






AMBONI, TANGA.

Pango la Amboni ndilo pango kubwa zaidi kwa ukanda wa Afrika Mashariki lakini ni pango namba mbili zaidi kwa ukubwa duniani. Ni moja ya mapango ambayo ni kivutio kikubwa duniani lakini kuna nadharia nyingi huwa zinatengenezwa kuhusu pango hilo kama vile kuingia na wanyama kama mbwa hairuhusiwi kwa imani zisizo thibitishwa lakini kuna watu wanadai ni eneo takatifu kwa ajili ya mizimu ambayo imekuwepo hapo mamilioni ya miaka hivyo kukiuka kwake ni kama kwenda kinyume hivyo kuna matatizo yanaweza kukupata kama kupotea ama kufa kabisa usije kuonekana tena kama simulizi ya wazungu wawili ambao walipotea jumla na hawakuwahi kuonekana tena.
Kuna nadharia pia zimetengenezwa kwamba eneo hilo limetokezea mpaka ndani ya mlima Kilimanjaro likidaiwa kuwa na njia nyingi mno ndani yake lakini wengine huwa wanadai kwamba njia mojawapo imetokezea lilipo ziwa Tanganyika. Zinaweza kuwa habari za kweli kutokana na kwamba zamani eneo hilo lilikuwa sehemu ya maji miaka mingi iliyopita, hapa nazungumzia mamilioni ya miaka.
Huko ndiko ambako alitakiwa kufika Edison, IRINA ESPANOVICH alidaiwa kuwepo kwenye hilo eneo na NOVACK NYANGASA ambao walikuwa wameanzisha makazi yao huko kwa miaka mingi iliyopita wakiwa wanaiendesha nchi kwa kutumia mlango wa nyuma. Safari ya kutoka Msata mpaka kufika huko yalikuwa ni masaa matatu na dakika ishirini na tatu lakini yeye alitumia masaa mawili na nusu hivyo alifika huko majira ya saa nane kasoro usiku.
Ni wakati ambao kulitulia isivyokuwa kawaida, alijua kabisa wakati huo asingekutana na changamoto yoyote hivyo aliiacha gari yake kwa mbali kidogo kisha akawa anaifuata ramani kama simu yake ilivyokuwa inamwelekeza. Alivipita vibanda kadhaa akamulika mbele, sehemu hiyo ilikuwa inatisha mno ndipo mbele yake alifanikiwa kuyaona mawe ya kale, akajua kabisa ni sehemu za kuta za hayo mapango.
Hakujua watu hao walikuwa wanaingilia wapi ila baada ya kutembea kwa muda alikutana na bango ambalo lilikuwa linatangaza utalii wa eneo hilo likiwa limechorwa kwenye kuta za pango hilo lakini pembeni yake paliandikwa bango lingine ambalo lilisimamishwa kwa chuma likidai kwamba eneo hilo shughuli za utalii zilikuwa zimesimamishwa. Bila shaka alihisi kwamba huenda ni wahusika ama wenyeji wake ndio ambao walifanya jambo hilo hivyo alielewa wazi kwamba alikuwa anasubiriwa eneo hilo kufika ama huenda walitegemea kwamba kuna siku atafika ndiyo maana walifanya maandalizi ya mapema.
Pango lilikuwa linatisha mno, alifika mbele kidogo sehemu ambayo mtandao ulikuwa unatoka na kurudi, ramani yake ilikuwa inampa maelekezo ya kuelekea kushoto, hakuwa na namna zaidi ya kufanya hivyo ambapo kwa mbele yake ndipo ilikuwa inagotea alama nyekundu kama ishara kwamba alikuwa amefika eneo husika. Aliyainua macho yake na kuona mwanga kwa mbali, bila shaka ilikuwa ni taa ile. Alikuwa anashika pembezoni mwa ukuta kupapasa asije kukosea njia kwani aliona ingemchoresha wenyeji wake wakajua kwamba alikuwa kwenye hilo eneo.
Kwenye ule ukuta alishika kitu kinacho nesa nesa ikabidi akibamize kwenye ukuta kwa nguvu, sauti ya kuhaha ndiyo ilimpa ishara kwamba alishika ni nyoka. Alikumbuka kwamba aliwahi kulisoma pango hilo na kugundua kwamba lilikuwa na mashimo mengi ambayo yalikuwa na nyoka wakali hivyo alitakiwa kuwa makini zaid ya hapo. Alikutana na ile kona ambayo ilikuwa inatoa mwanga, alichungulia na kumuona mwanaume mmoja akiwa amevaa mavazi ambayo yalimfunika kasoro kichwani tu akiwa anapata sigara silaha yake nzito ikiwa begani kwake.
Alitembea kwa kunyata mpaka alipofike ile sehemu bila kugundulikwa, alimshtua kijana yule ambaye aligeuka kwa hofu, alikuwa akiangaliana na silaha kwenye paji lake la uso. Aliangaza kila sehemu ila hakuona dalili za makazi hapo.
“Bosi wako yuko wapi?” mwanaume huyo hakujibu kitu zaidi ya kuonyesha hofu, mwanaume ikamlazimu kuikoki silaha yake.
“Makazi yake yapo karibu na upande wa nje”
“Nje?”

