SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE
Roma aliona ana bahati mbaya sana na Mage , kwani kila mara wanavyokuwa wanakutana inakuwa sio kwa heri bali ni kwa shari.
“Naomba ushuke kwenye gari haraka?”Alimrisha Afande Mage kwa hasira , huku baadhi ya watu waliokuwa karibu na hili eneo wakishangaa , na kilichokuwa kikiwashangaza kwanza kabisa ni gari aliokuwa akiendesha Roma, walikuwa wakijiuliza inakuwaje mtu anaendesha gari kama hii halafu anafanya makosa na kusimamishwa na polisi.
“Nipo na mgonjwa na siwezi kushuka mpaka nimfikishe hospitalini”Alizidi kumpanisha Mage hasira.
“Unajifanya mjuaji sio,Shuka kwenye gari”Aliongea tena na Roma alimwangalia Mage na kisha akafunga kioo jambo ambalo lilimkasirisha Zaidi Mage , wakati Mage akifikiria cha kufanya alishangaa Roma akitoa gari kwa spidi na kupelekea kumpushi Mage na kusogea pembeni.
Watu waliokuwa ndani ya hili eneo walishangilia kwa tukio hilo kitendo ambacho kilimuongezea Zaidi Mage hasira.
Mage alianza kuifukuzia gari ile kwa miguu kwa spidi na kufanya mpododo wake utingishike pwa pwaa.., lakini alikuwa amechelewa kwani gari ile ilikuwa ikipotelea kwenye macho yake , lakini hakukubali kushindwa , alikimbilia Pikipiki lake la kifahari na kisha kuanza kukimbiza ile gari , na kusahau kabisa kuwa alikuwa akiongoza magari wakati huo . watu waliokuwa pembeni walishangilia
“Sh**t huyu mpumbavu ama zake ama zangu leo lazima nimkamate”Aliongea Mage kwa hasira huku akifunga helmeti.
Pikipiki hii ilitoa mlio wa ajabu kiasi kwamba iliwafanya watu waliokuwepo stendi ya daladala hii eneo hili la misheni wapige mayowe ya shangwe , maana ni tukio ambalo hawakuwahi kulishuhudia na nikama walikuwa wakiangalia muvi ya kimarekani.
“Sema yule mwamba anaendesha ile ndinga ni mwehu na kakutana na kichaa mwenzake”Aliongea jamaa mmoja aliekuwa akiuza Samaki.
“Unadhani atamkamata?”
“Athu mimi sidhani kama ataweza kumkamata ila ngoja tuone, kama atakamatwa lazima tutajua tu”Aliongea bwana huyu huku wakiendelea na kazi zao.
Upande wa Roma alitumia dakika mbili na nusu tu na alikuwa akiingia ndani ya geti la mbele la hospitali hii ya Zakhiem , baada ya kuegesha gari hii alikimbilia nyuma na kufungua mlango na kumtoa Juma na kumkimbiza eneo la Mapokezi na haraka sana akapokewa na manesi hao na kuingizwa Wodini.
“Amefanya nini huyu?”Aliuliza Dockta lakini Roma hakuwa na majibu ya kueleweka na aliwataka watimtibu majeraha yake kwanza.
Madaktari hawa walishangazwa na alama zilizokuwa kwenye mwili wa Juma na kwa kuangalia tu waligundua kuwa mtu huyo alifanyiwa vitendo vya kikatili sana ila hawakutaka kulizungumza hili haraka , walichofanya ni kuanza kumuwekea Juma dripu ya maji wakichanganya na Dextrose ili kumuongezea nguvu , kwani alionekana kuwa mnyonge sana.
Baada ya Roma kuona ashakamilisha kumkabidhi Juma kwa madaktani , aliona atoke arudi kwanza kazini ili kukabidhi hela alizokuwa nazo kwenye gari maana zilikuwa nyingi sana na hakutaka kuendelea kukaa nazo.
Lakini ile Roma anatoka tu , aliwekwa chini ya ulinzi na afande wawili wa kiume pamoja na Mage.
“Upo chini ya Ulinzi kwa makosa mawili , la kwanza ni kuendesha gari bila ya pleti namba , kosa lako la pili ni kuidharau sheria ya nchi hii”Roma alimwangalia mrembo huyu huku akitabasamu na kisha akafungwa pingu.
“Afande Sepengo chukua funguo tukague gari yake , huenda ameficha madawa huyu”Aliongea Mage na Sepengo alifanya kama alivyoambiwa na alichukua funguo na kufungua milango wa ndinga hii,Sepengo baada ya kufungua mlango kwanza alianza kunusa nusa gari hii kama mbwa.
“Ma**mae hii gari inanukia vizuri hii , humu hata ufanyie uzinzi au dhambi yoyote malaika wanaweza wakakukingia kifua mbele ya Mungu”Aliwaza Sepengo na huyu Afande alikuwa akifanana na jina lake , kwanza alikuwa na meno yaliopishana ila ya njano , alikuwa ni kijana ila kutokana na uvutaji wa sigara anaonekana kuwa mzee.
Mage baada ya kuona Sepengo badala ya kukagua anashangaa uzuri wa gari aliona kazi hio aifanye mwenyewe , alilisogelea begi lililokuwa kwenye siti ya nyuma na kisha akalifungua na macho yalimtoka baada ya kuona maburungutu ya hela na Mage alitabasamu.
“Utakatishaji fedha kosa lingine”Mage aliwaza huku akitoa tabasamu la ushindi, lakini pia hakuishia hapo tu , aliendelea kufukunyua begi hilo , kwani kuna kitu kilimwambia kuna jambo la ziada atalipata na ni kweli ile anafungua kajizipu kadogo , alikumbana na kajimfuko ka unga unga kama wa chumvi.
