FEBIANI BABUYA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 1,916
- 3,850
- Thread starter
- #261
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 88
“Yuko wapi baba yangu?” aliuliza lakini hakuna ambaye alijihangaisha kuweza kumjibu.
“Nawauliza yuko wapi baba yangu?”
“Kuna kazi nahitaji uifanye kwa ajili yangu ndiyo maana upo hai mpaka sasa”
“Siwezi kuongea na wewe lolote mpaka nijue hali ya baba yangu”
“Baba yako amerudishwa nyumbani, kazi yake ilikuwa rahisi tu kukuleta wewe kwangu kisha nikamalizana naye baada ya wewe kufika. Kwa sasa familia yako itakuwa salama kwa muda mfupi tu kama utakubali kuifanya kazi hii basi mimi nitaiacha salama ila kama utagoma basi nitaua kila mtu kwenye familia yako nadhani unajua kabisa kwamba kwa sasa mimi sina cha kupoteza kwenye huu ulimwengu” Damasi alimeza mate kwa shida akiwa anahema kwa wasiwasi mwingi.
“Kazi gani hiyo?”
“Nahitaji unikutanishe na Yohani Mawenge pamoja na bosi wake au Yohani mwenyewe tu atatosha”
“Hilo ni jambo ambalo haliwezekani kwa sababu bosi sijawahi kupata nafasi ya kukutana naye hata Yohani anako kaa sikujui, huwa anatutafuta mara moja moja sana kukiwa na kazi maalumu ya kufanya”
“Mpaka huwa anawatafuta maana yake una namna ya kuweza kumfikia, nahitaji unikutanishe naye kwa namna yoyote ile kama hautaweza kufanya hivyo basi unajua kinacho enda kutokea”
“Na ukikutana nao una mapango gani?”
“Kinacho fuatia huko mbele wewe hakikuhusu, nimeingia makubaliano na baba yako kwamba ukikubali kufanya kazi yangu nitakuacha uishi na siri yako ya kudanganya kifo utabaki nayo mwenyewe ila kama ukigoma basi inatakiwa kurudi maiti nyumbani kwake”
“Nitaifanya ila naomba sana usiifanye chochote familia yangu”
“Natarajia baada ya hapa utakuwa mtu mwema, sitegemei kuja kukutafuta tena kwa sababu kama hii ambayo imetukutanisha leo” Damasi alitikisa kichwa chake. Edison alimfungulia mwanaume huyo na kumpa vidonge vya kutuliza maumivu kwani mwili wake bado ulikuwa na maumivu makali, alikunywa dawa hizo na kujinyoosha. Alimtoa mpaka nje na kumruhusu aweze kuondoka lakini jambo hilo Nicola hakufurahishwa nalo kabisa.
“Hili ni kosa kubwa unalifanya kumruhusu aweze kupafahamu tunapo ishi, huoni kama anaweza kurudi kwa mara nyingine tena hapa akiwa na mpango mwingine kichwani?”
“Atakuwa hayapendi maisha yake kwa sababu atakuwa amejichimbia kaburi ambalo nina uhakika kwa kilicho tokea hayupo tayari kufanya hivyo lakini kama akifanya hivyo pia atakuwa kanisaidia mimi kuwapata kirahisi watu hao hivyo waache waje” Edison alionekana kujiamini isivyokuwa kawaida hali iliyo anza kuleta mashaka kwa Nicola, wanadamu hawakutakiwa kuwekewa imani.
Aaliyah alikuwa ofisini kwake akiwa mwingi wa mawazo, ni asubuhi hiyo tu alikuwa ametoka kushuhudia mauaji ya makamu wa raisi namna yalivyokuwa, kichwa chake hakikuwa sawa. Edison alikuwa anaonekana wa kawaida machoni ila matukio yake yalikuwa ni ya kutisha isivyokuwa kawaida, alipiga hesabu zake zikagoma, yaani mtu anamuua makamu wa raisi halafu anataka sura yake ionekane? Kivipi? Hakuwa na jibu la moja kwa moja lakini alihisi kwamba mtu huyo huenda alijua hawawezi kutangaza hadharani kwamba yeye amehusika kwa sababu umma ulikuwa unajua kwamba amekufa ama watu hao kufanya hivyo wangekuwa wanaanza kutoboa siri zake mwenyewe.
