SURA YA ISHIRINI NA NANE
TANZANIA 2013 -JULY
Ilikuwa ni mwezi July ndani ya jiji la Dar pilika pilika zilikuwa za hali ya juu ndani ya jiji hili , si kwa wanausalama ,sio kwa majeshi , sio kwa wananchi , kwa mara ya kwanza jiji la Dar linaonekana kuwa safi kuliko siku zote.lakini haikuwa kwa swala la usafi tu , lakini pia ulinzi ulikuwa umeimarishwa kila kona ya jiji hili, huku makachero wa kizungu pia wakionekana kulandalanda huku na huko kuhakikisha hali ya usalama.
Naam hii yote nikutokana na ujio wa Raisi wa taifa kubwa duniani , taifa lenye ushawishi kila kona ya dunia , taifa ambalo lina uchumi mkuwa duniani , taifa ambalo linaongoza kwa teknolojia kubwa duniani,Raisi ambaye kwa mara ya kwanza anazuru ndani ya taifa la Tanzania na kufanya dunia isimame na kushangaa tukio hili la kipekee kabisa kutokea ndani ya taifa hili.
Ni baada ya masaa kadhaa ya ndege kubwa ya Raisi kutua ndani ya uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na mheshimiwa Raisi Kigombola raisi wa Tanzania akiongozana na viongozi wakubwa wa Tanzania walionekana kuwa katika hali ya furaha maa baada ya kumpokea raisi Barrack Mabo.
Mheshimiwa Raisi Kigombola alijisikia fahari sana , na katika Maisha yake ya uongozi alijihisi ni jambo kubwa sana ambalo amelitimiza , kwa kumtoa raisi wa dunia ambaye alikuwa na majukumu mengi duniani na kuja kutembelea taifa dogo la Tanzania.
“Ndoto zangu zimetimia nina uhakika maadui zangu ndani ya taifa hili wataelewa uwenzo na nguvu niliokuwa nao.,kumleta raisi wa Dunia Tanzania sio jambo dogo”Aliwaza mheshimiwa huyu wakati wimbo wa Taifa ukiendelea , licha ya kwamba mzee huyu alikuwa akiimba wimbo huu lakini akili yake iilikuwa ikiwaza maadui zake na mipango yake.
“Tanzania itakuwa yangu milele na milele ,m nitaacha mizizi ambayo hakuna kiumbe yoyote ambaye ataweza kuingoa”Aliendelea kuwaza.
Baada ya shamra shamra za aina yake hatimae safari ya kuelekea ikulu ilianza huku asilimia tisini ya ulinzi wa raisi huyu ulikuwa ukiratibiwa na vikosi vyake ambavyo vilikwisha kutangulia nchini kuhakikisha hali ya usalama.
“Karibu sana Rafiki yangu ndani ya Tanzania”Aliongea mheshimiwa Kigombola .
“Asante sana Kigombola , nimefurahi na mapokezi ya watanzania”aliongea na kumfanya mheshimiwa Kigombola aendelee kujiona yeye ndio yeye na ndio Raisi wa Tanzania ambaye ana akili nyingi kuliko raisi yoyote yule.
Baada ya chakula mheshimiwa Bamo alipewa ofisi yake kwa ajili ya kuendelea na majukumu ya kazi , kwani bwana huyu hakuwa ni mwenye kupumzika kabisa , muda wote alikuwa macho akifanya kazi , alikuwa ni raisi wa Taifa la Marekani , lakini alikuwa akitoa maamuzi na maelekezo yanayoenda kutekelezwa na maraisi wa mataifa mengine na hii yote inaifanya kazi yake kuwa ngumu sana na kumfanya kuwa bize.
Wakati akiendelea na kazi ndani ya ikulu ya Tanzania aliingia bwana mmoja alievalia mavazi ya kikachero yenye nembo ya taifa la Marekani, bwana huyu alionekana kuwa kijana mdogo , lakini alikuwa na nafasi kubwa katika kikosi cha ulinzi cha mheshimiwa huyu.
“Nipe Ripoti Chriss?”Aliongea mheshimiwa huyu na kisha akampatia mheshiwa Bahasha aliokuwa ameishikilia mkononi na Raisi huyu aliifungua na kuangalia kilichomo ndani , na alikuta ni picha, alizitoa na kuanza kuziangalia na bwana huyu macho yalimtoka.