UKURASA WA 104 unafika mwisho
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 105

“Ndiyo ila njia yake ipo huku ndani, makazi yapo chini ya ardhi ndiyo maana ukiwa nje huwezi kuona kwa sababu njia huwa zinafunguliwa bosi akihitaji kutoka tu”
“Nipeleke huko” hakuwa na namna zaidi ya kukatiza kwenye chochoro moja ambayo njiani ilikuwa na taa kadhaa ambazo zilikuwa zinatoa mwanga na kuifanya chochoro hiyo kuonekana vyema kabisa. Mbele yake aliona kuna mlango wa shaba ambao uliungana na kuta za mawe ya lile pango ukiwa umesimamiwa na wanaume wawili wenye silaha nzito. Alikuwa kwa nyuma hivyo wale walinzi hawakuwa wakimuona vyema, alitokezea ghafla na kuwatandika risasi wote wawili kisha akamtaka yule mlinzi ambaye aliongozana naye afungue geti la humo ndani ambapo alifungua kwa kuingiza namba kadhaa lakini ile panafungulia tu yule mlinzi ambaye alikuwa naye alipigwa risasi ya kichwa yeye mwenyewe akabaki kwenye mshangao.
Alikuwa anasubiriwa kwa muda mrefu, mtu ambaye alimtandika risasi hiyo alikuwa ni Nikolai Gibson, alimpa ishara Edison amfuate. Si aliwataka watu hao? Ni kweli walikuwepo hapo wakiwa wanamngoja kwa hamu kubwa. Alianza kutembea kwa wasiwasi kupitia kwenye njia ambazo zilikuwa zinatisha, alikuwa makini kuangaza kila hatua ambayo walikuwa wanapiga akiamini kwamba baadae njia hizo zingemsaidia kuweza kutoka humo ndani.
Hakuwa amemwangalia mwanaume huyo ambaye alimpokea mpaka walipofika kwenye lango lingine ambalo baada ya kufunguliwa walitokezea kwenye nyumba, hakuamini kama bado walikuwa ndani ya lile pango ambalo ni la Amboni. Ndani kulikuwa kunavutia isivyo kawaida, kulikuwa na mbavu wengi humo ndani ambao walikuwa kwa ajili ya ulinzi. Nikolai aligeuka kumuangalia Edison hapo ndipo alimhisi mwanaume huyo, huyo ndiye ambaye mama yake alimwambia kwamba kama akifanikiwa kumdondosha basi atakuwa amemaliza kazi yake. Runinga kubwa ziliwashwa humo ndani, aliwaona wale wawili ambao alikuwa amewafuata hapo ndani yaani IRINA ESPANOVICH na NOVACK NYANGASA.
Wanadamu ambao walikuwa wanaratibu namna nchi inatakiwa kuendeshwa wao wakiwa wanaishi kwa starehe huko hata hawakujua maumivu ambayo wananchi walikuwa wanayapitia. Irina ndiye ambaye alikuwa chanzo cha kila kitu mwanamama huyo ambaye umri wake ulikuwa umekwenda kwa wakati huo ila kwa sababu pesa ilikuwepo alikuwa bado ni mgumu ila kama sio kuwa na pesa huenda alitakiwa kuwa mzee zaidi ya alivyokuwa anaonekana.
Alikuwa anamshangaa mwanamama huyo ambaye aliishia kuzisikia simulizi zake tu, hakubahatika hata siku moja kujua alipo, wala alama ya uwepo wake wala kumuona ila wakati huo alikuwa mbele yake kwenye runinga ikiwa ni ishara ya kwamba alikuwa ndani ya jumba hilo hilo huenda kwenye vyumba vya karibu tu.
“Karibu Edison. Nina imani ulikuwa unatamani kukutana na sisi siku moja huenda kwa kutaka kujua sababu ya haya yote kutokea, inawezekana una majibu lakini ulitaka kuyathibitisha kupitia vinywa vyetu sisi moja kwa moja lakini leo uwanja ni wako kuweza kulidhihirisha hilo japo naweza kukupa sifa zako kwamba wewe ni mtu ambaye umepiga zaidi hatua kwenye suala hili kuliko binadamu yeyote yule na pole sana kwa kumpoteza mama yako” ni sauti ya IRINA ESPANOVICH mwenyewe ikiwa inasikika kwa lafudhi yake ya Kirusi lakini alikuwa anaongea kiswahili fasaha kabisa, bila shaka miaka ambayo alikaa Tanzania ilimfanya kufanikiwa kujifunza lugha hiyo kwa ufasaha.
“Why all this?” Lilikuwa swali la Edison kwenda kwa mwanamama huyo ambaye hakumjibu zaidi ya kucheka tu na hapo ndipo alishuhudia katikati ukuta ukijiachia. Mbele kulikuwa na dunia kama peponi, kulikuwa na kila kitu ambacho binadamu wa maisha ya juu anastahili kuwa nacho. Kwa mbele yake aliona sofa moja ya gharama ikiwa kama inaelea kuja upande ule ambao alikuwepo.
Baada ya kuangalia kwa umakini aligundua kwamba sofa hiyo haikuwa inaelea bali ilikuwa inaendeshwa kwa rimoti na wanawake wa warembo wanne. Kwenye sofa hiyo alikuwa ameketi mwanamama IRINA mwenyewe na mumewe NOVACH umri ukiwa unazidi kuwatupa mkono. Sofa hiyo ilisimamishwa eneo ambalo lilikuwa kama steji ya muziki wao wakawa wanaiangalia kwa juu yake huku Nikolai akiwa karibu yao.
“Mimi nilikuwa nafanya kila kitu kwa ajili yangu mimi na niliyajua madhara yake ndiyo maana nikawa tayari kuzikabili athari zake. Huenda ulikuwa ubinafsi kulisaliti taifa langu kuwauzia siri wamarekani lakini nakiri kwamba sijawahi kujutia maamuzi yangu kwa sababu kiasi cha pesa ambacho niliwekewa mezani ni watu wachache wanaweza kuwa wazalendo na wakafanikiwa kukihimili. Lakini mimi niliichagua pesa kwanza nikiamini kwamba pesa ndicho kitu ambacho kingenipa maisha ambayo nilikuwa nayaota kila siku ila kwa bahati mbaya licha ya kufanya kila namna ya siri walifanikiwa kunitambua na nimshukuru yule mlinzi wa mume wangu ambaye aliniwezesha mimi kupata taarifa nikafanikiwa kutoroka”
“Baada ya kuja kwenye nchi hii ambayo niliipenda kutokana na historia yake na nikiri kwamba huenda ndiyo ncho bora zaidi duniani japo mifumo yake ya uongozi ni dhaifu sana, sikutaka kuwa mtu mnyonge nilihitaji kuwa mtu mwenye nguvu zaidi kwenye ukanda huu ila nikiwa nayafanya mambo yangu kwa siri kubwa. Nilijua kabisa namna KGB walivyokuwa hatari kwahiyo kuwa mzembe hata dakika moja tu lazima wangenipata ndiyo maana nikawa adimu na kupotea kabisa kwenye macho ya watu wengi ikawa ni watu wachache tu ndio walikuwa wana nafasi ya kuniona akiwemo mama yako mzazi pamoja na Nikolai ambaye amesimamia shughuli nyingi na mama yako mzazi”
