Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 461.

Profesa Clark wakati Roma anafika aliteleza na kugonga kwenye kabati lakuhifadhia vitabu pamoja na vifaa vya kufanyia majaribio.

Roma baada ya kuingia ndani alishangaa kumkuta chini na vitabu vikiwa vimesambaa , ilionyesha alikuwa akisoma baadhi ya tafiti ambazo ziliachwa na Profesa Shelukindo.

Profesa Clark alikuwa amevalia miwani ndogo ya kusomea pamoja na gauni la kulalia , mwonekano wake na namna nywele zilivochanguka na kumfunika uso Roma alijikuta akiishia kucheka tu.

“Acha kucheka bwana nisaidie kuokota vitabu”Aliongea kwa kulalamika huku akijinyanyua kivivu

“Imekuwaje mpaka ukadondoka sehemu kama hii?”

“Nilikuona wakati ukiingia na nilitaka kukimbilia kukusalimia lakini nilijikuta nikiteleza nilishikilia hilo kabati kama sapoti lakini lilionekana liliegeshwa tu na nimedondoka nalo”Aliongea na kumfanya Roma akohoe kwa namna ya kuigiza na kisha aliinamanna kulibeba na akaanza kupangilia vitabu vilivyokuwepo chini.

Baada ya kumaliza aliokota Headphone iliokuwa na mwonekano wa kipekee .

“Hizi ni Headphone za aina gani?”

“Ni Headphone ambazo zinatumia teknolojia mpya nilioigundua , jaribu kuvaa uone”Aliongea na Roma akafanya hivyo..

“Nini kinafuata baada ya hapa?”Aliuliza Roma maana hazikuwa zikitoamziki wowote.

Profesa Clark alifikiria kidogo na kisha alibadili lugha na kuanza kuongea kwa Lugha ya kiebrania.

“Hizo ni Headphone ambazo zinatumia teknolojia ya kipekee kutafsiri sauti”Aliongea na Roma aliweza kushangazwa na kubadili lugha lakini palepale alielewa alichokuwa akijaribbu kufanya kwani sauti ilitoka kwenye zile Headphone kwa lugha ya kiswahili.

“Is it real time translation divices?”Aliuliza Romakwamba je ni kifaa cha kutafsiri sauti

“Upo sahihi ni Headphone ambayo inatumia Artificial intelligence kutafsiri lugha ya maongezi ya wakati husika, ina uwezo wa kutafsiri lugha zaidi ya mia moja hivyo kurahisisha baadhi ya mazungumzo, ni mbadala wa wakalimani katika lugha, Vipi unaonaje?”Aliuliza na Roma alitingisha kichwa kukubali , hata hivyo alijua kulikuwepo na vifaa vya kutafsiri lugha , lakini kwa alivyokuwa akimwamini Profesa Clark aliamini ni kifaa ambacho kingekuwa na uwezo mkubwa sana.

Alijikuta akimkumbuka Lanlan , Bi Wema alikuwa akipata shida ya kuongea na Lanlan kutokana na kutokuelewa lugha ya kingereza na kuna hata muda Edna alifikiria kumfundisha Lanlan kuongea lugha ya kiswahili.

“Hiki kifaa kinaweza kutoa changamoto za watu kuwasiliana kwa lugha tofatu , kwanini hujavitengeneza kwa uwingi?”Aliuliza

“Niligundua teknolojia yake miaka miwili iliopita lakini nilishindwa kuiweka wazi”

“Kwanini?”

“Gharama ya kuitengeneza hii Headphone moja ni sawa na gharama zilizotumika kutengeneza I phone 14 , hivyo inamaanisha kama nitaizindua ni nusu ya watu duniani kote ambao watamudu gharama , lakini licha ya hivyo kuna mamilioni ya watu wanaingiza kipato kwa kutafsiri lugha , kama hii bidhaa itaingia sokoni wataathirika moja kwa moja , lakini kubwa zaidi ukijifunza lugha ya jamii husika ni rahisi pia unajifunza tamaduni ya jamii hio , hivyo nikaona ni bora niache dunia iendelee kama ilivyo”Aliongea na kumfanya Roma aone ana mantiki kwenye maneno yake.

Clark alizichukua na kuzihifadhi kwenye kabati na kuanza kumuonyesha Roma teknolojia nyingine ambazo amegundua.

Kila kitu alichoonyeshwa kilimfanya Roma kushangaa kwani ni gunduzi za juu sana ambazo zimeweza kufanywa na mwanamke ambaye hajatimiza hata miaka ishirini na tano.

Alijikuta akimwangalia Clark ambaye sura yake ilionekana kuwa na furaha kuliko siku zote , tokea swala la ndoa yake kughairishwa alionyesha kama amepewa uhai mwingine.

“Kwanini unaniangalia hivyo? Au maelezo yangu yamekuywa mengi ,hivi vitu nimetengeneza nikiwa sina mudi ya kufanya chochote”

“Nikiri kwamba ijapokuwa nilikuwa nikikuchukulia kama mwanasayansi mkubwa lakini kuna vitu vingi sijavifahamu kutoka kwako , una heshima yangu”.

“Nikajua ungeniita mwanamke kichaa”

“Kwaninni nikuite kichaa wakati kazi yako ni kubwa , hata hivyo nimejikuta hata nipata ahueni ya kupunguza mawazo kwa kusikiliza maelezo yako”Aliongea Rom.

“Una mawazo gani wakati umezungukwa na watu wanaokupenda?”Aliuliza huku akionyesha hali yakutaka kujua nini kimemsibu Roma mpaka kuwa kwenye mawazo.

Roma ilibidi amuelezee Clark kuhusu Rufi namna ambavyo alifanya makusudi kudukua mawasiliano ya frequency za Tv Chanel yao lakini pia namna alivyogongwa na Edna mpaka kufanikiwa kuweka ukaribu lakini pia namna alivyomharibia siku yake nzuri..

Mpaka Roma anamaliza Clark alishangazwa na maelezo hayo , hakuamini siku ile mdukuzi alikuwa ni mtu ambaye alikuwa na mahusiano na Roma.

“Clark nipo najidharau hapa kwa kushindwa kujizuia na nahisi ubongo wangu umejaa Protini na sio akili”

“Sio kama umeshindwa kujizuia Roma, kama ni hivyo basi ungekuwa ushanigusa na mimi au huyo Rufi ni mrembo kuliko mimi?”

“Nishakuambia wewe ni wa tofauti kwangu”

“Jibu lako ndio linaelezea hali uliopo nayo kwa sasa , ukweli ni kwamba hukutaka kujizuia mara baada ya kumuona Rufi”

“Unamaanisha nini kusema hivyo?”

“Sijui sana kuhusu wanaume wengine lakini wewe nakufahamu ,kipindi cha nyuma licha ya kwamba ulikuwa ukishindwa kujizuia kwa sababu ya ukali wa Devine light kwenye mwili wako lakini hata hivyo ulikuwa ukichagua wanawake wa kulala nao , hivyo maelezo ya kwamba kwanini ulilala nae na sio mimi ni kwasababu Rufi ulimchukulia kama mwanamke ambaye hana umuhimu kwako , ulimchukulia kama Malaya wa kupumzisha akili na asubuhi kumpotezea ni kama kipindi kile ulivyokuwa Ninja wanawake hawakuwa na umuhimu kwako na hukujiuliza hata mara mbilimbili kuyachukua maisha yao wanapovuka mpaka”

“Wanawake niliowaua hawakuwa wanawake kwangu bali maadui , unapaswa kuwatofautisha”

“Sawa na ndio maana nakuambia ulivyomuona Rufi hukumzingatia kama mwanamke muhimu kwako hivyo ukaruhusu hisia zako kukuongoza na matokeo yake ni kwamba alikuwa ni mwanamke mwenye akili tofauti na ulivyomdhania, hivyo ulichomfanyia Edna ni usaliti wa kimwili na sio usaliti wa kihisia”

“Wewe pekee ndio unaweza kuelewa hivyo lakini sio Edna, matendo yangu yamemuumiza kihisia kwani moja kwa moja anamchukulia Riufi kama mwanamke ninaempenda”

“Ndio!, hawezi kukuelewa labda angefahamu hata nusu ya maisha yako ya nyuma huenda angekuelewa na hata mimi pia nisingekuelewa”

“Kwanini?”

“Kuna sababu moja tu, ulishaacha tabia ya kulala na kila mwanamke unaekutamanisha , hivyo naweza kuamini moja kwa moja hisia zako kwa Rufi hazielezeki na haumchukulii kama malaya tena na kama ingekuwa hivyo huenda muda huu angekuwa ni marehemu kwa kukuchokoza”

“Kwahio kimsingi ni kwamba mimi ni mbwa”

“Sio kila mmoja atakuona kama mbwa , Mimi mwenyewe natamani uendelee kutokuwa mwaminifu huenda nikapata nafasi kuwa mpenzi wako, ndoa ni ustaarabu wa kibinadamu zaidi na unachotakiwa kuelewa mwanamke yoyote anavutiwa na mwanaume mwenye nguvu na kujiamini , kwa mfano tu marafiki zako Sauroni na Makedoni wana wapenzi wengi kuliko hata wewe , mimi kwa uwezo wako naona bado ni muaminifu”

“Kwahio ndio unavyoniona?”

“Unafikiri ni mimi tu , naamini hata wapenzi wako wengine , Rose , Nasra , Amina na Dorisi wamekupenda kutokana na kutokuwa mtu wa kawaida , unafikiri ungeweza kuwa nao kama ungekuwa mtu wa kawaida ambaye unafanya kazi ndani ya kampuni ya Vexto?”

“Naona hii ni kama mbinu yako ya kuzitakasa dhambi zangu?”

“Ninachofanya hapa ni kukuelewesha tu namna ninavyokuchukulia lakini maono yangu kwako ni tofauti na Edna atakavyokuona”

“Kwanini?”

“Kwasababu Edna tayari ni mkeo na wapenzi wako wengine wanamfanya kukosa haki zote kama mke , yeye ni mke aliekamilika kwako lakini wewe ni mume ambaye hujakamilika kwake kutokana na kuwa na wanawake wengi, hivyo anakuvumilia kwasababu anaogopa kukuacha ,nakupenda kama lakini ukweli unachomfanyia Edna ni ukatili”

“Daah! I feel so too that’s why I’m so disgusted with myself”Aliongea Roma huku akivuta pumzi.

“Ndio hivyo Mister Disgusting, unajua ni maneno gani matatu hupaswi kusema kwa mkeo pale unapomkosea?”

“Maneno gani?”

“I am sorry”Aliongea na kumfanya Roma kuona labda kukutana na Edna kwenye maisha yake ni jambo baya sana , kwani muda wote alikuwa akiongea hilo neno.

“Kwanini sasa hukuniambia mapema”

“Kwanini nikupe ushauri unaoimarisha ndoa yako, wakati na mimi ni mwanamke ninaekuwinda, ninaweza kuwa mwanasayansi lakini mimi ni binadamu mwenye hisia na hisia zangu zinaniambia ukiachana na Edna mfaidika mkuu aakuwa mimi”

“Nisaidie namna ya kutatua hili tatizo napanga kufunga nae ndoa mwezi ujao”

“Kwanini usimpe talaka tu”

“Acha ujinga ! Haitokuja ikatokea siku nikamuacha yule mwanamke labda yeye mwenyewe alazimishe kufanya hivyo , Kama ningekuwa simpendi nisingeishi nae mpaka sasa , unajua ni vita gani baridi nimepitia kukaa nae nyumba moja , yote ni kwasababu ameujaza moyo wangu kuliko mwanamke yoyote yule”Aliongea Roma akiweka usiriasi.

“Lakini hivyo sio Edna anavyofikiria , unachotakiwa kujua mapenzi ni kama Manati , unavyomuumiza kihisia ni kama vile unavyoivuta na kadri unavyoendelea kuivuta itaishia kukatika na haiwezi kurudi kwenye mwonekano wake wa mwanzo”

“Nitaiunganisha hata kwa kuifunga na mpira mwingine”Aliongea Roma na kumfanya Clark kukosa usemi kutokana na jibu lake.

“Hii ni mara yangu ya kwanza kukuona ukiwa na wasiwasi namna hii inaonekana kweli unampenda sana”

“Nisamehe kama maneno yangu yamekuwa makali lakini nahitaji kutatua hii changamoto”

“Usijali hata sijakasirika”

“Kwahio unanisaidiaje sasa?”

“Unamuuliza mtu ambaye maisha yake yote hakuwahi kuwa kwenye mahusiano , nawezaje kutoa ushauri kwa mwanaume mwenye mke? Ila nina wazo lakini naona kama la kijinga”Aliongea na kisha akamnong’oneza“

*****

Molin ndio aliekuwa wa kwanza kumsogelea Edna , lakini kikumbo alichokutana nacho kilimfanya kutupwa upande wa pili wa mchanga.

Lanlan siraha yake kubwa ni mwili wake na ndio alichokifanya baada ya kuona Molin kutaka kumgusa mama yake.

“Why are you following Mama?, if you’re bad guys I’ll kill you”Aliongea Lanlan huku akianza kuminya minya pua zake kama vile anataka kutoa makamasi.

Wanajeshi wa The Eagles walikuwa wakifahamu Lanlan alikuwa na uwezo usio kawaida mara baada ya miezi kadhaa iliopita Edna waliposhambuliwa na misukule ya Yan Buwen iliofufuliwa kwa Ressurrection Fluid , sasa siku ile waliweza kuangalia ’footage’ za CCTV za tukio zima na ndipo walipogundua Lanlan hakuwa mtoto wa kawaida.

Lanlan aliwaangalia mmoja mmoja kwa namna ya kuwachunguza na alivyoweza kuona sura ya Adeline aligundua alishawahi kumuona nyumbani kwao.

The Eagles wakati wakiangaliana kwa tahadhari kwa kujiuliza cha kufanya walijikuta wakitoa macho mara baada ya kumuona Lanlan akimshika Edna masikio kwa kuyaingiza vidole pande zote na palepale Edna alishituka kama mtu ambaye alikuwa kwenye ndoto.

Afande Adeline na wenzake walijikuta wakiangaliana wakishindwa kuzuia mshangao wao, lakini hata hivyo walijikuta wakivuta pumzi za ahueni mara baada ya Edna kurudiwa na fahamu.

“Madam uko sawa, tunaomba tukupeleke hospitalini kwa ajili ya kufanyiwa vipimo” Aliongea Adeline mara baada ya kutoka kwenye mshituko.

“Nipo sawa na sihitaji ulinzi wenu, mnaweza kurudi na muambieni aliewaagiza sitaki kumuona tena”Aliongea Edna kwa kiburi.

“Madam hupaswi kuongea hivyo , Mfalme Pluto hatopenda tukukuache bila ya ulinzi”Aliongea Adeline

“Ndio Madam ,jambo lolote baya lilikupata hatoweza kutusamehe”Aliongezea Fanny.

“If mama tells you to go you must go and if you don’t I will kill you both”Aliongea Lanlan kuingilia yale mazungumzo huku akimshika Edna mkono

Maneno ya Lanlan yalimfanya Edna amwangalie Lanlan kwa mshangao kwani kauli zake zilikuwa za kibabe sana , kuna muda alifikiria huenda Roma na Lanlan ni kitu na baba yake , kwani walikuwa wakifanana kwenye mambo mengi.

Lanlan alikuwa anapenda chakula sana na hivyo hivyo Roma alikuwa akipenda kula sana ,wote walionekana sana kupenda kuua sana na kutoa kauli za ugomvi.

Ijapokuwa walikuwa wakiongea na Edna lakini macho yao yote yalikuwa kwa Lanlan , walimwangalia kwa wasiwasi.

Molini bado alikuwa akiugulia maumivu kwani mwili wake ni kama uligongwa na jiwe .

“Tunapaswa kuondoka , Madam hatopatwa na tatizo kutokana na uwepo wa Lanlan hapa , Huyo mtoto anaonekana kuwa na nguvu kuliko sisi wote hapa”Aliongea Molin kinyonge akiwashauri wenzake.

“But..”

“We ‘ll head back and report to Captain Diego , From there we will await for further orders”Aliendelea kuongea akimaanisha kwamba wanapaswa kurudi wakatoe ripoti kwa Kapteni Diego na kusubiria oda nyingine.

****

Roma akiwa ameketi eneo la sebuleni ndipo alipopigiwa simu na Diego na kupewa taarifa ya kile kilichotokea , alishangazwa sana na kuwa na wasiwasi kwa kile kilichotokea mara baada ya kuambiwa Edna alidondoka na kupoteza fahamu na kisha Lanlan akamshika masikio na akazinduka.

Alijua Lanlan alikuwa na uwezo usiokuwa wa kawaida lakini kitendo cha kumzindua mama yake baada ya kupoteza fahamu kilimshanganya ,lakini kubwa zaidi ni kwanini Edna adondoke na kupoteza fahamu au ni kwasababu alimuumiza kihisia ,alijikuta moyo wake ukiuma mara baada ya kuhisi huenda yeye ndio chanzo.

“Ndio unaondoka?”

“Ndio shukrani kwako umenisaidia kupoteza mawazo”

“Mpango wako ni upi sasa?”

“Umeniambia nisubiri mpaka atakapokuwa sawa mwenyewe , hivyo sitofanya chochote na zaidi yoyote nawajibika pia kwa wapenzi wangu wengine”

“Ngoja nikupe kuna chupa za pombe zipo kwenye friji , maana siruhusiwi kunyw apombe”

“Mbona kuna ile chupa ambayo ipo wazi?”

“Nilipunguza upweke ile siku nilivyotoka kwako nikiwa na hasira baada ya Edna kuniambia niolewee na Maksim , ila situmii pombe kabisa”

“Clark nisingekuwa nimemuoa Edna ningekuoa wewe”

“Nah Being Clark suits me more than being Edna”

“Umeeleweka”Aliongea Roma na kisha alipunga mkono na kutoka ndani ya nyumba hio.

“Pumbavu kama ningekuwa mpenzi wako nisingependa kuwa Clark tu”Aliongea Clark baada ya kujibwaga kwenye Sofa.

*****

Edna aliondoka eneo la ufukweni kutokana na kukosa amani kwani watu wengi walikuwa wakimwangalia kwa mshangao kutokana na tukio la kudondoka lakini pia Lanlan kumpiga Molin kikumbo mpaka kudondoka.

Safari yao ya kwanza ilikuwa ni Mlimani na alimnunulia Lanlan baadhi ya zawadi ikiwemo mdoli na kisha akaianza safari ya kurudi nyumbani.

Uwepo wa Lanlan ilikuwa ni nafuu kwake kwani mawazo yalikuwa yamepungua kwa kiasi kikubwa lakini hasira na Roma hazikuwa zimeisha na alitamani asimuone kwa zaidi ya wiki nzima.

Aliendesha gari huku akifikiria tukio lilomtokea , haikuwa mara yake ya kwanza kupoteza fahamu , mara ya kwanza ilikuwa ni Hongkong na hisia zilikuwa zinafanana, lakini awamu hii ilikuwa tofauti kidogo.

Alivyopoteza fahamu ni kama alikuwa akiota ndoto akiwa aneo la msituni katikati ya mbuga huku akimuona mwanamke mwenye mwonekano wa kufanana kabisa na yeye lakini mwanamke aliekuwa mbele yake hakuwa peke yake , alikuwa akimwangalia Lanlan ambaye amepanda juu ya mnyama mkubwa mwenye kufanana na Tembo lakini muda uleule ghafla yule mwanamke aligeuka nyuma na kumuona yeye na kuanza kuonyesha mshituko uliojaa hofu na palepale alimkimbilia Lanlan huku akiita jina lake.