“Wanafanana kwa asiliamia kubwa na Agent no 17, Umefuatilia ni nani baba wa mtoto huyu?”
“Mheshimiwa tumekusanya ripoti kadri tulivyoweza , huyo mwanadada anaitwa Edna ni mtoto wa Rahel na Adebayo wanafamilia wanaomiliki kampuni changa ya VEXTO”.
“Lakiini imekuwaje huyu Edna akafanana kwa asilimia mia moja na Agent 17?”.
“Hilo ndio swali lililofanya tuendelee kufatilia kwa ukaribu kama kuna muunganiko wowte kati ya 17 na Edna na katika uchunguzi tuliofanya tulibaini watu waliohusika kumfanyia matibabu Rahel kipindi cha ujauzito wake , wote walifariki vifo visivyoleweka lakini swala hilo halikuweza kutukwamisha kupata taarifa na kutokana na uwepovyanzo vingi vya taarifa tulivyovipandikiza hapa nchini tumegundua Agent 17 na Edna walizaliwa mapacha wa kufanana”.
“Nini, unahakika na hio taarifa Chriss”
“Ndio mheshimiwa”.
“Sawa Chriss , kazi nzuri kaendelee na majukumu yako mengine , ila hili swala kwa sasa nitampatia mtu mwingine ashughulike nalo , kwasasa hatupaswi kufanya jambo lolote lile”Aliongea Mheshimiwa naChriss alitoka ndani ya ofisi.
Baada ya Chriss kutoka mheshimiwa alirudia kuangalia zile picha mezani kwake kwa umakini mkubwa huku akionekana kuwaza sana.
“Hapana kwa namna yoyote ile siwezi kuruhusu tundu lolote ambalo litafanya Operation LADO kufichuka, Uwepo wa Edna duniani utamfanya Agent 13 na 17 kutaka kufahamu ukweli uliotokea katika Maisha yao ya nyuma kama watabahatika kumuona Edna na suluhisho la haya yote ni Edna kufa”Aliwaza mheshimiwa huyu huku akiangalia picha hizo.
Baada ya lisaa kukaa kwenye ofisi yake hatimae mheshimiwa Kigombola aliingia ndani ya ofisi hio na kukaa kwa ajili ya mazungumzo na mheshimiwa , swala la kwanza ni juu ya mipango yao , ambayo imemfanya bwana huyu mwenye madaraka makubwa duniani kufika ndani ya taifa , lakini pia swala la pili ni jambo binafsi alilokuwa akitaka kuomba msaada kwa Kigombola .
“Kigombola , kuna jambo la ziada unapaswa kunisadia”Alianzisha maongezi.
“Jambo gani hilo mheshimiwa wewe ni Rafiki yangu na nipo tayari kukusaidia jambo lolote hata kama unataka kasehemu ndani ya hii nchi naweza kukupatia”.Alitabasamu na kisha akatoa picha na kumpa Kigombola.
“She need to die and you as my friend utanisaidia katika hili”Aliongea Bamo na kumfanya Raisi wa watanzania ashangae nini tatizo.
“Mheshimiwa kuna haja gani ya mtoto kama huyu kufa?”.
“Kigombola fanya kama ninavyokuambia huyu msichana lazima afe la sivyo mafanikio yangu ambayo nimeyajenga kwa miaka na miaka yanaweza kuwa hatarini na uwepo wa huyu msichana”Aliongea na kumfanya Kigombola kumwangalia mheshimiwa mwenzake na kutingisha kichwa kwamba jambo hilo atalifanyia kazi.
Wakati hayo yakiendelea upande wa pili nchini Rwanda Jeremy anapokea taarifa kutoka kwa shushu wake ikulu iliokuwa kwa mfumo wa ujumbe wa sauti.
“Edna yupo hatarini kubaki nchini Tanzania”
“Nilitegemea swala hilo , ngoja niwasiliane na upande wa pili wa mpango wetu”Alijibu na simu ilikatwa.
“Fu**ck you Amerika , I must pay for what you Did , nitachimba na kuujua ukweli wote”Aliongea kwa hasira Jeremy.
