Simulizi ya kijasusi: Nafsi zilizotelekezwa

Simulizi ya kijasusi: Nafsi zilizotelekezwa

HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 40

“Hivyo kitu ambacho kimeniweka mimi hapa ni kwamba nahitaji jambo hili lipatiwe majibu, nataka mtu huyu achunguzwe kwa umakini bila kuumizwa au kuvamiwa kutekwa. Nataka taarifa zake zote, nahitaji historia yake sahihi na kama kuna ndugu zake basi wapatikane, nahitaji kila taarifa juu ya ukuaji wake na maisha yake ya nyuma na nijue hizi habari yeye alikuwa anazipatia wapi. Baada ya hapo nitafanya maamuzi ya nini cha kufanya juu yake, Aaliyah nakupa masaa arobaini na nane, utajua namna ya kufanya na vijana wako ila nayahitaji hayo majibu kwa huo wakati ambao nimeutaja hapo” Alimaliza bila kuruhusu swali lolote kutoka kwa hao vijana wake, alitoka humo ndani. Hakuonekana kuwa na amani, jambo hilo lilimvuruga pakubwa na kumpa hofu kwa wakati mmoja, lilikuwa jambo zito kutokana na aina ya mtu ambaye walikuwa wanaingia naye kwenye ulingo huo. Mwanaume ambaye aliijua sheria vilivyo nayo ikamtii, alikuwa ana uwezo wa kufanya lolote kwenye sheria na kila kitu kinaenda atakavyo yeye, ungemwambia nini JACK kuhusu sheria? Mkurugenzi hakujali kama mwanaume huyo alikuwa sahihi au hakuwa sahihi ila jambo hilo kufanyika hatari yake ilikuwa ni kubwa kuliko faida ndiyo maana alihitaji kulizuia haraka kabla halijatokea.
Aalyah alisimama na kusogea mbele, ni yeye ambeye alikuwa kiongozi wa wanaume hao. RIGHT HAND, ndilo jina ambalo walikuwa wanalitumia ikiwa na maana ya mkono wa Kulia, kwanini? Kwa sababu waliamini wao ndiyo ilikuwa nguzo mhimu kwenye shirika hilo, wao ndio walikuwa kama mkono wa kulia wa mkurugenzi na kamwe hawakuwahi kumuangusha na ndiyo sababu haswa aliamua kuwapa kesi hiyo akiwa na imani kwamba walikuwa wanaweza kuishughulikia kwa usahihi kuliko mtu yeyote yule.
Wote walibaki kimya kila mmoja akiwa anamtazama mwenzake kwa vituo, kilicho washangaza sio kusikia kuhusu kesi hiyo hapana, walikuwa wanaijua kesi hiyo kwa muda mrefu na ni kesi ambayo walijua kwamba ni serikali iliifuta makusudi kwa sababu ambazo hazikuwahi kuwekwa wazi ila wao kama wapelelezi walijua kabisa mambo hayakuwa sawa ila haikuwa kazi yao hivyo nao wakaachana nayo. Jambo ambalo hata wao liliwashtua ni aina ya mtu ambaye aliamua kulivalia njuga swala hiyo, mwanasheria ambaye hata wao walikuwa mashabiki zake wakubwa kwa namna alivyojua kucheza na kalamu yake pamoja na ubongo wake kwa wakati mmoja.
Hawakuijua sababu ya mwanasheria huyo kujiingiza kwenye sakati zito na baya kama hilo ambalo ni lazima lingeisha vibaya kwa upande wake yeye;
“Mimi nilijua tu ipo siku hili jambo litafufuta. Moja kati ya makosa makubwa ambayo huwa yanafanyika serikalini ni kufanya kila kitu kimazoea, viongozi wakubwa huwa wanahisi kwamba watu wote ndani ya taifa hili akili yao ni moja. Sio kila mtu ni mjinga ila kuna watu huwa wanainamisha vichwa kama hawapo na muda wao sahihi unapofika basi wanaweza kukushangaza kwa mengi na ndiyo haya ambayo yanaanza kutokea. Kosa lililofanywa ni pale ambapo wahusika walilizima jambo hili kiholela wakiamini kwamba halitakuwa na madhara yoyote yale ila walipaswa kuwa smart zaidi ya hapa” Jumapili Magawa, moja kati ya mmoja wa kikosi hicho aliongea kwa masikitiko kuhusu jambo hilo.
“Kuna kitu unahisi labda Jumapili?”
“Ndiyo, Kwenye ile miaka mitano ambayo imepita komando mmoja tena mwenye mafunzo ya hali ya juu hakupatikana eneo la tukio zaidi ya damu yake huku watu ambao walitumwa nao miili yao haikukutwa, nyie hamhisi kwamba kuna kitu hakipo sawa hapo? Mtu huyo licha ya kutafutwa lakini bado hakukuwa na dalili zozote za uwepo wake hapa duniani jambo ambalo lilifanya vyombo vya dola kupoteza matumaini ya kumpata na kuamua kuachana na habari yake ukizingatia wakati huo huo mtu huyu anapotea kulikuwa na habari kwamba aligundulika kuwa mtoto wa yule mwanasayansi wa zamani ambaye naye alipotea kwenye mazingira ya kutatanisha kwa kudaiwa kupelekwa Israeli”
“Wakati huo huo anakuja kugundulika mchungaji akiwa anaingia katikati ya haya, halafu baadae baada ya komando huyo kupotea anatokea mwanasheria nguli anadai kwamba ana ushahidi wa mambo yote hayo ambayo yalitokea tena akiwa anajiamini kabisa na mtu yule hajawahi kuongea jambo ambalo hana uhakika nalo ndiyo sababu hajawahi kupoteza kesi hata moja kwenye maisha yake na nina uhakika serikali wakikubali kwenda naye mahakamani basi lazima serikali ipoteze”
“Maana yako ni ipi hasa?”
“Nina uhakika huu unaweza kuwa mpango wa yule komando ambaye alipotea kwa sababu ndiye alikuwa na taarifa zote hivyo huenda ndiye alimpatia huyu mtu taarifa hizo, uzembe mkubwa ulifanyika kuruhusu yule mchungaji kuuawa kwa sababu angeturahisishia jambo hili. Na kama haipo hivyo basi huyu mtu atakuwa na taarifa za namna ya kumpata huyo komando” maelezo yake yaliwafungua wenzake kiasi fulani kiasi kwamba kila mtu akawa anawaza mara mbili mbili.
Wanaume wawili walikuwa wametulia wakiwa wanasikiliza kwa umakini mazungumzo ya wenzao, wanaume hao walikuwa ni mmoja kutoka ardhi ya watu wajivuni, mhaya David Mbatina pamoja na mkurya mmoja Ruben Magesa jitu la miraba minne ambalo lilikuwa linajiamini kwa kiasi kikubwa. Mjivuni David Mbatina alisogea mbele na kujikohoza kidogo ili kuwapa ishara wenzake kwamba alikuwa na jambo.
“Kwa sasa kuna jambo la mhimu hapa katikati ambalo linaweza kutupatia msaada mkubwa, kwenye moja kati ya habari za ajabu ambazo huyu mwanasheria aliwahi kuzitoa ni kuvujisha siri kwamba anaishi kwenye sura ya mtu mwingine. Habari hii ilionekana kama kiki tu na maneno ya kuzushwa ila ndani yake huenda ina maaan kubwa, nadhani hapa ndipo tunaweza kuanzia kufanyia uchunguzi ili tujue kama anaishi kwenye sura ya mtu mwingine kweli, ni sura ya na nani na kwanini afanye hivyo? Jibu likiwa ni kweli basi tuna asilimia themanini mpaka sasa za kuupata ukweli wa jambo hili haraka na mapema” jambo hilo lilionekana kuwa la maana hivyo walikubaliana kuingia kazini na asubuhi hiyo hiyo alitakiwa Aaliyah kwenye kwenye ofisi ya mwanasheria huyo ili kuteta naye jambo kama mwanzo wa kufanya uchunguzi wao ambao walitakiwa kuukamilisha ndani ya masaa arobaini na manane tu.

JACK THE LAWYER asubuhi alikuwa ndani ya ofisi yake, alikuwa ametulia kwa ajili ya kuweza kuianza siku hiyo mpya. Nje ya jengo hilo la ghorofa ambalo ndipo ilikuwepo ofisi yake kulikuwa na kelele nyingi za watu wakiwa wanamshangilia, watu hao walikuwa wanalitaja jina lake kwa msisitizo huku wakilinadi na kumuona kama shujaa wa taifa. Alikuwa amezisikia kelele hizo tangu anafika ila hakutaka kwenda, sio kwa sababu aliwapuuza wananchi hao, lahasha! Bali kwa sababu aliupa muda nafasi na angewaonyesha na kuja kufanya mahojiano yake baada ya serikali kutoa jibu la kueleweka, hakuwa mtu wa kuyafanya mambo kwa haraka.
Aliingia katibu muhtasi wake, mwanamke mrembo ambaye kwa mwonekano wake miaka ilikuwa inaelekea thelathini.
“Bosi kuna mtu hapa anadai kwamba ni askari anahitaji kuonana na wewe, nimempa taarifa kwamba hauna muda saivi ila kasisitiza hivyo nimekuja kukuuliza kama utaongea naye au nimtoe aondoke” sauti hiyo ilimfanya aache kila alichokuwa anakifanya, alisimama na kusogea pembezoni mwa dirisha ambalo lilikuwa na vioo vilivyo mfanya auone mji kwa usahihi.
“Mwambie aingie” alijibu akiwa hajajisumbua hata kuangalia nyuma. Mlango ulifunguliwa, aliye ingia, alikuwa ni Aaliyah Beka.
“Naitwa Warda Abdul, ni askari mpelelezi kutoka ndani ya ofisi ya afisa upelelezi wa mkoa; Naomba muda wako kidogo niweze kukuuliza maswali kadhaa” Aaliyah aliongea kwa kujiamini kwa sababu hakuwa na papara na kazi yake, Jack bado alikuwa amempa mgongo lakini hakuchukua muda, aliogeuka akiwa na tabasamu usoni kwake huku akiwa anamwangalia kwa umakini mwanamke ambaye alikuwa mbele yake akiwa amezifunika vyema nywele zake kiasi kwamba yale maadili yaliendana na jina lake ambalo alilitambulisha hapo.
“Nambie kilicho kuleta kwenye ofisi yangu asubuhi yote hii Aaliyah Beka” Alibaki ameduwaa kiasi kwamba alilegea na kuyumba ila alijikaza kukaa vizuri. Alibaki ametweta kwenye uso wake asielewe lile jambo ambalo lilikuwa linaendelea pale wakati ule, maisha yake yalikuwa ya usiri mkubwa lakini mwanaume huyo alikuwa akilifahamu jina lake. Sasa kivipi? JACK alisogea kwenye kiti chake na kuketi huku akimuonyesha ishara mwanamke huyo ambaye aliishiwa pozi naye aketi.
“Nadhani umenielewa vibaya, umenitajia jina ambalo sio langu na sijui ni mtu yupi ambaye unamaanisha” Aaliyaha alijitetea.