“Lanla…!!!”Edna kabla hajamaliza ndoto alijikuta akirudiwa na fahamu na ni muda ambao Lanlan alimuwekea vidole masikioni.

Alijikuta akimgeukia Lanlan aliekuwa pembeni akicheza na mdoli wa kike , alijiambia mwonekano wa Lanlan pembani yake si kiasi cha pesa chochoe ambacho kinaweza kukamilisha hilo, alijikuta akiwa ni mwenye faraja , uwepo wa Lanlan kwenye maisha yake ni kama sababu nyingine ambayo inamfanya kuyapenda sana maisha yake.

Dakika chache mbele aliweza kufika Ununio na kuingiza gari ndani na ni muda huo huo na Roma na yeye aliweza kuingia hapo ndani baada ya kushushwa na Taksi nje ya geti.

Edna alivyoshuka kwenye gari na kumuona Roma anaingia alijikuta sura akiikunja na hasira zikianza kujikusanya upya.

“Kwanini upo hapa?”Aliuliza Edna akiwa na sura iliojaa usiriasi.

“Edna mke wangu sidhani kama ndio unanifukuza ndani ya hii nyumba?”

“Unaweza kwenda popote unapojisikia , kwanza una wanawake wengi hivyo hukosi pakulala, Hapa ilikuwa ni nyumbani kwako na si sasa na kama hutaki kuondoka hapa nitaondoka mimi na Lanlan”Aliongea kwa kufoka.

“Edna hatuwezi kukaa chini na kuongea?”

“Sitaki maongezi na wewe”

“Edna najua una hasira na mimi , lakini kilichotokea mimi na Rufi ni kitendo cha mara moja tu na hakiwezi kujirudia tena na hata sijui ni sababu gani ametaka kutuvurugia , hata hivyo sio mwanamke wa kawaida na wasiwasi wangu angekuwa hatari zaidi kwako na huenda angekuumiza”

“Wewe ndio umeziumiza hisia zangu sio Rufi”

“Okey basi nitaondoka na nitarudi ukiwa umetulia”Aliongea Roma na kisha alichukua ufunguo wa gari yake kwenye mikono ya Edna na kisha akaliwasha na kuondoka , muda huo ilikuwa ni saa kumi na mbili na nusu kwenda saa moja na kigiza kishaanza kuingia.

Edna alisimama palepale pasipo kuamini Roma anaondoka kweli , alimwambia aondoke kwasababu alikuwa na hasira lakini hakuwa akimaanisha kwenye moyo wake, alitaka kuona Roma akiomba msamaha na kujielezea , lakini akaondoka nje ya mategemeo yake.

“Mama don’t cry”Lanlan alimwangalia mama yake kwa huzuni na Edna alijikuta akiyafuta machozi haraka haraka na kisha alimwangalia kwa tabasamu na kumwambia halii.











SEHEMU YA 462

Upande wa juu ghorofa ya pili Qiang Xi alikuwa akishuhudia wana ndoa wakigombana na alijikuta hata yeye moyo ukimuuma , hasa alipomwangalia Lanlan alieshikwa mkono na Edna.

Waliingia ndani na nyumba ilikuwa imetulia kuliko isivyokuwa kawaida ,maana wanafamilia walikuwa wamepungua kwa kiasi kikubwa , Yezi alikuwa ashaondoka kwa zaidi ya miezi kadhaa , Sophia kahama, Blandina alikuwa anaishi Masaki nyumbani kwao , hivyo waliobaki ni Bi Wema na Qiang Xi.

“Sister Edna kama ukija kuwa na mtoto mwingine wa kike unadhani atakuwa ni kama Lanlan?”Aliuliza Qiang Xi na haikueleweka kwanini ameuliza hilo swali.

“Mama , Don’t get me a sister I want a brother”Aliongea Lanlan na kumfanya Edna kushangazwa na jibu lake na Bi Wema ndio ambaye hakuelewa pekee na ilibidi Edna atafsiri.

Edna hakuwahi kuwaza kupata mtoto mwingine bado na hakuelewa namna alivyojisikia mara baada ya kumsikia Lanlan kusema anataka mdogo wake wa kiume na sio wa kike.

*****

Roma mara baada ya kutoka nyumbani safari yake ya kwanza ilikuwa ni mjini na alipitia njia ya Kawe na kwenda kusimamisha gari nje ya jengo la Apartment za PalmVillage Mikocheni kwa Warioba.

Alikuwa na mpango wa kuonana na Rufi kwa mara nyingine , haikujulikanaa ni sababu ipi ya kuonana nae tena , lakini sasa kwasababu hakuwa akijua ni Apartment namba ngapi aliokuwa akiishi alishindwa kushuka na kuingia ndani.

Baada ya kuwaza kwa muda mfupi alikumbuka Mika alikuwa na ukaribu na Rufi lakini hata hivyo hakuwa na mawasiliano yake hivyo moja kwa moja alimkumbuka Benadetha na palepale alitoa simu yake na kumpigia.

“Roma siamini kama umenikumbuka leo?”Sauti laini ya kike ilisikika upande wa pili huku ikionyesha kufurahishwa na simu hio.

“Kwanini useme hivyo wakati sina sababu ya kukupigia simu” Aliongea Roma.

“Oh! Kwahio ni sababu gani umepata leo mpaka ukanikumbuka?”

“Nahitaji namba ya simu ya mdogo wako Mika , nitumie kwa meseji”Aliongea Roma.

“Mh! Haya”Aliongea Benadetha na kisha simu ilikatwa na dakika hio hio namba ya Mika ilitumwa kwa meseji na Roma alipiga simu palepale

“Dogo niambie ni Apartment namba ngapi Rufi amechukua ndani ya hili jengo”

“Shemeji Roma..Aaa Bro!”Sauti upande wa pili ilisikika na Roma aliweza kufahamu Mika yupo Bar kama sio Claub kutokana na sauti za watu na mziki lakini alishangazwa kuitwa shemeji.

“Ndio ni mimi Roma na sio Shemeji yako”

“Okey Bro , Anaishi number 101 floor 14 , Password ni siku, mwezi na mwaka mliokutana”Aliongea Mika kwa sauti.

“Wewe dogo ndio kakuambia uniambie na Pasword”

“Bro nimesema hivyo kwasababu sifahamu hata mmekutana lini hivyo hata mimi hio Pasword siiijui”Aliongea na Roma alikata simu na kisha alitoka kwenye gari na kuzama ndani kupitia upande wa Supermarket.

Dakika chache mbele alikuwa kwenye Korido ya Floor 14, hili jengo halikumpa shida kwasababu Nasra alikuwa akiishi hapo pia hivyo watu wa usalama walikuwa wakimfahamu.

Roma mara baada ya kufika mbele ya mlango uliokuwa na kibao cha namba anuani 101 pembeni yake , alifikiria kwa muda kuminya kengele au kuingiza Password ,lakini akili yake ilimwambia aingize Pasword kwa kukumbuka tarehe aliokuana na Rufi L.A kwa kutumia mfumo wa tarehe na kweli palepale mlango ulifunguka.

Alijikuta akitabasamu na kisha akaingia ndani taratibu na kuita jina la Rufi lakini hakujibiwa , kulikuwa kimya kama hakukuwa na mtu lakini kutokana na uwezo wake usio kuwa wa kawaida alihisi uwepo wa mtu akiwa bafuni hivyo alisogelea dirisha lililokuwa likiangaliana na jiji kwa muda na kisha akarudisha pazia na kujibwaga kwenye sofa.

Rufi hakujua kuna uwepo wa mtu hivyo mara baada ya kumaliza kuoga moja kwa moja alitoka mpaka sebuleni akiwa uchi huku taulo mkononi akijifura maji.

“Ahh..!”Sauti ya kike ilisikika upande wa kulia kwake na alipomuona Rufi akiwa uchi ameziba sehemu zake za siri kuzificha na kukimbilia chumbani alikotoka.

Roma alijikuta mawazo yake yakisafiri kurudi nyuma mpaka siku ambayo alikutana na mrembo huyo ndani ya jiji la Loss Angeles na hatimae kumvua nguo na kufanya nae mapenzi

“Umeingiaje nyumbani kwangu?”Rufi aliongea mara baada ya kuvaa tisheti na kijikaptura kilichoishia kwenye magoti.

“Unafikiri wewe ndio mwenye akili nyingi ndani ya dunia hii?”Aliuliza Roma maana hakuwa tayari kumtaja Mika.

“Nadhani ni swali la kijinga , kama umeweza kuniponyesha sumu iliokuwa mwilini mwangu kwa muda mrefu naweza kukufananisha na wazee wa jamii za kijini”Aliongea na kumfanya Roma kumwangalia kwa mshangao kidogo.

“Lakini siamini kama unatokea jamii za kijini kama ingekuwa kweli usingeoa binadamu kwani usingeweza hata kumpa ujauzito”Aliongea na kuzidi kumshangaza Roma na kujiuliza kama Rufi alikuwa ametokea kwenye jamii hizo za kijini lakini alikaa vilevile kwenye Sofa bila ya kumjibu swali hata moja , haikueleweka alikuwa akiwaza nini.

“Roma naomba nikuulize swali?”Aliongea

“Umeuliza maswali mengi na umejijibu mwenyewe “Roma aliongea huku akitoa kicheko hafifu bila kuelewa hata yeye mwenyewe anacheka nini.

“Nataka kujua kama unanichukia na upo hapa kuniadhibu?”Aliuliza kwa wasiwasi.

“Kwanini nikuchukie ?”

“Kwasababu nimekugombanisha na mkeo?”

“Kwani tulishawahi kufanya mapenzi?”

“Acha kunidhalilisha , Ndio tumefanya tena mara nyingi , mchana wote”Aliongea kwa hasira.

“Kama ndio hivyo basi hatuna ugomvi , ulichomwambia mke wangu haujatunga na uliongea ukweli, ijapokuwa sijafurahishwa lakini sina sababu ya kukuchukia”Aliongea .

“Roma you are so nice to me”Aliongea huku akianza kutoa machozi.

“Wewe ni mtu mzuri ambaye nishawahi kukutana nae kwenye maisha yangu yote nimekugombanisha na mkeo lakini bado hunichukii , nilikaa nikawaza labda ndio mwisho wa kukuona tena kwa nilichokufanyia”

“Acha maigizo kwa mwonekano wako usingekosa mwanaume wa kukupenda na akawa mzuri kwako”

“Wewe hufahamu nilipotoroka nyumbani na kufika Marekani nilikutana na wanaume ambao asilimia kubwa walinisogelea kwa kunihitaji kingono pekee , hata wale ambao walijifanyisha kuwa marafiki zangu hawakuweka wazi lakini nia zao zilionekana wazi”

“Ulimwengu huu sio wa giza kama unavyofikiria watu wazuri na wabaya wapo”

“Kuwa na bahati ya kuzungukwa na watu wazuri haimaanishi kila mtu anaweza kuzungukwa na watu wazuri , mimi ni mwenye bahati mbaya”Aliongea na Roma alishindwa kujua cha kuongea na kuamua kuanzisha maongezi ya kile kilichomfikisha hapo.

“Umeuliza maswali mengi , hivyo ni zamu yangu na mimi kukuuliza . Niambie unataka nini kutoka kwangu na wewe ni nani haswa , maana matendo yako yanaonyesha unatafuta ‘attention’ yangu hivyo niweke wazi?”

“Kama nitakuelezea ukweli wote , je unaweza kuniahidi kitu kimoja?”

“Kitu gani?”

“Kunisaidia kulipiza kisasi?”

“Nini?”

“Nimesema kunisaidia kulipiza kisasi , ukiniahidi katika hilo nitahakikisha nafanya kila utakachotaka kutoka kwangu, nilichokuambia kuhusu mama yangu mzazi kutokea Afrika Mashariki ni kweli lakini sababu yangu ya kukufuata Tanzania ni kwa ajili ya kutaka msaada wa kulipiza kisasi”Aliongea .

“Unamaanisha nini?”

“Unatakiwa kukubali kwanza kuahidi ndipo nitakapokuelezea nimetokea wapi?”Aliongea kibishi.

“Wewe mwanamke ijue mipaka yako , huna haki ya kunilazimisha kufanya chochote kwa ajili yako , nikiamua kukuua hutokuwa na uwezo wowote wa kujitetea na kama unajihisi wewe ni mrembo na unaweza kunitega nadhani tayari ushamuona mke wangu”Aliongea Roma huku awamu hii akiwa siriasi mno.

“Nilijua tu hutotaka kunisaidia?”

“Nilishakuelezea mara ya mwisho usinikaribie tena kwasababu sikutaka ugomvi, hunidai wala sikudai lakini ukaamua kunivuruga ..”

“Ni kwasababu naogopa watanikamata tena?”

“Unamaanisha kuna watu wanataka kukuua?”

“Bora ingekuwa ni kifo ingekuwa afadhali lakini wakinikamata wataishia kunipa mateso makali ya muda mrefu pasipo ya kuniua”Aliongea na kuanza kutokwa na machozi

“Okey huna haja ya kutoa machozi mbele yangu na sitokuuliza maswali mengine hata hivyo uvumilivu wangu unakikomo , nataka uondoke Tanzania kwanzia siku ya kesho , umenunua hii Apartment nitakurudishia hela zako”

“Mbona unakuwa mkatili namna hio?”

“Unahisi ni wapi nimekuwa mkatili?”

“Umeniponyesha maumivu niliokuwa nayo kwa zaidi ya miaka ishirini na juu ya yote umesema hunichukii , inaonyesha kabisa unanipenda na hutaki kukubali ukweli”

“Unaongea ujinga ,kwangu wewe ni kama mwanamke wa kutumia na kuacha tu na sio wa kurudia mara ya pili , acha kujipa umuhimu kwangu”

“Wewe…!!”Aliongea huku akionyesha hasira waziazi.

“Sina haja ya kuongea na wewe mimi , ninachotaka ni wewe kuondoka hapa Tanzania , ikitokea umekuja kunivuruga tena itakuwa ndio mwisho wa uhai wako”Aliongea Roma na kisha alipiga hatua kuelekea mlangoni ili kutoka nje, hakuwa tayari kukubaliana na mwanamke huyo juu ya kitu ambacho hakuwa akikifahamu , hata hivyo alikuwa sio wa kawaida alijiambie je kama ni jambo litakalomwingiza kwenye matatizo.

Rufi alijikuta machozi yakimtoka mfululizo huku akimwangalia Roma akifungua mlango na kutoka nje.

“You Coward man the more you try to get rid of me the harder it will be”

“Wewe mwanaume muoga , kadri unavyojitahidi kuniondoa ndivyo itakuwa ngumu zaidi”Aliongea kwa hasira bara baada ya kufungua mpango akimwangalia Roma aliekuwa kwenye Lift ilioanza kujifunga..

Roma hakujali maneno yake , baada ya kurudi kwenye gari aliwaza ni wapi akamalize usiku maana amefukuzwa , hakuwa na mpango wa kutembelea mwanamke yoyote ambaye yupo karibu na nyumbani kwani alijua lazima Edna angefahamu hivyo kumuongezea hasira zaidi.

Wakati akiwa anawaza ni safari ya wapi aanzishe, simu yake ilianza kuita na baada ya kuangalia namba ilikuwa ni ngeni , lakini ilikuwa ni ya Kitanzania.

“Roma za siku nyingi”Sauti laini ya kike ilisikika kwenye masikio ya Roma , ni sauti ambayo haikuwa ngeni lakini ni kama ameisahau”

“Naongea na nani?”

“Ni Mimi Nadia Alfonso , tunaweza kuonana?”Aliongea Nadia na kumfanya Roma kushangaa na kujiuliza mwanamke huyu alijuaje yupo nje ya nyumba muda huo sa saa mbili za usiku.

“Nadia nadhani unajua nimeoa na muda kama huu nipo na familia”

“Najua haupo nyumbani kwako ndio maana nikakupigia simu”Aliongea na kumfanya Roma kuanza kuchungulia mazingira ya nje na kuangalia mbele zaidi mita kadhaa aliweza kuona mwanamke mrembo alievalia suruali ya jeans rangi ya bluu , viatu vyeupe high heels na kijiblazier cha mikono mirefu rangi ya pink isiokoleza.

Alikuwa ni Nadia ndio akiwa ameangalia gari yake huku akiwa ameshikilia simu na mkono mmoja na mkoba wa Brand ya Hermes mkono mwingine.

“Nilipanga nikutafute kesho asubuhi , lakini imekuwa bahati upo maeneo haya”Aliongea huku akipunga mkono kw akuinua mkoba wake juu.
 
SEHEMU YA 463.

Roma na Nadia waliketi kwenye eneo la mgahawa chini ya jengo hili la Apartment , ilikuwa sehemu tulivu hivyo Roma hakuona shida kuongea na Nadia , hata hivyo ni muda mrefu walikuwa hawajaonana.

Mwonekano wa Nadia ni kama umeimarika zaidi licha ya kuonyesha kukonda kidogo lakini uzuri wake wa rangi nyeusi ya chocolate ulimfanya kuwa mrembo zaidi.

Alikuwa amesuka nywele zake kwa mtindo wa Knot kama rasta na kumfanya kuwa mwamke wa kisasa zaidi.

Roma alitumia nafasi hio kuagiza kabisa chakula maana muda ulikuwa umeenda , ilikuwa imetimia saa mbili na nusu usiku hivi kwenda saa tatu.

“Nadia mbona unaniangalia sana bila ya kuongea?”Roma alivunja ukimya mara baada ya kuona Nadia haongei chochote zaidi ya kumwangalia , kauli yake ilimfanya Nadia kutoa tabasamu hafifu.

“Nimefurahi kukuona unaendelea vizuri , tofauti na mara ya mwisho tulivyoachana mwonekano wako umebadilika”Aliongea na kumfanya Roma kushangazwa na kauli yake.

“Nimekuwaje?”

“Erm,,,, naweza kusema unaonekana siriasi zaidi , More matured.. ule ukawaida umekupotea”Aliongea Roma na kisha alimwangalia Nadia na kutabasamu kidogo, hata hivyo ni kweli tokea apigwe na Radi za mipangilio tisa na kupanda levo ule ukawaida ni kweli ulikuwa umepotea ni kama mvuto wake uliongezeka maradufu.

“Kama ndio unavyoniona hivyo naweza kusema tunalingana”

“How!”Aliuliza akishangaa.

“Wewe pia licha ya kwamba unaonekana kupungua mwili lakini unavutia zaidi”

“Wow! Really!!|”

“Huamini maneno yangu?”

“Huwezi amini kila mtu ameniambia hivyo lakini kauli hii imekuwa tofauti zaidi ulivyoongea wewe , nahisi kama umenijengea kuamini kama nina mabadiliko”Aliongea na muda huo huo Roma chakula alichoagiza kilitetwa , tofauti ya Nadia yeye hakuagiza chochote akitoa sababu ameshakula , hivyo alichukua juisi ya matunda.

“So… nieleze nini unahitaji kuongea kabla sijamaliza chakula changu”Aliongea Roma huku akishika uma na kisu.

Nadia alionyesha kama mtu ambaye alikuwa akijishauri na Roma aligundua na kumwangalia.

“Roma unakumbuka mara ya mwisho tulivyokutan?”Aliuliza Nadia na kumfanya Roma kufikiria kidogo na alikumbuka hivyo alitingisha kichwa.

“Nipo Tanzania kwa misheni maalumu”Aliongea.

“Misheni!?”Roma aliongea huku akionyesha kushangazwa na kauli ya Nadia.

“Ndio”Aliongea na kisha alichukua mkoba wake alioweka pembeni na kufungua ndani na kisha alitoa picha ndogo na kumpatia Roma.