****
Edna kama kawaida yake alikuwa amekaa chumba chake cha kujisomea akiwa anafanya baadhi ya kazi za hapa na pale kama ilivyokuwa kawaida ya mwanadada huyu kutokupumzika , lakini ufanyaji kazi wake wa leo mwanadada huyu haukuwa kama wa siku zote , alikuwa ni mwenye kuwaza mambo kadha wa kadha lakini kubwa lililokuw andani ya kichwa chake ni juu ya Roma.
Aliinua simu yake na kisha kuangalia picha zilizotumwa na Suzzane zikimuonesha Roma akiwa na Doris siku kadhaa nyuma wakionekana wameshikana viuno , lakini pia picha ya pili ilikuwa ikimuonesha Roma akitoka ndani ya nyumba ya Rose , lakini picha nyingine ikimuonesha Roma akiwa amekumbatiwa na mwanadada ambaye sura yake haikuonekana , lakini pia picha nyingine Roma akibusiana na Nasra kwenye gari , lakini pia picha nyingine Roma akiingia ndani ya chumba cha hoteli na Neema luwazo , Picha zote hizi zilitumwa na mwanadada Suzzane mlinzi wa siri wa Edna.
“Suzzane anafanya mambo ambayo sijamwagiza , haikuwa na haja ya kumfatilia Roma , ni mume wangu ndio lakini sio kwa mapenzi ila kwa mkataba na ukiisha tunaachana , sitaki kuyaingilia sana Maisha yake” Aliwaza
Licha ya kuona picha hizo lakini kwa Edna hakuonyesha kukasirika alichukulia kawaida tu lakini alionekana kuna kitu hakipo sawa , aliona licha ya Roma kuwa mume wake kisheria ,, lakini hakuwa akiishi kama mume wake ,vitendo ambavyo aliona Roma anafanya vitamletea shida kama watu watagundua kuwa Roma ana mahawala wengi
Wakati akiendelea kufikiria mala mlango wake uligongwa na alinyanyuka na kwenda kuufungua na uso kwa uso na Roma.
“Honey Darling Chakula tayari , twende tukale”Aliongea Roma huku akiwa ametabasamu na Edna alimwangalia Roma na hakummaliza.
“Sijisikii kula” Aliongea na kisha akafunga mlango kwa hasira , ila Roma hakuondoka alisimama na kugonga tena na awamu hii mlango ukafunguliwa tena na mwanadaa huyu huku akionekana ni mwenye kuwa na hasira.
“Hivi Roma nini , si nimekuambia sijisikii kula , unaweza kwenda kuendelea”
“Namimi siwezi kula peke yangu, na nitaendelea kugonga mlango mpaka ushuke tukale” Edna alimwangalia Roma na kwa alivyokuwa ana muona Roma aliamini bwana huyu alichokiongea alikuwa anaaanisha.
“Kale na Bi Wema , kama huwezi kula peke yako”
“Bi wema kasema hajisikii vizuri atakula baadae,Mke wangu mbona huna heshima kwa mumeo twende basi”
“Yaani Roma wewe sijui ni mwanaume wa aina gani huelewi”Aliongea Edna huku akitoka na kufunga mlango na kuelekea chini akitangulia huku Roma akimwangalia kwa nyuma na kuishia kutabasamu.
Bi Wema aliekuwa akiingia kutoka nje alijikuta akitabasamu na moyo wake kuwa wa moto mara baada ya kuona Roma na Edna wakiwa kwenye meza wakila chakula , ilikuwa ni picha ambayo ilimvutia sana, kwake na alitamani iwe kila siku kuona wanandoa hao wanafanya mambo kwa pamoja , hakupenda namna Maisha ambayo Edna alikuwa akiyaishi , alikuwa akiamini mwanamke hawezi kukamilika pasipo ya kuwa na mume na pia Mume hawezi kukamilika pasipo ya kuwa na Mke.
“Roma ..!!!”Aliita Edna na Roma alimwangalia Edna.
“Ndio mke wangu”
“Kwanini haupo kama wanaume wengine”.
“Unamaanisha nini mke wangu , usiniambie ushaanza kunifananisha na wanauame wengine?”