Aliachana na hayo mawazo na kuingia kwenye chumba cha mikutano ambako wenzake watatu Jumapili Magawa, Davidi Mbatina na Ruben Magesa walikuwepo. Hatua zake za kinyonge ziliwapa ishara wenzake kwamba mambo hayakuwa sawa hata yeye alikuwa anawaangalia watu hao kwa macho ya mawenge makubwa kwa sababu hakuwa akiwaamini tena, alihisi watu hao walikuwa wanamzunguka na kula sahani moja na bosi wake na muda wowote bomu lilikuwa linamlipukia hivyo alitakiwa kwenda nao kwa akili hususani baada ya kugundua kwamba usiku wa jana alikuwa anafuatiliwa na Jumapili ambaye alikuwa amejikausha kama hakuna jambo ambalo lilikuwa limetokea kabisa.
“Jumapili unaweza ukaniambia uliishia wapi kwenye ile kazi ya kuifuatilia familia ya Damasi kujua kilicho tokea mpaka akadanganya kifo?”
“Ndiyo nilifuatilia kwa umakini lakini familia yake inaonekana kutojua lolote na kaburi lake lipo vile vile”
“Lakini kuna taarifa kwamba askari polisi ambaye alikuwa anaitwa Julius alifukua kaburi hilo na kwenda kufanya vipimo juu ya ukweli wa jambo hilo lakini usiku huo huo alikutwa amekufa huko ufukweni, una taarifa yoyote kuhusu hili labda?” walikuwa kama wanachorana sasa kila mtu hakuwa na uhakika na mwenzake.
“Hizo ni taarifa ngeni kabisa kwangu kwani mzee Kazimoto anasema kwamba askari huyo alienda huko tu kufuatilia jambo hilo lakini hakufanya hayo yote ya kufukua kaburi”
“Una uhakika?”
“Ndiyo kiongozi”
“Sawa, kuna taarifa mbili mbaya” wote walibaki wamemtumbulia macho kusubiri atoe taarifa hizo”
“Ya kwanza ni kifo ambacho kimefichwa ila ni kwamba bondia maarufu Wilson Ndamaru alikutwa amekufa ila inaonekana kuna watu wanajaribu kuhitaji kulificha jambo hili” wote walibaki wametulia bila hata kushtuka maana yake hiyo taarifa walikuwa nayo, alishangazwa na jambo hilo kwamba vijana wake wanapataje taarifa ambayo hata yeye hana? Alibaki ameduwaa tu akaishia kujicheka maana alionekana kama mjinga mbele yao.
“Kwahiyo mnajua hata ambao wapo nyuma ya hili?”
“Hapana”
“Mbona mna taarifa hizi na hakuna hata mmoja wenu ambaye amethubutu kuniambia?”
“Tulijua utakuwa nazo”
“Basi nina uhakika hata hizi habari zingine mtakuwa nazo haina haja ya kuwaambia” aliongea kwa hasira ila alijaribu kujizuia kwa sababu wenzake ni moja kwa moja walikuwa wanamtenga halafu kibaya alikuwa ndiye kiongozi. Angeweza kuwawajibisha kama angejua mkurugenzi yupo upande wake lakini alijua kabisa mkurugenzi hawezi kumuelewa ukzingatia kwa yale ambayo aliyasikia kwa kiongozi huyo kwenye simu.
Aliukunja mkono wake kwa hasira huku akiwa anauma meno yake lakini akiwa hajanongeza neno lolote aliingia kijana mmoja akiwa kwenye suti na kifaa cha mawasiliano kwenye sikio lake humo ndani.
“Team leader mkurugenzi anakuhitaji haraka ofisini” aliwaangalia wenzake kwa awamu, hakuongea kitu na kuelekea alikokuwa ameitwa na mkurugenzi wake. Aliingia ofisini na kumkuta mwanamama huyo akiwa anaangalia nje ya dirisha la kioo kizito cha shaba, aligeuka baada ya kugundua kwamba binti huyo alikuwa ameingia humo ndani.
“Umeishia wapi kwenye kesi ambayo nilikupatia?”
“Mwanasheria ameuawa, wananchi wamepaniki wanahitaji majibu ya sababu za kuuawa kwake lakini kwa bahati mbaya imeenda kutengenezwa stori ambayo siyo ya kweli ili kumchafua yeye na Edison bila sababu za msingi kwanini usinge subiri tufanye uchunguzi ndipo tutoe majibu bosi?” mwanamama huyo alimwangalia kwa jicho kali baada ya kutamka kauli hiyo, ni kama alikuwa anaingilia majukumu ya bosi wake na kumuona hajui anacho kifanya.
“Vipi unaona kwamba mimi sijui kuifanya kazi yangu?”
UKURASA WA 88 unafika mwisho.