“Kwenye kazi yangu sikuhitaji mtu ambaye angekuwa ni hatari kwangu, baba yako niliona kabisa kwamba angekuja kuwa hatari kwa upande wangu hivyo nikafanya hisani kumpeleka huko mashariki ya kati kuwasaidia MOSSAD na CIA kama kulipiza kwa taifa langu. Akili ya baba yako ingekuja kunipindua siku moja ndiyo maana sikumhitaji awe hai na ukumbuke kabisa mimi ndiye nilimtengeneza mama yako na kumtuma huko chuo kumfuata baba yako baada ya kumchunguza na kuona atafaa kwa muda fulani na kazi yake ikiisha afe. Mama yako alikuwa na maisha magumu hivyo nikamuahidi kila kitu akakubali, kiuhalisia ni kwamba wewe ulitakiwa kufa lakini aliahidi angekulea kwenye mikono yake na usingekuwa hatari kwa baadae na kama ungekuwa hivyo basi angekuja kukuua mwenyewe. Mambo yalibadilika baada ya wewe kutekwa” mama huyo alitabasamu na kuendelea
“Sina haja ya kuendelea mbele kwa sababu nina imani uliipata ile frash na umekutana na mama yako ambapo nina uhakika kama kuna maswali ulihitaji majibu yake basi ulishayapata hususani hilo la makomando wenzako kuuawa ambapo mwanasheria yule aliamua kuandaa jina la kesi hiyo kama NAFSI ZILIZO TELEKEZWA Lakini nasikitika kwamba nafsi yako pekee ndiyo haikutelekezwa ndiyo maana upo hapa leo. Kuna wanaume wenzako hapo mbele kama utahitaji kumhoji mume wangu kwa chochote basi malizana nao kwanza awe nafsi iliyogoma kuteketezwa ila huwa sipendi matumizi ya silaha kwa sababu huwa yananiumiza kichwa na sipendi makelele hivyo tumia uwezo wako huku ukijua kabisa kwamba leo ni siku yako ya kuweza kuzikwa kama ambavyo imetokea kwa familia yako” aliongea huyo mama kwa dhihaka akiwa anacheka kwa lafudhi yake ya Kirusi
Edison alijisikia vibaya mno, huyo ndiye alikuwa chanzo cha kila tatizo ambalo lilitokea, alitamani angemmeza mwanamama huyo ila alikumbuka kwamba aliahidi kumrudisha akiwa hai Dar es salaam ili akabidhiwe kwa KGB, wakati ulikuwa unasoma saa kumi kasoro ya usiku kwenye saa kubwa ya dhahabu ambayo ilikuwa ukutani.
Alirudi nyuma hatua kadhaa bila kutarajia ambapo alinyofoa koromeo la mbavu mmoja aliyekuwa amesimama kihasara hasara akadondoka chini. Aligeuka mbele akapishana na ngumi ya shingo aliudaka ule mkono na kuuvunja, mwanaume yule alitaka kupiga kelele vidole viliwi vilizama kwenye jicho lake likatoboka vibaya kisha alizamishiwa vidole kwenye masikio yake ambayo yalitoboka vibaya shingo ikazungushwa akatupwa pembeni. Ni ndani ya sekunde zipatazo kumi tu mbevu wawili hawakuwa na maisha huku Edison akiwangalia Nikolai kwa hasira, wanaume hao walikuwa wakijiamini mno kwa sanaa ya mikono yao kiasi kwamba hawakuhitaji kabisa kutumia silaha ambazo kwao zilikuwa ni kama matusi.
Walipewa ishra ya kumshambulia, hakuwa anawapiga bali alikuwa anatumia vidole vyake, alipokea ngumi ya mgongo iliyo mpenya vilivyo alibendi mbele kidogo akageuka na vidoke vyake ambapo aliikamata sehemu ya kifua kwenye moyo na kuitoboa kwa vidole vyake, aliutoboa moyo wa mwanaume huyo kisha akakita ngumi kali ambayo ilihitimisha safari yake moja kwa moja. Aliwaona wakimjia kwa wingi, alisubiria wakati ambao walikuwa wamemfukia, alichana msamba wake chini wakapigana wenyewe alinyanyuka na buti zito ambalo lilizitawanya sehemu za siri za mwanaume mmoja ambaye alianza kupiga makelele ulimi wake ukadakwa, ulivutwa mpaka ukakatika akawa anazunguka kila sehemu akilia kwa kujutia kuzaliwa, alikimbilia nje ambako alienda kujichomeka kwenye jiwe lililo chongoka ili afe sio kuvumilia yake maumivu.
Mwanaume mmoja aligeuka kwa sarakasi ya hewani, buti moja lilitosha kuuvunja vunja uti wake wa mgongo, alitua chini kama mfuko wa unga wa ngano. Alipigwa kama mpira na kusogezwa pembeni habari yake ikaisha. Walikuwa wamebaki kama watano lakini kipindi ambacho Edison anamshambulia huyo mwanaume, Nikolai alikuwa anaifunga bunduki zake mbili viwambo wa kuzuia sauti kwa sababu mabosi zake hawakuwa wakipenda kabisa kelele. Aliwangoja wanaume wale watano waanze kumsogelea Edison ndipo aliwapiga risasi wote, hata Edison alishangazwa na tukio hilo.
Nikolai alifanya hivyo kurahisisha mambo kwani walikuwa wanapoteza muda tu jambo ambalo lilihitajika kuisha mapema na hakuna kitu wangeweza kufanya kwakuwa walikuwa wanauawa kama watoto wadogo. Hivyo zoezi lilikuwa limebakia moja tu kuweza kumdondosha Nikolai ambaye yeye binafsi alijua kabisa Edison ni kinda mno kwake hakuwa na cha kukifanya.
Nikolai aliinyoosha mikono yake na kuzirushia mbali silaha zake hizo, alimuita kwa mkono wa dharau Edison kwani alihisi alikuwa anawaonea watoto wadogo japo hakuwahi kutokea mwanadamu yeyote kwa namna yoyote ile wa kufanikiwa kuua watu karibia wote mpaka akafanikiwa kuijua hiyo sehemu na kufika ama kugusa hata mlangoni hivyo mpaka hapo alikuwa anastahili sifa nyingi kwa hiyo hatua ambayo aliipiga. Edison akiikung’uta damu ambayo ilikuwa kwenye mkono wake na kuhitaji kusogea kwa kasi ila alirudi nyuma akitikisa kichwa chake.
Nikolai alikuwa na kasi kama mara mbili yake ndiyo maana alishtukia amechezea ngumi nzito ya uso na siku hiyo alijua kabisa alikutana na mtu ambaye hakuwa wa kawaida. Kwa mara ya kwanza aliipanga mikono yake akiwa amezikunja ngumi zake, alisogea kwa mahesabu kwani alijua mpinzani wake ana uwezo mkubwa huenda kuliko yeye hivyo nidhamu ingemlinda. Mkono ulimkosa Nikolai akamdokoa Edison na ngumi nyingine ya mbavu ile sehemu ambayo ilikuwa na jeraha akazidi kulitonesha na damu ikaanza kuvuja tena.