“Sio kukufananisha na wanaume wengine , lakini wewe upo tofauti kabisa , haupo siriasi na Maisha , kazi umepata lakini unaishai kucheza gemu na kufanya uzinzi”Aliongea Edna huku akionesha yupo siriasi ila Roma hakujali kwanza alitabasamu.
“Mke wangu nitakuwaje siriasi na pesa zote hizo ulizonazo , nani wakuzitumbua, wote tukiwa na pesa hainogi bebi , mmoja akiwa tajiri mwingine asiwe na pesa ili kuwe na mtu wa kutumbua pesa na kula bata ,Bebi Edna tuseme wewe umeolewa na mimi na ukanikuta na mipesa kama hii yako, kwanini uanze kujihangaisha na Maisha badala ya kula bata”
“Kwa hio wewe kazi yako ni kutumbua pesa zangu ?”
“Halafu mke wangu sio pesa zako ni za kwetu , ushasahau sisi ni mwili mmoja”Edna alimwangalia Roma kwa hasira kali mno , alishindwa kuelewa Roma ni mtu wa aina gani yeye yupo siriasi kumwambia mambo ya maana lakini anaanza kuongea ujinga juu ya maswala ya kutumbua hela.
“Kama unawaza kutumbua pesa zangu sahau , usipo tafuta zako hutipata chochote kutoka kwangu”
“Mke wangu kama hutaki nikitumia pesa zako nani atazitumia ...Halafu mke wangu mbona kama unampango wako kichwani wa sisi kutafuta mtoto halafu huniambii nijiandae”Edna alimwangalia Roma huku akishangazwa na uroppokaji wake , ‘Neno mtoto ‘ ni swala ambalo hakuwahi kulifikiria hapo kabla .
“Nani mimi … Mtoto ,, hata kama nitake mtoto siwezi kuzaa na mwanaume asiye siriasi na maisha Watoto wataiga nini”.
“Bebi kama hutaki kuzaa na mimi mumeo unataka uzae nje ya ndoa ?”Edna baada ya kuona topic ambayo hakuwa akiipenda Roma kaikomalia , alinyanyuka na kupandisha Ngazi kuelekea chumbani kwake huku Roma akiwa ni mwenye kutabasamu.
“Huyu mwanaume muda wote anafikiria ujinga tu , nifanye nini ili angalau kumbadilisha ili hata niwe na kujiamini nikimtambulisha mbele za watu”Aliwaza Edna huku akiwa amesimama kwenye dirisha chumbani kwake.
Ukweli ni kwamba kuna muda Edna alitamani kumuona Roma abadilishe mfumo wake wa kimaisha , alitamani awe kama wanaume wengine ambao wako bize na kutafuta Maisha na kuongoza biashara hatimae aweze kujivunia kuwa na mume mwenye mafanikio , lakini haikuwa hivyo , Roma alikuwa Roma kama alivyomtoa kule kwenye kazi yake ya ubeba mizigo , hakuwa amebadilika hata kidogo ,tabia yake ilikuwa vilevile
Edna wakati akiendelea kufikiria akiwa anaangalia eno la Nje alimuona mwamba Roma akaitoka tena awamu hii akiwa amepigilia miwani ya jua kabisa na haikueleweka katioa wapi , alimwangalia namna ambavyo anaingia kwenye gari yake na kuwasha na mpaka lilipotokomea nje ya geti.
“Lazima anaenda kutafuta mwanamke pale”Aliwaza Edna huku akirudi kitandani na kukaa.
SURA YA ISHIRINI NA TISA
Roma hakuwa ni mwenye kujali sana kuhusu maneno ya Edna kwani muda huo alichokuwa anawaza ni kiwanja gani anaweza kwenda kula bata , na angalau kujipatia kitumbua ambacho kinaweza kumtuliza kwa siku hio ya Wikiend.
Wakati akiwa anaingia kwenye Daraja la Kigambomi kuna gari aliitilia mashaka kwani hisia zake zilimwambia kabisa gari hio ilikuwa ikimfatilia , lakini licha ya kuwa na hisia hizo alitamani kulithibitisha hilo na ndio maanba alianza kuchukua chocho ambazo zilikuja kumfikisha mtaa wa Chang`ombe , lakini Gari ile bado ilikuwa nyuma yake.