Roma alijikuta akishangaa mara baada ya kumuona Mage akitoka na kajimfuko kaunga na hapo hapo alijikuta akinywea na kuona wale mabwege huenda walificha unga wao kwenye hilo begi na yeye hakulikagua vizuri.
“Nilijua tu wewe ni Jambazi ,Afande Marko huyu tunampeka moja kwa moja kituo kikubwa cha wilaya Temeke kule”Aliongea Mage na kisha akatoa simu yake ya upepo.
“Naripoti kutoka Mbagala Zakhem ,Jambazi kuu lipo chini ya ulinzi , Narudia jambazi kuu lipo chini ya ulinzi , tunahitahi usafiri haraka Ova”Aliongea Mage
“Kwa kulikamata hili Jambazi nadhani nitapongezwa sana na nitaweza kurudishwa kwenye kazi yangu ya upolisi,Mungu ni wa ajabu sana ,yaani huwa anajibu Maombi kwa namna ambavyo hata hutegemei”Aliwaza Mage huku akimwangalia Roma aliekuwa hana wasiwasi akiwa amegamia gari.
“Mrembo hio gari inakuja saa ngapi? , nina njaa sio poa”Aliongea Roma na kumfanya Mage amwangalie kwa hasira.
Lakini wakati wakiwa wamesimama hapo ndani , huku baadhi ya watu wakishangaa mara alikuja mwanamke na kumkimbilia Roma na kumkumbatia , ni kitendo ambacho hata Mage hakukiona kilivyofanyika, kwani Roma alikuwa amekumbatiwa na mwanamke mzuri mno.
“Najma … !,Unafanya nini hapa?”Aliongea Roma huku akimshangaa Najma aliekuwa amemkumbatia , kumbatio ambalo lilimfanya ahisi kitu cha tofauti katika mwili wake.
“Roma kaka .. kaka.. Jumaa kanitelekeza ..Roma.. hihiii hii….”Najma alikuwa akilia kama mtoto,alionekana ni mwenye huzuni kweli.
Unajua nini , Baada ya Juma kumfikisha Najma Hospitalini na yeye kuondoka siku mbili nyuma , baada ya vipimo kutoka Najma aligundulika kuwa na Malaria kali , kiasi kwamba ilibidi alazwe kwa ajili ya kupata dawa kali za Malaria .
Baada ya masaa nane ya dozi ya kwanza kuisha alipatwa na ahueni kiasi cha kumpelekea kuinuka na kukaa kitako ndani ya wodi hii ya wanawake ,muda nao ulizidi kusonga na Najma alijikuta akilala tena na kuja kushituliwa na Mama Debora ambaye alikuja kumtembelea , akiwa amebeba chakula na hakuwa peke yake alikuwa na mpangaji aliemleta hospitalini aliekua akifahamika kwa jina la Mama Bedo.
“Najma Juma alikuja? , nimejaribu kumpigia simu lakini hakuwa akipatikana”Aliongea Mama Bedo baada ya kupeana salamu za pole kwa mgonjwa na mama Debora.
“Mh! Hajaja , lakini labda atakuwa kazini kwake”.
“hata kama ndio azime mpaka simu jamani huku mdogo wake anaumwa , kukitokea shida nani wa kuambiwa sasa , halafu pia aliondoka kabla hata vipimo vyako havijatoka”Aliongea Mama Bedo huku akionekana kusikitishwa na matendo ya Juma.
Walijaribu kujipa sababu ambazo huenda Juma anazo ndio maana hakuwa ameonekana mpaka muda huo , kwa ajili ya kumuona lakini muda ulizidi kusonga Juma hakuonekana Mama Debora alienda nyumbani na kurudi tena kumletea Najma chakula lakini bado hakumuona .
“Hivi kweli kaka Juma anaweza kubanwa na kazi kiasi cha kutokuja kunitembelea mdogo wake jamani , mpaka muda huu?”Aliwaza Najma huku akiwa ni mwenye kusikitishwa na matendo ya kaka yake,Mwanadada huyu hakuwa akijua kuwa kaka yake alikuwa ametekwa na alichokuwa akijua ni kwamba kaka yake alikuwa akithamini mambo yake kuliko yeye na ndio maana alionekana ni mwenye kulalamika.
Siku ya kwanza ilipita . huku Najma akiendelea na matibabu na kuanza kupata nafuu , lakini bado mwanadada huyu hakuweza kumuona kaka yake , jambo ambalo lilizidi kumsononesha na kuona kaka yake hakuwa akimjali , aliumia sana moyoni licha ya Mama Debora kumwambia kuwa kaka yake hakurudi nyumbani kabisa kwa Najma bado aliona kaka yake alikuwa bize na kazi na wala hakukuwa na jambo ambalo lilikuwa likimuweka bize kiasi cha kutofika hospitalini kumtembelea.
Ile hali ya Najma kutokumuona kaka yake ilianza kuibua jina lingine katika akili yake na jina hilo halikuwa la mtu mwingine bali ni la mwanaume aliekuwa anampenda kwa mapenzi ya Dhati kabisa.
“Roma ndio mtu pekee anaenijali,amekuja kuniokoa bila ya woga wowote lakini kaka yangu kuja tu kunisalimia ameshindwa , sasa ndio najua nani ananijali kati ya kaka yangu na Roma”Aliwaza Najma huku akisahau miaka yote iliopita nyuma walivyoishi na kaka yake na alichokuwa akiwaza muda huo ni kwamba Roma ndie anaemjali na kaka yake hakuwa akimjali.