UKURASA WA 105 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

MWISHO………………………..
Edison alifanya kosa dogo kupandwa na jaziba wakati wa mpambano, hiyo ni seehmu ambayo huwa inahitaji utulivu hususani unapokutana na fundi wa hiyo sanaa ya mapigano. Alikuja vibaya akiwa amekunjuka kwa sarakasi ambapo hesabu zake zilikuwa ni kutua na buti lake kwenye kichwa cha Nikolai kisha mguu mmoja ungecheza na kifua cha mwanaume huyo lakini kabla hajafika aliwahiwa hewani ambapo aliguswa ngumi kama tano na kurushwa mbali akiwa anatokwa damu nyingi kwenye lile jeraha lake na mdomoni damu ilikuwa inamtoka kwani ngumi zilipigwa kitaalamu.
Alinyanyuka mwili ukiwa na maumivu, ngumi za mwanaume huyo zilikuwa kama sumu kali kila zikigusa mahali, alijaribu bahati yake kwa mara nyingine tena lakini alipigwa kama mtoto mdogo. Mkono wake ulidakwa akaachiwa, ikadakwa shingo ambapo alizungushwa kama mara kumi kwa kasi kiasi kwamba akapoteza kabisa network kichwani kisha alikutanishwa na viganja vingi usoni alipigwa ngumi akavutwa tena, alikutana na buti la uso kisha akasindikizwa na ngumi mbili ambazo zilirushwa pamoja kwenye tumbo lake.
Ndani ya muda mfupi alipigwa ngumi sio chini ya ishirini, mwili ulikuwa unawasha kila sehemu lakini alirushwa mbali hali ikizidi kuwa mbaya. Alitikisa kichwa chake akiwa ananyanyuka kwa taabu kubwa ili kutuliza kichwa maana alikuwa anaona watu sitasita mbele yake. Nikolai alihitaji kumaliza hiyo kazi mapema, alizunguka mara moja akaruka juu, alitua kwa goti chini ili kuuvunja mguu wa Edison ambaye alikuwa amefumba macho yake akitumia hisia kwani macho yalimsaliti kwa muda. Alijivuta pembeni goti likatua chini ya sakafu, wakati anauafumbua macho yake kuna ngumi ilishonwa kwenye uso wake aliiona akarudi nyuma akiwa hoi ameinama, kila kiungo kilikuwa kinamuwasha.
“Ulifanya kosa kuwaua vijana ambao nimetumia muda mrefu kuwafundisha akiwepo Yohani Mawenge hivyo kwa sasa nakuua” aliongea kwa hasira akiwa anasogea alipokuwepo Edison, alifumba macho yake tena akahema kwa nguvu kupata utulivu wakati anayafumbua alikuwa anaangaliana na buti ambalo lililenga uso wake na lingempata angeishia sehemu mbaya, aliunyoosha mkono wake na kukita mbele ya buti hilo na kuufanya mkono wake kukutana na mguu wa Nikolai, Nikolai alisikika akiguna ni wazi mkono ulimfikia mguuni.
Wakati anaguna aliutua mguu wake chini kuuangalia, alifanya kosa alihisi upepo unakuja upande wake, aliinama akapishana na buti zito ambapo kuinama kwake kulimfanya akutanishwe na buti la mguu mwingine naye akatupwa mbali. Edison alivua shati ambayo ilikuwa kwenye mwili wake kwa sababu damu ilikuwa inamtoka kwa wingi kwenye mbavu yake. Nikolai alinyanyuka akiwa anavuja damu pua ilipasuka na mdomo, hakuwa akiamini kwamba ni yeye ambaye alikuwa amefanyiwa jambo hilo. Aliilegeza tai yake ambayo ilienda kumponza.
Alikimbia kwa nguvu akaruka sarakasi na kutua kwa nguvu kubwa akamkosa Edison, alijigeuza kwa sarakasi kali ya nyuma kumfuata Edison pembeni ambako alisogea ila naye aliwahiwa, ile tai ilimkosesha balansi baada ya kudakwa akashuka chini vibaya. Uso wake ulifunikwa kama mpira yai ikiwa imeshikwa hivyo hakuwa na uwezo wa kumponyoka Edison, alipigwa mabuti matano mfululizo mpaka pale ambapo alichomoa kisu chake na kukikita tumboni kwa Edison ndipo alimuachia kwa kumsindikiza na buti zito lingine la uso ambao ulichakaa mno kwani ilikuwa ni kama anapiga danadana kwenye uso huo.