“Kuna wapuuzi wananifatilia”Aliwaza Roma huku akiendelea kukumbuka kuwa gari ile ilikuwa karibu na nyumba anayoishi na kwa namna yoyote ile ni kwamba watu hao wanataarifa la eneo ambalo anaishi nah ii aliona ni hatari kwa yeye na kwa familia yake yaani Bi Wema na Edna.
“Ngoja kwanza niwapoteze “Aliwaza huku akiongeza spidi ya gari na muda huu magari yalikuwa mengi barabarani kwani ilikuwa ni muda wa jioni jioni hivi watu wakirejea majumbani , lakini licha ya magari hayo mengi haikumsumbua Roma kuendesha gari kwa spidi na kuanza kupita kila apatapo nafasi na alitumia dakika chache tu gari iliokuwa inamfatilia alikuwa ameipoteza , lakini sasa alijishgaa kuona ameendesha gari umbali mrefu mpaka kufika Kawe.
“Bora niende zangu Beach”Aliwaza Roma na kuendesha gari kuelekea upande ilipo kuwepo Ufukwe wa Kawe.
Wakati anaingiza gari yake eneo maalumu la kuegeshea magari wapo watu wengi waliokuwa wakimkodolea macho kutokana na uzuri wa gari yake.
“Bosi kuna boti zipo hapa kama utahitaji”Aliongea kijana flani mara baada ya kumuona Roma akitoka kwenye gari, kijana huyo alionekana kuvaa tisheti flani hivi ya kampuni iliokuwa imeanzishwa hivi karibuni ndani ya jiji la Dar es salaam ambayo ilikuwa ikikodisha SpeedBoat , boti flani hivi zipo kama pikipiki.
Roma alijikuta akitamani kweli kuendesha boti na aliongozana na kijana yule mpaka upande ambao Boti hizi hukodishwa.
Baada ya kufanya malipo ya awali , alionyeshwa upande ambao boti hizo zilikuwa zimeegeshwa na Roma alisogea upande huo na kuchagua boti ambayo ilimvutia na alionekana alikuwa akijua kweli boti hizo.
Baada ya kuridhika na chaguo lake alirudi na kubadilisha nguo na kupewa mavazi ya ziada kwani hakuwa na mpango wa kuja ufukweni hivyo hakuwa na nguo za fukwe.
Siku hii ndani ya eneo la fukwe kulikuwa kumechangamka mno kiasi kwamba kulikuwa kumependeza , kuna waliokuwa wachumba wakiwa ndani ya hili eneo , kuna waliokuwa ndani ya fukwe hii kama wanafamilia na pia kuna waliokuwa wapo ndani ya fukwe hii wakiwa peke yao kubarizi.
Roma hakujali sana juu ya watu hao, ila kwake muda huo ni kufurahia maji ya baharini kwa kutumia speedboat.
Upande mwingine kwenye maegesho ya magari , iliingia gari aina ya Nissani nyeusi na kupaki pembeni ya gari ya Roma na wakashuka mwanamke mmoja wa kizungu pamoja na mwanaume wa kizungu , wote wakiwa wamevalia Track suit pamoa na tisheti , baada ya kushuka waliangalia gari ya Roma na kisha wakatingishiana vichwa kama ishara na kisha walisogea upande wa fukwe.
Baada ya kufika kwenye fukwe walianza kuangaza macho yao kulia na kushoto kama watu waliokuwa wakitafuta jambo Fulani na ndani ya dakika kama mbili hivi walijikuta wakipeana ishara mara baada ya kuona boti iliokuwa kwenye spidi ikipotelea katikati ya maji.
Ni kitendo cha haraka sana mzungu yule wa kike alirudi kwenye gari na kutoa begi flani dogo na kisha kutoka na kuungana na mzungu wa kiume na kuelekea kwenye kampuni ambayo ilikuwa ikikodisha Speedboat na kulipia moja na dakika chache tu walionekana wakiwa kwenye boti ile huku wakiitoa kwa spidi kiasi kwamba watu walianza kushangaa kwa umahili wao. Na kwa jinsi walivyokuwa wanaonekana kama ungewaangalia ungesema watu hao watakuwa ni wapenzi kwa namna yoyote ile ,kwani walikuwa wamependezana.