“Lakini Roma hafananii na nilivyokuwa nikimfahamu ,lakini hapana yote yale yalitokea kwasababu yangu , ananipenda sana na ndio maana alionekana kuuwa , ni hasira tu zile ,Roma sio muuaji ,Roma sio Mkatili yote ameyafanya kutokana na hasira , atakuwa ananipenda sana”Hayo ndio mawazo aliokuwa nayo Najma siku ya pili yake baada ya kulazwa muda wa asubuhi.
Yale mapenzi ambayo alidhania yalipotea katika moyo wake baada ya kumshuhudia Roma akiwa kikatili , yalirudi upya tena awamu hii yalionekana kuwa na nguvu kubwa sana , kiasi kwamba mwanadada huyu alitamani kumuona tena Roma , alikuwa ni mwenye wasiwasi sana , kwani alikuwa akikumbuka mara ya mwisho Roma alimuacha kituo cha polisi
“Sijui alitoka jamani ?”Roho ya Najma haikutulia tena , alikuwa na mawazo mchanganyiko mazuri na mbaya kwa wakti mmoja , lakini mawazo yaliokuwa na nguvu kwa wakati huo ni yaliokuwa mazuri juu ya Roma , alitamani sana kujua ni hali gani anayo Roma , wakati akiendelea kuwaza alikumbuka simu yake , lakini baada ya kukumbuka hakuwa akifahamu ni mahali gani ameicha baada ya kutekwa na wale watekaji alizidi kusononeka.
“Binti hali yako sasa imetengemaa na dozi yako ya kwanza imekamilika na kwa sasa utatumia dawa za kumeza , hivyo haina haja ya kubakia hapa hospitalini , utaendelea nazo ukiwa nyumbanni , lakini kama ukijisikia hali yoyote mbaya unaweza kurudi”Aliongea Daktari wa raundi ya asubuhi na kumfanya Najma apatwe na furaha kwani alikuwa amechoka kukaa ndani ya hii wodi kwani harufu yake haiukuwa ikimfurahisha hata kidogo.
Baada ya Najma kupewa taarifa hio , hakuwa na haraka ya kuondoka lakini pia hakuwa amelipia gharama za matibabu mpaka wakati huo na hakuwa na hela ya kutosha , baada ya kukaa kwa takribani lisaa akiwa na mawazo ya Roma pamoja na namna ya kumaliza matibabu hatimae alikuja Mama Bedo.
“Mama Bedo nisharuhusiwa tayari , bado kulipia gharama tu za matibabu nirudi nyumbani , lakini hela niliokuwa nayo haitoshi na kaka Juma haonekani mpaka leo hii”Aliongea Najma na mama Bedo alimhurumia lakini pia alimlaani Juma kwa kutoonekana ,alimwangalia.
Mwanadada huyu mrembo , mwenye haiba ya utoto alionekana kuwaza jambo na ghafla wazo lilimuingia kwenye kichwa chake.
“Mama Bedo umekuja na simu?”
“Ndio hii hapa Najma , tena ina salio , unataka kumpigia nani?”
“Rafiki yangu mmoja hivi” Aliongea huku akichukua simu kwenye mikono ya mama Bedo kwa ajili ya kupiga.
“Hellow! “Sauti nyororo ilisikika upande wa pili.
“Twin ni mimi Najma”.
“Haan..jamani shosti mbona unapenda kunipa wasiwasi namna hio , nimekutafuta siku mbili zote sikupati hewani”.
“Ni stori ndefu pacha na ndio maana nakupigia na simu nyingine , nipo hospitalini nimelazwa unaweza kuja kuniona sasa hivi , nina shida mpenzi”.
“Naja.. Shida nini nisubiri Najna muda si mrefu nisubiri..”Ilisikika sauti upande wa pili ilionekana kuwa na wasiwasi.
Najma alivuta pumzi mara baada ya kufanya mawasiliano hayo na kurudisha simu kwa Mama Bedo.
Ni ndani ya masaa mawili waliokuwa wamesubiri mara alionekana mwanamke mrembo sana akiingia ndani ya hospitali hii na gari zuri sana aina ya BMW M4 ya pink na kufanya watu wamkodolee macho , kwani alikuwa mrembo haswa , na wanaume waliokuw a ndani ya eneo hili waliambizana.
“Sema mzee kuna wanaume wanakojolea pazuri aisee , yaani hii pisi ikinipa raundi moja tu Maisha yangu yatakuwa ya baraka sana”.
“Acha kuwaza sana Shaba , hivyo ni vya wakubwa , usione pisi kama hio inaendesha gari kali na inapendeza jua kuna mwamba nyuma anafanya kazi kwa juhudi , Waswahili wanakuambia usione vya elea jua vimeundwa”.
“Ni kweli tupige kazi tu”Hawa walikuwa ni wafanyakazi wa usafi ndani ya hospitali hii na muda wote walikuwa wakiangalia pisi hio ikipotelea mapokezi na mabwana hawa waliokuwa wamevalia glovusi na Mabuti makubwa , waliendelea na kazi yao ya kukusanya takataka.
Ndani ya wodi ya wanawake aliingia mrembo huyu huku akitembea kwa madaha kabisa na kusababisha harufu yake ya perfume kali ya bei ya juu isambae ndani ya eneo hili , mwanadada huyu alitembea na baada ya kumuona mtu anaemtafuta alikimbia na kwenda kumkumbatia huku akianza kulia na waliambizana kulia hawa warembo wote.
Naam mrembo huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni Nasra Mhasibu mkuu wa makampuni ya Vexto na inaonekana mwanadada huyu alivyomuacha Roma Mtongani hakuwa akija kuonana na mteja bali alikuwa akija kuonana na Najma.