Nikolai alidondokea mbali akiwa amechakaa usoni, macho yake alikuwa anayafumbua kwa shida kwakuwa uso ulipasuka kila kona na kila sehemu ilikuwa unavuja damu. Edison mwenyewe hakuwa kwenye hali nzuri naye kwa sababu alizamishiwa kisu kwenye mwili wake akawa anayumba yumba, mwili ulikuwa una maumivu kila sehemu na damu yake ilikuwa inaendelea kutoka kwa sifa kubwa. Alikichomoa kile kisu akiwa bado anayumba yumba lakini wakati anafanya lile jambo alihisi kama kuna hatua za mtu ndipo akageuka nyuma yake.
Aligundua kwamba yule mzee Novack Nyangasa alikuwa anaikimbilia bastola moja baada ya shughuli kuonekana kuwa nzito upande wao. Alikuwa karibu kuifikia bastola moja nyingine ikiwa upande mwingine lakini aliwahiwa kabla hajaigusa bastola ile kisu kilipenya kwenye kiganja cha mkono wake na kuutoboa katikati. Edison alisogea akiwa anayumba yumba pale chini ambapo mzee yule alikuwa akipiga makelele, aliikota ile bastola pamoja na kisu alikitoa kwa nguvu, alimkanyaga kifuani kwa nguvu kwani alikuwa dhaifu tu akammiminia risasi mbili za kichwa mzee mpumbavu ambaye alilisaliti taifa lake kwa sauti ya uchi wa Mrusi.
Kifo cha mzee yule ambaye hawakuongea lolote ndicho kilimuinua mkewe IRINA akiwa anapiga kelele kumkimbilia Edison, mwanaume aligeuka na kuachia risasi moja ambayo ilitua kwenye goti na Irina na kulivunja goti hilo. Alikuwa kwenye mwendo hivyo alidondoka chini vibaya akajibamiza kwa kishindo, alitamani kuachia risasi nyingine ndipo akagundua kwamba silaha hiyo ilikuwa imeisha risasi ila hata hivyo hakutakiwa kumuua mwanamama huyo ambaye alibaki anatambaa kumkimbilia mumewe kipenzi aliye msaidia kuishi ndani ya taifa hili bila bug-u-dha kwa miaka mingi.
Alisikia kelele kali za ujio wa mtu, alikuwa ni Nikolai, aligeuka kwa kasi na kutuliza kelele hizo ambazo zilikuwa zinamjia upande wake baada ya kugeuka na kile kisu ambacho alikikota pale chini kwa yule mzee. Kisu hicho alikizamisha kifuani sehemu ambayo ilikuwa na moyo wa Nikolai, alikuwa anaichana sehemu hiyo kushuka chini akiwa amemkazia macho usoni kwake. Alikichomoa na kukichana chana kifua hicho bila huruma na mwisho alikizamisha kwenye shingo akakisindikiza na ngumi ambapo kilipitiliza mpaka kikatokea nyuma. Nikolai alikuwa ameumaliza mwendo.
Edison alijongea kuelekea ilipo bastola nyingine, kwa hesabu zake zile bastola zilikuwa zinahifadhi risasi sita sita na zilitumika kuulia watu watano maana yake risasi zilitumika tano kipindi Nikolai anawashambulia vijana wake. Tatu alizitumia yeye wakati ule hivyo alijua kwamba risasi nne zilikuwa zimebaki kwenye ile bastola nyingine, alichechemea mpaka ilipo akaiokota kisha akamrudia IRINA ESPANOVICH. Alimnyooshea ile bastola usoni akiwa na uchungu mkubwa, aliona kabisa mwanamama huyo alistahili kufia kwenye mkono wake ila yasingekuwa maamuzi sahihi.
“Nilipaswa kukuua lakini unatakiwa kurudi kwenye mikono ya KGB nadhani hamkumalizana mahojiano yenu bado”
“Noooooo, naomba uniue tafadhali usinipeleke huko” ilikuwa sauti ya Irina akibembeleza kwa sababu aliwajua KGB walivyo kama angeingia kwenye mikono yao angekutana na mambo ya kutisha isivyo kawaida huku akiwa hata hajui mtoto ambaye alimuacha huko Urusi alikuwa kwenye hali gani. Edison hakumsikiliza ambapo aliachia risasi mbili kwenye mguu mwingine wa Irina akatoa kile kiwambo cha sauti na kuachia risasi mbili zilizokuwa zimebaki karibu na kichwa cha mwanamama huyo ambaye mlio wa bastola ulimfanya apige kelele na kuzimia.