UKURASA WA 40 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 41

“Usitake tupoteze muda kwenye jambo ambalo mimi na wewe tunaujua ukweli wake, haina ulazima nikupe taarifa zako kuanzia uliko zaliwa mpaka uliko patia mafunzo yako, haina sababu ya msingi ya mimi kukutajia vijana ambao wapo nyuma yako wale watatu ndipo uwe na uhakika kwamba nina taarifa zako zote. Niambie kilicho kuleta kisha uende maana nina mambo mengi ya kufanya” Alimjibu mwanamke huyo akiwa amemkazia uso mkavu kabisa, Aaliyah aliguna na kumeza mate maana utambulisho wake bandia ulikuwa ni kupoteza muda tu.
“Umefanikiwa vipi kulifahamu jina langu na kazi yangu?”
“Nina taarifa nyingi za hili taifa, nina taarifa za watu wengi ambazo nikiamua kuziweka wazi basi unaweza ukakuta hata Ikulu inaweza kuanguka na kuleta machafuko kwenye taifa hili. Kuwa na taarifa nyingi na sahihi ndiko ambako huwa kunanifanya nafanya mambo yangu kwa uhakika kwa sababu nachagua taarifa ambayo naihitaji, naangalia wakati ambao ni sahihi kisha naamua kuiachia”
“Mara ya kwanza nakuona kwa macho yangu nilikuchukulia kama mwanasheria wa kawaida tu ambaye uliamua kuzipambania ndoto zako na kuziishi kwenye ujana wako. Lakini baadae japo sikutilia maanani, baada ya lile tukio la milipuko kule Gongo la Mboto nilikuona kwenye halaiki ukiwa umejitokeza kusaidia watu wasio jiweza, wewe ni miongoni mwa watu ambao walisaidia watu wengi zaidi japo jambo hili huenda halifahamiki kwa sababu hupendi kuishi kwenye maisha ya picha. Kwenye lile tukio niliona kitu cha tofauti, kuna mtoto alikuwa amezidiwa kama anaelekea kufa, ulichanganyikiwa kabisa ukiwa unahaha kumsaidia kiasi kwamba nikabaki nashangaa na kutaka kujua kama labda ni mtoto wako ila niligundua kwamba hakuwa mtoto wako bali ni mtu tu ambaye uliamua kumsaidia. Kuanzia siku ile ulinigusa nikawa mmoja wa mashabiki zako ila nahisi ile hofu huenda ilikuwa na jambo nyuma yake”
“Upo sahihi, sikujua kama ulikuwa unanichunguza kuanzia wakati ule. Miaka kadhaa huko nyuma niliwahi kufanya jambo ambalo huwa linanifanya najuta mpaka leo unapo niona na huu umri wangu. Ufahari wangu na kujivuta vuta kulisababisha mama na mtoto wakafa, mwanamke yule alinifuata na kuhitaji msaada lakini mazingira ambayo tulikutana ndiyo yalinipa wasiwasi hivyo nikahitaji nijipe muda kwanza nijiridhishe ili nisije kufanya kosa lolote lakini kumbe ule muda ambao nilikuwa nautumia kujivuta vuta nilikuwa nachelewa hali ambayo ilipelekea yeye na mtoto wake kupoteza maisha”
“Kwa maana hiyo ni kwamba kama ingetokea nikamsaidia mapema basi kulikuwa kuna uwezekano wa kuyaokoa maisha yake. Lile ni tukio ambalo lilinikaa kichwani mwangu kwa muda mrefu hivyo nikawa natumia muda mwingi kulijutia, ile hali ilinifanya kusaidia watu kwa wingi zaidi na kuwa mwepesi pindi mtu anapo nihitaji ndiyo maana baada ya kuona wale watoto wakiwa kwenye ile hali ya mateso na njaa, iliniuma kwa sababu nilikuwa nikilikumbuka tukio lile kwenye akili yangu. Kwenye maisha yako ukipata nafasi ya kusaidia watu, achana na mawazo ya kwamba watanisaliti, hawatanisaidia baadae au wao watanikataa wewe wasaidie tu kwa sababu msaada hauna malipo bali moyo wako ndiyo unatoa”
“Unatakiwa kuacha unacho kifanya Jack”
“Hicho ndicho ambacho wamekutuma wakubwa wako?”
“Nimekuja hapa kama mimi binafsi kwa sababu nahitaji uniambie ukweli, wewe ni nani?”
“Kabla ya kuhitaji kujua kwamba mimi ni nani jambo ambalo nina uhakika haliwezekani nataka kujua wewe na wenzako mmefikia wapi kwenye kesi ya watu ambao wanaliendesha taifa hili ingali sio watanzania?” swali la Jack kilikuwa kama kisu mfupani kilivyo mchoma Aaliyah.
“Nchi inaongozwa na raisi mtanzania na hata wote ambao wapo madarakani ni watanzania sasa unanipa habari gani hizo?”
“Mimi na wewe wote tunajua kwamba kuna viongozi huwa wanawekwa pale kama mapazia tu ila kuna watu ambao wanaliendesha taifa wakiwa kwenye mlango wa nyuma. Nina uhakika unaelewa juu ya uwepo wa LUNATIC SOCIETY!”
“Hapana”
“Bibie naona upo kwenye mlengo wa kuwalinda wakubwa zako si ndiyo? Naweza kukupa nafasi ya maisha wewe na wenzako kama mtakubali kufanya kazi chini yangu”
“Hahaha sina imani kama wewe ni mtumiaji wa pombe lakini nahisi leo utakuwa umelewa”
“Mimi sijawahi hata kuijua ladha yake, nakwambia haya kwa sababu hautapata nafasi nyingine kama hii, nyie wote mtahitajika kufa kwani hamtakuwa na umuhimu wowote kwa taifa hili”
“Kwamba unanitisha?” Jack hakuongeza neno bali alitoa picha kwenye mfuko wake wa koti na kuirushia mezani alipokuwa ameketi mrs Beka. Picha hiyo ilikuwa na sura ya mwanamke ambaye alikuwa na asili ya nchi ya Urusi.
“Picha ina maana gani hii?”
“Hiyo ndiyo picha ambayo imeleta matatizo mengi ndani ya nchi hii, ndiyo picha ambayo ni sababu ya kila kitu kilicho tokea na bila shaka najua unaeleewa nazungumzia nini. Huyo mwanamke sishangai wewe kutomfahamu kwa sababu maisha yake ni ya usiri mkubwa na wanayajua watu wachache wa kuhesabika na mimi nikiwemo. IRINA ESPANOVICH, ni mpelelezi wa zamani wa KGB lakini alifanya uasi kwa kuuza taarifa za nchi yake kwa Marekani hali ambayo ilipelekea kuanza kutafutwa ili auawe lakini alifanikiwa kutoroka. Alikuwa mke wa ofisa mkubwa ndani ya KGB hivyo alihatarisha usalama wa taifa lake kwa asilimia nyingi na ni miongoni mwa watu ambao walisababisha kwa kiwango kikubwa umoja wa kisovieti kudondoka kwenye ile vita baridi”
“Huyo ndiye mwanzilishi wa jamii ya Wendawazimu hapa nchini. Baada ya kutoroka alikuja Tanzania ambapo alianzisha maisha mapya, wakati anaanzisha jamii hiyo alipata upinzani kutoka kwa raisi ambaye alikuwa madarakani Justin Nyangasa hali ambayo ilipelekea raisi huyo kuuawa kwa kutumia sumu ambayo ilitengenezwa na mwanasayansi Dr Christian Edison. Baada ya hapo aliwaweka watu wake kwenye nafasi za mhimu za serikali hivyo naweza kusema yeye ndiye ambaye amekuwa akiliendesha taifa hili kwa miongo kama mitatu sasa na kupanga kila kitu ila kitu kimoja kuhusu mwanamke huyu ni kwamba hajawahi kuonekana wala kujulikana kama bado yupo hai au kama amekufa kisha watu wengine wakaimu nafasi yake ila kuna mtu mmoja tu ambaye anajua ni wapi alipo huyu mwanamke” Licha ya kuwa na nafasi kubwa ndani ya shirika la IBA lakini taarifa ambazo alikuwa anapewa Aaliyah nyingi zilikuwa ngeni kwake, aliwahi kusikia stori kadhaa kuhusu jambo hilo ila hakuwa na mengi kama ambavyo alikuw anayo mwanasheria huyo.
“Unaweza ukaniambia ni nani huyo?”
“Hapana, siwezi kukwambia hiyo ni kazi yako wewe kutafuta jibu kwa sababu hata mtu huyo kwa sasa hajulikani kwamba ni wapi yupo. Hivyo nimekupa taarifa hizo ili uifanye kazi hiyo na kama ukiifanya kazi hiyo basi mimi na wewe tunaweza kuwa kwenye meza moja”
“Hapo ndipo unakosea Jack, unahisi kwamba labda mimi nimekuja kukubembeleza hapa? Unahisi kwamba labda ninaweza kuagizwa na mtu kama wewe na nikafanya vile ambavyo unataka wewe? Nimekupa nafasi ya kujielezea kwa sababu yanaweza kukupata mabaya muda sio mrefu”
“Mwambie huyo bosi wako aje kuzungumza na mimi kama ana shida ya kujibiwa hayo maswali ambayo yanamfanya ajifiche nyuma ya vijana wake. Umekuja hapa kwa sababu kubw ambili, ya kwanza ni kuhitaji kujua mimi ni nani kwa sababu nawachanganya, lakini unatamani kujua sababu ya mimi kuyafanya haya na kama ikiwezekana kujua kama kuna mtu nyuma yangu ambaye ananifanya mimi nazipata taarifa nyingi kuliko hata nyie ambayo ndiyo kazi yenu. Lakini jambo la pili umekuja hapa kuzuia kile ambacho nakifanya hususani cha kuhitaji kuishtaki serikali pamoja na viongozi wenu wapuuzi ambao wamesababisha na wanaendelea kusababisha maafa kwa watu wasio na hatia kwa mgongo wa kudai nchi itaingia kwenye machafuko. Hauna huo ubavu wa kunifanya chochote binti au kunishauri mimi cha kufanya kwa sababu hata uwezo wako kichwani bado ni mdogo hivyo kafanye kazi ambayo nimekupa na kama ukiikamilisha utarudi hapa nitaangalia namna ya kuwasaidia na kuwasikiliza ila kama huwezi basi toka nje ya ofisi yangu” Aaliyah alishangaa namna mwanaume huyo alivyokuwa anajiamini. Shirika lao lilikuwa likiogopeka mahali popote pale ambapo lilikuwa likitajwa lakini ilikuwa tofauti kabisa kwa Jack, aliwaona watu wa kawaida tu mbele yake na sasa alimtaka mwanamke huyo atoke ndani ya ofisi yake.

UKURASA WA 41 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 42

“Hii siku ya leo nitaiweka akilini JACK, dharau yote ambayo umeionyesha mbele yangu nitailipa na nakuahidi utaijutia hii nafasi ambayo umeipoteza” Aaliyah aliongea kwa hasira akiwa anaondoka na kuhitaji kutoka lakini alisimama baada ya mwanasheria huyo kumuita na kunyanyuka kisha akamsogelea mwanamke huyo na kumkumbatia kwa nyuma bila ridhaa yake kisha akamnong’oneza kwenye sikio lake.
“Iangalie hiyo mihemko yako bibie kwa sababu unatakiwa kuipeleka kitandani sio kwenye dunia ya mtu kama mimi, hili ni jambo la hatari kwako. Muda huu unatakiwa kuufanyia kazi ushauri wangu ikiwemo kuwatafuta watu wengine wawili, Damas Kazimoto mwanajeshi ambaye aliigiza kifo chake na juzi ameonekana kwenye tukio la pale uwanja wa ndege lakini pia unatakiwa kumtafuta Nicola Aidan Semzaba ambaye alitekwa pale uwanja wa ndege. Unafaa tukiwa kitandani ila usije ukajaribu kuhitaji kunipima na kujua nipoje, sihitaji kumuua mwanamke mrembo kama wewe kwa kutumia mkono wangu. Lizingatie neno hili HII KAULI IISHIE KWANGU TU NA SIO KWAKE ATAKUUA BILA KUKUULIZA CHOCHOTE” Maelezo aliyasikia vizuri akiwa amekumbatiwa, yalimtisha na kumshangaza kwani alianza kuona dalili kabisa kwamba mwanasheria huyo hakuwa yule ambaye watu wengi walikuwa wanamjua na kumuona mahakamani bali kulikuwa na dunia yake ya siri ambayo ilimpa hiyo hali ya kujiamini kupitiliza. Hayo yote hayakuwa ya mhimu ila ile kauli ambayo aliambiwa aizingatie ndiyo ilimfanya moyo wake uanze kupiga kwa nguvu, alihisi jasho linamtoka kwenye mwili wake kwa kasi japo alikuwepo ndani ya chumba ambacho kilikuwa na hali safi na ubaridi usio kera. Aliwaza kwamba je kulikuwa na mtu mwingine? Ni nani hasa mpaka apewe tahadhari ya kuto mwambia kauli hiyo ya kitisho? Moyo ulitahamaki, nafsi ikatahayari kwa kile alicho kisikia ila hakuwa na uwezo wa kuuliza kwani mazungumzo yalikuwa yameisha na mtu huyo alimpa ishara ya kuweza kutoka ndani ya chumba hicho akiwa mwingi wa mawazo. Alipewa mengi ambayo hakuyajua lakini aliongezewa mtihani wa kuchambua baadhi ya taarifa zingine.