Roma mara baada ya kushika picha ile palepale kuna tukio alilikumbuka , lilikuwa ni tukio ambalo lilimtokea Edna na Suzzane ndani ya mji wa kisasa , tukio lilomhusisha Chriss ambaye alitaka kumuua mke wake.

“Unamjua?”

“Namfahamu kwa uchache sana , labda uniambie huyu ni nani haswa maana alitaka kumdhuru Edna”Aliongea Roma huku akiweka uma chini , awamu hii akiwa siriasi kidogo.

“Huyu mwanaume anafahamika kwa jina la Chriss Alton ni Ajenti mstaafu wa Secret service ndani ya ikulu ya Marekani , Stori yake inafanana sana na ya Mellisa”Aliongea kwa ufupi.

Roma alikuwa akimfahamu sana Chriss Altoni, faili la maongezi ya mheshimiwa Barrack Mabo , Raisi Kigombola na Chriss alishalisikiliza tayari na kumfahamu Chriss kama Secret Service Ajent , lakini jambo ambalo Roma hakulijua kuhusu Chriss ni stori ya maisha yake ambayo Nadia anasema inafanana na ile ya Mellisa iliomtokea nchini Bolivia.

“Ilikuwaje mpaka akafika nchini Tanzania na kutaka kumuua mke wangu?”Aliuliza Roma.

“Chriss alifanya kazi ndani ya ikulu ya Marekani na alikuwa ni moja ya vijana waliokuwa na ukaribu mkubwa sana na mheshimiwa Barrack Mabo, kama nilivyosema Chriss stori yake inafanana kabisa na ya Mellisa licha ya kwamba mazingira yalikuwa tofauti”

“Inafanana sehemu gani?”Aliongea Roma.

“Nadhani inabidi nikuelezee kwa ufupi kwa kile ninachofahamu kuhusu Chriss”Aliongea na kisha kuanza kusimulia.

Sehemu iliomvutia Roma ni pale Nadia aliposema Chriss hakuhusika katika kurekodi sauti za mheshimiwa Barack Mabo.

Swala hili Roma lilikuwa likimtekenya kwa muda mrefu hata yeye , tokea siku apate kusikiliza sauti iliokuwa ikizungumzia mpango LADO lakini pia ikizungumzia kuhusu Edna kuuliwa huku maagizo akipewa mheshimiwa Kigombola.

Roma hata yeye hakuamini kabisa kwamba Chriss aliweza kurekodi maongezi yale kwani alijua protokali za kiulinzi kwa raisi wa Marekani..

Nadia anasema wakati mheshimiwa Barrack Mabo anakaribia kuhitimisha ziara yake nchini Tanzania, Chriss aliweza kugundua uwepo wa Flashdisk ndani ya mfuko wa suruali upande wa kushoto.

Mwanzoni yeye mwenyewe alishangaa juu ya uwepo wa Flash kwenye mfuko wake kwani hakuwa na kumbukumbu kufika nchini Tanzania akiwa na Flash Disk.

Kutokana na shauku ya kutaka kujua ndani ya Flash ile kulikuwa na kitu gani ndipo alipotumia mwanya wa muda wa mapumziko kutafuta tarakishi ya mapakato na kuangalia kilichohifadhiwa kwenye hio flash kwani alikuwa na uhakika haikuwa ya kwake.

Kitendo cha kuifungua ile Flash ndani aliweza kukutana na mafaili matatu , la kwanza lilikuwa ni faili la Document na mafaili mawili ya mwisho yalikuwa ni Voice recording , jambo lile lilimshangaza Chriss na palepale alifungua kwanza faili ambalo ni la Document na ndipo alipokiutana na ujumbe ambao ulimshitua sana , ujumbe ambao ndio uliompelekea kumpatia Flash Disk hio Suphina Kangasi mfanyakazi wa Ikulu kintengo cha IT.

“Kwahio unasema Chriss hakuhusika bali ni mtu mwingine kabisa na huyo mtu ndio ambaye alimpa maagizo Chriss kumkabidhi Kangasi hio Flash Disk?”Aliuliza Roma.

“Ndio alivyosema, faili la Document lilimpa maelekezo ya nanmna hio , ijapokuwa hakuweka wazi ni nini kilichowekwa kwenye Document lakini ilionyesha pia alipewa vitisho ndio maana akafanya kama maelekezo yalivyokuwa yakimwambia”

“Nini kiliendelea baada ya hapo?”Aliuliza Roma huku akionyesha kuanza kuvutiwa na maongezi.

“Alifanikiwa kumkabidhi Suphian Kangasi kama alivyoelekezwa na baada ya hapo siku za ziara ya mheshimiwa zilifikia ukomo nchini Tanzania na akarudi Marekani na siku chache mbele ndipo Chriss alipokamatwa mara baada ya kugundulika yeye ndio alihusika kurekodi sauti za maongezi ya raisi, alipewa mateso ya kutaja mshirika wake na namna ambavyo alifanikisha lakini kwakuwa sio muhusika na hata aliempatia kazi hakujitambbulisha kwake alishindwa kutoa majibu na ilibidi apelekwe kwenye gerezani mara baada ya CIA kushindwa kupata chochote kutoka kwake na ndio huko Gerezani alipotoroshwa na kwenda kuishi katika Visiwa vva nchi ya Kiribati”

“Nani alimtorosha?”

“Hio ndio sehemu niliosema inafanana na Mellisa”Aliongea Nadia na Roma alifikiria kidogo na kisha akavuta pumzi.

Unajua Roma licha ya kwamba alikuwa na cheo cha Hades lakini hakuwa akijua mambo mengi ambayo Hades wa zamani alifanya , kwa mfano vitendo vya Hades wa zamani kuwapa watu machata kwenye mwili ya visiwa vya wafu hakuwahi kufahamu maana yake hata hivyo aliamini kuishi kwa Hades miaka mingi kuna mambo mengi ambayo amefanya ndani ya dunia hivyo hata kama atapenda kufahamu kila kitu uwezo huo hana.

Historia itakufuata nyuma yako na utajua kila kitu kuhusu mimi”Ndio kauli pekee ambayo Hades wa Zamani alimwambia Roma.

“Mpaka sasa watu wenye stori kama Mellisa na Chriss wamefikia wangapi mnaowafahamu?”Aliuliza Roma na kumfanya Nadia kushangaa kidogo ni kama hakutegemea swali hilo kutoka kwa Roma.

“Huenda wapo wengi sana , ila ninaowafahamu mpaka sasa wanafika 150”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa.

“Unasema 150!!”

“Tunaamini wapo wengi zaidi”

“Mellisa alionyesha kuwa na kisasi na serikali ya Marekani , je na hao wote wana visasi?”.

“Hapana mpaka sasa kinachoendelea ni zaidi ya kuwa na chuki na Marekani , jumuia ni yenye malengo mapana zaidi”

“Ukiachana na hio jumuia yenu , nataka kujua kwanini Chriss alitaka kumuua mke wangu?”

“Chriss bado hakuwa ametambulishwa katika Umoja na kupokelewa rasmi , kwani hakuwa amemaliza misheni yake na pia hakutuweka wazi juu ya misheni hio inahusiana na nini lakini tulichokuwa tukifahamu ina uhusiano mkubwa sana na mke wako Edna”Aliongea.

“Roma misheni yangu hapa nchini Tanzania ni kutaka kujua kwanini Chriss alikufa na kutaka kumuua Edna na ndio nilichotaka kuongea na wewe , viongozi wapo kwenye wasiwasi kwa kile ambacho amekifanya Chriss , ijapokuwa hawakua wakifahamu Chriss misheni yake ilikuwa ni ipi lakini alichokifanya kimetushangaza sana kwani ni nje ya ramani ya mipango yetu”Aliongea .

“Kwahio Chriss alikuwa na misheni iliomuhusisha mke wangu na nyie mkamuamini na kuacha aendelee na misheni yake bila kujua inahusiana na nini, nadhani mnipe maelezo ya kutosha kabla sijaanza kuua washirika wote wa Chriss”

“Moja ya sheria kuu ya Umoja wetu ni Imani kati ya mwanachama na mwanachama, pili kila mwanachama ana siri ambayo umoja hawezi kufahamu na hawezi kulazimishwa kuitoa kwasababbu za kiusalama, hivyo hata Chriss aliposema misheni yake hataki kuiweka wazi hakuna aliemhofia kwamba angefanya mambo kinyume”.

“Nadhani mpaka kutaka kuongea na mimi mnafahamu sijahusika na kifo cha Chriss?”

“Hilo ni kweli na ndio misheni yangu kubwa hapa nchini Tanzania, tunahitaji kujua nini kilitokea”Aliongea Nadia na Roma alifikiria kidogo na kisha akamwelezea kwa ufupi kile kilichotokea Nadia.

“Kuhusu namna alivyokufa sijui lakini muhusika alimpatia Edna zawadi ya Blue Ghost Orchid”

“Blue Orchids?”Aliongea kwa mshangao Nadia.

“Kwa mshangao wako naamini unafahamu kuhusu Blue Orchid?”

“Ndio Blue Orchid ni utambulisho wa taasisi ya siri ambayo ipo chini ya The Doni”Aliongea Nadia huku akionyesha wasiwasi.

“Nadia nakushauri ujitoe kwenye hayo mambo na uendelee na maisha yako ya kutafsiri sheria unajiingiza hatarini na hakuna ambae anaweza kukupatia ulinzi”Aliongea Roma.

“Najua ninachofanya ni hatari lakini kama ndio njia pekee ya kujenga ukaribu kwako nitafanya chochote”Aliongea Nadia na kumfanya Roma kushangaa kwa kauli yake.

“Unamaanisha nini kujenga ukaribu na mimi kwa kujiingiza kwenye matatizo?”

“Roma mpaka siku ambayo nimekuja kufahamu upo hapa Tanzania nimefanya mambo mengi ya hatari zaidi ya unavyofikiria , nilijinigiza kwenye hatari nyingi na yote hayo ni kutokana na msukumo uliopo hapa”Aliongea huku akishikilia eneo la moyo.

Roma hakuwa mjinga tokea muda mrefu alijua Nadia alikuwa akimpenda kimapenzi lakini hakuwa tayari kuanzisha mahusiano na Nadia kwa sababu alizokuwa akizijuia yeye.

“Kwahio unaamini kwa kujiingiza kwenye hio jumuia yenu ndio utakuwa karibu na mimi?, Nadia sijui nini unakipenda kutoka kwangu lakini nikueleze tu mimi sio yule uliekutana nae miaka ya nyuma sasa hivi nimebadilika na siwezi kuwa na mahusiano na wewe, natumaini utapata mwaname bora zaidi yangu”Aliongea Roma na kusimama.

Maeno yake yalionekana kuwa makali lakini alijiambia hataki kuongeza kabisa matatizo na mke wake Edna na akiendelea kuwa mpole mbele ya wanawake hatopata faida zaidi ya hasara.

“Roma subiri”Aliongea Nadia aliekuwa kwenye Bumbuwazi lakini Roma hakusimama.

Muda ulikuwa umeenda sana ilikuwa ikikaribia saa nne kamili za usiku , Roma hakuwa akijua aende kulala wapi usiku huo maana mke wake amemfukuza.

Baada ya kutoa gari lake taratibu na kuingia barabaranni alimtafuta Mage na simu yake iipokelewa ndani ya dakika chache tu.

Dakika chache nyingine mbele Roma alisimamisha gari nje ya geti ya nyumba ya Afande Tozo na kusubiri kwa dakika kadhaa tu hatimae Mage alievalia pigo za kitomboy alitoka.

Mavazi yale yalimshangaza Roma na kutamani kucheka lakini hata hivyo alipendeza, Mage alikuwa amevalia tisheti kubwa ya rangi nyeupe yenye chata kwa mbele la mpira wa Basketball , suruali alipiga pensi ya Timberland raba ya converse na kofia ya chepelu kampuni ya Nike.

“Mbona unanishangaa hivyo?”

“Ukichana na mavazi yako naweza kusema mwili wako umeanza kuimarika , muda wowote unaweza kupata ufunuo wa levo ya nusu Mzunguko”Aliongea Roma.

“Hata mimi najiona nina mabadiliko makubwa , kichwa kimekuwa chepesi kufanya maamzi mpaka kazini wanashangaa , lakini kubwa zaidi nguo nilizokuwa nikivaa mwanzonni naona sizipendi”Aliongea na kumfanya Roma kucheka.

“Kwahio staili hii ndio unahisi inakupendeza”

“Unaweza kusema hivyo , hata mama ananishangaa kwa mavazi yangu , nilivyomuaga nakuja kuonana na wewe alinikataza kuvaa hii staili”Aliongea Mage na Roma alitabasamu.

“Kadri utakavyofanya tahajudi na kupata ufunuo wa kubalansi nishati ya Yin and Yang ndio utazidi kuufahamu mwili wako kwa kiwango cha juu , ni siri nyingi zilizojificha ndani ya miili yetu na kadri unavyofumbua mafumbo ya siri hizo ndio unavyouelewa zaidi, hivyo kupenda uvaaji wa aina hii na kuchukia nguo zako za zamani ni mwanzo wa safari”Aliongea Roma na kisha alianza kuondoa gari eneo hilo taratibu taratibu.

“Jana niliamka asubuhi asubuhi na kuanza kufanya kwa kanuni ulizoniekeza na nilihisi kila kitu kilichokuwa kimenizunguka kinaelea juu angani, ni hisia za ajabu mno ambayo nimeweza kuzipata kwa mara ya kwanza katika maisha yangu Roma”Aliongea na kumfanya Roma kufikiria kidogo.

“Kuna kitu gani kingine cha ajabu uliweza kuona ?”

“Sijaona kingine cha ajabu , lakini nilisikia sauti za ambazo sio za kawaida”Aliongea.

“Kama nini?”Aliuliza Roma kwa shauku.

“Nilihisu mvumo wa sauti za wadudu kama nyuki”Aliongea Mage na Roma alitabasamu.

“Maendeleo mazuri , nina hamu ya kujua ni aina gani ya ufunuo utakaopata , awamu nyingine ukisikia mvumo wa sauti za nyuki hakikisha unapotezea kile unachokiona na kuweka umakini kwenye sauti”.

“Kwanini?”

“Sina uhakika na ninachokiwaza ila jaribu kufanya hivyo na uniambie baada ya kuzingatia sauti hizo ni kipi unaweza kuona zaidi”Aliongea Roma na Mage alitkubali.

Dakika chache mbele Roma aliingiza gari ndani ya hoteli ya Golden Tulip na kumuachia muegesha magari ufunguo kwa ajili ya kupaki gari yake.

Wakari Roma anafika mapokezi alikutana na sura ya Abubakari Hamadi akiwa na mwanamke wanatoka ndani ya hoteli hio.

Abubakari ndio aliekuwa wa kwanza kumuona Roma na alimwangalia kwa tahadhari na kisha akapita , lakini macho yake yote yalikuwa kwa Mage.

Roma hakumzingatia sana Abubakari na baada ya kuchukua chumba walinyoosha moja kwa moja mpaka kwenye Lift.

Roma walizungushana usiku mzima na Mage na saa kumi kumi ndio muda ambao walipotelea usingizini na Roma alikuja kushituka saa nne za asubuhi na kilichomuamsha ni simu yake iliokuwa ikiita.

Aliichukua na kuangalia jina la mtu anaepiga na aliona ni Recho , alishangazwa na simu hio na kupokea palepale.

“Recho kuna nini?”Aliongea Roma kivivu.

“Roma Boss Edna upo nae?”Aliuliza Recho na kumfanya Roma kufikicha macho na kukaa vizuri.

“Edna sipo nae, si atakuwa kazini muda huu”Aliongea Roma akiangalia saa ya ukutani.

“Hajafika kazini leo na nikimpigia simu haipokelewi , nikajua labda upo nae”Aliongea Recho kwa wasiwasi na kumfanya Roma kuhisi kuna kitu hakipo sawa na alitoka kitandani haraka, lakini alijiambia kama kuna tatizo The Eagles wangempigia simu.

“Usiwe na wasiwasi , hakikisha hili swala unalifanya kuwa siri na mtu yoyote hapo kazini akiulizia mwambie yupo na mimi”Aliongea Roma na Recho alikubali na kisha akakata simu.

“Mpenzi nini tatizo?”Aliuliza Mage aliekuwa amekaa akimwangalia Roma aliempa mgongo na Roma alimwelezea kwa ufupi.

“Au ni washindani wake wa kibiashara?”

“Sidhani kama kuna tatizo lazima ningepata taarifa kwani kuna watu wanampatia ulinzi, ngoja nielekee kwanza ofisini nikaangalie kinachoendelea”Aliongea Roma na Mage alimwambia atangulie kuondoka.

Roma alioga haraka haraka na kisha akavaa na kutoka ndani ya hoteli hio , baada ya kuingia kwenye gari lake alitafuta namba ya Diego na kupiga.

“Your Majesty Pluto , what are your orders for me today?”

“Edna yupo wapi?, Hajafika kazini na simu yake haipo hewani?”

“Mfalme Pluto sijapatiwa taarifa kama haonekani kwani vijana wapo kazini, ametoweka?”

“Ndio nakuuliza?”Aliongea Roma huku akionyesha kukasirika na Diego aliwasiliana na wanajeshi wake na ndani ya muda mfupi tu alimrudishia Roma jibu huku akionyesha kukosa utulivu.

“Mfalme Pluto nisamehe kwa kufanya kosa , nimejaribu kuwasiliana nao hapa hakuna majibu lakini vifaa vyao bado vinaonyesha kupokea mawasiliano , kuna uwezekano wakawa wamekufa”Alionge Diego.

“Damn it”Roma alijikuta akitoa tusi alitamani simu kuitupia nje, hapo hapo alijua kama kweli Edna ametekwa baada ya kuuliwa kwa wanajeshi wa The Eagles basi ni uhakika kwamba aliemteka Edna hakuwa na mpango wa kumuua.

“Sitokuwajibisha kwa hili kwani naamini adui atakuwa na uwezo mkubwa wa kuwaua bila hata ya wao kutoa taarifa ya tahadhari , hakikisha maiti zao zinafanyiwa mchakato wa kurudishwa nyumbani, wasiliana na Sautoni aidhinishe Euro milioni tano kwa kila familia kama fidia lakini unapaswa kujifunza kwa kosa ulilofanya leo”Aliongea Roma.

ITAENDELEA -SEE ME WATSAPP 0687151346.
 
Achana nae atawasumbua wengine ndivyo tulivyo waafrika tunapenda sana kupigiwa magoti kwa vitu vidogo mwanzoni hakuwa bize ila sasa baada ya fan base kuwa kubwa kawa bize sikatai kabisa kuwa ni haki yake kupata kile ambacho kinastahili anapokosea anawapa ahadi za uongo pia mara atarudia siyo poa.

Singano ni mwandishi mzuri sana nakubali ila rekebisha hayo hii dunia tulipofika wasio bize naamini wachache.
Sasa wewe si ndio mwafrika Halisi , kumchangia mwandishi 3000 tu kumsapoti unaona kuubwa na itamtajirisha .

Hebu jipe muda wa kufatilia wenzetu wa mataifa ya Ulaya , Asia na Marekani uone walivyokuwa supportive kwa waandishi wao, wewe unafikiri tunakaa chini kukuandikia ili kukufurahisha bure bure tu

NB:Jifunze kuthamini kazi za watu hata kama unaziona ni ndogo vipi itakusaidia sana.

TUSIWE NA WASIWASI SIMULIZI ITAISHA HII MPAKA MWISHO HATA KAMA NI MWAKANI
 
SEHEMU YA 463.

Roma na Nadia waliketi kwenye eneo la mgahawa chini ya jengo hili la Apartment , ilikuwa sehemu tulivu hivyo Roma hakuona shida kuongea na Nadia , hata hivyo ni muda mrefu walikuwa hawajaonana.