Roma alikuwa akiendesha mdogo mdogo huku akiwa ni mwenye kufurahia upepo uliokuwa ukimpepea machon kiasi cha kumpelekea kufumba macho.
“Hey! Bro , ilisikika sauti iliomwita Roma akiwa katikati ya maji kiasi cha kufumbua macho , kwani muda wote alikuwa ameyafunga akifurahia upepo, Na Romaa baada ya kugeuza macho yake alimuona msichana mrembo akiwa kwenye boat kama yake , alikuwa ni mrembo haswa kiasi kwamba Roma pepo la ngono liliibuka hapo hapo
Kimakadirio mwanamke aliekuwa mbele yake alikuwa mdogo sana kiumri kati ya miaka ishirini hivi kushuka na Roma alimkadiria mwanadada huyo kama mwanafunzi wa chuo kama tu atakuwa anasoma.
“Mambo mrembo?”
“Poa! Tunaweza kushindana?”
“Kushindana kufanya nini?”
“Kuendesha”Hapo Roma alimuelewa na kisha akatabasamu.
“Hautoweza kunishinda wewe”
“Hata mimi hautoweza kunishinda”Aliongea Mrembo na wote hawa wawili licha ya kwamba walikuwa wamekaribiana na boti zao ,lakini walikuwa wakuiongea kwa sauiti kubwa ili kusikilizana kwani upepo ulikuwa mkali kiasi kwamba sauti ilikuwa ikipotea.
“Sawa lakini lazima kuwe na zawadi kwa mshindi , ukiweza kunishinda nakupatia gari yangu niliokuja nayo”Aliongea Roma.
“Gari aina gani umekuja nayo ambayo unaamini ninaweza kuikubali kama sehemu ya zawadi kwa mshindi?”
“Aud Q8”Aliongea roma na kumfanya mwanadada huyu atabasamu kwani gari hio alikuwa akiijua vyema ugharama wake katika soko la magari duniani , ni gari ambayo sio chini ya milioni 200.
“Mimi ukiweza kunishinda nakupa mwili wangu leo?”Aliongea yule mwanadada kwa kujiamini na kumfanya Roma acheke.
“Hehe.. unaonekana unajiamini sana mremb?,o kumbuka kutimiza ahadi ”
“Ndio hakuna ambaye ashawahi kunishinda kwenye mbio za baharini , nina medali nyingi nilizopata chuoni”
“Chuo gani unasomea?”
“Yale university”Aliongea manadada huyu na kumfanya Roma atabasamu .
“Okey ! deal ule wako uende kinyume na ahadi yako”
“Siwezi kwenda kinyume na ahadi yangu ni moja ya sharia nilizojiwekea”
“Karembo sana haka nitahakikisha nashinda nikakavue nguo nione kamebeba nini?”Aliwaza Roma huku wakijiandaa kuanza mtanange na kuamua mstari wa ushindi , mwanadada huyu mrembo ambaye jina bado hatumjua alionekana kujiamini mno.
“Ukute anafurahi mwenyewe atanishinda Looh! yaani nikuvulie nguo mimi”Aliwaza mrembo huyu na muda huo huo wakaanza kuendesha kwa spidi huku membo huyu akionekana kuwa imara kweli , kwani ni ndani ya dakika moja tu alikuwa amemuacha mbali kidogo Roma , lakini kwa Rroma hakuwa na wasiwasi hata kidogo ,alikuwa akiendesha kama hataki vile.
Mwanadada aliekuwa mbele , alionekana kumdharau Roma na kuona hakuwa saizi yake , lakini ghafla wakati akiendelea na mawazo hayo , alipitwa na Roma kwa spidi ambayo haikuwa ya kawaida na kumfanya mrembo huyu ashangae na kuanza kuongeza Spidi, kwani Roma alikuwa ashamuacha hatua kadhaa mbele.
“Shi**t Atanishinda huyu”Aliongea huku akiichochea boti yake na ikaanza kusererka kiasi kwamba kulionekana povu la maji ya baharini likiwa limejitengeneza kwa nyuma.