Wagonjwa wlaiokuwa wamelazwa ndani ya hii wodi walishangazwa na mapenzi yaliokuwepo baina ya wadada hawa warembo , kitendo chao cha kulia hapa hospitalini kilimfanya Mama Bedo na baadhi ya wagonjwa kuguswa na tukio hilo kiasi cha kuwafanya watokwe na machozi.
“Nisamehe sana Najma , nisamehe mpenzi , sikujua ulikuwa unaumwa hivi”Aliongea Nasra huku akionekana alikuwa ni mwenye huzuni mno na kuumizwa na kuumwa kwa Rafiki yake
Wawili hawa walionekana kufahamiana sana sana na ilionekana sio kufahamiana kwa siku chache , bali urafiki wao ulionekana ni wa muda.
Baada ya wawili hawa kubembelezana hatimae Najma alianza kumwambia yaliokuwa yamemtokea mpaka kupoteza simu.
“Kwa hio unamaanisha The chosen one ndio alikuja kukuokoa?”Aliuliza Nasra huku akimtaja Roma kama The Chosen one yaani kwa tafsri ya ‘Aliechaguliwa’ na Najma alitingisha kichwa.
“How Romantic ….jamanii natamani na mimi initokee Twin”
“Wee ,, muangalie unavyofikiria ujinga sasa , nilikuwa nikiogopa balaa”.
“Hapo ndio penye point sasa Naj.. yaani unatekwa unaogopa mpaka unataka kujikojolea halafu pale unapojiona umekata tamaa , mara vuup .. bebi huyo anatoa kichapo then anakuokoa kwenye mikono ya watekaji .. how Romantic.. haha .,Najma nikwambie tu hakuna mwanamke ambaye hapendi hio Fantansy .. you know I cant picture how things was ..but I know for sure it was real amaizing scene .. I wish someday jambo kama hilo linitokee Naj… Your love Experience is far more exciting Twin, you should be happy”Mwanadada huyu mrembo alionekana kufurahishwa san ana tukio hilo na alisahau kabisa uhatari ambao ungemkuta Najma kama tu Roma asingetokea kumuokoa ,Nasra aliegemea upande wa mazuri yaliomtokea Najma,
Maneno ya Nasra kwa Najma ni kama yalilipua bomu la huba ndani ya moyo wa Najma , mwanadada huyu alijona kama mjinga kwa wakati mmoja , siku zote alikuwa ni mwenye kujifunza kutoka kwa Rafiki yake huyu , alichojilaumu ni pale kuegemea upande wa mambo ya kutisha yaliotokea katika tukio lile na kuacha yale mambo mazuri maana ni kweli Roma alihatarisha Maisha yake kwake.
“Twinie .. I have always been one to tell you to focus only to good thing that happn around you .. I know you were frightened at the moment but the Ending was good .. ungewezaje kujua ni kiasi gani The Chosen anakupenda ,, hii yote ni mipango ya Mungu Naj.. be happy” Maneno aliokuwa anaongea mwanadada huyu yalionekana kumuingia vizuri na alijikuta akianza kumuwaza Roma tena na kuona ule uuaji wa Roma ni Swaga na sasa zilikuwa zinausuuza moyo wake.
Wawili hawa walipiga stori za hapa na pale , mpaka pale Nasra alivyopigiwa simu kurudi kazini haraka kuna dharula inayomuhitaji na kwakuwa alimuona Najma alikuwa amepona , wasiwasi wake ulipungua , alilipia gharama zote na kisha akaaga huku akimwambia asiwe na wasiwasi kaka yake anamjali na asimfikirie vibaya .
“Kila siku ninapopata shida inayosumbua akili yangu , nikionana na Nasra huwa Napata kitu kipya na wasiwasi wote kuisha ,Nasra kabarikiwa kweli kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuingoza akili yake , tokea utoto wetu nilipokutana na Nasra nimekuwa mtu wa furaha sana kuwa na Rafiki kama yeye” Aliwaza mwanadada huyu mrembo sana ambaye hajawahi kuwa na mpenzi kwenye Maisha yake Zaidi ya kuwa na Roma ambaye alikuwa akimzingua .
Najma hakuwa amemueleza Rafiki yake kama Roma alikuwa ameoa na ana mwanamke ambaye alikuw aamepotezana nae kwa miaka mingi nyuma , lakini mwanadada huyu licha ya Roma kuwa na mwanamke mwingine lakini bado hakuwa ni mwenye kuacha kumpenda Roma , alimfikiria kila siku na aliamini kabisa Mungu wake hakufanya makosa kumkutanisha na Roma na kwamba siku moja atakuja kuishi na Roma kama mke na mume.
“Mpaka sassa nimejua ni kiasi gani Roma ananipenda , na nitaishi kwa kumpenda Maisha yangu yote na nitamlindia heshima na nafasi yake ndani ya moyo wangu”
Aliwaza huyu mwanamke mrembo wakati akitoka mapokezi kwa ajili ya kuelekea nyumbani kwani walikuwa washakamilisha taratibu zote , lakini ndipo moyo wa Najma ulipopiga kwa nguvu mara baada ya kumuona mwanaume wa Maisha yake na hakutaka kujiuliza mara mibili aliona yes , hii ndio Chance na lazima aitumie vizuri , hakujali Pingu alizokuwa nazo Roma , alichojali ni kile kilichomjaa moyoni mwake .
Na kama muvi la kuchi kuchi hotae hee , mrembo huyu kwa spidi maridhawa kabisa , alikimbia , akakimbia na kwenda kutua kwa mwanaume , mwambaaa Roma Ramoni .
Je unadhani ndoto za mwanamke huyu zitatimia … Endelea kula mtori nyama zipo chini.
SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO.