Mwonekano wa Nadia ni kama umeimarika zaidi licha ya kuonyesha kukonda kidogo lakini uzuri wake wa rangi nyeusi ya chocolate ulimfanya kuwa mrembo zaidi.

Alikuwa amesuka nywele zake kwa mtindo wa Knot kama rasta na kumfanya kuwa mwamke wa kisasa zaidi.

Roma alitumia nafasi hio kuagiza kabisa chakula maana muda ulikuwa umeenda , ilikuwa imetimia saa mbili na nusu usiku hivi kwenda saa tatu.

“Nadia mbona unaniangalia sana bila ya kuongea?”Roma alivunja ukimya mara baada ya kuona Nadia haongei chochote zaidi ya kumwangalia , kauli yake ilimfanya Nadia kutoa tabasamu hafifu.

“Nimefurahi kukuona unaendelea vizuri , tofauti na mara ya mwisho tulivyoachana mwonekano wako umebadilika”Aliongea na kumfanya Roma kushangazwa na kauli yake.

“Nimekuwaje?”

“Erm,,,, naweza kusema unaonekana siriasi zaidi , More matured.. ule ukawaida umekupotea”Aliongea Roma na kisha alimwangalia Nadia na kutabasamu kidogo, hata hivyo ni kweli tokea apigwe na Radi za mipangilio tisa na kupanda levo ule ukawaida ni kweli ulikuwa umepotea ni kama mvuto wake uliongezeka maradufu.

“Kama ndio unavyoniona hivyo naweza kusema tunalingana”

“How!”Aliuliza akishangaa.

“Wewe pia licha ya kwamba unaonekana kupungua mwili lakini unavutia zaidi”

“Wow! Really!!|”

“Huamini maneno yangu?”

“Huwezi amini kila mtu ameniambia hivyo lakini kauli hii imekuwa tofauti zaidi ulivyoongea wewe , nahisi kama umenijengea kuamini kama nina mabadiliko”Aliongea na muda huo huo Roma chakula alichoagiza kilitetwa , tofauti ya Nadia yeye hakuagiza chochote akitoa sababu ameshakula , hivyo alichukua juisi ya matunda.

“So… nieleze nini unahitaji kuongea kabla sijamaliza chakula changu”Aliongea Roma huku akishika uma na kisu.

Nadia alionyesha kama mtu ambaye alikuwa akijishauri na Roma aligundua na kumwangalia.

“Roma unakumbuka mara ya mwisho tulivyokutan?”Aliuliza Nadia na kumfanya Roma kufikiria kidogo na alikumbuka hivyo alitingisha kichwa.

“Nipo Tanzania kwa misheni maalumu”Aliongea.

“Misheni!?”Roma aliongea huku akionyesha kushangazwa na kauli ya Nadia.

“Ndio”Aliongea na kisha alichukua mkoba wake alioweka pembeni na kufungua ndani na kisha alitoa picha ndogo na kumpatia Roma.

Roma mara baada ya kushika picha ile palepale kuna tukio alilikumbuka , lilikuwa ni tukio ambalo lilimtokea Edna na Suzzane ndani ya mji wa kisasa , tukio lilomhusisha Chriss ambaye alitaka kumuua mke wake.

“Unamjua?”

“Namfahamu kwa uchache sana , labda uniambie huyu ni nani haswa maana alitaka kumdhuru Edna”Aliongea Roma huku akiweka uma chini , awamu hii akiwa siriasi kidogo.

“Huyu mwanaume anafahamika kwa jina la Chriss Alton ni Ajenti mstaafu wa Secret service ndani ya ikulu ya Marekani , Stori yake inafanana sana na ya Mellisa”Aliongea kwa ufupi.

Roma alikuwa akimfahamu sana Chriss Altoni, faili la maongezi ya mheshimiwa Barrack Mabo , Raisi Kigombola na Chriss alishalisikiliza tayari na kumfahamu Chriss kama Secret Service Ajent , lakini jambo ambalo Roma hakulijua kuhusu Chriss ni stori ya maisha yake ambayo Nadia anasema inafanana na ile ya Mellisa iliomtokea nchini Bolivia.

“Ilikuwaje mpaka akafika nchini Tanzania na kutaka kumuua mke wangu?”Aliuliza Roma.

“Chriss alifanya kazi ndani ya ikulu ya Marekani na alikuwa ni moja ya vijana waliokuwa na ukaribu mkubwa sana na mheshimiwa Barrack Mabo, kama nilivyosema Chriss stori yake inafanana kabisa na ya Mellisa licha ya kwamba mazingira yalikuwa tofauti”

“Inafanana sehemu gani?”Aliongea Roma.

“Nadhani inabidi nikuelezee kwa ufupi kwa kile ninachofahamu kuhusu Chriss”Aliongea na kisha kuanza kusimulia.

Sehemu iliomvutia Roma ni pale Nadia aliposema Chriss hakuhusika katika kurekodi sauti za mheshimiwa Barack Mabo.

Swala hili Roma lilikuwa likimtekenya kwa muda mrefu hata yeye , tokea siku apate kusikiliza sauti iliokuwa ikizungumzia mpango LADO lakini pia ikizungumzia kuhusu Edna kuuliwa huku maagizo akipewa mheshimiwa Kigombola.

Roma hata yeye hakuamini kabisa kwamba Chriss aliweza kurekodi maongezi yale kwani alijua protokali za kiulinzi kwa raisi wa Marekani..

Nadia anasema wakati mheshimiwa Barrack Mabo anakaribia kuhitimisha ziara yake nchini Tanzania, Chriss aliweza kugundua uwepo wa Flashdisk ndani ya mfuko wa suruali upande wa kushoto.

Mwanzoni yeye mwenyewe alishangaa juu ya uwepo wa Flash kwenye mfuko wake kwani hakuwa na kumbukumbu kufika nchini Tanzania akiwa na Flash Disk.

Kutokana na shauku ya kutaka kujua ndani ya Flash ile kulikuwa na kitu gani ndipo alipotumia mwanya wa muda wa mapumziko kutafuta tarakishi ya mapakato na kuangalia kilichohifadhiwa kwenye hio flash kwani alikuwa na uhakika haikuwa ya kwake.

Kitendo cha kuifungua ile Flash ndani aliweza kukutana na mafaili matatu , la kwanza lilikuwa ni faili la Document na mafaili mawili ya mwisho yalikuwa ni Voice recording , jambo lile lilimshangaza Chriss na palepale alifungua kwanza faili ambalo ni la Document na ndipo alipokiutana na ujumbe ambao ulimshitua sana , ujumbe ambao ndio uliompelekea kumpatia Flash Disk hio Suphina Kangasi mfanyakazi wa Ikulu kintengo cha IT.

“Kwahio unasema Chriss hakuhusika bali ni mtu mwingine kabisa na huyo mtu ndio ambaye alimpa maagizo Chriss kumkabidhi Kangasi hio Flash Disk?”Aliuliza Roma.

“Ndio alivyosema, faili la Document lilimpa maelekezo ya nanmna hio , ijapokuwa hakuweka wazi ni nini kilichowekwa kwenye Document lakini ilionyesha pia alipewa vitisho ndio maana akafanya kama maelekezo yalivyokuwa yakimwambia”

“Nini kiliendelea baada ya hapo?”Aliuliza Roma huku akionyesha kuanza kuvutiwa na maongezi.

“Alifanikiwa kumkabidhi Suphian Kangasi kama alivyoelekezwa na baada ya hapo siku za ziara ya mheshimiwa zilifikia ukomo nchini Tanzania na akarudi Marekani na siku chache mbele ndipo Chriss alipokamatwa mara baada ya kugundulika yeye ndio alihusika kurekodi sauti za maongezi ya raisi, alipewa mateso ya kutaja mshirika wake na namna ambavyo alifanikisha lakini kwakuwa sio muhusika na hata aliempatia kazi hakujitambbulisha kwake alishindwa kutoa majibu na ilibidi apelekwe kwenye gerezani mara baada ya CIA kushindwa kupata chochote kutoka kwake na ndio huko Gerezani alipotoroshwa na kwenda kuishi katika Visiwa vva nchi ya Kiribati”

“Nani alimtorosha?”

“Hio ndio sehemu niliosema inafanana na Mellisa”Aliongea Nadia na Roma alifikiria kidogo na kisha akavuta pumzi.

Unajua Roma licha ya kwamba alikuwa na cheo cha Hades lakini hakuwa akijua mambo mengi ambayo Hades wa zamani alifanya , kwa mfano vitendo vya Hades wa zamani kuwapa watu machata kwenye mwili ya visiwa vya wafu hakuwahi kufahamu maana yake hata hivyo aliamini kuishi kwa Hades miaka mingi kuna mambo mengi ambayo amefanya ndani ya dunia hivyo hata kama atapenda kufahamu kila kitu uwezo huo hana.

Historia itakufuata nyuma yako na utajua kila kitu kuhusu mimi”Ndio kauli pekee ambayo Hades wa Zamani alimwambia Roma.

“Mpaka sasa watu wenye stori kama Mellisa na Chriss wamefikia wangapi mnaowafahamu?”Aliuliza Roma na kumfanya Nadia kushangaa kidogo ni kama hakutegemea swali hilo kutoka kwa Roma.

“Huenda wapo wengi sana , ila ninaowafahamu mpaka sasa wanafika 150”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa.

“Unasema 150!!”

“Tunaamini wapo wengi zaidi”

“Mellisa alionyesha kuwa na kisasi na serikali ya Marekani , je na hao wote wana visasi?”.

“Hapana mpaka sasa kinachoendelea ni zaidi ya kuwa na chuki na Marekani , jumuia ni yenye malengo mapana zaidi”

“Ukiachana na hio jumuia yenu , nataka kujua kwanini Chriss alitaka kumuua mke wangu?”

“Chriss bado hakuwa ametambulishwa katika Umoja na kupokelewa rasmi , kwani hakuwa amemaliza misheni yake na pia hakutuweka wazi juu ya misheni hio inahusiana na nini lakini tulichokuwa tukifahamu ina uhusiano mkubwa sana na mke wako Edna”Aliongea.

“Roma misheni yangu hapa nchini Tanzania ni kutaka kujua kwanini Chriss alikufa na kutaka kumuua Edna na ndio nilichotaka kuongea na wewe , viongozi wapo kwenye wasiwasi kwa kile ambacho amekifanya Chriss , ijapokuwa hawakua wakifahamu Chriss misheni yake ilikuwa ni ipi lakini alichokifanya kimetushangaza sana kwani ni nje ya ramani ya mipango yetu”Aliongea .

“Kwahio Chriss alikuwa na misheni iliomuhusisha mke wangu na nyie mkamuamini na kuacha aendelee na misheni yake bila kujua inahusiana na nini, nadhani mnipe maelezo ya kutosha kabla sijaanza kuua washirika wote wa Chriss”

“Moja ya sheria kuu ya Umoja wetu ni Imani kati ya mwanachama na mwanachama, pili kila mwanachama ana siri ambayo umoja hawezi kufahamu na hawezi kulazimishwa kuitoa kwasababbu za kiusalama, hivyo hata Chriss aliposema misheni yake hataki kuiweka wazi hakuna aliemhofia kwamba angefanya mambo kinyume”.

“Nadhani mpaka kutaka kuongea na mimi mnafahamu sijahusika na kifo cha Chriss?”

“Hilo ni kweli na ndio misheni yangu kubwa hapa nchini Tanzania, tunahitaji kujua nini kilitokea”Aliongea Nadia na Roma alifikiria kidogo na kisha akamwelezea kwa ufupi kile kilichotokea Nadia.

“Kuhusu namna alivyokufa sijui lakini muhusika alimpatia Edna zawadi ya Blue Ghost Orchid”

“Blue Orchids?”Aliongea kwa mshangao Nadia.

“Kwa mshangao wako naamini unafahamu kuhusu Blue Orchid?”

“Ndio Blue Orchid ni utambulisho wa taasisi ya siri ambayo ipo chini ya The Doni”Aliongea Nadia huku akionyesha wasiwasi.

“Nadia nakushauri ujitoe kwenye hayo mambo na uendelee na maisha yako ya kutafsiri sheria unajiingiza hatarini na hakuna ambae anaweza kukupatia ulinzi”Aliongea Roma.

“Najua ninachofanya ni hatari lakini kama ndio njia pekee ya kujenga ukaribu kwako nitafanya chochote”Aliongea Nadia na kumfanya Roma kushangaa kwa kauli yake.

“Unamaanisha nini kujenga ukaribu na mimi kwa kujiingiza kwenye matatizo?”

“Roma mpaka siku ambayo nimekuja kufahamu upo hapa Tanzania nimefanya mambo mengi ya hatari zaidi ya unavyofikiria , nilijinigiza kwenye hatari nyingi na yote hayo ni kutokana na msukumo uliopo hapa”Aliongea huku akishikilia eneo la moyo.

Roma hakuwa mjinga tokea muda mrefu alijua Nadia alikuwa akimpenda kimapenzi lakini hakuwa tayari kuanzisha mahusiano na Nadia kwa sababu alizokuwa akizijuia yeye.

“Kwahio unaamini kwa kujiingiza kwenye hio jumuia yenu ndio utakuwa karibu na mimi?, Nadia sijui nini unakipenda kutoka kwangu lakini nikueleze tu mimi sio yule uliekutana nae miaka ya nyuma sasa hivi nimebadilika na siwezi kuwa na mahusiano na wewe, natumaini utapata mwaname bora zaidi yangu”Aliongea Roma na kusimama.

Maeno yake yalionekana kuwa makali lakini alijiambia hataki kuongeza kabisa matatizo na mke wake Edna na akiendelea kuwa mpole mbele ya wanawake hatopata faida zaidi ya hasara.

“Roma subiri”Aliongea Nadia aliekuwa kwenye Bumbuwazi lakini Roma hakusimama.

Muda ulikuwa umeenda sana ilikuwa ikikaribia saa nne kamili za usiku , Roma hakuwa akijua aende kulala wapi usiku huo maana mke wake amemfukuza.

Baada ya kutoa gari lake taratibu na kuingia barabaranni alimtafuta Mage na simu yake iipokelewa ndani ya dakika chache tu.

Dakika chache nyingine mbele Roma alisimamisha gari nje ya geti ya nyumba ya Afande Tozo na kusubiri kwa dakika kadhaa tu hatimae Mage alievalia pigo za kitomboy alitoka.

Mavazi yale yalimshangaza Roma na kutamani kucheka lakini hata hivyo alipendeza, Mage alikuwa amevalia tisheti kubwa ya rangi nyeupe yenye chata kwa mbele la mpira wa Basketball , suruali alipiga pensi ya Timberland raba ya converse na kofia ya chepelu kampuni ya Nike.

“Mbona unanishangaa hivyo?”

“Ukichana na mavazi yako naweza kusema mwili wako umeanza kuimarika , muda wowote unaweza kupata ufunuo wa levo ya nusu Mzunguko”Aliongea Roma.

“Hata mimi najiona nina mabadiliko makubwa , kichwa kimekuwa chepesi kufanya maamzi mpaka kazini wanashangaa , lakini kubwa zaidi nguo nilizokuwa nikivaa mwanzonni naona sizipendi”Aliongea na kumfanya Roma kucheka.

“Kwahio staili hii ndio unahisi inakupendeza”

“Unaweza kusema hivyo , hata mama ananishangaa kwa mavazi yangu , nilivyomuaga nakuja kuonana na wewe alinikataza kuvaa hii staili”Aliongea Mage na Roma alitabasamu.

“Kadri utakavyofanya tahajudi na kupata ufunuo wa kubalansi nishati ya Yin and Yang ndio utazidi kuufahamu mwili wako kwa kiwango cha juu , ni siri nyingi zilizojificha ndani ya miili yetu na kadri unavyofumbua mafumbo ya siri hizo ndio unavyouelewa zaidi, hivyo kupenda uvaaji wa aina hii na kuchukia nguo zako za zamani ni mwanzo wa safari”Aliongea Roma na kisha alianza kuondoa gari eneo hilo taratibu taratibu.

“Jana niliamka asubuhi asubuhi na kuanza kufanya kwa kanuni ulizoniekeza na nilihisi kila kitu kilichokuwa kimenizunguka kinaelea juu angani, ni hisia za ajabu mno ambayo nimeweza kuzipata kwa mara ya kwanza katika maisha yangu Roma”Aliongea na kumfanya Roma kufikiria kidogo.

“Kuna kitu gani kingine cha ajabu uliweza kuona ?”

“Sijaona kingine cha ajabu , lakini nilisikia sauti za ambazo sio za kawaida”Aliongea.

“Kama nini?”Aliuliza Roma kwa shauku.

“Nilihisu mvumo wa sauti za wadudu kama nyuki”Aliongea Mage na Roma alitabasamu.

“Maendeleo mazuri , nina hamu ya kujua ni aina gani ya ufunuo utakaopata , awamu nyingine ukisikia mvumo wa sauti za nyuki hakikisha unapotezea kile unachokiona na kuweka umakini kwenye sauti”.

“Kwanini?”

“Sina uhakika na ninachokiwaza ila jaribu kufanya hivyo na uniambie baada ya kuzingatia sauti hizo ni kipi unaweza kuona zaidi”Aliongea Roma na Mage alitkubali.

Dakika chache mbele Roma aliingiza gari ndani ya hoteli ya Golden Tulip na kumuachia muegesha magari ufunguo kwa ajili ya kupaki gari yake.

Wakari Roma anafika mapokezi alikutana na sura ya Abubakari Hamadi akiwa na mwanamke wanatoka ndani ya hoteli hio.

Abubakari ndio aliekuwa wa kwanza kumuona Roma na alimwangalia kwa tahadhari na kisha akapita , lakini macho yake yote yalikuwa kwa Mage.

Roma hakumzingatia sana Abubakari na baada ya kuchukua chumba walinyoosha moja kwa moja mpaka kwenye Lift.

Roma walizungushana usiku mzima na Mage na saa kumi kumi ndio muda ambao walipotelea usingizini na Roma alikuja kushituka saa nne za asubuhi na kilichomuamsha ni simu yake iliokuwa ikiita.

Aliichukua na kuangalia jina la mtu anaepiga na aliona ni Recho , alishangazwa na simu hio na kupokea palepale.

“Recho kuna nini?”Aliongea Roma kivivu.

“Roma Boss Edna upo nae?”Aliuliza Recho na kumfanya Roma kufikicha macho na kukaa vizuri.

“Edna sipo nae, si atakuwa kazini muda huu”Aliongea Roma akiangalia saa ya ukutani.

“Hajafika kazini leo na nikimpigia simu haipokelewi , nikajua labda upo nae”Aliongea Recho kwa wasiwasi na kumfanya Roma kuhisi kuna kitu hakipo sawa na alitoka kitandani haraka, lakini alijiambia kama kuna tatizo The Eagles wangempigia simu.

“Usiwe na wasiwasi , hakikisha hili swala unalifanya kuwa siri na mtu yoyote hapo kazini akiulizia mwambie yupo na mimi”Aliongea Roma na Recho alikubali na kisha akakata simu.

“Mpenzi nini tatizo?”Aliuliza Mage aliekuwa amekaa akimwangalia Roma aliempa mgongo na Roma alimwelezea kwa ufupi.

“Au ni washindani wake wa kibiashara?”

“Sidhani kama kuna tatizo lazima ningepata taarifa kwani kuna watu wanampatia ulinzi, ngoja nielekee kwanza ofisini nikaangalie kinachoendelea”Aliongea Roma na Mage alimwambia atangulie kuondoka.

Roma alioga haraka haraka na kisha akavaa na kutoka ndani ya hoteli hio , baada ya kuingia kwenye gari lake alitafuta namba ya Diego na kupiga.