JACK THE LAWYER baada ya kuhakikisha Aaliyah ameondoka ndani ya eneo lile, alisogea kwa kabati kubwa ambalo lilikuwa limejaa tuzo ambazo alizipata kwenye maisha yake ya kuiongoza sheria. Aliweka kidole chake kwenye sehemu ndogo ya kioo ambayo ilikuwa pembezoni mwa kabati hilo, kabati likajisogeza pembeni ambapo ulitokea mlango. Pembeni kulikuwa na namba za kuingiza, alingiza namba kadhaa kwa kuzichanganya kama kumi na sita ndipo mlango ukafunguka naye akaingia huko ndani.
Kilikuwa chumba kizuri ambacho kilipambwa kwa kitanda, kabati kubwa, friji moja, kompyuta kadhaa ukutani pamoja na kioo kikubwa ambacho kilibandikwa ukutani. Alisogea kwenye kioo hicho na kujitazama kwa muda mrefu, kwenye mfuko wake wa koti upande wa kushoto kulikuwa na picha, picha ambayo aliitoa na kuiangalia kwa umakini naye akiwa anajitazama kwenye kile kioo kikubwa. Picha ile ilikuwa ni ya Edison Christian, haikujulikana sababu ya msingi ya yeye kuwa na picha ya mtu huyo ambaye alikuwa anatafutwa kila kona ya jiji. Aliitazama kwa muda na kutamka

“Uko wapi Edjr, nahitaji kwenda kupumzika, muda wangu wa kufa umefika sasa ebu jitokeze uichukue nafasi yako haya maisha sio sehemu yangu” aliongea kwa uchungu kiasi kwamba chozi lilimshuka usoni taratibu. Alionekana kuwa na mengi yaliyokuwa yakipita akilini mwake kiasi kwamba hata kuendelea kuishi yalikuwa maumivu makali upande wake. Hisia zake zilimrudisha miaka ya nyuma;

Miaka mingi iliyopita eneo la Tukuyu kijana mmoja wa kiume wa miaka kumi na mitano alikuwa akiishi na baba yake mzazi. Kijana huyo hakuwa na furaha kabisa kwenye maisha yake kwa sababu kuu mbili, sababu ya kwanza ulikuwa ni umaskini ulio kithiri kwao lakini sababu ya pili ni kwa yale ambayo yalikuwa yamewatokea miaka kadhaa ambayo ilipita. Baba yake alikuwa mchuuzi wa samaki ambapo alikuwa analazimika kwenda ziwa Nyasa kwa ajili ya kuvua hususani upande wa fukwe ya Matema lakini muda mwingine alikuwa akijishughulisha na biashara ya nafaka maeneo ya Tukuyu mjini.
Ukiachana na umaskini ambao ulimfanya kila awapo na wenzake aishie kuchekwa kitu ambacho kwake hakikumuumiza ila jambo ambalo liliwakuta kwenye maisha yao ndilo ambalo lilikuw alinajirudia kichwani mwake. Baba yake alikuwa mzaliwa wa Zambia lakini mama yake alikuwa ni Mnyakyusa wa Kyela, baba yake alikuja miaka kadhaa huko nyuma kwa ajili ya kutafuta maisha ndani ya jiji la Mbeya lakini kutokana na sifa nzuri za huko Kyela akaamua kuchangamkia fursa na kwenda kujaribu bahati yake.
Kuishi kwake huko hususani maeneo ya fukwe ya Ngonga kulimsaidia kukutana na mwanamke mrembo wa Kinyakyusa, hakuwa na kikubwa cha kumpa lakini aliziweka wazi hisia zake kwa mwanamke huyo naye akazielewa na kuzipokea. Mwanzo wao ukafunguliwa rasmi kwa penzi zito baina ya watu hao wawili ambao walionewa gere na watu wengi hususani watu ambao walikuwa na kipato kikubwa kumzidi, watu walishangaa kwanini mwanamke mrembo kama huyo awakatae wao na kisha kukubali kuwa na mwanaume kapuku asiye na chochote? Wengi wakawa wanamfingia mwanaume huyo na mrembo huyo na kuwapa onyo kama watafika popote pale na hayo mapenzi yao hata hivyo hawakujali zaidi ya kuyaanza maisha.
Nkole Mwanawasa ndilo lilikuwa jina la mzambia huyo ambaye alikimbia kwao ambapo alikuwa anaishi karibu na mipaka ya boda ya Tunduma. Kukimbia kwake huko ni baada ya kusingiziwa kesi ya kuhujumu pesa za wafanya biashara ambao huwa wanabadili kwacha pale mpakani. Hakutenda kosa ila aliona kabisa kwamba akizubaa basi alikuwa anaishia jela na hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kumsaidia kwa kesi hiyo hivyo akaamua kuacha kila kitu na kwenda kuyaanza maisha mengine mapya huko Tukuyu.
Upambanaji wake mkubwa ambao alikuwa nao ulimsogeza mbele, wahenga walisema kosea vyote ila sio kuoa, alibahatika kumpata mwanamke ambaye alikuwa ana mipango mikubwa na maisha hivyo wakawa na lengo moja. Walilima mipunga huku akiendelea kuchuuza samaki, mafanikio yakawagongea hodi mlangoni kwao na wakati huo walikuwa wamepata mtoto wa kiume, kwa sababu yeye alikuwa mzambia wakaona ili mtoto asije kupata taabu kwa baadae basi wampatie ukoo wa mama yake hivyo akaitwa Chrispin Mwambano.
Alipendwa mno na wazazi wake kwenye ukuaji wake, licha ya vita ambayo walikuwa wanakumbana nayo kwa watu wa jamii hiyo kwa sababu hawakutaka wazazi wao kuwa pamoja ila bado alisimama kwa sababu wazazi wake walikuwa imara. Baba yake akawa miongoni mwa watu ambao walipata mafanikio makubwa, maisha yakakubali upande wake akawa mtu tofauti jambo ambalo lilimpa maadui wapya ambao walimuona kama tishio kwao kwa sababu walitamani kumuona akiwa anafeli siku zote za maisha yake.
Vita hiyo iliwafanya kupitia mambo mengi kwenye ukuaji wake ikiwemo kuharibiwa mazao na mali zao lakini baba yake hakukata tamaa mpaka alipo amua kuhama sehemu alikokuwa anaishi kwa muda na kwenda Kyela mjini ambako ndiko ulikuwa mwanzo wa historia mbaya ya maisha yao. Miaka ilikimbia lakini bado hawakuwa na amani, ndipo usiku mmoja likaokea jambo baya ambalo lilikuwa gumu kufutika kwenye kichwa cha Chrispin. Jambo hilo lilikuwa ni kuvamiwa kwa familia yao majira ya usiku wa manane, kuvamiwa haikuwa tatizo ila shida ilikuwa ni kile ambacho kilitokea baada ya kuvamiwa kwao siku hiyo.
Baba yake alifungwa na mama yake alikamatwa na watu ambao hakuwajua sura kwa sababu sura zao zilifunikwa kwa vitambaa vyeusi. Watu hao walimtesa baba yake na kumfunga huku yeye akiwa hana cha kufanya zaidi ya kukamatwa na wanaume waliokuwa na nguvu kwenye miili yao kisha akawa anatazama kinacho endelea akishusha machozi taratibu. Alilazimishwa kuangalia mama yake mzazi akiwa anabakwa mbele yake, lile tukio lilimuathiri pakubwa sana saikolojia yake, lile jambo liliharibu yale mazuri ambayo ubongo uliweza kuyahifadhi kwenye nafsi yake. Watu hao baada ya kukamilisha hilo walitoweka.
Alimuangalia mama yake pale chini akiwa anashusha machozi, alimuita mara moja wakati anamuona mama yake anananyuka na kuanza kukimbilia nje lakini hakuwa na cha kufanya zaidi ya kuzimia kwani alikuwa amepigwa na kitu kizito muda sio mrefu. Fahamu zake zilirudi majira ya asubuhi huku nyumbani kwao kukiwa na watu wengi, alishangaa kunani? Ndipo zile kumbukumbu zikaanza kurudi kwa kile ambacho kilitokea jana yake, alikurupuka na kuanza kumtafuta mama yake ila watu wazima wenye busara walimtuliza, walimtuliza ili kumjibu swali lake la wapi alipo mama yake mzazi. Habari ambazo aliambiwa, alitamani usiwe ukweli kwani kwake aliona kama ni ngumu kukubaliana moja kwa moja na jambo hilo ila ndio ulikuwa ukweli kwamba mama yake alikutwa akiwa amejinyonga juu ya mti ambao ulikuwa nje ya nyumba yao kwa kutumia kanga yake.

UKURASA WA 42 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 43

Lilikuwa pigo zito kwenye moyo wake, moyo wake ulikuwa unagala gala kwa maumivu makali huku lawama zote akiwapa wanadamu ambao walikuwa wanamzunguka ila angefanya nini? Alifuga kisasi kwenye moyo wake, alichukizwa na jambo hilo isivyo kawaida ila baba yake ndiye pekee ambaye alibaki naye. Baada ya msiba waliamua kuhama eneo hilo na kwenda kuyaanza maisha yao Kiwira ambako walianza upya na kila kitu na baba yake akawa mchuuzi akiwa anaenda kufuata samaki kule kule Kyela ambako ndiko mkewe aliuawa, je ilikuwa ni kweli? Hapana, hakuwa akifuata samaki tu bali alikuwa anawataka watu ambao walihusika kwenye mauaji ya mkewe kipenzi. Hakujali kwamba familia ya mkewe ilimtenga yeye na mwanae kabisa na waliapa kutowataka kwenye maisha yao yote kwa sababu ndugu yao aliolewa na mtu huyo bila ruhusa yao ila aliamua kulipa kwa ajili ya mkewe, malipo ambayo yalimuwahisha yeye mwenyewe kaburuni miaka mitatu baadae kwani akiwa anahangaika kuwatafuta waliamua kumuua.
Mwili wa baba yake uliokotwa ndani ya fukwe ya Mwamnyange ambaye aliwahi kuwa CDF wa jeshi la Tanzania. Chrispin akiwa na miaka kumi na minane alikuwa amebaki pekeyake. Alikuwa amemaliza kidato cha nne ila hakuona hata umuhimu wa elimu yenyewe, moyo wake ulighafilika pakubwa, majina ya watu ambao walikuwa wamehusika na hilo yalikuwa masikioni mwake kwani aliwahi kuyasikia kwa baba yake hivyo akaamua kujivika bomu kwenye moyo wake. Kwanza alitafuta mali zote za watu hao kama viwanda vidogo na mashamba ya mipunga pamoja na maduka alichoma vyote na kisha akahangaika na kuwaua wahusika wote bila kuacha ushahidi kisha akakimbia ndani ya eneo hilo na kupotelea kusiko julikana.
Kukimbia kwake hakuona sababu ya kuendelea kuishi tena kwa sababu maisha yake hayakuwa na thamani hata kidogo, kukata tamaa ya kuishi kukamfanya achukue hatua ya kuamua kuyatoa maisha yake kwa kwenda kujitupa juu ya daraja ili afie kwenye maji. Hakuna ambacho alikibakiza kwenye maisha yake yeye hivyo akaamua kufanya hivyo ila wakati anafanya jambo hilo ambalo alilifanyia Tukuyu kwa bahati iliyo njema mtumishi wa Mungu wa kanisa katoliki alikuwa amesafiri kutoka Shinyanga na kutembelea moja ya jimbo la huko Tukuyu.
Edward Pande ambaye ndiye alikuwa mlezi wa Edison alikuwa yupo huko kwa ziara za kulitangaza neno la Mungu na majira ya jioni alihitaji kidogo kuangaza mazingira yalivyo na alihitaji kuachwa pekeyake. Wakati akiwa anapita katikati ya daraja moja alimuona kijana mmoja mdogo akiwa amesimama kwenye kingo moja ya daraja na bila shaka alikuwa anahitaji kujirushia chini ya maji. Alishangazwa pakubwa na kijana wa umri mdogo kama ule kuhitaji kufanya maamuzi magumu namna ile, alikimbia kumuwahi ila alichelewa kwani wakati amebakisha hatua kadhaa kumfikia kijana yule alijiachia na kuelekea kwenye maji. Alivua lile vazi lake la utambulisho na kujitupa chini ya daraja lile bila kujali hatari iliyopo chini akafanikiwa kumuokoa kijana yule japo alikuwa kwenye hali mbaya kwani maji alikuwa ameyanywa ya kutosha.
Baada ya kijana yule kupata nafuu alimsimulia hatua ambazo alipitia kwenye maisha yake na yale ndiyo maamuzi sahihi ambayo yangemfanya apumzike kwa amani. Licha ya Mr Pande kumshawishi kijana yule lakini hakukubali kwa sababu aliomba kuwa anahitaji kufa. Mr Pande hakuwa na namna ila alimuomba ampe msaada wa kitu kimoja kwa sababu anahitaji kufa, msaada huo ndio ambao ulimfanya amhitaji kijana huyo aweze kuigiza na kudanganya maisha yake kwa baadae aje kujulikana kama mtu mwingine ili kumlinda kijana wake ambaye alikuwa ni Edison. Kwa sababu yeye alitamani kufa basi kuna siku angekufa ila alitakiwa kufa akiwa anayasaidia maisha ya kijana huyo mwingine, haikujalisha ni miaka mingapi ila kuna siku kujitoa kwake uhai ndiko ambako kungemfanya Edison kubaki salama.
Ilikuwa ni kazi ngumu kumshawishi ila mwisho wa siku alikubali hivyo akamtaka mtu huyo ampe maelekezo ya nini alitakiwa kukifanya na ni lini hasa alitakiwa kuifanya kazi hiyo ya kuja kufa ili kuyaokoa maisha ya mwenzake. Na hapo ndipo rasmi ulipo zaliwa mpango wa kumtengeneza CHRISPIN MWAMBANO kama IMPOSTER ili kuja kuuhadaa ulimwengu uje uamini kama yeye ndiye Edison Christian, kuuhadaa kwake ulimwengu ni pale ambapo angekufa basi dunia ingeamini moja kwa moja kwa Edison alishakufa tayari na wakati huo zingekuwa zimetengenezwa sura bandia ambazo ni mfanano wa uhalisia kwa asilimia tisini kwa kutumia teknolojia ya Three-Dimensional Printing (3DP) ili kuja kuwa na uwezo wa kubadili sura kulingana na mazingira na nafasi ambayo alitakiwa kuwa nayo kwa wakati huo.
Alikuwa kijana mpya wa siri ambaye Edward Pande aliamua kumsomesha kwa gharama kubwa na kumpatia mafunzo makali kwa usiri mkubwa kwa sababu ulikuwa ni mpango wa pili wa kumlinda mtoto wa rafiki yake kipenzi ambaye wakati anazijua siri zilizokuwa nyuma ya mzee huyo alikuwa tayari amekufa. Jack ndiye ambaye alihusika kwenda kumsaidia Edison kule Somalia na ndiye ambaye alimfutia kumbukumbu kichwani mwake ili asiweze kukumbuka matukio yoyote ambayo yangemuweka kwenye wakati mgumu lakini vivyo hivyo yeye ndiye ambaye alikuwa na uwezo wa kuzirudisha kumbukumbu zake.
Hizo ni kumbukumbu ambazo alikuwa anazikumbuka JACK THE LAWYER akiwa ndani ya chumba chake hicho cha siri ndani ya ofisi yake. Alikaa muda mrefu humo akiwa anamsubiri kwa hamu Edison aweze kumkabidhi yale ambayo alikuwa nayo kichwani kisha yeye akapumzike kwa kufa kama alivyokuwa akidai mwenyewe. Alishtuka baada ya kengere kugonga kwa nguvu kupiti alamu ya kwenye chumba hicho, aliangalia kwenye kamera na kugundua kwamba nje ya ofisi yake katibu wake muhtasi alikuwa anabisha hodi kwa muda mrefu na hapo ndipo akakumbuka kuangalia saa yake. Ulikuwa usiku tayari maana yake alitumia muda mrefu ndani ya chumba hicho bila kutambua huku nje kukiwa hakuna taarifa yake yoyote na kwa sababu hakuwa akipokea simu katibu wake alienda kuwaita walinzi ambao walikuwa wamejazana nje ya mlango wa bosi wao. Alifanya haraka na kutoka ndani ya chumba hicho kisha akatoka mpaka nje kabisa akiwa na mkoba wake na hakutaka kuongea jambo lolote hali ambayo iliwafanya walinzi wake wabaki wanamshangaa lakini hakuwajali, akawa anatoweka hilo eneo.