Mage kwanza kabisa alishangazwa na urembo wa Najma kiasi kwamba alijiulizaje huyu Jambazi akapata pisi kama hio kwenye Maisha yake , lakini hakukuwa na majibu sahihi yaliopatikanan katika halmashari ya kichwa chake.
“Najma usilie tena .. kaka yako alipatwa na matatizo na kwasasa yupo kalazwa anapatiwa matibabu , mimi naenda na hawa polisi kuna jambo la kuweka sawa , hakikisha kaka yako anapatiwa matibabu sawa?”Aliongea Roma kama mwanaume na mwanadada huyu aliekuwa ametokewa na machozi kutingisha kichwa kwa kukubaliana nae , lakini licha ya kumuuelewa alionekana hakuwa tayari kumuachia Roma.
“Eti kuna jambo la kuweka sawa .. yaani huna aibu unamuongopea mwanamke mrembo kama huuyu hahaha.. wewe mwambie unaenda jela na atafute bwana mwingine”aliongea Mage kwa kebehi na kumfanya Nama amwangalie mwanadada huyo kwa hasira.
“Wewe dada wa kitrafiki , mimi namjua Roma sio Jambazi na hayo maneno yote unayoongea hayakai kwenye Maisha ya Roma”Aliongea Najma na kumfanya Roma amwangalie mwanamke huyu na kutabasamu.
“Hilo litajulikana mrembo eh na Ushahidi tulionao , hakuna mengi ya kuzungumza na nitahakikisha hili Jambazi halirudi mtaani kuwarubuni Watoto wakike kama wewe , Mrembo wewe ni mhanga huyu jamaa kakubuhu hivyo shukuru ninamtoa kwenye Maisha yako , nakwambia utanishukuru baadae”
Aliongea Mage na baada ya kumaliza tu Difenda ya polisi iliingia hapo ndani na Mage aliwaamrisha polisi wengine waendeshe gari ya Roma na Mage akapanda kwenye pikipiki yake huku wakimwacha Najma anaetokwa na machozi.
“Najma nitarudi baadae sawa , usiwe na wasiwasi . hakikisha kaka yako anapatiwa matibabu”aliongea Roma na kufanya watu waliokuwa eneo hili la hospitali washangazwe na Roma maana maneno yake yalikuwa na nguvu sana kwenye mioyo ya watu hawa.
Ni baada ya lisaa limoja tokea Roma aingizwe ndani ya kituo kikubwa cha polisi wilaya ya Temeke alionekana mwanamke mmoa mrembo sana maarufu sana hapa nchini akiingia akiwa ameshikilia mkoba wake , huyu mwanadada alikuwa mrembo sio kawaida , ila licha ya urembo wake wote hakuwa akimfikia mrembo Edna.
Mwanadada huyu hakuwa mwingine bali alifahamika kwa jina la Nadia Alfonso , lakini nchini na duniani wengi walikuwa wakimuita kwa jina la ‘Goddes of law’ umaarufu wa jina hili mwanamke huyu hakupewa tu , ila yote hayo ni kutokana na heshima aliojijengea katika ulingo wa kutafsiri sheria, usomi wa mwanadada huyu pamoja na kipaji chake kilichangia pakubwa heshima aliokuwa nayo .
Nsdia Alfonso ni mwanasheria aliemaliza masomo yake ndani ya chou kikuu cha Harvard kuanzia digrii yake ya kwanza mpaka ngazi ya juu yabisa ya PhD , unaweza ukajiuliza inakuwaje mwanamke mdogo kama huyu kuwa na mafanikio makubwa kama hayo , lakini yote hayo ni kutokana na juhudi binafsi za mwanadada huyu tokea alipkuwa mdogo , lakini pia ukijumlisha na uwezo mkubwa wa akili Mungu aliombariki nao.
Umaarufu wake unakuja mara baada ya kusimamia kesi ya Raisi mstaafu wa Korea kusini , kesi ambayo ilikuwa ni gumzo sana duniani , kesi ambayo ilikuwa ikimtuhumu raisi huyo kwa ufisadi , lakini kwa uwezo mkubwa wa Nadia raisi huyo alipata haki yake na Dunia ikatambua kuwa raisi huyo sio kama walivyomdhania kwani alisafisha jina lake , lakini kufanikiwa huko kunazua gumzo baada ya Raisi huyo kutoa hotuba ya shukrani mbele ya waandishi wa habari na kumshukuru Nadia Alfonso kama mwanasheria mkuu alisimama kidete katika kufanikisha kwake kupata haki yake kisheria , lakini pia kusafishika kwa kile alichokiita kusingiziwa kesi ya ufisadi , kwanzia siku hio ndipo jina la Nadia liliposambaa duniani ,umahiri wake uliotukuka aliounesha katika kesi hio , kwanzia kukusanya Ushahidi ulimpa heshima kubwa sana., umaarufu ulimfanya mwanadada huyu kutafutwa na watu wengi maarufu duniani kwa ajili ya kusimamia kesi zao hayo ni machache kuhusu Nadia A.k.a Goddes of Law.
Polisi waliokuwa wakimjua mwanadada huyu ambaye alikuwa akipewa heshima kubwa na Taifa kwakuwa mtanzania wa kwanza kung`ara katika fani ya sheria , walihaha , walikuwa wakijiuliza imekuwaje mwanasheria huyu akaja kwenye kituo chao , na si hao tu , hata Mage aliekuwa yupo kituoni hapo kuhakikisha Roma hachomoki alishangazwa sana.