Mchezo huu walikuwa wamewekeana umbali ambao walitakiwa kufika , kwa mbele kabisa kulionekana kukiwa na mnara ambao ndio mwanadada huyu alipendekeza , japo ilikuwa katikati ya bahari kwenye maji mengi ila hawakuongopa , lakini sasa , kadri alivyokuwa akijitahidi kuendesha hakuwa akimfikia Roma na hapa akili yake ilianza kupata moto na kujiuliza huyu mtu ni wa namna gani kwani katika Maisha yake yote hajawahi kushindwa kwenye mchezo huo na anazo medali.
Mwanadada huyu mrembo alianza kujutia maamuzi ya kuuweka mwili wake Rehani aliona kabisa dalili za kuliwa zinaenda kutimia.
Roma na yeye hakuwa na utani kabisa mbele ya kitumbua , alihakikisha anashinda na hilo alilikuwa akikaribia kulifanikisha kwani alikuwa akikaribia eneo ambalo ndio mstari wa ushindi.
Mrembo huyu alijikuta macho yakimtoka mara baada ya kumuona mwamba Roma akipita mnara kwa spidi na kuwa mshindi.
“Shi**t nishaliwa leo”Aliongea huku akipunguza mwendo lakini ghafla alimuona Roma akipiga kona ya hatari sana kuzunguka mnara ule na kuja upande ambao yupo kwa spidi ya hali ya juu sana kiasi kwamba mwanadada huyu alianza kujawa na hofu na kujiuliza ni kitu gani mwanaume huyu asiemjua anafanya , lakini alikuja kujua baada ya dakika chache , kwani ile Roma anamfikia yule mrembo aliisukuma bot ya yule mrembo kwa kutumia boat yake kwa nguvu na kuacha uwazi na hapo hapo ikapita Boat nyinngine sehemu ambayo boti ya mrembo yule alikuwa ameisimamisha na ikawa ponea ya mrembo huyu.
“Pumbavu wana siraha”Aliongea Roma baada ya kuona mwanadada wa kizungu kutoa bundiki yake kubwa na kumlenga , yule mrembo mwanzoni hakuwa akielewa kinachoendelea ila alipoangalia kwa umakini aliona bunduki na kuanza kupatwa na hofu na kujiambia leo anakufa katikati ya bahari , na eneo walilokuwepo ni kama vile watu hawa walikuwa wakiwasubiria waende mbali ili kuanza kuwashambulia wakina Roma kwani ilikuw ani mbali na fukwe.
Roma aliona yule mzungu akivuta Triga , lakini hakutaka kufa kizembe , aliipindisha Boti ile kwa upande mmoja wa kulia ina ikainama kiasi ambacho bega la Roma liligusa maji huku yeye akiinama na kichwa pia kugusa maji na boti ile kubinuka upande mmoja na kilichosikika hapo ni risasi mbili mfululizo zilizotua upande wa chini kabisa wa Boti.
Kwa jinsi Roma alivyokinga risasi ile kwa Boti ni kitendo ambacho mrembo aliekuwa pembeni hakuwahi kukishuhudia katika Maisha yake aliona kama yupo kwenye muvi.
Mzungu yule wa kike alishindwa kumlenga Roma kwani hakuwa akimuona kwa upande ambao walikuwa wapo ,kwa kitendo cha boti ya Roma kubinuka upande na nikama Roma alikuwa akifanya makusudi , baada ya wao kuona Roma amejiwekea kinga kwa kutumia boti ile , waligeuza kwa spidi kwenda upande mwingine na hapo mrembo yule alijikuta akizidi kupagawa , lakini alikuja kupiga mshangao mara ya boti ya Roma kurudi katika usawa wake , lakini kwenye boti hakukuwa na mtu na hata wale wazungu walishangaa kwa wakati mmoja na kujiuliza ni kitu gani kimetokea , walionekana kuhaha.
Umbali ambao Roma alikuwa amesimama na umbali ambao wazungu walikuwa wamesimama ilikuwa mita kama ishirini hivi.
Mrembo yule alikuwa kwenye hali ya mshangao na alijiambia huenda mwanaume yule Kazama chin na Risasi ile imempata ., hakutaka kujiuliza mara mbilimbili na yeye alijitupa ndani ya bahari huku akidhamiliia kufanya jambo la kiuokozi.