Mwanaume alipiga simu polisi akiwataka wafike eneo hilo kisha akambeba mwanamama huyo na kutoweka naye kurudi Dar es salaa ambako alipokea habari njema kwani mpenzi wake alikuwa amerudi kwenye fahamu zake baada ya oparesheni kufanyika na ilikuwa ni siku nyingine asubuhi akawa amefanikiwa kumkabidhi Irina kwa raisi.
Mheshimiwa raisi aliitisha mkutano wa dharura na serikali na nchi ya Uganda na kuwapa onyo kali kwa kile ambacho walikifanya kushirikiana na mwanamama huyo tena bila yeye kushirikishwa hivyo aliwataka kuomba msamaha kabla hajavunja mahusiano ya kidiplomasia wakati huo aliwaambia kabisa kwamba alikuwa na ushahizi wa uchafu wa viongozi wake wote ambao walikuwa nyuma ya mgongo wa LUNATIC SOCIETY zikiwemo zile video za ngono na kama wangekuja kucheza na Tanzania hata kwa kubipu tu basi angeziachia hadharani kila mtu akaziona. Hali hiyo ilipelekea habari kuvuja Uganda ambapo raia waliandamana, serikali ikavunjwa na kuundwa nyingine
Hilo onyo halikuishia kwa Uganda pekee bali hata kwa raisi wa Bulgaria Hristo Radoslav ambaye alisababisha kukatika kabisa kwa mahusiano baina ya nchi hizo mbili kwa kukubali kufanya biashara za siri na IRINA kwa kumtumia Madam Kate ama Cersie Mhina ikiwa ni amri ya raisi wa Tanzania hivyo naye alipewa onyo kali kuhusu kunusa rasilimali za Tanzania, hali hiyo ilipelekea mahusiano ya kidiplomasia ambayo yalikuwa yameanza kukua baina ya nchi hizo mbili kufia hapo.
Wananchi wa Tanzania walipata amani baada ya kupatiwa ukweli lakini walihitaji serikali iwajibike ambapo kila ambaye alikuwa kwenye mfumo wa ile Jamii ya siri aliwajibishwa vikali na ni watu wengi walikamatwa kwa sakata hilo na uongozi ukabadilisha mfumo mzima wa utawala. Raisi Faraji Asani alikubali kujiuzulu nafasi yake lakini wananchi waliandamana kugoma kwa kumtaka kuendelea na nafasi hiyo kwa sababu kama yeye alikuwa mtu wa kwanza kuleta mabadiliko basi ndiye alitakiwa kuyasimamia mabadiliko hayo huku wakiahidi kumpatia ushirikiano wa kutosha kabisa.
Majina wa watu wote ambao walikufa na kuchafuliwa yalipewa heshima yake, majina yalisafishwa na watu hao ikaahidiwa kwamba wataandikwa kwenye vitabu vya historia ya nchi ili dunia ije iwasome hata kwa vizazi vijavyo huko mbeleni. Hususani zile NAFSI KUMI ZILIZO TELEKEZWA lakini nafsi moja ikafanikiwa kuishi tena, watu hao walipewa heshima kubwa mno kiasi kwamba majina yao yaliandikwa kwenye nembo ya utambulisho wa taifa kama heshima kwao huku Edison Christian jina lake likitambulika kama ndiyo ishara ya ushujaa wa taifa, zilitengenezwa t-shirt zake, yalitengenezwa mabango yake kila kona hata viwanja vikubwa vya nchi vilipewa jina lake na kila sehemu ya jeshi jina lake lilikuwa nembo ya ushujaa na uzalendo yeye pamoja na mpenzi wake Nicola ambaye naye hakusahaulika kwa sababu alikuwa mhanga wa mambo hayo.
Irina alikabidhiwa kwenye mikono ya wanaume wa KGB ambao walishangazwa na jambo hilo kwani ni kazi ambayo wao walifanya kwa miaka mingi bila mafanikio lakini ilikuja kukamilishwa na mtanzania. Walitoa heshima kubwa kwa Edison lakini kwa taifa la Tanzania ambapo jambo hilo lilifungua milango mipya ya mahusiano makubwa zaidi ya kidiplomasia baina ya hizi nchi mbili huku wakiahidi kuwa tayari kufanya jambo lolote kwa ajili ya Tanzia kwa huo msaada mkubwa ambao walipatiwa.