“Your Majesty Pluto , what are your orders for me today?”

“Edna yupo wapi?, Hajafika kazini na simu yake haipo hewani?”

“Mfalme Pluto sijapatiwa taarifa kama haonekani kwani vijana wapo kazini, ametoweka?”

“Ndio nakuuliza?”Aliongea Roma huku akionyesha kukasirika na Diego aliwasiliana na wanajeshi wake na ndani ya muda mfupi tu alimrudishia Roma jibu huku akionyesha kukosa utulivu.

“Mfalme Pluto nisamehe kwa kufanya kosa , nimejaribu kuwasiliana nao hapa hakuna majibu lakini vifaa vyao bado vinaonyesha kupokea mawasiliano , kuna uwezekano wakawa wamekufa”Alionge Diego.

“Damn it”Roma alijikuta akitoa tusi alitamani simu kuitupia nje, hapo hapo alijua kama kweli Edna ametekwa baada ya kuuliwa kwa wanajeshi wa The Eagles basi ni uhakika kwamba aliemteka Edna hakuwa na mpango wa kumuua.

“Sitokuwajibisha kwa hili kwani naamini adui atakuwa na uwezo mkubwa wa kuwaua bila hata ya wao kutoa taarifa ya tahadhari , hakikisha maiti zao zinafanyiwa mchakato wa kurudishwa nyumbani, wasiliana na Sautoni aidhinishe Euro milioni tano kwa kila familia kama fidia lakini unapaswa kujifunza kwa kosa ulilofanya leo”Aliongea Roma.

ITAENDELEA -SEE ME WATSAPP 0687151346.
Asante sana, nitarudi tena hapa jumamosi panapo uzima
 
Sasa wewe si ndio mwafrika Halisi , kumchangia mwandishi 3000 tu kumsapoti unaona kuubwa na itamtajirisha .

Hebu jipe muda wa kufatilia wenzetu wa mataifa ya Ulaya , Asia na Marekani uone walivyokuwa supportive kwa waandishi wao, wewe unafikiri tunakaa chini kukuandikia ili kukufurahisha bure bure tu

NB:Jifunze kuthamini kazi za watu hata kama unaziona ni ndogo vipi itakusaidia sana.

TUSIWE NA WASIWASI SIMULIZI ITAISHA HII MPAKA MWISHO HATA KAMA NI MWAKANI
Lazima nikuchangie ila wape watu ahadi zinazoendana na ukweli
 
Nimeandika nikafuta , nikaandika tena nikafuta anyway nimeamua nikae kimya
Kuna jambo ningekwambia ila siwezi andika humu ndo ujue namna gani tunathamini kazi za waandishi hadi naandika pale sikukurupuka na sijawahi kukwambia Chochote.
 
Kuna jambo ningekwambia ila siwezi andika humu ndo ujue namna gani tunathamini kazi za waandishi hadi naandika pale sikukurupuka na sijawahi kukwambia Chochote.
Sawa mkuu tupo Pamoja , Endeleeni kutusapoti
 
SEHEMU YA 454.

Mwanaume yule alitoa tabasamu huku akimwangalia Denisi ,lilikuwa tabasamu ambalo liliashilia kuridhika nae.

“Umebadilika sana , Yan Buwen amekufunza vizuri”Aliongea kwa lugha ya kingereza, lakini Denisi maneno yale aliyachukulia kama tusi kwani palepale alimsogelea kwa spidi na kumkwida tai kwa namna ya kumminya.

“Acha kufanya maigizo mbele yangu ,mimi ni tofauti na wewe , nina jitegemea kwenye mambo mengi mwenyewe na kwako wewe…. Unaishi kwasababu ya baba yak”Aliongea Denisi huku akiweka sura yenye usiriasi kwenye macho yake.

“Usiwe mwepesi wakukasirika ,wote tunatambua kama sio kwa Master wetu Yan Buwen , tusingekuwa hai mpaka muda huu”Aliongea huku akionyesha hana hasira na Denisi , licha ya kwamba alikuwa amemkwida kwenye shingo.

“Wanachama wawili kutoka kundi la Camarilla watafika hapa muda si mrefu , Nadhani unafahamu Yan Buwen amekupa maagizo usionyeshe uwezo wako mpaka muda utakapowadia”

“Una uhakika utaweza kuwadhibiti ukiwa peke yako?”Aliuliza Denisi akionyesha wasiwasi kidogo na uwezo wa mwenzake na kumfanya yule bwana Vampire kupiga mwayo huku akimwangalia.

“Ingekuwa ni Zamani ningewahofia , lakini sasa hivi hata waungane na wazazi wao , hakuna ambaye anaweza kunizidi”Aliongea kwa majigambo na palepale Denisi alipotea kwa spidi na sekunde chache alionekana akifungua mlango wa gari yake aina ya V8 na kuondoka kwenye nyumba hio.

Muda huo huo wakati akitokomea , Lilith na Lefayette waliweza kutua ndani ya nyumba hio kwenye eneo la sebuleni sehemu ile ile aliokuwa amesimama Denisi mwanzoni.

“Karibuni sana , Ni kitambo kidogo bila ya kuonana na wewe mrembo Lilith pamoja na Marquess Lefayette”Aliongea na kumfanya Lefayette kumwambagalia kwa hasira.

“Nilijua tu ni wewe Drogba , upumbavu wako umepitiliza na awamu hii hakuna ambaye anaweza kujitokeza kukuokoa”

“Don’t be such a buzzkill , Shouldn’t we just sit and enjoy the view ? its rare for two of us to meet , The gracefull princess of the Venture clan, the mighty heir of the Brujah Clan and I , a minion of the sabbbat from the Tzimisce clan , Care for glass of blood?”

Aliongea huku akiweka tabasamu lake ambalo lilikuwa likiashria unafiki, akiwakaribisha huku akiwaambia kama watajali kupata angalau glass moja ya damu.

Sasa hapa unatakiwa kuelewa kimiminika cha rangi nyekundu kilichokuwepo kwenye glasi ilikuwa ni damu.

“Hatuna haja ya kuungana na wewe kwenye kijisherehe chako cha kuua mtu , nadhani ingekuwa kipaumbele chako kukimbia”Aliongea Lilith.

“Unafahamu ni kwanini Vampire ilipotea kwenye uso wa dunia kwa kuangamaizwa na binadamu?”Aliuliza Drogba na kumfanya Lilith na Lefayette kuangaliana ikionyesha hawakuwa na majibu.

“Ni kwasababu ya mitazamo yao ya kiburi kwa binadamu ndio ilikuwa anguko lao , nyie wawili mnaonekana kuwa wapole mno na hamfahamu mambo mengi,hivi mnadhania nimekaa hapa kuwasubiria kwasababu nawaogopa?”

“Unaongea ujinga na leo ndio mwisho wako”Aliongea Lilith na palepale ulionekana upanga wa kung’aa kwenye mikono yake maarufu kama Massace Blade au upanga wa maafa.

Drogba aliweka glasi ya damu kwenye meza na kuanza kunyoosha mabega yake kwa mbwembwe.

“Niliwauliza kama mnapenda mandhari ya hapa , lakni ukimya wenu huenda ndio jibu “

“Vizuri sana , unaonekana kuwa na nguvu nyingi ambazo zinakufanya ujihisi ni mwenye kujiamini , naamini awamu hii utajitahidi angalau hata kunipiga ngumi moja na isiwe kila siku mimi ndio ninakubutua”Aliongea Lefayette na palepale na yeye mkono wake ulionekana kushikilia siraha ya kichawi ambayo ipo muundo wa shoka lenye makali pande zote huku ikiwa na mpini wa mita kama moja na nusu hivi.

“Hio siraha yako inavutia sana kwa macho ,lakini kwa bahati mbaya sasa hivi haina athari kwangu”

“Unaweza kujaribu tuone kama haina athari”Aliongea na palepale alimsogela kwa kasi na kutaka kumpiga nayo lakini Drogba alikuwa mwepesi kwani sekunde tu alikuwa nje eneo la bustani na wote kwa pamoja walitoka nje huku Lefayette akiwa na hasira kwani alipelekea mashambulizi kwa kasi akidhamiria kumdhuru Drogba lakini adui yake alionekana kuwa na spidi isio na kifani.

Kwa spidi ambayo walikuwa wakitumia binadamu huenda macho yake yasingeweza kuona kile kinachoendelea na labda kuhisi eneo kuwa na upepeo usiokuwa wa kawaida peke yaeke..

Namna Lefayette alivyokuwa akishambulia ilikuwa tofauti kabisa na namna ambavyo Lilith na yeye anashambulia , lakini matokeo yalikuwa sio haba , kwani walimpelekesha Drogba kwa kiasi chake.

“Imekuawaje akabadilika kwa muda mfupi spidi yake sio tulioizoea”aliongea Lefayete kwa hamaki mara baada ya kugundua kila pigo analopeleka linapita hewani licha ya kwamba alijaribu kutumia spidi kubwa.

“Haijalishi unaspidi kiasi gani lakini nakuhakikishia siku ya leo huwezi kuondoka hapa ukiwa hai”Aliongea Lilith na muda ule ule Lefayette alipiga chini shoka lake na kukusanya upepo usiokuwa wa kawaida ambao ulikuwa kama kimbunga na kwa spidi kali sana alimsogelea nao Drogba.

Drogba licha ya kwamba alikuwa na spidi lakini alikuwa amechelewa kwani spidi ya kimbunga ilikuwa ni kali kuliko ya kwake na palepale ilimvaa , lakini hakutaka kuzembea , alichokifanya nikujiokoa kwa kutaka kuruka kwenda juu , lakini Lilith alikuja kwa spidi ya ajabu akiwa na panga lake na kushambulia , na kwasababu spidi ya ya Lilith ilikuwa kubwa kuliko ya Lefayette ilimuwia vigumu Drogba kukwepa pigo lake na kumkata Drogba mkono kuanzia begani na Drogba alitoa ukulele huku akidondoka pembeni, Lefayyete hakutaka kumpa nafasi nyingine alimsogelea na kumcharanga na lile shoka lake eneo la tumboni na kusababisha damu na nyama nyama kusambaa eneo zima.

Mpaka hapo aliamini ndio mwisho wa Drogba na walijikuta wakivuta pumzi za ahueni kwani mwanzo walihofia spidi yake.

Lakini sasa palepale walijikuta wakishangaa mabadiliko yalioanza kutokea kwenye mwiliwa Drogba , kila tone la damu na nyama zilizosambaa zilianza kujikusanya kwa spidi kubwa huku zikivutwa eneo moja kwa nguvu isiokuwa ya kwaida na kilikuwa ni kitendo cha dakika tu Drogba alirudi kwenye uhai wake.

“Play time is over , Time to get serious”Aliongea

“How… How can this be possible”Lilith alijawa na mshangao na hofu isiokuwa na kifani kwani ni mara yake ya kwanza kushuhudia tukio la namna hio.

“Ilitakiwa mpaka sasa awe ameshakufa kutokana na laana iliokuwa kwenye mwili wake, lakini kwanini akaweza kujirudisha hai”Lefayette nae aliongea huku akimwangalia Lilith.

“Nishawaambia ukiburi na ukale ndio anguko la jamii ya Vampire , ndio maana haijatokea hata siku moja mkapiga hatua kwenye kujikomboa na kujiweka huru , not only you guys but even the maing god will also face the true Rangarok”

“Unaongea ujjinga , usifikirie ndio tumekushindwa”Aliongea Lilith huku akivuta pumzi nyingi na kuzishusha na kusababisha kifua chake kupanda na kushuka.

“Naona hamtaki kuelewa sasa ni muda wa kuweza kuonja radha kamili ya ghadhabu yangu”Aliongea na palepale alipotea na ile anakuja kuibuka alikuwa mbele ya Lefayette na alimramnba ngumi yenye uzito wa tani eneo la shavuni na Lefayette alipeperushwa kama mpira na kwenda kuvaa mnara wa tanki la maji ambao ulipondeka palepale na kufanya tanki kumdondokea na maji yote kumwagika.

Lilith baada ya kuona vile alijiandaa kwa ajili ya kujilinda , lakini ilikuwa amechelewa kwani alijikuta akipokea mateke mawili mazito ambayo yalimrusha na kwenda kujipiza kwenye ukuta .

Lilith hakutaka kushindwa palepale alisimama na kupaa juu huku akitema mate na kumsogelea Drogba kwa kasi ya kutaka kumshambulia na panga lake la Maafa , lakini alikuwa amecheelewa kwani Drogba kwa kasi ya upepo alimvaa Lilith na kupaaa nae na ile anafika juu alimpiga ngumi yenye uzito watani mbili na kumfanya apepesuke na kwenda kutua kwenye maji ya bahari.

Akiacha hewani matone ya damu kama mvua yakidondoka chini kwenye mchanga wa fukwe.

Lefayette alipigika lakini haikumaanisha alishindwa .hivyo kushuhudia mchumba wake Llith akishambuliwa kwa namna ambayo ilimfanya kudhania amepoteza maisha alipandwa na jazba kwa kiasi kikubwa na palepale aliamka kwa spidi na kumfuata Drogba kwa kumshambulia na shoka lake.

“Blood Avalanche”

Aliongea kwa sauti kubwa akiita nguvu za kichawi na palepale wingu kama la moshi unaozunguka kwa spidi ulimsogelea Drogba kwa spidi kubwa huku akifuatia Lefayette kwa nyuma

“Inatia aibu dhana hio ya kichawi ikipotelea kwenye mikono yako”Aliongea Drogba na palepale alinyanyua mikono yake na kuzuia pigo lile la kichawi kwa kunyumbulisha Anga kutengeneza wigo.

Lefayette alishangazwa na tukio lile na kuhofia kwa wakati mmoja na kujiuliza inawezekana vipi Dogba kuwa na uwezo wa kutumia kanuni za anga ,mpaka hapo alijua kabisa kuna utofauti mkubwa kati yake na yeye , mwili wa Drogba umepitia mabadiliko makubwa yasiotamithilika.

Lakini hakutaka kukata tamaa , alifyatua shoka lake kuelekewa kwa Drogba , huku akiwa na asilimia chache za kufanikiwa na Drogba alitoa tabasau la kejeli.

“Dhaifu sanaa”

Aliongea na kumsogelea Lefayette kwa kasi na kumpiga ngumi nzito kwenye eneo la kifuati ambayo ilichangua mbavu zake na kumsababishia kushindwa kupumua palepale kutokana na kifua kujaa damu, hakuwa amekufa kwani moyo wake haukuwa umeathrika lakini hakuwa na nguvu za kuendelea kupambana zaidi ya kumwangalia Drogba kwa kumlaani, lakini kilichomfanya kuwa na wasiwasi na kukiona kifo chake ni kwamba mwili wake ulishindwa kujiponyesha wenyewe kama ilivyo kwa Vampire na kuna nguvu iliokuwa ikizuia kitendo hicho kutokea.

“Hii ni nguvu nguvu .. gani , Wewe bado ni Vampire kweli?” Aliuliza kinyonge lakini Drogba hakumjali zaidi ya kugeukia bahari na kumwangalia lilith ambaye alishatoka kwenye maji huku akiwa amepiga magoti akihema kama mbwa huku maji yaliolawanisha nywele zake pamoja na nguo yakitiririka kwenye mchanga.

“Lilith unajua kwamaba nilikuwa nikikupenda sana na mpaka sasa bado na kupenda , hivyo nipo tayari kukupa dili , kama utakubali kuwa kijakazi wangu nitakuacha uendelee kuwa hai”Aliongea Drogba.

“Ukoo wa Tzimsce licha ya kuwa kwenye umoja wa kishetani wa Sabbat na wanachama wake kuwa wenye roho mbaya , lakini bado wewe ni Vampire , Drogba wewe ni mjinga kweli kuitelekeza nafasi yako kama mrithi na kuamua kuruhusu mwili wako kutumika kama siraha ya kibailojjia”Aliongea Lilith.

“Mwanamke usipoteze pumzi yako kunijali mimi , nani anajali kuhusu urithi, uwezo na nguvu ndio urithi pekee , sio wewe tu hata wazazi wako hawana uwezo wa kuweza kushindana na mimi , nikitoka hapa naenda kuwaua wote na kuchukua mamlaka yote , ninakwenda kuwa mfalme na sio kupata urithi wa kipuuzi”Aliongea huku akianza kucheka.

“Usifanyishe kijogoo unaweza kweli umenishindwa mimi lakini kuna mtu huna uwezo wa kupambana nae maana umemkosea pia na huyo ndio atakuwa ni mwenye kutoa hukumu yako”Aliongea

“Oh you are saying the ever great Pluto ,Mr Roma Ramoni?”Aliongea bila hofu na kumfanya Lilith kuwa na wasiwasi , alikuwa akiamini mpaka muda huo mtu pekee ambaye anaweza kumshinda Drogba ni Roma pekee lakini kwa namna alivyokuwa akijiamini alijawa na wasiwasi.

“Lilith unaonaje tukishambulia wote , mpaka sasa anaonekana kutumia kiasi kiukubwa cha nguvu zake”Aliongea Lefayeytte aliekuwa akijitahidi kusimama.

“Usiwe mjinga wewe mrithi kutoka ukoo wa Brujah , kama kweli una nguvu za kushindana na mimi anza kunishambulia tuone utatumia dakika ngapi kuhimili”Aliongea na kumfanya Lefayette kuwa ni mwenye hasira kali mno na alijaribu kukusanya nguvu zake kusogea lakini aliishia kudondoka , muda huo huo breki za gari zilisikika mita kadhaa kutoka walipo.

Lilith ndio aliekuwa wa kwanza kuangalia ni mtu gani kaweza kufika na alijikuta akipata ahueni mara baada ya kuona ni Roma akiwa kwenye gari aina ya Lexus.

“Haha… nadhani nimekuwa na bahati kufika ndani ya muda muafaka , msongamano wa magari Kivukoni ndio umenipa changamoto”Aliongea Roma huku akimwangalia Drogba na kumfanya Lilith kutoa tabasamu hafifu.



.









SEHEMU YA 455.

Lefayette licha ya kumuona mwokozi wake alionyesha kutofurahishwa na ujio wake , aliamini huenda Lilith ndio alifanya mawasiliano na Roma na kumwambia eneo walipo, hivyo aliona kabisa Lilith alikuwa akidharau uwezo wake wa kupigana.

“Pluto nilikuwa nikikusubiria sana”Aliongea Drogba.

Roma hakumjali sana Drogba zaidi ya kumsogelea Lefayette aliekuwa akihema kwa tabu .

“Bado hujafa tu?”Aliuliza Roma.

“Usinisogelee kama kweli una uwezo pigana nae na ushinde”Aliongea .

“Ineonyesha bado una nguvu kiasi za kupigana , unaonaje nikiyakatisha maumivu yako?”Aliongea Roma na palepale aliinua mkono wake na kumpiga karate ya kichwa na kilichotokea Lefayette kichwa chake kilichanguka kama tikiti maji na Roma alitumia uchawi wake na palepale alianza kuungua kwa kasi ya ajabu mno na mwili wake kupukutika kama majivu.

“Why!!?”Lilith alijikuta akitoa macho ya mshangao kwa kitendo alichokifanya Roma.

“Mfalme Pluto kwnaini umemuua Lefayette , Adui wetu ni Drogba kutoka ukoo wa Tzimsce?”

“Lefayette amevunja sheria yangu kubwa , hua sipendi kutishiwa kwenye maisha yangu kama nakumbuka vizuri alisema angevunja shingo yangu na nilijizuia muda ule kwasababu mke wangu alikuwa amenilalia la sivyo asingefika hata hapa”Aliongea Roma na kumfanya Lilith kutetemeka , hakuamini kauli tu inaweza kupelekea mtu kuuliwa.