UKURASA WA 43 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 44

UPANGA
Hali ilikuwa shwari kutokana na eneo hilo kuupokea vyema upepo wa bahari. Dunia ilikuwa inashangilia kwa hali kuwa safi, anga liliwazoemea wale wote ambao maisha yalikuwa yakiwachapa bakora ndani ya jiji hili la mzizima hali ambayo ilikuwa tofauti kwenye nyumba moja ndani ya eneo la Upanga.
Ilionekana familia yenye furaha tele, baba mama na watoto wawili wa kike. Baba alikuwa mtanzania mwenye asili ya India, mama wa familia alikuwa ni mtanzania halisi kabisa na watoto rangi zao zilikuwa zimeibia kwa baba ila zililalia zaidi kwa mama yao. Majira hayo walikuwa wametulia wakipata chakula cha pamoja nyuma ya jumba hilo kubwa la kifahari. Sehemu ambayo walikuwepo walionekana wakiwa watano, mwanamke mmoja ambaye aliongezeka alikuwa mfanyakazi wao wa ndani ambaye muda mwingi alikuwa akipambana kubadilisha vyombo na kuongeza aina mpya ya vyakula mezani ili kumpa furaha mwajiri wake.
Walionekana kuzama kwenye furaha kubwa kwa sababu ni wazi chakula cha usiku kupata pamoja kama familia ndilo lilikuwa takwa la kuiweka kwa ukaribu bondi ya familia yao izidi kukua siku hadi siku. Furaha iliwasahaulisha matatizo yote ya nyuma, walijikuta wapya, tabasamu likawa sehemu yao huku pembeni kukiwa na redio ambayo ilikuwa inapiga mziki wa taratibu kusindikiza furaha ya watu hao wanne.
Ilkuwa ni familia ya daktari NAMAKI PRASAD, daktari bingwa ambaye alikuwa anatumika zaidi kutibu watu mashuhuri na watu wakubwa serikalini. Alikuwa na miaka zaidi ya thelathini na mitano ya uzoefu wa kazi yake hiyo ambayo alikuwa anaijua vyema, ni kwa miaka hiyo ambayo alihudumu kwa kuwatibu maraisi watatu wa Tanzania na viongozi wengine wakubwa wa serikali. Huduma yake ilimfanya kuwa mtu wa kuheshimika mno na kutengeneza pesa nyingi za kumfanya yeye na familia yake kuishi yale maisha ya ndotoni ambayo watanzania wengi huwa wanaishia tu kuyaota ama kuyaona kwenye filamu za magharibi huko.
Nyumba yake ilikuwa na walinzi wanne pamoja na mfungua geti mmoja, walinzi wawili walikuwa upande wa mbele ya jengo hilo lakini upande ambao ilikuwepo familia, hatua kadhaa kutokea pale ambapo walikuwa wamekaa walikuwepo wanaume wawili wakiwa kwenye suti zao na vifaa vya mawasiliano kwenye masikio yao wakiwa makini na silaha zao mikononi. Usalama ulikuwa wa kutosha eneo hilo hivyo hawakuwa na wasiwasi.
Nje ya jumba hilo ulikuwa unaonekana moshi, moshi ambao ulitoka kwenye sigara ya bei ghali. Cigar ilikuwa imeshikwa vizuri kwenye mikono ya mtu ambaye alijifunika kwa kofia usoni, moshi wa milo kadhaa ya watu wa mtaani ilikuwa inapotelea hewani na mtu huyo asiwe na mawazo hata kidogo. Alivaa koti la kijivu ambalo lilipeperushwa kidogo na upepo zikaonekana bastola mbili kwenye kiuno cha mwamba aliekuwa anapata na kuufaidi moshi huo kwani aliuvuta kwa hisia isivyokuwa kawaida. Kwenye miguu yake alivaa buti la ngozi nalo la kijivu kama lilivyokuwa kati lake, ndani alivaa vest nyeupe ambayo ni kama ilivalishwa kwa lazima kwani mwili uliizidia kwa sababu ulituna vilivyo, suruali yake nyeusi ya kutanuka ilimkaa vyema kwenye mwili wake hakuwa na wasi huku mkononi akiwa na kisu ambacho kilikuwa na mduara katikati na pembe zake zote zilikuwa na nchi kali.
Aliuinua uso wake juu sura yake ikaonekana, Yohani Mawenge ambaye tulimuona akiingia ndani ya serikali ya Uganda na kusababisha matatizo ndiye alikuwa amefika hilo eneo. Aliirusha cigar yake hewani na wakati unakaribia kutua chini aliitawanyisha kwa kisu chake, hakupoa wala kuboa alikimbia kwa kasi, akaenda kutua mguu wake mmoja karibu na lilipokuwa geti ya nyumba ile na kwa sababu ukuta ule haukuwa mbali na juu; hatua tatu zilimfanya kuwa juu ya ukuta ule ambapo alidunda na kutua kwa ndani.
Eneo ambalo alitua lilikuwa hatua chache kufika pale ambapo alikuwepo mlinzi, alihisi kama kuna kivuli kimakatiza nyuma yake kwa sababu ya mwanga ambao ulikuwepo wa umeme hivyo akageuka akiwa na silaha yake mkononi. Wakati anageuka alikutana na kisu cha kwenye moyo huku akizibwa mdomo na mkono mmoja, alitingishika kidogo wakati mwanaume huyo anaendelea kukichomoka chomeka mpaka pale alipo tulia, akamuachia akiwa anaendelea kuvuja damu kwa wingi ambazo ziliendelea kuchafua nyasi za gharama zilizokuwa pale chini.
Wale walinzi wawili walikuwa wamezuiwa na ukuta mdogo ambao uliifanya nyumba ile kuwa pembeni kidogo kutoka getini ila mmoja wa wale walinzi alishangaa baada ya kutomuona mlinzi kwani eneo ambalo alikuwepo alikuwa anaweza kumuona mlinzi wa getini vyema kama akisimama. Hali hiyo ilimfanya asogee taratibu bila kumshtua mwenzake ili kuona hali inaendaje, alishtuka alipo karibia lile eneo baada ya kumuona mlinzi akiwa chini anavuja damu kwenye sehemu yake ya moyo.
Aligeuka haraka ili kumpa mwenzake ishara ila kwa bahati iliyokuwa mbaya kwake wakati anageuka alikutana na kisu kwenye mkono wake ambao ulikuwa na silaha. Kisu ambacho kilirushwa kwa nguvu kiasi kwamba kikaondoka na vidole vyake viwili na kumfanaya aidondoshe bastola yake. Alipiga mluzi ila hakuumalizia kwa sababu Yohani aliteleza kwenye zile nyasi ambazo zililowa kwa maji na kumfikia mwanaume yule ambaye alikwepa buti lililokuwa limelenga kumpiga mtama.
Alisogea nyuma akiwa anasikilizia maumivu ya mkono wake. Alikuja kwa kuchangaya miguu yake ila kwa bahati mbaya mhusika hakutaka kupoteza muda wake, alimpiga risasi nyingi za kwenye moyo kwa kutumia silaha yake ambayo aliifunga kiwambo cha kuzuia sauti kisha akairudisha kiunoni kuelekea kwa yule mwingine ambaye alikuwa amesimama upande wake. Mwanaume yule alikuwa anasogelea kwenye kona moja ila alishtuka baada ya kuguswa begani, alijua ni mwenzake hivyo aligeuka bila mahesabu. Kisu kilizama kwenye jicho lake moja, alihitaji kupiga kelele kupunguza uchungu wa maumivu ila alizibwa mdomo na kupigwa risasi nyingi kwenye miguu yake huku Yohani akiwa naampa ishara ya kutulia kimya silaha akiwa ameielekezea eneo la moyo likiwa ni onyo kwamba kama akifanya ujinga wowote ule basi alikuwa anamuua.
“Dokta yuko wapi?”
“Yupo nyuma ya nyumba na familia yake”
“Wapo walinzi wangapi?”
“Wawili” mlinzi yule alikuwa akijibu kwa hofu na hisia za maumivu makali, hata hivyo hakuachwa hai alipigwa risasi moja ya kwenye moyo hata Yohani alipo hitaji kuongeza risasi nyingine aligundua kwamba risasi zilikuwa zimeisha. Alisonya na kukiweka kisu chake kiunoni huku akiwa na hizo silaha zake mbili ambazo hazikuwa na risasi hata moja”
Yohani alijitokeza hadharani kwenye lile eneo ambalo familia ya dokta Prasad ilikuwepo akiwa amenyoosha bastola zake kuelekea lile eneo ambalo walikuwepo, ilikuwa ni ghafla hali ambayo iliwafanya hata wale walinzi kushtuka na kumnyooshea bastola zao kwa umakini wakiwa wanakaribi alipokuwepo bosi wao kwani Yohani alikuwa anasogea lile eneo pia.
“Msije mkafanya hilo kosa kwa sababu mnajua kabisa kwamba nikiachia risasi zangu zote hapa naua familia nzima hivyo tupeni silaha zenu kwa sababu sina mpango wa kumuua kwa sasa nina mazungumzo naye na kwa nyie hapo sina haja ya kutumia silaha” aliongea akiwa anamaanisha kutokana na jinsi uso wake ulivyokuwa, wale walinzi hawakufanya hivyo kwa sababu bado walikuwa wanajishauri kufanya maamuzi japo mtu ambaye aliitoa hiyo kauli alikuwa siriasi.
Jambo hilo lilimshtua dokta Prasad kiasi kwamba wanae walianza kupiga kelele za uoga huku mkewe akiwa anatetemeka na kuwakumbatia wanae ambao walimsogelea yeye alipo wakatoka kwenye viti vyao. Daktari huyo hakuwa na taarifa za ujio wa huyo mtu wala hakuwahi kuonana naye sehemu yoyote ile hivyo alihitaji kujua kwamba alikuwa nani hasa mpaka avamie nyumbani kwake kwa silaha kwani kama alikuwa anataka huduma angeomba kuonana naye kistaarabu akamsikiliza. Alijua akifanya maamuzi ya kijinga angeipoteza familia yake hivyo aliwataka walinzi wake washushe bastola zao chini ila Yohani alisisitza kwamba walitakiwa kuzirushia umbali kadhaa na walipo kwa sababu hakuwa mjinga.
Ilikuwa ni amri ya bosi wao hivyo zoezi hilo lilitekelezeka kwa haraka ila wakati wanafanya hivyo Yohani alirusha bastola yake moja kwenye kwa mwanaume mmoja huku akiwa anamfuata mwingine kwa spidi ya mwendo wa farasi. Wakati anakaribia kumfikia alidunda chini akajigeuza kwa sarakasi ambapo miguu yake ilitua kwenye bega la mwanaume huyo alifanikiwa kuupangua mmoja ila mmoja ulimpata kwenye shingo ambapo aliyumba kidogo ila kabla hajatua ule mwingine ambao aliupangua ulitua kwenye mbavu zake. Yalikuwa ni mateke mazito ambayo yalimpeleka mbali akiwa anaugulia maumivu makali.