Kwanza kabisa Nadia kwake alikuwa ni Role Model , kwani katika Maisha yake Mage alikuwa akipenda sana sheria na alipigania sana ndoto yake hio kuja kuwa mwanasheria huku nguvu kubwa ya kimsukumo ikitoka kwa Nadia ambaye watu wengi katika sheria walimuita ‘Chain Breaker’ yaani mkata minyororo au kwa tafsiri ya haraka haraka yaa maana hi ni kwamba mtu ambaye ameshinda vizuizi vyote yeye kama mwanamke na kuudhihirishia ulimwengu kama mshindi , sasa wewe jaribu kuwaza mtu ambaye ulimhudusu kwenye Maisha yako yote akatokea mbele yako ghafla tu , basi hio ndio namna ambavyo Mage alishituka na hakuwa akiamini kwamba mtu aliekuwa mbele yake alikuwa ni ‘Goddes of law’ mwanamke aliekuwa akimpenda na kumpenda Zaidi ya neno lenyewe.
Mage machozi yalianza kumtoka , alikumbuka miaka kadhaa nyuma alivyokuwa akipambania kusoma sheria , lakini kutokanana na kile alichokiita mweyewe uwezo wake mdogo kiakili alikuwa akifeli kila mara na kumpelekea kukata tamaa na kuachana na sheria na kujiunga na jeshi la polisi huku akiamini kwamba polisi na wanasheria wanafanana kwa vitu vingi ,aliamini licha ya kufeli kuwa mwanasheria kuwa polisi sio mbali sana na ndoto zake.
Mkuu wa kituo cha polisi ndio wa kwanza kutoka kwa ajili ya kuonana na Nadia ili kumpa heshima zote kubwa , kwani mwanadada huyo hakuwa mdogo kabisa ndani ya taifa hili, lakini licha ya hivyo polisi wengine wote walijipanga mstari kwa ajili ya kutoa heshima kwa Goddes of law.
“Karibu sana mheshimiwa ,, Ini furaha kwangu kufamiana na mrembo kama wewe na mtu mkubwa sana duniani karibu kituoni kwetu”.
“Asante sana , lakini sijaja hapa kimatembezi nipo hapa kama mwanasheria na nina mteja wangu hapa”Aliongea Nadia kwa sauti yake tamu na kuwafanya polisi wote washangae , anachozungumza Nadia , kwanza hapo polisi hakukuwa na mtuhumiwa mwenye hadhi ya juu kama anavyoongea mwanadada huyu , kwani hakuwa na taarifa ya mtu wa hadhi alieshikiliwa na kituo chake Zaidi ya vikapuku tu waliowafunga.
“Mheshimiwa Labda umekosea , hapa hatuna mtu tuliemshikilia ambaye ni wa hadhi kuhudumiwa na wewe kisheria”
“Kwangu kila mtu anaehitaji sheria anapaswa kuhudumiwa na mimi na sijawahi kubagua watu kutokana na nafasi zao katika jamii”Baada ya kuongea hivyo alimpita mkuu huyu wa kituo .
“Pumbavu nimeongea ujinga”Aliwaza mkuu huyu wakituo huku akifatisha nyuma na waliingia kwenye ofisi ya kuonana na wageni.
“Nipo hapa kwa ajili ya mteja wangu anaefahamika kwa jina la Roma Ramoni”Aliongea na kumfanya Mheshimiwa ashituke na kujiuliza Roma ni nani mpaka mtu mkubwa duniani kama huyu aje kumtoa.
“Mheshimiwa mtu unayemzungumzia ni jambazi ambalo tulikuwa tukilitafuta kwa muda mrefu sana na leo tumemkamata hatuwezi kumuachia kirahisi” Aliongea Mkuu wa kituo na hakuwa tayari kumuachia Roma kizembe hivyo , kwani alishuhudia yale maburungutu ya pesa na alikuwa ashayapigia plani kabisa wa kulipa deni ambalo alikuwa akidaiwa na anaemdai kumkalia kooni , lakini pia alikuwa akipanga kulipa kodi ya nyumba anayoishi maana hakuwa akiishi kwenye nyumba za polisi maaruufu kama kota , lakini pia alikuwa akisumbuliwa na mchepuko wake juu ya hela ya mtaji na alikuwa amenyimwa kitumbua na mchepuko huyo kwa muda wa mwezi mmoja , pia mke wake alikuwa akidaiwa vikoba sasa kwa matatizo hayo yote aliona kwa pesa hizo zilizofika kwenye ofisi yake , aliona ni Mungu ndio kaleta fursa , sasa hakuwa mzembe kiasi hicho licha ya kwamba mtu aliekuwa mbele yake alikuwa mkubwa tu katika sheria, tamaa ya pesa ikisukumwa na matatizo aliokuwa nayo aliona asimamie msimambo wake
“Nishatangulia kusema sipo hapa kaa mtu maarufu , ila nimekuja kwa ajili ya mteja wangu na nina Ushahidi wa kutosha ambao unamfanya mteja wangu kutokuwa na makosa”
Aliongea mwanadada huyu kwa upole na kujiamnini kisha akatoa Ushahidi wake na kwa namna ambavyo mwanadada huyu alielezea na kuoonyesha uhahidi Mkuu wa kituo alijisemea moyoni yes hapa kakutana na profesheno mwenyewe.
“Naomba kwanza kuonana na mteja wangu”Aliongea Nadia na mkuu wa kituo hakuwa na sababu ya kumzuia .
Huku upande wa nje Mage alikuwa kwenye mshangao mara baada ya kusikia kuwa Mrembo Nadia amekuja kwa ajili ya Roma , alishangaa sana sana , inakuwaje choko kama Roma kuja kupata huduma ya kisheria kutoka kwa mwanasheria nguli duniani na hapo hapo swali la Roma ni nani lilianza kuibuka kwenye kichwa chake.
“Pluto!” Aliita Nadia na kumfanya Roma anyanyuie uso wake na kuangalia sauti tamu inayomwita kwa jina ambalo hajalisikia muda mrefu.