Lakini sio hivyo tu Roma na Camarila hawakuwa na ugomvi, hata kama hawakuwa na ushirika lakini washawahi kushirikiana kule Ufaransa , lakini Roma hakujali kabisa kama Lefayette alikuwa ni mwanachama wa Camarila lakini wakati huo huo akiutokea kwenye koo yenye nguvu ya Brujah.

“Anatokea ukoo wa Brujah na ni mtoto wa mfalme , Ulichofanya mfalme Pluto kinaweza kuku,,”

“Sijali anatokea wapi , kama familia yake inataka kulipa kisasi nipo hapa Tanzania , lakini kama wana akili ya kuchanganua mambo nadhani ni bora wapotezee”Aliongea na kumgeukia Dtogba.

“Haishangazi kwa ukoo wa Tzimsce kupenda kutumia miili ya wengine , mwili wako unatisha na ulivyo ungua ungua , Kwanini usingemuomba Yan Buwen angalau akakuchagulia mwili mzuri wakati anakufanyia majaribio?”

“Sipendi unachoongea , lakini nimependezwa na ulichomfanyia Lefayette”Aijibu Drogba.

“Kama unaonyesha humfahamu Yan Buwen , vipi kuhusu Denisi hakuwepo hapa kwa ajili ya kukupa msaada?”

“Denisi ndio nani, simjui mtu huyo mim”

“Unaonekana kweli unakitafuta kifo , unadhani nguvu aliokupa Yan Buwen inaweza kukuokoa muda huu?’

“Hapana m sifikirii kabisa kupambana na wewe kama Clone aliotuma Yan Buwen ilionyesha kushindwa kwanini mimi nishinde , nilishaandaa mpango wa kujiokoa muda mrefu tu”Aliongea kwa kujiamini na kumfanya Roma kumsogelea.

“Ilinichukua mapigo manne kuipiga na kuiua Clone , vipi kuhusu wewe ni mapigo mangapi utaweza kuhimili?”

“Mfalme Pluto kabla hatujaendelea , unaonaje kwanza ukipiga simu nyumbani luona kama wapo salama”Aliongea na kumfanya Roma kushituka baada ya kusikia neno nyumbani , alikuwa ashatuma wanajeshi wa The Eagles kutoa ulinzi sasa alijiuliza nini hakijaenda sawa.

“Ni juu yako kunishambulia, lakini naomba nikwambie kwamba inaweza kugharimu maisha ya wanafamilia wako?” Aliongea na kumfanya Roma kusita , hata hivyo alijiambia kwamba Drogba hawezi kumponyoka kwa namna yoyote ile , hivyo alitoa simu yake kujaribu kupiga nyumbani.

“Hello !”Sauti ya Blandina mama yake ilisikika lakini haikuwa sawa ni kama alikuwa akitetemeka.

“Mama kuna nini kimetokea?”

“Roma kuna mwanaume amekuja nyumbani akiwa amebeba wanaume wawili wa kizungu ambao hawana fahamu na ametuzuia tusiondoke hapa nyumbani , imekuwa bahati Sophia kaondoka mapema”Aliongea Blandina kwa wasiwasi na kumfanya Roma kupagawa na kujiuliza je ni kazi ya Yan Buwen.

Hata hivyo kusikia wazungu wawili wamepoteza fahamu alielewa kabisa ni The Eagles ambao amewatuma kwa ajili ya kuipa ulinzi familia yake.

Roma wasiwasi umemjaa na kuhisi huenda Yan Buwen akawa ameunda jeshi la watu wenye miili isio kawaida pamoja na nguvu za kucheza na kanuni za anga..

“Mama mpe simu aongee na mimi”

“Your Majesty Pluto , bado unakumbuka sauti yangu”Ilisika sauti upande wa pili na Roma kutoa macho.

“Mourihno?”Aliongea Roma na sasa kuanza kuelewa fumbo ambalo alikuwa akijaribu kulifumbua tokea siku ya jana .

“Ndio ni mimi , shukrani zikuendee ewe mfalme Pluto kwa kunisaidia kujiokoa kutoka kwa Lilith na Lefayette na kuja kuingia kwenye nyumba yako na sasa ipo chini yangu”

“Kwahio unasema ulikuwa na ushirikiano na Drogba muda wote?”

“Bingoo.. Mfalme Pluto unaonaje ujuzi wangu wa kuigiza, nadhani naweza kushinda tuzo ya Oscar , nilivyoona umeweza kununua maneno yangu nilitaka hata kucheka lakini niliishia kujizuia”

“Mfallme Pluto , Mourihno si ndio Peasant ambaye ulitaka sisi tumuachie pindi tutakapo mkamata , nini kimeenda kombo?”Aliuliza Lilith mara baada ya kusikia jina la Mourihno.

“Ngoja nikuambie miim kilichomkuta mfalme wako”

“Roma aliweza kudanganywa na Mourihno kwa kuambiwa na Mouihno alitaka kulipiza kisasi kwa kifo cha mpenzi wake wakati alipomkamata lakini huo sio ukweli, Dina alikuwa ni mpenzi wa Mourihno lakini alijifanyisha mjanja kwa kutaka kutoa siri kwenda kwa Nessa juu ya sababu ya kifo cha mama yake, nakiri Mourihno alikuwa mpumbavu kumwambia Dina siri zote , lakini hata hivyo Dina hakuwa na pakwenda kwani wakati anataka kuweka ukaribu na Nessa kwa kumwambia siri iliofukiwa miaka mingi aliweza kumzuia , Lilith mwanaume unaejisifia kumwita Mfalme hana lolote na ameweza kudanganyika kirahisi”Aliongea Drogba huku akainza kucheka.

Ujio wa Nessa Nchini Tanzania haukuwa wa bahati mbaya hata kidogo, ni kweli msanii wa kimaifa Nessa alikuwa kwenye Tour dunia nzima , lakini ratiba yake haikuwa ikimwambia kwamba angeweza kufika nchini Tanzania , maamuzi ya kuja Tanzania akitokea nchini China aliweza kuyafanya mara baada ya kupokea ujumbe kutoka kwa mtu asiojulikana unaosema kwamba alikuwa na siri nzito iliokuwa ikihusiana na kifo cha mama yake mzazi Ms Doleres.

Mpaka leo hii kifo cha Ms Doleres kutoka Ireland kilikuwa kina utata mwingi licha ya taarifa iliotolewa kuonyesha alijizamisha kwenye swimming Pool akiwa hotelini kutokana na tatizo la Sonono.

Kama ijulikanayvo kundi la Cranberries ilikuwa ni Band maarufu ambayo ilikuwa ikipigania sana haki za raia kupitia nyimbo zao , ni kama hata Tanzania uwafananishe na msanii Roma Mkatoliki ambaye hana uwoga kuwaponda wanasiasa, basi ndivyo ilivyokuwa kwa Ms Doleres, haikueleweka ni siri gani ambayo ilifasababisha kifo chake lakini ni dhahiri kwamba aliuliwa na wahusika wakuu ni jamii ya watu wanaojiita Vampire.

Ikumbukwe kwamba mume wa Ms Doleres pia alikuwa ni Vampire hivyo pia kwa mtoto wao Nessa ambaye ni msanii.

Sasa Dina aliweza kupata ubuyu wote kutoka kwa Mourihno juu ya sababu ya kifo cha Ms Doleres na baada ya kupata siri hio aliona nikama kadi muhimu sana ya kuicheza kama tu atataka kuwa na ukaribu na msanii mkubwa duniani ,ni rahisi kusema kwamba Dina msukumo wake ulikuwa ni kutokana na kuogopa kufunikwa na kimuziki na Sophia , hivyo alitaka kumtumia Nessa ambaye alikuwa tishio kubwa kwenye mziki kwa kutumia siri aliopata kwa Mourihno , lakini asichokifahamu ni kwamba mchezo wake uligundulika mapema tu mara baada ya taarifa kumfikia Mourihno baada ya ujio wa Nessa nchini Tanzania, hivyo kuuliwa kabla hajaweza kutoa siri,

Hivyo hitimisho tamaa ndio iliomuua msanii Dina na hivyo kujibu maswali ya Roma kwamba kama kweli Dina alikuwa akibadilishwa kuwa Vampire kwanii Vampire hao hao wamuue.

Lilith alijikuta akishangaa mara baada ya kusikia habari hio kwamba Roma aliweza kuchezewa akili na Mourihno.

Upande wa Roma alijikua akikunja ngumi yake kwa hasira, ilikuwa ni sahihi kwake kufikiria kwamba The Eagles wameweza kuzibitiwa kirahisi kutokana na kwmaba Vampire ni viumbe ambavyo vina uwezo mkubwa wa kumlewesha binadamu na kumuamuru kufanya watakvyo.

Lakini kitu kingine ambacho Roma kilimkasirisha zaidi ni namna ambavyo alidanganywa na kuingizwa kwenye mtego bila ya yeye mwenyewe kujua na kumuachia mhusika kundoka bila ya yeye mwenyewe kufahamu.

“Vipi naweza sasa kuondoka.?, Naamini kabisa mfalme Pluto huwezi kuhatarisha maisha ya wanafamilia wako kwasababu tu unahitaji kuniua”Aliongea Drogbs

Mpango wao ulikuwa mwepesi sana , Drogba alifahamu kwamba hana uwezo wa kushindana na Roma hivyo walipanga kwanza kuiteka familia ili Drogba atakapotoweka na Mourihno angeiteka familia ya Roma na kukimbia nayo mpaka msaada wa Yan Buwen utakapo wafikia na hapo ndipo Lilith atakuwa hana uwezo wa kuwanasa na kifaa chake na wataweza kucheza na Roma kupitia udhaifu wa familia.

“Mfalme Pluto kwanini tusimuache tu akaondoka, sio kosa lako , ni tabia yake kuwa mjanja , familia yako kwasasa tuiweke kipaumbele”Aliongea Lilith lakini Roma bado hakujibu , alionekana kuwa kwenye tafakari

“Mfalme Pluto nakushauri uzingatie hili , Drogba ni mtoto wa Prince Raphaeli kutoka koo ya Tzimsce , ukimuua inamaanisha kwamba unatangaza vita na ukoo wetu hawapo kwenye ushirikiano mzuri na kundi la Sabbat na baba sikuzote amesema hatupaswi kumchokoza Prince Raphaeli kutokana na uwezo wake mkubwa wa mapambano”Aliendelea kuongea Lilith.

“Lilith asante kwa maneno yako , lakini niseme tu kwamba siku hizi mbili nilisahau kwamba viumbe hivi damu yao ni ya baridi tofauti na binadamu ndio maana nikadanganyika kirahisi”Aliongea Roma na kumfanya Lilith kuguna lakini Roma alitabasamu kifedhuli.

“Unajua ni kosa gani kubwa ambalo umeweza kufanya?”Alimuuliza Drogba ambaye aliishia kushangaa.

“Kosa gani?”Aliuliza kwa hofu.

“Vizuri , siwezi sana kukulaumu kwa kutokufahamu , na nimekuja hapa kwa kutumia usafiri kwa kuogopa malipizi”Aliongea na kumfanya Drogba asielewe

“Acha majigambo na kujifanyisha, huna lolote la kunifanya , ukijaribu kunishambulia Mourihno ataweza kugundua mapema kwani kuna kifaa maalumu ambacho kitafanya kuona nguvu zangu zikiniishia na hapo hapo atachukua hatua ya kummaliza mama yako , sina muda wa kucheza mchezo na wewe mim”Aliongea.

“Hili sio mchezo” Aliongea Roma na palepale alipotea na kumfanya Drogba kuchanganyikiwa , lakini kabla hajaelewa kinachoendelea Roma huyu hapa na alitumia staili ile ile aliomshambulia Lefayette lakini awamu hii aliongeza nguvu kidogo na kufanya kichwa cha Drogba kuvunjika palepale na kugeukia mgongoni.

Kitendo kile kilimuacha na hamaki Lilith kwa kudhania kwamba Mourihno angeua familia ya Roma, lakini ile anaangalia vizuri , Roma hakuonekana tena mbele yake akawa amepotea mara baada ya kumpiga Drogba.

Upande mwingine ndani ya sekunde ile ile upande wa Ununio , mkono mrefu ambao haukujulikana umetokea wapi , ulitokezea kwenye hewa na kuishika shingo ya Morihno kwa nguvu wakati akijiandaa kumcharanga Blandina kwa panga.

Hata yeye alishangaa nguvu ya ajabu ikimvuta , lakini alichelewa kwani mkono ule ulikuwa na nguvu sana na ulienda moja kwa moja eneo la moyo na kubomoa kifua na kuunyofoa moyo wote nje na ikawa mwisho wa maisha ya Mourihno.

Blandina na Bi Wema walitoa ukulele kwa tukio lile kwani walishangaa midamu ikiwarukia pasipo ya kuelewa nini kimetokea.

Upande wa huku Kigamboni wakati Drogba alipojirudisha hai kwa mara nyingine palepale Roma alijitokeza mbele yake tena na Drogba alishindwa kujilinda kwani ilitokea ghafla sana na sekunde ya pili ni kwamba moyo wake uliachana na mwili wake palepale na kuwa kwenye mikono ya Roma,

Lilith kitendo kile kilimfanya apige magoti pasipo ya kuelewa mwenyewe huku mdomo ukiwa wazi akishindwa kuamini namna hali ilivyogeuka na kuanza kumuogopa Roma palepale.

Drogba bado hakuwa amekufa , licha ya moyo wake kutolewa lakini ilimaanisha kwamba hana dakika nyingi angepoteza maisha kama moyo wake usingerudishwa kwenye kifua chake, hivyo aliishia kumwangalia Roma kwa macho ya kumwambia anaomba moyo wake tafadhari.

“Niambie Yan Buwen yuko wapi, unadakika moja tu kabla moyo wako haujapoteza uwezo wake?”Aliuliza Roma huku akitishia kuuyeyusha moyo wa Drogba.

Alitaka kujua alipo Yan Buwen kutokana na kwamba watu wake waliweza kutafuta kona zote za dunia pasipo ya kupata taarifa ya mahali alip.

“Hahaha… Hahahaa….”

Alichena na kisha alidondoka chini na kupiga magoti huku akitema damu , hakua na uwezo wa kujiponyesha tena kwasababu mwili wake hauna moyo na ni nguvu ya jiwe la kimungu pekee ambalo lilimpa uwezo wa kuongea kwa dakika chache.

“Kabla sijakufa naomba nikuambie hivi , Hades huna uwezo wa kumzidi Yan Buwen kwa namna yoyote na siku atakayorudi ndio itakuwa mwisho wako , sijutii kufa kwa ajili yake kwani naamini kisasi changu atakilipi… za.”Aliongea na palepale alidondoka chini akionyesha hayupo tayari kutaja mahali Yan Buwen alipo.

“Huwe….wezi, kumpata … Yan Buwen mpaka siku atakayokutafuta ,, ye ..ye mwenye,,, kwa ajili ya kuku.. kuku..”Alishindwa kumalizia kauli na palepale ikawa ndio mwisho wa uhai wwake

Roma hakuona haja ya kuendela kushikilia moyo wake zaidi ya kutumia nguvu ya kimaandiko kuuyeyusha pale pale na kisha akamkausha na Drogba palepale na kuwa majivu pasipo kuacha ushaihidi wa aina yoyote.

Lilith kuona namna Drogba alivyomalizwa na kuwa majivu ,alijihisi kukosa pumzi, alikuwa akijua uwezo wa Roma kuwa mkubwa lakini namna alivyodhibiti watu wawili waliopo sehemu mbili tofauti kwa wakati mmoja ilikuwa ni jambo la kushangaza

Ukumbuke sasa hapa Roma macho yake yalikuwa ni ya njano kama jua licha ya kwamba mwili wake haukubadilika kama ilivyokuwa miezi kadhaa nyuma kabla hajapitia steji za kupanda levo za nguvu ya kimaandiko za kijini.

Lilith hisia zake alizokuwa nazo juu ya Roma zilikata palepale kwa kumugopa na alijiambia ni kheri akawa na urafiki wa kawaida tu na sio wa kimapenzi alikuwa ashashuhudia watu wenye uwezo wa ajabu lakini kwa Roma alijawa a hofu hata ya kumsogelea tena.

…………………….

Baada ya Mourihnno na Drogba kudhibitiwa ilibidi Mage kwa kushirikiana na jeshi la polisi watengeneze ushahidi ambao ulithibitisha kwamba Recho hakuhusika na mauaji ya msanii Dina.

Wanasema hata kama vyombo vya habari viwe na ukubwa gani lakini mwisho wa siku vipo kwenye mikono ya serikali , hivyo ushahidi feki uliotolewa ulisambazwa kwa kasi mno na ndani ya muda mfupi swala la Recho kumuua msanii Dina lilipotelea hewani.

Lilith alimuaga Roma na kusema atarudi nyumbani na kuhakikisha kwamba hakuna kitu kitatokea kwa kuhusika na kifo cha Lefayette na Roma hakujali sana alimwambi aafanye vile atakavyoona inafaa.

“Nguvu alizoniachia Hades nilidhani hazitofanya kazi , lakini inaonyesha uwezo wa kucheza na kaununi za anga pia ninao, nilihofia muda mrefu kuzitumia nahisi ni wakati wa kujifunza kutumia mbinu zote”Aliwaza Roma wakati akiendesha gari kuelekea nyumbani kwake.

Ndio Roma alishawahi kuachiwa nusu ya nguvu za kunyumbulisha kanuni za anga na Hades wa Zamani lakini hakuwahi kuzitumia kutokana na kwamba alihisi zisingefanya kazi kwa upande wake.

Kitendo cha kumshambuliaMourihno na Drogba kwa wakati mmoja licha ya kwamba walikuwa sehemu mbili tofauti ilikuwa ni kutokana na kucheza na kanuni za anga na ku’fold space’ hivyo kumpelekea kuwa sehemu moja kwa wakati mmoja lakini kuwa kwenye maeneo tofauti , ulikuwa ni uwezo wa ajabu sana lakini jaribio lake lilimfumbuliajambo jipya kuhusu kanuni za anga.

Lakini licha ya hivyo mbinu zake zilikuwa za chini mno kufananisha na zile ambazo anatumia Athena..

Roma kutokana na kusikia habari za Yan Buwen alizidi kuhimiza watu wake kuongeza kasi ya kumtafuta , lakini wakati huo huo akiongeza wanajeshi ndani ya Tanzania kwa ajili ya ulinzi.

Hatimae mwezi mmoja ulipita tokea tukio la kifo cha Dina na Vampire Drogba na Mourihno.

Lanlan aliweza kuandikishwa shule ndani ya mwezi huo huo mmoja , shule ambayo ilikuwa maarufu kwa watoto wa vigogo wengu kusoma hapo na wale wa matajiri , iliokuwa ikitumia mtaala wa Cambridge, ilimchukua siku chache tu kwa Lanlan kuzoea mazingira ya shule na hatimae kuweza kupata rafiki.

Lakini licha ya hivyo Lanlan alileta gumzo na mshangao kwa wengi kwani licha ya umri mdogo aliokuwa nao alionyesha uwezo mkubwa mno wa akili , jambo ambalo liliwafanya Roma na Edna kufika shuleni kwa majadiliano na walimu na makubaliano yalifanyika Lanlan asianzie chekechea bali aanze darasa la kwanza kabisa.

Kitendo cha Lanlan kupata rafiki ndio mwanzo wa mwanafunzi mmoja kupigwa mpaka kuzimia.

Itaendelea siku kesho tumalize tukio la kumuona mshrika mkuu waAthena then twende sasa Korea Kusini.

Nawakumbusha Kuna jiwe moja ambalo lina Roho ya Gaia halijapatkana lakini pia kuna kisa kilichopelekea Athena kumuua Hades wa Zamani.