UKURASA WA 44 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 42

“Hii siku ya leo nitaiweka akilini JACK, dharau yote ambayo umeionyesha mbele yangu nitailipa na nakuahidi utaijutia hii nafasi ambayo umeipoteza” Aaliyah aliongea kwa hasira akiwa anaondoka na kuhitaji kutoka lakini alisimama baada ya mwanasheria huyo kumuita na kunyanyuka kisha akamsogelea mwanamke huyo na kumkumbatia kwa nyuma bila ridhaa yake kisha akamnong’oneza kwenye sikio lake.
“Iangalie hiyo mihemko yako bibie kwa sababu unatakiwa kuipeleka kitandani sio kwenye dunia ya mtu kama mimi, hili ni jambo la hatari kwako. Muda huu unatakiwa kuufanyia kazi ushauri wangu ikiwemo kuwatafuta watu wengine wawili, Damas Kazimoto mwanajeshi ambaye aliigiza kifo chake na juzi ameonekana kwenye tukio la pale uwanja wa ndege lakini pia unatakiwa kumtafuta Nicola Aidan Semzaba ambaye alitekwa pale uwanja wa ndege. Unafaa tukiwa kitandani ila usije ukajaribu kuhitaji kunipima na kujua nipoje, sihitaji kumuua mwanamke mrembo kama wewe kwa kutumia mkono wangu. Lizingatie neno hili HII KAULI IISHIE KWANGU TU NA SIO KWAKE ATAKUUA BILA KUKUULIZA CHOCHOTE” Maelezo aliyasikia vizuri akiwa amekumbatiwa, yalimtisha na kumshangaza kwani alianza kuona dalili kabisa kwamba mwanasheria huyo hakuwa yule ambaye watu wengi walikuwa wanamjua na kumuona mahakamani bali kulikuwa na dunia yake ya siri ambayo ilimpa hiyo hali ya kujiamini kupitiliza. Hayo yote hayakuwa ya mhimu ila ile kauli ambayo aliambiwa aizingatie ndiyo ilimfanya moyo wake uanze kupiga kwa nguvu, alihisi jasho linamtoka kwenye mwili wake kwa kasi japo alikuwepo ndani ya chumba ambacho kilikuwa na hali safi na ubaridi usio kera. Aliwaza kwamba je kulikuwa na mtu mwingine? Ni nani hasa mpaka apewe tahadhari ya kuto mwambia kauli hiyo ya kitisho? Moyo ulitahamaki, nafsi ikatahayari kwa kile alicho kisikia ila hakuwa na uwezo wa kuuliza kwani mazungumzo yalikuwa yameisha na mtu huyo alimpa ishara ya kuweza kutoka ndani ya chumba hicho akiwa mwingi wa mawazo. Alipewa mengi ambayo hakuyajua lakini aliongezewa mtihani wa kuchambua baadhi ya taarifa zingine.

JACK THE LAWYER baada ya kuhakikisha Aaliyah ameondoka ndani ya eneo lile, alisogea kwa kabati kubwa ambalo lilikuwa limejaa tuzo ambazo alizipata kwenye maisha yake ya kuiongoza sheria. Aliweka kidole chake kwenye sehemu ndogo ya kioo ambayo ilikuwa pembezoni mwa kabati hilo, kabati likajisogeza pembeni ambapo ulitokea mlango. Pembeni kulikuwa na namba za kuingiza, alingiza namba kadhaa kwa kuzichanganya kama kumi na sita ndipo mlango ukafunguka naye akaingia huko ndani.
Kilikuwa chumba kizuri ambacho kilipambwa kwa kitanda, kabati kubwa, friji moja, kompyuta kadhaa ukutani pamoja na kioo kikubwa ambacho kilibandikwa ukutani. Alisogea kwenye kioo hicho na kujitazama kwa muda mrefu, kwenye mfuko wake wa koti upande wa kushoto kulikuwa na picha, picha ambayo aliitoa na kuiangalia kwa umakini naye akiwa anajitazama kwenye kile kioo kikubwa. Picha ile ilikuwa ni ya Edison Christian, haikujulikana sababu ya msingi ya yeye kuwa na picha ya mtu huyo ambaye alikuwa anatafutwa kila kona ya jiji. Aliitazama kwa muda na kutamka

“Uko wapi Edjr, nahitaji kwenda kupumzika, muda wangu wa kufa umefika sasa ebu jitokeze uichukue nafasi yako haya maisha sio sehemu yangu” aliongea kwa uchungu kiasi kwamba chozi lilimshuka usoni taratibu. Alionekana kuwa na mengi yaliyokuwa yakipita akilini mwake kiasi kwamba hata kuendelea kuishi yalikuwa maumivu makali upande wake. Hisia zake zilimrudisha miaka ya nyuma;

Miaka mingi iliyopita eneo la Tukuyu kijana mmoja wa kiume wa miaka kumi na mitano alikuwa akiishi na baba yake mzazi. Kijana huyo hakuwa na furaha kabisa kwenye maisha yake kwa sababu kuu mbili, sababu ya kwanza ulikuwa ni umaskini ulio kithiri kwao lakini sababu ya pili ni kwa yale ambayo yalikuwa yamewatokea miaka kadhaa ambayo ilipita. Baba yake alikuwa mchuuzi wa samaki ambapo alikuwa analazimika kwenda ziwa Nyasa kwa ajili ya kuvua hususani upande wa fukwe ya Matema lakini muda mwingine alikuwa akijishughulisha na biashara ya nafaka maeneo ya Tukuyu mjini.
Ukiachana na umaskini ambao ulimfanya kila awapo na wenzake aishie kuchekwa kitu ambacho kwake hakikumuumiza ila jambo ambalo liliwakuta kwenye maisha yao ndilo ambalo lilikuw alinajirudia kichwani mwake. Baba yake alikuwa mzaliwa wa Zambia lakini mama yake alikuwa ni Mnyakyusa wa Kyela, baba yake alikuja miaka kadhaa huko nyuma kwa ajili ya kutafuta maisha ndani ya jiji la Mbeya lakini kutokana na sifa nzuri za huko Kyela akaamua kuchangamkia fursa na kwenda kujaribu bahati yake.
Kuishi kwake huko hususani maeneo ya fukwe ya Ngonga kulimsaidia kukutana na mwanamke mrembo wa Kinyakyusa, hakuwa na kikubwa cha kumpa lakini aliziweka wazi hisia zake kwa mwanamke huyo naye akazielewa na kuzipokea. Mwanzo wao ukafunguliwa rasmi kwa penzi zito baina ya watu hao wawili ambao walionewa gere na watu wengi hususani watu ambao walikuwa na kipato kikubwa kumzidi, watu walishangaa kwanini mwanamke mrembo kama huyo awakatae wao na kisha kukubali kuwa na mwanaume kapuku asiye na chochote? Wengi wakawa wanamfingia mwanaume huyo na mrembo huyo na kuwapa onyo kama watafika popote pale na hayo mapenzi yao hata hivyo hawakujali zaidi ya kuyaanza maisha.
Nkole Mwanawasa ndilo lilikuwa jina la mzambia huyo ambaye alikimbia kwao ambapo alikuwa anaishi karibu na mipaka ya boda ya Tunduma. Kukimbia kwake huko ni baada ya kusingiziwa kesi ya kuhujumu pesa za wafanya biashara ambao huwa wanabadili kwacha pale mpakani. Hakutenda kosa ila aliona kabisa kwamba akizubaa basi alikuwa anaishia jela na hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kumsaidia kwa kesi hiyo hivyo akaamua kuacha kila kitu na kwenda kuyaanza maisha mengine mapya huko Tukuyu.
Upambanaji wake mkubwa ambao alikuwa nao ulimsogeza mbele, wahenga walisema kosea vyote ila sio kuoa, alibahatika kumpata mwanamke ambaye alikuwa ana mipango mikubwa na maisha hivyo wakawa na lengo moja. Walilima mipunga huku akiendelea kuchuuza samaki, mafanikio yakawagongea hodi mlangoni kwao na wakati huo walikuwa wamepata mtoto wa kiume, kwa sababu yeye alikuwa mzambia wakaona ili mtoto asije kupata taabu kwa baadae basi wampatie ukoo wa mama yake hivyo akaitwa Chrispin Mwambano.
Alipendwa mno na wazazi wake kwenye ukuaji wake, licha ya vita ambayo walikuwa wanakumbana nayo kwa watu wa jamii hiyo kwa sababu hawakutaka wazazi wao kuwa pamoja ila bado alisimama kwa sababu wazazi wake walikuwa imara. Baba yake akawa miongoni mwa watu ambao walipata mafanikio makubwa, maisha yakakubali upande wake akawa mtu tofauti jambo ambalo lilimpa maadui wapya ambao walimuona kama tishio kwao kwa sababu walitamani kumuona akiwa anafeli siku zote za maisha yake.
Vita hiyo iliwafanya kupitia mambo mengi kwenye ukuaji wake ikiwemo kuharibiwa mazao na mali zao lakini baba yake hakukata tamaa mpaka alipo amua kuhama sehemu alikokuwa anaishi kwa muda na kwenda Kyela mjini ambako ndiko ulikuwa mwanzo wa historia mbaya ya maisha yao. Miaka ilikimbia lakini bado hawakuwa na amani, ndipo usiku mmoja likaokea jambo baya ambalo lilikuwa gumu kufutika kwenye kichwa cha Chrispin. Jambo hilo lilikuwa ni kuvamiwa kwa familia yao majira ya usiku wa manane, kuvamiwa haikuwa tatizo ila shida ilikuwa ni kile ambacho kilitokea baada ya kuvamiwa kwao siku hiyo.
Baba yake alifungwa na mama yake alikamatwa na watu ambao hakuwajua sura kwa sababu sura zao zilifunikwa kwa vitambaa vyeusi. Watu hao walimtesa baba yake na kumfunga huku yeye akiwa hana cha kufanya zaidi ya kukamatwa na wanaume waliokuwa na nguvu kwenye miili yao kisha akawa anatazama kinacho endelea akishusha machozi taratibu. Alilazimishwa kuangalia mama yake mzazi akiwa anabakwa mbele yake, lile tukio lilimuathiri pakubwa sana saikolojia yake, lile jambo liliharibu yale mazuri ambayo ubongo uliweza kuyahifadhi kwenye nafsi yake. Watu hao baada ya kukamilisha hilo walitoweka.
Alimuangalia mama yake pale chini akiwa anashusha machozi, alimuita mara moja wakati anamuona mama yake anananyuka na kuanza kukimbilia nje lakini hakuwa na cha kufanya zaidi ya kuzimia kwani alikuwa amepigwa na kitu kizito muda sio mrefu. Fahamu zake zilirudi majira ya asubuhi huku nyumbani kwao kukiwa na watu wengi, alishangaa kunani? Ndipo zile kumbukumbu zikaanza kurudi kwa kile ambacho kilitokea jana yake, alikurupuka na kuanza kumtafuta mama yake ila watu wazima wenye busara walimtuliza, walimtuliza ili kumjibu swali lake la wapi alipo mama yake mzazi. Habari ambazo aliambiwa, alitamani usiwe ukweli kwani kwake aliona kama ni ngumu kukubaliana moja kwa moja na jambo hilo ila ndio ulikuwa ukweli kwamba mama yake alikutwa akiwa amejinyonga juu ya mti ambao ulikuwa nje ya nyumba yao kwa kutumia kanga yake.

UKURASA WA 42 unafika mwisho.
Duuh
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 45