“Haha.. Nadia unafanya nini hapa?”Roma alishangaa sana na alionekana alikuwa akimfahamu vyema Nadia na mrembo huyu aliachia tabasamu ambalo ungekuwa mwanaume rijali kama Roma ungekuwa hoi.
“Za siku nyingi The Great Pluto nimefurahi sana kukuona tena , hujui tu nilivyokuwa nikitamani kupata nafasi ya sisi kuonana tena tokea tulivyo achana nchini Korea Kusini”
“Nadia hayo mambo tuache kuyaongelea sasa hivi , nataka uniambie unafanya nini hapa”Aliongea Roma kwa usiriasi na mwanadada huyu alimwangalia na kuonekana kama hajafurahia , kwani alitamani kumuona Roma akiwa kwenye mshangao na furaha ya wao kukutana tena baada ya miaka mingi.
“Nipo hapa kama mwanasheria mpya wa kampuni unayofanyia kazi, na nipo kukutoa”Aliongea mwanadada huyu na kumfanya Roma ashangae.
“Okey! Basi fanya hima nitoke hapa maana nina njaa sio poa”Aliongea Roma huku akijigusa tumbo , yaani kwa Roma alionekana hakuwa akimchukulia kabisa Nadia kama mtu mkubwa vile tofauti na wengi walivyokuwa wakimchukulia , kwani Nadia alikuwa akipewa heshima ya jiuu mpaka na maraisi wa Afrika , lakini kwa Roma alimuona Nadia kama wa kawaida.
“Tayari mpaka sasa upo huru”Aliongea Nadia na mlango ulifunguliwa na akaingia mkuu wa kituo akiwa ni mwenye kutoa jasho jingi usoni.
“Mheshimiwa mteja wako yupo huru”Aliongea mkuu huyu huku akionekana ni mwenye kuhema , sijui nini kimemtokea maana ujasiri aliokuwa nao umeisha wote.
“Daah ! Afadhali maana sio kwa njaa hii ,Nadia uko vizuri sana kwenye kazi yako”Aliongea Roma huku akiamka wa kwanza na kutangulia mlangoni akimuacha Nadia aliekuwa akimwangalia mwanaume huyo kwa hali ya hudhuni inaonekana alitarajia kitu kikubwa Zaidi kutoka kwa Roma.
“Niletewe begi langu lenye pesa niondoke nina njaa ”Aliongea Roma huku akimwangalia Mage aliekuwa akimwangalia bwana huyu pasipo kummaliza na alionekana ni mwenye maswali mengi sana katika kichwa chake.
“Boss begi lako hili hapa”Aliongea Afande mmoja kwa heshima na kumpatia Roma begi lake na Roma alilibeba lakini akasita.
“Huu uzito ni tofauti , kuna kiasi cha pesa kimepungua”Aliongea Roma na kuwafanya mapolisi hawa wote waangaliane kama kondoo.
“Rudisheni pesa zote zilizokuwa humu ndani , najua kiasi kamili cha hizi pesa , mkigoma nitakaa hapa nakuhesabu zote na hakuna mtu kuondoka nikihakikisha hela ni pungufu nitawasachi wote”
“Rudisheni pesa , acheni kuvunja sheria la sivyo swala hili sitoliacha lipite hivi hivi”Aliongea Nadia baada ya kumuona Roma anaongea na Polisi wote walitoa jasho akiwemo mkuu wa kituo.
“Huyu jamaa mahela yote hayo kajuaje nimepunguza vibunda viwili”Aliwaza mkuu wa kituo huku akikumbuka vibunda alivyoficha ofisini kwake,wakati akiendelea kutoa jasho simu yake iliingia ujumbe na kufungua na kuangalia meseji ilitoka kwa jina la ‘Mke Wangu’
“BABA LEAH MWENYE NYUMBA ANAKUSUBIRI NA ANASEMA HAONDOKI MPAKA UTOE PESA YAKE , HALAFU GESI IMEISHA MPAKA SASA HATUJUI TUNAPIKA NA NINI” ilikuwa ni meseji kutoka kwa mke wake iliandikwa kwa herufi kubwa kabisa kuonesha msisitizo , mzee huyu jasho lilizidi .
“Hapana sitoi zile pesa nitakuwa mjinga wa karne” Uasiri uliongezeka.
“Narudia nataka pesa zangu zote ili niondoke”Aliongea Roma akianza kuwangalia polisi mmoja mmoja na baada ya macho yake kutua kwa mkuu wa kituo , aliona jambo na kumsogelea.
“Nataka pesa zangu” Aliongea Roma huku akiwa amemkaribia mkuu wa kituo karibu kabisa.
“Sijachukua pesa mimi , siwezi kuiba , mimi ni mkuu wa kituo na nachukia wezi” Aliongea kwa kujiamini na muda huo huo Simu yake iliingia ujumbe mwingine na aliinua simu yake na kuangalia ujumbe huo ulitoka kwa jina la “Fundi cherehani’
“ WEWE MWANAUME VIPI MBONA HUTUMI HIO HELA , AU ULIKUWA UNAJIGAMBA BURE UMEPATA PESA NYINGI LEO , KAMA HUNA HELA USEME UACHE KUNISUMBUA MIMI KUNA WANAUME WENZIO WANAWEZA KUNIHUDUMIA , NITUMIE HIO HELA NIKANUNUE WIGI”
Baada ya mkuu huyu wa kituo kuona meseji hio alikunja ngumi na kusema liwalo na liwe pesa sitoi.
Roma baada ya kuona mkuu wa kituo anakataa , alimsukuma na kisha alimpita na kuingia kwenye ofisi yake , baada ya kuingia tu , alivuta mtoto wa Meza na kuibuka na mabuda mawili ya pesa na kutoka.