Edison na mkewe Nicola Aidan ambaye aliamua kumuoa waliamua kurudi Rujewa Mbarali ambako ndilo ilikuwa asili ya mwanaume huyo. Alihitaji kuishi karibu na makaburi ya familia yake baada ya kuhakikisha amemaliza kazi yake, walijenga mijengo ya gharama huko kwenye eneo ambalo lilibakia kwenye mikono ya serikali kwa miaka kadhaa lakini mwisho wa siku mhusika alikuwa amerejeshewa huku akiwa kama shujaa wa nchi. Kila siku ya asubuhi na jioni watu walikuwa wanajaa nje ya geti lake kubwa wakiwa wanamtakia kheri ya kuwa salama yeye na familia yake naye alikuwa akipanda juu ya jengo lake na kuwasabahi raia wake ambao walimpenda sana na aliwasaidia sana mpaka kuibadilisha sehemu hiyo kwa ukubwa na maisha ya wananchi wake kwa ujumla.
“Ulitamani siku moja kuwa na maisha ya utulivu kama haya nadhani ndoto imetimia japo sio yote ila kiasi chake” ilikuwa ni sauti tamu ya mkewe.
“Nakupenda mke wangu” ndilo jibu pekee ambalo alimjibu mkewe kwenye mkono wake akiwa na ile nyaraka ambayo iliandikwa NAFSI ZILIZO TELEKEZWA. Ilikuwa imeandaliwa na mwanasheria JACK THE LAWYER ambaye aliitoa nafsi yake kwa ajili yake yeye hivyo aliapa kuitunza nyaraka ile kama kumbukumbu yake na kuwakumbuka makomando wenzake wale tisa ambao nafsi zao zilichukuliwa. Wakati huo alikuwa ameegamia tumbo la mke wake ambalo lilionekana kuwa kubwa kwa sababu alikuwa mjamzito.

MWISHO

Tulikuwa na wakati mwema mimi na wewe msomaji wangu lakini siku zote lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho. Niliungana nawe kwenye hili andiko ambalo bila shaka limekuwa bora kwako na limekupa furaha ya kutosha hivyo kwa sasa sina la ziada la kuongezea, panapo majaaliwa tukutane wakati ujao huenda kwenye andiko jipya (IDAIWE MAITI YANGU)

CIAO.
 
Nimemwaga vipande vyote mpaka mwisho.....

Ni matumaini yangu umepata burudani ya kutosha.


Next time usisahau pia kuwasupport waandishi, sio lazima mimi bali mwandishi yeyote. Mara Moja Moja toa chenji mfukoni nunua kukuza tasnia kwa sababu itakuja kufa hii maana Bongo uandishi umekuwa kama upotezaji wa muda tu.

Wengi huwa nawaona wanavyo wakebehi waandishi hapa na kuwapangia kuletewa simulizi muda wanao taka wao bila kujali waandishi wanapitia nini ila uhalisia ni kwamba uandishi ni kazi ngumu kuliko wengi wenu mnavyo hisi au kuambiwa na kuupambanua humu......

Ukitaka kuamini hilo andaa kazi ya kueleweka ambayo inaweza kuwafanya watu 10 tu wapoteze muda wao kukesha nayo ... Utanielewa vyema.

So wasomaji tunawapenda sana ila mnaweza kuwa sababu kubwa ya kuwakatisha tamaa waandishi wengi japo huwa hawasemi kwa sababu wanaogopa mtaanza kuwananga....

Msikunje sana, tuikuze hii tasnia iliyo sahaulika.

Binafsi niseme asanteni sana kwa kuwa pamoja nami mpaka sasa. Wale ambao walilike, walio-comment, walio pita kimya lakini waliyapenda maandishi..... Wote nawaheshimu sana.

Me i got much love for you guys....

No Hard Feelings..... Love ❤️

CIAO 👋
 
Nimemwaga vipande vyote mpaka mwisho.....

Ni matumaini yangu umepata burudani ya kutosha.


Next time usisahau pia kuwasupport waandishi, sio lazima mimi bali mwandishi yeyote. Mara Moja Moja toa chenji mfukoni nunua kukuza tasnia kwa sababu itakuja kufa hii maana Bongo uandishi umekuwa kama upotezaji wa muda tu.

Wengi huwa nawaona wanavyo wakebehi waandishi hapa na kuwapangia kuletewa simulizi muda wanao taka wao bila kujali waandishi wanapitia nini ila uhalisia ni kwamba uandishi ni kazi ngumu kuliko wengi wenu mnavyo hisi au kuambiwa na kuupambanua humu......

Ukitaka kuamini hilo andaa kazi ya kueleweka ambayo inaweza kuwafanya watu 10 tu wapoteze muda wao kukesha nayo ... Utanielewa vyema.

So wasomaji tunawapenda sana ila mnaweza kuwa sababu kubwa ya kuwakatisha tamaa waandishi wengi japo huwa hawasemi kwa sababu wanaogopa mtaanza kuwananga....

Msikunje sana, tuikuze hii tasnia iliyo sahaulika.

Binafsi niseme asanteni sana kwa kuwa pamoja nami mpaka sasa. Wale ambao walilike, walio-comment, walio pita kimya lakini waliyapenda maandishi..... Wote nawaheshimu sana.

Me i got much love for you guys....

No Hard Feelings..... Love ❤️

CIAO 👋
Hongera
 
Nimemwaga vipande vyote mpaka mwisho.....

Ni matumaini yangu umepata burudani ya kutosha.


Next time usisahau pia kuwasupport waandishi, sio lazima mimi bali mwandishi yeyote. Mara Moja Moja toa chenji mfukoni nunua kukuza tasnia kwa sababu itakuja kufa hii maana Bongo uandishi umekuwa kama upotezaji wa muda tu.

Wengi huwa nawaona wanavyo wakebehi waandishi hapa na kuwapangia kuletewa simulizi muda wanao taka wao bila kujali waandishi wanapitia nini ila uhalisia ni kwamba uandishi ni kazi ngumu kuliko wengi wenu mnavyo hisi au kuambiwa na kuupambanua humu......

Ukitaka kuamini hilo andaa kazi ya kueleweka ambayo inaweza kuwafanya watu 10 tu wapoteze muda wao kukesha nayo ... Utanielewa vyema.

So wasomaji tunawapenda sana ila mnaweza kuwa sababu kubwa ya kuwakatisha tamaa waandishi wengi japo huwa hawasemi kwa sababu wanaogopa mtaanza kuwananga....