Mwenzake ambaye aliipangua bastola alikuwa anakuja nyuma ya Yohani, alirusha ngumi ya mgongoni ambayo haikufua dafu kwa sababu mhusika alisogea mbele ikaishia kumgusa kwenye koti lake tu bila kuleta madhara, aligeuka kwa kulizungusha hilo koti lake ila wakati anafanya hayo alikuwa amechomoa kisu chake ambacho kilikita kwenye shingo ya yule mwanaume, alikufa pale pale akiwa amesimama.
Mauaji yale ya kikatili ndiyo yalimpa onyo dokta Prasad kwamba aliyekuwa amekuja nyumbani kwake hakuja kwa ajili ya mazungumzo bali alikuwa muuaji hivyo alihitahi kuitoa familia yake ndani ya hilo eneo. Aliwainua na kutaka kukimbia nao ila tukio hilo Yohani alikuwa akilishuhudia vizuri, aliruka sarakasi ya chini kwenda mbele yake hatua kadhaa eneo ambalo wanaume wale walidondoshea bastola zao akaipata moja, aliachia risasi ambayo ilitua kwenye mguu wa mke wa dokta Prasad akandondoka chini. Kundondoka kwake kulifanya eneo lile kuwa na kelele za vilio na sio kukimbia tena, yule mwanaume ambaye alipigwa na mabuti kadhaa ya shingo na mbavu alinyanyuka kwa pupa ili kulipa na kumlinda bosi wake ila hasira zilimponza. Bila kugeuka nyuma Yohani alinyoosha bastola yake na kuachia risasi zote zilizokuwepo ndani ambazo ziliishia kwenye paji ya uso la mlinzi yule akandoka chini. Yohani alisogea taratibu alipokuwepo yule daktari na familia yake wakiwa wanahaha pale chini, aliiokota bastola nyingine ambayo ilikuwa na risasi akasogeza kiti kimoja na kuketi karibu na ilipokuwa ile familia wakiwa wanalia zamu kwa zamu huku wakiomba kuachwa hai ili wamuwahishe mama yao hospitali.
“Sikuwa na mpango wa kumuumiza mkeo au wanao ila umetaka iwe hivi na kama ukinilazimisha basi nitawaua moja kwa moja” Yohani sauti yake ilikuwa juu tena yenye mamlaka isiyo na mzaha hata kidogo.
“Wewe ni nani na unataka nini kwangu na familia yangu?”
“Mimi sina shida na familia yako, nina shida na wewe hapo. Ni ajabu usikute hata familia yako haijui unafanya kazi gani mzee wangu!”
“Kazi yangu inakuhusu nini wewe?”
“Inanihusu ndiyo maana nipo hapa” Yohani alitamka na kumgeuki mke na watoto wa dokta Namaki Prasad
“Msikute hata hamjui kwamba kiongozi wa familia yenu ni muuaji?” wote walibaki wanashangaa huku mkewe akiwa na maumivu makali mguuni kwake ambapo alipigwa risasi. Yohani aliendelea
“Huyu ndi dokta mkubwa ambaye amefanya makubwa kwenye taifa hili lakini haiondoi maana ya kwamba yeye ni muuaji. Unamkumbuka raisi Justin Nyangasa?” swali hilo lilionekana kushtua daktari huyo
“Najua unamkumbuka vizuri, kwa mkono wako ulimchoma sindano yenye sumu kwa ajili ya kumuua, sumu ambayo ilitengenezwa na mwanasayansi Christina Edison. Ulimuua raisi wa Tanzania kwa mikono yako kwa kufuata maagizo bila kukosea na jambo hilo likaisha, umeachwa uishi miaka mingi ambayo bila shaka umeifurahia na kuyafaidi maisha vilivyo kama posho ya ulicho kifanya lakini imefikia hatua uwepo wako duniani unakuja kuwa hatari kwa upande wetu kwani tunaamini kwamba kwa haya ambayo yanaendelea ipo siku utakuja kutafutwa na kuna uwezekano ukauweka ukweli bayana” maelezo ya Yohani yaliwashangaza wote ila sio Namaki, lugha hiyo alianza kuielewa vizuri na kutambua kwamba huyo mtu alikuwa ametumwa na nani kuweza kumfauata hapo alipokuwepo.
“Kwahiyo wamekutuma uweze kuniua?”
“Ndiyo”
“Unahisi ukiniua mimi ndiyo suluhisho la haya yote? Mimi nimeishi na hii siri kwa miaka mingi bila hata familia yangu kujua leo unaniambia mimi naweza kuisaliti jamii yangu ambayo imenipa nafasi kubwa ya maisha?”
“Natamani mimi ndiye ningekuwa natoa amri ila unajua vizuri namna sheria zilivyo na hakuna kitu cha kupindua haya maamuzi ambayo yametoka ngazi za juu hivyo ili kuilinda siri hii unatakiwa kufa hapa hapa. Familia yako siwezi kuiua kwa sababu hawana ushahidi wa kusema watathibitisha ila kama nao kwa baadae watakuwa hatari basi nitakuja kuwaua kwa mkono wangu mwenyewe hivyo ni vyema kabla hujafa uwaonye kwa hilo” alionekana kumaanisha kile ambacho alikuwa anakiongea na asingeweza kurudi nyuma. Dokta Namaki alibaki ametahamaki akiwaza namna sahihi ya kuweza kuiomba familia yake msamaha kwani hata wao walishangaa maelezo ya kwamba baba wa familia ndiye alikuwa nyuma ya mauaji ya raisi.
Kuduwaa huko kulimfanya daktari huyo bingwa kupokea risasi nyingi za kifuani kisha Yohani akanyanyuka na kuondoka hilo eneo akiiacha familia kwenye majonzi na kilizo kizito. Huyo ndiye daktari ambaye alifanikisha lile zoezi la kumuua raisi Justin Nyangasa kipindi LUNATIC SOCIETY inazaliwa rasmi na kwa ambayo yalianza kutokea likiwemo ya mwanasheria JACK THE LAWYER liliwatisha watu hao wakaamini kwamba linaweza kutokea jambo lolote lile mtu huyo akaja kusema ukweli hivyo ilikuwa ni lazima apunguzwe.
Muda mfupi tangu tukio hili liweze kutokea kuna gari ya kifahari ilipaki nje, jambo la kushangaza ni kwamba aliyefika hapo alikuwa ni JACK THE LAWYER mwenyewe. Alishangaa kuona geti lipo wazi usiku huo na baada ya kuangalia vyema aligundua kwamba walinzi walikuwa wameuawa hivyo eneo hilo akajua kabisa kwamba halikuwa salama. Aliitoa bastola yake kiunoni na kuanza kusogea upande wa nyuma wa nyumba hiyo kwa sababu kwa mbali alisikia mziki eneo hilo.
Kadri alivyokuwa anasogea karibu ndivyo alivyokuwa akishangazwa na alichokuwa anakiona. Mama mtu mzima alikuwa analia huku wanae wakiwa wamemkumbatia, alisogea eneo hilo ndipo akashtuka baada ya kuuona mwili wa daktari huyo ambaye alikuwa maarufu ukiwa chini unamwaga damu. Haikuchukua muda mtoto mmoja wa yule mama akawa anatoka ndani akiwa anakimbia mkononi akiwa na simu, bila shaka alikuwa anapiga simu polisi.
Akiwa anashangazwa na tukio hilo hata familia hiyo ilionekana kumshangaa yeye, walizoea kumuona mtu huyo kwenye mitandao tu ila siku hiyo walikuwa wanamuona mbele yao ila wakati ambao walikuwa wanamuona ulikuwa ni wakati mbaya. Hawakujua mwanasheria huyo nguli alikuwa amefuata nini ndani ya hiyo nyumba hivyo walibaki wanamwangaia yeye kusubiri kile ambacho angekitamka kwenye kinywa chake, Alipakia bastola yake kiunoni kisha akainama pale ulipokuwepo mwili wa Namaki Prasad akiwa anaukagua kwa umakini.
“Nini kimetokea hapa?”
“Kuna mtu amekuja akaua walinzi wote kisha akamuua mume wangu na kunipiga mimi risasi”
“Amejitambulisha kwamba anaitwa nani?”
“Hapana” alitamka mama huyo kwa kitetemeshi lakini uso wake ulikuwa unapingana na kauli yake.
“Najua hali mliyo nayo kwa sasa sio nzuri na siwezi kabisa kuwalaumu kwa hilo ila mimi lengo langu hapa nilikuja kistaarabu tu kuongea na mume wako na sasa hayupo, naweza kujua kama labda kuna taarifa ambazo ninaweza kuzijua zikanisaidia kwenye kesi yangu?”
“Ulikuwa unajua kuhusu hili?” mama yule aliuliza kwa msisitizo
“Ndiyo, nina taarifa nyingi kuhusu hili ambalo lilikuwa linaendelea ila kuna vitu ambavyo nilitaka kuvisikia kutoka kwa dokta mwenyewe kwa sababu yeye alipewa kazi ya kumuua raisi ila bado sijajua mtu ambaye alimpa hiyo amri”
“Ni kweli mume wangu aliyafanya haya kama nilivyo sikia mtu aliyekuja hapa akimwambia?”
“Ndiyo mumeo hajamuua raisi tu bali ameua watu wengi mno. Imekuwa rahisi wkake kufanya hivyo kwa sababu ni daktari mkubwa na anaaminika na hiyo ndiyo nafasi ambayo alikuwa anaitumia kuua watu bila kushtukiwa na mtu yeyote yule”
“Ulikuwa na mpango wa kumfanya nini kama ungemkuta hai?”
“Alikuwa na machaguo mawili ambapo alitakiwa kunipa moja tu, kama angekubali kunisaidia basi ningemuacha salama bila kumfunga ila kama angegoma basi ningemjumuisha kwenye kundi la watu ambao wanatakiwa kuishia jela au kuuawa”