“Mimi siibiwi kizembe ohoo..”Aliongea huku mkuu wa kituo akimtukana moyoni na kuona mkeka umechanika.
“Hawa ndio majambazi ambao unatakiwa kuwakamata kama unajali sana sheria , sio raia wema kama sisi mrembo eh” Aliongea Roma wakati akiwa amemsogelea Mage karibu kabisa na Mage hakuwa na la kuongea kwani wakati huo alionekana kuwa kwenye mawazo mengi sana kwa wakati mmoja.
Roma baada ya kutoka alifanya mawasiliano na Nasr ana kumuuliza yuko wapi na mwanadada huyo alimjibu bado yupo ofisni , Roma alishangaa kwani muda ulikuwa umeenda sana , lakini alijua huenda mwanadada huyo kabanwa na majukumu mengi Zaidi.
Ndani ya masaa machache Roma alikuwa ashafika ndani ya kampuni , haikueleweka waliachana vipi na mrembo Nadia ila Roma alikuwa ni aina flani ya wanaume ambao hawakujali sana baadhi ya mambo na ilionekana anahistoria kubwa san ana mwanadada huyo.
******
MASAA MACHACHE NYUMA
Kitendo cha Roma kufanikisha kazi ya kurudisha feza kutoka PANZ Security kilimfurahisha sana Edna, na kwa mara ya kwanza alijihisi kweli ana mume.
“Nitampikia chakula leo ,ananidharau sana sijui kupika ananiona sistahili kuwa mke ”Aliwaza mrembo huyu wakati akiwa ndani ya ofisi yake
“Bosi Miss Nadia amefika?” ilikuwa ni sauti ya Monica akitoa taarifa kwa bosi wake.
“Okey mruhusu aingie”
“Wow! You are beutifull Edna as the rumors”
“Asante sana Nadia , na wewe pia umrembo”
Wawili hawa walikaribishana na kuanza mazungumzo ya kibiashara.
“Nimekubali ombi la kuwa mwanasheria wa Kampuni yako”Edna alishangaa maana haikuwa kazi rahisi kumfanya mwanasheria mkubwa duniani kuwa mwanasheria wa kampuni change kama Vexto maana Nadia alikuwa akifanya kazi na makampuni makubwa kama Sumsung
“Nashukuru sana Nadia kwa kuchagua kufanya kazi na kampuni yangu na niseme tu nitahakikisha unafurahia kufanya kazi na sisi”.
Nadia alitabasamu huku akihusudu urembo aliokuwa nao Edna , alikiri kuwa hakuwa akiingia kwa urembo wa mwanadada huyo hata kidogo.
Basi wawili hawa walikutana kwa ajili ya kusaini mkataba wa Nadia kusimamia kampuni ya Edna kisheria yaani VExto.
Wakati wakiagana mara simu ya CEO Edna iliita na alipoangalia jina aliona ni ‘Mbakaji’ na bahati mbaya ni kwamba simu ilikuwa mezani hivyo Nadia aliona jia hilo na kujiuta akishangaa.
“Hello!”
“Bebi nimekamatwa tena na polisi”Ilikuwa ni sauti ya Roma na Edna alishangaa.
“Ilikuwaje “
“Nina kesi ya utakatishaji fedha , nimedharau sharia za nchi”Aliongea Roma na Edna hakuongea chochote .
“Bebi mbona huongei , usiniambie mapenzi siku hizi yamepungua kiasi cha kutaka mumeo nikae jela”Edna alimwangalia Nadia.
“Natuma mwanasheria aje kukutoa” Baada ya kukata simu Edna alivuta pumzi.
“Nitaenda mimi” Aliongea mwanadada Nadia. Nadna alishangaa
“Lakini..”
“Usiwe na wasiwasi , najua unachofikiria lakini nitaenda mimi iweke kama kazi yangu ya kwanza kwa kampuni”Baada ya kuongea maneno hayo Nadia alichukua mkoba wake na kushuka hadi kwenye maegesho ya gari na kuingia .
“Evans nipe taarifa?” Aliongea mwanadada huyu na kupewa taarifa na mtu anaefahamika kwa jina la Evans.
“Okey ! nikusanyie ushahidi wote na tukutane”
“Sawa madam” ilisikika sauti upande wa pili wa simu .
Baada ya smu hio kukatwa mwanadada huyu alifatufa jina lingine na kupiga .
“ Ndio boss nishasaini mkataba, anaonekana kufurahia sana kwa mimi kufanya kazi ndani ya kamupini”
“Hongera sana Nadia ni mwanzo mzuri nadhani ni wakati sasa wa kuendelea mipango yetu” ilisikika sauti nyingine kwenye simu , sauti nzito.
TUKO SEHEMU YA 36 KWA GRUPU .. ENDELEA KUTOA SAPOTI YAKO KWA KUCHANGIA KIASI KIDOGO TU CHA SHILINGI 2000 TUKUUNGE GRUPU AU TUKUTUMIE INBOX WATSAPP SIMULIZI HII KILA SIKU VIPANDE VITATU FULL DOZI.
LIPIA NAMBA 0687151346 AIRTEL AU 0623367345 HALOPESA AU 0657192492 TIGO JINA ISSAI SINGANO , UKISHALIPA NICHEKI TU WATSAPP NA MESEJI YA MUAMALA AU JINA LA WAKALA , HAINA HAJA YA KUPIGA SIMU WATSAPP NIPO ONLINE MASA YOTE MPAKA SAA SITA USIKU TUNAKUJIBU
WITO WA HII SIMULIZI NI ;ENDELEA KULA MTORI NYAMA ZIPO CHINI.