Huku nje wale wazungu walishangazwa na tukio hilo , lakini pia na wao walidhania mtu aliekuwa wakimshambulia atakuwa Kazama , lakini haikuwa hivyo kwani ile wanapunguza spidi ya boti yao kulitokea tukio kama la Dolpin kuruka sarakasi kwa kutokezea nje ya maji na yule mwanamke alivutwa kwa kushikwa kwenye mkono kwa nguvu na kuachia libunduki lake na baada ya kuvutwa alizamishwa kwenye maji na kukatulia tuli.
Wakati hayo yakiendelea mrembo yule mwingine alikuwa akitokelezea kwenye maji huku akionekana kuvuta pumzi na kurudi tena kupiga mbizi , huku akiacha kuangalia upande walikokuwa wale wazungu aliowaacha , alirudi tena ndani ya maji kwa ajili ya kumtafuta Roma .
Yule mzungu aliekuwa amebakia baada ya kuona tukio lile na yeye alijitosa katika maji, huku akiwa amevalia miwani ambayo ilionesha kumsaidia kuona akiwa ndani ya maji kama anavyokuwa nje , na hapo ndipo aliposhuhudia jambo la kutisha kabisa kwani alishuhudia Roma akiwa amemzamisha mwenzake chini kabisa ya maji. Kina ambacho hata yeye mwenywe hakuwa na ujasiri wa kwenda , kwani walikuwa wamegusa eneo la sakafu kwenye mawe .
Mzungu yule alimuona Roma akimvunja shingo mwenzake na aliishia kutoa kilio .
“Noo ..Nancy “wakati amepanua mdogo kumuita mwenzake , Roma alipanda kama mshale au unaweza kusema kama zile roketi zinazoenda masafa ya juu na ni kitendo cha kufumba macho na kufumbua Roma alimfikia yule mzungu na kwakua mzungu yule hakuwa kwenye kujiandaa kutokana na kushuduhudia tukio la mwenzake kuvunjwa shingo. Alijikuta ameshikwa na yeye kwa staili ya Roba shingoni na kuzamishwa chini ya maji .
Upande wa huku nje mrembo ambaye alionekana kuwa jasiri licha ya kuona bunduki na majambazi yale ya kizungu ambayo yalikuwa yanamshambulia Roma alitokezea nje tena , lakinni awamu hii akiwa amekata tamaa kwani alikuwa amemkosa Roma chini , lakini ile anaangalia upande wa wale wazungu hakuona mtu kwenye ile boti na kushangaa Zaidi , wakati akiendela kushangaa , aliaona mtu akitokezea kama samaki ma kuvuta boti na kuketi huku akiwa anavuja maji mwilini
Yule mrembo alipanda kwenye boti huku akiwa ni mwenye kushangaa na akiendelea kutafuta wale wazungu wamepotelea wapi , lakini hakuwaona .
“Vipi mrembo , mbona unashangaa hivyo”Aliongea Roma kama kawaida yake utadhani hakukuwa na tukio lililokuwa limetokea
Yule mwanamke bado alionekana kuwa nah ofu , alikuwa akiangalia ili wawaone wale wazungu , lakini kwake ni kama walikuwa wamepotea na alikuwa haamini kama wale wazungu wamepotea maana ni ghafla sana.
“Unaitwa nani mrembo?”Aliuliza Roma na kumfanya yule mwanadada amwangalie Roma kwa mshangao.
“Naitwa Donyi”Aliongea mwanadada huyu na Roma akatabasamu.
“Sasa Donyi nadhani ni muda wa kutawaza mshindi na mwenye kupata zawadi yake apate”
CHANGIA KAZI HII KWA KULIPIA KUANZIA 2000 KUENDELEA NIKUUNGANISHE NA GRUPU UIFATILIE KWA VIPANDE VITATU KILA SIKU TUPO SEASON 2 KWENYE GRUPU
GRUPU NI KWA AJILI YA SIMULIZI HAKUNA KUCHAT
LIPIA NAMBA 0687151346 AIRTEL AU 0623367345 HALOPESA AU 0657195492 TIGOPESA JINA ISSAI SINGANO UKILIPA TUMA MESEJI YA MUAMALA NAMBA 0687151346 WATSAPP