UKURASA WA 45 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 46

“Mimi hakuna ninalo lijua zaidi ndiyo nasikia leo mume wangu akiambiwa kwamba ni muuaji naomba msaada wako tafadhali hawa watu ambao wamehusika na hili waweze kupatikana” mwanasheria huyo alimwangalia sana mwanamke huyo mtu mzima, hakumjibu zaidi ya kumuuliza swali
“Naweza kuipata sura ya mtu ambaye alikuja hapa kufanya mauaji?” simu ilitolewa na mtoto mmoja wa dokta, simu hiyo ilikuwa imeunganishwa na mfumo wa ulinzi wa nyumba hiyo. Alisimama JACK kisha akasikitika na kutoka eneo hilo, ilikuwa ni baada ya kukosa alichokuwa amekifuata kwa kuchelewa kidogo ila angewahi huenda angefanikiwa kuyaokoa maisha ya daktari huyo ambaye angempa majibu ya maswali ambayo yalikuwa yanamhusu. Kuondoka kwake ilikuwa ni baada ya kusikia milio ya ving’ora vya polisi ambavyo vilikuwa vinakuja eneo lile bila shaka ni ile simu ambayo yule binti wa dokta Namaki aliipiga ila alifanikiwa kuondoka na simu moja kwa ajili ya kwenda kumchunguza huyo mhusika ambaye alikuja kufanya hayo mauaji ambayo hakuwa na maswali mengi juu ya nani alikuwa nyuma ya mpango huo zaidi ya kuhitaji kumfahamu aliyeenda kutekeleza, watoa amri alikuwa anawajua ila muuaji halisi ndiye alikuwa na shida naye kubwa.
Baada ya kutoka pale aliingia kwenye gari kichwa kikiwa bado hakijatulia, aliliondoa gari kichwani akiwa anawaza mambo mengi. Hakuelewa ilikuwaje mpaka muuaji akamuwahi kufika eneo lile na kutekeleza kilicho mpeleka na hapo ndipo akakumbuka ile simu ambayo alipewa. Alisogeza karibu yake na kuangalia picha kubwa ambayo ilikuwa juu ya skrini ya simu ile sura ilikuwa ngeni kwake, hakuitambua sura hiyo na hakujua ni wapi angefanikiwa kuipatia. Akiwa kwenye hiyo tafakuri ndipo aligundua kwamba msafara ulikuwa umeongezeka, kulikuwa na gari zingine mbili ambazo zilikuwa zimeunga kwa msafara wake, huenda ni kwa sababu ya mawazo juu ya ile picha ndiyo yalimfanya kukosa umakini kiasi kwamba hakuyaona hayo magari tangu mwanzo. Alisonya akiwa anaachana na ile njia ya kuelekea Karume ambako alijua angekatisha na kutokezea Buguruni apitilize moja kwa moja nyumbani kwake.
Alikunja kama anaenda gerezani kisha akakata kona ya mkono wake wa kulia baada ya kufika kwenye mataa ya mtaa wa Congo pale bila kusimama tangu atoke Upanga, njia aliyo ikunja ilikuwa inampeleka moja kwa moja mpaka Machinga Complex. Lengo la kufanya hivyo alihitaji kujirishisha kama ule msafara wa zile gari mbili bado ulikuwa unamfuatilia, alijirishisha kwamba watu hao bado walikuwa naye hivyo walikuwa wamekuja kwa ajili yake. Baada ya kuwa na uhakika huo, alipofika Machinga aliamua kukunja kulia na kisha baada ya hatua kadhaa akakunja kushoto kwake barabara ya kukunjia Ilala sokoni.
Watu wake walikuwa nyuma wakija kwa kasi ikamlazimu kuongeza mwendo wa gari yake, hakuhitaji kuwakimbia bali alihitaji kufanya nao mazungumzo kwa namna ambayo wangeitaka wao ila mazingira hayakuwa rafiki kwake. Aliendesha gari kwa fujo mpaka alipo karibia Rozana ambapo barabara ilikuwa inaendelea kutengenezwa alipunguza kidogo kwa sababu eneo hilo lina kituo cha polisi, huenda alihisi tukio hilo linaweza kuwavutia polisi ambao wangekuwepo usiku huo likampotezea mahesabu yake ila baada ya kuvuka tena aliongeza kasi kubwa na baada ya kufika mataa alikunja kushoto barabara ya kuelekea lilipo daraja ya Mfugale ila hakufika kule.
Gari yake ilikutwa imetelekezwa chini ya barabara ya teni ya umeme (standard gauge) ikiwa bado inaunguruma ila ilifungwa. Watu hao ambao walikuwa wanamfuatilia walishuka kwenye magari yao, hawakuwa wanaume wa kubeza kwa sababu miili yao ilikuwa imara.
“Namhitaji akiwa hai” ilikuwa sauti ya kike kutokea kwenye gari ya nyuma ambayo mhusika hakushuka hivyo mpaka wakati huo hakufahamika kwamba alikuwa ni nani. Kwa mbali mwanaume mmoja aliona kwenye barabara ya chini ya treni ya kawaida kukiwa na mtu ambaye ni kama alichepuka kutoka relini kusogea pembezoni karibia na yalipo majengo ya pembezoni. Aliwapa ishara wenzake wanne ambao kwa ujumla wao walikuwa watano, ishara ilikuwa ni kwamba alimuona mtu wao hivyo walitakiwa kwenda kumchukua na kumletea bosi wao kama alivyokuwa ameagiza.
Walitembea kwa kutawanyika kidogo ili kuangalia kwa umakini, kuna sehemu walifika ambayo ilikuwa na vifaa kadhaa pembezoni mwa reli hiyo kukiwa na kokoto nyingi karibu yake alisimama na kuanza kuongaza huku na huko. Mwanaume mmoja alihisi kama kuna mtu ameongozeka miongoni mwao, alihitaji kuwashtua wenzake ndipo alivutwa kwa nguvu, wakati analeta ubishi alipigwa buti la mguu ambalo lilimzoa na kumkosesha balansi, akiwa anaelea elea alipokea buti la shingo ambalo lilimbeba mpaka relini, kichwa kilijipigiza kwenye kuta za reli kikapasuka vibaya na kusambaratisha ubongo wake.
Ile kashkashi ndiyo iliwashtua wenzake ambao walikuwa wanaendelea kuangaza pembeni hivyo wote wakakimbilia ile sehemu kumsaidia mwenzao ambaye kiuhalisia hakuwa na uhai tena. Walienda kwa pupa na hasira baada ya kugundua kwamba mwenzao alikuwa chini na singeweza kurudi tena, wawili ambao walikuwa mbele walikuja kwa jazba ambapo mkoja alirusha ngumi zake huku mwingine akijigeuza kwa teke kali la tumbo. Kilicho fanikiwa kumgusa ni teke tu baada ya kuzipangua zile ngumi hata hivyo teke halikufua dafu sana kwake kwani alilikaza mno tumbo lake.
Wakati anajiandaa kuwafanyia shambulizi watu hao, wale wengine wawili wa nyuma walikuwa eneo la tukio, walimhambulia kwa ngumi kadhaa ambazo zilimzoa nyuma akakosa balansi kidogo, mmoja aligeuka na sarakasi iliyo msaidia kuikunjua miguu yake kwa ufasaha ambayo ilitua kifuani kwa mwanasheria, mwanasheria alibebwa na nguvu ya mateke yake, almanusura aligongeshe kwenye kuta za reli kwa kutumia mgongo wake lakini hakuwa mzembe mpaka kufikia hatua hiyo. Alitua kwa mkono wake mmoja na kujirudi kwa sarakasi na kubakia amesimama wima bila presha.
Hawakuwa na muda wa kusubiri walimsogelea kwa kasi, aliinama chini mithili ya mtu ambaye anapiga magoti baada ya kuona buti moja linakuja kwa nguvu upande wake, buti hilo lilipishwa kisha akairusha ngumi yake ambayo ilitua kwenye goti la mwanaume huyo na kulivunja goti hilo. Wakati yule mwanaume anatoa sauti ya maumivu alinyanyuka naye ambapo alimgongesha kwa kutumia viganja vyake kwenye masikio yake ambayo yalianza kutoa damu kwa kasi, alimshindilia ngumi ya kwenye koo na kumshushia kwenye goti lake. Hilo tukio lilitekelezeka ndani ya sekunde nane tu pekee mwanaume huyo aliachiwa chini kama mzoga.
Wakati anaachiwa mmoja wao alichomoa upanga mfupi na mnene kwenye koti lake, hali haikuwa sawa kwa upande wao. Upanga wake ulimpa imani ya kuja akitoa sauti ya muungurumo ndani yake mithili ya beberu aliyeona jike mbele yake. Alihitaji kugawanyisha upande wa bega la mwanasheria lakini alikwepa, wakati mwanaume yule anahitaji kuugeuza upanga ule ngumi ilipenya kwenye ukwapa wake, hakuwa na uwezo wa kuendelea kuushikilia tena ule upanga hivyo akauachia ila kwa bahati mbaya ulifikia kwenye mikono ya mwanasheria ambapo alimgeuza mtu yule mnofu. Alimkata mara mbili pande zake za shingo kisha akaigandamizia ngumi yake kwenye kifua cha mwanaume yule ambaye alidondokea mbali huku kichwa chake kikiwa kinacheza cheza kikiwa tayari kujitioa kwenye kiwili wili chake kwa namna ule upanga ulivyokuwa umetenganisha ile mihimili ya ile shingo ila bahati ilikuwa upande wake kwa sababu alikufa kichwa kikiwa hakijatoka.
Wawili wale waliamua kuja kwa pamoja ili kumchanganya, walikuwa wanaviziana, yeye aliwatisha kama anarusha ule upanga hivyo wakasita na kuinama mkukwepa wakati hakurusha. Ule muda yeye aliutumia kujigeuza na kutua nyuma yao wakati wanainuka hakuwepo mbele yao, waligeuka haraka ila aliyebahatika kuona kilicho fanyika ni yule ambaye alikuwa nyuma yake kwani wa mbele alikutana na ule upanga uso kwa uso kwenye shingo yake. Ulichomolewa kwa nguvu akasukumiziwa pembeni. Aliyekuwa nyuma alitaka kuchomoa bastola yake kwani licha ya kuambiwa mtu huyo anahitajika akiwa hai ni kama zoezi hilo aliona haliwezekani hivyo njia pekee kushindana naye ilikuwa ni kutumia silaha ya moto ila kujiuliza kwake mara mbili kulimchelewesha kufanya maamuzi alipigwa risasi tano za kichwa.
Wakati mwanasheria anamaliza kazi ya kuua watu hao alihisi mchakacho wa bastola nyuma yake, kuna mtu ambaye alimsahau alikuwa amemuwahi na kumuweka mtu kati. Aliishika bastola yake upande kisha akaidondosha chini na kunyoosha mikono juu, ni wazi alitii amri bila hata kuambiwa kisha akageuka ili kumuona huyo ambaye aliamua kuyatoa maisha yake sadaka kwa kumfuatilia usiku huo. Sura kwake haikuwa ngeni kwa sababu alikuwa anamjua mpaka jina mtu huyo, Nicola Aidan Semzaba ndiye alikuwa hapo, mwanamke ambaye alikuwa anamtafuta Edison kwa udi na uvumba kwa sababu aliamini kwamba ndiye ambaye alihusika na mauaji ya kaka yake ambaye alikuwa ni komando. Alikuwa mbele ya mwanasheria na bila shaka alikuwa na mazungumzo naye kwa njia ya amani au ya lazima ili atekeleze ambacho kilimuweka hapo.

UKURASA WA 46 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 47

“Sikutegemea mwanasheria kama wewe ungekuwa muuaji katili namna hii, hii inaonekana sio mara yako ya kwanza kufanya haya kwa sababu mtu ambaye anaua kwa mara ya kwanza hawezi kuwa mkatili na kuua wenzake kama kuku namna hii. Wewe ni nani?” lilikuwa swali kutoka kwa mwanamke huyo ambaye siku kadhaa zilizokuwa zimepita alitekwa ndani ya uwanja wa ndege.
“Nicola Aidan, huo muda ambao umeruhusu nigeuke nilikuwa naweza kukuua ila nilitamani kwanza nikufahamu wewe ni nani hasa ambaye unajiamini namna hii kunivamia na una shida ipi kwangu?” Mwanasheria Jack aliongea akiwa anauachia upanga ambao aliulaza usawa wa mkono wake hivyo wakati amegeukia upande mwingine mtu wa nyuma yake asingeweza kuuona, ina maana alikuwa anaweza kuutumia upanga huo kumuua Nicola ila alihitaji kumfahamu kwanza. Alitulia akiwa anaishusha mikono yake na kuendelea
“Unataka nini kwangu?”
“Umenijulia wapi mimi mpaka unaniita jina langu?”
“Bibie nazijua siri hadi za raisi wa nchi ambaye sehemu anayo kaa kunywa tu juisi inalindwa kiasi kwamba hata nzi hawezi kupenya itakuwa wewe hapo ambaye unaigiza michezo ya kitoto ya kutekwa?”
“Who are you?”
“Unahitaji kunifahamu kwa sababu ulisikia kuna taarifa zinadai kwamba mimi ninaishi kwenye sura ya mtu mwingine ili ujiaminishe kama mimi ndiye yule mtu ambaye alimuua kaka yako kule Somalia kwa kuhisi mimi ni Edison? Halafu baada ya hapo ufanye maamuzi ya kuniua si ndiyo? Nina imani hicho ndicho kimekuleta hapa ila kwa bahati mbaya leo sio siku ambayo naweza kufa kwa sababu kuna kazi ndogo imebakia sijaimaliza bado”
“Wewe umejuaje kama hicho ndicho ninacho kihitaji?”
“Kwa sababu ndicho ulicho aminishwa ili ukiamini”
“Una maana gani kusema hayo yote?” mwanaume huyo alimwangalia mwanamke huyo kwa muda kidogo kisha akajishika usoni kwake ambapo alijigusa na kubandua sehemu ndogo ya shingo yake hali iliyo mfanya kuwa na uwezo wa kuivua ile sura ambayo ilikuwa nje. Nicola alitahamaki alichokuwa anakiona mbele yake, hakuwa yule mwanasheria JACK THE LAWYER ambaye yeye alizoea kumuona kwenye mitandao na vyombo vya habari bali alikuwa ni yule Clyton Lameck ambaye baadae aligundulika kwamba alikuwa ni EdJr.
Bado nafsi yake ni kama ilikuwa ikigoma kuamini kile kitu kwa sababu hakuhitaji kufanya kosa la aina yoyote lile la kuua mtu asiye husika.
“Binti hii dunia ni nzuri mambo mazuri yakiwa upande wako na yakaenda kwa namna ambayo unaitaka wewe ila hii dunia ni mbaya kama kila kitu kwako kinaenda kinyume na matarajio yako hususani yale matarajio yanapokwamishwa na wanadamu ambao unawaona wanadunda na hawajali maumivu yako. Kaka yako sikumuua mimi hapa kwa sababu hata mimi nilipaswa kuuawa na nilipigwa risasi mbili ila nilifanikiwa kuishi wakati vijana wangu wakiuawa, unaamini kwamba ni kweli ningewaua watu ambao nilishi nao kama ndugu halafu kwa wakati mmoja kirahisi tu? Unatakiwa kufikiria mara mbili, watu ambao wamekupa hizi taarifa hazikuwa sahihi, mpango ulikuwa sisi wote tufe hivyo kupona kwangu mimi likawa kosa kwa sababu nina siri zao nyingi kuliko mtu yeyote ndiyo maana unaona waliamua kunichafua na kunipa hiyo kesi ili nisije kupata msaada sehemu yoyote ile ndani na nje ya nchi hii. Tumia zaidi akili na sio hisia kwa sababu kaka yako hayupo, mimi naweza kukusaidia wewe kuujua ukweli wote na kinacho endelea mpaka sasa kwa sababu hata hivyo watakuua” maneno ya mwanasheria huyo aliyekuwa ni Edison kwa sura alikuwa akiyasikia vyema lakini hakuwa na maamuzi sahihi ya kuyafanya kwenye halmashauri ya kichwa chake.
Mambo ambayo yalikuwa yanamchanganya yalikuwa ni mawili, kwanza ilikuwa ni sababu ya mtu huyo kuishi kwenye sura isiyo yake na akaliaminisha taifa zima kwa miaka mingi huku akiwa hajui kilichopo nyuma ya hilo lakini jambo la pili ni kwamba kama huyo alikuwa Edison mwenyewe alikuwa anaweza vipi kujigawa kwenye kazi ya ukomando ambako alipatikana kila alipo hitajika lakini wakati huo huo alipatikana muda wote kama mwanasheria na mahakamani hakuwahi kukosa hata siku moja kama ana kesi ya kuishughulikia.
Yale mawazo yake yalimpotezea umakini, kwenye kuzichuja fikra yake aliyumba kimawazo likawa kosa. Mwanasheria alichota kokoto kwa mguu wake kwa nguvu ambazo ziliruka na kwenda kumkita Nicola kwenye mkono na kifuani, hakutarajia kukutana na hali hiyo hivyo aliyumba. Kuyumba kwake kukamkosesha balansi nzuri hali iliyo mpelekea kupigwa na kiganja kwenye bega lake kwa nguvu maana bastola ilikuwa imedondoka chini, aliongezwa ngumi ya kwenye mishipa ya shingo akapoteza fahamu. Mwanasheria alimbeba mwanamke huyo mpaka kwenye gari ambazo alikuja na vijana wake, alimuingiza kwenye gari moja bila kumfanya chochote kisha yeye akapotea hilo eneo. Hakutaka kumuua mwanamke huyo kwa sababu hakuwa na hatia bali alikuwa anakurupukia mambo ambayo hakuwa na taarifa nayo.