Najma anaendeleaje huko alipo Aluta Continuara kesho mapema , vipande vitatu.
Actually good
 
SEHEMU YA 459.

Roma alisimama mara baada ya Hermes kumwambia ana uhakika gani alichomwambia alikuwa akidanganya.

“Mpaka sasa nipo kwenye mshangao , Aphrodite aliniambia ukiachana na Zeus na Athena , Poseidon ndio mwenye nguvu zaidi anaefuatia lakini nikikuangalia naona unao uwezo mkubwa kuliko wa Poseidon mathalani kwenye mbinu yako ya kuweza kumdhibiti mtu kupitia ndoto, hio ni zaidi ya kanuni za anga na nina wasiwasi kama tukipigana hapa nitaweza kukushinda na kama pia ungeamua kunikimbia nisingeweza kukukamata kwani wewe ni Vampire na mnasifika kwa mbinu mbinu nyingi likija swala la kujificha.

“Kwa hio huo ndio mchanganuo wako?”Aliuliza Hermes.

“Kuna zaidi ya nilichosema?”

“Bila shaka , Hao wazee muda mwingi wanajichukulia kama ndio wenye nguvu kuzidi wengine lakini nikwambie wana nguvu kwasababu binadamu wanawaogopa , Vampire wana uwezo mkubwa zaidi kuliko kiumbe chochote , nilikuwa ndani ya huu mwili kwa miaka elfu moja, wakati wao wakizaliwa upya kwenye miili mingine mimi bado nilikuwa nikiendelea kuishi , unaweza kusema pia nilikuwa dhaifu lakini nilipokuja kuwa Vampire nguvu zangu zilikuwa maradufu zaidi kuliko Poseidon”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa kwani tofauti na wengine wote walikuwa wakivaa miili tofauti tofauti ya binadamu kila pale unapozeeka na kuhamia mwingine , lakini kwa Hermes alimaaisha kwamba yeye mwili wake ni huo huo na hajaubadilisha kwa milenia moja kwasababu alikuwa ni Vampire.

“Kama kweli umeweza kuishi kwa kuwa Vampire naweza kuamini kwamba una cheo kubwa katika jamii yako , lakini kwanini sijawahi kukusiakia hapo kabla?”Aliuliza Roma.

“Nadhani ushawahi kunisikia , jina langu la kibinadamu ni Raphaeli”Aliongea na Roma sasa kuelewa lakini alijikuta akishangaa.

“Raphaeli ! Unamaanisha kiongozi mkuu wa kundi la Tzimsce ?’

“Upo sahihi , siku nyingi nilikuwa nikiishi kwa kuficha ubini wangu kwa wengine kwani niliona haina maana , hivyo maisha yangu yamekuwa ya siri , Drogba ni mtoto wangu niliemzaa miaka zaidi ya mia mbili iliopita”Aliongea

Roma alishangaa kwani miaka kadhaa iliopita alishawahi kukutana na mtoto wa Christen afahamikae kwa jina la Judy hivyo ikawa mara yake ya kwanza kushuhudia mtoto wa miungu , lakini kusikia Drogba alikuwa mtoto wa mojawapo ya miungu ilimshangaza.

Judy ni mtoto wa Christen na Hades wa Zamani na kipindi cha nyuma wakati Roma akiwa bado ni Agent code 13 alimuua baada ya kuingia kwenye kumi nane zake , ilikuwa ni taarifa ya kusikitisha kwa Christen na Hades lakini kwasababu mwenye makosa wakati huo alikuwa ni Judy Roma hakulaumiwa.

Roma pia ashawahi kusikia kwamba ukoo wa Tzimsce ulikuwa mkubwa likija jamii za Vampire au wanywa damu na hata Prince Sergeras baba yake Lilith alikuwa akiogopa sana ukoo huo , lakini Roma hakuwahi kujua aliekuwa akiogopwa ni Hermes , ilikuwa ikiletea maana sasa.

“Kwahio umekuja Tanzania kwa ajili ya kulipiza kisasi kwa kile nilichomfanyia mtoto wako?”

“Huyo ashakufa tayari kuna haja gani ya mimi kulipiza kisasi , alikuwa akinichukiza na tamaa yake ya madaraka na ndio maana nilimfukuza kwenye ukoo”Aliongea na kumfanya Roma kutabasamu.

“Lakini ukweli ni kwamba hata kama ningejaribu kupigana na wewe nina wasiwasi naweza nisikushinde lakini naamini usingeweza kuniua pia na mimi nisingeweza kukua hivyo haileti maana kupigana na wewe, Hivyo Mr Roma Ramoni nirudishie Headphone zangu”Aliongea.

“Hizi Headphone siwezi kukupatia na kingine usije ukaingilia mambo yangu tena kama ulivyofanya leo”Alitoa onyo

“Lakini hizo ndio chaguo langu la muda wote huwezi kuzichukua”

“Ninaondoka”Aliongea Roma na Hermes alimkimblia akitaka kumpokonya lakini Roma aliita nguvu za kijini na kuzigeuza siraha kisha akampiga nayo Hermes tumboni na kuishia kuugulia maumivu , lakini Hermes na yeye palepale aliita uwezo wake na kisha kuanza kucheza na kanuni za anga na kutengeneza matabaka ya anga msambo na kisha alirudishwa nyuma kwa spidi , Roma alijikuta akishangazwa na kitendo kile kwani kutumia kanuni za anga ni nguvu kubwa iliohitajika lakini kwa Hermes ilionyesha rahisi kwake.

“Damn it Hades, are you seriously doing this?”Aliuliza kwa kuchuki.

“I’m not interested playing games”Aliongea Roma akimaansiha havutiwi na michezo michezo.

“Okey tufanye umeshinda , Headphone zangu hizo ni za gharama sana hivyo ninakupatia kama zawadi, nimekuja kukupa tahadhari lakini naona haunichukulii siriasi , kwa heri”Aliongea na palepale aliita mabawa yake maarufu kama Sandals Talaria na kupaa huku akionekana angani kama malaika wa mabawa mawili.

Roma alijua kabisa kama angepambana na Hermes huenda ingemchukua muda mwingi kushinda kwani alikuwa na mbinu nyingi za kutoroka ukizingatia na uwezo wake wa anga lakini pia uwezo wake wa kujitengenezea mabawa lakini pia kuwa Vampire.

Roma hakutaka kukaa eneo hilo kwa dakika nyingi zaidi , kwani alijua familia yake ingekuwa kwenye wasiwasi , hivyo alipotea na kutokezea nje ya geti na kisha akaingia ndani.

“Mjomba ulienda wapi kila mmoja alikuwa na wasiwasi”Aliongea Donyi baada ya kufungua geti.

“Si nilisema naenda kukutana na mtu?”Aliongea Roma na kupita na kisha alisogea mpaka kwenye meza na kuweka zile Headphone juu yake.

“Mnaonaje hizo ni nzuri?”Aliuliza akiwafanya wote kuangalia zile Headphone

“Hizi si Headphone..?”Aliongea Sophia kwa namna ya kushangaa.

“Sophia mbona umeshangaa hivyo , ni Headphone ndio?”Alijibu Donyi

“Ah.. ninachotaka kumaanisha ni kwamba hizi ni za utofauti sana , hata ninazotumia sio kama hizi , inaonyesha hizi ni gharama kubwa”

“Uko vizuri Sophia inaonyesha fani yako ya mziki inakufanya kutofautisha baadhi ya vitu, hizi ni ‘electrostatic headphone’ kutoka Ujerumani zinazofahamika kwa jina la Sennheiser’s Orpheus , zipo jumla ya 300 dunia nzima ambazo zimewahi kutengenezwa , Ninakupatia kama zawadi yangu kwako”Aliongea Roma.

“Brother kwa hio hizi ndio Orpheus nishawahi kuzisikia kutoka kwa rafiki yangu nilipokuwa masomoni nje ya nchi inasemekana moja thamani yake ni zaidi ya milioni mia moja na nusu za kitanzania”Aliongea Kasimu na kumfanya Sophia kutetemeka na kuziweka chini na kumpatia Roma.

“Bro kwanini usizitumie wewe , ni ghali sana kwangu”Aliongea

“Usijali mimi na dada yako Edna hatusikilizi sana mziki hivyo zinakufaa wewe msanii , Edna ndio ambaye siku zote amekuwa akikupatia zawadi lazima na mimi angalau nitoe zawadi kama shemeji yako?’Aliongea Roma.

Ni kweli Sophia aliweza kuzawadiwa gari na Edna yenye thamani kubwa kampuni ya Bentley. ni aina ya gari ambazo ni chache sana ndani ya Tanzania hivyo Roma aliona itakuwa sawa na yeye kutoa zawadi.

Sophia alijikuta moyo wake ukipiga kwa nguvu mara baada ya kusikia neno Shemeji , ilikuwa mara yae ya kwanza Roma kuongea hivyo na ilikuwa ni kama anaweka mpaka kati yake na yeye.

Watu wote walielewa maeneno ya Roma na kuishia kumuonea huruma Sophia , hata Edna aliona maneno yake yamekaa kikatili lakini aliona ni afadhali kwani hakujua angejisikiaje kama Sophia akiwa mpenzi wa Roma.

Kama Sophia angekubali zawadi hio inamaana angehesabika kwanzia siko hio kama shemeji rasmi na kuachana hata na jina la Bro.

“Bro kwahio unataka nikuite shemeji kwa kunipa hizi Headphone pekee?”Aliuliza Sophia na kufanya hali ya hewa kubadilika , lakini hakujali zaidi ya kuzichukua na kuzikumbatia.

“Asante kwa zawadi lakini hazitoshi kama zawadi kutoka kwa Shemeji , unatakiwa kuelewa mimi ni mtu maarufu mwenye hadhi hivyo nategemea kitu kikubwa zaidi”Aliongea huku akiweka tabasamu kuonyesha kwamba amekubali na kila mtu alivuta pumzi ya ahueni.

Na ndio hivyo Sophia ukawa mwanzo wa kumuita Roma Shemeji kutoka kwenye jina la Bro Roma.

Baada ya kuongea ongea kwa muda mfupi kidogo ilikuwa ni saa kumi hivyo kila mmoja aliaga na kuondoka na wa mwisho kabisa alikuwa ni Omari Tozo.

“Nipigie muda wowote ukiwa na shida,, hata mrembo Queen hapa akikusumbua niambie tu nitakusaidia”.

“Una uhakika utanisaidia katika hilo?”

“Ndio nitahakikisha nakufariji”

“Aah.. Nikajua unasema utanisaidia kumrudisha kwangu”

“Hio sio kazi yangu ukiachwa umeachwa na mimi kama rafiki yako nitahakikisha nakusaidia lesso ya kufutia machozi”Aliongea Roma na Omari alionekana kutopenda maneno yake na kufungua gari lake mlango.

“Shemeji Edna nitakupigia wa kwanza kukutaarifu siku ya harusi yangu na Queen”Aliongea Omari.

“Nitarufahi nikiwa wa kwanza”Aliongea Edna akipunga mkono na kisha akamgeukia Roma na kumwangalia kwa dakika kadhaa na kisha akaingia kwenye gari lake na kuondoka.

Roma alitambua kitendo cha Omari kupigana na Denisi ilikuwa ni kumsaidia maana wakati ule hata yeye hakujua namna ya kumchukulia Denisi hatua lakini ni shukrani kwa Omari aliweza kutatua tatizo kwa kumshugjulikia kisawa sawa Denisi , ijapokuwa alikuwa ametoroka lakini aliamini ilikuwa ni adhabu ya kutosha kwake.

Siku iliofuata Sophia alihamia rasmi katika nyumba ya kigamboni, upande wa Blandina na yeye baba yake afya yake haikuwa sawa hivyo ilimbidi kuondoka kwenda kumhudumia kwa muda, hivyo familia ikabakia watu wachache sana , lakini hata hivyo haikupoa kwasababu ya uwepo wa Lanlan.

Ilikuwa siku ya jumapili Roma , Edna na mtoto wao Lanlan walitoka kwenda matembezini , sehemu walioichagua siku hio ilikuwa ni kwenye hoteli moja iliokuwepo Kigamboni ambayo ilikuwa na Zoo ya wanyama, walichagua sehemu hio kutokana na Lanlan kutaka kwenda kuona wanyama.

Safari yao ilianza asubuhi, ilikuwa siku nzuri sana kwa Edna kutoka kama hivyo akiwa yupo na Roma pamoja na mtoto wao wa kumlea.

Ktuokana na mazingira ya hoteli hii maarufu kuwa tulivu sana na ya kuridhisha ilimfanya Edna kuwa na utulivu wa akili wa hali ya juu sana na kufurahia mazingira , walifanya mambo mengi ya kufarahisha na kuwa kivutio kwa wageni kadhaa waliokuwa wapo pia katika maeneo hayo.

Jambo ambalo liliwafanya watu wengi kushangaa ni pale Lanlan alipokataa kupanda na Roma kuendesha farasi akitaka yeye kuendesha mwenyewe.

“Lanlan anataka kuendesha mwenyewe farasi”

“Lanlan utadondoka , panda na baba yako”

“Lanlan hawezi kudondoka na babu aliniacha nikapanda mwenyewe”Aliongea Lanlan na kumfanya Edna kumwangalia Roma , walijua jina la babu lilikuwa likitokea wapi , walijua lazima angekuwa ni Afande Kweka.

Edna ilibidi amuangalie Roma kuona anasemaje na Roma alimwambia amuache afanye anavyotaka , Edna alikuwa na wasiwasi lakini Roma hakuwa na wasiwasi , kwanza alikuwa akijua Lanlan hakuwa mtoto wa kawaida.

Lanlan ilionyesha kweli alikuwa na uwezo wa kuendesha farasi , kilichoashangaza watu hata yule ambaye anawahudumia wanyama na kuongoza wageni katika Zoo ni namna pekee ya Lanlan kuamrisha Farasi kutembea kwa namna ya tofauti kabisa , hata Roma mwenyewe alishangazwa na kitendo hicho, ijapokuwa halikuwa jambo jipya kuliona kwenye maisha yake lakini kwa umri wa Lanlan kuweza kuwasiliana na wanyama lilimfanya kujiuliza maswali, aliamini huenda ndio maana muda mwingi Lanlan alikuwa akipenda kuona wanyama kuliko kitu kingine.

“Lanlan nani kakufundisha kuongea na wanyama?”Aliuliza Roma

“Ni mama yake Lanlan” Alijibu kwa Kingereza huku akimshika Edna akionyesha kufurahia sana kuja eneo hilo kwa siku hio.

Sasa muda huo huo wakati wakipata chakula cha mchana, upande mwingine ndani ya hoteli hio hio Rufi alikuwepo akiwa ameambatana na Mika na walikuwa wamekaa upande mwingine , muda wote ambao Roma alikuwa akimsaidia Edna kupanda kwenye Farasi alikuwa akiona kila kitu.

Wakati wakiwa wamemaliza kula ,Edna alipokea simu kutoka kwa Rufi na haikujulikana alikuwa akiongea nae nini , lakini Roma alijua Edna anaongea na Rufi na ile anamaliza kuongea alirudisha simu chini.

“Alikuwa anaongea nini?”Aliuliza Roma kwa shauku ya kujua mke wake alikuwa akiongea nini na Rufi.

“Aliniambia kuna kitu anataka kuniambia , ambacho alipaswa kuniambia siku ile ile niliokutana nae”Aliongea na kumfanya Roma moyo wake kupiga Paah.

“Edna yule msichana sio mtu mzuri na anakutumia tu”Aliongea Roma na kumfanya Edna kumwangalia Romakwa mshangao.

“Unamaanisha nini kusema ananitumia?”Aliuliza Edna na kumfanya Roma kujilaumu na kuona ametumia kauli ambayo hakupaswa kuongea , lakini hata hivyo alikuwa na hofu kama Rufi ataongea ukweli kabla yake..

“Edna kuna kitu sijakuambia kuhusu Rufi… , najua unaweza kukasirika lakini nilishawahi kukutana nae L.A Marekani”Aliongea Roma kwa upole sana kama sio yeye vile , ijapokuwa alifahamu hakupaswa kuliongelea jambo hilo kwa muda kama huo ambao wamekuja kufurahi ,lakini aliona ni kheri Edna kufahamu mapema kuliko Rufi kumwambia.

Kauli ya Roma ni kama ilitafisirka kwa namna ya tofauti kwenye kichwa cha Edna , kwa mwonekano wa kirembo wa Rufi aliamini kama kweli Roma aliweza kukutana na Rufi basi ni lazima ilikuwa zaidi ya kukutana.

“Edna nilipaswa kukuambia pale hospitalini lakini ukweli alikudanganya alijifanyisha kugongwa na gari ili kujenga ukaribu na wewe”Aliongea Roma na kumfanya Edna kumkata jicho na palepale alichukua simu yake kwenye meza na kumpigia Rufi.

“Sitojali kama ulijifanyisha kugongwa na gari yangu kwa makusudi , lakini nipe jibu moja ni uhusiano gani unao na mume wangu?”Aliuliza Edna baada ya simu kupokelewa.

“I… we,,,we met in LA”Rufi alisikika akijing’ata ng’ata meneno akimaanisha kwamba wamekutana Loss Angeles.

“Ilikuwa ni lini?”

“Miezi miwili na wiki tatu zilizopita”Alijibu na kumfanya Edna akili yake kufanya kazi kama mashine , alikumbuka mara ya mwisho Roma kwenda Marekani ni miezi miwili iliopita.

“Na mlifanya nini mlivyokutana?”Aliuliza Edna kwa kingereza.

“We…we.. did that..”Aliongea na kumfanya Edna kukunja sura .

“That!?”Alijuliza na kufikiria kwa muda na alijikua akielewa alichomaanisha.

“Miss Edna naomba unisamehe kwa kutokukuambia , lakini .. lakini nampenda sana Roma, tulipiga hata picha tukiwa kitandani, ninaweza kukutumia uzione”Sauti ya Rufi ilisikika , ilionyesha alidhamiria kwa asilimia mia moja kumharibia Roma kwa mke wake , sasa haikueleweka ni wivu alioupata alivyowaona wakiwa wapo pamoja au alipanga kuongea ukweli , baada ya simu kukatwa picha zilitumwa palepale na Edna alifungua moja moja na alipojaribu kuchunguza mazingira aligundua kabisa ni picha zilizokuwa zimepigwa hotelini.

Mpaka hapo Roma aliamini kabisa Rufi alikuwa akimfanyia makusudi lakini muda huo hakuwa na namna ya kuchukulia swala hilo hatua, Edna aliona picha na Rufi hakutuma vidio yenyewe lakini hata hivyo ulikuwa ushahidi wa kutosha kabisa ambao hata hivyo Roma alikiri mwenyewe kwamba amekutana nae LA.

Edna alijikuta akiinua macho yake na kumwangalia Roma na chozi hakuelewa hata machozi yalimtoka wapi , lakini yalianza kujitengeneza na kutiririka kama mto.

Hakuamini mwanaume anaefahamika kwa jina la mume wake ndio huyo ambaye yupo uchi kwenye picha akiwa kitandani na msichana Rufi.





SEHEMU YA 460

Roma alijikuta akiumia kumuona Edna kutoa machozi namna hio , alishukuru Lanlan alikuwa akicheza upande mwingine hivyo hakusikia hayo mazungumzo.

“Kwanini hukuniambia tokea mwanzo kama alikuwa na yeye ni mwanamke wako , unao wanawake wengi na umekuwa hata na ujasiri wa kuwakaribisha mpaka nyumbani umeshindwaje kuniambia na huyu ni wa kwako au kwasababu unao wengi sana kiasi cha kusahau mahesabu si ndio”Aliongea Edna huku sauti yake ilikuwa kavu mno akimfokea mfalme Pluto.