Msikunje sana, tuikuze hii tasnia iliyo sahaulika.

Binafsi niseme asanteni sana kwa kuwa pamoja nami mpaka sasa. Wale ambao walilike, walio-comment, walio pita kimya lakini waliyapenda maandishi..... Wote nawaheshimu sana.

Me i got much love for you guys....

No Hard Feelings..... Love ❤️

CIAO 👋
Nianze kuisoma sasa
 
Nimemwaga vipande vyote mpaka mwisho.....

Ni matumaini yangu umepata burudani ya kutosha.


Next time usisahau pia kuwasupport waandishi, sio lazima mimi bali mwandishi yeyote. Mara Moja Moja toa chenji mfukoni nunua kukuza tasnia kwa sababu itakuja kufa hii maana Bongo uandishi umekuwa kama upotezaji wa muda tu.

Wengi huwa nawaona wanavyo wakebehi waandishi hapa na kuwapangia kuletewa simulizi muda wanao taka wao bila kujali waandishi wanapitia nini ila uhalisia ni kwamba uandishi ni kazi ngumu kuliko wengi wenu mnavyo hisi au kuambiwa na kuupambanua humu......

Ukitaka kuamini hilo andaa kazi ya kueleweka ambayo inaweza kuwafanya watu 10 tu wapoteze muda wao kukesha nayo ... Utanielewa vyema.

So wasomaji tunawapenda sana ila mnaweza kuwa sababu kubwa ya kuwakatisha tamaa waandishi wengi japo huwa hawasemi kwa sababu wanaogopa mtaanza kuwananga....

Msikunje sana, tuikuze hii tasnia iliyo sahaulika.

Binafsi niseme asanteni sana kwa kuwa pamoja nami mpaka sasa. Wale ambao walilike, walio-comment, walio pita kimya lakini waliyapenda maandishi..... Wote nawaheshimu sana.

Me i got much love for you guys....

No Hard Feelings..... Love ❤️

CIAO 👋
Umetisha sana mkuu, wewe na wenzako msiache kutuletea vitu. Puuzieni wote wanaoleta kebehi na kutaka kuwavunja moyo. Respect 🙏🙏
 
Nimemwaga vipande vyote mpaka mwisho.....

Ni matumaini yangu umepata burudani ya kutosha.


Next time usisahau pia kuwasupport waandishi, sio lazima mimi bali mwandishi yeyote. Mara Moja Moja toa chenji mfukoni nunua kukuza tasnia kwa sababu itakuja kufa hii maana Bongo uandishi umekuwa kama upotezaji wa muda tu.

Wengi huwa nawaona wanavyo wakebehi waandishi hapa na kuwapangia kuletewa simulizi muda wanao taka wao bila kujali waandishi wanapitia nini ila uhalisia ni kwamba uandishi ni kazi ngumu kuliko wengi wenu mnavyo hisi au kuambiwa na kuupambanua humu......

Ukitaka kuamini hilo andaa kazi ya kueleweka ambayo inaweza kuwafanya watu 10 tu wapoteze muda wao kukesha nayo ... Utanielewa vyema.

So wasomaji tunawapenda sana ila mnaweza kuwa sababu kubwa ya kuwakatisha tamaa waandishi wengi japo huwa hawasemi kwa sababu wanaogopa mtaanza kuwananga....

Msikunje sana, tuikuze hii tasnia iliyo sahaulika.

Binafsi niseme asanteni sana kwa kuwa pamoja nami mpaka sasa. Wale ambao walilike, walio-comment, walio pita kimya lakini waliyapenda maandishi..... Wote nawaheshimu sana.

Me i got much love for you guys....

No Hard Feelings..... Love [emoji3590]

CIAO [emoji112]
Kazi nzuri sana mkuu. Ila usikubali baadhi ya watu wakafifisha talent uliyonayo, kuna baadhi ya members humu wana tabia chafu sana na ukifatilia kwa makini hata huko majumbani mwao hutukana wazazi wao, so jitenge nao na ufocus kwenye malengo yako.
 
Nimemwaga vipande vyote mpaka mwisho.....

Ni matumaini yangu umepata burudani ya kutosha.


Next time usisahau pia kuwasupport waandishi, sio lazima mimi bali mwandishi yeyote. Mara Moja Moja toa chenji mfukoni nunua kukuza tasnia kwa sababu itakuja kufa hii maana Bongo uandishi umekuwa kama upotezaji wa muda tu.

Wengi huwa nawaona wanavyo wakebehi waandishi hapa na kuwapangia kuletewa simulizi muda wanao taka wao bila kujali waandishi wanapitia nini ila uhalisia ni kwamba uandishi ni kazi ngumu kuliko wengi wenu mnavyo hisi au kuambiwa na kuupambanua humu......

Ukitaka kuamini hilo andaa kazi ya kueleweka ambayo inaweza kuwafanya watu 10 tu wapoteze muda wao kukesha nayo ... Utanielewa vyema.

So wasomaji tunawapenda sana ila mnaweza kuwa sababu kubwa ya kuwakatisha tamaa waandishi wengi japo huwa hawasemi kwa sababu wanaogopa mtaanza kuwananga....

Msikunje sana, tuikuze hii tasnia iliyo sahaulika.

Binafsi niseme asanteni sana kwa kuwa pamoja nami mpaka sasa. Wale ambao walilike, walio-comment, walio pita kimya lakini waliyapenda maandishi..... Wote nawaheshimu sana.

Me i got much love for you guys....

No Hard Feelings..... Love ❤️

CIAO 👋
KAZI Bora kabisa,
Shukrani sana mtunzi. 🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝
 
Back
Top Bottom