SURA YA TANO
ISO
Shirika la kijasusi la Uganda, The Internal Security Organization (ISO) liliweza kuwasiliana na serikali ya Tanzania kuhusu uvamizi ambao ulifanywa na raisi ambaye bila shaka waliamini kwamba alikuwa ni mtanzania lakini habari hizo zilikuwa ngeni kabisa kwa serikali ya Tanzania. Watu hao walionyesha mpaka ushahidi wakati mtuhumiwa huyo akiomba kufanya mawasiliano na kamishna wa jeshi la polisi nchini au raisi moja kwa moja na aliwasiliana nao mbele yao sasa iweje serikali idai kwamba haikuwa na taarifa hizo? Hapo ndipo wakagundua kwamba Yohani alikuwa anajua kila ambacho alikuwa anakifanya, yale mawasiliano ambayo waliyafanya hayakuwa kwa ajili ya viongozi bali waliwasiliana na watu wake ambao walikuwa wamejiandaa juu ya jambo hilo na lengo lake hasa kubwa lilikuwa ni kufika Dark Site ya shirika hilo hivyo walichezewa akili na raia wa kawaida.
Walipo jaribu kufuatilia jina na sura ya mtu huyo huyo hazikuonyesha kwamba ziliwai kutokea eneo lolote lile duniani, wakabaki na mshangao. Waliomba serikali ya Tanzania iweze kuwasaidia kwa kuwapa ushirikiano katika hilo ili wafanikiwe kumpata mtu huyo ama endapo wangepata taarifa za kumhusu kwani alifanya tukio la kigaidi nchini kwao ambalo liliacha athari kubwa na ilikuwa historia mbaya kwa shirika hilo kudhalilishwa namna hiyo lakini mpaka ofisi ya raisi wao hivyo alihitajika kupatikana mtu huyo ambaye hawakuelewa kwamba wangempatia wapi mpaka wakati huo.
Nakasero, Kampala Uganda yalipo makao makuu ya shirika hilo ndipo kikao kizito kilipokuwa kinafanyika. Kikao hicho ulikuwa ni mstakabali mzima juu ya kile ambacho kilifanyika, serikali ya Uganda ilikuwa inaamini kwamba huenda kile ambacho kilitokea ni serikali ya Tanzania ilikuwa inahusika, kivipi? Mtu ambaye walikuwa wamemkamata na kumhifadhi ndani ya Dark Site alikuwa ni mtanzania tena ambaye alikamatwa kwenye tukio kubwa la kihalifu halafu siku kadhaa mbele wakiwa wanaendelea kumhoji anajitokeza mtu kwa kudai anahitaji kuwasiliana na serikali yake kitu ambacho walikifanikisha lakini anafanya tukio la kutisha kama lile huku maafisa wengi wakiuawa na mwisho wake akafanikisha kumuua mtu wake na kutoweka kirahisi tu? Haikuwaingia akilini, waliamini kwamba kulikuwa na namna ambayo haikuwa sawa.
Mtu pekee ambaye alikutwa yupo hai kwenye lile jengo alikuwa ni mkuu wa kituo cha polisi cha Entebe bwana Akello Odong, hata wale ambao walifungiwa sehemu moja waliuawa. Mwanaume huyo baada ya kukutwa hai tena akiwa amezimia iliwashangaza, jambo ambalo liliwashangaza ni kwamba kwanini yeye hakuweza kuuawa kama wengine! Kwamba ilikuwa bahati mbaya? Hapana mtu makini kama yule asingeweza kufanya kosa la namna hiyo la kumuacha mtu hai eti kwa sababu ya bahati mbaya hivyo njia pakee ya kupata majibu yake ilikuwa ni kumkamata na kumhoji bwana Odong ambaye mpaka wakati huo alikuwa chini ya ulinzi ndani ya makao makuu ya shirika hilo.

UKURASA WA 47 unafika mwisho.
 
Voila....kudos
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 39

Asubuhi wakati kunakucha, nchi iliamka na habari hizo, habari ambayo ilianza kusambaa kwa nguvu kutokana na aina ya mtu ambaye alikuwa ameitoa taarifa hiyo. Mwanasheria nguli zaidi nchi ndiye alitoa hizo taarifa, mtu ambaye jamii ilikuwa ikimuamini kwa jambo lolote ambalo lilikuwa linatoka kwenye mdomo wake. Watu walianza kutoa lawama kwa serikali hususani suala la kupotea kwa mwanasayansi mashuhuri ambaye ni miaka mingi sana ilikuwa imepita lakini serikali haikuwahi kuonyesha kuguswa na jambo hilo hata kidogo lakini pia watu waliihitaji serikali itolee ufafanuzi juu ya tuhuma kutoka kwa mwanasheria huyo za kuhusika kwenye mauaji ya hao makomando tisa na mmoja ambaye alisadikika kuwa hai bila kujulikana alikuwa wapi ambaye aliuziwa hiyo kesi.
Taarifa hiyo ilifika mpaka ndani kabisa kwenye shirika la kijasusi ya nchi, IBA (INVESTIGATION BREAUCRACY AGENCY). Haikuwa habari njema kwao, ilikuwa ni habari mbaya ambayo ilikuwa inaenda kuwachafua wao, ofisi ya raisi lakini mpaka jeshi la nchi kwa wote kuoekana kutowajibika vya kutosha juu ya mambo ya hatari ambayo yalikuwa yanatokea nchini ukizingatia ni siku chache tu zilikuwa zimepita tangu kutokea kwa utekaji na mauaji uwanja wa ndege na bado watu hawakuwa wamepata taarifa zozote za kuridhisha, haukupita muda tena askari ambaye aliishika ile kesi ya kufuatilia jambo lile alikutwa akiwa ameuawa na wenzake wakiwa wameuliwa eneo jingine. Hali hiyo iliwafanya wananchi waanze kuandamana na kudai kwamba viongozi wa juu walitakiwa kutoa majibu na kama hawakuwa na majibu basi walitakiwa kuachia nafasi zao kwani hawakuwa na sifa stahiki za kuweza kuisimamia nchi yao na kupigania haki za watu wanyonge maskini.
Taarifa hiyo ambayo haikuwa njema ndiyo ilimtoa mwanamama Lionela Philson ambaye alikuwa mkurugenzi wa shirika la kijasusi la IBA nyumbani kwake na kumuwahisha ofisini akiwa mwingi wa hasira. Ofisi hizo za shirika hilo zilikuwa mita chache kutoka kilipo chuo cha mafunzo ya usalama wa taifa wa nchi huko Mbweni ambako wanapatikana watu wenye ukwasi wa kutosha hasa wale viongozi wa ngazi za juu serikalini na wafanya biashara wakubwa. Aliingia ofisini akiwa anawahitaji vijana wake ambao alikuwa anawaamini awakute wamejikusanya kwenye ukumbi wa mikutano.
Jengo lilikuwa ni kubwa la ghorofa mbili, lilitengenezwa kwa uzio mrefu na pembani yake hakuna mtu ambaye aliruhusiwa kujenga nyumba ya ghorofa kwa sababu wizara ya ardhi ilipiga marufuku kwa kudai kwamba eneo hilo halikuwa salama kulingana na aina ya udongo wake hata hilo ghorofa ambalo lilikuwepo lilikuwa kimakosa lakini watu wa maeneo ya mbali na eneo hilo walikuwa wanaruhusiwa kuweza kujenga nyumba ya aina yoyote ile kulingana na ukubwa wa mfuko wako. Lengo la kuzuia ujengaji wa majengo marefu, hawakuhitaji mtu yeyote aweze kutambua kitu ambacho kilikuwa kinaendelea humo ndani.
Mambo yao mengi yalikuwa yanafanyika chini ya ardhi ambako kulikuwa na vyumba na maofisi mengi na kila kitu kilimalizikia huko huku juu watu wachache wakiwa wanazuga kama wanayaendeleza maisha ya kila siku ambapo hata kama kwa bahati mbaya mtu angehoji basi asingekuwa na taarifa za jambo lolote ambalo lilikuwa linafanyika humo ndani. Akiwa amefura kwa hasira ambazo zilijidhihirisha kwa ndita zilizo jichora kwenye uso wake, alifika ofisini kwake na kuutua chini mkoba wake mdogo huku akiwa amevaa suti ya blue na koti lake akiwa amejifunikia tu bila kulivaa! Simu yake iliita.
Baada ya kuangalia vizuri aligundua kwamba simu ambayo ilikuwa inaita haikuwa ya ofisini bali namba yake binafsi, aliisogelea mahali ambapo alikuwa ameibwaga na kuipokea baada ya kugundua kwamba ilikuwa inapigwa na CDF.
“Kichwa changu hakipo sawa, tutaongea baadae”
“Hili jambo ni mhimu halihitaji hata kusubiri, sio muda hapa raisi atahitaji taarifa kwa skendo hii chafu ambayo inaendelea hivyo nahitaji kujua kama kuna taarifa zozote za mhimu ambazo unazo?”
“Hapana, hata mimi nimeshangazwa na taarifa hizi, huyu mwanasheria hajawahi kuonyesha dalili zozote za kulijua jambo hili sasa iweje aibuke tu ghafla baada ya miaka mingi kupita tena akiwa anaongelea habari za ukweli na kudai kwamba ana ushahidi wa kutosha? Hili sio bure kuna namna na hatari kubwa inaweza kuwa inajisogeza hali ambayo inaweza kuliingiza taifa kwenye majanga makubwa mbele ya macho yetu”
“Nadhani huyu anapaswa kuuawa” CDF alitamka kwa sauti ya nguvu
“Halafu?”
“Habari hiyo itakuwa imeishia hapo”
“Muda mwingine uwe unatumia akili, umepewa jeshi uliongoze nina imani sio kwa bahati mbaya. Huyo ni mtu ambaye anapendwa na watu na kwa hili ambalo limetokea kama akipata tatizo lolote lile basi moja kwa moja tutadhihirisha kwamba serikali imehusika moja kwa moja kwenye hilo jambo. Halafu ukizingatia yule ni gwiji wa sheria hauna huo uwezo wa kumkamata kijinga namna hiyo hivyo kwa sasa anatakiwa kuachwa kama alivyo”
“Yaani tumuache aendelee kufanya hiki anacho kifanya?”
“Jambo la msingi tunatakiwa kujua sababu ya yeye kuyaleta haya yote ni ipi na alikuwa wapi wakati wote mpaka ajitokeze saivi? Kuna kitu ambacho huenda hukifahamu kwa huyu bwana. Kuna taarifa zinadai kwamba ni mtu ambaye anaishi kwenye sura ya mtu mwingine na taarifa hizi kuna vyanzo vinadai kwamba alizivujisha yeye mwenyewe makusudi hivyo kabla ya kukurupuka kuna mengi ambayo tunatakiwa kuyajua kumhusu yeye. Ni muuji pia wa kutisha wa siri ambapo haijulikani haya mambo alijifunzia wapi lakini pia ni daktari mzuri tu na hilo wanalijua watu wachache”
“Hivi unamzungumzia ni huyu mwanasheria JACK THE LAWYER au mtu mwingine?”
“Ndiye huyo huyo mwenyewe, ndiyo maana nakwambia kwamba hatutakiwi kukurupuka huenda anajua kwamba tutafanya hivyo ili afanye anacho kitaka. Watu wenye akili ni hatari sana kama ukiamua kutumia mihemko kupambana nao hivyo kwa sasa usije ukathubutu hata kutuma watu wako kwake kwa sababu utazua mambo mengine ambayo siyo. Kuhusu raisi naenda kuongea naye kuhusu hili mimi mwenyewe” mwanamama huyo alikata simu baada ya kuona CDF anazidi kumhoji utadhani alikuwa mtuhumiwa wake. Alichukua kifaa chake kidogo cha mawasiliano mithili ya kalamu ya wino na kuelekea nayo kwenye chumba cha mkutano.
“Nadhani wote mnakumbuka vyema tukio la miaka mitano iliyopita, tukio ambalo lilileta mtikisiko mkubwa kwenye idara na nchi kwa ujumla baada ya makomando tisa kufariki na mmoja kupotelea kusiko julikana na kupewa kesi ya kuhusika na mauaji ya wenzake pamoja na kuuza siri za nchi. Jambo hilo limerudi tena kupitia mwanasheria JACK THE LAWYER” Aliweka kituo huku akiibonyeza ile kalamu yake katikati ambayo ilikuwa kama rimoti. Kwenye ukuta mkubwa paliwaka pakiwa na picha ya mwanasheria huyo ambaye alikuwa ndani ya suti ya gharama akiwa mwingi wa tabasamu. Mama huyo aliyaanzisha mazungumzo hayo bila hata kujibu salamu ya vijana wake wanne ambao walikuwa wakimsubiri ndani humu, watatu walikuwa wa kiume na mmoja wao ambaye ndiye alikuwa kiongozi wao alikuwa ni mwanamke! Aaliyah Beka.
“Anaadai kwamba kesi hii inatakiwa kufunguliwa upya na serikali ndiyo mshtakiwa, hili ni jambo baya kwa sababu kama serikali ikishindwa kwenye kesi hii ni kwamba viongozi wakubwa watahitajika kuachia nafasi zao na watu wengi watakosa kazi huku wengine wakitakiwa kufungwa. Ukiachana na jambo hilo, jambo la hatari zaidi ni kwamba nchi itapata mpasuko mkubwa ambao utakuwa ni hatari kwani unaweza ukachochea vurugu nyingi kama sio kuleta vita vya wenyewe kwa wenyewe”
“Sanjari na hilo, mwanasheria huyu huwa haongei vitu kwa kubahatisha, mpaka amefikia hatua ya kuongea mambo mazito kama hayo basi jua ana ushahidi wa kutosha. Kilicho zidi kueleta hofu kubwa ni baada ya kuifufua kesi ya miaka mingi iliyopita, kesi ya mwanasayansi Christian Edison ambaye serikali ilikubali kumpeleka huko MOSSAD kwa ajili ya kwenda kulisaidia taifa la Israeli kutengeneza nyuklia ila mpaka sasa haijawahi kurudi taarifa yoyote kumhusu na jambo hili halieleweki liliishia wapi ila mtu huyu anadai yeye anazo taarifa”

UKURASA WA 39 unafika mwisho.
❤️❤️
 
Back
Top Bottom