Roma alifumba macho yake na kuvuta pumzi nyingi , hata hivyo ndio alienzisha hayo maongezi hivyo alitakiwa kujitetea na kumtuliza.

“Edna ni kweli nilikutana nae Marekani na kwangu nilimchukulia kama ‘Onenight stand’ lakini nakuapia sina hisia zozote na yeye, unaweza kusema ni ajali , huwezi kusema ni mpenzi wangu .. alichokuambia ni kujaribu kunisingizia tu”

“Kimyaa!!”

“Rufi ni msichana wa kawaida unawezaje kusema anakusingizia ukijumlisha na uwezo usio wa kawaida uliokuwa nao , unanifanya mimi ni mtoto mdogo si ndio?”Aliuliza na kumfanya Roma kukosa jibu , ukweli ni kwamba siku aliokutana na Rufi alijua uwepo wa zile Kamera za siri ,lakini kwasababbu alijua asingeweza kukutana na Rufi tena ndio maana hakuchukua hatua yoyote..

“I’m sorry”Aliongea .

“Unaomba msamaha tena , unasaidia nini kwenye hali kama hii , kama hili lingetokea zamani ningekubali lakini ni juzi hapo tu , kama huna mpango wa kuachana na tabia yako kwanini unataka kufunga ndoa na mimi?”Aliongea huku machozi yakiwa yanamtoka lakini Roma alishindwa kujjitetea.

“Nina weza kupotezea swala la wewe kuwa na wanawake wengine ambao unawapenda kupitiliza lakini siwezi kuvumilia kitendo chako cha kunidanganya, umenidanganya umeenda Loss Angeles kumsaidia Christen kumbe ulimfuata mwanamke”

“Edna .. najua umekasirika na lilishatokea tayari lakini Rufi ni mwanamke hatari na nilitaka kukuambia mapema”

“Wewe ndio hatari zaidi kwangu , siku zote unaniambia kwamba utakuwa muwazi kwangu kwa kila kitu lakini kumbe maneno yako ni tofuati na vitendo, Wewe ni muongo Romaa”.

Uzuri wa hoteli hii ni kwamba kila nyumba ilikuwa ikijitegemea na ilikuwa imejitenga na nyumba zingine hivyo hakuna ambaye alikuwa akiona ugomvi huo kwani ni hoteli iliokuwa ikipokea wageni wa kifamilia.

Edna alishindwa kuongea zaidi na alichukua mkoba wake na kutoka akimuacha Roma ,mpango ulikuwa ni kuamkia ndani ya hoteli hio lakini hakuwa na uwezo wa kumvumilia Roma ambaye muda huo alihisi kumchukia.

Alijifuta machozi na kutoka nje kuelekea eneo la maegesho ya magari, wakati akiwa anafungua mlango wa gari waliokuja nalo alijikuta akikumbatiwa miguuni na alipogeuka alijikuta akimwangalia Lanlan ambaye alikuwa akitoa machozi na alichuchuma chini na kisha akamkumbatia huku akijiona mkosaji kumsahau kwasababu ya hasira zake.

Hasira zake zilimfanya kumsahau Lanlan na alijiuliza kama Lanlan aliweza kusikia ugomvi wao na Roma.Dakika chache mbele Edna aliondoka na Lanlan ndani ya hoteli hio, na siku yake ilioanza vizuri ikawa imeingia doa..

Roma akili yake ilikuwa ikizunguka na alijikuta hata akijilaumu kumwambia mke wake ukweli , aliona huenda angemdhibiti Rufi kabla hata hawajakutana na mke wake , huenda ingekuwa afadhali lakini kwasababu ambazo yeye mwenyewe hakuwa akizijua aliamua kuchukua maamuzi ya kumwambia.

Alijilaumu kwa kutochukua tahadhari siku ile ile pale hospitalini lakini kwa stori ya Rufi kutaka kumtafuta mzazi wake nchini Tanznai ndio iliomfanya kusita kutokuchukua hatua.

Wakati akiendelea kuwaza mlango ulifunguliwa na aligeuka kwa kudhania ni Edna karudi lakini bahati mbaya ile sura ya mtu aliemuharibia na mke wake ilitokeza mbele yake.

Roma alijjikuta akimwangalia Rufi huku akishindwa hata kujielewa , alijikuta hata yeye akijidharau na kujiuliza kwanini maisha yake yamebadilika kiasi hicho na kuendeshwa na mwanamke, ilikuwa kama sio yeye , lakini alijua kabisa yeye ni binadamu licha ya kwamba alikuwa akifahamika kwa jina la Hades na matatizo yanayomtokea ni kwasababu aliamua kuishi kama binadamu wa kawaida , huenda angeishi kama Hades angeweza kuchukua tahadhari na kuendelea kumfurahisha mke wake hata kama ni kwa kumficha baadhi ya vitu kwa kutumia uwezo wake.

“Umeridhika ? Ndio ulichotaka?”Aliuliza Roma , hakutaka kujua Rufi kafikaje hapo ndani wala ndani ya hoteli hio.

“Ndio! tokea mara ya mwisho tulivyoachana pale hotelini ulionyesha kutonipenda tena , nilidhania ungenitafuta ila ukaamua kunipotezea moja kwa moja na kunifanya niishi kama mgonjwa , hivyo nimeamua kuyafanya maisha yako kuwa magumu”Aliongea kwa Kingereza.

“Tulikubaliana nini , kwanini ukaamua kuvunja ahadi yako?”

“Unachekesha, nani kavunja makubalino?, wewe ndio umeamua kumwambia mkeo ukweli na akanipigia simu kuulizia kuuthibitisha ulitaka mimi nifanyeje”Aliongea kwa Kingereza.

Ijapokuwa ni kweli Rufi alimwambia Edna kuna kitu anapaswa kumwambia , lakini haikumaanisha kwamba ni mahusiano yake na Roma , huenda alitaka kumwambia kitu kingine.

Ukweli ni kwamba Rufi mara baada ya kuona Edna na Roma wanafurahi huku wakiwa na mtoto ambaye alijuwa kabisa ni mtoto wao , alijikuta akijawa na wivu mkali sana , kubwa zaidi ni kitendo cha Roma kumpotezea kabisa tokea walivyo achana.

Kitendo cha kumpigia Edna kwamba kuna kitu anahitaji kumwambia, ulikuwa ni mtego, alijua Edna amepokea simu mbele ya mume wake , hivyo alijua lazima Roma angeweza kuhisi moja kwa moja kile ambacho anakwenda kumwambia hivyo angechukua nafasi ya kumtafuta kabla hajaonana nae.

Yaanni kwa lugha nyepesi Rufi alitaka atumie siri ya kukutana na Roma Marekani kama udhaifu wa kumwendesha Roma , lakini matokeo yake yakawa tofauti , Roma akaweka wazi kila kitu jambo ambalo hakuwa amelitegemea wala kutaka litokee, hivyo baada ya Edna kumpigia simu na kumuuliza swali la uhusiano wake na Roma alishangaa na kuona aliharibu na Roma ameshindwa kuingia kwenye mtego wake hivyo ilibidi kuweka ukweli wazi.

Roma hata yeye alijua Rufi anajaribu kumuigiza mtegoni na ndio maana aliamua kumwambia Edna palepale lakini ndio hivyo ukweli ulikuwa mchungu kwa Edna na kuishia kugombana, lakini alijiambia ni swala ambalo angemalizana na Edna , kwani aliamini hata kama asingemwambia Edna ukweli ungekuja kujulikana tu.

“What will you get out of this?”Aliuliza Roma kwamba angefadika nini.

“Nothing”Alijibu Rufi.

“You’re Crazy woman”Aliongea Roma akimwabia Rufi kwamba ni kichaa.

“Ndio unachosema ni kweli mimi ni Chizi”

“Huogopi nitakuua muda huu?”

“Nilikupatia mwili wangu ukanitoa bikra yangu , unafikiri ninaogopa nini kukupa na maisha yangu?”Aliongea Rufi huku akicheka kwa kejeli.

“Usicheke”Aliongea Roma na palepale alimsogelea kwa spidi na kumshika shingo na kuanza kuiminya , alikuwa na hasira mno lakini alijitahidi kujizuia kwani angeongeza nguvu kuiminya zaidi basi angeivunja palepale.

Rufi alijikuta akianza kukosa hewa na macho yalimtoka huku kile kiini chake cheusi kilianza kupungua ukubwa kwa namna kama kilikuwa kinapotea ndani, Roma alijikuta akimwachia palepale , alishangazwa na kile alichokiona kwenye macho ya Rufi na kujiuliza kwanini amekuwa hivyo ghafla.

“Kwanini umeshindwa kuniua?”Aliuliza Rufi huku akitoa tabasamu la kejeli.

“Nimesema usitabasamu”

“Nataka kutabasamu kwanini unizuie”

“Unaweza kulia ila sio kutabasamu”Aliongea Roma huku akijikuta hasira zikishuka.

“Naomba uniue , siwezi kutabasamu kama nitakuwa nimekufa”Aliongea huku akiwa ametoa tabasamu vilevile lakini wakati huo huo machozi yakimtoka.

Ni ngumu binadamu kutoa machozi huku akionyesha tabasamu na akifanya hivyo ujue ni kwamba tabasamu limeambatana na maumivu makali.

“Wewe mwanamke hukiogopi kifo?”

“Kifo..!!”Aliongea na kuanza kucheka sana kwa zaidi ya dakika moja nzima

“Nimekufa zaidi ya mara elfu moja , kipi kinakufanya uamini naweza kuogopa kifo”Aliongea na kumfanya Roma kuvuta pumzi na kumwangalia.

Ni kweli alijua Rufi hakuwa akiogopa kifo , ukizingatia na maisha yake, kwa sumu iliokuwa ndani ya mwili wake kipindi anakutana nae ilikuwa ni miujiza mikubwa akawa anaendelea kuishi.

“Hutaki kuniua?”

“Sijui kwanini umeamua kuja Tanzania na kuvuruga maisha yangu lakini sitaki kukuona tena , Uhai kwako ni zaidi ya Adhabu kuliko hata ya kifo”Aliongea Roma na kisha alichukua kila kitu chake na kutoka hapo ndani

“Umesema unataka kuniua , lakini ukashindwa kufanya hivyo , umesema huna hisia na mimi lakini ulivyoona mwonekano wangu wakati wakunikaba hasira zako zikaisha … Looh! Wanaume ndio mlivyo siku zote ni waongo sana”Aliongea wakati akiwa ameugeukia mlango

Roma hakutaka kukaa kabisa hapo ndani kwenye hio hoteli , ijapokuwa alikuja na gari akiwa na mke wake na mtoto wake , lakini alikuwa akiondoka peke yake tena kwa mguu , ilihuzunisha lakini hakuwa na jinsi kwa muda huo.

Hakujali sana nini Rufi angefanya zaidi ya hapo lakini hakutaka kujihusha nae tena na alijiambia kwake Rufi ni mwanamke aliejipigia mbususu na kusepa tu na asingeeweza kuwa na mahusiano yoyote.

Huku nyuma muda ule ule Mika alimfuata Rufi akiwa ni mwenye wasiwasi sana .

“Hajakuua?”Aliuliza huku akivuta pumzi nyingi za ahueni na Rufi aliachia tabasamu pana la ushindi.

“Nilikuambia asingeweza kuniua na hukuniamini , tuondoke sitaki kuendelea kubakia hapa”Aliongea na kisha alipiga hatua kueleka upande wa maegesho ya magari na kumfanya Mika kusimama huku akimwangalia Rufi kwa nyuma.

Ijapokuwa Rufi alikuwa na baba mchina lakin umbo halikuwa la kichina , umbo lilikuwa la kitanzania kabisa , hakuwa na umbo kubwa lakini Shepu yake ilijitengeneza vizuri mno , Rufi urembo wake ulikuwa ni wa kipekee , ule ambao haukuwa ukikinasha mbele ya mwanaume rijali.

Mika alimwangalia Rufi na kujikuta akitingisha kichwa na kutabasamu kwa wakati mmoja , alikumbuka na nyumbani kwao baba yake alivyokuwa akimlazimisha Benadetha kuhakikisha anakuwa hata mchepuko wa Roma.

“Baba siwezi kuwa mahusiano na Roma kwani ni mume wa bosi wangu”

“Benadetha naomba unisikilize mimi baba yako , sijali Roma anaweza kukuoa au hatokuoa lakini nataka uwe sehemu ya wanawake zake ikibidi umzalie hata mtoto”

“Baba Benadetha kwanini unamlazimisha mtoto kuwa na mahusinao na mwanaume alieoa?”

“Mke wangu huwezi kunielewa mara moja hata nikikuelezea kila kitu hapa , lakini Roma ni zaidi ya binadamu ambaye mimi Samweli Nguluma lazima nimfanye kuwa ndugu yangu kama ninayahitaji mafanikio”

“Lakini Benadetha hawezi kuwa na mwanaume ambaye hampendi?”

“Hahaha.. mke wangu hebu muulize , akiniambia hampendi Roma nipo tayari kupokea mahali ya mwanaume yoyote”

“Benadetha anayo ongea baba yako ni kweli?”

“Mamaa..!”

“Nipe majibu kama unampenda au humpendi huyo Roma?”

“Mama hata kama nampenda inasaidia nini, kwani mtu mwenyewe siwezi kuwa nae kwenye mahusiano , hii mada sitaki iendelee”Alijibu na kukimbilia ngazi na kwenda chumbani kwake.

“Mke wangu unaona sasa?, Mika hakikisha dada yako anakuwa na mahusiano na Roma”

“Sawa baba”

“Yaani hata siwaelewi , huyu Roma ana nini mpaka mnataka mwanangu awe mchepuko”

“Tunamsaidia Benadetha , kaa nae uongee vizuri la sivyo atazeekea hapa nyumbani bila kuleta mwanaume”

Mika alijikuta akirudi kutoka kwenye mawazo ya mazungumzo ya mama yake na baba yake, ni kweli alikuwa akijua Roma hakuwa mtu wa kawaida kutokana kushuhudia yeye mwenyewe uwezo wake , lakini hakujua kwanini kila mwanamke anamtaka.

Roma hakuchukua hata taksi , alitembea kwenye barabara inayotoka eneo hilo kwa mguu huku akionyesha ni mwenye kuwaza , ilikuwa ni saa kumi za jioni lakini hakuwa na hamu ya kurudi nyumbani kuonana na Edna kwani alijua asingeweza kupata namna ya kumtuliza.

Alitoa simu yake mfukoni na kumpigia Diego na kumpa maagizo ya kuhakikisha Edna anakuwa salama kwa kufuatiliwa kwa ukaribu.

Baaada ya kuwaza namna ya kuimaliza siku hio , alijikuta akijipiga kibao na kukumbuka jambo moja ambalo ni kama amelisahau , wiki iliiopita Clark alimtaarifu amerudi Tanzania lakini hakuwa amemtafuta.

Roma alitafuta usafiri haraka na kuanza safari ya kuelekea Makongo juu na ndani ya dakika chache tu Taksi iliweza kumfikisha na alifunguliwa mlango na mlizi na kisha akaingia ndani.

Baada ya kufika eneo la sebuleni nyumba ilionekana kuwa tulivu kama haikuwa na mtu , lakini mezani aliweza kuona chupa ya maji iliofunguliwa nusu na kuona Clark yupo , alinyoosha moja kwa moja kwenda chini ya maabara na slishangaa kukutana milango ya kwenda chini ya maabara hio ilikuwa wazi.

Wakati anakarribia kufika ndani kabisa ya maabara hio ambayo hakuweza kupata kizuizi cha aina yoyote , alisikia sauti za kudondoka kwa vitu mfululizo zikitokea ndani ya maabara na kumfanya moyo wake kushituka na kuogopa jambo baya kumkuta Clark.

********

Edna mara baada ya kuondoka na Lanlan alienda kusimamisha gari kwenye fukwe maarufu iliokuwa ndani ya Kigamboni , alikuw a na mawazo hivyo hakutaka kuendesha gari mpaka nyumbani akiwa kwenye hali hio.

Eneo lilichangamka kwasababu alikuwa ni Weekend , lakini Edna hakuenda moja kwa moja upande wa mikusanyiko ya watu wengi bali alichagua upande wa hotelini.

Lanlan alifurahi kufika Beach na Edna alimzuia asijichanganye na watu hivyo alisimama akiwa amemshikilia mkono , ilikuwa ahueni, zile hasira zimepungua kutokana na uwepo wa Lanlan lakini mawazo yalikuwa yakimwendesha.

Alitamani kumpotezea moja kwa moja Roma , lakini alivyokuwa akijihisi kwenye moyo wake ni kama hakuwa na uwezo wa kuachana na Roma kabisa , hakuelewa hata yeye imekuwaje akawa hivyo kwani mwaka mmoja uliopita hakuwa ni mwenye kujali kuhusu wanaume zaidi ya kampuni.

Lanlan aliona mama yake alikuwa kwenye mawazo hivyo na yeye alisimama pembeni yake pasipo ya kuongea , alionyesha hali ya kuwa mtiifu.

Wanaume waliokuwepo kwenye hilo eneo waliishia kumwangalia Edna kwa macho ya kimatamanio kuna waliokuwa wakimfahamu na kuna ambao hawakuwa wakimfahamu , gauni la rangi nyeupe na nyeusi lililokuwa na muundo kama wa Dera halikuficha uzuri wake na umbo lake, Lanlan pia uzuri wake aliorithi kwa mama , ulifanya pia wanawake waliokuwa eneo hilo kumwangalia kwa macho ya kumuonea wivu.

Na kuna wale walioenda mbali kwa kumlaumu Mungu kumbariki Edna kwa kila kitu , hela alikuwa nazo , uzuri alikuwa nao na mtoto alikuwa nae mzuri tu.

Licha ya Edna kuangaliwa sana ni kama hakuweza kufahamu kwani alikuwa kwenye mawazo na hakujua pia kwamba uwepo wake hapo ndani uliwafanya watu kukosa amani.

Roma kitendo cha kutoa maagizo ya Edna kulindwa kwa ukaribu kiliwafanya Molin, Adeline na Fanny kuweka umbali wa mita chache na yeye , mbaya zaidi siku hii wote walivalia suti nyeusi na kila mtu alikuwa amekaa upande wake huku wakiwa na Earpices masikioni.

Uwepo wa wazungu eneo hili wakiwa wapo na umakini wa hali ya juu kumlinda Edna ndio uliofanya watu kukosa amani na utulivu na hata baadhi ya watu Edna aliokuwa akiwakaribia walimpisha kwa tahadhari.

Ilikuwa ni tukio la kuvutia na la kushangaza kuona mwaftika kupewa ulinzi na wazungu , ijapokuwa watu hawakushangaa sana kutokana na kwamba Edna alikuwa mwanamke tajiri , lakini swala la wazungu lilikuwa sio la kawaida.

Kwa wale waliokuwa wakifuatilia baadhi ya maswala ya walinzi kwa ukaribu huenda mwafrika alionekana hadharani akilindwa kwa ukaribu na wazungu ni Raisi wa Afrika ya Kati.

Sasa Edna akiwa haelewi kile kilichokuwa kikiendelea hapo ufukweni ghafla tu alishikwa na kizunguzungu kikali sana kilichoambatana na maumivu ya kichwa na alijikuta akikosa balansi na palepale alishuka chini mzima mzima na kupoteza fahamu.

Kitendo kile kiliwafanya Walinzi kumsogelea kwa kasi lakini lilikuwa kosa kubwa ambalo wamelifanya kwani Lanlan aliwachukulia kama maadui na ndio waliomfanya mama yao kudondoka.
Hatariii
 
Back
Top Bottom